Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Ecclesiastes 1

Ecclesiastes 1:1

Kama mvuke wa ukungu, kama upepo mwanana katika upepo

Hii ni misemo miwili inayomaanisha kitu kimoja na vimeunganishwa kwa ajili ya msisitizo.

Ni faida gani wanadamu huipata ... chini ya jua?

"Binadamu hapati faidi ... chini ya jua."

Ecclesiastes 1:4

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaonesha hali halisi ya mpangilio wa maisha jinsi aelewavyo..

Ecclesiastes 1:7

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendela na mpangilio halisi wa mtazamo.

Kila kitu huwa uchovu

Kwa kuwa binadamu hawezi kueleza vitu hivi, inakuwa haina maana kujaribu. "kila kitu kinachosha"

Jicho halishibi na kile linachokiona

Mtu hawezi kufikia maelezo rahisi kwa kila anachokiona. "Mtu haridhiki na kile ambacho macho yake yanaona"

wala sikio halishibi na kile linachosikia

Mtu hawezi kufikia maelezo rahisi kwa kila anachosikia. "wala mtu haridhiki na kile ambacho masikio yake yanasikia""

Ecclesiastes 1:9

Taarifa ya Jumla:

Hakuna kitu jipya kuhusu binadamu na shughuli zake.

kila kilichofanyika ndicho kitakachofanyika

"kile ambacho watu wamefanya ndicho ambacho watu watafanya siku za usoni"

Je kuna jambo lolote ambalo watu wanaweza kusema, 'Tazama, hili ni jipya'?

"Hakuna kitu ambacho mtu anaweza kusema, 'Tazama, hiki ni kipya."

nayo hayatakumbukwa

"watu wanaweza wasiyakumbuke pia"

Ecclesiastes 1:12

Nilitia akili yangu

"Nikusudia" au "Niliamua"

kusoma na kutafuta

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na inasisitiza alisoma kwa bidii.

wana wa watu

"binadamu"

matendo yote ambayo yanafanyika

"kila kitu ambacho watu hufanya"

mvuke

"umande" au "pumzi." Haidumu. "cha muda" au "haina maana." Kile ambacho watu wanafanya ni kama umande kwa sababu hakidumu na hakina maana.

kujaribu kuuchunga upepo

Mwalimu anasema kwamba vitu ambavyo watu hufanya ni kama kujaribu kuushika upepo au kuuzuia upepo kupuliza.

Palipopinda hapawezi kunyoshwa! Kisicho kuwepo hakiwezi kuhesabiwa!

"watu hawawezi kunyosha vitu vilivyopinda! Hawawezi kuhesabu kisichokuwepo!"

Ecclesiastes 1:16

nimetia moyo wangu

"Nikusudia" au "Niliamua"

upumbavu na ujinga

Maneno "upumbavu" na "ujinga" yana maana ya kufanana na zinamaanisha kufikiri kwa kijinga na matendo.

kujaribu kuuchunga upepo

Mwalimu anasema kwamba vitu ambavyo watu hufanya ni kama kujaribu kuushika upepo au kuuzuia upepo kupuliza.

Ecclesiastes 2

Ecclesiastes 2:1

Nikasema moyoni

"Nikajiambia"

nitakujaribu kwa furaha

Hapo atakayejaribiwa inamaanisha ni yeye mwenyewe. "Nitajijaribu mwenyewe na vitu vinavyonipa furaha"

Kwa hiyo furahia

"Kwa hiyo nitafurahia vitu vinavyo nipendeza"

Nikasema juu ya kicheko, "Ni wazimu,"

"Nikasema kuwa ni wazimu kucheka wakati mwingine"

Yafaa nini?

"ni batili"

Ecclesiastes 2:3

Nikajipeleleza moyoni mwangu

"Nikawaza sana kuhusu"

kutimiza hamu yangu kwa mvinyo

"kutumia mvinyo kujipa furaha"

Nikaruhusu akili yangu iongozwe na hekima

"Nikawaza kuhusu vitu amabvyo watu wenye hekima walinifundisha"

wakati wa siku za maisha yao

"ili mradi wakiwa hai"

Ecclesiastes 2:4

Nilijenga nyumba kwa ajili yangu na kupanda miti ya mizabibu

Huenda mwandishi aliwaambia watu kuifanya hiyo kazi. "Niliwafanya watu wanijengee nyumba na kunipandia miti ya mizabibu"

bustani na viwanja

Maneno haya mawili yana maana zikukaribiana na zinamaanisha mashamba mazuri ya miti ya matunda.

kumwagilia msitu

"kutoa maji kwa ajili ya msitu"

msitu mahali miti ilikuwa imepandwa

"msitu ambapo miti huota"

Ecclesiastes 2:7

nilikuwa na watumwa waliozaliwa katika ikulu yangu

"watumwa wangu walizaa watoto nao pia walikuwa watumwa wangu"

hazina ya wafalme na majimbo

Hii inamaanisha dhahabu na utajiri mwingine ambao nchi jirani ulilazimishwa kulipa kwa mfalme wa Israeli.

kufurahia kutoka kwa wana wa wanadamu, masulia na wanawake

"Niliwafurahia sana wake wangu wengi na masulia kama mwaname yeyote ambavyo angewafurahia"

Ecclesiastes 2:9

hekima yangu ilikuwa ndani yangu

"nikaendelea kutenda matendo kwa hekima" au "nikaendelea kuwa na hekima"

Lolote ambalo macho yangu yalikitamani

"Chochote nilichoona na kutamani"

sikuyazuia

Hii naweza kuweka katika hali chanya. "nilijipatia"

Sikuuzuia moyo wangu katika furaha yeyote

Hii naweza kuweka katika hali chanya. "Nilijiruhusu kufurahia kila kitu kilichonipa furaha"

moyo wangu ulifurahi

"Nilifurahi"

Ecclesiastes 2:11

matendo yote ambayo mikono yangu iliyokwisha kuyatimiliza

"yote niliyotimiza"

mvuke na kujaribu kuuchunga upepo

walimu anasema kwamba vitu ambavyo watu hufanya ni kama kujaribu kuushika upepo au kuuzuia upepo kupuliza.

upumbavu na ujinga

Maneno "upumbavu" na "ujinga" yana maana ya kufanana na zinamaanisha kufikiri kwa kijinga na matendo.

Kwa maana ni kitu gani mfalme anayekuja baada yangu afanye ... ambacho hakijafanyika?

Mwandishi anatumia swali hili kusisitiza wazo kuwa mfalme ajaye hatawezi kufanya jambo lolote la maana zaidi la yale aliyokwisha yafanye yeye. "Kwa kuwa mfalme ajaye hawezi kufany a kitu ... ambacho tayari hakijafanyika."

mfalme anayekuja ... baada yangu

"mfalme ... anayemridhi mfalme aliyepo." Hii huenda iliandikwa na mfalme aliyekowepo katika utawala, kwa hiyo "baada ya mfalme" inaweza kutafsiriwa "baada yangu"

Ecclesiastes 2:13

hekima ina faida kuliko upumbavu, kama nuru ilivyo bora kuliko giza

hekima ni bora kuliko upumbavu, kama vile nuru ilivyo bora kuliko giza.

