Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Genesis 1

Genesis 1:1

Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na nchi

"Hii inahusu jinsi gani Mungu aliumba mbingu na nchi hapo mwanzo." Kauli hii inafupisha sura iliyobaki. Lugha zingine huitafsiri kama "Hapo zamani sana Mungu aliziumba mbingu na nchi."

Hapo mwanzo

Hii inalenga kuanza kwa dunia na kila kitu ndani mwake.

mbingu na nchi

"anga, ardhi, na kila kitu ndani yao"

mbingu

Hapa inamaanisha anga

Bila umbo na tupu

Mungu alikuwa hajaweka dunia katika mpangilio.

vilindi

"maji" au "maji ya kina kirefu" au "maji mengi"

maji

"maji" au "uso wa maji"

Genesis 1:3

Na kuwe na nuru

Hii ni amri. Kwa kuamuru kuwepo na nuru, Mungu alifanya iwepo.

Mungu akaona nuru, kuwa ni njema

"Mungu aliifikiria nuru na kufurahishwa nayo." Hapa "Njema" inamaanisha "kufurahisha" au "inayofaa."

akaigawa nuru na giza

"alitenganisha nuru na giza" au "alifanya kuwepo na nuru wakati mmoja na giza wakati mwingine." Hii inamaanisha Mungu aliumba wakati wa mchana na usiku.

Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza

Mungu alifanya vitu hivi katika siku ya kwanza ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

Genesis 1:6

Na kuwe na anga kati ya maji ...na ligawe

Hizi ni amri. Kwa kuamuru kwamba anga kati ya maji iwepo na igawe maji, Mungu alifanya iwepo na kugawa maji na maji.

anga

"anga tupu na wazi". Watu wa Kiyahudi walichukulia uwazi huu kuwa na umbo kama la kuba au bakuli lililofunikwa.

kati ya maji

"ndani ya maji"

Mungu alifanya anga na kugawanya maji

"kwa namna hii, Mungu alifanya anga na kugawa maji." Mungu alipozungumza, ilitokea. Sentensi hii inaeleza kitu gani Mungu alifanya alipokuwa akizungumza.

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

siku ya pili

Hii inamaanisha siku ya pili ambapo ulimwengu ulipoanza kuwepo.

Genesis 1:9

Maji yaliyo chini ..yakusanyike

Hii inaweza kutafsiriwa kama kitenzi endelevu. Hii ni amri. Kwa kuamuru maji yakusanyike, Mungu aliyafanya yakusanyike pamoja.

na ardhi kavu ionekane

Maji yalikuwa yamefunika ardhi. Basi maji yalisogea pembeni na baadhi ya ardhi kubaki wazi. Hii ni amri. Kwa kuamuru kwamba ardhi kavu ionekane, Mungu alifanya ionekane. "na ardhi kavu ionekane" au "na ardhi kavu iwe wazi" au "na ardhi ifunuliwe"

ardhi kavu

Hii inamaanisha ardhi ambayo haijafunikwa kwa maji. Haimaanishi ardhi ambayo ni kavu sana kwa ajili ya kilimo.

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

nchi

"ardhi" au "chini"

Akaona kuwa ni vyema

Hapa "ni" inamaanisha nchi na bahari.

Genesis 1:11

Na nchi ichipushe mimea

Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba mimea ichipuke juu ya ardhi, Mungu alifanya ichipuke. "Mimea na ichipuke juu ya ardhi" au "Mimea na iote juu ya ardhi"

mimea: miche inayotoa mbegu na miti ya matunda izaayo matunda

"mimea, kila mche unaozaa mbegu na kila mti unaozaa matunda" au "mmea. Kuwe na mimea itoayo mbegu na matunda ya miti yazaayo matunda". Mimea hutumika hapa kama msemo wa jumla inaojumlsiha mimea na miti yote.

miche

Hii ni aina ya mimea ambayo ina mashina laini, na sio kama ya mbao

miti ya matunda izaayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani yake

miti izaayo matunda yenye mbegu ndani yake

kila kitu kwa namna yake

Mbegu zingezaa mimea na miti ambayo ingekuwa kama zile zilipotokea. Kwa namna hii, mimea na miti zingejizalisha zenyewe.

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

Mungu akaona kuwa ni vyema

Hapa "ni" inamaanisha mimea, mazao na miti.

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

siku ya tatu

Hii inamaanisha siku ya tatu ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.

Genesis 1:14

Kuwe na mianga katika anga

Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba mianga iwepo, Mungu alifanya iwepo

mianga katika anga

"vitu ving'aavyo katika anga" au"vitu vitoavyo mwanga katika anga". Hii inaamanisha jua, mwezi na nyota

katika anga

"katika uwazi wa anga" au "katika uwazi mkubwa wa anga"

kutenganisha mchana na usiku

"kutenganisha mchana na usiku." Hii inamaanisha "kutusaidia kutambua tofauti kati ya mchana na usiku." Jua inamaanisha ni mchana, na mwezi na nyota humaanisha ni usiku.

na ziwe kama ishara

Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba ziwe kama ishara, Mungu alizifanya zitumike kama ishara. "Na zitumike kama ishara" au "na zioneshe"

ishara

Hapa inamaanisha kitu kinachofunua au kinacholenga jambo

majira

"Majira" inamaanisha nyakati zitakazotengwa kwa sikukuu na mambo mengine ambayo watu hufanya.

kwa majira, kwa siku na miaka

Jua, mwezi, na nyota huonyesha muendelezo wa muda. Hii inatusaidia kutambua ni wakati gani tukio hutokea kila wiki, mwezi au mwaka.

ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi

Hii ni amri. Kwa kuamuru ziwe mianga juu ya nchi, Mungu alifanya zimulike juu ya nchi

kutoa mwanga juu ya nchi

"kutoa mwanga juu ya nchi" au "kuangazia nchi". Nchi haitoi mwanga yenyewe bali hupata mwanga na kurudisha mwanga.

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

Genesis 1:16

Mungu akafanya mianga mikuu miwili

"Kwa njia hii Mungu akafanya mianga miwili mikuu" Sentensi hii inaelezea Mungu alichofanya alipozungumza.

mianga miwili mikuu

"mianga miwili mikuu" au "mianga miwili ing'aaro". Mianga miwili mikuu ni jua na mwezi.

kutawala mchana

"kuongoza mchana kama mtawala angozapo kundi la watu" au "kuweka alama katika siku"

siku

Hii inamaanisha masaa ya mchana pekee

mwanga mdogo

"mwanga mdogo" au "mwanga hafifu"

katika anga

"katika mbingu" au "katika uwazi wa angani"

kutenganisha mwanga na giza

"kutenganisha mwanga na giza" au "kutoa mwanga kwa kipindi kimoja na giza kwa kingine.

Mungu akaona kuwa ni vyema

Hapa "ni" inamaanisha jua, mwezi na nyota.

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

siku ya nne

Hii inamaanisha siku ya nne ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.

Genesis 1:20

Na maji yajae idadi kubwa ya viumbe hai

Hii ni amri. Kwa kuamuru viumbe hai wajaze maji, Mungu alifanya viwepo. Baadhi ya lugha huweza kuwa na neno moja linalomaanisha aina wote wa samaki na viumbe wa baharini. "Maji yajae viumbe wote" au "viumbe wengi wanao ogelea waishi baharini".

na ndege waruke

Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba ndege waruke, Mungu alifanya waruke.

ndege

"wanyama warukao" au "vitu vinavyoruka"

anga tupu ya angani

"nafasi iliyo wazi ya angani" au "anga"

Mungu aliumba

"kwa njia hii Mungu aliumba"

viumbe wa majini wakubwa

"wanyama wakubwa wanaishi ndani ya bahari"

kwa aina yake

Vitu hai vya "aina" moja ni sawa na kule vilivyotokea.

kila ndege mwenye mabawa

"kila kitu kipaacho chenye mabawa." Iwapo neno kwa ajili ya ndege linatumika, linaweza kuwa kawaida kwa baadhi ya lugha kusema "kila ndege" kwa maana kila ndege ana mabawa.

Mungu akaona kuwa ni vyema

Hapa "ni" inamaanisha ndege na samaki.

Genesis 1:22

akavibariki

"alibariki wanyama aliowaumba"

zaeni na muongezeke

Hii ni baraka ya Mungu. Aliwaambia wanyama wa baharini kuzalisha wanyama wengine wa baharini kama wao wenyewe, ili kwamba wawe wengi baharini. Neno "ongezeka" linafafanua jinsi gani wanapaswa "kuongezeka"

ongezeka

"ongezeka kwa idadi kubwa" au "kuwa wengi"

Ndege waongezeke

Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba ndege waongezeke, Mungu aliwafanya ndege waongezeke.

ndege

"wanyama warukao" au "vitu virukavyo"

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

siku ya tano

Hii inamaanisha siku ya nne ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.

Genesis 1:24

nchi na itoe viumbe hai

"Nchi na itoe vitu hai" au "na viumbe hai vingi viishi juu ya nchi". Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba nchi itoe viumbe hai, Mungu alifanya nchi itoe viumbe hai.

kila kiumbe kwa aina yake

"ili kwamba kila aina ya mnyama izae aina yake zaidi"

mnyama wa kufugwa, vitu vitambaavyo, na wanyama wa nchi

Hii inaonyesha ya kwamba Mungu aliumba kila aina ya wanyama. Iwapo lugha yako inayo namna nyingine ya kuunganisha wanyama wote katika kundi, basi waweza tumia hilo neno, au tumia kundi hili.

mnyama wa kufugwa

"wanyama wanaotunzwa na binadamu"

vitu vitambaavyo

"wanyama wadogo"

wanyama wa nchi

"wanyama mwitu" au "wanyama hatari"

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

Mungu akafanya wanyama wa nchi

"Kwa njia hii Mungu aliwafanya wanyama wa nchi"

Akaona kuwa ni vyema

Hapa "ni" inamaanisha viumbe hai wa nchi.

Genesis 1:26

na tufanye

Hapa neno "tumfanye" lina maana ya Mungu. Mungu alisema alichokusudia kukifanya. Kiwakilishi nomino "tu" ni wingi. Uwezekano wa sababu za wingi ni 1) wingi huu unaweza maanisha Mungu anajadili jambo na malaika ambao hukamilisha baraza lake la mbinguni au 2) wingi huu unaonyesha dalili baadae katika Agano Jipya kuhusisha ya kwamba Mungu yupo katika Utatu Mtakatifu. Baadhi hutafsiri kama "Na nifanye" au "Nitafanya". Kama utafanya hivi, basi zingatia kuweka maandishi mafupi kusema kuwa neno lina wingi.

mtu

"binadamu" au "watu". Neno hili hapa halimaanishi jinsia ya kiume pekee.

katika mfano wetu, wa kufanana na sisi

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza kuwa Mungu alifanya binadamu awe kama yeye. Mstari huu hausemi ni kwa njia zipi Mungu alifanya watu wawe kama yeye. Mungu hana mwili, kwa hiyo haimanishi watu watafanana na Mungu. "na kufanana na sisi".

wawe na mamlaka juu ya

"kutawala" au "kuwa na mamlaka juu"

Mungu akamuumba mtu ...alimuumba

Sentensi hizi mbili zina maana moja na zinasisitiza ya kwamba Mungu aliumba watu katika mfano wake.

Mungu akamuumba mtu

Namna Mungu alivyoumba binadamu ni tofauti na jinsi alivyoumba vitu vingine vyote. Usieleze bayana ya kwamba aliumba binadamu kwa kuongea, kama mistari ya nyuma inavyoonyesha.

Genesis 1:28

Mungu akawabariki

Neno "akawabariki" lina maana ya mwanamume na mwanamke aliowaumba Mungu.

zaeni na kuongezeka

Mungu alimwambia mwanamume na mwanamke kuzalisha watu zaidi kama wao wenyewe ili kwamba wawe wengi kama wao. neno "kuongezeka" linaelezea namna wanavyotakiwa "kuzaa".

Jazeni nchi

jazeni nchi na watu.

Genesis 1:30

Taarifa ya jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza

kila ndege wa angani

"ndege wote wanaopaa angani"

chenye pumzi ya uhai

"kinachopumua". Msemo huu unasisitiza ya kwamba wanyama hawa walikuwa na uhai tofauti na mimea. Mimea haiwezi kupumua, na ilipaswa kutumika kama chakula cha wanyama. Hapa "uhai" una maana ya uhai wa mwili.

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

Tazama

"hasa". Hapa neno "tazama" linaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata.

kikawa chema sana

Mungu alipotazama kila kitu alichokiumba, "kikawa chema sana".

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

siku ya sita

Hii inamaanisha siku ya sita ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.

Genesis 2

Genesis 2:1

mbingu

"anga" au "mbingu"

na viumbe hai vyote vilivyo jaza

"na viumbe hai vingi ambavyo vimo ndani yao" au "na makundi ya viumbe hai vinavyoishi ndani mwao"

zilimalizika

Hii inaweza kutajwa katika njia endelevu "Mungu alimaliza kuviumba"

Siku ya saba Mungu alifikia mwisho wa kazi yake

Mungu hakufanya kazi kabisa katika siku ya saba.

alifikia mwisho wa

Hii ni lahaja. "alikuwa amemaliza"

alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote

"katika siku hiyo hakufanya kazi"

Mungu akaibarikia siku ya saba

Yawezekana maana ni 1) Mungu alisababisha siku ya saba kutoa matokeo mazuri au 2) Mungu alisema ya kwamba siku ya saba ilikuwa nzuri.

na akaitakasa

"na akaiweka kando" au "na kuifanya iwe yake"

katika siku hiyo alipumzika kutoka kwenye kazi yake yote

"katika siku hiyo hakufanya kazi"

Genesis 2:4

Taarifa ya jumla

Sura ya pili iliyobaki ya Mwanzo inaelezea juu ya Mungu alivyoumba watu katika siku ya sita.

Haya yalikuwa ni matukio yahusuyo mbingu na nchi

"Hii ni habari ya mbingu na nchi" au "Hii ni simulizi ya mbingu na nchi" Yawezekana maana ni 1) ni kifupisho cha matukio yaliyoelezwa katika Mwanzo 1:1-2:3 au 2) inakaribisha matukio yaliyoelezwa katika Mwanzo 2.

vilipoumbwa

Yahwe Mungu aliviumba". Katika sura ya 1 mwandishi kila mara anamzungumzia Mungu kama "Mungu", lakini katika sura ya 2 kila mara anamzungumzia Mungu kama "Yahwe Mungu".

katika siku ambayo Yahwe Mungu aliumba

"Yahwe Mungu alipoumba". neno "siku" linamaana ya muda wote wa uumbaji na siyo siku hiyo moja pekee.

Yahwe

Hili ni jina la Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la Kale.

Hapakuwa na msitu wa shambani

hapakuwa na vichaka vimeavyo msituni ambayo wanyama wangeweza kula

hapakuwa na mmea wa shambani

hapakuwa na mimea ya majani kama mboga au mboga za kijani ambazo wanyama na binadamu wangeweza kula

kulima

kufanya kila kitu alichopaswa kufanya ili kwamba mimea iweze kuota vizuri

ukungu

Yawezekana maana yake ni 1) kitu kama umande au ukungu wa asubuhi au 2) chemichemi kutoka mikondo chini ya ardhi.

uso wote wa ardhi

dunia nzima

Genesis 2:7

aliumba

"alifinyanga" au "alifanya" au "aliumba"

mtu ... mtu

"binadanu ... mtu" au "mwanadamu" sio lazima wa kiume.

tundu la pua

"pua yake"

pumzi ya uhai

"pumzi inayofanya vitu kuishi". Hapa "uhai" una maana ya uhai wa mwili.

bustani

Hii yaweza kuwa shamba la miti ya matunda au eneo lenye kila aina ya miti.

upande wa mashariki

"mashariki"

Genesis 2:9

mti wa uzima

"mti unaowapa watu uzima"

uzima

Hapa ina maana "uzima wa milele" au maisha yasiyokuwa na mwisho.

mti wa ujuzi wa mema na mabaya

"mti unaowapa watu uwezo wa kuelewa mema na mabaya" au "mti unaowafanya watu wale matunda yake na kuwafanya kuelewa mema na mabaya"

mema na mabaya

Huu ni msemo ambao una maana mbili tofauti kabisa na kila kitu katikati. "kila kitu kujumlisha yote mema na mabaya"

katikati ya bustani

"katikati ya bustani". Yawezekana miti hii miwili haikuwa katikati ya bustani kabisa.

Mto ukatoka nje ya Edeni kuitia maji bustani

Bustani ilikuwa Edeni. Mto uliendelea kutiririka kutoka Edeni. "Mto ukatoka kupitia Edeni na kumwagilia bustani"

Genesis 2:11

Pishoni

Huu ni wakati pekee ambapo mto huu unatajwa katika Biblia.

nchi yote ya Havila

"nchi yote inaitwa Havila". Ilikuwa mahali katika jangwa la Arabia.

ambapo kuna dhahabu

Msemo huu unatoa taarifa kuhusu Havila. Baadhi ya lugha hutafsiri kwa sentensi nyingine tofauti. "Kuna dhahabu Havila"

pia kuna bedola na jiwe shohamu

Neno "kuna" lipo kwenye sentensi kwa kuonyesha msisitizo. "Hapa pia ni mahali ambapo watu waweza kupata bedola na mawe ya shohamu"

bedola

Utomvu huu hutoka katika mti na hutoa harufu nzuri. Bedola hunata na hutoka katika mti fulani na yaweza kuwaka moto.

jiwe shohamu

"mawe ya shohamu". Shohamu ni aina fulani ya mawe ya urembo.

Genesis 2:13

Gihoni

Hii ni sehemu pekee ya mto huu katika Biblia.

unatiririka kupitia nchi yote ya Kushi

Mto haukufunika nchi yote, lakini ulipanda katika sehemu za nchi.

nchi yote ya Kushi

"nchi nzima inayoitwa Kushi"

ambao unatiririka mashariki mwa Ashuru

"ambao unatiririka katika nchi mashariki mwa mji wa Ashuru." Mto wa Hidekeli unatiririka kutoka kaskazini hadi kusini. Msemo "unatiririka mashariki mwa Ashuru" unatoa taarifa kuhusu mahali mto Hidekeli ulipo. Baadhi ya lugha hutafsiri katika sentensi tofauti. "na hutiririka mashariki mwa Ashuru"

Genesis 2:15

bustani ya Edeni

"bustani iliyokuwa Edeni"

kuilima

"kuilima". Hii ina maana ya kufanya kila kitu cha muhimu ili mimea iweze kuota vizuri.

kuitunza

kuilinda dhidi ya mambo mabaya yanayoweza kuikuta

kutoka kwenye kila mti bustanini

"Tunda katika kila mti la bustani"

wewe

kiwakilishi ni cha kipekee

waweza kula kwa uhuru ...usile

Katika baadhi ya lugha ni kawaida kusema kile ambacho hakiruhusiwi na kisha kusema kile ambacho hakiruhusiwi.

waweza kula kwa uhuru

"waweza kula bila kizuizi"

mti wa ujuzi wa mema na mabaya

"mti unaowapa watu uwezo wa kuelewa mema na mabaya" au "mti unaowafanya watu wanaokula matunda yake kujua mambo mazuri na mambo mabaya.

usile

"sitakuruhusu ule" au "haupaswi kula"

Genesis 2:18

Nitamfanyia msaidizi anaye mfaa

"nitafanya msaidizi ambaye ni sahihi kwa ajili yake"

kila mnyama wa kondeni na kila ndege wa angani

Misemo ya "wa kondeni" na "wa angani" inatuambia mahali ambapo wanyama na ndege hupatikana mara kwa mara. "kila aina ya wanyama na ndege"

wanyama wote

"wanyama wote ambao watu huwachunga"

hapakuwa na msaidizi wa kumfaa yeye

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "hapakuwa na msaidizi aliyekuwa sahihi kwa ajili yake"

Genesis 2:21

akaleta usingizi mzito kwa mtu huyu

"alisababisha mwanamume kulala sana." Usingizi mzito ni wakati ambapo mtu kalala na hawezi kubughudhiwa kirahisi au kuamshwa.

Kwa ubavu ... akafanya mwanamke

"Kutoka ubavuni... alimuumba mwanamke." Ubavu ni nyenzo ambayo Mungu alimuumba mwanamke.

kwa sasa, huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu

"Hatimaye, mifupa ya huyu ni kama ya kwangu, na nyama yake ni kama nyama yangu". Baada ya kutazama miongoni mwa wanyama wote kwa ajili ya mwenzi na kukoswa, hatimaye akamwona mtu kama yeye ambaye angeweza kuwa mwenzi wake. Yawezekana mwanamume alionyesha hisia za faraja na furaha.

nyama

Hii inamaanisha sehemu laini za mwili kama ngozi na msuri.

ataitwa 'mwanamke,' kwa sababu ametwaliwa katika mwanaume

"Neno la Kihebrania la 'mwanamke' linafanana na neno la Kihebrania kwa ajili ya 'mwanamume'.

Genesis 2:24

Taarifa ya jumla

Kinachofuata kimeandikwa na mwandishi. Mwanamume hakusema vitu hivi.

Kwa hiyo

"Hii ni kwa sababu"

mwanaume atawaacha baba yake na mama yake

"mwanamume ataacha kuishi kwenye nyumba ya baba na mama yake." Hii inahusu wanamume kwa ujumla. Hailengi mwanamume fulani katika muda fulani.

watakuwa mwili mmoja

Lugha hii inaongelea tendo la ngono kana kwamba miili inakutana pamoja na kuwa kama mwili mmoja. "miili yao miwili itakuwa mwili mmoja"

Wote wawili walikuwa uchi

Neno "walikuwa" linamaana ya mwanamume na mwanamke ambao Mungu aliwaumba.

uchi

"kutovaa mavazi"

lakini hawakuona aibu

"hawakuona aibu kwa kuwa uchi"

Genesis 3

Genesis 3:1

Sasa

Mwandishi anaanza sehemu mpya ya simulizi.

mwerevu kuliko

"mjanja zaidi" au "mwenye akili ya kupata kile atakacho kwa kusema uongo"

Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile ... bustanini?

Nyoka anajifanya kushangazwa ya kwamba Mungu alitoa sheria hii. Swali hili la balagha laweza kutafsiriwa kama kauli. "Nashangaa ya kwamba Mungu, "Msile ... bustanini."

Msile

Neno "msile" ni wingi na linamaasha mwanamume na mwanamke

Twaweza kula ... Mungu amesema, 'msile'

Hawa alimwambia nyoka ambacho Mungu aliwaruhusu kufanya kwanza na kisha kile Mungu alichowazuia kufanya. Baadhi ya lugha zingesema kile walichozuiwa kufanya kwanza na kisha kusema kile walichoruhusiwa kufanya.

Twaweza kula

"Tunaruhusiwa kula" au "Tunayo ruhusa ya kula"

Msile ... wala ... mtakufa

Neno "msile" ni wingi na linamaasha mwanamume na mwanamke

Msile

"Hampaswi kula" au "Msile"

msiuguse

"na hampaswi kuigusa" au "na msiuguse"

Genesis 3:4

Wewe ... yenu ... hamtakufa

Maneno haya yanamaanisha mwanamume na mwanamke na kwa hiyo yako katika matumizi mawili au wingi.

macho yenu yatafumbuliwa

"macho yenu yatafumbuliwa." Lugha hii ina maana "utakuwa na utambuzi wa mambo." Maana hii yaweza kutajwa wazi. "Itakuwa kana kwamba macho yenu yamefumbuliwa"

mkijua mema na mabaya

Hapa "mema na mabaya" ni msemo ambao unalenga maana zote mbili kabisa na kila kitu katikati. "kujua kila kitu, ikiwemo mema na mabaya"

na kuwa unapendeza macho

"mti ulipendeza kutazama" au"ulikuwa mzuri kuangalia" au "au ulikuwa mzuri sana"

na kwamba mti ulitamanika kwa kumfanya mtu awe mwerevu

"naye alitaka matunda ya mti kwa sababu ingeweza kumfanya mtu awe mwerevu" au "naye alitaka matunda yake kwa sababu yangemfanya kuelewa kipi kizuri na kibaya kama vile Mungu afanyavyo.

Genesis 3:7

Macho ya wote wawili yalifumbuliwa

"Kisha macho yao yakafumbuliwa" au "Wakapata ufahamu" au "Wakaelewa"

Wakashona

"wakakaza" au"wakaunganisha"

majani ya miti

Iwapo watu hawajui majani ya miti yakoje, hii yaweza kutafsiriwa kama "majani makubwa ya mti" au kwa wepesi "majani makubwa"

na wakatengeneza vya kujifunika kwa ajili wao wenyewe

Walifanya hivi kwa sababu walikuwa na aibu. Taarifa hii inayojitokea yaweza kufanywa dhahiri kama itahitajika. "na wakajivika navyo kwa sababu walikuwa na aibu"

majira ya kupoa kwa jua

"katika kipindi hicho cha siku ambapo hewa tulivu huvuma"

kutoka kwa uwepo wa Yahwe Mungu

"kuepuka uwepo wa Yahwe Mungu" au "ili kwamba Yahwe Mungu asiweze kuwaona" au "kutoka kwa Yahwe Mungu"

Genesis 3:9

uko wapi?

"Kwa nini unajaribu kujificha kwangu?" Mungu alijua mwanamume alikuwa wapi. Mwanamume alipojibu, hakusema yupo wapi bali alisema kwa nini amejificha.

"uko"

Katika mstari wa 9 na 11, Mungu alikuwa akizungumza na mwanamume.

nilikusikia

"Nilisikia sauti uliyokuwa unaifanya"

Ni nani alikwambia

Mungu alijua jibu la swali hili. Aliuliza ili kumlazimisha Adamu akiri kuwa hakumtii Mungu.

Je umekula ... kutoka?

Kwa mara nyingine, Mungu alijua kuwa hiki kimetokea. Tafsiri hili swali katika namna ambayo inaonyesha Mungu anamlaumu Adamu kwa kutokutii kwake. Sentensi yaweza kutafsiriwa kwa kauli hii. "Umekula ..kutoka."

Genesis 3:12

Nini hiki ulichofanya?

Mungu alikwishajua ni nini mwanamke alichofanya. Alipouliza swali hili, alikuwa akimpatia nafasi ajieleze kuhusu lile jambo, na alikuwa akionyesha kusikitishwa kwake kwa kile alichokifanya.Lugha nyingi hutumia maswali ya balagha kwa ajili ya kukemea na kukaripia. "Umefanya jambo baya"

Genesis 3:14

umelaaniwa wewe mwenyewe

"wewe peke yako umelaaniwa." Neno "laana" lipo kwanza kwa Kiebrania ili kuweka msisitizo ya tofauti kati ya baraka ya Mungu kwa wanyama na laana juu ya nyoka. Hii ni laana, au namna ambavyo laana zilitamkwa. Kwa kutamka laana hii, Mungu alifanya itokee.

wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni

"wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwitu"

Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda

"Utasogea kwenye ardhi kwa kutumiatumbo lako". Maneno "itakuwa kwa tumbo lako" huja kwanza kuweka msisitizo ya tofauti kati ya njia ya wanyama wengine wanavyosogea kwa kutumia miguu yao na njia ya nyoka atakavyotelezateleza kwa tumbo lake. Hii pia ni sehemu ya laana.

mavumbi utakula

"utakula mavumbi". Maneno "ni mavumbi" huja kwanza kuweka msisitizo ya tofauti kati ya mimea juu ya ardhi ambayo wanyama wengine hula na chakula kichafu cha ardhi ambacho nyoka angekula. Hii ni sehemu ya laana.

uadui kati yako na mwanamke

Hii inamaana ya kwamba nyoka na mwanamke wangekuja kuwa maadui.

uzao

"mtoto" au "kizazi". Neno "uzao" linamaanisha nini mwanamume huweka ndani ya nwanamke kusababisha mtoto kukua ndani ya mwanamke. Kama neno la "mtoto" linaweza kumaanisha zaidi ya mtu mmoja, kama neno "vizazi".

Atakujeruhi ... kisigino chake

Maneno "wako" na "wake" yanamaanisha uzao wa mwanamke. Iwapo "uzao" ulitafsiriwa kwa wingi, hii yaweza tafsiriwa kama "watajeruhi .. visigino vyao"; kwa hali hii, "wao" na "yao" hutumika kutafsiri kiwakilishi kimoja.

Atakujeruhi

"ponda" au "kujeruhi" au "shambulia"

Genesis 3:16

nitaongeza uchungu wako sana

"Nitafanya maumivu yako kuongezeka sana" au "Nitafanya maumivu yako kuwa makali sana"

wakati wa kuzaa watoto

"katika kuzaa watoto" au "utakapozaa watoto"

Tamaa yako itakua kwa mume wako

"Utakuwa na tamaa kubwa kwa mume wako." Maana yake yaweza kuwa 1) "Utataka kuwa na mume wako sana" au 2) "Utataka kumuongoza mume wako"

atakutawala

"atakuwa bwana wako" au "atakuongoza"

Genesis 3:17

Adamu

Jina Adamu ni sawa na jina la Kiebrania kwa ajili ya neno "mwanamume". Baadhi ya tafsiri husema "Adamu" na baadhi husema "mwanamume". Unaweza kusema yoyote kati yao maana hulenga mtu mmoja.

umesikiliza sauti ya mke wako

Hii ni lahaja. "umetii kile mkeo kakuambia"

umekula kutoka katika mti

Unaweza kusema ni nini kile walichokula. "wamekula tunda la mti" au "wamekula sehemu ya matunda ya mti"

usile matunda yake

"Hutakiwi kula kutoka kwake" au "Usile matunda yake"

ardhi imelaaniwa

Neno "laana" hujitokeza kwenye sentensi kuweka msisitizo ya kwamba ardhi, ambayo ilikuwa "nzuri" imekuwa chini ya laana ya Mungu sasa. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Ninalaani ardhi"

kupitia kazi yenye maumivu

"kwa kufanya kazi ngumu"

utakula

Neno "utakula" linamaanisha ardhi ambayo ni ufafanuzi wa sehemu ya mimea, ambayo huota ardhini na watu hula. "utakula kile kiotacho kutoka kwake"

mimea ya shambani

Maana yaweza kuwa 1) "mimea unayoitunza shambani mwako" au 2) "mimea ya mwitu inayoota katika mashamba yako"

Kwa jasho la uso wako

"Kwa kufanya kazi ngumu na kufanya uso kutoka jasho"

utakula mkate

Hapa neno "mkate" ni kiwakilishi kwa chakula kwa ujumla. "utakula chakula"

mpaka utakapo irudia ardhi

"hadi utakapokufa na mwili wako unawekwa ndani ya ardhi." Kwa baadhi ya tamaduni, waliweka miili ya watu waliokufa kwenye shimo ardhini. Kazi ya mwanamume haikamiliki hadi kipindi cha kifo na kuzikwa kwake.

kwa kuwa wewe ni mavumbi na kwenye mavumbi utarudi

Nimekufanya kutoka kwenye udongo, kwa hiyo mwili wako utakuwa udongo tena".

Genesis 3:20

Mwanamume

Baadhi ya tafsiri husema "Adamu".

akaita mke wake jina Hawa

"alimpa mke wake jina la Hawa" au "alimuita mkewe Hawa"

Hawa

Neno Hawa linafanana na neno la Kihebrania lenye maana ya "wenye uhai".

wote wenye uhai

Neno hapa "wenye uhai" linamaanisha watu. "watu wote"

mavazi ya ngozi

"mavazi yanayotengenezwa kwa ngozi ya wanyama"

Genesis 3:22

Mwanamume

Maana yaweza kuwa 1) Mungu alimaanisha binadamu mmoja, mwanamume au 2) Mungu alikuwa akimaanisha binadamu kwa ujumla, kwa hiyo ilimaanisha mwanamume na mke wake. Hata kama Mungu alikuwa akizungumza kuhusu mtu mmoja, alichosema kiliwahusu wote wawili.

kama mmoja wetu

"kama sisi". Kiwakilishi "sisi" ni wingi.

ajuaye mema na mabaya

Hapa "mema na mabaya" ni msemo ambao unamaana ya tofauti zote mbili na kila kitu katikati. "kujua kila kitu, ikiwemo mema na mabaya"

hataruhusiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Sitamruhusu"

mti wa uzima

"mti unaowapa watu uzima"

ardhi ambayo kwahiyo alikuwa ametwaliwa

"ardhi kwa maana alichukuliwa kutoka ardhini". Hii haimaanishi sehemu moja husika katika nchi ambayo Mungu alimchukua.

Kwa hiyo Mungu akamfukuza mtu huyu nje ya bustani

"Mungu alimlazimisha mwanamume aondoke bustanini." Hii inamaanisha tukio la 3:22, ambapo inasema "Yahwe Mungu alimfukuza kwenye bustani ya Edeni". Mungu hakumfukuza mwanamume mara ya pili.

kulima

Hii ina maana kinachohitajika ili mimea iweze kuota vizuri.

ili kulinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima.

"ili kuzuia watu wasiende kwenye mti wa uzima"

upanga wa moto

Maana yaweza kuwa 1) upanga ambao unatoa moto au 2) moto ulikuwa na umbo kama upanga.

Genesis 4

Genesis 4:1

Mwanume

"binadamu" au "Adamu"

akalala na

"akamjua"

nimezaa mwanaume

Neno la "mwanamume" linamuelezea binadamu wa kiume, tofauti na mtoto mchanga au kijana. Kama hiyo italeta kuchanganya, inaweza kutafsiriwa kama "kijana wa kiume" au "mvulana" au "mtoto mchanga wa kiume" au "

Kaini

Watafsiri wanaweza kuweka taarifa fupi ambayo inasema "Jina la Kaini linafanana na neno la Kiebrania linalmaanisha "zaa". Hawa alimuita Kaini kwa sababu alimzaa.

Kisha akazaa

Hatujui ni muda gani ulipita katikati ya kuzaliwa kwa Kaini na Habili. Yawezekana walikuwa mapacha, au Habili alizaliwa baada ya Hawa kupata mimba tena. Kama

alilima

Hii ina maana alifanya kila kitu alichopaswa kufanya ili kwamba mimea iweze kuota vizuri.

Genesis 4:3

Ikawa kwamba

Msemo huu unatumika kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi. Kama lugha yakoin njia ya kufanya hivi, basi tumia njia hii.

baada ya muda

Maana yake yaweza kuwa 1) "baada ya muda kupita" au 2) "kwa muda sahihi"

mazao ya ardhi

Hii inamaanisha chakula kilichotoka kwa mimea aliyoitunza."mazao" au "mavuno"

sehemu zilizonona

Hii inamaanisha sehemu zilizonona za kondoo alizoua, ilikuwa ni sehemu bora zaidi ya mnyama. "baadhi ya sehemu zao zilizonona"

akamkubali

"alipendezwa naye" au "alifurahishwa naye"

alikasirika sana

Baadhi la lugha zina lahaja kwa neno hasira kama "aliwaka" au "hasira yake iliwaka".

ukakunjamana

Hii ina maana muonekano wa uso wake ulionyesha ya kuwa alikuwa amekasirika au ana wivu. Baadhi ya lugha zina lugha ambayo inaelezea sura inavyoonekana anapokuwa na hasira.

Genesis 4:6

kwa nini umekasirika na kwa nini uso wako umekunjamana?

Mungu alitumia maswali haya la balagha kumwambia Kaini ya kwamba hakuwa sahihi kuwa na hasira na kukunjamana sura. Yawezekana yalitumika kumpatia Kaini nafasi ya kutubu makosa yake.

Kama ... je hutapata kibali?

Mungu alitumia swali hili la balagha kumkumbusha Kaini juu ya jambo ambalo Kaini alipaswa kulifahamu. "Unajua ya kwamba ukifanya lilio sahihi, nitakukubali"

lakini kama hutafanya ... inakupasa uishinde

Mungu anazungumzia dhambi kana kwamba ni binadamu. "Lakini kama hutafanya kilicho sahihi, utatamani kufanya dhambi zaidi, na kisha utatenda matendo ya dhambi. Unatakiwa kukataa kuitii"

dhambi iko inakuotea ... kukutawala

Hapa dhambi inazungumziwa kama mnyama mwitu hatari anayesubiri nafasi ya kumshambulia Kaini. "utakuwa na hasira sana utashindwa kuizuia dhambi"

dhambi

Lugha ambazo hazina nomino yenye maana ya "dhambi" zaweza kutafsiri hii kama "tamaa yako kutenda dhambi" au "mambo mabaya unayotaka kufanya".

inakupasa uishinde

Yahwe anazungumzia tamaa ya Kaini kutenda dhambi kana kwamba ni mtu ambaye Kaini anapaswa kumtawala. "unapaswa kuitawala ili usitende dhambi"

Genesis 4:8

Kaini akamwambia Habili ndugu yake

Baadhi ya lugha zinahitaji kuongeza taarifa inayojitokeza ya kwamba Kaini alizungumza na ndugu yake kuhusu kwenda mashambani.

ndugu

Habili alikuwa ndugu yake Kaini. Baadhi ya lugha zinaweza kutumia neno kwa ajili ya "ndugu mdogo"

aliinuka dhidi

"alimshambulia"

Ndugu yako Habili yuko wapi?

Mungu alijua ya kwamba Kaini alimuua Habili, lakini alimuuliza Kaini swali hili ili Kaini aweze kujibu.

Je mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

Kaini alitumia swali hili la balaghaili kukwepa kusema ukweli. Hii yaweza kutafsiriwa katika msemo. "Mimi sio mlinzi wa ndugu yangu!" au "Kumtunza ndugu yangu sio kazi yangu!"

Genesis 4:10

umefanya nini?

Mungu alitumia swali la balagha kumkaripia Kaini. Hii yaweza kutafsiriwa kama msemo. "Ulichofanya ni kibaya"

damu ya ndugu yako inaniita mimi

Damu ya Habili ni lugha kwa ajili ya kifo chake, kana kwamba ni mtu anayemwita Mungu kumuadhibu Kaini. "Damu ya ndugu yako ni kama mtu akiniita kumuadhibu yule aliyemuua"

sasa umelaaniwa wewe kutoka ardhini

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Ninakulaani ili usiweze kuotesha chakula kutoka ardhini"

ambayo imefungua kinywa chake kupokea damu ya ndugu yako

Mungu anazungumzia ardhi kana kwamba ni mtu awezaye kunywa damu ya Habili. "ambayo imelowa kwa damu ya ndugu yako"

kutoka mikononi mwako

Mungu anazungumzia mkono wa Kaini kana kwamba umemwaga damu ya Habili katika "mdomo" wa ardhi. "iliyomwagwa ulipomuua" au "kutoka kwako"

ilima

Hii inamaanisha kufanya kila liwezekanalo ili mimea iweze kuota vizuri.

haita kuzalia wewe nguvu yake

Ardhi inapewa utu kana kwamba ni binadamu anayepoteza nguvu. "ardhi haitakuzalia chakula cha kutosha kwa ajili yako"

mkimbizi na mtu asiye na makao

Unaweza kuunganisha maneno haya pamoja. "mkimbizi asiye na makao"

Genesis 4:13

sitaonekana mbele ya uso wako

Msemo wa "uso wako" unawakilisha uwepo wa Mungu. "Sitaweza kuzungumza na wewe"

mkimbizi na mtu nisiye na makao

mtu asiye na makao

kisasi kitakuwa juu yake mara saba

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nitachukua kisasi juu yake mara saba" au "Nitamuadhibu mtu yule mara saba kwa ukali kama navyokuadhibu"

asimshambulie

"hatamuua Kaini"

Genesis 4:16

akatoka mbele ya uwepo wa Yahwe

Ingawa Yahwe yupo kila mahali, lahaja hii inamzungumzia Kaini kana kwamba alienda mbali sana. "aliondoka kutoka mahali ambapo Yahwe alizungumza naye"

Nodi

Neno Nodi linamaana ya "mkimbizi"

akamjua

akamjua

Akajenga mji

"Kaini akajenga mji"

Genesis 4:18

Kwa Henoko akazaliwa Iradi

Inasemekana ya kwamba Henoko alikuwa na kuoa mwanamke. "Henoko alikua na kuoa na akawa baba kwa mtoto ambaye alimuita Iradi"

Iradi akamzaa Mehuyaeli

"Iradi alipata mtoto na kumuita Mehuyaeli"

Ada ... Sila

majina ya wanawake

Genesis 4:20

Ada ... Sila

majina ya wanawake

alikuwa baba yao na wale walioishi hemani

Maana yake yaweza kuwa 1) "Alikuwa binadamu wa kwanza kuishi hemani" au 2) "Yeye na uzao wake waliishi hemani"

walioishi hemani ambao wanafuga wanyama

watu wanaoishi hemani na kufuga wanyama

alikuwa baba yao na wale wapigao kinubi na filimbi

Maana yake yaweza kuwa 1) "Alikuwa mtu wa kwanza kupiga kinubi na filimbi" au 2) "Yeye na uzao wake walipiga kinubi na filimbi".

Tubal Kaini, mfua vyombo vya shaba na chuma

"Yubal Kaini. alitengeneza vyombo vya shaba na chuma"

chuma

Hii ni metali yenye nguvu sana iliyotumika kutengeneza vyombo, vifaa na silaha.

Genesis 4:23

Ada .. Sila

majina ya wanawake

sikieni sauti yangu ... sikilizeni nisemacho

lameki alisema jambo moja mara mbili kuonyesha msisitizo. Sauti yake ni lugha nyingine kwa utu wake wote. "nisikilizeni kwa makini"

mtu ... kijana

Lameki alimuua mtu mmoja tu

kwa kunijeruhi ... kwa kunichubua

"kwa sababu alinijeruhi ... kwa sababi alinichubua" au "kwa sababu aliniumiza"

Ikiwa Kaini atalipiwa kisasi mara saba, ndipo Lameki

Lameki anajua ya kwamba Mungu atalipa kisasi kwa ajili ya Kaini mara saba. "Kwa maana Mungu atamuadhibu yeyote atakayemuua Kaini mara saba, Lameki"

ndipo Lameki atalipiwa kisasi mara sabini na saba

mara saba - Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "yeyote atakayeniua, Mungu atamuadhibu mara sabini na saba"

sabini na saba

saba - 77

Genesis 4:25

akamjua

akamjua

na akasema, " Mungu amenipatia mtoto mwingine wa kiume

Hii ni sababu ya yeye kumuita Sethi. Hii inaweza kuwekwa dhahiri. "na ikaeleza, 'Mungu amenipa mtoto mwingine'"

Sethi

Hili jina linaonekana kama neno la Kiyahudi lenye maana ya "amenipatia"

Mtoto wa kiume alizaliwa kwa Seth

Hii inaweza kuwekwa dhahiri. "mke wa Sethi alimzalia mtoto wa kiume"

kuliitia jina la Yahwe

Hii ni mara ya kwanza watu wanamuita Mungu kwa jina la Yahwe. Hii inaweza kuwekwa dhahiri. "kumuabudu Mungu kwa kutumia jina la Yahwe"

Genesis 5

Genesis 5:1

Taarifa ya jumla:

Huu ni mwanzo wa orodha ya uzao wa Adamu.

katika mfano

Msemo huu unamaanisha ya kwamba Mungu aliumba binadamu amfanane yeye. Mstari huu hausemi ni kwa namna gani Mungu aliumba wanadamu wawe kama yeye. Mungu hana mwili, kwa hiyo haimaanishi watu wangekuwa kama Mungu. "kuwa kama sisi"

walipoumbwa

Hii inaweza kufanywa katika hali ya kutenda. "alipowaumba"

Genesis 5:3

130 ... mia nane

Watafsiri wanaweza kuandika tarakimu "130" na "800" au maneno "mia moja na thelathini" na "mia nane".

akamzaa mwana katika sura yake

"akamzaa mwana wa kiume"

katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake

Misemo hii miwili inamaana moja. Inatumika kama kumbukumbu ya kwamba Mungu alimuumba binadamu katika mfano wake.

Sethi

Sethi

Akawazaa wana wengi waume na wake

"Akawa na wana zaidi wa kiume na kike"

kisha akafariki

Msemo huu utarudiwa katika sura yote. "Kisha akaafa"

Adamu akaishi miaka 930

Watu walikuwa wakiishi muda mrefu sana. "Adamu aliishi jumla ya miaka 930"

Genesis 5:6

akawa baba wa Enoshi

Hapa "baba" inamaana ya baba mzazi, na sio babu. "akamzaa mwana wake wa kiume Enoshi"

Enoshi

Hili ni jina la mtu

naye akawa baba wa wana wengi waume na wake

"na akawa na wana zaidi wa kiume na kike"

Sethi akaishi miaka 912

"Sethi aliishi jumla ya miaka 912"

kisha akafariki

"Kisha akafa"

Genesis 5:9

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu za Mwanzo 5:6-27 zina mfumo mmoja.

Genesis 5:12

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu za Mwanzo 5:6-27 zina mfumo mmoja.

Genesis 5:15

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu za Mwanzo 5:6-27 zina mfumo mmoja.

Genesis 5:18

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu za Mwanzo 5:6-27 zina mfumo mmoja.

Genesis 5:21

akawa baba wa Methusela

"akapata mwana wake wa kiume Methusela"

Methusela

Hili ni jina la mwanamume

Henoko akaenenda na Mungu

Kuenenda na mtu ni sitiari ya kuwa na uhusiano wa karibu na yeye. "Henoko alikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu" au "Henoko aliishi kwa umoja na Mungu"

Akawa baba wa wana zaidi wa kiume na kike

"Akawa na wana zaidi wa kiume na kike"

Henoko aliishi miaka 365

"Henoko aliishi jumla ya miaka 365"

kisha alitoweka

Neno "alitoweka" linamaanisha Henoko. Hakuwa duniani tena.

kwa kuwa Mungu alimtwaa

Hii inamaana Mungu alimtwaa Henoko awe naye.

Genesis 5:25

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu za Mwanzo 5:6-27 zina mfumo mmoja.

Lameki

Lameki huyu ni tofauti na Lameki wa 4:18

Genesis 5:28

akawa baba wa mwana wa kiume

"akapata mwana wa kiume"

Nuhu

Jina hili linafanana na jina la Kiyahudi lenye maana ya "pumziko".

katika kazi yetu na kutoka katika kazi ya taabu ya mikono yetu

Lameki anasema jambo hilo hilo mara mbili kusisitiza jinsi kazi ilivyo ngumu. "kwa kufanya kazi sana kwa mikono yetu"

Genesis 5:30

Lameki aliishi miaka 595

"Lameki aliishi jumla ya miaka ya 777"

Genesis 5:32

akawa baba wa

"akazaa watoto wake wa kiume". Hii haituambii kama wana wa kiume walizaliwa katika siku moja au mika tofauti.

Shemu, Hamu, na Yafethi

Yawezekana wana hawa wa kiume hawajaorodheshwa kufuata kuzaliwa kwao. Kuna mjadala kuhusu nani alikuwa mkubwa. Epuka kutafsiri haya majina na kuonyesha ya kwamba orodha ipo katika mpangilio wa umri wao.

Genesis 6

Genesis 6:1

Ikawa wakati

Msemo huu unatumika hapa kuonyesha alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

wana wa kike wakazaliwa kwao

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wanawake wakazaa mabinti"

wana wa Mungu

Haipo wazi kama hii inamaanisha viumbe wa mbinguni au wanadamu. Kwa vyovyote vile, walikuwa viumbe ambao Mungu aliumba. Baadhi wanaamini maneno haya yanamaanisha malaika waliomuasi Mungu, yaani, roho chafu au mapepo. Wengine wanadhani hii inamaanisha watawala wa kisiasa wenye nguvu, na wengine wanadhani hii inamaanisha uzao wa Sethi.

roho yangu

Hapa Yahwe anaongelea kuhusu yeye mwenyewe na roho wake, ambaye ni Roho wa Mungu.

nyama

Hii ina maana wana mwili ambayo itakufa siku moja

Wataishi miaka 120

Maana yaweza kuwa 1) urefu wa kawaida wa watu ingepungua hadi miaka 120. "Hawataishi zaidi ya miaka 120" au 2) katika miaka 120 kila mtu atakufa. "Wataishi miaka 120 tu"

Genesis 6:4

Majitu makubwa

warefu sana, watu wakubwa

Hii ilitokea wakati

"Hawa majitu makubwa walizaliwa kwa sababu"

wana wa Mungu

Haipo wazi kama hii inamaanisha viumbe wa mbinguni au wanadamu. Kwa vyovyote vile, walikuwa viumbe ambao Mungu aliumba. Baadhi wanaamini maneno haya yanamaanisha malaika waliomuasi Mungu, yaani, roho chafu au mapepo. Wengine wanadhani hii inamaanisha watawala wa kisiasa wenye nguvu, na wengine wanadhani hii inamaanisha uzao wa Sethi.

Hawa walikuwa watu hodari zamani

"Majitu makubwa walikuwa wanaume hodari walioishi zamani" au "Hawa watoto wakakua kuja kuwa wapiganaji hodari walioishi zamani"

watu hodari

wanaume ambao ni wajasiri na washindi katika vita

watu wenye sifa

"watu maarufu"

Genesis 6:5

mwinamo

"mwelekeo" au "tabia"

mawazo ya mioyo yao

Mwandishi anazungumzia juu ya moyo kana kwamba ni sehemu ya mwili unaofikiri. "mawazo yao ya ndani ya siri"

ikamuhuzunisha moyo wake

Mwandishi anazungumzia juu ya moyo kana kwamba ni sehemu ya mwili unaoweza kuhisi huzuni. "alikuwa na huzuni sana mno juu ya hili"

Genesis 6:7

Nitamfutilia mbali mwanadamu ... katika uso wa nchi

Mwandishi anamzungumzia Mungu kuua watu kana kwamba Mungu alikuwa akisafisha uchafu katika nchi tambarare. "Nitawaangamiza wanadamu ..ili kwamba kusiwepo na watu katika nchi"

Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba

Baadhi ya lugha hutafsiri hii kama sentensi mbili. "Niliumba mwanadamu. Nitamfutilia mbali"

Nitamfutilia

"kuangamiza kabisa". Hapa "kuangamiza" inatumika katika hali ya hasi, kwa maana Mungu anazungumzia juu ya kuangamiza watu kwa sababu ya dhambi yake.

Nuhu akapata neema ya upendeleo machoni pa Yahwe

"Yahwe alimtazama Nuhu kwa upendeleo" au "Yahwe alifurahishwa na Nuhu"

machoni pa Yahwe

Hapa "machoni" inamaana ya mtazamo au mawazo. "katika mtazamo wa Yahwe" au " katika mawazo ya Yahwe"

Genesis 6:9

Taarifa ya Jumla:

Hii inaanza simulizi ya Nuhu, ambayo inayoendelea mpaka kwenye sura ya 9.

Haya yalikuwa matukio yanayomhusu Nuhu

"Hii ni taarifa ya Nuhu"

alitembea na Mungu

Kutembea na mtu ni sitiari ya kuwa na uhusiano wa karibu na yeye. "Nuhu alikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu" au "Nuhu aliishi kwa umoja na Mungu"

Nuhu akafanyika baba wa wana watatu wa kiume

"Nuhu akawa na wana watatu wa kiume" au "Mke wa Nuhu akawa na wana watatu wa kiume"

Shemu, Hamu, na Yafethi.

"Wana wa kiume hawajaorodheshwa katika mpangilio wa kuzaliwa"

Genesis 6:11

Nchi

Maana yaweza kuwa 1) watu walioishi duniani au 2) "Dunia yenyewe"

iliharibika

Watu waliokuwa wakifanya uovu inazungumziwa kana kwamba walikuwa chakula kilichooza. "ilioza" au "ilikua na ouvu sana"

mbele za Mungu

Maana yaweza kuwa 1) "machoni pa Mungu" au 2) "katika uwepo wa Yahwe" kama 4:16.

na ilijaa ghasia

Mwandishi anazungumzia ghasia kana kwamba ni kitu kinachoweza kuwekwa ndani ya chombo na nchi kama chombo. "na kulikuwa na wanadamu wenye vurugu sana nchini" au "kwa sababu ilikuwa imejaa watu waliofanya mambo maovu baina yao"

tazama

Neno "tazama" hapa linatutahadharisha kuwa msikivu kwa taarifa ya kushtukiza inayofuata.

wote wenye mwili

Maana yaweza kuwa 1) wanadamu wote au 2) viumbe vyote vyenye mwili, ikijumlisha wanadamu na wanyama.

wameharibu njia zao

Namna mtu anavyoishi inazungumzwa kana kwamba ilikuwa njia au barabara. "waliacha kuishi kwa njia ambayo Mungu alitaka" au "waliishi katika njia ya uovu"

Genesis 6:13

wenye mwili

Maana yaweza kuwa 1) wanadamu wote au 2) viumbe vyote vyenye mwili, ikijumlisha wanadamu na wanyama.

inchi imejaa ghasia kutokana na wao

"watu nchini kote wana vurugu"

nitawaangamiza wao pamoja na nchi

"Nitawaangamiza wao pamoja na nchi" au "Nitawaangamiza wao nitakapoiangamiza nchi"

safina

Hii inamaanisha sanduku kubwa sana ambalo lingeweza kuelea juu ya maji hata katika dhoruba mbaya. "mtumbwi mkubwa" au "meli" au "tishali"

mti wa mvinje

Watu hawajui haswa huu ulikuwa mti wa aina gani. "mbao iliyotumika kuunda mitumbwi" au "mbao nzuri"

vifunike kwa lami

"sambaza lami juu yake" au "paka lami juu yake". Sababu ya kufanya hivi yaweza kuwekwa wazi: "kufanya isipitishe maji"

lami

Hiki ni kimiminiko chenye mafuta, kizito, na kinatacho ambacho watu huweka nje ya mtumbwi kuzuia maji kupenya katika nafasi za mbao hadi kwenye mtumbwi.

dhiraa

Dhiraa ilikuwa ni namba ya kipimo, kiasi kidogo tu kwa mita moja.

dhiraa mia tatu

"mita 138". Dhiraa mia tatu ni sawa na mita 138"

dhiraa hamsini

"mita ishirini na tatu"

dhiraa thelathini

"mita kumi na nne"

Genesis 6:16

paa la safina

Inawezekana hii lilikuwa paa lililochongeka au lililolala. Kusudi lake lilikuwa kulinda kila kitu ndani ya safina dhidi ya mvua.

dhiraa

Dhiraa ilikuwa ni namba ya kipimo, kiasi kidogo tu kwa mita moja.

ya chini, ya pili na ya tatu

"dari ya chini, ya katikati, na ya juu" au "dari tatu ndani"

dari

"sakafu" au "daraja"

Sikiliza

Mungu alinena hivi ili kusudi kusisitiza ya kuwa angefanya kile alichotarajia kukifanya. "Sikiliza" au "Sikiliza kile nachosema"

nimekaribia kuleta gharika ya maji

"Nimekaribia kutuma mafuriko ya maji" au "ninakaribia kusababisha mafuriko"

mwili wote

Hapa "mwili" inawakilisha viumbe vyote vya mwili, kujumlisha binadamu na wanyama.

wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai

Hapa "pumzi" inawakilisha uhai. "inayoishi"

Genesis 6:18

nitalifanya thabiti agano langu na wewe

"fanya agano kati yako na mimi"

na wewe

pamoja na Nuhu

Utaingia ndani ya safina

"Utaingia ndani ya safina" Baadhi ya tafsiri husema "Utaingia ndani mwa safina".

Kwa kila kiumbe hai chenye mwili, viwili vya kila aina utavileta ndani ya safina

"Unapaswa kuleta aina mbili ya kila aina ya kiumbe ndani ya safina"

kiumbe

mnyama ambaye Mungu aliumba

chenye mwili

Maana yaweza kuwa 1) wanadamu wote au 2) viumbe vyote vyenye mwili, ikijumlisha wanadamu na wanyama.

Genesis 6:20

kwa jinsi yake

"wa kila aina tofauti"

kitambaacho ardhini

Hii inamaana ya wanyama wadogo ambao hutambaa juu ya ardhi

viwili vya kila aina

Hii inamaana ya ain mbili ya kila aina ya ndege na mnyama.

viwe salama

"ili uweze kuwaweka wawe hai"

kwako ... kwa ajili yako .. chako

Hii inamaana ya Nuhu na ni katika umoja

chakula kinacholiwa

"chakula ambacho watu na wanyama hula"

Kwa hiyo Nuhu akafanya hivi. kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya

Sentensi hizi mbili zinamaanisha jambo moja. Sentensi ya pili inafafanua ya kwanza na kuweka msisitizo ya kwamba Nuhu alimtii Mungu. Sentensi hizi zilizo sambamba zinaweza kuunganishwa kuwa kitu kimoja. "Kwa hiyo Nuhu alifanya kila kitu alichoambiwa na Mungu kufanya"

Genesis 7

Genesis 7:1

Taarifa ya jumla:

Matukio ya sura hii yanatokea baadaya Nuhu kujenga safina, kukusanya chakula, na kukiweka ndani ya safina.

Njoo ...katika safina ...utakuja nao

"Ingia ... ndani ya safina .. chukua". Tafsiri nyingi husema "Nenda .. ndani ya safina .. chukua"

wewe

Neno hapa "wewe" linamaana ya Nuhu la lipo katika umoja.

nyumba yako

"familia yako"

mwenye haki mbele yangu

Hii inamaana ya kwamba Mungu alimwona Nuhu kuwa mwenye haki.

katika kizazi hiki

Hii inamaana ya watu wote ambao walikuwa wakiishi katika muda huo. "Kati ya watu wote wanaoishi sasa"

mnyama aliye safi

Huyu alikuwa ni myama ambaye Mungu aliruhusu watu wake wamle na kutoa sadaka.

wanyama wasio safi

Hawa ni wanyama ambao Mungu hakuruhusu watu wale au kutoa sadaka.

kuhifadhi kizazi chao

"ili kwamba waweze kuwa na kizazi kitakachoishi" au "ili kwamba, baada ya gharika, wanyama waendelee kuishi"

Genesis 7:4

siku arobaini mchana na usiku

Hii ilikuwa siku arobaini kamili. Haikuwa jumla ua siku themanini. "siku arobaini mchana na usiku"

hai

Hii inamaana ya uhai wa mwili

Genesis 7:6

Taarifa ya jumla

Mistari ya 6-12 inarudia kwa mara ya pili na kutoa kwa utondoti jinsi gani Nuhu alivyoinbgia ndani ya safina na familia yake pamoja na wanyama katika 7:1. Hili sio tukio jipya.

ilipokuja juu ya nchi

"ilipotokea" au "ikaja juu ya nchi"

kwa sababu ya maji ya gharika

"kwa sababu ya gharika itakayokuja" au "kutoroka maji ya gharika"

Genesis 7:8

Taarifa ya jumla:

Mistari ya 6-12 inarudia kwa mara ya pili na kutoa kwa utondoti jinsi gani Nuhu alivyoinbgia ndani ya safina na familia yake pamoja na wanyama katika 7:1. Hili sio tukio jipya.

Wanyama ambao ni safi

Hawa walikuwa wanyama ambao Mungu aliruhusu watu wake kuwala na kuwatoa kama sadaka kwake.

wanyama ambao si safi

Hawa walikuwa wanyama ambao Mungu hakuruhusu watu wake wale au kuwato kama sadaka kwake.

wawili wawili

Wanyama waliingia kwenye safina katika makundi ya dume mmoja na jike mmoja.

Ikawa kwamba

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama kuhusu tukio muhimu katika simulizi hii. Mwanzo wa gharika.

baada ya zile siku saba

"baadaya siku saba" au"siku saba baadaye"

maji ya gharika yakaja juu ya nchi

Habari inayojitokeza, "ikaanza kunyesha" inaweza kufanywa kuwa wazi. "ikaanza kunyesha na maji ya gharika yakaja juu ya nchi"

Genesis 7:11

Taarifa ya jumla:

Mistari ya 6-12 inarudia kwa mara ya pili na kutoa kwa utondoti jinsi gani Nuhu alivyoinbgia ndani ya safina na familia yake pamoja na wanyama katika 7:1. Hili sio tukio jipya.

Katika mwaka wa mia sita wa maisha yake Nuhu

"Nuhu alipokuwa na umri wa miaka 600"

mwezi wa pili, katika siku ya kumi na saba ya mwezi

Kwa kuwa Musa aliandika kitabu hiki, inawezekana inamaanisha mwezi wa pili katika kalenda ya Kiebrania. Lakini hii haina uhakika

katika siku iyo hiyo

Hii ina maana siku bayana ambapo mvua ilianza. Msemo huu unasisitiza jinsi gani matukio yote makubwa yalivyotokea haraka muda ulipowadia.

chemchemi zote za vilindi vikuu zilipasuka na kufunguka

"maji kutoka chini ya ardhi yalifunguka juu kwenye sakafu ya nchi"

vilindi vikuu

Hii ina maana ya bahari ambalo inasadikiwa lilikuwa chini ya ardhi.

madirisha ya mbinguni yakafunguka

Hii ina maana ya mvua. Inaelezea anga kama dari ambalo hutunza maji juu yake kutodondoka ardhini. Madirisha, au milango, ya anga yalipofunguliwa, maji yalifunguka chini kupitia kwao. "anga ikafungua" au "milango ya anga ikafunguka"

mvua

Mvua kubwa

Genesis 7:13

Taarifa ya jumla

Mistari ya 13-18 inarudia kwa mara ya tatu na kutoa kwa undani kuhusu jinsi gani Nuhu aliingia katika safina pamoja na familia yake na wanyama katika 7:1. Hili si tukio jipya.

Katika siku iyo hiyo

"Katika siku hiyo hasa". Hii ina maana ya siku ambayo mvua ilianza kunyesha. Mistari ya 13-16 inaeleza Nuhu alichofanya kabla tu ya mvua kuanza.

mnyama wa mwitu ... mnyama wa kufugwa ... kila kitambaacho ... ndege

Vikundi hivi vinne vinaorodheshwa kuonyesha ya kwamba kila aina ya mnyama alijumuishwa.

kila kitambaacho

Hii ina maana ya wanyama watambaao juu ya ardhi, kama wanyama wagugunaji, wadudu, mjusi na nyoka.

kwa jinsi yake

"ili kwamba kila aina ya mnyama azalishe zaidi ya kila aina yake"

Genesis 7:15

Taarifa ya Jumla:

Mistari ya 13-18 inarudia kwa mara ya tatu na kutoa ufafanuzi zaidi jinsi gani Nuhu aliingia katika safina pamoja na familia yake na wanyama. Hili sio tukio.

Viwili viwili katika kila chenye mwili

Hapa "mwili" inawakilisha wanyama.

ambacho kilikuwa na pumzi ya uhai

Hapa "pumzi" inawakilisha uhai. "alivyoishi"

kilikuja kwa Nuhu

Neno "kilikuja" linaweza kutafsiriwa kama "alikwenda".

wote wenye mwili

Hapa "mwili" inawakilisha wanyama. "katika kila aina ya mnyama"

akawafungia

Maana kamili yaweza kutajwa wazi. "walipoingia ndani ya safina"

Genesis 7:17

Taarifa ya Jumla:

Mistari ya 13-18 inarudia kwa mara ya tatu na kutoa ufafanuzi zaidi jinsi gani Nuhu aliingia katika safina pamoja na familia yake na wanyama. Hili sio tukio.

na maji yakaongezeka

Hii ilitokea katika kipindi cha siku arobaini wakati maji yalipokuwa yakija. "na maji yakawa na kina kirefu sana"

na kuinua safina

"na ikasababisha safina kuelea"

kuinua juu ya nchi

inasababisha safina kuinuka juu ya nchi" au "safina ilielea juu ya maji ya kina kirefu"

Genesis 7:19

Maji yakaongezeka zaidi juu ya nchi

"Maji yalishinda kabisa nchi"

dhiraa kumi na tano

"mita sita"

Genesis 7:21

vilitembea juu

"vilisogea kote kote" au "vilitangatanga"

viumbe hai vyote kwa wingi vilivyoishi juu ya nchi

Hii ina maanisha wanyama wote wanatembea kote kote juu ya nchi kwa makundi makubwa.

vilivyo pumua pumzi ya uhai kwa njia ya pua

Hapa "pua" inawakilisha mnyama mzima au mwanadamu. "kila mtu apumuaye"

pumzi ya uhai

Maneno "pumzi"na "uhai" yanawakilisha nguvu inayosababisha watu na wanadamu kuwa na uhai.

vilikufa

Hii ina maana kifo cha kimwili

Genesis 7:23

Hivyo kila kilichokuwa hai ... kilifutwa

Ikiwezekana, hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kwa hiyo kila kiumbe hai ... kikatoweka" au "Kwa hiyo gharika iliangamiza kabisa kila kiumbe hai"

Vyote viliangamizwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu aliwaangamiza wote"

kutoka kwenye nchi

"kwa hiyo hawakuwa katika nchi"

na wale waliokuwa naye

"na watu pamoja na wanyama waliokuwa naye"

walisalia

"walibaki" au "waliishi" au"walibaki hai"

Maji yalitawala nchi

"Maji yenye kina kirefu yalifunika nchi yote" au "Maji yalibaki na gharika kubwa juu ya nchi"

Genesis 8

Genesis 8:1

akamtazama

"akamkumbuka" au "alimfikiria"

safina

Hii inamaanisha sanduku kubwa sana ambalo lingeweza kuelea juu ya maji hata katika dhoruba mbaya. "mtumbwi mkubwa" au "meli" au "tishali"

Chemichemi za vilindi pamoja na madirisha ya mbingu vikafungwa

"Maji yaliacha kutoka chini ya ardhi na mvua zikaacha kunyesha." Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu alifunga chemichemi za vilindi na madirisha ya mbinguni"

chemichemi za vilindi

"maji kutoka chini ya ardhi"

madirisha ya mbingu vikafungwa

Hii ina maana ya mvua kuacha kunyesha. Hii ina maana ya mvua. Inaelezea anga kama dari ambalo hutunza maji juu yake kutodondoka ardhini. Madirisha, au milango, ya anga yalipofunguliwa, maji yalifunguka chini kupitia kwao. "anga ikafungua" au "milango ya anga ikafunguka"

Genesis 8:4

ikatulia

"ikatua" au "ikasimama juu ya ardhi ngumu"

katika mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya ... mwezi wa kumi

Kwa sababu Musa aliandika kitabu hiki, inawezekana ana maana ya mwezi wa saba na mwezi wa kumu kwa kalenda ya Kihebrania, lakini hii haipo wazi.

