Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

1 Kings 1

1 Kings 1:1

walimfunika kwa nguo

Waliweka blanketi nyingi juu yake ili apate joto.

1 Kings 1:3

Kwa hiyo wakatafuta

"Kwa hiyo watumishi wa mfalme wakatafuta"

Katika mipaka yote ya Israeli

"katika nchi yote ya Israeli"

Abishaagi Mshunami

"Abishagi kutoka Shunami"

Mshunami

Mtu kutoka katika mji wa Shunami

mfalme

Mfalme Daudi

1 Kings 1:5

Adoniya mwana wa Hagithi

Hagithi alikuwa mke wa Daudi

alijiinua

"alianza kujivuna"

wapanda farasi

Watu wanaoendesha magari yanayovutwa na Farasi

magari na wapanda farasi hamsini ili wapige mbio mbele yake

Hawa watu walienda walitangulia mbele ya magari ili kuwaandalia njia na kuwalinda

alikuwa hajawahi mumsumbua, kwa kusema

"Alikuwa hajawahi kumsumbua. Alikuwa hajawahi hata kumwuliza" au "alikuwa hajawahi hata kutaka kumfanya awe na hasira, kwa hiyo hakuwahi hata kumwuliza"

Kwa nini umefanya hili na lile?

"Unapaswa kutambua kuwa kile ulichokifanya hakiko sawa."

aliyezaliwa baada ya Absalomu

Daudi alikuwa mzazi wa wote Absalomu na Adoniya, lakini walikuwa na mama zao tofauti. Absalomu alizaliwa, kisha Adoniya.

1 Kings 1:7

Akashauriana n a Yoabu

"Adoniya alijadili mipango yake na Yoabu"

Yoabu ... Seruya ... Abiathari ... Adonya ... Sadoki ... Benaya ... Yehoyada ... Nathani ... Shemei ... Rei

Mainaya wanaume

wakumfuata Adoniya

"wakamfauata na kumsaidia Adoniya" au "waliahidi kumsadia Adoniya"

1 Kings 1:9

ndama walionona

"ndama waliokuwa wamepewa chakula cha kutosha ili wanenepe" au "ng'ombe wachanga waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya sadaka"

jiwe la Sohelethi

Hili ni eneo lenye mwamba lililokaribu na Yerusalemu.

Eni Rogeli

Hili liliuwa jina la kisima ambacho watu walipata maji

ndugu zake wote, watoto wa mfalme

virai hivi viwili vinamaanisha kitu kilekile

wanaume wote wa Yuda, na watumishi wa mfalme

Virai hivi viwili vinamaanisha jambo lilelile.

1 Kings 1:11

Je, haujasikia kuwa ... hilo?

"unaonekana kuwa haujasikia ...hilo" au "Je, umesikia juu ... hilo?

Kuwa Adonya mwana wa Hagathi amekuwa mfalme

"Kwamba mwana wa Hagathi Adoniya amekuwa mfalme"

Hagathi

mama wa Adoniya na mke wa Dsudi.

1 Kings 1:13

Taarifa kwa ujumla

Nabii Nathani anendelea kuongea na Bathisheba

Je, haukumwapia mtumishi ... enzi?

"ulimwapia mtumishi wako ... enzi"

mtumishi wako

"kwangu, mtumishi wako"

ataketi kwenye kiti changu cha enzi

"atakuwa mfalme kama nilivyokuwa"

Kwa nini basi Adoniya anatawla?

"Kwa hiyo basi, Adoniya anapaswa kutokutawala"

kuthibitisha hayo

"mwambie kuwa hayo uliyosema ni ya kweli"

1 Kings 1:15

chumbani kwa mfalme

"chumba ambacho mfalme alilala"

Abishagi Mshunami

Tazama 1:3

akainama kifudifudi mbele ya mfalme

"akainama kuikaribia sakafu mbele ya mfalme"

una haja gani?

"unataka nikufanyie ini?"

ulimwapia mtumishi wako

Kiwakilishi cha "u" ni kinasisitiza kuwa "wewe mwenyewe uliapa"

mtumishi wako

Tazama 1:3

ataketi kwenye kiti changu cha enzi

Tazama 1:3

1 Kings 1:18

Taarifa kwa ujumla

Bathisheba anaendelea kuoongea na Daudi

Tazama

"Sikiliza kwa makini ninachotaka kukuambia"

Makaisai, ndama walionona,, na kondoo"

"makiisai wengi, ndama walionona na kondo wengi"

1 Kings 1:20

Taarifa kwa ujumla

Bathisheba anaendelea kuongea na Daudi

macho yote ya Israeli yako kwako

Neno "macho" liinamaanisha watu. "watu wote wa Israeli wanakutazama wewe"

atakayeketi kwenye kiti cha enzi

Tazama 1:13

wakati bwana wangu atakapolala na baba zake

"utakapolala na baba zako"

atakapolala na baba zake

Hii ni tafsida ya neno "kufa"

Mimi na mwanangu Sulemani kuhesabiwa wahaini

"Mfalme mpya atatuhesabu mimi na mwanangu Sulemani kuwa ni wahaini"

1 Kings 1:22

Taarifa kwa ujumla

Nabii Nthani anaongea na Daudi

akalala kifudifudi

"akasujudu chini sana"

1 Kings 1:24

Taarifa kwa ujumla

Nabii Nathani anaendelea kuongea na Daudi

ataketi kwenye kiti changu cha enzi

Tazama 1:3

wanakula na kunywa

"wanankula na kunywa pamoja naye"

1 Kings 1:26

Taarifa kwa ujumla

Nabii Nthani anandea kuongea na Daudi

bwana wangu mfalme

Nathani anaongea na Daudi kana kwamba mfalme Daudi ni mtu mwingine ili kuonesha heshima kwa Daudi

ataketi kwenye kiti changucha enzi

Tazama 1:13

1 Kings 1:28

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Daudi anamwahidi Bathisheba

akaja akasimama mbele ya mfalme

"akaja mbele ya mfalme" au "akarudi kwa mfalme"

akafanya kiapo

"akafanya ahadi "

atakayeketi kwenye kiti changu cha enzi

Tazama 1:13

Bwana wangu mfalme Daudi na aishi milele

Bathisheba alijua kuwa Daudi hataishi milele, hii ni namna ya kusema kuwa Daudi ni mfalme mwema.

1 Kings 1:32

Taarifa kwa ujumla

Daudi anampaka mafuta Sulemani kuwa mfalme

uwachukue watumishi wangu

"watumishi wangu"

Gihoni

Hilini jiina la kisima

1 Kings 1:35

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Daudi anaendelea kuongea kwa niaba ya Sulemani kuwa yeye ndiye atakayekuwa mfalme

atakuja kukaa kwenye kiti changu

Tazama 1:13

Na iwe hivyo

Walikubali na kufanya kama vile mfalme Daudi alivyosema

BWANA, Mungu wa mafalme bwana wangu, alithibitishe hilo

"Bwana wangu mfalme, BWANA, Mungu wako na alithibitishe"

alivyokuwana mfalme bwana wangu

"amekuwa na wewe, bwana wangu mfalme, kwa hiyo"

na kuifanya enzi yake kuwa kubwa kuliko enzi ya bwana wangu Daudi.

neno "enzi" linamaanisha 1) mtu anayekaa kwenye kiti cha enzi. "kumfanya yule anayekaa kwenye kiti cha enzi kuwa mkubwa kuliko bwana wangu Daudi" au 2) ufalme ambao yule aketiye kwenye kiti cha enzi anatawala, au "kuufanya ufame wake kuwa mkubwa kuliko ufame wa bwana wangu Daudi"

enzi ya bwana wangu Daudi

"enzi yako, bwana wangu mfalme Daudi"

1 Kings 1:38

Taarifa kwa ujumla

Watu wa Israeli wanampaka mafuta Sulemani kuwa mfalme wa Israeli.

Wakerethi ... Wapelethi

majina ya makundi ya watu

Gihoni

jina la kisima, mahali ambapo maji baridi hutoka katikta ardhi

akachukua pembe lenye mafuta hemani

alichukua pemba maalumu la mnyama lililokuwa limejaa mafuta ya mizeituni ambayo makuhani walikuwa wameyatunza kwenye hema maalumu ya BWANA.

pembe ya mafuta

Hii inaweza kumaanisha 1) pembe ya mnyama iliyojaa mafuta ya mizeiituni au 2) choombo ambacho kilitumika badala ya pembe lakini watu bado waliendelea kuita pembe, "chombo cha mafuta"

1 Kings 1:41

Taarifa kwa ujumla

Adoniya anasikia kelele na anasubiri habari.

1 Kings 1:43

Taarifa kwa ujumla

Adoniya anagundua kuwa Sulemani ndiye mfalme mpya

Wakerethi ... Wapelethi

majina ya makundi ya watu.

1 Kings 1:46

Taarifa kwa ujumla

Yonathani anaenedelea kumwambia Adoniya juu ya Sulemani

amaeketi kwenye kiti cha enzi cha ufalme

Tazama 1:35

mtu kuketi kwenye enzi yangu

Tazama 1:35

1 Kings 1:49

Taarifs kwa ujumla

Adoniya anamwogopa mfalme Sulemani

Wakasimama

"Walianza kufanya mabo yao haraka"

Adoniya ... akasimama kisha

"Adoniya kwa haraka"

Adoniya ... akachukua pembe la madhabahuni

"pembe la madhabahuni" inaonyesha ulinzi wa BWANA.

amemwogopa mfalme Sulemani

"anakuogopa, Mfalame Sulemani"

hatamwua mtumishi wake

"hataniua"

1 Kings 1:52

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anaghairi kumwua Adoniya

hakunahata unywele mmoja utakaoanguka

"Nitamlinda awe sakama"

uovu utaonekana kwake

"atakapofanya uovu"

1 Kings 2

1 Kings 2:1

Mimi sas ninnaiendea njia ya dunia yote

Hii ni tafsida ya kusema "Mimi naelekea kufa"

ujionyeshe mwenyewe kama mwanamume

"Mwonyeshe kila mmoja kuwa wewe ni mwanamume" au ":uishi maisha ambayo kila mmoja atakuona kuwa wewe ni mwanamume mwema"

ukitembea katika njia zake

"uishi maisha anayokuamuru"

ufanikiwe

"kufanikisha" au "kufanya vizuri"

atayatimiza maneno yake

"atafanya kila kitu alichoahidi kufanya"

kama wanao ... hawatakoma

BWANAanamwambia Daudi, kwa hiyo maneno "o" na "wa" yanamwakilisha Daudi.

wakatembea mbele yangu kwa uaminifu

BWANA anamwabia Daudi. kwa hiyo neno "yangu" linamwakilisha BWANA.

kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote

kujitoa kikamilifu

hawatakoma kuwa na mtu katika kiti cha enzi cha Israeli

"Mmoja wa wana wa kizazi chako ataendelea kuwa mfalme."

1 Kings 2:5

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Daudi anaendelea kumwambia Sulemani jinsi ya kuingoza Israeli.

kile Yoabu ...alichonifanyia, na kike alichowafanyia

Dudi anamaanisha kitu kilekile mara mbili. "kile Yoabu ... alichonifanyia, hiyo maanisha,kile alichofanya"

alimwaga damu vitani wakati wa amani

Yaweza kumaanisha 1) "aliwaua wale wanaume wakati wa amani kama vile ilikuwa wakati wa vita" au 2) "aliwalipizia kisasi wale wanaume wakati wa amani kwa sababu walikuwa wameuwa watu vitani"

na kuiweka ile damu kwenye mshipi na kwenye vie viatu miguuni mwake

Yoabu alikuwa karibu sana na wale wanaume wakati alipokuwa akiuwaua kiasi kwamba damu yao ilirukia kwenye mshipi wake na kwenye viatu vyake.

viatu

kile ambacho watu huvaa miguuni

usiache mvi zake ziingie kaburini kwa amani

"hakikisha Yoabu anakufa kifo cha kuuawa kabla hajazeeka."

1 Kings 2:7

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Daudi anaendelea kumwambia Sulemani jinsi ya kuingoza Israeli.

Barizilai

jiina la mwanamume

uwaache wawe miongoni mwa wale wanaokula mezani mwako

"uwakaribishe kula mezani kwako"

1 Kings 2:8

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Daudi anaendelea kumwambia Sulemani jinsi ya kuingoza Israeli.

Shimei ... Gera

Haya nimajina ya wanaume

Wabenjamini

Wana wa uzao wa Benjamini

Bahurimu ... Mahanaimu

Majina ya mahali

usimwache aiepuke adhabu

"hakikisha unamwadahibu

Uatkileta hicho kichwa chenye mvi kaburini

"hakikisha anakufa kifo cha kuuawa"

1 Kings 2:10

Taarifa kwa ujumla

Daudi anakufa na Sulemani anakuwa mfalme mpya wa Israeli.

alipolala na mababu zake

"alipokufa"

Daudi ... na alizikwa

"Daudi ... na wakamzika"

Siku ambazo Daudi alitawala Israeli zilikuwa ni

"Muda ambao Daudi alitawala Israeli walikuwa" au "Daudi alitawala Israeli kwa muda wa "

akaketi kwenye kiti cha enzi cha baba yake Daudi

"kiti cha enzi kinawakilisha mamlaka ya mfalme

akaketi kwenye kiti cha babayake Daudi

"akawa mfalme, kama vile Daudi baba yake alivyokuwa"

1 Kings 2:13

Taarifa kwa ujumla

Adoniya anakuja kuongea na Bathisheba

kwa amani

"bila kuwa na kusudio la kusababisha maumivu"

mambo yamebadilika

"Kile kilichokusudiwa kutokea hakikutokea"

ufalme umegeuzwa na umekuwa wa ndugu yangu

"BWANA alimpatia ufalme ndugu yangu" au "ndugu yangu amekuwa mfalme"

1 Kings 2:16

Taarifa kwa ujumla

Adoniya anamshirikisha Bathisheba ombi lake

Usinikatalie ... hatakukatalia

"Tafaadhali fanya kama ninavyofanya ... kwa hakika atafanya kama unavyosema"

Abishagi Mshunami

Tazama 1:3

1 Kings 2:19

Taarifa kwa ujumla

Bathisheba anaenda kwa mfalme Sulemani akiwa na ombi la Adoniya

kiti kingine cha enzi kilicholetwa

"alimwagiza mtu kuleta kiti cha enzi

sitakukatalia

"Nitakupa utakachoomba"

1 Kings 2:22

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Sulemani anatoa jibu la ombi la Adoniya

Kwa nini unamwombea ... Adoniya? Kwa nini usimwombea na ufalme pia ... Sruya?

"Umekosea kumwombea ... Adoniya! Hii ni sawa na kumwombea ufalme pia ... Seruya!" au "Nadhani nimruhusu kuwa mtawala wa ufalme pia!"

Mungu wangu na anifanyie hivyo, na zaidi pia, k ama Adoniya hajayasema hayo kinyume na maisha yake

Mungu atakuwa na haki zote za kuniua na hata kunifanyia hata mabaya zaidi kama sitamwuwa Adoniya kwa sababu ametoa ombi hili"

1 Kings 2:24

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Sulemani anamwua Adoniya

na kunipa kiti cha enzi

"Neno "kiti cha enzi" linamaanisha mamlaka ya Sulemani ya muwa mtawala kama alivyokuwa amepewa na BWANA.

ambaye amenifanyia nyumba

Neno "nyumba" linamaanisha uzao ambao Mungu alikuwa amempa mfalme Sulemani, ambao utaendelea kutawala baada ya Yake.

1 Kings 2:26

Taarifa kwa ujumla

Abiatahari amefukuzwsa kwenye ukuhani na mfalme Sulemani.

na kujitaabisha kwa namna mbalimbali kama baba yangu alivyopata tabu

Abiathari alijitabisha pamoja na mfalme Daudi kabla Daudi hajawa mfalme.

ili kwamba atimilize

Neno "a" linamwakilisha mfalme Sulemani

alivyokuwa amesema

neno "a" linamwakilisha BWANA

1 Kings 2:28

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Sulemani anamwagiza Benaya kumwusa Yoabu

Habari hizo zikamfikia Yoabu

"Yaabu akasikia kile ambacho Sulemani alifanya baada ya kuwa mfalme"

pembe za madhabahuni

pembe za madhabahuni zinamaanisha mamlaka ya BWANA na ulinzi.

