Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Isaiah 1

Isaiah 1:1

Maono ya Isaya ... ambayo aliyaona

"Hili ni Ono la Isaya ... ambalo Yahwe alimwonyesha" au "Hiki ndicho Mungu alichomwonyesha Isaya"

Amozi

Amozi alikuwa baba wa Isaya

Yuda na Yerusalemu

"Yuda" ina maana ya ufalme wa kusini mwa Israeli. "Yerusalemu" ulikuwa mji wake muhimu zaidi. "wale wanaoishi Yuda na Yerusalemu" au "watu wa Yuda na Yerusalemu"

katika siku za Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.

Hii ni lahaja na ina maana ya kipindi ambacho kila mfalme alitawala. Walitawala mmoja baada ya mwingine, na sio wote kwa kipindi kimoja. "Pale Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia walipokuwa wafalme wa Yuda"

Isaiah 1:2

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Sikieni, enyi mbingu, na sikilizeni, enyi nchi

Ingawa unabii huu ulikusudiwa kwa ajili ya watu wa Yerusalemu na Yuda kusikiliza, Isaya anafahamu hawatasikiliza. Maana zawezekana kuwa 1) anazungumza kwa kifupisho, kana kwamba "mbingu" na "nchi" zingeweza kusikiliza kile Yahwe alichosema, au 2) maneno "mbingu" na "nchi" ni mifano ya maneno na neno la ujumla kwa ajili ya viumbe vyote hai kila sehemu. "wewe ambaye unaishi katika mbingu ... wewe ambaye unaishi juu ya nchi"

Yahwe

Hili ni jina la Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la Kale.

Nimewarutubisha ... haielewi

Maneno ambayo Yahwe alizungumza na ambayo Isaya anazungumza kwa Waisraeli kwa niaba ya Yahwe.

Nimewarutubisha na kuwakuza watoto

Yahwe anazungumza kana kwamba maneno yake yalikuwa chakula na kana kwamba Waisraeli walikuwa watoto wake. "Nimewatunza watu wanaoishi Yuda kama walikuwa watoto wangu"

punda kihori cha kulisha cha bwana wake

Unaweza kuiweka wazi taarifa inayoeleweka. "punda anajua kihori cha kulisha cha bwana wake" au "punda anajua ni wapi bwana wake humpatia chakula"

lakini Israeli haijui, Israeli haielewi

Yawezekana hii ina maana ya "lakini watu wa Israeli hawanijui, hawaelewi ya kuwa mimi ndiye ninayewatunza"

Israeli

Huu ni mfano wa maneno kwa ajili ya watu wa Israeli. Yuda ni sehemu ambayo ilikuwa taifa la Israeli. "watu wa Israeli"

Isaiah 1:4

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Taifa, wenye dhambi

Maana zawezekana kuwa 1) Isaya anasema mambo mawili tofauti juu yao. "Taifa la Israeli, nyie wenye dhambi" au 2) anasema jambo moja tu kuhusu wao. "Taifa la wenye dhambi"

watu waliolemewa kwa udhalimu

Kitu kizito sana ambacho mtu anweza kubeba ni sitiari ya dhambi nyingi. "dhambi yao ni kama mfuko mzito juu ya mabega yao unaowafanya vigumu kwao kutembea"

mtoto wa waovu

Neno "mtoto" ni sitiari ya watu ambao hufanya kile wengine walichokwisha fanya. "watu ambao hufanya uovu ule ule wanaouona wengine wakifanya"

tenda mabaya

fanya mambo maovu

Wamemtelekeza Yahwe

"Wameondoka mbali kutoka kwa Yahwe"

wamemdharau

"wamekataa kutii" au "wamekataa kuheshimu"

Israel

Yuda ni sehemu ya iliyokuwa taifa la Israeli.

Wamejitenganisha kutoka kwake

Ingawa katika kipindi kimoja walikuwa marafiki, kwa sasa wanamtendea kana kwamba hawamjui.

Isaiah 1:5

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Kwa nini bado mnapigwa? Kwa nini mnaasi zaidi na zaidi?

Isaya anatumia maswali haya kuwakaripia watu wa Yuda. Maswali haya yanaweza kutafsiriwa kama kauli. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Unaendelea kufanya mambo ambayo Yahwe anatakiwa kukuadhibu. Unaendelea kuasi dhidi yake"

mnapigwa

Hapa neno "mnapigwa" ina maana ya watu ambao huishi Yuda na kwa hiyo ni katika wingi.

Kichwa kizima kimeugua, moyo wote ni dhaifu

Sitiari hii inalinganisha taifa la Israeli na mtu ambaye amepigwa. "Wewe ni kama mtu ambaye kichwa chake kimejeruhiwa na ambaye moyo wake ni dhaifu" au "Wewe ni kama mtu ambaye akili na moyo wake wote ni mgonjwa"

Hakuna sehemu iliyodhuriwa

Hii inaweza kuwekwa katika hali ya chanya. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kila sehemu ya kwako imejeruhiwa" au "mtu amejeruhi kila sehemu ya kwako"

vilikuwa havijafunikwa, safishwa, kufungwa bendeji, wala kutibiwa kwa mafuta

Sitiari hii inalinganisha adhabu ambayo Mungu amewapa Israeli na vidonda halisi. Inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu aliyefunga, safisha, kufunga bendeji, au kuwatibu kwa mafuta"

Isaiah 1:7

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Nchi yako imeharibiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Wameharibu nchi yako" au "Adui zako wameharibu nchi yako"

Miji yako imeungua

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wameunguza miji yenu"

mashamba yenu - mbele yenu, wageni wanaingamiza

"watu ambao si wa nchi yenu wenyewe wanaiba mazao kutoka kwenye mashamba yenu huku mkitazama"

uharibifu uliotelekezwa

"tupu na kuharibiwa". Msemo huu wa nomino dhahania unaweza kuelezwa kama misemo ya kitenzi. "wameangamiza nchi na hakuna mtu anayeishi pale"

kupinduliwa na wageni

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wageni wamepindua nchi yako" au "jeshi la kigeni limeitwaa kabisa"

binti Sayuni amabaki

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nimemuacha binti wa Sayuni"

binti Sayuni

"binti" wa mji ina maana ya watu wa mji. "Watu wa Sayuni" au "Watu wanaoishi Sayuni"

ameachwa kama kibanda cha shamba la mizabibu, kama kivuli katika bustani ya matango

Maana zawezekana kuwa 1) "amekuwa mdogo kama kibanda katika shamba la mizabibu au kivuli katika bustani ya matango" au 2) "ameachwa kwa mtindo ambao mkulima huacha kibanda katika shamba la mizabibu au kivuli katika bustani ya matango anapokuwa kamalizana nayo"

kama ... matango, kama mji uliozingirwa

Maana nyingine yaweza kuwa "kama ... matango. Yeye ni mji uliozingirwa"

Isaiah 1:9

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Kama Yahwe

Hii inaelezea jambo amabalo lingeweza kutokea zamani lakini halikutokea.

mabaki wachache

"waliokoka wachache"

ametuachia ... tungekuwa

Hapa maneno haya yana maana ya Isaya na yanajumuisha watu wote wa Yuda na Yerusalemu.

tungekuwa kama Sodoma, tungekuwa kama Gomora

Jinsi ambavyo Yuda angekuwa kama Sodoma na Gomora inaweza kufanywa wazi. "Mungu angetuangamiza, kama alivyoangamiza miji ya Sodoma na Gomora"

Isaiah 1:10

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

nyie watawala wa Sodoma ... nyie watu wa Gomora

Isaya analinganisha watu wa Yuda na Sodoma na Gomora kusisitiza jinsi walivyokuwa wenye dhambi. "nyie watawala ambao mna dhambi kama watu wa Sodoma ... nyie watu ambao ni waovu kama wale walioishi Gomora"

"Wingi wa sadaka zako kwangu ni upi?"

Mungu anatumia swali kukaripia watu. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Sadaka zako nyingi hazina maana yoyote kwangu!"

Isaiah 1:12

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

ni nani ametaka kutoka kwako, kukanyaga mahakama yangu?

Neno "kukanyaga" lina maana ya kukanyaga juu ya na kuponda kwa mguu wa mtu. Mungu anatumia swali kukaripia watu wanaoishi Yuda. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "hakuna aliyekuambia kukanyanga katika uwanja wangu wa mahakama!"

Usilete sadaka zisizo na maana

"Usiniletee zawadi zako zaidi zisizo na maana"

ubani ni chukizo kwangu

Hapa nomino dhahania ya "chukizo" inaweza kuelezwa kama kitenzi "chuki". "Ninachukia ubani makuhani wanayochoma"

siwezi kustahimili mikusanyiko hii ya kiovu

Maana zawezekana kuwa 1) "Siwezi kuwaruhusu kukusanyika pamoja kwa sababu ya mambo maovu mnayofanya" au 2) "Siwezi kujiruhusu kuwatazama mkikusanyika pamoja kwa sababu ya mambo maovu mnayofanya"

Isaiah 1:14

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

mbala miezi yenu mipya, na sikukuu mlizochagua

Maneno "mbala miezi mipya" ni mfano wa maneno kwa sherehe za mwezi mpya. Pia ni maneno yenye maana sawa na sherehe za kawaida. "sherehe zako za mbala miezi mipya na sikukuu zingine mpya"

mbala miezi mipya

Mbala mwezi mpya ni pale ambapo mwezi unapoanza kutoa mwanga baada ya kuwa giza.

ni mzigo kwangu; nimechoka kivivumilia

Hii inalinganisha namna Mungu anavyojisikia kuhusu sherehe za watu kwa kubeba kitu kizito. "wao ni mzigo mzito ambao nimechoka kuubeba"

ninaficha macho yangu kwako

Lahaja hii niu njia ya kusema "Sitakutazama" au "Sitakutazama kwa uangalifu"

mikono yako imejaa damu

Hii ni sababu ambayo Mungu hatasikia maombi yao. Damu inawezekana kumaanisha vurugu ambayo wamefanya dhidi ya watu. "kwa sababu ni kama mikono yako imefunikwa na damu ya wale uliowadhuru" au "kwa sababu una hatia ya vurugu"

Isaiah 1:16

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Jioshe, jisafishe

Hapa Mungu analinganisha mtu anayeacha kutenda dhambi na mtu ambaye anaosha mwili wake. "Tubu na uoshe dhambi kutoka moyoni mwako kama uanvyoosha uchafu kutoka mwilini mwako"

ondoa uovu wa matendo yako kutoka machoni pangu

Mungu hakuwa anawaambia kufanya matendo yao maovu sehemu nyingine, lakini kuacha kuyafanya. "acha kufanya matendo maovu ambayo naona mnafanya"

nyosha wima ukandamizaji

Mungu anazungumza na watu ambao huwakandamiza wengine kana kwamba wamefanya kitu kupinda ambacho kilitakiwa kuwa wima, na anawaita kukifanya kitu hicho kuwa wima tena. Nomino dhahania "ukandamizaji" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "hakikisha ya kwamba wale watu wasiojiweza uliowadhuru hawateseki kutoka na mambo mabaya uliyofanya kwao"

toa haki kwa yatima

"uwe na haki kwa watoto ambao hawana baba"

walinde wajane

"walinde wanawake ambao waume zao wamefariki"

Isaiah 1:18

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

Njooni sasa, na

Yahwe anawakaribisha kwa upendeleo na upendo watu kusikiliza kile anachotaka kusema. "Tafadhali mnisikilize. Na" au "Zingatia kwa makini; Ninataka kukusaidia".

tutafakari pamoja

"Tufikirieni juu ya hili pamoja" au "tunahitaji kujadili hili" au "tutaenda kufanya nini?". Yahwe anawakaribisha watu kujadili siku za usoni. Hapa neno "tutafakari" lina maana ya Yahwe na linajumuisha watu wa Yuda.

ingawa dhambi zako ni rangi nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji; ingawa ni nyekundu kama nyekundu iliyoiva, zitakuwa kama sufu

Isaya anazungumza na watu kana kwamba walikuwa wanavaa nguo ambazo zilitakiwa kuwa sufu nyeupe na dhambi zao kana kwamba zilikuwa mabaka mekundu ya dhambi juu ya nguo. Iwapo Yahwe anasamehe dhambi zao, itakuwa kana kwamba nguo zao zitakuwa nyeupe tena.

ni rangi nyekundu

Rangi nyekundu ni rangi nyekundu inayong'aa "nyekundu inayong'aa"

nyeupe kama theluji

Nyeupe mara kwa mara ni alama ya utakatifu au usafi. "Theluji" ina maana ya kitu kama mvua iliyoganda ambayo ni nyeupe sana. Kwa kuwa hii

nyekundu iliyoiva

Nyekundu hii ni nyekundu iliyoiva "nyekundu iliyoiva"

kama sufu

Sufu ni manyoya ya kondoo au mbuzi. Jinsi zitakavyokuwa kama sufu inaweza kufanywa wazi. "nyeupe kama sufu"

Isaiah 1:19

Taarifa ya Jumla

Mungu anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

Kama u mtiifu na tayari

Hapa, "tayari" na "mtiifu" inatumika pamoja kumaanisha wazo moja. "Kama upo tayari kutii"

utakula mema ya nchi

"nchi itazaa chakula kizuri kwa ajili yako kula"

lakini kama utakataa na kuasi

"lakini kama ukikataa kusikiliza na badala yake kutonitii mimi"

upanga utakumeza

Neno "upanga" lina maana ya maadui wa Yuda. Pia, neno "kumeza" inalinganisha maadui wa Yuda kuja kuwaua kama mnyama pori ambaye hushambulia na kula wanyama wengine. "maadui wako watakuua"

kinywa cha Yahwe kimesema hivi

Neno "kinywa" kinasisitiza ya kwamba Yahwe amasema na kile anachosema hakika kitatokea. "Yahwe amezungumza" au "Yahwe amesema ya kwamba hiki kitatokea"

Isaiah 1:21

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Jinsi mji mwaminifu

Neno hili la mshangao linaonyesha hasira na huzuni ya Isaya juu ya watu wa Yerusalemu. "Tazama jinsi watu wa Yerusalemu, ambao wamekuwa waaminiufu kwa Mungu"

ulivyokuwa kahaba

Isaya analinganisha watu na mwanamke ambaye sio mwaminifu kwa mumewe lakini analala na wanamume wengine kwa pesa. Watu hawakuwa waaminifu kwa Mungu lakini walikuwa wakiabudu miungu ya uongo. "kutenda kama kahaba"

Alikuwa amejaa haki

Neno "alikuwa" ina maana ya Yerusalemu na watu wake. Wale waliondika Biblia mara kwa mara walimaanisha miji kama wanawake. "Watu wa Yerusalemu walikuwa wa haki na walifanya kilicho sahihi"

lakini sasa amejaa wauaji

Neno "amejaa" lina maana ya Yerusalemu na watu wake. Wale waliondika Biblia mara kwa mara walimaanisha miji kama wanawake. "lakini sasa watu wa Yerusalemu ni wauaji"

Fedha yako imekuwa chafu, divai yako imechanganywa na maji

Maana zawekekana kuwa ya kwamba Isaya anatumia fedha na divai kama sitiari ya 1) watu wa Yerusalemu. "Wewe ni kama fedha ambayo sio safi tena, na kama divai ambayo imechanganywa na maji" au 2) matendo mema ambayo watu walifanya awali. "Mlikuwa mkifanya matendo mema, lakini sasa matendo yenu mabaya yanafanya matendo yenu mema kutokuwa na maana".

fedha ... chafu

Mtu huhitaji kusafisha fedha mara kwa mara au haitang'aa tena.

divai ... maji

Divai na maji ndani yake ina ladha kidogo na kwa hiyo haitofautiani na maji.

Isaiah 1:23

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shair.

Wakubwa wenu ni waasi

"Viongozi wao wanaasi dhidi ya Mungu"

wenzi wa wezi

"wao ni marafiki wa watu ambao huiba kutoka kwa wengine"

rushwa ... malipo

Watu hutoa "rushwa" kama zawadi kwa watawala wasio waaminifu kwa hiyo watawala hapohapo watatenda kinyume na haki. Watawala hupokea "malipo" kama zawadi kutoka kwa wale hutengeneza faida kutoka kwa sheria zisizo haki ambazo mtawala amezipitisha.

hukimbilia malipo

Mtu anapokuwa na shauku sana mtu ampatie rushwa inazungumzwa kana kwamba malipo yanakimbia na mtu anayafukuza. "kila mtu hutamaniu mtu kumlipa pesa kufanya maamuzi yasiyo ya kweli"

Hawawalindi yatima

"hawawalindi wale ambao hawana baba"

wala maombi ya haki ya mjane hajaji mbele zao

"wala hawasikii pale ambapo wajane huenda kwao kupata msaada dhidi ya wale wanaovunja sheria" au "na hawasaidii wajane wanaokwenda kwao kupata msaada dhidi ya wale wanaovunja sheria"

Isaiah 1:24

Taarifa ya Jumla

Isaya anaanza kuzungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Kwa hiyo

"Kwa sababu hiyo"

Hili ni tamko la Mungu

Nomino dhahania "tamko" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "hivi ndivyo ambavyo Mungu anatamka"

Nitafanya kisasi dhidi ya washindani wangu, na kujilipiza kisasi dhidi ya adui zangu

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja. Maneno "chukua kisasi dhidi ya maadui wangu" huzungumza zaidi juu ya Yahwe kufanya chochote anachohitaji kufanya kwa wale wanaofanya kazi dhidi yake ili aweze kuwa na furaha. Maneno "kujilipiza kisasi dhidi ya adui zangu" yanazungumza zaidi juu ya Yahwe kuadhibu kwa haki adui zake. "Nitaadhibu wale ambao wananipinga" au "Nitafanya kile kinachonipendeza kwa wale wanaofanya kazi dhidi yangu, na nitaadhibu kwa haki adui zangu"

Nitageuza mkono wangu dhidi yako

Hapa "mkono" ina maana ya nguvu ya Mungu ambayo angetumia kuadhibu watu wake. "Nitaanza kutumia nguvu yangu yote dhidi yako"

safisha takataka zako kwa maji magadi

Hapa hatua ambayo Mungu hutoa dhambi za watu wake inazungumziwa kana kwamba anatenganisha chuma kutoka kwa vitu vibaya vilivyochanganywa navyo. Maneno "kwa maji magadi" yanaongeza sitiari nyingine, kwa sababu maji magadi hutumika ndani ya sabuni, sio kusafisha chuma. "na kama vile moto unavyotoa uchafu kutoka kwa fedha, nitatoa uovu wote kutoka miongoni mwao"

takataka

Huu ni uchafu na mambo mengine ambayo watu hutoa kutoka kwenye vyuma ili chuma kiwe safi.

Isaiah 1:26

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

hapo mwanzo ... hapo mwanzo

Hizi ni njia mbili za kuzungumzia sehemu ya kwanza au mwanzo wa historia ya Israeli, pale ambapo Israeli ilipokuwa taifa.

utaitwa

Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "watu watakuita"

mji wa utakatifu, mji mwaminifu

Hapa "mji" una maana ya watu wanaoishi Yerusalemu. "mji ambao watu ni watakatifu na waaminifu kwa Mungu"

Isaiah 1:27

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Sayuni itakombolewa kwa haki, na waliotubu kwa utakatifu

Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. Maana zawezekana kuwa 1) " Yahwe atakomboa Sayuni kwa sababu watu pale hufanya kilicho haki, na atawakomboa wale wanaotubu kwa sababu wanafanya kile ambacho Yahwe anasema ni sahihi" au 2) "Yahwe atakomboa Sayuni kwa sababu ana haki, na atakomboa wale wanaotubu kwa sababu ni mtakatifu"

Sayuni

Huu ni mfano wa maneno wa "watu wanaoishi juu ya Mlima Sayuni".

Waasi na wenye dhambi wakandamizwa pamoja

Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Mungu ataangamiza wale ambao huasi na kutenda dhambi dhidi yake"

wale wanaomuacha Yahwe watatoweka kabisa

Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "na Yahwe atawaondoa kabisa wale wanaogeuka kutoka kwake" au "na Yahwe atawaua wote wanaomkataa"

Isaiah 1:29

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Miti ya mwaloni mitakatifu ... bustani

Misemo hii ina maana ya sehemu ambapo watu wa Yuda waliabudu sanamu.

utaaibika kwa

Baadhi ya tafsiri husema, "utaona aibu kwa sababu ya". Mtu huona aibu uso wake unapochemka, mara kwa mara kwa sababu anahisi amefanya kitu kibaya.

Kwa maana utakuwa kama mwaloni ambao majani hufifia, na kama bustani ambayo haina maji

Maji hutoa uhai kwa miti na bustani. Watu wamejikata kutoka kwa Yahwe, ambaye hutoa uhai.

Isaiah 1:31

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Mtu mwenye nguvu

"Mtu mwenye nguvu" au "Yeyote mwenye nguvu". Hii inaweza kumaanisha watu ambao ni muhimu na wana ushawishi kwa watu wengine"

vitu vinavyoshika moto haraka

vitu vilivyokauka vinavyowaka kirahisi

na kazi yake kama cheche

Hii inalinganisha matendo ya mtu au kazi zake za uovu na cheche ambazo huanguka juu ya vitu vinavyoshika moto haraka na kuiwasha moto. "kazi yake itakuwa kama cheche ambayo huanzisha moto"

Isaiah 2

Isaiah 2:1

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Yuda na Yerusalemu

"Yuda" na "Yerusalemu" ni mifano ya maneno kwa ajili ya watu wanaoishi pale. "wale wanaoishi katika Yuda na Yerusalemu"

katika siku za mwisho

"katika siku za usoni"

mlima wa nyumba ya Yahwe utaimarishwa

Hii inaweza kuwekwa 1) kama ufafanuzi. "Mlima wa nyumba ya Yahwe utasimama" au 2 katika hali ya kutenda. "Yahwe ataimarisha mlima ambapo hekalu lake linajengwa"

kama kilele cha milima

Isaya anazungumzia umuhimu kana kamba ni urefu wa kihalisia. "sehemu muhimu zaidi ya milima" au "sehemu muhimu zaidi duniani"

itainuliwa juu zaidi ya vilima

Isaya anazungumzia heshima kama sitiari kana kwamba ilikuwa urefu halisi. Hii inaweza kuwekwa 1) katika hali ya kutenda. "Yahwe atuheshimu kuliko kilima kingine" au 2) kama mfano wa maneno kwa ajili ya watu wanaoabudu pale. "Yahwe atawaheshimu watu ambao wanaabudu pale kuliko vile anavyoheshimu watu wengine wowote"

na mataifa yote

Hapa "mataifa" ni mfano wa maneno kwa ajili ya watu wa mataifa hayo. "na watu kutoka mataifa yote"

yatatiririka kwake

Watu kuzunguka duniani kwenda katika mlima wa Yahwe inalinganishwa na jinsi mto unavyotiririka. Hii inasistiza ya kuwa watu wengi watakuja, sio tu watu wachache.

Isaiah 2:3

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Yakobo, ili aweze kufundisha ... na tuweze kutembea

Maana nyingine ni "Yakobo . Atafundisha ... na tutatembea"

aweze kutufundisha baadhi ya njia zake, na tuweze kutembea katika njia zake

Neno "njia" ni sitiari kwa namna mtu anavyoishi. Kama lugha yako ina neno moja tu kwa ardhi ambayo watu wanatembea, unaweza kunganisha miseo hii miwili. "aweze kutufundisha mapenzi yake ili kwamba tuweze kumtii"

Kwa maana kutoka kwa Sayuni sheria itakwenda, na neno la Yahwe kutoka Yerusalemu

Misemo hii ina maana ya kitu kiimoja. Isaya alikuwa akisisitiza ya kwamba mataia yote yataelewa ya kwamba ukweli unapatikana Yerusalemu. "Watu wa Sayuni watafundisha sheria ya Mungu, na watu wa Yerusalemu watafundisha neno la Yahwe"

Kwa maana kutoka kwa Sayuni sheria itakwenda

"Kwa maana sheria itakwenda kutoka Sayuni". Isaya anazungumza kana kwamba sheria ilikuwa kitu kama mto ambao husogea bila watu kufanya lolote. "Wale ambao wanafundishwa sheria watatoka nje kutoka Sayuni" au "Yahwe atatangaza sheria yake kutoka Sayuni"

neno la Yahwe kutoka Yerusalemu

"neno la Yahwe litatoka kutoka Yerusalemu". Isaya anazungumza kana kwamba neno la Yahwe lilikuwa kitu kama mto ambacho kinasogea bila watu kufanya lolote. Unaweza kufanya taarifa inayoeleweka wazi. "Wale ambao wanafundishwa sheria watatoka nje kutoka Yerusalemu" au "Yahwe atatangaza sheria yake kutoka Yerusalemu"

Isaiah 2:4

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

Atawahukumu

"Yahwe atawahukumu"

atatoa maamuzi

"atatatua ugomvi"

watatwanga panga zao katika majembe, na mikuki yao katika ndoano za kupogolea

Watu wa mataiufa watageuza silaha zao za vita kuwa vifaa kwa ajili ya ukulima.

panga ... mikuki ... upanga

Maneno haya ni maana sawa ya silaha za aina yoyote.

majembe ... ndoano za kupogolea

Maneno haya ni maana sawa ya vifaa vya aina yoyote ambavyo watu hutumia katika shughuli za amani.

watatwanga panga zao katika majembe

"watafanya panga zao kuwa vifaa kwa ajili ya kuoanda mbegu". Jembe ni ubapa ambao watu hutumia kuchimba katika ardhi iuli waweze kupanda mbegu pale.

na mikuki yao katika ndoano za kupogolea

"watatwanga mikuki yao kuwa ndoano za kupogolea" au "watafanya mikuki yao kuwa vifaa kwa kutunza mimea". Ndoano ya kupogolea ni kisu ambacho watu hutumia kukata matawi ambayo hayahitajiki kutoka kwa mimea.

taifa halitainua panga lake dhidi ya taifa

"hakuna taifa litainua panga lake dhidi ya taifa lingine". Panga ni mfano wa maneno kwa ajili ya vita. "taifa moja halipigana vita dhidi ya taifa lingine"

wala hatafanya maandalizi kwa ajili ya vita

"wala hawatafanya maandalizi kupigana vitani". Mwandishi anatarajia msomaji kuamiini ya kwamba wale wanaopigana vita hufanya maandalizi kabla ya kupigana na kwamba baadhi wanaofanya maandalizi hawapigani.

Isaiah 2:5

Taarifa ya Jumla

Katika 2:5 Isaya anazungumza na watu wa Yuda, na katika 2:6 anazungumza na Yahwe. Nyakati zote mbili anazungumz katika mtindo wa shairi.

Nyumba ya Yakobo

"Nyie uzao wa Yakobo". Neno "nyumba" ni mfano wa maneno kwa ajili ya watu wanaoishi katika nyumba, familia. Hapa "Yakobo" inawakilisha taifa la Yuda, lakini itafaa zaidi kutumia "Yakobo" hapa.

njooni

kutumainisha kwa upole kufanya kile mwandishi anataka kumwambia msikilizaji kufanya.

na tutembee katika nuru ya Yahwe

Isaya anazungumza na watu kujifunza na kisha kufanya kiile Yahwe anachotaka wao kufanya kana kwamba walikuwa wakitembea usiku na nuru ambayo Yahwe aliwapatia ili waweze kuona njia. "na tujifunze jinsi Yahwe anatutaka tuishi na kisha tuishi namna hiyo"

Kwa kuwa mmetelekeza watu wako

"Kwa kuwa mmewaacha watu wako" na haujali nini kitatokea kwao. Hapa neno "mmetelekeza" lina maana ya Yahwe ni kwa hiyo ni katika umoja.

wamejazwa kwa tamaduni kutoka mashariki

Isaya anazungumza kana kwamba watu walikuwa vyombo ambavyo vilikuwa vimejaa na kitu kutoka mashariki. Maana zaweza kuwa anazungumza 1) matendo ambayo watu wa mashariki hufanya. "wanafanya kila wakati matendo maovu ambayo watu wanaoishi katika nchi za mashariki mwa Israeli hufanya" au 2) watu, haswa wale wanaotangaza kuzungumza na wafu, ambao wanatoka mashariki kufanya matendo maovu. "waaguzi wengi wanatoka mashariki na sasa wanaishi pale"

wasoma ishara

watu wanaotangaza ya kwamba wanaweza kutabiri muda ujao kwa kutazama vitu kama sehemu ya wanyama na majani.

na wanashika mikono na wana wa wageni

Kushika mikono pamoja ni ishara ya urafiki na amani. "wanafanya amani na kufanya kazi pamoja na watu ambao hawatoki Israeli"

Isaiah 2:7

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na Yahwe katika mtindo wa shairi.

Nchi yao imejaa fedha ... nchi yao pia imejaa farasi ... Nchi yao pia imejaa sanamu

Isaya anazungumza kana kwamba nchi ilikuwa chombo ambacho mtu ameweka fedha, farasi, na sanamu. Neno "nchi" ni mfano wa maneno kwa ajili ya watu wenyewe, na maneno "imejaa" ni sitiari kwa ajili ya watu kumiliki vifaa hivi. "Wanamiliki fedha nyingi ... pia wanamiliki farasi nyingi ... Pia wanamiliki sanamu nyingi"

ufundistadi wa mikono yao wenyewe, vitu ambavyo vidole vya wenyewe vimetengeneza

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza ya kwamba hivi sio miungu ya kweli. Kama lugha yako haina maana ya jumla kwa kitu ambacho mtu ametengeneza, unaweza kuunganisha misemo hii miwili katika moja. "vitu ambavyo wao wenyewe umetengeneza"

ufundistadi wa mikono yao wenyewe

Neno "mikono" ina maana sawa na watu wenyewe. "ufundistadi wao wenyewe" au "kazi yao wenyewe" au "vitu ambavyo wametengeneza kwa mikono yao"

vitu ambavyo vidole vya wenyewe vimetengeneza

Neno "vidole" ina maana sawa na watu wenyewe. "vitu ambavyo wametengeneza kwa vidole vyao wenyewe"

Isaiah 2:9

Taarifa ya Jumla

Katika 2:9 Isaya anamaliza kuzungumza na Yahwe. Katika 2:10-11 Isaya anazungumza na watu wa Yuda. Nyakati mbili anazungumza katika mtindo wa shairi.

Watu watainamishwa, na kila mtu binafsi ataanguka chini

Hapa kuwa chini mpaka ardhini inawakilisha watu ambao wameaibishwa kabisa kwa sababu wamegundua yote waliyoamini hayana maana, na hawawezi kufanya kitu kujisaidia wenyewe. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "'Mungu atafanya watu waaibike, na watagundua ya kwamba waliamini katika vitu visivyo na maana"

Watu

binadamu, tofauti na wanyama

mtu binafsi

"kila mtu"

usiwainue juu

Maneno "kuwainua juu" ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kusamehe watu. "usiwasamehe"

Nenda katika sehemu za mawe

Maana zaweza kuwa watu wanapaswa kwenda katika 1) mapango juu ya teremko za upande wa milima au 2) sehemu ambapo kuna mawe makubwa mengi ambapo mtu atajificha.

jifiche katika ardhi

Maana zaweza kuwa ya kwamba watu wanapaswa kujificha 1) katika shimo la kawaida katika ardhi au 2) katika shimo ambalo wanachimba katika ardhi.

kutoka kwa hofu kuu ya Yahwe

Hapa nomino dhahania "hofu kuu" inaweza kuelezwa na kitenzi "kuogofya". "kutoka kwa uwepo wa kuogofya wa Yahwe" au "Kutoka kwa Yahwe kwa sababu utamwogopa sana"

utukufu wa ufalme wake

"uzuri wake mkuu na nguvu ambayo anayo kama mfalme" au "ufahari wake wa kifalme"

mtazamo wa kiburi wa mwanamume kutashushwa chini

"Yahwe atashusha chini mtazamo wa kiburi wa mwanamume". Mwanamume mwenye "mtazamo wa kiburi" anatazama juu ya kila mtu kuwaonyesha ya kwamba ni bora kuliko wao. Hapa watu wote wana hatia ya kufikiri wapo bora kuliko Yahwe, na jinsi wanavyotazama wale wanaomwabudu Yahwe, ni mfano wa maneno wa kiburi chao. "Yahwe atawaibisha watu wote kwa sababu wanafikiri wako bora kuliko yeye"

kiburi cha wanamume kutashushwa chini

Yahwe atawafanya wanamume wenye kiburi kuaibiika wao wenyewe. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atashusha chini kiburi cha wanamume" "Wanamume wenye kiburi" ni mfano wa maneno wa watu wenye kiburi. "Yahwe atawashusha chini watu wenye kiburi"

Yahwe peke yake atainuliwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu watamsifu Yahwe tu"

katika siku hiyo

Hii ni lahaja. "katika siku ambayo Yahwe anahukumu kila mtu"

Isaiah 2:12

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.

ambaye ana kiburi na ameinuliwa

Yule ambaye "ameinuliwa" ana majivuno na kujichukulia kuwa bora kuliko watu wengine. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambaye anajisifu na anajiinua juu ya watu wengine" au "ambaye anajivuna na kufikiri ya kwamba yuko bora kuliko watu wengine"

ambaye ana kiburi ... ambaye anajisifa

Mtu ambaye ana majivuno anaongeza na kutenda kana kwamba yupo bora kuliko watu wengine. Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kusisitiza ya kwamba Yahwe atawaadhibu wao"

na yeye atashushwa chini

"na kila mtu mwenye kiburi atashushwa chini". Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atamnyenyekeza"

dhidi ya mierezi ya Lebanoni ... dhidi ya mwaloni ya Bashani

"Siku ya Yahwe wa Majeshi" itakuwa dhidi ya mierezi na mwaloni. Maana zaweza kuwa 1) miti hii ni sitiari kwa watu wenye kiburi ambao Mungu atawahukumu au 2) Mungu kwa uhakika ataangamiza miti hii mikuu.

Isaiah 2:14

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi. Anaendelea kufafanua kile kitakachotokea katika siku ya Yahwe wa Majeshi.

na dhidi ya

Katika 2:14-16 Isaya anaorodhesha viitu ambavyo Mungu ataangamiza. Maana zaweza kuwa 1) hivi vina maana ya watu wenye kiburi ambao Mungu atawashusha au 2) Mungu atawaangamiza kabisa vitu hivi katika orodha.

milima ... vilima

Maneno haya ni sitiari kwa ajilii kiburi cha Waisraeliu. Pia zinajitokeza katika 2:1.

ambayo imeinuliwa juu

Hii ni lahaja. "ambayo iko juu sana"

mnara wa juu ... ukuta usioshindika

Hii ina maana ya vitu ambavyo watu watajenga kuzunguka miji yao ilii waweze kujilinda dhidi ya adui zao. Ni sitiari kwa ajili ya kiburi cha Waisraeli na waliamini hawakuwa na hitaji la Yahwe na wangeweza kusimama dhidi ya adhabu yoyote Yahwe angewapimia kwao kwa ajili ya dhambi zao.

ukuta usioshindika

"ukuta ambao hakuna kitu kinachoweza kuvunja au kupita katikati"

meli za Tarshishi ... vyombo vizuri vya matanga

Hizi zina maana ya meli kubwa ambazo watu walitumia kusafiri mbali juu ya bahari na kuleta bidhaa katika miji yao.

meli za Tarshishi

"meli ambazo wanatumia kwenda Tarshishi"

Isaiah 2:17

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi. Anaendelea kufafanua kile kitakachotokea katika siku ya Yahwe wa Majeshi.

Kiburi cha mtu kitashushwa chini

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Atawashusha chini watu wenye kiburi" au "Atamuwaibisha kila mwanamume mwenye kiburi"

Kiburi cha wanamume kitaanguka

Nomino dhahania "kiburi" inaweza kutafsiriwa kama kivumishi. "wale watu ambao wana kiburi na wataacha kuwa na kiburi"

Yahwe pekee ayainuliwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu watamsifu Yahwe tu"

Hizo sanamu zitapita mbali kabisa

"Sanamu zote zitatoweka" au "Hapatakuwa na sanamu zaidi"

Wanamume watakwenda ... kutoka kwa hofu kuu

Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Wanamume watakwenda .. kujificha kutoka kwa hofu kuu"

mapango ya mawe

"mapango katika mawe". Haya ni mawe makubwa, sio mawe madogo ambayo yanaweza kushikiliwa katika mkono.

kutoka kwa hofu kuu ya Yahwe, na kutoka kwa utukufu wa ukuu wake wa enzi

Hapa nomino dhahania "hofu kuu" inaweza kuelezwa na kitenzi "kuogofya". "kutoka kwa uwepo wa kuogofya wa Yahwe" au "Kutoka kwa Yahwe kwa sababu utamwogopa sana"

kutoka kwa hofu kuu ya Yahwe

kwa sababu walikuwa wanamuogopa sana Yahwe

kutoka kwa utukufu wa ufalme wake

Hapa neno "utukufu" kufafanua "ufalme". "uzuri ambao anao kama mfalme"

atakapoinuka kuogofya dunia

"pale Yahwe atakapochukua hatua na kusababisha watu wa dunia kumuogopa sana"

Isaiah 2:20

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi. Anaendelea kufafanua kile kitakachotokea katika siku ya Yahwe wa Majeshi.

kwa fuko na popo

Fuko ni wanyama wadogo ambao huchimba na kuishi chini ya ardhi. Popo ni wanyama wanaopaa wadogo ambao mara nyingi huishi ndani ya mapango. "kwa wanyama"

mianya katika mawe .. nyufa za mawe yaliyopasuka

Kama lugha yako haina maneno mawili tofauti kwa ajili ya "mianya" na "nyufa", nafasi inayojitokeza katikati ya sehemu mbili ya jiwe linapogawanyika, unaweza kuunganisha misemo hii miwili kuwa moja.

kutoka kwa hofu kuu ya Yahwe

kwa sababu walikuwa wakuimuogopa sana Yahwe.

utukufu wa ukuu wake wa enzi

"uzuri wake mkuu na nguvu ambayo anayo kama mfalme" au "ukuu wake wa enzi wa kifalme"

atakapoinuka kutisha dunia

"pale Yahwe anapochukua hatua na kusababisha watu wa dunia kumuogopa sana"

ambaye pumzi yake ya uhai ipo katika pua zake

pumzi ipo ndani ya pua zake Pua ni dhaifu na shimo za pua ni nzuri, kwa hiyo pia ni mfano wa watu, ambao ni dhaifu. "ni nani ambaye ni dhaifu na atakufa" au "nani anahitaji pumzi katika pua yake kuishi"

pua

mashimo katika pua ambapo watu hupumulia

kwa maana ataambulia wapi?

Isaya anatumia swali kuwakumbusha watu kitu ambacho wanapaswa kuwa wanakijua tayari. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "kwa maana mtu ataambulia patupu!" au "kwa maana mtu hana faida yoyote!"

Isaiah 3

Isaiah 3:1

Tazama

Neno "tazama" hapa linaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata. Pia inaweza kutafsiriwa kama "Sikiliza" au "Hasa".

tegemeo na nguzo

Maneno haya mawili yana maana ya fimbo ya kutembelea, ambayo mtu huegemea kwa msaada. Wazo hili lina maana ya vitu ambavyo watu wanahitaji zaidi ili waishi: chakula na maji. "kila kitu ambacho kinakukimu" au "kila kitu ambacho unategemea"

mtu hodari ... mchawi wa kiume mwenye ujuzi

Hii ni orodha ya makundi ya watu ambao wengine wanawategemea. Kwa kuwa hazimaanishi watu binafsi hasa, inaweza kutafsiriwa na nomino za wingi. "wanamume hodari

msoma ishara

Hawa ni watu ambao wanadai ya kwamba wanaweza kujua mambo yajayo kwa kuangalia vitu kama sehemu za wanyama na majani.

nahodha wa hamsini

Hii lahaja ina maana ya nahodha ambaye anasimamia wanajeshi hamsini. Inaweza kutafsiriwa kwa msemo wa jumla zaidi. "afisa wa jeshi" au "jemadari wa jeshi"

hamsini

"50"

Isaiah 3:4

Nitaweka vijana wadogo kuwa viongozi wao, na watoto watatawala juu yao

Misemo hii ina maana ya kitu kimoja. Maana zaweza kuwa 1) "Nitaweka watu wachanga kama viongozi wao, na hao watu wachanga watatawala juu yao" au 2) "vijana" ni sitiari kwa ajili ya wanamume wapumbavu. "Nitawawekea juu yao viongozi ambao hawajakomaa, kama watu wachanga, na wale viongozi wabaya watatawala juu yao"

Nitaweka vijana wa kawaida

Hapa neno "Nitaweka" ina maana ya Yahwe. Hii inaweza kuwekwa wazi. "Yahwe anasema, "Nitaweka vijana wa kawaida kama viongozi wao""

Watu watakandamizwa, kila mmoja kwa mwingine, na kila mmoja kwa jirani yake

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kila mtu atakuwa mkatili kwa wengine na atamtendea ubaya jirani yake"

walioshushwa

"watu ambao hawana heshima" au "watu ambao hakuna mtu anayewashimu"

waliotukuka

"watu wenye heshima" au "watu ambao kila mtu anawaheshimu"

Isaiah 3:6

na uharibifu huu uwe mikononi mwako

Hapa "mikono" inawakilisha mamlaka. "chukua usimamizi wa uharibifu huu" au "tawala juu ya uharibifu huu"

uharibifu huu

Maana zaweza kuwa 1) majengo mengi katika mji wa Yerusalemu yaliangamizwa au 2) watu katika Yerusalemu hawana mafanikio tena au uongozi. "mji huu, ambao sasa umeharibiwa"

sitakuwa mponyaji

Kutatua matatizo ya watu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kuwaponya. "Hapana, siwezi kutengeneza tatizo hili" au "Hapana, siwezii kukusaidia"

Isaiah 3:8

Kauli Kiunganishi

Nabii anaanza kutoa neno juu ya hii hali

Yerusalemu imejikwaa, na Yuda imeanguka

Kutomtii Mungu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa ikijikwaa na kuanguka

macho ya utukufu wake

Hapa "macho" ina maana ya Mungu mwenyewe, ambaye ni mtukufu.

Mtazamo katika uso wao unashuhudia dhidi yao

Mionekano wa majiivuno katika nyuso za watu inazungumziwa kana kwamba mionekano ilikuwa watu ambao wanaweza kushuhudia dhidi ya watu wanaojivuna. "Mionekano ya kiburi juu ya nyuso zao zinaonyesha ya kwamba wanapingana na Yahwe"

wanasema juu ya dhambi yao kama Sodoma; hawaifichi

Hapa watu wa Yuda wanasemekana kuwa kama watu wa Sodoma, kwa sababu walijivuna wazi wazi kuhusu dhambi zao. "kama watu wa Sodoma, wanazungumza kuhusu dhambi zao na kuwaruhusu kila mtu ajue juu yao"

Kwa maana wamekamilisha maangamizi kwa ajili yao

Maangamizi bado yanakuja, lakini watu walimaliza kufanya kile kitakachosababisha kufuatia. Sababu za maangamizi zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa ni balaa zenyewe. "Kwa maana wamefanya kila kitu ambacho kitasababisha maangamizi kutokea"

Isaiah 3:10

Mwambie mtu mwenye haki ya kwamba itakuwa ni salama

"Mwambie yule ambaye anafanya kilicho haki ya kwamba nitafanya mambo kuwa mazuri kwake"

mtu mwenye haki

Hii ina maana ya watu wenye haki kwa ujumla. "watu wenye haki"

kwa maana watakula matunda ya matendo yao

Matendo yazungumziwa kana kwamba yalikuwa miti itoayo matunda yanayoweza kuliwa. Tunda ina maana ya dhawabu ya kufanya matendo mema. "kwa maana watapokea dhawabu yao kwa ajili ya matendo yao mazuri" au "kwa maana watapokea dhawabu yao kwa ajili ya mambo mazuri waliyofanya"

watakula matunda ya matendo yao

Maandishi ya Kiebrania yana wingi wa kiwakilishi nomino hapa, lakini yana maana ya mtu mwenye haki yeyote. Watafsiri wanaweza kuchagua kutafsiri katika umoja. "atakula tunda la matendo yake"

kwa maana fidia ya mikono yake itafanyika kwake

Hapa "mikono" ina maana ya matendo ambayo mtu amefanya. "kwa kile ambacho mtu mwovu amefanya kwa wengine itafanyika kwake"

Watu wangu ... watu wangu

Maana zaweza kuwa 1) Isaya anazungumza na "wangu" kumaanisha Isaya, au 2) Yahwe anazungumza na "wangu" kumaanisha Yahwe.

watoto ndio wakandamizaji wao

Maana zawvza kuwa 1) "watu wachanga wamekuwa viongozi wao na wanakandamiza watu" au 2) "viongozi wao hawajakomaa kama watoto na wanakandamiza watu"

wanawake wanatawala juu yao

Maana zaweza kuwa 1) "wanawake wanatawala juu ya watu" au 2) "viongozi wao ni wadhaifu kama wanawake"

wale wanaokuongoza wanakuongoza nje ya mstari na kuchanganya muelekeo wa njia yako

Ilikuwa kawaida katika Mashariki ya Kati ya Zamani kuzungumza juu ya viongozi wa taifa kana kwamba walikuwa wachungaji. Mchungaji huongoza kondoo katika njia nzuri katika usalama, viongozi wanapaswa kuwafunza watu ukweli na kuwasaidia kufanya kilicho sahihi. Viongozi wa Yuda hawakuwa wakifanya hivi. "viongozi wako ni kama wachungaji wabaya na hawakuonyeshi mahali pa kwenda"

Isaiah 3:13

Yahwe husimama kwa ajili ya mashtaka; anasimama kuwashtaki watu

Isaya anazungumzia uamuzi wa Yahwe kudhuru watu kana kwamba Yahwe alikuwa akileta mashtaka halali katika mahakama dhidi ya watu wa Israeli. Sehemu ya pili ya mstari huu una maana hiyo hiyo na sehemu ya kwanza, lakini inasema kikamilifu zaidi. "ni kana kwamba Yahwe amechukua nafasi yake katika mahakama na alikuwa tayari kushtaki watu"

atakuja na hukumu

Hukumu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni kitu ambacho mtu anawez kuleta kwa mtu mwingine. "atatangaza hukumu yake" au "atatamka hukumu yake"

Umeharibu shamba la mizabibu

Hapa "umeharibu" ina maana ya wazee na watawala. Yahwe anazungumzia juu ya watu wake kana kwamba walikuwa shamba la mizabibu. Kama mtu anayeshindwa kutunza shamba la mizabibu ili kwamba mizabibu zishindwe kuzaa matunda, wazee na viongozi wanakatisha tamaa Waisraeli kutomtumikia Mungu. "Watu wangu ni kama shamba la mizabibu, na umeliharibu"

Uporaji kutoka kwa maskini upo katika nyumba zenu

"vitu ulivyochukua kutoka kwa maskini zipo ndani ya nyumba zenu"

maskini

Kivumishi kidogo hiki kinaweza kuwekwa kama kivumishi. "wale ambao ni maskini"

Kwa nini unaponda watu wangu na kusaga nyuso za maskini?

Yahwe anauliza swali hili ili kwamba awashataki viongozi wa watu. Mashtaka haya yanaweza kuelezwa kama kauli. "Nina hasira na nyie watu waovu kwa sababu mnaponda watu wangu na kusaga nyuso za maskini"

unaponda watu wangu

Kufanya watu wangu kuteseka inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kuwaponda na uzito mkubwa sana. "kuwaumiza watu wangu kwa ukatili"

kusaga nyuso za maskini

Kuwafanya watu kuteseka inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kufuta nyuso zao katika ardhi. "kudhuru maskini na kuwafanya wateseke"

Isaiah 3:16

binti wa Sayuni

Sayuni, ina maana hapa mji wa Yerusalemu, anazungumzia kana kwamba ilikuwa mwanamke na binti zake. "wanawake wa Sayuni"

na vichwa vyao vikiwa juu

Hii ina maana kwa namna ya majivuno.

onyesha mapenzi kwa macho yao

Hapa "macho yao" yanawakilisha jinsi wanawaka wanavyowatazama. "wakijaribu kuwafurahisha wanamume kwa namna wanavyowatazama"

kutembea kwa maringo huku wakienda

"kuchukua hatua ndogo sana wanapotembea"

na kutoa mlio kama njuga kwa miguu yao

"kwa hiyo bangili katika vifundo vya miguu yao" au "kwa hiyo kengele katika vifundo vya miguu yao zilipiga kelele"

Isaiah 3:18

Taarifa ya Jumla

Hii inaendelea kumfafanua jinsi Yahwe atakavyohukumu wanawake wa Yerusalemu.

Bwana ataondoa

Hapa "ataondoa" inawakilisha kusababisha wengine kuondoa kitu. "Bwana atasababisha wengine kuondoa"

mapambo ya vito vya kifundo cha mguu

Pambo ambalo wanawake huvaa katika kifundo cha miguu, juu kidogo ya mguu.

ukanda wa kichwani

Pambo ambalo wanawake huvaa juu ya vichwa na nywele

mapambo yenye umbo la mwezi mwandamo

Mapambo yenye umbo la mwezi ambao watu huvaa kwa imani ya kwamba yatamlinda mtu kutoka na uovu.

lozi ya kidani ya sikioni

mapambo ya vito ambayo huning'inia kutoka kwenye sikio au juu ya sikio

bangili

Pambo ambalo wanawake huvaa katika mikono

shela

nyenzo nyembamba sana inayotumika kufunika kichwa na uso wa mwanamke

hijabu

vipande vyembamba vya nguo, virefu ambavyo wanawake hujifunga kuzunguka kichwa au nywele.

mkufu wa kifundo cha mguu

Haya ni mapambo ambayo wanawake huvaa karibu na miguu. Mara kwa mara mikufu huning'inia chini na kutoa sauti ya chini.

mishipi

kipande cha nguo ambacho watu huvaa kuzunguka kiuno au kupita kifuani.

visanduku vya manukato

kisanduku kidogo au mfuko unaokuwa na manukato ambayo wanawake walivaa juu ya mikufu au kamba kuzunguka shingo zao ili watoe harufu nzuri.

hirizi ya bahati

mapambo ya vito ambayo watu huvaa kwa imani ya kwamba italeta bahati nzuri

Isaiah 3:21

pete

pambo ambalo huvaliwa kuzunguka kidole

mapambo ya vito ya puani

pambo ambalo huvaliwa ndani ya au katika pua

joho la sikukuu

vazi refu linalolegea lenye mapambo ambalo lilivaliwa juu ya nguo zingine kwa kila mtu kuona

majoho

nguo inayovaliwa juu ya mabega kwa nje ya nguo

shela

nyenzo nyembamba sana inayotumika kufunika kichwa na uso wa mwanamke

mifuko ya mikononi

mfuko uliotumika kubeba vitu vidogo vidogo

vioo vya mkononi

uso mdogo, unaobebwa mkononi na kutumika kujitazama mwenyewe

kitani safi

kitambaa laini kinachovaliwa na watu matajiri

vipande vya kichwani

kitambaa au kofia ndogo inayovaliwa juu ya nywele

vifungashio

pambo la nguo ambalo mwanamke hujiviringishia kujifanya awe mzuri

Isaiah 3:24

mshipi

kipande cha nguo ambacho watu huvaa kuzunguka kiuno au kupita kifuani.

kamba

Hii inaweza kumaanisha kamba ambayo maadui wangefunga watu wa Yuda pale walipowakamata. Au inaweza kumaanisha ya kwamba wanawake wa Yerusalemu wangekuwa hawana kitu cha kuvaa ila nguo zilizochafuka zilizoshikwa kwa kamba.

nywele iliyopangwa vizuri, upaa

nywele zilizopangwa, upaa - "nywele nzuri, vichwa vyao vitakuwa na upaa"

Wanamume wenu wataanguka kwa upanga, na wanamume wenu wenye nguvu wataanguka vitani

Kuanguka ina maana ya kuuawa, na upanga inawakilisha vita. "Wanamume wenu watauawa vitani, na wanamume wenu wenye nguvu watauawa katika vita" au "Maadui wako watawaua wanajeshi wako katika vita"

malango ya Yerusalemu yataomboleza na kulia

Isaya anazungumzia malango ya mji kulia kana kwamba yalikuwa watu kama mfano wa maneno kwa ajili ya watu ambao watalia katika maeneo ya wazi karibu na malango. "Watu wa Yerusalemu watakaa katika malango ya mji na kulia na kuomboleza"

atakuwa peke yake na atakaa juu y ardhi

UIsaya anazungumzia watu wa Yerusalemu, ambao hakuna mtu atakayewaokoa kutoka kwa adui zao, kana kwamba walikuwa mji wao wenyewe na kana kwamba walikuwa mwanamke ambaye hukaa juu ya ardhi kwa sababu marafiki zake wote wamemuacha"

Isaiah 4

Isaiah 4:1

turuhusu tuchukue jina lako

Msemo huu una maana ya "turuhusu tukuoe"

tawi la Yahwe litakuwa zuri

Maana zawezekana kuwa 1) "tawi" ni neno lenye maana sawa na neno linalowakilisha mazao ambayo Yahwe atasababisha kuota katika nchi ya Israeli. "Yahwe atasababisha mazao katika Israeli kuwa mazuriu" au 2) "tawi" ni sitiari ambayo ina maana ya Masihi.

litakuwa zuri na lenye utukufu

"litakuwa limejaa uzuri na utukufu"

matunda ya nchi yakuwa matamu na ya kupendeza sana kwa wale waliosalia Israeli

"Matunda" mara kwa mara inawakilisha chakula kinachozalishwa katika nchiu, na mara nyingi inawakilisha baraka za kiroho. Maana hapa zawezekana kuwa 1) Mungu atasababisha nchi kutoa chakula kizuri tena. "watu ambao bado wapo Israeli watafurahia chakula bora kutoka katika nchi" au 2) Masihi ajaye ataleta baraka za kiroho kwa watu katika nchi.

Isaiah 4:3

yule ambaye amebaki Sayuni na yule ambaye anabaki Yerusalemu

Kauli hizi mbili zina maana moja. Hapa "yule ambaye" haimaanishi mtu dhahiri lakini watu kwa ujumla ambao bado wako hai Yerusalemu. "kila mtu ambaye anabaki Yerusalemu"

ataitwa mtakatifu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Bwana atawaita watakatifu" au "watakuwa wa Bwana"

kila mmoja ambaye ameandikwa chini kama aishiye Yerusalemu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kila mmoja ambaye jina lake lipo katika orodha ya watu ambao wanaishi Yerusalemu"

Bwana atakapokuwa ameosha uchafu wa binti wa Sayuni

Msemo huu unazungumzia dhambi kana kwamba ilikuwa uchafu halisi. "baada ya Bwana kuondoa dhambiu ya binti wa Sayuni kama vile mtu anavyoosha uchafu"

binti wa Sayuni

Maana zawezekana kuwa 1) wanawake wa Yerusalemu au 2) watu wa Yerusalemu

na atakuwa amesafisha madoa ya damu kutoka miongoni mwa Yerusalemu

"Madoa ya damu" hapa yanawakilisha vurugu na mauaji. "na atakuwa amewaondoa wale walioko Yerusalemu ambao huwadhuru watu wasio na hatia"

kwa njia ya roho wa hukumu na roho anayewaka moto

Hii ni jinsi Mungu atakavyotoa dhambi kutoka Yerusalemu. Hapa "roho" huenda inawakilisha tukio la kuhukumu na kuchoma. "kwa hukumu na moto unaowaka"

roho wa hukumu

Maana zawezekana kuwa 1) Yahwe atawaadhibu watu au 2) Yahwe atawatangaza kuwa na hatia

roho awa moto uwakao

Maana zawezekana kuwa 1) hii ni sitiari ambayo inamaanisha Yahwe ataondoa wenye dhambi kutoka Sayuni kama moto uondoavyo uchafu au 2) "moto unaowaka" ni mfano wa maneno yanayowakilisha uharibifu kwa ujumla wa wenye dhambi wote.

Isaiah 4:5

kivuli juu ya utukufu wote

Maana zaweza kuwa 1) kivuli cha kulinda mji mtukufu, au 2) kivuli kinachojumuiusha utukufu wa Mungu ambao utalinda mji. Kama maana ya kwanza inafuata, basi inaweza kumaanisha zaidi ya kwamba mji ni tukufu kwa sababu Yahwe yupo mudo huo ndani yake.

kivuli

Hiki ni kitambaa ambacho huning'inizwa juu ya kitu kukifunika kwa ajili ya ulinzi.

Isaiah 5

Isaiah 5:1

Taarifa ya Jumla

Isaya anasema fumbo juu ya mkulima na shamba lake la mizabibu. Mkulima anawakilisha Mungu na shamba la mizabibu linawakilisha watu wa Yuda, ufalme wa kusini wa Waisraeli.

ninayempenda

"rafiki yangu kipenzi"

juu ya kilima chenye rutuba

"juu ya kilima ambapo mazao mazuri yanaweza kuota"

akachimbua kwa sepeto

"Ameandaa udongo". Msemo huu una maana ya kutumia kifaa kuchimba katika ardhi kuiandaa kwa ajilii ya kupanda.

Akajenga mnara katikati yake

"Alitengeneza jengo refu katikati ya shamba la mizabibu kuutazama". Mtu alikuwa akisimama juu ya mnara kutazama shamba la mizabibu na kuhakikisha hakuna wanyama au watu watakaoingia ndani mwake. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi.

kujenga kishinikizo cha zabibu

"alichimba shimo kuminya juisi ya zabibu". Kishinikizo cha zabibu ni sehemu ya chini iliyochongwa kwa jiwe katika ardhi ambapo wafanyakazi hukanyaga juu ya zabibu kuisaga kwa miguu yao, ili kutoa juisi ya zabibu.

zabibu mwitu

"zabibu zisizo na thamani" au "zabibu zenye ladha mbaya"

Isaiah 5:3

Taarifa ya Jumla

Katika fumbo la Isaya ya shamba la mizabibu, mmiliki wa shamba la mizabibu, ambaye anawakilisha Mungu, inazungumzia watu wa Yerusalemu na Yuda juu ya shamba lake la mizabibu.

wakazi wa Yerusalemu na mtu wa Yuda

Misemo hii ina maana ya ujumla watu wote wanaoishi Yerusalemu na Yuda, kwa hiyo iinaweza kutafsiriwa na nomino za wingi. "nyie wote ambao mnaishi Yerusalemu na Yuda"

Yerusalemu ... Yuda

"Yuda" ilikuwa jina la ufalme wa kusini wa Waisraeli, na Yerusalemu ulikuwa mji mkuu.

amua kati yangu na shamba langu la mizabibu

Wazo la nafasiii kugawanyisha vitu viwili mara kwa mara lilitumiika kueleza wazo la kuchagua moja kati ya nyingine ya vitu hivyo. "amua ni nani ametenda sahihi, mimi au shamba langu la mizabibu"

Ni kipi zaidi ambacho kingeweza kufanywa kwa ajili ya shamba langu la miiizabibu, ambalo sijafanya kwa ajili yake?

Mmilikii anatumia swali hili kutoa kauli juu ya shamba lake la mizabibu. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Nimefanya kila nachoweza kwa ajili ya shamba langu la mizabibu"

Nilipoitazama kuzaa zabibu, kwa nini ilizaa mizabibu mwtu?

Mmiliki anatumia swali kusema ya kwamba shamba lake la mizabibu limezaa zabibu nzuri. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Nilitaka kutengeneza zabibu nzuri, lakini ilizaa zabibu zisizo na thamani"

Isaiah 5:5

Taarifa ya Jumla

Katika fumbo hili, mmiliki wa shamba la mizabibu anaendelea kuzungumza juu ya shamba lake la mizabibu.

ondoa kitalu

"ondoa mpaka wa vichaka". Kitalu ni safu ya vichaka au miti midogo ambayo ilipandwa ili kulinda bustani au eneo lingine lolote. Hapa "kitalu" huenda ina maana ya vichaka vya miiba ambavyo vilipandwa kuota katika ukuta wa mawe unaozunguka shamba la mizabibu.

nitaibadili kuwa malisho

"nitaruhusu wanyama kwenda pale na kula". Hili ni eneo lenye nyasi ambapo wanyama hula.

itakanyagwa chini

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wanyama watapakanyaga chini"

nitailaza kuwa takataka

"nitapaangamiza"

haitapogolewa wala kupaliliwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu atapapunguza au kupapalilia" au "hakuna mtu atapakata matawi ambayo hayahitajiki, na hakuna mtu wa kutunza udongo"

mbigili na miiba itachipua juu

Mbigili na miiba mara kwa mara hutumika kama alama za miji na nchi zilizoharibiwa.

Isaiah 5:7

Taarifa ya Jumla

Isaya anafafanua fumbo la shamba la mizabibu.

Kwa ajili ya shamba la mizabibu la Yahwe wa majeshi ndiyo nyumba ya Israeli

"Kwa maana shamba la mizabibu la Yahwe wa majeshi linawakilisha nyumba ya Israeli" au "Watu wa Israelii ni kama shamba la mizabibu la Yahwe, Bwana wa majeshi ya malaika"

nyumba ya Israeli

Mataifa na makundi ya kikabila yanazungumziwa mara kwa mara katika Biblia kana kwamba yalikuwa nyumba, yaani, familia. "watu wa Israeli"

mtu wa Yuda mmea wake wa kufurahisha

"watu wa Yuda ni kama shamba la mizabibu ambalo huwapa watu starehe"

mtu wa Yuda

Hapa "mtu" inawakilisha watu wote wa Yuda. "watu wa Yuda"

alisubiri kwa ajili ya haki, lakini badala yake, kukawa na mauaji

Hii inaweza kubadilishwa ili kwamba nomino dhahania "haki" iweze kuelezwa kwa kitenzi "fanya kilicho haki". Nomino dhahania "mauaji" iuanweza kuelezwa kama "walijiua wao kwa wao". Yahwe alisubir watu kufanya kilicho haki, lakini badala yake walijiua wao kwa wao"

kwa ajili ya haki

Msemo "alisubiri" umeachwa lakini unaeleweka. Taarifa hii inayoeleweka inaweza kufanya maana kuwa wazi. "Alisubiri kwa ajili ya haki" au "Alisubiri kwa ajili yao kufanya kilicho haki"

badala yake, kelele za msaada

"badala yake, kulikuwa na kelele za msaada". Sababu ya watu kupiga kelele ya msaada inaweza kuwekwa wazi. "badala yake, wale ambao walikuwa dhaifu walipiga kelele kwa mtu kuwasaidia kwa sababu wengine walikuwa wakiwashambulia"

kelele

Msemo huu huenda una maana ya kelele nyingi.

