Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Job 1

Job 1:1

nchi ya Usi

Inawezekana maeneo haya ni 1) eneo katika Edomu mashariki ya mto Yordani mahali fulani magharibi ya Yordani ya sasa au 2) eneo mashariki ya mto Frati katika Irani ya sasa.

haki na mkamilifu

Neno "haki" na "mkamilifu" yana maana sawa na yanaeleza kwamba Ayubu alikuwa muadilifu. "Alitenda yaliyo mema mbele za Mungu."

mmoja aliyemcha Mungu

"mmoja aliyemheshimu Mungu"

kuepukana na uovu

Hapa uovu unazungumziwa kama vile eneo ambalo mtu ataepuka kwenda huko, badala ya kufanya matendo maovu. "alikataa kufanya uovu"

watoto saba wakiume na mabinti watatu

"wakiume 7 na mabinti 3"

Alimiliki kondoo elfu saba

"Alikuwa na kondoo 7,000"

ngamia elfu tatu

"ngamia 3,000"

jozi mia tano za maksai

"jozi 500 za maksai"

mkuu

"tajiri"

watu wote wa Mashariki

Inahusu maeneo yaliyokuwa mashariki ya Kanaani. "watu wote wanaoishi katika nchi zilizokuwa mashariki ya Kanaani"

Job 1:4

Kwa siku yake kila mtoto wa kiume, hufanya

Neno "siku" labda linahusu siku ambayo walisherehekea kuzaliwa kwa mtoto wa kiume. Lakini angalau inahusu wazo la kila mtoto wa kiume kuchukua mwelekeo katika kufanya sherehe. "Katika sherehe ya siku ya kila mtoto wa kiume, mwana hutoa" au " Kila mtoto wa kiume kwa upande wake hutoa"

hufanya ... Wakatuma ... Ayubu hutuma ... kuwatakasa ... Aliamka asubuhi na mapema ... na kusema

"kwa desturi alitoa ... kwa desturi walituma ... Ayubu kwa desturi alituma ... kwa desturi aliwaweka wakfu ... Kwa desturi aliamka mapema ... kwa desturi alisema"

yeye huwatakasa

Hapa "weka wakfu" humaanisha kumsihi Mungu kuondoa ibada yoyote chafu ambayo watoto wa Ayubu huenda waliileta juu yao wenyewe wakati wakisherekea kwa furaha pamoja. Ayubu alifanya haya kwa kuwatolea sadaka kwa Mungu.

pamoja nao

Neno "wao" linahusu watoto saba wa kiume na mabinti watatu lakini halimjumuishi Ayubu.

Baada ya siku za karamu zilipokuwa zimetimia

"Wakati sherehe zilipomalizika" au "Baada ya sherehe"

Ayubu hutuma kwao

"Kwa desturi Ayubu alituma mtu kuwaita waje kwake mwenyewe"

kumkufuru Mungu mioyoni mwao

Mara nyingi mawazo hayo huja bila kukusudia, bila mtu kusubiri kuyafikiri. "kumkufuru Mungu mawazoni mwao"

Job 1:6

siku ambayo

Hii haikuwa siku maalumu. Kusanyiko lilifanyika mara kwa mara. "wakati ambapo" au "siku moja wakati"

watoto wa Mungu

Hii inamaanisha malaika, viumbe wa mbinguni.

kujihudhurisha mbele za BWANA

"kusimama pamoja mbele za BWANA kama alivyo waagiza kufanya"

Natoka kuzunguka zunguka duniani, kutembea huku na huko humo

Msemo "kuzunguka zunguka" na "kutembea huku na huko" inakusudia kazi moja ya kusisitiza ukamilifu wake. "Kutoka mahali popote duniani."

BWANA

Hili ni jina la Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la Kale. Tazama ukurasa wa tafsiri ya Neno Yahweh kuhusu namna ya kulitafsiri

kutembea huku na huko humo

"huku na huko" inahusian na kusafiri juu ya dunia yote.

Je umemwangalia mtumishi wangu Ayubu?

"Je umefikiri kuhusu mtumishi wangu Ayubu?" Hapa Mungu alianza kuzungumza na Shetani kuhusu Ayubu. "Angalia mtumishi wangu Ayubu"

mtu mwenye haki na mkamilifu

Neno "mwenye haki" na "mkamilifu" yana maana sawa na yanaeleza kwamba Ayubu alikuwa muadilifu. "Alitenda yaliyo mema mbele za Mungu."

mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu

"mmoja aliyemheshimu Mungu" na "alikataa kufanya uovu." Hapa uovu unazungumziwa kama vile eneo ambalo mtu ataepuka kwenda huko, badala ya kufanya matendo maovu

Job 1:9

Je Ayubu amcha Mungu bila sababu?

"Je Ayubu anamheshimu Mungu bila sababu?" Shetani akamjibu Mungu kwa kuwasilisha na kujibu maswali yake mwenyewe. Akasema kwamba Ayubu anamheshimu Mungu tu kwa sababu Mungu anambariki yeye. "Ayubu ana sababu ya kumtii Mungu."

Wewe hukumwekea kinga pande zote, kuzunguka nyumba yake, na kuzunguka vitu vyote alivyo navyo kutoka kila upande

Shetani anaeleza ukweli kuunga mkono hoja yake. "Wewe umemlinda yeye, familia yake na kila kitu anachomiliki."

kumwekea kinga pande zote, kuzunguka nyumba yake

kama kizuizi kama vile ukuta au uwa wa miti iliyooteshwa kuzunguka na kulinda ardhi ya mtu, Mungu amemzungushia Ayubu na ulinzi wake. "akamlinda yeye na nyumba yake"

kazi za mikono yake

"Kila kitu ambacho anafanya"

mifugo yake imeongezeka katika nchi

"ana mifugo zaidi na zaidi katika nchi"

Lakini sasa nyosha mkono wako na uguse yote hayo aliyonayo, na uone kama hatakufuru mbele ya uso wako.

Shetani anamaanisha kwamba kama Mungu atamshambulia Ayubu, ataona namna ambavyo Ayubu atajibu. "Lakini sasa, kama utanyosha mkono wako na uguse vyote alivyonavyo, utaona atakavyo kufuru mbele ya uso wako"

Lakini sasa nyosha mkono wako

Hapa "mkono" unahusiana na uwezo wa Mungu wa kutenda. "Lakini sasa zitumie nguvu zako"

uguse yote hayo aliyonayo

Hapa "gusa" linawakilisha tendo la kudhuru au kuangamiza. "shambulia vyote alivyonavyo" au "angamiza vyote alivyonavyo"

ya uso wako.

Hii inahusu muda ambao Mungu yuko makini. "katika uwezo wake wa kusikia"

Tazama

"Tazama" au "kuwa makini na yote ambayo na kwenda kukuambia"

hayo yote aliyonayo yamo mkononi mwako

Hapa "mkono" unawakilisha uwezo wa mtu kudhibiti kitu fulani. "una uwezo juu ya yote aliyonayo."

juu yake yeye mwenyewe

"dhidi ya mwili wake" "lakini usimdhuru kimwili" au "usiudhuru mwili wake"

akatoka mbele za BWANA.

"aliondoka kutoka kwa BWANA" au "Akamwacha BWANA"

Job 1:13

Waseba

Hili lilikuwa eneo lililopo katika Yemeni ya siku hizi. Hapa linawakilisha kundi la wavamizi au wanyang'anyi kutoka Sheba.

wakawaangukia

Hapa "kuangukia" inawakilisha wazo la shambulizi. "wakawashambulia"

wamewaua

Hapa kushangaza inawakilisha mauaji.

makali ya upanga

Hapa "mdomo" unawakilisha sehemu ya jambia ambayo huua watu, ambayo ni, labda ncha au ukingo mkali. Pia, majambia yote ya watu kutoka Seba yaliongea kama vile walikuwa na jambia moja tu.

Job 1:16

Wakati alipokuwa akiendelea kusema

"yeye" linarejea mjumbe wa kwanza

akatokea mwingine

"mjumbe mwingine pia alifika"

Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari.

Tafsiri kama katika 1: 13

Kwa wale watumishi, wamewaua kwa makali ya upanga. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari.

Tafsiri kama katika 1: 13

Job 1:18

Wana wako wa kiume na binti zako walikuwa wakila na kunywa mvinyo nyumbani mwa ndugu yao mkubwa

Tafsiri kama katika 1: 13

Upepo wenye nguvu

"kimbunga" au "dhoruba jangwani"

pembe nne za nyumba

"mihimili ya muundo wa nyumba"

Ikawaangukia vijana

"Nyumba ikawaangukia wana wako wa kiume na mabinti zako"

Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari.

Tafsiri kama katika 1: 13

Job 1:20

akalirarua joho lake, akanyoa kichwa chake

Haya yalikuwa matendo ya taratibu za ibada ya maombolezo, kuashiria huzuni kumbwa.

Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu ni uchi, nami nitakuwa uchi wakati nitakaporudi huko

"Wakati wa kuzaliwa kwangu, si kuleta kitu duniani, na wakati wa kifo changu nitarudi udongoni bila kitu."

Katika mambo hayo yote

"Kuhusu haya yote yaliyotokea"

hakumwazia Mungu kwa uovu.

"kusema kwamba Mungu alifanya makosa"

Job 2

Job 2:1

Habari za jumla:

Mistari hii ipo sawa na 1: 6 na inawezekana kutafsiriwa katika namna moja.

Kisha kulikuwa na siku

Tafsiri kama katika 1: 6

siku ambayo

Hii haikuwa siku maalumu. Kusanyiko lilifanyika mara kwa mara. "wakati ambapo" au "wakati wa siku moja"

wana wa Mungu

Tafasiri kama katika 1: 6.

kujihudhurisha mbele za BWANA

Tafasiri kama katika 1: 6.

Natoka kuzunguka zunguka duniani, kutembea huku na huko humo.

tafasiri kama katika 1: 6.

Job 2:3

Habari za Jumla:

Mistari hii ipo sawa na 1: 6, isipokuwa kwa ongezeko la "Yeye anashikamana na utimilifu wake, japokuwa ulinichochea dhidi yake, nimwangamize pasipo sababu."

Je umemwangalia mtumishi wangu Ayubu?

Hili swali la kejeli kwa kweli inatengeneza maelezo. Tafasiri kama katika 1: 6. "Angalia mtumishi wangu Ayubu."

mtu mwenye haki na mkamilifu

Neno "haki" na "mkamilifu" yana maana sawa na yanaeleza kwamba Ayubu alikuwa muadilifu. "Alitenda yaliyo mema mbele za Mungu."

mmoja aliye mcha Mungu na kuepukana na uovu.

Hapa uovu unazungumziwa kama vile eneo ambalo mtu ataepuka kwenda huko, badala ya kufanya matendo maovu. "alikataa kufanya uovu" (Tafasiri kama katika 1: 1)

Hata sasa anashikamana na utimilifu wake

"amesalia amejitoa kikamilifu kufanya yale yaliyo ya haki na kweli"

ulinichochea juu yake

"ulinishawishi bila sababu nimshambulie"

nimwangamize

Hapa "angamiza" linawakilisha "kumfanya awe maskini." "kumfanya yeye awe mtu maskini"

Job 2:4

Ngozi kwa ngozi, hasa

"Ngozi" ni mfano wa maisha ya Ayubu. "Mtu atafanya chochote kuokoa maisha yake, hata kukubali kupoteza mali zake na wapendwa."

Lakini nyosha mkono wako sasa na uguse mifupa yake na nyama yake, na uone kama hatakufuru mbele ya uso wako.

Shetani anamaanisha kwamba kama Mungu atamshambulia Ayubu, yeye ataona namna Ayubu atakavyojibu. "Lakini sasa, kama utanyosha mkono wako na uguse mifupa yake na nyama yake, utaona utakavyokufuru mbele ya uso wako"

nyosha mkono wako

Hapa "mkono" unahusu uwezo wa Mungu kutenda. "Lakini sasa tumia nguvu zako." Tafsiri kama katika 1: 9.

gusa

Hapa "gusa" huwakilisha kitendo cha kudhuru. "shambulio"

mifupa yake na nyama yake

Maelezo haya yanawakilisha mwili wa Ayubu.

kufuru mbele ya uso wako

Tafasiri kama katika 1: 9.

uso wako

Hii inahusiana na wakati ambao Mungu yupo makini. "katika uwezo wako wa kusikia"

Job 2:7

Kisha Shetani akatoka mbele ya uso wa BWANA.

Tafasiri kama katika 1: 9.

akampiga

"kushambuliwa" au "athiriwa na"

majipu mabaya

makubwa, yanayowasha na maambukizi machungu ya ngozi

kipande cha kigae kujikunia

kusugua mikwaruzo ya ngozi ili kupunguza mwasho.

akaketi chini majivuni.

Hii yawezekana inahusiana na eneo ambalo takataka hutupwa na pengine huchomwa. kukaa katika eneo kama hilo ilikuwa alama ya maombolezo mazito. "kukaa kwenye rundo la takataka"

Job 2:9

Je hata sasa wewe unashikamana na utimilifu wako?

Hili swali la kejeli kwa kweli linatengeneza taarifa. Tafasiri kama katika 1: 6. "Angalia mtumishi wangu Ayubu."

Umkufuru Mungu

"Kumkataa Mungu"

unaongea kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu

Ayubu akasema unaongea kama mwanamke mpumbavu. "Unaongea kana kwamba wewe ni mwanamke mpumbavu."

Je sisi tupate mema toka kwa Mungu na tusipate mabaya?

Swali hili la kejeli kwa kweli linawasilisha taarifa. "Bila shaka lazima tungelipata mabaya kutoka kwa Mungu pamoja na mazuri."

tupate mema

"kunufaika na mambo yote mazuri"

mema

Hili linawakilisha mambo yote mazuri ambayo Mungu hutupa.

tupate mabaya

"teseka na mateso yote mabaya bila kulalamika"

mabaya

Hili linawakilisha mambo yote mabaya ambayo Mungu hufanya au huruhusu ili sisi tupate maarifa.

tenda dhambi kwa midomo yake.

Hapa "midomo" inawakilisha tendo la kuongea. "dhambi kusema kwa kushindana na Mungu"

Job 2:11

Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi

Elifazi, Bildadi, na Sofari ni majina ya wanaume. Temani ulikuwa mji katika Edomu. Washuhi ni uzao wa Ibrahimu na Ketura (tazama Mwanzo 25: 1). Naamathi ulikuwa mji katika Kanaani.

Wakatenga muda

"walikubaliana juu ya wakati"

kuomboleza naye na kumfariji.

Hapa neno "omboleza" na "fariji" yana maana sawa. Rafikize wanajaribu kumfariji Ayubu na kuomboleza naye. "kuhuzunika na Ayubu ili kusaidia kupoza mateso yake."

Job 2:12

Walipoinua macho yao

"walikaza macho" au "walitazama kwa makini"

hawakuweza kumtambua

Hii yawezekana inamaanisha kwamba wageni wa Ayubu hawakuweza kumtambua kwanza, wakati walipo muona kwa mbali. Ayubu alionekana tofauti kuliko kawaida kwa sababu ya huzuni yake na kwa sababu ya kuwashwa mwili mzima. "kwa shida walimtambua"

Wakapaza sauti zao na kulia

"wakalia kwa sauti kubwa " au "wakalia sana"

akararua joho lake

Hii ilikuwa ishara ya maombolezo.

kurusha majivu hewani na juu ya kichwa chake

Hizi zilikuwa ishara za maombolezo.

Job 3

Job 3:1

akafunua kinywa chake

"alianza kusema"

Na ipotelee mbali siku niliyozaliwa mimi, usiku

Ayubu anaongea juu ya siku na usiku kana kwamba walikuwa watu. "Na tamani kwamba nisingekuwa nimezaliwa."

usiku uliosema, 'Mimba ya mtoto wa kiume imetungwa.'

kujieleza huku kunazidi maelezo ya huzuni ya Ayubu kwa kwenda wakati wa nyuma zaidi kutoka kuzaliwa kwake hadi kutungwa mimba yake. "usiku ambao ulisema, "Mtoto wa kiume amechukuliwa mimba' potevu."

usiku uliosema

Hapa usiku umeongelewa kana kwamba walikuwa watu ambao wanaweza kuongea. ... "usiku ule ambao watu walisema."

Mimba ya mtoto wa kiume imetungwa.'

Hii inaweza kuwekwa katika muundo hai. " mama yake amechukuwa mimba ya mtoto wa kiume."

Job 3:4

Habari za Jumla:

Semi zote katika mistari hii ni matamanio kwamba siku ya kuzaliwa kwake Ayubu isingekuwako tena. Hii inaweza husika na siku, japokuwa katika wakati uliopita, hata kuwepo kwa namna fulani. ... "Natamani kwamba siku nilipozaliwa ingelikuwa giza."

Siku hiyo na iwe giza ... wala mwanga usiiangazie

Vifungu hivi viwili vinaelezea giza la siku ya kuzaliwa kwake Ayubu, hivyo kurudia majuto ya Ayubu ya kuwa alikuwa amezaliwa.

Siku hiyo na iwe giza

Hili ni tamanio la kutokuwepo tena siku hiyo. "ikiwezekana siku hiyo itoweke."

Ishikwe na giza na kivuli la mauti liwe lake

Hapa giza na kivuli cha mauti vinazungumziwa kana kwamba ni watu ambao wanaweza kudai chochote kuwa ni mali yao. Neno "hii" inahusiana na siku ya kuzaliwa kwa Ayubu.

kivuli cha mauti

Hapa kivuli kinawakilisha mauti yenyewe. "kifo kama kivuli"

Wingu na likae juu yake

Hapa wingu linazungumziwa kana kwamba ni mtu ambaye anaweza kuishi juu ya siku ya kuzaliwa kwake Ayubu. "Ikiwezekana wingu liifunike hivyo hakuna mtu anayeweza kuiona"

kila kitu kiifanyacho siku kuwa giza

Hii inamaanisha vitu vizuiavyo nje mwanga wa jua na kutengeneza giza. Hapa "nyeusi" inawakilisha giza.

kiitishe

"itishe siku hiyo." Siku inazungumziwa kana kwamba ni mtu ambaye anaweza kutishwa na giza.

Job 3:6

na ukamatwe na giza tororo

Giza hili tena linazungumziwa kana kwamba ni mtu ambaye anaweza kuushika na kuuzuia usiku. "ikiwezekana giza nene kulifanya litoweke"

giza tororo

"giza sana" au "giza kabisa"

shangwe isiwe ndani yake.

Neno "hii" linahusiana na usiku wa kuzaliwa kwake Ayubu au mimba yake. Usiku wa mimba ya Ayubu unazungumziwa kana kwamba mtu ambaye hata kuwa na furaha. "Ikiwezekana usiku huo utoweke kwenye kalenda."

usiwekwe katika hesabu

Usiku huo unazungumziwa kana kwamba mtu ambaye anaweza kutembea. "ikiwezekana asiwepo mtu wa kuuweka katika hesabu"

usiku huo na uwe tasa

Usiku wa kuzaliwa kwake Ayubu unazungumziwa kana kwamba ni mwanamke. "ikiwezekana asizaliwe mtoto katika usiku huo"

sauti ya shangwe isiwe ndani yake.

Hapa usiku wa kuzaliwa kwake Ayubu unazungumziwa kana kwamba ni muda ambao ulikuwa bado unawezekana kwa mtu kuwa na furaha. "ikiwezekana asiwepo mtu wa kusikia kilio cha furaha wakati wa kuzaliwa mwana"

sauti ya shangwe kuja

Hapa sauti inasimama kwaajili ya mtu mwenye furaha. "Ikiwezekana asiwepo mtu wa kuwa na furaha katika hili milele"

Job 3:8

hao wafahamuo namna ya kumuamsha lewiathan

Hapa huenda Ayubu anamaanisha wachawi na waganga, ambao yeye anawaamini wanaweza kuwa na uwezo wa kumchochea Lewiathani katika kueneza machafuko. Lewiathani alikuwa mnyama bora aliyejulikana wakati wa Kale Karibu Mashariki ya mithiolojia, ambaye alifikiri kuwa dhamana kwa aina zote za uharibifu, maradhi, na machafuko.

Nyota za mapambazuko yake zitiwe giza

Hii inahusiana na sayari ambayo mara kwa mara huonekana sawasawa kabla ya mapambazuko. "Inawezekana nyota ambazo huonekana kabla ya siku hiyo kwanza mwanga uwe giza"

Siku hiyo iutafute mwanga, lakini isiupate

Siku ya kuzaliwa kwake Ayubu inazungumziwa kana kwamba ni mtu anayetazama kitu. "Inawezekana siku hiyo ilitarajia mwanga, lakini haikuupata."

wala makope ya mapambazuko isiyaone

Mapambazuko yanazungumziwa kana kwamba yana kope kama alizonazo mtu. "wala kuona mwanga wa kwanza wa mapambazuko."

kwasababu haikuifunga milango ya tumbo la mama yangu

Tumbo la uzazi la mwanamke linazungumziwa kana kwamba ni chombo chenye milango. "kwasababu siku hiyo haikulifunga tumbo la uzazi la mama yangu"

kwasababu haikunifichia taabu machoni pangu.

Siku ya kuzaliwa kwake Ayubu inazungumziwa kana kwamba ni ni mtu ambaye anaweza kuficha kitu.

machoni pangu.

Hapa "macho" yanawakilisha mtu ambaye anaonana nao. "kutoka kwangu"

Job 3:11

Habari za Jumla:

Kifungu hiki kina maswali manne ya kejeli, ambayo Ayubu anauliza ili kufanya mfululizo wa kweli wa maelezo.

Kwanini si-kufa wakati lipotokeza katika tumbo la uzazi?

"kwa nini sikufa wakati wa kuzaliwa?" Ayubu anauliza swali hili ili kulaani siku ya kuzaliwa kwake na kueleza majuto yake. "Natamani ningelikufa siku nilipozaliwa"

Kwanini sikuitoa roho yangu hapo mama aliponizaa?

Ayubu anamaanisha kusema kwamba yeye asingelizaliwa hai. "Natamani ningelikufa wakati nilipotoka nje ya tumbo la uzazi."

kuitoa roho yangu

Hii inahusiana na kifo.

kwanini magoti yake yalinipokea?

Labda hii inahusiana na paja la mama yake Ayubu. Magoti ya mama yake yamezungumziwa kana kwamba ni watu ambao wanaweza kumkaribisha mtoto mchanga. "Natamani kusingelikuwa na paja la kunipokea mimi."

Kwanini maziwa yake yanipokee hata ninyonye?

Maziwa ya mama yake Ayubu yanazungumziwa kana kwamba ni watu ambao wanaweza kumkaribisha mtoto mchanga. "Natamani kusingelikuwa na maziwa kwaajili ya kuninyoshesha."

Job 3:13

Kwa sasa ningelikuwa nimelala chini kimyakimya. Ningelala usingizi na kupata pumziko

Ayubu anatumia sentensi mbili kufikiri kuhusu ingelikuwaje kama yeye asingelizaliwa au angelikufa wakati wa kuzaliwa.

ningelikuwa nimelala chini kimya kimya

Ayubu anafikiria kitu ambacho kingeliweza kutokea katika siku za nyuma lakini hakikutokea, kama ilivyoelezwa hapo juu. "Ningelikuwa nimelala chini kimyakimya"

nimelala chini kimya

"lala, kupumzika kwa amani"

na kupata pumziko

Neno "pumziko" hapa linamaanisha kulala kwa amani, lakini pia huyo Ayubu asingelikuwa anapitia maumivu ambayo anayapata

pamoja na wafalme na washauri wa dunia,

"na wafalme na washauri wao"

Job 3:15

Habari za Jumla:

Ayubu anaendelea na fikira zake kuhusu kufa kabla ya kuzaliwa.

Au Ningelikuwa nimelala pamoja ... wasio uona mwanga kabisa.

Hii inaelezea kitu ambacho kingetokea lakini hakikuweza kutokea.

Au Ningelikuwa nimelala pamoja na wakuu

"Ningelikuwa nimepumzika na wakuu." Katika kifungu hiki, neno "lala" na "kupumzika" ni njia ya heshima kusema "haishi tena."

wenye dhahabu, waliozijaza nyumba zao fedha

Ayubu anatumia ulinganishaji kusisitiza kile anachosema.

Au pengine ningekuwa sijazaliwa, kama watoto wachanga wasio uona mwanga kabisa.

Ayubu anatumia ulinganishaji kusisitiza anachosema.

ningekuwa sijazaliwa

"Ningelikuwa nimekufa tumboni mwa mama yangu"

kama watoto wachanga wasio uona mwanga kabisa

"kama watoto wachanga ambao hawangelizaliwa"

watoto wachanga

"watoto" au "watoto wadogo sana"

Job 3:17

Habari za Jumla:

Ayubu anabadilisha mazungumzo yake kutoka kufa mpaka uzima baada ya kifo.

Huko waovu huacha kusumbua; huko waliochoka hupumzika.

Ayubu anatumia usambamba kusisitiza kuwa wanyonge watapata pumziko kutoka kwa wale walio wasababishia magumu.

Huko waovu huacha kusumbua

Ayubu anaongea kuhusu sehemu ambayo watu huenda baada ya wao kuacha kuishi. "Katika sehemu hiyo, watu waovu huacha kusumbua"

sauti ya msimamizi wa watumwa

Hapa "sauti" ni mfano wa nguvu ambayo msimamizi wa watumwa anakuwa nayo juu ya watumwa. "Hawako tena chini ya udhibiti wa watumwa"

wadogo na watu maarufu

Hii ni tamathali ya usemi ambayo humaanisha "watu wote, watu masikini na watu matajiri."

mtumishi yuko huru kwa bwana wake huko.

Mtumishi hana wajibu wa kumtumikia bwana wake.

Job 3:20

Kwa nini yeye aliye mashakani kupewa mwanga? Kwa nini hao wenye uchungu moyoni kupewa uhai

Maswali mawili ya Ayubu kimsingi humaanisha kitu kimoja. Yeye anashangaa kwanini hao ambao hukabili magumu huendelea kuishi.

Kwa nini yeye aliye mashakani kupewa mwanga?

Hapa Ayubu anashangaa kwanini lazima watu wabaki hai na kuteseka. "Mimi sielewi kwa nini Mungu hutoa uhai kwa mtu ambaye anateseka"

mwanga

Hapa mwanga unawakilisha uhai

Kwa nini hao wenye uchungu moyoni kupewa uhai ... hazina iliyofichika?

"je kwa nini Mungu hutoa uhai kwa mtu mwenye taabu? "Mimi sielewi kwa nini Mungu anatoa uhai kwa mtu mwenye huzuni sana ... hazina iliyofichika"

ambao hutamani mauti lakini hawapati

Hapa kifo kinazungumziwa kana kwamba kuna kitu kinakuja kikimwelekea mtu fulani. "kwa mtu ambaye haitaji tena kuwa hai, lakini bado yu-hai"

ambao huyachimbulia mauti zaidi ya kutafuta hazina iliyofichika

Mtu anayetumainia kufa anazumgumziwa hapa kana kwamba anachimbua hazina iliyozikwa. "kwa mtu ambaye anahitaji kufa zaidi ya yeye kutafuta hazina iliyofichika"

Kwa nini kupewa mwanga ambao hushangilia mno na kufurahi walionapo kaburi

Hapa Ayubu anatumia swali kufanya kauli. "Mimi sielewi kwa nini Mungu anaruhusu mtu kuendelea kuishi wakati mtu huyo angefurahi kuzikwa katika udongo"

ambao hushangilia mno na kufurahi

Msemo wa "hufurahia sana" kimsingi unamaanisha kitu kimoja kama "furaha." Pamoja, misemo yote miwili inatilia mkazo wa nguvu ya furaha. "mtu ambaye ana furaha sana"

alionapo kaburi

Hii ni njia ya heshima ya kumaanisha kufa. "wakati yeye akifa na anaweza kuzikwa"

kaburi

Hapa kaburi linawakilisha kifo.

Job 3:23

Kwanini kupewa mwanga mtu ambaye njia zake zimefichika, mtu ambaye Mungu amemzungushia uwa?

Ayubu anauliza hili swali ili kutengeneza habari. "Mungu hatoi uhai kwa mtu na kisha kuzichukua mbali siku zake za baadaye na kumwekea mpaka yeye."

Kwanini kupewa mwanga mtu

Hapa mwanga unawakilisha uhai. "Je kwa nini Mungu humweka mtu hai"

ambaye njia zake zimefichika

Hapa Ayubu anaongelea siku zake za baadaye, ambazo yeye hazijui mapema, kana kwamba Mungu alikuwa amezificha kutoka kwake.

mtu ambaye Mungu amemzungushia uwa

Hapa kuwa katika matatizo na hatari yanasemwa kana kwamba walikuwa wamefungwa ndani ya mipaka finyu.

kushusha kwangu pumzi kwatokea badala ya kula; kuugua kwangu kumemiminika kama maji

Ayubu anaelezea maumivu yake makubwa katika njia mbili.

kushusha kwangu pumzi kwatokea badala ya kula

"Badala ya kula, mimi naomboleza"

kuugua kwangu kumemiminika kama maji.

ubora wa maadili na hisia kama vile huzuni mara kwa mara huongelewa kana kwamba yalikuwa maji.

Job 3:25

jambo lile niliogopalo limenipata; nalo linitialo hofu limenijilia

misemo hii miwili ina maana moja. "kile nikiogopacho sana kimenitokea mimi" au "liniogopeshalo vibaya sana limenijilia kweli.

Mimi sioni raha, sipati utulivu, na sipati pumziko;

Ayubu anaelezea maumivu yake katika misemo mitatu inayotenganishwa. "Nina mashaka sana" au "mimi nimeteseka kihisia na kimwili

badala yake huja taabu

Taabu imezungumziwa kana kwamba lilikuwa jambo ambalo lingeweza kumwijia Ayubu. "badala yake msiba unanitesa mimi"

Job 4

Job 4:1

Elifazi

Elifazi ni jina kiume.

Mtemani

Mtemani ni mtu wa kabila la Temani.

je utakosa ustahimilivu?

Elifazi anauliza swali hili ili kutengeneza maelezo. "wewe kweli utakosa uvumilivu."

je utakosa ustahimilivu?

"Hicho kitakukera wewe?"

ni nani anaweza kujizuia asizungumze?

Elifazi anauliza swali hili kusema kwamba hakuna mtu ambaye amuonaye rafiki yake anateseka akakaa kimya. "Hakuna mtu awezaye kujizuia mwenyewe kuongea (kwa rafiki yake katika hali hiyo kama uliyonayo wewe mwenyewe)" au "Mimi lazima nizungumze na wewe, (kwa kukuona kuwa upo katika hali ya majonzi)."

Tazama, wewe umewafunza wengi; wewe imeipa nguvu mikono iliyokuwa dhaifu.

Mstari huu unaeleza wazo moja katika njia mbili tofauti.

umeipa nguvu mikono iliyo dhaifu.

Hapa "mikono dhaifu" inawakilisha watu ambao wanahitaji msaada. "wewe uliwasaidia wengine wakati walipohitaji msaada"

Job 4:4

Habari za Jumla:

Mwandishi anatumia ulinganishaji katika kila mistari hii kutengeneza wazo moja akitumia habari mbili tofauti kusisitiza 1) kuunga mkono kwamba Ayubu aliwasaidia wengine siku zilizopita, 2) madhara juu yake kwa taabu zake za sasa, na 3) unyenyekevu wake mbele za Mungu.

yamemsaidia

mtu fulani ambaye alishawahi kutiwa moyo anazungumziwa kana kwamba yeye alishikwa asianguke chini.

umeyaimarisha magoti dhaifu

Hapa kukatisha tamaa kunazungumziwa kana kwamba ni mtu ambaye magoti dhaifu hayawezi kumweka yeye wima.

Lakini sasa matatizo yamekuja kwako

Hapa matatizo yanazumziwa kana kwamba ni jambo ambalo linaweza kumfika mtu. "Lakini sasa wewe unateseka na masaibu"

wewe umechoka

"umekata tamaa"

hofu yako

"ni kweli kwamba una mweshimu Mungu"

Je si hofu yako imani yako, na ukamilifu wa njia zako tumaini lako?

Elifazi anauliza maswali haya ili kutengeneza usemi kwa Ayubu kwamba dhambi zake zimemsababishia yeye kuteseka. "Kila mmoja anafikiri kwamba unamheshimu Mungu; kila mmoja anafikiri kwamba wewe ni mtu mwaminifu. Lakini mambo haya lazima hayawezi kuwa kweli, kwa sababu wewe humwamini Mungu tena."

hofu yako

Elifazi anamaanisha hofu ya Ayubu kwa Mungu. "hofu yako kwa Mungu"

njia zako

Hapa "njia zako" inawakilisha "mwenendo wako," "namna unavyoenenda."

Job 4:7

ni nani aliyeangamia akiwa hana kosa?

Elifazi anatumia swali hili kumshawishi Ayubu kuchunguza dhambi katika maisha yake (na hukumu takatifu ya Mungu) kama kisababishi cha yeye kupotea. "Hapa mmoja aliyeangamizwa wakati hana kosa."

ni lini watu wakamilifu walikatiliwa mbali

Swali hili pia linamaanisha kutengeneza maelezo, na yanaweza kuwekwa katika umbo la kufaa. "Hakuna hata mmoja aliyewahi kumkatilia mbali mtu mkamilifu."

katiliwa mbali

Hapa kukatiliwa mbali inamaanisha kuangamizwa.

walimao uovu ... kupanda taabu ... huvuna

Hapa matendo ya kulima na kupanda yanawakilisha kinacho sababisha taabu kwa watu wengine. Tendo la kuvuna ni mfano wa mateso ya taabu ambazo mtu huzisababisha mwenyewe.

Kwa pumzi ya Mungu huangamia; kwa mlipuko wa hasira zake huteketea

Mwandishi anaeleza wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti. Huu ni muundo wa ushairi wa kiebrania utumikao kwa kusisitiza, udhahiri, mafundisho, au yote matatu.

pumzi ya Mungu

Hii inaweza kuwa mfano wa tendo la Mungu la kutoa amri.

mlipuko wa hasira

Usemi huu unaashiria upumuaji mkubwa ambao mtu wakati fulani huufanya kupitia pua zake wakati akiwa na hasira.

pumzi ... mlipuko

msemo wa pili umejengwa juu ya wa kwanza. Zinaunda wazo moja kwa kutumia maana ambazo zinaongeza matokeo. "Kwa mpumuo wa mdomo wa Mungu wanafariki; mwendo kasi wa upepo wa hasira zake huwateketeza wao."

huangamia ... huteketea.

Fungu la pili limejengwa juu ya la pili. Yanaunda wazo moja. "Kwa mpumuo wa mdomo wa Mungu wanafariki; mwendo kasi wa upepo wa hasira zake huwateketeza wao."

huteketea.

Hapa kuteketezwa au kuliwa ni mfano wa kuuliwa.

Job 4:10

Habari za Jumla:

Mwandishi anatumia ulinganishaji katika mistari hii, anawasilisha wazo moja akitumia maelezo tofauti kutilia mkazo uharibifu wa Mungu kwa watu waovu.

Kuunguruma kwa simba, sauti ya simba mkali, meno ya simba wadogo - yamevunjika.

Hapa muungurumo wa simba, sauti yake, na meno yake yamevunjika vinatumika kama mfano wa kuangamizwa kwa waovu.

yamevunjika

Hii inaweza kuwekwa katika umbo halisi. "kitu fulani kimeyavunja"

Simba mzee huangamia kwa kukosa wahanga; watoto wa simba jike wametawanyiko kila mahali

Elifazi anatumia picha ya simba mzee anayekufa kwa njaa na familia yake imetawanyika kama sitiari ya kuangamizwa kwa waovu

wametawanyika

"kitu fulani kimetawanya watoto wa simba"

Job 4:12

Sasa nililetewa kwangu jambo fulani kisiri ... sikio langu likapokea uvumi kuhusu hilo

vifungu hivi vinaelezea wazo sawa katika njia tofauti. Vinawasilisha wazo kuwa Elifazi amesikia ujumbe uvumao kwake. Urudiaji huu ni muundo wa ushairi wa kiebrania umetumika mara kwa mara kwa kusisitiza, kufundisha, au udhahiri.

nililetewa kwangu jambo fulani kisiri

"kitu fulani kimeleta kwangu jambo fulani kwa siri"

maono wakati wa usiku

"ndoto"

wakati uwaangukiwapo usingizi mzito watu

"wakati watu wakisinzia sana"

Job 4:14

Habari za Jumla:

Mwandishi anatumia ulinganishaji katika mistari hii, kuwasilisha wazo moja akitumia maelezo tofauti kusisitiza hofu ya Elifazi.

nilipopatwa hofu na kutetemeka

Hapa hofu na kutetemeka yanazungumziwa kana kwamba ni mambo ambayo yanaweza kumwijilia mtu. "Mimi nikanza kuogopa na kutetemeka."

nywele zangu za mwili zilisimama

Hii inaonyesha hofu kubwa.

nywele za mwili wangu

"Nywele juu ya mwili wangu"

Job 4:16

Habari za Jumla:

Mwandishi anatumia ulinganishaji katika mstari wa 17, kuwasilisha wazo moja akitumia maelezo mawili tofauti kutilia mkazo swali kuhusu utakatifu wa mwanadamu mbele za Mungu.

Umbo lilikuwa mbele ya macho yangu

"Kitu fulani kilikuwa mbele ya macho yangu," "nimeona kitu fulani"

nami nikasikia

"Kisha nikasikia"

Je binadamu mwenye kufa anaweza kuwa mwenye haki zaidi kuliko Mungu?

Elifazi anatoa swali hili ili kwamba Ayubu akumbuke, "Naweza kujiangalia mimi mwenyewe kama mwenye haki zaidi ya Mungu?" au "Je nimethibitika mbele za Mungu?" "Binadamu mwenye kufa hawezi kuwa mwenye haki zaidi ya Mungu" au "Binadamu mwenye kufa hawezi kuwa mwenye haki mbele za Mungu."

Je mtu anaweza kuwa msafi zaidi kuliko Muumba wake?

Swali hili lina lengo sawa kama swali lililotangulia. "Binadamu hawezi kuwa msafi zaidi kuliko Muumba wake."

Muumba

"Mfanyaji"

Job 4:18

wale waishio katika nyumba za udongo, ambao misingi yao ipo katika vumbi

Huu ni utumiaji wa lugha ya picha kumwelezea mtu, ambaye aliumbwa kutokana na vumbi la udongo na ambao miili yao iko kama nyumba, ambazo zimejengwa kwa udongo na kuwa na misingi mibovu.

hupondwa mapema kuliko nondo

Kirai "mapema zaidi" kwa kawaida inatafasiriwa kama "kabla." "hupondwa kabla ya nondo" au " hupondwa sawa na nondo"

wameangamizwa

"kitu fulani kinawaangamiza wao"

wameangamizwa

"wameuawa"

Job 4:20

Habari za Jumla:

Mistari hii inaendeleza matumizi ya awali ya ulinganishaji, hapa inasisitiza katika njia tofauti wazo kwamba watu hufa ghafla pasipo kupata hekima na wala usumbufu kutoka kwa wengine.

Kati ya asubuhi na jioni wameangamizwa

Hii inamaanisha wazo la kitu fulani kinachotokea upesi.

wameangamizwa

Hii pia inaweza kuwekwa katika umbo hai. "wamekufa"

Je kamba za hema yao hazikung'olewa kati yao?

Hii inaweza kuwekwa katika umbo hai. "Si adui zao waliong'oa kamba za hema zao kutoka miongoni mwao?"

kamba za hema yao

Hapa kamba za hema zinawakilisha hema. Wakati mwingine nyumba ya mtu na familia zinafananishwa kama hema yake, ambayo inaweza pia kuwakilisha mali zake zote.

Job 5

Job 5:1

Utamrudia yupi katika watakatifu hao?

Elifazi anatoa swali hili kutengeneza hoja kuwa hakuna hata mmoja Ayubu anaweza kumgeukia kwa ajili ya msaada. "Je kuna mtakatifu yeyote ambaye unaweza kumgeukia?" au "Hakuna mtakatifu yeyote ambaye unaweza kumgeukia kwa ajili ya msaada."

watakatifu

Hii imaanisha viumbe bora kwa asili katika baadhi ya tabia, kama malaika au roho zingine

mjinga ... mtu mpumbavu

Hii inahusiana na mtu yeyote mjinga na mtu yeyote mpuuzi.

wivu huua mjinga

"wivu huua yeyote ambaye anatenda kijinga na maamuzi ya ghafla"

mtu mpumbavu akishika mzizi

Hapa mtu anazungumziwa kana kwamba ni mmea, huenda anakuwa mpuuzi zaidi kadri muda unavyosogea. "mtu mpuuzi anakuwa amejengwa katika ujinga zaidi"

makazi yake

Hii inahusiana na familia ya mtu na mali zake zote.

Job 5:4

Habari za Jumla:

Mistari hii inaendeleza matumizi ya awali ya ulinganishaji, hapa inatilia mkazo katika njia tofauti wazo kwamba watoto wa watu wajinga hawapo salama.

Watoto wake wako mbali na uzima

"yake" inahusiana na mtu mjinga au watu wajinga katika 5:1. "Watoto wao si salama milele"

wameangamia

Hapa kuangamizwa ni mfano wa kuonewa, kutumiwa vibaya, katika mahakama. Wazo hili linaweza kuwekwa katika umbo hai. "mtu fulani amewaangamiza"

lango la mji.

Lango la mji, linafanya kazi kama mahakama, ilikuwa sehemu ambayo ugomvi uliamuliwa na hukumu kutolewa.

Hakuna yeyote atakaye waponya.

"Hakuna yeyote wakuwaokoa watoto wa watu wapuuzi kutoka kwenye dhiki zao"

hata huyachukua katikati ya miiba

Inawezekana huu ni mfano wa kipande cha shamba ambapo mazao mabaya sana humea, kwasababu ya uwepo wa mimea yenye miba.

Wenye kiu huzitaka sana mali zao

Hapa watu waroho wanaongelewa kana kwamba wanakiu, na utajiri wa mtu mpumbavu unazungumziwa kana kwamba ni kitu fulani ambacho wanaweza kunywa.

Job 5:6

Kwa kuwa magumu hayatoki udongoni; wala taabu haichipuki katika nchi

Hapa magumu na taabu yanazungumziwa kana kwamba ni mimea.

wanadamu huzaliwa kwaajili ya taabu, kama cheche za moto zirukavyo juu.

Ni kama asili ya watu, mara tu wazaliwapo, kuwa na taabu kama ilivyo kwa cheche za moto zirukavyo juu.

Job 5:8

Habari za Jumla:

Katika mistari hii, Elifazi anaendeleza hotuba toka 4: 1. Mwandishi anaenedelea kutumia ulinganishaji katika kila mstari, kuwasilisha wazo moja akitumia maelezo mawili tofauti kusisitiza kwamba Ayubu lazima akiri hali yake kwa Mungu ambaye hutenda mambo ya kustajabisha.

makuu na mambo yasiyochunguzika, mambo ya ajabu yasiyo na hesabu

"Mambo makuu ambayo hayawezi fahamika, maajabu ambayo hayahesabiki"

mambo yasiyochunguzika

Hii inamaanisha mambo ambayo wanadamu hawezi kuyaelewa.

makuu na mambo yasiyochunguzika

Hapa mwandishi anatumia maneno mawili yanayojitegemea na kuunganishwa kwa "na" kusisitiza ukuu wa matendo ya Mungu. "mambo makuu sana yenye kuhitaji maarifa mengi"

mambo ya ajabu

"mambo ya kustajabisha" au "maajabu"

Job 5:11

Habari za Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika kila mstari, kuwasilisha wazo moja akitumia maelezo mawili tofauti kusisitiza namna Mungu anavyo wainua wale ambao ni wanyonge na kuwashusha wale ambao ni werevu.

Hufanya haya kwaajili ya kuwainua juu hao walio chini

Watu wanyenyekevu wakati wa dhiki wanazungumziwa kana kwamba wako katika nafasi ya chini. Wakati Mungu akiwaokoa, wanapokea heshima. wakati hili likitendeka, wanazungumziwa kuwa kama wamepandishwa juu na kuweka katika nafasi ya juu. "Mungu hufanya hili ili kuwaokoa na kuwaheshimu wanyenyekevu ambao wamekuwa wakitaabika"

Yeye huharibu mipango

Hapa kuzuia mipango ya watu mwenye hila inazungumziwa kana kwamba ni vitu ambavyo vinaweza kuharibika kihalisia.

Yeye huwanasa watu wenye hekima katika matendo ya hila zao wenyewe

Hapa kuwafanya watu wenye hekima wataabike kwasababu ya matendo yao maovu inazungumziwa kana kwamba wamekamatwa katika mitego. Matendo yao wenyewe yanazungumziwa kana kwamba ni ile mitego.

watu waliogeuzwa

Hapa kuwa muovu kwa njia ya akili inazungumziwa kana kwamba umegeuzwa. "wale ambao ni werevu" au "wale ambao ni wajanja" au "wale ambao makini"

Job 5:14

Habari za Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika kila mstari, kuwasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kusisitiza namna Mungu anavyowashusha wale ambao ni werevu na kuwaokoa wale ambao ni masikini.

hupatwa na giza wakati wa mchana

Hapa mwerevu, watu waovu ambao Mungu amewachanganya wanazungumziwa kana kwamba bila matarajio wakawa gizani wakati wa adhuhuri, wakati jua likiwa sehemu ya katikati ya anga. Hawawezi kufanya chochote wanachotamani kufanya, kwasababu hawawezi kuona. "Wale ambao ni werevu wako gizani, hata wakati wa muda wa adhuhuri"

kupapasa

papasa kwa mikono pande zote kama mtu kipofu

wakati wa mchana

"saa sita mchana"

Lakini yeye huokoa maskini kwa upanga wa vinywa vyao

Hapa mambo ya matusi na vitisho ambayo watu husema yanazungumziwa kana kwamba ni upanga vinywani vyao. "Lakini humwokoa mtu masikini kutokana na vitisho vya mwenye uwezo" au "Lakini yeye humwokoa mtu masikini wakati mwenye uwezo anapowatisha au kuwatukana wao"

udhalimu hufumba kinywa chake mwenyewe.

Watu ambao husema mambo yasiyo haki wanazungumziwa kana kwamba wao ni wadhalimu, ambao lazima waache kuongea. "Hata hivyo ni kama mdhalimu afunge mdomo wake."

Job 5:17

Habari za Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika mstari wa 18 na 19, kuwasilisha wazo moja akitumia maelezo mawili tofauti kusisitiza matendo ya Mungu ya kuongoza na kuponya.

kutiwa adabu na Mungu ... uongozi wa Mwenyezi

Mungu ni mfano wa mzazi atiavyo adabu au aelekezavyo mtoto.

amebarikiwa

"umependelewa"

usidharau

"usikatae au " au "usiwangalie wasio na thamani"

uongozi

"mafunzo" au "ukusanyaji" au "adilisha"

Kwa kuwa yeye hujeruhi na kisha huuguza; yeye hutia jeraha na kisha mikono yake huponya

"kwa kuwa yeye hujeruhi lakini hufunga zaidi; yeye huangamiza lakini mikono yake huponya"

mikono yake huponya

Hapa "mikono yake" ni mfano wa Mungu.

Yeye atakuokoa na mateso sita; kweli, katika mateso saba, hakuna uovu utakao kugusa

matumizi ya ongezeko la hesabu kama vile "sita" na "saba" ni mfano wa wazo la wengi, mara nyingi. "Yeye atakuokoa kutoka katika taabu zaidi na zaidi; kwa kweli, muda baada ya muda, hakuna uovu utakao kugusa wewe"

Job 5:20

Habari za Jumla:

Mabadiliko katika kiwakilishi kutoka (yeye" hadi "wewe" ambayo yalianzia katika 5:17 yanaendelea hadi mwisho wa usemi ya Elifasi katika 5: 26.