1 Kings 2:30

Taarifa kwa ujumla

Benaya anaenda kumwua Yoabu

uitoe kwangu na kwenye nyumba ya baba yangu damu ambayo Yoabu alimwaga bila sababu

"uiondoe hatia ya mauaji ambayo Yoabu aliyafanya kutoka kwangu na familia yangu"

1 Kings 2:32

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Sulemani anaeleza sababu ya Yoabu kuuawa

BWANA na amrudishie damu yake kichwani mwake

"Neno "mwake" linamaanisha Yoabu. "Damu" linamaanisha hatia.

wasio na hatia na wema kuliko yeye

Maneno haya mawili yanamaanisha kitu kilekile na yanatia msisitizo kuwa Abineri na Amasa walikuwa wanaume wema kuliko Yoabu.

Yoabu kichwani pake na kwenye kichwa cha uzao wake

Neno "kichwa " linatumika kumaanisha mtu kamili

na nyumba yak,e na kwenye kiti chake cha enzi

Neno "nyumba" na "kiti cha enzi" linamaanisha uzao wa Daudi na utawala wa Daudi."

1 Kings 2:34

Taarifa kwa ujumla

Benaya anamwua Yoabu na anakuwa na akuwa mkuu wa jeshi la mfalme Sulemani

Alizikwa kwenye nyumba yake

"Yoabu alizikwa kwenye nyumba yakae

1 Kings 2:36

Taarifa wa ujumla

Mfalme Sulemani anamwambia Shimei kubaki Yerusalemu vinginevyo atakufa

Damu yako itakuwa juuy a kichwa chako

Neno "damu: linawakilisha hatia.

1 Kings 2:39

Taarifa kwa ujumla

Shimei anaondoka Yerusalemu

Akishi ... Maaka ... Gathi

Akishi na Maaka nii majina ya wanaume; Gathi ni jina lamji wa Filisti

1 Kings 2:41

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Sulemani anamhukumu Shimei kwa kuondoka Yerusalemu

Je, sikukuapisha ... nikisema, Tambua ...utakufa?

"Unatambua vizuri sana kuwa nilikuapisha ...Nikisema, 'Tambua ... utakufa'!"

1 Kings 2:43

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Sulemani anatoa hukumu juu ya Shimei kwa sababu ya kuondoka Yerusalemu.

Kwa nini basi umeshindwa kulinda kiapo chako ... nuliyokupa?

Inaweza kumaanisha 1) Sulemani anataka kjua jibu au 2)"umefanya makosa kwa kuvunja kiapo chako ... wewe"

kichwani pako

Neno "kichwa" linamaanisha mtu kamili. "juu yako"

1 Kings 2:45

Taarifa kwa ujumla

Mfalme Sulemani anatoamari ya kumwua Shimei

na enzi ya Daudi itaimrika mbele ya BWANA milele

Neno "enzi ya Daudi" linamaanisha mamlaka na utawala wa Daudi na uzao wake wote milele.

Kwa mkono wa Sulemani

matumizi ya "mkono" unawakilisha nguvu ya Sulemani

1 Kings 3

1 Kings 3:1

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anamwoa mwanamke wa Kimisri

Sulemani akawa na ushirikiiano ... na Farao mfalme wa Misri

Sulemani anaanzisha uhusiano na Farao

nyumba ya BWANA

"hekalu"

mahali pa juu

"mahali ambapo watu huabudu na kufanya makafara kwa miungu"

1 Kings 3:4

Taarifa kwa ujumla

Mungu anamwuliza Sulemani kuwa amfanyie nini:

eneo kuu la juu

"eneo linalofahamika sana kwa kutolea kafara" au "madahabu ya muhimu sana"

Omba! unataka nikupe nini?

"Niombe unalotaka nami nitakupa" au "Unataka nini?

1 Kings 3:6

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anajibu swali la Mungu

Umeonesha uaminifu wa agano mkuu

"Umekuwa mwaminifu kwa makubaliano yako"

kwa sababu alitembea mbele yako kwa ukweli na uaminifu, katika haki ya moyo

"kwa sababu alikuwa mwaminifu, mwenye haki na mkweli"

kuketi kwenye kiti chake cha enzi

"kutawala mahali pake"

1 Kings 3:7

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anaomba hekima

Mimi ni mtoto mdogo

Sulemani anasema kuwea yeye ni kama mtoto mdogo ambaye hajui kama baba yake anavyojua.

Sijui namna ya kuingia na kutoka

"Sijui njia sahihi ya kufikiri" au "Sijui namna ya kuwa mfalme"

Kwani ni nani awezaye kuwahukumu watu watu wako hawa walio wengi?

Sulemani anauliza swali ambalo jibu lake liko wazi. Jibu lake ni kwamba "hakuna awezaye." "Hakuuna awezaye kuwahukumuhawa watu wako wakuu"."

1 Kings 3:10

Taarifa kwa ujumla

Munga anampatia Sulelmani hekima na vitu vingine.

uhai wa adui zako

Sulemai hakumwamba Mingu ampe uwezo dhidi ya adui zake. "adui zako wauawe" au "uwezo wa kuwaua adui zako"

Tazama sasa nitafanya yote uliyoomba wakati uliponipa ombi lako

"Nitafanya kile ulichoomba nifanye pale uliposema nami"

1 Kings 3:13

kama utataembea katika njia zangu na kuyatunza maagizo

"kuishi kama nianvyotaka na ktii"

nitakapoziongeza siku zako

"siku" linamaanisha siku za Sulemani. "nitakufanya uishi maisha marefu"

1 Kings 3:15

ndoto

Ndoto ni kitu ambacho huwapata watu katika akili zao wanapokuwa katika usingizi. Hutokea na watu wakaona kama ni katu halisi na kumbe sivyo. Wakati mwingine Mungu hutumia ndoto kufikisha ujumbe kwa watu wake.

Yerusalemu

Kwa asili Yerusalmu ulikuwa mji wa Wakanaani ambao b aadaye ulikuja kuwa mji wa muhimu wa Israeli. Mjihuu uko kilomita 34 magharibi mwa bahari ya chumvi na kaskazini kidogo mwa Bethelehemu. Mpaka sasa bado ni mji mkuu wa Israeli.

sanduku la agano la Bwana, sanduku laamri ya agano, sanduku la BWANA

sentensi hizi zinamaanisha sanduku maalumu ambalo limesakafiwa kwa dhahabu, ambalo ndani mwake kulikuwa na vile vidonge viwili vya mawe vilivyokuwa vimeandikwa amri kumi za Mungu. Pia lilikuwa na fimbo ya Haruni pamoja na jagi la mana.

Bwana

Neno "Bwana" linamaanisha mtu aliye naumiliki fulani pia mwenye mamlaka juu ya watu. Lina hili linapoanza kwa herufi kubwa humaanisha Mungu.

sadaka za kuteketezwa, sadaka za moto

sadaka za kuteketezwa zilikuwa ni aina za sadaka ambazo zilikuwa zimechomwa kwa moto madhabahuni. Zilitengenezwa kwa ajili ya fidia ya dhambi za watu. Sadaka hizi zilijulikana pia kama "sadakaza moto."

sadaka za amani

"sadaka za amani" zilikuwa ni moja kati ya sadaka nyingi ambazo Mungu aliwaamuru Waisraeli kutoa. Pia ziliitwa "sadaka za shukurani" au "sadaka za amani"

sherehe

Neno "sherehe" linamaanisha tukio ambalo makundi ya watu walikula chakula kingi kwa pamoja kwa lengo la kufurahia jambo fulani. Wakati mwingine kunakuwa na chakula maalumu.

mtumishi, mtumwa, utumwa

Neno "mtumishi" linaweza kumaanisha "mtumwa" lenye maana ya mtu anayetumika kwa mtu mwingine kwa kupenda yeye au kwa kulazimishwa.

1 Kings 3:16

Taarifa kwa ujumla

Makahaba wawili wanamwomba Sulemani awaamue

1 Kings 3:18

Taarifa kwa ujumla

Wale makahaba wawili wanamsimulia Sulemani kisa chao

alimlalia

"kwa bahati mbaya alijigeuza juu ya yule mt

1 Kings 3:21

Taarifa kwa ujumla

Makahaba wawili wanaendelea kumweleza kisa chao Sulemani

kumhudumia mwanangu

Hii inamaanisha kumnyonyesha mtoto kwa maziwa yake.

mbele ya mfalme

"mbele ya Sulemani"

1 Kings 3:23

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anafanya uamuzi kwa wale wanawake wawili.

1 Kings 3:26

Taarifa kwa ujumla

Yule mama halisi wa yule mtoto anamwomba mfalme asimwue yule mtoto.

moyo wake ulikuwa na huruma sana kwa mwanae

"alimpenda sana mtoto wake"

1 Kings 4

1 Kings 4:1

Taarifa kwa ujumla

wakuu wa ofisi ya Sulemani

Azaria ... Sadoki ... Elihorefu ... Ahiya ... Shisha ... Yehoshafati ... Ahiludi .. Benaya ... Yehoyaida ... Abiathari

Haya yote ni majina ya wanaume

1 Kings 4:5

Taarifa kwa ujumla

Wakuu wengine wa Ofisi ya Sulemani

Azaria ... Nathani ... Zabudi ... Adoniramu ... Abda

Haya yote ni majina ya wanaume

1 Kings 4:7

Taarifa kwa ujumla

Mwendelezowa wakuu wa ofisi ya Sulemani

Beni Huri ... Beni Dekeri ... Beni Hesedi

Haya ni majina ya wanaume. Neno "Beni" nyuma ya jina inamaanisha "mwana wa" kwa hyo "Beni Huri" inamaanisha "mwana wa Huri."

Efraimu ... Makazi ... Shaalibimu ... Bethi Shemeshi ... Elonbethi Hanani ... Arubothi ... Sokohi Hefa

Haya ni majina ya mahali

1 Kings 4:11

Sentensi unganishi

Mwendelezo wa wakuu wa ofisi ya Sulemani

Beni Abinadabu ... Beni Geberi ... Yairi ... Manase ... Ahinadabu ... Ido

Haya ni majina ya wanaume

Tafathi

Hili ni jina la mwanamke

Dori ... Bethi Shani ... Zarethani ... Yezreeli ... Bethi Shani hadi Abeli Mehola ... Jokimeamu ... Ramothi Gileadi ... Arigobu ... Bashani ... Mahanaimu

Haya ni majina ya mahali

1 Kings 4:15

Taarifa kwa ujumla

Mwenedelezo wa wakuu wa ofisi ya Sulemani

Ahimaazi

Yeye alikuwa anatoka kabila la Naftali na laimwoa Basemathi

Baana

Baba yake, Husahi, alikuwa anatoka kabila ya Asheri na alimwoa Bealothi.

Yehoshafati

Baba yake, Parua, alikuwa anatoka kabila ya Isakari.

1 Kings 4:18

Taarifa kwa ujumla

Mwenedelezo wa wakuu wa ofisi ya Sulemani

katikanchi

Neno "nchi" linamaanisha nchi ya Yuda; wale wakuu wa ofifi ya Sulemani walikuwa wanatoka sehemu mbalimabli za Israeli

1 Kings 4:20

wengi kama mchanga wa bahariini

Hii ni lugha ya umbo

Mto

"Mto Frati"

Nchi ya Wafilisti

Eneo walimoishi Wafilisti

Kori thelathini

Kori moja kilikuwa kipimo cha mzigo mmoja

ayala, paa, na kulungu

"hawa ni aina ya ayala"

1 Kings 4:24

Tifsa

Hili ni eneoambalo leoliko Kaskazini mashariki mwa Ashuru

Yuda na Israeli

Majinaya Yuda na Israeli hutumika kumaanisha watu wa Israeli na wa Yuda.

kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake

"kilafamilia ilikuwa na bustani yake ya mizabibu na mitini," ahaii inamaanisha kuwa watu waliishi kwa amani kwa sababu hawakuishi wakati wa vita na hivyo walikuwa na muda kwa ajili ya kufanya shughuli za bustanini.

Kutoka Dani mpaka Bereerisheba

Hii inamaanisha nchi yote ya Israeli kwa maana ya kutokaDani ambako ni kaskazinihadi Beerisheba ambako ni kusini.

1 Kings 4:26

mabanda ya farasi

Banda ni mahali ambapo hukaa wanyama kama vile punda

Walihakikisha hakuna kilichopungua

"walitoa kila kitu ambacho Sulemani alihitaji"

1 Kings 4:29

ufahamu na upana wa kuelewa kama mchanga wa baharini

Ule ukubwa wa uelewa wa Sulemani umefananishwa na mchcanfa wa baharini, ambao kimsingi hakuna awezaye kuuhesabu

watu wote wa mashariki

Hii inamaanisha nchi zilizokuwa mashariki mwa nchi ya Israeli kama vile Arabia na Mesopotamia.

Etheni ... Hemani ... Kaliko Darda... Maholi

Haya ni majina ya wanaume

1 Kings 4:32

Mierezi ... Hisopo

Majina ya miti

1 Kings 5

1 Kings 5:1

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anaongea na mfalme Hiramu juu ya ujenzi wa hekalu

kwani Hiramu alimpenda Daudi

"kwa kuwa Hiramu alikuwa rafiki wa karibu wa Daudi"

kwa kuwa wakati wa uhai wake BWANA alikuwa akiwaweka adui zake chini ya nyayo za miguu yake

"BWANA alikuwa akimsadia Daudi kuwashinda adui zake" au"Daudi alikuwa na majukumu mengi kwa kuwa BWANA alikuwa akimpatia ushindi dhidi ya adui zake."

kujenga nyumba kwa jina la BWANA

"kujenga hekalu ambalo kwalo tutamwabudu BWANA"

1 Kings 5:4

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anaendelea kuongea na mfalme Hiramu juu ya ujenzi wa hekalu

amenipa mimi pumziko toka pande zote

wakati wamfalme Daudi natu wa Israeli kulikuwa na vita, lakini sasa mafalme Sulemani na watu walikuwa na pumziko na amani.

nitamweka kwenye kiti chako cha enzi

"nitamfanya kuwa mfalme baada yako"

1 Kings 5:6

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anaendelea kuongea na mfalme Hiramu juu ya ujenziwa hekalu

Lebanoni

Mfalme Hiramu alikuwa mfalme wa mji wa Tiro, ambao ulikuwa kwenye eneo hilohilo ambalo kwa leo linaitwa Lebanoni

Hakuna mtu miongoni mwetu anayejua kukata miti kama Wasidoni

"Wafanya kazi wako wanajua kukati miti kuliko watu wangu"

Wasidoni

"Watu wa Sidoni"

1 Kings 5:7

Taarifa kwa ujumla

mfalme Hiramu anamjibu Sulemani

maneno ya Sulemani

"Kile ambacho Sulemani alisema"

BWANA na abarikiwe leo

"Ninamsifu BWANA leo"

Mierezi

Mierezi ni aina fulani ya miti ambayo itatumika katika ujenzi wa hekalu

1 Kings 5:9

Taarifa kwa uumla

Mfalme Hiramu anaendelea kumjibu Hiramu

nami nitaileta katika makundi

"kuifunga kwa pamoja ili iweze kuelea kwa makundi

Nitaigawa pale

"nitayafungua hayo makundi ya miti"

Utafanya kile ninachohitaji

"Unaweza kufanya kile ninachotaka" au " unaweza kunilipa"

1 Kings 5:10

Miberoshi

Neno "Miberoshi" linamaanisha aina nyingi ya miti ikiwemo mierezi

Kori za ngano

Hiki kilikuwa kipimo cha vitu vikavu ambapo mafuta ndiyo yaliyokuwa kipimo cha kimiminika.

mwaka kwa mwaka

"kila mwaka"

1 Kings 5:13

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anawashurutisha watu kujenga hekalu

akaandaa wafanyakazi kutoka Israeli yote

"akawashurutisha toka Israeli yote"

kwa zamu

Wafanyakazihawakwenda wote kwa pamoja; makundi yalienda moja baada ya lingine ili kushirikiana katika kazi.

Kwa mwezi mmoja walienda Lebanoni na miezi miwili walikaa nyumbani

Kila yale makundi matatu walitumia mwezi mmoja wakifanya kazi Lebanoni na kisha walikaa miezi miwili nyumbani Israeli.

1 Kings 5:15

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anaendelea kuwashurutisha watu kujenga hekalu

mizigo

"vitu vizito"

wakata mawe milimani

"wanaume waliochimba mawe kutoka ardhini na kuyachonga"

1 Kings 5:17

Taarifa kwa ujumla

Sulemani anaendelea kuwashururtisha watu kujenga hekalu

walileta mawe makubwa ya thamani

"walichimba mawe mazuri kutoka mlimani n a kuyachonga katika sura takiwa"

Wagebaliti

"Hawa ni wanaume toka mji wa Gebali" Gebali ulikuwa mji uliokuwa mlimani karibu na Tiro huko Lebanoni.