Isaiah 5:8

Taarifa ya Jumla

Isaya anatangaza hukumu ya Mungu.

kwa wale ambao wanaunga nyumba kwa nyumba, ambao wanaunga shamba kwa shamba

"kwa wale ambao huchukua nyumba zaidi na zaidi, na yule ambaye huchukua mashamba zaidi na zaidi". Isaya anachukulia ya kwamba wasikilizaji wake wanajua ya kwamba sheria inakataza mtu kuchukua ardhi kutoka kwa familia kwa kudumu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi.

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli.

bila wakazi

"bila mtu yeyote anayeishi pale"

shamba la mizabibu la nira kumi

nira ya shamba la mizabibu Ukubwa wa shamba la mizabibu linawakilishwa na namba ya jozi za maksai ambao wanaweza kulilima katika siku moja. Kila jozi huunganishwa kwa nira. "shamba la mizabibu ambalo ni kubwa vya kutosha kwa jozi kumi za maksai kulilima"

bathi moja

"bathi moja ya divai" au "lita 22 ya divai"

homeri moja ya mbegu itatoa efa moja tu

"lita 220 za mbegu ztazaa lita 22 tu za nafaka". Homeri moja ni sawa na efa kumi.

Isaiah 5:11

wale ambao huamka mapema alfajiri ... ambao hukawia usiku kwa kuchelewa

Hii ina maana ya watu ambao hawafanyi lolote siku nzima lakini hunywa vinywaji vya kulewa.

mpaka divai inapowachoma

Hapa nguvu ya mvinyo kuwafanya wanywaji wake kulewa inazungumziwa kana kwamba ilikuwa ikiwachoma, yaani, kuwawasha moto. "hadi walewe kwa mvinyo"

kinubi, zeze, tari, filimbi na mvinyo

Hivi vyombo vya muziki na mvinyo zinaonyesha ya kwamba watu wanaofurahia vitu hivi wanasherehekea sana.

tari

Chombo cha muziki chenye kichwa kama ngoma ambacho kinaweza kupigwa kwa mkono. Huenda kilikuwa na vipande vya chuma vikizunguka upande ambao ilitoa sauti mpigaji alipokitikisa. Tari ilikuwa kidogo kwa mpigaji kukishika na kukitikisa kwa mkono mmoja.

kufikiria

"walifikiri kwa uzito juu ya"

matendo ya mikono yake

Hii inaweza kuandikwa tena ili kwamba nomino dhahania "matendo" yaelezwe kama kitenzi "kufanya" au "kuunda". "Kile alichofanya" au "kile alichounda"

matendo ya mikono yake

Hapa mifano ya maneno "mikono" inawakilisha mtu ambaye amefanya kitu. "Kile Yahwe alichofanya"

Isaiah 5:13

Taarifa ya Jumla

Mistari hii inasema kile kitakachotokea kwa watu kwa sababu hawajamtii Mungu.

watu wangu wamekwenda katika kifungo

Katika unabii vitu ambavyo vitatokea katika siku za usoni mara kwa mara vilimaanisha kana kwamba vilikwisha tendeka. Hii inasisitiza ya kwamba unabii utakuja kuwa kweli hakika. "maadui kutoka nchi zingine zitachukua watu wangu, Israeli, kama watumwa"

kwa ukosefu wa ufahamu

Kile ambacho hawaelewi inaweza kuwekwa wazi. "kwa sababu hawamuelewi Yahwe au sheria yake"

Kuzimu imefanya hamu yake kubwa zaidi na imefungua kinywa chake wazi sana

Msemo huu unazungumzia kuzimu, ambayo hapa ina maana ya kaburi, kwa mnyama ambaye yupo tayari kula wanyama wengine. Inasemekana ya kwamba watu wengi, wengi watakufa. "kifo ni kama mnyama mwenye njaa ambaye amefungua kinywa chake wazi kumeza watu wengi"

watu wao wenye uwezo, viongozi wao, na wale ambao wana furaha miongoni mwao, wanashuka kuzimu

Nabii anazungumzia kuhusu siku za usoni kana kwamba kinatokea sasa. "Watu wengi wa Israeli, watu wake muhimu na watu wa kawaida, viongozi wao na wale wanaofurahia sherehe, wataingia kuzimu"

Isaiah 5:15

Mtu atalazimishwa kuinama chini, na binadamu atashushwa

Misemo inayotumika pamoja ina mana moja na inatumika pamoja kwa msisitizo. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu atafanya kila mtu kuinama chini na kuwa wanyenyekevu".

Mtu atalazimishwa kuinama chini, na binadamu atashushwa

Matukio ya siku za usoni yanazungumziwa kana kwamba vimekwisha tendeka.

Mtu atalazimishwa kuinama chini

Kuinama chini mara kwa mara inaashria kuaibishwa.

macho ya mwenye majivuno yatakuwa chini

Kuangalia chini mara nyingi ni ishara ya kuaibishwa. "macho ya watu wenye kiburi wataangalia chini kwa aibu" au "watu ambao wanamajivuno sasa wana aibu".

mwenye majivuno

Hapa watu wenye kiburi, majivuno wanazungumziwa kana kwamba wapo juu zaidi ya watu wengine. "kiburi"

Yahwe wa majeshi atainuliwa katika haki yake

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu watamsifu Yahwe wa majeshi kwa sababu ni mwenye haki"

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli

atainuliwa

Kuheshimiwa inazungumziwa kana kwamba ni kuinuliwa juu. "ataheshimiwa sana"

kondoo watakula kama kwenye malisho yao wenyewe

Yahwe ataangamiza mji wa Yerusalemu, ambao uliitwa "shamba la mizabibu" katika 5:1. Litakuwa zuri bila chochote ila kwa ajili ya kondoo kula nyasi pale.

lisha

kula nyasi

katika uharibifu, kondoo watalisha kama wageni

Yaani, kondoo watalisha pale. Nchi itakuwa haina thamani kwa shughuli nyingine yoyote.

Isaiah 5:18

Ole wao ambao huvuta udhalimu kwa kamba zisizo na thamani na kuvuta dhambi kana kwamba iliikuwa kwa kamba ya mkokoteni

Misemo hii ina maana moja. Inazungumzia watu ambao wanaendelea kufanya dhambi kwa makusudi kana kwamba walikuwa wakitumia nguvu yao kuvuta mkokoteni mzito. Mungu atawaadhibu kwa ajili ya dhambi yao". "Ole wao ambao hufanya kazi kwa bidii kutenda dhambi kama mtu ambaye huvuta mkokoteni kwa kamba"

wale ambao husema

Hii ina maana ya wale ambao wanaendelea kutenda dhambi (mstari wa 18) na kisha kwa dhihaka kumpa na Mungu changamoto ya kuwazuia. "wale wadhihaki ambao husema"

acha mipango ya Mtakatifu wa Israeli aje

Mipango ya Mungu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa vitu ambavyo vinaweza kuja vyenyewe. "acha Mtakatifu wa Israeli atimize mipango yake"

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

Isaiah 5:20

ambao huwakilisha giza kuwa nuru, na nuru kuwa giza ... uchungu kuwa utamu, na utamu kuwa uchungu

Wale wanaofanya vitu hivi ni sawa na wale ambao "huita uovu wema, na wema uovu". Vitu hivi ni kinyume na watu wanajua tofauti kati yao, lakini baadhi ya watu hudanganya na kusema mambo mabaya kuwa ni mema. "Wao ni kama watu ambao huita giza nuru na nuru giza. Wao ni kama watu wanaoita vitu vichungu vitamu na vitu vitamu vichungu"

kwa wale ambao wan hekima katika macho yao

Hapa mfano wa maneno "macho" una maana ya mawazo yao. "kwa wale ambao hujichukulia kuwa na hekima"

na wenye busara katika ufahamu wao

"na kufikiri wanaelewa kila kitu"

Isaiah 5:22

ambao huachilia waovu kwa malipo

Sehemu hii inasungumzia kuhusu hukumu iliyopotoshwa katika mahakama ya sheria.

huachilia waovu

"tamka wenye hatia kutokuwa na hatia"

hunyima asiye na hatia haki zake

"usiwatende watu wasio na hatia kwa haki"

Isaiah 5:24

ulimi wa moto

"mwale wa moto" au "mwale"

kama vile ulimi wa moto unavyomeza mashina ya mabua, na kama vile nyasi kavu zinavyoshuka chini katika mwale

Misemo hii ina maana moja. Mungu ataadhibu watu wanaoelezwa katika 5:18. "kama vile moto unavyochoma mashina ya mabua na nyasi"

mashina ya mabua

"mashina ya mazao yaliyokauka". Hii ina maana ya sehemu ya mmea ambao umebaki katika shamba kufa baada ya mkulima kukusanya chakula.

mzizi wao utaoza, na maua yao yatapulizwa mbali kama vumbi

Isaya anazungumzia watu hawa kana kwamba walikuwa mmea unaokufa. "watakufa kama mmea ambao mizizi yake imeoza na ambao maua yake yamekauka na kupulizwa katika upepo"

Isaiah 5:25

hasira ya Yahwe imewashwa

Isaya anazungumzia hasira ya Yahwe kana kwamba ilikuwa moto. "Yahwe ana hasira sana"

Amenyosha nje kwa mkono wake dhidi yao na amewaadhibu

Nabii anazungumza kuhusu siku za usoni kana kwamba imekwsha tokea. Anafanya hivi kusisitiza ya kwamba unabii utatokea kwa hakika. "atawaadhibu kwa mkono wake wenye nguvu"

amenyosha nje kwa mkono wake dhidi yao

Hapa "mkono" una maana ya nguvu ya Mungu na utawala. "ameonyesha nguvu yake dhidi yao"

mizoga

"miili iliyokufa"

mizoga yao ni kama takataka katika mitaa

Miili iliyokufa inaruhusiiwa kulala chini mitaani kana kwamba ilikuwa takataka. Hii inaonyesha ya kwamba wengi watakufa lakini hakuna mtu atakayekuwepo kuwazika. Neno "takataka" linaweza kutafsiriwa kama "iliyokataliwa" au "mbolea".

Katika haya yote, hasira yake haizimiki, badala yake, mkono wake

"Ingawa vitu hivi vyote vimetokea, bado ana hasira, na mkono wake"

mkono wake bado unanyoshwa nje

Hapa "mkono" unawakilisha nguvu na utawala wa Mungu. Isaya anazungumza kana kwamba Yahwe alikuwa mtu aliyekuwa tayari kumpiga mtu mwingine kwa ngumi yake. Hii ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kuadhibu Israeli. "bado atakuwa tayari kuwaadhibu"

Isaiah 5:26

Atainua shara ya bendera kwa ajili ya mataifa ya mbali na atapiga mluzi kwa wale walio mwisho wa dunia

Isaya anasema jambo moja kwa njia mbili tofauti. Mungu kusababisha majeshi ya mataifa ambayo yapo mbali kutoka Yuda kuja na kushambulia inazungumziwa kana kwamba angeinua bendera na kupiga mluzui kuwaita kuja Yuda. "Atawaita majeshi ya mataifa ambayo yapo mbali kutoka Yuda na kuwaambia kuja"

piga mluzi

sauti ya juu ambayo mtu hufanya kwa mdomo wake kumuita mtu au mnyama ambaye yupo mbali.

watakuja

"jeshi la maadui litakuja"

kwa mbio na haraka sana

Maneno haya yana maana moja na yanasisitiza jinsi watavyokuja kwa haraka. "haraka sana"

Isaiah 5:27

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua jeshi ambalo litashambulia Yuda. Anafafanua kana kwamba tayai lilikuwepo.

huchoka ... huanguka ... husinzia ... hulala

Maneno haya manne yanaendelea kutoka kwenye kuchoka na kazi kwenda kutoweza kutembea vizuri, kwenda kutoweza kubaki macho, hadi kulala kabisa, kwa hiyo yote manne hutokea katika tafsiri.

Wala mikanda yao haijalegea

Wanajeshi waliweka nguo zao hali ya kubana ili iwe rahisi kusogea na kupigana.

mikanda ya ndara zao

"mikanda ya ndara zao"

kwato za farasi wao ni kama jiwe gumu

"kwato zao ni kama jiwe gumu". Isaya analinganisha sehemu ngumu ya mguu wa farasi kwa jiwe gumu, ambalo linaweza kusababisha cheche linapopigwa. Maana zaweza kuwa 1) Isaya analinganisha kwako zao ili kufafanua picha ya kutisha ya miguu yao kusababisha cheche wanapokimbia au 2) Isaya analinganisha kwato kwa jiwe gumu kusisitiza jinsi kwato zao ziilivyo na nguvu na zinavyomuwezesha farasi kufanya chochote bwana wake anachotaka kufanya.

na magurudumu ya vibandawazi vyao ni kama dhoruba

Isaya analinganisha matairi ya kibandawazi na dhoruba ili kuonyesha ya kwamba wataangamiza kila kitu katika njia yao. "na magurudumu ya vibandawazi yatazunguka kama dhoruba ya upepo"

magurudumu ya kibandawazi

Magurudumu haya mara kwa mara yana upapa uliochongoka ulionganishwa kwao ambao hukata mtu yeyote ambaye atapita karibu yake.

Isaiah 5:29

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua jeshi ambalo litaishambulia Yuda.

Kunguruma kwao kutakuwa kama simba, wataunguruma kama simba wachanga

Misemo hii miwili ina maana moja. Isaya analinganisha jeshi la adui kwa simba kuonyesha jinsi sauti ya shambulio lao litasababisha watu wa Yuda kuwa na hofu sana. "Pale ambapo jeshi lao linapiga kelele katika vita watakuwa kama simba anayeunguruma"

simba wachanga

Umri mdogo ni mfano wa maneno kwa ajili ya nguvu. "simba wenye nguvu"

Wataunguruma na kukamata mawindo

Isaya analinganisha adui kuwaua watu wa Yuda kwa simba kuwaua wanyama dhaifu. Maana zaweza kuwa 1) simba hutoa sauti isiyo ya juu kama ngurumo kabla hawajashambulia, au 2) mwandishi anatumia maneno mawili kumaanisha jambo moja.

mawindo

wanyama ambao wanyama wengine hutaka kuwshika na kuwala

bila mtu kuwaokoa

"na hakuna mtu atakayeweza kuwaokoa"

wataunguruma ... bahari inavyounguruma

Haya ni maneno yale yale yanayotafsiri "unguruma" katika mstari wa 29. Tumia neno ya lugha yako kwa sauti ya mawimbi katika dhoruba au mvua kubwa.

hata nuru itafanywa giza kwa mawingu

Hapa giza linawakilisha mateso na maafa. Sitiari hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "mawingu meusi yatafunika kabisa nuru kutoka kwa jua"

Isaiah 6

Isaiah 6:1

alikuwa juu na kunyanyuliwa

Maneno "juu" na "kunyanyuliwa" yanasisitiza ya kwamba kiti cha enzi kilikuwa juu sana na juu ya kila kitu kukizunguka. Urefu wa kiti cha enzi unawakilisha jinsiu Bwana alivyo mkuu na mwenye nguvu.

ulijaza hekalu

"ulijaza kasri". Neno linalotumika kwa ajili ya hekalu hapa mara kwa mara linatumika kumaanisha kasri ya wafalme.

Juu yake palikuwa na maserafi

Neno "maserafi" ni wingi wa serafi. Hii ina maana Bwana alikuwa amekaa juu ya kiti cha enzi na maserafi walikuwa wamesimama au wakipaa karibu na Bwana tayari kumtumikia.

maserafi

Neno hili linaashiria ya kwamba viumbe hawa wanaweza kuwa na muonekano wa ukali au kufanana na nyoka. Kwa sababu hatujui haswa nini "maserafi" inamaanisha, unaweza kutafsiri hili kama "viumbe wa mabawa" au "vitu vyenye uhai vyenye mabawa". Au unaweza kuazima neno na kutumia katika lugha yako.

kila mmoja wao alikuwa na mabawa sita

"kila serafi alikuwa na mabawa sita" au "kila kiumbe alikuwa na mabawa sita"

na mawili kila moja likifunika uso wake, na mawili yakifunika miguu yake, na mawili alipaa

Maneno "mabawa" na "serafi" yanaeleweka. "kwa mabawa mawili kila serafi alifunika uso wake, na kwa mabawa mawili alifunika miguu yake, na kwa mabawa mawili alipaa"

Isaiah 6:3

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuelezea maono yake.

Kila mmoja alisema kwa mwingine na kusema

"Serafi aliita kwa mwingine na kusema" au "viumbe wenye mabawa walitamka kwa mwingine"

Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, ni Yahwe wa majeshi

Kurudia neno "mtakatifu" mara tatu inaashiria Mungu ni mtakatifu kikamilifu. "Yahwe wa majeshi ni mtakatifu kuzidi kla kitu" au "Yahwe wa majeshi ni mtakatifu kabisa"

Dunia nzima imejaa utukufu wake

Hii inazungumzia dunia kana kwamba ilikuwa chombo na utukufu ulikuwa ujazo katika chombo. "Kila kitu juu ya dunia ni ushahidi wa utukufu wa Mungu"

Isaiah 6:4

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua maono yake.

Misingi ya vizingiti ilitetemeka kwa sauti ya wale waliokuwa wakilia kwa sauti

"Pale ambapo maserafi walitoa sauti, sauti zao zilitetemesha milango na misingi yao"

na nyumba ilijaa na moshi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na moshi ulijaza hekalu" au "na moshi ulijaza kasri"

Ole wangu! Maana nimeangamia

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nipo katika matatizo makubwa! Mambo mabaya yatatokea kwangu"

wenye midomo michafu

Hapa "midomo" inawakilisha kile ambacho mtu anazungumza. Na, watu kusema mambo ambayo hayakubaliki kwa Mungu inazungumziwa kana kwamba midomo yao ilikuwa michafu kimwili.

Yahwe, Yahwe wa majeshi

Yahwe, mtawala wa jeshi la malaika

macho yangu yameona

Hapa "macho" yanawakilisha mtu mzima. "Nimeona"

Isaiah 6:6

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua maono yake.

maserafi

Neno hili linadokeza ya kwamba viumbe vinaweza kuwa na muonekano wa kutisha au kufanana na nyoka. Kwa sababu hatujui haswa nini "maserafi" ina maana gani, unaweza kutafsiri haya kama "viumbe" au "vitu hai" au "kiumbe". Au unaweza kuazima neno na kutumia katika lugha yako.

koleo

chombo kinachotumika kushika au kunyakua vitu

hatia yako imeondolewa, na dhambi yako imelipiwa

Misemo hii miwili kimsingi inasema kitu kimoja. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Yahwe ameondoa hatia yako na amesamehe dhambi zako"

hatia yako imeondolewa

Yahwe kutomchukulii tena mtu kuwa na hatia inazungumziwa kana kwamba "hatia" ilikuwa kitu ambacho mtu anaweza kuondoa kutoka kwa mtu mwingine.

Isaiah 6:8

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua ono lake.

sauti ya Bwana inasema

Hapa "sauti" inawakilisha Bwana mwenyewe. "Bwana anasema"

nimtume nani

Inadokezwa ya kwamba Yahwe atamtuma mtu kuzungumza ujumbe wake kwa watu wa Israeli. "Nani nitamtuma kuwa mjumbe kwa watu wangu"

nani ataenda kwa ajili yetu

Inaonekana "yetu" ina maana ya Yahwe na washiriki wa baraza lake la mbinguni.

watu hawa

"watu wa Israeli"

Sikilizeni, lakini msielewe; tazameni, lakini msitambue

Maana zawezekana kuwa 1) vitenzi vya kuamuru "msielewe" na "mstambue" vinaeleza kile Mungu anasababisha kufanyika. "Utasikia, lakini Yahwe hatakuruhusu uelewe; utatazama kwa makini, lakini Yahwe hataruhusu uelewe" au 2) vitenzi vya kuamuru "Sikiliza" na "tazama" zinaeleza wazo la "kama". "Hata kama ukisikiliza hautaelewa; hata kama utatazama kwa makini, hautaelewa"

Sikilizeni, lakini msielewe; tazameni, lakini msitambue

Unaweza kueleza taarifa inayoeleweka kwa uwazi. "Sikiliza ujumbe wa Yahwe, lakini usielewe maana yake; tazama kile Yahwe anachofanya, lakini usigundue maana yake"

Isaiah 6:10

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kumwambia Isaya anachotakiwa kufanya pale ambapo Yahwe atamtuma kuhubiri kwa watu.

Fanya mioyo ya watu hawa kutokuhisi

Hapa "moyo" unawakilisha akili ya mtu. Mtu ambaye hafikiri kwa ufasaha na hawezi kuelewa na kujali juu ya kile kinachotokea inazungumziwa kana kwamba moyo wake hauna hisia. "Wafanye watu hawa kutoweza kuelewa" au "Fanya akili za watu hawa kufifia"

Fanya moyo wa watu hawa

Inaweza kuwa kawaida zaidi kutafsiri "moyo" na "hawa" kama wingi. "Fanya mioyo ya watu hawa"

Fanya moyo ... kutokuhisi

Amri hii ina maana ya kwamba Yahwe atatumia ujumbe wa Isaya kusababisha watu kuelewa kwa upungufu na kuwafanya kutojali kile Yahwe anachofanya.

masikio yao kufifia, na pofusha macho yao

"fanya ya kwamba wasiweza kusikia, na fanya ya kwamba wasiweze kuona". Isaya kufanya watu kutoelewa ujumbe wa Yahwe au kile anachofanya kinazungumziwa kana kwamba Isaya alikuwa akiwafanya kuwa viziwi na vipofu.

waweze kuona kwa macho yao, kusikia kwa masikio yao

Watu kuweza kuelewa ujumbe wa Yahwe na kile anachofanya inazungumziwa kana kwamba kama watu waliweza kuona na kusikia kimwili.

kuelewa kwa moyo wao

Hapa "moyo" unawakilisha akili ya mtu. Kuelewa kwa ukweli jambo na kujali juu ya kile kinachoendelea inazungumziwa kana kwamba watu walipaswa kuelewa kwa mioyo yao.

kisha kugeuka

Kutubu na kuanza kumtii Yahwe inazungumzwa kana kwamba watu waligeuka kwa Mungu kimwili. "mnifuate tena" au "kisha muanze kuniamini tena"

kuponywa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Ningewaponya"

Isaiah 6:11

Mpaka miji ianguke katika uharibifu na iwe bila wakazi, na nyumba iwe bila watu

"Mpaka miji yote na nyumba ziharibike na hakuna mtu anayeishi pale"

nchi huanguka katika takataka ya ukiwa

Hapa "huanguka katika" ni lahaja ambayo ina maana ya kuwa kitu kibaya zaidi. "nchi inakuwa takataka ya upweke"

Mpaka Yahwe awaondoe watu mbali, na upweke wa nchi ni mkubwa

Hapa Yahwe anazungumza kuhusu yeye mwenyewe katika mtu wa utatu. "Hadi mimi, Yahwe, nimewatuma watu wote mbali kabisa mwa nchi yao, ili kwamba hakuna mtu anayebaki"

Isaiah 6:13

itaangamizwa tena

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "majeshi yataangamiza nchi ya Israeli tena"

kama mvinje na mwaloni inapokatwa na mashina kubaki, mbegu takatifu ipo katika kisiki chake

Tashbihi hii ina maana ya kwamba hata baada ya Yahwe kuangamiza Israeli, atawatenga kando watu kutoka miongoni mwa Waisraeli kumtumikia.

mvinye

aina ya mti wa mwaloni

shina ... kisiki

Shina ni shina nene la mti. Kisiki ni sehemu ya mti ambayo inasalia kwenye ardhi baada ya mti kukatwa chini.

mbegu takatifu

Watu ambao watamtumikia Yahwe baada ya majeshi kuangamiza Israeli inazungumziwa kana kwamba walitengwa kando kama mbegu takatifu.

Isaiah 7

Isaiah 7:1

Katika siku za Ahazi ... mfalme wa Yuda

"Pale Ahazi... alipokuwa mfalme wa Yuda" Huu ulikuwa wakati matukio yalitokea.

Resini ... Peka ... Remalia

majina ya wanaume.

Resini ... na Peka ... alikwenda juu

Mwandishi anazungumza kana kwamba wafalme walikuwa majeshi walioyaongoza. "Resini ... na Peka ... waliongoza majeshi yao juu"

kufanya vita dhidi yake

Mwandishi anazungumza kana kwamba mji wenyewe ulikuwa watu ambao huishi ndani yake. "kupiga vita dhidi ya watu wa Yerusalemu"

Ikasemekana katika nyumba ya Daudi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nyumba ya Daudi ikasikia taarifa" au "mtu alitoa taarifa kwa nyumba ya Daudi"

nyumba ya Daudi

Neno "nyumba" ni mfano wa maneno kwa ajili ya familia inayoishi katika nyumba. "Mfalme Ahazi na washauri wake"

ya kwamba Aramu alishirikiana na Efraimu

Hapa "Aramu" na "Efraimu" wanatambua wafalme wao. Efraimu anatumiwa hapa kumaanisha ufalme mzima wa kaskazini wa Israeli. "ya kwamba Resini, mfalme wa Aramu alikuwa akimsaidia Peka, mfalme wa Israeli"

Moyo wake ulitetemeka, na moyo wa watu wake, kama miti ya msituni inavyotetemeka katika upepo

Kutetemeka kwa mioyo yao katika habari hii inalinganishwa na namna miti hutikisika pale upepo unapovuma katikati yao. "Ahazi na watu wake waliogopa sana"

Isaiah 7:3

Maelezo ya Jumla

Isaya anaandika juu ya kile kilichotokea kwake kana kwamba kilitokea kwa mtu mwingine.

Shear-yashubu

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi kwa chini ambayo yanasema, "Jina la Shear-yashubu ina maana ya 'waliobakia watarudi'". Maana inaweza kuwa imempatia matumaini Ahazi.

katika mwisho wa mfereji wa dimbwi la juu

"ambapo maji huingia katika dimbwi la juu"

mfereji

mtaro wa kutengenezwa na mtu au chini mwa chini mwa mlima ambmo maji hutiririka

barabara

barabara laini kama la lami.

shamba la dobi

Maana zaweza kuwa 1) hii ni jina la kufaa ambalo watu waliita shamba au 2) hii ni nomino ya kawaida ambayo watu walitumia kuongea juu y shamba, "shamba la dobi" au "shamba ambapo watu huosha sufu"

shamba la dobi

Dobi huwa ni 1) mwanamume ambaye hufua sufu ambayo mtu kanyoa katika kondoo, "Shamba la Mfuaji wa Sufu" au 2) mwanamke ambaye hufua nguo chafu, "Shamba la Mfuaji wa Nguo"

Mwambie

"Mwambie Ahazi"

usiogope au kutishwa kwa mikia ya moto miwili ya kichiniichini, kwa hasira kali ya Resini na Aram, na ya Peka mwana wa Remalia

Mungu analinganisha Resini na Peka kwa njiti zinazowaka ambao moto wake umezimika na kufanya moshi. Mungu anasisitiza ya kwamba sio vitisho vya kweli. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "usimruhusu Resini na Peka kukutisha; hasira yao katili ni kama kijiti kiwakacho ambacho moto wake umezimika na kuna moshi pekee"

usiogope au kutishwa

Maneno "ogopa" na "tishwa" yana moja na yanaweza kutafsiriwa kama neno moja.

Isaiah 7:5

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kumwambia Isaya kile anachotakiwa kumwambia Ahazi.

Aramu, Efraimu, na mwana wa Remalia

Maneno "Aram" na "Efraimu" yana maana ya wafalme wa nchi hizi. Pia, "Efraimu" ina maana ya ufalme wa kaskazini wa Israeli. "Resini mfalme wa Aramu na Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli"

Remalia

Hili ni jina la mwanamume.

wamepanga uovu dhidi yako

Hapa "yako" ni umoja na ina maana ya Ahazi.

mwana wa Tabeeli

Haijulikani mwanamume huyu ni nani.

Isaiah 7:7

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kumwambia Isaya kile anachotakiwa kumwambia Ahazi.

na mkuu wa Dameski ni Resini

"na mfalme wa Dameski ni Resini, ambaye ni mtu dhaifu"

miaka sitini na tano

miaka mitano "miaka 65"

Efraimu atavunjwavunjwa na hatakuwa kundi la watu tena

Hapa "Efraimu" ina maana wote wa ufalme wa kaskazini wa Israeli. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "jeshi litaangamiza Efraimu, na hapatakuwa tena na watu wa Israeli"

mkuu wa Samaria ni mwana wa Remalia

Hii ina maana Peka ni mfalme wa Samaria na Israeli yote. "mfalme wa Samaria ni Peka, ambaye n mwanamume dhaifu"

kama hautabaki imara katika imani, hakika hautabaki salama

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Ukiendelea kuamini ndani yangu, hakika utabaki salama"

kama hautabaki

"hadi ubaki"

Isaiah 7:10

iombe kwa kina au katika maref ya juu

Yahwe anatumia neno "kina" na "urefu" kumaanisha Ahazi anaweza kumuuliza jambo lolote.

kina ... marefu

Nomino dhahania "kina" na "urefu" inaweza kutafsiriwa kwa vihusishi. "sehemu mbali chini yako ... sehemu mbali juu yako"

sitaiomba

"sitamuomba Yahwe kwa ajili ya ishara"

Isaiah 7:13

nyumba ya Daudi

Neno "nyumba" ni mfano wa maneno kwa ajili ya familia nayoishi katika nyumba. "Mfalme Ahaz, wewe na washauri wako"

Je! haitoshi kwenu watu kujaribu uvumilivu wa watu? Je! ni lazima mjaribu uvumilivu wa Mungu wangu?

Maswali haya yanasisitza ya kwamba mflme ametenda dhambi sana. "Unajaribu uvumilivu wa watu! Sasa unajaribu uvumilivu wa Mungu wangu!"

mwanamke kijana atapata mimba

Baadhi ya tafsiri za zamani na tafsiri za kisasa hutafsiri, "bikira atapata mimba", huku zingine "mwanamke kijana atapata mimba"

jina lake Imanueli

Watafsiiri wanaweza kuongeza maandishi ambayo yanasema: "Jina Imanueli lina maana 'Mungu pamoja nasi'".

Atakula magandi na asali anapojua kukataa uovu na kuchagua mema

Maana zaweza kuwa 1) "Hadi kufikia muda huyo mtoto amekua vya kutosha kula magandi na asali, ataweza kukataa kilicho kiovu na kuchagua kilicho chema." Hii inasisitiza ya kwamba mtoto atakuwa mdogo sana atakapojua kuchagua kipi ni sahihi badala ya kibaya au 2) "Hadi kufikia muda mtoto amekua vya kutosha kukataa kilicho kiovu na kuchagua kilicho chema, atakuwa anakula magandi na asali". Watu wa Yuda walichukulia mtoto kuwajibika kwa kufanya mema aliipokuwa na umri wa miaka 12. Hii inasisitiza ya kwamba ndani ya miaka kumi na mbili watu wataweza kula magandi na asali kwa sababu watu wengi zaidi wa Israeli watauliwa au kuchukuliwa kama mateka.

magandi

maziwa ambayo watu wameyatengeneza kutengeneza kuwa ugumu laini

kukataa uovu na kuchagua mema

"kataa kufanya matendo maovu na chagua kufanya mambo mema"

Isaiah 7:16

Maelezo ya Jumla

Hii ina maana ya watu wa Yuda

kukataa uovu na kuchagua mema

"kataa kufanya matendo maovu na kuchagua kufanya mambo mema".

unaowahofia

"unaogopa". Hapa "unaowahofia" ni umoja na ina maana ya Ahazi.

watu wako

Hii ina maana ya watu wa Yuda.

Efraimu alijitoa kutoka kwa Yuda

"watu wa Efraimu kugawanya kutoka kwa watu wa Yuda"

Isaiah 7:18

Kwa kipindi hicho

kabla mtoto kujua kukataa uovu na kuchagua mema

Yahwe atapiga mluzi kwa

"Yahwe atawaita" au "Yahwe atawaita mahakamani"

kwa ajili ya inzi aliyeko katika vijito vya mbali vya Misri, na kwa ajilii ya nyuk kutoka nchi ya Ashuru

"kwa maana majeshi ya Misri na Ashuru, na wanajeshi wao yatakuwa kila sehemu kama inzi na nyuki"

Isaiah 7:20

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua kipindi ambacho jeshi la Ashuru litavamia Israeli.

Bwana atanyoa kwa wembe ambao ulikodiwa upande wa pili wa Mto Frati - mfalme wa Ashuru

Neno "wembe" ni sitiari kwa ajili ya mfalme wa Ashuru na jeshi lake, na Yahwe anazungumzia mfalme kana kwamba mfalme alikuwa mwanamume ambaye angefanya kazi ya Yahwe na kisha kupokea fedha kutoka kwa Yahwe. "Bwana atamuita mfalme wa Ashuru kutoka ng'ambo ya Mto Frati kufanya kazi kwa ajili yake kukunyoa"

ambao ulikodiwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambao alinunua"

kichwa ... nywele za miguuni ... pia ... ndevu

Ilikuwa vibaya kwa mtu kunyoa sehemu ya juu ya kichwa chake; ilikuwa vibaya zaidi kwa mtu kunyoa "nywele za miguu"; ilikuwa vibaya kuliko zote kwa mtu kunyoa ndevu.

kichwa ... nywele za miguuni ... ndevu

Isaya hasemi ni kichwa cha nani, nywele, na ndevu ambazo Bwana anakwenda kunyoa, lakini Ahazi na msomaji wataelewa ya kwamba huyu ni mwanamume; mwanamume ni sitiari kwa ajili ya watu wanaoishi katika nchi ya Yuda.

kichwa

"nywele katika kichwa"

nywele za miguuni

Maana zaweza kuwa 1) hii ni njia ya upole kuzungumza juu ya nywele katika sehemu ya chini ya mwili au 2) hii inazungumzia nywele katika miguu.

pia itafyeka

"wembe utafyeka pia". Iwapo lugha yako inahitaji mtu kuwa mhusika wa "atafyeka", unaweza kusema, "Bwana pia atafyeka".

kwa sababu y wingi wa maziwa ambayo watayatoa

Nomino dhahania "wingi" unaweza kutafsiriwa kama kishazi. "kwa sababu watatoa maziwa mengi sana"

Isaiah 7:23

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua kipindi ambacho jeshi kutoka Ashuru litashambulia nchi ya Israeli.

palipokuwa na mizabibu elfu moja ... mibigili na miiba

"kulikuwa na mizabibu 1,000". Yaani, Isaya alipoandika, kulikuwa na mashamba ya mizabibu, ambazo baadhi yao kulikuwa na mizabibu 1,000 au zaidi. Anasema ya kwamba mashamba haya ya mizabibu yatajaa mibigili na miiba"

shekeli elfu moja za fedha

"shekeli 1,000 za fedha". Shekeli ni sarafu ya fedha yenye thamani ya mshahara wa siku 4. "sarafu 1,000 za fedha"

mibigili na miibaa

Maneno "mibigili" na "miiba" yote ina maana ya kutokuwa na thamani, mimea ya miiba. "vichaka vya miiba" au "vichaka vya mibigili"

kwa sababu nchi yote itakuwa mibigili na miiba

Kwa nini wawindaji watakuja katika nchi hizi inaweza kuwekwa wazi. "kwa sababu hakutakuwa na kitu katika nchi hizi ila mibigili, miiba, na wanyama pori"

Watakaa mbali na vilima vyote ambavyo vililimwa kwa jembe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu watakaa mbali na vilima ambamo hapo awali ziliandaa udongo kupanda mazao"

Isaiah 8

Isaiah 8:1

Yahwe alisema kwangu

Hapa neno "kwangu" ina maana ya Isaya.

Nitawaita kortini mashahidi waaminifu kushuhudia kwa ajili yangu

Maana zaweza kuwa 1) Yahwe anazungumza "Nitawaita watu waaminifu kuwa mashahidi" au 2) Isaya anazungumza: "Niliwaita wanamume waaminifu kuwa mashahidi" au 3) Yahwe anamuamuru Isaya: "Waite wanamume waaminifu kuwa mashahidi"

Isaiah 8:3

Nilikwenda kwa nabii wa kike

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba Isaya alimuoa nabii wa kike. "Nililala na mke wangu, nabii wa kike"

utajiri wa Dameski na nyara za Samaria zitachukuliwa na mfalme wa Ashuru

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "mfalme wa Ashuru atabeba hazina zote za Dameski na Samaria"

Isaiah 8:5

Kwa sababu watu hawa wamekataa maji ya pole pole ya Shiloa

Maneno "maji ya pole pole" ni sitiari kwa ajili ya sheria ya Mungu. "Kwa sababu watu hawa wamekataa sheria ya Yahwe, ambayo ni kama maji ya pole pole ya Shiloa"

watu hawa

"kundi hili la watu". "watu hawa wamekataa ... wana furaha"

na wana furaha juu Resini na mwana wa Remalia

Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "na wana furaha ya kwamba majeshi ya AShuru yameshinda Resini, mfalme wa Aramu, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli.

kwa hiyo Bwana

Yahwe anazungumza juu yake kana kwmba alikuwa mtu mwingine kuwakumbusha watu yeye ni nani. "kwa hiyo, Mimi, Bwana, ni"

kuleta juu yao

Kitenzi ni "kuleta juu"; kielezi ni "juu yao".

juu yao

"ju ya watu wa Yuda"

maji ya Mto, yenye nguvu na mengi, mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote

Mto unaashiria jeshi la Ashuru. "jeshi kutoka Ashuru, ambalo lina nguvu kama mto wenye nguvu"

Mto

Mto Frati katika Ashuru

Isaiah 8:8

Maelezo ya Jumla

Bwana anaendelea kufafanua jeshi la Ashuru kama mto ambao utafurika Yuda.

Mto utafagia mbele mpaka Yuda, kufurika na kupitiliza mbele, hadi ufike shingoni mwako

Jeshi la Ashuru ni kama maji yafurikayo. "Wanajeshi zaidi na zaidi watakuja kama mto unaopanda juu ya shingo yako"

Mto

Mto Frati katika Ashuru. Huu ni mfano wa maneno kwa ajili ya wanajeshi wa Ashuru, ambao watakuja kutoka katika nyumba zao kwa Mto Frati.

mabawa yake yaliyonywoshwa yatajaza

Maana zaweza kuwa 1) kama "Mto" kwa sitiari kuinua, "mabawa" yake kutiririka juu na kufunika kile kilichokuwa nchi kavu au 2) Isaya anabadili sitiari na sasa anazungumza juu ya Yahwe kama ndege anayelinda nchii, "Lakini mabawa yake yaliyonywoshwa yatafunika"

Imanueli

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi yanayosema: "Jina Imanueli lina maana ya 'Mungu pamoja nasi'"

Isaiah 8:9

Watu wako watavunjwa vipande vipande

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nitavunja majeshi yako vipande vipande"

Sikiliza, nyie nchi za mbali

Isaya anazungumza kana kwamba watu katika nchi zingine wanaweza kumsikiliza. "Sikiliza, nyie watu wote mlio sehemu za mbali"

jiwekeni tayari kwa ajili ya vita na mvunjike vipande vipande; jiwekeni tayari na mvunjike vipande vipande

Hii ina maana ya jambo moja, inatajwa mara mbili kwa msisitizo. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "unaweza kujiandaa kwa ajili ya vita, lakini nitakushinda"

Unda mpango, lakini hautatekelezwa; toa amri, lakini haitatekelezwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Unaweza kujiandaa kushambulia Yuda, lakini hautafanikiwa"

haitatekelezwa ... haitatekelezwa

"Kutekeleza" mpango au amri ni kufanya kile ambacho mtu aliyefanya mpango au amr anataka msikilizaji afanye. Vishazi hivi vinaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "hautaweza kufanya kile unachopanga kufanya ... wanajeshi wako hawataweza kufanya kile makamanda wao wanawaambia kufanya"

Isaiah 8:11

Yahwe alizungumza kwangu, kwa mkono wake wa nguvu juu yangu

"Yahwe alizungumza kwangu kwa njia ya nguvu sana"

na kunionya nisitembee katika njia ya watu hawa

Hii ni nukuu isiyo moja kwa moja ambayo huisha katika 8:17. "na kunionya na kusema, 'Usitende kama watu hawa'"

Usiite njama kitu chochote ambacho watu hawa wanaitwa njama

Watu wanawaza kuna njama, na inawafanya wawe na wasiwasi. "Usiwe na wasiwasi kama watu ambao wanadhani mtu anajaribu kuwadhuru muda wote"

Ni Yahwe wa majeshi ambaye utamheshimu kama mtakatifu; yeye ndiye unayepaswa kumuogopa, na yeye ndiye unapaswa kumhofia

Kama utatafsiri hii kama nukuu ya moja kwa moja, pia unaweza kutafsiri na Yahwe kuzungumza katika mtu wa kwanza. "Lakini utanifikiria, Yahwe wa majeshi, kama mtakatifu. Na utaniogopa na kuwa na hofu kwangu"

Isaiah 8:14

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendeleza nukuu isiyo moja kwa moja ya Yahwe ambayo ilianza katika 8:11. Inaweza kutafsiriwa kama nukuu ya moja kwa moja na Yahwe akizungumza katika mtu wa kwanza.

Atakuwa mahali patakatifu

Neno "mahali patakatifu" ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kuwaweka watu wake salama na kuwalinda. "Atawalinda watakapokwenda kwake"

atakuwa jiwe la kupiga, na mwamba wa kujikwaa

Maneno "jiwe la kupiga" na "mwamba wa kujikwaa" yote ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kudhuru watu wake. Baadhi wanatafsiri "kupiga" na "kujikwaa" kama "kujikwaa" na "kuanguka"; wengine wanatafsiri kama "kosa" na "kujikwaa". "atawadhuru watu wake, kama mwamba ambao watu hupiga miguu yao na kujikwaa, na kama mwamba ambao husababisha watu kuanguka"

atakuwa mtego na kikwazo kwa watu wa Yerusalemu

Maneno "mtego" na "kikwazo" ina maana karibu na kitu kimoja na inasisitiza ya kwamba pale ambapo Yahwe ataamua kuadhibu watu wa Yerusalemu hawataweza kutoroka. "atawatega watu wa Yerusalemu ili wasiweze kumtoroka"

mtego

chombo ambacho hukamata ndege katika wavu au kikapu

kikwazo

mtego ambao hukamata na kushika mguu wa mnyama au pua

Wengi watajikwaa juu yake na kuanguka na kuvunjika, na kutegwa na kukamatwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wengi watajikwaa ju ya jiwe, na watakapoanguka hawatainuka. Na watu wengi watakanyaga katika mtego, na hawataweza kutoka"

kutegwa na kukamatwa

Maneno haya mawili yana maana moja na yanasisitiza ya kwamba watashikwa katika mtego.

Isaiah 8:16

Ufunge ushuhuda wangu, wekea muhuri kumbukumbu halali

Misemo hii miwili ina maana moja. "Funga kwa nguvu hati ya kukunja kwa ujumbe huu ulioandikwa juu yake"

ushuhuda wangu ... wanafunzi wangu

Haipo wazi ni kwa nani neno "wangu" ina maanisha nini. Inaweza kuwa Isaya au Yahwe. Ni vyema kuacha kiwakilishi kuwa na maana nyingi.

Nitamsubiri Yahwe

Hapa "nitamsubiri" ina maana ya Isaya.

ambaye huficha uso wake kutoka katika nyumba ya Yakobo

"uso" wa Yahwe ni mfano wa maneno kwa ajili ya baraka au fadhila yake. "ambaye amechukua baraka yake kutoka katika nyumba ya Yakobo" au "ambaye hatazami kwa fadhila tena juu ya nyumba ya Yakobo"

nyumba ya Yakobo

watu wa Israeli

Mimi na wana ambao Yahwe amenipatia ni kwa ajili ya ishara na maajabu katika Israeli

"Mimi na wana ambao Yahwe amenipatia ni kama isihara kuwaonya watu wa Israeli". Wana ni Shear-yashubu na Maher-shalal-hash-bazi, ambao majina yao ni ujumbe kwa watu wa Israeli.

Isaiah 8:19

Maelezo ya Jumla

Isaya anazungumza

Watasema kwako, "Shauriana na watu wanaowasiliana na mizimu na wachawi", wale ambao hulia na nung'unika dua. Lakini watu wasitafute ushauri kwa Mungu wao? Je! watafute ushauri kwa wafu kwa niaba ya walio hai? Kwa sheria na kwa ushuhuda!

Maana zingine zaweza kuwa 1) "Watasema kwako, 'Watashauriana na wanaowasiliana na mizimu na wachawi, wale ambao hulia na ung'unika dua. Lakini watu wasitafute ushauri kwa Mungu wao? Je! watafute ushauri kwa wafu kwa niaba ya walio hai? Kwa sheria na kwa ushuhuda!'" au 2) "Watakaposema kwako, 'Watashauriana na wanaowasiliana na mizimu na wachawi, wale ambao hulia na ung'unika dua. Lakini watu wasitafute ushauri kwa Mungu wao? Je! watafute ushauri kwa wafu kwa niaba ya walio hai? Kwa sheria na kwa ushuhuda!

Watasema kwako

Neno "watasema" lina maana ya wale ambao humtumaini Yahwe. Neno "kwako" ni wingi na lina maana ya wale ambao wanamtumaini Yahwe.

Shauriana na watu wanaowasiliana na mizimu na wachawi

"Waulize wanaowasiliana na mizimu na wachawi unachpaswa kufanywa"

wanaowasiliana na mizimu na wachawi

wale ambao hudai kuzungumza na wale ambao wameshakufa

wale ambao hulia na nung'unika dua

Maneno "hulia" na "nung'unika" yana maana ya sauti ambazo wanaowasiliana na mizimu na wachawi hufanya wanapojaribu kuzungumza na wafu. "wale ambao hunong'oneza na kunung'una maneno yao ya kichawi kujaribu kuzungumza na watu waliokufa"

hulia

kufanya sauti kama ya ndege

Lakini watu wasitafute ushauri kwa Mungu wao? Je! watafute ushauri kwa wafu kwa niaba ya walio hai?

Maswali haya yanaonyesha ya kwamba watu wanaweza kushauriana na Mungu badala ya matendo yao ya kipumbavu ya kujaribu kuzungumza na watu waliokufa. "Lakini watu wanapaswa kumuuliza Yahwe kuwaongoza. Hawapaswi kutafuta majibu kutoka kwa wale waliokufa"

Kwa sheria na kwa ushuhuda!

Maana zaweza kuwa 1) "Kuwa makini na maelekezo ya Mungu na mafunzo" au 2) "Kisha unatakiwa kukumbuka mafundisho na ushuhuda niliokupatia"

sheria

Hili ni neno hilo hilo lililotafsiriwa "kumbukumbu halali" katika 8:16

ushuhuda

Inaweza kuwa Isaya au Yahwe. Ni vyema kuacha kiwakilishi kuwa na maana nyingi.

Iwapo hawatasema vitu hivi

"Kama hawatazungumza juu ya sheria na ushuhuda"

ni kwa sababu hawana nuru ya alfajiri

Isaya anazungumzia watu ambao hawamjui Mungu kana kwamba walikuwa watu wanaotembea katika giza bila mwanga wowote. "ni kwa sababu wao ni kama mtu aliyepotea gizani"

Isaiah 8:21

utusitusi wa kukandamiza

"huzuni mbaya"

Wataendeshwa katika nchi ya giza

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawaondoa nje katika giza kamili"

Isaiah 9

Isaiah 9:1

Huzuni itaondolewa kutoka kwake ambaye alikuwa katika maumivu makali

Isaya anazungumzia watu ambao wamepotea kiroho kana kwamba walikuwa wakitembea katika giza tupu. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe ataondoa giza kutoka kwake aliyekuwa katika maumivu makali"

Huzuni

Neno hili lina maana ya "giza kidogo au giza tupu".

kwake ambaye alikuwa katika maumivu makali

"yeye ambaye alikuwa akiteseka maumivu makali na huzuni". Huenda hii ni sitiari kwa ajili ya watu wa Yuda

Katika kipindi cha awali aliabisha nchi ya Zabulonii na nchi ya Naftali

"Nchi" ina maana ya watu ambao wanaishi katika eneo. "Kipindi cha nyuma, Bwana aliwashusha waleabuloni na Naftali"

lakini katika kipindi cha baadaye ataifanya iwe tukufu, njia ya baharini, mbele ya Yordani, Galilaya ya mataifa

Hapa "ataifanya" ina maana ya Galilaya ambayo inawakilisha watu wanaoishi kule. "lakini katika siku za usoni, Bwana ataheshimu watu wa Galilaya wa mataifa, ambayo ipo katika barabara kati ya Bahari ya Mediteranea na Mto Yordani"

Galilaya ya mataifa

Hapa "mataifa" yanawakilisha watu kutoka mataifa mengine ambao wanaishi Galilaya. "Galilaya, ambapo wageni wengi huishi"

waliotembea gizani ... walioishi katiika nchi ya kivuli cha kifo

isaya anazungumzia watu kuishi maisha ya dhambi na mateso kwa sababu yake kana kwamba walikuwa wakitembea katika nchi ya giza na yenye kivuli cha kifo.

mwanga mkubwa ... mwanga umewaka

Hapa "mwanga" unawakilisha matumaini na ukombozi.

nchi ya kivuli cha kifo

Msemo "kivuli cha kifo" ni lahaja ambayo ina maana ya giza nene. "nchi yenye giza zito"

Isaiah 9:3

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuelezea kipindi ambapo Mungu atawaokoa watu wa Israeli. Ingawa matukio haya yatatokea katika siku za usoni (9:1), Isaya anayafafanua kana kwamba yamekwisha tokea. Hii inasisitiza ya kwamba yatatokea hakika.

Umezidisha taifa; umeongeza furaha yao

Neno "umezidisha" ina maana ya Yahwe. Neno "yao" ina maana ya watu wa Israeli, lakini Iisaya anajijumlisha kama sehemu ya Israeli. "Bwana, utaongeza sana watu wetu na furaha yetu"

Wanafurahi mbele yako kama furaha ya kipindi cha mavunno, kama wanamume wanavyofurahi wanapogawana nyara zao

"Watafurahi mbele yako kama watu wanavyofurahi wanapokusanya mazao yao au pale vita inakamilika na wanajeshi kugawanya kiile walichochukua"

Isaiah 9:4

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua kipindi ambacho Mungu ataokoa watu wa Israeli. Ingawa matukio haya yatatokea katika kipindi cha usoni. Isaya anayafafanua kana kwamba yalikuwa yametokea tayari. Hii inasisitiza ya kwamba hakika itatokea.

Kwa maana nira ya mzigo wake ... umeharibika kabisa kama katika siku ya Midiani

Isaya anazungumzia Waisraeli, ambao ni watumwa wa Ashuru, kana kwamba walikuwa ng'ombe anayevaa nira. Hii itatokea katika siku za usoni, lakini anazungumza kana kwamba tayari imetokea tayari. "Kwa maana kama katika siku ya Midiani utawaweka watu wa Israeli huru katika utumwa kwa wakandamizaji wao kama mtu anavyotoa nira kutoka mabegani mwa mnyama"

Kwa maana nira ya mzigo wake .... bega lake ... mkandamizaji wake

Isaya anazungumzia watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja. "Kwa maana nira ya mzigo wao ... mabegani mwao ... wakandamizaji wao"

mhimili katika bega lake

Mhimili ni sehemu ya nira ambayo huenda juu ya mabega ya ng'ombe

mhimili

Maana nyingine yaweza kuwa "gongo", kipande kirefu cha mbao ambacho mtu hutumia kupiga ng'ombe ili wafanye kazi na ishara ya nguvu ya mtu kutawala watu wengine.

kiboko cha mkandamizaji wake

Isaya anazungumzia nguvu ya mkandamizaji ambayo anayo juu ya watu wa Yuda kana kwamba kilikuwa kipande cha mbao kilichotumiwa kupiga ng'ombe ili aweze kufanya kazi.

kama katika siku ya Midiani

Neno "siku" ni lahaja ambayo inaweza kumanisha tukio ambalo linachukua zaidi ya siiku moja kufanyika. "kama pale mlipowashinda Wamidiani"

kila buti inayokanyaga katika ghasia na mavazi yaliyobiringishwa katika damu yatachomwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "utachoma buti za wanajeshi na nguo zao, ambazo zimefunikwa na damu"

yatachomwa, mafuta kwa ajili ya moto

Hii inaweza kuwekwa wazi kwa kutafsiri kama sentensi mpya. "kuchomwa. Utafanya buti na mavazi mafuta kwa ajili ya moto"

Isaiah 9:6

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua kipindi ambapo Mungu atawaokoa watu wa Israeli (9:1). Ingawa matukiio haya yatatokea katika siku za usoni za Isaya, anaelezea kana kwamba yamekwisha tokea. Hii inasisitiza ya kwamba hakika vitatokea.

Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, kwetu mwana ametolewa

Misemo hii miwili ina maana moja. Neno "yetu" ina maana ya wote msemaji na mskilizaj na kwa hiyo ziko pamoja. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kwa maana Bwana atatoa kwetu mtoto"

utawala utakuwa juu ya bega lake

"atakuwa na mamlaka ya kutawala kama mfalme" au "Yahwe atamfanya awe na wajibu wa kutawala"

Mshauri

yule ambaye anashauri wafalme

Katika ongezeko la ufalme wake na wa amani hatukauwa na mwisho

"Kadri muda unavyopita atatawala juu ya watu zaidi na zaidi na kuwawezesha kuishi kwa amani zaidi na zaidi"

anapotawala katika kiti cha enzi cha Daudi

Kukaa katika "kiti cha enzi cha Daudi" ni mfano wa maneno ya kuwa na haki ya kutawala; uzao wa Daudi pekee unweza kuwa mfalme juu ya Israeli. "ana haki ya kutawala kama uzao wa Daudi"

ufalme wake, kuuimarisha na kuuhimili kwa haki na kwa haki

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "ufalme wake". Ataimarisha na kulinda ufalme wake, na atafanya kilicho haki"

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi wa Israeli

Isaiah 9:8

Bwana alituma neno dhidi ya Yakobo, nalo likaanguka juu ya Israeli

"Tuma neno" ina maana ya kuzungumza. "Bwana amezungumza dhidi ya watu wa Israeli"

Yakobo ... Israeli ... Efraimu ... Samaria

Majina haya yana maana ya watu wa ufalme wa kaskazini wa Israeli.

Watu wote watajua, hata Efraimu na wakazi wa Samaria

Kile watakachojua kinaweza kuwekwa wazi. "Watu wote watajua ya kwamba Bwana amewahukumu wao, hata wale wa Efraimu na Samaria"

Matofali yameanguka, lakini tutaijenga tena kwa mawe ya kuchonga; mkuyu umekatwa chini, lakin tutaweka mkangazi katika nafasi yao

Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Tutarudishia mahali pake matofali ya kawaida ya miji yetu iliyoangamizwa kwa mawe ya gharama ya kuchongwa, na tutapanda miti mikubwa ya mikangazi ambapo miti ya kawaida ya mkuyu iliota"

Isaiah 9:11

Kwa hiyo Yahwe atamuinua dhidi yake Resini, mshindani wake

Hapa "Resini" inawakilisha jeshi lake. "Kwa hiyo, Yahwe atamleta Resini na jeshi lake dhidi ya watu wa Israeli"

Resini

Hili ni jina la mwanamume.

na atawatikisa maadui zake

Msemo "tikisa" ni lahaja ambayo ina maana ya kuwachochea kushambulia. "na Yahwe atasababisha adui wa Israeli kushambulia"

Watameza Israeli kwa mdomo wazi

"Kumeza" ni jinsi ambavyo wanyama pori hula mawindo. "Kama mnyama mwitu anavyokula mawindo yake, jeshi la adui litaangamiza watu wa Israeli"

Katika vitu hivi vyote, hasira yake haipungui; badala yake, mkono wake

"Hata kama vitu hivi vyote vimetokea, bado ana hasira, na mkono wake"

mkono wake bado unanyoshwa nje

Isaya anazungumza kana kwamba Yahwe alikuwa mtu ambaye anataka kumpiga mtu mwingine kwa ngumi yake. Hii ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kuadhibu Israeli. "atakuwa tayari kuwaadhibu"

Isaiah 9:13

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli.

kichwa mpaka mkia

Isaya anafafanua sitiari hii katika mstari wa 15. "Kichwa", sehemu ya mnyama ambayo mtu angetaka kuwa, ni "kiongozi na mtu mwadilifu", na "mkia" sehemu chafu ya mnyama, ni "nabii anayefundisha uongo"

tawi la mnazi na matete

"Tawi la mnazi" huota juu ya mti na sitiari kwa ajili ya watu ambao ni muhimu na hutawala wengine. "Tete" huota katika maji ya kina kifupi na sitiari kwa ajili ya watu ambao ni maskini na hawana umuhimu na hutawaliwa na wengine.

Isaiah 9:16

Wale ambao wanaongoza watu hawa wanawapotosha

Viongozii kusababisha watu kutotii inazungumziwa kana kwamba viongozi waliwaongoza katika njia isiyo sahihi. "Viongozi wa Israeli wamesababisha watu kutomtii Mungu"

na wale ambao wanaongozwa wanamezwa

Hii ni sitiari ambayo inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. Maana zaweza kuwa 1) "na wale ambao wanaongozwa wanachanganyikiwa" au 2) "na Yahwe huangamiza wale ambao wanaongoza"

kila kinywa kinazungumza vitu vya kipumbavu

Neno "kinywa" lina maana ya mtu. "kila mtu huzungumza vitu vya kipumbavu"

Katika vitu hivi vyote, hasira yake haipungui; badala yake, mkono wake

"Ingawa vitu hivi vyote vimetokea, bado ana hasira, na mkono wake"

mkono wake bado unanyoshwa nje

Isaya anazungumza kana kwamba Yahwe alikuwa mtu ambaye anataka kumpiga mtu mwingine kwa ngumi yake. Hii ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kuwaadhibu Israeli. "bado atakuwa tayari kuwaadhibu"

Isaiah 9:18

Uovu unawaka kama moto; unameza mibigili na miiba; pia unawasha vichaka vya msitu

Matendo ya uovu ya watu yanazungumziwa kana kwamba yalikuwa moto mharibifu kabisa. Moto huu huchoma hata mibigili na miiba, mimea ambayo huota katika maeneo ambayo hawaishi tena, na "vichaka vya msituni" ambapo hakuna mtu aliyewahi kuishi, kwa sababu ulikuwa umeangamiza maeneo ambapo watu walikuwa wakiishi.

mibigili ... miiba

Maneno "mibigili" na "miiba" yote ina maana mimea ya miiba isiyo na thamani; inaweza kutafsiriwa kutumia neno moja. "vichaka vya miiba"

Katika ghadhabu ya Yahwe wa majeshi nchi inachomwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kama moto ambao unachoma nchi, hasira kali ya Bwana itaangamiza watu wa Israeli"

Hakuna mtu amwachaye ndugu yake

"Hakuna mtu afanyaye kitu chochote kusaidia mtu mwingine yeyote kutoroka"

Isaiah 9:20

Watanyakua chakula katika mkono wa kuume ... katika mkono wa kushoto

Msemo huu una maana ya kwamba watu watanyakua chakula popote watakapokikuta.

Kila mmoja hata atakula nyama ya mkono wake mwenyewe

Maana zaweza kuwa 1) watu watakuwa na njaa sana hadi watataka kula au hatimaye watakula mikono yao wenyewe au 2) neno "mkono" ni sitiari kwa ajili ya jirani wa mtu.

Katika vitu hivi vyote, hasira yake haipungui; badala yake, mkono wake

"Ingawa vitu hivi vyote vimetokea, bado ana hasira, na mkono wake"

mkono wake bado unanyoshwa nje

Isaya anazungumza kana kwamba Yahwe alikuwa mtu ambaye anataka kumpiga mtu mwingine kwa ngumi yake. Hii ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kuwaadhibu Israeli. "bado atakuwa tayari kuwaadhibu"

Isaiah 10

Isaiah 10:1

kwa wale ambao hufanya sheria zisizo za haki na kuandika maagizo yasiyo ya haki

Misemo hii miwili ina maana moja. "kwa wale ambao hutengeneza sheria na maagizo ambayo sio haki kwa wote"

Watawanyima wahitaji haki, kunyanganya maskini wa watu wangu haki zao

Misemo hii miwili ina maana moja. "hazina haki kwa maskini na wahitaji miongoni mwa watu wangu"

wahitaji

"watu maskini"

kupora wajane

"chukua kila kitu kutoka kwa wanawake ambao waume zao wameshakufa"

na kufanya wasio na baba mawindo yao

Isaya inalinganisha yatima kwa wanyama ambao wanyama wengine huwinda na kula. Hii inasisitiza ya kwamba yatima hawana uwezo na waamuzi wanaweza kuwadhuru kiurahisi. "na kuwadhuru watoto ambao hawana wazazi kama mnyama anayemfuata windo lake"

mawindo

wanyama ambao wanyama wengine hutaka kuwshika na kuwala

Isaiah 10:3

Mtafanya nini katika siku ya hukumu ... mbali?

Isaya anatumia swali kukaripia wale ambao Yuda anadhuru maskini na watu dhaifu. "Utaweza kutofanya kitu katika siku ya hukumu ... mbali!"

siku ya hukumu

"siku ambayo Yahwe anakuja kukuhukumu" au "siku ambayo Yahwe anakuadhibu"

Utatoroka kwa nani kwa ajili ya msaada, na utaacha utajiri wako wapi?

Isaya anatumia swali kukaripia wale ambao wapo yuda ambao hudhuru maskini na watu dhaifu. "Hauna sehemu ya kukimbilia kwa msaada, na hautakuwa na sehemu ya kuficha utajiri wako!"

Hakuna kinachobaki

"Hakuna kitu kinachobaki kwa ajili yako kufanya"

na unajikunyata miongoni mwa wafungwa au kuanguka miongoni mwa waliouliwa

"'na adui zako watakuchukua kama wafungwa au watakuua"

Katika haya yote, hasira yake haishuki

"Hata kama vitu hivi vyote vikitokea, bado ana hasira".

mkono wake bao unanyoshwa nje

Isaya anazungumza kana kwamba Yahwe alikuwa mtu aliyetaka kumpiga mtu mwingine kwa ngumi yake. Hii ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kuadhibu Israeli. "atakuwa tayari kuwaadhibu"

Isaiah 10:5

Ole

neno hili linaweka alama mwanzo wa tangazo la Mungu kuhusu adhabu kali dhidi ya Ashuru.