Mwenye hekima hutumia macho yake katika kichwa chake kuona mahali anakoenda

"Mtu mwenye hekima ni kama mtu anayetumia macho yake kuona anapoenda"

hutumia macho yake katika kichwa chake

"anaona"

mpumbavu hutembea katika giza

"mpumbavu ni kama mtu anayetembea katika giza"

Ecclesiastes 2:15

nikasema moyoni mwangu

"nikajiambia"

Hivyo kuna utofauti gani kama mimi ni mwenye hekima sana?

Mwandishi anatumia swali kusisitiza wazo lake kuwa hakuna faida ya kuwa na hekima. "Kwa hivyo haina tofauti kama nina hekima sana."

Nikahitimisha moyoni mwangu

"nikahitimisha"

mvuke

"umande" au "pumzi." Haidumu. "cha muda" au "haina maana." Kile ambacho watu wanafanya ni kama umande kwa sababu hakidumu na hakina maana.

mwenye hekima, kama mpumbavu, hakumbukwi kwa muda mrefu

"watu hawatamkumbuka mwenye hekima kwa muda mrefu, kama tu ambavyo hawamkumbuki mpumbavu kwa muda mrefu"

kila kitu kitakuwa kimesahauliwa

"watu watakuwa wamekishwa sahau kila kitu"

Ecclesiastes 2:17

kazi zote zilizofanyika

"kazi zote ambazo watu hufanya"

mvuke na kujaribu kuuchunga upepo

Mwalimu anasema kwamba vitu ambavyo watu hufanya ni kama kujaribu kuushika upepo au kuuzuia upepo kupuliza.

Ecclesiastes 2:19

Na ni nani ajuaye kama atakuwa mwenye hekima au mpumbavu?

"Kwa kuwa hakuna ajuaye kama atakuwa mwenye hekima au mpumbavu."

atakuwa

Hapa inamaanisha mtu yule atakaye rithi utajiri wa Sulemani.

moyo wangu ukaanza kukata tamaa

"Nikaanza kusononeka"

Ecclesiastes 2:21

hatari kubwa

"janga kubwa"

Kwa maana ni faida gani mtu hupata ambaye hufanya kazi kwa juhudi na kujaribu moyoni mwake kutimiza kazi zake chini ya jua?

"Kwa kuwa mtu anayefanya kazi sana na kujaribu moyoni mwake kukamilisha kazi zake chini ya jua hafaidi kitu."

ambaye hufanya kazi kwa juhudi na kujaribu moyoni mwake

Misemo hii miwili inamaana moja na inasisitiza jinsi gani mtu anavyofanya kazi kwa nguvu nyingi.

kujaribu moyoni mwake

"kujaribu kwa wasiwasi"

maumivu na masikitiko

Maneno haya mawili yana maana sawa na yanasisitiza jinsi gani kazi ya mtu ilivyo ngumu.

roho yake haipumziki

"akili yake haipumziki" au "anaendelea kuwa na wasiwasi"

Ecclesiastes 2:24

ukweli huu unatoka kutoka mkononi mwa Mungu

"ukweli huu unatoka kwa Mungu"

Kwa kuwa ni nani anaweza kula au anaweza kupata furaha yoyote tofauti na Mungu?

"Kwa kuwa hakuna awezaye kula au kuwa na furaha yoyote tofauti na Mungu."

Ecclesiastes 2:26

ili kwamba ampe mtu anayempendeza Mungu

Yule amabaye "ampaye" inaweza kumaashiria ni Mungu au mtenda dhambi. Kinachopewa ni kila ambacho mwenye dhambi amekusanya na kutunza. Tafsiri ifuatayo njia moja ya kusema hivi bila kuweka wazi ni nani anayegawa vitu vilivyotunzwa. "ili kwamba yule anayempendeza Mungu awe navyo"

mvuke na kujaribu kuuchunga upepo

Mwalimu anasema kwamba vitu ambavyo watu hufanya ni kama kujaribu kuushika upepo au kuuzuia upepo kupuliza.

Ecclesiastes 3

Ecclesiastes 3:1

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anahama na kuanza kueleza tofauti za maisha.

Kwa kuwa kila kitu na wakati wake, na majira kwa kila kusudi

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na imeunganishwa kuleta msisitizo.

kuzaliwa na ... kufa ... kuua na ... kuponya

Hizi ni sehemu mbali mbali za maisha kama zinavyoelezwa kutoka tofauti moja kabisa hadi nyingine.

wakati wa kung'oa yaliyopandwa

Maana zinazowezekana ni 1) "wakati wa kuvuna" au 2) "wakati wa kutoa magugu" au 3) "wakati wa kung'oa."

Ecclesiastes 3:4

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea na tofauti za maisha.

kulia na ... kucheka ... kuombolezana ... kucheza

Hizi ni sehemu mbali mbali za maisha kama zinavyoelezwa kutoka tofauti moja kabisa hadi nyingine.

Ecclesiastes 3:6

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea na tofauti za maisha.

Ecclesiastes 3:8

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendelea na tofauti za maisha.

Ni faida gani mfanyakazi aipatayo katika kazi yake?

Hili ni swali la kumfanya mtu kufikiri ili kumelekeza msomaji katika mada yamajadiliano yafuatayo.

Ecclesiastes 3:11

ameweka umilele ndani ya mioyo yao

Hapa "yao" inamaanisha binadamu. "ameweka umilele ndani ya mioyo ya binadamu"

Ecclesiastes 3:12

anapaswa kuelewa jinsi ya kufurahia

Mwandishi anasisitiza zoezi la mtu kufurahia kazi yake, sio ufahamu wa kiakili ya jinsi ya mtu kufurahia kazi yake.

Ecclesiastes 3:14

Chochote kilichopo kimekwisha kuwepo

Hakuna kitu jipya kuhusu binadamu na shughuli zake.

Ecclesiastes 3:16

nimeona ... ubaya upo ... ina ubaya

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na inasisitiza jinsi gani tabia ya uovu ni kawaida.

ubaya upo

"kawaida watu wanapata ubaya"

Nikasema moyoni mwangu

"Nikajiambia"

kila jambo na kila tendo

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na zinaashiria kila tendo wafanyao binadamu.

Ecclesiastes 3:19

Hakuna faida kwa mwanadamu zaidi ya wanyama

"Binadamu hayuko bora zaidi ya wanyama"

kuwa hakuna kila kitu isipokuwa pumzi?

"Kila kitu ni pumzi tu"

Ecclesiastes 3:21

Ni nani ajuaye kama roho ... chini ya nchi?

Mwandishi anadai kuwa wanyama wana roho. "Hakuna ajuaye kama roho ... chini ya nchi."

hakuna lililo jema kwa yeyote zaidi ya

Mwandishi anasisitiza zoezi la mtu kufurahia kazi yake, sio ufahamu wa kiakili ya jinsi ya mtu kufurahia kazi yake.

Ni nani awezaye kumleta ... baada yake?

Hakuna yeyote aliyewahi kumfufua mtu au mnyama kutoka wafu. "Hakuna awezaye kumleta ... baada yake."

Ecclesiastes 4

Ecclesiastes 4:1

Nguvu iko katika mikononi mwa watesaji

"Watesi wao wana mamlaka makubwa"

lakini wateswaji hawana mfariji

Hakuna mwenye mamlaka anayewatetea wanao teswa"

Ecclesiastes 4:2

bahati zaidi kuliko wote wawili ni yule ambaye hajaishi

"yule ambaye bado hajazaliwa ni bora zaidi yao"

Ecclesiastes 4:4

wivu wa jirani ya mtu

Maana zinazowezekana ni 1) Jirani ana wivu na kitu alichounda jirani yake au 2) jirani ana wivu na ufundi alionao jirani yake.

mvuke na kujaribu kuchunga upepo

Hakuna awezaye kuchunga upepo kama vile wanyama. Mwalimu anasema kwamba vitu ambavyo watu hufanya ni kama kujaribu kuushika upepo au kuuzuia upepo kupuliza.

