Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Judges 1

Judges 1:1

Sentensi unganishi

Kitabu cha Waamuzi kinaendeleza simulizi ya Yoshua na pia ni mwanzo wa simulizi nyingine mpya.

atawashambulia Wakanaani kwa ajili yetu,

Neno "yetu" linamaanisha wana wa Israeli

Yuda atawashambulia

Hapa "Yuda" linawakilisha watu wa kabila la Yuda. Mungu anawaamuru watu hawa kushambulia kwanza. "Watu wa Yuda watashambulia kwanza"

Tazama

"Angalia" au "kweli". Hii inaongeza msisitizo wa kile kinachofuata.

Nchi hii

Hii inamaanisha nchi ambayo Wakanaani waliishi. "nchi ya Wakanaani"

Ndugu zao

"waisraeli wenzao" au "ndugu zao"

Njooni pamoja nasi

Watu wa kabila la Yuda na Simeoni waliweka kambi pamoja na Waisraeli katika bonde la mto Yordani. Yuda alipewa nchi ambayo ipo kwenye vilima juu ya bonde. Lugha zingine hazijaelezea kama watu walikwenda juu au chini. "njooni pamoja nasi" au "twendeni pamoja"

ambalo tulipewa... ambali mlipewa

"Ambalo Bwana alitupa sisi... ambalo Bwana aliwapa ninyi"

Tutakwenda pamoja nanyi

"sisi pia tutakwenda pamoja nanyi" au "kwa namna ile ile tutakwenda pamoja nanyi"

Judges 1:4

Watu wa Yuda wakavamia

Inamaanisha kwamba watu wa Simoni walivamiwa na watu wa Yuda.

Wakawaua watu elfu kumi

"waliwaua watu takribani 10,000" au "waliua idadi kubwa ya watu"

Hao

"askari Wakanaani na Waperizi" au "maadui"

Bezeki

Hili ni eneo la milima ya Kanaani

Adoni Bezeki

Alikuwa kiongozi wa jeshi la Wakanaani na Waperizi

Wakapigana naye

"naye" inamuelezea Adoni Bezeki na jeshi lake. "walipigana naye pamoja na jeshi lake"

Judges 1:6

Wakamfuata

"wakamkimbiza"

Wafalme sabini

"Wafalme 70"

walikusanya chakula chao chini ya meza yangu

"walikula vipande vya chakula chili ya meza yangu." Aliwalazimisha hawa wafalme kula vipande vya chakula inaonesha namna gani Adoni Bezeki alivyowanyanyasa hawa wafalme.

ambao na vidole gumba vyako na vidole vikubwa vilikatwa

"niliwaambia watu wangu wavikate vidole gumba vyao na vidole vikubwa"

Judges 1:8

jiji la Yerusalemu na kulichukua

Hapa "jiji" lina maanisha watu. "watu wanaoishi Yerusalemu na kuwashinda"

Walishambulia

Walishambulia jiji linaliwakilisha watu wa mji. "Walishambulia watu wa jiji"

kwa makali ya upanga

Hapa "Upanga" inamaanisha upanga au silaha nyingine inayotumiwa na askari vitani. "na upanga wao" au "na silaha zao"

watu wa Yuda walikwenda chini kupigana

Ilikuwa kawaida kutumia neno chini ikiwa ina maanisha kusafiri toka Yerusalemu. "Watu wa Yuda walikwenda kupigana"

Negebu

Kusini mwa jangwa la Yuda

Milima

vilima vilivyo chini ya mlima.

jina la Hebroni hapo awali ilikuwa Kiriath-arba

Hii ni taarifa. baadhi ya watu ambao walisoma kitabu hiki mwanzoni yamkini walisikia juu ya Kiriath-arba lakini hawakufahamu kuwa ilikuwa ni mji wa Hebroni.

Sheshai, Ahimani na Talmai

Haya ni majina ya viongozi watatu wa Kikanaani wa Hebroni. Kila kiongozi anawakilisha jeshi lake.

Judges 1:11

Maelezo ya jumla

Tazama: tafsiri ya majina

jina la Debiri hapo awali ilikuwa Kiriath-seferi

Mwandishi aliandika hivi kwa kuwa yamkini wasomaji wake walifahamu juu ya mji wa Debiri. lakini wakati ambao Israeli walivamia palikuwa pakiitwa Kiriath-seferi.

Awali

"siku za nyuma" au "wakati wa nyuma"

Yeyote atakayeivamia Kiriath-seferi na kuichukua

"Kiriath-seferi" ina maanisha watu. Yeyote atakayeivamia na kuiteka Kiriath-seferi na kuchukua mji wao"

Aksa

Jina la binti wa Kalebu

Otinieli, mwana wa Kenazi

Haya ni majina ya wanaume

Judges 1:14

Akamsihi

"Aksa akamsihi Othnieli"

akampa nchi ... kwa kuwa umenipa nchi

Hii inaelezea kuwa Kalebu alimpa nchi aliyoiomba katika sura ya 14. Katika sura ya 15 anaomba sasa na chemichemi ya maji.

Nibariki

"Nepe neema" au "Nifanyie hivi"

Kwa kuwa umenipa nchi ya Negebu

Kalebu alimpa Aksa aolewe na Othnieli, hivyo aliishi pamoja na Othnieli katika mji waliouteka Negebu.

Judges 1:16

Mkwe wake na Musa

"mkwe" "baba yake na mke wa musa"

Mkeeni, mkwe alikwenda

"mkwe ambaye alikuwa ni moja ya watu wa Keeni, alikwenda"

walikwenda kutoka mji wa Mitende ... mpaka jangwa

"aliondoka kwenye mji wa mitende ... akaenda jangwani"

Mji wa mitende

Hili ni jina lingine la mji wa Yeriko

Arad

Hili ni jina la mji wa Kanaani

wana wa Simeoni ndugu zao

"ndugu" hii inamaanisha ndugu waliopo katika kabila lingine la Israeli.

Zefathi

Hili ni jina la mji wa Kanaani

Mji uliitwa Horma

Baada ya Israeli kuiharibu Zefathi, walibadilisha jina na kupaita Horma. Jina Horma lina maana ya "uharibifu kamili."

Judges 1:18

Yahweh alikuwa pamoja na watu wa Yuda

"alikuwa pamoja" ina maana ya kwamba Bwana aliwasaidia watu wa Yuda.

Bonde

eneo kubwa lisilo na miti

Judges 1:20

Hebroni alipewa Kalebu (kama Musa alivyosema)

"Musa alimkabidhi Hebroni kwa Kalebu"

wana watatu wa Anaki

Viongozi wa watu wa kundi wamezoea kumaanisha kundi zima. "wana watatu wa Anaki na watu wao"

Anaki

Hili ni jina la mtu. Uzao wake wana sifa ya kuwa warefu sana wa kimo.

Hata leo

"mpaka sasa" Hii inamaanisha wakati kitabu cha Waamuzi kilipokuwa kinaandikwa.

Judges 1:22

Nyumba ya Yusufu

Hapa "Nyumba" inamaanisha uzao. Manase na Efraimu walikuwa watoto wa Yusufu na "nyumba ya Yusufu" inaweza kuwa na maana ya uzao wa Manase na Efraimu. "uzao wa Manase na Efraimu"

kushambulia Betheli

"Betheli" inamaanisha watu wanaoishi Betheli.

peleleza

kupata taarifa kwa siri

jiji lililoitwa Luzu

Hii ni taarifa. watu wengine waliosoma kitabu hiki kwa mara ya kwanza yamkini walisikia kuhusu Luzu ila hawakufahamu kuwa ni sawa na mji ulioitwa Betheli.

Wapelelezi

Watu wanaopata taarifa kwa siri

Judges 1:25

Waliuteka mji

"mji" inamaanisha watu. " Waliwateka watu wa mji"

kwa makali ya upanga

Hapa "Upanga" inamaanisha upanga au silaha nyingine inayotumiwa na askari vitani. "na upanga wao" au "na silaha zao"

Waondoke

"toroka"

Luzu

Mji huu mpya ulianza katika nchi ya Wahiti.

ambalo jina lake hata leo.

"ambalo bado ni jina lake.

Judges 1:27

Bethsheani ...Taanaki ... Dori ... Ibleamu ... Megido

Haya ni majina ya miji

kwa sababu Wakanaani walikuwa wameamua kuishi katika nchi hiyo

"kwa sababu Wkanaani waliamua kwa dhati kuwa hawataiacha hiyo nchi"

Israeli ipokuwa na nguvu

"Israeli" inamaanisha watu. "Watu wa Israeli walipokuwa na nguvu"

waliwalazimisha Wakanaani wawatumikie kwa kazi ngumu

"Waliwalazimisha wakaanani wawafanyie kazi ngumu"

Judges 1:29

Efraimu hakuwafukuza

"Efraimu" ni watu au askari wa kabila la Efraimu.

Gezeri

Jina la mji katika Efraimu.

Judges 1:30

Zebuloni hakuwafukuza

"Zebuloni" ni watu au askari wa kabila la Zebuloni.

Kitroni ... Nahaloli

Haya ni majina ya mji katika nchi ya Kanaani.

lakini Zebuloni akawalazimisha

"Zebuloni" ni watu wa kabila la Zebuloni.

kazi ngumu

"kazi ngumu"

Judges 1:31

Asheri hakuwafukuza

"Asheri" linamaanisha watu au askari wa kabila la Asheri.

Aka ... Sidoni ...Alabu, Akzib, Helba, Afeka ... Rehobu.

Haya ni majina ya miji katika nchi ya Kanaani.

Judges 1:33

Bethshemeshi ... Bethanathi.

Hata ni majina ya miji

wenyeji wa Bethshemeshi na Bethanathi walilazimishwa kufanya kazi ngumu kwa Naphthali.

Hii inaweza kutafsiriwa kama "watu wa Naftali walilazimishwa na watu wa Bethshemeshi naa Bethanathi kuwafanyia kazi kama watumwa.

Judges 1:34

Maelezo ya jumla

Tazama; tafsiri ya majina

hawakuwaruhusu kuja bondeni

"aliwakataza kushuka bondeni"

bonde

eneo kubwa la ardhi lisilo na miti

Mlima wa Heresi

Hili ni jina la mlima mkubwa ambapo mji wa Aiyaloni ulijengwa.

Aiyaloni... Shaalbimu,

Haya ni majina ya miji

nguvu za kijeshi za nyumba ya Yusufu ziliwashinda

"kabila la watu wa uzao wa Yusufu waliweza kuwashinda kwa sababu walikuwa na jeshi lenye nguvu"

Nyumba ya Yusufu

Hapa "Nyumba" inamaanisha uzao. Manase na Efraimu walikuwa watoto wa Yusufu na "nyumba ya Yusufu" inaweza kuwa na maana ya uzao wa Manase na Efraimu. "uzao wa Manase na Efraimu"

kilima cha Akrabimu

Hiki kilikuwa njiani kusini mashariki na Bahari ya shamu. Pia inaitwa "njia ya nge"

Sela

Hili ni jina la mji

Judges 2

Judges 2:1

Malaika wa Bwana

yaweza kuwa na maana ya 1) "malaika anayemuwakilisha Bwana" au 2) "malaika anayemtumikia Bwana" au 3) yaweza kumaanisha Bwana mwenyewe, aliyeonekana kama malaika akiwa anazungumza na mtu.

akatoka Gilgali, akaenda Bokimu

"akaondoka Gilgali akaenda Bokimu"

Bokimu

Wana wa Irsaeli walipaita mahali hapa katika sura ya 2:5 baada ya malaika kuwakemea watu. "Bokimu" ina maana ya "kilio"

akasema

inaeleweka kuwa malaika wa Bwana alikuwa akizungumza na wana wa Israeli. "akasema na wana wa Israeli"

Nimekuleta kutoka Misri

"nimekutoa Misri"

Baba zako

"mababu zako"

kuvunja agano langu na wewe

"kushindwa kufanya yale niliyopaswa kufanya kwako"

Haukuisikiliza sauti yangu

"sauti" ina maanisha alichokisema Bwana. "haukusikiliza ammri zangu"

Ni nini hiki ulichokifanya?

Swali hili linaulizwa ili kuwafanya wana wa Israeli wagundue kuwa hawajamtii Mungu na watateseka kwa sababu hiyo. "Mmefanya jambo baya"

Judges 2:3

Maelezo ya jumla

Malaika wa Bwana anaendelea kuzungumza na wana wa Israeli.

Basi sasa nasema, "Sitawafukuza... miiba kwenu

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. "Basi sasa nawaambia sitawafukuza ... miiba kwenu.'"

watakuwa miiba kwenu

Wakanaani wanaowasumbua Waisraeli wanazungumzwa kuwa Wakanaani watakuwa miiba kwa Waisraeli. "watawasababishia matatizo"

Miiba

Kipande cha mbao chenye ncha kali mpaka sentimeta 7 ambacho huchomoza pembeni ya mmea.

miungu yao itakuwa mtego kwa ajili yenu

Waisraeli kuabudu miungu ya Wakanaani ni sawa na miungu ya uongo inayofananishwa na mtego wa mwindaji unaowakamata wanyama na kusababisha madhara.

wakapiga kelele na kulia

"wakalia machozi mengi"

Judges 2:6

Sasa Yoshua

"Sasa" imetumika kama alama ya kituo toka kwenye simulizi. Hapa mwandishi anaanza kwa kuelezea uzao wa Israeli baada ya Yoshua kuasi na kuabudu miungu ya uongo na Bwana akawaadhibu, lakini atawatuma waamuzi kuja kuwaokoa.

Yoshua alipo ... alikufa akiwa na umri wa miaka 110

Matukio ya 1:1-2:5 yalitokea baada ya Yoshua kufa. Hapa inahesabu matukio yaliyotokea mwishoni mwa kitabu cha Yoshua.

mahali alipopewa

"Mahali alipopewa na Bwana"

wakati wa maisha

Ina maana ya wakati ambao mtu alikuwa hai. "wakati wa uhai"

Wazee

Inamaanisha watu waliosaidia kuingoza Israeli, walioshiriki katika mambo ya kijamii na kidini kama vile kutii amri ya Musa.

Walioendelea baada yake

Hii inamaanisha kuishi mda mrefu zaidi ya mtu mwingine. "Kuishi mda mrefu zaidi yake"

Nuni

Hili ni jina la mwanamume.

Judges 2:9

Aliyopewa

"Ambayo Mungu alimpa"

Timnath Heresi

Hili ni jina la eneo.

Mlima Gaash

Hili ni jina la mlima

Kizazi hicho chote kilikusanyika kwa baba zao

Sentensi "kilikusanyika kwa baba zao" ina maanisha kwamba watu wa kizazi kile walikufa, nafsi zao zikaenda sehemu ile ile ambayo mababu zao waliokufa kwanza walienda. Ni namna nzuri ya kusema walikufa.

Baba

Hapa ina maanisha mababu wa mtu au kikundi fulani cha watu.

Kukua

"kuongezeka umri" au "kuwa mzee"

Ambao hawakumjua Bwana

"hawakumjua" ina maanisha hawakumtambua Bwana au nguvu zake kama ambavyo kizazi kilichopita kilimtambua.

Judges 2:11

Yaliyo mabaya machoni mwa Bwana

"machoni mwa Bwana" inawakilisha kile ambacho Bwana alikifikiria.

Mabaali

Huu ni wingi wa Baali. Baali ni jina la mungu wa uongo.

Wakaondoka kwa Bwana

Waisraeli hawakutii tena anayosema Bwana hivyo wakawa wameondoka mbele ya Bwana.

Baba

"Mababu"

Wakaifuata miungu mingine

Waisraeli kuanza kuabudu miungu ya uongo wanafananishwa kama Waisraeli walioondoka na kuifuata miungu ya uongo.

Wakaisujudia

Hili ni tendo la kuabudu au kutoa heshima kwa mtu.

Wakamkasirisha Bwana

Wakasababisha Bwana akasirike"

Maashtoreti.

Huu ni wingi wa Ashtoreti, aliyeabudiwa kama mungu kwa namna nyingi.

Judges 2:14

Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli

Hasira ya Bwana inaelezewa kama moto uwakao. "Bwana akakasirika juu ya wana wa Israeli"

akawapa washambuliaji walioiba mali zao kutoka kwao

"Akawaacha washambuliaji waibe mali zao"

Aliwauza kama watumwa waliofanyika kwa nguvu za maadui zao waliowazunguka, hivyo hawakuweza kujikinga dhidi ya adui zao

Bwana akaruhusu adui zao wawachukue Waisraeli kama watumwa, wakauzwa utumwani. "Aliwaruhusu adui zao kuwashinda na kuwachukua kama watumwa na hawakuweza kuishinda nguvu ya adui"

mkono wa Bwana ulikuwa dhidi yao kuwashinda

"Mkono" inawakilisha nguvu ya Bwana. "Bwana aliwasaidia adui zao kuwashinda"

walikuwa katika shida kali

"Waliteseka sana"

Judges 2:16

Ndipo Bwana akawainua waamuzi

Bwana aliwachagua watu kuwa waamuzi akawainua.

katika mikono ya wale

"mikono" ni nguvu. "Toka kwenye nguvu za adui zao"

Hawakuwasikiliza waamuzi wao

"hawakuwatii waamuzi wao"

wakajitoa wenyewe kama makahaba kwa miungu mingine na kuabudu

Watu kumsaliti Mungu na kuiabudu miungu mingine wanafananishwa na makahaba. "walimsaliti kwa kuiabudu miungu ya uongo"

Waligeuka upesi na kuiacha njia waliyoishi baba zao

Watu hawakufanya kama vile babu zao walivyomuabudu Bwana, waligeukia upande mwingine.

Baba zao

"mababu zao"

Judges 2:18

Bwana aliinua waamuzi.

Bwana alichagua watu kuwa waamuzi kwa njia ya kuwainua juu.

waamuzi kwa ajili yao ... kuwaokoa

"yao" ina maanisha Waisraeli.

mikono ya adui zao

"mkono" ina maanisha nguvu za adui za kuwaumiza Waisraeli.

siku zote muamuzi aliishi

"kwa muda muamuzi alioishi"

Huruma

Kuwa na huruma juu ya kitu fulani au mtu

walipougua

Huu ni mlio unatolewa na mtu anayeteseka, inatumika kuelezea maumivu ya Waisraeli.

Waligeuka

Watu hawakuendelea kumtii Bwana waligeuka.

Baba zao

"mababu zao"

Wakaenda kuifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu

Waisraeli kuiabudu miungu mingine inafananishwa kama vile walitembea kuifuata miungu mingine. "Waliitumikia na kuabudu miungu mingine"

Walikataa kuacha matendo yao yote mabaya au njia zao za ukaidi.

"Walikataa kuacha kufanya mambo maovu na wakawa wakaidi."

Judges 2:20

Hasira ya Bwana iliwaka juu ya Israeli

Hasira ya Bwana inaelezewa kama moto uwakao.

Taifa hili limevunjika

"taifa" inawakilisha watu. "watu hawa wamevunjika" au "Waisraeli wamevunjika"

Baba

Hapa inamaanisha mababu wa mtu fulani au wa kundi fulani la watu.

Hawakuisikiliza sauti yangu

"sauti" inawakilisha yale aliyosema Bwana. "hawajatii niliyowaamuru" au "hawajanitii mimi"

Taifa lolote

"taifa" inawakilisha kundi la watu walioishi Kanaani kabla ya Waisraeli.

Watashika njia ya Bwana na kuifuata

Namna ambavyo Bwana anataka watu waishi inafananishwa kama vile wapo njiani. Watu kumtii Bwana ni sawa na kutembea katika njia zake.

Hakumruhusu Yoshua kuwashinda

"hakumuacha Yoshua kuwashinda"

Hakumruhusu Yoshua

Hapa "Yoshua" anawakilisha jeshi lake. Hakumruhusu Yoshua na jeshi lake.