Ashuru

Hii ina maana ya mflame wa Ashuru.

rungu ya hasira, fimbo ambayo ninatawala ghadhabu yangu

Misemo hii miwili ina maana moja. Yahwe analinganisha mfalme wa Ashuru kwa silaha ambayo mtu hubeba mkononi na kupiga watu wengine. Inasisitiza ya kwamba mfalme wa Ashuru na jeshi lake ni chombo ambacho Yahwe hutumia kuadhibu Israeli. "nani atakuwa kama silaha mikononi mwangu ambayo nitaitumia kuponyesha hasira yangu"

ninamtuma ... ninamuamuru

Neno "ninamtuma" hapa pia ina maana ya mflame wa Ashuru. Lakini haimaanishi Mungu anamtuma mfalme pekee; anamtuma pamoja na jeshi la Ashuru. "Ninatuma jeshi la Ashuru ... ninawaamuru"

dhidi ya taifa lenye kiburi na dhidi ya watu ambao wanabeba ghadhabu yangu ya kumwagikia

"kushambulia taifa lililojaa watu wenye kiburi ambao wamenifanya niwe na hasira sana"

ambao wanabeba ghadhabu yangu ya kumwagikia

Yahwe anazungumzia ghadhabu yake kana kwamba ilikuwa kimiminiko kuzidi chombo ambacho kilibeba; "watu" wanajaribu kubeba chombo chake, lakini ni kizito, na Yahwe anamwaga kimiminiko ndani hata baada ya kuanza kumwagikia nje. "ambao ninaendela kuwa na hasira nao hata baada ya kuwaadhibu"

kuchukua mateka

"kuchukua kila kitu walichonacho"

kuchukua mawindo

kuwachukua watu kama mawindo.

kuwakanyaga kama tope

Maana zaweza kuwa 1) Yahwe analinganisha jeshi la Ashuru kushambulia Israeli na watu kukanyaga katika tope ambao hawajali nini kinatokea kwa matope. "wakanyage mpaka wawe kama matope" au 2) watu wanakanyaga juu ya watu wengine kwa hiyo wanalala kwenye matope na kushindwa kuinuka. Hii ni sitiari ya kuwashinda kabisa. "kuwashinda kabisa"

Isaiah 10:7

Lakini hivi sivyo kile anachokusudia, wala hawazi kwa namna hii

Maana ya "hivi" na "namna hii" zinaweza kuwekwa wazi. "lakini mfalme wa Ashuru hakusudii kufanya kile ninachomuambia, na wala hafikirii ya kwamba ninamtumia kama silaha"

Ni katika moyo wake kuangamiza na kuondoa mataifa mengi

Maneno "angamiza" na "ondoa" ina maana moja. Zinatumiwa kwa ajili ya msisitizo. "Anataka uangamize kabisa mataifa mengi"

Je! wakuu wangu wote sio wafalme?

Mfalme wa Ashuru anatumia swali kusisitiza kile anachoamini kila mtu anatakiwa kuwa anakifahamu. "Nimefanya makapteni kutoka kwa wafalme wa jeshi langu juu ya nchi nilizozishinda!"

Je! Kalno sio kama Karkemishi? Hamathi sio kama Arpadi? Je! Samaria sio kama Damesk?

Mfalme wa Ashuru anatumia maswali haya kwa ajili ya msisitizo. "kalno sio tofauti na Karkemishi. Hamathi sio tofauti na Arpadi. Samaria sio tofauti na Dameski. Nimezishinda zote!"

Kalno ... Karkemishi ...

Haya ni majina ya miji.

Isaiah 10:10

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kunukuu kile mfalme wa Ashuru anachosema.

Kama mkono ulivyoshinda

"Mkono" ni kumbukumbu kwa nguvu ya jeshi. "Kama jeshi langu lenye nguvu lilivyoshinda" au "Kama nilivyoshinda"

wangu

Hii ina maana ya mfalme wa Ashuru.

ambao sanamu zao za kuchonga zilikuwa kubwa kuliko

Katika kipindi hiki watu waliamini ya kwamba ukubwa wa sanamu ulionyesha jinsi ufalme ulivyokuwa na nguvu ambayo iliijenga. Mfalme wa Ashuru kusema kuwa kwa sababu sanamu katika Yerusalemu sio kubwa kama sanamu za falme alizozishinda, Yerusalemu ingekuwa na uwezo mdogo zaidi kumshinda kuliko zingine.

kama nilivyofanya kwa Samaria na sanamu zake sizizo na thamani

Neno "Samaria" lina maana ya watu ambao waliishi pale, na "zake" ina maana ya mji wa Samaria. Miji na mataifa mara kwa mara ilizungumziwa kana kwamba ilikuwa wanawake. "'kama nilivyofanya kwa watu wa Samaria na sanamu zao sizizo na thamani"

sitafanya hivyo hivyo pia kwa Yerusalemu na kwa sanamu wake?

Mfalme wa Ashuru anatumia swali kusisitiza uhakika ya kwamba atashinda watu wa Israeli. "Hakika nitafanya kile kile kwa Yerusalemu na sanamu wake!"

Isaiah 10:12

Bwana atakapomaliza kazi yake juu ya Mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitaadhibu

Yahwe anajizungumzia kana kwamba alikuwa mtu mwingine. "Pale Mimi, Bwana, nitakapomaliza kazi yangu juu ya Mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitaadhibu"

kazi yake juu ... na juu ya

kazi yake ya kuadhibu. "kuadhibu ... na kuadhibu"

Nitaadhibu usemi wa moyo wa kujisifu wa mfalme wa Ashuru na muonekano wake wa kiburi

"Nitaadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya mambo ya kiburi aliyosema na muonekano wa kiburi katika uso wake"

Kwa maana anasema

"Kwa maana mfalme wa Ashuru anasema"

Nimeondoa mipaka ya watu

Hapa neno "nimeondoa" ina maana ya mfalme wa Ashuru. Alikuwa kiongozi wa jeshi la Ashuru na kuchukua sifa kwa kile jeshi lilifanya kwa amri yake. "jeshi langu limeondoa mipaka ya watu"

kama ng'ombe dume

"na nguvu kama ng'ombe dume". Baadhi ya tafsiri husoma, "kama mwanamume mwenye nguvu"

Nimewaweka chini

"Mimi na jeshi langu tumewaweka"

Nimewaweka chini wakazi

Maana zaweza kuwa 1) mfalme wa Ashuru amewaaibisha watu wa nchi alizozishinda au 2) ameondoa wafalme wa mataifa ili zisiweze kutawala tena.

Isaiah 10:14

Maelezo ya Jumla

Yahwe bado anamnukuu mfalme wa Ashuru.

Mkono wangu umekamata

Mkono ni mfano wa maneno kwa nguvu ya mfalme au jeshi lake. "Katika nguvu yangu nimekamata" au "Mkono wangu umekamata"

Mkono wangu umekamata, kama katika kiota, utajiri wa mataifa

Mfalme wa Ashuru analinganisha kuchukua hazina kutoka katika mataifa kwa mtu anayechukua mayai nje ya kiota cha ndege. Hii inasisitiza jinsi ilivyo rahisi kwake na jeshi lake kushinda falme hizi zingine. "Jeshi langu limeiba utajiri kutoka mataifa kwa urahisi kama mwanamume anayechukua mayai kutoka kwenye kiota"

na kama mtu anayekusanya mayai yaliyotelekezwa, nilikusanya dunia yote

"na vile tu kama mtu anayechukua mayai kutoka katika kiota pale ndege hayupo kuyalinda, jeshi langu limechukua hazina ya kila taifa"

Hakuna aliyepigapiga mabawa au kufungua mdomo wao au kulia

Hii inalinganisha mataifa kwa ndege ambaye hukaa kwa utulivu huku mayai yake yanachukuliwa. Hii inasisitiza ya kwamba mataifa hayakufanya kitu wakati jeshi la Ashuru lilipochukua mali zao zote. "Na kama ndege ambaye hatoi sauti au kupiga mabawa yake pale mtu anapoiba mayai yake, mataifa hayakufanya chochote tulipokuwa tukichukua hazina zao"

Isaiah 10:15

Je! shoka litajivunia lenyewe dhidi ya yule anayelitumia? Je! msumeno utajisifu zaidi kuliko yule anayekata kwa kulitumia?

Msemaji anatumia maswali haya kukejeli mfalme wa Ashuru. "Shoka haliwezi kujivuna ya kwamba ni bora kuliko yule anayelishikilia. Na msumeno haupati utukufu zaidi ya yule anayekata kwa kulitumia"

msumeno

kifaa chenye ncha kali kiinchotumiwa kukata mbao

Ni kana kwamba kiboko kinaweza kuwainua wale ambao huiinua, au kana kwamba rungu ya mbao inaweza kumuinua mtu

Misemo hii ina maana moja na inatumika kuimarisha maana ya maswali mawili kabla yao. Inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Na wala fimbo au gongo haviwezi kumwinua yule anayeziokota"

Kwa hiyo Bwana Yahwe wa majeshi atatuma udhoofishaji katika mahodari wake wa juu

Haipo wazi kama Yahwe au Isaya anazungumza. Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "kudhoofika" inaelezwa kama kitenzi "kufanya dhaifu". Kwa hiyo, Mimi, Bwana wa Yahwe wa majeshi, atafanya wanajeshi wenye nguvu wa mfalme kuwa dhaifu"

chini ya utukufu wake kutachochewa mwako kama wa moto

Yahwe analinganisha adhabu yake kwa moto. Hii inasisitiza ya kwamba adhabu yake utaangamiza kabisa ufahari wote na ukubwa wa ufalme wa Ashuru. "Nitaangamiza ukubwa wake kana kwamba nilikuwa nikianzisha moto kuchoma kila kitu anachojivunia"

Isaiah 10:17

Nuru ya Israeli itakuwa moto

Msemo "nuru ya Israeli" ina maana ya Yahwe. Haipo wazi kama Yahwe an Isaya anazungumza. "Mimi, Yahwe, nuru ya Israeli, atakuwa kama moto"

moto

"Moto" unasisitiza nguvu ya Yahwe kuangamiza kila kitu ambacho hakimpi utukufu.

Mtakatifu wake mwale

"Mimi, Yahwe, Mtakatifu wa Israeli, atakuwa kama mwale".

utaunguza na kumeza miiba na mibigili yake

"Moto utaunguza na kumeza miiba na mibigili ya mfalme wa Ashuru" Msemaji analinganisha jeshi la mfalme wa Ashuru kwa miiba na mibigili. Hii inasisitiza ilivyo rahisi kwa Mungu kuwaangamiza. "Nitaangamiza Ashuru kama moto unaochoma miiba na mibigili"

miiba ... mibigili

Maneno "mibigili" na "miiba" yote yana maana mimea isiyo na thamani y miiba; inaweza kutafsiriwa kutumia msemo mmoja.

Yahwe atateketeza utukufu wa msitu wake na nchi yake inayozaa

Maana zaweza kuwa 1) "Yahwe ataangamiza misitu mikubwa na mshamba katika taifa la Ashuru" au 2) "Yahwe ataangamiza jeshi la Ashuru kama moto unavyochoma misitu mikubwa na mashamba"

zote nafsi na mwili

Maana zaweza kuwa 1) hii inasisitiza ya kwamba Mungu ataangamiza kabisa misitu na mshamba. "kabisa" au 2) hii ina maana Mungu atangamiza kabisa watu wa Ashuru. Msemo "nafsi na mwili" ina maana ya sehemu ya roho na sehemu ya mwili ya mtu.

itakuwa kama pale maisha ya mtu mgonjwa unavyotokomea

Hii inalinganisha aidha misitu na mashamba ya Ashuru au jeshi la Ashuru kwa mtu mgonjwa anapolala kitandani akifa. Hii inasisitiza jinsi jambo kubwa sana linaweza kuwa dhaifu na kufa. "watakuwa kama mtu mgonjwa anayekuwa dhaifu na kufa"

Masalio ya miti y msitu wake utakuwa mchache sana

"Vile vinavyosalia vya miti katika msitu wa mfalme vitakuwa vichache sana"

Isaiah 10:20

Katika siku hiyo

Hii ina maana kipindi ambacho Mungu anafanya mambo ambayo yanaelezwa katika 10:15. "Katika kipindi hicho"

ambayo imetoroka

Maana inaweza kuwekwa wazi. "ambaye ametoroka kutoka katika jeshi la Ashuru"

haitategemea tena kwa yule ambaye aliwashinda

"hatategemea tena mfalme wa Ashuru, ambaye aliwadhuru"

Mtakatifu

Mtakatifu wa Israeli

Isaiah 10:22

watu wako, Israeli, ni

Hapa "wako" ni umoja. Tafsiri zinazowezekana ni 1) Mungu anazungumza kwa Isaya na "wako" ina maana ya Isaya. "watu wako Israeli ni" au 2) Isaya au Mungu anazungumza kwa taifa la Israeli na "wako" ina maana ya taifa. "watu wako, O Israeli, ni"

ni kama mchanga wa pwani

Hii inasisitiza ya kwamba kulikuwa na idadi kubwa ya watu wa Israeli. "ni wengi mno kuhesabu, kama mchanga wa pwani"

Uharibifu umeagizwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe ameagiza ya kwamba ataangamiza wengi wa wale wanaoshi Israeli"

kadri haki inayomwagikia inavyodai

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Hii inapaswa kufanywa kwa ajili ya haki timilifu" au "Yahwe anatakiwa kufanya hili kwa sababu ni mwenye haki kabisa"

kutekeleza uharibifu uliobainishwa katika nchi

Maana zaweza kuwa 1) "kuangamiza kila kitu katika nchi kama alivyoamua kufanya" au 2) "kuangamiza watu katika nchi kama alivyoamua kufanya"

uliobainishwa

"kuamuliwa"

Isaiah 10:24

Ashuru

Isaya anazungumzia mfalme wa Ashuru na jeshi lake kana kwamba alikuwa mtu mmoja. "mfalme wa Ashuru na jeshi lake"

Atakupiga kwa fimbo na kuinua gongo lake dhidi yako

Neno "lake" ina maana ya "Ashuru", utambulisho wa mfalme wa Ashuru na jeshi lake. Maneno "fimbo" na "gongo" ina maana ya vipande vya mbao ambavyo watu hutumia kama rungu kupiga wanyama na watu wengine. Isaya anazungumzia njia ambayo Ashuru atatawala juu ya Waisraeli kana kwamba Ashuru alikuwa akiwapiga Waisraeli kwa rungu. "Ashuru atatawala juu yako na kukufanya mtumwa"

kama Mmisri alivyofanya

Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "kama Wamisri walivyotawala juu ya mababu zako na kuwafanya watumwa"

hasira yangu utapelekea uharibifu wake

Nomino dhahania "uharibifu" unaweza kutafsiri kama kitenzi. "Nitamwangamiza kwa sababu nina hasira juu yake"

Isaiah 10:26

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi wa Israeli

atainua mjeledi dhidi yao

"atapiga Ashuru kwa mjeledi". Mungu hatatumia mjeledi kihalisia. Hii ina maana ya nguvu ya Mungu kuadhibu Ashuru kwa ukalii. "nitaadhibu Ashuru kwa ukali kana kwamba kwa mjeledi"

kama pale alipowashinda Midiani katika mwamba wa Orebu

Hii ina maana ya pale Mungu alipomsaidia mtu aliyeitwa Gideoni kuwashinda jeshi la Midani.

Atainua fimbo yake juu ya bahari na kuinua kama alivyofanya kwa Misri

Hii ina maana ya fimbo pale Mungu aliposababisha maji ya Bahari ya Shamu kugawanyika ili watu wa Israeli waweze kutoroka kutoka kwa jeshi la Misri na ili kwamba jeshi la Misri lizame ndani yake. "Atakusaidia kutoroka kutok katika jeshi la Ashuru kama alivyowasaidia mababu zako kutoroka jeshi la Misri"

mzigo wake unainuliwa kutoka kwenye bega lako na nira yake kutoka shingoni mwako

"Yahwe atabeba mzigo ambao Ashuru ameweka katika bega lako, na atatoa nira ambayo wameweka juu ya shingo yako". Misemo hii miwili ina maana moja. Maneno "mzigo" na "nira" ina maana ya utumwa. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe ataondoa Ashuru ambaye huwakandamiza na atawazuia kuwafanya kuwa watumwa"

nira itaangamizwa kwa sababu ya unene

Msemo huu unaashiria ya kwamba shingo ya mnyama ambayo inavaa nira itakuwa nene sana kutosha nira tena. Hii ni sitiari kwa Israeli kuwa na nguvu sana hadi Ashuru kutowatawala tena. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "shingo yako itakuwa nene sana hadi itavunja nira" au "mtakuwa na nguvu sana hadi hamtakuwa tena watumwa wa Ashuru"

Isaiah 10:28

amekuja ... amepita ... ametunza ... wamevuka ... kupanga ... hutetemeka ... amekimbia

Isaya anazungumzia matukio haya ya mbeleni kana kwamba yamekwisha tokea.

Aiath ... Migroni ...Mikmashi ... Geba ... Rama ... Gibea

Hii yote ni miji na vijiji karibu na Yerusalemu ambazo jeshi la Ashuru lilipita katikati na kusababisha shida.

Rama hutetemeka na Gibea wa Sauli amekimbia

"Watu wa Rama hutetemeka na watu wa Gibea wa Sauli wamekimbia"

Isaiah 10:30

binti wa Galimu

Neno "binti" hapa lina maana ya watu ambao huishi katika mji. "Galimu" au "watu wa Galimu"

Galimu ... Laisha ... Anathothi ... Madmena ... Gedimu ... Nobu

Haya ni majina ya miji zaidi na vijiji karibu na Yerusalemu ambayo jeshi la Ashuru lilisafiri katikati kusababisha hofu miongoni mwa watu. Zote hizi zina maana ya watu ambo huishi katika maeneo haya.

atasimama Nobu na kutikisa ngumi yake

Hapa "atasimama" na "yake" ina maana ya mfalme wa Ashuru na wanajeshi wake. Watu walikuwa wakitikisa ngumi zao kwa watu ambao walikuwa wakiwatisha. "jeshi la Ashuru litasimama Nobu na kutisha"

mlima wa binti wa Sayuni, kilima cha Yerusalemu

Maneno "mlima" na "kilima" ni mfano wa maneno kwa ajili ya watu ambao wanaishi ndani yao. "watu wa Mlima Sayuni na watu wanaoishi katika kilima kilicho Yerusalemu". Maneno "mlima wa binti wa Sayuni" ina maana ya kitu kimoja kama maneno "kilima cha Yerusalemu".

Isaiah 10:33

Tazama

HIi inaweza kutafsiriwa kama "Angalia" au "'Sikiliza" au "Zingatia kwa makini kile ninachotaka kukuambia".

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli

atapogoa matawi ... na Lebanoni katika ufahari wake utaanguka

Isaya anazungumzia jeshi la Ashuru kana kwamba lilikuwa miti mirefu katika Lebanoni. Mungu ataangamiza jeshi kama watu wanvyokata chini miti mikubwa ya Lebanoni. Hii inasisitiza ya kwamba ingawa jeshi lina nguvu, Mungu ana uwezo wa kuliangamiza.

atapogoa matawi

"atakata matawi makubwa ya miti". Ataangamiza jeshi la Ashuru kama wanamume wenye nguvu wanavyokata matawi makubwa ya miti"

kwa kishindo cha kutisha

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "kishindo" inaelezwa kama kitenzi "kupiga kelele". "na matawi yataanguka chini katika ardhi na kutoa sauti ya kutisha" au "na matawi yataanguka katika ardhii kwa sauti kubwa sana"

miti mirefu zaidi itakatwa chini

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "'atakata chini miti mirefu zaidi"

miti mirefu zaidi

Hii ni sitiari kwa ajili ya "wanajeshi wenye nguvu zaidi"

wenye kiburi watashushwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "atawashusha chini watu wenye kiburi"

wenye kiburi

mjivuno

vichaka vya msitu

"vichaka vinene katika msitu". Hii inawezekana kuwa sitiari kwa wale watu ambao hawajulikani"

Lebanoni katika ufahari wake utaanguka

"misitu ya Lebanoni haitakuwa mikubwa tena". Hii inaweza kuwa sitiari kwa ajili ya jeshi la Ashuru. "Yahwe atawashinda jeshi la Ashuru, kama jinsi lilivyo na nguvu"

Isaiah 11

Isaiah 11:1

Chipukizi litachipuka kutoka kwenye kisiki cha Yese ... tawi kutoka katika mizizi yake litazaa matunda

Isaya anamzungumzia Yese na uzao wake kana kwamba walikuwa mti ambao ulikuwa umekatwa chini. Misemo hii miwili inaelezea juu ya uzao wa Yese ambaye atakuwa mfalme. "Kama vile chipukizi linavyochipuka kutoka kwenye kisiki cha mti, vile vile uzao wa Yese utakuja kuwa mfalme juu ya kinachobaki cha Israeli"

kisiki cha Yese

Kisiki ni kile kinachobaki kwenye mti baada ya kukatwa chini. "Kisiki" cha Yese kinawakilisha kile kinachobaki katika ufalme ambao mwana wa Yese Daudi aliwahi kuwa mfalme.

Roho wa Yahwe atatua juu yake

Kutua juu yake inawakilisha kuwa pamoja naye na kumsaidia. Neno "yake" ina maana ya yule ambaye angekuja kuwa mfalme.

roho ya hekima ... roho ya mafunzo ... roho ya maarifa ... hofu ya Yahwe

Hapa neno "roho" ina maana ya uwezo au sifa ambayo Roho wa Yahwe angempatia. "na atasababisha kuwa na hekima na uelewa, mafunzo na uwezo, maarifa na hofu ya Yahwe"

Isaiah 11:3

Kauli Unganishi

Isaya anaendelea kumfafanua mfalme.

hatahukumu kwa kile ambacho macho yake yanaona

Msemo "kile ambacho macho yake yanaona" ina maana ya kuona vitu ambavyo sio muhimu kwa kuhukumu mtu kwa sahihi. "hatahukumu mtu kwa kumtazama tu vile ambavyo mtu anavyoonekana"

wala kuamua kwa kile masikio yake yanasikia

"na hataamua kwa kile ambacho masikio yake husikia". Msemo "kile ambacho masikio yake husikia" yana maana ya kusikia kile ambacho watu wanasema juu ya mtu. "na hatahukumu mtu kwa kusikia kile ambacho wengine wanasema juu yake"

maskini ... wanyenyekevu ... waovu

Misemo hii ina maana ya watu ambao wana sifa hizi. "watu maskini ... watu wanyenyekevu ... watu waovu"

Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake ... kwa pumzi ya midomo yake atawachinja waovu

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja.

Ataipiga nchi kwa fimbo ya kinywa chake

Neno "nchi" hapa linawakilisha watu wa dunia. Kuwapiga kwa fimbo ya kinywa chake inawakilisha kuwahukumu, na hukumu hiyo italeta adhabu. "Atahukumu watu wa dunia, na wataadhibiwa"

kwa pumzi ya midomo yake atawachinja waovu

"pumzi ya midomo yake" inawakilisha yeye kuwahukumu. "atahukumu watu waovu, nao watauwawa"

mkanda wa kiuno chake ... mkanda unaozunguka kiunoni kwake

Maana zaweza kuwa 1) mkanda unatumika kuimarisha nguo za mtu ili aweze kufanya kazi, au 2) mkanda ni nguo ya ndani, au 3) mkanda ni mshipii ambao mfalme huvaa kuonyesha mamlaka yake.

Haki itakuwa mkanda wa kiuno chake

Kuvaa haki kama mkanda inawakilisha kuwa mwenye haki. Maana zaweza kuwa 1) haki ya mfalme itamuwezesha kutawala. "Haki yake itakuwa kama mkanda unaozunguka kiuno chake" au 2) haki ya mfalme itaonyesha mamlaka yake ya kutawala. "Atatawala kwa haki"

uaminifu mkanda unaozunguka nyonga yake

Maneno "utakuwa" inaeleweka katika msemo huu. "uaminifu utakuwa mkanda unaozunguka nyonga yake"

uaminifu mkanda unaozunguka nyonga yake

Kuvaa uaminifu kama mkanda inawakilisha kuwa mwaminifu. Maana zaweza kuwa 1) uaminifu wa mfalme utamwezesha kutawala, au 2) uaminifu wa mfalme utaonyesha mamlaka yake ya kutawala. "uaminifu wake utakuwa kama mkanda unaozunguka nyonga yake" au "atatawala kwa uaminifu"

Isaiah 11:6

Taarifa ya Jumla

Isaya anafafanua kile ambacho dunia itakavyokuwa mfalme atakavyotawala. Kutakuwa na amani kamili duniani. Hii inaonyeshwa kwa amani ambayo itakuwepo hata kwa wanyama. Wanyama ambao kawaida huwaua wanyama wengine hawatawaua, na watakuwa salama pamoja.

Mbwa mwitu ... chui ... simba mchanga ... dubu ... Simba

Misemo hii ina maana ya hawa wanyama kwa ujumla, sio kwa mbwa mwitu au chui bayana. Hawa ni wanyama wenye nguvu ambao hushambulia na kula wanyama wengine. "Mbwa mwitu ... chui .. simba wachanga ... dubu ... Simba"

mwanakondoo ... mbuzi mchanga ... ndama ... ndama aliyenenepeshwa ... Ng'ombe ... maksai

Misemo ina maana ya wanyama hawa kwa ujumla, sio mwanakondoo au mbuzi bayana. Hawa wote ni wanyama ambao hula nyasi na majani makavu. Wanyama wengine mara nyingine huwashambulia na kuwala. "mwanakondoo ... mbuzi mchanga ... ndama ... ndama aliyenenepeshwa ... Ng'ombe ... maksai"

chui

paka mkubwa mwenye manyoya ya njano na madoa meusi ambaye huwaua na kuwala wanyama wengine.

ndama, simba mchanga na ndama aliyenenepeshwa, kwa pamoja

Msemo "watakuwa" unaeleweka. ndama, simba, na ndama aliyenenepeshwa watakuwa pamoja

dubu

mnyama mkubwa sana mwenye nywele nene na makucha makali ambaye huwaua na kuwala wanyama wengine.

mtoto mdogo atawaongoza

Mtoto atawatunza na kuwaongoza katika sehemu nzuri kunywa maji na kula nyasi au nyasi kavu.

watachunga pamoja

"watakula nyasi pamoja"

watoto wao

Hii ina maana ya watoto wa wanyama muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Isaiah 11:8

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua amani kamili katika dunia pale mfalme atakapotawala.

mtoto mchanga atacheza juu ya shimo la nyoka

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba mtoto mchanga atakuwa salama kwa sababu nyoka hatamng'ata. "Watoto wachanga watacheza kwa usalama juu ya shimo la nyoka"

nyoka ... tundu la nyoka

Misemo hii ina maana ya nyoka wenye sumu kwa ujumla. "nyoka ... matundu ya nyoka"

mtoto aliyeachishwa ziwa

mtoto ambaye hanywi tena maziwa ya mama yake

katika milima yangu mitakatifu

"Mlima mtakatifu" ni Mlima Sayuni, katika Yerusalemu. "katika mlima mtakatifu wote wa Yahwe"

dunia itakuwa imejaa maarifa ya Yahwe

Msemo "maarifa ya Yahwe" yanawakilisha watu wanaomjua Yahwe. "dunia itakuwa imejaa wale ambao wanamjua Yahwe" au "wale ambao wanamjua Yahwe watafunika dunia"

kama maji yanavyofunika bahari

Msemo huu unatumika kuonyesha jinsi dunia itakavyojaa na watu ambao wanamjua Yahwe. Inaweza kuwa wazi ya kwamba inafanya hivi kama maneno yanafanana na maneno katika msemo uliopita. "kama bahari zilivyojaa na maji"

Isaiah 11:10

mzizi wa Yese

Hii ina maana ya uzao wa Yese na Mfalme Daudi ambaye atakuja kuwa mfalme ambaye alizungumziwa katika 11:1. "Uzao wa wa Yese mfalme" au "mfalme alitokana kwa Yese"

itasimama kama bango kwa ajili ya watu

bango ni bendera ambayo mfalme huinua kama ishara kwa watu kuiona na kuja kwake. "utakuwa kama ishara kwa ajili ya watu" au "itavuta watu kuja kwake"

mataifa

"watu wa mataifa"

Bwana atanyosha tena mkono wake kurejesha aliyesalia wa watu wake

Mkono ni marejeo ya nguvu ya Mungu. "Bwana atatumia tenanguvu yake kuwaleta waliosalia wa watu wake"

Pathrosi ... Elamu .. Hamathi

Haya ni majina ya mahali

Isaiah 11:12

Ataandaa bango kwa ajili ya mataifa

Maana zaweza kuwa 1) "Bwana ataandaa mfalme kama bango kwa ajili ya mataifa" au 2) "Mfalme ataandaa bango kwa ajili ya mataifa"

bango kwa ajili ya mataifa

"bendera kwa ajili ya mataifa kuona" au "bendera kuwaita mataifa kwa ajili yake"

waliotawanywa wa kutoka Yuda

"watu wa Yuda ambao walitawanyika duniani kote"

kutoka pembe nne za dunia

Dunia inapewa taswira ya kwamba ina pembe nne, na pembe hizo ndizo umbali mkubwa kabisa. Hii ina maana ya kila sehemu duniani ambao watu hao wanaweza kuwepo. "kutoka hata sehemu za mbali kabisa za dunia" au "kutoka duniani kote"

Atageuza upande wivu wa Efraimu

Efraimu hapa ina maana ya uzao wa ufalme wa kaskazini wa Israeli. Nomino "wivu" inaweza kuelezwa kama kivumishi. "Atawazuia watu wa Efraimu kutokuwa na wivu"

Yuda hatakuwa na uadui tena kwa Efraimu

Yuda hapa ina maana ya uzao wa ufalme wa kusini wa Israeli. Msemo huu unaweza kuwekwa katika halii ya kutenda. "atawazuia watu wa Yuda kutokuwa na uadui" au "atawazuia wtu wa Yuda kutochukia"

Isaiah 11:14

watashuka chini kwa kasi juu ya vilima vya Wafilisti

Watu wa Israeli na Yuda wanawekewa taswira kana kwamba wao ni ndege ambao wanaweza kupaa chini kwa haraka kumshambulia mtu au mnyama. "watakwenda kwa haraka katika vilima vya Wafilisti kushambulia watu kule"

ghuba ya Bahari ya Misri

"ghuba" ni eneo kubwa la maji ambalo huzungukwa kidogo na nchi kavu.

Kwa upepo wake unaochoma atapunga mkono wake juu ya Mto Frati

Kupunga mkono juu ya kitu inawakilisha nguvu yake kuibadili. "Kwa nguvu yake atasababisha upepo uchomao kuvuma juu ya Mto Frati"

upepo wake unaochoma

Huu ni upepo wenye nguvu na wa moto ambao husababisha sehemu ya maji katika mto kukauka.

ili iweze kuvukwa juu kwa ndara

"ili kwamba watu waweze kuvuka juu hata kama wanavaa ndara zao"

Isaiah 11:16

Kutakuwa na njia

Njia ni barabara kubwa ambayo watu wengi wanaweza kusafiri juu yake."Yahwe atafanya barabara"

katika ujio wao kutoka katika nchi ya Misri

"walipokuja kutoka katika nchi ya Misri"

Isaiah 12

Isaiah 12:1

Taarifa ya Jumla

Hapa Isaya anaendelea kuelezea jinsi itakavyokuwa pale mfalme ambaye Mungu amemchagua anatawala.

Katika siku hiyo

Inaweza kuwekwa wazi ni wakati gani unaomaanishwa. "Katika kipindi hicho" au "Pale mfalme anapotawala"

hasira yako imegeuka

Hasira ya Mungu inazungumziwa kana kwamba mtu anaweza kugeuka na kuondoka. Ina maana ya kwamba Mungu ameacha kuwa na hasira. "Hauna hasira na mimi tena"

Mungu ni wokovu wangu

Mungu anasababisha wokovu wa mtu inazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa huo wokovu. Nomino dhahania "wokovu" inaweza kuelezwa na nomino "mwokozi" au kitenzi "okoa". "Mungu husababisha wokovu wangu" au "Mungu ni mwokozi wangu" au "Mungu ndiye anayeniokoa"

Yahwe ni nguvu yangu

Mungu kusababisha mtu kuwa na nguvu inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa nguvu yao. "Yahwe hunifanya niwe na nguvu"

na wimbo

Neno "wimbo" hapa linawakilisha kile mtu anachokiimba. "na yule ambaye nayemwimba kwa furaha"

Amekuwa wokovu wangu

"Ameniokoa"

Isaiah 12:3

Kwa furaha utateka maji kutoka kwenye visima vya wokovu

Isaya anazungumzia watu kukombolewa kana kwamba walikuwa wakipata wokovu kwa namna ambavyo watu hupata maji kutoka kisimani. "utafurahi pale atakapokukomboa, kama watu wanavyofurahi wanapoteka maji kutoka kisimani"

kuliita jina lake

Hapa "jina lake" lina maana ya Yahwe. Kuliita jina lake lina maana ya aidha kumsifu au kumwomba msaada. "kumsifu kwa sauti" au "kumwita akusaidie"

kutamka matendo yake miongoni mwa watu

Nomino ya "matendo" inaweza kuelezwa na msemo "kile aliuchofanya". "Waambie watu juu ya mambo makubwa aliyofanya"

kutamka ya kuwa jina lake limeinuliwa

Hapa "jina lake" lina maana ya Yahwe. "tangaza ya kuwa ameinuliwa" au "tangaza ya kwamba ni mkuu"

Isaiah 12:5

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kusema kile ambacho watu watasema pale ambapo wafalme wanatawala.

kwa maana miongoni mwenu yupo Mtakatiufu wa Israeli

"kwa sababu Mtakatifu wa Israeli, ambaye huishi miongoni mwenu, ana uwezo" au "kwa sababu Mtakatifu wa Israeli ana uwezo ana uwezo na anaishi miongoni mwenu"

Isaiah 13

Isaiah 13:1

kuhusu Babeli

Jina la mji lina maana ya watu wa Babeli. "kuhusu watu wa Babeli"

Amozi

Amozi alikuwa baba wa Isaya.

lia kwa sauti kwao

Neno "kwao" ina maana ya wanajeshi kutoka nchi nyingine.

malango ya waadilifu

Maana zaweza kuwa 1) "malango ya Babeli ambapo waadilifu wanaishi" au 2) "malango ya nyumba kubwa za waadilifu"

waadilifu

"watu wanaoheshimiwa" au "watawala"

watakatifu wangu

"wale ambao nimewaweka kando kwa ajili yangu" au "jeshii ambalo nimeliweka kando kwa ajili yangu"

Nmewaita wanamume wangu wenye uwezo kutekeleza hasira yangu

Kutekeleza hasira ya Mungu inawakilisha kuadhibu watu kwa sababu ya hasira ya Mungu. "Nimewaita wanajeshi wenye nguvu kuadhibu watu wa Babeli kwa sababu wamenikasirisha"

hata wanaoshangilia kwa kujisifu

"hata wale ambao wanashangilia kwa majivuno". Sababu ya wao kushangilia kwa majivuno inaweza kuwekwa wazi. "hata watu wangu ambao hushangilia kwa majivuno kwa sababu ya mambo makubwa nayofanya"

Isaiah 13:4

Kelele za kundi katika milima, kama watu wengi

Neno "kelele" linaeleweka. Misemo "kundi" na "watu wengi" ina maana moja. "kuna kelele ya watu wengi katika milima" au "Kuna kelele ya kundi kubwa la watu katika milima"

Kelele za ghasia ya falme kama mataifa mengi yaliyokusanyika pamoja

MaNeno "kuna" linaeleweka. Maneno "falme" na "mataifa" hapa yana maana ya jambo moja. "Kuna ghasia ya kelele ya falme nyingi zilizokusanyika pamoja"

anawakutanisha

"anawakusanya"

kutoka mbali juu ya upeo wa macho

"kutoka sehemu mbali kupita upeo wa macho" au "kutoka sehemu za mbali sana"

vyombo vyake vya hukumu

Wanajeshi ambao Mungu anawatuma kushambulia Babeli wanazungumziwa kana kwamba walikuwa silaha. "Hukumu" inawakilisha adhabu kwa sababu Mungu alihukumu Babeli. "'jeshi ambalo atalitumia kuadhibu Babeli"

Isaiah 13:6

Lia kwa kelele

"Paza sauti ya juu"

siku ya Yahwe ipo karibu

Jambo ambalo linatarajia kufanyika hivi karibuni linazungumziwa kana kwamba linakuja karibu. "siku ya Yahwe itatokea hivi karibuni"

inakuja na uhariibifu kutoka kwa Mwenyezi

Neno "inakuja" ina maana ya siku ya Yahwe. "Inakuja na uharibifu" ina maana uharibifu utatokea katika siku hiyo. "Uharibifu kutoka kwa Mwenyezi" ina maana ya kwamba Mwenyezi atawaangamiza. "katika siku hiyo, Mwenyezi Mungu atawaangamiza"

mikono yote huning'inia kwa ulegevu

Hii inaonyesha ya kwamba watu wote ni dhaifu sana na hawawezi kufanya jambo lolote.

kila moyo huyeyuka

Watu kuwa na hofu sana inazungumzwa kana kwamba mioyo yao huyeyuka. "kila mmoja anaogopa sana"

uchungu na maumivu utawakamata

Watu kujisikia maumivu mabaya ghafla na majonzi inazungumziwa kana kwamba maumivu na majonzi yalikuwa watu ambao huwakamata. "ghafla watahisi maumivu makubwa na uchungu"

kama mwanamke katika uchungu

Kuwa katika uchungu inawakilisha kuzaa mtoto. "kama mwanamke anayezaa mtoto" au "kama maumivu ya mwanamke ambaye anazaa mtoto"

nyuso zao zitawaka

Nyuso zao kuwa za moto na nyekundu inazungumziwa kana kwamba zilikuwa zikiungua. Sababu zinazowezekana za nyuso zao kuwa za moto ni 1) watu wanaogopa sana au 2) watu wanajisikia aibu au 3) watu wanalia. "nyuso zao zitakuwa za moto na nyekundu"

Isaiah 13:9

siku ya Yahwe inakuja kwa ghadhabu katili na hasira ya kumwagikia

Siku kuja kwa ghadhabu na hasira ina maana ya kwamba kutakuwa na ghadhabu na hasira katika siku hiyo. Nomino dhahania "ghadhabu" na "hasira" inaweza kuelezwa kwa vivumishi "ghadhabu" na "hasira". "katika siku ya Yahwe, atakuwa na ghadhabu na hasira sana"

hasira ya kumwagikia

Hasira hapa inazungumziwa kana kwamba yule ambaye ana hasira ni chombo kiliichojazwa na hasira. Hasira inayomwagikia ina maana ya kwamba ana hasira sana.

kufanya nchi kutiwa ukiwa

Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "tia ukiwa" inaelezwa kwa kitenzi "haribu". "kuharibu nchi"

Nyota za mbinguni na vilimia

"Nyota katika anga"

havitatoa mwanga wao

Kutoa mwanga inawakilisha "kung'aa". "haitang'aa"

Jua litafanywa kuwa giza

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atauwekea giza jua" au "Jua litakuwa na giza"

Isaiah 13:11

Kauli Kiunganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya kile atakachofanya katika siku ya Yahwe.

ulimwengu

Hii ina maana ya "watu wa ulimwengu"

waovu ... wanaojivuna ... wakatili

Misemo hii ina maana ya watu ambao wana sifa hizi. "watu waovu ... watu wanaojivuna ... watu wakatili"

wakatili

"watu wakatili"

na nitashusha chini kiburi cha wakatili

Kuwa chini mara nyingi inawakilisha kuwa mnyenyekevu. Kushusha kiburi cha watu chini inawakilisha kufanya wawe chini. "na nitawashuhsa wakatili"

Nitawafanya wanamume kuwa adimu kuliko dhahabu safi

Kwa nini kutakuwa na watu wachache sana inaweza kuwekwa wazi. "Nitasababisha watu wengi sana kufa mpaka watu wanaoishi watakuwa adimu zaidi kuliko dhahabu safi"

wanamume kuwa adimu kuliko dhahabu safi ... binadamu mgumu kumpata kuliko dhahabu safi ya Ofiri

Misemo hii miwili ina maana moja.

dhahabu safi ya Ofiri

Ofiri lilikuwa jina la sehemu ambapo kulikuwa na dhahabu safi.

Isaiah 13:13

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Kama swala anayewindwa au kama kondoo asiyekuwa na mchungaji

"Kama swala ambaye hukimbia haraka pale watu wanapomwinda, na kama kondoo ambaye hana mchungaji anavyokimbia kutoka kwa wanyama pori"

swala

mnyama ambaye anafanana na mbawala. Watu huwawinda, na wanyama pori mara nyingine huwashambulia na kuwaua.

kama kondoo asiyekuwa na mchungaji

Kondoo ambao hawana mchungaji hawana mtu wa kuwalinda kutoka kwa wanyama pori ambao huwashambulia na kuwaua.

Isaiah 13:15

Yeyote atakayepatikana atauawa ... kila mmoja ambaye anakamatwa atakufa kwa upanga

Misemo hii miwili ina maana moja. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Adui ataua kwa upanga kila mtu anayempata"

Watoto wao wachanga pia watakatwa vipande

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Adui atawakata pia watoto wao wachanga katika vipande" au "Adui atawapiga watoto wao wachanga mpaka wafe"

mbele ya macho yao

"Mbele ya macho yao" ina maana ya "katika uwepo wao" au "huku wakitazama". Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba wazazi hawakuw\vza kuwasaidia watoto wao wachanga. "huku wazazi wao wakitazama bila msaada"

Nyumba zao zitaporwa

Hii ina maana ya kwamba kila kitu chenye thamani kitaibiwa kutoka katika nyumba zao. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Adui atapora nyumba za watu" au "Adui ataiba kila kitu chenye thamani kutoka kwa nyumba za watu"

wake zao kubakwa

Hii ina maana ya kwamba maadui watashambulia wanawake na kuwalazimsha kufanya ngono pamoja nao. Maneno "watabakwa" yanaeleweka. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wake zao watabakwa" au "maadui wao watawabaka wake zao"

Isaiah 13:17

Kauli Kiunganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Ninakaribia kuwatikisa Wamedi kuwashambulia

Kuwafanya watu kutaka kufanya kitu inazungumziwa kama kuwaamsha. "Ninataka kufanya Wamedi watake kuwashambulia"

Isaiah 13:19

Kauli Kiunganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza.

falme zinazoshangaza zaidi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ufalme ambao watu hushangaa zaidi"

ufahari wa kiburi cha Wakaldayo

Nomino "kiburi" inaweza kuelezwa kwa kivumishi "kujivuna". "mji mzuri ambao Wakaldayo wanajivunia"

itapinduliwa

"itaangamizwa"

kama Sodoma na Gomora

"kama Sodoma na Gomora walivyopundiliwa".

haitakaliwa au kuishi kwake

Vitenzi hivi viwili vina maana moja. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Hakuna mtu ataishi ndani yake"

kwake kutoka kizazi mpaka kizazi

Msemo "kizazi mpaka kizazi" una maana ya vizazi vyote vya watu ambavyo vitaishi katika siku za usoni. "milele" "wakati wowote tena"

Mwarabu

Hii ina maana ya watu wa Kiarabu kwa ujumla, sio mtu mmoja. "Waarabu" au "watu wa Kiarabu"

Isaiah 13:21

Kauli Kiunganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza kuhusu kile kitakachotokea kwa Babeli.

watalala pale

"watalala Babeli"

Nyumba zao

"'nyumba za watu"

bundi

Bundi ni ndege pori ambao huwinda usiku.

mbuni

Mbuni ni ndege pori wakubwa ambao hukimbia haraka na hawawezi kupaa.

Fisi

Fisi ni wanyama pori wakubwa ambao hufanana na mbwa na hula wanyama waliokufa. Sauti zao zaa juu husikika kama mtu achekavyo.

na mbweha katika kasri nzuri

Maneno "watalia" inaeleweka. "Na mbweha watalia ndani ya kasri nzuri"

mbweha

mbwa mwitu

Muda wake umekaribia, na siku zake hazitacheleweshwa

Misemo hii miwili ina maana moja. "Muda wake" na "siku zake" yote ina maana ya kipindi ambacho Mungu alichagua Babel kuangamizwa. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kipindi ambacho yote haya yatatokea kwa watu wa Babeli kimekaribia, na hakuna kitu kitazuia"

Isaiah 14

Isaiah 14:1

Yahwe atakuwa na huruma kwa Yakobo

Hapa "Yakobo" ina maana ya vizazi vya Yakobo. "Yahwe atakuwa na huruma juu ya vizazi vya Yakobo"

kujishikiza katika nyumba ya Yakobo

Nyumba ya Yakobo ina maana ya vizazi vya Yakobo, Waisraeli. "jiunge na vizazi vya Yakobo"

Mataifa yatawaleta katika sehemu zao wenyewe

"Mataifa yatarudisha vizazi vya Yakobo katika nchi ya Israeli"

nyumba ya Israeli

Hii ina maana ya Waisraeli, vizazi vya Israeli. "vizazi vya Israeli"

Watachukua mateka wale ambao waliwakamata

"Wanajeshi wa Israeli watachukua kama mateka wale ambao waliwakamata Waisraeli"

Isaiah 14:3

kutoka katika mateso yako na maumivu makali

Neno "yako" ni umoja, lakini lina maana ya watu wa Israeli. Pia, "mateso" na "maumivu makali" ina maana moja na inatumika pamoja kwa msisitizo. "kutoka kwa vitu ambavyo uliteseka navyo sana"

Jinsi mkandamizaji alivyofikia mwishoni

"Mkandamizaji amefikia mwisho". Hii ni hali ya mshangao.

ghadhabu ya wenye kiburi ikaisha

Maneno "jinsi" na "umeisha" inaeleweka. "jinsi ghadhabu ya wenye kiburi imefika mwisho" au "kiburi na ghadhabu yake imekamilika"

ghadhabu ya wenye kiburi ikaisha

"ghadhabu ya wenye kiburi" ina maana ya mfalme wa Babeli kuwa na kiburi na kuwatendea mataifa mengine ukatili. "ukatili wake umefikia mwisho" au "hawezi tena kukandamiza watu"

Isaiah 14:5

Kauli Kiunganishi

Hii ni sehemu ya wimbo wa dhihaki ambao Waisraeli wataimba kwa mfalme wa Babeli.

Yahwe amevunja gongo la waovu

Gongo la waovu huenda lina maana ya kijiti ambacho watu waovu wangepigia watu wengine. Kuvunja kijiti hicho inawakilisha kuangamiza nguvu yao ya kufanyia watu ukatili. "'Yahwe ameangamiza nguvu ya waovu"

fimbo ya kifalme ya hao watawala

Fimbo ya kifalme inawakilisha nguvu ya mtawala kutawala. Kuvunja fimbo ya kifalme inawakilisha kuangamiza nguvu ya watawala. "Yahwe ameangamiza nguvu ya watawala waovu"

iliyowapiga watu

"ambaye aliwapiga watu". Watu waovu walipiga watu kwa gongo lao.

kwa mapigo yasiyokoma

"bila kukoma" au "tena na tena"

iliyotawala mataifa

"ambaye alishinda mataifa mengine"

kwa shaambulio ambalo halikuzuilika

"kuwashambulia bila kuacha"

Isaiah 14:7

Kauli Kiunganishi

Hii ni sehemu ya wimbo wa dhihaki ambao Waisraeli wataimba kwa mfalme wa Babeli.

Dunia nzima

Hii ina maana ya kila mtu duniani. "kila mtu juu ya dunia"

Hata mti wa mvinje unashangilia juu yako pamoja na mierezi ya Lebanoni

Isaya anazungumzia miti kana kwamba ilikuwa watu ambao wanaweza kushangilia. Hii inasisitiza ya kwamba ni jambo kubwa ya kwamba Mungu amezuia mfalme wa Babeli hadi asili inashangilia kama ingeweza. "Itakuwa kana kwamba hata miti ya mvinje na mierezi ya Lebanoni hushangilia juu yako"

unashangilia juu yako

Kwa nini wanashangilia inaweza kuwekwa wazi. "furahia ya kwamba Mungu amekufanya bila nguvu"

Kwa maana umelazwa chini

Kulazwa chini inawakilisha kufanywa bila nguvu na kutokuwa na umuhimu. "Kwa kuwa umekuwa bila nguvu"

Kuzimu chini pana shauku ya kukutana na wewe

Kuzimu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa mtu ambaye ana shauku ya kukutana na wageni wake. Hii inadokeza ya kwamba mfalme amekufa. "Kuzimu ni kama mwenyeji mwenye shauku ya kukutana nawe"

Inaamsha wafu kwa ajili yako, wafalme wote wa dunia

"Inaamsha wafu kwa ajili yako, wafalme wote wa dunia". Kuzimu inazungumzia kana kwamba ilkuwa mtu ambaye anaweza kumsha wale ambao wamo ndani yake". "Wafalme wote waliokufa wa dunia wa kuzimu huamka kukusalimia"

Isaiah 14:10

Kauli Kiunganishi

Hii ni sehemu ya wimbo wa dhihaki ambao Waisraeli wataimba kwa mfalme wa Babeli. Hapa wanaimba juu ya wafalme waliokufa wa kuzimu watakavyosema kwake.

Wote watazungumza na kusema kwako

Neno "wata" lina maana ya wafalme waliokufa wa kuzimu, na neno "kwako" lina maana ya mfalme wa Babeli.

Ufahari wako umeletwa chini mpaka kuzimu

Wafalme waliokufa watazungumza na mfalme wa Babeli kutokuwa na ufahari tena kana kwamba ufahari wake umeshuka chini kuzimu. "Ufahari wako umekwisha pale Mungu alipokutuma hapa kuzimu"

kwa sauti ya nyuzi za vinanda

Watu walifanya muziki kwa njuzi za vinanda kumheshimu mfalme. Wafalme waliokufa hawatawazungumzia watu tena kuheshimi mfalme wa Babeli kwa muziki kana kwamba muziki ulikwenda kuzimu. "pamoja na sauti ya watu wakicheza muziki kukuheshimu"

Funza wanasambazwa chini yako

Funza chini ya mwili wake uliokufa inazungumziwa kana kwamba zilikuwa kitanda. "Unalala juu ya kitanda cha funza" au "Unalala ju funza wengi"

funza hukufunika

Funza katika mwili wake wote inazungumziwa kana kwamba walikuwa wakimfunika kama blangeti. "Funza wanakufunika kama blangeti" au "Kuna funza ju ya mwili wako wote"

Isaiah 14:12

Kauli Kiunganishi

Hii ni sehemu ya wimbo wa dhihaki ambao Waisraeli wataimba kwa mfalme wa Babeli.

Jinsi ulivyonguka kutoka mbinguni, nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi

Nyota ya alfajiri ni nyota inayong'aa ambayo inainuka kabla tu ya asubuhi. Watu wa Israeli watamchukulia mfalme wa Babeli kwa msemo wa hii nyota ili kuonyesha ya kwamba aliwahi kuwa mkuu, lakini sasa hayupo. "Ulikuwa kama nyota inayong'aa ya asubuhi, lakini umeanguka kutoka angani"

Jinsi ulivyokatwa chini ardhini

Watu wa Israeli watazungumzia mfalme wa Babeli kana kwamba alikuwa mti ambao ulikuwa ulikatwa chini. "Umeshindwa kama mti ambao mtu ameukata chini ardhini"

Nitakaa juu ya mlima wa kusanyiko

Hii inagusia kisasili ya kwamba watu wengi katika Mshariki ya Karibu ya Zamani, miungu wa Wakaanani walikutana baraza juu ya mlima katiika sehemu ya kaskazini ya Ashuru. Kukaa juu ya mlima inawakilisha kutawala kwa miungu. "Nitatawala juu ya mlima ambao miungu hukusanyka"

katika mipaka ya mbali ya kaskazini

"katika sehemu za kusni zaidi"

Isaiah 14:15

Kauli Kiunganishi

Hii ni sehemu ya wimbo wa dhihaki ambao Waisraeli wataimba kwa mfalme wa Babeli.

Ingawa sasa unaletwa chini kuzimu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Lakini sasa Mungu amekutuma chini mpaka kuzimu"

Je! huyu ni mtu

Watu watatumia swali hili aidha kumdhihaki mfalme wa Babeli, au kuonyesha mshangao wao ya kile kilichotokea kwake. "Hakika, huyu siye mwanamume"

aliyefanya dunia kutetemeka

Maana zaweza kuwa 1) dunia inatetemeka jeshi la mfalme lilipotembea kuwashinda watu, au 2) hii ina maana ya watu wa dunia kutetemeka kwa hofu juu yake.

kutikisa falme

Maana zaweza kuwa 1) hii sitiari kwa ajili ya "falme zilizodhindwa" au 2) huu ni mfano wa maneno kwa ajili ya "alitisha watu wa falme".

aliyeifanya dunia kama nyika

"ambaye alifanya maeneo ambao watu waliishi kuwa nyika"

Isaiah 14:18

Kauli Kiunganishi

Huu ni mwisho wa wimbo wa dhihaka ambao Waisraeli wataimba kwa mfalme wa Babeli.

wote watalala chini kwa heshima

Hii ina maana ya kwamba miili yao itazikwa kwa naman ya heshima. "wafalme wote ambao wamekufa wanazikwa kwa namna ya heshima"

Lakini umerushwa nje ya kaburi lako

Kurushwa nje ya kaburi inawakilisha kutozikwa. "lakini haujazikwa. Mwili wako umeachwa juu ya ardhi"

kama tawi lililotupwa

Tawi lilitupwa linawakilisha kitu kisichokuwa na thamani. "kama tawi lisilo na thamani ambalo hutupwa kando"

wafu wamekufunika kama vazi

Hii inawakilisha maiti nyingi kuwa juu ya mwili wake. "Miili ya wafu inafunika kabisa mwili wako" au "Miili ya wanajeshi waliokufa imerundikwa juu ya mwili wako"

wale waliochomwa kwa upanga

Hii inaelezea "wafu" ni kina nani katika mwanzo wa sentensi. Kuchomwa na upanga inawakilisha kuuliwa vitani. "wale ambao waliuliwa vitani"

wanaoshuka chini katika mawe ya shimo

Shimo lina maana aidha ya jehanamu, au shimo kubwa katika ardhi ambapo miili mingi ya wafu inatupwa.

Hautajiunga nao katika kuzikwa

Neno "nao" lina maana ya wafalme wengine ambao walikufa na kuzikwa vizuri. Kuwaunga katika kuzikwa inawakilisha kuzikwa kama wao. "hautazikwa kama wafalme wengine walivyozikwa"

Watoto wa waovu hawatatajwa tena

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu atayezungumza tena kuhusu uzao wa waovu"

Isaiah 14:21

Andaa machinjio yako kwa ajili ya watoto wake

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "machinjio" ilelezwa kwa kitenzi "ua"."Jiandae kuwaua watoto wa mfalme wa Babeli"

kwa maana udhalimu wa mababu zao

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "udhalimu" inaelezwa kama kitenzi "tenda dhambi sana". "kwa sababu babu zao walitenda dhambi sana"

ili wasiweze kuinuka juu

Hapa "kuinuka juu" inawakilisha aidha kuwa na nguvu au kushambulia. "ili wasiweze kuwa na nguvu" au "ili wasishambulie"

kumiliki dunia

Hii inawakilisha kutawala juu ya watu wa dunia, katika suala hili kwa kuwashinda wao. "tawala juu ya watu wa dunia" au "washinde watu wa dunia"

na kuijaza dunia nzima kwa miji

Hii inawakilisha kusababisha dunia kuwa na mijij mingi. "na kujenga miji duniani kote"

Nitainuka juu dhidi yao

Hii ina maana ya kwamba Mungu atafanya jambo dhidi yao. neno "yao" lina maana ya watu wa Babeli. "Nitawashambulia" au "Nitatuma watu kuwashambulia"

hili ni tamko la Yahwe wa majeshi

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "tamko" lielezwa kama kitenzi "tamka" au "sema kwa dhati". "hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyotamka" au "hivi ndivyo kile Yahwe wa majeshi alivyosema kwa dhati"

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi wa Israeli.

Nitakata jina la Babeli, uzao, na watoto

"Kukata" inawakilisha kuangamiza. Hapa "Babeli" ina maana ya watu wa Babeli. Pia, "jina" ina maana ya aidha umaarufu wa Babeli au Babeli yenyewe kama ufalme. "Nitaangamiza Babeli, pamoja na watoto wa watu na wajukuu"

Pia nitaifanya

Neno "nitaifanya" ina maana ya mji wa Babeli. Miji mara kwa mara ilizungumziwa kana kwamba ilikuwa wanawake. "Pia nitaifanya"

milki ya bundi

Hii inawakilisha wanyama pori wanaoishi katika mji kwa sababu hakuna watu pale. "sehemu ambayo bundi huishi" au "sehemu ambayo wanyma pori huishi"

na kuwa dimbwi za maji

Kusababisha kuwepo vinamasi au madimbwi ya maji yaliyotulia ambapo mji ulikuwepo inazungumziwa kama kufanya mji kuwa vitu hivyo. "na katika sehemu ambapo kuna madimbwi yaliyotulia"

nitaifagia kwa ufagio wa uharibifu

Hii inawakilisha kuangamiza Babeli kabisa na kuifanya isiwepo tena kana kwamba ilikuwa uchafu usiokuwa na thamani ambao watu hufagia. "Nitaangamiza kabisa, kama kufagia kwa ufagio"

Isaiah 14:24

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli

kama nilivyodhamiria, ndivyo itakavyokua; na kama nilivyokususida, basi ndivyo itakuwa

Misemo hii miwili ina maana moja. "vitu ambavyo nimepanga hakika vitatimia"

nitavunja Ashuru katika nchi yangu

Kuvunja inawakilisha kushinda. "Nitashinda Ashuru katika nchi yangu" au "Nitasababisha Ashuru katika nchi yangu kushindwa"

Ashuru

Hii inawakilisha mfalme wa Ashuru na jeshi lake. "mfalme wa Ashuru na jeshi lake" au "jeshi la Ashuru"

kumkanyaga chini ya mguu

Hii inawakilisha kumshinda kabisa

Kisha nira yake itainuliwa kutoka kwao na mzigo wake kutoka katika bega lao

Hii inaweza kuelezwa kwa kitenzi cha kutenda. "Kisha nitainua nira yake kutoka kwao na mzigowake kutoka katika bega lao"

Kisha nira yake itainuliwa kutoka kwao na mzigo wake kutoka katika bega lao

Misemo hii miwili ina maana moja. Kuinua nira na mzigo inawakilisha kuwaweka watu huru katika utumwa. "Kisha nitawaweka Waisraeli huru kutoka katikautumwa wa Ashuru kama kutoa mzigo mzito kutoka katika mabega yao"

nira yake ... mzigo wake

Neno "yake" ina maana ya Ashuru.

kutoka kwao ... kutoka katika bega lao

Maneno "kwao" na "lao" ina maana ya watu wa Israeli.

Isaiah 14:26

Taarifa ya Jumla

Huyu anaweza kuwa Isaya akizungumza au inaweza kuwa Yahwe akizungumza.

Huu ni mpango ambao umekususdiwa kwa ajili ya dunia nzima

Wazo la "umekusudiwa" linaweza kuelezwa kwa kitenzi cha kutenda."Hu ni mpango ambao Mungu anakududia kwa ajili ya dunia nzima"

na huu ndio mkono ambao umeinuliwa juu ya mataifa yote

Mungu kuwa tayari kuadhibu mataifa inazungumziwa kana kwamba aliinua mkono wake ili kuwapiga. Neno "mkono" unaweza kuwakilisha nguvu yake. "na hii ndiyo nguvu ya Yahwe kuadhibu mataifa yote" au "hivi ndivyo Yahwe atakavyoadhibu mataifa"

ni nani atakayemzuia?

Swali hili linasisitiza ya kwamba hakuna mtu wa kumzuia Yahwe. "hakuna mtu ambaye anaweza kumzuia"

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli.

mkono wake umeinuliwa

Hii inawakilisha Yahwe kuwa tayari kuadhibu mataifa. "Yupo tayari kuwaadhibu"

ni nani atakayeurudhisha?

Swali hili linatumika kusema ya kwamba hakuna mtu anayeweza kugeuza mkono wa Yahwe. Kugeuza mkono wake inawakilisha kumzuia kuadhibu mataifa.

Isaiah 14:28

rungu iliyokupiga imevunjika

Rungu ambayo ilimpiga Filisti inawakilisha mfalme aliyetuma jeshi lake kuwashambulia. Kuvunjika inawakilisha aidha kufa au kushindwa. "mfalme aliyetuma jeshi lake dhidi yako amekufa" au "jeshi ambalo lilikushambulia limeshindwa"

Kwa maana katika mzizi wa nyoka kutaota kifutu ... mtoto wake atakuwa nyoka mkali anayepaa

Misemo hii miwili yote ni taswira ya mtoto wa nyoka kuwa na madhara zaidi ya nyoka. Inawakilisha mrithi wa mfalme kuwa na nguvu zaidi na katili kuliko mfalme wa kwanza.

kifutu

aina ya nyoka mwenye sumu

nyoka mkali anayepaa

Hapa neno "kali" huenda ina maana ya kung'atwa na sumu ya nyoka, na neno "kupaa" ina maana ya kusogea kwake kwa haraka. "nyoka mwenye sumu anayesogea kwa haraka"

mzaliwa wa kwanza wa maskini

Hii inawakilisha maskini zaidi wa watu. "Maskini zaidi wa watu" au "maskini zaidi wa watu wangu"

Nitaua mzizi wako kwa njaa ambaye itawaua wote waliopona wa kwako

Hapa "mzizi wako" ina maana ya watu wa Filisti. "Nitawaua watu wako kwa njaa ambayo itawaua wote waliopona wa kwako"

Isaiah 14:31

Vuma, lango; lia, mji

Hapa "lango" na "mji" inawakilisha watu katika malango ya mji katika miji. "Vuma, enyi watu katika malango ya mji; lieni, nyie watu katika miji"

utayeyuka mbali

Kuyeyuka inawakilisha kuwa dhaifu kwa sababu ya uoga. "utakuwa dhaifi kwa uoga"

Kwa maana katika kaskazini linakuja wingu la moshi

Hii inadokeza ya kwamba jeshi kubwa linakuja kutoka kaskazini. "Kwa maana kutoka kaskazini linakuja jeshi kubwa pamoja na wingu la moshi"

wingu la moshi

Maana zaweza kuwa 1) hii inawakilisha wingu la vumbi ambalo jeshi hutengeneza wanaposafiri katika njia za vumbi. "wingu la vumbi" au 2) kuna moshi mwingi kwa sababu ya vitu vyote ambavyo jeshi linaangamiza na kuchoma. "moshi mwingi"

hakuna mchelewaji katika safu zake

"hakuna aliye katika safu zake anayetembea poole pole nyuma ya wenzake"

Je! mtu atajibu nini kwa wajumbe wa taifa hilo?

