Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Psalms 1

Psalms 1:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

ambaye hatembei katika ushauri wa waovu

"Ushauri wa waovu" unazungumziwa kana kwamba ni njia ya kufuata. "ambaye hafuati ushauri wa waovu"

kusimama katika njia ya watenda dhambi

Hapa neno "njia" inaonesha namna watu wanavyoishi. Neno "simama" liko sambamba na "tembea." "kuiga tabia za watu watenda dhambi"

au kuketi katika kusanyiko la wenye dhihaka

Kuketi na watu wanao mdhihaki Mungu inaonesha kuwaunga watu wanao mdhihaki Mungu. "au kuwaunga wale wanao mdhihaki Mungu" au "au kumdhihaki Mungu na wale wanaomdhihaki"

furahi

"kuridhika" au "furaha"

Yahwe

Hili ni jina la Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la kale.

Psalms 1:3

Taarifa ya Jumla:

Kifungu hiki kinatambulisha picha iliyo fafanuliwa kwa undani ambayo mtu mtakatifu anawaziwa kama mti unao stawi.

Atakuwa kama mti ... matunda katika msimu wake

Katika Biblia, watu mara nyingi wanazungumziwa kama miti. Watu wanaofurahi katika sheria ya Yahwe wanaweza kufanya yote ambayo Mungu anataka wafanye kama mti uliopandwa kandokando ya maji uwezavyo kutoa matunda mazuri. "Atafanikiwa kama mti ... matunda katika msimu wake"

uliopandwa kandokando ya vijito vya maji

Mti ulipandwa kandokando ya kijito unaweza kupata maji ya kutosha kuwa na afya.

unaotoa matunda yake katika msimu wake

Miti yenye afya inatoa matunda mazuri kwa wakati sahihi.

ambao majani yake hayakauki

Mti ukipaata maji yakutosha, majani yake hayakauki na kufa.

chochote afanyacho kinafanikiwa

"atafanikiwa kwa chochote afanyacho"

Psalms 1:4

Waovu hawako hivyo

Jinsi wasivyo hivyo inaweza kuwekwa wazi. "Waovu hawana mafanikio" au "Waovu hawafanikiwi"

lakini ni kama makapi

Jinsi walivyo kama nyasi inaweza kuwekwa wazi. "lakini hawana faida kama makapi"

hawatasimama katika hukumu

Kupona wakati Mungu anahukumu inazungumziwa kama "kusimama." "hawatapona wakati Mungu anawahukumu" au "watalaaniwa Mungu atakapo wahukumu"

wala watenda dhambi katika kusanyiko

"wala watenda dhambi kusimama katika kusanyiko"

wala watenda dhambi katika kusanyiko la wenye haki

Kukubaliwa na Mungu kama mwenye haki inazungumziwa kama kusimama na kundi la watu wenye haki. "na Mungu hatawakubali watenda dhambi pamoja na watu wenye haki"

Psalms 1:6

Kwa kuwa Yahwe anakubali njia ya watakatifu, bali njia ya waovu itapotea

Vishazi hivi viwili vinaonesha tofauti kwa yale yanayowatokea watu watakatifu na yale yanayowatokea watu waovu.

njia ya mwenye haki

Jinsi watu wanavyoishi inazungumziwa kama vile ni "njia" au "barabara" ambayo walikuwa wakitembea. "jinsi wenye haki wanavyoishi"

njia ya waovu itapotea

Hapa "njia" inamaanisha waovu, ambao kimafumbo wanatembea katika hiyo njia. "Waovu wataangamia kwa sababu ya njia yao" au "waovu watakufa kwa sababu ya jinsi wanavyoishi"

Psalms 2

Psalms 2:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa nini mataifa yako katika ghasia ... kwa nini watu wanafanya mipango itakayoshindwa?

Vishazi hivi viwili vina maana zakufanana, na "mataifa" na "watu" linamaanisha kundi hilo hilo la watu. Maneno "mataifa" na "watu" yanaweza kumaanisha viongozi wao. "Kwa nini viongozi wa mataifa wako katika ghasia na kufanya mipango itakayoshindwa?"

Kwa nini mataifa yako katika ghasia, na kwa nini watu wanafanya mipango itakayoshindwa?

Maswali haya yanatumika kuonesha mshangao kwamba watu wanafanya jambo baya sana na laki pumbavu. "Mataifa yako katika ghasia na watu wanafanya mipango itakayoshindwa."

mataifa yako katika ghasia

Hii inaweza kumaanisha kuwa mataifa yalikuwa yakifanya vurugu ya kelele na hasira.

mipango itakayoshindwa

Hii inawezekana kuwa mipango dhidi ya Mungu na watu wake.

Wafalme wa nchi wafanya msimamo wa pamoja ... viongozi wao wanafanya njama pamoja.

Vishazi hivi viwili vina maana ya kufanana.

wafanya msimamo wa pamoja

"kukusanyika kupambana" au "kuungana na kujiaanda kupinga"

Tupasue pingu ... tutupe minyororo yao

Watu wa mataifa mengine wanamzungumzia utawala wa Yahwe na Masihi juu yao kama pingu na minyororo. "Tujiweke huru kutoka kwenye utawala wao; tusiwaruhusu watutawale tena!"

Psalms 2:4

Yeye ... Bwana

Maneno haya yanamaanisha Yahwe. Yahwe mara nyingi huitwa "Bwana" lakini maneno kwa ajili ya "Yahwe" na "Bwana" ni tofauti.

aketiye mbinguni

Hapa kuketi inamaanisha kutawala. Kile anachokalia kinaweza kuelezwa vizuri. "anatawala mbinguni" au "anaketi katika kiti chake cha enzi mbinguni"

Bwana anawadhihaki

"Bwana anawadhihaki hao watu." Kwa nini anawadhihaki inaweza kuelezwa vizuri. "Bwana anawadhihaki kwa mipango yao yakipumbavu"

na kuwatisha katika gadhabu yake

"gadhabu" inamaanisha kuwa na hasira kali.

kuwatisha

"kuwaogofya"

Psalms 2:6

Mimi mwenyewe

Yahwe anasisitiza kuwa yeye, na sio mtu mwingine, ndiye aliyemtia mafuta mfalme wake.

mtia mafuta mfalme wangu

"kumchagua mfalme wangu kutawala"

Nitatangaza amri ya Yahwe

Mtu anayesema haya ni mfalme. Hii inaweza kuelezwa vizuri. "Mfalme anasema, 'Nitatangaza amri ya Yahwe'"

Akaniambia

"Yahwe akaniambia"

Wewe ni mwanangu! Siku hii nimekuwa baba yako

Kati ya watu wengi katika sehemu hiyo ya dunia kipindi hicho, wanaume waliweza kuamua kupanga watoto kisheria, ambao watakuwa warithi wao. Hapa Yahwe anamtwaa mwanamme na kumfanya kuwa mfalme wa Israeli. "Nitakufanya mwanangu. Siku hii nimekuwa baba yako" au "Sasa u mwanangu na mimi baba yako"

Psalms 2:8

Kauli Unganishi:

Yahwe anaendelea kuzungumza na mfalme mpya wa Israeli.

mataaifa kwa urithi wako ... sehemu za mbali za nchi kwa mali yako

Mafungu haya yanaonesha mawazo ya kufanana sana.

sehemu za mbali za nchi

"ardhi iliyo mbali kabisa"

Utawavunja kwa fimbo ya chuma; kama chupa ya mfinyanzi, utawaponda vipande vipande.

Vifungu hivi vinanaonesha mawazo ya kufanana sana.

Utawavunja kwa fimbo ya chuma

Kuyashinda mataifa inazungumziwa kama kuyavunja, na nguvu yake inazungumziwa kama fimbo ya chuma. "Utawashinda kabisa kwa nguvu yako"

utawaponda vipande vipande

Kuangamiza mataifa inazungumziwa kana kwamba yanaweza kupondwa kama chupa ya udongo. "utawaangamiza kabisa kama chuma ya udongo"

chupa ya mfinyanzi

Mfinyanzi ni mtu anayetengeneza vyungu vya udongo na chupa. Hizi ni nyepesi kuvunjika. "chupa ya udongo" au "chungu cha udongo"

Psalms 2:10

Kwa hiyo sasa, nyie wafalme, muonywe; muwekwe sasa, nyie watawala wa nchi

Mafungu haya mawili yana maana za kufanana. "Kwa hiyo sasa, nyie wafalme na watawala wa nchi, muonywe na kurekebishwa"

muonywe

Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "sikiliza onya hili" au "muwe na hekima"

muwekwe sasa

Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "sikiliza masahihisho haya" au "chukua masahihisho haya"

Psalms 2:12

Mbusu mwana

Watu walimwonesha mfalme wao kuwa walikuwa waaminifu kwake kwa kumbusu, labada miguuni. "Mwonesheni mwana kuwa kweli ni waaminifu kwake" au "Sujuduni kwa unyenyekevu kwa mwanaye"

mtakufa njiani

Hii inaweza kumaanisha kufa hapo hapo, kabla hajapata nafasi ya kuondoka. "utakufa hapo hapo"

hasira yake inapowaka kwa muda tu

Hasira ya mfalme inazungumziwa kama vile ni moto unaoweza kuwaka. "anapokasirika sana ghafla"

wanaotafuta usalama kwake

Kumuomba mfalme ulinzi inazungumziwa kama kutafuta usalama kwake. "wanaomuomba mfalme kuwalinda"

Psalms 3

Psalms 3:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Yahwe, maadui zangu ni wangapi!

Tamko hili linaonesha kuwa Daudi anawaogopa maadui wake. "O Yahwe, nina maadu wengi sana!"

wameinuka dhidi yangu

Kupigana na mtu inazungumziwa kama kuinuka dhidi yake. "wamekuja dhidi yangu"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 3:3

wewe, Yahwe, ni ngao yangu

Ngao humlinda askari. Daudi anazungumza kana kwamba Mungu ni ngao inayomlinda. "wewe, Yahwe, unanilinda kama ngao"

utukufu wangu

"wewe ni utukufu wangu." Kwa kumuita Mungu utukufu wake, Daudi anasema kuwa Mungu ndiye anayempa utukufu. Kwa kuwa Daudi amemaliza tu kuwazungumzia maadui zake na Mungu kuwa mlinzi wake, inawezekana alimaanisha kuwa Mungu anampa utukufu kwa kumpa ushindi juu ya maadui wake. "wewe ndiye unipaye utukufu" au "wewe ndiye unipaye ushindi"

unayenyanyua kichwa changu

"wewe ndiye unayenyanyua kichwa changu." Kumpa mtu ujasiri inazungumziwa kama kumnyanyua kichwa chake. "unayenitia moyo"

Nainua sauti yangu

Mtu kutumia sauti yake kulia inazungumziwa kama kuinua sauti yake.

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 3:5

waliojipanga dhidi yangu kila upande

"wamenizunguka kuniangamiza"

Psalms 3:7

Inuka

Daudi anazungumzia kuanza kufanya kitu kama kuinuka. "Chukua hatua" au "Fanya kitu"

utawapiga maadui wangu wote ... utavunja meno ya waovu

Vifungu hivi vinasema vitu vya kufanana sana. Misemo "maadui wangu" na "waovu" inamaanisha kundi moja la watu.

Kwa kuwa utawapiga maadui wangu kwenye taya

Hii ilikuwa ni njia ya kuwatukana watu. Daudi anazungumza kana kwamba Yahwe atakuja na kuwapiga kimwili adui zake. "Kwa kuwa utawafedhehesha adui zangu wote kama mtu anawapiga kwenye taya.

utavunja meno ya waovu

Wanyama huvamia kwa meno yao. Kuvunja meno yao inawaondolea nguvu ya kuvamia. Daudi anazungumza kana kwamba Yahwe atakuja na kupambana kimwili na waovu. "utawafanya waovu washindwe kunidhuru kama mtu kuvunja meno ya mnyama mkali"

Wokovu unatoka kwa Yahwe

Nomino dhahania ya "Wokovu" inaweza kuelezwa na kitenzi "okoa." "Yahwe anawaokoa watu wake"

Psalms 4

Psalms 4:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

kwenye vyombo vya nyuzi

"watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Nijibu ninapoita

"Nisaidie ninapoita"

Mungu wa haki yangu

"Mungu, unayeonesha kuwa ni mwenye haki"

nipe nafasi ninapozungukwa

Kuwa hatarini inazungumziwa kama kuwa katika nafasi finyu. "niokoe ninapokuwa hatarini"

Psalms 4:2

Taarifa ya Jumla:

Daudi anaimba sehemu hii ya wimbo kana kwamba anazungumza na adui zake.

Nyie watu, mtageuza heshima yangu kuwa aibu hadi lini?

Daudi anatumia swali hili kuwakemea adui zake. "Nyie watu mnaendela kugeuza heshima yangu kuwa aibu!"

mtageuza heshima yangu kuwa aibu

Kumwaibisha badala ya kumheshimu inazungumziwa kama kuifanya heshima yake kuwa aibu. "kuniaibisha badala ya kuniheshimu" au "kuniletea aibu badala ya kuniletea heshima"

Hadi lini mtapenda kile kisicho na dhamani na kutafuta uongo?

Daudi anatumia swali hli kuwakemea adui zake. "Mnaendela kupenda vitu visivyo na dhamani na kutafuta uongo."

mtapenda kile kisicho na dhamani ... kutafuta uongo

Misemo hii miwili inamaana ya kufanana. Uongo hauna dhamani. "mtapenda uongo usio na dhamani"

Yahwe anawatenga watauwa kwa ajili yake

"Yahwe anawachagua watauwa kwa ajili yake"

Psalms 4:4

Mtetemeke kwa hofu

Uhusiano kati ya "kutetemeka" na "hofu" na ni nani watu wanapaswa kumhofu unaweza kuelezwa vizuri. "Mche Yahwe sana hadi utetemeke" au "Simama kwa kumshangaa Yahwe"

Mtetemeke

"Mtikisike"

Tafakari moyoni mwako

Moyo unaashiria mawazo ya mtu. Kuwaza kwa umakini inazungumziwa kama kutafakari ndani ya moyo wa mtu. "Waza kwa umakini:

Toa sadaka za haki

"Toa sadaka zilizo sawa"

weka imani yako kwa Yahwe

Imani inazungumziwa kama vile ni kitu kinachoweza kuweka sehemu. "muamini Yahwe"

Psalms 4:6

Nani atatuonesha chochote kizuri?

Swali hili linatumika kwa mojawapo kati ya kuuliza kwa ajili ya kitu au kuonesha matamanio kuhusu jambo ambalo bado halijatokea. "Tafadhali tuonesha jambo zuri" au "Tunatamani mtu atuoneshe jambo zuri"

Nani atatuonesha chochote kizuri?

Kuonesha kitu kizuri inaweza kumaanisha kuleta vitu vizuri au kusema kwamba vitu vizuri vimetokea. "Nani ataleta vitu vizuri kwetu?" au "Nani atasema kwamba kitu chochote kizuri kimetokea?"

inua mwanga wa uso wako kwetu

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwatendea mazuri kana kwamba uso wa Yahwe ulimulika mwanga kwao. "kutenda mema kwetu"

Umeupa moyo wangu furaha zaidi

Moyo unaashiria mtu. "Umenipa furaha zaidi"

Umeupa moyo wangu furaha zaidi kuliko wengine walivyo

Furaha inazungumziwa kama kitu kinachoweza kupewa. "Umenifanya kuwa mwenye furaha zaidi kuliko wengine"

nafaka zao na divai yao mpya inapozidi

"Divai mpya" inaweza kumaanisha mizabibu. "wanapovuna mavuno mengi ya nafaka na mizabibu"

Ni kwa amani nitalala chini

Amani inazungumziwa kana kwamba ni sehemu. "Nitakuwa na amani ninapolala chini" au "Sitaogopa hatari ninapolala"

unanifanya salama

"unanifanya salama

Psalms 5

Psalms 5:1

Taarifa ya Jumla

Usambamba ni jambo la kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

na vyombo vya upepo

"Wimbo huu unapaswa kuandamana na watu wanaocheza vyombo vya upepo

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Sikia wito wangu kwako

Huu ni wito wa msaada. "Nisikie mimi ninapokuita sasa kwa ajili ya msaada"

sauti ya kulemewa

sauti ndogo watu wanazofanya wanapohangaika

asubuhi unasikia kulia kwangu ... asubuhi nitaleta dua yangu kwako

Vifungu hivi viwili vinamaana ya kufanana.

nitaleta dua yangu kwako

"Nitafanya ombi langu" au "Nitakuomba ninachohitaji"

kutazamia

"matumaini"

Psalms 5:4

Yahwe anawachuki watu wenye vurugu na waongo

Kwa kuwa Daudi anazungumza na Mungu katika zaburi hii, sentensi hii inaweza kuelezwa na neno "wewe." "Yahwe, wewe unawachukia watu wenye vurugu na waongo" au "Yahwe, wewe unachukia watu wanaofanya matendo ya vurugu na kuwadanganya wengine"

Psalms 5:7

nyumba yako

Hii inamaanisha hekalu la Mungu. "hekalu lako"

niongoze katika haki yako

Daudi anazungumzia haki kana kwamba ni njia na kufundisha kama kuongoza. Msemo "haki yako" unamaanisha kuwa Mungu ni mwenye haki. "nifundishe kufanya kilicho na haki kama wewe ufanyavyo"

nyosha njia yako mbele yangu

Daudi anazungumzia haki kana kwamba ni njia. Njia iliyonyoka ni rahisi kuona na kutemebelea. "nionesha vizuri jinsi ya kuisha njia sahihi" au "ifanye rahisi kwangu kufanya yaliyo sawa"

Psalms 5:9

Taarifa ya Jumla:

Daudi anawazungumzia adui zake

Kwa kuwa hakuna ukweli midomoni mwao

Ukweli kuwa midomoni mwao inamaanisha kuongea ukweli. "Kwa kuwa huwa hawasemi ya kweli"

utu wao wa ndani ni uovu

Utu wao wa ndani inamaanisha mawazo ya watu na tamaa zao. "mawazo yao na tamaa ni mbaya"

koo yao

Koo inaashiria maneno ya watu. "maneno yao" au "kile wanchosema"

koo yao ni kaburi lililo wazi

Koo yao inazungumziwa kana kwamba ni kaburi lililo wazi, tayari kwa ajili ya maiti kuwekwamo. Maana zinazowezekana ni 1) "wanasema watawaua watu" au 2) "Wanachosema huua watu"

wanijipendekeza na ulimi wao

"wanasema vitu vizuri kuhusu watu wengine bila kumaanisha"

ulimi wao

Ulimi unaashiria kile wanachosema watu.

njama zao ziwe anguko lao

"njama zao ziwasababishe kupitia maafa" au "wapunguze umuhimu wao kwa sababu ya njama zao"

njama

mipango ya kuwadhuru watu

anguko

Hili ni jambo linalowafanya watu kupitia maafa na kupoteza nguvu. Kupitia maafa au kupoteza umuhimu inazungumziwa kama kuangaku.

Psalms 5:11

wote wanaokukimbilia wafurahi

Mungu anazungumziwa kana kwamba ni kambi, sehemu ambayo watu wanaweza kulindwa. "Wote wanaokuja kwako kwa ulinzi wafurahi"

wote wanaokukimbilia wafurahi ... wapige kelele za shangwe kwa sababu unawalinda

Vishazi hivi viwili vina wazo la kufanana.

wanaokukimbilia

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi kunazungumziwa kama kumkimbilia yeye. "kwenda kwako kwa ulinzi"

wale wanaolipenda jina lako

Jina la Mungu linamwakilisha yeye. "wale wanaokupenda"

utawazunguka na fadhila kama ngao

Fadhila za Mungu zinazungumziwa kama ngao. "utawaonesha fadhila na kuwalinda kama askari wanavyojilina kwa ngao" au "kwa sababu u mkarimu kwao, utawalinda"

Psalms 6

Psalms 6:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

kwenye vyombo vya nyuzi

"watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu"

weka kwa mtindo wa Sheminithi

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

mifupa yangu inatetemeka

Mifupa inaashiria mwili wote. Mwili wake unaweza kuwa unatetemeka kwa sababu alikuwa mgonjwa au amechoka sana. "mwili wangu wote unatetemeka"

Psalms 6:3

imetaabika sana

"ogopa" au "wasiwasi"

hii itaendelea hadi lini?

Daudi anatumia swali hili kuonesha kuwa hataki kuendelea kujisikia mdhaifu na mwenye taabu. "tafadhali, usiruhusu hii iendelee!"

Rudi, Yahwe

Daudi anazungumzia Mungu kumtendea wema kama Mungu kurudi kwake. "Yahwe, rudi kwangu" au "Nione huruma, Yahwe"

Kwa kuwa katika kifo hakuna kumbukuku lako. Nani atakupa shukrani kuzimu?

Sentensi hizi mbili zina maana ya kufanana.

Kwa kuwa katika kifo hakuna kumbukuku lako.

Kumbukumbu inaashiria sifa. "Kwa kuwa watu wanapokufa, hawakusifu tena"

Nani atakupa shukrani kuzimu?

Daudi anatumia swali hili kusisitiza kuwa hakuna mtu anayetoa shukrani kwa Mungu toka kuzimu. "Hakuna mtu kuzimu atayekupa shukrani!" au "Wafu hawawezi kukusifu"

Psalms 6:6

Nimechoka na kulia kwangu kwa sauti ya kuelemewa

Kulia kwake kwa sauti ya kuelemewa inaonesha maumivu na mateso aliyoyasikia. "Nimechoka sana kwa sababu ya maumivu

ninaloanisha kitanda changu kwa machozi: ninaosha jilanza langu kwa machozi

Sentensi hizi zina maana moja.

ninaloanisha kitanda changu kwa machozi

"Ninafanya kitanda changu kilowe kwa machozi" au "Kitanda changu kimelowana kwa sababu ya machozi yangu"

ninaosha jilanza langu kwa machozi

"Nilifanya jilaza langu lilowane kwa machozi yangu"

macho yangu yanachoka

Uwezo wa kuona unazungumziwa kwa njia ya macho. "Kuona kwangu kumefifia" au "Siwezi kuona vizuri"

kutokana na huzuni

Huzuni hapa inamaanisha kulia. "kutokana na kulia" au "kwa sababu nalia sana"

Psalms 6:8

Yahwe amesikia ombi langu la huruma ... Yahwe amekubali ombi langu

Mistari hii miwili ina maana ya kufanana.

Yahwe amekubali ombi langu

Kuwa tayari kufanya ambacho Daudi ameomba inazungumziwa kama kukubali ombi lake. "Yahwe atajibu ombi langu"

Psalms 7

Psalms 7:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Utunzi wa kimuziki wa Daudi

"Huu ni wimbo ambao Daudi aliaandika"

kuhusu maneno ya Kushi Mbenyamini

Usemi "maneno ya Kushi" yanamaanisha alichosema. "kuhusu Kushi, mwanamme kutoka kabila la Benyamini alichosema"

wanaokimbia kwako

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi kunazungumziwa kama kumkimbilia. "kwenda kwako kwa ulinzi!"

watanirarua vipande vipande kama simba

Daudi anawazungumzia adui zake kumshambulia kana kwamba wanamrarua mwili wake na kumwacha vipande vipande kama simba afanyavyo. "wataniua kikatili kama simba anavyorarua mwili wa mawindo yake na kuugawa vipande vipande" au "wataniua kikatili"

bila kuwa na yeyote mwingine kuniletea mahali salama

"na hakuna mwingine atakayeweza kuniokoa"

Psalms 7:3

hakuna udhalimu mikononi mwangu

Mikono inaashiria jambo analofanya mtu. Kuwa na udhalimu juu yake inamaanisha kuwa amefanya kitu kisicho cha haki. "hakuna udhalimu ni kile nilichofanya" au "sijafanya chochote kisicho cha haki kwa yeyote"

Psalms 7:5

maisha yangu

Maisha yanaashiria mtu. "mimi"

kuyapita

"kufikia" au "kuipata." Hii inamaanisha kumshika. "kunikamata"

acha akanyage mwili wangu ulio hai ardhini

Hapa "mwili wangu ulio hai" unamaanisha mwandishi. "waruhusu adui zangu kuniangamiza"

nimelala bila heshima kwenye vumbi

Hii inamaana kulala akiwa amekufa na bila kuzikwa katika aibu.

Psalms 7:6

Inuka, Yahwe, katika hasira yako

Kuinuka inamaanisha kufanya jambo au kuchukua hatua. "Fanya jambo katika hasira yako" au "Wakasirikie adui zangu na uchukue hatua"

simama dhidi ya gadhabu ya adui zangu

Kupambana na watu kunazungumziwa kama kusimama dhidi yao. "pambana dhidi ya gadhabu ya adui zangu" au "shambulia adui zangu wenye gadhabu juu yangu"

gadhabu ya adui zangu

Gadhabu yao inaashiria mashambulizi yao. "mashambulizi ya adui zangu" au "adui zangu wanaonishambulia"

amka

Kuamka kunaashiria kuanza kufanya jambo au kuchukua hatua. "Chukua hatua" au "Fanya kitu"

kwa ajili yangu

"kunisaidia"

Mataifa yamekusanyika

Hapa neno "mataifa" linamaanisha majeshi yote yaliokusanyika kushambulia.

chukua tena nafasi yako unayostahili juu yao

Kutawala watu kunazungumziwa kama kuwa juu yao. Sehemu anayostahili Yahwe inamaanisha mojawapo kati ya mbinguni au kutawala kwa ujumla. "Tawala juu yao kutoka mbinguni" au "Tawala juu yao"

Psalms 7:8

nithibitishe

"waoneshe kuwa sina hatia"

imarisha watu wenye haki

"wafanye watu wenye haki kuwa imara" au "wafanye watu wenye haki wafanikiwe"

wewe unayechunguza mioyo na akili

Mioyo na akili zinaashiria tamaa na mawazo ya watu. "wewe unayejua mawazo yao ya ndani"

Psalms 7:10

Ngao yangu inatoka kwa Mungu

Neno "ngao" inamaanisha ulinzi wa Mungu.

Mungu anayeudhika kila siku

Ambaye Mungu anahasira naye inaweza kuelezwa vizuri. "Mungu aliye na hasira na waovu kila siku"

Psalms 7:12

Mungu atanoa upanga wake na kuandaa upinde wake kwa ajili ya mapambano

Katika mistari ya 12 na 13, Daudi anazungumzia juu ya Mungu kuamua kuwaadhibu waovu kana kwamba Mungu ni mpambanaji anayejianda kupigana dhidi yao kwa silaha. "Mungu atachukua hatua juu yao kama mpambanaji anaye noa upanga wake na kuanda upinde wake kwa ajili ya mapambano"

Psalms 7:14

yule ambaye yuko mimba na uovu ... anajifungua mipango haribifu ... anazaa uongo wenye madhara

Daudi anazungumzia vitu ambavyo mtu mwovu anafanya kama mtu mwenye mimba na uovu ndiye mtoto. "mtu mwovu. Anafanya mipango ya kuangamiza watu kusabisha uongo wenye

Mipango yake ya uharibifu yanarudia kichwa chake mwenyewe, kwa kuwa vurugu zake zinashuka chini ya kichwa chake

Uharibifu na vurugu zinazungumziwa kana kwamba zinagonga kichwa cha mtu au kumdondokea. "Mipango yake ya uharibifu inamuangamiza, kwa kuwa vurugu yake inamshambulia" au "Anapopanga kuangamiza wengine, wengine wanamuangamiza; anaposhambulia wengine, wengine wanamshambulia"

Psalms 8

Psalms 8:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika

weka kwa mtindo wa gittithi

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

jina lako lililovyo tukufu duniani kote

"Jina" la Mungu linaashiria asili yake yote. "watu duniani kote wanajua kuwa wewe ni mkuu sana"

Kutoka katika midomo ya watoto na wachanga umeumba sifa

Kusababisha watoto kumsifu Mungu kunazungumziwa kana kwamba sifa ni kitu kilichoumbwa ndani ya midomo ya watoto na kufanywa kutoka nje. "Umewapa watoto na wachanga uwezo wa kukusifu"

Psalms 8:3

mbingu zako, ambazo vidole vyako

Vidole vya Mungu vinaashiria ni yeye. "mbingu ulizoumba"

binadamu ana umuhimu gani hadi umtambue, au mtu hadi umwangalie?

Misemo hii inaelezwa kwa njia ya swali kuongeza msisitizo. "Ni ajabu kuwa unawawaza watu na kuwajali!"

binadamu ... mtu

Misemo hii yote inamaanisha watu kwa ujumla.

umewavika taji la utukufu na heshima

Utukufu na heshima zinazungumziwa kana kwamba ni mataji. Maneno "utukufu" na "heshima" yanakaribiana kwa maana. "umewapa utukufu na heshima" au "umewasababisha kuwa kama wafalme"

Psalms 8:6

Unamfanya kutawala juu ya kazi yako ... umeweka vitu vyote chini ya miguu yake

Vishazi hivi viwili vinaeleza maana ya kufanana.

Unamfanya ... chini ya miguu yake

Vishazi hivi viwili vinaeleza maana ya kufanana

kazi ya mikono yako

Mikono inaashiria yale Mungu aliyoyatenda. "vitu ulivyoumba"

umeweka vitu vyote chini ya miguu yake

Kuwa na mamlaka kutawala wengine na madaraka juu ya vitu inazungumziwa kama kuwa na hivyo vitu chini ya miguu yake. Hii inamaanisha Mungu aliwapa watu mamlaka juu ya uumbaji wote. "umempa mamlaka juu ya vitu vyote"

Psalms 8:9

Jina lako limetukuka duniani kote

Kwa mshangao huu, Daudi anaonesha furaha yake na heshima yenye uoga kuhusu Mungu alivyo mkuu. "jina lako limetukuka vizuri duniani kote" au "watu duniani kote wanajua ulivyotukuka"

jina lako

"Jina" la Mungu linamaanisha yeye au sifa yake. "sifa yako"

limetukuka

"zuri" au "kuu"

Psalms 9

Psalms 9:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka kwa mtindo wa Muthi Labeni

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Nitampa shukrani Yahwe kwa moyo wangu wote

Kwa sababu wimbo huu ameandikiwa Yahwe, Yahwe anaweza kupelekea kumita "wewe." "Yahwe, nitakupa wewe shukrani kwa moyo wangu wote"

matendo yako ya ajabu

Nomino "matendo" inaweza kuelezwa na kitenzi "kufanya." "matendo yote ya ajabu unayofanya" au "matendo yote ya ajabu uliyofanya"

Nitaimbia sifa jina lako

Hapa jina la Mungu linamaanisha ni Mungu. "Nitakuimbia sifa"

Psalms 9:3

geuka

"kurudi" au "kukimbia kwa uoga"

umeketi kwenye kiti cha enzi, hakimu mwenye haki

Wafalme walikuwa na mamlaka ya kuhukumu watu, na waliketi katika kiti cha enzi walipokuwa wakihukumu. Daudi anazungumza kana kwamba Mungu alikuwa mfalme wa kidunia. "unahukumu kama mfalme anayeketi katika kiti chake cha enzi, na u mwenye haki"

Psalms 9:5

umelifuta jina lao milele na milele

Kusababisha watu kusahaulika inazungumziwa kama kufuta jina lake. "umesababisha wasahaulike kana kwamba umefuta majina yao" au "hakuna atakaye wakumbuka tena daima"

umelifuta

"umeondoa"

Adui alivunjika kama uharibifu

Adui anazungumziwa kana kwamba alikuwa mji uliojaa majinge yaliyovunjika. "Adui zetu waliangamizwa"

ulipopindua miji yao

"Ulipoangamiza miji yao"

Kumbukumbu yao yote imepotea

Kumbukumbu inazungumziwa kana kwamba kilikuwa kiumbe hai kinachoweza kufa. "Kumbukumbu yao imesimama" au "Hakuna tena kumbukumbu yao"

Kumbukumbu yao yote imepotea

Kumbukumbu inaweza kuelezwa na kitenzi "kumbuka." "Hakuna mtu anaye wakumbuka kabisa"

Psalms 9:7

Yahwe anabaki milele

"Kubaki" inaweza kuashiria kuketi kwenye kiti cha enzi kama mfalme. "Yahwe anaketi kwenye kiti chake cha enzi milele" au "Yahwe anatawala milele"

ameweka kiti chake cha enzi kwa jili ya haki

Msemo "kiti chake cha enzi" unaashiria utawala wa Mungu. Maana zinazowezekana ni 1) "Anatawala ili ahukumu watu" au "Anatawala juu ya watu kwa haki"

Atahukumu ulimwengu kwa haki ... atatekeleza hukumu kwa ajili ya mataifa kwa kutopendelea.

Vishazi hivi viwili vinaeleza kitu kimoja.

Atahukumu ulimwengu kwa haki

Hapa "ulimwengu" unamaanisha watu wote duniani. "Atahukumu watu wote duniani kwa haki"

Psalms 9:9

Yahwe pia atakuwa ngome kwa wanaokandamizwa

Mungu anazungumziwa kana kwamba alikuwa ni sehemu ambapo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya usalama. "Yahwe pia atawalinda wanaokandamizwa" au "Yahwe atawapa usalama wale wanaokandamizwa"

ngome

"pa kukimbila" au "kivuli"

Wale wanaolijua jina lako

Hapa maneno "jina lako" yanamaanisha Mungu. "Wale wanaokujua"

usiwatelekeze

"usiwaache"

Psalms 9:11

anaye tawala Sayuni

"anayeishi Yerusalemu"

waambie mataifa

Hapa "mataifa" yamaanisha watu wote.

Kwa kuwa Mungu anayelipiza kisasi cha damu iliyo mwagika hukumbuka

Kile anachokumbuka kinaweza kuwekwa wazi. "Kwa kuwa Mungu anaye lipiza kisasi umwagaji damu anawakumbuka wale waliouliwa" au "Kwa kuwa Mungu hukumbuka anawakumbuka wale waliouliwa na kuwaadhibu wauwaji"

hasahau kilio chao

"Anajali kilio chao"

Psalms 9:13

tazama jinsi ninavyokandamizwa na wale wanaonichukia

Hii inawezwa kuelezwa katika hali ya kutenda. "tazama wale wanaonichukia wanavyonikandamiza" au "tazama jinsi adui zangu wanavyonitendea vibaya"

wewe unayeweza kuniokoa kutoka malango ya mauti

Mauti inazungumziwa kana kwamba ni mji ulio na malango ambayo watu huingia. Kama mtu yuko karibu na malango ya mauti, inamaanisha kuwa atakufa punde. Kumzuia mtu kutokufa inazungumziwa kama kumwondoa kwenye malango ya mji. "wewe unayeweza kuniokoa na mauti" au "wewe unayeweza kuzuia nisife"

Psalms 9:15

Mataifa yamezama chini kwenye shimo walilotengeneza

Watu huchimba mashimo ili kukamata wanyama wanaoanguka humo. Hapa kuchimba shimo inaashiria kufanya mipango ya kuangamiza watu. "Mataifa ni kama watu wanaochimba mashimo kwa ajili ya wengine na kisha kuanguka humo"

miguu yao imenaswa kwenye wavu walioficha

Watu huficha nyavu ili kukamata wanyama wanaonaswa humo. Hapa kuficha wavu inaashiria kufanya mipango ya kuangamiza watu. "ni kama watu wanaoficha wavu na kunaswa humo"

ametegwa

"kunaswa" au "kushikwa." Hii inamaanisha kuangamizwa. "kuangamizwa"

Psalms 9:17

wanageuzwa

"wanakataliwa"

hatima ya mataifa yote yanayomsahau Mungu

"pale ambapo mataifa yote yanayomsahau Mungu yatakapokuwa"

Kwa kuwa wahitaji hawatasahauliwa daima

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu hatawasahau wahitaji daima" au "Mungu atawakumbuka wahitaji"

wala matumaina ya waliokandamizwa kufutwa

Matumaini yanazungumziwa kana kwamba ni vitu vinavyoweza kuvunjika au kuharibika. Matumaini kuangamizwa inaashiria mambo ambayo watu wanatumaini kutokutokea. "na wanaokandamizwa hawatatumaini milele bila kuona matokeo" au "na siku moja kile wanaokandamizwa wanachotumaini kitatokea"

Psalms 9:19

Inuka

Kuinuka kunaashiria kuanza kufanya kitu. "Fanya kitu" au "Chukua hatua"

mwanadamu

"watu"

yahukumiwe

Hapa kuhukumu kunaashiria kuadhibu. "yaadhibiwe"

machoni pako

Hapa machoni inamaanisha uwepo. "katika uwepo wako"

mataifa yahukumiwe machoni pako

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hukumu mataifa katika uwepo wako" au "yapeleke mataifa katika uwepo wako na uyaadhibu"

Psalms 10

Psalms 10:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa nini, Yahwe, unasimama mbali? Kwa nini unajificha nyakati za taabu?

Mwandishi anatumia maswali haya kuonesha huzuni yake kuwa Mungu hajamsaidia. "Yahwe, inaonekana kana kwamba uko mbali na mimi na unajificha kwangu kila ninapokuwa kwenye

njama

"mipango"

mtu mwovu

Hii inamaanisha watu waovu kwa ujumla. "watu waovu"

tamaa yake ya nafsi

Nomino "tamaa" inaweza kuelezwa na kitenzi "kutaka." "vitu anavyotaka sana kufanya"

walafi

"watu wenye tamaa"

Psalms 10:4

Mtu mwovu

Hii inamaanisha watu waovu kwa ujumla. "watu waovu"

ana uso ulioinuka

Uso ulioinuka inaashiria kiburi. "Ana tabia ya kiburi" au "ana kiburi"

hamtafuti Mungu

Kumtafuta Mungu inamaanisha kati ya 1) kumwomba Mungu msaada au 2) kumwaza Mungu na kumtii. "hamwombi Mungu msaada" au "hamwazi Mungu"

Yuko salama muda wote

Hayuko salama kweli ila anadhani yuko salama.

amri zako za haki ziko juu sana kwake

Jambo lililogumu kuelewa linazungumziwa kana kwamba liko juu sana kufikia. "hawezi kuelewa amri zako za haki"

anawakoromea adui zake

Watu hukoromea adui zao wanapodhani kuwa adui zao ni wanyonge na hawana faida. "anafikiri kuwa adui zake wote ni wanyonge na wasio na faida" au "anawakoromea adui zake wote"

anawakoromea

Hii inamaanisha kuwa anapuliza hewa kwa sauti kutoka puani mwake.

Psalms 10:6

Anasema

"Mtu mwovu anasema"

katika vizazi vyote

Hii inaweza kumaanisha "milele."

sitakutana na taabu

Kupitia taabu inazungumziwa kama kukutana nayo. "Sitakuwa na shida zozote"

Mdomo wake umejaa laana na maneno ya uongo na ya kudhuru

Kile watu wanachosema kinazungumziwa kama kuwa mdomoni mwao. "huwa anawalaani watu na kusema vitu ambavyo ni vya uongo na vya kudhuru" au "Huwa analaani watu, kusema uongo, na kutishia kuwadhuru watu"

ulimi wake huumiza na kuangamiza

Hapa ulimi unaashiria kuongea. au "kile anachokisema kinaumiza na kuangamiza watu" au "anazungumza maneno yanayowatisha na kuumiza watu"

Psalms 10:8

Anasubiri tayari kwa kuvamia

Anayesubiri ni mtu mwovu

macho yake hutafuta mhanga asiyejiweza

Macho yamamwakilisha yeye. "anatafuta mhanga asiyejiweza"

Hujificha sehemu ya siri kama simba kwenye kichaka

Hii inamzungumzia mtu mwovu kana kwamba ni simba. "Anajificha wakati akisubiri wangyonge wapite karibu yake, kama simba anavyosubiri kwa utulivu katika kichaka kwa ajili ya mnyama anayetaka kushambulia"

Hujificha

Kujificha na kusudi la kudhuru au kuua.

hulala na kusubiri

"hulala chini akisubiri" au "anajificha na kusubiri"

Anashika waliokandamizwa anapovuta wavy wake

Mwandishi anazungumzia mtu mwovu kuwashika watu kana kwamba ni mwindaji anatumia wavu kushika wanyama. "Anawashika walio kandamizwa kama mwindaji anayomshika mnywama kwenye wavu na kumvuta.

wanaanguka kwenye nyavu zake imara

Mwandishi anaendelea kumzungumzia mtu mwovu kuwashika watu kana kwamba ni mwindaji, mipango yake ni nyavu, na watu ni wanyama wanaoangukia kwenye wavu. "wahanga wake wanakamatwa na mipango yake kama wanyama wanaoanguka kwenye wavu imara wa mwindaji"

Psalms 10:11

Asema

Anayesema ni mtu mwovu na watu waovu kwa ujumla.

Mungu amesahau

Kukataa kuzingatia kile ambacho watu wanafanya inazungumziwa kama kusahau. "Mungu hazingati" au "Mungu hajali kuhusu kile nachofanya"

anafunika uso wake

Kukataa kuzingatia kitu ambacho mtu anafanya kama kufunika uso wa mtu. "Mungu anakataa kuona kinachotokea"

hatahangaika kutazama

Kuzingatia kile ambacho mtu anafanya inazungumziwa kama kukiangalia. "hatahangaika kuzingatia" au "hatajali"

Inuka

Kuanza kufanya kitu inazungumziwa kama kuinuka. "Fanya kitu"

Inua mkono wako

Hapa kuinua mkono kumpiga mtu inaashiria kumwadhibu. "kumpiga kwa nguvu" au "kumwadhibu mtu mwovu"

Psalms 10:13

Kwa nini mtu mwovu anamkataa Mungu na kusema ... "Hutaniwajibisha"?

Mwandishi anatumia swali hili kuonesha kuwa anachosema ni cha kusikitisha sana kuwa watu waovu wanafanya vitu hivi. "Watu waovu humktaa Mungu kila wakati na kusema .. 'Hautaniwajisbisha.'"

Hutaniwajibisha

"Hutaniomba kukueleza kwa nini ninafanya ninachokifanya." Kumwajibisha mtu hapa inaashiria kumwadhibu. "Hautaniadhibu"

Psalms 10:15

Kuvunja mkono wa mwovu na mtu mbaya

Hapa "mkono" unaashiria nguvu. "Kuangamiza nguvu ya mwovu na mtu mbaya" au "Kumfanya mtu mwovu na mbaya kuwa mnyonge"

mwovu na mtu mbaya

Maneno haya yana maana sawa.

Kumfanya awajibike kwa matendo yake maovu

Kumfanya mtu awajibike kwa matendo yake maovu inaashiria kumwadhibu. "Muadhibu kwa mambo maovu aliyotenda"

mataifa yanatolewa kwenye nchi yake

"Yahwe anawalazimisha watu wa mataifa kuondoka nchini kwake"

Psalms 10:17

umesikia mahitaji ya wanao kandamizwa

Inaonesha kuwa watu wanao kandamizwa walilia kwa Mungu. "watu wanao kandamizwa wakilia kwako, uliwasikiliza wakikuambia walichohitaji"

unautia nguvu moyo wao

Moyo imara inaashiria ujasiri, na kufanya mioyo ya watu kuwa imara inaashiria kuwatia moyo. "unawatia moyo" au "unawafanya kujiamini"

hakuna mtu ... atakaye sababisha hofu tena

"hakuna mtu ... atakaye sababisha watu kuogopa tena"

Psalms 11

Psalms 11:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

ninamkimbilia Yahwe

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi kunazungumziwa kama kumkimbilia. "kwenda kwa Yahwe kwa ulinzi"

utasemaje kwangu, "Kimbia kama ndege milimani?"

Swali hili linaulizwa kutoa msisitizo. Linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Kwa hiyo usiniambie kukimbia!"

Maana tazama! Waovu wanaanda upinde wao. Wanafanya tayari mishale yao kwenye nyuzi kupiga gizani kwa wanyofu moyoni.

"Tazama! waovu wanajiandaa kuvamia watu wanyofu"

wanyofu moyoni

Hapa "wanyofu moyoni" inamaanisha watu wanaomcha Mungu au wenye haki.

Psalms 11:3

Maana misingi imeharibika, mwenye haki atafanya nini?

Hapa "misingi" inaweza kumaanisha sheria na utaratibu. Swali hili la balagha linaulizwa kuongeza msisitizo. Linaweza kutafsiririwa kama kauli. "Watu wenye haki hawawezi kufanya lolote pale watu waovu wasipoadhibiwa wanapokeuka sheria!"

Macho yake yanatazama, macho yake yanachunguza watoto wa binadamu

Yahwe anajua kila kitu kinachotokea. "Anachunguza yote wanayofanya wanadamu"

watoto wa binadamu

"wanadamu"

Psalms 11:5

anachunguza

"kuangalia kwa umakini"

wanaofanya fujo

"kuumiza wengine"

Anawanyeshea moto wa makaa na kibiriti juu ya waovu; upepo unaochoma utakua sehemu yao kutoka kwenye kikombe chake!

Adhabu ya Mungu inaelezwa kana kwamba yalikuwa makaa ya moto na kibiriti kutoka kwenye volkano. "Anawaadhibu waovu; hakutakuwa na nafuu kwao!"

kibiriti

Hili ni jina lingine la salfa

wataona uso wake

"kuwa kwenye uwepo wake"

Psalms 12

Psalms 12:1

Taarifa ya Jumla:

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka kwa mtindo wa Sheminithi

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Nisaidie, Yahwe

"Yahwe, njoo unisaidie"

waaminifu wamepotea

"watu waaminifu wamepotea wote"

Psalms 12:2

Kila mmjoa anasema ... kila mmoja anazungumza

Kurudiwa mara mbili kwa "kila mmoja" ni kukuza maneno, yanatumika kusisitiza kuwa tatizo lilikuwa kubwa.

midomo ya

"sifa ya uongo"

moyo mara mbili

"maneno yanayopotosha"

kata midomo yote ya kujipendekeza

"wazuie kuzungumza sifa za uongo"

kila ulimi unaotangaza mambo makuu

Hapa "ulimi" unaashiria maneno ya kujidai. "kila mtu anayejidai"

Kwa ndimi zetu tutashinda

Hapa maneno "ndimi zetu" yanamaanisha maneno mengi wanayoyazungumza. "Kuzungumza maneno mengi kutatufanya washindi"

tutashinda

"tutafanikiwa"

nani anaweza kuwa mkuu juu yetu?

Hili swali la balagha linaulizwa kusisitiza kuwa waliamini kuwa hakuna anayeweza kuwatala. Inaweza kutafsiriwa kama kauli. "hakuna anayeweza kutawala juu yetu!"

Psalms 12:5

mgumio

Hizi ni sauti nzito ambazo watu hufanya kwa sababu ya maumivu au hisia kali

nitainuka," asema Yahwe

Hii inamaanisha Yahwe atatenda kitu kuwasaidia watu.

Psalms 12:6

kama shaba iliyosafishwa kwenye tanuu duniani, kusafishwa mara saba

Maneno ya Yahwe yanalinganizhwa na shaba iliyosafishwa. "wako bila kasoro"

Unawatunza

"Unawatunza watu wenye haki"

wanatembea kila upande

"wametuzunguka"

wakati uovu unapotukuzwa miongoni mwa watoto wa wanadamu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wakati watu kila sehemu wanasifu uovu"

watoto wa wanadamu

"binadamu" au "watu"

Psalms 13

Psalms 13:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Hadi lini, Yahwe, utakuwa ukinisahau?

Swali hili linaulizwa kushika ufahamu wa msomaji na kuongeza msisitizo. Linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Yahwe, inaonekana kuwa umenisahau!

Hadi lini ... uso wako kwangu?

Maneno "uso wako" yanaashiria Mungu kamili. Swali hili balagha linaulizwa kuongeza msisitizo. Linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Inaonekana unajificha kwangu!"

Hadi lini adui yangu atashinda juu yangu?

Swali hili la balagha linaulizwa kuongeza msisitizo. Linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hakika adui zangu hawatanishinda daima!"

Psalms 13:3

Nitazame na unijibu

"Nizingatie na unisikilize"

Nipe mwanga machoni mwangu

Hii ni njia ya kuomba nguvu. "Nifanye kuwa na nguvu tena"

au nitalala kifoni

"Kulala kifoni" inamaanisha kufa.

Usimruhusu adui yangu aseme ... ili adui yangu asiseme

"Usimruhusu adui yangu aseme kunihusu ... ili adui yangu asiseme kunihusu"

ninapoletwa chini

"ninapoanguka" au "wanaponishinda"

Psalms 13:5

Nimetumaini katika uaminifu wako wa agano

Kwa kuzungumzia uaminifu wa Yahwe wa agano, Daudi anatumaini kuwa Yahwe atampenda daima. "Nina imani kuwa utanipenda kwa uaminifu"

moyo wangu unafuahi ndani ya wokovu wako

Hapa "moyo wangu" unaashiria mtu mzima. "Nitafurahi kwa sababu umeniokoa"

Psalms 14

Psalms 14:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Mpumbavu husema moyoni mwake

Hii ni lahaja inayomaanisha kuzungumza mwenyewe au kujiwazia mwenyewe. "Mtu mpumbavu anajiambia"

Wameharibika

walioharibika inaashiria binadamu wapumbavu wanaosema hakuna Mungu.

Psalms 14:2

watoto wa wanadamu

Msemo huu unamaanisha wanadamu wote.

wanaonitafuta

Hii inafafanua wote wanaotamani kumjua Mungu kana kwamba walikuwa wanamfuata kabisa kwenye njia. "wanaotamani kumjua"

Wote wamegeuka

Hii inaelezea watu waliomkataa Mungu kana kwamba waliacha kutembea kwenye njia sahihi na wameenda upande mwingine. "Wote wamemgeuka Yahwe"

Psalms 14:4

Kwani hawajui chochote ... ambao hawamwiti Yahwe?

Swali hili la balagha linaulizwa kuongeza msisitizo. Linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Wanatenda kana kwamba hawajui chochote ... wasiomwita Yahwe. Lakini wanajua wanachokifanya!"

wale wanaotenda udhalimu

Hapa "udhalimu" unamaanisha matendo maovu. "wale wwnye tabia mbovu.

wale wanaowala watu wangu

Hii inamaanisha wale wanaofanya vitu viovu na wanawaangamiza watu wa Mungu kana kwamba wanakula chakula.

Psalms 14:5

Wanatemeka

Wanaotetemeke ni wale wanaotenda maovu.

Mungu yuko pamoja na mkusanyiko wa wenye haki

Kusema kuwa "Mungu yuko pamoja" na mkusanyiko wa wenye haki inamaanisha kuwa atawasaidia. HIi inaweza kuwekwa wazi. "Mungu huwasaidia wale wanaotenda haki" au "Mungu anawasaidia wale wanaotenda yaliyo sawa"

Mnataka

Wanaotaka ni watu waovu.

kumwaibishi mtu maskini

"kumfanya mtu aliye maskini kuona aibu"

Yahwe ni kimbilio lake

Hii inazungumzia ulinzi ambao Yahwe anatoa kana kwamba ulikuwa kivuli ambacho mtu atatufuta wakati wa dhoruba. "Yahwe ni kama kivuli cha ulinzi kwake"

Psalms 14:7

O, wokovu wa Israeli utatoka Sayuni

Mwandishi anasema kuwa anatamani Mungu aje kutoka Yerusalemu kuisaidia Israeli. "Ninatamani kwamba Yahwe aje kutoka Yerusalemu na kuwasaidia watu wake!"

kisha Yakobo atashangilia na Israeli kufurahi

Misemo hii miwili ina maana moja. Hapa "Yakobo na"Israeli" inawakilisha watu wa Israeli. "kisha watu wote wa Israeli watafurahi sana"

Psalms 15

Psalms 15:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Nani aishi kwenye kilima chako kitakatifu?

"Kilima kitakatifu" hapa kinaashiria hekalu la Mungu, ambalo lilikuwa kwenye mlima Sayuni. "Nani aishi kwenye sehemu yako takatifu?"

anazungumza ukweli kutoka moyoni mwake

"anazungumza ukweli"

Psalms 15:3

Hakashifu

Hii inaashiria mtu mwenye haki katika 15:1.

Hakashifu kwa ulimi wake

Hapa "ulimi" unaashiria maneno maovu. "Hasemi mambo maovu kuhusu watu wasio na hatia"

Hadhuru

"kuumiza" au "kuharibu"

Psalms 15:4

Mtu asiyefaa ni chukizo machoni pake, lakini anawaheshimu wale wanaomcha Yahwe

"Watu wenye haki wanachukia wale waliomkataa Mungu, lakini wanawaheshimu wale wanaomheshimu Mungu"

Mtu asiyefaa

"Mtu mwovu" au"Mtu aliyemkataa Yahwe"

hatatikisika

Hapa "kutikisika" kunaashiria kutokuishi kwa usalama tena. Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "wataishi katia usalama"

Psalms 16

Psalms 16:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Hii inaweza kuandikwa kama: "Hii ni zaburi ambayo Daudi aliandika."

kukimbilia wewe

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia yeye. "kwenda kwako kwa jili ya ulinzi"

watu watakatifu waliomo duniani

Hapa "watu watakatifu" inaashiria watu wa Mungu wanaomuamini. "watu wako wanaoishi katika nchi hii"

Psalms 16:4

Taabu zao zita... miungu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Taabu za wale wanaotafuta miungu mingine zitaongezeka"

sitamwaga ... damu kwa miungu wao

"kutoa sadaka kwa miungu yao"

kuinua majina yao na midomo yangu

Kuinua "majina yao na midomo yangu" inamaanisha kusifu miungu mingine au kuomba kwao.

Psalms 16:5

sehemu yangu niliyochagua

Hapa Daudi anamzungumzia Yahwe kana kwamba alikuwa ni sehemu ya nchi ambayo alipewa.

kikombe changu

Hapa Daudi anamzungumzia Yahwe kana kwamba alikuwa ni kikombe chenye baraka nyingi. "ambaye hunibariki"

Unashikilia hatima yangu

"Unaamua siku zangu za usoni"

Kamba za kupima ... katika sehemu nzuri

Baraka za Mungu kwa Daudi zinazungumziwa kana kwamba ni sehemu ya nchi iliyochunguzwa kwa jili yake kumiliki. "Kamba za kupima" zinaashiria kamba za mchunguzi wa ardhi. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Sehemu uliyonipa inapendeza"

hakika urithi wa kupendeza ni wangu

Hapa Daudi anazungumzia baraka za Yahwe kana kwamba zilikuwa ni urithi ambao alipokea. "Nimefurahi kwa vitu vyote alivyonipa"

Psalms 16:7

Nimemuweka Yahwe mbele yangu muda wote

"Daima nakumbuka kuwa Yahwe yuko pamoja na mimi"

ili nisitikiswe kutoka mkono wake wa kuume

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna kitu kitakachonitoa upande wake"

Psalms 16:9

Taarifa ya Jumla:

Daudi anaendelea kuzungumza na Mungu.

Kwa hiyo moyo wangu una furaha; utukufu wangu unashangilia

Msemaji anasema kwamba kuweza kumsifu Mungu kunamletea yeye heshima. Vishazi hivi viwili vinaeleza vitu vya kufanana. "Kwa hiyo nina furaha, nina heshima kumsifu"

moyo wangu

Hapa "moyo" unaashiria mawazo na hisia za msemaji.

utukufu wangu

Matoleo mengi yanatafsiri "utukufu wangu" kumaanisha moyo wa mwandishi, anayekuwa na heshima kushangilia kwa sababu ya Mungu.

Psalms 16:11

tele

"kubwa" au "kiasi kikubwa cha"

furaha ... inakaa katika uwepo wako

Mwandishi anazungumzia "furaha" kana kwamba ni mtu.

katika mkono wako wa kuume

Maneno "mkono wako wa kuume" yanaonesha kuwa katika uwepo maalum wa Mungu. "Ninapokuwa karibu na wewe"

Psalms 17

Psalms 17:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Ombi la Daudi

"Hili ni ombi ambalo Daudi aliaandika."

Nipe sikio ombi langu kutoka midomo isiyo na uongo

Msemo "nipe sikio" unamaanisha kusikiliza, na neno "midomo" inaashiria maneno ambayo mtu huongea. "Sikiliza ombi langu ambalo halitoki katika midomo ya uongo"

Acha uthibitisho wangu uje kutoka katika uwepo wako

Hapa "uwepo" inaashiria Yahwe. "Nitamke kuwa sina hatia"

acha macho yako yaone kilicho sawa!

Hapa "macho yako" inaashiria kile ambacho Yahwe anajua kuwa kweli. "unajua kuwa ninakuambia ukweli!"

Psalms 17:3

Ukiujaribu moyo wangu, ukija kwangu usiku

Hapa " ukiujaribu moyo wangu" inamaansiha kupima mawazo na nia. "ukipima mawazo yangu usiku"

mdomo wangu hutatenda dhambi

Hapa mdomo unazungumziwa kana kwamba unaweza kutenda wenyewe. Pia inawakilisha maneno ambayo mtu huzungumza. "Sitasema uongo au kutenda dhambi kwa maneo yangu

Psalms 17:4

ni kwa neno la midomo yako nimetunza kutoka katika njia za wahalifu

Hapa "neno la midomo yako" inamaanisha maelekezo ya Mungu. "maelekezo yako yamenisabisha kuepuka kufanya mambo maovu"

Hatua zangu zimeshikilia kwa nguvu kwenye njia zako; miguu yangu yaijateleza

Vishazi hivi viwili vinamaanisha kitu kimoja. Kurudia kunaongeza msisitizo.

miguu yangu yaijateleza

Mwandishi anazungumzia kumtii Mungu kana kwamba anatembea katika mjia. "nimedhamiria kufuata njia zako"

Psalms 17:6

geuza sikio lako kwangu ... sikiliza ninapozungumza

Misemo hii miwili ina maana sawa. Hapa "sikio lako" linamaanisha utayari wa Mungu kumsikiliza mtu anayemuomba. "nizingatie ... nisikilize ninapozungumza"

mkono wako wa kuume

"Mkono wa kuume" unaashiria nguvu ya Mungu. "uwezo wako mkuu"

kukimbilia

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. "kwenda kwako kwa ajili ya ulinzi"

Psalms 17:8

Nilinde kama mboni la jicho lako

"mboni la jicho lako" inaashiria kitu kilicho na thamani. "Nilinde kama utakavyolinda kitu cha thamani sana"

nifiche chini ya kivuli cha mbawa zako

Daudi anazungumzia ulinzi wa Mungu kana kwamba alikuwa ni ndege anayelinda watoto wake chini ya mbawa zake. "Niweke salama kama ndege anavyolinda makinda yake chini ya mbawa zake"

midomo yao inazungumza kwa majivuno

Hapa "midomo yao inazungumza" inamaanisha kile ambacho watu wanasema. "huwa wanajidai"

Psalms 17:11

Wamezunguka hatua zangu

Hapa "wamezunguka hatua zangu" inaashiria jinsi adui wa Daudi walivyomfuata kila mahali ili kumkamata. "Adui zangu wamenizunguka"

kama simba mwenye hamu kwa ajili ya mhanga, kama simba mchanga aliyejikunyata katika maficho

Misemo hii miwili inaonesha mawazo ya kufanana. Kurudia kunaongeza mkazo.

Wao ni kama simba ... kama simba mchanga

Mwandishi inahisi kufuatiliwa kama simba anavyowinda windo lake.

Psalms 17:13

Okoa maisha yangu kutoka kwa mwovu kwa upanga wako ... Niokoe kutoka kwa watu kwa mkono wako, Yahwe, kutoka kwa wanaume wa dunia hii

Vishazi hivi viwili vina maana ya kufanana. Kurudiwa kunaongeza mkazo wa maneno ya mwandishi.

kwa upanga wako ... kwa mkono wako

Hapa "upanga" na "mkono" yote inaashiria nguvu ya Yahwe.

Utajaza matumbo ya hazina yako na utajiri

Maandiko ya zamani yanapotosha. Maana zinazowezekana ni 1) Yahwe atatoa baraka nyingi kwa watu wake. "Utawabariki watu wako sana" au 2) Yahwe atawaadhibu kwa nguvu watu waovu hadi watoto na wajukuu wao.

Psalms 17:15

Nitauona uso wako katika haki

Hapa "uso" unamwakilisha Yahwe. Daudi anaujasiri kuwa atamuona Yahwe. "kwa sababu ninatenda yaliyo sawa, nitakuwa na wewe siku moja"

Nitaridhika nitakapoamka, na kukutazama wewe

Daudi anaamini kuwa baada ya kufa, atakuwa na Yahwe. Hii naweza kuweka wazi. "Baada ya kufa, nitafurahi kuamka katika uwepo wako"

Psalms 18

Psalms 18:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

akamwimbia Yahwe maneno ya wimbo huu

"aliimba wimbo huu kwa Yahwe"

katika siku ambayo Yahwe aliniokoa

"baada ya Yahwe kumwokoa"

kutoka katika mkono wa Sauli

Hapa "mkono" unamaanisha nguvu ya Sauli. "kutoka katika nguvu ya Sauli"

Psalms 18:2

Yahwe ni mwamba wangu

Daudi anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni mwamba. Neno "mwamba" ni picha ya sehemu salama.

mwamba wangu, boma langu

Hapa maneno "mwamba" na "boma" zinamaana ya kufanana na zinasisitiza kuwa Yahwe anatoa usalama kutoka kwa adui.

mkimbilia

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi kunazungumziwa kama kumkimbilia. "kwenda kwake kwa ajili ya ulinzi"

ngao yangu, pembe la wokovu wangu, na ngome yangu

Daudi anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni "ngao," "pembe" la wokovu, na "ngome" yake. Yahwe ndiye anayemlinda na mabaya. Hapa wazo la kufanana linarudiwa kwa njia tatu kwa ajili ya mkazo.

Nitaokolewa kutoka kwa adui zangu

"Nitaokolewa kutoka kwa adui zangu"

Psalms 18:4

Kamba za mauti zinanizunguka

Daudi anazungumzia kifo kana kwamba ni mtu anayeweza kukamata na kumfunga kwa kamba. "Nilikuwa nataka kuuwawa"

maji yanayokimbia ya yasiyofaa

Daudi ni mnyonge kana kwamba anabebwa na mafuriko ya maji yanayokimbia. "Nilihisi kuwa mnyonge kabisa"

Kamba za kuzimu zinanizunguka; mitego ya mauti imeninasa

Hapa "kuzimu," sehemu ya wafu, na "mauti" zinazungumziwa kana kwamba ni watu wanaoweza kumzunguka na kumtega. Vishazi hivi viwili vina maana ya kufanana na wazo linarudiwa kwa ajili ya mkazo. "Nilihisi kubanwa na nikadhani ninaenda kufa"

Psalms 18:6

Katika huzuni yangu

"katika hitaji langu kubwa" au "katika kukata tamaa kwangu"

kilio changu kikaenda katika uwepo wake

Hapa Daudi anazungumzia "kilio" chake kana kwamba ni mtu anayeweza kuja katika uwepo wa Yahwe. "Nikamuomba"

kikaenda katika maskio yake

Hapa Daudi anazungumzia jinsi Yahwe alivyosikia kilio chake cha msaada. Wazo linarudiwa kwa ajili ya mkazo. "akasikia maombi yangu"

Psalms 18:7

Kisha ulimwengu ... ikatikiswa kwa sababu Mungu alikuwa na hasira

Mungu kuwa na hasira inazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni tetemeko baya. "Mungu alikuwa na hasira sana hadi ikawa kama dunia ... ikatikisika"

ulimwengu ukatikisika na kutetemeka

Maneno "kutikisika" na "kutetemeka" yana maana sawa na yanasisitiza jinsi dunia ilivyotikisika. "nchi ikasogea huku na kule" au "ardhi ikasogea juu na chini" au "kulikuwa na tetemeko kali"

misingi ya milima pia ikatetemeka na kutikiswa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "misingi ya milima pia ikatetemeka na kutikisika"

Moshi ukatoka kwenye tundu zake za pua ... Makaa ikawashwa nao

Daudi anamzungumzia Yahwe kana kwamba alikuwa akipumua moto. Hii ni picha ya jinsi Mungu alivyokasirika.

moto ukatoka mdomoni mwake. Makaa ikawashwa nao.

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "moto ukatoka katika mdomo wake na kuwasha makaa"

Psalms 18:9

Akafungua

Aliyefungua ni Yahwe.

giza nene lilikuwa chini ya miguu yake

Ingawa Yahwe sio binadamu, mwandishi anampa sifa za binadamu. "giza nene lilikuwa chini yake"

mabawa ya upepo

Hapa mwandishi wa zaburi anazungumzia upepo kana kwamba una mabawa kama malaika.

Psalms 18:11

Akafanya giza ... yeye

Hapa neno "yeye" linamaanisha Yahwe

Akafanya giza hema

Hapa giza linazungumziwa kana kwamba ni hema. "Akafanya giza kitu cha kufunikia" au "Akafanya giza sehemu ya kujifichia"

mawingu mazito ya mvua

"mawingu na mvua kubwa" au "mawingu manene, meusi"

Mvua ya mawe

"mawe ya barafu"

Psalms 18:13

Yahwe akaunguruma mbinguni

Sauti ya Yahwe ilikuwa kama ya radi

Aliye juu

"Aliye juu" inamaanisha Yahwe.

Akapiga mishale yake na kuwatawanya adui zake ... miale ya radi ikawatawanyisha

Vishazi hivi viwili vina maana ya kukaribiana.

Akapiga mishale yake na kuwatawanya adui zake

Hapa miale ya radi inazungumziwa kana kwamba ni mishale.

ikawatawanyisha

"ikawapeleka pande tofauti"

Psalms 18:15

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuzungumzia uwezo wa Yahwe.

Kisha mikondo ya maji ikatokea; misingi ya dunia ikawekwa wazi.

Vishazi hivi viwili vina maana ya kukaribiana. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kisha mikondo ya maji ikatokeza na chini ya bahari pakaonekana; ukaweka wazi misingi ya dunia"

kwa mlipuko wa pumzi wa tundu zako za pua

Ingawa Mungu hana sifa za kimwili kama za binadamu zilizoelezwa hapa, picha hii inaonesha uwezo wake mkuu. Upepo unazungumziwa kana kwamba ulikuja kama mlipuko mkubwa kutoka katika tundu za pua za Mungu.

Psalms 18:16

Akafika chini ... akanishika ...Akanivuta

Anayezungumziwa hapa ni Yahwe.

maji yaliyokuwa yakienda mbele

Hapa mwandishi wa zaburi anazungumzia hatari ya adui zake kana kwamba walikuwa mawimbi makubwa au maji ya nguvu, ambapo Yahwe alimwokoa.

Psalms 18:18

Wakaja dhidi yangu

Wanazungumziwa ni adui wenye nguvu katika msatari wa 17.

Wakaja dhidi yangu katika siku ya dhiki yangu lakini Yahwe alikuwa msaada wangu

Neno "dhiki" linaeleza hali ya mtu mwenye shida nyingi. "Adui wenye nguvu walinivamia katika siku niliyokuwa na taabu nyingi, lakini Yahwe alinilinda"

Psalms 18:20

mikono yangu ilikuwa misafi

Hapa kuwa na "mikono misafi" inamaanisha mtu hana hatia. "matendo yangu yote yalikuwa sawa"

Nimetunza njia za Yahwe

Sheria za Yahwe zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa njia ambazo mtu anapaswa kutembea. "Nimetii sheria za Yahwe"

sijageuka kwa uovu kutoka njia ya Mungu

Hapa kuwa mwovu inazungumziwa kama mtu kuacha njia sahihi na kufuata njia isiyo sahihi. "sijafanya uovu kwa kugeuka kutoka kwa Mungu wangu"

Psalms 18:22

Kwa amri zake zote za haki ... sijazigeuka

Vishazi hivi viwili vina maana ya kufanana. Mwandishi anarudia mawazo haya kwa ajili ya mkazo.

zimekuwa mbele yangu

"zimeniongoza" au "nimezikumbuka"

Pia nimekuwa bila hatia ... nimejitenga na dhambi

Vishazi hivi viwili vina maana ya kufanana. Mwandishi anarudia mawazo haya kwa ajili ya mkazo.

bila hatia mbele yake

"bila hatia kulingana na yeye"

nimejitenga na dhambi

"sijatenda dhambi"

mikono yangu ilikuwa misafi

Kuwa na "mikono misafi" inamaanisha kuwa mtu hana hatia na kosa. "matendo yangu yote yalikuwa sawa"

mbele ya macho yake

Hii inamaanisha uwepo wa Mungu. "mbele yake" au "kulingana na yeye"

Psalms 18:25

Taarifa ya

Mwandishi anazungumza na Yahwe

Kwa yeyote aliye mwaminifu

Hapa "mwaminifu" inamaanisha kufanya kile ambacho Mungu anamuamuru mtu kufanya. "kwa wale walio wanaotii kwa uaminifu amri zako" au "kwa wale wanaofanya agano lako kwa uaminifu"

kwa mwanamme asiye na lawama ... ujioneshe msafi

Vishazi hivi viwili vina maana ya kufanana. Mwandishi anarudi mawazo haya kwa ajili ya mkazo.

una akili kwa yeyote aliye mkaidi

"Unamshinda kwa akili yeyote asiye wazi"

Psalms 18:27

unawaleta chini

"unawanyenyekesha"

wenye macho ya majivuno yaliyoinuka

lahaja hii inaashiria wale walio na majivuno. "wenye majivuno"

Kwa kuwa unaipa nuru taa yangu; Yahwe Mungu wangu huipa nuru giza langu

Mwandishi anazungumzia uwepo wa Yahwe kana kwamba alikuwa nuru. Vishazi hivi vina maana ya kukaribiana.

Kwako ninaweza kuruka kizuizi

"Kwa msaada wako ninaweza kuvuka kikwazo chochote"

Psalms 18:30

Yeye ni ngao kwa kila mmoja anaye

Ngao humlinda askari. Daudi anazungumza kana kwamba Mungu alikuwa ni ngao inayomlinda. "Wewe, Yahwe, unamlinda kila mtu anayekukimbilia wewe kama kimbilio"

Kwa kuwa ni nani Mungu ila Yahwe? Nani ni mwamba ila Mungu wetu?

Jibu linalodokezwa ni hakuna mtu. "Yahwe pekee ndiye Mungu! Mungu wetu pekee ndiye mwamba!"

mwamba

Daudi anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni mwamba anaoweza kupanda kuwatoroka adui zake.

anayeniwekea nguvu juu yangu kama mshipi

Mungu anampa nguvu Daudi kana kwamba ilikuwa ni kipande cha nguo.

anayemuweka mtu asiye na lawama katika njia yake

Hapa Daudi anazungumzia kuishi maisha yanaompendeza Mungu kana kwamba ni kuwa katika njia sahihi. "humsababisha mtu asiye na lawama kuishi maisha ya haki"

Psalms 18:33

hufanya miguu yangu miepesi

Hii inaashiria kumwezesha mtu kukimbia haraka zaidi. "hunifanya nikimbie haraka sana"

kama mbawala na kuniweka pa juu

Mbawala ana kasi na mtulivu milimani.

hufunza mikono yangu

Hapa "mikono yangu" inamaanisha mtu. "Hunifunza"

mikono yangu

Hii inaashiria mtu. "mimi"

Psalms 18:35

ngao ya wokovu wako

Hapa mwandishi anazungumzia ulinzi wa Mungu kana kwamba ni ngao. Nomino dhahania ya "wokovu" inaweza kuelezwa kama kitenzi "okoa." "ulinzi wako na kuniokoa"

Mkono wako wa kuume ... fadhili zako

Zote hizi ni njia zingine za kumwakilisha Mungu mwenyewe.

sehemu pana kwa ajili ya miguu yangu chini yangu

Mwandishi anazungumzia ulinzi ambao Mungu ameutoa kana kwamba ni eneo pana kwa ajili yake kusimama. "sehemu salama kwa ajili yangu"

miguu yangu haijateleza

Hapa "miguu yangu" inamaanisha mtu mwenyewe. Mwandishi anazungumzia usalama wa ulinzi wa Mungu kana kwamba alikuwa akisimama mahali ambapo hawezi kuteleza wala kuanguka. "Sijateleza" au "Niko salama"

Psalms 18:37

Nimewaponda

"Nimewavunja vipande vipande"

hawakuweza kuinuka

"hawakuweza kusimama"

wameanguka chini ya miguu yangu

Lahaja hii inamaansiha kuwa mwandishi wa zaburi amewashinda adui zake. "nimewashinda wote"

umeweka nguvu juu yangu kama mshipi

Mwandishi wa zaburi anasema kuwa Yahwe amempa nguvu inayomzunguka na kumstahimili kama mshipi.

umewaweka chini yangu

Hapa mwandishi wa zaburi anazungumzia kushindwa kwa adui zake kama kusimama juu yao. "unawashinda kwa ajili yangu"

wale wanaojiinua dhidi yangu

Hii inamaansiha wale wanaompinga mwandishi wa zaburi. "wale ambao ni adui zangu"

Psalms 18:40

sehemu za nyuma za shingo za adui zangu

Hii inaashiria ushindi juuya maadui wa mtu. "ushindi juu ya adui zangu"

Nimewaangamiza wale wanaonichukia

"Niliwashinda wale walionichukia" au "Niliwaangamiza kabisa wale walionichukia"

lakini hakuwajibu

Hii inamaanisha Yahwe hakutoa msaada wowote. "lakini hakuwasaidia"

Niliwapiga hadi vipande kama vumbi mbele ya upepo

Adui wa mwandishi wa zaburi wanalinganishwa na vumbi kuonesha jinsi alivyowashinda.

Nikawarusha nje kama tope katika mitaa

Adui wa mwandishi wa zaburi wanalinganishwa na tope la kwenye mitaa kuonesha jinsi alivyowashinda.

Psalms 18:43

mabishano

"kutokuelewana"

umenifanya kichwa juu ya mataifa

Hapa "kichwa" kinamaanisha mtawala. "umeniweka mimi kuwa mtawala juu ya mataifa

wageni walilazimika kusujudu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu aliwalazimisha wageni kusujudu"

wageni walikuja wakitetemeka

hapa "kutetemeka" inaonesha kuwa walikuwa wanaogopa sana. "wageni walikuja wakitetemeka, wakionesha kuwa walikuwa wanaogopa sana"

Psalms 18:46

na mwamba wangu usifiwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "yeye ni mwamba wangu na anapaswa kusifiwa" au "watu wasifu mwamba wangu"

mwamba wangu

Hapa mwandishi anazungumzia ulinzi wa Yahwe kana kwamba alikuwa ni mwamba uliozuia adui zake kumfikia.

Na Mungu wa wokovu wangu ainuliwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na watu wamtukuze Mungu wa wokovu wangu"

Mungu wa wokovu wangu

Hii inamaanisha kuwa Mungu amemuokoa. "Mungu aliyeniokoa"

Mungu anayetekeleza kisasi kwa ajili yangu

"Kutekeleza kisasi" inamaana kuwaadhibu watu kwa matendo yao maovu. "Mungu anayewaadhibu watu kwa matendo maovu waliyotenda kwangu"

Psalms 18:48

Nimewekwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu ameniweka

umeniinua

Ulinzi wa Yahwe kwa mwandishi unazungumziwa kana kwamba amemuinua mwandishi juu sana hadi adui zake hawakuweza kumfikia na kumdhuru. "umeniweka sehemu salama juu"

walioinuka dhidi yangu

"walionivamia" au "walioasi dhidi

wanaume wenye vurugu

"wanaume wakatili" au "watu wenye hasira sana"

miongoni mwa

Hapa mwandishi anamaana kuwa atampa Yahwe shukrani ili watu wote wasikie ukuu wa Yahwe. "ili mataifa yote yasikie kuhusu hili"

kwa jina lako

Hapa "jina" linamwakilisha Mungu mwenyewe. "kwa heshima ya jina lako" au "kwako"

Psalms 18:50

ushindi kwa mfalme wake

Kwa kutumia maneno "mfalme wake," Daudi anamaanisha yeye mwenyewe kama mfalme.

anaonesha uaminifu wake wa agano kwa mtiwa mafuta wake ... kwa vizazi vyake milele

"ananipenda kwa uaminifu kama alivyoahidi katika agano lake, na ataupenda uzao wangu milele"

Psalms 19

Psalms 19:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Mbingu zinatangaza

Mbingu zinaelezwa kana kwamba ni mtu. "Mbingu zinaonesha" au "Mbingu zinaonekana kama zinatangaza"

anga zinafanya kazi yake ya mikono kujulikana

Anga zinaelezwa kana kwamba ni mwalimu. "anga zinaonekana kufanya kazi ya mikono ya Mungu kujulikana kwetu"

kazi yake ya mikono

"uumbaji wake" au "ulimwengu alioutengeneza"

maneno humwagika

Kilicho kizuri kuhusu uumbaji kinafananishwa na kuzungumza, kana kwamba uumbaji ni mtu. Kisha maneno hayo yanalinganishwa na maji wanayotiririka kila mahali. "Uumbaji ni kama mtu anayezungumza na kila mtu"

Hakuna mazungumzo au maneno ya kusemwa; sauti yao haisikiki

Misemo hii inaelza wazi kuwa mistari miwili ya kwanza ilikuwa sitiari. "Hakuna mazungumzo ya kweli wala maneo ya kusemwa; hakuna anyesikia sauti halisi kwa masikio yao"

sauti yao haisikiki

Tafsiri zingine zinasoma "ambapo sauti yao haisikiki," kusisitiza kuwa "mazungumzo" ya uumbaji yanapatikana kila sehemu.

Psalms 19:4

Taarifa ya Jumla:

Daudi amemaliza tu kusema kuwa uumbaji unaonesha utukufu wa Mungu.

maneno yao ...kusema kwao

Hii namaansiha "maneno" yasiyozungumzwa ya uumbaji yanayoonesha utukufu wa Mungu.

maneno yao huenda

Maneno yanaelezwa kana kwamba ni watu ambao wanatoka na ujumbe. "maneno amabyo uumbaji unazungumza ni kama watu wanaoenda nje"

kusema kwao hadi mwisho wa dunia

"kusema kwao kunaenda hadi mwisho wa dunia"

Ameweka hema kwa ajili ya jua

Hapa mwandishi anazungumzia sehemu ambayo Yahwe aliumba kwa ajili ya jua kana kwamba ni hema. "Aliumba sehemu kwa ajili ya jua"

miongoni mwao

Neno "mwao" inaweza kuwa inamaanisha mbingu.

Jua ni kama bwana arusi anayetoka katika chumba chake

Mwandishi anazungumzia kuchomoza kwa jua kana kwamba ni bwana arusi. "jua ni kama bwana arusi akitembea kwa furaha kwenda kwa bibi arusi wake"

kama mwamme menye nguvu anayefurahi anapokimbia mbio yake

Hii inalinganisha jua na mwanariadha kusisitiza nguvu na mwanga wa jua.

mwanamme mweye nguvu

"mkimbiaji mwenye kasi"

upeo wa macho

mstari ambao ardhi na anga hukutana

hadi mwingine

Hapa "mwingine" inamaanisha upeo wa macho. "hadi kwenye upeo wa macho mwingine"

hakuna kinachotoroka joto lake

Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "kila kitu kinahisi joto lake"

Psalms 19:7

nafsi ... moyo ... macho

Maneno yote haya matatu yanamaanisha mtu mzima.

wa kawaida

"wale wasiokuwa na uzoefu" au "wale ambao hawajajifunza"

ni sahihi

"ni za kweli" au "ziko sawa"

huleta nuru

"huleta uelewa"

Psalms 19:9

pamoja ni sawa

"sahihi kabisa"

Zina thamani zaidi ya dhahabu ... nitamu zaidi ya asali

Amri za Yahwe zinazungumziwa kana kwamba zinaweza kununuliwa na kuonjwa. "Kama unaweza kuzinunua, zitakuwa na dhamani zaidi ya dhahabu ... kama unaweza kuzionja, zitakuwa tamu zaidi ya asali"

hata zaidi ya dhahabu safi

"hata thamani zaidi ya dhahabu nyingi safi"

dhahabu safi

"dhahabu halisi" au "dhahabu ya gharama"

Psalms 19:11

Ndio

"Pia" au "Kweli"

kwazo mtumishi wako huonywa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "zinamuonya mtumishi wako" au "ni onyo kwa mtumishi wako"

kwazo ...kwa kuzitii

Zinazozungumziwa hapa ni amri za Yahwe za haki.

mtumishi wako huonywa

Daudi anajiita "mtumishi wako" anapozungumza na Mungu kama ishara ya heshima. "nimeonywa"

Nani anaweza kutambua makosa yake yote?

Hii inaonekana katika hali ya swali kuongeza mkazo na inaweza kutafsiriwa na kauli kali. "Hakuna mtu anayeweza kutambua makosa yake mwenyewe!"

na makosa yaliyojificha

"na makosa ya siri niliyofanya"

Psalms 19:13

Muweke mtumishi wako pia mbali na

Lahaja hii inaonesha mtumishi kama ametolewa kwenye dhambi ambazo hataki kutenda. "Pia, mlinde mtumishi wako kutokufanya" au "Pia, hakikisha sifanya"

mtumishi wako

Daudi anajiita "mtumishi wako" anapozungumza na Mungu kama ishara ya heshima. "mimi"

usiziache zinitawale

Dhambi zinaelezwa kana kwamba ni mfalme anayeweza kutawala juu ya mtu. "usiache dhambi zangu ziwe kama mfalme anayetawala juu yangu"

sina hatia na makosa mengi

"sina hatia ya kuasi dhidi yako" au "sina hatia ya kutenda dhambi nyingi"

maneno ya mdomo wangu na mawazo ya moyo wangu

Misemo hii pamoja inaeleza kile ambacho mtu anasema na kuwaza. "vitu ninavyosema na vitu ninavyowaza"

yakubalike machoni pako

"yapokee kukubaliwa machoni pako" au "yakupendeze wewe"

machoni pako

Hii inamaanisha Mungu mwenyewe. "kwako"

Yahwe, mwamba wangu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni mwamba ambao mtu anaweza kupanda kujilinda dhidi ya adui zake. "Yahwe, wewe ni kama mwamba wangu"

Psalms 20

Psalms 20:1

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii inaanza na kundi la watu wakizungumza na mfalme wa Israeli.

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

ukusaidie

Anayesaidiwa hapa ni mfalme.

siku ya shida

Hapa "siku" inamaanisha muda mrefu zaidi. "nyakati za shida"

jina la Mungu wa Yakobo

Hapa "jina" linamaanisha Mungu mwenyewe. "Mungu"

Mungu wa Yakobo

hii inamaanisha babu yao Yakobo, aliyemwabudu Yahwe.

tuma msaada kutoka sehemu takatifu

Mungu kuwasaidia kutoka sehemu yake takatifu inazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa anatuma msaada. "na Yahwe awasaidie kutoka sehemu yake takatifu"

sehemu takatifu ... Sayuni

Zote hizi zinamaansiha hekalu la Mungu Yerusalemu.

Psalms 20:3

Na atilie akilini

Msemo huu "atilie akilini" ni njia nyingine ya kusema "akumbuke." Haimaanishi kuwa Mungu alisahau. Inamaanisha kutafakari au kuwazia. "Na akumbuke"

Na atilie

Hapa anayezungumziwa ni Yahwe.

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Na awape

"Na awapatie"

hamu ya moyo wako

Hapa "moyo" unamaanisha mtu mzima. Nomino dhahania "hamu" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "unachotamani" au "unachotaka"

kutimiza mipango yako yote

Nomino dhania ya "mipango" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "na akusaidie kutimiza kila jambo ulilopanga kufanya"

Psalms 20:5

tutafurahi katika ushindi wako

Hapa watakaofurahi ni watu. Watufurahi katika ushindi wa mfalme.

katika jina la Mungu wetu

Hapa "jina" linamaanisha heshima na sifa. "kwa heshima ya Mungu" au "kwa sifa ya Mungu wetu"

tutanyanyua bendera

"tutanyanyua mabango"

akupe maombi yako yote

"kukupa kila kitu unachomuomba"

Sasa

Neno hili linatumika kuweka mapumziko katika zaburi. Inahama kutoka kwa watu kuzungumza hadi kwa mfalme kuzungumza.

Ninajua

Anayejua inawezekana ni mfalme katika kipengele hiki.

mtiwa mafuta wake ... atamjibu ... atamuokoa

Mfalme anajizumzia mwenyewe katika hali ya mtu wa tatu. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya mtu wa kwanza. "mimi, mtiwa mafuta wake ... nijibu .. niokoe"

kutoka mbingu yake takatifu

Mungu anaishi mbinguni pamoja na kwenye hekalu Yerusalemu.

kwa nguvu ya mkono wake wa kuume unaoweza kumwokoa

Mkono wa kuume wa Mungu unaashiria nguvu yake kumwokoa mfalme. "kwa nguvu yake kubwa atamwokoa"

Psalms 20:7

Wengine wanatumaini vibandawazi na wengine farasi

Hapa "vibandawazi" na "farasi" zinamaanisha jeshi la mfalme.

na wengine farasi

Neno "tumaini" linaeleweka. "na wengine wantumaini farasi"

tunaita

Wanaoita ni mfalme na watu wake.

Wataletwa chini na kuanguka

Wanaoletwa chini ni watu wanaotumaini vibandawazi na farasi. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu atawaleta chini na kuwafanya waanguke"

kuletwa chini na kuanguka

Vitenzi hivi viwili vinamana sawa. Zote mbili zinamaanisha kushindwa kwenye mapambano.

tutanyanyuka na kusimama wima

"tutainuka na kusimama wima." Misemo hii miwli inamaana ya kufanana. Zote mbili zinamaanisha ushindi katika mapambano.

Psalms 20:9

Yahwe, muokoe mfalme

Tafsiri zinazowezekana ni 1) watu wanamwomba Mungu kumlinda mfalme au 2) mfalme anaendelea kujizungumzia katika hali ya mtu wa tatu.

mfalme; tusaidie tunapokuita

Tafsiri zingine zinaelewa Kiebrania tofauti. Zingine zinatafsiri kama watu kuzungumza na Yahwe mfalme wao. "Mfalme, tusaidie tunapokuita"

Psalms 21

Psalms 21:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

katika nguvu yako, Yahwe

Inadokezwa kuwa hii ni nguvu ambayo Yahwe amempa mfalme kuwashinda adui zake. "kwa sababu wewe, Yahwe, umempa nguvu ya kutosha kuwashinda adui zake"

Jinsi gani anafurahi

"Anafurahi sana"

katika wokovu unaoutoa

Inadokezwa kuwa Mungu amemwokoa mfalme kutoka kwa adui zake. Nomini dhahania ya "wokovu" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "kwa sababu umemwokoa kutoka kwa adui zake"

hamu zake za moyo

"matamanio ya moyo wake." Hapa "moyo" unamaanisha mtu mzima. "hamu yake" au "alichokuwa anatamani"

hujazuia

"haujamkatalia." Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "umempa"

maombi ya midomo yake

Hapa "midomo" inaashiria mtu mzima. "maombi yake" au "kile alichokuomba"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 21:3

unamletea baraka nyingi

Nomino dhahania "baraka" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "unambariki sana" au "unampa vitu vingi vizuri"

umeweka kichwani mwake taji la dhahabu safi

Kuweka taji juu ya kichwa cha mtu ni ishara ya kumfanya kuwa mfalme.

taji la dhahabu safi

Hapa "dhahabu safi" inaashiria heshima kubwa anayopewa mfalme.

Aliomba uhai; ukampa

Nomino dhahania ya "uhai" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "Alikuomba kuwa umfanye aishi kwa muda mrefu, ukaifanya itokee"

siku ndefu milele na milele

Maana zinazowezekana ni 1) maisha marefu sana au 2) masiha ya milele au 3) uzao mrefu.

Psalms 21:5

Utukufu wake

"heshima ya mfalme" au "umaarufu wa mfalme"

umeweka kwake fahari na utukufu

Kusababisha mfalme kuwa na utajiri na nguvu inazungumziwa kama fahari na utukufu ni vitu vilivyowekwa kwake. "umemfanya kuwa na utajiri na nguvu"

umempa

"umemruhusu kuwa na" au "umekubali kumpa"

baraka za kudumu

"baraka itakayodumu" au "baraka itayobaki"

furaha ya uwepo wako

"furaha ya kuwa katika uwepo wako" au "furaha inayokuja kwa kuwa karibu na wewe"

Psalms 21:7

katika uaminifu wa agano la aliye juu

"kwa kuwa aliye juu ni mwaminifu kwa agano lake"

hatasogezwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu atakaye msogeza kama mfalme"

Mkono wako utakamata

Hapa "mkono" unaashiria nguvu. "Nguvu yako itakamta" au "Utawakamata kwa nguvu"

Mkono wako ... unachukia

Maana zinazowezekana za anaye zungumziwa ni 1) mfalme au zinamaanisha ni 2) Mungu.

Mkono wako wa kuume utawakamata wale wanaokuchukia

Hii inamaanisha kitu sawa kama sehemu ya kwanza ya sentensi. Inawekamkazo kuwa Mungu atampa mfalme uwezo wa kuwazuia adui zake.

Psalms 21:9

Katika kipindi cha hasira yako

"Utakapotokea katika hasira yako"

hasira yako ... Utaangamiza

Maana zinazowezekana za anaye zungumziwa ni 1) Mungu au ni 2) mfalme.

utawachoma kama tanuu ya moto

Yahwe au mfalme kuwaangamiza adui inazungumziwa kana kwamba adui ni mbao na Yahwe au mfalme atawatupa katika tanuu.

Yahwe atawamaliza katika gadhabu yake, na moto utawateketeza

Vishazi vyote viwili vina maana sawa. Yahwe kuwaangamiza kabisa adui zake inazungumziwa kana kwamba gadhabu yake ni moto unaowaunguza kabisa adui zake.

kutoka duniani ... kutoka kwa wanadamu

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja. Inaweka mkazo kuwa hakuna adui yao hata mmoja atakayepona.

Psalms 21:11

walikusudi

"walipanga." Waliopanga ni adui wa Mungu na mfalme.

maovu dhidi yako

"kufanya vitu viovu"

wakatunga njama

"wakafanya mpango" au "wakiunda hila"

Kwa kuwa utawageuza; utachukua upinde wako mbele yao

Maana zinazowezekana za anaye zungumziwa ni 1) mfalme au ni 2) Mungu na zinamzungumzia kana kwamba alikuwa ni shujaa mwenye upinde na mishale.

utawageuza

Hii ni njia ya kusema kuwa Mungu na mfalme watawashinda adui zao vitani.

utachukua upinde wako mbele yao

Hii inaashiria kuwa anawapiga adui zake kwa mishale.

Psalms 21:13

Utukuzwe, Yahwe, katika nguvu yako

Maana zinazowezekana ni 1) "Yahwe, tuoneshe kuwa una nguvu sana" (UDB) au 2) "Yahwe, kwa sababu una nguvu, tutakutukuza"

tutaimba na kusifu uwezo wako

Maneno "tutaimba" na "kusifu" yana maana ya kukaribiana. Hapa neno "uwezo" linamaanisha Mungu na uwezo wake. "kwa kuimba tutakusifu kwa sababu una uwezo"

Psalms 22

Psalms 22:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Mapigo ya mbawala

Hii inaweza kumaanisha aina ya muziki.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Mungu wangu, Mungu wangu

Mwandishi anarudia "Mungu wangu" kusisitiza kuwa anatamani sana Mungu amsikie.

Mungu wangu, kwa nini umeniacha?

Mwandishi anatumia swali kusisitiza kuwa anahisi kama vile Mungu amemwacha. Ni bora zaidi kuiacha hii kama swali. Inaweza pia kuwekwa kama kauli. "Mungu wangu, nahisi kama umeniacha!"

umeniacha

"umeniacha peke yangu"

Kwa nini uko mbali sana na kuniokoa na mbali na maneno yangu ya uchungu?

Mwandishi anatumia tena swali kusisitiza kuwa anahisi kama vile Mungu yuko mbali naye. Ni bora zaidi kuiacha hii kama swali. Inaweza pia kuwekwa kama kauli. "Uko mbali na kuniokoa na mbali na maneno ya uchungu wangu!"

mbali na maneno yangu ya uchungu

Mwandishi kuhisi kana kwamba Mungu hamsikilizi kunazungumziwa kana kwamba Mungu yuko mbali na maneno ya uchungu wake. Hapa "maneno" yanamaanisha chochote ambacho mwandishi anasema. "kwa nini hausikilizi ninapozungumza kwako kuhusu uchungu ninaoupitia" au "nimekuambia kuhusu mahangaiko yangu lakini haujaja kwangu"

mchana ... usiku

Mwandishi anatumia maneno "mchana" na "usiku" kumaanisha kuwa humwomba Mungu kila wakati.

siko kimya

Hii inaweza kuwekwa katika hali chanya. "Bado ninazungumza"

Psalms 22:3

umeketi kama mfalme na sifa za Israeli

"sifa za Israeli ni kiti cha enzi ambacho unaketi kama mfalme." Sifa za Israeli zinaelezwa kana kwamba ni kiti cha enzi ambacho Mungu anaketi na kutawala, au nyumba ambayo Mungu anaweza kuishi. "wewe ni mfalme na watu wa ISraeli wanakusifu"

za Israeli

Hapa "Israeli" inamaanisha watu wa Israeli.

hawakuvunjwa matarajio

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na haukuvunja matarajio yao" au "haukuwaangusha"

hawakuvunjwa matarajio

Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "na ukawaokoa" au "ukawafanyia walichohitaji uwafanyie"

Psalms 22:6

mimi ni mnyoo na sio mtu

Mwandishi anajizungumzia kana kwamba alikuwa ni mnyoo. Hii inaonesha mkazo kuwa alijihisi hafai au kuwa watu walimtenda kana kwamba hana faida. "Lakini ni kama mimi ni mnyoo na sio binadamu"

aibu kwa wanadamu na kuchukiwa na watu

Misemo hii miwili inamaana sawa. Msemo "kuchukiwa na watu" unaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kila mtu anadhani sina faida na watu wananichukia"

wananidhihaki, wananifanyia mzaha; wanatikisa vichwa vyao kwangu

Misemo hii mitatu ina maana ya kukaribiana na inasisitiza jinsi watu walivyomdharau.

wanatikisa vichwa vyao kwangu

Hii inaelezea tendo ambalo watuwalitumia kumdhihaki mtu.

Anamtumaini Yahwe ... anamfurahia

Watu wanasema hivi kumdhihaki mwandishi. Hawaamani kweli kuwa Yahwe atamwokoa.

Acha amwokoe

"Acha Yahwe amwokoe"

kwa kuwa anamfurahia

Maana zinazowezekana ni 1) "kwa kuwa Yahwe anamfurahia" au 2) "kwa kuwa anamfurahia Yahwe"

Psalms 22:9

Kwa kuwa

Mwandishi anatumia neno "Kwa" kuanza kueleza kwa nini amechanganyikiwa na kumwuliza Mungu kwa nini haji kumsaidia.

umenitoa kwenye tumbo

Hii ni njia ya kusema "umesababisha nizaliwe"

nilipokuwa katika kifua cha mama yangu

Hii inamaanisha kuwa amekuwa akimtumaini Yahwe tangu yuko mchanga. "hata tangu wakati nilipokunywa maziwa kutoka kifua cha mama yangu"

Nimetupwa kwako kutoka tumboni

Msemo "nimetupwa" ni njia ya kusema kuwa Yahwe amemtunza kana kwamba Yahwe alimpanga utoto kama mwana wake. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Ilikuwa kana kwamba umenipanga utoto tangu nilipozaliwa"

wewe ni Mungu wangu

Hii inadokeza kuwa Yahwe daima amekuwa akimctunza mwandishi. "wewe, Mungu, umenitunza"

tangu nimo tumboni mwa mama yangu

"tangu kabla sijazaliwa"

Psalms 22:11

Usiwe mbali na mimi

Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "Njoo karibu yangu"

kwa kuwa taabu iko karibu

Mwandishi anazungumzia "taabu" kana kwamba ni kitu kilicho karibu yake. "kwa kuwa adui zangu wako karibu yangu"

hakuna msaada

"hakuna msaidizi"

Mafahali wengi wamenizunguka; mafali hodari wa Bashani wamenizunguka

Mwandishi anawazungmzia adui zake kana kwamba ni mafahali. Hii inaweka mkazo wa jinsi adui zake walivyo na nguvu. "Nina adui wengi na wako kama mafahali wanaonizunguka; wako kama mafahali hodari kutoka Bashani wanaonizunguka"

Wamefungua midomo yao wazi dhidi yangu

Mwandishi anawazungumzia adui zake kana kwamba ni simba wenye midomo wazi tayari kumla. Adui zake wanaweza kuwa wanazungumza uongo kumpunguzia sifa. Au wanaweza kuwa wanamtisha na kumvamia.

kamasimba anayeunguruma akimrarua mhanga wake

Mwandishi anawazungumzia adui zake kana kwamba ni simba. Hii inasisitiza jinsi adui wake walivyokuwa na nguvu na hatari.

Psalms 22:14

Ninamwagwa nje kama maji

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Ni kama mtu ananimwaga nje kama maji"

Ninamwagwa nje kama maji

Mwandishi anazungumzia kuhusu kujihisi kuchoka na munyonge kana kwamba alikuwa maji akimwagwa nje ya chupa

mifupa yangu yote imeteguka

"mifupa yangu yote iko nje ya sehemu zake." Inawezekana mwandishi yuko katika aina flani ya maumivu ya kimwili. Au anaweza kuwa anazungumzia maumivu ya hisia kana kwamba ni maumivu ya kimwili.

Moyo wangu ni kama nta ... sehemu zangu za ndani

Mwandishi anazungumzia kutokuwa na ujasiri kana kwamba moyo wake umeyeyuka kama nta. Hapa "moyo" unaashiria "ujasiri."

nta

kitu laini kinacho yeyuka kwa joto dogo.

ndani ya sehemu zangu za ndani

"ndani yangu"

Nguvu yangu imekauka kama kipande cha ufinyanzi

Mwandishi anazungumzia kujisikia mdhaifu kana kwamba nguvu yake ilikuwa kama kipande cha ufinyanzi kilichokauka na chepesi kuvunjika.

kipande cha ufinyanzi

kitu kilichoundwa kwa udongo wa kuoka kinachoweza kutumika ndani ya nyumba.

ulimi wangu unatokeza hadi kwenye paa ya mdomo wangu

"ulimi wangu unatokeza hadi juu ya mdomo wangu." Mwandishi anaweza kuwa anaelezea kiu yake kali. Au anaweza kuwa anaendelea kuzungumzia kuwa mdhaifu kana kwamba amekauka kabisa.

Umenilaza kwenye vumbi la mauti

Maana zinazowezekana kwa ajili ya "vumbi la mauti" ni 1) inamaanisha mtu kugeuka kuwa vumbi baada ya kufa. "Unataka kuniacha nife na niwe vumbi" au 2) ni njia ya kuzungumzia kaburi, ambayo inamaanisha Mungu anamsababisha mwandishi kufa. "Umenilaza kwenye kaburi langu"

Umenilaza

Aliyemlaza ni Mungu.

Psalms 22:16

mbwa wamenizunguka

Mwandishi anazungumza kuhusu adui zake kana kwamba ni mbwa. Adui zake wanakuja karibu yake kama mbwa pori wanavyofanya kwa mnyama anayekufa. "adui zangu ni kama mbwa walionizunguka"

kundi la watenda maovu

"kikundi cha watenda maovu"

wamenizunguka

"wamenizingira"

wametoboa mikono yangu na miguu yangu

Hii inaendeleza mfano wambwa. Mwandishi anazungumzia adui zake kana kwamba ni mbwa wanao mng'ata na kutoboa mikono na miguu yake kwa meno yao.

toboa

kuchoma na kifaa chenye ncha kali

Ninaweza kuhesabu mifupa yangu yote

Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi ni mwembamba sana hadi anaweza kuona mifupa yake. "Ninaweza kuona mifupa yangu yote" au "Ninaweza kuihisi mifupa yangu yote" au 2) hii inaendeleza mfano wa mbwa na mwandishi anaweza kuona mifupa yake baade ya mbwa kurarua nyama yake.

Wananitazama na kunikazia macho

Maneno "wananitazama" na "kunikazia macho" ina maana sawa na inasisitiza kuwa watu wanamwangalia kwa ajabu na kumtania.