Ecclesiastes 4:5

hukunja mikono yake na hafanyi kazi

kukunja mikono ni ishara ya uvivu na ni njia nyingine ya kusema kuwa mtu amekataa kufanya kazi.

hivyo chakula chake in mwili wake

"matokeo yake ni kusababisha uharibifu wake mwenyewe."

kazi ambayo hujaribu kuuchunga upepo

Sio kila kiza ina faida. Kazi zingine hazina faida kama kuchunga upepo.

Ecclesiastes 4:7

hana mwana, wala ndugu

Mtu huyu hana familia.

macho yake hayatosheki

"haridhiki"

Ninajisumbua na kuharibu furaha yangu kwa ajili ya nani?

"Kuna mtu atakaye faidi kutokana na mimi kufanya kazi kwa bidii na kutofurahi?" au "Kazi yangu hamfaidishi yeyote na sina furaha"

Ecclesiastes 4:9

kama wawili wakilala pamoja, wanaweza kupata joto

Mwandishi anazungumzia watu wawili kupatiana joto kwenye usiku wa baridi.

mtu mmoja anawezaje kupata joto akiwa mwenyewe?

"mtu hawezi kuwa na joto akiwa mwenyewe."

Ecclesiastes 4:12

kusimama katika shambulio

"kujilinda dhidi ya mashambulio"

na kamba ya nyuzi tatu haikatika upesi

kamba yenye meno haikatika kwa wepesi "watu hawawezi kukata kwa wepesi kamba ya meno matatu"

Ecclesiastes 4:13

alizaliwa masikini katika ufalme wake

"alizaliwa kwa wazazi masikini walioishi katika nchi ambayo siku moja atatawala"

Ecclesiastes 4:15

Taarifa ya Jumla:

Badala ya kuchagua vijana wenye hekima, watu wanamchagua mwana wa mfalme ambaye anaweza asiwe na hekima zaidi.

hai na kuzunguka

Maneno "hai" na "kuzunguka" yanamaanisha kitu kimoja na yamewekwa pamoja kwa ajili ya msisitizo.

Hakuna mwisho kwa watu wote

"Kuna watu wengi sana"

mvuke na kujaribu kuuchunga upepo

Mwalimu anasema kwamba vitu ambavyo watu hufanya ni kama kujaribu kuushika upepo au kuuzuia upepo kupuliza.

Ecclesiastes 5

Ecclesiastes 5:1

Nenda kule usikilize

Ni muhimu zaidi kwenda hekaluni kusikiliza na na kujifunza sheria ya Mungu ili kumtii Mungu kuliko kutoa sadaka lakini kuendelea kutenda dhambi dhidi ya Mungu.

Ecclesiastes 5:2

kuongea kwa mdomo wako

Kuweka ahadi au kiapo kwa Mungu.

Usiwe mwepesi sana ... usiufanye moyo wako uwe mwepesi sana

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja.

maneno yako yawe machache

"usiseme sana"

Ecclesiastes 5:4

kwa kuwa Mungu hafurahii wapumbavu

Tabia moja ya mpumbavu nikuweka ahadi au viapo ambazo hawana mpango wakutimiza.

Ecclesiastes 5:6

Usiuruhusu mdomo wako kusababisha mwili wako kutenda dhambi

"Usiruhusu kile unenacho kikusababishe utende dhambi"

kwa nini kumfanya Mungu ...mikono

"Itakuwa upumbavu kumfanya Mungu akasirike ... mikono

aharibu kazi ya mikono yako

"aharibu kila kitu ufanyacho"

Kwa kuwa katika ndoto nyingi, kama ilivyo katika maneno mengi, kuna mvuke ubatili

"Kuzidisha maneno haiipi umbo, kama vile kuwa na ndoto nyingi haizifanyi kuwa kweli zaidi."

Ecclesiastes 5:8

masikini akiteswa na kunyang'anywa

"watu kuwatesa watu masikini na kuwaibia"

haki na kutendewa vibaya

Hii inamaanisha aina ya matendo ambayo watu wanastahili. "kutendwa sawa."

usishangae

"usishtuke"

kuna watu katika mamlaka

"kuna watu wenye mamlaka"

hata walio juu yao

Kuna wanaume wengine wana utawala juu ya wanaume walio kwenye madaraka. "wanaume walio na mamlaka zaidi yao"

uzalishaji wa ardhi

"chakula ambacho ardhi inazalisha"

Ecclesiastes 5:10

Huu pia ni mvuke

Kama vile mvuke hauna umbo, vivyo hivo hakuna kuridhika katika kutamani pesa.

Kadri mafanikio yanapoongezeka

"Kadri mtu anavyofanikiwa"

ndivyo wanavyoongezeka watu wanaotumia

Maana zinazowezekana ni 1) "ndivyo mtu anavyotumia pesa zaidi" au 2) "ndivyo pia watukuwepo watu zaidi wakutumia utajiri wake."

Kuna faida gani katika utajiri kwa mmiliki isipokuwa kuutazama kwa macho yake?

"Faida pekee ambayo mmiliki alionao kutokana na utajiri wake ni kwamba anaweza kuutazama tu"

Ecclesiastes 5:12

Usingizi wa mfanyakazi ni mtamu

mtu ambaye anafanya kazi nzuri au ya ukweli anaweza kuridhika akijua alifanya kazi nzuri bila kujali malipo.

kama anakula kidogo au sana

"kama anakula chakula kidogo au chakula kingi"

haumuruhusu yeye kulala vizuri

mtu tajiri haridhiki na utajiri wake. Anabaki macho usiku akiwaza pesa zake. "humweka macho usiku"

Ecclesiastes 5:13

mali iliyowekwa akiba na mwenye nayo

"mwenye mali anatunza utajiri"

kwa bahati mbaya

Maana zinazowezekana ni 1) "kupitia bahati mbaya" au 2) "kwa makubaliano mabovu ya kibiashara."

mwana wake ... habakiziwi chochote mikononi mwake

Hapa usemi "mikononi mwake" inamaanisha umiliki. "haachi mali kwa ajili ya mwana wake"

Ecclesiastes 5:15

mtu azaliwavyo uchi ... ataondoka katika maisha haya akiwa uchi

Kwa kuongezea na kutokua na nguo, neno"uchi" hapa linasisitiza kuwa watu wanazaliwa bila kitu chochote. "mtu yu uchi na hamiliki kitu anapozaliwa ...ataondoka maisha haya kwa njia vivyo hivyo.

ataondoka katika maisha haya

"atakufa"

Hachukui chochote

"hachukui chochote mkononi mwake"

kama mtu alivyo kuja ni lazima aende vivyo hivyo

Hii inamaanisha kuzaliwa na kufa kwa mtu na inaashiria wazo sawa na mstari uliopita.

Hivyo ni faida gani mtu yeyote aipatayo katika kufanya kwa ajili ya upepo?