1 Kings 6

1 Kings 6:1

Taarifa kwa ujumla

Maandiko yanaorodhesha vipimo vya hekalu

Sulemani akaanza kujenga

Sulemani hakujenga pekee yake; watumishi wake ndio waioifanya hiyo kazi

wa 480 ... wa nne

wa 480 ... wa4

katika mwezi wa Zivi, ambao ndio mwezi wa pili

"Zivi" ni jiina la mwezi wa pili wa kalenda ya Kihebrania. Mwezi huu uko kati ya sehemu ya mwisho wa mwezi wa Aprili na mwanzo wa sehemu ya mwezi Meyi wa kalenda ya Kimagharibi.

dhiraa

Dhiraa moja ni sawa na sentimenta 46

1 Kings 6:3

Taarifa kwa ujumla

Maandiko yanaorodhesha vipimo vya hekalu

ukumbi

ni sehemu ya jengo yenye safu na paa inayoonyesha uelekeo na kuunganisha jengo na sehemu ya mlango kuingilia.

1 Kings 6:5

Taarifa kwa ujumla

Maandiko yanaorodhesha vipimo vya hekalu

Kile chumba cha chini ... cha kati ... cha tatu

Hii inaonyesha vyumba vya kila sehemu ya jengo

Aupande wa nje akaupunguza upande wa nyumba

Walitengeneza kuta kuzunguka jengo ili kuzilinda nguzo za vyumba vidogovidogo

boriti

Hiki ni kipande kirefu na kizito cha ubao unaotenengenezwa ili kulinda jengo.

1 Kings 6:7

nyumba

Neno "nyumba" limetumika kumaanisha nyumba ya Mungu, hekalu

mawe yaliyokuwa yamechongwa chimboni

Chimo ni sehemu ambayo mawe makubwayalikuwa yakichimbwa huko mlimani na kuchongwa kwa vifaa ili kuyalainisha. Mawe yaliandaliwa chimboni na kuletwa hekaluni.

1 Kings 6:9

Sulemani akalijenga hekalu akalimaliza

Sulemai ahakulijenga hekalu pekee yake; watumishi wake ndio walioifanya hiyo kazi

Akavijenga na vyumba vya pembeni

Hivi ni vyumba vilevile ambavy ovimeonyeshwa kwenye jengo.

kwa boriti na mbao za mwerezi

boriti ni kipande kirefu na kizito cha ubao unaotengenezwa ili kulinda jengo. Papi ni kipande cha mti uliobapa ambao pia hutumika katika ujenzi.

vyumba vya ndani

"kuta za ndani"

mbao za mierezi

Neno "mbao" ni neno la jumla ambalo linatumika kuonesha ubao unaotumika kwa kujengea, kama vile boriti na papi

1 Kings 6:11

Neno la BWANA

"BWANA alinena ujumbe wake"

Nno la BWANA

Hapa "neno" linawakailisha ujumbe wa BWANA.

utatembea katika maagizo yangu

"utaendelea kutii maagizo yangu yote"

kuhukumu kwa haki

kutii na kufuata sheria za Mungu

kutunza amri zangu na kuishi kwa hizo

"kuwa mwangalifu na kufanya kila kitu nilichokuambia"

nitakapozithibitisha ahadi zangu

Muungu atazithibitisha ahadi zake kwa kutimiza kile alichoahidi kufanya.

Nitaishi

"Roho yangu itakaa hekaluni"

1 Kings 6:14

Sulemani

"wafanya kazi wa Sulemani"

za ndani

"ndani"

mierezi

mierezi ni aina ya miti iliyotumika kujenga hekalu

1 Kings 6:16

Dhiraa

Dhiraa moja ni kama sentimita 46

ukumbi mkuu

"chumba kikuu"

vibuyu

ni aina ya mboga za majani zenye umbo la duara ambazo hupandwa kwenye mizabibu

maua yaliyochanua

"maua yaliyofunguka"

1 Kings 6:19

madhabahu aliifunika kwa mbao za mierezi

Madhabau ilitumika kwa kuchoma ubani

1 Kings 6:21

Akaisakafia

"aliifunika"

madhabahu yote ya chumba cha ndani

"madhabahu ya uvumba iliyokuwa kwenye lango la kuingia chumba cha ndani"

1 Kings 6:23

mbao za mizeituni"

mbao zinazotokana na miti ya mizeituni

bawa mojahadi jingine

umbali uliokuwepo toka bawa moja hadi jingine

vipimo

"kiasi cha ukubwa"

1 Kings 6:27

Sulemani aliliweka ... Sulemani aliwafunika

"Sulemani" kwa maneno haya inamaanisha wafanyakazi wake

chumba cha ndani kabisa

jina jingine la patakatifu sana

aliwafunika

"alisakafia"

1 Kings 6:29

sura

umbo

1 Kings 6:31

Sulemani akatengeneza

"Wafanyakazi wa Sulemani walitengeneza"

vizingiti

sehemu ya juu inayoshikilia miimo ya mlango

kwenye pande tano

mashikio yaliyo katika pande za milango

Akasakafia

"akafunika"

1 Kings 6:33

Kwa njia hii, akalitengenezea hekalu miimo

Sulemani alitengeneza pia miimo kwenye lango la hekalu

yenye pande

yenye mashikio

Zile mbao mbili za mlanago mmoja

Inamaanisha kuwa kila mlango ulikuwa na sehemu mbilia ambazo zilikuwa zimefungwa pamoja.

1 Kings 6:36

Akalijenga korido la ndani

"Sulemani alizijenga kuta za korido la ndani" au "wafanya kazi wa Sulemani wakazijenga kuta za korido la ndani"

mihimili ya mierezi

Hizi ni mbao kubwakubwa za mierezi ambazo ziliwekwa kwa ajili ya kulinda kuta

1 Kings 6:37

mwaka wa nne ... mwaka wa kumi na moja

Hii ni miaka inayohesabiwa tangu Sulemani alipokuwa mfalme

Nyumba ya BWANA

"hekalu"

katika mwezi wa Ziv

Tazama 6:1

Katika mwezi wa Buli

"Buli" ni mwezi wa nane wa kalenda Kihebrania. Mwezi huu uko katika ya sehemu ya mwezi Oktoba na sehemu ya kwanza ya mwezi wa Novemba.

1 Kings 7

1 Kings 7:1

Taarifa kwa ujumla

Mwandishi anaandika juu ya ikulu ya Sulemani

Iliimchukua Sulemani miaka kumi na tatu kujenga ikulu yake

Kwa Sulemani alikuwa mfalme, wafanyakazi wake walifanya kazi kwa niaba yake.

ikulu yake

nyumba ya utawala

ikulu iliyoitwa mwitu wa Lebanoni

nyumba ya mwitu wa Lebanoni

Dhiraa

kiasi cha sentimita 46

mihimili

Hizi ni mbao kubwakubwa za mierezi ambazo ziliwekwa kwa ajili ya kulinda paa

1 Kings 7:3

Taarifa kwa ujumla

Baadhi ya taarifa ziinazohusu jengo la ikulu zinatolewa.

Paa la ikulu lilezekwa kwa mierezi

"kuliwekwa mihimili ya mierezi kwa lengo la kulinda paa"

mihimili

Hizi ni mbao kubwakubwa za mierezi ambazo ziliwekwa kwa ajili ya kulinda paa

Milango na miimo yake ilikuwa ya mraba

"fremu ngumu za umbo la mstatili"

1 Kings 7:6

Taarifa kwa ujumla

Mwandishi anaandika juu ya muundo wa ukumbi wa nguzo.

baraza

sehemu ya jengo ambayo imejengwa kwa safu ambayo inaunganisha sehemu zingine za jengo pamoja na lango.

1 Kings 7:7

Taarifa kwa ujumla

Mwandishi anaandika juu ya ukumbi wa ikulu

Sulemani akaijengabaraza yenye kiti cha enzi

"Sulemani alijenga nyumba iliyoitwa "nyumba ya kiti cha mfalme"

ilikuwa imeezekwa kwa mierezi

"wafanyakazi waliizeka ile nyumba kwa mierezi"

kutoka sakafu moja hadi nyingine

sakafu yote ilikuwa ya mierezi, kutoka ukuta mmoja hadi mwingine.

1 Kings 7:8

Taarifa kwa ujumla

Mwandishi anaendelea kuandika juu ya eneo la ikulu.

1 Kings 7:9

Taarifa kwa ujumla

Mwandishi anaandika juu ya mawe yaliyotumika kujengea hayo majengo

Majengo hayo yalipambwa kwa vitu vya thamani, mawe ya thamani

"Wafanyakazi waliyanakishi hayo majengo kwa mawe ya thamani na vitu vya thamani"

mawe ya thamani, yaliyochongwa na kukatwa kwa msimeno kufuata vipimo sahihi na kulainishwa

Wafanyakazi waliyapima mawe na kuyakata kwa usahihi na kuyalainisha"

Mawe ya namna hii ndiyo yaliyotumika

"wafanyakazi waliyatumia mawe hayo"

kuwanzia kwenye msingi hadi juu, pia na nje hadi kwenye baraza

Mwandishi anasisitiza kuwa wafanyakazi walitumia mawe ya thamani kwenye msingi na hata jengo lote kwa ujumla.

Msingi ulijengwa

"Wale wafanyakazi waliujenga msingi"

Dhiraa

Takribani sentimita 46

1 Kings 7:11

mihimili ya mierezi

Mhimili ni ubao mrefu unaojengwa kwa lengo la kushikilia kitu fulani kwenye mfumo wa ujenzi

safu tatu za mawe yaliyokatwa na safu moja ya mihimili ya mierezi

Tazama 6:36.

1 Kings 7:13

Kumleta Huramu kutoka Tiro

Huramu aliupokea wito wa Sulemani wa kuja Yerusalemu

mwana wa mjane ... baba yake alikuwa mtu wa Tiro

Mjane ni mwanamke ambaye mume wake alishafariki, na tunajiridhisha kuwa baba yake kweli alishakufa.

Huramau alikuwa mwingi wa hekima na ufahamu na stadi

Neno "hekima naufahamu" yanamaanisha kitu kilekile, yametumika kuonyesha msisitizo. "Mungu alimjaza Huramu kwa hekima, ufahamu na stadi"

1 Kings 7:15

Dhiraa kumi na nane

Dhiraa moja ni sentimita 46

mzingo wa mita 5.5

"mzingo" ni kipimo cha urefu wa kitu cha duara.

Akatengeneza taji mbili

Neno "taji" linamaanishapamba linalowekwa juu ya nguzo.

shaba

Shaba iling'aishwa ili kuaksi mwanga wa jua

Kulikuwa na nyavu za kuwa kama kaziy a kusuka

"Mikufu ya vyuma iliyosukwa"

1 Kings 7:18

safu mbili za komomanga

Komamanga ni tunda lenye ganda gumu, rangi nyekundu kwa ndani na mbegu nyingi zenye maji matamu. Huramu hakutumia makomamanga halisi kupamba hizo nguzo. Atengeneza kwa kutumia shaba.

Zile taji ...zilikuwa zimepambwa kwa maua, vyenye vimo vya mita 1.8

"Huramu alizipamba zile taji ... kwa maua ya shsaba, yenye vimo mita 1.8"

vichwa vya nguzo za ukumbi

Tazama 7:6

1 Kings 7:20

makomamanga mia mbili

"makomamanga 200"

Alisimamisha nguzo

Neno "Ali" linamaanisha wafanyakazi wa Huramu. "Wafanyakazi wa Huramu walisimamisha nguzo"

Ile nguzo ya kuume akaipa jina la Yakini

"jina la nguzo ya kuume illitwa Yakini"

Ile nguzo ya kushoto ilikuwa inaitwa Boaz

"Jna la nguzo ya kushoto iliitwa Boazi"

Hivyo ndivyo zile nguzo zilivyotengenezwa

"Hivyo ndivyo Huramu alivyozipamba zike nguzo"

1 Kings 7:23

bahari ya kusubu

Hi inamaanisha kalai la shaba ambalo liliweza kubeba maji.

vyuma vya kusubu

Huramu aliyeyusha shaba na kuvitengeneza

mita 2.3 kutoka ukingo hadi ukingo

kutoka ukingo mmoja hadi mwingine

mzingo wake ulikuwa mita 13.7

"mzingo" ni kipimo cha urefu wa mzunguko wa kitu cha dauara.

na vibuyu vilivyoizunguka

Kibuyu ni aina ya mboga yenye ganda gumu na lenye duara ambalo huoteshwa kwenye shamba la mizabibu.

wakati bahari inapokuwa kalibu

"wakati Huramu alipoitengeneza bahari"

1 Kings 7:25

Bahari

Bahari ya kutengeneza ya shaba

Bahari ilikaa juu ya

"ilikuwa juu ya"

Ile bahari iliwekwa juu yao

"Wafanyakazi wa Huramu walliweka bahari juu ya wale makiasai wa shaba

pande zao zote za nyuma

Hii ni sehemu ya nyuma ya mwili wa mnyama mwenye miguu minne

na ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, kama ua l a yungi

"Huramu aliitengeneza ukingo ukafanana n a ukingo wa kikombe, ukapinda kwa nje kama ua"

bathi elfu mbili

bathi moja ni sawa na lita 22.

1 Kings 7:27

urefu wa mita 1.8

Huo ni urefu wa kalio moja

Hivi ndivyo kazi za makalio zilivyofanywa

Hii inamaanisha kuwa mwandishi atayafafanua makalio katika maneno yafuatayo.

na juu ya papi na vipandio kulikuwa na simba, makisai, na makerubi

Kulikuwa na vipande vya nakshi katikasura za simba, makisai, na makerubi yaliyokuwa yameunganishwa katika pande za makalio.

masongo ya kazi y a kufuliwa

Neno "masongo" linamaanishsa vipande vya shaba vyenye sura ya kusokotwa.

1 Kings 7:30

magurudumu ya shaba na vipini, na pande zake nne

kulikuwa na pini moja kwa kila jozi yamagurudumu. "magurudumu manne napini mbili"

pande zake nne

"pande nne za kila kwa kila kalio"

Chini ya birika yalikuweko mataruma ya kusubu yenye masongo

"Huramu aliweka mataruma yenye vipande vya sura ya masongo"

na ile taji ilikuwa

Neno "taji" inamaanisha kipande cha mviringo kilichokuwa kimesimama wazi ili kibebe yale makalai.

na papi zake zilikuwa za maraba

Tazama 7:27

1 Kings 7:32

yalikuwa ndani ya makalio

neno "yao" linamaanha zile papi na neno "ndani" linamaanisha jinsi ile mikono ilivyokuwa ilivyokuwa imechomekwa kwenye zile papi.

Yale magurudumu yalikuwa kama ya gari.

"Huramu alitengeneza yale magrurdumu kuwa kama magurudumu madogo ya gari"

Mikono yake, na maduara, matindi yake, na vipande vya ndani

Neno "yake" limaanishsa yale magurudumu.

1 Kings 7:34

Kulikuwa na mataruma manne katika pande zake nne za makaliio

"Kulikuwa na mataruma katika kila upande wa kalio"

kina cha sentimita ishirini na tatu

sentimita ishirini na tatu ni sawa na "nusu ya dhiraa moja"

na juu ya makalio mashikio yake na papi zakae zikawa zimeshikanishwa

"Huramu alishikamanisha mashikio yake na papi na juu ya kila kalio"

1 Kings 7:36

nayo ilikuwa imezungukwa

Neno "nayo" linamaanisha Makerubi, simba, n a miti ya mitende.

ilikuwa imezungukwa na masongo

Neno "masongo" linamaanisha sura za kusukwa za vipande vya masongo.