Psalms 22:18

nguo zangu

"mavazi yangu"

Usiwe mbali

Hii inawezwa kuelezwa katika hali chanya. "Uwe karibu sana"

nguvu yangu

Hapa "nguvu" inaashiria Yahwe anayempa nguvu. "wewe unayenipa nguvu" au "wewe unayenisaidia"

Psalms 22:20

Okoa nafsi yangu

Hapa "nafsi" inamaanisha mtu mzima. "Niokoe"

upanga

Upanga ni njia ya kawaida ya kumaanisha adui mwenye vurugu. "wale wanaotaka kuniua" au "adui zangu"

maisha yangu pekee

"maisha yangu ya dhamani" au "maisha pekee niliyonayo"

makucha ya mbwa pori ... mdomo wa simba ... mapembe ya nyati

Mwandishi anawazungumzia adui zake kana kwamba ni mbwa, simba, na nyati kuweka mkazo jinsi adui zake walivyo hatari. Pia, makucha, mdomo, na mapembe yanamaanisha myama mzima. Mwandishi anasisitiza sehemu hizi za wanayama kwa sababu ndio sehemu ambazo wanyama hao hutumia kuua mtu.

mbwa pori ... nyati

Neno "pori" linamaanisha kuwa hakuna mtu aliyemshika na kumfuga huyu mnyama.

Psalms 22:22

Nitatangaza jina lako

"Nitafanya jina lako lijulikane." Hapa "jina" linaashiria tabia na sifa ya Mungu. "Nitazungumza kuhusu tabia yako"

ndugu zangu

Hapa "ndugu" inamaanisha "Waisraeli wezangu" au "waabudu wezangu wa Yahwe"

katikati ya kusanyiko

"Waisraeli wezangu na mimi tukikutana pamoja" au " ninapozungukwa na waabudu wezangu wa Yahwe"

Nyie mnayemwogopa

Hapa anazungumza na watu wengi.

Nyie wote uzao wa Yakobo ...nyie wote uzao wa Israeli

Zote hizi zinamaansiha kundi moja la watu.

Simameni kwa kumshangaa

"Mjawe na kumshangaa yeye" au "Acheni nguvu ya Mungu iwashangaze"

Psalms 22:24

hajadharau wala kuchukizwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "amependa na kuona bora kabisa"

hajadharau wala kuchukizwa na mateso ya aliyeteswa

Hapa "mateso" inamaanisha mtu anayeteseka. "hajamdharau wala kumchukia yule anayeteseka"

hajadharau wala kuchukizwa

Maneno haya mawili yana maana ya kufanana na yanasisitiza kuwa Mungu hajamsahau mwandishi.

hajadharau

"chukia sana"

kuchukizwa

"kukemea"

mateso ya aliyeteswa ...kwake ... aliyeteswa alipolia

Hii inaweza kuelezwa ili imaanishe yeyote anayeteseka. "wale wanaoteseka ... kwao ... wale wanaoteseka walilia"

hajaficha uso wake

Hii ni lahaja. "hajageuza usikivu wake" au "hajaacha kunizingatia"

alisikia

"alisikiliza." Inadokezwa kuwa alijibu aliposikia kilio chao. "alijibu" au "alisaidia"

kwa sababu yako

Anayezungumziwa hapa ni Yahwe.

nitatimiza viapo vyangu

Hii inamaanisha sadaka ambazo mwandishi aliahidi kumtolea Mungu.

mbele yao

Ambaye wanamcha ni Yahwe. Inaweza kuelezwa kama "wewe." "mbele yao wanaokugopa wewe"

Psalms 22:26

Walidhulumiwa watakula na kuridhika

Hii inamaanisha mlo wa ushirika unaotokea baada ya mwandishi kumpa Mungu sadaka alizoahidi. Atawakaribisha wale waliokuwa wanateseka kula sehemu ya mnyama aliyemtoa sadaka.

wale wanaomtafuta Yahwe

Wale wanaotaka kumjua Yahwe na kumpendeza wanazungumziwa kana kwamba wanamtafuta Yahwe kwa uhalisia.

Mioyo yenu iishi milele

Hapa "mioyo" inawakilisha mtu mzima. "Na uishi milele"

Mioyo yenu

Hapa "yenu" inamaanisha watu walio dhulumiwa.

watakumbuka na kumgeukia Yahwe

Kuanza kumtii Yahwe kunazungumziwa kana kwamba watu wanamgeukia Yahwe kimwili. "watamkumbuka Yahwe na kumtii"

familia zote za mataifa zitasujudu chini mbele yako

Hii inamaanisha kitu kimoja na sehemu ya kwanza ya sentensi. Mwandishi anasisitiza kuwa kila mtu kutoka kila sehemu atamwabudu na kumtii Yahwe.

zitasujudu chini mbele yako

Hii ni alama ya kumpa utkufu na heshima mtu.

mbele yako

Hapa "yako" inamaanisha Yahwe. Inaweza kutafsiriwa katika hali ya mtu wa tatu ili ilingane na sehemu ya kwanza ya sentensi. "mbele yake"

Psalms 22:28

Kwa kuwa ufalme ni wa Yahwe

Hapa "ufalme" unaashiria utawala wa Mungu kama mfalme. "Kwa kuwa Yahwe ni mfalme"

yeye ni mtawala juu ya mataifa

Hapa "mataifa" yanaashiria watu wa mataifa. "anawatawala watu wa mataifa"

wata kuwa na karamu

Watu watakula pamoja kwenye karamu. "watakula pamoja" au "watakula chakula cha sherehe pamoja"

wale wote wanaoenda chini kwenye vumbi ... wale ambao hawawezi kuhifadhi maisha yao wenyewe

Misemo hii miwili inaashiria kundi moja. Zote zinamaanisha watu wote kwa kuwa watu wote watakufa.

wale wote wanaoshuka kwenye vumbi

Hapa "vumbi" linamaanisha kaburi. Msemo "wanaoshuka kwenye vumbi" ni njia ya kusema mtu anakufa. "wale wanaokufa" au "wale waliokufa"

wale ambao hawawezi kuhifadhi maisha yao wenyewe

"wale ambao hawawezi kuokoa maisha yao" au "wale ambao hawawezi kujizuia kufa"

Psalms 22:30

Kikazi kitakajokuja

Hapa "kizazi" kinawakilisha watu wa kizazi. "Msemo "kitakajokuja" inazungumzia muda wa baadaye kanakwamba ni kitu kinachosafiri na kufika sehemu. "watu wa vizazi vya baadaye"

kizazi kijacho

Hapa "kizazi" kinaashiria watu wa kizazi hicho. "watu wa kizazi kijacho" au "watoto wao"

cha Bwana

"kumhusu Bwana" au "kuhusu kile Bwana amefanya"

kusema kuhusu haki yake

Nomino dhahania ya "haki" inaweza kuelezwa kama kivumishi. "kusema kuhusu vitu vya haku alivyofanya"

Psalms 23

Psalms 23:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Yahwe ni mchungaji wangu

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kana kwamba alikuwa mchungaji. Hii inasisitiza jinsi Mungu anavyowajali watu kama mchungaji anavyowajali kondoo wake. "Yahwe ni kama mchungaji kwangu" au " Yahwe ananijali kama mchungaji anavyojali kondoo wake"

sitapungukiwa kitu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nina kila kitu ninachohitaji"

Ananifanya kulala chini kwenye malisho ya kijani

Mwandishi anajizungumzia kana kwamba ni kondoo, na anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni mchungaji. "Ananipa mapumziko kama mchungaji anavyowaongoza kondoo wake kulala chini kwenye malisho ya kijani"

ananiongoza kando kando na maji yaliyotulia

Mwandishi anajizungumzia kana kwamba ni kondoo, na anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni mchungaji. "ananipa ninachohitaji kama mchungaji anayewaongoza kondoo wake kando kando ya maji matulivu"

maji yaliyotulia

"maji yanayotiririka taratibu." Maji haya ni salama kunywa.

Psalms 23:3

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii inaendelea kueleza jinsi Mungu anavyotujali kama kondoo anavyowajali kondoo wake.

Hurudisha maisha yangu

Hii inamaanisha Mungu anamfanya mtu aliyenyonge na mchovu kuwa na nguvu na kupumzika tena.

huniongoza katika njia zilizonyooka

Kumwonyesha mtu jinsi ya kuishi katika njia inayo mpendeza Mungu inazungumziwa kana kwamba ni mchungaji anaonesha kondoo njia sahihi ya kuchukua. "Ananionesha jinsi ya kuishi sawa"

kwa ajili ya jina lake

Msemo "jina lake" hapa unamaanisha sifa yake. "kwa ajili ya jina lake" au "ili watu wamheshimu"

Psalms 23:4

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii inaendelea kueleza jinsi Mungu anavyotujali kama mchungaji anavyojali kondoo wake.

Ingawa ninatembea katika bonde la kivuli cha giza zaidi

Mwandishi anamwelezea mtu anayepitia matatizo makubwa kana kwamba ni kondoo anayetembea kwenye bonde hatari la giza. Huko kondoo anaweza kupotea au kuvamiwa na mnyama pori. "Ingawa maisha yangu ni kama kutembea katika bonde hatari la giza"

sitaogopa madhara

Nomino dhahania ya "madhara" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "Sitaogopa kitu kunidhuru"

uko nami

Aliye pamoja naye ni Yahwe.

gongo lako na fimbo yako hunifariji

Gongo na fimbo inaashiria ulinzi kwa sababu wachungaji walizitumia kuwalinda kondoo wao kutoka hatarini. "Siogopi kwa sababu unanilinda kama mchungaji anavyolinda kondoo wake kwa gongo na fimbo"

Psalms 23:5

Taarifa ya Jumla:

Sasa mwandishi anaeleza jinsi Mungu ni kama mtu anayemkaribisha mgeni nyumbani kwake na kumlinda.

Unaandaa

Meza inaashiria karamu kwa sababu watu huweka chakula chote mezani.

mbele ya adui zangu

Maana hapa ni kwamba mwandishi hana wasiwasi kuhusu adui zake kwa sababu yeye ni mgeni wa heshima wa Bwana na kwa hiyo analindwa na madhara. "licha ya uwepo wa adui zangu"

unatia kichwa changu mafuta

Watu wakati mwingine huweka mafuta kwenye vichwa vya wageni wao ili kuwapa heshima.

kikombe changu kinamwagikia

Hapa kikombe cha divai kinachotiririka kinaashiria baraka nyingi. "Unajaza kikombe changu sana hadi kinamwagikia" au "unanipa baraka nyingi"

Psalms 23:6

Hakika wema na uaminifu wa agano utanifuata

Yahwe kuwa mwema na mwaminifu kwa mtu inazungumziwa kana kwamba wema na uaminifu wa agano ni vitu vinavyomfuata mtu. "Hakika utakuwa mwema na mwaminifu kwangu"

siku zote za maisha yangu

Nomino dhahania ya "maisha" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "maadamu nina ishi"

nyumba ya Yahwe

Maana zinazowezekana ni kwamba 1) hii inamaanisha nyumba ya milele ya Yahwe, au 2) hii inamaanisha hekalu la Yahwe Yerusalemu.

kwa muda mrefu sana

Maana zinazowezekana ni 1) "milele" au 2) "maadamu nina ishi."

Psalms 24

Psalms 24:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

na ujao wake

Nomino dhahania "ujao" inaweza kuelezwa kama kitenzi "kujaza." "na kila kitu kinachoijaza"

Kwa kuwa ameiweka juu ya bahari na kuiweka juu ya mito

Wahebrania wa wakati huo waliamini kuwa nchi ilishikiliwa na bahari na mito ya chini ya ardhi. "Kwa kuwa aliumba misingi yake kwenye bahari na kuijenga juu ya maji mrefu"

bahari ... mito

Misemo hii miwili inatumika kumaanisha bahari kubwa yenye kina kirefu chini ya dunia.

juu ya mito

"maji yaliyo chini kwenye kina kirefu"

Psalms 24:3

Nani ataupanda mlima ... katika sehemu yake takatifu?

Maswali yote haya mawili ya maana moja. Mwandishi anauliza kuhusu nani anayefaa kwenda kumwabudu Yahwe.

kupanda

"kwenda juu"

mlima wa Yahwe

Hii inamaanisha mlima Sayuni ndani ya Yerusalemu

sehemu yake takatifu

Hii inamaanisha hekalu la Yahwe. Hekalu lake liko katika mlima Sayuni ulioko Yerusalemu.

Yeye aliye ...aliye ... na haja...

Hapa haimzungumzii mtu bayana. "Wale ambao ...walio ... na hawaja..."

aliye na mikono safi

Neno "mikono" inawakilisha kile ambacho mtu anafanya. Kwa "mikono" kuwa safi inamaanisha anafanya kilicho sawa. "anafanya kilicho sawa"

moyo safi

Hapa "moyo" inamaanisha mawazo au nia ya mtu. "anawaza mawazo mazuri" au "hawazi kuhusu yaliyo mabaya"

ambaye hajainua juu uongo

Hapa "uongo" inawakilisha sanamu ya uongo. "Kuinua juu" inamaanisha kuabudu. "ambaye hajaabudu sanamu"

Psalms 24:5

Atapokea baraka kutoka kwa Yahwe

Hapa hazungumziwi mtu yeyote bayana. Inamaanisha wale wenye mioyo safi waliotajwa kwenye mstari uliopita. Nomino dhahania ya "baraka" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "Yahwe atawabariki"

na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake

Nomino dhahania ya "haki" inaweza kuelezwa kama "kwa haki." Na "wokovu" unaweza kuelezwa kama "okoa." "na Mungu atatenda kwa haki naye na kumwokoa"

Ndivyo kilivyo kizazi cha wale wanaomtafuta

Hapa "kizazi" inawakilisha watu kwa ujumla. "Watu wanaomtafuta wako hivi"

wale wanaomtafuta, wale wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo

Misemo yote miwili ina maana moja. Yote inamaanisha wale wanaoenda hekaluni kumwabudu Mungu. "wale wanaomkaribia Mungu, wao ndio wanaweza kumwabudu Mungu, yule ambaye sisi Waisraeli tunamwabudu"

wale wanaomtafuta

Kwenda hekaluni kumwabudu Yahwe inazungumziwa kana kwamba mtu anatafuta kwa uhalisia kumpata.

uso wa Mungu wa Yakobo

Hapa "uso" unamaanisha mtu mzima. "Mungu wa Yakobo"

Psalms 24:7

Inueni vichwa vyenu, nyie malango; muinuliwe, malango ya milele

Misemo miwili ina maana za kukaribiana. "Malango" ni ile ya hekaluni. Mwandishi anazungumza na malango kana kwamba ni mtu. Mtu anayetunza malango ndiye huwepo kufungua malango. "Fungukeni, enyi malango ya zamani" au "Fungueni milango hii ya zamani"

Inueni vichwa vyenu

Haikowazi ni sehemu gani bayana ya lango ndio "kichwa." Lakini inawakilishi mlango mzima kwa ujumla.

Yahwe, mwenye nguvu na hodari; Yahwe, hodari vitani

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni shujaa hodari anapigana vitani.

Psalms 24:9

Inueni vichwa vyenu, nyie malango; muinuliwe, malango ya milele

Misemo miwili ina maana za kukaribiana. "Malango" ni ile ya hekaluni. Mwandishi anazungumza na milango kana kwamba ni mtu. Mtu anayetunza malango ndiye huwepo kufungua malango. "Fungukeni, enyi malango ya zamani" au "Fungueni malango haya ya zamani"

Inueni vichwa vyenu

Haikowazi ni sehemu gani bayana ya lango ndio "kichwa." Lakini inawakilishi lango lote kwa ujumla.

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 25

Psalms 25:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

nainua maisha yangu

Msemo "nainua maisha yangu" ni sitiari. Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi unajitoa kwa Yahwe, ambayo inamaanisha anamtegemea Yahwe kabisa. "nitajitoa kwako" au 2) aleta maombi na heshima kwa Yahwe. "ninakuabudu na kukuheshimu"

Usiniache niaibike

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Usiwaache adui zangu waniaibishe"

niaibike

"kudhalilika"

wafurahi kwa ushindi juu yangu

Msemo "juu yangu" unadokeza kuwa adui zake wamemshinda na kusima juu kwa ushindi. "wanishinde na kufurahia"

Na mtu yeyote anayekutumaini asiaibike

"Usiwaache wale wanaokutumaini waaibike." Aibu inaweza kuja kwa kushindwa na dui zao. Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "Usiwaache adui wawashinde wale wanaokutumaini"

anayekutumaini

"wanaokuamini"

fanya udanganyifu

"fanya uongo" au "fanya ujanja"

bila sababu

"bila chanzo"

Psalms 25:4

Unijulishe njia zako, Yahwe; nifundishe njia zako

Kauli hizi mbili zina maana moja. Mungu kumfundisha mtu jinsi anavyotakiwa kutenda inazungumziwa kana kwamba alikuwa akimwonyesha mtu njia sahihi ambayo mtu anapaswa kusafiria.

Nakutumaini

"Nakutegemea" au "Nakusubiri kwa uvumilivu"

Niongoze kwenye kweli yako na unifundishe

Niongoze na unifundishe zina maana sawa, kutoa maagizo. "Nielekeze kusimamia maisha yangu kwa kutii ukweli wako"

Mungu wa wokovu wangu

Nomino dhahania ya "wokovu" inaweza kuelezwa kama "'huokoa." "yule anayeniokoa"

Psalms 25:6

Kuweka

Hii ni lahaja. Hii haimaanishi kuwa Mungu amesahau kitu. Mwandishi anamuomba kufikiria na kuzingatia matendo yake ya huruma na uaminifu. "Kumbuka" au "Fikiria kuhusu"

matendo yako ya huruma na uaminifu wako wa agano

Nomino dhahania za "huruma" na "uaminifu" zinaweza kuelezwa kama vivumishi. "jinsi ulivyokuwa na huruma na mwaminifu kwangu kwa sababu ya agano lako"

kwa kuwa wamekuwepo daima

Hapa zinazozungumziwa ni huruma na uaminifu wa Mungu. "kwa kuwa hivyo ndivyo ulivyokuwa daima"

Usiwaze kuhusu dhambi za ujana wangu

Nomino dhahania ya "dhambi" inaweza kuelezwa kama "kutenda dhami." "Usiwaze jinsi nilivyotenda dhambi dhidi yako nilipokuwa mdogo"

au ukaidi wangu

Nomino dhahania ya "ukaidi" unaweza kuelezwa kama "kukaida." "au kusuhu jinsi nilivyokaidi dhidi yako"

Weka akilini

Hii ni lahaja. Hii haimaanishi kuwa Mungu amesahau kitu. Hii haimaanishi kuwa Mungu alisahau kitu. Mwandishi anamwomba Mungu kumwaza. "Nikumbuke" au "Nifikirie"

na uaminifu wa agano kwa sababu ya wema wako

Nomino dhahnia za "uaminifu" na "wema" zinaweza kuelezwa kama vitenzi. "na uwe mwaminifu kwangu kwa sababu ya agano lako, kwa kuwa u mwema"

Psalms 25:8

njia ... njia yake

Jinsi amabvyo Mungu anataka mtu kuwa inazungumziwa kana kwamba ni njia ambayo mtu anasafiri.

wanyenyekevu

Hiki kivumishi kidogo kinaweza kuelezwa kama kivumishi. "watu wanyenyekevu" au "wale ambao ni wanyenyekevu"

Psalms 25:10

Njia zote za Yahwe ni upendo imara na uaminifu

"Yahwe hutupenda daima kwa sababu ya agano lake na ni mwaminifu daima"

Kwa ajili ya jina lako

Msemo "jina lako" hapa unamaanisha sifa ya Yahwe. "Kwa ajili ya sifa yako" au "Ili kwamba watu wakuheshimu"

samehe dhambi yangu, kwa kuwa ni kubwa

Nomino dhahania ya "dhambi" inaweza kuelezwa ka "kutenda dhambi." "tafadhali nisamehe, kwa kuwa nimetenda dhambi sana"

Psalms 25:12

Ni nani mtu anayemcha Yahwe?

Swali linatumbulisha "mtu anayemcha Yahwe" kama mada mpya. "Nitakuambia kuhusu mtu anayemcha Yahwe"

mtu anayemcha ... mwelekeza ... anapaswa ... Maisha yake ...uzao wake

Hii haimaanisha mtu bayana. "ni wale wanaomcha ... anawaelekeza ... wanapaswa ... Maisha yao ... uzao wao"

Bwana atamuelekeza katika njia anayopaswa kuchagua

Yahwe kuwafundisha watu jinsi wanavyopaswa kuwa inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa akiwafundisha watu ni njia gani wanapaswa kuifuata.

Maisha yake yataenda katika wema

"Mungu atamsababisha kufanikiwa" au "Mungu atawasababisha kufanikiwa"

Psalms 25:14

Urafiki wa Yahwe ni kwa wale

"Yahwe ni rafiki kwa wale." Wengine wanatafsiri hii kama "Yahwe anawaambia siri wale." Kuwaambia siri inaonesha urafiki wa karibu alionao nao.

Macho yangu daima yako kwa Yahwe

Hapa "macho" yawakilisha kuangalia. kumwangalia Yahwe ni njia ya kusema anamuomba Yahwe msaada. "Huwa natazama kwa Yahwe" au "Huwa namuomba Yahwe msaada"

kwa kuwa ataokoa miguu yangu kwenye wavu

Wavu ni mtego. Mtu aliye hatarini anazungumziwa kana kwamba miguu yake imekwama katika wavu. "Ataniokoa katika

Geukia kwangu

Yahwe kuzingatia mtu kwa makini inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa akigeuka kimwili kuelekea kwa mtu huyo.

Psalms 25:17

Taabu za moyo wangu zimekuwa

Hapa "moyo" unawakilisha hisia za mtu. "Najihisi kutaabika zaidi na zaidi"

nitoe katika dhiki yangu

"nitoe kwenye dhiki yangu." Hii inazungumzia dhiki kana kwamba ni sehemu ambayo mtu anaweza kutolewa. "niokoe na dhiki yangu" au "nipumzishe na dhiki yangu"

dhiki zangu

Neno "dhiki" ni nomino dhahania. "vitu vinavyonipa dhiki" au "vitu vinavyosababisha niogope"

Tazama mateso yangu

"Tambua mateso yangu"

mateso yangu

Nomino dhahania ya "mateso" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "vitu vinavyonitesa" au "jinsi nilivyoteseka"

taabu zangu

Neno "taabu" ni nomino dhahania. "vitu vinavyonipa taabu"

wananichukia na chuki ya kikatili

"wananichukia kwa ukatili" au "wananichukia kwa ukali"

Psalms 25:20

usiniache niaibike

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Usiwaache adui zangu waniaibishe"

ninakukimbilia wewe!

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. "kwenda kwako kwa ajili ya ulinzi!"

Na uadilifu na unyofu unihifadhi

Hii inazungumzia "uadilifu" na "unyofu" kana kwamba ni watu wanaoweza kumweka mtu mwingine salama. Nomino dhahania hizi zinaweza kuelezwa kama vivumishi. "Na kuwa mwaminifu na kufanya kilicho sawa kilihifadhi" au "Nihifadhi, Bwana, kwa kuwa mimi ni mwaminifu na hufanya kilicho sawa"

unihifadhi

"uniweke salama"

Psalms 25:22

Iokoe Israeli

"Komboa Israeli"

Israeli ... shida zake

Hapa "Israeli" inawakilisha watu wa Israeli. "watu wa Israeli ... shida zetu"

Psalms 26

Psalms 26:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Nimetembea

Neno "kutembea" ni sitiari ya tabia. "Nimeenenda"

Yahwe

Matumizi ya mtu wa tatu wa "Yahwe" inaweza kuelezwa katika hali ya mtu wa pili. "wewe"

bila kuyumba

Mashaka yanazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni kuyumba na kupepea mbele na nyuma. "bila kuwa na shaka"

Nichunguze

"Nijaribu"

jaribu usafi wa sehemu zangu za ndani na moyo wangu

Hapa "sehemu za ndani" na "moyo" inamaanisha nia. "jaribu kama nia zangu ni nzuri"

Kwa kuwa uaminifu wako wa agano uko mbele ya macho yangu

Hapa "macho" yanawakilisha mawazo ya mtu. "Kwa kuwa huwa nawaza kuhusu jinsi ulivyo mwaminifu kwangu kwa sababu ya agano lako"

ninatembea katika uaminifu wako

Neno "kutembea" ni sitiari ya tabia. "Ninaendesha maisha yangu kulingana na uaminifu wako" au "Ninaenenda jinsi nilivyo kwa sababu ya uaminifu wako"

Psalms 26:4

Sijihusishi

"Sikai kundi moja na" au "Siketi na"

na watu waongo

"na wale wanao wadanganya wengine"

wala kujichanganya na watu wasio wakweli

Hii ina maana sawa na sehemu ya kwanza ya sentensi. "na sijiungi na watu wasio wakweli"

watu wasio wakweli

"wanafiki" au "wale wanao wadanganya wengine"

mkusanyiko wa watenda maovu

"wale wanao kusanyika kutenda maovu"

waovu

Hiki ni kivumishi kidogo. "watu waovu" au "wale walio waovu"

Psalms 26:6

Ninanawa mikono yangu katika sehemu isiyo na hatia

Hii inaonekana kumaanisha utaratibu wa kunawa mikono kwatika maji kuashiria uhuru kutoka dhambini au hatia.

kuizunguka madhabahu yako

Hili lilikuwa tendo la kuabudu amablo Waisraeli walizoea kufanya.

nyumba unayoishi

Maana zinazowezekana ni 1) kama mtu aliandiki hii baada ya wakati wa Daudi, basi mwandishi anamaanisha hekalu liliko Yerusalemu. au 2) kama Daudi aliandiki hii, basi hii inamaanisha hema ambalo Mungu aliwaambia watu wake kuandaa ili wamwabudu humo.

sehemu ambayo utukufu wako huishi

Hapa "utukufu" unawakilisha uwepo na nguvu ya Mungu, ambayo inakaribiana na mwanga mweupe sana. "sehemu ambayo watu wanaweza kuona mwanga wako mtukufu wa uwepo wako"

Psalms 26:9

usinifagie na watenda dhambi

"kufagia" ni sitiari ya maangamizi. "Usiniangamize pamoja na watenda dhambi"

au maisha yangu

Neno "fagia" linaeleweka. "au usifagie maisha yangu"

watu wenye kiu ya damu

Maneno "kiu ya damu" yanawakilisha mtu anayetaka kuua watu wengine. "watu wenye hamu ya kumwaga damu ya wengine" au "watu wauaji"

ambamo minono yao

"Mikono" inashiria mtu mzima. "watu ambao"

njama

"mpango uovu"

Psalms 26:11

Lakini kwangu

Msemo huu unaonesha kuwa mwandishi anabadilisha kutoka kuwazungumzia watu waovu na kujizungumzia mwenyewe.

nitatembea kwa uadilifu

"Kutembea" ni sitiari ya tabia. "Nitaenenda kwa uadilifu"

Mguu wangu unasimama

Hapa "mguu" unawakilisha mtu mzima. "Nina simama"

ardhi tambarare

Maana zinazowezekana ni kwamba "ardhi tambarare" inawakilisha 1) sehemu salama au 2) tabia iliyo sawa

katika makusanyiko nitambariki Yahwe

"nitakapowakusanya watu wa Israeli nitakusifu"

Psalms 27

Psalms 27:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Yahwe ni nuru yangu

Hapa "nuru" inawakilisha maisha. "Yahwe ni chanzo cha maisha yangu"

nimwogope nani?

Swali hili linaweka mkazo kuwa hakuna mtu ambaye Daudi anapaswa kumwogopa. "sitamwogopa mtu yeyote"

Yahwe ni kimbilio langu

Hii inamzungumzia Yahwe kana kwamba ni sehemu ambapo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya usalama. "Yahwe ndiye anayeniweka salama"

nimhofu nani?

Swali hili linaweka mkazo kuwa hakuna mtu ambaye Daudi anapaswa kumwogopa. "sitamhofua mtu yeyote"

Psalms 27:2

kuteketeza mwili yangu

Kumwangamiza mtu kabisa inazungumziwa kana kwamba ni kuangamiza mwili wa mtu. Hamaanishi kwamba walitaka kula mwili wake. "kuniangamiza"

washindani wangu na adui zangu

Maneno haya yana maana sawa. Hawa ndio watenda maovu walisogea karibu yake.

walijikwaa na kuanguka

Hii inaashiria adui wa mwandishi kushindwa kutimiza mipango yao kumdhuru mwandishi. "hawakufanikiwa"au "walishindwa"

Ingawa jeshi linweka kambi dhidi yangu

"ingawa jeshi linanizunguka" au "ingawa jeshi linanizunguka na mahema"

moyo wangu hautaogopa

Hapa "moyo" unawakilisha mtu mzima. "Sitaogopa"

ingawa vita zinainuka

Adui wa mwandishi wanazungumziwa kana kwamba wao wenyewe wako vitani. "ingawa adui zangu wanakuja kupigana na mimi"

nitabaki na ujasiri

"nitaendelea kumtumaini Mungu kunisaidia"

Psalms 27:4

nimemuomba Yahwe

"nimemuomba Yahwe kuniruhusu"

nitaitafuta hiyo

Mtu anayetaka kitu sana na kumwomba Mungu mara kwa mara kwa ajili yake inazungumziwa kama kutafuta kitu.

kuona uzuri wa Yahwe

Tabia nzuri ya Mungu inazungumziwa kana kwamba ni uzuri ya kimwili. "kuona jinsi Yahwe alivyo mzuri"

kutafakari katika hekalu lake

Maana zinazowezekana ni 1) "kumwuliza Mungu anataka nifanye nini" au 2) "kumtafakari Mungu kwa makini katika hekalu lake"

Psalms 27:5

katika siku ya taabu

Hapa "siku" inawakilisha muda mrefu zaidi. "katika wakati wa taabu" au "ninapokuwa na taabu"

atanificha

"atanilinda"

kivuli chake ... hema lake

Zote hizi zinamaanisha hema ambamo mwandishi anamwabudu Mungu.

katika mfuniko wa hema lake

Neno "mfuniko" inawakilisha kitu kinachoficha na kulinda.

Ataniinua juu ya mwamba

Mungu kumweka salama mwandishi kutoka kwa adui zake inazungumziwa kanakwamba Mungu alimuweka katika mwamba wa juu ambapo adui zake hawakuweza kumfikia.

kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu

Hii inawakilisha mwandishi kupokea sifa au heshima anapowashinda adui zake. Inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu wataniheshimu nitakaposhinda pambano langu dhidi ya adui zangu" au "Mungu atanipa heshima kwa kuniwezesha kuwashinda adui zangu"

Psalms 27:7

Sikia, Yahwe, sauti yangu

Hapa "sauti" inamaanisha kuwa mwandishi anasema. "Nisikie, Yahwe"

nijibu

Hii inaashiria kuwa Yahwe anasikia maombi ya mwandishi na Yahwe atafanya kile mwandishi anachoomba. "jibu ombi langu" au "fanya ninachokuomba"

Moyo wangu unasema

Hapa "moyo" unawakilisha akili na mawazo ya mtu. "Moyoni mwangu nasema" au "Ninajiambia"

Utafute uso wake

Mtu kwenda hekaluni kumwomba Yahwe inazungumziwa kana kwamba mtu huyo anamtafuta Yahwe. "Hapa "uso" unamwakilisha Mungu. "Nenda ukaombe kwa Yahwe"

Nautafuta uso wako, Yahwe

Mtu kwenda hekaluni kumwomba Yahwe inazungumziwa kana kwamba mtu huyo anamtafuta Yahwe. "Hapa "uso" unamwakilisha Mungu. "Nitakuja kwenye hekalu lako na kuomba kwako"

Psalms 27:9

Usiufiche uso wako kwangu

Uso unawakilisha usikivu wa Yahwe. Msemo "Usiufiche uso wako" ni njia kumwomba Mungu asimkatae. "Usinikatae" au "Usiache kunitunza"

usimgeuza mtumishi wako kwa hasira

Daudi alisema "mtumishi wako" kumaanisha ni yeye mwenywe kwa njia ya unyenyekevu. "usinikasirikie"

usiniache wala kunitupa

Maneno "kuacha" na "kutupa" yana maana sawa. Mwandishi anasisitiza kuwa hataki Mungu amuache.

wala kunitupa

"na usinitupe" au "na usiniache"

Mungu wa wokovu wangu

Nomino dhahania ya "wokovu" inaweza kuelezwa kama "okoa." "Mungu anayeniokoa" au "kwa kuwa wewe ni Mungu unayeniokoa"

Hata kama baba na mama yangu wakiniacha

Hasemi kuwa kweli wamefanya hivi au kwamba watafanya hivi. Wazo lake ni kwamba hata kama wangefanya hivyo, Mungu asingemuacha.

Yahwe atanichukua

"Yahwe atanitunza"

Psalms 27:11

Nifundishe njia yako

Jinsi mtu anavyopaswa kuenenda inazungumziwa kana kwamba ni njia ambayo mtu anapaswa kusafiri. "Nifundishe jinsi unavyotaka niishi" au "Nifundishe unachotaka nifanya"

Niongoze katika njia tambarare

Yahwe kumweka mwandishi salama na adui zake inazungumziwa kana kwamba Yahwe anamwongoza mwandishi katika njia tambarare ambapo hatajikwaa na kuanguka. "Niweke salama"

Usiniweka katika hamu za adui zangu

Nomino dhahania ya "hamu" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "Usiwaache adui zangu wafanye kwangu wanachotamani"

wameinuka dhidi yangu

"Kuinuka" ni lahaja inayomaanisha kuwa shahidi alisimama mahakamani kutoa ushuhuda. "wamesimama ili kuzungumza dhidi yangu"

wanapumua vurugu

Hapa vurugu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni kitu ambacho mtu anaweza kupumua nje. "wanasema kwamba watafanya vitu vya vurugu kwangu"

Psalms 27:13

Nini kingetokea kwangu

Swali hili balagha linaweza kuelezwa katika hali chanya. "Kitu kibaya kingetokea kwangu"

uzuri wa Yahwe

Nomino dhahania ya "uzuri" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "vitu vizuri ambavyo Yahwe hufanya"

katika nchi ya walio hai

Hii inamaanisha kuwa hai. "wakati niko hai"

Msubiri Yahwe ... msubiri Yahwe!

Mstari huu unaweza kuwa 1) mwandishi anazungumza mwenyewe au 2) mwandishi anazungumza na wengine au 3) mtu anazungumza na mwandishi.

acha moyo wako uwe na ujasiri

Hapa "moyo" unawakilisha mtu mzima. "uwe mjasiri"

Msubiri Yahwe!

Mstari huu umerudiwa mwishoni mwa zaburi kama njia ya kumalizia zaburi.

Psalms 28

Psalms 28:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

ninalia

"ninaita kwa sauti"

mwamba wangu

Hii ni sitiari ya nguvu. "nguvu yangu"

usiache kunijali

"usiwe kimya kwangu" au "usiniache mwenyewe"

Nitaungana na wale wanaoenda chini kaburini

Watu wanaokufa wanazungumziwa kana kwamba wanaenda kaburini. "Nitakufa kama wale waliomo kaburini"

Sikia sauti ya dua yangu

Hapa "sauti" inamaanisha maneno ya ombilake. "Sikia ombi langu kuu"

Napainulia mikono yangu mahali pako patakatifu

Kuinua mikono ni ishara ya kuabudu. Mwandishi haabudu mahali patakatifu, bali Yahwe anayeishi katika sehemu hiyo takatifu.

mahali pako patakatifu

Maana zinazowezekana ni 1) kama Daudi aliandika hii, basi hii inamaanisha hema ambalo Mungu aliwaambia watu wake kuandaa ili wamwabudu humo, au 2) kama ni mtu aliandika baada ya wakati wa Daudi, basi mwandishi anamaanisha hekalu lililoko Yerusalemu.

Psalms 28:3

Usinikokote

Mungu kuwaadhibu inazungumziwa kana kwamba anawakokota kimwili. Katika sitiari hii, Yahwe anaweza kuwa anawakokota kwenda gerezani, uhamishoni, au kifoni. "Usinitoe"

ambao wanazungumza amani na majirani zao

Hapa "majirani" inamaanisha watu kwa ujumla. "wanazungumza kwa amani na watu wengine"

lakini wana uovu mioyoni mwao

Hapa "mioyo" inawakilisha akili au mawazo ya mtu. "lakini wanawaza kitu kiovu kuwahusu"

Wape kile ambacho matendo yao maovu yanastahili ... walipe kile ambacho uovu wao unadai

Misemo hii miwili ina maana sawa. Inatumika pamoja kusisitiza kuwa wanastahili kuadhibiwa na Mungu.

kazi ya mikono yao

Hapa "mikono" inawakilisha kile ambacho mtu amaefanya"

warudishie wanachostahili

"wape wanachostahili"

Kwa sababu hawaelewi ... usiwajenge tena

Haiko wazi kama mstari wa 5 unaeleweka kama kauli au ombi.

hawaelewi matendo ya Yahwe

Inadokezwa kuwa "hawaelewi" inamaanisha hawajali au kuheshimu kazi za Yahwe. "hawajali kwa heshima kile ambacho Yahwe amefanya"

kazi ya mikono yake

Hapa "mikono" inawakilisha kile ambacho Yahwe amefanya au kuumba. "alichoumba"

atawavunja chini na hatawajengea tena

Adhabu ya watu waovu inazungumziwa kana kwamba walikuwa wakijenga mji utakaoangamizwa.

Psalms 28:6

amesikia sauti ya dua yangu

Hapa "sauti" inawakilisha kile mwandishi alichosema. "amesikia nilichosema nilipomwomba"

Yahwe ni nguvu yangu

"Yahwe ananifanya kuwa na nguvu"

ngao yangu

Hii inawakilisha ulinzi wa Yahwe kwa mwandishi.

moyo unamtumaini

Hapa "moyo" unamwakilisha mtu mzima. "Ninamwamini"

ninasaidiwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali yakutenda. "ananisaidia"

moyo unafurahi sana

Hapa "moyo" unamwakilisha mtu mzima. "ninafurahi sana"

Yahwe ni nguvu ya watu wake

"Yahwe anawafanya watu wake kuwa na nguvu"

ni kimbilio la wokovu la mtiwa mafuta wake

Yahwe kumweka mfalme salama inazungumziwa kana kwamba Yahwe ni sehemu ambayo mfalme anaweza kwenda kwa ajili ya usalama. "anamuweka salama yule aliyemchagua kuwa mfalme"

mtiwa mafuta wake

Hii inamaanisha mfalme.

Psalms 28:9

urithi wako

Hii inazungumzia watu wa Mungu kana kwamba walikuwa kitu ambacho Mungu alirithi. "mali yako" au "wale walio wako"

Uwe mchungaji wao na uwabebe milele

Mwandishi anazungumza kumhusu Yahwe kana kwamba ni mchungaji na watu ni kondoo wake. Mchungaji humbeba kondoo kama anahitaji msaada au ulinzi. "Uwe kama mchungaji na uwalinde milele"

Psalms 29

Psalms 29:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

wana wa Mungu

Msemo "wana wa" ni njia ya kusema "kuwa na sifa za." "nyie watu hodari"

Mpeni sifa kwa Yahwe kwa utukufu wake na nguvu

Nomino dhahania ya "utukufu" na "nguvu" zinaweza kuelezwa kama vitenzi. "Mpeni heshima Yahwe kwa kuwa ana utukufu na nguvu"

Mpeni Yahwe utukufu ambao jina lake linastahili

Nomino dhahania ya "heshima" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "Mheshimu Yahwe kama ambavyo jina lake linastahili" au "Tangazeni kuwa Yahwe ni mtukufu kama jina lake linavyostahili"

ambao jina lake linastahili

Msemo "jina lake" unamaanisha Yahwe au sifa yake. "kama ilivyo sahihi kwa sababu alivyo"

Psalms 29:3

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii inaonesha nguvu na utukufu wa Yahwe.

Sauti ya Yahwe inasisikika juu ya maji

Sauti ya Mungu ni kubwa na inasikika vizuri zaidi ya sauti na kelele zingine. Inaweza kusikika juu ya sauti zingine kubwa kama sauti ya maji. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe akizungumza sauti yake ni kubwa zaidi ya sauti ya bahari" au "Yahwe anapaza sauti zaidi ya sauti ya maji"

juu ya maji

Hii inamaanisha bahari. Maji haya hutoa sauti kubwa sana mawimbi yanapopanda na kushuka.

Sauti ya Yahwe

"Sauti" katika sehemu zote hapa inamwakilisha Yahwe akizungumza. Mwandishi anasisitiza kuwa wakati Yahwe anazungumza, sauti ni kubwa sana inasikika juu ya maji, na ina nguvu sana inaweza kuangamiza miti mikubwa . "Yahwe akizungumza, sauti yake"

Mungu wa utukufu anapiga radi

Hii inazungumzia juu ya Mungu kuzungumza kana kwamba ilikuwa ni sauti ya radi. Kama tu sauti ya radi, sauti ya Yahwe inaweza kusikika umbali mrefu. "Sauti ya Mungu wa utukufu ni kama radi kubwa" au "Wakati Mungu wa utukufu akizungumza inaunguruma kama radi"

juu ya maji mengi

"juu ya maji mengi"

Psalms 29:6

Kauli Unganishi:

Mwandishi anaendelea kuelezea nguvu ya sauti ya Mungu.

Anaifanya Lebanoni kurukaruka kama ndama

Lebanoni inazungumziwa kana kwamba ni ndama mchanga. Hii inasisitiza kwamba Yahwe akizungumza, nguvu ya sauti yake hutikisa ardhi. "Hufanya nchi ya Lebanoni kutikisika kama ndama anaye rukaruka"

kurukaruka

kuruka kidogo hapa na pale

Sirioni kama kama ng'ombe mdogo

Sirioni inazungumziwa kana kwamba ni ng'ombe mchanga. Hii inasisitiza kuwa Yahwe akizungumza, nguvu ya sauti yake hutikisia ardhi. "Huifanya Sirioni kuruka kama ng'ombe mchanga"

Sirioni

Huu ni mlima Lebanoni. Pia unaitwa mlima Hermoni.

Sauti ya Yahwe inatuma miali ya moto

Sehemu zote zenye "sauti" zinamaanisha Yahwe anazungumza. "Yahwe akizungumza husababisha miali ya radi kuonekana angani"

miali ya moto

hii inamaanisha mwale wa radi.

Psalms 29:9

Sauti ya Yahwe husababisha

Hapa "sauti" inamaanisha Yahwe anazungumza. "Yahwe akizungumza, sauti husababisha"

mwaloni kujikunja

"miti mikubwa kutikisika"

na kuuvua msitu

Kutoa majani ya miti inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kuvua nguo zao. "hutoa majani kwenye miti"

Yahwe ameketi kama mfalme

Hii inamaanisha kuwa Yahwe anatawala. "Yahwe anatawala" au "Yahwe ni mfalme"

juu ya mafuriko

Hapa "mafuriko" yanamaanisha maji yanayofunika dunia.

Psalms 29:11

Yahwe anawabariki watu wake na amani

Neno "amani" ni nomino dhahania. Yahwe huwabariki watu wake kwa kuwasababisha kufanikiwa na kuishi kwa amani"

Psalms 30

Psalms 30:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wakati wa kuweka wakfu hekalu

"Huu wimbo uliimbwa wakati hekalu linawekewa wakfu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

umeniinua

Mwandishi anazungumzia Mungu kumwokoa na kumwepusha na kufa kana kwamba Mungu amemuinua kutoka katika kisima kirefu. "umeniokoa"

umeinua nafsi yangu kutoka kuzimu

Kwa kuwa "kuzima" ilikuwa sehemu ambapo wafu huenda, inamaanisha kifo. "umeniepusha na kifo"

umeinua nafsi yangu

Hapa "nafsi yangu" inamaanisha mwandishi. "umenileta juu"

na kwenda chini kaburini

"Kaburi" linawakilisha kifo. "na kufa"

Psalms 30:4

Mpeni shukrani mnapo kumbuka utakatifu wake

Nomino dhahani "utakatifu" inaweza kuelezwa kama "takatifu." "Kumbukeni kuwa Mungu ni mtakatifu na mshukuruni" au "Kumbukeni kile ambacho Mungu amefanya kwa kuwa ni mtakatifu na mshukuruni"

hasira yake ni kwa muda tu

"hasira ya huduma kwa muda tu." Nomino dhahania ya "hasira" inaweza kuelezwa kama "kasirika." Anakasirika kwa muda tu"

muda

Hapa "muda" inaashiria muda mdogo. "muda mfupi"

lakini fadhila zakeni milele

Nomino dhahania ya "fadhila" inaweza kuelezwa kama kivumishi "mwema." "lakini yeye ni mwema kwetu maisha yetu yote"

Kulia kunakuja usiku, lakini furaha huja asubuhi

Hii inazungumzia "kulia" na "furaha" kana kwamba ni vitu vinavyo safiri na kufika kwa wakati fulani. "Tunaweza kulia wakati wa usiku, lakini asubuhi ijayo tutakuwa na furaha"

Psalms 30:6

Kwa ujasiri

Neno "ujasiri" ni nomino dhahania. Mwandishi anakumbuka kipindi alipokuwa akifanikiwa na kujihisi kuwa na ujasiri na salama. "Nilipokuwa na ujasiri" au "Nilipojihisi kuwa salama"

Sitatikiswa kamwe

Neno "kutikiswa" ni sitiari ya kushindwa. "Hakuna atakayenishinda"

kwa fadhila zako

Nomino dhahania "fadhila" inaweza kuelezwa kama kitenzi "pendelea" au kivumishi "huruma". "uliponipendelea" au "ulipokuwa na huruma kwangu"

umeniweka kama mlima imara

Usalama wa mwandishi unazungumziwa kana kwamba alikuwa mlima imara. "umenifanya salama kama mlima ulio juu"

ulipoficha uso wako

Hii ni lahaja. "ulipoacha kunisaidia" au "uliponikataa"

nilipata taabu

"niliogopa" au "nilikuwa na wasi wasi"

nikatafuta fadhila kutoka kwa Bawana wangu

Msemo "nikatafuta fadhila" inamaanisha kuomba msaada. "nilikuomba unisaidie"

kutoka kwa Bawana wangu

Mwandishi anamaanisha Yahwe katika hali ya mtu wa tatu. Inaweza kuelezwa katika hali ya mtu wa pili. "kutoka kwako, Bwana wangu"

Psalms 30:9

Kuna faida gani ... kuwa msaidizi wangu

Hii inaweza kuelezwa kama nukuuya moja kwa moja.

Kuna faida gani katika kifo changu, kama nikienda kaburini?

Mwandishi anatumia swali hili kusisitiza kuwa hatakuwa wa faida kwa Mungu kama akifa. "Hakuna faida katika kufa kwangu na kwenda chini kaburini"

Je, mavumbi yatakusifu? Yatatangaza uaminifu wako?

Mwandishi anatumia maswali haya kusisitiza kuwa mwili wake uliokufa na kuoza hauwezi kumsifu Mungu. "Mavumbi yangu hakika hayatakusifu au kuwaambia watu jinsi ulivyo mwaminifu"

mavumbi

Hii inamaanisha mwili wa mwandishi utakaooza na kuwa mavumbi atakapokufa. "mwili wangu uliooza"

Psalms 30:11

Umegeuza kuomboleza kwangu kuwa kucheza

Ili kuwa ni utamaduni kwa Wayahudi kucheza walipokuwa na furaha. Nomino dhahania "kuomboleza" na "kucheza" zinaweza kuelezwa kama vitenzi. "Umenisababisha niache kuomboleza na badala yake kucheza kwa furaha"

umeliondoa gunia langu

Gunia liliambatanishwa na kuomboleza na huzuni. "Umenisababisha kutokuwa na huzuni tena"

umenivika furaha

Mwandishi anazungumzia furaha kana kwamba ni vazi ambalo linaweza kuvaliwa. "umenisababisha kuwa na furaha"

utukufu wangu utakuimbia wewe sifa

Hapa "utukufu wangu" unamaanisha nafsi ya mwandishi au moyo wake. Hii inamaanisha mwandishi mzima, anaye mwabudu Mungu kwa sababu amemfanya kuwa na furaha. "nitakuimbia wewe sifa"

Psalms 31

Psalms 31:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Katika wewe Yahwe, ninakukimbilia

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. "Naenda kwako Yahwe, kwa ajiliya ulinzi"

usiniache niaibike kamwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "usiwaache wengine waniaibishe"

uwe mwamba wangu wa kukimbilia; ngome ya kuniokoa

Mseno "uwe mwamba wangu wa kukimbilia" ni ombi kwa ajili ya ulinzi. Msemo wa pili unawekea mkazo msemo wa kwanza.

mwamba wangu wa kukimbilia

Yahwe anazungumziwa kana kwamba yeye ni mwamba mkubwa ambao utamlinda mwandishi na mashambulio. "kama mwamba mkubwa ambao nitakuwa salama"

ngome ya kuniokoa

Yahwe anazungumziwa kana kwamba yeye ni ngome imara ambayo mwandishi anaweza kulindwa dhidi ya adui zake.

Psalms 31:3

mwamba wangu

Yahwe anazungumziwa kana kwamba ni mwamba mkubwa utakao mlinda mwandishi na shambulio. "kama mwamba mkubwa ambao nitakuwa salama"

ngome yangu

Yahwe anazungumziwa kana kwamba ni ngome imara ambao mwandishi atalindwa kutoka kwa adui zake.

kwa ajili ya jina lako

Katika msemo huu "jina" inamwakilisha Yahwe. "ili jina lako lipewe heshima" au "ili nilikuabudu"

niongoze na unichunge

Maneno "kuongoza" na "kuchunga" yana maana sawa na yana imarisha ombi kwambaYahwe amuongoze. "niongoze pale unapotaka niende"

Ning'oe kutoka kwenye wavu walioficha kwa jili yangu

Mwandishi anazungumziwa kana kwamba ni ndege aliye naswa katika wavu, na kumsubiri Yahwe kumweka huru kutoka kwenye mtego.

wewe ni kimbilio langu

Yahwe anazungumziwa kana kwamba ni sehemu ambayo mwandishi anaweza kujificha kutoka kwa watu wanao mshambulia. "wewe hunilinda daima" au "huwa unanipa ulinzi wakati wote"

Psalms 31:5

Katika mikono yako

Mungu ni roho, lakini hapa anazungumziwa kana kwamba ana mikono. Hapa "mikono yako" inamaansiha matunzo ya Yahwe. "katika matunzo yako"

ninaiweka roho yangu

Hapa "roho yangu" inamaanisha mwandishi. "ninajiweka"

Mungu wa uaminifu

"wewe ni Mungu ninayeweza kumtumaini"

Nawachukia wale wanaotumikia sanamu zisizo na faida

"Sanamu hazina faida. Nawachukia wale wanaoziabudu"

umeona mateso yangu ... ulijua dhiki ya nafsi yangu

Misemo hii miwili inaeleza wazo moja kuwa Mungu anajua kuhusu taabu za mwandishi.

dhiki ya nafsi yangu

Hapa "nafsi yangu" inamaani mwandishi. "dhiki yangu"

Psalms 31:8

Umeweka miguu yangu

Hapa "miguu yangu" inamaanisha mwandishi. "Umeniweka"

sehemu ya wazi pana

Waebrania waliona sehemu za wazi pana kama sitiari ya usalama na uhuru. "sehemu ambayo niko huru"

niko katika dhiki

"ninateseka sana"

nafsi yangu na mwili wangu

Maneno "nafsi" na "mwili" yanatumika kumwelezea mtu kamili.

Psalms 31:10

Kwa kuwa maisha yangu yamechoshwa

Hapa "maisha yangu" inamaanisha mwandishi. "Nimekuwa mnyonge sana"

na huzuni ... kwa kugumia

"kwa sababu ya huzuni yangu ... kwa sababu ya kugumia kwangu"

miaka yangu kwa kugumia

Msemo "kuchoka" haumo, ila unadokezwa. "miaka yangu imechoshwa kwa kugumia"

Nguvu yangu inashindwa

Hapa "Nguvu yangu" inamaanisha mwandishi. "Nimekuwa mnyonge"

mifupa yanguinapotea

Hapa "mifupa" inamaanisha afya ya kimwili ya mwandishi. "afya yangu inashindikana"

watu wananidharau

"watu wananitukana"

wanatishwa na hali yangu

"wanashtushwa na hali yangu"

Psalms 31:12

kama mtu mfu ambaye hakuna mtu

Mwandishi anasema kuwa watu wamemsahau sana hadi inakuwa kana kwamba ameshakufa tayari.

kama chungu kilicho vunjika

Mwandishi anajizungumzia kana kwamba hafai kabisa. "sifai kama chungu kilichovunjika"

kunong'ona kwa wengi

Inadokezwa kuwa "wengi" inamaanisha watu. "watu wengi wananisema"

habari za kuogofya kutoka kila upande

"taarifa za kutisha kutoka vyanzo vingi"

kuchukua maisha yangu

Lahaja hii inamaanisha kuua mtu. "kuniua"

Psalms 31:14

Hatima yangu iko mkononi mwako

Hapa "mkononi mwako" inamaanisha nguvu ya Yahwe. "Una nguvu ya kuamua hatima yangu"

wale wanaonifuatilia

"kutoka kwa watu wanaojaribu kunishika"

Fanya uso wako ung'ae kwa mtumishi wako

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kumtendea kwa fadhila kana kwamba uso wa Yahwe unang'aa mwanga juu yake. "Tenda kwa fadhili kwa mtumishi wako"

Psalms 31:17

Usiniache niaibike

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Usiwaache wengine wanifanye nijisikie aibu"

Na waovu waaibike!

"Natamani kwamba Mungu awaaibishe watu waovu!"

waovu

Hii inamaanisha watu waovu.

Na wawe kimya kuzimu. Midomo ya uongo inyamazishwe

Wazo hili linarudiwa kusisitiza hamu ya mwandishi kwamba sauti za waovu hazisikiwi.

Na wawe kimya kuzimu

Hapa "kuzimu" inawakilisha kifo. "Acha wafe ili wasiweze kuzungumza"

Midomo ya uongo

Hii inawakilisha watu waongo. "watu wanaodanganya"

inayozungumza dhidi ya wenye haki kwa ujasiri

"wanaosema mambo mabaya kuhusu watu wenye haki"

kwa dharau na kubeza

Maneno haya yana maana ya kufanana. "na dharau sana"

Psalms 31:19

Wema wako

Hii inaweza kuelezwa kama kitenzi. "ni vitu vizuri unavyofanya"

uliutunza

Wema wa Yahwe unazungumziwa kana kwamba ni kitu kinachoweza kutunzwa kama mazao. "unayoweka tayari kwa ajili ya matumizi"

wale wanao kuheshimu

"wale wanao kuheshimu sana"

wanao kukimbilia

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. "wale wanaoenda kwako kwa ajili ya ulinzi"

Katika kivuli cha uwepo wako; unawaficha... Unawaficha katika kivuli

Misemo hii miwili inamaanisha kuwa Mungu anawalinda.

katika kivuli

Uwepo wa Yahwe unazungumziwa kana kwamba ni jengo imara ambapo mwandishi atakuwa salama.

Unawaficha katika kivuli

Hapa "kivuli" kinawakilisha sehemu salama. "Unatoa sehemu salama kwa ajili yao"

dhidi ya vurugu ya ndimi

Hapa "ndimi" zinawakilisha watu wanaozungumza mambo makali sana dhidi ya mwandishi. "ambapo adui zao hawawezi kuzungumza uovu kwao"

Psalms 31:21

Nimekataliwa kutoka machoni pako

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Umenitoa katika uwepo wako"

machoni pako

Hapa "macho" yanamaanisha uwepo wa Yahwe. "uwepo wako"

ulisikia ombi langu la msaada

Hapa "ombi" linaweza kuelezwa na kitenzi. "ulinisikia nikiomba msaada"

Psalms 31:23

waaminifu

Hii inamaanisha watu waaminifu. "watu walio waaminifu"

huwalipa wenye kiburi kikamilifu

Hapa "kulipa" ni lahaja inayomaanisha kuwaadhibu. "anawapa watu wenye kiburi adhabu yote wanayostahili"

Psalms 32

Psalms 32:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

ambaye makosa yake yamesamehewa, ambaye dhambi zake zimefunikwa

Misemo hii ina maana ya kufanana. Inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambaye Mungu husamehe makosa yake na kufunika dhambi zake"

dhambi zake zimefunikwa

Hapa dhambi iliyosamehewa inazungumziwa kana kwamba imefunikwa ili isionekane. "ambaye dhambi yake haijaliwi" au "ambaye dhambi yake inasahauliwa makusudi"

ambaye Yahwe hamhesabii hatia

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambaye Yahwe anaona hana hatia" au "ambaye hana hatia kulingana na Yahwe"

ambaye rohoni mwake hakuna hila

Hapa "roho" inamaanisha mtu. "ambaye hakuna hila" au "ambaye ni mkweli kabisa"

Psalms 32:3

mifupa yangu ilikuwa inachakaa

Hapa "mifupa yangu" inamaanisha mwandishi. "nilikuwa nachakaa" au "nilikuwa nakuwa mdhaifu"

siku nzima

Lahaja hii inamaanisha "endelevu." "wakati wote"

mchana na usiku

Tofauti hizi zinajumlisha kila kitu katikati. "wakati wote"

mkono wako ulikuwa mzito juu yangu

Hapa "mkono" inamaanisha Yahwe. Msemo wote ni lahaja inayomaanisha "umenitesa." "umenifanya niteseke sana"

Nguvu yangu ilinyauka kama kwenye ukame wa majira ya joto

Nguvu ya Daudi inalinganishwa na mmea mdogo wa kijani unaogeuka kuwa wa rangi ya kahawia na kuanguka katika majira ya kiangazi.

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kihebrabia, na zingine haziliweki.

Psalms 32:5

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

katika kipindi cha dhiki kuu

"wakati wako katika taabu kubwa"

Kisha maji yakifurika, hayatawafikia hao watu

Matatizo yanazungumziwa kana kwamba ni mafuriko ya maji. "Kisha matatizo yatakapokuja kama mafuriko ya maji, watu hao watakuwa salama"

Psalms 32:7

Wewe ni maficho yangu

Yahwe anazungumziwa kana kwamba ni sehemu salama dhidi ya mashambulizi ya adui wa mwandishi. "Wewe ni kama sehemu ambayo naweza kujificha dhidi ya adui zangu"

Utanizunguka na wimbo wa ushindi

Sitiari hii inamaanisha kuwa ulinzi wa Yahwe kwa mwandishi ndio sababu ya nyimbo za ushindi alizoimba. "Kwa sababu yako nitaimba nyimbo za ushindi"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kihebrabia, na zingine haziliweki.

Nitakuelekeza na kukufundisha katika njia

Maneno "kuelekeza" na "kufundisha" zinamaana sawa na zinasisitiza maelekezo makini. "Nitakufundisha kila kitu kuhusu njia"

Nitakuelekeza

Hapa anayesema hivi ni Yahwe akimwambia Daudi.

katika njia unayopaswa kwenda

Kuishi katika njia sahihi inazungumziwa kana kwamba ni njia ambayo mwandishi anapaswa kutembea. "jinsi ya kuishi maisha yako"

na jicho langu juu yako

Hapa "jicho langu" linamaanisha Yahwe kuzangatia kwa umakini. "na kuweka umakini wangu kwako" au "kukuangalia"

Psalms 32:9

Usiwe kama farasi ... hawana uelewa

Mwandishi anawafananisha watu wasio na uelewa na farasi au nyumbu. Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi anazungumza maneno ya Yahwe kwa wasomaji wake, "Mnapaswa wote kutokuwa kama farasi ... hawana uelewa" au2) Yahwe anazungumza na mwandishi kana kwamba ni kundi la watu.

hatamu na lijamu

Vifaa viwili vinavyotumiwa na watu kuwaongoza farasi na nyumbu kwenda anapotaka mtu.

unapotaka

"popote mtu anapotaka waende."

zitamzunguka

Uaminifu wa Yahwe "utakaomzunguka" unasababisha ulinzi na uongozo."zitamwongoza" au "zitamlinda"

Psalms 32:11

Furahi katika Yahwe

Hapa "katika Yahwe" inamaanisha kile ambacho Yahwe aliwatendea. "Uwe na furaha kwa sababu ya kile ambacho amefanya Yahwe"

wenye haki

Hii inamaanisha watu. "watu wako watakatifu"

piga kelele ya furaha

"piga kelele kwa furaha" au "piga kelele kwa sababu ya furaha"

walio wanyofu moyoni

Hapa "moyo" inamaanisha mtu. "watu walio wanyofu"

Psalms 33

Psalms 33:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Furahi katika Yahwe

Hapa "katika Yahwe" inamaanisha kile ambacho Yahwe aliwatendea. "Furahini kwa sababu ya kile ambacho amefanya Yahwe"

kusifu kunawafaa wanyofu

"kumsifu Yahwe kunafaa kwa watu walio wanyofu"

Psalms 33:4

Taarifa ya Jumla:

Kila mstari una mistari miwili yenye maana za kufanana.

Neno la Yahwe ni imara

Hapa "imara" ni sitiari kwa jambo lililo la kweli. "Yahwe daima hufanya anachosema atafanya"

Anapenda haki na hukumu

Nomino hizi dhahania zinaweza kuelezwa kama vitendo. "Anapenda kufanya kilicho cha haki na sawa" au "Anawapenda wale wanaofanya kilicho cha haki na sawa"

Dunia imejaa uaminifu wa agano la Yahwe

Hapa "Dunia imejaa" ni lahaja inayomaanisha kwamba uaminifu wa agano unaweza kuonekana duniani kote. "Uaminifu wa agano la Yahwe unaweza kupitia duniani kote"

Kwa neno la Yahwe mbingu ziliumbwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kwa kutumia neno lake, Yahwe aliziumba mbingu"

kwa pumzi ya mdomo wake

Hii inamaanisha neno la Yahwe. "kwa neno lake"

Psalms 33:7

Taarifa ya Jumla:

Kila mstari una mistari miwili yenye maana za kufanana.

kama rundo

"kama nyuma ya bwawa." Mwandishi anaelezea uumbaji wa bahari kana kwamba Mungu anarundika maji yote pamoja.

anaweka bahari katika ghala

Mwandishi anaelezea uumbaji wa bahari kana kwamba Mungu anayaweka katika ghala. "anaweka bahari katika sehemu yake, kama mtu anayeweka mbegu katika ghala"

Acha dunia yote

Hii inamaanisha watu wa duniani. "Acha kila mtu duniani"

isimame kwa kumstaajabu yeye

Hapa "isimame kwa kumstaajabu" ni lahaja inayomaanisha "kustaajabu." "kumheshimu"

ikasimama

Hapa "ikasimama" ni lahaja inayomaanisha "iliumbwa." "kuanza kuwepo"

Psalms 33:10

Taarifa ya Jumla:

Kila mstari una mistari miwili yenye maana za kufanana.

Yahwe huzuia

"Yahwe huangamiza" au "Yahwe huvunja"

mwungano wa mataifa

Hapa "mataifa" yanamaanisha watu wa mataifa haya. "mwungano wa watu wa mataifa tofauti"

mwungano

Mwungano ni makubaliano kati ya mataifa mawili au zaidi kusaidiana katika vita dhidi ya adui mmoja.

mipango ya watu

"dhamira ya watu" "mipango ya uovu ya watu"

inasimama milele

Hapa "kusimama" ni lahaja inayomaanisha "kudumu."

mipango ya moyo wake kwa vizazi vyote

Neno ambalo halipo "kusimama" linadokezwa. "mipango ya moyo wake inasimama vizazi vyote"

mipango ya moyo wake

Hapa "moyo wake" inamaanisha Yahwe. "mipango yake"

kwa vizazi vyote

"kwa vizazi vyote vya mbeleni." Hii ni lahaja inayomaanisha "milele"

Limebarikiwa taifa

Hapa "taifa" linamaanisha watu wa taifa hilo. "Wamebarikiwa watu wa taifa"

ambalo Yahwe ni Mungu wake

"wanao mwabudu Yahwe kama Mungu"

kama urithi wake

Watu ambao Yahwe amewachagua kumwabudu wanaelezwa hapa kana kwamba ni urithi ulioupokea.

Psalms 33:13

anatazama chini

Sehemu ambayo Yahwe huishi inazungumziwa kana kwamba iko juu ya dunia wanayoishi watu.

anyeunda mioyo yao wote

Hapa "mioyo" inamaanisha kuwaza kwa hawa watu. Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuongoza kufikiri kwa watu kana kwamba alikuwa ni mfinyanzi anayeunda bakuli. "huongoza mawazo yao kama mfinyanzi anavyounda bakuli"

Psalms 33:16

Hakuna mfalme anayeokolewa kwa jeshi kubwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Jeshi kubwa sicho kinachomwokoa mfalme"

Farasi ni usalama wa uongo

Hapa "farasi" inawakilisha sehemu yenye nguvu zaidi ya jeshi. "Kuwa na jeshi lenye farasi imara halitoi usalama"

Psalms 33:18

Tazama

Neno hili linaonesha kuwa wazo jipya linaanza katika zaburi hii. "Angalia" au "Sikiliza" au "Zingatia ninachotaka kukuambia"

jicho la Yahwe

Hapa "jicho" linamaanisha umakini au usikivu wa Yahwe. "Usikivu wa Yahwe"

wanao tegemea

"wanaosubiri" au "wanaotumaini"

kuokoa maisha yao na mauti

Hapa "maisha yao" inamaanisha watu. "kuwaepusha na kufa"

Psalms 33:20

Tunamsubiri Yahwe

"Kusubiri" hapa ni lahaja inayomaanisha kutumaini. "Tunamwamini Yahwe" au "Tunamtumaini Yahwe"

yeye ni msaada wetu na ngao yetu

Hapa Yahwe anazungumziwa kana kwamba ni ngao inayowalinda askari vitani. "yeye ni msaada wetu na hutulinda kama ngao"

Mioyo yetu inafurahi

Hapa "mioyo" inamaanisha watu. "Tunafurahi"

katika jina lake takatifu

Hapa "jina takatifu" linamaanisha tabia takatifu ya Yahwe. "katika tabia yake takatifu" au "katika yeye kwa sababu ni mtakatifu"

Psalms 33:22

kuwa nasi

Lahaja hii inamaanisha "tusaidie." "tenda kwa faida yetu" au "tusaidie" au "tulinde"

tunapoweka tumaini letu kwako

"tunapotumaini msaada wako"

Psalms 34

Psalms 34:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

kujifanya kuwa mwenye wazimu

"kuigiza kama mtu chizi"

mbele ya Abimeleki

Hii inamaanisha tukio bayana la kihistoria ambalo Wahebrania wanafahamu vizuri. "alipokuwa katika nyumba ya Abimeleki" au "alipokuwa mfungwa wa Abimeleki"

mfukuza

"mwondoa kwa nguvu"

sifa yake daima itakuwa mdomoni mwangu

Hapa "mdomoni mwangu" inamaanisha Daudi kumzungumzia Mungu. "daima nitamsifu kwa sauti"

Psalms 34:2

walio kandamizwa

Hii inamaanisha watu walio kandamizwa. "watu walio kandamizwa"

Msifuni Yahwe pamoja na mimi

Kitenzi "msifuni" ni amri kwa kikundi. "Kila mtu anapaswa kumsifu Yahwe pamoja na mimi"

inueni jina lake

Hapa "inueni" ni lahaja inayomaanisha kumtukuza Yahwe. "waambieni watu jinsi alivyo mkuu"

jina lake

Hapa "jina lake" linammanisha tabia ya Yahwe. "tabia yake"

Psalms 34:4

Nilimtafuta Yahwe

Hapa "Nilimtafuta Yahwe" inamaanisha kuwa Daudi alikuwa akimwomba Yahwe msaada. "Niliomba kwa Yahwe" au "Nilimwomba Yahwe msaada"

Wale wanaomtazama

Hapa "wanaomtazama" inawakilisha kutafuta msaada kutoka kwake. "Wale wanaomtazama yeye kwa ajili ya msaada" au "wale wanaotegemea msaada kutoka kwake pekee"

wanang'aa

Lahaja hii inamaanisha mwonekano wao kuwa wa furaha. "wana furaha"

nyuso zao hazina aibu

Hapa "nyuso zao" inamaanisha watu wanaomtazama Yahwe. Inaweza pia kuelezwa katika hali chanya. "hawana aibu" au "wana majivuno"

Mtu huyu aliye kandamizwa

Daudi anajieleza kama mtu aliye kandamizwa. "Nilikandamizwa na"

Yahwe akamsikia

Hapa "kusikia" inamaana kuwa Yahwe alimsaidia. "Yahwe alinisikia" au "Yahwe alinisaidia"

Psalms 34:7

huzungusha kambi

Malaika wa Yahwe anazungumziwa kana kwamba alikuw ani jeshi linalozungusha kambi kwa mtu ili kuwalinda. "hulinda"

Onjeni mwone Yahwe yu mwema

Wema wa Yahwe unazungumziwa kana kwamba ni kitu kinachoweza kuonjwa na kuonwa. "Jaribuni na mwone kuwa Yahwe ni mwema"

anaye mkimbilia

Yahwe anazungumziwa kana kwamba ni sehemu ambayo watu wanaweza kujificha kwa ajili ya ulinzi kutoka kwa adui zao. "mwamini kuwalinda"

Hakuna upungufu kwa wale wanaomcha yeye

Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "Wale wanaomcha daima watakuwa na kile wanachohitaji"

Psalms 34:10

hawatapungukiwa chochote kizuri

Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "daima watakuwa na vitu vizuri wanavyohitaji"

wana

Hapa hii haimaanishi wana wa mwandishi halisi, lakini watu anaowafundisha kuhusu Yahwe. "wanafunzi wangu"

Psalms 34:12

Kuna mtu gani anayetamani maisha na kupenda siku nyingi, ili aone mema?

Jibu linalodokezwa la swali hili ni "kila mtu." Swali hili balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Kila mtu anatamani maisha na anatamani kuishi siku nyingi na kuwa na maisha mazuri"

weka ulimi wako mbali na uovu ... weka midomo yako mbali na kuongea uongo

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na inasemwa katika njia tofauti ili kusisitiza umuhimu wake.

Basi weka ulimi wako mbali na uovu

Hapa "ulimi" inamaanisha mtu mzima. "Basi, usizungumze uongo"

weka midomo yako mbali na kuongea uongo

Hapa "midomo" inamaanisha mtu anayezungumza. "usizungumze uongo"

Ugeuke uovu

Hapa "ugeuke" ni sitiari ya kuepuka na uovu. "Kataa kufanya uovu"

Tafuta amani

Hapa "kutafuta" inamaanisha kujihusisha na amani. "Jaribu kwa bidii kuishi kwa amani na watu wengine"

Psalms 34:15

Macho ya Yahwe yako juu ya wenye haki

Hapa "macho ya Yahwe" inamaanisha kutazama kwake kwa makini. "wenye haki" inamaanisha watu wenye haki. "Yahwe huwatazama kwa makini watu wenye haki"

mskio yake yameelekezwa kwa kilio chao

Hapa "maskio yake" inamaanisha hamu ya Yahwe kuwajibu. "anazingatia kilio chao" au "anajibu kilio chao"

kukata kumbukumbu yao duniani

Yahwe atawasababisha watu wawasahau kabisa watakapokufa hadi inakuwa kana kwamba ametumia kisu kuikata kumbukumbu yao. "ili watakapokufa, watu watawasahau kabisa"

Yahwe husikia

Hapa "husikia" inamaanisha kuwa Yahwe anatamani kuwajibu. "Yahwe anawazingatia"

Psalms 34:18

Yahwe yuko karibu

Hapa "yuko karibu" inamaana "tayari kusaidia." "Yahwe yuko tayari kusaidia"

walio vunjika moyo

Huzuni kubwa inazungumziwa kana kwamba moyo wa mtu umevunjika. "watu walio na huzuni sana"

wale walio pondeka rohoni

Watu waliokata tamaa sana wanazungumziwa kana kwamba roho zao zimepondwa. "watu waliokata tamaa sana"

wenye haki

Hii inamaanisha watu wenye haki. "watu wenye haki"

Anatunza mifupa yake yote, hakuna hata moja itakayovunjika

Hapa "mifupa yake" ni halisia, lakini pia inaashiria kuwa yahwe anamtunza mtu mzima. "Anatoa ulinzi kamili kwake, hatadhuriwa kwa njia yoyote"

Psalms 34:21

Uovu utawaua waovu

Uovu unazungumziwa kana kwamba mtu anayeweza kuua watu. "Matendo maovu ya watu waovu yatawaua"

waovu

Hii inamaanisha watu waovu.

Wale wanaowachukia wenye haki watahukumiwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawahukumu wale wanaowachukia wenye haki"

wenye haki

Hii inamaanisha watu wenye haki.

Hakuna atakaye hukumiwa kwa wanaomkimbilia

Hii inaweza kutafsiriwa katika hali ya kutenda. Inaweza pia kutafsiriwa katika hali chanya. "Yahwe atawasamehe wote wanaomkimbilia"

wanaomkimbilia

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. 'kwenda kwake kwa ajilil ya ulinzi"

Psalms 35

Psalms 35:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Kamata ngao yako ndogo na ngao kubwa ... mkuki wako na shoka ya vita

Misemo hii inamwelezea Mungu kama shujaa ambaye anajiandaa kwa ajili ya vita.

ngao yako ndogo na ngao kubw

hizi ni silaha za kujilinda

mkuki wako na shoka ya vita

hizi ni silaha za mashambulizi

wale wanaonifukuza

Maana zinawezekana ni 1) hawa ni adui wanaomfukuza mwandishi kiuhalisia au 2) hii ni sitiari ya watu ambao ni adui wa mwandishi.

sema kwa nafsi yangu

Hii inamaanisha mwandishi. "sema kwangu"

Mimi ni wokovu wako

"Mimi ni mwokozi wako" au "Nitakuokoa"

Psalms 35:4

Na wale wanaotafuta maisha yangu waaibike na kunyimwa heshima

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na Yahwe awaaibishe na kuwanyima heshima wale wanaotafuta maisha yangu"

Na

"Natamani kwamba"

wanaotafuta maisha yangu

Hapa "maisha yangu" inamaana wanatamani kumuua mwandishi. "wanaojaribu kuniua"

Na wale wanaopanga kunidhuru wageuzwe na washangazwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na Yahwe awageuze na kuwashangaza wale wanaopanga kunidhuru"

wageuzwe

"wageuzwe" ni sitiari ya kushindwa kutimiza lengo lao. "kushindwa kufanikiwa"

washangazwe

"wachanganyikiwe" au "kuwafadhaisha"

kama makapi mbele ya upepo

Adui wa mwandishi wanazungumziwa kana kwamba ni nyasi ambayo inapulizwa kwa urahisi. "kupulizwa na upepo kama makapi"

njia yao

Hapa "njia yao" inamaanisha maisha yao. "maisha yao"

giza na utelezi

Hii inamaanisha njia iliyojificha na hatari. "imejificha na imejaa hatari"

anawafukuza

Hii inamaanisha malaika wa Yahwe kuwa kinyume na adui wa mwandishi. "anaenda kinyume nao" au "anawapinga"

Psalms 35:7

wanaliandaa wavu wao kwa ajili yangu

Njama za waovu zinazungumziwa kana kwamba ni wavu walioweka kumnasa mwandishi.

walichimba shimo kwa ajili ya maisha yangu

Njama za waovu zinazungumziwa kana kwamba ni shimo walilochimba kumkamata mwandishi. "walitaka kunishika katika shimo kama mnyama mkubwa"

maisha yangu

Hii inamaanisha mwandishi. "mimi"

Acha maangamizi yawapite kwa kushtukiza

Maangamizi yanazungumziwa kana kwamba ni mnyama hatari ambaye atawavamia ghafla. "Acha waangamizwe ghafla" au "Acha washtukizwe kwa sababu umewaangamiza ghafla"

wavu waliouandaa

Njama za waovu zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa ni wavu walioweka kumnasa mwandishi. "wavu walioweka ili kuninasa kama mnyama na kunidhuru"

Acha waanguke humo

Hii ni sitiari kama mstari wa 7. Wavu umekusudiwa kumnasa mwandishi. "Acha waanguke katika shimo walilo nichimbia"

waanguke humo

Maana zinazowezekana ni 1) kuanguka katika shimo la mstari wa 7 au 2) kuanguka katika uharibifu.

maangamizi yao

"ili waangamizwe" au "hivyo ndivyo unavyopaswa kuwaangamiza"

Psalms 35:9

katika wokovu wake

Nomino dhahania "wokovu" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "kwa kuwa umeniokoa"

Mifupa yangu yote

Hapa "mifupa" inamaanisha undani zaidi wa mtu. "Undani wangu wote"

Yahwe, ni nani aliye kama wewe ... wale wanao jaribu kuwaibia?

Jibu linalodokezwa kwa hili swali ni kwamba hakuna aliye kama Yahwe. "Yahwe, hakuna aliye kama wewe ... wale wanaojaribu kuwaibia"

maskini na wahitaji

Maneno "maskini" na "wahitaji" yana maana ya kufanana na yanasisitiza kuwa Yahwe anawaokoa wengi wanaohitaji msaada wake.

Psalms 35:11

inuka

Hii inamaanisha kuwa wanashuhudia katika majaribu. "kujitolea kutoa ushuhuda"

Wananilipa maovu kwa mema

Hii ni sitiari inayomaanisha wanarudisha marejeo maovu kwa mema waliyopokea. "Kwa kunirudishia kutenda wema wangu, wanafanya vitu viovu kwangu"

maovu ... mema

Nomino dhahania hizi zinaweza kuelezwa katika hali zingine. "vitu viovu ... vitu vizuri"

Nina huzuni

"Nina huzuni sana"

Psalms 35:13

walipokuwa wagonjwa

Wagonjwa hapa inamaanisha "mashahidi waovu"

Nilivaa gunia

"Nilionesha kuwa nina huzuni"

na kichwa changu kikiwa kimeinamishwa kifuani mwangu

Hii ilikuwa ishara ya maombi. "na kichwa changu kimeinama chini katika maombi"

katika majonzi kama kwa ndugu yangu

Mwandishi alikuwa na huzuni kana kwamba ndugu yangu amekufa. "kuhuzunika kana kwamba ndugu yangu mwenyewe alikuwa ameugua"

Niliinama katika kuomboleza kama kwa mama yangu

Mwandishi aliomboleza kana kwamba mama yake amekufa. "Niliomboleza kana kwambamama yangu amekufa"

Niliinama

Hii ilikuwa alama ya maumivu na mateso.

Psalms 35:15

wakakusanya pamoja

"kukusanyika pamoja" au "wakaja pamoja"

dhidi yangu

Hii inamaanisha walikuja pamoja kwa kusudi la kumshambulia mwandishi. "kufanya mipango dhidi yangu" au "kupanga uharibifu"

Wakanirarua

Hapa walimtendea mwandishi kana kwamba alikuwa kipande cha nguo walichoweza kurarua vipande vipande. "Walinivamia"

Bila heshima yoyote wakanidhihaki

"Walinidhihaki na watu wasio na faida kabisa" au 2) "walinikejeli bila heshima"

wakanisagia meno

Hii ni alama ya hasira na chuki. "walinifanyia sauti za kusaga kwa meno yao"

Psalms 35:17

hadi lini utanitazama?

Hili swali la balgha linaashiria kuwa mwandishi anamtaka Mungu kuacha tu kumtazama na kuanza kumsaidia. "hadi lini utawatazama tu wakifanya hivi" au "utanisaidia lini"

Okoa nafsi yangu

Hapa "nafsi" inamaanisha mwandishi. "Niokoe"

maisha yangu kutoka kwa simba

Neno "okoa" linadokezwa. "okoa maisha yangu kutoka kwa simba"

maisha yangu

Hii inamaanisha mwandishi. "mimi"

kutoka kwa simba

Hapa mwandishi anazungumzia adui zake kana kwamba ni simba wakali. "kutoka kwa adui zangu wanaonivamia kama wanyama pori"

Psalms 35:19

Usiache adui zangu waongo

"Usiache adui zangu, wanaosema uongo kunihusu,"

njama zao za uovu

"mipango yao ya uovu"

hawazungumzi amani

"hawazungumzi kwa amani na watu"

kupanga maneno ya uongo

"wanatafuta njia za kusema uongo"

wale katika nchi yetu wanao ishi kwa amani

"wale wanaoishi kwa amani katika nchi yetu"

ishi kwa amani

"usimdhuru yeyote"

Psalms 35:21

Wanafungua midomo wazi yao dhidi yangu

Sababu ya kufungua midomo yao ni kumshtaki mwandishi. "Wananipigia kelele ili wanashtaki"

Aha, Aha

Huu ni mshangao unaotumika wakati kitu kinaonekana ghafla au kueleweka. Unaweka mkazo katika kauli inayofuata.

macho yetu yameona

Hapa "macho yetu" inamanisha macho ya adui. Inadokezwa kuwa wanasema kwamba wamemwona mwandishi anafanya kitu kibaya. "tumeona" au "tumeona makosa uliyofanya"

Umeiona

Hapa walichoona ni mashtaka ya uongo ya adui wa mwandishi. "Umeona jinsi walivyonishtaki kimakosa"

usiwe kimya

"usiache kujali walichonifanyia." Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "wahukumu kwa sababu ya kile walichofanya"

usiwe mbali na mimi

Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "uwe karibu sana na mimi"

Jiinue na uamke

Hii haimaanishi kuwa Mungu kweli yuko usingizi. Mwandishi anataka Mungu aingilie kati. Maneno yote yana maana moja na yanasisitiza uharaka wa ombi hili. "Nahisi kama umelala! Amka"

kwa utetezi wangu

"kunilinda"

madai yangu

Hii inamaanisha mwandishi. "mimi"

Psalms 35:24

usiwaache wafurahi juu yangu

"usiwaache wafurahi kwa sababu ninateseka"

waseme moyoni mwao

Hii ni lahaja inayomaanisha kujisemesha. "wajisemeshe"

Aha

Huu ni mshangao unaotumika wakati kitu kinaonekana ghafla au kueleweka. Unaweka mkazo katika kauli inayofuata. "Ndio"

tumepata tunalichokuwa tunataka

Inadokezwa kuwa adui wa mwandishi walitaka atangazwe kuwa na hatia. "ametangazwa kuwa na hatia kama tulivyokuwa tunatamani!"

Tumemmeza

Adui wa mwandishi wanazungumzia uharibifu wake kana kwamba waoni wanyama pori waliommeza. "Tumemwangamiza"

shangaze

"aibishe" au "fadhaishe"

Na wale wanao nidhihaki wafunikwe na aibu na kukosa heshima

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na uwafunike kwa aibu na kukosa heshima wale wanao nidhihaki"

nidhihaki

kumtukana mtu ili kumkasirisha

wafunikwe na aibu na kukosa heshima

Hapa aibu na kukosa heshima zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa nguo za aibu ambazo mwandishi aliweza kuvaa. Nomini dhahania hizi zinaweza kuelezwa kama vitenzi. "waaibishwe na kukosa heshima"

aibu na kukosa heshima

Haya maneno yana maana za kukaribiana na yanatumika kuonesha ni kiasa gani watashushwa.

Psalms 35:27

uthibitisho wangu

Hapa "uthibitisho" unamaanisha Yahwe kumtangaza au kumhukumu mwandishi wa zaburi kuwa hana hatia.

na waseme kwa kuendelea

"na daima waseme"

Yahwe asifiwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Acha tumsifu Yahwe"

anaye furahi katika

"anayefurahishwa na" au "anayefurahishwa kwa"

ustawi

hali njema, furaha

sema kuhusu haki yako

"kutangaza kuwa unatenda yaliyo sawa"

Psalms 36

Psalms 36:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi mtumishi wa Yahwe

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Dhambi inazungumza kama mwaguzi

Dhambi inaelezwa kana kwamba ni nabii wa uongo. "Dhambi ni kama nabii wa uongo anayezungumza"

katika moyo wa mtu mwovu

Hapa "moyo" inamaanisha hali ya ndani wa mtu. "hali ya ndani ya mtu mwovu"

mtu mwovu

Hii haimaanishi mtu bayana, lakini kwa watu waovu kwa ujumla. "watu waovu"

katika macho yake

Hapa "macho" yanamaanisha mtu mwovu. "ndani yake"

anajifariji, akifikiri

"anapendelea kuamini" au "anataka kufikiri"

dhambi yake haitagunduliwa na kuchukiwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu hatagundua na kuchukia dhambi yake"

Psalms 36:3

Maneno yake ni

Hii inamaanisha kauli zake. "Anachosema ni"

kufanya mema

"kufanya vitu ambavyo ni vyema"

anaenda katika njia ya uovu

Vitendo vya dambi vyamtu vinazungumziwa kana kwamba alikuwa akitembea kwenye njia ambayo ilikuwa na uovu.

hapingi uovu

"hapingi tabia za uovu"

Psalms 36:5

unafika mbinguni

Ukuu wa uaminifu wa Mungu wa agano unazungmziwa kana kwamba uko juu sana. "uko juu kama mbingu" au "ni mkuu sana"

unafika kwenye mawingu

Ukuu wa uaminifu wa Mungu unazungumziwa kana kwamba uko juu sana. "uko juu kama mawingu" au "ni mkuu sana"

kama milima ya Mungu ... kama kina kirefu

Misemo hii inaeleza ukuu wa haki ya Mungu na hukumu zake kana kwambazilikuwa juu zana na zenye kina kirefu. "juu kama mlima ya juu zaidi ... mrefu kama bahari lenye kina kirefu zaidi"

unatunza

"unasaidia" au "unaokoa"

Psalms 36:7

Jinsi ulivyo wa thamani uaminifu wako wa agano

Uaminifu wa Agano wa Mungu unazungumziwa kana kwamba kilikuwa kito adimu na cha gharama. "Uaminifu wako wa agano ni wa thamani kama kito adimu.

Wanadamu hukimbilia

"Watu watatafuta ulinzi"

Wanadamu hukimbilia chini ya kivuli cha mbawa zako

Mungu hana mbawa kweli. Hii ni sitiari ya ulinzi wa Mungu. "Wanadamu hukimbilia kwako kama ndege wadogo wanavyotafuta ulinzi chini ya mbawa za mama yao"

Wataridhishwa tele

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Utawaridhisha tele"

kwa wingi wa chakula katika nyumba yako

Hii haimaanishi kuwa Mung ana nyumba yenye chakula. Hii ni sitiari ya utoaji wa vitu tele. "kana kwamba wanakula chakula kizuri kutoka katika nyumba yako" au "kwa baraka zako nzuri"

utawaacha wanywe kutoka katika mto wa baraka zako za thamani

Kuna sitiari mbili hapa. Baraka tele za Mungu zinazungumziwa kana kwamba ni maji yanayotiririka katika mto. Pia, wale wanaopokea hizo baraka wanazungumziwa kana kwamba wanazinya kama maji. "baraka zako za thamani ni kama mto ambao utawaruhusu wanywe kutokea humo"

chechemi ya uzima

"chanzo cha maisha"

katika nuru yako tunaona nuru

Hapa "nuru" ni sitiari ya maarifa ya kweli. "unapotuelimisha, tutajua ukweli" au "nuru yako ndio inayotuwezesha kujua ukweli kukuhusu"

Psalms 36:10

Endeleza uaminifu wa agano lako kikamilifu

"Endeleza uaminifu wako wa agano"

ulinzi wako kwa wanyofu wa moyo

"Endelea" inadokezwa kutoka katika msemo uliopita. "Endelea kuwalinda wanyofu wa moyo"

wanyofu wa moyo

Hapa "moyo" inamaanisha watu. "wanyofu" au "watu wanaoenenda kwa haki"

mguu wa aliye na majivuno ... mkono wa mwovu

Hapa "mguu" na "mkono" inamaanisha watu waovu. Hawa sio watu bayana. Hii inamaanisha watu waovu kwa ujumla. "watu wenye majivuno ... watu waovu"

uniondoe

"unifanye niondoke sehemu yangu"

watenda maovu wameanguka; wameangushwa chini na hawawezi kuinuka

Misemo hii mitatu inaeleza watenda maovu kama watu walioshindwa.

wameangushwa chini

"umewaangusha chini" au "umewaangamiza"

hawawezi kuinuka

"hawawezi kuinuka"

Psalms 37

Psalms 37:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Usikasirike kwa sababu ya watenda maovu

"Usiwaruhusu watu waovu wakukasirishe" au "Usisumbuliwe na kile ambacho watu waovu wanafanya"

watakauka kama nyasi ... kunyauka kama mimea ya kijani

Watenda maovu wanazungumziwa kana kwamba ni nyazi na mimea iliyokauka na inakufa katika hali ya hewa ya joto. Mifanano hii miwiliyote inamaana kuwa watakufa. "kufa" au "kufika mwisho"

Psalms 37:3

chunga katika uaminifu

Uaminifu unazungumziwa kana kwamba ni mnyama atakepata nguvu kwa kula katika malisho mazuri. "rutubisha uaminifu" au "zidisha uaminifu wako"

hamu zako za moyoni

Hapa "moyo" unawakilisha hali ya ndani ya mtu na mawazo. "hamu zako za ndani" au "vitu unavyotamani zaidi"

Psalms 37:5

Mpe Yahwe njia zako

Hapa "kumpa njia zako" ni lahaja inayomaanisha kumwomba Yahwe kuongoza maisha yako. "Mwombe Yahwe aongoze matendo yako katika maisha"

atatenda kwa niaba yako

Hii ni kumwakilisha mwingine katika mambo ya kisheria. Hapa, mtu anayemtumaini Yahwe, atamlinda mtu huyo na kumpa haki mtu huyo.

kama mchana ... kama siku mchana

Misemo hii yote ina maana ya kufanana.

kama mchana

Hii inamaanisha "mbele ya watu wote." "wazi kuona kama mwanga wa mchana"

kama siku mchana

HIi inamaanisha "kuonekana kama jua la mchana." "kuonekana kama nuru wakati wa mwanga zaidi mchana"

Psalms 37:7

Uwe mtulivu

"Uwe kimya"

Psalms 37:8

watakatwa

Uharibifu wa waovu unazungumziwa kana kwamba walikuwa ni matawi ya mmea uliokatwa na kutupwa.

lakini wale wanaomsubir yahwe

"lakini wale wanaomtumaini Yahwe"

watarithi nchi

Kumiliki nchi kunazungumziwa kana kwamba itapokelewa kama urithi. "watapokea nchi kama urithi wao" au "wataishi kwa usalama katika nchi"

atapotea

Lahaja hii inamaanisha kifo cha mtu mwovu. "atakufa na hautamwona tena"

Psalms 37:11

wapole

Hii inamaanisha watu walio wapole. "watu wapole"

watarithi nchi

Kumiliki nchi kunazungumziwa kana kwamba itapokelewa kama urithi. "watapokea nchi kama urithi wao" au "wataishi kwa usalama katika nchi"

mtu mwovu

Hii haimaanishi mtu bayana. Inamaanisha watu waovu kwa ujumla. "mtu mwovu"

mwenye haki

Hii haimaanishi mtu bayana. Inamaanisha watu wenye haki kwa ujumla. "mtu mwenye haki"

kusaga meno

Mtu mwovu anamchukia mtu mwenye haki sana hadi anasaga meno yake pamoja kuonesha hasira yake.

siku yake inakuja

Inadokezwa kuwa "siku yake" itakuwa siku ya hukumu. "siku inakuja ambapo Yahwe atamhukumu na kumwadhibu" au "siku inakuja ambapo Yahwe atamhukumu na kumwadhibu mtu mwovu"

Psalms 37:14

Waovu

Hii inamaanisha watu waovu. "Watu waovu"

wametoa upanga wao ... wamekunja upinde wao

"Upanga" na "upinde" zote ni silaha zinazotumika kushambulia watu. Kitendo kwamba zimetolewa na kukunjwa inamaanisha kuwa wako tayari kushambulia. "wameandaa silaha zao ili kushambulia"

kuwatupa chini

Uharibifu wa watu wahitaji unazungumziwa kana kwamba ni vyombo vya udongo vinavyoweza kuvunjika katika vipande vikitupwa chini. "kuwaangamiza"

waliokandamizwa na wahitaji

Misemo hii inamaana watu wale wale wasio na uwezo wa kujilinda. "watu wasio weza kuwapinga"

Panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe

Panga ni mfano wa silaha na "mioyo" inawakilisha watu. "Kuchoma moyo" ni lahaja inayomaanisha "kuua." "Silaha zao zitageuzwa kwao na watajiua wenyewe"

Psalms 37:16

Bora kidogo alichonacho mwenye haki kuliko kingi cha watu waovu wengi

Hapa mstari wa pili ni tofauti na wa kwanza. "Ni bora kuwa mwenye haki, hata kama inamaanisha utakuwa maskini, kuliko kuwa mwovu na utajiri mkubwa"

Bora kidogo alichonacho mwenye haki

"Ni bora kuwa mwenye haki, hata kama inamaanisha utakuwa maskini"

kidogo

Hii inamaanisha kuwa na mali kidogo.

mwenye haki

Hii inamaanisha mtu mwenye haki. "mtu mwenye haki ana"

kingi

Hii inamaanisha utajiri wa watu waovu.

Kwa kuwa mikono ya watu waovu itavunjwa

Hapa "mikono" inawakilisha nguvu ya watu waovu. Kuvunja mikono yao inawakilisha kuwanyanganya nguvu yao. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kwa kuwa Yahwe ataondoa uwezo wa watu waovu"

Psalms 37:18

huwaangalia wasio na lawama

"Kuangalia" inamaanisha kumlinda mtu. Hapa 'wasio na lawama" inamaanisha watu wasio na lawama. "huwalinda watu wasio na lawama"

siku kwa siku

"kila siku" au "kwa kuendelea"

wakati nyakati ni mbaya

Msemo huu unamaanisha maafa, kama njaa. "maafa yanapotokea"

Psalms 37:20

Adui wa Yahwe watakuwa kama utukufu wa malisho

Mwandishi analinganisha adui wa Yahwe na maua yanayo chanua katika mashamba.

watateketezwa na kupotea katika moshi

Mwandishi anazungumzia uharibifu wa waovu kwana kwamba ni magugu au maua yaliyo nyauka shambani yanayochomwa baada ya mavuno. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawaangamiza kama moto unavyogeuza magugu ya shamba kuwa moshi"

ni mkarimu na hugawa

Hizi zina maana moja na zinasisitiza ukarimu wa wenye haki.

Psalms 37:22

Wale walio barikiwa na Mungu

"Wale ambao Mungu anawabariki"

watarithi nchi

Umiliki wa nchi unazungumziwa kanakwamba umepokelewa kama urithi. "watapokea nchi kama mali yao" au "wataruhusiwa kuishi kwa usalama katika nchi"

wale waliolaaniwa naye

"wale ambao Yahwe amewalaani"

watakatwa

Uharibifu wa watu waovu unazungumziwa kana kwamba ni tawi la mmea uliokatwa na kutupwa.

Ni kupitia Yahwe hatua za mtu zinaimarishwa ... inpendeza machoni pa Mungu

"Kama mtu anaishi katika njia ya kupendeza machono pa Yahwe, Yahwe ataimarisha njia zake"

Ni kupitia Yahwe hatua za mtu zinaimarishwa

"Yahwe ndiye anayemwezesha mtu kufanikiwa"

mtu ... mtu

Hii haimaanishi mtu bayana, lakini kwa watu kwa ujumla.

hatua za mtu

Hatua zinawakilisha jinsi mtu anavyoishi. "jinsi mtu anavyoishi"

Ingawa anajikwaa, hataanguka

Hapa "kujikwaa" na "kuanguka" inamaanisha jinsi mtu anavyojibu katika vipindi vigumu. "Ingawa ana vipindi vigumu, hatashindwa kabisa"

anamshika kwa mkono wake

Hapa "mkono wake" inamaanisha nguvu ya Yahwe, na "kumshika" inamaanisha kumlinda. "kumlinda na nguvu yake"

Psalms 37:25

mtu mwenye haki ameachwa

"Yahwe amwacha mtu mwenye haki"

mtu mwenye

Hii haimaanishi mtu bayana. Ni kauli ya ujumla.

wakiomba mkate

Hapa "mkate" inwakilisha chakula kwa ujumla. "kuomba chakula"

Siku nzima

Lahaja hii inamaanisha tendo hili ni tabia ya maisha yake.

watoto wake wanakuwa baraka

"watoto wanakuwa kuwabariki wengine"

Geuka

Kuacha kufanya kitu inazungumziwa kana kwamba mtu ankigeuka. "Acha kufanya"

Psalms 37:28

Wanatunzwa milele

"Yahwe atawalinda milele"

watakatwa

Uharibifu wa waovu unazungumziwa kana kwamba walikuwa tawi la mmea uliokatwa na kutupwa.

wenye haki

"watu wenye haki"

watarithi nchi

Umiliki wa nchi unazungumziwa kana kwamba umepokelewa kama urithi. "watapokea nchi kama urithi wao" au "wataruhusiwa kuishi katika nchi kwa usalama"

Mdomo wa mtu mwenye haki

Hapa "mdomo" unawakilisha mtu mzima anayezungumza. "Mtu mwenye haki"

huzungumza hekima

"huwapa wengine ushauri wa hekima"

huongeza hukumu

"huwatia moyo watu wengine kuishi kwa haki"

Psalms 37:31

Sheria ya Mungu wake moyoni mwake

Hapa "moyo" unamaanisha hali yake ya ndani zaidi. "Anathamini amri za Mungu wake ndani mwake"

miguu yake haitateleza

Kushindwa kwake kumtii Yahwe kunazungumziwa kama kuteleza kwenye njia salama au kuanguka. "atatembea salama katika njia ambayo Mungu anataka atembee" au "atafanya kwa usalama vitu ambavyo Mungu anataka afanye"

Mtu mwovu ... mtu mwenye haki ... mtu mwovu

Hawa sio watu bayana. Inamaanisha aina hii ya watu kwa ujumla.

humtazama mtu mwenye haki

Hapa kutazama inaashiria kuwaangalia wenye haki ili kuwadhuru. "husibiri ili kumvamia mtu mwenye haki"

mkono wa mtu mwovu

Hapa "mkono" unawakilisha uwezo au nguvu. "uwezo wa mtu mwovu"

anapohukumiwa

Hii inamaanisha Yahwe kumhukumu mtu mwenye haki. "Yahwe atakapomhukumu"

Psalms 37:34

atakuinua kumiliki nchi

Hapa "kuinuka" inamaanisha Mungu kuwapa heshima wale wanaomsubiri. "atakuheshimu kwa kukupa nchi"

waovu

"watu waovu"

wanakatwa

Uharibifu wa waovu unazungumziwa kana kwamba walikuwa tawi la mmea uliokatwa na kutupwa.

Psalms 37:35

waovu na mtu wa kutisha

Hii haimaanishi mtu bayana. Ni kauli ya ujumla.

wanasambaa kama mti wa kijani katika udongo wake wa asili

Hapa mafanikio ya mtu mwovu yanazungumziwa kana kwamba ni mti wenye afya unaoota kwatikaudongo mzuri.

hakupatikana

"Sikuweza kumpata" au "Yahwe alimchukua"

Psalms 37:37

mtu wa uadilifu

Hii haimaanishi mtu bayana. Ni kauli ya ujumla.

mwekee alama mnyofu

"waangalia kwa makini watu wazuri"

siku za usoni za mtu mwovu zimekatwa

"Mungu atasitisha uzao wake" au "hatakuwa na uzao"

siku za usoni

Hii inamaanisha uzao wake. "uzao wake"

mtu mwovu

Hii haimaanishi mtu bayana. Ni kauli ya ujumla.

zimekatwa

Uharibifu wa waovu unazungumziwa kana kwamba walikuwa tawi la mmea uliokatwa na kutupwa.

Psalms 37:39

Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Yahwe

"Yahwe huokoa watu wenye haki"

wenye haki

"watu wenye haki"

huwasaidia ... huwaokoa ... huwaokoa

Wazo hilo hilo linarudiwa kwa njia tofauti kusisitiza kuwa Yahwe ni wa kutegemewa na anaweza kutoa msaada.

wamemkimbilia

Kwenda kwa Yahwe kunazungumziwa kama kumkimbilia. "wameenda kwake kwa ajili ya ulinzi"

Psalms 38

Psalms 38:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

usinikemee katika hasira yako ... usiniadhibu katika gadhabu yako

Misemo hii inamaana moja na wazo linarudiwa kwa ajili ya mkazo.

mishale yako inanichoma

Ukali wa adhabu ya Yahwe kwa mwandishi unazungumziwa kana kwamba Yahwe amepiga mishale kwa mwandishi. "Adhabu yako ina maumivu kana kwamba umepiga mishale kwangu"

mkono wako unanikandamiza chini

Adhabu ya Yahwe kwa mwandishi inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa akimponda mwandishi kwa mkono wake.