Mwandishi anatumia swali hili kutambulisha maagizo yake juu ya jinsi Waisraeli wanatakiwa kuzungumza kwa wajumbe. "Hivi ndivyo tutakavyojibu wajumbe wa Filisti"

Yahwe ameianzisha Sayuni

"Yahwe alianzisha Sayuni"

na ndani mwake

"na Yerusalemu" au "kule"

walioteseka wa watu wake

"wale watu wake ambao walikuwa wameteswa"

Isaiah 15

Isaiah 15:1

Taarifa ya Jumla

Mara kwa mara katika unabii, matukio yajayo yanaelezwa kama yanatokea sasa au katika kipindi cha nyuma. Hii inasisitiza ya kwamba tukio hakika litatokea.

Tamko

"Hiki ni kile ambacho Yahwe anatamka" au "Huu ni ujumbe utokao kwa Yahwe"

Ari ... Kiri ... Diboni ... Nebo ... Medeba

Haya ni majina na miji ya Moabu.

Ari ya Moabu imewekwa kama takataka na kuangamizwa

Maneno "imewekwa kama takataka" na "kuangamizwa" ina maana moja na inasisitiza ya kwamba mji uliharibiwa kabisa. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Majeshi ya adui yataangamiza kabisa Ari ya Moabu"

kwenda juu kileleni kulia

Hapa "juu kileleni" ina maana ya katika hekalu au dhabahu ambalo limejengwa juu ya nchi kama kilima au upande wa mlima. "kwenda juu hekaluni juu ya juu ya kilima kulia"

Moabu huomboleza juu ya Nebo na juu ya Madeba

Majina ya sehemu hizi ina maana ya watu wanaoishi kule. "watu wa Moabu watalia kwa sababu ya kile kilichotokea kwa miji ya Nebo na Medeba"

Vichwa vyao vyote vimenyolewa wazi na ndevu zao zote zimekatwa

Wanafanya hivi kuonyesha huzuni yao kuu. "Wote watanyoa vichwa vyao na kukata ndevu zao na kuhuzunika"

Isaiah 15:3

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza unabii kuhusu watu wa Moabu. Mungu anafafanua matukio ambayo yatatokea wakati ujao kana kwamba inatokea katika wakati wa sasa.

wanavaa nguo ya gunia

Wanafanya hivi kuonyesha huzuni yao kuu. "wanavaa nguo za gunia na kuomboleza"

Heshboni ... Eleale ...Yahasa

Haya ni majina ya miji mikubwa na miji midogo.

Heshboni na Eleale zikapaza sauti

Majina ya miji hii inawakilisha watu wa miji hii. "Watu wa Hebroni na Eleale wanapaza sauti"

wanatetemeka kati yao

Kutetemeka kimwili ni dalili ya hofu. "watakuwa wamejazwa kabisa kwa hofu"

Isaiah 15:5

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza unabii kuhusu watu wa Moabu. Mungu anafafanua matukio ambayo yatatokea katika muda ujao kana kwamba yanatokea katika wakati wa sasa.

Moyo wangu unalia kwa ajili ya Moabu

Moyo unawakilisha hisia. Mungu anazungumzia huzuni yake kubwa kana kwamba moyo wake ulilia kwa sauti. "Nina huzuni sana juu kile kinachoendelea Moabu"

wakimbizi wake hutoroka

"wakimbizi kutoka Moabu watatoroka". Mkimbizi ni mtu ambaye hutoroka ili kwamba adui zake wasiweze kumkamata.

Soari ... Eglathi Shelishiya ... Luhithi ... Horonaimu ... Nimrimu

Haya ni majina ya miji mikubwa na miji midogo.

juu ya uharibifu

Hii inaweza kuelezwa ili kwamba nomino dhahania "uharibifu" inaelezwa kama kitenzi "kuangamizwa". "kwa sababu mji wao umeangamizwa"

wingi

"Kila kitu"

kijito cha mipopla

Hii inaweza kumaanisha mto katika mpaka wa kusini wa Moabu.

Isaiah 15:8

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza unabii kuhusu watu wa Moabu. Mungu anafafanua matukio ambayo yatatokea katika muda ujao kana kwamba inatokea katika muda wa sasa.

Kilio kimeenda kuzunguka eneo la Moabu

Watu kulia na wengine kusikia inazungumziwa kana kwamba kilio kimetoka nje. "Watu juu ya eneo lote la Moabu wanalia"

maombolezo yamefika mbali mpaka Eglaimu na Beer-Elimu

Maneno "yamefika" yanaeleweka. Watu kulia na wengine kusikia inazungumzwa kana kwamba kilio kimetoka na kufika mbali hadi maeneo haya mawili. "kilio kimefika mbali mpaka Eglaimu na Beer-Elimu" au "watu hata umbali wa Elaimu na Beer-Elimu wanalia"

Eglaimu ... Beer-Elimu ... Dimoni

Haya ni majina ya miji mikubwa na miji midogo. Dimoni ulikuwa mji mkuu wa nchi ya Moabu. Baadhi ya tafsiri za kisasa zina "Diboni" badala ya "Dimoni".

lakini nitaleta zaidi juu ya Dimoni

Hapa "nitaleta" ina maana ya Yahwe. Pia, "juu ya Dimoni" ina maana ya watu. "lakini nitasababisha hata matatizo zaidi kwa watu wa Dimoni"

Isaiah 16

Isaiah 16:1

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza unabii kuhusu watu wa Moabu. Mungu anaelezea matukio yatakayotokea katika siku za usoni kana kwamba yanatokea wakati wa sasa. Mstari wa kwanza huenda ndicho Mungu anasema watawala wa Moabu watasema kwao wenyewe.

Tuma kondoo dume kwa mtawala wa nchi

Wamoabu watatuma kondoo dume kwa mfalme wa Yuda ili kwamba aweze kuwalinda kutoka kwa jeshi la adui.

Sela

Hili ni jina la mji.

binti Sayuni

"binti" wa mji ina maana ya watu wa mji. "Watu wa Sayuni" au "Watu wanaoishi Sayuni"

Kama ndege wanaozurura, kama kiota kilivyosambaa, kwa hiyo wanawake wa Moabu watakuwa katika vivuko vya Mto Arnoni

Watu wote wa Moabu, ambayo inajumlisha wanawake, wanalazimishwa kutoroka kutoka kwenye nyumba zao. "Kama ndege wasio na nyumba, wanawake wa Moabu watatoroka kupitia mto hadi nchi nyingine"

Kama ndege wanaozurura, kama kiota kilivyosambaa

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja.

Isaiah 16:3

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza unabii kuhusu watu wa Moabu. Mungu anafafanua matukio ambayo yatatokea katika siku za usoni kana kwamba yatatokea wakati wa sasa. Mistari ya 3 na 4 huenda ni ujumbe ambao watawala wa Moabu hutuma kwa mfalme wa Yuda.

toa kivuli kama usiku katikati ya siku

Joto la katikati ya siku linawakilisha mateso ya Wamoabu kutoka kwa adui zao, na kivuli kinawakilisha ulinzi kutoka kwa maadui wao. Kufafanisha kivuli na usiku inaonyesha ya kwamba wanataka ulinzi imara. "tulinde kikamilifu kutoka kwa adui zetu kama kivuli kikubwa kinavyolinda watu kutoka na jua kali"

Waruhusu waishi miongoni mwenu, wakimbizi kutoka Moabu

"Ruhusu wakimbizi kutoka Moabu kuishi pamoja nawe". Hapa "mwenu" ina maana ya watu wa Yuda.

uwe sehemu ya maficho kwa ajili yao kutoka kwa mharibifu

Kutoa sehemu ya maficho inazungumziwa kama kuwa sehemu ya kujificha. "wapatie sehemu ya kujificha kutoka kwa wale ambao wanajaribu kuwaangamiza" au "wafiche kutoka kwa wale wanaotaka kuwaangamiza"

Isaiah 16:5

ufalme utaimarishwa katika agano la uaminifu

Hapa "ufalme" una maana ya nguvu ya kutawala kama mfalme. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yahwe atakuwa mwaminifu kwa agano na atamteua mfalme"

na mmoja kutoka katika hema la Daudi atakaa pale kwa uaminifu

Hapa "hema la Daudi" inawakilisha familia ya Daudi, ikijumlisha uzao wake. Kukaa juu ya kiti cha enzi inawakilihsa kutawala. "na uzao wa Daudi utatawala kwa uaminifu"

atakapotafuta haki

Kutafuta haki inawakilisha kutaka kufanya kile ambacho ni haki.

Isaiah 16:6

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza unabii kuhusu watu wa Moabu. Mungu anafafanua matukio ambayo yatatokea katika siku za usini kana kwamba yanatokea katika wakati wa sasa.

Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu, majivuni yake, kujidai kwake, na hasira yake

Maneno haya "cha Moabu" na "yake" yana maana ya watu wa Moabu. "Tumesikia ya kwamba watu wa Moabu wana kiburi na majivuni, wanajidai na wana hasira"

Tumesikia

Maana zaweza kuwa 1) Isaya anazungumza na "Tumesikia" ina maana ya kwake na watu wa Yuda, au 2) Mungu anazungumza na "Tumesikia" ina maana ya Mungu.

Lakini kuringa kwake ni maneno matupu

"Lakini kile wanachosema kuhusu wao haina maana yoyote" au "Lakini kile wanachojidai nacho sio cha kweli"

Kwa hiyo Moabu anaomboleza kwa ajili ya Moabu - wote wanaomboleza

"Moabu" inawakilisha watu wa Moabu. "Kwa hiyo watu wa Moabu watalia kwa sauti juu ya kile kilichotokea kwa miji yao"

kwa maana keki ya zabibu kavu ya Kir-Haresethi

"kwa sababu hakuna keki za zabibu kavu katika Kir-Haresethi"

keki ya zabibu kavu

Neno la Kiebrania linalotumiwa hapa lina maana aidha ya "keki ya zabibu kavu" au "wanamume".

Kir-Haresethi

"Kir-Haresethi" ni jina la mji.

Isaiah 16:8

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza unabii kuhusu watu wa Moabu. Mungu anafafanua matukio ambayo yatatokea katika siku za usoni kana kwamba zilitokea katika kipindi cha nyuma.

Heshboni

Haya ni majina ya miji mikubwa na miji midogo.

Sibma ... Yazeri

Haya ni majina ya miji.

Watawala wa mataifa wamekanyaga mizabibu iliyo bora

Nchi ya Moabu ilijulikana kwa mashamba yake ya mizabibu. Hapa Mungu anafafanua nchi ya Moabu kama shamba moja kubwa la mizabibu. Hii inasisitiza ya kwamba watawala, ambao ina maanisha majeshi, waliangamiza kabisa kila kitu ndani ya Moabu.

Isaiah 16:9

Taarifaya Jumla

Hii inaendeleza kufafanua nchi ya Moabu kama shamba kubwa la mizabibu. Mungu anaelezea matukio yatakayotokea katika siku za usoni kana kwamba yanatokea katika wakati wa sasa.

Hasa nitalia

Katika 16:9-10 neno "nitalia" lina maana ya Yahwe.

nitakumwagilia kwa machozi yangu

Mungu anazungumza kuhusu majonzi yake kwa miji hii kana kwamba angelia sana na machozi yake mengi yataanguka juu yao. "Nitalia sana juu yako"

Yazeri ... Sibma

Haya ni majina ya miji

Heshboni ... Eleale

Haya ni majina ya miji mikubwa na miji midogo.

Kwa maana katika mashamba yako ya matunda ya kipindi cha joto na mavuno nimemaliza keleleza shangwe

"kelele za shangwe" zinawakilisha watu kupiga kelele za shangwe juu ya mavuno ya matunda ya miti. "Kwa sababu ya kile nitakachofanya, hautapiga kelele tena ya shangwe utakapovuna mashamba yako ya matunda ya kipindi cha joto"

Nimeweka mwisho kelele za yule ambaye hukanyaga

Hapa "kelele" ina maana ya furaha ya watu wanaokanyaga mizabibu kutengeneza divai. "kwa hiyo watu wanaokanyaga mizabibu hawapigi kelele za furaha"

Isaiah 16:11

Taarifa ya Jumla

Hiiinaendeleza unabii kuhusu watu wa Moabu. Mungu anafafanua matukio ambayo yatatokea katika siku za usoni kana kwamba yanatokea kipindi cha sasa.

Kwa hiyo moyo wangu unashuhsa pumzi kama kinubi cha Moabu

Msemo "moyo wangu" unawakilisha Yahwe na hisia zake za huzuni. Analinganisha kushusha pumzi kama sauti ya wimbo wa huzuni unaochezwa katika kinubi. "Kwa hiyo ninashusha pumzi kama wimbo wa huzuni katika kinubi"

Moabu .. mwenyewe ... lake

Maneno haya yote yana maana ya watu wa Moabu.

kiumbe changu cha ndani kwa ajili ya Kir-Haresethi

Msemo "kiumbe changu cha ndani" inawakilisha Yahwe. Neno "kushusha pumzi" linaeleweka kutoka kwa msemo uliopita. "kiumbe changu cha ndani kwa ajili ya Kir-Haresethi" au "Nina huzuni sana kwa ajili ya watu wa Kir-haresethi"

maombi yake hatatimiza kitu

"maombi yake hayatajibiwa"

Isaiah 16:13

Hili ni neno

"Huu ni ujumbe". Hii ina maana ya kile kilichosemwa katika 15:1-16:12

kuhusu Moabu

Neno "Moabu" lina maana ya watu wa Moabu.

utukufu wa Moabu utatoweka

"Nchi ya Moabu haitakuwa na utukufu tena"

Isaiah 17

Isaiah 17:1

kuhusu Dameski

Dameski ni jina la mji.

miji ya Aroeri itatelekezwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Watu wote watatelekeza miji ya Aroeri"

hakuna atakayewatisha

Neno "atakayewatisha" ina maana ya kondoo

Miji iliyoimarishwa itatoweka kutoka Efraimu

Efraimu ilikuwa kabila kubwa zaidi la Israeli. hapa linawakilisha ufalme wote wa kaskazini wa Israeli. "Miji imara itatoweka kutoka Israeli"

itatoweka

Hii haimaanishi ya kwamba zitapotelea, lakini miji ile itaangamizwa.

ufalme wa Dameski

Maneno "itatoweka" inaeleweka kutoka kwa msemo uliopita. Dameski ilikuwa mahali ambapo mfalme wa Aramu alitawala. Ufalme kutoweka unawakilisha mflame kutokuwa tena na nguvu za kifalme. "ufalme utatoweka kutoka Dameski" au "hapatakuwa na nguvu ya kifalme Dameski"

Aramu

Aramu ni jina la taifa.

watakuwa kama utukufu wa watu wa Israeli

Kwa kuwa watu wa Israeli hawakuwa na utukufu tena, hii ilimaanihsa ya kwamba waliosalia wa Aramu hawatakuwa na utukufu tena. "hawatakuwa na utukufu tena, kama watu wa Israeli" au "Nitaleta aibu juu yao kama nilivyofanya kwa watu wa Israeli"

tamko la Yahwe wa majeshi

Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "tamko" ielezwe kama kitenzi "alitamka" au "alisema kwa dhati". "Hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyotamka" au "hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyosema kwa dhati".

Isaiah 17:4

Itakuja kuwa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya tukio muhimu ambalo litatokea.

utukufu wa yakobo utakuwa mwembamba, na unene wa mwili wake utadhoofika

Hapa "Yakobo" ina maana ya ufalme wa Israeli. Israeli hatakuwa na utukufu tena. Ila atakuwa dhaifu na maskini.

itakuwa kama pale ambapo wavunaji walikusanya nafaka iliyosimama ... katika bonde la Warefai

Hakutakuwa na kitu kinachobaki katika nchi baada ya Mungu kuadhibu watu wa Israeli.

bonde la Warefai

Hili ni bonde ambapo watu kawaida kuotesha na kuvuna chakula kingi.

Isaiah 17:6

Taarifa ya Jumla

Hii inaendelea kulinganisha taifa la Israeli na shamba baada ya kuvunwa.

Masazo ya mavuno yatabaki

Neno "masazo ya mavuno" hapa yanawakilisha watu ambao bado wanaishi Israeli. "Lakini kutakuwa na watu wachache waliosalia Israeli"

kama pale mzeituni unapotikiswa

Watu walivuna mizeituni kwa kutikisa ili kwamba matunda yaweze kudondoka. "kama matunda machache ambayo yanabaki juu ya mizeituni baada ya watu kuivuna"

manne au matano

Neno "matunda" linaeleweka kutoka kwa msemo kabla ya huu. "matunda manne au matano"

hili ni tamko la Yahwe

Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "tamko" ielezwe kama kitenzi "alitamka" au "alisema kwa dhati". "Hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyotamka" au "hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyosema kwa dhati".

wanamume watamtazama kuelekea Muumba wao ... watamtazama Mtakatifu wa Israeli

Kutazama kuelekea Mungu hapa inawakilisha kuwa na tumaini kuwa atawasaidia. "wanamume watakuwa na tumaini ya kwamba Muumba wao, Mtakatifu wa Israeli, atawasaidia"

wanamume watamtazama

Neno "wanamume" linawakilisha watu kwa ujumla. "watu watamtazama"

macho yao yatatazama

Hapa "macho" yanawakilisha watu ambao wanatazama. "watatazama" au"watu watatazama"

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli.

Isaiah 17:8

Hawataangalia katika madhabahu

Kutazama madhabahu kunawakilisha kuabudu sanama kwa tumaini ya kwamba sanamu zitawasaidia. "hawataabudu sanamu katika madhabahu yao" au "Watu wa Israeli hawatakwenda katika madhabahu yao na kuuliza sanamu zao kuwasaidia"

kazi ya mikono yao

Kuzungumzia mikono hapa inasisitiza ya kwamba watu walitengeneza madhabahu au sanamu. "ya kwamba walitengeneza kwa mikono yao" au "ambayo walitengeneza wao wenyewe"

kile vidole vyao kimetengeneza ... nguzo za Ashera au sanamu za jua

Msemo wa pili unatambua vitu ambavyo watu walitengeneza. Kuzungumzia vidole hapa inasisitiza ya kuwa watu walizitengeneza, kwa hiyo vitu hivi sio miungu ya kweli. "nguzo za Ashera au sanamu za jua, ambayo walitengeneza wao wenyewe"

walitelekezwa kwa sababu ya watu wa Israeli

Inaweza kuwekwa wazi ni nani aliacha nchi hii. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ya kwamba Wahivi na Waamori waliacha baada ya watu wa Israeli kuja"

Isaiah 17:10

Kwa kuwa umesahau

Hapa "umesahau" ina maana ya watu wa Israeli. Neno "kusahau haimaanishi hawakuwa na kumbukumbu ya Mungu. Ina maana hawakumtii tena. "Kwa kuwa hamtii tena"

Mungu wa wokovu wako

"Mungu ambaye anakuokoa"

na umepuuzia mwamba wa nguvu yako

Hii inalinganisha Mungu na jiwe kubwa ambalo watu wanweza kupanda kutoka kwa adui zao au kujificha nyuma. "na wamemsahau Mungu, ambaye ni kama mwamba unaowalinda" au "na wamemsahau yule ambaye anawalinda"

mavuno yatashindwa

"hapatakuwa na matunda mengi kwa ajili yako kuvuna"

Isaiah 17:12

Vurumai ya watu wengi, kelele hiyo kama kelele za bahari

Vurumai ni sauti kubwa sana. "Sauti ya watu wengi, ambayo ni kubwa sana kama ya bahari"

kushuka kwa mataifa, kushuka huko kama kushuka kwa maji mengi

Majeshi ya maadui yanaonekana kuwa na nguvu sana ambayo hakuna awezaye kuwazuia. "mataifa wanakuja wakishuka kama maji mengi"

kushuka kwa mataifa

Neno "mataifa" lina maana ya majeshi ya mataifa hayo. "kushuka kwa majeshi ya maadui"

kama majani yaliyokufa juu ya milima kabla ya upepo ... kama majani yanavyozunguka kabla ya dhoruba

Misemo hii miwili ina maana moja. Majeshi wa maadui inaonekana kuwa na nguvu lakini Mungu atawazuia kwa urahisi na kuwafukuza mbali. "kama majani yaliyokufa juu ya milima ambayo upepo huipuliza mbali ... kama majani ambayo huzunguka na kupulizwa mbali ambapo dhoruba hukaribia"

hii ni sehemu ya wale

Kile kinachotokea kwao inazungumziwa kana kwamba ni sehemu ambayo wanarithi. "Hiki ndicho kinachotokea kwa wale"

wanaotupora ... wanaotuibia

Neno "..tupora ...tuibia" lina maana ya Isaya na watu wa Yuda.

Isaiah 18

Isaiah 18:1

Ole nchi yenye mchakarisho wa mabawa, ambayo ipo kando mwa mito ya Kushi

Maana za "mchakarisho wa mabawa" zawezekana kuwa 1) mabawa yanawakilisha mitumbwi ambayo ina matanga. "Ole wao ambao huishi katika nchi ng'ambo ya pili ya mito ya Kushi, ambao meli zao nyingi huonekana kama wadudu juu ya maji" au 2) mchakarisho wa mabawa una maana ya kelele ya wadudu wenye mabawa, huenda nzige.

katika bahari

Mto ulikuwa mpana sana, na watu wa Misri na Kushi waliutaja kama "bahari". "katika mto mkuu" au "katika Mto"

vyombo vya mafunjo

Mafunjo ni mmea mrefu ambao huota kando na Mto mkuu. Watu walifunga pamoja mafungu ya mafunjo kutengeneza makasia. "makasia ya mafunjo" au "makasia yanayotengenezwa kwa matete"

taifa refu na laini ... watu wanaogopwa mbali na karibu ... taifa lenye nguvu na kukanyaga chini, ambayo nchi yake mito huigawanya

Misemo hii yote inaelezea watu wa taifa moja.

taifa refu na laini

Neno "taifa" hapa lina maana ya watu wa taifa hilo. "taifa ambalo watu ni warefu na wana ngozi laini"

watu wanaogopwa mbali na karibu

Maneno "mbali" na "karibu" yanatumika pamoja kumaanisha "kila mahali". "watu ambao wanaogopwa kila mahali" au "watu ambao kila mtu duniani huwaogopa"

taifa lenye nguvu na kukanyaga chini

Kukanyaga chini inawakilisha kushinda mataifa mengine. "taifa ambalo lina nguvu na hushinda mataifa mengine"

mito huigawanya

Huenda hii ina maana ya mito mingi ambayo hutiririka katika taifa ili igawanye katika sehemu tofauti.

Isaiah 18:3

Kauli Kiunganishi

Mstari wa 3 unasema kile wajumbe katika 18:1 wanapaswa kusema kwa watu wa dunia.

Enyi wakazi wote wa duniani ... nyie mnaoishi juu ya dunia

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja. "Nyie watu wote wa duniani"

ishara itakapoinuliwa juu ya milima, tazama; na tarumbeta itakapopulizwa, sikiliza

Ishara na tarumbeta ilikuwa kuwaita watu vitani. Amri za kutazama na kusikiliza ni amri za kuzingatia kwa makini na kujiandaa kwa vita. "zingatia kwa makini pale ambapo ishara inainuliwa juu ya milima na tarumbeta inapopulizwa"

ishara itakapoinuliwa juu ya milima, tazama

Ishara ilikuwa bendera iliyotumika kuwaita watu vitani. Inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. Zingatia kwa makini pale utakapoona bendera ya vita juu ya milima".

tarumbeta itakapopulizwa, sikiliza

Tarumbeta zilitumika kuwaita watu vitani. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "zingatia kwa makini utakaposikia sauti ya tarumbeta za vita".

Isaiah 18:4

Taarifa ya Jumla

Mungu anatumia fumbo kuhusu mkulima katika shamba la mizabibu ili kufafanua kile atakachofanya kwa taifa fulani. Taifa hilo ni kati ya Kushi au adui wa Kushi.

Hiki ndicho Yahwe alichosema kwangu

"Yahwe aliniambia". Hapa neno "kwangu" ina maana ya Isaya.

Nitachunguza kwa utulivu kutoka kwenye nyuma yangu

Kile Mungu atakachochunguza kinaweza kuwekwa wazi. "Nitachunguza taifa hilo kwa utulivu kutoka nyumbani kwangu" au "Kutoka nyumbani kwangu, nitatazama kwa utulivu kile ambacho watu wa taifa hilo wanachofanya"

kama joto linalochemka pole pole katika mwanga wa jua, kama wingu la umande katika joto la mavuno

Misemo hii inaonyesha jinsi gani Mungu atazama taifa kwa utulivu.

Kabla ya mavuno

"Kabla ya mavuno ya zabibu"

pale ambapo uchanuzi umekamilika

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba hii ina maana ya kuchanuka juu ya mizabibu. "pale ambapo maua yamekamilisha kuota juu ya mizabibu"

atayakata matawi

Kama mkulima anaona ya kwamba tawi jipya halizai tunda, atalikata. "mkulima atakata matawi ambayo hayazai matunda"

makasi ya kupogolea

Mkasi wa kupogolea ni kisu ambacho watu hutumia kukata matawi katika mizabibu au mimea mingine.

atakata chini na kuondoa matawi yaliyotawanyika

Kama mkulima anaona ya kwamba tawi limeota sana na linafanya mzabibu wote kutozaa matunda mengi, ataukata na kuutupa.

Isaiah 18:6

Wataachwa pamoja

Inaonekana Mungu anabadilisha kutoka kuelezea fumbo na kuzungumzia moja kwa moja juu ya taifa. Hii inaweza kuwekwa wazi. "Wale ambao wanauawa wataachwa pamoja" au "Kama matawi yanayokatwa na kutupwa, miili ya wale ambao wameuawa wataachwa juu ya nchi"

Ndege watakuwa juu yao wakati wa kiangazi

"Ndege zitawala wakati wa kiangazi". Maneno "ndege" yana maana ya ndege ambao hula nyama ya miili iliyokufa.

wanyama wote wa duniani

"aina zote za wanyama pori"

watakuwa juu yao wakati wa baridi

"watawala katika kipindi cha baridi"

watu warefu na laini ... watu wanaogopwa mbali na karibu .... taifa lenye nguvu na kukanyaga chini, ambayo nchi yake imegawanywa na mito

Misemo hii yote inaelezea watu wa taifa kubwa.

watu warefu na laini

"watu ambao ni warefu na wenye ngozi laini"

watu wanaogopwa mbali na karibu

Maneno "mbali" na "karibu" yanatumika pamoja kumaanisha "kila mahali". "watu ambao wanaogopwa kila mahali" au "watu ambao kila mtu duniani anawaogopa".

taifa lenye nguvu na kukanyaga chini

Kukanyaga chini inawakilisha kushinda mataifa mengine. "taifa ambalo lina nguvu na hushinda mataifa mengine"

mpaka mahali penye jina la Yahwe wa majeshi, kwa mlima Sayuni

Neno "jina" lina maana ya Yahwe. "mpaka Mlima Sayuni, ambapo Yahwe wa majeshi hukaa"

Isaiah 19

Isaiah 19:1

Tazama

"Angalia" au "Sikiliza". Neno hili linaongeza msisitizo kwa kile kinachosemwa baadaye.

Yahwe anaendesha juu ya wingu jepesi

Yahwe anaonekana kupigwa picha hapa akiendesha juu ya wingu kana kwamba alikuwa akiendesha katika kibandawazi.

sanamu za Misri zinatetemeka mbele zake

Sanamu zinaelezwa kama kuwa na hisia za uoga Yahwe anapokaribia. "sanamu za Misri zinatetemeka kwa uoga mbele za Yahwe"

na mioyo ya Wamisri zinayeyuka ndani mwao

Moyo kuyeyuka kunawakilisha kupoteza ujasiri wake. "na Wamisri hawana ujasiri tena"

mwanamume dhidi ya jirani yake

Maneno "atapigana" inaeleweka kutoka kwa msemo uliopita. "mwanamume atapigana dhidi ya jirani yake"

mji utakuwa dhidi ya mji

Neno "mji" unawakilisha watu wa mji. "watu wa mji mmoja watapigana dhidi ya watu wa mji mwingine" au "watu kutoka miji tofauti watapigana dhidi yao wenyewe"

ufalme dhidi ya ufalme

Manebo "utakuwa" au "utapigana" inaeleweka kutoka kwa misemo ya nyuma. "ufalme utakuwa dhidi ya ufalme" au "ufalme utapigana dhidi ya ufalme"

ufalme dhidi ya ufalme

Neno "ufalme" una maana ya ufalme mdogo ndani ya Misri. Pia inaweza kuitwa mkoa. Inawakilisha watu wa ufalme huo au mkoa. "watu wa mkoa mwingine watakuwa dhidi ya watu wa mko mwingine" au "watu kutoka mikoa tofauti watapigana dhidi yao wenyewe"

Isaiah 19:3

Roho ya Misri itadhoofishwa kutoka kwa ndani. Nitaangamiza ushauri wake

Taifa la Misri linazungumziwa hapa kana kwamba lilikuwa mtu.

Roho ya Misri itadhoofishwa kutoka kwa ndani

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nitadhoofisha roho ya Misri kwa ndani"

Nitaangamiza ushauri wake

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "ushauri" inaelezwa kama kitenzi "shauri". "Nitawachangnaya wale amabo wanamshauri mfalme"

ingawa

"ingawa" hata kama"

waganga ... wachawi

Hawa ni watu ambao wanadai kuzungumza na wale ambao wamekufa.

Nitawapa Wamisri katika mikono ya bwana mkali

Hapa "mkono" ina maana ya nguvu na tawala. "Nitatoa Wamisri katika utawala wa bwana mkali"

hili ni tamko la Bwana , Yahwe wa majeshi

Nomino dhahania "tamko" linaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "hivi ndivyo Bwana, Yahwe wa majeshi, anavyosema"

Isaiah 19:5

Maji ya bahari yatakauka, na mto utakauka na kuwa tupu

Wamisri walimaanisha Mto Nile kama "bahari". Misemo hii miwiwli ina maana. "Mto Nile utakauka kabisa"

itakuwa chafu

"kutoa harufu mbaya" au "kunuka"

itafifia

"kuwa chini"

matete na mianzi itasinyaa

"Matete" na "mianzi" ina maana ya aina mbili ya mimea ya maji. "mimea katika mto itakufa na kuoza"

Isaiah 19:7

mashamba yaliyopandwa ya Nile

"mashamba karibu na Mto Nile ambapo watu wamepanda mazao"

wavuvi watalia na kuomboleza, na wote ambao hurusha ndoano katika Mto wataomboleza, na wale ambao hutawanya nyavu katika maji watahuzunika

Misemo hii mitatu ina maana moja. Ikibidi, sababu ya wao kuhuzunika inaweza kuwekwa wazi. "Wavuvi ambao hushika samaki kwa ndoano au nyavu watabeba kwa kufa moyo kwa sababu samaki wa Nile watakuwa wamekufa"

hurusha ndoano katika Mto Nile

Ili kukamta smaki, baadhi ya watu waliweka chakula kidogo katika ndoano, kufunga ndoano katika kamba, na kurusha ndoano katika maji. Samaki anapojaribu kula chakula, mdomo wake unanaswa katika ndoano, na mtu huvuta samaki nje ya maji.

hurusha

"rusha"

kutawanya nyavu juu ya maji

Ili kukamata samaki, baadhi ya watu hutupa wavu juu ya maji. Samaki anapokamtwa ndani yake, wanavuta wavu na samaki nje ya maji.

Isaiah 19:9

Watumishi katika kitani kilichochanwa na wale ambao hufuma nguo nyeupe watakwajuka. Watumishi wa nguo wa Misri watapondwa

Misemo hii miwili ina maana moja. Ikibidi, sababu ya wao kufadhaika inaweza kuwekwa wazi. "Watengeneza kitani wa Misri wataaibishwa kwa sababu hakuna kitani"

Watumishi katika kitani kilichochanwa

"Wale ambao wanafanya kazi na kitani iliyochanwa"

kitani kilichochanwa

Kitani ni mmea ambao huota katika Mto Nile. Watu kuchana utembo wake ili kuzigawanyisha, na kuzitumia kutengeneza uzi kwa ajili ya nguo ya kitani.

watakwajuka

"wataaibika"

Watumishi wa nguo

"Watu wa Misri ambao hutengeneza nguo"

watapondwa

Kupondwa inawakilisha hali ya kukata tamaa. "atavunjika moyo"

wanaofanya kazi ya kuajiriwa

"wanaofanya kazi kwa malipo"

watahuzunika ndani mwao

"watajisikia huzuni sana"

Isaiah 19:11

Wakuu wa Soani ni wapumbavu kabisa. Ushauri wa washauri wenye hekima kabisa wa Farao umekuwa hauna maana

Misemo hii miwili ina maana moja. Aidha wakuu wa Soani ndio washauri wenye hekima kabisa au Farao, au kuna kundi lingine la watu ambalo pia linaonyeshwa kuwa pumbavu.

Soani

Huu ni mji katika Misri ya kaskazini.

Unawezaje kusema kwa Farao ... wafalme?

Isaya anatumia swali kukejeli wale walio Misri wanaodai kuwa na hekima. "Mnasema kwa upumbavu kwa Farao ... wafalme"

Wako wapi basi wanaume wenu wenye hekima?

Isaya anatumia swali kukejeli wanaume wenye hekima. Neno "wenu" ina maana ya Farao. "Hauna wanaume wowote wenye hekima" au "Wanaume wako wenye hekima ni wapumbavu"

Waache wakuambie na kufanya kujulikana kile Yahwe wa majeshi anapanga kuhusu Misri.

isaya anadokeza ya kwamba wanamume wenye hekima wanatakiwa kuweza kuelewa mipango ya Mungu, lakini Isaya haamini kiukweli kuwa wana hekima. "kama walikuwa na hekima kweli, wangeweza kukuambia kile Yahwe wa majeshi anavyopanga kuhusu Misri"

Isaiah 19:13

wamefanya Misri ipotoke, ambayo ni jiwe la pembeni la makabila yake

Wakuu wa Soani na Nofu wanazungumziwa kana kwamba wao ni jiwe la pembeni la majengo kwa sababu wao ni sehemu muhimu katika jamii. "viongozi wamefanya Misri kupotoka"

wakuu wa Soani

Soani ni mji kaskazini mwa Misri.

Nofu

Huu ni mji katika sehemu ya kaskazini ya Misri.

wamefanya Misri ipotoke

Neno "Misri" linawakilisha watu wa Misri. Kupotoka kunawakilisha kufanya kilicho kibaya. "kufanya watu wa Misri kupotoka" au "kufanya watu wa Misri kufanya kilicho kibaya"

Yahwe amechanganya roho ya upotoshaji miongoni mwake

Isaya anazungumzia hukumu ya Yahwe kana kwamba Misri ilikuwa kikapu cha divai. Anazungumzia Yahwe kusababisha mawazo ya viongozi kupotoshwa kana kwamba mawazo yao yaliyopotoka yalikuwa kimiminiko ambacho Yahwe alichanganya kwa divai. "Yahwe amewahukumu kwa mawazo yao yaliyopotoka" au "Yahwe amewahukumu Misri kwa kupotosha mawazo ya viongozi wao, kama vinywaji vinavyolewesha huchanganya mawazo ya watu"

upotoshaji

"upotovu" au "mchafuko"

miongoni mwake

Hapa "mwake" ina maana ya Misri. Mataifa mara kwa mara huzungumziwa kana kwmaba ilikuwa wanawake. "ndani ya Misri"

wameiongoza Misri kupotea

Hapa "wameiongoza" ina maana ya viongozi wanaoelezwa katika mistari iliyopita. Neno "Misri" inawakilisha watu wa Misri. "wakuu wamewaongoza watu wa Misri kupotoka"

wameiongoza Misri kupotea

Kuongoza watu kupotoka inawakilisha kuwashawi kufanya kilicho kibaya.

kama mlevi anayepepesuka katika matapishi yake

Isaya anazungumzia watu wa Misri kufanya kilicho kibaya kana kwamba walifanywa kuzurura kama mtu mlevi.

kama kichwa au mkia

"Kichwa" ni sehemu ya mnyama au mtu anayopenda awe, inawakilisha kiongozi. "Mkia" ni kinyume na inawakilisha watu wanaofuata. "kama kiongozi au mfuasi"

tawi la mnazi au tete

"tawi la mnazi" huota juu ya mti na linawakilisha watu ambao ni tajiri na muhimu. "Tete" huota katika maji mafupi na inawakilisha watu ambao ni maskini na wasio na umuhimu. "kama wao ni muhimu au sio muhimu" au "kama ni tajiri au maskini"

Isaiah 19:16

Wamisri watakuwa kama wanawake

Hii inasisitiza ya kwamba watu wa Misri wataogopa na kutojiweza Mungu anapowaadhibu.

kwa sababu ya mkono wa Yahwe wa majeshi usiosifiwa

Hapa "mkono" una maana ya nguvu ya Mungu, na kuinua mkono dhidi yao inawakilisha kuwaadhibu wao. "kwa sababu Yahwe wa majeshi ameinua mkono wake wa nguvu kuwaadhibu"

nchi ya Yuda itakuwa sababu ya kupepesuka kwa Misri

"nchi ya Yuda" na "Misri" ina maana ya watu katika maeneo hayo. Wamisri watapepesuka kwa sababu wanaogopa. "Watu wa Yuda watasababisha Wamisri kupepesuka" au "Watu wa Yuda watasababisha Wamisri kuogopa sana"

Wakati wowote mtu yeyote anawakumbusha juu yake, wataogopa

Hapa, "anawakumbusha" na "wataogopa" ina maana ya Wamisri na "yake" ina maana ya watu wa Yuda. "Wakati wowote mtu yeyote anawakumbusha Wamisri wa watu wa Yuda, Wamisri wataogopa"

Isaiah 19:18

kutakuwa na miji mitano katika nchi ya Misri ambayo inazungumza

Hii ina maana ya watu wa miji ile. "watu katika miji mitano ya Misri watazungumza"

lugha ya Kaanani

Hii ina maana ya Kiebrania, lugha ya watu wa Mungu wanaoishi katika nchi ya Kanaani. "lugha ya watu wa Kanaani"

kutoa kiapo cha utii

"ahidi kuwa mwaminifu"

Moja ya miji hii itaitwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wataziita moja ya miji hii"

itaitwa Mji wa Jua

Haipo wazi kama neno la Kiebrania linalotafsiriwa "Jua" hapa lina maana ya "jua" au "uharibifu". Haipo wazi ni nini jina linasema juu ya mji. "mji unoitwa 'Mji wa Jua'" au "mji unaoitwa "Mji wa Uharibifu"

Isaiah 19:19

jiwe la nguzo katika mpaka wa Yahwe

Msemo "mpaka" ina maana ya mpaka wa Misri. "jiwe la nguzo kwa Yahwe katika mpaka wa Misri"

itakuwa kama ishara na shahidi kwa Yahwe wa majeshi katika nchi ya Misri

Nomino dhahania "ishara" na "shahidi" inaweza kuelezwa kwa vitenzi "onyesha" na kuthibitisha. "Dhabahu itaonyesha na kuthibitisha ya kwamba Yahwe wa majeshi yupo katika nchi ya Misri"

kwa Yahwe wa majeshi katika nchi ya Misri

Yahwe kuwa katika nchi ya Misri inawakilsiha watu wa Misri kumuabudu yeye. "ya kwamba watu katika nchi ya Misri humwabudu Yahwe wa majeshi"

Watakapomlilia

"Wamisri watakapolia"

kwa sababu ya wakandamizaji

"kwa sababu watu wanatendea kwa ukatili" au "kwa sababu wengine wanasababisha wao wateseke"

atawatumia mkombozi na mtetezi

"Yahwe atamtuma mtu kuwaokoa na kuwatetea Wamisri"

atawaokoa

Nani ambaye Yahwe atatetea kwao inaweza kuwekwa wazi. "Yahwe atawaokoa Wamisri kutoka kwa wakandamizaji wao"

Isaiah 19:21

Yahwe atajulikana kwa Misri

Hapa "Misri" ina maana ya watu wa Misri. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawafanya watu wa Misri kumjua"

watamtambua Yahwe

"watapokea ukweli juu ya Yahwe" au "watakubaliana na ukweli juu ya Yahwe"

Watamwabudu

Kitu cha ibaada yao kinaweza kuwekwa wazi. "Watamwabudu Yahwe"

watatoa viapo kwa Yahwe na kuzitimiza

'"watatoa ahadi kwa Yahwe na kuzishika" au "'watatoa ahadi kwa Yahwe na watafanya kile walichokiahidi kufanya"

Yahwe ataiumiza Misri

Hapa, "Misri" ina maana ya watu wa Misri. "Yahwe ataumiza watu wa Misri"

umiza

"kupiga" au "kuadhibu"

kuwaumiza na kuwaponya

Neno "wao" linaeleweka katika msemo huu. "kuwaumiza wao na kuwaponya wao"

kuwaumiza na kuwaponya

Jinsi msemo huu unavyohusiana na msemo kabla yake unaweza kuwekwa wazi kwa maneno '"baada" na "pia". "na baada yake kuwaumiiza, pia atawaponya"

Isaiah 19:23

kutakuwa na barabara

Barabara ni njia kubwa ambayo watu wanaweza kusafiri

Muashuru atakuja

"Muashuru" ina maana ya mtu kutoka Ashuru lakini inawakilisha yeyote kutoka Ashuru ambaye anatoka Misri. "Waashuru atakuja"

na Mmisri mpaka Ashuru

Neno "atakuja" linaeleweka. "na Mmisri atakuja mpaka Ashuru"

Mmisri

Hii ina maana ya mtu kutoka Misri, lakini inawakilisha yeyote kutoka Misri ambaye anakuja Ashuru. "Wamisri"

Mmisri ataabudu pamoja na Waashuru

Kitu cha ibaada yao kinaweza kuwekwa wazi. . "Wamisri na Waashuru watamwabudu Yahwe"

Isaiah 19:24

Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru

Majina ya mataifa matatu yanawakiliisha watu wa mataifa hayo. "Waisraeli watakuwa wa tatu pamoja na Wamisri na Waashuru"

atakuwa wa tatu pamoja na

Maana zaweza kuwa 1) "kujiunga pamoja na" au 2) "kuwa na baraka ya tatu pamoja na" au 3) "'kuwa sawa na"

Misri na ibarikiwe, watu wangu; Ashuru, kazi ya mikono yangu; na Israeli, urithi wangu

Majina ya mataifa matatu yana maana ya watu wa mataifa yale. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nimekubariki, watu wa Misri, kwa sababu wewe ni mtu wangu; na nimekubariki, watu wa Ashuru, kwa sababu nimekuumba; na nimekubariki, watu wa Israeli, kwa sababu ninakumiliki kwa usalama"

kazi ya mikono yangu

Hapa "mikono" ina maana ya nguvu ya Mungu na matendo.

Isaiah 20

Isaiah 20:1

jemadari yule

Jina la kamanda mkuu wa majeshi ya Ashuru

Sargoni

jina la mfalme wa Ashuru

alipigana dhidi ya Ashdodi na kuuchukua

Ashdodi ina maana ya jeshi la Ashdodi. "alipigana dhidi ya jeshi la Ashdodi na kulishinda"

kutembea uchi na peku

"kutembea tembea bila nguo na bila ndara". Hapa neno "uchi" huenda ina maana ya kuvaa nguo zake za ndani pekee.

Isaiah 20:3

na ishara

"na tahadhari"

kuhusu Misri na kuhusu Kushi

Majina ya sehemu yana maana ya watu wake. "kuhusu watu wa Misri na watu wa Kushi"

mfalme wa Ashuru atawaongoza mbali mateka

Mfalme huamrisha jeshi lake kufanya kazi hii. "mfalme wa Ashuru atalifanya jeshi lake kuwaongoza mbali mateka"

atawaongoza mbali mateka wa Misri, na walio hamishwa wa Kushi

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba watashambulia kwanza na kukamata watu. "watashambulia Misri na Kushi na kukamata watu wake na kuwaongoza mbali"

kwa aibu ya Misri

Misri ina maana ya watu wa Misri. "ambayo italeta aibu juu ya watu wa Misri"

Isaiah 20:5

watafadhaishwa na kuaibika

"kuogopa na kupata aibu"

kwa sababu ya Kushi tumaini lao na ya Misri utukufu wao

Tumaini na utukufu ina maana ya imani yao katika nguvu ya jeshi ya nchi hizi. "kwa sababu waliamini katika nguvu ya majeshi ya Kushi na Misri"

wakazi wa pwani hizi

watu ambao waliishi katika nchi zinazopakana na Bahari ya Mediteranea

ambapo tulikimbilia kwa ajili ya msaada kukombolewa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambapo tuliporokea ili kwamba waweze kutukomboa"

na sasa, tutatorokaje?

Mwandishi anatumia swali hili kusisitiza jinsi hali yao ilivyokosa tumaini. "Sasa hakuna njia kwa ajili yetu kutoroka!"

Isaiah 21

Isaiah 21:1

Tamko

"Hivi ndivyo Yahwe anavyotamka" au "Huu ni ujumbe wa Yahwe"

kuhusu jangwa karibu na bahari

Hii ina maana ya watu ambao wanaishi babeli kama kuwa jangwa, ingawa Mungu bado hajapafanya kuwa jangwa. Tukio hili hakikalitatokea. "kuhusu watu wanaoishi katikanchi ambayo punde itakuwa jangwa"

Kama upepo wa dhoruba unavyofyeka katikati ya Negebu

Isaya analinganihsa jeshi ambalo litashambulia watu na dhoruba yenye upepo mkali. Watakuwa na kasi na nguvu.

kutoka nyikani

Hapa "nyikani" ina maana ya nyika ya Yuda.

kutoka katika nchi ya kutisha

Jeshi linatokana na watu ambao husababisha hofu kubwa.

maono ya kudhihikisha yameletwa kwangu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yahwe alinionyesha maono ya kusumbua akili"

mwanamume mdanganyifu anafanya udanganyifu

"wale wanaodanganya watadanganya"

na mharibifu huharibu

"na wale wanaoharibu wataharibu"

Nenda juu na ushambulie, Elamu; izingire, Umedi

Katika maono yaliyopatiwa Isaya, Yahwe anazungumza kwa majeshi ya Elamu na Umedi kana kwamba walikuwa wakimsikiliza.

Nenda juu na ushambulie, Elamu; izingire, Umedi

Inaeleweka ya kwamba wanapaswa kushambulia Wababeli. "Nenda juu na ushambulie Wababeli, nyie wanajeshi wa Elamu; nendeni na muwazingire Wababeli, nyie wanajeshi wa Umedi"

Elamu ... Umedi

Hapa "Elamu" na "Umedi" inawakilisha wanajeshi kutoka maeneo haya.

Nitakomesha minung'uniko yake yote

Hapa "yake" inawakilisha watu wote ambao wanateseka kwa sababu ya Wababeli. Yahwe atasababisha kuacha kulalamika atakapotuma majeshi ya elamu na Umedi kuangamiza Wababeli.

Isaiah 21:3

viuno vyangu vimejaa maumivu

Maono haya ambayo Isaya anayaona yanasumbua yanasababisha maumivu kwake. Hapa anaelezea maumivu na mkakamao katika sehemu ya kati ya mwili wake.

maumivu kama maumivu ya mwanamke katika uchungu vimenikamata

Isaya analinganisha maumivu yake na maumivu ya mwanamke anayezaa. Hii inasisitiza maumivu makubwa anayosikia.

nimeinama chini kwa kile nilichosikia

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kile nilichosikia kimenisababisha kuinama chini kwa maumivu"

nimesumbuliwa kwa kile nilichokiona

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kile nilichoona kimenisumbua sana"

Moyo wangu unadunda, ninatetemeka kwa hofu

"Moyo wangu unapiga haraka na ninatetemeka"

Isaiah 21:5

Wanaandaa

Hapa "wanaandaa" ina maana ya viongozi wa Babeli.

andaa meza

Hapa "meza" inawakilisha chakula ambacho watu watakula katika karamu.

inuka, wakuu

Hapa "wakuu" ina maana kwa ujumla wanamume wenye mamlaka na sio lazima wana wa wafalme.

pakeni ngao zenu kwa mafuta

Wanajeshi wangepaka mafuta juu ngao zao za ngozi ili kwamba ziweze kuwa laini na zisipasuke wakati wa vita.

Isaiah 21:6

weka mlinzi

"mwambie mlinzi asimame juu ya ukuta wa Yerusalemu"

kibandawazi, jozi ya wapanda farasi

"mwanajeshi anaendesha katika kibandawazi, jozi ya farasi ikiivuta"

Isaiah 21:8

Bwana, nasimama juu ya mnara

Hapa "Bwana" ina maana ya mtu mwenye mamlaka ambaye alimuamuru mlinzi kusimama juu ya ukuta wa Yerusalemu.

Babeli imeanguka, imeanguka

Babeli kushindwa kabisa na adui zake inazungumziwa kana kwamba Babeli imeanguka. Hapa "Babeli" ni mfano wa maneno unawakilisha watu wa Babeli. "Watu wa Babeli wameshindwa kabisa"

imeanguka, imeanguka

Neno "imeanguka" inarudiwa kusisitiza ya kwamba watu wa Babeli walishindwa kabisa na adui zao.

Isaiah 21:10

Wale niliowapukuta na kuwapembua, watoto wa sakafu yangu ya kupukuchua

Watu wa Israeli kuteseka kwa sababu ya Wababeli inazungumziwa kana kwamba watu walikuwa nafaka ambayo ilipukukutwa na kupembuliwa.

niliowapukuta

neno "yangu" ina maana ya Isaya.

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli.

Isaiah 21:11

Tamko

"Hivi ndivyo Yahwe anavyotamka" au "Huu ni ujumbe kutoka kwa Yahwe"

kuhusu Duma

Hili ni jina lingine kwa ajili ya Edomu. Hapa "Duma" inawakilisha watu wanaoishi kule. "kuhusu watu wa Duma" au "kuhusu watu wa Edomu"

Mtu ananiita kwangu

Hapa "ananiita" ina maana ya Isaya.

Seiri

Hili ni jina la milima ya magharibi mwa Edomu.

Mlinzi, nini kimebaki usiku? Mlinzi, nini kimebaki usiku?

Hii inarudiwa kusisitiza ya kwamba mtu yule anayeuliza swali ana wasiwasi na woga.

kama unataka kuuliza, basi uliza; na urudi tena

"Niulize sasa kile unachotaka kujua, lakini pia uje baadaye uniulize tena"

Isaiah 21:13

Tamko

"Hivi ndivyo Yahwe anavyotamka" au "Huu ni ujumbe kutoka kwa Yahwe"

kuhusu Arabuni

Arabuni ina maana ya idadi ya watu wa Arabuni. "kuhusu watu wa Arabuni"

Katika nyika ya Arabuni

Arabuni haina msitu. "mbali kutoka na barabara ya Arabuni" au "Nje katika vichaka vya Arabuni"

misafara

kikundi cha watu wanaosafiri pamoja

Wadedani

Hili ni kundi la watu ambao wanaishi Arabuni.

nchi ya Tema

Hili ni jina la mji Arabuni.

wakimbizi

Mkimbizi ni mtu ambaye hukimbia mbali ili adui wake asimkamate.

kwa mkate

Hapa "mkate" inawakilisha chakula kwa ujumla.

kutoka kwa upanga, kutoka kwa upanga uliotolewa, kutoka kwa upinde uliopindwa

Hapa "upanga" na "upinde" unawakilisha wanajeshi wanaoshambulia wakazi wa Tema. "kutoka kwa adui zao ambao huwashambulia kwa upanga na upinde"

kutoka kwa uzito wa vita

Hofu kuu na mateso ambayo inapitiwa wakati wa vita inazungumziwa kana kwamba vita ilikuwa uzito mkubwa juu ya watu. "kutoka na vitisho vya vita"

Isaiah 21:16

kama mwajiriwa alivyoajiriwa kwa mwaka atakavyoona

"kama mwajiri aliyeajiriwa atakavyohesabu siku za mwaka". Mtumishi aliyeajiriwa ni mwangalifu kuhesabu siku ili kwamba afanye kazi kwa muda husika anaolipwa kufanya. Hii ina maana Kedari itashindwa ndani ya mwaka mmoja kamili.

wa Kedari

Hili ni eneo kule Uarabuni. Kedari inawakilisha idadi ya watu wa Kedari. "ya watu wa Kedari"

Isaiah 22

Isaiah 22:1

Tamko

"Hivi ndivyo Yahwe anachotamka" au "Huu ni ujumbe wa Yahwe"

juu ya bondo la maono

Hapa "Bonde" ina maana ya wale ambao wanaishi katika bonde, yaani, Yerusalemu. "juu ya wale ambao wanaishi katika Bonde la Maono" au "kuhusu wale ambao wanaishi Yerusalemu"

Ni sababu ipi ambayo wote mmekwenda juu ya dari za nyumba

Isaya anatumia swali kukaripia watu wa Yua. "'Hautakiwi kwend na kusimama juu ya dari za nyumba"

mji uliojaa shangwe

"mji uliojaa watu wanaoshangilia"

Wafu wako hawakuawa kwa upanga

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Wanajeshi maadui hawakuwaua watu wako"

kwa upanga

Hapa "upanga" inawakilisha wanajeshi ambao hupigana vitani.

Isaiah 22:3

lakini walikamatwa bila upinde

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "lakini adui aliwakamata watawala wako ambao hata hawakuwa wakibeba upinde"

wote walikamatwa na kushikwa pamoja

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "adui aliwakamata na kuwashika wote pamoja"

Kwa hiyo nikasema

Hapa "Mimi" ina maana ya Isaya

wa binti wa watu wangu

Hapa "binti" inawakilisha watu na inaweza kudokeza hisia za Isaya za upendo kwa ajili yao. "'wa watu wangu ambao nampenda" au "wa watu wangu"

Isaiah 22:5

Kwa maana kuna siku

Hapa "siku" ina maana ya kipindii kirefu cha muda. "Kwa maana kutakuwa na muda"

ya ghasia, kukanyagwa chini, na kuchanganyikiwa kwa ajili ya Bwana, Yahwe wa majeshi

"pale Yahwe wa majeshi atasababisha hofu kubwa, kukanyagwa chini, na kuchanganyikiwa

kukanyagwa chini

Maana zaweza kuwa 1) hii ina maana ya wanajeshi wakitembea au 2) watu kwa ujumla wanakimbia kwa hofu kubwa na kutokuwa na uhakika wapi pa kwenda.

katika Bonde la Maono

Hapa "Bonde" ina maana ya wale ambao wanaishi katika bonde, yaani, Yerusalemu. "juu ya wale ambao wanaishi katika Bonde la Maono" au "kuhusu wale ambao wanaishi Yerusalemu"

watu kulia katika milima

Maana zaweza kuwa 1) "watu katika milima watasikia sauti zao" au 2) "milio ya watu inasikika katika milima"

Elamu anabeba podo

Podo ni mfuko wa kubeba mishale na inawakilisha silaha za mpiga mshale. "Wanajeshi wa Elamu huchukua upinde zao na mishale"

Kiri anaweka wazi ngao

Hapa "Kiri" inawakilisha wanajeshi. "wanajeshi wa Kiri watabeba ngao zao nje ya makasha yao"

Kiri

Kiri ni mji wa Media.

mabonde yako mazuri

Hapa "yako" ina maana ya watu wa Yerusalemu. Isaya hajijumlishi mwenyewe kama mmoja wa watu wa Yerusalemu. "mabonde yetu mazuri"

Isaiah 22:8

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua kipindi katika siku za usoni ambapo jeshi litashambulia watu wa Yerusalemu. Vitenzi vya wakati uliopita vinaweza kutafsiriwa kwa vitenzi vya wakati unaokuja.

Aliondoa ulinzi wa Yuda

Nomino dhahania "ulinzi" inaweza kuwekwa kama kitenzi. "Yahwe atachukua kila kitu ambacho kiliwalinda watu wa Yuda"

ukaangalia katika siku hiyo kwa ajili ya silaha

Hapa msemo "kuangalia" ina maana ya kuamini katika jambo. "ili kujilinda utachukua silaha"

Kasri ya Msitu

Hii ilikuwa sehemu ya hekalu Yerusalemu ambapo walihifadhi silaha zao.

ulikusanya maji ya dimbwi la chini

Watu watahifadhi maji ili kwamba waweze kuwa na maji ya kunywa ya kutosha huku adui zao wakizunguka mji.

Isaiah 22:10

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua kipindi katika siku za usoni ambapo jeshi litashambulia watu wa Yerusalemu.

Ulihesabu nyumba

Hapa "hesabu" ina maana ya walikagua nyumba kutafuta nyezno kuwasaidia kujenga tena ukuta wa mji.

Ulitengeneza bwawa

"Ulitengeza sehemu ya kuhifadhi"

katikati ya kuta mbili

Haipo wazi Isaya alikuwa akimaanisha nini kwa kuta mbili. Cha msingi ni kwamba walijenga bwawa katikati ya kuta za mji.

anayetengeza mji

Hii ina maana ya Yahwe.

Isaiah 22:12

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli.

kwa vichwa vilivyonyoa

Hii ilikwa ishara ya maombolezo na kutubu.

na tule na kunywa, kwa maana kesho tutakufa

Hapa "kula na kunywa" inawakilisha kuwa na sherehe na kuendekeza kula chakula na divai. "bora tupate starehe sasa kwa kula na kunywa vyote tunavyotaka, kwa maana tutakufa hivi punde"

Hii ilifunuliiwa masikioni mwangu na Yahwe wa majeshi

Hapa "masikio" inawakilisha Isaya kama kamili. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe wa majeshi alifunua hili kwangu"

Hakika udhalimu huu hautasamehewa, hata utakapokufa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Hakika sitakusamehe kwa ajili ya vitu hivi vya dhambi ulivyofanya, hata utakapokufa"

hata utakapokufa

Maana zaweza kuwa 1) Yahwe hatawasamehe, hata baada yao kufa au 2) Yahwe hatawasamehe mpaka wafe.

Isaiah 22:15

Shebna

Hili ni jina la msimamizi wa kasri ya mfalme huko Yerusalemu.

ambaye yupo juu ya nyumba

Hapa "nyumba" inawakilisha wale walio katika kasri ya mfalme. "ni nani aliye msimamizi wa wale ambao wanafanya kazi katika kasri"

Unafanya nini hapa na nani amekupa ruhusa ... katika mwamba?

Yahwe anatumia swalii hili kumkaripia Shebna. "Hauna haki ... katika mwamba!"

kukata kaburi ... kuchonga kaburi ... kuchonga sehemu ya kupumzika

Misemo hii mitatu yote ina maana ya kutengeneza kaburi la kuzika.

juu ya marefu

Watu muhimu zaidi wa Israel walikuwa na makaburi katika sehemu za juu.

Isaiah 22:17

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza ujumbe wa Mungu kwa Shebna.

Hakika atakuzungushazungusha, na kukurusha kama mpira kwa nchi kubwa mno

Wanajeshi maadui kuja na kumchukua Shebna kama mateka kwa nchi ya kigeni inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa akimrusha kama mpira katika nch nyingine.

utakuwa aibu ya nyumba ya bwana wako

Hapa "nyumba" inawakilisha watu ambao wanafanya kazi katiika kasri ya mfalme. "utasababisha aibu kwa wale wote walio ndani ya kasri ya bwana wako"

Nitakusukuma kutoka katika ofisi yako na kutoka katika kituo chako. Utavutwa chini

Yahwe kusababisha Shebna kutofanya kazi tena katika kasri ya mfalme inazungumzwa kana kwamba Yahwe atamtupa katika ardhi.

Utavutwa chini

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nitakuleta chini kutoka katika nafasi yako ya juu"

Isaiah 22:20

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza ujumbe wa Mungu kwa Shebna.

Itakuja kuwa katika siku hiyo

Hapa "siku" inawakilisha kipindi kwa ujumla. "'Itatokea katika kipindi hicho"

Eliakimu ... Hilkia

Haya ni majina ya wanamume.

Nitamvisha kwa gwanda lako na kumwekea juu yake mshipi wako

Yahwe kusababisha Eliakimu kuchukua nafasi ya Shebna katika kasri ya mfalme inazungumziwa kana kwamba Yahwe atamvisha Eliakimu katika nguo za Shebna ambazo zinawakilisha mamlaka yake katika kasri ya mfalme.

gwanda lako ... mshipi wako

Hapa gwanda na mshipi inawakilisha mamlaka katika kasri ya mfalme.

mshipi

Hii ni kipande cha nguo ambacho watu huvaa kuzunguka kiuno au kupita kifuani.

katika mkono wake

Hapa "mkono" unawakilisha nguvu na utawala. "kwake"

Atakuwa baba

Eliakimu kutunza na kulinda watu wa Yuda inazungumziwa kana kwamba angekuwa baba yao. "Atakuwa kama baba"

katika nyumba ya Yuda

Hapa "nyumba" inawakilisha watu. "kwa watu wa Yuda"

Nitaweka ufunguo wa nyumba ya Daudi juu ya bega lake ... hakuna atakayefungua

Hapa "ufunguo" inawakilisha mamlaka. Hii inazungumzia Eliakimu kuwa na mamlaka ambayo hakuna mtu awezaye kumzuia kana kwamba alikuwa na ufunguo wa kasri na hakuna mtu mwingine awezaye kufunga au kufungua mlango. "Nitamweka kuwa msimamizi wa wale ambao hufanya kazi katika kasri ya mfalme, na anapofanya maamuzi hakuna atakayeweza kumpinga"

Isaiah 22:23

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kufafanua Eliakimu, ambaye atachukua nafasi ya Shebna katika kasri ya mfalme.