Katika siku ya kwanza ya mwezi

"Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kumi"

vikaonekana

Hii inaweza kuwekwa wazi: "ikaonekana juu ya uso wa maji"

Genesis 8:6

Ikatokea kwamba

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi. "Ikawa kwamba"

Ikatokea kwamba ... dirisha la safina ambayo aliitengeneza

Msemo "ambayo alitengeneza" unazungumzia kuhusu madirisha. Baadhi ya lugha zaweza kufanya msemo huu kuwa sentensi tofauti. "Nuhu alitengeneza dirisha katika safina. Ikaja kuwa baada ya siku arobaini ndipo dirisha likafunguliwa"

kunguru

ndege mweusi anayekula zaidi nyama ya mizoga ya wanyama

akaruka mbele na nyuma

Hii ina maana ya kwamba kunguru aliendelea kuacha safina na kurejea.

hadi maji yalipo kauka

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "hadi pale upepo ulipokausha maji" au "hadi maji yalipokauka"

Genesis 8:8

kutua unyayo wake

"kutua" au "kutulia juu ya". Ina maana ya kutua juu ya kitu ili kupumzika kupaa.

unyayo wake ... akarudi ... akamchukua

Neno "njiwa" kwa lugha ya mwandishi ni la kike. Unaweza kutafsiri msemo huu na kiwakilishi cha "hiki ... huyu ... hii" au "yake ... yeye ... yeye" kulingana na namna gani lugha inamfafanua njiwa.

Akanyoosha ... naye

Ukitumia kiwakilishi cha kiume kwa neno "njiwa" inaweza kuhitaji kuongeza jina la Nuhu ili kukwepa mchanganyo. "Nuhu alimtuma njiwa," "Nuhu alinyosha mkono wake mbele" n.k.

Genesis 8:10

Tazama

"Sikiliza kwa makini" au "Hii ni muhimu"

jani bichi la mzeituni lililochumwa

"jani ambalo njiwa alichuma kutoka katika mzeituni"

lililochumwa

"kunyofoa"

Akasubiri siku saba zingine

"Alisubiri tena siku saba"

Njiwa hakurudi kwake tena

Iwapo watu hawataelewa unaweza kutoa sababu wazi: "Hakurudi tena kwake kwa sababu alipata sehemu ya kutua".

Genesis 8:13

Ikawa kwamba

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

katika mwaka wa mia sita na mwaka wa kwanza

"Nuhu alipokuwa na umri wa miaka 601"

mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi

Kwa sababu Musa aliandika kitabu hiki, inawezekana ana maana ya mwezi wa saba na mwezi wa kumu kwa kalenda ya Kiebrania, lakini hii haipo wazi.

maji yalikuwa yamekauka katika nchi

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "maji yaliyofunika nchi yalikauka" au "upepo ulikausha maji yaliyofunika nchi"

kifuniko cha safina

Hii ina maana ya kifuniko kilichozuia maji ya mvua kuingia ndani ya safina.

tazama

Neno "tazama" linatuambia kuwa makini kwa ajili ya taarifa muhimu inayafuatia.

Katika mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi

siku ya saba ya mwezi - "Katika siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili." Hii inaweza kuwa na maana ya mwezi wa pili katika kalenda ya Kihebrania, lakini haipo wazi.

nchi ilikuwa imekauka

"ardhi ilikuwa imekauka kabisa"

Genesis 8:15

Toka nje ... 17Wachukuwe

"Ondoka ...Chukua" Baadhi ya tafsiri husoma "Njoo nje ... Leta nje".

kila kiumbe hai chenye mwili

"kila aina ya kiumbe hai" Maana yaweza kuwa 1) wanadamu wote au 2) viumbe vyote vyenye mwili, ikijumlisha wanadamu na wanyama.

kwa kuzaliana na kuongezeka

Hii ni lahaja. Jazeni nchi na watu. Mungu alitaka wanadamu na wanyama kuzaliana, ili waweze kuwa wengi wa aina yao.

Genesis 8:18

Nuhu akatoka nje

Baadhi ya tafsiri husoma "Nuhu akaja nje"

kwa kabila zao

"katika makundi ya aina yao wenyewe"

Genesis 8:20

akajenga madhabahu kwa Yahwe

"akajenga madhabahu kwa makusudi ya Yahwe" au "akajenga madhabahu kwa ajili ya kumuabudu Yahwe." Inawezekana alijenga kwa mawe.

wanyama walio safi ... ndege walio safi

Hapa "safi" ina maana ya kwamba Mungu aliruhusu wanyama hawa kutumika kama sadaka. Baadha ya wanyama hawakutumika kwa ajili ya sadaka na waliitwa "wasio safi".

kutoa sadaka ya kuteketezwa

Nuhu aliwaua wanyama na kuwachoma kabisa kama sadaka kwa Mungu. "aliwachoma wanyama kama sadaka kwa Yahwe"

harufu nzuri ya kuridhisha

Hii ina maana ya harufu nzuri ya nyama ya kuchomwa.

akasema moyoni mwake

Hapa neno la "moyo" lina maana ya mawazo na hisia za Mungu.

laani ardhi

"kuleta madhara makubwa kwenye nchi"

kwa sababu ya mwanadamu

Hii inaweza kuwa wazi: "kwa sababu mwanadamu ni mwenye dhambi"

nia za mioyo yao ni mbaya tokea utoto

"kutoka miaka yao ya utotoni wanakuwa wakifanya mambo maovu" au "walipokuwa wadogo, walitaka kufanya mambo maovu"

nia za mioyo yao

Hapa neno "mioyo" lina maana ya mawazo, hisia, haja na ridhaa ya watu. "mwelekeo wao" au "tabia yao"

tokea utoto

Hii ina maana ya mtoto mwenye umri mkubwa. "kutoka ujana wao"

Wakati nchi isaliapo

"wakati nchi inapoendelea kudumu" au "Kadri nchi inavyoendelea kuwepo"

majira ya kupanda mbegu

"msimu wa kupanda"

baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi

Misemo hii miwili ina maana ya aina mbili za majira katika mwaka.

kiangazi

kipindi kikavu na cha joto cha mwaka

majira ya baridi

kipindi cha baridi kidogo na theluji katika mwaka

havitakoma

"havitaacha kuwepo" au "havitaacha kutendeka" . Hii inaweza kuelezwa katika hali ya chanya. "vitaendelea"

Genesis 9

Genesis 9:1

Zaeni, mkaongezeke, na muijaze nchi

Hii ni baraka ya Mungu. Alimwambia Nuhu pamoja na familia yake kuzaliana wanadamu wengine kama wao, ili kwamba wawe wengi wa aina yao. Neno "mkaongezeke" linafafanua jinsi gani wanapaswa "kuzaana"

Hofu na utisho wenu vitakuwa juu ya kila mnyama aliye hai ... na juu ya samaki wote wa baharini

Mwandishi anazungumzia hofu na utisho kana kwamba ni vitu vya mwili ambavyo vingeweza kuwa juu ya wanyama. "Kila mnyama hai ... na samaki wote wa baharini watakua na hofu kubwa sana juu yako"

Hofu na utisho wenu

maneno "hofu" na "utisho" zina maana moja na husisitiza jinsi wanyama walivyokuwa wanaogopa binadamu. "Hofu ya utisho kwako" au "Hofu ya kutisha kwako"

kila mnyama aliye hai juu ya nchi

Hili ni moja kati ya makundi manne ya wanyama ambayo mwandishi ameorodhesha, na sio ufupisho wa wanyama waliosalia atakaowataja hapo baadae

ndege

Huu ni msemo wa jumla kwa vitu vinavyopaa. "wanyama warukao" au "vitu vinavyoruka"

juu ya kila kitu kiendacho chini juu ya ardhi

Hii inajumuisha aina yote ya wanyama.

Vimetolewa katika mikono yenu

Mkono ni lugha mbadala kwa mamlaka ambayo mkono ulikuwa nayo. Hii inaweza kuwa katika hali ya kutenda. "Vimetolewa katika mamlaka yako" au "Nimeviweka chini ya mamlaka yako"

Genesis 9:3

Taarifa ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu pamoja na watoto wake.

uhai ... damu

"Damu ni alama ya uhai". "Mungu alikuwa akiwaamuru watu wasile nyama ambayo bado ina damu ndani yake. Walipaswa kutoa kwanza damu"

Genesis 9:5

Taarifa ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu pamoja na watoto wake.

Lakini kwa ajili ya damu yenu

Hii inatofautisha damu ya mwanadamu na damu ya wanyama

kwa ajili ya damu yenu

Inaonyesha ya kwamba damu imemwagwa, au imemwagika, au mwagikia. "iwapo yeyote atasababisha damu yako kumwagika" au "iwapo yeyote atamwaga damu yako" au "iwapo yeyote atakuua"

uhai

Hii ina maana ya uhai wa mwili.

nitataka malipo

Malipo haya yana maana kifo kwa yule muuaji, sio fedha. "Nitataka yeyote atakayekuua kulipa"

Kutoka katika mkono

Hapa neno "mkono" lina maana ya yule mtu anayehusika na jambo kutendeka.

Kutoka katika mkono wa kila mnyama nitaitaka

"Nitataka mnyama yeyote atakayetoa uhai wako kulipa"

Kutoka katika mkono wa kila mtu, yaani, kutoka katika mkono wa yule ambaye amemuua ndugu yake, nitataka fidia kwa ajili ya uhai wa mtu huyo.

"Nitataka mtut yeyote atakayetoa uhai wa mtu mwingine kulipa"

Kutoka katika mkono

Msemo huu una maana ya mtu katika hali ya ukaribu sana. "Kutoka kwa mtu huyo kabisa"

ndugu

Hapa "ndugu" inatumika kama kumbukumbu ya jumla kwa jamaa, kama wanajumuiya wa kabila moja, ukoo au kikundi cha watu.

Yeyote amwagaye damu ya mtu, kwa njia ya mtu damu yake itamwagwa

Kumwaga kwa damu ni sitiari kwa ajili ya kuua mtu. Hii ina maanisha kama mtu atamuua mtu, mtu mwingine anapaswa kumuua muuaji. japokuwa, "damu" ina umuhimu sana katika kipengele hichi na inapaswa kutumiwa katika tafsiri ikiwezekana.

kwa sababu ilikuwa ni katika mfano wa Mungu kwamba Mungu alimuumba mtu

"kwa sababu Mungu aliumba watu wafanane na yeye" au "kwa sababu niliumba watu katika mfano wangu"

zaeni na kuongezeka

Hii ni baraka ya Mungu. Alimwambia Nuhu na familia yake kuzaa wanadamu wengine kama wao wenyewe, ili kusudi waweze kuwa wengi zaidi. Neno "kuongezeka" linafafanua jinsi ya wao "kuzaa"

Genesis 9:8

Kisha Mungu akazungumza na Nuhu na wanae pamoja naye

Mungu alikuwa akizungumza nao tayari. Msemo huu unaweka alama ya mabadiliko juu ya kile Mungu alichokuwa akienda kukizungumzia. "Mungu aliendelea kuzungumza na Nuhu pamoja na watoto wake" au "Kisha Mungu akaendelea kusema"

Kwa ajili yangu

Msemo huu unatumika kwa Kiingereza kuweka alama ya mabadiliko juu ya kile Mungu alichokuwa akizungumzia juu ya Nuhu na wanawe walichopaswa kufanya na kuzungumzia juu ya nini Mungu angefanya.

kulithibitisha agano langu pamoja nawe

"fanya agano kati yako na mimi"

Genesis 9:11

Maelezo ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu na wanawe.

ninalithibitisha agano langu pamoja nanyi

"kwa kusema hivi, ninafanya agano langu pamoja na wewe"

mwili

Maana zaweza kuwa 1) binadamu wote au 2) wenye viumbe wote, kujumlisha binadamu na wanyama.

Tena hapatatokea gharika ya kuangamiza nchi

"Hakutakuwa tena na gharika ambalo litaangamiza nchi". Kutakuwa na gharika, lakini hazitaangamiza dunia nzima.

ishara

Hii ina maana ya ukumbusho wa jambo lililoahidiwa.

agano ... kwa vizazi vyote vya baadaye

Agano hili linamhusu Nuhu na familia yake na pia vizazi vyote vitakavyofuata.

Genesis 9:14

Maelezo ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu na wanawe.

itakuwa nitakapoleta

"Itakapokuwa". Ni jambo ambalo hutokea mara nyingi.

upinde wa mvua ukaonekana

Haipo wazi ni nani atauona upinde wa mvua, lakini kwa sababu agano upo kati ya Yahwe na watu, iwapo utataka kusema nani atauona upinde wa mvua, ni vyema kuwataja wote Yahwe na watu. Hii inaweza kutafsiriwa katika hali ya kutenda. "watu pamoja na mimi tunauona upinde wa mvua"

upinde wa mvua

mstari wa rangi wenye mwanga unaojitokeza katika mvua ambapo jua hungaa kutoka nyuma ya mtazamaji.

nitakumbuka agano langu

Hii haimaanishi ya kwamba Mungu angesahau kwanza. "Nitafikiria juu ya agano langu"

yangu na ninyi

Neno "ninyi" ni wingi. Mungu anazungumza na Nuhu na wana wa Nuhu.

kila kiumbe hai cha wote mwenye mwili

"kila aina na kiumbe hai"

mwenye mwili

Maana zaweza kuwa 1) binadamu wote au 2) wenye viumbe wote wenye mwili, kujumlisha binadamu na wanyama.

Genesis 9:16

Maelezo ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu na wanawe.

ili kukumbuka

"ili kwamba nikumbuke" au "ili kwamba nitafikiria juu ya"

kati ya Mungu na kila kiumbe

Mungu anazungumza hapa. "kati yangu na kila kiumbe hai"

kila kiumbe hai cha wote wenye mwili

"kila aina ya kiumbe hai"

Kisha Mungu akamwambia Nuhu

Mungu alikuwa tayari anazungumza na Nuhu. Msemo huu unaweka alama ya sehemu ya mwisho ya kile Mngu alichokuwa akisema. "Mungu alimalizia kwa kusema kwa Nuhu" au "Kwa hiyo Mungu akasema kwa Nuhu"

Genesis 9:18

Maelezo ya Jumla

Mistari ya 18-19 inatambulisha wana watatu wa Nuhu, ambao watakuwa sehemu muhimu katika simulizi ifuatayo.

baba

Hamu alikuwa baba wa Kaanani wa halisi.

Genesis 9:20

mkulima

"mtu wa ardhi"

akalewa

"alikunywa divai nyingi sana"

uchi

Maandishi haisemi jinsi gani mwili wa Nuhu ulikuwa uchi alipokuwa amelala kalewa. Mapokeo ya wanawe yalionyesha ya kwamba ilikuwa suala la aibu.

Genesis 9:22

baba yake

Hii ina maana ya Nuhu.

Genesis 9:24

Maelezo ya Jumla:

Katika mistari ya 25-27 Nuhu anatamka laana juu ya mwana wa Hamu na baraka juu ya ndugu za hamu. Kile alichokisema Nuhu juu yao pia iliwahusu uzao wao.

Maelezo ya Jumla:

Misemo tofauti katika mistari hii inakusudiwa kuonyesha ya kwamba hii ilikuwa shairi.

alipozinduka kutoka katika ulevi wake

"akawa mtulivu"

mtoto wake mdogo

Hii ina maana ya Hamu. "mwanawe mdogo, Hamu"

Alaaniwe Kanaani

"Ninakulaani Kaanani" au "Na mambo mabaya yafanyike kwako Kaanani"

Kanaani

Huyu alikuwa mmoja wa wana wa Hamu. "mwana wa Hamu Kaanani"

mtumishi kwa watumishi wa ndugu zake

"mtumishi wa chini wa kaka zake" au "mtumishi mwenye umuhimu wa chini kabisa kati ya ndugu zake"

ndugu zake

Hii inaweza kumaanisha ndugu zake Kaanani au ndugu zake kwa ujumla.

Genesis 9:26

Maelezo ya Jumla:

Hii ni shairi.

Yahwe , Mungu wa Shemu, abarikiwe

"Yahwe na asifiwe, Mungu wa Shemu" au "Yahwe, Mungu wa Shemu, anastahili sifa" au "Ninamsifu Yahwe, Mungu wa Shemu"

Kanaani na awe mtumishi wake

"Na Kaanani awe mtumishi wa Shemu". Hii inajumlisha uzao wa Kaanani na Shemu.

Mungu na apanue mipaka ya Yafethi

Maana zaweza kuwa 1) "Mungu na afanya mipaka ya Yafethi mikubwa" au 2) "Mungu na asababishe Yafethi kuwa na uzao mwingi"

na afanye makazi yake katika hema za Shemu

"na mfanye aishi kwa amani na Shemu". Hii inajumlisha uzao wa Yafethi na Shemu.

Kanaani na awe mtumishi wake

"Na Kaanani awe mtumishi wa Yafethi". Hii inajumlisha uzao wa Kaanani na Yafethi.

Genesis 10

Genesis 10:1

Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya wana wa Nuhu

"Hii ni habari ya wana wa Nuhu." Sentensi hii inatambulisha habari ya vizazi vya Nuhu katika Mwanzo 10:1-11:9

Genesis 10:2

Kutoka kwa hawa watu wa pwani waligawanyika na

"Wana wa yafethi na vizazi vyake waligawanyika na kuhamia pwani na visiwani"

watu wa pwani

Hii ina maana ya watu waliokuwa wakiishi kando ya pwani na visiwani.

ardhi zao

"makazi yao". Hizi ni sehemu ambazo watu waliohama waliishi.

kila mtu na lugha yake

"Kila kundi la watu lilizungumza lugha yake" au " Makundi ya watu walijigawa kulingana na lugha zao"

Genesis 10:6

Misraimu

Misraimu ni jina la Kihebrania la "Misri".

Genesis 10:8

hodari

Maana zaweza kuwa 1) "hodari mwenye nguvu" au 2) "mwanamume mwenye nguvu" au 3) "mtawala mwenye uwezo".

mbele za Yahwe

Maana zaweza kuwa 1) "machoni pa Yahwe" au 2) "kwa msaada wa Yahwe"

Hii ndiyo sababu hunenwa

Hii inatambulisha methali. Lugha yako yaweza tambulisha methali na misemo kwa namna tofauti. "Hii ni sababu watu husema"

Miji ya kwanza

Maana zaweza kuwa 1) miji ya kwanza aliyoijenga au 2) miji muhimu.

Genesis 10:11

alikwenda Ashuru

Nimrodi alikwenda Ashuru

Misraimu akawa

orodha ya vizazi vya Nuhu inaendelea.

Misraimu

Misraimu alikuwa mmoja wa wana wa Hamu. Vizazi vyake vikawa watu wa Misri. Misraimu ni jina la Kihebrania la Misri.

Genesis 10:15

Myebusi ... Mwamori ... Mgirgashi

Majina haya yana maana ya makundi makubwa ya watu walioshuka kutoka Kanaani.

Genesis 10:19

mpaka

"eneo" au "mpaka wa eneo"

ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza

Mwelekeo wa kusini waweza elezwa wazi kama itahitajika. "Kutoka mji wa Sidoni magharibi hata mji wa Gaza, ambao uko karibu na Gerari"

na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha

Mwelekeo ni "mashariki" au "bara" inaweza kuelezwa wazi kama itahitajika. "kisha mashariki mwa miji ya Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hata Lasha"

Hawa walikuwa wana wa Hamu

Neno "hawa" lina maana ya watu na makundi ya watu waliorodhoshwa katika mistari ya 10:6

kwa lugha zao

"waligawanyika kulingana na lugha zao tofauti"

katika ardhi zao

"katika makazi yao"

Genesis 10:24

Arfaksadi

Arfaksadi alikuwa mmoja wa wana wa Shemu.

Pelegi

Jina Pelegi lina maana ya "mgawanyiko"

nchi iligawanyika

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "watu wa duniani walijigawa wenyewe" au "watu wa duniani waligawanyika kati yao" au "Mungu aligawanya watu wa duniani"

Genesis 10:26

Yoktani

Yoktani alikuwa mmoja wa wana wa kiume wa Eberi.

Hawa

Hapa "hawa" ina maana ya wana wa kiume wa Yoktani.

Genesis 10:30

Mpaka wao

"ardhi walioitawala" au "ardhi walipoishi"

Hawa walikuwa wana wa Shemu

Neno "hawa" ina maana ya vizazi vya Shemu.

Genesis 10:32

Hizi zilikuwa koo

Hii inarudi nyuma kwa watu wote waliorodheshwa katika 10:1

kulingana na

"imeorodheshwa kwa"

kwa hawa mataifa yaligawanyika na kwenda juu ya nchi

"kutoka kwa koo hizi mataifa yaligawanyika na kusambaa nchini kote" au "Koo hizi ziligawanyika baina yao na kuunda mataifa ya dunia"

baada ya gharika

Hii inaweza kuelezwa dhahiri au kwa uwazi zaidi. "baada ya gharika kuangamiza nchi"

Genesis 11

Genesis 11:1

Sasa

Neno hili linaonyesha kuwa mwandishi anaanza sehemu mpya ya simulizi.

nchi yote

watu wote juu ya nchi

inatumia lugha moja na ilikua na usemi mmoja

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza ya kwamba watu wote walizungumza lugha moja.

waliposafiri

"walihama" au "sogea pande zote"

upande wa mashariki

Yawezekana maana ni 1) "mashariki" au 2) "kutoka mashariki" au 3) "kuelekea mashariki". Chaguo linalofaa ni "mashariki" kwa sababu Shinari ipo upande wa mashariki ambapo wasomi wanaamini safina ilikuja kutulia.

wakakaa

waliacha kusogea kutoka sehemu moja hadi nyingine na wakaanza kuishi sehemu moja.

Genesis 11:3

haya njooni

"haya njooni"

tuyachome kikamilifu

Watu hutengeneza matofali kwa udongo na kuyachoma ndani ya joko la moto sana ili yawe magumu na imara.

lami

kimiminiko kinene, kinachonata, cheusi kinachotoka ardhini.

chokaa

hiki ni kiini kinene kinachoundwa kwa unga wa ndimu, udongo, mchanga, na maji inayotumika kufanya mawe au matofali kugandamana.

tujifanyie jina

"tujifanyie sifa yetu kuwa kubwa"

jina

"sifa"

tutatawanyika

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "tutajigawanya baina yetu na kuishi sehemu tofauti"

Genesis 11:5

wazao wa Ibrahimu

"watu"

akashuka

Habari kuhusu mahali aliposhuka inaweza kuwekwa wazi. "akashuka kutoka mbinguni". Hii haielezi jinsi gani alishuka kutoka mbinguni.

kuona

"angalia kwa makini" au "kutazama kwa makini zaidi"

watu hawa ni taifa moja na lugha moja

Watu wote walikuwa katika kundi moja kubwa na wote walizungumza lugha moja.

wanaanza kufanya hivi

Yawezekana maana kuwa 1) "wameaanza kufanya hivi" ikimaanisha ya kwamba wameanza kujenga mnara lakini haijakamilika au 2)"hili ni jambo la kwanza walilofanya", ikimaanisha ya kwamba katika siku za usoni watafanya mambo makubwa zaidi.

halitashindikana jambo watakalo kusudia kulifanya

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kila jambo wanalikusudia kufanya litawezekana kwao"

Haya! Njooni

"haya! njooni"

tushuke

Neno "tushuke" ni wingi ingawa ina maana ya Mungu. Tafsiri zingine husema "na nishuke" au "nitashuka"

tuvuruge lugha yao

Hii ina maana ya kwamba Yahwe angesababisha watu wote wa nchi kukoma kuzungumza lugha moja. "kuchanganya lugha yao"

ili kwamba wasielewane

Hii ilikuwa lengo la kuchanganya lugha yao. "ili kwamba wasiweze kuelewa kile mwingine anachokisema"

Genesis 11:8

kutoka pale

"kutoka katika mji"

jina lake ukaitwa Babeli, kwa sababu hapo Yahwe alivuruga

Jina la "Babeli" linaonekana kama neno lenye maana ya "kuchanganyikiwa"

alivuruga lugha ya nchi yote

Ina maana ya kwamba Yahwe alisababisha watu wote katika nchi kutozungumza lugha moja. "alichanganya lugha ya nchi yote"

Genesis 11:10

Taarifa ya jumla

Sura iliyosalia inaorodhesha mtiririko wa vizazi vya Shemu mpaka vya Abramu.

Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Shemu

Sentensi hii inaanza orodha ya vizazi vya Shemu.

gharika

Hii ilikuwa gharika kutoka kipindi cha Nuhu ambapo watu walikuwa waovu sana mpaka Mungu akatuma gharika nchi yote kufunika nchi.

akawa baba wa Alfaksadi

"akapata mwana wake wa kiume Alfaksadi" au "mwana wake wa kiume Alfaksadi alizaliwa"

Alfaksadi

jina la mwanamume

mia moja ... miwili ... mia tano

Watafsiri wanaweza kuandika maneno au namba "100", "2", and "500".

Genesis 11:12

akawa baba wa Shela

"mwana wa kiume wake Shela alizaliwa"

Shela

jina la mwanamume

Genesis 11:14

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu katika Mwanzo 11:12-25 zilikuwa na mfumo huo huo.

Genesis 11:16

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu katika Mwanzo 11:12-25 zilikuwa na mfumo huo huo.

Genesis 11:18

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu katika Mwanzo 11:12-25 zilikuwa na mfumo huo huo.

Genesis 11:20

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu katika Mwanzo 11:12-25 zilikuwa na mfumo huo huo.

Genesis 11:22

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu katika Mwanzo 11:12-25 zilikuwa na mfumo huo huo.

Genesis 11:24

Taarifa ya Jumla:

Kumbukumbu katika Mwanzo 11:12-25 zilikuwa na mfumo huo huo.

Abramu, Nahori, na Harani

Hatujui mpangilio wa kuzaliwa kwa watoto wake.

Genesis 11:27

Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Tera

Sentensi hii inatambulisha habari ya vizazi vya Tera. Mwanzo 11:27-25:11 unazungumzia kuhusu vizazi vya Tera, mahsusi mwanae Abrahamu. "Hii ni habari ya vizazi vya Tera"

Harani akafa machoni pa baba yake Tera

Hii ina maana ya kwamba Harani alikufa wakati baba yake akiwa hai. "Harani alikufa wakati baba yake, Tera, alipokuwa naye"

Genesis 11:29

wakajitwalia wake

"akaoa wake"

Iska

hili ni jina la kike

Sasa

Neno hili linatumiwa kutambulisha habari mpya kuhusu Sarai ambayo itakuwa muhimu baadae katika sura.

tasa

Lugha hii inaelezea mwanamke ambaye kimwili hawezi kutunga mimba au kuzaa mtoto.

Genesis 11:31

akamtwaa

Hapa neno "mwana wa" lina maana ya Tera.

Sarai mkwewe, mke wa mwanawe Abramu

mkwewe, mwanawe mke wa Abramu - "mkwe wa Sarai, ambaye alikuwa mke wa mwanawe Abramu.

Harani ... Harani

Haya ni majina mawili tofauti na yanaandikwa tofauti Kihebrania. Moja lina maana ya mtu na lingine lina maana ya mji.

Genesis 12

Genesis 12:1

Sasa

Neno hili linatumika kuweka alama sehemu mpya ya simulizi.

Nenda utoke katika nchi yako, na toka kwa ndugu zako

"Nenda kutoka nchini kwako, kutoka katika familia yako"

Nitakufanya uwe taifa kubwa

Hapa "nitakufanya" ni umoja na ina maana ya Abramu, lakini Abramu anawakilisha vizazi vyake. "Nitaanzisha taifa kubwa kupitia kwako" au "Nitawafanya vizazi vyako kuwa taifa kubwa"

na kulifanya jina lako kuwa kubwa

Neno "jina" linawakilisha sifa ya mtu. "na kukufanya uwe maarufu"

na utafanyika baraka

neno "jina" linawakilisha sifa ya mtu. "na kukufanya uwe maarufu"

asiye kuheshimu nita mlaani

"Nitamlaani yeyote atakayekutendea jambo kwa njia ya aibu" au "iwapo kuna mtu atakayekutendea jambo lisilofaa, nitamlaani"

Kupitia kwako familia zote za nchi zitabarikiwa

Hii inaweza kufanywa katika hali ya kutenda. "Nitabariki familia za nchi kupitia kwako"

Kupitia kwako

"Kwa sababu yako" au "Kwa sababu nimekubariki"

Genesis 12:4

walivyomiliki

Hii inajumlisha wanyama na mali isiyokuwa na uhai

Watu ambao wamewapata

Maana yaweza kuwa 1) "watumwa ambao wamewakusanya" au 2) "watu ambao wamewakusanya kuwa pamoja nao"

Genesis 12:6

Abramu akapitia katikati ya nchi

Ni jina la Abramu pekee linatajwa kwa sababu alikuwa kichwa cha familia. Mungu alimpatia amri ya kuchukua familia yake na kwenda kule. "Kwa hiyo Abramu na familia yake walikwenda katikati ya nchi"

nchi

"nchi ya Kanaani"

mwaloni wa More

Yawezekana More ilikuwa jina ya sehemu

Yahwe aliyemtokea Abramu

"Yahwe, kwa sababu alimtokea"

Genesis 12:8

alipiga hema yake

Abramu alikuwa na watu wengi pamoja naye alipokuwa akisafiri. Watu waliokuwa wakihama kutoka sehemu moja hadi nyingine waliishi ndani ya mahema. "walitengeneza mahema yao"

kuliitia jina la Yahwe

"waliomba kwa jina la Yahwe" au "kumuabudu Yahwe"

Kisha Abram akaendelea kusafiri

"Kisha Abramu alichukua hema lake na kuendelea na safari"

upande wa Negebu

"kuelekea eneo la Negebu" au "kuelekea kusini" au "kusini ya jangwa la Negebu"

Genesis 12:10

Kulikuwa na njaa

Mazao hayakuota vizuri msimu huo.

katika nchi

"katika eneo" au "katika nchi ambapo Abramu alikuwa akiishi"

akaenda chini kuingia

Maana zaweza kuwa 1) "alikwenda kusini zaidi" au 2) "aliondoka mbali na Kaanani kuingia". Ingependeza kutafsiri kwa kutumia maneno ya kawaida ya kutoka eneo la juu kuelekea eneo la chini.

wataniua mimi ... wewe hai

Sababu watakayomuua Abramu inaweza kufanywa wazi. "wataniua ili kwamba wakuoe"

ili kwamba niwe salama kwa sababu yako

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ili kwamba, kwa sababu yako, hawataniua mimi"

Genesis 12:14

Ikawa kwamba

Maana zaweza kuwa 1) Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya wapi tukio linaanza, na kama lugha yako ina namna ya kufanya hivi basi tumia njia hiyo, au 2) "Na hivyo ndivyo kilichotokea"

Wakuu wa Farao wakamuona

"Wakuu wa Farao walimwona Sarai" au "wakuu wa Farao walimwona"

mwanamke akachukuliwa kupelekwa nyumbani mwa Farao

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Farao akamchukua mpaka nyumbani kwake" au "Farao aliwaamuru askari wake kumpeleka nyumbani kwake"

mwanamke

Sarai

nyumbani mwa Farao

Maana zaweza kuwa 1)"Familia ya Farao", yaani kama mke au 2) "Nyumba ya Farao" au "Hekalu la Farao" ni tasifida ya Farao kumfanya awe mmoja wa wake zake.

kwa ajili yake

"kwa ajili ya Sarai" au "kwa sababu yake"

Genesis 12:17

kwa sababau ya Sarai, mke wa Abramu

Hii inaweza kufanywa kwa uwazi zaidi. "Kwa kuwa Farao alitaka kumchua Sarai , mke wa Abramu, aweze kuwa mke wake mwenyewe"

Farao akamwita Abramu

"Farao akamuita Abramu" au "Farao akamuamuru Abramu kuja kwake"

Nini hiki ambacho umenifanyia?

Farao alitumia lugha hii ya balagha kuonyesha jinsi gani alivyokasirika juu ya kile Abramu alichomfanyia. Inaweza kuelezeka kwa namna ya mshangao. "Umedanya jambo baya kwangu!"

Kisha Farao akatoa amri kwa watu wake kuhusiana naye

"Kisha Farao akawaongoza wakuu wake kuhusu Abramu"

na wakamuondoa, yeye pamoja na mke wake na vyote alivyokuwa navyo

"na wakuu wakamfukuza Abramu kutoka kwa Farao, pamoja na mke wake na alivyokuwa navyo"

Genesis 13

Genesis 13:1

akaondoka kutoka

"kwenda" au "kuondoka kutoka"

akaenda Negebu

Negebu ilikuwa ni eneo la jangwa kusini mwa Kanaani, magharibi mwa Misri. Hii inaweza kufanywa kwa uwazi. "akarudi katika jangwa la Negebu"

Abram alikuwa tajiri wa wanyama, fedha na dhahabu

"Abramu alikuwa na wanyama wengi, fedha nyingi na dhahabu nyingi"

wanyama

"mifugo" au "ng'ombe"

Genesis 13:3

Aliendelea na safari yake

Abramu na familia yake walisafiri kwa hatua, kwenda kutoka sehemu hadi sehemu. Hii inaweza kufanywa wazi. "Waliendelea na safari yao"

mahali ambapo hema yake ilikuwa tangu mwanzo

Watafsiri wanaweza kuweka maandishi machache yanayosema "Tazama Mwanzo 12:8." Muda wa safari yake unaweza kuwekwa wazi. "katika eneo alipotenga hema lake kabla hajakwenda Misri"

akaliitia jina la Yahwe

"aliomba katika jina la Yahwe" au"alimuabudu Yahwe"

Genesis 13:5

Sasa

Neno hili linatumika kuonyesha kitakachofuatia ni taarifa ya nyuma kumsaidia msomaji kuelewa matukio yatakayofuata.

Nchi haikuwatosha wote

Hapakuwa na ardhi ya kutosha ya malisho na maji kwa ajili ya wanyama wao.

mali zao

Hii inajumuisha mifugo, ambayo inahitaji malisho na maji.

hawakuweza kukaa pamoja

"hawakuweza kuishi pamoja"

Wakanaani pamoja na Waperizi walikuwa wakiishi katika nchi ile wakati huo

Hii ni sababu nyingine ya nchi kutoweza kuwahimili wote.

Genesis 13:8

Pasiwe na ugomvi kati yako na mimi,

"Tusigombane"

ugomvi

"chuki" au "ugomvi" au "malumbano"

na kati ya wachunga wanyama wako na wachunga wanyama wangu

"na tuwazuie wanaume wanaochunga wanyama wetu kulumbana"

licha ya hayo sisi ni familia

"kwa sababu sisi ni familia"

familia

"ndugu" au "jamaa". Lutu alikuwa mpwa wa Abramu.

Je nchi hii yote haiko mbele yako?

Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa katika hali ya chanya. "nchi nzima ipo wazi kwa matumizi yako"

Nenda na ujitenge na mimi

Abrahamu alizungumza kwa huruma na Lutu na kumtia moyo afanye jambo litakalowasaidia wote. "Tugawanyike".

Ikiwa utakwenda kulia, mimi nitakwenda kushoto

Maana zaweza kuwa 1) "ukienda njia moja, basi na mimi nitaenda njia nyingine" au 2) "ukienda kaskazini, nitaenda kusini." Abramu alimruhusu Lutu kuchagua sehemu ya nchi aliyoitaka, na Abramu angechukua kile kilichobaki.

Genesis 13:10

nchi yote tambarare ya Yorodani

Hii ina maana ya eneo la jumla la mto Yordani.

ilikuwa na maji kila mahali

"ilikuwa na maji mengi"

kama vile bustani ya Yahwe, na kama nchi ya Misri

"kama bustani ya Yahwe au kama nchi ya Misri". Haya yalikuwa maeneo mawili tofauti.

bustani ya Yahwe

Hili ni jina lingine kwa bustani ya Edeni.

bustani

Hii yaweza kuwa shamba la miti ya matunda au eneo lenye kila aina ya miti.

Hii ilikuwa ni kabla Yahwe hajaiangamiza Sodoma na Gomora

Hii inatazamia jambo litakalotokea baadae. Hapa ni muhimu kwa sababu inaeleza kwa nini Lutu alikaa katika eneo ambalo baadae halikuwa na mbolea.

ndugu

"ndugu wa karibu" au "familia". Hii ina maana ya Lutu na Abramu pamoja na nyumba zao.

Genesis 13:12

akaishi

"akatulia" au "akakaa"

nchi ya Kanaani

"nchi ya watu wa Kanaani"

Akatandaza hema zake hadi Sodoma

Maana zaweza kuwa 1) "alitandaza mahema yake karibu na Sodoma" au 2) "Alisogeza mahema yake kuzunguka eneo lililofika hadi Sodoma".

Genesis 13:14

baada ya Lutu kuondoka kwake

"baada ya Lutu kumuacha Abrahamu"

Genesis 13:16

tembea katika urefu na upana wa nchi hii,

"kutembea tembea juu ya ardhi nzima"

Mamre

Hii ilikuwa jina la mwanamume aliyemiliki miti ya mwaloni.

Hebroni

jina la sehemu

madhabahu ya Yahwe

"dhabahu la kumuabudu Yahwe"

Genesis 14

Genesis 14:1

Taarifa ya Jumla:

Maeneno katika 14:1 yote ni miji inayojitegemea

ikaja kuwa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

katika siku

"katika muda wa"

walifanya vita

"walienda vitani" au "walianzisha vita" au "walijiandaa kwa vita"

Genesis 14:3

Hawa wafalme watano wa mwisho waliungana pamoja

Taarifa ya kwamba majeshi yao walikuwa pamoja nao inaweza kuwekwa wazi. "Wafalme hawa watano wa nyuma na majeshi yao waliungana"

miaka kumi na mbili walimtumikia

Matukio katika mistari ya 4-7 yalitokea kabla ya mstari wa 3. Lugha yakoinaweza kuwa na namna ya kuonyesha hivi.

walimtumikia Kedorlaoma

Inawezekana walitakiwa kumlipa kodi na kumtumikia jeshini. "walikuwa chini ya utawala wa Kedorlaoma"

waliasi

"walikataa kumtumikia" au "walisitisha kumtumika"

walikuja na kuwashambulia

Walifanya hivi kwa sababu wafalme wengine waliasi.

Warefai ... Wazuzi ... Waemi ... Wahori

Haya ni majina ya makundi ya watu.

Ashteroth Karnaimu ... Hamu ... Shawe Kiriathaimu ... Seiri ...El Parani

Haya ni majina ya sehemu.

El Parani iliyo karibu na jangwa

Huu msemo unasaidia wasomaji kuelewa El parani ilikuwa wapi. Inaweza kutafsiriwa katika sentensi tofauti kama italazimu. "El Parani. El Parani ipo karibu na jangwa"

Genesis 14:7

Taarifa ya Jumla:

Mistari ya 8 na 9 inarudia kile kilichosemwa katika 14:3 na kuendelea kueleza yaliyojiri baada ya wafalme kukutana pamoja kupigana.

wakarudi wakaja

Neno "wakarudi" lina maana ya wafalme wanne wageni ambao walikuwa wakishambulia eneo la Kanaani. Majina yao yalikuwa Amrafeli, Arioko, Kadorlaoma na Tidali. "wakageuka na kuondoka"

Waamori ambao waliishi Hasasoni Tamari

Msemo huu unaelezea juu ya watu wa Waamori walioshindwa. Hawa walikuwa Waamori wengine walioishi katika maeneno mengine.

na mfalme wa Bela (pia ikiitwa Soari)

Mji wa Bela pia ulikuwa unaitwa Soari. Taarifa hii inaweza kuwekwa mwishoni mwa sentensi. "na mfalme wa Bela akaondoka na kujiandaa kwa vita. Bela pia inaitwa Soari.

kujiandaa kwa vita

"kujiunga vitani" au "kuanza mistari ya vita" Baadhi ya watafsiri wanaweza kusema kuwa majeshi yalipigana.

afme wanne dhidi ya wale watano

Kwa kuwa wafalme watano waliorodheshwa kwanza, baadhi ya lugha inaweza kutafsiri hii kama "wafalme watano dhidi ya wanne".

Genesis 14:10

Sasa

Neno hili linatambulisha taarifa ya nyuma kuhusu bonde la Sidimu. Lugha yako inaweza kuwa na njia nyingine ya kutambulisha taarifa hii ya nyuma.

lilikuwa limejaa mashimo ya lami

"ilikuwa na mashimo ya lami mengi". Haya yalikuwa mashimo katika ardhi ambayo yalikuwa na lami ndani mwao.

lami

kimiminiko kinene, kinachonata, cheusi kinachotoka ardhini.

wafalme wa Sodoma na Gomora

Huu ni usemi mwingine kwa ajili ya wafalme na majeshi yao. "wafalme wa Sodoma na Gomora na majeshi yao"

wakaanguka pale

Maana zaweza kuwa 1) baadhi ya wanajeshi wao walianguka ndani ya mashimo ya lami au 2) wafalme wenyewe walianguka ndani ya mashimo ya lami. Kwa kuwa 14:17 unasema ya kwamba mfalme wa Sodoma alikwenda kukutana na Abramu, maana ya kwanza yaweza kuwa sahihi zaidi.

Wale waliosalia

"Wale ambao hawakufa vitani na hawakuanguka ndani ya mashimo"

adui

Hii ina maana ya mfalme Kedorlaoma na wafalme wengine na majeshi yao aliokuwa nao waliokuwa wakishambulia Sodoma na Gomora.

mali zote za Sodoma na Gomora

Maneno "Sodoma" na "Gomora" ni lugha nyingine kwa ajili ya watu walioishi katika miji ile. "utajiri wa watu wa Sodoma na Gomora" au "mali za watu wa Sodoma na Gomora"

vyakula vyao vyote

"chakula na vinywaji vyao"

wakaenda zao

"wakaenda njia zao"

wakamchukua pia Lutu, mtoto wa ndugu yake na Abramu ambaye aliishi Sodoma, pamoja na mali zake zote

Misemo ya "mwana wa kaka wa Abramu" na "aliyekuwa akiishi Sodoma" unamkumbusha msomaji juu ya mambo yaliyoandikwa mapema kuhus Lutu. "walimchukua Lutu pia, pamoja na na mali zake zote. Lutu alikuwa mwana wa kaka wa Abramu na alikuwa akiishi Sodoma kwa kipindi hicho"

Genesis 14:13

Mmoja ambaye alitoroka alikuja

"Mwanamume alitoroka vitani na kuja"

Alikuwa anaishi

"Abramu alikuwa anaishi" Hii inatambulisha taarifa ya nyuma.

walikuwa washirika wa Abram

"walikuwa washirika wa mkataba na Abramu" au "alikuwa na makubaliano ya amani na Abramu"

ndugu yake

Hii inahusu mpwa wa Abramu Lutu

wanaume waliofunzwa

"wanamume waliofunzwa kupigana"

wanaume waliozaliwa nyumbani mwake

"wanamume waliozaliwa nyumbani mwa Abramu". Walikuwa watoto wa watumishi wa Abramu.

akawafukuza

"akawafukuza"

Dani

Huu ni mji wa kaskazini wa Kanaani, mbali ya kambi ya Abramu.

Genesis 14:15

Akawagawanya watu wake dhidi yao usiku na kuwavamia

Yawezekana hii ina maana ya mipango ya vita. "Abramu aliwagawa wanamume katika makundi kadhaa, na wakawashambulia maadui zao katika pande zote"

mali zote

Hii ina maana ya vitu ambavyo maadui waliiba kutoka miji ya Sodoma na Gomora.

mali zake

"na mali za Lutu ambazo maadui waliiba kutoka kwa Lutu"

pamoja na wanawake na watu wengine

"pamoja na wanawake na watu wengine ambao wafalme wanne waliwakamata"

Genesis 14:17

kurudi

Taarifa inayodokezwa kuhusu wapi alipokuwa anarudi inaweza kuwekwa wazi. "alirudi hadi pale alipokuwa akiishi"

Melkizedeki, mfalme wa Salemu

Hii ni mara ya kwanza mfalme huyu anatajwa.

mkate na divai

Watu hula mkate na divai mara kwa mara.

Genesis 14:19

Alimbariki

Mfalme Melkizedeki alimbariki Abramu.

Abarikiwea Abramu na Mungu aliye juu sana, muumba wa mbingu na nchi

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na nchi, ambariki Abramu"

mbingu

Hii ina maana ya sehemu ambayo Mungu huishi.

Mungu aliye juu sana, ambaye amekupatia

"Mungu aliye juu sana, kwa sababu amekupatia". Msemo unaoanza na "ambaye amekupatia" unatueleza jambo zaidi kuhusu Mungu aliye juu sana.

Abarikiwe Mungu aliye juu sana

Hii ni njia ya kumsifu Mungu.

mikono yako

"ndani ya utawala wako" au "ndani ya uwezo yako"

Genesis 14:21

Nipatie watu

Msemo "watu" unaweza kuwa na maana ya watu wa Sodoma ambao maadui waliwakamata. Abramu aliwaokoa alipomuokoa Lutu.

Nimeinua juu mkono wangu

Hii ina maana "nimetoa kiapo" au "nimefanya ahadi".

Sitachukua chochote isipokuwa kile ambacho vijana wamekula

"Ninachukua kutoka kwako kile tu vijana wangu walishakwisha kula". Abramu alikuwa akikataa kupokea chochote kwa ajili yake, lakini alikiri kuwa wanajeshi wake wamekula sehemu ya akiba wakati wa safari ya kurudi Sodoma baada ya vita.

sehemu za watu waliokwenda nami.

Maana kamili ya kauli hii yawezwa kuwekwa wazi. "sehemu ya mali iliyokombolewa iliyokuwa ya wanamume walionisaidia kurudi"

Aneri, Eskoli, na Mamre

Hawa ni washirika wa Abramu (14:13). Kwa kuwa walikuwa washirika wa Abramu walipigana vita pamoja naye. Maana kamili ya kauli inaweza kufanywa wazi. "washirika wangu Aneri, Eskoli na Mamre"

Genesis 15

Genesis 15:1

Baada ya mambo haya

"Mambo haya" ina maana ya pale ambapo wafalme walipigana na Abramu akamuokoa Lutu.

neno la Yahwe likamjia

Lahaja hii ina maana ya Yahwe akazungumza. "Yahwe alizunguza ujumbe wake"

neno la Yahwe

Hapa "neno" inawakilisha ujumbe wa Yahwe. "ujumbe wa Yahwe"

ngao ... thawabu

Mungu alitumia sitiari hizi mbili kumwambia Abramu juu ya tabia yake na uhusiano wake na Abramu.

mimi ni ngao yako

Wanajeshi hutumia ngao kujilinda kwa maadui zao. "Nitakulinda kama ngao" au "Mimi ni ngao yako kukulinda"

thawabu

"malipo". Hii ina maana ya malipo yanayostahili kwa mtu. Maana mbili zaweza kuwa 1) "Mimi ni yote unayohitaji" au 2) "Nitakupa yote unayohitaji".

Abram akasema, "Kwakuwa hujanipatia

"Abramu aliendelea kuzungumza na kusema, "Kwa kuwa umenipatia"

Genesis 15:4

Kisha, tazama

Neno "tazama" linasisitiza ukweli ya kwamba neno la Yahwe lilikuja kwa Abrahamu tena.

neno la Yahwe likaja

Lugha hii ina maana ya kuwa Mungu alizungumza. "Yahwe alizungumza ujumbe wake"

neno la Yahwe

Hapa "neno" linawakilisha ujumbe wa Yahwe. "Ujumbe wa Yahwe"

Mtu huyu

Hii ina maana ya Eliezeri wa Dameski.

atakaye toka katika mwili wako ndiye

"yule utakayekuwa baba yake" au "mwana wako kabisa". Mwana wa Abramu atakuwa mrithi wake.

uzihesabu nyota

"hesabu nyota"

ndivyo uzao wako utakavyokuwa

Kama vile Abramu atavyoshindwa kuhesabu nyota zote, hataweza kuhesabu uzao wake wote kwa sababu utakuwa mwingi sana.

Genesis 15:6

Akamwamini Yahwe

Hii ina maana alipokea na kuamini kile Yahwe alichosema ni kweli.

akamuhesabia jambo hili kuwa mwenye haki

"Yahwe alimhesabia imani ya Abramu kama haki" au "Yahwe alimchukulia Abramu kuwa na haki kwa sababu Abramu alimuamini"

Mimi ni Yahwe, niliye kutoa katika Uru

Yahwe alikuwa akimkumbusha Abrahamu kile alichokuwa amefanya ili Abrahamu aweze kumjua Yahwe alikuwa na nguvu kumpatia Abramu kile alichomuahidi.

kuirithi

"kukipokea" au "ili kwamba ukimiliki"

nitajua je

Abramu alikuwa akiulizia ushahidi zaidi ya kwamba Yahwe atampatia ile nchi.

Genesis 15:9

mizoga

"miili iliyokufa ya wanyama na ndege"

Abram akawafukuza

"Abramu aliwafukuza ndege". Alihakikisha ndege hawakula wanyama waliokufa.

Genesis 15:12

Abramu akalala usingizi

Hii ni lahaja. "Abrahamu alilala usingizi mzito"

giza zito na la kutisha

"giza kubwa sana lililomtisha"

ikamfunika

"ikamzunguka"

wageni

"wageni"

watatumikishwa na kuteswa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "na wamiliki wa nchi ile watawatumikisha na kuwatesa"

Genesis 15:14

Taarifa ya Jumla:

Yahwe aliendelea kuzungumza na Abramu wakati Abramu alipokuwa akiota.

Nitahukumu

Hapa "hukumu" ni lugha nyingine kwa kile kitakachotokea baada ya Mungu kutoa hukumu. "Nitaadhibu"

wataowatumikia

Maana kamili ya kauli hii inawezwa kufanywa wazi. "ambao vizazi vyako watawatumikia"

mali nyingi

Hii ni lahaja. "mali nyingi" au "utajiri mkubwa"

utakwenda kwa baba zako

Hii ni njia ya upole ya kusema "utakufa"

baba

Neno "baba" lina maana sawa na mababu. "mababu"

utazikwa katika uzee mwema

"utakuwa mzee sana utakapokufa na familia yako itazika mwili wako"

Katika kizazi cha nne

Hapa kizazi kimoja kina maana ya urefu wa miaka 100. "Baada ya miaka mia nne"

watakuja tena hapa

"vizazi vyako watakuja hapa tena". Vizazi vya Abrahamu vitakuja katika nchi ampabo Abramu alikuwa akiishi, nchi ambayo Yahwe aliahidi kumpatia.

haujafikia mwisho wake

"haijakamilika" au "itakuwa mbaya zaidi kabla sijawaadhibu"

Genesis 15:17

tazama

Neno "tazama" hapa linatuamsha kuwa makini kwa taarifa ya kushangaza inayofuata.

moshi wenye moto na miali ya mwanga ilipita kati ya vile vipande

Mungu alifanya hivi kumuonyesha Abramu ya kuwa alikuwa akifanya agano na yeye.

ilipita kati ya vile vipande

"ilipita katikati ya mistari miwili ya vipande vya wanyama"

agano

Katika agano hili Mungu alimuahidi kumbariki Abramu, naye ataendelea kumbariki ikiwa Abramu ataendelea kumfuata yeye.

Ninatoa nchi hii

Kwa kusema hivi, Mungu alikuwa akiwapa uzao wa Abramu nchi. Mungu alikuwa akifanya hivi, lakini uzao hawakuweza kwenda katika nchi hadi baada ya miaka mingi baadae.

mto mkuu, Frati

"mto mkubwa, Frati". Hizi ni njia mbili zinazoelezea mto mmoja.

Mkeni , Mkenizi, na Mkadmoni, Mhiti, Mperizi, Mrefai, Mwamori, Mkanaani, Mgirgashi, na Myebusi.

Haya ni majina ya makundi ya watu ambao waliishi katika nchi. Mungu angeruhusu uzao wa Abrahamu kuwashinda watu hawa na kuchukua nchi yao.

Genesis 16

Genesis 16:1

Sasa

Neno hili linatumika kutambulisha sehemu mpya ya simulizi na taarifa ya nyuma kuhusu Sarai.

mtumishi wa kike

"mtumwa wa kike". Mtumwa wa namna hii alikuwa akimtumikia mwanamke wa nyumbani.

kutopata watoto

"kutoweza kuzaa watoto"

niweze kupata watoto kupitia yeye

"Nitajenga familia yangu kupitia kwake"

Abram akasikiliza sauti ya Sarai

"Abramu alifanya kile Sarai alichosema"

akamdharau bibi yake

"alimdharau bibi yake" au "alifikiria alikuwa na thamani zaidi ya bibi yake"

bibi yake

Hapa ina maana ya Sarai. Bibi alikuwa na uwezo juu ya mtumwa wake. "mmiliki wake" au "Sarai"

Genesis 16:5

Jambo hili baya kwangu

"Udhalimu huu dhidi yangu"

ni kwa sababu yako

"ni wajibu wako" au "ni kosa lako"

Nilimtoa mtumishi wangu wa kike katika kumbatio lako

Sarai alitumia neno "kumbatia" hapa kumaanisha yeye kulala naye. "Nilimpa mtumishi wangu ili uweze kulala naye"

nilidharaulika machoni pake

Hii inaweza kuwa katika hali ya kutenda. "alinichukia" au"alianza kunichukia" au "alidhani yeye ni bora zaidi yangu"

Na sasa acha Yahwe aamuwe kati yangu na wewe

"Ninataka Yahwe aseme kama hili ni kosa langu au lako" au "Nataka Yahwe kuamua nani kati yetu yupo sahihi." Msemo "aamue kati ya" una maana ya kuamua nani yuko sawa katika ugomvi kati yao"

Tazama, hapa

"Nisikilize mimi" au "Sikiliza kwa makini"

katika uwezo wako

"chini ya mamlaka yako"

Sarai akakabiliana naye kwa ukatili

"Sarai alimtendea Hajiri vibaya sana"

na akatoroka

"na Hajiri akatoroka kwa Sarai"

Genesis 16:7

Malaika wa Yahwe

Maana zinaweza kuwa 1) Yahwe alijifanya kuonekana kama malaika au 2) huyu alikuwa mmoja wa malaika wa Yahwe au 3) huyu alikuwa mjumbe maalumu kutoka kwa Mungu (baadhi ya wasomi wanadhani alikuwa Yesu). Kwa sababu msemo hauleweki vizuri, ni bora kutafsiri kama "malaika wa Yahwe" kwa kutumia neno la kawaida linalotumika kwa "malaika".

jangwa

Eneo la jangwa aliloenda lilikuwa ni nyikani. "jangwa"

Shuri

Hii ilikuwa jina ya sehemu kusini mwa Kaanani mashariki mwa Misri.

bibi yangu

Hapa ina maana ya Sarai. Bibi alikuwa na mamlaka juu ya mtumwa wake. "mmiliki wangu".

Genesis 16:9

Malaika wa Yahwe akamwambia

"Malaika wa Yahwe alimwambia Hajiri"

Malaika wa Yahwe

Maana zinaweza kuwa 1) Yahwe alijifanya kuonekana kama malaika au 2) huyu alikuwa mmoja wa malaika wa Yahwe au 3) huyu alikuwa mjumbe maalumu kutoka kwa Mungu (baadhi ya wasomi wanadhani alikuwa Yesu). Kwa sababu msemo hauleweki vizuri, ni bora kutafsiri kama "malaika wa Yahwe" kwa kutumia neno la kawaida linalotumika kwa "malaika".

bibi yako

Hapa ina maana ya Sarai. Bibi alikuwa na uwezo juu ya mtumwa wake. "mmiliki wake" au "Sarai"

Kisha Malaika wa Yahwe akamwambia, "Nita

Aliposema "Nita" alikuwa ana maana ya Yahwe.

Nitazidisha uzao wako maradufu

"Nitakupatia uzao mwingi sana"

wengi wasioweza kuhesabika

"wengi sana hadi hakuna mtu atakayeweza kuwahesabu"

Genesis 16:11

Malaika wa Yahwe

Maana zinaweza kuwa 1) Yahwe alijifanya kuonekana kama malaika au 2) huyu alikuwa mmoja wa malaika wa Yahwe au 3) huyu alikuwa mjumbe maalumu kutoka kwa Mungu (baadhi ya wasomi wanadhani alikuwa Yesu). Kwa sababu msemo hauleweki vizuri, ni bora kutafsiri kama "malaika wa Yahwe" kwa kutumia neno la kawaida linalotumika kwa "malaika".

Tazama

"Angalia" au "Sikiliza" au "Sikiliza kwa makini"

utazaa mtoto kiume

"kuzaa mtoto wa kiume"

utamwita jina lake

"utamuita jina lake". Neno "utamuita" linamlenga Hajiri.

Ishmaeli, kwa sababu Yahwe amesikia

Watafsiri wanaweza kuweka maelezo mafupi yanayosema "Jina la 'Ishmaeli' lina maana ya 'Mungu amesikia'".

mateso

Alikuwa ameteswa na mawazo na mateso.

Atakuwa punda mwitu wa mtu

Hili halikuwa tusi. Inaweza kumaanisha Ishmaeli angekuwa anajitegemea na mwenye nguvu kama punda mwitu. "Atakuwa kama punda mwitu miongoni mwa watu"

Atakuwa adui dhidi ya kila mtu

"Atakuwa adui wa kila mtu"

kila mtu atakuwa adui yake

"Kila mtu atakua adui yake"

na ataishi kando na

Hii inaweza pia kumaanisha "ataishi kwa uadui pamoja na"

ndugu

"ndugu wa karibu"

Genesis 16:13

Yahwe aliye zungumza naye

"Yahwe, kwa sababu alizungumza naye"

je ninaendelea kweli kuona, ... mimi?

Hajiri alitumia swali hili la balagha kuonyesha mshangao wake wa kuwa hai hata baada ya kukutana na Mungu. Watu walitarajia iwapo wanakutana na Mungu, wangekufa. "Ninashangaa ya kwamba bado nipo hai, ... mimi"

Kwa hiyo kisima kiliitwa Beerlahairori

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi yanayosema "Beerlahairori ina maana ya 'kisima cha yule anayeniona mimi"

Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi.

Neno "tazama" hapa linavuta ukweli kwamba kisima kilikuwa katika eneo ambalo mwandishi na wasomaji wake walijua. "tena, ilikuwa kati ya Kadeshi na Beredi"

Genesis 16:15

Hajiri akamzalia

Ujio wa Hajiri kwa Sarai na Abramu unajitokeza wazi. Unaweza kufanya hivi kuwa wazi. "Kwa hiyo Hajiri alirudi na kuzaa"

akamwita mwanawe, ambaye Hajiri amemzaa

"alimwita mtoto wake kwa Hajiri" au "alimuita wake na mtoto wa Hajiri"

Abram alikuwa

Hii inatambulisha taarifa ya nyuma kuhusu umri wa Abramu ambapo vitu hivi vilipotokea. Lugha inaweza kuwa na namna maalumu ya kutaja taarifa ya nyuma.

alipomzaa Ishmaeli kwa Abram

Hii inamaanisha "alimzaa mtoto wa Abramu, Ishmaeli." Lengo lipo kwa Abramu kupata mtoto.

Genesis 17

Genesis 17:1

Abram alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa

miaka mia tisa na tisa - Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

Mungu wa uwezo

"Mungu mwenye uweza wote" au "Mungu ambaye ana uwezo wote"

Uende mbele yangu

Kuenda ni sitiari kwa ajili ya kuishi, na "mbele yangu" au "katika uwepo wangu" hapa ni sitiari kwa ajili ya kutii. "Ishi kwa namna nayotaka uishi" au "Kunitii"

Kisha nitalithibitisha

"Iwapo utafanya hivi, basi nitathibitisha"

nitalithibitisha agano langu

"Nitatoa agano langu" au "Nitafanya agano langu"

agano

Katika agano hili Mungu anamuahidi kumbariki Abramu lakini pia anataka Abramu amutii.

nitakuzidisha sana

"nitazidisha kwa wingi idadi ya vizazi vyako" au "nitakupatia vizazi wengi sana"

Genesis 17:3

Abramu akainama uso wake hadi chini ardhini

"Abramu alijirusha uso chini ya ardhi" au "Abrahamu aliinama chini mara moja uso ukiwa ardhini." Alifanya hivi kuonyesha ya kuwa alimheshimu Mungu na angemtii.

Mimi

Mungu alitumia msemo huu kutambulisha kile alichoenda kukifanya kwa Abramu kama sehemu ya agano lake na Abramu.

tazama, agano langu liko nawe

Neno "tazama" hapa linasema ya kwamba kinachofuata ni cha uhakika: "agano langu na wewe ni la uhakika"

baba wa mataifa mengi

"baba wa idadi kubwa ya mataifa" au "yule ambaye mataifa mengi yatajiita"

Abrahamu

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi yafuatayo: Jina "Abramu" lina maana ya "baba aliyeinuliwa" na jina "Abrahamu" linafanana na "baba wa kundi"

Nitakufanya uwe na uzao mwingi

"Nitakusababisha uwe na vizazi vingi sana"

nitakufanya mataifa

"Nitasababisha vizazi vyako kuwa mataifa"

wafalme watatoka kwako

"miongoni mwa vizazi vyako kutakuwa na wafalme" au "baadhi ya vizazi vyako kutakuwa na wafalme"

Genesis 17:7

Taarifa ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Abrahamu.

katika vizazi vyao

"katika kila kizazi"

kwa agano la milele

"kama agano ambalo litadumu milele"

Mungu kwako na kwa wazao wako baada yako

"kuwa Mungu wako na vizazi vyako" au "agano"

Kanaani, kuwa miliki ya milele

"Kanaani, kama miliki ya milele" au"Kanaani, kuimiliki milele"

Genesis 17:9

nawe

Mungu anatumia msemo huu kutambulisha kile Abramu alichokuwa akielekea kufanya kama sehemu ya agano la Mungu na yeye.

ulishike agano langu

"fuata agano langu" au "heshimu agano langu" au "tii agano langu"

Hili ndilo agano langu

"Hili ni hitaji la agano langu" au "Hii ni sehemu ya agano langu". Sentensi hii inatambulisha sehemu ya agano ambayo Abramu ilimpasa afanye.

Kila mwanaume wa kwenu lazima atahiriwe

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Unapaswa kutahiri kila mwanamume miongoni mwako"

Kila mwanaume

Hii ina maana ya wanadamu wa kiume

Lazima mtatahiriwa katika nyama ya govi la ngozi ya mbele

Baadhi ya jamii inaweza kutumia lugha nyepesi zaidi kama "Unatakiwa kutairiwa." Iwapo tafsiri yako ya "fanya tohara" inajumlisha neno la govi la ngozi ya mbele, hauhitaji kurudia.Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Unatakiwa kuwatahiri wanamume wote miongoni mwenu"

ishara ya agano

"ishara inayoonyesha ya kwamba agano lipo"

ishara

Maana zaweza kuwa 1) "ishara" au 2) "ishara". Maana ya kwanza inaonyesha kulikuwa na ishara moja, na maana ya pili inaonyesha kulikuwa na ishara zaidi ya moja. Hapa neno "ishara" ina maana ya ukumbusho kuhusu jambo ambalo Mungu aliahidi.

Genesis 17:12

Taarifaya Jumla

Mungu anaendelea kuzungumza na Abrahamu.

Kila mwanaume

"Hii ina maana ya wanadamu wa kiume"

katika vizazi ya watu wenu

"katika kila kizazi"

yeye ambaye amenunuliwa kwa fedha

Hii ina maana ya watumwa. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mwanamume yeyote utakayemnunua"

agano langu litakuwa katika mwili wenu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "utaweka alama ya agano langu juu ya mwili wako"

kuwa agano la milele

"kama agano la kudumu". Kwa sababu iliwekwa juu ya mwili, hakuna aliyeweza kuifuta.

Mwanaume yeyote asiye tahiriwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda, na unaweza kuacha maneno ambayo yanaweza kuleta maana mbaya katika lugha yako. "mwanamume ambaye haujamtahiri"

Mwanaume yeyote asiye tahiriwa ... govi la ngozi yake ya mbele atatengwa na watu wake

Maana zaweza kuwa 1) "nitamtenga mwanamume yeyote asiyetahiriwa ... govi la mbele kutoka kwa watu wake" au 2)"Ninataka umtenge mwanamume yeyote asiyetahiriwa ... govi la mbele kutoka kwa watu wake"

atatengwa na watu wake

Maana zaweza kuwa 1) "aliuawa" au 2) "kufukuzwa kutoka kwenye jamii".

Amevunja agano langu

"Hajatii amri za agano langu." Hii ni sababu itakayomfanya atengwe kutoka kwa watu wake.

Genesis 17:15

kwa habari ya Sarai

Maneno "kwa habari ya" zinatambulisha mtu anayefuata ambaye Mungu anamzungumzia.

nitakupatia mtoto wa kiume kwake

"Nitamfanya azae mtoto kupitia kwake"

atakuwa mama wa mataifa

"atakuwa mama wa mataifa mengi" au "uzao wake watakuwa mataifa"

Wafalme wa watu wa mataifa watapatikana kutokana na yeye

"Wafalme wa watu watatokana kwake" au "Baadhi ya uzao wake watakuwa wafalme wa watu"

Genesis 17:17

akasema moyoni mwake

"akawaza mwenyewe" au "akasema mwenyewe kimya kimya"

Je yawezekana mtoto azaliwe kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka mia moja?