Psalms 38:3

Taarifa ya Jumla:

Daudi anaendelea kueleza kile amabacho hatia na aibu yake inavyoufanya mwili wake. Anatumia kauli iliyokuzwa kuweka mkazo madhara ya somo hili.

hakuna afya katika mifupa yangu kwa sababu ya dhambi yangu

Hapa "mifupa yangu" inawakilisha mwili wa mwandishi. "mwili wangu wote unaugonjwa kwa sababu ya dhambi yangu"

udhalimu wangu unanilemea

Udhalimu wa mwandishi unazungumziwa kana kwamba ni mafuriko ya maji yanayomfunika. "udhalimu wangu unanifunika kama mafuriko"

ni mzigo mzito sana kwangu

Udhalimu wa mwandishi unazungumziwa kana kwamba ni mzigo asioweza kuinua. "ni kama mzigo ulio mzito sana kwangu kunyanyua"

Psalms 38:5

Taarifa ya Jumla:

Daudi anaendelea kueleza kile amabacho hatia na aibu yake inavyoufanya mwili wake. Anatumia kauli iliyokuzwa kuweka mkazo madhara ya somo hili.

Vidonda vyangu vimeathirika na vinanuka

Hapa "kunuka" inamaanisha vidonda vyake kuwa na harufu mbaya inayoambatana na kuoza kwa nyama. "Vidonda vyangu vimeathirika na vinanuka vinavyooza"

Nimeinama

Maumivu ya mwandishi yamemsababisha ainame kana kwamba ni mzee aliyechoka. "Nimeinama kwa maumivu"

Psalms 38:7

nimejawa na kuungua

Mwandishi ana homa sana hadi inakuwa kana kwamba anaungua ndani. "Mwili wangu unachemka kwa homa"

hakuna afya katika mwili wangu

Hapa "mwili" unamaanisha mwandishi. "Ninaumwa sana"

kupondeka kabisa

Ugonjwa wa mwandishi ni mkali sana hadi inakuwa kana kwamba uzito unamkandamiza chini.

uchungu wa moyo wangu

Hapa "moyo wangu" unamaanisha mwandishi. "uchungu wangu"

Psalms 38:9

haja zangu za moyo za ndani

Hapa "moyo" unamaanisha mwandishi. "Hamu zangu kuu" au "kuwa natamani uniponye"

magumio yangu hayajafichwa kwako

Hii inaweza kuelzwa katika hali ya kutenda. "unaweza kuona

moyo wangu unadunda

"unaweza kuona kulia kwangu kwa huzuni"

nguvu yangu inapotea

"ninakuwa mnyonge sana"

kuona kwangu kunafifia

"Siwezi kuona vizuri tena"

Psalms 38:11

wanalaza mitego kwa ajili yangu

Mipango ya waandishi wa adui wanazungumziwa kana kwamba ni mitego walitega kumshika kama mnyama. "kuweka mitego kunishika"

huzungumza maneno ya uharibifu na kusema maneno ya udanganyifu

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na inasisitiza uasili wa kuumiza wa kile ambacho watu hawa wanasema.

Psalms 38:13

Niko kama kiziwi ... sisikii ... asiyesikia

Mistari ya kwanza ya mstari wa 13 na 14 inatumia tashbihi kuwakilisha picha moja ya mtu kiziwi. Mwandishi anaumwa sana hadi hasikii.

Mimi ni kama bubu ... hasemi kitu ... hana jibu

Mistari ya kwanza ya mstari wa 13 na 14 inatumia tashbihi kuwakilisha picha moja ya mtu bubu. Mwandishi anaumwa sana hadi hazungumzi.

bubu

mtu asiyeweza kuongea

Psalms 38:15

utajibu

Maana zinazowezekana ni 1) "utanijibu" au 2) "utawajibu adui zangu."

wasinicheke

"hawatafurahi juu ya shida yangu"

Kama mguu wangu ukiteleza

Hapa "mguu" unmwakilisha mwandishi. Kuteleza kwa mguu wake ni sitiari inayomaanisha matatizo ya mwandishi na bahati mbaya. "Kama nikifanya makosa ya kunisababishia taabu"

Psalms 38:17

ninataka kujikwaa

Maana zinazowezekan kwa sitiari hii ni 1) "ninaumwa sana hadi ninataka kufa" au 2) "nitaangamia hivi karibuni."

niko kwenye maumivu endelevu

"niko kwenye maumivu daima"

Psalms 38:19

Lakin adui wangu ni wengi ... ni wengi

Misemo hii miwili inamaana sawa.

Wananilipa uovu kwa uzuri

Matendo ya adui wa mwandishi yanazungumziwa kama mapatano ya kibiashara ambapo walimpa vitu viovu kwa kubadilishana na vitu vizuri. "Wananipa matendo maovu kwa kubadilishana na matendo yangu mazuri kwao"

wanatupa mashtaka kwangu

Jinsi adui wa mwandishi wanavyomshtaki inazungumziwa kana kwamba wanatupa mashtaka kwake kama mawe.

nimefuata kilicho chema

Hamu ya mwandishi kwa kilicho chema kinazungumziwa kana kwamba anakimbilia vitu vizuri.

Psalms 38:21

Usiniache ... usikae mbali na mimi

Misemo hii miwili ina maana za kufanana sana.

usikae mbali na mimi

Kwa sababu Yahwe bado hajajibu ombi la mwandishi, anamzungumzia Yahwe kana kwamba yahwe alikuwa amesimama mbali na mwandishi.

Njoo upesi kunisaidia

Mungu anazungumziwa kana kwamba anakimbia kwenda kwa mwandishi kumsaidia.

wokovu wangu

"wewe ndiye unayeniokoa"

Psalms 39

Psalms 39:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Yeduthuni

Mmoja wa wanamuziki wakuu wa Daudi alikuwa na jina hili. Hii inaweza kumaanisha ni yeye.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Nitachunga ninachozungumza

"Nitakuwa msikivu katika vitu nitakavyosema"

ili nisitende dhambi kwa ulimi wangu

Hapa "ulimi" inamaanisha maneno ya mwandishi. "ili nisizungumze maneno mabaya dhidi ya Yahwe"

nitajitia lijamu

Hii inamaanisha kufunga mdomo. Hapa Daudi anamaanisha kuwa hatazungumza akiwa na mtu mwovu.

Psalms 39:2

Nilikaa kimya; nilitunza maneno yangu

Misemo hii miwili inamaana moja na inasisitiza kuwa mwandishi hakuzungumza kabisa. "Nilikuwa kimya kabisa"

nilitunza maneno yangu

Hapa "maneno yangu" inamaanisha maneno ya mwandishi. "sikuzungumza"

Moyo wangu ukachemka ... ukawaka kama moto

Hapa "moyo" unamwakilishi mtu mzima. Mawazo ya wasiwasi ya mwandishi yanazungumziwa kana kwamba ni moto unaomuunguza ndani yake. "Nikawa na wasiwasi sana nilipowaza hivi vitu"

Psalms 39:4

mwisho wa maisha yangu ... kiasi cha siku zangu

Misemo hii inamaana moja.

Nioneshe jinsi nilivyo wa kupita

"Nioneshe jinsi maisha yangu yalivyo mafupi" au "Nioneshe nitakavyokufa mapema"

upana wa mkono wangu tu

Mwandishi anazungumza kana kwamba yanaweza kupimwa na upana wa mkono wake. "muda mdogo sana"

maisha yangu ni kama bure mbele yako

Tashbihi hii inaeleza kuwa urefu wa maisha ya mwandishi ni mafupi sana hadi hayapo. Hii ni kukuza kwa neno kuonesha jinsi yalivyo mafupi. "urefu wa maisha ni muda kidogo sana"

Hakika kila mtu ni pumzi moja

Ufupi wa maisha unazungumziwa kana kwamba ulikuwa ni sawa na muda unaochukua mtu kupumua mara moja. "Muda ambao wanadamu huishi ni mfupi kama pumzi moja ya mtu"

Psalms 39:6

Hakika kila mtu anatembea kama kivuli

Maisha ya watu yanazungumziwa kana kwamba sio ya muhimu kama vivuli. "Kila mtu anapotea kama vivuli vinavyofanya"

ingawa hawajui nini atawapokea

Hapa inadokezwa kuwa hawajui kitakachotokea kwa utajiri watakapokufa.

Sasa, Bwana, ninasubiri nini?

Mwandishi anauliza hili swali kusisitiza kuwa watu hawawezi kumsaidia. "Kwa hiyo, Yahwe, sitegemei kupokea kitu kutoka kwa mtu mwingine"

Psalms 39:8

Niko kimya ... siwezi kufungua mdomo wangu

Misemo hii inamaana moja.

kwa sababu ni wewe uliyekifanya

""kwa sababu adhabu yangu inatoka kwako"

Psalms 39:10

Acha kuniumiza

Adhabu ya Mungu kwa mwandishi inazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa akimuumiza kwa silaha. "tafadhali acha kuniadhibu!"

nimelemewa

"nimeshindwa kabisa"

pigo la mkono wako

Adhabu ya Mungu kwa mwandishi inazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa akimpiga kwa mkono wake. Hapa "mkono" unawakilisha hukumu ya Mungu. "hukumu yako kwangu"

unameza vitu wanavyotamani kama nondo

Mungu atachukua vitu wanavyojali katika njia moja nondo anavyokula kipande cha nguo. "unameza vitu wanavyotamani kama nondo anavyokula nguo"

watu wote sio kitu ila mvuke

Mwandishi anazungumza udhaifu wa watukana kwamba ni umande unaopotea haraka. "kila mtu ni dhaifu kabisa"

Psalms 39:12

Sikia ombi langu ... nisikilize ... sikia kilio changu

Misemo hii mitatu inamaana moja na inaonesha jinsi mwandishi anavyotaka Mungu amjibu.

Usiwe kiziwi kwangu

Mwandishi anazungumzia Yahwe kutomjibu kana kwamba ni kiziwi. "Usiache kunijali kana kwamba huwezi kunisikia"

Mimi ni kama mgeni kwako, mkimbizi

Mwandishi anazungumzia Yahwe kutomjibu kana kwamba Yahwe alikuwa akimchukulia kama mgeni kabisa kwake. "Mimi ni kama mgeni kabisa kwako"

Usinikazie macho

Hapa "kukazia macho" inawakilisha adhabu ya Yahwe. "Tafadhali acha kuniadhibu"

ili ni tabasamu tena

Hapa "kutabasamu" inahusishwa na kuwa na furaha. "ili niweze kuwa na furaha tena"

Psalms 40

Psalms 40:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Nilimsubiri Yahwe kwa uvumilivu

Hii inamaanisha mwandishi alimsubiri Yahwe kumsaidia.

alinisikiliza ... kusikia kilio changu

"alinisikia nilipomwita"

nje ya shimo baya, nje ya udongo wa tope

Sitiari hizi mbili zinamaanisha kitu kimoja. Hatari ya mwandishi inazungumziwa kana kwambani shimo hatari la tope. Hii inawekea mkazo hatari. "kutoka kunaswa kwenye shimo baya lililojaa tope ya kunata.

ameweka miguu yangu kwenye mwamba

Hapa "miguu" inamaanisha ni mwandishi, na "mwamba" inamaanisha sehemu ya usalama. "alitoa usalama kwa ajili yangu"

Psalms 40:3

Ameweka wimbo mpya mdomoni mwangu

Maana zinazowezekana ni 1) "Amenifundisha maneno ya wimbo mpya" au 2) "Amenipa sababu mpya ya kuimba"

mdomoni mwangu

Hapa "mdomo wangu" inamaanisha mwandishi. "ndani yangu"

sifa kwa Mungu wetu

"wimbo wa kumsifu Mungu wetu"

Wengi wataona

Hapa "wataona" inamaanisha kumsikia mwandishi akiimba wimbo kuhusu kile ambacho Mungu amemtendea. "Watu wengi watasikia kile ambacho Yahwe amefanya"

Amebarikiwa mtu anayemfanya Yahwe tumaini lake

"Amebarikiwa mtu anayemtumaini Yahwe" au "Wale wanaomtumaini Yahwe wamebarikiwa"

wenye kiburi

Hii inamaanisha watu walio na kiburi.

uongo

Maana zinazowezekana ni 1) "uongo" au 2) "miungu ya uongo"

Psalms 40:5

Mawazo yako juu yetu hayahesabiki

"hakuna mtu awezaye kuhesabu vitu vyote unavyotuwazia"

hayahesabiki ... zaidi ya yanayoweza kuhesabika

Misemo hii inamaana sawa. Ya kwanza imeelezwa katika hali hasi na ya pili katika hali chanya.

Haupendezwi na dhabihu na sadaka

Hii ni kukuza kwa neno ili kuonesha kuwa vitu hivi havikuwa muhimu zaidi kwa Mungu. "Dhabihu na sadaka zingine sio vitu vinavyokufurahisha zaidi"

umefungua maskio yangu

Hapa "maskio" inamaanisha uwezo wa kusikia. "umeniwezesha kusikia amri zako"

hujaomba sadaka za kuchoma au sadaka za dhambi

Hii ni kukuza kwa neno ili kuonesha kuwa vitu hivi havikuwa muhimu zaidi kwa Mungu. "wanyama wanaotolewa kwenye madhabahu na sadaka zingine kwa ajili ya dhambi zetu sio unachotaka zaidi"

Psalms 40:7

gombo la nyaraka

Hii inamaanisha gombo ambapo kuna neno la kuandikwa la Yahwe. "gombo lililoandikwa"

sheria zako ziko moyoni mwangu

Hapa "moyo" inamaanisha undani wa mwanshishi. "Huwa ninawaza kuhusu sheria zako ndani mwangu"

Nimetangaza habari njema za haki yako katika mkusanyiko mkuu

"Nimewaambia mkusanyiko mkubwa wa watu habari njema za haki yako"

habari njema za haki yako

Hii inamaanisha habari njema kuwa Mungu huokoa watu wake. "habari njema kwa sababu u mwenyehaki, unaokoa watu wako"

midomo yangu yaijajizuia kufanya hili

Hapa "midomo" inamaanisha maneno ya mwandishi. "Sijajizuia kutangaza hivi vitu"

Psalms 40:10

Sijaficha haki yako moyoni mwangu

"Sijafanya haki yako kuwa siri" au "Nimemweleza kila mtu kuhusu haki yako"

moyoni mwangu

Hapa inamaanisha hali ya ndani.

Sijaficha uaminifu wako wa agano au uaminifu wako kwenye mkusanyiko mkuu

"Nimemwambia watu wote katika kusanyiko kuu kuhusu uaminifu wako wa agano au uaminifu wako"

uaminifu wako wa agano

"jinsi ulivyo mwaminifu kutunza ahadi zako"

uaminifu wako

"jinsi ulivyo mwaminifu"

acha uaminifu wako wa agano na uaminifu wako unitunze

Hapa "uaminifu wa agano" na "uaminifu" zinazungumziwa kana kwamba ni binadamu hai wanaoweza kumlinda mwandishi. "nataka uaminifu wako wa agano na uaminifu wako unilinde daima"

Psalms 40:12

Taabu zisizoweza kuhesabika zinanizunguka

Hapa taabu zinazungumziwa kana kwamba ni vitu vinavyomzunguka na kumtega mwandishi. "kuna taabu nyingi zimenizunguka kuliko navyoweza kuhesabu" au "taabu nyingi huja kwangu kuliko navyoweza kuhesabu"

zisizoweza kuhesabika

Hii imeelezwa katika hali hasi kuweka mkazo wa idadi. "zilizo nyingi kwa idadi"

udhalimu wangu

Hii inamaanisha matokeo ya dhambi. "matokeo ya udhalimu wangu"

umenishika

Udhalimu wa mwandishi unazungumziwa kana kwamba ni adui zake wanaomdhuru.

siwezi tena kuona kitu

Matoleo yanatofautiana katika kuelewa msemo huu. Inaweza kuwa inamaanisha kuwa mwandishi analia sana hadi hawezi kuona chochote kwa sababu ya machozi yake.

moyo wangu umeshinda

Hapa "moyo" inamaanisha ujasiri wa ndani wa mwandishi.

Psalms 40:14

Acha ... wanaofuatilia maisha yangu kuyachukua

"Tafadhali wafanye wale wanaojaribu kuniua waaibike na kuvunjwa matumaini"

wanaofuatilia maisha yangu kuyachukua

Hapa "wanaofuatilia maisha yangu" inamaanisha hamu ya kumuua mwandishi. "wanaojaribu kuniua"

Acha ... wanaofurahi kuniumiza

"Tafadhali wasimamishe wale wanaofurahi kuniumiza na uwatolea heshima"

wageuzwe

Kuzuiliwa inazungumziwa kama kugeuzwa kutoka katika mashambulizi yao. "kuzuiwa"

Acha ... wanaosema, "Aha, aha!"

"Acha wale wanaosema kwangu, 'Aha, aha!' washtuke kwa sababu ya aibu yao"

Acha washtuke kwa sababu ya aibu yao

"Natamani washtuke utakapowaaibisha"

wale wanaosema kwangu, "Aha, aha!"

"Aha, aha!" ni kitu wanachosema watu wakati wakimdhihaki mtu.

Psalms 40:16

washangilie na kuwa na furaha

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na inasisitiza uzito wa furaha. "wawe na furaha sana"

wanaopenda wokovu wako

"wanaokupenda kwa sababu umewaokoa"

maskini na mhitaji

Maneno haya yanamaanisha kitu kimoja na yanasisitiza jisni mwandishi asivyojiweza. "mhitaji sana"

Bwana ananiwaza

"Bwana ananijali"

Wewe ni msaada wangu ... unakuja kwa ukombozi wangu

Misemo hii inamaanisha kitu kimoja.

Wewe ni msaada wangu

"Wewe ndiye unaye nisaidia"

unakuja kwa ukombozi wangu

"unakuja kunioka"

usichelewe

"unijibu upesi"

Psalms 41

Psalms 41:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

yeye ... atamwokoa ... zake

Anayezungumziwa hapa ni mtu anayejihusisha na wanyonge.

wanyonge

"watu wanyonge" au "watu maskini"

Yahwe atamsaidia katika kitanda cha mateso

Msemo "kitanda cha mateso" inamaanisha mtu anapolala kitandani kwa sababu ni mgonjwa. "Akiwa mgonjwa na kitandani, Yahwe atamlinda"

utakifanya kitanda cha magonjwa yake kuwa kitanda cha uponyaji

Msemo "kitanda cha uponyaji" inamaanisha mtu anapopumzika kitandani na kupona ugonjwa wake. "wewe, Yahwe, utamponya ugonjwa wake"

Psalms 41:4

jina lake lipotee

Kama jina la mtu linakufa, inamaanisha kuwa watu wanasahau kuwa aliwahi kuishi. "jina lake litapotea lini" au "watu watasahau lini jina lake"

Kama adui wangu akija kuniona

Maneno "adui wangu" inamaanisha adui yeyote kwa ujumla, na sio kwa adui bayana yeyoto.

anasema vitu visivyofaa

Maana zinazowezekana ni 1) "anasema vitu vya kipuuzi" au 2) adui zake wanasema vitu kumfanya afikiri kuwa ni rafiki zake wakati sio. "anasema vitu vya udanganyifu" au "wanajifanya kumjali"

moyo wake unajikusanyia wenyewe maafa yangu

Adui zake wanajaribu kujifunza vitu vyote vibaya kumhusu. Hapa neno "moyo" linamaanisha mtu mzima. Matukio mabaya yanazungumziwa kana kwamba ni vitu vinavyoweza kukusanywa. "anajaribu kujifunza kuhusu maafa yangu yote"

Psalms 41:7

wanatamani niumie

Maana zinazowezekana ni 1) "wanatamani kwamba vitu vibaya sana vinikute" au 2) "wanapanga kunidhuru"

Ugonjwa uovu ... kwake

Adui zangu wanazungumzia "ugonjwa" kana kwamba ni mtu aliyemkamata. "Ni mgonjwa na ugonjwa hatari"

Ugonjwa uovu

Maana zinazowezekana ni 1) "ugonjwa wa mauti" au 2) "Kitu kiovu"

kwa sasa amelala chini, hatainuka tena

Hapa maneno "amelala chini" inamaanisha kulala kitndani kwa sabau ya ugonjwa. Kuwa "hatainuka" inamaanisha ataendelea kulala chini, ambayo pia tasifida ya kifo. "kwa kuwa sasa yuko kitandani, atakufa hapo"

ameinua kisigo chake dhidi yangu

Hii ni lahaja inayomaanisha rafiki yake amemsaliti. "amenisaliti" au "amegeuka dhidi yangu"

Psalms 41:10

Lakini wewe, Yahwe, unahuruma kwangu na unaniinua

Hili ni ombi. "Tafadhali, Yahwe, uwe na huruma kwangu na niinue"

unaniinua

Hii inamaanisha kumwinua kutoka kitandani, au kumponya kutoka kwenye ugonjwa wake.

ili niweze kuwalipa

Mwandishi anazungumzia kisasi kwa adui zake kana kwamba ni kuwalipa anachodaiwa. "ili kwamba nilipe kisasi kwao"

Kwa hili najua kuwa unafurahishwa na mimi, kwa kuwa adui wangu hanishindi

Neno "hili" inamaanisha kile ambacho mwandishi atasema baadaye. "Kwa sababu adui wangu hanishindi, natambua kuwa unafurahishwa na mimi"

Kwa hili najua kuwa unafurahishwa na mimi, kwa kuwa adui wangu hanishindi

"Ukiniwezesha kutenda hilo, kwa matokeo ya adui zangu kushindwa kunishinda, nitajua kuwa umefurahishwa na mimi"

unanibeba katika uadilifu wangu

"unanilinda kwa sababu ya uadilifu wangu"

utaniweka mbele ya uso wako

Mwandishi anazungumzia kuwa katika uwepo wa Yahwe kama kuwa sehemu ambayo Yahwe anaweza kumuona na kuona uso wa Yahwe. "utaniweka pamoja na wewe"

Psalms 41:13

Taarifa ya Jumla:

Mstari huu ni zaidi ya mwisho wa zaburi hii. Ni kauli ya kufunga ya kiabu chote cha kwanza cha Zaburi, kinachoanzia katika Zaburi 1 na kuishia na Zaburi 41.

kutoka milele na milele

Hii inamaanisha tofauti mbili na inamaanishwa wakati wote. "milele"

Amina na Amina

Neno "Amina" linarudiwa kusisitiza kukubaliwa kwa kilichosemwa. "Na hakika iwe hivyo"

Psalms 42

Psalms 42:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Kama mbawala anavyotweta kwa ajili ya kijito cha maji, vivyo hivyo ninakiua na wewe , Mungu

Mwandishi analinganisha shauku yake kwa ajili ya Mungu na shauku ya mbawala kwa ajili ya maji.

anavyotweta

kupumua kwa nguvu kutoka kwa mnyama au mtu aliyechoka sana au mwenye kiu

ninakiua na wewe , Mungu ... Ninakiu na Mungu

Mwandishi anazungumzia hamu yake kubwa kwa ajili ya Mungu kana kwamba ni kiu kikali kwa ajili ya maji.

nitakuja lini nakutokea mbele za Mungu?

Mwandishi haulizi swali hili ili kupata jibu bali kuonesha shauku yake kubwa ya kuwa mbele za Mungu.

Psalms 42:3

Machozi yangu yamekuwa chakula changu

Mwandishi anazungumzia machozi yake kana kwamba ni chakula anachokula. Hii inamaanisha kuwa ana huzuni sana hadi hawezi kula. "Machozi yangu ni kama chakula changu na sili kitu kingine"

mchana na usiku

Msemo huu unamaanisha siku nzima kwa kutaja mwanzo wake na mwisho wake. "siku nzima"

adui zangu daima wanasema kwangu

Huku ni kukuza kwa neno. Adui zake hawasemi haya muda wote; wanasema mara kwa mara.

Yuko wapi Mungu wako?

Adui wa mwandishi wanatumia swali hili kumkejeli na kuonesha kuwa hawaoni Mungu wake akimsaidia. "Mungu wako hayuko hapa kukusaidia"

itisha akilini

Hii ni lahaja inayomaanisha kuwaza au kukumbuka kitu. "kumbuka"

Ninamwaga nafsi yangu

Hapa neno "nafsi" inamaanisha hisia. Mwandishi anazungumzia nafsi yake kana kwamba ni kimiminiko anachomwaga. Msemo unamaanisha kuwa anaeleza uchungu wake wa hisia. "ninaeleza huzuni yangu"

msongamano

"kundi la watu"

furaha na sifa

Msemo huu unatumia maneno mawili tofauti kueleza wazo moja.

Psalms 42:5

Kwa nini umeinama chini, nafsi yangu? Kwa nini umefadhaika ndani yangu?

Mwandishi jizungumzia undani wake kama "nafsi" yake. Anajiuliza maswali haya kujikemea. "Sitakiwi kuinama chini. Sitakiwa kuwa na wasiwasi"

umeinama chini

Mwandishi anazungumzia huzuni au kukata tamaa kana kwamba nafsi yake imeinama. "kukata tamaa"

Mtumaini Mungu

Mwandishi anaendelea kuzungumza na nafsi yake na kuiamuru kumtumaini Mungu.

Mungu wangu, nafsi yangu

Mwandishi anaanza kuzungumza na Mungu kuhusu nafsi yake.

Nina kuiitisha akilini

Msemo huu unamaanisha kukumbuka au kuwaza kuhusu kitu. "Nina kuwaza"

nchi ya Yordani

Hii inaweza kumaanisha Israeli ya kaskazini, ambapo mto Yordani huanzia. "nchi ambayo mto Yordani huanzia"

vilele

juu ya milima

kilima cha Mizari

Hili ni jina la kilima kwenye kitako cha mlima Hermoni.

Psalms 42:7

Kilindi huita kilindi katika kelele cha maporomoko

Neno "kilindi" inmaanisha maji yenye kina kirefu, ambapo hapa inawezekana ni vijito vinavyo tiririka chini ya mlima Hermoni. Mwandishi anavizungumzia kana kwamba ni watu wanaitana wanaposikia sauti yao ya kushuka katika mlima.

mawimbi yako yote ... yameenda juu yangu

Mwandishi anazungumzia bahati yake mbaya na huzuni kana kwamba ni maji yenye kina kirefu yanayo mzamisha kwa wimbi moja baada ya jingine.

mawimbi yako na gharika

Maneno haya mawili yanatumika pamoja kusisitiza ukubwa wa mawimbi. "mawimbi yako yote makubwa"

Yahwe ataamuru uaminifu wake wa agano

Mwandishi anazungumzia uaminifu wa agano wa Yahwe kana kwamba ni mtu anayemwamuru kuwa naye. "Yahwe atanionesha uaminifu wake wa agano"

wimbo wake

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo anaonipa" au "wimbo kumhusu"

Mungu wa uhai wangu

"Mungu anayenipa uhai"

Psalms 42:9

Nitasema kwa Mungu, mwamba wangu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni mwamba mkubwa utakaotoa ulinzi dhidi ya mashambulizi ya adui.

Kwa nini ninaenda kuomboleza

"Kwenda kuomboleza" nikufanya desturi zinazokaribiana na kuwa huzuni sana.

Kama na upanga ndani ya mifupa yangu

Mwandishi anaelezea kukemea kwa adui zake kama kupokea kidondo hatari.

huwa wanasema kwangu

Hii ni ukuzaji wa neno; adui zake hawasemi hivi kila wakati bali wanasema mara kwa mara.

Yuko wapi Mungu wako?

Adui wa mwandishi wanatumia swali hili kumkejeli na kuonesha kuwa hawaoni Mungu wake akimsaidia. "Mungu wako hayuko hapa kukusaidia"

Psalms 42:11

Kwa nini umeinama chini, nafsi yangu? Kwa nini umefadhaishwa ndani yangu?

Mwandishi jizungumzia undani wake kama "nafsi" yake. Anajiuliza maswali haya kujikemea. "Sitakiwi kuinama chini. Sitakiwa kuwa na wasiwasi"

umeinama chini

Mwandishi anazungumzia huzuni au kukata tamaa kana kwamba nafsi yake imeinama. "kukata tamaa"

Mtumaini Mungu

Mwandishi anaendelea kuzungumza na nafsi yake na kuiamuru kumtumaini Mungu.

Psalms 43

Psalms 43:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Mungu wa nguvu yangu

Maana zinazowezekana ni 1) "Mungu unayenilinda" au 2) "Mungu unayenipa nguvu"

Kwa nini umenikataa? Kwa nini ninaomboleza kwa sababu ya ukandamizaji wa adui?

Mwandishi anauliza maswali haya ili kulalamika kwa Mungu na kuonesha hisia yake, sio kupata jibu.

Kwa nini ninaomboleza

"Kuomboleza" ni kufanya matendo yana onesha kuwa na huzuni sana.

kwa sababu ya ukandamizaji wa adui

Neno "ukandamizaji" linaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "kwa sababu adui zangu wananikandamiza"

Psalms 43:3

tuma nuru yako na ukweli wako

Mwandishi anazungumzia ukombozi wa Mungu kana kwamba ni nuru inayo mwonyesha njia na ukweli unaomfundisha jinsi ya kuishi. "niongoze kwa nuru yako na kweli"

mlima ... mtakatifu

Hii inamaanisha mlima ulioko Yerusalemu ambapo hekalu lipo kwa hiyo ni hekalu lenyewe.

kwenye makazi yako

"mahali ambapo unaishi"

Mungu furaha yangu inayozidi

"Mungu ambaye ni furaha yangu kubwa sana" au "Mungu anayenipa furaha kubwa"

Psalms 43:5

Kwa nini umeinama chini , nafsi yangu? Kwa nini umekasirika ndani yangu?

Mwandishi anaelezea uwepo wake wa ndani kama "nafsi" yake. Anauliza maswali haya kujikemea mwenyewe. "Sitakiwi kuinama chini. Sitakiwi kuwa na wasiwasi"

umeinama chini

Mwandishi anazungumzia huzuni au kukata tamaa kana kwamba nafsi yake imeinama.

Mtumaini Mungu

Mwandishi anaendelea kuzungumza na nafsi yake na kuiamuru kumtumaini Mungu.

wokovu wangu na Mungu wangu

Msemo "wokovu wangu" inamaanisha Mungu. Ikibidi, misemo miwili inaweza kuunganishwa. "Mungu wangu anayeniokoa"

Psalms 44

Psalms 44:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kihebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya wana wa Kora

"Hii ni zaburi ambayo wana wa Kora waliandika."

Maschili

Hii inaweza kuwa mtindo wa muziki.

Tumeskia kwa maskio yetu, Mungu

Neno "maskio" linaongeza mkazo kwa kauli waliosikia na kuelewa vitu ambavyo mwandishi anataka kueleza. Mwandishi anaeleza kauli hii kwa Mungu. "Mungu, tumesikia vizuri"

katika siku zao, katika siku za kale

Misemo yote hii miwili inatumia neno "siku" kumaanisha wakati ambao mababu wa watu wa Israeli walipokuwa hai.

Uliondoa mataifa

"Ulilazimisha watu wa mataifa mengine kuondoka"

kwa mkono wako

Hapa neno "mkono" linamaanisha nguvu ya Mungu. "kwa nguvu yako"

uliwapanda watu wetu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kusababisha Waisraeli kuishi katika nchi kana kwamba aliyokuwa akiwapanda katika udongo kama ambavyo angepanda mti. "uliwasababisha watu kuishi huko"

Psalms 44:3

kwa upanga wao wenyewe

Neno "upanga" linamaanisha nguvu ya kijeshi. "kwa kupigana na panga zao" au "kwa nguvu ya jeshi lao wenyewe"

mkono wao wenyewe

Hapa neno "mkono" linamaanisha nguvu. "nguvu yao wenyewe"

na nuru ya uso wako

"na nuru ya uso wako uliwapatia nchi kuwa mali yao"

mkono wako wa kuume, mkono wako

Hapa neno "mkono" linamaanisha nguvu ya Mungu. Kwa pamoja zinaweka mkazo kwa ukuu wa nguvu ya Mungu. "nguvu yako kuu"

nuru ya uso wako

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwaangalia kwa fadhila na kuwa na huruma kwao kana kwamba ni uso wa Yahwe ulitoa nuru kwa ajili yao. "huruma yako" au "fadhila zako"

ushindi kwa Yakobo

Watu wa Israeli wanajulikana kwa jina la babu yao "Yakobo"

Psalms 44:5

Kupitia kwako ... kupitia

"Kwako ... kwa"

tutasukuma ... kuwakanyaga chini ... inuka juu

Mwandishi anazungumzia kushindwa kwa adui zake kana kwamba wako "chini" na kujiandaa kwao kupigana kana kwamba wako "juu."

kupitia jina lako

Hapa neno "jina" linamaanisha nguvu na mamlaka ya Mungu. "kwa nguvu yako"

kuwakanyaga chini

"kuwakanyaga chini ya miguu yako" au "kutembea juu yao"

Psalms 44:7

tumefanya majivuno yetu

"tumejivuna"

tutatoa shukrani kwa jina lako

Hapa neno "jina" linamaanisha Mungu mwenyewe. "tutakupa shukrani wewe"

Psalms 44:9

umetutupa

Mwandishi anazungumzia kukataliwa kwa Israeli kana kwamba alikuwa akitupa nguo ambayo haitaki. "kutukataa"

ngawira

mali ambazo jeshi hukusanya baada ya kushinda vita

Umetufanya kama kondoo waliokusudiwa kuwa chakula

Mwandishi anafananisha Waisraeli na kondoo ambao watu huua na kula. Kama kondoo wasiojiweza mbele ya wale wanaowaua, kwa hiyo Waisraeli hawajiwezi mbele ya adui zao. "Umewaruhusu adui zetu kutuua kama wanavyoua kondoo na kumla"

waliokusudiwa kuwa chakula

"tumekusudiwa kuwa chakula ambacho watu wanakula"

kututawanya miongoni mwamataifa

"kutusababisha kuishi katika mataifa mengi tofauti"

Psalms 44:12

Unawauza watu wako bure

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwaruhusu adui wa Israeli kuwashinda kana kwamba alikuwa akiwauza watu wa Israeli kwa adui zao lakini hahitaji malipo kutoka kwa adui zao.

Unatufanya kuwa lawama kwa jirani zetu, kudhihakiwa na kukejeliwa na wale waliotuzunguka

Misemo hii miwili ina usambamba ikisisitiza jinsi watu wanaoishi miongoni mwao wanavyowakejeli.

Unatufanya kuwa lawama kwa jirani zetu

"Unatufanya kuwa kitu ambacho jirani zetu wanakemea"

kudhihakiwa na kukejeliwa na wale waliotuzunguka

"wale waliotuzunguka wanatudhihaki na kutukejeli"

fedheha miongoni ... kutikisa kichwa

Misemo hii miwili ina usambamba ikisisitiza jinsi watu wanavyowakejeli kwa nguvu.

Umetufanya fedheha miongoni mwa mataifa

Unayafanya mataifa yaliyo tuzunguka kutufedhehesha"

kutikisa kichwa miongoni mwa watu

"jambo ambalo watu hutikisa vichwa"

kutikisa kichwa

Hiki ni kitendeo ambacho watu walitumia kuonesha dharau wengine.

Psalms 44:15

fedheha yangu iko mbele yangu

Mwandishi anazungumzia fedheha kana kwamba ni kitu ambacho daima kiko mbele yake kwa ajili yake kuona. Msemo unamaanisha kuwa huwa anafikiria fedheha yake. "ninafikiria fedheha yangu"

aibu ya uso wangu umenifunika

Mwandishi anazungumzia aibu yake kana kwamba ni kitu kinachomfunika kama blangeti. "aibu ya uso wangu imenilemea"

aibu ya uso wangu

"aibu inayoonekana katika uso wangu." Hii inamaanisha mwonekano wa sura ambao unasababishwa na aibu yake.

kwa sababu ya sauti ya yule anyenikemea na kunifedhehesha

Hapa neno "sauti"linamaanisha kitu ambacho mtu anasema. "kwa sababu ya kile ambacho mtu anasema anyenikemea na kunifedhehesha"

anyenikemea na kunifedhehesha

Maneno haya yana maaza za kufanana na yanasisitiza uhalisia mbaya wa kile ambacho mtu huyu anasema.

Psalms 44:18

Moyo wetu haujageuka ... hazijatoka kwenye njia yako

Misemo hii miwili in usambamba. Mwandishi anazungumzia uaminifu kwa Mungu kana kwamba ilikuwa kumfuata, na kutokuwa mwaminifu kana kwamba ni kumgeuka.

Moyo wetu haujageuka

Hapa neno "moyo" linamaanisha hisia, hasa za uaminifu. "Hatujaacha kuwa waaminifu kwako"

umetuvunja sana

Mwandishi anazungumzia adhabu za Mungu kana kwamba ilikuwa ni kuvunja chombo rahisi kuvunjika. "umetuadhibu vikali"

katika nafasi ya mbweha

Mwandishi anazungumzia Israeli baada ya adhabu ya Mungu kana kwamba ilikuwa sehemu ya pori, ambapo mtu hawezi kuishi. "umefanya nchi yetu kama sehemu ambayo mbweha huishi"

mbweha

aina ya mbwa pori

kutufunika na kivuli cha mauti

Mwandishi anazungumzia mauti kana kwamba ni kitu kinachotoa kivuli juu ya wale wanaotaka kufa. "umetufanya ili tuwe karibu kufa"

Kama tumesahau jina la Mungu wetu

Hapa neno "jina" linamaanisha Mungu mwenyewe. Kumsahau Mungu ni kuacha kumwabudu. Hili ni jambo ambalo halikutokea. "Kama tungemsahau Mungu wetu" au "Kama tungeacha kumwabudu Mungu wetu"

kusambaza mikono yetu kwa mungu mgeni

Kusambaza mikono ni ishara ambayo watu walitumia kuabudu na kuomba kwa mungu yeyote. "waliabudu mungu mgeni" au "kuomba kwa mungu mgeni"

Je, Mungu hatalichunguza hili?

Mwandishi anatumia swali hili kueleza kuwa Mungu atajua kama watamwabudu mungu mwingine. "Hakika Mungu atagundua"

anajua siri zatunauwawa siku nzima moyo

Hapa neno "moyo" unamaanisha akili na mawazo. "anajua kile ambacho mtu anawaza kwa siri"

tunauwawa siku kutwa

Msemo "siku kutwa" ni kukuza maneno kusisitiza kuwa watu wao wanauwawa mara kwa mara. "watu wanatuua kila wakati"

tumefanywa kuwa kondoo wa machinjo

"watu wanatuona kama kondoo kwa ajili ya machinjo"

kondoo wa machinjo

Mwandishi anafananisha Waisraeli na kondoo ambao watu huua na kula. Kama kondoo wasivyojiweza mbele ya wale wanaowaua, hivyo ndivyo Waisraeli wasivyojiweza mbele ya adui zao.

Psalms 44:23

Amka, kwa nini unalala, Bwana?

Hii haimaanishi ya kuwa Mungu amelala kweli. Mwandishi anazungumzia Mungu kuonekana kama hatendi kitu kana kwamba amelala. Anauliza swali hili kumkemea Mungu kwa kuonekana kutokujali kuhusu taabu zao. "Amka! Naona kama umelala, Bwana!"

usitutupe

Mwandishi anamzungumzia Mungu kuikataa Israeli kwamba alikuwa akitupa nguo ambayo haitaki. "usitukatae"

Kwa nini unaficha uso wako ... kukandamizwa kwetu?

Mwandishi anatumia hili swali kulalamika kuwa Mungu anaonekana kutowajali. "Usifiche uso wako ... kukandamizwa kwetu."

unaficha uso wako

Mwandishi anasungumzia Mungu kutowajali kana kwamba Mungu alikuwa akificha uso wake ili asiwaone. "kutujali"

kusahau mateso yetu na kukandamizwa kwetu

Maneno "mateso" na "kukandamizwa " inamaanisha kitu kimoja na inaweka mkazo ya ukali wa mateso. "kusahau kuwa watu wanatutesana kutukandamiza" au "kusahau kuwa watu wanatutesa sana"

Psalms 44:25

Kwa kuwa tumeyeyuka kwenye mavumbi; miili yetu inang'ang'ania nchini

Misemo hii ya usambamba ina maana za kufanana. Mwandishi anaelezea watu wake kama wamelala ardhini katika mkao wa kushindwa na kudhalilishwa.

Kwa kuwa tumeyeyuka kwenye mavumbi

Mwandishi anazungumzia kudhalilishwa kwao kana kwamba miili yao ni vitu, kama barafu, inayoyeyuka na kulowa kwenye mchanga.

miili yetu inang'ang'ania nchini

Mwandishi anazungumzia kudhalilishwa kwao kana kwamba miili yao ilikuwa imekwama kwenye ardhi na hawakuweza kujinyanyua juu.

inuka

Hii ni amri ya kusimama. Msemo huu unamaanisha kuanza kutenda kitu. "Tenda jambo"

Psalms 45

Psalms 45:1

Taarifa ya jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Shoshannimu

Hii inaweza kuwa mtindo wa mlio wa muziki. wakati mwingine inatafsiriwa kama "weka katika mlio wa 'yungiyungi.'"

Zaburi ya wana wa Kora

"Hii ni zaburi ambayo wana wa Kora waliandika."

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Wimbo wa upendo

"Wimbo wa mapenzi"

Moyo wangu umefurika kwa neno zuri

Mwandishi anazungumzia moyo wake kana kwamba ni chombo kinachofurika na kimiminiko. Neno "moyo" linawakilisha hisia zake, amabzo zinafurahishwa kwa nyimbo anazoimba. "Hisia zangu zinafuraha juu ya neno zuri"

neno zuri

"wazo lenye uadilifu." Hii inamaanisha wimbo alioandika.

niliyotunga

kuandika au kuunda wimbo

ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi aliye tayari

Mwandishi anazungumzia ulimi wake kana kwamba ni kalamu. Anazungumza kwa ujuzi kama mwandishi mwenye uzoefu anavyoandika. "ulimi wangu ni kama kalamu ya mtu anayeandika vizuri" au "ninapozungumza kwa ujuzi kama mwandishi mwenye uzoefu anavyoweza kuandika maneno"

Wewe ni mzuri kuliko watoto wa wanadamu

Msemo huu ni kukuza kwa neno na inasisitiza kuwa mfalme ni mzuri kwa mwonekano kuliko mtu mwingine. Msemo "watoto wa watu" ni lahaja inayomaanisha watu wote. "Una uzuri zaidi ya mtu mwingine yeyote"

neema imemwagwa katika midomo yako

Mwandishi anazungumzia neema kana kwamba ni mafuta ambayo mtu ametumia kuitia mafuta midomo yake. Neno "midomo" linamaanisha maneno ya mfalme. Msemo huu unamaanisha kuwa mfalme anazungumza kwa ufasaha. "ni kana kwamba mtu ametia mafuta midomo yako kwa mafuta" au "unazungumza kwa ufasaha"

Psalms 45:3

Weka upanda wako pembeni yako

Mashujaa walibeba mapanga yao katika makundi yalioning'inia kwenye mshipi katika viuno vyao. Upanga utakaa pembeni mwao. Msemo huu unaeleza tendo la mtu kujiandaa kwa ajili ya viti. "Jiandaeni kwa ajili ya vita"

uende kwa ushindi

Mwandishi anamwambia mfalme kumpanda farasi wake au kibandawazi kuelekea katika ushindi.

kwa sababu ya uaminifu, upole, na haki

Maana zinazowezekana ni 1) hizi ni sifa za mwenye nguvu. "kwa sababu u mwaminifu, mpole, na mwenye haki" au 2) sifa hizi anazopambana kushikilia kwa ajili ya watu anaowatawala. "ili kushika uaminifu, upole, na haki"

mkono wako wa kuume utakufundisha mambo ya kuogofya

Askari walio wengi walishikia mapanga yao kwa mkono wao wa kuume walipopigana, ambayo mwandishi anazungumzia kana kwamba ni mtu anayeweza kumfunza mfalme kupitia uzoefu anaopitia vitani. "Utajifunza kutimiza matendo makubwa ya kijeshi kwa kupigana katika vita nyingi"

mambo ya kuogofya

"matendo ya ajabu." Hii inamaanisha ushindi wa kijeshi unaowasababisha adui zake kumwogopa na rafiki zake kumheshimu sana.

Psalms 45:5

watu wanaanguka chini yako

Msemo huu unamaanisha mfalme kuwashinda adui zake. Maana zinazowezekana ni 1) "watu wanaanguka miguuni mwako kwa kusalimu amri" au 2) "watu wanaanguka wakiwa wamekufa miguuni mwako."

mishale yako iko mioyo ya adui wa mfalme

"mishale yako imechoma mioyo ya adui zako." Mwandishi anazungumza kwa mfalme huku akimweleza mfalme katika nafasi ya mtu wa tatu.

Kiti chako cha enzi ... ni wa milele na milele

maneno "Kiti chako cha enzi" yanawakilisha ufalme na utawala wa mfalme. "Ufalme wako ... ni wa milele na milele" au "Utatawala ... milele na milele"

Kiti chako cha enzi, Mungu

Maana zinazowezekana ni kwamba neno la "Mungu" 1) ni jina kwa ajili ya mfalme, ambaye ni mwakilishi wa Mungu au 2) linaboresha maneno "kiti cha enzi" na linamaanisha "Ufalme wako ambao Mungu amekupa"

fimbo ya hukumu ni fimbo ya ufalme wako

Neno "fimbo" linawakilisha mamlaka ya mfalme kutawala ufalme wake. "unatawala ufalme wako kwa haki"

Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta ya furaha

Mwandishi anazungumzia furaha kana kwamba ni mafuta ambayo Mungu alitumia kumtia mafuta mfalme. Mungu kumtia mafuta ni ishara inayowakilisha kwamba Mungu amemchagua kuwa mfalme. "Mungu alipokuchagua kama mfalme, alikufanya kuwa na furaha sana"

Psalms 45:8

Taarifa ya Jumla:

Hapa mwandishi anaanza kueleza kile kinachoonekana kuwa sherehe ya arusi ya mfalme na bibi arusi wake.

manemane, mshubiri ,na mdalasini

Hii ni mimea yenye harufu nzuri ambayo watu hutumia kutengeneza manukato.

majumba ya mapembe

Mapembe ni meno meupe magumu ya nje ya mnyama. Msemo huu unaelezea jumba lenye kuta na samani ambazo watu wamepamba kwa mapembe.

vyombo vya nyuzi vimekupa furaha

Maneno "vyombo vya nyuzi" yanamaanisha muziki ambao watu hutengeneza kwa kucheza vyombo vya nyuzi. "muziki wa vyombo vya nyuzi umekufanya kuwa na furaha"

wanawake wenye heshima

Hawa wanawake ni wake wa mfalme waliopokea kibali hiki.

malkia

Hii inamaanisha mwanamke atakaye kuwa malkia. "bibi arusi wako, malkia" au "bibi arusi wako, atakaye kuwa malkia"

Ofiri

Hili ni jina la sehemu iliyokuwa ikijulikana kwa dhahabu yake safi. " Mahali hapajulikani.

Psalms 45:10

Sikiliza, binti

Mwandishi anaanza kuzungumza na malkia na anamuita kama "binti" yake kwa sababu ni msichana mdogo.

tega sikio lako

Mwandishi anazungumzia kusikiliza kitu kwa makini kana kwamba ni kuinamisha sikio la mtu kuelekea kwa mtu anayezungumza. "sikiliza kwa makini"

wasahau watu wako mwenyewe

Mwandishi anamzungumzia malkia kuacha kufuata imani na desturi za watu wake wa asili kana kwamba ni kuwasahau. "usifuate tena desturi za watu wako"

nyumba ya baba yako

Hapa neno "nyumba" linamaanisha familia. "ndugu zako"

Katika njia hii

"na" au "kwa hiyo"

mfalme atatamani uzuri wako

Hii ni njia ya ustarabu ya kusema kuwa mfalme atataka kulala na malkia kama mke wake.

Psalms 45:12

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuzungumza na malkia.

Binti wa Tiro

Mwandishi anazungumza na watu wanaoishi Tiro kana kwamba ni watoto wa Tiro. "Watu wa Tiro"

binti wa kifalme

Hii inamaanisha mwanamke ambaye mfalme atamuoa. "Bibi arusi wa mfalme"

amependeza

"mzuri sana." Hii inamaanisha mwonekano wa mwanamke.

mavazi yake yameundwa kwa dhahabu

Mavazi yake yamepambwa au kushonwa kwa dhahabu. "anavaa mavazi ambayo mtu ameshona kwa uzi wa dhahabu"

Psalms 45:14

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuzungumza kuhusu malkia lakini anaanza kwa kuzungumza na mfalme kwanza.

Ataongozwa kwenda kwa mfalme na nguo ya tarizi

"Watu watamwongoza kwenda kwa mfalme akiwa amevaa nguo ya tarizi"

tarizi

mtindo ulioundwa kwa kushona nyuzi za rangi kwenye nguo

wanawali, wenzake wanaomfuata, wataletwa kwako

Hapa neno "kwako" inamaanisha mfalme. "watu watakuletea wanawali, wenzake wanaomfuata"

Wataongozwa kwa furaha na shangwe

Msemo huu unaeleza "furaha na shangwe" kama mtu anayewaongoza wengine kusherehekea. "Furaha na shangwe zitawaongoza" au "Wataenda kwa furaha na shangwe"

furaha na shangwe

Maneno haya mawili yana maana moja na yanasisitiza ukali wa furaha. "furaha kubwa"

Psalms 45:16

Kauli Unganishi:

Mwandishi anaendelea kuzungumza na mfalme.

Katika sehemu ya baba zako watakuwa watoto wako

Hii inamaanisha wana wa mfalme watachukua nafasi yake kama mfalme, kama yeye alivyochukua nafasi ya mababu zake.

utafanya wakuu duniani kote

Msemo "duniani kote" ni kukuza kwa neno kusisitiza kwamba atatawala juu ya mataifa mengi. "utafanya watawala juu ya mataifa mengi"

Nitalifanya jina lako likumbukwe katika vizazi vyote

Hapa "atakayefanya" ni mwandishi. Neno "jina" linamaanisha tabia ya mfalme na sifa yake. "Nitawasababisha watu katika kila kizazi kujua kuhusu ukuu wako"

Psalms 46

Psalms 46:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya wana wa Kora

"Hii ni zaburi ambayo wana wa Kora waliandika"

weka katika Alamothi

Hii inaweza kumaanisha aina ya muziki.

Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni sehemu ambapo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya usalama. "Mungu hutupa ulinzi na nguvu"

milima itikiswe katika moyo wa bahari

Mwandishi anazungumzia kilindi cha chini zaidi ya bahari kana kwamba ni moyo wa bahari. Hapa anaelezea tetemeko la dunia linalo sababisha milima kumeng'enya na kuanguka baharini. "milima inatakiwa kutikisika kwa nguvu sana hadi ianguke kwenye vilindi vya bahari"

ingawa maji yake yanaunguruma na kukasirika

"ingawa maji ya bahari wanaunguruma na kukasirika." Maneno "kuunguruma" na "kukasirika" yanaelezea kusogea kwa nguvu kwa bahari wakati wa dhoruba kali.

milima inatetemeka katika kuvimba kwake

Msemo "kuvimba kwake" kinamaanisha maji ya bahari yanapoinuka na kugonga milima. "kuvimba kwa maji kunasababisha milima kutetemeka"

Psalms 46:4

Kuna mto, mikondo ambayo huufanya mji wa Mungu kuwa na furaha

"Kuna mto ambao mikondo yake huufanya mji wa Mungu kuwa na furaha." Hii picha ya mto unaotiririka inaashiria amani na mafanikio kwa ajili ya mji wa Mungu.

huufanya mji wa Mungu kuwa na furaha

Msemo "mji wa Mungu" unamaanisha yerusalemu, ambao mwandishi anauzungumzia kama mtu anayeweza kuwa na furaha. "huwafanya watu wanaoishi Yerusalemu kuwa na furaha"

sehemu takatifu za hema takatifu za Aliye juu

Msemo huu unaelezea "mji wa Mungu." Wingi wa mahema unaweka mkazo katika wazo kwamba hapa ni mahali patakatifu pa Mungu kuishi. "sehemu takatifu anapoishi Aliye juu"

katikati yake; hatasogezwa ... atamsaidia.

Panapozungumziwa na "mji wa Mungu."

hatasogezwa

Hapa neno "kusogezwa " ni sawa na neno linalotafsiriwa "kutikiswa" katika 46:1. Mwandishi anazungumzia uharibifu wa Yerusalemu kwa majeshi kana kwamba tetemekolingeuangamiza. "hakuna kitu kitakachoweza kuuangamiza"

Psalms 46:6

mataifa yalikasirika

Hapa neno "kukasirika" ni neno sawa mwandishi alilotumia katika 46:1 kuelezea maji ya bahari. Mwandishi anazungumzia uoga wa mataifa kana kwamba ni kusogea kwa fujo kwa bahari wakati wa dhoruba. "mataifa yanaogopa"

falme zilitikiswa

Hapa neno "kutikiswa" ni neno sawa ambalo mwandishi alitumia katika 46:1 kuelezea madhara ya tetemeko kwenye milima. Mwandishi anazungumzia kuangushwa kwa falme na majeshi kana kwamba tetemeko litawaangamiza. "majeshi yanapindua falme"

akainua sauti yake

"Mungu akainua sauti yake." Mwandishi anazungumzia "sauti" kana kitu amabcho mtu anaweza kuinua na kuweka hewani. Hii inamaanisha kwamba sauti inakua ya sauti zaidi. "Mungu alipaza sauti"

dunia ikayeyuka

Mwandishi anazungumzia dunia kama kitu, kama barafu, inayoweza kuyeyuka. Hapa "'dunia" inawakilisha binadamu, na kuyeyuka inawakilisha uoga. "watu wa duniani wanatetemeka kwa uoga"

Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni sehemu ambayo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya ulinzi. "Mungu wa Yakobo anatupa ulinzi"

Mungu wa Yakobo

Maana zinazowezekana ni 1) "Mungu ambaye Yakobo alimwabudu" au 2) "Yakobo: ni njia nyingine ya kusema taifa la Israeli na inamaanisha "Mungu wa Israeli."

Psalms 46:8

Hufanya vita kukoma

"Hufanya mataifa kuacha kupigana vita"

hadi mwisho wa dunia

Huu ni msemo wa nahau unaomaanisha sehemu zote duniani. "sehemu zote duniani"

huvunja upinde ... huunguza ngao

Njia moja ambayo Yahwe atakomesha vita vyote kwa kuangamiza silaha ambazo majeshi hutumia kupigania.

Psalms 46:10

Kuwa kimya na ujue kuwa mimi ni Mungu

Hapa, Mungu anaanza kuzungumza.

Kuwa kimya

Katika hali hii, maneno haya yanawezekana kuwa ni amri kwa mataifa kukomesha vita vyao. "Acheni kupigana"

ujue kuwa mimi ni Mungu

Hapa neno "kujua" inamaanisha kuelewa na kukiri kuwa Yahwe ndiye Mungu wa kweli.

Nitatukuzwa katika mataifa; nitatukuzwa duniani

Misemo hii miwili inamaana sawa na inasisitiza kuwa watu wa kila taifa duniani watamtukuza Mungu. "Watu katika kila taifa watanitukuza; watu duniani kote watanitukuza"

Yahwe wa majeshi yuko nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni sehemu ambayo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya ulinzi.

Psalms 47

Psalms 47:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya wana wa Kora

"Hii ni zaburi iliyoandikwa na wana wa Kora"

Piga makofi

Kupiga makofi inahiusishwa na sherehe. "Piga makofi kwa kusherehekea"

piga kelele kwa Mungu na sauti ya ushindi

piga kelele kwa Mungu na sauti za furaha." Hapa neno "ushindi" inamaanisha furaha inayohusiana na ushindi

Psalms 47:3

Anawatiisha watu chini yetu na mataifa chini ya miguu yetu.

Misemo hii miwili ina usambamba na inamaanisha kuwa Mungu aliwezesha Israeli kuwashinda adui zake.

Anawatiisha

Kushinda na kuweka chini ya mamlaka ya mwingine

chini yetu ... chini ya miguu yetu

Mwandishi anazungumzia kuyashinda mataifa mengine kana kwamba ilikuwa kuyaweka mataifa hayo chini ya miguu yao.

Anatuchagulia urithi wetu

Mwandishi anazungumzia nchi ya Israeli kana kwamba ilikuwa ni urithi ambao Mungu aliwapa watu kama mali ya milele. "Anachagua nchi hii kama urithi wetu"

utukufu wa Yakobo

Hapa neno "utukufu" inmaanisha chanzo cha majivuno na linaashiria nchi ambayo Mungu amewapa watu wake kama urithi. "nchi ambayo Yakobo anajivunia"

Yakobo aliyempenda

Neno "Yakobo" linaashiria taifa la Israeli.

Mungu ameenda juu kwa shangwe

Mwandishi anamzungumzia Mungu kuyashinda mataifa kana kwamba Mungu alikuwa mfalme anaye panda kwenye kiti chake cha enzi, kilicho kuwa hekaluni. "Mungu ameenda juu kwenye hekalu wakati watu wakipiga shangwe" (UDB) au "Mungu amepanda kwenye kiti chake cha enzi wakati watu wakipiga shagngwe"

Yahwe kwa sauti ya tarumbeta

Msemo huu uko sambamba na msemo uliopita. Kitenzi kinaweza kuwekwa kuweka wazi. "Yahwe ameenda juu wakati watu wakipuliza tarumbeta"

Psalms 47:6

Mwimbieni sifa Mungu, imbeni sifa; imbeni sifa kwa mfalme wetu, imbeni sifa

Msemo "imbeni sifa" unarudiwa kwa ajili ya msisitizo. "Mwimbieni, mwimbieni sifa Mungu; imbeni, imbeni sifa kwa mfalme wetu"

Psalms 47:8

Wakuu wa watu

"Viongozi wa mataifa yote"

wamekusanyika pamoja kwa watu

Maana zinazowezekana ni kwamba watawala wa mataifa 1) "wanakusanyika mbele ya mataifa" (UDB) au 2) "walikusanyika pamoja na watu" ili wote wamwabudu Mungu kama mfalme.

ngao za ulimwengu ni za Mungu

Maana zinazowezekana ni kwamba "ngao" 1) zinamaanisha vifaa vya vita. "Mungu ana uwezo zaidi ya silaha za wafalme wote dunia" (UDB) au 2) inamaanisha viongozi wa mataifa ambao wanazungumzia kama ngao ambazo zinalinda mataifa yao. "wafalme wa duniani wako chini ya Mungu"

Psalms 48

Psalms 48:1

Taarifa ya Jumla:

Huu ni wimbo kuhusu Yerusalemu kuwa sehemu ya kuishi ya Mungu.

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

zaburi ya wana Kora

"hii ni zaburi ambayo wana wa Kora waliandika"

mwenye kusifiwa sana

"watu wanapaswa kumsifu sana"

mji wa Mungu wetu katika mlima wake mtakatifu

Hii inamaanisha Yerusalemu, iliyojengwa katika mlima Sayuni.

mji wa Mungu wetu

Maana zinazowezekana ni 1) "mji ambao Mungu wetu huishi" au 2) "mji ulio wa Mungu wetu"

Mzuri katika kuinuka

"Mzuri na juu." Neno "kuinuka" linamaanisha jinsi mlima Sayuni ulivyo juu.

furaha ya dunia yote, ni mlima Sayuni

Hapa neno "dunia" linamaanisha kila mtu anayeishi duniani. "Mlima Sayuni huwapa watu wote duniani furaha" au "watu wote wanafurahi kwa sababu ya mlima Sayuni"

katika pande za kaskazini

Maana zinazowezekana ni kwamba msemo huu 1) unamaanisha mwelekeo wa kaskazini au 2) ni jina jingine la mlima sayuni linalomaanisha "mlima wa Mungu."

Mungu amejifanya kujulikana katika majumba yake kama sehemu ya kukimbilia

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni sehemu ambapo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya usalama. "Mungu amejifanya kujulikana kama yule anayetoa usalama kwa watu katika majumba ya mlima Sayuni"

Psalms 48:4

tazama

Neno "tazama" hapa linataka tuwe macho na kuzingatia taarifa ya kushangaza inayofuata.

wamejikusanya

Hii inamaanisha kwamba wafalme wa mataifa walikusanya majeshi yao. "walikusanya majeshi yao"

wakapita pamoja

"kwa pamoja walipita Yerusalemu"

Wakaona

"Wakaona Yerusalemu"

hawakufadhaika

"taabika sana"

Kutetemeka kuliwashika

Mwandishi anazungumzia hofu ya wafalme kana kwamba ni mtu aliyesababisha wafalme na majeshi yao kutetemeka. "Huko walitetemeka kwa hofu"

maumivu kama ya mwanamke mwenye uchungu wa kuzaa

Mwandishi anazungumzia hofu ya wafalme kana kwamba ni maumivu ambayo mwanamke hupitia wakati wa kuzaa na kuzungumzia maumivu haya kana kwamba ni mtu. "maumivu yaliwashika, kama mwanamke aliye katika uchungu wa kuzaa" au "wakaogopa, kama mwanamke anavyoogopa kupitia maumivu ya kuzaa"

Psalms 48:7

Na upepo wa mashariki unavunja meli za Tarshishi

Maana zinazowezekana ni 1) hii ni sitiari ambayo mwandishi anawaelezea wafalme kuwa na hofu kana kwamba ni meli zinazotikisika kwa sababu Mungu anaziangamiza kwa upepo mkali. "Walitikisika kwa hofu, kama meli za Tarshishi zinavyotikisika unapozivunja na upepo wa mashariki" au 2) hii ni alama ya kifupisho ambayo mwandishi anaelezea nguvu kuu ya Mungu.

upepo wa mashariki

Maana zinazowezekana ni 1) "upepo unaopuliza kutoka mashariki" au 2) "upepo mkali."

meli za Tarshishi

Maana zinazowezekana ni kuwa hii inamaanisha 1) meli zinazosafiri kwenda Tarshishi au zimetengenezwa katika mji wa Tarshishi au 2) meli yoyote kubwa ya kwenda baharini.

Kama tulivyosikia

Inadokezwa kuwa kile walichosikia ni mambo makubwa ambayo Mungu ametenda kipindi cha nyuma. "Kama tulivyosikia kuhusu mambo makubwa ambayo Mungu ametenda"

ndivyo tulivyoona

Hii inamaanisha kuwa wameona kithibitisho kuwa vitu walivyosikia ni vya kweli. "kwa hiyo tumeona Mungu akifanya mambo makuu sasa"

katika mji wa Yahwe wa majeshi, katika mji wa Mungu wetu

Misemo hii miwili inamaanisha Yerusalemu. "katika mji wa Mungu wetu, Yahwe wa majeshi"

imarisha

"ifanye kuwa imara." Hapa neno "imarisha" linamaanisha kutunza na kufanya kitu kuwa salama.

Psalms 48:9

katikati ya hekalu lako

"kama tulivyo kwenye hekalu lako"

Kama jina lako lilivyo ... ndivyo ilivyo sifa yako hadi mwisho wa dunia

Hapa neno "jina" linawakilisha tabia ya Mungu na sifa yake. Misemo hii miwili inalinganisha ukuu wa sifa ya Mungu na jinsi watu wanavyomsifu sana. "Jina lako ni kuu sana ... na kwa hiyo watu duniani kote wanakusifu sana" au "Watu duniani kote wamesikia kukuhusu ... kwa hiyo watu duniani kote wanakusifu"

hadi mwisho wa dunia

Huu ni msemo wa nahau unaomaanisha sehemu zote duniani.

mkono wako wa kuume umejaa haki

Mwandishi anazungumzia haki kana kwamba ni kitu ambacho Mungu anaweza kushika mkononi mwake. Hapa neno "mkono" unamaanisha uwezo na mamlaka ya Mungu kutawala. "unatawala kwa haki" au "wewe ni mwenye haki unapotawala"

Psalms 48:11

Acha mlima Sayuni ufurahi

Mwandishi anazungumzia mlima Sayuni kana kwamba ni mtu anayeweza kufurahi. Msemo unamaanisha watu wanaoishi Yerusalemu. "Acha wale wanaoishi mlima Sayuni wafurahi"

acha binti wa Yuda wafurahi

Mwandishi anazungumzia miji ndani ya Yuda kana kwamba ni watoto wa Yuda. Msemo huu unamaanisha watu wanaoishi katika miji hio. "acha watu wanaoishi katika miji ya Yuda wafurahi"

Psalms 48:12

Tembeeni katika mlima Sayuni, mzungukeni

Misemo hii miwli ina usambamba. "Tembeeni kote mkiuzunguka mlima Sayuni"

angalieni vizuri

"angalieni kwa umakini"

Psalms 48:14

atakuwa mwongozo wetu

"atatuongoza"

hadi kifo

Maana zinazowezekana ni 1) "hadi tufe" au 2) "milele."

Psalms 49

Psalms 49:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya wana wa Kora

"Hii ni zaburi ambayo wana Kora waliandika"

Sikieni haya, enyi watu wote; toeni maskio, wakazi wote

Misemo hii miwili ina usambamba. Kwa pamoja inaimarisha amri kwa watu wote kusikiliza.

toeni maskio

Huu ni msemo wa nahau unaomaanisha kutumia maskio kusikiliza. "sikilizeni"

wote wa chini na juu

Mwandishi anazungumzia watu walio wanyonge au wasio wa muhimu katika jamii kama kuwa chini na watu walio muhimu na wenye uwezo kama kuwa juu. Kwa pamoja, maneno "chini" na "juu" wanawakilisha watu wote. "wote watu muhimu na watu ambao sio wa muhimu" au "watu wa daraja katika jamii"

tajiri na maskini pamoja

Kwa pamoja, maneno "tajiri" na "maskini" yanamaanisha watu wote, bila kujali mali. "watu wote"

Psalms 49:3

Mdomo wangu utazungumza hekima

Hapa neno "mdomo" inamaanisha mtu anayezungumza. "Nitazungumza maneno ya hekima"

kutafakari kwa moyo wangu kutakuwa kwa uelewa

Hapa neno "moyo" linawakilisha akili na mawazo. "mawazo ambayo ninatafakari yatanielekeza kwenye uelewa"

tega sikio langu

Mwandishi anazungumzia kusikiliza kitu kwa makini kana kwamba ni kuinamisha sikio la mtu kwa mtu anayezungumza. "sikiliza kwa makini"

kwa kinubi

"kama ninavyocheza kinubi"

Kwa nini niogope ... visigino vyangu?

Mwandishi anatumia wali hili kuweka mkazo kwamba hakuna sababu ya kuogopa vitu vibaya vinapotokea. "Sina sababu ya kuogopa ...visigino vyangu."

siku za uovu

"vitu viovu vikitokea." Hapa neno "siku" linamaanisha nyakati kwa ujumla.

udhalimu unaponizunguka katika visigino vyangu

Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi anazungumzia hamu za uovu za adui zake kana kwamba ni mnyama anayewinda wanyama wengine aliye tayari kumpita. "wakati udhalimu wa watu wenye dhambi unapokuwa tayari kunishinda" au 2) adui wa mwandishi wanamzunguka wakati wanatenda udhalimu wao. "adui zangu wanaponizunguka"

Psalms 49:6

wale wanaotumaini katika mali zao

Watu hawa wanatumaini kuwa mali zao zitawaepusha na mateso.

kuhusu kiasi cha utajiri wao

kiasi kikubwa cha kitu

Ni hakika kuwa hakuna mtu

"Hakuna namna ambayo yeyote anaweza" au "Hakuna anayeweza"

hakuna mtu anayeweza kumkomboa ndugu yake au kumlipa Mungu kwa ajili yake

Misemo yote hii inaeleza kuwa mtu hawezi kumpa Mungu fedha ya kutosha ya kuepuka kifo. "hakuna mtu anayeweza kulipa fedha kwa Mungu ili ndugu yake asife"

ukombozi wa maisha ya mtu ni gharama

"inagharimu sana kukomboa maisha ya mtu"

Psalms 49:9

ili mwili wake usioze

Hii inamaanisha mwili kuoza katika kaburi.

ataona uozo

Mwandishi anazungumzia kupitia kitu kana kwamba ilikuwa ni kukiona hicho kitu. "atakufa na mwili wake kuoza"

Watu wenye hekima hufa; mpumbavu na mjinga wote wanaangamia

Mwandishi anamaanisha watu wote kwa kuwataja wale walio na hekima nyingi zaidi na kidogo zaidi.

mjinga

mtu ambaye hajui kitu

Psalms 49:11

Mawazo yao ya ndani

"Imani yao"

nasehemu wanazoishi, kwa vizazi vyote

"na sehemu wanazoishi zitaendelea vizazi vyote"

wanaita ncho baada ya majina yao

"wanaita nchi zao kwa majina yao wenyewe." "wanamiliki nchi zao wenyewe"

Psalms 49:12

Lakini mtu, akiwa na mali

"Lakini mtu, hata kama ana mali"

Hii, njia yao, ni upuuzi wao

Mwandishi anazungumzia hatima ya wapumbavu kana kwamba ni mwisho wao katika njia wanayotembea. "Hii ndio hatima ya wale wanaotenda upuuzi"

lakini baada yao

"lakini baada ya kufa"

Psalms 49:14

Taarifa ya jumla:

Mwandishi anaendelea kuwaelezea watu wanaoamini kuwa mali yao itawaokoa.

Kama kondoo

Mwandishi anawafananisha watu watakaokufa kama kundi la kondoo. Kama kondoo amabvyo hawawezi kutoroka wakati bucha anapoamua kuwachinja, kwa hiyo watu hawatatoroka ukifika wakati wao kufa.

wamechaguliwa

"Mungu amewachagulia"

mauti itakuwa mchungaji wao

Mwandishi anazungumzia watu kufa kwa kutaja mauti kama mtu ambaye ni mchungaji anayewaongoza katika kaburi. "mauti itawapeleka kama mchungaji anavyowaongoza kondoo kwenda machinjioni"

asubuhi

Hapa neno "asubuhi" ni sitiari inayomaanisha wakati ambapo Mungu atawathibitisha watu wenye haki na kuwaokoa kutoka kwa watu waovu.

miili yao itamezwa kuzimu

Mwandishi anazungumzia kuzimu, sehemu ya wafu, kana kwamba ni mtu au mnyama. Anazungumzia uozo wa miili iliyokufa kana kwamba kuzimu inaila. "miili yao itaoza kaburini"

Mungu atakomboa maisha yangu kutoka kwenye nguvu ya kuzima

Mwandishi anazungumzia kuzimu kana kwamba ni mtu aliye na nguvu juu ya wale walio kufa. Kutokana na muktadha, inadokezwa kwamba uwezo huu unamaanisha kuteketeza miili ya wafu.

Mungu atakomboa maisha yangu

Hapa neno "maisha" linamaanisha mtu mzima. "Mungu atanikomboa"

Psalms 49:16

utukufu wa nyumba yake unaongezeka

neno "utukufu" hapa unamaanisha mali au utajiri. Maana zinazowezekana ni 1) "atakapopata utajiri zaidi katika nyumba yake" au 2) "familia yake inapokuwa tajiri zaidi."

hatachukua kitu

"hatachukua kitu chochote kwenda nacho kaburini"

utukufu wake hautamfuata chini

Msemo "kwenda chini" unamaanisha wakati mtu anapokufa. "utukufu wake hautamfuata atakapokufa" au "hatatunza sifa yake atakapokufa"

Psalms 49:18

Akabariki nafsi yake

Hapa neno "nafsi" linamaanisha mtu mzima. Msemo huu unamaanisha kuwa alijiona kuwa na furaha na mafanikio kwa sababu ya utajiri wake. "Akajipongeza mwenyewe"

na watu wanakusifu unapoishi kwa ajili yako mwenyewe

Hapa mwandishi anatoa kauli ya ujumla kuhusu jinsi watu wanavyozungumza kuhusu watu wengine waliofanikiwa kulingana na mtazamo wa kidunia.

unapoishi kwa ajili yako mwenyewe

Msemo huu unamaanisha kuishi kwa mafanikio kulingana na mtazamo wa kidunia. "fanya vyema kwa ajili yako" au "ishi kwa mafanikio"

ataenda katika kizazi cha baba zake

"ataenda mahali kizazi cha baba yake kilipo." Hii ni tasifida inayomaanisha kwamba mtu tajiri atakufa na kuungana na mababu zake kaburini. "ataungana na mababu zake kaburini"

hawataona nuru tena

wale ambao "hawataona" ni mtu tajiri na mababu zake. Neno "nuru" inaweza kuwa inamaanisha jua au ni sitiari ya uhai. "hawataliona jua tena" au "hawataishi tena"

Psalms 50

Psalms 50:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii ni wimbo unaofundisha watu.

Zaburi ya Asafu

"Hii ni zaburi ambayo Asafu aliandika."

Mwenye nguvu, Mungu, Yahwe

Mwandishi anatumia majina matatu tofauti kumzungumzia Mungu.

akaiita dunia

Hapa neno "dunia" inamaanisha watu ambao wanaishi duniani. "akawaita watu wote"

kutoka kuchomoza kwa jua hadi kuzama kwake

Msemo huu unamaanisha upande wa mashariki, ambapo jua huchomoza, na magharibi, ambapo jua huzama. Mwandishi anatumia tofauti hizi mbili kuwakilisha sehemu zote duniani. "kila sehemu duniani"

Sayuni, ukamilisho wa uzuri

Maana zinazowezekana 1) "Sayuni, ambayo uzuri wake ni kamili" au 2) "Sayuni, mji mzuri zaidi."

Mungu ameng'aa

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni nuru inayong'aa. Hii inamaanisha Mungu kusababisha watu kujua kuhusu utukufu wake. "Utukufu wa Mungu unang'aa kama taa"

Psalms 50:3

habaki kimya

Mwandishi anatumia kauli hii hasi kusisitiza kitu chanya. "huzungumza ili kila mtu aweze kumsikia"

moto unameza mbele yake

Mwandishi anazungumzia moto kuunguza vitu kana kwamba ulikuwa ukiwala. "moto unachoma mbele yake"

kuna tufani inayomzunguka

"kuna tufani kubwa imemzunguka"

Huita mbingu juu na dunia

Maana zinazowezekana ni 1) Mungu anawaita wote wanaoishi mbinguni na duniani kuwa mashuhuda akiwa anawahukumu watu wake au 2) Mungu anazungumza na mbingu na dunia kana kwamba ni watu, na anawaita kuwa mashahidi wakati anawahukumu watu wake.

Psalms 50:6

Mbingu zitatangaza

Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi anatumia neno "mbingu" kumaanisha malaika wanaoishi huko. au 2) mwandishi anazungumzia "mbingu" kana kwamba ni mtu anayeshuhudia kuhusu haki ya Mungu.

Psalms 50:7

Sita kulaumu kwa sadaka zako

"Nitakulaumu, ila sio kwa sadaka zako." Mungu anaeleza kuwa sadaka zao sio sababu ya kuwalaumu.

laumu

"kemea" au "karipia"

sadaka zako za kuteketeza daima ziko mbele yangu

Hii inaelezea kwa nini Mungu hawalaumu kwa ajili ya sadaka zao. Msemo huu " daima ziko mbele yangu" unamaanisha kuwa katika uwepo wa Mungu na unamaanisha kuwa watu wake daima wanatoa sadaka zao cha kuteketeza kwake. "huwa mnatoa sadaka zenu za kuteketeza kwangu"

Psalms 50:9

mazizi

"kizimba"

ng'ombe kwenye vilima elfu

Msemo "kwenye vilima elfu" haiwakilishi idadi kamili ya ng'ombe ambazo Mungu anamiliki. Namba ni kukuza kwa neno ambayo inasisitiza kuwa Mungu anamiliki ng'ombe wote duniani. "ng'ombe wote duniani ni wangu"

vilima elfu

"vilima 1,000"

Nawajua ndege wote

Hapa neno "nawajua" inadokeza umiliki. "Ninamiliki ndege wote"

Psalms 50:12

Kama nina njaa

Hii inaelezea kitu ambacho hakiwezi kutokea, kwa kuwa Mungu huwa hapati njaa.

Je! Nitakula nyama ya mafahali au kunywa damu ya mbuzi?

Mungu anauliza swali hili balagha kusisitiza kuwa huwa hafanyi hivi vitu na kwa hiyo haitaji sadaka zao. "Sili nyama ya mafahali au kunywa damu ya mbuzi."

Psalms 50:14

Mtolee Mungu

Hapa Mungu inamaanisha mwenyewe. "Nitolee mimi"

lipi nadhiri zako kwa Aliye juu

Mwandishi anazungumzia "nadhiri" kana kwamba ni fedha ambayo mtu analipa kwa Mungu. "timiza nadhiri zako kwa Aliye juu" au "fanya kile ulichomwahidi aliye juu kufanya"

katika siku ya shida

Hapa neno "siku" linamaanisha wakati wowote. "unapokuwa na taabu"

Psalms 50:16

Lakini kwa waovu Mungu anasema

Hapa Mungu bado anazungumza na anajizungumzia mwenyewe katika hali ya mtu wa tatu. "Lakini kwa waovu nasema"

kwa waovu

Neno "waovu" inamaanisha watu waovu kwa ujumla. "kwa watu waovu"

Una nini na kutangaza sheria zangu ... na kutupa maneno yangu?

Mungu anatumia swali hili kukemea watu waovu. Swali hili linaweza kugeuzwa kuwa kauli. "Haina maana kwamba unatangaza sheria na agano langu, kwa kuwa unachukia maagizo yangu na kutupa maneno yangu." au "Sio sawa kwako kutangaza sheria zangu"

kwamba umechukua agano langu mdomo mwako

Mungu anazungumzia watu waovu kutongoa maneno ya agano kana kwamba wanaweka agano midomoni mwao. "kuzungumza kuhusu agano langu"

kutupa maneno yangu

Mungu anazungumzia watu waovu kukataa anachosema kana kwamba walikuwa wakitupa nje takataka. "kukataa ninachosema"

Psalms 50:18

unakubaliana naye

Maana zinazowezekana ni 1) kwamba wanakubaliana na matendo ya mwizi. "unamkubali" au 2) kwamba wanamuunga mwizi katika matendo yake. "unamuunga"

Unatoa mdomo wako kwa uovu

Mungu anamzungumzia mtu kuongea vitu vya uovu kana kwamba mdomo wa mtu ni mjumbe ambaye mtu anamtuma kufanya vitu viovu. "Daima huwa unasema vitu viovu"

ulimi wako unaeleza uongo

Neno "ulimi" linawakilisha mtu anayezungumza. "huwa unasema uongo daima"

Unakaa na kuzungumza dhidi ya ndugu yako; unamkashifu mtoto wa mama yako

Misemo hii miwili ina maana moja lakini inatumia maneno tofauti. Mungu anawashtaki kwa kuongea uongo dhidi ya watu wa familia yao wenyewe.

Unakaa na kuzungumza

"Kukaa na kuzungumza" dhidi ya mtu inaashiria kuwa mtu huyu anawaza kwa makusudi vitu vibaya vya kusema kwa mtu. "Huwa unawaza namna ya kuongea"

Psalms 50:21

ulifikiri kuwa mimi ni mtu kama wewe

kwa kuwa Mungu amekaa kimya na bado hajawakemea watu waovu kwa matendo yao, walidhani kuwa Mungu amekubaliana na walichofanya. "ulifikiri kuwa mimi ni mtu nayetenda kama nyie"

shutumu

"kemea" au "karipia"

kuleta ... vitu vyote ulivyofanya

Mungu anazungumzia kuorodhesha mambo maovu yote waliyotenda. "orodhesha ... vitu vyote mlivyofanya"

mbele ya macho yako

Hapa, kuwa "mbele ya macho yako" inamaanisha kuwa ni sehemu wanayoweza kuona. Hii inamaanisha kuwa hawataweza kukana mashtaka ambayo Mungu anawaletea. "mbele yenu" au "ili usiweze kuyakana"

nyie mnaomsahau Mungu

Mungu anawazungumzia waovu kumkataa kana kwamba wamemsahau. "Anajizungumzia katika hali ya mtu wa tatu. "nyie mlio nikataa"

nitawararua katika vipande

Mungu anazungumzia kuwaangamiza waovu kana kwamba ni simba anakula mawindo yake. "nitakuangamiza"

Psalms 50:23

hupanga njia yake katika namna sahihi

Mungu anazungumzia jinsi mtu anavyoishi kana kwamba ni njia ambayo mtu anasafiri. "huishi maisha yake katika njia sahihi"

Nitaonesha wokovu wa Mungu

Hapa Mungu anazungumzia kumwokoa mtu kana kwamba ilikuwa ni kumsababisha mtu kuona wokovu wake. Anajizungumzia katika hali ya mtu wa tatu. "Nitamwokoa"

Psalms 51

Psalms 51:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Katika zaburi hii Daudi anamwomba Mungu msamaha.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

wakati nabii Nathani alipokuja kwake

Inaweza kuelezwa wazi Nathani alifanya nini alipokuja kwa Daudi, kwa sababu zaburi hii ni majibu ya hayo. "wakati nabii Nathani alipokuja kwa Daudi na kumkemea"

alipolala na Bathsheba

"baada ya Daudi kulala na Bathsheba"

kwa ajili ya umati wa matendo yako ya huruma

"kwa sababu unafanya mambo mengi sana ya huruma"

weka doa makosa yangu

Kusamehe dhambi inazungumziwa kana kwamba ni kati ya 1) kuwekea doa au 2) kufuta kumbukumbu za dhambi. "samehe dhambi zanguu kama mtu anazifuta" au "sahau dhambi zangu kama mtu anayefuta kumbukumbu za dhambi"

Nioshe kikamili kutokana na udhalimu wangu ... nisafishe na dhambi zangu

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja.

Nioshe kikamili kutokana na udhalimu wangu

Kukubaliwa na Mungu kunazungumziwa kama kuwa msafi. Mungu huwafanya watu kukubalika kwa kusamehe dhambi zao. "Osha dhambi zangu zote" au "Samehe dhambi zangu zote ili nikubalike kwako"

kikamili

"kikamilifu"

nisafishe na dhambi zangu

Kukubalika kwa Mungu kunazungumziwa kama kuwa msafi. Mungu huwafanya watu kukubalika kwa kusamehe dhambi zao. "Nifanye kuwa msafi na dhambi yangu" au "nisamehe kwa dhambi yangu ili niwe msafi"

Psalms 51:3

dhambi yangu daima iko mbele yangu

Kutoweza kusahau dhambi zake inazungumziwa kana kwamba zilikuwa mbele yake wakati wote ambapo anaweza kuziona. "huwa nina ufahamu wa dhambi zangu" au "siwezi kusahua dhambi zangu"

na kufanya kilicho kiovu mbele yako

"na nimefanya kilicho kiovu"

Psalms 51:5

Tazama, nilizaliwa katika udhalimu ... tazama, unatamani uaminifu

Matumizi mawili ya "Tazama" hapa yanavuta nadhari kati ya tofauti ya mambo haya mawili. "Hakika nilizaliwa katika udhalimu ... Lakini unatamani uaminifu"

Tazama, nilizaliwa katika udhalimu ... mara tu mama yangu alipochukua mimba yangu, nilikuwa katika dhambi

Misemo hii miwili inamaana moja na inatumika pamoja kuleta msisitizo.

nilizaliwa katika udhalimu

Kuwa mwenye dhambi inazungumziwa kama kuwa kwenye udhalimu. "nilikuwa mwenye dhambi tayari wakati nazaliwa"

mara tu mama yangu alipochukua mimba yangu, nilikuwa katika dhambi

Kuwa mwenye dhambi inazungumziwa kama kuwa kwenye dhambi. "hata mama yangu alipobeba mimba yangu, nilikuwa mwenye dhambi"

unatamani uaminifu moyoni mwangu

Moyo unawakilisha kati ya 1) hamu za mtu au 2) mtu mzima. "Unataka nitamani uaminifu" au "unataka niwe mwaminifu"

Psalms 51:7

Nitakase ... nitakuwa msafi ... nioshe ... nitakuwa mweupe zaidi ya theluji

Kukubalika kwa Mungu kunazungumziwa kama kuwa msafi au mweupe. Mungu huwafanya watu kukubalika kwa kusamehe dhambi zao.

Nitakase kwa hisopo

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba Mungu ni kuhani ambaye humwaga maji juu yake kumfanya akubalike kwa Mungu. "Nifanye nikubalike kwa kunimwagia maji na hisopo" au "Nisamehe kwa dhambi zangu ili nikubalike kwako"

hisopo

Huu ni mmea ambao kuhani alitumia kunyunyizia maji au damu juu ya watu au vitu kuvifanya visafi kiutaratibu, yaani, kukubalika kwa Mungu.

mweupe zaidi ya theluji

Kutokuwa na dhambi kunazungumziwa kama kuwa mweupe. "mweupe sana"

furaha na shangwe

Maneno haya mawili yana maana moja na yana sisitiza hamu yake kusikia mambo ya furaha.

ili kwamba mifupa uliyovunja ifurahi

Kujisikia huzuni kali inazungumziwa kana kwamba mifupa yake imevunjika. "Kwa kuwa umesababisha huzuni kali ndani yangu. Acha nifurahi tena!"

Ficha uso wako mbali na dhambi zangu

Kufikiria kuhusu dhambi za mtu inazungumziwa kama kuziona. Kusamehe au kukataa kuwaza kuhusu dhambi inazungumziwa kama kuchagua kutoziona. "Usizitazame dhambi zangu" au "Usikumbuke dhambi zangu"

wekea doa udhalimu wangu

Kusamehe au kukataa kuwaza kuhusu dhambi inazungumziwa kama kati ya 1) kuziwekea doa au 2) kufuta kumbukumbu iliyoandikwa ya dhambi. "samehe dhambi zangu kama mtu anafuta kitu" au "samehe dhambi zangu kama mtu anayefuta kumbukumbu ya dhambi"

Psalms 51:10

Umba ndani yangu moyo msafi

Hapa "moyo" unawakilisha hisia na hamu. Kujitoa kamili na kuwa mtiifu kwa Mungu inazungumziwa kama na kuwa na moyomsafi. "Unifanye nijitoe kamili kwako" au "Nifanye nitake kukutii wewe daima"

fanya upya roho safi ndani yangu

Hapa "roho" inawakilisha mtazamo na hamu za Daudi. "fanya mtazamo wangu kuwa sawa" au "nifanye nitake daima kufanya kilicho sawa"

Usiniondoe mbali na uwepo wako

"Usinilazimishe kwenda mbali na wewe." Kukataliwa na Mungu kunazungumziwa kama kulazimishwa kwendambali naye. "Usinikatae mimi kama mmoja wa watu wako"

Psalms 51:12

na uniendeleza

"na unishike" au "unisaidie"

njia zako

"jinsi unavyotaka watu waishi" au "unachotaka watu wafanye"

watenda makosa ... watenda dhambi

Maneno haya mawili yanamaanisha watu wale wale.

Psalms 51:14

kumwaga damu

Msemo huu unamaanisha kumua mtu mwingine.

Bwana, fungua midomo yangu, na mdomo wangu utaeleza sifa yako

Kuwa na uwezo wa kuongea inazungumziwa kama midomo kuwa wazi. Hapa kutoweza kuongea ni ishara ya kuwa na hatia ya dhambi na kutoweza kujitetea. "Bwana, nifanye niweze kuongea, na nitakusifu"

hupendezwi na sadaka ... hauna furaha na sadaka za kuteketeza

Hii inamaanisha kwamba Mungu anataka kitu cha muhimu zaidi ya hivi vitu. "Sadaka haitoshi kukupendeza ... unataka kitu zaidi ya sadaka za kuteketeza"

Psalms 51:17

Sadaka za Mungu

"Sadaka zinazompendeza Mungu"

roho iliyovunjika

Roho iliyovunjika inawakilisha mtazamo wa unyenyekevu. "unyenyekevu" au "mtu anayekuwa mnyenyekevu"

moyo ulio vunjika na wenye majuto

Kuwa mnyenyekevu na majuto juu ya dhambi za mtu inazungumziwa kama kuwa na moyo ulio vunjika na wa majuto. Moyo unawakilisha hisia na nia. "huzuni na unyenyekevu" au "mtu anayejuta kwa ajili ya dhambi zake na ni mnyenyekevu"

uzijenge kuta za Yerusalemu

Kuta za mji huulinda mji na watu waliomo. Maana zinazowezekana ni 1) "utuwezeshe kujenga kuta za Yerusalemu" au 2) "ilinde Yerusalemu na uifanye kuwa imara"

watu wetu watatoa mafahali katika madhabahu yako

Fahali ni ng'ombe dume. Mafahali mara nyingi hutumika kama wanyama wa sadaka, kulingana na maagizo ya Mungu.

Psalms 52

Psalms 52:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Katika zaburi hii anayezungumziwa ni Doegi. Wakati Sauli alipotaka kumuua Daudi, Doegi alimwambia Sauli mahali alipokuwa Daudi ili Sauli ampate.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Doegi ... Mwedomi

Haya ni majina ya wanaume.

Kwa nini unajivunia kufanya fujo, wewe mwanamme shujaa?

Swali hili linaonesha jinsi Daudi alivyokuwa na hasira na yule aliyeleta matatizo. "Hutakiwi kuwa na majivuno sana kwa kutengeneza matatizo, wewe mwanamme shujaa."

wewe mwanamume shujaa

Inawezekana Daudi alikuwa akitumia kejeli alipokuwa anamwita Doegi hivi. "wewe, unadhani una uwezo sana"

Uaminifu wa agano wa Mungu unakuja

Daudi anazungumzia uaminifu wa Mungu wa agano kana kwamba ni kitu kilichoweza kuja. Inawezekana alikuwa akimaanisha ahadi za Mungu kuwalinda watu wake na watu waovu. Hii inaweza kuelezwa wazi. "Mungu ni mwaminifu kutunza ahadi za agano lake" au "Mungu huwalinda kwa uaminifu watu wake kutoka kwa watu waovu kama wewe"

wembe mkali

ubapa mkali

Ulimi wako unapanga maangamizi kama wembe mkali, unafanya udanganyifu

Hapa ulimi unalinganishwa na wembe mkali ambao unauwezo wa kusababisha madhara makubwa. "Ulimi wako unadhuru watu kama wembe mkali ufanyavyo, unapopanga maangamizi na kudanganya wengine"

Ulimi wako

Hapa "ulimi wako" unaashiria mtu ambaye Daudi anazungumza naye. "Wewe"

Psalms 52:3

Kauli Unganishi:

Daudi anaendelea kuzungumza na "mwanamme shujaa" wa 52:1

kudanganya kuliko kuzungumza haki

"unapenda kudanganya zaidi ya kusema kilicho sawa"

Psalms 52:4

maneno yanayomeza wengine

Hapa maneno yanayowadhuru wengine yanazungumziwa kana kwamba yalikuwa wanyama wanayo wameza watu. "maneno yanadhuru wengine"

wewe ulimu wa uongo

Hii inamaanisha mtu ambaye mwandishi anazungumza naye. "wewe msemaji wa uongo" au "wewe muongo"

atakuchukua juu ... kukunyofoa ... kukung'oa

Misemo hii yote mitatu ni njia tofauti ya kusema "kukutoa"

kukung'oa katika nchi ya walio hai

Kuwa hai duniani inazungumziwa kana kwamba watu ni mimea yenye mizizi ardhini. Mungu kumuua mtu inazungumziwa kama kuchimba mizizi ya mmea na kuitoa ardhini. "atakutoa katika nchi ya walio hai" au "Atakuua ili usiwepo tena dunia pamoja na watu waishio"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 52:6

Mwenye haki pia ationa na kuogopa

"Wenye haki pia watamwona Mungu akimuondoa na watamwogopa"

Tazama

"hakika"

hakumfanya Mungu kuwa kimbilio lake

Hapa anayekimbiliwa inamaanisha mlinzi. "hakumfanya Mungu kuwa mlinzi wake" au "hakumwomba Mungu kumlinda"

Psalms 52:8

mti wa kijani wa mzeituni

Majani ya kijani ya mizeituni yana nguvu na ni imara. Hayaanguki.

mimi ni kama mti wa kijani wa mzeituni ndani ya nyumba ya Mungu

Kuwa salama inazungumziwa kama kuwa mti imara. "Nina nguvu katika nyumba ya Mungu, kama mti wa kijani wa mzeituni" au "Kwa sababu naabudu katika nyumba ya Mungu, niko salama kama mti wa kijani wa mzeituni"

ndani ya nyumba ya Mungu

Hii inamaanisha hekalu la Mungu

Nitasubiri jina lako, kwa sababu ni zuri

Jina la Mungu linamaanisha Mungu mwenyewe. Kumsubiri Mungu inaashiria kumsubiri Mungu kumsaidia. "Nitakusubiri, kwa sababu u mwema" au "Nitakusubiri unisaidie, kwa sababu u mwema"

Psalms 53

Psalms 53:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Mahalathi

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

watoto wa wanadamu

Hii inamaanisha watu wote

anayemtafuta

Kumtafuta Mungu kama mtu inazungumziwa kama "kumtafuta" Mungu. Maana zinazowezekana ni 1) kutaka kumjua Mungu. "wanaotaka kumjua yeye" au 2) kumwabudu Mungu. "wanao mwabudu yeye"

Wote wamegeuka

Kumkataa Mungu na kilicho sawa kinazungumziwa kama kugeuka. "Wote wamegeuka kutokakufanya kilicho sawa" au "Wote wamemkataa Mungu"

Psalms 53:4

Je wale wanaotenda udhalimu hawana uelewa - wale ... Mungu?

Swali hili linatumika kuonesha mshtuko ambao mwandishi anahisi kwa sababu watu wanatenda dhambi sana. Inaweza kuandikwa kama kauli mbili. "Wale wanaotenda udhalimu kana kwamba hawajui chochote. Wanawameza watu wangu kana kwamba wanakula mikate, na hawamwiti Mungu!

wale wanao wameza watu wangu kana kwamba wanakula mkate

Kuangamiza watu inazungumziwa kama kuwameza. Kufanya kana kwamba walikuwa wakila mikate inaashiria kuwa walifanya kwa urahisi sana bila kuhisi hatia. "wale wanaowaangamiza watu wangu kwa uhuru kana kwamba wanakula mikate"

Mungu ataitawanya mifupa ya yeyote atakayeweka kambi dhidi yako

Kutawanya mifupa ya watu inamaanisha kuwaua na kuruhusu mifupa yao kubaki walipofia na bila kuwazika vizuri. "Mungu atamwangamiza kabisa yeyote atakaye weka kambi dhidi yako, na mifupa yao italala imetawanyika kwenye ardhi"

yeyote atakayeweka kambi dhidi yako

Kuweka kambi dhidi ya watu inamaanisha kuwashambulia. Majeshi ya adui yalikuwa yakisafiri na kuweka kambi na kuishi kwa muda karibu na watu waliotaka kuwavamia. "yeyote atakaye wavamia"

Psalms 53:6

O, kwamba wokovu wa Israeli uje

Neno "O" hapa linatambulisha mshangao unaoonesha matumaini au ombi. "Natumaini kuwa wokovu wa Israeli utakuja" au "Ninaomba kwamba wokovu uje"

wokovu wa Israeli uje kutoka Sayuni

Wokovu unaashiria Mungu, mwokozi, ambaye hekalu lake liko Sayuni. "mwokozi wa Israeli utakuja kutoka Sayuni" au "Mungu atakuja kutoka Sayuni na kuokoa Israeli"

Mungu atakapo warudisha watu wake kutoka mateka

"Mungu atakapo okoa watu wake wafungwa"

Yakobo atasherehekea na Israeli kufurahi!

Misemo hii miwili ina maana moja.

Yakobo

Hapa "Yakobo" inamaanisha uzao wa Yakobo, Waisraeli.

Psalms 54

Psalms 54:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii ni ombi kwa ajili ya msaada.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

kwenye vyombo vya nyuzi

"watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu"

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Wafizi

Watu kutoka mji wa Zifu katika milima ya Yuda, kusini mashariki mwa Hebroni.

Kwani Daudi hajifichi pamoja na sisi?

Swali hili linatumika kuonesha kuwa hili ni jambo muhimu ambalo Sauli anapaswa kujua. "Daudi anajificha na sisi."

Niokoe, Mungu, kwa jina lako

Hapa jina la Mungu linaashiria tabia yake. Inaweza kumaanisha zaidi uwezo wake au haki yake. "niokoe, Mungu, kwa uwezo wako"

nihukumu katika uwezo wako

Kumhukumu Daudi hapa inaashiria kuwaonesha watu kuwa Daudi hana hatia. Mungu anapotumia nguvu zake kumwokoa Daudi, watu watajua kuwa Mungu amemhukumu na hana hatia. "Kwa uwezo wako, waoneshe watu kuwa sina hatia" au "Waoneshe watu kuwa sina hatia kwa kutumia nguvu zako kuniokoa"

yape masikio maneno ya

Kumpa mtu masikio inaashiria kumsikiliza. "sikiliza maneno yangu"

maneno ya mdomo wangu

Msemo huu unamaanisha kile alichosema mnenaji. "maneno yangu" au "ninachosema kwako"

wameinuka dhidi yangu

Kuinuka dhidi ya mtu inaashiria kujiandaa kumshambulia au kumshambulia kabisa. "wamejiandaa kunishambulia" au "wananishambulia"

watu wasio na huruma

"wanaume wasio na huruma"

wametafuta maisha yangu

Kutafuta maisha ya mtu inamaanisha kujaribu kumuua. "wamejaribu kuniua" au "wanataka kuniua"

hawajamuweka Mungu mbele yao

Kumweka Mungu mbele yao inaashiria kuwa makini na Mungu. "hawamzingatii Mungu" au "hawamjali Mungu"

Psalms 54:4

anaye nishikilia

Kumtetea Daudi na kumweka salama inazungumziwa kama kumshikilia. "anaye nitetea" au "anaye niweka salama"

Atawalipa adui zangu kwa uovu

Adhabu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni malipo. "Atafanya uovu kwa adui zangu ambao walioufanya kwangu" au "Atasababisha uovu ambao adui zangu walifanya kwangu ufanywe kwao"

katika uaminifu wako, waangamize

Hapa Daudi anabadilisha kutoka kuzungumza kumhusu Mungu na kuongea naye. "Mungu, waangamize kwa sababu wewe ni mwaminifu kwangu"

Psalms 54:6

Nitatoa shukrani kwa jina lako, Yahwe, kwa kuwa ni zuri

Jina la Yahwe linamwakilisha yeye. "Nitatoa shukrani kwako, Yahwe, kwa kuwa u mwema"

jicho langu limetazama

Jicho linamaanisha mtu. "Nimetazama"

jicho langu limetazama kwa ushindi juu ya adui zangu

Maana zinazowezekana ni 1) kuona kuwa adui zake wameshindwa. "Nimeona kuwa adui zangu wameshindwa" au 2) kuwashinda adui zake. "Nimewashinda adui zangu"

Psalms 55

Psalms 55:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

kwenye vyombo vya nyuzi

"watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu"

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Toa sikio kwa ombi langu

Kutoa sikio kwa mtu inamaanisha kusikiliza. "Sikiliza ombi langu"

usijifiche kwa ombi langu

Kukataa kuvutia nadhari ombi lake inazungumziwa kama kujificha mbali na hilo ombi. "usiache kujali ombi langu"

kwa sababu ya sauti ya adui zangu

Hapa "sauti" inawakilisha walichosema. "kwa sababu ya kile ambacho adui zangu wanasema"

wanaleta shida kwangu

Kusababisha taabu inazungumziwa kama kuleta taabu. "wananisababisha kuwa na taabu kubwa" au "wanafanya vitu viovu kwangu na kwa hiyo nateseka"

Psalms 55:4

Moyo wangu unatetemeka ndani yangu

Hapa, "moyo unatetemeka" inamaansiha maumivu yake ya kihisia au kuteseka. Kuteseka huku ni kwa sababu ya uoga. "Ninateseka kwa sababu ninaogopa sana"

hofu yangu ya mauti imeniangukia

Kuwa na hofu sana inazungumziwa kana kwamba hofu ni kitu kinachomwangukia mtu. "Ninaogopa sana kuwa nitakufa" au "Ninahofu kuwa nitakufa"

Uoga na kutetemeka zimeniangukia

Kuwa na hofu na kutetemeka kunazungumziwa kana kwamba hofu na kutetemeka ni vitu vinavyokuja kwa mtu. "Nimekuwa na hofu sana na kutetemeka"

kitisho kimenilemea

Kuhisi kitisho inazungumziwa kana kwamba kitisho ni kitu kinachoweza kuwafunika watu. "Ninahisi kitisho kibaya" au "Ninahofu sana"

Psalms 55:6

O, ningekuwa na mbawa kama njiwa!