Yote yalikuwa yametengenezwa kwa kufanana

"Huramu alitenegeneza makalio yote katika mfumo uleule"

na yalikuwa na vipimo sawa, na sura inayofanana

"makalio yote yalikuwa na vipimo sawa na sura sawa"

1 Kings 7:38

bathi arobaini

Bathi moja ni sawa na lita 22

upande wa mashariki, ukielekea upande wa kusini wa hekalu

"upande wa kusini mashariki wa hekalu"

1 Kings 7:40

lile besini la kuwa kama taji

mataji yalikuwa na sura kama ya beseni

mapambo ya kufunika

"mikufu ya vyuma iliyosukwa"

1 Kings 7:42

makomamanga mia nne

"makomamanga 400"

1 Kings 7:44

Akatengeneza

neno "aka" linamaanisha Hurama na wasaidizi wake.

na vyombo vingine vyote

"zana zingine zote"

shaba iliyosuguliwa

shaba inayong'aa na kuaksi mwanga

1 Kings 7:46

Mfalme alivisubu

"Mfalme alimruhusu Huramu awaagize wafanyakazi wake kuvisubu"

uwanda wa Yorodani

Hii inamaanisha eneo lililo tambarare karibu na Mto wa Yorodani.

kati ya Sukoti na Zarethani

"Sukoti" ni mji ulio upande wa mashariki mwa Mto Yorodani

Sulemani hakuvipima vyombo vyote

"Sulemani hakumwambia Huramu na wafanyakazi wake kuvipima vyombo vyote"

kwa sababu uzani wa shaba ulikuwa hauwezi kupimwa

"hakuna ambaye angeweza kuupima uzani wa shaba"

1 Kings 7:48

Sulemani akatengeneza

"Wafnyakazi wa Sulemani walitengeneza"

ile meza ambayo iliwekwa mikate ya wonyesho

"ambayo makuhani waliweka mikate ya wonyesho"

maua, na taa

"maua" na "taa" vilikuwa sehemu ya vinara.

1 Kings 7:50

Vile vikombe ... vilikuwa vimetengenezwa kwa dhahabu

"Wafanyakazi walivitengeneza vikombe ... kwa kutumia dhahabu halisi"

Na bawaba ... vyote vilitengenezwa kwa dhahabu

"Pia walizitengeneza bawaba ... kwa kutumia dhahabu"

bawaba za milngo

bawaba in aweza kumaanisha ima 1)bawaba ambazo huruhusu milango kugeuka, au 2) mashikio mabayo hushikilia milango.

1 Kings 7:51

kazi yote ambayo mfalme Sulemani kwa ajili ya hekalu ilimalika

wafanyakazi waliimaliz kaziyote ambayo Sulemani aliwataka wafanye kwa ajili ya nyumba ya BWANA"

1 Kings 8

1 Kings 8:1

akawakusanya wazee wa Israeli

"aliwaita pamoja viongozi wa Israeli"

wanaume wote

Hii yaweza kumaanisha 1) watu ambao Sulemani aliwaita kule Yerusalemu ambao pia wameorodheshwa kwenye 8:1 au 2) kwa wale ambao walisafiri kwenda Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu, na siyo lazima kuwa ni wanaume wote walioishi Israeli.

Kwenye sikukuu

Hii inamaanisha sikukuu ya vibanda

Katika mwezi wa Ethanimu, ambao ndio mwezi wa saba

"Ethanimu" ni m Huu mwezi ulikuwa kati ya mwezi wa saba wa kalenda ya Kihebrania. Huu mwezi ulikuwa kati ya sehemu ya mwisho wa mwezi wa Septemba na mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba kwa kalenda ya Magharibi.

1 Kings 8:3

ambazo hazikuweza kuhesabiwa

"ambazo hakuna mtu aliyekuwa na uwezo wa kuzihesabu"

1 Kings 8:6

ndani ya chumba cha ndani, mahali patakatifu sana

Sentensi ya pili inatumika kufafanua sentensi ya kwanza.

miti yake kwani ilitumika kulibebea

"miti ambayo makuhani walitumia kulibebea"

haikuweza kuonekana

"hakuna aliyeweza kuwaona"

1 Kings 8:9

ilitokea kwamba

Kirai hiki kimetumika hapa ili kuonyesha tukio la muhimu katika habari. Kama lugha yako ina namna ya kuonyesha hilo, unaweza kuitumia

1 Kings 8:12

makao ya kujivunia

"Nyumba iliyoinuliwa"

1 Kings 8:14

BWANA, Mungu wa Israeli, asifiwe

"Msifuni BWANA, Mungu wa Israeli"

kwa mkono wake

"kwa nguvu zake"

1 Kings 8:17

ilikuwa kwenye moyo wa Daudi

"ilikuwa hamu ya Daudi"

mmoja wa wanao atakayezaliwa toka viunoni mwako

"mmoja mabye atakuwa mzaliwa wa wana wako" au "mmoja ambaye wewe utakuwa baba kwake"

1 Kings 8:20

nimeketi kwenye kiti cha enzi cha Israeli

"Ninatawala juu ya Israeli"

1 Kings 8:22

hutembea mbele yako kwa mioyo yao yote

"kuishi kwa moyo wote ambao wewe unapenda waishi"

umetimiza kwa mkono wako

"kwa nguvu zako umetimiza ulichosema"

1 Kings 8:25

ataketi katika kiti cha enzi cha Israeli

"kuitawala Israeli"

kutembea mbele yangu

"kuishi kwa kunitii mimi"

1 Kings 8:27

Je, ni kweli Mungu ataishi duniani?

"Lakiini kwa hakika haiwezekani kuwa Mungu ataishi duniani!"

maombi haya ya mtumishi wako na haja yake

Neno "maombi" na "haja" yanamaanisha kitu kilekile. Yametumika kuonesha msisitizo wa maombi yake.

uyajali maombi haya ya mtumishi wako ... sikiliza kilio na maombi ambayo mtumishi wako anakuomba leo

sehemu ya kwanza na ya mwisho ya sentensi hizi zinamaanisha kitu kilekile. Sehemu zote zinaonesha maombi ya Sulemani.

1 Kings 8:29

Naomba ulitazame hekealu hili

"Naomba uliangalie"

mchana nausiku

"wakati wote" au "kila mara"

Jina langu na uwepo wangu

Maneno haya kwa pamoja yanasisitiza kuwa BWANA ataishi hekaluni.

1 Kings 8:31

anapewa sharti la kiapo

mtu mmoja anamtaka aape

kichwani mwake

kichwa kinamaanisha mtu kamili. "juu yake"

thawabu yake ya haki

"kile anachohitaji kwa sababu ya kutokuwa na hatia"

1 Kings 8:33

Watu wako Israeli watakapopigwa na adui

adui amewashinda watu wako Israeli

1 Kings 8:35

mbingu zitafungwa na mvua hazinyeshi

Virai vyote viwili vinamaanisha kitu kilekile

njia njema itakayowapasa

"ambayo kwayo wanatakiwa kuishi"

1 Kings 8:37

magonjwa au ukungu

haya nimajina ya magonjwa ya mazao ya kilimo yanayomaanisha kifo cha mazao kutokana uhaba wa mvua au mvua iliyozidi.

nzige au funza

"nzige" niaainaya panzi ambaye husababisha uharibifu kwa njia ya kula mazao, Neno "funza" ni hatua ya mwanzo wa kukua kwa nzige.

na kama kuna mtu au watu wataomba

mtu au watu wako wote wa Israeli, wataomba na kukupa dua"

akaijua hiyo tauni katika moyo wake

Hii inaweza kumaanisha 1) "kuijua dhambi katika moyo wake" au 2) "kujua katika moyo wake kwamba ile tauni ni matokeo ya dhambi yake

1 Kings 8:39

mbinguni, angani

mbinguni ni mahali ambapo Mungu huishi. Pia linaweza kumaanisha angani kutemea na mukhutadha. Lakini mbinguni ni mahali pa juu ya ardhi au dunia.

uhai, kuishi, maisha, aliye hai

maneno haya yote yanamaanisha kuwa hai kimwili.

samehe, msamaha

kumsamehe mtu kunamaanisha kutokushikilia hasira dhidiya mtu aliyekuumiza.

zawadi

zawadi linamaanisha kitu ambacho mtu hupokea kwa sababu ya kufanya kitu fulani

moyo

katika biblia, neno "moyo" limetumika kama lugha ya umbo kumaanisha mawazo, hisia, tamaa au utashi.

hofu, kuogopa, hofu ya BWANA

Nno "hofu" na "kuogopa" yanamaanisha hisisa hasi ambazo mtu huwa nazo pale kunapokuwepo na kitisho. Lakini pia neno "hofu" linamaanisha heshima ya ndani kabisa kwa mtu mwenye mamlaka.

1 Kings 8:41

mkono wako wenye nguvu, na mkono wako ulioinuliwa

Virai hivi viwili vinamaanisha kitu kilekile na vivnalenga mamlaka ya Mungu.

nyumba hii niliyoijenga inaitwa kwa jina lako

Kirai kinachosema "inaitwa kwa jin lako" kinamaanisha umiliki. "wewe ndiye mmiliki wa nyumba hii ambayo nimeijenga"

1 Kings 8:44

maombi yao, na dua zao

Neno "maombi" na "dua" yana maana moja yametumika kuonyesha juhudi ya kile ambacho watu wanamwomba BWANA awafanyie.

1 Kings 8:46

kutokea katika nchi ya watekaji

"ambako adui zao wamewapeleka kama mateka"

katika nchi ya watekaji

Neno "watekaji" linamaasha wale watu ambao huwafanya watu kuwa mateka.

Tuemetenda kwa ukaidi, na tumefanya dhambi. Tumetenda kwa uovu.

Virai hivi viwili vinvamaanisha kitu kimoja na vimetumika kuonyesha msisitizo wa jinsi hawa watu walivyofanya mabaya.

tumetenda kwa ukaidi, na tumefanya dhambi

Maneno haya mawili ya namaanisha kitu kilekile na yametumika kuonyesha jinsi wale watu walivyofanya uovu.

1 Kings 8:48

kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote

Tazama 2:1

kuelekea nchi yao

Neno "nchi yao" linamaanisha nchi ya walke wanaoomba, nayo ni, Israeli.

1 Kings 8:49

maombi yao, dua zao

Tazama 8:44

Wasamehe watu wako waliotenda dhambi dhidi yako, na dhambi zao zote ambazo kwazo, wamekukosea wewe dhidi ya amri zako

Sulemani anamwomba BWANA mara mbili kuwasamehe watu. Hii inasisitiza ile juhudi ya dua yake.

1 Kings 8:51

tanuru ambamo vyuma huyeyushwa

"tanuru ambalo watuhuyeyusha vyuma"

macho yako yatazame

"utazingatia"

1 Kings 8:54

Asiwe BWANA

"Msifuni BWANA"

1 Kings 8:57

Asituache wala kututelekeza

Virai hivi viwili vinamaanisha kitu kilekile na vinasisitza hamu ya BWANA ya kuwa pamoja na watu.

aunganishe mioyo yetu na yeye

"atufanye tujitoe kwake"

tuishi katika njia zake

"kuishi kama anavyotutaka kufanya"

1 Kings 8:59

mchana na usiku

"muda wote"

mioyo yenu iwe ya haki

"kujitoa kikamilifu"

1 Kings 8:62

watu pamoja naye

Tazama 8:1

1 Kings 8:64

madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele yakae

"madhabahu ya shaba iliykuwa mbele ya BWANA"

1 Kings 8:65

Israeli yote pamoja naye

Tazama 8:62

siku saba ... siku saba ... siku kumi na nne

"siku 7 ... siku 7 ... siku 14"

kwa furaha na mioyo ya shangwe

Virai hivi viwili vinmaanisha kitu sawa

1 Kings 9

1 Kings 9:1

Sulemani

Sulemani alikuwa mwana wa mfalme Daudi ambaye alikuwa mtoto wa Bthisheba.

nyumba

neno nyumba limetumika kama lugha ya umbo katika biblia. Wakati mwingine limemaanisha "wanafamilia", wakati mwingine limemaanisha uzao wa mtu fulani, na wakati mwingine limemaanisha Hekalu au masikani ya BWANA. Pengine limemaanisha watu wa Mungu na wakati mwingine taifa la Israeli.

BWANA

Neno "BWANA" ni jina binafsi la Mungu ambalo lilijifunua wakati wa Mungu alipojidhihirisha kwa Musa kwenye kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto.

mfalme

Neno "mfalme" linamaanisha mtu mwenye mamlaka makubwa ya mji, serikali au ya nchi.

Ikulu

Neno "ikulu" linamaanisha nyumba anayoishi mfalme, pamoja n a wanafamilia wake, na watumishi wake.

Gibioni, Wagibioni

Gibioni ni mji uliokuwa umbali wa kilomita 13 kaskazini m ashariki mwa Yerusalemu. Watu waliokuwa wakiishi kwenye huo mji waliitwa Wagibioni.

1 Kings 9:3

ili niweke jina langu humo milele

"ili kuishi humo na kuwa mmliki milele na milele"

Macho yangu na moyo wangu utakuwa humo nyakati zote

"Nitalilinda na kulitunza"

1 Kings 9:4

kama utatembea mbele yangu kama baba yako Daudi alivyotembea

"Kama utaisha kama ninavyokutaka uishi, kama vile Daudi baba yako alivyofanya"

kwa haki na unyofu katika moyo

Virai hivi viwili vinamaanisha kitu kilekile, vimetumika kuonyesha msisitizo wa jinsi Daudi alivyokuwa.

kiti chako cha enzi

"utawala wako"

uzao wako hautaondoka katika kiti cha enzi cha Israeli

"daima utatawala katika Israeli"

1 Kings 9:6

amri zangu na maagizo yangu

"maagizo" na "amri" yanamaanishakitu kilekile yametumika kusisitiza kuwa BWANA aliamuru.

kuabudu miungu mingine na kusujudu

Virai hivi vinamaanisha kitu kilekile, na vimeunganiswa kwa ajili ya msisitizo.

niliyoitakasa kwa jina langu

"niliyoitenga kwa ajili yangu"

Nitaitupilia mbali

"Nitaikataa"

1 Kings 9:8

Ijapokuwa hekalu hili limetukuka sasa

"japokuwa hekalu hili ni kubwa na zuri"

atasituka na kuzomea

"ataonyesha mshangao na kutoa sauti ya dharau"

wameinamia na kuiabudu

Virai hivi vinamaanisha kitu kilekile. Kirai "kuiinamia" kinaonyesha kitendo ambacho watu hutumia wa wakati wa kuabudu.

1 Kings 9:10

Ilitokea

Nneo hili limetumika ili kuonesha mwanzo mpya wa habari. Unaweza kutumia neneo ambalo lugha yako huwa inatumia.

mwishoni mwa miaka ishirini

"baada ya miaka 20"

Sulemani alikuwa amemaliza kuyajenga

"Wafanyakazi wa Sulemani walikua wamemaliza kuyajenga"

1 Kings 9:12

Ndugu yangu, ni miji gani hii uliyonipa?

"Hii miji uliyonipa ni mizuri lakini haina faida yeyote."

akaiita nchi ya Kabuli mpaka leo

"Na watu bado huiita hivyo mpaka leo"

tani alfu nne za dhahabu

"kiasi cha kilogramu 4000"

1 Kings 9:15

vigezo ambavyo Sulemani aliweka ili kujenga hekalu

"sababu ambazo Sulemani aliweka kwa wafanyazi ili wajenge hekalu"

kuijenga Milo

Inaweza kumaanisha "kujenga ule mfumo wa ngazi"

Farao mfalme wa Misiri alikuwa ameenda

"Jeshi la Farao, mfalme wa Misri, lilikuwa limeenda"

1 Kings 9:17

Kwa hiyo Sulemani akaijenga Gezeri

"Wafanyakazi wa Sulemani wakaijenga Gezeri"

1 Kings 9:20

makundi ya watu, watu wengi, watu, mtu

Hayao ni , makundi ya watu wenye lugha moja na utamaduni mmoja.

Mwamori

Waamori walikuwa watu wenye nguvu ambao walikuwa wanatokana na mjukuu wa Nuhu aliyeitwa Kanaani.

Mhiti

Wahiti walitokana na uzao wa Hamu kupitia mwanae Kanaani. Baadaye walikuja kuwa dola kubwa ambayo leo iko kwenye eneo la Uturuki na Palestina y a kaskazini.

Waperezi

Waperezi walikuwa moja ya makundi ta watu waliokuwa katika nchi ya Kanaani. Tunafahamu machache sana juu ya mababu wa hili kundi na hata sehemu hasa walikoishi huko Kanaani

uzao, walitokana n a

"uzad" ni mtu ambaye ana uhusiano wa moja kwa moja au uhusiano wa damu na mtu katika historia.

Yebuse, Wayebuse

Wayebuse walikuwa ni moja ya makundi ya watu walioishi katika nchi ya Kanaani. Walitokana na mtoto wa Hamu aliyeitwa Kanaani.

kazi, wafanya kazi

Neno "kazi" linamaanisha kufanya kazi fulani ngumu.