Mwandishi anatumia swali hili kusisitiza wazo lake kuwa hakuna faida kufanya kazi kwa ajili ya upepo. "Hakuna anayepata faida yoyote kwa kufanyia kazi upepo."

kufanya kwa ajili ya upepo

Maana zinazowezekana ni 1) "kujaribu kuushika upepo" au 2) "kufanyia kazi pumzi apumuayo"

Wakati wa siku zake anakula gizani

Hapa neno "giza" linamaanisha hali ya huzuni. Maana zinazowezekana ni 1) "Wakati wa maisha yake anakula kwa kuomboleza" au 2) "Maisha yake anaishi kwa kuomboleza"

na anafedheheshwa sana na magonjwa na hasira

"na kuteseka sana, kwa kuugua na hasira"

Ecclesiastes 5:18

Tazama

"kuwa makini" au "sikiliza"

kile nilichokiona kuwa kizuri kufaaa

Hapa maneno "kizuri" na "kufaa" zinamaana moja. Ya pili inakazia maana ya ile ya kwanza. "kile nilichokiona kuwa bora zaidi kufanya."

wakati wa siku za maisha haya ambayo Mungu ametupa

"kadri Mungu atakavyo turuhusu kuishi"

wajibu wa mtu

Maana zinazowezekana ni 1) "dhawabu ya mtu" au 2) "fungu la mtu maishani"

Ecclesiastes 5:19

mali na utajiri

Maneno haya mawili yana maana moja. Yanamaanisha pesa na vitu ambavyo anaweza kununua kwa pesa.

kupokea sehemu yake na kufurahi katika kazi yake

Hii inaonesha uwezo wa kuridhika na mtu kufurahia kazi yake.

hakumbuki

Ambaye hakumbuki ni mtu ambaye Mungu amempa zawadi.

siku za maisha yake

"vitu vilivyotokea wakati wa maisha yake.

kuhangaika

"kushughulika"

Ecclesiastes 6

Ecclesiastes 6:1

ni mbaya kwa watu

"inasababisha ugumu kwa watu"

mali na utajiri

Maneno haya mawili yana maana moja. Yanamaanisha pesa na vitu ambavyo anaweza kununua kwa pesa.

hakosi chochote

"ana kila kitu"

Mungu ... hampi uwezo wa kukifurahia

Kukusanya utajiri na mali na kushindwa kuufaidi ni bure.

Huu ni mvuke, teso baya

Mtu kutoweza kufaidi mali yake ni teso baya au laana.

Ecclesiastes 6:3

akizaa watoto mia moja

"akizaa watoto 100"

kuishi miaka mingi, ili kwamba siku za miaka yake ni nyingi

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na imeunganishwa kuleta msisitizo.

moyo wake hautosheki kwa mema

"haridhika na vitu vizuri"

hazikwi kwa heshima

Maana zinazowezekana ni 1)"hakuna atakayemzika" au 2) "hakuna atakayemzika vizuri"

Hata mtoto huyo amezaliwa bila faida

"mtoto wa hivyo amezaliwa bure"

anapita katika giza

Hapa neno "giza" linaweza kumaanisha kati ya dunia ya wafu au kitu ambacho ni kigumu kuelewa. "anakufa bila kuelewa"

jina lake linabaki limefichika

"hakuna ajuaye jina lake"

Ecclesiastes 6:5

ana pumziko ingawa mtu huyo hakupumzika

Mtoto ambaye hakuzaliwa hapitia taabu, anabaki katika mapumziko. wakati mtu aliyeishi miaka mingi bila kuridhika anakosa pumziko.

Hata kama mtu akiishi miaka elfu mbili

Hii ni kukuza neno kuonesha kuwa haijalishi ni muda gani mtu ataishi kama hatafurahia vitu vizuri maishani.

miaka elfu mbili

"miaka 2000"

lakini hajifunzi kufurahia vitu vizuri

Hili ndilo lengo, kuwa mtu anapaswa kufaidi vitu vizuri kutoka katika maisha.

Ecclesiastes 6:7

kujaza mdomo wake

"kuweka chakula mdomoni mwake" au "kula"

hamu yake haishibi

"haridhishi hamu yake"

ni faida gani aliyo nayo mwenye hekima kuliko mpumbavu?

Hekima ya mtu mwenye hekima haimfanyi kuwa na starahe za ziada. "mtu mwenye hekima hada nafuu juu ya mpumbavu."

Ni faida gani aliyo nayo masikini hata kama anajua jinsi ya kutenda mbele ya watu?

"Mtu masikini hana nafuu hata kama anajua kutenda mbele ya watu wengine."

Ecclesiastes 6:9

kile ambacho macho hukiona

Mtu anaweza kuona vitu kwa sababu tayari anavyo. "kile ambacho mtu anacho"

kutamani kile ambacho hamu isiyo tulia inatamani

Hii inamaanisha vitu ambavyo mtu anatamani ila hana. "kutamani kile ambacho hana"

mvuke na kujaribu kuuchunga upepo

Mwalimu anasema kwamba vitu ambavyo watu hufanya ni kama kujaribu kuushika upepo au kuuzuia upepo kupuliza.

Chochote ambacho kimekuwepo

"Watu tayari wameshavipatia majina vitu vilivyopo"

vile mtu alivyo ni kama tayari amekwisha fahamika

"watu tayari wanajua vile binadamu alivyo"

Ecclesiastes 7

Ecclesiastes 7:1

Jina zuri

"Sifa nzuri"

watu wanaoishi ni lazima waweke hili moyoni

Wanahitaji kuzingatia ni aina gani ya jina au sifa waliyonayo na watakayoacha wakifa. "wale walio hai wanapaswa kufikiri kwa makini kuhusu hili."

Ecclesiastes 7:3

uso wa huzuni

Hii inamaanisha kuwa na huzuni. "tukio linalomfanya mtu kuwa na huzuni"

furaha ya moyo

Hapa neno "moyo" linamaanisha mawazo na hisia ya mtu. Furaha inafafanua hali ya hisia ya kuwa mwenye furaha na amani . "kufikiri sawa"

Moyo wa mwenye hekima uko katika nyumba ya maombolezo

"Watu wenye hekima huwaza kwa makini kuhusu kifo"

lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya karamu

"lakini mpumbavu anawazu tu jinsi ya kufurahi"

nyumba ya maombolezo ... nyumba ya karamu

Misemo hii inamaanisha nini kinatokea katika sehemu hizi.

Ecclesiastes 7:5

maonyo ya mtu mwenye hekima

"watu wenye hekima wakikuonya"

kusikiliza wimbo wa wapumbavu

"kusikiliza wapumbavu wakiimba"

kama mlio wa miiba chini ya chungu, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu

"kicheko cha wapumbavu" kinalinganishwa na kuchomwa kwa miba ambayo ina kelele ila inateketea upesi.