Mshangao huu unaelezea kitu ambacho mwandishi anatamani sana. "Ninatamani sana ningekuwana mbawa kama njiwa"

Basi ningepaa

"Kama ningekuwa na mbawa, ningepaa"

Tazama

"Hakika"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 55:8

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anamaliza kueleza alichokisema.

tufani

dhoruba kali

Wameze

Kuangamiza kitu inazungumziwa kama kukila chote. Maana zinazowezekana ni "Angamiza mipango ya adui zangu" au "Waangamize adui zangu"

changanya lugha yao

"Lugha" hapa inawakilisha kile ambacho watu walikuwa wakiambiana, na inaweza kumaanisha hasa wao kuzungumzia mipango ya kufanya uovu. Kuwachanganya inawaklisha kuwafanya watu washindwe kuelewana. "wachanganye wanapozungumza pamoja" au "changaya mipango yao"

Psalms 55:10

wanazunguka kuta zake

"vurugu na ugomzihuzunguka kuta zake." Vurugu na ugomvi zinazungumziwa kana kwamba ni watu. Hii inaweza kuelezwa kwa kuelezea watu wanaosababisha vuruguna ugomvi. "watu wanatembea kwenye kuta za mji, wakiwa na vurugu na kupigana"

kuta zake

"juu ya kuta za mji" Miji ilikuwa imezungukwa na kuta nene za kuwalinda na adui. Watu waliweza kutembea juu ya kuta kuona kama kuna adui wanaokuja kwenye mji.

udhalimu na shida ziko katikati yake

Udhalimu na shida zinazungumziwa kana kwamba ni watu. "watu hufanya udhalimu na kuleta shida.katikati ya mji" au "watu hufanya matendo ya dhambi na kusababisha shida ndani yake"

shida

"taabu"

Uovu uko katikati yake

Uovu unazungumziwa kana kwamba ni mtu. "Watu hufanya vitendo vya uovu katikati ya mji" au "watu huteketeza vitu katika mji"

dhuluma na uongo haziondoki mitaa yake

Dhuluma na uongo zinazungumziwa kana kwamba ni watu. "Watu hudhulumu na kuwadanganya wengine katika mitaa ya mji, na hawaondoki" au "Watu huwadhulumu na kuwadanganya wengine katika mitaa ya mji"

mitaa yake

Hii inaweza kumaanisha sehemu za masoko katika mji.

Psalms 55:12

ningeweza kuibeba

Kuvumilia kukemewa inazungumziwa kama kuubeba. "ningeweza kubeba kukemewa" au "nisingekuwa na huzuni sana kuhusu kukemewa"

aliyejiinua dhidi yangu

Kuwa na majivuno na kumtusi mwingine inazungumziwa kama kujiinua dhidi ya mwingine. "kanitukana mimi" au "kanichukia"

Lakini ilikuwa ni wewe

Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba mtu aliyemkemea na kumsuta alikuwa hapo akimsikiliza.

mwenzangu na rafiki wangu wa karibu

"Wewe ulikuwa mwenzangu na rafiki wa karibu"

Sisi

Neno "sisi" inamaanisha mwandishi wa zaburi na rafiki yake.

pamoja na umati

Maana zinazowezekan ni 1) "pamoja" au 2) "pamoja na kundi"

Psalms 55:15

Acha mauti ije kwao ghafla

Mauti inazungumziwa kana kwamba ni mtu anayeweza kushambulia watu. "Acha adui zangu wafe ghafla"

acha waende chini kuzimu wakiwa hai

Kufa ghafla inazungumziwa kana kwamba watu walitakiwa kwenda kuzimu haraka sana hadi hawakufa kwanza. "acha waende kuzimu ghafla'

uovu ndipo wanapoishi

Uovu unazungumziwa kana kwamba ni kitu kinachoweza kuwa sehemu fulani. Tabia ya uovu ya adui zake inazungumziwa kana kwamba uovu ulikuwa pamoja nao au akribu yao. "huwa wanafanya vitu viovu wanapoishi"

katikati yao

Msemo huu unawekea mkazo wazo la uovu kuwa karibu yao sana. Hapa uovu unazungumziwa kama kutokuwa tu kwenyenyumba zao, bali mahali walipo. "Huwa wanafanya vitu viovu popote walipo" au "popote walipo"

Psalms 55:16

Mimi

Msemo huu unaonesha kuwa mwandishi ameacha kuzungumzia kitu kimoja na sasa ameanza kujizungumzia mwenyewe.

kuguna

"kulia"

atasikia sauti yangu

Hapa "sauti" inawakilisha kati ya 1) mwandishi wa zaburi au 2) malalamiko ya mwandishi wa zaburi au kilio chake. "atanisikia" au "atasikia kuguna kwangu"

maisha yangu

Hapa "maisha" inamwakilisha mwandishi wa zaburi. "mimi"

kwa kuwa wale waliokuwa wakipigana dhidi yangu walikuwa wengi

"kwa kuwa watu wengi walipigana dhidi yangu"

Psalms 55:19

atawasikia

"atawasikia adui zangu" au "atasikia kile ambacho adui zangu wanasema." Tafsiri zingine zinasema "watanisikia."

kuwaaibisha

"atawashinda na kuwaaibisha"

Psalms 55:20

ameinua mikono yake dhidi ya wale

Kuinua mkono dhidi ya watu inawakilisha kuwashambulia. Hii inaweza kuwa sitiari ya kusema vitu vinavyowaweka watu katika hatari au kuwasababisha kuwa katika shida. "amewashambulia wale" au "amewasiliti wale"

Mdomo wake

"Mdomo" wa mtu unawakilisha anachosema. "Kile ambacho rafiki yangu amesema"

Mdomo wake ulikuwa laini kama siagi

Maneno yanayopendeza au mazuri kusikia yanazungumziwa kana kwamba ni malaini na mepesi kumeza. "Alichosema kinapendeza kama siagi laini" au "Alisema vitu vizuri"

uhasama

"ovyo" au "chuki"

maneno yake

"Maneno" ya mtu yanawakilisha anachosema. "Alichosema"

maneno yake yalikuwa laini kuliko mafuta

Watu huweka mafuta kwenye ngozi zao kuifanya ijisikie vizuri, na huweka kwenye vidonda kuviponya. Maneno yaliyo yenye huruma au yenye msaada yanazungumziwa kana kwamba yalikuwa laini au ya kumbembeleza. "aliyosema yalikuwa yenye huruma na ya kumbembeleza kama mafuta" au "alisema vitu venye huruma"

yalikuwa panga zilizo chomolewa

Maneno yanayosababisha shida kwa watu yanazungumziwa kana kwamba ni panga zinazoweza kuumiza watu. "kile alichosema kiliwaumiza watu kama panga zilizochomolewa zifanyavyo" au "alichosema kiliwasababishia watu shida"

panga zilizo chomolewa

Neno "chomolewa" hapa linamaanisha kuwa panga zimetolewa kwenye makasha yake tayari kwa kutumiwa.

Psalms 55:22

Weka mizigo yako

Hapa mwandishi anazungumza na watu wanyofu wengine.

Weka mizigo yako kwa Yahwe

Hapa taabu zinazungumziwa kana kwamba ni mizigo ambayo watu wanatakiwa kubeba. Kumtumaini Mungu kutusaidia wakati tuna shida inazungumziwa kama kumwekea mizigo yetu juu yake ili atubebee. "Mpe Yahwe shida zako" au "Mwamini Yahwe kukusaidia na taabu zako zote kama mtu anavyomwamini mtu mwenye nguvu zaidi kubeba mzigo wake"

atakuchukua

Kumtunza mtu au kumsaidia mtu akiwa na shida inazungumziwa kama kumsaidia. "atakutunza" au "atakulinda"

kamwe hataruhusu mtu mwenye haki kupepesuka

Mtu ambaye anataka kudhuriwa vibaya na maafa fulani inazungumziwa kana kwamba anapepesuka au kuyumba na anataka kuanguka. "hatamuacha mtu mwenye haki ayumbe na kuanguka" au "hataacha mtu mwenye haki aangamizwe"

Lakini wewe, Mungu

Mwandishi anazungumza na Yahwe sasa.

shimo la uharibifu

Hii inaweza kumaanisha kaburi au jahannamu.

utawaleta waovu chini kwenye shimo la uharibifu

Hii inawakilisha kuwasababisha watu kufa. "utawasababisha waovu wafe" au "utawasababisha watu waovu kufa na kwenda sehemu ambapo wafu wapo"

wenye kiu ya damu na watu waongo

"watu wanadanganya na wanaotaka kuwaua wengine" au "wauaji waongo"

hata nusu ya urefu wa wengine

hata nusu ya urefu wa uhai wa wengine

Psalms 56

Psalms 56:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Yothani elemu rehokimu

Hii inaweza kuwa inaeleza mtindo au tuni ya muziki ya kutumia wakati wa kuimba zaburi hii. "Imba zaburi hii kwa kutumia tuni ya "Yothani elemu rehokimu" au "Imba kwa kutumia mtindo wa Yothani elemu rehokimu"

Yothani elemu rehokimu

Hii inaweza kumaanisha "Njiwa katika Miti ya Mwaloni ya Mbali."

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Michtamu

Maana ya neno "michtamu" haieleweki. Hii inaweza kuandikwa kama: "Hii ni zaburi ambayo Daudi aliandika."

wakati Wafilisti walipomchukua Gathi

"Wafilisti walipomkamata Gathi"

wanakandamiza shambulio lao

"wanakuja karibu na karibu ili kunishambulia"

Adui zangu wananikanyaga

Shambulio kali la adui linazungumziwa kana kwamba walikuwa wakitumia mwili wake kutembea. "Adui zangu wananishambulia sana"

Psalms 56:3

kwako

Neno "kwako" linamaanisha Mungu.

mtu tu anaweza kufanya nini kwangu?

Hapa swali linatumika kuonesha kuwa mwandishi wa zaburi haogopi watu, kwa sababu hawawezi kumdhuru kabisa. "watu tu hawawezi kufanya kitu kwangu!" au "watu tu hawawezi kunidhuru vibaya!"

mtu tu

"watu." Hii inadokezwa kuwa watu hawana nguvu, lakini Mungu ana uwezo.

Psalms 56:5

Siku nzima

"wakati wote"

wanapindisha maneno yangu

Kurudia kile ambacho mtu amesema lakini kubadilisha kidogo ili imaanishe kitu tofauti inazungumziwa kama kupindisha maneno yao. "wanasema kuwa nimesema vitu ambavyo sijasema" au "wanadai kuwa nimesema vitu, lakini wanadanganya"

mawazo yao yote yako dhidi yangu kwa uovu

"daima huwa wanan mawazo maovu dhidi yangu" au "daima huwa wanawaza mambo maovu ya kunifanyia"

wanaangalia hatua zangu

Kuangalia kile ambacho mtu anafnya ili kuona jinsi ya kumsababishia shida inazungumziwa kama kuangalia hatua zake, kama mtu anavyotaka kumkamata mtu anavyoangalia mtu anapotembea. "wanaangalia kila kitu nachofnaya"

kama tu walivyo subiri kwa ajili ya maisha yangu

Kusubiri kumua mtu inazungumziwa kama kusubiri maisha yake. "wanaposubiri kuniua"

Psalms 56:7

Usiache watoroke kufanya udhalimu

"Usiwaache watoroke adhabu yako kwa ajili ya udhalimu wao" au "Usiwaache watoroke unapowaadhibu kwa mambo maovu wanayofanya"

Uwalete chini watu

Kuwashinda adui inazungumziwa kama kuwaleta chini. "Washinde watu"

Unahesabu kuzurura kwangu

Kujishughulisha kwa Mungu juu ya mwandishi wa zaburi inazungumziwa kana kwamba Mungu alihesabu kila wakati ambao mwandishi wa zaburi alite

na kuweka machozi yangu kwenye chupa yako

Kujishughulisha kwa Mungu juu ya mwandishi wa zaburi inazungumziwa kana kwamba Mungu alitunza machozi ya mwandishi wa zaburi kwenye chupa. Machozi yanawakilisha kulia. "na unajua jinsi nilivyolia na unanijali"

hazimo kwenye kitabu chako?

Kujishughulisha kwa Mungu juu ya mwandishi wa zaburi inazungumziwa kana kwamba aliandika idadi ya machozi ya mwandishi wa zaburi katika kitabu chake. Swali hili linatumika kumkumbusha Mungu jinsi anavyomjali sana mwandishi. "umeandika kuyahusu katika kitabu chako" au "unakumbuka machozi yangu"

Psalms 56:9

watageuka

"watakimbia" au "watageuka na kukimbia"

Mungu yu upande wangu

Hii inamaanisha kuwa Mungu anamwonesha fadhila. Katika hali hii inadokezwa kuwa Mungu anapambana dhidi ya adui wa mwandishi wa zaburi ili kumlinda. "Mungu ananipigania"

Yeyote anaweza kunifanya nini?

Swali linatumika hapa kuonesha kuwa mwandishi wa zaburi haogopi watu, kwa sababu hawawezi kumuumiza sana. "Watu hawawezi kunifanya kitu!" au "Watu hawawezi kuniumiza vibaya!"

Psalms 56:12

Jukumu la kutimiza nadhiri zangu kwako liko juu yangu

Kuwajibika kufanya kitu inazungumziwa kana kwamba jukumu lakufanya kitu liko juu yamtu. "Lazima nitimize nadhiri zangu kwako" au "Lazima nifanye nilichoahidi kwako kufanya"

umiitunza miguu yangu na kuanguka

Hapa miguu inamwakilisha mtu. Kuanguka hapa inaweza kuwakilisha kuuwawa na adui zake. "umenepusha na kuanguka" au "umeniepusha na kuuwawa na adui zangu"

ili kwamba nitembee mbele za Mungu

Kuishi na kuonwa na Mungu inazungumziwa kama kutembea mbele ya Mungu. "ili kwamba niishi mbele ya uwepo wa Mungu"

katika nuru ya walio hai

Hapa "nuru ya walio hai" inaweza kuwa inawakilisha Mungu kuwawezesha watu kuishi. "na uhai unaotoa" au "kwa sababu unaniwezesha kuishi"

Psalms 57

Psalms 57:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Al Tashhethi

Hii inawezakuwa inaeleza mtindo wa muziki au tuni ya kutumia wakati wa kuimba zaburi hii. "imba zaburi hii kwa kutumia tuni ya 'Al Tashhethi'" au

Al Tashhethi

Hii inamaanisha "Usiangamize."

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Michtamu

Maana ya neno "michtamu" haiko wazi. Hii inaweza kuandikwa kama: "Hii ni zaburi aliyoandika Daudi."

alipotoroka kutoka kwa Sauli, katika pango

"Hii ina husu Daudi alipojificha kwenye pango akimkimbia Sauli" au "Hii ina husu wakati mfalme Sauli alipokuwa anamfukuza Daudi, na Daudi akajificha kwenye pango"

ninakukimbilia

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. "ninaenda kwako kwa ajili ya ulinzi"

ninakaa chini ya mbawa zako kwa ajili ya ulinzi

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni ndege anayelinda makinda yake kwa kuwaficha chini ya mbawa zake. "nakuamini wewe kunilinda"

hadi uharibifu wake uishe

Mwandishi wa zaburi anazungumzia hamu ya Sauli kumuua kana kwamba Sauli alikuwa akitafuta kumwangamiza adui. "hadi shida hii iishe" au "hadi nitakapo kuwa siko hatarini tena"

Psalms 57:2

anayefanya vitu hivi vyote kwa ajili yangu

Hii inaeleza kwa nini atalia kwa Mungu. "kwa sababu hufanya vitu vyote kwa ajili yangu"

wale wanao niponda

Mashambulizi makali ya adui yanazungumziwa kana kwamba yalikuwa wakikandamiza mwili wake kwa kutembea juu yake. "wale wanaonishambulia kwa ukali"

Mungu atanitumia upendo wake wa huruma na uaminifu wake

Huruma na uaminifu wa Mungu unazungumziwa kana kwamba anatuma huruma yake na uaminifu wake. "Mungu atakuwa na huruma kwangu na mwaminifu"

Psalms 57:4

Maisha yangu yako katikati ya simba

Mwandishi anazungumzia adui zake kana kwamba ni simba. "Ninaishi katikati ya adui wakali" au "Adui wakali wananizunguka kama simba"

wale walio tayari kunimeza

Kuangamiza inazungumziwa kama kumeza au kula kitu. Tafsiri zingine zinaelewa neno la Kihebrania kumaanisha "wanyam wa moto." Picha zote zinazungumzia adui zake kana kwamba ni wanyama pori. "wale walio tayari kuniangamiza"

watu ambao meno yao ni mikuki na mishale

Mikuki na mishale ya wanyama inazungumziwa kana kwamba ni meno ya simba. Mwandishi wa zaburi anaendelea kuzungumzia adui zake kana kwamba ni simba. "watu wanaowaua wengine kwa mikuki na mishale kama simba wanavyoua kwa meno yao makali"

mikuki na mishale

Hizi ni silaha za vita.

ambao ndimi zao ni panga kali

Ulimi unawakilisha kile ambacho mtu anasemam na maneno mabaya ya adui yanazungumziwa kana kwamba ni panga. "ambao maneno yao ni kama panga kali" au "wanaosababisha taabu kubwa kwangu kwa sababu ya kile wanachosema"

Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu

Mwandishi anamwomba Mungu kuonesha kuwa ameinuliwa. Kuinuliwa juu ya mbingu inawakilisha kuwa mkuu. "Mungu, onesha kuwa umeinuliwa juu ya mbingu" au "Mungu, onesha kuwa wewe ni mkuu katika mbingu"

acha utukufu wako uwe juu ya dunia

Mwandishi wa zaburi anamwomba Mungu kuonesha utukufu wake. "onesha utukufu wako duniani kote"

Psalms 57:6

Wanasambaza wavu kwa ajili ya miguu yangu

Mipango ya adui zake kumshika inazungumziwa kana kwamba walisambaza wavu kwenye ardhi ili kumnasa. "Ni kana kwamba adui zangu wamesambaza wavu kwa ajili ya kuninasa" au "Walipanga kunishika kama watu wanavyosambaza wavu kumnasa mnyama"

Walichimba shimo mbele yangu

Mipango ya adui zake kumshika inazungumziwa kana kwamba walichimba shimo kwa ajili yake kuangukia. "Ni kana kwamba walichimba shimo kwa ajili yangu kuangukia" au "Walipanga kunishika kama watu wanaochimba shimo kwenye ardhi kumnasa mnyama"

Wao wenyewe wameanguka katikati yake

Madhara yaliyokuja kwa adui zake walivyojaribu kumnasa inazungumziwa kana kwamba walianguka kwenye mtego walioandaa kwa ajili yake. "Wao wenyewe walianguka katika shimo walilochimba kwa ajili yangu" au "Lakini wao wenyewe waliumizwa kwa kile walichojaribu kufanya kwangu"

Psalms 57:7

Moyo wangu ni thabiti, Mungu, moyo wangu ni thabiti

Kuwa jasiri inazungumziwa kama moyo wa mtu kuwa imara badala ya kutikiswa au kusogezwa kirahisi. Msemo huu unarudiwa kuonesha kuwa ana imani kamili kwa Mungu na hata badilika. "Nina imani kamili kwako, Mungu"

Nitaimba sifa

"Mimi nitaimba sifa kwako, Mungu"

Amka, moyo wangu ulio heshimiwa

Kuamka inaweza kuwa sitiari ya kuanza au kujiandaa kufanya kitu. Moyo unamwakilisha mwandishi wa zaburi au hisia zake. "Amka, moyo wangu ulio heshimiwa, imba sifa kwa Mungu" au "Nina heshima kuamka na kuimba sifa kwa Mungu"

amka, kinanda na kinubi

Mwandishi anazungumza kana kwamba kinanda na kinubi ni watu wanaoweza kuimba sifa kwa Mungu. "Amka, kinanda na kinubu na imbeni sifa kwa Mungu" au "Nitacheza kinanda na kinubi huku ninaimba sifa kwa Mungu"

Nitauamsha alfajiri

Alfajiri inazungumziwa kana kwamba iko hai, na kuamka kabla ya alfajiri inazungumziwa kama kuuamsha. Lengo la kuamka kabla ya alfajiri ni kumsifu Mungu. "Nitaamka kabla ya alfajiri" au "Nitaamka kabla jua halijachomoza"

Psalms 57:9

Kwa kuwa upendo wako usio koma ni mkuu, unafika mbinguni ... uaminifu wako hadi mawinguni

Misemo hii miwili inamaana ya kukaribiana. Ukuu wa upendo wa Mungu usio koma na ukuu wa uaminifu wake zinazungumziwa kana kwamba zinaweza kupimwa kwa umbali.

Kwa kuwa upendo wako usio shindwa ni mkuu, unafika mbinguni

Ukku wa upendo usio shindwa wa Mungu unazungumziwa kana kwamba unaweza kupimwa kwa umbali. "Upendo wako usio shindwa ni mkuu kama umbali wa kutoka duniani hadi mbinguni"

na uaminifu wako hadi mawinguni

"na uamonifu wako ni mkuu, unafika mawinguni" au "na uaminifu wako ni mkuu kama umbali wa kutoka duniani hadi mawinguni"

Utukuzwe, Mungu, juu ya mbingu

Mwandishi anamwomba Mungu kuonesha kuwa ameinuliwa. Kuinuliwa juu ya mbingu inawakilisha kuwa mkuu. "Mungu, onesha kuwa umeinuliwa juu ya mbingu" au "Mungu, onesha kuwa wewe ni mkuu katika mbingu"

utukufu wako uinuliwe juu ya dunia wote

Mwandishi wa zaburi anamwomba Mungu kuonesha utukufu wake. "onesha utukufu wako juu ya dunia yote"

Psalms 58

Psalms 58:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii ni wimbo kuhusu watu waovu.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Al Tashhethi

Hii inaweza kuwa inaeleza mtindo wa muziki au tuni ya kutumia wakati wa kuimba zaburi hii.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Michtamu

Maana ya neno "Michtamu" haiko wazi. Hii inaweza kuandikwa kama: "Hii ni zaburi ambayo Daudi aliandika"

Je, watawala wenu wanazungumza haki?

Mwandishi anatumia swali hili kukemea watawala kwa sababu hawazungumzi kwa haki. "Nyie watawala hamsemi kilicho haki!"

nyie ... mwenu

Hapa wanaozungumziwa ni watu wenye nguvu ambao ni waamuzi.

Huwa mnahukumu kwa unyofu, nyie watu?

Mwandishi anatumia swali hili kukemea waamuzi ambao awahukumu kwa unyofu. "Nyie watu huwa hamhukumu watu kwa unyofu!"

Hapana

Mwandishi anajibu maswali mawili aliyouliza.

unatenda uovu katika moyo wako

Moyo unawakilisha mawazo au mipango ya watu. "mnatenda uovu katika mawazo yenu" au "mnawaza kuhusu kufanya vitu viovu"

unasamba vurugu katika nchi nzima kwa mikono yako

Kufanya vurugu katika sehemu mbali mbali katika nchi inazungumziwa kama kusambaza vurugu kwenye nchi, kana kwamba vurugu ni aina fulani ya kitu. "nyie wenyewe huwa mnafanya matendo ya vurugu kila sehemu katika nchi"

Psalms 58:3

Waovu wanapotoka hata walipokuwa tumboni ... wanaenda pembeni tangu kuzaliwa

Hili ni wazo moja linaloelezwa kwa njia mbili tofauti.

wanapotoka

Kufanya vitu vibaya inazungumziwa kana kwamba watu wanatembea kwenye barabara, na wanageuka na kukosea njia. "wanafanya makosa"

Sumu yao ni kama sumu ya nyoka

Vitu viovu ambavyo watu wanasema vinazungumziwa kana kwamba ni sumu. "Maneno yao maovu yanasababisha shida kama sumu ya nyoka inavyowadhuru watu"

ni kama fira kiziwi anayezuia maskio yake

watu waovu wasiosikia ushauri au kukemewa wanazungumziwa kana kwamba ni nyoka ambazo haziitikii muziki wa mganga. "wanakataa kusikiliza kama fira kiziwi inayozuia maskio yake"

fira kiziwi anayezuia maskio yake

Fira asiyeitikia muziki wa mganga anazungumziwa kana kwamba inaweza kuweka kitu katika maskio yake ili kwamba isisikie. "fira asiye sikia"

fira

aina ya nyoka mwenye sumu

waganga

watu wanaocheza au kuimba muziki ili kumwongoza nyoka

haijalishi ujuzi wao ulivyo

"haijalishi ujuzi walionao waganga katika kumwongoza nyoka"

Psalms 58:6

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuorodhesha vitu ambavyo anapenda Mungu awafanyie watu waovu.

Vunja meno yao ... vunja nje meno makuu ya simba wachanga

Katika misemo hii miwili, watu waovu wanazungumziwa kana kwamba ni simba, na kuwafanya wanyonge kuua watu inazungumziwa kama kuvunja meno yao. "Chukua nguvu yao ya kuua. Uwafanye kuwa wanyonge kama simba wachanga ambao meno yao yamevunjwa na kuanguka nje"

Acha wayeyuke kama maji yanayotiririka

Watu waovu wanazungumziwa kana kwamba ni barafu au maji. Kutokuwepo tena inazungumziwa kama kuyeyuka au maji kutiririka kwenye ardhi kavu. "Wafanye wapotee kama maji yanayotiririka" au "Wafanye wapotee kama barafu inayoyeyuka na kutiririka kwenye ardhi"

acha wawe kana kwamba hawana ncha

"acha mishale yao iwe kama haina ncha"

Acha wawe kama konokono inayoyeyuka na kupita

Kutokuwepo tena inazungumziwa kama kuyeyuka na kupotea. "Acha waovu wapotee kama konokono anayeyuka na kutokuwepo tena"

konokono

"koa"

kama mtoto wa mwanamke aliyezaliwa kabla ya muda ambaye hajaliona jua

Kutokuwepo kunazungumziwa kama kuwa kama mtoto anayezaliwa akiwa amekufa. "kama mtoto anayezaliwa mapema sana kuishi na kuona mwanga wa jua" au "kama mtoto alizaliwa akiwa amekufa"

Psalms 58:9

Kabla masufuria yenu hayajajaza moto wa kuchoma wa miiba ... miiba ya kijana na miiba ya kuchoma pamoja

Waovu wanazungumziwa kana kwamba walikuwa matawi ya miti ya miiba, na hukumu ya haraka ya Mungu juu yao inazungumziwa kana kwamba atawapuliza au kuwafagia haraka. "Mungu atawaangamiza watu waovu haraka zaidi ya kimbunga kinavyoweza kupuliza matawi ya miiba yaliyowekwa chini ya sufuria la kupikia na kuchomwa na moto"

yenu

Daudi anazungumza na watu wa Mungu.

mwiba

"matawi ya miiba"

Mwenye haki atafurahi atakapoona

Msemo "mwenye haki" inamaanisha watu wenye haki kwa ujumla. "Watu wenye haki watafurahi watakapoona"

ataosha miguu yake kwenye damu ya waovu

Kuloanisha miguu ya mtu kwa kutembea kwenye damu inazungumziwa kama kuosha miguu katika damu. "wenye haki wataloanisha miguu yao katika damu ya waovu" au "wenye haki watatembea katika damu ya waovu"

ataosha miguu yake kwenye damu ya waovu

Idadi kubwa ya watu waovu wanaokufa inaelezwa kwa kutumia kukuza kwa neno la watu wenye haki kuosha miguu yao katika damu ya watu waovu. "watu wengi sana waovu watakufa hadi wenye haki watakapotembea kwenye damu yao, itaonekana kana kwamba wanaweza kuosha miguu yao humo"

Psalms 59

Psalms 59:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Al Tashhethi

Hii inaweza kuwa inaeleza mtindo wa muziki au tuni ya kutumia wakati wa kuimba zaburi hii.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Michtamu

Maana ya neno "michtamu" haiko wazi. Hii inaweza kuandikwa kama: "Hii ni zaburi ambayo Daudi aliandika"

Sauli alipotuma, na wakaangalia nyumba kumuua

"katika kipindi Sauli alipowatuma askari wake kwenda na kuangalia nyumba ya Daudi kwa ajili ya nafasi ya kumuua"

niweke juu

Sehemu ya juu inawakilisha sehemu salama ambapo adui zake hawawezi kumfikia. "niweke sehemu salama"

inuka dhidi yangu

Kuinuka dhidi ya mtu inawakilisha kumshambulia. "wananishambulia"

watu wenye kiu ya damu

""watu wenye hamu ya kuua" au "watu wanaopenda kuua watu"

Psalms 59:3

wanasubiri kunivamia ili kuchukua uhai wangu

Adui wa Daudi wako katika maficho na wanasubiri kwa utulivu kwa muda ambao watamvamia.

amka

Kuamua kufanya kitu na kuanza kukifanya inazungumziwa kama kuamka. "fanya kitu" au "chukua hatua"

na uone

"na tazama kinachotokea kwangu" au "na uone wanachonifanyie mimi"

Psalms 59:5

inuka

Kuamua kufanya kitu na kuanza kukifanya inazungumziwa kama kuamka. "fanya kitu" au "chukua hatua"

mataifa yote

Neno "mataifa" hapa yanawakilisha watu wa mataifa ambao hawamtukuzi Mungu. "watu wa mataifa yote"

Psalms 59:6

Wanarudi jioni

Wanaorudi ni watenda maovu.

wanalia kama mbwa

Mwandishi anazungumzia vitishio vya adui zake kushambulia watu kana kwamba walikuwa ni mbwa wanaolia, kunguruma, au kubweka kwa watu. "wanatishia kushambulia watu"

kuuzunguka mji

"kuuzunguka mji kumshambulia yeyote watakayemkuta"

Tazama

Hapa neno "Tazama" linatumika kuvuta nadhari kwa kitu. "Sikia"

wanateuka kwa midomo yao

Kusema vitu viovu inazungumziwa kama kuteuka. Vitu hivi vibaya vinaweza kuwa ni matusi au vitisho. "wanasema vitu vibaya" au "wanapiga kelele kwa kusema vitu vibaya"

teuka

kutoa pumzi kwa nguvu kutoka mdomoni; kuruhusu hewa kutoka tumboni kupitia mdomoni kwa sauti kubwa ya kuudhi.

panga ziko kwenye midomo yao

Vitu vya ukatili ambavyo watu waovu walikuwa wakisema vinazungumziwa kana kwamba ni panga. "wanasema vitu vya ukatili vinavyosababisha watu taabu kama panga zinavyoangamiza watu"

Nani anatusikia?

Swali hili linatumika kuonesha kuwa waliamini kuwa Mungu hatawasikia na kuwaadhibu. "Hakuna mtu anayetusikia!" au "Mungu wenu hatusikii!"

Psalms 59:8

wachekee

"wachekee kwa dharau" au "wadhihaka." Mungu aliwachekea kwa sababu walikuwa hawafai na dhaifu.

unashilia mataifa yote katika dhihaka

"unafanyia mzaha mataifa yote" au "unajua kuwa watu wa mataifa ni wapumbavu"

dhihaka

"fanyia mzaha" au "kejeli"

nguvu yangu

Mungu kuwa nguvu ya mwandishi wa zaburi inawakilisha Mungu kumlinda. "wewe ni nguvu yangu" au "wewe ni mlinzi wangu"

wewe ni mnara wangu wa juu

Mnara wa juu ni sehemu ambapo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya kivuli kutoka kwa adui zao. Mwandishi wa zaburi anamzungumzia Mungu kumlinda kana kwamba Mungu ni kivuli imara na salama. "unanilinda kama mnara wa juu"

Psalms 59:10

Mungu wangu atakuna na mimi

Mungu kumwokoa mwandishi wa zaburi inazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa anatakiwa kukutana naye. "Mungu wangu ataniokoa"

hamu yangu kwa adui zangu

"nachotaka kitokee kwa adui zangu"

Watawanye

"Wasababishe wazurure"

ngao yetu

Mungu kumlinda mwenye haki inazungumziwa kana kwamba Mungu ni ngao. "mlinzi wetu" au "yule anyetulinda kama ngao"

Psalms 59:12

Kwa dhambi za midomo yao na maneno ya midomo yao

Midomo inawakilisha vitu ambavyo watu husema. "Kwa sababu wanatenda dhambi kwa kile wanachokisema" au "Kwa sababu ya maneno ya dhambi wanayoyasema"

acha wakamatwe katika kiburi chao

"acha watu wawashike kwa sababu ya kiburi chao"

wanayoonesha

"wanayosema"

Wameze katika gadhabu yako, wameze ili wasiwepo tena

Kuwaangamiza kabisa inazungumziwa aidha kati ya kuwachoma au kuwala. "Kuwa na hasira nao na waangamize kabisa ili wasiwepo tena"

katika Yakobo

Yakobo hapa inamaanisha Israeli. "katika Israeli"

hadi mwisho wa dunia

"hadi sehemu za mbali zaidi duniani." Hii inawakilisha sehemu zote duniani. "sehemu zote duniani"

Psalms 59:14

kulia kama mbwa

Mwandishi anazungumzia adui zake kutishia kushambulia watu kana kwamba ni mbwa wanalia, wanaunguruma, au wanawabwekea watu. "wanatishia kutushambulia" au "wanatishia kutushambulia kama mbwa pori"

ridhika

"tosheki"

Psalms 59:16

umekuwa mnara wangu wa juu na kimbilio langu

Minara ya juu na sehemu za kukimbilia ni mahali ambapo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya kivuli kutoka kwa adui zao. Mwandishi anazungumzia Mungu kumlinda kana kwamba Mungu alikuwa kivuli imara na salama. "umenilinda kama mnara wa juu na kimbilio.

katika siku ya dhiki yangu

"Neno "siku" hapa inamaanisha kipindi katika wakati. "wakati nina taabu"

Kwako, nguvu yangu, nitaimba sifa

"Wewe ni nguvu yangu, kwa hiyo nitaimba sifa kwako"

nguvu yangu

Mungu kuwa nguvu ya mwandishi wa zaburi inazungumziwa kama Mungu kumlinda. "mlinzi wangu"

kwa Mungu ni mnara wangu wa juu

Minara ya juu na sehemu za kukimbilia ni mahali ambapo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya kivuli kutoka kwa adui zao. Mwandishi anazungumzia Mungu kumlinda kana kwamba Mungu alikuwa kivuli imara na salama. "umenilinda kama mnara wa juu na kimbilio.

Mungu wa agano la umanifu

Hii inaweza kuelezwa katika sentensi tofauti. "Yeye ni Mungu wa agano la uaminifu" au "Wewe ni Mungu wa agano la uaminifu"

Psalms 60

Psalms 60:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Shushani Eduthi

Hii inaweza kuwa inaeleza tuni au mtindo wa muziki wa kutumia wakati wa kuimba zaburi hii. "imba zaburi hii kwa kutumia tuni ya 'Shushani Eduthi'" au "imba hii kwa kutumia mtindo wa Shushani Eduthi"

Shushani Eduthi

Hii inamaanisha "Yungiyungi ya Ahadi"

Michtam

Maana ya neno "michtamu" haliko wazi. Hii inaweza kuandikwa kama: "Hii ni zaburi ambayo Daudi aliandika"

Aramu Naharaimu ... Aramu Soba

"Aramu wa mito miwili ... taifa la Aramu la Soba." Hizi ni sehemu.

Yoabu

Hii inamaanisha Yoabu na jeshi aliloongoza.

watu elfu kumi na mbili wa Edomu

watu wa Edomu 12,000"

umetutupa

Mungu kuwakataa watu inazungumziwa kana kwamba amewatupa. "umetukataa"

umevunja kwenye ulinzi wetu

Mungu kuwaruhusu adui wa Israeli kuvunja kwenye ulinzi wao inazungmziwa kama Mungu mwenyewe amefanya hivyo. "umewaruhusu adui zetu kuvunja kwenye ulinzi wetu"

Psalms 60:2

Kauli Unganishi:

Mwandishi wa zaburi anaendelea kuzungumza na Mungu.

Umeifanya nchi kutetemeka; umeichana

Mwandishi wa zaburi anazungumzia maafa katika nchi yake kana kwamba ni tetemeko.

ponya nyufa zake

Kuwafanya watu kuwa na nguvu tena inazungumziwa kama kurekebisha nyufa chini na kwenye kuta.

nyufa

upenyo mkubwa chini au kwenye kuta

Umewafanya watu wako waone vitu vigumu

Hapa "tazama" inawakilisha "kupitia" au "kuteseka"

kunywa divai ya kupepesuka

"divai inayotufanya tupepesuke." Kutojiweza inazungumziwa kama kupepesuka, kushindwa kusima wima vizuri.

Psalms 60:4

umeweka benderea

Mungu kuwaongoza watu wake vitani inazungumziwa kana kwamba Mungu ni binadamu mfalme au kamanda mkuu aliyeweka bendera kwa ajili ya jeshi lake. "wewe ni kama mfalme anayeweka bendera" au "unatuagiza vitani kama mfalme anayeinua bendera"

bendera

"bendera ya vita." Hii ni bendera ambayo mfalme au kamanda huinua kwenye nguzo kuonesha kuwa jeshi linapaswa kukusanyika.

kuonesha dhidi ya wale waliobeba upinde

"kuonesha dhidi ya wale waliobeba upinde."

kuonesha dhidi ya wale waliobeba upinde

Msemo huu "wale waliobeba upinde" unamaanisha jeshi la adui vitani. "kuonesha wakati akipeleka jeshi lake vitani dhidi ya adui zako"

kwa mkono wako wa kuume

Mkono wa kuume wa Mungu unaashiria nguvu. "kwa nguvu yako"

nijibu

Kumjibu hapa inawakilisha kuitikia ombi lake. "itikiaombi langu" au "jibu ombi langu"

Psalms 60:6

Efraimu pia ni kofia yangu ya chuma

Mungu anazungumzia kabila la Efraimu kana kwamba ni jeshi lake. Kofia inaashiria kifaa cha vita. "Efraimu ni kama kofia yangu ya chuma niliyochagua" au "kabila la Efraimu ni jeshi langu"

kofia ya chuma

kofi ngumu ambayo askari huvaa kulinda kichwa chake dhidi ya ajali

Yuda ni fimbo yangu

Mungu alichagua wanaume kutoka kabila la Yuda kuwa wafalme wa watu wake, na anazungumzia kabila hilo kana kwamba ni fimbo yake. "kabila la Yuda ni kama fimbo yangu" au "Yuda ni kabila ambalo natawalia watu wangu"

Psalms 60:8

Moabu ni bakuli langu la kunawia

Mungu anazungumzia Moabu kutokuwa muhimu kana kwamba Moabu ni bakuli la kunawia au mtumishi wa chini. "Moabu ni kama bakuli nilalotumia kunawia"

juu ya Edomu nitarusha kiatu changu

Inawezekana Mungu alikuwa akizungumzia kuimiliki Edomu kana kwamba anatupa kiatu kwa ishara katika nchi kuonesha kuwa inaimiliki. Ingawa tafsiri zingine hapa ziko tofauti. "Ninachukua umiliki wa nchi ya Edomu" au "Ninatupa kiatu changu katika nchi ya Edomu kuonesha kuwa ni yangu"

Psalms 60:10

Lakini wewe, Mungu, haujatukataa?

Mwandishi anatumia swali hili kueleza huzuni yake kuwa inaonekana kwamba Mungu amewakataa. "Lakini Mungu, inaonekana kama umetukataa." au "Mungu, inaonekana kama umetuacha"

Hauendi vitani na jeshi letu

Mwandishi anazungumzia Mungu kusaidia jeshi lao kana kwamba Mungu huwa anapigina pamoja nao. "huwa husaidii jeshi letu tunapoenda vitani"

haufai

"hauna maana"

tutashinda

"kuwa na ushindi"

atawakanyaga chini adui zetu

Mwandishi anazungumzia Mungu kusaidia jeshi lao kuwashinda adui zao kana kwamba Mungu alikuwa akiwakanyaga adui zao. "atatusaidia kuwakanyaga chini adui zetu" au "atatuwezesha kuwashinda adui zetu"

Psalms 61

Psalms 61:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Huu ni wimbo kuhusu uaminifu wa Mungu.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

kwenye vyombo vya nyuzi

"watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Sikia kulia kwangu; jali ombi langu

Vishazi hivi viwili vinamaana sawa. "Mungu, nisikilize na ujibu ombi langu"

umezidiwa

"umeshindwa"

niongoze kwenye jiwe lililo juu zaidi yangu

Hapa mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni mwamba mkubwa anaoweza kupanda kwa ajili ya ulinzi.

mnara imara kutoka kwa adui

Maneno yanayodokezwa "unaonilinda" yanaweza kuongezwa. "umekuwa kama mwamba imara unaonilinda dhidi ya adui wangu"

mnara imara

Hapa mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni "mnara imara" unaotoa ulinzi dhidi ya adui zake.

Psalms 61:4

nitakimbilia chini ya kivuli cha mbawa zako

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. Hata kuna sitiari ya pili inayozungumzia ulinzi wa Yahwe kana kwamba ni kuku analinda vifaranga wake chini ya mbawa zake. "kwenda kwako kwa ajili ya ulinzi kama kifaranga alivyo salama chini ya mbawa za mama yake"

umenipa urithi

Mwandishi anazungumzia baraka za Mungu kana kwamba ni urithi aliopokea. "umenipa baraka"

wanaoheshimu jina lako

Hapa "jina lako" linamaanisha Mungu mwenyewe. "wanaokuheshimu wewe" au "walio na heshima ya ajabu kwa ajili yako"

Psalms 61:6

Utarefusha ... vizazi vingi

Vishazi hivi viwili vina maana ya kufana. Wazo linarudiwa kwa ajili ya mkazo.

Utarefusha maisha ya mfalme

"Utasababisha maisha ya mfalme kudumu muda mrefu"

miaka yake itakuwa kama vizazi vingi

Hapa "miaka" inamaanisha muda ambao mfalme ataishi. "ataishi kwa vizazi vingi"

Atabaki mbele ya Mungu milele

Hapa "kubaki mbele ya Mungu" inamaana kuwa katika uwepo wa Mungu au kuwa pamoja na Mungu. "Mungu atakuwa naye milele" au "Mungu atakuwa na mfalme milele"

Psalms 61:8

Nitaimba sifa kwa jina lako milele

Hapa "jina" linamaanisha Mungu mwenyewe. "Nitaimba sifa kwako milele"

nadhiri zangu

Hii zinamaanisha ahadi ya kutoa sadaka kwa Mungu kila siku.

Psalms 62

Psalms 62:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii ni wimbo kuhusu uaminifu wa Mungu.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Yeduthuni

Mmoja wa wanamuzi wakuu wa Daudi alikuwa na jina hili. Hii inaweza kumaanisha ni yeye.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

wokovu wangu unatoka kwake

"yeye ndiye anayeniokoa"

Yeye pekee ni mwamba wangu na wokovu wangu

Mwandishi anazungumzia uwezo wa mungu kumlinda kana kwamba Mungu ni mwamba. "Yeye pekee ndiye anayeweza kunilinda na kuniokoa"

yeye ni mnara wangu wa juu

Mwandishi uwezo wa Mungu kumlinda kana kwamba Mungu ni mnara wa juu. "ananiepusha na kushikwa na adui"

sitasogezwa sana

"hakuna kitu kinachoweza kunisogeza kamwe"

Psalms 62:3

nyie wote

"adui zangu" au "adui zangu wote"

Hadi lini ... utamshambulia mtu ... au ua inayotikisika?

Hakuna mtu anayetarajiwa. "Inaonekana kama adui zangu hawataacha kunishambulia. Nijishisi kuwa myonge dhidi yako kama ukuta ulioegemea au ua uliovunjika."

utamshambulia mtu

"utanishambulia"

Watashauriana naye ili

Wanakusudia" au "Wanapanga"

Watashauriana naye ... kumletachini ... wanambariki ... mlaani

Katika mistari hii, Daudi alieleza mwenyewe kama mtu mwingine.

kwa midomo yao

Hii inamaanisha hotuba ya maneno yao.

mioyoni mwao

Hii inamaanisha mawazo yao.

Psalms 62:5

kwa kuwa matumaini yangu yako kwake

"kwa kuwa ninaweka matumaini yangu kwake"

Yeye pekee ni mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni mnara wangu wa juu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni mwamba na mnara wa juu. Sitiari zote hizi mbili zinaonesha jinsi Mungu anavyotoa ulinzi kutoka kwa adui wa mtu. Hapa "wokovu" inamaanisha Mungu anamwokoa mwandishi.

sitasogezwa

"hakuna kitu kinachoweza kunisogeza"

Psalms 62:7

mwamba wa nguvu yangu na kimbilo langu liko katika Mungu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni mwamba unaomlinda mtu dhidi ya adui zake. Anamzungumzia Mungu pia kana kwamba ni kivuli kinachotoa ulinzi. "Mungu huwa ananipa nguvu na ulinzi"

mwaga moyo wako

Hii inamaanisha kumwambia Mungu hisia zako za ndani kana kwamba ni kumwaga kimiminiko. "mpe Mungu mawazo yako ya ndani"

kimbilio letu

Neno "letu" linamaanisha Daudi na watu anaozungumza nao.

Psalms 62:9

wa msimamo wa chini ... watu wa msimamo wa juu ni uongo

Hii inamaanisha viwango vya utajiri na umuhimu. Misemo "ni ubatili" na "ni uongo" ina maana moja. Mtu hawezi kumwamini mtu kwa ujasiri. "huwezi kuweka imani yako kwa watu, hata kama wana umuhimu gani"

kupimwa pamoja, ni nyepesi kuliko ubatili

Ukiwaweka watu wote wa aina hii pamoja katika mizani, hawatakuwa na uzito. Hii inamaanisha kuwa hawana uthamani wa kweli kwako.

udhalimu au wizi

Maneno haya mawili yana maana moja. Huwezi kutumaini katika fedha unayochukua kutoka kwa watu wengine.

kwa kuwa hawatazaa matunda

Mwandishi anazungumzia utajiri kana kwamba ni miti au mizabibu inayoweza kuzaa matunda. "kwa kuwa hawatatoa chochote kizuri kwa ajili yako"

usiweke moyo wako kwao

Hapa "kuweka moyo wako" ni lahaja inayomaanisha kutamani kitu sana. "usiwatamani"

Psalms 62:11

Mungu amezungumza mara moja, mara mbili nimesikia hivi

Hii inamaanisha kuwa Mungu amesema hivi zaidi ya mara moja.

nguvu ni ya Mungu

"Mungu ndiye myenye nguvu kweli kweli"

Pia kwako, Bwana, ni uaminifu wa agano

"yeye ndiye anayetupenda kwa uaminifu, kama alivyoahidi"

kwa kuwa unamlipa kila mtu kwa kile alichokifanya

Mwandishi anazungumzia dhawabu za Mungu kana kwamba analipa mshahara wa kazi.

Psalms 63

Psalms 63:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

kwa bidii

"kwa uaminifu"

nafsi yangu ina kiu na wewe, na mwili wangu una shuku na wewe

Vishazi hivi viwili vinamaana mojana vinatumikapamoja kusisitiza jinsi mwandishi anavyotamani kuwana Mungu. "mwili wangu wote unatamani kuwa na wewe"

nchi kavu na iliochoka

"jangwa kavu lenye joto"

Psalms 63:3

midomo yangu itakusifu

Hapa "midomo" inamwakilisha mtu mzima. "nitakusifu"

nitainua mikono yangu katika jina lako

Hapa "katika jina lako" inamaanisha "kwako." "nitakuabudu wewe na kuomba kwako"

Psalms 63:5

Itakuwa kana kwamba nimekula mlo wa uboho na mafuta

Hapa mwandishi anazungumzia kumjua na kumwabudu Mungu kama kuridhisha zaidi ya kula chakula kizuri. "Nitakuwa na furaha zaidi ya mtu anayekula mlo wa mafuta na chakula kizuri"

kwa midomo ya furaha mdomo wangu utakusifu

Hapa "kwa midomo ya furaha mdomo wangu" inamwakilisha mtu mzima atakayemsifu Mungu kwa furaha"

ninapokuwaza kitandani mwangu ... katika masaa ya usiku

Vishazi hivi viwili vina maana sawa. Mawazo yanarudiwa kusisitiza jinsi mwandishi anavyowaza kuhusu Mungu.

Psalms 63:7

nitafurahi katika kivuli cha mbawa zako

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni ndege anayelinda makinda yake chini ya mbawa zake. "ninafurahi kwa sababu unanilinda"

Nang'ang'ania kwako

"Ninakuhitaji" au "Ninakutegemea"

mkon wako wa kuume unanibeba

Hapa, mkono wa kuume unatumika kama ishara ya nguvu na uwezo. "unanibeba" au "unaniinua juu"

Psalms 63:9

wataenda chini kwenye sehemu za chini zaidi za dunia

Hii inamaanisha kuwa watakufa na kwenda sehemu ya wafu. "watakufa na kushuka katika sehemu ya wafu" au "watakufa na kwenda chini katika sehemu ya wafu"

watapewa kwa wale ambao mikono yao hutumia upanga

Hapa "upanga" inawakilisha kifo vitani, na "wale ambao mikono yao hutumia upanga" inamaanisha adui ambao wanawaua vitani. "Mungu atawasababisha kufa vitani"

watakuwa chakula cha mbweha

Hapa wanaozungumziwa ni maiti za wale wanaokufa vitani. "mbweha watakula miili yao iliyokufa"

mbweha

"mbweha" ni aina ya mbwa pori mwenye miguu mirefu. Huwa wanakula mizoga, mawindo, na matunda.

Psalms 63:11

mfalme

Daudi anajizungumzia mwenyewe. "Mimi, mfalme wa Israeli"

anayeapa kwake ... atajivunia naye

Neno "kwake" inamaanisha Mungu.

lakini mdomo wa wale wanaozungumza uongo utasitishwa

Hapa "mdomo" inamwakilisha mtu mzima. "lakini Mungu atawanyamazisha waongo wote" au "lakini Mungu atawanyamazisha wale wanaodanganya"

Psalms 64

Psalms 64:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii ni ombi la msaada.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

hifadhi

"okoa"

Nifiche na hila za siri ... ghasia za watenda udhalimu

Vishazi hivi viwili vina maana ya kufanana. Kishazi cha pili kinatoa taarifa zaidi kwa kuelezea "hila za siri" zina sauti gani.

na vurugu

"nifiche na ghasia"

ghasia

sauti ya kuchanganya ya kelele na msisimko.

Psalms 64:3

wamenoa ndimi zao kama panga

Mwandishi anazungumzia ndimi wa adui zake kana kwamba zilikuwa zimechongeka kama panga. Hapa "ndimi" inawakilisha maneno makali ambayo aduizake wamezungumza. "Vitu vikali wanavyosema vinaniumiza kama upanga mkali"

mishale yao, maneno machungu

Mwandishi anazungumzia maneno machungu ya adui zake kana kwamba ni mishale inayopigwa kwake. "maneno machungu yanayonichoma mishale"

Psalms 64:5

Nani atatuona?

Watenda maovu hawategemi jibu kwa ajili ya swali lao kwa sababu wanafikiri hakuna mtu atakaye waona. "hakuna atakayeona tunachokifanya"

Mawazo ya ndani na mioyo wa watu yana kina

Mwandishi anazungumzia "mawazo ya ndani" na "mioyo ya watu" kana kwamba ni vilindi vya maji ambavyo hakuna mtu anayeweza kuvichunguza hadi chini.

Mawazo ya ndani ... mioyo ya watu

Misemo yote hii miwili inamaanisha mawazo ya siri au ya ndani ya mtu.

Psalms 64:7

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuwazungumzia "watenda maovu" wa 64:1.

Lakini Mungu atawapiga ... kwa mishale

Mwandishi anazungumzia adhabu ya Mungu kwa watenda maovu kana kwamba Mungu anapiga mishale kwao.

Watafanywa kujikwaa

Mwandishi anazungumzia Mungu kusababisha mipango ya kushindwa kana kwamba Mungu alikuwaakiwafanya kujikwaa katika njia zao. "Mungu atawafanya wajikwae" au "Mungu atasababisha mipango yao kushindwa'

kwa kuwa ndimi zao wenyewe ziko dhidi yao

Hapa "ndimi" inawakilisha maneno wanayosema. "kwa kuwa maneno wanayosema yako dhidi yao"

alichofanya

"kile ambacho Mungu amefanya"

Psalms 64:10

watamkimbilia yeye

Kwend akwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. "enda kwake kwa ajili ya ulinzi"

wanyofu wote wa moyo tajivunia kwake

Hapa "wanyofu moyoni" ni lahaja inayomaanisha wanyofu na wenye haki. "watu wote wanyofu watamsifu yeye"

Psalms 65

Psalms 65:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii ni wimbo wa sifa.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi. Zaburi ya Daudi

"Hii ni zaburi aliyoandika Daudi"

Kwako, Mungu uliye Sayuni, sifa zetu zinakusubiri

Hii inazungumzia sifa kana kwamba ni mtu anayeweza kutenda kitu mwenyewe. "Kwako pekee, Mungu uliye Sayuni, tutatoa sifu zetu"

nadhiri zetu zitabebwa kwako

"tutafanya tulichokuahidi kufanya"

Udhalimu unatushinda

Mwandishi anazungumzia udhalimu kana kwamba ni mtu anayeweza kushinda au kukandamiza. "ni kana kwamba dhambi zetu wenyewe zinatushinda"

utawasamehe

Watakao "samehewa" inamaanisha ni "udhalimu."

Psalms 65:4

unayemchagua ... nyuani mwako

Maneno "unaye" na "mwako" yanamaanisha Yahwe.

aishi nyuani mwako

Hii haimaanisha kuwa mtu huyo anaishi kweli kwenye hekalu lakini ni kwamba yuko huko mara kwa mara kumwabudu Yahwe. "aabudu mara kwa mara katika hekalu lako"

Tutaridhika na uzuri wa nyumba yako, hekalu lako takatifu

"Uzuri wa nyumba yako, hekalu lako takatifu, utaturidhisha"

Tutaridhika

Hapa anayezungumziwa ni Daudi na watu anaozungumza nao.

nyumba yako, hekalu lako takatifu

"nyumba yako, ambalo ni hekalu lako takatifu"

Psalms 65:5

Katika haki

"Kwa sababu u mwenye haki"

wewe ambaye ni

"wewe ni"

wa mwisho wote wa dunia ... upande wa pili wa bahari

Misemo hii inamaana za kufanana. "kwa watu wote wanaoishi duniani kote na upande wa pili wa bahari"

wa mwisho wote wa dunia

Hii inamaanisha watu wote wanaoishi duniani kote.

Psalms 65:6

wewe uliyefungwa na nguvu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba alivaa nguvu yake kama mshipi. "kuonesha kuwa una uwezo sana"

kuunguruma kwa bahari, kuruka kwa mawimbi yake

Misemo hii miwili inamaana moja na inatumika pamoja kuleta hisia dhahiri kwa msikilizaji na msomaji. "mwendelezo wa bahari kuunguruma"

kuunguruma

sauti kubwa inayosababishwa na upepo na mawimbi

na ghasia

"na kutuliza ghasia"

ghasia

sauti kubwa

Psalms 65:8

ushahidi

kithibitisho au kitu cha kuonesha kuwa kitu kingine ni kweli

unafanya mashariki na magharibi kufurahi

Msemo "mashariki na magharibi" inamaanisha watu wanaoishi duniani kote. "unasababisha watu wanoishi kote kupiga kelele kwa furaha"

kusaidia dunia

Hii inamaanisha udongo wa dunia.

unairutubisha sana

"unaufanya udongo kuwa mzuri sana ili vitu vizuri visitawi juu yake"

mto wa Mungu umejaa maji

Hii inamaanisha maji yaliyoko angani ambayo Mungu hutuma kumwagilia dunia na kuijaza mikondo. "unaijaza mikondo na maji"

Psalms 65:10

Unamwagilia ... lako

Anayezungumziwa hapa ni Yahwe.

mitaro yake

"mitaro ya dunia"

mitaro

Mtaro ni mfereji mrefu mwembamba unatengenezwa kwenye ardhi kwa ajili ya kupanda mbegu au kwa ajili ya kumwagilia shamba ambapo nafaka zimepandwa.

migongo

makali

Unauvika taji mwaka kwa uzuri wako

Hapa "mwaka" umepewa sifa ya kibinadamu ya kuvaa taji. "Umeupa heshima mwaka kwa mavuno mazuri"

hudondosha unono chini duniani

Neno "unono" unaashiria urutubisho au uzuri. Kama inavyotumika katika mesmo huu, inaonesha jinsi Yahwe anavyoufanya udongo kuwa mzuri sana na wenye urutubisho hadi unatoa mavuno mengi.

Malisho ... dondosha umande

Kuna umande mwingi sana katika malisho hadi yanasemwa kuudondosha. "Malisho ... yamejaa umande" au "Umande mwingi unadondoka katika malisho ya nyikani"

vilima vimevikwa na furaha

Mwandishi anazungumzia uzuri wa vilima kana kwamba ni watu wenye furaha, na furaha kana kwamba ni mavazi. "vilima ni kama watu waliovaa furaha" au "vilima ni kama watu wenye furaha"

Psalms 65:13

Malisho yamevikwa kundi

Mwandishi anazungumzia malisho kama vile yamefunikwa na kundi la kondoo hadi inakuwa kama malisho yamevaa vazi.

malisho

kiwanja kikubwa ambapo wanyama hula nyasi

kundi

kundi la wanyama, kama kondoo na mbuzi

yanapiga kelele kwa furaha, na yanaimba

Malisho, vilima na mabonde ni mengi sana hadi yanaonekana kama yanapiga kelele na kuimba kwa furaha. "ni kama watu wanaoimba kwa furaha"

yanapiga kelele

Yanayopiga "kelele" ni malisho na mabonde.

Psalms 66

Psalms 66:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii ni wimbo wa sifa.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Fanya sauti ya furaha kwa Mungu, dunia yote

"Sauti ya furaha kwa Mungu" inawakilisha kuimba na kupiga kelele za kumsifu Mungu. "Acha dunia yote iimbe na kupiga kelele kwa furaha kwa Mungu"

dunia yote

Hii inamaanisha watu wote wanaoishi duniani. "watu wote duniani"

Imba utukufu wa jina lake; fanya sifa yake kuwa tukufu

Misemo hii inamaana za kufanana na inatumika kwa pamoja kusisitiza jinsi Mungu alivyo wa ajabu. "Imba kuhusu jinsi jina la Mungu lilivyo la ajabu; imba sifa ya ajabu ya jinsi Mungu alivyo mkuu"

utukufu wa jina lake

JIna la Mungu hapa linamwakilisha Mungu mwenyewe. "utukufu wake"

Psalms 66:3

Matendo yako yanaogofya

Matendo ya Mungu yanatusababisha kuwa katika mshangao na kuogopa kwa sababu tunajua kuwa ana uwezo na ni mtakatifu.

Kwa ukuu wa uwezo wako

"Kwa sababu una uwezo mkuu"

Dunia yote itakuabudu

Hii inamaanisha watu wote wanaoishi duniani. "Watu wote duniani watakuabudu"

wataimba kwa jina lako

Hapa "jina lako" linamaanisha Mungu mwenyewe. "watakusifu na kukupa heshima"

Psalms 66:5

anatisha ... yake ... kwake

Hapa anayezungumziwa ni Mungu.

anatisha

"wa ajabu"

wanadamu

"binadamu"

Aligeuza bahari kuwa nchi kavu; walipita mto kwa miguu

Hii inamaanisha kuvuka bahari ya Shamu.

walipita

Waliopita ni watu wa Mungu, Waisraeli.

tulifurahi

Waliofurahi ni Waisraeli, mababu zao, Daudi, na watu anaozungumza nao.

macho yake yanatazama

Msemo huu "macho yake" inamaanisha Mungu mwenyewe. "anaona"

usiwaache wakaidi wajiinue

"usiwaache watu wakaidi wajiinue" au "usiwaache watu wakaidi wawe na kiburi"

Psalms 66:8

Mpe Mungu baraka ... acha sauti ya sifa yake isikike

Misemo hii miwili ina maana za kufanana. Wazo linarudiwa kusisitiza umuhimu wa kumsifu Mungu.

yetu

Katika mstari huu "yetu" inajumuisha Daudi na watu anaozungumza nao.

haruhusu miguu yetu kuteleza

Mwandishi anazungumzia ulinzi wa Mungu kama kuwaepusha watu wake kuteleza wanapotembea au kuanguka katika mteremko wa ghafla. "hajaturuhusu kuanguka katika maafa"

Psalms 66:10

Umetuleta kwenye wavu

Mwandishi anazungumzia adhabu ya Mungu kana kwamba Mungu aliwashika watu wake katika wavu.

wavu

mtego kwa ajili ya ndege au mnyama

umeweka mzigo mkubwa viunoni mwetu

Mwandishi anazungumzia kile ambacho watu wamestahamili kama kulazimika kubeba mizigo mizito migongoni mwao.

Umewafanya watu kuendesha juu ya vichwa vyetu

Hii ni picha ya kushindwa vibaya vitani. "Ni kana kwamba adui zetu wametushinda vitani na wameendesha vibandawazi vyetu juu ya miili yetu iliyoanguka"

tulipita katika moto na maji

Mungu aliwajaribu kwa maafa ya asili kama moto na mafuriko. "tuliteseka kama watu wanavyoteseka kutokana na moto na mafuriko"

sehemu yenye nafasi

Mwandishi anazungumzia baraka walizonazo sasa watu wa Israeli kana kwamba wameletwa katika nafasi kubwa ya wazi ambapo wako salama. "nafasi ya wazi ambapo tuko salama"

Psalms 66:13

ambazo midomo yangu iliahidi na mdomo wangu kuzungumza

Hapa "midomo" na "mdomo" inamaanisha maneno ya ahadi yaliyozungumzwa. "niliyoahidi"

harufu nzuri ya kondoo dume

"harufu ya moshi wa kondoo dume wa sadaka"

Psalms 66:16

Nitatangaza alichofanya kwa ajili ya nafsi yangu

Neno "nafsi" linamwakilisha mtu mzima. "Nitakwambia alichofanya kwa ajili yangu"

Nililia kwake kwa mdomo wangu

Neno "mdomo" linamwakilisha mtu mzima. anayelia kwa Mungu.

alisifiwa kwa mdomo wangu

Hpa "ulimi" unawakilisha maneno au hotuba. "Nilimsifu kwa ulimi wangu" au "Nilimsifu"

ningeona dhambi

"ningependa dhambi" au "kutunza udhalimu"

asinge nisikiliza

Hapa "asinge nisikiliza" inadokeza kuwa Mungu asinge jibu ombi lake. "asinge nisikia nikimwita" au "asinge jibu ombi langu"

Psalms 66:19

Lakini hakika Mungu amesikia; amevuta nadhari

Vishazi hivi viwili vina maana za kufanana na zinatumika pamoja kusisitiza kuwa Mungu amesikia ombi lake. "Lakini hakika Mungu amesikia ombi langu"

sauti ya ombi langu

Hapa ombi la mwandishi limepewa sifa ya kuwa na sauti. "ombi langu"

au uaminifu wake wa agano kutoka kwangu

"au kugeuza uaminifu wake wa agano kutoka kwangu"

Psalms 67

Psalms 67:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

kwenye vyombo vya nyuzi

"watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu"

kusababisha uso wake ung'ae kwetu

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwatendea fadhila kana kwamba uso wa Yahwe uling'aa mwanga juu yao. "kututendea fadhili"

njia zako zijulikane duniani

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu wajue njia zako duniani"

wokovu wako miongoni mwa mataifa yote

Mwandishi anatamani kila mtu ajue kuwa Mungu ana uwezo wa kuwaokoa. Hii inaweza kuwekwa wazi. "na watu wa mataifa yote wajue kuwa una uwezo wa kuwaokoa"

Psalms 67:3

Achawatu wakusifu ... acha watu wakusifu

Kishazi cha pili kinaogenza uzito wa maana ya ile ya kwanza kwa kusisitiza umuhimu wa kumsifu Mungu.

acha mataifa ... tawala mataifa

Hapa "mataifa" yanamaanisha watu wanaoishi katika mataifa yote duniani.

kwa haki

"kwa usawa"

Psalms 67:5

Achawatu wakusifu ... acha watu wakusifu

Kishazi cha pili kinaogenza uzito wa maana ya ile ya kwanza kwa kusisitiza umuhimu wa kumsifu Mungu.

Nchi imetoa mazao yake

Hapa mwandishi anazungumzia "dunia" kana kwamba imechagua kutoa mazao kwa watu. "Tumevuna mazao mengi kutoka kwenye mazao yetu.

Psalms 67:7

na mwisho wote wa dunia unamheshimu

Hii inamaanisha kwamba watu kila sehemu wanapaswa kumheshimu Mungu kwa sababu ya baraka zake. "ninatamani kwamba watu wote kila mahali duniani wawe na heshima ya ajabu kwake"

Psalms 68

Psalms 68:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Acha Mungu ainuke

Mungu kuanza kutenda inazungumziwa kana kwamba anasimama. "Acha Mungu aanze kutenda"

acha adui zake watawanyike

"acha Mungu awafukuze adui zake"

Kama moshi unavyopeperushwa, ndivyo hivyo uwapeperushe

Adui wa Mungu wanazungumziwa kana kwamba ni moshi unaoweza kupeperushwa kwa urahisi na upepo. "Waondoe kama upepo unavyopuliza moshi"

kama nta inavyoyeyuka mbele ya moto

Adui wa Mungu wanazungumziwa kana kwamba ni nta inayoyeyuka kwa wepesi na moto. "wasababishe kupotea kama nta inavyoyeyuka mbele ya moto.

waovu

Hii inamaanisha watu waovu kwa ujumla.

wenye haki

Hii inamaanisha watu wenye haki kwa ujumla.

wafurahi na kushangilia

Hii inamaanisha kitu kimoja na inasisitiza kiasi cha furaha walichokuwanacho.

Psalms 68:4

jina lake

Hii inamaanisha Mungu. "kwake"

yule anayeendesha katika sehemu za wazi

Uwepo wa Mungu katikati ya watu unazungumziwa kana kwamba anaendesha juu ya dunia katika farasi au kibandawazi.

Baba wa wasio na baba

Mungu anazungumziwa kama Mungu mwenye huruma anayekuwa kama baba kwa yatima. "Yule anayekuwa kama baba kwa watoto wasio na wazazi"

mwamuzi wa wajane

Mungu anazungumziwa kama Mungu anayewlinda wajane. "mlinzi wa wajane"

Mungu huwaweka wapweke katika familia

Mungu anazungumziwa kana kwamba huwaweka watu wapweke katika familia. "Mungu huwapa familia wale waiokuwa na mtu wa kuishi nao"

huwaleta nje wafungwa kwa kuimba

Mungu anazungumziwa kama yule anayewaongoza wafungwa kutoka katika vifungo vyao. "Mungu huwaweka huru wafungwa na huwafanya waimbe kwa furaha"

wakaidi

Hii inamaanisha watu wakaidi. "wale wanaokaidi dhidi yake"

nchi kavu

Adhabu ya Mungu kwa wakaidi inazungumziwa kana kwamba anawalazimisha kuishi katika jangwa lenye joto. "nchi kavu na yenye joto kali"

Psalms 68:7

Taarifa ya Jumla:

Daudi anaanza kueleza hadithi ya Mungu kuwaongoza Waisraeli katika jangwa hadi mlima Sinai.

ulipotoka nje ... ulipotembea katika

Misemo hii miwili inamaanisha tukio lile lile.

ulipotoka nje mbele ya watu wako

"uliwaongoza watu wako"

ulipotembea katika nyika

Mungu anazungumziwa kana kwamba ni askari anayetembea mbele ya watu wa Israeli.

mbingu pia zikadondosha mvua ... uwepo wa Mungu

"Mungu alisababisha inyeshe"

katika uwepo wa Mungu

Lahaja hii inamaanisha kutokea kwa Mungu mbele ya Waisraeli. "Mungu alipotokea kwa Waisraeli"

Psalms 68:9

uliimarisha urithi wako ulipochoka

Nchi ya Israeli inazungumziwa kana kwamba ni mtu anayeweza kuchoka, au kuptat nguvu. "ulisababisha nchi kutoa mazao mazuri"

urithi wako

Nchi ambayo Mungu aliwapa Waisraeli inazungumziwa kana kwamba ni urithi ambao baba alipitisha kwa watoto wake. "nchi uliyotupa sisi Waisraeli"

maskini

Hii inamaanisha watu maskini kwa ujumla. "watu maskini"

Psalms 68:11

Taarifa ya Jumla:

Daudi anaendelea hadithi ya safari ya Waisraeli katika jangwa. Katika sehemu hii ya hadithi, Waisraeli wanashinda vitani dhidi ya adui zao.

wale walioyatangaza ... jeshi kubwa

Idadi kubwa ya watu walisema ujumbe wa Bwana kwa wengine. Wanazungumziwa kana kwamba ni jeshi kubwa. Kwa kuwa msemo huu ni wa kike, tafsiri zingine hutafsiri hii kama, "wanawake walioyatangaza ... jeshi kubwa."

Wafalme wa majeshi ... kwa nini mlifanya hivi?

Taarifa hii katika 68:11 imepangwa vingine ili maana yake ieleweke kwa wepesi zaidi.

Wafalme wa majeshi wanatoroka, wanatoroka

Wafalme wanawakilisha majeshi kamili. Inaeleweka kuwa wanatoroka kwa sababu wameshindwa na jeshi la Israeli. "Wafalme na majeshi yao wanatutoroka kwa sababu wameshindwa"

nyara

mali vinavyochukuliwa kutoka kwa jeshi lililoshinwa na kuletwa kwa maskani ya jeshi lililo shinda.

njiwa waliofunikwa kwa fedha ... dhahabu

Hii inamaanisha kuwa baadhi ya vitu vilivyotekwa nyara ni vya thamani sana kwa sabau vimefunikwa kwa mawe ya thamani.

Wakati baadhi ya nyie watu mlipobaki katika zizizi za kondoo, kwa nini mlifanya hivi?

Swali hili linatumika kukemea watu ambao hawakushiriki vitani. "Wale waliobaki katika zizi za kondoo wasinge baki; wangeenda vitana."

Psalms 68:14

aliwatawanya wafalme huko ... anguka theluji juu wa mlima Salmoni

Kuna wafalme na askari wengi sana waliokufa katika mlima hadi wanazungumziwa kana kwamba ni theluji iliyofunika mlima. "aliwashinda wafalme na askari wengi sana huko hadi wakawa kama chembe za theluji imefunika mlima Salmoni."

aliwatawanya wafalme

Hapa "wafalme" inamaanisha majeshi pia. "aliwatawanya wafalme adui na majeshi yao"

mlima Salmoni

HIli ni jina la mlima.

Mlima mkuu ni ... mlima wa juu ni

Misemo hii miwili inamaana za kufanana na inatumika pamoja kuimarisha nyingine. "mlima mkuu na wa juu ni nchi ya kilima cha Bashani"

Kwa nini unaangalia kwa wivu ... kwa ajili ya sehemu atakayoishi?

Swali hili linawezakuandikwa kama kauli. "Nchi ya kilima cha juu cha Bashani hakitakiwa kuangalia kwa wivu mlima wa ambao Mungu anatamani kwa ajili ya sehemu atakayoishi."

Psalms 68:17

elfu ishiri, maelfu juu ya maelfu

Hii inawezekana haimaanishi idadi kamili, lakini kuashiria idadi kubwa. "maelfu mengi"

unapanda

Hii ni kwenda juu kuelekea angani.

Psalms 68:19

hubeba mizigo yetu kila siku

"hubeba mizigo yetu mizito kila siku." Kujali kwa Bwana kwa ajili ya watu wake inazungumziwa kana kwamba alikuwa akibeba kwa uhalisia matatizo yao kama mzigo.

Mungu ambaye ni wokovu wetu ... Mungu wetu ni Mungu anayeokoa

Misemo inamaanisha kitu kimoja. "Mungu anayetuokoa ... Mungu wetu ni Mungu anayeokoa"

atapiga katika vichwa vya adui zake

Mungu anazungumziwa kana kwamba ni shujaa ambaye ataua adui zake kwa kuwapiga vichwani ili kuwaua. "atawaua adui zake kwa kuwapiga kichwani"

ngozi ya kichwa na nywele nyingi

Inaonekana kuwa utamaduni wa wanajeshi kutonyoa nywele zao wakati wa vita. "mafuvu yenye nywele ndefu"

wanaotembea katika makosa dhidi yake

Kumkosea Mungu inazungumziwa kama kutembea kwenye makosa. "kumkosea mara kwa mara"

Psalms 68:22

nitawarudisha

Watakaorudishwa ni adui wa Mungu.

vilindi vya bahari

Hii ni lahaja inayomaanisha sehemu za mbali za duniani ambapo watu watajaribu kumtoroka Mungu.

uwaponde adui zako

Uharibifu wa adui wa Israeli unazungumziwa kana kwamba Waisraeli waliwagandamiza chini ya miguu yao. "kuwashinda kabisa adui zako"

unachovya mguu wako kwenye damu

Vurugu ya kutoka kwenye uharibifu wa adui unazungumziwa katika njia ya picha kali, kana kwamba Waisreali watakuwa wakisimama katika damu ya adui zao waliokufa. "kukanyaga katika damu yao"

ndimi za mbwa wako wawe na gao lao

Umwagaji wa damu katika vita dhidi ya adui wa Israeli unazungumziwa kana kwamba ni mkubwa sana hadi mbwa watalamba damu inayotiririka kwa ndimi zao.

Psalms 68:24

maandamano

Maandamano ni kundi kubwa la watu wanaotembea pamoja kwa mpangilio kama sehemu ya sherehe.

wapiga vinanda

watu wanopiga vyombo vya muziki

Psalms 68:26

Mbarikini Mungu katika mkusanyiko; msifuni Yahwe, nyie uzao wa kweli wa Israeli

"Nyie ambao ni kizazi cha kweli cha Israeli, msifuni Yahwe na mbarikini Mungu katika kusanyiko.

makundi yao

"kundi lao." Neno "lao" linamaanisha viongozi wa Yuda.

Psalms 68:28

Mungu wenu, Israeli, ameagiza nguvu yenu

Tafsiri zingine zinaelewa maandiko ya Kihebrania tofauti. "Amrisha (au tumia) nguvu yako, Mungu"

Mungu wenu, Israeli, ameagiza

"Watu wa Israeli, Mungu wenu ameagiza"

kwetu

Neno "kwetu" linamaanisha watu ambao Daudi anazungumza nao na yeye mwenyewe.

Onesha uwezo wako kwetu kutoka katika hekalu lako Yerusalemu

Unapokuwepo katika hekalu lako Yerusalemu, tuoneshe uwezo wako"

Onesha uwezo wako

"Tuonesha kuwa una nguvu"

Psalms 68:30

wanyama pori katika matete

Wasomi wengi wanaamini wanyama pori hawa ni sitiari inayomaanisha watu wa Misri. "watu wa Misri ambao ni kama wanyama pori katika matete"

watu, makundi ya mafahali na ndama

Watu wa mataifa mengine wanazungumziwa kana kwamba ni kundi kubwa la ngombe. "mataifa yenye nguvu, ambao ni kama makundi ya mafahali"

watawanye

kusambaza au kusababisha kitu kusambaa haraka katika pande tofauti

Wakuu watatoka kutoka Misri

Inadokezwa kuwa wakuu wanatoka Misri ili kumpa Mungu zawadi Yerusalemu. "Kisha viongozi wa Misri wataleta zawadi kwako"

Kushi

Hii inamaanisha watu wa Kushi. "Watu wa Kushi"

anafika kwa mikono yake kwa Mungu

Hili tendo linaloashiria kumwabudu Mungu. "anainua mikono yake kumsifu Mungu"

Psalms 68:32

nyie falme za duniani

Hapa "falme" inamaanishwa wakazi wa falme. "nyie watu ambao ni wakazi wa falme duniani kote"

Kwake anayeendesha juu ya mbingu ya mbingu

Neno "Imbeni" linadokezwa kama mwanzo wa mstari huu. Hapa Mungu anaelezwa kana kwamba anaendesha kibandawazi angani. "Imbeni kwa Mungu anayeendesha juu ya anga katika kibandawazi chake"

anainua sauti yake kwa nguvu

Lahaja hii inamanisha anazungumza kwa nguvu. "anapiga kelele kwa nguvu" au "anazungumza kwa sauti kubwa"

Psalms 68:34

Mhesabieni Mungu nguvu

"Mhesabieni" inamaanisha kumpa mtu sifa. "Nguvu ni ya Mungu"

nguvu yake iko angani

"katika anga pia anaonesha kuwa ana uwezo"

Mungu, wewe unatisha katika sehemu yako takatifu

Hapa mwandishi anazungumza moja ka moja na Mungu.

nguvu na uwezo

Maneno haya mawili yana maana moja. Yanasisitiza kiasi ambacho Mungu anawapa nguvu watu wake.

Psalms 69

Psalms 69:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii ni ombi la msaada.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Shoshannimu

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

kwa kuwa maji yameweka maisha yangu hatarini

Mwandishi anaelezea matatizo maishani mwake kana kwamba alikuwa akizama kwenye mafuriko ya maji. "kwa kuwa ni kama ninazama katika maji"

ninazama katika matope mengi

Mwandishi anaelezea matatizo maishani mwake kana kwamba anazama katika matopemengi. "Kwa kuwa ni kama ninazama katika matope mengi na nitakufa"

matope

udongo wa maji maji

hakuna sehemu ya kusimama

Mwandishi anatumia kauli hasi kusisitiza jinsi hali ilivyokuwa haiko imara na haileweki.

Nimekuja katika maji marefu, ambapo mafuriko yanapita juu yangu

Mwandishi anaelezea matatizo yake kana kwamba anazama katika mto mrefu wenye vurugu. "nahisa kama niko kwenye maji marefu, na mafuriko ya maji yanapita juu yangu"

Psalms 69:3

nimechoka

kuchoka sana

macho yangu yameshindwa

Lahaja hii inamaanisha kuwa mwandishi amaelia sana hadi macho yake hayaoni vizuri tena. "macho yangu yamevimba kutokana na machozi"

zaidi ya nywele kichwani mwangu

Hii ni kukuza kwa neno kuonesha ni kisasi gani cha adui alichonacho mwandishi. "zaidi ya niwezavyo kuhesabu, kama nywele kichwani mwangu"

nikata

Lahaja hii inamaanisha "niue."

Psalms 69:5

upumbavu wangu

"vitu vya kipumbavu ambavyo nimefanya"

dhambi zangu hazijafichwa kutoka kwako

"unajua dhambi zangu zote"

wale wanaokusubiri wewe waaibishwe ... wale wanakutafuta wakose heshima

Misemo hii miwli inamaana moja na inasisitiza hamu ya mwandishi ya kwamba Mungu awalinde watu wake.

Usiache wale wanaokusubiri wewe waaibishwe kwa sababu yangu

"Tafadhali usiwaaibishe wale wanaokusubiri wewe kwa sababu yangu"

Usiache wale

"Usiwaache wale"

usiache wale wanakutafuta wakose heshima kwa sabau yangu

"Tafadhali usiwenyime heshima kwa sababu yangu wale wanaokutafuta wewe"

wale wanakutafuta

Kumtafuta Mungu inawakilisha kati aya 1) kumwomba Mungu msaada au 2) kuwaza kumhusu Mungu na kumtii. "wale wanao omba msaada wako" au 2) wale wanaokuabudu na kukutii wewe"

Psalms 69:7

Kwa ajili yako

"Kwa niaba yako"

Nimebeba lawama

Lawama za adui wa mwandishi zinazungumziwa kana kwamba ni mzigo mzito ambapo alitakiwa kubeba. "Nimevumilia matusi ya adui zangu"

aibu imefunika uso wangu

Mwandishi anazungumzia aibu anayoihisi kana kwamba ni kitu kibaya usoni pake ambacho kila mtu anakiona vizuri. "Nimeaibika sana"

Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu

Mwandishi anajizungumzia mwenyewe kana kwamba hakuwa sehemu ya familia yake mwenyewe. "Ndugu zangu hawanijui tena au kunikubali kabisa"

mgeni kwa ndugu zangu ... mgeni kwa watoto wa mama yangu

Misemo hii miwili inamaana moja. Inarudiwa kusisitiza mtengano na familia yake mwenyewe.

mgeni kwa watoto wa mama yangu

Mwandishi anajizungumzia mwenyewe kana kwamba hakuwa sehemu ya familia yake mwenyewe. "ndugu zangu hawanijui tena au kuniamini kabisa"

ari ya nyumba yako imenila

Mwandishi anazungumzia ari kwa ajili ya hekalu la Mungu kana kwamba ni mnyama pori unaommeza mwandishi. "ari niliyonayo kwa ajili ya nyumba yako inanimeza"

imenila

Lahaja hii inamaanisha ari ya mwandishi kwa ajili ya hekalu inateka mawazo na matendo yake yote. "inatawala kabisa kila kitu nachowaza na kufanya"

lawama ... zimeniangukia

Mwandishi anazungumzia lawama za adui wa Mungu kana kwamaba ni mawe yaliyopondwa kwa mwandishi. "wale wanaokulaumu piwa wanatuma lawama zao kwangu"

Psalms 69:10

Nililia na sikula chakula

Ukweli kuwa mwandishi alikuwa akifunga inaashiria kuwa alikuwa na huzuni kuhusu jinsi watu walivyolitendea hekalu la Mungu.

walinidhihaki

"adui zangu walinilaumu kwa sababu yake"

nilipofanya magunia kuwa mavazi yangu

Kuvaa vnguo mbaya, za thamani ndogo ni ishara ya kuomboleza juu ya dhambi.

nikawa kitu cha mithali

Mwandishi anajizungumzia kana kwamba alikuwa ndiye mtu mwenye huzuni au mpumbavu katika mithali. "nikawa mfano wa mtu mwenye huzuni anayezungumziwa katika mithali" au "wananicheka"

Wale wanokaa katika lango la mji

Hapa "lango la mji" unahusishwa na uongozi wa mji. "Watu muhimu wa mji"

mimi ni wimbo wa walevi

Mwandishi anajizungumzia kana kwamba alikuwa ndiye mtu ambaye walevi walimkejeli kwa myimbo. "walevi wa mji wanaimba nyimbo za kuudhikunihusu mimi"

Psalms 69:13

katika muda utakaokubali

"katika muda wako uliokubalika" au "utakapokuwa tayari"

nijibu katika uaminifu wa wokovu wako

"niokoe kwa sababu unanipenda kwa uaminifu, kama ulivyoahidi kufanya"

Nivute nje ... usiniache nizame

Misemo hii miwili ina maana moja.

Nivute nje ya matope, na usiniache nizame

Mwandishi anazungumzia hatari yake kutoka kwa adui zake kana kwamba alikuwa akizama katika shimo la matope. "Usiniruhusu niendelee kuzama katika matope"

acha nichukuliwe

Hapa "kuchukuliwa" inamaanisha kutolewa kutoka hatarini. "nitoe" au "niokoe"

niokolewe kutoka

"tafadhali niokoe kutoka"

maji marefu ... mafuriko ya maji ... kilindi

Misemo hii ina maana moja.

niokoa kutoka kwenye maji marefu

Mwandishi anazungumzia hatari yake kutoka kwa adui zake kana kwamba anazama katika maji marefu.

mafuriko ya maji yamenilemea

Mwandishi anazungumzia hatari yake kutoka kwa adui zake kana kwamba mafuriko ya maji yalikuwa yakimfunika kabisa.

kilindi kinanimeza

Mwandishi anazungumzia kilindi kana kwamba ni mnyama hatari aliyekuwa tayari kumla. "maji marefu yananimeza kama mnyama hatari"

Usiruhusu shimo lifunge mdomo wake kwangu

Hapa "shimo" linazungumziwa kana kwamba lina mdomo kama mtu na linaweza kumla mwandishi. "Usiruhusu shimo linimeze" au "Usiache shimo la mauti lifunge juu yangu"

Psalms 69:16

uaminifu wako wa agano ni mzuri

"wewe ni mwema na unanipenda kwa uaminifu"

huruma zako kwangu ni nyingi

"una huruma sana kwangu"

geukia kwangu

Wazo la kumgeukia mtu linamaanisha kumvutia nadhari kwao au kuwasaidia. "nisaidie"

Usifiche uso wako kwa mtumishi wako

Kuficha uso wa mtu inamaanisha kukataa kumsikiliza au kumsaidia mtu. "Tafadhali msaidie mtumishi wako" au "Tafadhali nisaidie"

katika dhiki

"katika taabu kubwa"

Psalms 69:18

niokoe

Mwandishi anamwomba Mungu kumwokoa kana kwamba mwandishi alikuwa ni mtumwa ambaye uhuru wake ungewezz kununuliwa na Mungu.

nikomboe mateka

Mwandishi anazungumzia kulipia fidia maisha yake kana kwamba alikuwa mtumwa ambaye uhuru wake ungeweza kununuliwa kwa fedha.

lawama yangu, aibu yangu, na fedheha yangu

"jinsi watu walivyonilaumu, niaibisha, na kunifedhehesha"

adui zangu wote wako mbele zako

Hapa "mbele zako" inamaanisha kuwa Mungu anaona na kujua yote kuwahusu. "unajua adui zangu wote ni kinanani"

Psalms 69:20

imevunja moyo wangu

Lahaja hii inamaanisha mtu ana huzuni sana. "imenikosea sana"

nimeja uzito

huzuni kuu ya mwandishi inazungumziwa kana kwamba alikuwa amejaa uzito. "nimejaa uzito wa huzuni"

kunihurumia

kusikia maombolezo au huzuni

Walinipa sumu kama chakula changu

Hii inaweza kuwa fumbo. Chakula ambacho watu walimpa mwandishi kilikuwa kibaya sana hadi kilikuwa na ladha kama ya sumu. "Walinipa chakula chenye ladha kama ya sumu"

Psalms 69:22

Acha meza yao mbele yao iwemtego ... acha iwe tanzi

Mwandishi angependa kuona chakula cha adui zake kinawaharibu kabisa kana kwamba ni wanyama wadogo walionaswa katika mtego au tanzi. "Na chakula chao kiwaharibu kama mtego ... na kiwaangamize kama tanzi"

meza yao

Hii inamaanisha chakula kilichowekwa mezani, inawezekana katika karamu. "chakula chao wenyewe" au "karamu za sadaka"

Acha macho yao yatiwe giza

Mwandishi anazungumzia macho yasiyoweza kuona vizuri kana kwamba yametiwa giza. "Tafadhali uwafanye wasiweze kuona kitu"

ufanye viuno vyao vitetemeke

Migongo midhaifu inazungumziwa kana kwamba inatetemeka katika udhaifu. "sababisha migongo yao kuwa minyonge kwao kufanya lolote"

viuno vyao

"pembeni kwao" au "migongo yao"

Psalms 69:24

Mwaga gadhabu yako juu yao

Mungu kuonesha hasira yake inaelezwa kana kwamba aliimwaga juu ya adui zake kama maji.

gadhabu

"hasira kali" au "hasira'

ukali wa hasira yako

"hasira yako ya moto" au "hasira yako kali"

uwapite

Hukumu ya Mungu kwa adui zake unaelezwa kana kwamba aliwafukuza na kuwashika.

iwe ya kuhuzunisha

"kuwa imetelekezwa"

Psalms 69:26

walimtesa yule

"walimtesa mtu"

uliyempiga chini

Hapa "kupiga chini" inamaanisha adhabu. "ulimwadhibu"

wale uliowaumiza

Hapa "kuumizwa" inamaansiha kuwasababisha kuteseka. "wale uliowasababisha wateseka"

Washtakaki kwa kufanya udhalimu baada ya udhalimu

"Endelea kuweka kumbukumbu ya dhambi zao zote"

udhalimu baada ya udhalimu

"dhambi nyingi sana"

usiwaache waje katika ushindi wako wa haki

Kuja katika ushindi wa Mungu ni lahaja inayomaanisha kupokea dhawabu kutoka kwake. "usiwaache wapokee dhawabu yako ya haki"

Psalms 69:28

Acha wawekewe doa katika

Kinachozungumziwa hapa ni majina ya adui. "Futa majina yao katika"

wasiandikwe chini

"usiandike majina yao"

acha wokovu wako, Mungu, uwaweke juu

"Mungu, niokoe na uniweke katika sehemu salama"

Psalms 69:30

jina la Mungu

Hapa "jina" linamaanisha Mungu mwenyewe. "Mungu"

kwa shukrani

"kwa kumshukuru"

zaidi ya ng'ombe au fahali

"bora zaidi ya kutoa sadaka ya ng'ombe au fahali"

fahali mwenye pembe na kwato

Msemo huu unatofautisha fahali wazima na ndama wadogo. "fahali mzima mweye pembe na kwato"

Psalms 69:32

Wapole

Hii inamaanisha watu wapole kwa ujumla. "Watu wapole"

nyie mnaomtafuta Mungu

Kumtafuta Mungu inawakilisha kati ya 1) kumwomba Mungu msaada au 2) kumuwaza Mungu na kumtii. "nyie mnaomwomba Mungu msaada" au "nyie mnaomuwaza Mungu"

acha mioyo yenu iishi

Hapa "mioyo" inamaanisha watu. Hapa "kuishi" ni lahaja inayomaanisha kutiwa moyo. "na utiwe moyo"

Yahwe huwasikia

Hapa "huwasikia" inamaanisha hujibu. "Yahwe hujibu"

wahitaji

Hii inamaanisha watu wahitaji kwa ujumla. "watu wahitaji"

wafungwa wake

"wale walioteseka kwa ajili yake"

Psalms 69:34

Acha mbingu na nchi zimsifu ... bahari

Hapa mbingu na nchi na bahari zinazungumziwa kana kwamba ni watu wanaoweza kumsifu Mungu.

bahari na kila kitu kinachoenda ndani yake

"acha bahari na kila kitu kinachoenda ndani yake kimsifu Mungu"

Mungu ataiokoa Sayuni

Hapa "Sayuni" inamaanisha watu wa Sayuni. "Mungu atawaokoa watu wa Sayuni"

kuwa nayo kama mali ya kumiliki

Hapa neno "nayo" linamaanisha nchi ya Yuda.

wanaopenda jina lake

Hapa "jina" linamaanisha Mungu mwenyewe. "wanaompenda Mungu"

Psalms 70

Psalms 70:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

kuleta katika kumbukumbu

"zaburi hii iliandikwa kuwasababisha watu kukumbuka"

wale ambao

"watu ambao"

kuchukua maisha yangu

Lahaja hii inamaanisha "kuniua"

waaibike na kudhalilishwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu awaweke katika aibu na kuleta fedheha juu yao"

acha wageuzwe nyuma na kuletwa kwenye fedheha

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu awageuze na kuwafanya waaibike kwa yale waliyotenda"

acha wageuzwe nyuma

Kusimamishwa inazungumziwa kama kugeuzwa kutoka kwenye mashambulizi yao. "kusimamishwa"

wale wanaosema, "Aha, aha"

Hii inaonesha kudhihaki kicheko. "wale wanao nidhihaki na kunicheka"

Psalms 70:4

wanaokutafuta

Kumtafuta Mungu inaashiria kati ya 1)kumwomba Mungumsaada au 2) kumwaza Mungu na kumtii. "kukuomba msaada" au"kukuwaza na kukutii"

washereheke na kufurahi

Misemo hii miwili inamaana sawa na inasisitiza uzito wa furaha. "kufurahi sana" au "kuwa na furaha sana"

wanaopenda waokovu wako

Nomino dhahania ya "wokovu" inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wanaokupenda kwa sababu umewaokoa"

daima waseme

Hapa ni kukuza kwa neno ili kusisitiza umihimu wa kumsifu Mungu mara kwa mara.

Mungu asifiwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Acha kila mtu amsifu Mungu"

maskini na mhitaji

Hapa maneno "maskini" na "mhitaji" yanamaana ya kufanana na yanasisitiza kuwahakuweza kujihudumia mwenyewe. "mhitaji sana"

harakisha kwangu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba anamkimbilia mwandishi ili amsaidie. "njoo upesi unisaidie!"

wewe ni msaada wangu na unaniokoa

Hapa msemo "unaniokoa" unaeleza jinsi Mungu alivyo msaada wake. "unanisaidia kwa kuniokoa"

usichelewe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "tafadhali njoo upesi"

Psalms 71

Psalms 71:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Zaburi hii ni ombi kwa ajili ya msaada.

Katika wewe, Yahwe, ninakimbilia

Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. "kwenda kwako, Yahwe, kwa ajili ya ulinzi"

acha nisiaibishwe kamwe

"usiwaruhusu kamwe adui zangu kuniaibisha"

unifanya kuwa salama katika haki yako

Maana zinazowezekana ni 1) "nifanye kuwa salama kwa sababu daima huwa unafanya kilocho sawa" au 2) "nifanye kuwa salama ninapofanya kile unachotaka nifanye"

geuza sikio lako kwangu

Hapa "sikio lako" inamaanisha utayari wa Mungu kumsikiliza mtu anaye omba kwake. "kuwa msikivu kwangu"

Uwe kwangu mwamba wa kukimbilia

Mwandishi anaomba kwamba Yahwe amfanye kuwa salama kama ambavyo angekuwa kama angejificha kwenye mwamba mkubwa au jabali ambapo adui zake wasingempata.

mwamba ... mwamba

Hivi ni vilima au milima, sio mawe ambayo mtu anaweza kushika mkononi.

umetoa amri

"umewaamuru malaika wako"

kuniokoa

"niweke salama"

wewe ni mwamba wangu na ngome yangu

Mwandishi wa zaburi anaamini kuwa Yahwe atamlinda na kumfanye kuwa salama kana kwamba anajificha juu ya mlima mkubwa au kwenye ngome iliyotengenezwa na mwanadamu.

Psalms 71:4

kutoka kwenye mkono wa mwovu, kutoka kwenye mkono wa asiye na haki

Maana zinazowezekana ni 1) neno "mkono" ni njia nyingine ya kusema nguvu. "kutoka katika nguvu ya wasio na haki" au 2) "mkono" unamaanisha mtu mwenyewe. "kutoka kwa watu waovu, kutoka kwa watu wasio na haki" au "ili kwamba watu waovu na watu wasio na haki hawawezi kunidhuru"

mwovu, kutoka kwenye mkono wa asiye na haki

"mwovu; niokoe kutoka kwenye mkono wa asiye na haki."

mwovu ... asiye na haki ... mkatali

"watu waovu... watu wasio na haki ... watu wakatili"

wewe ni matumaini yangu

Hapa "matumaini" ni njia nyingine ya kusema yule ambaye mwandishi wa zaburi anamtumaini. "wewe ndiye ninayekutegemea unisaidie"

Psalms 71:6

Kupitia wewe nimebebwa tangu tumboni

"Umenibeba tangu tumboni" au "Umenitunza tangu nitoke tumboni mwa mama yangu"

wewe ndiye

"wewe ndiye yule"

Mimi ni mfano kwa watu wengi

"Watu wengi wanaona ninavyoishi na wanataka kuishi kama mimi"

Psalms 71:8

Mdomo wangu umejaa na sifa yako ... na heshima yako

Mwandishi wa zaburi anazungumzia hamu yake ya kumsifu na kumpa heshima Yahwe kwa maneno anayoyazungumza kana kwamba mdomo wake umejaa maneno kama unavyoweza kujaa chakula. "Mdomo wangu utajaa maneno yanayokusifu wewe ... yanayo kuheshimu wewe" au "Nitakusifu daima ... nitakupa heshima daima"

sifa yako

"maneno yanayo waambia watu jinsi ulivyo mkuu"

heshima yako

"maneno yanayo wasababisha watu wakupe heshima"

siku nzima

"wakati wote"

Usinitupe ... usiniache

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika kwa pamoja kwa ajili ya mkazo.

Usinitupe

"Usinilazimisheniende mbali na wewe." Kwa Mungu kumkataa inazungumziwa kana kwamba Mungu anamlazimisha kwenda mbali. "usinikatae"

usiniache

"usiniache milele"

Psalms 71:10

angalia maisha yangu

"wanasubiri nafasi ya kuniua"

Wanasema

"Wanasema kunihusu"

mfuatilieni na kumchukua

"mfuateni anapokimbia na muueni"

Psalms 71:12

usiwe mbali nami

"kaa karibu nami"

harakisha kunisaidia

"nisaidie mapema"

Acha waaibike na kuangamia, wale walio na uhasama na maisha yangu

"Acha wale walio na uhasama na maisha yangu waaibike na kuangamizwa"

Acha waaibike na kuangamia

"Waaibishe na kuwaangamiza"

wale walio na uhasama na maisha yangu

"wale wanaonishtaki kwa kufanya kosa"

acha wafunikwe na lawama na fedheha, wale wanaotafuta kuniumiza

"acha wale wanaotafuta kuniumiza wafunikwe na lawama na fedheha"

acha wafunikwe kwa lawama na fedheha

"wafunike kwa lawama na fedheha." "na kila mtu awalaumu, na mtu yeyote asiwape heshima"

wale wanaotafuta kuniumiza

"wale wanaotafuta njia za kunidhuru"

Psalms 71:14

zaidi na zaidi

"zaidi wakati wote" au "daima zaidi ya nilivyofanya kabla"

Mdomo wangu utaeleza

Mdomo ni njia nyingine ya kumwakilisha mtu mzima. "Nitaeleza" au "Nitazungumza kwa mdomo wangu na kueleza"

haki yako

"jinsi ulivyo mwenye haki" au "vitu vyote vizuri unavyovifanya"

wokovu wako

"jinsi ulivyoniokoa" au "jinsi unavyookoa watu"

ingawa

"hata kama"

Nitakuja

Maana zinazowezekana ni 1) "Nitaenda mahali ambapo watu wanamwabudu Yahwe" au 2) "Nitaenda kwa adui zangu"

kwa matendo makuu ya Bwana Yahwe

Maana zinazowezekana ni 1) "nitawaambia kuhusu matendo makuu aliyoyafanya Bwana Yahwe" au 2) "kwa sababu Bwana Yahwe amenipa nguvu kufanya matendo makuu"

nita taja

"nitazungumzia"

Psalms 71:17

umenifundisha

"umenifundisha vitu vingi"

Mungu, usiniache

"Mungu, tafadhali usiniache"

nimekuwa nikitangaza nguvu yako

"nimekuwa nikiwaambia watu jinsi ulivyo na nguvu"

kwa kizazi kifuatacho

"kwa wale ambao ni watoto leo"

uwezo wako kwa kila mtu atakeyekuja

"na kama ninavyotangaza uwezo wako kwa kila mtu atakayekuja"

kila mtu atakeyekuja

Hii ni kukuza kwa neno. "ili watu wengi niwezavyo kuwaambia wajue"

Psalms 71:19

Haki yako pia, Mungu, iko juu sana

Mwandishi wa zaburi anazungumzia vitu vizuri ambavyo Mungu amefanya kana kwamba viliwekwa pamoja kama jengo kubwa au mlima.

ni nani kama wewe?

Hili ni swali balagha linaloweza kutafsiriwa kama kauli. "hakuna mtu kama wewe!"

taabu saba

"taabu mbaya"

fufua

imarisha au kufanya kuishi tena

kutoka pande za chini ya dunia

"Pande za chini ya dunia" ni sitiari ya mahali ambapo watu huenda wanapokufa. Mwandishi wa zaburi hakuwa amekufa bado, lakini anazungumza kana kwamba alikuwa amekufa. "tunapokaribia kifo"

Psalms 71:21

Na uzidishe ... geuka tena na unifariji

"Nita unizidishie ... nataka ugeuka tena na kunifariji." Tafsiri zingine zinasoma, "Utanizidishia ... utageuka tena na kunifariji"

geuka tena na unifariji

Hii inaeleza tendo moja katika misemo miwili. "nifariji tena"

kwa uaminifu wako

"kwa sababu ninaweza kukutumaini"

nitaimba sifa kwako kwa kinubi, Mtakatifu wa Israeli

"kwako, ambaye ni Mtakatifu wa Israeli, nitaimba sifa huku nikicheza kinubi"

Psalms 71:23

Midomo yangu itapiga kelele ya furaha

"Midomo" ni njia nyingine ya kusema mtu mzima. "Nitapiga kelele ya furaha"

hata nafsi yangu, ambayo umeikomboa

"na nafsi yangu, ambayo umekomboa, itaimba sifa"

nafsi yangu

Hapa "nafsi" inamaanisha mtu mzima"

Ulimi wangu pia utazungumza

Hapa "ulimi" unamaanisha mtu mzima. "nitazungumza pia"

wameaibishwa na kuchanganywa, wale waliotafuta kuniumiza

"wale walio tafuta kuniumiza wameaibishwa na kuchanganywa"

kwa kuwa wameaibishwa na kuchanganywa

"kwa kuwa Mungu amewaaibisha na kuwachanganya"

wale waliotafuta kuniumiza

Hii inamaanisha adui wa mwandishi.