Nitamkaza, kigingi katika sehemu salama

Yahwe kusababisha mamlaka ya Eliakimu kuwa na nguvu na salama katika kasri ya mfalme inazungumziwa kana kwamba Eliakimu alikuwa kigingi na Yahwe atamweka kwa uthabiti katika kuta wa kasri.

atakuja kuwa kiti cha utukufu kwa ajili ya nyumba ya baba yake

Hapa "kiti cha utukufu" inawakilisha sehemu ya heshima. "Eliakimu ataleta heshima kwa familia yake"

nyumba ya baba yake

Hapa "nyumba" inawakilisha familia. "familia ya baba yake" au "familia yake"

Watamng'ang'ania yeye utukufu wote wa nyumba ya baba yake

Yahwe kusababisha familia nzima ya Eliakimu kuheshimiwa kwa sababu ya Eliakimu inazungumziwa kana kwamba Eliakimu alikuwa kigingi katika ukuta na familia yake ilikuwa kitu ambacho kinaning'inia juu ya kigingi. "Watatoa heshima kwa familia yake yote kwa sababu yake"

kila chombo kidogo kutoka katika vikombe kwa majagi yote

Hii inaendeleza kuzungumza juu ya Eliakimu kama kigingi. Mtoto wake atakuwa kama vikombe ambavyo vitaning'inia juu ya kigingi. Hii ina maana vizazi vyake vitaheshimika kwa sababu yake.

vikombe kwa majagi yote

Kikombe ni chombo kidogo ambacho kinashikilia maji. Jagi ni chombo kikubwa ambacho kinashikilia maji.

Isaiah 22:25

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza picha kutoka katika mistari ya nyuma.

Katika siku hiyo

Hapa "siku" inawakilisha kipindi kwa ujumla. "Katika kipindi hicho"

tamko la Yahwe wa majeshi

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "tamko" ielezwe kama kitenzi "tamka" au "sema kwa dhati". "hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyotamka" au "hivi ndivyo kile Yahwe wa majeshi alivyosema kwa dhati"

kigingi kuzamishwa katika sehemu imara ... utakatwa

Yahwe kusababisha Shebna kupoteza mamlaka yake katika kasri ya mfalme inazungumziwa kana kwamba Shebna ilikuwa kigingi katika ukuta ambacho hupasuka na kuanguka ardhini. Hii inasisitiza ya kwamba Shebna alifikiri mamlaka yake yalikuwa salama lakini Mungu atamwondoa.

uzito ambao ulikuwa juu yake utakatwa

Hapa "uzito" inawakilisha nguvu ya Shebna na mamlaka. Inazungumzia kana kwamba ilikuwa kitu kinachoning'inia juu ya kigingi ambacho kinachowakilisha Shebna. Yahwe kusababisha Shebna kupoteza nguvu yake na mamlaka inazungumziwa kana kwamba mtu alikuwa akikata kitu ambacho kilikuwa kinaning'inia juu ya kigingi.

Isaiah 23

Isaiah 23:1

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kusema kile ambacho Mungu amehukumu dhidi ya mataifa katika 13:1-23:18

Tamko kuhusu Tiro

"Hivi ndivyo Yahwe anavyotamka kuhusu Tiro"

Lia kwa sauti kali, enyi meli za Tarshishi

Hapa "meli" inawakilisha wanamume katika meli hizo. Isaya anazungumza na wanamume katika meli za Tarshishi kana kwamba zinaweza kumsikia. "Paza sauti kwa kukata tamaa enyi wanamume katika meli za Tarshishi"

bandari

eneo la bahari ambalo lipo karibu na nchi na salama kwa ajili ya meli

kutoka katika nchi ya Kupro imefunuliwa kwao

Msemo huu unaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "wanamume walisikia kuhusu Tiro walipokuwa katika nchi ya Kupro"

Kaeni kimya, nyie wakazi wa pwani

Isaya anazungumza na watu wanaoishi katika pwani kana kwamba wanaweza kumsikia.

Kaeni kimya

Hii ni lahaja. Hapa ukimya una maana ya kuashiria mshtuko na mshangao. "Ushtuke"

katika pwani

"pwani" ni nchi ambayo ipo karibu an inazunguka bahari. Hapa ina maana ya watu wanaoishi Wafinisia wanaopakana na bahari ya Mediteranea.

mfanya biashara wa Sidoni, ambaye anasafiri juu ya bahari, amekujaza

Hapa "mfanya biashara" ina maana ya "wafanya biashara wengi". "wafanya biashara wa Sidoni, ambao wanasafiri juu ya bahari, wamekufanya uwe tajiri"

Juu ya maji makuu kulikuwa na nafaka ya Shihori

Shihori ilikuwa jina la bonde karibu na Mto wa Nile katika Misri lijulikanalo kwa uzalishaji wake wa nafaka. "Wanamume walisafiri juu ya bahari kuu kusafirisha nafaka kutoka Shihori ndani ya Misri"

mavuno ya Nile yalikuwa mazao yake

Nafaka ilivunwa karibu na Mto na kusafirishwa katika mto na kisha mpaka Wafinisia.

mazao yake

"mazao yake". Ilikuwa kawaida kumaanisha mto kama "yake"

ikaja kuwa kitivo cha biashara cha mataifa

Kitivo cha biashara ni tendo la kununua na kuuza bidhaa. Hapa "mataifa" inawakilisha watu. "ulikuwa pale ambapo watu kutoka mataifa mengine walikuja kununua na kuuza bidhaa"

Isaiah 23:4

kwa maana bahari imeongea, mwenye uwezo wa bahari ... wala kukuza wanawake wachanga

Maana zaweza kuwa 1) Yahwe anaelezea mji wa Tiro kama mama ambaye huzungumza kuhusu watu wanaoishi katika mji kama watoto wake, au 2) Yahwe anafafanua Bahari ya Mediteranea kama ikizungumza. Watu wa Tiro walichukulia bahari mungu wao na baba. Katika maana mojawapo msemaji anaomboleza kwa sababu watoto wake wameangamizwa.

Isaiah 23:6

Vuka mpaka Tarshishi

"Tengeneza njia yako mpaka Tarshishi". Tarshishi ilikuwa nchi ya mbali watu wa Tiro walisafiri kufanya biashara. Itakuwa sehemu pekee ya usalama kwa wale wanaotoroka kutoka Tiro.

Je! hiki kimetokea kwako, mji wenye furaha, ambao asili yake inatoka kipindi cha zamani ... kukaa?

Yahwe anatumia swali kukejeli Tiro. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hili hasa limetokea kwako ambaye ulikuwa umejaa furaha katika mji wa zamani wa tiro .. kukaa."

mji wenye furaha

Hapa "mji" unawakilisha watu. "watu wenye furaha ambao waliishi katika mji wa Tiro"

ambao miguu yake iliibeba mbali sana katika sehemu za kigeni kukaa

Hapa "miguu" inawakilisha mtu mzima. "ambaye alikwenda katika sehemu za mbali kuishi na kutengeneza pesa"

iliibeba mbali sana

Hapa "iliibeba" ina maana ya mji wa Tiro ambayo inawakilisha watu wa Tiro.

Isaiah 23:8

Ni nani aliyepanga hili dhidi ya Tiro ... wa dunia?

Isaya anatumia swali kukejeli Tiro. Neno "hili" lina maana ya mipango ya Mungu kuangamiza Tiro ambayo Isaya alielezea katika 23:1-7. Pia, "Tiro" ina maana ya watu wanaoishi Tiro. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Alikuwa Yahwe ambaye alipanga kuangamiza watu wa Tiro ... wa dunia"

mtoaji wa taji

Hapa "taji" ina maana ya nguvu ambayo mtu anayo kama mtawala juu ya watu. "ambaye huwapa watu nguvu ya kutawala juu ya wengine"

ambao wafanya biashara wake ni wakuu

Wafanya biashara wanalinganishwa na wakuu kusisitiza jinsi walivyo na nguvu walipokwenda katika nchi tofauti. "ambao wafanya biashara wao ni kama wakuu"

ambao wauzaji wake wanaheshimika katika dunia

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambao wauzaji wake watu wa dunia wanatoa heshima kubwa zaidi"

kupunguza kiburi chake na utukufu wake wote

"kutowaheshimu kwa sababu walikuwa na kiburi kwa utukufu wao wenyewe"

kiburi chake ... utukufu wake ... walioheshimiwa wa kwake

Hapa "kwake" ina maana ya mji wa Tiro ambao unawakilisha watu wanaoishi kule. "kiburi chao .. utukufu wao ... walioheshimiwa wa kwao"

Isaiah 23:10

Lima nchi yako, kama mtu alimavyo Nile, binti wa Tarshishi. Hakuna tena soko ndani ya Tiro

Maana zaweza kuwa 1) Isaya anawaambia watu wa Tarshishi kuanza kupanda mazao kwa kuwa hawawezi tena kufanya biashara na Tiro au 2) Isaya anawaambia watu wa Tarshishi ya kuwa wapo huru kutoka na utawala wa Tiro."Pita katika nchi kama mto, binti wa Tarshishi. Watu wa Tiro hawana nguvu yoyote tena"

binti wa Tarshishi

"Binti" wa mji inawakilisha watu wa mji. "watu wa Tarshishi" au "watu ambao wanaishi Tarshishi"

Yahwe amenyosha mkono wake juu ya bahari, na ametikisa falme

Yahwe kutumia nguvu yake kuongoza bahari na watu wenye falme zenye uwezo inazungumziwa kana kwamba Yahwe alinyosha mkono wake na kutikisa falme.

amenyosha mkono wake juu ya bahari

Hapa "mkono" ina maana ya nguvu na uongozi wa Mungu. "ameonyesha nguvu yake juu ya bahari"

bikira binti wa Sidoni uliyekandamizwa

Hapa "binti bikira" inawakilisha watu wa Sidoni. "watu wa Sidoni, kwa sababu watu wengine watakukandamiza"

Isaiah 23:13

Tazama nchi ya Wakaldayo

"Wakaldayo" ni jina lingine la Wababeli. "Tazama kile kinachotokea kwa nchi ya Wababeli" au "Tazama kile kinachotokea kwa Babeli"

minara ya kuzingira

Wanajeshi walijenga minara au matuta ya udongo kushambulia juu ya kuta za mji

Lia kwa uchungu, enyi meli za Tarshishi

Hapa "meli" inawakilisha wanamume katika meli.

kwa maana kimbilio lenu limeangamizwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kwa maana maadui wameangamiza kimbilio lako"

Isaiah 23:15

Katika siku hiyo

Hapa "siku" inawakilisha kipindi cha muda kwa ujumla. "Katika kipindi hicho" au "Pale"

Tiro itasahaulika kwa miaka sabini

Kwa kuwa watu hawatakwenda tena Tiro kununua au kuuza bidhaa, itakuwa kana kwamba wamesahau kuhusu mji ule. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kwa miaka sabini itakuwa kana kwamba watu wamesahau kuhusu Tiro"

kwa miaka sabini

"kwa miaka 70"

kama siku za mfalme

Hapa "siku" inawakilisha kipindi kirefu zaidi cha muda. Muda wa wastani ambao mfalme aliishi ulikuwa kama miaka 70. "kama miaka ya mfalme" au "ambao ni kama urefu ambao mfalme huishi"

kama katika wimbo wa kahaba ... ili kwamba uweze kukumbukwa

Hii inazungumzia kuhusu watu wa Tiro kana kwamba walikuwa kahaba. Kama vile kahaba ambaye sio maarufu tena anaweza kuimba katika mitaa kurudisha wapenzi wake wa zamani, watu wa Tiro watajaribu kutafuta watu kutoka mataifa mengine kurudi kwao kuendelea kufanya biashara ili kwamba watu wa Tiro wawe matajiri na wenye uwezo tena.

ili kwamba uweze kukumbukwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ili kwamba watu wakukumbuke" au "ili kwamba watu warudi kwako"

Isaiah 23:17

Itakuja kuwa ya kwamba

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya tukio muhimu ambalo litatokea.

miaka sabini

"miaka 70"

Yahwe ataisaidia Tiro

Hapa "Tiro" inawakilisha watu ambao wanaishi Tiro. "Yahwe atawasaidia watu wa Tiro"

ataanza kupata pesa tena kwa kufanya kazi ya ukahaba ... wa dunia

Isaya analinganisha watu wa Tiro na kahaba. Kama vile kahaba anavyojiuza kwa ajili ya pesa kwa mwanamume yeyote, watu wa Tiro watanunua na kuuza tena kwa falme zote."Na kama kahaba watanunua na kuuza na falme zote za duniani"

Haitatunzwa au kuwekwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Wafanya biashara hawatatunza pembeni pesa yao"

Wale wanaoishi ndani ya uwepo wa Yahwe

"Wale wanaomtii na kumtumikia Yahwe"

kwa ajili yao kula na kuwa na mavazi ya kudumu

"kwa wao kupata chakula cha kutosha kwa kula na nguo ambazo zitadumu muda mrefu"

Isaiah 24

Isaiah 24:1

kufanya dunia kuwa tupu

"kufanya dunia kuwa na ukiwa" au "kuangamiza kila kitu juu ya dunia"

Itakuja kuwa ya kwamba

Msemo huu unaweka alama kwa tukio muhimu.

kama itakavyokuwa ... ndivyo itakuwa

Kile Yahwe atakachofanya hakielezwi hapa, lakini kinaeleweka. Hiii inaonyesha ya kwamba Mungu atawafanya watu kw njai moja. "kama Yahwe anavyotawanya ... kw hiyo atatawanya"

kuhani ... mtoaji wa riba

Katika 24:2 Isaya anaorodhesha madaraja ya watu. Yanaweza kuwekwa kama nomino za wingi. "makuhani ... wale ambao hutoa riba"

mpokeaji wa riba

"yule ambaye hudaiwa fedha". Neno "riba" lina maana ya fedha ya ziada ambayo mtu anatakiwa kulipa ili aweze kukopa fedha.

mtoaji wa riba

"yule ambaye anadaiwa fedha"

Isaiah 24:3

Dunia itaharibiwa kabisa na kuvuliwa kabisa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atahariibu kabisa dunia na ataondoa kila kitu chenye thamani"

Yahwe amanena neno hili

Hapa "neno" linawakilisha kile Yahwe alichosema. "Yahwe amesema angefanya"

Dunia inakauka na kunyauka, dunia inakauka na kutokomea

Misemo hii miwili ina maana moja. "Kila kitu juu ya dunia kitakauka na kufa"

Dunia ... ulimwengu

Zote hizi zinawakilisha kila kiitu ambacho kipo juu ya dunia.

Dunia inachafuliwa na wakazi wake

Watu kutenda dhambi na kufanya dunia kutokubalika kwa Mungu inazungumziwa kana kwamba watu walifanya dunia kuwa chafu kimwiili. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wamechafua dunia"

wamevunja sheria, kukiuka amri, na kuvunja agano la milele

"hawajatii sheria na amri za Mungu, na wamevunja agano la milele la Mungu"

Isaiah 24:6

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua kipindi katika siku za usoni ambapo Mungu atahukumu dunia. Manabii mara nyingine hufafanua tukio la siku za usoni kama kitu cha nyuma au cha sasa. Hii inasisitiza tukio kufanyika kwa uhakika.

laana humeza dunia

Yahwe kulaani dunia na kuiangamiza inazungumziwa kana kwamba laana ilikuwa aidha mnyama pori ambaye anakula kabisa dunia au moto ambao huchoma kabisa dunia.

na wakazi wake wanakutwa na hatia

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na Yahwe atatamka ya kwamba watu wana hatia"

Isaiah 24:8

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua kipindi katika siku za usoni ambapo Mungu atahukumu dunia. Manabii mara nyingine hufafanua tukio la siku za usoni kama kitu cha nyuma au cha sasa. Hii inasisitiza tukio kufanyika kwa uhakika.

vigoma ... kinubi

Hivi ni vyombo vya muziki.

Isaiah 24:10

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua kipindi katika siku za usoni ambapo Mungu atahukumu dunia. Manabii mara nyingine hufafanua tukio la siku za usoni kama kitu cha nyuma au cha sasa. Hii inasisitiza tukio kufanyika kwa uhakika.

Mji wa uharibifu umevunjwa chini

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atavunja chini mji wa uharibifu"

Mji wa uharibifu

Maana zaweza kuwa 1) mji ulikuwa katika uharibifu kabla Mungu hajauvunja chini; watu hawakumtii Mungu, serikali ilikuwa imeharibika, na mji ulikuwa umejaa unywaji na sherehe, au 2) mji utakuwa katika uharibifu baada ya Mungu kuuvunja chini. Kuta na majengo ambayo hapo awali yalikuwa na nguvu na marefu sasa yapo katika uharibifu juu ya ardhi. Kwa maana zote mbili, ina maana ya miji kwa ujumla na sio mji mmoja.

kila nyumba inafungwa na kuwa tupu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu watafunga nyumba zo na kuziacha tupu"

kwa sababu ya mvinyo

"kwa sababu hakuna divai"

furaha yote inawekwa giza, shangwe ya nchi imepotea

Misemo hii miwili ina maana moja. "furaha yote itaondoka kutoka duniani"

shangwe ya nchi

Hapa "nchi" inawakilisha watu wa dunia.

Isaiah 24:12

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua kipindi katika siku za usoni ambapo Mungu atahukumu dunia. Manabii mara nyingine hufafanua tukio la siku za usoni kama kitu cha nyuma au cha sasa. Hii inasisitiza tukio kufanyika kwa uhakika.

Ndani ya mji kunaachwa ukiwa

Nomino dhahania "ukiwa" inaweza kuandikwa kama "tia ukiwa" au "tupu". "Mji umetiwa ukiwa" au "Mji umeachwa tupu"

Ndani ya mji

Huu sio mji mmoja lakini miji kwa ujumla.

kama pale mzeituni unapigwa, kama vile masazo ya mavuno baada ya mavuno ya zabibu kukamilika

Hii inalinganisha mataifa baada ya Yahwe kuharibu nchi kwa miti na mizabibu baada ya matunda kuchukuliwa. Hii ina maana kutakuwa na watu wachache sana waliosalia katika nchi.

Isaiah 24:14

Watainua juu sauti zao na kupiga kelele utukufu wa Yahwe

Msemo "inua juu sauti zao" ni lahaja ambayo ina maana ya kuongea kwa sauti kubwa. "Wataimba na kupiga kelele kuhusu utukufu wa Yahwe"

Wata

Hapa "wata" ina maana ya wale ambao bado wapo hai baada ya Yahwe kuharibu dunia.

na watapiga kelele kwa shangwe kutoka baharini

Hapa "bahari" ina maana ya Bahari ya Mediteranea ambayo ipo magharibi mwa Israeli. "na wale wa magharibi kuelekea bahari watapiga kelele za shangwe"

Kwa hiyo katika mashariki mtukuze Yahwe

Msemo "katika mashariki" inawakilisha watu wanaoishi mashariki mwa Israeli. Isaya anaamuru watu hawa kana kwamba walikuwa plae pamoja naye. Lakini, anazungumza na watu katika siku za usoni baada ya Mungu kuharibu dunia. "Kwa hiyo kila mtu kutoka nchi za mbali za mashariki watamtukuza Yahwe"

na katika visiwa vvya bahari mpatie utukufu

Isaya anawaamuru watu ambao wanaishi katika visiwa katika bahari ya Meditarenea kana kwamba walikuwa pale pamoja naye. Lakini, anazungumza kwa watu katika siku za usoni baada ya Mungu kuharibu dunia. "na kila mtu katika visiwa atatoa utukufu

kwa jina la Yahwe

Hapa "jina" inawakilisha Yahwe. "kwa Yahwe"

Isaiah 24:16

tumesikia

Hapa "tumesikia" ina maana ya Isaya na watu wa Israeli. Isaya anafafanua kitu katika siku za usoni kana kwamba kimekwisha tokea. "tutasikia"

Nimeisha, nimeisha

Isaya anarudia msemo huu kusisitiza uchungu wake. Alijihangaisha sana kwa sababu aliwaona watu ambao walidanganya wengine na hawakufanya kile walichoahidi kufanya. "Nimekuwa dhaifu sana"

Wadanganyifu wamefanya udanganyifu; ndio, wadanganyifu wamefanya udanganyifu

Isaya anarudia msemo huu kusisitiza uchungu wake. "Kweli, wale ambao hudanganya sasa wanadanganya wengine" au "Kweli, wadanganyifu wametenda udanganyifu"

Isaiah 24:17

Hofu kuu, shimo, na mtego upo juu yako, wakazi wa dunia

"Nyie watu wa dunia mtapitia hofu kuu, shimo, na mtego"

shimo, na mtego ... atakamatwa katika mtego

Hapa "shimo" na "mtego" inawakilisha mambo mabaya yote tofauti ambayo yatatokea kwa watu. Watu watatoroka kitu kimoja kibaya lakini watapitia kitu kingine kibaya.

sauti za hofu kuu

"sauti ya kutisha"

atakamatwa katika mtego

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "mtego utamkamata"

Madirisha ya mbinguni yatafunguliwa

Hii inazungumzia kiasi kikubwa cha mvua kunguka kutoka angani kana kwamba Yahwe alifungua dirisha katika anga na kuruhusu maji kumwagika. "Anga itafunguka wazi na mvua nyingi itamwagika"

misingi ya dunia itatikisika

Neno "msingi" kawaida lina maana ya umbo la mawe ambalo hutoa mhimili kwa jengo kutok kwa chini. Hapa inaelezea umbo la kufanana ambalo lilidhaniwa kushikilia dunia katika sehemu yake. "dunia itatikisika kwa kutisha" au "kutakuwa na tetemeko la kutisha"

Isaiah 24:19

Dunia itavunjwa kabisa, dunia itararuliwa kabisa; dunia itatikiswa kwa nguvu

Vishazi hivi vinaweza kuwa katika hali ya kutenda. "Dunia itavunjika na kugawanyika; dunia itatikisika kwa nguvu"

Dunia itapepesuka kama mwanamume mlevi na itayumba huku na kule kama kibanda

Tashbihi hizi zinasisitiza jinsi dunia itakavyotikisa huku na kule.

Dhambi yake itakuwa nzito juu yake na itaanguka na haitainuka tena

Hii inazungumzia dunia kana kwamba ilikuwa mtu na wadanganyifu walikuwa vyombo vizito. Mtu hujaribu kubeba mzigo mzito lakini uzito unasababisha mtu kunguka na kutoweza kusimama juu. Hapa dunia inawakilisha watu wa dunia ambao husababisha Yahwe kuangamiza dunia kwa sababu ya dhambi zao. "Dhambi za watu ni nyingi na kwa hiyo Yahwe ataangamiza dunia, na dunia itakuwa kama mtu ambaye huanguka na hawezi kusimama juu"

Isaiah 24:21

Itakuja kuwa

Hii inaweka alama kwa tukio muhimu.

katika siku hiyo

Hapa "siku" ina maana ya kipindi cha muda kwa ujumla. "katika kipindi hicho"

wingi wa walio juu

Msemo "wingi" au "jeshi" ni neno ambalo lina maana ya idadi kubwa ya kitu. Hapa ina maana ya viumbe viovu vya kiroho katika mbingu. "viumbe viovu vya kiroho" au "malaika ambao waliasi dhidi yake"

walio juu

Hapa "juu" inawakilisha mbinguni au anga. "katika mbingu" au "katika anga"

Watakusanywa pamoja, wafungwa katika shimo, na watafungwa katika gereza

Hapa "shimo" ina maana ya chumba chenye giza au shimo katika gereza. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawakusanya pamoja kama wafungwa wake na kuwafunga katika gereza la chini"

wataadhibiwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawaadhibu"

Kisha mwezi utaaibishwa, na jua kufedheheshwa

Jua na mwezi inaelezwa kama mtu ambaye anaona aibu ya kuwa mbele ya mtu mwenye nguvu kubwa. Katika uwepo wa Yahwe, nuru ya mwezi na jua itaonekana na mwanga mdogo.

Isaiah 25

Isaiah 25:1

nitasifu jina lako

Hapa "jina" inawakilisha Yahwe. "ninakusifu"

vitu vilivyopangwa zamani

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "vitu ulivyovipanga zamani"

katika uaminifu kamilifu

Nomino dhahania "uaminifu" inaweza kuwekwa kama "mwaminifu". "kwa sababu wewe ni mwaminifu uliye mkamilifu"

mji ule

Hii haimaanishi mji fulani. Ina maana na miji kwa ujumla.

ngoma ya wageni

"ngome ambayo ni ya wageni"

mji wa mataifa katili

Hapa "mji" na "mataifa" inawakilisha watu ambao wanaishi pale.

Isaiah 25:4

umekuwa sehemu ya usalama ... hifadhi ... hifadhi kutoka kwa dhoruba ... kivuli kutoka kwa joto

Yahwe kuwalinda watu wake inazungumziwa kana kwamba alikuwa sehemu ambayo watu wanaweza kwenda kuwa salama na kufarijiwa.

Pale ambapo pumzi ya wakatili ulipokuwa kama dhoruba dhidi ya ukuta

Watu wakatili kuwakandamiza watu wa Mungu inazungumziwa kana kwamba walikuwa dhoruba inayopiga dhidi ya ukuta.

Pale ambapo pumzi

"Pale upepo" au "Pale mlipuko"

wakatili

Hiki ni kitenzi kidogo."watu wakatili" au "wale ambao ni wakatili"

kama joto katika nchi kavu

Hii inalinganisha adui wa watu wa Mungu kwa joto ambalo hukausha nchi. Hii inasisitiza jinsi maadui wanavyosababisha watu wa Mungu kuteseka.

kama joto linapotulizwa ... wakatili unajibiwa

Yahwe kuwasimamisha watu wakatili kutokuimba na kujivuna inalinganishwa na wingu kutoa kivuli katika siku ya kiangazi. Hii inasisitiza ya kwamba Yahwe huwafariji watu wake kwa kusimamisha wale ambao husababisha wao wateseke.

kama vile joto linavyotulizwa kwa kivuli cha wingu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kama vile wingu linavyopita juu kichwani na kutuliza joto"

wimbo wa wakatili unajibiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "utawazuia watu wakatili kutokuimba"

Isaiah 25:6

Katika mlima huu

Hii ina maana ya Yerusalemu au Mlima Sayuni.

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli.

karamu ya vitu vinono

Hapa "vitu vinono" ina maana ya vyakula bora.

karamu katika masimbi

"divai ya zamani". Hii ina maana ya divai bora.

kifuniko juu ya watu wote, utando ulifumwa juu ya mataifa

Kifo, mateso, na huzuni inazungumziwa kana kwamba vilikuwa wingu jeusi au utando ambao hufunika kila mtu juu ya dunia.

Ataimeza mauti milele

Yahwe kusababisha watu kuishi milele inazungumziwa kana kwamba angeweza kumeza kifo.

aibu ya watu wake ataiondoa kutoka dunia nzima

Yahwe kusababisha watu kutokuwa na aibu tena inazungumziwa kana kwamba aibu ilikuwa kitu ambacho Yahwe angeweza kuondoa mbali.

Isaiah 25:9

Itasemwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Watu watasema"

katika siku hiyo

Hapa "siku" inawakilisha kipindi cha muda kwa ujumla. "katika kipindi hicho"

Kwa kuwa katika mlima huu mkono wa Yahwe utapumzika

"mkono" unawakilisha nguvu ya Mungu. Kwa maana mkono wa Yahwe kupumzika juu ya "mlima huu" ina maana atawalinda watu wake. "Nguvu ya Yahwe itakuwa juu ya mlima huu" au "Kwa maana juu ya Mlima Sayuni Yahwe atalinda watu wake"

Moabu itakanyagwa chini katika nafasi yake, hata kama majani makavu yanavyokanyagwa chini katika shimo lililojaa mbolea

Yahwe kuangamiza watu wa Moabu inazungumziwa kana kwamba angewakanyaga na kuwasaga. Hii inalinganishwa na jinsi watu wanavyokanyaga majani makavu kuchanganya na mbolea.

Moabu itakanyagwa chini katika nafasi yake

Hapa Moabu anawakilisha watu wa Moabu. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yahwe atakanyaga watu wa nchi ya Moabu"

Isaiah 25:11

Watatawanya mikono yao ... mikono yake kuogelea

Tashbihi hii inasisitiza jinsi gani Yahwe atawaibisha watu wa Moabu. Watatawanya mikono yao katika kinyesi cha mnyama kama mwogeleaji anavyotawanya mikono yake majini.

Watatawanya mikono yao katikati yake

"Watu wa Moabu watasukuma mikono yao katikati ya kinyesi cha mnyama"

kama mwogeleaji anavyotawanya mikono yake kuogelea

"kana kwamba walikuwa wakiogelea"

atashusha chini kiburi chake

Yahwe kuaibisha mtu mwenye kiburi inazungumziwa kana kwamba kiburi ilikuwa kitu cha juu na Yahwe angekisababisha kuwa chini.

pamoja na ujuzi wa mikono yao

Hapa "mikono" inawakilisha nguvu ya kufanya au kutengeneza kitu. "pamoja na vitu vikubwa walivyotengeneza" au "pamoja na vitu vikubwa walivyofanya"

ngome yako ya juu ya kuta atazishusha chini mpaka kwenye ardhi, kwenye vumbi

Hii inazungumzia Yahwe kusababisha majeshi kuzileta chini kuta kana kwamba yeye mwenyewe alikuwa akienda kuzileta chini. "Atatuma jeshi kuleta ngome yako iliyo juu ya kuta ardhini, katika mavumbi"

Ngome yako ya juu

Hapa "yako" ina maana ya watu wa Moabu. Inaweza kuwekwa katika mtu wa tatu kuwe na mlingano na mstari uliopita. "Ngome yao iliyo juu"

Isaiah 26

Isaiah 26:1

Katika siku hiyo

Hapa "siku" inawakilisha kipindi cha muda kwa ujumla. "Katika kipindi hicho"

wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "watu katika nchi ya Yuda wataimba wimbo huu"

Tuna mji imara

Hii ina maana ya mji wa Yerusalemu.

Mungu amefanya wokovu ukuta na boma lake

Nguvu ya Mungu kuwalinda na kuwaokoa watu wake inazungumziwa kana kwamba wokovu wake ulikwa ukuta unaozunguka mji.

taifa lenye haki linaloshikilia imani

Hapa "taifa" inawakilisha watu. "watu wenye haki na waaminifu"

Isaiah 26:3

Akili ambayo imekaa kwako

Hapa "akili" inawakilisha mawazo ya mtu. Pia, "kwako" ina maana ya Yahwe. Msemo "Akili ambayo imekaa kwako" ni lahaja ambayo ina maana "Mtu ambaye huwaza kwa kuendelea juu yako"

Yah, Yahwe

Yah ni jina lingine kwa ajili ya Yahwe.

Yahwe, ni mwamba wa milele

Yahwe kuwa na nguvu ya kuwalinda watu wake inazungumziwa kana kwamba alikuwa jiwe refu ambapo watu wanaweza kwenda kutoroka maadui zao.

Isaiah 26:5

atawashusha chini wale ambao wanaishi kwa kujiinua

Yahwe kuwaaibisha wale ambao wanajiinua inazungumziwa kana kwamba watu wenye kiburi walikuwa juu na angeweza kusababisha washuke chini.

miji iliyoimarishwa

Hii ina maana miji iliyoimarishwa kwa ujumla sio mji fulani.

ataiweka chini ... atasambaratisha

Yahwe kusababisha jeshi kuangamiza miji iliyoimarishwa inazungumziwa kana kwamba yahwe angefanya mwenyewe.

itakanyagwa chini kwa miguu ya maskini na kutembea kwa wahitaji

Kauli mbili zina maana moja. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Maskini na watu walioteswa watakanyaga juu ya uharibifu wa mji"

Isaiah 26:7

Njia ya wenye haki ina usawa ... njia ya wenye haki umefanya iwe wima

Misemo hii miwili ina maana moja. Watu kumtii Yahwe inazungumziwa kana kwamba walikuwa wakitembea juu ya njia yake. Yahwe kuhakikishia watu ya kwamba kile wanachofanya ni sahihi inazungumziwa kana kwamba alikuwa akifanya njia kuwa sawa na wima kwa ajili yao.

katika njia ya hukumu zako, Yahwe, tunakusubiri

Kufanya kile Yahwe amehukumu kuwa sahihi inazungumziwa kutembea katika njia yake. "tunakusubiri, Yahwe, tunapoendelea kufanya kile ulichohukumu kuwa sahihi"

ya hukumu zako

"ya sheria zako" au "ya mafundisho yako"

tunakusubiri

Hapa "tunakusubiri" ina maana ya Isaya na watu wote wenye haki ambao wanazungumza na Yahwe.

jina lako na sifa yako ni shauku yetu

Hapa "jina" na "sifa" inawakilisha silika ya Yahwe ambayo inawakilisha Yahwe mwenyewe. "shauku yetu pekee ni kukuheshimu"

roho yangu ndani yangu inakutafuta kwa bidii

Kutaka kumjua Yahwe na sheria zake zaidi inazungumziwa kana kwamba mtu alikuwa akitaka kumtafuta Yahwe. "Ninataka kukujua zaidi kwa bidii"

roho yangu ndani yangu inakutafuta kwa bidii

Hapa "roho" inawakilisha msemaji kwa yeye mzima.

Isaiah 26:10

Acha fadhila ionyeshwe kwa mtu muovu, lakini hatajifunza haki

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Hata kama Yahwe ni mwema kwa watu waovu, bado hawajifunzi kufanya kile kilicho sahihi"

mtu muovu

Hii ina maana watu waovu kwa ujumla.

katika nchi ya wenye haki

Hapa "nchi" inawakilisha watu ambao wanaishi kule. "Katika nchi ambapo watu hufanya kile kilicho sahihi"

haoni ukuu wa enzi wa Yahwe

Hapa "kuona" inawakilisha kutambua kitu. "hatambui ya kwamba Yahwe ni mkuu"

Isaiah 26:11

mkono wako umeinuliwa juu

Yahwe kujiandaa kuwaadhibu watu waovu inazungumziwa kana kwamba mkono wake uliinuliwa na unataka kuwapiga watu waovu.

lakini hawagundui

"lakini watu waovu hawagundui"

wataona ari yako kwa ajili ya watu

Hapa "kuona" inawakilisha kugundua kitu. "watagundua ya kwamba una hamu ya kuwabariki watu wako"

kuaibishwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wataaibishwa"

moto wa adui zako utawaangamiza

Yahwe kuwaadhibu na kuwaangamiza kabisa adui zake inazungumziwa kana kwamba angetuma moto ambao utawachoma kabisa.

moto wa adui zako

Hapa "wa" haimaanishi moto ni wa maadui lakini ya kwamba moto umekusudiwa kutumiwa dhidi ya maadui. "moto wako utawachoma kabisa"

kwa ajili yetu

Hapa "yetu" ina maana ya Isaya na inajumlisha watu wote wenye haki.

Isaiah 26:13

lakini tunasifu jina lako pekee

Hapa "jina" inawakilisha nafsi ya Mungu. "lakini tunakusifu wewe peke yako"

hawatainuka

"hawatarudi katika uhai"

kufanya kila kumbukumbu yao kutoweka

Yahwe kusababisha watu kutokumbuka wale aliowaangamiza inazungumziwa kana kwamba Yahwe alifanya kumbukumbu yao kutoweka au kufa.

Isaiah 26:15

Umeongeza taifa, Yahwe, umeongeza taifa

Kishazi hiki kinarudiwa kwa ajili ya msisitizo. Hapa "taifa" inawakilisha watu. "Umeongeza sana idadi ya watu katika taifa letu"

Isaiah 26:16

walikuangalia wewe

Hapa "walikuangalia" ina maana ya watu wa Israeli. Hii ingeweza kujumuisha Isaya. "tuliangalia kwako"

walikuangalia wewe

Lahaja hii ina maana walimuuliza Yahwe kwa msaada.

nidhamu yako ilipokuwa juu yao

Nomino dhahania "nidhamu" inaweza kuwekwa kama kitenzi. "unapowaadhibisha"

Kama mwanamke mwenye mimba .. anapolia katika maumivu yake ya uchungu

Hii inalinganisha watu kwa mwanamke kuzaa. Hii inasisitiza mateso na kulia kwao Yahwe alipowaadhibisha"

Isaiah 26:18

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kulinganisha mateso ya watu wa Yuda na mwanamke anayezaa.

lakini ni kana kwamba tumezaa tu upepo

"lakini ni kana kwamba tumezaa tu hewa" au "ni kana kwamba tumezaa utupu".Hii ni tashbihi ambayo inasisitiza ya kwamba mateso ya watu hayajaleta kitu chochote. "lakini hakuna kitu kizuri kilichotokana kwake"

Hatujaleta wokovu katika dunia, na wakazi wa ulimwengu hawajaanguka

Hapa "dunia" inawakilisha watu ambao wanaishi juu ya dunia. Maana haiko wazi, lakini inaonekana kumaanisha ya kwamba watu wa Israeli hawakuweza kujiokoa wenyewe au watu wengine kwa kuwashinda adui zao vitani.

Hatujaleta wokovu katika dunia

Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "wokovu" ielezwe kama kitenzi "kuokoa". "Hatujaokoa wakazi wa dunia"

na wakazi wa ulimwengu hawajaanguka

"wala hatujasababisha watu waovu wa ulimwengu kuanguka katika vita"

Isaiah 26:19

Wafu wako wataishi

Hii inawezwa kuandikwa upya ili kwamba kivumishi kidogo "wafu" kinaelezwa kama kitenzi "wamekufa". "Watu wako ambao wamekufa wataishi tena"

Wafu wako

Maana zaweza kuwa 1) "wako" ina maana ya Yahwe au 2) "Wako" ina maana ya watu wa Israeli. Iwapo utachagua chaguo la pili unaweza kutafsiri kama "Wafu wetu"

Inukeni

Hii inazungumzia watu waliokufa kurudi katika uhai kana kwamba walikuwa wakiamka kutoka usingizini.

nyie mnaoishi katika vumbi

Hii ni njia ya upole ya kumaanisha wale waliokufa. "wale ambao wamekufa na kuzikwa"

kwa maana umande wako ni umande wa mwanga

Yahwe kuwa mwema kwa watu wake na kuwaleta katika uhai inazungumziwa kana kwamba ilikuwa umande ambao unasababisha mimea kuishi.

kwa maana umande wako

Maana zaweza kuwa 1) "wako" ina maana ya Yahwe na huu ni umande ambao Yahwe hutoa au 2) "wako" ina maana ya watu wa Israeli na huu ni umande wanaopata kutoka kwa Yahwe.

umande wa mwanga

Maana zaweza kuwa 1) "mwanga" ina maana ya nguvu ya Yahwe kufanya watu waliokufa kuishi tena. "umande kutoka kwa Yahwe" au 2) "mwanga" ina maana ya kipindi cha asubuhi ambapo umande upo juu ya mimea. "umande wa asubuhi"

dunia italeta mbele wafu wake

"dunia itazaa wale waliokufa". Yahwe kusababisha watu waliokufa kuja katika uzima inazungumziwa kana kwamba dunia ingeweza kuzaa wale waliokufa. "na Yahwe atasababisha wale ambao wamekufa kuinuka kutoka katika dunia"

Isaiah 26:20

watu wangu

Hapa "wangu" ina maana ya Isaya. Pia "watu" ina maana ya watu wa Israel.

hadi pale hasira itakapopita

"hadi Yahwe atakapokuwa hana hasir ana sisi tena"

dunia itafunua damu yake, na haitaficha tena waliouwawa wa kwake

Yahwe kufunua mauaji yote ambayo yamefanyika duniani ili kwamba aweze kuadhibu inazungumziwa kana kwamba dunia yenyewe itamfunua kila mmoja ambaye alikuwa ameuawa.

Isaiah 27

Isaiah 27:1

Katika siku hiyo

Hapa "siku" inawakilisha kipindi cha muda kwa ujumla.

Yahwe kwa mkono wake, kwa upanga mkubwa na mkali ataadhibu

Yahwe kuwa na nguvu ya kuangamiza adui zake inazungumziwa kana kwamba alikuwa na upanga imara, na mkubwa.

jitu la kutisha ambalo limo katika bahari

Hii ina maana ya Lewiathani

Shamba la mizabibu la mvinyo, litaimba kwa ajili yake

"Imba juu ya shamba la mizabibu la mvinyo".Hii inazungumzia kuhusu watu wa Israeli kana kwamba walikuwa shamba la mizabibu ambalo lilizaa matunda. "Imba kuhusu watu wa Israeli kana kwamba walikuwa shamba la mizabibu ambalo lilizaa mizabibu kwa ajili ya mvinyo"

Mimi, Yahwe, ni mlinzi wake

"Mimi, Yahwe, hulinda shamba la mizabibu"

usiku na mchana

Maneno "usiku" na "mchana" yanaunganishwa hapa kumaanisha "wakati wote". "wakati wote" au "kwa kuendelea"

Isaiah 27:4

Kauli Kiunganishi

Hii inaendelea kuzungumza kuhusu watu wa Israeli kana kwamba walikuwa shamba la mizabibu.

Sina hasira, Oh, hata kuwe na mibigili na miiba! Katika vita nitatembea dhidi yao

"Sina hasira. Kama kulikuwa na mibigili na miiba ningetembea dhidi yao katika vita"

Sina hasira

Inaeleweka ya kwamba Yahwe hana hasira na watu wake tena. "Sina hasira na watu wangu tena"

hata kuwe na mibigili na miiba

Adui za watu wa Israeli wanazungumziwa kana kwamba walikuwa mibigili na miiba inayoota katika shamba la mizabibu.

mibigili na miiba

Mibigili na miiba hutumika mara kwa mara kama alama ya miji na nchi zilizoharibiwa

Katika vita nitatembea dhidi yao

Yahwe kupigana na adui zake inazungumziwa kana kwamba alikuwa mwanajeshi katika jeshi.

Ningetembea dhidi yao; Ningewachoma wote kwa pamoja

Hapa Isaya anaunganisha picha tofauti kuzungumzia maadui wa Yahwe. Anazungumza juu yao kana kwamba walikuwa mibigili na miiba lakini pia kama wanajeshi katika jeshi.

isipokuwa washike ulinzi wangu

Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "ulinzi" ielezwe kama kitenzi "kulinda". "Isipokuwa waniulize kuwalinda wao"

na kufanya amani pamoja na mimi; waache wafanya amani pamoja na mimi

"na waombe kuishi kwa amani pamoja nami; ninataka waishi kwa amani pamoja nami"

Isaiah 27:6

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza. Anaendelea kufafanua watu wa Israeli kama shamba la mizabibu.

Katika siku ijayo

Hii inazungumza juu ya siku kana kwamba inasafiri na kufika sehemu. "Katika siku za usoni"

Yakobo atachuku mzizi; Israeli atachanua na kuchomoza

Yahwe kubariki watu wa Israeli na kusababisha waweze kufanikiwa inazungumziwa kana kwamba walikuwa mzabibu unaota mizizi na kuchanua. "uzao wa Israeli utafanikiwa kama mzabibu ambao umeshika mizizi na kuchanua"

Yakobo ... Israeli

Hapa "Yakobo" na "Israeli" ni mfano wa maneno ambao yanawakilisha uzao wa Yakobo.

watajaza uso wa nchi kwa matunda

Yahwe kusababisha watu wa Israeli kufanikiwa sana ili kwamba waweze kuwasaidia watu wengine inazungumziwa kana kwamba walikuwa mzabibu ambao huotesha matunda mengi sana hadi kufunika dunia.

Isaiah 27:7

Je! Yahwe amemshambulia Yakobo na Israeli kama alivyoshambulia mataifa ambayo yaliwashambulia?

Swali linatumika kutofautisha ukali wa adhabu ya Mungu. "Yahwe kwa uhakika aliadhibu adui wa mataifa zaido na alivyoadhibu watu wa Israeli"

Yakobo ... Israeli

Haya yanawakilisha vizazi vya Yakobo.

Je! Yakobo na Israeli wameuwawa kama katika kuchinja kwa mataifa yale ambayo yaliuwawa na wao?

Swali hili pia linatumika kutofautisha ukali wa adhabu ya Mungu. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yahwe hajawaua watu wa Israeli kama alivyowaua adui zake kutoka kwa mataifa mengine"

Kwa kipimo sahihi umepambana

Hapa "umepambana" ina maana ya Mungu. Yahwe kuadhibu watu wake kama walivyohitaji inazungumziwa kana kwamba adhabu ya Mungu ilikuwa kity ambacho kiliweza kupimwa. "Lakini uliwaadhibu kama ilivyohitajika"

kuwatuma mbali Yakobo na Israeli

Hii inawakilisha uzao wa Yakobo "kuwatuma Waisraeli mbali"

aliwafukuza mbali kwa upepo wake mkali, katika siku ya upepo wa mashariki

Nguvu ya Yahwe kuwatuma watu wake mbali katika nchi ya kigeni inazungumziwa kana kwamba Yahwe alitumia upepo kuwapuliza mbali mpaka nchi ya kigeni. "nguvu ya Yahwe kuwaendesha nje kama upepo mkali kutoka mashariki"

Isaiah 27:9

Kwa hiyo kwa njia hii

Maana zaweza kuwa 1) "hii" ina maana ya Yahwe kuwatuma watu uhamishoni kama Isaya alivyosema katika mstari uliopita au 2) "hii" ina maana ya matendo ambay Isaya atayataja katiika sehemu inayofuata ya mstari wa 9.

udhalimu wa Yakobo utalipiwa kosa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe ataondoa dhambi kutoka kwa Waisraeli" au "Yahwe atasamehe dhambi ya Waisraeli"

udhalimu wa Yakobo ... kuondolewa kwa dhambi yake

Hapa "Yakobo" inawakilisha uzao wa Yakobo. "udhalimu wa Waisraeli ... kuondolewa kwa dhambi zao"

kwa maana hii itakuwa

Hapa "hii" ina maana ya matendo ambayo Isaya atafafanua katika sehemu inayofuata ya mstari wa 9.

tunda kamili

Hii inazungumzia matokeo ya matendo kana kwamba ilikuwa tunda ambalo huota juu ya mti au mzabibu. "tokeo"

atafanya mawe yote ya madhabahu kama chokaa na kupondwa vipande vipande, na hakuna nguzo za Ashera au ubani wa madhabahu utabaki ukisimama

Hapa "atafanya" ina maana ya Yakobo ambaye anawakilisha vizazi vyake. "Wataangamiza kabisa madhabahu yote ambayo wanatoa sadaka kwa miungu ya uongo, na watatoa sanamu zote za Ashera na madhabahu ambayo wanachoma ubani kwa miungu ya uongo"

Isaiah 27:10

Kwa maana mji ulioimarishwa una ... kumaliza matawi yake

Hapa isaya anafafanua tukio ambalo litatokea katika siku za usoni kana kwamba limeshatokea. Hii inasisitiza ya kwamba hakika litatokea.

Kwa maana mji ulioimarishwa una ukiwa, na makazi yametelekezwa na kuachwa kama nyika

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Miji ambayo ilikuwa na nguvu na ilikuwa na watu wengi wanaoishi ndani mwao itakuwa tupu kama jangwa"

mji ulioimarishwa ... makazi

Hii haimaanishi mji bayana au makazi lakini miji au makazi kwa ujumla.

ndama hula, na pale hulala chini na kumaliza

Hapa "ndama" inawakilisha ndama au ng'ombe kwa ujumla. "ndama hula, na pale wanalala chini na kumaliza"

matawi ... sio watu wenye uelewa

Watu hawa kuwa dhaifu sana kwa sababu hawamtii Yahwe ili kwamba maadui waweze kuwaangamiza kwa urahisi inazungumziwa kana kwamba walikuwa matawi makavu ambayo wanawake huvunja kutoka kwenye mti.

Matawi yatakaponyauka, yatavunjwa. Wanawake watakuja na kutengeneza moto kwao

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Matawi yatakaponyauka, wanawake watakuja na kuyavunja na kutengeneza moto nayo"

hawa sio watu wenye uelewa

Hii inaweza kuwekwa wazi zaidi. "hawa sio watu ambao wanamwelewa Yahwe au sheria yake"

watu

Maana zaweza kuwa 1) "watu" ina maana ya watu wa Israeli au 2) "watu" ina maana ya watu wa mataifa ya kigeni ambao hukandamiza watu wa Israeli.

Kwa hiyo Muumba wao hatakuwa na huruma juu yao, na yule aliyewaumba hatakuwa na rehema kwao

Vishazi hivi viwili vina maana moja. "Kwa sababu hawaelewi, Yahwe, yule aliyewaumba, hatakuwa na rehema kwao"

Isaiah 27:12

Itakuja kuwa

Msemo huu unaweka alama kwa tukio muhimu ambalo litatokea.

katika siku hiyo

Hapa "siku" inawakilisha kipindi cha muda kwa ujumla.

Yahwe atapura

Yahwe kukusanya watu wake kuwarudisha kutoka mataifa ya kigeni katika nchi ya Israeli inazungumziwa kana kwamba alikuwa akipura mtama kugawanya nafaka kutoka kwa makapi.

kutoka Mto Frati, mpaka kwenye korongo kavu la mto la Misri

Isaya anataja Mto Frati na Korongo kavu la Misri kumaanisha ya kwamba Yahwe atawarudisha watu wa Israeli ambao walikuwa uhamishoni katika nchi karibu na maji hayo, yaani, Ashuru na Misri. Mto Frati ni kaskazini mashariki mwa Israeli, na Korongo Kavu la Misri ni kusini magharibi mwa Israeli.

korongo kavu la mto la Misri

"kijito kidogo cha Misri"

wewe ... utakusanywa mmoja baada ya mwingine

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawakusanya mmoja mmoja"

tarumbeta kubwa itapulizwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "mtu atapulizwa tarumbeta kwa sauti"

wanaoangamia katika nchi ya Ashuru watakuja, na waliotengwa katika nchi ya Misri

Taarifa inayoeleweka inaweza kuwekwa wazi. "wale ambao wapo uhamishoni na kufa katika nchi ya Ashuru na nchi ya Misri watarudi katika nchi ya Israeli"

mlima mtakatifu

"mlima mtakatifu" ni Mlima Sayuni, katika Yerusalemu.

Isaiah 28

Isaiah 28:1

Ole wake shada la maua lenye kiburi ...juu ya kichwa cha Bonde linalositawi ya wale ambao wamezidiwa na mvinyo

"shada la maua" ni taji linalotengenezwa kwa maua. Hapa linawakilisha mji wa Samaria, mji mkuu wa Israeli, ambao upo juu ya bonde lenye rutuba. Samaria na watu wake kuangamizwa inazungumziwa kana kwamba shada la maua litazeeka na kuacha kuwa zuri.

Tazama

"Sikiliza" au "Zingatia kwa makini"

ambao wamezidiwa na mvinyo

"ambao wamelewa kwa mvinyo"

Bwana humtuma yule ambaye ana uwezo na nguvu

Hapa "yule" ina maana ya mfalme mwenye nguvu ambaye pia anawakilisha jeshi lake lenye nguvu. "Bwana hutuma mfalme pamoja na jeshi lake lenye nguvu"

dhoruba ya mvua ya mawe

"Dhoruba ya mvua ya mawe" inatokea pale ambapo vipande vigumu vya barafu kutoka angani huanguka. Hapa ni tashbihi ambayo ina maana ya jeshi la adui ambalo Yahwe atatuma kuangamiza watu wa Samaria.

atatupa kila taji la shada la maua chini katika ardhi

Mfalme na jeshi lake lenye nguvu kuangamiza watu wa Samaria na mji wao inazungumziwa kana kwamba mfalme atarusha mashada ya maua ya watu chini ardhini.

Isaiah 28:3

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza juu ya watu na mji wa Samaria kana kwamba walikuwa shada la maua.

Shada la maua lenye kiburi la walevi wa Efraimu watakanyagwa chini ya miguu

Isaya anaendelea kuzungumza juu ya watu na mji wa Samaria kana kwamba walikuwa shada la maua.

shada la maua lenye kiburi ... wa Efraimu ... ambao uko juu ya kichwa cha bonde tajiri

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Jeshi la adui litaponda walevi wenye kiburi wa Samaria kana kwamba walikuwa wakiponda maua chini ya miguu yao"

litakuwa kama mtini ulioiva ... hugugumia chini

Hii inazungumzia wanajeshi wa adui kuona uzuri wa Samaria na kupora kwa haraka kana kwamba walikuwa mtu ambaye huona mtini wa kwanza wa msimu na kula haraka.

Isaiah 28:5

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli.

atakuwa taji zuri na taji lenye uzuri

Yahwe anazungumziwa kana kwamba alitakiwa kuwa taji zuri ambalo watu wanaomheshimu kama mfalme wao wa kweli wangevaa.

taji zuri na taji lenye uzuri

Hii ina maana ya kitu kimoja. "taji zuri"

watu wake, roho ya haki kwa ajili yake ambaye hukaa katika hukumu, na nguvu

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "haki" inaelezwa kama kitenzi "kuwa na haki". "watu". Yahwe atasababisha waamuzi kuwa na haki na kutoa nguvu"

roho ya haki

Mtu ambaye ana "roho ya haki" ni mtu ambaye ana sifa za haki na ni mtu mwenye haki.

hukaa katika hukumu

Lahaja hii ina maana ya mtu ambaye ana mamlaka ya kuhukumu.

na nguvu kwa wale ambao huwageuza maadui zao katika malango yao

Hapa "kuwageukia" ni lahaja ambayo ina maana ya kushinda vitani. "na Yahwe atasababisha wanajeshi kuwa na nguvu ili kwamba wawashinde adui zao pale ambapo maadui wanashambulia mji wao"

Isaiah 28:7

Lakini hata hawa

"Lakini hata viongozi"

Kuhani na nabii

Hii haimaanishi kuhani mmoja au nabii. Ina maana ya makuhani na manabii kwa ujumla. "Makuhani na manabii"

hupepesuka kwa mvinyo, na kuyumbayumba kwa kinywaji kikali

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza ya kwamba makuhani na manabii hawawezi kufanya kazi yao kwa sababu wamelewa sana. "kujikwaa kwa sababu wamelewa"

wanamezwa kwa mvinyo

Kunywa kwao sana hadi wanashindwa kufikiri kwa usahihi inzungumziwa kana kwamba mvinyo imewameza. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "divai inawafanya kuchanganyikiwa"

wayumbayumba katika kuangalia na kupepesuka katika maamuzi

Kama ambavyo wamelewa sana kutembea sawa sawa, wamelewa sana kuelewa maono Mungu anayowapatia au kufanya maamuzi sahihi.

Isaiah 28:9

Ni kwa nani atamfundisha maarifa, na kwa nani ataelezea ujumbe?

Manabii na makuhani walevi wanatumia swali kumkosoa Isaya, ambaye anajaribu kuwasahisha. "Manabii walevi na makuhani wanasema, 'Isaya hatakiwi kujaribu kutufundisha kuhusu ujumbe wa Yahwe!'"

Kwa wale ambao wameachishwa maziwa au kwa wale ambao wameondolewa tu kutoka kwenye titi?

Manabii na makuhani walevi wanatumia swali kumkosoa Isaya, kwa sababu wanahisi ya kwamba anawafanya kama watoto. "Hatakiwi kutufanya kama watoto!"

Kwa maana ni amri baada ya amri, amri juu ya amri; utawala juu ya utawala, utawala juu ya utawala; hapa kidogo, pale kidogo

Manabii na makuhani walevi wanamkosoa Isaya kwa sababu wanahisi Isaya anarudia amri za kawaida kana kwamba alikuwa akiongea kwa mtoto.

Isaiah 28:11

kwa midomo ya kukejeli na ulimi wa kigeni atazungumza kwa watu hawa

Hapa "midomo" na "ulimi" inawakilisha wageni ambao huongea lugha tofauti na wanayozungumza Waisraeli. Inadokezwa ya kwamba hii ina maana ya jeshi la Ashuru ambalo litashambulia Israeli. "Yahwe atazungumza kwa watu hawa kupitia majeshi ya maadui ambao wataongea lugha ya kigeni"

midomo ya kukejeli

"midomo yenye kigugumizi"

Haya ni mapumziko

Nomino dhahania "pumziko" inaweza kuandikwa kama kivumishi. "Hii ni sehemu ya kupumzika"

toa mapumziko kwake ambaye amechoka

Nomino dhahania "pumziko" inaweza kuwekwa kama kitenzi. "acha yule ambaye amechoka aje na apumzike"

hiki ni kiburudisho

Nomino dhahania "kiburudisho" inaweza kuwekwa kama kitenzi. "hii ni seheu ambayo unaweza kuburudika"

Isaiah 28:13

Kwa hiyo neno la Yahwe

Hapa "neno" linawakilisha ujumbe. "Kwa hiyo ujumbe wa Yahwe"

amri juu ya amri, amri juu ya amri; utawala juu ya utawala, utawala juu ya utawala; hapa kidogo, pale kidogo

Haya ni maneno ambayo makuhani na manabii walevi walitumia jinsi Isaya anawafundisha wao.

ili kwamba waweze kuondoka na kuanguka nyuma, na kuvunjika, kutegwa na kukamatwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ili kwamba jeshi la Ashuru litakuja na kuwashinda na kuwachukua kama mateka"

kuondoka na kuanguka nyuma

Watu kushindwa vitani kwa jeshi la adui linazungumziwa kana kwamba watu wataanguka chini na kuvunjika.

kutegwa

Wanajeshi wa adui kukamata watu wa Israeli inazungumziwa kana kwamba walikuwa wawindaji ambao hushika mnyama katika mtego.

Isaiah 28:14

Kwa hiyo sikiliza neno la Yahwe

Isaya sasa anazungumza kwa viongozi wa Yerusalemu. Hapa "neno" linawakilisha ujumbe. "Kwa hiyo sikiliza kwa ujumbe wa Yahwe"

Tumefanya agano na kifo, na kwa kuzimu tumefikia makubaliano

Kauli hizi mbili zina maana moja. Maana zinaweza kuwa 1) viongozi wa Yerusalemu wametumia mazingaombwe au uchawi kujaribu kufanya makubaliano na miungu ya sehemu za wafu ili kwamba miungu hawa wawalinde kutokufa au 2) hii ni sitiari ambayo inazungumzia viongozi kufanya makubaliano na viongozi wa Misri. Viongozi wa Yerusalemu walikuwa wanajiamini sana hadi Wamisri wangewalinda na kuonekana kana kwamba walifanya makubaliano na miungu wa sehemu ya wafu.

Kwa hiyo mjeledi mkubwa kabisa utakapopita katikati, hautatufikia sisi

Hii inazungumzia hukumu ya Yahwe na adhabu kana kwamba ilikuwa mjeledi ambao ungewapiga watu. Na mjeledi unazungumziwa kana kwamba ulikuwa mafuriko ambayo yangepita katikati ya Yerusalemu. "Kama matokeo, ambapo wengine wote wanateseka na kufa, hakuna kitu kitatudhuru"

Kwa kuwa tumetengeneza uongo kimbilio letu, na kujiweka hifadhi katika uongo

Misemo hii miwili ina maana moja. "Uongo" unazungumziwa kana kwamba ilikuwa sehemu ambayo mtu angeweza kwenda kujificha. Viongozi wa Yerusalemu wasingesema wanatumaini katika uongo. Waliamin walikuwa salama kabisa. Lakini Isaya anajua hawako salama, kwa sababu wanaamini katika uongo. "Kwa maana uongo umekuwa kama sehemu ambayo tunaweza kujificha kutoka hatarini"

uongo kimbilio letu ... kujiweka hifadhi katika uongo

Maana zaweza kuwa 1) viongozi wanaamini katika uongo ambao wamesema ili kujilinda wenyewe au 2) viongozi huamini ya kwamba agano walilofanya na miungu ya uongo ya sehemu ya wafu itawaweka salama au 3) viongozi huamini ya kwamba makubaliano ambayo wameyafanya na Wamisri itawaweka salama.

Isaiah 28:16

Tazama

"Sikiliza hili"

Nitatandaza Sayuni jiwe la msingi ... msingi wa hakika

Yahwe kumtuma mtu mwenye nguvu kusaidia watu wa Israeli inazungumziwa kana kwamba Yahwe anajenga msingi wa nguvu kwa ajili ya jengo.

jiwe lililojaribiwa

"jiwe ambalo ni thabiti"

msingi wa hakika

"mhimili imara"

Yule ambaye huamini hataaibika

"Yeyote ambaye huamini katika jiwe hili la msingi hatajilaumu"

Isaiah 28:17

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kulinganisha kile atakachofanya kwa ajili ya watu wa Yerusalemu kwa mjenzi kuandaa jengo.

Nitafanya hukumu fimbo ya kupimia, na haki timazi

Yahwe kujaribu kulingana na hukumu yake na haki kuthiibitisha kama watu wana haki inazungumziwa kana kwamba alikuwa mjenzi akitumia vifaa kuthibitisha ya kwamba kitu ni urefu sahihi na usawa wa kamili.

fimbo ya kupimia

Mjenzi hutumia fimbo ya kupimia kubainisha kama kitu kina urefu sahihi.

timazi

Mjenzi hutumia fimbo ya kupimia kubainisha kama kitu kipo wima na usawa.

Mvua ya mawe itaondoa

Yahwe kusababisha kiasi kikubwa cha mvua ya mawe kuanguka inazungumziwa kana kwamba itakuwa mafuriko makubwa. "Mvua za mawe zitaangamiza"

Mvua ya mawe ... maji ya mafuriko

Maana zaweza kuwa 1) maneno yenye maana sawa yanayowakilisha kitu chochote kwa ujumla ambacho kitasababisha uharibifu au 2) hizi ni sitiari kwa jeshi la adui ambalo Yahwe atalituma kuangamiza watu wa Yerusalemu.

Mvua ya mawe

Vipande vikubwa vigumu vya barafu ambavyo huanguka kutoka angani

kimbilio la uongo ... sehemu ya kujificha

Hii inazungumzia kuhusu "uongo" kana kwamba ulikuwa sehemu ambao mtu angeweza kwenda kujificha. Inawakilisha kile viongozi wa Yerusalemu waliamini kuwaweka salama kwa adhabu ya Yahwe. Maana zaweza kuwa 1) viongozi wanaamini katika uongo wao wenyewe ambao wamesema ili kujilinda wenyewe au 2) viongozi wanaamini ya kwamba agano walilofanya na miungu ya uongo ya sehemu ya wafu itawaweka salama au 3) viongozi wanaamini ya kwamba makubaliano na Wamisri yatawaweka salama.