1 Kings 9:22

Sulemai hakuwafanya kuwa shokoa watu wa Israeli

"Sileani hakuwashurutisha watu wa Israeli kufanya kazi"

1 Kings 9:23

watu 550

"watu mia tano na hamsini"

1 Kings 9:24

akaijenga Milo

Tazama 9:15

1 Kings 9:25

madhabahu iliyokuwa mbele ya BWANA

Tazama 8:64

Kwa hiyo akalimaliza hekalu

"Kwa hiyo wafanya kazi wake wakalimaliza hekalu"

1 Kings 9:26

Sulemani alitengeneza

"Wafanyakazi wa Sulemani walijenga"

Merikebu

"kundi kubwa la meli"

tani 14.5 za dhahabu

"kiasi cha kilo 14,000 za dhahabu

1 Kings 10

1 Kings 10:1

Uvumi wa Sulemani kuhusu jina la BWANA

Inaweza kumaanisha 1) "Uvumi wa Sulemani uliomtukuza BWANA" au 2) "Uvumi wa Sulemani aliopewa na BWANA"

yote yaliyokuwa moyoni mwake

"vyote alivyotaka kujua"

1 Kings 10:3

kuketi kwa watumishi wake

Inaweza kumaanisha 1) "Jinsi watumishi wake walivyokuwa wameketi kuzunguka meza" au 2) "Mahli ambapo watumishi wake waliishi"

roho yake ilizimika

"aliishiwa pumzi"

1 Kings 10:6

maneno yako na hekiima yako

Neno "hekima" linbeba uzito wa "maneno". "hekima ya semi zako"

macho yangu yamejionea

"Nimejionea"

Hata nusu ya hekima na utajri wako umezidi uvumi ambao nilikuwa nimesikia

"watu waliniambia kidogo sana"

1 Kings 10:8

ambao daima husimama mbele yako

"ambao wako katika uwepo wako wakisubiri kukutumikia"

BWANA, Mungu wako atukuzwe

"Watu na wamtukuze BWANA Mungu wako"

alikuweka kwenye kiti cha enzi cha Israeli

"Aliyekufanya kuwa mfalme"

1 Kings 10:10

kilo za dhahabu elfu nne na miatano

kilo 4500 za dhahabu

Hapakuwahi kutokea kiasi kikubwa cha viungo ... alitoa kwa mfalme Sulemani kuwahi kutolewa tena

"Hakuna tena mtu aliyetoa kwa mfalme Sulemani viungo kama vile ambavyo malkia wa Sheba alimpa"

1 Kings 10:11

Mfalme alitengeneza nguzo

"Wafanyakazi wa mfalme walitengeneza nguzo za hekalu"

kimewahi kutokea hadi leo

"wala hakuna aliyewahi kuona kiasi kikubwa tena"

1 Kings 10:13

kila kitu ambacho alihitaji, na kila kitu alichoomba

Virai hivi viwili vinamaanisha kitu kilekile na vitumika kwa pamoja kuonyesha msisitizo.

kwa ukarimu wake

"kutokana na ukarimu wake"

1 Kings 10:14

kwa mwaka mmoja

Hii inamaanisha kwa kila mwaka katika utawala wa Sulemani, na wala siyo mara moja tu. "kila mwaka"

kilo elfu ishrini na tatu za dhahabu

kilo 23,000za dhahabu

1 Kings 10:16

Mfalme Sulemani alitengeneza

"wafanyakazi wa mfalme Sulemani walitengeneza"

ngao kubwa mia mbili

"ngao 200 kubwa"

shekeli mia sita za dhahabu

Shekeli moja ina kipimmo ch a gramu 11. "Ni kama kiasi cha kilo 6.6 cha dhahabu"

shekeli mia sita

ni sawa na kilo tatu

ngao mia tatu

"ngao 300"

Mane tatu za dhahabu

Mane moja ni kipimo kilicho karibu sawa na gramu 600."sawa na kiasi cha kilo 1.8 za dhahabu"

ikulu ya mwitu wa Lebanoni

Tazama 7:1

1 Kings 10:18

mfalme akafanya

"wafanyakazi wa mfalme walifanya"

enzi kwa pembe

Pembe ni vitu vigumu vyeupe ambavyo vinatokana na pembe za tembo.

1 Kings 10:21

ikulu ya mwitu wa Lebanoni

Tazama 7:1

1 Kings 10:23

wote ulimwenguni

"watu kutoka sehemu zote"

ilitafuta uwepo wa Sulemani

"walitafuta kumtembelea Sulemani"

ambayo Mungu alikuwa ameweka katika moyo wake

"ambacho Mungu alikuwa ameweka katika akili zake" au "ambacho Mungu alikuwa amempatia"

1 Kings 10:26

magari 1,400 na wapanda farasi elfu kumi na mbili

"magari 1,400 na wapanda farasi 12,000"

1 Kings 10:28

waliokuwa wamenunuliwa kutoka Misri

"amabao wachuuzi wake waliwanunua Misri"

Magari yalinunuliwa

"Wachuuzi wake walinunua magari"

kwa shekeli mia sita za fedha ... shekeli 150

Shekeli moja ina uzani wa ulioswa na gramu 11. "karibu sawa na kilo 6.6 za fedha ... sawa na kilo 1.7"

Vitu vingi katika hivi baadaye viliuzwa

"Wachuuzi wake baadaye waliviuza vitu hivi"

1 Kings 11

1 Kings 11:1

Wamoabu, Waamori, Waedomu, Wasidoni na Wahiti

Haya ni majina ya makundi ya watu

Basi mfalme Sulemani

Neno "basi" linaonyesha mwanzo wa habari mpya.

wataigeuza mioyo yenu ili mfuate miungu yao

"watawashawishi kuabudu miungu wanayoiabudu"

1 Kings 11:3

wanawake halali mia saba namasuria mia tatu

"wanawake halali 700 na masuria 300"

waliugeuza moyo wake

"waliugeuza moyo wake toka kwa BWANA" au "walimgeuza akaacha kumwabudu BWANA"

hakuutoa moyo wake wote

"hakuwa amejito akikamilifu"

1 Kings 11:5

Ashitorethi, Milikomu

Haya ni majina ya miiungu ya uongo

Wasidoni

Hili jinala kundi la watu

maovu mbele ya BWANA

"kile ambacho BWANA alikiona kuwa ni kiovu"

alimfuata Milikomu

"Milikomu" ni jina lingine la "Moleki"

1 Kings 11:7

walifukiza uvumba na kuwatolea sadaka

Neno "kuwa" linamaanisha hao miungu ambao Sulemani aliwajengea.

1 Kings 11:9

Moyo wake ulikuwa umemwacha Mungu

"Sulemani alimwacha kumwabudu BWANA"

alikuwa amejionyesha kwake mara mbili

"BWANA alikuwa amejionyesha kwa Sukemani mara mbili"

1 Kings 11:11

nitaugawa ufalme kutoka kwako

Mungu atauondo ufalme kutoka kwenye uzao wa Sulemani kama vile mtu achanavyo kipande cha nguo.

ukiwa chini ya mwanao

"mamlaka ya mwanao"

1 Kings 11:14

Daudi alipokuwa Edomu ... Hadadi alipokuwa mtoto mdogo

Hii ni habari ya historia iliyotokea hapo kale.

Yoabu na Israeli yote

"Yoabu na jeshi lote la Israeli"

Hadadi alichukuliwa na Waedumu wengine na watumishi wa baba yake

"watumishi wa baba wa Hadadi walimchukua pamoja na Waedomu wengine"

1 Kings 11:18

Taarifa kwa ujumla

Tazama 4:11

Waliondoka Midiani

Tazama 11:14

1 Kings 11:20

Daudi alishalala na mababu zake

"Daudi alikuwa amekufa"

1 Kings 11:23

Daudi aliwapiga

Wakati jeshi la Daudi lilkipowaua

Rezoni akawachukia Israeli

"Rezoni aliwachukia sana Waisraeli"

1 Kings 11:26

akainua mkono wake dhidi ya mfalme

"akamwasi mfalme"

Sulemani kujenga Milo

Tazama9:15

1 Kings 11:28

Mtu hodari na shujaa

Inaweza kumaanisha 1) "shuja mkuu" 2) "mtu mwenye uwezo mkubwa" au 3)mtu tajiri na mwenye ushawishi."

akampa kuwa na mamlaka

"akamfanya kuwa kamanda"

1 Kings 11:31

Akamwabia

Neno "a" linamaanisha Ahiya

Nitaugawa ufalme

Tazama 11:11

mkono wa Sulemani

"mamalaka ya Sulemani

Sulemani atabaki

"Mwana wa Sulemani a" au "Uzao wa Sulemani utabaki"

kilicho chema katika macho yangu

"Ninachokiona kuwa sawa"

1 Kings 11:34

Taarifa kwa ujumla

Ahiya anaendelea kumwambia Yeroboamu kile ambacho BWANA alisema.

Sitauchukua

"Neno "si" linamaanisha BWANA

kwenye mkono wa Sulemani

"toka kwenye mamlaka ya Sulemani"

Nitampa

Neno "m" Yeroboamu.

atabaki kuwa nuru mbele yangu

"daima kutakuwa na kizazi kitakachotawala ili kuwa ukumbusho wa familia ya Daudi"

1 Kings 11:37

Taarifa kwa ujumla

Ahiya anaendeleea kumwambia Yeroboamu kile ambacho BWANA amesema.

Nitakuchukua

Neno "ni" linamaanisha BWANA na neno "ku" linamaanisha Yeroboaomu.

kinachopendeza mbele yangu

Tazama 1:31

nitakujengea nyumba ya uhakika

"Nitakuanzia ufalme wa milele"

1 Kings 11:40

Yeroboamu

Yeroboamu mwana wa Nebati ndiye aliyekuwa mfalme wa kwanza wa dola ya kaskazini ya Israeli kati ya mwaka 910 - 900 KK. Yeroboamu mwingine, mwana wa Yehoashi, alitawala Israeli baada ya miaka 120

Misri, Wamisri

Misri ni nchi iliyo kasikazini mwa Afrika, kusini magharibi mwa nchi ya Kanaani.

kifo. kufa, aliyekufa

Neno hili linatumika kuonyesha kifo cha kimwili na cha kiroho.

1 Kings 11:41

je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio y a Sulemani?

"unaweza kuyapata kwenye kitabu cha matukio ya Sulemani."

Kitabu cha matukio ya Sulemani

hiki ni kitabu ambacho kwa sasa hakipo tena

Naye akalala na mababu zake

"Akafa"

alizikwa

"watu wakamzika"

1 Kings 12

1 Kings 12:1

Israeli yote walikua wanaenda

"Wanaume wote wa Israeli"

Ikatokea kuwa

Neno hili linaonyesha mwanzo wa habari mpya. Waweza kutumia neno lililo katika lugha yako.

1 Kings 12:3

kumwita

Herufi "m" inamaanisha Yeroboamu

ailiifanya nira yetu kuwa nzito

"alitutendea kwa ukatili" au "alitushurutisha kufanya kazi"

1 Kings 12:6

kwa wazee waliokuwa wamesimama mbele ya Sulemain

"wazee waliomshauri Sulemani" au "wazee waliohudhuria kwa Sulemani"

1 Kings 12:8

wakasimama mbele yake

"waliomshauri" au "waliohudhuria kwake"

ifanye nyepesi nira ambayo baba yako alituwekea"

"usitutenee kwa ukatilii kama baba yako alivyotutendea" au "usitushurutishe kufanya kazi kama baba yako alivyotufanyia"

1 Kings 12:10

kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu

Maana yake ni kwamba Rehoboamu ni mkali na mwenye kuogofya kuliko baba yake.

Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini mimi nitawaadhibu kwa nge

Hii inamaanisha kuwa adhabu ambayo Rehoboamu ataitoa ni mbaya kuliko alitoa baba yake.

nitawaadhibu kwa nge

Neno "nge" linaweza kumaanisha 1)mjeredi wenye ncha za vyuma, au 2) kiumbe mwenye mkia wa sumu.

1 Kings 12:12

baba yangu aliwatwika kongwa zito ... mimi nitawaadhibu kwa nge

Tazama 12:10

1 Kings 12:15

kwa kuwa ilikuwa zamu ya tukio lililoletwa na BWANA

"BWANA alisababisha hili litokee"

1 Kings 12:16

Israeli yote

"watu wote wa Israeli waliokuwepo"

Je, tuna sehemu gani kwa Daudi?

"hatutakuwa na sehemu katika familia ya Daudi"

Hatuna urithi kwa mwana wa Yese"

"Hatutakuwa na chochote cha kufanya katika uzao wa Yese"

"Nenda kwenye hema zako

"Nendeni nyumbani kwenu, enyi watu wa Israeli"

sasa tazama kwenye nyumba yako

"Sasa uuangalie utawala wako, uzao wa Daudi"

1 Kings 12:18

Waisraeli wote wakampiga kwa mawe

"Watu wote wa Israeli waliokuwepo pale"

nyumba ya Daudi

"Wafalme wanaotokana na uzao wa Daudi"

1 Kings 12:20

Ndipo Israeli

Neno hili limetumika kuonesha kuwa kuna tukio la muhimu kwenye habari. Waweza kutumia neno lolote lililo kwenye kabila yako lenye mukhutadha huo.

Israeli yote

"Viongozi wote wa Israeli waliposikia"

kuwa mfalme wa Israeli

"mfalme wa makabila yote 10 ya Israeli"

familia ya Daudi

"Uzao wa Daudi"

kabila ya Yuda

"watu wa kabila ya Yuda"

1 Kings 12:21

nyumba ya Yuda

Watu kutoka kabil ya Yuda

wanaume wanajeshi 180,000

"askari 180,000 waliochaaguliwa kwa uangalifu" au "askari wazuri 180,000"

nyumba ya Israeli

watu kutoka makabila 10 ya Israeli yaliyokuwa kaskazini

1 Kings 12:22

Neno la Mungu lkamjia

"Mungu alisema neno lake"

mtu wa Mungu

Hili jina lingine la nabii, "Nabii"

kwa nyumba yote ya Yuda na Benjamini

"watu wote wa kabila Yuda na Benjamini"

ndugu zako watu wa Israeli

Neno "ndugu" na "watu wa Israeli" vyote vivnamaanisha wanaume wa makabila kumi ya kaskazini mwa Israeli na vinatoa msisitizo wa uhusiano wa kifamilia kati yao na Rehoboamu.

kwa kuwa jambo hili nimelisababisha mimi

"Kwa sababu mimi ndiye niliyelifanya litokee"

1 Kings 12:25

Yeroboamu akaijenga Shekemu

"Wafanyakazi wa Yeroboamu wakaijenga Shekemu"

akafikiri moyoni mwake

"mwenyewe akafikiri"

nyumba ya Daudi

"wafalme waliotokana na Daudi"

Kama hawa watu wataenda

Neno "watu hawa" linamaanisha wale watu wa makabila kumi ya Waisraeli wa kaskazini.

basi mioyo ya hawa watu itarudi tena kwa bwana wao, kwa Rehoboamu mfalme wa Yuda ... na kurudi kwa Rehoboamu mfalme wa Yuda

Virai hivi vina maana moja ambavyo vimetumika pamoja kuonesha msisitizo.