Wakati wa njaa atakukomboa

"wakati wa njaa Mungu atakuokoa wewe"

atakukomboa wewe

"atakukomboa wewe" au "atakuokoa wewe" au "atakunusuru"

uharibifu

"madhara kutoka kwa maadui"

hutatishika na wanyama mwitu

"wewe hutaogopa wanyama mwitu"

wanyama mwitu

wanyama ambao hawajafugwa au hawajafundishwa.

Job 5:23

Habari za Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika kila mistari hii, akiwakilisha wazo moja kwa kutumia maelezo mawili tofauti kusisitiza usalama na kuhusu ulimwengu wa asili, nyumba ndani ya shamba, na vizazi vya mmoja.

utakuwa na mapatano na mawe ya shambani mwako

Sentensi hii inatumia lugha ya picha kuwasilisha ulingalifu na ulimwengu wa asili. "mapatano yako na mawe ya shambani"

wewe utakuwa na amani na wanyama wa mwituni

"wanyama mwitu watakuwa na amani na wewe"

wanyama wa mwituni

Wanyama ambao hawajawahi kufungwa au kufundishwa

utajua kwamba hema lako lina usalama

"utafahamu kwamba hema lako lina amani"

utatembelea zizi la kondoo wako na hutakosa kitu chochote

"wewe utatembelea kundi lako na kukuta hakuna kilichopotea"

Pia utafahamu kwamba uzao wako utakuwa mwingi, na vizazi vyako vitakuwa kama nyasi juu ya ardhi

Katika usemi huu, "kizazi" ni mfano wingi sana kama bapa la majani. "pia wewe utafahamu kwamba uzao wako utakuwa mwingi, kwamba kizazi chako kitakuwa kama majani juu ya ardhi"

Job 5:26

Wewe utafika kaburini kwako mwenye umri kamili

"wewe utakufa katika umri wa uzee sana"

kama vile rundo la mashuke ya nafaka ambalo limembebwa juu kupelekwa kwenye uwanja wa kupuria

Elifazi anatumia ulinganifu kutengeneza wazo lake kwamba Ayubu atakufa wakati muda wake wa kufa ukifika. "Kama tu nafaka zivunwavyo kwa wakati, hivyo wewe utakufa wakati wako ukifika."

Tazama, tumelipeleleza jambo hili; ndivyo lilivyo; lisikie, na ulifahamu kwa ajili yako mwenyewe.

"Sisi" inamhusu rafiki zake Ayubu, akiwemo Elifazi, amabaye anazungumza. "Tazama, Sisi tumefikiri kuhusu jambo hili. Sikiliza kile ninsema na ufahamu kwamba ni kweli."

Job 6

Job 6:1

laiti maumivu yangu makubwa yangepimwa; laiti misiba yangu yote mikubwa ingewekwa kwenye mizani!

Hapa mwandishi anatumia maelezo mawili tofauti kuwasilisha wazo moja, mzigo wa mateso ya Ayubu.

kwenye mizani

"kwenye kipimo"

Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa baharini

Ayubu analinganisha mzigo wa mateso yake na uzito wa mchanga wenye majimaji; vyote vinaweza kumwangamiza mtu. "Mzingo wa maumivu yangu makubwa na taabu ni mazito kuliko mchanga wa ufukweni."

Job 6:4

Habari za Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika kila moja ya mistari hii, akiwasilisha wazo moja akitumia maelezo mawili tofauti kusisitiza maumivu makali sana ya Ayubu kama sababu ya malalamiko yake.

Kwa kuwa vitisho vya Mungu vimejipanga vyenyewe dhidi yangu

Huu ni ulinganishi wa mateso ya Ayubu. Yeye analinganisha taabu zake nyingi na mishale ambayo choma mwili wake.

moyo wangu umelewa sumu

Ulinganishaji unaendelea. Maumivu yamepenya hadi moyoni mwa Ayubu. "Nasikia maumivu ndani ya moyo wangu."

Vitisho vya Mungu vimejipanga vyenyewe dhidi yangu

"mambo yote mabaya sana ambayo yameweza kutokea dhidi yangu yamekuja kwa wakati mmoja."

kwa mishale

"kama kikosi cha jeshi chini ya kanali" u "kama kundi la wanajeshi"

Je punda mwitu hulia akiwa na malisho? Au ng'ombe huwa dhaifu wakati wa njaa ambapo anachakula?

Ayubu anatoa maswali haya kusisitiza kwamba ana maana nzuri kulalamika. " Tafadhari mimi ningelilalamika kama kila kitu kipo vizuri?" au "Tafadhari mimi nisingelilalamika bila sababu."

mlio

ni sauti aitoayo punda

dhaifu

sauti aitoayo ng'ombe

chakula

chakula cha mifugo

Je inawezekana kitu kisicho na ladha kulika bila chumvi? Au kuna radha yoyote katika ute mweupe wa yai?

Hata chakula, au hali ya mambo, katika maisha ya Ayubu ni ya kuhuzunisha. Ayubu analinganisha maisha yake na mlo ambao hauna viungo au ladha. "Maisha yangu hayana mwokoaji; ni kama ute mweupe wa yai usio na ladha."

Je inawezekana kitu kisicho na ladha kulika

Swali hili la kutoonyesha hisia linaweza kutafasiriwa kama maelezo hai: "Mtu hawezi kula chakula chenye ladha mbaya bil chumvi."

Job 6:7

Habari ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika kila mistari hii, kuwasilisha wazo moja akitumia maelezo mawili tofauti kusisitiza mateso yake makali sana na haja yake ya kufa.

Nakataa kuvigusa

"Wao" inahusu chakula chenye ladha mbaya. Hapa Ayubu anaendelea kutumia sura ya chakula kibaya kama sitiari kwa hali ya mambo yasiyokubalika.

Oo, kama nigeweza kupata haja yangu; oo, kama Mungu angeridhia jambo nilitamanilo sana

"Oo kwamba Mungu angefanya kile ambacho nimemwomba yeye kufanya"

kama Mungu ingempendeza kuniangamiza mara moja

"Kwamba Mungu angelisonga mbele na kuniangamiza mimi"

kwamba angeulegeza mkono wake na kuyakatilia mbali maisha yangu

"kwamba angelitenda haraka na kufupisha maisha yangu"

angeulegeza mkono wake

"tenda haraka"

Job 6:10

Hii inaweza kuwa faraja yangu hata sasa

"Hata hivyo hii inaweza kuwa faraja yangu" au "Hii inaweza kuniletea faraja"

hata kama nafurahia sana maumivu ambayo hayapungui

"Mimi nita ruka kwa furaha katika maumivu yasiyokwisha" au "Mimi nitavumilia maumivu ambayo hayapungui"

nafurahia sana

"furahi"

yasiyopungua

"hayapungui"

kwa kuwa sikuyakana maneno yake Mtakatifu

"hivyo sikumkana Mungu"

Nguvu yangu ni ipi, hata nijaribu kusubiri? Mwisho wangu ni upi, utakao refusha maisha yangu?

Ayubu anatoa maswali haya kusisitiza kwamba hakuna maana ya yeye kuendelea kuishi. "Zaidi, kuna nini tena kipo kwaajili yangu kuishi na kukitumainia?" au "Mimi sina nguvu za kuendelea kuishi; Mimi sina sababu ya kuwa mstahamilivu"

Job 6:12

Habari ya Jumla:

Mwandishi anatumia maswali ulinganishi ya kejeli katika kila mistari hii, akiwasilisha wazo moja kutumia maelezo mawili tofauti kusisitiza ukosefu wa nguvu za kustahamili mateso.

Je nguvu zangu ni nguvu za mawe? Au mwili wangu umeumbwa kwa shaba nyeusi?

Ayubu analinganisha udhaifu wa mwili wake na ugumu, vifaa vya ujenzi vya kudumu sana kusisitiza ukosefu wake wa nguvu. "Mimi siko imara kama mawe. Mwili wangu hujaumbwa kwa kokoto za kutengenezea barabara."

Je si kweli kwamba sina msaada ndani yangu ... nami?

"Ni kweli kwamba sinanguvu zilizobaki ... mimi."

hekima imeondolewa mbali nami?

"mafanikio yangu yameondolewa kwangu" au "au "nguvu za ndani zimeondolewa kwangu" Hii inaweza kutajwa katika muundo hai. "Nguvu zangu za ndani zienda."

Job 6:14

Kwa mtu ambaye yu karibu kuzirai, inapasa uaminifu uonyeshwe na rafiki zake

"Rafiki anatakiwa kuwa na huruma kwa mtu ambaye anajihisi kukata tamaa"

hata kwake yeye aachaye kumcha Mwenyezi

"hata kama ataacha kumweshimu Mwenyezi Mungu" Maana za kufaa ni 1) mtu hana hofu ya Mungu au 2) rafiki zake hawamwogopi Mungu.

Lakini ndugu zangu wamekuwa waaminifu kwangu kama mkondo wa maji jangwani

Ayubu anawaelezea rafiki zake kuwa wamekuwa kama "bondejangwa" ambalo hupitiwa na mto katikati yake ambao unaweza kukauka ghafra na si wa kutumainika.

mfano wa mifereji ya maji ipitayo mpaka pasipo kitu

"mfano wa mito ya maji ambayo hukauka"

ambayo imetiwa giza kwa sababu ya barafu juu yake

"ambayo ni giza kama barafu"

na kwa sababu ya theluji ambayo hujificha yenyewe ndani yake

"na theluji hujificha ndani yake" au "barafu hupotea ndani yake"

Wakati zikiyeyuka, hutoweka

"Wakati zikipata joto, hutoweka"

kukiwa na joto, hutoweka mahali hapo.

"wakati wa joto, hukauka"

Job 6:18

Misafara ambayo husafiri kwa njia hiyo hugeuka kwaajili ya maji

Ayubu anaendelea na maelezo yake kuhusu rafiki zake kuwa si wa kutegemewa kama mito ambayo hukauka. "Njia ya wasafiri hubadili njia kwa ajili ya kutafuta maji"

Misafara

Kifungu hiki kinaweza pia kutafsiriwa kama "njia za misafara" au "njia za wasafiri" au "wasafiri."

huzurura jangwani na kisha huangamia

"hawakwenda popote na kisha hufariki"

Tema

Hili ni jina la mahali. Watu wa mahali pale walitumia misafara kufanya biashara ya vitu na watu kutoka nchi zingine.

wakati majeshi ya Sheba huitarajia

"wakati wasafiri kutoka Sheba waliwatumainia"

Sheba

Hili ni jina la mahali. Watu wa mahala pale walitumia misafara kufanya biashara ya vitu na watu kutoka nchi zingine.

waliwatarajia

"walitumaini kwaajili yao" au " waliweka matumaini yao kwao

Wamevunjika moyo kwa sababu walitumaini kupata maji

"Walichanganyikiwa kwasababu waliamini kwamba wangeweza kupata maji"

lakini walidanganywa

"lakini walipoteza matumaini" au "lakini hawakuridhika"

Job 6:21

Habari za Jumla:

Katika mistari hii, Ayubu anatoa maswali manne kuwakaripia rafiki zake na kusisitiza kwamba yeye hakuomba msaada kutoka kwa yeyote kati yao.

Kwa sasa

Ayubu anatumia kifungu hiki kuanza sehemu kuu ya kile anachosema.

ninyi rafiki si kitu kwangu

"hamtendi kama rafiki zangu"

nanyi mwaogopa

"na ninyi mnaogopa kwamba Mungu anaweza kuwafanyia mambo hayahaya." Hapa inaweka bayana zaidi habari ya kutisha kwamba rafiki zake wanaogopa kuadhibiwa na Mungu.

Je nilisema kwenu, 'Nipeni kitu furani?'

"Sijamuomba yeyote kati yenu kitu chochote."

nitoleeni zawadi katika mali zenu?

"Mimi sijawaomba mnipe pesa." au "Mimi sijawaomba kutoa bibi harusi kwaajili yangu kutoka katika mali zenu."

Niokoeni toka mkononi mwa mtesi wangu?

"Mkono wa mtesi wangu" ni mfano ambao unasimama badala ya nguvu ya mtu fulani ambaye anashindana kwa nguvu sana na Ayubu. "Mimi sijawahi kumwomba mmoja kati yenu kuniokoa kutoka kwa adui zangu"

Niokoeni toka mkononi mwa mtesi wangu?

"Mkono wa mtesi wangu" ni mfano ambao unasimama badala ya nguvu za watu ambao wanamtendea Ayubu vibaya. 'Mimi sijawaomba kuniokoa kutoka kwa wale ambao wananitendea vibaya."

Niokoe

"nisaidie"

Job 6:24

Nifundishe

Kitenzi "kufundisha" ipo katika sehemu ya nafsi ya pili wingi.

nami nitaishika amani yangu

" na mimi nitakuwa kimya"

nifanye nifahamu

"wewe umenifanya mimi nielewe." Kitenzi kipo katika sehemu ya nafsi ya pili wingi.

Jinsi gani maneno ya kweli yanavyo umiza

ULB na UDB zina maana zinazopingana kwa kifungu hiki. Hii ni kwasababu maana mbili zinazofaa kwa Kiebrania ni 1) Maneno ya kweli yanaumiza kuyasikia au 2) Maneno ya mtu mkweli hayaumizi kuyasikia.

Lakini hoja zenu, jee hasa zimenionya nini mimi?

Ayubu anatumia swali hili kuwa karipia rafiki zake na kusisitiza kwamba kile wanachosema hakimhusu. "Sababu zenu hazinihusu japokuwa mmenikosoa bila huruma."

hoja zenu

"Sababu zenu" au "madai yenu." "-ako, - enu" ipo katika sehemu ya nafsi ya pili wingi.

Job 6:26

Je mnapanga kuyapuuza maneno yangu, mnayachukulia maneno ya mtu mwenye kukata tamaa sawa na upepo?

Ayubu anatumia swali hili kuwakemea rafiki zake. "Mmeyapuuza maneno yangu, na kuyachukulia maneno yangu kama si kitu."

Je mna

"wewe, ninyi" ipo katika sehemu ya nafsi ya pili wingi.

mnayachukulia maneno ya mtu mwenye kukata tamaa sawa na upepo

Ayubu analinganisha maneno ya kukata tamaa ya mtu asiye na tumaini kwaajili ya msaada na upepo usio na kitu; yote hayana manufaa.

mna piga kura kwa ajili ya yatima

"hata mna cheza kamari kumpata yatima"

mna piga kura ... kupatana bei juu ya rafiki yenu

Hapa "wewe, ninyi" na "-ako, -enu" yapo katika sehemu ya nafsi ya pili wingi.

na kupatana bei juu ya rafiki yenu kama bidhaa.

"na kuchimba shimo kwaajili ya rafiki yenu"

Job 6:28

Sasa

Neno hili limetumiwa na Ayubu kuleta habari mpya.

tafadhari tazama

Kitenzi "kutazama" lipo katika sehemu ya nafsi ya pili wingi.

usoni penu

"-ako, -enu" lipo katika sehemu ya nafsi ya pili wingi.

punguzeni ukali, nawasihi

"Tafadhari kuwa na huruma nami" au "Tafadhari geuka"

ukali kidogo

Kitenzi hiki kipo katika sehemu ya nafsi ya pili wingi.

lisiwepo neno la uonevu na nyinyi

"nitendeeni kwa haki"

Hasa, punguzeni ukali, sababu zangu ni za haki

"Badilisheni namna mnavyonitendea mimi tena; Mimi niko sawa katika hili" au " Badilisheni namna mnavyonitendea; Mimi bado niko sawa katika hili"

kali kidogo

Kitenzi hiki kipo katika sehemu ya nafsi ya pili wingi.

Je mna uovu ulimini mwangu?

"Je nimesema mabo maovu?" Ayubu anatumia hili swali kuwakemea rafiki zake na kusisitiza kwamba yeye siyo mbaya. "Mimi sisemi mambo maovu."

Je mna uovu ulimini mwangu?

Kiuhalisia ulimi hauwezi kuwa na uovu, kwa hiyo ni mfano uliotumika kuelezea kauli mbaya.

Je kinywa changu hakiwezi kungundua madhara?

Ayubu anatumia swali hili kuwa kemea rafiki zake na kusisitiza kwamba yeye anaweza kuwaambia tofauti kati ya wema na ubaya. "Mimi naweza kuwaambia tofauti kati ya uzuri na ubaya."

Job 7

Job 7:1

Habari za Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika kila mistari hii, kuwasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kusisitiza kwamba mateso ya mtu binafsi ni sehemu ya mateso ya watu wote ambayo watu wote huyapitia.

Je mtu hana kazi ngumu juu ya nchi?

Ayubu analeta swali hili kusisitiza ufahamu wake kwamba watu wote huyapitia mateso. "Je si kila mtu ana kazi ngumu katika nchi?" au "Kila mmoja ana kazi ngumu katika nchi"

Je siku zake si kama siku za mwajiriwa?

Ayubu anatoa swali hili kuunga mkono ufahamu wake kwamba watu wote hupambana katika maisha. "Na siku zake ni kama siku za mwajiriwa."

Kama mtumwa ... kama mwajiriwa

Ayubu anajilinganisha mwenyewe (mstari 3) na wale ambao hufanya kazi kwa bidii hawana msaada (mstari 2).

kivuli cha jioni

"giza"

mwajiriwa

Huyu ni mtu ambaye hufanya kazi kwa siku kwa muda na hulipwa kutwa ya kila siku. "kibaruwa"

hivyo nami nimeumbwa kuvumilia miezi ya taabu; Nami nimepewa taabu - zimeujaza usiku

kuujaza usiku- "kwa hiyo mimi nimevumilia miezi ya mateso na taabu-zimeujaza usiku"

miezi ya taabu

"miezi ya msiba" au "miezi ya kufirisika"

Job 7:4

Lini nitatoka kitandani na lini usiku utatoweka?

Ayubu analeta swali hili kusisitiza mateso yake makali sana wakati wa masaa ya kulala. "Natamani ningeweza kuamka, lakini usiku unaendelea."

Nimejawa na kujitupa huku na huko

Hii inaonyesha kwamba Ayubu alikuwa anahamahama kitandani usiku kucha bila kupumzika. "Mimi nimechoka kujisukasuka na kujigeuza bila kutulia."

madonda yenye vumbi

uvimbe mchafu

Job 7:6

Habari ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika mistari hii, kuwasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kusisitiza hisia za Ayubu juu ya ufupi wa maisha.

Siku zangu zinakimbia kuliko chombo cha kufumia

"Maisha yangu yanapita haraka sana"

mfumaji

mtu ambaye hutengeneza nguo kwa kupishanisha uzi au kitani

chombo cha kufumia

ni kipande ambacho kinatembea mbele na nyuma haraka sana katika mashine au chombo kwa ajili ya kutengeneza nguo

zinapita bila tumaini

"zinafika mwisho bila matumaini kabisa"

Mungu, anakumbuka

Neno "Mungu" liliongezwa katika kifungu hiki kwa sababu watu ambao watasikia "kumbuka" waliweza kuelewa kwamba Mungu ameandikiwa.

maisha yangu ni pumzi tu

Katika msemo huu, Ayubu analinganisha ufupi wa maisha yake na upungufu wa pumzi. "Maisha yangu ni mafupi kama kupumua mara moja"

jicho langu halitaona mema tena

"Sitapata tena furaha"

Job 7:8

Habari za Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika kila mtistari hii, kuwasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kusisitiza fikira za Ayubu kwamba, baada ya kufa, si Mungu wala watu yeye alifahamu wataonana naye tena.

Macho ya Mungu yatanitazama, lakini sitakuwako

Neno "Mungu" liliongezwa katika kifungu hiki kwasababu muktadha unaonyesha kwamba Ayubu anaongea na Mungu. "Macho ambayo yananiona mimi hayataniona tena."

Macho ya Mungu yatanitazama, lakini sitakuwako

"Macho yako yatakuwa juu yangu, lakini mimi sitakuwako."

kama vile wingu liishavyo na kutoweka, hivyo wale waendao sheoli hawatarudi tena kabisa

Ayubu anaelezea kifo katika hali ya mawingu yanavyotoweka. "Kama mawingu yatowekavyo, hivyo yeye ambaye anakufa hutoweka" au "Mara wewe uwapo kaburini, hutaweza kuinuka."

kama vile wingu liishavyo

"Kama wingu linavyotoweka"

Job 7:11

Nitasema juu ya maumivu makubwa ya roho yangu; Nitanung'unika juu ya uchungu wa nafsi yangu

Ayubu anawasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kuelezea sababu za yeye kutokukaa kimya.

sitakizuia kinywa changu

"Mimi sitaacha kuongea"

maumivu makubwa ya roho yangu

"mateso ya moyo wangu" au "maumivu makali ya mateso yangu"

uchungu wa nafsi yangu

"uchungu wa moyo wangu"

Je mimi ni bahari au kiumbe cha kutisha baharini hata ukaweka mlinzi juu yangu?

Ayubu anatoa swali hili kuelezea hasira yake kwa Mungu. Kwa kujilinganisha yeye mwenyewe na bahari au kiumbe cha kutisha baharini, Ayubu anamaanisha kwamba Mungu anamchukulia yeye kama kiumbe cha kutisha. 'Mimi siyo bahari au kiumbe cha baharini ambacho huitaji mlinzi wa kukilinda."

Job 7:13

Habari za Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika mistari miwili ya kwanza, kuwasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kuelezea maumivu makali sana ya Ayubu.

kitanda changu kitanifariji, na malazi yangu yatatuliza manung'uniko yangu

Hapa "kitanda" na "malazi" ni mifano wa "kulala." Kwa kulala chini, Ayubu alitarajia faraja. Mfano pia una sifa za kibinadamu; wana uwezo wa kumriwadha na kumfariji mtu.

wewe unanitisha mimi

"wewe" inamaanisha Mungu ambaye Ayubu anamlalamikia.

kunyonga

kuua mtu kwa kumkaba koo lake na kuzuia asipumue.

hii mifupa yangu

Hapa Ayubu anatumia neno "mifupa" kumaanisha mwili wake. "Huu mwili wangu"

Job 7:16

Habari unganishi:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika mistari hii, kuwasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kusisitiza matokeo ya mateso ya Ayubu juu ya hisia zake kuwa mwenye thamani.

Ninayachukia kabisa maisha yangu

"Mimi naya-dharau maisha yangu"

siku zote kuwa hai

"kuishi milele"

siku zangu hazifai

"siku zangu hazina maana" au "siku zangu hazina thamani"

hata ukatia bidii kwake

"kwamba wewe utamwangalia yeye"

utaweka akili yako kwake

"kwamba wewe utayaelekeza bidii zako kwake"

na kumwangalia

"kwamba wewe utamwangalia vizuri yeye"

Job 7:19

Je itachukuwa muda gani kabla hujaacha kuniangalia, wala kunisumbua muda wa kutosha kwaajili ya kumeza mate yangu?

Hapa Ayubu anawasilisha wazo moja akitumia maswali mawili ya kejeri kusisitiza matamanio yake kwamba Mungu angeliacha kumwangalia yeye. "Usinitazame! Niache peke yangu kiasi cha kumeza mate yangu mwenyewe!"

Hata kama nimefanya dhambi, itakusaidia nini, wewe ulindaye wanadamu?

Ayubu analeta swali hili kumkaripia Mungu. "Hata kama nimefanya dhambi, kwamba haitakusaidia kitu wewe, ambaye uwalinda watu."

Kwa nini umenifanya shabaha yako, ... kwako?

"Kwanini umenifanya mimi shabaha kwa ajili yako mwenyewe?"

Job 7:21

Kwa nini hunisamehi makosa yangu na kuniondolea uovu wangu?

Hapa Ayubu analeta vishazi viwili tofauti ndani ya swali la kejeri kusisitiza matamanio yake kwamba Mungu atazisamehe dhambi zake. Yeye analeta swali hii kumkaripia Mungu kwa kumfanya ateseke. "Samehe makosa yangu na uniondolee uovu wangu."

Kwa nini wewe husamehi makosa yangu

"Kwa nini husamehi makosa yangu?"

niondolea

"ondoa"

sasa nitalala mavumbini

Kifungu "lala chini katika mavumbi" ni upole au njia ya upole ya kusema "kufa." "sasa mimi nitakufa"

Job 8

Job 8:1

Habari ya Jumla:

Katika kila mstari wa habari yake, Bildadi anawasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti, moja kumkemea Ayubu na tena kumtetea Mungu.

Kisha Bildadi huyo Mshuhi akajibu

"Bildadi" ni jina la mtu ambaye mmoja wa kabila la Washuhi.

Kwa muda gani maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo wenye nguvu?

Bildadi analeta swali hili kumkaripia Ayubu kwa malalamiko yake kwa Mungu. Katika msemo huu, yote maneno ya Ayubu na upepo ni matupu na dhaifu. "Maneno ya mdomo wako ni upepo wenye nguvu."

Je Mungu hupotosha hukumu? Je Mwenyezi hupotosha haki?

Hapa mwandishi anatumia maswali mawili ya kejeri, ambayo Bildadi anayatumia kukaripia Ayubu. "Mungu hatendi yasiyo haki; Mwenyezi hashindwi kufanya mema."

Job 8:4

kwa kuwa amewatia mkononi kwa makosa yao

" ni kwasababu Mungu ameruhusu uwezo wa dhambi zao kuwaongoza wao" au "amewaadhibu kulingana na matokeo ya dhambi zao."

Lakini wewe unaonaje ukimtafuta Mungu kwa bidii na kufikisha haja yako kwa huyo Mwenyezi

Vifungu vyote hivi vinamtaja Ayubu akimwomba Mungu msaada, au akijitetea kwa Mungu kwa ajili ya msamaha.

ukimtafuta Mungu kwa bidii

"kwa bidii mwombe Mungu kwa ajili ya msaada"

Job 8:6

Ukiwa wewe ni msafi na mkamilifu

"Kama tu wewe ni msafi na mmwenye haki" au " Kama moyo na matendo yako ni mema"

Japokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, hata hivyo hali yako ya mwisho itaongezeka sana

"Hata kama wewe hukuwahi kuwa mwenye heri kabla, wakati wa mwisho wa maisha yako utakuwa tajiri sana."

Job 8:8

Habari ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika kila mistari hii, kuwasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kusisitiza uwezo wa watu kujifunza kutoka kwa wazazi, waliopewa ufupi wa maisha na utayari wa wazazi kuwapa mafundisho.

utie bidii katika hayo mababu zetu waliyojifunza

"Jifunze kwa makini yale waliyoyangundua wazazi wetu" au "zingatia yale ambayo mababu zetu waliyojifunza"

siku zetu duniani ni kivuli

Katika hii tashbiha, maisha yanalinganishwa na giza; yote yanapita kwa haraka.

Je hawatakufunza wao na kukuambia? Je hawatatamka maneno yatokayo mioyoni mwao?

Bildadi anatoa maswali haya kumkaripia Ayubu. "Watakufundisha na kukuambia wewe, na kutokana na uelewa wao unaleta maneno ya kutia moyo."

Job 8:11

Je hayo mafunjo yaota pasipo matope? Je mafunjo yaota pasipo maji?

Bidadi anatoa maswali ya kejeri kusisitiza hoja yake aliyoitoa katika 8:8: Watu wanahitaji mafundisho ya wazazi wao. "Mti wa mafunjo hayawezi kumea mbali na bwawa. Mafunjo hayawezi kumea bila maji."

nyauka

"kausha"

Job 8:13

Habari ya Jumla:

Mistari hii inaendeleza habari ya Bildadi. Katika mstari wa 14 - 15, mwandishi anatumia ulinganishaji, kuwasilisha wazo moja kwa kutumia taarifa mbili tofauti kusisitiza uharibifu wa wale ambao hawajayajenga maisha yao juu ya mafundisho ya wazazi wao.

Hivyo pia ni njia ya wote wamsahauo Mungu

"Kutembea kwenye njia" ni usemi wa kawaida ambao unahusu maisha ya mtu na uelekeo wake. Mara nyingi hii inahusiana na watu kama wanafuata njia ya Mungu au njia zao wenyewe.

matumaini yake ni dhaifu kama utando wa buibui

Hapa Bildadi analinganisha maisha ya waovu na utando wa buibui; nguvu kidogo itaharibu vyote.

atashikamana nayo

"yeye atajaribu kukisaidia hicho"

Job 8:16

Habari za Jumla:

Katika mstari wa 16 - 17, mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji, kuwasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kueleza ugumu, mfuko wa muda wa kusaidia wa waovu.

Yeye huwa mti mbichi chini ya jua, na machipukizi yake huenea katika bustani yake yote

Hapa Bildadi analinganisha waovu na mti ambao husitawi wakati wa mchana; mwanzoni vyote huonekana hai, mbichi, na bora.

Mizizi yake hujifunga funga kwenye rundo la mawe

Mizizi ya watu waovu hushikamana si katika udongo wenye rutuba lakini kwa mawe. ardhi ya mawe haisaidii mimea kumea. Mizizi ya mtu huyu itakufa mapema. "Mizizi yake hushika kwenye ardhi ya mawe."

huangalia mahali pazuri katikati ya mawe

Neno "wao" inahusu mizizi ya watu waovu. "hutafuta ardhi yenye rutuba miongoni mwa mawe" au "hutafuta udongo wenye rutuba miongoni mwa mawe"

Lakini mtu huyu aking'olewa mahali pake, kisha mahali pale patamkana, na kusema, 'mimi sikukuona

Watu waovu wanalinganishwa na mmea ambao, wakati ukiondolewa kutoka kwenye msingi wa mawe, hautambuliki mahali pote kwasababu hauwezi kustawi katika sehemu yoyote yenye rutuba. "kama hautaondolewa kutoka sehemu yake, utamkana yeye nakusema, 'Mimi sijawahi kukuona wewe."

mahali pale patamkana, na kusema

Uwezo wa mwanadamu kukana na kusema imetumiwa kwa ardhi ya mawe.

mahali pake

"ardhi ya mawe"

Job 8:19

furaha

zawadi, ni matokeo ya tabia ya uovu ya mtu ambayo Bildadi kwa dharau anaitamka kama 'furaha.'

tabia

"matendo" au "namna ya maisha"

mimea mingine itachipuka toka katika udongo ule ule mahali pake

Hapa mwandishi anaendelea na sitiari kutoka 8:16.Watu waovu wanalinganishwa na mimea ambayo huchukua sehemu ya kwanza ya ule ambao humea miongoni mwa mawe. "Wakati mtu muovu mmoja akifa, mwingine atachukua nafasi yake" au "kutoka kwenye udongo, mwingine utamea."

chupuka

"mea"

udongo ule ule

"ardhi ya mawe"

mahali pake

"katika sehemu ya mtu muovu"

wala hatawathibitisha watendao uovu.

"Mkono" ni mfano wa mwili mzima wa mtu. "hatawasaidia watenda maovu" au " hatawatia nguvu watenda mabaya"

Job 8:21

Yeye atakijaza kinywa chako na kicheko, midomo yako na shangwe

Bildadi anaendelea kusema na Ayubu. Neno "yeye" linahusu Mungu, na "-ako, -enu" linahusu Ayubu. Mwandishi anawasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kuwasilisha furaha ambayo Ayubu atapitia. "Mungu atakupa furaha tena."

midomo yako na shangwe

Maana kamili ya kifungu hiki inaweza kuwafahamika kutokana na mwanzo wa sentensi. "Mungu atakijaza kinywa chako na na kelele za furaha."

Wale ambao wanakuchukia wewe watavishwa aibu; nayo hema yake mwovu haitakuwepo tena

"Waovu watajawa na aibu; wabaya watakoma kuishi."

haitakuwepo tena

"hautadumu" au "utafika mwisho"

Job 9

Job 9:1

"kweli najua kwamba ndivyo hivyo.

"najua kwamba kile unachosema ni kweli"

ndivyo hivyo

Hapa neno "hii" linahusu kile alichosema Bildadi.

kwa namna gani mtu anakuwa na haki kwa Mungu?

"kwa namna gani mtu yeyote atakuwa hana kosa mbele za Mungu?"

hoji

"shindana"

hatamjibu yeye mara moja katika elfu zaidi

"Mara moja katika elfu zaidi" ni usemi unaomaanisha "hata kidogo." Maana zinazofaa ni 1) "hawezi kutoa jibu lolote kwa Mungu" au 2) "Mungu atamjibu yeye hata kidogo"

elfu zaidi

"mara 1,000"

Job 9:4

hekima moyoni

Hapa moyo unawakilisha utu wa ndani au fikira. "ana hekima katika maamuzi yake"

mwenye uwezo mwingi

Jina la kuwazika "nguvu" inaweza kuelezewa kama kisifa "imara." "mwenye nguvu kwa jinsi alivyo imara"

ni nani daima aliyejifanya mwenyewe kuwa mgumu dhidi yake na akafanikiwa?

Hili ni swali la kejeri ambalo linahitaji jibu la "hakuna hata mmoja." Linaweza kupangiliwa kama maelezo. "Hapa mmoja aliyewahi mwenyewe kujifanya mgumu dhidi yake na akafanikiwa."

aliyejifanya mwenyewe kuwa mgumu dhidi yake

Kujifanya mgumu inamaanisha kuwa mkaidi. "kumbishia yeye" au "kumpinga yeye"

ambaye huiondoa milima

"Mungu huhamisha milima"

katika hasira zake

"Hasira" ni jina la kufikirika tu linaweza kuelezewa kama "mwenye hasira" katika kivumishi cha sifa. "kwasababu yeye ni mwenye hasira"

ambaye huitikisa nchi

"Mungu hutikisa nchi"

mihimili yake hutikisika.

"hufanya misingi ya nyumba itikisike"

Job 9:7

ambaye huzihifadhi nyota

"ambaye huzuia nyota zisionekane"

ambaye peke yake ni mwenye kupanua mbingu

Mungu anaongelewa kama aliyeumba mbingu bila msaada wowote, kana kwamba mbingu ilikuwa mfumo kwamba yeye aliueneza.

kuyatuliza mawimbi ya bahari

Mungu anazungumziwa kama mtuliza bahari kana kwamba kwa miguu yake. "hukanyaga miguu yake juu ya mawimbi ya bahari" au " hutuliza mawimbi ya bahari"

Dubu, Orioni, kilima

Haya yanahusu kundi la nyota, ambalo ni kundi la nyota ambalo huonekana kama zimetengeza umbo fulani angani.

Orioni

ni maarufu kwa uwindaji katika elimu ya visasili ya kigiriki

Kilima

nyota nyingi zenye kung'aa ambazo huonekana kama zipo karibu karibu angani.

kundinyota

kundi la nyota ambalo huonekana kama limetengeneza umbo fulani angani

Job 9:10

Habari za Jumla:

Mwandishi anatumia ulinganishaji katika kila mistari hii, kuwasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili kusisitiza kwamba Mungu ni mkuu, asiyeonekana, na mwenye mamlaka.

mambo yasiyofahamika

"mambo yasiyochunguzika" au "mambo yasiyoeleweka"

yasiyohesabika

"ambayo hayahesabiki"

Tazama

"Tazama" au "kuwa makini"

hupita kwenda mbele

"yeye hupita" au "yeye huendelea mbele"

Kama akichukua kitu chochote, nani tamzuia? Nani awezaye kumuuliza, 'unafanya nini?'

Haya ni maswali ya kejeri ambayo hutarajia jibu la "Hata mmoja." Yanaweza kupangiliwa kama maelezo. "Kama akichukuwa kitu chochote mbali, hakuna wakumzuia. Hakuna wa kumuuliza, 'unafanya nini?""

Kama akichukua kitu chochote

"Kama yeye akichukua mbali kitu fulani" au "Kama akihitaji kunyakua mbali kitu chochote"

Job 9:13

wamsaidiao Rahabu kuinama chini yake

Hapa "kuinama mbele zake" inaashiria utii au ushindwaji. "yeye huangamiza wasaidizi wa Rahabu"

Rahabu

Neno hili "Rahabu" hapa linamaanisha dubwana la baharini.

Je ni upungufu kiasi gani mimi nitamjibu, je nichague maneno kuhojiana naye?

Ayubu anatoa maswali mawili yanayofanana kusisitiza kukataa kwake kumkabili Mungu. Yanaweza kupangiliwa kama maelezo. "Hivyo Bila shaka mimi nisingeweza kumjibu au kuchagua maneno ya kuhojiana na yeye."

Job 9:16

kwa kuwa yeye anidhoofishaye kwa dhoruba

Ayubu analinganisha mateso yake kutoka Kwa Mungu na athari za dhoruba. "Yeye hunijeruhi mimi kana kwamba kwa dhoruba."

dhoruba

lenye nguvu sana au tufani lenye nguvu sana

zidisha majeraha yangu

"hunipatia mimi majeraha mengi" au "hunijeruhi mimi tena na tena"

pasipo sababu

Hata kama sijaweza kumpa sababu ya kufanya hivyo" au "hata kama sina kosa"

kamata pumzi yangu

Hii ni lugha ambayo humaanisha "pumua" au "vuta pumzi"

yeye hunijaza uchungu

Mstari huu ni mfano wa Mungu kuyajaza maisha ya Ayubu na mambo ambayo humpa yeye uchungu. Jina la kufikirika "uchungu" linaweza kuelezewa kama kivumishi "-chungu." "yeye hunijaza mimi na mambo machungu"

Job 9:19

Kama ni habari ya nguvu

"Kama kuna mabishano ya nguvu"

tazama

"tazama" au "kuwa makini na kile nataka kukuambia"

yeye ni mwenye nguvu

"yeye ni hodari sana"

nani atakaye mhukumu?

Swali hili linatarajia jibu la "Hata mmoja" kutengeneza hoja kwamba hakuna hat mmoja awezaye kumfikisha Mungu mahakamani. Hili linaweza kupangiliwa kama kama maelezo. "hata mmoja anaweza kumuita yeye kortini."

Ingawa ni mwenye haki

Hapa "mimi nipo katika haki" inamaanisha mimi ni mmoja ambaye nimefanya mambo yaliyo haki. "Ijapokuwa mimi nimefanya mambo ya haki" au "Hata hivyo mimi sina kosa"

Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; na ingawa ni mtakatifu, maneno yangu yatashuhudia kuwa ni mwenye kosa.

mstari huu unaelezea wazo lile lile mara mbili kwa ajili ya kusisitiza.

kinywa changu mwenyewe kitanihukumu

Hapa "kinywa" mfano wa maneno ya Ayubu. "maneno yangu mwenyewe yatanishitaki" au "kile ninachosema kitanihukumu"

mtakatifu

"bila kosa"

maneno yangu yatashuhudia kuwa ni mwenye kosa

Hapa "maneno yangu" yameongelewa kana kwamba yanaweza kutenda jambo. "Mungu atatumia kile ninachosema kuthibitisha mimi ni mwenye kosa"

mwenye makosa

Neno hili hapa linamaanisha "kugeuzwa" au "mdanganyifu."

Job 9:21

Mimi ni mtakatifu

"Mimi ni kamili"

kuhusu mimi mwenyewe

"nini kinanitokea"

Haileti tofauti

"yote ni sawa" au "haina shida"

huangamiza watu wasio na makosa na waovu pia

"yeye huwafikisha kila mmoja mwisho, kama ni wasio na kosa au waovu"

Kama hilo pigo liliua ghafla

"Kama baa linaweza kuua watu ghafra"

mateso ya watu wasio na makosa

Jina la kufikirika "wasio na makosa" linaweza kutafasiriwa kama kitenzi "tesa." "wakati watu wasio na makosa wakiteswa"

Dunia imetiwa

Hii inaweza kusemwa katika hali halisi. "Mungu anatoa nchi"

Dunia

Hapa "nchi" imetumika kuwakilisha watu waishio juu ya nchi. "Watu wa ulimwengu ni"

mkononi mwa

Hapa "mkono" ni mfano wa "udhibiti." "chini ya udhibiti wa"

Mungu hufunika nyuso za waamuzi

Usemi huu unamaanisha Mungu huwasimamia waamuzi wa nchi katika kuweza kuona tofauti kati ya wema na uovu. "Mungu huwapofusha waamuzi" au "Mungu husimamia waamuzi katika kutoa hukumu kwa haki"

kama si yeye hufanya, ni nani basi?

"Kama si Mungu ambaye hufanya mambo haya, halafu nani hufanya haya?"

Job 9:25

Siku zangu zinapita haraka kuliko tarishi akimbiae

Ayubu analinganisha namna siku zake zinavyopita upesi na mkimbiaji mwenye kasi. "Siku zangu zinapita kwa haraka"

tarishi akimbiae

"mkimbiaji" au "mtu anayekimbia"

siku zangu zinakimbia mbali

Hii inazielezea siku za maisha ya Ayubu kama zinaweza kukimbia mbali kama mtu.

hazioni mema mahali popote

Hii inazielezea siku za maisha ya Ayubu kama zinaweza kuona kama mtu.

hakuna mema

"hakuna jambo jema"

Zinapita kwa kasi kama mashua zilizoundwa kwa mafunjo

Ayubu analinganisha namna siku zake zinavyopita kwa upesi na mwendo kasi wa mashua. "Zinapita haraka kama mashua zilizotengenezwa kwa mafunjo"

mashua zilizoundwa kwa mafunjo

"mashua iliyotengenezwa kwa mafunjo." Mafunjo ni majani yenye shimo ambayo humea pembezoni mwa kingo za mito.

zinakasi kama tai ashukaye upesi katika mawindo yake

Ayubu analinganisha namna siku zake zinavyopita upesi na ndege mkubwa ashukaye upesi kuelekea kwenye mawindo. "ana kasi kama tai ashukae chini kwa kasi kukamata chakula chake.

shuka chini kwa kasi

"kuharakisha kwenda chini"

Job 9:27

mimi nitasahau kuhusu manung'uniko yangu

Jina la kufikirika "nung'uniko" linaweza kutafasiriwa kama kitenzi "lalamiko." "Mimi nitaacha kulalamika" au "Mimi nitaacha kulalamika dhidi ya Mungu"

manung'uniko yangu

habari zilizo husika zinaweza kuongezwa. "malalamiko yangu dhidi ya Mungu"

nitaacha kuonyesha sura ya huzuni na kuwa na furaha

Sura yenye huzuni ya Ayubu inaongelewa hapa kana kwamba kitu fulani ambacho kinaweza kuondolewa. "Mimi nitaacha kuonekana mwenye huzuni na kutabasamu"

Mimi nitaziogopa huzuni zangu zote

Mstari wa 28 na 29 zinaelezea matokeo kama Ayubu atafanya yale anayosema katika mstari 27. "Tena mimi nitaogopa kwa ajili ya huzuni zangu"

huzuni zangu zote

Jina la kufikirika "huzuni" linaweza kuonyeshwa kama kitenzi. "nini kitanidhuru"

Nitahukumiwa

"Mimi nitashitakiwa na kuadhibiwa." Hili linaweza kusemwa katika sura ya kutenda. "Mungu atanihukumu"

kwa nini, basi, nitaabike bure?

Ayubu anatumia swali hili kusisitiza kwamba yeye hafikirii kama kuna maana yoyote kujaribu kuupata usikivu wa Mungu. Taarifa za kuashiria kuhusu kile Ayubu anajaribu zinaweza kufanywa wazi. "Haina maana kujaribu kuupata usikivu wa Mungu"

Job 9:30

Kama najiosha mwenyewe kwa maji ya theluj

"Kama nimeoga tu, maji safi"

kuitakasa mikono yangu na kuwa safi zaidi

"kuifanya mikono yangu safi sana." Baadhi ya tafsiri zingine za Biblia zinafasiri hiki na maana ya "nimeosha mikono yangu na sabuni kali sana."

nitumbukize shimoni

"nitupe shimoni"

nguo zangu mwenyewe zitanichukia

Nguo za Ayubu zinazungumziwa kana kwamba zina jibu hasi kwa Ayubu baada ya Mungu kumtumbukiza yeye shimoni. "Mimi nitakuwa mchafu sana kwa ajili ya nguo zangu mwenyewe"

Job 9:32

mjibu yeye

Taarifa za kuashiria zinaweza kuongezwa. "nitajibu mashitaka yake dhidi yangu" au "nitajitetea mwenyewe" au "nitahojiana naye hali yangu yakutokuwa na hatia"

tukaribiane katika hukumu

"tuwe pamoja kwenye hukumu." Hapa "mahakama" ni sehemu ambayo watu wanaweza kuja na hakimu ataamua ugomvi. Kuwa pamoja mahakamani" ni mfano wa kupingana kila mmoja kisheria mahakamani."kila mmoja kutetea upande wake mbele ya hakimu."

Hakuna hakimu baina yetu

Hii inamaanisha hakuna hakimu ambaye ni mkuu kuliko Mungu ambaye anaweza kuamua lipi ni jema kati yake na Ayubu.

weka mkono wake juu

Hapa "weka mkono wako juu ya" inamaanisha kuwa na uwezo au mamlaka zaidi. "uwezo wa kuamua" au "kuwa na mamlaka zaidi"

Job 9:34

Habari unganishi:

Mistari hii inaendeleza hoja ya kwanza kwamba hakuna hata mmoja aliye mkuu kuliko Mungu ambaye anaweza kutenda kama hakimu kati ya Mungu na Ayubu.

niondolee fimbo ya Mungu

Hapa "fimbo ya Mungu" ni mfano wa Mungu anamwadhibu au anamrekebisha Ayubu. "acha Mungu kuniadhibu mimi"

awezaye kuzuia kitisho chake kisinitie hofu

Jina la kufikirika "kitisho" inaweza kutafasiriwa kama kitenzi "tisha." "mzuie kunitisha na kuniogofya mimi"

kisha ningesema

"kisha ningeliweza kusema"

kama mambo yalivyo sasa

"kwasababu hivi ndivyo mambo yalivyo sasa"

Job 10

Job 10:1

Nimechoka na maisha yangu

"mimi nimechoka kuishi"

Nitanena wazi manung'uniko yangu

Jina la kufikirika "usemi" na "lalamiko" yanaweza kutafasiriwa kama vitenzi "eleza" na "nung'unika." "Mimi nitaeleza wazi kile ninachonung'unikia" au "Mimi nitahoji wazi"

nitasema kwa uchungu wa roho yangu

Namna gani Ayubu anavyojisikia inalinganishwa na ladha chungu. Jina la kufikirika "chungu sana" inaweza kutafasiriwa kama kielezi "chungu." "Utu wangu wa ndani utaongea kwa uchungu" au "Kwa uchungu nitasema sana"

ni vizuri kwako wewe kunionea mimi, kudharau kazi ya mikono yako wakati unafurahia juu ya mipango ya waovu?

Swali hili linahitaji jibu la "hapana" na inaweza kubadilishwa na kuwa habari. "Si vyema kwamba unaweza kunikandamiza mimi, kwamba unaweza kudharau kazi ya mikono yako, wakati ukifurahia juu ya mipango ya waovu."

kazi ya mikono yako

Hapa mikono inawakilisha uwezo wa kuumba wa Mungu. "kile ulicho kiumba"

unafurahia juu ya mipango ya waovu

Hapa usemi "ridhia" ni mfano wa kibali cha Mungu."kubali mipango ya waovu"

Job 10:4

Je wewe una macho ya kimwili? Je wewe unaona kama mtu aonavyo?

Mswali haya mawili yanamaana zinazo karibiana. Maswali haya yatarajia jibu hasi kusisitiza kwamba Mungu haoni au kuelewa mambo kama vile mtu aelewavyo. Yanaweza kuelezewa kama habari. "Wewe huna macho ya mwili, na hautazami kama mtu atazamavyo."

Je siku zako ni kama siku za wanadamu au miaka yako ni kama miaka ya watu ... na hapana mwingine awezaye kuniokoa mimi na mkono wako?