Isaiah 28:18

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

Agano lako na kifo litayeyushwa, na makubaliano yako na kuzimu hayatasimama

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nitafuta agano ambalo umefanya na kifo, na nitafuta makubaliano uliyofanya na kuzimu"

agano lako na kifo ... makubaliano na kuzimu

Maana zaweza kuwa 1) viongozi wa Yerusalemu wametumia mazingaombwe au uchawi kujaribu kufanya makubaliano na miungu ya sehemu za wafu ili kwamba miungu hawa wawalinde kutokufa au 2) hii ni sitiari ambayo inazungumzia viongozi kufanya makubaliano na viongozi wa Misri. Viongozi wa Yerusalemu walikuwa wanajiamini sana hadi Wamisri wangewalinda na kuonekana kana kwamba walifanya makubaliano na miungu wa sehemu ya wafu.

hayatasimama

"hayatadumu"

Pale ambapo mafuriko makali yatakapopita

Maana zaweza kuwa 1) "mafuriko" ni maneno yenye maana sawa na yanawakilisha kitu chochote kwa ujumla ambacho kitasababisha uharibifu au 2) "mafuriko" ni sitiari inayomaanisha jeshi la adui ambalo Yahwe atatuma kuangamiza watu wa Yerusalemu.

utazidiwa nayo

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "itakuzidia" au "itakuangamiza"

asubuhi kwa asubuhi

Hii ni lahaja. "kila siku"

kwa mchana na usiku

Hii ina maana "katika siku nzima"

Isaiah 28:20

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

Kwa maana kitanda ni kifupi sana kwa mtu kujinyosha juu, na blangeti ni nyembamba sana kwake kujifunika ndani yake

Huenda hii ilikuwa methali ambayo watu walijua katika kipindi hicho. Ina maana ya kwamba kile wanachoamini kitawaweka salama kutoka kwa adhabu Yahwe atawaangusha kama kitanda ambacho ni kifupi mno au blangeti ambayo ni nyembamba mno.

Yahwe atainuka

Yahwe kujiandaa kutenda inazungumziwa kana kwamba alikuwa amekaa na kisha kuinuka.

Mlima Perasimu ... Bonde la Gibeoni

Hii ina maana ya sehemu ambazo Mungu aliwashinda kwa miujiza majeshi ya adui.

atajiamsha yeye

"atakuwa na hasira sana"

kazi yake ya ajabu ... tendo lake la ajabu

Misemo hii miwili ina maana moja. Kazi hii ni ya ajabu kwa sababu Mungu anatumia jeshi geni kuwashinda watu wa Yerusalemu kuliko kusaidia watu wa Yerusalemu kushinda adui zao.

Isaiah 28:22

Sasa

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki", lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu ambalo linafuata.

vifungo vyako vitakazwa

Yahwe kuadhibu watu kwa ukali zaidi inazungumziwa kana kwamba angekaza vifungo vyao. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atakaza vifungo vyako" au "Yahwe atakuadhibu kwa ukali zaidi"

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli.

maagizo ya uharibifu katika dunia

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "uharibifu" uelezwe kama kitenzi "angamiza". "ya kwamba anakwenda kuangamiza watu katika nchi"

Isaiah 28:23

Taarifa ya Jumla

Hii inaanza mfano ambao unaisha katika 28:29

Zingatia kwa makini na sikilizia sauti yangu; uwe msikivu na sikiliza maneno yangu

Misemo hii miwili ina maana moja. Msemo wa pili unatumka kuimarisha wa kwanza.

sauti yangu

Hapa "sauti" inawakiliisha kile Isaya anasema. "kwa kile nachosema"

maneno yangu

Hapa "maneno" yanawakilisha ujumbe. "kwa ujumbe wangu"

Je! mkulima anayelima siku nzima kupanda, huwa analima tu? Je! huwa anaendelea kuvunja na kupiga haro shamba?

Isaya anatumia maswalii ya balagha kufanya watu wafikiri kwa undani. "Mkulima halimi ardhi tena na tena na kuendelea kufanya kazi bila kupanda mbegu"

Isaiah 28:25

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuwaambia mfano watu wa Yerusalemu.

Atakapokuwa ameandaa ardhi

"Mkulima alipolima udongo"

je! hatawanyi mbegu ya kisibiti, kupanda jira, kuweka ngano katika mistari na shayiri katika sehemu sahihi, na kusemethi katika mipaka yake?

Isaya anatumia swali kuwafanya watu wa Yerusalemu kuwaza kwa ndani. "hakika atapanda kila aina ya mbegu kwa njia sahihi katika seheu sahihi".

kisibiti ... jira

Haya ni majina ya mimea ambayo ni viungo.

ngano ... shayiri ... kusemethi

Haya ni majina ya mimea ambayo ni nafaka.

Mungu wake humwelekeza; humfundisha kw hekima

Misemo hii miwili ina maana moja. "Yahwe humsaidia mkulima kujua namna ya kutunza kila aina ya mmea"

Isaiah 28:27

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuwaambia mfano watu wa Yerusalemu.

mbegu ya kisibiti haipurwi kwa nyundo ya kupura

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "mkulima hagawanyish mbegu ya kisibiti kutoka kwa mmea kwa rungu nzito"

kisibiti

Haya ni majina ya mimea ambayo ni viungo.

wala gurudumu la gari huviringishwa juu ya jira

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wala waviringisha gurudumu ziito juu ya mbegu ya jira"

jira

Haya ni majina ya mimea ambayo ni viungo.

lakini kisibiti inapigwa kwa kijiti, na jira kwa rungu

Isaya anafafanua njia sahihi ya mkulima kutenganisha mbegu kutoka kwa mmea. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "lakini hupiga kisibti kwa fimbo, na hupiga jira kwa rungu"

Nafaka ni ardhi kwa mkate lakini sio kwa ubora sana

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mkulima husaga nafaka kwa ajili ya mkate lakini sio kwamba iwe ndogo sana"

Isaiah 28:29

Hii pia huja ... bora katika hekima

Hii inahitimisha mfano ulioanza katika 28:23. Somo linalodokezwa la mfano ni kwamba wakulima wana hekima ya kutosha kusikiliza maagizo ya Yahwe kuhusu kupanda na kupura. Lakini viongozi wa Yerusalemu ni wapumbavu kwa kutosikia maagizo ya Yahwe ya kwamba anazungumza kupitia Isaya.

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi wa Israeli.

Isaiah 29

Isaiah 29:1

Ole wa Arieli

Hapa "Arieli" inawakilisha watu ambao wanaishi katika mji wa Arieli. "Jinsi gani itakuwa vibaya kwa watu wa Arieli"

Arieli

Hili ni jina lingine kwa ajili ya Yerusalemu, na lina maana ya "madhabahu".

Daudi alipoweka kambi

"Daudi alikaa" au "Daudi aliishi"

Ongeza mwaka kwa mwaka; acha sikukuu ziwadie

"endelea kusherehekea sikukuu yako mwaka baada ya mwaka". Hili ni tamko la kejeli. Yahwe anawaambia watu kuendelea kusherehekea sikukuu zao ambapo wanatoa sadaka kwake, lakini anajua haitamzuia kuwaangamiza.

Lakini nitazingira

Neno "nitazingira" ina maana ya Yahwe. Hii inawakilisha Yahwe kusababisha jeshi la adui kuzingira Yerusalemu.

atakuwa

Hapa "atakuwa" ina maana ya Arieli, ambayo inawakilisha watu wa Arieli. "watu wa Arieli wata"

kulia na kuomboleza

Maneno "kulia" na "kuomboleza" ina maana moja na inasisitiza ukali wa maombolezo. "wataomboleza kwa uchungu"

kama Arieli

Jina la Arieli lina maana ya "madhabahu"

Isaiah 29:3

Nitapiga kambi dhidi yako

Neno "nitapiga" ina maana ya Yahwe. Hii inawakilisha Yahwe kusababisha jeshi la adui kuziingira Yerusalemu. "Nitaamuru jeshi la adui zako kukuzingira"

uzio ... kazi za kuzingira

"Uzio" ni mnara ambao majeshi hujenga kushambulia miji kwa kuta ndefu. Pia, "kazi za kuzingira" ina maana ya silaha za aina nyingine majeshi hujenga kushambulia miji.

Utawekwa chini

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Adui wako atakuleta chini" au "Adui wako atakushusha"

na utazungumza kutoka ardhini; usemi wako utakuwa chini kutoka mavumbini. Sauti yako itakuwa kama zimwi kutoka kwenye ardhi, na usemi wako utakuwa dhaifu sana kutoka mavumbini

Kauli hizi zote zina maana moja. Zinasisitiza ya kwamba watu ambao hapo awali walizungumza maneno ya kujivuna watakuwa dhaifu na kulia baada ya adui kuwashinda. "na utaweza tu kuonge kwa minong'ono dhaifu kama ya roho inayozungumza ambapo wafu huishi"

Isaiah 29:5

Umati wa wavamizi wako watakuwa kama vumbi dogo, na wingi wa walio wakatili kama makapi ya majani ambacho hupita mbali

Hii inasisitiza jinsi jeshi linalovamia ni dhaifu na lisilo na maana mbele za Mungu. "Yahwe ataondoa kirahisi umati wa wavamizi wako na wingi wa walio katili"

umati wa mavazi yako

"wanajeshi wengi watakushambulia"

walio wakatili kama makapi ya majani

"wanajeshi ambao hawataonyesha huruma watakuwa kama makapi ya majani"

Yahwe wa majeshi atakuja kwako

Neno "kwako" ina maana ya watu wa Yerusalemu. Maana zaweza kuwa 1) "Yahwe wa majeshi atakuja kukusaidia" au 2) "Yahwe wa majeshi atakuja kukuadhibu"

Isaiah 29:7

Itakuwa kama ndoto, maono ya usiku

Msemo "maono ya usiku" ni jambo sawa na "ndoto". Misemo hii inasisitiza ya kwamba hivi karibuni itakuwa kama jeshi linalovamia halikuwa pale.

Umati wa mataifa yote

"Majeshi makubwa kutoka mataifa yote"

watapigana dhidi ya Arieli

Jina "Arieli" ni jina lingine kwa Yerusalemu, na inawakilisha watu ambao wanaishi kule. "kupigana dhidi ya watu wa Arieli"

ngome yake. Watamshambulia na kuimarishwa kwake kugandamiza juu yake

Neno "yake" ina maana ya Arieli ambayo inawakilisha watu ambao wanaishi kule. "ngome zao. Watashambulia mji wa Arieli na ulinzi wake na kusababisha watu kuwa katika mateso makubwa"

itakuwa kama vile mtu mwenye njaa anavyoota anakula ... kiu yake haikatwi

Tashbihi ina maana ya kwamba adui atategemea ushindi lakini watashindwa kwa sababu Mungu hataruhusu wao kushinda Yerusalemu.

Ndio, ndivyo itakavyokuwa idadi kubwa ya mataifa ambayo hupigana dhidi ya Mlima Sayuni

Hapa "Mlima Sayuni" inawakilisha watu ambao wanaishi kule. "Ndio, hivi ndivyo itakavyotokea kwa majeshi kutoka kwa mataifa ambayo hupigana dhidi ya watu wanaoishi juu ya Mlma Sayuni"

Isaiah 29:9

Jishangaze mwenyewe na ushangazwe

Neno "mwenyewe" lina maana ya watu wa Yerusalemu. Kwa nini wanashangazwa inawvza kuwekwa wazi. "Ushangazwe kwa kile nachotaka kukuambia"

jipofushe na uwe kipofu

Watu kupuuza kile Yahwe anasema inazungumziwa kana kwamba wangeweza kujifanya vipofu wenyewe. "endelea kuwa mjinga na kipofu wa kiroho kwa kile nachokuonyesha"

Lewa, lakini sio kwa divai; pepesuka, lakini sio kwa mvinyo

Watu kutokuwa na ufahamu na kutoelewa kile Yahwe anafanya inazungumziwa kana kwamba walikuwa wamelewa. "Uwe bila ufahamu kama mtu mlevi, lakini sio kwa sababu umekunywa divai au mvinyo kupitiliza"

Kwa maana Yahwe amekumwagia juu yako roho ya usingizi mzito

Hapa " roho ya" ina maana "kuwa na sifa za" kuwa na usingizi. Yahwe kusababisha watu kuwa na usingizii inazungumziwa kana kwamba "roho" ilikuwa kimiminiko ambacho kilimwagwa juu ya watu. Pia "usingizi mzito" ni sitiari ambayo ina maana ya watu ambao hawana ufahamu na hawawezi kuelewa kile Yahwe anafanya. "Sababu hauna ufahamu ni kwa sababu Yahwe amesababisha uwe umelala kiroho"

Ameyafumba macho yako, manabii, na amefunika vichwa vyako, watazamaji

Yahwe kusababisha watu kutokuwa na ufahamu na kutoelewa kile anachofanya inazungumziwa kana kwamba alifumba macho yao na kufunika vichwa vyao ili wasiweze kuona. "Ni kana kwamba Yahwe amefumba macho ya manabii na kufunika vichwa vya watazamaji"

Isaiah 29:11

Ufunuo wote umekuwa kwako kama maneno ya kitabu kilichofungwa kabisa

Nabii mwingine Yerusalemu hawawezi kusikia au kuelewa ujumbe wa Mungu. "Yote ambayo Yahwe amefunua kwako ni kama kitabu kilichofungwa kabisa"

kilichofungwa, ambacho watu wanaweza kutoa kwa yule ambayo amesoma

Hii inaweza kuandikwa kama sentensi mpya. "inafungwa kabisa. Mtu anaweza kuchukua kitabu kilichofungwa kabisa kwa mtu ambaye anaweza kusoma"

kama kitabu kinatolewa kwa yule ambaye hawezi kusoma

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kama mtu anachukua kitabu kwa mtu ambaye hawezi kusoma"

Isaiah 29:13

Watu hawa huja karibu na mimi kwa vinywa vyao na kuniinua mimi kwa midomo yao

Maneno "vinywa" na "midomo" inawakilisha kile watu wanasema. Hapa pia inawakilisha kusema kitu lakini sio kukimaanisha kihalisia. "Watu wa Yerusalemu wanavunga kuniabudu na kuniheshimu kwa kile wanachosema"

lakini moyo wao upo mbali na mimi

Hapa "moyo" ni neno linalowakilisha mawazo ya mtu na hisia. Watu kutokuwa na kujizatiti kwa Yahwe inazungumziwa kana kwamba mioyo yao ilikuwa mbali sana kutoka kwake. "lakini hawaniheshimu katika mawazo yao" au "lakini hawajizatiti kwangu kiukweli"

Heshima yao kwangu ni amri to ya watu ambayo imefundishwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Wananiheshimu tu kwa sababu hicho ndicho watu wanawaambia kufanya"

Kwa hiyo, tazama, nitaendelea kufanya jambo la ajabu katika hawa watu, ajabu baada ya ajabu

"Kwa hiyo, tazama na angalia! ninaenda kufanya mambo mazuri na ya ajabu miongoni mwako ambayo hutaweza kuyaelezea"

Hekima ya watu wenye hekima wao itatoweka, na uelewa wa watu wenye busara wao itapotea

Kauli hizi mbili zina maana moja. Yahwe kuonyesha ya kwamba watu wenye hekima hawawezi kuelewa au kufafanua kile Yahwe anafanya inazungumziwa kana kwamba hekima yao na uelewa utapotea.

Isaiah 29:15

Taarifa ya Jumla

Huyu anaweza kuwa Isaya akizungumza au inaweza kuwa muendelezo wa maneno ya Yahwe katika 29:13-14.

ambao huficha kwa chini kabisa mipango yao kutoka kwa Yahwe

Watu kujaribu kutengeneza mipango bila Yahwe kujua inazungumziwa kana kwamba kama wanaficha mipango yao katika sehemu ya chini ambapo Yahwe hawezi kuona. "ambao wanajaribu kumzuia Yahwe kutogundua kile wanachopanga kufanya"

ambao mateno yao yamo gizani

Inadokezwa ya kwamba wanafanya mambo maovu kwa siri. "ambao hufanya mambo maovu gizani ili mtu asiwaone"

Ambao hutuona, na ambao wanatujua sisi?

Wanatumia swali kusisitiza ya kwamba wanaamini hakuna mtu anayejua kile wanachofanya. "Hakuna mtu, hata Yahwe, anatuona au kujua kile tunachofanya!"

Isaiah 29:16

Unageuza vitu juu chini

Hii ni lahaja ambayo ina maana ya kupotosha kile kilicho cha ukweli. "Unafanya vitu kinyume na namna vinavyotakiwa kuwa" au "Unatakiwa kupotosha ukweli"

Je! mfinyanzi achukuliwe kama udongo, ili kwamba kitu ambacho kimetengenezwa kiweze kusema juu yake ambaye amekitengeneza ... "Yeye haelewi"?

Yahwe ambaye aliumba wanadamu inazungumziwa kana kwamba alikuwa mfinyanzi na wanadamu walikuwa udongo. Sitiari hi nasisitiza ya kwamba ni upumbavu kwa wanaamu kukataa au kukosoa yule ambaye aliviumba. "Je! utanichukulia, muumba wako, kuwa kama udongo badala ya mfinyanzi? Ni kana kwamba mfinyanzi aliumba kitu, na hicho kitu kikasema kuhusu mfinyanzi, "Hakuniiumba mimi", au "Haelewi"

e! mfinyanzi achukuliwe kama udongo ... "Yeye haelewi'"?

Swali hili linatumika kukaripia watu wa Yerusalemu. "Ni dhahiri, mfinyanzi hatakiwi kuchukuliwa kama udongo ... "Yeye haelewi'"

Isaiah 29:17

Lebanoni itageuzwa kuwa shamba, na shamba litakuwa msitu

Maana zaweza kuwa 1) huu ni uhalisi na Yahwe atasababisha maeneo ambapo miti iliota pori katika Lebanoni kuwa mashamba yanayozaa au 2) hii ni sitiari na misitu mikubwa ya Lebanoni inawakilisha wakandamizaji wenye nguvu, na mazao ambayo huota katika shamba na kuwa msitu ni watu wa kawaida ambao wanateseka. Hii ina maana Yahwe atawashusha wale ambao ni wenye nguvu, lakini atawainua wale ambao wanateseka.

Lebanoni itageuzwa kuwa shamba

Hapa "Lebanoni" inawakilisha msitu mkubwa wa mvinje wa Lebanoni. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu atageuza msitu mkubwa wa Lebanoni kuwa shamba"

kiziwi atasikia maneno ya kitabu, na macho ya kipofu yataona giza nene

Maana zaweza kuwa 1) huu ni uhalisi na Yahwe atasabisha watu viziwi kusikia na watu vipofu kuona au 2) hii ni sitiari ya kwamba Yahwe atawezesha watu kusikia na kuelewa ujumbe wake au 3) inaweza kumaanisha zote 1 na 2.

macho ya kipofu

Hapa "macho" yanawakilisha mti kamili. "wale ambao ni vipofu"

Waliokandamizwa watafurahi tena katika Yahwe, na maskini miongoni mwa watu watafurahi katika Mtakatiifu wa Israeli

Misemo hii miwili ina maana moja. "Maskini na watu waliokandamizwa watafurahi tena kwa sababu ya kile Yahwe , Mtakatifu wa Israeli, alichofanya"

Isaiah 29:20

Kwa maana wakatili watakoma

Kivumishi kiidogo "wakatili" kinaweza kuwekwa kama kivumishi. "Kwa maana watu wakatili watakoma" au "Kwa kuwa hapatakuwa tena na watu katili"

na mwenye dharau atatoweka

Kivumishi kidogo "mwenye dharau" kinaweza kuandikwa kama kitenzi. "na wale ambao hudharau watatoweka" au "na watu ambao hukejeli watapotea"

Wote wale ambao hupenda kutenda uovu wataondoshwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe ataondosha wote wale ambao hupenda kutenda uovu"

ambao kwa neno humfanya mtu kuwa mhalifu

Hapa "neno" linawakilisha ushuhuda mahakamani. "ambao husem mahakamani ya kwamba mtu asiye na hatia ana hatia ya kufanya jambo baya"

Wanalaza mtego kwa ajili yake atafutaye haki katika lango na kuiweka haki chini kwa uongo mtupu

Watu waovu kufanya chochote wawezacho kumzuia mtu mwema inazungumzwa kana kwamba watu waovu waliweka mtego kama mwindaji akikamata mawindo. "Wanadanganya na kujaribu kuzuia wale ambao wanataka kufanya kiilicho haki na sahihi"

atafutaye haki katika lango

Malango ya mji mara kwa mara yalikuwa sehemu ambapo viongozi wa mji walifanya maamuzi rasmi.

Isaiah 29:22

nyumba ya Yakobo

Hapa "nyumba" inawakiliisha familia. "vizazi vya Yakobo"

ambao walimkomboa Abrahamu

Hii huenda ina maana ya pale Yahwe alipomwita Abrahamu kutoka katika nchi yake ya nyumbani na kumtuma katika nchi ya ahadi.

Yakobo hata ... uso wake ...atakapowaona watoto wake

Hapa "Yakobo" inawakilisha vizazi vyake. "Vizazi vya Yakobo havitakuwa tena ... nyuso zao ... wataona watoto wao"

wala uso wake kupauka

Hii ni lahaja ambayo ina maana ya hawatakuwa na hofu tena. "wala hawataogopa"

Lakini atakapowaona watoto wake, kazi ya mikono yangu

Hapa "mikono" inawakilisha nguvu na matendo ya Yahwe. "Watakapowaona watoto wote niliowapatia na yote niliyofanya"

watafanya jina langu kuwa takatifu

Hapa "jina" linawakilisha Yahwe. "wataniinua mimi"

Watafanya jina kuwa takatifu la Mtkatifu wa Yakobo

Hapa "jina" linawakilisha Yahwe. Yahwe anajitambua mwenyewe kama "Mtakatifu wa Yakobo". "Wataninua mimi, Mtakatifu wa Yakobo"

wa Mungu wa Israeli

Yahwe anajitambua mwenyewe kama "Mungu wa Israeli". "wa kwangu, Mungu wa Israeli"

Wale wanaopotoka katika roho

Hapa "roho" inawakilisha undani wa mtu. "Wale ambao wamekosea kwa kiile wanachowaza" au "Wale ambao wanakosea katika mtazamo wao"

watapata uelewa

Hii inaweza kufanywa waz zaidi kufafanua kile watakachoelewa. "wataanza kumuelewa Yahwe na sheria zake"

walalamishi watajifunza maarifa

Hii inaweza kuwekwa wazi kufafanua ni maarifa yapi watajifunza. "wale ambao wanalalamika wataanza kujua ya kwamba kile Yahwe anawafundisha ni cha kweli"

Isaiah 30

Isaiah 30:1

watoto waasi

Yahwe anazungumzia kuhusu watu wake kana kwamba walikuwa watoto wake.

hili ni tamko la Yahwe

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "tamko" inaelezwa kama kitenzi "kusema kwa dhati". "hiki ndicho kile Yahwe anachotamka" au "hiki ndicho kile Yahwe amesema kwa dhati"

Wanafanya mipango, lakini sio kutoka kwangu

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "mipango" iweze kuandikwa kama kitenzi "kupanga". "Wanapanga kufanya mambo, lakini hawaniulizi nini nachotaka wao kufanya"

lakini hawakuongozwa kwa Roho wangu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "lakini Roho waangu hakuwaongoza"

wanaongeza dhambi kwa dhambi

Kuendelea kutenda dhamb inazungumziwa kana kwamba dhambi iliikuwa maumbo ambayo yaliweza kupangwa juu ya mengine. "wanaendelea kutenda dhambi zaidi na zaidi"

Wanatafuta ulinzi kutoka kwa Farao

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "ulinzi" inaelezwa kama kitenzi "linda". "Wanamuuliza Farao kuwalinda"

na kufuata kimbilio katika kifuli cha Misri

Ulinzi wa Misri kutoka kwa jeshi la adui unazungumziwa kana kwamba ulikuwa kivuli ambacho hulinda mtu kutoka na joto linalochoma la jua. "wanawategemea Wamisri kuwaweka salama"

Isaiah 30:3

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

Kwa hiyo ulinzi wa Farao utakuwa aibu yako, na kimbilio katika kivuli cha Misri, fedheha yako

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "ulinzi", "aibu", na "fedheha" zinaelezwa kama vivumishi au vitenzi. "Kwa hiiyo utaibika kwa sabbu ulimtegemea Farao kukulinda; utafedheheshwa kwa sababu uliwategemea Wamisri kukuweka salama"

kimbilio katika kivuli cha Misri

Ulinzi wa Misri kutoka kwa jeshi la adui inazungumziwa kana kwamba ulikuwa kivuli ambacho humlinda mtu kutoka na joto linalowaka la jua.

wakuu

Hapa "wakuu" ina maana ya afisa au balozi, sio lazima wana wa mfalme.

wao ... wata ... wao

Maneno haya yana maana ya watu wa Yuda.

Soani ... Hanesi

Hii ilikuwa miji katika sehemu ya kaskazini ya Misri.

wamekuja Hanesi

Hapa "kuja" inaweza kuandikwa kama "kuondoka"

kwa sababu ya watu

"kwa sababu ya watu wa Misri"

Isaiah 30:6

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza tamko la Mungu kuhusu watu wa Yuda.

tamko

"Hiki ndicho Yahwe anachotamka"

ya simba jike na simba, kipiribao na nyoka mkali anayepaa

Hii ina maana ya aina hawa ya wanyama kwa ujumla. "ambapo simba jike na simba huishi, na ambapo kuna kipiribao na nyoka"

nyoka mkali anayepaa

Hapa neno "mkali" huenda una maana ya sumu ya nyoka anapouma na neno "kupaa" lina maana ya kusogea kwake kwa haraka.

wanabeba utajiri wao

"watu wa Yuda wanabeba utajiri wao"

nimemuita Rahabu, ambaye hukaa kwa kutulia

Kulikuwa na simulizi maarufu kuhusu joka la baharini linaloitwa Rahabu. Jina Rahabu ina maana ya "nguvu" au "kiburi". "Ninaita Misri mwenye kiburi wa sauti ambaye hafanyi lolote"

Isaiah 30:8

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na Isaya.

Sasa

Neno hili linatumika hapa kuweka alama ya pumziko katika tamko la Yahwe kuhusu Yuda. Hapa anamwambia Isaya kufanya kitu.

katika uwepo wao

"katika uwepo wa watu wa Yuda"

kwa maana muda umefika

Hii inazungumzia kipindi kana kwamba kinasafiri na kufika mahali. "kwa kipindi cha siku za usoni"

watoto waongo, watoto ambao hawasikii maelekezo ya Yahwe

Hii inazungumzia watu wa Yahwe kana kwamba walikuwa watoto wake. Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi. "Wanaenenda kama watoto ambao hudanganya na kutosikiliza kile Yahwe anachoamuru"

Isaiah 30:10

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kuhusu watu wa Yuda.

Geuka upande kutoka katika njia, potea kutoka katika njia

Jinsi Yahwe anavyotaka watu wake kuenenda inazungumziwa kana kwamba ilikuwa njia au barabara ambayo inatembelewa. Kutomtii Yahwe inazungumziwa kana kwamba mtu hupotea kutoka katika njia ya Yahwe.

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

Isaiah 30:12

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

unakataa neno hili

Hapa "neno" inawakilisha ujumbe. "unakataa ujumbe huu"

kuamini katika ukandamizaji na udanganyifu na kuiegemea

Maana zaweza kuwa 1) viongozi wa Yuda wanaamini katika viongozi wa Misri mbao hutawala kwa kukandamiza na kudanganya wengine au 2) viongozi wa Yuda wamekandamiza na kudanganya watu wao wenyewe ili kuchukua fedha zao na kuituma kwa viongozi wa Misri kama malipo kwa ajili ya ulinzi.

kuiegemea

Hapa neno "kuiegemea" ina maana ya "ukandamizaji na udanganyifu". "kuziegemea"

egemea katika

Hii ni lahaja ambayo ina maana ya kuamini au kutegemea juu ya kitu.

kwa hiyo dhambi hii kwako itakuwa kama sehemu iliyovunjika ... kwa mara moja

Tashbihi hii ina maana ya kwamba Mungu ataangamiza watu wa Yuda ghafla kwa sababu ya dhambi zao.

kama sehemu iliyovunjka tayari kudondoka

Inaeleweka ya kwamba hii ni sehemu iliyovunjika ya ukuta. "kama sehemu iliyovunjika ya ukuta ambayo iko tayari kuanguka"

ambao anguko lake litatokea ghafla

Hii inaweza kundikwa ili kwamba nomino dhahania "anguka" inaelezwa kama kitenzi "anguka". "ambayo itaanguka ghafla"

ghafla, kwa mara moja

Hizi zina maana ya kitu kimoja na husisitiza jinsi ukuta utakavyoanguka kwa haraka.

Isaiah 30:14

Taarifa ya Jumla

Isaya anafafanua jinsi Yahwe ataangamiza watu wa Yuda.

Ativunja

Hapa "ataivunja" ina maana ya sehemu ya ukuta ambayo inakaribia kuanguka. Sehemu katika ukuta ni sitiari ambayo inawakilisha watu wa Yuda na dhambi yao iliyotajwa katika 30:12

kama chombo cha mfinyanzi kinavyovunjwa

Tashbihi hii ina maana ya kwamba kipande cha ukuta kitavunjika haraka na kikamilifu kama jagi la udongo linapoanguka chini.

mfinyanzi

Mfinyanzi ni mtu ambaye hutengeneza vyungu na majagi kwa udongo.

hakutapatikana

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu ataweza kupata" au "hapatakuwa"

kigae ambacho kitatumika kukwangua

"kigae kikubwa ya kutosha kukwangua"

moto kutoka katika meko

Neno "moto" hapa lina maana ya majivu. "majivu kutoka katika sehemu ya moto"

Isaiah 30:15

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

Katika kurudi na kupumzika utaokolewa

Kutubu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kurudi kwa Yahwe kihalisia. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nitakuokoa kutok kwa adui zako kama utatubu na kupumzika ukijua ya kwamba nitakutunza"

kupumzika

Inadokezwa ya kwamba watu hupumzika kwa sababu wanamwaminii Yahwe kuwatunza.

katika utulivu na katika imani itakuwa nguvu yako

Utulivu hapa ina maana ya kutokuwa na wasiwasi. Inadokezwa ya kwamba hawana wasiwasi kwa sababu wanamwamini Yahwe. "Utakuwa na nguvu kama utakuwa kimya na kuniamini mimi"

tutatoroka juu ya farasi

Ni wazi kwamba farasi hizi ndizo ambazo watu wa Yuda walipokea kutoka kwa Wamisri.

Isaiah 30:17

Elfu moja watatoroka katika tishio la mmoja; katika tishio la watano utatoroka

Neno "mwanajeshi" linaeleweka. "Wanajeshi elfu moja watatoroka katika tishio la mwanajeshi mmoja wa adui; katika tishio la wanajeshi watano wa adui wanajeshi wako wote watatoroka"

Elfu moja

"1,000"

mpaka aliyesalia wa kwako ataakuwa kama fimbo ya bendera juu ya mlima, au kama bendera juu ya kilima

Tashbihi hii ina maana ya kwamba kutakuwa na watu wachache sana waliobaki mpaka watakuwa kama bendera moja juu ya kilima.

Isaiah 30:18

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

hautalia ... kwako ... atakujibu

Hapa "kwako" ina maana ya watu ambao wanaishi Sayuni.

atakujibu

"atakusaidia"

Isaiah 30:20

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

mkate wa shida na maji ya mateso

Hapa "mkate" na "maji" huunda mlo wa mtu maskini sana. Msemo wote unawakilisha nyakati ngumu na umaskini wa watu.

mwalimu wako

Hii ina maana ya Yahwe.

utamwona mwalimu wako kwa macho yako mwenyewe

Hapa "macho" inawakilisha mtu mzima. "nyie wenyewe mtamwona mwalimu wenu"

Masikio yako yatasikia

Hapa "masikio" inawakilsha mtu mzima. "Utasikia"

neno nyuma yako likisema

Hapa "neno" linawakilisha mtu anayezungumza. "yule anayezungumza nyuma yako akisema"

Hii ndiyo njia, tembea juu yake

Jinsi Yahwe anavyotaka watu wake kuenenda inazungumziwa kana kwamba ilikuwa njia au barabara. Kumtii Yahwe inazungumziwa kana kwamba ilikuwa mtu akitembea katika njia yake.

utakapogeuka kulia au utakapogeuka kushoto

Kumkaidi Yahwe inazungumziwa kana kwamb mtu aligeuka kushoto au kulia katika njia ya Yahwe.

Isaiah 30:22

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

Utazitupa mbali kama kitambaa cha hedhi

Tashbihi hii ina maana watatupa mbali sanamu zao kana kwamba zilikuwa takataka.

Utasema kwao, "Ondoka hapa"

Hii inazungumzia sanamu kana kwamba zinaweza kusikia na kuinuka na kuondoka mahali. Yahwe ana maana ya kwamba watu hawatahitaji au kutaka tena sanamu.

Isaiah 30:23

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

Atatoa

"Yahwe atatoa"

mkate kwa wingi kutoka ardhini

Hapa "mkate" unawakilisha chakula kwa ujumla. "atasababisha ardhi kutoa chakula kingi kwa ajili yako kula"

Katika siku hiyo

Hapa "siku" inawakilisha kipindi cha muda kwa ujumla. "Katika kipindi hicho"

ambayo imepepetwa kwa koleo na uma

Makoleo na uma yalitumika kurusha nafaka angani ili upepo upulize makapi, kuacha tu sehemu ambayo inaweza kuliwa. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambayo umepepeta kwa koleo na uma ya nyasi"

Isaiah 30:25

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

Katika kila mlima wa juu ... mwanga wa jua wa siku saba

Isaya anafafanua kile itakayokuwa hali sahihi baada ya Yahwe kukomboa watu wake.

katika siku ya machinjo makubwa ambapo minara huanguka

"Yahwe anapochinja adui zako na kusababisha minara yao yenye nguvu kuanguka"

katika siku hiyo

Hapa "siku" inawakilisha kipindi cha muda kwa ujumla. "katika kipindi hicho"

mwanga wa jua utakuwa na mwanga mara saba, kama mwanga wa jua wa siku saba

"jua litang'aa kwa mwanga wa jua saba" au "jua litatoa mwanga mwingi katika siku moja kama linavyotoa katika siku saba"

Yahwe atafunga kuvunjika kwa watu wake na kuponya vilia vya kuwajeruhi kwake

Yahwe kufariji watu wake na kusababisha mateso yao kufika mwisho inazungumziwa kana kwamba angefunga vitambaa juu ya vidonda vyao.

Isaiah 30:27

jina la Yahwe ... kma moto unaoteketeza

Yahwe kuwa na hasira kali inzungumziwa kana kwamba alikuwa moto mkubwa.

jina la Yahwe linakuja

Hapa "jina" linawakilisha Yahwe. "Yahwe anakuja"

Midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni kama moto unaoteketeza

Hapa "midomo" na "ulimi" ni mifano ya maneno ambayo inawakilisha Yahwe akzungumza. Na, Yahwe anazungumza na hasira kubwa na uwezo ambao unazungumziwa kana kwamba ulimi wake ulikuwa moto. "Anapozungumza hasira yake ni kama moto ambao huangamiza kila kitu"

Pumzi yake ni mbubujiko wa nguvu unaomwagikia

Hii inalinganisha hewa inayotoka mdomoni mwa Yahwe kwa mafuriko kusisitiza nguvu yake ya kuangamiza.

kuchekecha mataifa kwa chungio la uharibifu

Yahwe kutenganisha watu wa mataifa na kuangamiza watu waovu inazungumziwa kana kwamba Yahwe huweka mataifa katika chungio. Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Yahwe atatenganisha na kuangamiza watu waovu wa mataifa"

Pumzi yake ni hatamu katika taya wa watu kusababisha wazurure mbali

Yahwe kuwa na nguvu ya kusbabisha mipango ya watu kushindwa au kusababisha waangamizwe inazungumziwa kana kwamba pumzi yake ilikuwa hatamu ambayo huongoza watu nje ya njia sahihi.

hatamu katika taya za watu

"hatamu" ni chombo ambacho watu huwek juu ya kichwa cha farasi kuiongoza. Hatamu huwa na kipande kidogo kinachoitwa "lijamu" ambayo huwekwa katika mdomo wa farasi. "hatamu juu ya vichwa vya watu" au "lijamu katika taya za watu"

Isaiah 30:29

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

Utakuwa na wimbo

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "wimbo" inaelezwa kama kitenzi. "Utaimba"

kama usiku ambapo sikukuu takatifu inazingatiwa

Tashbihi hii inasisitiza jinsi watu watakavyokuwa na furaha.

ambapo sikukuu takatifu inazingatiwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "utakapozingatia sherehe takatifu"

na furaha ya moyo

Hapa "moyo" unawakilisha uanadamu wa ndani wa mtu. "nawe utakuwa na furaha"

kama pale mtu huenda ... Mwamba wa Israeli

Tashbihi hii inasisitiza jinsi watu watakavyokuwa na furaha.

kwa Mwamba wa Israeli

Yahwe kuwa na nguvu ya kulinda watu wake inazungumziwa kana kwamba alikuwa mwamba ambao watu wanaweza kupanda na kutoroka kutoka kwa adui. "kwa mwamba wa ulinzi wa Israeli" au "ambao ni kama mwamba wa ulinzi wa Israeli"

Isaiah 30:30

kuonyesha kusogea kwa mkono wake

Hapa "mkono" unawakilisha nguvu ya Mungu. Inadokezwa ya kwamba Yahwe ataonyesha nguvu yake kwa kuangamiza maadui wa watu wake. "onyesha ya kwamba ana nguvu kwa kuangamiza adui zako"

katika dhoruba ya hasira na miale ya moto

Hasira ya Yahwe inazungumziwa kana kwamba ilikuwa dhoruba au moto. "katika hasira ambayo ni kama dhoruba na miale ya moto" au "katika hasira kuu"

kwa upepo wa dhoruba, mvua ya dhoruba, na mvua ya mawe

"kwa dhoruba iliyojaa upepo, mvua na mvua ya mawe"

mvua ya mawe

vipande vigumu vya barafu ambavyo huanguka kutoka angani kama mvua

Isaiah 30:31

Kwa maana kwa sauti ya Yahwe, Ashuru itapondwapondwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kwa maana Yahwe anapozungumza atapondaponda wanajeshi wa Ashuru"

Ashuru itapondwapondwa

Isaya anazungumzia hofu ya Ashuru kana kwamba Ashuru ni chombo ambacho sauti ya Yahwe hupondaponda. "Ashuru itaogopa"

Ashuru

Hapa hii inawakilisha wanajeshi wa Ashuru.

Kila pigo la kiboko kilichoteuliwa ambacho Yahwe atakilaza juu yao

Yahwe kusababisha jeshi kuwashinda Ashuru inazungumziwa kana kwamba Yahwe angewapiga Ashuru kwa fimbo.

itaungana

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu wa Yuda wataungana nayo"

kigoma

Hiki ni chombo cha muziki chenye kichwa kama ngoma ambacho kinaweza kupigwa na kina vipande vya chuma kuzunguka pande ambazo hutoa sauti pale chombo kinapotikiswa.

anapambana na kupigana pamoja nao

Yahwe kusababisha jeshi la adui kuwashinda Ashuru inazungumziwa kana kwamba Yahwe walikuwa shujaa ambaye angepigana pamoja na jeshi la adui.

Isaiah 30:33

Kwa maana sehemu ya kuchoma iliandaliwa zamani

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kwa maana zamani Yahwe aliandaa sehemu kwa ajili ya kuchoma"

sehemu ya kuchoma

Msemo huu ni maana ya neno "Tofethi". Tofethi ni sehemu katika Bonde la Hinomi, kusini mwa Yerusalemu, ambapo katika kipindi kimoja watu walichoma watoto wao kama sadaka kwa miungu ya uongo.

inaandaliwaa kwa ajili ya mfalme

Inadokezwa ya kwamba hii ina maana ya mfalme wa Ashuru. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe aliandaa kwa ajili ya mfalme wa Ashuru".

Rundo lipo tayari na moto na mbao nyingi

"Rundo lipo tayari kwa mbao nyingi kutengeneza moto"

Pumzi ya Yahwe, kama kijito cha salfa, kitaiwasha moto

Hii inazungumzia pumzi ya Yahwe kana kwamba ilikuwa mto wa moto ambao utawasha rundo katika moto.

Isaiah 31

Isaiah 31:1

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza kwa watu wa Yuda.

wanaokwenda chini mpaka Misri

Msemo "kwenda chini" inatumika hapa kwa sababu Misri ipo chini kwa kimo kuliko Yerusalemu.

wanaokwenda chini

"watu hao wa Yuda wanaokwenda chini"

kuegemea farasi

Hii inazungumza juu ya watu kutegemea farasi wao kuwasaidia kana kwamba walikuwa wakitegemea farasi wao. "kutegemea farasi wao"

Mtakatifu wa Israeli

"Wameondoka mbali kutoka kwa Yahwe"

wala hawamtafuti Yahwe

"wala hawamuulizi Yahwe kuwasaidia"

ataleta maafa

Hapa neno "ataleta" lina maana ya "kusababisha". "atasababisha maafa kutokea"

hatarudisha maneno yake

Msemo "kurudisha maneno yake" yanazungumzia juu ya mtu kutotimiza kile alichosema atafanya kana kwamba maneno ambayo alisema yalikuwa kitu ambacho angeweza kuvuta kuelekea kwake. Hapa inasema ya kwamba Yahwe hatafanya hivi, ikimaanisha atatekeleza kile alichosema. "atafanya kile alichosema kuwa atafanya"

kuinuka dhidi ya

"kuadhibu"

nyumba ovu

Hii ina maana ya watu waovu wanaoishi pale. "wote wanaofanya mambo maovu"

Isaiah 31:3

Misri ni mwanamume

Hapa Misri ina maana ya wanajeshi wa Misri. "Wanajeshi wa Misri ni wanamume"

farasi wao ni nyama na sio roho

Hii ina maana ya kwamba farasi wao ni farasi tu na sio viumbe vya kiroho. "farasi wao ni farasi tu; sio roho zenye uwezo!"

Yahwe atakapofikia kwa mkono wake

Msemo "mkono" mara kwa mara hutumika kwa kumbukumbu ya matendo na uwezo wa Mungu. "Yahwe hutumia uwezo wake dhidi yao"

wote yule anayesaidia atajikwaa, na yule anayesaidiwa ataanguka

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja. Kujikwaa na kuanguka ni sitiari ya kushindwa. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "vitu hivi viwili vitatokea: nitaiangamiza Misri, inayokusaidia, na nitakuangamiza wewe, ambaye Misri inasaidia"

yule anayesaidiwa ataanguka

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "yule ambaye anatafuta msaada"

Isaiah 31:4

Taarifa ya Jumla

Yahwe anazungumza na Isaya

Kama simba ... ndivyo Yahwe wa majeshi

"Simba ... kwa njia hiyo hiyo Yahwe wa majeshi". Hapa Yahwe anazungumza jinsi atakavyolinda watu ambao ni wake na kutokuogopa kwa kujilinganisha na simba ambaye hulinda mawindo yake"

ndivyo Yahwe wa majeshi atakashuka ... kilima hicho

Inaweza kuwa wazi zaidi kama ukiweka mstari wa mwisho kabla ya mstari wa kwanza. "Yahwe wa majeshi atashuka kupigana juu ya Mlima Sayuni, juu ya mlima huo, kama simba, hata simba mdogo"

simba, hata simba mdogo

"simba jike au simba muuaji". Hii ni jozi ya kufanana ikiwa na misemo miwili kumaanisha simba mkali. "simba"

huunguruma

huonya wengine kukaa mbali

kikundi cha wachungaji kinapoitwa dhidi yake

Msemo huu "kinapoitwa dhidi yake" una maana ya kutumwa kufukuza simba mbali. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "mtu anapowatuma wachungaji kufukuza simba mbali"

kutokana na sauti yao

Wachungaji hutoa sauti za juu kujaribu kufukuza simba mbali. "kutoka kwa sauti za juu ambazo wanazifanya"

atashuka

"watakuja chini". Hii ina maana kushuka kutoka mbinguni. "atakuja chini kutoka mbinguni"

juu ya Mlima Sayuni

Misemo yote miwili ina maana ya Mlima Sayuni. "juu ya Mlima Sayuni"

Isaiah 31:5

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

Kama ndege wapaavyo, ndivyo Yahwe wa majeshi atalinda Yerusalemu

Hapa njia ambayo Yahwe analinda Yerusalemu inalinganishwa na njia ambayo mama wa ndege hulinda makinda yake katika kiota chao.

atalinda na kuokoa atakapokuwa akipita juu yake na kuitunza

Hii inazungumza jinsi Yahwe anavyolinda na kukoa Yerusalemu, ikimueleza yeye kama ndege ambaye hupaa juu ya mji. "atalinda na kuokoa huo mji kutoka kwa maadui zake"

Yahwe wa majeshi

Hii inaelezea jambo amabalo lingeweza kutokea zamani lakini halikutokea.

Yerusalemu

Hii ina maana ya watu wanaoishi pale. "watu wa Yerusalemu"

Mrudie yeye ambaye ulimuacha kwa kina sana

"Rudi kwa yule ambaye umemuasi"

ambayo mikono yako mwenyewe ilitengeneza kwa dhambi

Hapa watu wanamaanishwa kwa "mikono" yao kusisitiza ya kwamba walitengeneza kitu kwa mikono yao. "ya kwamba umefanya dhambi kwa kutengeneza kwa mikono yako mwenyewe"

Isaiah 32

Isaiah 32:1

Tazama

Neno hili linatumika hapa kuwavuta nadhari ya watu kwa kile kinachosemwa baadaye. "Sikiliza"

Kila mmoja atakuwa kama hifadhi kutoka kwa upepo na kimbilio kutoka kwa dhoruba

Hii inalinganisha mfalme na waku ambao wanalinda watu katika hifadhi. "watawala watalinda watu kama hifadhi inavyofanya katika dhoruba"

kama vijito vya maji katika sehemu kavu

Huu ni ulinganisho mwingine ambao una maana ya watawala kutoa kwa ajili ya mahitaj ya watu. "watatoa kwa ajili ya watu kama vijito vya maji katika sehemu kavu"

kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi iliyochoka

Huu ni ulinganisho mwingine ambao una maana ya watawala kutoa faraja na pumziko kwa ajili ya watu. "watatoa pumziko kwa ajili ya watu kama mwamba mkubwa unaotoa kivuli kwa watu waliochoka"

Kisha macho ... kwa makini

Misemo hii miwili inasisitiza ya kwamba viongozi watawawezesha watu kuelewa ukweli wa Mungu.

hawatafifia

"wataona vizuri"

Isaiah 32:4

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua watu baada ya Mungu kuwarejesha watawala wenye haki wa Yuda.

Wenye pupa ... mwenye kigugumizi

Hii ina maana ya watu ambao hufanya kwa pupa na watu wenye kigugumizi. "Mtu mwenye pupa ... mtu mwenye kigugumizi"

Mpumbavu hataitwa tena mwenye heshima

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Hakuna mtu atakayetoa heshima kwa mpumbavu"

Kwa maana mpumbavu huongea upuuzi

"Mpumbavu" ina maana ya watu wapumbavu. Pia, "upuuzi" na "uovu" inaweza kuelezwa kama vivumishi. "Kwa maana mtu mpumbavu anasema vitu vya kipuuzi na moyo wake unapanga mambo maovu"

moyo wake unapanga uovu

Hapa mtu mpumbavu anamaanishwa kwa moyo wake kusisitiza mawazo yake ya ndani. "anapanga mambo maovu moyoni mwake"

wala mdanganyifu hataitwa mwenye msimamo

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mdanganyifu" ina maana mtu ambaye ni mdanganyifu. "wala hakuna mtu ataonyesha heshima kwa mtu anayedanganya"

Huwafanya

Neno "huwafanya" lina maana ya mtu mpumbavu.

wenye njaa kuwa tupu

"Wenye njaa" ina maana ya watu wenye njaa. Wana njaa kwa sababu wana matumbo tupu. "mtu mwenye njaa ana tumbo tupu"

wenye kiu huwafanya kukosa kinywaji

"Wenye kiu" ina maana ya watu ambao wana kiu. "anasababisha wenye kiu kutokuwa na kitu cha kunywa"

Isaiah 32:7

Mdanganyifu

Hii ina maana ya mtu ambaye hudanganya wengine. "udanganyifu wa mtu"

uharibifu wa maskini kwa uongo

"Maskini" ina maana ya watu maskini. Pia, msemo "kuharibu" haimaanishi kuwaua lakini kuwadhuru kwa kusema uongo juu yao. "kuwadhuru maskini kwa kusema uongo"

atasimama

Hii ina maana ya kwamba atafanikiwa. "atakuwa na mafanikio"

Isaiah 32:9

Inuka

"Simama" au "Zingatia kwa makini"

mliotulia

"salama" au "kuwa huru"

sauti yangu

Isaya ana maana yake mwenyewe kwa sauti yake kusisitiza kiile anachosema. "mimi kuongea"

imani yenu itavunjwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Pia, Isaya anazungumzia wao kutokuwa na imani kana kwamba imani ilikuwa kitu cha kimwili ambacho kinaweza kuvunjwa. "hautakuwa na imani tena"

mavuno ya zabibu yatashindwa

Hii ina maana ya kwamba hapatakuwa na mizabibu mizuri ya kuvuna. "hapatakuwa na mizabibu kwa ajili yako kuvuna"

makusanyo hayatakuja

"kipindi cha makusanyo ya nafaka hakutatokea"

Isaiah 32:11

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza.

Tetemekeni

"Tetemeka kwa woga"

wametulia

"salama" au "kuwa huru"

vua nguo zako nzuri na jiweke mwenyewe wazi

Hapa "wazi" haimaanishi kuwa uchi, lakini kujifunika kiasi kama vile kwa nguo za ndani. "vua nguo zako nzuri na ujifanye kutokuwa na nguo" au "vua nguo zako za kibunifu"

vaa gunia za nguo kuzunguka viunoni mwako

Hili ni tendo la kulia au kuomboleza. "vaa nguo ya gunia kiunoni unapolia"

Utaomboleza kwa ajili ya mashamba mazuri, kwa ajili ya mizabibu ya matunda

Hii ina maana ya kwamba watalia kwa sauti wanapoomboleza kile knachotokea kwa mashamba yao yaliyozaa na mizabibu. "Utalia kwa sababu ya kile kinachotokea kwa mashamba yako mazuri na mizabibu inayozaa"

miiba na mibigili

Mbigili na miiba mara kwa mara hutumika kama alama za miji na nchi zilizoharibiwa.

nyumba zilizokuwa na furaha mwanzo

Hapa nyumba inafafanuliwa kama kuwa na furaha kwa sababu ya watu wenye furaha ndani mwao. "nyumba zako ambamo mlikuwa na furaha awali"

mji wa furaha

"mji wako wa shangwe". Neno "furaha" ina maana ya kushangilia na kusherekea.

Isaiah 32:14

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza.

Kwa maana kasri litatelekezwa, miji iliyojaa itaachwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kwa maana watu wataacha kasri na makundi watatelekeza mji"

kilima

Hii ina maana ya ngome iliyojengwa juu ya kilima. "ngome juu ya kilima"

kilima na mnara wa mlinzi vitakuwa mapango

Hii inazungumzia ngoma na mnara kuachwa kana kwamba vimekuwa mapango. "kilima na mnara vitaachwa na kuwa tupu"

furaha ya punda mwitu, malisho ya makundi

Hii ina maana wanyama hawa watafurahiia nyasi ambayo huota miongoni mwa ngome na mnara. "punda mwitu na kundi la kondoo watakula nyasi pale"

milele

Hii ina maana ya muda mrefu sana. "muda mrefu mno"

hadi Roho anapomiminwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "mpaka Yahwe atakapomwaga Roho"

hadi Roho anapomiminwa juu yetu

Hii inazungumzia Yahwe kumpatia Roho kwa watu wake kana kwamba Roho alikuwa mmiminiko ambao unaweza kumwagwa juu yao. "Roho amepatiwa kwetu"

kutoka juu

Hapa mbinguni ina maana ya "juu". "kutoka mbinguni"

mashamba yanayozaa yanachuliwa kama msitu

Hii inaweza kuandikwa katika hali ya kutenda. Hii inalinganisha jinsi mashamba yalivyo na wingi na kuzaa kwa kulinganisha na msitu mnene na mkubwa.

Isaiah 32:16

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza.

hukumu itakaa ... haki itaishi

Isaya anafafanua "hukumu" na "haki" kama mtu ambaye anaishi katika maeneo haya. Hii ina maana ya watu ambao wanaishi katika maeneo haya watafanya kilicho haki na sahihi. "watu watafanya kwa haki katika nyika na watu watatenda kwa haki katika mashamba yenye rutuba.

Kazi ya haki itakuwa amani; na matokeo ya haki, utulivu na imani milele

Misemo hii miwili ni sambamba na yote hutoa matokeo ya haki. Inaweza ikajumlishwa. "Matokeo ya watu kutenda haki ni kwamba kutakuwa na amani, na utulivu na imani milele"

makazi

"sehemu"

Isaiah 32:19

mvua ya mawe

"Mvua ya mawe" hutokea pale ambapo vipande vya barafu huanguka kutoka kwenye anga.

msitu unaangamizwa, na mji unateketezwa kabisa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "inaangamiza msitu na kuangamiza mj kabisa"

wewe ambaye unapanda kando na vijito vyote vitabarikiwa, wewe ambaye unawatuma ng'ombe na punda wako kulisha

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Hii ina maana ya Yahwe kubariki watu wake wote na inazungumzia vitu ambavyo ni kawaida kwa watu wake kufanya. "Yahwe atakubariki, unapopanda mazao yako katika mashamba kando ya vijito na unatuma ng'ombe wako na punda kulisha katika malisho"

Isaiah 33

Isaiah 33:1

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza kwa shairi kwa ajili ya Yahwe kwa Waashuru.

ambaye haujaangamizwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambao wengine hawajawaangamiza"

utaangamizwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wengine watakuangamiza"

watakusaliti

"wengine watakusaliti"

Isaiah 33:2

kuwa mkono wetu

Hapa mkono wa Yahwe una maana ya nguvu yake. Hii inazungumzia Yahwe kuwaimarisha kana kwamba Yahwe angetumia nguvu yake kutenda kwa ajili yao. "tupatie nguvu"

kila asubuhi

Hii ina maana ya siku nzima, sio asubuhi tu. "kila siku"

wokovu wetu

Neno "wokovu" linaweza kuelezwa kwa kitenzi "okoa". "uwe wokovu wetu" au "tuokoe"

katika kipindi cha shida

Hii in maana ya kipindi ambapo wanapatia shida. "tunapokuwa na shida"

Isaiah 33:3

Kwa sauti kubwa watu wanatoroka

Maana zinazowezekana za "sauti kubwa" ni 1) ina maana ya sauti ya Yahwe. "Watu hutoroka kwa kelele ya sauti yako" au 2) ina maana ya kelele kubwa ya jeshi la Yahwe. "Watu hutoroka kwa sauti ya jeshi lako"

inuka

Hii ina maana kuanza kufanya kitu. "anza kufanya"

mataifa yanatawanywa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "mataifa yanagawanya"

Mali yako iliyoibiwa inakusanywa kama nzige zinavyojikusanya; kama nzige wanavyoruka, watu huruka juu yake

Hii inalinganisha jinsi watu wa Yahwe walivyo na haraka na shauku wanapokusanya mali iliyoibiwa kutoka kwa adui zao. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wako hukusanya mali za kuibiwa kutoka kwa adui zako kwa ukali huo huo kama nzige wanavyomeza mimea ya kijani"

Isaiah 33:5

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumzia watu wa Yuda

Yahwe anainuliwa

"Yahwe ni mkubwa kuliko mtu yeyote yule"

Ataijaza Sayuni kwa hukumu na haki

Hii inazungumzia Yahwe kutawala Sayuni kwa hukumu na haki yake kana kwamba alikuwa akijaza Sayuni kwa hukumu na haki. "Atatawala Sayuni kwa hukumu na haki"

Atakuwa uthibiti katika nyakati zako

Hii inazungumzia Yahwe kusababisha watu wake kuwa imara kana kwamba alikuwa uthabiti mwenyewe. Msemo "nyakati zako" una maana ya maisha yao. "Atakufanya salama maisha yako yote"

wingi wa wokovu, hekima, na maarifa

Maneno ambayo hayapo yanaweza kuongezwa. Pia "wokovu" inaweza kuelezwa kwa kitenzi "okoa". "na atakupatia wingi wa wokovu, hekima, na maarifa" au "atakuokoa na kukupa wingi wa hekima na maarifa"

hofu ya Yahwe ni hazina yake

Hii inazungumzia kumhofu Yahwe kana kwamba ilikuwa hazina ambayo Yahwe hutoa kwa watu wake. "kumcha Yahwe itakuwa kama hazina yenye thamani ambayo atakupatia wewe" au "kumcha Yahwe itakuwa na thamani kwako kama hazina"

Isaiah 33:7

Tazama

Neno hilii lnatumika hapa kuvuta nadhari ya wtu kwa kile kinasemwa baadaye. Inatumika hapa pia kuweka alama kwa sehemu mpya katika kitabu. "Sikiliza"

wajumbe

"majumbe"

wanadiplomasia wenye matumaini ya amani hulia kwa uchungu

Hii na maana wanalia kwa sababu hawafanikiwi kutengeneza amani. "wanadiplomasia wanatumaini kwa ajili ya amani lakini hawafanikiwi na kwa hiyo wanalia kwa uchungu"

Barabara zimetelekezwa; hakuna wasafiri tena

Misemo hii miwili inasisitiza ya kwamba hakuna msafiri katika barabara. Hii inaweza kuunganshwa na kuandika katika hali ya kutenda. "Watu hawasafiri tena katika barabara".

Maagano yanavunjwa, mashahidi wanadharauliwa, na mwanadamu haheshimiwi

Mstari huu una maana ya hali za ujumla za uharibifu wa Israeli, au inaweza kumaanisha kutoweza kwa taifa kufanya makubaliano yanayoaminika ya amani na Ashuru. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu huvunja maagano ambayo wameyafanya, watu kutojali ushuhuda wa mashahidi, na watu kutojiheshimu wao kwa wao"

Isaiah 33:9

Nchi inaomboleza na kunyauka

Hii inazungumzia nchi kuwa kavu kana kwamba ilikuwa mtu anayeomboleza. "Nchi kuwa kavu na mimea yake kunyauka"

anaona aibu na ananyauka

Hii inazungumzia miti ya Lebanoni kunyauka na kuoza kana kwamba Lebanoni ilikuwa mtu ambaye ameaibika. "Miti ya Lebanoni hunyauka na kuoza"

Sharoni ... Bashani ... Karmeli

Miti mingi na maua iliwahi kuota katika maeneo haya.

Sharoni ni kama jangwa wazi

Hii inalinganisha jinsi Sharoni ilivyo kavu kwa jangwa wazi. "Sharoni ni kavu kama jangwa wazi"

Bashani na Karmeli hutikisa majani yao

"hakuna majani tena katika miti ya Bashani na Karmeli"

Isaiah 33:10

inuka

"simama". Hapa neno hili lina maana ya kuanza kufanya jambo. Katika hali hii Yahwe sasa anajinua mwenyewe.

sasa nitainuliwa; sasa nitapandishwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza Yahwe kuinuliwa. "sasa nitajiinua na kuonyesha ya kwamba ninastahili kwa ajili ya kila mtu kuniheshimu"

Unachukua mimba ya makapi, na unazaa mashina ya mabua

Hii inazungumzia Ashuru kufanya mipango kana kwamba walikuwa wakitunga mimba na kuzaa mipango yao kama mama anavyozaa mtoto. Hii inazungumzia mipango yao kutokuwa na thamani kwa kulinganisha na majani makavu. "Unafanya mipango ambayo haina thamani kama makapi na majani makavu"

mashina ya mabua

"majani makavu"

pumzi yako ni moto ambayo itakuangamiza

Hapa mipango ya Ashuru ina maana ya "pumzi" yao. Hii inazungumzia mipango yao kusababisha wao kufa kana kwamba mipango yao ingechoma miili yao kihalisia. "mipango yako itasababisha ufe"

Watu watachomwa mpaka kuwa chokaa, kama miiba ya vichaka inavyokatwa chini na kuchomwa

Hii inalinganisha jinsi maiti za watu itakavyochomwa kwa njia ambayo vichaka vya miiba inachomwa. Pia, hi inaweza kuandikwa katika hali ya kutenda. "Moto utachoma miili ya watu kuwa chokaa kwa nja moja ambayo mkulima hukata chini vichaka vya miiba na kuvichoma"

chokaa

mjivu kutoka kwa mifupa iliyoungua

Isaiah 33:13

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

Wewe uliye mbali, sikiliza kile nilichofanya; na, wewe uliye karibu, kubali nguvu yangu

Yahwe anatumia maneno "mbali" na "karibu" kumaanisha watu wote. Neno "nguvu" linaweza kuelezwa kwa kivumishi "uwezo". "Watu wote kil sehemu watasikia kile nilichofanya na kukubali ya kwamba nina uwezo"

kutetemeka kumekamata wasio na Mungu

Hii inazungumzia watu wasio na Mungu kutetemeka kana kwamba kutetemeka kwao kulikuwa adui aliyewakamata. "wasio na Mungu wameingiwa kabisa na kutetemeka"

Nani kati yetu ... kuungua

Inadokvzwa ya kwamba mwenye dhambi wa Sayuni anauliza maswali haya. "Wanasema, 'Nani kati yetu ... kuungua"

Nani kati yetu anaweza kushindana na moto mkali? Nani kati yetu anaweza kushindana na kuungua kwa milele?

Maswali haya ya balagha yana maana moja na inasisitiza ya kwamba hakuna mtu anayeshi na moto. Hapa moto unwakilisha hukumu ya Yahwe. "Hakuna mtu anaweza kuishi kwa moto mkali! Hakuna mtu anaweza kuishi na moto wa milele!" au "Hakuna mtu anaweza kuishi kwa kubeba hukumu ya Yahwe, ni kama moto wa milele!"

kushindana

kuishi katiika eneo ambalo sio nyumba ya mtu

Isaiah 33:15

Yule anayetembea

Hapa kutembea ina maana ya kuishi. "Yule ambaye anaishi"

yule ambaye hudharau ongezeko la mali kwa dhuluma

Msemo wa nomino "ongezeko la mali kwa dhuluma" linaweza kuelezwa kama msemo wa kitenzi. "yule ambaye huchukia utajiri unaotokana na kudhuru watu wengine"

na haangalii uovu

"Kutazama" hapa ina maana ya kuidhinisha jambo. "na yule ambaye hakubaliani na kutenda uovu"

vilele

Hii ina maana ya kilima ch juu au upane wa mlima. "kilima cha juu" au "upande wa mlima"

ngome za miamba

Hii inazungumzia maeneo ya mawe ambayo ni rahisi kujilinda kana kwamba ilikuwa ngome kihalisia. "rundo kubwa la mawe"

itatolewa bila kikomo

"itakuwepo daima"

Isaiah 33:17

Macho yako yataona .. yatatazama

Hii ina maana ya watazamaji kwa "macho" yao. "Utaona ... utatazama"

mfalme katika uzuri wake

Majoho ya kifalme ya mfalme yanaelezwa kama "uzuri wake". "mfalme katika majoho yake mazuri"

Moyo wako utakumbuka hofu kuu

Hii ina maana ya watazamaji kwa "mioyo" yao. "Hofu kuu" ina maana ya vita yao na Ashuru. Hii inaweza kuandikwa wazi. "Utakumbuka hofu kuu ambayo Ashuru alisababisha kwako alipokushambulia"

yuko wapi mwandishi, yuko wapi yule ambaye alipima uzito wa fedha? Yuko wapo yule aliyehesabu minara?