1 Kings 12:28

iliyowatoa toka

"iliyowatoa mababu zenu toka"

1 Kings 12:31

Yeroboamu akajenga nyumba mahali pa juu

"Wafanyakazi wa Yeroboamu walijenga nyumba mahali pa juu"

kufanya makuhani

"aliwachagua watu kuwa makuhani"

watu wote

"watu wote wa makabila kumi ya kaskazini"

katika mweziwa , wa siku ya kumi na tano ya mwezi

Huu ni mwezi wa nane wa kalenda ya Wahebrania. Siku ya kumi na tano ni kaaribu na mwanzo wa mwezi wa Novemba wa kalenda ya kimagharibi. "siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane"

akaenda juu kwenye madhabahu

"akatoa sadaka kwenye madhabahu"

1 Kings 12:33

akaenda juu kwenye madhabahu

"akatoa sadaka madhabahuni"

ndio mwezialiokuwa amefikiri katika akili yake

"katika mwezi aliokuwa ameamua"

1 Kings 13

1 Kings 13:1

mtu wa Mungu

Hili jina lingine la nabii. "Nabii"

Alia kinyumem na zile madhabahu

"Alitoa unabii kwa sauti kubwa kinyume na zile madhdabahu"

Ee madhabau, madhabau

Nabii iliziambia zile madhabahu kama vile anamwambia mtu anyeweza kumsikia. Alisema mara mbili ili kusisitiza.

mwana aitwaye Yosia atazaliwa katikafamilia ya Daudi

"mwana wa uzao wa Daudi atakuwa na mwana aitwaye Yosia"

watachoma

Neno "wa" linamaanisha Yosia na watu atakaokuwa nao.

madhabahu zitavunjika, na majivu ylyo juu yatamwagika

"BWANA atazivunja madhabahu na atayasambaza majivu yaliyo juu yake"

1 Kings 13:4

Na ile madhabahu ikavunjika vipande vipande, na majivu yakamwagika kutoka madhabahuni

"Mungu akazivunja zile madhabahu na akayamwaga yale majivu kutoka madhabahuni"

kama iloivyokuwa imefafanuliwa kuwa ndiyo ishara ya kwamba mtu wa Mungu alikuwa amepewa kwa neno la Mungu

"kama ishara ambayo mtu wa Mungu alikuwa amefafanua kwa neno la BWANA"

1 Kings 13:6

mkono wangu urejee

" BWANA arejeshe mkoo wangu"

mkonio wa mfalme ukarejea

"BWANA alirejesha mkono wa mfalme"

1 Kings 13:8

Hata kama utanipa nusu ya milki yako. Sitaenda na wewe

"Unadhani kuwa kama utanipa nusu ya miliki yako nitaenda na wewe. Lakini hata kama utafanya hivyo, sitaenda na wewe"

1 Kings 13:11

Wale wanawe walikuwa wamemwona yule mtu Mungu kutoka Yuda njia aliyotumia

"wanawe walimwonyesha njia"

1 Kings 13:14

Yulenabii mzee

"Nabii kutoka Betheli"

akamwambia

"nabii mzee akamwambia mtu wa Mungu"

Naye akamjibu

"Mtu wa Mungu akamjibu"

mahali hapa

"Hapa Betheli"

1 Kings 13:18

malaika amesema nami neno la BWANA

"malaika ameniambia kile ammbacho BWANA amesema" au "malaika ameniambia ujumbe kutoka kwa BWANA"

1 Kings 13:20

Walipokuwa wamekaa mezani

"Walipokuwa wameketi mezani wakila"

Neno la BWANA likamjia yule nabii

Tazama 6:11

aliyemrudisha

Herufi "m" inamaanisha mtu wa Mungu

1 Kings 13:23

na mwili wake uliachwa barabarani

"na akaucha mwili wake barabarani"

walikuja wakaeleza

"walikuja wakawambia watu juu ya ule mwili"

1 Kings 13:26

neno la Mungu, neno la BWANA, neno la Bwana, maandiko

Katika biblia, "neno la Mungu" linamaanisha kitu chochite ambacho Mungu amesema kwa watu. Hii inajumuisha kilichoandikwa na kilichosemwa. Yesu pia anaitwa "neno la Mungu"

mwana, mwana wa

Neno "mwana" linamlenga mtoto wa kiume au mwanamume katiak uhusiano na mzazi wake. Inaweza pia kumaanisha mtoto wa kiume aliyeasiliwa.

1 Kings 13:29

wakamwombolezea

Hapa herufi "wa" inamaanisha yule nabii na wanawe.

Aa, ndugu yangu

Neno "Aa" linaonyesha huzuni kubwa

1 Kings 13:31

baada ya kumzika

alieyemzika ni yule nabii mzee, na herufi "m" inamaanisha yule mtu wa Mungu.

1 Kings 13:33

Jambo hiloi likawa dhambi kwenye familia ya Yeroboamu

"Familia ya Yeroboamu ikawa imefanya dhambi kwa kufanya jambo hili"

Jambo hili

Hii inamaanisha kitendo cha Yeroboamu kujenga madhabahu ya miungu na kuchagua makuhani.

na kusababishsa familia yake kuangamizwa na kuondolewa kabisa katika uso wa dunia

"Munugu aliiangamiza na kuiondoa familia ya Yeroboamu katika usowa dunia"

1 Kings 14

1 Kings 14:1

ili wasikutambue

"hakuna atakayekutambua"

1 Kings 14:4

Tazama, mke wa Yeroboamu

Neno "Tazama" linamaanisha "sikiliza kwa uangalifu"

Mwambie hivi na hivi

Neno "hivi" na "hivi" linamaanisha kuwa BWANA alikuwa amemwambia Ahiya kitu cha kusema. "mwabia hivi"

1 Kings 14:6

kwa nini unajifanya kuwa mtu mwingine?

Acha kujifanya kuwa mtu mwingine;Mimki najua kuwa wewe ni nani?

Nimetumwa kwako nikiwa na habari mbaya

"BWANA ameniambia nikwambie habari mbaya"

Niliugawa ufalme

Mungu aliugawa ufalme kama vile mtu achanavyo kipande cha nguo.

1 Kings 14:9

kunitupa nyumavyako

Yeroboamu ameacha kumheshimu BWANA amekuwa kama mtu anayetupa takataka

1 Kings 14:11

Yeyote ambaye ni mwanfamila yako ... ataliwa na mbwa

"Mbwa watawala kila mmojaambaye ni mwanafamilia yako atakayefia mjini"

na yeyote atakayefia ... ataliwa na ndege wa angani

"ndege wa angani watamla yeyote anyefia shambani"

je, kuna jambo lolote jema lililoonekana katika macho ya BWANA, Mungu wa Israeli.

"Je, BWANA, Mungu wa Israeli, ameona jambo lolote jema?"

1 Kings 14:14

kama vile majani yanavyotikiswa majini

"kama vile mto wa maji utikizavyo jani"

ataing'oa Israeli katika nchihii njema

BWANA anailingnisha Israeli na mmea ambao ataung'oa kutoka ardhini kwa mizizi yake

1 Kings 14:17

Israeli wote walimzika

"Idadi kubwa ya watu wa Israeli walikuwepo wakati watu walipomzika"

kama vile alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA

"kama vile BWANA alivyomwambia"

1 Kings 14:19

yameandikwa

"kuna mtua liyeyanadika"

naye akalala n abau zake

"kisha akafa"

1 Kings 14:21

miaka arobaiini na moja ... miaka kumina saba

"miaka 17 ... miaka 41"

ili aweke jina lake

Tazama 9:3

jina la mama yake

kiwakilishi "yake" kinamwakilisha Rehoboamu

1 Kings 14:23

kila mahali pa juuna katika kila mti wenye majani mabichi

"mahali pa juu na chini ya miti mibichi"

walifanya machukizo yaleyale kama wa mataifa yale ambayo

"mabo yale yale yenye kuchukiza ambayo watu walifanya, ambao"

1 Kings 14:25

akaja kinyume

"jeshi lake lilivamia

ambazo Sulemani alikuwa ametengeneza

"ambazo Sulemani aliwaamuru wafanyakazi wake kutengeneza"

1 Kings 14:27

Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao

"Wafanyakazi wa mfalme Rehoboamu walitengenza ngao"

mahali pake

"mahali pa ngao za dhahabu"

na akazikabidhi kwa wakuu wa walinzi

"akawapa kuwa jukumu la walinzi"

1 Kings 14:29

je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Yuda?

"Yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda"

Rehoboamu akalala na mababu zake n a watu wakamzika

"Rehoboamu akafa na watu wakamzika"

1 Kings 15

1 Kings 15:1

Katika mwaka wa kumi na nane

"katika mwaka wa 18"

miaka mitatu

"miaka 3"

"akatembea katika dhambi zote"

"Akaendelea kufanya dhambi zote"

moyo wake haukuwa mkamilifu

"alikuwa hajajitoa"

1 Kings 15:4

alimpa taa Yerusalemu ... ili kuimarisha Yerusalemu

"alimpa Daudi mwana wa Uazao kutawala Yerusalemu ka ukumbusho wa agano na familia ya Daudi"

yaliyo mema machoni pake

"Yale ambayo BWANA aliyaona kuwa mema"

Kati ya Rehoboamu na Yeroboamu

"Kati ya majeshi ya Rehoboamu na Yeroboamu"

1 Kings 15:7

yote aliyofanya, je, hayajaandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?

Tazama 14:29

Abiya akalala na mababu zake

"Abiya akafa"

1 Kings 15:9

mwaka wa Ishirini

"katika mwaka wa 20"

miaka arobaini na moja

"miaka 41"

akafanya yaliyo mema machoni mwa BWANA

"yale amabyo BWANA aliyaona kuwa mema"

1 Kings 15:12

Asa aliikata sanamu ya kuchukiza

"Wafanyakazi wa Asa waliiangusaha ile sanamu ya kuchuliza"

1 Kings 15:14

Lakini pale mahali pa juu hapakuchukuliwa

"Lakini Asa hakuwaamuru watu kupachukua mahali pa juu"

Moyo wa Asa ulikuwa mkamilifu mbele ya BWANA

"Asa alikuwa mkamilifu mbele ya BWANA"

1 Kings 15:16

akaivamia na kuitendea kwa ukatili Yuda

"aliivamia Yuda"

akaijenga Rama

"aliiteka na kuijengea ngome Rama"

1 Kings 15:18

Akaziweka katika mikono ya watumishi

"Akaiweka kwa mtumishi wake"

Akasema

"Akawaambia watumishi wake"

Tazama

Neno "Tazama" linaongeza msisitizo kwa kilke kinachofuata na kuhalalisha kile kilichokuwa kimesemwa, "Kama uhakika wa kuwa nahitaji mkataba na wewe"

uvunje agano lako na Baasha

"Vunja agano lako na Baasha na uaivamie Israeli"

1 Kings 15:20

Ikawa Baasha aliposikia

Kirai hiki kimetumika hapa kuonyeha tukio kubwa kwenye habari. Waweza kutumia neno lililo kwenye lugha yako.

akaacha kuijenga

"Aliwazuia wafanyakazi wake kujenga"

1 Kings 15:23

je, hayajaandikwa katikakitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?

Tazama 14:29

Akalala na mababu zake na akazikwa pamoja nao

Tazama 14:29

Daudi baba yake

"Daudi babu yake"

1 Kings 15:25

Akafanya yaliyo maovu mbele ya macho ya BWANA

"kile ambacho BWANA aliona kuwa ni maovu"

akatembea katika njia ya baba yake

"alkifanya sawa nakile ambacho baba yake alifanya"

1 Kings 15:27

akafanya hila dhidi ya Nadabu

"Afanya mbinu kwa siri kumwua Nadabu"

Nadabu na Israeli yote

"Nadabu na jeshi la Israeli"

1 Kings 15:29

Baasha aliwaua watu wote wa familia ya Yeroboamu. Hakumwaacha hata mmoja wa uzao wa Yeroboamu awe hai

Sentensi hizi mbili zinamaanisha jambo moja vimetumika kwa ajili ya kutia msisitizo.

ukoo wake wote

Neno "wake" linamaanisha Yeroboamu

Ahiyo Mshilo

Ahiya alikuwa anatoka Shilo

1 Kings 15:31

je, hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli

"Yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli"

1 Kings 15:33

yaliyo mabaya katika macho ya BWANA

"yale ambayo BWANA aliyaona kuwa maovu"

akatembea katika njia ya Yeroboamu

"aliishi katika njia za Yeroboamu" au "alifanya mabo yaleyale ambayo Yeroboamu alifanya"

katika dhambi yake

Neno "yake" linamwakilisha Baasha

1 Kings 16

1 Kings 16:1

Neno la BWANA lilimjia

Tazama6:11

kutoka kwenye mavumbi

"kutoka nafasi ya chini isiyo na thamani kabisa"

umetembea katika njia za Yeroboamu

"umefanya mambo yaleyale ambyao Yeroboamu alifanya"

1 Kings 16:3

nitaifanya familia yako

Neno "yako" linamwakilishsa Baasha

1 Kings 16:5

je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?

Tazama 15:31

akalala n a mababu zake na akazikwa

Tazama 14:29

1 Kings 16:7

Neno la BWANA lilimjia

Tazama 6:11

maovu yote aliyofanya mbele ya BWANA

"mambo aliyofanya ambayo BWANA aliyaona kuwa ni maovu"

kazi ya mikonko yake

"mambo ambayo alikuwa amefanya"

1 Kings 16:8

Mtumishi wake Zimri

Neno "wake" linamwakilisha Ela

1 Kings 16:11

kama alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA

"kama BWANA alivyokuwa amemwambia"

Mungu wa Israeli

Neno "Israeli linamaanisha watu wote wa makabila kmi na mbili ambayo yametoka kwa Yakobo

1 Kings 16:14

yote ambayo alifanya , je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?

Tazama 15:31

1 Kings 16:15

lile jeshi lililokuwa limeweka kamabi kule lilisikika likisema

Wale wanajeshi waliokuwa wameweka kambi kule walimsikia mtu akisema"

Israeli yote wakamtangaza

"watu wote wa jeshi wakamtangaza"

1 Kings 16:18

yale yalIyokuwa maovu machoni pa BWANA

"yale ambayo BWANA alyaona kuwa maovu"

alitembea katika njia ya Yeroboamu

"alifanya mambo yaleyale ambayo Yeroboamu alifanya"

je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?

Tazama 15:31

1 Kings 16:21

walimfuata Tibni ... walimfuata Omri

Walimsaidia Tibni ... walimsaidia Omri

walikuwa na nguvu kuliko wale waliomfuata Tibni

"waliwazidi nguvu wale waliomfuata Tibni

1 Kings 16:23

talanta mbili za fedha

karibu kiasi cha kilo 68 cha fedha

Akajenga mji

"wafanyakazi wa Omri walijenga mji"

1 Kings 16:25

akafanya maovu mbele ya BWANA

"yaliyokuwa maovu mbele ya macho ya BWANA"

akatembea katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati

"Akafanya mambo yaleyale ambayo Yeroboamu mwana wa Nebati alifanya"

ilI kumkasirisha BWANA ... kuwa na hasira juu yasanamu zao za ubatili

Tazama 16:11

1 Kings 16:27

je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli

Tazama 15:31

akalala na mababu zake na akazikwa

Tazama 14:29

1 Kings 16:29

Yale yaliyokuwa maovu mbele ya macho ya BWANA

"yale ambayo BWANA aliyona kuwa ni maovu"

1 Kings 16:31

Ikawa kidogo tu kwa Ahabu ayaendee makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati

Kama vile kutenda dhambi sawa na zile alizofanya Yeroboamu mwana wa Nebaati hazimkutosha Ahabu"

Ikawa kidogo tu

"kitu ambacho hakina umuhimu"

akamwabudu baali na akamsujudia

Virai hivi viwili vinamaanisha jambo lilelile. Kirai cha "akamwabudu" kinafafanua kile kitendo cha kuabudu ambacho watu walifanya wakati wa kuabudu.

1 Kings 16:34

siku zake

Neno "zake" linamwakilisha Ahabu

1 Kings 17

1 Kings 17:1

Mtishibi

Hili jina la kundi la watu kutoka Tishibi

Tishibi

Hili ni jina la mji katika mkoa wa Gileadi

Kama vile BWANA, Mungu wa Israeli aishivyo

Kirai hiki ni kiapo kinchomaanisha kuwa kile anachosema ni kweli.

ambaye mbele yake ninasimama

Hii ni nahau ambayo inamaanisha "kutumika" "ambaye ninamtumikia"

umande

matone ya mvua ambayo hutokea kwenye mmea wakati wa usiku

1 Kings 17:2

Neno la BWANA lilimjia

Tazama 6:11

Neno la BWANA

Neno linawakilisha ujumbe wa wa BWANA. "ujumbe wa BWANA"

Kerithi

Hili ni jina la kisima kidogo.

Nawe utakunywa

Kirai hiki kimetumika kuonyesha kuwa BWANA atamtunza Eliya wsakati wa ukame. "kule"

kunguru

ndege wakubwa, weusi

1 Kings 17:5

kama neno la BWANA lilivyoamuru

Hapa "neno" linamwakilisha BWANA mwenyewe. "kama BWANA alivyoamuru"

kijito

Tazama 17"2

katiaka nchi

"katika eneo hilo" au "katika nchi hiyo"

1 Kings 17:8

Neno la BWANA lililmjia

Tazama 6:11

Neno la BWANA

"Neno" linawakilisha ujumbe wa BWANA, "ujumbe wa BWANA"

lilimjia

Neno "m" linamwakiklisha Eliya.