Psalms 72

Psalms 72:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Maana zinazowezekana kwa ajili ya kichwa cha habari "zaburi ya Sulemani" ni 1) Daudi aliandika zaburi hii kwa ajili ya Sulemani("mwana wa mfalme") au 2) Sulemani (ambaye, kama mwana wa Daudi, alikuwa "mwana wa mfalme") aliandika zaburi hii kama maombi juu yake mwenyewe au 3) mfalme mwingine aliandika kumhusu mwanaye kwa mtindo wa Sulemani. Watu kipindi hicho mara nyingi walijizungumzia kana kwamba walikuwa mtu mwingine. Ingawa, itakuwa vyema zaidi kutafsiri hii kana kwamba mwandishi wa zaburi anamzungumzia mtu mwingine na sio yeye mwenyewe.

Mpe mfalme amri zako za haki, Mungu, haki yako kwa mwana wa mfalme

Maana zinazowezekana ni 1) "Nipe mimi, mfalme, amri zako za haki, Mungu, haki yako kwa mwana wa mfalme" au 2) "Nipe mimi, mfalme, amri zako za haki, Mungu, haki yako kwangu, mwana wa mfalme." Watu kipindi hicho mara nyingi walijizungumzia kana kwamba walikuwa mtu mwingine. Ingawa, itakuwa vyema zaidi kutafsiri hii kana kwamba mwandishi wa zaburi anamzungumzia mtu mwingine na sio yeye mwenyewe.

Mpe mfalme amri zako za haki

"Mwezeshe mfalme kuhukumu kwa haki"

haki yako kwa mwana wa mfalme

"Mwana wa mfalme aweze kutenda yanayokupendeza wewe"

Ahukumu

Kama ni Daudi aliandika hii, anamzungumzia mwana wake, "mwana wa mfalme," anazungumzia wakati ambao mwana wake atakuwa mfalme. Kama ni Sulemani aliyeandika hii, hata kama anaandika kujihusu, itakuwa vyema kuandika kana kwamba anaandika kumhusu mtu mwingine. Vyovyote vile, "mfalme ahukumu" ndio tafsiri bora zaidi.

watu wako ... maskini wako

Mwandishi wa zaburi anazungumza na Mungu.

na maskini wako

"na mfalme awahukumu watu wako maskini"

Milima itoe amani ... na vilima vitoe haki

Mwandishi wa zaburi anazungumzia watu wa Israeli kana kwamba ni milima na vilima ambapo wanaishi. Anazungumzia milima na vilima kana kwamba ni nchi nzima ya Israeli, kana kwamba nchi ni bustani itoayo matunda, na amani na haki kana kwamba ndio matunda. "Watu wa wa nchini waishi kwa amabi ... wafanye kila kitu kwa haki"

Psalms 72:4

awahukumu

Anayezungumziwa hapa ni mtu atakaye hukumu

kumvunja vipande vipande mkandamizaji

"kumwangamiza kabisa yule anayewakandamiza"

wakati jua bado linadumu, na wakati mwezi bado upo

Jua na mwezi ni mfano wa maneno kwa ajili ya mchana na usiku, ambayo pamoja ni maneno ya ujumla kwa ajili ya wakati wote.

Psalms 72:6

Aje chini kama mvua juu ya nyasi zilizofyekwa

Mfalme atakuwa mwema, na atafanya mambo mema kwa watu wake kana kwamba alikuwa mvua ikiifanyia mema nyasi zilizotoka kukatwa."

Aje

"Natamani kwamba aje"

kama mvua zinazomwagia

"Aje chini kama mvua zinazomwagia." Mfalme atakuwa mwema, na atafanya mambo mema kwa watu wake kana kwamba alikuwa mvua ikiifanyia mema ardhi.

mwenye haki

Kivumishi "haki" kinaweza kutafsiriwa kama msemo wa nomino. "mtu mwenye haki"

katika siku zake

Maana zinazowezekana ni 1) "wakati mfalme anatawala" au 2) "maadamu mtu mwenye haki anaishi" au "maadamu watu wenye haki wanaishi"

kuwepo amani tele

Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba amani ni kitu cha kugusa kama chakula. "Tele" ni wakati kuna kingi kwa kitu. "watu wenye haki waweze kuishi kwa amani ya kweli"

hadi mwezi usiwepo tena

"maadamu mwezi unang'ara" au "milele"

Psalms 72:8

Awe na mamlaka

"Mfalme awe na mamlaka"

kutoka bahari hadi bahari, na kutoka kwenye mto hadi mwisho wa nchi

Misemo hii miwili inazungumzia mifano miwli ya tofauti ikimaanisha dunia nzima.

kutoka bahari hadi bahari

kutoka bahari ya Chumvi na bahari ya Kinerethi mashariki mwa bahari ya Shamu magharibi.

mto

"mto Frati," ambao Waisraeli walisafari kwenda huko kwa nchi kwa kuelekea kaskazini.

mwisho wa nchi

hadi umbali ambao watu waliweza kusafiri ardhini kwa njia tofauti kufika kusini. Waisraeli walizungumzia dunia kana kwamba ilikuwa tambarare yenye mwisho.

rambe vumbi

Hii ni sitiari ya aibu kubwa. "wanafanye kila wawezacho ili awaruhusu waishi"

Tarshishi

jina la sehemu

onyesha

"toa"

toa zawadi

"onesha zawadi"

Seba

Hili ni jina la nchi. Sio nchi sawa na ile ya Sheba.

Psalms 72:11

wanguke chini mbele yake

"sujudu mbele yake" au "mheshimu yeye kama mfalme wao"

mataifa yote

"watu wanaoishi katika kila taifa"

hana msaidizi mwingine

"hakuna wa kumsaidia"

Psalms 72:13

Anahuruma kwa maskini na wahitaji

"Anataka kuzuia maskini na wahitaji kuhangaika"

maskini na wahitaji

Hapa maneno "maskini" na "wahitaji" yana maana ya kufanana na yanasisitiza kwamba hawawezi kujisaidia wenyewe.

Anaokoa maisha yao

"Anawaokoa" au "Anawakomboa"

ukandamizaji na vurugu

Maneno haya mawili yana maana zinazo fanana na yanasisitiza jinsi wahitaji wanavyohangaika. "wale wanao wakandamiza na kuwaumiza"

damu yao ni ya dhamani machoni pake

"anataka waishi vizuri"

damu yao

"maisha yao" au "hali yao"

machoni pake

"kwake"

Psalms 72:15

Aishi!

"Mfalme aishi muda mrefu!" au "Natamani kwamba mfalme aishi muda mrefu!"

dhahabu ya Sheba ipewe kwake

Hii inaweza kuelezwa kwa njia ya kutenda, "na wampe dhahabu ya Sheba" au "na apokee dhahabu ya Sheba"

siku nzima

"kwa kuendelea"

nafaka tele

"tele" ni wakati kuna wingi wa kitu. "nafaka nyingi" au "nafaka ya kutosha"

mazao

mimea ambayo watu huoteshi kwa ajili ya chakula

tikisike

majani yanaposogea wakati upepo mwepesi unapoyapuliza.

kama Lebanoni

"kama miti ya seda ya Lebanoni." Miti hii ilikuwa mizuri na ilikuwa na mbao iliyo kuwa nzuri kwa ajili ya ujenzi. Maana ya hii inaweza kuwekwa wazi.

watu wastawi katika miji kama nyasi shambani

Mafanikio ya watu mijini yanazungumziwa kana kwamba yalikuwa nyasi zinazoota mashambani.

Psalms 72:17

Jina lake lidumu milele

"Watu wajue kumhusu yeye daima" au "Watu wasisahau kamwe yeye ni nani"

Jina lake

"Jina la mfalme" au "sifa ya mfalme" au "umaarufu wa mfalme"

kama jua

"maadamu jua linang'aa"

watu wabarikwe kwake

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu amsababishe kufanya mambo mazuri kwa ajili ya watu"

wamuite aliye barikiwa

"watambue kuwa Mungu amembariki"

Psalms 72:18

Taarifa ya Jumla:

Mistari hii ni zaidi ya mwisho wa zaburi hii. Ni kauli ya kufunga ya kitabu kizima cha 2 cha Zaburi, kinachoaanza Zaburi 42 hadi Zaburi 72.

Yahwe Mungu, Mungu wa Israeli, abarikiwe

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Watu wambariki Yahwe Mungu, Mungu wa Israeli"

Jina lake tukufu libarikiwe milele

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Watu walibariki jina lake tukufu milele" au kufanya "jina" kama namna nyingine ya kusema Yahwe mwenyewe, "watu daima wajue jinsi alivyo mtukufu"

Jina lake tukufu libarikiwe

"yeye aliye mtukufu, abarikiwe"

dunia nzima ijazwe na utukufu wake

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "utukufu wake uijaze dunia yote" au "aijaze dunia yote na utukufu wake"

Amina na Amina

Neno "Amina" linarudiwa kusisitiza kukubali kilichosemwa. "Hakika iwe hivyo"

Maombi ya Daudi mwana wa Yese yanaisha

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Daudi mwana wa Yese amemaliza maombi yake" au "Haya ni maombi ya mwisho ya Daudi mwana wa Yese"

Psalms 73

Psalms 73:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Asafu

"Hii ni zaburi Asafu ambayo aliandika"

miguu yangu kidogo iteleze; miguu yangu kidogo iteleze chini yangu

Mwandishi wa zaburi anazungumzia kushindwa kumwamini Mungu na kutaka kutenda dhambi kama vile kidogo aanguke kwenye njia inayo teleza. "Kidogo niache kumwamini Mungu, kidogo niwe na hatia ya kutenda dhambi kubwa dhidi yake"

niliwaonea wivu wenye kiburi

"sikutaka watu wenye kiburi wawe na vitu vizuri walivyo kuwa navyo"

wenye kiburi

Kivumishi "kiburi" kinaweza kutafsiriwa kama msemo wa nomino. "watu wenye kiburi"

mafanikio ya waovu

Neno "mafanikio" linaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "jinsi waovu walivyo na vitu vingi vizuri"

waovu

Kivumishi "waovu" kinaweza kutafsiriwa kama msemo wa nomino. "watu waovu"

Psalms 73:4

Taarifa ya Jumla:

Asafu anaanza kueleza ambavyo wakati mwingine anataka kulalamika kwa Mungu kuhusu wale ambao wana "kiburi" na "waovu".

mizigo ya watu wengine

Neno "mizigo" ni njia nyingine ya kusema mahangaiko ya maisha ya kila siku (hitaji la chakula, pango, nguo, na afya)

hawateswi kama wanaume wengine

"hawateseki kama watu wengine wanavyoteseka"

Psalms 73:6

Taarifa ya Jumla:

Asafu anaendelea kueleza ambavyo wakati mwingine anataka kulalamika kwa Mungu kuhusu wale ambao wana "kiburi" na "waovu".

Kiburi kinawapamba kama mkufu shingoni; vurugu inawavika kama joho

Hii inamaanisha waovu wanawaonesha wote jinsi walivyo na kiburi na vurugu kana kwamba wamevaa mkufu au joho zuri.

mkufu ... joho

Hii inaonesha vitu ambavyo matajiri na watu muhimu huvaa.

mkufu

ni kama mnyororo mdogo uliotengenezwa na madini kama dhahabu ambayo huvaliwa shingoni.

Kutokana na upofu wa hivi huja dhambi

Kwa sababu ni kama watu vipofu ambao hawaoni waendako, wanatenda dhambi bila kujua. Kuwa kipofu ni njia nyingine ya kusema mtu hawezi kuona jinsi alivyo muovu.

mawazo maovu yanapitia mioyoni mwao

Hapa mwandishi wa zaburi anaelezea mawazo ya watu kana kwamba ni watu. Pia anaelezea uhalisia wa ndani wa watu waovu kana kwamba ni majengo ambao wanaweza kutembea humo. "ndani yao huwa wanawaza mambo mengine maovu ya kufanya"

Psalms 73:8

Taarifa ya Ujumla:

Asafu anaendela kueleza ambavyo wakati mwingine anataka kulalamika kwa Mungu kuhusu wale ambao wana "kiburi" na "waovu".

Hudhihaki

Yule ambaye wanamdhihaki inaweza kuelezwa vizuri. "Wanamdhihaki Mungu na watu wake"

Wanaweka mdomo wao dhidi ya mbingu

Hapa neno "mbingu" ni njia nyingine ya kusema Mungu, ambaye anaishi mbinguni. "wanazungumza dhidi ya Mungu aliye mbinguni"

Wanaweka mdomo wao

"kuzungumza vikali" au "kuzungumza na kusudi"

ulimi wao unatembea duniani

Neno "ulimi" ni njia nyingine ya kusema watu wenyewe. Maana zinazowezekana ni 1) "wanaenda duniani wakisema mambo mabaya kumhusu Mungu" au "wanaenda kila mahali na kujisifia."

Psalms 73:10

Taarifa ya Jumla:

Asafu anaendelea kueleza ambavyo wakati mwingine anataka kulalamika kwa Mungu kuhusu wale ambao wana "kiburi" na "waovu"

watu wake wanawageukia

Maana zinazowezekana ni 1) "Watu wa Mungu wanawapenda watu waovu" au "watu waovu wanarudi sehemu hii"

maji mengi yanatolewa

Maana zinazowezekana ni 1) "Watu wa Mungu wanasikiliza kwa furaha maneno ya watu waovu" au 2) "watu waovu wana chakula cha kutosha kula na divai ya kunywa"

Wanasema

watu waovu wanasema

Mungu anajuaje? Kuna ufahamu kwa Aliye juu?

Maswali haya yenye balagha yanaonesha dharau kwa Mungu. Maswali haya yanaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hakika Mungu hajui tunalolifanya. Aliye juu hana ufahamu wa hili."

Psalms 73:13

Taarifa ya Jumla:

katika mistari ya 13 na 14, Asafu anaendelea kueleza ambavyo wakati mwingine anataka kulalamika kwa Mungu kuhusu wale ambao wana "kiburi" na "waovu". katika mstari wa 15 anaanza kuzungumza kuhusu kile ambacho anakiwaza kweli.

nime

hapa anayezungumza ni Asafu.

ulinda moyo wangu

Asafu anazungumzia kulinda moyo wake kana kwamba analinda mji au jengo dhidi ya maadui. "nimekuwa na mawazo masafi"

kunawa mikono yako ndani ya pasipokuwa na hatia

Mwandishi anazungumzia usafi kama vile amenawa mikono yake kwa kutokua na hatia badala ya maji. "matendo yangu yamebaki masafi" au "nimenawa mikono yangu kuonehsa kuwa sina hatia"

siku nzima

"wakati wote"

nimeteseka

"uminifanya kuteseka."

kuadhibiwa

"nimepewa adhabu"

Kama ningesema, "nitasema vitu hivi," basi ningekuwa ninasaliti kizazi hiki cha wato wako.

Hii hali ya kubuni haikutokea. "Sijawahi kusema, 'nitasema vitu hivi,' kwa hiyo sikusaliti kizazi hiki cha watoto wako"

Psalms 73:16

vitu hivi

Vitu vizuri vinavyowatokea watu "waovu"

hatima yao

"nini hutokea kwa watu waovu wanapokufa"(UDB) au "watu waovu wanakufa je"

Psalms 73:18

umewaweka

Waliowekwa ni waovu.

sehemu telezi

"ardhi isiyo imara au salama"

Jinsi wanavyokuwa jangwa kwa muda mfupi

Neno "jangwa" ni njia nyingine ya kusema watu waliopoteza kila kitu kizuri. "Jinsi wanavyoangamizwa haraka"

kamandoto baada ya mtu kuamka

Waovu hawatadumu zaidi kama mtu anachoona kwenye ndoto. Inapotea mara tu mtu anapoamka.

Psalms 73:21

moyo wangu ulihuzunika

neno "moyo" ni njia nyingine ya kusema mawazo na hisia za mtu. "nilikuwa na huzuni sana"

niliumia sana

Mwandishi wa zaburi anazungumzia maumivu ya hisia kana kwamba ni maumivu ya mwili. "nilihisi kama mtu ameniumiza kwa kisu au mshale."

mjinga na kukosa utambuzi

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza kiasi gani hakujua. "mjinga sana"

kukosa utambuzi

"kutukuelewa kitu"

yako

Hapa anayemaanishwa ni Mungu.

Psalms 73:23

daima niko na wewe

Anayezungumza hapa ni Asafu. Anayezungumziwa ni Mungu.

unanishika mkono wangu wa kuume

hii inaonesha mahusiano ya karibu na Mungu yanayotoa uimara na ulinzi. "unanishika karibu"

kunipokea katika utukufu

Maana zinazowezekana ni 1) "unaniweka mahali ambapo watu wataniheshimu" au 2) "nipe heshima kwa kunipeleka mahali ambapo upo."

Psalms 73:25

Nina nani mbinguni ila wewe?

Unaweza kutafsiri hii kama kauli. "Hakuna mtu mbinguni kwa ajili yangu ila wewe" au "Wewe pekee ndiye niliye naye mbinguni"

mbinguni

mionngoni mwa miungi" au "miongoni mwa viumbe vya ajabu"

hakuna mtu duniani

"hakuna binadamu"

Mwili wangu na moyo wangu

Misemo hii miwili ina maana ya kufanana. Pamoja inamaanisha mtu kamili. "Mwili wangu na akili"

Psalms 73:27

Taarifa ya Jumla:

Asafu anaendelea kumzungumzia Mungu.

Wale walio mbali na wewe

Hapa wazo la kukaa mbali na Mungu linalinganishwa na kutokuwa tayari kumtii. "Wale wasiotaka kukutii"

kimbilio langu

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kana kwamba alikuwa sehemu ambayo mtu anaweza kutorokea kwa usalama.

Psalms 74

Psalms 74:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Maschili ya Asafu

Hii ni maschili ambayo Asafu aliandika."

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Mungu, kwa nini umetukataa milele?

Hii inaweza kutafsiriwa kama kauli. "Mungu, hatujafanya kosa, lakini umetukataa milele!"

Kwa nini hasira yako inawachoma kondoo wa malisho yako?

Hii inaweza kutafsiriwa kama kauli. "Sisi ndio ulio ahidi kututunza, na hatujafanya kosa, lakini sasa una hasira na sisi!"

kondoo wa malisho yako

Asafu anawazungumzia watu wa Israeli kana kwamba ni kondoo. "dhidi ya Israeli, ambao ni kama kondoo unaowalisha kwenye malisho yako"

Kumbuka

"Kuwa makini kwa." Mungu hajasahau watu wake, lakini haonekani kuwafikiria.

urithi wako mwenyewe

"wako milele"

Psalms 74:3

Taarifa ya Jumla:

Mistari hii inaeleza tukio halisi, shambulizi la kimwili lililofanyika katika hekalu la Israeli ndani ya Yerusalemu.

Njoo uone

Asafu anaongea na Mungu, anamuomba aje aangalie uharibifu.

wameunguruma

Maadui walipiga kelele kwa mlio mkubwa wa ushindi.

nakshi

Hii inamaanisha urembo wa kuchonga kwenye mbao, chuma au mawe ya hekaluni.

Psalms 74:7

Taarifa ya Jumla:

Asafu anaendelea kuelezea uharibifu wa hekalu.

waliweka ... walisema ... walichoma

Hapa wanaozungumziwa ni maadui waliotajwa.

walisema mioyoni mwao

Hii ni lahaja. "Wakajiambia" au "wakajiwazia"

Psalms 74:9

Taarifa ya jumla:

Asafu anamueleza Mungu kuhusu uharibifu anaouona.

Hatuoni ishara zingine tena

Maanza zinazowezekana ni 1) "Hatuoni tena ishara za miujiza kutoka kwa Mungu" au 2) "Alama zetu zote takatifu hazipo" au 3) kama kuzungumzia bendera na alama zajeshi, "Jeshi letu limeangamizwa kabisa."

Hadi lini, Mungu, adui atatupa matusi kwako?

Hii inaweza kutafsiriwa kama kauli. "Mungu, adui amekuwa akikurushia matusi kwa muda mrefu sana!"

Adui atakufuru jina lako milele?

Hii inaweza kutafsiriwa kama kauli. "Inaonekana kana kwamba hautamzuia adui kukufuru jina lako!"

atakufuru jina

Neno "jina" ni njia nyingine ya kusema Mungu mwenyewe. "anasema wewe ni mbaya" au "anakutukana"

Kwa nini unazuia mkono wako, mkono wako wa kuume?

Mwandishi wa zaburi anamzungumzia Mungu kana kwamba ana mwili. Hii inaweza kutafsiriwa kama kauli. "Acha kuzuia mkono wako, mkono wako wa kuume!"

unazuia mkono wako

Hapa neno "mokono" ni njia nyingine ya kusema nguvu. "usionesha nguvu yako" au "usitumie nguvu yako kuwaangamiza adui zako"

mkono wako wa kuume

"mkono wako wenye nguvu zaidi"

Toa mkono wako wa kuume kutoka kwenye vazi lako

Mwandishi wa zaburi anamzungumzia Mungu kana kwamba ana mwili. "Acha kuficha nguvu yako na uchukue hatua"

Psalms 74:12

Taarifa ya Jumla:

Hii inaanzisha wazo jipya: Asafu anatangaza ukuu wa matendo ya Mungu katika historia ya watu.

Mungu amekuwa mwema tangu nyakati za zamani

Maana zinazowezekana ni 1) Asafu anazungumza kama mwakilishi wa Israeli, "Mungu amekuwa mfalme wetu tangu Israeli lilipokuwa taifa" au 2) "Mungu, mfalme wangu, alikuwa hai hata katika nyakati za kale."

akileta wokovu

"kuokoa watu"

Uliligawa ... ndani ya maji

Asafu inawezekana anazungumzia wakati ambao Mungu aliitoa Israeli kutoka Misri, akagawa bahari, akawaongoza Waisraeli kwenye nchi kavu, kisha kuzamisha jeshi la Farao.

Uliligawa bahara kwa nguvu yako

Asafu anamzungumzia Mungu kana kwamba ana mwili. "Una nguvu sana uliweza kufanya nchi kavu katikati ya bahari.

bahari

"maji makuu"

uliponda vichwa vya wanyama wakubwa ndani ya maji

Inawezekana Asafu anamzungumzia Farao na jeshi lake kama vile walikuwa wanyama wa baharini. "Ulipoua jeshi la Farao, ilikuwa kama umeponda vichwa vya wanyama wakubwa ndani ya maji"

Psalms 74:14

Taarifa ya jumla:

Asafu anaendelea kuzungumzia kile Mungu alichofanya zamani. Inawezekana anazungumzia wakati Mungu alipoitoa Israeli kutoka Misri na kuangamiza jeshi la Farao baharini.

lewiathani

Lewiathani ni mnyama wa baharini. Inaashiria adui mkatili.

Ulipasua chemchemi na vijito

"Ulisababisha chechemi na vijito kutiririka kutoka kwenye ardhi ngumu iliyo kauka"

Psalms 74:16

Taarifa ya Jumla

Asafu anaendelea kukumbuka nguvu ya ajabu ya Mungu.

mipaka ya dunia

"mipaka ya nchi na bahari"

Psalms 74:18

Taarifa ya Jumla:

Asafu anaomba msaada wa Mungu.

Ita akilini

"Vuta nadhari."

adui alitupa matusi kwako

Asafu anazungumzia maneno ya matusi kana kwamba ni vitu , kama mawe, ambavyo adui alikuwaakitumia kumponda Yahwe. "adui walikutukana mara nyingi"

maisha ya njiwa wako

Asafu anajizungumzia kana kwamba ni njiwa, ndege asiyeweza kujilinda. "mimi, njiwa wako." Msemo huu pia ni sitiari kwa ajili ya watu wa Israeli.

njiwa

Ndege mdogo asiyeweza kujilinda na mara nyingi hutunzwa kama ndege wa kufuga.

mnyama pori

Msemo huu unaweza kuwa ni sitiari kwa ajili ya adui wa Israeli. "adui mkatili ambaye ni kama mnyama pori"

Usisahau maisha ya watu wako walio kandamizwa milele

Usiendelee milele kutokufanya kitu kuwasaidia watu wako walio kandamizwa" "Njoo upesi kuwasaidia watu wako walio kandamizwa"

Psalms 74:20

Taarifa ya Jumla:

Asafu anaendela kuomboleza kwa Yahwe.

sehemu zenye giza za nchi zimejaa sehemu za vurugu

Asafu anazungumzia "sehemu" kana kwamba ni chombo ambamo mtu anaweza kuweka "sehemu za vurugu." "watu wenye vurugu wanafanya matendo maovu katika sehemu za giza nchini pale wanapoweza"

sehemu zenye giza za nchi

Neno "giza" linaweza kuwa ni sitiari ya sehemu ambapo mambo mabaya yanatokea au nchi ambazo Waisraeli walipelekwa katika uhamisho.

Usiwaache walio kandamizwa warudi na aibu

"Usiwaache watu waovu wawashinde walio kandamizwa na kuwaaibisha"

walio kandamizwa

Hawa ni watu wanaotendewa ukatili na watu wenye nguvu.

maskini na walio kandamizwa

Maneno "maskini" na "walio kandamizwa" yanamaanisha kitu kimoja na yanasisitiza kuwa Yahwe anawaokoa wengi wanaohitaji msaada wake.

Psalms 74:22

tetea heshima yako mwenyewe

"onesha kila mtu kuwa uko sawa"

ita akilini

"Vuta nadhari." Mungu hajasahau jinsi wapumbavu wanavyomtukanu, lakini haonekani kuwa anafikiria hilo.

sauti ya adui zako

Neno "sauti" ni njia nyingine ya kusema maneno ambayo watu wanatumia wakati wakizungumza. "kile ambacho adui zako wanasema"

au ghasia ya wale wanaoendelea kukaidi

Mwandishi wa zaburi anazungumzia maneno ya wale wanaomkaidi Mungu kana kwamba yalikuwa na sauti kubwa ya wanyama au vitu ambavyo havina uhai kama maji au upepo. "na vuta nadhari kwa sauti kubwa na maneno yasiyo kuwa na maana ya wale wanao endelea kukukaidi"

kukaidi

kupinga kwa nguvu

Psalms 75

Psalms 75:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Watu wa Mungu wanazungumza katika 75:1, na Mungu anazungumza katika 75:2-3.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Al Tashhethi

Hii inaweza kuwa inamaanisha mtindo wa muziki.

Zaburi ya Asafu

"Hii ni zaburi ambayo Asafu aliandika"

wakazi wote

"watu wote wanaosishi ndani yake"

ninazifanya imara nguzo za dunia

"ninaiweka dunia kutoangamizwa" au "waweke watu wangu salama"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 75:4

Nilisema

Maana zinazowezekana ni 1) Mungu anazungumza au 2) Asafu anazungumza

Msiwe na kiburi ...Msiinue ... Msiinue ... msizungumze

Anaye zungumza anazungumza na watu wengi waovu.

na kwa waovu

"na nikasema kwa waovu"

Msiinue juu pembe

Asafu anazungumzia watu waovu kana kwamba ni wanyama wenye pembe vichwani mwao, wanonyosha shingo zao na kuweka vichwa vyao juu kutisha wanyama wengine. "Msiwe wajasiri" au "Msijivune jinsi mlivyo na nguvu"

Msiinue pembe yenu juu

Asafu anazungumzia watu waovu kana kwamba ni wanyama wenye pembe vichwani mwao, wanonyosha shingo zao na kuweka vichwa vyao juu kutisha wanyama wengine. "Kuweni waangalifu sana kutokuwa na majivuno kuwa mko bora zaidi ya Mungu"

na shingo yenye jeuri

Asafu anazungumzia watu waovu wanaomkaidi au kupingana na Mungu kana kwamba ni wanyama wenye pembe vichwani mwao, wanonyosha shingo zao na kuweka vichwa vyao juu kutisha wanyama wengine. "kwa kiburi"

Sio mashariki ... kuinuka kunakotokea

Asafu anamzungumzia yule anayeinua kana kwamba ndio tendo la kuinua. Anazungumzia pia Mungu kumpa nguvu na heshima mtu kana kwamba Mungu alikuwa akimnyanyua mtu kimwili. "Yule ambaye atakuinua hatakuwa mtu atokaye mashariki" au "Yule ambaye atakufanya kuwa na nguvu na kuwafanya watu wakuheshimu hatakuwa mtu anayetoka mashariki"

Psalms 75:7

Taarifa ya Jumla:

Asafu anamzungumzia Mungu.

huleta chini na huinua juu

"huwashusha watu wengine na kuwainua watu wengine." Maneno "huleta chini" na "huinua juu" ni sitiari ya Mungu kuwapa nguvu watu na kuchukua nguvu yao. "humfanya mtu mmoja mfalme katika nafasi ya mwingine" au "huondoa nguvu ya mtu mmoja na kumpa nguvu mtu mwingine"

kikombe cha divai ya povu ... imechanganywa na vikolezo

Yahwe anapowaadhibu watu watakuwa kama watu waliokunywa divai kali na kuugua.

divai ya povu

Povu ni sitiari ya nguvu ya divai kuwafanya watu walewe. "divai kali"

vikolezo

majani yaliyo kaushwa au mbegu za ardhini

kuimwaga nje

kuimwaga kutoka kwenye chombo kikubwa hadi kwenye vikombe ambavyo watu watatumia kunywa

watainya hadi tone la mwisho

"kunywa kila tone lake"

Psalms 75:9

Anasema

Mungu anasema

nitakata pembe zote za

Pembe za mnyama ni sitiari ya nguvu ya mtu. "ondoa nguvu yote kutoka kwa"

pembe za mwenye haki zitainuliwa juu

Pembe za mnyama ni sitiari ya nguvu ya mtu. "nitainua pembe za mwenye haki" au "nitamfanya mwenye haki kuwa na nguvu"

Psalms 76

Psalms 76:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

kwenye vyombo vya nyuzi

"watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu"

Zaburi ya Asafu

"Hii ni zaburi ambayo asafu aliandika"

amejifanya kujulikana katika Yuda

"amesababisha watu wa yuda kujua yeye ni nani" au "amejifanya kuwa maarafu katika Yuda"

jina lake ni kuu katika Israeli

Maneno "jina lake" ni njia nyingine ya kusema sifa yake. "watu wa Israeli wanamwona kuwa mwema na mwenye nguvu"

sehemu yake ya kuishi

"sehemu aliyochagua kuishi"

Huko alivunja mishale ya upinde, ngao, upanga, na silaha zingine za vita

Maneno haya yanaweza kuwa ni sitiari ya Mungu kuwasababisha watu wa Yuda kuishi katika amani bila ya kuwa na hofu ya adui zao kufanya vita dhidi yao.

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 76:4

Taarifa ya Jumla:

Asafu anamzungumzia Mungu kana kwamba Mungu alikuwa askari anayerudi kutoka katika mlima baada ya kushinda vita vikuu.

Unang'aa kwa nguvu na kuonesha utukufu wako

Mseno wa pili unaimarisha ule msemo wa kwanza ya kwamba utukufu wa Yahwe inaonesha Yahwe kung'aa kwa nguvu.

Unang'aa kwa nguvu

Maneno "unang'aa kwa nguvu" ni sitiari kwa ajili ya kuwa mkuu. "Unaonesha jinsi ulivyo mkuu"

wenye mioyo ya ujasiri walitekwa

"Watu wako waliwaua askari shupavu wa adui zao na kuchukua mali zao zote"

walisinzia

Hapa "walisinzia" ni tasifida ya kufa. "walikufa' au "walianguka chini na kufa"

Psalms 76:6

Kwa kukemea kwako

"Ulipowakemea"

walisinzia

"walikufa" au "walianguka chini na kufa"

nani anaweza kusimama mbele ya macho yako unapokuwa na hasira?

"Hakuna mtu anayeweza kusimama machoni pako unapokuwa na hasira" au "Unaweza kumwangamiza yeyote ambaye una hasira naye"

Psalms 76:8

ulifanya hukumu yako isikike

"ulitangaza hukumu" au "ulitangaza jinsi ambavyo ungeenda kuwaadhibu watu waovu"

dunia ili...

Hapa "dunia" ni njia nyingine ya kusema watu wanaoishi duniani. "watu wa duniani"

kutekeleza hukumu

"kupitisha hukumu" au "kuwaadhibu watu waovu"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 76:10

Hakika

"Hakika" inaeleza matarajio ya kwamba kinachofuata lazima kitatokea.

hukumu yako ya hasira dhidi ya wanadamu italeta sifa kwako

Maana zinazowezekana ni 1) "watu watakusifu kwa sababu una hasira na waovu na una wahukumu" au 2) "watu ambao wana hasira na wewe watafanya vitu vitakavyo sababisha watu wakusifi wewe"

unijifungwa na kile kilichobaki katika hasira yako

Hasira ya Yahwe inazungumziwa kama kitu ambacho anaweza kujifunga kama mshipi. "unajifunga kama mshipi hasira yako iliyobaki"

Psalms 76:11

kwake ambaye anapaswa kuogopwa

"Yahwe, ambaye wanapaswa kumwogopa"

Huzikata roho za wakuu

Msemo "Huzikata roho" ni lahaja inayomaanisha kuwa huvunja roho au huzinyenyekesha. "Huwanyenyekesha wakuu"

anaogopwa na wafalme wa duniani

"wafalme wa duniani wanamwogopa"

Psalms 77

Psalms 77:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Yeduthuni

Mmoja wa wanamuziki wakuu wa Daudi alikuwa na jina hili. Hii inaweza kuwa inamaanisha ni yeye.

Zaburi ya Asafu

"Hii ni zaburi ambayo Asafu aliandika"

Psalms 77:2

nilinyosha mikono yangu

"niliomba na mikono yangu ikiwa imenyoshwa"

Nafsi yangu ilikataa kufarijiwa

"Nafsi" ni njia nyingine ya kusema mtu. "Sikumruhusu yeyote kujaribu kunifariji"

Nilimuwaza Mungu na nikagumia; Nilimuwaza huku nikiishiwa nguvu

Misemo hii miwili ina maana za kufanana na inaunganishwa kwa ajili ya mkazo.

huku nikiishiwa nguvu

"wakati nafsi yangu ikiishiwa nguvu" au "wakati nafsi yangu ilipolemewa"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 77:4

Taarifa ya jumla:

Baada ya kuzungumza na Mungu, Asafu anazungmza na Mungu katika mstari wa 4 na kisha anarudi kusungumza kuhusu Mungu.

Uliyashika macho yangu wazi

"Nilisema kwa Mungu, 'Ulishika macho yangu wazi.'"

Uliyashika macho yangu wazi

Macho yaliyowazi ni njia nyingine ya kusema kushindwa kulala. "ulinizuia kulala"

siku za kale, kuhusu siku za zamani

"kuhusu vitu vilivyotokea siku za zamani sana"

Psalms 77:6

Nikaita akilini

Hii ni lahaja ya kukumbuka. "Nilikumbuka"

kilichotokea

Maana nyingine inayowezekana ni "nini kilikuwa kinatokea."

Je! Bwana atanikataa milele? Hatanionesha tena fadhila?

Misemo hii miwili inaeleza hisia ya kukataliwa na Bwana.

Hatanionesha tena fadhila

"kufanya vitu ambavyo vinaonesha kuwa amefurahishwa na mimi"

Psalms 77:8

Taarifa ya Jumla:

Kwa sababu Asafu hakuwa na uhakika ya jibu la maswali haya, inawezekana kuwa yalikuwa maswali halisi.

uaminifu wa agano

Katika kuzungumzia "uaminifu wa agano" wa yahwe, daudi anamtumaini Yahwe kuwa aampenda daima. "upendo wa uaminifu"

Je! Wokovu wake ulizima huruma yake

Asafu anazungumzia hasira kana kwamba ni mtu aanayefunga mlango kumzuia mtu mwingine au huruma kutoka nje. "Je! Mungu aliacha kutuonesha huruma kwa sababu ana hasira na sisi"

Psalms 77:10

Nilisema

Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi wa zaburi alikuwa akijizungumzia mwenyewe au 2) mwandishi wa zaburi alikuwa akimzungumzia Yahwe.

kubadilika kwa mkono wa kuume wa Aliye juu kwetu

"Mkono wa kuume" ni njia nyingine ya kusema, uwezo, mamlaka au nguvu. "Aliye juu hatumii tena nguvu yake kutusaidia"

Psalms 77:11

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaanza kuzungumza na Yahwe.

ita akilini

"kumbuka"

matendo yako makuu ya kale

"mambo ya ajabu uliyofanya zamani"

Nitatafakari matendo na nitayakumbuka

Misemo hii miwli inaeleza wazo la kutafakari juu ya kile ambacho Yahwe ametenda.

Nitatafakari

"kuwaza kwa kina kuhusu"

nitayakumbuka

"kuwaza yanacho maanisha"

Psalms 77:13

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuzungumza na Yahwe.

mungu gani analinganishwa na Mungu wetu mkuu?

"hakuna mungu anayelinganishwa na Mungu wetu mkuu."

onesha nguvu yako katikati ya watu

"onesha watu kutoka makundi mengi ya watu jinsi ulivyo mkuu"

uliwapa watu wako ushindi ... uzao

"ulitupa sisi, wato wako, ushindi ... sisi tulio uzao"

uliwapa watu wako ushindi

"uliwawezesha watu wako kuwashinda adui zao"

uzao wa Yakobo na Yusufu

Hii inamaanisha taifa zima la Israeli.

Psalms 77:16

Maji yalikuona ... yaliogopa ... vilindi vilitetemeka

Asafu anazungumzia maji kana kwamba ni mtu aliyeona kitu kilichomtisha.

Maji yalikuona, na yakaogopa; vilindi vilitetemeka

"maji" na "vilindi" zinamaanisha miili mikubwa ya maji kama bahari.

vilindi

"maji ya kina kirefu zaidi"

Mawingu yalimwaga chini maji

Asafu anazungumzia mawingu kana kwamba ni watu wanamwaga maji kutoka kwenye chombo. "Mvua nyingi ilianguka" au "Ilinyesha kwa nguvu sana"

mishale yako ilitapakaa

Hii ni sitiari inayoelezea radi kama mshale wa Mungu. "radi uliyotengeneza ilitoa mwanga kama mishale"

ilitapakaa

Mishale ilipaa hovyo ovyo.

Psalms 77:18

Sauti yako ya radi

Hii ni kuipa sifa ya mtu, sauti ya radi ya Mungu. "sauti, ambayo ilikuwa na sauti zaidi ya radi" au "sauti kubwa sana"

radi ilimulika ulimwengu

Radi ilionekana kama kuimulika dunia yote. "radi ilimulika kila kitu hadi mwisho wa upeo wa macho"

Njia yako ... njia yako

Misemo hii miwili inamaana za kufanana na imeunganishwa kwa ajili ya mkazo.

nyayo zako

Asafu anamzungumzia Yahwe kana kwamba Yahwe alikuwa ni mtu mwenye miguu.

nyayo zako hazikuonekana

"hakuna mtu aliyeona nyayo zako"

Uliwaongoza watu wako kama kundi

Tashbihi hii inawafananisha watu wa Mungu na kundi la wanyama.

kwa mkono wa

Msemo "kwa mkono" hapa unamaanisha "kwa matendo ya" au "kupitia matendo ya."

mkono

Hapa "mkono" ni njia nyingine ya kusema mtu mzima.

Psalms 78

Psalms 78:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Maschili ya Asafu

"Hii ni maschili ambayo Asafu aliandika."

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

mafundisho yangu

"mimi ninapokufunza"

maneno ya mdomo wangu

Neno "mdomo" ni njia nyingine ya kusema mtu anayezungumza kwao.

fungua mdomo wangu kwa mafumbo

"fungua mdomo wangu na useme mafumbo"

kuimba kuhusu

"sema"

vitu vilivyojificha

mafumbo

Psalms 78:3

Taarifa ya Jumla:

Mstari wa 3 unaendeleza sentensi ya mstari wa 2.

Hatutawatenga na uzao wao

"Hakika tutawaambia uzao wetu kuyahusu"

matendo ya kusifu ya Yahwe

"vitu ambavyo tunamsifia Yahwe"

Psalms 78:5

aliweka

Yahwe aliweka"

amri za agano

Maana zingine zinazowezzekana ni "shuhuda" au "sheria."

Psalms 78:7

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anazungumzia "watoto" wa 78:5.

Psalms 78:9

Waefraimu ... siku ya vita

Hii inawezekana ni sitiari ya kutokutunza agano (mstari wa 10).

Waefraimu

"askari wa Efraimu"

walikuwa na pinde

Inawezekana kuwa askari walikuwa na mishale. "walikuwa na pinde na mishale kwa ajili ya silaha"

Psalms 78:12

nchi ya Sayuni

Hii inamaanisha eneo lililozunguka mji wa Soani, ambao ulikuwa Misri.

Psalms 78:15

Aligawanya

"Mungu aligawanya"

ya kutosha kujaza vilindi vya bahari

"maji zaidi ya walivyoweza kunywa"

mikondo

mito midogo

Psalms 78:17

Walimjaribu Mungu

Walimtaka Mungu kuthibitisha kuwa aliweza kufanya alichosema atafanya kabla ya kumwamini.

mioyoni mwao

"kwa mioyo yao yote"

kuridhisha hamu zao

"ili wale kiasi walichotaka"

Psalms 78:19

Walizungumza

Waisraeli walizungumza

Kweli Mungu anaweza kuandaa meza kwa ajili yetu nyikani?

"Hatuamini kuwa kweli Mungu anaweza kuandaa meza kwa ajili yetu nyikani!" au "Mungu, jithibitishe kwetu kuwa kweli unaweza kuandaa meza kwa ajili yetu nyikani!"

kuandaa meza

"kutupa chakula"

maji yalitoka nje

maji mengi yalitoka haraka

Lakini anaweza kutupa mkate pia? Atatoa nyama kwa ajiil ya watu wake?

Watu wanamcheka Mungu kumtukana kwa maswali haya. "Lakini hatuta amini kuwa anaweza kutupa mkate pia au kutoa nyama kwa ajili ya watu wake hadi tumwone akifanya."

mkate ... nyama

chakula kutoka katika mimea au chakula kutoka katika wanyama. Ingawa hii neno moja linalojumuisha aina zote za chakula.

Psalms 78:21

hasira yake ilishambulia Israeli

"kwa kuwa alikuwa na hasira, alivamia Israeli"

hawakutumaini katika wokovu wake

"hawakumtumaini kuwaokoa"

Psalms 78:23

aliamuru anga

Asafu anazungumzia anga kana kwamba ilikuwa ni mtu anayeweza kusikia na kutii amri za Mungu. "alizungumza na anga'

anga

Maana zinazowezekana ni 1) "anga" au 2) "mawingu."

kufungua mzlango ya anga

Asafu anazungumzia anga kana kwamba ni ghala lenye mzlango. "kufungua anga kana kwamba ni ghala"

Aliwanyeshea mana kwa ajili yao kula, na kuwapa nafaka kutoka mbinguni

Mistari hii miwili inazungumzia tukio moja.

Aliwanyeshea mana

"Alisababisha mana kudondoka kutoka angani kama mvua"

mkate wa malaika

Hii inazungumzia mana. "aina moja ya chakula ambayo malaika hula"

chakula cha kutosha

"kiasi kikubwa cha chakula"

Psalms 78:26

Alisababisha

"Mungu alisababisha"

Aliwanyeshea nyama kama vumbi

"Alisababisha nyama kudondoka kutoka angani kama mvua, na ilikuwepo nyingi sana hadi ilifunika ardhi kama vumbi"

nyama

ndege

kama vumbi... wengi kama mchanga wa baharini

Kulikuwa na ndege zaidi ya ambavyo mtu angeweza kuhesabu.

Psalms 78:29

tamani

"kuwa shauku sana"

Psalms 78:31

Kisha

wakati chakula kilikuwa bado midomoni mwao (78:29)

hasira ya Mungu ikawashambulia

"Mungu alikuwa na hasira na akawashambulia."

akawaleta chini

"akawaua"

hawakuamini matendo yake ya ajabu

Neno "matendo" ni njia nyingine ya kusema Mungu, ambaye alifanya hayo matendo. "hawakuamini kuwa atawatunza licha ya kufanya mambo ya ajabu hivyo"

Psalms 78:33

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kueleza kile ambacho Mungu alitenda kwa Waisraeli.

alipunguza siku zao kuwa fupi

"aliwaua wakati bado wako wachanga"

miaka yao ilijaa na hofu

Asafu anazungumzia miaka kana kwamba ilikuwa ni vyombo. "mwaka baada ya mwaka walikuwa wakiogopa kila wakati"

kumtafuta

kumwomba walichohitaji afanye ili awalinde

alipowaumiza, walianza ... walirudi na kumtafuta

Hawa ni watu tofauti ambao Mungu "alipunguza siku zao". Baadhi yao walipokufa, wengine walianza "kumtafuta" Mungu.

walirudi

"walitubu" au "walijuta kweli kwa sababu ya dhambi zao"

kwa bidii

"kwa haraka" au "kadri ya uwezo wao"

Psalms 78:35

Taarifa ya Jumla:

Hii inaelezea kile ambacho Waisraeli walichofanya.

ita akilini

"kumbuka"

Mungu alikuwa mwamba wao

Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba alikuwa kilima au mlima ambapo watu walienda ili kuwa salama kutoka kwa adui zao. "Mungu ndiye aliyewalinda"

mkombozi wao

"yule aliyewakomboa"

walijipendekeza kwake

"walimwambia kuwa ni wa ajabu wakati hawakuamini hivyo"

kwa midomo yao

Neno "mdomo" ni njia nyingine ya kusema maneno waliyozungumza kwa midomo yao.

mioyo yao haikuwa thabiti kwake

"hawakumtumaini" au "hawakuwa waminifu kwake"

Psalms 78:38

alisamehe udhalimu wao

"aliwasamehe ingawa walifanya matendo maovu"

alizuia hasira yake

Asafu anazungumzia hasira ya Mungu kana kwamba ni mtu mwenye hasira ambaye Mungu alimzuia kushambulia yule aliyemkasirisha. "hakuwaadhibu ingawa alikuwa amekasirishwa nao"

hakutikisa gadhabu yake yote

Asafu anazungumzia gadhabu ya Mungu kana kwamba ni mtu aliyelala ambaye Mungu alimruhusu kulala na hakumwamsha. "hakujiruhusu kuwakasirikia kabisa"

Psalms 78:39

Aliita akilini

"Alikumbuka"

wameumbwa kwa nyama

Neno "nyama," ambalo ni dhaifu halafu hufa, ni njia nyingine ya kusema udhaifu na mauti. "Waisraeli walikuwa wanyonge na siku moja watakufa"

maeneo yenye ukame

"sehemu ambapo hakuna kitu kinachoota"

walimpinga Mungu

Walitaka Mungu kuthibitisha kuwa anaweza kufanya alichosema atafanya kabla hawajamwamini.

Psalms 78:42

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anazungumzia jinsi Mungu alivyowaokoa Waisraeli.

Soani

mji ndani ya Misri

Psalms 78:44

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaeleza alichokifanya Mungu.

makundi ya inzi

inzi wengi sana hadi ikaonekana kama wingu

yaliyo wameza

Inzi ziliwafanya Wamisri wakoswe furaha kama ambavyo wangekuwa kama zingewala Wamisri.

Akawapa panzi mazao yao na kazi yao kwa nzige

"Aliwaruhusu panzi kula mazao yao yote na kuwaruhusu nzige kula kila kitu walichofanyia kazi kupata"

enea

"walitanda kila mahali"

panzi

mdudu anayekula mimea mwenye miguu mirefu anayotumia kwa ajili ya kuruka

Aliwapa panzi mazao yao

Asafu anazungumzia mimea kama zawadi ambayo Mungu aliwapa panzi. "Aliwaruhusu panzi kula mimea yao"

kazi yao kwa nzige

"Aliwapa kazi yao kwa nzige." Asafu anazungumzia kazi ya watu kana kwamba ni zawadi ambayo Mungu aliwapa panzi. Neno "kazi" ni njia nyingine ya kusema mazao ambayo kazi yao ilipata. "Aliwaruhusu nzige kula mazao waliyofanyia kazi kupata"

Psalms 78:47

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alichofanya kwa Wamisri.

mkuyu

mti unaotoa matunda

miale ya radi

radi yenye ngurumo kubwa

Alinyeshea mvua ya mawe

"Alileta mvua ya mawe" au "Alisababisha mvua ya mawe kuanguka"

Ukali wa hasira yake uliwapiga

Asafu anazungumzia ukali kana kwamba ni mtu anayeweza kumvamia mtu mwingine. "Alikuwa na hasira nao, kwa hiyo aliwashambulia ghafla na kwa ukali"

Ukali wa hasira yake

"Hasira yake kali"

uliwapiga

"aliwavamia wakati hawakuwa wakitegemea chochote kutokea"

Alituma hasira, gadhabu, na taabu kama wakala wanaoleta maafa

Asafu anazungumzia hasira, gadhabu, na taabu kana kwamba ni watu ambao Mungu anaweza kuwatuma kufanya kazi yake. Alikuwa na hasira sana hadi alitaka kuwadhuru Wamisri, kwa hiyo aliwafanyia taabu na kuwapeleka katika maafa"

gadhabu

hasira inayomfanya mtu kutaka kuwadhuru wengine

Psalms 78:50

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alifanya kwa Wamisri.

Akasambaza njia kwa ajili ya hasira yake

Mwandishi wa zaburi anazungumzia hasira yake kana kwamba ni mtu anayeweza kumtazama Yahwe akijiandaa kuwaadhibu watu kana kwamba alikuwa akitengeneza barabara kwa ajili ya mtu kutembelea. "Alikuwa na hasira sana hadi alifanya yote awezayo kuwadhuru" au "Ilikuwa kana kwamba hasira yake ni jeshi na akalitengenezea barabara kwa ajili ya kutembelea"

hakuwaepusha na mauti

"hakuwaepusha Wamisri na kifo" au "hakuwaruhusu Wamisri kuishi"

aliwapa kwa mapigo

Asafu anazungumzia pigo kana kwamba ni mtu amabye alikuwa anaenda kuwadhuru Wamisri. "aliwafanya wote kuugua sana kwa pigo"

mzaliwa wa kwanza wa nguvu yao

"wanaume wao wa muhimu na bora zaidi"

katika mahema ya Hamu

"miongoni mwa familia za Misiri"

Psalms 78:52

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alifanya kwa watu wa Israeli.

kama kondoo ... kama kundi

Mwandishi anawazungumzia Waisraeli kana kwamba walikuwa kondoo. Hii inamaanisha kuwa Mungu aliwajali na kuwalinda watu kama mchungaji anavyofanya kondoo wake.

liliwalemea

"wafunika kabisa"

Psalms 78:54

Taarifa ya Jumla

Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alifanya kwa watu wa Israeli.

mkono wake wa kuume ulipata

Maneno "mkono wa kuume" ni njia nyingine ya kusema uweso. "alijishindia kwa kutumia uwezo wake mwenyewe"

akawagawia urithi wao

Maana zinazowezekana ni 1) Mungu aliwapangia Waisraeli urithi wao katika nchi ambayo mataifa mengine yaliwahi kuishi au 2) Mungu aliyapangia mataifa aliyoyaondoa urithi sehemu nyingine. "aliwapa nchi ambayo itakuwa yao daima"

katika mahema yao

Maana zinazowezekana ni 1) aliweka Israeli katika mahema yao wenyewekatika nchi au 2) aliwaweka Israeli katika mahema ambamo aliwaondoa mataifa mengine. "Mahema" mengi haya yalikuwa nyumba kabisa, wakati mataifa mengine yalipoishimo na Waisraeli walipoishimo.

Psalms 78:56

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alifanya kwa watu wa Israeli.

walipingana na kukaidi

Maneno haya yana maana ya kukaribiana. Mwandishi anayatumia yote kusisitiza kuwa Waisraeli hawakuamini kuwa Mungu atawap mahitaji au kuadhibu maovu kama alivyosema atafanya.

walipingana

Walitaka Mungu kuthibitisha kuwa anaweza kufanya kama alivyosema kabla hajamwamini.

kukaidi

"kataa kutii"

Hawakuwa waaminifu na kutenda kwa uongo

Maneno haya yana maana ya kukaribiana. Mwandishi anayatumia yote mawili kusisitiza kuwa Waisraeli hawakumfanyia Mungu walichosema watafanya.

Psalms 78:58

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alifanya kwa watu wa Israeli.

walimkasirisha na sehemu zao za juu na kumchokoza na wivu wa hasira kwa sanamu zao

Misemo hii miwli ina maana za kukaribiana.

Psalms 78:60

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alifanya kwa watu wa Israeli.

Aliruhusu nguvu yake kushikwa na kuwapa adui utukufu wake katika mkono wao

Asafu anazungumzia nguvu ya Mungu na utukufu wake kana kwamba zilikuwa vitu ambavyo watu waliweza kushika na kubeba. Maneno "nguvu" na "utukufu" inawezekana kuwa ni njia nyingine ya kusema sanduku la agano. Neno "mkono" ni njia nyingine ya kusema uwezo wa adui. "aliwaruhusu adui zake kulishika sanduku tukufu la agano lake; aliwapa ili wafanye nalo walichotaka"

Psalms 78:62

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alifanya kwa watu wa Israeli.

Aliwatoa watu wake kwa upanga

Asafu anawazungumzia watu wa Mungu kana kwamba walikuwa kitu kidogo.

alikasirishwa na urithi wake

"alikasirishwa na watu aliosema watakuwa wake milele"

Moto uliwameza vijana

Maana zinazowezekana ni 1) "Adui walitumia moto kuwaua vijana wao wote" au 2) "Vijana wao walikufa upesi vitani kama moto unavyochoma majani yaliyokauka."

wameza

"Kumeza" ni kula kila kitu haraka.

arusi

sherehe wakati watu wakioa

Psalms 78:64

makuhani walianguka kwa upanga

"adui waliua makuhani wengi wa Israeli kwa kutumia upanga"

wajane wao walishndwa kulia

Maana zinazowezekana ni 1) mtu aliwalazimisha wajane kutolia au 2) makuhani wengi sana walikufa hadi hakukuwa na mazishi sahihi.

wajane

wanawake ambao waume wao wamekufa

Bwana aliamka kama mtu kutoka usingizini

"ilikuwa kana kwamba Bwana aliamka kutoka usingizini"

kama shujaa anayepiga kelele kwa sababu ya mvinyo

Maana zinazowezekana ni 1) kama shujaa aliyekunywa mvinyo mwingi na akawa na hasira kwa sababu aliamshwa na kwa hio alitaka kupigana au 2) kama shujaa aliyekunywa sana mvinyo na sasa anaweza kufikiri na kupigana vizuri kwa sababu amelala.

Psalms 78:67

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alifanya kwa watu wa Israeli.

hema la Yusufu

"uzao wa Yusufu"

Yusufu ... Efraimu

Efraimu alikuwa mwana wa Yusufu.

Yuda ... mlima Sayuni

Mlima Sayuni ulikuwa katika nchi ambayo kabila la Yuda lilikuwa.

kama mbingu

"juu, kama mbingu"

kama dunia

"thabiti na imara, kama dunia"

Psalms 78:70

taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alifanya.

kutoka katika mazizi ya kondoo

"kutoka mahali ambapo alikuwa akifanya kazi katika mazizi ya kondoo"

mazizi ya kondoo

nafasi zenye kuta ambapo kondoo hutunzwa

kuwa mchungaji wa Yakobo, watu wake, na israeli, urithi wake

Neno "mchungaji" ni sitiari ya yule anayewaongoza na kuwalinda watu wengine. "kuwaongoza na kuwalinda uzao wa Yakobo, watu wake, na Israeli, urithi wake"

urithi wake

"wale aliowachagua kuwa wake milele"

Daudi aliwachunga

Neno "mchungaji" ni sitiari ya kuongoza na kulinda. "Daudi aliwaongoza na kuwalinda"

Psalms 79

Psalms 79:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Asafu

"Hii ni zaburi ambayo Asafu aliandika"

urithi wako

"nchi ilikuwa iwe yako milele"

Wamemwaga damu yao kama maji

Neno "damu" ni njia nyingine ya kusemamtu asiye na hatia. Kumwaga damu ni kuua watu wasio na hatia. Watu wengi waliona damu kila siku, kwa hiyo kwa damu kuwa ya kawaida kama maji, watu wengi wa hatia ilibidi wafe. "Wamewaua watu wengi sana wasio na hatia hadi damu iko kila sehemu, kama maji baada ya kunyesha"

hakuwepo wa kuwazika

"hakuna wa kuwazika walio kufa"

Psalms 79:4

Tumekuwa chukizo kwa jirani zetu, kejeli na dhihaka kwa wale waliotuzunguka

Maneno "chukizo," "kejeli," na "dhihaka" ni njia zingine za kusema watu ambao wanachukiza, kejeli, na kudhihaki. "Tumekuwa watu ambao jirani zetu wanatuchukia; wale waliotuzunguka wanatukejeli na kutudhihaki"

Tumekuwa

Wanaozungumziwa ni watu wa Mungu.

dhihaka

kicheko kikubwa cha kumwaibisha mtu

Hadi lini wivu wako wa hasira utawaka kama moto?

"Inaonekana kana kwamba wivu wako wa hasira hautaacha kuwaka kama moto"

wivu wako wa hasira utawaka

Maneno "wivu wako wa hasira" unazungumzia kuwa na wivu na hasira. "utakuwa na wivu na hasira"

utawaka kama moto

Tashbihi hii inalinganisha kuonesha kwa hasira ya Mungu na moto unaoangamiza vitu. "utatuangamiza"

Psalms 79:6

Taarifa ya Jumla:

Misemo hii miwili yote ina maana za kufanana na inaunganishwa kwa ajili ya kuweka mkazo.

Mwaga gadhabu yako kwa mataifa

Asafu anazungumzia gadhabu ya Mungu kana kwamba ilikuwa ni kimiminiko. "Kwa kuwa una hasira, adhibu mataifa"

haliiti jina lako

Neno "jina" ni njia nyingine ya kusema nguvu na mamlaka ya mtu. "sio wako" au "hawakuombi wewe kuwasaidia"

wamemmeza Yakobo

Neno "Yakobo" ni njia nyingine ya kusema uzao wako, watu wa Israeli. "wamewaangamiza kabisa watu wa Israeli"

Psalms 79:8

Usishikilie dhambi za baba zetu dhidi yetu

"Usiendelee kukumbuka dhambi za baba zetu na kutuadhibu kwa sababu yao" au "Tusamehe kwa dhambi za baba zetu"

tuko chini sana

"tumedhoofika sana"

Mungu wa wokovu wetu

"Mungu anayetuokoa"

kwa ajili ya utukufu wa jina lako

Neno "jina" ni njia nyingine ya kusema sifa yake, kwa kile ambacho watu wanachojua kumhusu. "ili watu wajue kuhusu utukufu wako"

kwa ajili ya jina lako

Jina la Mungu hapa linamwakilisha yeye na heshima anayostahili. "ili watu wakuheshimu" au "kwa ajili yako mwenyewe"

Psalms 79:10

Kwa nini mataifa yasema, "Yuko wapi Mungu wao?"

"Mataifa hayapaswi kusema, 'Yuko wapi Mungu wao?'"

Yuko wapi Mungu wao?

"Mungu wao hawezi kufanya chochote!"

Na damu ya watumishi wako iliyomwaga ilipizwe kisasi juu ya mataifa mbele ya macho yetu

Kumwaga damu ni njia nyingine ya kusema kuua watu wasio na hatia. "Walipize kisasi watumishi wako wasio na hatia ambao mataifa waliwaua ambapo tunaweza kukuona unapofanya hivyo."

mbele ya macho yetu

"machoni petu" au "wakati tupo"

Na kuguma kwa wafungwa kufike mbele yako

Asafu anazungumzia sauti ambayo wafungwa walitoa katika maumivu na huzuni kana kwamba alikuwa ni mtu aliyejitokeza mbele ya mfalme. "Sikiliza kwa usikivu kuguma kwa wafungwa na wasaidie"

wana wa mauti

"wale walio hukumiwa kufa"

Psalms 79:12

Lipa ... matusi yao ... Bwana

Asafu anazungumzia matendo ya uovu ambayo nchi jirani zilifanya dhidi ya Israeli kama "matusi" na kana kwamba ni vitu halisia. Anamwomba Mungu kuhesabu matendo hayo, na kwa kila moja ambayo mataifa jirani yalitenda, anamwomba Mungu kumfanya mtu awafanyie matendo ya uovu saba mataifa jirani.

Lipa

"Warudishie"

mapajani mwao

katika magoti yao na mapaja wakati wanakaa chini. Hii nisitiari ya "moja kwa moja na binafsi."

sisi watu wako na kondoo wa malisho tutakupa shukrani

Neno "kondoo" ni sitiari ya watu wasio jiweza ambao mchungaji anawalinda na kuwaongoza. sisi ambao ni watu wako, ambao unatulinda na kutuongoza, tutakushukuru"

kusema sifa zako kwa vizazi vyote

"hakikisha vizazi vyote vinakuja kufahamu mambo yote mema uliyotenda"

sifa zako

Hii ni njia nyingine ya kusema "mambo mazuri ambayo watu watakusifia"

Psalms 80

Psalms 80:1

Taarifa ya Jumla

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Shoshannimu

Hii inaweza kuwa inamaanisha mtindo wa muziki.

Zaburi ya Asafu

"Hii nizaburi ambayo Asafu aliandika."

Mchungaji wa Israeli

Asafu anamzungumzia Mungu kama yule anayeiongoza na kuilinda Israeli.

wewe uliyemwongoza Yusufu kama kundi

"wewe unayewaongoza uzao wa Yusufu kana kwamba ni kundi la kondoo"

Yusufu

Hapa Yusufu inamaanisha taifa la Israeli.

wewe uketiye juu ya makerubi

Mfuniko wa sanduku la agano hekaluni, ishara ya kiti cha enzi ambapo Mungu aliitawala Israeli, ilikuwa imeunganishwa na makerubi ya dhahbu, moja kila upande, zikitazamana.

ung'ae kwetu

Asafu anamzungumzia Mungu kana kwamba ni jua, linalotoa mwanga, sitiari ya unyofu. "tupe mwanga" au "tuoneshe njia sahihi ya kuishi"

tikisa nguvu yako

Msemo "tikisa" inamaanisha "weka katika matendo"

fanya uso wako ung'ae kwetu

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwatendea kwa fadhila kana kwamba uso wa Yahwe uling'aa mwanga kwao.

na tutaokoka

"na tafadhali tuokoe" au "ili utuokoe"

Psalms 80:4

watu wako

Israeli

Umewalishana mkate wa machozi na kuwapa machozi kunywa kwa wingi

Maneno "mkate wa machozi" na "machozi kunywa" ni sitiari ya huzuni endelevu. "Umehakikisha kuwa wana huzuni sana muda wote"

Psalms 80:7

Taarifa ya Jumla:

Asafu anazungumza kwa niaba ya Israeli. Anaanza katika mstari wa 8 kuzungumzia jinsi Mungu alivyowaweka Israeli katika nchi yao kana kwamba Mungu alikuwa ni mtu anayesafisha ardhi ili kupanda mzabibu.

fanya uso wake ung'ae kwetu

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwatendea kwa fadhila kana kwamba uso wa yahwe alimulika mwanga juu yao. "tenda kwa fadhila kwetu"

tutaokoa

"utatuokoa"

Unileta mzabibu kutoka Misri

Asafu anafananisha taifa la Israeli na mzabibu uliowekwatayari kwa kupandwa. "Ulituleta, kama mzabibu, kutoka Misri"

uliyaondoa mataifa na ukaupanda tena

Mwandishi wa zaburi anawazungumzia watu wake kana kwamba ni mmea ambao Yahwe alikuwa akiupanda tena. "Uliyaondoa mataifa kutoka katika nchi yao na kutupa sisi mzabibu, nakutupanda huko.

Psalms 80:9

Taarifa ya Jumla:

Asafu anazungumza kwa niaba ya Israeli. Anaanza katika mstari wa 8 kuzungumzia jinsi Mungu alivyowaweka Israeli katika nchi yao kana kwamba Mungu alikuwa ni mtu anayesafisha ardhi ili kupanda mzabibu.

Ulisafisha nchi kwa ajili yake

"Ulisafisha nchi kwa ajili ya mzabibu"

ikasika mzizi

""mzabibu ulikamata mzizi" au "mzabibu ulianza kuota"

kuijaza nchi

"matawi yake yakafunika nchi"

Milima ilifunikw kwa kivuli chake, seda za Mungu kwa matawi yake

"kivuli chake kilifunika milima, matawi yake seda za Mungu"

seda za Mungu kwa matawi yake

"na seda za Mungu zilifunikwa kwa matawi yake" "namatawi yake yalifunika seda za Mungu"

seda za Mungu

Maana zinazowezekana ni 1) "miti ya seda mirefu zaidi," miti ya seda iliyoota kwenye "milima" katika nchi ya Lebanoni kaskazini mwa Israeli, au 2) "Miti ya seda ya Mungu."

bahari

bahari ya Mediteranea magharibi mwa Israeli

vichipukizi

sehemu za mimea ambazo zinaanza kutokeza kutoka ardhini

Psalms 80:12

Taarifa ya Jumla:

Asafu anazungumza kwa niaba ya Israeli. Anaanza katika mstari wa 8 kuzungumzia jinsi Mungu alivyowaweka Israeli katika nchi yao kana kwamba Mungu alikuwa ni mtu anayesafisha ardhi ili kupanda mzabibu.

kuta zake

kuta za mawe, sio za mbao

nguruwe wa msituni

nguruwe pori wanaharibu bustani na mashamba na kuvamia watu.

msitu

ardhi ambapo kuna miti mingi

wanyama

hawa ni wanyama pori wa aina yoyote

shambani

ardhi ambapo kuna mimea mingi lakini hakuna miti

Psalms 80:14

Taarifa ya Jumla:

Asafu anazungumza kwa niaba ya Israeli. Anaanza katika mstari wa 8 kuzungumzia jinsi Mungu alivyowaweka Israeli katika nchi yao kana kwamba Mungu alikuwa ni mtu anayesafisha ardhi ili kupanda mzabibu.

Geuka

"Geuka kwetu" au "Njoo utusaidie tena"

na ugundue

"na uangalie"

mzabibu huu

Mwandishi anaendelea kufananisha taifa la Israeli na mzabibu.

Huu ni mzizi ambao mono wako wa kuume ulipanda

Mkono wa kuume unawakilisha uwezo na nguvu ya Yahwe. "Huu ndio mzizi ambao wewe, Yahwe, ulipanda"

kichipukizi

sehemu za mimea ambazo zinaanza kutokeza kutoka ardhini

chini; wanaangamia kwa sababu ya lawama yako

Maana zinazowezekana ni 1) chini; watu wako wanaangamia kwa sababu ya lawama yako." au 2) "chini. Na adui zako waangamie kwa sababu ya lawama yako!"

Psalms 80:17

mkono wako

Hii inamaanisha uwezo na nguvu ya Yahwe.

mtu wa mkono wako wa kuume

taifa la Israeli, ambalo Yahwe amelichagua kama watu wake

mkono wako wa kuume

Mtu katika Israeli alipotaka kumpa heshima mtu mwingine, alimweka mtu mwingine kusimama katika upande wake wa kuume, karibu na mkono wake wa kuume.

hatutakugeuka

"hatutaacha kukuabudu na kukutii" au "daima tutakuabudu na kukutii wewe"

Psalms 80:19

ung'ae kwetu

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwatendea kwa fadhila kana kwamba uso wa Yahwe uling'aa mwanga kwao. "tenda kwa fadhila kwetu"

tutaokoka

"utatuokoa"

Psalms 81

Psalms 81:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Zaburi ya Asafu.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Gitithi

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Zaburi ya Asafu

"Hii ni zaburi ambayo Asafu aliandika"

Mungu nguvu yetu

"Mungu anayesababisha tuwe na nguvu"

Mungu wa Yakobo

Hapa "Yakobo" inawakilisha uzao wake wote. "Mungu wa israeli, taifa la uzao wa Yakobo"

pigeni tari, kinubi kizuri

Hivi ni vyombo vya muziki.

tari

chombo cha muziki chenye kichwa kama ngoma kinachoweza kugongwa na kina vipande vya chuma vimezunguka pembeni vinavyotoa sauti chombo kinapotikiswa.

mwandamo wa mwezi

Huu ni mwanzo wa mwezi.

siku ya mbalamwezi

Hapa ni katikati ya mwezi.

sikukuu zetu zinapoanza

"na katika siku ambapo sikukuu zetu zinapoanza"

Psalms 81:4

Kwa kuwa

Hapa kinachozungumziwa ni sikukuu.

amri iliyotolewa na Mungu wa Yakobo

"Mungu wa Yakobo aliamrisha" au "Mungu wa yakobo aliamuru"

Mungu wa Yakobo

Hapa "Yakobo" inawakilishwa uzao wake wote. "Mungu wa Israeli, taifa la uzao wa Yakobo"

aliitoa kama kanuni

"aliitoa kama sheria"

katika Yusufu

Hapa "Yusufu" inawakilisha Waisraeli. "kwa Waisraeli"

alipoaende dhidi ya nchi ya Misri

Hii inamaanisha matukio ya kihistoria katika Misri wakati watu wa Israeli walipokuwa watumwa na Mungu akawaokoa.

nchi ya Misri

Hapa "nchi" inawakilisha watu. "watu wa Misri"

Psalms 81:6

Taarifa ya Jumla:

Hapa Mungu anaanza kuzungumza.

Nilitoa mzigo kutoka mabegani mwake

Hapa "mzigo kutoka mabegani mwake" inawakilisha kazi za kulazimishwa ambazo Waisraeli iliwalazimu kufanya kama watumwa Misri.

mikono yake iliwekwa huru na kushikilia kikapu

Hapa "kushikilia kikapu" inawakilisha kazi za kulazimishwa ambazo Waisraeli iliwalazimu kufanya kama watumwa Misri.

katika dhiki yako

"katika mateso yako makuu"

Nilikujibu kutoka katika wingu la giza la radi

Mungu alipokuja kwa Waisraeli, alificha ukamili wa uwepo wake na utukufu katika wingu lenye giza na la kutisha.

Nilikujaribu katika maji ya Meriba

Mungu aliwajaribu wana wa Israeli kuona kama watamtumaini kuwapa maji katika jangwa la Meriba.

Psalms 81:8

Taarifa ya jumla:

Yahwe unawakumbusha watu alichosema wakati wako jangwani.

kwa kuwa nitawaonya

"kwa sababu ninakupa onyo"

Israeli

Hapa "Israeli" inawakilisha watu wa Israeli. "Waisraeli" au "watu wa Israeli"

kama tu utanisikiliza!

"jinsi ninavyotamani kuwa mnisikilize" au "lakani inabidi muanze kunisikiliza!"

Fungua mdomo wako wazi, na nitaujaza

Mungu kujali mahitaji ya watu inazungumziwa kana kwamba alikuwa ni ndege anawalisha makinda yake.

Psalms 81:11

Taarifa ya Jumla:

Sasa Yahwe anaeleza nini kilitokea baada ya kuwaonya watu.

maneno yangu

Hapa "maneno" yanawakilisha kile ambacho Mungu alisema. "kwa kile nilichosema" au "kwangu"

Kwa hiyo nikawapa kwa njia yao wenyewe ya usumbufu

Mungu kuwaruhusu watu kubaki wasumbufu inazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa akiwapa kwa adui kumwacha adui awadhuru. "Kwa hiyo, ninawaacha wawe wasumbufu"

Psalms 81:13

O, kama watu wangu watembee katika njia zangu

Mungu kutaka watu kumtii inazungumziwa kana kwamba alitaka watu kutembea katika njia yake au mabarabara. "natamani kuwa watii sheria zangu"

geuza mkono wako dhidi

Hapa "mkono" inawakilisha uwezo wa yahwe. "nitawaangamiza" au "Nitawaangamiza"

Psalms 81:15

wanaomchukia Yahwe ... mbele zake

Yahwe anajizungumzia mwenyewe katika hali ya mtu wa tatu. ""wanaonichukia ... mbele yangu"

wajikunyate kwa hofu

"inama chini kwa hofu" au "anguka chini kwa hofu"

Na waaibishwe milele

"Nitawaaibisha milele" au "Nitawaadhibu milele"

Nitawalisha israeli kwa ngano safi

Mungu kusababisha ngano bora zaidi kuota Israeli inazungumziwa kana kwamba angewalisha watu ngano kiuhalisia. "Nitawaruhusu Waisraeli kula ngano bora zaidi"

Nitawalisha Israeli ... nitakuridhisha

Hapa pote wanaozungumziwa ni watu wa Israeli.

asali kutoka kwenye mwamba

Hii inamaanisha asali ya porini. Nyuki hujenga mizinga katika mashimo kwenye miamba na kutengeneza asali humo.

Psalms 82

Psalms 82:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Asafu

"Hii ni zaburi ambayo Asafu aliandika"

mkusanyiko mtakatifu

"baraza la mbinguni" au "mkutano wa mbinguni"

anapitisha hukumu

"anatoa hukumu." Nomino dhahania "hukumu" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "anahukumu"

miungu

Maana zinazowezekana ni 1) hivi ni viumbe vingine vya kiroho vinavyoishi mbinguni. "viumbe vitakatifu" au "mahakimu wa mbinguni" au 2) hawa ni mahakimu binadamu ambao Mungu amewachagua. Vyovyote vile, haimaanishi ni miungu kama Yahwe alivyo Mungu. Inamaanisha Mungu amewapa uwezo mkubwa na mamlaka. "watawala"

Hadi lini utahukumu bila haki na kuonesha upendeleo kwa waovu?

Yahwe anatumia swali kukemea miungu kwa kutowahukumu watu kwa haki.

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 82:3

maskini na wasio na baba

Hapa "maskini" na "wasio na baba" vivumishi vidogo. Vinaweza kuelezwa kama vivumishi. "wale walio maskini na walio yatima"

tunza haki za

"fanya iliyo haki kwa"

walioteswa na fukara

Hapa "walioteswa" na "fukara" ni vivumishi vidogo. Vinaweza kuelezwa kama vivumishi. "wale wanaoteseka na wale wasiokuwa na kitu"

maskini na wahitaji ... waovu

Hivi ni vivumishi vidogo. Vinaweza kuelezwa kama vivumishi. "wale walio maskini na wale walio wahitaji ... wale walio waovu"

watoe katika mkono wa waovu

Hapa neno "mkono" inawakilisha nguvu au uwezo. "uwadhibiti waovu kuwadhuru"

Psalms 82:5

Hawaelewi

Maana zinazowezekana ni 1) wasioelewa ni miungu au 2) wasioelewa ni watu waovu.

wanazurura gizani

Kufanya kilicho kiovu kinazungumziwa kana kwamba walikuwa wakitembea sehemu yenye giza sana.

misingi yote ya duniani inaanguka

Miungu kuharibu mpangilio wa uadilifu ambao Yahwe aliweka inazungumziwa kana kwamba miungu ilikuwa inatikisa dunia na kuifanya ibomoke.

inaanguka

"kubomoka"

Psalms 82:6

Nyie ni miungu, na nyie wote ni wana wa Aliye juu

Hapa "miungu" inamaanisha kundi sawa na la Zaburi 82:1. Kama hii inamaanisha viumbe wa kiroho au binadamu, sio miungu kama Yahwe alivyo Mungu, na sio wana wake kihalisi. Kwa kuwaita "miungu" na "wana wa Aliye juu," Yahwe anakiri kuwa amewapa uwezo mkuu na mamlaka.

wana wa Aliye juu

Yahwe anajizungumzia mwenyewe kama "Aliye juu."

Hata hivyo

"Ingawa"

na kuanguka

Hii ni njia ya kuzungumzia mtu anayekufa.

Psalms 82:8

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anazungumza tena.

hukumu ulimwengu

Hapa "ulimwengu" unawakilisha watu. "hukumu watu wa ulimwengu"

kwa kuwa una urithi katika mataifa yote

"kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako." Yahwe kuwachukua watu wote kama wake na kuwatawala inazungumziwa kana kwamba mataifa ni mali aliyorithi. "kwa kuwa unatawala juu ya watu wote wa kila taifa"

maataifa yote

Hapa "mataifa" inawakilisha watu wa mataifa.

Psalms 83

Psalms 83:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Wimbo. Zaburi ya Asafu

"Hii ni zaburi ambayo Asafu aliandika"

na kubaki bila kusogea

"na kutokufanya kitu kutusaidia"

Tazama, adui zako wanafanya ghasia

Hapa "kufanya ghasia" inamaanisha kufanya fujo au kukaidi. "Tazama, adui zako wanakaidi dhidi yako"

wale wanokuchukia wameinua vichwa vyao

Msemo "wameinua vichwa vyao" ni njia ya kusema kuwa wamekaidi dhidi ya Mungu. "wale wanaokuchukia wanakukaidi"

Psalms 83:3

uliowalinda

"wale unaowalinda" Hii inamaanisha Waisraeli.

jina la Israeli halitakumbukwa tena

Hapa "jina" linawakilisha sifa au kumbukumbu ya mtu. "hakuna mtu atakye kumbumbuka Waisraeli walikuwepo"

Wamepanga hila kwa pamoja na mkakati mmoja

"Adui zako wamekubali pamoja kwa mpango mmoja"

dhidi yako wamefanya mwungano

"wameungana pamoja dhidi yako"

Psalms 83:6

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuorodhesha makundi ya watu yanayotaka kuangamiza Israeli.

mahema ya Edomu

Hii inamaanisha watu wa Edomu walioishi katika mahema.

Wahagari

Hili ni jina la kundi la watu walioishi upande wa mashariki wa mto Yordani.

Gebali, Amoni, Amaleki ... FIlisti

Majina haya yote yanawakilisha watu wa kila eneo au kabila. "watu wa Gebali, Waamoni, Waamaleki ... Wafilisti"

Gebali

Hili jina la eneo kusini mwa bahari ya Chumvi.

Psalms 83:8

Ashuri

Hii inawakilishwa watu wa ashuri. "watu wa Ashuri"

uzao wa Lutu

Hii inamaanisha watu wa mataifa ya Moabu na Amoni.

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 83:9

Fanya kwao ...kwa ajili ya dunia

Mwandishi anamwomba Mungu kuwashinda adui wa Israeli kama alivyofanya kipindi cha nyuma.

ulivyofanya kwa Midiani

Hapa "Midiani" inawakilishwa watu wa Midiani. "ulivyofanya kwa Wamidiani"

Sisera ... Yabini

Haya ni najina ya wanaume. Yabini alikuwa mfalme wa Hazori. Sisera alikuwa kamanda wa jeshi la Yabini.

mto Kishoni

Hili ni jina la mto kaskazini mwa israeli

Endori

Hili ni jina la mji kaskazini mwa Israeli,

wakawa kama mbolea kwa ajili ya dunia

Hii inamaanisha miili ya Sisera na Yabini haikuzikwa lakini iliachwa kuoza.

Psalms 83:11

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anamwomba Mungu kuwashinda adui wa Israeli kama alivyofanya kipindi cha nyuma.

Orebu ... Zeebu ... Zeba ... Zalmuna

Haya yote ni majina ya wafalme.

Wakasema

Hapa "Wakasema" inamaanisha Orebu, Zeebu, Zeba na Zalmuna.

malisho ya Mungu

Mwandishi anazungumzia nchi ya Israeli kana kwamba ni nchi kwa ajili ya kondoo kula na Mungu alikuwa mchungaji wao aliyekuwa akiwachunga.

Psalms 83:13

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anatumia tashbihi kuelezea uharibifu kamili wa Mungu kwa adui wa Israeli.

wafanya kuwa kama mavumbi yanayozunguka, kama makapi mbele ya upepo

Kauli zote mbili zinazungumzia Mungu kuangamiza adui zake kana kwamba alikuwa upepo mkali unaowapuliza kwa urahisi.

kama moto unaochoma msitu, na moto unaoweka milima katika moto

Kauli zote mbili zinazungumzia adhabu ya Mungu kana kwamba ni moto, na adui wa Mungu ni vitu vinavyoungua katika moto.

Wafukuze kwa upepo wako wenye nguvu, na watishe kwa dhoruba yako

Kauli zote mbili zinamwomba Mungu kuangamiza adui kwa dhoruba.

Psalms 83:16

Jaza nyuso zao na aibu

Hapa "nyuso"zinawakilishwa mtu mzima. "Wafanye waaibike sana"

watafute jina lako

Hapa "jina" linawakilisha uwezo wa Mungu. Adui wa Mungu kukiri kuwa Mungu ana uwezo inazungumziwa kana kwamba wanatafuta kumpata yahwe. "wakubali kuwa una uwezo"

watafute jina lako

Maana zinazowezekana ni 1) adui wa Mungu wanakiri kuwa Mungu ana uwezo au 2) adui wa mungu wanamwomba Mungu msaada au 3) adui wa Mungu wanaanza kumwabudu na kumtii.

Na waaibishwe na kuogofywa milele

"Wafanye waaibike na kuogopa milele"

waangamie kwa aibu

"na wafe wakiwa wameaibika"

Psalms 83:18

Kisha watajua

"Wafanye wajue"

ndiye Uliye juu, juu ya dunia yote

Mungu kutawala juu kila kitu duniani inazungumziwa kana kwamba ameinuliwa juu zaidi ya vingine vyote. "ndiye mkuu, na unatawala vitu vyote duniani"

Psalms 84

Psalms 84:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika Gitithi

Hii inaweza kuwa inamaanisha mtindo wa muziki.

Zaburi ya wana wa Kora

"Hii ni zaburi ambayo wana wa Kora waliandika"

Panapendeza kiasi gani

"Ni pazuri kiasi gani"

na shauku na nyua za Yahwe

"Ninatamani sana kuwa katika nyua za Yahwe"

nyua za Yahwe

Hapa "nyua" inawakilisha hekalu.

hamu yangu kwa kwa hizo imanichosha

"hamu yangu imenichosha" au "nimechoka kwa sababu ninaitaka sana"

Moyo wanguna kila kitu ndani yangu kinamwita

Hapa "moyo" unawakilisha mtu mzima. "Niita kwa kila kitu ndani yangu"

Mungu aliye hai

Hii inamaanisha kuwa Mungu yu hai na pia ana uwezo wa kusababisha vitu vingine kuishi.

Psalms 84:3

shorewanda ... mbayuwayu

Hawa ni aina ya ndege.

amepata nyumba

"amejipatia makazi" au "ametengeneza makazi"

mbayuwayu kioto

"mbayuwayu amepata kioto" au "mbayuwayu ametengeneza kioto"

ambapo anaweza kuweka makinda yake

"ambapo anaweza kutaga mayai na kutunza makinda yake"

wale wanaoishi nyumbani kwako

Maana zinazowezekana ni 1) "wale' inamaanisha makuhani ambao hutumika muda wote hekaluni au 2) "wale" inamaanisha watu kwa ujumla ambao hua wanakuja kuabudu hekaluni.

kwa uendelevu

"tena na tena"

Psalms 84:5

Amebarikiwe mtu

Hapa "mtu" inamaanisha watu kwa ujumla.

ambaye nguvu yake iko katika wewe

Mungu anazungumziwa kana kwamba nguvu kweli ilipatikana ndani yake. "ambaye unamtia nguvu"

ambaye moyoni mwake ni njia za kwenda Sayuni

Msemo huu unahusu hamu ya kweli kutoka moyoni. "Wanaopenda kwenda juu Sayuni" au "Wanaotaka kwa dhati kwenda juu Sayuni"

njia

"barabara kuu"

za kwenda Sayuni

Hekalu lilikuwa Yerusalemu juu ya kilima kirefu zaidi, kiitwacho mlima Sayuni.

mabonde ya Machozi

Hii inamaanisha sehemu iliyokauka. Biblia zingine zina "bonde la Baka." neno "Baka" linamaanisha kulia."

Mvua za mapema

Hii inamaanisha mvua inayodondoka katika majira ya kupukutika kwa majani kabla ya majira ya baridi. Hiki ni kipindi cha miezi ya Oktoba na Novemba katika kalenda za magharibi.

baraka

"mabwawa ya maji"

Psalms 84:7

Huenda kutoka nguvu hadi nguvu

Hii ni njia ya kusema wanapata nguvu.

Huenda

Hapa wanaoenda inamaanisha wale wanaotamani kwenda hekaluni kumwabudu Mungu.

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Mungu, angalia ngao yetu

Mfalme anayewalinda watu wake anazungumziwa kana kwamba ni ngao. "Mungu, mwangalie mfalme wetu"

Kwa kuwa siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu pengine

"Ni bora niwe katika nyua zako kwa siku moja badala ya kuwa sehemu nyingine kwa siku elfu moja"

elfu

"1,000"

niwe bawabu

"niwe mlinzi mlangoni" au "nisimame mlangoni"

waovu

"watu waovu" au "wale ambao ni waovu"

Psalms 84:11

Kwa kuwa Yahwe Mungu ni jua letu na ngao

Yahwe anayewaongoza na kuwalinda watu wake anazungumziwa kana kwamba alikuwa jua na ngao. "Kwa kuwa Yahwe hutuongoza kama mwanga wa jua, na hutulinda kama ngao"

Yahwe atatoa neema na utukufu

"Yahwe atakuwa na huruma kwetu na kutupa heshima"

wanaotembea katika uadilifu

Jinsi mtu anavyoenenda maisha yake inazungumziwa kana kwamba mtu huyo alikuwa akitembea. "wanaoishi kwa uadilifu" au "walio wa kweli"

amebarikiwa mtu

Hapa "mtu" inamaanisha mtu kwa ujumla. "wamebarikiwa wale"

Psalms 85

Psalms 85:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya wana wa Kora

"Hii ni zaburi ambayo wana wa Kora waliandika."

umeonesha fadhila kwa nchi yako

Hapa "nchi" inawakilisha taifa na watu wa Israeli.

ustawi

Hii inamaanisha mtu kuwa na furaha, mwenye afya na mafanikio.

wa Yakobo

Hapa "Yakobo" inawakilisha uzao wa Yakobo, Waisraeli.

umefunika dhambi zao zote

Hapa dhambi iliyosamehewa inazungumziwa kana kwamba imefunikwa ili isionekane. "umesahau kwa makusudi dhambi zao"

dhambi zao

Mwandishi alijifikiria kama kuwa miongoni mwa watu wa Mungu. "dhambi zetu"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 85:3

Umeondoa gadhabu yako yote

Mungu kutowaadhibu tena Waisraeli inazungumziwa kana kwamba gadhabu ni kitu ambacho Yahwe anaweza kuondoa kutoka kwa Waisraeli.

umegeuka kutoka katika hasira yako ya moto

Mungu kutokuwa na hasira tena na Waisraeli inazungumziwa kana kwamba hasira ni moto kutoka kwa Mungu ambao Mungu ameuguza.

Mungu wa wokovu wetu

"Mungu anayetuokoa"

achia chuki uliyonayo kwetu

Kumwomba Mungukuacha kuwa na hasira na Waisraeli inazungumziwa kana kwamba chuki ni kitu ambacho mwandishi anataka Mungu aachie.

Je! Utakuwa na hasira na sisi milele? Utabaki na hasira katika vizazi vyote?

Mwandishi anatumia maswali haya kusisitiza kwamba anamwomba Mungu kuacha kuwa na hasira nao. "Tafadhali usibaka na hasira na sisi milele."

Psalms 85:6

Je! Hautahuisha tena?

Mwandishi anatumia swali hili kusisitiza kwamba anamwomba Mungu kuwafanya watu wa Israeli wafanikiwe na wawe na furaha tena. "Tafadhali tufanye kuwa na mafanikio tena"

Tuoneshe uaminifu wako wa agano

"Kuwa mwaminifu kwa sababu ya agano lako na sisi"

tupe wokovu wako

"tupe wokovu wako kwa kutuokoa"

Psalms 85:8

atafanya amani na watu wake

"atakuwa na mahusiano ya amani na watu wake" au "ataleta amani kwa watu wake"

Bali wasirudie tena njia zao za upumbavu

Mtu anayebadili tabia yake anazungumziwa kana kwamba alikuwa akigeukia kimwili upande mwingine. "Bali hawatakiwa kuanza kufanya mambo ya upambavu tena"

Hakika wokovu wake uko karibu na wale

Mungu kuwa tayari kumwokoa mtu inazungumziwa kana kwamba wokovu ni kitu ambacho Mungu ameweka karibu na mtu. "Hakika Mungu yuko tayari kuwaokoa wale"

kisha utukufu utabaki katika nchi yetu

Hapa "utukufu" unawakilisha uwepo wa Mungu. "kisha uwepo wake wa utukufu utabaki katika nchi yetu"

Psalms 85:10

Uaminifu wa agano na uaminifu umekutana pamoja

Maana zinazowezekana ni 1) Mungu atakuwa mwaminifu kwa sababu ya agano lake na atafanya alichoahidi au 2) Mungu atakuwa mwaminifu kwa sababu ya agano lake na watu wataitikia kwa kuwa waaminifu kwake. Vyovyote vile uaminifu unazungumziwa kana kwamba ni mtu anayeweza kukutana na mwenzake.

umekutana pamoja ... zimepigana busu

Inawezekana kuwa mwandishi anazungumzia wakati wa mbele ambapo Mungu atawasababisha watu wake kufanikiwa tena. zitakutana pamoja ... zitapigana busu"

haki na amani zimepigana busu

Maana zinaziwezekana ni 1) watu watafanya kilicho sawa na mungu atawasababisha watu kuishi kwa amani au 2) Mungu atafanya kilicho sawa na kuwasababisha watu kuishi katika amani. Vyovyote vile, haki na amani zinazungumziwa kana kwamba ni watu wanajipiga busu.

zimepigana busu

Hii ni njia ya kawaida ya marafiki kusalimiana.

Uaminifu unachomoza kutoka kwenye ardhi

Watu wa duniani kuwa waaminifu kwa Mungu inazungumziwa kana kwamba uaminifu ni mmea unaoota ardhini. "Hapa duniani, tutakuwa waaminifu kwa Mungu"

haki inaangalia chini kutoka angani

Mwandishi anaelezea haki kama mtu anatazama chin kama Mungu afanyavyo. "Mungu atatuangalia kwa fadhila na kutupa ushinid"

Psalms 85:12

Haki itamtangulia na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake

Mungu kufanya kilicho sawa kila sehemu aendayo inazungumziwa kana kwamba haki ni mtu ambaye humtangulia Mungu na kuandaa njia ya Mungu kupitia.

hatua zake

Hapa "hatua" inawakilisha ambapo Mungu anapita.

Psalms 86

Psalms 86:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

maskini na niliye kandamizwa

"mnyonge na mhitaji"

mwokoe mtumishi wako

Daudi anajizungumzia kama "mtumishi wako," yaani, mtumishi wa Mungu. "niokoe mimi, mtumishi wako"

Psalms 86:3

siku nzima

Hii ni kukuza kwa neno. Daudi halii siku nzima kwa uhalisia. Hii inasisitiza kuwa huwa analia kwa uendelevu. "kwa uendelevu"

Mfanye mtumishi wako kuwa na furaha

Daudi anajizungumzia kama "mtumishi wako," yaani, mtumishi wa Mungu. "Nifanye mimi, mtumishi wako" au "Nifanye"

Psalms 86:5

Katika siku ya taabu yangu

Hapa "siku" inawakilisha muda mrefu zaidi. "Wakati wa kipindi changu cha taabu"

ninakuita wewe

"nina omba kwako"

Psalms 86:8

kati ya miungu

Mwandishi hakiri kuwa miungu hii mingine ipo. Anamaanisha miungu ya uongo ambayo watu wa mataifa mengine huabudu.

Mataifa yote

Hapa "mataifa" inawakilisha watu. "Watu kutoka mataifa yote"

Watatukuza jina lako

Hapa "jina" linamwakilisha mtu mzima. "Watakutukuza"

Psalms 86:10

mambo ya ajabu

"vitu vizuri sana vinavyo tushangaza"

wewe pekee ni Mungu

"wewe ndiye Mungu pekee"

Nifundishe njia zako, Yahwe. Kisha nitatembea katika kweli yako

Mtu anayetii kile ambacho Mungu anataka anazungumziwa kana kwamba anatembea katika njia au barabara la Mungu. "Nifundishe ukweli wako, Yahwe. Kisha nitatii unachosema"

Unganisha moyo wako kukucha wewe

Hapa "moyo" unawakilisha mawazo, hisia na nia ya mtu. Kumwomba Mungu kumsababisha mtu kumtii kikamilifu inazungumziwa kana kwamba moyo wa mtu ulikuwa katika vipande vingi na kwamba Mungu anaviunganisha pamoja. "Nisababishe nikuheshimu kwa moyo wangu wote" au "Nisababishe nikuheshimu kwa dhati"

nitakusifu kwa moyo wangu wote

Hapa "moyo" unawakilisha mawazo, hisia na nia ya mtu. "Nitakusifu kikamilifu na kwa dhati"

nitalitukuza jina lako

Hapa "jina" linamwakilisha mtu mzima. "nitakutukuza"

Psalms 86:13

Kwa kuwa uaminifu wako wa agano ni mkuu kwangu

"Kwa kuwa wewe ni mwaminifu kwangu kwa sababu ya agano lako"

umeokoa maisha kutoka vilindi vya kuzimu

Hii haimaanishi kuwa Mungu alimfufua baada ya kufa. Inamaanisha kuwa Mungu alimwokoa alipotaka kufa.

wenye kiburi

"watu wenye kiburi"

wameinukadhidi yangu

"wanakuja pamoja kunidhuru"

wanatafuta maisha yangu

Hii ni njia ya kusema wanataka kumuua.

Psalms 86:15

umejaa uaminifu wa agano na uaminifu

Mungu kuwa mwaminifu kila wakati inazungumziwa kana kwamba uaminifu ni kitu ambacho Mungu ana kiasi kikubwa chake.

Geuka kwangu

Kumwomba Mung kumzingatia inazungumziwa kana kwamba alimtaka Mungu amgeukie na kumwangalia.

mpe mtumishi wako nguvu yako

"mwimarishe mtumishi wako" au "mfanye mtumishi wako kuwa imara"

mtumishi wako ... mwana wa mjakazi wako

Mwandishi anajizungumzia mwenyewe katika hali ya mtu wa tatu.

na kuaibishwa

"na wataaibika"

Psalms 87

Psalms 87:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya wana wa Kora; wimbo

"Hii ni zaburi ambayo wana wa Kora waliandika"

malango ya Sayuni

Hapa "malango ya Sayuni" inawakilisha mji mzima wa Yerusalemu. "mji wa Yerusalemu"

mahema yote ya Yakobo

Watu waliishi katika mahema walipokuwa wakizurura jangwani. Hapa mwandishi anatumia "mahema ya Yakobo" kuwakilisha mahali Waisraeli wanapoishi sasa. "sehemu yoyote ya kuishi ya Waisraeli"

Mambo yenye utukufu yanasemwa juu yako, mji wa Mungu

Mwandishi anazungumza na mji wa Yerusalemu kana kwamba ulikuwa unamsikiliza. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nyie watu katika Yerusalemu, watu wengine wanasema vitu vizuri kuhusu mji wenu"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 87:4

Ninamtaja

"Nitawaambia kuhusu." Anyezungumza hapa ni Yahwe.

Rahabu na Babeli

Hapa "Rahabu" ni njia ya kishahiri ya kumaanisha Misri. Zote "Rahabu" na "Babeli" zinawakilisha watu. "watu wa Misri na Babeli"

kwa wafuasi wangu

"kwa wale wanaoniabudu"

Filisti, na Tirohopia, pamoja na Kushi

Majina ya mataifa haya yanawakilisha watu. "watu kutoka Filist na Tiro, pamoja na watu wa Kushi"

Huyu alizaliwa huko

"Huyu" inamaanisha watu kutoka mataifa ambayo mwandisha ameyataja. Ingawa hawakuzaliwa kimwili Sayuni, wale wanaomfuata Mungu ni wakazi wa Yerusalemu kiroho.

Psalms 87:5

Kwa Sayuni itasemwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu watasema kuhusu Sayuni"

Kila mmoja wa hawa alizaliwa ndani yake

Watu kutoka mataifa mengine wanaomwabudu Yahwe wanazungumziwa kana kwamba walizaliwa Yerusalemu. "Ni kana kwamba watu hawa wote walizaliwa Yerusalemu"

ndani yake

Ilikuwa kawaida kuelezea miji kama mtu.

Aliye juu mwenyewe

Mwandishi anatumia kiwakilishi cha kujirudia "mwenyewe" kusisitiza kuwa Aliye juu ndiye anafanya hiki.

atamuimarisha

"ataifanya Yerusalemu kuwa imara"

Yahwe anaandika katika kitabu cha sensa cha mataifa

Yahwe kukubali kuwa watu kutoka mataifa mengine ni wake inazungumziwa kana kwamba yeye ni mfalme anayeandika majina ya watu wanaoishi katika mji wake.

Huyu hapa alizaliwa huko

"Huyu" inamaanisha watu kutoka mataifa ambayo mwandishi ametaja. Ingawa hawakuzaliwa kimwili Sayuni, wale wanaomfuata Mungu ni wakazi wa Mji wa Yerusalemu kiroho.

Psalms 87:7

Chemchemi zangu zote ziko ndani yako

Yerusalemu kuwa sehemu ambayo watu hupokea baraka zao zote inazungumziwa kana kwamba Yerusalemu ni chemchemi inayotoa maji kwa watu.

Psalms 88

Psalms 88:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Wimbo, zaburi ya wana wa Kora

"Hii ni zaburi ambayo wana wa Kora waliandika"

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

weka katika mtindo wa Mahalathi Leanothi

Hii inaweza kuwa inamaanisha mtindo wa muziki.

Maschili

Hii inaweza kuwa inamaanisha mtindo wa muziki.

Hemani

Hili ni jina la mwanamume

Mwezrahi

Hili ni jina la kundi la watu. Inaweza kumaanisha mwana au uzao wa Zera.

Mungu wa wokovu wangu

"wewe ndiye unaye niokoa"

mchana na usiku

Mwandishi anatumia maneno haya yenye maana tofauti kumaanisha kuwa analia kwa uendelevu.

Psalms 88:3

Kwa kuwa nimejaa taabu

Mwandishi anajizungumzia kana kwamba ni chombo na taabu ni vitu vinavyojaza hicho chombo. "Kwa kuwa nina taabu sana"

maisha yangu yamefika kuzimu

Hapa "maisha" yanamwakilisha mwandishi na "kuzimi" kunawakilisha mauti. Inawezekana mwandishi anajizungumzia mwenyewe kufa mapema kana kwamba kuzimu ni sehemu na amefika hiyo sehemu. "nimekaribia kufa"

Watu wananifanyia kama wale wanaoenda chini shimoni

Neno "shimo" linamaana moja kama "kuzimu." Msemo "wanaoenda chini kuzimu" inawakilisha kufa. "watu wananifanya kana kwamba tayari nimekufa"

Psalms 88:5

Nimeachwa miongoni mwa wafu

Watu kumfanyia mwandishi kana kwamba tayari amekufa inazungumziwa kana kwamba ni maiti ambayo imeachwa bila kuzikwa. "Nimeachwa peke yangu kana kwamba nimekufa"

mimi ni kama mfu niliyelala kaburini

Mwandishi kuhisi kana kwamba watu na Mungu wamemwacha anajizungumzia kana kwamba alikuwa tayari ni mtu aliyekufa amelala kaburini.

mfu niliyelala

"mtu aliyekufa mabaye amelala" au "watu waliokufa ambao wamelala"

ambao huwajali tena

"watu ambao umeacha kuwajali"

wamekatwa kutoka katika nguvu yako

Mungu kuacha kutumia nguvu yake kuwasaidia wafu inazungumziwa kana kwamba Mungu amemkata au amemtoa kutoka kwenye nguvu yake. "hautumii tena nguvu yako kuwaokoa"

Umeniweka katika sehemu ya chini zaidi ya shimo, katika vina vya china vyenye giza

Mwandishi kuhisi kama Mungu kumwacha anajizungumzia kana kwamba Mungu amemweka katika kaburi kina kirefu zaidi na lenye giza.

Psalms 88:7

Gadhabu yako ni nzito kwangu

Hii inazungumzia jinzi Mungu alivyo na hasira sana na mwandishi kana kwamba gadhabu ya Mungu ni kitu kizito kilicho juu ya maji. "Ninahisi hasira yako kuu" au "Ninahisi jinsi ulivyo na hasira kali na mimi"

njia zako zote zinanikandamiza

Hii inazungumzia Mungu kuwa na hasira sana na mwandishi kana kwamba hasira ya Mungu ni mawimbi makubwa yanayoinuka kutoka baharini na kutua kwa mwandishi.