Judges 3

Judges 3:1

Sasa Bwana

"sasa" inaonesha mwanzo wa simulizi.

Mataifa haya

Hili ni kundi la watu wanaozungumzwa katika 3:3.

ambaye hakushiriki vita yoyote huko Kanaani

Inaweza kuanza kama "ambaye hakupigana vita yoyote huko Kanaani.

Alifanya hivyo ili kuwafundisha vita kizazi kipya cha Waisraeli ambao hawakujua kabla

Msimuliaji anatoa taarifa kwanini Bwana aliwaacha baadhi ya watu Kanaani. "Bwana aliyaacha mataifa kati ya Israeli ili awafundishe vijana ambao hawakupigana vita"

Wafalme watano

Wafalme hawa watano wanawakilisha watu wao. "wafalme watano na watu wao"

Mlima Baali Hermoni

Huu ni mlima mrefu sana Israeli.

Hamathi

Hili ni jina la eneo kaskazini mwa mpaka wa Kanaani.

Judges 3:4

Mataifa haya yaliachwa

Inaweza kuanza kama "Bwana aliyaacha mataifa haya Kanaani" au "Bwana aliruhusu mataifa haya kuendelea kuishi Kanaani"

kama njia

"kama namna"

kama watazitii ... alizowapa babu zao

Maneno "wao" na "zao" yanawaelezea wana wa Israeli.

amri alizowapa

"amri ambazo Bwana aliwapa"

Judges 3:7

yaliyo mabaya machoni pa Bwana

"machoni mwa Bwana" inawakilisha kitu ambacho Bwana anakifikiria au kuwaza juu ya jambo fulani.

wakamsahau Bwana, Mungu wao

"kumsahau" ni fumbo lenyhe maana ya "waliacha kumtii"

hasira ya Bwana ikawaka

Bwana kuwa na hasira inafananishwa na kitu ambacho kinaweza kuwaka moto. "Bwana akakasirika sana"

akawauza mkononi mwa Kushan-rishathaimu

Akaruhusu wana wa Israeli kutekwa inazungumzwa kama vile Bwana amewauza kwa Kushan-rishathaimu. "Akaruhusu Kushan-rishathaimu na jeshi lake kuwashinda"

mkononi mwa Kushan-rishathaimu

"mkono" ina maanisha nguvu ya kutawala. pia Kushan-rishathaimu inawakilisha jeshi lake.

Kushan-rishathaimu

Hili ni jina la mwanaume.

Aram Naharaimu

Hili ni jina la nchi.

Judges 3:9

Bwana akamuinua mtu

Bwana akamchagua mtu kufanya kazi maalumu kwa ajili yake.

Othnieli ... Kenazi

Majina haya ni ya wanaume.

akamtia nguvu

Maneno haya yanamaanisha kwamba Bwana akamsaidia Othnieli kukuza sifa alizozitaka ili awe kiongozi bora.

akahukumu Israeli

"kuhukumu" inamaanisha kuwaongoza wana wa Israeli.

naye akatoka kwenda vitani

"naye" inamuelezea Othnieli ambaye anawakilisha jeshi la Israeli. "Othnieli na jeshi la Israeli wakatoka kwenda kupigana na jeshi la Kushan-rishathaimu"

Bwana akampa kuishinda Kush-rishataimu mfalme wa Aramu

"Kush-rishataimu" anawakilisha jeshi lake. "Bwana akalisaidia jeshi la Israeli kulishinda jeshi la Kush-rishataimu mfalme wa Aramu"

Mkono wa Othnieli

Hapa neno "mkono" limesimama badala ya jeshi. "Jeshi la Othnieli"

Nchi ilikuwa na amani

"nchi" imetumika kuelezea watu waishio ndani yake. "Watu waliishi kwa amani"

Miaka arobaini

"miaka 40"

Judges 3:12

yaliyo mabaya machoni pa Bwana

"machoni mwa Bwana" inawakilisha kitu ambacho Bwana anakifikiria au kuwaza juu ya jambo fulani

Bwana akampa Egloni mfalme wa Moabu nguvu

"Bwana akamfanya Elgoni mfalme wa Moabu kuwa na nguvu"

Egloni mfalme wa Moabu, kuwashinda Waisraeli

"Egloni mfalme wa Moabu" inawakilisha jeshi lake. "Egloni mfalme wa Moabu na askari wake wakavamia jeshi la Israeli"

Egloni

Hili ni jina la mfalme.

mji wa Mitende.

Hili ni jina lingine la mji wa Yeriko.

Miaka kumi na nane

"miaka 18"

Judges 3:15

walipomwomba Bwana

Hii inamaanisha walipaza sauti kwa nguvu kwa mtu aliye mbali. pia inaweza kumaanisha mtu anaomba msaada hasa kwa Mungu.

akamwinua mtu

Bwana akamchagua mtu kufanya kazi maalumu kwa ajili yake.

Ehudi ... Gera

Haya ni majina ya wanaume.

mtu shoto

shoto. Ehudi alikuwa na uwezo wa kutumia upanga kwa mkono wa kushoto.

Judges 3:16

dhiraa moja

Kama kuna ulazima wa kutumia njia za kisasa za kupima urefu, kuna njia mbili za kufanya hivyo. "urefu sentimeta 46" au "urefu zaidi ya mita moja na nusu"

aliufunga chini ya nguo zake juu ya mguu wake wa kulia

"aliufunga kwenye mguu wake wa kulia chini ya nguo"

mguu

"paja"

Egloni alikuwa mtu mnene sana

Hapa msimuliaji anatupa taarifa juu ya Elgoni.

Judges 3:19

alipofikia mahali ambapo sanamu za kuchonga zilitengenezwa karibu na Gilgali,

"Alipofika mahali karibu na Gigali sehemu ambapo sanamu za kuchongwa hutengenezwa"

katika chumba cha juu cha baridi

Hiki ni chumba cha juu kilichotumika kwa ajili ya kupumzika na chenye ubaridi hata wakati wa joto.

Mfalme akasimama kutoka katika kiti chake

Kusimama ni ishara ya kumheshimu Mungu wakati wa kusikiliza ujumbe wake.

Judges 3:21

nao ukatokea nyuma yake

"ncha ya upanga ikatokea nyuma yake"

hakuutoa

"hakuuvuta"

ukumbi

Hiki ni chumba cha nje chenye ukuta mdogo na kilichoezekwa.

Judges 3:24

Hakika atakuwa anajitoa mwenyewe

Hii ni hali ya kuzungumza kwa upole kuhusu mtu ambaye anataka kujisaidia.

hata walipoanza kuhisi kuwa walikuwa wakipuuza wajibu wao

Walisubiri mpaka wakaanza kuwa na wasiwasi kuwa kuna kitu hakipo sawa na ulikuwa wajibu wao kufungua mlango katika chumba binafsi cha mfalme wao.

walichukua ufunguo wakawafungua

"walichukua ufunguo na kufungua mlango"

Judges 3:26

Wakati watumishi wakisubiri ... Ehudi alikimbia

Hii inaeleza nini kilitokea kabla watumishi hawajafungua mlango wa chumba cha juu na kukuta mfalme amekufa. "Wakati watumishi walipokuwa wakisubiri nje ya chumba cha juu ... Ehudi alikimbia"

Seira.

Hili ni jina la mji.

Alipofika

"Alipofika Seira"

Judges 3:28

Maelezo ya jumla:

Ehudi anazungumza na watu wa Israeli huko Efraimu.

kwa kuwa Bwana atawashinda adui zenu

Bwana aliwasaidia Waisraeli kuwashinda adui zao kama vile Bwana ndiye shujaa anayepigana na kuwashinda adui zao.

wakakamata vivuko

"Wakamiliki vivuko"

Vivuko

Sehemu ya mto ambayo ni rahisi kupita kuwenda upande mwingine.

hawakuruhusu mtu yeyote kuvuka

"hawakuacha mtu yeyote avuke"

Watu elfu kumi

"watu 10,000"

Watu wenye uwezo

"watu wenye uwezo wa kupigana vizuri"

Moabu ilishindwa na nguvu ya Israeli

Hii inaweza kuanza "jeshi la Waisraeli liliwashinda Wamoabu"

Nguvu ya Israeli

Hapa "nguvu" inawakilisha jeshi la Israeli.

nchi ilikuwa na amani

Hapa "nchi" inawakilisha watu. "Waisraeli waliishi kwa amani"

Miaka themanini

"miaka 80"

Judges 3:31

Mwamuzi

Mungu alichagua mwamuzi kuwaongoza wana wa Israeli katika nyakati za shida baada ya kuingia katika nchi ya ahadi na kabla ya kuwa na wafalme. mara nyingi waamuzi waliwaokoa Waisraeli toka kwa maadui.

Shamgari

Ni jina la mwanaume.

Athani

Ni jina la mwanaume.

konzo

"kusogeza" au "kuongoza"

Pia aliwaokoa Israeli kutoka kwenye hatari.

"Hatari" inamaanisha maadui waliotaka kuwadhuru Waisraeli.

Judges 4

Judges 4:1

Ehudi

Hili ni jina la mwanaume.

yaliyo mabaya machoni pa Bwana.

"machoni mwa Bwana" inawakilisha kitu ambacho Bwana anakifikiria au kuwaza juu ya jambo fulani

Bwana akawatia mkononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani

Hapa "mkono" ina maanisha nguvu za Yabini juu ya Israeli.

Yabini ... Sisera

Haya ni majina ya wanaume

Hasori ... Harosheti

Haya ni majina ya miji au mahali.

magari ya chuma mia tisa

"magari ya chuma 900"

miaka ishirini

"miaka 20"

Judges 4:4

Sasa

hapa msimuliaji anatuelezea habari kuhusu Debora.

Debora

Hili ni jina la mwanamke.

Lapidothi

Hili ni jina la mwanaume.

Mwamuzi

Mungu alichagua mwamuzi kuwaongoza wana wa Israeli katika nyakati za shida baada ya kuingia katika nchi ya ahadi na kabla ya kuwa na wafalme. mara nyingi waamuzi waliwaokoa Waisraeli toka kwa maadui.

mtende wa Debora

Mti huu ulipewa jina la Debora.

Judges 4:6

Taarifa ya jumla

Mwandishi wa Waamuzi anaelezea watu, miji, milima na mito kwa majina yake.

Baraka ... Abinoamu

Haya ni majina ya wanaume.

mlima wa Tabori

Hili ni jina la mlima.

watu elfu kumi

"watu 10,000"

Mimi nitamfukuza

"Mimi" linamaanisha Mungu.

Nitamfukuza Sisera

Hapa "sisera" inawakilisha jeshi lake. "nitamfukuza Sisera na jeshi lake"

Kufukuza

Kuwatoa watu waondoke sehemu salama.

Sisera ... Yabini,

Haya ni majina ya wanaume.

Kishoni

Hili ni jina la mto.

Judges 4:8

Taarifa ya jumla:

Baraka anafanya majadiliano na Debora.

Baraka

Hili ni jina la mwanaume.

njia unayoienda haitakupa heshima

Maamuzi aliyoyafanya Baraka yanafananishwa kama njia aliyoichagua Baraka kusafiria. Pia "heshima" inazungumzwa kama mwisho wa safari.

kwa kuwa Bwana atamuuza Sisera mkononi mwa mwanamke

Hapa "mkono" imetumika kama nguvu za kumuua. "Kwa maana Bwana atasababisha mwanamke amshinde Sisera"

Sisera

Hili ni jina la mwanaume.

Debora

Hili ni jina la mwanaume.

Judges 4:10

Watu elfu kumi

"watu 10,000"

Judges 4:11

Sasa

hapa msimuliaji anatuelezea habari kuhusu Heberi.

Heberi ... Hobabu

Haya ni majina ya wanaume.

Mkeni

Huyu ni mmoja ya watu wa Keeni.

Mkwe wa Musa

"Baba yake na mke wa Musa"

Saanaimu

Hili ni jina la mji.

Judges 4:12

Walipomwambia Sisera

Hapa haijambainisha mtu moja kwa moja. "mtu alipomwambia Sisera"

Sisera

Hili ni jina la mwanaume.

Baraka ... Abinoamu ... mlima wa Tabori

Baraka na Abinoamu ni majina ya mwanaume. Na mlima wa Tabori ni jina la mlima.

Sisera akayaita magari yake yote

"magari" yanawakilisha askari wanaoendesha magari.

magari ya farasi mia tisa

"Magari ya farasi 900"

Haroshethi

Hili ni jina la mahali.

Mto Kishoni.

Hili ni jinala mto.

Judges 4:14

Bwana amekupa ushindi

Debora ana uhakika na ushindi. anazungumza kama vile Baraka ameshapata ushindi. "Bwana atakupa ushindi"

Je! si Bwana anayekuongoza?

Debora anamuuliza hili Swali Baraka ili kumkumbusha kuwa wanapigana wakiwa upande wa Bwana. "Kumbuka Bwana anakuongoza"

Kumi elfu

"10,000"

Judges 4:15

Bwana alifanya jeshi la Sisera kuchanganyikiwa

"Bwana akamfanya Sisera ashindwe kufikiri vizuri" au Bwana akalifanya jeshi la Sisera kuchanganyikiwa"

magari yake yote

"magari" yanawakilisha askari wanaoendesha magari.

Baraka akayafuata

"Baraka" anawakilisha jeshi lake. Baraka na jeshi lake wakayafuata"

Haroshethi

Hili ni jina la mji.

jeshi lote la Sisera likauawa kwa upanga

Hapa neno "upanga" linawakilisha upanga au siliha nyingine ambayo askari hutumia vitani.

Judges 4:17

Sisera ... Yabini ... Hazori

Sisera na Yabini haya ni majina ya wanaume bali Hazori hili ni jina la mji.

akakimbia kwa miguu

Hii ina mana ya kuwa alikuwa anatembea kwa miguu na sio kutumia farasi.

Yaeli

Hili ni jinala mwanaume.

Heberi

Hili ni jina la mwanaume.

Mkeni

Huyu ni mmoja ya watu wa Keeni.

nyumba ya Heberi Mkeni

Hapa "nyumba" inawakilisha familia. "familia ya Heberi mkeni"

Akageuka kando

Hii inamaanisha kupumzika katika safari.

Bushuti

Ni shuka kubwa analojifunika mtu ili mwili upate joto wakati wa kulala, hutengenezwa kwa sufu au ngozi ya mnyama.

Judges 4:19

Akamwambia

"Sisera akamwambia Yaeli"

Judges 4:21

kigingi cha hema

Kipande cha mbao au chuma, kama sindano kubwa ambayo inachomekwa chini na kushikilia kona ya hema.

Nyundo

Kifaa kizito kinachotumika kugongea kigingi cha hema chini.

Usingizi mzito

Kama mtu aliye katika shimo kubwa hawezi kupanda juu, mtu aliye katika usingizi mzito haweze kuamka haraka.

kupenya

"ikatengeneza shimo"

Baraka alimfuata

"Baraka alimkimbilia" au "Baraka alimfuata kwa nyuma"

Judges 4:23

Mungu alimshinda Jabin, mfalme wa Kanaani, mbele ya watu wa Israeli

Mungu aliwafanya Waisraeli wamshinde Yabini pamoja na jeshi lake.

Uwezo

"Nguvu za jeshi"

wakamwangamiza yeye

"yeye" inamaanisha Yabini na jeshi lake. "Wakamwangamiza Yabini na jeshi lake"

Judges 5

Judges 5:1

Siku hiyo

Maana halisi ya sentensi hii yaweza kuwa "Siku hiyo Waisraeli walilishinda jeshi la Yabini"

Debora

Hili ni jina la mwanamke.

Baraka ... Abinoamu

Haya ni majina ya wanaume.

watu wanapojitolea kupigana vita

"watu walipokubali kupigana vitani"

Judges 5:3

Taarifa za jumla:

wimbo wa Debora na Baraka kwa kutumia ushairi unaendelea.

Sikiliza, ninyi wafalme! Sikiliza kwa makini, ninyi viongozi

Debora na Baraka wanazungumza na wafalme na viongozi kama vile wanawasikilizisha wimbo.

Ninyi wafalme ... ninyi viongozi

Hii inamaanisha wafalme na viongozi kwa ujumla, na sio viongozi au wafalme fulani.

wakati ulipotoka Seiri, ulipokwenda kutoka Edomu

Hii inarejea wakati ambao Waisraeli waliondoka Edomu na kuanza kuwateka watu wa Kanaani. Bwana aliwatia nguvu watu wake wakawashinda watu wa Kanaani.

Seiri

Huu ni mlima uliopo mpakani mwa Israeli na Edomu.

nchi ilitetemeka, na mbingu pia ilitetemeka; pia mawingu yalitoa maji.

Yaweza kuwa na maana ya 1) Hii ni lugha ya kishairi ambayo inasisitiza nguvu ya Bwana ambazo zina uwezo wa kusababisha tetemeko la ardhi au 2) watu wa Kanaani walianza kuogopa baada ya Waisraeli kutaka kuwavamia inafananishwa kama vile mbingu na nchi zinatetemeka.

Judges 5:5

Taarifa za jumla:

wimbo wa Debora na Baraka kwa kutumia ushairi unaendelea.

Milima inatetemeka

Imerejea tetemeko la ardhi ili kuonesha kuwa milima inatetemeka kwa sababu inamuogopa Bwana.

mbele ya uso wa Bwana

"uso" ina maanisha uwepo wa Bwana. "kwenye uwepo wa Bwana"

hata Mlima Sinai ukatetemeka

Musa na Waisraeli walipokuwa mlima Sinai ulitetemeka. "Hapo zamani hata mlima Sinai ulitetemeka"

Katika siku za

Hapa "siku" inawakilisha muda mrefu uliopita.

Shamgari ... Anathi ... Jael

Haya ni majina ya watu.

Mwana wa Anathi

Baba yake na Shamgari anatajwa ili kusaidia kumtambua Shamgari.

barabara kuu ziliachwa

"Watu waliacha kutumia barabara kuu kwa sababu waliwaogopa maadaui wa Israeli.

njia za upepo

Hizi ni njia ndogo ambazo watu wachache walizitumia.

Judges 5:7

mama alichukua amri katika Israeli

Hii inazungumzia juu ya uongozi wa Debora kama mama wa Israeli. "Aliwajali Waisraeli kama ambavyo mama anawajali watoto wake"

Walichagua miungu wapya

"Wana wa Israeli waliabudu miungo mipya"

kulikuwa na vita katika malango ya jiji

Neno "malango" linawakilisha mji mzima. "maadui waliwashambulia watu ndani ya miji ya Israeli"

hapakuwa na ngao au mikuki iliyoonekana kati ya watu elfu arobaini nchini Israeli.

Hii sentensi inaelezea ni kwa kiasi gani Waisraeli walikuwa na silaha chache.

elfu arobaini nchini Israeli

"40,000 nchini Israeli"

Judges 5:9

Moyo wangu unawaendea wakuu wa Israeli

"moyo" unawakilisha hisia za mtu. Debora anatoa shukrani kwa wakuu wa Israeli.

ninyi ambao hupanda punda weupe ... nanyi mnaotembea njiani.

Maelezo haya yanawaelezea matajiri na masikini, zote hizi zimetumika ili kumuelezea kila mtu.

mmeketi kwenye mazulia

Mazulia yalitumika kuweka kwenye mgongo wa punda ili kumfanya mtumiaji wa punda kuwa huru zaidi.

Judges 5:11

Taarifa ya jumla:

Wimbo wa Debora na Baraka unaendelea.

Sikiliza sauti za wale

"sauti" inawakilisha watu wakiimba.

wakashuka kwenye malango ya mji.

"malango" inawakilisha mji mzima. "wakarudi kwenye miji yao"

Judges 5:12

Taarifa ya jumla:

wimbo wa Debora na Baraka kwa kutumia ushairi unaendelea.