Sarepta

Huuni mji

Tazama

Neno "Tazama" linaongeza msisitizo kwa kile kiniachofuata

1 Kings 17:11

Kama BWANA Mungu wako aishivyo

Kirai hii ni kiapo kinachosisitiza kuwa kile atakachokisema ni kweli.

konzi moja ya unga tu

ni kidogo tu kwa ajili ya mlo mdogo

unga

"unga uliotumika kutengeneza mkate

kuni mbili

Hii inamaanisha vijiti viwili

ili tule, na tusubiri kufa

"kwamba tuweze kula na baada ya hapo tusubiri kufa"

Ndipo baadaye ujitengenezee wewe na mwanao

Hii iko wazi kabisa kuwa kutakuwa na unga wa kutosha na mafuta kwa ajili ya mikate zaidi.

1 Kings 17:14

BWANA atakapotuma mvua

"BWANA ndiye asababishaye mvua kunyesha"

kama vile neno la BWANA lilivyosema

"kama vile BWANA alivyokuwa amesema"

1 Kings 17:17

mwana , yule mwanamke, yule mwanamke mwenye nyumba

"mwana wa yule mwanamke mwenye nyumba"

akaishiwa pumzi kabisa

Hii ni tafsuda ya kusema kuwa mtoto alikuwa amekufa. "Alikoma kupumua" au "alikufa"

mtu wa Mungu

Mtu wa Mungu ni aina nyingine ya kusema nabii

dhambi zangu

Hii inamaanisha kuwa dhambi ni kitu cha jumla wala si kitu mahususi. "juu ya dhambi zangu"

1 Kings 17:19

alimokuwa akikaa

Herufi "mo" inamwakilisha Eliya

kitandani pake

Neno "pake" linamaanisha Eliya

umeleta majanga kwa mjane ambaye mimi nikaa, kwa kumwua mwanae

Inaweza kumaanisha 1) Eliya anauliza swali kweli. "kwa nini unamsababishia mjane ambaye mimi ninakaa kupata majanga zaidi kiasicha kumwua mwanae? au 2) Eliya anatumia swali kueleza huzuni aliyo nayo, "Kwa kweli hungemsbsbia majanga mjane ambaye mimi ninakaa kwa kumwua mwanae."

umeletea majanga kwa mjane

kumsababishia mjane maumivu ndiko kunakoongelewa kama "majanga" hiki ni kitu ambacho kiliwekwa kwa mjane.

pia umeleta majanga

neno "pia" nyongeza ya majanga ambayo ukame umesababisha

akajinyosha mwenyewe juu ya mtoto

"akalala juu ya mtoto"

1 Kings 17:22

BWANA akaisikiliza sauti ya Eliya

"BWANA akajibu maombi ya Eliya"

uhai wa mtoto ukamrudia, na akawa hai.

"mtoto akarudia uhai wake"

chumbani kwake

"kwake" Eliya

Tazama, mwanao yuko hai

Neno "Tazama" linatuandaa kuwa makinii kwa taarfa ambazo ziinafuata.

Neno la BWANA kinywani mwako ni la kweli

"Neno" linawakilisha ujumbe. Pia "kinywani" linamaanishsa kile Eliya alichosema kutoka kwa BWANA ni cha ukweli"

1 Kings 18

1 Kings 18:1

Neno la BWANA lilimjia

Tazama 6:11

nitainyeshea ardhi mvuva

"nitasababisha mvua iinyeshee ardhi

sasa njaa ilikuwa kali sana

Neno "sasa" limetumika kuonyesha mwanzo wa katika habari kuu. Na hapa mwandishi anaeleza madhara yaliyosababishwa na njaa huko samaria

1 Kings 18:3

Obadia alimheshimu sana BWANA

Hapa mwandishi anaeleza juu ya mtu mwingine katika habari.

manabii mia moja akawaficha katika makundi ya hamsini hamsini

"manabii 100 akawaficha katika makundi ya 50"

1 Kings 18:5

tuwaokoe hawa farasi na nyumbu ... ili tusiwakose wanyama wote

"tuzuie kifo kwa farasi na nyumbu hawa"

Ahabuakaenda njia yke mwenyewe na Obadia naye akaenda njia yake

Ahabu akaongoza Kikosi kuelekea upande mwingine na Obadia akaongoza kikosi kuelekea upande mwingine.

1 Kings 18:7

Ndiye wewe bwana wangu Eliya?

"Eliya Bwana, umekuja!"

bwana Eliya

Neno "bwana" limetumika kuonesha heshima

Nenda umwambie bwana wako, 'Tazama, Eliya yuko hapa."

Neno "bwana" linamaanisha Ahabu

Tazama

Neno "Tazama" hapa linonesha msisitizo wa kile kinachofuata.

1 Kings 18:9

Nimekoseaje ... ili aniue?

"Sijakukosea wewe ... kwa yeye kuniua,"

umtoe mtumishi wako katika mkono wa Ahabu

"umtoe mtumishi wako kwa Ahabu"

mtumishi

Obadia anjiona mwenyewe kuwa ni mtumishi wa Eliya ili kumheshimu Eliya

Kama BWANA Mungu wako aishivyo

Hiki ni kiapo ambacho kilitumika kuonyesha kuwa kile anachosema ni cha kweli.

hakuna taifa wala ufalme ... ambapo bwana wangu hajatuma watu

"bwana wangu ametuma watu kila mahali"

Na sasa wewe

Neno hili limetumika kuonyesha hatari ya kile ambacho Eliya anamwambia Eliya kufanya.

1 Kings 18:12

Je, haujaambiwa ... kwa mikate na maji

"Kwa hakika umeshambiwa juu y a kile nilichokifanya ... kwa mikate na maji,"

bwana wangu

neno "bwana" ni neno la heshima inayotolewa kwa Eliya

manabii miamoja wa BWANA katika makundi ya hamsini

"manabii 100 wa BWANA katika makundi ya 50"

1 Kings 18:14

Nenda umwambie bwana wako kwamba Eliya yuko hapa

Tazama 18:9

bwana wako

Neno "bwana" hapa linamaanisha Ahabu

kama vile BWANA wa majeshi aishivyo

Hiki ni kiapo kinachomaanisha kuwa anachokisema ni cha kweli

ambaye mimi ninasimama

"ambaye ninamtumikia"

1 Kings 18:16

na kumwambia

"Obadia akamwambia Ahabu kile ambacho Eliya amemwambia kusema"

"Je, ni wewe? mtabishaji wa Israeli!"

"Kwa hiyo leo nimekuona . Wewe mtabishaji wa Israeli!"

1 Kings 18:18

Israeli yote

Hii inamaanisha viongozi na watu wote wa makabila kumi ya Israeli yaliyoko kwenye utfalme wa kaskazini.

manabii 450

"manabii mia nne na hamsini"

manabii mia nne

"manabii 400"

1 Kings 18:20

akatuma neno

"akatuma ujumbe"

Mtaendelea kubadilisha mawazo yenu mpaka lini?

"Mmesitasita katikati ya mawazo kwa muda mrefu sana"

Lakini watu hawakumjibu neno

"hawakusema chochote" au "walibaki kimya"

1 Kings 18:22

Mimi, pekee yangu, ndiye niliyebaki

Neno "Mimi" limerudiwa kwa aji;li ya msisitizo.

kisha mtaliita jna la mungu wenu ... nitaliita jiina la BWANA

"mwiteni mungu wenu ... nitamwita BWANA"

Watu wote wakajibu na kusema, "Hilo ni jambo jema"

watu wote wakasema, "hili ni jambo jema"

1 Kings 18:25

kumwandaa

"mfanyeni tayari kwa sadaka"

ninyi ni wengi

Neno "ninyi" ni la wingi.

Nao wakamchukua yule nfahari

"manabii wa baali wakamchukua yule fahari"

waliyekuwa wamepewa

yule fahari ambaye mtu aliwapa

Lakini hapakuwepo na sauti, wala aliyejibu

"Lakini Baali hakusema wala kufanya chochote"

1 Kings 18:27

Labda

"yawezekana" au "inaweza kuwa"

anapumzika

"bafuni"

sharti aamushwe

"lazima mwamshe"

bado walikuwa wakiendelea

"waliendelea na tabia yao isiyo ya kawaida"

wakati wa jioni wa kutoa dhabihu

kutoa dhabihu ya jioni

jioni

wakati jua linapoanza kutoweka na giza kuanza kuingia

lakini hapakuwepo na sauti wala mtu wa kujibu; wala hapakuwepo na yeyote wa kujibu wala wa kuangalia.

"lakini Baali hakusema wala kufanya chochote wala kuangalia"

lakini hapakuwepo na sauti wala mtu wa kujibu;

Tazama 18:25

1 Kings 18:30

mawe kumi na mbili

"mawe 12"

katika jina la BWANA

Inaanisha 1) "kumheshimu BWANA" au 2) "kwa mamlaka ya BWANA."

mfereji

ni njia ndogo ya maji

1 Kings 18:33

akaweka kuni kwa ajili ya moto

"akaweka kuni kwa ajili ya moto madhabahuni"

vyombo vinne

"vyombo 4"

pipa

pipa ni chombo cha kuwekea maji

mfereji

Tazama 18:30

1 Kings 18:36

Ikawa

Neno hili hutumika kuonyesha tukio la muhimu katika historia. Waweza kutumia neno jingine linalofaa katika lugha yako

Jioni

Tazama 18:27

BWANA, Mungu wa Ibrahimu, wa Isaka, na wa Yakobo

Hapa "Israeli" inamaanisha Yakobo. Mungu alilibadilisha jina la Yakobo likiwa Israeli (Mwanzo 32:28). Pia Mungu aliwaita wana wa uzao wa Yakobo "Israeli."

na ijulikane leo kuwa

"kuwafanya hawa watu wajue leo"

Nisikie ... nisikie

Neno hili limerudiwa kwa ajiloi ya kutia msisitizo

umerudisha mioyo yao kwako tena

"umewafanya wakuabudu tena"

1 Kings 18:38

moto wa BWANA ukashuka

"moto wa BWANA ukashuka chini"

BWANA, ndiye Mungu! BWANA, ndiye Mungu

Neno limerudiwa kwaajiliya kusisitiza

kijito cha Kishoni

"kijito" ni chemichemi ndogo za maji.

1 Kings 18:41

kuna sauti ya mvua kubwa

"kuna sauti kama ya mvuva kubwa itakayonyesha"

akasujudu chini na akaweka uso wake katikati ya magoti

Hiki ni kitendo kilichokuwa kikitumika waktati wa kuabudu.

1 Kings 18:43

mara saba

"mara 7"

dogo kama mkono wa mtu

kutoka mbali, wingu linaweza kuonekana kama mkono wa mtu.

1 Kings 18:45

Ikatokea

Neno hili limetumika hapa ili kuonyesha mahali ambapo tendo linaanzia. waweza kutumia neno linalotumika katika lugha yako

mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Eliya

"BWANA alimpa Eliya mkono wake"

Akalikaza vazi lake kwa mshipi

Eliya alilikaza vazi lake kiunoni iloi kwamba miguu yake iwe tayari kukimbia.

1 Kings 19

1 Kings 19:1

miungu wanifanye hivyo na mimi, na zaidi

"miungu waniue na nawanifanyie mabaya zaidi"

muda kama huu sitayafanya maisha yako kuwa kama mmooja wa hao manabii waliokufa.

"kama sitakua kama ulivyowaua hao manabii"

akainuka

"akasimama"

1 Kings 19:4

Lakini ye ye mwenyewe akaenda mwendo wa siku moja

"altembea mwenyewe kwa siku moja"

mti wa mretemu

"huu ni mtiunaokua kwenye jangwa"

Akajiombea mwenyewe kufa

"Akaomba kwamba afe"

Sasa yatosha, BWANA

"Mateso haya ni makubwa sana kwangu, BWANA" au "Sasa ninamashaka sana, BWANA"

Inuka

"amka"

mkate uliokuwa umeokwa kwa mkaa

"mkate ambao mtu alikuwa ameuoka kwenye jiwe lenye joyo"

gudulia la maji

"chombo cha maji"

1 Kings 19:7

safari bado ndefu kwako

"itakuwa ndefu sana kwako"

akasafri kwa nguvu ya chaku;a hicho kwa muda wa siku arobaini mchana na usiku

"chakua hicho kilimpa nguvu ya kusafiri siku 40"

1 Kings 19:9

kwenye pango akakaa humo

Neno "humo" linamaanisha Mlima Horebu. Pango ni sehemu iliyowazi maaeneo ya milima ambayo hufanya kitu kama chumba cha asili au chumba kilicho chini aridhini.

Neno la BWANA lilimjia likimwambia

Tazama 6:11

Unafanya nini hapa Eliya

"Hapa si mahali unapotakiwa kuwa, Eliya"

Mimi, pekee yangu, nimebaki

Neno "mimi" limerudiwa kwa aji;i ya msisitizo.

1 Kings 19:11

kwenye mlima mbele yangu

"mlimani katika uwepo wangu"

ukaupige mlima

"upige mlima"

1 Kings 19:13

akaufunika uso wake kwa vazi lake

Akuficha uso wake kwa vazi lake" au"akaficha macho yake asimwone Mungu"

lango

ule uwaziambao mtu huutumia kuingilia pangoni au kwenye chumba"

Na sauti ikaja kwake

"Kisha akaisikia sauti"

unafanya nini hapa? ... wanajaribu kuichukua roho yangu

Tazama 19:9

1 Kings 19:15

kuwa nabii mahali pako

"nabii badala yako"

1 Kings 19:17

Itakuwa hivi

"Kitakachotokea ni"

atakayejaribu kutoroka upanga wa Hazaeli

"ambaye Hazaeli hatamwua kwa upanga"

ntawaacha kwa ajili yangu

Neno "ni" linamaanishsa BWANA. "Nitawaokoa kutoka kwenye kifo"

watu elfu saba

"watu 7000"

ambao magoti yao hayajawahi kupigwa kwa Baali, na ambao midomo yao haijambusu."

"Ambao hawajawahi kumwabudu na kumbusu Baali"

1 Kings 19:19

akilima

akilima kwa jembe la kukokotwa na wanyama linlovunja vunja udongo ili kwamba mbegu zipandwe.

jozi za makisai kumi na mbili

"jozi 12 za makisai"

yeye mwenyewe alikuwa akilima na ile ozi ya kumi na mbili

Neno "mwenyewe" linaonyesha kuwa Elisha alikuwa akilima na ile jozi ya mwisho, wakati wale wanume wengine walikuwa wakilima na zile jozi kumi na moja.

akamwambia, "tafadhali"

Neno "mwa" linamaanisha Elisha

1 Kings 19:21

akawapa watu

Elisha aliwapa nyama iliyopikwa wale watu wa mji.

1 Kings 20

1 Kings 20:1

Beni Hadadi

Hili jina la mwanamume

wafalme thelathini na mbili wasaidizi

"wafalme wasaidizi 32"

wafalme wasaidizi

"wafalme wanaotawala makundi madogo madogo ya watu"

1 Kings 20:4

iwe kama unavyosema

"ninakubaliana n a wewe"

kesho wakati kama huu

"kesho wakati wa saa kama huu wa sasa"

kila wakipendacho machoni mwao

"chochote kinachowapendeza"

1 Kings 20:7

wa nchi

"wa watu wa Israeli"

Hebu angalieni

"agalieni kwa makini"

sijamkatalia

"Nimekubaliana na matakwa yake"

watu wote

"watu wote waliokuwepo"

1 Kings 20:9

matakwa yako haya ya pili

"vitu vile ulivyoomba mara ya pili"

basi miungu inifanye hivyo na zaidi

Tazama 19:1

kama mavumbi ya Samaria yatawatosheleza watu wote wanaonifuata kuchukuc angalau kila mmoja angalau konzi mkononi mwake

Bebi Hadadi anasema kuwa jeshi lake litaangamiza kabisa kila kitu Samaria.

1 Kings 20:11

Mwambieni Bebi Hadadi, 'Hakuna abaebaye silaha yake, atakayejivuna kama wakati wa kuishusha

"Mwambieni Beni Hadadi, 'usijivune kana kwamba tayari umekwisha kushinda vita ambavyo bado hujapigana."

1 Kings 20:13

Tazama

Neno "tazama" linatuandaa kuonekana kwa mtu mwingine kwenye hii habari. Lugha yako inaweza kuwa na neno zurizaidi.

Je, umeliona hili jeshi kubwa?

"Tazama hili jeshi kubwa"

Tazama, nitaliweka katika mkono wako leo

Neno "tazama" linatuandaa kusikiataaraifa za kushangaza zinazofuatia.