Abrahamu alitumia swali hili la balagha kwa sababu hakuamini ya kuwa hili lingeweza kutokea. "Hakika mwanamume mwenye umri wa miaka mia moja hawezi kuwa baba wa mtoto!"

Je Sara, ambaye ana umri wa miaka tisini anaweza kuzaa mwana?

Tena Abrahamu alitumia swali la balagha kwa sababu hakuamini ya kuwa hili lingeweza kutokea. msemo "ambaye ana umri wa miaka tisini" unasema kwa nini Abrahamu hakuamini ya kwamba Sarai hataweza kuzaa mtoto. "Sarai ana umri wa miaka tisini. Hakika hawezi kuzaa mtoto wa kiume!"

Lau Ishmaeli angeweza kuishi kabla yako!

"Tafadhali muache Ishmaeli arithi agano ulilofanya pamoja na mimi" au "Huenda Ishmaeli anaweza kupokea baraka ya agano lako" Abrahamu alipendekeza jambo ambalo aliamini lingeweza kutokea"

Genesis 17:19

Hapana, Sarai mkeo atakuzalia

Mungu alisema hili kusahisha imani ya Abrahamu juu ya Sarai kupata mtoto.

utamwita jina lake

Neno "utamwita" linamlenga Abrahamu.

Na kwa habari ya Ishmaeli

Maneno "na kwa habari" yanaonyesha ya kwamba Mungu anabadilisha maongezi kuhusu mtoto ambaye angezaliwa na kumuongelea Ishmaeli.

Tazama

"Angalia" au "Sikiliza" au "Sikiliza kwa makini kwa kile nachotaka kukuambia"

nitamfanya kuwa na uzao

Hii ni lahaja inayokuwa na maana ya "nitamsababisha awe na watoto wengi"

na kumzidisha maradufu

"na nitamsababisha awe na uzao mwingi"

viongozi wa makabila

"machifu" au "watawala". Hawa viongozi sio wana kumi na mbili na wajukuu wa Yakobo ambao wataongoza makabila kumi na mbili ya Israeli.

Lakini agano langu nitalifanya imara na Isaka

Mungu anarudi kuongelea juu ya agano lako na Abrahamu na kusisitiza ya kwamba atatimiza ahadi yake na Isaka, na sio Ishmaeli.

Genesis 17:22

Alipo kuwa amemaliza kuzungumza naye

"Mungu alipomaliza kuzungumza na Abrahamu"

Mungu akaondoka kwa Abraham

"Mungu akamuacha Abrahamu"

kila mwanaume miongoni mwa watu wa nyumba ya Abraham

"kila binadamu wa kiume katika nyumba ya Abrahamu" au "kila mtu wa kiume katika nyumba ya Abrahamu". Ina maana ya wanadamu wa kiume wa umri wote: watoto wachanga, wavulana na wanamume.

Genesis 17:24

ni pamoja na wale waliozaliwa katika nyumba ile na wale walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni

"Hii inajumlisha wale waliozaliwa katika nyumba yake na wale walionunuliwa kutoka kwa wageni"

wale walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni

Hii ina maana ya watumishi au watumwa

wale walionunuliwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wale ambao amekwisha wanunua"

Genesis 18

Genesis 18:1

Mamre

Hili lilikuwa jina la mwanamume aliyemiliki mialoni.

mlangoni pa hema

"katika uwazi wa hema" au "katika kuingilia kwa hema"

joto la mchana

"wakati wa jua kali la mchana"

Akatazama juu na, tazama, akaona wanaume watatu wamesimama.

"Alitazama juu na kuona, tazama, wanamume watatu walikuwa wamesimama"

tazama

"ghafla". Neno "tazama" hapa linatuonyesha kitakachofuata ni cha kushangaza kwa Abrahamu.

mbele yake

"karibu" au "pale". Walikuwa karibu na yeye, lakini umbali wa kutosha kwa yeye kuwakimbilia.

kuinama

Hii ina maana kuinama chini na kuonyesha unyenyekevu na heshima kwa mtu.

Genesis 18:3

Bwana

Hili ni jina la heshima. Maana zaweza kuwa 1) Abrahamu alijua ya kuwa mmoja wa wanamume hawa alikuwa Mungu au 2) Abrahamu alijua ya kwamba wanamume hawa walikuja kwa niaba ya Mungu.

machoni pako

Abrahamu anazungumza na mmoja wa wanamume.

usinipite

"tafadhali msiendelee kupita"

mtumishi wako

"mimi". Abrahamu ana maanisha yeye mwenyewe katika njia hii kuonyesha heshima kwa mgeni wake.

Naomba maji kidogo yaletwe

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Niruhusu nikuletee maji" au "Mtumishi wangu atakuletea maji"

maji kidogo ... chakula kidogo

"maji kidogo ... chakula kidogo." Kusema "kidogo" ilikuwa lugha ya upole ya kuonyesha ukarimu. Abrahamu angewapatia maji na chakula cha kutosha zaidi.

mnawe miguu yenu

Utamaduni huu uliwasaidia wasafiri waliochoka kujiburudisha baada ya kutembea umbali mrefu.

wenu ... mji...

Abrahamu anazungumza na wanamume wote watatu, kwa hiyo "wenu" na "mji..." ni katika hali ya wingi.

Genesis 18:6

vipimo vitatu

kama lita 22

mkate

Mkate huu yawezekana ulikuwa umepikwa haraka katika jiko la moto. Inawezekana ulikuwa tambarare au duara kama mikate midogo midogo ya duara.

kwa haraka

"mtumishi aliharakisha"

akaiandaa

"kuukata na kuubanika"

siagi

Hii ina maana ya sehemu ngumu ya maziwa yaliogandishwa. Inawezekana ilikuwa mtindi au jibini.

ndama aliye kwisha andaliwa

"ndama aliyebanikwa"

mbele yao

"mbele ya wageni watatu"

Genesis 18:9

Wakamwambia

"Kisha wakamwambia Abrahamu"

akasema, "Hakika nitarejea kwako

Neno "akasema" lina maana ya mwanamume ambaye Abrahamu alimwita "Bwana" katika 18:3.

majira ya machipuko

"pale ambapo majira kama haya yatakapowadia mwaka kesho" au "muda kama huu mwaka kesho"

na tazama

Neno "tazama" hapa linatutahadharisha kuwa makini kwa taarifa ya kushangaza inayofuata.

mlangoni pa hema

"katika uwazi wa hema" au "katika kiingilio cha hema"

Genesis 18:11

baada ya kuwa nimechakaa na bwana wangu ni mzee, je ni tapata furaha hii?

nimechakaa na bwana wangu ni mzee, je nitapata furaha hii ya kupata mtoto? Sarai alitumia swali hili la balagha kwa sababu hakuamini angeweza kupata mtoto. "Siamini ya kuwa nitapitia furaha ya kupata mtoto. Bwana wangu ni mzee sana"

bwana wangu ni mzee

Hii ina maana ya "kwa kuwa mume wangu ni mzee pia".

bwana wangu

Hili ni jina la heshima ambalo Sarai alimpa mumewe Abrahamu.

Genesis 18:13

Kwa nini Sara amecheka na kusema, Je ni kweli nitazaa mtoto, nikiwa mzee'?

Mungu alitumia swali la balagha kuonyesha ya kwamba alifahamu alichokuwa akikifikiria Sarai na ya kwamba hakufurahishwa nacho. Anarudia swali la balagha la Sarai (18:11) kutumia maneno tofauti. "Sarai hakuwa sahihi kucheka na kusema, "Sitazaa mtoto kwa sababu mimi ni mzee sana!"

Je kuna jambo lolote gumu sana kwa Yahwe?

"Je kuna jambo lolote ambalo Yahwe hawezi kufanya?" Yahwe anazungumzia juu yake mwenyewe kana kwamba anazungumzia mtu mwingine kumkumbusha Abrahamu ya kwamba yeye, Yahwe, ni mkuu na anaweza lolote. "Hakuna jambo ambalo mimi, Yahwe, siwezi kufanya!"

katika wakati nilioweka mimi majira ya machipuko

"Katikamuda huo niliouweka, ambao ni wakati wa machipuko"

Kisha Sarai akakataa na kusema

"Kisha Sarai aliukana kwa kusema"

akajibu

"Yahwe alijibu"

hapana ulicheka

"Ndio, ulicheka." Hii ina maana ya "Hapana, hiyo sio kweli; kweli umecheka."

Genesis 18:16

kuwaaga

"kuwaaga kwenda njia yao" au "kusema 'Kwaheri' kwao". Ilikuwa ni jambo la upole kuwasindikiza wageni umbali fulani wakati wanapoondoka.

Je ni mfiche Abraham kile ninacho kusudia kufanya ...yeye?

Mungu alitumia swali hili la balagha kusema ya kwamba alikuwa akizungumza na Abrahamu kuhusu jambo muhimu sana na kwamba ilimpasa yeye kufanya hivyo. "Sipaswi na sitamficha Abrahamu kile ninachotaka kufanya .... yeye." au "Ninatakiwa na nitamwambia Abrahamu kile ninachotaka kufanya ... yeye"

Je ni ... kufanya, kwa kuwa ... yeye?

"Sitakiwi ... kufanya. Hii ni kwa sababu .. yeye"

katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nitawabariki mataifa yote ya duniani kupitia Abrahamu.

katika yeye watabarikiwa

"watabarikiwa kwa sababu ya Abrahamu" au "watabarikiwa kwa sababu nimembariki Abrahamu".

ili awaelekeze

"ya kwamba atawaongoza" au "ili kwamba awaamuru"

waishike njia ya Yahwe ... Yahwe ampatie ... aliyo yasema

Yahwe anazungumza juu yake mwenyewe kana kwamba alikuwa mtu mwingine. "kutii kile ambacho mimi, Yahwe nahitaji....mimi, Yahwe, nitaleta ... nimesema"

waishike njia ya Yahwe

"kutii amri za Yahwe"

watende utakatifu na haki

"kwa kufanya utakatifu na haki" Hii inaelezea namna ya kushikilia njia ya Yahwe.

ili kwamba Yahwe ampatie Abraham yale aliyo yasema kwake

"ili kwamba Yahwe aweze kumbariki Abrahamu kama alivyosema angefanya" Hii ina maana ya ahadi ya agano ya kumbariki Abrahamu na kumfanya kuwa taifa kubwa.

Genesis 18:20

kilio cha Sodoma na Gomora ni kikuu

Hii inaweza kuelezwa kwa maneno mengine ili maana halisi ya "kilio" linaloelezwa kama kitenzi cha "kushtaki". "watu wengi sana walikuwa wakishtaki watu wa Sodoma na Gomora kufanya uovu mwingi"

dhambi yao ni kubwa

"wamefanya dhambi sana"

sasa nitashuka pale

"Nitashuka pale sasa hadi Sodoma na Gomora"

nitashuka pale na kuona

"nitashuka pale kujua" au "nitashuka pale kuamua"

kuona kilio ... kilicho nifikia

Yahwe anazungumzia kana kwamba alijua kuhusu jambo hili kwa sababu alisikia kilio na mashtaka yakija kutoka kwa watu waliokuwa wameteseka. Hii inaweza kuwekwa kwa maneno mengine ili kitenzi cha "kilio" kiweze kuelezwa kama kitenzi cha "kushtaki". "waovu kama wale wanaowashtaki wanasema kuwa wako vile"

ikiwa kweli

"kama sio waovu kama kilio kinavyoashiria"

Genesis 18:22

wakageuka toka pale

"aliondoka kutoka katika hema la Abrahamu"

Abrahamu akabaki amesimama mbele ya Yahwe

"Abrahamu na Yahwe walibaki pamoja"

alikaribia

"alimkaribia Yahwe" au "alisogea karibu na Yahwe"

utawafutilia mbali

Abrahamu anazungumzia kuwaangamiza watu kana kwamba alikuwa akifagia takataka kwa ufagio. "kuangamiza"

watakatifu pamoja na waovu

"watu watakatifu na watu waovu"

Genesis 18:24

Taarifa ya Jumla:

Abrahamu anaendelea kuzungumza na Yahwe

Huenda wakawepo

"Chukulia wakawepo"

Je utawakatilia mbali na usiuache mji kwa ajili ya hao watakatifu hamsini walioko hapo?

Abrahamu alikuwa na tumaini ya kwamba Yahwe angesema, "Sitaikatalia mbali". "Nadhani hautaikatalia mbali. Badala yake, utaiacha kuiharibu sehemu kwa sababu ya watakatifu hamsini ambao wapo pale"

utawakatilia mbali

"kuingamiza". Abrahamu anazungumzia kuwaangamiza watu kana kwamba alifagia uchafu na ufagio. "kuangamiza watu waliokuwa wakiishi pale"

na usiuache mji kwa ajili ya hao watakatifu hamsini walioko hapo?

Abrahamu alikuwa akitumaini ya kwamba Mungu angesema, "Nitaacha kuangamiza sehemu kwa niaba ya watu watakatifu hamsini walioishi pale"

usiuache mji

"ruhusu watu waishi"

kwa ajili ya hao

"kwa sababu ya"

Hasha usifanye hivyo

"Sitapenda ufanye jambo kama hilo" au "Haupaswi kutaka kufanya jambo kama hilo"

hivyo, kuwauwa

"jambo kama hili kama kuwaua" au "jambo kama hilo, yaani, kuwaua"

watakatifu watendewe sawa na waovu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "unatakiwa kuwatendea watakatifu sawa sawa na waovu"

Je Mhukumu wa ulimwengu wote hatatenda haki?

Abrahamu alitumia swali hili la balagha kusema kile alichotarajia Mungu kukifanya. "Mhukumu wa ulimwengu wote hakika atafanya kilicho haki" au "Kwa kuwa wewe ni Mhukumu wa ulimwengu wote, hakika utafanya lililo sahihi!"

Mhukumu

Mungu anasemwa kama mhukumu kwa sababu yeye ni mhukumu aliye kamilika ambaye hufanya maamuzi ya mwisho kuhusu mema na mabaya.

Genesis 18:27

Tazama

Msemo wa "tazama" hapa unavuta nadhari juu ya taarifa ya kushangaza inayofuata.

Nimeshika kusema

"Niwie radhi kwa kuwa wazi na kuzungumza na wewe" au "Samahani kwa kudiriki kuzungumza"

kwa Bwana wangu

Abrahamu anaonyesha heshima kwa Yahwe kwa kuzungumza na Yahwe kana kwamba alikuwa akizungumza na mtu mwingine. "kwako wewe, Bwana wangu"

mavumbi na majivu

Sitiari hii inamuelezea Abrahamu kama binadamu, ambaye atakufa na mwili wake kugeuka kuwa vumbi na majivu. "ni binadamu pekee" au "kama vile vumbi na majivu yasivyokuwa na umuhimu"

watano pungufu katika idadi ya hao watakatifu hamsini

"watu arobaini na tano tu watakatifu"

kwa upungufu wa hao watano

"iwapo kuna watu watano pungufu watakatifu"

Sitaangamiza

"Sitaangamiza Sodoma"

Genesis 18:29

Akaongea naye

"Abrahamu akazungumza na Yahwe"

ikiwa arobaini watapatikana pale

Hii ina maana ya "ikiwa ukapata watu watakatifu arobaini Sodoma na Gomora"

Akajibu

"Yahwe akajibu"

Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini

"Sitaangamiza miji iwapo nitakuta watu watakatifu arobaini pale"

thelathini

"watu thelathini watakatifu" au "watu thelathini wazuri"

Tazama

Msemo wa "tazama" hapa unavuta nadhari juu ya taarifa ya kushangaza inayofuata.

Nimeshika kusema

"Niwie radhi kwa kuwa wazi na kuzungumza na wewe" au "Samahani kwa kudiriki kuzungumza"

ishirini

"watu ishirini watakatifu" au "watu ishirini wazuri"

Genesis 18:32

Huenda kumi wakaonekana kule

"Huenda utakuta watu kumi watakatifu pale"

kumi

"watu kumi watakatifu" au " watu kumi wazuri"

Kisha akasema

"Na Yahwe akajibu"

kwa ajili ya hao kumi

"ikiwa nikipata watu kumi watakatifu pale"

Yahwe akaendelea na njia yake

"Yahwe aliondoka" au "Yahwe alienda"

Genesis 19

Genesis 19:1

Malaika wawili

Mwanzo 18 unasema ya kwamba wanamume wawili waliondoka kwenda Sodoma. Hapa tunajifunza ya kwamba ni kweli walikuwa malaika.

langoni mwa Sodoma

"malango wa mji wa Sodoma." Mji ulikuwa na kuta ukiuzunguka, na watu iliwabidi kupitia malango ili kuingia. Hii ilikuwa sehemu muhimu sana katika mji. Watu muhimu mara kwa mara walitumia muda wao pale.

akainama uso wake chini ardhini

Aliweka goti lake juu ya ardhi na kisha kugusa ardhi kwa kipaji cha uso wake na pua.

Bwana zangu

Huu ulikuwa usemi wa heshima Lutu alitumia kwa malaika.

nawasihi mgeuke mwende kwenye nyumba ya mtumishi wenu

"Tafadhali njooni na mkae ndani ya nyumba ya mtumishi wenu"

nyumba ya mtumishi wenu

Lutu anajitambulisha kama mtumishi ili kuonyesha heshima kwao.

muoshe miguu yenu

Watu walipenda kuosha miguu yao baada ya kusafiri.

muamke asubuhi

"muamke mapema"

usiku tutalala

Malaika wawili waliposema hivi, walikuwa wakimaanisha wao wenyewe, na sio Lutu. Wao wawili walipanga kukaa usiku pale mjini.

mjini

Hili ni eneo la wazi, lililo nje katika mji.

wakaondoka pamoja nae

"waligeuka na kuondoka pamoja naye"

Genesis 19:4

kabla hawaja lala

"kabla watu ndani mwa nyumba ya Lutu walipolala usingizi"

wanaume wa mji, wa Sodoma

"wanamume wa mji, yaani, wanamume wa Sodoma" au "wanamume wa mji wa Sodoma"

nyumba

"nyumba ya Lutu"

vijana kwa wazee

"kutoka kwa vijana hadi wazee". Hii ina maana "wanamume wa umri wote" na ina maana ya wanamume wa Sodoma ambao walikuwa wakizunguka nyumba ya Lutu.

walioingia kwako

"waliongia ndani ya nyumba"

kulala nao

"kushiriki tendo la ngono pamoja nao". Lugha yako yaweza kuwa na namna ya upole zaidi ya kusema hivi. "kuwajua karibu zaidi"

Genesis 19:6

nyuma yake

"nyuma yake" au "baada ya kuingia ndani"

Nawasihi, ndugu zangu

"nawaomba, ndugu zangu"

ndugu zangu

Lutu alizungumza kwa njia ya kirafiki kwa wanamume wa mji akitarajia wangemsikiliza. "rafiki zangu"

msitende uovu

"msifanye jambo la uovu hivi" au "msifanye jambo la uovu kama hili"

Tazama

"Sikiliza kwa makini" au"Angalia hapa"

hawajawahi kulala na

"hawajashiriki tendo la ngono na" Lugha yako inaweza kuwa na njia ya upole ya kusema hili. "hawajawajua"

lolote muonalo kuwa jema machoni penu

"lolote mnalotamani" au "lolote mnalofikiria ni sahihi"

chini ya kivuli cha dari yangu

Wanamume wawili walikuwa wageni katika nyumba ya Lutu, kwa hiyo alihitaji kuwalinda. Neno "dari" ni maana nyingine ya kusema nyumba na sitiari kwa Lutu kuwalinda. "ndani ya nyumba yangu, na Mungu anatarajia mimi niwalinde"

Genesis 19:9

Simama nyuma!

"Simama pembeni!" au "Toka katika njia yetu!"

huyu alikuja kukaa hapa kama mgeni

"Huyu hapa alikua hapa kama mtu wa nje" au "Huyu mgeni alikuja kuishi hapa"

huyu

"Lutu". Wanamume wanazungumza wao kwa wao. Kama hii haitakuwa wazi katika lugha yako, unaweza kuwafanya wanamume wazungumze na Lutu hapa.

na sasa amekuwa mwamuzi wetu

"na sasa anadhani ana mamlaka ya kutuambia kipi ni sahihi na kipi sio sahihi" au "lakini hatutamruhusu atuzuie kufanya kile tunachotaka kufanya"

na sasa ame...

"na ingawa hana sababu nzuri, amekuwa"

Sasa tuta...

"Kwa sababu unatuambia ya kwamba tunafanya uovu, tuta.."

tutakushugulilia vibaya wewe kuliko wao

Wanamume walikasirika kwa Lutu kusema, "Msitende uovu hivi" (19:6) kwa hiyo wanamtishia kutenda uovu zaidi ya vile Lutu alivyohofia mara ya kwanza. "tutakushughulikia uovu zaidi na wewe zaidi ya wao"

Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, na wakakaribia kuvunja mlango

Maana zaweza kuwa 1) "walizidi kuja karibu na mwanamume, kwa Lutu, hadi wakawa karibu sana kuweza kuvunja mlango" au 2) walimsukuma Lutu kwa mwili dhidi ya ukuta au mlango wa nyumba na walikuwa wakitaka kuvunja mlango.

huyo mtu ... Lutu

Hizi ni njia mbili zinazomfafanua Lutu.

Genesis 19:10

Lakini wale wanaume

"Lakini wageni wawili wa Lutu" au "Lakini malaika wawili"

wanaume wakamkamata Lutu na kumweka ndani na wakafunga

Lugha yako inaweza kuongezea ya kwamba wanamume walifungua mlango kwanza. "wanamume walifungua mlango vya kutosha mpaka kunyosha mikono yao na kuvuta ... na kisha wakafunga"

wageni wa Lutu wakawapiga kwa upofu wale wanaume

Msemo "wakawapiga kwa upofu" ni sitiari; wageni hawakuwapiga kwa mwili wanamume. "Wageni wa Lutu waliwapofusha wanamume" au "waliondoa uwezo wao wa kuona"

vijana na wazee kwa pamoja

"wanamume wa umri wote". Hii lugha unasisitiza ya kwamba wageni walipofusha wanamume wote. Hii inaweza kumaanisha uwakilishi wa kijamii kuliko umri. "vijana na wazee kwa pamoja"

Genesis 19:12

Basi wale watu wakamwambia

"Kisha wale wanamume wawili wakasema" au "Kisha malaika wawili wakasema"

Je una mtu mwingine yeyote hapa?

"Je una mtu mwingine wa familia yako ndani ya mji?" au "Je una mtu mwingine wa familia katika eneo hili?"

yeyote mwingine katika huu mji

"mtu mwingine katika familia yako anayeishi katika mji huu"

tunakaribia kuiangamiza

Neno "tunakaribia" hapa linajitegemea. Ni malaika wawili pekee wangeenda kuangamiza mji; Lutu hakuwa anaenda kuangamiza mji. Iwapo lugha yako ina namna ya kutenganisha "tunakaribia" basi itumike hapa.

mashitaka dhidi yake mbele ya Yahwe yamezidi

Hii inaweza kusemwa kwa namna nyingine ili kwamba nomino ya "mashtaka" inaelezwa kama kitenzi. "kwa hiyo watuwengi walikuwa wakimwambia Yahwe ya kwamba watu wa mji wanafanya mambo ya uovu"

Genesis 19:14

Lutu akatoka

"Kwa hiyo Lutu aliondoka nyumbani"

wakwe zake, wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake

wakwe zake, wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake Msemo wa "wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake" unafafanua maana ya "mkwe" hapa. "wanamume waliokuwa wakielekea kuwaoa binti zake" au "wachumba wa binti zake"

Alfajiri

"Kabla jua halijachomoza"

ondoka

"Ondoka sasa"

usipotelee katika adhabu ya mji huu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ili Yahwe asikuangamize pia atakapowaadhibu watu wa mji huu"

usipotelee katika adhabu

Mungu kuangamiza watu wa mji unazungumzwa kana kwamba mtu anafagia vumbi.

ya mji

Hapa "mji" una maana ya watu.

Genesis 19:16

Lakini akakawia-kawia

"Lakini Lutu alisita" au "Lakini Lutu hakuanza kuondoka"

Kwa hiyo watu wale wakamshika

"kwa hiyo wanamume wawili walimkamata" au "Kwa hiyo malaika walimkamata"

alimhurumia

"akawa na huruma kwa Lutu". Yahwe anaelezwa kama kuwa na "huruma" kwa sababu alikuwa akitunza uhai wa Lutu na familia yake badala ya kuwaangamiza alipoangamiza watu wa Sodoma kwa maovu waliofanya.

Walipowatoa nje

"Wanamume wawili walipowatoa familia ya Lutu nje"

jiponye nafsi yako!

Hii ilikuwa namna ya kuwaambia wakimbie ili wasife. "Kimbia na uokoe maisha yenu!"

usitazame nyuma

Msemo "katika mji" unaeleweka. "Usitazame nyuma katika mji" au "Usitazame nyuma katika Sodoma"

kwenye hili bonde

Hii ina maana bonde la Mto Yordani. Hii ina maana ya jumla ya eneo la Mto Yordani.

usije ukatoweshwa mbali

Inaeleweka ya kwamba watatoweshwa pamoja na watu wa mji. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "la sivyo Mungu atawaangamiza pamoja na watu wa mji"

ukatoweshwa mbali

Mungu kuwaangamiza watu wa mji inazungumziwa kana kwamba mtu anafagia vumbi.

Genesis 19:18

Mtumishi wenu amepata kibali machoni pako

Kupendezwa na mtu inazungumziwa kana kwamba "fadhila" ni kitu kinachoweza kupatikana. Pia, "machoni" ni lugha nyingine inayowakilisha mawazo au fikra za mtu. "Umependezwa na mimi"

Mtumishi wenu ame...

Lutu alikuwa akionyesha heshima kwa kumaanisha mwenyewe kama "mtumishi wako". "Mimi, mtumishi wako, nime..."

umenionesha wema ulio mkuu kwa kuokoa maisha yangu

Kitenzi cha "wema" kinaweza kuelezwa kama "wema". "Umekuwa mwema sana kwangu kwa kuokoa maisha yangu"

sitaweza kutorokea milimani, kwa sababu mabaya yataniwahi na nitakufa

Kutoweza kufika umbali wa kutosha mwa Sodoma pale ambapo Mungu anaangamiza mji unazungumziwa kana kwamba "uhalifu" ni mtu ambaye atamfukuza na kumfikia Lutu. "Familia yangu na mimi hakika tutakufa Mungu atakapoangamiza watu wa Sodoma, kwa sababu milima ipo mbali sana na sisi kufika kule salama"

maisha yangu ... sitaweza kutorokea ... yataniwahi na nitakufa

Inaonyesha ya kwamba familia ya Lutu itakufa pamoja naye. "maisha yetu ... hatuwezi kutoroka ... yataniwahi, na tutakufa"

niacheni nikimbilie pale ( Je Siyo mdogo ule?), na maisha yangu yataokolewa

Lutu alitumia swali hili la balagha kuwafanya malaika kutambua ya kwamba ule mji ni mdogo kweli. "acha nitoroke kule. Unaona jinsi gani ni mdogo. Ukituruhusu kufika pale tutaishi"

niacheni nikimbilie pale

Ombi kamili la Lutu linaweza kuwekwa wazi. "badala ya kuangamiza mji ule, niruhusu nitoroke pale"

maisha yangu yataokolewa

Inaonyesha ya kwamba maisha ya familia ya Lutu yataokolewa pamoja naye. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ili kwamba tuweze kuishi" au "ili kwamba tuweze okoka"

Genesis 19:21

nimekubali ombi hili pia

"nitafanya kile ulichokiomba"

sitafanya chochote

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "sitaangamiza miji mingine"

Soari

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi yanayosema "Jina la Soari linafanana na neno la Kiebrania lenye maana ya "ndogo". Lutu aliuita mji huu "mdogo" katika Mwanzo 19:20.

Genesis 19:23

Jua lilikuwa limekwisha chomoza juu ya nchi

"Jua limechomoza juu ya nchi". msemo wa "juu ya nchi" unaweza kuachwa wazi.

Lutu alipofika Soari

Inaonyesha ya kwamba familia ya Lutu ilikuwa pamoja naye. "Lutu na familia yake walipofika Soari"

Yahwe akanyesha juu ya Sodoma na Gomora kiberiti na moto toka kwa Yahwe mbinguni

Msemo wa "kutoka kwa Yahwe" una maana ya nguvu ya Mungu kusababisha kiberiti na moto kuanguka juu ya mji. Yahwe alisababisha kiberiti na moto kuanguka kutoka mbinguni juu ya Sodoma na Gomora"

kiberiti na moto

Maneno haya yanatumika pamoja kuelezea umbo moja. "kiberiti kiwakacho" au "mvua kali"

miji ile

Kimsingi hii ina maana ya Sodoma na Gomora, lakini pia miji mingine mitatu.

vilivyomo katika miji

"watu waliokuwa wakiishi katika miji ile"

Genesis 19:26

akawa nguzo ya chumvi

"akawa kama sanamu ya chumvi" au "mwili wake ukawa kama jiwe refu la chumvi". Kwa sababu hakutii malaika aliyemwambia asitazame nyuma ya mji, Mungu alimfanya awe kama sanamu iliyotengenezwa na jiwe la chumvi.

tazama

Msemo wa "tazama" hapa unavuta nadhari juu ya taarifa ya kushangaza inayofuata.

kama moshi wa tanuru

Hii inaonyesha ya kwamba ulikuwa ni moshi mkubwa sana. "kama moshi utokao katika moto mkubwa sana"

Genesis 19:29

Taarifa ya Jumla:

Mstari wa 29 ni ufupi wa sura hii.

Mungu akamkumbuka Abrahamu

Hii inasema kwa nini Mungu alimuokoa Lutu. "kukumbuka" ni namna ya kusema "alimkumbuka". Hii haimaanishi Mungu alisahau juu ya Abrahamu. Ina maana alimfikiria Abrahamu na kuwa na huruma juu yake. "Mungu alimfikiria Abrahamu na kuwa na huruma juu yake"

katika maangamizi

"kutoka kwa maangamizi" au "kutoka kwa hatari"

Genesis 19:30

Lutu akapanda juu kutoka Soari na kwenda kuishi katika milima

Msemo "akapanda juu" unatumiwa kwa sababu Lutu alienda sehemu ya juu mlimani.

Genesis 19:31

Yule wa kwanza

"Binti wa kwanza wa Lutu" au "Binti mkubwa"

yule mdogo

"Binti mdogo" au "mdogo wake"

kulingana na desturi ya dunia yote

Hapa "dunia" ina maana ya watu. "kama watu sehemu zote hufanya"

kunywa mvinyo

Hii inaweza kuelezwa kwa uwazi ya kwamba lengo lao lilikuwa kumfanya alewe. "kunywa mvinyo hadi alewe" au "alewe kwa mvinyo".

ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu

Hii inazungumzia kuhusu kumpatia Lutu uzao kana kwamba familia yake ilikuwa na mtiririko mrefu. "ili kwamba tuweze kuzaa watoto ambao watakuwa uzao wa baba yetu"

hakujua ni wakati gani alikuja kulala, wala wakati alipo amka

"hakujua chochote kuhusu hili" au "hakujua ya kwamba alilala pamoja naye"

Genesis 19:34

Na tumnyweshe mvinyo ... wala wakati alipoamka

Hii inaweza kuelezwa kwa uwazi ya kwamba lengo lao lilikuwa kumfanya alewe. "kunywa mvinyo hadi alewe" au "alewe kwa mvinyo".

tumnyweshe mvinyo

Hii inaweza kuelezwa kwa uwazi ya kwamba lengo lao lilikuwa kumfanya alewe. "kunywa mvinyo hadi alewe" au "alewe kwa mvinyo".

Ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu

Hii inazungumzia kuhusu kumpatia Lutu uzao kana kwamba familia yake ilikuwa na mtiririko mrefu. "ili kwamba tuweze kuzaa watoto ambao watakuwa uzao wa baba yetu"

hakujua ni wakati gani alilala, wala wakati alipoamka

"hakujua chochote kuhusu hili" au "hakujua ya kwamba alilala pamoja naye"

Genesis 19:36

wakapata mimba kwa baba yao

"wakawa mimba kupitia baba yao" au "wakapatawatoto kwa baba yao"

Akawa

"Yeye ndiye"

wamoabu hata leo

"Wamoabu ambao wanaishi sasa"

hata leo

Neno "leo" lina maana ya kipindi ambapo mwandishi wa Mwanzo alipokuwa hai. Mwandishi alizaliwa na kuandika haya miaka mingi baada ya familia ya Lutu kuishi na kufa.

Benami

Hili ni jina la mwanamume.

watu wa Waamoni

"uzao wa Amoni" au "Watu wa Amoni"

Genesis 20

Genesis 20:1

Shuri

Hili ni eneo la jangwa upande wa mashariki wa mpaka wa Misri.

akatuma watu wake kumchukua Sara

"aliwafanya wanamume wake kumfuata Sara na kumleta kwake"

Mungu akamtokea Abimeleki

"Mungu akamtokea Abimeleki"

Tazama

Hapa neno "tazama" linaongeza msisitizo kwa kile kifuatacho. "Nisikilize"

wewe ni mfu

Hii ni njia ya nguvu ya kusema mfalme atakufa. "hakika utakufa hivi karibuni" au "Nitakuua"

mke wa mtu

"mwanamke aliyeolewa"

Genesis 20:4

Basi ... hajamkaribia

Neno hili linatumika hapa kuweka alama ya kubadilisha kutoka kwenye simulizi kwenda kwa taarifa kuhusu Abimeleki.

Abimeleki alikuwa bado hajamkaribia

Hii ni njia ya upole ya kusema hakufanya ngono pamoja naye. "Abimeleki hakulala na Sara" au "Abimeleki hakumgusa Sara"

hata taifa lenye haki

Hapa "taifa" lina maana ya watu. Abimeleki ana wasiwasi ya kwamba Mungu atawaadhibu sio yeye tu, lakini watu wake pia. "hata watu wasio kuwa na hatia"

Je si yeye mwenyewe aliye niambia, 'Sara ni dada yangu?' Hata Sara mwenyewe alisema, 'ni kaka yangu.'

Hii ina nukuu ndani ya nukuu. Zinaweza kutajwa kwa nukuu isiyo dhahiri. "Je sio yeye mwenyewe aliyeniambia ya kwamba huyo ni dada yaek? Hata yeye mwenyewe alinimbia ya kwamba ni kaka yake"

Je si yeye mwenyewe aliye niambia, 'Sara ni dada yangu?

Abimeleki alitumia swali la balagha kumkumbusha Mungu juu ya jambo alilokuwa akilifahamu tayari. Hii inaweza kufanywa kuwa kauli. "Abrahamu mwenyewe aliniambia 'Huyu ni dada yangu'" au "Abrahamu alisema ya kwamba ni dada yake".

Je si yeye mwenyewe aliye niambia, ...Hata Sara mwenyewe

Maneno "yeye mwenyewe" na "Sara mwenyewe" yanatumika kuweka msisitizo kuleta nadhiri kwa Abrahamu na Sara na kuwalaumu kwa kilichotokea.

Nimefanya hili katika uadilifu wa moyo wangu na katika mikono isiyo na hatia.

Hapa "moyo" una maana ya mawazo yake au nia zake. Pia "mikono" hapa ina maana ya matendo yake. "Nimefanya hili kwa nia njema na matendo mema" au "Nimefanya hivi bila mawazo au matendo ya uovu"

Genesis 20:6

Mungu akasema naye

"Mungu akasema kwa Abimeleki"

umefanya hili katika uadilifu wa moyo wako

Hapa"moyo" una maana ya mawazo na nia zake. "ulifanya hivi kwa nia njema" au "ulifanya hivi bila kuwa na nia ya uovu"

umshike

Hii ni lugha ya upole kwa kufanya ngono na Sara. "kulala naye"

mke wa mtu

"Mke wa Abrahamu"

utaishi

"Nitakuruhusu uishi"

wote walio wa kwako

"nyie watu wote"

Genesis 20:8

Akawasimulia mambo haya yote

"Aliwaambia kila kitu ambacho Mungu alimwambia"

Umetufanyia jambo gani?

Abimeleki alitumia swali hili la balagha kumshtaki Abrahamu. "Umefanya jambo hili baya kwetu!" au "Tazama ulichokifanya kwetu!"

Umetufanyia

Neno "umetufanyia" hapa linajitegemea na halimhusu Abrahamu na Sara.

Ni kwa jinsi gani nimekutenda dhambi kwamba umeniletea ... dhambi?

Abimeleki alitumia swali hili la balagha kumkumbusha Abrahamu ya kwamba hakufanya dhambi dhidi ya Abrahamu. "Sijafanya jambo dhidi yako kusababisha wewe ulete ... dhambi."

kwamba umeniletea mimi na ufalme wangu dhambi hii kubwa

Kumsababishia mtu awe na hatia ya kutenda dhambi inazungumzwa kana kwamba "dhambi" ilikuwa jambo linaloweza kuwekwa juu ya mtu. "ya kwamba umetufanya mimi na ufalme wangu kuwa na hatia kwa dhambi hii mbaya"

ufalme wangu

Hapa "ufalme" ina maana ya watu. "juu ya watu wa ufalme wangu"

Umenifanyia mimi jambo ambalo halipaswi kufanywa

"Usingefanya jambo hili kwangu"

Genesis 20:10

Nini kilikushawishi wewe kutenda jambo hili?

"Nini kilisababisha ufanye hivi?" au "Kwa nini ulifanya hivi?" Kile ambacho Abrahamu alifanya kinaweza kuwekwa wazi. "Kwa nini uliniambia ya kwamba Sara ni dada yako?"

kwasababu nilifikiri hakika hakuna hofu ya Mungu katika sehemu hii, na kwamba wataniua kwa ajili ya mke wangu.

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kusemwa katika nukuu tofauti. "Kwa sababu nilidhani ya kwamba kwa kuwa hakuna mwenye hofu ya Mungu hapa, mtu anaweza kuniua ili amchukue mke wangu"

hakuna hofu ya Mungu katika sehemu hii

Hapa "sehemu" ina maana ya watu. "hakuna mtu hapa Gerari mwenye hofu ya Mungu"

hofu ya Mungu

Hii ina maana ya kumheshimu Mungu sana na kuonyesha heshima hiyo kwa kumtii.

Licha ya kwamba kweli ni dada yangu

"Pia, ni kweli ya kwamba Sara ni dada yangu" au "Pia, Sara ni dada yangu ki ukweli"

binti wa baba yangu, ingawa si binti wa mama yangu

"tuna baba mmoja, lakini mama tofauti"

Genesis 20:13

Taarifa ya Jumla:

Mstari wa 13 ni muendelezo wa jibu la Abrahamu kwa Abimeleki.

nyumba ya baba yangu

Hapa "nyumba" ina maana ya familia ya Abrahamu. "baba yangu na familia yangu yote" au "nyumba ya baba yangu"

nilimwambia mke wangu, kwa kila sehemu tutakayo kwenda, unioneshe uaminifu wako kama mke wangu: Kila mahali tutakapo kwenda, useme juu yangu kuwa, "Ni kaka yangu."'''

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kusemwa katika nukuu tofauti. "Nilisema kwa Sara ya kwamba nataka awe mwaminifu kwangu kwa kuwaambia watu kila mahali tuendapo ya kwamba mimi ni kaka yake"

Abimeleki akatwaa

"Abimeleki akaleta baadhi"

Genesis 20:15

Abimeleki akasema

"Abimeleki akasema kwa Abrahamu"

Tazama

Hapa na katika mstari wa 16 neno "tazama" linaongeza msisitizo kwa kile kifuatacho.

Nchi yangu i mbele yako

Hii ni njia ya kusema "ninaifanya nchi yangu yote iwe wazi kwako"

Kaa mahali utakapopendezewa

"ishi popote upendapo"

elfu

"1,000"

ni kwa ajili ya kufunika kosa lolote dhidi yako machoni pa wote walio pamoja na wewe

Kutoa fedha kuthibitisha kwa wengine ya kwamba Sara hana hatia inazungumzwa kana kwamba anaweka mfuniko juu ya kosa ili mwingine asilione. "Ninampatia hili kwake, ili kwamba wale ulionao wajue haujafanya kosa"

machoni

Hapa "macho" ina maana ya mawazo na fikra za mtu.

mbele ya kila mtu ambaye umemfanya kuwa na haki

Msemo huu wa "umemfanya kuwa na haki" unaweza kuwa katika hali ya kutenda. "kila mtu atajua ya kwamba huna hatia"

Genesis 20:17

tasa kabisa

"kutoweza kupata watoto kabisa"

kwa sababu ya Sara, mke wa Abraham

Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "kwa sababu Abimeleki alimchukua mke wa Abrahamu Sara"

Genesis 21

Genesis 21:1

Yahwe akamsikiliza Sara

Hapa msemo "kumsikiliza" una maana ya Yahwe kumsaidia Sara kupata mtoto. "Yahwe alimsaidia Sara"

akamzalia Abrahamu mtoto wa kiume

"akamzaa mtoto wa kiume wa Abrahamu"

katika uzee wake

"Abrahamu alipokuwa mzee sana"

katika muda ule ule ambao Mungu alikuwa amemwambia

"katika muda haswa ambao Mungu alimwambia ingekuja kutokea"

Abrahamu alimuita mwanawe wa kiume, yule ambaye alizaliwa kwake, ambaye Sara alimzaa, Isaka

"Abrahamu alimuita mtoto wake wa kiume, yule ambaye Sara alimzaa, Isaka" au "Abrahamu alimuita mtoto wao wa kiume Isaka"

Abrahamu akamtahiri mwanawe Isaka alipofikisha siku nane

"Mwanae Isaka alipofikisha umri wa siku nane, Abrahamu alimtahiri"

siku nane

"siku 8"

amemwagiza

"alimuamuru Abrahamu kufanya"

Genesis 21:5

mia moja

"100"

Mungu amenifanya nicheke

Sara alikuwa akicheka kwa sababu alishangazwa na alikuwa na furaha. Hii inaweza kuwekwa wazi. "Mungu alinisababisha nicheke kwa furaha"

kila mtu atakaye sikia

Kile ambacho watu wangesikia kinaweza kuwekwa wazi. "kila mtu asikiaye kuhusu kile Mungu amefanya kwangu"

Nani angesema kwa Abraham kwamba Sara atalea mtoto

Hili swali la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hakuna ambaye angeweza kusema kwa Abrahamu ya kwamba Sara atalea watoto"

atalea mtoto

Hii ni lugha ya upole ikimaanisha kunyonyesha watoto. "mnyonyeshe mtoto maziwa yake mwenyewe"

Genesis 21:8

Mtoto akakua ... Isaka aliachishwa

"aliachishwa" ni lugha ya upole ya kusema mtoto alimaliza kunyonyeshwa. "Isaka akakua, na pale alipokuwa hahitaji tena kunyonya, Abrahamu aliandaa karamu kubwa"

mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alikuwa amezaliwa kwa Abrahamu

Jina la mwana wa Hajiri linaweza kuwekwa wazi. "Ishmaeli, mwana wa Hajiri Mmisri na Abrahamu"

akidhihaki

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba alimzomea au alimcheka Isaka. "alimcheka Isaka"

Genesis 21:10

akamwambia Abrahamu

"Sara akamwambia Abrahamu"

Mfukuze

"mfukuze aende zake" au "mtoweshe"

mwanamke huyu mtumwa pamoja na mtoto wake

Hii ina maana ya Hajiri na Ishmaeli. Sara hakuwatambua kwa majina kwa sababu alikuwa amekasirishwa nao.

pamoja na mwanangu Isaka

"pamoja na mwanangu Isaka"

Jambo hili likamuhuzunisha sana Abrahamu

"Abrahamu alikuwa na huzuni kuhusu kile alichosema Sara"

kwa sababu ya mwanawe

"kwa sababu ilikuwa inahusu mwanawe" Inamaanisha mwanawe, Ishameli"

Genesis 21:12

Usihuzunike kwa sababu ya kijana huyu, na kwa sababu ya mwanamke huyu mtumwa wako

"Usifadhaike kuhusu mvulana na mjakazi wako"

Sikiliza maneno asemayo Sara juu ya jambo hili

Hapa "maneno" yana maana ya kile kinachosemwa. "Fanya kila kitu ambacho Sara anakuambia kuhusu wao"

itakuwa kupitia Isaka kwamba uzao wako utaitwa

Msemo "utaitwa" una maana ya wale watakaozaliwa kupitia Isaka ndio wale Mungu anawatambua kuwa uzao ambao alimuahidi Abrahamu. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Isaka ndiye atakayekuwa baba wa uzao niliokuahidi kwako"

Nitamfanya pia mtoto wa mjakazi kuwa taifa

Neno "taifa" lina maana ya Mungu atampatia uzao mwingi ili kwamba wawe taifa kubwa la watu. "Nitamfanya mwana wa mwanamke mjakazi pia awe baba wa taifa kubwa"

Genesis 21:14

akachukua mkate

Maana zaweza kuwa 1) hii inaweza kumaanisha chakula kwa ujumla au 2) hii ina maana ya mkate mahususi.

kiriba cha maji

"mfuko wa maji". Chombo cha maji kilitengenezwa kwa ngozi ya mnyama.

Maji yalipokwisha kwenye kiriba

"Mfuko wa maji ulipokuwa tupu" au "Walipokunywa maji yote"

umbali kama wa kutupa mshale

Hii ina maana ya umbali ambao mtu anaweza kutupa mshale kwa upinde. Hiini kama mita 100.

nisitazame kifo cha mtoto

Kitenzi hiki cha kujitegemea "kifo" kinaweza kuwekwa kama "kufa". "Sitaki kutazama mwanangu akifa"

akapaza sauti yake akalia

Hapa "sauti" ina maana ya sauti ya kilio chake. "kupaza sauti yake" ina maana ya kulia kwa sauti kubwa. "alipaza kwa sauti kubwa na kulia" au "alilia kwa sauti"

Genesis 21:17

kilio cha kijana

"kilio cha kijana". Hapa "kilio" ina maana ya sauti ambayo kijana alilia au alizungumza. "sauti ya Ishmaeli"

malaika wa Mungu

"mjumbe kutoka kwa Mungu" au "Mjumbe wa Mungu"

kutoka mbinguni

Hapa "mbinguni" ina maana ya sehemu ambapo Mungu huishi.

Nini kinakusumbua

"Tatizo ni nini" au "kwa nini unalia"

kilio cha kijana mahali alipo

Hapa "kilio" ina maana ya sauti ambayo kijana alilia au alizungumza. "sauti ya kijana alipokuwa amelala pale chini"

msimamishe mtoto

"msaidie kijana asimame"

nitamfanya kuwa taifa kubwa

Kumfanya Ishamaeli kuwa taifa kubwa ina maana Mungu atampa uzao mwingi ambao utakua taifa kubwa. "Nitafanya uzao wake kuwa taifa kubwa" au "Nitamfanya awe baba wa taifa kubwa"

Genesis 21:19

Mungu akayafunua macho ya Hajiri

Mungu kumfanya Hajiri aweze kuona kisima inazungumzwa kana kwamba alimfungua macho kihalisia. "Mungu alisababisha Hajiri kuona" au "Mungu alimuonyesha Hajiri"

kiriba

"chombo kilichoundwa na ngozi" au "mfuko"

kijana

"mvulana" au "Ishameli"

Mungu akawa pamoja na kijana

Hapa msemo wa "akawa pamoja" ni lahaja ambayo ina maana ya Mungu alimsaidia au alimbariki mvulana. "Mungu alimuongoza mvulana" au "Mungu alimbariki mvulana"

akawa mwindaji

"akawa na uwezo sana wa kutumia upinde na mishale"

akampatia mke

"akapata mke"

Genesis 21:22

Ikawa kwamba katika wakati ule

Msemo huu unaweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

Fikoli

Hili ni jina la mwanamume.

kamanda wa jeshi lake

"kamanda wa jeshi lake"

jeshi lake

neno "lake" lina maana ya Abimeleki.

Mungu yuko pamoja na wewe katika yote uyatendayo

Hapa msemo "yuko pamoja nawe" ni lahaja yenye maana ya Mungu husaidia au humbariki Abrahamu. "Mungu hubariki kila kitu ufanyacho"

Sasa basi

Neno "Sasa" halimaanishi "katika muda huu", lakini linatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata. "Sasa basi"

niapie hapa kwa Mungu

Hii ni lahaja yenye maana ya kutoa kiapo cha dhati kinachoshuhudiwa na mamlaka ya juu, kwa hali hii ni Mungu. "niahidi mimi na Mungu kama shahidi"

kwamba hutanifanyia baya

"ya kwamba hutanidanganya"

kwamba hutanifanyia baya ... pamoja na uzao wangu

Hii inaweza kuelezwa kwa njia ya chanya. "utanifanyia haki mimi na uzao wangu"

Onesha kwangu ... gano lile lile la uaminifu ambalo nimekuonesha wewe

Wanamume wawili walifanya agano kati yao. Kitenzi kinachojitegemea "umaninifu" kinaweza kuelezwa kama "mwaminifu" au "mtiifu". "Uwe mwaminifu kwangu na kwa nchi kama nilivyokuwa kwako"

kwa nchi

Hapa "nchi" ina maana ya watu. "kwa watu wa nchi"

nina apa

Hii inaweza kuelezwa kwa taarifa iliyoeleweka. "Ninaapa kuwa mwaminifu kwako na kwa watu wako kama ulivyokuwa kwangu"

Genesis 21:25

Abraham pia akamlalamikia Abimeleki

Maana zaweza kuwa 1) Abrahamu alikuwa akilalamika kuhusu kile kilichotokea au 2) "Abrahamu pia alimkaripia Abimeleki"

kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamekinyang'anya

"kwa sababu watumishi wa Abimeleki walichukua kisima kimoja cha visima vya Abrahamu"

wamekinyang'anya kwake

"kuchukua kutoka kwa Abrahamu" au "wamekitawala"

sijalisikia hadi leo hii

"Hii ni mara ya kwanza nimesikia kuhusu jambo hili"

Abrahamu akachukua kondoo na ng'ombe maksai akampatia Abimeleki

Hii ni ishara ya urafiki na ya kwamba Abrahamu amekubali kuweka agano na Abimeleki.

Genesis 21:28

Abraham akatenga wanakondoo wa kike saba peke yao

"Abrahamu aligawanya kondoo saba wa kike kutoka kundini"

saba

"7"

Nini maana ya hawa wanakondoo wa kike saba ambao umewatenga peke yao?

"Kwa nini umegawanya hawa kondoo saba kutoka kundini?"

utawapokea

"utachukua"

kutoka mkononi mwangu

Hapa "mkononi" una maana ya Abrahamu. "kutoka kwangu"

iwe ushahidi

Neno "iwe" ina maana ya zawadi ya kondoo saba.

ili kwamba iwe ushahidi kwangu

Kitenzi kinachojitegemea "shahidi" kinaweza kuelezwa kama "kuthibitisha". "Kuthibitisha kwa kila mtu"

Genesis 21:31

akaita mahali pale

"Abrahamu akapaita mahali pale"

Beerisheba

"Beerisheba inaweza kuwa na maana ya "kisima cha kiapo" au "kisima cha saba".

wote

"Abrahamu na Abimeleki"

Fikoli

Hili ni jina la mwanamume.

wakarudi katika nchi ya Wafilisti

"wakarudi katika nchi ya Wafilisti"

Genesis 21:33

mti wa mkwaju

Huu ni mti wa kijani ambao unaota jangwani. Inaweza kusemwa kwa ujumla zaidi. "mti"

Mungu wa milele

"Mungu aishiye milele"

siku nyingi

Hii ina maana ya muda mrefu zaidi

Genesis 22

Genesis 22:1

Ikawa kwamba

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

baada ya mambo hayo

Msemo huu una maana ya matukio katika sura ya 21.

Mungu akampima Abrahamu

Inasemekana Mungu alimpima Abrahamu kujifunza kama Abrahamu atakuwa mwaminifu kwake. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. Mungu alipima uaminifu wa Abrahamu.

Mimi hapa

"Ndio, nasikiliza" au "Ndio, kuna nini?"

mwanao wa pekee

Inasemekana ya kwamba Mungu anajua ya kuwa Abrahamu ana mtoto mwingine, Ishmaeli. Hii inasisitiza ya kwamba Isaka ni mwana ambaye Mungu alimuahidi kumpa Abrahamu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "mwana wako wa pekee ambaye nilikuahidi"

umpendaye

Hii inasisitiza upendo wa Abrahamu kwa mwanawe, Isaka.

nchi ya Moria

"nchi inayoitwa Moria"

akatandika punda wake

"akambebesha punda wake" au "akaweka juu ya punda kile kilichohitajika kwa ajili ya safari"

vijana wake

"watumishi"

kisha akapanga safari

"alianza safari yake" au "alianza kusafiri"

Genesis 22:4

Katika siku ya tatu

Neno "tatu" ni nambari ya mpango kwa ajili ya tatu. "Baada ya kusafiri kwa siku tatu"

akaona mahali pakiwa mbali

"akaona kwa mbali sehemu ambayo Mungu alizungumzia"

vijana wake

"watumishi"

Tutaabudu

Neno "tutaabudu" ina maana ya Abrahamu pekee na Isaka.

tutarudi hapa penu

"nitarudi kwako"

akaziweka juu ya Isaka mwanawe

"akamfanya Isaka, mwanawe, kuibeba"

Mkononi mwake

Hapa "mkononi mwake mwenyewe" inasisitiza ya kwamba Abrahamu mwenyewe alibeba vitu hivi. "Abrahamu mwenyewe alibeba"

moto

Hapa "moto" ina maana ya sufuria yenye mkaa unaowaka au tochi au taa. "kitu cha kuanzishia moto"

wote wawili wakaondoka pamoja

"waliondoka pamoja" au "wote wawili waliondoka pamoja"

Genesis 22:7

Baba yangu

Hii ni njia ya upendo ya mwana kuongea kwa baba yake.

Nipo hapa

"Ndio, nasikiliza" au "Ndio, kuna nini?"

Mwanangu

Hii ni njia ya upendo ya baba kuongea kwa mwanawe.

moto

Hapa "moto" ina maana ya sufuria yenye mkaa unaowaka au tochi au taa. "kitu cha kuanzishia moto"

mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa

"mwanakondoo ambaye utamtoa kama sadaka wa kuteketezwa"

Mungu mwenyewe

Hapa "mwenyewe" inasisitiza ya kwamba Mungu atatoa mwanakondoo.

atatupatia

"atatupatia sisi"

Genesis 22:9

Walipofika mahali

"Abrahamu na Isaka walipofika katika sehemu ile"

akamfunga

"akamfunga kamba"

juu ya madhabahu, juu ya zile kuni

"juu ya kuni zilizokuwa juu ya madhabahu"

akanyoosha mkono wake akachukua kisu

"akaokota kile kisu"

Genesis 22:11

malaika wa Yahwe

Maana zinaweza kuwa 1) Yahwe alijifanya kuonekana kama malaika au 2) huyu alikuwa mmoja wa malaika wa Yahwe au 3) huyu alikuwa mjumbe maalumu kutoka kwa Mungu (baadhi ya wasomi wanadhani alikuwa Yesu). Kwa sababu msemo hauleweki vizuri, ni bora kutafsiri kama "malaika wa Yahwe" kwa kutumia neno la kawaida linalotumika kwa "malaika".

kutoka mbinguni

Hii ina maana ya sehemu ambapo Yahwe anaishi.

Mimi hapa

"Ndio,ninasikiliza" au "Ndio, kuna nini?"

usinyooshe mkono wako juu ya kijana, wala usifanye jambo lolote kumdhuru

Msemo "usinyooshe mkono wako juu ya" ni namna ya kusema "usimdhuru". Mungu alisema kitu kile kile mara mbili kusisitiza ya kwamba Abrahamu hakupaswa kumdhuru Isaka. "usimdhuru kijana kwa njia yoyote ile"

sasa najua ... kwa ajili yangu

Maneno "najua" na "yangu" yana maana ya Yahwe. Unapotafsiri kilichomo ndani ya nukuu, sema kwa namna ambayo Yahwe alitumia maneno ya "najua" na "yangu" alipomaanisha Yahwe.

unamcha Mungu

Hii ina maana ya kumheshimu Mungu kwa undani na kuonyesha heshima hiyo kwa kumtii yeye.

kuona

"kwa sababu ninaona"

hukumzuilia mwanao ... kwa ajili yangu

"haujamshikilia nyuma mwanao ... kwangu" Hii inaweza kusemwa kwa njia ya chanya. "ulikuwa tayari kumtoa mwanao ... kwangu"

mwanao, mwanao wa pekee

Inasemekana ya kwamba Mungu anajua ya kuwa Abrahamu ana mtoto mwingine, Ishmaeli. Hii inasisitiza ya kwamba Isaka ni mwana ambaye Mungu alimuahidi kumpa Abrahamu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "mwana wako wa pekee ambaye nilikuahidi"

Genesis 22:13

tazama

Neno "tazama" hapa linatuamsha kuvuta nadhari kwa taarifa ya kushangaza inayofuata.

kulikuwa na kondoo mume amenaswa pembe zake kichakani

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kulikuwa na kondoo dume aliyekwama pembe zake kichakani" au "kulikuwa na kondoo dume aliyekwama kichakani"

akaenda akamchukua kondoo

"Abrahamu alienda kwa kondoo dume na kumchukua"

atatoa ... itatolewa

"atatupatia sisi"

hata leo

"hata sasa". Hii ina maana ya hata katika kipindi ambacho mwandishi alikuwa akiandika kitabu hiki.

itatolewa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yeye atatoa"

Genesis 22:15

Malaika wa Yahwe

Maana zinaweza kuwa 1) Yahwe alijifanya kuonekana kama malaika au 2) huyu alikuwa mmoja wa malaika wa Yahwe au 3) huyu alikuwa mjumbe maalumu kutoka kwa Mungu (baadhi ya wasomi wanadhani alikuwa Yesu). Kwa sababu msemo hauleweki vizuri, ni bora kutafsiri kama "malaika wa Yahwe" kwa kutumia neno la kawaida linalotumika kwa "malaika".

mara ya pili

Neno "pili" ni namba ya mpango kwa ajili ya mbili

kutoka mbinguni

Hapa neno "mbinguni" lina maana ya sehemu anapoishi Mungu.

na kusema - Hiki ni kiapo cha Yahwe

"na kuzungumza ujumbe huu kutoka kwa Yahwe" au "na kutamka maneno haya ya Yahwe". Hii ni njia ya fasaha ya kusema ya kwamba maneno yanayofuata yanatoka moja kwa moja kwa Yahwe.

Kwa ajili ya nafsi yangu nimeapa

"Nimeahidi na mimi ni shahidi wangu mwenyewe". Msemo "kuapa kwa" una maana kutumia jina la kitu au mtu kama msingi au nguvu ambayo kiapo kinafanyika. Hakuna kitu chenye nguvu zaidi ya Yahwe kuapa kwa jina lake mwenyewe.

umefanya jambo hili

"umenitii"

hukunizuilia mwanao

"hukumzuia nyuma mtoto wako wa kiume". Hii inaweza kuwekwa katika hali ya chanya. "ulikuwa tayari kumtoa mwanao kwangu"

mwanao, mwanao wa pekee

Inaonyesha ya kwamba Mungu anajua ya kuwa Abrahamu ana mtoto mwingine, Ishmaeli. Hii inasisitiza ya kwamba Isaka ni mwana ambaye Mungu alimuahidi kumpatia Abrahamu.

hakika nitakubariki

"hakika nitabariki"

nitakuzidishia uzao wako

Nitasababisha uzao wako kuongezeka tena na tena" au "Nitasababisha uzao wako kuwa mwingi"

kama nyota za angani, na kama mchanga ulioko kwenye ufukwe wa bahari

Mungu alifananisha uzao wa Abrahamu na nyota na mchanga. Kama vile watu wasivyoweza kuhesabu idadi kubwa ya nyota au chembe za mchanga, kwa hiyo kutakuwa na uzao mwingi wa Abrahamu ambao watu wasingeweza kuwahesabu. "zaidi ya kile uwezavyo kuhesabu"

kama nyota za angani

Hapa neno "mbinguni" ina maana ya kila kitu tunachoona juu ya dunia, kujumlisha jua, mwezi na nyota.

watamiliki lango la adui zao

Hapa "lango" linawakilisha mji wote. "Kumiliki lango la adui zake" ina maana ya kuangamiza adui zake. "atawashinda adui zake kabisa"

Genesis 22:18

Taarifa ya Jumla

Malaika wa Yahwe anaendelea kuzungumza na Abrahamu.

mataifa yote ya dunia watabarikiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mimi, Bwana, nitabariki watu wote wanaoishi mahali pote"

mataifa ya dunia

Hapa "mataifa" ina maana ya watu wa matiafa.

umetii sauti yangu

Hapa "sauti" ina maana ya kile ambacho Mungu alisema. "umetii kile nilichosema" au "umenitii"

Abraham akarejea

Ni Abrahamu pekee aliyetajwa kwa sababu alikuwa baba, lakini imeonekana ya kwamba mwanawe alikwenda naye. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Abrahamu na mwanawe walirejea"

vijana

"watumishi"

wakaondoka

"waliondoka sehemu ile"

akakaa Beerisheba

Ni Abrahamu pekee aliyetajwa kwa sababu alikuwa kongozi wa familia yake na watumishi wake, lakini imeonekana walikuwa pamoja naye. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Abrahamu na watu wake alikaa Beerisheba"

Genesis 22:20

Ikawa kwamba baada ya mambo haya

"Baada ya matukio haya". Msemo "mambo haya" una maana ya matukio ya Mwanzo 22:1-19

Abraham aliambiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mtu alimwambia Abrahamu"

Milka amemzalia pia watoto

"Milka pia alizaa watoto"

Milka

Hili ni jina la mwanamke

walikuwa ni Usi mzaliwa wa kwanza, Busi ndugu yake

"Jina la mwanawe wa kwanza lilikuwa Usi, na majina ya watoto waliosalia walikuwa Busi ndugu yake"

Usi ... Busi ... Kemueli ... Aramu ...Kesedi, Hazo, Pildasi, Yildashi, na bethueli

Haya yote ni majina ya wanamume. Hawa wote kasoro Aramu walikuwa watoto watoto wa nahori na Milka.

Genesis 22:23

Bethueli akawa baba wa Rebeka

"Baadae Bethueli akawa baba wa Rebeka"

Hawa walikuwa ni wale watoto wanane ambao Milka alizaa kwa Nahori, ndugu yake na Abraham

"hawa walikuwa watoto wanane wa Milka na Nahori, ndugu yake Abrahamu" Hii ina maana ya watoto waliorodheshwa katika 22:20.

nane

"8"

Suria wake

"Suria wa Nahori"

Reuma

Hili ni jina la mwanamke.

pia akamzaa

"pia akajifungua"

eba, Gahamu, Tahashi, na Maaka

Haya yote ni majina ya wanamume

Genesis 23

Genesis 23:1

Sara akaishi mika mia moja na ishirini na saba

miaka saba - 'Sara aliishi miaka 127"

Hii ndiyo ilikuwa ni miaka ya maisha ya Sara

Baadhi ya watafsiri hawajumlishi sentensi hii.

Kiriathi Arba

Hili ni jina la mji.

Abraham akaomboleza na kumlilia Sara

"Abrahamu alikuwa na huzuni sana na akalia kwa sababu Sara alikufa"

Genesis 23:3

akainuka na kutoka kwa mkewe aliye kufa

"akasimama na kuacha mwili wa mke wake"

watoto wa kiume wa Hethi

Hapa "watoto" ina maana ya wale waliotokana na Hethi. "uzao wa Hethi" au "Wahiti"

miongoni mwenu

Wazo hili linaweza kuelezwa kwa lugha ya eneo. "katika nchi yako" au "hapa"

Tafadhari nipatieni mahali

"Niuzie sehemu ya nchi" au "Niruhusu kununua kipande cha nchi"

wafu wangu

Kivumishi kidogo "wafu" kinaweza kuelezwa kama kivumishi au kitenzi. "mke wangu aliyekufa" au "mke wangu ambaye amekufa"

Genesis 23:5

Wana wa Hethi

Hapa "wana" ina maana ya wale waliotokana na Hethi. "uzao wa Hethi"

bwana wangu

Msemo huu unatumika kuonyesha heshima kwa Abrahamu.

mwana wa Mungu

Hii ni lahaja. Hii yaweza kuwa na maana ya "mwanamume mwenye mamlaka" au "kiongozi mwenye nguvu"

wafu wako

Kivumishi kidogo cha "wafu" kinaweza kusemwa kama kitenzi au kwa njia ya urahisi kama "mke". "mke wako ambaye amekufa" au "mke wako"

katika makaburi yetu utakayochagua

"sehemu bora kabisa ya makaburi yetu"

atakaye kuzuilia kaburi lake

"kuzuia sehemu ya makaburi kwako" au " kukataa kukupatia makaburi"

Genesis 23:7

kusujudu

Hii ina maana ya kuinama au kupiga goti chini kabisa kwa kuonyesha unyenyekevu wa heshima na taadhima kwa mtu.

kwa watu wa nchi ile, kwa wana wa Hethi

"kwa wana wa Hethi waliokuwa wakiishi katika eneo lile"

wana wa Hethi

Hapa "wana" ina maana ya wale amabo wametoka kwa Hethi. "uzao wa Hethi"

wafu wangu

Kivumishi kidogo "wafu" kinaweza kuelezwa kama kivumishi au kitenzi. "mke wangu aliyekufa" au "mke wangu ambaye amekufa"

Efroni .... Sohari

Haya ni majina ya wanamume.

pango la Makpela, ambalo analimiliki, ambalo liko mwishoni mwa shamba lake

"pango lake ambalo lipo mwishoni mwa shamba lililoko Makpela"

pango la Makpela

"pango lililoko Makpela". Makpela ilikuwa jina ya eneo au sehemu. Efroni alimiliki shamba katika Makpela na pango ambalo lilikuwa katika shamba.

ambalo analimiliki

Hii inatueleza jambo kuhusu pango lile. Efroni alimiliki pango lile.

ambalo liko mwishoni mwa shamba lake

Hii pia inatumabia jambo kuhusu pango lile. Pango lilikuwa mwishoni mwa shamba la Efroni.

aniuzie waziwazi

"niuzie mbele yenu wote" au "niuzie mbele ya uwepo wenu"

kama miliki

"kama kipande cha nchi ambacho nitamiliki na kutumia"

Genesis 23:10

Sasa Efroni alikuwa ameketi miongoni mwa wana wa Hethi

Hapa "Sasa" inatumika kuweka alama ya badiliko ya habari kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Efroni.