Ecclesiastes 7:7

Kuchukua kwa nguvu (jeuri)

Hii ina maanisha kumlazimisha mtu kumpa pesa au vitu vingine vya dhamani mtu mwingine ili asimdhuru. Hii inadhaniwa kuwa kosa.

humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu

Maana zinazowezekana ni 1) "humgeuza mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu" au 2) "hufanya ushauri wa mwenye hekima kuonekana kama ushauri wa kipumbavu."

huharibu moyo

Hapa neno "moyo" inamaanisha akili. "huharibu uwezo wa mtu kuwaza na kuamua vizuri"

Ecclesiastes 7:8

watu wenye uvumilivu ni bora kuliko wenye majivuno rohoni

Hapo neno "rohoni" inamaanisha mwenedao wa mtu. "watu wenye subira ni bora kuliko watu wenye majivuno" au "tabia ya uvumilivu ni bora kuliko tabia ya majivuno"

Usikasirike haraka rohoni mwako

"Usiwe mwepesi wa hasira" au "Usiwe na hasira kali"

hasira hukaa katika mioyo ya wapumbavu

Hasira inalinganishwa na kitu kinachoishi ndani ya wapumbavu. "watu wapumbavu wamejaa hasira"

Ecclesiastes 7:10

Kwa nini siku za zamani zilikuwa bora kuliko siku hizi?

Mtu anauliza swali hili ili kulalamika kuhusu wakati wa sasa. "Vitu vilikuwa nafuu zamani kuliko sasa"

sio kwa sababu ya hekima kwamba unauliza swali hili

Mtu anayesema maneno haya halinganishi wakati wa sasa na wa zamani kwa mantiki, lakini kulingana na uelewa wake. "ungekuwa na hekima usingeuliza swali hili" au "kuuliza swali hili inaonesha kuwa hauna hekima"

Ecclesiastes 7:11

wale wanaoliona jua

"wale walio hai"

faida ya maarifa ni kwamba hekima humpa uhai

Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi anatumia maneno "maarifa" na "hekima" kumaanisha kitu kimoja, au 2) "faida ya kujua hekima ni kwamba inakupa uhai."

humpa uhai kwa yeyote aliye nayo

Inayompa uhai ni hekima. Maarifa na hekima "humpa uhai" kwa njia tofauti. Kuchagua uwekezaji mwema, kuwa na marafiki wazuri, kuchagua hali nzuri ya kuishi kiafya, kuishi kwa amani na wengine ni baadhi ya njia amabvyo hekima "humpa uhai."

Ecclesiastes 7:13

Ni nani awezaye kuimarisha chochote alichokipindisha?

"Hakuna awezaye kunyoosha kitu alichokikunja."

Ecclesiastes 7:14

Wakati nyakati ni njema ... wakati nyakati ni mbaya

"Vitu vizuri vinapotokea ... vitu vibaya vinapotokea"

ishi kwa furaha katika hali hiyo

"uwe na furaha kuhusu vitu hivyo vizuri"

zote ziwepo pamoja

"zote ziwepo kwa wakati mmoja"

chochote kinacho kuja baada yake

Maana zinazowezekana ni 1) "chochote kitakachotokea siku za usoni" au 2) "chochote kitakachotokea duniani baada ya yeye kufa" au 3) "chochote kitakachotokea kwake baada ya kufa."

Ecclesiastes 7:15

licha ya kwamba wana haki

"hata kama wana haki"

mwenye haki katika macho yako mwenyewe

mwenye haki, hekima machoni mwako mwenyewe -Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na imeunganishwa kuleta msisitizo.

Usiwe mwenye haki

haki - "Usidhani una haki zaidi ya ambavyo ulivyo"

hekima machoni mwako

"mwenye hekima kwa mawazo yako"

Kwa nini kujiharibu mwenyewe?

Mwandishi anatumia swali kusisitiza kwamba kujiona una haki ni kujiangamiza. "Hakuna sababu ya kujiangamiza."

Ecclesiastes 7:17

Kwa nini ufe kabla ya wakati wako?

"Hakuna sababu ya wewe kufa kabla ya unavyotakiwa"

ushike hekima hii

"jikabidi kwa hekima"

usiache haki iende zake

"usiache kujaribu kuwa mwenye haki" au "unapaswa kuendelea kujaribu kuwa mwenye haki"

atatimiza ahadi zake zote

"atafanya kila kitu ambacho Mungu anatarajia kwake"

Ecclesiastes 7:19

zaidi ya watawala kumi katika mji

Hekima inalinganishwa na watawala wengi wa miji. Hekima inaweza kumfanya mtu kuwa wa muhimu zaidi kuliko watawala wa miji.

anayefanya mema na hatendi dhambi

"anayefanya matendo mazuri na hatendi dhambi"

Ecclesiastes 7:21

kila neno linaongelewa

"kila kitu wanachosema watu"

unafahamu mwenyewe

"wewe mwenyewe unafahamu." Hapa "mwenywe" inatumika kusisitiza "unafahamu."

ndani ya moyo wako

"katika mawazo yako"

Ecclesiastes 7:23

Haya yote nimeyathibitisha

"Hivi vyote amabvyo nimekwisha andaki nimevithibitisha"

ilikuwa zaidi ambavyo ningekuwa

"ilikuwa zaidi ya uwezo wangu kuelewa"

mbali na kina sana

Hekima ilikuwa ngumu kushika. Wakati ulipokuwepo uelewa, ulikuwa mdogo. Ilihitaji utambuzi wa kina zaidi ya vile ambavyo mwandishi aliweza kupata. "ngumu kuelewa"

Ni nani awezaye kuipata?

Mwandishi anatumia swali hili kusisitiza ugumu wa kuelewa hekima. "Hakuna awezaye kuelewa."

Nikageuza moyo wangu

Hapa neno "moyo" inamaanisha akili. "Nikageuza mawazo yangu" au "nikakusudi"

Ecclesiastes 7:26

mwanamke yeyote ambaye moyo wake umejaa mitego na nyavu, na ambaye mikono yake ni minyororo

Mwandishi anasema mwanamke mshawishi ni kama mitego ambayo mwindaji anatumia kushika wanyama.

ambaye moyo wake umejaa mitego na nyavu

Hapa neno "moyo" linamaanisha mawazo na hisia. Huyu ni mwanamke ambaye anajali ya kwake tu. "anayetaka kumtega mtu"

mitego na nyavu

Maneno haya mawili yote yanaonesha njia ambazo watu wanatega wanyama. Anaendelea kufikiria njia za kuwatega wanaume ili wampe vitu.

mikono yake ni minyororo

Hapa neno "mikono" inamaanisha nguvu au mamlaka ya kuongoza. "ambaye hakuna awazaye kutoroka"

mwenye dhambi atachukuliwa naye

"atamkamata mwenye dhambi"

Ecclesiastes 7:27

nikiongeza uvumbuzi mmoja hadi mwingine

"kugundua kitu kimoja baada ya kingine"

ili kwamba nipate ufafanuzi wa ukweli

"ili niweza kufafanua maisha"

mwanamme mmoja mwenye haki miongoni mwa elfu

Mwanamme mmoja tu mwenye haki aliweza kupatikana kati ya wanaume 1,000. "1 mwenye haki kati ya wanaume 1,000"

mwanamke miongoni mwa wale wote

Hakuwepo mwanamke yeyote mwenye haki aliyepatikana katika kundi la wanawake 1,000.

Ecclesiastes 7:29

wametoka katika hali ya unyofu wakitafuta magumu mengi

Maana zinazowezekana ni 1) "wamefanya mipango mingi ya dhambi" au 2) "wamefanya maisha yao wenyewe kuwa magumu."

wametoka

Hapa waliotoka ni wanadamu.

Ecclesiastes 8

Ecclesiastes 8:1

Ni mtu gani mwenye hekima? Ambaye anafahamu matukio yana maana gani katika maisha?