Swali hili linatarajia jibu hasi kusisitiza kwamba Mungu ni waa milele na siku za mtu ni ndogo. Linaweza elezewa kama habari. "Siku zako si kama siku za mwanadamu na miaka yako si kama miaka ya watu ... na hapana yeyote ambaye ataweza kuniokoa mkoni mwako."

siku zako ni kama siku za wanadamu ... miaka yako ni kama miaka ya watu

Vifungu hivi viwili vina maana zinazokaribiana.

siku zako

"hesabu ya siku zako"

miaka yako

"hesabu ya miaka yako"

ukauliza habari za uovu wangu ...kutafuta dhambi yangu

Vifungu hivi viwili vinamaana zinazo karibiana.

hata ukauliza

"tena ukatafuta"

kutoka mkoni mwako

Hapa "mkono wako" ni mfano nguvu za Mungu. "kutoka nguvuni mwako"

Job 10:8

Mikono yako

Hapa "mikono" ni mfano wa Mungu na ubunifu wake wa kufanya. "Wewe"

Mikono yako imeniumba na kunifinyanga kwa wakati mmoja nawe kunizunguka

Ayubu anatumia sitiari ya mfinyanzi atengenezaye udongo kuelezea namna Mungu alivyo muumba yeye kwa uangalifu mkubwa.

imeniumba na kunifinyanga

"amenipa umbo na kunitengeneza." Maneno "umbwa" na "finyangwa" yana maana inayolandana.

fikiri

"kumbuka"

utanirudisha mavumbini tena

"nirudishe tena mavumbini"

Job 10:10

Habari za Jumla:

Katika mistari hii, Ayubu anatumia lugha ya ushairi kuelezea namna Mungu alivyo muumba yeye katika tumbo la uzazi.

Je wewe hukunimimina kama maziwa na kunigandisha mfano wa jibini?

Hili ni swali ambalo linatarajia jibu halisi. "Wewe ulinimimina kama maziwa na kunigandisha kama jibini." au "Wewe umenitengeneza mimi katika tumbo la uzazi kama maziwa yamiminavyo na kuwa jibini."

Wewe

Hapa "wewe" linahusiana na Mungu.

mimi

Hapa "mimi" linahusiana na Ayubu.

Umenivika ngozi na nyama

Mungu kuweka ngozi na nyama juu ya mwili wa Ayubu inaongelewa kana kwamba Mungu alimvisha nguo yeye. "Wewe umeweka ngozi na nyama juu ya mwili wangu"

niunganisha pamoja

"umenifuma." Mungu anaunganisha mwili wa Ayubu katika tumbo la uzazi inaongelewa kana kwamba Mungu alikuwa anafuma au anashona kipande cha nguo."niunganishe"

misuri

"mikano." Hizi ni sehemu za mwili ambazo huunganisha misuli na mifupa au sehemu zingine za mwili na ziko kama kwamba ni ngumu, utepe mweupu au kamba nyembamba.

Job 10:12

Wewe umenizawadia mimi uhai na ahadi ya upendeleo

Hapa jina la kufikirika "maisha" linamaanisha maisha ya mwili na "ahadi ya upendeleo" inahusiana na Mungu kuwa mwaminifu kwa ahadi zake. Yanaweza kutafsiriwa kama vitenzi. "Wewe umeniruhusu kuishi na kwa uaminifu hunilinda mimi"

usaidizi wako

"utunzaji wako"

umeilinda roho yangu

Hapa "moyo" inahusiana na maisha ya Ayubu. "umenikinga mimi" au "umenichunga kwa uangalifu sana mimi" au "umeniweka mimi salama"

mambo haya uliyaficha moyoni mwako

Hapa "mambo haya" yanahusiana na mambo yaliyoongelewa katika mistari inayofuata.

mambo haya uliyaficha moyoni mwako

Hapa "umeficha moyoni mwako" inamaanisha Mungu ameyaweka siri au umeyaficha. "mambo haya umeyaweka siri"

wewe utaizingatia

"wewe utanilinda mimi"

Job 10:15

Kama mimi ni muovu

"Kama mimi ni muovu" au "Kama mimi nafanya mambo maovu"

ole wangu

"jinsi ngani itakuwa ya kutisha kwangu"

hata kama ni mwenye haki

"hata kama mimi mara zote hufanya mambo vizuri"

inua kichwa changu

Msemo huu unamaanisha kuwa na uhakika or tumaini. "nitazidi kutazama juu" au "kuwa na tumaini" au "kuwa na uhakika kuhusu mimi mwenyewe"

nimejaa aibu

Jina la kufikirika "aibu" linaweza kutafsiriwa kwa kutumia kivumishi "aibika." "Mimi nimejawa na kuaibika"

aibu

"fedheha"

na ninayaangalia mateso yangu

Jina la kufikirika "mateso" linaweza kutafsiriwa kwa kutumia kitenzi "teseka." "na ninaangalia jinsi gani mimi nateseka"

na ninayaangalia

Neno linalokosekana linaweza kuwa kuongezwa. "na mimi ninatazama"

Kama kichwa changu kikijiinua chenyewe

Msemo huu unamaanisha kuwa kujiamini au kujiona. "Kama nitakuwa na kiburi"

waniwinda kama simba

Maana zinazofaa ni 1) Mungu anamwinda Ayubu kama simba awindavyo mawindo yake au 2) Ayubu ni kama simba awindwaye na Mungu.

mara nyingine tena wajionyesha mwenyewe kuwa ni mwenye nguvu kwangu.

Kifungu hiki kinaelezea kejeri jinsi gani ma ajabu ya nguvu za Mungu yaonekanavyo kwa namna yeye anavyotenda dhidi ya Ayubu.

Job 10:17

Wewe unaleta mashahidi wapya dhidi yangu

Taabu za Ayubu kutoka kwa Mungu zinazungumziwa kana kwamba ni watu ambao wanatoa ushahidi dhidi yake.

na kuzidisha hasira zako dhidi yangu

Jina la kufikirika "hasira" linaweza kutafsiriwa kama kivumishi "mwenye hasira." "na mwenye hasira na mimi zaidi na zaidi"

wanishambulia na majeshi mapya.

Mungu kutuma taabu dhidi ya Ayubu kunazungumziwa kana kwamba Mungu mara kwa mara anatuma majeshi mapya dhidi yake.

Job 10:18

ulinitoa kwenye tumbo la uzazi

Hapa kutolewa nje la tumbo la uzazi kunahusiana na kuzaliwa duniani. "kunitoa mimi nje la tumbo la uzazi la mama yangu" au " kunileta mimi duniani"

ningekata roho

Kukata roho kwa mtu kunahusiana na kufa. "fariki"

na ili jicho lolote lisinione

Ayubu anatumia "jicho" hapa akirejea watu wote. Anatamani yeye angelikufa wakati wa kuzaliwa, kabla hajaonekana na yeyote. "kabla mtu yeyote hajaniona mimi" au "kabla ya kuzaliwa kwangu"

kuwepo

"kuishi"

ningelikuwa nimechukuliwa

"Mwili wangu ungelikuwa umechukuliwa"

Job 10:20

Je si siku zangu pekee ni chache?

Hapa "siku zangu" zinahusiana na urefu wa maisha ya Ayubu. Swali hili linataraji jibu halisi, kusisitiza kwamba Ayubu anatazamia tu kuishi siku chache zaidi. Inaweza kutafsiriwa kama taarifa. "Mimi nina siku chache tu za kuishi zilizobaki."au "Maisha yangu hivi karibuni yatafikia mwisho."

nchi

Hapa sehemu ambayo roho za watu waliokufa huenda inazungumziwa kana kwamba ilikuwa nchi. "sehemu"

kwenye nchi ya giza na kivuli cha mauti

Kifungu "kivuli cha mauti" inaongeza wazo la "giza." Vifungu vyote vinaelezea wapi roho za watu waliokufa huenda.

kivuli cha mauti

Fasiri kifungu hiki kama katika 3:4

giza kama usiku wa manane

Giza la sehemu ambapo roho za watu walio kufa huenda inalinganishwa na giza la usiku wa manane.

bila mpangilio

Hiki kifungu cha kukanusha kinaweza kuelezewa katika hali halisi. "wasiwasi mwingi" au "sehemu ambayo wote wamechanganyikiwa"

ambayo nuru yake ni kama usiku wa manane

Mwanga wa sehemu ambayo roho za watu waliokufa huenda inalinganishwa na usiku wa manane. "ambapo hakuna nuru"

Job 11

Job 11:1

Sofari Mnaamathi

Sofari kutoka sehemu ya Naamathi

Huo wingi wa maneno haupaswi kujibiwa?

Sofari anauliza swali kinyume chake kusisitiza kuwa maneno ya Ayubu lazima yakosolewe."Ni lazima tuyajibu maneno haya yote" au "Mtu yeyote angeyajibu mameno haya yote"

Mtu huyu, aliyejaa maneno mengi awe wa kuaminiwa?

Sofari anatumia swali hili kusisitiza kuwa hawapaswi kuamini kile ambacho Ayubu anachosema. "Mtu huyu amejaa maneno mengi , lakini yeye watu hawapaswi kumwamini" au " Maneno yako mengi peke yake hayamaanishi huna hatia."

Kujivuna kwako kunapaswa kuwafanya wengine wabaki wamenyamaza? "Umeyadharau mafundisho yetu.Sasa tutakufanya wewe ujisikie mweye aibu!

Sofari anatumia swali hili kumkemea Ayubu."Kwa sababu wewe umeongea maneno mengi, hii haimaanishi kuwa wengine lazima wabaki wamenyamaza."

Wakati unapoyadhihaki mafundisho yetu, hakuna awaye yote atakayekufanya wewe ujisikie mwenye aibu?

Sofari anatumia swali hili kumkemea Ayubu "

Job 11:4

Imani yangu ni safi,

"Ufahamu wangu ni sahihi"

Mimi sina waa lolote machoni pako.'

Macho yanawakilisha kuona , ni tashbiha ya tathimini juu ya Mungu kwa Ayubu. Maana zaweza kuwa 1) Ayubu anasema kwamba Mungu amemhukumu yeye kama asiye na hatia" au 2) kwamba Ayubu anaamini yeye amekuwa asiye na hatia na kwamba Mungu anapaswa kumhukumu yeye kama mwenye hatia. "Mnapaswa kutambua kwamba mimi sina hatia."

laiti, Mungu huyo angesema na kufungua midomo yake dhidi yako;

Maneno "kufungua midomo yake" ni ishara ambayo inamaanisha zungumza. Sentensi hizi mbili zinamaanisha kitu kilekile zimetumika pamoja kusisitiza shauku ya Sofari kuwa Mungu angezungumza kwa kumuumiza Ayubu.

hivyo angekuonyesha wewe siri za hekima1

Ni nini "siri za hekima". Zinaweza kuelezwa wazi hivi: "kwamba yeye angekuonyesha wewe kuwa wewe unateseka kwa sababu ya dhambi yako"

Mungu anataka kutoka kwako kidogo kuliko uovu wako unavyostahili.

Kutaka kutoka kwa Ayubu inawakilisha kuadhibiwa kwa Ayubu. "Mungu anakuadhibu wewe kidogo kuliko wewe unavyostahili"

Job 11:7

Je, wewe unaweza kumfahamu Mungu kwa kumtafuta yeye? Unaweza kumtambua aliye mkuu kwa ukamilifu?

Haya maswali mawili ya mfano yanauliza kitu kile kile. Mwandishi anatumia mfumo wa maswali kuongeza msisitizo."Wewe huwezi kumfahamu Mungu kwa kumtafuta yeye, na wewe hautaweza kabisa kumfahamu aliye mkuu"

Upeo

Hii inamaanisha kumfahamu Mungu.

uko juu kama mbingu; unaweza kufanya nini wewe ? Ni wenye kina kirefu kuliko kuzimu;

Kutokuweza kumfahamu Mungu kumezungumzwa kuwa kama vile ilikuwa haiwezekani kwenda mbali mahali pa kuzimu. "haifikiwi kama mahali pa juu mbinguni ....haifikiwi zaidi kuliko mahali pa chini pa kuzimu"

unaweza kufanya nini wewe ?

Sofari anatumia swali hili kuonyesha kuwa mtu hawezi kufanya chochote kumfahamu Mungu kabisa."wewe huwezi kufanya chochote" au " wewe huwezi kumfahamu yeye kikamilifu"

waweza kufahamu nini wewe?

Sofari anatumia swali hili kuonyesha kwamba mtu hawezi kumfahamu Mungu kwa ukamilifu."Wewe huwezi kumfahamu Mungu kwa ukamilifu" au wewe huwezi kufahamu yale yote ya kufahamu"

Vipimo vyake

Ukuu wa Mungu, au ukuu wa hekima

ni virefu kuliko nchi, na vipana kuliko bahari.

Ukuu wa Mungu au hekima umezungumzwa kama unaweza kupimwa katika umbali.

Job 11:10

kama yeye.... kumyamazisha mtu yeyote,

"Kama Mungu ...akimfunga mtu yeyote gerezezani"

kama yeye akimwita mtu yeyote hukumuni,

Jina dhahania "hukumu" laweza kutafsiriwa pamoja na tendo "hukumu." "kama Mungu akimwita mtu yeyote kwake hivyo kwamba Mungu angemhukumu yeye"

ni nani anayeweza kumzuia yeye?

Swali hili linasisitiza kuwa hakuna hata mmoja awezaye kumzuia Mungu. "Hakuna awezaye kumzuia yeye!"

hawezi yeye kuukumbuka?

Hii kinasisitiza kuwa Mungu anakumbuka dhambi. "Hakika yeye huikumbuka !

Lakini watu wapumbavu hawana ufahamu;

Jina dhahania "ufahamu" laweza kuelezwa pamoja na kitenzi "fahamu." "Lakini watu wapumbavu hawafahamu"

wataupata wakati punda mwitu atakapozaa mtu.

Kwa kuwa punda mwitu hawezi kuzaa mtu, maneno haya yanamaanisha kwamba watu wapumbavu hawatapata ufahamu. "ni pale tu ikiwa punda mwitu atakapozaa mtu ndipo watu wapumbavu watapata ufahamu" au "haiwezekani kwa mtu mpumbavu kupata ufahamu kama ilivyo kwa punda kuzaa mtu."

Job 11:13

ikiwa umeuelekeza moyo wako kwa haki

Moyo huwakilisha fikra na mitazamo. Kuuelekeza inawakilisha kuusahihisha. "hata kama wewe umeusahihisha mtazamo wako."

na umeunyosha mkono wako karibu na Mungu;

Hiki ni kitendo cha ishara kuwakilisha kumwomba Mungu msaada. "na amefanya kusihi, ameomba kwa Mungu.

ikiwa huo uovu ulikuwa katika mikono yako

Mkono unawakilisha kile ambacho mtu anakifanya. "hata ikiwa wewe umefanya vitu viovu katika wakati uliopita."

lakini hivyo tena unauweka mbali nawe,

Kuiweka dhambi nyuma inawakilisha kuacha kutenda dhambi. "lakini kwamba tena wewe unaacha kufanya dhambi."

haukuruhusu kutokuwa mwenye haki kukaa hemani mwako.

Maisha yasiyo ya haki yanawakilisha watu kufanya mambo yasiyo ya haki. "na wewe hukuwaruhusu watu wa nyumba yako kufanya mambo yasiyo ya haki."

Job 11:15

inua juu uso wako bila ishara ya aibu;

"Inua juu uso wako" inawakilisha mtazamo wa mtu mwenye kujiamini na ujasiri"

ungeyakumbuka hayo tu kama maji ambayo yametiririka mbali.

Sofari analinganisha ukiwa na maji ambayo hutiririka chini na yanapotea. "Wewe ungeyakumbuka, lakini mateso yatatoweka kama maji ambayo yametiririka mbali.

Maisha yako yangekuwa angavu kuliko adhuhuri;

Sofari anarudia wazo lile lile kwa msisitizo.

Maisha yako yangekuwa angavu kuliko adhuhuri

mga'o unawakilisha kuwa mwenye mafanikio na furaha. "Maisha yako yangefanikiwa na furaha kama adhuhuri"

japokuwa kulikuwa na giza,

giza linawakilisha mahangaiko na huzuni."Ingawa kulikuwa ya giza na huzuni"

itakuwa kama asubuhi.

Asubuhi inawakilisha mwanga, ambao unawakilisha mafanikio na furaha. "yatakuwa mafanikio na furaha kama asubuhi"

Job 11:18

Ungekuwa salama...utachukua pumziko lako katika usalama.

Sofari anarudia wazo lilelile kwa msisitizo na anaelezea uwezekano.

utachukua pumziko lako katika usalama

"Chukua pumziko lako" ni nahau kwa "pumziko" maneno" katika pumziko" yanaweza kuelezwa pamoja na neno" salama" ungepumzika salama"

Pia ungelala chini katika pumziko,

Sofari anarudia wazo lilelile kwa msisitizo na anaelezea uwezekano.

ungelala chini katika pumziko

jina dhahania "pumziko" kinaweza kuelezwa pamoja na kitenzi "pumzika" "wewe ungelala chini na kupumzika"

Job 11:20

macho ya watu waovu yatashindwa;

Macho yao yanawakilisha ufahamu wao. "ufahamu wa watu waovu utashindwa" au "watu waovu hawataweza kufahamu"

tumaini lao la pekee litakuwa pumzi yao ya mwisho ya uhai.

Jina dhahania "tumaini" chaweza kuelezwa pamoja na kitenzi "tumaini" pumzi ya mwisho ya uhai inawakilisha kufa. " "Tumaini lao pekee litakuwa pumzi yao ya mwisho" au " watatumaini kufa tu"

Job 12

Job 12:1

Hakuna shaka

"Hakika"

ninyi wanadamu

"ninyi ni watu muhimu mnafahamu kila kitu"

Hakuna shaka ninyi wanadamu; Hekima mtakufa nayo

Ayubu anawadhihaki jinsi gani wanavyotenda na kuonyesha jinsi walivyo wenye kudhihaki. "Hakika ninyi ni watu muhimu kwamba hekima haiwezi kuwepo bila ninyi" au " Ninyi nyote mnatenda kama ninyi ni watu wenye hekima peke yenu, na kwamba wakati mtakapokufa hekima itapotea"

ninyi

Huu ni wingi hapa na katika sentensi mbili zifuatazo.

Ni dhahiri, ni nani asiyefahamu vitu hivyo kama hivi?

Ayubu anatumia swali hili kuelezea ukweli ambao unapaswa kuwa wazi kwa wasikilizaji wake. Sentensi hii inaweza kuelezwa kwa jinsi hii: Ni dhahiri hakuna awaye yote ambaye hafahamu vitu kama hivi" au "kila mtu anafahamu vitu hivi"

Job 12:4

Mimi ni kitu cha kuchekwa na jirani-Mimi, ni mmoja aliyemwita Mungu na ambaye alijibiwa na yeye!

Uhusiano baina ya tungo hizi unaweza kufafanuliwa na maneno " japokuwa" "Mimi ni kitu cha kuchekwa na jirani zangu-ingawa ni mmoja aliye mwita Mungu na yeye alinijibu mimi"

Mimi, ni mwenye haki na mtu asiyekuwa na hatia-Mimi sasa nimekuwa kitu cha kuchekwa.

Uhusiano kati ya tungo hizi "japokuwa" "Japokuwa mimi ni mwenye haki na mtu asiyelaumika, sasa watu ananicheka"

Katika mawazo yake mtu fulani aliye katika kufurahi, kuna kudharau kwa mashaka;

Maneno " mawazo", "rahisi" "dhihaka" "bahati mbaya"yaweza kuelezwa pamoja na tungo zingine. "Mtu anayeishi katika maisha rahisi humchukia mtu anayeteseka"

huleta mambo mabaya zaidi kwa wale ambao miguu yao inateleza.

Kuleta mambo mabaya ina maanisha kuyasababisha kutokea. "kusababisha vitu vibaya zaidi kutokea"

ambao miguu yao inateleza

Mguu kuteleza inamaanisha kuwa katika hatari au mahangaiko"

Hema za wezi hufanikiwa,

Kufanikiwa kwa hema zao kunawakilisha wezi kufanikiwa katika hema zao. "Wevi huishi katika kufanikiwa ndani ya hema zao wenyewe"

mikono yao wenyewe ni miungu wao.

"Mikono yao wenyewe" kiwakilishi cha "nguvu na " na "miungu yao" ni tashbiha kuelezea kiburi chao. "wao wanajivuna sana kwa uwezo wao wenyewe"

Job 12:7

7Lakini sasa waulize... watakuambia wewe.

Tungo hizi nne zote zinaelezea wazo moja kwamba wanyama wa mwituni, ndege, ardhi, na samaki, wanamfahamu Mungu vizuri kuliko rafiki za Ayubu wanavyofanya.

waulize hao wanyama wa mwituni, na watakufundisha wewe;

Kiambishi tashihisi katika sehehemu ya kwanza ya sentensi kinatumika kuonyesha hali ya kutokuwa na uhakika wa jambo kutokea. "Lakini ungewauliza hayawani wangekufundisha wewe"

waulize ndege wa angani, na watakuambia wewe

Tashihisi katika sentensi hii inatumika kuonyesha hali ya kutokuwa na hakika ya jambo kutokea. "kama wewe ungewauliza ndege wa angani, wao wangekuambia wewe"

Au iambie ardhi, na itakufundisha wewe;

Kiambishi tashihisi katika sehemu ya kwanza ya sentensi hii kinatumika kuonyesha hali ya kutokuwa na uhakika wa jambo kutokea "Au kama ungeiambia ardhi ingekufundisha wewe"

samaki wa baharini watakutangazia wewe.

Kiambishi tashihisi "Waulize samaki wa baharini" kimefahamika kutoka katika sentensi zilizotangulia."na kama ungeliwauliza samaki wa baharini, wangekutangazia wewe"

Job 12:9

Ni myama yupi miongoni mwa hawa asiyefahamu kuwa mkono wa Yahwe umetenda haya

Swali hili linasisitiza mantiki ya kwamba wayama wote wanatambua kuwa Yahwe amefanya haya. Ina maanisha , "Kila mnyama anafahamu....haya."

mkono wa Yahwe umetenda haya?

Mkono wa Yahwe unawakilisha nguvu zake. "Yahwe ametenda haya kwa nguvu zake"

Katika mkono wake mna uzima...na pumzi ya wanadamu wote.

Mkono wa Yahwe unawakilisha udhibiti wake au nguvu. Vitu kuwa katika mikono yake inawakilisha uweza wake kuvidhibiti. "ambaye anadhibiti uhai wa kila kiumbe hai na ataoa uhai kwa kila mwanadamu"

pumzi ya wanadamu

"Pumzi" inawakilisha uzima au uwezo wa kuishi

Job 12:11

Je, sikio haliyajaribu maneno kama vile kaakaa lionjavyo chakula chake?

Ayubu anatumia swali hili kusisitiza kuwa watu husikiliza kile ambacho watu husema na kuhukumu ikiwa ni vizuri au hapana. Sikio na kaakaa ni mfano wa kusikia na kuonja. " Huwa tunasikia kile ambacho watu husema na kukionja kama vile tunavoonja chakula"

Kwa wazee mna hekima;

"Watu wazee wana hekima" kivumishi cha jina "hekima" chaweza kuelezwa pamoja na "ufahamu." Neno "watu" linamaanisha watu wote kwa ujumla. "watu wazee ni wenye hekima"

katika wingi wa siku mna ufahamu.

Tungo "wingi wa siku" ni kuonyesha kuishi kwa muda mrefu.Ufahamu uko katika wingi wa siku kuwakilisha watu kupata ufahamu wakati wanapoishi muda mrefu. Kivumishi cha jina "ufahamu" kinaweza kuelezwa na tungo "ufahamu mwingi" "Watu hupata ufahamu mwingi wakati wanapoishi muda mrefu" au " Watu ambao huishi muda mrefu hufahamu mengi"

Job 12:13

habari za Jumla:

Mstai wa 13 unasema kuwa Mungu ni mwenye hekima na mkuu. Mwisho wa sura hii inaonyesha kuwa hii ni kweli kwa kuzungumza kuhusu mwenye hekima na vitu vikuu ambavyo Mungu hufanya.

Pamoja na Mungu mna hekima na ukuu

Kivumishi cha jina "hekima" na" ukuu" vyaweza kuelezwa na kivumishi "busara" na "ukuu Mungu ni mwenye hekima na "ukuu"

Tazama

Neno hili linamkumbusha Ayubu wakati Ayubu alipohitaji msikilizaji kuwa na mwitikio maalumu.

haiwezekani kujengwa tena;

Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa jinsi hii: "Hakuna awezaye kujenga tena"

kama yeye akimtia gerezani mtu yeyote, hakutakuwa tena kufunguliwa

Kama Mungu akimfunga mtu yeyote, hakuna awezaye kumfungua yeye."

kama yeye akiyazuia maji, yanakauka

Maana zaweza kuwa: 1)kuizuia mvua isinye. "kama akiizuia mcvua isinyeshe ardhi hukauka" au 2) kuzuia maji yasitiririke . " "kama yeye akiyazuia maji yasitiririke, ardhi hukauka"

kama akiyaachilia nje yanaitaabisha nchi

Maana zaweza kuwa: 1)kufanya mvua inyeshe) 2"kama akaiifanya mvua kubwa kunyesha, huigharikisha nchi" au" kuyafanya maji yafurike "kama akiyafanya maji mengi kufurika, huigharikisha nchi"

Job 12:16

Pamoja na yeye mna nguvu na hekima;

"Mungu ni mwenye nguvu na hekima"

watu ambao wamedanganywa na mdanganyi wote pamoja wako katika nguvu zake.

Kuwa katika nguvu za Mungu inawakilisha Mungu anatawala juu yao. "Watu ambao wanauamini uongo, na watu ambao huwadanganya wengini wote pamoja wako katika nguvu zake" au " Mungu anatawala juu ya wote wanaouamini uongo na watu ambao huwadanganya wengine"

Yeye huwaongoza washauri mbali bila kuvaa viatu

Kuwaongoza washauri mbali bila kuvaa viatu huwakilisha kuondolea mbali hekima yao na mamlaka yao.

katika huzuni;

Kielezi cha jina "huzuni" kinaweza kuelezwa pamoja na maneno "majonzi" msiba" "na wanajisikia wenye huzuni sana" au na wana majonzi"

huwarudisha hakimu katika upumbavu.

"yeye huwafanya wahukumu kuwa wapumbavu"

Yeye Huondoa minyororo ya mamlaka kutoka kwa wafalme;

Maaana zaweza kuwa: 1) kuwafanya wafalme kutokuwa na mamlaka tena. "Yeye huondoa mamlaka ya wafalme" au 2) huu ni mfano wa kuwaweka watu huru kutoka katika minyororo ambayo wafalme wameiweka juu yao) "yeye huondoa utumwa ambao wafalme wameuweka juu yao."

yeye hufunika viuno vyao kwa nguo.

Nguo hii huenda ambayo mtumwa huvaa. Kuvaa nguo hizi kwa wafalme inawakilisha kuwafanya wafalme kuwa watumwa" au " yeye huwafanya kuwa watumwa"

Job 12:19

Yeye huwaongoza makuhani mbali bila kuvaa viatu

Kuwaongoza makuhani mbali bila kuvaa viatu inawakilisha kuondolea mbali mamlaka yao.

Yeye humwaga aibu

"aibu" inaweza kuelezwa kuwa ni huzuni, au majonzi." na wanajisikia wenye huzuni zana"

kuwapindua watu wakuu.

"huwashinda watu wenye nguvu"

Yeye huondoa hotuba ya wale waliokuwa wameaminiwa

Kuondoa hotuba zao kunawakilisha kuwafanya wao washindwe kuzungumza."Yeye huwafanya wale waliokuwa wameaminiwa kutoweza kuzungumza" au "Yeye huwanyamazisha watu ambao wengine wanawatumainia"

huondoa mbali ufahamu wa wazee

Kuondolea mbali uafahamu wao kunawakilisha kutoweza kufahamu au kufanya maamuzi sahihi. "huwafanya wazee washindwe kufahamu: au " huwafanya wazee wasiweze kufanya maamuzi sahihi"

wazee.

"watu wazee" au" wazee"

Yeye humwaga aibu juu ya binti za wafalme

Kumwaga aibu juu ya binti za wafalme ni kuwasababishia watu kujisikia wenye huzuni juu yao." Yeye huwafanya watu kutowaheshimu sana wale wanaotawala"

hufungua mishipi ya watu wenye nguvu.

Mshipi ni alama ya nguvu.Kufungua mshipi wa mtu menye nguvu huwakilisha kuondolea mbali nguvu zake na kumfanya awe dhaifu"

Job 12:22

Yeye huweka wazi vitu vya kina kutoka katika giza

Kuviweka wazi vitu ikiwa ni kuvifanya vijulikane. " Vitu vya kina kutoka katika giza" huwakilisha siri ambazo watu hawazijui. "Yeye huzifanya siri kujulikana ambazo watu hawazifahamu"

kuvileta nje kumuika vivuli mahali ambapa watu waliokufa wapo

Kuvileta vitu nje inawakilisha kuvifanya vijulikane."hufanya mahali ambapo wafu waliko pajulikane"

huyafanya mataifa kuwa na nguvu

"Yeye hufanya kupanuka kwa nchi ya watu waliojikusanya pamoja kuwa kubwa" au " Yeye hufanya mataifa kuchukua ardhi zaidi"

pia yeye huyaongoza mbali kama wafungwa.

Mungu kuyaongoza mataifa kunawakilisha Mungu kuwafanya adui za mataifa kuwaongoza. Neno "wao" linawakilisha watu wa mataifa hayo. " Yeye pia huwafanya adui zao kuwaongoza wao mbali kama wafungwa"

Job 12:24

Yeye huondoa mbali ufahamu kutoka kwa viongozi wa watu wa nchi

Kuondolea mbali ufahamu wao inawakilisha kuwafanya wao wasiweze kufahamu"Yeye huwafanya viongozi wa watu wa nchi kutoweza kufahamu.

kutangatanga msituni mahali pasipo na njia.

Kutangatanga nyikani mahali pasipo na njia kunawakilisha kuwa katika wakati mgumu na kutokujua nini cha kufanya. "kuwa na hakika ya nini cha kufanya kama mtu anayetangatanga katika nchi ya uharibifu pasipo na njia.

Wao wanapapasa katika giza bila kuwa na mwanga

Kuwa katika giza bila mwanga kunawakilisha kukosa maarifa ."Wao wanahangaika kufanya maamuzi bila kuwa na maarifa kama vile watu wanavyohangaika kutembea katika giza bila mwanga.

yeye huwafanya wao kuweweseka kama mtu mlevi.

Kuweweseka au kutangatanga kama mtu mlevi kunawakilisha kuishi bila matumaini kama mtu mlevi ambaye huweweseka anapotembea.

Job 13

Job 13:1

Sentensi Unganishi:

Sentensi unganishi: Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Tazama

"Kuwa msikivu" au "Sikiliza" "maneno haya yanakumbusha pale Ayubu anapowataka rafiki zake kusikiliza kwa makini"

jicho langu limeyaona haya yote;

Ayubu anajisema yeye mwenyewe kama macho yake kwa kuwa ni macho yake ambayo yanaona vitu hivi. "Mimi nimeyaona haya yote"

sikio langu limeyasikia na kuyaelewa hayo.

Ayubu anasema yeye mwenyewe kama sikio lake kwa kuwa kwa masikio yake yeye mwenyewe amesikia vitu hivi. "Mimi nimesikia na kuvielewa"

Kile mnachokifahamu, ndicho hicho mimi pia ninachokifahamu;

Kile mnachokifahamu, Mimi pia ninakifahamu" au "Mimi ninafahamu mengi kama vile ninyi"

Job 13:3

Mimi natamani kusemezana na Mungu.

Rafiki za Ayubu wanamhukumu yeye, lakini hawazungumzi ukweli. Ayubu zaidi angehojiana na Mungu kuhusu malalamiko yake .

ninyi mnauficha ukweli kwa uongo;

Kuweka uongo au kuufunika uongo inawakilisha kuupuuza ukweli. "ninyi mnauficha ukweli kwa uongo" au " niniyi mnadanganya na kuupuuza ukweli"

ninyi nyote ni tabibu msiokuwa na thamani

Kuwa tabibu inawakilisha kuwa mtu ambaye huwafariji wengine. Kuwa asiye na thamani ina maanisha kwamba wao hawafahamu jinsi ya kufanya kile wanachopaswa. "Ninyi nyote ni kama tabibu ambao hawajui kuwaponya watu" au " ninyi nyote mnakuja kunifariji mimi, lakini hamtambui jinsi ya kufanya, kama tabibu asiyekuwa na weledi"

shikilieni amani yenu!

Inamaanisha: "nyamazeni "au acheni kuzungumza"

Hilo lingekuwa hekima yenu ninyi.

Walidhani kuwa walikuwa wanasema vitu vya busara lakini Ayubu alikuwa anasema kwamba wanapaswa kuwa wenye busara kama wangeacha kuzungumza. Kielezi cha jina "hekima" Chaweza kuelezwa na neno "busara" "kama niniyi mngefanya hivyo, ninyi mngekuwa wenye busara" au " kama ninyi mngeacha kuzungumza, niniyi mngeonekana wenye busara"

Job 13:6

Sentensi Unganishi:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Sikiliza kusihi kwa midomo yangu mwenyewe

Hapa neno "midomo" linawakilisha mtu anayezungumza. "sikiliza kile ambacho mimi mwenyewe nikusihi"

Ninyi mtazungumza visivyo haki kwa ajili ya Mungu, na ninyi mtazungumza udanganyifu kwa yeye?

Ayubu anatumia maswali haya mawili kuwakemea rafiki zake kwa kuzungumza visivyo haki. "Ninyi mnafikiri kwamba mnazungumza kwa Mungu, lakini mnazungumza visivyo haki." Ninyi mnazungumza udanganyifu"

mtazungumza udanganyifu

"uongo", sema "uongo"

Ni kweli ninyi mngetetea katika mahakama kama mawakili wa Mungu?

Kuonyesha upole kwa Mugnu kunawakilisha kumsaidia Mungu au kumtetea Mungu dhidi ya malalamiko ya Ayubu. Ayubu anatumia maswali haya mawili kuwakemea rafiki zake kwa kufikiri kwamba wanaweza kumtetea Mungu. " Ninyi mnafikiri kuwa mnaweza kumtetea Mungu. Ninyi mnafikiri mnaweza kutetea kama mawakili wa Mungu katika mahakama"

Job 13:9

Je, kweli ingekuwa vizuri kwenu wakati yeye akiwatafuta ninyi

"Kuwathibitisha ninyi" ni tashbiha inayomaanisha " jitathimini ninyi" Ayubu anatumia swali hili kuwatahadharisha rafiki zake kuwa ikiwa Mungu angewatathimini wao, yeye angesema kwamba matendo yao ni mabaya. "Kama Mungu angewatathimini ninyi, isingekuwa vyema kwenu"

Mngeweza ninyi kumdanganya yeye kama mlivyoweza kuwadanganya watu?

Ayubu anatumia swali hili kuwaonya rafiki zake kuwa Mungu anaujua ukweli kuhusu wao. "Ninyi mngeweza kuwadanganya wanadamu, lakini ninyi hamuwezi kumdanganya Mungu"

mjithibitisha ninyi

"mjisahihisha ninyi"

ikiwa katika siri ninyi mmeonyesha kutokukamilika.

Kuonyesha kutokukamilika inamaanisha kusema tu mambo mazuri ili kwamba hakimu atasema kwamba mtu yule ni mwema. Kufanya hivi kwa siri inamaanisha kujifanya kuzungumza kwa haki, lakini kiukweli kumpendelea mtu mmoja dhidi ya mwingine. "kama ninyi mnaonyesha upendeleo kwa siri kwa mwingine"

Job 13:11

Je, ukuu wake usingewafanya ninyi muogope? Je, utisho wake usingeshuka juu yenu?

Ayubu anatumia swali hili kuwakemea rafiki zake: Sentensi hii yaweza kutafsiriwa hivi: 1) Ayubu anasema kuwa wanapaswa kumhofu Mungu " Ukuu wake unapaswa kuwafanya ninyi muogope, na ukuu wake unapaswa kushuka juu yenu" au 2) Ayubu anasema kwamba wao watamhofu Mungu." Ukuu wake utawafanya ninyi muogope na utisho wake utashuka juu yenu"

Je, utisho wake usingeshuka juu yenu?

Utisho wake kushuka juu ya watu inawakilisha wao kuogopa sana "Ninyi hamtaogopeshwa sana" au " Ninyi hamtaogoa sana?

Hadithi zenu za misemo ya kukariri, ni mithali zimetengenezwa kwa majivu;

Majivu yanawakilisha vitu ambavyo havina thamani na havidumu. "Hadidhi zenu hazina thamani kama majivu" au "Misemo yenu ya kukariri itasahaulika kama majivu yaliyomwagwa mbali"

utetezi wenu ni utetezi uliotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi.

Ayubu anazungumza kile ambacho wanasema kama vile kilikuwa kama ukuta kuzungumza mji uliotengenezwa kwa majivu; Hauwezi kuwalinda watu kwa sababu udongo wa mfinyanzi huvunjika kirahisi."Ninyi mnasema nini katika utetezi kama vile ni upuuzi kama ukuta wa udongo wa mfinyanzi.

utetezi wenu

Hii inamaanisha kwa kile wanachokisema kujitetea wao wenyewe. au 2) kile wanachokisema kumtetea Mungu.

Job 13:13

Shikilieni amani yenu

Hii ni nahau ionayomaanisha "Nyamaza" au Acha kuzungumza"

mniache peke yangu,

Hii ni nahau yenye maana ya "acheni kunivunja moyo mimi au " acheni kunizuia mimi"

acheni yaje yale yanayoweza kuja kwang

Vitu vinakuja juu ya mtu inawakilisha vitu vinavyotokea kwa mtu. Ni kuonyesha kinachoanza na "Acha" maana yake yeye hajali kile kinachoweza kutokea kwake. " Acheni chochote kinachoweza kutokea kwangu kitokee" au " Sijali kile ambacho kinaweza kutokea kwangu"

Nitaichukua nyama yangu mwenywewe katika meno yangu;

"Nyama" kuwakilisha maisha. "Meno" na "mikono" ni kiwakilishi cha udhibiti wake. Tungo hizi mbili pamoja zinasisitia kuwa Ayubu yuko tayari kuhatarisha maisha yake kwa kutetea hoja yake pamoja na Mungu. " Niko tayari kuyahatarisha maisha yangu"

Job 13:16

Hiki kitakuwa sababu ya kutohesabiwa hatia,

Kielezi cha jina "kutohesabia hatia" chaweza kuelezwa pamoja na kitenzi " kutohesabia hatia" "Hii ndiyo sababu Mungu hatanihesabia hatia mimi " au " Hii ni sababu ambayo Mungu atasema kwamba mimi sina hatia"

Mungu, sikiliza kwa makini

Ayubu anaanza kuelekeza hoja yake moja kwa moja kwa Mungu.

sikiliza kwa makini kuzungumza kwangu; ruhusu kutangaza kwangu kuje kwenye masikio yako.

Mistari hii miwili kimsingi inamaanisha kitu kilekile na kinatilia uzito wa ombi la Ayubu kwa Mungu kumsikiliza yeye.

ruhusu kutangaza kwangu kuje kwenye masikio yako.

Kielezi cha jina "tangazo" Chaweza kuelezwa pamoja na kitenzi "tangaza." Masikio yanawakilisha kusikiliza. "sikiliza kutangaza kwangu" au sikia kile ninachotangaza"

Job 13:18

Habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza na Mungu

Tazama sasa

Huu ni msisitizo wa kile kinachofuata." Sikiliza sasa" au "tafadhali, kipekee, sikiliza."

Nimeuweka utetezi wangu katika mpangilio,

Ameupangilia utetezi wake ni kuamua kile ambacho angesema kujitetea yeye mwenyewe. " Mimi nimefikiria jinsi nitakavyojitetea mwenyewe" au "Mimi nimeamua jinsi nitakavyojieleza mimi mwenyewe"

Ni nani anayeweza kushindana na mimi katika mahakama?

Ayubu anatumia swali hili kueleza imani yake kwamba kwa kuwa yeye yuko sahihi, hakuna awaye yote angeshindana na yeye. "Mimi siamini kuwa mtu yeyote atahojiana na mimi katika mahakama."

Ikiwa mlikuja kufanya hivyo,

"kama mlikuja kushindana dhidi yangu mimi"

ikiwa ninyi

"Ninyi" hapa ina maanisha Mungu mwenyewe.

kama mimi nilithibitishwa kukosea,

"Kama niniyi mngethibitisha mimi kuwa nimekosea"

kuyatoa maisha yangu.

"Kuyatoa maisha ya mtu ni tashbiha inayomaanisha kufa"

Job 13:20

Habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa Mungu.

kutoka katika uso wako.

"Uso" unawakilisha mtu. "kutoka kwako wewe"

Ondoa kutoka kwangu mkono wako unaotesa,

Kuondoa mkono unaotesa ni tashbiha inayomaanisha kuacha kufanya vitu hivyo. "acha kunitesa mimi"

usiache utisho wako unifanye mimi kuogopa.

Tungo "utisho wako" inamaanisha kile kinachosababisha watu kumwogopa Mungu"

Job 13:23

Habari za Jumla"

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa Mungu.

Kwa nini unaficha uso wako kutoka kwangu mimi na kunitendea mimi kama adui yako?

Ayubu anauliza swali hili kulalamika kuhusu jinsi Mungu anavyomtendea yeye. Yeye huenda anategemea jibu.

unaficha uso wako kutoka kwangu mimi

Mtu kuficha uso wake inawakilisha kukataa kumtazama yeye au kumpuuza yeye. Wewe unakaa kunitazama mimi" au " wewe unanipuuza mimi"

Je, wewe utalitesa jani linalopeperushwa

Ayubu anatumia swali hili kumwambia Mungu kuwa Ayubu si wa muhimu na ni dhaifu, ni hasara kumtesa yeye"

jani linalopeperushwa....bua kavu

"Jani" na "bua" ni tashbiha ikielezea udhaifu wa Ayubu, kutokuwa wa muhimu, na kutokuwa mwenye nguvu. "Wewe unanitesa mimi, lakini niko dhaifu kama jani lililopeperushwa na upepo na si wa maana kama bua kavu"

Job 13:26

Habari za Jumla:

Ayubu anamaliza kutoa hoja yake kwa Mungu.

Kwa maana wewe unaandika chini vitu vichungu dhidi yangu mimi;

"Vitu vichungu" vinawakilisha mashitaka. " wewe waandika chini mashitaka dhidi yangu"

wewe unanifanya mimi kurithi uovu wa ujana wangu.

maanza zaweza kuwa 1) kuwa mwenye hatia kwa dhambi za ujana wangu au 2) Kuwa ameadhibiwa kwa dhabi za ujana wake. "wewe waniadhibu mimi kwa dhambi za ujana wangu"

uovu wa ujana wangu.

kielezi cha jina "ujana" kinawezakutafsiriwa pamoja na neno" kijana." "Dhambi ambazo mimi nilitenda wakati nilipokuwa kijana"

Wewe pia unaiweka miguu yangu katika nguo nyembamba

Kufanya hivi kunawakilisha kumwadhibu Ayubu na kumzuia kuishi kwa uhuru kama vile Ayubu ametenda kosa la kihalifu na alikuwa mfungwa. " Ni kama vile wewe unaniweka miguu yangu katika gunia."

nguo nyembamba

Ni kitu ambacho huzuia miguu ya mfungwa kwamba hawezi kabisa kujongea hata kidogo. au ni mnyororo kuzunguka miguu ya mfungwa ambayo humfanya atembee kwa shida. Hivi vimetumika kama ishara ya hukumu.

wewe waangalia njia zangu zote;

Njia huwakilisha vitu ambavyo Ayubu hufanya. " kila kitu ninachokifanya"

wewe wachunguza chini mahali ambapo nyayo za miguu yangu zimekanyaga.

Nyayo za miguu yake vinawakilisha mtu anyetembea " wew wachunguza chini mahali ambapo nimekanyaga"

wewe wachunguza chini mahali ambapo nyayo za miguu yangu zimekanyaga.

Kuchunguza hapa chini kunawakilisha kuchunguza yote ambayo Ayubu amefayafanya. "Ni kama vile ingawa wewe unachunguza chini mahali ambapo nimetembea" au Wewe wachunguza kila kitu inachokifanya kama mtu anavyochunguza nyayo za mtu alizokanyaga chini ya ardhi"

kama kitu kilichooza ambacho hutupwa mbali,

Ayubu analinganisha maisha yake kama kitu kile ambacho kinaoza. Yeye anakufa pole pole.

kama vazi lile ambalo nondo wamelila.

Ayubu anajilinganisha yeye mwenyewe na nguo iliyotoboka toboka kwa sababu nondo wa wamelila sehemu zake.

Job 14

Job 14:1

Habari za Jumla:

Sura hii ni mwendelezo wa hotuba ya Ayubu, iliyoanza 12:1. Ayubu anazungumza kwa Mungu.

Mwanadamu, ambaye amezaliwa na mwanamke,

Sentensi hii ina maanisha watu wote,wanaume na wanawake wote wamezaliwa katika ulimwengu huu.

huishi siku chache tu

hapa imetumika lugha ya kukuza jambo ili kutoa msisitizo kwamba watu huishi muda mfupi tu. " hushi muda mfupi sana"

amejaa mahangaiko.

Kujaaa "mahangaiko" inaonyesha kupata mateso mengi. "yeye ana mahangaiko mengi" au " anateseka sana"

Yeye huchanua kutoka katika ardhi kama ua na kukatwa chini;

Kama maisha ya ua, maisha ya mtu ni mafupi na ni rahisi kuuawa.

yeye hukimbia kama kivuli na hawezi kudumu.

Maisha mafupi ya mwanadamu yamelinganishwa na kivuli ambacho hutoweka haraka.

Je, wewe unatazama chochote katika hivi?

Ayubu ana maanisha kuwa yeye hahitaji Mungu amsikilize sana." Wewe hautazami chochote haya" au " Wewe haunisikilizi sana mimi "

tazama katika hivi

Kumtazama mtu kunawakilisha kuwa makini kumsikiliza ili kumhukumu yeye. "Kuwa tayari kusikiliza" au " tazama makosa ndani yake"

Mnanileta mimi hukumuni pamoja nanyi?

Ayubu anatumia swali hili kuonyesha kushangaa kwake kuwa Mungu anamhukumu yeye ingawa Ayubu si wa thamani kama ua."Lakini wewe wanihukumu mimi"

Job 14:4

Habari za Jumla:

Habari za Jumla: Ayubu anaendelea kuzungumza kwa Mungu.

Ni nani anayeweza kukileta kitu safi kutoka katika kitu kichafu? Hakuna awaye yote.

Ayubu anatumia swali hili kumshawishi Mungu kufanyia kazi kile ambacho yeye anakifahamu kuhusu vitu visivyo safi kwa Ayubu."Hakuna hata mmoja ambaye anaweza kukileta kitu kilicho safi kutoka kwenye kitu kichafu"

Siku za mwanadamu zimeamriwa

"Wewe unaziamuru siku za mwanadamu" au "Wewe unaamua siku za kuishi mwanadamu"

Idadi ya miezi yake unayo wewe;

Idadi ya miezi ya mwanadamu kuwa na Mungu inawakilisha Mungu kuamua idadi ya miezi ambayo mtu ataishi," Wewe waamua ni miezi mingapi yeye ataishi"

umekiweka kikomo chake ambacho hawezi kukivuka

Kuweka kikomo inawakilisha kuishi muda uliopita ambao Mungu ameuweka kwa mtu kufa. "Wewe umeuweka wakati ambao yeye atakufa", na yeye hawezi kuishi zidi ya hapo.

mtu aliyekodishwa

mtu aliyekodishwa kufanya kazi na huenda nyumbani baadaye.