Efroni

Hili ni jina la mwanamume.

wana wa Hethi

Hapa "wana" ina maana ya wale ambao wametoka kwa Hethi. "uzao wa Hethi"

alipowasikia wana wa Hethi

Nomino inayojitegemea "alipowasikia" inaweza kuwekwa kama "kusikia" au "kusikiliza". "ili kwamba wana wote wa Hethi waweze kumsikia" au "wakati wana wote wa Hethi walipokuwa wakimsikiliza"

wote ambao walikuwa wamekuja langoni mwa mji wake

Hii inaelezea ni wana wapi wa Hethi walikuwa wakisikiliza. "wale wote waliokusanyika langoni mwa mji"

langoni mwa mji wake

Lango la mji ilikuwa mahali ambapo viongozi wa mji walikutana kufanya maamuzi muhimu.

mji wake

"mji ambao aliishi". Msemo huu unaonyesha ya kwamba Efroni alikuwa wa mji ule. Haimaanishi ya kwamba aliumiliki.

bwana wangu

Huu msemo umetumika kuonyesha heshima kwa Abrahamu.

mbele ya wana wa watu wangu

Hapa "mbele ya" ina maana ya watu waliokuwa kama mashahidi. "pamoja na wananchi kama mashahidi"

wana wa watu wangu

Hii ina maana ya "wananchi wenzangu" au "Wahiti wenzangu"

watu wangu

"watu wangu". Msemo huu unaonyesha ya kwamba efroni alikuwa sehemu ya kundi la watu. Haimaanishi ya kwamba alikuwa kiongozi wao.

Ninakupatia uzike wafu wako

"Ninakupatia. Zika wafu wako"

wafu wako

Kivumishi kidogo "wafu" kinaweza kuelezwa kama kitenzi. "mke wangu aliyekufa" au "mke wangu ambaye amekufa"

Genesis 23:12

akasujudu chini

Hii ina maana ya kuinama au kupiga goti chini kabisa kwa kuonyesha unyenyekevu wa heshima na taadhima kwa mtu.

watu wa nchi

"watu wanaoishi katika eneo lile"

watu wa nchi ile wakisikiliza

Nomino inayojitegemea "wakisikiliza" inaweza kusemwa kama "sikia" au "sikiliza". "ili kwamba watu wanaoishi katika eneo lile waweze kusikia" au "wakati watu waliokuwa wakiishi katika eneo lile wakisikiliza"

ikiwa uko radhi

Neno "lakini" linaonyesha tofauti. Efroni alitaka kutoa shamba kwa Abrahamu; Abrahamu alitaka kulipia. "hapana, lakini kama upo tayari" au "Hapana, lakini kama unakubaliana na hili"

Nitalipia shamba

"Nitakupa fedha kwa ajili ya shamba"

wafu wangu

Kivumishi cha "wafu" kinaweza kuelezwa kama kitenzi au "mke". "Mke wangu aliyekufa" au "mke wangu"

Genesis 23:14

Efroni

Hili ni jina la mwanamume.

Tafadhali bwana wangu, nisikilize

"Nisikie, bwana wangu" au "Nisikilize, bwana mwema"

bwana wangu

Msemo huu unatumika kuonyesha heshima kwa Abrahamu.

Kipande cha ardhi kinathamani ya shekeli mia nne za fedha, na hiyo ni kitu gani kati yangu mimi na wewe?

Efroni alimaanisha ya kwamba kwa kuwa yeye na Abrahamu walikuwa matajiri wote, shekeli 400 za dhahabu zilikuwa kiwango kidogo. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Kipande cha shamba kina thamani cha shekeli mia nne za fedha tu. Kwako na mimi, hii si kitu"

shekeli mia nne za fedha

Hii ni kama kilogramu 4.5 za fedha

mia nne

"400"

wazike wafu wako

Kivumishi cha "wafu" kinaweza kuelezwa kama kitenzi au "mke". "Nenda kamzike mke wako ambaye amekufa"

Abrahamu akampimia Efroni kiwango cha fedha alizosema

"Abrahamu alipima fedha na kumpatia Efroni kiwango" au "Abrahamu alimhesabia Efroni kiwango cha fedha"

kiwango cha fedha alizosema

"kiwango cha fedha ambacho Efroni alikitaja"

wana wa Helthi wakisikiliza

Nomino inayojitegemea "wakisikiliza" inaweza kusemwa kama "sikia" au "sikiliza". "ili kwamba wana wa Hethi walimsikia" au "wakati wana wa Hethi walikuwa wakisikiliza"

wana wa Helthi

Hapa "watoto" ina maana ya wale waliotokana na Hethi. "uzao wa Hethi"

kwa mujibu wa viwango vya vipimo vya kibiashara

"kwa kutumia viwango vya vipimo vya uzito ambao wafanyabiashara walitumia." Hii inaweza kuelezwa kama sentensi mpya. "Alipima fedha kwa njia ile ile ambayo wafanyabiashara walikuwa wakitumia kupima"

Genesis 23:17

Makpela

Makpela lilikuwa jina la eneo au mahali.

Mamre

Hii ilikuwa jina jingine kwa mji wa Hebroni. Inawezekana iliitwa baada ya Mamre, rafiki yake Abrahamu aliyeishi pale"

shamba pamoja na pango lililokuwamo ndani yake na miti yote

Msemo huu unafafanua kile ambacho mwandishi alimaanisha alipoandika "shamba la Efroni". Halikuwa shamba tu, lakini pia pango na miti katika shamba.

kwa Abraham kwa njia ya manunuzi

"ikawa mali ya Abrahamu alipoinunua" au "ikawa ya Abrahamu baada ya kuinunua"

mbele ya wana wa Hethi

Hapa "mbele ya" ina maana ya watu kutumika kama mashahidi. "pamoja na watu wa Hethi wakitazama kama mashahidi"

wana wa Hethi

Hapa "wana" ina maana ya wale amabo wametoka kwa Hethi. "uzao wa Hethi"

wote waliokuja malangoni pa mji wake

Hii inaeleza ni wana wapi wa Hethi waliomwona Abrahamu akinunua mali ile. "wale wote waliokusanyika langoni mwa mji"

malangoni pa mji wake

Malango ya mji palikuwa pale ambapo viongozi wa mji walikutana kufanya maamuzi muhimu.

mji wake

"mji aliokuwa akiishi". Msemo huu unaonyesha Efroni alikuwa wa mji ule. Haimaanishi ya kwamba aliumiliki.

Genesis 23:19

Baada ya haya

"Alipomaliza kununua shamba lile"

pango la shamba

"pango katika shamba lile"

shamba la Makpela

"shamba katika Makpela"

ambayo ni Hebroni

Maana zaweza kuwa 1) Mamre lilikuwa jina lingine la Hebroni au 2) Hebroni alikuwa akijulikana kama Mamre au 3) Mamre alikuwa karibu sana na mji mkubwa wa Hebroni, kwa hiyo watu waliuita Hebroni mara kwa mara.

kwa Abraham kama milki na eneo la kuzikia

"ikawa mali ya Abrahamu ya makaburi aliponunua kutoka kwa wana wa Hethi"

wana wa Hethi

Hapa "wana" ina maana ya wale amabo wametoka kwa Hethi. "uzao wa Hethi"

Genesis 24

Genesis 24:1

Sasa

Neno hili linatumika hapa kuweka alama ya kuonyesha mapumziko kwa simulizi kuu. Hapa mwandishi anaanza kueleza sehemu mpya ya simulizi.

Weka mkono wako chini ya paja langu

Abrahamu alikuwa akitaka kumuliza mtumishi wake kuapa kufanya jambo. Kuweka mkono chini ya paja la Abrahamu ingeonyesha ya kwamba hakika angefanya kile alichotaka kuapa kukifanya.

nitakufanya uape

Hii inaweza kuelezwa kama amri. "apa"

uape kwa Yahwe

Msemo "uape kwa" una maana ya kutumia jina la kitu au mtu kama msingi au nguvu ambayo kiapo kinafanywa. "niahidi mimi pamoja na Yahwe kama shahidi wako"

Mungu wa Mbingu na Mungu wa nchi

"Mungu wa mbingu na nchi". Maneno "mbingu" na "nchi" yanatumika pamoja kumaanisha kila kitu ambacho Mungu aliumba. "Mungu wakila kitu mbinguni na nchini"

mbingu

Hii ina maana ya sehemu ambayo Mungu anaishi.

kutoka kwa mabinti wa Wakanaani

"kutoka kwa wanawake wa Kanaani" au "kutoka kwa Wakaanani". Hii ina maana ya wanawake wa Kanaani.

miongoni mwao wale nikaao kati yao

"miongoni mwao wale namoishi" Hapa "nikaapo" ina maana ya Abrahamu na familia yake yote na watumishi. "miongoni mwao tunapoishi"

Lakini utakwenda

Hii inaweza kuelezwa kama amri. "Apa ya kwamba utakwenda" au "Lakini ondoka"

ndugu zangu

"familia yangu"

Genesis 24:5

Itakuwaje

"nitafanyaje iwapo"

hatakuwa tayari kufuatana nami

"hatanifuata" au "akikataa kurudi pamoja nami"

Je nitamrudisha mwanao katika nchi ambayo ulitoka

"Je nimchukue mwanao kuishi katika nchi ambayo umetoka"

Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu kule

Msemo "hakikisha" unasisitiza amri inayofuata. "Kuwa mwangalifu usimpeleke mwanangu kule" au "Hakika hautakiwi kumpeleka mwanangu kule"

ambaye alinitoa mimi kutoka katika nyumba ya baba yangu

Hapa "nyumba" ina maana ya watu katika familia. "aliyenichukua kutoka kwa baba na familia yangu yote"

aliniahidia kwa kiapo maalumu

"aliapa kiapo kwangu"

akisema, 'Nitawapa uzao wako nchi hii,'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "akisema kwamba angempataia nchi hii kwa uzao wake"

atatuma malaika wake

Maneno "atatuma" na ":wake" yana maana ya Yahwe.

Genesis 24:8

Taarifa ya Jumla:

Mstari wa 8 ni muendelezo wa maelekezo Abrahamu alimpatia mtumishi wake.

Lakini ikiwa mwanamke hatakuwa tayari kukufuata

"Lakini kama mwanamke anakataa kurudi pamoja nami." Abrahamu alikuwa akijibu swali la mtumishi wake kutoka 24:5.

utakuwa huru katika hiki kiapo changu

"utafunguliwa kutoka kwa kiapo ulichokifanya kwangu". Kutokamilisha kiapo inazungumziwa kana kwamba mtu anakuwa huru kutoka kwa kitu ambacho kimemkamata. "hautapaswa kufanya kile ulichoapa kwangu ambcho ulipaswa kufanya"

akaweka mkono wake jini ya paja la Abrahamu bwana wake

Hii ilikuwa ikionyesha ya kwamba hakika angefanya kile alichoapa kufanya.

akaapa kwake

"akafanya kiapo kwake"

kuhusiana na jambo hili

"kuhusu ombi la Abrahamu" au "ya kwamba angefanya kile alichoambiwa na Abrahamu"

Genesis 24:10

na akaondoka. Akachukua pia

Sentensi inayoanza na "Akachukua pia" inatupa taarifa ya nyongeza kuhusu nini mtumishi alichukua katika safari. Alivikusanya kabla ya kuondoka.

Akachukua pia aina zote za zawadi kutoka kwa bwana wake

Hii ina maana alichukua pia vitu vingi ambavyo bwana wake alitaka akawapatie familia ya mwanamke.

Akaondoka na kwenda

"akajiandaa na kuondoka" au "aliondoka na kwenda"

mji wa Nahori

Maana zaweza kuwa 1) "mji ambapo Nahori aliishi" au 2) "mji ulioitwa Nahori".

Akawapigisha magoti ngamia

Ngamia ni wanyama warefu wenye miguu mirefu. Aliwafanya wainamishe miguu yao na kushusha miili yao ardhini. "Aliwafanya ngamia kulala chini"

kisima cha maji

"kisima cha maji" au "kisima"

kuchota maji

"kufuata maji"

Genesis 24:12

Kisha akasema

"Kisha mtumishi akasema"

anijalie kufanikiwa leo na aoneshe agano la uaminifu kwa bwana wangu Abrahamu

Unaweza kuiweka hii kwa neno kiunganishi "kwa". Hii inaonyesha kwa uwazi jinsi mtumishi anataka Mungu amuonyeshe uaminifu wake. "Onyesha agano la uaminifu kwa bwana wangu Abrahamu kwa kunipatia mafanikio leo"

anijalie kufanikiwa

"nipatie mafanikio". Mtumishi alitaka kupata mke mwema kwa mwana wa Abrahamu. Nomino inayojitegemea ya "mafanikio" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "nisaidie nifanikiwe" au "nifanye niweze kufanya kile nilichokuja kukifanya"

aoneshe agano la uaminifu kwa bwana wangu Abrahamu

Huu ni uaminifu kwa sababu ya agano ambalo Mungu alifanya na Abrahamu. Nomino inayojitegemea ya "uaminifu" inaweza kuelezwa "uwe mwaminifu". "Uwe mwaminifu kwa bwana wangu Abrahamu kwa sababu ya agano lako"

Tazama

Hapa neno "tazama" linaongeza msisitizo kwa kile kifuatacho.

chemchemi ya maji

"chemichemi" au "kisima"

binti za watu wa mji

"wanawake vijana wa mji ule"

Na itokee kama hivi

"Na itokee kwa namna hii" au "Fanya hii ifanyike"

Nikimwambia msichana, 'tafadhari tua mtungi wako ili niweze kunywa maji,'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Hii inaweza kuelezwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Ninapomuuliza msichana aniruhusu kunywa maji kutoka kwenye mtungi wake"

tafadhari tua mtungi wako

Wanawake walibeba mitungi juu ya mabega yao. Alitakiwa kushusha na kumpatia mwanamume anywe.

mtungi

chombo cha ukubwa wa kati kilichoundwa na udongo kinachotumika kubeba na kumwaga vimiminikio.

kuwa umeonesha agano la uaminifu kwa bwana wangu

Nomino inayojitegemea "uaminifu" inawezakuelezwa kama "alikuwa mwaminifu". "ya kwamba ulikuwa mwaminifu kwa bwana wangu kwa sababu ya agano lako"

Genesis 24:15

Ikawa kwamba

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama

tazama

Neno "tazama" hapa linatuamsha kusikiliza taarifa ya kushangaza inayofuata.

mtungi

chombo cha ukubwa wa kati kilichoundwa na udongo kinachotumika kubeba na kumwaga vimiminikio.

Rebeka alizaliwa na Bethueli mwana wa Milka, mke wa Nahori, ndugu yake na Abrahamu

"Baba yake Rebeka alikuwa Bethueli. Wazazi wa Bethueli walikuwa Milka na Nahori. Nahori alikuwa kaka yake Abrahamu"

Bethueli

Bethueli alikuwa baba yake Rebeka.

Nahori

Hili ni jina la mwanamume.

Milka

Milka alikuwa mke wa Nahori na mama yake Bethueli.

kashuka kisimani ... na kupanda juu.

Kisima kilikuwa sehemu ya chini katika muinuko wa chini ambapo mtumishi alikuwa amesimama.

Genesis 24:17

kumlaki yule msichana

"kukutana na yule msichana"

maji kidogo

"maji kiasi"

mtungi

chombo cha ukubwa wa kati kilichoundwa na udongo kinachotumika kubeba na kumwaga vimiminikio.

bwana wangu,

"bwana". Hapa mwanamke anatumia msemo huu wa heshima kwa mwanamume, ingawa yeye sio mtumwa wake.

kwa haraka akatua mtungi wake juu ya mkono wake

"alishusha mtungi wake haraka". Alikuwa akibeba mtungi juu ya bega lake. Ilimbidi ahushe ili apate maji kwa ajili ya mtumishi.

Genesis 24:19

Nitachota maji

"Nitafuata maji"

Hivyo akaharakisha akamwaga maji yaliyokuwa mtungini

"Kwa hiyo aliyatoa maji ndani ya mtungi haraka"

chombo cha kunywshea mifugo,

"chombo cha kunywshea wanyama". Chombo cha kunyweshea wanayma ni chombo kilicho wazi kinachoshikilia maji kwa ajili ya wanyama kunywa.

Genesis 24:21

Yule mtu

"Mtumishi"

akamtazama msichana

"akamtazama Rebeka" au "alimtazama yule msichana"

kuona

Kujifunza jambo huwa kunazungumzwa kana kwamba kinaweza kuona. "kujua" au "kukusudia"

amefanikisha njia yake

"Kutimiza lengo la safari yake" au "alifanya safari yake iwe ya mafanikio". Unaweza kuiweka wazi nini mtumishi alijaribu kukusudia. "alimwonyesha mwanamke nani ambaye angekuwa mke wa Isaka"

au la

unaweza kuweka kwa uwazi taarifa inayoeleweka. "au kutofanikiwa katika safari yake"

pete ya pua ya dhahabu yenye uzito wa nusu shekeli

"pete ya pua ya dhahabu ambayo ilikuwa na uzito wa gramu sita". Uzito unaonyesha thamani ya pete hiyo. "pete ya pua ya dhahabu ya gharama"

bangili mbili za dhahabu kwa ajili ya mikono yake zenye uzito wa shekeli kumi

"bangili mbili za dhahabu kwa ajili ya mikono yake zenye uzito wa gramu 110". Uzito unaonyesha ukubwa na thamani yao. "bangili mbili za dhahabu kwa ajili ya mikono yake"

wewe ni binti wa nani

"Nani baba yako"

Je kuna nafasi nyumbani mwa baba yako

"Je kuna nafasi katika nyumba ya baba yako"

kwa ajili yetu

Ni wazi ya kwamba wanamume wengine walikuwa katika safari hii na mtumishi wa Abrahamu. Hapa "yetu" ina maana mtumishi na wale aliokuwa amesafiri pamoja naye.

kupumzika usiku

"kukaa usiku huu" au "kukaa usiku wa leo"

Genesis 24:24

Akamwambia

"rebeka alisema" au "msichan yule alisema"

kwake

"kwa mtumishi"

Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, ambaye alimzaa kwa Nahori

"Bethueli ni baba yangu, na wazazi wake ni Milka na Nahori"

Tunayo malisho tele na chakula

Inaeleweka ya kwamba malisho na chakula yalikuwa kwa ajili ya ngamia. "Tuna malisho na chakula cha kutosha kwa ajili ya ngamia"

kwa ajili yako kulala usiku

"kwa ajili yako kulala usiku" au "ambapo utalala kwa usiku huu"

kwa ajili yako

Hapa "yako" ina maana ya mtumishi na wale aliosafiri naye"

Genesis 24:26

yule mtu

"mtumishi"

akainama chini

Hii ni ishara ya unyenyekevu mbele za Mungu.

hakuacha agano lake la uaminifu na kweli yake mbele ya bwana wangu

"hakuacha kuonyesha agano lake la uaminifu na kweli kwa bwana wangu." Nomino zinazojitegemea "uaminifu" na "kweli" zinaweza kuelezwa kama "kuwa mwaniminfu na mkweli". "ameendelea kuwa mwaminifu na mkweli kwa sababu ya agano lake na bwana wangu"

hakuacha

Hii inaweza kuelezwa kwa namna ya chanya. "anaendelea kuonyesha"

ndugu zake

"familia" au "ukoo"

Genesis 24:28

akakimbia na kwenda kuwaeleza watu wa nyumba ya mama yake

Hapa "nyumba" ina maana ya watu waliokuwa wakiishi katika nyumba ya mama yake. "alikimbia katika nyumba na kumwambia mama yake na kila mtu pale"

mambo yote haya

"kila kitu ambacho kilitokea"

sasa

Neno hili linatumika hapa kuweka alama kuweka mapumziko katika simulizi kuu. hapa mwandishi anaelezea taarifa ya nyuma kuhusu Rebeka. Mwandishi anamtambulisha kaka yake, Labani, katika simulizi.

Akisha kuona hereni ya puani ... na kusikia maneno ya Rebeka dada yake

Mambo haya yalitokea kabla hajakimbia nje kwa mwanamume. Hii inatuambia kwa nini Labani alikimbia nje kwa mwanamume yule.

na kusikia maneno ya Rebeka dada yake, "Hivi ndivyo yule mtu alicho niambia,"

Hii inaweza kuelezwa kama nukuu isiyokuwa moja kwa moja. "alipokuwa amesikia ya kuwa dada yake Rebeka amemwambia nini mwanamume amekisema kwake"

tazama

"naam". Neno "tazama" hapa linaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata.

Genesis 24:31

Njoo

"Njoo ndani" au "Ingia"

uliye barikiwa na Yahwe

"wewe ambaye Yahwe amekubariki"

uliye

Hapa neno la "uliye" lina maana ya mtumishi wa Abrahamu.

Kwa nini umesimama nje?

Labani alitumia swali hili kumkaribisha mtumishi wa Abrahamu katika nyumba yake. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hauhitaji kubaki nje"

Kwa hiyo yule mtu akaingia ndani ya nyumba

Neno "akaingia" linaweza kutafsiriwa kama "akaenda"

kashusha mizigo kutoka kwa wale ngamia

Haipo wazi nani alifanya kazi hii. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtumishi wa Labani alishusha mizigo kutoka kwa ngamia" au "ngamia walishushwa mizigo"

Ngamia wakapatiwa malisho na chakula, na maji yakatolewa

Hii haisemi nani alifanya kazi hii. Iwapo utaweka hii katika hali ya kutenda basi sema "watumishi wa Labani" kama jambo. "Watumishi wa Labani waliwapa malisho na chakula ngamia, na wakatoa maji"

kuosha miguu yake ... naye

"kwa watumishi wa Abrahamu na wanamume waliokuwa naye kuosha miguu yao"

Genesis 24:33

Wakaandaa

Hapa neno "wakaandaa" lina maana ya watu wa familia ya Labani au watumishi wa nyumbani.

chakula mbele yake

"kumpatia mtumishi chakula"

niseme kile ninacho paswa kusema

"kuzungumza maneno yangu" au "nimekuambia kwa nini nipo hapa"

amekuwa mtu mkuu

Hapa neno "amekuwa" lina maana ya Abrahamu.

amekuwa mkuu

"amekuwa tajiri sana"

Amempatia

Neno "amempatia" lina maana ya Yahwe.

Genesis 24:36

Taarifa ya Jumla:

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

alimzalia mwana bwana wangu

"alimzaa mtoto wa kiume"

amempatia ... mwanawe

"bwana wangu amempatia ... kwa mtoto wake wa kiume"

Bwana wangu aliniapisha, akisema

"Bwana wangu amenifanya niape ya kwamba nitafanya kile alichonimabia kufanya. Alisema"

kutoka kwa mabinti wa Wakanaani

Hii ina maana ya wanawake wa Kaanani. "kutoka kwa wanawake wa Kaanani" au "kutoka kwa Wakaanani"

ambao kwao nimefanya makazi

"miongoni mwa wale ninamoishi". Hapa "ninamoishi" ina maana ya Abrahamu na familia yake yotena watumishi wake. "miongoni mwa wale tuishipo"

kwa ndugu zangu

"kwa ukoo wangu"

Genesis 24:39

Taarifa ya Jumla:

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

pengine mwanamke huyo asikubali kufuatana nami

Hili ni jambo ambalo linaweza kutokea. "Je kama mwanamke hatakuja pamoja nami" au "Nitafanyaje iwapo mwanamke huyu hatakuja pamoja nami?"

mbaye ninakwenda mbele yake

Kumtumikia Yahwe inazungumzwa kana kwamba Abrahamu alikuwa akitembea ndani ya uwepo wa Yahwe. "ambaye namtumikia"

atakufanikisha njia yako

"atafanya safari yako kufanikiwa"

ukoo wa baba yangu

"familia"

Lakini utakuwa huru katika kiapo changu ikiwa utafika kwa ndugu zangu na wasikuruhusu kuja naye. Ndipo utakuwa huru katika kiapo changu

Hii ni nadharia tete ambayo Abrahamu alifikiri isingeweza kutokea. Maana zaweza kuwa 1) "Kuna njia moja tu ya kuwa huru na kiapo changu: iwapo utakuja kwa ndugu zangu na hawatakupatia mwanamke kwako, basi utakuwa huru kutoka kwa kiapo changu" au 2) kujengea mstari wa 40, "iwapo utaenda kwa familia ya baba yangu na kumuuliza msichana, utakuwa umefanya kile nilichokuomba ufanye. Iwapo hawatakupatia msichana kwako, basi utakuwa huru kwa kipao ulichoapa kwangu"

Lakini utakuwa huru katika kiapo changu

"utafunguliwa kutoka kwa kiapo ulichofanya kwangu". Kushindwa kutimiza kiapo inazungumzwa kana kwamba mtu yupo huru na kitu kilichomfunga. "hautapaswa kufanya kile ulichoapa kwangu ambacho ungefanya"

ikiwa utafika kwa ndugu zangu

Lugha zinatumia maneno "njoo" na "kwenda" tofauti. "iwapo utafika kwa nyumba ya ndugu zangu" au "utakapokwenda kwa ndugu zangu"

Genesis 24:42

Taarifa ya Jumla:

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

kisima

"kisima"

niko hapa nimesimama karibu na kisima cha maji

Mtumishi alikatisha kile alichokuwa akimuuliza Mungu kwa kuvuta nadhari ya Mungu kwa pale alipokuwa amesimama.

na iwe kwamba binti ajaye ... nitakayemwambia ... mwanamke atakayeniambia

Mtumishi alirudia kueleza ombi lake, na alikuwa na mambo matatu kusema juu ya mwanamke ambayo alitumaini yangekuja.

kuchota maji

"kuchukua maji"

mtungi

chombo cha ukubwa wa kati kilichoundwa na udongo kinachotumika kubeba na kumwaga vimiminikio.

awe ndiye mwanamke

Mtumishi alikamilisha ombi lake.

Genesis 24:45

Taarifa ya Jumla

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

kuzungumza moyoni mwangu

Kuomba kimoyo moyo katika akili ya mtu inazungumzwa kana kwamba alikuwa akizungumza ndani ya moyo wake. Neno "moyo" lina maana ya mawazo yake na fikra zake. "kuomba" au"kuomba kimya kimya"

tazama

"naam" au "ghafla". Neno "tazama" hapa linatuamsha kusikiliza taarifa inayoshangaza inayofuata.

mtungi

chombo cha ukubwa wa kati kilichoundwa na udongo kinachotumika kubeba na kumwaga vimiminikio.

akashuka chini kisimani

Msemo "akashuka chini" unatumika kwa sababu kisima kilikuwa sehemu ya chini zaidi ya mahali watumishi walipokuwa wamesimama.

kisimani

"kisima"

akawanywesha ngamia

"wakawapa ngamia maji"

Genesis 24:47

Taarifa ya Jumla

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

Binti wa Bethueli, Mwana wa Nahori, ambaye Milka alizaa kwake

"Baba yangu Bethueli. Wazazi wake ni Nahori na Milka"

pete ... bangili

Katika simulizi hii, vitu vyote hivi vilikuwa vya dhahabu.

nikainama

Hii ni ishara ya unyenyekevu mbele za Mungu.

ameniongoza katika njia sahihi

"amenileta hapa"

ambaye ameniongoza

Neno la kiunganishi "kwa sababu" linaweza kutumika kuonyesha hii ni sababu mtumishi alimuabudu Mungu. "kwa sababu Yahwe aliniongoza"

ndugu za bwana wangu

Hii ina maana ya Bethueli, mwana wa Abrahamu kaka yake Nahori.

Genesis 24:49

Taarifa ya Jumla:

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

Kwa hiyo

"Kwa hiyo". Hapa "kwa hiyo" haimaanishi "katika muda huu", lakini unatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimi linalofuata.

ikiwa mko tayari kumfanyia rehema na kweli, niambieni

Namna gani wangeonyesha uaminifu wao na ukweli inaweza kuelezwa kwa uwazi. "niambie kama utakuwa mwaminifu na mkweli kwa bwana wangu kwa kunipatia Rebeka awe mke wa mwana wake"

mko

Neno "mko" ina maana ya Labani na Bethueli.

uaminifu na kweli

Hizi nomino zinazojitegemea zinaweza kuelezwa kama "umanifu na ukweli"

uaminifu wa familia

Huu ni uaminifu wa watu wa familia

Lakini kama sivyo

Taarifa inayoeleweka inaweza kuelezwa kwa uwazi. "Lakini kama haujajiandaa kumtendea bwana wangu kwa uaminifu na ukweli wa familia"

ili kwamba niweze kwenda upande wa kulia, au kushoto

Maana zaweza kuwa 1) kuamua nini cha kufanya kunazungumzwa kana kwamba mtu atageuka upande mmoja au mwingine. "ili kwamba nijue nini cha kufanya" au 2) mtumishi anataka kujua kama anahitaji kusafiri sehemu nyingine. "ili kwamba niendelee na safari yangu"

Genesis 24:50

Bethueli

Huyu alikuwa baba wa Labani na Rebeka.

Jambo hili limetoka kwa Yahwe

"Yahwe alisababisha haya yote kutokea"

hatuwezi kusema kwako aidha neno baya au zuri

Wanasema hawana mamlaka ya kuamua kwamba aliyofanya Mungu ni mema au mabaya. "hatuthubutu kuhukumu kile ambacho Yahwe anatenda"

Tazama

Neno "tazama" hapa linaongeza msisitizo kwa kile kifuatacho.

Rebeka yu mbele yako

"Huyu hapa Rebeka"

Genesis 24:52

maneno yao

"Maneno ya Labani na Bethueli". Hapa "maneno" ina maana ya kile walichosema. "kile ambacho Labani na Bethueli walisema"

akainama mwenyewe chini

Kuinama chini mbele ya Mungu ni ishara ya kumuabudu yeye.

vipande vya fedha na vipande vya dhahabu

"vipande vya fedha na dhahabu" au "vitu vilivyotengenezwa kwa fedha na dhahabu"

zawadi zenye thamani

"zawadi za gharama" au "zawadi za thamani"

Genesis 24:54

yeye na watu aliokuwa nao

"Watumishi wa Abrahamu na wanamume wake"

wakakaa pale mpaka usiku

"walilala pale usiku ule"

walipoamka asubuhi

"waliamka asubuhi iliyofuata"

Niruhusuni niende

"Niruhusu niondoke na kurudi"

kwa siku chache zingine, angalau siku kumi

"angalau siku kumi zaidi"

kumi

"10"

baada ya hapo

"Kisha"

Genesis 24:56

akasema

"Mtumishi wa Abrahamu akasema"

kwao

"kwa kaka wa Rebeka na mama yake"

msinizuie

"Msinikawize" au "Msinifanye nisubiri"

Yahwe amefanikisha njia yangu

Hapa "njia" ina maana ya safari. "Yahwe amefanya nifanikiwe katika lengo la safari yangu"

Niruhusuni niende

"Niruhusu niondoke"

Genesis 24:59

Kwa hiyo wakampeleka dada yao Rebeka

"Kwa hiyo familia ilimpeleka Rebeka"

dada yao

Rebeka alikuwa dada wa Labani. "ndugu yao" au "dada wa Labani"

mtumishi wake wa kike

Hii ina maana ya mtumishi wa kike ambaye alimlisha Rebeka alipokuwa mtoto mchanga, akamtunza alipokuwa mtoto, na alimtumikia.

Dada yetu

Rebeka hakuwa adad kwa kila mtu katika familia yake. Lakini walimuita kwa jinsi hii kuonyesha walimpenda. "Dada yetu Rebeka"

na uwe mama wa maelfu na wa makumi elfu

Hapa "mama" ina maana ya mama. "na uwe mama wa mamilioni wa watu" au "na uwe na uzao mkubwa"

maelfu na wa makumi elfu

Hii ina maana ya idadi kubwa au idadi isiyohesabika.

uzao wako upate kumiliki lango la wale wanao wachukia

Majeshi huvunja katika malango ya miji ya adui zao na kuwashinda watu. "na uzao wako wawashinde kabisa wale wawachukiao"

Genesis 24:61

Kisha Rebeka akasimama, yeye na watumishi wake wakawapakia ngamia

"Kisha Rebeka akasimama, yeye na watumishi wake wakawapakia ngamia"

Hivyo watumishi wakamchukua Rebeka, na wakaenda zao

"Katika njia hii mtumishi wa Abrahamu alimchukua Rebeka pamoja naye na kurudi naye mahali alipotoka"

Nyakati hizo

Neno hili linaweka alama ya kubadili simulizi. Ilikuwa inaeleza juu ya mtumishi kutafuta mke, na sasa itaanza kueleza kuhusu Isaka.

Beerlahairoi

Hili ni jina la maji ya kisima kule Negebu.

Genesis 24:63

Isaka akaenda kutafakari shambani jioni

"jioni moja Isaka alitoka shambani kufikiri". Hii inaweza kuwa muda mrefu baada ya mtumishi na Rebeka kuondoka nyumbani kwake kwa maana walisafiri umbali mrefu.

Alipotazama akaona, natazama, kulikuwa na ngamia wakija!

Hili neno "tazama" hapa linatumasha kusikiliza kwa taarifa ya kushangaza inayofuata. "Alipotazama juu akashangaa kuona ngamia wakija"

Rebeka akatazama

"Rebeka akatazama juu"

akaruka kutoka kwenye ngamia

"alishuka juu ya ngamia haraka"

akachukua shela yake akajifunika

"Kwa hiyo alijifunika uso na shela yake". Hii ni ishara ya heshima na adabu kwa mwanamume atakayemuoa. Maana kamili inaweza kuelezwa wazi.

shela

Kipande cha kitambaa kilichotumika kufunika kichwa cha mtu, mabega na uso.

Genesis 24:66

akamchukua Rebeka, na akawa mke wake

Misemo hii miwili ina maana ya kwamba Isaka alimuoa Rebeka. "na akamuoa Rebeka" au "na akamchukua kama mke wake"

Kwa hiyo Isaka akafarijika

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kwa hiyo Rebeka alimfariji Isaka"

Genesis 25

Genesis 25:1

Taarifa ya Jumla:

Taarifa kuhusu Abrahamu.

Hawa wote

Hii ina maana ya watu waliotajwa katika mistari ya 2-4.

Genesis 25:5

Abrahamu akampatia Isaka vitu vyote alivyokuwa navyo

"Isaka alirithi kila kitu alichomiliki Abrahamu". Ilikuwa kawaida kwa baba kugawanya utajiri wake alipokuwa mzee na sio kuacha hivyo kwa wengine kufanya baada ya yeye kufariki.

Genesis 25:7

Hizi ndizo zilikuwa siku za miaka ya uhai wake Abrahamu alizoishi, miaka 175

"Abrahamu aliishi miaka 175"

Abrahamu akapumua pumzi ya mwisho na akafa

"Abrahamu alivuta pumzi yake ya mwisho na akafa". Misemo ya "alivuta pumzi ya mwisho" na "akafa" ina maana ya kitu kimoja. "Abrahamu alikufa"

akapumua pumzi ya mwisho

Hii ni njia ya upole ya kusema mtu alikufa.

katika uzee mwema, mzee aliye shiba siku

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza ya kwamba Abrahamu aliishi muda mrefu sana. "alipomaliza kuishi muda mrefu na akawa mzee sana"

mzee aliye shiba siku

Kuishi maisha marefu sana inazungumzwa kana kwamba maisha yalikuwa chombo kinachoweza kujaa.

akakusanywa kwa watu wake

Hii ina maana ya kwamba Abrahamu alikufa, nafsi yake ilikwenda sehemu ile ile ndugu zake waliokufa kabla yake. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "aliwaunga familia yake ambao walikuwa wameshakufa"

Genesis 25:9

pango la Makipela, katika shamba la Efroni

Efroni alimiliki shamba Makpela na pango ambalo lilikuwa ndani ya hilo shamba. Abrahamu alinunua shamba lile kutoka kwa Efroni.

Makpela

Makpela lilikuwa jina la eneo au sehemu.

Efroni ... Soari

Haya ni majina ya wanamume.

lililokuwa karibu na Mamre

Makpela ilikuwa karibu na Mamre.

Mamre

Hii ilikuwa jina jingine kwa mji wa Hebroni. Inawezekana iliitwa baada ya Mamre, rafiki yake Abrahamu aliyeishi pale"

Shamba hili Abrahamu alilinunua

"Abrahamu alinunua shamba hili"

watoto wa Hethi

Hapa "wana" ina maana ya wale amabo wametoka kwa Hethi. "uzao wa Hethi"

Abrahamu akazikwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Walimzika Abrahamu"

mwanae

"Mwana wa Abrahamu"

Beerlalahairoi

Jina hili lina maana ya "kisima cha yule aliye hai anionaye mimi"

Genesis 25:12

Na sasa

Hili neno linatumika kutambulisha sehemu mpya ya simulizi na taarifa kuhusu Ishameli.

Genesis 25:13

Taarifa ya Jumla:

Taarifa ya jumla

Hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, na haya ndiyo majina yao, kwa vijiji vyao, na katika vituo vyao; Maseyidi kumi na wawili kufuatana na kabila zao

Hii inaweza kuwekwa kama sentensi mbili. "Haya yalikuwa majina ya wana kumi na wawili wa Ishmaeli. Waliongoza kabila ambazo ziliitwa baada yao, na kila mmoja wao alikuwa na vijiji vyao na kambi zao"

kumi na wawili

"12"

Maseyidi

Hapa neno "maseyidi" ina maana ya wanamume waliokuwa viongozi au watawala wa makabila; haimaanishi ya kwamba walikuwa watoto wa mfalme.

Genesis 25:17

Hii ndiyo ilikuwa miaka ya Ishimaeli, miaka 137

"Ishmaeli aliishi miaka 137"

akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa

Msemo "akapumua pumzi yake ya mwisho" na "akafa" zina maana moja. "alikufa"

akakusanywa pamoja na watu wake

Hii ina maana ya kwamba ishmaeli alikufa, nafsi yake ilikwenda sehemu ile ile ndugu zake waliokufa kabla yake. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "alijiunga na familia yake ambao tayari walikuwa wamekufa"

Walioshi

"Uzao wake walikaa"

toka Havila mpaka Shuri

"kati ya Havila na Shuri"

Havila

Havila Ilikuwa mahali katika jangwa la Arabia.

kama yule aelekeaye mbele

"katika upande wa"

Waliishi kwa uadui kati yao

Maana zaweza kuwa 1) "hawakuishi kwa amani pamoja" au 2) "waliishi mbali kutoka kwa ndugu zao wengine"

Genesis 25:19

Haya ndiyo yalikuwa matukio kumuhusu Isaka

Sentensi hii inatambulisha habari ya uzao wa Isaka katika Mwanzo 25:19-35:29. "Hii ni habari ya uzao wa Isaka, mwana wa Abrahamu"

umri wa miaka arobaini

"umri wa miaka 40"

alipomuoa Rebeka kuwa mke wake

"alipomuoa Rebeka"

Bethueli

Bethueli alikuwa baba wa Rebeka.

Padani Aramu

Hili lilikuwa jina lingine la eneo la Mesopotamia, ambalo lipo eneo lile lile na Iraq ya sasa.

Genesis 25:21

alikuwa tasa

"hakuwa na uwezo wa kupata mimba"

Rebeka mkewe akabeba mimba

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba Rebeka alikuwa mimba na watoto wawili katika wakati mmoja. "Rebeka, mke wake, akawa mimba na mapacha"

Watoto hawa walipokuwa tumboni mwake wakasumbuka,

"watoto ndani mwake wakaendelea kugusana baina yao" au "Watoto walisukumana dhidi yao wenyewe ndani mwake"

Watoto ... tumboni mwake

Rebeka alikuwa mimba na mapacha.

Akaenda kumuuliza Yahwe kuhusu jambo hili

"Alienda kumuuliza Yahwe kuhusu suala hili". haipo wazi alienda wapi. Inawezekana alienda sehemu ya siri kuomba, au alienda sehemu kutoa sadaka.

Genesis 25:23

akamwambia

"akamwambia Rebeka"

Mataifa mawili ... atamtumikia mdogo

Hii ni lugha ya kishairi.

Mataifa mawili yako katika tumbo lako

Hapa "mataifa mawili" yana maana ya watoto wawili. Kila mtoto atakuwa baba wa taifa moja. "Mataifa mawili yatakuja pamoja kutoka kwa mapacha ndani yako"

na mataifa haya mawili yatatengana ndani yako

Hapa "mataifa mawili" ina maana ya watoto wawili. Kila mtoto atakuwa baba wa taifa moja. Hii inaweza kutafsiriwa kama kitenzi cha kutenda. "na utakapozaa hawa watoto wawili watakuwa wapinzani"

mkubwa atamtumikia mdogo

Maana zaweza kuwa 1) "mkubwa atamtumika mdogo" au 2) "uzao wa mkubwa utamtumikia uzao wa mdogo"

Genesis 25:24

tazama

Neno la "tazama" hapa linaongeza msisitizo kwa kile kifuatacho. "naam"

mwekundu mwili wote kama vazi la nywele

Maana zaweza kuwa 1) ngozi yake ilikuwa nyekundu na alikuwa na nywele nyingi katika mwili wake au 2) alikuwa na nywele nyingi nyekundu katika mwili wake. "nyekundu na yenye nywele kama nguo iliyotengenezwa na nywele ya mnyama"

Esau

"Jina Esau linafanana na neno "nywele"

umeshika kisigino cha Esau

"kushika sehemu ya nyuma ya mguu wa Esau"

Yakobo

"Jina Yakobo lina maana ya "anashika kisigino"

umri wa miaka sitini

"umri wa miak 60"

Genesis 25:27

akawa mwindaji hodari

"akawa hodari katika uwindaji na kuua wanyama kwa chakula"

mtu mkimya

"mtu wa amani" au"mtu asiyekuwa na mambo mengi"

aliye tumia muda wake akiwa katika mahema

Hii inazungumzia kuhusu muda kana kwamba ilikuwa bidhaa ambayo mtu angetumia. "aliyebaki katika mahema sehemu kubwa ya muda"

Kisha

Neno hili linatumika kuweka alama ya kubadili mwelekeo, kutoka katika simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Isaka na Rebeka.

Isaka akampenda

Hapa neno "akampenda" ina maana "alimpendelea" au "kumpenda zaidi"

kwa sababu alikula wanyama ambao alikuwa anawinda

"kwa sababu alikula wanyama ambao Esau aliwinda" au "kwa sababu alifurahia kula wanyama pori ambao Esau alikamata"

Genesis 25:29

Yakobo akapika

Kwa kuwa huu ni mwanzo wa simulizi kuhusu jambo lilitokea kipindi kimoja, baadhi ya watafsiri wanaweza kuanza na msemo wa "Siku moja, Yakobo alipika".

akapika mchuzi

"alichemsha chakula kiasi" au "alipika mchuzi kiasi". Mchuzi ulipikwa kwa dengu za kuchemsha.

akiwa dhaifu kutokana na njaa

"alikuwa dhaifu kwa sababu alikuwa na njaa sana" au "alikuwa na njaa sana"

nimechoka

"Nimechoka kwa sababu ya njaa" au "Nina njaa sana"

Edomu

Jina Edomu lina maana ya "nyekundu"

Genesis 25:31

haki yako ya mzaliwa wa kwanza

"haki ya mwana wa kwanza kurithi sehemu kubwa ya utajiri wa baba yake"

nakaribia kufa

Esau alitiachumvi kuweka msisitizo jinsi alivyokuwa na njaa. "Nina njaa mno nahisi kama vile ntakufa"

Ni nini kwangu haki ya mzaliwa wa kwanza?

Esau alitumia swali kuweka msisitizo ya kwamba kula ilikuwa muhimu zaidi ya haki ya mzawa wa kwanza. Hii inaweza kutafsiriwa kama kauli. "Urithi wangu haunisaidii iwapo nitakufa kwa njaa!"

Kwanza uape kwangu mimi

Kile ambacho Yakobo alimtaka Esau aape kinaweza kuwekwa wazi. "kwanza apa kwangu ya kwamba utaniuzia haki yako ya mzaliwa wa kwanza"

dengu

Haya ni kama maharage, lakini mbegu zake ni ndogo sana, na kama vile tambarare.

Esau akawa ameidharau haki yake

"Esau alionyesha ya kwamba hakuthamini haki yake ya kuzaliwa"

Genesis 26

Genesis 26:1

Basi

Neno hili linatumika kuweka alama kwa sehemu mpya ya simulizi.

njaa ikatokea

"kukawa na njaa" au "kukawa na njaa nyingine"

katika nchi

Unaweza kusema wazi ya kwamba nchi inayozungumziwa. "katika nchi ambayo Isaka na familia yake waliishi"

iliyotokea siku za Ibrahimu

Msemo "katika siku" ina maana ya wakati ambapo Abrahamu alikuwa hai. "ambayo ilitokea wakati wa uhai wa Abrahamu"

Genesis 26:2

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaanza kuzungumza na Isaka.

akamtokea

"akamtokea Isaka"

Usishuke kwenda Misri

Ilikuwa kawaida kuzungumzia kuondoka nchi ya ahadi kama "kushuka chini" kwenda sehemu nyingine.

kwani kwako wewe na uzao wako, nitawapa nchi hii yote

"kwa maana nitakupa nchi hizi zote kwako na kwa uzao wako"

nitatimiza kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako

"Nitafanya kile nilichoahidi kwa Abrahamu baba yako kukifanya"

Genesis 26:4

Taarifa ya Jumla:

Yahwe anaendelea kuzungumza na Isaka

Nitauzidisha uzao wako

"Nitasababisha uwe na uzao mwingi"

kama nyota za mbinguni

Hii inazungumzia kuhusu uzao wa Isaka kana kwamba walikuwa sawa na idadi ya nyota.

mbinguni

Hii ina maana ya kila kitu juu ya dunia ikijumlisha jua, mwezi na nyota.

mataifa yote ya dunia yatabarikiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nitabariki mataifa yote ya dunia"

Abrahamu aliitii sauti yangu na kutunza maelekezo yangu, amri zangu na sheria zangu

Misemo hii "alitii sauti yangu" na "kutunza maelekezo yangu, amri zangu na sheria zangu" zina maana moja. "Abrahamu alinitii na kufanya kila kitu nilichomuamuru kufanya"

aliitii sauti yangu

Hapa "sauti" ina maana ya Yahwe. "Alinitii"

Genesis 26:6

Hivyo Isaka akakaa Gerari

Isaka pekee ndiye aliyetajwa kwa sababu ni kiongozi wa familia, lakini familia yake yote ilikuwa pamoja naye. "Kwa hiyo Isaka na familia yake walikaa Gerari"

Aliogopa kusema

Hapa "aliogopa" ina maana ya hisia isiyofaa inayompata mtu wakati akipata tishio la kudhuriwa kwake au kwa wengine. "Aliogopa kusema"

wamchukue Rebeka

"ili kwamba wamchukue Rebeka"

Tazama, akamwona Isaka

Neno "tazama" linaonyesha ya kwamba kile alichokiona Abimeleki kilimshangaza. "Na alishangazwa kuona ya kwamba Isaka"

akimpapasa Rebeka

Maana zaweza kuwa 1) alikuwa akimgusa kwa njia ambayo mume humgusa mkewake au 2) alikuwa akicheka na kuzungumza pamoja naye kwa namna ambayo mume huzungumza na mkewe.

Genesis 26:9

Abimeleki akamwita Isaka kwake

Yawezekana Abimeleki alimtuma mtu kumwambia Isaka ya kwamba alihitaji kumuona. "Abimeleki alimtuma mtu kumleta Isaka kwake"

Kwa nini ulisema, 'Yeye ni dada yangu?"

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuelezwa kama nukuu isiyokuwa moja kwa moja. "Kwa nini ulisema ya kwamba ni dada yako?"

amchukue

"ili amchukue"

Ni jambo gani hili ulilotufanyia?

Abimeleki alitumia swali hili kumkaripia Isaka. "Haukupaswa kufanya jambo hili kwetu!"

ungeweza kuleta hatia juu yetu

Hii inazungumzia kuhusu kumsababisha mtu kuwa na hatia kana kwamba "hatia" ilikuwa ni kitu kinachowekwa juu ya mtu. "ungeweza kusababisha tuwe na hatia ya kuchukua mke wa mtu"

juu yetu

Hapa "yetu" ina maana ya Abimeleki na watu wake.

Mtu yeyote atakayemgusa mtu huyu

Hapa "atakayemgusa" ina maana ya kumgusa kwa namna ya kumdhuru. "Yeyote atakayemdhuru mwanamume huyu"

hakika atauwawa

Inawezekana Abimeleki alikusudia kumwambia mtu kumuua yeyote ambaye angemdhuru Isaka au Rebeka. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nitamuua" au "Nitawaamuru wanamume wangu kumuua"

Genesis 26:12

Taarifa ya Jumla

Hii inaanza sehemu mpya ya simulizi. Inabadilisha kutoka kueleza kuhusu Isaka kumuita Rebeka dada yake, na inaanza kuelezea kuhusu jinsi Isaka alivyokuwa tajiri na Wafilisti wakawa na wivu kwake.

katika nchi hiyo

"Gerari"

vipimo mia

Hii ina maana ya "mara mia zaidi ya alivyopanda"/Inaweza kuelezwa kwa ujumla zaidi kama "zao kubwa sana"

Mtu huyo akawa tajiri

"Isaka akawa tajiri" au "Akawa tajiri"

akaongezeka zaidi hata akawa mkuu sana

"na akapata zaidi na zaidi hadi akawa tajiri sana"

kondoo

Hii inaweza kujumuisha mbuzi pia.

familia kubwa

Hapa "familia" ina maana ya wafanya kazi au watumishi. "watumishi wengi"

Wafilisiti wakamwonea wivu

"Wafilisti walikuwa na wivu kwake"

Genesis 26:15

Basi

Hapa neno hili halimaanishi "katika kipindi hiki". Inaonyesha wapi matukio ya simulizi yanapoanzia. Inaweza kutafsiriwa kwa neno unganishi "Kwa hiyo" kuonyesha ya kwamba hii ni tokeo la kilichotokea katika 26:12.

katika siku za Ibrahimu baba yake

Msemo wa "katika siku za" ina maana ya maisha ya mtu. "wakati Abrahamu, baba yake, alipokuwa akiishi"

Abimeleki akamwambia

Maana zaweza kuwa 1) hili ni tukio lingine kumlazimisha Isaka na watu wake kuondoka. "Kisha Abimeleki akasema" au "Hatimaye Abimeleki akasema" au 2) Abimeleki alifanya uamuzi huu kwa sababu aliona ya kwamba watu wake walikuwa na wivu na walitenda uhasama dhidi ya Isaka. "Basi Abimeleki akasema"

nguvu kuliko sisi

"mwenye nguvu zaidi ya sisi"

Hivyo Isaka akaondoka

Isaka pekee ametajwa kwa sababu yeye ni kiongozi, lakini familia yake na watumishi wake walienda naye. "Kwa hiyo Isaka na nyumba yake waliondoka"

Genesis 26:18

Isaka akachimba

Hapa "Isaka" ina maana ya Isaka na watumishi wake. "Isaka na watumishi wake wakachimba"

vilivyokuwa vimechimbwa

"ambao watumishi wa Abrahamu walichimba"

siku za Abrahimu baba yake

Msemo "katika siku za" ina maana ya maisha yote ya binadamu. "ambapo Abrahamu, baba yake, alipokuwa anaishi"

Wafilisiti walikuwa wamevizuia

Hii ndio ilikuwa sababu ya Isaka kuvichimba. Njia kadhaa za kutafsiri hii ni 1) Kwa kuwa hili lilitokea kwanza, sentensi hii inaweza ikaja kabla ya sentensi juu ya Isaka kuvichimba au 2) Sentensi hii inaweza kuanza na "Isaka alifanya hivi kwa sababu Wafilisti waliwazuia"

wamevizuia

"walizijaza na udongo"

Genesis 26:19

maji yaliyokuwakuwa yakibubujika

Msemo huu una maana ya chemichemi ya maji ya asili waliyofunua walipokuwa wakichimba kisima kipya. Ilitoa maji safi ya muendelezo kwa ajili ya kunywa.

Wachungaji

"wanamume wanaotunza mifugo"

Haya ni maji yetu

Hapa "yetu" ina maana ya wafugaji wa Gerari"

Eseki

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi mafupi yanayosema "Jina la Eseki lina maana ya "malumbano" au "mabishano".

Genesis 26:21

Wakachimba

"Kisha watumishi wa Isaka wakachimba"

wakakigombania

"wafugaji wa Gerari walibishana na wafugaji wa Isaka"

hivyo akakiita

"kwa hiyo Isaka akakiita"

Sitina

Watafsiri wanaweza kuweka maandishi mafupi yanayosema. "Jina la Sitna ina maana ya "kupinga" au "kushtaki"

Rehobothi

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi mafupi yanayosema "Jina la Rehobothi lina maana ya "kuweka nafasi kwa ajili ya" au "nafasi wazi".

ametufanyia ... tutafanikiwa

Isaka alikuwa akijizungumzia mwenyewe na nyumba yake.

Genesis 26:23

Kisha Isaka akaenda Beersheba

Hapa "kwenda juu" inaweza kumaanisha kwenda kaskazini. "Isaka aliondoka pale na kwenda Beersheba"

kuvidisha vizazi vyako

"atasababisha vizazi vyako kuongezeka maradufu" au "atasababisha vizazi vyako kuwa wengi sana"

kwa ajili ya mtumishi wangu Abrahimu

"kwa mtumishi wangu Abrahamu" au unaweza kuweka maana yote wazi zaidi. "kwa sababu nilimuahidi mtumishi wangu Abrahamu kuwa nitafanya hili"

Isaka akajenga madhabahu pale

Unaweza kuweka wazi kwa nini Isaka alijenga dhabahu. "Isaka alijenga dhabahu pale kutoa sadaka kwa Yahwe"

akaliita jina la Yahwe

"Kuita" ina maana ya kuomba au kuabudu. Hapa "jina" lina maana ya Yahwe. "aliomba kwa Yahwe" au "alimuabudu Yahwe"

Genesis 26:26

akamwendea

"akaenda kwa Isaka"

Ahuzathi

Hili ni jina la mwanamume.

rafiki yake

Maana zaweza kuwa 1) "rafiki yake Abimeleki" au 2) "mshauri wa Abimeleki"

Fikoli

Hili ni jina la mwanamume.

Genesis 26:28

Nao wakasema

Hii ina maana ya Abimeleki, Ahuzathi na Fikoli. Mmoja wao aliongea na wengine wawili walikubaliana na kile alichosema. Haikumaanisha waliongea kwa wakati mmoja. "mmoja wao alisema"

Tumeona yakini

"Tunajua" au "Tuna uhakika"

Hivyo na tufanye agano

"Kwa hiyo tunataka kufanya agano"

na kama sisi tulivyokutendea vema wewe

Hii inaweza kutafsiriwa kama mwanzo wa sentensi mpya. "Tumetenda mema tu kwako"

umebarikiwa na Yahwe

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yahwe amekubariki"

Genesis 26:30

Isaka akawaandalia sherehe, na wakala na kunywa

Kula chakula pamoja ilikuwa sehemu ya kufanya agano na mtu mwingine.

akawaandalia

Hapa "akawaandalia" ina maana ya "Abimeleki, Ahuzathi na Fikoli"

wakala

Hapa "wakala" ina maana ya Isaka, Abimeleki, Ahuzathi, na Fikoli. "walikula wote"

Wakaamuka mapema

"Waliamka mapema"

Genesis 26:32

Akakiita kile kisima Shiba

"Kwa hiyo alikiita kisima Shiba". Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi mafupi yanayosema "Jina la Shiba linafanana na neno lenye maana ya "kiapo".

Beersheba

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi mafupi yanayosema "Beersheba inaweza kumaanisha "kisima cha kiapo" au "kisima cha saba"

Genesis 26:34

Taarifa ya Jumla

Sehemu kubwa ya Mwanzo 26 inahusu Isaka. Mistari hii inamhusu mtoto wake mkubwa Esau.

arobaini

"40"

akajitwalia mke

"alioa". Unaweza kusema kwa uwazi ya kwamba alioa wanawake wawili. "alioa wake wawili"

Yudithi ... Basemathi

Haya ni majina ya wake wa Esau.

Beeri ... Eloni

Haya ni majina ya wanamume.

Mhiti

"vizazi vya Hethi" au "mzawa wa Hethi"

Wakamhuzunisha Isaka na Rebeka

Hapa "wakamhuzunisha" ina maana ya Yudithi na Basemathi. Kumhuzunisha au kumsikitisha mtu inazungumziwa kana kwamba "huzuni" ni chombo ambacho mtu anaweza kukileta kwa mtu. "Walimfanya Isaka na Rebeka wawe na huzuni" au "Isaka na Rebeka walimsikitisha kwa sababu yao"

Genesis 27

Genesis 27:1

macho yake kuwa mazito

Hii inazungumzia kuhusu kuwa karibu na kupofuka kana kwamba macho yalikuwa taa na mwanga ulikuwa ukitoweka. "alikaribia kupofuka" au "kidogo apofuke"

akamwambia

"Na Esau akajibu"

Mimi hapa

"Nipo hapa" au "Ninasikiliza'

Akamwambia

"Kisha Isaka akasema"

Tazama hapa

Msemo wa "tazama hapa" unaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata. "Sikiliza kwa makini"

Sijui siku ya kufa kwangu

Inasemekana Isaka anajua atakufa hivi karibuni. "Naweza kufa siku yoyote toka sasa"

kufa

Hii ina maana ya kifo cha mwili.

Genesis 27:3

Taarifa ya Jumla

Isaka anaendelea kutoa maelekezo kwa mwanae mkubwa Esau.

silaha zako

"vifaa vyako vya kuwindia"

podo lako

Podo ni kasha la kushikilia mishale. "podo lako la mishale"

ukaniwindie mnyama

"winda mnyama pori kwa ajili yangu"

Uniandalie chakula kitamu, aina ile niipendayo

Neno "kitamu" lina maana ya kitu chenye ladha nzuri sana. "Nipikie nyama tamu ninayoipenda"

kukubariki

Kipindi cha Biblie, baba mara nyingi hutamka baraka juu ya watoto wake.

Genesis 27:5

Basi

Neno "basi" linaonyesha badiliko la msisitizo kwa Rebeka na Yakobo.

Rebeka akasikia Isaka alipoongea na Esau mwanawe

"Rebeka alimsikia Isaka akizungumza na mwanawe Esau"

Esau akaenda ... kuja nayo

Neno "kwa hiyo" inaweza kuongezwa kuonyesha ya kwamba Rebeka anazungumza na Yakobo kwa sababu ya kile alichosikia, na anaongea naye wakati Esau ameondoka. "Kwa hiyo Esau alipokuwa ameondoka ...kuja nayo"

na Esau mwanawe ... na Yakobo mwanawe

Esau na Yakobo walikuwa wote wawili watoto wa Isaka na Rebeka. Wanaitwa "mtoto wake" na "mwanawe" kusisitiza ya kwamba mzazi mmoja alimpendelea mtoto mmoja juu ya mtoto mwingine.

Tazama

Msemo "tazama hapa" unaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata. "Sikiliza kwa makini"

Akasema, 'Niletee mnyama na unitengenezee chakula kitamu, ili nikile na kukubariki mbele za Yahwe kabla ya kufa kwangu

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kusemwa katika hali isiyo moja kwa moja. Alimwambia Esau "kuwinda mnyama pori, na kumtengenezea nyama tamu anayoipenda". Kisha kabla hajafa, Isaka atambariki Esau mbele ya Yahwe.

'Niletee mnyama

"Niletee mnyama pori utakayemwinda na kumuua"

unitengenezee chakula kitamu

"nipikie nyama tamu ninayoipenda"

kukubariki mbele za Yahwe

"kukubariki mbele ya Yahwe"

kabla ya kufa kwangu

"kabla sijafa"

Genesis 27:8

Taarifaya Jumla

Rebeka anaendelea kuzungumza kwa mtoto wake mdogo Yakobo.

sasa

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

usikilize sauti yangu kama ninavyokuagiza

Rebeka alisema "sauti yangu" kumaanisha kile alichokuwa akisema. "unitii na ufanye kile nachokuambia"

nitaandaa chakula kitamu kutokana nao kwa ajili ya baba yako, kwa namna aipendayo

Neno "kitamu" ina maana ya kitu chenye ladha nzuri sana.

Utakipeleka kwa baba yako

"Kisha peleka kwa baba yako"

ili kwamba akile, na kukubariki

"na atakapokila, atakubariki"

kukubariki

Neno "kubariki" lina maana ya baraka maalumu ambayo baba hutamka kwa watoto wake.

kabla hajafa

"kabla hajafa"

Genesis 27:11

mimi ni mtu lain

"Mimi ni mwanamume mwenye ngozi laini" au "Mimi sina manyoya"

nami nitaonekana kama mdanganyifu kwake

"na atafikiri ya kwamba mimi ni muongo" au "atajua ya kwamba ninamdanganya"

nitajiletea laana badala ya baraka

Kulaaniwa au kubarikiwa inazungumziwa kana kwamba laana na baraka ni vitu vinavyowekwa juu ya mtu. "Kisha kwa sababu ya hili, atanilaani na hatanibariki"

Genesis 27:13

Mwanangu, acha laana yoyote iwe juu yangu

"acha laana yako na iwe juu yangu, mwanangu". Kulaaniwa inazungumziwa kana kwamba laana ni kitu kinachowekwa juu ya mtu. "acha baba yako anilaani badala yako, mwanangu"

sikiliza sauti yangu

Rebeka akasema "sauti yangu" kumaanisha kile alichokuwa akizungumza. "utii kile ninachokuambia" au "unitii"

uniletee

"niletee mwanambuzi mchanga"

akaandaa chakula kitamu, kama alichokipenda baba yake

Neno la "kitamu" lina maana ya kitu chenye ladha nzuri sana.

Genesis 27:15

Akamvalisha ngozi ya mwanambuzi katika mikono yake

Ngozi ya mbuzi ilikuwa bado ina manyoya juu yao.

Akaweka katika mikono ya Yakobo kile chakula kitamu na mkate aliokuwa ameuandaa.

"Alimpatia mtoto wake Yakobo chakula kitamy na mkate aliokuwa ameandaa"

Genesis 27:18

akasema

"Na baba yake akajibu" au "Isaka akajibu"

Mimi hapa

"ndio, nasikiliza" au "Ndio, kuna nini?"

nimefanya kama ulivyoniagiza

"Nimefanya kile ulichonimbia kufanya"

sehemu ya mawindo yangu

Neno "windo" lina maana ya wanyama pori ambayo mtu huwinda na kuua.

Genesis 27:20

akamwambia

"Yakobo alijibu"

ameniletea

Hii ni lahaja yenye maana ya kwamba Mungu alisababisha itokee. "alinisaidia kufanikiwa nilipokuwa nawinda"

kama kweli wewe ni mwanangu Esau au hapana

"kama kweli wewe ni mwanangu Esau"

Genesis 27:22

Yakobo akamkaribia Isaka baba yake

"Yakobo alimkaribia Isaka baba yake"

Sauti ni sauti ya Yakobo

Isaka anafananisha sauti ya Yakobo na Yakobo mwenyewe. "Unasikika kama Yakobo"

lakini mikono ni mkikono ya Esau

Isaka analinganisha mikono ya Esau kwa Esau mwenyewe. "lakini mikono yako inaonekana kama mikono ya Esau"

Genesis 27:24

Akasema

Isaka anauliza swali hili kabla hajambariki mwanawe. "Lakini kwanza Isaka alimuuliza Isaka"

nile mawindo yako

Neno "windo" lina maana ya mnyama pori ambaye watu huwinda na kuua.

akanywa

"na Isaka akainywa"

Genesis 27:26

akanusa harufu ya nguo zake na kumbariki

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba nguo zilinuka kama nguo za Esau. "alinusa nguo zake na zilinuka kama nguo za Esau, kwa hiyo Isaka akambariki"

naye akanusa

"na Isaka akanusa"

harufu

"marashi"

na kumbariki

"na kisha akambariki". Hii ina maana ya baraka maalumu ambayo baba hutamka kwa watoto wake.

Tazama, harufu ya mwanangu

Neno "tazama" linatumika kama msemo wa mkazo kumaanisha "ni kweli". Hakika, harufu ya mwanangu"

alilolibariki Yahwe

Hapa neno "alilolibariki" lina maana ya Yahwe alisababisha mambo mazuri kutokea kwenye shamba na ikawa na matunda. "ambayo Yahwe amesababisha kuzaa sana"

Genesis 27:28

Taarifa ya Jumla

Hii ni baraka ya Isaka. Alifikiri alikuwa akizungumza na Esau, lakini alikuwa akizungumza na Yakobo.

akupe

Hapa "akupe" ni katika hali ya umoja na ina maana ya Yakobo. Lakini baraka ingeweza kuhusika kwa vizazi vya Yakobo.

umande wa mbinguni

"umande" ni matone ya maji yanayounda juu ya mimea wakati wa usiku. Hii inaweza kuwekwa wazi. "umande wa usiku kutoka mbinguni kumwagilia mimea yako"

unono wa nchi

Kuwa na nchi yenye mbolea inazungumziwa kana kwamba nchi ilikuwa nene au tajiri. "udongo mzuri kwa ajili ya kuzaa mimea"

wingi wa nafaka na mvinyo mpya

Kama "nafaka" na "mvinyo" havijulikani, vinaweza kuwekwa kwa ujumla zaidi. "chakula na kinywaji kingi"

Genesis 27:29

wakutumikie ... zako

Hapa hivi viwakilishi vipo katika umoja na vina maana ya Yakobo. Lakini baraka pia inalenga vizazi vya Yakobo.

mataifa yainame

Hapa "mataifa" ina maana ya watu. "watu kutoka mataifa yote yainame"

yainame

Hii ina maana ya kuinama na kutoa heshima na taadhima ya unyenyekevu kwa mtu.