Amka, amka

Wazungumzaji wanaweza kuwa 1) wana wa Israeli au 2) Debora anajiambia mwenyewe au 3) mshairi aliyeandika wimbo.

Debora

Hili ni jina la mwanamke.

Baraka ... Abinoamu

Hya ni majina ya wanaume.

kwangu pamoja na mashujaa

"kwangu" inamaanisha Debora.

Judges 5:14

kutoka Efraimu, ambao mizizi yao iko katika Amaleki

Wana wa Efraimu waliokuwa wakiishi walikuwa uzao wa Amaleki.

walikufuata wewe

"wewe" inamaanisha watu wa Efraimu.

Mariki

Hili ni eneo ambalo uzao wa Mariki waliishi. Mariki alikuwa mwana wa Manase na mjukuu wa Yusufu.

kutoka Zebuloni wale wanaobeba fimbo ya afisa.

Viongozi wa kivita walitambulika kwa fimbo kama ishara ya mamlaka. "Kiongozi wa kivita wa Zebuloni"

Judges 5:15

Na wakuu wangu katika Isakari walikuwa pamoja na Debora

"wangu" ina maanisha Debora. Sentensi hii inaweza kuandikwa "Na wakuu wangu katika Isakari walikuwa pamoja nami"

Debora

Hili ni jina la mwanamke.

Isakari alikuwa na Baraka

"Isakari" ni kabila la Isakari.

Baraka

hili ni jina la mwanaume.

waliingia bondeni kwa kasi chini ya amri yake.

"kutii amri zake na kumfuata bondeni"

Kumfuata

"kumfuata nyuma kwa kasi"

kulikuwa na utafutaji mkubwa wa moyo.

"moyo" inawakilisha fikra. Watu kujadili wao kwa wao lakini wakashindwa kuamua nini cha kufanya inafananishwa na kutafuta mioyo yao.

Judges 5:16

Kwa nini uliketi katikati ya moto, ukisikiliza wachungaji wakipiga filimbi yao kwa makundi yao?

Hili swali limeulizwa ili kuwapinga wana wa Rubeni kwa sababu hawakuamua kwenda vitani. Pia inaweza kutafsiriwa "Mngetusaidia kupigana badala ya kukaa nyumbani na kusikiliza wachungaji wakipiga filimbi kwa makundi yao"

Moto

Tafsiri zingine za Biblia zinatafsiri "mazizi ya kondoo"

kulikuwa na utafutaji mkubwa wa moyo.

"moyo" inawakilisha fikra. Watu kujadili wao kwa wao lakini wakashindwa kuamua nini cha kufanya inafananishwa na kutafuta mioyo yao.

Judges 5:17

Gileadi alikaa

"Gileadi" inawakilisha watu wa Gileadi ambao walitakiwa kwenda vitani kupigana.

upande wa pili wa Yordani

Huuni upande wa mashariki wa Yordani.

na Dani, kwa nini alizunguka juu ya meli?

Swali hili liliulizwa ili kuelezea hasira kwa sababu watu wa Dani hawakupigana kwa ajili ya Israeli. "Na watu wa kabila la Dani hawakutusaidia vitani, badala yake walikuwa wakizunguka juu ya meli."

Dani, kwa nini

"Dani" inawakilisha watu wa Dani waliopaswa kwenda vitani kupigana.

kuzunguka juu ya meli

Kabila la Dani waliishi karibu na bahari ya Mediteraniani. Walifanya biashara kupitia bahari pamoja na uvuvi.

Asheri alibakia pwani na akaishi karibu na bandari zake

"Watu wa kabila la Asheri hawakutusaidia. walibaki pwani karibu na bandari zao."

Asheri alibaki

"Asheri" inawakilisha watu waliopaswa kwenda kwenda vitani kupigana.

Bandari

Pwani ya bahari yenye maji yenye kina kirefu ambapo meli huwekwa.

Naftali, pia

"Naftali lilikuwa kabila ambalo lilitoa maosha yake hata hatua ya kufa"

Judges 5:19

Wafalme walikuja, wakapigana ... wafalme wa Kanaani wakapigana

Mfalme wa kundi la watu hutumika kuelezea jeshi ambalo analiamuru.

Wakapigana ... wakapiagana

"Wakapigana nasi"

Taanaki ... Megido

Haya ni majina ya mahali

hakuna fedha kama nyara

"fedha" inawakilisha mali kwa ujumla.

nyara

Kitu kinachochukuliwa kwa nguvu, hasa katika vita au na wezi.

Nyota zilipigana kutoka mbinguni, kutoka katika njia zao za mbinguni zilipigana na Sisera

Bwana anawasaidia Waisraeli kumshinda Sisera na jeshi lake kama vile nyota zenyewe zinavyopigana na Sisera na jeshi lake. Mara nyingi Bwana hutumia vitu vya kawaida kama mvua ya radi kuipiga Sisera.

Dhidi ya Sisera

"Sisera" inawakilisha jeshi lake lote.

Sisera

Hili ni jina la mwanaume.

Judges 5:21

Mto Kishoni uliwaondoa

Kwa sababu ya mvua kubwa mto ulijaa haraka na ukasababisha magari yakwame kwenye tope na askari wengi kukwama.

Kishoni

Hili ni jina la mto.

Endelea mbele nafsi yangu, jipe nguvu

"nafsi" inamaanisha mtu. "yangu" ina maanisha Debora.

Kisha sauti za hofu za farasi-kupiga mbio, kupigana kwa watu wake wenye nguvu.

Hii inaelezea sauti ya farasi wengi wakikimbia toka vitani.

kupiga mbio

kukimbia haraka

Judges 5:23

Ilaani Merozi

"Merozi" inawakilisha watu waliokuwa wakiishi huko.

Merozi

Hili ni jina la mji.

Wenyeji

Watu waishio mahali fulani

Judges 5:24

Yaeli

Hili ni jina la mwanamke.

Heberi

Hili ni jina la mwanaume.

Mkeni

Moja ya mtu wa Keeni.

akamletea siagi

"siagi" ni maziwa mazito. Haya yalikuwa maziwa mazuri na kinywaji pendwa kwa watu wa Yaeli.

sahani inayofaa kwa wakuu

Hii inamaanisha kuwa sahani ile ilikuwa ya thamani sana kwa sababu wakuu walitumia vitu vya thamani.

Judges 5:26

Aliweka mkono wake kwenye kigingi cha hema

"Yaeli alitoa kigingi cha hema kwa mkono wake wa kushoto"

kigingi cha hema

Kipande cha mbao au chuma, kama sindano kubwa ambayo inachomekwa chini na kushikilia kona ya hema.

na mkono wake wa kuia katika nyundo ya mfanyakazi

"akachukua nyundo kwa mkono wake wa kulia"

Nyundo

Kifaa kizito kinachotumika kugongea kigingi cha hema chini.

Sisera

Hili ni jina la mwanaume

Akalala

Bila nguvu

aliuawa kwa ukatili

"alimuua" au "alikufa"

Judges 5:28

kamba

Huu ni mwonekano wa dirisha lililotengenezwa kwa mbao.

Kwa nini gari lake limechelewa kuja? Kwa nini viboko vya farasi vinavyovuta magari yake vimechelewa

Maswali haya yote yanamaana moja. "Kwa nini imemchukua Sisera mda mrefu kurudi nyumbani?"

gari lake limechukua ... nini viboko vya farasi vinavyovuta magari yake

Hivi vyote vinamuwakilisha Sisera. "Kumchukua Sisera ... kwa nini yeye"

Judges 5:29

Binti mfalme mwenye hekima

Huyu ni binti wa mfalme lakini pia anaweza kuwa mshauri wa kike wa familia ya kifalme.

akajibu jibu lile

"akajiambia mwenyewe kitu kile kile"

Je, hawakupata na kugawanya nyara?

"Watakuwa na nyara nyingi sana ndio maana wanachukua mda mrefu kugawana"

Tumbo, matumbo mawili kwa kila mtu ... kwa wale waliopora?

Wanawake wanatumia swali kusisitiza kuwa wanaamini hili ndilo lilitokea.

Tumbo, matumbo mawili kwa kila mtu

"tumbo" linawakilisha mwanamke. "Kila askari atapata mwanamke mmoja au wawili"

Nguo za rangi

"ngio zenye rangi"

Iliyofumwa

"imeshonwa vizuri"

misumari ya wale waliopora

"misumari" inawakilisha askari wa Sisera.

Judges 5:31

Waache wale wanaompenda

"Waache wale wanaompenda Bwana"

kama jua wakati linapoongezeka katika uwezo wake

Watu wa Israeli walitamani kuwa kama jua linapowaka kwa sababu hakuna jeshi lolote lenye nguvu ya kulizuia jua.

Nchi ilikuwa na amani

"nchi" inawakilisha watu wa Israeli.

Kwa miaka arobaini

"kwa miaka 40"

Judges 6

Judges 6:1

yaliyo mabaya machoni pa Bwana

"machoni mwa Bwana" inawakilisha kitu ambacho Bwana anakifikiria au kuwaza juu ya jambo fulani

mikononi mwa Midiani

"Midiani" inawakilisha watu wa Midiani. Pia "mkono" unawakilisha kutawala. "utawala wa watu wa Midiani"

Uwezo wa Midiani uliwanyanyasa Israeli

"uwezo wa Midiani" inamaanisha watu wa Midiani. "Watu wa Midiani walikuwa na nguvu kuliko watu wa Israeli na waliwanyanyasa"

Mabwawa

Eneo lenye miamba linaloweza kuwa makazi.

Judges 6:3

Waliweza kutengeneza jeshi

"Jeshi lao liliweka kambi" au "jeshi lao lilitengeneza hema"

Judges 6:5

Kila wakati wao na mifugo yao na mahema walipokuja

Nchi ya Midiani ilikuwa kusini mwa nchi ya Israeli pembeni mwa bahari ya Shamu.

walikuja kama kundi la nzige

Wamidiani wanafananishwa na kundi la nzige kwa sababu walikuja na kundi kubwa la watu na wanayama wao walikula kilakitu kilichopandwa.

Haikuwezekana kuhesabu

Hii inaonesha kuwa namba ilikuwa kubwa sana.

Midiani iliwadhoofisha

"Midiani" inawakilisha watu wa Midiani.

Wakamwita Bwana

"wakamwomba Bwana msaada"

Judges 6:7

walipomwomba Bwana

"wakamwomba Bwana msaada"

Kwa sababu ya Midiani.

"Midiani" inawakilisha watu wa Midiani.

Nimekuleta kutoka Misri

"Nimekuongoza kutoka Misri"

Nyumba ya utumwa

Musa anaizungumzia Misri kama nyumba ambayo watu waliwahifadhi watumwa. "sehemu ambayo mlikuwa watumwa"

Judges 6:9

Kutoka kwenye mkono

"mkono" unawakilisha nguvu na mamlaka.

Kutii sauti yangu

"sauti yangu" inawakilisha kitu ambacho Bwana ameamuru.

Judges 6:11

Sasa

Hapa msimuliaji anaanza kueleza sehemu mpya ya simulizi.

Malaika wa Bwana

Bwana anamtokea Gidioni kwa mfano wa malaika.

Ofra

Hili ni jina la mji.

Abiyezeri

Hili ni kundi la watu waliojiita baada ya babu yao Abiyezeri.

akitenganisha ngano katika sakafu

Hii ni hatua ya kupura nafaka. Gidioni alipura nafaka katika sakafu ili kutenganisha ngano na makapi.

Akamtokea

"akamwendea"

Judges 6:13

bwana wangu

Gidioni anatumia neno "bwana" kama njia ya unyenyekevu ya kumsalimia mgeni. Hakugundua kuwa anazungumza na Bwana kwa namna ya malaika.

Je, yako wapi matendo yake yote mazuri ambayo baba zetu walituambia, waliposema, 'Je! si Bwana aliyetukomboa kutoka Misri?'

Gidioni anatumia swali ili kuipinga sentensi ya mgeni kuwa Bwana yuko pamoja naye. Sentensi hii yaweza kuwa moja kwa moja kama "Hatujaona matendo makuu kama tuliyoambiwa na baba zetu kwamba Bwana aliwatoa Misri"

kututia mikononi mwa Midiani.

"kututia" inamaanisha Bwana aliruhusu Waisraeli washindwe.

kututia mikononi

"mkono" inawakilisha nguvu na utawala.

mwa Midiani

"Midiani" inawakilisha watu wa Midiani.

Judges 6:14

Bwana akamtazama.

"Bwana akamtazama Gidioni"

kutoka mkononi

"mkono inawakilisha nguvu au utawala.

Mwa Midiani

"Midiani inawakilisha watu wa Midiani"

Je, sikukutuma?

Bwana anatumia hili swali ili kumuhakikishia Gidioni kuwa amametuma. "kumtuma" inamaanisha kuwa Bwana amemchagua Gidioni kwa kazi maalumu.

Tafadhali, Bwana

Gidioni sasa anamuita Bwana. Inaonesha kuwa inaonekana Gidioni anatambua au anahisi kwamba anazungumza na Bwana.

Nawezaje kuwaokoa Israeli?

Gidioni aliuliza swali ili kusisitiza kuwa anafikiri hawezi kuwaokoa Waisraeli.

Tazama

"tafadhali elewa" au "sikiliza"

Katika Manase

"katika kabila la manase"

Katika nyumba ya baba yangu

"nyumba" inawakilisha familia. "katika familia ya baba yangu"

Judges 6:16

Nitakuwa pamoja nawe.

Hii inamaanisha kuwa Bwana atamsaidia na kumbariki Gidioni.

kama mtu mmoja

Hii yaweza kuwa na maana ya "itakuwa rahisi kama vile unapigana na mtu mmoja tuu.

kuiweka mbele yako

"kukuwekea mbele yako"

Judges 6:19

efa ya unga

Kama kuna ulazima wa kutumia njia za kisasa za kuonesha vipimo, hii ni moja wapo ya kufanya hivyo. "lita 22 za unga"

Mchuzi

Maji yaliyochanganywa na mboga kama vile nyama na kupikwa pamoja.

kumletea

"kumletea malaika wa Bwana"

Malaika wa Mungu.

Hii ni sawa na malaika wa Bwana. "Mungu aliye kama mfano wa Malaika"

Judges 6:21

Malaika wa Bwana.

Bwana akamtokea Gidioni kwa mfano wa Malaika.

Akaondoka

"akapotea"

Judges 6:22

Malaika wa Bwana

Bwana akamtokea Gidioni kwa mfano wa Malaika.

Ewe Bwana MUNGU!

"ewe" hii inaonesha kuwa Gidioni alikuwa na hofu.

nimemwona malaika wa Bwana uso kwa uso

Hii inaelezea namna ambavyo watuu wawili wapo karibu. "nimemwona kabisa malaika wa Bwana"

Bwana akamwambia

Bwana alizungumza na Gidioni toka mbinguni.

Hadi leo

Hii inamaanisha wakati ambao kitabu kitabu cha Waamuzi kimeandikwa.

Ofra

Hili ni jina la mji.

jamaa ya Abiezeri

Hili ni kundi la watu wa Abiezeri.

Judges 6:25

Ng'ombe wa pili

Hii inaonesha idadi kwamba kulikuwa na ng'ombe mwingine.

Karibu nayo

"karibu na madhabahu ya Baali"

juu ya mahali pa kukimbilia

Mji wa Ofra ulikuwa juu ya mlima. Waisraeli walikumbilia huko toka kwa Wamidiani ili wapate makazi.

kuijenga kwa njia sahihi

"weka matofali sehemu sahihi" au "ijenge vizuri"

Judges 6:27

Kufanya kama Bwana alivyomwambia

Hapa anatekeleza agizo la Bwana aliloambiwa katika 6:25

Judges 6:28

Alipoamka

"alipoinuka toka kitandani"

madhabahu ya Baali imebomolewa, na Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na ng'ombe wa pili ametolewa sadaka kwenye madhabahu iliyojengwa

Hii inaweza kutafsiriwa kuwa "waligundua kuwa kuna mtu ameibomoa madhabahu ya Baali, akaikatakata Ashera iliyokuwa pembeni na akajenga madhabahu na kutoa kafara ng'ombe wa pili juu yake"

Judges 6:30

ili auawe

"tumuuwe kama adhabu"

Judges 6:31

Je, ninyi mtamsihi Baali?

Yoashi anatumia swali kusisitiza kuwa mwanadamu hatakiwi kuiokoa miungu.

Mtamsihi

"mtamtetea" au "mtatoa sababu"

Je mtamuokoa?

Yoashi anatumia swali kusisitiza kuwa mwanadamu hatakiwi kuiokoa miungu.

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gidioni likiwa na maana ya "Baali ajitetee mwenyewe"

Kwa sababu alisema.

"Kwa sababu Yoashi alisema"

Judges 6:33

Sasa

Hapa msimuliaji anaanza kueleza sehemu mpya ya simulizi.

Walikusanyika pamoja.

"walikusanyika pamoja kama jeshi"

Judges 6:34

Akaja juu ya Gideoni.

"kumtawala Gideoni"

Jamaa ya Abiezeri.

Hili ni kundi la watu wa Abiezeri.

ili wamfuate

"ili wamfuate katika vita"

na wao pia, waliitwa nje kumfuata

"waliitwa nje wamfuate"

Asheri, Zabuloni, na Naftali

Yote haya yanawakilisha watu wa kila kabila. "kabila la Asheri, Zebuloni na Naftali"

Judges 6:36

ngozi ya samazi

Nguo itokanayo na ngozi ya kondoo.

umande

maji yanayotoka kwenye mimea wakati wa usiku.

basi nitajua kwamba utanitumia

Maana halisi ya sentensi hii yaweza kuwa "Hii itakuwa ishara toka kwako, kisha nitajua kwamba utanituma"

Judges 6:38

Gideoni aliamka

Gideoni alitoka kitandani

akatoa

kukamua kitu au kusogeza ili kuondoa maji.

Judges 7

Judges 7:1

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gideoni.

Wakaweka kambi

"wakatengeneza kambi yao"

Chemchemi ya Harodi ... kilima cha More

Haya ni majina ya mahali.

Kambi ya Midiani ilikuwa kaskazini mwao

"Midiani" inawakilisha jeshi la Wamidiani. "Jeshi la Wamidiani liliweka kambi kaskazini mwa jeshi la Israeli"

Judges 7:2

kwa mimi kukupa ushindi juu ya Wamidiani

"kwa mimi kukuruhusu wewe uwashinde wa Midiani"

Nguvu zetu zimetuokoa

"nguvu" inawakilisha watu wenyewe. "Tumejiokoa wenyewe bila msaada wa Mungu"

Sasa

Hii haimaanishi "wakati huu" bali inatengeneza usikivu wa jambo muhimu linalofuata.

tangaza masikioni mwa watu

Neno "masikio" hapa linamaanisha mtu mwenyewe. "watangazie watu"

Yeyote anayeogopa, anayetetemeka

Maneno haya yote yana maana sawa.

Kutetemeka

neno hili linaelezea namna ambavyo hofu inaweza kusababisha mtu akatetemeka.

Muache arudi

"muache arejee nyumbani kwake"

Mlima Gileadi

Hili ni jina la mliama uliopo katika mji wa Gileadi.

Elfu ishirini na mbili

"22,000"

Elfu kumi wakabaki

"watu 10,000 wakabaki"

Elfu kumi

"10,000"

Judges 7:4

nitafanya idadi yao iwe ndogo kwa ajili yako

"idadi" inawakilisha jeshi. Sentensi hii yaweza kuwa "nitakuonesha ni akina nani wa kuwarudisha nyumbani ili jeshi liwe na watu kidogo"

Judges 7:5

Gideoni akawapeleka

"kuwapeleka" inaweza kutafsiriwa kama "kuwachukua" au "kuwaongoza"

kulamba

"kunywa maji kwa kuyalamba kutumia ulimi"

Watu mia tatu

"watu 300"

Judges 7:7

Watu mia tatu

"watu 300"

nitakuokoa na kukupa ushindi

Hapa alikuwa anamwambia Gideoni ila akimaanisha Gideoni na Waisraeli.