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 88:8

wanaonifahamu

"wale wanaonijua"

Umenifanya kitu cha kushangaza kwao

"Umenifanya kitu cha kuchukiza machoni kwao" au "Kwa sababu yako, wanashangaa wanaponiona"

Nimezungukwa

Hali ya kimwili ya mwandishi inayomfanya kuwa chukizo kwa rafiki zake inazungumziwa kana kwamba alikuwa amefungwa katika nafasi yenye mipaka. "Ni kana kwamba nilikuwa gerezani" au "Nimenaswa"

Psalms 88:9

Macho yangu yanachoka kutokana na taabu

Hapa "macho" yanawakilisha uwezo wa mtu kuona. Kwa macho yake kuchoka kutokana na taabu ni njia ya kusema kwamba matatizo yake yanamsababisha kulia sana hadi inakuwa kazi kwake kuona.

Ninanyosha mikono yangu kwako

"Ninainua mikono yangu kwako." Hiki ni kitendo kinachoonesha kuwa anamtegemea Mungu kabisa.

Je! Utafanya maajabu kwa wafu?

Mwandishi anatumia swali kusisitiza kuwa kama Mungu akimwacha afe basi Mungu hataweza tena kufanya mambo ya ajabu kwa ajili yake. "Wewe hufanyi maajabu kwa awatu waliokufa."

Je! Wale waliokufa watafufuka na kukusifu

Mwandishi anatumia swali kusisitiza kuwa kama Mungu akimwacha afe basi hataweza kumsifu Mungu tena. "Unajua kuwa waliokufa hawataweza kusimama na kukusifu"

Psalms 88:11

Je! Uaminifu wako wa agano utatangazwa kaburini, uaminifu wako katika sehemu ya wafu?

Maswali yote yanamaanisha kitu kimoja. Mwandishi anatumia maswali kusisitiza kuwa mtu aliyekufa hawezi kusifu uaminifu wa Mungu. "Hakuna atakaye tangaza uaminifu wako wa agano au uaminifu wako kutoka kaburini"

kaburini ... sehemu ya wafu ... gizani ... sehemu ya usahaulifu

Majina haya yote yanawakilisha mahali ambapo watu huenda baada ya kufa.

uaminifu wako katika sehemu ya wafu?

"Je! Uaminifu wako utatangazwa katika sehemu ya wafu?" au "Wale waliokufa hawatatangaza uaminifu wako."

Je! Matendo yako ya ajabu yatajulikana gizani, au haki yako katika sehemu ya haki?

Maswali yote yanamaanisha kitu kimoja. Mwandishi anatumia maswali kusisitza kuwa wale walio kufa hawawezi kupitiia au kutangaza mambo makuu ambayo Mungu hufanya. "Watu hawazungumzii kuhusu matendo yako ya ajabu na haki katika sehemu ya giza ya watu walio sahaulika."

au haki yako katika sehemu ya haki?

"Je! Haki yako itajulikana katika sehemu ya walio sahaulika?" au "Wale walio katika sehemu ya usahaulifi hawatajua kuhusu mambo ya haki unayofanya."

Psalms 88:13

ombi langu linafika mbele yako

Mwandishi kuomba kwa yahwe inazungumziwa kana kwamba ombi lenyewe linaenda kuzungumza na Yahwe.

Kwa nini unaficha uso wako kwangu?

Hii inazungumzia mwandishi kuhisi kama Mungu amemkataa au kumwacha kana kwamba Mungu alikuwa akificha sura yake au kugeuka kiuhalisia kumwepuka mwandishi.

Psalms 88:15

Matendo yako ya hasira yamepita juu yangu

Hii inamzungumzia Mungu kumwadhibu mwandishi kana kwamba matendo ya Mungu ni wimbi kubwa linaloinuka kutoka baharini na kumwangukia na kumkandamiza mwandishi. "ni kana kwamba matendo yako ya hasira yananikandamiza"

matendo yako ya kutisha yameniangamiza

Hii inazungumzia Mungu kumwadhibu mwandishi kana kwamba Mungu alimwangamiza kabisa mwandishi. "vitu vya kutishi unavyofanya vimeniangamiza" au "vitu vya kustisha unavyofanya kidogo viniangamize"

Psalms 88:17

Yamenizunguka kama maji siku nzima

Mwandishi anafananisha m"matendo ya hasira" ya Mungu na "matendo ya kutisha" na mafuriko ya maji. "Siku nzima wananitisha kuniangamiza kama mafuriko"

Yamenizunguka

Kinachozungumziwa ni "matendo ya hasira" ya Mungu na "matendo ya kutisha" kutoka katika mstari uliopita.

yamenizunguka yote

Mwandishianazungumzia "matendo ya hasira" na "matendo ya kutisha" kana kwamba ni adui waliokuwa wakijaribu kumshika na kumuua. "wamenizunguka kama askari adui"

kila rafiki na anaye nijua

"kila mtu ninayempenda na kumjua"

Anijuae pekee ni giza

Hii inazungumzia giza kana kwamba ni mtu ambaye anaweza kuwa rafiki na mtu mwingine. Mwandishi anasisitiza kuwa anajihisi upweke. "Kila sehemu ninayoenda ni giza"

Psalms 89

Psalms 89:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

Ethani

Hili ni jina la mwandishi.

Mwezrahi

Hili ni jina la kundi la watu. Inaweza kumaanisha mwana au uzao wa Zera.

matendo ya uaminifu wa agano

"matendo ya uaminifu" au "matendo ya upendo"

Uaminifu wa agano umethibitishwa milele

Mungu kufanya alichoahidi kufanya inazungumziwa kana kwamba uaminifu wake ni jengo ambalo Mungu amejenga na kuimarisha. "Daima utakuwa mwaminifu kwa sababu y agano lako na sisi"

ukweli wako umethibitisha mbinguni

Mungu kufanya alichoahidi kufanya inazungumziwa kana kwamba uaminifu wake ni jengo ambalo Mungu amejenga na kuimarisha.

mbinguni

Maana zinazowezekana ni 1) hii inamaanisha makazi ya Mungu. Hii inamaanisha Mungu hutawala kutoka mbinguni na huwa anafanya kile alichoahidi au 2) hii inamaanisha anga. Hii inamaanisha kuwa wahadi za Mungu hazibadiliki na ni za kudumu kama anga.

Psalms 89:3

Nimefanya agano na niliye mchagua

"Nimempa ahadi Daudi, yule niliye mchagua"

Nimefanya

Yahwe anazungumza katika 89:3-4.

Nitawathibitisha uzao wako milele

Yahwe kuwasababisha uzao wa Daudi daima kuwa wafalme inazungumziwa kana kwamba uzao wa Daudi ni jengo ambalo Yahwe atajenga na kuimarisha.

Nitathibitisha kiti chako cha enzi katika vizazi vyote

Hapa "kiti cha enzi" kinawakilisha uwezo wa kutawala kama mfalme. Mwandishi wa zaburi anazungumzia Mungu kuahidi kuwa mmoja wa uzao wa Daudi atatawala daima kama mfalme kana kwamba Mungu atajenga kiti cha enzi cha Daudi na kukiimarisha. "Nitahakikisha kwamba mmoja wa uzao wako atatawala kama mfalme juu ya kila kizazi cha watu wangu"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 89:5

Mbingu zinasifu

Hapa "mbingu" inawakilisha wale walio mbinguni.

zinasifu maajabu yako, Yahwe

"zinakusifu, Yahwe, kwa sababu ya mambo ya ajabu unayotenda"

ukweli wako unasifiwa katika kusanyiko la watakatifu wako

"Mkusanyiko wa watakatifu hukusifu kwa sababu daima huwa unafanya ulichoahidi kufanya"

kusanyiko la watakatifu wako

Hii inamaanisha malaika mbinguni.

Kwa kuwa ni nani angani anaweza kulinganishwa na Yahwe? Nani miongoni mwa wana wa miungu ni kama Yahwe?

Maswali haya yote yana maana moja. Mwandishi anatumia swali hili kusisitiza kuwa hakuna mtu kama Yahwe mbinguni.

wana wa miungu

Hapa "wana" inamaanisha kuwa na sifa za. HIi ni njia ya kumaanisha viumbe vya kiroho vinavyoishi mbinguni. "malaika" au "viumbe vitakatifu"

Psalms 89:7

Yeye ni Mungu anayetukuzwa sana katika baraza la watakatifu

"Baraza la watakatifu lamtukuza sana Mungu"

baraza la watakatifu

"mkusanyiko wa viumbe wa mbinguni" au "mkusanyiko wa malaika"

nani mwenye nguvu kama wewe, Yahwe?

Mwandishi anauliza hili swali kusisitiza kuwa hakuna mtu mwenye nguvu kama Yahwe.

Ukweli wako unakuzunguka

Yahwe kufanya kile alichoahidi kufanya inazungumziwa kana kwamba ukweli wake ni joho au nguo inayozungushwa kwake.

Psalms 89:9

Unatawala bahari lenye hasira kali

"Una madaraka na bahari lenye hasira kali"

Ulimponda Rahabu kama mtu aliyeuawa

Neno "Rahabu" hapa linamaanisha mnyama mkubwa wa baharini.

kwa mkono wako imara

Hapa "mkono" inawakilisha uwezo. "kwa uwezo wako mkuu"

Psalms 89:11

kaskazini na kusini

Mwandishi anatumia maneno "kaskazini" na "kusini" kwa pamoja kumaanisha kuwa Mungu aliumba kila kitu kila sehemu.

Tabori na Hermoni wanafurahi katika jina lako

Tabori ni mlima kusini magharibi mwa bahari la Galilaya na Hermoni ni mlima kaskazini mashariki mwa bahari la Galilaya. Mwandishi anaelezea milima hii kana kwamba ni watu wanaoweza kufurahi. "Ni kana kwamba mlima Tabori na mlima Hermoni ilikuwa ikifurahi katika jina lako"

katika jina lako

Hapa "jina" linamaanisha mtu mzima. "katika wewe"

Psalms 89:13

Una mkono wenye uweza na mkono imara, na mkono wako wa kuume uko juu

Maneno "mkno wenye uweza," "mkono imara," na "mkono wa kuume" yote inawakilisha nguvu ya Mungu.

mkono wako wa kuume uko juu

Kuinua mkono wa kuume angani ni ishara inayoonesha nguvu.

Haki na hukumu ni msingi wa kiti chako cha enzi

Mungu kutawala kama mfalme na kufanya kilicho sawa na haki inazungumziwa kana kwamba kiti cha enzi cha Mungu ni jengo, na haki na hukumu ndio msingi wake.

kiti chako cha enzi

Kiti cha enzi kinawakilisha utawala wa Mungu kama mfalme.

Uaminifu wa agano na uaminifu unakuja mbele zako

Mungu kuwa mwaminifu daima na kufanya alichoahidi kufanya inazungumziwa kana kwamba uaminifu wa agano na uaminifu huja pamoja na kukutana na Mungu.

Psalms 89:15

wanao kuabudu

Hapa neno "kuabudu" inaashiria kupiga kelele na kupuliza pembe. Haya yalikuwa matendo ya kawaida wa kuabudu wakati wa sikukuu za Waisraeli.

wanatembea

Hapa watu kuishi maisha yao inazungumziwa kana kwamba wanatembea.

katika mwanga wa uso wako

Mwandishi anazumzungumzia Yahwe kuwatendea fadhila kana kwamba uso wa Yahwe ulimulika mwanga kwao. "wakijua kuwa unawatendea fadhila"

katika jina lako

Hapa "jina" linamwakilisha mtu. "katika wewe"

katika haki yako wanakutukuza

"wanakutukuza kwa sababu daima huwa unafanya kilicho sawa"

Psalms 89:17

Wewe ni nguvu yao ya fahari

"Wewe huwafanya kuwa na nguvu ya ajabu"

Wewe ni nguvu yao

Hapa "yao" inamaanisha Waisraeli. Mwandishi angejiweka pamoja kama mmoja wa Waisraeli. "Wewe ni nguvu yetu"

sisi ni washindi

Hapa "sisi" inamaanisha mwandishi na Waisraeli.

Kwa kuwa ngao yetu ni ya Yahwe

Mfalme ambaye huwalinda watu wake na ambaye Yahwe amemchagua anazungumziwa kana kwamba ni ngao ya Yahwe.

Psalms 89:19

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anachukulia kuwa msomaji anafahamu historia ya jinsi Daudi alivyochaguliwa kuwa mfalme.

Nimeweka taji kwa aliye hodari

Kuweka taji juu ya kichwa cha mtu ni ishara ya kumfanya kuwa mfalme. "Nimemfanya mtu hodari kuwa mfalme"

Nimeweka taji kwa aliye hodari

Tafsiri zingine za Biblia zina "kumpa nguvu aliye hodari" au "kumsaidia aliye hodari."

Nimemwinua mmoja niliyemchagua miongoni mwa watu

Hapa "nimemwinua" inamaanisha kuchagua. Inadokezwa kuwa Mungu alimchagua mtu huyu kuwa mfalme. "Nimemchagua mmoja miongoni mwa watu kuwa mfalme"

kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka

Hapa kumwaga mafuta juu ya kichwa cha mtu ni ishara kuwa Mungu anamchagua huyo mtu kuwa mfalme.

Mkono wangu utamshika; mkono wangu utamtia nguvu

Hapa "mkono" unamaanisha nguvu na mamlaka ya Yahwe. "nitamshika na kumfanya kuwa na nguvu"

mwana wa uovu

Mwandishi anawazungumzia wale wenye sifa au tabia ya uovu kama "wana wa uovu." "mtu mwovu"

Psalms 89:24

Kauli Unganishi:

Yahwe anaendelea kumzungumzia Daudi.

Ukweli wangu na uaminifu wangu wa agano utakuwa naye

Mungu kuwa mwaminifu daima na kufanya alichomwahidi Daudi inazungumziwa kana kwamba ukweli na uaminifu ni vitu ambavyo vitakuwa na Daudi.

kwa jina langu atashinda

Hapa "jina" linawakilisha nguvu ya Mungu. "Mimi, Mungu, nitamsababisha awe na ushindi"

Nitaweka mkono wake juu ya bahari na mkono wake wa kuume juu ya mito

Hapa "mkono" na "mkono wake wa kuume" inawakilisha uwezo na mamlaka, Hapa "bahari" inaonekana kumaanisha bahari ya Kati magharibi mwa Israeli, na "mito" inamaanisha mto Frati ulio mashariki. Hii inamaanisha kuwa Daudi atakuwa na mamlaka juu kila kitu kutoka baharini hadi kwenye mto. "Nitampa mamlaka juu ya kila kitu kutoka bahari ya Kati hadi mto Frati"

Ataniita, 'Wewe ni baba yangu, Mungu wangu, na mwamba wa wokovu wangu'

Hii ina nukuu ndani ya nukuu. "Atasema kuwa mimi ni baba yake, Mungu wake, na mwamba wa wokovu wake"

mwamba wa wokovu wangu

Yahwe kumlinda na kumwokoa daudi inazungumziwa kana kwamba Yahwe ni mwamba wa juu ambao Daudi aliweza kusimama juu yake kwa ajili ya ulinzi kutoka kwa adui.

Psalms 89:27

Kauli Unganishi:

Yahwe anaendelea kumzungumzia Daudi.

Pia nitamweka kama mzaliwa wa kwanza

Yahwe kumpa Daudi cheo maalumu na faida zaidi ya watu wengine wote inazungumziwa kana kwamba Daudi atakuwa mzaliwa wa kwanza wa Yahwe.

kiti cha cha enzi cha kudumu kama anga zilizo juu

Mtu kutoka familia ya Daudi kutawala daima kama mfalme inazungumziwa kana kwamba kiti chake cha enzi kitadumu muda sawa kama anga itakavyodumu.

kiti cha cha enzi

Hapa "kiti cha enzi" kinawakilisha uwezo wa kutawala kama mfalme.

Psalms 89:30

watoto wake

"uzao wa Daudi"

nitaadhibu uasi wao kwa fimbo

Mungu kuadhibu uzao wa Daudi inazungumziwa kana kwamba atawapiga kwa fimbo. "nitawaadhibu kwa kuasi dhidi yangu"

na udhalimu wao kwa mapigo

Mungu kuadhibu uzao wa Daudi inazungumziwa kana kwamba Mungu atawapiga kiuhalisia. "na nitawaadhibu kwa sababu wametenda dhambi dhidi yangu"

Psalms 89:33

Sitaondoa upendo wangu thabiti kutoka kwake wale kutokuwa mwaminifu kwa ahadi yangu

"Daima nitampenda Daudi, na nitafanya nilichomwahidi"

maneno ya midomo yangu

Hapa "maneno" yanawakilisha alichosema. Pia "midomo" inawakilisha mdomo wote na mtu anayezungumza. "nilichosema"

Psalms 89:35

Nimeapa kwa utakatifu wangu

Yahwe anatumia utakatifu wake kama msingi wa kiapo chake. Hii ni njia ya kuhakikisha kuwa hakika atafanya alichoahidi kufanya.

na kiti chake cha enzi kitakuwa kama jua mbele yangu

"na kiti chake cha enzi kitaendelea kama jua mbele yake"

kiti chake cha enzi

Hapa "kiti cha enzi" kinawakilisha uwezo wa kutawala kama mfalme. Mungu anaahidi kuwa mmoja wa uzao wa Daudi daima atakuwa mfalme.

kama jua mbele yangu

Mungu anafananisha utawala wa Daudi kama mfalme na jua kusisitiza kuwa mtu kutoka uzao wa Daudi atatawala daima kama mfalme.

kitaimarishwa milele

Hapa kinachozungumziwa ni kiti cha enzi au uwezo wa kutawala kama mfalme. "nitakisababisha kudumu milele"

milele kama mwezi

Mungu anafananisha utawala wa Daudi kama mfalme na mwezi kusisitiza kuwa mtu kutoka uzao wa Daudi atatawala daima kama mfalme.

mwezi, shahidi wa uaminifu wa angani

Mwezi unazungumziwa kana kwamba ni mtu anayeshuhudia Mungu akifanya ahadi yake kwa Daudi. "mwezi, ambao ni kama shahidi mwaminifu aliye angani"

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.

Psalms 89:38

umekatata na kutupa

"umemkataa na kumtupa mfalme"

na mfalme wako mtiwa mafuta

"na mfalme uliye mchagua"

Umekanusha agano la mtumishi wako

"Umelikataa agano"

umetia najisi taji lake ardhini

Kusukuma ardhini au mavumbini ni ishara ya aibu kubwa. "umetia najisi taji lake ardhini" au "Umesababisha taji lake kuanguka mavumbini"

taji lake

Hii inawakilishwa uwezo wa mfalme kama mfalme na haki yake ya kutawala.

Umevunja chini kuta zake zote. Umeharibu ngome zake

Hii inadokeza kuwa Mungu aliwaruhusu adui zake kuangamiza ulinzi wa Yerusalemu. "Umewaruhusu adui kuvunja chini kuta na kuharibu ngome katika Yerusalemu"

Psalms 89:41

kwa majirani zake

Hapa "majirani" inamaanisha watu mataifa ya karibu.

Umeinua mkono wa kuume wa adui zake

Hapa "mkono wa kuume" unawakilisha uwezo. "Kuinua mkono wa kuume" inamaanisha kuwa Yahwe aliwafanya adui zake kuwa na nguvu ya kutosha ya kumshinda mfalme aliye chaguliwa na Mungu.

geuza nyuma makali ya upanga wake

Hapa "upanga" unawakilisha nguvu ya mfalme vitani. Kugeuza upanga inawakilisha kumfanya mfalme kushindwa kushinda vitani.

makali ya upanga wake

Hapa "makali" inawakilisha upanga wote. "upanga wake"

hujamfanya asimame wakati akiwa vitani

Hapa "asimame" inawakilisha kuwa mshindi vitani. "Hujamsaidia kuwa mshindi vitani"

Psalms 89:44

umeleta chini kiti chakecha enzi hadi ardhini

Hapa "kiti cha enzi" kinawakilisha uwezo wa kutawala kama mfalme. "wewe, Yahwe, umemaliza utawala wake kama mfalme"

Umefupisha siku zake za ujana

Hii ni njia ya kusema Mungu alimfanya mfalme kuonekana mzee wakati alikuwa bado ni kijana. "Hata wakati bado ni kijana umemfanya kuwa mnyonge kama mzee"

umemfunika na aibu

Yahwe kumwaibisha kabisa mfalme inazungumziwa kana kwamba aibu ni vazi ambalo Mungu alitumia kumfunika mfalme.

Psalms 89:46

Hadi lini, Yahwe? Utajificha, milele?

Mwandishi anatumia maswali haya kusisitiza kuwa hataki Mungu aendelee kumkataa mfalme. "Tafadhali, Yahwe, usikatae kumsaidia mfalme milele."

Utajificha

Mungu kutomsaidia mfalme inazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa anajificha kwake. "Je! Utakataa kumsaidia mfalme"

Hadi lini hasira yako itawaka kama moto?

Mwandishi anatumia swali kusisitiza kuwa hataki Mungu aendelee kubaki na hasira. "Tafadhali usiendelee kuwa na hasira"

hasira yako itawaka kama moto

Mungu kuwa na hasira sana inazungumziwa kana kwamba hasira yake ilikuwa moto mkali.

kwa ubatili gani umewaumba watoto wote wa mwanadamu

"kwamba umewaumba watu wote kufa kibatili"

watoto wote wa mwanadamu

Hii inamaanisha wanadamu kwa ujumla. "wanadamu" au "watu"

Nani anaweza kuishi na asife, au kuokoa maisha yake mwenyewe kutoka katika mkono wa kuzimu?

Mwandishi anatumia maswali haya kusisitiza kuwa watu wote watakufa. "Hakuna mtu anayeweza kuishi milele au kujifufua baada ya kufa"

kuokoa maisha yake mwenyewe kutoka katika mkono wa kuzimu

Hapa "mkono" unamaanisha uwezo. Mwandishi anazungumzia kuzimu kana kwamba ni mtu aliye na nguvu juu ya wale waliokufa. Maana zinazowezekana ni 1) mtu hawezi kujifufua baada ya kufa au 2) mtu hawezi kujizuia kufa.

Psalms 89:49

Bwana, yako wapi matendo yako ya kale ya uaminifu wako wa agano ulioahidi kwa Daudi katika ukweli wako?

Mwandishi anatumia swali kumwomba Bwana kuwa mwaminifu kwa agano lake na Daudi. "Bwana, kuwa mwaminifu kwa agano lako na Daudi kama ulivyokuwa kipindi cha nyuma"

Ita akilini

Mwandishi anamwomba Mungu kuleta hili katika kumbukumbu yake. "Kumbuka" au "Zingatia"

kejeli iliyolengwa kwa watumishi wako

Hapa "watumishi wako" inamaanisha watu wa Israeli. "jinsi wanavyotukejeli, watumishi wako"

jinsi ninavyobeba moyoni mwangu matusi mengi sana kutoka kwa mataifa

Hapa "moyo" unawakilisha hisia za mtu. "Ninavumilia matusi mengi sana kutoka kwa watu wa mataifa" au " Ninateseka kwa sababu watu wa mataifa wananitukana"

kutoka kwa mataifa

Hapa "mataifa" inawakilisha watu wa mataifa.

Adui zako wanatupa matusi

Adui kupiga kelele za matusi kwa mfalme inazungumziwa kana kwamba matusi ni kitu ambacho adui wanamtupia mfalme kwa nguvu.

wanakejeli hatua za watiwa mafuta wako

Hapa "hatua" inawakilisha pale ambapo mfalme anaenda. "wanamkejeli mtiwa mafuta wako popote aendapo"

Psalms 89:52

Taarifa ya Jumla:

Mstari huu ni zaidi ya mwisho wa zaburi hii. Ni kauli ya kufunga ya kitabu kizima cha 3 cha Zaburi, ambacho kinaanza katika Zaburi 73 na kuishia na Zaburi 89.

Abarikiwe Yahwe milele

"Watu wamsifu Yahwe milele"

Amina na Amina

Neno "Amina" linarudiwa kusisitiza kukubali kilichosemwa.

Psalms 90

Psalms 90:1

Taarifa ya Jumala:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Ombi la Musa

"Hili ni ombi ambalo Musa aliandika"

Bwana, umekuwa kimbilio letu

Mungu kuwalinda watu wake inazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa kimbilio au kivuli. "Bwana, umekuwa kama kivuli kwa ajili yetu"

katika vizazi vyote

"daima"

Kabla milima haijaumbwa

"Kabla hujaumba milima"

umbwa

"tengeneza"

dunia

Hii inawakilisha kila kitu kilichomo duniani.

kutoka milele hadi milele

Msemo huu unawakilisha muda wote wa zamani, wa sasa, na wa baadaye.

Psalms 90:3

Unamrudisha mtu mavumbini

Hii inadokezwa kuwa kama jinsi Mungu alivyoumba binadamu wa kwanza, Adamu, kutoka mavumbini, Mungu atasababisha miili ya watu kurudi mavumbini baada ya kufa. "Unawarudisha watu kwenye mavumbi wanapokufa"

Unamrudisha mtu

Hapa "mtu" inamaanisha watu kwa ujumla.

Rudini, nyie uzao

"Rudini mavumbini, nyie uzao" au "Rudini kwenye mchanga, nyie uzao"

nyie uzao wa wanadamu

Hii ni njia ya kumaanisha watu kwa ujumla. "nyie wanadamu" au "nyie watu"

Kwa kuwa miaka elfu moja machoni pako ni kama siku ya jana inavyopita, na kama kesha la usiku

Mwandishi anamaanisha kuwa kipindi kirefu cha muda kinaonekana kama kipindi kifupi kwa Mungu. "Unaona miaka elfu moja sawa na siku moja ya nyuma, au kama masaa machache ya usiku" au "Hata miaka elfu moja sio muda mrefu kwako"

miaka elfu moja

"miaka 1,000"

machoni pako

Hapa "machoni" inawakilisha mawazo. "kwako"

Psalms 90:5

Unawafagia kama na mafuriko wanapolala

Mungu kuwasababisha watu kufa kabla inazungumziwa kana kwamba aliwafagia na mfagio. Kufagia huku pia kunazungumziwa kana kwamba ni mafuriko yaliyowabeba watu. "Bwana, unawaangamiza watu kama na mafuriko na wanakufa"

wanapolala

Hii ni jia ya ya ustarabu ya kuzungumzia watu kufa.

asubuhi ni kama nyasi ... jioni linanyauka na kukauka

Watu wanafananishwa na nyasi kusisitiza kuwa watu hawaishi muda mrefu sana.

linachanua na kuota

Misemo hii miwli inamaanisha jinsi nyasi zinavyoota. "linaanza kuota na kukua"

linanyauka na kukauka

Misemo hii miwili inamaanisha jinsi nyasi zinavyokufa. "linafifia na kukauka"

Psalms 90:7

tumemezwa katika hasira yako

Mungu kuwaangamiza watu katika hasira yake inazungumziwa kana kwamba hasira ya Mungu ni moto unaowaunguza kabisa watu. "Unatuangamiza katika hasira yako"

na katika gadhabuyako tunaogopa

"na unapokasirika tunaogopa sana"

Umeweka udhalimu wetumbele zako, dhambi zetu zilizofichwa katika nuru ya uwepo wako

Mungu kuzingatia dhambi za watu inazungumziwa kana kwamba dhambi ni vitu anavyoweza kuweka mbele yake na kuzitazama. "Unaona kila kitu kiovu tunachofanya, hata vitu vya dhambi tunavyofanya sirini"

Psalms 90:9

Maisha yetu yanapita chini ya gadhabu yako

"Maisha yetu yanafika mwisho kwa sababu ya gadhabu yako"

kama kite

Mwandishi anafananisha maisha ya mtu na kite kusisitiza kuwa maisha ni mafupi sana.

sabini

"70"

themanini

"80"

hata miaka yetu mizuri yana alama ya taabu na huzuni

"Hata katika miaka yetu mizuri tunapitia taabu na huzuni"

tunapaa

Hii ni njia ya ustaarabu ya kusema watu wanaokufa.

Psalms 90:11

Nani ajuaye ukali wa hasira yako, na gadhabu yako ambayo inalingana na kukucha wewe?

Mwandishi anatumia swali kusisitiza kuwa hakuna mtu aliyepitia kikamilifu hasira ya Mungu. Kwa hiyo hakuna mtu anayemheshimu Mungu na kuogopa hasira yake watu wanapotenda dhambi. "Hakuna mtu anayejua ukali wa hasira yako. Kwa hiyo hakuna mtu anayeogopa gadhabu yako wanapotenda dhambi."

Geuka, Yahwe! Hadi lini?

Kumwomba Yahwe kutokuwa na hasira tena inazungumziwa kana kwamba mwandishi anataka Mungu ageuke kimwili kutoka katika hasira yake. "Yahwe, tafadhali usiwe na hasira na sisi tena'

Hadi lini?

Mwandishi anatumia swali kueleza kuwa anataka Mungu aache kuwa na hasira.

Kuwa na huruma kwa watumishi wako

Hapa "watumishi wako" inamaanisha watu wa Israeli. "Kuwa na huruma kwetu, watumishi wako"

Psalms 90:14

Turidhishe asubuhi

"Turudhishe kila asubuhi"

na uaminifu wako wa agano

"kwa kuwa mwaminifu kwa sababu ya agano lako na sisi"

kwa kulingana na siku ulizotutesa na kwa miaka tuliyopitia taabu

Misemo yote hii miwili inamaanisha kitu kimoja. Mwandishi anamwomba Yahwe kuwafanya kuwa na furaha kwa kisai kile kile cha muda alichowaadhibu. "kwa kiasi sawa cha muda ulichotuumiza na kutusababisha kuteseka"

Acha watumishi wako

Hapa "watumishi wako" inamaanisha watu wa Israeli. "Acha sisi, watumishi wako" au "Acha sisi"

acha watoto wako

Hapa "watoto" inamaanisha watoto na uzao.

waone fahari yako

"waone mambo makuu unayoyafanya"

Psalms 90:17

Na fadhila ya Bwana Mungu wetu iwe yetu

"Na Bwana Mungu wetu awe na huruma kwetu"

fanikisha kazi ya mikono yetu

Hapa "mikono" inawakilisha mtu mzima. "tusababishe tufanikiwe"

Psalms 91

Psalms 91:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Yeye anayeishi ... atabaki ... ya Mwenyezi

"Aliye juu, Mwenyezi, atawajali wote wanaoishi mahali anapoweza kuwalinda"

anayeishi katika kivuli cha Aliye juu

Neno "kivuli" ni sitiari ya ulinzi. "anayeishi mahali ambapo Aliye juu humlinda"

Aliye juu

Maneno "Aliye juu" yanamaanisha Yahwe.

atabaki katika kivuli cha Mwenyezi

Neno "kivuli" hapa ni sitiari ya ulinzi. "atabaki mahali ambapo Mwenyezi anaweza kumlinda"

Mwenyezi

yule mwenye uwezo na mamlaka juu ya kila kitu

Nitasema ya Yahwe

"Nitasema kumhusu Yahwe"

kimbilio lnagu na ngome yangu

"Kimbilio" ni sehemu ambapo mtu anaweza kwenda na kuwa na mtu au kitu kinachomlinda. "Ngome" ni kitu ambacho watu hutengeneza ili wajilinde wao na mali zao. Asafu anayatumia hapa kama sitiari ya ulinzi. "yule ambaye ninaweza kwenda kwake na atanilinda"

Psalms 91:3

Kwa kuwa atakuokoa kutoka katika mtego wa mwindaji na kutoka katika tauni hatari

"Kwa kuwa Mungu atakuokoa kutoka katika mtego wa mwindaji na atakuokoa kutoka katika tauni zinazoweza kuua"

mtego wa mwindaji

"kutoka katika mtego ambao mwindaji aliweka kukushika"

Atakufunika kwa mbawa zake, na chini ya mbawa zake utapata kimbilio

Ulinzi wa Mungu hapa unazungumziwa kama "mbawa" ambazo ndege hutumia kufunika makinda yake dhidi ya hatari. "Atakufunika na mbwa zake" na "chini ya mbawa zake" zina maana moja. "Atakuweka salama na atakulinda"

Uaminifu wake ni ngao na ulinzi

Uaminifu wa Mungu hapa unazungumziwa kama "ngao" ambayo inaweza kuwalinda watu wanaomtegemea. "Unaweza kumtumaini akulinde"

ulinzi

Hakuna mtu anayejua kwa uhakika maana ya neno hili. Maana zinazowezekana ni 1) ngao ndogo iliyofungwa kwenye mkono wa askari inayotumika kujilinda dhidi ya mishale na panga au 2) ukuta wa mawe uliowekwa katika duara ambayo askari wanaweza kujificha na kupiga mishale.

Psalms 91:5

hofu wakati wa usiku

Mwandishi anazungumzia "hofu" kana kwamba ni roho au mnyama mkali ambaye anaweza kushambulia usiku na kuwatisha watu. "vitu vitakushambulia usiku"

wakati wa usiku ... mchana

Misemo hii miwli imewekwa pamoja kumaanisha nyakati zote zinazowezekana za usiku na mchana.

mshale unaopaa mchana

"Mshale" ni njia nyingine ya kusema watu wanaopiga mishale. "watu wanao kushambulia kwa mishale mchana"

au tauni inayozurura

Mwandishi wa zaburi anazungumzia ugonjwa kana kwamba ni mtu aliyetoka usiku na kuua watu wengine. "Hautaogopa kufa kutokana na ugonjwa"

inayozurura

anayeenda popote atakapoa kwenda na wakati wowote

gizani ... mchana

Misemo hii miwli imewekwa pamoja kumaanisha nyakati zote zinazowezekana za usiku na mchana.

ugonjwa

ugonjwa unaowafanya watu kuuguwa kwa wakati mmoja

Watu elfu wanaweza kuanguka katika upande wako na elfu kumi katika mkono wako wa kuume

"Watu wengi wanaweza kuanguka pembeni yetu."

haitakufikia

"uovu hauta kudhuru"

Psalms 91:8

Utatazama na kuona

"Wewe mwenyewe hautateseka, lakini utatazama kwa makini, na utaona"

adhabu ya waovu

"jinsi Mungu anvyowaadhibu waovu"

Yahwe ni kimbilio langu

"Yahwe ndiye ninayemfuata ninapohitaji mtu wa kunilinda"

Mfanye Aliye juu kimbilio lako pia

"Unapaswa kumfanya Aliye juu awe kimbilio lako pia." Mwandishi anaacha kuzungumza na Mungu na anaanza kuzungumza na msomaji.

Psalms 91:10

Hakuna uovu utakaokupita

"Hakuna kitu kiovu kitakachotokea kwako"

hakuna mateso yatakayo kuja karibu na nyumba yako

Mwandishi anawazungumzia watu wanaowatesa wengine kana kwamba walikuwa ndio madhara waliyoyasababisha. "hakuna mtu atakayeweza kudhuru familia yako"

Kwa kuwa atawaongoza

"Yahwe ataamuru"

katika njia zako zote

Mwandishi anazungumzia jinsi mtu anavyoishi kana kwamba ni njia ambayo mtu alitembea. "katika kila kitu unachofanya" au "wakati wote'

Psalms 91:12

Watakuinua

"Malaika wa Yahwe watakuinua"

hautajikwaa mguu wako kwenye jiwe

Malaika hawatalinda mguu wa msomaji pekee bali na mwili wake mzima. "hautaogonga mguu wako kwenye jiwe" au "hakuna kitu kibaya kitakachotokea kwako"

Utawaponda simba na vifutu chini ya miguu yako; utakanyaga juu ya simba wadogo na nyoka

Ambapo "atajikwaa mguu wako kwenye jiwe" ni tatizo dogo, simba na nyoka ni mnifano ya hatari kubwa. Mwandishi anazungumzia zimba na nyoka kana kwamba walikuwa ni wadogo ya kutosha kukanyagwa chini ya mguu wa mtu. "Utaweza kuwaua simba na nyoka kana kwamba ni wanyama wadogo ambao unaweza kuwakanyaga chini ya miguu yako"

vifutu

aina ya nyoka wenye sumu.

kanyaga

kuponda kwa kutembea kwa nguvu

Psalms 91:14

Kwa sabau amejitoa kwangu

"Kwa sababu ananipenda mimi"

Nitakuwa naye katika taabu

"Nitakuwa naye wakati yuko katika taabu"

nitampa ushindi

"nitamwezesha kuwashinda adui zake"

nitamridhisha na maisha marefu

Mwandishi anazungumzia maisha kana kwamba ni kitu ambacho mtu anaweza kula. Nitamruhusu kuishi maisha marefu na yenye furaha"

na kumwonesha wokovu wangu

"na nitamwonesha wokovu wangu." Mwandishi wa zaburi anazungumzia kazi ambayo Mungu hufanya kuwaokoa watu kana kwamba ni kitu chenye umbo. "Nitamwokoa ili ajue kuwa mimi ndiye niliyemwokoa"

Psalms 92

Psalms 92:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

kuimba sifa kwa jina lako

Maneno "jina lako" ni njia nyingine ya kusema "wewe." "kuimba sifa kwako"

kutangaza uaminifu wako wa agano

"kuwaambia watu kuwa wewe ni mwaminifu kutunza agano alko"

ukweli wako

"kuwa kila kitu unachosema ni kweli"

Psalms 92:4

furaha

furaha"

kupitia matendo yako

"kwa kile ulichofanya"

matendo ya mikono yako

Neno "mikono" ni njia nyingine ya kumaanisha mtu mzima. "Kile ulichofanya"

matendo yako

"kile ulichofanya"

Mawazo yako ni marefu sana

"Hatuwezi kuelewa unachopanga kufanya hadi ukifanye"

Mawazo yako

"Unachowaza" au "Unachopanga"

Psalms 92:6

katili

"mwenye vurugu na mjinga"

Wakati waovu wanpochipuka kama nyasi

Hii inafananisha watu waovu na nyasi, ambayo huota upesi na sehemu nyingi. "Wakati watu waovu wanapotokea haraka na kuonekana kuwa kila sehemu, kama nyasi"

wamehukumiwa kwa kuangamizwa milele

"Mungu ameamua kuwa atawaangamiza kabisa"

Psalms 92:8

Hakika, watazame adui zako, Yahwe

Maandishi mengi hayana maneno haya.

Wataangamia

"Watakufa" au "Utawaua"

Wale wote wanaofanya maovu watatawanywa

"utawatawanya wote wanaofanya uovu"

watatawanywa

Maandishi mengi yameandikwa, "wametawanywa."

watatawanywa

"wataondolewa"

Psalms 92:10

Umeinua pembe langu kama pembe la nyati

Mwandishi wa zaburi anamzungumzia Mungu kana kwamba Mungu amemfanya kuwa na nguvu kama mnyama wa porini. "Umenifanya kuwa na nguvu kama nyati"

Umeinua ... pembe

"Umenifanya kuwa na nguvu"

Nimetiwa mafuta na mafuta mapya

Maana zinazowezekana ni kwamba mafuta ambayo Mungu ameweka juu ya mwandishi wa zaburi ni sitiari ya Mungu 1) kufanya kuwa mwenye furaha, "umenifanya kuwa na furaha sana" au 2) kumfanya kuwa na nguvu, "umenifanya kuwa na nguvu" au 3) kumwezesha kuwashinda adui zake, "umeniwezesha kuwashinda adui zangu."

Macho yangu yameona anguko la adui zangu; masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu

Maneno "macho" na "masikio" ni njia nyingine ya kumaanisha mtu anayesikia na kuona. "Nimeona na kusikia kuhusu kushindwa kwa adui zangu waovu"

Psalms 92:12

Wenye haki watastawi kama mtende

Maana zinazowezekana ni kwamba watu wenye haki watakuwa kama mtende wenye afya kwa sababu 1) watakuwa imara au 2) wataishi muda mrefu.

wataota kama mti wa seda ya Lebanoni

Maana zinazowezekana no kwamba watu wenye haki watakuwa kama mti wa seda unaoota katika nchi ya Lebanoni kwa sababu 1) watakuwa imara au 2) watu watawaheshimu.

Wamepandwa

"Yahwe amewapanda" au "Yahwe anawatunza kana kwamba ni miti aliyoipanda"

katika nyumba ya Yahwe ... katika nyua za Mungu wetu

Mwandishi wa zaburi anawazungumzia watu wanaomwabudu Mungu kwa ukweli kana kwamba walikuwa miti inayoota katika nyumba ya Yahwe.

wanastawi

Mwandishi wa zaburi anawazungumzia watu wenye haki kana kwamba ni miti yenye afya. "wanakua vizuri" au "wana nguvu sana"

katika nyua za Mungu wetu

katika baraza la hekalu Yerusalemu.

Psalms 92:14

Wanazaa matunda

Mwandishi anawazungumzia watu wenye haki kana kwamba walikuwa miti ambayo inatoa matunda. "Wanampendeza Mungu"

wanabaki na ubichi na kijani

Mwandishi anawazungumzia watu wenye haki kana kwamba walikuwa miti. "wanabaki imara na wenye afya" au "huwa wanafanya kinachompendeza Mungu"

kijani, kutangaza kwamba

Maana zinazowezekana ni 1) kijani, ili watangaze" au 2) "kijani. Hii inaonesha kwamba"

Yeye ni mwamba wangu

"Yahwe ndiye anayenilinda." Mwandishi wa zaburi anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni mwamba ambao utamlinda.

Psalms 93

Psalms 93:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

amevikwa na adhama; Yahwe amemvika na kujifunga na nguvu

Mwandishi wa zaburi anazungumzia nguvu ya Yahwe na adhama yake kana kwamba vilikuwa vitu ambavyo Yahwe alivaa. "anawaonesha wote kuwa ni mfalme mwenye uwezo" au "adhama yake ipo kwa ajili ya kila mtu kuona, kama joho ambalo mfalme huvaa; kila kitu kumhusu Yahwe kinaonesha kuwa ana nguvu na yuko tayari kufanya kazi kubwa"

adhama

uwezo wa mfalme na jinsi mfalme anavyotenda

kujifunga

kufunga mshipi — ukanda wa ngozi au kitu kingine ambacho mtu huvaa kiunoni — kujianda kwa ajili ya kazi au mapambano

Dunia imewekwa imara

Hii inaweza kuelezwa kwatika hali ya kutenda. "Umeiweka imara dunia"

haiwezi kusogezwa

Hii inaweza kuelezwa kwatika hali ya kutenda. "hakuna atakaye isogeza"

Kiti chako cha enzi kimewekwa tangu nyakati za kale

Hii inaweza kuelezwa kwatika hali ya kutenda. "Ulikiweka kiti chako cha enzi tangu nyakati za kale"

wewe ni tangu milele

"ulikuwepo siku zote"

Psalms 93:3

bahari ... bahari

Tafsiri zingine zinasoma "mafuriko ... mafuriko." Neno hili mara nyingi humaanisha mto, lakini "bahari ... bahari" limechaguliwa hapa kwa sababu mabahari, na sio mito, huwa ina "mawimbi" yenye "kishindo na kuunguruma."

zimeinua sauti zao; mawimbi ya bahari ya kishindo na kuunguruma

Mwandishi wa zaburi anazungumzia bahari kana kwamba ni mtu anayeweza kuzungumza. "zimefanya sauti kuu kwa sababu mawimbo yao yana kishindo na kuunguruma"

kuunguruma

kupaza sauti ndefu ya kelele.

Juu ya vishindo vya mawimbi mengi, mawimbi makubwa yaumkayo ya bahari

Msemo huu "wavunjaji wakuu wa bahari" inamaana moja na "mawimbi mengi" na inasisitiza jinsi mawimbi yalivyo. "Juu ya vishindo vya mawimbi makubwa ya baharini"

mawimbi makubwa yaumkayo

mawimbi makubwa yajayo kwenye nchi

Aliye juu

Mwandishi wa zaburi anazungumzia mahali anapoishi Mungu kana kwamba palikuwa juu ya nchi. "mbinguni"

Psalms 93:5

makini

kuwa wa dhati

ni zakuaminika sana

"daima zinabaki hivyo hivyo" au "hazibadiliki"

utakatifu unapamba nyumba yako

Mwandishi wa zaburi anazungumzia nyumba ya Yahwe kana kwamba ilikuwa ni mwanamke aliyevaa nguo nzuri au mapambo ya vito na utakatifu wa Yahwe kama zile nguo nzuri na mapambo ya vito. "nyumba yako ni nzuri kwa sababu wewe ni mtakatifu" au "utakatifu wako unaifanya nyumba yako kuwa nzuri kama nguo nzuri na mapambo ya vito yanavyomfanya mwanamke kuwa mzuri zaidi"

nyumba yako

hekalu liliko Yerusalemu

unapamba

unafanya kuwa nzuri

Psalms 94

Psalms 94:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

ng'aa juu yetu

"jioneshe" au "dhihirisha hukumu yako"

Inuka, mwamuzi wa ulimwengu, wape walio na kiburi wanachostahili

"Njoo, mwamuzi wa ulimwengu, na uwaadhibu wenye kiburi"

Inuka

Mwandishi wa zaburi anazungumzia kuanza kufanya kitu kama kuinuka. "Chukua hatua" au "Fanya kitu"

Psalms 94:3

Hadi lini waovu, Yahwe, hadi lini waovu watashangilia?

Mwandishi wa zaburi anarudia wali kuonesha kuwa hana furaha na muda ambao Yahwe amewaruhusu waovu washangilie. "Umesubiri muda mrefu sana Yahwe; umesubiri muda mrefu sana kuwazuia waovu kushangilia."

waovu watashangilia

"Je! Waovu watashangilia kwa sababu huwaadhibu kwa matendo maovu wanayofanya"

Wanamwaga

"Wale wote wanaofanya uovu wanamwaga"

Wanamwaga nje maneno yao kiburi

Mwandishi wa zaburi anaandika kuhusu waovu kuzungumza kana kwamba maneno yao yalikuwa kimiminiko kinachomwagwa nje.

wale wote wanaofanya majivuno ya uovu

"Wale wote wanaofanya uovu wanajisifu juu ya matendo yao ya uovu na tabia zao"

Psalms 94:5

wanalitesa taifa

Hapa "taifa" linamaanisha watu wa hilo taifa. "wanawatesa watu wa taifa"

Wanawaponda

Mwandishi anawazungumzia watu wenye uwezo kuwatenda vibaya watu wanyonge kana kwamba ilikuwa kuwaponda au kuwabomoa katika vipande. "Wanawaangamiza kabisa" au "Wanawadhuru sana."

mjane

"wanawake ambao waume zao wamekufa"

wasio na baba

"watoto bila baba"

Mungu wa Yakobo hagundui

"Mungu wa Israeli haoni tunachokifanya"

Psalms 94:8

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi sasa anawaeleza watu waovu.

mtajifunza lini?

Swali hili la balagha linasisitiza hasira ya mwandishi na watu waovu anaozungumza nao. "acheni jia zenu za kipumbavu!" au "jifunzeni kutoka katika makosa yenu!"

Yeye aliyeumba sikio, je hasikii? Yeye aliyeumba jicho, hauoni?

Maswali haya balagha "Mungu aliumba masikio, kwa hiyo anaweza kusikia. Mungu aliumba macho, kwa hiyo anaweza kuona." au "Mungu aliumba masikio, kwa hiyo acheni kujifanya kana kwamba hasikii. Mungu aliumba macho, kwa hiyo acheni kujifanya kana kwamba haoni."

Psalms 94:10

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea kuwaeleza watu waovu.

Yeye anayeyaadibu mataifa, je harekebishi?

Inadokezwa kuwa yahwe anawarekebisha watu wake. "Mnajua kuwa Yahwe huyarekebisha mataifa, kwa hiyo kuweni na uhakika kuwa atawarekebisha watu wake" au "atawaadhibu watu wake"

je harekebishi

Maana zinazowezekana ni 1) Mungu hurekebisha. "hurekebisha" au 2) Mungu huadhibu. "huadhibu"

kuwa ni mvuke

Hapa mawazo ya watu yanalinganishwa na mvuke unaopotea hewani. Hii ni sitiari inayoonesha jinsi wasivyo wa muhimu na wasivyo na faida.

mvuke

"umande"

Psalms 94:12

Taarifa ya Jumla:

Sasa mwandishi anazungumza na Yahwe tena.

hadi shimo lichimbwe kwa ajili ya waovu

Mwandishi anazungumzia yahwe kuwaadhibu waovu kana kwamba Yahwe anamtega mnyama shimoni. "hadi uchimbe shimo kwa ajili ya waovu" au "hadi uwaangamize waovu"

Psalms 94:14

urithi wake

"wale alio wachagua kuwa naye milele"

hukumu itakuwa ya haki tena

Mwandishi anawazungumzia wale wanaohukumu kana kwamba walikuwa ndiyo maamuzi wanayoyafanya. "waamuzi watahukumu tena kwa haki" au "waamuzi watafanya tena maamuzi ya haki"

wanyofu wa moyo

"wale ambao mioyo yao iko sawa na Mungu"

wanafuata

"watataka waamuzi wahukumu kwa haki"

Nani atainuka kunitetea mimi dhidi ya watenda maovu? Nani atasimama kwa ajili yangu dhi ya waovu

"Hakuna mtu atakaye nitetea dhidi ya watenda maovu. Hakuna mtu atakaye nisaidia kupigana dhidi ya waovu"

waovu

"watu waovu"

Psalms 94:17

Kama Yahwe asingekuwa msaada wangu ... ukimya

Hii ni hali ya kubuni. Yahwe alimsaidia, kwa hiyo hakuwa amelala katika sehemu ya ukimya.

Kama Yahwe asingekuwa msaada wangu

"Kama Yahwe asingenisaidia"

ningekuwa nimelala chini hivi punde kwenye sehemu ya ukimya

Hapa" ningekuwa nimelala chini" inamaanisha "mauti" na "sehemu ya ukimya" inamaanisha "kaburi." "katika muda mfupi, nitakuwa nimekufa, nikiwa nimelala kaburini"

Wasiwasi ndani yangu ukiwa mwingi, faraja zako hunifurahisha

Mwandishi anazungumzia wasiwasi kana kwamba anaweza kuhesabu kwa kutenganisha wasiwasi. "Ninapokuwa na wasiwasi kuhusu mambo mengi, umenifariji na kunifanya kuwa na furaha"

Psalms 94:20

Je! Kiti cha enzi cha uharibifu kinaweza kushirikiana na wewe, yule anayetengeneza udhalime kwa amri

Hili ni swali la balagha linalotumika kueleza wazo. "Linaweza kuelezwa kama kauli. "Mtawala mwovu anayeunda sheria zisizo za haki sio rafiki yako"

Kiti cha enzi cha uharibifu

Hapa "kiti cha enzi" kinawakilisha mfalme au mtawala. "mtawala mwovu" au "mwamuzi mwovu"

Wanapanga njama

kufanya mpango wa siri na mtu wa madhara au kitu kisicho halali

kuchukua maisha ya

Hii ni lahaja inayomaanisha kumuua mtu.

Psalms 94:22

Yahwe amekuwa mnara wangu wa juu

Hapa "mnara" ni sitiari ya ulinzi. "Yahwe amenilinda dhidi ya adui zangu"

Mungu amekuwa mwamba wangu na ngome yangu

Mwandishi anazungumzia Mungu kumlinda kana kwamba Mungu ni sehemu ambayo mwandishi wa zaburi anaweza kwenda ili kuwa salama. "Nimemwomba Mungu kunilinda, na ameniweka salama kwa uwezo wake"

Atawaletea juu yao udhalimu wao wenyewe

Maana zinazowezekana ni 1) "Atawafanyia vitu viovu walivyowafanyia wengine" au 2) "Atawaadhibu kwa matendo maovu yote aliyowatendea wengine."

atawakata

Hii ni lahaja inayomaanisha "atawaua"

katika uovu wao wenyewe

Maana zinazowezekana ni 1) "wakati wanafanya mambo maovu" au 2) "kwa sababu wamefanya mambo maovu."

Psalms 95

Psalms 95:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

mwamba wa wokovu wangu

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni mlima ambao watu wanaweza kupanda ili wawe salama. "mwamba ambao tunaweza kwenda na Mungu atatuokoa."

tuingie katika uwepo wake

Mwandishi anazungumza kana kwamba anawaambia wasomaji kwenda katika chumba cha enzi cha mfalme. "nenda mahali alipo"

kwa shukrani

"kwa kumshukuru tunapoingia katika uwepo wake"

mkuu kwa miungu yote

Maana zinazowezekana ni kwamba Yahwe ni mfalme mkuu 1) "ambaye anatawala juu ya miungu wengine yote," au 2) "ambaye ni bora zaidi ya miungu wengine yote."

Psalms 95:4

Katika mikono yake

Hii ni lahaja inayomaanisha "katika miliki yake" au "anawajibika kwa ajili ya."

vina

sehemu za vina virefu

vinara

sehemu za juu

mikono yake iliunda

Neno "mijono" ni njia nyingine ya kusema Yahwe mwenyewe. "yeye mwenyewe aliunda"

Psalms 95:6

tupige magoti

kuweka magoti yote ardhini, mara nyingi kuonesha unyenyekevu

watu wa malisho yake

Neno "malisho" ni njia nyingine ya kusema chakula ambacho watu wanakula katika malisho, ambayo pia inamaanisha kila kitu ambacho yahwe anatoa kwa ajili ya watu wake. "sisi ni watu ambaye huwa anatupa mahitaji yetu"

malisho

eneo ambalo wanyama hupata nyasi za kula

kondoo wa mkono wake

Neno "mkono" hapa linamaanisha jinsi Yahwe anavyowalinda watu wake kama mchungaji anavyowalinda kondoo wake. "watu ambao anawalinda kama mchungaji anavyowalinda kondoo wake"

Leo—o, kwamba usikie sauti yake!

"O, kwamba usikie sauti yake leo!" Mwandishi anajiingilia makusudi katika kile alichokuwa akikisema.

utasikia sauti yake

Hapa "sauti yake" inamaanisha kusikiliza kwa makini neno la Mungu. "msikilize kwa makini"

Psalms 95:8

Taarifa ya Jumla:

Sasa mwandishi anaandika maneno ambayo Yahwe alizungumza.

Usikaze moyo wako

"Usiwe msumbufu"

Meriba, ... Masa

Haya ni maeneo jangwani ambayo Musa aliyataja kwa sababu Waisraeli waliasi dhidi ya Mungu.

walinijaribu ... kunipima

Misemo hii miwili yote ni sitiari ya watu kuangalia ni kiasi gani cha uovu wanaweza kufanya kabla Mungu hajawaadhibu. Misemo hii inasema kitu kimoja na inaweza kuunganishwa. "walinijaribu" au "walitaka kuona kama wanaweza kufanya uovu bila ya adhabu yangu ... walinipima kama nitaendelea kuwa mvumilivu nao"

matendo yangu

"vitu vya ajabu nilivyofanya"

Psalms 95:10

Taarifa ya Jumla:

Yahwe anaendelea kuzungumza moja kwa moja na watu wake.

miaka arobaini

"miaka 40"

kizazi hicho

"watu hao wote" au "kizazi hicho chote cha watu"

zurura pembeni

Mungu anawazungumzia watu kana kwamba ni kondoo ambao wataenda popote wanapotaka na hawatabaki karibu na mchungaji. "sogea mbali na mimi" au "kwenda njia yao wenyewe"

hawajajua njia zangu

"hawajanitii"

njia zangu

"jinsi ninavyotaka waishi"

sehemu yangu ya kupumzika

"sehemu ambayo ningewaruhusu wapumzike'

Psalms 96

Psalms 96:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo mpya

wimbo ambao hakuna mtu aliyewahi kuimba

dunia yote

Hii inamaanisha watu wa duniani. "nyie watu wote mnaoishi duniani"

barikini jina lake

neno "jina" linamaanisha Yahwe mwenyewe. "mbarikini Yahwe" au "fanya kinachomfanya Yahwe afurahi."

tangazeni wokovu wake

"tangazeni kwamba ametuokoa" au "waambie watu kuwa yeye ndiye aokoae"

Psalms 96:3

Tangazeni utukufu wake katika mataifa

"Waambie watu katika kila taifa kuhusu utukufu wake mkuu"

Yahwe ni mkuu na ni wakusifiwa sana

"Yahwe ni mkuu. Msifuni sana" au "Yahwe ni mkuu, na watu wanapaswa kumsifu sana"

Yeye ni wa kuogopwa zaidi ya miungu mingine yote

"Mcheni zaidi ya miungu mingine yote"

Psalms 96:5

katika uwepo wake

"ambapo alipo"

Uzuri na fahari ziko katika uwepo wako

Mwandishi anazungumza kana kwamba uzuri na fahari ni watu wanaoweza kusimama mbele ya mfalme. "Kila mtu anajua kuhusu uzuri wake na fahari"

Nguvu na uzuri ziko katika mahali pake patakatifu

Maneno "nguvu" na "uzuri" ni njia nyingine ya kusema agano la sanduku la amri, ambayo ipo katika mahali patakatifu. "Ni mahali pake patakatifu ambapo kuna sanduku la agano la amri"

Psalms 96:7

Mpeni Yahwe sifa ... mpeni Yahwe kwa utukufu wake na nguvu

"Msifuni Yahwe ... msifuni Yahwe kwa kuwa anautukufu na nguvu."

Mpeni Yahwe utukufu ambao jina lake linastahili

"Mpeni heshima Yahwe kama jina lake linavyostahili" au "Tangaza kuwa Yahwe ni mtukufu kama jina lake linavyostahili."

jina lake

"jina" linamaanisha Mungu. "yeye"

nyua zake

baraza la hekalu ambapo makuhani walitoa sadaka ya wanyama kwa Yahwe

Psalms 96:9

Yahwe mkiwa mmevaa mavazi yanayotukuza utakatifu wake

Mtu anapaswa kuvaa mavazi yanayoonesha kuwa anelewa kwamba Yahwe ni mtakatifu. "Yahwe, na vaeni nguo za kufaa kwa sababu yeye ni mtakatifu."

Tetemekeni

kutetemeka kwa sabau ya hofu

dunia yote

"watu wote wa duniani"

Dunia pia imethibitishwa

Alithibitisha pia dunia"

haiwezi kutikiswa

"hakuna kitu kinachoweza kuitikisa"

Psalms 96:11

Acha mbingu zifurahi, na dunia ishangilie

Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba "mbingu" na "dunia" zina hisia kama watu. "Acha iwe kana kwamba mbingu zimefurahi na dunia kushangilia" au 2) "Acha wale wanaoishi mbinguni wafurahi na wale wanaoishi duniani washangilie"

acha bahari liungurume na kile kinacholijaza kipige kelele ya furaha

"acha sauti iwe kama watu wengi wanamsifu Yahwe, na acha iwe kana kwamba wale wanaoishi baharini na kupiga kelele kwa furaha"

Acha mashamba yashangilie na vyote vilivyomo

"Acha mashamba na vyote vilivyomo vishangilie." Mwandishi anazungumza kana kwamba "mashamba" na wanyama wanaoishi humo wana hisia kama watu. "Acha iwe kana kwamba mashamba yenyewe na wanyama wote wanaoishi humo washangilie"

Kisha acha miti yote msituni ipige kelele

"Kisha miti yote msituni zitapiga kelele"

Anakuja kuhukumu dunia. Atahukumu dunia ... na watu

Misemo hii mitatu ina maana za kufanana; misemo miwili ya mwisho inatumika kuimarisha ule wa kwanza.

kuhukumu ... atahukumu

Maana nyingine inayowezekana ni "kutawala ... atatawala"

Ataihukumu dunia kwa haki yake

Hapa "dunia" inamaanisha watu wa duniani. "Atawahukumu watu wote wa dunia kwa haki."

watu kwa uaminifu wake

"atawahukumu watu kwa uaminifu wake"

kwa uaminifu wake

Maana zinazowezekana ni 1) "kwa usawa, kulingana na kile anachojua kuwa kweli" au 2) "kutumia kigezo kile kile kwa watu wote."

Psalms 97

Psalms 97:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

acha dunia ishangilie; acha fukwe nyingi zifurahi

Dunia na fukwe zinasemwa kuwa na hisia kama watu. "Shangilieni muwe na furaha kila mtu duniani na karibu na bahari"

fukwe

Maana zinazowezekana ni 1) "nchi karibu na bahari" au 2) "visiwa."

Mawingu na giza vinamzunguka

"Hatuwezi kumwona; ni kana kwamba alikuwa amekaa gizani na mawingu yamemzunguka"

Haki na hukumu ni msingi wa kiti chake cha enzi

Neno "kiti cha enzi" ni njia nyingine ya kusema matendo na maneno ya yule anayeketi hapo. Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba haki na hukumu ni vitu halisi vilivyopafanya kiti cha enzi kuwa imara. "Yeye ana haki katika kila kitu anachofanya" au "Anaweza kutawala kwa sababu anatawala kwa haki"

msingi wa kiti chake cha enzi

Hapa "msingi wa kiti chake cha enzi" unamaanisha jinsi Yahwe anavyotawala ufalme wake.

Psalms 97:3

Moto huenda mbele yake

Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba alikuwa ni mtu anayetembea mbele ya mfalme Yahwe na kuwaambia watu kuwa mfalme anakuja.

kuwameza adui zake

"anawaunguza adui zake"

dunia huona na kutetemeka

"dunia" inamaanisha watu wanaoishi duniani. "watu wa duniani wanaona na kutetemeka"

kutetemeka

"anatetemeka kwa uoga"

Milima inayeyuka kama nta mbele ya Yahwe

"Milima haiwezi kusimama wakati Yahwe anakuja karibu" au "Milima inaporomoka katika uwepo wa Yahwe"

Psalms 97:6

Anga zinatangaza haki yake

Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba anga ni wajumbe wa Yahwe wanaotangaza kuwa Yahwe ni wa haki. "Kila mtu anaweza kuona kuwa Mungu ni wa haki, kwa njia ilie ile ambayo wote wanaliona anga" au 2) anga inamaanisha viumbe vinavyoishi mbinguni. "Wale wote wanaoishi mbinguni wanatangaza kwamba Yahwe ni wa haki"

Wale wote wanaoabudu sanamu za kuchonga wataaibika, wale wanaojivunia katika sanamu zisizofaa

"Mungu atawaaibisha wale wote wanaojivunia katika sanamu zisizofaa na kuabudu sanamu za kuchonga"

Sayuni ikasikia ... miji ya Yuda

Hii inamaanisha watu wanaoishi katika nchi hizi. "Watu wa Sayuni walisikia ... watu wa Yuda"

Psalms 97:9

uko juu zaidi ya dunia yote

Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba wale wenye nguvu ya kutosha ya kutawala walikuwa juu zaidi kimwili zaidi ya wengine. "unatawala juu ya watu wote wanaoishi"

Umetukuzwajuu zaidi

Mwandishi anazungumza kana kwamba wale wenye nguvu ya kutosha ya kutawala walikuwa juu zaidi kimwili zaidi ya wengine. "Uko juu, mbali"

mkono wa mwovu

"nguvu ya waovu"

Nuru imepandwa kwa ajili ... na furaha kwa ajili ya

Misemo hii miwili ina maana za kufanana na inatumika pamoja kwa ajili ya kuweka mkazo. "Yahwe anapanda nuru kwa wale wanaofanya ya haki, na anapanda furaha kwa ajili ya wale wenye unyoofu wa mioyo"

Nuru imepandwa kwa ajili ya wenye haki

Neno "kupanda" ni sitiari ya matendo yenye matokeo ya mbeleni. "Nuru" ni sitiari ya vitu vizuri. "Yahwe anapanga vitu vizuri viwatokee watu wenye haki mbeleni"

wenye haki

"watu wenye haki"

na furaha kwa wale wenye mioyo ya uaminifu

"na furaha inapandwa kwa ajili ya wale wenye unyoofu wa mioyo." Neno "kupanda" ni sitiari ya matendo yenye matokeo ya mbeleni. "Yahwe anapanga kwa ajili ya watu wake wenye unyoofu wa mioyo kuwa na furaha siku za mbele"

wale wenye mioyo ya uaminifu

Moyo unamaanisha mtu mzima. "mtu mnyoofu"

Psalms 97:12

Taarifa ya Jumla:

Mstari huu una amri unaofuatwa na sababu ya amri hiyo. "Kwa sababu ya kile ambacho Yahwe amewafanyia, nyie watu wenye haki, kuweni na furaha na mpeni shukrani mnapokumbuka utakatifu wake"

Furahini katika Yahwe

"Furahini kwa sababu ya kile ambacho Yahwe amewatendea"

mnapokumbuka utakatifu wake

Maana zinazowezekana ni 1) "mnapokumbuka jinsi alivyo mtakatifu" au 2) "kwa jina lake tukufu," ni njia nyingine ya kusema "kwake."

Psalms 98

Psalms 98:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo mpya

wimbo ambao hakuna mtu amewahi kuimba.

mkono wake wa kuume na mkono wake mtakatifu umempa

Maneno "mkono wake wa kuume" na "mkono wake mtakatifu" zinamaanisha nguvu ya Yahwe. Pamoja zinasisitiza ukuu wa nguvu yake ulivyo. "uwezo wake mkuu sana umempa"

mkono wake wa kuume

mkono wenye nguvu na ujuzi zaidi

mkono wake mtakatifu

Hapa "mkono" ni sitiari ya uwezo. "uwezo ulio wake pekee"

umempa ushindi

Maana zinazowezekana ni 1) "kumwezesha kuwashinda adui zake" au 2) "kumwezesha kuwaokoa watu wake"

amefanya wokovu wake kujulikana

Nomini dhahania "wokovu" inaweza kutafsiriwa kwa kutumia kitenzi "oka." "amewaonesha watu kuwa huokoa watu wake"

ameonesha haki yake kwa mataifa yote

Neno "mataifa" ni njia nyingine ya kusema watu wanaoishi katika mataifa yote. "amewaonesha watu wanaoishi katika mataifa yote kuwa yeye ni wa haki"

Psalms 98:3

Anaitisha akilini

"anakumbuka"

mwisho wote wa dunia ... dunia yote

Hizi ni njia zingine za kusema watu wa duniani. "watu kutoka duniani kote .. watu wote duniani"

wataona utukufu wa Mungu wetu

Nomino dhahania inaweza kutafsiriwa na kitenzi "kushinda." "watamwona Mungu wetu akiwashinda adui zake"

pasukeni katika wimbo

"kuanza kuimba ghafla kwa furaha"

imbeni kwa furaha

"imbeni kwa sababu mnafuraha"

imbeni sifa

"imbeni sifa kwa Mungu"

Psalms 98:5

tuni

sauti nzuri ya muziki ya kupendeza

baragumu

pembe la mnyama linalotumika kama chombo cha muziki

fanyeni kelele ya shangwe

"inueni shangwe"

Psalms 98:7

Acha bahari ipige kelele na kila kitu kilichomo

Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba bahari ni mtu anayeweza kupaza sauti kwa Mungu. "Iwe kana kwamba bahari na kila kitu kilichomo kinapiga kelele"

dunia na wote wanaoishi ndani yake

Mwandishi wa zaburi anazungumzia dunia kana kwamba ni mtu. "na acha dunia na wote wanaoishi ndani yake wapige kelele"

Acha mito ipige makofi, na milima ipige kelele ya shangwe

Mwandishi anazungumza kana kwamba mito na milima ni watu wanaoweza kupiga makofi na kupiga kelele. "Iwe kana kwamba mito inapiga makofi na milima inapiga kelele ya furaha"

dunia ... mataifa

Misemo hii ni njia nyingine ya kusema "watu wa duniani" na "watu wanaoishi katika mataifa"

mataifa kwa usawa

"atahukumu mataifa kwa usawa"

kwa usawa

"ukweli" au "kutumia kigezo sawa kwa kila mmoja"

Psalms 99

Psalms 99:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

mataifa

Hii inamaanisha watu wa mataifa. "watu wa mataifa yote"

yatetemeke

kutetemeka kwa hofu

Ameketi amesimikwa juu ya makerubi

Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba kiti cha enzi ambacho yahwe hukaa ni juu ya makerubi kwenye mfuniko wa amri za sanduku la agano hekaluni.

inatetemeka

inatikisika

Yahwe ni mkuu Sayuni; ameinuliwa juu ya mataifa yote

"Sio tu kwamba Yahwe ni mkuu sayuni, ametukuka juu ya mataifa yote" au "Sio tu kwamba Yahwe anatawala Sayuni, anatawala juu ya mataifa yote"

ameinuliwa juu ya mataifa yote

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu katika mataifa yote wanamtukuza" au "watu katika mataifa yote wanamsifu sana"

Acha walisifu jina lako kuu na la ajabu

Hapa mwandishi anahama kutoka kumzungumzia Mungu na kuzungumza na Mungu. Ingawa baada ya msemo huu, anarudi tena kumzungumzia Mungu.

Psalms 99:4

anapenda haki

Nomino dhahania "haki" inaweza kutafsiriwa kutumia msemo "kilicho cha haki." "anapenda kufanya kilicho cha haki"

Umeimarisha usawa

Nomino dhahania ya "usawa" ni njia nyingine ya kusema sheria zilizo na usawa. "Sheria ulizoweka zina usawa"

miguuni pake

"mbele ya kiti chake cha enzi"

Psalms 99:6

dhabiti

"takatifu"

Psalms 99:8

Ukawajibu

"ukawajibu watu wako"

kilima chake kitakatifu

"Mlima Sayuni"

Psalms 100

Psalms 100:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Piga kelele ya furaha kwa Yahwe

"Paza kelele kwa Yahwe."

dunia yote

Hii inamaanisha watu tote wa duniani. "kila mtu duniani"

njooni mbele zake

Mwandishi wa zaburi hii anazungumza kana kwamba anawaambia watu kwenda kwenye chumba chenye kiti cha enzi cha mfalme. "nenda mahali alipo kwa kuimba kwa furaha" au "anaweza kukusikia, kwa hiyo imba kwa furaha"

Psalms 100:3

kondoo wa malisho yake

Watu wa Mungu ni kama kondoo. "watu ambao Mungu anawahudumia na kuwalinda"

malisho

sehemu yenye nyasi ya kulishia wanyama

Psalms 100:4

na shukrani

"wakati ukimshukuru" au "huku ukimpa shukrani"

barikini jina lake

Neno "jina" ni njia nyingine ya kusema Yahwe mwenyewe. "mbariki Yahwe" au "fanya yale yatakayo mfurahisha Yahwe."

ukweli wake katika vizazi vyote

"ukweli wake unadumu katika vizazi vyote"

katika vizazi vyote

"kizazi baada ya kizazi."

Psalms 101

Psalms 101:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Psalms 101:2

Nitatembea katika njia ya uaminifu

Hapa Daudi anazungumza kuhusu "kuishi" kana kwamba ni "kutembea." "Nitaishi kwa namna ambayo ni ya uaminifu na sawa" au "Nitaishi maisha yaliyo jaa uaminifu"

Nitatembea na uaminifu ndani ya nyumba yangu

Hapa Daudi anazungumza kuhusu "kuishi" kana kwamba ni "kutembea." Pia, Daudi anazungumzia kuhusu kuangalia nyumba yake kwa uaminifu , kana kwamba uaminifu ni kitu cha kimwili kinachokaa ndani ya nyumba yake. "Nitaichunga nyumba yangu kwa uaminifu"

Sitaweka uovu mbele ya macho yangu

"Uovu" ni nomino dhahania inayoweza kuandikwa kama msemo. Lahaja, "weka uovu mbele ya macho yangu," inamaanisha kuukubali. "Sitakubali mtu kufanya kisicho sawa mbele yangu"

haitang'ang'ania kwangu

Daudi anaelezea "uovu" kana kwamba ni kitu kinachoweza kumng'ang'ania. Hii inamaanisha ataepuka vitu viovu na watu wanaofanya vitu viovu. "Nitajiepusha kabisa na uovu"

ng'ang'ania

kushikilia kitu au mtu kwa nguvu.

Psalms 101:4

uovu

"chochote kilicho kiovu"

mwenye mwenendo wa dharau na kiburi

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza jinsi watu wa hivyo walivyo na kiburi.

mwenendo

"fikra" au "tabia"

Nitamtazama mwaminifu wa nchi kuketi pembeni kwangu

Hii inamaanisha kuwa Daudi angewaruhusu wale watu hao kuwa karibu naye na kuishi naye. "Nitawaruhusu waaminifu wa nchi kuishi na mimi"

mwaminifu

Hii inamaanisha watu walio waaminifu kwa Mungu. "watu waaminifu"

wanaotembea katika njia ya uadilifu

Hapa Daudi anazungumzia "kuishi" kana kwamba ilikuwa "kutembea." "ishi kwatika njia iliyo ya uwazi na sawa" au "wanaoishi maisha yaliyojaa uadilifu"

Psalms 101:7

Watu waongo hawata ... waongo hawata..

Misemo hii miwili ina wazo moja na inatumika pamoja kusisitiza jinsi Daudi atakavyoshindwa kuwavumilia watu waongo.

waongo hawatakaribishwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Sitawakaribisha waongo"

mbele ya macho yangu

Hapa "macho yangu" yanaashiria Daudi mwenyewe. "mbele yangu" au "mbele ya uwepo wangu"

Asubuhi kwa asubuhi

"Kila siku"

waovu

Hii inamaanisha watu waovu. "watu waovu"

kutoka mji wa Yahwe

Daudi anamaanisha mji aliumo kama "mji wa Yahwe." Hii inaweza kuwekwa wazi. "kutoka kwenye mji, ambao ni mji wa Yahwe"

Psalms 102

Psalms 102:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

aliyeteswa

Hii inamaanisha mtu aliyeteswa. "mtu aliyeteswa"

anapolemewa

"dhaifu" au "mnyonge"

kumwaga maombolezo yake mbele ya Yahwe

Jinsi mtu anavyoeleza maombolezo yake inafananishwa na kumwaga kimiminiko. "anaeleza huzuni yake kwa uhuru kwa Yahwe"

Psalms 102:3

siku zangu zinapita kama moshi

Hapa "siku zangu" inamaanisha maisha ya mwandishi na wazo la "moshi" ni kitu kinachopotea upesi. "maisha yangu yanapita upesi"

mifupa yangu kama moto

Hapa mwandishi anazungumzia "mwili" wake kama "mifupa." "nahisi mwili wangu ni kama kitu kinachoungua"

Moyo wangu umepondeka

Hapa mwandishi anajizungumzia mwenyewe kama "moyo"wake. "Niko katika huzuni"

niko kama nyasi ziizonyauka

Hii ni njia nyingine ya kuelezea huzuni yake. "nahisi kama vile nakauka kama nyasi zilizonyauka"

Psalms 102:5

Nimekuwa kama mwari wa jangwani

Analinganisha upweke wake na ule wa mwari, ambayo mara nyingi huonekana yenyewe badala ya kuwa ndege wengine. "Nimekuwa mpweke na niliyechukiwa kama mwari jangwani"

mwari

ndege mkubwa anaye kula samaki

nimekuwa kama bundi katika maanguko

Mwandishi anaendelea kufafanua upweke kwa kujifananisha mwenyewe na bundi katika maanguko yaliyotelekezwa. "nimekuwa mwenyewe kama bundi katika maanguko yaliyo telekezwa"

bundi

Huyu ni ndege anayekuwa macho wakati wa usiku. "ndege wa usiku"

Psalms 102:7

Ninalala macho kama ndege mpweke

Mwandishi anajifananisha na ndege kusisitiza hisia yake ya upweke.

Psalms 102:9

Ninakula majivu kama mkate

Daudi angekuwa amekaa katika majivu kama kitendo cha kuomboleza, kwa hiyo majivu yangeanguka kwenye chakula chake. "Ninakula majivu kama ninavyokula mkate" au "Ninapoomboleza, majivu hudondoka kwenye mkate ninaokula"

na kuchanganya kinywaji changu na machozi

Daudi hakuchanganya kwa makusudi kinyaji chake na machozi; bali chozi lake lingedondoka katika kikombe chake wakati akiomboleza na kulia. "na machozi yangu yanadondoka kwenye kikombe ninachonywea"

umeniinua juu kunitupa chini

Mungu hajainua kiuhalisia mwili wa Daudi na kuutupa ardhini; bali Daudi anasema hivi kuelezea anachojisikia na kupitia. "ni kana kwamba umeniinua juu ili kunitupa chini"

Psalms 102:11

Siku zangu ni kama kivuli kinachofifia

Daudi anafananisha muda aliobakiza kuishi duniani na kivuli kinachofifia. "Muda wangu wa kubaki hai ni mfupi kama kivuli cha jioni ambacho kitapotea punde"

nimenyauka kama nyasi

Wakati mwili wa Daudi unakuwa mdhaifu na anakaribia mwisho wa maisha yake, anajilinganisha na nyasi zinazonyauka. "mwili wangu umedhofika kama nyasi zilizonyauka"

nyauka

kukauka na kujikunja

umaarufu wako ni wa vizazi vyote

"utatambulika katika vizazi vyote vitakavyokuja"

umaarufu

kujulikana na watu wengi

Psalms 102:13

kuwa na huruma juu ya Sayuni

Hapa "Sayuni" inamaanisha watu wanaoishi Sayuni. "kuwa na huruma na watu wanaoishi Sayuni"

juu yake

Neno "yake" inamaanisha Sayuni.

hushika mawe yake karibu

"Mawe" inamaanisha mawe yaliyokuwa sehemu wa kuta za mji kabla ya kuangamizwa. "bado wanapenda mawe yaliyokuwepo katika kuta za mji"

jina lako

Hapa "jina lako" linamaanisha Yahwe. "wewe"

wataheshimu utukufu wako

Watu watumheshimu Yahwe kwa sababu ya utukufu wake. Hapa Yahwe anazungumziwa kwa utukufu wake. "watakuheshimu wewe kwa sababu una utukufu"

atatokea katika utukufu wake

"ataonekana kama mtukufu" au "watu wataona utukufu wake"

Psalms 102:17

fukara

Hii inamaanisha watu fukara.

hatakataa maombi yao

"Yahwe atakubali maombi yao"

Hii itaandikwa kwa ajili ya vizazi vya baadaye

"Nitaandika hii kwa ajili ya vizazi vya baadaye"

Psalms 102:19

Kwa kuwa ametazama chini kutoka katika patakatifu pake pa juu; kutoka mbinguni Yahwe ametazama

Misemo hii miwili ina maana za kufanana na inatumika pamoja kusisitiza jinsi Mungu anavyotazama chini kutoka mbinguni.

patakatifu pake pa juu

"mahali pake patakatifu juu ya dunia"

wale walio hukumiwa kufa

"wale ambao mamlaka yaliwaamuru kuhukumiwa kufa"

Psalms 102:21

tangaza jina la Yahwe katika Sayuni na sifa zake katika Yerusalemu

Misemo hii miwili inamaana moja na inasisitiza wazo la kusifu jina la Yahwe.

na sifa zake

"na tangazeni sifa zake"

Psalms 102:23

amechukuwa nguvu yangu

Daudi anazungumzia Mungu kumsababisha kuwa mnyonge kana kwamba nguvu yake ni kitu cha kihalisia kinachoweza kuondolewa kutoka kwake. "amenisababisha kuwa mnyonge"

siku zangu

Neno "siku" hapa linamaanisha maisha. "maisha yangu"

usichukue

Daudi anamwomba Mung asimwache afe. "usinitoe kutoka duniani" au "usiniache nife"

upo hapa katika vizazi vyote

"uko katika vizazi vyote"

Psalms 102:25

wote watazeeka

Neno "wote" linamaanisha "dunia" na "mbingu."

miaka yako haitakuwa na mwisho

Hapa Daudi anaelezea urefu wa muda ambao Mungu yuko hai kama "miaka" yake. "utaishi milele"

Psalms 102:28

wataishi

"wataendelea kuishi"

wataishi katika uwepo wako

Hapa Daudi anaelezea uzao kulindwa na Yahwe kama kuwa katika uwepo wake. "watalindwa wanapoishi katika uwepo wako"

Psalms 103

Psalms 103:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Nitamsifu Yahwe na maisha yangu yote, na kwa vyote vilivyo ndani yangu, ninatoa sifa kwa jina lake takatifu, ninatoa sifa kwa jina lake takatifu

Misemo hii miwili inamaana moja na inasisitiza jinsi atakavyomsifu Yahwe. "Nitamsifu Yahwe kwa moyo wangu wote"

ninatoa sifa kwa jina lake takatifu

Hii inamaanisha kusifu jina la Yahwe kama Yahwe.

vyote vilivyo ndani yangu

"kila kitu ndani yangu." Daudi anatumia msemo huu kujizungumzia mwenyewe na kusisitiza mapenzi kwa Yahwe.

Psalms 103:3

zako ... yako

Tafsiri nyingi zinaeleza hii na "mimi."

Anakomboa maisha yako kutoka katika uharibifu

Hii inamaanisha kuwa Yahwe anamweka kuwa hai. "Ananiokoa kutoka na kifo"

anakuvika taji

Hapa "baraka' inaelezwa kana kwamba ni "kuvikw taji." "anakubariki"

Anakuridhisha maisha yako na vitu vizuri

Msemo "maisha yako" inamaanisha "wewe," lakini inasisitiza kuwa Yahwe hutoa baraka katika maisha yote. "Anakuridhisha na vitu vizuri katika maisha"

ujana wako unafanywa kuwa mpya kama tai

Kuwa na "ujana wako kufanywa kuwa mpya" inamaanisha kujihisi kijana tena. Hapa Daudi anafananisha hisia hii ya ujana na wepesi na nguvu ya tai. "unajihisi kijana na mwenye nguvu kama tai"

ujana wako

"ujana" unamaanisha nguvu ambayo alikuwa nayo kama kijana.

Psalms 103:6

anafanya vitendo vya hukumu kwa ajili ya

"anasababisha hukumu kutokea"

wote walio kandamizwa

"wote walio kandamizwa na watu"

matendo yake kwa uzao

"alifanya matendo yake yajulikane kwa uzao"

ana uaminifu mkuu wa agano

amejaa huruma na upendo"

Psalms 103:9

Hataadabisha wakati wote; hakasiriki kila mara

Misemo hii miwili ina maana za kufanana. Msemo wa pili unaimarisha wazo la kwanza.

Hatufanyii ... au kutulipa

Misemo hii miwili ina usambamba na inasisitiza kwamba Mungu hatuadhibu kama tunavyostahili. "Hatulipi kwa adhabu tunayostahili kwa ajili ya dhambi zetu"

Hatufanyii

"Hautuadhibu"

Psalms 103:11

Kwa kuwa kama anga zilivyo juu ... kuelekea wale ambao humheshimu

Tashbihi inalinganisha umbali mkubwa kati ya mbingu na dunia kwa ukuu wa upendo wa Mungu kwa ajili ya watu wake.

Kama vile mashariki ilivyo mbali ... alivyoondoa hatia ya dhambi zetu kutoka kwetu

Umbali kati ya mashariki na magharibi ni mbali sana mpaka haiwezi kupimika. Katika tashbihi hii, umbali huo unalinganishwa kwa jinsi Mungu anavyosogeza mbali hatia yetu kutoka kwetu.

Kama vile baba alivyo na huruma ... juu ya wale amabo humheshimu

Hapa mwandishi analinganisha huruma ya baba kwa watoto wake kwa huruma ya Yahwe kwa wale ambao wanamheshimu.

Psalms 103:14

jinsi tulivyoumbwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "jinsi miili yetu ilivyo" au "jinsi alivyoumba miili yetu"

anajua ya kuwa sisi ni vumbi

Yahwe alipomuumba Adamu mtu wa kwanza alimuumba kutoka na vumbi. "anakumbuka ya kwamba alituumba kutoka na vumbi"

Na kwa mtu, siku zake ni kama nyasi

Katika tashbihi hii, urefu wa maisha ya mtu unalinganishwa na urefu mfupi ambao nyasi huota kabla hazijafa. "Urfeu wa maisha ya mtu ni kama yale ya nyasi"

hustawi kama ua katika shamba

Katika tashbihi hii, jinsi mtu hukua katika muda inalinganishwa kwa jinsi ua huota.

hustawi

"Kustawi" ni kuota vizuri na kuwa na afya.

Upepo huvuma juu yake, na linatoweka ... ni wapi liliwahi kuota

Misemo hii inaendelea kuongea juu ya maua na nyasi. Inalinganisha jinsi maua na nyasi hufa kwa jinsi mtu hufa. "Upepo huvuma juu ya maua na nyasi na inapotea, na hakuna awezaye kujua wapi zilianza kuota - ni sawa na mwanadamu"

Psalms 103:17

ni kutoka milele mpaka milele

Hii ina maana ya kwamba upendo wa Yahwe huendelea milele. "utaendelea milele"

vizazi vyao

"vizazi vya wale ambao humuinua yeye"

Wanashika agano lake na kukumbuka kutii maelekezo yake

Misemo hii miwili ina maana za kufanana.

Yahwe ameimarisha kiti chake cha enzi katika mbingu

Hapa utawala wa Yahwe kama mfalme unamaanishwa kama "kiti chake cha enzi". "Yahwe amechukua kiti chake katika mbingu ambapo hutawala kama mfalme"

ameimarisha

"alifanya"

ufalme wake hutawala

Hapa Yahwe anaelezwa kuwa "ufalme wake" kusisitiza mamlaka yake kama mfalme. "hutawala"

Psalms 103:20

hutekeleza mapenzi yake

Hii ni lahaja ikimaanisha "kufanya mapenzi yake". "fanya mapenzi yake"

katika sehemu zote ambazo hutawala

"msifu yeye katika sehemu zote ambapo hutawala"

kwa maisha yangu yote

"na moyo wangu wote" au "na nafsi yangu yote". Msemo huu una maana ya kwamba atamsifu Yahwe kwa moyo wote na unatumika kusisitiza utii wake kwake.

Psalms 104

Psalms 104:1

Taarifa ya Jumla

Usambaba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla

Zaburi hii ni wimbo wa sifa.

kwa maisha yangu yote

"kwa moyo wangu wote" au "kwa nafsi yangu yote". Msemo huu una maana ya kwamba atamsifu Yahwe kwa moyo wote na inatumika kusisitiza utii wake kwake.

umevaa ufahari na utukufu

Maneno "ufahari" na "utukufu" ina maana moja na inasisitiza ukuu wa utukufu wa Yahwe. Inaelezwa kama kumvisha Yahwe kama vazi. "una ufahari na utukufu kukuzunguka kote"

Unajifunika kwa mwanga kama vile vazi

Yahwe anafafanuliwa kama kufunikwa na mwanga kana kwamba mwanga ulikuwa vazi kukuzunguka. "Unafunikwa na mwanga"

unatandaza nje mbingu kama pazia la hema

Hapa Mungu anafafanuliwa kama kutandaza nje mbingu kama mtu anavyotandazwa nje ya hema wakati inaandaliwa. "unatandaza nje mbingu kama mtu anayetengeneza hema"

Unalaza nguzo za chumba chako juu ya mawingu

"Unajenga vyumba vyako vya juu katika mbingu". Hii ina maana ya nyumba yake kuwa ndefu ya kwamba sakafu yake ya juu inatanuka mapka katika mawingu.

unafanya mawingu kuwa kibanda wazi chako

Hapa mawingu yanaelezwa kumbeba Yahwe kana kwamba yalikuwa kibandawazi. "unafanya mawingu kukubeba kama kibandawazi"

unatembea juu ya mabawa ya upepo

Hapa kuvuma kwa upepo inaelezwa kama mabawa ambayo Yahwe hutembea. "unatembea juu ya upepo"

Psalms 104:4

Hufanya upepo kama wajumbe wake

Maana zaweza kuwa 1) anasababisha upepo kuweza kubeba ujumbe kama mjumbe, "Hufanya upepo kuwa kama wajumbe wake" au 2) "Huwafanya wajumbe wake kuwa na haraka kama upepo"

miale ya moto watumishi wake

Maana zaweza kuwa 1) "anasababisha miale ya moto kuwa kama watumishi wake". Husababisha moto kumtumikia kama mtumishi angefanya au 2) "hufanya mtumishi wake kuwa kama miale ya moto".

miale ya moto watumishi wake

Hii inaweza kuandikwa na taarifa ya kudokezwa kutoka katika mstari wa nyuma. "Hufanya miale ya moto watumishi wake"

Alilaza misingi ya dunia

Hapa msemo "kulaza misingi" ina maana ya "kuumbwa". "Aliumba dunia nzima"

Psalms 104:6

Ulifunika dunia kwa maji kama vazi

Hapa maji ambayo yalifunika dunia inalinganishwa na jinsi vazi kubwa linavyoweza kufunika kabisa kitu. "Umefunika kabisa dunia kwa maji"

Kukaripia kwako hufanya maji ... yalitoroka

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kusisitiza jinsi Mungu alivyozungumza na maji yalivyoondoka.

kurudi nyuma

"kukimbia" au "kusogea nyuma"

yalitoroka

Hapa mtunga zaburi anazungumza juu ya maji kurudi nyuma kana kwamba yalitoroka kama mnyama baada ya kusikia sauti ya Yahwe. Neno "kutoroka" lina maana ya kukimbia mbali haraka. "kukimbia haraka"

Psalms 104:8

Milima ikainuka, na mabonde yakasambaa

Hapa mtunga zaburi anazungumza juu ay Mungu kusababisha milima na mabonde kusogea na kubadilika kana kwamba zilichagua kusogea zenyewe. Inaelezewa kwa njia hii kusisitiza uwezo wa Mungu.

mpaka kwa ajili yao ili wasivuke

Hapa mtunga zaburi anazungumza juu ya Mungu kusababisha maji kutovuka mpaka ambao alitengeneza kwa ajili yao kana kwamba maji yenyewe yalichagua kutovuka. Yaneelezewa kwa naman hii kusisitiza mamlaka ya Mungu juu yao. "mpaka kwa ajili yao ambao hawawezi kuvuka"

mpaka

"mstari" au "mpaka"

kwa ajili yao

Neno "yao" ina maana ya maji.

Psalms 104:10

vijito

mito midogo

punda pori huzima kiu yao

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba wanazima kiu yao kwa kunywa maji. "punda pori hunywa maji kuzima kiu yao"

ukingo wa mto

ardhi katika ukingo wa mto

wanaimba miongoni mwa matawi

Hapa Daudi anafafanua ndege kulia kana kwamba walikuwa wakiimba. "wanalia miongoni mwa matawi ya mti"

Psalms 104:13

Humwagilia milima kutoka katika vyumba vyake vya maji vya angani

Hii ina maana ya kwamba Mungu husababisha mvua kunyesha. Maji yanaelezwa kama kurudi nyuma katika vyumba vya angani. "Humwagilia milima kwa kusababisha mvua kuanguka kutoka angani"

matunda ya kazi yake

"mambo mengi mazuri ambayo unaumba"

na mimea kwa ajili ya mtu kulima

Maneno ambayo hayapo yanweza kuongezwa. "na hufanya mimea kuota kwa ajili ya mtu kulima"

Psalms 104:16

Miti ya Yahwe hupata mvua nyingi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe alitoa mvua nyingi kwa ajili ya miti yake"

Pale ndege hutengeneza viota vyao

Wanatengeneza viota vyao katika seda. Hii inaweza kuwekwa wazi. "Ndege hutengeneza viota vyao katika seda"

korongo

Huyu ni aina ya ndege. "ndege"

pimbi

Pimbi ni mnyama mdogo ambaye hufanana na panya mkubwa. "melesi wa mawe"

Psalms 104:19

nyakati

Neno hili lina maana ya hali za hewa tofauti zinazobadilika katika mwaka. Baadhi ya sehemu zina nyakati za mvua kubwa na kiangazi, wakati zingine zina majira ya kuchipua, majira ya bubujiko, majira ya joto na majira ya baridi.

jua linajua wakati wake

Hapa Daudi anafafanua jua kana kwamba anajua ni wakati gani wa siku. "alifanya jua kuzama muda ukiwadia"

Unafanya

"Yahwe, unafanya". Hapa mwandishi anabadilisha kutoka kuzungumza juu ya Yahwe kwa kuzungumza kwake.

Psalms 104:21

mawindo

Huyu ni mnyama ambaye ni chakukla kwa ajili mnyama mwingine.

na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu

"lakini wanamtegemea Mungu kutoa chakula chao"

kurudi nyuma

"rudi" au "ondoka mbali"

mapango

nyumba za baadhi ya mamalia na wanyama wadogo

Psalms 104:23

humwagikia kwa kazi zako

Hapa Daudi anafafanua kiasi cha vitu ambavyo Yahwe aliviumba kana kwamba vilikuwa kimiminiko kumwagikia nje ya chombo. "inajazwa na kazi yako!"

Psalms 104:25

kirefu na kipana

"ina kina kirefu sana na ni pana sana". Urefu na upana wa bahari unasisitiza jinsi ilivyo kubwa.

inayojaa

"inayomwagikia"

visivyohesabika

"isiyohesabika"

wote wadogo na wakubwa

Hii ina maana ya viumbe vya kila aina ya ukubwa.

Meli husafiri pale

"Meli husafiri juu ya bahari"

Psalms 104:27

Hawa wote

"Viumbe hawa wote"

kuwapa chakula chao kwa wakati

"kuwapa chakula chao wanapokihitaji"

Utakapowapatia, wanakusanya

Inaweza kusaidia kuandika ya kwamba ni chakula ambacho kinapewa. "Unapotoa chakula kwao, wanakikusanya"

wanakusanya

"kusanya"

unapofungua mkono wako

Hii inaelezea Yahwe kama kufungua mkono wake kutoa chakula kwa viumbe. "unapofungua mkono wako kuwalisha"

Psalms 104:29

utakapoficha uso wako

Hii ina maana ya kwamba Yahwe hawatazami wao au kuwaangalia kwa makini. "pale ambapo hautazami juu yao" au "unapowadharau"

kurudi mavumbini

Hii ina maana ya kwamba miili yao huoza na huwa udongo tena. "miili yao huoza na kurudi ardhini"

Unapotuma nje Roho wako

Hii ina maana ya Roho wake kutumwa kutoa uhai kwa viumbe.

wanaumbwa

Ni roho ya Yahwe ambayo iliwaumba.

unafanya upya uso wa nchi

"unasababisha nchi kujaa na uhai mpya"

Psalms 104:33

mawazo yangu kuwa matamu

Analinganisha mawazo yake na kitu ambacho ni kitamu. "mawazo yangu yawe mazuri"

Psalms 104:35

wapoteleaa

"kupotelea"

acha waovu wasiwepo tena

Msemo huu "waovu" una maana ya watu waovu. "na watu waovu wapotelee"

Psalms 105

Psalms 105:1

Taarifa ya Jumla

Usambamba ni kawaida katika shairi ya Kiebrania.

liite jina lake ... Jivunie katika jina lake takatifu

Hapa "jina" inawakilisha Yahwe. "muite yeye ... Jivunie ndani ya Yahwe"

mataifa

Hii ina maana ya watu katika mataifa. "watu wa mataifa"

acha moyo wa wale ambao humtafuta Yahwe washangilie

Hapa "moyo" inawakilisha mtu ambaye humtafuta Yahwe. "acha watu ambao humtafuta Yahwe washangilie"

Psalms 105:4

Mtafute Yahwe na nguvu yake

"kutafuta nguvu ya Yahwe" ina maana ya kumuuliza kukuimarisha.

Kumbuka

"kumbuka"

miujiza yake na

Inaweza kusaidia kuongeza maneno ambayo hayapo. "kumbuka miujiza yake na"

maagizo kutoka mdomoni mwake

Hapa "mdomoni" ina maana ya mambo ambayo alizungumza. "maagizo ambayo ameyazungumza"

vizazi vyako vya Abrahamu ... nyie watu wa Yakobo

Mwandishi anazungumza kwa Waisraeli, kuwaita majina haya.

Abrahamu mtumishi wake

"Abrahamu, mtumishi wa Yahwe"

Psalms 105:7

Huweka akilini ... neno ambalo aliloliamuru

Misemo hii miwili inatumia maana ya kufanana na inatumika pamoja kwa ajili ya msisitizo. Neno "neno" lina maana ya agano. "Huweka akilini agano lako milele, ahadi aliyoifanya"

huweka akilini

Hii ina maana ya kukumbuka na kufikirir juu ya jambo. "hukumbuka"

vizazi elfu moja

"vizazi 1,000"

Psalms 105:9

Huweka akilini

Msemo huu "kuweka akilini" ina maana ya kukumbuka jambo. "anakumbuka"

agano ambalo alilifanya na Abrahamu ... kiapo chake kwa Isaka

Misemo hii miwili "agano" na "kiapo" ina maana ya ahadi moja ambayo Yahwe alifanya kwa watu wake.

kiapo chake kwa Isaka

Inaweza kusaidia kuongeza maneno ambayo hayapo. "kiapo chake ambacho alitoa kwa Isaka"

Psalms 105:12

Kauli Kiunganishi

Mtunga zaburi anaandika kuhusu Israeli.

walipokuwa wachache tu kwa idadi

Neno "walipokuwa" ina maana ya Waisraeli.

na wageni katika nchi

Inadokezwa ya kwamba "nchi" ina maana ya Kaanani. "na walikuwa wageni katika nchi ya Kaanani"

Waliondoka kutoka

"Waliendelea kutangatanga"

kutoka taifa kwa taifa na kutoka ufalme mmoja kwa mwingine

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kwa msisitizo.

Psalms 105:14

Kauli Kiunganishi

Mtunga zaburi anazungumza kuhusu Israeli.

kwa ajili yao

"kwa ajili ya ustawi wao". Hii ina maana ya Israeli.

Usiwaguse watiwa mafuta wangu

Hapa "kugusa" ina maana ya kudhuru, ni kukuza ambapo Yahwe alitumia kuimarisha onyo lake kutowadhuru watu wake. "Usiwadhuru watu ambao niwewatia mafuta"

Psalms 105:16

Akaamuru njaa

"Alituma". Hii ina maana ya kwamba alisababisha njaa kutokea katika nchi.

akiba yote ya mkate

Hapa "mkate" ina maana ya chakula kwa ujumla. "akiba yote ya chakula"

Alimtuma mtu mbele yao; Yusufu

Inaweza kusaidia kuandika ya kwamba alimtuma mbele yao Misir. "Alimtuma mwanamume mbele yao Misri; alimtuma Yusufu ambaye"

Yusufu aliuzwa kama mtumishi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Ndugu za Yusufu alimuuza kama mtumwa"

Psalms 105:18

minyororo

vizuizi vya chuma vinavyotumika kushika vifundo vya mfungwa au vifundo vya mguu pamoja

Miguu yake ilifungwa kwa minyororo; shingoni mwake kuliwekwa kola ya chuma

Kauli hizi zinaweza kuandikwa kama hali ya kutenda. "Wamisri walimfunga miguu yake kwa minyororo; waliweka kola ya chuma shingoni mwake".

neno la Yahwe likamjaribu

Hapa "neno" lina maana ya ujumbe wa Yahwe. "ujumbe wa Yahwe ulimjaribu"

Psalms 105:20

Mfalme alituma watumishi kumweka huru; mtawala wa watu akamweka huru

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kwa msisitizo ya kwamba mfalme alimweka huru.

Kisha Israeli akaja mpaka Misri

Hapa "Israeli" ina maana ya Yakobo. Yakobo alileta familia yake pamoja naye. "Kisha Israeli na familia yake kuja Misri"

Psalms 105:24

Yahwe aliwafanya watu wake kuzaliana

Mwandishi anazungumza juu ya ongezeko la Israeli kana kwamba walikuwa mmea ambao ulizaa matunda mengi. "Mungu aliongeza idadi ya watu wake sana"

kuwachukia watu wake, kuwatendea vibaya watumishi wake

"kuchukia watu wake na kuwatendea vibaya watumishi wake"

Walitelekeza ishara zake ... maajabu yake katika nchi ya Hamu

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kwa ajili ya msisitizo. "Musa na Haruni walitekeleza miujiza ya Yahwe Misri miongoni mwa vizazi wa Hamu"

maajabu yake

Maneno ambayo haypo yanaweza kuongezwa. "na wakatekeleza maajabu yake"

Psalms 105:28

alifanya nchi hiyo kuwa giza

"alifanya anga giza"

vyura

reptilia mdogo anayeruka

katika katika vyumba vya watawala wao

"hata walikuwa ndani ya vyumba vya watawala wao"

Psalms 105:31

Kauli Kiunganishi

Mtunga zaburi anaendelea kufafanua hukumu ya Yahwe kwa Misri.

kundi kubwa

makundi makubwa yanayopaa

chawa

wadudu wadongo wanaopaa kama nzi lakini wadogo zaidi

mvua ya mawe

barafu ambayo huanguka kutoka angani kama mvua

Aliangamiza ... alivunja

Mungu alisababisha mvua ya mawe, mvua, na radi kuharibu mizabibu na miti. "Alisababisha iangamize ... na kuvunja"

Psalms 105:34

nzige wengi sana

"kulikuwa na nzige wengi sana"

Nzige walikula mimea yote ... Walikula mazao yote ya ardhini

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kwa ajili ya msisitizo. "Wadudu walikula mimea yote na mazao yote katika nchi"

Alimuua kila mzaliwa wa kwanza katika nchi, malimbuko ya nguvu zao

Hapa msemo wa pili kuhusu "malimbuko" unatumika kufafanua "mzaliwa wa kwanza" katika msemo wa kwanza. "Aliua kila mzaliwa wa kwanza katika nchi yao, ambao walikuwa malimbuko ya nguvu zao" au "Kisha Yahwe aliwaua wana wenye umri mkubwa katika kila nyumba ya watu wa Misri"

Psalms 105:37

Aliwaleta Waisraeli nje wakiwa na fedha na dhahabu

Waisraeli walipoondoka Misri walichukua fedha na dhahabu pamoja nao. "Aliwatoa Waisraeli kutoka Misri pamoja na fedha na dhahabu katika milki yao"

hakuna wa kabila lake waliojikwaa njiani

Hakuna aliyebaki nyuma. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya chanya. "makabila yake yote yaliweza kufanya safari hiyo"

Misri ilifurahi

Hapa "Misri" ina maana ya watu ambao wanaishi Misri. Watu wa Misri alifurahi.