Mwandishi anauliza haya kama maswali yanayoongoza kutoa majibu katika yale atakayoyasema baadaye.

husababisha uso wake kung'ara

Hii inamaanisha kwamba uso wa mtu utaonesha kuwa ana hekima. "inaonekana usoni mwake"

ugumu wa uso wake

"muenekano wake usiopendeza"

Ecclesiastes 8:2

kiapo cha Mungu cha kumlinda yeye

"kiapo ulichoapa mbele za Mungu kumlinda"

Usiharakishe kuondoka mbele ya uwepo wake

Maana zinazowezekana ni 1) usiwe mwepesi kuondoka kimwili katika uwepo wake au 2) kubaki mwaminifu kwa Mfalme, usimuache kwa haraka kwa ajili ya mwingine.

Neno la mfalme hutawala

"Asemacho mfalme ni sheria"

ni nani atakaye mwambia

"hakuna awazaye kumwambia"

Unafanya nini?

"Haupaswi kufanya unachofanya."

Ecclesiastes 8:5

Moyo wa mwenye hekima hutambua

"moyo" unamaanisha mawazo. "Mtu mwenye hekima anatambua"

Ni nani awezaye kumwambia nini kinacho kuja?

Swali hili linasisitiza kuwa hakuna ajuaye kitakachotokea baadaye. "Hakuna awazaye kumwambia kinachokuja."

Ecclesiastes 8:8

Hakuna aliye mtawala wa pumzi yake hata kuizuia pumzi ... hakuna aliye na nguvu juu ya siku yake ya mauti.

Kama vile ambavyo mtu hana uwezo wa kujizuia kupumua, mtu hawezi kuendelea kuishi pale muda wake wa kufa ukifika.

uovu hautawasaidia wale amabao ni watumwa wake

Mwandishi anazungumzia uovu kana kwambani mkuu aliye na watumwa.

nimetia moyo wangu

"Nikusudia" au "Niliamua"

kila aina ya kazi ambayo inafanywa

"kila aina ya kazi ambayo watu hufanya"

Ecclesiastes 8:10

wabaya wakizikwa hadharani

Watu waovu waliokufa walipewa mazishi ya heshima. Inaashiria kuwa miili yao ilipaswa kutupwa katika rundo lililokataliwa la mji au kitu kama hicho. "watu wanawazika waovu hadharani"

Waliondolewa mahali patakatifu na kuzikwa mahali waliposifiwa na watu

"Watu waliwatowa kutoka eneo takatifu na kuwazika na kuwasifu"

Wakati hukumu dhidi ya tendo ovu halihukumiwi haraka

"Wakati watu katika madaraka hawatoi upesi hukumu dhidi ya tendo la uovu"

hushawishi mioyo ya wanadamu

Hapa neno "moyo" linamaanisha mapenzi. "humshawishi binadamu"

Ecclesiastes 8:12

mara mia moja

"Mara 100"

itakuwa vyema kwa wale wanao muheshimu Mungu

"maisha yataenda vyema kwa wale wanaomheshimu Mungu"

wanao mheshimu Mungu, wanaouheshimu uwepo wake

Misemo hii miwili ina maana moja na imeunganishwa kwa ajili ya msisitizo.

maisha yake hayatarefushwa

"Mungu hatarefusha maisha yake"

Siku zake kama kivuli kitowekacho

Maana zinazowezekana ni 1) mwandishi analinganisha urefu wa maisha mtu muovu na kivuli kinachopita upesi au 2) ubora au furaha ya maisha hutoweka kama mtu muovu, hakuna kitu dhabiti katika maisha yake.

Ecclesiastes 8:14

Kuna mvuke mwingine usio faa

"kutokuwa na maana" au "ubatili". Vitu vinatokea ila havipaswi. Kama vile vitu vizuri kuwatokea watu waovu na vitu vibaya kuwatokea watu wema.

jambo jingine linaofanyika juu ya dunia

"kitu kingine ambacho watu wanafanya duniani"

kwa siku zote za maisha yake ambayo Mungu amempa

"kadri Mungu anavyomruhusu kuishi"

Ecclesiastes 8:16

Nikauweka moyo wangu

"Nikusudia" au "Niliamua"

kazi inayofanyika juu ya nchi

"kazi ambayo watu wanafanya duniani"

pasipo kufumba macho

"bila kulala"

kazi inayofanyika chini ya jua

Maana zinazowezekana ni 1) "kazi ambayo Mungu anafanya chini ya jua" au 2) "kazi ambayo Mungu anaruhusu watu kufanya chini ya jua"

Ecclesiastes 9

Ecclesiastes 9:1

nilifikiri haya yote katika akili yangu

"Niliwaza kwa kina sana kuhusu haya yote"

Wote wako katika mikono ya Mungu

Hapa neno "wote" inamaanisha "wenye haki na watu wenye hekima" pamoja na "matendo yao"

mikono ya Mungu

Hapa neno "mikono" linamaanisha nguvu na mamlaka. "chini ya umiliki wa Mungu"

Ecclesiastes 9:2

watu wenye haki na waovu

x

walio safi na wasio safi

x

yeye atoaye dhabibu na yule asiye dhabihu

x

Kama vile watu wema ... wenye dhambi nao watakufa vivyo hivyo

x

yule anayeapa ... vivyo hivyo mtu yule aogopaye kuweka kiapo

x

Ecclesiastes 9:3

kila kitu kinachofanyika

"kila kitu amabacho watu hufanya"

mwisho mmoja

hapa neno "mwisho" linamaanisha kifo.

Mioyo ya wanadamu imejaa uovu, na wazimu uko katika mioyo yao

Hapa neno "mioyo" linamaanisha mawazo na hisia. "Wanadamu wamejaa uovu, na fikra zao ni wazimu"

wanaenda kwa wafu

"wanaenda sehemu ya wafu" au "wanakufa"

Ecclesiastes 9:4

kumbukumbu yao imesahaulika

"watu huwasahau"

Ecclesiastes 9:6

chochote kinachofanyika chini ya jua

"chochote ambacho watu hufanya chini ya jua"

kula mkate wako kwa furaha, na kunywa mvinyo wako na moyo wa furaha

Misemo hii miwili inamaana za kufanana na inasisitiza umuhimu wa kufurahia mambo ya msingi ya maisha.

kula mkate wako kwa furaha

"furahia chakula chako"

kunywa mvinyo wako na moyo wa furaha

Hapa neno "moyo" linamaanisha hisia. "kunywa mvinyo kwa furaha"

Nguo zako ziwe nyeupe siku zote, na kichwa chako kipake mafuta

Kuvaa nguo nyeupe na kupaka kichwa mafuta zilikuwa ishara ya furaha na kusherehekea.

kichwa chako kipake mafuta

"pakaa kichwa chako mafuta"

Ecclesiastes 9:9

Ishi kwa furaha na mwanamke umpendaye

Mtu anapaswa kumpenda mke aliye naye. "Kwa sababu una mke umpendaye, ishi naye kwa furaha"

Chochote mkono wako utakachopata kufanya

"Chochote utakachoweza kufanya"

hakuna kazi, au ufafanuzi au ujuzi au hekima

"wafu hawafanyi kazi au kufafanua au kujua au kuwa na hekima"

Ecclesiastes 9:11

muda na bahati huwaathiri wao wote

"kinachotokea na kitakapotokea huwaathiri wote"

huwaathiri wao wote

Hapa maneno "wao wote" inamaanisha mbio, vita, mkate, utajiri, na upendeleo.

kama vile samaki ... kama ndege ... Kama wanyama, wanadamu

Kifo huwashika wanadamu wakati wasiotarajia, kama vile watu wanavyokamata wanyama wakati wasipotarajia.

katika nyakati mbaya ambazo ghafla huwaangukia

Maana zinazowezekana ni 1) "katika hali mbaya ambayo inawatokea ghafla" au 2) "kwa kifo kinachowapata ghafla."