Uwe bwana juu ya ndugu zako

"Kuwa bwana juu ya ndugu zako"

ndugu zako ... wana wa mama yako

Isaka anazungumzia baraka hii moja kwa moja kwa Yakobo. Lakini, inahusika kwa vizazvi vya Yakobo ambao watatawala vizazi vya Esau na vizazi vya ndugu yeyote wa Yakobo ambaye anaweza kuwa naye.

na wana wa mama yako wainame chini yako

"na wana wa mama yako watakusujudu"

Kila anayekulaani na alaaniwe

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Na Mungu alaani kila mtu anayekulaani"

kila anayekubariki abarikiwe

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Na Mungu abariki kila mtu anayekubariki"

Genesis 27:30

ametoka mbele ya Isaka baba yake

"ameondoka tu katika hema la Isaka baba yake"

chakula kitamu

"nyama tamu nayoipenda"

baadhi ya mawindo ya mwanao

Hapa "ya mwanao" ilikuwa njia ya upole ya Esau kumaanisha chakula chake mwenyewe alichokiandaa.

mawindo ya mwanao

Neno "windo" lina maana ya wanyama pori ambao watu huwinda kwa ajili ya kula.

kunibariki

Hii ina maana ya baraka maalumu ambayo baba hutamka kwa watoto wake.

Genesis 27:32

akamwambia

"akamwambia Esau"

Isaka akatetemeka

"Isaka akaanza kutetemeka"

aliyewinda mawindo

Windo ina maana ya mnyama pori ambao watu huwinda na kuua.

Genesis 27:34

akalia kwa kilio kikubwa na cha uchungu sana

Uchungu wa Esau ulikuwa sawa na ladha ya kitu kichungu. "alilia kwa sauti kubwa"

amechukua baraka yako

Huu ni msemo wenye maana ya Yakobo alichukua kilichokuwa cha Esau. "Nimembariki badala yako"

Genesis 27:36

Je hakuitwa Yakobo kwa haki?

Esau anatumia swali kuweka msisitizo juu ya hasira yake kwa Yakobo. "Yakobo ni jina sahihi kwa kaka yangu!"

Yakobo

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi mafupi yanayosema: "Jina la Yakobo lina maana ya "yeye akamataye kisigino". Katika lugha ya asili jina la "Yakobo" linatamkika kama neno la "mdanganyifu"

Alichukua ... baraka

Hii inazungumzia kuhusu haki ya mzaliwa wa kwanza kana kwamba ilikuwa kitu ambacho mtu anaweza kukichukua. "Alinidanganya kumpatia mara mbili ya urithia ambayo ningepaswa kupokea kama mzawa wa kwanza!"

sasa amechukua baraka yangu

Hii inazungumzia juu ya baraka kana kwamba ilikuwa kitu ambacho mtu anaweza kuchua. "na sasa amekudanganya kumbariki yeye badala yake"

Je haukuniachia baraka

Esau anajua ya kwamba baba hawezi kumbariki na vitu vile vile alivyombariki Yakobo. Esau anauliza kama kuna kitu kinachosalia kusemwa kwake ambacho Isaka hakusema alipokuwa akimbariki Yakobo.

Je nikufanyie nini mwanangu?

Isaka anatumia swali kuweka msisitizo ya kwamba hakuna kilichobaki atakachofanya. "Hakuna kitu kingine nachoweza kufanya kwako!"

Genesis 27:38

Je hauna hata baraka moja kwa ajili yangu, babangu

Hii inaweza kuelezwa kwa njia ya chanya. "Baba yangu, je hauna baraka moja zaidi kwa ajili yangu"

Genesis 27:39

kumwambia

"akasema kwa Esau"

Tazama

Hii inaongeza msisitizo kwa kile Isaka anachosema baadae. "Sikiliza" au "Vuta nadhari kwa kile nachokwenda kukuambia"

mbali na utajiri wa nchi

Huu ni msemo unaomaanisha nchi yenye rutuba. "mbali na udongo wenye rutuba"

yako ... nawe

Katika 27:39-40 hivi viwakilishi vipo katika umoja na vina maana ya Esau, lakini kile Isaka anachosema pia kinaashiria kwa vizazi vya Esau.

umande juu angani

"umande" ni matone ya maji yanayounda juu ya mimea wakati wa usiku. Hii inaweza kuwekwa wazi. "umande wa usiku kutoka mbinguni kumwagilia mimea yako"

Kwa upanga wako utaishi

Hapa "upanga" ina maana ya vurugu. "Utaiba na kuua watu ili kupata kile unachohitaji kuishi"

utaiondoa nira yake shingoni mwako

Hii inazungumzia juu ya mtu kuwa na bwana kana kwamba utawala wa bwana juu ya mtu ulikuwa ni nira ambayo mtu anaweza kubeba. "utajifanya huru kutoka kwa utawala wake"

Genesis 27:41

Esau akajisemea moyoni

Hapa "moyoni" ina maana ya Esau mwenyewe. "Esau alijisemea mwenyewe"

Siku za maombolezo kwa ajili ya baba yangu zinakaribia

Hii ina maana ya idadi ya siku mtu huomboleza pale ambapo mmoja wa familia anapokufa.

Rebeka akaambiwa maneno ya Esau mwanawe mkubwa

Hapa "maneno" yana maana ya kile Esau alichosema. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu alimwambia Rebeka kuhusu mpango wa Esau"

Tazama

"Sikiliza" au "Vuta nadhari"

anajifariji

"anajifanya ajisikie vizuri"

Genesis 27:43

sasa

Hii haimaanishi "katika muda huu", lakini inatumika kuvuta nadhari kwa jambo muhimu linalofuata.

kukimbilia kwa Labani

"ondoka hapa haraka na uende kwa Labani"

kwa muda

"kwa kipindi cha muda"

mpaka hasira ya ndugu yako itakapopungua

"hadi kaka yako atakapopoa"

hata hasira ya ndugu yako itakapokuondokea

Kutokuwa na hasira inazungumziwa kana kwamba hasira hugeukia upande tofauti kutoka kwa mtu. "hadi pale atakapokuwa hana hasira na wewe"

Kwa nini niwapoteze ninyi nyote katika siku moja?

Rebeka anatumia swali kuweka msisitizo juu ya mawazo yake kwa suala hili. "Sitaki kuwapoteza wote wawili katika siku moja!"

niwapoteze ninyi nyote katika siku moja

Inasemekana ya kwamba iwapo Esau atamuua Yakobo, basi watamuua Esau kama muuaji.

niwapoteze

Hii ni njia ya upole inayomaanisha wanawe kufa.

Genesis 27:46

Nimechoka na maisha

Rebeka anatia chumvi kuweka msisitizo jinsi alivyofadhaishwa kuhusu mwanamke Mhiti ambaye Esau alimuoa. "Nimefadhaishwa sana"

binti za Hethi

"hawa wanawake wahiti" au "vizazi vya Wahiti"

kama wanawake hawa, baadhi ya binti za nchi

Msemo "binti wa nchi" ina maana ya wanawake wenyeji. "kama wanawake hawa wanaoishi katika nchi hii"

maisha yatakuwa na maana gani kwangu?

Rebeka anatumia swali kuweka msisitizo jinsi atakavyofadhaishwa iwapo Yakobo atamuoa mwanamke Mhiti". "Maisha yangu yatakuwa mabaya!"

Genesis 28

Genesis 28:1

Usichukuwe

"Usichukue"

Inuka, nenda

"Nenda mara moja"

Padani Aramu

Hili lilikuwa jina lingine kwa ajili ya eneo la Mesopotamia, ambalo lipo eneo sawa na Iraq ya sasa.

nyumba ya

Hii ina maana ya vizazi vya mtu au ndugu wengine. "familia"

Bethueli

Bethueli alikwa baba wa Rebeka.

baba wa mama yako

"babu yako"

mmojawapo wa binti

"kutoka kwa mabinti"

kaka wa mama yako

"mjomba wako"

Genesis 28:3

Taarifa ya Jumla:

Isaka anaendelea kuzungumza na Yakobo

akupe uzao na akuzidishe

Neno "kuongeza" unaelezea jinsi Mungu angemfanya Yakobo "azidishiwe". "akupe uzao na watoto wengi"

Na akupe baraka ya Ibrahimu, wewe, na uzao wako baada yako

Hii inazungumzia kuhusu kubariki mtu kana kwamba baraka ni kitu ambacho mtu anaweza kutoa. Nomino inayojitegemea "baraka" inaweza lusemwa kama "bariki". "Na Mungu akubariki wewe na uzao vyako kama alivyombariki Abrahamu" au "Na Mungu akupatie wewe na uzao wako kile alichoahidi kwa Abrahamu"

kwamba uweze kumilki nchi

Mungu kutoa nchi ya Kaanani kwa Yakobo na uzao wake inazungumziwa kana kwamba mtoto alikuwa akirithi fedha au mali kutoka kwa baba yake.

nchi ambapo umekuwa ukiishi

"nchi ambayo ulikuwa ukiishi"

ambayo Mungu alimpa Abrahamu

"ambayo Mungu aliahidi kwa Abrahamu"

Genesis 28:5

Padani Aramu

Hili lilikuwa jina lingine kwa ajili ya eneo la Mesopotamia, ambalo lipo eneo sawa na Iraq ya sasa.

Bethueli

Bethueli alikwa baba wa Rebeka.

Genesis 28:6

Taarifa ya Jumla:

Simulizi inabadilika kutoka kwa Yakobo kuelekea kwa Esau

Basi

Neno hili linatumiwa hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Esau.

Padani Aramu

Hili lilikuwa jina lingine kwa ajili ya eneo la Mesopotamia, ambalo lipo eneo sawa na Iraki ya sasa.

kuchukua mke

"kuchukua mke kwa ajili yake"

akaona kwamba Isaka alikuwa amembariki

"Esau aliona pia ya kwamba Isaka alimbariki Yakobo"

Usichukue

"Usichukue"

wanawake wa Kanaani

"binti wa Kaanani" au "wanawake wa Kaanani"

Genesis 28:8

Taarifa ya Jumla:

Hii inaendeleza taarifa ya nyuma kuhusu Esau.

Esau akaona

"Esau akagundua"

wanawake wa Kanaani hawakumpendeza Isaka baba yake

"baba yake Isaka hakuidhinisha wanawake wa Kaanani"

wanawake wa Kanaani

"binti wa Kaanani" au "wanawake wa Kaanani"

Hivyo

"Kwa sababu hiyo"

mbali na wake aliokuwa nao

"kwa kuongeza juu ya wake aliokuwa nao tayari"

Mahalathi

Hili ni jina la mmoja wa binti wa Ishmaeli.

Nebayothi

Hili ni jina la mmoja wa vijana wa Ishmaeli.

Genesis 28:10

Taarifa ya Jumla:

Simulizi inabadilika kurudi kwa Yakobo

Akaja mahali fulani na akakaa pale usiku kucha, kwa kuwa jua lilikuwa limekuchwa

"Akaja katika eneo fulani na kwa sababu jua lilikuwa limezama, aliamua kukaa usiku"

Genesis 28:12

Akaota

"Yakobo alipata ndoto"

imewekwa juu ya nchi

"chini yake ikigusa ardhini"

ilifika hata mbinguni

Hii ina maana ya sehemu ambapo Mungu anaishi.

Tazama

Neno la "tazama" hapa linatuamsha kuvuta nadhari kwa taarifa ya kushtukiza inayofuata.

Yahwe amesimama juu yake

Maana zaweza kuwa 1) "Yahwe alikuwa amesimama juu ya ngazi" au 2) "Yahwe alikuwa amesima kando na Yakobo"

Abrahamu baba yako

Hapa "baba" ina maana ya "babu". "Abrahamu babu yako" au "Abrahamu babu yako"

Genesis 28:14

Taarifa ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Yakobo ndotoni.

Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya ardhi

Mungu analinganisha uzao wa Yakobo na vumbi la ardhi kuweka msisitizo ya idadi kubwa. "Utakuwa na uzao mkubwa zaidi ya utakavyoweza kuhesabu"

na utaenea mbali kuelekea magharibi

Hapa neno "utaenea" lipo katika hali ya upekee lakina lina maana ya uzao wa Yakobo. Inazungumzia kuhusu Yakobo kwa maana yeye ni kiongozi wa familia. "na uzao wako utasambaa hadi magharibi"

na utaenea mbali

Hii ina maana ya watu wataongeza mipaka ya ardhi yao na kukaa

katika maeneo makubwa zaidi.

kuelekea magharibi, mashariki, kaskazini, na kusini Misemo hii inatumika pamoja kumaanisha "pande zote". "katika pande zote"

Kupitia kwako na kupitia uzao wako familia zote za dunia zitabarikiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nitabariki familia zote juu ya dunia kupitia kwako na uzao wako"

Tazama

Hii inaongeza msisitizo kwa kile kinachosemwa baadae. "Tazama" au "Sikiliza" au "Vuta nadhari kwa kile nachotaka kukuambia"

kwani sitakuacha. Nitafanya kila

"kwa kuwa sitakuacha mpaka nitende yote"

nitakulinda

"Nitakuweka salama" au "Nitakulinda"

Nitakurudisha katika nchi hii tena

"Nitakuleta katika nchi hii"

Genesis 28:16

akaamka katika usingizi

"aliamka kutoka katika usingizi wake"

nyumba ya Mungu ... lango la mbinguni

Msemo wa "lango la mbinguni" linaelezea ya kwamba sehemu hii ni kiingilio cha "nyumba ya Mungu" na "mlango wa mahali Mungu anapoishi"

Hili ni lango la mbinguni

Hii inazungumzia kuhusu mlango ambapo Mungu anaishi kana kwamba ilikuwa ni ufalme halisi ambao ulikuwa na lango ambalo mtu anatakiwa kufungua kuruhusu watu ndani.

Genesis 28:18

nguzo

Hii ni nguzo ya kumbukumbu, yaani, jiwe kubwa au jabali lililowekwa mwishoni pake.

kumimina mafuta juu yake

Tendo hili linaashiria ya kwamba Yakobo anaweka wakfu nguzo kwa Mungu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "alimwaga mafuta juu yake ili kuiweka wakfu nguzo kwa Mungu"

Betheli

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi mafupi yanayosema "Jina la Betheli lina maana 'nyumba ya Mungu."

Luzu

Hili ni jina la mji.

Genesis 28:20

akatoa nadhiri

"akafanya kiapo" au "alimuahidi Mungu kwa dhati"

Ikiwa Mungu atakuwa ... ndipo Yahwe atakapokuwa Mungu wangu

Yakobo anazungumza na Mungu katika lugha ya mtu wa utatu. Hii inaweza kusemwa katika lugha ya upili wa mtu. "Iwapo uta ... basi wewe, Yahwe, utakuwa Mungu ambaye nitamuabudu"

katika njia nipitayo

Hii ina maana ya safari ya Yakobo kutafuta mke na kurudi nyumbani. "katika safari hii"

atanipa mkate wa kula

Hapa "mkate" una maana ya chakula kwa ujumla.

katika nyumba ya baba yangu

Hapa "nyumba" ina maana ya familia ya Yakobo. "kwa baba yangu na familia yangu iliyosalia"

jiwe takatifu

Hii ina maana ya kwamba jiwe litaweka alama ya sehemu ambayo Mungu alijitokeza kwake na itakuwa sehemu ambapo watu watamuabudu Mungu. "nyumba ya Mungu" au "sehemu ya Mungu"

Genesis 29

Genesis 29:1

watu wa mashariki

Hii ina maana ya watu wa Paddani Aramu, ambayo ni nchi mashariki mwa nchi ya Kaanani.

na, tazama, makundi matatu ya kondoo yalikuwa yamelala kando yake

Neno "tazama" linaweka alama ya mwanzo wa tukio lingine katika simulizi kubwa.

Kwani kutoka katika hicho kisima

"Kwani kutoka katika kisima hicho". Msemo huu unaweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu jinsi wafugaji waliwanywesha mifugo"

wangeyanywesha

"wafugaji wangewanywesha" au "wale waliokuwa wakitunza kondoo wangewanywesha"

mdomo wa kisima

Hapa "mdomo" ni njia ya kuelezea uwazi. "uwazi wa kisima"

Genesis 29:4

Yakobo akawambia

"Yakobo aliwaambia wafugaji"

Ndugu zangu

Hii ni njia ya upole ya kumsalimia mgeni.

Labani mwana wa Nahori

Hapa "mwana" ina maana ya uzao wa kiume. Maana nyingine yaweza kuwa "Labani mjukuu wa Nahori".

na, tazama pale, Raheli binti yake anakuja na kondoo

"Tazama sasa! Raheli binti yake anakuja na kondoo"

Genesis 29:7

ni mchana

"jua bado lipo juu angani" au "jua bado linawaka kwa mwanga"

wakati wa kukusanya kondoo pamoja

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kwako kukusanya mifugo"

kukusanya pamoja

Hii ina maana ya kuwakusanya pamoja ndani ya uzio ili wakae kwa usiku. Maana kamili ya hii inaweza kuwekwa wazi.

kuwaacha wachunge

"waache wale nyasi shambani"

Hatuwezi kuwanywesha

"Inatubidi kusubiri ili kuwanywesha". Hii inahusu suala la muda, na sio ruhusa.

Hatuwezi kuwanywesha mpaka makundi yote yakusanyike pamoja

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "hadi pale wafugaji wengine watakapokusanya mifugo yao"

kutoka mlangoni mwa kisima

Hapa "mlangoni" ni njia ya kuelezea uwazi. "kutoka kwa kisima" au "kutoka kwa uwazi wa kisima"

na ndipo tutakapowanywesha kondoo

"kisha tutawanywesha kondoo"

Genesis 29:9

kaka wa mama yake

"mjomba wake"

mlangoni mwa kisima

Hapa "mdomo" ni njia ya kuelezea uwazi. "kisima" au "uwazi wa kisima"

Genesis 29:11

Yakobo akambusu Raheli

Nyakati za kale Mashariki ya Karibu, ilikuwa kawaida kumsalimu ndugu na busu. Ingawa, inafanywa baina ya wanamume.

akalia kwa sauti

Yakobo analia kwa sababu amefurahi sana. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi.

ndugu wa baba yake

"ana undugu na baba yake"

Genesis 29:13

mwana wa dada yake

"mpwa wake"

akamkumbatia

"alimkumbatia"

akambusu

Nyakati za kale Mashariki ya Karibu, ilikuwa kawaida kumsalimu ndugu na busu. Ingawa, inafanywa baina ya wanamume.

Yakobo akamwambia Labani mambo haya yote

"kisha Yakobo alimwambia Labani kila kitu alichomuambia Raheli"

mfupa wangu na nyama yangu

msemo huu una maana zinaoana moja kwa moja. "ndugu yangu" au "mmoja wa familia yangu"

Genesis 29:15

Je unitumikie bure ... ndugu yangu?

Labani anatumia swali kusisitiza ya kwamba anatakiwa kumlipa Yakobo kwa kumtumika. Swali linawezakutafsiriwa kama kauli. Pia linaweza kuwekwa katika njia ya chanya. "Hakika ni sahihi ya kwamba nikulipe kwa kunitumikia ingawa wewe ni ndugu yangu."

Basi Labani alikuwa

Neno "basi" linatumika hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Labani na binti zake"

Macho ya Lea yalikuwa dhaifu

Maana zaweza kuwa 1) "Macho ya Lea yalikuwa mazuri" au 2) "Macho ya Lea yalikuwa ya kawaida"

Yakobo alimpenda Raheli

Hapa neno "alimpenda" lina maana ya mvuto wa kimahaba kati ya mwanamume na mwanamke.

Genesis 29:19

kuliko kumpa mwanamume mwingine

"kuliko kumpa kwa mwanamume mwingine"

nayo ilionekana kwake kama siku chache tu

"lakini muda ulionekana kwake kama siku chache tu"

kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake

"kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake" au "kwa sababu ya upendo wake kwake"

Genesis 29:21

Nipe mke wangu, kwani siku zangu zimetimia

Hapa "siku" ina maana ya muda mrefu zaidi. Msemo "zimetimia" unaweza kuwekwa katika hali ya chanya. Kauli hii ina mkazo. Nipatie Raheli ili kwamba niweze kumuoa, kwa maana nimekufanyia kazi miaka saba!"

kuandaa sherehe

"kuandaa sherehe ya harusi". Yawezekana Labani alikuwa na watu walioandaa sherehe hii. "alikuwa na watu waliondaa sherehe ya harusi"

Genesis 29:23

aliyelala naye

Inadokezwa ya kwamba Yakobo hakujua alikuwa na Lea kwa sababu ilikuwa giza na hakuweza kuona. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi.

Labani akampa mtumishi wake wakike Zilpa ... mtumishi wake

Hapa mwandishi anatoa taarifa ya nyuma kuhusu Labani kumpa Zilfa kwa Lea. Inawezekana alimpa Zilfa kwa Lea kabla ya harusi.

Zilpa

Hili ni jina la mtumishi wa Lea.

tazama, kumbe ni Lea

"Yakobo alishangazwa kuona ilikuwa ni Lea kitandani pamoja naye". Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Yakobo alishtushwa na kile alichokiona"

Ni nini hiki ulichonifanyia?

"Yakobo alishangazwa kuona alikuwa Lea kitandani pamoja naye." Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Yakobo alishtushwa na kile alichoona.

Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli?

Yakobo anatumia maswali haya kuonyesha maumivu yake ya kwamba Labani alimdanganya. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Nimekutumikia kwa miaka saba kumuoa Raheli"

Genesis 29:26

Siyo utamaduni wetu kumtoa

"Huwa hatutoi kwenye familia yetu"

Timiza juma la bibi arusi

"Kumaliza kusherehekea harusi ya Raheli"

na tutakupa yule mwingine pia

Maana kamila inaweza kuwekwa wazi. "na wiki ijayo tutakupatia Raheli pia"

Genesis 29:28

Yakobo akafanya hivyo, na akatimiza juma la Lea

"Na Yakobo akafanya alichosema Labani, na akamaliza kusherehekea wiki ya harusi ya Lea"

Bilha

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Raheli.

Yakobo akalala na Raheli

Hii ni njia ya ustarabu ya kusema kuwa walikutana kimwili. "Yakobo akamuoa Raheli"

akampenda Raheli

Hii inamaanisha upendo wa kimahaba kati ya mwanamme na mwanamke.

Genesis 29:31

Lea hakupendwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yakobo hakumpenda Lea"

hakupendwa

Hii ni kuza jambo kusisitiza kuwa Yakobo alimpenda Raheli zaidi ya Lea. "alimpenda kwa uhafifu kuliko Raheli"

hivyo akalifungua tumbo lake

Mungu kumsababisha Lea kuwa na uwezo wa kuwa na mimba inazungumziwa kama kwamba Mungu alifungua tumbo lake.

hakuwa na mtoto

"hakuweza kuwa mjamzito"

Lea akashika mimba na kuzaa mwana

"Lea alipata mimba na kumzaa mwana wa kiume"

naye akamwita Rubeni

Jina Rubeni linamaanisha "Tazama, mwana wa kiume."

Yahwe ameliangalia teso langu

Lea alipitia uchungu wa hisia kwa sababu Yakobo alimkataa.. Nomino "teso" inaweza kuwekwa kama kitenzi. "Yahwe aliona kuwa nateseka"

Genesis 29:33

Kisha akashika mimba

"Lea akawa mjamzito"

kuzaa mwana

"akazaa mwana wa kiume"

Yahwe amesikia kwamba sipendwi

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yahwe amesikia kuwa mme wangu hanipendi"

akamwita Simoni

Jina Simoni linamaanisha "kusikiwa."

mume wangu ataungana nami

"mume wangu atanikumbatia"

nimemzalia wana watatu

"nimezaa wana watatu wa kiume kwa ajili yake"

akaitwa Lawi

Jina Lawi linamaanisha "ambatishwa."

Genesis 29:35

Akashika mimba tena

"Lea akawa na mimba tena"

kuzaa mwana

"Akazaa mwana wa kiume"

akamwita jina lake Yuda

Jina Yuda linamaanisha "sifa."

Genesis 30

Genesis 30:1

Raheli alipoona kwamba hamzalii Yakobo watoto

"Wakati Raheli alipogundua ya kwamba hawezi kupata mimba"

nitakufa

Raheli anatumia ukuzaji kuonyesha jinsi alivyohuzunika ya kuhusu kutopata watoto. "Nitajisikia sina maana yoyote kabisa"

Nipe watoto

"Nisababishie kupata mimba"

Hasira ya Yakobo ikawaka juu ya Raheli

Hasira ya Yakobo inazungumziwa kana kwamba ilikuwa moto. "Yakobo alimkasirikia sana Raheli"

Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia usipate watoto?

Hili ni swali la balagha ambalo Yakobo anatumia kumkaripia Raheli. Inaweza kutafsiriwa kama kauli. "Mimi si Mungu! Mimi siye ninayekuzuia kupata watoto"

Genesis 30:3

Akasema

"Raheli akasema"

Tazama

"Sikiliza" au "Vuta nadhari kwa kile nachotaka kukuambia". Hii inaongeza msisitizo kwa kile Raheli anachosema baadae"

kuna mjakazi wangu Bilha ... nami nitapata watoto kwake

Katika kipindi hicho, njia hii ilikuwa inakubalika kwa mwanamke tasa kupata watoto ambao kisheria wangekuwa wa kwake. Maana kamili inaweza kuwekwa wazi.

Bilha

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Raheli.

magotini pangu

Hii ni namna ya kusema ya kwamba mtoto ambaye Bilha anamzaa atakuwa wa Raheli. "wa kwangu"

nami nitapata watoto kwake

"na kwa njia hii atanifanya niwe na watoto"

Genesis 30:5

Bilha

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Raheli.

kumzalia Yakobo mwana

"akazaa mtoto wa kiume kwa Yakobo"

akamwita jina lake

"Raheli akmpatia jina"

akamwita jina lake Dani

"Jina la Dani lina maana ya "alihukumu".

Genesis 30:7

Bilha ... akashika mimba tena

"Bilha ... akawa mimba tena"

na kumzalia Yakobo mwana wa pili

"na akazaa mtoto wa kiume wa pili kwa Yakobo"

Kwa mashindano yenye nguvu nimeshindana na dada yangu

Msemo huu "mashindano nimeshindana" ni msemo unaotumiwa kwa msisitizo. Pia ni sitiari inayozungumzia jaribio la Raheli kupata mtoto kama dada yake kana kwamba alikuwa akigombana kimwili na Lea. "nimepambana sana kupata watoto kama dada yangu, Lea"

na kushinda

"na nimeshinda" au "nimefaulu"

Akamwita jina lake Naftali

"Jina la Naftali lina maana ya 'mapambano yangu'"

Genesis 30:9

Lea alipoona kwamba

"Lea alipopata ufahamu wa jambo hilo"

akamchukua Zilpa, mjakazi wake, na kumpa Yakobo kama mke wake

"alimpatia Zilpa, mtumishi wake, kwa Yakobo kama mke"

Zilpa

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Lea.

akamzalia Yakobo mwana

"akazaa mtoto wa kiume kwa Yakobo"

Hii ni bahati njema!

"Bahati gani!" au "Bahati gani hii!"

akamwita jina lake Gadi

"Jina la Gadi lina maana ya "mwenye bahati"

Genesis 30:12

Zilpa

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Lea.

akamzalia Yakobo mwana wa pili

"akazaa mtoto wa pili wakiume kwa Yakobo"

Nina furaha!

"Jinsi nilivyobarikiwa!" au "Jinsi nilivyo na furaha!"

mabinti

"wanawake" au "wanawake wadogo"

akamwita jina lake Asheri

"Jina la Asheri lina maana ya "furaha"

Genesis 30:14

Rubeni akaenda

"Rubeni alitoka nje"

Siku za mavuno ya ngano

Hapa msemo "siku za" ni sitiari yenye maana ya majira au kipindi cha mwaka. "katika kipindi cha mwaka cha mavuno ya ngano" au "wakati wa mavuno ya ngano"

tunguja

Hili ni tunda ambalo linasemekana kuongeza uwezo wa kuzaa na kuongeza hamu ya mtu kulala na mpenzi wake. "tunda la upendo"

Je ni jambo dogo kwako ... mme wangu?

"Je haujali ... mume wangu?" Hili ni swali la balagha limetumika kumkaripia Raheli. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli, "ni mbaya sana .. mume wangu"

Je na sasa unataka ... pia?

Hili ni swali la balagha limetumika kumkaripia Raheli. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli, "Na sasa unataka ... pia?"

Basi atalala nawe

"Basi Yakobo atalala" au "Basi nitamruhusu Yakobo alale"

Genesis 30:16

kwa tunguja za mwanangu

"kwa bei ya tunguja za mwanangu"

akashika mimba

"akawa mimba"

na kumzalia Yakobo mwana wa tano

"na akazaa mtoto wa kiume wa tano kwa Yakobo"

Mungu amenipa ujira wangu

Mungu kumzawadia Lea inazungumzwa kana kwamba alikuwa bosi anayelipa mshahara kwa mtu anayefanya kazi kwake. "Mungu amenipa stahiki yangu" au "Mungu amenizawadia"

Akamwita jina lake Isakari

"Jina la Isakari lina maana ya "kuna dhawabu"

Genesis 30:19

Lea akashika mimba tena

"Lea akawa mimba tena"

na kuzaa mwana wa sita kwa Yakobo

"na kuzaa mtoto wa kiume wa sita kwa Yakobo"

Akamwita jina lake Zabuloni

"Jina la Zabuloni lina maana ya "heshima"

na kumwita jina lake Dina

Hili ni jina la binti wa Lea.

Genesis 30:22

Mungu akamkumbuka Raheli na kumsikiliza

Msemo huu "akamkumbuka" una maana kukumbuka. Hii haimaanishi Mungu alimsahau Raheli. Ina maana alimfikiria juu ya ombi lake. "Mungu alimfikiria Raheli na kumpatia kile alichokitaka"

Mungu ameiondoa aibu yangu

Mungu kusababisha Raheli kutosikia aibu tena inazungumziwa kana kwamba "aibu" ni kitu ambacho mtu anaweza kukichukua kutoka kwa mtu mwingine. Nomino inayojitegemea "aibu" inaweza kuwekwa kama "kuona aibu". "Mungu amenisababishia nisione aibu tena"

Akamwita jina lake Yusufu

"Jina la Yusufu maana yake ni "na aongeze"

Yahwe ameniongeza mwana mwingine

watoto wa kwanza wa Raheli walitokana na mtumishi wa kike wa Bilha.

Genesis 30:25

Baada ya Raheli kumzaa Yusufu

"Baada ya Raheli kumzaa Yusufu"

na uniache niondoke

"ili niondoke"

unafahamu nilivyokutumikia

Yakobo anamkumbusha Labani kuhusu mkataba wake (29:26) Nomino inayojitegemea "huduma" inaweza kusemwa kama "kutumika". "unafahamu ya kwamba nimekutumikia muda wa kutosha"

Genesis 30:27

Labani akamwambia

"Labani akamwambia Yakobo"

Ikiwa nimepata kibali machoni pako

Msemo wa "machoni pako" ni lugha inayomaanisha mawazo na maoni ya Yakobo. Iwapo nimepata kibali na wewe" au "Iwapo unapendezwa na mimi"

nimepata kibali

Hii ni lahaja yenye maana ya mtu amekubalika na mtu mwingine.

subiri, kwa sababu

"tafadhali kaa, kwa sababu"

nimejifunza kwa kutumia uaguzi

"Nimegundua kwa desturi yangu ya kiroho na uchawi"

kwa ajili yako

"kwa sababu yako"

Taja ujira wako

Hii inaweza kuwekwa wazi. "Niambie nahitaji kukulipa kiasi gani kukuweka hapa"

Genesis 30:29

Yakobo akamwambia

"Yakobo alimwambia Labani"

jinsi ambavyo mifugo wako wamekuwa nami

"jinsi mifugo wako walivyokuwa vizuri tangu nimeanza kuwatunza"

Kwani walikuwa wachache kabla sijaja

"mifugo wako walikuwa wadogo kabla sijakutumikia"

na wameongezeka kwa wingi

"lakini sasa utajiri wako umeongezeka sana"

Je ni lini mimi nitaandaa kwa ajili ya nyumba yangu pia?

"Basi ni lini nitatunza familia yangu?" Yakobo anatumia swali kuweka msisitizo ya kwamba anataka kujitoa kwa familia yake. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "basi ninataka kutunza familia yangu!"

Genesis 30:31

Je nikulipe nini

"Nitakulipa nini" au "Nikupatie nini". Hii inaweza kuwekwa wazi zaidi. "Nitakulipa nini ili kwamba ubaki na kunitumikia"

Ikiwa utafanya jambo hili kwa ajili yangu

Neno la kiunganishi "ikiwa" inaweza kuongezwa kuonyesha ya kwamba hili ni jambo moja ambalo Yakobo anataka. "Ikiwa utafanya jambo hili kwa ajili yangu"

nitawalisha tena kondoo wako na kuwatunza

"nitalisha na kuwatunza mifugo wako"

kuondoa kila kondoo mwenye milia na mabaka, na kila kondoo mweusi kati yao, na kati ya wenye mabaka na milia katika mbuzi

"na kutoa kila kondoo wa madoia, kila kondoo mweusi, na kila mbuzi mwenye madoa"

Hawa watakuwa ujira wangu.

"Hii itakuwa gharama ya kuniweka hapa"

Genesis 30:33

Uadilifu wangu utashuhudia kwa ajili yangu hapo baadaye

Neno "uadilifu" lina maana ya "uaminifu". Hii inazungumzia kuhusu uadilifu kana kwamba ni mtu ambaye anaweza kushuhudia kwa ajili au dhidi ya mtu mwingine. "Na baadae utajua kama nimekuwa mwaminifu na wewe au la"

Kila ambaye hana milia na hana madoa miongoni mwa mbuzi, na mweusi kati ya kondoo, ikiwa wataonekana kwangu, watahesabiwa kuwa wameibwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Iwapo utakuta mbuzi yeyote asiyena madoa au kondoo yeyote ambaye sio mweusi, utawahesabu kuwa wameibiwa"

Na iwe kama yalivyo maneno yako

Hapa "neno" ina maana ya kitu kilichosemwa. "Itakuwa kana kwamba unasema" au "Tutafanya kile ulichosema"

Genesis 30:35

yaliyokuwa na milia na madoa

"ambazo zilikuwa na milia na madoa"

yaliyokuwa na milia na madoa

"yaliyokuwa na madoa"

kila aliyekuwa mweupe

"kila mbuzi ambaye alikuwa na weupe ndani yake"

na weusi wote katika kondoo,

"na kondoo wote weusi"

akawakabidhi katika mikono

Hapa "mikono" ina maana ya kutawala au kutunza. "akawafanya wanawe kuwatunza"

Genesis 30:37

mipopla .... mlozi ... mwaramoni

Hii yote ni miti ya mbao nyeupe

akatoa maganda ili michilizi myeupe ionekane, na akaifanya sehemu nyeupe ya ndani ya mti iliyokuwa ndani ya fito ionekane

"na kutoa maganda ya mti ili kwamba mbao nyeupe ya chini ionekane"

mabirika yakunyweshe

vyombo virefu vya wazi vinavyoshikilia maji kwa ajili ya wanyama kunywa

Genesis 30:39

Wanyama wakapandana

"Wanyama wa mifugo walizalishana" au "Wanyama walipandana"

wakazaa watoto wenye milia, mabaka na wenye madoa

"wakazaa watoto weney milia na madoa"

Yakobo akawatenga

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba hii ilitokea katika kipindi cha miaka kadhaa. "Katika kipindi cha miaka kadhaa iliyofuata, Yakobo akawagawanya"

kuelekea

"kutazama kuelekea"

kayatenga makundi yake mwenyewe pekee

"aliwatenganisha mifugo wake"

Genesis 30:41

mbele ya macho ya kundi

Hapa "macho" ina maana ya "kuona". "ili kwamba mifugo waweze kuona"

kati ya fito

"mbele ya fito"

wanyama waliodhaifu

"wanyama wenye nguvu chache"

Hivyo wanyama dhaifu wakawa wa Labani, na wenye nguvu wakawa wa Yakobo

"Kwa hiyo wanyama dhaifu wakawa wa Labani, na wale wenye nguvu wakawa wa Yakobo". Unaweza kuiweka wazi zaidi. "Kwa hiyo wanyama dhaifu hawakuwa na milia au madoa na wakawa wa Labani, na wale wenye nguvu hawakuwa na milia au madoa na wakawa wa Yakobo"

Genesis 30:43

Mtu huyo

"Yakobo"

akastawi sana

"akafanikiwa sana" au "akawa tajiri sana"

Genesis 31

Genesis 31:1

Basi

Neno hili linatumika hapa kuweka alama kuweka nafasi katika simulizi kuu. Hapa mwandishi anaanza kueleza sehemu mpya ya simulizi.

Yakobo akasikia maneno ya wana wa Labani, wakisema

Hapa "maneno" yana maana ya kwa yale waliokuwa wakisema. "Yakobo alisikia ya kwamba wana wa Labani wakisema"

Yakobo amechukuwa yote yaliyokuwa ya baba yetu

Wana wa Labani walikuza kwa sababu walikuwa na hasira. "Kila kitu ambacho Yakobo anacho ametoa kwa baba yetu"

Yakobo akaona mwonekano katika uso wa Labani. Akaona kwamba nia yake imebadilika

Sentensi hizi mbili zina maana moja. Ya pili inaelezea muonekano ambao Yakobo aliona kwa uso wa Labani. "Yakobo aligundua ya kwamba Labani hakufurahishwa naye tena"

baba zako

"baba yako Isaka na babu yako Abrahamu"

Genesis 31:4

Yakobo akatuma kuwaita Raheli na Lea uwanjani katika kundi lake la mifugo

"Yakobo akatuma kuwaita Raheli na Lea uwanjani katika kundi lake la mifugo"

katika kundi lake la mifugo naye akawambia

Hii inaweza kuwekwa kama sentensi mbili fupi. "katika mifugo yake. Akawaambia"

Naona nia ya baba yenu kwangu imebadilika

"Nimegundua baba yenu hafurahishwi na mimi tena"

mnajua kwamba ni kwa nguvu zangu zote nimemtumikia baba yenu

Neno "mnajua" hapa lina maana ya wote Raheli na Lea. Pia linaongeza msisitizo. "Nyie wenyewe mnajua ya kwamba nimetumikia baba yenu kwa nguvu zangu zote"

Genesis 31:7

amenidanganya

"amenidanganya" au "hajanitendea haki"

ujira wangu

"alichosema atanilipa"

kunidhuru

Maana zaweza kuwa 1) kudhuru kwa mwili au 2) kusababisha Yakobo ateseke kwa namna yoyote.

Wanyama wenye mabaka

"Wanyama wenye madoa"

kondoo wote walipozaa

"mifugo wakazaa"

wenye milia

"Wanyama wenye milia"

Kwa njia hii Mungu amemnyang'anya mifugo baba yenu na kunipa mimi

"Hivi ndivyo Mungu aliwapatia wanyama wa baba yenu kwangu"

Genesis 31:10

Taarifa ya Jumla

Yakobo anaendelea simulizi yake kwa wake zake Lea na Raheli.

Wakati fulani wa majira ya kupandana

"Wakati wa msimu wa kupandana"

yaliyowapanda kundi

Hapa "kundi" ina maana ya mbuzi wa kike. "kupandana na mbuzi wa kike wa kundi"

yalikuwa ya milia, mabaka na madoa

"walikuwa na milia, madoa kidogo,na mabaka makubwa"

Malaika wa Mungu

Maana zaweza kuwa 1) Mungu mwenyewe alijitokeza kama mtu au 2) mmoja wa wajumbe wa Mungu alijitokeza. Kwa maana msemo haueleweki vizuri, ni vyema kutafsiri kama "malaika wa Mungu" kwa kutumia neno la kawaida linalotumika kwa "malaika".

Nikasema

"Na nikajibu"

Mimi hapa

"Ndio, ninasikiliza" au "Ndio, kuna nini?"

Genesis 31:12

Taarifa ya Jumla:

Malaika wa Bwana anaendelea kuzungumza na Yakobo.

Inua macho yako

Hii ni namna ya kusema "Tazama juu"

wanaolipanda kundi

Hapa "kundi" lina maana ya mbuzi wa kike. "ambao wanawapanda na mbuzi wa kike wa kundi"

Wana milia, madoa na na mabaka

"wana milia na madoa"

mahali ulipoitia nguzo mafuta

Yakobo alimwaga mafuta juu ya nguzo kuiweka wakfu kwa Mungu.

nchi uliyozaliwa

"nchi ambayo ulizaliwa"

Genesis 31:14

Raheli na Lea wakajibu na kumwambia

Hii haimaanishi walizungumza katika wakati mmoja. Inasisitiza ya kwamba walikubaliana wao kwa wao.

Je kuna sehemu yoyote au urithi wetu katika nyumba ya baba yetu?

Raheli na Lea wanatumia swali kusisitiza ya kwamba hakuna kitu kilichosalia kutoka kwa baba yao kuwapatia. "Hakuna kitu chochote kabisa kilichobaki kwa ajili yetu kurithi kutoka kwa baba yetu!"

Je hatutendei kama wageni?

Wanatumia swali kuonyesha hasira yao kuhusu jinsi baba yao anavyowatendea. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Baba yetu anatutendea kama wanawake wageni badala ya binti zake!"

Kwa maana ametuuza na kwa ujumla ametapanya pesa zetu. 16Mali zote

Hii inaweza kuwekwa kwa uwazi zaidi. "Ametuuza kwa manufaa yake mwenyewe"

na kwa ujumla ametapanya pesa zetu

Labani kutumia fedha yote ambayo alipaswa kuwapatia binti zake inazungumziwa kana kwamba alikuwa mnyama pori aliyekula fedha yote kana kwamba ilikuwa chakula. "alitumia fedha yetu yote"

na sasa ni zetu na watoto wetu

"inakuwa ya kwetu na watoto wetu"

Sasa basi

Hapa "sasa" haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

lolote Mungu alilokuambia, fanya

"fanya yote ambayo Mungu alikuambia kufanya"

Genesis 31:17

wanawe

Yakobo aliwachukua watoto wake wote. Inataja watoto wa kiume pekee kwa sababu walikuwa muhimu kama warithi wake.

Akawaongoza mifugo wake wote

"Akawaongoza mifugo wake wote" Hapa "mifugo" ina maana ya wanyama wake wote wa kufuga.

wakiwemo wanyama aliowapata huko Padani Aramu

"wakiwemo mifugo wengine ambao aliwachukua umiliki alipokuwa Padani Aramu"

Kisha akaenda kuelekea kwa Isaka baba yake katika nchi ya Kanaani

"Alienda katika nchi ya Kaanani, ambapo Isaka baba yake alikuwa akiishi"

Genesis 31:19

Labani alipokuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo wake

"Wakati Labani alipoondoka kukata manyoya ya kondoo"

mto

Hii ina maana ya mto wa Frati.

akaenda kuelekea

"kusafiri kuelekea"

vilima ya Gileadi

"milima ya Gileadi" au "Mlima Gileadi"

Genesis 31:22

Labani akaambiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mtu mmoja akamwambia Labani"

Siku ya tatu

Ilikuwa utamaduni wa Kiyahudi kuhesabu siku ya kuanza safari kama siku ya kwanza. "Siku mbili baada ya kuondoka"

kwamba Yakobo amekimbia

Yakobo pekee ndiye anayetajwa kwa sababu ndiye kiongozi wa familia. Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba familia yake ilikwenda naye. "ya kwamba Yakobo alitoroka na wake zake na watoto wake"

Hivyo akawachukua

"Kwa hiyo labani akachukua"

na kumfuatia

"na kumfukuza Yakobo"

kwa safari ya siku saba

Labani alitumia siku saba akitembea kumfikia Yakobo.

Akampita

"Alimfikia"

Genesis 31:24

Basi Mungu akaja kwa Labani Mwarami katika ndoto usiku

Neno "basi" linatumika kuweka alama kwa badiliko kutoka kwenye simulizi ya taarifa ya nyuma kuhusu Labani. "usiku huo Mungu alikuja kwa Labani ndotoni"

Ujiadhari kumwambia Yakobo jambo lolote liwe jema au baya

Msemo huu "jema au baya" unatumika pamoja kumaanisha "chochote". "Usiseme chochote kujaribu kumsimamisha Yakobo kuondoka"

Labani akampata Yakobo. Basi Yakobo alikuwa amepiga hema yake katika nchi ya vilima. Labani pia akapiga kambi pamoja na ndugu zake katika nchi ya kilima ya Gileadi

Neno "basi" inatumika hapa kuweka alama ya badiliko ya simulizi kwa taarifa ya nyuma kuhusu Yakobo na Labani. "Labani alipomfikia Yakobo, Yakobo aliweka hema lake katika nchi ya vilima. Kisha Labani na ndugu zake pia waliweka mahema katika nchi ya Gileadi.

Genesis 31:26

umewachukua binti zangu kama mateka wa vita

Labani anamzungumzia Yakobo kuchukua familia yake pamoja naye mpaka katika nchi ya Kaanani kana kwamba Yakobo aliwachukua mateka baada ya vita na anawalazimisha wao kuondoka nao. Labani anatia chumvi kwa sababu ana hasira na anajaribu kumfanya Yakobo asikie hatia kwa kile alichokifanya.

umekimbia kwa siri

"kukimbia kwa siri"

kwa sherehe

"kwa furaha"

kwa matari na vinubi

Vyombo hivi ni vya muziki. "na kwa muziki"

matari

chombo cha muziki chenye kichwa kama ngoma ambacho kinapigwa na kina vipande vya chuma kimekizunguka pembeni vyenye sauti pale chombo kikitikiswa.

niwabusu wajukuu wangu

Hapa "wajukuu" wanajumlisha wajukuu wote wakiume na kike. "kubusu wajukuu wangu"

Basi umefanya upumbavu

"umefanya upumbavu"

Basi

Hapa haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

Genesis 31:29

Iko katika uwezo wangu kukudhuru

Neno "kukudhuru" ni wingi na una maana ya kila mmoja aliyekuwa na Yakobo. "Nina watu wa kutosha pamoja nami kuwadhuru nyote"

Jiadhari usimwambie Yakobo neno la heri wala shari

Maneno "heri au shari" yanatumika pamoja kumaanisha "chochote". "Usiseme chochote kujaribu kumzuia Yakobo kuondoka"

umeondoka

Hapa "umeondoka" ni umoja na ina maana ya Yakobo.

nyumba ya baba yako

Hapa "nyumba" ina maana ya familia. "kuwa nyumbani na baba yako na familia yako yote"

miungu yangu

"sanamu zangu"

Genesis 31:31

kwa sababu niliogopa na kudhani kuwa ungeninyang'anya binti zako kwa nguvu ndiyo maana nikaondoka kwa siri

"Niliondoka kwa siri kwa sababu niliogopa ya kwamba ungewachukua binti zako kutoka kwangu kwa lazima"

Yeyote aliyeiiba miungu yako hataendelea kuishi

Hii inaweza kuwekwa katika hali ya chanya. "Tutamuua yeyote aliyechukua miungu yako"

Mbele ya ndugu zetu

Neno "zetu" lina maana ya ndugu wa Yakobo na inajumuisha ndugu za Labani. Ndugu wote watatazama kuhakikisha kila kitu ni cha haki na kweli.

onesha chochote kilichochako nilichonacho na uchukue

"tafuta chochote tulichonacho ambacho ni chako na uchukue"

Kwa maana Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameviiba

Hii inabadilisha kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Yakobo.

Genesis 31:33

wajakazi wawili

Hii ina maana ya Zilfa ba Bilha.

hakuviona

"hakupata sanamu zake"

Genesis 31:34

Basi Raheli ... juu yake

Neno "basi" linatumika hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Raheli.

tandiko

kiti kinachowekwa mgongoni mwa mnyama ili mtu aweze kukaa juu yake.

bwana wangu

Kumuita mtu "bwana wangu" ni njia ya kumheshimu.

siwezi kusimama mbele yako

"kwa sababu siwezi kusimama mbele zako"

kwani nipo katika kipindi changu

Hii ina maana ya kipindi cha mwezi ambapo mwanamke hutokwa na damu kutoka kwenye uzazi wake.

Genesis 31:36

Akamwambia

"Yakobo alimwambia Labani"

Kosa langu ni nini? Dhambi yangu ni ipi, hata ukanifuatia kwa ukali?

Misemo ya "Kosa langu ni nini" na "Dhambi yangu ni ipi" zina maana moja. Yakobo anamuuliza Labani amwambie ni kipi alichokosea. "Kosa langu ni lipi mpaka unifuate namna hii?"

ukanifuatia kwa ukali

Hapa neno la "ukali" ina maana ya Labani kumfukuza kwa haraka kwa lengo la kumkamata.

Umeona nini kati ya kitu chochote cha nyumbani mwako

"Umepata nini ambacho ni cha kwako?"

Viweke hapa mbele ya ndugu zetu

Hapa neno "zetu" ina maana ya ndugu wa Yakobo na inajumuisha ndugu wa Labani. "Laza chochote ulichokuta mbele ya ndugu zetu"

waamue kati yetu wawili

Hapa "yetu wawili" ina maana ya Yakobo na Labani. Msemo "waamue kati" ina maana ya kuamua mtu yupi yupo sahihi katika ugomvi huu. "wanaweza kuhukumu kati yetu"

Genesis 31:38

Taarifa ya Jumla:

Yakobo anaendelea kuzungumza na Labani.

miaka ishirini

"miaka 20"

Kondoo

kondoo wa kike

hawakutoa mimba

Hii ina maana ya kwamba hawajawa na mimba iliyokatishwa mapema na bila matarajio na mwanakondoo au mbuzi kuzaliwa amekufa.

Kilichoraruliwa na mnyama sikukuletea

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mnyama pori alipowaua mmoja wa wanyama wako sikukuletea kwako"

Badala yake, nilichukua upotevu huo

Kwa Yakobo kuhesabu wanyama wa Labani waliokufa kama hasara kutoka kwa mifugo wake inazungumzwa kana kwamba ilikuwa mzigo ambao angeubeba begani mwake. "badala ya kuhesabu hasara kutoka kwa mifugo yako, nimehesabu kama hasara kutoka kwa mifugo yangu"

Nilikuwepo wakati wote; mchana joto lilinipata, na baridi wakati wa usiku

Kuteseka wakati wa jua kali na halijoto chini inazungumzwa kana kwamba halijoto ilikuwa wanyama waliokuwa wakimla Yakobo. "Nilikaa na mifugo wako hata wakati wa joto kali la siku na wakati wa baridi wa usiku"

Genesis 31:41

Taarifa ya Jumla

Yakobo anaendelea kuzungumza na Labani.

Miaka hii ishirini

"Miaka hii 20 iliyopita"

miaka kumi na nne

"miaka 14"

Umebadili ujira wangu mara kumi

"amebadili kile alichosema angenilipa mara kumi"

Isipokuwa Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu, yule Isaka anayemwofu, amekuwa nami

Yakobo ana maana ya Mungu yule yule na sio kwa miungu watatu tofauti. "Kama Mungu wa Abrahamu, na Isaka, baba yangu, asingekuwa na mimi"

Mungu wa baba yangu

Hapa neno "baba" lina maana ya mzazi wake, Isaka.

yule Isaka anayemwofu

Hapa neno "anayemwofu" lina maana ya "hofu ya Yahwe" ambayo ina maana ya kumheshimu kwa ndani na kuonyesha heshima hiyo kwa kumtii yeye.

mikono mitupu

mikono Hii ina maana kutokuwa na kitu. "bila kitu chochote"

Mungu ameliona teso langu na jinsi nilivyofanya kazi kwa bidii

Nomino inayojitegemea "teso" inaweza kuwekwa kama "kuteswa". "Mungu ameona jinsi nilivyofanya kazi kwa bidii na jinsi ulivyonitesa"

Genesis 31:43

akini nitafanya nini leo kwa hawa binti zangu, au kwa watoto wao waliowazaa?

Labani anatumia swali kusisitiza ya kwamba hakuna awezalo kufanya. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Lakini hakuna kitu nachoweza kufanya kuwarudisha binti zangu na wajukuu wangu kwangu"

liwe shahidi

Hapa neno "shahidi" haimaanishi mtu, lakini linatumika kwa mfano na lina maana ya agano ambalo Yakobo na Labani walifanya. Agano linazungumzwa kana kwamba lilikuwa mtu ambaye alikuwa pale wakati walipokubaliana kufanya amani kati yao.

Genesis 31:45

nguzo

Hii ina maana ya kwamba jiwe kubwa liliwekwa mwishoni pake kuweka alama ya sehemu ambapo tukio hili la muhimu lilitokea.

kufanya rundo

"kuzipangilia juu ya nyenzake"

Kisha wakala pale kati ya lile rundo

Kula chakula pamoja ilikuwa sehemu ya kufanya agano baina yao. Maana kamili ya hii inaweza kuwekwa wazi.

Yega Saha Dutha

"Jina la Yega Saha Dutha lina maana ya "fungu la mashahidi" kwa lugha ya Labani.

Galedi

"Jina la Galedi lina maana ya "fungu la mashahidi" kwa lugha ya Yakobo.

Genesis 31:48

Rundo hili ni shahidi kati yangu nawe leo

Mawe hayawi mashahidi halisi kwa ajili ya mtu. "Rundo hili litakuwa ukumbusho kati yangu na wewe"

Galedi

"Jina la Galedi lina maana ya "fungu la mashahidi" kwa lugha ya Yakobo.

Mispa

"Jina la Mispa lina maana ya "mnara".

tunapokuwa hatuonani

Hapa "nje ya macho" ina maana ya kutokuwa machoni pa mwenzako. "tutakapokuwa hatupo machoni mwetu sisi wawili"

japokuwa hakuna mwingine yupo nasi

Hapa "nasi" ina maana ya Labani na Yakobo. "hata kama hakuna mtu wa kutuona"

tazama

"kumbuka". Hii inaongeza msisitizo kwa kile kinachosemwa baadae.

Genesis 31:51

Rundo hili ni shahidi

Marundo haya ya mawe yalikuwa tendo ya kumbukumbu na alama ya mpaka kwa Yakobo na Labani kuhusu makubaliano yao ya amani. Yanazungumzwa kana kwamba ni mashahidi kama watu.

Mungu wa Ibrahimu, na mungu wa Nahori, miungu ya baba zao, waamue kati yetu

Abrahamu ni babu yake Yakobo. Nahori ni babu yake Labani. Baba wa Abrahamu na Nahori ni Tera. Sio wote walimuabudu Yahwe.

Hofu ya Isaka baba yake

Hapa neno "Hofu" lina maana ya Yahwe, ambaye Isaka alimheshimu kwa ndani na kuonyesha heshima hiyo kwa kumtii yeye.

Genesis 31:54

akawaita ndugu zake kula chakula

Kula chakula pamoja ilikuwa sehemu ya kufanya agano baina na mtu. Maana kamili ya hii inaweza kuwekwa wazi.

asubuhi na mapema ... kurudi kwake

Mstari wa 55 ni mstari wa kwanza wa sura ya 32 katika maandishi ya asili ya Kihebrania, lakini mstari wa mwisho wa suraya 31 katika Biblia za sasa. Tunashauri kufuata hesabu ya Biblia ya lugha yako.

kuwabariki

Hii ina maana ya kuweka nia kwa mambo chanya na yenye manufaa yanayotokea kwa mtu.

Genesis 32

Genesis 32:1

Mahanaimu

"Jina la Mahanaimu lina maana ya "kambi mbili"

Genesis 32:3

Seiri

Hili ni eneo lenye milima katika eneo la Edomu.

Hivi ndivyo mtakavyosema kwa bwana wangu Esau: Hivi ndivyo mtumishi wako Yakobo asemavyo: 'Nimekuwa ... mbele zako

Hii ina nukuu ndani ya nukuu. Nukuu ya moja kwa moja inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Hivi ndivyo nataka ukamwambie bwana wangu Esau. Mwambie nimekuwa ... machoni pake."

bwana wangu Esau

Yakobo anatumia lugha ya upole na anamtaja kaka yake kama "bwana wangu".

mtumishi wakoYakobo

Yakobo anatumia lugha ya upole na anajiita mwenyewe kama "mtumishi wako".

ili kwamba nipate kibali mbele zako.

Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo ya mtu. "ili kwamba unithibitishe"

Genesis 32:6

watu mia nne

"wanamume 400"

alipoogopa

HIi ina maana ya hisia zisizo nzuri ambazo mtu anazo pale anapopata tishio la kudhuriwa kwake au wengine.

kutaabika

"tia wasiwasi" au "kutaabishwa"

kambi moja, ndipo kambi nyingine itakaposalimika

Hapa "kambi" ina maana ya watu. "kuwashambulia watu katika kambi moja, kisha watu wa kambi nyingine watatoroka"

Genesis 32:9

Mungu wa baba yangu Ibrahimu, na Mungu wa baba yangu Isaka, Yahwe

Hii haimanishi mungu wawili, lakini kwa Mungu mmoja wanaomuabudu wote. "Yahwe, ambaye ni Mungu wa babu yangu Abrahamu na baba yangu Isaka"

Yahwe, aliyeniambia, 'Rudi katika nchi yako na kwa jamaa yako, nami nitakustawisha

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isyo moja kwa moja. "Yahwe, wewe uliyesema ya kwamba nirudi katika nchi na kwa jamaa yangu, na kwamab utanifanikisha"

na kwa jamaa yako

"na kwa familia yako"

nitakustawisha

"Nitafanya mema kwako" au "Nitakutendea mema"

Mimi sistahili matendo yako yote ya agano la uaminifu na ustahilifu wote uliomfanyia mtumishi wako

Nomino zinazojitegemea "uaminifu" na "mkweli" inaweza kuwekwa kama "mwaminifu". "Sistahili wewe uwe mwaminifu kwa agano lako au kwako kuwa mwaminifu kwangu, mtumishi wako"

mtumishi wako

Hii ni njia ya upole ya kusema "mimi"

sasa nimekuwa matuo mawili

Hapa "nimekuwa" inamaana ya kile ambacho anacho sasa. "na sasa nina watu wa kutosha, mifugo, na mali kutengeneza kambi mbili"

Genesis 32:11

niokoe

"niokoe"

kutoka katika mikono ya ndugu yangu, mikono ya Esau

Hapa neno "mikono" ina maana ya nguvu. Misemo miwili ina maana moja. Msemo wa pili unaelezea ya kwamba kaka ambaye Yakobo alikusudia ni Esau. "kutoka kwa nguvu ya kaka yangu, Esau" au "kutoka kwa kaka yangu, Esau"

namwogopa, kwamba

"Ninaogopa ya kwamba"

Lakini ulisema, 'hakika nitakufanya ufanikiwe. Nitaufanya uzao wako ... hesabu.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Lakini ulisema ya kwamba utanitafanikisha, na kwamba utafanya uzao wangu .. hesabu"

nitakufanya ufanikiwe

"kufanya mema kwako" au "kukutendea mema"

Nitaufanya uzao wako kuwa kama mchanga wa bahari

Hii inazungumzia hesabu kubwa ya uzao wa yakobo kana kwamba hesabu yake itakuwa kama chembe za mchanga za pwani za baharini.

ambao hauwezi kuhesabika kwa hesabu yake

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambayo hakuna mtu awezaye kuhesabu kwa sababu ya hesabu yake"

Genesis 32:13

mia mbili

"200"

ishirini ... thelathini ... arobaini ... kumi

"20 ... 30 ... 40 ... 10"

na wana wao

"na watoto wao"

Akawaweka katika mikono ya watumishi wake, kila kundi peke yake.

Hapa "katika mikono" ina maana ya kutoa mamlaka juu yao. "Aliwagawa katika makundi madogo, na kuwapa kila mmoja wa watumishi wake mamlaka juu ya makundi"

mwache nafasi kati ya makundi ya wanyama

"na kila kundi lisafiri kwa umbali kutoka kwa kundi lingine"

Genesis 32:17

Akamwagiza

"Akamuamuru"

kukuuliza .... ambao wako mbele yenu?

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "kukuuliza bwana wako ni nani, unakwenda wapi, na nani anamiliki wanyama walio mbele yako"

ni wa nani?

"Bwana wako ni nani?"

wanyama hawa mbele yenu ni wa nani?

"Nani anamiliki wanyama hawa ambao wako mbele yako?"

Ndipo umwambie, 'Ni wa mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi wanaopelekwa kwa bwana wangu Esau. Na tazama, yeye pia anakuja nyuma yetu."

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Kisha ntataka kumwambia ya kwamba vitu vyote hivi ni vya Yakobo, mtumishi wake, na anampatia bwana wake, Esau. Na mwambie ya kwamba Yakobo yupo njiani kukutana naye"

mtumishi wako Yakobo

Yakobo anajifafanua kwa njia ya upole kama mtumishi wa Esau.

kwa bwana wangu Esau

Yakobo anajifafanua kwa Esau kwa njia ya upole kama bwana wake.

anakuja nyuma yetu

Hapa "yetu" ina maana ya mtumishi akizungumza na watumishi wengine kuleta mifugo kwa Esau.

Genesis 32:19

akatoa maelekezo kwa kundi la pili

"akaamuru kundi la pili"

Mnapaswa pia kusema, 'mtumwa wako Yakobo

Maana zaweza kuwa 1) "Utasema pia, 'Mtumishi wako Yakobo"' au 2) 'Utasema, "Pia, Mtumishi wako Yakobo"'.

nitamtuliza

"Nitamtuliza" au "Nitafanya hasira yake itoweke"

atanipokea

"atanikaribisha kwa upole"

Hivyo zawadi zikatangulia mbele yake

Hapa "zawadi" ina maana ya watumishi kupeleka zawadi zile.

Yeye mwenyewe akakaa

Hapa "mwenyewe" inasisitiza ya kwamba yakobo hakuwenda pamoja na watumishi wake.

Genesis 32:22

wajakazi wake wawili

"watumishi wake wawili wake zake". Hii ina maana ya Zilpa na Bilha.

kijito

sehemu ya kina kifupi ya mto ambayo ni rahisi kuvuka.

Yaboki

Hili ni jina la mto.

mali yake yote

"kila kitu alichokuwa nacho"

Genesis 32:24

mpaka alfajiri

"mpaka alfajiri"

nyonga

"kiungo cha paja". Hii ni sehemu ambapo mfupa wa juu wa mguu unaungana na nyonga.

Nyonga ya Yakobo ikatenguka alipokuwa akishindana naye

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mwanamume alijeruhi nyonga ya Yakobo aliposhindana naye"

kwani kunakucha

"jua litachomoza hivi karibuni"

umenibariki

Hapa "umenibariki" ina maana ya kutamka baraka maalumu juu ya mtu na kusababisha mambo mazuri kutokea kwa huyo mtu.

sitakuacha uende mpaka uwe umenibariki

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya chanya. "Haiwezekani! Lazima unibariki kwanza, ndipo nitakuacha uondoke"

Genesis 32:27

Israeli

"Jina la Israeli lina maana ya 'Anayeshindana na Mungu'"

na wanadamu

Hapa "wanadamu" ina maana ya "watu" kwa ujumla.

Genesis 32:29

Akasema, "Kwa nini kuniuliza jina langu?"

Akasema, "Kwa nini kuniuliza jina langu?" Swali hili la balagha lilitakiwa kushtua, kukaripia na kumfanya Yakobo awaze juu ya kilichotokea kati yake na mtu mwingine aliyeshindana naye. "Usiniulize jina langu!"

Penieli

"Jina la Penieli lina maana ya "uso wa Mungu".

uso kwa uso

Kuwa "uso kwa uso" ina maana ya watu wawili kutazamana ana kwa ana, kwa umbali mfupi.

na maisha yangu yamesalimika

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "na bado akasalimisha maisha yangu"

Genesis 32:31

Ndiyo maana wana hadi siku ya leo

Hii inafanya mabadiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu vizazi vya Israeli.

hadi siku ya leo

Hii ina maana siku ambayo mwandishi alikuwa akiandika hivi.

kano za nyonga

Hii ina maana ya msuri unaonganisha mfupa wa paja na kiungo cha paja.

kiungo cha nyonga

"kiungo cha paja"

alipotegua

"alipokuwa akipiga"

Genesis 33

Genesis 33:1

tazama

Neno "tazama" hapa linatuamsha kuvuta nadhari juu ya sehemu mpya ya simulizi ya kushangaza.

watu mia nne

"wanamume 400"

Yakobo akawagawanya watoto ... wajakazi wawili wakike

Hii haimaanishi Yakobo aliwagawanya watoto wake sawa sawa ili kwamba kila mwanamke awe na idadi sawa ya watoto pamoja nao. Yakobo aliwagawa watoto ili kila mmoja aondoke na mama yake.

watumishi wa kike

"watumishi wa kike wake zake". Hii ina maana ya Bilha na Zilpa"

Yeye mwenyewe akatangulia mbele yao

Hapa "mwenyewe" inasisitiza ya kwamba Yakobo aliondoka peke yake mbele ya wenzake.

Akasujudu

Hapa neno "sujudu" lina maana ya kuinama chini kuonyesha kwa unyenyekevu heshima na taadhima kwa mtu.