Swali hili la balagha linaulizwa kusisitiza ya kwamba maafisa wa Ashuru wametoweka. Maswali haya yanweza kuandikwa kama kauli. "Maafisa wa Ashuru ambao walihesabu fedha za kodi ambayo ililazimishwa kulipwa kwao imepotea! Wanamume hao ambao walihesabu minara yetu wametoweka!"

alipima uzito wa fedha

Fedha ilikuwa chuma yenye thamani; uthamani wake ulithibitshwa kwa uzito wake.

watu wenye lugha ya ajabu

"watu ambao walizungumza lugha ya ajabu"

hamuwaelewi

"kuelewa"

Isaiah 33:20

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

mji wa sikukuu zetu

Hii ina maana ya kwamba wana sikuku zao na sherehe katika mji. "mji ambapo tuna sikuku zetu" au "mji ambao tunasherehekea karamu zetu"

macho yako yataona

Watu wanajulikana kwa "macho" yao kusisitiza kile wanachoona. "utaona"

hema ambalo halitaondolewa

Hii inazungumzia Sayuni kuwa salama na kuimarishwa kana kwamba ilikuwa hema lililo salama. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda na kuandikwa kama sentensi mpya. "itakuwa salama, kama hema ambalo hakuna mtu atakayeliondoa kamwe"

ambalo viging vyake havitawah kuvutwa wala kamba zake kukatwa

Hii ni sehemu ya sitiari ambayo inalinganisha Sayuni kwa hema salama. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambalo vigingi hakuna mtu atawahi kuvivuta juu na ambalo kamba zake hakuna awezaye kuvikata"

Yahwe katika utukufu atakuwa pamoja nasi, katika sehemu ya mito mipana na vijito

Hapa "nasi" ina maana ya Isaya na inajumuisha watu wa Yuda. Hii inazungumzia usalama wa kuishi na Yahwe kana kwamba ilikuwa sehemu ambayo ina mito ikizunguka ili kwamba maadui wasiweze kuishambulia. "Yahwe ambaye ni mtukufu atakuwa pamoja nasi, na tutakuwa salama kana kwamba tupo katika sehemu inayozungukwa kwa mito mipana"

utausafiria

"utasafiri juu ya mto"

Isaiah 33:22

wetu ... atatuokoa

Hii ina maana ya Isaya na inajumlisha watu wa Yuda.

Isaiah 33:23

Kamba zako ni goigoi; haziwezi kushikilia mlingoti mkuu katika sehemu yake; hawawezi kulitandaza tanga

Maana zaweza kuwa 1) jeshi la Ashuru ni kama mtumbwi ambao hauwezi kusogea katikati ya maji: kamba ambazo hushikilia mlingoti mkuu na tanga zimekuwa legevu na hazishiki tena mlingoti mkuu, kwa hiyo tanga halina faida (33:1) au 2) watu wa Yuda hawapo vitani tena. "Umelegeza kamba ambazo zilishikilia nguzo zako za bender; bendera haipepei tena"

mlingoti mkuu

nguzo ndefu ambazo hushikilia tanga

tanga

kitambaa kikubwa ambacho hujazwa na upepo na kusogeza mtumbwi katikati ya maji

mali kubwa iliyoibiiwa itakapogawanywa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watakapogawanya hazina"

vilema

Hii ina maana ya watu ambao hawawezi kutembea. "wale ambao ni vilema"

watu wanaoishi pale watasamehewa kwa udhalimu wao

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atasamehe dhambi za watu wanaoishi pale"

Isaiah 34

Isaiah 34:1

Taarifa ya Jumla

Yahwe anazungumza katika shairi.

Dunia na kila kitu kinachoijaza wanapaswa kusikiliza, ulimwengu, na vitu vyote vitokanavyo nao

Hapa dunia inazungumziwa kama inahitajika kumsikiliza Yahwe kusisitiza ya kwamba ipo chini ya mamlaka ya Yahwe. Misemo hii miwili ya sambamba ni mifano ya maneno kwa ajili ya watu wote wanaoishi ulimwenguni. "Katika sehemu zote duniani, kila mtu anapaswa kusikiliz kile nachosema"

ulimwengu, na vitu vyote vitokanavyo nao

Hii ni misemo ya sambamba ya pili. Maneno ambayo hayapo yanaweza kuongezwa katika msemo huu. "ulimwengu, na vitu vyote viunavyotoka kutoka kwake vinapaswa kusikiliza"

ameyaangamiza kabisa, ameyakabidhi kwa ajili ya kuchinjwa

Mara kwa mara manabii huzungumzia vitu ambavyo vitatokea katika siku za usoni kana kwamba vimekwisha tokea. Hii inasisitiza tukio litatokea hakika. "atawaangamiza kabisa, atawakabidhi katika machinjo"

Isaiah 34:3

Miili ya wafu wao itatupwa nje

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Hakuna ambaye atazika wafu wao"

wafu wao

Hii ina maana ya watu waliokufa. "wale ambao wamekufa"

milima itafyonza damu yao

"milima itafunikwa katika damu yao"

mbingu itakunjwa kama hati ya kukunja

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Hii inalinganisha kile ambacho Yahwe atafanya kwa mbingu kama mtu akikunja hati ya kukunja. "Yahwe atakunja hati ya kukunja kwa njia moja ambavyo mtu hukunja hati ya kukunja"

na nyota zao zote zitafifia, kama jani linavyofifia kutoka katika shina, na kama tini ilioiva kutoka kwenye mtini

Hii inasisitiza hata vitu katika mbingu ambavyo watu walidhani vingekuwa kule milele vitaanguka kwa urahisi kama jani. "na nyota zote zitaanguka kutoka mbinguni kama jani linavyoanguka kutoka katika shina au tini unavyoanguka kutoka katika mti"

Isaiah 34:5

pale upanga wangu utakapokuwa umekunywa ujazo wake mbinguni

Yahwe anajifafanua kama shujaa anayebeba upanga. Msemo "umekunywa ujazo wake" unazungumzia upanga wa Yahwe kana kwamba ulikuwa mtu ambaye amekula na kutosheka. Yahwe anatumia picha hii kusisitiza ya kwamba kutakuwa na uharibifu mwingi mbinguni na kutaja ukamilifu wake. "nitakapomaliiza kuangamiza vitu mbinguni"

tazama

Neno hili linatumika hapa kuwavuta wasikilizaji na kuwafanya wawaze mambo yanayosemwa. "sikiliza" au "na kisha"

sasa itashuka chini mpaka Edomu, juu ya watu naowaweka kando kwa ajili ya uharibifu

Neno "itashuka" ina maana ya upanga wa Yahwe. Hii inaendeleza sitiari kuhusu Yahwe kuangamiza vitu kwa upanga. "Nitakuja kuadhibu watu wa Edomu, watu ambao nimewaweka kando kwa ajili yangu kuangamiza"

juu ya Edomu

Edomu ina maana ya watu ambao wanaishi kule. "juu ya watu wa Edomu"

upanga wa Yahwe unadondoka kwa damu na kufunikwa na mafuta... wa kondoo dume

Hii inazungumzia Yahwe kuwaua watu kana kwamba alikuwa kuhani akitoa wanyama sadaka. Anafanya hivi kwa kufafanua upanga wa kuhani. "Yahwe anawatoa sadaka kama vile kuhani anavyotoa sadaka za wanyama, ambaye upanga wake unadondoka na damu na mafuta ya kondoo, mbuzi na kondoo dume"

Kwa maana Yahwe ana sadaka Bozra na machinjio makubwa katika nchi ya Edomu

Maneno "sadaka" na "machinjio" yanaweza kuelezwa hapa kama vitenzi. "

Bozra

Huu ni mji muhimu katika Edomu

Isaiah 34:7

Maksai pori watachinjwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mimi, Yahwe nitachinja maksai pori"

Nchi yao italewa kwa damu

Hii inaelezea kiwango cha damu ambacho italowa katika ardhi kwa kulinganisha nchi na mtu mlevi. "Nchi yao italowa kwa damu"

vumbi lao lilifanya nono kwa unene

Hapa "vumbi" ina maana ya udongo juu ya ardhi. Hii inaelezea kiwango cha mafuta ambacho kitalowanisha katika udongo kwa kumlinganisha kwa mtu ambaye amenenepa kwa kula sana mafuta ya mnyama. "udongo utakuwa umejaa mafuta ya wanyama"

Isaiah 34:8

itakuwa siku ya kisasi kwa ajili ya Yahwe

Hapa "siku" ni lahaja kwa ajili ya kipindi katika wakati; sio "siku" halisi. "itakuwa wakati ambapo Yahwe atapata kisasi"

atawalipa kwa ajili ya Sayuni

Hii ina maana ya kwamba atachukua kisasi juu yao kwa jinsi walivyofanya vita kipindi cha nyuma dhidi ya watu wa Yerusalemu. "atawapa adhabu wanayostahili kwa kile walichofanya kwa watu wa Sayuni"

vijito vya Edomu vitageuzwa kuwa lami nyeusi ... kuwa lami inayowaka

Maji na nchi kutokuwa na thamani kwa ajili ya kunywa au kuotesha chakula kwa sababu imeungua na kufunikwa katika lami na salfa inazungumziwa kana kwamba vijito vyake na nchi itakuwa lami na salfa. "Vijito vya Edomu vitajaa lami na ardhi itafunikwa na salfa inayowaka na lami inayowaka"

vumbii lake ... nchi yake

"Vumbi la Edomu ... nchi ya Edomu"

lami

dutu nene, nyeusii ambayo inawaka kwa muda mrefu

itawaka usiku na mchana

Hii iina maana wakati wote. "Itawaka usiku wote na mchana" au "Itawaka kwa muendelezo, usiku wote na mchana wote"

kutoka kizazi mpaka kizazi

Msemo "kizazi mpaka kizazi" una maana ya vizazi vyote vya watu ambao wataishi katika siku za usoni.

Isaiah 34:11

wataishi kule

"wataishi katika nchi ya Edomu"

bundi

Bundi ni ndege pori wanaowinda usiku

kunguru

Huyu ni ndege mkubwa mweusi. Ni vigumu kutambua baadhi ya aina haswa za ndege zinazotajwa katika sehemu hii. Hata hivyo, wote walikuwa ndege ambao walipendelea kuishi katika maeneo ambayo hapakuwa na watu, kwa hiyo waliashiria sehemu zilizotelekezwa.

ndani mwake

"kule". Hii ina maana ya Edomu.

Naye atanyosha juu yake kamba ya kupimia ya uharibifu na timazi ya uvunjifu

Hii inamzungumzia Yahwe kana kwamba alikuwa mjenzi mwangalifu kama akisababisha uharibifu katika Edomu. "Yahwe atapima nchi kwa uangalifu; atapima kuamua wapi kusababisha uharibifu na uvunjifu"

kamba ya kupimia ... timazi

Hivi ni vifaa vya mjenzi.

Waadilifu wake ... wakuu wake

"Waadilifu wa Edomu ... wakuu wa Edomu"

wakuu wake wote hawatukuwa kitu

Hii inakuza kuhusu wakuu kupoteza nafasi yao ya ufalme kwa kusema watakuwa si kitu. "wakuu wake wote hawatatawala tena"

Isaiah 34:13

Miiba ... upupu ... mbaruti

Haya yote ni magugu yenye miiba. Miiba ya upupu ina sumu inayosababisha mwasho.

mbweha ... mbuni ... wanyama pori ... fisi ... Bundi ...

mbweha ... mbuni ... wanyama pori ... fisi ... Bundi

Wanyama wa usiku

Wanyama ambao wapo macho na wanashughulika usiku

mwewe

ndege ambao wanaua wanyama wadogo kwa ajili ya chakula

Isaiah 34:16

Tafuteni katika hati ya kukunja ya Yahwe

Msemo "hati ya kukunja ya Yahwe" ina maana ina ujumbe unaozungumzwa na Yahwe. "Soma kwa uangalifu kile kilichoandikwa katika hati hii ya kukunja ambayo ina ujumbe wa Yahwe"

hakuna moja kati hawa

"hakuna mmoja wa wanyama"

Hakuna mmoja wao atakosa mwenzi

Hii inaweza kuandikwa kama kauli chanya. "Kila mnyama atakuwa na mwenzi"

kwa maana kinywa chake kimeiamuru

Yahwe anatajwa kwa "kinywa" chake kusisitiza kile alichosema. "kwa maana Yahwe ameiamuru"

Amepiga kura kwa nafasi zao

Hii inazungumzia kuhusu Yahwe kuamua wapi kusababisha wanyama kuishi kana kwamba alipiga kura kihalisia kwa ajili ya sehemu zao. "Amekusudia wapi wataishi"

na mkono wake umepima kwa ajili yao kwa mkanda

Hii ina maana ya njia ambayo watu walipima viutu kipindi cha Biblia. "na amewapa wanyama sehemu zao"

kutoka kizazi mpaka kizazi wataishi

Msemo huu "kizazi mpaka kizazi" una maana ya vizazi vyote vya watu ambao wataishi katika siku za usoni. "milele wataishi" au "wataendelea siku zote"

Isaiah 35

Isaiah 35:1

Nyika na mahali penye ukiwa patafurahi; na jangwa litashangilia

Misemo hii miwili kimsingi iuna maana moja. Sehemu hizi inaelezwa kama kuwa na furaha, kama mtu anavyokuwa na furaha, kwa sababu zimepokea maji na zinachanua. "Itakuwa kama nyika na mahali penye ukiwa pana furaha na jangwa litashangilia"

na kuchanua

Hii inazungumzia mimea katika jangwa kuchanua kana kwamba jangwa lenyewe lilikuwa likichanua. "na mimea yake itachanua"

Kama waridi, litachanua kwa wingi

Hii inalinganisha namna ya mimea ya jangwa huchanua kwa namna ambavyo waridi unavyochanua kwa wingi. "Jangwa litaota mimea na miti mipya mingi"

na kushangilia kwa furaha na kuimba

Hii inazungumzia jangwa kana kwamba ilikuwa na furaha na kuimba kama mtu. "itakuwa kana kwamba kila kitu kinashangilia na kuimba!"

utukufu wa Lebanoni utapewa kwake

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Hii inazungumzia Yahwe kulifanya jangwa kuonekana na utukufu kama wa Lebanoni kana kwamba alikuwa akilipa jangwa utukufu wa Lebanoni. "Yahwe ataupatia Lebanoniu utukufu wake" au "Yahwe ataufanya uwe mzuri kama Lebanoni"

uzuri wa Karmeli na Sharoni

Maneno ambayo hayapo yanaweza kuongezwa. Pia, hii inamzungumzia Yahwe kulifanya jangwa kuonekana zuri kama Karmeli na Sharoni kana kwamba alikuwa akilipa jangwa uzuri wake. "uzuri wa Karmeli na Sharoni utapewa kwake" au "Yahwe ataufanya uwe mzuri kama Karmeli na Sharoni"

utukufu wa Yahwe, uzuri wa Mungu wetu

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja na inasisitiza kutokea kwa Yahwe.

Isaiah 35:3

Taarifa ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Yuda.

Imarisha mikono iliyolegea, na nyosha magoti yanayotetemeka

Maneno "mikono iliyolegea" na "magotiu yanayotetemeka" yanawakilisha mtu ambaye ana hofu. "Imarisha wale ambao mikono yao ni dhaifu na ambao magoti yao hutetemeka kwa hofu"

wale wenye moyo wa uoga

Hapa watu wanamaanishwa kwa mioyo yao, ambayo inasisitiza hisia zao za ndani. "kwa wale ambao wana hofu"

Tazama

Hii ni lahaja. Neno hili linatumika hapa kuwavuta wasikilizaji kwa kile kinachosemwa baadaye. "Sikilizeni"

Mungu wako atakuja na kisasi, kwa fidia ya Mungu

Hii inaweza kusemwa kwa neno lingine ili kwamba nomino dhahania "kisasi" na "fidia" inaelezwa kama kitenzi "adhibu". Maneno haya "kisasi" na "fidia" yana maana moja na yanasisitiza ya kwamba Mungu atawaadhibu maadui wa Yuda. "Mungu wako ataadhibu adui zako kwa kile walichokifanya"

Isaiah 35:5

Taarifa ya Jumla

Mistari hii inaanza maelezo ya utukufu ujao wa watu wa Mungu.

macho ya vipofu yataona

"Vipofu" ina maana ya watu ambao ni vipofu. Wanamaanishwa kwa "macho" yao kusisitiza uponyaji wao. "watu vipofu wataona"

masikio ya viziwi yatasikia

"Viziwi" ina maana wa watu ambao hawawezi kusikia. Wanamaanishwa kwa "masikio" yao kusisitiuza uponyaji wao. "watu viziwi watasikia"

mtu kilema ataruka kama mbawala

Hii ina maana mtu ambaye hawezi kutembea ataweza kuruka. Uwezo wake kuruka inakuzwa kwa kusema ya kwamba anaweza kuruka kama mbawala. "mtu kilema ataruka juu"

ulimi usiozungumza utaimba

Hii ina maana ya watu ambao hawawezi kuongea. Wanamaanishwa kwa "ndimi" zao kusisitiza uponyaji wao. "bubu wataimba"

vijito katika nyika

Maneno ambayo hayapo yanaweza kuongezwa. "vijito vitatiririka katika nyika"

mchanga unaochoma utakuwa dimbwi

Hii ina maana ya kwamba dimbwi la maji litajitokeza katika mchanga wa moto. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Dimbwi litajitokeza katika mchanga unaochoma"

ardhi yenye kiu

Hapa ardhi kavu inaelezwa kama kuwa na kiu. "ardhi iliyokauka"

ardhi yenye kiu kuwa chemchemi za maji

Hii ina maana ya kwamba chemchemi itajitokeza katika ardhi ngumu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "chemchemi za maji zitatokea katika ardhi yenye kiu"

mbweha

mbwa mwitu

mafunjo na matete

Hii ni mimea ambayo huota katika maeneo yaliyoloana.

Isaiah 35:8

Taarifa ya Jumla

Mistari hii naendeleza ufafanuzi wa utukufu ujao wa watu wa Mungu.

Barabara itakuwa pale inayoitwa Njia Takatifu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Barabara itakuwa pale ambayo iatkuwa na jina Njia Takatifu"

barabara

Mtoto mdogo atawatunza na kuwaongoza katika sehemu nzuri kunywa maji na kula nyasi.

wachafu

Hii ina maana ya watu wasio safi. Mtu ambaye Mungu humchukulia kutokubalika kiroho au najisi anazungumziwa kana kwamba mtu alikuwa mchafu kimwili. "Wale ambao na wachafu" au "Watu ambao hawakubaliki kwa Mungu"

yule atembeaye ndani yake

Hii ni lahaja. Hapa "kutembea" ina maana ya "kuishi". Hii ina maana ya mtu ambaye anaishi maisha matakatifu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "yule ambaye anaishi katika njia ya utakatifu" au "yule ambaye huishi maisha ya utakatifu"

hawatapatikana pale

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu atakayewakuta kule"

waliokombolewa

Hii ina maana ya watu ambao Mungu amewakomboa. "wale ambao wamekombolewa" au "wale ambao Mungu kawakomboa"

Isaiah 35:10

Waliofidiwa wa Yahwe

"kufidia" ina maana ya "kukoa". Hii ina maana ya watu ambao Yahwe kawakomboa. "Wale ambao Yahwe amewaokoa"

furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao

Hii inatumia kichwa cha mtu kumaanisha mtu kwa ujumla. "watakuwa na furaha ya milele"

furaha na shangwe ... huzuni na tanafusi

Maneno "furaha" na "shangwe" kimsingi ina maana moja, kama vile "huzuni" na "kutanafusi". Kwa pamoja yanasisitiza mkazo wa hisia hizi.

furaha na shangwe itawapita wao

Hii inazungumzia watu kushindwa kabisa na furaha na shangwe kwa kuzipatia hisia hizi sifa za kibinadamu ya kuweza kumpita mtu kwa lazima. "watashindwa kabisa kwa shangwe na furaha"

huzuni na tanafusi itatoroka

Hii inazungumzia juu ya watu kutokuwa na huzuni na kutanafusi kwa kuzipa hisia hizi uwezo wa kibinadamu wa kukimbia. "hawatakuwa na huzuni na kutanafusi"

Isaiah 36

Isaiah 36:1

mwaka wa kumi na nne

"mwaka wa 14"

Mfalme Hezekia

Hezekia alikuwa mfalme wa Yuda

Senakeribu

Hili ni jina la mfalme wa Ashuru.

Senakeribu ... alishambulia miji yote iliyoimarishwa

Jeshi la Senakeribu lilivamia miji. "Senekeribu na jeshi lake ... walivamia miji yote iliyoimarishwa"

kamanda mkuu

Baadhi ya tafsiri za Biblia zinatafsiri kuwa hii ni ""Rabshake". Hili ni neno la Ashuru kwa yule mwenye nafasi ya juu kabisa ya viongozi wa kijeshi Ashuru.

Lakishi

Huu ni mji kusini magharibi mwa Yerusalemu.

mfereji wa dimbwi la juu katika barabara ya kuelekea shamba la dobi

"ambapo maji huingia katika dimbwi la juu"

Hilkia ... Eliakimu

Haya ni majina ya wanamume.

Shebna

Hili ni jina la msimaizi wa kasri ya mfalme Yerusalemu

Asafu ... Yoa

Haya ni majina ya wanamume.

Isaiah 36:4

akasema kwao

"akasema kwa Eliakimu, Shebna, na Yoa"

Chanzo cha matumaini yenu ni nini?

Mfalme wa Ashuru anatumia swali hili kutoa changamoto kwa Hezekia na kusema ya kwamba hana chanzo kizuri cha imani. Swali hili linaweza kuandikwa kama kauli. "Hauna chanzo cha kutegemea cha imani yako"

kuna ushauri na nguvu kwa ajili ya vita

"una ushauri na nguvu ya kwenda vitani". Msemo "nguvu kwa ajili ya vita" ina maana ya kuwa na jeshi kubwa la kutosha na la nguvu ya kutosha yenye silaha. "una ushauri wa kijeshi wa kutosha, wanamume wenye nguvu, na silaha za kwenda vitani"

Basi sasa ni nani mnayemwamini? Ni nani kawapa ujasiri kuasi shidi yangu?

Mfalme wa Ashuru anatumia maswali kumdhihaki Hezekia kwa kuamini ya kuwa ana nguvu ya kuasi. Swali hili linaweza kuandikwa kama kauli. "Haijalishi unamwamini nani, hautakuwa na ujasiri wa kuasi dhidi yangu".

Isaiah 36:6

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza ujumbe wa mfalme wa Ashuru kwa Hezekia. Kamanda mkuu anazungumza ujumbe kwa wanamume wa Hezekia.

Tazama

Senakeribu anatumia lahaja kumvuta Hezekia kwa kile anachotaka kusema hivi punde.

unamtegemea Misri

Hapa "Misri" ina maana ya jeshi la Misri. "kuamini katika jesgi la Misri"

hilo tete lililochanikachanika ambalo unatumia kama gongo la kutembelea, lakini kama mtu akaliegemea, litaganda mkononi mwake na kuuchuma

Hii inazungumzia Misri, haswa jeshi lake na Farao wake, kana kwamba lilikuwa tete lililochanikachanika kusisitiza ya kwamba kuwategemea hakuwezi kuwasaidia lakini kutawadhuru tu. "hiyo ni kama kutembea kwa tete lililochanikachanika kwa ajili ya gongo. Kama mtu ataliegemea, litanga'ang'ani kwenye mkono wake na kuuchoma"

tete lililochanikachanika

tete ni shina refu la mmea kama nyasi ndefu. Kama limechanikachanika au kuharibika haliwezi kubeba uzito wowote.

gongo la kutembelea

Hiki ni kijiti ambacho mtu anaweza kutumia kama mhimili anapotembea, kimetengenezwa kwa mti wa aina yoyote ambao hukutwa njiani.

je! yeye siye yule ambaye sehemu zake za juu na madhabahu zimeondolewa na Hezekia ... Yerusalemu"?

Mfalme wa Ashuru anatumia swali hili kudhihaki watu na kuonyesha ya kwamba Yahwe alikuwa amekasirika juu ya Hezekia alichofanya na asingewalinda. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "yeye ndiye ambaye sehemu zake za juu na madhabahu yameondolewa na Hezekia ... Yerusalemu" au "yeye ndiye ambaye sehemu zake za juu na madhabahu ... Yerusalemu".

akamwambia Yuda na Yerusalemu, "Unatakiwa kuabudu mbele ya dhabahu hili katika Yerusalemu"?

Hii inaweza kuandikwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Yuda" na "Yerusalemu" ina maana ya watu ambao wanaishi humo. "amewaambia watu wa Yuda na Yerusalemu ya kwamba wanapaswa kuabudu katika dhabahu hili tu Yerusalemu"

Isaiah 36:8

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza ujumbe wa mfalme wa Ashuru kwa Hezekia kwa kuzungumnza ujumbe kwa wanamume wa Hezekia.

farasi elfu mbili

"farasi 2,000"

kama unaweza kupata wafunza farasi kwa ajili yao

Kamanda mkuu anaendelea kumdhihaki Hezekia na jeshi lake kwa kudokeza ya kwamba hakuwa na wanajeshi wengi.

Isaiah 36:9

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza ujumbe wa mfalme wa Ashuru kwa Hezekia kwa kuzungumnza ujumbe kwa wanamume wa Hezekia.

Unawezaje kumpinga hata nahodha mmoja ... watumishi?

Kamanda mkuu anaendelea kumdhihaki Hezekia na jeshi lake. Anaposema "unawezaje" kumaanisha Hezekia, kihalisia anamaanisha jeshi la Hezekia. Swali hili linaweza kuandikwa kama kauli. "Jeshi lako hata haliwezi kushinda nahodha mmoja ...watumishi".

Basi sasa, sijasafiri hapa bila Yahwe kupigana dhidi ya nchi hii na kuiangamiza?

Kamanda mkuu anatumia swali lingine kumdhihaki Hezekia na watu wa Yuda. swali hili linaweza kuandikwa kama kauli. "Nilikuja hapa pamoja na amri ya Yahwe kuangamiza Yerusalemu"

bila Yahwe

Hapa "Yahwe" ina maana ya amri za Yahwe. "bila amri ya Yahwe"

dhidi ya nchi hii na kuiangamiza ... Shambulia nchi hii na uiangamize

Hii ina maana kupigana dhidi ya watu na kusababisha uharibifu katika eneo ambalo wanaishi. Nchi inamaanishwa hapa ni Yerusalemu. "dhidi ya watu hawa na kuangamiza nchi yao ... Shambulia watu hawa na angamiza nchi yao"

Isaiah 36:11

Eliakimu ... Hilkia ... Shebna

Haya ni majina ya wanamume.

Shebna

Hili ni jina la msimaizi wa kasri ya mfalme Yerusalemu

Yoa ...kamanda mkuu

Yoa ni jina la mwanamume. Kama mkuu ni mwenye nafasi ya juu kabisa ya viongozi wa kijeshi Ashuru.

Tafadhali zungumza kwa mtumishi wako

Eliakimu, Shebna, na Yoa wanajitambulisha kama watumishi wa makamanda wakuu. Hii njia ya upole ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka ya makubwa.

lugha ya Kiashuri, Kiyahudi

"Ashuru" ni jina la kundi la watu. "Kiashuri" ni jina la lugha yao

masikioni mwa watu ambao wapo katika ukuta

Lahaja "kuzungumza katika masikio ya mtu" ina maana ya kuzungumza pale ambapo watasikia. "ambapo watu walio juu ya ukuta waweze kutusikia"

ambao wapo katika ukuta

Hii ina maana wanasimama katika ukuta. Juu ya ukuta palikuwa papana na sehemu ambayo watu wanaweza kukaa au kusimama. Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "ambao wanasimama juu ya ukuta"

Je! bwana wangu amenituma kwa bwana wako na kwako kuzungumza maneno haya?

Kamanda mkuu anatumia swali hili kusisitiza ya kuwa ujumbe huu ni kwa ajili ya watu wote wa Yuda. Swali hili linaweza kuandikwa kama kauli. "Hakika, bwana wangu amenituma kuzungumza ujumbe huu kwako na wote wanaoweza kuusikia".

Je! hajanituma kwa wanamume ambao wanakaa juu ya ukuta, ambao ... wewe?

Kamanda mkuu anatumia swali hili kusisitiza tusi lake. "Bwana wangu amenituma kwa kila mmoja anayesikia hili, ambaye atapaswa ... wewe".

watapaswa kula kinyesi chao wenyewe na kunywa mkojo wao wenyewe pamoja na wewe

Hii ni kauli ya kuchukiza sana. Anadokeza ya kwamba watahitaji kula vitu hivi kwa sababu hawatakuwa na kitu kingine kula kwa sababu mji wao utashambuliwa. "hivi punde watahitaji kula kinyesi chao wenyewe na kunywa mkojo wao wenyewe, kama utakavyofanya, kwa sababu hautakuwa na kitu chochote cha kula"

Isaiah 36:13

kamanda mkuu

Baadhi ya tafsiri za Biblia zinatafsiri kuwa hii ni "Rabshake". Hili ni neno la Ashuru kwa yule mwenye nafasi ya juu kabisa ya viongozi wa kijeshi Ashuru.

mji huu hautakabidhiwa mikononi mwa mfalme wa Ashuru

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe hatawapatia Yerusalemu katika mkono wa mfalme wa Ashuru"

mkono wa mfalme

"mkono" wa mfalme una maana ya "utawala" wake. "utawala wa mfalme"

Isaiah 36:16

Maelezo ya Jumla

Kamanda mkuu anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda.

Fanya amani na mimi

Lahaja hii ina maana ya kukubali rasmi kutenda kwa amani kwa mtu mwingine. "Tukubaliane kuwa na amani"

jitokeze uje kwangu

Lahaja hii ina maana ya kujisalimisha. "jisalimishe kwangu"

hadi ntakapokuja na kuchukua

Hapa mfalme wa Ashuru anamaanihsa kwa jeshi lake kama yeye mwenyewe. "hadi jeshi langu litakapokuja na kuchukua"

nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kwa ajili ya msisitizo jinsi nchi itakavyokuwa na mafanikio.

nchi ya nafaka ... nchi ya mkate

Hii ina maana ya kwamba nchi imejaa rasilimali, kama vile nafaka. "nchi ambapo kuna nafaka nyingi ... nchi ambapo kuna mkate mwingi"

Isaiah 36:18

Taarifa ya Jumla

Kamanda mkuu anaendelea kuzungumza ujumbe wa mfalme wa Ashuru kwa watu wa Yuda.

Je! kuna miungu yoyote ya watu iliyowaokoa kutoka .... Ashuru?

Kamanda mkuu anatumia swali hili kudhihaki watu wa Yuda. Swali hili linaweza kuandikwa kama kauli. "hakuna kati ya miungu ya watu iliyowaokoa wao kutoka .... Ashuru"

mkono wa mfalme

Utawala wa mfalme una maana ya "mkono" wake. "utawala wa mfalme"

Wako wapi miungu wa Hamathi na Arpadi? Wako wapi miungu wa Sefarvaimu? Je! wameokoa Samaria kutoka katika nguvu yangu?

Kamanda mkuu anatumia maswali haya kudhihaki watu wa Yuda. Maswali haya yanaweza kuunganishwa na kuandikwa kama kauli. "Miungu ya hamathi, Arpadi, Sefravaimu, na Samaria haikuokoa watu wao kutoka katika nguvu yangu"

Hamathi ... Arpadi

Haya ni majina ya miji.

Sefarvaimu

Hili ni jina la mji.

Je! kuna mungu yeyote ambaye amekuokoa ... kana kwamba Yahwe anaweza kuokoa Yerusalemu kutoka katika nguvu yangu?

Kamanda mkuu anatumia swali hili kudhihaki watu wa Yuda. Swali hili linaweza kuandikwa kama kauli. "Hakuna mungu ambaye amekuokoa ... na Yahwe hatakuokoa Yerusalemu kutoka katika nguvu yangu"

nchi yake

Hii ina maana ya watu ambao wanaishi katika nchi. "watu wake"

Isaiah 36:21

Eliakimu ... Hilkia ... Sheban ... Yoa ... Asafu

Haya ni majina ya wanamume.

juu ya nyumba

Lahaja hii ina maana ya kwamba alikuwa msimamizi wa masuala ya kasri. "msimamizi wa kasri"

kwa nguo zao zilizochanika

maafisa wa Hezekia walichana nguo zao kama ishara ya kuomboleza na mateso. Maana ya hii inaweza kuwekwa wazi. "huku nguo zao zikiwa zimechanika kwa sababu walikuwa na wameteseka sana"

Isaiah 37

Isaiah 37:1

Ikaja kuwa kwamba

Msemo huu unatiwa hapa kuweka alama kwa tukio muhimu katika simulizi.

alichana nguo zake, akajifunika kwa nguo ya gunia

Hii ni ishara ya kuomboleza na dhiki. "alichana nguo zake na kujifunika kwa nguo ya gunia kwa sababu alikuwa na dhiki sana"

Eliakimu ... Shebna

Haya ni majina ya wanamume.

juu ya nyumba

Hii ni lahaja ambayo ina maana ya kwamba alikuwa akisimamia masuala ya kasri ya nyumba. "aliyesimamia kasri"

wote wakajifunika na nguo ya gunia

Hii ni ishara ya kuomboleza na kuhuzunika.

Isaiah 37:3

Walisema kwake

"Wanamume waliotumwa na Hezekia walisema kwa Isaya"

kama pale ambapo mtoto yupo tayari kuzaliwa, lakini mama hana nguvu ya kuzaa mtoto wake

Kulinganisha huku kunafanywa kusisitiza ya kwmba wapo katika kipindi kigumu sana. "Ni mateso kama siku ambapo mtoto yupo tayari kuzaliwa, lakini mama hana nguvu ya kuzaa mtoto wake"

Inaweza kuwa pale ambapo Yahwe Mungu wako atasikia maneno

Hezekia anadokeza sio moja kwa moja ya kwamba kama watu wataomba Yahwe anaweza kusikiliza na kutenda juu ya kile kamanda mkuu alichosema. Maana kamili ya kauli hii inaweza kufanywa wazi. "Huenda kama ukiomba kwa Yahwe Mungu wako atasikia ujumbe"

kamanda mku

Baadhi ya tafsiri za Biblia zinatafsiri kuwa hii ni ""Rabshake". Hili ni neno la Ashuru kwa yule mwenye nafasi ya juu kabisa ya viongozi wa kijeshi Ashuru.

bwana wake

Msemo huu una maana ya kwamba mfalme ni bwana wa kamanda mkuu.

na atakemea maneno ambayo Yahwe Mungu wako ameyasikia

Hapa msemo "maneno ambayo Yahwe Mungu wako amesikia" ina maana ya kile mfalme wa Ashuru amesema. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "na Yahwe Mungu wako atakemea mfalme wa Ashuru kwa kile alichosema"

inua maombi yako

Kuomba kwa Yahwe inaelezwa kwa njia hii kusisitiza ya kwamba Yahwe yupo mbinguni. Maombi yanazungumziwa kana kwamba yalikuwa vitu ambavyo vinaweza kuinuliwa juu angani. "omba"

kwa aliyesalia ambaye bado yupo pale

Hii ina maana ya watu ambao wamebaki Yerusalemu. "kwa wachache wetu ambao bado tupo hapa"

Isaiah 37:5

Nitaweka roho ndani yake, naye atasikia taarifa fulani na kurudi katika nchi yake

Msemo huu "kuweka roho ndani yake" ina maana ya kwamba Mungu atamshawishi kufanya maamuzi bayana. Neno "roho" hapa lina maana ya mtazamo wa nguvu au hisia. "Nitamshawishi ili kwamba atakaposikia taarifa fulani, atarudi katika nchi yake mwenyewe"

Tazama

Neno hili ni lahaja na linatumika hapa kuvuta nadhari ya watu kwa kile kinachosemwa baadaye. "Sikiliza"

Nitamsababisha aanguke kwa upanga katika nchi yake mwenyewe

Msemo "kuanguka kwa upanga" ni lahaja ambayo ina maana ya kwamba adui yake atamuua kwa upanga. "Na pale katika nchi yake mwenyewe, nitasababisha adui zake kumuua kwa panga zao"

Isaiah 37:8

Lakishi

Huu ni mji kusini magharibi mwa Yerusalemu.

Senakeribu

Hili ni jina la mfalme wa Ashuru.

Libna

Huu ni mji kusini mwa Yuda.

Tirhaka mfalme wa Ethiopia na Misri wamehasamisha kupigana dhidi yao

"Tirhaka" ni jina la mwanamume. Aliwahamasisha jeshi lake ili wawe tayari kupigana. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Tirhaka mfalme wa Ethiopia na Misri alihamasisha jeshi lake"

kupigana dhidi yake

Neno "yake" inawakilisha Senakeribu. Msemo huu una maana ya kupigana dhidi ya jeshi la Senakeribu"

Yerusalemu haitatolewa katika mkono wa mfalme wa Ashuru

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Neno "mkono" lina maana ya nguvu ya kijeshi ya mfalme. "Mfalme wa Ashuru na jeshi lake halitakushinda katika Yerusalemu"

Isaiah 37:11

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza ujumbe wa mfalme wa Ashuru kwa Hezekia.

Tazama, umesikia

Hii ni lahaja. Neno "tazama" hapa linatumika kuongeza msisitizo kwa kile kinachosemwa baadaye. "Hakika umesikia"

Kwa hiyo utakombolewa?

Mfalme wa Ashuru anatumia swali hili kumdhihaki Hezekia na jeshi lake. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Kwa hiyo na wewe hautaokolewa" au "Kwa hiyo hakuna mtu atakayekuokoa pia!"

Je! miungu wa mataifa wamewaokoa ... Telasari?

Mfalme wa Ashuru anatumia swali hili kumdhihaki Hezekia na jeshi lake. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Miungu ya mataifa hawakukomboa mataifa ambayo baba zangu waliangamiza ... Telasari!"

ambayo baba zangu waliangamiza

Wanamume hawa waliangamiza miji iliyoorodheshwa kwa kuishinda kwa majeshi yao. Hapa neno "baba" ina maana ya baba yake na babu zake wengine ambao walikuwa wafalme. "ambao baba zangu waliangamiza kwa majeshi yao"

Gozani ... Harani .... Resefu ... Adini ... Telasari ... Hena ... Iva

Hizi ni sehemu ambazo Ashuru alizishinda.

Yuko wapi mfalme ... Iva?

Mfalme wa Ashuru hutumia swali hili kumkejeli Hezekia na jeshi lake. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Pia tulimshinda mfalme ... Iva!"

Hamathi ... Arpadi ... Sefarvaimu

Haya ni majina ya miji.

Isaiah 37:14

katika mkono wa wajumbe

Hapa wajumbe wanamaanishwa kwa "mkono" wao kusisitiza ya kwamba walimpatia mfalme wao binafsi. "ambayo wajumbe walimpatia"

akaelekea juu katika nyumba ya Yahwe

Nyumba ya Yahwe ilikuwa katika sehemu ya juu Yerusalemu, kwa hiyo inazungumziwa kama "juu".

kuikunjua mbele yake

"kuikunjua barua mbele ya Yahwe". Kuwa katika nyumba ya Yahwe inachukuliwa sawa na kuwa katika uwepo wa Yahwe. Barua ilikuwa hati ya kukunja ambayo inaweza kufunulia na kutandikwa.

wewe unayekaa juu ya makerubi

Hapa Hezekiia anazungumza kuhusu Yhwe kuwepo ndani ya hekalu. Maana ya hii inaweza kuwekwa wazi. "wewe ambaye upo hapa pamoja na makerubi"

wewe ni Mungu pekee

"wewe tu ni Mungu"

juu ya falme zote

Lahaja hii ina maana ya kuwa na mamlaka na kutawala juu ya falme zote. "kuwa na mamlaka juu ya falme zote"

Ulitengeneza mbingu na dunia

Hii ina maana ya kwamba aliumba kila kitu. "Uliumba kila kitu"

Isaiah 37:17

Taarifa ya Jumla

Hezekia anaendelea kuomba kwa Yahwe.

ambaye alimtuma

Hezekia anamaanisha barua kutoka kwa Senakeribu. Maana ya hii inaweza kuwekwa wazi. "katika ujumbe aliotuma"

Geuza sikio lako

"Tega sikio lako" au "Geuza kichwa chako". Hii ina maana kugeuza kichwa chako ili kwamba uweze kusikia jambo vizuri.

Senakeribu

Hili ni jina la mfalme wa Ashuru.

mataifa yote na nchi zao

Huku ni kukuza. Wafalme walikuwa wameangamiza nchi nyingi za karibu, lakini sio nchi zote. "mataifa mengi na nchi zao"

Isaiah 37:19

Taarifa ya Jumla

Hezekia anaendelea kuomba kwa Yahwe.

kwa maana hawakuwa miungu lakini kazi ya mikono ya watu, mabao na mawe tu

Hii inasisitiza ya kwamba wanadamu walifanya sanamu hizi kwa mikono yao wenyewe na kwa hiyo hazina thamani. "kwa sababu ilikuwa miungu ya uongo ambayo watu walitengeneza kwa mbao na mawe"

kutoka katika nguvu yake

"kutoka kwa mfalme wa nguvu ya Ashuru"

falme zote

Hii ina maana ya watu katika falme. "watu wote katka falme"

wewe ni Yahwe pekee

"wewe tu, Yahwe, ni Mungu"

Isaiah 37:21

akatuma ujumbe

Hii ina maana ya kwamba alituma mjumbe kutoa ujumbe kwa mfalme. "alimtuma mtu kutoa ujumbe"

ni neno ambalo Yahwe amenena

"ni kile Yahwe ambacho alisema"

anakucheka kwa kubeza

"anakucheka" au "kukudhihaki"

anatikisa kichwa chake

Hii ni ishara ya dharau.

Binti bikira wa Sayuni ... binti wa Yerusalemu

Hizi ni lahaja. Misemo hii miwili ina maana moja. "binti" wa mji ina maana watu ambao wanaishi katika mji huo. "Watu wa Sayuni ... watu wa Yerusalemu"

Ni nani umemkataa na kumtukana? ... Dhidi ya Mtakatifu wa Israeli

Yahwe anatumia maswali haya ya balagha kumkejeli mfalme wa Ashuru. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Umemkataa na kumtukana Yahwe, umepiga kelele na kutenda kwa kiburi dhidi ya Mtakatifu wa Israeli!"

umeinua sauti yako

Hii ina maana ya kuongea kwa sautii kana kwamba sauti ya mtu ilikuwa kitu ambacho walikiinua juu. "je! umepiga kelele"

kuinua macho yako kwa kiburi

Hii ni lahaja ambayo ina maana ya kutazama kitu kwa kiburi, kujichukulia muhimu zaidi kuliko unavyotakiwa. "kutazama kwa kiburi" au "alitenda kwa kiburi"

Isaiah 37:24

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza ujumbe wa Yahwe kwa mfalme wa Ashuru

Kwa watumishi wako

Hii ina maana ya watumishi ambao aliwatuma kwa Hezekia na ujumbe. Hii inaweza kuwekwa wazi. "Katika ujumbe uliotuma na watumishi wako"

Nimekwenda ... Nitakata... Nitaingia ... Nmechimba ... Nilikausha ... miguu yangu

Hapa Senakeribu anajizungumzia kushinda vitu vingi. Kiuhalisia anawashinda kwa majeshi yake na vibandawazi. "Tumekwenda ... Tutakata ... Tutaingia ... Tumechimba ... Tulikausha ... miguu yetu"

mierezi yake mirefu

"mierezi mirefu ya Lebanoni"

misitu yake inayozaa zaidi

Hapa neno "inayozaa" ina maana ya msitu kuwa mzito na kujaa miti yenye afya. Maneno ambayo hayapo yanaweza kuongezwa kufanya maana kuwa wazi. "na katika msitu wake unaozaa zaidi"

Nilikausha mito yote ya Misri chini ya nyayo za miguu yangu

Hapa Senakeribu anakuza ushindi wake na kusafiri kupitia mito ya Misri kwa kudai kukausha mito alipotembeza jeshi lake mtoni. "Nimetembeza katikati ya mito yote ya Misri kana kwamba ilikuwa nchi kavu chini ya miguu yangu"

Isaiah 37:26

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza ujumbe wa Yahwe kw mfalme wa Ashuru.

Je! haujasikia jinsi ... nyakati?

Yahwe anatumia swali hili la balagha kumkumbusha Senakeribu kuhusu taarifa ambayo alipaswa kuwa anaifahamu. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Hakika mmesikia jinsi ... nyakati".

Upo hapa kupunguza miji isioingilika katika marundo ya uharibifu

Yahwe alikuwa amepanga kwa jeshi la Senakeribu kuangamiza miji ambayo walikuwa wameangamiza. Hii inaweza kuwekwa wazi zaidi. "Nilipanga ya kwamba jeshi lako lingeangamiza miji na kuisababisha kuwa rundo la kifusi"

isioingilika

imara na yenye ulinzi mkali

wenye nguvu ndogo

"ambao ni dhaifu"

wamepondwapondwa

"kuvunjwa moyo"

Ninaifanya itimie

Lahaja "kufanya kitu kutimia" ina maana ya kusababisha kitu dhahiri kutokea. "Ninasababisha itokee" au "Ninasababisha vitu hivi kutendeka"

Wao ni mimea katika shamba, nyasi za kijani, nyasi juu ya paa au katika shamba, mbele ya upepo wa mashariki

Hii inazungumzia jinsi miji ilivyo dhaifu na kutoweza kujilinda mbele ya jeshi la Ashuru kwa kulinganisha miji na nyasi. "Miji ni dhaifu kama nyasi katika mashamba mbele ya majeshi yako. Wao ni dhaifu kama nyasi ambayo huota juu ya paa za nyumba na kuchomwa na upepo mkali wa mashariki"

upepo wa mashariki

Upepo wa mashariki ni wa moto na mkavu kutoka katika jangwa na mimea hufa unapovuma.

Isaiah 37:28

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza ujumbe wa Yahwe kwa mfalme wa Ashuru.

Lakini ninajua kukaa kwako chini, kutoka kwako, kuingia kwako

Hii ina maana ya vitendo vyote vya maisha. "Ninajua kila kitu unachofanya"

na hasira yako dhidi yangu

Neno "hasira" linaweza kuelezwa kama kitenzi. "jinsi unavyokasirika dhidi yangu"

kiburi chako

Hapa "kiburi" cha mfalme kina maana ya maneno yake ya kiburi. "maneno yako ya kiburi"

kiburi chako kimeyafikia masikio yangu

Hii inazungumzia yahwe kusikia maneno ya mfalme kana kwamba maneno ya mfalme yalikuwa kitu ambacho kilisafiri mpaka katika sikio lake. "Nimesikia ukizungumza kwa kiburi"

nitaweka ndoano yangu katika pua yako, na lijamu katika mdomo wako

Mtu hutumia ndoano na lijamu kuongoza mnyama. Hii inazungumzia Yahwe kutawala mfalme kana kwamba mfalme alikuwa mnyama yahwe aliyetawala kwa lijamu na ndoano. "Nitakutawala kama mwanamume anavyotawala mnyama wake kwa ndoano katika pua yake na lijamu katika mdomo wake"

Nitakurudisha katika njia uliyotoka

Hii ina maana ya kusababisha mfalme kurudi katika nchi yake ya nyumbani. Maana ya hii inaweza kuwekwa wazi. "Nitakulazimisha kurudi katika nchi yako mwenyewe"

Isaiah 37:30

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza ujumbe wa Yahwe kwa Hezekia.

ishara kwako

"ishara kwako, Hezekia". Hapa "kwako" ni umoja na ina maana ya Hezekia.

utakula ... unapaswa kupanda

Hapa "utakula" ni wingi na ina maana ya watu wa Yuda.

mwaka wa pili

"mwaka wa pili"

katika mwaka wa pili kile kitakachoota

maneno ambayo hayapo yanaweza kuongezwa. "katika mwaka wa pili utakula kile kinachoota"

kile kitakachoota kutokana na hicho

"kile kitakachoota pori kutokana na hicho" au "kile kitakachoota pori"

Isaiah 37:31

Taarifa ya Jumla

Hii inaendeleza ujumbe wa Yahwe kwa Hezekia.

waliobaki

"aliyesalia" ni sehemu ya kitu ambacho hubaki baada ya wengine kuondoka. Hapa ina maana ya watu ambao wamebaki Yuda.

nyumba ya Yuda

Hapa "nyumba" ya Yuda ina maana ya vizazi vyake. "vizazi vya Yuda"

atachipua tena mzizi na kuzaa matunda

Hii inazungumzia watu wa Yuda kuwa na mafanikio kana kwamba walikuwa mimea ambayo ingetoa mzizi na kuzaa matunda. "itafanikiwa kama mmea ambao huota mzizi na kuzaa matunda"

Kwa maana kutoka Yerusalemu aliyesalia atajitokeza; kutoka Mlima Sayuni waliokoka watakuja

Misemo hii miwili ina maana moja na inatumika pamoja kusisitiza watu waliosalia ambao waliokoka.

Ari ya Yahwe wa majeshi itafanya hivi

Hii inazungumzia Yahwe kufanya kitu kwa sababu ya ari yake kana kwamba "ari" yake ilikuwa ikifanya tendo kihalisia. "Kwa sababu ya ari yake, Yahwe wa majeshi atafanya hivi" au "Yahwe wa majeshi atafanya hivi kwa sababu ya ari yake"

Isaiah 37:33

Hatakuja ... Wala hatakuja

Hapa mfalme wa Ashuru anamaanisha wote yeye na jeshi lake. "Jeshi lake halitakuja ... Wala hawatakuja"

kwa ngao

"kwa ngao"

tuta la kuzingira

kilima kikubwa cha mchanga kilichojengwa dhidi ya ukuta wa mji ambacho huwezesha jeshi kushambulia mji

alikuja ... hataingia

Hapa mfalme wa Ashuru anamaanisha wote yeye na jeshi lake. "walikuja .. hawataingia"

Hili ni tamko la Yahwe

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "tamko" lielezwa kama kitenzi "tamka" au "sema kwa dhati". "hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyotamka" au "hivi ndivyo kile Yahwe wa majeshi alivyosema kwa dhati"

Isaiah 37:35

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

kwa ajili ya

"kwa sababu"

Isaiah 37:36

kuwaua

Hii lahaja ina maana ya kua. "kuua"

Senakeribu mfalme wa Ashuru aliondoka Israeli na kwenda nyumbani na kukaa Ninawi

Hapa Senakeribu ina maana ya wote yeye na jeshi lake. Wote aliondoka Israeli na kurudi nyumbni Ashuru. Senakeribu alirudi katika mji wa Ninawi. "Senakeribu na jeshi lake aliondoka Israeli na kwenda nyumbani, na Senakeribu alibaki Ninawi"

Senakeribu

Hili ni jina la mfalme wa Ashuru.

Isaiah 37:38

alipokuwa akiabudu

"Senakeribu alipokuwa akiabudu"

Nsiroki

Hili ni jina la mungu wa uongo.

Adrameleki ... Shareza ... Esar-hadoni

Haya ni majina ya wanamume.

kwa upanga

"kwa panga zao"

Isaiah 38

Isaiah 38:1

Upange nyumba yako vizuri

Hii ina maana ya kuandaa familia yako na wale wanaosimamia masuala yako ili kwamba wajue cha kufanya baada ya kufa. Hii inaweza kuandikwa wazi. "Unatakiwa kuwaambia watu katika kasri kile unachotaka wao kufanya baada ya kufa"

weka akilini

Lahaja hii ina maana ya kukumbuka "kumbuka"

nilitembea kwa uaminifu mbele yako

Hii ni lahaja. Hapa "kutembea" ina maana ya "kuishi". Msemo una maana ya kuishi kwa njia ambayo inampendeza Yahwe. "aliishi kwa uaminifu mbele yako" au "alikutumikia kwa uaminifu"

kwa moyo wangu wote

Hapa "moyo" una maana ya undani wa mtu ambayo inawakilisha mtu kuwa na mapenzi ya dhati. "kwa utu wangu wote wa ndani" au "kwa mapenzi yangu yote"

kilichokuwa chema machoni pako

Msemo huu "machoni pako" ina maana ya kile Yahwe anachofikiri. "kile kinachokupendeza" au "kile unachokichukulia kuwa kizuri"

Isaiah 38:4

neno la Yahwe likaja

Hii ni lahaja ambayo inatumiwa kutambulisha kitu ambacho Mungu alimwambia manabii wake au watu wake. "Yahwe alizungumza ujumbe huu" au "Yahwe alizungumza maneno haya"

Tazama

Hii ni lahaja. Inatumika kuuliza wasikilizaji kuzingatia kwa makini kwa kile kinachosemwa. "Sikiliza"

miaka kumi na tano

"miaka 15"

mkono wa mfalme wa Ashuru

Hapa "mkono" wa mfalme una maana ya nguvu yake. "nguvu ya mflame wa Ashuru"

Isaiah 38:7

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na Hezekia.

Tazama

Hii ni lahaja. Yahwe anatumia neno hili kuvuta wasikilizaji kwa kile kinachosemwa baadaye.

ngazi za Ahazi

Ngazi hizi zina maana ya njia hii kwa sababu zilijengwa wakati Ahazi alikuwa mfalme.

Isaiah 38:9

hivyo katikati mwa maisha yangu

"ya kuwa kabla sijawa mzee". Hii ina maana ya kufa katika umri wa kati, kabla ya kuzeeka.

Nitapita katikati ya malango ya kuzimu

Hii inazungumzia kufa kana kwamba kuzimu ilikuwa ufalme ambao una malango ambayo mtu huingia. "Nitakufa na kuelekea kuzimu"

Nimetumwa kule kwa miaka yangu iliyobaki

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kabla sijaishi miaka yangu yote nitaenda kaburini"

katika nchi ya wanaoishi

"Wanaoishi" ina maana ya watu ambao wapo hai" au "katika dunia hii ambamo watu wapo hai"

Isaiah 38:12

Maelezo yaJumla

Hezekia anaendelea maombi yake ya maandishi.

Maisha yangu yameondolewa na kubebwa mbali na mimi kama hema la mchungaji

Hii inazungumzia jinsi Yahwe anamaliza uhai wa Hezekia kwa haraka kwa kulinganisha kwa jinsi mchungaji anavyotoa hema lake kutoka ardhini. "Yahwe amechukua uhai wangu kutoka kwangu haraka kama mchungaji anavyopanga hema lake na kulibeba mbali"

Maisha yangu yameondolewa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe amechukua uhai wangu"

Nimekunjua maisha yangu kama mfumaji; unanikata kutoka katika kitanda cha mfumi

Hii inazungumzia Yahwe kumaliza uhai wa Hezekia haraka kwa kulinganisha na jinsi mfumaji hukata nguo yake kutoka katika kitanda cha mfumi na kukikunjua juu. "unamaliza uhai wangu haraka, kama mfumaji anavyokata nguo yake kutoka katika kitnda inapokamilika"

unakata

Hapa "unakata" ni umoja na ina maana ya Mungu.

kitanda cha mfumi

chombo kinachotumika kufuma uzi pamoja kutengeneza nguo.

kama simba anavunja mifupa yangu yote

Hezekia anazungumza jinsi alivyo katika maumivu makala kwa kulinganisha kuwa na mwili wake kuraruriwa na simba. "maumivu yangu ni kana kwamba nimeraruliwa na simba"

Isaiah 38:14

Maelezo ya Jumla

Hezekia anaendelea maombi yake ya maandishi.

Kama mbayuwayu ninalia; ninalia polepole kama njiwa

Vishazi hivi vyote viwili vina maana moja na vinasisitiza jinsi milio ya huzuni na kusikitisha ya Hezekia ilivyokuwa. Mbayuwayu na njiwa ni aina ya ndege. "Milio yangu ni ya kusikitisha - inasikika kama mlio wa mbayuwayu na sauti kama ya njiwa"

macho yangu

Hapa Hezekia ana maana ya yeye mwenyewe. "macho" yake yanasisitiza ya kwamba anatafuta kitu.

kwa kutazama juu

Hii ina maana ya Hezekia kutazama mbinguni kwa ajili ya Mungu kumsaidia. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "kwa kusubiri msaada unaokuja kutoka mbinguni" au "kwa kusubiri kwa ajili yako kunisaidia"

Ninaonewa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ugonjwa wangu unanitesa mimi"

Niseme nini?

Hezekia anatumia swali kusisitiza hana chochote cha kusema. "Sina chochote kilichobaki cha kusema"

Nitatembea polepole

Hii ni lahaja. Hapa "kutembea" ina maana ya kuishi. "Nitatembea kwa unyenyekevu"

miaka yangu yote

Hii ina maana ya maisha yake yote yaliyobaka. "maisha yangu yaliyobaki"

kwa sababu nimezidiwa na majonzi

"kwa sababu nimejaa majonzi" au "kwa sababu nina huzuni sana"

Isaiah 38:16

Maelezo ya Jumla

Hezekia anaendelea maombi yake ya maandishi.

na maisha yangu yarudishwe kwangu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na unipatiea uhai wangu kwangu"

kutoka katika shimo la uharibifu

Hezekia hakufa lakini alikuwa karibu ya kufa. Hii ina maana Yahwe kumuokoa katika kufa. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "kutoka katika kifo na kwenda katika shimo la uharibifu" au "ili kwamba nisiweze kufa"

kwa kuwa umezitupa dhambi zangu nyuma ya mgongo wako

Hezekia anazungumzia Yahwe kusamehe dhambi zake kana kwamba zilikuwa vitu ambavyo Yahwe alitupa nyuma yake na kuvisahau. "kwa maana umesahau dhambi zangu zote na hauvifikirii tena"

Isaiah 38:18

Maelezo ya Jumla

Hezekia anaendelea maombi yake ya maandishi.

Kwa maana kuzimu haikushukuru wewe; kifo haikusifu wewe

Hapa "kuzimu" na "kifo" ina maana ya "watu waliokufa". "Kwa wale walio Kuzimu hawakushukuru; watu waliokufa hawakusifu"

wale waendao chini shimoni

"wale ambao hushuka katika kaburi"

hawatumaini katika uaminifu wako

"usiwe na matumaini katika uaminifu wako". Hapa "wako" ni umoja na ina maana ya Yahwe.

Mtu anayeishi, mtu anayeishi

Hezekia anarudia msemo huu kusisitiza ya kuwa mtu hai pekee, na sio mfu, anaweza kutoa shukurani kwa Yahwe.

Isaiah 38:20

Maelezo ya Jumla

Hezekia anaendelea maombi yake ya maandishi.

niokoe

Hii ina maana ya kuokolewa kutoka katika kufa. Inawez akuwekwa wazi zaidi. "niokoe katika kufa"

tutashangilia

Hapa "tutashangilia" ina maana ya Hezekia na watu wa Yuda.

Isaiah 38:21

Sasa

Neno hili linatumika kuweka alama ya pumziko katika simulizi kuu. Hii inatoa taarifa ya nyuma kuhusu Isaya na Hezekia.

Na wachukue

"Na watumishi wa Hezekia"

bonge la tini

Hii ilitumika kama lihamu. Maana inaweza kuwekwa wazi. "tumia lihamu ya tini ya kupondwa"

kuchemsha

eneo linalouma juu ya ngozi ambayo imeathirika

Isaiah 39

Isaiah 39:1

Merodaki-Baladani ... Baladani

Haya ni majina ya wanamume.

Hezekia alifurahiswah na mambo haya

Hii inaweza kuwekwa wazi zaidi. "Wajumbe wa mfalme walipofika, Hezekia alifurahishwa na kile walicholeta kwake"

aliwaonywesha wajumbe ghala yake yenye vitu vya thamani

"aliwaonyesha wajumbe kila kitu cha thamaniu alichokuwa nacho"

ghala

jengo ambapo bidhaa hukaa

kila kilichopatina ndani ya ghala yake

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kila kitu ambacho kilikuwa ndani ya ghala zake"

Hapakuwa na kitu katika nyumba yake, wala katika ufalme wake, ambacho Hezekia hakuwaonyesha

Huku ni kukuza kidogo maana Hezekia aliwaonyesha vitu vingi, lakini sio kila kitu. Pia, hii inaweza kuelezwa kwa chanya. "Hezekia aliwaonyesha karibu kila kitu ndani ya nyumba yake na ndani ya ufalme wake"

Isaiah 39:3

Wameona kila kitu ndani ya nyumba yangu. Hakuna kitu miongoniu mwa vitu vyangu vya thamani ambacho sijawaonyesha

Sentensi hizi mbili zina maana moja na hutumika pamoja kusisitiza jinsi gani Hezekia aliwaonyesha wanamume.

kila kitu ndani ya nyumba yangu

Huku ni kukuza kidogo maana Hezekia aliwaonyesha vitu vingi, lakini sio kila kitu. "karibu ya kila kitu katika nyumba yangu"

Hakuna kitu miongoniu mwa vitu vyangu vya thamani ambacho sijawaonyesha

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya chanya. "Niliwaonyesha vitu vyangu vyote vya thamani katika kasri yangu"

Isaiah 39:5

Yahwe wa majeshi

Hili ni jina la Mungu wa watu wa Israeli.

neno

"ujumbe"

Tazama

Neno hili linatumika hapa kama lahaja kuvuta usikivu wa Hezekia kwa kile kinachofuatwa kusemwa. "Sikilizeni"

ambapo kila kitu katika kasri yako ... kitabebwa mpaka Babeli

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya chanya. "pale ambapo jeshi la adui litachukua kila kitu katika kasri yako ... kurudi Babeli"

Isaiah 39:7

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza ujumbe wa Yahwe kwa Hezekia.

wana watakaozaliwa kwako

"wana wako"

watawachukua

"Wababeli watawachukua"

Isaiah 40

Isaiah 40:1

Fariji, fariji

Neno "fariji" linarudwa kwa ajili ya msisitizo

asema Mungu wako

Hapa "wako" ni wingi na ina maana ya wale ambao nabii anawaambia kufariji watu wa Mungu.