Alitandaza wingu kuwa mfuniko

Hapa mtunga zaburi anafafanua Yahwe kuweka wingu angani kana kwamba alikuwa akitandaza nje vazi. Wingu lilikuwa "linafunika" kuwalinda kutoka na jua. "Aliweka wingu angani kuwalinda kutoka na jua na joto"

kutengeneza moto kutoa mwanga usiku

Yahwe aliweka nguzo ya moto angani kutoa mwanga wakati wa usiku. "aliweka moto angani kutoa mwanga usiku"

Psalms 105:40

naye akaleta kware

Inaweza kuwa msaada kuweka wazi ya kwamba kware ni ndege wadogo Yahwe alituma kwa ajili yao kula. "na Yahwe alituma ndege wadogo wa kula"

na mkate kutoka mbinguni

Yahwe alisababisha mana, aina ya mkate, kuanguka kutoka angani. "kwa mkate ambao ulianguka kutoka angani"

yalitiririka

"maji yalitiririka"

aliweka akilini

Hii ina maana kukumbuka. "alikumbuka"

Psalms 105:43

Akawaongoza watu wake nje ... wateule wake kwa kelele za ushindi

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kusisitiza ya kwamba watu wa Mungu walikuwa na furaha alipowaongoza kutoka Misri. Watu walikuwa wakipiga kelele kwa furaha. "Aliwaongoza watu wake wateule kwa kelele za furaha na ushindi"

wateule wake

Hapa "wateule" ina maana ya watu wateule wa Yahwe. "watu wake wateule"

ushindi

"sherehe" au "furaha"

kuzishika amri zake na kutii sheria zake

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kwa ajili ya msisitizo. "Kushika" amri zake ina maana ya kuzitii. "kutii sheria zake na maagizo"

Psalms 106

Psalms 106:1

Taarifa ya Jumla

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Nani awezaye kuhesabu tena matendo makuu ya Yahwe ... matendo?

Mwandishi anauliza swali hili kumsifu Mungu na hategemei jibu. "Hakuna mtu awezaye kuhesabu tena matendo makuu ya Yahwe ... matendo".

matendo yake yanayostahili sifa

"matendo ambayo yanastahili sifa"

Psalms 106:3

Niite akilini

Msemo "kuita akilini" ina maana ya kukumbuka jambo. "nikumbuke"

ya chaguo lako

Neno "aliyechaguliwa" ina maana ya watu waliochaguliwa wa Yahwe. "wa watu waliochaguliwa"

nitashangilia katika furaha ... na nitakuwa na utukufu

Haya ni mambo ambayo Daudi anasema atafanya, pamoja na "kuona mafanikio ya waliochaguliwa wako". Maneno ambayo hayaonekani yanaweza kuongezwa. "Nitashangilia katika furaha ... na nitakuwa na utukufu"

furaha

"furaha" au "shangwe"

utukufu na urithi wako

Hapa msemo "urithi wako" ina maana ya Waisraeli, ambao ni watu wa Yahwe waliochaguliwa. Hapa "utukufu" ina maana ya "kujivunia" juu ya kitu; katika hali hii wanajivunia juu ya Yahwe. "kujivunia katika ukuu wako na watu wako"

Psalms 106:6

hawakutambua mambo yako ya ajabu

"hatuna shukurani kwa ajili ya mambo ya ajabu uliyofanya"

katika bahari ... Bahari ya Matete

Misemo hii miwili ina maana ya kitu kimoja. Ya pili ni jina la bahari.

Psalms 106:8

Hata hivyo

"ingawa" au "hata hivyo"

kwa ajili ya jina lake

Hapa "jina lake" lina maana ya Yahwe. "kwa ajili ya sifa yake mwenyewe"

katikati ya vina, kama vile katikati ya nyika

Hapa Daudi analinganisha njia ambayo Yahwe aliwaongoza Waisraeli katikati ya Bahari ya Matete kwa namna watu wanaweza kuongozwa katika ardhi kavu ya nyika. "Vina" ina maana Yahwe aligawanya maji. "katikati ya Bahari ya Matiti katika ardhi kavu"

Psalms 106:10

Aliwaokoa kutoka katika mkono ... na akawaokoa kutoka katika mkono

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja na inatumika pamoja kusisitiza ya kwamba Yahwe aliwaokoa kutoka kwa adui zao.

mkono wa wale ambao walimchukia

Hapa "mkono" una maana ya uwezo na utawala. "uwezo wa wale ambao walimchukia" au "utawala wa wale ambao walimchukia"

yaliwafunika wapinzani wao

Hii ni njia ya upole ya kuzungumza kuhusu yao kuzama majini. "alizamisha majini maadui zake"

Kisha wakaamini maneno yake

Hapa nano "wakaamini" ina maana ya "mababu zao" na neno "yake" ina maana ya "Yahwe".

Psalms 106:13

hawakusubiri maelekezo yake

Inadokezwa ya kwamba walifanya mambo bila kusubiri kujua Yahwe alitaka waende wapi. "walifanya mambo bila kwanza kusubiri maelekezo ya Yahwe"

uchu usiotosheka

"uchu ambao hauwezi kutoshelezwa"

walishindana na Mungu

"Waliasi dhidi ya Mungu"

uliteketeza

"uliwapita" au "ulichukua"

lakini akatuma ugonjwa

Hapa Daudi anazungumza kuhusu Yahwe kusababisha watu kuumizwa kwa ugonjwa kana kwamba Yahwe alituma ugonjwa kwao kwa njia moja ambayo mtu hutuma mtu au mjumbe. "lakini alisababisha ugonjwa kuteketeza miili yao"

Psalms 106:16

Katika kambi

Hii ina maana ya kambi ya Waisraeli katika nyika. "Katika kambi nyikani"

Dunia ilifunguka na kummeza

Hapa jinsi ardhi inavyofunguka na kuwazika watu inalinganishwa kwa jinsi kiumbe kinavyomeza kitu. "Dunia ilifunguka na kuzika"

Dathani

Huyu alikuwa afisa aliyeasi thidi ya Musa.

na kuwafunika wafuasi wa Abiramu

Wafuasi wa Abiramu walizikwa pia dunia ilipofunguka na kumzika Dathani. "pia ikafunuka wafuasi wa Abiramu" au "na pia ikazika wafuasi wa Abiramu"

Abiramu

Huyu alikuwa afisa aliyeasi dhidi Musa.

Moto ukaanza miongoni mwao; moto ukawateketeza waovu

Misemo hii miwili ina maana kimoja na inaandikwa pamoja kusisitiza jinsi watu waovu waliuawa kwa moto.

Psalms 106:19

Walitengeneza ndama Horebu na kuabudu sanamu ya chuma ya kuchonga

Taarifa hii inaweza kuandikwa kwa mpangilio ili kwamba iwe wazi ya kwamba ndama alikuwa sanamu ya chuma ya kuchonga. "Horebu, walitengeneza sanamu ya chuma ya ndama na kuiabudu"

Walibadilisha utukufu wa Mungu kwa mfano wa fahali

Hii ina maana ya kwamba badala ya kumwabudu Mungu waliabudu sanamu ya fahali.

utukufu wa Mungu

Hapa Mungu anajulikana kwa utukufu wake. "Mungu wao mtukufu" au "Mungu ambaye ana utukufu"

Psalms 106:22

nchi ya Hamu

Hii ina maana ya nchi ambapo vizazi vya Hamu waliishi. "nchi ambayo uzao wa Hamu waliishi"

matendo makuu

"mambo ya ajabu"

akaingilia kati naye katika upenyu ... kutowaangamiza

Hapa Daudi anazungumzia kuhusu Musa kumshawishi Yahwe kutowaangamiza Israeli kama kuingilia kati na yeye kuwa katika upenyo. "alisimama katikati ya Yahwe na Waisraeli na kumsihi Yahwe kutowaangamiza"

Psalms 106:24

walinung'unika

"walilalamika"

ahadi yake

Hii ina maana ya ahadi ya Yahwe ya kwamba atawaruhusu kuchukua nchi ya Kaanani kama milki yao.

Psalms 106:26

akainua mkono wake

Neno "wake" ina maana ya Yahwe. Pia, ilikuwa utamaduni kuinua mkono wakati wa kutoa kiapo.

kutawanya uzao wao ... katika nchi za kigeni

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kwa ajili ya msisitizo. "na ya kwamba angefanya uzao wao kuishi katika nchi za kigeni"

kutawanya

Hii ina maana ya kutawanya au kusambaza kitu

Psalms 106:28

sadaka zilizotolewa kwa wafu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "sadaka ambazo walitoa kwa wafu"

kwa wafu

"Wafu" ina maana ya sanamu na miungu ambayo Waisraeli walikuwa wakiabudu. "Kwa miungu ambao wamekufa" au "kwa miungu ambayo haina uhai"

tauni ikazuka

"tauni ikasambaa"

Wakachochea hasira yake

"ikamkasirisha"

Psalms 106:30

Kisha Finehasi akainuka kuingilia kati

Finehasi aliingilia kati miongoni mwa watu, kuwaadhibu kwa dhambi zao. Hii inaweza kufanywa wazi. "Kisha Finehasi akainuka kuingilia kati miongoni mwa watu kwa sababu ya dhambi yao"

Ilihesabika kwake kuwa tendo la haki

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu walitambua lile kuwa tendo la haki"

Psalms 106:32

Meniba

Hii ni sehemu.

aliteseka kwa sababu yao

Musa aliteseka kwa sababu ya dhambi za watu. Hapa neno "yao" ni kiwakilishi nomino kwa ajili ya watu na mfano wa maneno kumaanisha dhambi yao. "aliteseka kwa sababu ya matendo yao"

lakini walichangamana na mataifa

Hapa Daudi anazungumzia watu kuoana na wanawake kutoka mataifa mengine kama "kujichanganya" pamoja nao. "lakini walijichanganya katika ndoa na mataifa mengine"

ambayo ikawa mtego kwao

Sanamu zikawa mtego kwao.

Psalms 106:37

Walimwaga damu isiyo na hatia, damu ya wana wao na binti zao

Msemo "kumwaga damu" ni tasifida inayoelezeka kutumika kwa ajili ya "mauaji". "Walimwaga damu isiyo na hatia walipowaua wana na binti zao"

Walinajisiwa kwa matendo yao

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Matendo yao yaliwachafua"

katika matendo yao wakawa kama kahaba

Hapa Daudi analinganisha kutokuwa waaminifu kwao kwa Yahwe kwa kutokuwa waaminifu kwa kahaba. "walikuwa hawana uaminifu kwa Yahwe kama kahaba"

Psalms 106:40

Kwa hiyo Yahwe alikuwa na hasira na watu wake ... akawadharau watu wake mwenyewe

"Kwa hiyo Yahwe alikuwa na hasira na watu wake na akawadharau"

Akawakabidhi katika mkono wa mataifa

Hapa "mkono" una maana ya uwezo na utawala. "Mungu aliruhusu mataifa kuwatawala"

wale waliowachukia

"watu waliowachukia"

Psalms 106:42

na wakaletwa chini ya mamlaka yao

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na adui zao walisababisha wao kuwa chini ya mamlaka yao"

wakashushwa chini kwa dhambi yao wenyewe

Hapa msemo "kushushwa chini" ina maana ya kuangamizwa. Pia, hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "dhambi yao iliwaharibu"

Psalms 106:44

Hata hivyo

"Ingawa" au "hata hivyo".

dhiki yao

"mateso yao"

akaweka akilini

Msemo "kuweka akilini" ina maana ya kukumbuka jambo. "alikumbuka"

na akatulia

"na akawa na rehema kwao"

wanaowashinda

"waliowakamata". Hii ina maana ya maadui wa Waisraeli ambao waliwakamata.

kuwa na huruma kwao

"kuwa na huruma kwao"

Psalms 106:47

Taarifa ya Jumla

Hapa 106.48 ni zaidi ya mwisho wa zaburi. NI kauli ya kufunga kwa kitabu chote cha 4 cha Zaburi, ambacho kinaanaza katika Zaburi 90 na kukamilika na Zaburi 106.

Na Yahwe Mungu wa Israeli asifiwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na watu wamsifu Yahwe Mungu wa Israeli"

kwa jina lako takatifu

Hapa Yahwe ina maana ya "jina lake takatifu". "kwako"

kutoka milele mpaka milele

Hii ina maana ya tofauti kubwa na ina maana ya muda wote. "kwa milele yote"

Psalms 107

Psalms 107:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

uaminifu wa agano lako huduma milele

"upendo wake wa uaminifu kwangu hautaisha"

waliokombolewa na Yahwe

"Waliokombolewa" inamaanisha watu ambao Yahwe amewaokoa. "wale ambao Yahwe amewaokoa"

waongee

Hii inamaanisha kuwaambia wengine kuhusu kitu. "waambie yale Yahwe aliyofanya"

kutoka mkono wa adui

Hapa "mkono" unamaanisha nguvu. "kutoka kwenye nguvu ya adui"

kutoka mashariki ... na kutoka kusini

Hapa pande nne zinatolewa kusisitiza kwamba atawakusanya kutoka kila sehemu. "kutoka kila upande" au "kutoka kila sehemu ya dunia"

kutoka mashariki na kutoka magharibi, kutoka kaskazini na kutoka kusini

Hii inafafanua sehemu ambapo Yahwe anawakusanyia watu wake. "amewakusanya kutoka mashariki na kutoka magharibi, kutoka kaskazini na kutoka kusini"

Psalms 107:4

walizurura

"Baadhi ya watu walizurura"

katika njia ya jangwani

"kwenye barabara lililokuwa jangwani"

wakuishi

"Ambayo wanliweza kuishimo"

Kisha wakamuita Yahwe katika shida yao

Inaashiriwa kuwa wanaomba kwa Yahwe ili awasaidie. "Kisha wakaomba kwa Yahwe kuwasaidia katika shida yao"

dhiki

"tabu" au "mateso"

Psalms 107:8

O watu wamsifu Yahwe kwa uaminifu wake wa agano

"Acha watu wamsifu Yahwe kwa sababu anawapenda kwa uaminifu" au "Watu wanapaswa kumsifu Mungu kwa sababu ya upendo wake wa uaminifu." Hapa neno "O" linatumika kuonesha hamu kubwa ya watu kumsifu.

wanadamu

"watu"

Kwa kuwa anaridhisha hamu za wale walio na kiu

"Kwa kuwa anawapa maji wanaotamani - kwa wale walio na kiu"

na hamu za wale walio na njaa anawajaza na vitu vizuri

"na kwa wale walio na njaa sana na hamu ya chakula, anawapa vitu vizuri vya kula"

kwa wanadamu

"kwa watu wote"

Baadhi waliketi

Inadokezwa kwamba hawa ni watu ambao Yahwe aliwaokoa. "Yahwe pia aliwaokoa watu walioketi"

gizani na kwenye utusitusi

"Gizani" na "utusitusi" zina maana sawa na zinatumika kusisitiza jinsi gereza lilivyokuwa giza. "katika giza kabisa"

Psalms 107:11

waliasi dhidi ya neno la Mungu ... kukataa maagazi ya Aliye juu.

Misemo hii ina maana sawa na inasisitiza jinsi walivyomuasi Mungu, ambayo ndio sababu ya kufungwa.

Alinyenyekesha mioyo yao kupitia ugumu

Hapa moyo unamaanisha mtu, lakini mahususi mapenzi yake. "Aliwanyenyekesha kwa kuwaruhusu wapitie magumu"

ugumu

Maana zinazowezekana ni 1) "tabu" au 2) "kazi ngumu"

walijikwaa na hakuwepo mtu kuwasaidia kuinuka

Neno "kujikwaa" linamaanisha wakati watu hawa walijikuta kwenye nyakati ngumu sana. "waliingia taabuni na hakuwepo mtu wakuwakomboa"

Kisha wakamuita Yahwe katika tabu yao

Inaashiriwa kuwa wanaomba kwa Yahwe ili awasaidie. "Kisha wakaomba kwa Yahwe kuwasaidia katika shida yao"

dhiki yao

"taabu" au "mateso"

akawatoa

Hapa Daudi anaelezea Yahwe kuwaokoa kutoka dhiki yao kana kwamba dhiki ilikuwa sehemu ya kimwili ambayo alikuwa akiwatoa.

Psalms 107:14

Akawatoa

"Yahwe akawaleta wale walikuwa gerezani"

gizani na kwenye utusitusi

"Gizani" na "utusitusi" zina maana sawa na zinatumika kusisitiza jinsi gereza lilivyokuwa giza. "katika giza kabisa"

O watu wamsifu Yahwe kwa uaminifu wake wa agano

"Acha watu wamsifu Yahwe kwa sababu anawapenda kwa uaminifu" au "Watu wanapaswa kumsifu Mungu kwa sababu ya upendo wake wa uaminifu." Hapa neno "O" linatumika kuonesha hamu kubwa ya watu kumsifu.

Kwa kuwa

"Kwa sababu"

Kwa kuwa amevunja malango ya shaba na kukata mapingo ya chuma

Misemo hii miwili inaelezea Yahwe anavyowafungua watu kutoka gerezani na inatumika kusisitiza kwamba Yahwe kweli aliwaweka huru. "Aliwaweka huru watu wake kutoka gerezani"

Psalms 107:17

Walikuwa wapumbavu katika njia zao za uasi

"Walikuwa wapumbavu jinsi walivyoasi dhidi ya Yahwe"

na kuteswa

"na waliteseka." Kwa bayaba waliteseka kwa kuugua. "na wakawa wagonjwa"

wakaja karibu na malango ya kifo

Hapa tendo la "kufa" linaelezwa kama sehemu, "malango ya kifo" "kidogo wafe"

Kisha wakamuita Yahwe katika tabu yao

Inaashiriwa kuwa wanaomba kwa Yahwe ili awasaidie. "Kisha wakaomba kwa Yahwe kuwasaidia katika shida yao"

Psalms 107:20

Alituma neno lake na kuwaponya

Hapa Daudi anaeleza Yahwe kuzungumza kama kutuma maneno yake kana kwamba yalikuwa mjumbe. Maana zinazowezekana ni 1) "Aliamuru waponywe na wakaponywa" au 2) "Aliwatia moyo na kuwaponya"

O watu wamsifu Yahwe kwa uaminifu wake wa agano

"Acha watu wamsifu Yahwe kwa sababu anawapenda kwa uaminifu" au "Watu wanapaswa kumsifu Mungu kwa sababu ya upendo wake wa uaminifu." Hapa neno "O" linatumika kuonesha hamu kubwa ya watu kumsifu.

ya shukrani

"zinazoonesha kuwa wanashukuru"

kwa kuimba

"kwa kuimba kuyahusu"

Psalms 107:23

na kufanya biashara ng'ambo

Walikuwa wakisafari sehemu za ng'ambo na kununua na kuuza vitu na watu huko. "kuuza vitu kwenye miji ya mbali"

Psalms 107:25

aliamuru na kuamsha dhoruba unaotikisa bahari

"aliamuru upepo na kuusababisha kuwa dhoruba kubwa iliyolitikisa bahari"

dhoruba

upepo wenye nguvu nyingi sana ambao mara nyingi unaambatana na mvua kali

unaotikisa bahari

Hapa Daudi anaelezea upepo unaosababisha mawimbi kuwa juu kana kwamba mawimbi ni kitu kinachokoroga kitu kwa nguvu. ""uliosababisha mawimbi ya baharini kuwa juu sana"

Wakafika juu mbinguni; wakashuka chini vilindini

Hii inaelezea kuinuka na kushuka kwa meli na mawimbi. Kupanda juu kabisa hadi mawinguni na kushuka chini kwenye vilindi ni kukuza maneno ili kuonesha jinsi dhoruba ilivyokuwa mbaya. "meli zao ziliinuka juu sana kwenye mawimbi na kisha kudondoka chini sana katikati ya mawimbi"

Maisha yao yaliyeyuka kwa dhiki

Lugha hii inaelezea uoga wa mabaharia. "Wanaume waliogopa sana na kuwa na dhiki sana"

walikuwa wamechanganyikiwa

Msemo "kuchanganyikiwa" unamaanisha hawakujua nini cha kufanya. "na hawakujua chakufanya." au "hawakuwa na wazo la nini cha kufanya"

Psalms 107:28

Kisha wakamuita Yahwe katika tabu yao

Inaashiriwa kuwa wanaomba kwa Yahwe ili awasaidie. "Kisha wakaomba kwa Yahwe kuwasaidia katika shida yao"

Kisha waka...

Wanaozungumziwa hapa ni mabaharia.

Akatuliza dhoruba

"Akafanya upepo ukome"

mawimbi yakatulia

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "akafanya mawimbi yatulie"

akawaleta

"akawaongoza"

bandari waliyotaka

"kwenye bandari waliotaka kwenda"

Psalms 107:31

O watu wamsifu Yahwe kwa uaminifu wake wa agano

"Acha watu wamsifu Yahwe kwa sababu anawapenda kwa uaminifu" au "Watu wanapaswa kumsifu Mungu kwa sababu ya upendo wake wa uaminifu." Hapa neno "O" linatumika kuonesha hamu kubwa ya watu kumsifu.

wamsifu katika baraza la wazee

"wazee wanapokaa pamoja." Wazee waliketi pamoja kuzungumzia maswala ya jamii na kufanya maamuzi kwa ajili ya jamii.

Psalms 107:33

Anageuza

"Yahwe anafanya"

kwa sababu ya uovu wa watu wake

"kwa sababu watu wanaoishi hapo ni waovu"

Anageuza jangwa kuwa bwawa la maji na nchi kavu kuwa chechemi za maji

Misemo hii yote miwili ina maana ya kufanana na inasisitiza jinsi Yahwe anavyofanya maji yatokee jangwani. "Hufanya chemchemi na maziwa katika ardhi iliyokuwa jangwa"

Psalms 107:36

Anawatuliza walio na njaa huko

Hapa neno "huko" linamaanisha sehemu ambazo Yahwe alifanya chechemi na maziwa kutokea. Pia msemo "walio na njaa" inamaanisha watu walio na njaa. "Yahwe anafanya watu walio na njaa kuishi huko"

kupanda mashamba ya mizabibu

"ya kupandia mizabibu"

na kuleta mavuno tele

"ili walete mavuno tele"

kwa hiyo wanakuwa wengi sana

"ili watu wao wawe wengi sana"

Haachi ng'ombe wake wapungue idadi

Hii inaweza kuelezwa katika hali chanya. "Huweka ng'ombe wao kuwa wengi sana"

Psalms 107:39

Walipunguzwa

Wanaozungumziwa hapa ni watu waliokuwa na njaa na Yahwe kuwatuliza katika nchi. Sentensi hii inaeleza jinsi walivyokuwa kabla ya Yahwe kuwatuliza katika nchi.

Walipunguzwa na kuletwa chini

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Viongozi wao walipunguza idada yao na kuwaleta chini"

Walipunguzwa

"wakawa wachache kwa idadi"

kuletwa chini

Hiiinamaanisha kuaibishwa. "kuaibishwa"

Humwaga dharau

Hapa Daudi anazungumzia Yahwe kuwaonesha dharau viongozi kana kwamba dharau ni kuletwa chini alichowamwagia. "kuwaonesha dharau"

kwa viongozi

"wakubwa." Hii namaanisha viongozi waliowakandamiza watu. "viongozi waliowakandamiza"

ambapo hakuna mabarabara

"ambapo watu hawaendi"

Psalms 107:41

Lakina ana...

"Lakini Yahwe"

wahitaji

Hii inamaanisha watu wahitaji. "watu wahitaji" au "watu maskini"

hujali familia zake kama kundi

Hapa Daudi analinganisha jinsi Yahwe anavyowajali watu wake na jinsi mchungaji anavyojali kondoo wake. Maana zinazowezekana ni 1) "hufanya idadi ya watu kwatika famila zao kuongezeka kama kundi" au 2) "huwajali kama mchungaji anavyojali kondoo wake"

Wanyofu

Hii inamaanisha watu wanaoishi maisha ya unyofu. "Watu wanyofu" au "Watu wanaofanya kilicho sawa"

uovu wote

Hapa watu waovu wanazungumziwa kama "uovu." "watu wote waovu"

huziba mdomo

hii inamaanisha kutokujibu kitu. "hana kitu cha kumjibu Yahwe"

ayaangalie mambo haya yote

Hii namaanisha kuwaza vitu hivi. "kuwaza kuhusu hivi vitu" au "kukumbuka hivi vitu"

Psalms 108

Psalms 108:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Moyo wangu uko thabiti, Mungu

Hapa Daudi anajitambulisha kwa moyo wake. Pia, neno "thabiti" inamaanisha kuamini kabisa. "Moyo wangu uko thabiti kwako, Mungu" au "Nakuamini wewe kabisa, Mungu"

Nitaimba sifa pia na moyo wangu uliotukuzwa

Hapa Daudi anajitambulisha kama kuwa na heshima ya kumsifu Mungu. "Unaniheshimu kwa kuniruhusu kukuimbia sifa"

Amka, kinanda na kinubi

Hapa Daudi anaeleza kucheza vyombo kama kutembea kutoka usingizini. "Nitakusifu kwa kucheza kinanda na kinubi"

Nitaamsha alfajiri

Hapa Daudi anaeleza alfajiri kuamka kama mtu kuamka asubuhi. "Nitakuwa nikikusifu alfajiri ifikapo"

alfajiri

jua linapochomoza.

Psalms 108:3

Kwa kuwa uaminifu wako wa agano ni mkuu ... uaminifu wako unafika mawinguni

Misemo hii miwli ina maana ya kufanana. Inalinganisha ukuu wa uaminifu wa agano wa Yahwe na uaminifu wake kwa ukuu wa jinsi mbingu zilivyo juu ya nchi. "uaminifu wako wa agano na uaminifu wako ni zaidi ya umbali kati ya mbingu na nchi"

Psalms 108:5

Utukuzwe Mungu, juu ya mbingu

Mwandishi wa zaburi anamuomba Mungu kuonesha kuwa ametukuzwa. Kutukuzwa juu ya mbingu inaonesha kuwa mkuu. "Mungu, onesha kuwa umetukuzwa juu ya mbingu" au "Mungu, onesha kuwa umetukuzwa juu ya mbingu" au "Mungu, onesha kuwa wewe ni mkuu mbinguni"

utukufu wako uinuliwe

Hapa Yahwe anaoneshwa kwa "utukufu" wake. "utukuzwe"

Ili wale uwapendao waokolewe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kwa sababu wale uwapendao wanahitaji kuokolewa" au "Okoa wale unaowapenda"

kwa mkono wako wa kuume

Hapa "mkono wa kuume" wa Yahwe unamaanisha nguvu yake. "kwa nguvu yako"

nijibu

Kumjibu hapa inamaanisha kujibu ombi lake. "jibu ombi langu"

Psalms 108:7

Mungu amezungumza katika utakatifu wake

Hapa Daudi anaeleza Mungu kusema kitu kwa sababu ni mtakatifu kama kuzungumza "katika utakatifu wake," kana kwamba utakatifu wake ni kitu ambacho yuko ndani yake. "Mungu, kwa sababu ni mtakatifu, amesema"

Nitaigawa Shekemu na kuligawa bonde la Sukothi

Hapa Mungu anazungumza kuhusu kuigawa nchi ya Shekemu na bonde la Sukothi.

kugawa

kugawa katika vipande

Efraimu ni kofia yangu pia

Mungu analizungumzia kabila la Efraimu kana kwamba lilikuwa jeshi lake. Kofia ya chuma inaashiria kifaa cha vita. "Efraimu ni kama kofia ya chuma niliochagua kwa ajili ya vita" au "Kabila la Efraimu ni jeshi langu"

kofia ya chuma

Kofia ngumu ambayo askari huvaa kulinda vichwa vyao dhidi ya majeraha.

Yuda ni fimbo yangu

Mungu alichagua watu kutoka kabila la Yuda kuwa wafalme wa watu wake, na analizungumzia hilo kabila kama vile ni fimbo yake. "Kabila la Yuda ni kama fimbo yangu" au "Yuda ni kabila ambayo natawalia watu wangu"

Psalms 108:9

Moabu ni bakuli langu la kunawia

Mungu anaizungumzia Moabu kutokuwa muhimu kana kwamba Moabu ilikuwa bakuli la kunawia au mtumishi wa chini sana. "Moabu ni kama bakuli ninalotumia kunawa"

juu ya Edomu niturusha kiatu changu

Inawezekana kwamba Mungu alikuwa akizungumzia kuimiliki Edomu kana kwamba alikuwa akitupa kiatu chake kama ishara ya kuonesha kuwa anapamiliki. Lakini matoleo mengine yana tafsiri tofauti. "Ninaimiliki nchi ya Edomu" au "Ninarusha kiatu changu katika nchi ya Edomu kuonesha kuwa ni yangu"

Psalms 108:11

Taarifa ya Jumla:

lakina angalia kuwa 108:11 haina maneno "Lakini wewe," kama mwanzo wa 60:10.

Mungu, je haujatukataa?

Mwandishi wa zaburi anatumia swali hili kuonesha huzuni yake kwamba inaonekana Mungu amewakataa. "Inaonekana kama umetukataa" au "Mungu, unaonekana kututelekeza"

Hauendi vitani na jeshi letu

Mwandishi wa zaburi anazungumzia Mungu kulisaidia jeshi lao kana kwamba Mungu alikuwa akienda kupiga pamoja nao. "haulisaidii jeshi letu tunapoenda kupambana"

hauna maana

"batili"

tutashinda

kuwa na ushindi

atawakanyaga chini adui zetu

Mwandishi wa zaburi anamzungumzia Mungu kusaidia jeshi lao kuwashinda maadui kana kwamba Mungu alikuwa wa kuwaganyaga chini maadui." "atatuwezesha kuwakanyaga chin maadui" au "atatufanya tuweze kuwashinda maadui wetu"

Psalms 109

Psalms 109:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Kwa waovu na waongo

Maneno "uovu" na "uongo" inamaanisha watu. Zina maana yakufanana na inasisitiza jinsi watu hawa walivyo waovu. "Kwa wanaume waovu na waongo"

Psalms 109:4

Baada ya upendo wangu wananikashifu

"Ingawa niliwapenda, wananishtaki"

upendo wangu

"upendo wangu kwao"

wananikashifu

Wanaomkashifu ni wale watu waovu na waongo.

Psalms 109:6

Weka mtu mwovu ... weka mshitaki

Misemo hii miwili iko sambamba na misemo "mtu mwovu" na "mshitaki" inamaanisha mtu yule yule.

kwenye mkono wake wa kuume

"kwenye mkono wake wa kuume wa adui yangu"

Akihukumiwa, akutwe na hatia

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Anapokuwa anashtakiwa, hakimu ampate na hatia"

maombi yake yafikiriwa kuwa ya dhambi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "fikiria maombi yake kama dhambi"

Psalms 109:8

Siku zake ziwe chache

Usemi huu "Siku zake" unamaanisha urefu wa maisha yake. "Asiishi maisha marefu"

ofisi yake

"nafasi yake ya mamlaka"

misaada

chakula au fedha inayopewa kwa ombaomba

nyumba zao zilizoharibika

"waliangamiza nyumba"

Psalms 109:11

Mdai

mtu anayeazimisha fedha kwa mtu mwingine lakini anategemea huyo mtu alimpe.

wapore

"waibe"

Watoto wake wakatwe; jina lao lifutwe

Misemo hii miwili inamaana ya kufanana na inasisitiza watoto wake kuangamizwa.

Watoto wake wakatwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kusababisha watoto wake kukatwa" au "Kusababisha watoto wake kufa"

jina lao lifutwe katika kizazi kijacho

Hapa wazo la kutokuwepo na mtu kuendeleza jina la familia inazungumziwa kama "jina lao kufutwa." "asiwepo mtu kuendeleza jina lake"

Psalms 109:14

Dhambi za mababu yake zitajwe kwa Yahwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na ukumbuke dhambi za mababu zake, Yahwe"

na dhambi ya mama yake isisahaulike

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na usisahau dhambi ambazo mama yake alitenda"

Na hatia yao daima iwe mbele ya Yahwe

Hapa Daudi anazungumzia Yahwe kuwaza kuhusu hatia yao kana kwamba hatia yao ni kitu cha kimwili kilicho mbele yao. "Na Yahwe aendelee kufikiria kuhusu dhambi zao"

Yahwe akate kumbukumbu yao kutoka duniani

Daudi anatumia neno "dunia" kumaanisha watu wote wanaoishi duniani. Pia, msemo "kumbukumbu yao" inamaanisha watu kuwakumbuka baada ya kufa. "na Yahwe afanye kwamba watu duniani wasiwakumbuke"

mtu huyu hajawahi kuhangaika kuonesha uaminifu wowote wa agano

Hii inamaanisha yeye kuonesha uaminifu wa agano kwa watu. "mtu hakuhangaika kuonesha uaminifu wa agano kwa watu"

waliokandamizwa, wahitaji

Hii inamaanisha watu waliokandamizwa na wahitaji. "watu waliokandamizwa, watu wahitaji"

waliovunjika moyo

Hii inamaanisha watu waliovunjika moyo. "watu waliovunjika moyo" au "watu waliokata tamaa"

hadi kifo

"hadi wafe." Hii inamaanisha kuwa aliwatesa hadi walipokufa.

Psalms 109:17

na imrudie juu yake

"laana zake zije juu yake"

Alijivika kwa kulaani kama vazi lake

Daudi anazungumzia tabia ya mtu mwovu kana kwamba ni vazi lake. "Aliwalaani watu wengine mara nyingi kama avaavyo nguo. au "Aliwalaani watu muda wote"

kama vazi lake

"kana kwamba yalikuwa mavazi yake"

laana ikaja kwake kama maji, kama mafuta kwenye mifupa yake

Maana zinazowezekana ni: 1) Alizungumza laana sana hadi zikawa sehmu ya utambulisho wake. "laana anazozungumza ni sehemu yake alivyo" au 2) laana alizozizungumza zilimtokea yeye. "yeye mzima alilaaniwa kwa laana aliyozungumza"

kama maji

Hii inamaanisha jinsi mtu alivyokunywa maji. "kama maji ambayo mtu hunywa"

kama mafuta kwenye mifupa yake

Hii inamaanisha jinsi mafuta yanavozama kwenye mifupa yanapopakwa kwenye ngozi. "kama mafuta ya mzeituni yanavyozama kwenye mifupa ya mtu yanapopakwa kwenye ngozi yake"

Psalms 109:19

Laana zake ziwe kwake kama nguo avaazo kujifunika

Watu walivaa nguo zao kila siku. Daudi anamzungumzia yeye kufunikwa na laana kama kufunikwa na nguo. "Acha laana zake ziwe juu yake kila siku kama nguo avaazo"

kama mshipi ambao hua huvaa

Maneno haya yanaweza kuongezwa. "na acha laana zake daima ziwe juu yake kama mshipi auvaao"

Na hii iwe dhawabu yake

"Na laana hizi ziwe dhawabu yake"

Psalms 109:21

unitendee kwa fadhila

Hili ni ombi kwa Yahwe kumtendea kwa fadhila. "nitendee kwa fadhili"

kwa ajili ya jina lako

"kwa ajili ya sifa yako"

nimekandamizwa na muhitaji

Maneno haya mawili yana maana ya kufanana na yanasisitiza kuwa hawezi kujisaidia.

moyo wangu umeumia ndani yangu

Hapa daudi anazungumzia kukata tamaa kama moyo wake kuumia. "nimejaa majonzi na kukata tamaa"

Ninafifia kama kivuli ... kama nzige

Daudi anahisi kama anataka kufa na anaeleza hisia hii kwa kujifananisha na kivuli kinachofifia na jinsi upepo unavyopuliza nzige. "Nahisi kama nataka kufa, kama kivuli cha jioni kitakacho potea punde, kama nzige anavyopulizwa kirahisi na upepo"

Psalms 109:24

Magoti yangu yamechoka

Hii inamaanisha kuwa ameishiwa nguvu na vigumu kwake kusima. "Nina wakati mgumu kusima" au "Mwili wangu umechoka"

kutokana na kufunga

"kwa sababu sili chakula chochote"

Ninageuka kuwa ngozi na mifupa

Hii inamaanisha amepoteza uzito mwingi. "mwili wangu umekonda sana"

Ninadharauriwa na washtaki wangu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "washtaki wangu wananidhihaki"

wanatikisa vichwa vyao

Hili ni tendo la kutokukubali.

Psalms 109:26

Na wajue

Wanaozungumziwa ni washtaki wa Daudi na watu wanaosema vitu vibaya kumhusu.

umefanya hili

"umeniokoa"

Psalms 109:28

Ingawa wananilaani

Wanaozungumziwa ni watu wanaomshtaki Daudi na kusema vitu vibaya kumhusu.

na waaibishwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na waaibike" au "acha waaibike"

lakini watumishi wako wafurahi

"lakini mimi, mtumishi wako, nifurahi" au "mimi ni mtumishi wako, acha nifurahi." Daudi anatumia msemo "mtumishi wako" kumaanisha ni yeye.

Na washindani wangu wavikwe ... na wavae

Misemo hii miwili ina maana ya kufanana na inatumika kusisitiza jinsi anavyotamani sana waaibishwe.

wavikwe aibu

Hapa Daudi anawazungumzia kuaibika kana kwamba ilikuwa vazi walilovaa. "waaibike sana"

na wavae aibu yao kama joho

Daudi anawazungumzia kuaibika kana kwamba ilikuwa joho walilovaa. "na aibu yao iwafunike kama joho walilojifunika"

Psalms 109:30

Kwa mdomo wangu natoa

Hii inamaanisha kuwa atazungumza. "Nitazungumza na kutoa"

atasimama mkono wa kuume wa yule aliye mhitaji

Hii inamaanisha atamsaidia na kumtetea mtu maskini. "atamtetea mtu aliye mhitaji"

Psalms 110

Psalms 110:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Keti mkono wangu wa kuume

Msemo "mkono wangu wa kuume" unamaanisha sehemu ya heshima. "Keti sehemu ya heshima niliyokuandalia"

niwaweke adui zako chini ya miguu yako

Hapa Dauddi anamuelezea Yahwe kuwaweka adui wa bwana wake chini ya uwezo na mamlaka yake kama kuwaweka chini ya miguu yake. "umewaweka adui zako chini ya uwezo wako"

Psalms 110:2

Taarifa ya jumla:

Daudi anaendelea kuzungumza na mfalme

Yahwe ataishikilia fimbo ya nguvu yako

Hapa Daudi anamzungumzia Yahwe kupanua eneo analotawala mfalme kama kushikilia fimbo yake. "Yahwe atapanua eneo ambalo unatawala kwa uwezo"

tawala juu ya adui zako

"Mfalme, tawala kati ya adui zako." Hii inasemwa kwa mfalme kama amri.

kwa hiari yao wanyewe

"kwa uamuzi wao." Hii inamaanisha watachagua kumfuata mfalme.

katika siku ya uwezo wako

Hii inamaanisha siku ambayo mfalme atawaongoza watu wake vitani. Hii inaweza kuelezwa wazi. "katika siku utakapoliongoza jeshi lako vitani"

kutoka tumbo la alfajiri ... kama umande

Daudi anaelezea umande kama mtoto ambaye anazaliwa na umande. "asubuhi ... kama umande"

kutoka tumbo la alfajiri ujana wako utakuwa kwako kama umande

Daudi anamwambia mfalme kuwa atakuwa na nguvu za ujana kila asubuhi kwa kumfananisha na jinsi umande unavyotokeza mapema kila asubuhi. "kila asubuhi utajazwa na nguvu za ujana kukuhimili kama kila asubuhi umande unavyotokea kumwagilia na kuhimili ardhi"

Psalms 110:4

Wewe ni

Yahwe anazungumza na bwana.

hautabadilika

Hii inamaanisha kwamba hatabadili alichosema. "hatabadili mawazo yake" au "hatabadili alichosema"

baada ya mfano wa Melkizedeki

Maneno yasiyokowepo yanaweza kuongezwa. "baada ya mfano alivyokuwa kuhani Melkizedeki" au "katika njia ile ile alivyokuwa kuhani Melkizedeki"

Psalms 110:5

Bwana yu mkono wako wa kuume

Bwana anapokwenda vitani, Yahwe husimama mkono wake wa kuume ili kumsaidia. "Bwana anakusaidia vitani"

Bwana

Neno "Bwana" linamaanisha Yahwe.

Atawaua

Atakaye waua ni Yahwe. Atasababisha wafalme washindwe na kufa, lakini ataruhusu majeshi ya mfalme kuwaua waflame maadui. "Atasababisha wafalme wafe" au "Ataruhusu jeshi lako liwaue wafalme wote"

wafalme

Hii inamaanisha adui zake. "wafalme adui"

katika siku ya hasira yake

Hapa Daudi anazungumzia siku ambayo Yahwe atakasirika na kuwaangamiza wafalme kama "siku ya hasira yake." "katika siku ya hukumu ambapo uvumilivu wake utageuka kuwa hasira"

atajaza viwanja vya mapambano na miili iliyokufa

Hii inamaanisha kuwa Yahwe atasababisha hiki kitokee, sio kwamba atawaua watu wote mwenyewe watakaokufa vitani. "atasababisha viwanja vya mapambano kujazwa na miili iliyokufa"

atawaua viongozi katika nchi nyingi

Hii inamaanisha kuwa Yahwe atasababisha hiki kitokee, sio kwamba atawaua viongozi wenyewe. "atasababisha viongozi katika nchi nyingi kuuawa" au "ataruhusu viongozi katika nchi nyingi kufa"

Psalms 110:7

Atakunywa kwenye kijito njiani

Mfalme anasimama kidogo tu kwa ajili ya kinywaji na kisha anaendelea kuwafuatilia adui zake. "Akiwa anawafuatilia adui zake, atasimama tu kunywa kwenye kijito"

kwenye kijito

Hii inamaanisha kuwa atakunywa maji kutoka kwenye kijito. Kijito ni mto mdogo. "atakunywa maji kutoka kwenye kijito"

na kisha

"kwa hiyo"

atainua kichwa chake

Maana zinazowezekana ni 1) mfalme anainua kichwa chake mwenyewe au 2) Yahwe anainua kichwa cha mfalme.

atainua kichwa chake juu baada ya ushindi

Watu waliinua vichwa vyao walipokuwa washindi, walipojiamini na walipokuwa wenye furaha. "atainua kichwa chake kwa kujiamini baada ya ushindi" au "atakuwa mshindi"

Psalms 111

Psalms 111:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kihebrania.

kwa moyo wangu wote

Hapa neno "moyo" inawakilisha mtu kamili na hisia. "kwa kila kitu nilivyo"

katika kusanyiko la wanyofu, katikati yao

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na inaweza kuunganishwa kama ikihitajika. "katika mkusanyiko wa watu wanyofu"

yanasubiriwa kwa hamu na wale wote wanaoyatamani

Yanaosubiriwa ni "matendo ya Yahwe." HIi inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wale wote wanaotamani kazi za Yahwe wanasubiri kwa hamu"

yanasubiriwa kwa hamu

Maana zinazowezekana ni 1) "kutafuta" au 2) "kusoma"

Psalms 111:4

ambayo yatakumbukwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambayo watu watakumbuka daima"

atakumbuka

"ataitisha akilini"

matendo yake makuu

"matendo yake yaliyoonesha nguvu yake"

urithi wa mataifa

Mwandishi anazungumzia nchi iliyokuwa ya mataifa ya Kanaani kana kwamba ilikuwa urithi wao. "nchi iliyokuwa ya mataifa mengine"

Psalms 111:7

Kazi za mikono yake

Hapa neno "mikono" inamaanisha Yahwe, mwenyewe. "Kazi anazofanya"

Imethibitika milele

Hii inamaanisha kuwa maelezo ya Yahwe hayabadiliki na yanadumu milele. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Amezithibitisha milele" au "Zitadumu milele"

kuangaliwa kwa uaminifu na vizuri

Maana zinazowezekana ni 1) Yahwe ametoa maelezo yake katika namna ya uaminifu na iliyo sawa au 2) watu wake wanapaswa kuangalia maelezo ya Yahwe kwa namana ya uaminifu na iliyo sawa. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa watu wake kuziangalia kwa uaminifu na vizuri"

mtakatifu na la ajabu ni jina lake

Hapa neno "jina" linamaanisha Yahwe mwenyewe. "Yahwe ni mtakatifu na waajabu"

Psalms 111:10

mwanzo wa hekima

Neno "hekima" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "hatua ya kwanza ya kuwa na hekima" au "kitu muhimu zaidi kuwa na hekima"

wale wanaobeba maelekezo yake

"wale wanaotii maelezo yake"

Sifa yake huduma milele

Neno "sifa" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "Watu watamsifu milele"

Psalms 112

Psalms 112:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

anayefurahi sana

"unafurahia sana"

uzao wa mnyofu utabarikiwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe ataubariki uzao wa mtu mnyofu"

Psalms 112:3

Taarifa ya Jumla:

Mtu anayeimba wimbo huu anaendelea kumwelezea mtu anaye mheshimu sana Yahwe.

Mali na utajiri uko nyumbani mwake

Hapa neno "nyumba" inamaanisha familia. Maneno "Mali" na "utajiri" yanamaanisha kitu kimoja na yanaashiria utajiri mkubwa. "Familia yake ilikuwa tajiri sana"

Nuru hung'aa gizani kwa ajili ya mtu mnyofu

Mwandishi anamzungumzia Mungu kumbariki mtu mnyofu katika nyakati ngumu kana kwamba ilikuwa ni nuru inang'aa gizani. "Baraka ambayo mtu mnyofu anapokea kutoka kwa Mungu ni kama nuru inayong'aa gizani"

hukopesha fedha

Taarifa inaweza kuwekwa wazi. "anakopesha fedha zake kwa watu wengine."

Psalms 112:6

Taarifa ya Jumla:

Mtu anayeimba wimbo huu anaendelea kumwelezea mtu anaye mheshimu sana Yahwe.

Kwa kuwa hatasogezwa

hatasumbuliwa au kuzidiwa kwa hali yoyote kwa kuwa imani yake iko katika Yahwe. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa kuwa hakuna kitu kitakachomsogeza"

kwa kuwa mtu mwenye haki atakumbukwa milele

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu watamkumbuka mtu mwenye haki milele"

Psalms 112:8

Taarifa ya Jumla:

Mtu anayeimba wimbo huu anaendelea kumwelezea mtu anaye mheshimu sana Yahwe.

Moyo wake ni tulivu

"Moyo wake umethibitika." Hapo neno "moyo" inaashiria mtu. Maana zinazowezekana ni 1) "yuko na amani" au 2) "Anajiamini"

haki yake hudumu milele

"matendo yake yatadumu milele."

atatukuzwa na heshima

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atamtukuza kwa kumpa heshima"

Psalms 112:10

ataona hili

"ataona kuwa vitu vinaenda vizuri kwa mtu mnyofu." Neno "hili" linamaanisha kila kitu kizuri ambacho mwandishi alieleza katika mstari ulipoita kuhusu mtu mnyofu.

atasaga meno

Kusaga meno ilikuwa ni ishara ya daharu.

kuyeyuka

Mwandishi anamzungumzia hatima ya kifo cha mtu mwovu kana kwamba huyo mtu ni kitu, kama barafu inayoweza kuyeyuka. "hatimaye atakufa"

hamu ya watu waovu itaangamia

Maana zinazowezekana za "hamu" ni 1) hamu ya kihisia waliyo nayo watu waovu. "vitu ambavyo watu waovu wanataka kufanya havitawahi kutokea" au 2) ni njia nyingine yakusema vitu ambavyo watu waovu wanatamani. "watu waovu watapoteza vitu wanavyotamani"

Psalms 113

Psalms 113:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

jina la Yahwe

Hapa neno "jina" linamaanisha Yahwe mwenyewe. "Yahwe"

Psalms 113:3

Kutoka maawio ya jua hadi kuzama kwake

Hii inamaanisha upande wa mashariki ambapo jua linachomoka, na magharibi, ambapo jua linazama. Mwandishi anatumia tofauti hizi kuashiria kila sehemu duniani. "Kila sehemu duniani"

Jina la Yahwe linapaswa kusifiwa

Hapa neno "jina" linamaanisha Yahwe mwenyewe. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu wanapaswa kumsifu Yahwe"

utukufu wake unafika juu ya mbingu

Utukufu wa Mungu unazungumziwa kana kwamba ulikuwa juu sana. "utukufu wake uko juu zaidi ya mbingu" au "utukufu wake ni mkuu sana"

Psalms 113:5

Ni nani kama Yahwe Mungu wetu ... duniani?

Mwandishi anauliza swali kusisitiza kuwa hakuna mtu kama Yahwe. Hili swali la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hakuna kama Yahwe Mungu wetu ... duniani."

aliye na kiti chake juu

"aliyesimikwa juu" au "anayetawala katika nafasi ya juu zaidi"

Psalms 113:7

Anawainua maskini ... kutoka kwenye lundo la

Misemo hii miwili ina usambamba. Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwasaidia na kuwatukuza watu walio maskini kana kwamba Yahwe aliwasababisha kusimama kutoka kuketi kwenye vumbi na majivu.

kutoka mavumbini ...kutoka kwenye lundo la majivu

Kukaa kwenye mavumbi au majivu kunaashiria kati ya umaskini au kukata tamaa.

ili aketi na wakuu , na wakuu wa watu wake

Hapa msemo wa pili unaewka wazi kuwa msemo wa kwanza unamaanisha wakuu wa watu wa Yahwe. Misemo hii miwili inaweza kuunganishwa. "ili Yahwe amkalishe pamoja na wakuu wa watu wake"

Psalms 113:9

Anampa nyumba mwanamke aliyetasa

Hapa "nyumba" inamaanisha watoto wanaoishi nyumbani. "Anampa watoto mwanamke ambaye hakuwanao"

Psalms 114

Psalms 114:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Israeli iliondoka Misri, nyumba ya Yakobo kutoka kwa wageni

Mistari hii miwili ina usambamba, "Israeli" na "nyumba ya Yakobo" inamaanisha kitu kimoja na "Misri" na "watu wageni" inamaanisha watu wale wale.

nyumba ya Yakobo kutoka kwa wageni

Neno "nyumba" hapa linamaansiha familia au uzao. Kitenzi kinaweza kuwekwa kwa ajili ya huu msemo. "uzao wa Yakobo ukaondoka kutoka kwa watu wageni"

Yuda pakawa mahali pake patakatifu, Israeli ufalme wake

Maana zinazowezekana kwa ajili ya "Yuda" na "Israeli" ni 1) zinamaanisha nchi. "Nchi ya Yuda ikawa sehemu takatifu ya Yahwe, nchi ya Israeli ikawa ufalme wake" au 2) ni njia nyingine ya kusema watu wa Yuda na Israeli. "Watu wa Yuda wakawa miongoni mwa wale ambapo Yahwe aliishi, watu wa Israeli wakawa wale ambao aliwatala"

Psalms 114:3

Bahari lilitazama na kutoroka

Mwandishi anazungumzia bahari la Matete kana kwamba lilikuwa ni mtu aliyetoroka wakati Yahwe akiwaongoza watu wa Israeli kupita nchi kavu. "Ni kana kwamba bahari lilitazama na kutoroka"

Yordani ikageuka

Mwandishi anazungumzia mto Yordani kana kwamba ni mtu aliyerudi nyuma wakati Yahwe akiwaongoza watu wa Israeli kwenye nchi kavu. "ilikuwa kana kwamba Yordani ilirudi"

Milima ikaruka kama kondoo dume, vilima vikaruka kama wanakondoo

Mwandishi anazungumzia milima na vilima kana kwamba zilikuwa hai. Inawezekana anazungumzia tetemeko anapoelezea uoga wao kwenye uwepo wa Yahwe jinsi wanavyoruka kama kondoo dume na wanakondoo. "Ilikuwa kana kwamba milima ilitikisika kama kondoo dume wanaoruka na vilima vilitikisika kana kwamba wanakondoo wanavyoruka.

Psalms 114:5

Taarifa ya Jumla:

Mistari ya 5-6 ina maswali manne ya balagha. Jibu linalotarajiwa kwa kila swali linapatikana katika mstari wa 7, "kwa sababu ya uwepo wa Bwana."

uliruka kama kondoo dume ...uliruka kama wanakondoo

Mwandishi anazungumzia milima na vilima kana kwamba zilikuwa hai. Inawezekana anazungumzia tetemeko anapoelezea uoga wao kwenye uwepo wa Yahwe jinsi wanavyoruka kama kondoo dume na wanakondoo. "Ilikuwa kana kwamba milima ilitikisika kama kondoo dume wanaoruka na vilima vilitikisika kana kwamba wanakondoo wanavyoruka.

Tetemeka dunia, mbele ya Bwana, kwenye uwepo wa Mungu wa Yakobo

Misemo miwili ya mwisho ina usambamba. Kitenzi kinaweza kuwekwa kwenye mstari wa pili. "Tetemeka dunia, mbele ya Bwana, tetemeka mbele ya uwepo wa Mungu wa Yakobo"

Tetemeka dunia

Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi anazungumzia dunia kana kwamba ni mtu na anaiamuru kutetemeka kwa uoga mbele za Mungu au 2) neno "dunia" ni njia nyingine ya kusema wale wanaoishi duniani. "Tetemekeni, watu wote duniani"

Psalms 114:8

Akageuza jiwe kuwa bwawa la maji, jiwe gumu kuwa chechemi ya maji

Misemo hii mwili ina usambamba. Mwandishi anamuelezea Yahwe kusababisha maji kutiririka kutoka kwenye jiwe kana kwamba aliligeuza jiwe kuwa maji.

mwamba mgumu kuwa chechemi ya maji

Kitenzi kinaweza kutolewa kuwekwa kwenye msemo uliopita. "Akageuza jiwe gumu kuwa chemchemi ya maji"

Psalms 115

Psalms 115:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Sio kwetu, Yahwe, sio kwetu

Mwandishi anarudia msemo "sio kwetu" ili kusisitiza kwamba hawastahili kupokea heshima anayostahili Yahwe pekee. "Usilete heshima kwetu, Yahwe"

kwetu

Neno "kwetu" linamaanisha watu wa Israeli.

lakini kwa jina lako leta utukufu

Hapa neno "jina" linaashiria Yahwe mwenyewe. "lakini leta utukufu kwako mwenyewe"

kwa ajili ya uaminifu wako wa agano

"kwa sababu ya uaminifu wako wa agano"

Kwa nini mataifa yaseme, "Yuko wapi Mungu wao?"

Hili swali la balagha linasisitiza kuwa hakuna sababu ya mataifa kusema wanayosema. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Watu wa mataifa hawatakiwa kuwa na uwezo wa kusema, 'Yuko wapi Munguwao?'"

Yuko wapi Mungu wao?

Watu wa mataifa mengine wanatumia swali hili kuwadhihaki watu wa Israeli na kuonesha kuwa hawaoni Yahwe akiwasaidia. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Mungu wenu hayupo hapa kuwasaidia"

Psalms 115:3

kazi ya mikono ya watu

Hapa neno "mikono" inaashiria watu waliotengeneza hizo sanamu. "vitu ambavyo watu wametengeneza"

Psalms 115:5

Hizo sanamu zina midomo

Sanamu hazina midomo ya kweli, macho, maskio, au pua za kweli. Lakini, watu wamewaunda na mifano ya midomo, macho, maskio, na pua. Mwandishi anasisitiza kuwa sanamu haziko hai kweli. "Watu wamezipa midomo hizo sanamu"

Psalms 115:7

Hizo sanamu zina midomo

Sanamu hazina midomo ya kweli, macho, maskio, au pua za kweli. Lakini, watu wamewaunda na mifano ya midomo, macho, maskio, na pua. Mwandishi anasisitiza kuwa sanamu haziko hai kweli. "Watu wamezipa midomo hizo sanamu"

lakini hawahisi

"lakini mikono hio haihisi"

Wale wanaozitengeneza ni kama hizo sanamu, kama alivyo kila mtu anayezitegemea

Wale wanaounda na kuabudu sanamu wanakuwa bila uhai na wasio na nguvu , kama hizo sanamu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Wale wanaozitengeneza wanakosa uhai kama hizo sanamu, kama watu wengine wote wanaozitumaini"

Psalms 115:9

Israeli, mtumainini Yahwe

Neno "Israeli" linaashiria watu wa Israeli. "watu wa Israeli, mtumainini Yahwe"

msaada wenu na ngao

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni ngao kwa sababu anawalinda watu wake kama ngao inavyowalinda kutokana na madhara. "yule ambaye anawasaidia na kuwalinda"

Nyumba ya Haruni

Hapa neno "nyumba" linamaanisha familia au uzao. Msemo huu unamaanisha makuhani, walikuwa uzao wa Haruni. "Uzao wa Haruni" au "Makuhani"

Psalms 115:12

tuangali

"ametuangalia kwa makini"

familia ya Israeli

Hii inamaanisha watu wa Israeli, ambao ni uzao wa Yakobo, ambaye pia aliitwa Israeli. "watu wa Israeli"

familia ya Haruni

Hii inamaanisha makuhani, ambao ni uzao wa Haruni. "Uzao wa Haruni" au "Makuhani"

wote wachanga na wazee

"wote wadogo na wakubwa." Maana zinazowezekana ni kwamba hii inaashiria 1) hadhi katika jamii au 2) umri. Vyovyote vile, tofauti hizi mbili zinawakilisha kila mtu, bila kujali umri au hadhi katika jamii.

Na Yahwe aongeze idadi yenu zaidi na zaidi

Mwandishi anazungumzia idadi ya watoto ambayo watu wa Israeli watakuwa nayo. "Na Yahwe awazidishie idadi ya watoto wenu zaidi na zaidi"

yenu na ya uzao wenu

"wote watoto wenu na uzao wa watoto wenu." Mwandishi anaweka wazi kuwa ombi lake kwa ajili ya watoto zaidi halimaansihi kizazi cha sasa tu bali kwa uzao wao pia.

Psalms 115:15

Na mbarikiwe na Yahwe, aliyeumba mbingu na nchi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na Yahwe, aliyeumba mbingu na nchi, awabariki"

dunia amempa mwanadamu

Hii haimaanishi kuwa dunia si mali ya Yahwe, lakini amewapa binadamu dunia kama sehemu ya makao.

Psalms 115:17

Wafu

Kivumishi "wafu" kinaweza kutafsiriwa na msemo wa nomino. "Watu waliokufa"

wala yeyote anayeenda chini palipo nyamaza

Msemo huu wa usambamba unamaana sawa na msemo uliopita. Kitenzi kinaweza kuwekwa kutoka kwenye msemo uliopita kuweka maana yake wazi. "wala yeyote aendaye chini palipo nyamaza kumsifu Yahwe"

wala yeyote anayeenda chini kunyamaza

Mwandishi anazungumzia kaburi au sehemu ya wafu kama sehemu iliyo nyamaza ambapo hakuna awezaye kuzungumza. Hii ni tasifida ya kifo. "wala yeyote anayeenda sehemu ya wafu"

Lakini sisi

Neno "sisi" linamaanisha watu wa Israeli walio hai bado.

Psalms 116

Psalms 116:1

Taarifa ya jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

husikia saauti yangu na maombi yangu ya huruma

Hapa neno"sauti" linawakilisha mtu anayeongea. Msemo, "maombi yangu ya huruma" unaeleza anachokisema. "hunisikia ninapojieleza kwa ajili ya huruma"

Psalms 116:3

Taaarifa ya Jumla:

Mtu aliyetunga zaburi hii anaendelea kuzungumza.

Kamba za kifo zilinizunguka

Mwandishi anazungumzia kifo kanakwambani mtu anayeweza kumshika na kumfunga kwa kamba. "Nilihisa kama nataka kufa"

mitego ya kuzimu ilinikabili

Mwandishi anazungumzia "kuzimu," mahali pa wafu, kana kwambani mtu anayeweza kumtega kwamitego. "Nilihisi kama niko tayari kuingia kaburini"

nikalita jina la Yahwe

Hapa neno "jina" linaashiria Yahwe mwenyewe. "nikamwita Yahwe"

okoa maisha yangu

Hapa neno "maisha" linaashiria mtu. "niokoe" au "niepushe na kufa"

Psalms 116:5

Taarifa ya Jumla:

Mtu aliyetengeneza wimbo huu anaendelea kuzungumza.

wasio na hila

Hii inamaanisha watu wasikuwa na uzoefu au hawawezi kujitunza. Kivumizhi kinaweza kutafsiriwa kama msemo wanomino. "wale wasio na hila" au "wale wasiojiweza"

nililetwa chini

Mwandishi anazungumzia kunyenyekeshwa kama kuwa nafasi ya chini zaidi. "Nilikuwa sijiwezi"

Psalms 116:7

Taarifa ya Jumla:

Mtu aliyetunga zaburi hii anaendelea kuzungumza.

Nafsi yangu inaweza kurudi sehemu yake ya kupumzika

Mwandishi anazungumzia kuwa na amani na ujasiri kana kwamba ilikuwa ni sehemu ambapo nafsi yake ingeweza kupumzika. Neno "nafsi" linawakilisha mtu. "Ninaweza kupumzika kwa amani tena"

uliokoa maisha yangu na kifo

Aliyemwokoa ni Yahwe. Neno "maisha" yanaashiria mtu. "umeniokoa na kifo" au "umeniepusha na kifo"

macho yangu na machozi

Msemo wa kitenzi unawaweza kuwekwa kutoka msemo uliopita kuweka maana wazi. "umeokoa macho yangu na machozi" au "umeniepusha na kulia"

miguu yangu na kuanguka

Msemo wa kitenzi unawaweza kuwekwa kutoka msemo uliopita kuweka maana wazi. Miguu hapa inaashiria mtu. Kuanguka hapa inaweza kuwa inamaanisha kuuliwa na adui zake. "umeniokoa na kuanguka" au "umeniepusha na kuuliwa na adui zangu"

Psalms 116:9

Taarifa ya Jumla:

Mtu aliyetunga zaburi hii anaendelea kuzungumza.

katika nchi ya walio hai

"kwenye dunia hii ambapo watu wako hai." Hii ni tofauti na sehemu ya wafu.

Nimeumizwa sana

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Ninahangaika sana" au "Watu wananiumiza sana"

Nikasema haraka

"Nikasema haraka sana" au "Nikasema bila kutafakari"

Wanaume wote ni waongo

"Kila mtu ni muongo" au "Watu wote ni waongo"

Psalms 116:12

Taarifa ya Jumla:

Mtu aliyetengeneza wimbo huu anaendelea kuzungumza.

Nitamlipaje Yahwe ... kwangu?

Mwandishi anauliza swali hili kutambulisha jinsi atakavyojibu kwa yale Yahwe aliyofanya. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hivi ndivyo nitakavyomlipa Yahwe ... kwangu."

Nitainua kikombe cha wokovu

Hii inawezekana kuwa marejeo ya kinywaji, ambayo ilikuwa ni sadaka iliyohusisha kumwaga divai katika madhabahu, na ambayo mwandishi atatoa kwa Yahwe kwa kumwokoa. "Nitatoa sadaka ya kinywaji kwa yahwe kwa kuwa ameniokoa"

kuliita jina la Yahwe

Hap neno "jina" limwakilisha Yahwe mwenyewe. "kumwita Yahwe"

Ya thamani machoni pa Yahwe mauti ya watakatifu wake

Neno "thamani" hapa haimaanishi kuwa Yahwe anathamini vifo vya watakatifu wake, lakini vifo vya watakatifu wake vinamgharimu na kumhuzunisha. Msemo "machoni pa" inawakilisha moyo wa Yahwe kwenye kitu anachokiona. "Yahwe anaona kuwa vifo vya watakatifu wake ni jambo la gharama"

Psalms 116:16

Taarifa ya Jumla:

Mtu aliyetunga zaburi hii anaendelea kuzungumza.

mwana wa mtumishi wako mwanamke

Hii inawezekana kuwa mrejeo wa mama yake mwandishi na inaashiria kuwa alimwabudu Yahwe kwa uaminifu. Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "kama mama yangu alivyokuwa"

umenitolea pingu zangu

Mwandishi anazungumzia kuwa hatarini kufa kana kwamba alikuwa amefungwa gerezani."umeniokoa na kifo"

sadaka ya shukrani

"sadaka kuonesha shukrani yangu"

kuliita jina la Yahwe

Hapa neno "jina" linamwakilisha Yahwe mwenyewe. "kumwita Yahwe"

Psalms 116:18

Taarifa ya Jumla:

Mtu aliyeandika wimbo huu anaendelea kuzungumza.

Nitatimiza ... watu wake wote

"Nitatimiza nadhiri zangu kwa Yahwe ili watu wote waone"

katika baraza la nyumba ya Yahwe

Neno "nyumba" linamaanisha hekalu ya Yahwe. "katika baraza la hekalu ya Yahwe"

katikati yako, Yerusalemu

Mwandishi anazungumza na Yerusalemu kana kwamba anazungumza na mtu. "katika Yerusalemu"

Psalms 117

Psalms 117:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa

"Kwa sababu"

uaminifu wake wa agano ni mkubwa kwetu

"uaminifu wake wa agano kwetu ni mkubwa "

unadumu milele

"upo milele"

Psalms 118

Psalms 118:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Mpeni Yahwe shukrani, kwa kuwa ni mwema

"Mshukuruni Yahwe kwa mambo mema ambayo huwa anafanya"

Uaminifu wake wa agano unadumu milele

"Anatupenda kwa uaminifu milele"

Acha israeli iseme

Neno "Israeli" linawakilisha watu wa Israeli. "Acha watu wa Israeli waseme"

Psalms 118:3

Acha nyumba ya Haruni iseme

Hapa neno "nyumba" linawakilisha familia na uzao wa mtu. Msemo huu unamaanisha makuhani, ambao walikuwa uzao wa Haruni. "Acha uzao wa Haruni useme" au "Acha makuhani waseme"

Uaminifu wake wa agano unadumu milele

"Anatupenda kwa uaminifu milele"

wafuasi waaminifu wa Yahwe

"wale wanaomcha Yahwe" au "wale wanaomwabudu Yahwe"

Psalms 118:5

akaniweka huru

Mwandishi anazungumzia Yahwe kumwokoa kutoka kwenye huzuni kana kwamba Yahwe alimtoa kutoka sehemu ya kifungo hadi sehemu pana ya wazi ambapo angeweza kusogea kwa uhuru.

mtu atanifanya nini?

Mwandishi anauliza swali hili balagha kusisitiza kuwa hakuna kitu ambacho mtu anaweza kufanya kumuumiza kwa kuwa Yahwe yuko pamoja naye. "watu hawawezi kufanya chochote kunidhuru"

Yahwe yuko upande wangu kama msaidizi wangu

Kuwa upande wa mtu ni lahaja inayoashiria kuwa mtu anakubaliana na atamsaidia mtu mwingine. "Yahwe ananikubali na atanisaidia"

nitatazama kwa ushindi juu ya wale wanaonichukia

Inadokezwa kuwa Yahwe ndiye atakayewashinda adui wa mwandishi, wakati mwandishi akitazama. "Nitamwona Yahwe akiwashinde wote wanaonichukia"

Psalms 118:8

kujihifadhi kwa Yahwe

Mungu anazungumziwa kana kwamba ni kivuli, sehemu ambayo watu wanaweza kulindwa. "kutafuta ulinzi kutoka kwa Yahwe"

kumkimbilia Yahwe

Mstari huu una usambamba na ule uliopita. Mungu anazungumziwa kana kwamba ni kimbilio, sehemu ambayo watu wanaweza kulindwa. "kutafuta ulinzi kutoka kwa Yahwe"

Psalms 118:10

Mataifa yote

Hapa neno "mataifa" inawakilisha majeshi ya mataifa hayo. Mwandishi anatumi kukuza kwa neno kusisitiza idadi kubwa ya majeshi yaliyomzunguka. "Majeshi ya mataifa mengi"

katika jina la Yahwe

Hapa neno "jina" linawakilisha nguvu ya Yahwe. "kwa nguvu ya Yahwe"

ninawakata

Mwandishi anazungumzia kuyashinda majeshi ya adui kana kwamba alikuwa akiyakata kama mtu anavyokata tawi kwenye mmea. "niliwashinda"

wananizunguka kama nyuki

Mwandishi analinganisha majeshi ya adui na kundi kubwa la nyuki yatamzunguka mtu"

walipotea haraka kama moto kwenye miiba

Kama miiba iliyokauka inavyowaka upesi, mashambulizi ya majeshi ya adui yaliisha ghafla. "mashambulizi yao yalidumu kwa muda mfupi, kama moto unaoteketeza miiba unavyoisha upesi"

Psalms 118:13

kuniangusha chini

Mwandishi anazungumzia majeshi ya adui kujaribu kumshinda kana kwamba walikuwa wakijaribu kumsukuma ardhini. "ili kunishinda mimi"

Yahwe ni nguvu yangu na furaha yangu

"Yahwe hunipa nguvu na furaha"

Psalms 118:15

Sauti ya kelele ya ushindi inasikika katika mahema ya wenye haki

"Watu husikia kelele ya furaha katika mahema ya wenye haki" au "Wenye haki wanapiga kelele kwa furaha ya ushindi kwenye mahema yao"

mkono wa kuume wa Mungu unashinda

Hapa neno "mkono" linawakilishi uwezo wa Yahwe. "Yahwe ameshinda kwa nguvu yake kuu"

mkono wa kuume wa Mungu unashinda

Hapa, kuinua mkono ni ishara ya ushindi. "Yahwe ameinua mkono wake wa kuume" au "Yahwe ameinua mkono wake wa kuume kwa ushindi"

Psalms 118:17

Sitakufa, bali nitaishi

Mwandishi anaeleza wazo moja kwa njia hasi na chanya kusisitiza kuwa hakika ataishi.

Yahwe ameniadhibu

"Yahwe amenifundisha"

hajanikabidhi kwa mauti

Mwandishi anazungumzia mauti kana kwamba ni mtu ambaye Yahwe anaweza kumweka mtu chini ya uwezo wake. "hajaniruhusu kufa" au "hajawaruhusu adui zangu kuniua"

Psalms 118:19

Nifungulie malango ya haki

Nifungulie malango ambayo watu wenye haki hupita." Hii inamaanisha malango ya hekalu, na mwandishi anawaambia walinzi wa malango. "Nifungulieni malango ya hekalu"

lango la Yahwe

"lango unaowaongoza watu kuelekea katika uwepo wa Yahwe " au "lango la Yahwe"

nitatoa shukrani kwako

Hapa mwandishi anaanza kuzungumza na Yahwe.

umekuwa wokovu wangu

"uliniokoa"

Psalms 118:22

Jiwe ambalo wajensi walikataa limekuwa jiwe kuu la pembeni

Hii inaweka kuwa mithali ambayo mwandishi ametumia kuelezea mojawapo kati ya mfalme ya taifa la Israeli. Lile ambalo watu wameona halifai, Yahwe amelifanya kuwa la muhimu zaidi.

ni la ajabu machoni petu

Maana zinazowezekana ni 1) "ni jambo la ajabu kwetu kuona" au 2) "tunaona kuwa jambo la ajabu ."

Psalms 118:24

tutashangilia na kufurahi

Misemo hii inamaana moja na inasisitiza uzito wa furaha. "tutashangilia sana"

Psalms 118:26

Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Yahwe

Hapa makuhani wanaanza kuzungumza na mfalme.

anayekuja kwa jina la Yahwe

Hapa neno "jina" linawakilisha uwezo wa Yahwe. "yule anayekuja katika nguvu ya Yahwe"

tutakubariki kutoka katika nyumba ya Yahwe

Hapa makuhani wanazungumza na watu.

nyumba ya Yahwe

Neno "nyumba" linamaanisha hekalu. "hekalu la Yahwe"

ametupa nuru

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwabariki watu wake kana kwamba Yahwe anamulika mwanga juu yao. "ametubariki"

funga sadaka kwa kamba

"kaza sadaka kwa kamba"

Wewe ni Mungu wangu

Hapa mwandishi anaanza kuzungumza tena na anazungumza na Yahwe moja kwa moja.

Psalms 118:29

O

Huu ni mshangao.

mpeni Yahwe shukrani; kwa kuwa ni mwema

"Mshukuruni Yahwe kwa mambo mema ambayo huwa anafanya"

uaminifu wake wa aganounadumu milele

"anatupenda kwa uaminifu milele."

Psalms 119

Psalms 119:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

ALEFU

Hili ni jina la herufi ya kwanza ya alfabeti ya Kihebrania.

Wamebarikiwa wale

"Ni vizuri vikoje kwa wale"

wale ambao njia zao hazina lawama

Jinsi mtu anavyotenda inazungumziwa kama "njia." "wale ambao tabia zao hazina lawama" au "wale ambao hakuna anayeweza kuwalaumu kwa kutenda makosa"

wanao tembea katika sheria ya Yahwe

Jinsi mtu anavyoishi au kutenda inazungumziwa kama kutembea. "wanaoishi kulingna na sheria ya Yahwe" au "wanaotii sheria ya Yahwe." Msemo huu unaweka wazi maana ya "ambao njia zao hazina lawama."

wanaomtafuta kwa moyo wao wote

"Kumtafuta" Mungu inamaanisha kutaka kumjua.

kwa moyo wao wote

Hii ni lahaja inayomaanisha kwa nguvu au kwa ukweli. "kwa hali yao yote" au "kwa kila kitu ndani yao" au "kwa kweli"

Psalms 119:3

Taarifa ya Jumla:

Sehemu kubwa ya zaburi hii inaelekezwa kwa Mungu, na maneno "wewe" na "zako" mara nyingi zinamaanisha yeye.

Hawafanyi kosa

Hawamkaidi Yahwe

wanatembea katika njia zake

"wanatembea katika njia za Yahwe." Hapa tabia yao inazungumziwa kama "kutembea," na jinsi Mungu anavyoteka waenende inazungumziwa kama "njia zake." "wanaenenda kama Yahwe anavyotaka waenende"

kutunza maagizo wako

"kutii vitu vyote ambavyo umesema tunapaswa kufanya"

tuziangalie kwa uangalifu

Hii ni kujua kwa umakni na kuelewa amri na kuzitii hizo amri.

Psalms 119:5

nitawekwa thabiti

Mwandishi anazungumzia kuimarishwa katika amri za Mungu kana kwamba hakuna mtu anayeweza kumsogeza kimwili.

kuangalia sheria zako

"katika kutii sheria zako"

sitaaibishwa

Mwandishi hataki kuaibishwa akiwa katika uwepo wa Mungu.

amri zako zote

"yote uliyo tuamuru"

Psalms 119:7

moyomnyofu

"moyo wa ukweli." Mtu ambaye ni mkweli atafanya kilicho sawa. Moyo unamaanisha kiini cha hisia ndani ya mtu.

sheria zako

"Sheria" inamaanisha sheria au amri za Mungu.

Psalms 119:9

BETH

Hili ni jina la herufi ya pili ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari katika mistari ya 9-16 unaanza na herufi hii.

Kijana atasafishaje njia yake?

Swali hili linatumika kutambulisha faida mpya katika neno la Mungu. Swali hili balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hivi ndivyo kijana anavyoweza kusafisha njia yake"

atasafishaje njia zake

Mwandishi anafananisha kuishi kulingana na sheria ya Mungu kama njia unayowekwa wazi bila vikwazo.

Kwa moyo wangu wote

Hii ni lahaja. Moyo unawakilishi hisia, hamu, na mapenzi ya mtu. "kwa hali yangu yote" au "kwa kila kitu ndani yangu" au "kwa ukweli"

Usiniache nipotea kutoka katika amri zako

Hapa kutotii amri za Mungu inaelezwa kama kupotoka njia. "Usiniache nikaidi amri zako"

Psalms 119:11

Nimetunza neno lako moyoni mwangu

"Nimeweka maneno yako moyoni mwangu." Hii ni sitiari inayomaanisha "Nimekalili neno lako." Moyo unaoneshwa kama chombo kinachoweza kutunza kile ambacho watu wanafikiri.

Psalms 119:13

zaidi ya utajiri wote

"zaidi ya mali zote"

Psalms 119:15

Nitatafakari ... na kuzingatia

Haya ni mawazo ya usambamba yenye maana ya kufanana, zinazotenganishwa kwa ajili ya mkazo.

Nitatafakari maagizo yako

"kuwaza kwa umakini kuhusu ulichotuelekeza"

kuzingatia

Lahaja hii inamaanisha kuwaza vizuri kuhusu kinachojadiliwa. "kuwaza kwa makini"

Nafurahi

kufurahi katika

Psalms 119:17

GIMELI

Hili ni jina la herufi ya tatu ya alfabeti ya Kihebrabia. Katika lugha ya Kihebrania, kila mstari wa mistari ya 17-24 unaanza na herufi hii.

mtumishi wako

Mwandishi alijiita "mtumishi wako" kuonesha unyenyekevu.

Fungua macho yangu ili nione

Mwandishi anazungumzia kupata uelewa, maarifa na hekima kama kuweza kuona. "Nisaidie nielewe"

mambo ya ajabu katika sheria yako

Mwandishi anazungumzia utambuzi wa sheria kama vitu vya kustaajabu.

katika sheria yako

"katika maagizo yako" au "katika amri zako"

Psalms 119:19

Mimi ni mgeni katika nchi

Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi anazungumzia maisha yake mafupi duniani kana kwamba ni mgeni ambaye hatakuwa katika nchi kwa muda mrefu. "Mimi ni kama mgeni anayeishi kwa mudamfupi katika nchi" au 2) ujinga wa mwandishi wa sheria ya Mungu ni kana kwamba alikuwa mgeni ambaye hakuwa anajua sheria za nchi. "Sijui kama mgeni katika nchi"

Hamu zangu zinapondwa kwa shauku

Mwandishi anazungumzia hamu yake ya kuwa imara kama alikuwa katika maumivu. "Hali yangu ya ndani inatamani sana kukujua" au "Nafsi yangu inaumia kwa sababu nataka sana kujua"

Psalms 119:21

waliolaaniwa

Maana zinazowezekana ni 1) Mungu atawalaani au 2) wanastahili adhabu ya Mungu. "wanaostahili adhabu yako"

wanaopotea kutoka katika amri zako

Mwandishi anazungumzia kutotii amri za Mungu kana kwamba zilikuwa ni njia ambayo mtu anaweza kupotoka. "wanaoenda mbali na njia za amri zako" au "wanaokaidi amri zako"

Niepushe na

"Niweke mbali na" au "Niokoe na"

na aibu

"na kuhisi aibu na upumbavu"

Psalms 119:23

Ingawa watawala wanapanga hila na kunikashifu

"Ingawa watawala hufanya mipango ya kunidhuru na kusema vitu vibaya kunihusu"

Amri zako za agano ni furaha yangu

"Amri zako za agano zinanifanya kuwa na furaha sana"

na ni ushauri wangu

Amri za Mungu zinazungumziwa kana kwamba ni watu. "na ni kama washauri wenye hekima kwangu" au "na wananipa ushauri wa hekima"

Psalms 119:25

DALETI

Hili ni jina la herufi ya nne ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 25-32 unaanza na herufi hii.

Maisha yangu yanang'ang'ania kwenye mavumbi

Hii ni lahaja. Maana zinazowezekana ni kwamba 1) alidhani kuwa atakufa punde, au 2) alilala kwenye mavumbi kwa sababu alikuwa na huzuni sana, au 3) aligundua kuwa alitamani vitu visivyo na faida vya duniani.

Nipe maisha kwa neno lako

Hii ni lahaja. Hapa "maisha" inamaanisha kusudi na umuhimu, sio maisha ya kimwili tu.

kwa neno lako

"Neno" la Mungu linawakilisha alichokisema. Hapa linamaanisha alichoahidi. "kulingana na ahadi yako"

njia zangu

Kile ambacho mtu hufanya au jinsi anavyoenenda inazungumziwa kana kwamba ni barabara au njia. "nilichofanya"

Psalms 119:27

mafunzo ya ajabu

"mafunzo ya kushangaza"

kwa huzuni

"kwa sababu nina huzuni"

Nime nguvu

"Nifanye kuwa imara." Hii inaweza kumaanisha nguvu ya kimwili au nguvu ya kiroho.

Psalms 119:29

Nigeuze kutoka katika njia ya udanganyifu

Neno "njia" hapa linamaanisha namna ya kuenenda kitabia. "Niepushe na kufuata njia ya udanganyifu" au "Niepushe kutokuwa mdanganyifu"

udanganyifu

Maana zinazowezekana ni 1) kudanganya" au 2) "kuamini uongo" au "kufuata uongo"

njia ya uaminifu

Jinsi mtu anavyoenenda kitabia au kutenda inazungumziwa kana kwamba ni barabara au njia. "kuwa mwaminifu kwako"

Psalms 119:31

Nashilia amri zako za agano

Kuzishikilia kwa nguvu inamaanisha kuwa na nia ya kuzitii. "Ninashikilia kwa nguvu amri zako za agano" au "Nina nia ya kutii amri zako za agano"

amri za agano

Hii inamaanisha sheria za Musa.

Nitakimbia katika njia ya amri zako

Mwandishi anazungumzia kuwa makini au kuwa na nia ya kutii amri za Mungu kana kwamba mtu anakimbia katika njia. "Nitakuwa na nia ya kutii amri zako"

unaukuza moyo wangu

Hii ni lahaja. Maana zinazowezekana ni 1) "unanisaidia kupata uelewa mkubwa wa amri zako"

Psalms 119:33

HE

Hili ni jina la herufi ya tano ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 33-40 unaanza na herufi hii.

sheria zako

Hii ni njia nyingine ya kueleza sheria ya Musa.

hadi mwisho

Maana zinazowezekana ni 1) "kabisa" au 2) "hadi mwisho wa maisha yangu" au 3) "hadi mwisho wa wakati"

nitatunza sheria yako

"kutii sheria yako"

nitaiangalia kwa moyo wangu wote

"Hakika nitaifuata sheria yako" au "Nina nia kabisa ya kufanya isemacho"

kwa moyo wangu wote

Hii ni lahaja. "kwa hali yangu yote" au "kwa kila kitu ndani yangu" au "ki ukweli"

Psalms 119:35

Niongoze katika njia ya amri zako

"Niongoze kulingana na amri zako" au "Nifundishe kutii amri zako." Amri za Mungu zinalinganishwa na njia ambayo mtu anatembea akimtii Mungu.

Ongoza moyo wangu kuelekea

Hii ni lahaja. "Moyo" hapaunamaanisha nia, hamu, na maamuzi yanayoongoza maisha ya mtu. "Unifanye nitake"

amri zako za agano

"kutii amri zako za agano." Hii inamaanisha kutii amri za Musa.

kuongezeka pasipo haki

"hamu ya utajiri." Hii inamaanisha utajiri unaopatikana kwa njia zisizo sawa au kuwatendea ubaya wengine.

Psalms 119:37

Geuza macho yangu yasitazame vitu visivyo na faida

Hii ni sitiari inayomaanisha mtu anayetamani vitu ambavyo havina thamani ya milele.

nifufue katika njia zako

"nifanye niweze kuishi kama unavyotaka niishi"

nifufue

"fanya maisha yangu yawe imara" au "nipe nguvu"

Tekeleza kwa mtumishi wako ahadi yako uliyoahidi wale wanao kuheshimu

"Fanya kwa mtumishi wako kile ulichoahidi kufanya kwa wale wanao kuheshimu"

mtumishi wako

Mwandishi anajieleza kama mtumishi wa Mungu kuonesha unyenyekevu. "mimi, mtumishi wako"

Psalms 119:39

ninayo hofu

"ninaogopa sana"

hukumu zako za haki ni nzuri

Mungu anahukumu kwa haki na maamuzi yake ni mema. "Hukumu yako ni ya haki na njema"

Tazama

Hii ni lahaja. Hapa "Tazama" inamaanisha kuwa na ufahamu kuhusu jambo. Panapo lengwa ni maarifa na uelewa, na sio tu kutazama.

Nina shauku na maagizo yako

Maana zinazowezekana ni 1) "Ninataka sana kujua maagizo yako" au 2) "Ninataka sana kutii kile unachotufundisha kufanya"

nifufue katika haki yako

Neno "haki" ni nomino dhahania na inamaanisha kuwa mwenye haki. "nifufue kwa kuwa una haki"

nifufue

Maana zinazowezekana ni 1) "Niweke kuwa hai" au 2) "Nifanye kuwa na nguvu"

Psalms 119:41

VAV

Hili ni jina la herufi ya sita ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 41-48 unaanza na herufi hii.

nipe upendo wako usiokoma

Hili ni ombi. "tafadhali nipe upendo wako usiokoma"

wokovu wako

"nipe wokovu wako" au "niokoe"

jibu

"itikio"

Psalms 119:43

Usitoe neno la ukweli mdomoni mwangu

"mdomo wangu" inamaanisha kuzungumzia juu ya neno la Mungu. "Usinizuie kamwe kuzungumza ukweli wako"

kwa kuwa nimesubiri amri zako za haki

"kusubiri" kuna wazo la kuamini, kuwa na uhakika kuwa Mungu atafanya anavyoagiza.

Nitafuata

"Nitatii"

Psalms 119:45

NItatembea salama

Kutembea salama ni kuishi maisha kwa usalama. "Nitaishi kwa usalama katika Mungu"

natafuta maagizo yako

"Kutafuta" ni kutambua, au kupata uelewa wa maagizo ya Mungu kana kwamba mtu anaweza kuyaona.

amri zako makini mbele ya wafalme

"amri za dhati kwa wafalme" au "maagizo kwa wafalme"

Psalms 119:47

Ninafurahi katika amri zako

Maana zinazowezekana ni 1) "Ninapata furaha katika kusoma amri zako" au 2) "Ninafuraha kuwa nina nafasi ya kusoma amri zako"

nitainua mikono yangu

Hii ni lahaja inayomaanisha kutunza au kuheshimu amri za mungu.

Psalms 119:49

ZAYINI

Hili ni jina la herufi ya saba ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 49-56 unaanza na herufi hii.

Itisha akilini ahadi yako

"Kumbuka ahadi yako."

Hii nifaraja yangu katika mateso; kuwa ahadi yako imeniweka hai

"Sababu ya faraja yangu ni kwamba ahadi yako imeniweka hai katika mateso yangu"

Psalms 119:51

Wenye kiburi

"Watu wenye kiburi"

wamenikejeli

kumdhihaki mtu au kitu kinachodharauliwa, chenye wasiwasi, au kischo heshimiwa

za nyakati za zamani

Huu ni mrejeo kwa kipindi sheria zimepewa kwa Musa miaka mingi kabla.

Psalms 119:53

Hasira ya moto imenishika

Hii ni lahaja. Hasira inaelezwa kana kwamba ni mtu anayeweza kumkamata mtu mwingine. "Nimekuwa na hasira sana"

Sheria zako zimekuwa nyimbo zangu

"Nimetumia sheria zako kama maneno ya muziki wangu" au "Nimutunga nyimbo kutokana na sheria zako"

Psalms 119:55

Nafikiria kuhusu jina lako

Hapa neno "jina" linamwakilisha Yahwe mwenyewe. "Nakuwaza, Yahwe"

natunza sheria yako

Hii ni lahaja inayomaanisha kutii sheria. "Ninatii sheria yako"

zoezi langu

"tabia yangu"

nimefuata maagizo yako

"Nimetii maagizo yako"

Psalms 119:57

HETHI

Hili ni jina la herufi ya nane ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 57-64 unaanza na herufi hii.

Yahwe ni sehemu yangu

Hii inamaana kuwa Yahwe ndio kitu pekee anachotaka. Kama ambavyo Walawi hawapati maeneo makubwa ya nchi kwa kuwa Bwna ndiye alipaswa kuwa sehemu yao, kwa hiyo mwandishi anatamka kuwa Yahwe ni anayerithisha hamu zake.

Psalms 119:59

nikageuza miguu yangu

Hapa "miguu" inamwakilisha mtu mzima. Kutubu na kuchagua kutii sheria za Mungu ni kama kugeuza miguu kwenye njia na kuelekea upande mwingine. "nilibadilisha mwelekeo"

Ninaharakisha na sichelewi

Mwandishi anaeleza wazo moja katika hali chanya na hasi ili kusisitiza uharaka alionao katika kutii amri za Yahwe.

Psalms 119:61

Kamba za waovu zimeninasa

Katika sitiari hii, watu waovu walijaribu kumfanya mwandishi kutenda dhambi kama mwindaji anavyotafuta kumnasa mnyama kwa mtego. "Adui zangu wamejaribu kunishika"

Psalms 119:63

Mimi ni mwenzao wale wote waokuheshimu

"Mimi ni rafiki wa wale wote waokuheshimu"

Psalms 119:65

TETHI

Hili ni jina la herufi ya tisa ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 65-72 unaanza na herufi hii.

kwa mtumishi wako

Mwandishi anajieleza kama "mtumishi wako." "kwangu, mtumishi wako" au "kwangu"

kwa njia ya neno lako

Hii ni lahaja. "Neno lako" inamaanisha ahadi za Yahwe alizompa mwandishi. "kama ulivyoahidi"

Psalms 119:67

Kabla sijateseke

"Kabla haujanitesa" au "Kabla haujaniadhibu"

nilipotoka

Kumkaidi Mungu inazungumziwa kana kwamba mtu anatembea katika njia isiyofaa. "Sikukutii wewe"

ninafuata neno lako

Hapa "neno" linawakilisha amri. "ninatii amri zako"

Psalms 119:69

Wenye kiburi

"Watu wenye kiburi"

walinipaka na uongo

Watu kusema uongo kuhusu mtu inazungumziwa kana kwamba wamemfanya mtu kuwa mchafu kwa kumpaka uongo.

kwa moyo wangu wote

Hapa "moyo" unawakilisha nia ya mtu. "kwa umakini kamili" au "kabisa"

Mioyo yao imefanywa kuwa migumu

Hapa "mioyo" inawakilisha nia za watu. Mtu kuwa msumbufu inazungumziwa kana kwamba mioyo yao au nia zao ni ngumu kama jiwe. ""Ni wakaidi"

Psalms 119:71

Maagizo kutoka mdomoni mwako ni

Hapa "mdomo" unawakilisha anachosema Mungu. "Maagizo uliyozungumza ni" au Maagizo yako ni"

ya maelfu ya vipande vya dhahbu na shaba

"ya kiasi kikubwa cha fedha" au "utajiri mkubwa"

Psalms 119:73

YOD

Hili ni jina la herufi ya kumi ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 73-80 unaanza na herufi hii.

Mikono yako imeniumba na kunitengeneza

Mungu kumuumba mtu inazungumziwa kana kwamba Mungu alitumia mikono yake kumuunda mtu kama mtu anavyounda chombo cha udongo.

Mikono yako

Hapa "mikono" inawakilisha nguvu au matendo ya Mungu. "Wewe"

kwa sababu napata matumaini katika neno lako

Hapa "neno" linawakilisha anachosema Mungu. "kwa sababu ninaamini unachosema" au "ninaamini kwa ujasiri unachosema"

Psalms 119:75

katika uaminifu wako umenitesa

"umeniadhibu kwa sababu wewe ni mwaminifu." Mungu anaahidi kuwapa dhawabu wenye haki na kuwaadhibu watenda maovu, kwa hiyo ni mwaminifu kufanya alichosema atafanya.

mtumish wako

Mwandishi anajieleza kama "mtumishi wako." mimi, mtumishi wako" au "mimi"

Psalms 119:77

Acha wenye kiburi waaibishwe

"Waaibishe wenye kiburi" au "sababisha wale wenye kiburi waaibike"

wenye kiburi

"watu wenye kiburi" au "wale wenye kiburi"

Psalms 119:79

geuka kwangu

Watu kumrudia urafiki mwandishi inazungumziwa kana kwamba wanamgeukia yeye kimwili. "njoo kwangu" au "ungana na mimi"

wale wanaojua amri zako za agano

Maana zinazowezekana ni 1) hii inaendelea kuelezea wale wanaomheshimu Mungu au 2) hii inaashiria kusudi la wale wanaomheshimu Mungu kurudi kwa mwandishi. Maneno "ili kwamba" yanaweza kuongezwa kuashiria hili.. "ili kwamba wajifunze unachowaamuru"

Na moyo wangu usiwe na lawama

Hapa "moyo" unawakilisha mawazo ya mtu na nia yake. "Na nisiwe na lawama"

nisiaibishwe

"nisiaibike"

Psalms 119:81

KAFU

Hili ni jina la herufi ya kumi na moja ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 81-88 unaanza na herufi hii.

Ninamatumaini katika neno lako

Hapa "neno" linawakilisha kile anachokisema Mungu. "Ninaamini kwa ujasiri kile unachosema"

Macho yangu yanashauku ya kuona ahadi yako

Hapa "macho" yanawakilisha mtu mzima. "Nasubiri na kusubiri ili ufanye ulichoahidi kufanya"

Psalms 119:83

Nime kuwa kama kiriba katika moshi

Kiriba huaharibika kinaponing'inizwa muda mrefu kwenye sehemu ya moshi. Mwandishi anajifananisha na kiriba kilichoharibiwa na moshi kusisitiza kuwa anajihisi hana faida.

Hadi lini mtumishi wako avumilie hili, utawahukumu lini wale wanaonitesa?

Mwandishi anatumia swali kumwomba Mungu kuwaadhibu wale wanaomtesa. "Tafadhali usinifanye nisubiri zaidi. Waadhibu wale wanaonitesa."

mtumishi wako

Mwandishi analjielezea kama "mtumishi wako." "lazima ni, mtumishi wako" au "lazima ni"

Psalms 119:85

Wenye kiburi wamechimba mashimo kwa ajili yangu

Wenye kiburi wanatafuta kumshika mwandishi au kumsababisha kumfanya atende uovu. Hii inazungumziwa kana kwamba walikuwa ni wawindaji wanaochimba mashimo kumtega mwandishi kama mnyama.

Wenye kiburi

"Watu wenye kiburi" au "Wale walio na kiburi"

Psalms 119:87

Wamekaribia kuniwekea mwisho wangu duniani

Hii ni njia ya ustarabu ya kuzungumzia mtu kutaka kumuua mtu mwingine. "Wamekaribia kumuua"

Kwa upendo wako thabiti

"Kulingana na upendo wako thabiti." "kwa sababu unanipenda kwa uaminifu"

Psalms 119:89

LAMEDI

-Hili ni jina la herufi ya kumi na mbili ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 89-96 unaanza na herufi hii.

maneno yako milele

Hapa "neno" linawakilisha chochote ambacho Mungu amewasilisha kwa watu. "kile ulichosema kitakuwa kweli milele"

neo lako linawekwa thabiti mbinguni

Hapa "neno" linawakilisha chochote ambacho Mungu amewasilisha kwa watu. Hii inazungumzia kuhusu kile ambacho Mungu amesema kana kwamba ni chombo kinachoweza kusimama imara wima. "kile ulichosema kitakuwa cha kweli mbinguni milele"

kwa vizazi vyote

"kwa vizazi vyote vya baadaye." Hii ni lahaja inayomaanisha "milele"

Psalms 119:91

vitu vyote ni watumishi wako

Vitu vyote vilivyoumbwa vinazungumziwa kana kwamba ni watu wanaoweza kumtumikia Mungu. "vitu vyote vinakutumikia" au "vitu vyote vinatii amri zako"

Psalms 119:93

Kamwe sitasahau

"Daima nitakumbuka"

maana kwa hayo umeniweka hai

Inadokezwa kwamba mwandishi anatii maagizo ya Mungu. "kwa kuwa umeniweka kuwa hai kwa sababu ninazitii"

kwa kuwa natafuta maagizo yako

Kujaribu kutii maagizo ya Mungu inazungumziwa kana kwamba maagizo ni kitu ambacho mtu anatakiwa kutafuta.

Psalms 119:95

nitatafuta kuelewa

"nitajaribu sana kuelewa"

kila kitu kina mipaka yake

"vitu vyote vina mwisho"

amri zako ni pana, zaidi ya mipaka

Amri za Mungu daima kuwa kweli na hakika zinazungumziwa kana kwamba amri za mungu ni kitu kilicho kipana sana hadi hakina mwisho. "lakni amri zako hazina mipaka" au "lakini amri zako ni za milele"

Psalms 119:97

MEMU

Hili ni jina la herufi ya kumi na tatu ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 97-104 unaanza na herufi hii.

amri zako daima zako na mimi

Kuwaza daima kuhusu amri za Mungu inazungumziwa kana kwamba amri ni kitu ambacho mwandishi anakua nacho muda wote.

Psalms 119:101

Nimeweka miguu yangu mbali na njia ya uovu

Kuepuka kufanya kilicho kiovu kinazungumziwa kana kwamba ni kuepuka kutembea kwenye njia ambazo ni za uovu. "Nimeepuka kufanya kilicho cha uovu"

Nimeweka miguu

Hapa "miguu" inawakilisha mtu mzima. "nimejiweka"

nifuate neno lako

"nimetii neno lako"

neno lako

Hapa "neno" linawakilisha amri za Mungu.

Sijageuka pembeni kutoka katika amri zako za haki

Kuendelea kutii amri za haki za Mungu inazungumziwa kana kwamba mwandishi hajageuka kimwili kutoka katika amri za haki. "daima huwa natii amri zako za haki"

Psalms 119:103

Ni matamu kiasi gani maneno yako kwangu, ndio, matamu kuliko asali mdomoni mwangu!

Mwandishi kufurahi katika yale ambayo Mungu anasema inazungumziwa kana kwamba maneno ya Mungu ni chakula yaliyokuwa na ladha nzuri kwa mwandishi. "Maneno yako ni mazuri na yanapendeza!"

ninapata utambuzi

"ninajifunza kutambua kilicho sawa"

kwa hiyo ninachukia kila njia ya uongo

Tabia ya uovu inazungumziwa kana kwamba ni njia.

Psalms 119:105

NUN

Hili ni jina la herufi ya kumi na nne ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 105-112 unaanza na herufi hii.

Neno lako ni taa miguuni mwangu na nuru njiani mwangu

Misemo hii miwili ina maana za kufanana. Inazungumza kuhusu Mungu kumwambia mtu jinsi ya kuishi kana kwamba mtu alikuwa akitembea katika njia na neno la Mungu ni nuru inayomsaidia mtu kuona anapoenda. "Maneno yako yananieleza jinsi ya kuishi"

Neno lako

Hapa "neno" linawakilisha yote ambayo Mungu anwasiliana na watu.

Psalms 119:107

kwa ulivyoahaidi katika neno lako

Hapa "neno" linawakilisha kile ambacho Mungu anawasiliana na watu. "kama ulivyoahidi kufanya"

sadaka za kujitolea za mdomo wangu

Mwandishi anazungumzia ombi lake kana kwamba lilikuwa ni sadaka aliyokuwa akiitoa kwa Mungu. "ombi langu kama sadaka kwako"

za mdomo wangu

Hapa "mdomo" unawakilisha mtu mzima.

Psalms 119:109

Maisha yangu daima yako mkononi mwangu

Hii ni lahaja inayomaanisha maisha ya mwandishi yako hatarini wakati wote. "Adui zangu huwa wanajaribu kuniua"

Sisahau sheria yako

"Daima huwa nakumbuka sheria zako"

Waovu wameweka mtego mbele yangu

Watu waovu kujaribu kumshika na kumuua mwandishi inazungumziwa kana kwamba ni wawindaji wanaanda mtego kumshika mnyama.