Nitaliweka katika mkono wako

"Nitakupa ushindi dhidi ya jeshi hilo"

Ni nani?

"Utafanya hilo kwa kumtumia nani?"

Ndipo Ahabu alipowataarifu wale vijana

"Ahabu akawakusanyawale maofisa vijana"

232

"mia mbili thelethini na mbili"

wanajeshiwote, jeshi lote

Virai hivi vinmaanisha jambo lilelile. Vimetumia kwa ajili ya kuonesha msisitizo.

elfu saba

"7000"

1 Kings 20:16

Nao wakatka

Neno "wa" linamaanisha Waisraeli

wasaidiziwa wafalme

Tazama 20:1

Kisha Bebni Hadadi alitaarifiwa na wale wanaskauti aliokuwa amewatuma

"Wale wanaskauti ambao Beni Hadadi alikuwa amewatuma walimtaarifu"

Skauti

"Skauti" ni mwanjeshi anyetumwa kukusanya taarifa.

1 Kings 20:18

amani, kwa amani

Neno "amani" linamaanisha ile hali ya kutokuwa na machafuko, mashaka, au hofu.

Maisha, kuishi naishi ,yuko hai

Maneno haya yoe ynamaanisha ile hali ya kuwa hai kimwili wala siyo kufa.

1 Kings 20:20

Israeli ikawashinda

"Wale wanaume wa jeshi la Israwli likawashinda"

Kisha mfalme wa Israeli akaenda akawashambulia

Mfalme wa Israeli na wanajeshi wake walienda kuwashanbulia

1 Kings 20:22

ukajiimaishe mwenyewe

"imarisha majeshi yako

uelewe na kupanga

"fanaya uamuzi"

mwakani

inawezakumaanisha majira kama haya mwaka ujao.

hebu tupigane ... tutakuwa na nguvu

Kiwakilishi "tu" n a "tu"kinamaanisha watumishi, wafalme, a jeshi

1 Kings 20:24

waondoe wafalme; mwondoe kila mmoja mahali pake ukaweke majemedari

"lazima uwaondoe wale wasaidizi wa wafalme thelathini na mbili ambao wanaongoza vikosi"

1 Kings 20:26

Afeki

Hili ni jina la mji

kupigana na Israeli

"kupigana na jeshi la israeli"

watu wa Israeli walikuwa wamehesabiwa

Jeshi la Waisraeli lilikusanywa pamoja na walipewa vitu ambavyo walihitaji kwa ajili ya vita

kama makundi mawili madogo ya mbuzi

Jeshi l a Waisraeli linaonekana dogo nadhaifu kama mbuzi mchanga.

1 Kings 20:28

mtu wa Mungu

Hili jina lingiinela nabii. "Nabii"

nitaliweka hili jeshi kubwa mikononi mwako

"nitakupa ushindi juu ya hili jeshi kubwa"

1 Kings 20:29

siku saba

"siku 7"

100,000

"laki moja"

wanajeshi wa ardhini

"mwanjeshi wa ardhini" ni askari anayetenbea kwa mguu.

waliobaki walikimbilia Afeki

"wanajeshi wa Shamu waliobaki"

elfu ishirini na saba

"27,000"

1 Kings 20:31

Tazama sasa

"Sikiliza" au "Sikiliza kwa makini kile ninachotaka kukuambia"

tuvaeni magunia viunoni mwetu, na kamba vichwani mwetu

Hii ni ishara ya kjiachilia.

Je bado yuko hai?

"Ninashangaa kwamba bado yuko hai!"

Yeye ni ndugu yangu

"Ni kama ndugu yangu"

1 Kings 20:33

Sasa wale watu

Neno "sasa" halimaanishi "wakati huu," Bali limetumika ili kupata usikivu kwa ajili ya mambo yanayofufata.

ishara yeyote kutoka kwa Ahabu

"Kwa kuwa tendo lolote toka kwa Ahabu ambalo litawaonesha kuwa Ahabu anataka kuwa mwenye neema"

1 Kings 20:35

mmoja wa wana wa manabii

"mmoja wa wa kundila manabii

Kwa neno la BWANA

"kama BWANA alivyomwambia"

umekataa kutii sauti ya BWANA

"hujamtii BWANA"

1 Kings 20:37

Mfalme

Neno "mfalme" linamaanisha mtu ambaye ni kiongozi wa juu kabisa wa mji, serikali au nchi.

1 Kings 20:39

Mtumishi wako alienda

Nabii anajisemea yeye katika nafsiya tatu kama ishara ya kumheshimu mfalme

katikati ya pigano

"mahali pale ambapo pigano lilikuwa kali sana"

maishsa yako yatatolewa kwa ajili ya maisha yake

"basi utakufa kwa niaba yake"

talanta moja ya fedha

"kilo 34 za fedha"

akienda huku na kule

"akifanya mambo mengine" au "akifanya hili na lile

1 Kings 20:41

kwa kuwa umemwachia aende

"umemwachia" au "umemwacha hai"

maisha yako yatachukua nafasi ya maisha yake na watu wako kwa watu wake

"utakufa badala yake, na watu wako watakufa kwa nafasi ya watu wako"

moyo mzito na mwenye hasira

Maneno haya mawili yanamaanisha kitu kilekile. Yametumika kuonesha uzito wa hisia zake.

1 Kings 21

1 Kings 21:1

Basi ikawa baada ya hayo

Kirai hiki kimetumika kuonyesha mwanzo wa habari mpya. Kama lugha yako ina namna ya kuseema hili basi litumike hapa.

Nabothi Myezreeli

Hili ni jiina la mtu kutoka Yezreeli

Mfalme wa Samaria

Ahabu alitawala Israeli kutokea Samaria. "Mfalme wa Israeli"

1 Kings 21:3

BWANA na alizuie

"Natumaini BWANA atanilinda ili nisiharibu uaminifu huo"

akiwa mchovu

Tazama 20:41

1 Kings 21:5

Kwa nini moyo wako una huzuni

Hapa "moyo" unamaanisha hisia. "kwa nini una huzuni sana"

Je, wewe si mtawala wa ufalme wa Israeli?

Wewe bado ni mtawala wa utawala wa Israeli."

moyo wako uwe na amani

"uwe na furaha"

1 Kings 21:8

kwa jina la Ahabu

"na akaweka saini kwa jina la Ahabu"

watu tajiri alioketi nao

"watu tajiri walioketi na Nabothi"

juu mbele ya watu

"katika eneo la heshima miongoni mwa watu"

watoe ushahidi kinyume naye

"waambie hawa watu wamshitaki Nabothi kwa mashitaka ya kwamba amemlaani Mungu na mfalme"

1 Kings 21:11

watu tajiri waishio

watu tajiri wanaoishhi"

kama Yezebeli alivyowaeleza, kama ilivyoandikwa kwenye zile barua ambazo alikuwa amewatumia

Virai hivi viwili vinamaanisha jambo moja. Vimetumika kuonesha msisitizo

kama ilivyoandikwa kwenye zile barua

"kama alivyoandika kwenye hizo barua"

juu mbele ya watu

katiak eneo la heshima miongoni mwa watu

wakamchukua nje

Neno "wa" linamaanisha watu wa mji

Nabothi ameshapigwa mawe na amekufa

"Tumempiga mawe Nabothi na amekufa"

1 Kings 21:15

Nabothi ameshapigwa mawe na alikuwa amekufa

"kwamba watu walikuwa wamempiga mawe Nabothi na alikuwa amekufa"

Nabothi hayuko hai, bali amekufa

Maneno haya mawili yanafanana kwa maana. Yametumika kuonesha msisitizo kuwa Nabothi amekufa.

1 Kings 21:17

neno la BWANA likamjia

Tazama 6:11

1 Kings 21:19

Je, umeua na kujimilikisha?

Umemwua Nabothi na kuiba shamba lake la mizabibu?

damu yako, ndiyo, damu yako

Neno limerudiwa ili kusisitiza

Je, umenipatia, adui yangu

"umegundua kile nilichofanya, adui yangu!"

umejiuza mwenyewe kufanya yaliyo maovu

"umejitoa mwenyewe kufanya yaliyi maovu"

yaliyo maovu mbele ya macho ya BWANA

"yale ambayo BWANA huyaona kuwa ni maovu"

1 Kings 21:21

Tazama

"Sikiliza" au "angalia kwa makini kile ninachotaka kukuambia"

litakuangamiza kabisa na kukufutilia mbali

Senrwnsi hizi zina aana moja zinasisitiza kuangamiza kabisa kwa familia ya Ahabu.

Nitaifanya familia yako kama familia ya Yeroboamu ...na kama familia ya Baasha

BWANA ataiangamiz afamilia ya Ahabu kama alivyoaangamiza familia ya Yeroboamu na Baasha.

1 Kings 21:23

Yeyote ambaye ni mtu wa familia ya Ahabu

"Mtu yeyote ambaye ni wa familia ya Ahabu"

1 Kings 21:25

ambaye alijiuza mwenyewe kufanya maovu

"alijitoa mwenyewe kufanya maovu"

maovu mbele ya macho ya BWANA

"kile ambacho BWANA hukiona kuwa ni kiovu"

ambaye mke wake Yezebeli ... alimchochea

Neno "ambaye" linamwakilisha Ahabu

akawafukuza mbele ya watu wa Israeli

"akawafukuza kutoka katika uwepo wa watuwa Israeli"

1 Kings 21:27

Je, unamwona jinsi Ahabu anavyojinyenyekeza mbele yangu?

"Nimeona jinsi Ahabu anavyojinyenyekeza mbele yangu"

katika siku zake ... siku za mwanae

wakatiwa uhai wake ...wakati wa uhai wa mwanae"

1 Kings 22

1 Kings 22:1

Miaka mitatu

"Miaka 3"

Ikawa katika

Kirai hiki kimetumika hapa ili konesha mwanzo wa habari mpya. Wawea kutumia neno lililo kwenye lugha yako lenye maana ya mwanzo wa tukio jipya

1 Kings 22:3

Je, mnajua kuwa Ramothi Gileadi ni yetu, ila hatufanyi chochote kuitwaa ktoka kwenye mikono ya mfalme wsa Shamu?

Ramothi Gileadi ni yetu, Lakini hataujafanya lolote kuitwaa kutoka kwenye mikono ya mfalme wa Shamu."

Kuitwaa kutoka kwenye mikonao ya mfalme wa Shamu

"Kuitwaa kutoka kwenye utawala wa mfalme wa Shamu"

Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, na farasi wangu ni kama farasi wako

"Ninawatoa askari wangu, watu wangu, na farasi wangu kwako kuwatumia katika njia uzipendazo"

1 Kings 22:5

watu mia nne

"watu 400"

Bwana ataitoa katika mkono wa mfalme

"Bwana atamruhusu mfalme kuiteka"

1 Kings 22:10

akajitengenezea pembe

akatengeneza pembe kwa ajili yake

Kwa hili utawsukuma Washami mpaka watakapoisha

Anachokisema nabii ni kwamba jeshi la Ahabu litashinda kwa nguvu nyingi kama vilr fahari anavyomshambulia mnyama mwingine. "watatakapoisha" ni usemi unaomaanisha kuwa "kuangamiza"

mpaka watakapoisha

"mpaka uwaangamiza"akapo

ameiweka kwenye mkono wa mfalme

"amemruhusu mfalme kuivamia"

1 Kings 22:13

Tazama sasa

"Sikiliza" au "Uwe msikivu kwa jambo ninalotaka kukuambia"

maneno ya manabii kwa kinywa kimoa wanatabiri mambo mema kwa mfalme

Kirai cha "kwa kinywa kimoja" kinamaanisha kwamba wote wanasema jambo lilelile jema kwa mfalme"

Tafadhli maneno yako yawe kama yao

"yao" inamaanisha "maneno ya manabii." kile unachosema kifanane na kile walichosema"

je, twende

Neno "twe" linamaanisha Ahabu, Yehoshafati, na majaeshi yao lakini si Mikaya.

BWANA ataitoa kwenye mkono wa mfalme

Tazama 22:5

1 Kings 22:16

Je, nikutake mara ngapi ili nikuapia ukweli ... kwa jina la BWANA?

"Nimekutaka mara nyingi sana ...katika jina la BWANA."

katika jina la BWANA

"kama mwakilishi wa BWANA"

Ninaiona Israeli

"Ninaliona jeshi lote la Israeli"

kama kondoo wasiokuwa na mchungaji

Wanajeshi wamefananishwa na kondoo wasiokuwa na mtu wa kuwaongoza kwa zababu mchungaji wao, mfalme, ameuawa

1 Kings 22:18

Je, sikukuambia kuwa ...majanga tu?

"Nilikuambia ...majanga tu"

akafia Ramothi Gileadi

"akafa akiwa Ramothi Gileadi"

mtu mmoja ... mwiingine

"malaika wa mbinguni"

1 Kings 22:21

Tazama sasa

Neno "tazama" linaongeza msisitizo wa kile kinachofuata.

na kuwa roho idanganyayo katika vinywa vya manabii

Neno "roho" linamaanisha mtazamo wa manabii; "vinywa" inamaanisha kile watakachosema. "Nitawafanya manabii wote waseme uongo"

BWANA ameweka roho idanganyayokwenye vinywa vya hawa manabii wako

"amewafanya manabii wako wote kuongea uongo"

1 Kings 22:24

Je, yule roho wa BWANA alitokaje kwangu ili aseme na wewe?

"Usidhani kwamba roho wa BWANA ameniacha ili anene na wewe!"

Tazama

"Sikiliza" au "Uwe mwangalifu kwa kile ninachotaka kukuambia"

utatambua

"utajua kuwa ni nani anayetabiri ukweli"

1 Kings 22:26

Kama utarudi salama

Hii ineleza kitu ambacho kwa hakika hakitatokea. BWANA alikuwa amemwambia Mikaya keamba mfalme hatarudi salama.

1 Kings 22:31

majemedari thelethini na mbili

"majenedari 32"

Msimwangamize askari wa muhimu au ambaye si wa muhimu.

Msimvamie askari yeyote

Ikawa wakati

Hiki kirai kietumika hapa ili kuonyesha tukiola muhimu katiakhabari. Waweza kutumia neno lililo kwenye lugha yako kwa jambo kama hili.

1 Kings 22:35

mfalme akalazwa garini mwake

"mtu mmoja akamweka mfalme kwenye gari lake

kilio kiatawala

"wanajeshi walianza kupiga kelele

Kila mtu arudi kwenye mji wake; na kilamtu arudi kwenye mkoa wake

Senrensi hizi zinamaanisha jambo moja. Vimeunganishwa kwa ajili ya msisitizo.

1 Kings 22:37

akaletwa Samaria

"wanajeshi wake wakauleta mwili Samaria"

wakamzika

"watu wakamzika"

kama vile neno la BWANA lilivyokuwa limesema

kama vile BWANA alivyonena

1 Kings 22:39

je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya waflme wa Israeli?

Tazama 15:31

akalala pamoja na mababu zake

Tazama 14:29

1 Kings 22:41

miaka thelethini na tano

"miaka 35"

miaka ishirini natano

"miaka 25"

1 Kings 22:43

Akatembea katika njia za Asa

"Alifanya vituvilevile ambavyo Asa, baba yake alifanya"

akafanya yaliyo mema mbele ya macho ya BWANA

BWANA aliyoyaona kuwa ni mema

Lakini mahali pa juu palikuwa hapajabomolewa

Bado alikwa hajapabomowa mahali pa juu

1 Kings 22:45

je, hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?

Tazama 14:29

1 Kings 22:48

zile merikebu zilivunjika

"merikebu zilivunjika"

akalala na mababu zake na akazikwa

Tazama 14:29

1 Kings 22:51

akatawala kwa miaka miwili

"akatawala kwa miaka 2"

akafanya yaliyo maovu mbele za BWANA

"yale ambayo BWANA aliyaona kuwa ni maovu"

akatembea katika njia za baba yake, katikanjia za mama yake, na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati

"Alifanya sawa na baba yake alivyofanya, mama naYeroboamu mwana wa Nebati alivyofanya"

aliifanya Israeli kufanya dhambi

Neno "Israeli" linmaanisha makabila kumi ya dola ya Israeli iliyokuwa kaskazini

Alimtumika Baali na kumwabudu

"Alimtumikia" na "kumwabudu" maneno hayo yanamaanishakitu kimoja.

Mungu wa Israeli

"Israeli" linamaanishaWaisraeli wote waliotokana na Yakobo.