Ecclesiastes 9:13

katika mji kulikuwa na masikini, mtu mwenye hekima

"katika mji, watu walimkuta mtu masikini mwenye hekima" au "mtu masikini, mwenye hekima aliishi katika mji"

Ecclesiastes 9:16

hekima ya mtu masikini hudharauliwa

Kwa sababu mtu huyu alikuwa masikini, watu hawakuutambua hekima yake, wala kumheshimu kwa hekima yake. "watu husharau hekima ya mtu masikini"

maneno yake hayasikilizwi

Watu waliacha kumsikiliza. "hawasikiliza kile anachokisema" au "hawachukui ushauri wake"

Ecclesiastes 9:17

yanasikiwa vizuri zaidi

"yanaeleweka vizuri zaidi"

Ecclesiastes 10

Ecclesiastes 10:1

Kama nzi walio kufa ... hivyo hivyo upumbavu kidogo

Kama vile ambavyo nzi wanaweza kuharibu manukato, vivyo hivyo upumbavu unaweza kuharibu sifa ya mtu kwa hekima na heshima.

Moyo wa mtu mwenye hekima ... moyo wa mpumbavu

Hapa neno "moyo" inamaanisha akili na nia. "Jinsi mtu mwenye hekima anavyowaza ... jinsi mpumbavu anavyowaza"

huelekea kulia ... huelekea kushoto

Hapa maneno "kulia" na "kushoto" yanamaanisha yalio sawa na yasiyo sawa. "hufanya yaliyo sawa .. hufanya yasiyo sawa"

fikira zake zina upungufu

"ni mjinga"

Ecclesiastes 10:4

Kama jazba za mtawala zikiinuka kinyume na wewe

"kama mtawala akiwa na hasira na wewe"

Ecclesiastes 10:5

Wapumbavu wanapewa nafasi za uongozi

"Watawala wanawapa wapumbavu nafasi za uuongozi"

watu walio fanikiwa wanapewa nafasi za chini

"wanawapa nafasi za chini watu waliofanikiwa"

Ecclesiastes 10:8

Taarifa ya Jumla:

Kazi haikosi hatari.

anaweza kuumizwa nayo

"mawe hayo yanaweza kumuumiza"

Ecclesiastes 10:10

Taarifa ya Jumla:

Mithali kidogo

hekima hutoa faida kwa mafanikio

Mtu mwenye hekima angenoa bapa lake na asingelazimika kufanya kazi sana.

kabla hajafurahi

"kabla anayechezea nyoka hajamchamsha"

Ecclesiastes 10:12

Taarifa ya Jumla:

Mithali inaendelea.

Maneno ya kinywa cha mtu mwenye hekima yana huruma

"Vitu ambavyo mtu mwenye hekima husema vina huruma"

midomo ya mpumbavu humumeza mwenyewe

Hapa neno "kumeza" inaashiria kuteketeza. "Vitu ambavyo mtu mpumbavu hunena humteketeza"

Ecclesiastes 10:13

Kama maneno yanavyo anza kutiririka mdomoni mwa mpumbavu

"Kama mpumbavu anavyoanza kuongea"

mwisho mdomo wake hutiririka wazimu mbaya

"anapomaliza kuonge, anaongea wazimu mbaya"

Mpumbavu huongeza maneno

"Mpumbavu huendelea kuongea"

hakuna ajuaye kinachokuja

Swali hili linasisitiza kuwa hakuna ajuaye kitakachotokea baadaye. "Hakuna awazaye kumwambia kinachokuja."

Ni nani ajuaye baada yake?

Mwandishi anauliza hili swali kusisitiza kuwa hakuna ajuaye kitakachotokea baadaye. "Hakuna ajuaye kitakachokuja baada yake."

Ecclesiastes 10:15

huwachosha

"huwasababisha kujisikia uchovu"

hata hawajui barabara ya kwenda mjini

Maana zinazowezeka ni 1) kwamba mtu mpumbavu anachoka sana kutokana na kufanya kazi sana hadi anashindwa kujua njia ya kwenda popote, au 2) kwamba mtu mpumbavu anachoka kutokana na kufanya kazi sana kwa sababu hajui ya kutosha kwenda nyumbani.

Ecclesiastes 10:16

Ole wako ardhi ... umebarikiwa ardhi

Katika mstari huu, mwandishi anazungumza na taifa kana kwamba ni mtu.

kama mfalme wako ni kijana mdogo

Hii inamaanisha kuwa mfalme hana uzoefu au hajapevuka kiakili. Lakini tafsiri zingine za kisasa zinatafsiri neno la Kihebrania kama "mtumishi"

huanza karamu ahsubuhi

Hii huashiria kuwa viongozi wanajali zaidi kuwa na wakati mzuri kuliko kuongoza taifa.

mfalme wako ni mwana wa waungwana

Hii huashiria kuwa mwana huyu amefundishwa vizuri na wakubwa wake katika desturi za kuwa mfalme mzuri.

Ecclesiastes 10:18

Kwa sababu ya uvivu paa huanguka

Mtu mvivu hawezi kuitunza nyumba kwa kawaida.

kwa sababu ya mikono isiyo fanya kazi

"kwa sababu ya mtu asiye fanya kazi"

Watu huandaa chakula kwa ajili kicheko

"Watu huandaa chakula kwa ajili ya kucheka"

divai huleta furaha maishani

"divai husaidia watu kufurahia maisha"

fedha hutimiza hitaji kwa kila kitu

Maana zinazowezekana ni 1) "fedha husaidia kila hitaji" au 2) "fedha husaidia kwa ajili ya chakula na divai."

Ecclesiastes 10:20

hata katika akili

"hata katika mawazo yako"

wenye mali katika chumba chako

"watu matajiri ukiwa chumbani mwako." Hii inamaanisha usiwalaani watu matajiri hata katika sehemu yako ya faragha ambapo hakuna yeyote atakayekusikia.

Kwa kuwa ndege wa angani ... kinaweza kusambaza jambo

Mistari hii miwili inamaanisha kitu kimoja na imeunganishwa kwa ajili ya msisitizo. Mwandishi unatumia sitiari ya ndege kusema kuwa watu watajua ulichosema kwa njia moja au nyingine.

Ecclesiastes 11

Ecclesiastes 11:1

Peleka mkate wako juu ya maji, kwa kuwa utaupata tena baada ya siku nyingi

Maana zinazowezekana ni 1) kuwa mtu anapaswa kuwa mkarimu na mali yake na kisha atapokea ukarimu kutoka kwa wengine (UDB), au 2) kuwa mtu anapaswa kuwekeza mali zake ng'ambo na atapata faida humo.