Genesis 33:4

kumlaki

"kukutana na Yakobo"

akamkumbatia, akakumbatia shingo yake na kumbusu

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Esau aliweka mikono yake kumzunguka Yakobo, kumkumbatia, na kumbusu"

Kisha wakalia

Hii inaweza kusemwa kwa uwazi zaidi. "Kisha Esau na Yakobo wakalia kwa sababu walikuwa na furaha kuonana tena"

aliona wanawake na watoto

"akawaona wanawake na watoto waliokuwa na Yakobo"

Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako

Msemo "mtumishi wako" ni njia ya upole ya Yakobo akimaanisha yeye mwenyewe. "Hawa ni watoto ambao Mungu amenipatia mtumishi wako, kwa neema yake"

Genesis 33:6

watumishi wa kike

"watumishi wa kike wake zake". Hii ina maana ya Bilha na Zilpa.

wakasujudia

Hii ni ishara ya unyenyekevu na heshima mbele za mtu mwingine.

Unamaanisha nini kwa makundi haya yote niliyokutana nayo?

Msemo wa "makundi haya yote" una maana ya makundi ya watumishi ambao Yakobo aliwatuma kutoa zawadi kwa Esau. "Kwa nini ulituma makundi haya yote tofauti kuja kukutana nami?"

Kutafuta kibali machoni mwa bwana wangu.

Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo ya mtu. "Ili kwamba wewe, bwana wangu, ufurahishwe na mimi"

bwana wangu

Msemo "bwana wangu" ni njia ya upole inayomaanisha Esau.

Genesis 33:9

Ninayo ya kutosha

Neno "wanyama" au "mali" linaeleweka. "Nina wanyama wa kutosha" au "Nina mali ya kutosha"

ikiwa nimeona kibali machoni pako

Hapa "machoni" ina maana ya fikra au mawazo ya mtu. "Kama unapendezwa na mimi"

zawadi yangu kutoka mkononi mwangu

Hapa "mkononi" ina maana ya Yakobo. "zawadi hii nayokupatia"

mkononi mwangu, kwa maana

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "mkono wangu. Kwa uhakika"

nimeona uso wako, na ni kama kuona uso wa Mungu

Maana ya tashbihi hii haipo wazi. Maana zaweza kuwa 1) Yakobo amefurahi ya kwamba Esau amemsamehe kama Mungu alivyomsamehe au 2) Yakobo anashangazwa kumuona kaka yake tena kama alivyoshangazwa kumuona Mungu au 3) Yakobo ananyenyekea kuwa mbele ya Esau kama alivyonyenyekea kuwa mbele za Mungu.

nimeona uso wako

Hapa "uso" ina maana ya Esau. Ni vyema kutafsiri kama "uso" kwa sababu ya umuhimu wa neno "uso" hapa pamoja na "uso wa Mungu" na "uso kwa uso" katika 32:29.

uliyoletewa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambazo watumishi wangu wamekuletea"

Mungu amenitendea kwa neema

"Mungu amenitendea wema sana" au "Mungu amenibariki sana"

Hivyo Yakobo akamsihi, na Esau akamkubali

Ilikuwa utamaduni kukataa zawadi kwanza, lakini kukubali zawadi ile baadae kabla ya mtoaji kukwazika.

Genesis 33:12

Bwana wangu anajua

Hii ni njia ya upole na maalumu ya kumhusu Esau. "Wewe, bwana wangu, unajua"

watoto ni wadogo

Maana inaweza kuwekwa wazi zaidi. "watoto ni wadogo sana kusafiri haraka"

Ikiwa watapelekwa kwa haraka hata siku moj

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "tukiwalazimisha kwenda haraka sana hata kwa siku moja"

Tafadhari bwana wangu na amtangulie mtumishi wake

Hii ni njia ya upole na maalumu ya Yakobo kujitaja mwenyewe. "Bwana wangu, mimi ni mtumishi wako. Tafadhali nenda mbele yangu"

kwa kadili ya mifugo iliyo mbele yangu

"kwa kasi ya wanyama naowatunza wanaweza kwenda"

Seiri

Hili ni eneo lenye milima katika eneo la Edomu.

Genesis 33:15

Kwa nini kufanya hivyo?

Yakobo anatumia swali kuweka msisitizo ya kwamba Esau hahitaji kubakiza wanamume. "Usifanye hivyo!" au "Hahitaji kufanya hivyo!"

Bwana wangu amekuwa

Hii ni njia ya upole na maalumu ya kumaanisha Esau. "Wewe, bwana wangu, umekuwa"

Sukothi

"Jina la Sukothi lina maana ya "hifadhi".

akajijengea nyumba

Inasemekana ya kwamba nyumba ni ya familia yake pia. "alijenga nyumba kwa ajili yake mwenyewe na familia yake"

kwa ajili ya mifugo wake

"kwa wanyama aliowatunza"

Genesis 33:18

Taarifa ya Jumla:

Hii inaanza sehemu mpya ya simulizi. Mwandishi anaelezea kile Yakobo alichofanya baada ya kupumzika Sukothi.

Yakobo alipokuja kutoka Padani Aramu

"Baada ya Yakobo kuondoka Padani Aramu"

Yakobo ... alipokuja ... Akapiga kambi

Hii inamtaja Yakobo pekee kwa sababu ni kiongozi wa familia. Inasemekana ya kwamba familia yake ilikuwa pamoja naye.

Akapiga kambi karibu

"Aliweka kambi yake karibu"

sehemu ya ardhi

"kipande cha ardhi"

Hamori

Hili ni jina la mwanamume.

baba wa Shekemu

Shekemu ni jina la mji na jina la mwanamume.

mia

"100"

El Elohe Israeli

"Jina la El Elohe Israeli lina maana ya "Mungu, Mungu wa Israeli"

Genesis 34

Genesis 34:1

Basi

Hapa neno hili linatumika kuweka alama kwa sehemu mpya ya simulizi.

Dina

Hili ni jina la binti wa Lea.

Mhivi

Hili li jina la kundi la watu.

mwana wa mfalme wa nchi

Hii ina maana ya Hamori na sio Shekemu. Pia "mwana wa mfalme" hapa haimaanishi mtoto wa mfalme. Ina maana ya Hamori alikuwa kiongozi wa watu katika eneo hilo.

akamkamata kwa nguvu na kulala naye

Shekemu alimbaka Dina.

Akavutiwa na Dina

"Alivutiwa sana na yeye". Hii inazungumzia juu ya Shekemu kumpenda Dina na kutaka kuwa naye kana kwamba kuna jambo lililokuwa likimlazimisha kwenda kwa Dina. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Alitaka sana kuwa na Dina"

kuongea naye kwa upole

Hii ina maana aliongea naye kwa upole kumuaminisha ya kwamba alimpenda na kwamba alimtaka pia ampende yeye.

Genesis 34:4

Basi Yakobo

"basi" inatumika hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Yakobo.

Yakobo akasikia kwamba alikuwa

Neno "alikuwa" lina maana ya Shekemu

alikuwa amemchafua

Hii ina maana ya kwamba Shekemu alivunja sana heshima na kumuabisha Dina kwa kumlazimisha alale naye.

akawangoja

Hii ni namna ya kusema ya kwamba Yakobo hakusema au kufanya jambo kuhusu suala hili.

Genesis 34:6

Hamori ... akaenda kuongea na Yakobo

"Hamori ... akaenda kuongea na Yakobo"

Watu hawa walichukizwa

"Wanamume walikasirika"

Walikasirika sana ... halikupasa kutendeka

Hii inaweza kuwekwa kama nukuu ya moja kwa moja iliyozungumzwa na wana wa Yakobo.

amemwaibisha Israeli

Hapa neno la "Israeli" lina maana ya kila mtu katika familia ya Yakobo. Israeli kama kundi la watu liliabishwa."ameabisha familia ya Israeli" au "ameleta aibu juu ya watu wa Israeli"

kumlazimisha binti wa Yakobo

"kumvamia binti wa Yakobo"

kwa maana jambo kama hilo halikupasa kutendeka

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kwa maana hakupaswa kufanya jambo baya kama hilo"

Genesis 34:8

Hamori akaongea nao

"Hamori alizungumza na Yakobo na wanawe"

anampenda binti yenu

Hapa neno "anampenda" lina maana ya upendo wa kimahaba kati ya mwanamume na mwanamke. "anampenda na anataka kumuoa"

mpeni kuwa mke wake

Katika baadhi ya tamaduni, wazazi huamua watoto wao wataolewa na nani"

Mwoane nasi

Kuoana ni kuoa mtu wa jamii, kabila, au dini tofauti. "Ruhusu ndoa kati ya watu wako na wetu"

nchi itakuwa wazi kwa ajili yenu

"nchi itakuwa wazi kwako"

Genesis 34:11

Shekemu akamwambia baba yake

"Shekemu alimwambia baba yake Dina Yakobo"

Na nione kibari machoni penu, na chochote mtakachoniambia nitatoa

Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo ya mtu. "Kama utanipa kibali, basi nitakupa chochote utakachokiomba"

mahari

Katika baadhi ya tamaduni, ni kawaida kwa mwanamume kutoa fedha, mali, ng'ombe, na zawadi zingine kwa familia ya mwanamke katika kipindi cha ndoa.

Wana wa Yakobo wakamjibu Shekemu na Hamori baba yake kwa hila

Nomino inayojitegemea ya "hila" inaweza kuwekwa kama kitenzi cha "kudanganya". "Lakini wana wa Yakobo walimdanganya Shekemu na Hamori walipowajibu"

Shekemu alikuwa amemnajisi Dina

Hii ina maana ya kwamba Shekemu aliwavunjia heshima sana na kumuabisha Dina kwa kumlazimisha kulala naye.

Genesis 34:14

Wakawambia

"wana wa Yakobo waliwaambia Shekemu na Hamori"

Hatuwezi kufanya jambo hili, kumpa dada yetu

"Hatuwezi kukubali kumtoa Dina katika ndoa"

kwani hiyo ni aibu kwetu

"kwa maana hiyo itasababisha aibu kwetu". Hapa "kwetu" ina maana ya wana wa Yakobo na watu wote wa Israeli.

tutakapowapa binti zetu ... tutachukua binti zenu kwetu sisi wenyewe

Hii ina maana wataruhusu mtu kutoka familia ya Yakobo kuoa mtu anayeishi katika nchi ya Hamori.

Genesis 34:18

Maneno yao yakawafurahisha Hamori na Shekemu mwanaye

Hapa "maneno" ina maana ya kile kilichosemwa. "Hamori na mwanawe Shekemu walikubali na kile ambacho wana wa Yakobo walisema"

kufanya walichokisema

"kufanyiwa tohara"

binti wa Yakobo

"binti wa Yakobo Dina"

kwa sababu alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana katika nyumba ya babaye

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba Shekemu alijua wanamume wengine wangekubali kufanyiwa tohara kwa sababu walimheshimu sana. "Shekemu alijua wanamume wote katika nyumba ya baba yake watakubaliana naye kwa sababu alikuwa akiheshimiwa zaidi kati yao"

Genesis 34:20

lango la mji wao

Ilikuwa kawaida kwa viongozi kukutana katika lango la mji kufanya maamuzi rasmi.

Watu hawa

"Yakobo, wanawe, na watu wa Israeli"

wana amani nasi

Hapa "nasi" inajumlisha Hamori, mwanawe na watu wote waliozungumza nao langoni mwa mji.

waishi katika nchi na kufanya biashara humo

"waruhusu waishi na kufanya biashara katika nchi"

maana, kweli, nchi ni kubwa ya kuwatosha

Shekemu anatumia neno "kweli" kuongeza msisitizo kwa kauli yake. "kwa sababu, hakika, nchi ni kubwa ya kutosha kwa ajili yao" au "kwa sababu, haswa, kuna nchi ya kutosha kwa ajili yao"

tuwachukue binti zao ... tuwape binti zetu.

Hii ina maana ya ndoa kati ya wanawake wa kundi moja na wanamume wa kundi lingine.

Genesis 34:22

Taarifa ya Jumla:

Hamori na Shekemu mwanawe wanaendelea kuzungumza na viongozi wa mji.

Kwa sharti hili pekee watu hawa wanakubali kuishi nasi na kuwa wamoja: ikiwa kila mwanamme miongoni mwetu atatahiriwa, kama wao.

"Kwa sharti hili pekee iwapo kila mwanamume kati yetu atafanyiwa tohara, kama wanamume wa Israeli walivyotahiriwa, ndipo watakubali kusihi miongoni mwetu na kujiunga nasi kama kundi moja"

Je wanyama wao na vitu vyao - wanyama wao wote kuwa wetu?

Shekemu anatumia swali kusisitiza ya kwamba mifugo wa Yakobo na mali zitakuwa za watu wa Shekemu. Hii inaweza kutafsiriwa kama kauli. "Wanyama wao wote na mali zitakuwa zetu"

Genesis 34:24

Kila mwanamme alifanyiwa tohara

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kwa hiyo Hamori na Shekemu wakawa na mtu wa kufanya tohara kwa wanamume wote"

Katika siku ya tatu

"tatu" ni nambari za mpango kwa namba tatu. Inaweza kuwekwa bila nambari za mpango. "Baada ya siku mbili"

walipokuwa katika maumivu

"wakati wanamume wa mji walipokuwa bado na maumivu"

wakachukua kila mmoja upanga wake

"wakachukua panga zao"

kuushambulia mji

Hapa "mji" una maana ya watu. "waliwashambulia watu wa mji"

ulinzi wake, nao wakauwa wanamume wote

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "ulinzi. Simoni na Lawi waliwaua wanamume wote wa mji ule"

kwa makali ya upanga

Hapa "makali" yana maana ya ubapa wa upanga. "kwa ubapa wa panga zao" au "kwa upanga wao"

Genesis 34:27

maiti

"maiti ya Hamori, Shekemu na wanamume wao"

pora mji

"waliiba kila kitu chenye thamani katika mji ule"

kwa sababu watu wale walikuwa wamemnajisi dada yao

Shekemu pekee alimnajisi Dina, lakini wana wa Yakobo walichukulia familia yote ya Shekemu na kila mtu katika mji kuhusika na tendo hili.

walikuwa wamemnajisi

Hii ina maana ya kwamba Shekemu alimvunjia heshima na kumuabisha sana Dina kwa kumlazimisha kulala naye.

Wakachukua makundi yao

"wana wa Yakobo wakachukua mifugo ya watu wale"

utajiri wao wote

"mali zao zote na fedha"

Watoto na wake zao wote, wakawachukua

"Waliwakamata watoto wao na wake zao wote"

Genesis 34:30

Mmeleta shida juu yangu

Kusababisha mtu kupitia shida inazungumziwa kana kwamba shida ilikuwa kitu kinacholetwa na kuwekwa juu ya mtu. "mmesababisha shida kubwa kwangu"

kunifanya ninuke kwa wenyeji wa nchi

Kusababisha watu katika maeneo yanayozunguka kumchukia Yakobo inazungumziwa kana kwamba wana wa Yakobo walimfanya anuke vibaya kihalisia. Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Mmenifanya nionekane kwa kinyaa kwa watu wanaoishi katika nchi"

Mimi nina watu wachache ... dhidi yangu na kunishambulia, kisha nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu.

Hapa maneno "Mimi" na "yangu" yana maana ya nyumba yote ya Yakobo. Yakobo anasema "Mimi" au "yangu" kwa maana yeye ni kiongozi. "Nyumba yangu ni ndogo ... dhidi yetu na kutuvamia, kisha watatuangamiza sisi wote"

watajikusanya pamoja dhidi yangu na kunishambulia

"wataunda jeshi na kunishambulia" au "wataunda jeshi na kutushambulia"

kisha nitaangamizwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wataniangamiza" au "watatuangamiza"

Je Shekemu alipaswa kumtendea dada yetu kama kahaba?

Simoni na Lawi wanatumia swali kusisitiza ya kwamba Shekemu alifanya kosa na alistahili kufa. "Shekemu hakupaswa kumtenda dada yetu kama kahaba!"

Genesis 35

Genesis 35:1

panda kwenda Betheli

Msemo "panda" unatumika kwa sababu Betheli ipo sehemu ya juu kuliko Shekemu.

Unijengee madhabahu pale

Mungu anaongea kuhusu yeye mwenyewe katika lugha ya utatu. "Jenga madhabahu pale kwangu, Mungu wako"

akawambia nyumba yake

"akwaambia familia yake"

Wekeni mbali miungu yote ya kigeni iliyo kati yenu

"Tupa mbali sanamu zenu" au "Zitokomeze miungu yenu ya uongo"

jitakaseni wenyewe, na kubadili mavazi yenu

Hii ilikuwa utamaduni wa kujitakasa kimaadili na kimwili kabla ya kwenda kumuabudu Mungu.

kubadili mavazi yenu

Kuvaa mavazi mapya ilikuwa ishara ya kwamba walijifanya safi kabla ya kumkaribia Mungu.

katika siku ya shida yangu

Maana za "siku" zaweza kuwa 1) siku ambayo Yakobo alimtoroka Esau au 2) "siku" ina maana ya kipindi ambacho Yakobo alikuwa na mawazo. "nilipokuwa katika kipindi kigumu" au "nilipokuwa katika shida"

Genesis 35:4

Hivyo wakampa

"kwa hiyo kila mmoja katika nyumba ya Yakobo akatoa" au "kwa hiyo kila mtu katika familia na watumishi walitoa"

iliyokuwa mikononi mwao

Hapa "mikononi mwao" ina maana ya kile walichomiliki. "kilichokuwa mali yao" au "walivyokua navyo"

heleni zilizokuwa katika masikio yao

"heleni zao". Maana zaweza kuwa 1) dhahabu katika heleni zingeweza kutumika sanamu zingine au 2) walichukua heleni hizi kutoka kwenye mji wa Shekemu baada ya kuishambulia na kuwaua watu wote. Heleni zingewakumbusha juu ya dhambi yao.

Mungu akaifanya miji yote iliyokuwa karibu nao kuhofu

Mungu kusababisha watu wa miji kumuogopa Yakobo na familia yake inazungumziwa kana kwamba "hofu" ilikuwa kitu kilichoanguka juu ya miji. Nomino inayojitegemea "hofu" inaweza kuwekwa kama "kuogopa". "Mungu aliwafanya watu waliozunguka miji kumuogopa Yakobo na wote aliokuwa nao"

miji yote

Hapa "miji" ina maana ya watu wanaoishi katika miji.

wana wa Yakobo

Inasemekana ya kwamba hakuna mtu aliyeshambulia familia ya Yakobo. Lakini wana wawili, Simoni na Lawi walishambulia ndugu wa Wakaanani wa Shekemu baada ya kumkamata na kulala na binti wa Yakobo. Yakobo aliogopa wangelipiza kisasi katika 34:30. "Familia ya Yakobo" au "Nyumba ya Yakobo"

Genesis 35:6

Luzu

Hili ni jina la mji.

El Betheli

"Jina la El Betheli lina maana ya "Mungu wa Betheli"

Mungu alikuwa amejifunua kwake

"pale Mungu alijifunua kwa Yakobo"

Debora

Hili ni jina la mwanamke.

mlezi wa Rebeka

Mlezi ni mwanamke ambaye humtunza mtoto wa mwanamke mwingine. Mlezi aliheshimika na alikuwa muhimu sana kwa familia.

Akazikwa chini kutoka Betheli

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Walimzika chini kutoka Betheli"

chini kutoka Betheli

Msemo "chini kutoka" unatumika kwa sababu walimzika katika eneo ambalo lilikuwa chini kwa mwinuko kuliko Betheli.

Aloni Bakuthi.

"Jina la Aloni Bakuthi lina maana ya "Mwaloni ambapo kuna maombolezo"

Genesis 35:9

Yakobo alipokuja kutoka Padani Aramu

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba walikuwa Betheli. "Baada ya Yakobo kuondoka Padani Aramu, na wakati alipokuwa Betheli"

kumbariki

Hapa "kubariki" ina maana ya kutamka baraka maalumu juu ya mtu na kusababisha mambo mazuri kutokea juu ya mtu huyo.

lakini jina lako halitakuwa Yakobo tena

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "lakini jina lako halitakuwa Yakobo tena"

Genesis 35:11

Mungu akamwambia

"Mungu akamwambia Yakobo"

Uwe mwenye kuzaa na kuongezeka

Mungu akamwambia Yakobo kuzaa watoto ili kwamba waweze kuwa wengi wao. Neno "kuongezeka" unaelezea jinsi anavyotakiwa "kuzaa".

Taifa na wingi wa mataifa watakujia, na wafalme watatoka miongoni mwa uzao wako

Hapa "taifa" na "mataifa" yana maana ya vizazi vya Yakobo ambao wataunda mataifa haya.

Mungu akapanda kutoka

Hapa "akapanda kutoka" inatumika kwa sababu Mungu anapoishi inafikiriwa kuwa juu au juu ya dunia. "Mungu akamuacha"

Genesis 35:14

nguzo

Hii ni nguzo ya ukumbusho ambayo ilikuwa jiwe au jabali kubwa iliyowekwa mwishoni pake.

Akamimina juu yake sadaka ya kinywaji na akamimina mafuta juu yake

Hii ni ishara ya kwamba anaweka wakfu nguzo kwa Mungu.

Betheli

"Jina la Betheli lina maana ya "nyumba ya Mungu".

Genesis 35:16

Efrathi

Hili ni jina lingine la mji wa Bethelehemu.

akashikwa na uchungu

"Alikuwa na wakati mgumu wakati alipokuwa akimzaa mtoto"

Alipokuwa katika utungu mzito zaidi

"Uchungu ulipokuwa katika hatua mbaya zaidi"

mkunga

mtu anayemsaidia mwanamke anapojifungua mtoto

Hata alipokaribia kufa, kwa pumzi yake ya mwisho

"pumzi yake ya mwisho" ni pumzi ya mwisho ya mtu kabla mtu hajafa. "Hata kabla hajafa, alipovuta pumzi yake ya mwisho"

Benoni

"Jina la Benoni lina maana ya "mtoto wa majonzi yangu""

Benyamini

Watafsiri wanaweza kuweka maandishi mafupi yasemayo "Jina la Benyamini lina maana ya "mtoto wa mkono wa kuume". Msemo wa "mkono wa kulia" unalenga sehemu yenye upendeleo maalumu.

na kuzikwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "na wakamzika"

katika njia

"pembeni mwa barabara"

ndiyo alama ya kaburi la Raheli hata leo

"inaweka alama juu ya kaburi la Raheli mpaka siku hii"

hata leo

"mpaka wakati huu wa leo." Hii ina maana hadi wakati ambapo mwandishi alikuwa akiandika haya.

Genesis 35:21

Israeli akaendelea

Inasemekana ya kwamba familia ya Israeli na watumishi wake wako pamoja naye. Maana kamili ya taarifa hii inaweza kuwekwa wazi.

Bilha

Hii ni jina la mtumishi wa Raheli wa kike.

Basi Yakobo alikuwa na wana kumi na mbili

Sentensi hii inaanza ibara mpya, ambayo inaendeleza mistari inayofuata.

wana kumi na mbili

"watoto 12"

Genesis 35:23

Bilha

Hili ni jina la mtumishi wa Raheli wa kike.

Genesis 35:26

Zilpa

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Lea.

waliozaliwa kwake huko Padani Aramu

Inasemekana ya kwamba hii haimjumlishi Benyamini aliyezaliwa katika nchi ya Kaanani karibu na Bethelehemu. Inataja Padani Aramu tu kwa maana hapo ndipo wengi wao walizaliwa. Maana kamili ya hii inaweza kuwekwa wazi. "ambao walizaliwa kwake Padani Aramu, isipokuwa Benyamini ambaye alizaliwa katika nchi ya Kaanani"

Yakobo akaja kwa Isaka

Hapa "akaja" inaweza kuweka kama "akaondoka"

Mamre

Hili lilikuwa jina lingine la mji wa Hebroni. Inawezekana iliitwa baada ya Mamre, rafiki yake Abrahamu aliyeishi pale. Hii ilikuwa jina la mwanamume aliyemiliki miti ya mwaloni.

Kiriathi Arba

Hili ni jina la mji.

Genesis 35:28

miaka mia moja na themanini

"miaka 180"

Isaka akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa

"Isaka akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa". Misemo ya "alivuta pumzi ya mwisho" na "akafa" ina maana ya kitu kimoja. "Abrahamu alikufa"

akapumua pumzi yake ya mwisho

Hii ni njia ya upole ya kusema mtu alikufa.

akakusanywa kwa wahenga wake

Hii ina maana ya kwamba baada ya Isaka kufa, roho yake ilikwenda sehemu ile ile ndugu zake waliokufa kabla yake. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "alijiunga na familia yake waliokuwa wamekufa"

mtu mzee amejaa siku

Misemo ya "mtu mzee" na "amejaa siku" zina maan moja. Zinasisitiza ya kwamba Isaka aliishi muda mrefu sana. "baada ya kuishi muda mrefu sana na kuzeeka sana"

Genesis 36

Genesis 36:1

Hivi ndivyo vizazi vya Esau (aliyeitwa pia Edomu)

"Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ambaye pia anaitwa Edomu". Sentensi hii inatambulisha habari ya vizazi vya Esau katika Mwanzo 36:1-8. "Hii ni habari ya vizazi vya Esau, ambaye pia anaitwa Edomu"

Ada ... Oholibama

Haya ni majina ya wake wa Esau.

Eloni Mhiti

"Eloni kizazi cha Hethi" au "Eloni uzao wa Hethi". Hili ni jina la mwanamume.

Ana ... Zibeoni ... Nebayothi

Haya ni majina ya wanamume.

Mhivi

Hii ina maana ya kikundi kikubwa cha watu.

Basemathi

Hili ni jina la mke mmoja wa Esau.

Nebayothi

Hili ni jina la mtoto mmoja wa kiume wa Ishmaeli.

Genesis 36:4

Ada ... Basemathi ... Oholibama

Haya ni majina ya wake wa Esau.

Elifazi ... Reueli ... Yeushi ... Yalamu ... Kora

Haya ni majina ya wana wa Esau.

Genesis 36:6

aliyokuwa amekusanya katika nchi ya Kanaani

Hii ina maana ya vitu vyote vilivyokusanywa alipokuwa katika nchi ya Kaanani. "aliyokuwa amekusanya alipokuwa akiishi katika nchi ya Kanaani"

akaenda katika nchi

Hii ina maana ya kuhama katika sehemu nyingine na kuishi kule. "alikwenda kuishi katika nchi nyingine"

mali zao

"Mali za Esau na Yakobo"

isingeweza kuwafaa kwa mifugo yao. 8

Nchi haikuwa na ukubwa wa kutosha kuwatunza mifugo wote ambao Yakobo na Esau walimiliki. "haikuwa na ukubwa wa kutosha kuwatunza mifugo yao" au "haikuwa na ukubwa wa kutosha kwa mifugo ya Esau na Yakobo"

waliyokuwa wamekaa

Neno "wamekaa" lina maana ya kuelekea sehemu na kuishi pale. "pale walipohamia"

Genesis 36:9

Hivi ndivyo vizazi vya Esau

Sentensi hii inatambulisha habari ya vizazi vya Esau katika Mwanzo 36:9-43. "Hii ni habari ya vizazi vya Esau"

katika nchi ya mlima Seiri

Hii ina maana ya kwamba waliishi katika nchi ya mlima wa Seiri. Maana kamili ya hii inaweza kuwekwa wazi. "aliyeishi katika mlima wa nchi ya Seiri"

Elifazi ... Reueli

Haya ni majina ya wana wa Esau.

Ada ... Basemathi

Haya ni majina ya wake wa Esau.

Temani, Omari, Zefo, Gatamu, na Kenazi ... Amaleki

Haya ni majina ya wana wa Elifazi.

Timna

Hili ni jina la suria wa Elifazi.

Genesis 36:13

Reueli ... Yeushi, Yalamu, na Kora

Haya ni majina ya wana wa Esau.

Nahathi .... Zera ... Shama ... Miza

Haya ni majina ya wana wa Reueli.

Ana .... Zibeoni

Haya ni majina ya wanamume.

Basemathi ... Oholibama

Haya ni majina ya wake wa Esau.

Genesis 36:15

Elifazi

Hili ni jina la mwana wa Esau.

Temani, Omari, Zefo, Kenazi, Kora, Gatamu, na Amaleki

Haya ni majina ya wana wa Elifazi.

Ada

Hili ni jina la mmoja wa wake wz Esau.

Genesis 36:17

Reueli ... Yeushi, Yalamu, Kora

Haya ni majina ya wana wa Esau.

Nahathi, Zera, Shama, Miza

Haya ni majina ya wana wa Reueli.

katika nchi ya Edomu

Hii ina maana ya kwamba waliishi katika nchi ya Edomu. "walioishi katika nchi ya Edomu"

Basemathi ... Oholibama

Haya ni majina ya wake wa Esau.

Ana

Hili ni jina la mwanamume.

Genesis 36:20

Seiri

Neno la "Seiri" ni jina la mwanamume na nchi.

Mhori

Neno la "Mhori" lina maana la kundi la watu.

wakazi wa nchi hiyo

walioishi katika nchi ya Seiri, ambayo pia inaitwa Edomu.

Lotani, Shobali, Zibeoni, Ana, Dishoni, Ezeri, na Dishani ... Hori na Hemani

Haya ni majina ya wanamume.

Timna

Hili ni jina la mwanamke.

Genesis 36:23

Shobali ... Zibeoni

Haya ni majina ya wanamume.

Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu ... Aia na Ana

Haya ni majina ya wanamume.

Genesis 36:25

Ana ... Dishoni ... Ezeri ... Dishoni

Haya ni majina ya wanamume.

Oholibama

Hili ni jina la mwanamke.

Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani ... ilhani, Zaavani, na Akani ... Uzi na Arani

Haya ni majina ya wanamume.

Genesis 36:29

Timna

Hili ni jina la kundi la watu.

Lotani, Shobali, Zibeoni, na Ana, Dishoni, Ezeri, Dishani

Haya ni majina ya wanamume.

katika nchi ya Seiri

Hii ina maana ya kwamba waliishi katika nchi ya Seiri. "kwa wale walioishi katika nchi ya Seiri"

Genesis 36:31

Bela ... Beori ... Yobabu ... Zera

Haya ni majina ya wanamume.

jina la mji wake

Hii ina maana ya kwamba huu ulikuwa mji ambapo aliishi. "jina la mji alipoishi"

Dinhaba ... Bozra

Haya ni majina ya mahali.

Genesis 36:34

Yobabu

Hili ni jina la mwanamume.

Hushamu ... Hadadi ... Bedadi ... Samla

Haya ni majina ya wanamume.

Hushamu aliyekuwa wa nchi ya Watemani

Hii ina maanisha Hushani aliishi katika nchi ya Watemani. "Hushami aliyeishi katika nchi ya Watemani"

Avithi ... Masreka

Haya ni majina ya mahali.

Watemani

"vizazi vya Temani"

Jina la mji wake

Hii ina maana ya kwamba huu ulikuwa mji ambao aliishi. "Jina la mji ambao aliishi"

Samla wa Masreka

"Samra wa Masreka"

Genesis 36:37

Samla

Hili ni jina la mwanamume.

kisha Shauli wa Rehobothi kando ya mto alitawala mahali pake

Shauli aliishi Rehobothi. Rehobothi ilikuwa karibu na Mto Frati. Taarifa hii inaweza kuwekwa wazi. "kisha Shauli akatawala katika nafasi yake. Alikuwa akitoka Rehobothi ambayo ipo karibu na Mto Frati"

Shauli ... Baali Hanani ... Akbori ... Hadari ... Matredi ... Me Zahabu.

Haya ni majina ya wanamume.

Rehobothi ... Pau

Haya ni majina ya mahali.

Jina la mji wake

Hii ina maana ya kwamba huu ulikuwa mji ambao aliishi. "Jina la mji ambao aliishi"

binti wa Matredi, mjukuu wa Me Zahabu.

Taarifa ambayo haionekani inaweza kuongezwa. "alikuwa binti wa Matredi, na mjukuu wa Me Zahabu"

Mehetabeli

Hili ni jina la mwanamke.

Genesis 36:40

majina ya wakuu wa koo

"viongozi wa koo zao"

kwa kufuata koo zao na maeneo yao, kwa majina yao

Koo na maeneo yalitajwa kwa majina ya viongozi wa koo zao. "jina la koo zao na maeneo walipoishi yalitajwa baada yao. Haya ndio majina yao"

Timna, Alva, Yethethi, Oholibama, Ela, Pinoni, Kenazi, Temani, Mbza, Magdieli, na Iramu

Haya ni majina ya makundi ya watu.

makazi

"makazi ya kuishi" au "sehemu waliokuwa wakiishi"

Huyu alikuwa Esau

orodha hii inasemekana "kuwa" Esau, ambayo ina maana ni orodha nzima ya vizazi vya Esau"

Genesis 37

Genesis 37:1

nchi aliyokaa babaye, katika nchi ya Kanaani

"katika nchi ya Kaanani ambapo baba yake aliishi"

Haya ndiyo matukio yaliyomhusu Yakobo

Sentensi hii inatambulisha habari ya watoto wa Yakobo katika Mwanzo 37:1-50:26. Hapa "Yakobo" ina maana ya familia yake nzima. "Hii ni habari ya familia ya Yakobo"

umri wa miaka kumi na saba

"umri wa miak 17"

Bilha

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Raheli.

Zilpa

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Lea.

wake

"suria". Wanawake hawa walikuwa watumishi wa Lea na Raheli waliopewa kwa Yakobo kumzalia watoto.

akaleta taarifa yao mbaya kuhusu wao

"taarifa mbaya kuhusu kaka zake"

Genesis 37:3

Basi

Neno hili linatumika hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Israeli na Yusufu.

akampenda

Hii ina maana ya upendo wa kindugu au upendo wa kirafiki au kifamilia. Huu ni upendo wa kawaida wa binadamu kati ya marafiki na ndugu.

wa uzee wake

Hii ina maana ya kwamba Yusufu alizaliwa wakati Israeli alikuwa mzee. "aliyezaliwa wakati Israeli alipokuwa mtu mzee"

Akamshonea

"Israeli alimshonea Yusufu"

vazi zuri

"joho zuri"

hawakuongea naye vema.

"hawakuweza kuongea kwa namna ya upole kwake"

Genesis 37:5

Yusufu akaota ndoto, na akawambia ndugu zake. Wakamchukia zaidi

Huu ni ufupi wa matukio ambayo yatatokea katika 37:6-11.

Wakamchukia zaidi

"Na kaka zake Yusufu walimchukia zaidi ya walivyomchukia hapo awali"

Tafadhari sikilizeni ndoto hii niliyoiota

"Tafadhali sikilizeni ndoto hii niliyoipata"

Genesis 37:7

Taarifa ya Jumla:

Yusufu anaeleza kaka zake kuhusu ndoto yake.

Tazama

Neno la "tazama" hapa linatuamsha kuvuta nadhari kwa taarifa ya kushangaza inayofuata.

tulikuwa

Neo "tulikuwa" ina maana ya Yusufu na inajumuisha kaka zake wote.

tukifunga miganda ya nafaka

Nafaka inapovunwa inafungwa katika makundi na kupangwa katika rundo hadi muda wa kuzitenga nafaka kutoka kwa majani makavu.

na tazama

Hapa neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Yusufu alishangazwa na kile alichokiona.

mganda wangu ukainuka na kusimama wima ... miganda yenu ikasogea na kuuinamia mganda wangu

Hapa miganda ya nafaka inasimama wima na kupiga magoti kana kwamba ilikuwa watu. Miganda hii inawakilisha Yusufu na kaka zake.

Je ni kweli utatutawala? Je utatutawala juu yetu?

Misemo hii miwili ina maana moja. Kaka zake Yusufu wanatumia swali kumkejeli Yusufu. Inaweza kuandikwa kama kauli. "Hutaweza kuwa mfalme wetu, na hatutainama chini kwako!"

utatutawala juu yetu

Neno la "yetu" lina maana ya kaka zake Yusufu lakini sio Yusufu.

kwa ajili ya ndoto zake na maneno yake

"kwa sababu ya ndoto yake na kile alichokisema"

Genesis 37:9

Akaota ndoto nyingine

"Yusufu akapata ndoto nyingine"

nyota kumi na moja

"nyota 11"

baba yake akamkemea. Akamwambia

"Israeli alimkaripia, akisema"

Je umeota ndoto ya namna gani hii? Je mama yako ... kukuinamia mpaka chini?

Israeli anatumia swali kumrekebisha Yusufu. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Ndoto hii uliyoota sio ya kweli. Mama yako, kaka zako, na mimi hatutainama chini mbele yako!"

wivu

Hii ina maana kuwa na hasira kwa sababu mtu mwingine amefanikiwa au ana umaarufu zaidi.

akaliwema jambo hilo moyoni

Hii ina maana ya kwamba aliendelea kufikiria kuhusu maana ya ndoto ya Yusufu. "aliendelea kufikiria kuhusu maana ya ndoto ile"

Genesis 37:12

Je ndugu zako hawalichungi kundi huko Shekemu?

Israeli anatumia swali kuanza mazungumzo. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Ndugu zako wanachunga kundi huko Shekemu".

Njoo

Hapa inasemekana ya kwamba Israeli anamuomba Yusufu kujiandaa kuondoka kuonana na ndugu zake. "Jiandae"

nipo tayari

Yupo tayari kuondoka. "Nipo tayari kuondoka"

Akamwambia

"Israeli akamwambia Yusufu"

uniletee neno

Israeli anamtaka Yusufu kurudi na kumuambia kuhusu kaka zake na hali ya mifugo. "njoo uniambie utakakikuta" au "niletee taarifa"

kutoka katika bonde

"kutoka bondeni"

Genesis 37:15

Mtu mmoja akamwona Yusufu. Tazama, Yusufu alikuwa akizunguka kondeni

"Mtu mmoja akamkuta Yusufu akizunguka kondeni"

Tazama

Hii inaweka alama mwanzo wa tukio jingine katika simulizi kuu. Inaweza kuhusisha watu tofauti kuliko matukio ya nyuma.

Unatafuta nini?

"Ni nini unatafuta"

Tafadhari, niambie, wapi

"Tafadhali niambie wapi"

wananalichunga kundi

"wakichunga kundi"

Dothani

Hili ni jina la mahali ambalo lipo kama kilomita 22 kutoka Shekemu.

Genesis 37:18

Wakamwona kutokea mbali

"Ndugu zake Yusufu wakamwona alipokuwa bado yupo mbali"

wakapanga njama ya kumwua

"wakafanya njama ya kumuua"

mwotaji anakaribia

"anakuja yule mwenye ndoto zile"

Njoni sasa

Msemo huu unaonyesha ya kwamba kaka zake walitekeleza mipango yao. "Kwa hiyo sasa"

Mnyama mkali

"mnyama wa hatari" au "mnyama mkali"

amemmeza

amemla kwa hamu

Nasi tutaona ndoto zake zitakuwaje

Ndugu zake walipanga kumuua, kwa hiyo ni kejeli kuzungumzia kuhusu ndoto zake kuwa kweli, maana angekuwa amekwisha kufa. "Kwa njia hiyo tutahakikisha ndoto zake haziji kuwa kweli"

Genesis 37:21

alilisikia

"alisikia walichokuwa wakisema"

kutoka katika mikono yao

Msemo "mikono yao" una maana ya mipango ya kaka zake ya kumuua. "kutoka kwao" au "kutoka kwa mipango yao"

Tusiuondoe uhai wake

Msemo wa "kuondoa uhai wake" ni tasifida kwa kumuua mtu. "Tusimuue Yusufu"

Msimwage damu

Ukanushaji unaweza kuwekwa juu ya kitenzi. Pia "kumwaga damu" ni tasifida ya kuua mtu. "Usimwage damu yoyote" au "Usimuue"

msiweke mikono yenu juu yake

Hii ina maana ya kumdhuru au kumjeruhi. "msimdhuru"

ili kwamba aweze kumwokoa

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Rubeni alisema hivi ili aweze kumuokoa Yusufu"

mikono mwao

Msemo wa "mikononi mwao" una maana ya mpango wa kaka zake kumuua. "kutoka kwao" au "kutoka kwa mipango yao"

kumrudisha

"na kumrudisha"

Genesis 37:23

Ikawa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama juu ya tukio muhimu la simulizi.

walimvua vazi lake zuri

"walichana joho lake zuri kutoka kwake"

vazi lake zuri

"joho zuri"

Genesis 37:25

Wakakaa chini kula mkate

"Mkate" ni lugha nyingine kwa "chakula". "Walikaa chini kula chakula" au "Ndugu zake Yusufu walikaa chini kula"

Walipoinua macho yao na kuangalia, na, tazama, msafara

Hapa kuangalia juu inazungumziwa kana kwamba mtu aliinua macho yake juu kihalisia. Pia, neno "tazama" linatumika hapa kuvuta nadhari ya msomaji kwa kile walichokiona wanamume hawa. "Walitazama juu na ghafla wakaona msafara"

ulikuwa

"umebeba"

viungo

vikolezo

malhamu

kitu chenye mafuta chenye harufu tamu kinachotumiwa kwa ajili ya kuponya na kulinda ngozi. "dawa"

wakisafiri kuvichukua kuelekea Misri

"kuwaleta mpaka Misri". Hii inaweza kuwekwa wazi zaidi. "kuwaleta chini hadi Misiri kuviuza"

Ni faida gani kama tutamwua ndugu yetu na kufunika damu yake?

Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Hatupati faida yoyote kumuua ndugu yetu na kufunika damu yake"

kufunika damu yake

Huu ni msemo wenye maana ya kuficha kifo cha Yusufu. "kuficha mauaji yake"

Genesis 37:27

kwa Waishmaeli

"kwa wanamume hawa ambao ni vizazi vya Ishmaeli"

tusiweke mikono yetu juu yake

Hii ina maana ya kutomdhuru au kumjeruhi. "msimuumize"

ni ndugu yetu, nyama yetu

Neno la "nyama" ni lugha nyingine lenye maana ya ndugu. "ni ndugu wetu wa damu"

ndugu zake wakamsikiliza

"Kaka zake na Yuda walimsikiliza" au "Kaka zake Yuda walikubaliana naye"

Kimidiani ... Waishmaeli

Majina yote mawili yana maana ya kundi moja la wafanyabiashara ambao ndugu zake Yusufu walikutana nao.

kwa vipande ishirini vya fedha

"kwa bei ya vipande 20 vya fedha"

wakamchukua Yusufu mpaka Misri

"wakampeleka Yusufu Misri"

Genesis 37:29

Rubeni akarudi kwenye shimo, na, tazama, Yusufu hakuwemo shimoni

"Rubeni alirudi kwenye shimo, na akashangazwa kuona ya kwamba Yusufu hakuwepo mle" Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Rubeni alishangazwa kukuta ya kwamba Yusufu aliondoka.

Akararua mavazi yake

Hili ni tendo la mawazo na uchungu mkubwa. Hii inaweza kuandikwa kwa uwazi zaidi. "Alikuwa na majonzi mpaka akararua nguo zake"

Kijana yuko wapi? Na mimi, je niende wapi?"

Rubeni anatumia maswali kuweka msisitizo kwa tatizo ambalo Yusufu hapatikani. Hivi vinaweza kuandikwa kama kauli. "Kijana ametoweka! Siwezi kurudi nyumbani sasa!"

Genesis 37:31

vazi la Yusufu

Hii ina maana ya joho zuri ambalo baba yake alimtengenezea.

damu

"damu ya mbuzi"

wakalipeleka

"walileta joho lile"

amemrarua

"amemla"

Yusufu ameraruliwa katika vipande.

Yakobo anadhani ya kwamba mnyama pori amerarua mwili wa Yusufu vipande vipande. "hakika imemchana Yusufu katika vipande vipande"

Genesis 37:34

Yakobo akararua mavazi yake

Hili ni tendo la mawazo na uchungu mkubwa. Hii inaweza kuandikwa kwa uwazi zaidi. "Yakobo alikuwa na majonzi mpaka akararua nguo zake"

kuvaa mavazi ya magunia katika viuno vyake

Hapa "viuno" ina maana ya sehemu ya katikati ya mwili au kiuno. "akavaa magunia"

wakainuka

Hapa ujio wa watoto kwa baba yao inazungumziwa kama "kuinuka juu". "wakaja kwake"

lakini alikataa kufarijiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "lakini hakutaka wamfariji"

Hakika nitashuka kuzimu nikimwombolezea

Hii ina maana ataomboleza kutoka sasa hadi pale atakapokufa. "Kweli nitakapokufa na kwenda kuzimu bado nitakuwa naomboleza"

Wamidiani wakamwuza

"Wamidiani walimuuza Yusufu"

kepteni wa walinzi

"kiongozi wa wanajeshi waliokuwa wakimlinda mfalme"

Genesis 38

Genesis 38:1

Ikawa wakati ule Yuda

Hii inatambulisha sehemu mpya ya simulizi ambayo inamlenga Yuda.

Mwadulami fulani, jina lake Hira

Hira ni jina la mwanamume aliyeishi Adulami. Mwadulami ni utaifa wake.

jina lake Shua

Shua ni mwanamke wa Kaanani aliyeolewa na Yuda.

Genesis 38:3

Akawa mjamzito

"mke wa Yuda akawa mjamzito"

Akaitwa Eri

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Baba yake akamuita Eri"

Eri ... Onani ... Shela

Haya ni majina ya wana wa Yuda.

akamwita jina lake

"akamwita"

Kezibu

Hili ni jina la mahali.

Genesis 38:6

Eri

Hili ni jina la mmoja wa watoto wa Yuda.

alikuwa mwovu machoni pa Yahwe

Msemo "machoni pa" una maana ya yahwe kuona uovu wa Eri.. "alikuwa muovu na Yahwe akauona"

Yahwe akamwua

Yahwe akamuua kwa sababu alikuwa muovu. Hii inaweza kuwekwa wazi. "Kwa hiyo Yahwe akamuua"

Genesis 38:8

Onani

Hili ni jina la mmoja wa watoto wa Yuda.

Fanya wajibu wa shemeji kwake

shemeji kwake - Hii ina maana ya utamaduni ambao mwana mkubwa anapofariki kabla yeye na mkewe kupata mwana, ndugu anayefuata kiumri angemuoa na kulala na mjane. Mjane atakapozaa mwana wa kwanza, mtoto yule alijulikana kuwa mwana wa ndugu wa kwanza na angepokea urithi wa kaka wa kwaza.

lilikuwa ovu mbele za Yahwe

Msemo huu "machoni pa" una maana ya Yahwe kuona uovu wa Onani. "alikuwa muovu na Yahwe aliuona"

Yahwe akamwua pia

Yahwe akamuua kwa sababu alichofanya kilikuwa kiovu. Hii inaweza kuwekwa wazi. "Kwa hiyo Yahwe akamuua pia"

Genesis 38:11

mkwewe

mkwewe - "mke wa mwanawe mkubwa"

katika nyumba ya baba yako

Hii ina maana ya yeye kuishi katika nyumba ya baba yake. "na kuishi katika nyumba ya baba yako"

hadi Shela, mwanangu, atakapokuwa

Yuda anakusudia kwa Tamari kuja mumuoa Shela atakapokua mkubwa. "na pale ambapo Shela, mwanangu, atakapokua, ataweza kukuoa"

Shela

Hili ni jina la mmoja wa wana wa Yuda.

Kwani aliogopa, "Asije akafa pia, kama nduguze

Yuda aliogopa ya kwamba iwapo Shela atamuoa Tamari angekufa pia kama kaka zake walivyokufa. "Kwa maana alihofia, 'akimuoa na yeye angeweza kufa kama kaka zake walivyokufa"

Genesis 38:12

Shua

Hili ni jina la mwanamume.

Yuda akafarijika na

"Yuda alipokuwa haombolezi, ali"

wakatao kondoo wake manyoya huko Timna

"Timna, ambapo wanamume wake walikuwa wakinyoa manyoya ya kondoo"

Timna ... Enaimu

Haya ni majina ya mahali.

yeye na rafiki yake, Hira Mwadulami

"Rafiki yake Hirami, kutoka Adulami, alikwenda naye"

Hira Mwadulami

"Hira" ni jina la mwanamume, na "Adulami" ni jina la kijiji ambapo aliishi.

Tamari akaambiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu akamwambia Tamari"

Tazama, mkweo

mkweo - "Sikiliza". Hapa neno "tazama" linatumika kushika nadhari ya Tamari.

mkweo

mkweo - "baba wa mume wako"

ya ujane

"ambayo wajane huvaa"

ushungi

kitambaa chembamba sana kinachotumika kufunika kichwa na uso wa mwanamke.

na akajifunika

Hii ina maana alijificha kwa nguo yake ili kwamba watu wasiweze kumtambua. Kitamaduni, sehemu za nguo za wanawake zilikuwa kubwa walizojizungushia nazo. "na akajifunika na kitambaa chake ili watu wasiweze kumtambua"

kando ya njia

"kando ya barabara" au "njiani"

hakupewa kuwa mke wake

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yuda hakupatiwa kwa Shela kuwa mke"

Genesis 38:15

kwa maana alikuwa amefunika uso wake

Yuda hakufikiria ya kwamba alikuwa kahaba kwa sababu tu alifunika uso wake lakini pia kwa sababu alikuwa amekaa langoni. "kwa sababu alikuwa amefunika kichwa chake na kukaa mahali makahaba hukaa mara kwa mara"

Akamwendea kando ya njia

Tamari alikuwa amekaa kando ya njia. "Alikwenda mahali alipokuwa amekaa kando na njia"

Njoo

"Njoo kwangu" au "Njoo sasa"

Yuda alipomwona

"Yuda alipomwona Tamari"

mkwewe

mkwewe - "mke wa mwanawe"

Genesis 38:17

kutoka kwa kundi

"kutoka kwa kundi la mbuzi wangu"

Mhuri wako na mshipi ... fimbo

"Mhuri" ni sawa na sarafu yenye mchoro uliochongwa juu yake, unaotumika kuchapa nta iliyoyeyushwa. "Mshipi" uliwekwa katika mhuri ili kwamba mmiliki angeweza kuvaa shingoni mwake. Fimbo ilikuwa mti mrefu wa mbao uliosaidia kutembea juu ya ardhi ngumu.

Akawa na uja uzito wake

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "alimsababisha aweze kupata mimba"

Genesis 38:19

ushungi

kitambaa chembamba sana kinachotumika kufunika kichwa na uso wa mwanamke.

vazi la ujane wake

"ambayo wajane huvaa"

kutoka kundini

"kutoka katika kundi lake"

Mwadulami

"Adulami" ni jina la kijiji ambapo Hiramu aliishi.

aichukue rehani

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "chukua rehani"

kutoka katika mkono wa mwanamke

Hapa "mkono" unasisitiza ya kwamba vilikuwa katika umiliki wake. Mkono wa mwanamke una maana ya mwanamke. "kutoka kwa mwanamke"

Genesis 38:21

Mwadulami

"Adulami" ni jina la kijiji ambapo Hiramu aliishi.

watu wa sehemu

"baadhi ya wanamume ambao waliishi pale"

kahaba wa kidini

"kahaba aliyetumika katika hekalu"

Enaimu

Hili ni jina la mahali.

tusije tukaaibika

Watu wangekuja kugundua kilichotokea wangemkejeli Yuda na kumcheka. Hii inaweza kuwekwa wazi na kusemwa katika hali ya kutenda. "la sivyo watu watatucheka wakigundua kilichotokea"

Genesis 38:24

Ikawa

Msemo huu unatumika kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

Yuda akaambiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mtu akamwambia Yuda"

Tamari mkweo

mkweo - "Tamari, mke wa mwana wako mkubwa"

yeye ni mjamzito kwa tendo hilo

Hapa neno la "hilo" lina maana ya "ukahaba" alioufanya. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "limemfanya aweze kuwa na mimba" au "ana mimba"

Mleteni hapa

"Mleteni nje"

ili achomwe

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "tutamchoma mpaka kufa"

Alipoletwa nje

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Walipomleta nje"

mkwewe

mkwewe - "baba wa mume wake"

mhuri huu na mshipi na fimbo

"Mhuri" ni sawa na sarafu yenye mchoro uliochongwa juu yake, unaotumika kuchapa nta iliyoyeyushwa. "Mshipi" uliwekwa katika mhuri ili kwamba mmiliki angeweza kuvaa shingoni mwake. Fimbo ilikuwa mti mrefu wa mbao uliosaidia kutembea juu ya ardhi ngumu.

Shela

Haya ni majina ya wana wa Yuda.

Genesis 38:27

Muda ukafika

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

tazama

Neno "tazama" linatuamsha kwa mshtuko ya kwamba Tamari alikuwa amebeba mapacha, ambayo haikujulikana awali.

Muda wake wa kujifungua ukafika

Msemo huu "ukafika" unaweka alama kwa tukio muhimu katika simulizi.

mmoja akatoa mkono

"mmoja wa watoto akatoa mkono wake nje"

mkunga

Huyu ni mtu ambaye humsaidia mwanamke anayezaa mtoto.

kitambaa cha rangi ya zambarau

"kitambaa cha rangi nyekundu iliyoiva"

katika mkono wake

"kuzunguka kifundo cha mkono wake"

Genesis 38:29

Ikawa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

tazama

Neno "tazama" hapa linatuamsha kuvuta nadhari kwa habari ya kushangaza inayofuata.

Umetokaje

Hii inaonyesha mshangao wa mkunga kuona mtoto wa pili akitoka kwanza. "Kwa hiyo hivi ndivyo unavyojitokeza kwanza!" au "Umejitokeza nje kwanza!"

akaitwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "akamuita"

Peresi

Hili ni jina la mtoto wa kiume. "Jina la Peresi lina maana ya "kuvunja nje".

Zera

Hili ni jina la mtoto wa kiume. "Jina la Zera lina maana ya "kitambaa cha rangi nyekundu".

Genesis 39

Genesis 39:1

Yusufu akaletwa chini Misri

Kusafiri kwenda Misri inasemekana mara kwa mara kama "chini" tofauti na kwenda "juu" katika nchi ya ahadi. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Muishmaeli alimchukua Yusufu mpaka Misri"

Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu

Hii ina maana ya kwamba Yahwe alimsaidia Yusufu na alikuwa pamoja naye mara zote. "Yahwe alimuongoza Yusufu na kumsaidia"

Aliishi katika nyumba

Hapa mwandishi anazungumzia kufanya kazi ndani ya nyumba ya bwana wake kana kwamba alikuwa akiishi ndani ya nyumba ya bwana wake. Watumishi wanaoaminiwa pekee waliruhusiwa kufanya kazi ndani ya nyumba ya bwana wao. "alifanya kazi ndani ya nyumba".

Mmisri bwana wake

Yusufu sasa alikuwa mtumwa wa Potifa.

Genesis 39:3

Bwana wake akaona kwamba Yahwe alikuwa pamoja naye

Hii ina maana ya kwamba bwana wake aliona jinsi Yahwe alivyokuwa akimsaidia Yusufu. "Bwana wake aliona ya kwamba Yahwe alikuwa akimsaidia Yusufu"

kwamba Yahwe alifanikisha kila kitu alichokifanya

"Yahwe alisababisha kila kitu alichofanya Yusufu kufanikiwa"

Yusufu akapata kibali machoni pake

"Kupata kibali" ina maana ya kukubalika na mtu. Nomino ya "machoni pake" ina maana ya maoni ya mtu. Maana zaweza kuwa 1) "Potifa alifurahishwa na Yusufu" au 2) "Yahwe alifurahishwa na Yusufu"

Akamtumikia Potifa

Hii ina maana ya kwamba alikuwa mtumishi wa binafsi wa Potifa.

Potifa akamfanya msimamizi juu ya nyumba yake, na kila alichokimiliki

"Potifa alimweka Yusufu kusimamia nyumba yake na kila kitu kilichokuwa cha Potifa"

akakiweka chini ya uangalizi wake

Pale ambapo kitu "kinakuwa chini ya uangalizi wa mtu" ina maana ya kwamba mtu anawajibika na utunzanji na uhifadhi wake. "alimfanya Yusufu kutunza"

Genesis 39:5

Ikawa alipomfanya

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

alipomfanya msimamizi juu ya nyumba yake na juu ya kila kitu alichomiliki

"Potifa alimweka Yusufu kuwa msimamizi juu ya nyumba yake na juu ya kila kitu alichomiliki"

Baraka

Hapa "baraka" ina maana ya kusababisha mema na yenye manufaa kutokea kwa mtu au kitu kinachobarikiwa.

Baraka za Yahwe zilikuwa juu ya

Hapa mwandishi anazungumzia baraka ambayo Yahwe alitoa kana kwamba ilikuwa mfuniko wa kihalisia uliofunika kitu. "Yahwe alibariki"

kila kitu alichokuwa nacho Potifa nyumbani na shambani

Hii ina maana ya nyumba na nafaka na mifugo yake. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Nyumba ya Potifa na nafaka na mifugo yake yote"

Potifa akaweka kila alichokuwa nacho chini ya uangalizi wa Yusufu

Kitu kinachokuwa "chini ya uangalizi wa mtu" ina maana ya kwamba mtu huyo anawajibika kutunza na kulinda. "Kwa hiyo Potifa alimweka Yusufu kuwa mwangalizi wa kila kitu ambacho alikuwa nacho"

Hakuwa na haja ya kufikiri juu ya lolote isipokuwa chakula alichokula tu.

Hakuhitaji kuwaza juu ya jambo lolote katika nyumba yake; alipaswa kufanya maamuzi juu ya kile alichotaka kula. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya chanya. "Potifa alitakiwa kuwaza kuhusu kile alichotaka kula tu. Hakuhitaji kuwaza juu ya kitu kingine ndani ya nyumba yake"

Basi

Neno "basi" linaweka alama ya pumziko katika simulizi ambapo mwandishi anatoa taarifa ya nyuma kuhusu Yusufu.

mzuri na wa kuvutia

Maneno haya mawili yana maana moja. Yanalenga uzuri wa muenekano wa Yusufu. Yawezekana alikuwa mwenye sura nzuri na mwenye nguvu. "mwenye sura nzuri na nguvu"

Genesis 39:7

Ikawa baada ya hayo

"Na kwa hiyo". Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya tukio jipya katika simulizi.

Tazama

"Sikia". Yusufu anatumia neno hili kuvuta nadhari ya mke wa Potifa.

bwana wangu haangalii chochote nikifanyacho nyumbani

"bwana wangu hajishughulishi juu ya nyumba yake napokuwa msimamizi." Hii inaweza kuandikwa katika hali ya chanya. "bwana wangu ananiamini na nyumba yake"

ameweka kila kitu anachokimiliki chini ya uangalizi wangu

Kitu kinachokuwa "chini ya uangalizi wa mtu" ina maana ya kwamba mtu huyo anawajibika kutunza na kulinda. "Kwa hiyo Potifa alimweka Yusufu kuwa mwangalizi wa kila kitu ambacho alikuwa nacho"

Hakuna mtu aliye mkuu katika nyumba hii kuliko mimi

Hapa mwandishi anazungumzia juu ya mamlaka kana kwamba yalikuwa ukubwa. "Nina mamlaka katika nyumba hii kuliko mtu yeyote yule"

Hajanizuia chochote isipokuwa wewe

Hii inaweza kusemwa katika hali ya chanya. "Amenipatia kila kitu isipokuwa wewe"

Ni kwa namna gani basi naweza kufanya uovu mkuu namna hii na kumtenda dhambi Mungu?

Yusufu anatumia swali kuonyesha msisitizo. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Hakika siwezi kufanya jambo hili ovu na kutedna dhambi dhidi ya Mungu"

Genesis 39:10

Alizungumza na Yusufu siku baada ya siku

Hii ina maana ya kwamba aliendelea kumuuliza kulala naye. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Aliendelea kumuuliza Yusufu alale naye"

kuwa naye

"kuwa karibu naye"

Ikawa

"Na kwa hiyo". Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya sehemu mpya ya tukio katika simulizi.

Hakuna mtu yeyote wa nyumbani

"hakuna mwanamume yeyote aliyefanya katika nyumba"

akakimbia, na kutoka nje

"na akakimbia nje haraka" au "na kwa haraka akakimbia nje ya nyumba"

Genesis 39:13

Ikawa ... akawaita

"Kisha ... akawaita." Msemo "ikawa kwamba" unatumika hapa kuweka alama kwa tukio lifuatalo katika simulizi.

na kwamba amekimbia nje

"na kwa haraka alikimbia nje ya nyumba"

watu wa nyumbani mwake

"wanamume waliofanya kazi katika nyumba yake"

Tazama

"Sikiliza". Mke wa Potifa anatumia neno hili kuvuta nadhari ya watumishi wake.

Aliingia kulala nami

Hapa mke wa Potifa anamtuhumu Yusufu kwa kujaribu kumkamata na kulala naye.

Ikawa aliponisikia nikipiga kelele, akaniacha

"Ikawa aliponisikia nikipiga kelele, akaniacha". Msemo "ikawa kwamba" unatumika hapa kuweka alama kwa tukio lifuatalo la simulizi.

Genesis 39:16

bwana wake

"Bwana wa Yusufu." Hii ina maana ya Potifa.

Akamwambia maelelezo haya

"Alielezea namna hii"

uliyemleta kwetu

Neno hili "kwetu" ina maana ya Potifa, mke wake, na inamaanisha nyumba yake yote.

aliingia kunidhihaki

"alikuja ndani kunifanya mpumbavu". Hapa neno "dhihaki" ni tafisida ya "kumkamata na kulala naye". "alikuja nilipokuwepo na akajaribu kunilazimisha nilale naye"

Ikawa

"Kisha". Mke wa Potifa anatumiamsemo huu kuweka alama ya tukio linalofuata katika habari anayomwambia kuhusu Yusufu kujaribu kulala naye.

akakimbia nje

"alikimbia haraka nje ya nyumba"

Genesis 39:19

Ikawa

"Na kwa hiyo". Msemo huu unatumika kuweka alama ya tukio jipya katika simulizi.

bwana wake

"Bwana wake Yusufu". Hii ina maana ya Potifa. Taarifa hii inaweza kuwekwa wazi. "Bwana wake Yusufu, Potifa"

aliposikia maelezo aliyoambiwa na mkewe

"alimsikiliza mke wake akimuelezea kwake". Neno "wake" na "kwake" hapa yana maana ya Potifa.

alikasirika sana

"Potifa akawa na hasira sana"

mahali walipowekwa wafungwa wa mfalme

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mahali ambapo mfalme huweka wafungwa wake"

Akawa pale

"Yusufu alikaa pale"

Genesis 39:21

Lakini Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu

Hii ina maana ya namna Yahwe alivyomtunza Yusufu na kuwa mema kwake. "Lakini Yahwe alikuwa mwema kwa Yusufu" au "Lakini Yahwe alimtunza Yusufu"

Akampa kibali mbele ya mlinzi wa gereza

Hii ina maana Yahwe alisababisha mlinzi wa gereza kumkubali Yusufu na kumtendea wema. "Yahwe alisababisha mlinzi wa gereza kufurahishwa na Yusufu"

mlinzi wa gereza

"msimamizi wa gereza" au "mtu mwenye usamamizi na gereza"

akawaweka mikononi mwa Yusufu

Hapa "mkononi" unawakilisha nguvu ya Yusufu au uaminifu. "kumweka Yusufu juu ya"

Chochote walichokifanya, kilikuwa chini ya uangalizi wa Yusufu

"Yusufu alikuwa mwanaglizi wa kila kitu walichofanya pale"

kwa sababu Yahwe alikuwa pamoja naye

Hii ina maana ya jinsi Yahwe alivyomsaidia Yusufu na kumuongoza. "kwa sababu Yahwe alimuongoza Yusufu"

Yahwe akafanikisha kila alichokifanya.

"Yahwe alisababisha kila kitu ambacho Yusufu alifanya kufanikiwa"

Genesis 40

Genesis 40:1

Ikawa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya tukio jipya la simulizi.

mnyweshaji

Huyu ni mtu ambaye huleta vinywaji kwa mfalme.

mwokaji wa mfalime

Huyu ni mtu ambaye alitengeneza chakula cha mfalme.

walimkosa bwana wao

"walimkwaza bwana wao"

maafsa wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji

""mnyweshaji kiongozi na mwokaji kiongozi"

Akawaweka katika lindo katika nyumba ya kapteni wa walinzi

"Akawaweka katika gereza liliokuwa katika nyumba ambayo ilisimamiwa na kapteni wa walinzi"

Akawaweka

Mflame hakuwaweka gerezani lakini aliwaamuru wafungwe. "Akafanya wawekwe" au "Aliamuru walinzi wake kuwaweka"

katika gereza lile Yusufu alimofungwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Hili lilikuwa gereza lile lile ambalo Yusufu alikuwemo" au "Hili lilikuwa gereza lile lile ambalo Potifa alimweka Yusufu"

Genesis 40:4

Walikaa kifungoni kwa muda fulani

"Walikaa kifungoni kwa muda mrefu"

Genesis 40:6

Yusufu akaja kwao

"Yusufu akaja kwa mnyweshaji na mwokaji"

Tazama, walikuwa na uzuni

Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Yusufu alishangazwa na kile alichokiona. "Alishangazwa kuona ya kuwa walikuwa na huzuni"

maafsa wa Farao waliokuwa pamoja naye

Hii ina maana ya mnyweshaji na mwokaji"

kifungoni katika nyumba ya bwana wake

"Gerezani katika nyumba ya bwana wake". "Bwana wake" ina maana ya bwana wa Yusufu, kapteni wa walinzi.

Je tafsiri haitoki kwa Mungu?

Yusufu anatumia swali kuonyesha msisitizo. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "tafsiri ni za Mungu!" au "Ni Mungu ambaye anaweza kusema maana ya ndoto!"

Niambieni, tafadhari

Yusufu anawaomba wamumbie ndoto zao. "Tafadhali niambieni ndoto"

Genesis 40:9

Mkuu wa wanyweshaji

Mtu muhimu zaidi ambaye huleta vinywaji kwa mfalme.