Job 14:7

Kunaweza kuwa na tumaini kwa mti ;

Kielezi cha jina " Matumaini" chaweza kuelezwa pamoja na kitenzi " Tumaini." Tumaini limeelezwa katika mistari 7-9. "Sisi tunaweza kutumaini kuwa mti utaishi tena"

unaweza kuchipua tena

"Unaweza kuanza tena kukua"

hivyo chipukizi lake halitapotea.

Kupotelea mbali kunawakilisha kufa. "ili ya kwamba chipukizi lake halitakufa"

Japokuwa

"Ingawa" au "Hata kama"

shina

sehemu ya mti ambayo hubakia imetokeza nje kutoka ardhini baada ya mti kukatwa sehemu zingine za mti.

hata kama bado lina harufu ya maji

Sentensi hii yaweza kutafsiriwa hivi: shina linalokufa kama ikiwa linaharufu ya maji inawakilisha maji yako karibu nalo." hata kama maji kidogo yako karibu nalo"

litachipua tena

"litaanza kukua"

na kutoa nje matawi kama mche.

mtu kutoa majani inawakilisha matawi kukua katika mti. "na matawi yataanza kukua juu yake kama mche"

Job 14:10

na tena yuko wapi yeye? 11Kama maji

Ayubu anatumia swali hili kusisitiza kuwa wakati mtu anapokufa, yeye ametoweka. na hakuna hata mmoja anayefahamu aliko" au " na yeye ametoweka"

ma maji yanavyopotea kutoka ziwani, na kama vile mto upotezavyo maji na kukauka, vivyo hivyo watu hulala chini na hawaamki tena.

Ukweli kwamba kifo hakiwezi kurudishwa kimelinganishwa na maji ambayo hukauka na hayawezi kurudi.

Kama maji yanavyopotea kutoka ziwani, na kama vile mto upotezavyo maji na kukauka,

Tungo hizi mbili zinaeleza wazo moja na zimerudiwa kutoa msisitizo wa ukweli kwamba kifo ni mwicho.

vivyo hivyo watu hulala chini

Kulala chini kunawakilisha kufa." hivyo watu hufa"

na hawaamki tena

Kuinuka tena kunawakilisha kuishi tena. "na kutoishi tena"

hawataamka wala kuamshwa kutoka katika kulala kwao.

Hizi tungo mbili zinamaanisha kitu hiho hicho na zimetumiwa pamoja kusisitiza kuwa kifo ni mwisho. Kulala kunawakilisha kufa na kuamka kunaakilisha kuishi tena. " watu ambao wamekufa hawataishi tena na kufufunuliwa kutoka katika kifo.

Job 14:13

habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa Mungu.

Laiti, kwamba ungenificha mim

Huu ni mshangao kuonyesha kile ambacho Ayubu anataka sana lakini yeye hana matumaini ya hakika kutokea. " Mimi ningependa kwamba wewe ungenificha mimi"

ungenitunza mimi katika siri

"niache mimi nimefungiwa" au " niache mimi nimefichwa"

na kisha kuniita mimi katika fahamu

Kumwita mtu katika ufahamu ni nahau ikimaanisha kufikiri juu yake yeye. " na kisha nifikire mimi" au " na kisha unikumbuke mimi"

Ikiwa mwanadamu akifa, yeye ataishi tena?

jibu la hakika ni "hapana." "Kama mtu akifa, yeye hataishi tena"

Ikiwa hivyo

"hivyo" inamaanisha ufahamu kutoka katika mistari iliyotanguliza. " Kama yeye angeishi tena"

kusubiri kule muda wangu wote wa kuharibika

Maneno "muda wngu wa kuharibika" yanawakilisha muda ambao Ayubu angeharibika." kusubiri muda wangu wote kule ingawa ningeharibika"

mpaka kufunguliwa kwangu kutakapokuja

Kitenzi jina "kufunguliwa" chaweza kuelezwa na kitenzi "kufungua." "hadi hapo nitakapofunguliwa" au mpaka pale wewe utakaponiachilia"

Job 14:15

Habari za Jumla:

Habari za Jumla: Ayubu anaendelea kuzungumza kwa Mungu.

mimi ningekujibu

"Mimi ningeitikia kujibu"

Wewe ungekuwa na shauku ya

Jina " shauku" linaweza kuelezwa pamoja na kitenzi "shauku" au "kutamani." Wewe ungekuwa na shauku" au " Wewe ungehitaji"

ya kazi ya mikono yako.

Hapa mikono ya Mungu inamwakilisha yeye kufanya vitu. Ayubu anajisema mwenyewe kuwa kazi ya mikono ya Mungu. " kwa ajili yangu, ambaye umenitengeneza"

hesabu...na kutunza

Vitenzi hivi viwili kwa pamoja vinaeleza tendo moja."Kwa umakini tunza kwa ajili ya"

nyayo zangu;

Nyayo zinawakilisha maisha yake yeye au kile ambacho yeye anafanya."maisha yangu" au vitu ambavyo mimi huwa navifanya"

Wewe usingejali kumbukumbu ya dhambi yangu...wewe ungeufunga

Mistari hii mitatu inaeleza wazo lilelile na imetumika pamoja kusisitiza ujasiri wake yeye, Mungu angemsamehe yeye.

Wewe usingehifadhi mkoba wa dhambi yangu.

Kutunza mkoba wa dhambi ya Ayubu inawakilisha kufikiri juu ya dhambi yake. "wewe usingetazama dhambi yangu" au "wewe usingefikiri juu ya dhambi yangu"

Uovu wangu ungetiwa muhuri katika mkoba;

Kuutia muhuri uovu katika mkoba inawakilisha kuuficha na kukataa kufikiri juu yake. " Wewe ungekataa kufikiri juu ya uovu wangu kama mtu ambaye huficha kitu fulani katika mkoba"

wewe ungeufunika uovu wangu.

Kufunika uovu kwa kitu ili kwamba usiweze kuonekana ni kufikiri juu yake. "wewe ungeuficha uovu wangu" au " wewe ungeupuuza uovu wangu"

Job 14:18

Habari za Jumla:

Habari za Jumla: Ayubu anaendelea kuzunguza kwa Mungu.

milima huanguka na kuwa si chochote;

"Kuwa si chochote" ni nahau ikimaanisha kuharibiwa kabisa. Tungo hii inafafanua juu ya neno "anguka" na kusisitiza uharibifu. "milima imetupiliwa mbali"

miamba huhamishwa kutoka mahali pake;

"miamba kuporomoka chini kutoka mahali pake"

Kama hivi, ninyi mnavyoharibu matumaini ya mwanadamu.

"mnaharibu tumaini la mwanadamu kama vile..mavumbi ya ardhi"

matumaini ya mwanadamu.

"vitu ambavyo mwanadamu anvitumainia"

Job 14:20

Habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa Mungu.

Ninyi daima humshinda yeye,

Neno " yeye" linamaanisha kila mtu" Ninyi daima mnamshinda mwanadamu" au " Ninyi daima mnawashinda watu"

yeye hupita mbali;

Kupita mbali kunawakilisha kufa. " yeye hufa"

Ninyi mnabadilisha uso wake

Maana zaweza kuwa hizi: Maumivu kabla ya kufa humfanya uso wake kuwa angavu, au wakati mtu anapokufa, Mungu huufanya uso wa mtu kuwa tofauti.

kumtuma yeye mbali kufa

Sentensi hii inawakilisha kumsababishia yeye kufa.

na kama wakishushwa chini,

Kushushwa chini ni kuaibishwa. " kama wao wameaibishwa" au " ikiwa watu wakiwaaibisha wao"

Job 15

Job 15:1

Elifazi Mtemani

Hili ni jina la mtu. Watu kutoka temani wanajulikana kama Watemani.

Mtu mwenye hekima anapaswa kujibu kwa maarifa yasiyofaa na kujijaza mwenyewe na upepo wa mashariki?

Elifazi anatumia swali hili la kejeli kumkemea Ayubu. "Mtu mwenye busara hapaswi kujibu kwa maarifa yasiyo na faida wala kujilisha yeye mwenyewe na upepo wa mashariki"

kujijaza mwenyewe na upepo wa mashariki?

Upepo unawakilisha hakuna. Tungo hii inazungumzia mtu anyezungumza maneno yasiyo na maana.Mtu huyu ni kama amejaa upepo. "kujijaza yeye mwenyewe na maneno yasiyo na maana"

upepo wa mashariki?

"upepo wa joto" au "upepo wa jangwani"

Anapaswa kuhojiana na mazungumzo yasiyo na faida au na hotuba ambazo kwa hizo yeye hawezi kufanya mema?

Elifazi anatumia swali hili la kizushi kumkemea Ayubu. " Yeye hapaswi kuhojiana na kwa mazungumzo yasiyo na faida" au "Yeye hapaswi kushindana kwa kutumia maneno yasiyo na faida au kutoa hotuba ambazo mwisho wake ni hasara"

Job 15:4

fifisha

"haribu" au " kutostahilisha"

zuia

"fifisha" au "ondolea mbali"

heshima ya

"tafakari juu ya" au " fikiri juu ya"

uovu wako hufundisha midomo yako;

Sentensi hii yaweza kutafsiriwa hivi: "uovu"kama ulikuwa mwalimu wa midomo ya Ayubu umeelezwa kuwa kama vile midomo inajifunza. Hii ina maana kwamba usemi wake umeathiriwa na uovu wake kwa kiwango kikubwa. "uovu wako ni kama mwalimu na mdomo wako ni kama mwalimu" au " hii ni kwa sababu ya wewe kutenda dhambi kwamba unaongea kama vile wewe unavyofanya"

Mdomo wako

Mstari huu unamzungumzia Ayubu, lakini unarejea kwa "mdomo" wake kutilia mkazo kile anachokisema. "wewe pia wazungumza" au "wewe wasema kile ambacho wewe wasema"

kuwa na ulimi wa mtu mwenye hila

Sentensi hii inarejea jinsi mtu mwenye hila huzungumza kama "ulimi" wake. "kuzungumza katika njia ya mtu mwenye hila"

hila

"udanganyifu"

Mdomo wako mwenyewe hukukukumu wewe, siyo wangu;

Maneno haya yanamwelekea Ayubu na Elifazi kwa "midomo" yao kutilia mkazo kwa kile wanachosema. "Wewe umelaaniwa kwa kile ambacho unakisema, siyo kwa kile ambacho mimi ninachokisema, siyo mimi ninayekulaani wewe"

midomo yako mwenyewe hushuhudia

Ni "midomo" ya Ayubu kuweka msisitizo kwa kile ambacho anakisema. "maneno yako mwenyewe" au "wewe washuhudia"

Job 15:7

habari za Jumla

Kila mstari ni mfano ambao unabeba maswali mawili yenye kejeli .

Je, wewe ni mwanadamu wa kwanza ambaye aliyezaliwa?

Jibu dhahiri ni "hapana" Swali hili la kejeli linaweza kuwekwa katika hali isiyo ya kuuliza: Wewe siyo mtu wa kwanza aliyezaliwa"

Je, wewe ulizaliwa?

"Je, Mungu alikuleta"

Wewe ulikuwepo kabla ya vilima kuwepo?

Jibu sahihi ni "hapana" Hili ni swali la kejeli laweza kuwekawa hivi katika hali isiyo ya kuuliza: Wewe hujaletwa katika dunia kabla ya milima" au " Mungu hakukuleta wewe katika dunia kabla yeye hajaleta vilima katika dunia"

Wewe Umewahi kusikia maarifa ya siri ya Mungu?

Jibu dhahiri ni "hapana" Swali hili la kejeli laweza kuwekwa katika hali isiyo ya kuuliza hivi: "Wewe hujasikia siri za maarifa ya Mungu"

Je, wewe wajihesabia mwenye hekima wewe mwenyewe?

swali hili la kejeli linasisitiza kuwa yeye hawezi kujihesabia hekima yeye mwenyewe. "Wewe huwezi kujihesabia hekima wewe mwenyewe" au " Wewe siyo mtu pekee mwenye hekima"

Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho sisi hatukijui?

Jibu sahihi ni "hakuna"Hakuna chochote ambacho unakijua ambacho sisi hatukijui" au "Kila kitu unachokifahamu, hata sisi tunakifahamu"

Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho hakiko katika sisi?

"Kila kitu unachokifahamu , sisi pia tunakifahamu" au "Sisi tunakifahamu kila kitu unachokifahamu"

Job 15:10

Pamoja nasi wapo pia wenye mvi na watu wazee sana

wnye mvi na wazee sana- Elifazi anajiongelea yeye mwenyewe na watu wengine kuwa na hekima ya wazee ambao kwao walijifunza kana kwamba walikuwa pamoja nao katika mwili."Sisi tumepata hekima kutoka pia kwa watu wenye mvi na watu wazee sana"

wenye mvi na watu wazee sana ambao ni wazee

wenye mvi na watu wazeesana-tungo "wenye mvini ufafanuzi wakibinadamu "kwa watu ambao wamezeeka sana" "watu waliozeeka sana wana mvi"

wazee zaidi kuliko baba yako

Hii ni lugha ya kukuza jambo. "mzee kuliko baba yako"

faraja ya Mungu...ni ya upole dhidi yako wewe?

Hili ni swali la uzushi na kejeli ni shitaka lenye tumaini la jibu la "ndiyo"." Swali hili laweza kuweka katika hali isiyo ya kuuliza: Wewe ni sharti ufikiri kwamba faraja za Mungu ni ndogo mno kwako, maneno ambayo ni ya upole kwako.

faraja

"kufariji" au "kuchukuliana"

Job 15:12

Kwa nini moyo wako wewe unakupeleka mbali?

hapa " moyo" unawakilisha hisia za mtu. " kwa nini hisia zako zinakupeleka mbali" au Kwa nini wewe unaruhusu hisia zako kuongoza uamuzi wako?

Kwa nini macho yako yananga'ra

Sentensi hii imaanisha Ayubu kuonekana mwenye hasira Kwa uwazi kabisa muonekano wa mcho yake yeye. " Kwa nini macho yako yanaonekana mwenye hasira" au "Kwa nini wewe unakasirika"

kuirejesha roho yako

hapa neno "roho" linamaanisha utu wote wa mtu. "geuka wewe mwenyewe"

kuyatoa maneno hayo kutoka katika mdomo wako

hapa inamwelezea "yeye akizungumza na hivyo wewe wasema vitu vya kuumiza dhidi yake yeye"

Je, mwanadamu yeye ni nini kwamba yeye anapaswa kuwa safi?

Maswali haya mawili kimsingi ni kitu kimoja na yametumika pamoja kusisitiza kuwa mtu hawezi kuwa mkamilifu"

safi

mtu ambaye Mungu humfikiria kuwa kiroho amekubalika amezungumzwa kama mtu ambaye kimwili alikuwa safi.

mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ni nini kwamba yeye anapaswa awe mwenye haki?

Swali hili la kizushi limeulizwa kusisitiza kwamba mtu hawezi kabisa kuwa "mkamilifu." Bila kutumia swali sentensi hii yaweza kusomeka hivi: "Mtu aliyezaliwa kutoka kwa mwanamke kamwe hawezi kuwa mkamilifu."

Job 15:15

Tazama

Neno hili limetumika kuvuta usikivu wa Ayubu kwa kile ambacho kimezungumzwa hapo baadaye.

mmoja wake aliye mtakatifu;

"malaika wake yeye"

safi

mtu ambaye Mungu humfikiria kuwa kiroho amekubalika amezungumzwa kama mtu ambaye kimwili alikuwa safi.

machoni pake yeye;

Hapa machoni pake inawakilisha hukumu au tathimini.

mbaya na mla rushwa,

Maneno haya mawili kimsingi yanamaanisha kitu kilekile na linatia mkazo jinsi gani watu walivyo waovu.

ambaye hunywa uovu kama maji!

Sentensi hii inaelezea uovu kama vile ulikuwa maji unayokunywa. Inalinganisha mtu mwovu hutamani kutenda dhambi kwa vile jinsi gani yeye anavyokuwa na shauku ya kunywa maji ya uvuguvugu. "wao wapendao uovu ni zaidi kama vile wanapenda kikombe cha maji ya baridi" au "wao ambao ni kawaida yao kutenda matendo maovu kama wanavyokunywa maji ya baridi"

Job 15:17

Mimi nitakuonyesha wewe;

Hii ni nahau. "Mimi nitakuleza wewe" au " Mimi ninaweka wazi kwako wewe"

Mimi nitakutangazia wewe

"Mimi ntatangaza"

mababu zao hawakuvificha.

Elifazi anasisitiza kuwa mababu zao kwa makusudi waliwafundisha vitu hivi. " mababu zao waliwafundisha wao waziwazi"

Job 15:19

ambao kwao pekee nchi walipewa,

"kwa hao ambao Mungu pekee aliwapa nchi"

miongoni mwao hakuna mgeni aliyepita.

Hii inamaanisha kwamba hakuna mgeni aliyeishi kati yao, kwa uwazi ili kwamba wasiweze kuathiriwa na dini za kipagani. " hakuna mtu awaye yote kutoka katika nchi nyingine aliyekuja na kuwasababisha wao kufikiri vibaya juu ya Mungu"

hupitia katika maumivu

"kuteseka kwa maumivu mengi." Hii yaweza kuwa mayteso ya mwili au kihisia"

idadi ya miaka iliyowekwa juu

"miaka yote ambayo Mungu ameiweka juu"

iliyowekwa juu

Hii ni nahau. "ambavyo vimeandaliwa" au "vile vilivyoweka maalumu"

Sauti ya vitisho katika masikio yake;

"Yeye anasikia sauti za kuogofya siku zote"

Job 15:22

Sentensi Unganishi:

Elifazi anaendelea kumwelezea mtu ambaye ni mwovu anaanza kuelezea katika 15:19.

rudi kutoka katika giza;

Katika sentensi hii "giza" ni tashbiha kuonyesha mahangaiko au mambo mabaya" "epuka mambo mabaya"

Upanga humngojea yeye

katika tungo hii neno " upanga" inawakilisha adui ambaye anangojea kumuua mtu mwovu. Maana zaweza kuwa 1) yeye amehofu kwamba mtu fulani atamchinja yeye" "yeye anahofia kwamba mtu fulani yuko karibu kumwua yeye" au 2) ni dhahiri kwamba yeye anaenda kuuawa. "mtu fulani anamngojea kumtoa uhai"

kwa ajili ya mkate

Sehemu hii "mkate" unamaanisha chakula kwa ujumla" "kwa chakila"

siku ya giza

Hii ni nahau. "siku ya uharibifu" au "kipindi cha kifo chake"

iko mkononi.

Hii ni nahau. "inakuja hivi karibuni"

hushinda dhidi yake yeye,

"zidi nguvu" au "shinda"

kama mfalme tayari kwa vita.

Hii inaliganisha jinsi ukiwa wake na mateso yake makali kumshinda yeye kwa jinsi mfalme ambaye yuko tayari kwa vita, angeshinda dhidi yake. "kama ilivyo kwa mfalme , aliye tayari kwa vita, angeshinda dhidi yake yeye"

Job 15:25

yeye ameunyosha mkono wake dhidi ya Mungu

"yeye ameitikisa mikono yake dhidi ya Mungu." Hii ni ishara ya kukasirika.

hukimbia kwa Mungu

Sentensi hii inamhusu mtu mwovu anatenda kwa hila dhidi ya Mungu kama vile yeye alikuwa akikimbia kumkabili kumshambulia yeye" kumshambulia Mungu" au " kutenda kwa hila dhidi ya Mungu"

kwa vifundo vikubwa vya ngao.

kwa ngao yake yenye nguvu"

Job 15:27

Hii ni kweli,

Sentensi hii inamaanisha mtu mwovu kukimbia kwa Mungu kama ilivyoelezwa kutoka katika mistari iliyotangulia.

yeye amefunika uso wake kwa mafuta yake na amekusanya mafuta juu ya viuno vyake

Mtu huyu mwovu ameelezwa kama mtu mnene kna dhaifu wakati akijiamini mwenyewe kuwa ni mwenye nguvu vya kutosha kumshinda Mungu. "yeye ni dhaifu na uso mnene na viono vilivyowanda.

hakuna mwanadamu anayeishi humo

"ambazo zimetelekezwa"

magofu.

"mabaki" au "majalala"

Job 15:29

Yeye hatakuwa tajiri; utajiri wake yeye hautadumu

"yeye atakuwa masikini, fedha zake zote hazitaonekana"

hata kivuli chake hakitadumu katika nchi.

Sentensi hii inarudia wazo ambalo ni kwamba mali zote za mtu mwovu hazitaonekana."

nje ya giza;

Giza katika sentensi hii linamaanisha kifo. "nje ya giz la kifo"

mwali wa moto utakausha matawi yake;

Katika sentensi hii "mwali wa moto" unawakilisha hukumu ya Mungu na kukauka kwa ghala zake yeye kunawakilisha ukweli kwamba mali zake yeye kupotelea mbali, au kwamba yeye atakufa" Mungu atakitupilia mbali kila kitu ambacho yeye anachokimiliki" kama moto ukaushavyo majani ya mti mbichi"

pumzi ya kinywa cha Mungu

"Pumzi ya Mungu" inawakilisha hukumu yake yeye.

yeye ataenda zake.

Sentensi hii inamaanisha yeye mwenyewe kufa. "yeye atakufa"

Job 15:31

upuuzi utakuwa mshahara wake yeye.

"kwa maana kama yeye ataweka tumaini katika hvitu , upuuzi utakuwa ujira wake yeye"

tawi lake halitakuwa kijani.

Sentensi hii inazungumzia kuhusu mtu kuonekana tofauti na mfu kama vile ilivyokuwa ghala iliyokauka au tawi. " yeye ataonekana mfu, kama vile tawi la mti uliokufa lisivyoonekana kibichi"

Yeye atazipukutisha... yeye atayaondoa

Mistari hii miwili inatoa picha moja ambayo imerudiwa kusisitiza kuwa jambo hili litatokea kwa hakika.

Yeye atazipukutisha zabibu zake zisizovunwa kama kama mti wa mzabibu

Sentensi hii inazungumza juu ya mtu mwovu kuwa dahifu na kufa kama vile alikuwa mti wa mzabibu ukidondosha zabibu ambazo bado kuvunwa. "Kama vile mti wa mzabibu unavyoangushusha zabibu zake ambazo bado kuvunwa, viyo hivyo mtu mwovu atadondosha nguvu zake"

yeye atayaondoa maua yake kama mti wa mzeituni.

Sentensi hii inazungumza juu ya mtu mwovu kuwa dhaifu na kufa kama vile alikuwa mti wa mzabibu ukidondosha zabibu ambazo bado kuvunwa. "Kama vile mti wa mzabibu unavyoangusha zabibu zake ambazo bado kuvunwa, viyo hivyo mtu mwovu atadondosha nguvu zake"

Job 15:34

Kwa maana msaada wa watu wasiomcha Mungu

"kundi la watu wasiomcha Mungu"

moto utateketeza hema za rushwa.

Tungo "hema ya wala rushwa" ina maanisha kuwa watu waovu walizinunua hema hizi kwa pesa walizozipata kwa njia ya rushwa. "hema walizozinunua kwa rushwa zao, zitachomwa kwa moto"

Wao wanabeba mimba yenye ubaya na kuzaa uovu; tumbo lao hutunga mimba ya udanganifu.

Wazo hilihilo limerudiwa mara tatu kutoa msisitizo kwa kiwango gani watu hawa huzalisha waovu. Sentensi hii inamzungumzia mtu ambaye anapanga kufanya vitu viovu, na wanavifanya kama vile mtu aliyekuwa akibeba mimba na kuzaa vitu hivi kama vile mwanamke anavyotunga mimba na kuzaa mtoto. "Wao wanapanga kusababisha mambo maovu ya kitoto na kufanya vitu viovu; daima wao wanapanga kuwadanganya wengine"

tumbo lao hutunga mimba

Katika sentensi hii neno "tumbo" limetumika kumaanisha mtu na kusisitiza kuhusu kutunga mimba, kama ilivyo katika tumbo ambalo utungaji mimba hufanyika humo. "wao wanatunga mimba"

Job 16

Job 16:1

ninyi nyote ni wafariji wenye kuhuzunisha.

"Badala ya kunifariji mimi, ninyi nyote mnanifanya kuwa mwenye kuhuzunika"

Maneno yenye upuuzi daima yanaweza kuwa na mwisho?

Ayubu anatumia swali hili la kizushi kuonyesha kwamba yeye anapenda kwamba wao wangeacha kuzungumza maneno yasiyo na faida. "Jinsi gani mimi ningependa maneno yenu yasiyo na maana yakome.!

Nini kimeharibika kwenu kwamba mnajibu kama hivi?

Ayubu anatumia swali hili la kejeli kumkemea Elifazi. Neno "wewe" linamaanisha Elifazi ambaye amemaliza punde kuzungumza kwa Ayubu. "Elifazi, wewe unapaswa kuacha kunijibu mimi kama hivi"

Job 16:4

Mimi ningekusanya na kuunganisha maneno pamoja

"Mimi ningefikiri vitu vya kuzungumza"

tikisa kichwa changu

Hiki ni kitendo ambacho kinaonyesha kutokukubalika.

katika dhihaka

Neno "mzaha" laweza kuelezwa kama kitenzi "kukudhihaki wewe"

Laiti, jinsi gani Mimi ningewatia moyo na midomo yangu! Jinsi gani faraja kutoka midomo yangu ingenga'risha huzuni yenu!

Hapa Ayubu anazungumza kwa kumaanisha kinyume cha kile anachokizungumza. "Maneno yangu kwa hakika yangekuwa hayawatii moyo ninyi" Wao hakika hawaing'arishi huzuni yako wewe" au " Kwa uzungumza kwako kama mlivyozungumza kwangu hapa manzo, Mimi nisingewatia moyo ninyi au kuinga'risha huzuni yenu"

na midomo yangu!

katika sentensi hii "mdomo" wa Ayubu unawakilisha kile ambacho yeye anasema. "Kwa kile ambachop mimi ninasema"

faraja kutoka midomo yangu

Sentensi hii ina maanisha maneno yenye kutia moyo ambayo anayazungumza. "maneno yangu ya kutia faraja"

ingenga'risha huzuni yenu!

Hapa huzuni imezungumzwa kama ilikuwa mzigo mzito wa mwili. "ingepunguza huzuni yako " au " ingewasaidia kujisikia asiye na huzuni"

Job 16:6

kuomboleza

Ayubu amepitia majonzi mazito ya kupoteza familia yake na afya hiyo ni haielezeki na kwa hiyo, inamsababishia yeye "huzuni kubwa na maumivu ya hisia."

jinsi gani mimi ninasaidiwa?

Ayubu anatumia swali hili la kizushi kueleza kuwa kunyamaza kimya hakupunguzi huzuni yake yeye. Swali hili laweza kuandikwa bila kuwekwa katika hali ya swali. "hainisaidii mimi hata kidogo."

Lakini sasa, Mungu wewe

Ayubu sasa anarudisha lalamiko lake kwa Mungu.

umeifanya familia yangu yote kuwa ukiwa.

"umeharibu familia yangu yote"

Wewe umenifanya mimi kukauka,

Sentensi hii inamaanisha kuwa mwili wa Ayubu umekonda na kuwa na mikunjamano. "Wewe umeufanya mwili wangu kukonda"

ambayo yenyewe ni ushuhuda dhidi yangu mimi

Ayubu anaelezea kukonda kwa mwili wake kama vile ulikuwa kama mshitaki dhidi yake "na watu wanafikiri kuwa unanionyesha mimi kuwa ni mwenye dhambi"

kukonda kwa mwili wangu huinuka dhidi yangu, na kunashuhudia dhidi

Ayubu anaelezea hali ya kukonda kwa mwili wake kama vile ulikuwa mshitaki dhidi yake yeye. "Wote wanaona jinsi mwili wangu ulivyokonda, na wanafikiri hicho kinathibitisha kuwa mimi ni mwenye hatia"

dhidi ya macho yangu.

Hapa Ayubu anazungumzia kwa "uso "wake. "dhidi yangu mimi"

Job 16:9

Mungu amenirarua mimi katika ghadhabu yake na amenitesa mimi; Yeye amenisaga mimi kwa meno yake; Adui yangu amenikazia macho yake juu yangu kama yeye anavyonirarua mimi vipande.

Maneno haya yanazungumza juu ya Mungu kumsababishia Ayubu maumivu kama vile alikuwa mnyama wa porini na Ayubu alikuwa kama mawindo yake alikuwa akiua. Kwa sababu Mungu ana hasira kali na mimi, ni kama vile alikuwa mnyama wa mwituni ambaye anararua mwili wangu vipande vipande kwa meno yake kwa sababu alikuwa adui yangu"

Adui yangu

Sentensi hii inarejea kwa Mungu kama "adui"yake. Inaeleza jinsi yeyey alivyomsababishia yeye maumivu makali.

amenikazia macho yake juu yangu

Hii ni nahau."ananitazama mimi kwa hasira"

Watu wameachama na midomo iliyowazi

"Kuachama" ina maanisha kukazia macho katika mshangao na mdomo ulioachama.

Job 16:11

Mungu amenikabidhi mimi juu ya watu wasio mcha Mungu, na kunitupa mimi ndani ya mikono ya watu waovu

Mistari hii miwiwli kimsingi inamaanisha kitu kilekile. Kwa pamoja inasisitiza hisia za Ayubu za kuwa amesalitiwa na Mungu.

amenikabidhi mimi juu ya

Hii ni nahau. "ameniweka mimi chini ya himaya ya "

kunitupa mimi ndani ya mikono ya

Katika sentensi hii "mikono ya mtu" inamaanisha "udhibiti" wake "amenitoa mimi kwenye udhibiti"

na yeye amenivunjavunja mimi vipande.

Ayubu anazungumza juu ya maumivu yake na kukosa matumaini kama vile yeye alikuwa kitu ambacho kimevunjwavunjwa vipande. . "lakini kisha alikuwa yeye amenivunja mimi vipande vipande.

ameniponda mimi vipande vipande;

Ayubu anazungumza juu ya maumivu yake na kukosa matumaini kama vile yeye alikuwa kitu ambacho kimevunjwavunjwa vipande. " ni kama vile amenichukua mimi kwa shingo na kunivunjavunja vipande"

yeye pia ameniweka mimi juu kama shabaha yake.

Ayubu anajisema mwenyewe kuwa shabaha ya shambulizi la Mungu ikiwa kama Mungu amemweka yeye shabaha kumpiga upinde. "ni kama vile ameniweka mimi juu kama shabaha"

Job 16:13

Wapiga upinde wake wote wamenizunguka mimi;

Ayubu anajisema mwenyewe kuwa shabaha ya shambulizi la Mungu ikiwa kama Mungu amemweka yeye shabaha yake na Mungu alikuwa na wapiga upinde wakimzunguka yeye kumshambulia yeye. "ni kama vile wapiga upinde wake wamenizunguka mimi"

Mungu huzikata vipande vipande figo zangu, na haniokoi mimi; yeye humwaga nje nyongo yangu juu ya ardhi

Ayubu anazungumza juu ya maumivu ambayo yeye anajisikia kwa kuyalinganisha na Mungu kuchoma mwili wake yeye kwa upindeambao anaupiga. Hapa "Mungu "anawakilisha upinde umechoma figo na ini langu mimi, na kuimwaga nyongo yangu juu ya ardhi. Yeye hajanihifadhi mimi"

yeye hukanyaga kanyaga kupitia ukuta

Ayubu anazungumza juu ya maumivu ambayo anahisi kwa kujilinganisha yeye mwenyewe na ukuta ambao Mungu anapita kukanyagakanyaga." "Mimi ninajisikikia kama ukuta ambao kupitia huo Mungu huvunjavunja"

yeye hukimbia juu yangu mimi kama shujaa.

Ayubu anamwelezea Mungu kama askari ambaye anamshambulia yeye. "Ni kama shujaa ambaye hukimbia juu yangu kunishambulia"

Job 16:15

Mimi nimeshona nguo ya magunia juu ya ngozi yangu

"Kwa sababu mimi ninaomboleza, Mimi nimeshona pamoja nguo ya magunia kuvaa kama nguo yangu" au "Mimi navaa nguo ambayo nimeitengeneza kutoka katika magunia kwa sababu ninaomboleza"

Mimi nimeisukuma kwa nguvu pembe yangu ndani ya ardhi.

"Pembe" ya Ayubu inawakilisha nguvu na mamlaka aliyokuwa nayo kabla lakini sasa haipo tena. " Mimi nina simama hapa katika uchafu, mkiwa sana."

juu ya ngozi inayofunika macho kuna kivuli cha mauti

"kuna giza linazunguka macho yangu" au " macho yangu yana giza, kama jicho lamtu aliyekufa"

hakuna dhuluma katika mikono yangu,

"Mikono" inamaanisha uwezo wa mtu na utendaji kazi wake. "Mimi sijatenda kwa hila"

Job 16:18

Nchi, haifuniki juu damu yangu mimi

Ayubu anazungumza kwa " nchi"moja kwa moja japokuwa haiwezi kumsikia yeye, kutilia mkazo kwenye hoja yake. Nchi imepewa sifa za kutenda kama binadamu kuifunika juu damu yake baada ya yeye kufa. "Mimi ningependa damu yangu ilowane ndani ya ardhi lakini hiyo ingebaki juu ya ardhi kama uthibitisho wa jinsi nilivyokufa"

Nchi, haifuniki juu damu yangu mimi

Ayubu anajisema yeye mwenyewe akifa kama vile yee angechinjwa . "Damu" yake ni mfano kuonyesha kifo chake yeye. "Nchi, wakati nikifa , usifiche jinsi nilivyokufa visivystahili" au"na isiwe imefichika jinsi ninavyokufa isivyostahili"

acha kulia kwangu kuwe hakuna mahali pa kupumzika.

Ayubu anazungumzia juu ya kumtaka kila mmoja kujua kile kilichotoke kwake yeye kama "kilio" chake alikuwa mtu ambaye hakuacha kamwe kushuhudia kile ambacho kilitokea kwake yeye na hakupumzika kamwe. "Acheni kila mmoja asikie kuhusu kile ambacho kilitokea kwangu mimi"

tazama

Ayubu anatumia neno hili kuvuta usikivu kwa kile ambacho yeye anachokisema baadaye. "sikilizeni"

ushuhuda wangu uko mbinguni

Ayubu anatumaini kuwa mtu fulani atazungumza juu yake kwa Mungu.

ashuhudiaye

"hushuhudia"

yuko juu

Hii ni nahau. "mbinguni" au "juu mbinguni"

Job 16:20

wananicheka

"cheka au kejeli"

jicho langu linamwaga machozi

Ayubu anaeleza jinsi yeye anavyojisikia mwenye huzuni. Katika sentensi hii anaelezea kwa kulikuza jambo la jinsi gani mara nyingi machozi humwagika kutoka katika macho yake. "macho yangu yamejaa machozi wakati mimi ninapolia kwa sauti"

kwa ajili ya mtu huyu

Katika sentensi hii Ayubu anajisema yeye mwenyewe katika nafsi ya tatu"kwa ajili yangu mimi"

kama mwanadamu afanyavyo na jirani yake.

"Ayubu anaeleza jinsi anavyotaka yeye kwamba mmoja mbinguni kumwombea yeye.

mtu huyu

Ayubu anajisema yeye mwenyewe.

Mimi nitakwenda mahali

Pia katika sentensi hii Ayubu anajisema yeye mwenyewe anakufa. " Mimi nitakufa na kwenda mahali"

Job 17

Job 17:1

habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza.

Roho yangu imemezwa

Ayubu anajisema yeye mwenyewe kwa "roho" yake kusisitiza juu ya hisia zake za ndani. Anazungumza juu ya kukosa nguvu hata kidogo kama kitu ambacho kimetumika. " Mimi nimemezwa" au "mimi nimepoteza nguvu zangu zote"

siku zangu zimekwisha;

Ayubu anarejea kuhusu maisha yake "kama siku zake" muda wangu umekwisha" au " Mimi ninakwenda kufa hivi karibuni"

kaburi lipo tayari kwa ajili yangu mimi.

Tungo hii inaeleza "kaburi" kama vile ni mtu ambaye atampokea Ayubu kama mgeni. "nitakufa hivi karibuni na nitazikwa"

Hakika kuna wenye mzaha pamoja nami

"Wale wanaonizunguka mimi wananidhihaki mimi"

Hakika

"haswa"

ni lazima daima jicho langu litazame

Ayubu anajisema yeye mwenyewe kwa "macho yake" kusisitiza kile ambacho anakiona" Mimi ni lazima daima nione " au "Mimi ni lazima daima nisikie"

kukasirisha kwao

"kusimanga kwao" neno "kukasirisha kwa" laweza kuelezwa kama kitenzi. "wao wananikasirisha mimi" au "wa, wanajaribu kunifanya mimi nikasirike"

Nipe sasa ahadi, uwe uthibitisho kwangu mimi pamoja na wewe mwenyewe;

Hapa Ayubu anaanza kuzungumza na Mungu.Katika Sentensi hii yeye anazungumzia hali yake kama vile alikuwa gerezani. Anamwomba Mungu kutoa msamaha ili ya kwamba yeye aweze kufunguliwa."Mungu, toa sasa msamaha ili kwamba mimi nipate kufunguliwa kutoka katika gereza hili" au " lipa kwa ajili ya kufunguliwa kwangu mimi kutoka gerezani"

nani mwingine yuko pale ambaye atanisaidia mimi?

Ayubu anatumia swali hili la kejeli kusisitiza kwamba hakuna mwingine awaye yote wa kumsaidia yeye. Swali hili laweza kuandikwa bila hali ya kuuliza ikasomeka hivi" "hakuna mwingine awaye yote ambaye atanisaidia mimi"

Job 17:4

habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza.

umeitunza mioyo yao

Neno "yao" linamaanisha rafiki zake yeye. Wao wamesemwa kwa "mioyo yao" kusisitiza hisia zao."umewatunza wao" au "umewatunza rafiki zangu mimi"

hautawaheshimisha wao juu yangu mimi.

"wewe hautawaruhusu wao kushinda juu yangu"

Yeye ambaye

"Mtu yeyote ambaye"

huwapinga rafiki zake hadharani, kwa ajili ya tuzo

"kwa uongo anawashitaki rafiki zake kwa ajili ya kupata faida" au "huwasaliti rafiki zake ili kupokea tuzo"

macho ya watoto wake yatashindwa kuona.

Watoto wa mtu wamesemwa hapa kwa "macho yao." Tungo hii inawaelezea watoto wanateseka kwa sababu ya kile ambacho baba zao au mama zao walifanya. " watoto wake watateseka kwa ajili yake"

Job 17:6

Habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza.

amenifanya mimi kuwa neno la kuzungumziwa na watu;

Sentensi hii ina maanisha kwamba watu wanasema juu yake kwa kumkejeli na kulitumia jina lake kama masimango."kwa sababu yake yeye mwenyewe, watu hutumia jina langu kama masimango" au "kwa sababu yao, watu hutumia jina langu kama neno la kuzungumzwa na watu"

wao wananitemea mate katika uso wangu mimi.

"watu hunitemea mate usoni pangu" Katika utamaduni huu kumtemea mate mtu usoni ilikuwa ni dhihaka kubwa. "watu hunisimanga mimi sana , kwa kunitemea mate mimi usoni pangu"

jicho langu pia halioni vizuri kwa sababu ya huzuni;

Mungu nazungumza juu y uoni wake kama "macho yake" "Kuona kwangu kumefifia kwa sababu Mimi nina huzuni sana" au "Mimi ni kipofu kabisa kwa sababu ya huzuni yangu"

sehemu zangu zote za mwili wangu ni nyembamba kama kivuli

Kivuli hakina wembamba.Hii ni lugha iliyokuzwa kwa kuonyesha jinsi gani sehemu za mwili wa Ayubu zilivyokuwa nyembamba.

sehemu zangu zote za mwili

Huu ni mjumuisho uliotumiwa kusisitiza kuwa mwili wake wote ni mwembamba, lakini ina maanisha kwa uwazi zaidi mikono yake na miguu yake. "mikono yangu na miguu yangu"

watashtushwa

"tiwa mshtuko" fadhaishwa"

kwa hiki

"kwa kile ambacho kimetokea kwangu mimi"

atajitia yeye mwenyewe juu ya kushindana dhidi

Hii ni nahau. "wata kuwa wametiwa hofu kwa sababu ya" au" wao watakasirihwa sana na"

Job 17:9

Habari za Jumla:

Ayubu anaendeleza kuzungumza.

ataendelea katika njia yake;

Hii ni nahau. "ataendelea kuishi katika njia ya haki"

yeye ambaye ana mikono iliyo safi

Sentensi hii inazunguza juu ya mtu kuwa asiye na hatia kama mikono iliyo safi. "yeye ambaye hutenda haki" au "yeye ambaye hana hatia"

ataendelea kuwa mwenye nguvu zaidi na zaidi

Maneno haya hayamaanishi tu nguvu za kimwili lakini pia nguvu za utashi wa mtu na hisia.

ninyi nyote

Ayubu anazungumza kwa Elifazi, Bildadi, na Sofari.

njooni sasa

Ayubu anawakaribisha rafiki zake kuhojiana kile ambacho amekisema. "njoni sasa, mhojiane na mimi"

Job 17:11

habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza.

Siku zangu zimepita

Hii ni nahau. "Muda wangu umepita" au "Maisha yangu yamefikia mwisho"

mipango yangu imenyamazishwa

"mipango yangu kamwe haitatokea" au "mipango yangu kamwe haitatimizwa"

na hivyo ni matumaini

Katika sentensi hii "moyo" wa Ayubu unamaaanisha shauku yake kubwa. "Kama kwa vitu ambavyo mimi nimevionea shauku zaidi"

ya moyo wangu

Katika mstari huu Ayubu hakukamilisha maneno yake kuonyesha kuwa hakuwa na tumaini lolote kwa shauku yake. "kwa moyo wangu, hakuna tumaini lolote la hayo kutokea"

Watu hawa, wenye kukejeli,

Hizi ni tungo mbili zinamaanisha watu wale wale wanoitwa rafiki za Ayubu, Elifazi, Bildadi, na Sofari.Tungo ya pili inasisitiza mtazamo wao usio wa kirafiki.

badili usiku kuwa mchana;

Sentensi hii inazungimzia watu wanaodai kuwa usiku ni mchana kama vile kweli wameubadili usiku kuwa mchana."wao wanadai kuwa huu ni muda wa mchana wakati ni usiku" au "kile wanachosema ni kinyume cha ukweli kama vile usiku ulivyo kinyume na mchana"

mchana uko karibu kuwa giza.

"wanadai kuwa nuru iko karibu na giza" au "wanadai kwamba wakati inapokuwa usiku, hiyo inakuwa mchana"

Job 17:13

Habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza.

mimi nitazame katika Kuzimu kama nyumbani kwangu;

"Kutazama" ina maanisha "kufikiri" kwa jinsi hiyo. Mimi ninafikiri juu ya kuzimu kama nyumbani kwangu" au "Mimi sasa nafikiri kuzimu ni nyumbani kwangu mimi"

Mimi nimetandaza kiti changu katika giza;

Sentensi hii ina maanisha Ayubu kuwa amejiandaaa kufa kama vile kuwa amekitandika kitanda chake yeye katika giza." "nimejiandaa mwenyewe kwenda na kulala miongoni mwa waliokufa"

nimetandaza kiti changu

"nimekitengeneza kitanda changu"

Mimi nimesema na shimo....na kwa funza,

Mistari hii miwili inatofautiana na imetumiwa kwa pamoja kusisitiza jinsi gani Ayubu alikuwa mkiwa"

shimo

"kaburi"

Wewe ni baba yangu

Ayubu anazungumzia ule ukaribu atakaokuwa nao hivi karibuni na kaburi lake akilinganisha na ukaribu wa mtu alio nao na familia yake"wewe uko karibu na mimi kama baba yangu" au"Wakati mimi nitakapozikwa, wewe utakuwa karibu na mimi kama baba"

funza

"wadudu wadogo." minyoo ambayo ni viumbe wadogo ambao hula miili iliyooza.

Wewe ni mama yangu au dada yangu;

Ayubu anazungumzia ule ukaribu atakaokuwa nao hivi karibuni na kaburi lake akilinganisha na ukaribu wa mtu alio nao na familia yake"wewe uko karibu na mimi kama mama yake na dada zake. "Wew uko karibu na mimi kama mama yangu na dada yangu" au"Wewe utakuwa karibu na mimi kama mama au dada"

liko wapi tena tumaini langu?

Jibu dhahiri ni "hakuna popote," kwa sababu hana tumaini. Swali hili la kejeli linaweza kuandikwa pasipo kutumia swali hivi: "Mimi sina tumaini"

Kama kwa tumaini langu, nani awezaye kuona chochote?

Swali hili la kizushi limetumika kusisitiza kuwa hakuna mtu yeyote anayetarajia yeye kuwa na tumaini lolote. Swali hili la kejeli linaweza kuandikwa bila kutumia swali hivi: "hakuna awaye yote anayeweza kuona tumaini kwangu" au "Hakuna ategemeaye mimi kuwa na tumaini lolote"

Job 18

Job 18:1

Habari za Jumla:

Tazama uandishi wa ushairi na mifano

Habari za Jumla:

Bildadi Mshunami anazungumza kwa Ayubu.

Ndipo Bildadi Mshuhi alijibu na kusema

"Bildadi" ni jina la mtu ambaye ni mmoja wa watu wa kabila la Shua.

Je, lini utaacha kusema kwako

Hili swali la kizushi lina maanisha kuwa Ayubu amekuwa akizungumza kwa muda mrefu. Swali hili la kejeli linaweza kuandikwa bila kutumia swali hivi: "Acha kuzungumza!"

Fikiri,

"Kuwa mwenye kufikiri"au" tafakari juu ya vitu hivi"

Job 18:3

Habari za Jumla:

Bildadi anaendelea kuzungumza kwa Ayubu.

Kwa nini sisi tumehesabiwa kama wanyama

Bildadi anatumia swali hili la kejeli kusisitiza kwa Ayubu kuwa hapaswi kufikiria kuwa ni mpumbavu. Yeye anazungumzia wao kufikiriwa kuwa ni wapumbavu kwa kuwaita "wanyama hatari wa porini." Swali hili laweza kuandikwa billa hali ya kuuliza ikasomeka hivi: Wewe hupaswi kufikiri kuwa sisi ni wanyama hatari wa porini." au "Wewe hupaswi kufikiri kuwa sisi ni wapumbavu kama wanyama"

Kwa nini sisi

Neno "sisi" huenda lina maanisha Bildadi na rafiki wengine wa Ayubu.

kwa nini tumekuwa wapumbavu machoni pako?

Bildadi anatumia swali hili la kejeli kwamba yeye hapaswi kuwafikiria wao kuwa ni wapumbavu."Sisi hatuko wapumbavu kama wewe unavyofikiri kuwa tuko hivyo"

machoni pako?

Katika sentensi hii neno uoni linawakilisha hukumu au tathimini. "katika hukumu yako"

Wewe ambaye wajirarua mwenyewe katika hasira yako

hapa Bildadi anasema kwamba ni kwa sababu ya hasira ya Ayubu na kutokuwa mtiifu kwa hiyo amejeruhiwa, siyo kwa sababu ya hasira ya Mungu kama vile alivyodai hapo kabla. Neno "rarua" hapa linamaanisha "jeruhi" "Wewe umesababisha kujeruhiwa kwako kwa sababu ya hasira"

nchi haipaswi kuachwa kwa ajili yako au miamba inapaswa kuondolewa kutoka mahali pake?

Swali hili la kizushi linasema kwamba kumwacha Ayubu ambaye wanamfikiria kuwa ni mtu mwenye hatia, aende kwa uhuru itakuwa kama kuubadilisha ulimwengu wote. Ayubu anatumia lugha ya kukuza sana jambo jinsi gani inavyoshangaza waanavyofikiri jinsi iliyo. Swali hili laweza kuandikwa billa hali ya kuuliza ikasomeka hivi: Kumwomba Mungu akuache wewe, mtu mwenye hatia, uende kwa uhuru ni kama upumbavu, kama kuiomba ardhi kusamehewa kwa faida yako au kwa ajili ya Mungu kuhamisha miamba kutoka mahali pake kukufurahisha wewe"

nchi inapaswa kusamehewa

"kila mmoja anapaswa kuiacha nchi"

miamba inapaswa kuondolewa kutoka mahali pake?