Kwa hiyo wale waliochaguliwa

"kwa hiyo wale waliochaguliwa na Bwana"

walichukua vifaa vyao na tarumbeta zao.

"zao" inawakilisha askari wa Israeli walioondoka kwenye jeshi.

Sasa

Hili ni nenp linalotumiwa na msimuliaji kuanza sehemu mpya ya simulizi.

Judges 7:9

Kavamie kambi, kwa maana nitakupa ushindi juu yake

"kambi" inamaana ya jeshi zima la Wamidiani.

Anaogopa kushuka

"anaogopa kwenda chini kuvamia"

Pura

Hili ni jina la mwanaume

ujasiri wako utaimarishwa

"Na unayoyasikia yatakupa ujasiri"

Sehemu ya walinzi

Sehemu ambayo askari husimama kutizama jeshi la adui.

Judges 7:12

wengi kama wingu la nzige

Hapa "wingu" inamaanisha kundi. Mwandishi analizungumzia jeshi kama kundi la nzige ili kusisitiza kuwa idadi ya askari ilikuwa kubwa.

Ngamia zao walikuwa zaidi ... kuliko idadi ya mchanga katika bahari.

Mwandishi anasisitiza kuonesha idadi kubwa ya ngamia waliokuwepo.

Ngamia zao walikuwa zaidi ya mawingu

"Ngamia zao zilikuwa nyingi na walishindwa kuzihesabu"

Judges 7:13

Hii si kitu kingine isipokuwa upanga wa Gideoni

"upanga wa Gideoni" inamaanisha jeshi la Gideoni linavamia. "mkate wa shayiri katika ndoto yako ni jeshi la Gideoni.

Mungu amempa ushindi juu ya Midiani

Hili tukio la baadae linazungumzwa kama vile ni tukio lililopita. Inasisitiza kuwa lazima itatokea.

Judges 7:15

Watu mia tatu

"watu 300"

Judges 7:17

Kwa Bwana na Gideoni

"Tunapigana kwa ajili ya Bwana na Gideoni"

Judges 7:19

Watu mia moja

"watu 100"

hapo mwanzoni mwa saa ya kati.

Mwanzoni mwa saa ya kati yaweza kuwa saa 10 kamili usiku.

Judges 7:20

Upanga wa Bwana na wa Gideon

"upanga" inamaanisha mapigano. "Tunapigana kwa ajili ya Bwana na Gideoni"

Judges 7:22

tarumbeta mia tatu

"tarumbeta 300"

Bwana akaweka upanga wa kila mtu wa Midiani dhidi ya wenzake

"Upanga" ina maanisha kuwa kushambulia kwao ni kwa kutumia upanga. "Bwana akasababisha kila Mmidiani kupigana na askari mwenzake"

Bethshita ... Serera ... Abel ... Mehola ...Tabathi

Haya ni majina ya miji.

Watu wa Israeli kutoka Naftali, Asheri, na Manase wote waliitwa nje

Hii yaweza kuwa "Gideoni waliwaita nje Waisraeli toka kwenye kabila la Naftali, Asheri na Manase.

Judges 7:24

Bethbara

Hili ni jina la mji.

walikusanyika pamoja na kumiliki maji, mpaka Bethbara na Mto Yordani

"na kumiliki eneo la mto Yordani mpaka Bethbara"

Orebu ... Zeebu

Haya ni majina ya wanaume.

mwamba wa Orebu ... katika shinikizo la divai la Zeebu

Haya ni maeneo ambayo yalipewa majina baada ya Waisraeli kumuuwa Orebu na Beebu.

Judges 8

Judges 8:1

Ni nini hiki umetutenda?

Watu wa kabila la Efraimu wanamkemea Gideoni kwa kutumia swali kwa kuwa hakuwaweka katika jeshi lake.

Dhidi ya Midiani.

"Midiani" inawakilisha jeshi la Midiani.

Wakamwambia kwa nguvu

"wakamwambia kwa hasira" au "wakamkemea kwa nguvu"

Judges 8:2

Taarifa ya jumla

Gideoni anawajibu watu wa Efraimu.

Nimefanya nini sasa kulinganisha na mlichofanya ninyi?

Gideoni anatumia swali kuonesha heshima kwa watu wa Efraimu. "Nimefanya mambo madogo gasa ukilinganisha na mliyofanya"

Je! Mavuno ya zabibu za Efraimu si bora zaidi kuliko mavuno ya zabibu ya Abiezeri?

"Mavuno ya Zabibu zenu watu wa Efraimu ni bora kuliko yetu sisi watu wa Abiezeri"

Je! Mavuno ya zabibu za Efraimu si bora zaidi kuliko mavuno ya zabibu ya Abiezeri?

Gideoni na jeshi lake kuwashinda Wamidiani kunafananishwa na mavuno ya zabibu. Watu wa Efraimi kumuua Orebu na Zeebu kunafananishwa na mavuno ya zabibu katika kipindi cha mavuno. "Jambo ambalo ninyi watu wa Efraimu mmefanya mwishoni mwa vita ni muhimu kuliko jambo ambalo sisi uzao wa Abiezeri tumefanya mwanzoni"

Abiezeri

Hili ni jina la mababu wa Gideoni. Gideoni alilitumia kuelezea uzao wa Abiezeri na nchi yao.

Orebu na Zeebu

Haya ni majina ya wanaume.

Mimi nimefanya nini ukilinganisha na ninyi?

Gideoni anatumia swali kuonesha heshima kwa watu wa Efraimu. "Nimefanya mambo madogo gasa ukilinganisha na mliyofanya"

Ikashuka chini

"ikapungua"

Judges 8:4

Watu mia tatu

"watu 300"

bado waliendelea kufuatilia

"Kufuatilia" ni neno ambalo linaweza kutumika kama "waliendelea kuwafukuza adui zao"

Zeba na Salmuna

Haya ni majina ya wanaume.

Judges 8:6

Je, mikono ya Zeba na Salmuna sasa ipo mikononi mwako?

Viongozi wanatumia swali kusisitiza kuwa Waisraeli bado hawajawakamata Zeba na Salmuna.

mikono ya Zeba na Salmuna

Hapa "mikono inamaanisha mwili mzima.

sasa ipo mikononi mwako

"mkono" inawakilisha nguvu na mamlaka.

Kwa nini tulipe jeshi lako mikate?

Viongozi wanatumia swali hili kusisitiza kuwa hawana sababu yoyote ya kuwapa mkate Waisraeli.

nitairarua ngozi yenu kwa miiba ya jangwani na michongoma.

Nitatengeneza mjeledi kwa kutumia miiba na michongoma ya jangwani na kuitumia kukupiga"

Miiba na michongoma

Vipande vyenye ncha kali vinavyokuwepo kwenye miti ambavyo vinaweza kuchoma watu au wanyama.

Judges 8:8

Akatoka huko

Hapa anazungumziwa Gideoni pamoja na askari waliomfuata. "Gideoni na watu 300 wakatoka huko"

Penieli

Hili ni jina la mahali.

akawaambia watu maneno hayo hayo

"akaomba chakula hapo kwa namna ile ile" au " pia akawaomba chakula"

Nitakapokuja kwa amani

Hii ni namna ya heshima ya kuzungumza juu ya kumshinda adui. "Baada ya kumaliza kulishinda jeshi la Midiani"

nitauangusha mnara huu

"Mimi" inawakilisha Gideoni na watu wake. "Watu wangu na mimi tutauangusha mnara huu"

Judges 8:10

Sasa

Hapa msimuliaji anaanza kusimulia sehemu nyingine mpya ya simulizi.

Zeba na Salmuna

Haya ni majina ya wanaume.

Karkori

Hili ni jina la mji.

Watu elfu kumi na tano

"watu 15,000"

watu waliofundishwa kupigana na upanga

Hii ni njia nyingine ya kuwaelezea askari

Na upanga

"upanga" inawakilisha upanga au silaha nyingine ambazo askari huzitumia vitani.

walianguka

Hii ni lugha ya upole inayomaanisha watu waliokufa vitani.

Judges 8:11

Gideoni akapanda

"Gideoni" inawakilisha askari wake wote. "Gideoni na askari wake"

Akalishinda

"Gideoni na jeshi lake wakalishinda"

Noba na Yogbena

Haya ni majina ya miji.

Zeba na Salmuna

Haya ni majina ya wanaume.

Hofu

Uwoga uliopitiliza unaosababisha mtu akashindwa kufikiri vizuri.

Judges 8:13

kupitia Heresi

Hili ni jina la barabara inayopita katikati ya milima miwili.

Akamkimbilia kijana mmoja

"akakutana na kijana mmoja"

kutafuta ushauri kutoka kwake

"Alimuomba amtajie majina ya viongozi wote wa mji"

Watu sabini na saba

"watu 77"

Judges 8:15

Zeba na Salmuna

Haya ni majina ya wanaume.

Je! mmemshinda Zeba na Salmuna?

Gideoni anarejea swali kwa watu wa Sukothi ili kuwakejeli. "Bado hamjamshinda Zeba na Salmuna."

Gideoni akawachukua ... naye akawaadhibu ... akaangusha

Hapa "Gideoni" anawakilisha askari wake.

Miiba na michongoma.

Vipande vyenye ncha kali vinavyokuwepo kwenye miti ambavyo vinaweza kuchoma watu au wanyama.

Penueli

Hili ni jina la mji.

Judges 8:18

Zeba na Salmuna

Haya ni majina ya wanaume.

Tabori

Hili ni jina la mji.

Kama wewe ulivyo, ndivyo walivyokuwa

"walikuwa kama wewe ulivyo"

Kama Bwana aishivyo

Hiki ni kiapo cha dini kinachoonesha kuwa anachotaka kuzungumza ni ukweli.

Judges 8:20

Yetheri

Hili ni jina la mtoto wa Gideoni.

kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake

"Hii ni kazi ya mwanaume"

Makoja

Hili ni umbo ambalo hutokea wakati ambao mwezi umefunikwa kwa kiwango kikubwa na kivuli.

Mapambo

"mapambo"

Judges 8:22

wewe, mtoto wako, na mjukuu wako

Hii inaelezea kuwa walitaka uzao wa Gideoni kutawala juu yao baada ya yeye kufa.

umetuokoa mikononi mwa Midiani

"mkono" inawakilisha nguvu za Wamidiani juu ya Israeli.

Wamidiani

"Midiani" inawakilisha watu wa Midiani.

Judges 8:24

Gideoni akawaambia

"Gideoni akawaambia wana wa Israeli"

Hereni

dhahabu inayovaliwa sikioni

Nyara

Hivi ni vitu vilivyochukuliwa kwa nguvu au vilivyochukuliwa kwa watu waliokufa vitani.

Wamidiani walikuwa na pete za dhahabu kwa sababu walikuwa Waishmaeli

Hapa msimuliaji anatuelezea historia ya Wamidiani.

Vazi

Nguo kubwa inayotengenezwa kwa kipande kikubwa cha kitambaa na huvaliwa mabegani kama koti.

Judges 8:26

shekeli 1,700 za dhahabu

Ukitumia njia za kisasa kuonesha ukubwa wake yaweza kuwa "kilogramu 18.7 za dhahabu" au "karibu kilogramu 20 za dhahabu"

mapambo ya makoja

"mapambo"

Vidani

Ni pambo linaloning'inia shingoni.

Iliyovaliwa na wafalme wa Midiani.

"Ambazo Wafalme wa Midiani walivaa"

Judges 8:27

Gideoni akafanya efodi kutoka katika pete

"Gideoni alitumia dhahabu toka kwenye pete na kutengeneza efodi"

Ofra

Hili ni jina la mji.

Israeli wote wakaiandama kwa ukahaba na kuabudu

Kuabudu miungu ya uongo inafananishwa na ukahaba. "Waisraeli walimtenda Bwana dhambi kwa kuabudu efodi"

Waisraeli wote

Hii ni namna ya kusisitiza kuonesha kuwa idadi kubwa ya Waisraei waliabudu miugu.

Ilikuwa mtego kwa Gideoni na kwa wale walio nyumbani kwake.

Kuiabudu efodi inaelezwa kuwa ilikuwa mtego kwao. "ilikuwa jaribu kwa Gideoni na familia yake" au "Gideoni na familia yake walitenda dhambi kwa kuiabudu"

kwa wale walio nyumbani kwake

"nyumbani kwake" inawakilisha familia ya Gideoni.

Kwa hiyo Midiani ilishindwa mbele ya watu wa Israeli

Hii inaweza kuanza kama "Kwa hiyo Bwana akawafanya Wamidiani kushindwa mbele ya watu wa Israeli" au "kwa hiyo Bwana akawasaidia Waisraeli kuwashinda Wamidiani"

hawakuinua vichwa vyao tena

"Hawakuwavamia Waisraeli tena"

Na nchi ikawa na amani

"nchi" inawakilisha wana wa Israeli. "Na Waisraeli walikaa kwa amani"

Miaka arobaini

"miaka 40"

Siku za Gideoni

"siku" inamanisha kipindi cha uhai wake.

Judges 8:29

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gideoni.

Wana sabini

"wana 70"

Judges 8:32

uzee mzuri

"Alipokuwa mzee"

Akazikwa

Inaweza kuandikwa hivi "wakamzika"

Ofra

Hili ni jina la mji.

jamaa ya Abiyezeri

Hili ni kundi la watu toka katika uzao wa Abiezeri.

Ikawa

Hii hutumika kuonesha mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi. Kama lugha yako ina njia nyingine ya kufanya hivi unaweza kuitumia.

wakageuka tena

Watu walimkataa Bwana na hii imefananishwa na kitendo cha kugeuka toka kwake. "waliacha kumuabudu Bwana"

kujifanyia ukahaba wenyewe kwa kuabudu Mabaali

Kuabudu miungu ya uongo inafananishwa na ukahaba.

Baali Berith

Hili ni jina la mungu wa uongo

Judges 8:34

kutoka kwa mikono ya adui

"mkono" unawakilisha nguvu na utawala. "toka kwenye nguvu za adui zao wote"

Kila upande

"waliowazunguka"

Nyumba ya Yerubaali.

"nyumba ya" inawakilisha familia ya mtu.

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gideoni

Judges 9

Judges 9:1

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gideoni.

Tafadhali sema haya, ili wakuu wote wa Shekemu wasikie, Ni kipi bora kwako Je, wana sabini wote wa Yerubali kutawala juu yenu, au kwamba moja tu atawale juu yenu?

"Tafadhali waulize watu wa Shekemu kama wapo tayari kutawaliwa na wasa sabini wa Yerubaali au wana mmoja tuu atawale juu yao"

Sabini

"70"

mimi ni mfupa na nyama yenu.

"mifupa yenu na nyama yenu" inaelezea kuwa na undugu na mtu fulani.

Judges 9:3

Ndugu za mama yake waliongea kwa niaba yake kwa viongozi

Hii ina maana ya kwamba ndugu za mama yake Abimeleki walizungumza na viongozi, wakapendekeza wamfanye Abimeleki kuwa mfalme.

wakakubali kumfuata Abimeleki

"wakakubali Abimeleki awe kiongozi wao"

Nyumba

"nyumba" inawakilisha hekalu.

vipande sabini vya fedha

Hii inamaanisha shekeli. Shekeli ina uzito wa gramu 11. "karibia kilo moja ya fedha"

Sabini

"70"

Baali Berith

Hili ni jina la mungu wa uongo.

wasio na sheria na wajinga

"wakorofi na wajinga"

Judges 9:5

Ofra

Hili ni jina la mji.

Jiwe moja

"jiwe 1"

Sabini

"70"

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gideoni.

Beth Milo

Hili ni jina la mahali.

Judges 9:7

Taarifa ya jumla:

Yotamu anaanza kuelezea fumbo ambalo miti inafananishwa na makundi mbalimbali ya watu.

Yotamu alipoambiwa juu ya jambo hilo

"Yotamu aliposikia kuwa Abimeleki amemuua ndugu yake"

Mlima Gerizimu

Huu ni mlima.

Siku moja miti ilikwenda kumtia mafuta mfalme juu yao. Wakauambia mzeituni, tawala juu yetu.

Miti inazungumziwa kwa kufananishwa na watu.

kumtia mafuta mfalme juu yao

Kutia mafuta ni ishara ya kuwakilisha kitendo cha kumteua mtu kuwa mfalme.

Tawala juu yetu

"kuwa mfalme wetu"

Judges 9:9

Taarifa ya jumla:

Yotamu anaendelea kuelezea fumbo ambapo miti inawakilisha makundi mbalimbali ya watu.

mti wa mizeituni ukawaambia

Mti unafananishwa na mtu anayeweza kusikia na kuongea.

Je! Nitaacha mafuta yangu ... juu ya miti mingine?

Mzeituni unauliza swali la kukataa kuwa na huruma. Swali hili linaweza kuelezewa kama sentensi "Sitaacha mafuta yangu ... juu ya miti mingine"

Kuvuka juu

Mti unatumia maneno haya ukimaanisha "kutawala juu"

Mtini

Mti unafananishwa na mtu anayeweza kusikia na kuongea.

Je, nitaacha utamu wangu ... Je, nitaacha utamu wangu

Mtini unauliza swali la kukataa kuwa na huruma. "sitaacha utamu wangu ... juu ya miti mingine"

utamu wangu na matunda yangu

"utamu" ni neno linaloonesha kuwa matunda ya mti ule yamekomaa.

Judges 9:12

Taarifa ya jumla:

Yotamu anaendelea kuelezea fumbo ambapo miti inawakilisha makundi mbalimbali ya watu.

Mti ukasema

Mti unafananishwa na mtu anayeweza kusikia na kuongea.

Mzabibu

Mzabibu unafananishwa na mtu anayeweza kusikia na kuongea.

Je, nitaacha divai yangu mpya ... juu ya miti mingine?

Mzabibu unauliza swali la kukataa kuwa na huruma. "Sitaacha divai yangu mpya ... juu ya miti mingine."

Mti wa miiba

Hii ni miida ambayo ina ncha kali sana inayoumiza. kichaka hiki kina miiba mingi katika matawi yake.

Judges 9:15

Taarifa ya jumla:

Yotamu anaendelea kuelezea fumbo ambapo miti inawakilisha makundi mbalimbali ya watu.

Miti ya miiba

Miiba inafananishwa na mtu anayeweza kusikia na kuongea.

kunipaka mafuta niwe mfalme juu yako

Kupaka mafuta ni ishara ya kumteua mtu kuwa mfalme.

upate usalama

"uwe salama"

Acha moto utoke kwenye miti ya miiba

Hapa miti ya miiba inajielezea yenyewe. "acha moto utoke kwangu"

Acha moto utoke kwenye miti ya miiba na uiteketeze mierezi ya Lebanoni.

Hii inamaanisha acha miiba iwake moto ili iiteketeze mierezi.

Sasa

Hii inaleta umakini na kuonesha umuhimu wa jambo linalofuata.

ikiwa umefanya vizuri juu ya Yerubaali na nyumba yake, na ikiwa umemuadhibu kama anavyostahili

Yotamu anaonesha kuwa kwa namna moja walichokifanya ni kitu kizuri japokuwa Yotamu haamini moja kwa moja kuwa wamefanya jambo zuri.

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gideoni.

Nyumba yake

"nyumba" inawakilisha familia ya Gideoni.