Katika ndoto yangu, tazama, kulikuwa na mzabibu mbele yangu

"Katika ndoto yangu, tazama, kulikuwa na mzabibu mbele yangu!" Mnyweshaji anatumia neno "tazama" hapa kuonyesha ya kwamba alishangazwa kwa kile alichokiona katika ndoto yake na kumuamsha Yusufu avute nadhari.

kuzaa vichala vya zabibu

"vichala vyake vikaiva kuwa zabibu"

kuzikamua

Hii ina maana ya kwamba alikamua juisi kutoka kwao. "akakamua juisi kutoka kwao"

Genesis 40:12

Tafsiri yake ni hii

"Hivi ndivyo ndoto inavyomaanisha"

Yale matawi matatu ni siku tatu

"Matawi matatu yanawakilisha siku tatu"

Ndani ya siku tatu

"Katika siku tatu zaidi"

atakiinua kichwa chako

Hapa Yusufu anaongea na Farao kumuachia mnyweshaji kutoka gerezani kana kwamba Farao alisababisha yeye kuinua kichwa chake. "atakuachia kutoka gerezani"

kukurudisha katika nafasi yako

"atakurudishia kazi yako"

kama ulivyokuwa

Maneno ambayo hayapo yanaweza kuongezwa. "kama ulivyofanya ulipokuwa"

Genesis 40:14

unionesha wema

"na tafadhali unioneshe wema kwangu"

Unitaje kwa Farao na kuniondoa hapa gerezani

Yusufu ana maana ya mnyweshaji kumwambia Farao juu yake ili kwamba Farao amfungulie kutoka gerezani. "Nisaidie kutoka katika gereza hili kwa kumwambia Farao juu yangu"

Maana hakika nilitekwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Maana hakika watu walinichukua" au "Maana hakika Waishmaeli walinichukua"

nchi ya Waebrania

"nchi ambayo Waebrania huishi"

hapa sijafanya chochote kinachonipasa niwekwe gerezani

"na pia nilipokuwa hapa Misri, sijafanya jambo lolote ambalo nastahili kuwekwa gerezani"

Genesis 40:16

Mkuu wa waokaji

Hii ina maana ya mtu kiongozi aliyetengeneza chakula cha mfalme.

Mimi pia niliota ndoto, na

"Mimi pia nilipata ndoto, na ndani ya ndoto yangu"

tazama, vikapu vitatu vya mikate vilikuwa juu ya kichwa changu

"kulikuwa na vikapu vitatu vya mikate juu ya kichwa changu!" Mwokaji anatumia neno "tazama" hapa kuonyesha ya kwamba alishangazwa kwa kile alichokiona ndani ya ndoto yake na kumuamsha Yusufu kuvuta nadhari.

bidhaa ya kuokwa kwa Farao

"alioka vyakula kwa ajili ya Farao"

Genesis 40:18

Tafsiri ni hii

"Hii ndio maana ya ndoto"

Vikapu vitatu ni siku tatu

"Vikapu vitatu vinawakilisha siku tatu"

atakiinua kichwa chako kutoka kwako

Yusufu pia alitumia msemo huu "atainua kichwa chako" alipoongea kwa mnyweshaji katika 40:12. Hapa ina maana tofauti. Maana zaweza kuwa 1) "atainua kichwa chako na kuweka kamba katika shingo yako" au 2) "atainua kichwa chako kukikata"

mwili

Hapa "mwili" una maana ya sehemu laini katika mwili wa mtu.

Genesis 40:20

Ikawa

"Hapo baadae, katika siku ya tatu". msemo "ikawa" unatumika hapa kuweka alama kwa tukio jipya katika simulizi.

Akafanya sherehe

"Akawa na sherehe"

mkuu wa wanyweshaji

Huyu alikuwa mtu kiongozi ambaye aliandaa na kuhudumia vinywaji kwa mfalme.

mkuu wa waokaji

Huyu alikuwa mtu kiongozi ambaye aliandaa chakula kwa ajili ya mfalme.

Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika majukumu yake

"majukumu" wa mkuu wa wanyweshaji una maana ya kazi yake kama mkuu wa manyweshaji. "Alimrudishia mkuu wa wanyweshaji kazi yake"

Lakini akamtundika mkuu wa waokaji

Farao hakumnyonga mwokaji yeye binafsi, ila aliaamuru anyongwe. "Lakini aliamuru mkuu wa waokaji anyongwe" au "Lakini aliamuru walinzi wake kumnyonga mkuu wa waokaji"

kama Yusufu alivyokuwa amewatafsiria

Hii ina maana ya pale ambapo Yusufu alitafsiri ndoto zao. "kama vile Yusufu alivyosema kingetokea pale alipotafsiri ndoto za wanamume wale wawili"

Genesis 41

Genesis 41:1

Ikawa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

mwishoni mwa miaka miwili mizima

Miaka miwili ilipita baada ya Yusufu kutafsiri kwa usahihi ndoto za mnyweshaji wa Farao na mwokaji, ambao walikuwa gerezani pamoja na Yusufu.

Tazama, alikuwa amesimama

Neno "tazama" hapa linaweka alama ya mwanzo wa tukio jipya katika simulizi kuu.

amesimama

"Farao alikuwa amesimama"

Tazama

"Ghafla". Neno la "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Farao alishangazwa kwa kile alichokiona.

wakupendeza na wanene

"wenye afya na wanene"

wakajilisha katika nyasi

"walikuwa wakila nyasi kando kando ya mto"

nyasi

nyasi ndefu, nyembamba ambazo huota katika maeneo ya unyevunyevu

Tazama, ng'ombe wengine saba

Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Farao alishangazwa tena kwa kile alichokiona.

wasiopendeza na wamekondeana

"wagonjwa na wembamba"

ukingoni mwa mto

"kando kando ya mto" au "kando ya mto". Hii ni sehemu ya juu ya ardhi pembeni mwa mto.

Genesis 41:4

wasiopendeza na waliokonda

"dhaifu na nyembamba"

wanapendeza na walionenepa

"yenye afya na iliyolishwa vizuri"

akaamka

"aliamshwa"

mara ya pili

Neno "mara ya pili" ni mpangilio wa namba. "tena"

Tazama, masuke saba

Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Farao alishangazwa kwa kile alichokiona.

masuke ya nafaka

Vichwa ni sehemu ya mmea wa mahindi ambao mbegu huota.

yalichipua katika mche mmoja

"yaliota katika shina moja" Shina ni sehemu nene au ndefu ya mmea.

katika mche mmoja, mema na mazuri

"katika mche mmoja na ilikuwa yenye afya na nzuri"

membamba na yaliyokaushwa na upepo wa mashariki

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambayo ilikuwa nyembamba na kuchomwa kwa sababu ya upepo wa joto kutoka mashariki"

upepo wa mashariki

Upepo kutoka mashariki ulivuma kutoka jangwani. Joto la upepo wa mashariki mara kwa mara ulikuwa wenye uharibifu.

yakachipua

"yaliota" au "kukua"

Genesis 41:7

Masuke membamba

Maneno "ya mbegu" inaeleweka. "Vichwa vyembamba vya mbegu"

yakayameza

"wakala". Farao anaota ya kwamba mahindi ambayo hayana afya yanaweza kumeza mahindi yenye afya kama mtu anavyokula chakula.

masuke saba mema yote

"vichwa vyenye afya na vizuri"

akaamka

"aliamshwa"

tazama

Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Farao alishangazwa na kile alichokiona.

ilikuwa ni ndoto

"alikuwa akiota"

Ikawa

Msemo huu unatumika kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

roho yake ikafadhaika

Hapa neno "roho" lina maana ya utu wake na hisia zake. "alifadhaishwa ndani ya utu wake" au "alisononeshwa"

Akatuma na kuwaita

Inaeleweka ya kwamba aliwatuma watumishi. "Alituma watumishi wake kuwaita" au "Aliwatuma watumishi wake na kuwaita"

waganga na wenye hekima wote wa Misri

Wafalme wa zamani na watawala walitumia wachawi na wenye hekima kama washauri.

Genesis 41:9

mkuu wa wanyweshaji

Mtu muhimu zaidi ambaye huleta vinywaji kwa mfalme.

Leo ninayafikiri makosa yangu

Neno "Leo" linatumika kuonyesha msisitizo. "makosa" yake ni kwamba alitakiwa kumwambia Farao kitu mapema zaidi lakini hakufanya hivyo. "Nimegundua ya kwamba nimesahau kukuambia jambo"

Farao aliwakasirikia

Mnyweshaji ana maana ya Farao katika mtu wa utatu. Hii ni njia ya kawaida ya mtu mwenye nguvu ya chini kuzungumza na mtu mwenye nguvu zaidi. "Wewe, Farao, ulikuwa na hasira"

watumishi wake

Hapa "wake" ina maana ya Farao. Hapa "watumishi" ina maana ya mnyweshaji na mkuu wa waokaji. "na sisi, watumishi wako"

kuniweka kifungoni katika nyumba ya kapteni wa walinzi, mkuu wa waokaji na mimi

"kuniweka mkuu wa waokaji na mimi gerezani ambapo kapteni wa walinzi alikuwa msimamizi" hapa "nyumba" ina maana ya gereza.

kapteni wa walinzi

Askari msimamizi wa walinzi wa kifalme.

mkuu wa waokaji

Mtu muhimu zaidi ambaye alitengeneza chakula kwa ajili ya mfalme.

Tuliota ndoto usiku huo mmoja, yeye na mimi

"Usiku mmoja wote wawili tulipata ndoto"

Tuliota

Hapa "Tuliota" ina maana ya mkuu wa mnyweshaji na mkuu wa waokaji.

Kila mmoja aliota kwa kadili ya tafsiri yake

"Ndoto zetu zilikuwa na maana tofauti"

Genesis 41:12

Taarifa ya Jumla:

Mkuu wa wanyweshaji anaendelea kuzungumza na Farao.

Pamoja nasi kulikuwa

"Gerezani kulikuwa na mkuu wa waokaji na mimi"

kapteni wa walinzi

Askari msimamizi wa walinzi wa kifalme.

Tulimwambia na akatutafsiria ndoto zetu

"Tulimwambia ndoto zetu na kutueleza maana zake kwetu"

Alitutafsiria kila mmoja wetu kulingana na ndoto yake

Hapa "yake" ina maana ya mnyweshaji na muokaji mmoja mmoja, sio kwa yule anayetafsiri ile ndoto. "Alifafanua kile kilichokuwa kinakuja kutokea kwetu wawili"

Ikawa

Msemo huu unatumika kuweka alama ya tukio muhimu la simulizi.

alivyotutafsiria, ndivyo ilivyokuwa

"alivyotafsiri kuhusu ndoto ndivyo kilichotokea hapo baadae"

Farao alinirudisha katika nafasi yangu

Hapa mnyweshaji anatumia jina la Farao katika kuongea naye kama njia ya kumheshimu yeye. "Uliniruhusu nirudi katika kazi yangu!"

yule mwingine

"mkuu wa waokaji"

akamtundika

Hapa "akamtundika" ina maana ya Farao. Na ina maana ya maaskari ambao Farao aliwaamuru kumnyonga mkuu wa waokaji. "uliwaamuru maaskari wako kumnyonga"

Genesis 41:14

Farao alipotuma na kumwita

Inaeleweka ya kwamba Farao aliwatuma watumishi. "Farao aliwatuma watumishi wake kumfuata Yusufu"

wakamtoa gerezani

"nje ya gereza" au "nje ya ile jela"

Akajinyoa mwenyewe

Ilikuwa utaratibu wa kawaida kunyoa ndevu na nywele za kichwani mnapoandaa kwenda mbele ya Farao.

akaingia kwa Farao

Hapa "akaingia" inaweza kuwekwa kama "kwenda". "alikwenda mbele ya Farao"

hakuna wa kuitafsiri

"hakuna awezaye kueleza maana yake"

unaweza kuitafsiri

"unaweza kuelezea maana yake"

Siyo katika mimi

"Mimi siye ambaye naweza kueleza maana yake"

Mungu atamjibu Farao kwa fadhila zake

"Mungu atamjibu Farao kwa fadhila"

Genesis 41:17

tazama, nilisimama

Farao anatumia neno "tazama" kumfanya Yusufu kuvuta nadhari kwa habari ya kushangaza.

ukingo wa mto Nile

Hii ni ardhi iliyo juuzaidi katika ukingo wa Mto Nile.

Tazama, ng'ombe saba

Farao anatumia neno "tazama" kumfanya Yusufu kuvuta nadhari kwa habari ya kushangaza.

wanene na wakuvutia

"waliolishwa vizuri na wenye afya"

wakajilisha katika nyasi

"walikuwa wakila nyasi kando ya mto"

Genesis 41:19

Tazama, ng'ombe wengine saba

Farao anatumia neno "tazama" kumfanya Yusufu kuvuta nadhari kwa habari ya kushangaza.

wabaya, na wembamba

"dhaifu, na wembamba"

wabaya kama hao

Nomino inayojitegemea ya "kutotamanika" inaweza kutafsiriwa kwa kivumishi. "ng'ombe wabaya sana" au "ng'ombe wasiofaa kabisa"

ng'ombe wanene

"ng'ombe waliolishwa vizuri"

haikujulikana kama walikuwa wamewala

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "hakuna aliyeweza kutambua ya kwamba ng'ombe wembamba waliwameza ng'ombe wanene"

Genesis 41:22

Taarifa ya Jumla:

Farao anaendelea kumwambia Yusufu ndoto zake.

Niliona katika ndoto yangu

Hii inaanza sehemu inayofuata ya ndoto ya Farao baadaya kuamka na kurudi kulala. "Kisha nikaota tena"

tazama, masuke saba

Farao anatumia neno "tazama" kumfanya Yusufu kuvuta nadhari kwa habari ya kushangaza.

masuke saba

Maneno "ya masuke" inaeleweka. "masuke saba"

yakatoka katika bua moja

"yakatoka katika bua moja". Shina ni sehemu ya mmea mnene na mrefu.

Tazama, masuke saba zaidi

Farao anatumia neno "tazama" kumfanya Yusufu kuvuta nadhari kwa habari ya kushangaza.

yaliyonyauka, membamba na yamekaushwa na upepo wa mashariki

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "yalinyauka, yamekaushwa, myembamba, na kukaushwa na jua kwa sababu ya upepo wa joto kutoka mashariki"

kunyauka

"kuoza" au "nyauka"

upepo wa mashariki

Upepo unaotoka kutoka mashariki ulivuma kutoka jangwani. Joto la upepo wa mashariki mara kwa mara ulikuwa uharibifu kwa mazao.

yakachipua

"yakaota" au "kustawi"

masuke membamba

Maneno "ya masuke" yanaeleweka. "masuke membamba"

yakayameza

"yakala". Farao anaota ya kwamba mahindi dhaifu yanaweza kumeza mahindi yenye afya kama mtu anavyokula chakula.

hakuna aliyeweza

"hapakuwa na mtu mmoja ambaye" au "hakuna kati yao ambaye"

Genesis 41:25

Ndoto za Farao zinafanana

Inadokezwa ya kwamba maana zinafanana. "Ndoto zote mbili zina maana moja"

Mungu amemwambia Farao kuhusu jambo analokwenda kulifanya

Yusufu anazungumza na Farao katika utatu. Kwa njia hii anaonyesha heshima. Inaweza kuwekwa katika upili wa mtu. "Mungu anakuonyesha kile atakachofanya hivi karibuni"

masuke saba mema

Maneno ya "masuke" yanaeleweka. "masuke saba mazuri"

Genesis 41:27

Taarifa ya Jumla

Yusufu anaendelea tafsiri yake kwa ndoto za Farao.

ng'ombe saba wembamba na wabaya

"ng'ombe wembamba na dhaifu"

masuke saba membamba yaliyokaushwa na upepo wa mashariki

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Masuke saba yaliyokaushwa na jua kwa sababu ya upepo wa joto kutoka mashariki"

Hilo ni jambo nililomwambia Farao ... nililomwambia Farao

Yusufu anazungumzia kwa Farao katika utatu. Hii ni njia ya kuonyesha heshima. Inaweza kuwekwa katika lugha ya upili. "Matukio haya yatatokea kama nilivyokuambia ... imefunuliwa kwako, Farao"

amemfunulia

"amefanya ijulikane"

Tazama

hii inatumika kuweka msisitizo kile ambacho Yusufu anachosema baadae. "Vuta nadhari kwa kile nachosema"

miaka saba yenye utele mwingi inakuja katika nchi yote ya Misri

Hii inazungumzia kuhusu miaka ya wingi kana kwamba muda ni kitu kinachosafiri na kufika mahali. "kutakuwa na miaka saba ambayo kutakuwa na chakula kingi katika nchi yote ya Misri"

Genesis 41:30

Taarifa ya Jumla

Yusufu anaendelea tafsiri ya ndoto za Farao.

miaka saba ya njaa itakuja baada yake

Hii inazungumzia kuhusu miaka saba ya njaa kana kwamba miaka ni kitu kinachosafiri na kufika mahali. "Kisha kutakuwa na miaka saba ambayo kutakuwa na chakula kichache"

wingi wote katika nchi ya Misri utasahaulika ... na njaa itaiaribu nchi. Wingi hautakumbukwa ... kwa sababu ya njaa itakayofuata

Yusufu anaonyesha wazo kwa njia mbili kusisitiza umuhimu wake.

wingi wote katika nchi ya Misri utasahaulika

Hapa "nchi" ina maana ya watu. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "watu wa Misri watasahau kuhusu miaka saba ambayo kulikuwa na chakula kingi"

itaiaribu nchi.

Hapa "nchi" ina maana ya udongo, watu, na nchi nzima.

kwa sababu ya njaa itakayofuata

Hii inazungumzia kuhusu njaa kana kwamba ilikuwa kitu kinachosafiri na kufuata nyuma ya kitu kingine. "kwa sababu ya muda wa njaa utakaotokea hapo baadae"

Kwamba ndoto ilijirudia kwa Farao sababu ni kwamba jambo hili limeanzishwa na Mungu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu alikupatia ndoto mbili kukuonyesha ya kwamba hakika atasababisha mambo haya kutokea"

Genesis 41:33

Maelezo ya Jumla:

Yusufu anaendelea kuongea na Farao.

Basi

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

Farao atafute

Yusufu anazungumza na Farao katika lugha ya utatu. Hii ni namna ya kuonyesha heshima. Inaweza kuwekwa katika lugha ya upili. "Wewe, Farao, unapaswa kutafuta"

kumweka juu ya nchi ya Misri

Msemo "kumweka juu" una maana ya kumpatia mtu mamlaka. "kumpatia mamlaka juu ya ufalme wa Misri" au "kumpa usimamizi juu ya ufalme wa Misri"

nchi ya Misri

Hapa "nchi" ina maana ya watu wote na kila kitu ndani ya Misri.

Na wachukue sehemu ya tano ya mazao ya Misri

Neno "tano" ni sehemu. "Na wagawanishe nafaka ya Misri katika sehemu tano za kufanana, kisha wachukue moja ya sehemu hizo"

katika miaka saba ya shibe

"katika miaka saba ambayo kutakuwa na wingi wa chakula"

Genesis 41:35

Maelezo ya Jumla

Yusufu anaendelea kumshauri Farao.

Na wakusanye

"Waruhusu wageni kukusanya"

cha hii miaka myema ijayo

Hii inazungumzia miaka kana kwamba ni kitu kinachosafiri na kufikia mahali. "katika miaka mizuri ambayo hivi karibuni itatokea"

kuitunza nafaka chini ya mamlaka ya Farao

Msemo "chini ya mamlaka ya Farao" ina maana ya Farao kuwapa mamlaka. "tumia mamlaka ya Farao kutunza nafaka"

Wakiifadhi

Hifadhi nafaka kwa muda wakati ambao kuna chakula kidogo. "Wasimamizi wanatakiwa kuwaacha walinzi pale kulinda nafaka"

Chakula kitakuwa akiba ya nchi

Hapa "nchi" ina maana ya watu. "Chakula hiki kitakuwa kwa ajili ya watu"

Kwa njia hii nchi haitaaribiwa na njaa

Hapa "nchi" ina maana ya watu. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kwa njia hii watu hawatashinda njaa kipindi cha njaa"

Genesis 41:37

Ushauri huu ukawa mwema machoni pa Farao na machoni pa watumishi wake wote

Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo ya mtu. "Farao na watumishi wake walifikiri huu ulikuwa mpango mzuri"

watumishi wake

Hii ina maana ya watumishi wa Farao.

mtu kama huyu

"mtu kama vile Yusufu alivyomfafanua"

ambaye ndani yake kuna Roho wa Mungu

"ambaye Roho wa Mungu anaishi ndani mwake"

Genesis 41:39

hakuna mtu mwenye ufahamu

"hakuna mtu mwenye uwezo wa kufanya maamuzi"

Utakuwa juu ya nyumba yangu

Hapa "nyumba" ina maana ya kasri ya mfalme na watu ndani ya kasri. Msemo "utakuwa juu" una maana ya Yusufu kuwa na mamlaka juu ya. "Utakuwa na mamlaka juu ya kila mtu ndani ya kasri yangu"

watu wangu watatawaliwa kwa kadili ya neno lako

Hapa "neno" lina maana ya amri au kilichosemwa. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "utatawala juu ya watu wangu na wao watafanya kile unachoamuru"

kiti cha enzi peke yake

Hapa "enzi" ina maana ya utawala wa Farao kama mfalme. "Katika nafasi yangu pekee kama mfalme"

Tazama, nimekuweka

Neno "Tazama" linaweka msisitizo kwa kile Farao anachosema baadae. "Tazama, nimekuweka"

nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri

Msemo "nimekuweka juu" una maana ya kutoa mamlaka. Hapa "nchi" ina maana ya watu. "Nimekuweka kuwa na mamlaka ya kila mtu ndani ya Misri"

Genesis 41:42

Farao akavua pete yake ya mhuri ... mkufu wa dhahabu shingoni mwake

Matendo haya yote yanaashiria ya kwamba Farao anampatia Yusufu mamlaka kufanya kila kitu ambacho Yusufu alipanga.

pete ya mhuri

Pete hii ilikuwa na mhuri wa Mfalme uliochongwa juu yake. Hii ilimpatia Yusufu mamlaka na fedha iliyohitajika kutekeleza mipango yake.

mavazi ya kitani safi

"Kitani" ni kitambaa kilaini, kigumu kinachotengenezwa na mmea wa kitani.

Akataka apandishwe katika kibandawazi cha pili alichokuwa nacho

Tendo hili linadhihirisha wazi kwa watu ya kwamba Yusufu ni wa pili tu kutoka kwa Farao.

Pigeni magoti

"Inama chini na mheshimu Yusufu". Kupiga goti na kuinama chini ilikuwa ishara ya heshima na taadhima.

Farao akamweka juu ya nchi yote

Msemo "kukuweka juu" una maana ya kumpatia mamlaka. Hapa "nchi" ina maana ya watu. "Nimekupa mamlaka juu ya kila mmoja ndani ya Misri"

Genesis 41:44

Mimi ni Farao, mbali na wewe

Farao anasisitiza mamlaka yake. "Kama Farao, ninaamuru hivi mbali na wewe"

mbali na wewe, hakuna mtu atakayeinua mkono wake au mguu wake katika nchi ya Misri

Hapa "nchi" na "mguu" zina maana ya matendo ya mtu. "hakuna mtu ndani ya Misri ataweza kufanya kitu chochote bila ruhusa yako" au "kila mtu ndani ya Misri lazima akuombe ruhusa kabla hajafanya jambo lolote"

hakuna mtu

Hapa "mtu" ina maana ya binadamu kwa ujumla, iwe wa kiume au wakike.

Zafenathi Panea

Jina la Zafenathi Panea kina maana ya "mfunuaji wa siri"

Akampa Asenathi, binti wa Potifera kuhani wa On, kuwa mke wake

Makuhani wa Misri walikuwa tabaka la juu kabisa na upendeleo. Ndoa hii inaashiria nafasi ya Yusufu ya heshima na upendeleo.

Akampa Asenathi

"Asenathi" ni jina la mwanamke ambaye Farao alimpatia Yusufu kuwa mke wake.

binti wa Potifera

"Potifera" ni baba wa Asenathi.

kuhani wa Oni

Oni ni mji, ambao pia unajulikana kama Heliopolisi, ambao ulikuwa "Mji wa Jua" na makao ya kumuabudu mungu wa jua Ra.

Yusufu akaenda juu ya nchi yote ya Misri

Yusufu alisafiri katika nchi kusimamia maandalizi ya ujio wa ukame.

Genesis 41:46

umri wa miaka thelathini

"umri wa miaka 30"

aliposimama mbele ya Farao

Hapa "aliposimama" ina maana ya Yusufu kuanza kumtumikia Farao. "alipoanza kumtumikia Farao"

kwenda katika nchi yote ya Misri

Yusufu anakagua nchi anapoandaa kutekeleza mipango yake.

Katika miaka saba ya shibe

"Katika miaka mizuri saba"

nchi ilipozaa kwa wingi

"nchi ilizaa mavuno makubwa"

Genesis 41:48

Akakusanya ... kukiweka

Hapa "Akakusanya" ina maana ya watumishi wa Yusufu. "Yusufu aliwaamuru watumishi wake kukusanaya ... Wakaweka"

Yusufu akahifadhi nafaka kama mchanga wa bahari

Hii inalinganisha nafaka na mchanga wa bahari kuweka msisitizo wa idadi yake kubwa. "Nafaka ambayo Yusufu alihifadhi ilikuwa nyingi kama mchanga wa baharini.

Yusufu akahifadhi ... akaacha

Hapa "Yusufu" na "akahifadhi" ina maana ya watumishi wa Yusufu. "Yusufu aliwafanya watumishi wake wahifadhi ... wakaacha"

Genesis 41:50

Kabla miaka ya njaa kuingia

Hii inazungumzia kuhusu miaka saba kana kwamba ni kitu kinachosafiri na kuja kutulia mahali. "kabla ya miaka saba ya njaa kuanza"

Asenathi

"Asenathi" ni jina la mwanamke ambaye Faro alimpatia Yusufu kama mke wake.

binti wa Potifera

"Potifera" ni baba wa Asenathi.

kuhani wa Oni

Oni ni mji, ambao pia unajulikana kama Heliopolisi, ambao ulikuwa "Mji wa Jua" na makao ya kumuabudu mungu wa jua Ra.

Manase

"Jina la 'Manase' lina maana ya "kusababisha kusahau""

nyumba ya baba yake

Hii ina maana ya baba wa Yusufu Yakobo na familia yake.

Efraimu

"Jina la 'Efraimu' lina maana ya 'kuwa na uzao' au 'kupata watoto'"

amenipa uzao

Hapa "uzao" ina maana ya kufanikiwa au kupata watoto.

katika nchi ya mateso yangu

Nomino inayojitegemea "mateso" inaweza kuwekwa kama "nimeteseka". "katika nchi hii ambayo nimeteseka".

Genesis 41:53

katika nchi yote

Katika mataifa yanayozunguka mbele zaidi ya Misri, kujumuisha na nchi ya Kanaani.

lakini katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula

Inasemekana ya kwamba kulikuwa na chakula kwa sababu Yusufu aliwaamuru watu wake kuhifadhi chakula katika kipindi cha miaka saba mizuri.

Genesis 41:55

Nchi yote ya Misri ilipokuwa na njaa

Hapa "nchi" ina maana ya watu. "Ambapo Wamisri waliposhikwa na njaa"

Njaa ilikuwa juu ya uso wote wa nchi

Neno "uso" lina maana ya sehemu ya juu ya ardhi. "Njaa ilisambaa katika nchi yote"

Yusufu akafungua ghala zote na kuuza chakula kwa Wamisri

Hapa "Yusufu" ina maana ya watumishi wa Yusufu. "Yusufu aliwafanya watumishi wake kufungulia maghala yote na kuuza nafaka kwa Wamisri"

Dunia yote ilikuwa inakuja Misri

Hapa "dunia" ina maana ya watu kutoka maeneo yote. "Watu walikuwa wakija Misri kutoka maeneo yaliyozunguka"

katika dunia yote

"katika nchi yote". Inawezekana ya kwamba wafanyabiashara tofauti na mataifa ambayo yalikuwa sehemu ya njia za biashara na Misri yalioguswa na ukame walikuja Misri kwa ajili ya nafaka.

Genesis 42

Genesis 42:1

Basi Yakobo akafahamu

Neno "basi" inaweka alama ya sehemu mpya ya simulizi.

Kwa nini mnatazamana?

Yakobo anatumia swali kukaripia watoto wake kwa kutofanya kitu chochote kuhusu nafaka. "Msikae hapo tu!"

Shukeni huko ... chini

Ilikuwa kawaida kuzungumza kuhusu kwenda kutoka Kaanani mpaka Misri kama kwenda "chini"

kutoka Misri

Hapa "Misri" ina maana ya watu kuuza nafaka. "kutoka kwa wale wauzao nafaka ndani ya Misri"

Benjamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumtuma

Benyamini na Yusufu walikuwa na baba mmoja na mama. Yakobo hakutaka kuthubutu kumtuma mwanawe wa mwisho wa Raheli.

Genesis 42:5

Wana wa Israeli wakaja kununua miongoni mwao waliokuja

Neno "wakaja" inaweza kutafsiriwa kama "kwenda". Pia, maneno "nafaka" na "Misri" inaeleweka. "Wana wa Israeli walikwenda kununua nafaka pamoja na watu wengine waliokwenda Misri"

Basi Yusufu

"Basi" inaweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa maelezo ya nyuma kuhusu Yusufu.

juu ya nchi

Hapa "nchi" ina maana ya Misri. "juu ya Misri"

watu wote wa nchi

Hapa "nchi" inajumlisha Misri na nchi zingine zinayoizunguka. "watu wote wa mataifa yote waliokuja kununua nafaka"

Ndugu zake Yusufu wakaja

Hapa "wakaja" inaweza kutafsiriwa kama "walikwenda"

kumwinamia na nyuso zao hata chini

Hii ni njia ya kuonyesha heshima.

Genesis 42:7

Yusufu akawaona ndugu zake na kuwatambua

"Yusufu alipowaona ndugu zake, aliwatambua"

alijibadili kwao

"alijifanya kana kwamba hakuwa kaka yao" au "hakuwafahamisha ya kwamba alikuwa kaka yao"

Mmetoka wapi?

Hili halikuwa swali la balagha ingawa Yusufu alijua jibu. Ilikuwa sehemu ya maamuzi yake kuficha utambulisho wake kwa ndugu zake.

Genesis 42:9

Ninyi ni wapelelezi

Wapelelezi ni watu ambao kwa siri hujaribu kupata taarifa kuhusu nchi ili kuisaidia nchi nyingine.

Mmekuja kuona sehemu za nchi

Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "Mmekuja kujua ni wapi hatulindi nchi yetu ili kwamba muweze kutushambulia"

bwana wangu

Hii ni njia ya kuonyesha heshima kwa mtu.

Watumishi wako wamekuja

Ndugu hawa wanajitambulisha kama "watumishi". Hii ni njia maalumu ya kuongea na mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi. "Sisi, watumishi wako, tumekuja" au "Tumekuja"

Genesis 42:12

Akawambia

"Yusufu akawaambia ndugu zake"

Hapana, mmekuja kuangalia sehemu za nchi

Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "Hapana, mmekuja kujua ni wapi hatujalinda nchi yetu ili kwamba muweze kutuvamia"

ndugu kumi na wawili

"ndugu 12"

Tazama, mdogo

"Tusikilize, mdogo". Neno "Tazama" linatumika kusisitiza kile walichosema baadae.

mdogo yupo na baba yetu leo hii

"kwa sasa ndugu yetu mdogo yupo na baba yetu"

Genesis 42:14

Ndivyo nilivyowambia; ninyi ni wapelelezi

"kama nilivyotangulia kusema, nyinyi ni wapelelezi"

Mtajaribiwa kwa njia hii

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Hivi ndivyo nitakavyowajaribu"

aishivyo Farao

Msemo huu unaashiria kiapo maalumu.

Mtumeni mmoja wenu amlete mdogo wenu

"Chagueni mmoja wenu kumfuata mdogo wenu"

Mtabaki gerezani

"Mliosalia mtabaki gerezani"

hata maneno yenu yatakapothibitishwa, kama kuna ukweli ndani yenu.

Hapa "maneno" ina maana ya kile alichosema. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ili kwamba niweze kujua kama mnaniambia ukweli"

kifungoni

"gerezani"

Genesis 42:18

Katika siku ya tatu

Neno "tatu" ni mpangilio wa namba."baada ya siku ya pili"

Fanyeni hivi nanyi mtaishi

Taarifa inayotambulika inaweza kuwekwa wazi. "Kama utafanya kile nilichosema, nitakuruhusu uishi"

ninamcha Mungu

Hii ina maana ya kumheshimu Mungu kwa dhati na kuonyesha heshima hiyo kwa kumtii yeye.

mmoja wenu atazuiliwa hapa gerezani

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "muache mmoja wa ndugu zako hapa gerezani"

lakini ninyi nendeni

Hapa "ninyi" ni wingi na ina maana ya ndugu wote ambao hawatakaa gerezani. "lakini ninyi mliosalia"

chukueni nafaka kwa ajili ya nyumba zenu

Hapa "nyumba" ina maana ya familia. "beba nafaka hadi nyumbani kusaidia familia zenu wakati wa njaa hii"

ili kwamba maneno yenu yathibitishwe

Hapa "maneno" yana maana ya kile kilichosemwa. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ili niweze kujua kile mnachosema ni kweli"

nanyi hamtakufa

Hii inaashiria ya kwamba Yusufu angewafanya maaskari wake kuwaua ndugu iwapo angetambua ya kwamba walikuwa wapelelezi.

Genesis 42:21

kwani tuliona tabu ya nafsi yake

Neno "nafsi" ina maana ya Yusufu. "kwa sababu tuliona jinsi gani Yusufu alivyotaabika" au "kwa sababu tuliona ya kwamba Yusufu aliteseka"

Kwa hiyo taabu hii imeturudia

Nomino inayojitegemea "taabu" inaweza kuwekwa kama kitenzi "kuteseka" "Ndio maana tunateseka hivi sasa"

Je sikuwambia, 'Msitende dhambi juu ya kijana,' lakini hamkusikia?

Rubeni anatumia swali kuwakaripia ndugu zake. "Niliwaambia kutomuumiza kijana, lakini hamkunisikiliza!"

Je sikuwambia, 'Msitende dhambi juu ya kijana'

Hii inaweza kuwa nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Je sikuwaambia msimtendee dhambi kijana" au "Niliwaambia msimdhuru kijana"

Basi, tazama

Hapa "basi" haimaanishi "katika muda huu" lakini yote maneno "Sasa" na "tazama" yanatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

damu yake inatakiwa juu yetu

Hapa "damu" ina maana ya kifo cha Yusufu. Ndugu zake walidhani Yusufu alikufa. Msemo "inatakiwa juu yetu" una maana wanatakiwa kuadhibiwa kwa kile walichokifanya. "tunapata kile tunachostahili kwa kifo chake" au"tunateseka kwa kumuua yeye"

Genesis 42:23

hawakuja ... mkalimani kati yao

Hii inabadilisha kutoka kwenye simulizi kuu kwenda kwenye taarifa ya nyuma ambayo inaelezea kwa nini ndugu walidhani Yusufu hakuweza kuwaelewa.

mkalimani

"Mkalimani" ni mtu ambaye hutafsiri kile mtu anazungumza katika lugha nyingine. Yusufu aliweka mkalimani kati yake na ndugu zake kufanya ionekane kana kwamba hakuzungumza lugha yake.

Akatoka kwao na kulia

Inasemekana ya kwamba Yusufu alilia kwa sababu alipatwa na hisia baada kusikia walichosema ndugu zake.

kuongea nao

Yusufu aliendelea kuzingumza katika lugha nyingine na kutumia mkalimani kuzungumza na ndugu zake.

kumfunga mbele ya macho yao

Hapa "macho" ina maana ya machoni mwao. "alimfunga machoni mwao" au "alimfunga huku wakitazama"

na kuwapa mahitaji

"kuwapatia mahitaji waliyohitaji"

Wakatendewa hivyo

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. Watumishi walifanya kwao kila kitu ambachoYusufu aliwaamuru"

Genesis 42:26

Mmoja wao alipofungua gunia lake ili kumlisha punda wao katika sehemu waliyokuwa, akaona pesa yake. Tazama, ilikuwa mdomoni mwa gunia lake

"Waliposimama mahali usiku huo, mmoja wa ndugu alifungua gunia lake kupata chakula kwa ajili ya punda wake. Ndani ya gunia akakuta fedha!"

Tazama

Neno "tazama" hapa linatuamsha kuvuta nadhari kwa taarifa inayoshangaza inayofuata.

Pesa yangu imerudishwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu amerudisha fedha yangu"

Tazama

"Tazama ndani ya gunia langu!"

Mioyo yao ikazimia

Kuwa na hofu inazungumziwa kana kwamba mioyo yao ilikuwa ikizama. Hapa "mioyo" ina maana ya ujasiri. "Wakawa na hofu sana"

Genesis 42:29

bwana wa nchi

"bwana wa Misri"

aliongea nasi kwa ukali

"aliongea kwa jazba"

kuwa wapelelezi

Wapelelezi ni watu ambao kwa siri hujaribu kupata taarifa kuhusu nchi ili kuisaidia nchi nyingine.

Tukamwambia, 'Tu watu wa kweli sisi. Sisi siyo wapelelezi. Tupo ndugu kumi na wawili, wana wa baba yetu. Mmoja hayupo hai tena ... nchi ya Kanaani

Hii ina nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Tulimwambia ya kwamba sisi ni watu waaminifu na sio wapelelezi. Tulisema kwamba tu ndugu kumi na wawili, wana wa baba yetu, na kwamba ndugu yetu hayupo hai tena ... nchi ya Kaanani"

Mmoja hayupo hai tena

Neno "ndugu" linaeleweka. "Ndugu mmoja hayupo hai tena"

mdogo yupo na baba yetu

Neno "ndugu" linaeleweka. "ndugu yetu mdogo yupo na baba yetu kwa sasa"

Genesis 42:33

bwana wa nchi

"bwana wa Misri"

chukueni chakula kwa ajili ya njaa katika nyumba zenu

Hapa "nyumba" ina maana ya "familia". "chukua nafaka isaidie familia yenu wakati wa njaa"

mwondoke

"nendeni nyumbani" au "ondokeni"

na mtafanya biashara katika nchi

"na nitawaruhusu mnunue na kuuza katika nchi hii"

Genesis 42:35

Ikawa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama kwa tukio muhimu katika simulizi.

tazama

"kwa mshangao wao". Neno "tazama" hapa inaonyesha ya kwamba ndugu walishangazwa kwa kile walichokiona.

Mmeniharibia watoto wangu

"umeninyima watoto wangu" au "umesababisha kupoteza watoto wangu wawili"

Mambo haya yote ni kunyume changu

"mambo haya yote yaliniumiza"

Genesis 42:37

Mweke mikononi mwangu

Hili ni ombi la Rubeni kumchukua Benyamini pamoja naye na kumtunza katika safari hiyo. "Niweke kama msimamizi juu yake" au "Niache nimtunze"

Mwanangu hatashuka pamoja nanyi

Ilikuwa kawaida kutumia msemo "kushuka" walipokuwa wakizungumzia safari ya Kaanani kuelekea Misri. "Mwanangu, Benyamini, hatakwenda nawe hadi Misri"

pamoja nanyi

Hapa "nanyi" ni wingi na ina maana ya wana wa yakobo wakubwa.

Kwani ndugu yake amekufa na yeye peke yake amebaki

Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "Kwa maana mke wangu, Raheli, alikuwa na watoto wawili pekee. Yusufu amekufa na Benyamini amebaki mwenyewe tu"

katika njia mnayoiendea

"utakapokuwa ukisafiri kwenda Misri na kurudi" au "utakapokuwa mbali". Hapa "njia" ina maana ya kusafiri.

ndipo mtakapozishusha mvi zangu kaburini kwa huzuni

"mtakapozishusha ... kuzimu" ni njia ya kusema watamsababisha afariki na kushuka kuzimu. Anatumia neno "chini" kwa sababu iliaminika kuzimi ni sehemu chini ya ardhi. "basi mtanisababisha, mtu mzee, kufariki na huzuni"

mvi zangu

Hii ina maana ya Yakobo na inasisitiza umri wake mkubwa. "mimi, mtu mzee"

Genesis 43

Genesis 43:1

Njaa ilikuwa kali katika nchi

Neno "Kaanani" linaeleweka. Taarifa hii inaweza kuwekwa wazi. "Njaa ilikuwa kali katika nchi ya Kaanani"

Ikawa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

walipokuwa wametumia chakula

"Yakobo na familia yake walipokuwa wamekula"

walichokitoa

"wana wakubwa wa Yakobo walileta"

mtununulie

Hapa "mtununulie" ina maana ya Yakobo, wanawe, na familia yake iliyobaki.

Genesis 43:3

Yuda akamwambia

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "alituonya ya kwamba hatutauona uso wake hadi tumlete ndugu yetu mdogo pamoja nasi"

Yule mtu

Hii ina maana ya Yusufu, lakini ndugu hawakujua alikuwa Yusufu. Walimtaja kama "mtu" au "yule mtu, bwana wa nchi" kama katika 42:29.

alituonya, "Hamtauona uso wangu ndugu yenu asipokuwa nanyi"

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "alituonya ya kwamba hatutauona uso wake hadi tumlete ndugu yetu mdogo pamoja nasi"

alituonya kwa ukali

"alikuwa na hali ya ukali alipotuonya, akisema"

Hamtauona uso wangu

Yuda anatumia msemo huu mara mbili katika 43:3-5 kuweka msisitizo kwa baba yake ya kwamba hawawezi kurudi Misri bila Benyamni. Msemo "uso wangu" una maana ya yule mtu, ambaye ni Yusufu. "Hamtaniona"

ndugu yenu awe nanyi

Yuda ana maana ya Benyamini, mtoto wa Raheli wa mwisho kabla yeye hajafa.

hatutashuka

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "kushuka" kuzungumzia safari ya Kaanani kwenda Misri.

Genesis 43:6

Kwa nini mlinitendea mimi vibaya hivyo

"Kwa nini mlinisababishia matatizo makubwa hivi"

Yule mtu alituuliza habari zetu

"Yule mtu aliuliza maswali mengi"

juu yetu

Hapa "yetu" inajitegemea na ina maana ya ndugu waliokwenda Misri na kuzungumza na"yule mtu".

Akasema, 'Je baba yenu bado yuko hai? Je mnaye ndugu mwingine?

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Alituuliza kwa kuzunguka kama baba yetu alikuwa bado yu hai na kama tuna ndugu mwingine".

Tukamjibu kulingana na maswali haya

"Tulimjibu maswali aliyotuuliza"

Tungejuaje kwamba angetwambia, 'Mleteni ndugu yenu

Wana hawa wanatumia swali kuweka msisitizo ya kwamba hawakujua ni kitu gani yule mtu angewaambia kufanya. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hatukujua ya kwamba angetuambia ... chini!"

angetwambia, 'Mleteni ndugu yenu?"

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "angetuambia kumfuata ndugu yetu huku chini Misri"

Mleteni ndugu yenu chini

Ilikuwa kawaida kutumia neno la "chini" katika kuzungumzia safari ya kutoka Kanaani kwenda Misri.

Genesis 43:8

Tutainuka na kwenda ili kwamba tuishi tusife, wote sisi, wewe, na hata watoto wetu

Misemo hii "ili kwamba tuishi" pamoja na "tusife" ina maana moja. Yuda anaweka msisitizo ya kwamba wanalazimu kununua chakula Misri ili kwamba waishi. "Tutakwenda Misri na kupata nafaka ili familia yetu yote iweze kuishi"

Tutainuka

Hapa "tutainuka" ina maana ya ndugu ambao watasafiri kwenda Misri.

ili kwamba tuishi

Hapa "tuishi" ina maana ya ndugu, Israeli na familia nzima.

wote sisi

Hapa "sisi" ina maana ya hawa ndugu.

sisi, wewe

Hapa "wewe" ni umoja na ina maana ya Israeli.

na hata watoto wetu

Hapa "wetu" ina maana ya hawa ndugu. Hii ina maana ya watoto wadogo ambao wangeweza kufa katika kipindi cha njaa.

Mimi nitakuwa mdhamini wake

Nomino inayojitegemea "mdhamini" inaweza kuwekwa kama kitenzi "ahidi". "Ninaahidi kumrudisha"

Utaniwajibisha mimi

Jinsi ambavyo Yakobo atamuwajibisha Yuda inaweza kuwekwa wazi. "Utanifanya niwajibike kwako kuhusu kitakachotokea kwa Benyamini"

basi nibebe lawama

Hii inazungumzia kuhusu "lawama" kana kwamba ilikuwa kitu ambacho mtu anaweza kubeba. "Unaweza kunilaumu"

Kwani kama tusingekawia

Yuda anaelezea jambo ambalo lingetokea hapo nyuma lakini halikutokea. Yuda anamkaripia baba yake kwa kusubiri muda mrefu sana kuwatuma wanawe Misri kufuata chakula zaidi.

tungekuwa tumekwisha rudi mara ya pili

"tungekuwa tumerudi mara mbili"

Genesis 43:11

Kama ni hivyo, basi fanyeni hivi

"Iwapo huu ni uchaguzi wetu pekee, basi fanyeni"

Mchukulieni

Ilikuwa kawaida kutumia neno "chini" katika kuzungumzia safari ya Kaanani kwenda Misri.

malhamu

kitu chenye mafuta chenye harufu tamu kinachotumiwa kwa ajiliya kuponya na kulinda ngozi. "dawa"

viungo

vikolezo

jozi

karanga ndogo, itokayo kwenye mti wa kijani

lozi

karanga ya mti yenye ladha tamu

Chukueni pesa mara mbili mikononi mwenu

Hapa "mkononi" ina maana ya mtu mzima. "Chukua mara mbili ya pesa pamoja nawe"

Pesa iliyorudishwa katika magunia yenu, muichukue tena katika mikono yenu

Hapa "mikononi" ina maana ya mtu mzima. Msemo wa "iliyorudishwa" unaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "pesa iliyowekwa kwenye magunia yenu na mtu, muirudishe Misri"

Genesis 43:13

Mchukueni ndugu yenu pia

"Mchukueni pia Benyamini"

mwende tena

"mrudi"

Mungu Mwenyezi na awape kuona rehema mbele ya huyo mtu

Nomino inayojitegemea "rehema" inaweza kuwekwa kama kivumishi "huruma". "Mungu mwenye uwezo asababishe yule mtuawe na huruma kwenu"

ndugu yenu mwingine

"Simoni"

Kama nikipotelewa na watoto, nimepotelewa

"Kama nikipoteza watoto wangu, basi nipoteze watoto wangu". Hii ina maana ya kwamba Yakobo anajua inapaswa akubali kitakachotokea kwa watoto wake.

mikono yao wakachukua

Hapa "mikono" ina maana ya mtu mzima. "Wakachukua"

wakashuka Misri

Ilikuwa kawaida kutumia msemo "kushuka" pale ambapo inazungumziwa safari ya kutoka Kaanani kwenda Misri.

Genesis 43:16

Benjamini akiwa nao

"Benyamini pamoja na ndugu wa Yusufu wakubwa"

mtunzaji wa nyumba yake

"Mtunzaji" aliwajibika na kusimamia matukio ya nyumba ya Yusufu.

Akawaleta wale watu

Hapa "akawaleta" inaweza kutafsiriwa kama "kuwachukua"

nyumbani kwa Yusufu

"ndani ya nyumba ya Yusufu"

Genesis 43:18

Wale ndugu wakaogopa

"Ndugu wa Yusufu waliogopa"

walivyoletwa katika nyumba ya Yusufu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "walikwenda ndani ya nyumba ya Yusufu" au "mtunzaji aliwapeleka ndani ya nyumba ya Yusufu"

Ni kwa sababu ya pesa iliyorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tulipoletwa ndani

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtunzaji anatuleta ndani ya nyumba kwa sababu ya pesa ambayo mtu alirudisha ndani ya magunia yetu"

kwamba atafute nafasi kinyume chetu. Kwamba aweze kutukamata

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Anasubiria nafasi ya kutushtaki, ili kwamba aweze kutukamata"

tulikuja

Ilikuwa kawaida kutumia msemo "kushuka" pale ambapo inazungumziwa safari ya kutoka Kaanani kwenda Misri.

Genesis 43:21

Kauli Kiunganishi:

Ndugu wanaendelea kuzungumza na mtunzaji wa nyumba.

Ikawa

Msemo huu unatumika kuweka alama ya tukio muhimu la simulizi.

tulipofika katika eneo la kupumzikia

"tulipofika mahali ambapo tulikwenda kukaa usiku ule"

tazama

Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba ndugu walishangazwa kwa kile walichokiona.

pesa ya kila mtu ilikuwa katika gunia lake, pesa yetu kwa kiasi kamili

"kila mmoja wetu alikuta pesa kamili katika gunia lake"

Tumeileta katika mikono yetu.

Hapa "mikono" ina maana ya mtu mzima. "Tumerudisha pesa pamoja nasi"

Tumekuja na pesa nyingine pia mikononi mwetu ili kununua chakula

Hapa "mikono" ina maana ya mtu mzima. "Tumekuja na pesa zaidi pia kununua chakula zaidi"

Tumekuja na

Ilikuwa kawaida kutumia msemo "kushuka" pale ambapo inazungumziwa safari ya kutoka Kaanani kwenda Misri.

Amani iwe kwenu

Nomino inayojitegemea "Amani" inaweza kuwekwa kama kitenzi. "Tulia" au "Tulieni"

Mungu wenu na Mungu wa baba yenu

Mtunzaji hazungumzi kuhusu Mungu wawili tofauti. "Mungu wenu, Mungu ambaye baba yenu anamwabudu"

Genesis 43:24

wakaosha miguu yao

Utamaduni huu ulisaidia wasafiri waliochoka kujiburudisha baada ya kutembea umbali mrefu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi.

Akawalisha punda wao

"malisho" ni chakula kilichokauka ambacho huwekwa kando kwa ajili ya wanyama.

Genesis 43:26

wakaleta nyumbani zawadi iliyokuwa mikononi mwao

Hapa "mikononi" ina maana ya mtu mzima. "ndugu hawa walileta zawadi ambazo walikuwa nazo"

wakainama mbele yake

Hii ni njia ya kuonyesha heshima na taadhima.

Genesis 43:28

Mtumishi wako baba yetu

Walimuelezea baba yao kama "Mtumishi wako" kuonyesha heshima. "Baba yetu anayekutumikia"

Wakajinyenyekeza na kuinama chini

Maneno haya yana maana moja. Walilala chini mbele ya yule mtu kumuonyesha heshima. "Waliinama chini mbele yake"

Alipoinua macho yake

Hii ina maana "alitazama juu"

mwana wa mamaye, naye akasema

Hii inaweza kutafsiriwa na sentensi mpya. "mwana wa mamaye. Yusufu akamwambia"

Je huyu ndiye mdogo wenu ... mliyemsema?

Maana zaweza kuwa 1) Yusufu anauliza kwa dhati swali kupata uthibitisho ya kwamba mtu huyu ni Benyamini, au 2) ni swali la balagha. "Kwa hiyo huyu ndiye ndugu yenu mdogo ... mliyesema?"

mwanangu

Hii ni njia ya kirafiki mtu huzungumza kwa mtu mwingine wa cheo cha chini. "kijana"

Genesis 43:30

akaharakisha kutoka chumbani

"aliharakisha nje ya chumba"

kwani aliguswa sana kuhusu nduguye

Msemo "aliguswa sana" una maana ya kuwa na huruma kubwa au hisia ambapo jambo muhimu hutokea. "kwa maana alipatwa na hisia kali za huruma kwa nduguye" au "kwa maana akawa na hisia za upendo kwa ndugu yake"

akasema

Inaweza kuwekwa wazi ni kwa nani Yusufu anazungumza. "na akasema kwa watumishi wake"

karibuni chakula

Hii ina maana ya kusambaza chakula ili kila mtu aweze kula.

Genesis 43:32

Watumishi wakamhudumia Yusufu peke yake na wale ndugu peke yao. Wamisri pale wakala pamoja naye peke yao

Hii ina maana ya kwamba Yusufu, ndugu zake, na Wamisri wengine wanakula katika sehemu tatu tofauti ndani ya chumba kimoja. "Watumishi walimhudumia Yusufu peke yake na ndugu zake peke yao na Wamisri, ambao walikuwa wakila naye, peke yao"

Wamisri pale wakala pamoja naye peke yao

Inawezekana hawa ni maafisa Wamisri wengine ambao walikula pamoja na Yusufu, lakini bado waliketi tofauti kutoka kwake na ndugu zake wa Kiebrania.

kwa sababu Wamisri hawakuweza kula mkate na Waebrania, kwani hilo ni chukizo kwa Wamisri

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Walifanya hivi kwa sababu Wamisri walidhani ilikuwa aibu kula pamoja na Waebrania"

hawakuweza kula mkate

Hapa "mkate" ina maana ya chakula kwa ujumla.

Wale ndugu wakakaa mbele yake

Inasemekana ya kwamba Yusufu alipanga ni wapi kila ndugu angeketi. Unaweza kuweka wazi taarifa iliyodokezwa. "Ndugu walikaa upande wa pili na yule mtu, kulingana na jinsi alivyopanga nafasi zao"

mzaliwa wa kwanza kwa kulingana na haki yake ya uzaliwa, na mdogo kulingana na ujana wake

"mzaliwa wa kwanza" na "mdogo kuliko wote" inatumika pamoja kumaanisha ya kwamba ndugu wote walikaa kulingana na umri wao.

Wale watu wakashangaa wote

"Hawa watu walishangazwa walipogundua hili"

Lakini sehemu ya Benjamini ilikuwa mara tano zaidi ya kila ndugu zake

Msemo "mara tano" unaweza kuwekwa kwa ujumla zaidi. "Lakini Benyamini alipokea sehemu ambayo ilikuwa kubwa zaidi ya kile walichopokea ndugu zake"

Genesis 44

Genesis 44:1

Maelezo ya Jumla:

Hii inaanza sehemu mpya ya tukio katika simulizi. Inawezekana hii ni asubuhi iliyofuata baada ya sherehe.

msimamizi wa nyumba yake

"msimamizi" alikuwa na wajibu wa kusimamia matukio ya nyumba ya Yusufu.

pesa ya kila mtu

Pesa yao ilikuwa sarafu za fedha yawezekana ndani ya mfuko mdogo.

katika mdomo wa gunia lake

"katika gunia lake"

Uweke kikombe changu, cha fedha

"Weka kikombe changu cha fedha"

katika mdomo wa gunia la mdogo

Neno "ndugu" linaeleweka. "ndani ya gunia la ndugu mdogo"

Genesis 44:3

Kukapambazuka asubuh

"Mwanga wa asubuhi ulionekana"

wale watu wakaruhusiwa kuondoka, wao na punda zao

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "waliwatuma watu waondoke, pamoja na punda zao"

Kwa nini mmelipa uovu badala ya mema?

Swali hili linatumiwa kukaripia wale ndugu. "Mmetutendea vibaya, baada ya sisi kuwa wema kwenu!"

Je hiki siyo kikombe ambacho bwana wangu hukinywea, na kikombe akitumiacho kwa uaguzi?

Swali hili linatumika kukaripia wale ndugu. "Tayari mnafahamu ya kwamba hiki ni kikombe ambacho bwana wangu hutumia kunywea na kwa uaguzi!"

Mmefanya vibaya, kwa jambo hili mlilolifanya.

Hii inarudia "mmefanya" kuonyesha msisitizo. "Kile mlichofanya ni kibaya sana"

Genesis 44:6

kuwambia maneno haya

Hapa "maneno" yana maana ya kile kilichosemwa. "alizungumza kile Yusufu alichomuambia kusema"

Kwa nini bwana wetu anasema maneno kama haya?

Hapa "maneno" yana maana ya kile kilichosemwa. Ndugu wanataja msimamizi kama "bwana wangu". Hii njia maalumu ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi. Inaweza kuwekwa katika lugha ya upili. "Kwa nini unasema hivi, bwana wangu?"

Na iwe mbali na watumishi wako kwamba wanaweza kufanya jambo hili

Ndugu wanajitambua wenyewe kama "watumishi wako" na "wao". Hii ni njia maalumu ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi. "Hatuwezi kufanya jambo kama hilo!"

Na iwe mbali na watumishi

Jambo ambalo mtu hawezi kufanya inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kitu ambacho mtu anataka kukiweka mbali nacho.

Genesis 44:8

Tazama

Hii inaongeza msisitizo kwa kile ndugu wanasema baadae.

pesa tulizozikuta katika midomo ya magunia yetu

"unajua pesa ambayo tumeipata ndani ya magunia yetu"

tulizileta kwako kutoka katika nchi ya Kanaani

"tumerudisha kwako kutoka Kaanani"

Ni kwa jinsi gani basi tunaweza kuiba katika nyumba ya bwana wako fedha au dhahabu?

Ndugu wanatumia swali kuweka msisitizo ya kwamba hawawezi kuiba kutoka katika bwana wa Misri. "Kwa hiyo hatuwezi kuchukua kitu chochote kutoka kwenye nyumba ya bwana wako!"

fedha au dhahabu

Maneno haya yanatumiwa pamoja kumaanisha ya kwamba hawawezi kuiba kitu chochote chenye thamani yoyote.

Yeyote kitakayeonekana kwake miongoni mwa watumishi wako

Ndugu wanajitambua wao kama "watumishi wako". Hii njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. Inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu mmoja. Pia, "kitakayeonekana" linaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Ukikuta ya kwamba mmoja wetu ameiba kikombe"

nasi sote tutakuwa watumwa wa bwana wangu

Msemo "bwana wangu" una maana ya mtunzaji. Hii inaweza kuwekwa katika lugha ya upili. "Unaweza kutuchukua kama watumwa wako"

Basi na iwe kwa kadiri ya maneno yenu

Hapa "basi" haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata. Pia "maneno" ina maana ya kile kilichosemwa. "Vizuri sana. Nitafanya kile ulichosema"

Yeye ambaye kikombe kitaonekana kwake atakuwa mtumwa wangu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kama nikikuta kikombe ndani ya moja ya magunia yenu, mtu huyo atakuwa mtumwa wangu"

Genesis 44:11

kulishusha gunia lake chini

"akateremsha gunia lake"

mkubwa ... kwa mdogo wa wote

Neno "ndugu" linaeleweka. "ndugu mkubwa ... ndugu mdogo wa wote"

mdogo wa wote, na kikombe kikaonekana katika gunia la Benyamini

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya na katika hali ya kutenda. "mdogo wa wote. Mtunzaji alikuta kikombe ndani ya gunia la Benyamini"

Wakararua mavazi yao

Neno "wakararua" ina maana ya wale ndugu. Kurarua nguo ilikuwa ishara ya dhiki na majonzi makubwa.

nao wakarudi

"na wakarudi"

Genesis 44:14

Bado alikuwepo pale

"Yusufu alikuwa bado yupo pale"

wakainama mbele zake

"wakaanguka mbele yake". Hii ni ishara ya ndugu kutaka bwana awe na huruma kwao.

Je hamjui kwamba mtu kama mimi anafanya uaguzi

Yusufu anatumia swali kukaripia ndugu zake. "Hakika mnajua ya kwamba mtu kama mimi naweza kujifunza mambo kwa uaguzi!"

Genesis 44:16

Je tunaweza kumwambia nini bwana wangu? Tuseme nini? au ni jinsi gani twaweza kujithibitisha wenyewe?

Maswali yote 3 yana maana moja. Wanatumia maswali haya kuweka msisitizo ya kwamba hakuna kitu wanaweza kusema kuelezea kilichotokea. "Hatuna kitu cha kusema, bwana wangu. Hatuwezi kuzungumza jambo lolote la maana. Hatuwezi kujithibitisha"

Je tunaweza kumwambia nini bwana wangu ... watumwa wa bwana wangu

Hapa "bwana wangu" ina maana ya Yusufu. Hii njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. Inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa pili. "Tunaweza kusema nini kwako ... watumwa wako"

Mungu ameona uovu wa watumishi wako

Hapa "ameona" haimaanishi Mungu ameona tu kile ndugu walichofanya. Ina maana Mungu sasa anawaadhibu kwa kile walichofanya. "Mungu anatuadhibu kwa dhambi zetu za zamani"

uovu wa watumishi wako

Ndugu wanajitambulisha wenyewe kama "watumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. Inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa kwanza. "dhambi zetu"

na yule ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake

Hapa "mkononi" ina maana ya mtu mzima. Pia, "kimeonekana" inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "na yule ambaye alikuwa na kikombe"

Na iwe mbali nami kwamba naweza kufanya hivyo

Kitu ambacho mtu hawezi kufanya inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kitu mtu anataka kuweka mbali na yeye. "sio kawaida yangu kufanya jambo kama hili"

Mtu ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake

Hapa "mkononi" ina maana ya mtu mzima. Pia, "kimeonekana" inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "mtu aliyekuwa na kikombe changu"

Genesis 44:18

alipomkaribia

"akakaribia"

mwache mtumishi wako

Yuda anajitambulisha kama "mtumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza kwa mtu mwenye mamlaka zaidi. Hii inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa kwanza. "niruhusu mimi, mtumishi wako"

aseme neno katika masikio ya bwana wangu

Hapa "neno" ni lugha nyingine yenye maana ya kile kilichosemwa. Na "masikio" ni lugha nyingine yenye maana ya mtu mzima. "kuzungumza na wewe, bwana wangu"

masikio ya bwana wangu

Hapa "bwana wangu" ina maana ya Yusufu. Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka zaidi. Hii inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa pili. "kwako"

na usiziache hasira zako kuwaka dhidi ya mtumishi wako

Kuwa na hasira inazungumzwa kana kwamba ilikuwa moto unawaka. "tafadhali usiwe na hasira na mimi, mtumishi wako"

kwani wewe ni kama Farao

Yuda anamlinganisha bwana yule na Farao kusisitiza nguvu kubwa ambayo bwana yule alikuwa naye. Pia anadokeza ya kwamba hakutaka bwana kuwa na hasira na kumuadhibu. "kwa maana wewe kama Farao mwenye mamlaka na unaweza kuwaamuru askari wako kuniua"

Bwana wangu aliwauliza watumishi wake, kusema, Je mnaye baba au ndugu?'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Bwana wangu alituuliza kama tuna baba na ndugu"

Bwana wangu aliwauliza watumishi wake

Yuda anamtambua Yusufu kwa maneno haya "bwana wangu" na "wake". Pia anajitambulisha mwenyewe na ndugu zake kama "watumishi wake". "Wewe, bwana wangu, alituuliza, watumishi wako" au "Ulituuliza"

Genesis 44:20

Maelezo ya Jumla:

Yuda anaendelea kuzungumza mbele ya Yusufu.

Nasi tukamwambia bwana wangu, 'Tunaye baba ... baba yake anampenda.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Nasi tukamwambia bwana wetu ya kwamba tuna baba ... baba yake anampenda"

tukamwambia bwana wangu

Yuda anamtambua Yusufu kama "bwan wangu". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. "tulisema kwako, bwana wangu"

baba yake anampenda

Hii ina maana ya upendo kwa rafiki au mmoja wa familia.

Nawe ukawambia watumishi wako, 'Mleteni ili nimwone.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Nawe ukasema kwa mtumishi wako ya kwamba tunapaswa kumleta ndugu yetu mdogo kwako ili uweze kumuona"

Nawe ukawambia watumishi wako

Yuda anajitambulisha mwenyewe na ndugu zake kama "watumishi wako". "Kisha ulisema kwetu, watumishi wako"

Mleteni ili nimwone

Ilikuwa kawaida kutumia neno "chini" pale ilipozungumziwa safari ya kutoka Kanaani kwenda Misri. "Mleteni kwangu"

Baada ya hapo, tukamwambia bwana wangu, 'Kijana hawezi ... baba yake angekufa.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Kwa kujibu, tulisema kwa bwana wangu ya kwamba kijana hawezi ... baba yake angekufa"

baba yake angekufa

Inadokezwa ya kwamba baba yao angekufa kwa huzuni.

Genesis 44:23

Maelezoya jumla:

Yuda anaendelea simulizi yake kuhusu Yusufu.

Na ukawambia watumishi wako, 'Mdogo wenu asipokuja pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Kisha ulisema kwa watumishi wako ya kwamba hadi pale ndugu yetu mdogo aje pamoja nasi, hatutaweza kukuona tena"

Na ukawaambia watumishi wako

Yuda anajitambulisha mwenyewe na ndugu zake kama "watumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka zaidi. "Kisha ukasema kwetu, watumishi wako"

asipokuja ... kushuka

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "kushuka" kuzungumzia safari ya Kaanani kwenda Misri.

hamtauona uso wangu tena

Hapa "uso" ina maana ya mtu mzima. "Hamtaniona tena"

Ikawa

Msemo huu unatumika kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

tulipokwenda kwa mtumishi wako baba yangu

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "kwenda" kuzungumzia safari kutoka Misri kwenda Kaanani.

tulimwambia maneno ya bwana wangu

Yuda anamtambua Yusufu kama "bwana wangu". Pia "maneno" yana maana ya kile kilichosemwa. "tulimwambia ulichosema, bwana wangu"

Na baba yetu akasema, Nendeni tena, mkatununulie chakula

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Baba yetu alituambia kurudi tena Misri kununua chakula kwa ajili yetu na familia zetu"

Nasi tukasema, "Hatuwezi kushuka. Ikiwa mdogo wetu ... pamoja nasi,

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Kisha tukamwambia ya kwamba hatuwezi kushuka Misri. Tulimwambia ya kwamba iwapo ndugu yetu mdogo atakuwa pamoja nasi ... pamoja nasi"

kuuona uso wa mtu

Hapa "uso" ina maana ya mtu mzima. "kumuona yule mtu"

Genesis 44:27

Maelezo ya Jumla:

Yuda anaendeleza simulizi yake kwa Yusufu

akatuambia, 'Mnajua kwamba mke wangu alinizalia wana wawili. Na mmoja akatoka kwangu nami nikasema, "Bila shaka ameraruliwa vipande, na tangu hapo sijamwona." Nanyi mkimchukua huyu naye kutoka kwangu mabaya yanaweza kumpata, mtashusha mvi zangu kwa kaburini kwa huzuni.