Neno "mwamba" katika sentensi hii lina maanisha miamba mikubwa, kama vile milima. "Mungu anapaswa kuihamisha milima kutoka mahali pake " au"Mungu aihamishe milima inayozungunguka mahali pale"

Job 18:5

habari za Jumla:

Bildadi anaendelea kuzungumza kwa Ayubu.

Ni dhahiri, nuru ya watu waovu itawekwa nje; cheche ya moto wake haitanga'ra.

Bildadi anazungumza juu ya mtu mwovu kufa kama vile taa yake ilikuwa imewekwa nje. "Kitakachotokea ni kwamba maisha ya watu waovu kama wewe hutoweka haraka kama vile tunavyoweka nje taa au kuzima mwali wa moto"

itawekwa nje;

"itaenda nje"

Nuru itakuwa giza katika hema yake; taa yake juu yake yeye itawekwa

Bildadi anaendelea kuzungumza juu ya maisha ya mtu mwovu kama vile yalikuwa kama mwanga katika hema yake. Itakuwa kama mwanga katika hema yake imerudishwa katika giza, kama taa juu yake iliyozimika.

Job 18:7

habari za Jumla:

Bildadi anaendelea kumwelezea mtu mwovu.

Hatua za nguvu zake yeye zitafanywa kuwa fupi;

maneno haya yanamhusu mtu mwovu ghafla anapatwa na janga kama vile yeye hakuwa na nguvu za kutembea. "Itakuwa kama yeye hakuwa na nguvu za kutembea"

mipango yake yeye mwenyewe itamwangusha yeye chini.

"Ushauri wake mwenyewe unamfanya yeye kuanguka chini." maneno haya yanamzungumzia mtu mwovu akipitia majanga kama vile anavyoanguka chini. "mipango yake yeye mwenyewe itamwongoza yeye katika janga"

Kwa maana yeye atatupwa katika mtego kwa miguu yake mwenyewe; yeye atatembea katika mahangaiko.

"Miguu yake mwenyewe itamwongoza katika mtego." Bibldadi anatumia picha hii kusema kwamba njia ambayo mtu mwovu anaishi maisha yake inamwongoza yeye katika janga la ghafla. " Itakuwa ingawa amejiongoza mwenyewe katika mtego, kama vile yeye alitembea katika mahangaiko"

mtego

ni nguo au kamba ambayo watu huunganisha pamoja kutengeneza kizuio. Watu walitumia mitego kunasa wanyama.

shimo la mahangaiko.

shimo lina matawi na majani juu yake ili kwamba mnyama atapita juu ya matawi yake na majani na kuanguka ndani ya shimo.

Job 18:9

habari za Jumla:

Bildadi anaendela kuzungumza na anatumia picha ya mifano mitatu kuelezea jinsi gani mtu mwovu ghafla atapitia kwenye majanga.

Tanzi litamchukua yeye...mtego utabaki ...Tanzi ime... kwa ajili yake.... katika njia

Tungo hizi nne zinazungumza juu ya mtu mwovu anayepitia majanga kama vile alikuwa amekamatwa na mtgo. "Itakuwa kama mtego utamchukua yeye...mtego uta....Tanzi ina....na mtego kwa ajili yake katika njia"

Tanzi

Watu walitumia aina hii ya mtego kukamata ndege. Mtego umenasa na kufunga na kushikilia kwenye miguu ya ndege.

litamchukua yeye kwa kisigino;

Katika sentensi hii "kisigino" kinamaanisha mguu wote" utaushikilia mguu wake"

Tanzi limefichwa kwa ajili yake chini ya ardhi;

"Mtu fulani ameficha mtego katka ardhi ili kumkamata yeye"

mtego

kamba yenye tundu ambalo hushikilia mguu wa wanyama wakati mnyama anapotembea katikati ya tundu.

na mtego kwa ajili yake

"na mtego umefichwa katika njia kumkamata yeye" au" na mtu fulani atauficha mtego kumkamata yeye katka njia"

Watishao watamfanya yeye aogope juu ya sehemu zote

"watishao wote wanaomzunguka watamfanya yeye aogope"

watamkimbiza yeye kwenye visigino vyake.

Sentensi hii inazungumzia vitu ambavyo vitamfanya mtu mwovu aogope kama vile kulikuwa na adui zake ambao walimfukuza yeye"

Job 18:12

Habari za Jumla:

Bildadi anaendelea kumwelezea mtu mwovu.

Utajiri wake utageuka kuwa njaa,

Maneno haya yanamzungumzia mtu mwovu atakuwa maskini na mwenye njaa kwa kuwa utajiri wake umerudishwa kuwa kitu kingine. "Badala ya kuwa na utajiri, yeye atakuwa maskini na mwenye njaa"

na majanga yatakuwa tayari upande wake.

Maneno "tayari" na kuwa upande wake" ni nahau inayomaanisha kuwa kitu fulani kinaendelea sasa. "na yeye ataendelea kupitia majanga" au "na yeye hataweza kuyaepuka majanga"

sehemu za mwili wake zitakuwa zimemezwa

Pia maneno haya yanazungumzia ugonjwa unaoharibu mwili kama vile ulikuwa mnyama ambaye amemshambulia yeye na alikuwa akimla yeye. Ugonjwa utakula pale katika mwili wake" au " Ugonjwa utaharibu ngozi yake"

mzaliwa wa kwanza wa kifo atazila sehemu zake yeye.

Katika sentensi hii ugonjwa umelinganishwa na "mzaliwa wa kwanza wa kifo." Kusema ugonjwa unaoharibu mwili wake kama vile ulikuwa mnyama ambaye amemshambulia yeye na alikuwa akimla yeye. "ugonjwa hatari utaharibu sehemu tofauti tofauti za mwili wake"

Job 18:14

habari za Jumla:

Bildadi anaendelea kumwelezea mtu mwovu.

Yeye ameraruliwa kutoka kwenye usalama wa hema yake

"Majanga yamemtoa yeye kutoka katika hema yake, mahali ambapo yeye alikuwa salama"

hakuweza kutembea

"na hakuweza kutembea" au"ilimlazimu yeye kuondoka"

mfalme mwenye utisho.

Hili ni rejeo kwa "Mfalme Kifo'" mungu mpagani ambaye alikuwa ameaminiwa kutawala juu ya kifo" "mmoja ambaye anatawala juu ya waliokufa" "mfalme wa kifo"

Watu ambao siyo wa kwake

"watu ambao si wa familia yake"

baada ya kuona ule moto umesambaa ndani ya nyumba yake yeye

Watu walitumia kemikali ya salfa kujikinga na magonjwa yoyote kutoka kwa mgonjwa anayekufa. "baada ya kumwaga kemikali ya salfa juu ya nyumba yake yote"

Job 18:16

Habari za Jumla:

Bildadi anaendelea kumwelezea mtu mwovu.

Mizizi yake itanyauka juu yake ... tawi lake litakatwa.

Sentensi hii inamzungumzia mtu mwovu kufa bila kuwa na uzao kama vile mti ambao mzizi wake umekauka, na matawi kusinyaa na hayatoi matunda. "Yeye atakufa na hataacha uzao, yeye atakuwa kama mti ambao mizizi yake imekauka na ambao matawi yake yote yamenyauka"

tawi lake yeye litakatwa.

""matawi haya yatanyauka"

kumbukumbu lake yeye litapotea kutoka katika nchi; yeye hatakuwa na jina katika mtaa.

Tungo hizi zinabeba maana moja na zimetumiwa pamoja kusisitiza ukweli kwamba hakuna mtu ambaye atamkumbuka yeye baada ya yeye kufa"

Kumbukumbu lake yeye litapotea kutoka katika nchi

Maneno haya yametafsiriwa hivi: "kumbukumbu" za mtu mwovu kama vile zilikuwa mtu aliyekufa" "Hakuna hata mmoja katika nchi ambaye atamkumbuka yeye"

hatakuwa na jina katika mtaa.

Hii ni ni nahau: "hakuna hata mmoja atembeaye katika mtaa atakayeweza hata kukumbuka jina lake yeye"

Job 18:18

habari za Jumla:

Bildadi anaendelea kumwelezea mtu mwovu.

Yeye atafukuzwa kutoka katika nuru mpaka kwenye giza na kuwa amefukuzwa nje na ulimwengu huu

maneno haya pamoja yanasisitiza ukweli kuwa mtu mwovu atapelekwa kuzimuni, mahali pa waliokufa.

Yeye atafukuzwa kutoka katika nuru mpaka kwenye giza

"Mungu atamfukuza mtu mwovu kutoka kwenye nuru kwenda kwenye giza"

na kuwa amefukuzwa nje na ulimwengu huu.

Sentensi hii inamaanisha Mungu kumfanya yeye aiache nchi na kwenda mahali ambapo watu waliokufa huenda. Na kama vile alikuwa kama akimfukuza yeye" "na M ungu atamfanya yeye kuuacha ulimwengu" au Mungu atampeleka yeye mahali ambapo watu waliokufa huenda"

amefukuzwa nje

"Mungu atamfukuza yeye"

Hatakuwa na mtoto wa kiume wala mjukuu miongonni mwa watu wake, wala kizazi chochote kitakachobakia mahali alipokuwa amekaa.

Kwa pamoja tungo hizi zinasisitiza kuwa yeye hatakuwa na familia au uzao ulioachwa"

mtoto wa mtoto wa kiume

"mjukuu"

uzao

"ndugu"

Wale wanaoishi upande wa magharibi watakuwa wametiwa hofu kwa kile kitakachotokea kwake siku moja; wale wanaoishi upande wa mashariki watakuwa wameogopeshwa kwa hicho.

Maneno "upande wa magharibi" na "upande wa mashariki" yote kwa pamoja yanamaanisha watu wote wanaoishi kila mahali. Lugha ya kukuza jambo imetumika kila mtu kaitka nchi atasikia kuhusu kile kilichotokea kwa mtu mwovu anayejulikana. "Kila mtu katika ulimwengu atashtushwa na kushangazwa wakati watakapoona kilichotokea kwa mtu mwovu." au"watu wengi wanaoishi upande wa mashariki na upande wa magaharibi watashtushwa na kushangazwa wakati watakapoona kinachotokea kwa mtu mwovu"

siku moja;

"siku fulani"

Job 18:21

Habari za Jumla:

Bildadi anazidi kumzungumzia mtu mwovu.

nyumba za watu wasio haki, ni sehemu ya wale wasiomjua Mungu

Tungo hizi mbili zina maana moja kwa watu walewale. Katika sentensi hii watu hawa wamezungumzwa kwa mahali ambapo wao wanaishi. "watu wasio haki, wale ambao hawamfahamu Mungu"

Job 19

Job 19:1

Sentensi Unganishi:

Ayubu anazungumza kwa rafiki zake watatu.

Habari za Jumla

Tazama uandishi wa ushairi na mifano ya miti wa mitini

mpaka lini mtanifanya mimi kuteseka na kunivunja vunja mimi vipande vipnde kwa maneno?

Ayubu anatumia swali hili kulalamika kuhusu jinsi rafiki zake wanavyomtemdea yeye. "Acheni kunifanya mimi niteseke na kunikatakata mimi vipande vipande kwa maneno."

kunivunja vunja mimi vipande vipande

Ayubu anatumia picha hii kusema kwamba maneno yao yanamfanya yeye ajisikie mwenye huzuni sana na asiyekuwa na tumaini. "na kunitesa kwa maneno"

Job 19:3

Habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Mara kumi hivi mmenishutumu mimi

Tungo "Mara kumi hivi" inamaanisha jinsi ambavyo rafiki zake wamemkemea kabisa Ayubu"Ninyi mmenidhihaki mimi" au" Ninyi mmenidhihaki mimi mara nyingi"

ninyi hamuoni aibu kwamba mmenitendea mimi kwa ukatili.

Ayubu anawakemea wao hivi. "Ninyi mnapaswa kuona aibu kwamba mmenitendea mimi kwa ukatili"

mmenitendea mimi kwa ukatili.

"mmenikejeli mimi"au "mmenidhihaki mimi hadharani"

nimekosa,

"nimetenda dhambi kwa bahati mbaya" au" kwa kufanya makosa nimetenda dhambi"

makosa yangu

"dhambi yangu" au" makosa yangu"

makosa yangu hubaki kuwa wajibu wangu.

Ayubu anamaanisha kwamba rafiki zake hawapaswi kuendelea kumdhihaki yeye" makosa yangu ni juu yangu mimi mwenyewe, hivyo hampaswi kuendelea kunikemea mimi" au " makosa yangu hayakuwaumiza ninyi, hivyo hampaswi kuendelea kunikekemea mimi"

Job 19:5

habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafikiz ake watatu.

Kama ni dhahiri ninyi mtajiinua juu yangu mimi

"Kama mnafikiri ninyi ni bora kuliko mimi" au" Kwa maana mnatenda kana kwammba ninyi ni bora kuliko mimi nilivyo"

na kuutumia uvumilivu wangu kunipinga mimi

"na kudai kuwa uvumilivu wangu ushahidi dhidi yangu" au"na kuutumia uvumilivu wangu kama ushahidi kwamba mimi ni mwenye hatia"

kuutumia uvumilivu wangu kunipinga mimi

Jina dhahania "uvumilivu" laweza kuelezwa pamoja na kitenzi"vumilia". "dai kwamba kile ambacho kimetokea kwangu kinathibitisha kwamba mimi ni mwenye hatia"

amenikamata mimi katika mtego wake yeye.

Ayubu anazungumza kama Mungu alikuwa mwindaji ambaye amemnasa Ayubu katika mtego wake. Tashbiha hii inamwakilisha Mungu akichukua udhibiti wa hisia za Ayubu za kukosa tumaini. "ameninasa mimi" au "amechukua udhibiti wangu mimi" au" anadhibiti kile kinachotokea , hivyo mimi sina msaada"

Job 19:7

Habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake watatu.

Tazama,

Neno hili "Tazama" linatia mkazo unaofuata."Haswa"

dhuluma!"

Hiki ni kilo cha ajili ya msaada. "dhuluma! Msaada! Mimi nimekuwa nikishambuliwa!"

Mimi ninaita kwa ajili ya msaada,

Mimi ninapiga kelele kwa ajili ya msaada" "Ninalia kwa ajili ya msaad"a

lakini hakuna haki.

Jina dhahania "haki"linaweza kutafsiriwa katika tungo hivi: "lakini hakuna hata mmoja anayenilinda mimi kutoka kwa hao wanaotenda mabaya kwangu"

Yeye ameiwekea ukuta .... giza katika njia yangu

"Mungu ameweka ukuta katika njia ambayo kwayo Mimi ninapita juu yake" au "Yeye ameifunga njia hivyo siwezi kuendelea kupita"

Yeye ameiwekea ukuta njia yangu, ili kwamba mimi nisiweze kupita, na yeye ameweka giza katika njia yangu

Ayubu anatumia picha hii kusema kwamba Mungu amemfanya yeye kujisikia kukosa msaada na bila tumaini.

Yeye ameniondoa Mimi kutoka katika utukufu wangu

Ayubu anatumia picha hii kusema kwamba Mungu amechukua heshima yake njema, mali, na mafanikio mbali kutoka kwake.

Yeye ameniondoa Mimi kutoka katika utukufu wangu

Ayubu anazungumza juu ya uttukufu wake kana kwamba kulikuwa na mwizi yule Mungu.

ameichukua taji kutoka kwenye kichwa changu mimi

Taji inaashiria utu wa Ayubu au heshima. "yeye ameiondolea mbali taji ya kichwa changu"

Job 19:10

Habari za Jumla:

Ayubu anaendeleza kuzungumza kwa rafiki zake watatu.

Yeye amenivunjavunja mimi chini kwa kila upande,

Ayubu nazungumza juu ya Mungu akimharibu yeye kana kwamba alikuwa jengo ambalo Mungu analiangusha chini. "Yeye ameniharibu mimi kwa njia zote" au amenishambulia mimi katika nia zote"au "amenishambulia mimi katika kila njia"

na Mimi nimetoweka

Kuwa" umekwenda"linawakilisha kuharibiwa kabisa. "na mimi nimeharibiwa kabisa"

yeye amelikokota juu tumaini langu kama mti.

Ayubu anazungumza juu ua Mungu kusababisha Ayubu kukosa tumaini kana kwamba Ayubu alikuwa mti, Mungu ameukokota mti wote na mizizi yake kutoka katika ardhi. ""yeye ametupilia mbali tumaini lake lote"au " kw sababu ya kile ambacho yeye amefanya, Mimi siwezi tena kutumaini kitu chochote kizuri"

yeye pia ameiongeza ghadhabu yake dhidi yangu mimi

Ayubu anazungumza juu ya hasira ya Mungu kana kwamba ilikuwa kama moto. "Mungu pia amemwaga moto wa hasira dhidi yangu mimi" au" Mungu pia amenikasirikia mimi"

yeye ananihesabu mimi kama mmoja wa adui zake.

"yeye anafikiri juu yangu mimi kama adui yake"

Majeshi yake huja juu pamoja;

Ayubu anazungumza juu ya Mungu kumshambulia yeye kana kwamba Ayubu alikuwa mji na Mungu alikuwa anatuma jeshi kushambulia. "Mungu anatuma jeshi lake kunishambulia mimi"

kuniteka nyara kwa kundi kubwa kupigana na mimi

Mungu anazungumza juu ya Mungu kumshambulia yeye kana kwamba Ayubu alikuwa kama ukuta wa mji na jeshi la Mungu lilikuwa likiuangusha vibaya ukuta na kuuteka mji. "wanajeshi walikuwa wakiuharibu vibaya ukuta ili kupanda juu ya ukuta"

wakizunguka hema yangu.

Mungu anazungumza juu ya Mungu kumshambulia yeye kana kwamba Ayubu alikuwa hema yake na jeshi la Mungu likipiga kambi kumzunguka yeye na kujiandaa kumshambulia yeye. "wanapiga kambi kuzunguka hema yangu na kujiandaa kunishambulia mimi"

Job 19:13

Habari za Jumla:

Ayuba anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake watatu.

Yeye amewaweka ndugu zangu mbali kutoka kwangu mimi;

kuwa mbali "mbali kutoka" kwa mtu fulani inawakilisha kutokutaka kuhusiana na yeye au kumsaidia yeye" Mungu amewasababisha ndugu zangu kukaa mbali na mimi" au " Mungu kuwasababisha ndugu zangu kukataaa kunisaidia mimi"

watu wangu wa karibu wote wamejitenga kutoka kwangu mimi

wasaidizi wangu wamejitenga wao wenyewe kuto kwangu" au " rafiki zangu hunitendea mimi kama mgeni"

Vizazi vyangu vimeniangusha mimi

"ndugu zangu mimi wameniacha bila msaada"

rafiki zangu wa karibu

"rafiki zangu wa karibu"

wamenisahamu mimi

Hii ina maana kwamba wao wamekataa kumtenda yeye kulingana na jinsi yeye na wao wamekuwa wakihusiana kwa kila mmoja wakati uliopita. Inamaanisha kwamba wao wanamtelekeza yeye. "wamenitelekeza mimi" au"kunipuuza mimi"

Job 19:15

habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake watatu.

hunihesabu mimi

"kunifikiria mimi"

Mimi nimekuwa mgeni katika macho yao

Kuona kwao kunawakilisha mtzazamo wao dhidi yake. "wao wanafikiri juu yangu mimi kama mgeni"

lakini yeye hanipi jibu

Jibu ni mwitiko wa kuita kwa Ayubu. "lakini yeye hajibu kwangu mimi" au " lakini yeye haji kwangu mimi"

japokuwa Mimi nimemsihi yeye kwa midomo yangu.

Tungo"kwa midomo yangu" inamaanisha Ayubu anazungumza" ingawa Mimi ninazungumza kwake yeye na kumwomba yeye."

Job 19:17

habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake watatu.

Pumzi yangu mimi ni chukizo kwa mke wangu;

Katika sentensi hii neno "pumzi" linawakilisha harufu ya pumzi yake yeye. Kama mtu fulani analaumika kwa mtu mwingine, ina maanisha kwamba yeye anaichukia. "Mke wangu anaichukia harufu ya kinywa changu"

wale ambao walizaliwa kutoka katika tumbo la mama yangu mimi.

Ayubu anamaanisha kaka zake na dada zake kwa njia hii kuonyesha kwamba wao ni watu ambao wanapaswa kumpenda yeye."kaka zangu mimi mwenyewe" au"kaka zangu na dada zangu"

wananichukia mimi;

"kunichukia mimi" au kunitenga mimi"

huzungumza dhidi yangu mimi.

"wao wananikejeli mimi" au" wananicheka mimi"

Rafiki zangu wote

"rafiki zangu wote wa karibu" au"rafiki zangu wote ambao huwaambia mambo yangu ya siri"

huzungumza dhidi yangu mimi

"wamenichukia mimi"

wamegeuka kinyume na mimi.

"wamenisaliti mimi"

Job 19:20

habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake watatu.

Mifupa yangu inashikamana kwenye ngozi yangu na kwenye mwili wangu;

Ayubu anazungumza juu ya mifupa yake, ngozi na nyama yake kuelezea mwonekano wake.Yeye alikuwa amekonda sana, na watu wangeweza kuona kwa urahisi mifupa yake yeye ilivyo. Lungha zingine zina nahau katika hili. " "Mimi sasa ni ngozi na mifupa" au " ngozi yake inashikamana na mifupa yangu"

Mimi ninaishi tu kwa ngozi ya meno yangu.

Hii nahau inamaanisha kwamba yeye anaishi kwa bahati tu, kuwa yeye karibia haishi."Mimi ninaishi kwa shida"

Iweni na huruma juu yangu mimi,

"muwe na huruma juu yangu"

kwa maana mkono wa Mungu umenigusa mim

Katika sentensi hii neno"alinigusa mimi" ni kiwakilishi cha neno "nipige mimi" Hii ni tashbiha kwa kufanya vitu ambavyo vinasabisha Ayubu ateseke. "kwa sababu Mungu amenitesa mimi"

Kwa nini mnanitesa mimi?

Ayubu anatumia swali hili kulalamika kuhusu jinsi rafiki zake wanavyomtendea yeye. "usinitese mimi....Mungu!"

kwa nini hamjatosheka bado kwa kula mwili wangu?

Ayubu anatumia swali hili kulalamika kuhusu jinsi rafiki zake wanavyomtendea yeye. Ninyi meumeza mwili wangu vya kutosha!" au "Acheni kuumeza mwili wangu mimi"

kwa nini hamjatosheka bado kwa kula mwili wangu?

Ayubu anazungumza juu ya rafiki zake wanaozungumza kwa ukatili kwake yeye kama vile walikuwa wanyama wakali wa porini wanakula wanyama wenzao. "Acheni kunishambulia mimi kwa maneno"

Job 19:23

Habari za Jumla"

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake watatu.

Laiti, hayo maneno yangu yangekuwa yameandikwa chini!

Mshangao huu unaeleza kile ambacho Ayubu anatamani kwa ajili yake."Mimi ninatamani kuwa mtu fulani angeyaandika chini maneno yangu"

maneno yangu

Tungo hii inawakilisha kile ambacho Ayubu anasema. "kile ambacho mimi ninakisema"

Laiti, hayo yangekuwa yameandikwa katika kitabu!

Mshangao huu unaeleza kile ambacho Ayubu anatamani kwa ajili yake."Mimi ninatamani kuwa mtu fulani angeyaandika katika kitabu"

Laiti, kwa kalamu ya chuma na risasi hayo yangekuwa yamechorwa katika mwamba siku zote!

Mshangao huu unaeleza kile ambacho Ayubu anatamani kwa ajili yake. "Mimi ninatamani kuwa mtu fulani angetumia kalamu ya chuma na risasi na kuyatunza katika pango siku zote"

kalamu ya chuma

Hiki kilikuwa kitendea kazi kilichotumika kuandika. kilikuwa kimetengenezwa kwa chuma ya kwamba watu waweze kuyaficha maneno katika mwamba"ni kifaa cha chuma"

risasi

Risasi ni madini laini ya chuma.Hatufahamu jinsi watu walivyotumia risasi wanapouchonga mwamba.Wanaweza kuwa wameijaza barua ya maandishi kwa risasi ili kuyafanya maandishi yadumu siku nyingi.

Job 19:25

Habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake watatu.

mkombozi wangu

Katika sentensi hii neno"mkombozi" linamaanisha mtu ambaye atamwokoa Ayubu kwa kthibitisha kuwwa Ayubu hana hatia., kurudisha heshima yake, na kumpa yeye haki. "Mtetezi wangu"

hata mwisho atasimama katika nchi;

Sentensi hii inamaanisha kusimama katika mahakama. Mkombozi atakuwa wa mwisho kuzungumza katika mahakama. "Yeye atahukumu ikiwa mimi ni mwenye hatia au hapana"mwisho atanitetea mimi katika mahakama"

baada ya ngozi yangu, hivyo ndivyo, mwili huu, unaharibiwa,

mwili wake yeye kuwa umeharibiwa au mwili wak kuoza baada ya yeye kuwa amekufa.

katika mwili wangu mimi Nitamwona Mungu.

Nyama yake inawakilisha mwili wake , na "katika nyama yangu" inamaanisha katika kuwa hai. Waakati Mimi ninaishi katika mwili wangu, Mimi nitamwona Mungu"

macho yangu mwenyewe-Mimi, na siyo mtu mwingine....nitamwona yeye

Neno"macho yangu"yanawakilisha Ayubu. Na tungo "macho yangu" "na" na "siyo mtu mwingie" kusisitiza kuwa Ayubu kwa hakika atamwona Mungu. Na siyo mtu mwingine atamwona Mungu na kumwambia Ayubu kuhusu yeye.

Figo zangu hushindwa ndani yangu

Watu walifikiri kwamba kwenye figo ndipo palipo na hisia. Hivyo figo kushindwa kufanya kazi inawakilisha yeye kuwa mwenye hisia nyingi sana. "Mimi ni mwenye hisia kali juu yake" au hisia zangu zinanitaabisha mimi kama vile nifikirivyo juu yake"

Figo zangu hushindwa ndani yangu

Maana za za sentensi hii zaweza kuwa : Ayubu anajisikia mwenye matumaini sana, mwenye shukrani, na mwenye furaha au Ayubu anajisikia mwenye kuchoka sana kusubiri kumwona mkombozi wake.

Job 19:28

habari za Jumla:

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Kwa jinsi gani tutamtesa yeye?

Huu ni mshangao! Kumaanisha kuwaa wao kwa hakika watamtesa Ayubu au watamtesa yeye vikali sana.

Mzizi wa mahangaiko yake unakaa katika yeye;

"Mzizi" unawakilisha chanzo. "Yeye ni chanzo cha mahangaiko yake" au " Yeye amekuwa na matatizo haya yote kwa sababu ya kile ambacho yeye amekitenda"

ndipo uwe umeogopeshwa kwa ule upanga,

Sentensi hii ina maanisha hivi: Mungu anawahukumu wao, au Mungu anawaua wao. "kisha uwe na hofu kwamba Mungu anawaua", au "kisha uogope kwamba Mungu atakuua wewe"

kwa sababu ghadhabu huleta hukumu ya upanga,

Katika sentensi hii maneno "huleta" ni tashbiha kwa neno "matokeo" au "chanzo" Majina dhahania "ghadhabu" na "hukumu" yaweza kuelezwa na kivumishi "kasirika" na kitenzi "adhibu." Maana zaweza kuwa hizi: Hasira ya Mungu inaleta hukumu. "kwa sababu Mungu atakukasirikia wewe na kukuadhibu wewe" au " hasira ya rafiki za Ayubu inaleta hukumu. "kama mna hasira sana na mimi, Mungu atawaadhibu ninyi"

kuna hukumu."

Jina dhahania "hukumu" laweza kuelezwa na kitenzi "hukumu""Mungu huwahukumu watu"

Job 20

Job 20:1

habari za Jumla:

Sofari anamjibu Ayubu.

Sofari, Mnaamathi

Sofari wa mkoa wa Naamathi

Mawazo yangu yananifanya mimi nijibu kwa haraka

Mawazo ya Sofari kumfanya yeye kutenda jambo ina maanisha shauku yake kubwa kutenda jambo. "Mimi nahitaji sana kukujibu wewe haraka"

kwa sababu ya mashaka yaliyomo ndani yangu mimi.

Jina dhahania "hofu" laweza kuelezwa pamoja na kivumishi "kuhofu"Sababu ya hofu hii yaweza kuelezwa "Kwa sababu mimi naogopeshwa sana na wewe" au "kwa sababu nimeogopeshwa sana na kile ambacho umesema"

Mimi ninasikia kukemewa ambako kunaniondolea heshima mimi

Jina dhahania "kemea" laweza kuelezwa pamoja na kitenzi "kemea." "Mimi ninasikia wewe unanikemea mimi, na kile unachokisema kinaniondolea heshima mimi" au "wewe wanidhalilisha mimi kwa jinsi ambavyo unanikemea mimi"

roho kutoka katika ufahamu wangu hunijibu mimi.

katika sentensi hii "roho" inamaanisha fikra au wazo" wazo kutoka katika ufahamu wangu linanijibu mimi"

roho kutoka katika ufahamu wangu hunijibu mimi.

"roho" au wazo imesemwa kama vile ilikuwa mtu ambayo inaweza kumjibu Sofari. "Mimi nina wazo kutoka katika ufahamu wangu na sasa Mimi ninafahamu kile ambacho nilihitaji kufahamu"

roho kutoka katika ufahamu wangu hunijibu mimi.

yaliyomo katika jibu yanaweza kuelezwa kwa ufasaha. "wazo kutoka katika ufahamu wangu hunijibu mimi kuhusu namna nitakavyojibu kwako" au Mimi nina wazo kutoka katika ufahamu wangu , na sasa Mimi ninafahamu namna nitakavyokujibu wewe"

roho kutoka katika ufahamu wangu hunijibu mimi.

Kielezi cha jina "roho"chaweza kuelezwa pamoja na kitenzi "fikiri" na "fahamu" Kwa sababu ninavifahamu vitu, Mimi nimefikiri, na sasa Mimi ninafahamu jinsi nitakavyokujibu wewe.

Job 20:4

Habari za Jumla:

Sofari anaendelea kuzungumza na Ayubu.

Je, unafahamu kwamba ukweli huu kutoka enzi za kale kwa kitambo?

Sofari anatumia swali hili kumfanya Ayubu afikiri kwa kina kwa kile ambacho sasa atazungumza. "Hakika wewe unafahamu kile ambacho kimekuwa cha kweli tangu siku za mababu....kwa kitambo"

ushindi wa mtu mwovu ni mfupi,

jina dhahania"mshindi" laweza kuelezwa pamoja na vitenzi "ushindi" au "sherehekea." mtu mwovu hushinda kwa muda mfupi tu" au " mtu mwovu husherehekea kwa muda kidogo tu"

na furaha ya mtu asiyemcha Mungu hudumu kwa kitambo tu?

jina dhahania "furaha" laweza kuelezwa pamoja na kitenzi "furahia" au kivumishi "furaha"." Neno "kitambo" ni baragha kusisitiza kuwa muda ni mfupi sana ."mtu asiye mcha Mungu hufurahia kwa kitambo tu" au "mtu asiye mcha Mungu ana furahi kwa muda mfupi sana"

Job 20:6

Habari za Jumla:

Sofari anaendelea kuzungumza na Ayubu

Ingawa urefu wake

""Ingawa urefu wa mtu mwovu"

Ingawa urefu wake yeye hufikia juu kwenye mbingu,

Kielezi cha jina "urefu" chaweza kuelezwa pamoja na kivumishi "refu". Ingawa yeye ni mrefu kama mbingu"

Ingawa urefu wake yeye hufikia juu kwenye mbingu,

Urefu wa mtu mwovu unawakilisha heshima yake, au kiburi chake."Ingawa heshima yake inafika mpaka mbinguni" au "Ingawa kiburi chake kinafika mbinguni"

Ingawa urefu wake yeye hufikia juu kwenye mbingu,

katika sentensi hii "kufika mbinguni" kunawakilisha kuwa mkubwa sana "Ingawa heshima yake yeye ni kubwa" au Ingawa kiburi chake ni kikubwa"

Ingawa urefu wake yeye hufikia juu kwenye mbingu,

Kielezi cha jina "urefu" kinawakilisha heshima yake yeye au kiburi. Mawazo yote haya yanaweza kuelezwa pamoja na aina nyingine ya tungo."Japkuwa watu hufikiri kuwa yeye ni mtu mkuu sana" au" Japokuwa yeye ni mkuu"

na kichwa chake yeye kufikia kwenye mawingu

"japokuwa kichwa chake ni kirefu kama mawingu" " Hii pia iinawakilisha heshima yake yeye au kiburi chake kwa kuwa mkuu. Hii inamaana kama ile ya mistari iliyotangulia.

atapotea siku zote kama mavi yake yeye mwenyewe;

Mavi huchanganikana na udongo na kupotea. Rejeo hili kuhusu mavi linaweza pia kumaanisha kuwa mtu mwovu hana thamani. "atapotea siku zote kama mavi yake, ambayo hupotea kabisa katika udongo.

atapotea siku zote kama mavi yake yeye mwenyewe;

"atapotea siku zote kama mavumbi ambayo upepo huyapeperusha mbali"

Job 20:8

Habari za Jumla:

Sofari anaendelea kuzungumza kwa Ayubu.

Yeye ata

"Mtu mwovu ata"

atapaa mbali kama ndoto .... yeye atakuwa amefukuzwa mbali kama ono la usiku.

Katika sentensi hii neno "paa mbali" na "kufukuzwa mbali" yanawakilisha kutoonekana au kusahauliwa, kwa maana ndoto na maono hupotea wakati watu wanapozisahau. "Yeye hataonekana kama ndoto ....yeye atasahaulik akama ono la usiku"

na hataonekana tena

"na hakuna mtu yeyote atayemuona"

Jicho ambalo lilimuona yeye

Macho yanawakilisha mtu. "Mtu yeyote ambaye amemuona yeye", au "Watu waliomuona yeye"

mahali pake

Tungo "mahali pake yeye" inawakilisha wale walioishi katika sehemu yake yeye" "watu ambao huishi katika sehemu yake yeye' au" familia yake"

Job 20:10

Habari za Jumla:

Sofari anaendelea kuzungumza kwa Ayubu.

Watoto wake

"Watoto wa mtu mwovu"

mikono yake itaweza kurudisha utajiri wake.

Katika sentensi hii "mikono"inamaanisha watoto wa mtu mpumbavu. Wakati atakapokufa watoto wake watapaswa kurudisha kila kitu ambacho yeye alikichukua kwa watu wengine.

Mifupa yake imejaa nguvu za ujanani,

"Mifupa" yake inawakilisha mwili wake. Kuwa "umejawa" na nguvu za ujanani kunawakilisha kuwa na nguvu kama mtu kijana."Mwili wake una nguvu kama mwili wa mtu kijana"

lakini zitalala naye chini katika mavumbi.

Sentensi hii inamaanisha nguvu zake za ujanani "kulala chini katika mavumbi" kunawakilisha kupotelea mbali. " lakini nguvu zake za ujanani zitakufa maoja naye" au "lakini nguvu zake za ujanani hazitaonekana wakati atakapokufa"

Job 20:12

habari za Jumla:

Sofari anaendelea kuzungumza na Ayubu.

japokuwa uovu ni mtamu katika mdomo wake

Katika sentensi hii "uovu ni mtamu" tungo hii inawakilisha mtu ambaye anafurahia kufanya vitu. "Japokuwa kufanya vitu viovu inafurahisha, kama kuonja chakula kitamu katika mdomo"

japokuwa yeye anauficha yeye... hauruhusu kwenda

Tungo hii inawakilisha kutaka kuendelea kufurahia uovu kama vile mtu atakavyo kuendelea kuonja chakula kwa kukitunza katika mdomo.

chakula katika koromeo lake yeye hugeuka kuwa uchungu;

Wakati chakula kinapogeuka kuwa uchungu katika tumbo, inasababisha maumivu na ladha chungu. Hii ni tashbiha kwa mtu anayepitia mateso ya kufanya vitu viovu. Vito hivyo viovu, huwa kama chakula ambacho kimegeuka uchungu katika tumbo." au" cha maumivu kama chakula kilichogeuka kuwa kichungu ndani ya tumbo.

hugeuka kuwa sumu ya majoka ndani yake yeye.

Hii picha ni mbaya kuliko hata chakula chenye uchungu katika tumbo. Hii ni tashbiha inayoonyesha mtu akipitia mateso makali kwa kutenda vitu viovu. Madhara ya kufanya vitu viovu ni makali kama sumu ya majoka ndani yake"

majoka

"ni nyoka wenye sumu kali"

Job 20:15

Habari za Jumla:

Sofari anaendelea kuzungumza kwa Ayubu.

Yeye humeza chini utajiri, lakini yeye atautapika tena; Mungu atautoa nje kutoka katika tumbo lake

Sofari anazungumza juu ya kupata au kupoteza utajiri kana kwamba kilikuwa chakula ambacho mtu hula na kukitapika. "Mtu mwovu huwa mwenye mali nyingi lakini hpoteza utajiri wake kama mtu ambaye hukitapika chakula chake yeye. Mungu anamfanya kupoteza vyote"

Yeye humeza chini utajiri,

Maana zaweza kuwa hizi: kujikusanyia utajiri na kuunza kwa ubinafsi. "Mtu mwovu hupata hupata mali nyingi na huutuza wote kwa ajili yake yeyey mwenyewe" au" kujikusanyia mali katika njia za uovu""Mtu mwovu huiba mali nyingi"

Mungu atautoa nje kutoka katika tumbo lake yeye.

Katika sentensi hii: tungo: "kuutapika nje ya tumbo lake" ni ishara ya kumsababisha kuvitapika. Hii ni tashbiha inayoelezea kumsababisha mtu kupoteza utajiri wake.

toa

"tupa"

yeye atamumunya sumu ya majoka;

"kumumunya sumu ya majoka" kunawakilisha kufanya vitu viovu. Vyote ni hatari sana. Kufanya vitu viovu ni kuhatarisha maisha yake kama mtu anayemumunya sumu ya majoka"

majoka;

"nyoka wenye sumu kali"

ulimi wa nyoka mwenye sumu utamwua yeye.

Swira ni nyoka mwenye sumu kali . Ulimi wake unawakilisha mnga'to wake wenye sumu. Mng'ato wa Swira mwenye sumu unawakilisha mnga'to wake wenye sumu."Mng'ato wa Swira mwenye sumu utamwua yeye" au"Swira atamuuma yeye na yeye atakufa"

ulimi wa nyoka mwenye sumu utamwua yeye.

Swira anawakilisha uovu wa mtu. "uovu wake utamwua yeye kama kung'atwa na Swira.

Job 20:17

Hbari za J umla:

Sofari anaendelea kuzungumza kwa Ayubu.

vijito vya maji, wingi wa asali na siagi.

Vijito vya maji na wingi wa asali ni tashbiha kuwakilisha wingi. Asali na siagi kuwakilisha vitu vizuri ambavyo Mungu huwapa watu. ""wingi wa vitu vizuri ambavyo Mungu huwapa watu"

matunda ya kazi yake

"matunda ya kazi yake" inamaanisha matokeo ya kazi yake.Katika hoja hii inamaanisha vitu ambavyo mtu mwovu ameiba."vitu ambavyo amefanya kazi kuvipata" au"vitu ambavyo ameviiba"

Job 20:20

Hakuna chochote kilichoachwa ambacho yeye hakukimeza;

"Yeye alimeza kila kitu, na hakuna kitu chochote kilichobakia" au"hakuna kitu chochote kilichobakia kwa sababu yeye amemeza kila kitu"

Hakuna chochote kilichoachwa ambacho yeye hakukimeza;

"kumeza"kunawakilisha kuchukua vitu kwa ajili yake mwenyewe. "Hakuna chochote ambacho hakukichukuwa kwa ajili yake mwenyewe" au" Yeye alichukua kila kitu kwa ajili yake mwenyewe, na hakuna kitu chochote kilichobakia"

yeye ataanguka katika mahangaiko

"ghafla yeye atapittia mahangaiko"

mkono wa kila mmoja ambaye yuko katika umaskini utakuja kinyume chake yeye.

katika sentensi hii "mkono" unawakilisha nguvu, na "mkono... utakuja dhidi yake" unawakilisha watu kumshambulia yeye. Kielezi cha tendo "umaskini"chaweza kuelezwa pamoja na kivumishi "maskini" "kila mtu aliye katika umaskini atamshambulia yeye" au "kila mtu ambaye ni maskini atamshambulia yeye"

Job 20:23

Habari za Jumla:

Sofari anaendelea kuzungumza kwa Ayubu.

kulijaza tumbo lake

"kulijaza tumbo lake" inamaanisha kula sana.

Mungu atatupa hasira ya ghadhabu yake juu yake yeye

"katika hasira ya ghadhabu yake" ina maanisha hasira ya Mungu na adhabu yake.Kutupa adhabu juu yake ni kumwadhibu yeye vikali sna. "Mungu atakuwa mwenye hasira na kutupa chini adhabu yake juu yake"au"Mungu atakasirika na kumwadhibu yeye vikali sana"

Mungu ataunyeshea chini juu yake yeye

"Mungu ataisababisha inyeshe chini juu yake." "kunyesha chini juu yake" inawakilisha kusababisha adhabu nyingi kutokea kwa mtu. "Mungu atamwadhibu yeye vikali"

atakimbia kutoka katika silaha ya chuma,

Silaha ya chuma inawakilisha mtu kuibeba yenyewe. "atakimbia kutoka kwa mtu anayebeba silaha ya chuma"

upinde wa shaba utampiga yeye

Upinde unawakilisha mtu anayepiga upinde kwa kutumia upinde. "Mtu mwenye upinde wa shaba atampiga yeye"

ini

Hii ni sehemu yenye muhimu wake mkubwa katika mwili. Ikiwa mtu atapiga upinde kwenye ini, mtu aliyepigwa atakufa.

watesi huja tena juu yake.

Maneno haya yanamwakilisha yeye kwa ghafla anakuwa amefadhaishwa"

Job 20:26

Giza lililo kamilika limetunzwa kwa akiba zake;

"Giza lililokamailika" ni tashbiha kuonyesha uharibifu. "Uharibifu umetunzwa kwa ajili ya akiba zake yeye"au"Akiba zake yeye mwenyewe zitaharibiwa"

moto usiopulizwa utamla yeye

katika tungo hii neno "kumeza" ni tashbiha inayomaanisha kuharibu."mto ambao haukupulizwa utamharibu yeye"

moto usiopulizwa utamla yeye

Tungo "haukupulizwa" inamaanisha kuwa kuwa hakuna mwanadamu ambaye atauwasha moto. Ni Mungu atauleta moto. "moto ambao haukuwashwa na mwanadamu utamharibu yeye"au" Mungu atauleta moto kumharibu yeye"

utameza

Neno hili lemetafsiriwa hivi: "kumeza" ni tashbiha kumaanisha kuharibu."mto utaharibu"

Mbingu...na nchi

Tungo hii inaweza kutafsiriwa hivi: Wale anaoishi katika mbingu na juu ya nchi, au Sofari anazielezea mbingu na nchi kana kwamba ni binadamu ambaye atashuhudia katika mahakama dhidi ya mtu mwovu.

Job 20:28

Habari za Jumla:

Sehemu hii ni hitimisho la hotuba ya Sofari kwa Ayubu.

toweka

"kutoonekana" au "enda mbali"

bidhaa zake zitamwagika mbali

Maneno "mwagika mbali" yanawakilisha kuondolewa mbali kutoka kwake."bidhaa zake zitachukuliwa mbali kutoka kwake, kama bidhaa zinazoelea katika mafuriko"

siku ya ghadhabu ya Mungu.

Neno "ghadhabu" linawakilisha kuadhibiwa. Kielezi cha jna "ghadhabu" chaweza kuelezwa pamoja na kitenzi "adhibu""siku ambayo Mungu huwadhibu watu"

Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kutoka kwa Mungu,

Maneno "sehemu kutoka kwa Mungu" yanawakilisha kile ambacho Mungu amekikusudia kitokee kwa mtu fulani. Kimezungumzwa kana kwamba kilikuwa kitu ambacho Mungu angempa yeye. "Hiki ndicho ambacho Mungu amekikusudia kitokee kwa mtu mwovu"

urithi uliotunzwa akiba na Mungu kwa ajili yake yeye."

Tungo hii inawakilisha kile ambacho ameamua kinapaswa kitokee kwa mtu fulani. Kimezungumzwa kana kwamba kilikuwa kitu ambacho Mungu angempa yeye hapo kabla kama urithi. "Kile ambacho Mungu amekipanga kumpa yeye" au "kile ambacho Mungu amekikusudia lazima kitokee kwake"

Job 21

Job 21:1

Sentensi unganishi

Ayubu anaanza kujibu mashitaka ya Sofari

Univumilie

"Uniruhusu" au " uwe mstahimilivu kwangu"

Endelea kunidhihaki

" unaweza kuendelea kunidhihaki"

Job 21:4

Sentensi Unganishi.

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Je mimi, malalamiko yangu ni dhidi ya mtu? Kwa nini nisiwe mvumilivu?

Ayubu anatumia maswali kusisitiza kuwa ni hali ya kawaida kwake kumlalamikia Mungu.KT: "Simlalamikii mtu . ninahaki ya kutokuwa na uvumilivu"

weka mkono wako juu ya kinywa chako

"funika kinywa chako kwa mkono wako" Maneno haya yanaweza kumaanisha kwamba 1) huu ni mwitikio wa kuwa katika mshangao. KT: " funika kinywa chako kwa mkono wako" au 2) hiki ni kiashiria kuwa mtu hataongea . KT: "usiseme lolote"

mashaka yameushika mwili wangu

" hofu inasababisha mwili wangu kutetemeka" au "ninatetemeka kwa hofu"

Job 21:7

Sentensi unganishi

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Kwa nini watu waovu wanaendelea kuishi na kuwa wazee na kustawi katika nguvu nyingi?

Ayabu anatumia swali hili kuonesha kuwa rafiki zake walikosea kudhani kwamba watu waovu mara nyingi hupatwa na mateso. KN: " watu waovu huendelea kuishi, huzeeka, na kuwa na utajiri zaidi"

Wazao wao huimarika pamoja nao katika upeo wao...kizazi chao mbele ya macho yao.

Vishazi hivi viwili vinamaana ya jambo moja na vinaweka msisitizo kuwa jambo hili ni la kweli.

katika upeo wao... mbele ya macho yao

Misemo hii inamaanisha jambo moja kwa sababu "macho" yanahusiana na upeo wa kuona. Watu waovu huwaona wazoa wao wakistawi na kutajirika.

Nyumba zao

Hapa "nyumba" inamaanisha wanafamilia wanaoishi humo. KT: "Familia zao"

fimbo ya Mungu

inamaanisha adhabu ya Mungu.

Job 21:10

Sentensi unganishi

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

hapotezi ndama wake mchanga

" haharibu mimba" au " ndama wake huzaliwa mathubuti na mwenye afya"

watoto wao kama kundi

Ayubu anawalinganisha watoto hawa na wanakondoo ili kusisistiza kwamba hukimbia, hucheza, na wanafuraha.

tari

ni chombo cha muziki chenye ngoma inayoweza kupigwa pamoja na vipande vya chuma pembeni ambavyo hutoa sauti wakati chombo hicho kinapotikiswa.

Job 21:13

Sentensi unganishi

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

siku zao

"muda wao wa kuishi"

Hushuka taratibu kwenda kuzimu

KT: "hufa kwa amani"

njia zako

inamaanisha jinsi Mungu anavotaka watu waenende.