Judges 9:17

Taarifa ya jumla:

Yotamu anafanya maombi juu ya hali iliyopo mda ule na sehemu ile.

na kufikiri kwamba baba yangu alipigana kwa ajili yenu ... kutoka kwenye mkono wa Midiani

Yotamu anaelezea ni kwa jinsi gani haamini vitendo vyao vibaya walivyovifanya watu wa Shekemu kwa Gideoni na familia yake japokuwa Gideoni alipigana ili kuwaokoa watu wa Shekemu.

kutoka kwenye mkono wa Midiani

"mkono" unawakilisha nguvu na utawala.

umeamka juu ya

"umeipinga" au "umeasi juu ya"

Nyumba ya baba yangu

"nyumba" inawakilisha familia.

Sabini

"70"

Jiwe moja

"jiwe 1"

Mtumishi wake wa kike

"wake" inasimama badala ya Gideoni.

Judges 9:19

Ikiwa mlifanya kwa uaminifu na uelekevu pamoja na Jerubalai na nyumba yake

Yotamu anaonesha kuwa kwa namna moja walichokifanya ni kitu kizuri japokuwa Yotamu haamini moja kwa moja kuwa wamefanya jambo zuri.

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gideoni

Nyumba yake

"nyumba" inawakilisha familia.

Lakini ikiwa sio

Yotamu anaonesha upande mwingine kuwa wakichokifanya ni makosa na anatoa laana. Yotamu anaamini kuwa walichokifanya ni makosa.

moto utoke kwa Abimeleki, ukawaangamize watu wa Shekemu

Yotamu anatoa laana. anazungumza juu ya Abimeleki kuwaharibu watu wa Shekemu kwa kuwaangamiza kwa moto.

Basi moto utoke kwa watu wa Shekemu na Beth Milo, ili kumteketeza Abimeleki.

Yotamu anatoa laana. anazungumza juu ya Shekemu na Beth Milo kumteketeza Abimeleki kwa kumuangamiza kwa moto.

Beth Milo

Hili ni jina la mahali.

Beeri

Hili ni jina la mji

Judges 9:22

tatu

"3"

Mungu alituma roho mbaya kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu

Hii inamaanisha kuwa Mungu aliifanyia kazi laana aliyoitoa Yotamu kwa kutuma roho mbaya isababishe tatizo kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu.

Mungu alifanya hivyo ili uhalifu uliofanywa ... walimsaidia kuua ndugu zake.

"Mungu alifanya hivi ili kulipiza kisasi cha wana sabini ambao waliuawa na Abimeleki na watu wa Shekemu wakamsaidia"

Sabini

"70"

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gideoni.

Judges 9:25

wakawaweka wanaume wakimsubiri juu ya vilima ili wamwangamize

"akatuma watu wajifiche kwenye vilima na wasubiri kumuangamiza Abimeleki"

Hii iliripotiwa kwa Abimeleki

"kuna mtu alimwambia Abimeleki kuhusu watu wanaomsubiri ili wamwangamize"

Judges 9:26

Gaali ... Ebedi

Haya ni majina ya wanaume.

walimwamini

Hiki ni kitendo cha kumwamini mtu.

Wakaenda shambani

Hapa Gaali na ndugu zake na watu wa Shekemu ndio wanaozungumziwa.

wakazikanyaga

Walifanya hivi ili kupata maji ya matunda ya mizabibu kwa ajili ya kutengeneza mvinyo.

kukanyaga

"kuponda"

katika nyumba

"nyumba" inawakilisha hekalu.

Judges 9:28

Gaali ... Ebedi

Haya ni majina ya wanaume.

Abimeleki ni nani, na Shekemu ni nani, hata tumtumikie?

Gaali anatumia swali kusisitiza kuwa watu wa Shekemu hawawezi kumtumikia Abimeleki.

Abimeleki ni nani, na Shekemu ni nani,

Maswali haya yanamaana moja. Gaali anamuelezea Abimeleki kama Shekemu maana mama yake na Abimeleki alitoka Shekemu.

Je, si mwana wa Yerubaali? Na Zebuli si afisa wake?

Gaali anatumia swali kusisitiza kuwa watu wa Shekemu hawawezi kumtumikia Abimeleki.

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gideoni.

Zebuli

Hili ni jina la mwanaume.

Watumikieni watu wa Hamori, baba yake Shekemu

Gaali anamaanisha watu wa Shekemu wawatumikie watu wa uzao wa Hamori.

Kwa nini tunapaswa kumtumikia?

Gaali anatumia swali kusisitiza kuwa watu wa Shekemu hawawezi kumtumikia Abimeleki.

Laiti watu hawa wangekukuwa chini ya amri yangu

"natamani ningekuwa nawatawala watu wa Shekemu"

Judges 9:30

Zebuli

Hili ni jina la mwanaume.

aliposikia maneno ya Gaali, mwana wa Ebedi

"maneno" inawakilisha kile alichokisema.

Gaali ... Ebedi

Haya ni majina ya wanaume.

hasira yake ikawaka

Kitendo cha kuwa na hasira kinafananishwa na moto unaoanza kuwaka.

ili wapate kudanganya

Zebuli anamdanganya Gaali na watu wa Shekemu.

nao wanauchochea mji dhidi yako

"wanawashawishi watu wa mji waasi dhidi yako"

mji

"mji" inawakilisha watu wa mjini.

Judges 9:32

Taarifa ya jumla:

Mjumbe wa Zebuli anaendelea kuzungumza na Abimeleki.

Sasa

Neno hili linaonesha umuhimu wa jambo linalofuata.

uvamizi

"kujificha na kushambulia ghafla"

fanyeni chochote mnachoweza

Hii inamaanisha wanaweza kufanya jambo lolote ili kuwaangamiza wafuasi wa Gaali.

Judges 9:34

watu wote waliokuwa pamoja

"na watu wote wakamsindikiza Abimeleki"

wakaandaa uvamizi dhidi ya Shekemu

"Shekemu" inawakilisha watu wa Shekemu.

wakagawanyika vitengo vinne

"wakagawanyika katika makundi 4"

Gaali ... Ebedi

Haya ni majina ya wanaume.

Judges 9:36

Gaali

Hili ni jina la mwanaume.

Zebuli

Hili ni jina la mwanaume.

Wewe unaona vivuli juu ya vilima kama vile watu

Zebuli anajaribu kumchanganya Gaali na kusababisha asijiandae na vita. "Hao sio watu ni vivuli tuu juu ya vilima"

kitengo kimoja

"kundi 1"

Judges 9:38

Zebuli

Hili ni jina la mwanaume.

Je, maneno yako ya kiburi yako wapi sasa?

"maneno" yanawakilisha kile alichosema. "kiburi chako kiko wapi sasa."

wewe uliyesema, 'Abimeleki ni nani, ili tumtumikie?

Zebuli ananukuu swali la Gaali kwa Gaali mwenyewe. "wewe ndiye uliyesema kwamba tusimtumikie Abimeleki."

Je, hao sio watu ambao uliwadharau?

Swali hili linaweza kuwekwa katika senytensi kama "Hawa ndo watu ambao uliwadharau"

Aliwadharau

"aliwachukia" au "hakuwapenda"

Gaali

Hili ni jina la mwanaume

Na wengi wakaanguka na majeraha ya mauti

"na wengi wakafa kwa sababu ya majeraha"

Judges 9:41

Aruma

Hili ni jina la mji.

Zebuli

Hili ni jina la mwanaume.

Gaali

Hili ni jina la mwanaume.

hii ikamfikia Abimeleki

"kuna mtu alimfikishia taarifa Abimeleki"

akawagawanywa katika vitengo vitatu

"Akawatenganisha kati ka vitengo 3"

wakaandaa uvamizi mashambani

"Walijificha mashambana na kuwavamia watu ghafla.

Akawakamata

Huyu ni Abimeleki anayewakilisha askari wake.

Judges 9:44

vitengo

"Makundi ya askari"

vingine viwili

"vingine 2"

Abimeleki alipigana ... Akabomoa

"Abimeleki" anawakilisha askari wake. "Abimeleki na askari wake walipigana... wakabomoa"

Dhidi ya mji

"mji" inawakilisha watu. "dhidi ya watu wa Shekemu"

Akabomoa

Akaharibu

kueneza chumvi juu yake

Kitendo cha kumwaga chunvi juu ya nchi ni kitendo cha kuzuia kitu chochote kisistawi hapo"

Judges 9:46

nyumba

Hii inawakilisha hekalu.

El Berithi

Neno "El" inamaana ya mungu. Hili ni jina la mungu wa uongo.

Abimeleki aliambiwa

"kuna mtu alimwambia Abimeleki"

Judges 9:48

Mlima Salmoni

Hili ni jina la mlima.

Wakayafungia

Kuyashikiza na kuyafunga pamoja.

Elfu moja

"1,000"

Judges 9:50

Thebezi

Hili ni jina la mji

akapiga kambi dhidi ya Thebezi

"akapiga kambi nje ya mji wa Thebezi"

Judges 9:52

kupigana nao

"kuwavamia"

jiwe la juu

Mawe makubwa mawili yaliyokuwa yanatumika kusagia nafaka. Jiwe la juu ni lile lililokuwa juu ambalo lilizungushwa ili kusaga nafaka.

mbeba silaha

Huyu ni mtu aliyekuwa anabeba silaha za Abimeleki.

akamchoma

Hii inamaanisha kuwa kijana alichomeka upanga kwenye mwili wa Abimeleki.

Judges 9:55

Sabini

"70"

akafanya uovu wote wa watu wa Shekemu ugeuke juu ya vichwa vyao wenyewe

"uovu wao ukawarudia juu ya vichwa vyao" "kuwaadhibu watu wa Shekemu kwa uovu waliofanya"

juu yao ilikuja laana ya Yothamu mwana wa Yerubaali

"laana ya Yothamu mwana wa Yerubaali ikawapata"

Yerubaali

Hili ni jina lingine la Gideoni.

Judges 10

Judges 10:1

Tola ... Pua ... Dodo

Haya ni majina ya wanaume.

Shamiri

Hili ni jina la mahali.

akaondoka ili kuwaokoa Israeli

"akaenda kuwaokoa Israeli" au "akawa kiongozi na kuwaokoa Israeli"

kuwaokoa Israeli

"Israeli" inawakilisha watu wa Israeli.

Akawa mwamuzi wa Israeli

"kuamua" inamaanisha kuwaongoza watu wa Israeli.

Miaka ishirini na tatu

"Miaka 23"

Akazikwa

"wakamzika"

Judges 10:3

Alifuatiwa na Yairi Mgileadi

"Yairi Mgileadi alikuwa kiongozi baada ya Tola"

Yairi

Hili mi jina la mwanaume.

Mgileadi

Yairi alitoka katika kabila la Gileadi.

Akawa mwamuzi wa Israeli.

"kuamua" inamaanisha kuwaongoza watu wa Israeli.

Israeli

"Israeli" inawakilisha watu wa Israeli.

Miaka ishirini

"miaka 20"

Thelathini

"30"

Hawoth Yairi

Hili ni jina la mji lililotokana na jina la mtu.

hata leo

Hii inamaanisha wakati ambao kitabu cha waamuzi kinaandikwa.

Akazikwa

"wakamzika"

Kamoni

Hili ni jina la mahali.

Judges 10:6

waliendelea kutenda maovu mbele za Bwana

"waliendelea kufanya mambo ambayo Bwana alisema ni uovu"

mbele za Bwana

"mbele za Bwana" inawakilisha kitu ambacho Bwana anakifikiria au kuwaza juu ya jambo fulani.

Maashtoreti

Huu ni wingi wa Ashtoreti aliyekuwa anaabudiwa kama mungu wa uongo kwa namna mbalimbali.

Wakamsahau Bwana na hawakamsujudia tena

"waliacha kabisa kumwabudu Bwana"

Wakamsahau Bwana

Kumtii na kumwabudu Bwana inazungumzwa kama kitendo cha watu kumwacha Bwana na kwenda mahali pengine.

Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli

Kitendo cha Bwana kuwa na hasira kinafananishwa na moto uwakao.

akawauza mikononi mwa Wafilisti na katika mikono ya wana wa Amoni

Bwana akaruhusu Wafilisti na Waamoni wawashinde Waisraeli.

mkononi mwa

"mkono" unawakilisha nguvu na utawala.

Judges 10:8

Kuwaangamiza na kuwadhulumu

Haya maneno mawili yana maana moja ya kusisitiza ni kwa namna gani wana wa Israeli walikuwa wanateseka.

Miaka kumi na nane

"miaka 18"

waliokuwa ng'ambo ya Yordani

Hii inamaanisha waliokuwa mashariki mwa mto Yordani.

iliyoko Gileadi

"huu mji pia uliitwa Gileadi"

Yuda ... Benyamini

"Yuda" na "Benyamini" inasimama badala ya watu waliotoka katika makabila haya. "watu wa kabila la Yuda ... watu wa kabila la Benyamini"

Nyumba ya Efraimu

"nyumba" inasimama badala ya kabila la Efraimu.

Israeli akasumbuliwa sana

"israeli" inasimama badala ya watu wa Israeli. "watu wa Israeli wakateseka sana"

Judges 10:10

wana wa Israeli wakamwita Bwana

Hii ina maana kuwa wana wa Israeli waliomba msaada kwa Bwana.

kwa sababu tumemwacha Mungu wetu

Watu waliacha kumtii na kumuabudu Bwana, walimuacha na kwenda kuabudu miungu mingine.

tumemwacha Mungu wetu

"kukuacha wewe, Mungu wetu"

Je, sikuwatoa ninyi ... Wasidoni?

Bwana aliwakemea wana wa Israeli kwa kitendo chao cha kuabudu miungu mingine.

Waamoni

Hawa ni watu wa familia ya Amoni.

kutoka katika nguvu zao

"Nguvu" inawakilisha Waamaleki na Wamaoni.

Judges 10:13

mliniacha tena

Watu waliacha kumtii na kumuabudu Bwana, walimuacha na kwenda kuabudu miungu mingine.

Kwa hiyo, sitawaokoa tena.

"Sitaendelea kuwaokoa tena na tena"

Judges 10:15

Wakaiacha miungu ya kigeni

Watu wakaacha kuabudu miungu ya uongo.

miungu ya kigeni waliyokuwa nayo

"miungu ya kigeni ambayo walimiliki sanamu zake"

Naye akawa na subira juu ya taabu ya Israeli.

"Naye hakutaka watu wa Israeli wateseke tena"

Judges 10:17

Ni nani atakayeanza kupigana na Waamoni?

"Nani ataongoza jeshi letu ili kupigana na Waamoni?"

Judges 11

Judges 11:1

Mgileadi

Huyu ni mtu anayetoka katika mji wa Gileadi.

Wana wa mkewe walipokua

"Wana wa mke wa Gileadi walipokuwa wakubwa"

nchi ya Tobu

Hili ni jina la mji.

wakaja na kwenda pamoja naye.

"wakamfuata" au "walienda kila sehemu pamoja"

Judges 11:4

Siku kadhaa baadae

"Siku zilizofuata"

walipopigana na Israeli

Waliwashambulia Waisraeli na kupigana vita pamoja nao.

ili tupigane na

"ili tupigane dhidi ya"

Judges 11:7

Nyumba ya baba yangu.

"nyumba" inawakilisha watu waishio nyumbani.

Ndiyo sababu tunakugeukia sasa

"tunakuja kwako sasa kwa sababu tupo kwenye shida"

pigana na watu wa Amoni

"pigana dhidi ya watu wa Amoni"

Judges 11:9

msimamizi na mkuu

Maneno haya yana maana moja na yanasisitiza ni kwa namna gani Yeftha alikuwa wa muhimu.

Alipokuwa mbele ya Bwana huko Mizpa, Yeftha akarudia ahadi zote alizozifanya.

"mbele ya Bwana" inamaanisha kuwa alirudia ahadi zake kama kiapo mbele za Bwana.

ahadi zote alizozifanya

Hizi ni ahadi alizozitoa kwa viongozi wa Gileadi kwa kuwa kiongozi wao.

Judges 11:12

Ni nini mgogoro huu kati yetu?

"Kwa nini kuna mgogoro kati yetu?" Yeftha anamuuliza mfalme kwa nini wana hasira na Israeli.

Kwa nini umekuja kwa nguvu kuchukua ardhi yetu?

"Kwa nini askari wako wamekuja kuchukua ardhi yetu"

umekuja kwa nguvu kuchukua

"kuja kuchukua kwa nguvu"

Arnoni ... Yaboki

Haya ni majina ya mito miwili.

mpaka Yordani

"Upande mwingine wa mto Yordani"

Kwa amani

"amani"

Judges 11:14

Akasema

Mjumbe ndiye anayezungumza na mfalme. "Yeftha alimwambia mjumbe aseme"

walitoka Misri

Waisraeli walipotoka Misri walikuwa njiani kuelekea katika nchi ya ahadi.

Judges 11:17

Taarifa ya jumla:

Mjumbe wa Yeftha anaendelea kuzungumza.

Israeli walipotuma wajumbe

Wajumbe hawa walitumwa na viongozi wa Israeli.

Kupita

"kipitia" au "kukatisha"

Walikataa

"kukataa" au "kutosikiliza ombi lao"

Wakawatuma wajumbe kwa mfalme wa Moabu

"pia walituma wajumbe kwa mfalme wa Moabu juu ya ombi hilo hilo"

lakini akakataa

Mfalme wa Moabu alikataa ombi la Waisraeli kupita katika Moabu.

Arnoni

Hili ni jina la mto.

Judges 11:19

Taarifa ya jumla:

Mjumbe wa Yeftha anaendelea kuzungumza.

Israeli wakatuma wajumbe kwa Sihoni

Wajumbe walitumwa na viongozi wa Israeli.

Sihoni

Hili ni jina la mtu.

Heshboni ... Yahasa

Haya ni majina ya miji.

Lakini Sihoni hakumwamini Israeli apite katika eneo lake

Sihoni hakumuamini Israeli apite katika nchi yake kwa amani.

Akapigana huko

Sihoni anawakilisha jeshi lake. "wakapigana huko" au "jeshi lake likapigana huko"

Judges 11:21

Taarifa ya jumla:

Mjumbe wa Yeftha anaendelea kuzungumza.

Sihoni

Hili ni jina la mwanaume.

akamtia Sihoni na watu wake wote mkononi mwa Israeli

"mkono" inamaanisha nguvu ya kushinda vitani.

Arnoni ... Yaboki

Haya ni majina ya mito.

Judges 11:23

Taarifa ya jumla:

Mjumbe wa Yeftha anaendelea kuzungumza.

na sasa mnataka kuimiliki nchi yao?

"kwa hiyo hamtakiwi kuchukua umiliki wa nchi yao."

Je, huwezi kuchukua nchi ambayo Kemoshi, mungu wako, anakupa?

Yeftha anamkemea mfalme wa Waamoni kwa kutumia swali. "mlipaswa kuchukua ardhi ambayo mungu wenu Kemoshi amewapa."

kuchukua

"kumiliki" au "kutawala"

Kemoshi

Hili ni jina la mungu wa uongo.

Sasa wewe ni bora zaidi kuliko Balaki, mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu?

Yeftha anamkemea mfalme wa Waamoni kwa kutumia swali. "wewe sio bora kama Balaki mwana wa Sipori mfalme wa Moabu."

Balaki ... Zipori

Haya ni majina ya wanaume.

Je, alidai kuwa na hoja na Israeli?

Yeftha anamkemea mfalme wa Waamoni kwa kutumia swali.

Je, yeye amewahi kupigana vita dhidi yao?

Yeftha anamkemea mfalme wa Waamoni kwa kutumia swali. "Hakupigana vita dhidi yao."

Judges 11:26

Taarifa ya jumla:

Mjumbe wa Yeftha anaendelea kuzungumza.

Miaka mia tatu

"miaka 300"

Heshboni

Hili ni jina la mji.

Aroeri

Hili ni jina la mji.

Arnoni

Hili ni jina la mji.

kwa nini hamkuwachukua tena wakati huo?