Shiriki mkate na watu saba, hata wanane

Maana zinazowezekana ni 1) kugawana mali zako na watu wengi, au 2) kuwekeza mali zako sehemu nyingi.

saba, hata wanane

"7, hata 8" au "wengi"

majanga gani yanayo kuja juu ya nchi

Hapa msemo "juu ya nchi" inamaanisha "duniani" au "katika jamii."

yanajivua yenyewe chini ya nchi

Hapa neno "nchi" inamaanisha "katika ardhi."

kuelekea kusini au kuelekea kaskazini

"katika upande wowote"

Ecclesiastes 11:4

Yeyote autazamaye upepo yawezekana asipande

Maana zinazowezekana ni 1) "Mkulima yeyote anayetilia maanani upepo hatapanda wakati upepo unapopuliza upande usiofaa" au 2) "Mkulima yeyote anayetilia maanani sana upepo hatapanda."

yeyote atazamaye mawingu yawezekana asivune

Maana zinazowezekana ni 1) "Mkulima yeyote anayetilia maanani mawingu hatavuna inapotaka kunyesha" au 2) "Mkulima yeyote anayetilia maanani sana mawingu hatavuna."

ambavyo mifupa ya mtoto ikuavyo

Maana zinazowezekana ni 1) "jinsi mtoto anavyokuwa" au 2) "jinsi mifupa ya mtoto inavyokua."

Ecclesiastes 11:6

kwa mikono yako

"endelea kufanya kazi"

jioni au asubuhi, au hii au ile

Misemo hii miwili inamaana moja na inasisitiza kuwa kazi ya mtu inaweza kufanikiwa, bila kujali ni muda gani aliifanya. "hata kama ni mbegu uliyoipanda asubuhi au mbegu uliyoipanda jioni."

nuru ni tamu

Hapa neno "nuru" inamaanisha kuweza kuona jua hivyo kuwa hai. "kuweza kuliona jua ni tamu" au "kuwa hai ni tamu."

kwa macho kuona jua

Msemo huu unamaana moja na usemi uliopita. "kwa mtu kuliona jua" au "kuwa hai."

aifurahie yote

Hapa neno "yote" inamaanisha miaka ambayo mtu yuko hai.

siku zijazo za giza

Hapa neno "giza" inamaanisha kifo. "atakuwa amekufa ziku ngapi."

kwa kuwa zitakuwa nyingi

Hapa "zitakuwa" inamaanisha "siku za giza." "kwa kuwa atakuwa amekufa siku nyingi zaidi ya zile atakavyokuwa hai au "kwa kuwa atakufa milele."

Kila kitu kijacho

Maana zinazowezekana ni 1) "Kila kitu kinachotokea baada ya kifo" au 2) "Kila kitu kitakachotokea baadaye."

Ecclesiastes 11:9

Furahia kijana, katika ujana wako, na moyo wako ufurahie siku za ujana wako

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na imeunganishwa kwa ajili ya msisitizo.

moyo wako ufurahie

Hapa neno "moyo" inamaanisha hisia. "uwe na furaha"

Fuatilia yale mema ya moyo wako

Hapa neno "moyo" inaweza kumaanisha akili au hisia. "Fuatilia vitu vizuri unavyotamani" au "Fuatilia vitu vyema ulivyokusudia kufuatilia"

chochote kilicho mbele ya macho yako

"Chochote unachoona na kutamani" au "chochote unachoona kinafaa"

Mungu atakuleta hukumuni kwa ajili ya vitu hivi vyote

"Mungu atakuwajibisha kwa matendo yako yote"

Ondoa hasira kutoka moyoni mwako

"Kataa kuwa na hasira"

Ecclesiastes 12

Ecclesiastes 12:1

mkumbuke

"kumbuka"

Mimi sina furaha katika hizo

Hapa neno "hizo" linamaanisha "miaka."

Ecclesiastes 12:3

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaelezea nyumba ambayo matendo mbali mbali yanakoma. Hii inaonekana kuwa sitiari ya mwili wa binadamu unapozeeka.

wanawake wanao saga kukoma, kwa sababu ni wachache

"wanawake wanaosaga nafaka wanaacha kusaga nafaka kwa sababu ni wachache"

Ecclesiastes 12:4

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendeleza sitiari yake.

milango imefungwa katika mtaa

"watu walifunga milango iliyoelekea katika mtaa"

wakati wanaume watasitushwa kwa mlio wa ndege

"wakati sauti ya ndege itakapowashtua"

Ecclesiastes 12:5

Taarifa ya Jumla:

Mwandishi anaendeleza sitiari yake.

wakati ambapo hamu za asili zitakaposhindwa

"wakati ambapo watu hawatamani tena kile walichokuwa wanatamani kwa asili"

wakati ambapo mlozi utachanua maua

mti wa "mlozi" ni mti unaochanua wakati wa baridi na maua meupe.

mtu aenda katika nyumba yake ya milele

inamaanisha kifo.

waombolezaji watelemka mitaani

Maana zinazowezekana ni 1) waombolezaji wanaenda katika mtaa kuhudhuria mazishi, au 2) kwamba waombolezaji wanaenda mtaani kwenye nyumba ya mtu anayekaribia kufa.

Ecclesiastes 12:6

Mkumbuke

"kumbuka"

kabla ya kamba ya fedha kukatwa ... au torori la maji kuvunjika kisimani

Mwandishi anafananisha kifo na vitu mbali mbali vilivyovunjika. Kifo kitavunja mwili ghafla kama watu wavunjavyo hivi vitu wakati wakivitumia.

kamba ya fedha kukatwa

"mtu anakata kamba ya fedha"

bakuli ya dhahabu kupasuka

"mtu anapasua bakuli la dhahabu"

gudulia kuvunjwa

"Mtu anavunja gudulia"

torori la maji kuvunjika

"mtu anavunja torori la maji"

mavumbi kurudia aridhini

Hapa neno "mavumbi" inamaanisha mwili wa binadamu uliooza.

Ecclesiastes 12:8

kila kitu ni mvuke upoteao

"kila kitu kinadumu muda mfupi tu, kama mvuke unapotea."

kutafakari na kupanga

"aliwaza sana kuhusu na kupanga" au "aliwaza sana na kuandika chini"

Ecclesiastes 12:10

Maneno ya watu wenye hekima ... yamefundishwa na mchungaji mmoja

Mwandishi anamfananisha mwalimu anayetumia maneno yake kuelekeza watu na mchungaji anayetumia vifaa vyake kuongoza kundi lake.

Maneno ya watu wenye hekima ni kama mchokoo

"Watu wenye hekima wanatutia moyo kutenda, kama fimbo iliyochongoka inavyo watia hamasa wanyama kusogea.

Kama misumari ilivyogongomewa kwa undani, ndivyo yalivyo maneno ya mabwana katika mkusanyiko wa mithali zao

"Kama vile unavyoweza kuutegemea msumari uliozamishwa chini, ndivyo unaweza kutegemea mithali zilizoandikwa na watu wenye hekima."

maneno ya mabwana katika mkusanyiko wa mithali zao

"maneno ya wale ambao ni mahiri katika mikusanyiko ya mithali"

yamefundishwa na mchungaji mmoja

"ambayo mchungaji mmoja anafundisha"

Ecclesiastes 12:12

utengezaji wa vitabu vingi, ambapo hakuna mwisho

"watu hawatakoma kutengeneza vitabu vingi"

huleta uchovu mwilini

"humchosha mtu"

Ecclesiastes 12:13

Mwisho wa jambo

"hitimisho la mwisho la jambo"

baada ya kila kitu kusikika

"baada ya kusikia kila kitu"