Mwenyezi ni kitu gani, hata itupase kumwabudu? Ni faida gani tungepata kama tungemwomba?

watu waovu hutumia maswali haya katika kumdhihaki Mungu. KT: Hatuamini kwamba huyu Mungu Mwenyezi anastahili tumwabudu. Hawezi kufanya chochote kwa ajili yetu"

Job 21:16

Sentensi unganishi

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Tazama, je kufanikwa kwao hakupo mikono mwao mwenyewe?

hapa "mikono" inamaanisha nguvu zao au utawala wao. Ayubu anatumia swali hili kutoa changamoto kwa rafiki zake. KT: "Tazama, watu hawa waovu wanasema kwamba wamesababisha mafaniki wao wenyewe!"

Je ni mara ngapi... msiba wao huwajilia?

Ayubu anatumia swali hili kusisitiza kuwa yeye anaona kwamba Mungu hawaadhibu waovu mara nyingi. KT: "si mara nyingi ... msiba wao huwapata "

taa ya watu waovu imezimwa

Ayubu analinganisha kuzima taa na kufa. KTN: "Mungu husababisha wafe ghafla"

Ni mara ngapi hutokea... katika hasira yake?

Ayubu anatumia swali hili la pili kuweka mkazo kuwa inaonekana mara nyingi Mungu huwa hawaadhibu waovu. KTN: "Si mara nyingi ... katika hasira yake."

Ni mara ngapi ... dhoruba huwabeba?

Ayubu anatumia swali hili la tatu kuweka mkazo kuwa inaonekana mara nyingi Mungu huwa hawaadhibu waovu.KTN: "Si mara nyingi ... dhoruba huwabeba."

wanakuwa kama mabua mbele ya upepo au kama makapi ambayo huchukuliwa na dhoruba

Kifo cha waovu kinaongelewa kana kwamba ni makapi yasiyofaa na mabua yapeperushwayo.KTN: "Mungu huwaondoa kama upepo upeperushao makapi"

Job 21:19

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Ninyi mwasema

maneno haya yanaonesha kuwa Ayubu anawanukuu rafiki zake.

Mungu huweka hatia ya mtu kwa ajili ya watoto wake kuilipa

Hatia inaongelewa kama kitu ambacho kinaweza kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Hapa kulipa inamaanisha adhabu kwa ajili ya dhambi. KTN: "Mungu hutunza kumbukumbu ya dhambi za mtu, kisha huwaadhibu watoto wa mtu huyo kwa matendo yake maovu"

alipe yeye mwenyewe

Ayubu anaanza kutoa mawazo yake. KTN: " Lakini mimi nasema, alipe yeye mwenyewe"

Macho yake mwenyewe yaone

"Macho" ni rejea kwa mtu.KTN: "aweze kuona yeye mwenyewe"

anywe ghadhabu Mwenyezi

Ghadhabu ya Mungu inasema kana kwamba ni kinywaji ambacho mtu anaweza kuonja. Ayubu anataka waovu wapate adhabu ya Mungu.

Kwani anajali nini kuhusu familia yake baada ya idadi ya miezi yake kuondolewa?

Ayubu anatumia swali kuonesha kuwa kuwaadhibu watoto wa mtu mwovu haina nguvu.KTN: "Kwani mtu mwovu hajali kuhusu familia yake baada ya kufa!"

idadi ya miezi yake kuondolewa

hii ni namna ya staha kusema anapofariki.

idadi ya miezi yake

Hii inarejea urefu wa miaka ya maisha yake.

Job 21:22

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Mtu yeyote anaweza kumfundisha Mungu maarifa ikiwa yeye huwahukumu hata wale walio wakuu?

Ayubu anauliza swali kusisitiza kwamba Mungu anajua kila kitu. KTN: "Ni wazi, hakuna mtu anayeweza kumfundisha Mungu chochote kwani yeye huwahukumu hata wale walioko mbinguni."

walio wakuu

inaweza kumaanisha kuwa 1) "wale walioko mbinguni" au 2) "watu mashuhuri"

mtu mmoja hufa katika nguvu zake kamili.

Ayubu anamlinganisha mtu huyu afaye katika afya na amani na mtu afaye katika hudhuni na maumivu. KTN: "Kama kuma watu wawili, mmoja anaweza kufa katika nguvu zake kamili"

mwili wake umejaa maziwa

hii inamaana kwamba mtu yupo katika afya njema.

mwili wake umejaa maziwa... uboho wa mifupa yake umarainishwa na katika afya nzuri.

hii inamaana kwamba mtu yupo katika afya njema.

mwili wake umejaa maziwa

Neno "maziwa" linamaana ya "mnene" KTN: "mwili wake umejaa mafuta"

uboho wa mifupa yake umarainishwa na katika afya nzuri.

hii ni nahau ikimaanisha kuwa mwili wake una ujana na afya njema.

Job 21:25

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

mtu mwingine hufa

Ayubu anamlinganisha mtu huyu na mtu ambaye hufa katika amani 21:22

katika uchungu wa roho

"Roho" inamaanisha mwanadamu kamili. KTN: 'kwa uchungu na majuto" au " baada ya kuishi maisha ya huzuni"

pasipo kuonja mema yoyote

KTN:"akiwa ameonja vitu vibaya tu"

Hao vilevile hulala chini katika mavumbi

Hii ni kusema kwa staha kuwa hao hufa. KTN: " Hao wote hufa na watu huwazika"

Minyoo huwafunika wote

minyoo huhusiana na kuoza kwa mizoga. KTN "katika uchafu minyoo hula mizoga ya miili yao"

Job 21:27

Sentensi unganishi

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Tazama

Ayubu anatumia neno hili kuleta usikivu kwenye maneno yanayofuata. KTN: " angalia "

Sasa nyumba ya mfalme ipo wapi? ipo wapi hema ambapo mtu mwovu aliishi hapo mwanzo?

Maswali yote hay yana maanisha jambo moja. KTN: "Tazama, nyumba ya mtawala mwovu haipo. Hema ya mtu mwovu imetoweka"

Job 21:29

Setensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Je hamjawaliza watu wasafirio? Je hamjui viashiria wavyoweza kuwaambia ... kwa siku ya ghadhabu?

Ayubu anawakemea rafiki zake kwa kutumia maswali haya kuwa hawajajifunza kwa watu wasafirio. KTN: "Ninyi mnapaswa kuwasikiliza wale waliosafiri hadi sehemu za mbali. watawaambia ... kwa siku ya ghadhabu."

mtu mwovu huindwa kwa siku ya msiba ... huongozwa kwa siku ya ghadhabu

virai hivi vina maana sawa: KTN: "Mungu humhifadhi mtu mwovu wakati anapoleta maafa"

Job 21:31

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.

Ni nani ataishutumu njia ya mtu mwovu kwenye uso wake?

Ayubu anatumia swali hili kupinga dhana ya kuwa waovu mara zote hupatwa na hukumu. KTN: ' Hakuna anayemshutumu mtu mwovu kwenye uso wake"

kwenye uso wake

Hapa inamaana kuwa hakuna mtu atakaye kwenda moja kwa moja kwake na kumshutumu.

Ni nani atamlipiza kwa yale aliyotenda?

Ayubu anatumia swali hili kupinga imani ya rafiki zake kuwa waovu mara zote hupatwa na hukumu. KTN: ' Hakuna mtu anayemlipiza mwovu kwa mambo mabaya aliyotenda"

atazikwa

KTN: " Watu watambeba"

Madonge ya bondeni yatakuwa matamu kwake

Maana yake ni kwamba mtu mwovu atakuwa na kifo chema na maziko mema baada ya kutimiza maisha yake. KTN: "atafurahia kufukiwa kwa uchafu wa bondeni" au " atafurahia kuzikwa katika uchafu wa bonde"

watu wote watamfuata, kutakuwa na watu wengi mbele yake

Ayubu anaweka makazo kuwa kundi kubwa la watu watakuwepo katika harakati za mazishi yake kutoa heshima. KTN: "idadi kubwa ya watu watakwenda kwenye eneo la makaburi; baadhi wakiwa mbele na wengine nyuma"

Job 21:34

Sentensi Unganishi

Hili ni hitimisho la mazungumzo ya Ayabu kwa rafiki zake.

imekuwa basi kunifariji kwa upuuzi, kwani katika majibu yenu hakuna kitu isipokuwa uongo?

Ayubu anatumia swali kuwakaripia rafiki zake. KTN: " haiwezekani mnifariji kwa upuuzi. majibu yenu yote ni uongo."

Job 22

Job 22:1

Elifazi Mtemani

Jina la mtu, angalia 2:11

Je mtu anaweza kumfaa Mungu? Je mtu mwenye busara anaweza kumfaa Yeye?

Elifazi anatumia maswali kuweka mkazo kuwa matendo ya mtu au hekima havina faida kwa Mungu. KTN: "Mtu hawezi kumfaa Mungu. Mtu mwenye busara hawezi kuwa na faida kwake faida kwa kwake"

Je kuna furaha yoyote kwa mwenyezi kama wewe ni mwenye haki? Je ni faida kwake kama utazifanya njia zako kuwa timilifu?

Sentensi zote zina maana moja. Elifazi anatumia maswali kukazia kuwa matendo yake Ayubu hayana msaada kwa Mungu.KTN: "Mwenyezi hapokei furaha yoyote kama wewe ni mwenye haki. Hafaidiki na chochote kama utazifanya njia zako kuwa timilifu"

Job 22:4

Sentensi Unganishi

Elifazi anaendelea kuongoa kwa Ayubu.

Je anakukemea na kukuhukumu kwa sababu ya kumcha yeye? Je uovu wako siyo mkuu? Je hapana mwisho wa maovu yako?

Elifazi anatumia maswali kumkaripia na kumlaumu Ayubu kwa kutenda dhambi za kutisha. KTN: "Ni kuwa kuwa hujajitoa kwake kikamilifu ndiyo maana Mungu anakukea na kukuhukumu! Hapana, kama ujuavyo, anakuhukunu kwa sababu uovu wako ni mkuu na unaendelea kutenda dhambi"

Job 22:6

Sentensi Unganishi

Elifazi anaendelea kuongoa kwa Ayubu.

Umedai dhamana ya mkopo

Maana yake mkopeshaji anachukua kitu kutoka kwa mkopaji ili kuhakikisha kwamba mkopaji atalipa.

umetwaa vazi kwa walio uchi

Elifazi anamshutumu Ayubu kuchukua nguo kutoka kwa watu masikini waliomkopa kama dhamana

ulimnyima mkate

hapa "mkate" unawakilisha chakula kwa ujumla

alimiliki nchi.. aliishi ndani yake

Elifazi anamshutumu Ayubu kuchukua eneo kutoka kwa watu masikini na wala hakuwaruhusu kuishi sehemu ile.

alimiliki nchi

"alimiliki eneo kubwa la ardhi"

Job 22:9

Sentensi Unganishi

Elifazi anaendelea kuongoa kwa Ayubu.

umewafukuza wajanae hali ya utupu

uliwafanya wajane waondoke bila kitu chochote

Wajane

wanawakea ambao waume zao wamefariki

mikono ya yatima imevunjika

hapa "mikono" inarejea nguvu. KTN: 'hata uliwakandamiza yatima"

mitego imekuzunguka ...kuna giza ..kwenye maji mengi.

sitiari zote hizi maana yake kuna shuda na hatari kumzunguka Ayubu kwa sababu ya dhambi zake.

kwenye maji mengi.

" kwenye mafuriko"

Job 22:12

Sentensi Unganishi

Elifazi anaendelea kuongoa kwa Ayubu.

Je Mungu hayupo kwenye kimo cha mbingu?

Elifazi anatumia swali hili kudokeza kwamba Mungu anaiona dhambi ya Ayubu na atamuhukumu. KTN: " Mungu yupo katika vimo vya mbingu na anaona kila kitu kinachotokea duniani"

tazama kimo kwenye kima cha nyota , je zipo juu kiasi gani!

Elifazi amaanisha kuwa Mungu yupo juu kuliko nyota. KTN: Angalia jinsi nyota zilivyo juu . Mungu yupo juu kuliko hizo nyota"

Je Mungu anajua nini? je anaweza kuhukumu kwenye mawingu mazito?

Elifazi anatumia maswali haya kumaanisha kwamba Ayabu amasema mambo haya dhudi ya Mungu. KTN: " Mungu hajui kitu gani kinatokea duniani. anakaa kwenye wingu la giza na hawezi kutuhukumu sisi."

yeye hutembea kwenye kuba ya mbingu

Kuba inarejea kwenye mpaka ambao watu wa kale waliamini ulitenganusha dunia na mbingu. KTN "anaishi mbali sana kwenye mbingu kuona ni nini kinatokea hapa"

Job 22:15

Sentensi Unganishi

Elifazi anaendelea kuongoa kwa Ayubu

utaendeza njia ya zamani ambayo walitembea watu waovu.

Kutenda matendo mabaya kunazungumziwa kama kutembea kwenye njia. KTN: " utaendelea kufanya mambo wafanyayo watu waovu"

wale ambao walinyakuliwa

"wale waliokufa" au wale ambao Mungu aliwaondoa"

wale ambao misingi yao imetoweshwa kama mto

kifo cha watu waovu kinaongeleawa kana kwamba ni majengo yaliyokuwa na misingi yake ambayo ilikwishwa haribiwa na mafuriko.

Mwenyezi anaweza kufanya nini

Elifazi ananukuu swali ambalo waovu hutumia kumdhihaki Mungu. KTN "Mwenyezi hawezi kufanya chochote kwetu!"

Job 22:18

Sentensi Unganishi

Elifazi anaendelea kuongoa kwa Ayubu

mipango ya waovu ipo mbali nami

"mbali nami" ni nahau ambayo inamaanisha kuwa Elifazi anawakana waovu. KTN: "lakini sitasikiliza mipango yao miovu"

huona maangamizi yao

"hujua kitakacho tokea kwa waovu"

huwcheka kwa dharau

"hudhihaki watu waovu"

wale walio inuka juu dhidi yetu wamekatiliwa mbali.

"walio inuka juu" inamaanisha watu waovu. KTN: "Mungu amewaharibu watu waovu waliotuumiza"

Job 22:21

Setensi Unganishi

Elifazi anaendelea kuongoa kwa Ayubu

Sasa

Elifazi anatumia neno sasa kutoa utangulizi wa jambo muhimu analotaka kusema.

maelekezo kutoka katika kinywa chake

"kutoka kwenye kinywa chake" inawakilisha yale ambayo Mungu amekwisha sema. KTN" "maelekezo ya ambayo Mungu a mekwisha kusema."

uyahifadhi maneno yake

KTN: "amri zake uziweke kuwa akiba"

moyo wako.

moyo unarejea mawazo ya Ayubu. KTN: "akili zako"

Job 22:23

Senensi unganishi

Elifazi anaendelea kuongoa kwa Ayubu

utajengwa

KTN: "atakuponya na kukufanikisha tena"

kama udhalimu utauweka mbali kutoka katika hema yako

picha ya udhalimu inaonyeshwa kana kwamba ni mtu anayeishi katika nyumba ya Ayubu ambaye anatakiwa kuondolewa. KTN: "ikiwa wewe na kila mtu katika nyumba yako mtakoma kutenda dhambi"

Hazina zako ziweke chini kwenye mavumbi

hazina kuiweka kwenye mavumbi ni kuitazama kama kitu ambacho hakina thamani.KTN: ufikirie utajiri wako kama ni kitu ambacho siyo cha muhimu kama vile mavumbi"

dhahabu ya ofiri miongo mwa mawe ya vijito.

kuiweka dhahabu katika mfereji ni kuiona kitu kisicho na thamani kama mawe. KTN: " dhahabu yako isiwe na thamani kama mawe kwenye kijito"

Ofiri

hili ni jina la ukanda maarufu kwa dhahabu yake.

Mwenyezi atakuwa hazina, fedha ya thamani kwako

hii inamaana Mungu atakuwa wa thamani zaidi kwa Ayubu kuliko hazina yoyote.

Job 22:26

Sentensi Unganishi

Elifazi anaendelea kuongoa kwa Ayubu

utainua uso wako kwa Mungu

Maana yake kwamba Ayubu hataona aibu tena bali atamwani Mungu. KTN: " utaweza kumkabili kwa ujasiri"

itathibitishwa kwako

KTN: "Mungu atakufanya ufanikiwe"

mwanga utang'aa juu ya njia zako

KTN: "itakuwa kama mwanga unaong'aa kwenye barabara mbele yako"

Job 22:29

Sentensi Unganishi

Elifazi anaendelea kuongoa kwa Ayubu

mwenye macho ya kujishusha

macho ya kujishusha inarejea unyenyekevu. KTN: ' mtu mnyenyekevu"

mtu ambaye hana hatia

hata mtu ambaye si mwungwana

utaokolewa kupitia usafi wa mikono yako

maana yake "Mungu atakuokoa kwa sababu ya usafi wa mikono yako"

kupitia usafi wa mikono yako

"usafi" inamaana ya kutokuwa na hatia "mikono" inamaana ya matendo afanyayo mtu. KTN: " kwa sababu unatenda yaliyo haki"

Job 23

Job 23:1

Hata leo malalamiko yangu ni mchungu

"Hata leo" ni msisistizo kuwa mabishano ya marafiki zake hawajabadili hali ya Ayubu kabisa. KTN: " pamoja na yote mliyosema, malalamiko yangu bado na uchungu"

mkono wangu ni mzito kwa sababu ya kuugua kwangu.

hii inaweza kumanisha kuwa1)" ninaweza kuinua mkono wangu kwa sababu ya kuugua kwangu" au 2) mkono wake unaendelea kuniteda pamoja na kuugua kwangu" neno mkono linarejea nguvu ya Mungu katika kuhukumu .

Job 23:3

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

Laiti, ningejua ambapo ... laiti, ningekuja

mistari hii miwili inamaana moja na inasisitiza hamu ya Ayubu kukutana na Mungu.

ningempata

" ningempata Mungu"

Ingeweka dawaa yangu ... kukijaza kinywa changu

mistari hii miwili inamaana moja na inasisitiza hamu ya Ayubu kueleza hali ya ke kwa Mungu.

kukijaza kinywa changu kwa hoja

KTN: "ningezungumza hoja za ngu zote"

Ningejifunza maneno ... ambacho angesema kwangu

mistari hii miwili inamaana moja na inasisitiza hamu ya Ayubu kusikia jibu la Mungu.

maneno ambayo angenijibu

"jibu ambalo angelinipa"

Job 23:6

Sentensi unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

Je

"Mungu angelieweza"

Ambapo

inarejea sehemu ambapo Mungu yupo

je angeona kuwa sina hatia milele katika kuhukumu kwangu

KTN: "kuhukumu kwangu kungeliniweka huru daima" au "Mungu, ambaye ni hakimu wangu, angesema kuwa sina hatia kabisa"

Job 23:8

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

mashariki... magharibi .. kaskazini ... kusini

kwa kutaja pande hizi nne, Ayubu anasisitiza kwamba alitazama kila mahali.

Job 23:10

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

anaijua njia ninayoiendea

KTN: "Mungu anajua ninachofanya"

nitatoka kama dhahabu

Ayubu anaamini kuwa jaribio litamthibitisha kuwa mkamilifu kama dhahabu iliyosafishwa. KTN: "ataona kuwa nipo mkamilifu kama dhahabu ambayo uchafu wake wote umechomwa"

Mguu wangu umeshikamana kwenye hatua zake

"mguu wangu" inarejea kwa Ayubu. KTN: '"Nimeifuata njia aliyonionyesha"

nimeitunza njia yake

utii wa Ayubu unazungumziwa kama kutembea katika njia ambayo Mungu amemwelekeza" KTN: "Nimefanya alichoniambia"

sikungeukia upande

"fuata kwa usahihi"

sikurudi nyuma kutoka kwenye

KTN: "nimetii alichoamuru"

ya midomo yake

tungo hii inarejea ujumbe ambao Mungu alisema.. KTN: "ambacho alisema"

Nimeyatunza kwenye moyo wangu

hapa "moyo wangu"inarejea kwenye utu wa ndani wa Ayubu. KTN: "nimetunza katika utu wangu wa ndani" au "daima nafikiria juu yake"

maneno ya kinywa chake

hii inarejea kauli ya Mungu. KTN: "alichosema"

Job 23:13

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

Lakini yeye ni wa namna ya pekee, ni nani awezaye kumgeuza?

Ayubu anatumia swali hili kusisitiza kuwa Mungu ni wa pekee. KTN: "Lakini hakuna mwingine kama yeye, na hakuna wa kubadilisha nia yake." au "lakini yeye peke yake ni Mungu, na hakuna anayeweza kumshawishi"

Anachotaka, hukifanya

"anatimiza chochote anachotaka kufanya"

yeye huzitimiza amri zake dhidi yangu

" ananitendea ambacho alisema angefanya"

yapo mengi kama hayo

"anamipango yenye kufanana kwa ajili yangu"

Job 23:15

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

Maelezo ya Jumla

mistari hii kila mmoja upo katika muundo sambamba ili kusisitiza wazo kuu analotoa Ayubu.

maana Mungu ameufanya moyo wangu dhaifu; mwenyezi amenitaabisha

Hii mistari miwili inamaanisha jambo moja na inasisitiza kuwa Ayubu anamwogopa sana Mungu.

ameufanya moyo wangu dhaifu

mtu ambaye moyo wake ni dhaifu ni yule ambaye tishika au kujaa hofu.KTN " amenifanya niogope"

sikufikishwa mwisho kwa giza

inaweza kumaanisha 1) "giza nene mbele yangu halikufanya ninyamaze" au 2) "siyo giza lilonitupa nje" au "Mungu amenikatilia mbali, wala siyo giza"

Uso wangu

inamaanisha "mimi"

Job 24

Job 24:1

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

kwa nini nyakati za kuwahukumu watu waovu hazijapangawa na Mwenyezi?

Ayubu anatumia swali hili kuelezea fadhaa zake kuwa Mungu hajawahukumu waovu. KTN: " Sielewi kwa nini Mungu hajapanga muda ambapo atawahukumu watu waovu." au "Mwenyezi angapnga muda ambapo angewahukumu watu waovu"

Kwa nini wale ambao ni waaminifu kwa Mungu huona siku zake za hukumu zikija?

Ayubu anatumia swali hili kuelezea fadhaa zake kuwa wenye haki hawajamwona Mungu akihukumu uovu. KTN: "Inaonekana kuwa wale ambao humtii Mungu hawamwoni akiwahukumu waovu" au "Mungu angeonyesha siku ambapo atawahukumu waovu kwa wale wenye kumjua"

Job 24:2

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

alama za mipaka

haya ni mawe au vitu vingine kunyesha mpaka kati ya maeneo yanayomilikiwa na watu mbalimbali.

malisho

"konde la majani" au "viwanja vya kuchungia"

hutwaa

"wanaiba"

ambao hawana baba

"yatima" au "watoto ambao wazazi wao wamefariki"

huchua ng'ombe wa mjane kama rehani

"huchukua ng'ombe wa mjane ili kuwa hakikisho kwamba wajane watalipa pesa walizowakopesha

mjane

mwanamke ambaye amefiwa na mume wake.

dhamana

mwazimishaji alichukua kitu chochote kutoka mwazimaji ili kuhakikisha kuwa mwazimaji huyo atalipa.

nje ya njia yao

toka kwenye njia

watu masikini nchi waote hujificha

watu wengi masikini huwaogopa watu waovu.

Job 24:5

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

Watu hawa msikini huenda kwenye kazi zao mithili ya punda mwitu kwenye nyika, wakitafuta chakula kwa bidii

watu hawa ambao ni masikini wanaongelewa kana kwamba ni punda mwitu wasiojua ni wapi watapata chakula. KTN: "watu hawa masikini huenenda wakitafuta chakula kama vile punda mwitu kwenye nyika"

punda mwitu

"punda wasiomilikiwa na mtu au kuangaliwa"

watu masikini huvuana usiku ... wanakimulika zabibu.

hii mistari miwili inaeleza jambo moja na yote inasisitiza kwamba watu hawa wananjaa sana hivyo wanalazimika kuiba chadkula wakati wa usiku.

Hulala uchi ...hawana cha kujifunika

hii mistari miwili inaeleza jambo moja na yote inasisitiza kwamba watu hawa hawana mavazi ya kutosheleza kujisitili.

Job 24:8

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

wamelowana kwa manyunyu ya milimani

" wanlowana wakati inaponyesha milimani"

yatima kutoka kwenye maziwa ya mama zao

"maziwa" inarejea kwa mama. maana yake kuwa yatima hawa bado wadogo sana. KTN: " yatima wachanga kutoka kwenye mikono ya mama zao au vichanga wasio na baba kutoka kwa mama zao"

yatima

hii inarejea kwa watoto ambao hawana wazazi. Hata hivyo hapa neno hili limetumika kumaanisha watoto ambao hawana mama wla baba.

huchukua watoto kama dhamana kutoka kwa watu masikini

"huchukua watoto wa watu wa masikini ili kuhakikisha kuwa watu masikini watalipa pesa walizokopa"

dhamana

mwazimishaji anachukua kitu kutoka kwa mwazimaji ili kuhakikisha kwamba atalipa tena.

huzunguka

"kutembea huku na kule"

uchi pasipo mavazi

"uchi pasipo mavazi" maana yake ni sawa na kuwa uchi.

hubeba miganda ya nafaka ya wengine

hii inamaanisha wanfanya kazi kuzalisha chakula kwa wengine wala si kwa ajili yao wenyewe.

Job 24:11

Sentensi unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

watu masikini hutengeneza mafuta

wanakamua zeituni ili kutoa mafuta ya zeituni

Ndani ya kuta wale watu waovu

"Kuta" inarejea nyumba nzima .KTN: " kwenye nyumba za wale watu waovu"

wanakanyaga mashinikizo ya divai ya watu waovu

wanazalisha shalibati ili kutengeneza divai.KTN: "wanakanyaga zabibu ili kutengeneza sjhalibati kwa ajili ya diva"

wenyewe huteseka kwa kiu

"huteseka kutokana na kiu au hupata kiu"

Job 24:13

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

huasi dhidi ya mwanga

maana ya mwanga

hawazijui njia zake, wala hawakai katika mapito yake

hii mistari miwili inaeleza kitu kile kile, na inatumika kwa pamoja kusisitiza kwamba hawataki kufuata njia ya mwanga. KTN: "hawajui jinsi ya kuishi maisha yenye maadili; hawataki kuisha maisha ya haki"

masikini na watu wahitajia

maneno "masikini" na "wahitaji" yanarejea kundi moja la watu na kusisitiza kuwa watu hawa ni watu ambao hawawezi kijisaidia wenyewe.

Job 24:15

Sentensi unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

jicho la mzinzi

"jicho" linarejea binadamu kwa ujumla wake. KTN: "mzinzi"

kwa giza gaza

"kwenye machweo"

hakuna jicho litakaloniona

"jicho" hapa linarejea mwanadamu kwa ujumla wake.KTN: "hakuna mtu atakaye niona"

watu waovu huchimba kwenye nyumba

wanachimba ili kuiba kwenye hizo nyumba .

wao hujifungia wenyewe

"hujificha ndani"

maana kwao wote, giza nene ni kama asubuhi

giza nene ni faraja kwa waovu kama mwanga wa asubuhi kwa watu wa kawaida.

vitisho vya giza nene

"vitu vya kuogofya vinavyotokea usiku"

Job 24:18

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

kama povu juu ya uso wa maji

povu hudumu kwa muda mchache. Hii inasisitiza kuwa Mungu atasababisha waovu wapotee upesi.

sehemu ya ardhi yao imelaaniwa

KTN: "Mungu hulaani sehemu ya ardhi ambayo wanamiliki"

Kama ukame na joto huyeyusha...wale ambao wamefanya dhambi

Ayubu anasema kwamba wenye dhambi watapotelea kuzimu kwa njia ile ile kama vile theluji inavyoyeyuka na kupotea inapokuwa joto.

ukame na joto

haya maneno mawili yanaelezea hali ya hewa inayofanana.

Job 24:20

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

Tumbo

hii inarejea kwa mama. KTN: "mama"

minyoo itamla na kuona utamu

hii inamaana kuwa atakufa na minyoo itaula mwili wake. KTN: minyoo itafurahia kula mzoga wake" au "atakufa na mwili wake utaliwa na minyoo"

hatakumbukwa tena

" hakuna mtu atakayemkumbuka tena"

utavunjwa kama mti

" Mungu atawaharibu waovu kama mti"

mwovu huteketeza

sitiari hii inasisitiza jinsi mtu mwovu asivyofaa. KTN: "Kama mnyama mwitu anavyoua mawindo yake, ndivyo mtu mwovu huleta maumivu"

wanawake tasa ambao hawakuzaa watoto

watu wa wakati ule waliamini kuwa mtu ambaye hakuzaa watoto alikuwa amelaaniwa na Mungu. Hii inawakilisha wanawake wenye bahati mbaya kabisa.

Job 24:22

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

kwa nguvu zake

"kwa kutumia nguvu zake" au "kwasababu yeye ni mwenye nguvu"

huinuka na wala hawatii nguvu katika maisha

"wala hawatii nguvu katika maisha"maana yake Mungu hawaachi hai. KTN: "Mungu huinuka na hawapi watu waovu nguvu za kuishi" au "Mungu huinuka na kuwasababisha wafe"

bali macho yake yapo juu ya njia zao

hapa "macho" nirejea kwa Mungu. KTN: "lakini daima huangalia watendayo"

Job 24:24

Sentensi unganishi

Ayubu anaendelea kuongea

watashushwa

"Mungu atawashusha" au "Mungu atawaharibu"

watakusanywa kama wengine wote

baadhi ya tafsiri zingine zinasema "watanyauka na kufifia kama magugu"

watakatwa kama masuke ya nafaka

KTN:"Mungu atawakata kama mkulima anavyokata masuke ya nafaka"

Kama ndivyo, je ni nani anaweza kuthibitisha kuwa mimi ni mwongo ; nani anaweza kufanya maneno yangu yasifae kitu?

Ayubu anatumia swali hili kuonyesha uzito wa hoja yake. KTN: "hii ni kweli, hakuna mtu anaweza kuthibitisha kuwa mimi ni mwongo; hakuna wa kuthibitisha kuwa mimi ni mkosaji"

kufanya maneno yangu yasifae kitu?

"kuthibitisha ninachosema ni makosa"

Job 25

Job 25:1

Bildadi Mshuhi

hili ni jina la mtu kama ilivyo katika 2:11

Milki na hofu vipo pamoja naye

"naye" inarejea kwa Mungu. majina ya dhahania "milki" na "hofu" yanaweza kutajwa kama vitenzi. KTN: "Mungu ni mtawala wa yote, na watu wanapaswa kumhofu yeye peke yake"

katika sehemu zake za juu mbinguni

"katika mbingu" au "kwenye mbingu juu"

Je kuna ukomo wa idadi ya majeshi yake?

Bildadi anatumia swali hili kueleza jinsi Mungu alivyo mkuu. KTN: "Hakuna ukomo wa idadi ya malaika katika jeshi lake" au Adui zake ni wakubwa sana kwamba hakuna awezaye kuwahesabu"

je ni juu ya nani mwanga wake haumuliki?

Bildadi anatumia swali hili kueleza kwamba Mungu hutoa mwanga kwa kila mtu. KTN: "Wala hapana mtu ambaye mwanga wake haumuliki" au "Mungu hufanya mwanga wake kung'aa juu ya kila mmoja"

Job 25:4

Sentensi Unganishi

Bildadi anaendelea kuongea.

Mtu anawezaje ... Mungu? Je anawezaje aliyezaliwa ... kwake?

maswali haya mawili yematumika pamoja kusisitiza kwamba haiwezekani kwa mtu mwema kiasi cha kutosha mkwa Mungu

Basi mtu anawezaje kuwa mwenye haki kwa Mungu?

"Mtu hawezi kuwa mwenye haki kwa Mungu"

Je anawezaje yeye aliyezaliwa... kukubalika kwa Mungu?

" yeye ambaye amezaliwa na mwanake hawezi kuwa msafi au kukubalika kwake"

nyota si safi kwenye macho yake

"safi" maana yake "kamilifu" KTN: "anafikiri hata nyota hazina ukamilifu"

Jinsi gani mtu ... mwana wa mtu, ambaye ni mnyoo

hii mistari miwili inasema jambo moja na inatumika pamoja kukazia kuwa mtu si mkamilifu.

ambaye ni mnyoo

Bildadi anaeleza kwmba mwanadamu ni wa thamani ndogo kama minyoo. KTN: "ambaye hana thamani kama mnyoo"

mwana wa mtu

hii ni namna nyingine ya kumaanisha mtu. KTN: "Mtu"

Job 26

Job 26:1

jinsi gani ulimsaidia yule ...mkono ambao hauna nguvu!

Ayubu anamshutumu Bildadi. Neno "yule" linamrejea yeye mwenyewe (Ayubu). KTN: "Mimi sina uwezo wal nguvu, lakini unajifanya kama umenisaidia- ukweli ni kwamba hujanisaidia kabisa!"

mkono ambao hauna nguvu

Ayubu anajielezea mwenyewe kuwa..."mimi, ni kama mkono ambao hauna nguvu au "yule ambaye ni dhaifu kabisa"

Jinsi gani umemshauri yule asiyekuwa na hekima na kumtangazia maarifa ya kweli!

Ayubu anasema kwamba Bildadi hajatoa ushauri mzuri wala maarifa kwake. KTN: " Umetenda kana kwamba hauna maarifa kwa njisi ulivyonishauri"

kumtangazia maarifa ya kweli

"kumpa ushauri mzuri"

Kwa msaada wa nani umeongea maneno haya? je ilikuwa roho ya nani... yako?

katika maswali haya Ayubu anaendelea kumdhihaki Bildadi. KTN: "lazima ulipata msaada kuongea maneno haya. Yamkini roho fulani ilikusaidia kuyaongea maneno haya"

Job 26:5

waliokufa

" wale ambao walikufa" au " roho za wafu"

tetemeka

wanatetemeka kwa sababu wanamwogopa Mungu. KTN: "kutetemeka kwa hofu" au "kutetemeka kwa hofu ya Mungu"

wale ambao wapo chini ya maji

Hii inaelezea watu waliokufa ambao hutetemeka"

wote wanaoishi ndani yake

hii nazungumzia kuhusu watu waliokufa ambao hutetemeka. neno "yake" linamaanisha kwenye maji

kuzimu ipo tupu mbele za Mungu; uharibifu mwenyewe hauna kifuniko

kuzimu inaongelewa kana kwamba ni mtu. kuwa "tupu" au kukosa" kifuniko" ni kuwa wazi kabisa na kushindwa kuficha chochote. KTN: " Ni kama kuzimu ilivyo wazi mbele za Mungu, maana hakuna kitu kuzimu, au sehemu ya uharibifu ambayo imejificha kwa Mungu"

uharibifu

hili ni neno jingine kumaanisha kuzimu. KTN: "sehemu ya uharibifu"

Job 26:7

hulinyosha anga la kaskazini juu ya nafasi wazi

anga la kaskazini linawakilisha mbingu, sehemu ambapo Mungu huishi pamoja na viumbe alivyoviumba huko.

huyafunga maji kwenye mawingu yake mazito

mawingu yanazungumziwa kana kwamba ni bulanketi kubwa ambapo Mungu huyafunga maji ya mvua. KTN: "Huyafunga maji katika mawingu yake mazito"

walakini mawingu hayapasuki chini yake

KTN: "Lakini uzito wa maji haupasui mawingu"

Job 26:9

na hutandaza mawingu yake juu yake

maneno haya yanasema jinsi huifunika sura ya mwezi. KTN: " kwa kutandaza mawingu yake mbele yake"

amechonga mpaka wa duara

Anasema kana kwmba Mungu aliweka alama ya mpaka juu ya bahari.

Job 26:11

Nguzo za mbingu hutetemeka na kustaajabu kwa kukemea kwake

Ayubu anaongelea watu kama nguzo ambazo hutetemeka kwa hofu wakati Mungu anapokasirika.

alimvunjavunja Rahabu

alimharibu Rahabu

Rahabu

Hili ni jina la kiumbe cha kutisha kilichoishi katika bahari.

Job 26:13

Kwa pumzi yake alisafisha anga

"pumzi" au "puliza" ni sura ya kuwakilisha kitendao cha Mungu kusababisha upepo yayasukume mawingu. KTN: " Kwa pumzi, Mungu alisafisha anga" au "Mungu aliyapuliza mawingi hata anga likawa safi"

mkono wake ulimemchoma nyoka mwenye kukimbia.

"mkono wake" unawakilisha upanga wa Mungu na 'kumchoma' linawakilisha mauaji. KTN: "Kwa upanga wake alimchoma nyoka mwenye kukimbia"

nyoka mwenye kukimbia.

" nyoka huyu alikuwa anajaribu kumtoroka" zingatia 26:11

Tazama, walakini hivi ni viunga vya njia zake

Hapa "viunga" vinawakilisha sehemu ndogo ya kitu kikubwa inayoweza kuonekana.KTN: "Tazama vitu hivi ambavyo Mungu amavifanya vinaonyesha sehemu ndogo sana ya uwezo wake mkuu"

ni mnong'ono mdogo kiasi gani tunasikia kutoka kwake

KTN: " Tunasikia tu mnong'ono wake wa utulivu"

ni nani anawezakufahamu ngurumo ya nguvu zake?

"ngurumo ya nguvu zake" inawakilisha ukuu wote wa yale anayoyafanya Mungu. Ayubu anaelezea kuwa nguvu za Mungu ni kuu sana kiasi kwamba hakuna mtu mwenye kuzifahamu. KTN: "hakuna mwenye kufahanu ukuu wa nguvu zake"

Job 27

Job 27:1

Hakika kama Mungu anavyoishi

Hii ni namna ya dhati ya kuweka ahadi. KTN: "Ninaapa kwa Mungu"

ameniondolea haki yangu

kuindoa haki inamaanisha kukataa kumtendea haki Ayubu

aliyefanya maisha yangu kuwa machungu

"amesababisha niwe na uchungu" au " amenifanya nikasirike kwa sababu alinitendea kwa namna isiyo nzuri"

wakati uhai wangu ukiwa ndani yangu

hii inamaana ya maisha yake yote. KTN: wakati wote ambapo uzima wangu ukiwa ndani yangu" au "kwa muda wote ambao uhai wangu bado upo ndani yangu"

pumzi kutoka kwa Mungu puani mwangu

pumzi puani inawakilisha uwezo wa kupumua, "pumzi kutoka kwa Mungu" inawakilisha kitendo cha Mungu kumfanya aweze kupumua. KTN: "Mungu ananiwezesha kupumua"

puani

"pua"

Job 27:4

Hakika midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu kusema uongo

"midomo yangu" na "ulimi wangu" vifungu hivi vyote vina maana moja na vimetumika kusisitiza kwamba Ayubu hatasema mambo yasiyofaa. KTN: "Hakika sitasema ouvu au uongo"

haitanena uovu...kusema uongo

"uovu" na "uongo" ni majina dhahania yanayoweza kuelezea "kwa uovu" na "kwa udanganya" KTN: "kunena kwa uovu... kusema kwa udanga udanganyifu"

Sitakubali kwamba ninyi watatu mpo sahihi

"sitakubaliana nanyi na kusema kwamba ninyi watatu mpo sahihi"

sitaukana uadilifu wangu

"sitaacha kusema ya kwamba mimi si mwenye hatia" au " daima nitasema ya kuwa mimi mwadilifu"

Job 27:6

nashikamana na haki yangu

" mimi nimedhamiria kuendelea kusema ya kwamba ni mwenyehaki"

sitaiacha

" sitaacha kusema kuwa mimi ni mwenye haki"

mawazo yangu hayatanisuta

"hata katika mawazo yangu sitajishutumu mwenyewe"

Adui yangu awe...yule anayeinuka dhidi yangu awe

hivi vishazi viwili vina maana moja. Vinaonyesha hamu ya Ayubu kutaka jambo hili litokee

Adui yangu na awe kama mtu mwovu

" Adui yangu na aadhibiwe kama mtu mwovu " au "Mungu amuadhibu adui yangu kam anavyowaadhibu watu waovu"

Yule ainukaye dhidi yangu na awe kama mtu asiye haki

" yule anyeinuka kinyume nami aadhibiwe kama mtu asiye haki"

yeye ainukaye dhidi yangu

"Yeye anayenipinga" au " mshitaki wangu"

Job 27:8

Maana ni nini tumaini la mtu kafiri wakati... wakati Mungu aondoapo uzima wake?

" hakuna tumaini kwa mtu kafiri wakati Mungu... aondoapo roho yake."

wakati Mungu amwondoapo, wakati Mungu aondoapo uzima wake

misemo yote miwili inamaana moja.KTN: "Wakati Mungu anapomkatilia mbali na kuondoa uzima wake" au "wakati Mungu anaposababisha afe"

amwondoapo

"anapomwua" au " aposababisha afe"

aondoapo uzima wake

"anapomwua" au " anapomfanya asiendelee kuishi"

Je Mungu atasikia kilio chake wakati taabu itakapokuja juu yake?

"Mungu hatasikia kilio chake wakati taabu itakapokuja juu yake" au " Wakati taabu itakapokuja juu yake na kulilia msaada, Mungu hatamsikia."

Mungu atasikia kilio chake

"Mungu atamwitikia kilio chake"

Je atamfurahia Mwenyezi na kumwita Mungu katika nyakati zote?

Ayubu anatumia swali hili kusema kuwa mtu kafiri hatamfurahia Mwenyezi na kumwita Mungu katika nyakati zote. au " hatayafurahia matendo ya Mwenyezi na wala hata mwomba Mungu mara kwa mara"

Job 27:11

nitawafundisha

"nitawa.." ni neno katika wingi kumaanisha marafiki watatu wa Ayubu.

mkono wa Mungu

Mkono wa Mungu unawakilisha nguvu zake. KTN: "Nguvu za Mungu"

Sitayaficha mawazo ya Mwenyezi

"mawazo" ni jina dhahani ambapo laweza dhahiri pamoja na kitenzi "fikiri".KTN: "Sitawaficha yale ambayo Mwenyezi hufikiri"

basi mbona mmeongoa upuuzi huu wote?

Ayubu anatumia swali hili kuwakemea arafiki zke kwa kuongea vitu vya kipumbavu. KTN: "walakini mmeongea upuu huu wote" au " Haikuwapasa kuongea kwa upumbavu"

Job 27:13

Hii ndiyo hatima ya mtu mwovu kwa Mungu

Hatima ya mtu mwovu kwa Mungu inahusiana na mpango wa Mungu kwa mtu huyo. KTN: " huu ndio mpango wa Mungu kwa mtu mwovu"

urithi wa mnyonyaji ambao hupokea kutoka kwa Mwenyezi

"urithi wa mnyonyaji" ni stiari kuonyesha kitu gani kitatokea kwa mnyonyaji. Mambo atakayopokea toka kwa Mungu yanaongelewa kama ndiyo urithi wake.

ni kwa ajili ya upanga

"watakufa katika mapigano"

Job 27:15

wale ambao husalia

Hii inahusu watoto wa mtu mwovu ambao huendelea baada ya baba zao kufariki. KTN: "Wale ambao huendelea kuishi baada ya baba zao waovu kufariki"

watazikwa kwa tauni

"watakufa kwa tauni"

wajane wao... yao

maneno "wao... yao" yanahusu wale watakaosalia, ambao ni watoto wa mtu mwovu

hurundika fedha kama mavumbi

"hurundika "maana yake hukusanya sana. Ayubu anasema kuwa ilikuwa rahisi kwa mtu huyu kujipatia fedha kama vile mavumbi.

hurundika mavazi kama udongo

"hurundika "maana yake hukusanya sana. Ayubu anasema kuwa ilikuwa rahisi kwa mtu huyu kujipatia mavazi kama vile kuzoa udongo.

Job 27:18

Huijenga nyumba yake kama buibui

" kama buibui ajengavyo mifumo yake"

Huijenga nyumba yake kama buibui

" kama buibui ajengavyo mifumo yake"

kama kibanda

kibanda ni nyumba ya muda ambayo si imara. KTN: "Kama kibanda cha muda mfupi"

hulala chini kitandani akiwa tajiri

" analala wakati wa usiku akiwa tajiri"

walakini hawezi kuendelea kufanya hivyo

"walakini hataendelea kulala kwenye kitanda akiwa tajiri" au "hataendelea kuwa tajiri"

hufumbua macho yake

"ataamuka"

na kila kitu kimetoweka

"utajiri wake wote utaondoka" au "kila kitu kitakuwa kimepotea"

Job 27:20

vitisho humkabili

" mambo ya kutisha humtokea kwa ghafula" au "ghafula atashikwa na woga"

kama maji

" kama mafuriki" au "kama maji jaa upesi"

dhoruba humtoa

"upepo mkali humpeperusha mbali"

humfagia mbali na sehemu yake

"upepo humfagia mbali na sehemu yake kama mwanamke anafagia uchafu kwenye nyumba" au " upepo humpeperusha kwa urahisi mbali na sehemu yake"

sehemu yake

"nyumba yake"

Job 27:22

Maelezo ya Jumla

mistari ya 22-23 Ayubu anazungumzia upepo kana kwamba ni mtu mwenye kumshambulia mtu mwovu

unajirusha wenyewe juu yake

hapa "unajilisha wenyewe " inamaanisha upepe. "unavuma kwa nguvu dhidi yake kama mtu mwenye kumshambulia"

anajaribu kuukimbia mko wake

" anajaribu kukimbia kutoka katika mamlaka yake"

Anapiga makofi yake kwa kumdhihaki.

" Upepo unato sauti kubwa kama ya mtu anayepiga makofi ili kudhihaki"

anazomewa mbali na sehemu yake

"amepeperushwa mbali na sehemu yake na anazomewa kwa dhihaka"

Job 28

Job 28:1

machimbo

hii ni sehemu ambapo watu huchimba miamba kwenye ardhi. Hii miamba inachuma ndani yake.

husafisha

mchakato wa kupasha joto chuma ili kuondoa uchafu wote ndani yake.

chuma huchukuliwa kwenye ardhi

"watu huchukua chuma kutoka kwenye ardhi"

shaba huyeyushwa kutoka kwenye mawe

" watu huyeyusha shaba kutoka kwenye mawe" au "watu huchoma mawe kuyeyusha shaba ndani yake"

shaba

chuma cha brauni ambacho ni muhimu

yeyusha

huu ni mchakato wa kuchoma miamba ili kuyeyusha madini ndani yake na kutoa madini hayo kwenye miamba

Job 28:3

Binadamu hukomesha giza

huweka nuru mahali penye giza. Watu waliweza kutumia miale, ama taa au tochi.KTN:" Bibadamu hubeba mwanga kwenye sehemu za giza"

kwenye mpaka wa mbali zaidi

"kwenye sehemu za mbali zaidi kwenye machimbo"

uvunguvungu ...giza nene

haya mafumbo mawili yametumika kuonyesha kuwa giza ni kuu sana

shimo

tundu jembambale lenye kina linalochimbwa ardhini au kwenye mwamba. Watu hushuka chini ya tundu ili kuchimba.

sehemu ambazo zimesahauliwa na mguu wa mtu yeyote

KTN: " ambapo hakuna mtu amewahi kupakanyaga"

Huning'inia mbali na watu

KTN:" Mbali na watu huning'inia kwenye kamba ndani ya shimo"

Job 28:5

ardhini ambamo hutoka mkate

mkate unawakilisha chakula kwa ujumla. chaakula hutoka kwenye ardhi ni sitiari kwmab chakuka hukua kwenye ardhi. KTN: "ardhini ambapo chakula hustawi"

hugeuzwa chini kama kwa moto

hii inaweza kumaanisha 1) watu waliwasha moto chini ardhi ili kubomoa sehemu za mwamba 2) huboma chini sana kama kwamba kuteketeza kwa moto"

hugeuzwa...mawe yake ...vumbi lake

maneno yake, lake yanamaana ya ardhi

Johari

neno hili linamaana ya jiwe la bluu lenye thamani sana.