"Mngewachukua tena wakati huo" au "sasa mmechelewa; mngewachukua wakati huo."

ijawafanyia vibaya, lakini mnanifanyia vibaya kwa kunishambulia

Yeftha anazungumza na Sihoni. "Waisraeli hawajakufanyia mabaya, lakini watu wako wanatutendea mabaya kwa kutushambulia.

kuwatenda mabaya ... kunitendea mabaya

Kumtendea mtu mabaya inamaana kumfanyia mtu jambo baya.

Judges 11:29

Roho wa Bwana akamjia Yeftha

"Roho wa Bwana akamtawala Yeftha"

akapita Gileadi na Manase ... kutoka Mispa ya Gileadi

Yeftha alipita maeneo haya akiorodhesha watu kwa ajili ya jeshi lake kwenda vitani na watu wa Amoni.

Nami nitatoa hiyo sadaka

Kutoa kitu kwa ajili ya sadaka. "Nitakitoa kwako"

Judges 11:32

Basi Yeftha akapita kwa ... Bwana akampa ushindi ... Akawashinda

"Basi Yeftha na jeshi lake wakapita kwa ... Bwana akawapa ushindi ... wakavamia"

Aroeri

Hili ni jina la mji.

Minithi ... Abeli Keramimu

Haya ni majina ya miji.

Miji ishirini

"Miji 20"

Judges 11:34

Ngoma

Hiki ni kifaa cha muziki kinachopigwa kwa kutumia vipande vya chuma.

alirarua nguo zake

Hiki ni kitendo cha kuonesha kuomboleza au huzuni kubwa.

Umenivunja kwa huzuni ... umekuwa mtu anayenisababishia maumivu yangu

"Yeftha anazungumza kitu kile kile kusistiza ni kwa kiasi gani aamehuzunika"

Umenivunja kwa huzuni

Yeftha anaizungumzia huzuni yake kama vile kitu kilichovunjwa. "Umenisababishia huzuni kubwa"

umekuwa mtu anayenisababishia maumivu yangu

Yeftha anazungumza juu ya shida aliyonayo akiifananisha na maumivu.

siwezi kurudisha ahadi yangu.

Yeftha hawezi kuacha kufanya alichoahidi kukifanya.

Judges 11:36

amekulipia kisasi juu ya adui zako, wana wa Amoni

"amekulipa kisasi juu ya adui zako, wana wa Amoni kwa kuwashinda wao"

Hebu ahadi hii ihifadhiwe kwa ajili yangu

"Itunze ahadi hii kwa ajili yangu" au "itunze ahadi hii kuhusu mimi"

kuomboleza juu ya ubikira wangu

"kuomboleza kwa sababu mimi ni bikira" au "kuomboleza kwa sababu sitaolewa"

Judges 11:38

Mgileadi

Yairi alitoka katika kabila la Gileadi.

Judges 12

Judges 12:1

Watu wa Efraimu walitoka pamoja

"Watu wa Efraimu waliitwa pamoja" au "Watu wa Efraimu waliwakusanya askari wao"

Zafoni

Hili ni jina la mji.

wakapitia ... umetangulia

"kusafiri kupitia" au "kusafiri"

Tutachoma nyumba yako.

Hii inamaanisha tutachoma moto nyumba yako na watu walioko ndani.

Nilipokuita,

Hii imetumika kama wingi ikimaanisha watu wa Efraimu.

hukuniokoa

Hapa Yeftha anawaelezea watu wa Gileadi kama yeye mwenyewe. "hamkutuokoa sisi"

Judges 12:3

hamkuniokoa

Yeftha anawazungumzia watu wa Gileadi pamoja na yeye mwenyewe.

nikaweka uhai wangu na nguvu yangu mwenyewe

Hii inamaanisha kuyatoa muhanga maisha yako na kutegemea nguvu zako mwenyewe.

Bwana alinipa ushindi

Yeftha anaonesha kuwa Bwana aliwapa ushindi watu wa Gileadi juu ya Waanoni.

akapigana na Efraimu

Yeftha na watu wote wa Gileadi walipigana na Efraimu.

Kwa nini mmekuja kupigana nami leo?

Yeftha inamaanisha watu wa Gileadi. "Kwa nini mmekuja kupigana nasi"

Ninyi Wagileadi ni wakimbizi

"ninyi Wagileadi hapa sio kwenu. Mmekuja hapa kuishi tuu"

kupita ili kupigana na wana wa Amoni

Hii inamaanisha walipigana na Waamoni walipokuwa wakipita Amoni.

Wagileadi

"watu kutoka Gileadi"

katika Efraimu-katika Efraimu na Manase

"katika mji wa Efraimu na manase" au "katika nchi ya Efraimu na Manase"

Judges 12:5

kwa Efraimu

"katika nchi ya Efraimu"

Wagileadi waliteketeza

"Wagileadi walitawala"

Vivuko

Sehemu ambazo unaweza kupita kuvuka mto kwa miguu.

Mwefraimu

"Mtu toka kabila la Efraimu"

Shiboleth ... 'Sibboleth

Maneno haya hayana maana yoyote.

kutamka

"sema"

Elfu arobaini na mbili

"42,000"

Waefraimu elfu arobaini na mbili waliuawa

"Waliwaua Waefraimu elfu arobaini na mbili"

Judges 12:7

Yeftha Mgileadi akafa na akazikwa

"Yeftha Mgileadi akafa na wakamzika"

Judges 12:8

Ibzani

Hili ni jina la mtu toka Betlehemu.

Aliwapeleka binti thelathini katika ndoa

Hii inamaanisha aliwaruhusu binti zake kuolewa.

naye akaleta binti thelathini kutoka nje kwa ajili ya wanawe

"aliandaa mabinti thelathini toka nje ya jamaa yake kwa ajili ya kuolewa na watoto wake wa kiume"

Judges 12:10

Alizikwa Bethlehemu.

"wakamzika Bethlehemu"

Eloni

Hili ni jina la mwanaume.

Mzabuloni

Mtu kutoka kabila la Zabuloni.

Aiyaloni

Hili ni jina la mahali.

akazikwa huko Aiyaloni

"wakamzika huko Aiyaloni"

Judges 12:13

Abdoni ... Hileli

Haya ni majina ya wanaume.

Mpirathoni ... Pirathoni

Pirathoni ni jina la mahali, na mtu anayetokea huko anaitwa Mpirathoni.

Walipanda punda sabini

Watu hawa walimiliki punda sabini ambao waliwapanda.

wana arobaini ... wajukuu thelathini ... punda sabini

"wana 40 ... wajukuu 30 ... punda 70"

Judges 13

Judges 13:1

yaliyo mabaya machoni pa Bwana

"machoni pa Bwana" inawakilisha kitu ambacho Bwana anakifikiria au kuwaza juu ya jambo fulani.

akawatia mikononi mwa Wafilisti

"mkono" inamaanisha nguvu ya kushinda vitani. "aliruhusu Wafilisti wawashinde"

Miaka arobaini

"miaka 40"

Sora

Hili lilikuwa jina la mji katika Israeli. Ilikuwa katika mji wa Yuda karibu na mpaka wa Dani.

Wadani

Watu wa kabila la Dani.

Manoa

Hili ni jina la mwanaume.

Judges 13:3

kuzaa mtoto mwanaume.

"kuzaa mtoto wa kiume" au "kuwa na mtoto wa kiume"

chochote kilicho najisi

Kitu ambacho Bwana amesema hakifai kuliwa kinaonekana kuwa ni najisi.

Tazama

"sikiliza"

Hakuna wembe itakayotumiwa juu ya kichwa chake

"kichwa" inamaanisha nywele. "Hakuna mtu atakayekata nywele zake"

Wembe

Ni kisu kikali kitumikacho kukata nywele karibu na ngozi.

Mnaziri wa Mungu

"alitolewa kwa Mungu kama Mnaziri"

kutoka tumboni

"kabla hajazaliwa"

mkono wa Wafilisti

"mkono" inamaanisha utawala. "kuwa chini ya utawala wa Wafilisti"

Judges 13:6

Mtu wa Mungu

Hii inamaanisha kuwa mtu huyu alitumwa na Mungu.

kuonekana kwake kulikuwa kama malaika wa Mungu, wa kutisha sana.

"Nilimwogopa kwa sababu alionekama kama malaika wa Mungu"

Tazama

"sikia"

Utazaa mtoto mwanaume

"kuzaa mtoto wa kiume" au "kuwa na mtoto wa kiume"

chakula chochote ambacho sheria inasema kuwa si safi

Kitu ambacho Bwana amesema hakifai kuliwa kinaonekana kuwa ni najisi.

Mnaziri wa Mungu.

"alitolewa kwa Mungu kama Mnaziri"

tangu alipokuwa tumboni mwako mpaka siku ya kufa kwake

Hii inasisitiza kuwa itakuwa hivi kwa kipindi chote cha maisha yake.

Judges 13:8

Manoa

Hili ni jina la mwanaume.

akamwendea mwanamke

"akamwendea mke wa Manoa"

Judges 13:10

Tazama

"Sikia" au "tega sikio na ninayotaka kukwambia"

Mtu

Hii inamaanisha malaika wa Mungu.

Judges 13:12

Maneno yako

Haya ni maneno ambayo yule mtu aliyasema. "maneno uliyosema"

kitu chochote kinachotokana na mizabibu

Hapa malaika anamaanisha chakula chochote kitokanacho na mizabibu.

chochote ambacho sheria inasema kuwa si safi

Kitu ambacho Bwana amesema hakifai kuliwa kinaonekana kuwa ni najisi

Judges 13:15

kuandaa mbuzi kwa ajili yako

"kupika mbuzi kwa ajili yako ili upate kula"

Judges 13:17

maneno yako yatakapotimia

"maneno yako" haya ni maneno ambayo malaika aliyasema.

Mbona unauliza jina langu?

Malaika anamuuliza swali kwa kumkemea. swali hili laweza kuwa "Hupaswi kuniuliza jina langu"

Ni ajabu

"Ni ajabu kwako kuelewa"

Judges 13:19

sadaka ya nafaka

Sheria hii inataka sadaka ya nafaka itolewe wakati sadaka ya kuteketezwa inatolewa.

juu ya mwamba

"juu ya madhabahu"

Alifanya jambo

"Malaika alifanya jambo"

malaika wa Bwana akapanda katika moto wa madhabahu

"malaika wa Bwana akarudi mbinguni kupitia miale ya moto juu ya madhabahu"

wakainamisha vichwa vyao chini

Hii ni ishara ya utii na heshima lakini pia inaonesha walikuwa na hofu ya Bwana.

Judges 13:21

kwamba yule ndiye malaika wa Bwana

"yule" inamuelezea yule mtu ambaye Manoa na mke wake walimuona.

Hakika tutakufa, kwa sababu tumemwona Mungu

"Mungu atatufanya tufe kwa sababu tumemuona yeye"

Judges 13:23

Asingetuonesha mambo haya yote, wala wakati huu asingeweza kuturuhusu tusikie mambo hayo.

Mke wa manoa alizungumza jambo lile lile.

Judges 13:24

Mwanamke

"Mke wa Manoa"

kuzaa mtoto mwanaume

"kuzaa mtoto wa kiume" au "kuwa na mtoto wa kiume"

alikua

"akawa kijana" au "akapevuka"

Roho wa Bwana akaanza kumchochea

"Roho wa Bwana akaanza kumchochea Samsoni"

Mahane Dani ... Eshtaoli

Mahane Dani ni jina la kambi ya muda ambayo kabila la Wadani waliishi hapo wakiwa wanatafuta makazi ya kudumu.

Sora

Hili ni jina la mji.

Judges 14

Judges 14:1

Samsoni akashuka kwenda Timna

Neno "kushuka" linatumika kwa sababu Timna ipo juu ya ilipokuwa nyumba ya baba yake na Samsoni. Timna ni jina la mji uliopo kwenye bonde la Soreki.

mmojawapo wa binti za Wafilisti.

"binti" ni njia moja wapo ya kuelezea kuwa mwanamke huyu alikuwa hajaolewa.

Sasa mkanichukulie awe mke wangu.

Samsoni aliwaomba wazazi wake wazungumze na wazazi wa yule mwanamke kuhusu ndoa.

Judges 14:3

Je, hakuna mwanamke kati ya binti za ndugu zako, au kati ya watu wetu wote?

Waliuliza swali kwa kutoa maoni kuwa wanaweza kumtaftia Samsoni mke kati ya jamaa zao.

binti za ndugu zako

"binti" ni njia moja wapo ya kuelezea kuwa mwanamke huyu alikuwa hajaolewa.

Je! Utachukua mke kutoka kwa Wafilisti wasiotahiriwa?

Swali hili linaulizwa ili kumkemea Samsoni. "Hutakiwi kuoa mwanamke wa Kifilisti kwa sababu Wafilisti hawamwabudu Bwana"

Nichukulie kwa ajili yangu

Samsoni aliwaomba wazazi wake wazungumze na wazazi wa yule mwanamke kuhusu ndoa.

Ananipendeza mimi

Samsoni alifikiri kuwa binti yule ni mzuri. "Ananipendeza kwa namna alivyo mzuri"

suala hili

Hili ni ombi la Samsoni kuoa wanamke wa Kifilisti.

kwa maana alitaka kutengeneza mgogoro na Wafilisti

Kwa maana Bwana alitaka kutengeneza mgogoro na Wafilisti.

Judges 14:5

Samsoni akashuka Timna

Neno "kushuka" linatumika kwa sababu Timna ipo juu ya ilipokuwa nyumba ya baba yake na Samsoni. Timna ni jina la mji uliopo kwenye bonde la Soreki.

Na, tazama, kuna simba mdogo wa alikuja

"Tazama" ni neno lililotumika ili kumfanya msomaji awe makini kwa tukio linalofuata katika simulizi.

alikuwa akiunguruma

"alikuwa akimtisha." Hii ni sauti ya simba ambayo huitoa akiwa anataka kuvamia kitu.

Roho wa Bwana ghafla akaja juu yake

Roho wa Bwana akamchochea Samsoni. Akamfanya kuwa na nguvu sana.

Kumrarua ... vipande

Akamrarua vipande viwili.

hakuwa na kitu mkononi mwake

Hakuwa na kitu mkononi mwake ikimaanisha kuwa hakuwa na silaha yoyote.

Judges 14:7

alimpendeza Samsoni

Samsoni anafikiri kuwa binti yule ni mzuri. "Ananipendeza kwa namna alivyo mzuri"

Akageuka

Hii inamaanisha aliiacha njia na kufanya jambo fulani.

Mzoga

"Kiumbe kilichokufa"

Na, tazama, kulikuwa na kundi la nyuki

"Tazama" ni neno lililotumika ili kumfanya msomaji awe makini kwa tukio linalofuata katika simulizi. "

Kundi

"kundi kubwa la wadudu"

Akaweka

"akakusanya"

Judges 14:10

Baba yake Samsoni akaenda chini alipokuwa mwanamke

Neno "kushuka" linatumika kwa sababu Timna ipo juu ya ilipokuwa nyumba ya baba yake na Samsoni. Hapa inaonesha kuwa alikuwa Timna pamoja na Samsoni.

desturi ya vijana

"desturi ya vijana waliokaribia kuoa"

rafiki zao thelathin

"rafiki zao 30"

Judges 14:12

Kitendawili

Huu ni mchezo ambao wachezaji wanatakiwa wagundue jibu kutokana na swali gumu.

anaweza kuipata

"Anaweza kuipata maana yake"

nguo za kitani thelathini na seti ya nguo thelathini

"nguo za kitani 30 na seti ya nguo 30"

Lakini ikiwa hamuwezi kuniambia

Anawaambia maneno haya wageni waliokuwa kwenye sherehe.

Kitani

Aina ya nguo.

Judges 14:14

Taarifa ya jumla:

Samsoni anawaambia kitendawili.

Kati ya mtu aliyekula kilikuwepo kitu cha kula

"kitu cha kula kilikuwepo ndani ya mtu aliyekula"

"aliyekula"

Inaweza kuelezewa kama "kitu kinachokula"

nje ya nguvu kilikuwa kitu tamu

"Kitu ambacho ni kitamu kimetoka kwenye kitu chenye nguvu"

yenye nguvu

"kitu chenye nguvu"

Wageni wake

"watu waliokuwepo kwenye shherehe"

Hawakupata jibu

"Hawakugundua jibu"

Judges 14:15

siku ya nne

"siku ya 4"

mdanganye

Kumdanganya mtu afanye jambo ambalo hataki kufanya.

Nyumba ya baba yako

Hii yaweza kuwa na maana ya 1) inamaanisha nyumba kabisa. 2)"nyumba" inamaanisha watu wanaoishi ndani yake.

Tutachoma moto

"kuchoma moto" inamaanisha kukiteketeza kutu kwa moto. Kama mtu akichomwa moto inamaana mtu huyo ameteketea kwa moto mpaka kufa.

Je, umetualika hapa ili kutufanya maskini?

Wanamuuliza swali hili kwa kumshataki kuwa amewaalika ili awafanye maskini. "umetuleta hapa ili kutufanya maskini"

kutufanya maskini

Watakuwa masikini kama watamnunulia nguo mpya ikiwa watashindwa kutegua kitendawili.

Judges 14:16

Yote unayoyafanya ni kunichukia! Hunipendi

"Hunipendi mimi kabisa"

Kitendawili

Huu ni mchezo ambao wachezaji wanatakiwa wagundue jibu kutokana na swali gumu.

Angalia hapa

"angalia" inamanisha "sikiliza" "nisikilize mimi" au "kuwa makini kwa ninachotaka kukwambia"

kama sijawaambia baba yangu au mama yangu, nikuambie wewe?

Samsoni anamkemea mke wake baada ya mkewe kumlazimisha amwambie jibu.

kwa siku saba ambazo sikukuu yao iliendelea

Yaweza kuwa na maana ya 1)"katika siku saba za sikukuu yao" au 2) "katika siku saba zilizobaki za sikukuu yao"

Siku ya saba

"siku ya 7"

Alimlazimisha sana

"Aliendelea kumlazimisha ili amwambie"

Judges 14:18

Siku ya saba

"siku ya 7"

Watu wa mji

Hawa ni ndugu wa mke wa Samsoni.

Ni nini kilicho bora zaidi kuliko asali? Ni kitu gani chenye nguvu kuliko simba?

Hili ndilo jibu la kitendawili. "asali ni tamu na simba ni mkali" au "asali ni tamu na imetoka kwa simba"

Ikiwa hamkulima na ng'ombe wangu

Samsoni anafananisha kumtumia mke wake kupata jibu kama kutumia ng'ombe wa mtu kulima shamba lake. "Kama msingemtumia mke wangu"

Kulima

Hiki ni kitendo cha kutumia mnyama kuvuta jembe kuandaa ardi kwa ajili ya kuweka mbegu.

Judges 14:19

akaja kwa Samsoni kwa nguvu

"akaja" hii inamaanisha kuwa roho wa Bwana alimchochea Samsoni. "akamfanya Samsoni kuwa na nguvu sana"

Akawauwa watu thelathini

"Akawauwa watu 30"

watu hao

"watu walioishi hapo"

Nyara

Vitu vinavyochukuliwa kwa nguvu, hasa baada ya mapigano vitani.

Seti ya nguo

"Seti ya nguo alizochukua"

alikasirika

"kukasirika sana"

akaenda nyumbani kwa baba yake

Samsoni alikuwa Timna ambapo kulikuwa juu kuliko sehemu ambayo nyumba ya baba yake ilikuwepo.

Na mke wake akachukuliwa na rafiki yake

"baba wa mke wake alimkabidhi kwa rafiki yake wa karibu"

Rafiki wa karibu

"rafiki wa karibu"

Judges 15

Judges 15:1

Akajiambia mwenyewe

"Akafikiri mwenyewe"

Nitaenda kwenye chumba cha mke wangu

"Nitaenda kwenye chumba cha mke wangu ili tulale pamoja"

hakumruhusu aingie

"jakumpa ruhusa aingie chumbani kwake"

hivyo nikampatia rafiki yako

"Hivyo nikampa aolewe na rafiki yako"

Je sio?