Hii ina madaraja mawili na daraja la tatu la nukuu. Yanaweza kuwekwa kama nukuu zisikzokuwa moja kwa moja. "akatuambia ya kwamba tunafahamu ya kuwa mke wake, Raheli, alimzalia watoto wawili tu, na kwamba mmoja wao alitoweka na mnyama alimrarua vipande vipande, na hajamuona tangu siku hiyo, kisha tutamfanya afe kwa huzuni"

akatuambia

Hapa "akatuambia" haimjumlishi Yusufu.

Mnajua

Hapa "mnajua" ni wingi na ina maana ya wale ndugu.

ameraruliwa vipande

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mnyama pori alimrarua vipande vipande"

mabaya yanaweza kumpata

Jambo baya linalotokea kwa mtu inazungumziwa kana kwamba "baya" lilikuwa kitu ambacho husafiri na kuja kwa mtu.

mtashusha mvi zangu kwa kaburini kwa huzuni

"kushusha ... Kuzimu" ni njia ya kusema watasababisha afariki na kushuka Kuzimu. Anatumia neno "shuka" kwa sababu iliaminika Kuzimu ilikuwa sehemu ya chini. "kisha mtanisababisha, mtu mzee, kufa kwa huzuni"

mvi zangu

Hii ina maana ya Yakobo na inasisitiza umri wake mkubwa. "mimi, mtu mzee"

Genesis 44:30

Kwa hiyo

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika hapa kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

basi, nitapokuja ... huzuni ya kuzimu

Yuda anaelezea kwa Yusufu suala la ukweli lakini la kubuni ambalo linatarajiwa kutokea kwa Yakobo atakaporudi bila Benyamini.

nitapokuja kwa mtumishi wako

Hapa "nitakapokuja" inaweza kutafsiriwa kama "kwenda" au "kurudi".

kijana hayupo nasi

"kijana hayupo pamoja nasi"

kwa kuwa uhai wake umefungamanishwa katika uhai wa kijana

Baba anasema ya kwamba atakufa iwapo mwanawe atangekufa inazungumziwa kana kwamba maisha yao mawili yaliunganishwa pamoja kimwili. "kwa maana alisema angekufa iwapo kijana hangerudi"

itakuwa

Yuda anazungumzia kuhusu suala la kubuni katika wakati wa mbele kana kwamba ingetokea kweli.

watumishi wako watazishusha mvi za mtumishi wako baba yetu kaburini kwa masikitiko

"watazishusha ... Kuzimu" ni njia ya kusema watasababisha afariki na kushuka Kuzimu. Anatumia neno "shuka" kwa sababu iliaminika Kuzimu ilikuwa sehemu ya chini. "kisha mtanisababisha, mtu mzee, kufa kwa huzuni"

watumishi wako

Yuda anajitambulisha mwenyewe na ndugu zake kama "watumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka zaidi. "Nasi, watumishi wako" au " Na sisi"

mvi za mtumishi wako baba yetu

Hapa "mvi" ina maana ya Yakobo na inasisitiza umri wake mkubwa. "baba yetu mzee"

Kwani mtumishi wako alikuwa mdhamini wa kijana kwa baba yangu

Nomino hii inayojitegemea "mdhamini" inaweza kuwekwa kama kitenzi "aliahidi". "Maana nimuahidi baba yangu kuhusu kijana huyu"

Kwani mtumishi wako

Yuda anajitambulisha kama "mtumishi wako". "Kwa maana mimi, mtumishi wako" au "Kwa maana mimi"

ndipo nitakapokuwa mwenye hatia kwa baba yangu

Kuchukuliwa mwenye hatia inazungumziwa kana kwamba "hatia" ilikuwa kitu ambacho mtu hubeba. "kisha baba yangu anaweza kunilaumu"

Genesis 44:33

sasa

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

mwache mtumishi wako

Yuda anajitambulisha mwenyewe kama "mtumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. "niruhusu mimi, mtumishi wako" au "niruhusu mimi"

kwa bwana wangu

Yuda anamtambua Yusufu kama "bwana wangu". "kwako, bwana wangu" au "kwako"

umwache kijana aende juu

Alikuwa akienda kutumia msemo wa "aende juu" pale alipozungumzia safari ya kutoka Misri kwenda Kaanani.

Kwa maana nitakwenda jinsi gani kwa baba yangu ikiwa kijana hayupo nami?

Yuda anatumia swali kuweka msisitizo wa majonzi ambayo angeyapata iwapo Benyamini asingerudi nyumbani. "Siwezi kurudi kwa baba yangu iwapo kijana hatakuwa pamoja nami"

Ninaogopa kuona mabaya yatakayompata baba yangu

Mtu anayeteseka vibaya inazungumziwa kana kwamba "uovu" ilikuwa kitu kinachokuja juu ya mtu. "Ninaogopa kumuona jinsi baba yangu atakavyoteseka"

Genesis 45

Genesis 45:1

hakuweza kujizuia mwenyewe

Hii ina maana hakuweza kuzuia hisia zake. Inaweza kuwekwa katika hali ya chanya. "alikuwa akitaka kuanza kulia"

kando yake

"karibu naye"

nyumba ya Farao

Hapa "nyumba" ina maana ya watu katika kasri ya Farao. "kila mtu ndani ya kasri ya Farao"

walitishwa na uwepo wake

"walimuogopa"

Genesis 45:4

mliyemwuza Misri

Maana inaweza kuwekwa wazi zaidi. "ambaye mlimuuza kama mtumwa kwa wafanyabiashara walionileta huku Misri"

msihuzunike

"msihuzunike" au "msiteseke"

mliniuza huku

Maana inaweza kuwekwa wazi zaidi. "ya kwamba mliniuza kama mtumwa na kunituma huku Misri"

kutunza uhai

Hapa "uhai" ina maana ya watu ambao Yusufu aliwaokoa na kifo wakati wa njaa. "Ili niweze kuokoa maisha ya wengi"

bado kuna miaka mitano ambayo hakutakuwa na kulima wala kuvuna.

"kutakuwa na miaka mitano zaidi bila ya kupanda au kuvuna". Hapa "bila ya kupanda au kuvuna" ina maana ya ukweli kwamba mimea haitaota kwa sababu ya ukame. "na njaa itadumu kwa miaka mitano zaidi"

Genesis 45:7

kuwahifadhi kama masalia duniani

"ili kwamba wewe na familia yenu msipotee kutoka duniani" au "kuhakikisha vizazi vyako vinaendelea kuishi"

kuwaweka hai kwa ukombozi mkuu

Nomino inayojitegemea "ukombozi" inaweza kuwekwa kama "kuokoa". "kukuweka hai kwa kuwaokoa kwa njia ya juu"

amenifanya baba kwa Farao

Yusufu kumshauri na kumsaidia Farao inazungumziwa kana kwamba Yusufu alikuwa baba wa Farao. "amenifanya niwe kiongozi kwa Farao" au "amenifanya kuwa mshauri mkuu kwa Farao"

nyumba yake yote

Hapa "nyumba" ina maana ya watu wanaoishi ndani ya kasri yake. "miongoni mwa nyumba yake yote" au "kati ya wote wa kasri yake"

mtawala wa nchi yote ya Misri

Hapa "nchi" ina maana ya watu. "mtawala juu ya watu wote wa Misri"

mtawala

Hapa Yusufu anamanisha ya kwamba yeye ni mtawala katika nafasi ya pili kutoka kwa Farao, mfalme wa Misri. Taarifa hii inayoeleweka inaweza kuwekwa wazi.

Genesis 45:9

mwende kwa baba yangu

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "kushuka" kuzungumzia safari ya Kaanani kwenda Misri. "kurudi kwa baba yangu"

mmwambie, 'Hivi ndivyo asemavyo Yusufu mwanao, "Mungu amenifanya ... yote uliyonayo

Hii ni nukuu yenye madaraja matatu. Inaweza kurahisishwa katika madaraja mawili. "muambieni ya kwamba hivi ndivyo nilivyosema: "Mungu amenifanya ... yote uliyonayo"

Shuka kwangu

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "shuka" kuzungumzia safari ya kutoka Kaanani kwenda Misri. "Njooni hapa kwangu"

ukaingia katika uhitaji

Hii inazungumzia kuhusu "uhitaji" kana kwamba ilikuwa kikomo cha safari. "kupotea bure" au "kushinda njaa"

Genesis 45:12

macho yenu yanaona, na macho ya Benjamini ndugu yangu

Neno "macho" ina maana ya mtu mzima. "Nyie wote na Benyamini mnaweza kuona"

kwamba ni kinywa changu kinachoongea nanyi

Neno "kinywa" ina maana ya mtu mzima. "ya kwamba mimi, Yusufu, nazungumza na nyinyi"

juu ya heshima yangu yote huku Misri

"jinsi watu wa Misri wanavyoniheshimu sana"

baba yangu huku chini

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "shuka" kuzungumzia safari ya kutoka Kaanani kwenda Misri. "baba yangu huku kwangu"

Genesis 45:14

Akaikumbatia shingo ya Benjamini ndugu yake na kulia, na Benjamini akalia shingoni mwake

"Yusufu alimkumbatia ndugu yake Benyamini, na wote wakalia"

Akawabusu ndugu zake wote

Katika kipindi cha zamani cha Mashariki ya Karibu, ilikuwa kawaida kumsalimia jamaa kwa busu.

kulia kwa ajili yao

Hii ina maana ya Yusufu alilia alipowabusu.

Baada ya hayo ndugu zake wakaongea naye

Awali walikuwa na hofu juu yake. Sasa walijisikia wanaweza kuongea naye kwa uhuru. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Baada ya hapo ndugu zake waliongea naye kwa uhuru"

Genesis 45:16

Habari ya jambo hili ikasemwa katika nyumba ya Farao: "Ndugu zake Yusufu wamekuja"

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. Pia hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kila mtu katika kasri ya Farao alisikia ya kwamba ndugu zake Yusufu walikuja"

nyumba ya Farao

Hii ina maana ya kasri ya Farao

Wambie ndugu zako, 'Fanyeni hivi: Wapakieni wanyama wenu na mwende katika nchi ya Kanaani. Mchukueni baba yenu na nyumba zenu mnijie. Nami nitawapa mema ya nchi ya Misri, nanyi mtakula unono wa nchi.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Waambie ndugu zako kupakiza wanyama wao na kwenda Kaanani kumfuata baba yao na familia zao. Waambie waje hapa, nami nitawapa ardhi nzuri katika Misri na chakula bora tunachoweza kutoa"

nitawapa mema ya nchi ya Misri

"Nitawapa sehemu bora ya nchi ya Misri"

mtakula unono wa nchi

Chakula bora ambacho nchi huzaa inazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni sehemu nene ya nchi. "utakula chakula bora katika nchi"

Genesis 45:19

Maelezo ya Jumla

Farao anaendelea kumwambia Yusufu kipi cha kuwaambia ndugu zake.

Basi

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

mmeamriwa, 'Fanyeni hivi, chukueni mikokoteni kutoka Misri kwa ajili ya watoto wenu na kwa ajili ya wake zenu. Mchukueni baba yenu na kuja. Msijari kuhusu mali zenu, kwani mema yote ya nchi ya Misri ni yenu

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "pia waambie kuchukua mikokoteni kutoka katika nchi ya Misri kwa ajili ya watoto na wake zao, na kumchukua baba yao aje hapa. Hawatakiwi kuwa na wasiwasi kuhusu kuleta mali zao, kwa maana nitawapatia mambo mazuri tuliyonayo ndani ya Misri"

mmeamriwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nami nakuamuru kuwaambia" au "pia waambie"

chukueni mikokoteni

"Mikokoteni" ni gari dogo la abiria na mizigo lenye magurudumu mawili au manne. Wanyama huvuta mikokoteni.

Genesis 45:21

na akawapa mahitaji ya safari

"na kuwapa walichohitaji kwa ajili ya safari yao"

Akawapa wote mavazi ya kubadilisha

Kila mtu alipokea idadi ya nguo mbili isipokuwa kwa Benyamini aliyepokea idadi ya nguo tano.

vipande mia tatu

"vipande 300"

punda kumi ... punda majike kumi

Punda walijumlishwa kama sehemu ya zawadi.

Genesis 45:24

msijemkagombana

Maana zaweza kuwa 1) "msibishane" na 2) "msiwe na hofu"

Wakapanda kutoka Misri

Ilikuwa kawaida kutumia neno "panda" kuzungumzia safari ya kutoka Misri kwenda Kaanani.

ndiye mtawala juu ya nchi yote ya Misri

Hapa "nchi ya Misri" ina maana ya watu wa Misri. "anatawala watu wote wa Misri"

moyo wake ulishikwa na mshangao

Hapa "moyo" ina maana ya mtu mzima. "na alishtuka" au "na alishangazwa sana"

hakuwaamini walichomuambia

"hakupokea kile walichosema kilikuwa ni cha kweli"

Genesis 45:27

Wakamwambia

"Wakamwambia Yakobo"

maneno yote ya Yusufu aliyokuwa amewaambia

Hapa "maneno" yana maana ya kile kilichosemwa. "kila kitu ambacho Yusufu alikisema kwao"

roho ya Yakobo baba yao ikafufuka

Neno la "roho" lina maana ya mtu mzima. "Yakobo baba yao alipona" au "Yakobo baba yao akawa na furaha sana"

Genesis 46

Genesis 46:1

akaja Beersheba

"alikuja Beersheba"

Mimi hapa

"Ndio, ninasikiliza"

kushuka Misri

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "shuka" kuzungumzia safari ya kutoka Kaanani kwenda Misri.

nitakufanya taifa kubwa

Hapa "nitakufanya" ni katika umoja na una maana ya Yakobo. Hii "nitakufanya" pia ina maana ya uzao wa Israeli ambao watakuwa taifa kubwa. "Nitakupatia uzao mkubwa, nao watakuwa taifa kubwa"

huko Misri

"huko Misri"

Nami nitakupandisha huku tena bila shaka

Ahadi ilifanywa kwa Yakobo, lakini ahadi hii ingetimizwa kwa uzao wote wa Yakobo. "Hakika nitaleta uzao wako kutoka Misri tena"

nitakupandisha huku tena

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "kupanda" kuzungumzia safari ya kutoka Misri kwenda Kaanani.

Na Yusufu akayafunika macho yako kwa mikono yake

Msemo huu "akayafunika macho yako kwa mikono yake" ni njia ya kusema ya kwamba Yusufu atakuwepo pale ambapo Israeli atakufa na Yusufu atauafumba macho ya Yakobo katika kipindi cha kifo chake. "Na Yusufu pia atakuwepo pamoja na wewe katika kipindi cha kifo chako"

akayafunika macho yako

Ilikuwa ni utamaduni kufunika kope za macho pale mtu anapokufa na macho yake wazi. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi.

Genesis 46:5

akainuka kutoka

"kuwekwa kutoka kwa"

katika mikokoteni

"Mikokoteni" ni gari dogo la abiria na mizigo lenye magurudumu mawili au manne. Wanyama huvuta mikokoteni.

walizokuwa wamezipata

"ambazo walikusanya" au "waliopata"

Akaja pamoja nao

"Yakobo akaja pamoja nao"

wanawe

"wajukuu wake"

wana wa binti zake

"wajukuu wake wa kike"

Genesis 46:8

Haya ni majina

Hii ina maana ya majina ya watu ambao mwandishi anataka kuwaorodhesha.

ya watoto wa Israeli

"ya watoto wa familia ya Israeli"

Hanoki na Palu na Hezroni na Karmi ... Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli ... Gershoni, Kohathi, na Merari

Haya ni majina ya wanamume.

Genesis 46:12

Eri, Onani, Shela

Hawa walikuwa wana wa Yuda kwa mke wake, Shua.

Shela na Zera

Hawa walikuwa wana wa Yuda kwa mkwe wake, Tamari.

Hezroni ... Hamuli ... Tola, Puva, Lobu ... Shimroni ... Seredi, Eloni ... Yahleeli

Haya ni majina ya wanamume.

Dina

Hili ni jina la binti wa Lea.

Wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu

watatu - Hapa "wanawe" na "mabinti" ina maana ya wana wa Yakobo, mabinti , na wajukuu wenye uhusuiano na Lea. "Kwa pamoja alikuwa na watoto 33, mabinti na wajukuu"

Genesis 46:16

Zifioni ... Hagi, Shuni ... Ezboni, Eri, Arodi ... Areli ... Imna ... Ishva, Ishvi ... Beria ... Heberi ... Malkieli

Haya ni majina ya wanamume.

Sera

Hili ni jina la mwanamke

Zilpa

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Lea.

Wana hawa aliomzalia Yakobo - kumi na sita kwa ujumla

Hii ina maana ya watoto 16, wajukuu, na watukuu ambao walikuwa na uhusiano na Zilpa.

Genesis 46:19

Asenathi

"Asenathi" ni jina la mwanamke ambaye Farao alimpa Yusufu kuwa mke wake.

Potifera

"Potifera" ni baba yake Asenathi.

kuhani wa Oni

Oni ni mji, ambao pia unajulikana kama Heliopolisi, ambao ulikuwa "Mji wa Jua" na makao ya kumuabudu mungu wa jua Ra.

Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu, na Ardi

Haya ni majina ya wanamume.

jumla yao kumi na wanne

Hii ina maana ya wana 14 na wajukuu waliokuwa wamehusiana na Raheli.

Genesis 46:23

Hushimu ... Yahzeeli, Guni, Yezeri ... Shilemi

Haya ni majina ya wanamume.

Bilha

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Raheli.

wote walikuwa saba

Hii ina maana ya wana 7 na wajukuu waliokuwa wamehusiana na Bilha.

Genesis 46:26

sitini na sita

sita - "66"

sabini

"70"

Genesis 46:28

kuonesha njia mbele yake kwenda Gosheni

"kuwaonyesha njia ya kuelekea Gosheni"

Yusufu akaandaa kibandawazi chake na akaenda

Hapa "Yusufu" ina maana ya watumishi wake. "Watumishi wa Yusufu waliaanda kibandawazi chake na Yusufu akenda juu"

akaenda kukutana na baba yake Israeli

Msemo wa "kwenda juu" unatumika kwa sababu Yusufu anasafiri kwenye kwenye mwinuko kukutana na baba yake" "akaenda kukutana na baba yake"

akaikumbatia shingo yake, na akalia shingoni mwake kwa muda mrefu

"akaweka mikono yake kumzunguka baba yake, na kulia kwa muda mrefu"

Basi na nife sasa

"Sasa nipo tayari kufa" au "Sasa nitakufa na furaha"

kwa kuwa nimeuona uso wako, kwamba bado uko hai

Hapa "uso" ina maana ya mtu mzima. Yakobo anaonyesha furaha ya kumuona Yusufu. "kwa maana nimekuona ukiwa hai tena"

Genesis 46:31

nyumba ya baba yake

Hapa "nyumba" ina maana ya familia yake. "familia ya baba yake" au "nyumba ya baba yake"

Nitakwenda na kumwambia Farao

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "kwenda juu" pale mtu azungumzapo na mtu mwenye mamlaka makubwa. "Nitakwenda kumwambia Farao"

kumwambia Farao, kusema, 'Ndugu zangu ... vyote walivyonavyo.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "mwambie Farao ya kwamba ndugu zangu ... vyote walivyonavyo"

Genesis 46:33

Itakuwa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama kwa tukio muhimu ambalo linataka kutokea katika simulizi.

na kuwauliza, 'Kazi yenu ni ipi?' mwambieni,

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "mwambieni, 'Watumishi wako wamekuwa ... sisi, na baba zetu."

mwambieni, 'Watumishi wako wamekuwa ...sisi, na baba zetu."

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "mwambieni, 'Watumishi wako wamekuwa ... sisi, na baba zetu."

Watumishi wako

Familia ya Yusufu wanajitambulisha kama "watumishi wako" wanapozungumza na Farao. Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. Inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa kwanza. "Sisi, watumishi wako"

kila mfugaji ni chukizo kwa Wamisri

Nomino inayojitegemea ya "chukizo" inaweza kutafsiriwa na kivumishi "yenye maudhi". "Wamisri wanadhani ufugaji ni maudhi"

Genesis 47

Genesis 47:1

Akawachukua watano katika ndugu zake

tafsiri inaorodhesha tukio pamoja na Farao katika mpangilio, wakati tafsiri zingine huorodhesha matukio kama mwandishi alivyoandika.

Genesis 47:3

Watumishi wako ni wafugaji

"Watumishi wako wanafuga mifugo"

Watumishi wako

Ndugu wa Yusufu wanajitambua kama "watumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi. Hii inaweza katika lugha ya mtu wa kwanza. "Sisi, watumishi wako" au "Sisi"

kama mababu zetu

"wote sisi na baba zetu" au "wote sisi na mababu zetu"

Tumekuja kukaa kwa muda katika nchi

"Tumekuja kukaa kwa muda mfupi Misri"

Hakuna malisho

"Hakuna nyasi ya kula"

Hivyo

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

Genesis 47:5

Nchi ya Misri iko mbele yako

"Nchi ya Misri ipo wazi kwako" au "Nchi yote ya Misri ipo wazi kwako"

Mkalishe baba yako na ndugu zako katika eneo zuri, nchi ya Gosheni

"Muweke baba yako na ndugu zako katika nchi ya Gosheni, ambayo ni sehemu bora zaidi"

Ikiwa unafahamu watu wenye uwezo miongoni mwao

Inasemekana ya kwamba walikuwa na uwezo wa kuchunga wanyama. "Kama unawajua wanamume wowote miongoni mwao wenye uwezo wa kutunza mifugo"

Genesis 47:7

Yakobo akambariki Farao

Hapa "kubarikiwa" ina maana ya kuonyesha hamu ya mambo chanya na yenye manufaa kutokea kwa mtu huyo.

Umeishi kwa muda gani?

"Una umri gani?"

Miaka ya safari zangu ni mia moja na thelathini

Msemo wa "miaka ya safari zangu" ina maana ya muda ambao aliishi duniani akisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine. "Nimesafiri duniani kwa miaka 130"

Miaka ya maisha yangu imekuwa mifupi ... Siyo kama miaka ya baba zangu.

Yakobo ina maana ya kwamba maisha yake ni mafupi kulinganisha na maisha ya Abrahamu na Isaka.

na ya maumivu

Yakobo ameonyesha maumivu mengi na matatizo wakati wa maisha yake.

Genesis 47:11

Kisha Yusufu akamweka baba yake na ndugu zake

"Kisha Yusufu akamweka baba yake na ndugu zake na kuwasaidia kuimarisha sehemu watakapoishi"

eneo la Ramesesi

Hili ni jina la nchi ya Gosheni.

kulingana na hesabu ya wahitaji wao

Hapa, neno "wahitaji" lina maana ya watoto wadogo katika familia. "kulingana na idadi ya watoto wadogo ndani ya familia zao"

Genesis 47:13

Basi

Neno hili linatumika hapa kuweka alama ya pumziko katika zimulizi kuu. Hapa mwandishi anaanza kuelezea sehemu mpya ya simulizi.

Nchi ya Misri na nchi ya Kanaani

Hii ina maana ya watu wanaoishi katika nchi hizi. "watu wa Misri na watu wa Kaanani"

ikaharibika

"ikawa nyembamba na dhaifu"

Yusufu akakusanya pesa yote iliyokuwa katika nchi ya Misri na nchi ya Kanaani, kwa kuwauzia wakaaji wake nafaka

"Watu wa Misri na Kaanani walitumia pesa yao kununua nafaka kutoka kwa Yusufu"

Yusufu akakusanya ... Yusufu akaleta

Inawezekana Yusufu aliwaamuru watumishi wake kukusanya na kuleta ile pesa"

Genesis 47:15

Pesa yote ya nchi za Misri na Kanaani ilipokwisha

Hapa "nchi" ina maana ya watu wanaoishi katika nchi zile. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Pale ambapo watu wa Misri na Kaanani watakapomaliza pesa yao yote"

ya nchi za Misri na Kanaani

"kutoka katika nchi ya Misri na kutoka katika nchi ya Kaanani"

Kwa nini tufe mbele zako kwa maana pesa yetu imekwisha?

Watu walitumia swali kuweka msisitizo jinsi gani walivyokuwa na haja ya kununua chakula kutokana na kukata tamaa. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Tafadhali, usituruhusu tufe kwa sababu tumetumia pesa yetu yote!"

Akawalisha kwa mkate

Hapa "mkate" una maana ya chakula kwa ujumla. "Aliwapatia chakula" au "Aliwagawia chakula"

Genesis 47:18

wakaja kwake

"watu wakaja kwa Yusufu"

Hatutaficha kwa bwana wangu

Watu wanamtambua Yusufu kama "bwana wangu". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. Inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa pili. "Hatutajificha kwako, bwana wetu" au "Hatutajificka kutoka kwako"

Hakuna kilichobaki machoni pa bwana wangu

Hapa "machoni" ina maana ya Yusufu mwenyewe. "Hatuna kitu kilichobaki kukupa, bwana wetu"

Kwa nini tufe mbele za macho yake, sisi na nchi yetu?

Neno la "macho" lina maana ya macho ya Yusufu. Watu hutumia swali kuweka msisitizo jinsi walivyo na hamu ya kununua chakula. swali hili linaweza kutasfiriwa kama kauli. "Tafadhali usitazame tu tunavyokufa na nchi yetu inaharibika!"

Kwa nini tufe ... wote sisi na nchi yetu?

Nchi inakuwa haina faida na inaharibika kwa sababu hakuna mbegu ya kupanda; kwa hiyo inazungumziwa kana kwamba nchi itakufa.

Genesis 47:20

Kwa njia hii, nchi ikawa mali ya Farao

"Kwa hiyo nchi ikawa ya Farao"

Ilikuwa ni nchi ya makuhani pekee ambayo Yusufu hakuinunua

"Lakini hakununua nchi ya makuhani"

makuhani walikuwa wakipewa posho

"Posho" ni kiasi cha pesa au chakula ambacho mtu hutoa mara kwa mara mtu mwingine. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Farao aliwapa makuhani kiasi fulani cha chakula kila siku"

Walikula katika sehemu aliyowapa Farao

"Walikula kutoka kwa kile ambacho Farao aliwapatia"

Genesis 47:23

nanyi mtapanda

"ili muweze kupanda"

Wakati wa mavuno, mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu

Neno la "tano" ni sehemu. "Wakati wa mavuno utagawanyisha mazao katika sehemu tano. Utatoa sehemu moja kwa Farao kwa ajili ya malipo na sehemu nne ni kwa ajili yenu"

wa chakula cha nyumba zenu na watoto wenu

Unaweza kuwekwa wazi taarifa inayoeleweka. "kwa chakula kwa ajili ya nyumba zenu na kwa chakula kwa ajili ya watoto wenu"

Genesis 47:25

Na tupate kibali machoni pako

Hapa "macho" ina maana ya fikra na mawazo. "Na ufurahishwe na sisi"

tupate kibali

Hii ina maana ya kwamba mtu anakubalika kwa mtu mwingine.

katika nchi ya Misri

"katika nchi ya Misri" au "katika nchi yote ya Misri"

hata leo

Hii ina maana katika kipindi ambacho mwandishi alikuwa akiandika haya.

moja ya tano

tano- Neno la "tano" ni sehemu. "Wakati wa mavuno utagawanyisha mazao katika sehemu tano. Utatoa sehemu moja kwa Farao kwa ajili ya malipo na sehemu nne ni kwa ajili yenu"

Genesis 47:27

Walikuwa wenye kuzaa na kuongezeka sana

Neno "kuongezeka" linaelezea jinsi walivyokuwa "wamezaana". "Walikuwa na watoto wengi sana"

Walikuwa wenye kuzaa

Hapa "kuzaa" ina maana ya kufanikiwa au kupata watoto.

miaka kumi na saba

"miaka 17"

kwa hiyo miaka ya maisha ya Yakobo ilikuwa miaka mia moja arobaini na saba

miaka saba - "kwa hiyo Yakobo aliishi hadi umri wa miaka 147"

Genesis 47:29

Wakati wa kufa kwake Yakobo ulipokaribia

Hii inazungumzia juu ya muda kana kwamba inasafiri na kutua mahali. "Muda wa Israeli kufariki ulipokaribia"

Ikiwa nimepata kibali machoni pako

Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo. "Kama nimepata kibali na wewe" au "Kama nimekufurahisha"

sasa

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

nimepata kibali

Hii ina maana ya kwamba mtu amekubalika na mtu mwingine.

weka mkono wako chini ya paja langu

Tendo hili ni ishara ya kufanya ahadi ya dhati.

unionyeshe uaminifu na kweli

Nomino inayojitegemea ya "uaminifu"na "kweli" zinaweza kutafsiriwa kama vivumishi. "nitendee kwa namna ya uaminifu na kweli"

Tafadhari usinizike Misri

Neno "tafadhali" linaongeza msisitizo kwa ombi lake.

Nitakapolala na baba zangu

Hapa "kulala" ni njia ya upole ya kumaanisha kufa. "Nitakapokufa na kujiunga na wa familia yangu waliokufa kabla yangu"

Niapie

"Niahidi" au "Fanya kiapo kwangu"

akamwapia

"allimuahidi" au "alifanya kiapo kwake"

Genesis 48

Genesis 48:1

Ikawa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

mmojawapo akamwambia Yusufu

"mtu akamwambia Yusufu"

Tazama, baba yako

"Sikiliza, baba yako". Hapa neno "tazama" linatumika kuvuta nadhari ya Yusufu.

Hivyo akaondoka

"Kwa hiyo Yusufu akaondoka"

Yakobo alipoambiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu alipomuambia Yakobo"

mwanao Yusufu amekuja kukuona

"mwanao Yusufu amekuja kwako"

Israeli akakusanya nguvu na kukaa juu ya kitanda

Hapa mwandishi anazungumzia juu ya Israeli kuhangaika kuketi kitandani kana kwamba alikuwa akikusanya "nguvu" kama vile mtu akusanyavyo vitu halisia. "Israeli alifanya bidii kubwa kukaa kitandani" au "Israeli alihangaika alipokaa juu kitandani"

Genesis 48:3

Luzu

Hili ni jina la mji.

katika nchi ya Kanaani. Akanibariki na kuniambia

Hii inaweza kutafsiriwa kwa sentensi mpya ikianzia katika sehemu mpya. "katika nchi ya Kaanani, na akanibariki. Na akasema kwangu"

akanibariki

Hii ina maana ya Mungu kutamka baraka rasmi kwa mtu.

na kuniambia, 'Tazama, nitakupa uzao mwingi, na kukuzidisha. Nitakufanya kuwa kusanyiko la mataifa. Nitakupa nchi hii wewe na uzao wako kuwa milki ya milele

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "na kusema kwangu ya kwamba angenifanya niwe na uzao mwingi na kunizidishia. Na akasema ya kwamba angenifanya kuwa kusanyiko la mataifa na angenipa nchi hii kwa uzao wangu kama milki ya milele".

Tazama

Mungu alitumia neno hili "tazama" hapa kumuamsha Yakobo kuvuta nadhari kwa kile alichokuwa akitaka kumwambia.

nitakupa uzao mwingi, na kukuzidisha

Msemo "kukuzidishia" unaelezea jinsi ambavyo Mungu angemfanya Yakobo "kupata uzao". "Nitakupatia uzao mwingi sana"

Nitakufanya kuwa kusanyiko la mataifa

Hapa "nitakufanya" ina maana ya Yakobo, lakini ina maana ya uzao wa Yakobo. "Nitafanya vizazi vyako kuwa mataifa mengi"

milki ya milele

"milki ya kudumu"

Genesis 48:5

sasa

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

Efrahimu na Manase watakuwa wangu

Efrahimu na Manase kila mmoja atapokea sehemu ya nchi kama ndugu zake Yusufu.

watahesabiwa katika majina ya ndugu zao katika urithi wao

Maana zinawezekana kuwa 1) watoto wale wengine wa Yusufu wangerithi nchi kama sehemu ya makabila ya Efrahimu na Manase au 2) Yusufu atatengewa nchi na Efraimu na Manase na watoto wengine wa Yusufu watarithi nchi hiyo. "na kwa urithi wao, utawaorodhesha chini ya majina ya ndugu zao"

Efrathi

Hili ni jina lingine la mji wa Bethlehemu.

ndio, Bethlehemu

Mwandishi huyu anatoa taarifa ya nyuma.

Genesis 48:8

Ni nani hawa?

"Hawa ni watoto wa nani?"

niwabariki

Baba huwa anatamka baraka rasmi juu ya watoto au wajukuu wake.

Basi macho ya Israeli ... hakuweza kuona

Neno "Basi" linatumika hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwenye simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Israeli.

akawabusu

"Israeli aliwabusu"

Genesis 48:11

kuuona uso wako tena

Hapa "uso" ina maana ya mtu mzima. "Kukuona mara nyingine"

katikati ya magoti ya Israeli

Yusufu alipowaweka wanawe juu ya mapaja ya Israeli au magotini ilikuwa ishara ya kwamba Israeli alikuwa akiwachukua. Hii iliwapa watoto hawa urithi maalumu kutoka kwa Yakobo.

kisha akainama na uso wake juu ya nchi

Yusufu aliinama chini kuonyesha heshima kwa baba yake.

Manase katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kulia wa Israeli

Yusufu anawaweka wavulana ili kwamba Israeli aweze kuweka mkono wake wa kuume juu ya Manase. Manase alikuwa ndugu mkubwa na mkono wa kulia ilikuwa ishara ya kwamba angepokea baraka kubwa.

Genesis 48:14

mkono wake wa kulia na kuuweka juu ya kichwa cha Efrahimu

Kuweka mkono wa kulia juu ya kichwa cha Efraimu ilikuwa ishara ya kwamba angepokea baraka kubwa.

Israeli akambariki Yusufu

Hapa "Yusufu" pia ina maana ya Efraimu na Manase. Kwa kuwa Yusufu ni baba, ni yeye pekee anayetajwa hapa.

Mungu ambaye mbele zake baba zangu Ibrahimu na Isaka walitembea

Kumtumikia Mungu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kutembea mbele za Mungu. "Mungu ambaye babu yangu Abrahamu na baba yangu Isaka alimtumikia"

aliyenitunza

Mungu alimtunza Israeli kama vile mfugaji anavyotunza kondoo wake. "ambaye alinitunza kama mfugaji atunzavyo wanyama wake"

malaika

Maana zinawezekana kuwa 1) hii ina maana ya malaika ambaye Mungu alimtuma kumlinda Yakobo au 2) hii ina maana ya Mungu aliyemtokea kama malaika kumlinda Yakobo.

aliyenilinda

"aliniokoa"

Jina langu na litajwe kwao, na majina ya baba zangu Abrahamu na Isaka

Hapa "jina" lina maana ya mtu mzima. Msemo "jina langu na litajwe kwao" ni lahaja ambayo ina maana ya kwamba mtu anakumbukwa kwa sababu ya mtu mwingine. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Watu wamkumbuke Abrahamu, Isaka, na mimi kwa sababu ya Efraimu na Manase"

Na wawe makutano ya watu juu ya nchi

Hapa "wawe" ina maana ya Efraimu na Manase, lakini ina maana ya uzao wao. "Na wawe na uzao mwingi ambao utaishi ulimwenguni kote"

Genesis 48:17

ameweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa

Mkono wa kulia ulikuwa ishara ya baraka kubwa ambayo mwana mkubwa alitakiwa kupokea.

Genesis 48:19

Yeye naye atakuwa watu, naye pia atakuwa mkuu

Hapa "yeye" ina maana ya Manase, lakini inahusu uzao wake. "Mwana wako mkubwa atakuwa na uzao mwingi, nao watakuja kuwa taifa kubwa"

siku hiyo kwa maneno haya

Hapa "maneno" ina maana ya kile kilichosemwa. "siku hiyo, akisema"

Watu wa Israeli watatamka baraka kwa majina yenu wakisema

"Watu wa Israeli watazungumza majina yenu pale wanapowabariki wengine"

kwa majina yenu wakisema, Mungu na akufanye kama Efrahimu na kama Manase

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "kwa majina yenu. Watamuuliza Mungu kuwafanya wengine kama Efraimu na kama Manase"

kama Efrahimu na kama Manase

Israeli kusema jina la Efraimu kwanza ni njia nyingine anaonyesha ya kwamba Efraimu atakuwa mkubwa kuliko Manase.

Israeli akamweka Efrahimu mbele ya Manase

Kumpatia Efraimu baraka kubwa na kumfanya awe wa muhimu kuliko Manase inazungumziwa kana kwamba Israeli amemuweka kihalisia wa mwili Efraimu mbele ya Manase.

Genesis 48:21

atakuwa nanyi ... atawarudisha ... baba zenu

Hapa "nanyi" na "zenu" ni wingi na ina maana ya watu wote wa Israeli.

atakuwa nanyi

Hii ni lahaja yenye maana ya Mungu atasaidia na kubariki watu wa Israeli. "Mungu atakusaidia" au "Mungu atakubariki"

atawarudisha

Hapa "atawarudisha" inaweza kutafsiriwa kama "kuchukua"

nchi ya baba zenu

"nchi ya mababu zenu"

Kwako wewe, kwa kuwa uko juu ya ndugu zako, ninakupa mtelemko wa mlima

Maana zinawezekana kuwa 1) Yusufu kuwa na heshima na mamlaka zaidi kuliko ndugu zake inazungumziwa kana kwamba alikuwa juu yao kiuhalisia wa kimwili. "Kwako, ambaye ni mkubwa kuliko ndugu zako, ninakupa mteremko wa mlima" au 2) Yakobo ana maanisha anatoa nchi zaidi kwa Yusufu kuliko anavyotoa kwa ndugu wa Yusufu. "Kwako, ninakupa kilima kimoja zaidi ya nayowapatia ndugu zako. Ninakupatia mteremko wa mlima"

Kwako wewe

Hapa "wewe" ni umoja na ina maana ya Yusufu.

mteremko wa mlima niliouchukuwa kutoka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu

Hapa "upanga" na "upinde" ina maana ya kupigana vitani. "sehemu ya nchi niliyopigania na kuchukua kutoka kwa Waamori"

Genesis 49

Genesis 49:1

Maelezo ya Jumla:

Hii inaanza baraka za mwisho za Yakobo kwa wanawe. Hii inaendelea hadi 49:27. Baraka za Yakobo zinaandikwa kwa namna ya shairi.

Kusanyikeni ninyi wenyewe na msikilize, enyi wana wa Yakobo. Msikilizeni Israeli, baba yenu

Sentensi mbili zinasema jambo moja kuweka msisitizo. "Njooni na msikilize kwa makini baba yenu"

wana wa Yakobo. Msikilizeni Israeli, baba yenu.

Yakobo anajitambua katika lugha ya mtu wa utatu. Inaweza kusemwa katika lugha ya mtu wa kwanza. "wanangu. Nisikilizeni, baba yenu"

Genesis 49:3

mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, na mwanzo wa uwezo wangu

Misemo ya "mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu" na "mwanzo wa uwezo wangu" zina maana moja. Maneno "uwezo" na "nguvu" yana maana ya uwezo wa Yakobo kuzaa watoto. Maneno "mzaliwa wa kwanza" na "mwanzo" ina maana ya kwamba Rubeni ni mwanawe wa kwanza. "mwanangu wa kwanza nilipokuwa mwanamume"

aliyesalia katika heshima na nguvu

Hii inaweza kuwekwa kama sentensi mpya. "Wewe ni wa kwanza kwa heshima na nguvu" au "Unawapita wengine wote kwa heshima na nguvu"

Asiyezuilika kama maji yarukayo

Yakobo anamlinganisha Rubeni na maji yenye mkondo mwenye nguvu kusisitiza ya kwamba hawezi kujizuia hasirayake na hayupo imara.

hautakuwa na umaharufu

"hautakuwa wa kwanza miongoni mwa ndugu zako"

kwa sababu ulikwenda juu ya kitanda cha baba yako. Hata ukakitia unajisi; ulipanda juu ya kitanda changu

Hapa "kitanda" na "juu ya kitanda changu" ina maana ya suria wa Yakobo, Bilha. Yakobo ana maanisha pale ambapo Rubeni alilala na Bilha. "kwa sababu ulipanda kitandani mwangu na kulala na Bilha suria wangu. Umeniaibisha"

ulikwenda juu ya kitanda cha baba yako ... ulipanda juu ya kitanda changu

Kaluli zote mbili zina maana moja.

Genesis 49:5

Simoni na Lawi ni ndugu

Hii haimaanishi tu ya kwamba wao ni ndugu kwa kuzaliwa. yakobo anasisitiza ya kwamba walishirikiana pamoja kuwaua watu wa Shekemu.

Panga zao ni silaha za vurugu

"Wanatumia panga zao kudhuru na kuua watu"

Ee nafsi yangu ... moyo wangu

Yakobo anatumia maneno "nafsi" na "moyo" kujitambulisha na kusema ya kwamba watu wengine, na labda Mungu pia, wanamheshimu sana ya kwamba hatamani kujiunga na wale wanaopanga kufanya uovu.

usiingie barazani pao; usiingie katika mikutano yao

Misemo hii miwili ina maana moja. Yakobo anaunganisha kuweka msisitizo ya kwamba hataki kushirikiana katika mipango yao miovu. "hakika sitajiunga nao kufanya mipango yoyote"

kuwakata visigino ng'ombe.

Hii ina maana ya Simoni na Lawi kulemaza ng'ombe kwa starehe tu.

kuwakata visigino

Hii ina maana ya kukata visigino vya miguu ya wanyama ili isiweze kutembea.

Genesis 49:7

Hasira yao na ilaaniwe, kwani ilikuwa kali - na ukali wao, kwani ulikuwa ni katili

Mungu kumlaani Simoni na Lawi inazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa akilaani hasira na ukali wao. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Bwana anasema, 'Nitawalaani kwa sababu ya hasira yao kali na ukali wao mkatili" au "Mimi, Bwana, nitawalaani kwa sababu ya hasira ya kali na ukali wao mkatili"

Hasira yao na ilaaniwe

Katika unabii, nabii mara nyingi huzungumza maneno ya Mungu kana kwamba Mungu mwenyenwe alikuwa akizungumza. Hii inasisitiza ukaribu ulivyo kati ya nabii na Mungu.

na ukali wao, kwani ulikuwa ni katili

Neno "nitalaani" linaeleweka. "nami nitalaani ukali wao, maana ulikuwa katili"

Nitawagawa katika Yakobo na kuwatawanya katika Israeli

Neno "Nitawagawa" lina maana ya Mungu. Neno "kuwatawanya" lina maana ya Simoni na Lawi lakini ni lugha nyingine yenye maana ya uzao wao. Maneno "Yakobo" na "Israeli" ni lugha nyingine yenye maana ya watu wote wa Israeli. "Nitawagawanya uzao wao na kuwasambaza miongoni mwa watu wote wa Israeli"

Genesis 49:8

ndugu zako watakusifu ... Wana wa baba yako watainama mbele zako

Kauli hizi mbili zina maana moja.

watakusifu. Mkono wako

Sentensi ya pili inaeleza sababu ya sentensi ya kwanza. Neno "kwa" au "kwa sababu" linaweza kuongezwa kuweka hii wazi. "nitakusifu wewe. Kwa mkono wako" au "nitakusifu kwa sababu mkono wako"

Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako

Hii ni njia ya kusema. "Utawashinda adui zako"

watainama

Hii ina maana kuinama kwa unyenyekevu kuonyesha heshima na taadhima kwa mtu.

Genesis 49:9

Yuda ni mwana simba

Yakobo anamzungumzia Yuda kana kwamba alikuwa mtoto wa simba. Yakobo anasisitiza nguvu ya Yuda. "Yuda ni kama mwana wa simba"

Mwanangu, umetoka katika mawindo yako

"Wewe, mwanangu, umerudi kutoka kula windo lako"

kama simba jike

Yakobo anamlinganisha Yuda na simba jike. Simba jike ni mwindaji na mlinzi wa msingi wa watoto wake.

Je nani atakayejaribu kumwamsha?

Yakobo anatumia swali kusisitiza jinsi Yuda anavyotisha watu wengine. "Hakuna atakaye kumuamsha"

Genesis 49:10

Fimbo haitaondoka katika Yuda, wala fimbo ya utawala kutoka katika miguu yake

"Fimbo" na "fimbo ya utawala" ni miti iliyopambwa ambayo wafalme hubeba. Hapa ni lugha nyingine yenye maana ya nguvu ya utawala. Na "Yuda" ina maana ya uzao wake. "Nguvu ya kutawala daima itakuwa ndani ya uzao wa Yuda"

hata atakapo kuja Shilo. Mataifa yatamtii

Maana zawezekana kuwa 1) "Shilo" ina maana "shukrani". "hadi pale mataifa yatamtii na kuleta shukrani kwake" au 2) "Shilo" ina maana ya mji wa Shilo. "hadi pale mtawala atakuja Shilo. Kisha mataifa yatamtii." Watu wengi huchukulia hili kama unabii kuhusu Mesia ambaye ni uzao wa Mflame Daudi. Daudi ni uzao wa Yuda.

Mataifa yatamtii

Hapa "mataifa" ina maana ya watu. "Watu wa mataifa watamtii"

Genesis 49:11

Kumfunga punda wake ... katika mzabibu mzuri

Kauli zote mbili zina maana moja. Inasemekana ya kwamba mizabibu imejaa zabibu ambayo bwana hajali kama punda inavila baadhi yao.

wake ... amefua

Maana za muonakano wa "wake" au "amefua" ni 1) ina maana ya uzao wa Yuda. "wake ... wame" au 2) ina maana ya mtawala katika 49:10, ambayo inaweza kumaanisha Mesia.

amefua ... katika damu ya vichala vya mzabibu

Kauli zote mbili zina maana moja. Inasemekana ya kwamba kuna zabibu nyingi sana hadi wanaweza kufua nguo zao kwa maji yake.

amefua

Mara nyingi katika unabii matukio yatakoyotokea hapo baadae yanaelezwa kama jambo lililokwisha tokea zamani. Hii inasisitiza ya kwamba tukio hili hakika litatokea. "watafua" au "atafua"

damu ya vichala vya mzabibu

HIi inazungumzia kuhusu maji ya zabibu kana kwamba yalikuwa damu. Hii inasisitiza jinsi gani maji yalikuwa mekundu.

Macho yake yatakuwa meusi kama mvinyo

Hii ina maana ya rangi ya macho ya mtu kulinganisha na rangi ya mvinyo mwekundu. Maana zaweza kuwa 1) macho meusi ina maana macho yenye afya au 2) macho ya watu yatakuwa mekundu kutokana na kunywa mvinyo mwingi

meno yake meupe kama maziwa

Hii inalinganisha rangi ya meno ya watu kwa weupe wa rangi ya maziwa. Hii inasemekana ya kwamba kutakuwa na ng'ombe wengi wenye afya na kuwa na maziwa mengi ya kunywa.

Genesis 49:13

Zabuloni atakaa

Hii ina maana ya uzao wa Zabuloni.

Atakuwa bandari

Hapa "atakuwa" ina maana ya miji ya baharini ambayo watu wa Zabuloni wataishi au kujenga. Miji hii itatoa hifadhi kwa meli.

bandari

sehemu ya bahari ambayo ipo karibu na nchi na ipo salama kwa ajili ya meli.

Genesis 49:14

Isakari ni punda mwenye nguvu

Yakobo anazungumzia kuhusu Isakari na uzao wake kana kwamba walikuwa punda. Hii inasisitiza ya kwamba watafanya kazi kwa bidii. "Uzao wa Isakari utakuwa kama punda mwenye nguvu"

Isakari ni

Mara nyingi katika unabii matukio ambayo yatatokea baadae inaelezwa kama kitu ambacho tayari kinaendelea. Hii inasisitiza ya kwamba tukio litatokea hakika. Inaweza kuwekwa kwa lugha ya baade. "Isakari atakuwa" au "Uzao wa Isakari utakuwa"

Isakari ... Anaona ... Atainamisha

Hapa "Isakari" ni lugha nyingine yenye maana ya uzao wake. "Uzao wa Isakari ... Wanaona .. Wataona"

ajilazaye kati ya kondoo

Maana zaweza kuwa 1) "ajilazaye chini katikati ya kundi walizokuwa wakibeba" au 2) "ajilazaye chini katikati ya zizi la kondoo".Kwa namna yoyote ile, Yakobo anazungumzia kuhusu uzao wa Isakari kana kwamba walikuwa punda ambao wamefanya kazi kwa bidii na wamejilaza chini kupumzika.

mahali pazuri pa kupumzikia na nchi ya kupendeza

"sehemu ya kupumzikia ambayo ni nzuri na kwamba nchi inapendeza"

Atainamisha bega lake kwa mzigo

Msemo huu "Atainamisha bega lake kwa mzigo" ni njia ya kusema "fanya kazi kwa bidii kubeba mzigo"

kuwa mtumishi wake kwa kazi ile

"watafanya kazi kwa wengine kama watumwa"

Genesis 49:16

Dani atawaamua watu wake

Hapa "Dani" ina maana ya uzao wake. "Uzao wa Dani utawaamua watu wake"

watu wake

Maana zinazowezekana za "watu wake" ni 1) "watu wa Dani" au 2) "watu wa Israeli"

Dani atakuwa nyoka kando ya njia

Yakobo anazungumza kuhusu Dani na uzao wake kana kwamba walikuwa nyoka. Ingawa nyoka ni mdogo, inaweza kumshusha aongozaye farasi chini ya farasi wake. Kwa hiyo Dani, ingawa kabila dogo, ni la kutisha sana kwa adui zake. "Uzao wa Dani utakuwa kama nyoka kando ya barabara"

Ninaungoja wokovu wako, Yahwe.

Nomino inayojitegemea "wokovu" inaweza kutafsiriwa kama "kuokoa". "Ninakusubiri, Yahwe, kunikoa"

Ninaungoja

Neno "Ninaungoja" ina maana ya Yakobo.

Genesis 49:19

Gadi ... Asheri ... Naftali

Hawa ina maana ya vizazi vya kila mwanamume.

katika visigino vyao

Hapa "visigino" ina maana ya wavamizi ambao wanatoroka kutoka kwa uzao wa Gadi.

Vyakula vitakuwa vingi

Hapa "vingi" ni njia ya kusema "vitamu"

Naftali ni dubu jike asiyefungwa

Yakobo anazungumzia kuhuus uzao wa Naftali kana kwamba walikuwa paa wa kike ambaye yupo huru kukimbia. Hii inaweza kusisitiza ya kwamba watakuwa wajumbe wepesi. "Uzao wa Naftali utakuwa kama paa aliyeachiwa huru"

atakuwa na watoto wa dubu walio wazuri

"mtoto wa paa". Maana kwa lugha ya Kihebrania haipo wazi. Baadhi ya tafsiri hutafsiri kama "ana maneno mazuri" au "kuzungumza mambo mazuri"

Genesis 49:22

Yusufu ni tawi lizaalo

Hapa "Yusufu" ni lugha nyingine yenye maana ya uzao wake. Yakobo anazungumzia uzao kana kwamba walikuwa shina la mti lizaalo matunda mengi. Hii inasisitiza ya kwamba wataongezeka sana kwa idadi.

tawi

shina kuu la mti

ambaye matawi yake yako juu wa ukuta

Shina ambalo litakuwa na kusambaajuu ya ukuta inazungumziwa kana kwamba ilikuwa inapanda.

Genesis 49:24

Maelezo ya Jumla:

Yakobo anaendelea kumbariki Yusufu na uzao wake.

upinde wake utakuwa imara

Mtu anayeshikilia upinde kwa umakini inazungumziwa kana kwamba uoinde mwenyewe utakuwa imara. Inasemekana anaushikilia kwa ustadi anapopima kwa adui wake. "ataushika upinde wake kwa uimara anapolenga adui wake"

upinde wake ... mikono yake

Hapa "wake" ina maana ya Yakobo anayesimama badala ya uzao wake. "upinde wake .. mikono yake"

mikono yake itakuwa hodari

Hapa "mikono" ina maana ya mikono ya mtu anaposhikilia upinde wake kwa makini. "mikono yake utabaki imara anapolenga upinde wake"

mikono ya Mwenye nguvu

"mikono" inaelezea nguvu ya Yahwe. "nguvu ya Mwenye Nguvu"

kwa ajili ya jina la Mchungaji

Hapa "jina" lina maana ya mtu mzima. "kwa sababu ya Mchungaji"

Mchungaji

Yakobo anamzungumzia Yahwe kana kwamba alikuwa "mchungaji". Hii inasisitiza ya kwamba Yahwe anawaongoza na kuwalinda watu wake.

Mwamba

Yakobo anazungumzia kuhusu Yahwe kana kwamba alikuwa "Mwamba" ambao watu wanaweza kuupanda kutafuta usalama kutoka kwa maadui. Hii inasisitiza ya kwamba Yahwe hulinda watu wake.

Genesis 49:25

Maelezo ya Jumla:

Yakobo anaendelea kumbariki Yusufu na uzao wake.

atakusaidia ... atakubariki

Hapa "atakusaidia" ina maana ya Yusufu inayomaanisha uzao wake. "saidia uzao wako ... wabariki"

baraka za mbinguni juu

Hapa "mbinguni juu" ina maana ya mvua ambayo husaidia mazao kuota.

baraka za vilindi vilivyo chini

Hapa "chini" ina maana ya maji chini ya ardhi ambayo hutosheleza mito na visima.

baraka za maziwa na tumbo

Hapa "maziwa na tumbo" ina maana ya uwezo wa mama kupata watoto na kuwanyonyesha maziwa.

Genesis 49:26

Maelezo ya Jumla

Yakobo anaendelea kumbariki Yusufu na uzao wake.

milima ya zamani

Maana ya lugha asili haipo wazi. Baadhi ya tafsiri za Biblia zina "mababu zangu" badala ya "milima ya zamani"

Na viwe katika kichwa cha Yusufu

Hapa "viwe" ina maana ya baraka za baba yake.

juu ya taji ya kifalme kichwani pa ndugu zake

Yakobo anatamani kwa baraka hizi kupitishwa hata kwa wale wazawa muhimu. "juu ya kichwa cha mzawa muhimu wa Yusufu"

mwana wa mfalme kwa ndugu zake

"mtu muhimu wa ndugu zake"

Genesis 49:27

Benjamini ni mbwamwitu mwenye njaa

Hapa "Benyamini" ni lugha nyingine ya uzao. Yakobo anazungumzia juu ya uzao wa Benyamini kana kwamba ulikuwa mbwa mwitu wenye njaa. Hii inasisitiza ya kwamba watakuwa wapiganaji hodari. "Uzao wa Benyamini watakuwa kama mbwa mwitu"

Genesis 49:28

Haya ni makabila kumi na mbili ya Israeli

"Haya" ina maana ya wana wa Yakobo waliotajwa katika 49:1-27. Kila mwana alikuwa kiongozi wa kabila lake mwenyewe.

alipowabariki

Hapa neno "alipowabariki" lina maana ya kuongelea baraka rasmi.

kila mmoja kwa baraka iliyomstahili

"Akawapa kila mtoto baraka inayomstahili"

akawaelekeza

"akawaamuru"

Ninakaribia kwenda kwa watu wangu

Hii ni njia ya upole ya kusema ya kwamba amekaribia kufa. "Nimekaribia kufa"

kwenda kwa watu wangu

Yakobo ana maanisha pale ambapo nafsi yake utakwenda atakapokufa. Anategemea kuwaunga Abrahamu na Isaka katika maisha ya baadae.

Efroni Mhiti

Hili ni jina la mwanamume. "Mhiti" ina maana ya "uzao wa Hethi".

Makpela

Makpela lilikuwa jina la eneo au mahali.

Mamre

Hili lilikuwa jina lingine la mji wa Hebroni. Inawezekana lilitajwa baada ya Mamre, rafiki wa Abrahamu aliyeishi kule.

Genesis 49:31

Maelezo ya Jumla:

Yakobo anaendelea kuzungumza na wanawe.

lililomo lilinunuliwa

Ununuzi unaweza kuwekwa wazi. "ndani mwake ulinunuliwa na Abrahamu"

kutoka kwa watu wa Hethi

"kutoka kwa Wahiti"

alipomaliza maagizo hayo kwa wanawe

"alimaliza kuwaagiza wanawe" au "alimaliza kuwaamuru wanawe"

akaiweka miguu yake kitandani

Yakobo alikuwa amekaa juu ya kitanda. Sasa, Yakobo anageuka na kuweka miguu yake kitandani ili aweze kulala chini.

akavuta pumzi ya mwisho

Hii ni njia ya upole ya kusema mtu amekufa.

akawaendea watu wake

Baada ya Yakobo kufa, nafsi yake ilikwenda sehemu ile ile kama ndugu zake waliokufa kabla yake.

Genesis 50

Genesis 50:1

akauangukia uso wa baba yake

Msemo "akauangukia" ni lahaja ya kuzidiwa. "hadi akaanguka juu ya baba yake kwa majonzi"

watumishi wake matabibu

"watumishi wake ambao waliangalia maiti"

kumtia dawa babaye

"kumtia dawa" ni njia maalumu ya kuhifadhi maiti kabla haijazikwa. "kuandaa mwili wa baba yake kabla ya mazishi"

Wakatimiza siku arobaini

"Wakatimiza siku 40"

siku sabini

"siku 70"

Genesis 50:4

Siku za maombolezo

"siku za kumuomboleza" au "siku za kumlilia"

Yusufu akaongea na watumishi wa baraza la kifalme

Hapa "baraza la kifalme" ina maana ya maafisa ambao huunda baraza la kifalme la Farao. "Yusufu alizungumza na maafisa wa Farao"

Ikiwa nimepata kibali machoni penu

Msemo "machoni penu" ni lugha nyingine yenye maana ya fikra na mawazo ya Yakobo. "Iwapo nimepata kibali kwako" au "kama umefurahishwa na mimi"

nimepata kibali

Hii ni lahaja yenye maana ya kwamba mtu amekubalika na mtu mwingine.

tafadhali ongeeni na Farao, kusema, 5'Baba yangu aliniapisha, kusema, "Tazama, ninakaribia kufa. Unizike katika kaburi nililolichimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani. Ndipo utakaponizika." Basi sasa niruhusu niende nimzike baba yangu, na kisha nitarudi."

Hii ina madaraja mawili ya nukuu na madaraja matatu ya nukuu. Hizi zinaweza kuwekwa kama nukuu zisizo moja kwa moja. "tafadhali mwambie Farao ya kwamba baba yangu alinifanya niape ya kuwa baada ya kufa kwake nitamzika katika kaburi ambalo alilichimba kwa ajili yake katika nchi ya Kaanani. Tafadhali muombe Farao aniruhusu niende kumzika baba yangu, na kisha nitarudi.

Tazama, ninakaribia kufa

"Tazama, ninakufa"

niruhusu niende juu

Ilikuwa kawaida kutumia msemo "kwenda juu" pale izungumzwapo safari ya kutoka Misri kwenda Kaanani.

Farao akajibu

Inasemekana ya kwamba wajumbe wa baraza walizungumza na Farao, na sasa Farao anamjibu Yusufu.

kama alivyokuwapisha

"kama ulivyoapa kwake"

Genesis 50:7

Yusufu akaenda juu

Ilikuwa kawaida kutumia msemo "kwenda juu" inapozungumziwa safari ya kutoka Misri kwenda Kaanani.

Maofisa wote ... washauri ... maofisa waandamizi

viongozi wote muhimu wa Farao walihudhuria tukio la mazishi.

washauri

Huyu mtu alikuwa mshauri wa kifalme.

washauri wa nyumba yake

Hapa "nyumba" ina maana ya baraza la kifalme la Farao.

nchi ya Misri, pamoja na nyumba yote ya Yusufu na ndugu zake, na nyumba yote ya baba yake

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "nchi ya Misri. Nyumba ya Yusufu, ndugu zake, na nyumba ya baba yake walikwenda naye"

nyumba ya Yusufu ... nyumba ya baba yake

Hapa "nyumba" ina maana ya familia zao.

Vibandawazi

Hapa ina maana ya wanamume wanaoendesha ndani ya vibandawazi.

Lilikuwa kundi kubwa sana la watu

"ulikuwa mkusanyiko mkubwa sana"

Genesis 50:10

Hata walipokuja

Neno "walipokuja" lina maana ya washiriki katika tukio la mazishi.

sakafu ya Atadi

Maana zaweza kuwa 1) neno la "Atadi" lina maana ya "mwiba" na lina maana ya sehemu ambapo kuna idadi kubwa ya miiba inayoota, au 2) inaweza kuwa jina la mtu anayemiliki sakafu ya kupigia.

wakaomboleza kwa majonzi ya huzuni kubwa

"walikuwana huzuni kubwa na walilia sana"

ya siku saba

"ya siku 7"

katika sakafu ya Atadi

"katika sakafu ya kupigia ya Atadi"

Hili ni tukio la kuhuzunisha sana kwa Wamisri

"maombolezo ya Wamisri ni mkubwa sana"

Abeli Mizraimu

"Jina la Abeli Mizraimu lina maana ya "maombolezo ya Misri"

Genesis 50:12

wanawe

"Kwa hiyo wana wa Yakobo"

kama alivyokuwa amewaagiza

"kama alivyokuwa amewaagiza"

Wanawe wakambeba

"Wanawe waliuchukua mwili wake"

Makpela

Makpela ni jina la jina la eneo au sehemu.

Mamre

Hili lilikuwa jina jingine la mji wa Hebroni. Inawezekana lilikuwa jina baada ya Mamre, rafiki wa Abrahamu aliyeishi kule.

Efroni Mhiti

Hili ni jina la mwanamume. "Mhiti" ina maana ya "uzao wa Hethi"

Yusufu akarudi Misri

"Yusufu alirudi Misri"

wote waliokuwa wamemsindikiza

"wale wote waliokuja pamoja nami"

Genesis 50:15

Itakuwaje ikiwa Yusufu atatukasirikia

Hapa hasira inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kitu cha kimwili ambacho Yusufu alikishika kwa mkono wake. "Je iwapo Yusufu atakuwa bado na hasira na sisi"

akataka kutulipa kikamilifu kwa ajili ya uovu tuliomtenda

Kulipiza mwenyewe dhidi ya mtu mwingine aliyemdhuru inazungumziwa kana kwamba mtu alikuwa akilipa mtu mwingine kile walichodai. "anataka kulipiza kwa uovu tuliofanya kwake"

Baba yako alitoa maelekezo kabla hajafa, kusema, 'Mwambieni hivi Yusufu, "Tafadhali samehe makosa ya ndugu zako na dhambi yao uovu waliokutenda."

Hii ina madaraja mawili ya nukuu na madaraja matatu ya nukuu. Zinaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Baba yako alituagiza kabla ya kufa tukuambie ya kwamba utusamehe kwa uovu tuliokufanyia kwako"

Baba yako alitoa maelekezo kabla hajafa, kusema

Yakobo alikuwa baba wa ndugu wote. Hapa wanasema "baba yako" kusisitiza ya kwamba Yusufu anahitaji kuvuta nadhari kwa kile baba yake alichosema. "Kabla baba yetu hajafa alisema"

na dhambi yao uovu waliokutenda

"kwa mambo maovu waliyokufanyia kwako"

Basi

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

Basi wasamehe watumishi wa Mungu wa baba yako

Ndugu wanajitambulisha kama "watumishi wa Mungu wa baba yako". Hii inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa kwanza. "tafadhali tusamehe, watumishi wa Mungu wa baba yetu"

Yusufu akalia walipomwambia.

"Yusufu alilia aliposikia ujumbe huu"

Genesis 50:18

kuinamisha nyuso zao mbele zake

Walilala chini kifudifudi kuelekea ardhini. Hii ni ishara ya unyenyekevu na heshima kwa Yusufu.

Je mimi ni badala ya Mungu?

Yusufu anatumia swali kuwatia moyo ndugu zake. "Mimi sipo katika nafasi ya Mungu" au "Mimi sio Mungu"

mlikusudia kunidhuru

"mlikusudia kutenda uovu dhidi yangu"

Mungu alikusudia mema

"Mungu alikusudia kwa wema"

Hivyo basi msiogope

"Kwa hiyo msiniogope"

Nitawahudumia ninyi na watoto wenu wadogo

"Nitahakikisha nyie pamoja na watoto wenu mnapata chakula cha kutosha"

aliwatia moyo na kuongea na mioyo yao kwa upole.

"Aliwatia moyo kwa kuzungumza nao kwa upole"

Genesis 50:22

miaka mia moja na kumi

"miaka 110"

Efraimu hata kizazi cha tatu

"Watoto na wajukuu wa Efraimu"

Makiri

Hili ni jina la mjukuu wa Yusufu"

waliowekwa katika magoti ya Yusufu

Msemo huu una maana ya kwamba Yusufu alitwaa watoto hawa wa Makiri kama watoto wake. Hii ina maana wangekuwa na haki ya urithi maalumu kutoka kwa Yusufu.

Genesis 50:24

atawajilia

Katika 50:24 neno "atawajilia" lina maana ya ndugu wa Yusufu, lakini pia lina maana ya uzao wake.

kuwaongoza kutoka katika nchi hii na kuwapeleka katika nchi

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "kupanda" kuzungumzia safari ya kutoka Misri kwenda Kaanani. "kuwaleta kutoka nchi hii na kuwapeleka katika nchi"

Wakampaka dawa

"kumpaka dawa" ni njia maalumu ya kuhifadhi maiti kabla haujazikwa.

akawekwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "walimweka"

katika jeneza

"ndani ya sanduku" au "katika kasha". Hili ni sanduku ambalo mtu aliyekufa kuwekwa ndani.