Job 28:7

Hakuna ndege mbua aijuaye njia yake ... wala hakuna jicho la tai halijaiona

KTN: "Hakuna ndege mbua au tai anayeijua au akwisha kuiona njia anayokwenda kwenye mgodi"

ndege mbua

ndege alaye wanyama wangine

tai

kipanga

wanyama wenye kujivuna hawajapita kwenye njia kama hiyo...wala simba mwenye hasira hajapita pale

Virai hivi vinaeleza maana zenye kufanana

wanyama wenye kujivuna

hii inamaanisha wanya mwitu wenye nguvu

Job 28:9

Binadamu huulaza makono wake juu ya mwamba mgumu

hii inamaanisha kupasua mwamba.KTN: "huchimba kwenye mwamba mgumu"

mwamba mgumu

" mwamba gumegume"

huipindua milima kwenye mizizi yake

"huipindua milima juu chini kwa kuvuita mizizi yake"

macho yake huona

"huona"

Huifunga mifereji ili istiririke

kuifunga mifereji inakilisha kuzuia majia au kuizuia mifereji ya maji.

kilichofichwa pale

hii inarejea vitu ambavyo watu hawawezi kuviona kwa sababu vipo chini ya ardhi au chini ya maji.

Job 28:12

Maelezo ya Jumla

kwenye 28:12-28, hekima na maarifa vimesemwa kama vitu ambavyo vipo mahali fulani na watu wanataka wavipate. kutafuta hekima na maarifa inawakilisha kuwa na busara na kujifunza kufahamu vitu kwa uzuri.

Je hekima itapatikana wapi? Je ni sehemu gani yenye maarifa?

Maswali haya yanamaana moja na yametumika kuonesha kuwa ni vigumu kupata hekima na maarifa.

Je hekima itapatikana wapi? Je ni sehemu gani yenye maarifa

Kuwa mwenye hekima na maarifa inazungumziwa kana kwamba ni kutafuta hekima ana maarifa: KTN: "Jinsi gani watu huwa na hekima? Jinsi gani watu hujifunza kufahamu vitu kwa uzuri?"

Binadamu hajui thamani yake

Hapa inaweza kumaanisha kuwa:- 1) "Watu hawajui uzuri wake" au 2) "Watu hawajui mahali ilipo"

wala haipatikani katika nchi ya walio hai

nchi ya walio hai inamaana ya ulimwengu huu ambapo watu wanaishi. KTN: "na hakuna mtu anayeweza kupata hekima katika ulimwengu huu "

Maji yenye kina... yanasema, 'haiapo ndani kwangu' bahari inasema, ' haipo kwangu'

vilindi vya maji na na bahari vinasimama kama watu wanaoweza kuongea. KTN: "Hekima haipo ndani ya vilindi vya maji chini ya ardhi, wala katika bahari"

Job 28:15

Haiwezi kupatikana kwa dhahabu

Hii inamaanisha kuwa hekima ina anathamani zaidi kuliko dhahabu. KTN: "Watu hawawezi kulipa dhahabu kwa ajili ya kupata hekima"

wala fedha haiweza kupimwa kwa thamani yake

Hii ina maana kwamba hekima inathamani sana kuliko fedha. KTN: "na watu hawawezi kupima fedha za kutosha ili kulipa kwa ajili ya hekima"

Haiwezia kuthaminishwa kwa ... johari

hii inamana kuwa hekima inathamani zaidi ya dhahabu ya ofiri, inathamani kuliko oni na johari.

ofiri

Hili ni jina la eneo ambako kulikuwa na dhahabu safi.

oni

jiwe jeusi lenye thamani

johari

jiwe la bluu lenye thamani sana.

Dhahabu na fuwele haziwezi kulingana nayo kwa thamani

Hapa inamaana kuwa hekima inathamani zaidi kuliko dhahabu na fuwele.

fuwele

jiwe la thamani lililo safi au angavu kwa rangi yake.

wala haiwezi kubadilishwa kwa kito cha dhahabu safi

na haiwezi kubadilishwa kwa kito cha dhahabu safi." Hii inamaana kuwa hekima ina thamani zaidi kuliko kito cha dhahbu safini.

kubadilishwa

"kuuzwa"

Job 28:18

Fedhalika au marijani havistahili kutajwa

"haifai kutaja marijani au fedhaluka" hii inamaan kuwa hekima inastahili zaidi kuliko marijani na fedhaluka wala Ayubu hahitaji kusema chochote juu ya hivi.KTN: "Sitajisumbua kutaja marijani au fedhaluka" au marijani na fedhaluka havina thamani vikilinganishwa na hekima"

marijani

Ni kitu kizuri na kigumu ambacho hustawi chini ya bahari.

fedhaluka...rubi...topazi

Haya ni mawe yenye thamani sana

topazi ya Ethiopia haiwezi kulingana nayo

Hii inamaanisha kwamba hekima inathamani zaidi kuliko topazi.

wala haiwezi thaminishwa kwa vigezo vya dhahabu safi

"na hekima haiwezi kuthaminishwa kwa vigezo vya dhahabu safi" hekima inathamani zaidi ya dhahabu safi.

Job 28:20

Basi, hekima hutoka wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi?

Ayubu anatumia maswali haya kudokeza jinsi gani watu hupata ufahamu na hekima> KTN: " Nitawaambia hekima hutoka wapi na mahali ufahamu ulipo" au "nitawaambia jinsi ya kuwa na busara na namna ya kujifunza vitu vya ufahamu"

Basi hekima hutoka wapi

hekima inaongelewa kana kwamba ipo mahali fulani na huwajia watu. hii inamaanisha watu kujipatia busara. KTN: "Basi watu hupata wapi hekima" au "basi namna gani watu hupata busara"

Mahali pa ufahamu ni wapi

Ufahamu umeongelewa kama kitu ambacho kipo hali. KTN: "Watu hupata wapi ufahamu" au "namna gani ya watu hufahamu vitu"

hekima imefichwa kutoka kwenye macho ya viumbe hai vyote

Viumbe hai haviwezi kuiona hekima. KTN: "Hakuna kiumbe hai chenye kuweza kuiona hekima"

na imefichwa kutoka kwa ndege wa mbinguni

"hata ndege ambao huruka katika anga hawawezi kuona hekima"

uharibifu na mauti husema

hapa "uharibifu" na "mauti" ni tamathali kwa sehemu ambapo watu huelekea wakati wanapofariki.

Job 28:23

Mungu inaifahamu njia yake; anapajua mahali pake

"Mungu anajua jinsi ya kuipata hekima. Anajua mahali ilipo"

miisho ya nchi

"sehemu za mbali za dunia"

aliyagawa maji kwa vipimo

Mungu hufanya maamuzi ni maji kiasi gani yanapaswa kuwepo kwa kila sehemu. KTN: "aliamua ni maji kiasi gani yanapaswa kuwepo kwa kila sehemu" au "ameweka kiwango cha maji ambacho alikipanga kwa kila sehemu"

Job 28:26

na njia kwa mwanga wa radi

maana yaake 1) aliamua namna yamapigo ya mwanga au 2) aliamua mahali pa kuelekea ngurumo za radi.

Hofu ya Bwana -ni hekima

"hofu" au "heshima" KTN: " ukimheshimu Bwana- utakuwa na busara"

kujitenga na uovu ni ufahamu

KTN: "Kukataa kutenda vitu viovu ni ufahamu" au " kama utaepuka kutenda vitu viovu, utaweza kufahamu mambo vizuri"

Job 29

Job 29:1

La, ningekuwa kama nilivyokuwa katika miezi iliyopita

"nitamani ningekuwa kama nilivyikuwa katika miezi ya kale"

wakati taa yake ilipong'aa juu ya kichwa changu

Taa ya Mungu kung'aa juu Ayubu inawakilisha Mungu kumbariki Ayubu. KTN: "Wakati baraka za Mungu zilipokuwa kama taa iking'aa juu ya kichwa changu"

wakati nilipotembea gizani kwa nuru yake

kutembe kwenye giza inawakilisha kukabiliwa na hali ngumu"

Job 29:4

katika kukomaa kwa siku zangu

"nilipokwa kijana na mwenye nguvu"

wakati urafiki na Mungu ulikuwa kwenye hema yangu

" Wakati Mungu alipokuwa rafiki yangu na alipoilinda nyumba yangu"

wakati njia yangu ilipooshwa katika malai

"wakati njia yangu ilipomiminika malai" au "wakati ng'ombe wangu walipotoa malai kwa wingi"

na mwamba ulinimiminia mito ya mafuta

" watumishi wangu walipo kamua mafuta ya mizeituni kwa wingi" au " wakati ambapo mafuta yalitiririka kama mito kutoka kwenye mwamba wa kusindikia"

Job 29:7

viunga vya mji

Hili ni eneo wazi katika kijiji au mji ambapo ni makutano ya miji miwili au zaidi.

waliinuka na kusimama kwa ajili yangu

hii ni alama ya heshima.KTN: "waliinuka na kusimama kwa kuniheshimu"

Job 29:9

nipokuja kwa wafalme wajizuia kuongea

hii ilikuwa alama ya heshima

waliweka mkono wao juu ya kinywa chao

hii ilikuwa alama ya heshima. Walifanya hivi kuonesha kuwa usingeweza kuongea.

sauti za waungwana zilinyamaza

"waungwana walinyamazisha sauti zao" au "waungwana waliacha kuongea"

na ulimi wao gandamana kwenye makaakaa ya vinywa vyao

maana yake walimweshimu Ayubu hadi kukosa neno la kusema. KTN: " walijihisi kushindwa kuongea" au "na hawakuwa na jambo lolote la kusema"

Job 29:11

baada ya masikio yao kunisikia.... baada ya macho yao kuniona

masikio yanawakilisha wale waliomsikia na macho yanawakilisha wale waliomwona. KTN: "baada ya kusikia nilichowaeleza ... baada ya kuniona"

waliweza kunishuhudia na kunithibitisha

"waliweza kunishuhudia kwa kunithibitisha"

nilimwokoa mtu masikini aliyenililia

Hapa"mtu masikini" inahusu mtu yeyote ambaye ni masikini. KTN: "niliwaokoa watu masikini ambao walinililia"

Baraka ya yule aliyekuwa karibu kupotea ilinijia

baraka ya mtu kwenda kwa mwingine inawakilisha kitendo cha huyi mtu kumbariki mwingine.KTN: "yule aliyekuwa karibu kupotea aliweza kunibariki"

yeye aliyekuwa karibu kuangamia

Mtu yeyote aliyekuwa anakaribia kufa. KTN: " wale ambao walikaribia kufa"

nilisababisha moyo wa mjane kuimba kwa furaha

"moyo wa mjane" inamaana ya mjane yoyote. KTN: "Niliwafanya wajane waimbe kwa furaha kuu"

Job 29:14

Nilivaa haki, nayo ikanifunika

watu wa wakati ule waliongelea haki kama vazi. KTN: "Nilitenda haki, nayo ikawa kama vazi la kujisitiri juu yangu"

uadilifu wangu ulikuwa kama joho na kilemba

watu wa wakati ule waliongelea uadilifu kama vazi. KTN: "Nilitenda kwa adili, na ilikuwa kama joho na kilemba juu yangu"

kilemba

vazi refu ambalo wanaume hufunga kuzunguka vichwa vyao, huvaa kama kofia.

nilikuwa macho kwa watu vipofu

Hii inamaanisha kuwasaidia watu vipofu. KTN: "nilikuwa kama macho kwa ajili ya watu vipofu" au "niliwaongoza watu vipofu"

nilikuwa miguu kwa watu viwete

"nilikuwa kama miguu kwa watu viwete" au "niliwasaidia watu viwete"

nilikuwa baba kwa watu wahitaji

hapa neno baba linawakilisha kutoa kwa ajili ya watu. KTN: "Nilitoa kwa ajili ya watu wahitaji kama baba anavyotoa kwa ajili ya watoto wake"

Job 29:17

Maelezoa ya jumla

katika mistari ya 18-28 Ayubu anasimulia mambo ambayo alifanya kabla mambo mabaya hajatokea kwake.

nilivunja taya za ... nilimng'oa mwathirika

" niliwafanya dhalimu waache kuwatesa watu, kam mtu anayevunja taya la mnyama mwitu na kuokoa mhanga kutoka katika meno yake"

nitakufa katika kiota changu

" nitakufa kwenye nyumba yangu pamoja na familia yangu" au "nitakufa katika usalama wa nyumbani kwangu"

nitazidisha siku zangu kama mchanga

"nitaishi maisha marefu" au "nitaishi miaka mingi "

Mizizi yangu ... matawi yangu

Ayubu anaongea juu ya nguvu zake, anasema yeye ni kama mti imara uliomwagiliwa vizuri.

Job 29:20

heshima ndani yangu ni mpya siku zote

"watu hunipa heshima daima" au "watu huniheshimu mara kwa mara"

upinde wa nguvu zangu ni mpya daima mkononi mwangu

"siku zote nipo imara kama upinde mpya"

hotuba yangu ilidondoka kama maji juu yao

"hotuba yangu burudisha mioyo yao kama matone ya maji yanavyoburudisha miili ya watu" au nichosema kwao kiliwaburudisha kama matone ya maji"

Job 29:23

walinisubiri daima kama walivyosubiri mavua

watu walimsubiri kwa subira na kutarajia kusikia mambo mema.

"walisubiri kwa hamu niongee ili wanufaike kutoka katika usemi wangu"

kama walivyofanya kwa mvua ya masika

"wakulima walisubiri kwa hamu mvua ya masika"

mvua ya masika

mvua ya masika

hii ni mvua kubwa ambayo hunyesha kabla ya majira ya ukame

nilitabasamu kwa ajili yao

"nilitabasamu kwa aji yao ili kuwafariji"

mwanga wa uso wangu

hii inawakilisha ukarimu waliouna katika sura ya Ayubu

Job 29:25

niliwachagulia njia zao

hii inamaanisha kuwaamulia jambo wanalopaswa kutenda

niliketi kama mkuu wao

"niliwaongoza kama mkuu wao"

niliishi kama mfalme kwenye jeshi lake

watu walimtii Ayubu kama mfalme na walikuwa kama jeshi lake.

nilikuwa kama mtu anayewafariji waombolezaji

"niliwafariji wakati wa kuomboleza kwao"

Job 30

Job 30:1

hawana kitu lakini mdhaha kwa ajili yangu

"hunidhihaki tu"

ambao baba zao nigewakataza kufanya kazi sambamba na mbwa wa kundi langu

"ambao baba zao niliwadharau na sikuwaruhusu kufanya kazi sambamba na mbwa wa kundi langu"

mbwa wa kundi langu

"mbwa ambao walilinda kundi langu"

Je nguvu za mikono ya baba zao zingewezaje kunisaidia mimi... zimeharibika?

"nguvu za mikono ya baba zao hazikunisaidia kunisaidia mimi... zimeharibika"

watu ambao nguvu zao za ukomavu wa umri wa o zimeharibika

"watu ambao wamezeeka na hawana nguvu" au "watu ambao wamekuwa wazee na dhaifu"

walikonda kwa umasikini na njaa

neno "wali.." ni kiambishi kwa kumaanisha baba wa vijana wenye dhihaka.

walikonda kwa umasikini na njaa

"walikonda sana kwa sababu walikuwa masikini na hawakupata mahitaji ya kutosha"

tafuna kwenye ardhi kavu

"walitafuna mzizi waliyoipata katika ardhi" au "kutafuna kwenye ardhi kavu" ni picha kuwa walikula chochote walichoweza kukipata katika ardhi kavu"

Job 30:4

Sentensi Unganishi

Ayubu anaendelea kuongea kuhusu baba zao wenye kudhihaki

mboga ya chumvi ...majani ya vichakani...mizizi ya miretemu

Hii ni mimea ambayo watu waliweza kula endapo hawakuwa kupata chakula kizuri.

mizizi ya miretemu kilikuwa chakula chao

(1) watu walikula mizizi ya miretemu au 2) watu waliota moto kwa kuchoma mizizi ya miretemu.

walifukuzwa kutoka kati ya watu ambao waliwapigia kelele... mwizi

"walipigiwa kelele na watu ...mwizi na kulazimishwa kuondoka"

waliwapigia kelele kama mtu anavyompigia kelele mwizi

"waliwapigia kelele kana kwamba walikuwa wezi"

Job 30:7

walilia kama punda

"walilia kwa kupata njaa"

walikuwa uzao wa wapumbavu, naam, wa watu wasiofaa

"walitenda kama watu wasiokuwa na akili"

walifukuzwa kwa mijeredi watoke kwenye nchi

"walifukuzwa watoke nje ya nchi kama waharifu"

Job 30:9

hawaachi kunitemea mate usoni

"hata hunitemea mate usoni"

Mungu amelegeza kamba ya upinde wangu na kunitesa

"Mungu ameziondoa nguvu zangu kwa ajili ya kujitetea mwenyewe"

Job 30:12

juu ya mkono wangu wa kuume huinuka umati

"kundi la vijana hushambulia nguvu zangu" au " makundi ya watu wanashabulia heshima yangu"

hujikusanya dhidi yangu kwa kunizunguka

...adui wamejiandaa kumshambulia Ayubu, kama jeshi linavyojiandaa kushambulia...

Job 30:14

kama jeshi kwenye ufa mpana katika ukuta wa mji

Ayubu analinganisha hali yake na mji ambao upo katika mashambulizi wakati ukuta wake wa ulinzi unaufa

heshima yangu imefukuziwa mbali kama kwa upepo

"upepo umepeperusha heshima yangu"

mafanikio yangu yanatoweka kama wingu

Mali ya Ayubu imepotea kama wingi ambalo huonekana ghafula na hutoweka kutoka angani.

Job 30:16

Sasa uhai wangu unamiminika kutoka ndani yangu

Ayubu anahisi yu karibu kufa

maumivu ambayo yanaguguna kwangu hayapumziki

Ayubu anaongelea maumivu yake kam kitu chenye uhai.

Job 30:18

amenitupa kwenye matope

Ayubu anasema amefedheheshwa na Mungu

Job 30:20

katili

neno hili linamaana ya kukosa huruma

kwa nguvu za mkono wako umenitesa

Neno "mkono" linawakilisha nguvu za Mungu

Job 30:22

unaniinu juu kwenye upepo ...unanirusha nyuma na mbele katika dhoruba

Hii inaelezea mateso makuu ambayo Mungu amfanya Ayubu avumilie

nyumba ya hatima kwa viumbe hai vyote

"nyumba" inawakilisha sehemu ambapo wafu huelekea

viumbe hai vyote

vitu vyote vilivyo hai kwa sasa lakini vitakufa siku moja

Job 30:24

je hapana mtu wa kufikisha mkono wake kuomba msaada wakati anapoanguka? Je mtu mwenye shida hawezi kuomba msaada?

(1) "Niliwasaidia watu ambao walianguka wakati waliponiomba msaada . Niliwasaidia waliokuwa na taabu walipoomba msaada". au (2) "Nimeanguka na Mungu hapaswi kuona kama ninakosea ninapoomba msaada wake. Niko kwenye shida, naomba msaada!"

Je sikulia...shida? Je sikusononeka...mtu?

"Unajua kwamba nililia ...shida, na nilisononeka ...mtu!"

Nilisubiri mwanga ...giza likaja

Hapa "mwanga" unawakilisha baraka na kibali cha Mungu na "giza" linawakilisha shida na mateso.

Job 30:27

Moyo wangu umetaabika na wala haupumziki

Ayubu anaongelea moyo wake kama ni mtu

Ninarandaranda na ngozi yenye giza lakini si kusababu ya jua

"Daima nipo katika hudhuni na giza"

ndugu wa mbwa mwitu, mshirika wa mbuni

Ayubu anafananisha mateso yake na kuomba kwake msaada kama kilio cha mbweha na mbuni.

Job 30:30

Mifupa yangu imeungua kwa joto

Hapa "mifupa" inawakilisha mwili wote, ambao unaugua katika homa

maombolezo

"maombolezo" ni sauti kuu ya kilio chenye huzuni au maumivu.

Job 31

Job 31:1

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kuzungumza

Nimefanya patano na macho yangu

"Nimejiahidi mwenyewe kwamba sitamwangalia mwanamke kwa tamaa"

kwa namna gani tena napaswa kumtazama mwanamwali kwa tamaa?

Ayubu anatumia swalli ili kutia mkazo kwamba hatavunja ahadi yake.

Ni sehemu gani kutoka kwa Mungu juu, na urithi gani kutoka kwake mwenye nguvu aliye juu?

sentensi hizi mbili zina maana moja. Ayubu anatumia swali ili kukazi kwamba Mungu asingempa kitu kizuri kama angefanya dhambi na kuvunja ahadi yake.

Job 31:3

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kuzungumza

Je Mungu hazioni njia zangu na kuzihesabu hatua zangu zote?

Mahali hapa "njia zangu" na "hatua zangu" zinarejelea tabia za Ayubu. Ayubu anatumia swali kwa ajili ya mkazo.

Job 31:5

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kuzungumza

kama nime...

Katika 31:5-40 Ayubu anafafanua hali mbalimbali ambazo angesitahili kupata hukumu ya Mungu. Lakini anajua kuwa si ya kweli na yeye hana hatia.

nimetembea katika udanganyifu, kama mguu wangu umeharakisha katika uongo

"kufanya kitu cha uongo au kumdanganya mtu kwa makusudi"

na nipimwe katika vipimo vilivyo sawa

Watu hutumia mizani ili kupima vitu na kutambua uthamani wake. "Mungu na anihukumu kwa uadilifu"

Job 31:7

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kufafanua hali ambazo alistahili kupata hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli.

Kama hatua zangu zimegeuka kutoka katika njia sahihi

"kama nimekoma kufanya kile kilicho sawa"

kama moyo wangu umetembea kwa kufuata macho yangu

"kama nimefanya mambo yoyote maovu"

na kama doa lolote la uchafu limeng'ang'ania katika mikono yangu

"kama nina hatia ya dhambi kabisa"

mavuno na yang'olewe katika shamba langu

"mtu mwingine zaidi na aje na kuchukua mavuno kutoka katika shamba langu"

Job 31:9

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kufafanua hali ambazo alistahili kupata hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli.

kama moyo wangu umevutiwa na mwanamke mwingine

"kama nimemwakia tamaa mke wa mwanaume mwingine"

ikiwa nimelala na mke wa jirani yangu katika hali ya kusubiria katika mlango wake

"na kama nimemsubiria aache nyumba yake ili niweleze kulala naye"

na ndipo mke wangu na asage nafaka kwa mwanaume mwingine

Maana zinazokubalika ni 1) hii ni njia ya kusema kuwa mwanaume atalala na mke wa Ayubu au 2) in maana kwamba atakuwa mtumwa na kufanya kazi kwa mwanaume mwingine.

Job 31:11

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kufafanua hali ambazo alistahili kupata hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli.

litakuwa ni kosa kubwa kuadhibiwa na waamuzi

"Litakuwa ni kosa ambalo kwa ajili yake waamuzi watakuwa sahihi kuniad

Kwa kuwa ni moto ambao unateketeza kila kitu kwa uharibifu, na kwamba utaunguza mavuno yangu yote

Ayubu anatia mkazo jinsi dhambi ya uzinzi iilivyo ya hatari na kuangamiza.

Job 31:13

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kufafanua hali ambazo alistahili kupata hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli.

kisha nini basi ningefanya wakati Mungu anapoinuka ili kunishitaki mimi? Atakapokuja kunihukumu, nitamjibuje?

Ayubu anatumia swali ili kutia mkazo. "kisha hakutakuwa na kitu kabisa nitakachoweza kusema ili kujilinda mwenyewe wakati Mungu atakapokuja kunihukumu"

Je yeye aliyenifanya mimi tumboni hakuwafanya wao pia? Je yeye si yeye yule aliyetuumba sisi wote katika tumbo?

"Mungu, ambaye alinifanya mimi na kwa namna ile ile aliwafanya na wao, atanihukumu kwa jinsi ya haki ile ile kama anavyowahukumu wao."

Job 31:16

Maelezo ya jumla .

Ayubu anaanza kufafanua hali ambazo angestahili kupata hukumu ya Mungu, (zimeelezwa katika 31:22) lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli

nimesababisha macho ya wajane yafifie kwa kulia,

Mahali hapa "yafifie" inarejelea mjane kuwa wa uwezo mbaya wa kuona kwasababu ya kulia sana.

kipande changu

"chakula"

tangu ujana wangu yatima walikua pamoja nami kama kuwa na baba, nami nimemwongoza mama yake, mjane, tangu katika tumbo la mama yangu mwenyewe.

Ayubu anaelezea jinsi alivyowatendea kweli mjane na yatima. "Niliwajali yatima na wajane tantu nilipokuwa mdogo sana"

Job 31:19

Maelezo ya jumla .

Ayubu anaanza kufafanua hali ambazo angestahili kupata hukumu ya Mungu, (zimeelezwa katika 31:22) lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli

ikiwa moyo wake haujanibariki kwasababu amekuwa hajatiwa joto na sufu ya kondoo zangu,

"Nimewapa watu wale nguo za sufu ili kupata joto, na hivyo wamenibariki, lakini kama ningekuwa sijafanya hivyo,"

nimeinua juu mkono wangu kinyume

"Nimetisha ili kudhuru"

katika lango la mji

Hapa ni mahali ambapo watu muhimu wa mji hukusanyika na kufanya maamuzi.

Job 31:22

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kufafanua hali ambazo alistahili kupata hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli.

Ndipo bega langu na lianguake kutoka katika sehemu yake, na mkono wangu uvunjike katika kiungo chake

"kisha mtu mmoja na alivunje bega langu na kuuvunja mkono wangu"

Job 31:24

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kufafanua hali ambazo alistahili kupata hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli.

kama ningesema kwa dhahabu safi, 'wewe unanifanya kuwa na tumaini';

Msitari huu una maana sawa na msitari uliotangulia. Kwa pamoja inasisitiza kwamba Ayubu hajategemea mali ili kumletea usalama.

mkono wangu umepata mali nyingi,

"Nimepata mali nyingi kwa uwezo wangu"

Job 31:26

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kufafanua hali ambazo alistahili kupata hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli.

mwezi ukitembea

"mwezi ukizunguka katika anga"

na kama moyo wangu umevutwa kwa siri

"kama kwa siri nimetamani kuviabudu"

mdomo wangu umeubusu mkono wangu

Hii ni ishara ya upendo na ibada.

kuadhibiwa na waamuzi,

"kwa ajili yake waamuzi wangekuwa sawa kuhukumu"

Job 31:29

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kufafanua hali ambazo alistahili kupata hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli.

Kwa kweli sijauruhusu hata mdomo wangu kutenda dhambi kwa kuuomba uhai wake kwa laana.

Ayubu anaelezea ukweli wa jinsi alivyowatendea wale anaowachukia. "kwa ukweli, sikujihusisha mwenye katika dhambi kwa kuilaani sik yake"

Job 31:31

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kufafanua hali ambazo alistahili kupata hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli.

Ikiwa watu wa hema yangu hawajasema,' Nani aweza kumpata mtu ambaye hayashibishwa na chakula cha Ayubu?

"Watu wangu siku zote wamekuwa na uwezo wa kusema,"Kila mtu tunayemjua amekula chakula kingi cha Ayubu kama alivyotaka' Kama hayo hayakuwa ya kweli,"

hata mgeni hajawahi kukaa katika pembe ya mji, kwa kuwa siku zote nimefungua milango yangu kwa ajili ya wasafiri

Ayubu anaelezea jinsi ambayo aliwatendea wageni."Wageni hawakuwahi kulala mitaani. Mara zote niliwakaribisha nyumbani kwangu"

Job 31:33

Maelezo ya jumla

Ayubu anaendelea kufafanua hali ambazo angestahili kupata hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa hayakuwa ni ya kweli.

kwa kuwa niliogopa kusanyiko kubwa, kwasababu ya matwezo ya familia yaliniogopesha

Kauli hizi zinamaanisha kitu kimoja. Kwa pamoja zinatia mkazo kwamba mtu anaweza kuificha dhambi yake kwasababu anahofu juu kile ambacho watu wangesema.

Job 31:35

hii ni saini yangu

Ayubu anaelezea malalamiko yake kwa Mungu kana kwamba aliyaandika katika nyaraka rasmi. Angeandika jina lake juu yake kama ahadi ambayo kila kitu katika nyaraka ni za kweli.

Ikiwa nilikuwa na shitaka rasmi ambalo adui yangu ameliandika!

"kama tu ningeweza kusoma mashitaka ya adui yangu dhidi yangu"

Hakika ningelibeba hadharani juu ya bega langu; ningeliweka juu kama taji

Hii ina maana kama Mungu angeyaandika mashitaka kinyume na Ayubu, kisha Ayubu angeziweka nyaraka mahali ambapo kila mtu angeweza kuzisoma.

hatua zangu

hii inarejelea matendo ya Ayubu

kama mwana wa mfalme mwenye kujiamini

Hii ina maana kwamba Ayubu angemkaribia Mungu bila hofu.

Job 31:38

Maelezo ya jumla

Hii inahitimisha maelezo ya Ayubu juu ya hali ambazo ndani yake angestahili hukumu ya Mungu, lakini anajua kuwa haikuwa kweli.

Kama nchi yangu ingelia dhidi yangu, na matuta yake yaomboleza pamoja

Ayubu anaielezea nchi kana kwamba alikuwa mtu ambaye analia kwasababu Ayubu ameiiba kutoka kwa mmliki halali.

Job 32

Job 32:1

katika macho yake mwenyewe

''katka ufahamu wake mwenyewe" au "katika mawazo yake"

Ndipo iliwaka hasira ya Elihu mwana wa Barakeli Mbuzi, wa familia ya Ramu, iliwaka dhidi ya Ayubu

Hii inalinganisha hasira ya Elihu na mtu anayewasha moto.

Elihu.....Barakeli.....Ramu

Haya ni majina ya wanaume

mbuzi

Hili ni jina la kikundi cha watu.

Job 32:3

Hasira ya Elihu iliwaka pia kinyume cha marafiki zake watatu

Hii inallingisha hasira ya Elihu na mtu anayewasha moto.

sasa

Neno hili limetumika hapa kuonesha pumziko fupi katika habari kuu. Hii inatueleza habari za nyuma kuha

uwa hapakuwa na jibu katika midomo ya watu hawa watatu

"kwamba watu hawa watatu walikuwa hawana kitu zaidi cha kusema"

hasira yake iliwaka

Hii tena inalinganisha hasira ya Elihu na mtu anayewasha moto. "alikuwa mwenye hasira sana"

Job 32:6

ninyi ni wazee

mahali hapa 'ninyi' ni wingi na inarejelea Ayubu na marafiki zake.

Urefu wa siku utazungumza; na wingi wa miaka utatufundisha hekima

Hii mistari miwili inamaanisha kitu kimoja. Elihu anatia mkazo kwa kuwa watu wazee ni wenye hekima kulika vijana, wanatakiwa kuwa wa kwanza kusema yale wanayoyajua.

Job 32:8

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza na Ayubu na marafiki zake.

roho.... pumzi ya Mwenye nguvu

Virai hivi vinamaanisha kitu kimoja. Elihu anakazia kwamba hekima ya watu hutoka kwa Mungu.

Job 32:11

niliyasubiria maneno yenu

Elihu anaongea na marafiki za Ayubu. "Nilisubiri nisikie yale ambayo mngesema"

Job 32:13

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza na marafiki zake na Ayubu.

Tumepata hekima

"sisi ni wenye hekima"

amemshinda Ayubu

"kumshawishi Ayubu" au "kumjibu Ayubu"

Job 32:15

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

Hawa watu watatu wamep igwa bumbuwazi; hawawezi kuendelea kumjibu Ayubu; hawana neno zaidi la kusema

Vipande vitatu vya mstari hii vinamaanisha kitu kimoja. Elihu anakazia kwamba marafiki wa Ayubu wamesema kile walichoweza kusema.

Je ninapaswa kusubiria kwasababu hawazungumzi, kwa kuwa wamesimama pale kimya na wala hawajibu zaidi?

Elihu anatumia swali kukazia kwamba hatasubiria tena ili azungumze

Job 32:17

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza kwa kutumia mtindo wa usambamba

nimejawa na maneno

"nina mengi sana ya kusema"

roho ndani yangu inanisukuma

"lazima niseme sasa"

kifua changu ni kama divai yenye chachu ambayo haina tundu; kama viriba vipya, kiko tayari kupasuka.

Wakati divai inapochacha, gesi hujikusanya katika chombo. Kama gesi hiyo yaitaondolewa, chombo kitapasuka . Elihu anamaanisha kwamba anayo mengi ya kusema na kama hatayasema anajisikia kama atapasuka.

Job 32:20

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza kwa kutumia mtindo wa usambamba

niweze kuburudishwa

"naweza kujisikia vizuri"

nitafungua kimya changu

"fungua mdomo wako"au "sema"

wala sitatoa sifa za majina kwa mtu yeyote

"wala sitamsifu mtu yeyote au kumpa mtu majina ya heshima"

Muumba wangu

"Mungu aliyeniumba"

Job 33

Job 33:1

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

usikilize hotuba yangu; sikiliza maneno yangu yote

Virai hivi viwili vinamaanisha kitu kimoja. Elihu anatia mkazo kwamba Ayubu lazima asikilize kwa makini.

nimeufumbua mdomo wangu; ulimi wangu umesema maneno ndani ya mdomo wangu

Kauli hizi zinamaanisha kitu kimoja. Elihu anatiza mkazo kwamba sasa ana utayari wa kuzungumza.

Maneno yangu yatasema uadilifu wa moyo wangu

"Nitazungumza kwa ukamilifu wa uadilifu"

yatasema kwa unyofu yale ambayo mdomo wangu unayajua.

"Nitakwambia kwa uaminifu mambo ninayoyajua"

Job 33:4

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza na Ayubu

Roho ya Mungu imeniumba..... imenipatia uhai

mistari hii miwili ina maana moja. Elihu inatia mkazo kwamba Mungu amemfanya yeye na kwa hivyo humpa mamlaka kwa kile anachokisema.

weka maneno yako katika mpangilio mbele yangu na kisha usimame

"andaa kile utakachokisema na unijibu"

Job 33:6

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuongea na Ayubu.

nimeumbwa pia kutoka katika udongo

"Mungu amenifanya kutokana na udongo"

wala mzigo wangu hautakuwa mzito kwako.

"Sitakutesa wewe kwa kile ninachokisema" au " nitazungumza na wewe kwa upole"

Job 33:8

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuongea na Ayubu

nimeisikia sauti ya maneno yako yakisema

"Nimekusikia ukisema"

'Mimi ni safi na bila hila; sina hatia, na hakuna dhambi ndani yangu.

Maelezo yote haya yanamaanisha kitu kile kile. "Mimi sina hatia ya kosa lolote"

Job 33:10

Elihu anaendelea kunukuru kile alichomsikia Ayubu akikisema

"akiba" ni vizuizi ya mbao ambayo ilitumika na bwana jela ambaye aliiweka katika miguu ya wafungwa kuwazuia wasitoke.

njia zangu

Hii inarejelea matendo ya Ayubu

nitakujibu

Elihu anazungumza na Ayubu

Job 33:13

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza na Ayubu

Kwanini unashindana naye?

"hatutakiwi hata kujaribu kushindana na Mungu"

Huwa hahesabu matendo yake yoyote.

"Yeye hawajibiki kutueleza sisi kila kitu anachokifanya"

Mungu huzungumza mara moja, naam, mara mbili,

"Mungu huzungumza tena na tena kwa njia mbalimbali

Katika ndoto, katika maono ya usiku,

Maneno haya yanamaanisha kitu kile kile. "ndoto ambayo katika maono ya usiku"

wakati usingizi mzito unapowapata watu, katika usingizi kitandani

"wakati watu wakiwa wamesinzia kweli kitandani mwao"

Job 33:16

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza na Ayubu

Mungu hufungua masikio ya watu

"ndipo Mungu hufunua mambo kwa watu"

Mungu huyaokoa maisha ya mwanadamu kutoka katika shimo, na uhai wake dhidi ya kifo.

Maelezo ya haya yanamaanisha kitu kile kile. "Mungu huwakoa watu kutoka katika kaburi na katika kifo."

Job 33:19

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuongea na Ayubu

Mtu huadhidibiwa pia

"Mungu pia humwadhibu mtu"

ili kwamba maisha yake yachukie chakula, na roho yake ichukie vyakula vizuri

Virai hivi viwili kimsingi vinamaanisha kitu kile kile, kwamba mtu ni yuko katika maumivu makali ambayo yanamfanya anashindwa hata kula.

ichukie vyakula vizuri

"kuchukia hata chakula chake anachokipendelea"

Job 33:21

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza na Ayubu

Nyama yake imeharibiwa ili kwamba usionekane; mifupa yake

"Ugonjwa huufanya mwili wake uwe dhaifu na ukonde hata kwamba mtu anaweza hata kuona mifupa yake"

roho yake inasogea shimoni

"yuko karibu kuingia katika kaburini"

uhai wake unasogea kwa wale wanaotaka kuuharibu.

Kirai "wale wanaotaka kuuharibu" yaweza kurejelea watu wale ambao wako tayari katika sehemu ambapo wafu huenda. Yaweza pia kurejelea malaika wa kifo ambaye huja na kumfanya mtu afe. "Yuko karibu na kufa"

Job 33:23

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuongea na Ayubu

kwa ajili yake

Hii haimrejelei mtu maalumu. Elihu anaendelea kuongea na mtu yeyote kwa ujumla.

mmoja miongoni mwa maelfu ya malaika,

"mmoja kutoka katika kundi kubwa la malaika"

Job 33:25

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuongea na Ayubu

kisha

"kama matokeo ya ombi la malaika kwa Mungu"

mwili wake utakuwa mororo kuliko mwili wa mtoto

"mwili wa mtu mgonjwa utakuwa mpya tena kama mwili wa mtu mdogo"

atazirudia siku za nguvu za ujana wake.

"atakuwa na nguvu tena"

auone uso wa Mungu akiwa mwenye furaha

"humwabudu Mungu kwa furaha"

Mungu atampa mtu ushindi wak

"Mungu atamwokoa mtu" au "Mungu atayafanya mambo ya mtu kuwa sawa" Hii pia yaweza kumaanisha kwamba mtu anatangaza kwa wengine jinsi Mungu alivyomwokoa.

Job 33:27

Maelezo ya jumla

Elihu anazidi kuzungumza na Ayubu

lakini dhambi yangu haikuadhibiwa

"lakini Mungu hakuniadhibu mimi kwa kutenda dhambi"

ameiokoa roho yangu

"aliniokoa mimi"

maisha yangu yataendelea kuuona mwanga

Atauona mwanga wa maisha badala ya giza ambalo angeliliona katika kifo. "nitaendelea kuishi"

Job 33:29

Maelezo ya jumla

Elihu anazidi kuzungumza na Ayubu

mara mbili, naam, hata mara tatu

"tena na tena"

roho yake

:yeye"

aweze kumlikwa na mwanga wa maisha.

"aweza kuwa na furaha ya kubaki kuwa hai"

Job 33:31

Maelezo ya jumla

Elihu anazidi kuongea na Ayubu

zingatia na unisikilize mimi;

Virai hivi vinamaanisha kitu kile kile. "Nisikilize kwa umakini, Ayubu"

Job 34

Job 34:1

Elihu

Angalia jinsi alivyofasiri katika 32:1

Sikilizeni maneno yangu

"Sikiliza kile ninachokisema"

ninyi watu wenye hekima....ninyi mlio na maarifa

Elihu anamkosoa Ayubu na marafiki zake. Hafikiri kama ni watu wenye hekima kweli.

Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno kama ambavyo kaakaa huonja chakula.

Elihu anamaanisha kwamba watu wasikilize kwa makini ili kujua kilicho cha haki au kibaya kama tu vile ambavyo tunaonja chakula kutambua kama ni chakula kizuri au kibaya.

Job 34:4

Maelezo ya jumla

Elihu anazidi kuongea

Na tujichagulie sisi

Hapa "sisi" inamrejelea Elihu, Ayubu, na marafiki wake watatu.

ameondoa haki zangu

"amekataa kunipa haki "

, ninaangaliwa kama mwongo

"marafiki zangu hudhani mimi ni mwongo" Hii huenda yaweza kumaanisha: "Mungu hasemi ukweli kuhusu mimi"

Kidonda changu hakiponyeki,

"mimi ni mgonjwa na hakuna awezaye kuniponya"

Job 34:7

Maelezo ya jumla

Elihu anazidi kuzungumza

Ni mtu gani aliye kama Ayubu

Elihu anatumia swali hili kumkaripia Ayubu. " Hakuna mwingine zaidi kama Ayubu"

ambaye hunywa dharau kama maji

Elihu anamshitaki Ayubu kwa kufurahia kuwadharau watu wengine.

ambaye hutembea pamoja na watu waovu

"ambaye anaenenda kama watu waovu"

Job 34:10

Maelezo ya jumla

Elihu anazidi kuongea

enyi watu wenye ufahamu

Elihu anamkosoa Ayubu na marafiki zake. Hadhani kabisa kama walikuwa ni watu wenye hekima.

iwe mbali na Mwenye enzi kwamba atatenda dhambi

Hii ina maana sawa na sehemu nyingine ya sentensi iliyotangulia. Elihu anakazia kwamba Mungu siku zote hufanya yaliyo ya haki.

humfanya mtu apate thawabu za njia zake mwenyewe

Hii inamaana sawa na sehemu nyingine ya sentensi iliyotangulia. Elihu anatia mkazo kwamba Mungu huwapa watu kile wanachostahili.

Mungu hatendi uovu, wala Mwenye nguvu hajaIpotosha haki.

Hii ina maana sawa na sehemu nyingine ya sentensi iliyotangulia. Elihu anakazia kwamba Mungu siku zote hufanya yaliyo ya haki.

Job 34:13

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

Ni nani aliyemweka kuwa mtawala wa dunia? Ni nani aliyeiweka dunia yote chini yake?

Kauli hii ina maana moja. "hakuna hata mmoja ambaye anahitaji kumpa Mungu ruhusa ili anaye majukumu yake juu ya dunia yote. Yeye ni mwenye haki katika kuutawala ulimwengu wote."

nafsi yake na pumzi yake

"nafsi yake na pumzi amabayo hutupa uzima"

miili yote

"viumbe hai vyote "

Job 34:16

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

sasa

Elihu anatumia neno hili ili kuleta usikivu wa kitu fulani muhimu ambacho alikuwa karibu kukisema.

sikilizeni sauti ya maneno yangu

Hii ina ina maana ile ile na ya sehemu iliyotangulia ya sentensi. "sikiliza kile ninachosema"

Je yeye anayeichukia haki aweza kutawala? Je mtamhukumu Mungu kuwa ni mwenye makosa, ambaye ni mwenye haki na mwenye nguvu?

"Yeye anayechukia haki hawezi kutegemea kuwa kiongozi juu

Job 34:18

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

Mungu ambaye humwambia mfalme, ' Wewe ni mbaya; au huwaambia wenye kuheshimiwa, 'Ninyi ni waovu'?

Hii inaendeleza swali kutoka katika mstari uliotangulia.

mbaya

"mwovu" au "asiyestahili"

, kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake

Mahali hapa neno "mkono" linamaanisha nguvu.

wakati wa usiku watu watatikiswa na watapita

"wakati wa usiku" ni wakati wa mwisho wa siku na mwanzo wa siku nyingine.

watu wenye nguvu watatwaliwa mbali,lakini si kwa mikono ya wanadamu.

"Ni Mungu wala si wanadamu anayewafanya watu wa muhimu wafe.

Job 34:21

Kwa kuwa macho ya Mungu yako juu ya njia za mtu;

"kwa kuwa Mungu huangalia kila kitu anakifanyacho mtu

anaziona hatua zake zote

"humwona kila aendako"

Hakuna giza, wala hakuna weusi mzito

Maneno "weusi mzito" kimsingi yanamaanisha kitu kile kile na yanatia uzito juu ya neno "giza"

Job 34:24

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

Huwavunja vipande vipande watu wenye nguvu

"Huwaharibu watawala"

kwa ajili ya njia zao ambazo hazihitaji uchunguzi zaidi

"kwasababu anajua tayari kile alichokifanya"

huwaweka watu wengine katika nafasi zao

"na anachagua watu wengine kutawala katika nafasi zao"

wakati wa usiku

"wakati wasioutarajia"

Job 34:26

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

dhahiri mbele za watu wengine

"katika sehemu ambayo kila mtu anaweza kuona"

wamegeuka na kuacha kumfuata yeye

"wangeacha kumtii yeye"

njia zake

Hii inarejelea maagizo ya Mungu kwa jinsi ambavyo watu wanapaswa kuenenda.

wamekifanya kilio cha watu masikini kimfikie

"waliwafanya watu masikini walie, na Mungu aliwasikia"

Job 34:29

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

Na wakati akaapo kimya, nani aweza kumhukumu kuwa mkosaji?

Elihu anatumia swali kwa ajili ya kumfundisha Ayubu. "Hakuna anayeweza kumkosoa Mungu kama akiamua kukaa kimya"

Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumjua?

Elihu anatumia swali jingine kwa sababu ile ile. "Hakuna hata mmoja anayeweza kwenda na kumwona kama akiamua kujificha mwenyewe."

asiwepo mtu wa kuwanasa watu.

Hii inawalinganisha watu watawaua na muwindaji ambaye hunasa nyara zake.

Job 34:31

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

nifunze kile ambacho siwezi kukiona

"nifundishe kile nilichokifanya vibaya na hata sikukijua"

Je unadhani kwamba Mungu ataiadhibu dhambi ya mtu huyo, kwa kuwa unayachukia yale ambayo Mungu huyatenda?

Elihu anatumia swali kwa ajili ya kutia mkazo. "Ingawa haupendi kile ambacho Mungu anakifanya, hakika hata haufikirii kwamba Mungu atamwadhibu mtu huyu"

Job 34:34

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

Job 34:36

Kama Ayubu alijaribiwa kwa kitu kidogo kabisa katika kesi yake

"kama tu tungeweza kumpeleka Ayubu mahakamani ili kwamba hakimu aweze kumsikia kwa malalamiko yake yote."

anapiga makofi ya dharau kati yetu

"Humdharau Mungu mbele yetu hasa"

anaweka maneno kinyume na Mungu

"anaendelea kusema mambo mabaya kumhusu Mungu"

Job 35

Job 35:1

Je unadhani hii ni sawa ....'Haki yangu mbele ya Mungu?

Elihu anatumia maswali ili kumtia changamoto Ayubu. "Lazima ufikiri wewe ni mwenye haki....haki yangu mbele za Mungu"

Je unadhani

hapa kiambishi 'u' ni umoja na kinamwakilisha Ayubu.

Kwa kuwa unauliza, 'Inafaa nini kwangu' na 'Ingekuwa nzuri kwangu kama ningekuwa nimetenda dhambi?

"kwa kuwa wasema haijalishi kuwa uko mwenye haki, na ya kwamba hakuna faida zaidi kwako kuliko kama ungekuwa umetenda dhambi"

Job 35:4

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

Job 35:6

Sentensi kiunganishi

Elihu anaendelea kuongea

Kama umetenda dhambi, ni madhara gani huwa unayafanya kwa Mungu?

Dhambi zako zote haziwezi kumharibu mtu au tabia za Mungu"

Ikiwa makosa yako yameongezeka zaidi, je huwa unafanya nini kwake?

Swali hili linarudia wazo lile lile kama swali lililotangulia. "Ingawa unaendelea kutenda dhambi pamoja na matokeo makubwa, dhambi zako hazina athari juu yake.