Anauliza swali hili kuonesha kuwa Samsoni anapaswa kukubali. "Natumaini unakubali"

Mchukue badala yake

"Mchukue awe mke wako badala yake"

Judges 15:3

sitakuwa na hatia juu ya Wafilisti wakati nikiwaumiza

Samsoni anafikiri kuwa kwa sababu Wafilisti wamemkosea hivyo hatakuwa na hatia akiwavamia.

Mbweha mia tatu

"mbweha 300"

Mbweha

Mbweha ni wanayama wadogo kama mbwa wenye mikia mirefu wanaokula wanyama wadogo wadogo na ndege.

Kila jozi

Jozi ni vitu viwili. Mfano mbweha wawili au mikia miwili.

Mkia kwa mkia

"kwa mikia yao"

Taa

Ni fimbo ya mbao inayowaka na kutoa mwanga ambayo mara nyingi hutumika usiku.

Judges 15:5

Nafaka

Nafaka ambazo zinaendelea kukua katika shamba.

Nafaka

Nafaka zilizokusanywa kabla hazijavunwa.

Mashamba

Hii ni sehemu ambayo miti ya matunda inakua.

Mtimna

Ni mtu anayetoka Timna.

Mkwe wa Mtimna

"mkwe"

alimchukua mke wa Samsoni akampa rafiki yake

"akamchukua mke wa Samsoni na kuruhusu aolewe na rafiki yake"

Wakamchoma

Hii inaonesha kuwa mtu alichomwa moto mpaka kufa.

Judges 15:7

akawaambia

"akawaambia Wafilisti"

Ikiwa ndivyo mnavyofanya

"kwa sababu mnafanya hivi"

akawakata vipande vipande, paja na mguu

"Akakata miili yao vipande vipande"

akashuka chini

"akashuka chini" au "akaenda"

pango

Sehemu ya wazi iliyopo mlimani.

Mwamba

mwamba uliopo kwenye mlima.

Etamu

Hili ni jina la mwamba karibu na Yerusalemu.

Judges 15:9

Wafilisti wakaja ... huko Yuda

Wafilisti walienda Yuda ambapo ni juu toka kwenye nchi yao.

kujiandaa na vita

"kujipanga wenyewe kwa ajili ya vita"

Lehi

Hili ni jina la mji uliopo Yuda.

tumtendee kama alivyotutendea

"tumuuwe kama alivyowaua watu wetu"

Judges 15:11

Watu elfu tatu wa Yuda

"watu 3,000 wa Yuda"

mwamba la Eatamu

Hili ni jina la mwamba lililopo karibu na Yerusalemu.

Je, hujui kwamba Wafilisti hutawala juu yetu? Je! umetutendea nini?

"Unajua kwamba Wafilisti wanatutawala lakini unafanya kama vile hawatutawali. Unayoyafanya yanatusababishia madhara makubwa."

Kwa kadiri walivyonitendea mimi, vivyo hivyo nimewatendea wao.

"Wamemuua mke wangu hivyo nimewaua na wao"

Judges 15:12

mikononi mwa Wafilisti

"Mikono" inamaanisha nguvu. "utawala wa Wafilisti"

kukupeleka kwao

"kukupeleka kwa Wafilisti"

kutoka kwenye mwamba

Huu ni mwamba wa Eatamu ambao Samsoni alienda.

Judges 15:14

Alipofika

"Samsoni hakusafiri pekeyake, alikuwa akiongozwa na watu waliokuwa wamemfunga kwa kamba"

Lehi

Hili ni jina la mji uliopo Yuda.

akaja juu yake kwa nguvu

Roho wa Bwana alimchochea Samsoni. "akamfanya Samsoni kuwa na nguvu"

Kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitambaa cha kuteketezwa

"Alizikata kamba zilizokuwa mikononi mwake kwa urahisi kama kitambaa kilichokuwa kinateketezwa"

Kitambaa

Hiki kimetokana na mmea ambacho hutumika kutengenezea nyuzi na nguo.

Judges 15:15

mfupa mbichi

Hii inamaanisha kuwa punda alikufa siku za karibuni na mfupa wake haukuanza kuharibika.

watu elfu moja

"watu 1,000"

taya ya punda

"taya ya punda"

Chungu juu ya chungu

Maneno haya yanaelezea ni kwa namna gani Samsoni aliwaua watu wengi sana.

Judges 15:17

Ramath Lehi

Hili ni jina la mahali. Lenye maana ya kilima cha taya.

alikuwa na kiu sana

"alihitaji maji ya kunywa"

Lakini sasa nitakufa kwa kiu na kuanguka

Yaweza kuwa na maana ya 1)Samsoni alikuwa na kiu sana kiasi cha kufa. 2)Samsoni alitia chunvi kuonesha ni kwa kiasi gani alikuwa na kiu.

kufa kwa kiu

Hii inamaanisha kuwa kufa kwa sababu hujanywa maji ya kutosha hivyo hauna maji ya kutosha mwilini.

kuanguka mikononi mwa wale wasiootahiriwa?

"kuanguka mikononi" Hii inamaanisha kukamatwa. "Wasiotairiwa" hawa ni Wafilisti, hii inasisitiza kuonesha kuwa hawakumwabudu Bwana.

Judges 15:19

akapafungua mahali pa shimo

"akapafungua mahali pa shimo" Hii ni sehemu ya chini ambayo Bwana alisababisha maji ya chemchemi yatoke.

Lehi

Hili ni jina la mji uliopo Yuda.

nguvu zake zikarejea na akahuishwa

"akapata nguvu tena" au "nguvu zake zikarejea"

Enhakore

Hili ni jina la chemchemi.

ni huko Lehi hadi leo

"chemchemi ipo mpaka leo huko Lehi"

katika siku za Wafilisti

"Katika wakati wa Wafilisti kuwatawala Waisraeli"

miaka ishirini

"miaka 20"

Judges 16

Judges 16:1

akalala pamoja naye

"Akalala naye"

Watu wa Gaza wakaambiwa

"Kuna mtu aliwaambia watu wa Gaza"

Watu wa Gaza wakazunguka mahali hapo ... wakamngoja usiku wote katika lango la jiji

Hii inaonesha kuwa Wagaza walizunguka sehemu ambayo Samsoni alikuwepo na wengine wakasubiri katika lango la jiji ili asiondoke.

Walikaa kimya usiku wote

"Hawakupiga kelele zozote usiku kucha" au "hawakutaka kumkamata usiku"

Judges 16:3

Usiku wa manane

"katikati ya usiku"

Miimo miwili

Yawezekana ilitengenezwa kwa magogo ya miti na ilichimbiwa chini ya ardhi kwa ajili ya kusikilia malango ya jiji.

Komeo na vyote

Komeo ni kifaa kizito cha chuma kinachounganishwa na mlango.

mabega

Hii ni sehemu ya mwili wa binadamu ambapo mikono na shingo vimeunganishwa pamoja.

Hebroni

Hili ni jina la mji.

Judges 16:4

Bonde la Sereki

Hili ni jina la bonde lililokuwa karibu na nyumba ya Samsoni.

Danganya

ni kitendo cha kumpotosha mtu ili afanye jambo ambalo hataki kufanya.

ili uone

"ili uelewe" au "ili ujifunze"

mahali zilipo nguvu zake kuu

"kinachomsababisha awe na nguvu"

kwa namna gani tunaweza kumshinda

"kwa jinsi gani tunaweza kumshinda"

Judges 16:6

kukufunga, ili aweze kukudhibiti

"kukufunga ili kukudhibiti"

kamba safi

Kamba hutengenezwa kwa kutumia wanyama. kamba safi ni zile ambazo zimetoka kwa mnyama ambaye amechinjwa na hajakauka bado.

ambazo hazijakauka

"ambazo hazijawa kavu"

Judges 16:8

ambazo hazijakauka

"ambazo hazijawa kavu"

akamfunga Samsoni

"Delila akamfunga Samsoni na kamba safi"

Sasa

Mwandishi anatueleza simulizi kuhusu Wafilisti na Delila wanavyosubiri kumkamata Samsoni.

Wafilisti wako juu yako

"Wafilisti wako hapa ili kukukamata"

akazikata kamba kama uzi wakati unapogusa moto

Mwandishi anaelezea ni kwa jinsi gani ilikuwa rahisi kwa Samsoni kuzikata kamba kama vile zinavyokatika zikiwa katika moto.

Judges 16:10

Ndivyo ulivyonidanganya mimi ... kuniambia uongo

"Umenidanganya"

Unaweza kufungwa

"watu wanaweza kukushinda"

Wafilisti wako juu yako

"Wafilisti wako hapa ili kukukamata"

waliokuwa wakisubiri

"wakimsubiri ili kumshambulia"

kama kilikuwa kipande cha uzi.

Mwandishi anaelezea ni kwa jinsi gani ilikuwa rahisi kwa Samsoni kuzikata kamba akifananisha na kipande cha uzi.

Judges 16:13

umenidanganya na kuniambia uongo

"Umenidanganya"

unaweza kufungwa

"watu wanaweza kukushinda"

Kufuma

Kupishanisha vipande pamoja ili vishikane.

vifungo vya nywele zangu

Vipande vidogo vya nywele

Kitambaa

nguo iliyotengenezwa kwa kufuma.

Kitanda cha mfumi

Hii ni mashine inayochanganya nyuzi na kutengeneza nguo.

kisha ukafunga kwenye kitanda cha mfumi

"kisha ukafunga kitambaa kwenye kitanda cha mfumi"

kufunga

Kufunga kitu sehemu moja.

nitakuwa kama mtu mwingine yeyote

"Nitakuwa na udhaifu kama mtu mwingine"

Wafilisti wako juu yako

"Wafilisti wako hapa ili kukukamata"

akang'oa kitambaa na pini zilizokuwa zimefungwa

"alizitoa nywele zake, pamoja akang'oa na pini zilizokuwa zimefungwa na kitambaa kilichokua kwenye kitanda cha mfumi"

Judges 16:15

Wawezaje kusema, 'Unanipenda', wakati hushiriki siri zako na mimi

Delila anauliza hili swali akiwa na maana ya kuwa kama Samsoni anampenda kwa dhati alipaswa kumwambia siri zake.

alisisitiza kwa bidii ... akamkemea sana

Hapa mwandishi anaonesha ni kwa kiasi gani Delila alimsisitiza Samsoni ili amwambie anachotaka kukifahamu.

na maneno yake

Haya ni maneno aliyosema Samsoni kwa Delila.

alitamani kufa

Hapa mwandishi ametia chunvi kuonesha ni jinsi gani Samsoni alichoshwa na maneno ya Delila.

Judges 16:17

alimwambia kila kitu

Alimwambia kila kitu juu ya asili ya nguvu zake.

wembe

Hiki ni kifaa chenye makali kinachotumika kinyolea nywele.

Mnaziri wa Mungu.

"alitolewa kwa Mungu kama Mnaziri"

kutoka tumboni mwa mama yangu

"kabla sijazaliwa"

Ikiwa kichwa changu kitanyolewa

"kama mtu atanyoa kichwa changu"

Kunyoa

Ni kitendo cha kukata nywele.

nguvu zangu zitaniacha

"sitakuwa na nguvu tena"

Judges 16:18

Delila alipoona

"kuona" inamaana ya alipotambua.

ukweli juu ya kila kitu

"ukweli juu ya nguvu za Samsoni"

Njooni tena

Delila anawaambia viongozi waende anapoishi.

wakaleta fedha mkononi mwao

Hii inamaanisha kuwa walimleta fedha walizomuahidi kuwa watampa ikiwa atawasaidia kumkamata Samsoni.

Alimfanya alale

"Alimsababisha alale usingizi"

kwenye mapaja yake

"alilaza kichwa chake kwenye mapaja yake"

Paja

Paja ni eneo la mguu wa juu.

Vifungo saba vya nywele zake

Samsoni alikuwa na vifungo saba katika nywele zake.

kumshinda

"kumtawala"

nguvu zake zilikuwa zimemwacha.

"nguvu zake ziliondoka" au "hakuwa na nguvu tena"

Judges 16:20

Wafilisti wako juu yako, Samsoni

Wafilisti wamekuja kukukamata.

Aliamka

"kuamka"

Nitatoka nje

"nitatoroka"

wakamng'oa macho yake

Hiki ni kitendo cha kutoa macho yake.

Wakampeleka Gaza.

Gaza ni sehemu iliyokuwa chini toka kwenye nyumba waliyomkamata.

wakamfunga kwa shaba

"wakamfunga kwa kutumia shaba"

Pingu

Hivi ni vifungo vinavyofungwa mwisho wa minyororo ili kushikilia miguu na mikono ya mfungwa.

Akisaga ngano

"kusaga ngano kuzunguka duara"

Jiwe la kusagia

Hili ni jiwe kubwa lenye umbo la duara ambalo hutumika kusagia nafaka. Huwa linazunguswa na wanyama kama ng'ombe au farasi.

baada ya kunyolewa.

"Baada ya Wafilisti kuzinyoa"

Judges 16:23

Dagoni

Alikuwa mungu wa uongo wa Wafilisti.

amemshinda

"amemshinda"

kumtia katika ufahamu

Mwandishi anaonesha kuwa Samsoni alikuwa chini ya utawala wa Wafilisti.

mharibifu wa nchi yetu

"mtu aliyeharibu nchi yetu"

aliwaua wengi wetu

"mtu aliyeua watu wetu"

Judges 16:25

Mwite Samsoni ... Walimwita Samsoni

Kwa kuwa Samsoni alikuwa mfungwa hakuitwa moja kwa moja, bali watu walimuomba mtu aliyekuwa muhusika ili amlete Samsoni.

Kijana

Huyu hakuwa mtoto mdogo lakini alikuwa kijana.

Niruhusu nishike nguzo zilizoshikilia nyumba hii, ili nipate kuegemea

"Niruhusu nishike nguzo zilizoshikilia nyumba"

Judges 16:27

Sasa

Hapa mwandishi anaelezea taarifa fulani kwa kukatisha simulizi.

wanaume na wanawake elfu tatu

"wanaume na wanawake 3,000"

Wakiangalia

"wakitazama"

wakati Samsoni alipokuwa akiwafurahisha

"Wakati Samsoni akiwafurahisha." "kufurahisha" ni kitendo cha kusimama katikati ya watu na kuwafanya wafurahi na kucheka.

Judges 16:28

Akamwita Bwana

"Akamwomba Bwana"

Nipe nia

"nikumbuke mimi"

mara moja tu

"kwa mara nyingine"

kwa wakati mmoja

Hii inamaanisha Samsoni anataka kulipiza kisasi ;lakini ili ikamilike inahitaji kitendo kimoja cha ngubu ambacho ni kuziangusha nguzo.

ambazo zinashikilia nyumba

"ambazo zinaishikilia jengo"

Judges 16:30

Alisukuma kwa nguvu zake

"alitumia nguvu zake kusukuma nguzo"

Waliouawa

"watu waliokufa"

walikuwa zaidi

"idadi yao ilikuwa kubwa sana"

nyumba yote ya baba yake

"familia yote ya baba yake"

Kisha ndugu zake na nyumba yote ya baba yake wakashuka

"Walishuka" kwa sababu sehemu ambayo familia ya Samsoni walitoka ilikuwa juu ya Gaza.

Sora ... Eshtaoli

Haya ni majina ya mahali.

mahali pa kuzikwa Manoa, baba yake

"mahali alipozikwa Manoa baba yake"

Manoa

Hili ni jina la mwanaume.

Samsoni alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini

"Samsoni alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini kabla hajafa"

Miaka ishirini

"miaka 20"

Judges 17

Judges 17:1

Kulikuwa na mtu

Hii ni njia ya kumtambulisha mtu mwingine katika simulizi.

Mika

Hili ni jina la mwanaume.

ambazo zilichukuliwa kutoka kwako

"ambazo mtu aliziiba toka kwako"

Nimeziiba

"mimi ndiye niliyezichukua"

Judges 17:3

Nimeweka

Hii inamaanisha kuweka kitu kwa ajili ya kusudi maalumu.

takwimu za chuma

Chuma kilichoyeyushwa na kutengeneza umbo maalumu.

Nakurudishia wewe

"Nairudisha kwako"

Vipande mia mbili vya fedha

"vipande 200 vya fedha"

Vikawekwa ndani ya nyumba ya Mika

"Mika akaviweka ndani ya nyumba yake"

Judges 17:5

nyumba ya sanamu

Hii ni nyumba ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuabudu sanamu. "alikuwa na nyumba ya kuabudia sanamu"

kila mtu alifanya yaliyo sawa machoni pake.

"kila mtu alifanya kile alichoona kilikuwa sawa"

Judges 17:7

Wa Bethlehemu

"toka Bethlehemu"

wa jamaa ya Yuda

Hii inamaana kuwa alikuwa akiishi kati ya familia ya Yuda, ambalo ni kabila la Yuda.

Alikaa huko ili kutimiza majukumu yake

"Alikaa na kufanya kazi huko"

kutafuta mahali pa kuishi

"kutafuta sehemu tofauti ya kuishi"

nipate kuishi

"ambapo nitaishi na kupata kazi"

Judges 17:10

baba na kuhani

Hapa "baba" imetumika kama mshauri. "mshauri na kuhani"

suti ya nguo

"suti ya nguo kila mwaka"

Basi Mlawi akaingia nyumbani mwake

"Hivyo Mlawi akakubaliana na alichoambiwa na akaingia kwenye nyumba yake"

huyo kijana kwa Mika akawa kama mmoja wa wanawe

Uhusiano kati ya Mika na Mlawi ukawa wa karibu sana kama uhusiano wa baba na mtoto wake.

Judges 17:12

Mika akamtenga Mlawi

"Kumtenga" maana yake ni kumtoa. "Mika akamtoa Mlawi"

katika nyumba ya Mika

"aliishi katika nyumba ya Mika"

Judges 18

Judges 18:1

Siku hizo ... miongoni mwa makabila ya Israeli

Haya ni maelezo juu ya Israeli na watu wa kabila la Dani.

Siku hizo

Hii inaonesha mwanzo wa tukio katika simulizi.

hawakupokea urithi wowote kutoka

"hawakupokea ardhi kama urithi"

kutoka kwa idadi yote ya kabila lao

"idadi yote" inamaanisha watu wa kabila lile.

wenye ujasiri

"wenye uzoefu wa kupigana"

ili kukagua ardhi kwa miguu

"miguu" inamaanisha kutembea.

Sora

Hili ni jina la mji.

Eshtaoi

Hili ni jina la mji.

Mika

Hili ni jina la mtu.

Judges 18:3

walitambua maneno ya Mlawi

Walimtambua yule mtu kwa namna alivyoongea.

Judges 18:7

Laishia

Hili ni jina la mji.

Hapakuwa na mtu aliyewashinda katika nchi hiyo

"Hapakuwa na adui yeyote aliyeishi kwenye nchi yao na kuwashinda"

hawakuwa na ushirikiano na mtu yeyote

"hawakuwa na mawasiliano na mtu yeyote wa nje" Hii inamaanisha kuwa walikuwa mbali sana na miji mingine.

Zora

Hili ni jina la mji.

Eshtaol

Hili ni jina la mji.

Judges 18:9

Je hamfanyi kitu?

Hili ni swali lenye maana ya kuwa mnapaswa kufanya jambo. "Mnapaswa kuchukua hatua sasa"

Msiwe wavivu kushambulia

"Shambulieni haraka"

nchi ni pana

"Nchi ni kubwa"

hapajapungukiwa kitu chochote duniani

"tutakuwa na kila kitu tunachokitaka"

hakujapungukiwa

"kuna kila kitu"

Judges 18:11

Watu mia sita

"watu 600"

Kiriath-yearimu

Hili ni jina la mji.