Waovu

"Watu waovu"

Sijapotea kutoka kwenye maagizo yako

Kutokaidi maagizo ya Mungu inazungumziwa kana kwamba mwandishi hajatembea mbali na maagizo ya Mungu. "Ninatii maagizo yako"

Psalms 119:111

Ninadai amri zako za agano kama urithi wangu milele

Mwandishi kutunza na kutii amri za Mungu inazungumziwa kana kwamba amri ni nchi au mali ambayo mwandishi atarithi. "Sheria zako zitakuwa zangu milele" au "Amri zako za agano ni kama urithi nitakaoutunza milele"

ni furaha ya moyo wangu

Hapa "moyo" unawakilisha mtu mzima. "zinanifanya kuwa na furaha" au "ninazifurahia'

Moyo wangu uko tayari kutii

Hapa "moyo" unawakilisha nia ya mwandishi. Msemo "Moyo wangu uko tayari" ni lahaja. Ni njia ya kusema mwandishi amekusudia. "Nimekusudi kutii"

hadi mwisho

Maana zinazowezekana ni 1) "kila moja" 2) "hadi mwisho wa maisha yangu" au 3) "hadi mwisho wa wakati"

Psalms 119:113

SAMEKHI

Hili ni jina la herufi ya kumi na tano ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 113-120 unaanza na herufi hii.

wenye akili mbili

Mtu asiye mkweli na kuwa na msimamo wa kumtii Mungu anazungumziwa kana kwamba ni mwenye akili mbili. "wasio na msimamo kabisa wa kukutii wewe" au "wasio wakweli"

maficho yangu

Mungu kumfanya mwandishi salama kunazungumziwa kana kwamba Mungu ni sehemu ambayo mwandishi anaweza kwenda na kujificha.

ngao yangu

Mungu kumlinda mwandishi kunazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa ni ngao ya mwandishi.

nasubiri neno lako

Hapa "kusubiri" inamaanisha kusubiri kwa kutarajia. Hii ina wazo la kutumaini au kuamini. "ninatumaini neno lako"

neno lako

Hapa "neno" linawakilisha kile ambacho Mungu anawasiliana kwa watu.

Psalms 119:115

Unitunze kwa neno lako

"Nishikilie kwa neno lako." Hapa "neno" linawakilisha kile ambacho Mungu anawasiliana kwa watu. "Nipe nguvu kama ulivyosema utafanya" au "Niwezeshe kuwa na nguvu kama ulivyoahidi"

na nisiaibike kwa tumaini langu

Hapa "tumaini langu" linawikilisha tumaini la mwandishi kwa Mugnu na ahadi zake. "Usinivunje matumaini." au "Usinisababishe niwe na aibu kwa kutokufanya kile ulichoahidi kufanya."

Psalms 119:117

Unisaidie mimi

"Nisaidie" au "Nitie nguvu"

watu hao ni waongo na sio wa kutegemea

Maana zinazowezekana ni 1) "watu hao wanadanganya na hakuna mtu anayeweza kuwaamini" au 2) "watu hao wanapanga mipango ya uongo lakini watashindwa"

Psalms 119:119

Unawaondoa waovu wote duniani kama takataka

Hapa "takataka" ni yale mabaki yanayobaki wakati wa kusafisha dhahabu au madini mengine ya chuma. Yahwe anawaondoa watu waovu kana kwamba ni takataka.

waovu

"watu waovu"

kama takataka

"kama uchafu"

Mwili unatetemeka kwa kukuogopa wewe

Hapa "mwili" unawakilisha mtu mzima. "Ninatetemeka kwa sababu ninakuogopa"

ninaogopa amri zako za haki

Inadokezwa kwamba mwandishi anaogopa amri za haki za Mungu kwa sababu Mungu anajua kuwa Mungu huwaadhibu wale wanaokaidi amri zake.

Psalms 119:121

AYINI

Hili ni jina la herufi ya kumi na sita ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 121-128 unaanza na herufi hii.

usiniache kwa wakandamizaji wangu

"usiwaruhusu watu wanikandamize"

Hakikisha ustawi wa mtumishi wako

Mwandishi anajizungumzia kama "mtumishi wako." "Hakikisha ustawi wangu" au "Nisaidie na unilinde mimi, mtumishi wako"

wenye kiburi

"wale walio na kiburi" au "watu wenye kiburi"

Psalms 119:123

Macho yangu yanachoka ninaposubiri

Hapa "macho" yanawakilisha mtu mzima. "Ninachoka kwa sababu ninasubiri na kusubiri"

kwa wokovu wako na kwa neno lako la haki

"ili uniokoe kama ulivyoahidi kufanya"

neno lako la haki

Hapa "neno" linawakilisha kile ambacho Mungu anawasiliana na watu. "ahadi yako ya haki"

Mwoneshe mtumishi wako

Mwandishi anajizungumzia mwenyewe kama "mtumishi wako." "Nioneshe" au "Nioneshe mimi, mtumishi wako"

uaminifu wako wa agano

"kwamba unanipenda kwa uaminifu" au "kwa kuwa wewe ni mwaminifu kwangu kwa sababu ya agano lako"

Psalms 119:125

nipe uelewa

"niwezeshe kuelewa kile unachotaka nijue"

Ni muda wa Yahwe kutenda

Mwandishi anazungumza na Yahwe katika hali ya mtu wa tatu. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya mtu wa pili. "Ni muda wako kutenda, Yahwe"

watu wamevunja sheria yako

Hii ni lahaja. Hapa "wamevunja" inamaanisha "kukaidi." Hii ni njia ya kusema kuwa watu wamekaidi sheria ya Mungu.

Psalms 119:127

Ninafuata maagizo yako yote kwa makini

Mtu kutii kwa makini maagizo yote ya Mungu inazungumziwa kana kwamba maagizo yanamwongoza mtu na mtu anayafuata kwa nyuma. "Ninatii kwa makini maagizo yako yote"

kila njia ya uongo

Watu kufanya kilicho kiovu inazungumziwa kana kwamba wanatembea njia mbaya. "njia zote mbaya ambazo baadhi ya watu huishi"

Psalms 119:129

PE

Hili ni jina la herufi ya kumi na saba ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 129-136 unaanza na herufi hii.

Ufunuo wa maneno yako hutoa mwanga

Mwandishi anazungumzia neno la Yahwe kana kwamba maneno hayo nikitambaa kilichokunjwa, na mtu anayefafanua maneno ya Yahwe kana kwamba wanafunua hicho kitambaa. "Ufafanuzi wa maneno yako hutoa mwanga" au "Mtu akifafanua maneno yako, hutoa mwanga"

Ufunuo wa maneno yako hutoa mwanga

Mwandishi anazungumzia maneno ya Yahwe kutoa hekima na mtu kana kwamba maneno yanatoa mwanga kwao. "Ufafanuzi wa maneno yako huwapa watu hekima"

Psalms 119:131

Ninafungua mdomo wangu na kuhema, kwa kuwa nina shauku na amri zako

Mwandishi anazungumzia hamu yake ya amri za Yahwe kana kwamba alikuwa mbwa anayehema kwa ajili ya maji. "nina shauku ya kweli na amri zako"

Nigeukie

Kumgeukia mtu inamaanisha kuvuta nadhari kwa mtu huyo. "Nizingatie"

wanaolipenda jina lako

Hapa neno "jina" linamwakilisha yahwe mwenyewe. "wanaokupenda"

Psalms 119:133

Ongoza hatua zangu

Hapa neno "hatua" inamwakilisha mwandishi anavyotembea. Anazungumzia jinsi anavyoishi, au mwenendo wake, kana kwamba alikuwa akitembea katika njia. "Niongoze" au "Nifundishe jinsi ya kuishi"

usiache dhambi yoyote initawale

Mwandishi anazungumzia dhambi kana kwamba ni mtu mwenye mamlaka juu yake. Maana zinazowezekana ni 1) "usiniache nifanye dhambi yoyote kwa mazoea" au 2) "usiache watu wenye dhambi wanitawale"

Niokoe na ukandamizaji wa wanadamu

"Niokoe na watu wanaowakandamiza wengine"

Psalms 119:135

Acha uso wako ung'ae kwa mtumishi wako

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kutenda kwa fadhila kwake kana kwamba uso wa Yahwe ulitoa mwanga juu yake. "Tenda kwa fadhila kwa mtumishi wako"

Mikondo ya machozi

Mwandishi anazungumzia machozi yake mengi kana kwamba ni mkondo wa maji. "Machozi mengi"

hawafuati sheria yako

"hawatii sheria yako"

Psalms 119:137

TSHADE

Hili ni jina la herufi ya kumi na nane ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 137-144 unaanza na herufi hii.

amri za agano

Maana zingine zinazowezekana ni "shuhuda" au "sheria."

Psalms 119:139

Hasira imeniangamiza

Hii ni lahaja. Msemo huu ni kukuza kwa neno na ni njia nyingine ya kusema "Nina hasira sana."

limejaribiwa sana

"Nimelijaribu neno lako mara nyingi"

mtumishi wako hulipenda

Mwandishi anajizungumzia kana kwamba alikuwa ni mtu mwingine. "mimi, mtumishi wako, hupenda" au "ninapenda"

Psalms 119:141

Mimi ... ninachukiwa

"Watu wananichukia"

Psalms 119:143

huzuni na maumivu yamenipata

Mwandishi anazungumzia huzuni na maumivu kana kwamba ni watu. "Nimekuwa na huzuni na maumivu" au "mwili wangu na akili yangu zinateseka"

Psalms 119:145

QOPHU

Hili ni jina la herufi ya kumi na tisa ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 145-152 unaanza na herufi hii.

kwa moyo wangu wote

Mwandishi anajizungumzia mwili ukamili wake kana kwamba ni moyo wake tu. "kabisa"

amri za agano

Maana zingine zinazowezekana ni "shuhuda" au "sheria"

Psalms 119:147

mapambazuko ya asubuhi

"kabla jua halijatokea"

Macho yangu yako wazi kabla usiku haujabadilika

Hii ni lahaja. Katika utamaduni wa Kihebrania, usiku uligawanyika mara tatu. "Niko macho usiku kucha"

Psalms 119:149

Sikia sauti katika uaminifu wako wa agano

Mwandishi anazungumzia anachokisema kana kwamba ni sauti anayotumia kuzungumzia. "Sikia ninachosema kwa sababu ya uaminifu wako wa agano"

wako mbali na sheria yako

"wamepotoka mbali na sheria yako" au "hawazingatii sheria zako"

Psalms 119:151

amri zako zote ni za uaminifu

"ninaweza kuamini amri zako"

amri za agano

Maana zingine zinazowezekana ni "shuhuda" au "sheria"

umeziandaa

Mwandishi wa zaburi anazungumzia amri za Yahwe kana kwamba ni nguzo zilizopangwa kwenye ardhi. "umewapa watu kutii"

Psalms 119:153

RESHI

Hili ni jina la herufi ya ishirini ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 153-160 unaanza na herufi hii.

Angalia mateso yangu

Mwandishi wa zaburi anazungumzia mateso kana kwamba ni kitu ambacho watu wanaweza kuona. "Ona jinsi ninavyoteseka"

Tetea haja yangu

"Nitetee dhidi ya wale wanao nishutumu"

niweke

"linda maisha yangu" au "nipe uhai"

Psalms 119:155

Wokovu u mbali na waovu

mwandishi anazungumzia wokovu kana kwamba ni kitu chenye umbo. "Hakika hautawaokoa waovu"

Matendo yako ya huruma ni mengi

"Umeonesha huruma kwa watu mara nyingi" au "Umefanya matendo mengi ya huruma"

kama hufanyavyo

Maana nyingine inayowezekana ni "kwa sababu unafanya kilicho cha haki"

Psalms 119:157

Watesi wangu

"Wale wanaonitesa mimi"

sijageuka

Hii ni lahaja. "Sijaacha kutii" au "Sijaacha kuamini"

amri za agano

Maana zingine zinazowezekana ni "shuhuda" au "sheria."

waongo

"watu waongo" au "wale wanaonisaliti" au "adui zangu"

hawatunzi

"hawatii"

Psalms 119:159

Tazama

"Angalia" au "Niangalie ili uone"

Asili ya neno lako ni ukweli

"Neno lako ni kweli kabisa" au "Neno lako linaweza kuaminika"

Psalms 119:161

SHINI

Hili ni jina la herufi ya ishirini na moja ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 161-168 unaanza na herufi hii.

moyo wangu unatetemeka, ukiogopa kutokutii neno lako

Mwandishi anazungumzia moyo kana kwamba unaweza kutetemeka na kuogopa. Moyo ni njia nyingine ya kusema mtu mzima. "Ninatetemeka kwa sababu ninaogopa kuwa nitakaidi neno lako"

mapato

Maana zinazowezekana ni 1) vitu ambavyo askari huchukua kwa wale waliowashinda katika vita au 2) vitu vya thamani kubwa au "hazina."

Psalms 119:163

chukia na kinyongo

Maneno haya mawili inamaanisha karibu kitu kimoja. "nachukia sana"

uongo

maana zinazowezekana ni njia nyingine ya kusema 1) "watu wanaodanganya" au 2) "vitu vya uongo ambavyo watu wanasema"

Psalms 119:165

hakuna kitu kinachowafanya wajikwae

Maana zinazowezekana ni 1) "hakuna kitu kinachowafanya kufanya kosa" au 2) "hakuna kitu kinachowaletea shida"

Psalms 119:167

Ninafuata amri zako makini

"Ninatii amri zako makini"

amri zako makini

Maana zingine zinazowezekana ni "shuhuda" au "sheria."

Ninatunza maagizo yako

"Ninatii maagizo yako"

Psalms 119:169

TAVI

Hili ni jina la herufi ya ishirin na mbiliya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 169-176 unaanza na herufi hii.

nipe uelewa katika neno lako

Mwandishi anazungumzia uwezo wa kuelewa kana kwamba ni kitu chenye umbo. "nisaidie nielewe neno lako"

Ombi langu lifike mbele yako

Mwandishi wa zaburi anazungumzia maneno anayoyasema kana kwamba ni watu wanaotaka kuzungumza kwa mfalme. "Na usikie ombi langu"

Psalms 119:171

Midomo yangu imwage sifa

Mwandishi wa zaburi anazungumzia midomo yake kana kwamba ni chombo na ni kimiminiko kinachoweza kumwagwa. Hapa neno "midomo" ni neno lingine linalowakilisha mtu mzima. "Ninatamani kukusifu sana"

ulimi wangu uimbe

Mwandishi anazungumzia ulimi wake aidha 1) kana kwamba ni mtu au 2) kama neno lingine la kuwakilisha yeye mzima. "mimi naimba"

Psalms 119:173

Mkono wako unisaidie

Mkono unawakilisha mtu mzima. "Tafadhali nisaidie"

nimechagua

"nimechagua kutii"

ukombozi wako

"unaniokoa"

sheria yako ni furaha yangu

"Ninafurahi sana kutii neno lako"

Psalms 119:175

amri zako za agano zinisaidie

Mwandishi anazungimzia amri za Yahwe kana kwamba ni mtu anayeweza kumsaidia. "naomba nisikilize amri zako za haki ili niwe na hekima na thabiti"

Nimezurura kama kondoo aliyepotea

"nimeacha njia yako kama kondoo aliyeacha kundi lake"

mtafute mtumishi wako

"kwa sababu mimi ni mtumishi wako, njoo unitafute"

Psalms 120

Psalms 120:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

Katika dhiki yangu

"katika taabu yangu" au "Wakati niko kwenye taabu"

Okoa maisha yangu

Hapa neno "maisha" linamwakilisha mtu. "Niokoe"

kwa wale wanaodanganya na midomo yao na kupotosha na ndimi zao

Hapa msemo "midom yao" na "ndimi zao" inawakilisha watu wanaozungumza uongo na kupotosha. "wale wanao nidanganya na kujaribu kunipotosha"

Psalms 120:3

Atakuadhibuje, na nini zaidi atafanya kwako, wewe mwenye ulimi wa udanganyifu?

Mwandishi anauliza swali hili kama mwongozo wa kueleza kitu ambacho Mungu atafanya kwa waongo. Swali linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hivi ndivyo Mungu atakavyo kuadhibu, hiki ndicho atakachofanya kwako, wewe mwenye ulimi wa udanganyifu."

wewe mwenye ulimi wa udanganyifu

Hapa "ulimi wa udanganyifu" inamwakilisha mtu anayezungumza uongo. "wewe unayesema uongo"

Atakuadhibu kwa mishale ya shujaa

Mwandishi anazungumzia Mungu kuwaadhibu kwa ukali waongo kana kwamba Mungu anawapiga kwa mishale. "Atakuadhibu kwa ukali, kana kwamba anawapiga kwa mishale ya shujaa"

iliyochongwa juu ya makaa ya moto ya mti wa mfagio

Hii inamaansiha jinsi watu walivyounda ncha ya mshale katika moto. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "aliyochonga juu makaa ya moto ya mti wa mfagio"

Psalms 120:5

Ninaishi Mesheki kwa muda; Niliishi kwa muda katika mahema ya Kedari

sehemu hizi mbili zilikuwa mbali. Mwandishi inawezekana anatumia majina kwa balagha kuashiria kuishi miongoni mwa watu wakatili. "Ni kana kwamba ninaishi Mesheki au katika mahema ya Kedari"

mahema ya Kedari

Msemo huu unawakilisha watu wa Kedari wanaoishi katika mahema hayo. "watu wanaoishi Kedari"

Mimi ni wa amani

"Ninataka amani"

wao ni wa vita

"wanataka vita"

Psalms 121

Psalms 121:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

nitainua macho yangu

Msemo huu unamaanisha "kutazama" au "kuvuta macho kwa"

Msaada wangu utatoka wapi?

Mwandishi anatumia swali kuvuta nadhari katika chanzo cha msaada wake. Swali hili la balagha linaweza kuelezwa kama kauli. "Nitakwambia msaada wangu unatoka wapi."

Msaada wangu unatoka kwa Yahwe

Hili ni jibu la swali lililopita.

Psalms 121:3

Taarifa ya Jumla:

Hapa ni uhamisho kwenda katika hali ya mtu wa pili. Hii inaweza kumaanisha 1) mwandishi anaanza kuzungumza na wtu wa Israeli au 2) mwandishi anamnukuu mtu mwingine akizungumza na mwandishi.

mguu wako kuteleza

Kuteleza kwa mguu kunahusishwa na kuanguka. "wewe kuanguka"

yeye anayekulinda ... mlinzi

Misemo hii miwli inamaana kitu kimoja, na inasisitiza nafasi ya Mungu kama mlinzi.

yeye anayekulinda hatalala

Hapa "kulala" inamaanisha kuacha kulinda. Hali yake hasi inaimarisha msemo. "Mungu hatalala na kuacha kuwalinda" au " Mungu atawalinda daima"

hatalala ... huwa halali wala kusinzia

Misemo hii miwli inamaana sawa. Msemo wa pili unaimarisha wazo la kwanza.

Tazama

Neno hili linatufanya kuzingatia kwa makini taarifa zinazofuata.

huwa halali wala kusinzia

Mananeo haya mawili yana maana sawa. Hapa "kulala" inamaana kuacha kulinda. Hali yake hasi inaimarisha msemo. "hatalala na kuacha kuwalinda" au "atawalinda daima"

Psalms 121:5

Yahwe ni kivuli katika mkono wako wa kuume

Hapa "kivuli" inamaanisha ulinzi. "Mungu yuko pembeni yako kukulinda dhidi ya vitu vinavyoweza kukudhuru"

mkono wako wa kuume

Hapa msemo huu unamaanisha kuwa pembeni au karibu na mwandishi.

Jua halitakudhuru mchana, wala mwezi usiku

Maneno haya ya tofauti ya "mchana" na "usiku" yanamaanisha tofauti hizo mbili na kila kitu katikati. "Mungu anakulinda na vitu vyote wakati wote"

wala mwezi usiku

Inadokezwa kuwa "hautakudhuru" ndio inadokezwa hapa. Maana kamili ya sentensi hii inaweza kuwekwa wazi. "wala mwezi hautakudhuru usiku"

Psalms 121:7

Yahwe atakulinda ... atalinda maisha yako ... Yahwe atakulinda

Misemo hii ina maana ya kufanana. Kurudia kunaimarisha mawazo.

maisha yako

Hii inamaanisha mwandishi. "wewe"

Psalms 122

Psalms 122:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

Yerusalemu, miguu yetu inasimama ndani ya malango yako!

Mwandishi anasitisha kuzungumza na wasikilizaji wake kwa muda na kuzungumza moja kwa moja na mji wa Yerusalemu. Yerusalemu inasemeshwa kana kwamba ni mtu anayeweza kusikia na kuandika.

miguu yetu inasimama

Hapa "miguu" inamaanisha mtu mzima. "tunasimama"

ndani ya malango yako

Hapa "malango" inamaanisha mji. "ndani yako, Yerusalemu"

Psalms 122:4

jina la Yahwe

Hapa "jina" linamaanisha Yahwe mwenyewe. "Yahwe"

nyumba ya Daudi

Hapa "nyumba" inamaanisha uzao wa Daudi. "uzao wa Daudi"

Psalms 122:6

Wale wanaokupenda wawe na amani ... amani ndani ya ngome yenu

Sehemu hii inaeleza ujao wa maombi ambayo mwandishi anataka wasikilizaji wake waombe. Anawaomba kuzungumza moja kwa moja na mji wa Yerusalemu, kana kwamba mji ni mtu anayeweza kuwasikia.

Iwepo amani ndani ... iwepo amani ndani

Misemo hii miwili ina maana sawa na pamoja kuimarishana. "watu wa Yerusalemu waishi kwa amani"

ndani ya kuta inayowalinda ... ndani ya ngome yenu

Hapa Yerusalemu inaelezewa kwa kuta zinazoilinda. "ndani ya Yerusalemu"

Psalms 122:8

Taarifa ya Jumla:

Katika sehemu hii, mwandishi anazungumza moja kwa moja na mji wa Yerusalemu, kana kwamba mji ni mtu anayeweza kuwasikia.

Kwa ajili yako

"Kwa faida yako"

Kuwe na amani ndani yako

"Ninaomba kwamba watu ndani yako waishi kwa amani"

nitatafuta mema kwa ajili yako

Nomino dhahania ya "mema" inaweza kuelezwa kama kitendo. "natama kwamba watu wawatende wema"

Psalms 123

Psalms 123:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

Nainua macho yangu

Hapa mwandishi anamaanisha macho yake kwa sababu ndiyo sehemu ya mwili inayotumika kuonea. "Nitakutazama"

umesimikwa

kuketi kwenye kiti cha enzi na kutawala kama mfalme

kama macho ya mtumishi ... kama macho ya mjakazi ...kwa hiyo macho yetu yanatazama

Misemo hii mitatu inamaana ya kufanana. Msemo wa tatu, unaohusu Waisraeli, unalinganishwa na jinsi watumishi na wajakazi wanavyowatazama bwana zao na bimkubwa wao kwa ajili ya msaada. "Macho" yanaashiria mtu mzima.

mkono wa bwana ... mkono wa bimkubwa

Hapa "mkono" unaashiria utoaji wa mahitaji. "utoaji wa bwana ... utoaji wa bibi"

wajakazi

"watumishi wasichana"

bimkubwa

mwanamke mwenye mamlaka juu ya watumishi wasichana.

awe na huruma kwetu

Nomino dhahania ya "huruma" inaweza kuelezwa kama kitendo. "kutendea kwa huruma"

Psalms 123:3

Uwe na huruma kwetu

Nomino dhahania ya "huruma" inaweza kuelezwa kama kitendo. "kutendea kwa huruma"

tumeshiba ... Tumeshiba zaidi

Misemo hii miwili inamaana ya kufanana, wa pili unaongeza ukali wa ile wa kwanza.

tumeshiba aibu

Hapa aibu inazungumziwa kana kwamba ni kitu kinachoweza kumjaa mtu. "tumefedheheka sana"

Tumeshiba zaidi

Lahaja hii inamaanisha idadi imezidi kwa ubaya. "tumepata kingi sana"

kejeli ... na dharau

Misemo hii miwili inamaana ya kufanana na inatumika pamoja kusisitiza jinsi gani walivyo dhihakiwa na watu.

kejeli

kudhihaki au kutukana

jeuri

Hii inaashiria watu wenye jeuri. "watu wasio na adabu na wenye kiburi"

wenye kiburi

Hii inaashiria watu wenye kiburi. "watu walio na kiburi"

Psalms 124

Psalms 124:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi.

Kama Yahwe asingekuwa upande wetu ... basi wangetumeza tukiwa hai

Hii ni kauli ya nadharia tete inayoeleza matokeo ambayo hayakutokea, kwa sababu Yahwe alikuwa upande wao. "Yahwe alikuwa upande wetu ... kwa hiyo hawakuweza kutumeza tukiwa hai"

Kama Yahwe asingekuwa upande wetu ... kama asingekuwa Yahwe aliyekuwa upande wetu

Misemo hii miwili inamaana moja. "Bila msaada wa Yahwe ... bila msaada wa Yahwe"

wangetumeza tukiwa hai

Sitiari hii inaeleza jinsi Waisraeli ambavyo wangeweza kufa kama mnyama mkali anavyoshambuli mnyama mdogo kumla. "wangetuua"

hasira yao ilipowaka dhidi yetu

Hapa "hasira yao" inamaanisha adui waliokuwa na hasira. "walikuwa wametukasirikia sana"

Psalms 124:4

Taarifa ya Jumla:

Katika mistari hii miwili mwandishi anafananisha adui wa Israeli na mafuriko ya maji.

Maji yangetubeba ... yangetuzamisha

Hii inaendela kauli ya nadharia tete kutoka mstari uliopita. Inaeleza matokeo ambayo hayakutokea, kwa sababu Yahwe alikuwa upande wao. "Maji hayakutubeba ... hayakutuzamisha"

Maji ... mbubujiko wa nguvu ... maji ya nguvu

Misemo hii ina maana sawa.

yangetubeba ... ungetulemea ... yangetuzamisha

Misemo hii ina maana sawa.

Maji yangetubeba

Hapa adui wa Mwandishi wanazungumziwa kana kwamba ni mafuriko ya mji. "Adui zetu wangetushinda kwa urahisi"

mbubujiko wa nguvu ungetulemea

Hapa adui wa Mwandishi wanazungumziwa kana kwamba ni mafuriko ya maji ambayo yangewazamisha Waisraeli. "adui zetu wangetulemea"

maji ya nguvu yangetuzamisha

Hapa adui wa Mwandishi wanazungumziwa kana kwamba ni mto wenye hasira kali ambao ungewazamisha Waisraeli. "adui zetu wangetuangamiza"

Psalms 124:6

kuchanwa na meno yao

Adui wanazungumziwa kana kwamba ni wanyama pori ambao wangewaangamiza Waisraeli kwa kuwala. "tuangamizwe kana kwamba tunaliwa na wanyama pori"

tumetoroka kama ndege kutoka kwenye kitanzi cha wawindaji wa ndege

Mwandishi anaelezea kutoroka kwake kutoka kwa adui zake kana kwamba likuwa ndege aliyetoroka kwenye mitego ya wawindaji. "tumetoroka kutoka kwa adui zetu kama ndege anavyotoroka mtego ambao mwindajia ametega"

kitanzi

mtego mdogo wa kamba au uzi unaotengenezwa kukamatia wanyama wadogo au ndege

kitanzi kimekatika

Mpango wa adui kumshika mwandishi umeshindwa kana kwamba ni kitanzi kilicho katika.

Psalms 125

Psalms 125:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kihebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

Wale wanaomtumaini Yahwe ni kama mlima Sayuni, hautikisiki, hudumu milele

Watu wanaomuamini Yahwe wanazungumziwa kana kwamba ni mlima Sayuni. Milima haiwezi kusogea.

Kama milima inavyoizunguka Yerusalemu, hivyo hivyo Yahwe anawazunguka watu wake

Ulinzi wa Yahwe unazungumziwa kana kwamba alikuwa ni milima ilyowazunguka. Yerusalemu ilikuwa imezungukwa na milima kadhaa, iliyoilinda dhidi ya mashambulizi. "Kama milima iliyoizunguka Yerusalemu inavyoilinda, kwa hiyo Yahwe anawalinda watu wake"'

sasa na milele

Hapa msemo huu unamaanisha "daima."

Fimbo ya uovu

Hapa fimbo ya uovu inaashiria utawala wa watu waovu. "watu waovu" au "Viongozi waovu"

Psalms 125:4

Fanya wema, Yahwe

Hili ni ombi. Nomino dhahania "wema" inaweza kuelezwa kama tendo. "Yahwe, tafadhali fanya vitu vizuri" au "Yahwe, nakusihi ufanye vitu vizuri"

walio sawa mioyoni mwao

Hapa "mioyoni" inamaanisha hamu. "hamu ya kufanya kilicho sawa"

geukia

Kukataa kumti Yahwe kunazungumziwa kama kugeuka kutoka njia nzuri. "acha kizuri na kwenda"

njia zao zilizopinda

Hapa njia za uovu zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa ni njia ambayo haiko wima. "njia zao za uovu"

atawaongoza

Watu wanaongozwa ili kuadhibiwa. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "kuwaongoza ili kuwaadhibu"

Psalms 126

Psalms 126:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kihebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

aliporejesha utajiri wa Sayuni

"alipoifanya Sayuni kufanikiwa tena"

Psalms 126:2

midomo yetu ilijawa na kicheko

Kucheka kunazungumziwa kana kwamba midomo yao ilikuwa ni chombo, na kicheko chao kilikuwa ndani yake. Inaweza kuwekwa wazi kuwa kicheko hiki kilikuwa na mrejesho wa furaha. "tulicheka kwa furaha"

ndimi zetu na kuimba

Kitenzi "kujawa" kinaweza kuelezwa vizuri. Kuimba kunazungumziwa kana kwamba ndimi zao zilikuwa vyombo, na kuimba kulikuwa ndani yake. "ndimi zetu zilijawa na kuimba" au "tuliimba nyimbo za furaha"

wakasema miongoni mwa mataifa

"watu wamataifa walisema miongoni mwao." Kiwakilishi nomino kinatumika kabla ya kutambulisha kinachozungumzia. Hii sio kawaida.

Yahwe alitutendea mambo makuu; tumefurahi sana!

"Tumefurahi sana, kwa sababu Yahwe ametenda mambo makuu kwa ajili yetu!"

Psalms 126:4

wale wanaopanda kwa machozi ... Anatoka akilia ... akileta miganda yake

Mistari hii miwili inausambamba. Sentensi ya pili inamaana sawa na sentensi ya kwanza, lakini inatoa maelezo zaidi.

wale wanaopanda kwa machozi

"wale wanaopanda wakiwa na machozi"

Psalms 127

Psalms 127:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kihebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

kuamka mapema, kukawia kurudi nyumbani

Mtu anayefanya kazi kwa bidii mara nyingi inambidi kuamka mapema asubuhi na kuchelwa kurudi nyumbani usiku.

kula mkate wa kazi ngumu

Hii ni lahaja. Mkate mara nyingi humaanisha chakula anachohitaji mtu kila siku ili kuishi. "fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya mahitaji yako ya kila siku"

Psalms 127:3

urithi

"zawadi" au "mali wa dhamani". Watoto kawaida hupokea urithi kutoka kwa wazazi wao. Urithi huenda kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto. Mstari huu unaonesha watoto kama urithi wa wazazi wao.

Kama mishale kwenye mkono wa shujaa, ndivyo walivyo watoto wa ujanani

Mishale ni ya muhimu sana kwa shujaa kwa sababu inamlinda vitani. Watoto wanazungumziwa kana kwamba ni mishale ya shujaa. "Kuwa na watoto wengi kutakulinda"

aliyejaza podo lake nao

Podo ni chombo kwa ajiil ya mishale. Kuwa na watoto wengi kunazungumziwa kana kwamba watoto walikuwa mishale ndani ya podo. "nyumba iliyojaa watoto" au" wato wengi"

Psalms 128

Psalms 128:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kihebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

Amebarikiwa kila mtu anayemheshimu Yahwe

Msemo huu unatoke katika sauti isiyotenda kuashiria kuwa Yahwe halazimiki kumbariki mtu anayemheshimu. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atambariki kila mtu anayemheshimu"

Kile ambacho mikono yako huleta

Mtu anaweza kutambulika kwa mikono yake kwa sababu hiyo ndio sehemu ya mwili anayotumia kufanyia kazi. "Unacholeta" au "Unachofanyia kazi"

utabarikiwa na kufanikiwa

Maneno "kubarikiwa" na "kufnikiwa" ina maana ya kukaribiana na inasisitiza fadhili za Mungu. "Yahwe atakubariki na kukufanikisha" au "Yahwe atakufanya ubarikiwe na ufanikiwe"

Psalms 128:3

kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako

Mke anazungumziwa kama mzabibu uzaao matunda mengi. Hii inaashiria kuwa watoto ni kama matunda na mke atakuwa na watoto wengi. "anazalisha sana na atakupa watoto wengi"

watoto wako watakuwa kama mimea ya mizeituni

Watoto wanalinganishwa na mimea ya mizeituni kwa sababu ya jinsi inavyokuwa na kuzunguka kitu. Watoto wataizunguka meza na kuijaza. "utakuwa na watoto wengi watakao kuwa na kufanikiwa"

wakiizungunka meza yako

Hii inamaanisha sehemu ambapo familia hukusanyika kula. Maranyingi, wote wanaokula kwenye meza ya mtu wako chini ya utawala wake.

mtu atabarikiwa anayemheshimu Yahwe

Hii inaweza kuelezwa katika kitenzi cha kutenda. "Yahwe atambariki mtu anayemheshimu"

siku zote za maisha yako

"maishani mwako mwote"

Amani iwe juu ya Israeli

"Israeli iwe na amani"

Psalms 129

Psalms 129:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

Wakulima wamelima mgongoni mwangu

Mikwaruzo kutokana na kupigwa inazungumziwa kama kulima kwa mkulima. Mkulima alilima mistari yenye kina kirefu kiwanjani. "Adaui zangu wamenikata sana mgongoni mwanga"

wakaifanya mifuo yao kuwa mirefu

Huu ni mwendelezo wa msemo wa ukulima. "Mfuo" ni mstari ambao mkulima aliulima. "walifanya mikwaruzo yao kuwa mirefu"

Psalms 129:4

amekata kamba za waovu

Israeli inazungumziwa kama imefungwa na watu waovu. "ametuokoa na adui zetu"

Wote waaibishwe na kugeuzwa

Yahwe hajatajwa wazi kama ndiye aliyefanya hivi vitu. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Yahwe awaaibishe na kuwashinda"

Psalms 129:6

Na wawe kama ... miganda

Mwandishi wa zaburi anawazungumzia adui zake kufa na kuwa wachache kwa idadi. Wanalinganishwa na nyasi ndogo zinazoota kwenye paa ya nyumba na kukauka na haitoshi kukata au kukusanya. "Na wafe na wawe wachache sana hadi wawe kama nyasi ... miganda"

baraka ya Yahwe iwe juu yako

"Yahwe akubariki"

Psalms 130

Psalms 130:1

Taarifa ya Ujumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kihebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

Toka vilindini

Huzuni ya mwandishi inazungumziwa kana kwamba ni chombo. Huzuni yake inatokea chini ya chombo. Huzuni mwara nyingi huzungumziwa kama chombo kinachojaa kutoka juu hadi chini. "Kwa sababu nina huzuni sana,"

acha maskio yako yawe masikivu

Masikio yanaashiria ni Yahwe, lakini kwa sababu mwandishi anafahamu kuwa Yahwe anasikia kila kitu, anachoomba ni kwa Yahwe kujibu. "tafadhali sikiliza" au "tafashali jibu"

kwa maombi yangu ya huruma

"Huruma" sio kitu kinachoweza kupewa kimwili kwa mtu. Mwandishi anazungumzia kuhusu Yahwe kuwa na huruma kwake. "kwa maombi yangu na kuwa na huruma kwangu"

Psalms 130:3

nani atasimama?

Mwandishi anatumia swali hili kuonesha ubatili wa kuwaza kuwa mtu yeyote anaweza kusimama katika hali hii. Hili swali balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "hakuna anayeweza kusimama."

nani atasimama

"Kusimama" mara humaanisha kutoroka au kupona wakati mtu anaposhambulia. Kwa hali hiyo, itamaanisha kutoroka kutoadhibiwa. "hakuna anayeweza kutoroka adhabu yako" au "hakuna anayeweza kupona adhabu yako"

Psalms 130:5

Nafsi yangu

"Nafsi yangu" inamaanisha mwandishi wa zaburi. "mimi"

Nafsi yangu inasubiri

Mwandishi wa zaburi anazungumziwa kana kwamba anasubiri kitu kwa kutarajia. "Natumaini" au "Nina amini" au "Ninatamani kitu"

Nafsi yangu inasubiri ... zaidi ya walinzi wanavyosubiri asubuhi

Mwandishi wa zaburi anazungumzia hamu yake Bwana kumsaidia kama kuwa zaidi ya ile hamu ya wale wanaofanya kazi usiku kucha wakisubiri asubuhi ifike.

walinzi

Hawa ni wanaume wanaolinda miji au viwanja dhidi ya adui na wezi. Hapa inamaanisha watu wanaokeshi uskiu kufanya hivi.

Psalms 130:7

Israeli ... dhambi zake

Watu wa Israeli wanazungumziwa kana kwamba walikuwa ni mtu. "watu wa Israeli ... zao"

Psalms 131

Psalms 131:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

moyo wangu hauna kiburi au macho yangu majivuno

Moyo na macho yanamwakilisha mtu. "Sina kiburi wala majivuno"

Sina matumaini makubwa kwa ajili yangu

Maana zinazowezekana ni "Sitegemei kufanya mambo makuu" au "Sidhani kuwa mimi ni mkuu"

vitu ambavyo viko njee ya uwezo wangu

Vitu vilivyo vigumu sana kwa mtu kuelewa vinazungumziwa kana kwamba viko nje ya uwezo wa mtu au mbali sana kutoka kwa huyo mtu kuweza kufikia. "vitu vilivyo vigumu sana kuelewa"

Psalms 131:2

Nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu

Nafsi inawakilisha mtu au hisia zake. Kuwa mtulivu na wa amani inazungumziwa kama kufanya nfasi ya mtu kutulia na kuwa kimya. "Nimetulia na nina amani"

nafsi yangu ndani yangu

Nafsi inawakilisha mtu au hisia zake. "mimi"

mtoto aliyeachishwa kifuani mwa mama yake

Mwandishi anajizungumzia kuridhika na kupumzika kana kwamba alikuwa mtoto mchanga ambaye haitaji tena maziwa kutoka kwa mama yake. "kuridhika kama mtoto mchanga ambaye halilii tena maziwa ya mama yake lakini anapumzika mikononi mwake" au "kuridhika na kupumzika"

Psalms 132

Psalms 132:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

kwa ajili ya Daudi

"kwa sababu ya kilichotokea kwa Daudi"

ita katika kumbukumbu

"kumbuka" au "fikiri kuhusu"

Hodari wa Yakobo

Hii inamaanisha Mungu.

Psalms 132:3

Akasema

"Mfalme Daudi alisema"

Sitayapa usingizi macho yangi wa kupumzika kwa vigubiko vya macho yangu

Usingizi na kupumzika zinazungumziwa kana kwamba ni vitu vinavyoweza kupewa. Hapa macho na vigubiko vya macho vinawakilisha mtu mzima. "Sitaruhusu macho yangu kulala wala vigubiko vya macho yangu kupumzika" au "sitalala wala kufunga macho yangu kupumzika"

hadi nipate sehemu kwa ajili ya Yahwe

Kujenga sehemu kwa ajili ya Yahwe inazungumziwa kama kumtafutia sehemu. "hadi nijenge sehemu kwa ajili ya Yahwe"

Hodari wa Yakobo

Hii inamaanisha Mungu.

Psalms 132:6

tulisikia kuihusu Efrata

Kitu kinachozungumziwa inawezekana ni sehemu ambapo sanduku takatifu la Mungu lilipokuwa. Msemo "Efrata" inawezekana kumaanisha sehemu waliyokuwa wakati wakisikia habari yake. Hii inaweza kuwekwa wazi. "sisi tuliokuwa Efrata tulisikia kuhusu ambapo sanduku takatifu lilipo" au " sisi tulioko Efrata tulisikia kuwa sanduku takatifu lilikuwa Yearimu"

viwanja vya Yearimu

Hii inaweza kumaanisha viwanja vinavyouzunguka mji.

tutaabudu miguuni pake

Kumwabudu Mungu katika sanduku la agano inazungumziwa kama kusujudu kwenye miguu ya mfalme anayeketi katika kiti chake cha enzi. Hii inaonesha unyenyekevu na usikivu kwa Mungu. "tutaenda kwenye sanduku la agano la Mungu na kumwabudu kama mfalme"

Inuka, Yahwe, kwenye sehemu yako ya kupumzikia

Kitenzi "njoo" kinaweza kuelezwa wazi. "Inuka, Yahwe, na uje kewnye sehemu yako ya kupumzika"

sehemu yako ya kupumzikia

Sehemu ambayo Mungu alichagua ya watu kumwabudu inazungumziwa kama sehemu anayopumzikia au anapoishi milele. "sehemu unayokaa" au "hema lako"

wewe na sanduku la nguvu yako!

Maana zinazowezekana ni 1) "njoo kwenye sanduku la nguvu yako" au 2) "njoo, na ufanye sanduku la nguvu yako lije."

sanduku la nguvu yako

"sanduku linaloonesha uwezo wako mkuu"

Psalms 132:9

Makuhani wako wavikwe na uadilifu

Uadilifu unazungumziwa kana kwamba ni nguo. "Watu watambue kuwa makuhani wako wana uadilifu" au "Nataka watu waone kuwa makuhani wako daima hufanya kilicho sawa"

Kwa ajili ya mtumishi wako Daudi

"Kwa sabau ya kilichotokea kwa mtumishi wako Daudi."

usigeuke kutoka kwa mfalme wake aliyetiwa mafuta

Hapa "kugeuka" inamaanisha kumkataa mtu. "usimuache mfalme uliyemtia mafuta"

Psalms 132:11

Nitamweka mmoja wa uzao wako kenye kiti chako cha enzi

Kumfanya uzao wa mfalme kuwa mfalme badala yake inazungumziwa kama kumweka katika kiti cha enzi cha huyo mfalme. "Nitasababisha mmoja wa uzao wako kutawala Israeli katika nafasi yako"

wataketi kwenye kiti chako cha enzi

Kutawala kama mfalme inazungumziwa kama kuketi kwenye kiti cha enzi.

watoto wako

Hapa "watoto wako" inawakilisha uzao wa Daudi watakao kuwa wafalme. "uzao wako"

Psalms 132:13

Taarifa ya Jumla:

Katika mstari wa 13 anayetamani ni Yahwe na mstari wa 14 anayezungumza ni Yahwe. Yule anayetamaniw ni Sayuni.

Sayuni ... amemtamani ... ninmtamani

Mwandishi anaandika kana kwamba mji wa Sayuni ulikuwa ni mwanamke.

amemtamani kwa ajili ya kiti chake

Hapa "kiti" kinaashiri kati ya 1) kiti chake cha enzi atakapotawala, au 2) sehemu atakayo ishi.

amemtamani kwa ajili ya kiti chake

Yahwe ametamani Sayuni kwa ajili ya kiti cha Yahwe." Hii inaonesha washiriki halisi.

sehemu yangu ya kupumzika

Sehemu ambayo Mungu alichagua ya watu kumwabudu inazungumziwa kama sehemu anayopumzikia au anapoishi milele. "sehemu ninayokaa" au "hema langu"

Psalms 132:15

Kauli Unganishi:

Mungu anaendelea kuzungumzia mji wa Sayuni kana kwamba Sayuni ni mwanamke.

Nitambariki sana

"Nitambariki sana Sayuni"

Nitawaridhisha maskini wake kwa mkate

Hapa "maskini" inamaanisha watu maskini waliomo Sayuni. Hapa "mkate" inaweza kumaanisha chakula kwa ujumla. "Nitawaridhisha watu wa Sayuni kwa chakula"

Nitawavika makuhani wake na wokovu

Wokovu unazungumziwa kana kwamba ni nguo. Maana zinazowezekana ni 1) "Nitawasababisha makuhani kuenenda kwa namna inayostahili ya wale niliowaokoa" au 2) "Nitawaokoa makuhani wake"

Psalms 132:17

Nitafanya pembe lichomoze kwa ajili ya Daudi

Mungu anazungumzia mwana mwenye nguvu wa Daudi kana kwamba alikuwa ni pembe lenye nguvu la mnyama. "Nitamfanya mwana wa Daudi awe mfalme baada yake" au "Nitamfanya Daudi awe na mwana katika uzao wake atakaye kuwa mfalme mwenye nguvu"

nitaweka taa kwa ajili ya mtiwa mafuta wangu

Mungu anazungumzia kusabisha uzao wa Daudi kuendelea kutawala kama wafalme kana kwamba walikuwa ni taa inayoendela kung'aa. "Nitafanya uzao wa mtiwa mafuta wangu kuendelea kutawala kama wafalme"

mtiwa mafuta wangu

"mfalme wangu niliye mchagua" au "mfalme niliye mchagua"

Nitawavika adui zake na aibu

Aibu inazungumziwa kana kwamba ni nguo. Aibu hii inatokana na kushindwa vitani. "Nitawafanya adui zake washindwe vitani na waaibike"

taji lake linatang'aa

Taji linawakilisha utawala wake, na ukuu unnazungumziwa kama kung'aa"

Psalms 133

Psalms 133:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

Tazama

Hili neno linatumika kusisitiza umuhimu wa kauli inayofuata.

kwa ndugu kuishi pamoja

Uhusiano miongoni mwa watu wa Mungu unazungumziwa kama ndugu. "kwa watu wa Mungu kuishi pamoja kwa amani kama ndugu"

Psalms 133:2

Ni kama mafuta mazuri kichwani

Uzuri wa umoja miongoni mwa watu wa Mungu unazungumziwa kana kwamba yalikuwa mafuta mazuri yaliyomwagwa kichwani pa Haruni. "Huu umoja ni wa dhamani kama mafuta yaliyomwagwa kwenye kichwa cha Haruni.

kama umande wa Hermoni

Uzuri wa umoja miongoni mwa watu wa Mungu unazungumziwa kana kwamba ulikuwa umande unaoburudisha. "unaburudisha kama umande wa hermoni"

Hermoni

Huu ni mlima katika Israeli wenye theluji mwaka mzima.

Psalms 134

Psalms 134:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

wimbo wa upaaji

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi."

watumishi wote wa Yahwe

"wote mnaomtumikia Yahwe"

Inueni mikono yenu

Hivi ndivyo watu walivyoomba au kumsifu Mungu.

kwenye sehemu takatifu

Maana zinazowezekana ni 1) "kwenye hekalu" au 2) "kwenye sehemu takatifu hekaluni"

Psalms 134:3

mbingu na nchi

Msemo "mbigu na nchi" hapa unaashiria vitu vyote. "vitu vyote mbinguni na duniani"

Psalms 135

Psalms 135:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Lisifuni jina la Yahwe

Jina la Yahwe linamwakilisha yeye. "Msifuni Yahwe" au "Msifuni yeye"

simama katika nyumba ya Yahwe

Hii inawakilisha kumtumikia Yahwe hekaluni mwake.

Yahwe ... Mungu wetu

"Mungu wetu" inamaanisha Yahwe.

Psalms 135:3

kwa kuwa ni vyema kufanya hivyo

"kwa sababu tunapata raha kwa kulisifu jina lake"

Yahwe amemchagua Yakobo

"Yakobo" hapa inamaanisha uzao wake, watu wa Israeli. "Yahwe amewachagua uzao wa Yakobo"

Israeli kama mali yake

"ameichagua Israeli kuwa mali yake"

Psalms 135:5

kuwa Bwana wetu yuko juu ya miungu yote

"ninajua kuwa Bwana wetu yuko juu ya miungu yote." Kuwa mkuu zaidi ya kitu inazungumziwa kama kuwa juu yake. "kuwa Bwana wetu ni mkuu zaidi ya miungu yote"

Psalms 135:7

kuleta upepo kutoka kwenye ghala lake

Ghala ni sehemu ambapo vitu hutunzwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Picha hii inaonesha nguvu ya Mungu kuumiliki upepo. "kuusababisha upepo kupuliza kwa uwezo wake"

Psalms 135:8

ishara na maajabu

Maneno haya mawili yana maana moja na yanamaanisha matatizo ya kimiujiza ambayo Mungu alisababishia Misri.

katikati yenu, Misri

Mwandishi anazungumza kana kwamba watu wa Misri walikuwa wakimsikiliza. "katikati yenu watu wa Misri" au "katikati ya watu wa Misri"

dhidi ya Farao

"kumwadhibu Farao"

Psalms 135:10

Sihoni ... Ogu

Haya ni majina ya wanaume wawili.

Psalms 135:12

Alitupa nchi yao kama urithi

Zawadi ya Mungu ya nchi kwa Wasiraeli inazungumziwa kana kwamba ni urithi kutoka kwa baba kwenda kwa mwana. "Alitupa nchi yao kuwa nayo milele" au "Alitupa nchi yao kuwa yetu milele"

Jina lako

Jina lake hapa linawakilisha umaarufu wake au sifa yake. "Umaarufu wako" au "Sifa yako"

Psalms 135:19

yeye anayeishi Yerusalemu

Mungu anazungumziwa kana kwamba aliishi Yerusalemu kwa sababu hekalu ambalo Waisraeli walimwabudia lilikuwa huko. "yeye ambaye hekalu lake liko Yerusalemu"

Psalms 136

Psalms 136:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

O

Huu ni mshangao.

Mungu wa miungu

Mungu aliye mkuu zaidi ya miungu mingine ambayo watu huabudu.

Psalms 136:4

kwa hekima

Kwa sababu ana hekima.

Psalms 136:6

aliyesambaza dunia juu ya maji

Waisraeli wa zamani walidhani kwamba nchi kavu ya dunia ilikuwa juu ya bahari. "aliyeweka dunia juu ya maji"

taa kuu

Hii inamaanisha vyanzo vya nuru kwa ajili ya dunia, hasa jua na mwezi. "jua na mwezi na nyota"

Psalms 136:8

kutawala machan ... kutawala usiku

Jua, mwezi, na nyota zinazungumziwa kana kwamba ni wafalme. "kuweka alama ya muda wa siku ... kuweka alama ya muda wa usiku"

Psalms 136:10

kutoka miongoni mwao

"kutoka miongoni mwa watu wa Misri"

kwa mkono wenye nguvu na ulioinuka

Hapa "mkono" inawakilisha uwezo. "kwa uwezo mkuu"

Psalms 136:13

bahari la Matete

wanajeshi wa Farao walizama katika bahari la Matete.

akampindua Farao

Hapa kushindwa kunazungumziwa kama kumpindua mtu. "akamshinda Farao" au "akamshinda mfalme wa Misri"

Farao

Jeshi la Farao.

Psalms 136:18

Sihoni ... Ogu

Wafalme hawa walikuwa wafalme wawili tu kati ya wengi ambao Mungu aliwawezesha Waisraeli kuwashinda.

Psalms 136:21

alituita akilini

"alituwaza"

kutusaidia katika aibu yetu

Hali ya kuhisi aibu inazungumziwa kana kwamba ni sehemu ambayo Waisraeli walikuwepo. Hii kumbukumbu ya nyakati nyingi ambapo adui wa israeli walishindwa katika vita na kuwaaibisha. "kutujali wakati tulipoaibishwa"

Psalms 136:24

ametupa ushindi juu adui zetu

Kusababisha watu kuwa washindi na kuwashinda adui zao inazungumziwa kama kuwapa ushindi, kana kwamba ushindi ni kitu kinachoweza kupewa. "ametufnay kuwa washindi juu ya adui zetu" au "ametufanya kuweza kuwashinda adui zetu"

Mungu wa mbinguni

Mungu anayeishi mbinguni" au "Mungu ambaye viumbe wa mbinguni wanamwabudu"

Psalms 137

Psalms 137:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kando ya mito ya Babeli

"Katika mto mmoja karibu na Babeli"

tulikaa ... kulia ... tulipo fikiria ... tulininginiza

Mwandishi hawajumuishi wasomaji.

Katika mpopla huko

Miti ya mpopla haioti Israeli. "Mpopla" hapa inaweza kuwakilisha miti yote Babeli. "Katika miti ndani ya Babeli"

Psalms 137:3

waliotuchukua mateka walitaka nyimbo kutoka kwetu

Hapa "nyimbo" inaashiria vitendo vya kuimba. "waliotuchukua mateka walitaka tuimbe"

walitaka tuwe na furaha

"walitufanya tujifanye kana kwamba tuna furaha"

moja ya nyimbo za Sayuni

Hii inaweza kumaanisha nyimbo ambazo Waisraeli walitumia katika kuabudu hekaluni Yerusalemu.

Psalms 137:5

Nikisahau kumbukumbu yako, Yerusalemu

Mwandishi anazungumza kana kwamba Yerusalemu inamsikiliza. "Nikifanya kana kwamba nimekusahau, Yerusalemu" au "Nikijaribu kukusahau, Yerusalemu"

mkono wa kuume

mkono ambao watu wengi hutumia zaidi

Psalms 137:7

Kuita akilini

"Kukumbuka" au "Kufikiria"

Kuita akilini, Yahwe, walichofanya Waedomu

Hapa kukumbuka kile ambacho Waedomu walichofanya inawakilisha kuwaadhibu kwa kile walichotenda. "Waadhibu Waedomu, Yahwe, kwa kile walichotenda"

siku ambayo Yerusalemu ilianguka

Yerusalemu kukamatwa na jeshi la adui inazungumziwa kana kwamba imeanguka. Aliyeikamata Israeli inaweza kuwekwa wazi. "siku ambayo Yerusalemu ilikamatwa" au "siku ambayo jeshi la Babeli liliingia Yerusalemu"

Psalms 137:8

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anawahutubia watu wa Babeli kana kwamba wanamsikiliza.

Binti wa Babeli

Hii inamaanisha mji wa Babeli na watu wake.

na mtu abarikiwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu ambariki mtu"

anayekulipa kwa kile ulichokifanya kwetu

Mwandishi anazungumzia mtu kuwatendea wengine alichotendewa kana kwamba ni malipo. "kufanya kwako ulichofanya kwetu"

kuwaseta wadogo wenu kwenye mwamba

"kuponda vichwa vya watoto wenu kwenye miamba"

Psalms 138

Psalms 138:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Nitakupa shukrani na moyo wangu wote

Hapa moyo unawakilisha hisia. Kufanya kitu kwa dhati au kamili inazungumziwa kama kukifanya kwa moyo wote. "Nitakushukuru kwa dhati"

mbele ya miungu

Maana zinazowezekana ni 1) "licha ya sanamu za uongo zilizopo" au 2) "mbele ya mkusanyiko wa mbinguni," ambayo inamaanisha "katika ufahamu wa malaika mbinguni"

Nitasujudu

Kusujudu ni kitendo cha ishara kinachowakilisha kuabudu au kutoa heshima. "Nitakuabudu"

kutoa shukrani kwa jina lako

"kukupa wewe shukrani"

neno lako

Hii inamaanisha kile ambacho Mungu amesema. "kile ulichosema" au "amri zako na ahadi zako"

jina lako

Maana zinazowezekana ni 1) "mwenyewe" au 2) "umaarufu wako"

Psalms 138:3

Wafalme wote wa ulimwenguni

"Viongozi wote wa duniani"

mdomo wako

Msemo huu unamwakilisha Mungu mwenyewe. "wewe"

Psalms 138:5

Yahwe yuko juu, lakini anawajali walio chini

Yahwe yuko juu ya uumbaji wote katika nguvu, nafasi, na mamlaka. Lakini shauku lake ni kwa wale walio wanyenyekevu wa moyo, watumishi kwa wote. Hii ni tofauti rahisi.

wenye majivuno anawajua kwa mbali

Msemo huu unaweza kuwa unamaanisha kuwa Mungu sio mwaminifu kwa wale wenye majivuno.

Psalms 138:7

natembea

kuishi

katikati ya hatari

Kuwa hatarini inazungumziwa kama kuwa katika sehemu ya kimwili.

utafika na mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu

Mungu anazungumziwa kana kwamba atawapiga adui kwa mkono wake.

hasira ya adui zangu

Hasira inazungumziwa kana kwamba ni kitu badala ya hisia. "adui zangu, ambao wana hasira"

mikono yako imeumba

Mungu anazungumziwa kana kwamba alitumia mikono yake kihalisia kuumba. "umeumba"

wale ambao mikono yako imeumba

Msemo huu unawezekana kumaanisha taifa la Israeli.

Psalms 139

Psalms 139:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

umenichunguza

"umenipima"

ninapoketi na ninapoinuka

Mwandishi wa zaburi anatumia vitendo hivi viwili kuwakilisha kila kitu afanyacho. "kila kitu ninachofanya" au "kila kitu kunihusu mimi"

Psalms 139:3

njia yangu na kulala kwangu

Hapa "njia" inamaanisha tabia. "Njia yangu na kulala kwangu" kwa pamoja zinamaanisha kila kitu kuhusu mwandishi wa zaburi.

kabla kuna neno kwenye ulimi wangu

Hapa "neno kwenye ulimi" linawakilisha maneno. "kabla sijasema kitu"

Nyuma yangu na mbele yangu unanizunguka

Maelezo haya yanamaanisha uwepo wa Mungu kila sehemu.

kuweka mkono wako juu yangu

Msemo huu unamaanisha uongozo na msaada. "unaniongoza na kunisaidia"

mwingi sana kwangu

"mwingi sana kwangu kuelewa"

uko juu sana; na siwezi kuufikia

Kuwa juu na nje ya uwezo ni usemi, kwa hali hii, kuhusu maarifa ambayo wanadamu hawawezi kuwa nao. "ni magumu sana kuelewa"

Psalms 139:7

Naweza kwenda wapi mbali na Roho yako? ... Naweza kuukimbia wapi uwepo wako?

Maswali haya mawili yana usambamba. Mwandishi wa zaburi anasema kwamba hawezi kuepuka uwepo wa Mungu. "Siwezi kuitoroka Roho yako."

nikitengeneza kitanda changu kuzimu

"Kutengeneza kitanda cha mtu" inamaanisha kuishi sehemu. "hata kama nikiishi kuzimu"

Psalms 139:9

Kama nikipaa kwenye mbawa za asubuhi na kwenda kuishi kwenye sehemu za mbali za bahari

Mwandishi aneleza kwamba popote alipo, Mungu yupo pia.

Kama nikipaa kwenye mbawa za asubuhi

Katika sehemu ya zamani karibu na mashariki, jua lilifikiriwa kana kwamba lina mbawa zilizoliwezesha kupaa juu ya anga. "Kama jua lingeweza kunibeba lenyewe juu ya anga"

kwenye sehemu za mbali za bahari

"mbali sana magharibi"

utanishikilia

"utanisaidia"

Psalms 139:11

Kama ningesema, "Hakika giza litanifunika

Mwandishi wa zaburi anazungumzia usiku kana kwamba ni blangeti inayoweza kumfunika.

Usiku utang'aa kama mchana

Usiku, ambao ni giza, unazungumziwa kana kwamba unang'aa mwanga.

Psalms 139:13

Umeunda sehemu zangu za ndani

"Sehemu za ndani" inamaanisha sehemu za ndani za mwili za mtu, lakini usemi huu hapa unaweza kuwa unamaanisha mwili mzima. "Umeumba mwili wangu wote"

Nafsi yangu inatambua hili vizuri

Hapa "nafsi" inaweza kumaanisha uwezo wa ndani wa mwandishi wa zaburi kuwa na uhakika na upendo na uongozo wa Mungu. "Ninajua hili kwa moyo wangu wote'

Psalms 139:15

nilipoumbwa kwa ustadi

"uliniumba kwa ustadi mkubwa"

katika sehemu za chini za nchi

Hii inawezekana kuwa namna kuzungumzia tumbo la mama mzazi.

siku zangu zote nilizopewa ziliandikwa kwenye kitabu chako hata kabla ya kwanza haijatokea

Msemo huu unashiria kuwa Waisraeli wa zamani walifikiri kuwa Mungu aliandika mipango yake kwenye kitabu.

Psalms 139:17

thamani

"muhimu"

Idadi yake ni kubwa kiasi gani!

"Mawazo yako ni mengi sana."

yatakuwa zaidi ya namba ya mchanga

"hayahesabiki"

Psalms 139:19

nendeni mabli na mimi, nyie watu wenye vurugu

Mwandishi wa zaburi anajifanya kuzungumza moja kwa moja na watu wenye vurugu ambao anao akilini.

Wanaasi dhidi wako

"Wanaasi dhidi ya mamlaka yako, Mungu"

adui zako wanasema uongo

"adui zako wanadanganya kukuhusu"

Psalms 139:21

Je, siwachukii wale, Yahwe, wanaokuchukia? Je, siwachukii wale wanaoinuka dhidi yako?

Sentensi hizi mbili zinamaana ya kufanana. Sentensi ya pili inaimarisha wazo la ya kwanza. Maswali yote haya mawili yanaweza kuunda kauli.

wanaoinuka dhidi

kuasi dhidi ya

Psalms 139:23

Nichunguze

Hili ni ombi kwa Mungu kumwambia mwandishi wa zaburi kuhusu mawazo yoyote ya dhambi anayoweza kuwa nayo. "Tafadhali nichunguze" au "Nakuomba unichunguze"

Nichunguze, Mungu, na ujue moyo wangu; nijaribu na ujue mawazo yangu

Sentensi hizi mbili zinamaana ya kufanana. Sentensi ya pili inaimarisha wazo la ya kwanza.

njia yoyote ya uovu

Hapa "njia" inamaanisha tabia.

njia ya milele

Hapa "njia" inamaanisha kumtumaini na kumtii Mungu. Yeyote "anayetembea" hivi atakuwa na maisha ya milele.

Psalms 140

Psalms 140:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Kwa mwanamuziki mkuu

"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

wanasababisha vita

Hapa "vita" inaweza kumaanisha ugomvi wa aina yoyote, yakiwemo mabishano.

Ndimi zao zinaumiza kama nyoka

Watu wanaosababisha ugomvi kwa yale wanayosema wanazungumziwa kana kwamba wana ndimi za nyoka. Ingawa nyoka hawadhuru kwa ndimi zao, lakini kwa kung'ata kwao na hasa kwa sumu. Wala mtu hawezi kuuchonga ulimi wake. Lakini, wazo la ulimi uliochongeka linamaanisha kuzungumza katika njia inayosababisha shida. Na wazo la nyoka kuwa na ulimi ulio chongeka inawakilisha ukweli kuwa nyoka wengi wana sumu.

Psalms 140:4

mikono ya waovu

nugu ya waovu

wameweka mtego ... sambaza wavu ... weka kitanzi

Aina bayana ya mitego sio muhumi kuliko wazo la kwamba"waovu ... watu wenye vurugu" wanapanga kusababisha shida kwa mwandishi wa zaburi.

Psalms 140:6

sikia vilio vyangu

Huu ni wito wa msaada. "nisikie ninapokuita sasa unisaidie"

unalinda kichwa changu katika siku ya vita

Kichwa cha mtu huwa kwenye hatari kubwa wakati wa vita. "unanilinda ninapoenda vitani"

vita

Hapa"vita" inaweza kumaanisha shida kubwa ya aina yoyote.

usitimize hamu za waovu

"tafadhali usiwaruhusu waovu kupata wanachotamani"

waovu

"watu waovu"

Psalms 140:9

wanainua vichwa vyao

Hii ni ishara ya kuwa na kiburi. "wana kiburi"

acha madhara ya midomo yao wenyewe iwafunike

Hili ni ombi kuwa Mungu atawafanya watenda maovu kuteseka kwa shida walizosababisha kwa maneno waliyosema.

madhara ya midomo yao wenyewe

Taabu walizosababisha wenyewe kwa yale waliyosema.

iwafunike

Basi, wazuie kusababisha shida zaidi.

Acha makaa ya moto yawadondokee; watupe katika moto

Picha ya moto inamaanisha adhabu kali kwa ajili ya waovu.

shimo lisilo na mwisho

Hii inaweza kumaanisha kuzimu, ulimwengu wa wafu.

watu wa ndimi

wale wanaozungumza uovu kuhusu wengine bila sababu.

salama katika nchi

"salama katika maisha haya"

na uovu umwinde mtu mwenye vurugu

Hapa uovu unazungumziwa kana kwamba ni mtu anayelipiza kisasi kwa mtu mwingine.

Psalms 140:12

atampa hukumu mhitaji

Hapa hukumu inazungumziwa kana kwamba ni kit kinachoweza kupewa kwa mtu. "Atatenda katika hali ya kuwasaidia wahitaji"

kwa jina lako

kwako

Psalms 141

Psalms 141:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

kulilia

"nakuomba msaada"

njoo upesi kwangu

Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba Yahwe ni mtu aliyehitaji kuja kutoka sehemu nyingine kumsaidia. "Njoo upesi kunisaidia"

Nisikie ninapokuita

"Tafadhali nisikie ninapokuita" au "Nakuomba unisikie ninapokuita"

Na maombi yangu yawe kama uvumba

"Na maombi yangu yakupendeze kama harufu nzuri ya uvumba unavyowapendeza watu"

maombi yangu

Mwandishi wa zaburi anataka Yahwe kupendeza naye kwa sababu anaomba na kwa sababu ya maneno ya ombi lake.

mikono yangu iliyoinuka

"mikono niliyoinua juu." Mikon iliyo inuka ni njia nyingine ya kusema maombi. Watu waliinua mikono yao walipoomba au kumsifu Yahwe.

iwe kama sadaka ya jioni

iwe kama mnyama aliyechomwa katika madhabahu jioni. Mwandishi anazungumza kana kwamba anataka Yahwe apendezwe naye kama anavyopendezwa na wanaoleta wanyama kwa ajili ya sadaka. Anataka Yahwe apendezwe kwa sababu mwandishi wa zaburi anaomba au kwa sababu ya maneno ya ombi lake.

Psalms 141:3

weka ulinzi juu ya mdomo wangu

Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba maneno maovu ni wafungwa wanaojaribu kutoroka kutoka mdomoni mwake. "tafadhali nisaidie nisiseme mambo yaliyo maovu"

weka ulinzi juu ya

"mwambie mtu alinde"

linda mlango wa midomo yangu

Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba maneno maovu ni wafungwa wanaojaribu kutoroka kutoka mdomoni mwake. "tafadhali nisaidie nisiseme mambo yaliyo maovu"

kushiriki katika vitendo vya dhambi

"kufanya vitendo vya dhambi"

vyakula vyao vitamu

"vyakula maalumu"

Psalms 141:5

anipige

Mwandishi anazungumza kana kwamba kukemewa ni kumpiga mtu kimwili. "nikemee" au "nipige ili nisikie anaponirekebisha"

itakuwa kama fadhili kwangu

"anaponipiga, nitajua kuwa yule anayenipiga ananitendea fadhila"

itakuwa kama mafuta kichwani kwangu

Maana zinazowezekana ni kwamba mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba mtu anayemsahihisha anamwekea mafuta kichwani mwake 1) kumpa heshima. "anaponisahihisha, nitajua kuwa yule anayenisahihisha ananitendea jambo jema" au 2) kufanya kichwa chake kipate unafuu.

na kichwa changu kisikatae kukubali

Kichwa kinamwakilisha mtu. "na niikubali kwa furaha"

maombi yangu daima ni dhidi ya matendo yao ya uovu

Maneno "matendo ya uovu" ni njia nyingine ya kusema watu waliotenda hayo matendo maovu. "Huwa naomba kwamba Yahwe awazuie watu waovu kutenda mambo maovu"

Viongozi wao watatupwa chini

Maana zinazowezekana ni 1) "Mtu atawatupa viongozi wao chini" au 2) "Viongozi wao watawatupa chini."

genge

ardhi yenye mteremko wa ghafla

mifupa yetu imetawanywa

Maana zinazowezekana ni 1) "watu wametupa mifupa yetu pande tofauti" au 2) kama matokeo ya kuanguka katika genge. "miili yetu imevunjika na mifupa yetu imelala ovyo.

Psalms 141:8

macho yangu yako kwako

Macho yanawakilisha mtu mzima. "ninaangalia kuona utakachofanya" au "nategemea unisaidie"

nakukimbilia wewe

"ninakuomba unisaidie"

nafsi yangu

Nafsi ni njia nyingine ya kusema mtu mzima. "mimi"

mitego waliyoniwekea

Mwandishi anazungumzia kumdanganya mtu mzuri ili kwamba mtu mzuri atende dhambi au ili watu waovu wamshinde kana kwamba ilikuwa kuweka mtego kwa ajili ya mnyama. Neno "mitego" ni njia nyingine ya kusema watu wenyewe. "watu wanaotafuta njia za kumdhuru"

vitanzi ... mitego

Vitanzi humnasa mnyama kwa njia ya kama wakati mitego humnasa mnyama kwenye kachumba kado, mara nyingi kaliko undwa kwa chuma au mbao.

mitego ya watenda uovu

"mitego ambayo wanaotenda maovu wametega"

Acha waovu waanguke kwenye nyavu zao wenyewe

Mwandishi wa zaburi anawazungumzia watu waovu kuwadanganya watu wazuri kana kwamba wawindaji wanatega wanyama. "Acha waovu waanguke kwenye mitego ya nyavu waliyoandaa kunasa watu wengine" au " Acha vitu viovu walichopanga waovu kwa ajili ya wenye haki viwatokee waovu wenyewe"

Psalms 142

Psalms 142:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Maschili

Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.

pango

sehemu ya wazi chini ya ardhi yenye ukubwa wa kutosha watu kutembea

Ninalilia msaada kwa Yahwe ... Ninaomba kwa ajili ya fadhili za Yahwe

"Ninalilia na kuomba msaada kwa Yahwe kwa ajili ya fadhili zake"

kwa sauti yangu

"kwa kutumia sauti yangu"

Ninamwagwa kilio changu mbele yake ... namweleza shida zangu

"Ninamwaga kilio changu na shida zangu mbele yake"

Ninamwagwa kilio changu mbele yake

Mwandishi anazungumzia kumweleza Yahwe kwa nini ana huzuni kana kwamba anamwaga kimiminiko kutoka kwenye chombo. "Namwambia yote kuhusu kwa nini nina huzuni"

namweleza shida zangu

"namwambia kuhusu yote yanayonifanya kuwa na wasiwasi"

Psalms 142:3

roho yangu imedhoofika ndani yangu

"niko mnyonge" au "nimekata tamaa sana"

unafahamu njia yangu

"unafahamu njia nayopaswa kuchukua." Mwandishi anazungumza kana kwamba afanyacho mtu ni njia ambayo mtu amepitia. "unafahamu namna ninavyopaswa kuishi"

Katika njia nayopita wameficha mtego kwa ajili yangu

Mwandishi wa zaburi anazungumzia watu kutaka kumdhuru kana kwamba walikuwa wakijaribu kutega mnyama. "Wanafanya mipango ili chochote nitakachofanya wanidhuru"

maisha yangu

Hii ni njia nyingine ya kusema "mimi."

Nikakuita

Huu ni wito wa msaada. "nikuita wewe kwa ajili ya msaada"

fungu langu

Maana zinazowezekana ni 1)"ninachotaka" au 2) "ninachohitaji" au 3) "nilichonacho"

katika nchi ya walio hai

"wakati niko hai"

Psalms 142:6

Sikia wito wangu

Huu ni wito wa msaada. "Nisikilize ninapokuita kwa ajili ya msaada"

Nimeshushwa chini sana

Maana zinazowezekana ni 1) "mimi ni mhitaji sana" na 2) "mimi ni mnyonge sana."

Leta nafsi yangu kutoka gerezani

Hili ni ombi. "nitoe gerezani"

nitoe shukrani kwa jina lako

Neno "jina" ni njia nyingine ya kusema mtu. "kutoa shukrani kwako"

Psalms 143

Psalms 143:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

Sikia ombi langu

Maneno "ombi langu" ni njia nyingine ya kusema mtu anaye omba. "Nisikilie ninapoomba kwako" au "Kuwa tayari kufanya ninachokuomba kufanya"

nijibu

"tafadhali fanya ninachokuomba ufanye"

Usiingie hukumuni

"Tafadhali usinihukumu" au "Nakusihi usinihukumu"

mtumishi wako

Mwandishi anajizungumzia mwenyewe kana kwamba anamzungumzia mtu mwingine. "mimi"

machoni pako hakuna aliye na haki

"haufikiri kuwa yeyote ana haki"

Psalms 143:3

amefuatilia nafsi yangu

"amenifukuza akijaribu kunishika"

amenisukuma chini hadi ardhini

"ameniangamiza kabisa"

Roho yangu imezidiwa ndani yangu

"Mimi mnyonge" au "Nimekata tamaa kabisa"

moyo wangu umekata tamaa

"sina matumaini tena"

Psalms 143:5

Naitisha akilini

"Nafikiria"

mafanikio yako

"yote uliyotimiza" au "mambo yote makuu uliyotenda"

natawanya mikono yangu kwako katika maombi

"naomba kwako na mikono yangu ikiwa imenyanyuka pembeni yangu"

nafsi yangu ina kiu na wewe katika nchi iliyokauka

Mwandishi wa zaburi anazungumzia kutaka kuwa na Mungu kana kwamba yuko katika nchi iliyokauka na pia alikuwa karibu ya kufa kwa kiu. "ninataka kuwa na wewe kama mtu aliye katika nchi iliyokauka mwenye kiu sana anavyotaka maji"

nafsi yangu ina kiu na wewe

Mwandishi anatamani kumjua Yahwe. Mkazo wa hamu yake kumjua yahwe ni kama mtu aliye na kiu sana. "na shauku na wewe"

nafsi yangu

Nafsi ni njia nyingine ya kusema mtu.

nchi iliyokauka

Ardhi ambayo kila kitu kimekufa kwa sababu hakuna maji.

Sela

Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kihebrabia, na zingine haziliweki.

Psalms 143:7

roho yangu ni dhaifu

"mimi ni mnyonge" au "nimekata tamaa sana"

Usifiche uso wako kwangu

Hili ni ombi. "Nakuomba usijifiche kwangu" au "Tafadhali usijifiche kwangu"

Usifiche uso wako kwangu

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kukataa kufanya kile ambacho mwandishi wa zaburi anaomba kana kwamba Yahwe alikuwa anakataa hata kumtazama. "Usikatae kunisikiliza" au "Tafadhali nisikilize"

Nitakuwa kama hao waendao shimoni

"Nitakuwa kama mtu mwingine tu aliyekufa"

Acha nisikie uaminifu wako wa agano

"Nisababishe kusikia uaminifu wako wa agano" au "Niambie uaminifu wako wa agano"

asubuhi

Maana zinazowezekana ni 1) asubuhi ni muda ambao watu wa wakati huo walidhani unafaa kuomba, au 2) "asubuhi kwa asubuhi," kila siku.

Nioneshe

"Niambie"

njia ninayopaswa kutembea

Mwandishi wa zaburi anazungumzia jinsi watu wanavyoishi kana kwamba ni njia ambayo wanatembea. "jinsi unavyotaka niishi"

kwa kuwa ninainua roho yangu kwako

Maana zinazowezekana ni 1) "ninaomba kwako" au 2) "ninaamini kuwa utaniongoza na kunilinda"

Psalms 143:9

Nakimbia kwako kujificha

Maana zinazowezekana ni 1) "Nakimbia kwako ili nijifiche" na 2) "Nakimbia kwako ili unifiche na kunilinda."

kufanya mapenzi yako

"kufanya unachotaka nifanye"

aniongoze katika nchi ya unyofu

Maana zinazowezekan ni 1) "nasaidie niishi kwa haki" au 2) "maisha yangu yawe huru na taabu"

nchi ya unyofu

Maana zinazowezekana ni 1) hii ni sititari ya kuishi maisha ya haki au 2) "nchi tambarare," sitiari ya maisha yasiyokuwa na taabu.

Psalms 143:11

kwa ajili ya jina lako

x

adui wa maisha yangu

"adui wanaotaka kuchukua maisha yangu"

Katika uaminifu wako wa agano wakate adui zangu

"Onesha uaminifu wako wa agano kwa kuwakata adui zangu"

adui wa maisha yangu

"adui wa nafsi yangu" au, kuchukua "maisha yangu" kama njia nyingine ya kusema "mimi", "adui zangu"

Psalms 144

Psalms 144:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Zaburi ya Daudi

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.

mwamba wangu

Maana zinazowezekana ni1) "yule ambaye ananiweka salama" au 2) "yule anayenipa nguvu"

anayefunza mikono yangu kwa ajili ya vita na vidole vyangu kwa mapambano

Maneno "mikono" na "vidole" zinamaana ya "mimi." "anayeniandaa kwa ajili ya vita" au ""anayeniandaa kwa ajili ya mapambano"

uaminifu wangu wa agano

"yule ambaye ananionesha uaminifu wa agano"

ngome yangu ... namkimbilia

Mwandishi wa zaburi anatumia sitiari kusisitiza kwamba Yahwe atamlinda.

mnara wangu wa juu

Daudi anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni ngome inayomlinda dhidi ya mashambulizi. Yahwe ndiye anayemlinda Daudi na hatari.

ngao yangu

Daudi anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni ngao inayomlinda askari. Yahwe ndiye anayemlinda Daudi dhidi ya hatari.

yule ambaye namkimbilia

Kwenda kwa Yahwe kunazungumziwa kama kumkimbilia. "yule ambaye ninaenda kwake kwa ajili ya ulinzi"

yule unayedhibiti mataifa chini yangu

"yule anayenisaidia kuyashinda mataifa mengine"

Psalms 144:3

Yahwe, mtu ni nini hadi unamtambua au mwanadamu hadi unamfikiria?

"Mwanadamu ni mdogo sana ukilinganisha na vingine vyote ulivyoumba hadi ninashangaa kwamba unamtambua na kumwaza"

mtu ... mwanadamu

maneno mawili yote yanamaanisha wanadamu

kama pumzi ... kama kivuli kipitacho

Mwandishi anawafananisha wanadamu na hivi vitu kuonesha jinsi maisha yao yalivyo mafupi.

Psalms 144:5

sababishe ... ije chini ... gusa ... ifanye ... Tuma ... uwatawanye ... piga ... warudishe

Haya maneno yanatakiwa kutafsiriwa kama maombi na sio amri kwa sababu mwandishi anatambua kuwa Mungu ni mkuu zaidi yake.

Sababisha anga izame

Maana zinazowezekana ni 1) pasua anga wazi au 2) kunja mbigu kama tawi la mti linavyojikunja mtu anapotembea juu yake au kama mtu anavyokunja upinde kabla ya kupiga mishale.

katika kuchanganyikiwa

"ili wasijue wawaze nini au wafanye nini"

Psalms 144:7

Nyosha mkono wako toka juu; niokoe na maji mengi

Daudi anazungumza kana kwamba Mungu alikuwa kwenye ardhi juu ya mafuriko na ana mikono ya kimwili ambayo angeweza kumvuta Daudi kutoka kwenye mafuriko. Mafuriko ni sitiari ya taabu zilizosababishwa na "wageni." "Unaweza kutenda, nisaidie nizishinde taabu zangu"

kutoka mkono wa wageni

Hapa "mkono" unaashiria nguvu."kutoka katika nguvu ya wageni"

Midomo yao inazungumza uongo

"Wanazungumza uongo"

mkono wao wa kuume ni uongo

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi anazungumzia utamaduni wa kuinua mkono wa kuume ili kuapa kuwa anachotaka kusema mtu mahakamani ni kweli, "wanadanganya hata wanapoapa kusema ukweli," au 2) "mkono wa kuume" ni sitiari ya nguvu, "kila kitu walichopata, wamepata kwa kusema uongo"

Psalms 144:9

wimbo mpya

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao hakuna mtu amewahi kuimba" au 2) "wimbo ambao sijawahi kuimba"

kwako, unayewapa ...wafalme, uliyemwokoa

"kwako. Ni wewe unayewapa ... wafalme. Ni wewe ulimwokoa"

Daudi mtumishi wako

Daudi anajizungumzia kana kwamba ni mtu mwingine. "mimi, Daudi, mtumishi wako"

na upanga mwovu

Daudi anawazungumzia watu waovu kana kwamba ni upanga wanaotumia kama silaha. "kutoka kwa watu waovu waliokuwa wanajaribu kumuua"

Niokoe na uniweke huru

"Tafadhali niokoe na uniweke huru"

kutoka katika mkono wa wageni

Hapa "mkono" unaashiria nguvu."kutoka katika nguvu ya wageni"

Midomo yao inazungumza uongo

"Wanazungumza uongo"

mkono wao wa kuume ni uongo

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi anazungumzia utamaduni wa kuinua mkono wa kuume ili kuapa kuwa anachotaka kusema mtu mahakamani ni kweli, "wanadanganya hata wanapoapa kusema ukweli," au 2) "mkono wa kuume" ni sitiari ya nguvu, "kila kitu walichopata, wamepata kwa kusema uongo"

Psalms 144:12

kama mimea inayokuwa kikanilifu

yenye afya na imara

katika ujana wao

muda ambao watu wanakua

binti zetu kama nguzo za pembeni zilizochongeka

"na binti zetu wachongeke kama nguzo za pembeni"

nguzo za pembeni zilizochongeka

"nguzo nzuri zinazobeba pembe za nyumba kubwa"

nguzo za pembeni zilizochongeka, zenye umbo zuri kama za hekalu

"nguzo zilizochengeka kufanya hekalu lipendeze"

maelfu na elfukumi katika mashamba yetu

"maelfu—hata makumi elfu!—na wajaze mashamba yetu"

Psalms 144:14

Hakuna mtu atakayepasua kwenye kuta zetu

"Hakuna mtu atakayeweza kuvamia mji wetu"

wala kilio

"hakuna mtu atakayelia kwa maumivu" au "hakuna mtu kuomba omba chakula" au "hakuna tu kuita hukumu"

Psalms 145

Psalms 145:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

zaburi ya kusifu ya Daudi

"Hii ni zaburi ya kusifu ambayo Daudi aliandika"

Nitakutukuza wewe

"Nitawaambia watu jinsi ulivyo wa ajabu"

Nitabariki jina lako

Neno "jina" ni njia nyingine ya kusema Yahwe mwenyewe. "jina lake tukufu libarikiwe", "ubarikiwe" au "fanya kinachokufurahisha"

Nitalisifu jina lako

Neno "jina" ni njia nyingine ya kusema Yahwe mwenyewe. "nitakusifu" au "nitawaambia watu jinsi ulivyo mkuu"

Psalms 145:4

matendo yako makuu

"vitu unavyoweza kufanya kwa sababu una nguvu"

Psalms 145:6

nitatangaza wema wako uliojaa tele

"nitawaambia watu jinsi ulivyo mwema sana"

Psalms 145:8

umejaa tele uaminifu wa agano

Mwandishi anazungumzia uaminifu wa agano kana kwamba ni kitu cha kimwili ambacho mtu anaweza kumiliki kiasi kikubwa chake. "ni mwaminifu kabisa kwa agano lako"

rehema zake ziko juu ya kasi zake zote

"watu wanaweza kumwona akionesha huruma katika kila kitu afanyacho"

Psalms 145:10

Yote ulivyoumba vitakupa shukrani

"Watu wote uliowaumba watakupa shukrani" au "Itakuwa kana kwamba kila kitu ulichoumba kitakupa shukrani"

Psalms 145:13

unadumu katika vizazi vyote

"unabaki milele"

Psalms 145:14

anashikilia wote wanaoanguka ... anawainua wote walioinama

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwatia moyo watu kana kwamba alikuwa akiwasaidia watu waliokuwa wandhaifu kimwili. "huwatia moyo wale walio kata tamaa"

Macho ya wote yanasubiri

"Kila mtu anasubiri"

Unafungua mkono wako

"Unatoa kwa ukarimu"

kuridhisha hamu za kila kiumbe hai

"unampa kila mtu zaidi ya anachohitaji na kiasi anachotaka"

Psalms 145:17

Yahwe ni wa haki katika njia zake zote

"Watu wanaweza kuona katika yote ambayo Yahwe anafanya kuwa yeye ni mwenye haki"

mwenye fadhili katika yote atendayo

"na ni mwenye fadhili katika yote atendayo" au "watu wanaweza kuona katika mambo yote ambayo Yahwe anafanya ya kuwa ni mwenye fadhili"

yuko karibu kwa wale wote wanaomwita

"anatenda upesi kuwasaidia wale wanaoomba"

wale wote wanaomwita kwa uaminifu

"kwa wale wanaosema ukweli tu wanapoomba" au "kwa wote wale anaowaamini wanapoomba"

Psalms 145:20

Mdomo wangu uta...

"Nita..."

utazungumza sifa za Yahwe

"Nitawaambia wote jinsi Yahwe alivyo mwema"

acha wanadamu wote wabariki jina lake

Neno "jina " njia nyingine ya kusema Yahwe mwenyewe. "jina lake tukufu libarikiwe," "acha watu wote wambariki" au "acha watu wote wafanye kinachomfurahisha"

Psalms 146

Psalms 146:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Msifu Yahwe, nafsi yangu

Hapa "nafsi" inawakilisha undani wa mwandishi. Mwandishi anajiamuru kumsifu Yahwe. "Nitamsifu Yahwe kwa nafsi yangu yote" au "Nitampa Yahwe sifa kwa maisha yangu yote"

kwa maisha yangu yote

"hadi nife" au "wakati ninaishi"

Psalms 146:3

kwa wana wa wafalme

Hapa "wana wa wafalme" inawakilishwa viongozi wote wanadamu.

kwa wanadamu, ambamo hakuna wokovu

"kwa mtu yeyote kwa sababu hawezi kukuokoa"

kwa wanadamu

"kwa watu"

Pumzi ya mtu inaposimama

Hii ni njia ya ustarabu ya kumaanisha mtu anakufa. "Mtu anapokufa"

anarudi mavumbini

Hii inamaanisha kamaMungu alivyomuumba binadamu wa kwanza, Adamu, kutoka mavumbini, hivyo pia mwili wa mtu utaoza na kuwa mavumbi tena atakapokufa.

Psalms 146:5

Yahwe ameumba mbingu na dunia

Maneno "mbingu" na "dunia" yanamaanisha kila kitu kilichopo ulimwenguni.

hufuata uaminifu

"hubaki mwaminifu"

Psalms 146:7

Anapitisha hukumu

"Anaamua mambo kwa usawa"

kwa waliokandamizwa

"kwa watu waliokandamizwa" au "kwa wale ambao watu wengine wamewakandamiza"

kwa wenye njaa

"kwa watu wenye njaa" au "kwa wale walio na njaa"

hufungua macho ya vipofu

Kumsababisha mtu kipofu kuona inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa anafungua macho yake. "husababisha vipofu kuona"

vipofu

"watu vipofu" au "wale walio vipofu"

Yahwe huwainua wale walioinama chini

Yahwe kumsaidia mtu inazungumziwa kana kwamba anamsaidia mtu kimwili kusimama. "Yahwe huwasaidia wale walio kata tamaa" au "Yahwe huwasaidia wale walio wanyonge"

walioinama chini

Hili ni tendo lenye ishara ya kukata tamaa na kuomboleza.

Psalms 146:9

huwainua

Mungu kumsaidia mtu kunazungumziwa kana kwamba alikuwa akiwanyanyua juu kimwili.

Mungu wako, Sayuni

Hapa "Sayuni" inawakilisha watu wote wa Israeli. Mwandishi anazungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa hapo wakimsikiliza. "Mungu wenu, watu wa Israeli"

katika vizazi vyote

"atatawala katika vizazi vyote" au "atatawala milele"

Psalms 147

Psalms 147:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

ni vyema

"ni vyema kuimba sifa"

sifa inafaa

"sifa inastahili"

Psalms 147:2

Huwaponya waliovunjika moyo na kuziba vidonda vyao

Mwandishi anazungumzia huzuni ya watu na kukata tamaa kana kwamba ni vidonda vya kimwili, na Yahwe kuwatia moyo kana kwamba anaponya vidonda vyao. "Huwatia moyo wale walio na huzuni na kuwasaidia kupona na vidonda vyao vya kihisia"

Psalms 147:4

uelewa wake hauwezi kupimwa

"hakuna mtu anayeweza kupima uelewa wake" au "uelewa wake hauna mwisho"

Psalms 147:6

Yahwe huwainua waliokandamizwa

Mwandishi anazungumzia yahwe kuwapa heshima wale walio kandamizwa kana kwamba Yahwe alikuwa akiwainua kutoka ardhini. "Yahwe huwapa heshima walio kandamizwa"

huwaleta waovu chini ardhini

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwaaibisha waovu kana kwamba Yahwe alikuwa akiwalazimisha kulala ardhini. "huwaaibisha waovu"

kwa kinubi

"huku wakicheza kinubi"

Psalms 147:8

na kwa wana wa kunguru wanapolia

"na huwapa chakula wana wa kunguru wanapolia"

wanapolia

"wanapoita"

Psalms 147:10

Hapendezwi na nguvu ya farasi

"Farasi wenye nguvu hawampendezi"

miguu yenye nguvu ya mtu

Maana zinazowezekana ni 1) "miguu yenye nguvu" ni njia nyingine inayowakilisha jinsi mtu anavyoweza kukimbia mbio. "watu wanaoweza kukimbia mbio" au 2) "miguu yenye nguvu" inawakilisha nguvu ya mtu mzima. "jinsi mtu alivyo na nguvu"

Psalms 147:12

Yerusalemu ... Sayuni

Mwandishi anazungumzana Yerusalemu, ambayo pia aniita Sayuni, kana kwamba ni mtu. Majina ya mji ni njia nyingine ya kuwaita watu wanaoishi humo. "watu wa Yerusalemu ... watu w Sayuni"

Kwa kuwa huimarisha vyuma vya malango yako

Msemo "vyuma vya malango yako" unawakilisha mji kwa ujumla. Yahwe ataifanya Yerusalemu kuwa salama kutoka kwa uvamizi wa adui. "Kwa kuwa huilinda Yerusalemu"

huwabariki ... miongoni mwenu

Mwandishi anawazungumzia wanaoishi Yerusalemu kana kwamba ni watoto wa Yerusalemu. "huwabariki wale wanaoishi Yerusalemu"

Huleta mafanikio

"Huleta amani." Maana zinazowezekana ni 1) Yahwe husababisha watu wanaoishi Yerusalemu kufanikiwa kwa mali na kwa fedha au 2) neno lililotafsiriwa kama "mafanikio" linamaanisha "amani" na Yahwe huitunza yerusalemu dhidi ya mashambulizi ya adui.

Psalms 147:15

amri yake inakimbia haraka sana

Mwandishi anaelezea amri za Mungu kana kwamba ni mjumbe anayekimbia haraka kufikisha ujumbe wa Mungu.

Huifanya theluji kama sufu, husambaza jalidi kama majivu

Hii inasisitiza jinsi ilivyo rahisi kwake kufanya hivi vitu. Hufunika ardhi kwa theluji kwa urahisi kama mtu anavyofunika kitu kwa blangeti wa sufu. Na huondoa jalidi kwa wepesi kama upepo unavyopuliza majivu.

Psalms 147:17

Huigawa mvua ya mawe kama makombo

Yahwe husambaza mvua ya mawe kwa wepesi kama mtu anavyosambaza chembechembe za mkate. "Huigawa mvua ya mawe kwa urahisi, kana kwamba ni makombo"

Huigawa

"Hutuma"

mvua ya mawe

mvua yenye vipande vidogo vya barafu kutoka angani

nani anawezakustahimili baridi anayoituma

Mwandishi anatumia swali hili kusisitiza kuwa ni vigumu kuvumilia hali ya hewa ya baridi ambayo Yahwe husababisha. "hakuna anayeweza kuishi katika baridi anayoituma"

Hutuma amri yake na kuyayeyusha

Mwandishi anazungumzia amri ya yahwe kana kwamba ilikuwa ni mjumbe wake. "Huamuru barafu kuyeyuka"

Psalms 147:19

Alitangaza neno lake kwa Yakobo, sheria zake na amri zake za haki kwa Israeli

Mistari hii miwili inamaana moja na inasisitiza kuwa Yahwe alitoa sheria yake kwa Israeli pekee.

sheria zake na amri zake za haki kwa Israeli

"Alitangaza sheria zake na amri zake za haki kwa Israeli"

sheria zake na amri zake za haki

Maneno "sheria" na "amri za haki" pamoja na "neno" katika mstari uliopita, yote yanamaanisha sheria ya Musa.

hawazijui

Mataifa mengine hayajui amri za Yahwe.

Psalms 148

Psalms 148:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Msifuni Yahwe, nyie mbinguni ... nyie mlio juu

"Msifuni Yahwe, nyie mbinguni ... nyie mlio angani." Mistari hii miwili ina usambamba. Msemo "juu" una maana sawa na "mbinguni" katika mstari uliopita"

Psalms 148:3

Msifuni, juana mwezi

Mwandishi anazungumza na jua na mwezi kana kwamba ni watu na anaziamuru kumsifu Yahwe. "Msifuni Yahwe, jua na mwezi, kama watu wafanyavyo"

msifuni, nyota zote zinazong'aa

Mwandishi anazungumza na nyota kana kwamba ni watu na anaziamuru kumsifu Yahwe. "Msifuni Yahwe, nyota wa kung'aa, kama watu wafanyavyo"

Msifuni, mbingu ya juu zaidi

Msemo "mbingu ya juu zaidi" ni lahaja ya kumaanisha mbingu yenyewe. Mwandishi anazungumza na mbingu kwan kwamba ni mtu na anaiamuru kumsifu Yahwe. "Msifu yahwe, mbingu iliyo juu zaidi, kama watu wafanyavyo"

nyie maji mlio juu ya anga

Mwandishi anazungumza na "maji mlio juu ya anga" kana kwamba ni watu na anayaamuru kumsifu Yahwe. "Msifuni Yahwe, maji mlio juu ya anga, kama watu wafanyavyo"

maji mlio juu ya anga

Mwandishi anazungumzia sehemu juu ya anga ambapo maji huhifadhiwa na mvua hutokea.

Psalms 148:5

Acha walisifu jina la Yahwe

Hapa neno "jina" linamwakilisha Yahwe mwenyewe. "Acha wamsifu Yahwe"

vikaumbwa

"aliviumba"

ametoa amri ambayo hatabadili

Maana zinazowezekana ni 1) "ametoa amri ambayo ni ya milele" au 2) "ametoa amri ambayo hawatakaidi"

ametoa

"kutoa" kama mfalme anavyotoa

Psalms 148:7

vilindi vyote vya bahari

Msemo huu unawakilisha kila kiumbe kinachoishi katika vilindi vya bahari. "viumbe vyote katika vilindi vya bahari"

moto na mvua ya mawe, theluji na mawingu, upepo wa dhoruba

Mwandishi anazungumza hivi vitu vya asili kana kwamba ni watu na kuviamuru kumsifu Yahwe.

upepo wa dhoruba unaotimiza neno lake

Msemo "neno lake" unawakilisha kile ambacho yahwe ameamuru. "upepo wa dhoruba unaofanya kile ambacho Yahwe ameamuru"

Psalms 148:9

Kauli Unganishi:

Mwandishi anaendelea kuzungumza na vitu ambavyo sio binadamu kana kwamba ni watu na kuviamuru kumsifu Yahwe.

wanyama pori na wakufugwa

"wanyama wote"

Psalms 148:11

Kauli Unganishi:

Mwandishi anawaamuru watu wote kumsifu Yahwe

mataifa yote

Neno "mataifa" linawakilisha watu wanoishi katika mataifa hayo. "watu wa mataifa yote"

vijana wanaume na wanawali, wazee na watoto

Mwandishi anatumia tofauti hizi za jinsia na umri kuwakilisha kila mtu.

Psalms 148:13

jina la Yahwe, kwa kuwa jina lake pekee

Hapa neno "jina" limwakilisha Yahwe mwenyewe. "Yahwe, kwa kuwa yeye pekee"

utukufu wake unasambaa juu ulimwengu na mbingu

Mwandishi anazungumzia ukuu wa Yahwe kama utukufu wake kuwa juu ya ulimwengu na mbingu.

Ameinua pembe za watu wake

Mwandishi anazungumzia nguvu kana kwamba ni pembe la mnyama. Kuinua pembe la mnyama ilikuwa ni ishara ilioshiria ushindi wa kijeshi. "Amewafanya watu wake kuwa na nguvu" au "Amewapa watu wake ushindi"

kwa ajili ya sifa kutoka kwa waaminifu wake wote

"ili kwamba waaminifu wake wote wamsifu"

watu karibu naye

Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwapenda watu wake kana kwamba watu wake wako karibu naye kimwili. "watu awapendao"

Psalms 149

Psalms 149:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi wa zaburi anazungumza na watu wote wa Mungu.

wimbo mpya

Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao hujawahi kuimba" au 2) wimbo ambao hakuna mtu aliyewahi kuimba.

imbeni sifa yake

"msifuni kwa nyimbo"

Psalms 149:2

ifurahi katika yeye aliyekuamba

Maana zinazowezekana ni 1) "furahi kwa sababu aliwaumba" au 2) "furahi kwa sababu aliyewaumba ni mwema."

wamfurahie mfalme wao

Maneno "mfalme wao" inawezekana kumaanisha Mungu. Maana zinazowezekana ni 1) "furahi kwa sababu ni mfalme wao" au 2) "furahi kwa sababu mfalme ni mwema."

wasifu jina lake

Neno "jina" ni njia nyingine ya kusema Yahwe mwenyewe. "msifuni yeye" au "waambie watu alivyo mkuu"

tari

chombo cha muziki chenye kichwa kama ngoma kinachoweza kugongwa na kina vipande vya chuma vimezunguka pembeni vinavyotoa sauti chombo kinapotikiswa.

Psalms 149:4

anawatukuza wanyenyekevu kwa wokovu

"anawapa utukufu wanyenyekevu kwa kuwaokoa kutoka kwa maadui zao"

vitandani mwao

"hata wanapolala chini kusinzia usiku"

Psalms 149:6

Sifa za Mungu ziwe kwenye midomo yao

Mdomo ni njianyingine ya kusema mtu mzima. "Daima wawe tayari kumsifu Mungu"

upanga wenye makali mawili mkononi mwao

upanga wenye makali mkononi mwao - Neno "upanga" ni njia nyingine ya kusema kuwa tayari kupigana vitani. "wawe tayari wakati wote kwenda vitani kwa ajili yake"

mataifa

Msemo "mataifa" ni njia nyingine ya kusema watu wanaoishi katika mataifa. "watu wa mataifa"

Psalms 149:8

minyororo

Hizi zinaundwa na vyuma vizito na zinazuia kusogea kwa mfungwa.

pingu

Kitu cha miduara miwili kilicho tengenezwa na chuma na mnyororo katikati yake zinazozuia kusogea kwa miguu au mikono ya mfungwa.

watatekeleza hukumu iliyoandikwa

kufanya kile ambacho Yahwe alimwambia Musa kuandika ili watu wafanye kwa wale wenye hati.

Psalms 150

Psalms 150:1

Taarifa ya Jumla:

Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.

Taarifa ya Jumla:

kuzingatia zaidi kusifu na kuabudu na jambo la kawaida hekaluni.

Msifuni Mungu katika mahali pake patakatifu

Hekalu la Mungu lilikuwa likijulikana zaida kama sehemu yake takatifu. Hii ilikuwa sehemu iliyotumika zaida kwenda kumwabudu Mungu.

matendo yake makuu

"mambo makubwa aliyotenda." "Matendo makubwa" ya Mungu yanaweza kumaanisha 1) ya asili kama radi na matetemeko au 2) miujiza kama uponyaji na ushindi mkubwa vitani.

Psalms 150:3

Taarifa ya Jumla:

Hiki kipande kinakazia kumsifu na kumwabudu Mungu kwa vyombo vya muziki na kucheza.

matari

Tari ni chombo cha muziki chenye kichwa kama ngoma kinachoweza kugongwa na kina vipande vya chuma vimezunguka pembeni vinavyotoa sauti chombo kinapotikiswa.

matoazi

sahani mbili nyembamba za chuma zinazogongwa pamoja kutengeneza sauti kubwa.

Psalms 150:6

Taarifa ya Jumla

Huu mstari ni zaidi ya mwisho wa zaburi hii. ni kauli ya kufunga kwa ajili ya kitabu chote cha 5 cha Zaburi, kinachoanzia Zaburi 107 na kuishia na Zaburi 150.

kila kitu kilicho na uhai

Maana zinazowezekana ni 1) watu wote walio hai wanapaswa kumsifu Mungu au 2) viumbe vyote vilivyo hai vinapaswa kumsifu Mungu.