Kama wewe ni mwenye haki, unaweza kumpa nini? Je atapokea nini mkononi mwako?

Maswali haya mawili kimsingi yanamaanisha jambo lile lile, kwamba haki ya Ayubu haikuongeza chochote kwa Mungu.

kutoka mkononi mwako

"kutoka kwako"

mwana wa mtu

"mwanadamu mwenza" au "mtu mwingine"

Job 35:9

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

katika mikono ya watu wenye nguvu

Mahali hapa "mikono" ina maana ya ya nguvu au uwezo.

Lakini hakuna hata mmoja asemaye, ' Mungu Muumba wangu yuko wapi....ndege wa angani?

"Lakini mtu wa haki kweli si mwenye kiburi hata kwa kusema kwamba Mungu amekataa kuwapa uwezo wa kuimba nyimbo za furaha, wakati wa mateso yao."

ambaye hutoa nyimbo wakati wa usiku,

Hii ina maana kwamba ahadi za Mungu huwapa watu sababu ya kuwa na furaha hata wakati wakiwa katika mateso.

Job 35:12

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

wanalia

" watu walioteswa wanalia"

Ni kwa namna gani atakujibu

"Hakika hatakujibu"

Job 35:15

Maelezo ya jumla

Elihu anaendelea kuzungumza

Ni kwa jinsi gani atakujibu

"Hakika hatakujibu"

huongeza maneno

"anaendelea kuongea"

Job 36

Job 36:4

maneno yangu hayatakuwa ya uongo;

"Nitasema yale ya kweli"

angalia

Neno 'angalia' mahali hapa linatia mkazo juu ya kile kinachofuata. "hakika"

yeye ni mwenye nguvu katika uweza wa ufahamu

Kirai "mwenye nguvu katika uweza" kina maana "kuwa na nguvu zaidi"

Job 36:6

Haondoi macho yake kwa wenye haki

"huwaangalia wale wenye haki"

huwaweka juu ya viti vya enzi kama wafalme

Yahweh huwaheshimu watu kama watu wanavyowaheshimu wafalme.

nao wameinuliwa juu

Maana zinazokubalika ni 1) anawafanya wengine" au 2)"anawafanya wengine wafanikiwe"

Job 36:8

wamefungwa minyororo

Hapa kiambishi 'wa' kinawarejelea watu kwa ujumla. "mtu mmoja aliwafunga kwa minyororo''

kunaswa katika kamba za mateso

Elihu anaongelea juu ya mateso kana kwamba yanaweza kuwanasa watu kwa kamba. "kama mtu atawafanya wateseke"

Job 36:10

Hufungua pia masikio yao kwa ajili ya agizo lake

"huwafanya wasikilize agizo lake"

siku zao....miaka yao

Virai hivi viwili rinarejelea kipindi cha maisha ya mtu.

wataangamia kwa upanga

"watakufa kifo cha vurugu"

Job 36:13

Na wale wasiomjua Mungu hutunza hasiria zao katika mioyo

Mahali hapa neno "moyo" linarejelea "fikra na hisia"

Job 36:15

hufungua masikio yao

angalia ulivyotafsiria katika 36:10

meza yenu ingewekwa

"Watumishi wako wangeiweka meza yako"

chakula kilichojaa mafuta

nyama yenye mafuta mengi ilikuwa ni ishara ya mafanikio kwasababu wanyama walikuwa na afya njema na walilishwa vizuri. "vyakula vizuri sana"

Job 36:17

wewe umejaa hukumu juu ya watu waovu

Maana zinazokubalika ni 1)" Mungu anakuhukumu kama ambavyo angewahukumu watu waovu" au 2) "umejawa na kushikwa na hukumu ambayo watu waovu wanastahili"

hukumu na haki umeziachilia

"Mungu amekuleta katika hukumu na amekupa haki"

Usiuache utajiri ukuvute katika udanganyifu;

Usimruhusu mtu akuvute katika udanganyifu kwa mali.

sehemu kubwa ya rushwa isikugeuze upande kutoka katika haki.

"Usimruhusu mtu akugeuze upande kutoka katika haki kwa rusha kubwa.

Job 36:19

Je utajiri wako waweza kukunufaisha, ili kwamba usiwe katika taabu, au nguvu zako zote za uwezo zaweza kukusaidia?

Elihu anauliza maswali haya ili kutia mkazo kwamba pesa na nguvu hazitaweza kumsaidia Ayubu kama atatenda isivyo haki.

nguvu zako zote za uwezo

"nguvu zako zote kubwa"

wakati ambapo mataifa hukatiliwa mbali katika nafasi zao

Maana zinazokubalika ni 1)" wakati makundi ya watu yatakapotoweka kutoka katika sehemu yake au 2) " wakati watu watakapowavuta kutoka katika nyumba zao,"

unajaribiwa kwa mateso

"Mungu anakujaribu wewe kwa kukufanya uteseke"

Job 36:22

Angalia

Neno 'angalia' mahali hapa linaongeza mkazo kwa kile kinachofuata

nani aliye mwalimu kama yeye?

Jibu lililofichwa kwa swali hili ni "hakuna" "Hakuna mwalimu kama yeye" au "hakuna awezaye kufundisha kama anavyofanya yeye"

Ni nani alishamwalekeza njia yake?

"Hakuna hata mmoja ambaye alishamwamuru yeye na kumwelekeza kitu cha kufanya.

Job 36:25

kwa mbali

""Isiyo kamili"

Tazama

Neno "tazama" mahalip hapa linaongeza kile kijacho.

hesabu ya miaka yake

"umri wake"

Job 36:27

kuna hata mmoja awezaye kuelewa kwa undani kusambaa kwa mawingu na radi kutoka katika nyumba yake?

Jibu lisilo la wazi ni "Hapana"

nyumba yake

Mahali hapa ni "nyumba yake" inawakilisha anga la juu mahali ambapo Mungu hudhani kuwa huiishi huko.

Job 36:30

Angalia

Neno 'angalia' mahali hapa linaongeza mkazo kwa kile kinachofuata.

Job 36:32

Yeye huuijaza mikono yake kwa mwanga

Maana zinazokubalika ni 1) kwamba Mungu anashikilia vifungo vya mwanga mkononi mwake ili aweze kuzitupa au 2) kwamba Mungu huuficha vifungo vya mwanga katika mikono yake hadi pale alipo tayari kuvitumia.

ngurumo zake

"Sauti ya mwangaza"

Job 37

Job 37:1

moyo wangu hutetemeka...umeondolewa kutoka katika sehemu yake

Virai hivi viwili kimsingi vina maana moja ile ile na kutia mkazo wa ukubwa wa hofu yake.

moyo wangu hutetemeka kwa hili

Neno 'hili' linarejelea dhoruba katika 36:32

umeondolewa kutoka katika sehemu yake

Mapigo ya moyo wa Elihu yanaongelewa kana kwamba yalikuwa yanaruka nje ya kifua chake.

kelele za sauti yake, sauti inayotoka katika mdomo wake.

Virai hivi viwili kimsingi vina maana ile ile. Elihu anaiongelea sauti ya radi kana kwamba ni sauti ya Mungu.

mipaka ya dunia

"sehemu yeyote katika dunia"

Job 37:4

Sauti huunguruma baada yake...mshindo wa mwanga wakati sauti yake inaposikika

Elihu anaendelea kuzungumzia radi kana kwamba ni sauti ya Mungu.

wakati sauti yake inaposikika

"wakati watu wanapoisikia sauti yake"

Job 37:7

Huuzuia mkono wa kila mtu

"humzuia kila mtu"

Dhoruba hutoka katika chumba chake upande wa kusini na baridi kutoka katika pepo zilizotawanyika katika upande wa Kaskazini.

Katika Israeli, upepo mkali wa dhoruba huvuma kutoka kusini na hewa ya baribi hufika kutoka kaskazini.

chumba chake upande wa kusini

Elihu anaongelea dhoruba kuwa ina sehemu inapokaa mpaka

Job 37:10

Barafu imetolewa kwa pumzi ya Mungu

Elihu anaongelea juu ya upepo wa baridi wa kaskazini kana kwamba ni pumzi ya Mungu. "Pumzi ya Mungu hufanya barafu"

umeganda kama chuma

wakati maji yanapoganda, huwa magumu kama chuma

Job 37:14

Je unajua ni kwa namna gani Mungu hushurutisha mawingu na kuufanya mwanga wa radi ung'ae ndani yake?

Jibu lililojificha la swali hili ni ''hapana''.

Job 37:16

Je unafahamu kuelea kwa mawingu, matendo ya ajabu ya Mungu, Je ni nani aliyemkamilifu katika maarifa?

"Haufahamu kuelea kwa mawingu, matendo ya ajabu ya Mungu, ambaye ni mkamilifu katika maarifa."

kuelea kwa mawingu

"jinsi mawingu yanavyoelea"

matendo ya ajabu ya Mungu

"njia za miujiza ambayo kwayo huyafanya mawingu yaelee katika anga"

Je unafahamu ni kwa jinsi gani mavazi yako huwa ya moto wakati nchi ikiwa imetulia kwasababu ya upepo unaotoka upande wa kusini?

"Wewe haufahamu jinsi ya kuzuia kutoka kwa jasho katika nguo zako; ni hatari sana wakati upepo wa joto kali unapokoma kuvuma kutoka kusini na majani yote katika miti hutulia"

Job 37:18

Je unaweza kulitandaza anga kama anavyofanya - anga ambalo lina nguvu kama kioo cha chuma kigumu?

"Hauwezi kulitandaza anga kama anavyoweza kwa anga ambalo ni gumu kama kioo cha chuma kigumu"

nguvu kama kioo cha chuma

Katika siku za Biblia, vioo vilitengenezwa kwa chuma. Elihu anaongelea anga kama anavyoangalia chuma kigumu wakati halitoi mvua.

chuma kigumu

Hii inarejelea chuma kilichoyeyushwa, na kumwagwa

Tufundishe sisi kile tunachopaswa kumwambia yeye

'mahali hapa maneno 'sisi' na kiambishi 'tu' yanamrejelea Elihu, Elifazi, Bildadi na Zofari, lakini si Ayubu. Elihu anatumia kirai hiki kwa kejeli.

kwasababu ya kiza katika akili zetu.

"kwasababu hatufahamu"

je anapaswa kuambiwa kwamba ninapenda kuongea naye?

"Sitakuwa na mtu wa kumwambia kwamba ninataka kuongea naye"

Je anapaswa kuambiwa

"je nipate mtu wa kumwambia"

Je mtu angependa kumezwa?

"Hakuna mtu ambaye angependwa kumezwa"

kumezwa

"kwa ajili ya Mungu kumwua"

Job 37:23

wale ambao ni wenye hekima katika akili zao wenyewe.

"wale wanaojidhania kuwa ni wenye hekima"

Job 38

Job 38:1

"Huyu ni nani ...... bila maarifa?

Yahweh anatumia swali hili ili kutia mkazo kwamba Ayubu alikuwa ameseam mambo ya kipumbavu. "Umeleta giza.... pasipo ufahamu."

aletaye giza katika mipango

Giza linawakilisha ushari wa kipumbavu.

kwa njia ya maneno bila maarifa?

"kwa kusema maneno lakini pasipokuwa na maarifa"

jifunge kiunoni mwako

"jifunge nguo yako kiuoni" Wanaume wajifunga nguo kuzunguka viunoni mwao, ili kwamba miguu iwe huru katika vita au mashindano.

kama mwanaume

"Kama shujaa"

lazima unijibu

"lazima animbie majibu"

Job 38:4

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu.

Wewe ulikuwa wapi... misingi

Yahweh anaumia swali hili il kutia mkazo kwamba Ayubu hakuwepo wakati Mungu alipoumba dunia, hivyo Ayubu haelewi jinsi Mungu alivyoiumba dunia.

ilipoitandaza misingi ya dunia

"Nilifanya misingi ya dunia" Yahweh anaelezea jinsi alivyoiumba dunia kana kwamba alikuwa akijenga jengo.

Niambie

"Niambie jibu"

kama unao ufahamu zaidi

"unadhani unajua sana"

ni nani aliyeamuru vipimo vyake

Yahweh anatumia swali hili kutia mkazo kwamba ni yeye anayeamua namna ukubwa wa dunia unavyopaswa kuwa, hivyo ni yeye pekee anayejua jinsi alivyoifanya.

alivinyosha vipimo juu yake

"aliipima dunia kwa kamba"

kipimo

kamba ambayo watu waliitumia ili kuhakiki kuwa wanajenga jengo kwa kipimo halisi na kwa muundo sahihi.

Job 38:6

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

Ni nani............jiwe la pembeni

Yahweh anatumia maswali haya kutia makazo kwamba Ayubu hajui jinsi Yahweh alivyoifanya dunia.

Misingi yake ilitandazwa juu ya nini?

Ni juu ya nini misingi ya dunia iliwekwa.

nyota za asubuhi

"nyota angavu ambazo huangaza asubuhi"

wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja

Yahweh anaelezea juu ya nyota kana kwamba walikuwa ni watu walioweza kuimba.

wana wa Mungu

"malaika"

kwa furaha

"kwasababu walikuwa na furaha imejaa"

Job 38:8

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu.

huifunga bahari

Yahweh anatumia swali hili ili kutia mkazo kwamba aliifanya bahari.

huifunga bahari kwa milango

Yahweh analinganisha njia aliyoitumia kuizuia bahari ili isiigharikishe dunia yote na kuishikilia bahari kwa nyuma.

kana kwamba inatoka katika tumbo

Yahweh analinganisha uumbaji wake wa bahari na uzazi.

mavazi yake

kama nguo kwa ajili ya bahari

giza nene

:mawingu meusi sana"

na giza nene kuwa mkanda wake wa kujifungia

"na kufunga katika mawingu mazito Kama mkanda wa kujifungia"

mkanda wake wa kujifungia

Hiki ni kipande cha nguo ambacho watu walikitumia kuwafunga watoto wachanga baada ya kuzaliwa.

Job 38:10

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

apo ilikuwa wakati nilipoweka bahari mpaka wangu,

Nlifanya mipaka kwa ajili ya bahari.

mpaka

Yahweh aliumba mpka kuzunguka bahari kwamba bahari haziruhusiwi kuuvuka.

nilipoweka makomeo yake na milango,

Yahweh analinganisha namna alivyotengeneza mpaka wa bahari na ya kwamba bahari ina milango na makomeo. "Hivyo niliweka vizuizi ili kwamba maji yasiweze kuvuka juu ya nchi."

makomeo

ni kpande kirefu cha ubao au chuma ambacho hutumika kwa ajili ya kufungia mlango.

kwa fahari ya mawimbi yako

Yahweh anazungumzia juu ya mawimbi kana kwamba walikuwa ni watu. Ina maana kwamba mawimbi yana fahari kwa kuwa yana nguvu.

Job 38:12

Maelezo ya jumla

Yahweh aendelea kumtia changamoto Ayubu.

Je tangu mwanzo wa siku zako, ulishawahi .....waovu watikiswe mbali nayo?

Yahweh anatumia swali hili kutilia mkazo kwamba ni Mungu tu anazo nguvu juu ya asubuhu na Ayubu hana hizo nguvu.

tangu mwanzo wa siku zako

Kirai hiki kina maana "tangu ulipozaliwa" au "katika siku

kuigiza asubuhi

Yahweh anaeilezea asubuhi kana kwamba alikuwa ni mtu ambaye angeweze kupokea maagizo.

a kuyafanya mapambazuko yajue sehemu yake katika mpangilio wa vitu

"uyaache mapambazuko yajue kule miliki yake iliko"

mapambazuko

ni mwanga unajitokeza asubuhi kabla ya jua halijachomoza.

ili kwamba ishikilie sehemu za dunia

Yahweh anaiongelea asubuhi kana kwamba ni mtu anayeshikila pembe za dunia kama pembe za mkeka. Mapambazuko yanaonekana kushikilia sehemu za dunia kwasababu mwanga wake huonekana kwanza pembezoni.

ili watu waovu watikiswe mbali nayo.

''na kuwatikisa watu waovu nje ya dunia." Mwanga wa mapambazuko huwafanya watu waovu waende mbali kama kutikisa kwa mkeka kunavyotoa uchafu juu yake.

Job 38:14

Dunia imebadilishwa katika mwonekano kama udongo unavyobadilika chini ya muhuri;

Watu hawawezi kuona vizuri kwa wakati wa usiku, lakini asubuhi hufunua wazi muundo wa kila kitu, kama vile muhuri unavyoumba mwonekano katika udongo.

Mwanga' wao umeondolewa kutoka kwa watu waovu

"Asubuhi huondolea mbali mwanga wa watu waovu"

mwanga wao

Watu waovu hudhani giza kuwa ndio mwanga wao, kwa kuwa wanafanya matendo yao maovu katika giza na wameizoelea giza.

mkono wao ulioinuliwa umevunjwa

Mkono ulioinuliwa wa watu waovu unaonesha kwamba wana nguvu na nia ya kufanya mambo maovu, lakini mwanga wa asubuhi huvunja mkono wa ili kwamba wasiwe na uwezo wa kufanya maovu.

Job 38:16

Maelezo ya jumla

Yahweh aendelea kumtia changamoto Ayubu.

Je ume...upana wake?

Yahweh anatumia maswali haya ili kutia mkazo kwamba vitu hivi ambavyo Ayubu hajavifanya na ya kwamba kuna vitu vingi sana ambavyo Ayubu havijui.

vyanzo

"chemichemi"

kilindi

"maji"j au "bahari" au "vilindi vya maji"

Je malango ya mauti yamefunuliwa kwako?

"Je kuna mtu amekuonesha malango ya kuzimu"

e umeifahamu dunia katika upana wake?

"Je umekiangalia kila kitu kkwa umakini katika njia zake kwa sehemu za mbali sana za dunia"

kama unayajua yote hayo

"kama umezoea dunia yote" au "kama unajua kila kitu kuhusu dunia"

Job 38:19

Maelezo ya jumla

Yahweh aendelea kumtia changamoto Ayubu.

sehemu ya kupumzikia kwa mwanga,

"sehemu ambayo mwanga hukaa" au " sehemu ambayo mwanga unaishi" Yahweh anauelezea mwanga kana kwamba alikuwa ni mtu.

sehemu zake za kazi

"kwa mpaka wake' Mpaka huizunguka sehemu ya mwanga na giza. Wakati usiku unapoisha, giza hurudi katika sehemu yake. Na wakati siku inapoisha, mwanga hurudi katika sehemu yake.

Bila shaka......kubwa sana!

Yahweh anatumia kejeli ya kinyume ili kutia mkazo kwamba Ayubu hauelewi mwanga na giza. "Ni wazi kwamba hauelewi kwa sababu ulikuwa bado haujazaliwa wakati nilipoviumba na haukuwa mtu mzima"

kwa kuwa ulizaliwa wakati huo

Neno 'wakati" linarejelea muda ambao mwanga uliumbwa na kutengwa na giza. "kwa kuwa ulikuwa umezaliwa wakati nilipouumba ulimwengu"

hesabu ya siku zako ni kubwa sana!

"umeishi miaka mingi sana ' au wewe ni mzee sana"

Job 38:22

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

ume....juu ya dunia?

Yahweh anatumea maswali haya kukazia kwamba Ayubu hajui jinsi ambavyo Yahweh hutuma barafu, mawe ya mvua, radi na upepo wa mashariki juu ya nchi.

mawe ya mvua

vipande vya mviringo vya barafu ambavyo huanguka ardhini kutoka angani.

Job 38:25

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu.

Ni nani aliyezitengeneza mifereji

Yahweh anatumia swali hili kutia mkazo kwamba yeye ndiye hufanya mambo haya yote.

gharika ya mvua

"mbubujiko wa nguvy wa mvua"

njia

"barabara'' au "sehemu za kupita"

milipuko ya radi

"sauti ya radi." Hii ni sauti kuu ya radi ambayo hutoka katika mawimbi ya hewa.

kuifanya mvua inyeshe

Yahweh hutengeneza mifereji ya chemichemi ya maji ili kwamba aweze kutuma maji juu ya nchi sehemu ambazo hakuna watu.

hakuna mtu aishiye ndani yake

"sehemu isiyo na watu"

ili kutimiza mahitaji

"ili kwamba mvua iweze kukidhi mahitaji"

mikoa iliyo kame na yenye ukiwa

"sehemu ambazo hazina mimea au wanyama au watu"

majani mororo

majani ambayo kwanza yameanza kukua na bado machanga na laini

kuyastawisha

"kuanza kukua"

Job 38:28

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu.

Je kuna baba wa mvua? Ni nani aliyeyafanya matone ya umande?

Yahweh anatumia maswa haya kukazia kwamba Ayubu hafahau jinsi Yahweh anavyoitengeneza mvua, umande, barafu, na theluji

Je kuna baba wa mvua?

Yahweh anaiongelea mvua kana kwamba alikuwa ni mtu.

aliyeyafanya

kazi ya baba katika kumfanya mtoto azaliwe

matone ya umande

matone ya umande ambayo huunda mtonesho katika mmea na katika vitu vingine

Na ni nani aliyeizaa theluji nyeupe

"ambaye ameizaa theluji nyeupe"

Maji hujificha menyewe

katika kipindi cha masika barafu huficha maji chini yake.

vilindi

Hii hurejelea maji ya kina kirefu kama vile maziwa, mito, na bahari

Job 38:31

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

Je unaweza kuzifunga minyororo.....juu ya dunia

Yahweh anatumia maswali haya kukazia kwamba Ayubu hajui jinsi ya kutawala na kuongoza nyota.

kuzifunga minyororo

"kukaza minyororo" au "kufunga vifungo"

Kilimia...Orioni...dubu

Haya ni majina ya makundi ya nyota.

kuvifungua vifundo vya Orioni

"kuvunja vifungo vinavyoshikilia Orioni"

nyota

Hii inarejelea aina kumi na mbili tofauti tofauti za nyota ambazo huonekana baada ya jua wakati linapozama. Mkusanyiko wa nyota huonekana nyuma ya jua kila mwezi.

kutokea katika nyakati zake

"ili kwamba zionekanae kwa wakati sahihi"

watoto wake

"vitoto vichanga vya dubu"

Job 38:34

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

Je waweza kupaza....sisi tupo hapa

Yahweh anatumia maswali haya kukazi kwamba Ayubu hawezi kutawala mawingu, mvua au mwanga wa radi.

ili kwamba maji mengi ya mvua yakufunike

"ili kwlamba maji mengi sana yatakufunika"

Je waweza kuagiza miali ya mwanga ili itokee

"waweza kuamuru miali ya radi kutokea mahali unapotaka itokee na kwa kweli itatokea'

kukwambia

"na watakwambia"

Sisi tupo hapa

Kirai hiki kina maana, "sisi tupo hapa ili kwamba wewe utuambia kila unachotaka sisi tufanye"

Job 38:36

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

Ni nani ameweka hekima...kushikama kwa pamoja

Yahweh anatumia maswali haya kukazi kwamba Mungu ana utawala juu ya mawingu na kwamba Ayubu hana uwezo huo

ameweka hekima katika mawingu

'ameyapa mawingu hekima" Yahweh anaelezea mawingu kana kwamba walikuwa ni watu na alikuwa ameyapa hekima ili kwamba yajue kile cha kufanya.

Nani anaweza kuyahesabu mawingu

Kirai hiki kina maana: "Ni nani awezaye kujua kuwa ni wembamba wa mawingu ni wa namna ganii katika anga"

viriba

Hivi ni vitu vilivyotengenezwa na watu ili viweze kuhifadhi maji. Yahweh anayarejeleamawingu mazito kama "viriba" kwasababu kwa kuwa yanashikilia maji mengi kama viriba vya maji.

wakati mavumbi yanapoungana kuwa kitu kigumu

"wakati matope ya mvua yanapoungana kwa pamoja kuwa kipande kimoja." Mvua huyafanay mavumbi makavu yaungane kwa pamoja kama kipande kimoja cha udongo.

mabonge ya dunia yanaposhikama kwa pamoja

Vipande vya udongo hushikana kwa pamoja"

Job 38:39

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

Je waweza kuwinda... kulala katika hali ya kuvizia

Yahweh anatumia maswali haya kukazia kwamba yeye anajua jinsi ya kulisha simba, lakini Ayubu hajui.

mawindo

"nyara" Huyu ni mnyama ambaye anaweza kuliwa na simba

simba jike

Huenda ni "simba"

au kutosheleza hamu ya watoto wadogo wa simba

"au kuwapa simba wadogo chakula cha kutosha ili kwamba waweze kuishi"

watoto wake wadogo

"simba wadogo." Hawa ni simba wadogo ambao wana umri unaotosha kuwinda wao wenyewe.

katika pango lao

"katika sehemu ambazo wanaishi" au "sehemu za makao yao"

kukaa katika kificho

"kulala katika uoto wa mimea minene"

kulala katika hali ya kuvizia

"ambayo ni sehemu ya kuvizia" au "ni sehemu ambayo wanajificha ili kukamata wanyama wengine." Simba hujificha katika katika mimea minene na kusubiria mnyama apite na ili wamrukie na kumkamata mnyama huyo.

Job 38:41

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

aletaye mawindo

Yahwe anatumia swali hili kukazi kwamba ni yeye aletaye chakula kwa kunguru na ya kwamba Ayubu halijui hilo.

mawindo

mnyama ambaye kunguru humtafuta na anaweza kumla

kunguru

ndege aina ya kunguru

wanapomlilia Mungu

"kumlilia Mungu ili kupata msaada" au " kumlilia Mungu ili awaokoe"

kutangatanga

"kuzunguka zunguka"

kwa kukosa chakula

"kwasababu hawana chakula" au "kwa kuwa hawana kitu cha kula"

Job 39

Job 39:1

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu.

Je unajua ni wakati gani .... muda ambao huzaa watoto wao

Yahweh anatumia maswali haya kutia mkazo kwamba anatunza mbuzi na paa ilihali Ayubu hawezi kufanya hivyo.

Je waweza kuwangalia paa wakati wanapozaa watoto wao?

"wakai paa wanapozaa je waweza kuhakikisha kwamba kila kitu kinaenda sawa"

wanapozaa watoto wao

"kuzaa"

"kuhesabu miezi ya kuchukua mimba

"kuhakikisha kuwa wanakamilisha muda wa mimba zao"

wa....

Kiambishi hiki kinarejelea mbuzi na paa

muda ambao huzaa watoto wao

wakati wao wa kuzaa"

Job 39:3

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

Wanainama chini

Kiambishi 'wa'inarejelea mbuzi na paa

kuzaa watoto wao

"kuwafanya watoto wao watoke ndani yao"

kisha maumivu yao ya uzazi yanaisha

Maneno "maumivu ya uzazi' yanarejelea uzao wa mbuzi na paa kwasababu ni matokeo ya kazi na maumivu ya mama zao.

uwanda wa wazi

"nchi ya mashamba" au "porini"

hawarudi tena

"hawatarudi tena kwao" au " kurudi kwa mama zao"

Job 39:5

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

nani.....nchi ya chumvi

Yahweh anatumia maswali haya ili kutia mkazo kwamba yeye huwalinda punda pori na ya kwamba Ayubu hawezi kufanya hivyo.

Punda mwtu.... punda wepesi

Haya ni majina tofauti ya aina ile ile ya punda

vifungo

kamba, minyororo ambayo hufunga mnyama na kumzuia asikimbie.

ni nyumba ya nani

Yahweh anaiongolea punda kana kwamba alikuwa ni mtu ambaye ana nyumba. "Nilimpta Araba kama nyumba ya kuishi"

nchi ya chumvi

nchi inayoizunguka Bahari ya Chumvi ambayo ina chumvi nyingi ndani yake.

Job 39:7

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

hu...

Kiambishi hiki kinarejelea punda mwitu

Hucheka kwa dharau

Yahweh anaiongelea punda kana kwamba alikuwa ni mtu. Punda walichekka kwasababu wale walikuwa katika mji lazima wasikie sauti kubwa, ingawa alikuwa akiishi sehemu ya ukimya.

mwongozaji

mtu ambaye anawalazimisha wanyama kufanya kazi.

malisho

sehemu ambazo wanyama wanaweza kula mimea inayokua katika mashamba

Job 39:9

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

je nyati...bonde kwa ajili yako?

Yahweh anatumia maswali haya ili kutia mkazo kwamba Ayubu hawezi kuwatawala nyati.

Nyati

Maana zinazowezekana ni 1) "ng'ombe wa porini" 2)"swala" aina fulani ya swala anayeonekana kama ng'ombe dume.

kuwa na furaha

"kuridhia"

atakubali kukaa katika zizi lako

"kukaa karibu na zizi wakati wote wa usiku"

hori/zizi

Katika mazingira ya Israeli, hiki kilikuwa ni chombo cha kulishia wanyama

mtaro

Ni mfereji mrefu uliotengenezwa katika sehemu chafu kwa kutumia plau.

kuchimba

"kulima kwa plau"

kwa ajili yako

"nyuma yako" wakati wa kulima kwa plau, mtu huongoza ng'ombe akiwa nyuma yake.

Job 39:11

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

waweza kumtumaini...uwanda wako wa kupuria

Yahweh anatumia maswali haya ili kutia mkazo kwamba Ayubu hawezi kuwatawala nyati.

kumtumaini

Kiambishi 'm' kinamrejelea 'nyati"

kumwachia kazi yako ili aifanye

"umwachie yeye aifanye kazi yako ngumu kwa ajili yako"

Job 39:13

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

Mabawa... ya upendo

Yahweh anatumia swali hii ili kutia mkazo kwamba Ayubu hawezi kuelezea kwanini mbuni wanaenenda jinsi wanavyofanya.

mbuni

huyu ni ndege mkubwa ambaye anaweza kukimbia haraka, lakini hawezi kupaa.

kwa majivuno

"kwenda kwa furaha"

mabawa

haya ni manyoya marefu juu ya mabawa ya ndege

manyoya

ni manyoya madogo yaliyoenea juu y mwili wote wa ndege

yana upendo

Maana zinazowezana 1) "uaminifu" 2) "ya kurungu" Jina hili lilimaanisha "mwaminifu mmoja" au mwenye kupenda, kwasababu kunguru huwajali sana watoto wake.

katika nchi

juu ya ardhi

kuyaharibu

Neno hili linarejelea mayai.

kuyakanyaga

"kukanyaga juu yao"

Job 39:16

Huyatendea vibaya

kiambishi 'hu' kinamrejelea mbuni jike

kazi yake

kazi ile ambayo huifanya wakati wa kulalia mayai na kuwahudumia vifaranga.

yaweza kupotea bure,

kama watoto watakufa, kazi yake yote itakuwa ni bure

amemnyima hekima

humfanya asahau hekima

ufahamu

Angalia ulivyofasiri katika 11:4

huwacheka...mpanda farasi wake

Ina maana kwamba hucheka kwasababu huenda kwa kasi kulliko farasi. "Hucheka... kwa mpanda farasi wake, kwasababu farasi hawezi kukimbia kwa kama yeye.

Job 39:19

Maelezo ya jumla

Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu

Je umempa farasi ... panzi?

Yahweh anatumia maswali haya kutia mkazo kwamba ni yeye ndiye huyafanya mambo haya ambayo Ayubu hayawezi.

umeivika shingo yake

Neno 'kuvika" ni njia ya kuelezea jinsi ambavyo Yahweh alivyoifanya shingo ya farasi.

manyoya yake

ni nywele ndefu ambazo hushuka chini kutoka katika shingo ya farasi na hutisika wakati farasi anapoondoka.

nzige

ni aina kubwa ya panzi ambayo yaweza kuruka kwenda mbali na kwa haraka sana.

mlio

ni sauti kubwa ambayo farasi huitoa katika pua zao.

Job 39:21

Hurarua

Kiambishi 'hu' kinarejelea farasi. Farasi huchimbua ardhi kwasababu anakuwa amesisimka kuanza kupigana.

hurarua

"kuchimbua ardhi kwa kutumia kwato"

hudharau

"kuchekelea"

hashangazwi

"kuogopeshwa'' au ''kuhofu''

harudi nyuma

"hakimbii mbali''

podo

ni chombo ambacho hutunza mishale

hugongagonga

"kutikisika na kutoa kelele''

ubavuni

sehemu za pembeni za farasi

fumo

ni mti mrefu uliochongoka mwishoni ambao watu huurusha kwa maadui zao.

Job 39:24

huimeza

Kiambishi 'hu' kinarejelea farasi

huimeza nchi

Farasi hukimbia kwa kasi juu ya ardhi na ya kwamba nchi hupita kama mtu anakunywa maji.

hasira na ghadhabu

"kwa miondoko mikubwa na ya haraka" Farasi anaposisimuka huondoka kwa haraka na kwa nguvu. Na kwasababu hii, farasi hukimbia kwa haraka.

katika sauti ya tarumbeta,

"wakati mtu fulani anapopuliza tarumbeta ili kutangaza kwamba vita imeanza."

hawezi kusimama sehemu moja

"mara kwa mara huwahi kwenye vita"

husema Ooo!

Watu hutoa Sauti Ooo! wakati wanapokuwa wamefurahia kitu fulani. Farasi huwa na furaha kwasababu huifurahia vita.

vishindo vya radi

Hii ina maana kwamba farasi huvisikia vitu hivi. "husikia sauti ya radi"

kelele

"Vita hupiga kelele" Watu huwa na kilio maalumu ambacho hukitumia kuonesha kuwa wao ni watu gani na nguvu zao kuu na ujasiri na kuwaogopesha maadui.

Job 39:26

Je ni kwa hekima ... kwa upande wa kusini?

Jibu lililofika la swali hili ni "hapana". Si kwa hekima yetu..."

Je ni kwa hekima yako kwamba mwewe hupaa

"si wewe unayemfunza mwewe kuruka"

huyanyosha mabawa yake

hupaa

kwa upande wa kusini

Katika jiografia ya kibiblia, ndegu hupaa na kuelekea upande wa kusini katika kipindi cha masika ili kuishi katika hali ya joto.

Job 39:27

Je ni kwa agizo lako ... kiota chake katika sehemu za juu?

Jibu lililofichika la swali hili ni ''hapana'' ''si kwa maagizo yako....kiota katika sehemu za juu"

Je ni kwa agizo lako

"je ni kwasababu wewe unaiambia kufanya hivyo"

huruka juu

"hupaa juu angani"

majabali

ni vifusi virefu ni makao ya tai kwasababu wanyama ambao wangetaka kuwala hawawezi kuwafikia.

Job 39:29

hutafuta mawindo

Kiambishi 'hu' kinarejelea tai

macho yake huyaona

huwaona wao

pale walipo wafu

"sehemu palipo na watu wafu'' Kirai hichi kinarejelea maiti zilizolala katika sehemu wazi, si miili iliyozikwa ardhini.

ndipo na yeye alipo.

"yuko pale kuwala wao"

Job 40

Job 40:1

Je mtu yeyote anayetaka kukosoa na ajaribu kumsahihisha Mwenye enzi?

Jibu linalotarajiwa hapa ni, 'hapana'

Job 40:3

mimi si mtu muhimu;

sina umuhimu

je nawezaje kukujibu?

"Siwezi kukujibu"

Job 40:6

Jifunge sasa mkanda kiunoni mwako kama mwanaume

Hii humlinganisha Ayubu na mtu anayejiweka tayari kwa ajili ya kazi. ''Jifunge mkanda kiunoni mwako'' ina maana ya kujifunga kipande cha nguo katika sehemu ya mkanda ili mtu aweze kufaya kazi.

Job 40:8

Je waweza kusema kwa hakika kwamba mimi si mwenye haki?

Unasema mimi si mwenye haki"

je utanihukumu mimi ili useme wewe ni mwenye haki?

Unanihukumu mimi ili wewe uweze kusema kwamba wewe ni mwenye haki."

mkono kama wa Mungu

"nguvu kama nguvu za Mungu

Je waweza kutoa kishindo kwa sauti kama yeye?

"Hakika hauna sauti ya nguvu kama ya Mungu, ambaye huileta radi.

Job 40:10

Sambaza ziada ya hasira yako

"Funua jinsi hasira yako ilivyo katika majivuno ya watu"

mtazame kila mmoja mwenye kiburi

"angalia watu wote wenye kiburi"

umshushe chini.

"mweke chini katika umuhimu"

Job 40:12

zifunge nyuso zao

"wafunge hao"

katika sehemu zilizositirika

Hii ni njia nyingine ya kusema 'sheoli' au sehemu ambapo watu wa agano la kale walienda baada ya kufa.

Job 40:15

anakula

Kiambishi 'a' kinarejelea kiboko.

kama ng'ombe

Hii inaelezea jinsi ambayo kiboko anavyokula majani

Job 40:17

kama mti wa mwerezi

"namna ambayo matawi ya mierezi yanavyokwenda.'

kama ya mirija ya shaba

Mahali hapa, mifupa yake inalinganishwa na mirija iliyotengenezwa kwa shaba ili kuonesha jinsi mnyama alivyo mgumu

kama kipande cha chuma

Huu mlinganisho wa mwisho unaelezea nguvu za mnyama mkubwa.

Job 40:19

milima humpatia chakula

Mwandishi anaongelea juu ya milima kana kwamba walikuwa ni watu wanaoweza kumpatia chakula.

mimea ya kivuli

Mmea wa kivuli ni mmea wenye maua ambayo huelea juu ya maji katika sehemu zenye maji maji na tope

mianzi

Majani marefu ambayo hupatikana katika sehemu za maji maji na matope au mabwawa.

Job 40:22

miti yenye vivuli

angalia jinsi ulivyotafsiri hii katika 40:19

kingo

pande za mto

hata kama Mto wa Yordani unajaa hadi katika pua yake

"hata kama gharika litakuja juu ya pua yake"

Je mtu yeyote aweza kumnasa kwa ndoano... kwa mtego?

Hili ni swali hili la kejeli hupaswa kujibiwa kwa jibu la kukanusha. "Hakuna yeyote awezaye kumkamata kwa ndoano au kwa mtego"

Job 41

Job 41:1

Maelezo ya jumla

Mungu anaendelea kuzungumza. Anatumia maswali mengi ya kejeli kumtia changamoto Ayubu.

Au kumfunga taya zake kwa kamba?

"Hauwezi kumvua mamba kwa ndoano ya samaki"

Au kumfunga taya zake kwa kamba?

Hii si sentensi kamili, lakini maana yake yaweza kufahamika kutoka katika muktadha kama " Au kumfunga taya zake kwa kamba? "au hauwezi kumfunga taya kwa kamba.

Je waweza kuweka kamba katika pua zake

"Hauwezi kuweka kamba katika pua yake, au kuchoma taya zake kwa ndoano"

Je atafanya maombi mengi kwako?

"Hawezi kufanya maombi kwako"

Je atazungumza na wewe kwa maneno laini?

"Hataweza kuzungumza maneno laini"

Job 41:4

Je atafanya agano na wewe, ili kwamba umchukue kwa ajili ya mtumishi milele?

"Hatafanya agano na wewe, kwamba hautamfanya kuwa mtumishi milele"

Je utacheza pamoja naye kama ambavyo ungecheza na ndege?

"Hautacheza naye kama ambavyo ungecheza na ndege"

Je utamfunga kwa ajili ya mtumishi wako wa kike?

"Hautamfunga kwa ajili wa watumishi wako wa kike"

Je makundi ya wavuvi waweza kumfanyia biashara?

"Makundi ya wavuvi hawataweza kufanya biashara naye"

Je watamgawanya ili kufanya biashara miongoni mwa wafanya biashara?

"Hawatamgawanya kwa wafanya biashara"

watamgawanya

"maundi ya wavuvi watamgawanya"

Job 41:7

e waweza kuijaza ngozi yake kwa vyusa au kichwa chake kwa mikuki ya kuvulia?

"Hauwezi kumchoma ngozi yake kwa silaha za kuwindia, wala kumchoma kichwa chake kwa zana za kuvulia"

vyusa au kichwa cha mikuki

chusa ni mkuki mkubwa ukiwa umechongoka ukitumika kuwindia samaki wakubwa au nyangumi.

je si kila mmoja atatupwa chini katika nchi mbele yake?

"kila mmoja atatupwa chini ardhini mbele yake"

Job 41:10

Ni nani basi awezaye kusimama mbele yake?

"Hakuna yeyote anayeweza kusimama mbele yangu/yake"

Ni nani kwanza aliyenipa kitu chochote ili kwamba niweze kumlipa?

"Hakuna yeyote ambaye kwanza amenipa kitu fulani, ili kwamba niweze kumlipa.

Sitanyamaza kimya

"Hakika nitasema"

miguu ya mamba, wala kuhusu jambo linalohusu nguvu zake

"mguu. Nitazungumza pia juu ya mambo yanayohusu nguvu zake"

nguvu zake, wala kuhusu umbo lake zuri.

"nguvu. Nitazungumzia pia juu ya umbo lake la neema"

Job 41:13

Nani awezaye kuiondoa ngozi yake?

"hakuna yeyote anayeweza kuondoa nguo yake ya nje"

Nani anaweza kumchoma kwa silaha mara mbili?

"Hakuna awezaye kumchoma katika ngovi yake nene"

Nani awezaye kuifungua milango ya uso wake, imezungukwa na meno yake ambayo yanaogofya?

Hakuna yeyote anaweza kuyapanua makanwa yake...yanaogofya"

yamefungwa kwa pamoja kama chapa

Hii ina maana kwamba magamba yamekaribiana kwa ukaribu na yameungana kwa pamoja.

Job 41:16

Moja li karibu na jingine

safu moja ya kinga iko karibu na nyingine.

hayawezi kutenganishwa

"watu hawawezi kuwatenganisha"

Job 41:19

Ndani ya mdomo wake hutoka miali ya mwanga, chembe za moto huruka nje

"katika mdomo wake hutoka miali, cheche za moto zikiruka nje ya mdomo wake." Mungu anafafanua wazo lile lile kwa njia mbili tofauti ili kutia mkazo juu ya mwonekano wa kutisha wa mamba.

Katika pua zake hutoka moshi kama chungu kinachotokota juu ya moto ambao umechochewa ili uwe na joto sana

Kutoka kwa moshi katika pua zake kunalinganishwa na chungu kinachochemshwa juu ya moto.

Job 41:22

yake...hu

Maneno ''yake'' na ''hu'' yanamrejelea mamba

haziwezi kuondolewa

"hakuna yeyote awezaye kuyaondoa"

Job 41:25

hata miungu huogopa;

"Hata watu wenye nguvu huwa waoga"

Yeye hufikiri juu ya chuma kana kwamba ni majani makavu

"Hufikiri juu ya silaha zilizotengenezwa kwa chuma kana kwamba zilikuwa ni silaha zilizotengenezwa kwa majani makavu" Hii inaonesha jinsi ambavyo vyuma imara huwa dhaifa kwa mamba.

hufikiri juu ya fedha kana kwamba ni ubao uliooza

"'Hufikiri juu ya silaha zilizotengenezwa kwa fedha kana kwamba zilikuwa ni silaha zilizotengenezwa kwa mbao zilizooza."

Job 41:28

kwake yeye mawe ya kombeo huwa kama makapi.

Hii ina kwamba mawe ya kombeo hayan matumizi tena kuliko makapi katika upepo dhidi ya mamba.

kwake yeye mawe ya kombeo huwa kama makapi.

Hii ina maana kwamba rungu haitakuwa na faida tena kuliko makapi katika kumpiga mamba.

yeye hucheka juu ya mkuki unaovuma

Mamba anafananishwa na mtu anayechekelea kushindana naye kusiko na maana kwa kumrushia mikuki.

Sehemu zake za chini zi kama vipande vilivyochongoka vya vyungu

Hii inazungumzia juu ya magamba yaliyo na ukali.

huacha alama zilizosambaa katika udongo kana kwamba alikuwa ni chombo cha kusagia.

Sentensi hii inalinganisha mkia wake na chombo cha kusagia ambacho husugua ardhi na kuacha alama kana kwamba kilikuwa kinaenda.

Job 41:31

Yeye hukifanya kilindi kichemke kama chungu cha maji ya moto

"wakati anapopita katika ya maji, huacha mchirizo wa alama ukiotoa povu nyuma yake, kama ni chungu cha maji kilichochemka na kutoa povu."

huifanya bahari kama chungu cha lihamu

Hii ina maana kwamba husuka suka bahari kama chupa ya marihamu ambavyo ingeonekana baada ya kutikiswa hasa.

mtu mmoja angedhani kilindi kuwa cheupe.

Hii ina maana kwamba maji yote hupinduliwa juu wakati mamba anapoogelea kwasababu ya ukubwa wake, naye husababisha mchirizo wa alama ukitoa mapovu.

Job 41:33

Hakuna cha kumlinganisha

"hakuna kiumbe kingine kama mamba"

Hukiona kila kitu chenye kiburi

"yeye ana kiburi sana sana"

yeye ni mfalme juu ya wana wote wa kiburi.

"Mamba ni kama mfalme wa viumbe vyenye kiburi"

Job 42

Job 42:1

"Ninajua kwamba unaweza kufanya mambo yote, ya kuwa hakuna kusudi lako linaweza kuzuiliwa.

"Ninajua kwamba wewe unaweza kufanya mambo yote. Ninajua kwamba hakuna kusudi lako lolote linaweza kuzuiliwa." Hili ni wazo lile lile limeelezwa kwa jinsi mbili tofauti.

hakuna kusudi lako linaweza kuzuiliwa

"hakuna yeyote awezaye kuzuia kusudi lako lolote"

Ni nani huyo ambaye pasipo maarifa huificha mipango?

Matoleo mengi ya kisasa hukubaliano kwamba Ayubu ananukuru maneno ya Mungu kutoka katika 38:1. Wafasiri wanaweza kuamua kuiweka wazi kwamba Mungu alimwuliza swali hili Ayubu, na ya kwamba Ayubu kwa sasa analikumbuka.

huificha mipango

Hii ina maana kwamba, kuficha au kutoiwakilisha mipango ya Mungu na ushauri wake.

Job 42:4

lakini sasa jicho langu linakuona wewe

"lakini sasa ninakufahamu wewe"

ninatubu kwa mavumbi na majivu

Hii ni njia ya kiutamaduni ya kuonesha majuto na toba

Job 42:7

Ilitokea baada ya kuwa

Kirai hiki kimetumika hapa kuonesha tukio kubwa katika habari hii. Kama lugha yako ina jinsi ya kuweza kusema hili unaweza kutumia.

Elifazi Mtemani

angalia ulivyofasiri hii katika 2:1

mafahari saba

mahafari 7

Bildadi Mshuhi

Angalia jinsi ulivyofasiri hii katika 2:11

Zofari Mnaamathi

Angalia jinsi ulivyofasiri hii katika 2:11

Mungu alimtakabali Ayubu

"Mungu anaipokea sala ya Ayubu kwa ajili ya marafiki zake watatu"

Job 42:10

Waliomboleza pamoja naye na walimfariji

Hizi kazi mbili za kuomboleza na kufariji hufanya kazi pamoja katika mchakato wa kumrejesha Ayubu.

Job 42:12

kuliko mwanzo wake

"zaidi sana kuliko sehemu ya kwanza ya maisha yake"

kondoo kumi na nne elfu

kondoo 14,000/=

ngamia elfu sita

ngamia 6,000

jozi elfu moja

jozi za ng'ombe 1,000

wana saba na mabinti watatu.

wana 7 na binti 3

Yemima

binti wa kwanza wa Ayubu

Kezia

binti wa pili wa Ayubu

Kerenihapuki

binti wa tatu anaitwa Kerenihapuki

Job 42:15

hawakupatikana wanawake wazuri kama mabinti wa Ayubu.

"Mabinti za Ayubu walikuwa wazuri zaida kuliko wanawake wengine" au "mabinti za Ayubu walikuwa ni wazuri sana"

akiwa mzee na akijawa na siku nyingi.

Maneno "kujawa na siku" kimsingi yanamaanisha kitu kile kile ya kuwa 'mzee" Virai hivi viwili vinatengeneza nahau moja "kuwa mtu mzee sana"