Mahane Dani

Hili ni jina la mji.

hata leo

Hii inamaanisha kuwa kitu kile kipo vile vile. "na mpaka leo ndio jina lake"

Judges 18:13

Laisha

Hili ni jina la mji.

Je, mnajua kwamba katika nyumba hizi kuna efodi ... sanamu za chuma? Amua utakachofanya.

Watu watano waliuliza hili swali kama njia ya kupendekeza na kuwahimiza wenzao ili waibe zile sanamu.

Judges 18:15

Wakarudi huko

"wakarudi"

wakamsalimu

"wakamsalimu Mlawi"

Wadani mia sita

"Wadani 600"

Judges 18:17

Watu mia sita

"Watu 600"

Judges 18:19

Je, ni bora kuwa wewe kuhani kwa ajili ya nyumba ya mtu mmoja ... jamaa katika Israeli?

"Ni vizuri kwako kuwa kuhani wakabila na jamaa wa Israeli kuliko kuwa kuhani wa mtu mmoja"

Moyo wa kuhani ulifurahi

"Kuhani alifurahi"

Judges 18:21

Wameweka watoto wadogo mbele yao wenyewe

Walisafiri kwa namna hii ili kuwalinda watoto.

umbali mzuri

Huu sio umbali mrefu lakini unatosha kupima namna mnavyoendelea.

watu waliokuwa ndani ya nyumba zilizo karibu na nyumba ya Mika waliitwa

"Mika aliwaita watu waliokuwa wakiishi katika nyumba zilizokuwa karibu na nyumba yake"

wakawafikia Wadani

"waliwakimbilia Wadani na wakawafikia"

wakageuka

"Wadani wakageuka"

Kwa nini mmewaita pamoja?

"Msingewaita watu wenu pamoja ili kutukimbiza"

mmewaita pamoja

"mmewaita watu hawa pamoja"

Judges 18:24

miungu niliyoifanya

Mika hakuitengeneza miungu lakini fundi aliitengeneza.

Je, nina nini tena?

"sijabakiwa na kitu" au "mmechukua kila kitu ambacho ni muhimu kwangu"

Unawezaje kuniuliza, 'Ni nini kinachokusumbua?

Mika anauliza hili swali akiwa na maana kuwa Wadani wanafahamu kitu kinachomsumbua.

Usiruhusu tusikie chochote unachosema

"Usirihusu tukagundua chochote ulichozungumza" au "usiseme chochote juu ya hili"

Kusikia ukisema chochote

"kukusikia ukisema chochote juu ya swala hili"

familia yako mtauawa

"na kuiuwa familia yako"

wakaenda zao

Hii ina maana ya kuwa wakaendelea na safari yao.

walikuwa na nguvu sana juu yake

Wadani walikuwa na nguvu sana juu ya Mika na watu wake.

Judges 18:27

kile alichokifanya Mika

Mika hakuitengeneza miungu lakini fundi aliitengeneza.

Laisha

Hili ni jina la mji.

kwa upanga

"upanga" unawakilisha upanga au silaha nyingine zinazotumiwa na askari vitani.

hawakuwa na uhusiano na mtu yeyote

Hii inamaanisha kuwa walikuwa wakiishi mbali na miji mingine hivyo walikuwa mbali na watu.

Beth Rehobu

Hili ni jina la mji.

Judges 18:30

Yonathani ... Gershomu ... Musa

Hili ni jina la Mlawi aliyekuwa kuhani wa Mika.

mpaka siku ya uhamisho wa nchi.

Hii ina maana ya kipindi ambacho watu wa Dani wachukuliwa mateka na adui zao. "mpaka siku ambayo adui waliiteka nchi yao"

aliyoifanya

Mika hakuitengeneza miungu lakini fundi aliitengeneza.

Judges 19

Judges 19:1

Katika siku hizo

Hii inaonesha mwanzo wa tukio lingine katika simulizi.

mbali

"mbali na mahali ambapo watu wengi waliishi"

hakuwa mwaminifu kwake

Hii inamaanisha kuwa hakuwa mwaminifu katika mahusiano yao na alianza kulala na wanaume wengine.

Judges 19:3

alimshawishi kukaa

"alizungumza naye ili aamue kukaa"

Judges 19:5

alijiandaa

Mlawi alijiandaa

Jipe nguvu na mkate kidogo

"Mkate" inamaanisha chakula. "Kula chakula kidogo ili upate nguvu ya kusafiri"

Tafadhali uwe tayari kukaa usiku

"Tafadhali kaa tena usiku huu"

Judges 19:7

Jitie nguvu mwenyewe, na usubiri mpaka alasiri

Baba mkwe alitoa mawazo kuwa ajipe nguvu kwa kula chakula. Pia alimuomba asubirie mpaka alasiri ndipo aondoke.

Judges 19:9

sasa mchana unaelekea jioni

"siku inakaribia kuisha" au "jioni inakaribia"

Judges 19:10

hiyo ni Yerusalemu

"Ambayo baadae iliitwa Yerusalemu"

Alikuwa na saruji katika punda

"Aliweka saruji katika punda wake wawili"

Njoo

"Nafikiri"

Tupate kwenda

Hii ina maana ya kupumzika na kusimama mahali katikati ya safari.

Judges 19:12

Tupate kwenda

Hii ina maana ya kupumzika na kusimama mahali katikati ya safari.

Njoo

"Nafikiri"

Judges 19:14

Wakageuka huko

Hii ina maana ya kupumzika na kusimama mahali katikati ya safari.

Naye akaingia

"Naye" inamzungumzia Mlawi lakini pia inazungumzia pamoja na watumishi wake na suria wake.

aliyewaingiza nyumbani kwake

"atakayenikaribisha nyumbani kwake usiku huo"

Judges 19:16

Wabenyamini

Hawa ni uzao wa Benyamini.

Aliinua macho

Hapa mtu aliangalia kwa makini kuona kilichopo pembeni yake. "alitizama juu"

Njia kuu ya mji

Ni sehemu ya soko ambayo watu hukusanyika wakati wa mchana, ni njia kuu za mji.

Judges 19:18

atakayenichukua nyumbani kwake

"atakayenikaribisha nyumbani kwake"

atakayenichukua

Hapa Mlawi alikuwa anamaanisha yeye pamoja na watumishi wake na masuria wake.

na kuna mkate na divai

"na kuna chakula cha kutosha na vinywaji"

yangu na mtumishi wako mwanamke hapa, na kwa kijana huyu pamoja na watumishi wako.

Mlawi anazungumza juu yake pamoja na wengine kama watumishi.

Hatujapungukiwa chochote

"Tuna kila kitu"

Judges 19:20

Usikae

Neno hili linasisitiza kuwa hakutaka Mlawi akae.

Njia kuu

Hii inamaanisha njia kuu za mji pia ni sehemu ya soko ambayo watu hukusanyika wakati wa mchana.

akamleta Mlawi nyumbani kwake

Hii inamaanisha kuwa akamkaribisha Mlawi ashinde nyumbani kwake usiku ule.

Judges 19:22

watu ... walizunguka nyumba

Watu wengi walizunguka pande zote za numba"

Judges 19:24

Angalia

"Sikiliza"

Lakini watu hawakumsikiliza

"watu hawakukipokea kile walichopewa"

huyo mwanamume akamshika yule mwanamke

"Mlawi akamshika mwanamke wake"

Asubuhi

"jua lilipoanza kuchomoza"

huyo mwanamume akamshika yule mwanamke

"mpaka jua lilipochomoza kabisa"

Judges 19:27

Lakini hakujibiwa

Mwanamke hakujibu chochote kwa sababu alikuwa amekufa.

Judges 19:29

Mguu kwa mguu

Mwandishi anatumua maneno haya kuonesha ni kwa namna gani Mlawi aliugawa mwili wa yule mwanamke vipande vipande.

Vipande kumi na mbili

"Vipande 12"

akapeleka vipande kila mahali katika Israeli

"akapeleka kila kipande maeneo tofauti katika Israeli"

Judges 20

Judges 20:1

mtu mmoja

Hii inazungumzia kundi la watu ambalo lipo kama mtu mmoja.

Dani mpaka Beer-sheba

Hii ni nchi kwa ujumla.

Mungu-watu 400,000 waendao kwa miguu

"Mungu na pia askari 400,000 walikuja"

tayari kupigana

"wenye uwezo wa kupigana." Hawakupigana wao kwa wao.

Judges 20:3

Sasa

Mwandishi anatuambia taarifa ya ni kitu gani wanachokifahamu Wabenyamini.

wamepanda Mispa

Mispa ilikuwa juu ya milima.

Ili tulale

"tukae usiku huu"

Judges 20:5

uovu na upumbavu

Huu ni uovu.

Sasa

Hili neno limetumika kuonesha mwisho wa maneno ya Mlawi

toeni maneno na ushauri wenu hapa

"amueni ni nini kifanyike kuhusu jambo hili"

Judges 20:8

kama mmoja

Hii inazungumzia kundi la watu ambalo lipo kama mtu mmoja.

Hakuna hata mmoja wetu atakayeenda hemani kwake ... hakuna hata mmoja wetu atakayerudi nyumbani kwake

Sentensi hizi mbili zina maana moja na hapa zinaonesha msisitizo. "Tutakaa hapa wote"

Lakini sasa

Maneno haya yanaonesha ni kitu gani watu walikuwa wanazungumza.

kama kura inavyotuongoza

Hii inahusisha kuzungusha mawe madogo ili kujua Mungu anataka nini.

Judges 20:10

watu kumi katika mia moja ... mia moja katika elfu ... elfu moja katika elfu kumi

"Watu 10 katika 100 ... 100 katika 1,000 .... 1,000 katika 10,000"

Chakula

"mahitaji"

wakakusanyika juu ya mji

"Wakakusanyika pamoja ili kuuvamia mji"

Judges 20:12

tupate kuwaua

"kuwaua"

sauti ya ndugu zao

"Sauti" inawakilisha ujumbe uliosemwa. "Kile ambacho ndugu yao alikisema"

Judges 20:15

Ishirini na sita elfu

"26,000"

Mia saba

"700"

shoto

Mtu mwenye shoto ni mtu mwenye uwezo wa kutumia mkono wake wa kushoto vizuri kuliko wa kulia.

angeweza kupiga unywele kwa mawe na asikose

"anaweza kupiga kwa kutumia jiwe vizuri"

Judges 20:17

Bila kuhesabu

"bila kujumuishwa"

wakaomba ushauri kutoka kwa Mungu

Wakamuomba Mungu awaambie ni nini cha kufanya"

Judges 20:19

wakahamisha kambi yao karibu na Gibea

"wakatoka na kutazamana na Gibea"

Elfu ishirini na mbili

"22,000"

Judges 20:22

walijitia nguvu wenyewe

Walijipa moyo wenyewe.

wakaunda mstari wa vita

Waisraeli waliandaa mistari yao ya kivita kwa ajili ya siku iliyofuata ya mapigano.

Walitaka mwongozo kutoka kwa Bwana

Kuhani alitegemea mapenzi ya Mungu.

Judges 20:24

Elfu kumi na nane

"18,000"

Judges 20:26

Mbele za Bwana

"kwenye uwepo wa Bwana"

Judges 20:27

wa sababu ya sanduku la agano la Mungu ... akihudumia mbele ya sanduku siku hizo

Mwandishi anatueleza ni kwa namna gani watu waliomba msaada kwa Bwana.

lilikuwapo siku hizo

"lilikuwepo Batheli siku hizo"

akihudumia mbele ya sanduku

"akihudumu kama kuhani mbele ya sanduku"

Wapigeni

"Wapigeni jeshi la Benyamini"

Judges 20:29

Israeli akaweka watu

"Israeli" inamaanisha watu wa Israeli. "Waisraeli"

mahali pa siri

"kwa kuvamia"

Judges 20:31

kupigana na watu

"Kupigana dhidi ya watu wa Israeli"

wakachukuliwa mbali na mji

"Watu wa Israeli wakawachukua nje ya mji"

Walianza kuua baadhi ya watu

"Watu wa Benyamini wakaanza kuwaua baadhi ya watu wa Israeli"

Judges 20:32

kama hapo awali

"kama hapo mwanzo"

Baal-Tamari

Hili ni jina la mji.

Maare-Geba

Hili ni jina la mahali.

Judges 20:34

Elfu kumi

"10,000"

waliochaguliwa

"Askari waliofundishwa vizuri"

msiba ulikuwa karibu nao

"muda si mrefu wataangamizwa kabisa"

Judges 20:36

Wana wa Israeli walikuwa wametoa ardhi kwa Benyamini, kwa kuwa walikuwa wakihesabu watu waliowaweka katika nafasi zilizofichwa nje ya Gibea.

Sentensi hii mpaka mstari wa 41 unaelezea ni kwa namna gani uvamizi ulisababisha Wabenyamini kushindwa.

wametoa ardhi kwa Benyamini

"Waliwaruhusu Wabenyamini kusogea mbele"

walikuwa wakihesabu watu

Waliwaamini watu wao.

Judges 20:39

Taarifa ya jumla:

mstari huu unaelezea ni kwa namna gani uvamizi ulisababisha Wabenyamini kushindwa.

wakageuka kutoka kwenye vita

"wakaondoka vitani"

wanapigwa mbele yetu

"tumewapiga wao"

Judges 20:40

Taarifa ya jumla:

mstari huu unaendelea kuelezea ni kwa namna gani uvamizi ulisababisha Wabenyamini kushindwa.

maafa

"majanga" au "matatizo"

yaliwajia

"yaliwapata"

Judges 20:42

Lakini vita viliwapata

"Lakini hawakuweza kuikimbia vita"

Judges 20:43

Noha

Hili ni jina la mahali.

Nao wakawakanyaga

"wakawaharibu kabisa"

wakawaua

"waliwaua walipokuwa wakikimbia"

Kumi na nane elfu

"18,000"

waliojulikana

"waliopigana kwa ujasiri katika vita"

Judges 20:45

Wakageuka na kukimbia

"Wabenyamini waliobakia waligeuka na kukimbia"

Elfu tano ... elfu mbili

"5,000 ... 2,000"

Gidomu

Hili ni jina la sehemu.

Elfu ishirini na tano

"25,000"

Judges 20:47

Mia sita

"600"

waliwarudia watu wa Benyamini

Watu hawa wa Benyamini ni wale waliokuwepo katika mji.

mji mzima

"mji" inamanisha watu wa mji ule. "kila mtu aliyekuwepo mjini"

katika njia yao

Hii inaelezea kila kitu walichokikuta walipokuwa wakielekea mjini.

Judges 21

Judges 21:1

Sasa watu wa Israeli walikuwa wameahidi huko ... kuolewa na Mbenyamini

Mwandishi anatuambia juu ya ahadi waliyoifanya Waisraeli kabla ya vita na Wabenyamini.

Mbenyamini

Hili ni jina la uzao wa Benyamini.

Kwa nini, Bwana, Mungu wa Israeli, amefanya jambo hili kwa Waisraeli, kwamba moja ya makabila yetu linapotea leo?

Waisraeli walitumia swali hili kuelezea ni kwa namna gani walikuwa na huzuni kubwa.

Judges 21:4

Watu wa Israeli wakasema, "Ni nani kati ya kabila zote za Israeli hawakuja katika mkutano wa Bwana?

Watu wanaukumbuka mkutano wa Waisraeli kule Mispa kabla ya kuwakamata Wabenyamini.

Kwa kuwa walikuwa wamefanya ahadi muhimu juu ya mtu yeyote ambaye hakuja kwa Bwana huko Mispa. Wakasema, "Hakika yeye atauawa."

Mwandishi anaeleza ahadi ambayo Waisraeli waliifanya huko Mispa kabla hawajakamatwa na Wabenyamini.

Judges 21:6

ndugu yao Benyamini.

"ndugu yao Benyamini" inamaanisha uzao uliobaki wa Benjamini.

kabila moja limekatiliwa mbali kutoka Israeli

Kuharibiwa kwa kabila la Benyamini kunafananishwa na kukatiliwa mbali kutoka katika Israeli.

Ni nani atakayewapa wale walioachwa wake, kwa kuwa tumeahidi kwa Bwana kwamba hatuwezi kuwaruhusu yeyote kati yao aoe binti zetu?

Waisraeli walitaka kuwapa wake Wabenyamini waliosalia lakini ahadi waliyoiweka Mispa iliwazuia kufanya hivyo.

Judges 21:8

Jabeshi-Gileadi

Hili ni jina la mji.

watu walipokuwa wamepangwa kwa utaratibu

"watu waliokuwa wamekusanyika huko Mispa walikuwa wamepangwa"

hakuna hata mmoja wa wenyeji wa Yabeshi Gileadi

"hakuna hata mmoja wa uzao wa Yabeshi Gileadi aliyekuwepo Mispa"

Kumi na mbili elfu

"12,000"

Waueni, hata wanawake na watoto.

Mistari inayofuata inaweka mipaka juu ya maelekezo haya.

Judges 21:11

Yabeshi-gileadi

Hili ni jina la mji.

kulala na mwanaume

Hiki ni kitendo cha kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Wanawake mia nne

"wanawake 400"

Judges 21:13

walikuwa wanawapa amani

"Walitaka kufanya amani pamoja nao"

Yabeshi Gileadi

Hili ni jina la mji.

hapakuwa na wanawake wa kutosha kwa wote

Kulikuwa na Wabenyamini mia sita na wanawake kutoka Yabeshi Gileadi walikuwa mia nne.

alifanya mgawanyiko kati ya makabila ya Israeli.

"alisababisha makabila ya Israeli yasiwe na umoja"

Judges 21:16

Mbenyamini

Huu ni uzao wa Benyamini.

wanawake wa Benyamini wameuawa

"tumewauwa wanawake wote wa Benyamini"

Lazima kuwe na urithi ... lisiharibiwe kutoka Israeli.

Waisraeli wanaongeza chunvi tuu. Tayari walishawapa Wabenyamini wake mia nne hivyo kabila halitaharibiwa moja kwa moja.

Judges 21:18

mke kwa Benyamini

"mke kwa watu wa Benyamini"

ambayo ni kaskazini ya Betheli, mashariki ya barabara inayopanda kutoka Betheli hadi Shekemu, na kusini mwa Lebona

Haya ni maelezo yanayotolewa ili kumuwezesha msomaji kuelewa ulipo mji wa Shilo.

Lebona

Hili ni jina la mji.

Judges 21:20

kila mmoja wenu anapaswa kunyakua mke ... rudi kwenye nchi ya Benyamini

"Kila mmoja wenu anapaswa kuchukua binti toka Shilo na kisha kuondoka nao kuwapeleka kwenye nchi ya Benyamini na kuwa wake zenu"

Judges 21:22

Tupeni neema

"tuonesheni upole sisi pamoja na watu wa Benyamini"

kwa sababu hatukupata wake kwa kila mtu wakati wa vita

"kwa sababu hatukupata wake kwa kila mtu wakati wa vita na Yabeshi Gileadi"

ninyi hamna hatia ... hamkuwapa wao binti zenu

Hapa wanaambiwa watu wa Shilo. Hawakuwatoa binti zao kwa watu wa Benyamini na hivyo hawakuvunja ahadi yao ya kutokufanya hivyo.

Judges 21:23

idadi ya wake waliowahitaji

Mke mmoja kwa kila Wabenyamini mia mbili ambao hawakupewa wake kutoka Yabeshi Gileadi.

Judges 21:25

hapakuwa na mfalme huko Israeli

"Bado Israeli haikuwa na mfalme"

yaliyo sawa machoni pake mwenyewe

"macho" inawakilisha mawazo ya mtu au fikra zake. "aliyoyaona kuwa ni sawa"