Zungumza kwa upole kwa Yerusalemu

Nabii anazungumzia Yerusalemu kana kwamba ilikuwa mwanamke ambaye Yahwe alimsamehe. Kwa hiyo, Yerusalemu inawakilisha watu wanaoishi katika mji huo. Zungumza kwa upole kwa watu wa Yerusalemu"

tamka kwake ...ustawi wake ... udhalimu wake amepokea ... dhambi zake

Viwakilishi nomino vina maana ya Yerusalemu lakini inaweza kubadilishwa kama "watu wa Yerusalemu" inaazimwa kama tafsiri. "tangaza kwao ... ustawi wao ... udhalimu wao ... wamepokea ... dhambi zao"

ustawi wake

Maana zaweza kuwa ya kwamba neno "ustawi" lina maana ya 1) kwa vita ya kijeshi au 2) kwa kazi ya kulazimishwa.

udhalimu wake umesamehewa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe amesamehe udhalimu wake"

kutoka mkononi mwa Yahwe

Hapa neno "mkono" inawakilisha Yahwe mwenyewe. "kutoka kwa Yahwe"

Isaiah 40:3

Sauti inalia

Neno "sauti" inawakilisha mtu ambaye analia. "Mtu analia"

Katika nyika andaa njia ya Yahwe; weka wima katika Araba njia kwa ajili Mungu wetu

Mistari hii miwili ni sambamba na ina maana moja. Watu kujiandaa kwa ajili ya msaada wa Yahwe inazungumziwa kana kwamba walikuwa wakiandaa njia kwa ajili ya Yahwe kusafiri juu yake.

Araba

Hili ni jangwa.

Kila bonde litainuliwa juu, na kila mlima na kilima kitasawazishwa

Misemo hii inaelezea jinsi watu wanapaswa kuandaa njia kwa ajili ya Yahwe. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Inua juu kila bonde, na sawazisha kila mlima na kilima"

Kila bonde litainuliwa juu

Kufanya mabonde kuwa sawasawa na ardhi iliyobakiai inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kuinua juu mabonde. "Kila bonde litajazwa"

na utukufu wa Yahwe utafunuliwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na Yahwe atafunua utukufu wake"

kwa maana mdomo wa Yahwe umenena

Neno "mdomo" unawakilisha Yahwe mwenyewe. " kwa maana Yahwe umeizungumza"

Isaiah 40:6

Nyama yote ni nyasi

Neno "nyama" lina maana ya watu. Msemaji anazungumza kuhusu wanadamu kana kwamba ni nyasi, kwa sababu wote hufa haraka. "Watu wote ni kama nyasi"

agano lao la uaminifu ni kama maua ya shambani

Msemaji analinganisha agano la uaminifu la watu kwa maua ambayo huchanua na kisha kufa haraka. "agano lao la uaminifu lote huisha haraka, kama ua wa shamba liinavyokufa haraka"

uaminifu wa agano

Maana zaweza kuwa 1) agano la uaminifu au 2) uzuri.

pumzi ya Yahwe itakapopuliza juu yake

Maana zaweza kuwa 1) "Yahwe atakapopuliza pumzi yake juu yake" au 2) "Yahwe atakapotuma upepo kupuliza juu yake".

ubinadamu ni nyasi

Msemaji anazungumzia wanadamu kana kwamba ni nyasi, kwa sababu wote hufa haraka. "watu hufa haraka kama nyasi"

neno la Mungu wetu litasimama milele

Msemaji anazungumza kile Mungu anasema kudumu milele kana kwamba neno lake husimama milele. "vitu ambavyo Mungu wetu wanasema vitadumu milele"

Isaiah 40:9

Panda katika mlima wa juu, Sayuni, mletaji wa habari njema

Mwandishi anazungumzia Sayuni kana kwamba ilikuwa mjumbe anayetmka habari njema kutoka katika kilele cha mlima.

Panda katika mlima wa juu

Wajumbe mara kwa mara husimama juu ya nchi iliyoinuka, kama vile milima, ili kwamba watu wengi waweze kusikia kile walichotangaza.

Sayuni

Hii ina maana ya watu ambao wanaishi Sayuni. "nyie watu wa Sayuni"

Yerusalemu. Wewe uletaye habari njema

Mwandishi anazungumzia Yerusalemu kana kwamba ilikuwa mjumbe ambaye hutangaza habari njema.

na mkono wake wa nguvu hutawala kwa ajili yake

Hapa neno "mkono" linawakilisha nguvu ya Mungu. "na anatawala kwa nguvu kubwa"

dhawabu yake ipo pamoja naye ... wale ambao amewaokoa huenda mbele zake

Misemo hii miwili ina maana moja. Wale ambao aliwaokoa ni "zawadi" yake. "anawaleta wale aliowaokoa pamoja naye kama zawadi yake"

Isaiah 40:11

Atalisha kundi lake kama mchungaji

Mwandishi anazungumzia watu wa Yahwe kana kwamba walikuwa kondoo na juu ya Yahwe kana kwamba alikuwa mchungaji wao. "Atawatunza watu wake kama mchungaji anavyolisha kundi lake"

Isaiah 40:12

Ambaye amepima ... au vilima juu ya mizani?

Maswali haya ya balagha yanatarajia jibu la kukana na linasisitiza ya kwamba ni Yahwe pekee anaweza kufanya vitu hivi. "Hakuna mwingine ila Yahwe amepima ... na vilima katika mizani".

aliyepima maji katika uwazi wa mkono wake

Yahwe kujua wingi wa maji uliomo katika bahari inazungumziwa kana kwamba Yahwe alishika maji katika mkono wake.

aliyepima anga kwa upana wa mkono wake

"upana" ni kipimo cha urefu katikati ya kidole gumba n kidole kidogo mkono unaponywoshwa. Yahwe kujua urefu wa anga inazungumziwa kana kwamba alipima kwa mkono wake.

aliyeshika vumbi la dunia katika kikapu

Yahwe kujua wingi wa vumbi ulivyo katika dunia inazungumziwa kana kwamba alilibeba katika kikapu.

aliyepima uzito wa milima katika mizani, au vilima katika mizani?

Yahwe kujua jinsi milima iilivyo mizito inazungumziwa kana kwamba alipiima kwa mizani.

Isaiah 40:13

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kutumia maswali kusisitiza utofauti wa Yahwe.

Ni nani ameelewa akili ya Yahwe, au kumwelekeza kama mshauri wake?

Swali hili la balagha linatarajia jibu la kukana na kusisitiza ya kwamba hakuna mtu aliyewahi kufanya vitu hivi. "Hakuna mtu aliyeelewa akili ya Yahwe, na hakuna mtu alimwelekeza kama mshauri wake".

ameelewa akili ya Yahwe

Hapa neno "akili" lina maana ya mawazo ya Yahwe, lakini pia na hamu na motisha zake.

Kutoka kwa nani alwahi kupokea maelekezo?

Swali hili la balagha linatarajia jibu la kukana na linasisitiza ya kwamba hakuna mtu aliyewahi kufanya hivi. "Hajawahi pokea maelekezo kutoka kwa mtu"

Nani alimfundisha njia sahihi ya kufanya mambo, na kumfundisha uelewa, au kumwonyesha njia ya maarifa?

Swali hili la balagha linatarajia jibu la kukana na kusisitiza ya kwamba hakuna mtu aliyewahi kufanya vitu hivi. "Hakuna mtu aliyemfundisha njia sahihi ya kufanya vitu. Hakuna mtu aliyemfundisha uelewa. Hakuna mtu aliyemwonyesha njia ya maarifa".

Isaiah 40:15

Tazama ... angalia

Maneno haya huongeza msisitizo kwa kile kinachofuata.

mataifa ni kama tone katika ndoo, na yanachukuliwa kama vumbi katika mizani

Nabii analinganisha mataifa kwa tone la maji na kwa vumbi ili kusisitiza jinsi yalivyo madogo na kutokuwa na umuhimu kwa Yahwe.

kama tone katika ndoo

Maana zaweza kuwa 1) tone la maji ambalo huanguka katika ndoo au 2) tone la maji ambalo hudondok nje ya ndoo.

na wanachukuliwa kama vumbi katika mizani

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na Yahwe anawachukulia kama vumbi juu ya mizani"

yanachukuliwa na yeye kama si kitu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "anayachukulia kutokuwa kitu"

Isaiah 40:18

Mtamlinganisha Mungu na nani? Kwa sanamu ipi mtamfananisha naye"

Isaya anatumia maswali mawili ya kufanana kusisitiza ya kwamba hakuna sanamu ambayo inaweza kufanana na Mungu. "Hakuna mtu ambaye unaweza kulinganisha na Mungu. Hakuna sanamu ambayo unaweza kumfananisha"

utamfananisha

Huu ni wingi na ina maana ya watu wote wa Mungu.

Fundistadi huichonga: sonara anavyoifunika kwa hahabu na kuichonga mikufu ya fedha kwa ajili yake

"Mtumishi mwenye ujuzi huiunda, mwingine huifunika kwa dhahabu, na kutengeneza mkufu wa fedha kwa ajili yake"

Isaiah 40:21

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Mungu.

Je! haujajua? Haujasikia? Haijaambiwa kwako toka mwanzo? Haujaelewa toka misingi ya dunia?

Isaya anatumia maswali haya kusisitiza ya kwamba watu wanapaswa kujua ukuu wa Yahwe kma muumba. "Kwa uhakika unajua na umesikia! Imeambiwa kwako toka mwanzo; umeelewa toka misingi ya dunia!"

Haijaambiwa kwako toka mwanzo?

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Je! watu hawajakuambia toka mwanzo?"

toka misingi ya dunia

Nabii anazungumzia Yahwe kuumba dunia kana kwamba dunia ilikuwa jengo ambalo Yahwe alilaza msingi. "kutoka kipindi ambacho Yahwe aliumba dunia"

Yeye ndiye ambaye hukaa juu ya upeo wa macho ya dunia

Nabii anazungumzia Yahwe kutawala dunia kana kwamba Yahwe alikuwa amekaa juu ya kiti cha enzi juu ya dunia.

wakazi ni kama panzi mbele zake

Nabii analinganisha namna ambavyo Yahwe anachukulia wanadamu kwa namna ambavyo wanadamu wangechukulia panzi. Kama vile panzi ni wadogo kwa binadamu, binadamu ni wadogo na dhaifu mbele za Mungu.

Ananyosha mbingu kama pazia na kuitawanya kama hema la kuishi ndani

Mistari hii miwili inatumia maana ya kufanana. Nabii anazungumzia Yahwe kuumba mbingu kana kwamba alisimamisha hema ambalo ataishi. "Anatawanya mbingu kwa urahisi kama mtu anavyonyosha pazia au kusimamisha hema ambalo anishi"

Isaiah 40:23

Hupunguza

"Yahwe hupunguza"

Tazama ... tazama ... tazama

Maneno haya yanaongeza msisitizo kwa kinachofuata.

wamepandwa muda si mrefu ... nao wananyauka

Nabii anazungumzia watawala kutojiweza mbele ya Yahwe kana kwamba walikuwa mimea mipya ambayo hunyauka pale upepo wa moto hupuliza juu yao.

wamepandwa muda si mrefu ... wameoteshwa muda si mrefu

Misemo hii miwili ina maana moja na inamaansha lengo ambalo mimea au mbegu inawekwa katika ardhi. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "baada tu ya mtu kuipanda ... baada tu ya mtu kusia"

anapuliza juu yao

Nabii anazungumzia Yahwe kuondoa watawala kutoka kwenye madaraka kana kwamba Yahwe alikuwa upepo unaochoma juu ya mimea na kusababisha inyeuke.

upepo unawapuliza kama majani makavu

Tashbihi hii inaongeza sitiari ya watawala kuwa mimea na Yahwe kama upepo ambao husababisha wao kunyauka. Hukumu ya upepo wa Yahwe utaondoa mimea iliyonyauka kirahisi kama upepo unavyopuliza majani makavu.

Isaiah 40:25

Ni kwa nani utanilinganisha mimi, ni nani nayefanana naye?

Yahwe anatumia maswali mawili ya kufanana ya balagha kusisitiza ya kuwa hakuna mtu kama yeye. "Hakuna mtu ambaye unaweza kulinganisha na mimi. Hakuna mtu ambaye ninamfanana".

Nani ameumba nyota hizi zote?

Hili ni swali la kufokeza ambalo linaashiria jibu, Yahwe. "Yahwe ameziumba nyota hizi zote!"

Yeye huongoza mpangilio wao

Hapa neno "mpangilio" una maana ya mpangilio wa kijeshi. Nabii anazungumzia nyota kana kwamba zilikuwa wanajeshi ambao Yahwe huamuru kujitokeza.

Kwa ukuu wa uwezo wake na kwa wingi wa nguvu zake

Misemo "ukuu wa uwezo wake" na "wingi wa nguvu zake" huunda mambo mawili ambayo husisitiza uweza wa Yahwe. "Kwa uwezo wake mkubwa na wingi wa nguvu"

hakuna mmoja asiyeonekana

Kauli hii ya kukana inasisitiza jambo chanya. "kila mmoja yupo"

Isaiah 40:27

Kwa nini unasema, Yakobo, na kutamka, Israeli ... uthibitisho"?

Swali linasisitiza ya kwamba hawatakiwi kusema wanachosema. "Hautakiwi kusema, enyi watu wa Israeli ... uthibitiisho'".

Kwa nini unasema, Yakobo, na kutamka, Israeli

Misemo hii miwili yote ina maana ya watu wa Israeli. "Kwa nini unasema, enyi watu wa Israeli"

Njia yangu imefichwa kutoka kwa Yahwe

Yahwe kutojua kinachotokea kwao inazungumziwa kana kwamba Yahwe hakuweza kuona njia ambayo ninasafiria. "Yahwe hajui kinatoke kwangu"

Mungu wangu hajihusishi juu ya uthibitisho wangu

Maana zaweza kuwa 1) "Mungu wangu hajihusishi juu ya wengine kunitendea kinyume n haki" au 2) "Mungu wangu hajihusishii juu kunitendea haki".

Je! haujajua? Haujasikia?

Isaya anatumia maswali haya kusisitiza ya kwamba watu wanatakiwaa kuja ukuu wa Yahwe. "Hakika unafahamu na umesikia!"

mwisho wa dunia

Sehemu katika dunia ambazo zipo mbali sana zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa sehemu ambapo dunia huwa mwisho. Msemo huu pia huunda neno moja kwa ajilii ya maneno mengiine kumaanisha kila sehemu katikati ya hizi mwisho. "sehemu za mbali za dunia" au "dunia nzima"

Isaiah 40:29

Hutoa nguvu kwa waliochoka; na kwa wadhaifu hutoa nguvu mpya

Mistari hii miwili inatuma maana za kufanana na husisitiza ya kwamba Yahwe hutia nguvu wale ambao hawana nguvu.

Hutoa nguvu

"Yahwe hutoa nguvu"

watapaa kwa mabawa kama tai

Watu kupokea nguvu kutoka kwa Yahwe inazungumziwa kana kwamba watu waliweza kupaa kama tai wanavyopaa. Tai ni ndege ambaye hutumiwa mara kwa mara kama alama ya uwezo na nguvu.

watakimbia na kuwatachoka; watatembea na hawazimia

Mistari hii miwili inatumia maana za kufanana. Watu kupata nguvu kutoka kwa Yahwe inazungumziwa kana kwamba waliweza kukimbia na kutembea bila kuchoka.

Isaiah 41

Isaiah 41:1

Sikiliza mbele zangu kwa utulivu

Hapa "zangu" ina maana ya Mungu.

enyi nchi za pwani

Hii ina maana ya watu ambao huishi katika visiwa na katika nchi zinazopatikana au ng'ambo ya pili ya Bahari ya Mediteranea.

wafanye upya nguvu zao

Yahwe hutia nguvu wale ambao hawana nguvu.

waache waje karibu na kuongea; tuache tukaribie pamoja kuamua mabishano

Misemo hii miwili hutumia maana moja. Msemo wa pili unafafanua sababu kwa ajili ya kwanza. "waache waje karibu ili wawvze kuzungumza na kuamua pamoja nami"

Ni nani aliyemwamsha yule kutoka mashariki, kumwita katika haki kwa huduma yake?

Yahwe anatumia swali hili kusisitiza ya kwamba yeye ndiye aliyesababisha mtawala huyu kutoka mashariki kuwa mshindi. "Mimi ndiye niliyemwita mtawala huyu wa nguvu kutoka mashariki na kumweka katika huduma nzuri"

Hukabidhi mataifa kwake

"Ninawapa mataifa kwake" au "Yule anayefanya mambo haya hukabidhi mataifa kwake"

Huyageuza kwa vumbi kwa upanga wake, kama mashina ya mabua yalipulizwa kwa upepo kwa upinde wake

Mataifa ambaye yule wa mashariki yanalinganshwa kwa vumbi na mashina ya mabua, kwa sababu yote yatakuwa madogo sana kama vitu hivi na kwa sababu jeshi lake litayasambaza kirahisi.

Isaiah 41:3

Taarif ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa nchi za pwani na mataifa

Huwafuatilia na kuwapita kwa usalama

"Mtawala kutoka mashariki hufuatilia mataifa"

kwa njia nyepesi ambayo miguu yake hugusa kwa nadra

Maana zaweza kuwa 1) hii ni sitiari ambayo yeye na jeshi lake kusogea haraka sana inazungumziwa kana kwamba miguu yake hugusa ardhii kwa nadra. "kwa njia ambayo anasogea kwa kasi kubwa" au 2) "miguu" ni sawa na msemo unaodokeza ya kuwa hii ni njia ambayo wamesafiri hapo awali. "kwa njia ambayo hajawahi kusafiria kabla"

Ni nani ametenda na kutimiza mambo haya?

Yahwe anatumia swali hili kusisitiza ya kwamba yeye ndiye ambaye amefanya mambo haya. "Nimefanya na kutimiza mambo haya"

Ni nani aliyeita vizazi kutoka mwanzo?

Hapa neno "vizazi" linawakiliisha wanadamu wote, ambao Yahwe aliwaumba na kuwaongoza katika historia. Swali la balagha linatarajia jibu, Yahwe. "Nimewaita vizazi vya wanadamu kutoka mwanzo"

ametenda na kutimiza

Maneno haya mawili yana maana moja na husisitiza ya kwamba Yahwe ndiye aliyefanya mambo haya.

wa kwanza, na wale wa mwisho

Maana zaweza kuwa 1) ya kuwa Yahwe alikuwepo kabla ya uumbaji na atakuwepo katika mwisho wa uumbaji au 2) ya kuwa Yahwe alikuwepo kabla ya kizazi cha kwanza ya wanadamu na atakuwepo katika kizazi cha mwisho cha wanadamu.

Isaiah 41:5

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Visiwa hivi ... mwisho wa dunia

Misemo hii inawakilisha watu ambao wanaishi maeneo hayo. "Watu ambao huishi katika vsiwa ... watu ambao huishi katika mwisho wa dunia"

Visiwa

Hii ina maana ya watu ambao huishi katika visiwa na katika nchi zinazopatikana au ng'ambo ya pili ya Bahari ya Mediteranea.

mwisho wa dunia

Sehemu katika dunia ambazo zipo mbali sana na zinazungumziwa kana kwamba ni sehemu ambapo dunia huwa mwisho. "sehemu za mbali za dunia"

vinakaribia na kuja

Hizi mbili zina maana ya kwamba watu hujikusanya pamoja. "wanakuja pamoja"

fuawe

kipande cha chuma ambacho mtu kuchonga chuma kwa nyundo

kusema juu ya kuchomelea

Hapa neno "kuchomelea" lina maana ya njia ya kukaza dhahabu kwa mbao pale ambapo watumishi humaliza kutengeneza sanamu.

Wanaikaza kwa misumari ili kwamba isianguke

Hapa "isianguke" ina maana ya sanamu ambayo walitengeneza.

Isaiah 41:8

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

wewe ambaye ninakurudisha kutoka katika mwsho wa dunia, na ambaye nilimwita kutoka sehemu za mbali

Mistari hii miwili ina maana moja na inasisitiza ya kwamba Yahwe analeta watu wa Israeli kutoka katika nch kutoka nchi za mbali.

mwisho wa dunia

Sehemu katika dunia ambazo zipo mbali sana na zinazungumziwa kana kwamba ni sehemu ambapo dunia huwa mwisho. "sehemu za mbali za dunia"

Nimekuchagua na sijakukataa

Misemo hii miwili ina maana moja. Wa pilii unaeleza katika maneno ya kukana kwa msemo wa kwanza unavyoeleza maneno ya chanya.

Isaiah 41:10

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Nitakuthibitisha kwa mkono wangu wa kuume wa haki

Yahwe kuimarisha watu wake inazungumziwa kana kwamba alikuwa akiwashikilia kwa mkono wake.

mkono wangu wa kuume wa haki

Hapa "mkono wa kuume" unawakilisha nguvu ya Yahwe. Maana zaweza kuwa 1) mkono wa kuume wa Yahwe ni wa haki yaani daima atafanya jambo sahihi. "nguvu yangu ya haki" au 2) mkono wa kuume wa Yahwe ni wa ushindi yaani atafanikiwa kwa kile anachofanya. "nguvu yangu ya ushindi"

Isaiah 41:11

Taarfa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

wataona haya na kuaibika, wote ambao walikuwa na hasira juu yako

"wote ambao walikuwa na hasira na wewe watapata haya na kuaibika"

wataona haya na kuaibika

Maneno haya mawili yana maana moja na husisitiza ukuu wa aibu yao.

watakuwa si kitu na kuangamia, wale wanaopingana na wewe

"wale ambao wanapingana na wewe watakuwa si kitu na wataangamia"

Isaiah 41:12

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Mimi ... nitashika mkono wako wa kiume

Yahwe kuwasaidia watu wa Israeli inazungumzwa kana kwamba alikuwa akishikilia mkono wao wa kulia.

Isaiah 41:14

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Yakobo wewe funza, na nyie watu wa Israeli

Hapa "Yakobo" na "watu wa Israeli" ina maana moja. "nyie watu wa Israeli ambao ni kama funza"

Yakobo wewe funza

Maana zaweza kuwa 1) ya kwamba ina maana ya mawazo ya mataifa mengine kuhusu watu wa Israeli au 2) ya kwamba hii ina maana ya mawazo ya Israeli wenyewe. Yahwe anazungumziwa umuhimu wao kana kwamba walikuwa funza.

tamko la Yahwe

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "tamko" linaelezwa kama kitenzi "tamka" au "kusema kwa dhati". "Yahwe alitamka" au "Yahwe alisema kwa dhati"

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

Ninakufanya kama chombo cha kupura yenye ncha kali ... utaifanya vilima kuwa kama makapi

Yahwe anazungumzia kuwawezesha Israeli kuwashinda adui zao kana kwamba alikuwa akifanya taifa kuwa chombo cha kupura ambayo itasawazisha milima.

chombo cha kupura yenye ncha kali

chombo cha kupura ilikuwa ubao wenye uma zenye ncha kali ambazo mtu huvuta juu ya ngano kugawanyisha nafaka kutoka na makapi.

makali pande mbili

Hii ina maana ya pande za uma ambazo ziliungwa katika chombo cha kupura. Ya kwamba walikuwa "makali pande mbili" ina maana walikuwa na makali sana.

utapura milima na kuikanyaga

Badala ya kupura nafaka, Israeli atapura milima, ambayo inawakilisha mataifa yenye nguvu ambayo yalikuwa adui wa Israeli. "utapura adui zako na kuwaponda kana kwamba walikuwa nafaka, ingawa wanaonekana kuwa kama milima imara"

utaifanya vilima kuwa kama makapi

Mstari huu una maana sawa na mstari wa nyuma lakini unawakilisha hatua inayofuata katika njia ya kupura nafaka.

Isaiah 41:16

Kauli Kiunganishi

Yahwe anaendelea kutumia sitiari ya kugawanyisha nafaka kwa makapi kufafanua jinsi Israeli atakavyoshinda adui zake.

Utawapepeta ... upepo utawatawanya

Hapa neno "utawapepeta" ina maana ya milima na vilima katika 41:14. Hii inawakilisha hatua inayofuata katika njia ya kupura nafaka, ambapo nafaka hupepetwa kuondoa makapi. Adui wa Israeli watatoweka kama makapi yanayopulizwa kwa upepo.

upepo utawabeba mbali; upepo utawatawanya

Misemo hii miwili ina maana moja. "upepo utawapuliza mbali"

Isaiah 41:17

Taarifa ya Jumla

Yahwe anazungumzia watu ambao wapo katika mahitaji makubwa kana kwamba walikuwa na kiu kubwa sana, na utoaji wake kwao kana kwamba alisababisha maji kutokeza katka maeneo ambapo kwa kawaida hayatokei.

Isaiah 41:19

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

mihadasi ... msonobari na miti ya mvinje

Hii ni aina ya miti

mkono wa Yahwe umefanya haya

Hapa neno "mkono" unawakilisha Yahwe mwenyewe. "Yahwe amefanya hivi"

Isaiah 41:21

Taarifa ya Jumla

Katika mistari hii, Yahwe anakejel watu na sanamu zao. Anazipa changamoto sanamu ziseme nini kitatokea katika siku za usoni, lakini anajua haziwezi.

Isaiah 41:23

Kauli Kiunganishi

Yahwe anaendelea kudhihaki sanamu na watu ambao huziabudu.

fanya kitu chema au kiovu

Maneno "chema" na "kiovu" huunda neno la maana moja na neno na linawakilisha kitu chochote. "fanya kitu chochote"

yule ambaye anakuchagua

Hapa "anakuchagua" ni wingi na ina maana ya sanamu. "mtu ambaye huchagua sanamu"

Isaiah 41:25

Taaarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Nimemwinua juu mmoja

Yahwe anazungumzia kumteua mtu kana kwamba alimwinua mtu huyo juu. "Nimemteua mmoja"

kutoka katika kuchomoza kwa jua

Hii ina maana ya mashariki, upande ambapo jua linachomoza. "kutoka mashariki"

yeye anayeliita jina langu

Maana zaweza kuwa 1) ya kwamba mtu huyu humwomba Yahwe kwa ajili ya mafanikio yake au 2) ya kwamba mtu huyu humwabudu Yahwe.

atawakanyaga watawala

Kushinda watawala wa mataifa mengine inazungumziwa kana kwamba likuwa kuikanyaga chini ya miguu. "atawashinda watawala hawa"

kama mfinyanzi ambaye kuknyaga juu ya udongo

Yahwe analinganisha njia ambayo mtu huyu atakanyaga watawala wengine kwa njia ambayo mfinyanzi hukanyaga juu ya udongo kuchanganya kwa maji.

Ni nani aliyetangaza hili kutoka mwanzo, ili tuweze kujua? Kabla ya muda huu, ili tuweze kusema, "Yupo sahihi"?

Yahwe anatumia maswali haya ya balagha kudhihaki sanamu amabazo watu huabudu. Jibu linalodokezwa ni 1) ya kwamba sanamu hazijafanya mambo haya na 2) ya kwamba Yahwe ndiye ambaye alifanya mambo haya. "Hakuna kati ya sanamu ametangaza hiki kutoka mwanzo, ili tuweze kujua. Na hakuna kati yao aliyetangaza hili kabla ya wakati, ili tuweze kusema, "Yupo sahihi".

"Kweli, hakuna kati ya sanamu aliagiza hivyo. Kweli, hakuna mtu aliyesikia nyie sanamu mkisema chochote"

"Kweli, hakuna kati ya sanamu alagiza hivyo. Kweli, hakuna mtu aliyesikia nyie sanamu mkisema chochote"

Isaiah 41:27

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

hakuna mmoja kati yao

"hakuna sanamu moja"

viumbe vyao vya chuma vilivyochongwa ni upepo na utupu

Yahwe anazungumzia kutokuwa na thamani kwa sanamu kana kwamba sanamu ni upepo na si kitu kabisa. "sanamu zao hazina thamani"

Isaiah 42

Isaiah 42:1

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

Tazama, mtumishi wangu

"Tazama, mtumishi wangu" au "Mtumishi wangu huyu hapa"

ndani yake ninafurahi

"ambaye ninayo furaha naye"

Isaiah 42:3

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Tete lililopondwa hataivunja, na utambi unowaka kwa chini hatauzima

Yahwe anazungumzia watu dhaifu na wasiojiweza kana kwamba walipondwa kama matete na kuwaka kwa chini kama utambi.

Tete lililopondwa

Tete ni shina la mmea refu na jembamba kama nyasi ndefu. Kama likipondwa, haliwezi kubeba uzito wowote.

hataivunja

"Mtumishi wangu hatavunja"

nchi za pwani

Hii ina maana ya watu ambao huishi katika visiwa na katika nchi zenye mipaka au ng'ambo ya pili ya Mediteranea. "watu ambao wanaishi katika nchi za pwani"

Isaiah 42:5

yule aliyeziumba mbingu na kzitandaza, yule ambaye alitengeneza dunia

Nabii anazungumzia Yahwe kuziumba mbingu na dunia kana kwamba mbingu na dunia ilikuwa akitambaa ambacho Yahwe alizitandaza.

hutoa pumzi kwa watu juu yake na uzima kwa wale wanaoishi ndani yake

Misemo hii ina maana moja na inasisitiza ya kwamba Yahwe hutoa uhai kwa kila mtu. Neno "pumzi" ni neno kwa ajili ya uhai. "hutoa uhai kwa watu ambao wanaishi juu ya dunia"

nimekuita

Hapa "nimekuita" ni umoja na ina maana ya mtumishi wa Yahwe.

Nita ... kukutenda kama agano kwa ajili ya watu

Hapa neno "agano" ni neno kwa ajili ya yule anayeimarisha au patanisha agano. "Nita ... kukufanya kuwa mpatanishi wa agano kwa watu"

nuru kwa Mataifa

Yahwe anazungumzia kumfanya mtumishi wake yule ambaye atakomboa mataifa kutoka kifungoni kana kwamba alikuwa akimfanya nuru ambayo hung'aa katika maeneo ya giza kwa Mataifa.

Isaiah 42:7

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kufafanua kile mtumishi wake atafanya.

kufungua macho ya vipofu

Kusababisha watu vipofu kuona inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kufungua macho yao. Pia, Yahwe anazungumzia mtumishi wake kuwaokoa wale ambao wamefungwa kimakosa kana kwamba mtumishi wke alikuwa akirejesha kuona kwa watu vipofu. "kuwezesha vipofu kuona"

kuwaacha huru wafungwa kutoka gerezani, na kutoka nyumba ya ulinzi mkali kwa wale wanaokaa gizani

Misemo hii miwili ina maana moja. Kitenzi kinaweza kutumka katika msemo wa pili. "kuwaacha huru wafungwa kutoka gerezani, na kuwaacha huru wale wanaokaa gizani kutoka nyumba ambayo wameshikiliwa"

Isaiah 42:8

wala sifa yangu pamoja na sanamu za kuchongwa

Kitenzi kinaweza kutumika kutoka msemo wa nyuma. "wala sitagawana sifa yangu na sanamu za kuchonga"

sifa yangu

Hii ina maana ya sifa ambayo Yahwe hupokea kutoka kwa watu.

nitakueleza

Hapa "nitakueleza" ni wingi na ina maana ya watu wa Israeli.

Isaiah 42:10

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

bahari, na vyote vilivyomo, nchi za pwani, na wale wanaoishi pale

"na viumbe wote ambao huishi katika bahari, na wale wote wanaoishi katika nchi za pwani"

Acha jangwa na miji ipaze sauti

Hii ina maana ya watu wanaoishi katika jangwa na miji.

Kedari

Hili ni eneo kule Uarabuni. Kedari inawakilisha idadi ya watu wa Kedari. "ya watu wa Kedari"

Sela

wakazi wa Sela - Sela ni mji wa Edomu.

Isaiah 42:12

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Waache watoe utukufu

Hapa "waache" ina maana ya watu katika nchi za pwani.

Yahwe atatoka nje kama hodari; kama mwanamume wa vita

Yahwe analinganishwa na hodari ambaye yupo tayari kuwashinda watu wa adui zake.

atamwamsha ari yake

Hapa "ari" ina maana ya uchu ambao hodari hupitia anapokaribia kupigana vita. Yahwe kuchangamsha ari yake inazungumziwa kana kwamba aliamsha kama upepo unapoamsha mawimbi ya maji.

Isaiah 42:14

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Nimekaa kimya kwa muda mrefu; Nilikuwa nimetulia n kujizuia

Mistari hii miwili inagawana maana ya kufanana. Kutulia kwa Yahwe kunafafanuliwa kama ukimya na utulivi.

Nilikuwa nimetulia n kujizuia

Misemo hii miwili inagawana jambo moja na hudokeza ya kwamba Yahwe amejizuia kutotenda. "Nimejizuia kutofanya chochote"

Nitalia kama mwanamke katika uchungu; nitahema na kutweta

Utulivu wa Yahwe kama hodari anayepaza sauti inalinganishwa na mwanamke mwenye mimba anayelia kwa maumivu ya uchungu. Hii inasisitiza tendo la ghafla lisilozuilika baada ya kipindi cha utulivu.

Nitafanya milima kuwa takataka ... Nitakausha mabwawa

Yahwe anatumia lugha hii ya kisitiari kufafanua nguvu yake kubwa kushinda adui zake.

mabwawa

Bwawa ni eneo laini, lililo tepe tepe lenye madimbwi ya maji

Isaiah 42:16

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Nitawaleta vipofu kwa njia ambayo hawajui; katika njia ambayo hawaijui nitawaongoza

Misemo hii miwili ina maana moja. "Nitawaongoza vipofu katika njia ambayo hawajui"

vipofu

Yahwe anazungumzia watu wake kutojiweza kana kwamba hawawezi kuona kwa sababu walikuwa vipofu.

ambayo hawaijui

Maana zaweza kuwa 1) "ya kwamba hawajawahi kusafiri" au 2) "ambayo hawana uzoefu nao"

Nitageuza giza kuwa nurur mbele yao

Yahwe anazungumzia watu wake kutojiweza kana kwamba hawakweza kuona kwa sababu walitembea gizani, na kusaidia kwake kana kwamba alisababisha mwanga kung'ara katika giza.

Isaiah 42:17

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

Watageuzwa; watafedheheshwa kabisa

Kuwakataa wale ambao huabudu sanamu inazungumziwa kana kwamba ni kuwalazimisha kugeuka na kuelekea upande mwingine. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nitawakataa na kuwatia aibu"

Isaiah 42:18

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

wewe kiziwi ... wewe kipofu

Hapa "wewe" ni wingi na ina maana ya watu wa Israeli. Yahwe anazungumzia kushindwa kwao kumsikliza na kumtii kana kwamba walikuwa viziwi na vipofu.

Ni nani aliye kipofu ila mtumishi wangu? Au kiziwi kama mjumbe wangu nayemtuma?

Yahwe anauliza maswali haya ya balagha kukaripia watu wake na kusisitiza ya kwamba hakuna mtu aliye kipofu au kiziwi kama walivyo. "Hakuna mtu aliye kipofu kama mtumishi wangu. Hakuna mtu aliye kiziwi kama mjumbe wangu ambaye namtuma"

Ni nani aliye kipofu kama mwenzangu wa agano, au kipofu kama mtumishi wa Yahwe?

Yahwe anauliza maswali haya ya balagha kukaripia watu wake na kusisitiza ya kwamba hakuna mtu aliye kipofu au kiziwi kama walivyo. "Hakuna aliye kipofu kama mwenzangu wa agano. Hakuna aliye kipofu kama mtumishi wa Yahwe".

Isaiah 42:20

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza wtu wa Israeli.

Unaona mambo mengi, lakini hauelewi

"Ingawa unaona mambo mengi, hauelewi kile wanachomaanisha"

masikio yapo wazi, lakini hakuna anayesikia

Uwezo wa kusikia inazungumziwa kana kwamba masikio yalikuwa wazi. Hapa neno "kusikia" ina maana ya kuelewa kile mtu anachosikia. "watu husikia, lakini hakuna mtu anayeelewa kile wanachosikia".

Ilimpendeza Yahwe kusifu haki yake na kufanya sheria yake kutukuka

"Yahwe alifurahishwa kuinua haki yake kwa kufanya sheria zake kutukuka". Sehemu ya pili ya msemo huu unafafanu jinsi Yahwe ametimiza sehemu ya kwanza.

Isaiah 42:22

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Lakini hawa ni watu walionyanganywa na kuporwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Lakini adui amenyanganya na kupora watu hawa"

walionyanganywa na kuporwa

Maneno haya mawili yana maana moja na husisitiza jinsi adui alivyowapora sana.

wote wametegwa ndani ya mashimo, kushikwa mateka ndani ya magereza

Misemo hii miwili ina maana moja. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "adui amewatega wote katika mashimo na kuwashika mateka katika magereza"

Isaiah 42:23

Taarifa ya Jumla

Hapa Isaya anaanza kuzungumza

Nani kati yenu

Hapa "yenu" ni wingi na ina maana watu wa Israeli.

Ni nani alimpatia Yakobo kwa mnyanganyi, na Israeli kwa waporaji?

Misemo hii miwili ina maana ya jambo moja. Isaya anatuma hii kama swali la kuongoza ili kusisitiza jibu ambalo atalitoa katika msemo unaofuata. "Nitakuambia ni nani aliwapa watu wa Israeli kwa wanyanganyi na waporaji"

Je! haikuwa Yahwe ... walikataa kutii?

Isaya anatumia swali hili la balagha kusisitiza ya kwamba Yahwe pekee alikuwa anawajibika kwa hali ya Israeli, na kufafanua sababu ambayo Yahwe alifanya vile. "Hakika alikuwa Yahwe ... walikataa kutii".

ambaye tumetenda dhambi dhidi yake

Hapa neno "tumetenda" ina maana ya watu wa Israeli na Isaya.

ambazo katika njia zake walikataa kutembea, na katika sheria yake walikataa kutii

Neno "walikataa" pia ina maana ya watu wa Israeli na Isaya. Misemo miwili ina maana moja. Katika ya kwanza, kutii sheria za Yahwe inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kutembea katika njia ambayo Yahwe aliamuru kutembea.

Isaiah 42:25

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza

Kwa hiyo ali

"Kwa hiyo Yahwe"

alimwaga ghadhabu yake kali dhidi yao

Isaya anazungumzia ghadhabu ya Yahwe kana kwamba ilikuwa kimiminikio ambacho kinaweza kumwagwa nje. "alionyesha ghadhabu yake kali kuwaelekea wao"

dhidi yao

"dhidi yetu". Hapa "yao" ina maana ya watu wa Israelii, lakini Isaya bado anajumlisha mwenyewe kama sehemu ya watu.

kwa uharibifu wa vita

Neno "uharibifu" linaweza kutafsiriwa kwa kitenzi. "kwa kuwaharibu wao kwa vita"

Uliwaka kuwazunguka ... ukawaunguza

Isaya anazungumzia ghadhabu kali ya Yahwe kana kwamba ilikuwa moto ambao uliwachoma watu.

hawakuliweka moyoni

Kuzingatia kwa makini kwa jambo na kujifunza kwake inazungumziwa kana kwamba walikuwa wakiweka jambo hilo juu ya moyo wa mtu. "hawakuzingatia kwa makini" au "hawakujifunza kutoka kwake"

Isaiah 43

Isaiah 43:1

yeye aliyekuumba wewe, Yakobo, na yeye aliyekutengeneza wewe, Israeli

Vishazi hivi vyote viwili vina maana moja. "yule ambaye amekuumba, Ee watu wa Israeli"

Isaiah 43:2

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Utakapopita katikati ya maji ... miale haitakuangamiza

Yahwe anazungumza kuteseka na kupitia ugumu kana kwamba ni maji marefu na moto ambayo watu hutembea. Maneno "maji" na "miale" huunda neno lenye maana ya mambo mengi na husisitza hali yoyote ngumu.

Utakapopita katikati ya maji, nitakuwa pamoja nawe; na katikati ya maji, hayatakushinda

Kauli hizi mbili zina maana moja na husisitiza y kwamba watu hawatapitia madhara kwa sababu Yahwe yupo pamoja nao.

hautachomwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "haitakuchoma"

Nimewapatia Msri kama fidia yako, Kushi na Seba kubadilishana kwa ajili yako

Misemo hii miwili inatumia maana moja na inasisitiza ya kwamba Yahwe ataruhusu adui wa Israeli kushinda mataifa haya badala ya Israeli.

Seba

Hili ni jina la taifa.

Isaiah 43:4

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Kwa maana una thamani na wa kipekee machoni mwangu

Maneno "thamani" na "kipekee" yana maana moja na yanasisitiza jinsi gani Yahwe huthamini watu wake. "Kwa sababu wewe ni wa thamani kwangu"

kwa hiyo nitawapa watu kwa kubadilishana kwa ajili yako, na watu wengine kwa kubadilishana kwa maisha yako

Misemo yote ina maana moja. "kwa hiyo nitaruhusu adui kuwashinda watu wengine badala yako"

Nitaleta watoto wako kutoka mashariki, kukukusanya kutoka magharibi

Pande "mashariki" na "magharibi" huunda neno lenye maana ya kundi na linawakilisha kila upande. "Nitakuleta wewe na wtoto wako kutoka kila upande"

Isaiah 43:6

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

nitasema kwa kaskazini ... kwa kusini

Yahwe anazungumza kwa "kaskazini" na "kwa kusini" kana kwamba anaamuru mataifa katka maeneo hayo.

wana wangu ... binti zangu

Yahwe anazungumzia wtu ambao wanakuwa wake kana kwamba walikuwa watoto wake.

kila mtu ambaye ameitwa kwa jina langu

Hapa kuitwa kwa jina la mtu inawakilisha kuwa mali ya mtu huyo. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kila mtu ambaye nimemuita kwa jina langu" au "kila mtu ambaye ni mali yangu"

ambaye nimemuumba, ndio, ambaye nimemtengeneza

Zote hizi zina maana moja na husisitiza ya kwamba ni Mungu ambaye aliwatengeneza watu wa Israeli.

Isaiah 43:8

watu ambao ni vipofu ... viziwi

Yahwe anazungumzia wale ambao hawamsikilizi au kumtii kana kwamba walikuwa vipofu na viziwi.

Ni nani kati yao angeweza kutamka hili na kutangaza kwetu matukio ya mapema?

Swali hili la balagha linatumika kwa miungu ambao watu wa mataifa huabudu. Jibu linalodokezwa ni kwamba hakuna kati yao angefanya hivi. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hakuna kati ya miungu yao ingeweza kutamka hili au kutangaza kwetu matukio ya mapema"

kutangaza kwetu matukio ya mapema

Msemo huu una maana ya uwezo wao kusema juu ya matukio ambayo yametokea kipindi cha nyuma kabla hayatokea. "alitangaza kwetu matukio ya mapema kabla hayajatokea"

Waache walete mashahidi wao kujithibitishia wenyewe kuwa sahihi, waache wasikilize na kukiri, "Ni ukweli'.

Yahwe anatoa changamoto kwa miungu ambao mataifa huabudu kutoa mashahidi ambao watashuhudia ya kwamba wameweza kufanya vitu hivi, ingawa anajua ya kwamba hawawezi kufanya hivyo. "Miungu hawa hawana mashahidi ambao watathibitisha kuwa sahihi, mashahidi ambao watasikiliza na kukiri, "Ni kweli"

Isaiah 43:10

Nyie ... mtumishi wangu

Hapa "nyie" ni wingi na ina maana ya watu wa Israeli. Msemo "mtumishi wangu" ina maana ya taifa, kwa ukamilifu.

Kabla yangu ... baada yangu

Kwa kuzungumza kwa njia hii, Yahwe hasemi ya kwamba kulikuwa na muda ambapo hakuwepo au kipindi ambacho hatakuwepo. Anasema ya kwamba yeye ni wa milele na kwamba miungu ambayo watu wa mataifa mengine huabudu hawako hivyo.

Kabla yangu hapakuwa na miungu aliyeumbwa

Hapa neno "kumba" inaonyesha ya kwamba Yahwe anazungumzia sanamu ambazo watu waliumba. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Hakuna kati ya miungu ambao watu walitengeneza walikuwepo kabla yangu"

na hapatakuwa naye baada yangu

"na hakuna kati ya miungu hao atakuwepo baada yangu"

Mimi, mimi ni Yahwe

Neno "Mimi" inarudiwa kusisitiza lengo kwa Yahwe. "Mimi pekee ni Yahwe" au "Mimi mwenyewe ni Yahwe"

hakun mkombozi ila mimi

Hii inaweza kuelezwa kwa chanya. "Mimi ni mkombozi pekee" au "Mimi ndiye pekee mbaye naweza kukuokoa"

Isaiah 43:12

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

hakuna atakayeweza kuokoa yeyote kutoka mkononi mwangu

Hapa neno "mkono" linawakilisha nguvu ya Yahwe. "hakuna mtu anaweza kuokoa yeyote kutoka kwa nguvu yangu"

nani anawvza kugeuza?

Yahwe anatumia swali hili kusema ya kwamba hakuna mtu anaweza kugeuza mkono wake. Inaweza kutafsiriwa kam kauli. Kugeuza mkono wake inawakilisha kumzuia kutofanya kitu. "hakuna ambaye ataigeuza" au "hakuna mtu anaweza kunizuia"

Isaiah 43:14

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

Nimetuma Babeli na kuwaongoza wote chini

Kitu cha kitenzi "tuma" kinaweza kutumika katika tafsiri. "Ninatuma jeshi Babeli"

kuwaongoza wote chinii kama wakimbizi

"ongoza Wababeli wote chini kama wakimbizi"

wakimbizi

Mkimbizi ni mtu ambaye hukimbia mbali ili adui yake asiweze kumkamata.

Isaiah 43:16

ambaye alifungua njia ... kama utambi unaowaka

Katika mistari hii, Isaya anazungumzia matukio yanayofuata safari kutoka Misri, Yahwe alipogawanya bahari kuruhusu Waisraeli kutembea katikati juu ya nchi kavu lakini kisha kuzamisiha jeshi la Wamisri. Maana kamili ya kauli inaweza kuwekwa wazi.

Walianguka chini pamoja; hawatainuka tena

Kufa inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kuanguka chini ardhini. "Wote walikufa pamoja; hawataishi tena"

wamezimwa, wamepozwa kama utambi unaowaka

Watu kufa inazungumziwa kana kwamba walikuwa wakichoma mshumaa wa utambi ambayo mtu ameuzima. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "maisha yao yamekwisha, kama mtu anavyozima mwale wa mshumaa unaowaka"

Isaiah 43:18

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Usiwaze juu ya vitu hivi vya awali, wala kufikiria vitu vya zamani sana

Misemo hii miwili ina maana moja na kusisitiza ya kwamba hawapaswi kuwa na wasiwasii juu ya kilichotokea kipindi cha nyuma.

Tazama

Hii ni lahaja. "Sikiliza" au "Zingatia kwa makini"

je! hauielewi?

Yahwe anatumia swali kufundisha watu wa Israeli. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "hakika umeigundua"

Isaiah 43:20

wanyama pori wa mashamba wataniinua mimi, mbweha na mbuni

Hapa wanyama wanamheshimu Yahwe kana kwamba walikuwa watu.

mbweha na mbuni

Hawa ni mifano ya aina ya wanyama ambao watamheshimu Yahwe. "mbweha na mbuni wataniheshimu"

Isaiah 43:22

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Isaiah 43:24

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

ufito wa mwanzi wenye manukato

ufito wa mwanzi wenye manukato Huu ni mmea wenye harufu nzuri inayotumika kutengeneza mafuta ya kupaka. Haikuota katika nchii ya Israeli kwa hiyo watu walitakiwa kuinunua kutoka mataifa mengine.

umenibebesha mzigo na dhambi zako, umenichosha na matendo yako maovu

Zote hizi zina maana moja na husisitiza malalamiko ambayo Yahwe anayo kwa watu wake.

umenibebesha mzigo na dhambi zako

"umenihangaisha na dhambi zako"

Isaiah 43:25

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Mimi, ndio, mimi

Neno "Mimi" linarudiwa kwa ajili ya msisitizo. "Mimi pekee"

anayefuta makosa yako

Kusamehe dhambi inazungumziwa kama kuwa aidha 1) kuziondoa au kuzipangusa mbali au 2) kufuta kumbukumbu iliyoandkwa ya dhambi. "ambaye husamehe makosa yako kama mtu anayepangusa kitu mbali" au "ambaye husamehe makosa yako kama mtu ambaye hufuta kumbukumbu ya dhambi"

kwa ajili yako

"kwa ajili ya heshima yangu" au "kwa ajili ya sifa yangu"

sitaweka akilini

"kumbuka"

wasilisha kesi yako, ili uweze kuthibitishwa hauna hatia

Yahwe anawapa changamoto watu kutoa ushahidi ya kwamba hawana hatia kwa mashtaka ambayo ameleta dhidi yao, ingawa anajua hawawezi kufanya hivyo. "wasilish kesi yako, lakini huwezi kuthibitisha kuwa hauna hatia"

ili uweze kuthibitishwa hauna hatia

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ili uweze kuthibitisha mwenyewe kuwa huna hatia"

Isaiah 43:27

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Baba yako wa kwanza alitenda dhambi

Hii ina maana ya mwanzilish wa Israeli na inaweza kuwakilisha aidha Abrahamu au Yakobo.

Nitamweka Yakobo katika uharibifu kamili

Hapa "nitamweka" inawakilisha kumweka mtu chini ya nguvu ya mwingine. Nomino ya "uharibifu" inaweza kutafsiriwa kwa msemo wa kitenzi. "Nitasababisha adui kumuangamzia Yakobo kabisa"

Israeli katiika aibu ya shutumu

Kitenzi kinaweza kutumika kutoka msemo wa nyuma, ambayo msemo huu ni sambamba. Nomino "aibu" inaweza kutafsiriwa na msemo wa kitenzi. "Nitaruhusu adui kutukana na kudhalilisha Israeli"

Isaiah 44

Isaiah 44:1

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Yakobo mtumwa wangu

Hii ina maana ya uzao wa Yakobo. "vizazi vya Yakobo, watumishi wangu"

yeye aliyekutengeneza na kukuumba ndani ya tumbo

Yahwe anazungumzia kuumba taifa la Israeli kana kwamba alikuwa akiumba taifa kama mtoto katika tumbo lake. "yeye aliyekutengeneza, kama navyoumba mtoto ndani ya tumbo"

na wewe, Yeshuruni, ambaye nimekuchagua

Kitenzii kinaweza kutumika kutoka kwa msemo uliopita. "na wewe, Yeshuruni, ambaye nimekuchagua, usiogope"

Yeshuruni

Hii pia ina maana ya watu wa Israeli.

Isaiah 44:3

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Nitamwaga maji katika ardhi yenye kiu, na vijito vinavyotiririka juu ya ardhi kavu

Yahwe anazungumza kutoa Roho wake kwa wtu wa Israeli kana kwamba alikuwa akisababisha mvua kuanguka na vjito kutiririka juu ya ardhi kavu.

ardhi yenye kiu

Ardhi kavu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa mtu mwenye wivu. "ardhi kavu"

nitamwaga Roho wangu juu ya watoto wako

Yahwe anazungumza kumtoa Roho wake kwa watu kana kwmba Roho wake alikuwa kimiminiko ambacho alimwaga juu yao. "Nitatoa Roho wangu kwa watoto wao"

na baraka yangu juu ya wtoto wako

Kitenzi kinaweza kutolewa kutoka katika msemo wa nyuma. "na nitamwaga baraka yangu juu ya watoto wako" au "na nitatoa baraka yangu kwa watoto wangu"

Watachipuka juu katika nyasi, kama mierebi kando na vijito vya maji

Watu wa Israeli kuwa na mafanikio na kuongezeka inazungumziwa kana kwamba walikuwa mimea ambayo huota kwa sababu wana majii mengi.

mierebi

Muerebi ni mti wenye matawi membamba ambayo huota kaaribu na maji.

Isaiah 44:5

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

mwingine ataita jina la Yakobo

"mtu mwingine atasema kuwa yeye ni uzao wa Yakobo"

kujiita mwenyewe kwa jina la Israeli

"kujita mwenyewe uzao wa Israeli"

Isaiah 44:6

Mkombozi wake

"Mkombozi wa Israeli"

Yahwe of majeshi

Yahwe of majeshi wa Israeli

Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho

Msemo huu unasisitiza asili ya Yahwe ya milele. Maana zaweza kuwa 1) "Mimi ndiye ambaye nilianzisha vitu vyote, na mimi ndiye ambaye humaliza vitu vyote" au 2) "Mimi ndiye yule ambaye niliishi daima, na mimi ndiye yule ambaye nitaishi daima"

Isaiah 44:7

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

Nani kama mimi? Na atangaze

Yahwe anatumia swali hili la balagha kusisitiza ya kwamba hakuna mtu kama yeye. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "kama yeyote anafikiri ni kama mimi, na atangaze"

Isaiah 44:8

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Usiwe na hofu au kuogopa

Yahwe anatumia misemo miwili ya kufanana ili kuimarisha faraja yake. "Usiogope"

Je! sijatamka kwako zamani, na kuitangaza?

Yahwe anatumia swali hili kusisitiza ya kwamba yeye ndiye ambaye alitabiri matukio ambayo yametokea sasa. Hii inaweza kutafsiriwa kama kauli. Neno "kutangaza" lina maana ya kitu kimoja kama "kutangaza". "Nimetangaza mambo haya kwako zamani"

Je! kuna Mungu yeyote kando ya mimi?

Yahwe anatumia swali tena kusisitiza ya kwamba hakuna Mungu mwingine. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hakuna Mungu kando ya mimi"

Hakuna Mwamba mwingine

Yahwe anajizungumzia kana kwamba alikuwa jiwe kubwa ambayo chini yake wtu wanaweza kupata hifadhi. Hii ina maana ya nguvu kulinda watu wake.

Isaiah 44:9

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

vitu wanavyofurahia navyo havina thamani

"sanamu wanazozifurahia hazina thamani"

mashahidi wao hawawezii kuona au kujua chochote

Msemo huu una maana ya wale ambao huabudu sanamu hawa na kudai kuwa mashahidi wa nguvu ya sanamu. Yahwe anazungumzia ukosefu wa uwezo wao kuelewa ukweli kana kwamba walikuwa vipofu. "wale ambao hutumika kama mashahidi kwa ajili ya sanamu hizi ni kama watu vipofu ambao hawajui chochote"

wataaibishwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wataaibika" au "sanamu zao zitaaibishwa"

Nan angeweza kuunda mungu au kuchonga sanamu ambayo haina thamani?

Yahwe anatumia swali hili kukemea wale ambao hutengeneza sanamu. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Ni wapumbavu pekee wanaweza kuunda mungu au kuchonga sanamu ambayo haina thamani"

kuchonga sanamu ambayo haina thamani

Neno "haina thamani" haitofautishi kutofaa kwa sanamu kwa sanamu ambazo zina thamani, kwa sababu sanamu zote hazina thamani. "kuchonga sanamu ambazo hazina thamani"

Isaiah 44:11

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

washiriki wake wote

Maana zaweza kuwa 1) hii ina maana kuwa washiriki wa fundistadii ambaye hutengeneza sanamu. "washiriki wote wa fundistadi" au 2) hii ina maana ya wale washiriki wenyewe pamoja na sanamu kwa kuiabudu. "wale wote ambao huabudu sanamu"

wataaibishwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ataaibika"

Acha wachukue msimamo wo pamoja

"Waache wote waje pamoja mbele zangu"

wataogopa

"watogopa". "kuogopa" ni kuinama mbele kwa hofu.

Isaiah 44:12

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

kuiunda

"kuunda sanamu" au "kutengeneza sanamu"

Isaiah 44:13

kwa kamba

Kamba iliyotumika kuchora mstari umbo la sanamu katika mbao.

sindano ya santuri

Hiki ni chombo chenye ncha kali kukwaruza mbao ili fundistadi aweze kuona wapi pa kukata.

bikari

Hiki ni chombo chenye ncha sehemu mbili ambacho hutandazwa kusaidia kuweka alama katika mbao kutengeneza sanamu.

Isaiah 44:14

Hukata chini

"Fundi seremala hukata chini" au "mchonga mbao hukata chini"

mvinje

mti mrefu wa majani ya kijani

Isaiah 44:15

Kisha mtu huitumia

"Mwanamume hutumia mbao"

hutengeneza sanamu na kuinama chini kwake

Sehemu hii ya sentensi kimsingi inasema jambo moja kama ya kwanza kusisitiza.

Isaiah 44:18

kwa maana macho yao ni vipofu na hayawezi kuona

Yahwe anazungumzia watu ambao hawawezi kuelewa upumbavu wa kuabudu sanamu kana kwamba walikuwa vipofu.

kwa maana macho yao ni vipofu

Hapa "macho yao" yanawakiilisha mtu mzima. "kwa maana ni vipofu"

mioyo yao haiwezi kutambua

Hapa neno "mioyo" inawakilisha akili na mawazo ya watu. "hawawezi kuelewa"

Isaiah 44:19

Sasa naweza kutengeneza ... kitu cha kuchukiza cha kuabudu? Je! nitainama chini kwa kipande cha mbao?

Yahwe anasema ya kwamba watu hawa wanatakiwa kujiuliza maswali haya ya balagha. Maswali yanatazamia majibu ya kukana na kusisitiza jinsi itakavyokuwa upumbavu kwa mtu kufanya mambo haya. Maswali haya yanaweza kutafsiriwa kama kauli. "Sitakiwi sasa kutengeneza ... kitu cha kuchukiza cha kuabudu. Sitakiwi kuinama chini kwa kipande cha mbao"

Isaiah 44:20

Ni kana kwamba alikuwa akila majivu

Yahwe anazungumzia mtu kuabudu sanamu kana kwamba mtu huyo alikuwa akila majivu yaliiyochomwa ya mbao kutoka pale alipotengenezea sanamu. Kama vile kula majivu haimpi mtu faida, wala kuabudu sanamu.

moyo wake uliodanganywa humpotosha

Moyo unawakilisha undani wa mtu. "anajipotosha kwa sababu amedanganywa"

Hawezi kujiokoa mwenyewe

"Mtu ambaye huabudu sanamu hawezi kujiokoa mwenyewe"

Isaiah 44:21

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

Yakobo, na Israeli

Hii ina maana ya watu waliotokana kwa Yakobo, Israeli. "nyie uzao wa Israeli"

hautasahaulika na mimi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Sitakusahau"

Nimefuta, kama wingu zito, matendo yako ya uasi, na kama wingu, dhambi zako

Kauli hizi mbili zina maana ya kitu kimoja. Mungu ameondoa dhambi zao kwa haraka na urahisi kama upepo uweze kupuliza mbali wingu.

na kama wingu, dhambi zako

Kitenzi kinaweza kutumika kutoka na msemo uliopita. "na kama wingu, nimefuta dhambi zako"

Isaiah 44:23

Imbeni, enyi mbingu ... utukufu wake katika Israeli

Hapa Isaya anazungumzia sehemu mbalimbali za uumbaji kana kwamba walikuwa watu na kuwaamuru kumsifu Yahwe.

enyi vina virefu vya dunia

"enyi sehemu za chini za dunia". Maana zaweza kwa 1) ya kwamba hii ina maana ya sehemu zenye vina virefu sana katika dunia kama vile mapango au makorongo na kuunda neno linalowakilisha kundi la maneno kama "mbingu" katika msemo uliopita au 2) ya kwamba hii ina maana ya sehemu ya wafu.

Isaiah 44:24

Mkombozi

Mkombozi wa Israeli

yeye aliyekuumba katika tumbo

Yahwe anazungumzia kuumba taifa la Israeli kana kwamba ilikuwa kuunda taifa kama mtoto katika tumbo la mama yake. "yeye aliyekuumba, kama navyouumba mtoto katika tumbo"

ambaye yeye peke yake alitandaza mbingu

Yahwe anazungumzia kuumba mbingu kana kwamba ilikuwa nguo ambayo ilitandazwa.

ishara

Hizi ni ishara ambazo watu walitumia kujaribu kutabiri siku za usoni.

waongea watupu

Hii ina maana ya watu ambao husema vitu ambavyo havina maana.

Isaiah 44:26

nani alithibitisha maneno ya mtumishi wake na kuyafanya kutendeka utabiri wa wajumbe wake

Yahwe anasema jambo moja mara mbili kusisitiza ya kwamba ni yeye pekee, Yahwe, ambaye husababisha unabii kutimia.

maneno ya mtumishi wake ... utabiri wa wajumbe wao

Nomino dhahania "maneno" na "utabiri" inaweza kutafsiriwa kama vitenzi. "kile mtumishi wake atakavyotamka ... kile wajumbe wake wanachotangaza"

Atafanyiwa makazi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wataishi pale tena"

Itajengwa tena

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wataijenga tena"

Nitainua uharibifu wao

Msemo "uharibifua" ina maana ya sehemu ambazo zimeangamizwa. Yahwe anazungumza kuijenga tena kana kwamba alikuwa akiinua. "Nitajenga tena kile wengine walichoangamiza"

Isaiah 44:28

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

Yeye ni mchungaji wangu

Yahwe anazungumzia Koreshi kutawala na kulinda watu wa Israeli kana kwamba Koreshi ni mchungaji wao.

Acha ijengwe tena

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. 'Acha watu wajenge tena mji"

Acha msingi wako ulazwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Acha watu walaze misingi yake"

Isaiah 45

Isaiah 45:1

ambao mkono wake naushikilia

Yahwe kuwasaidia Koreshi na kumsababishia kufanikiwa inazungumziwa kana kwamba alikuwa akishikilia mkono wake wa kuume.

Isaiah 45:2

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na Kosheri.

na kusawazisha milima

Yahwe anazungumza kuondoa vizuizi ambavyo vinaweza kukawiza mafanikio ya Koreshi kana kwamba ilikuwa kusawazisha milima mbele yake.

milima

Neno la Kiebrania linalotumika katika maandishi ni adimu na maana haileweki. Baadhi ya tafsiri zina "sehemu za kukwaruzakwaruza" au "sehemu zilizopinda".

nguzo zao za chuma

Hii ina maana ya nguzo za chuma katika malango ya shaba.

hazina za giza

Hapa "giza" ina maana ya sehemu ambazo ni za siri. "hazina katika sehemu za giza" au "hazina katika sehemu za siri"

Isaiah 45:4

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na Koreshi.

Yakobo ... Israeli

Zote hizi zina maana ya vizazi vya Israeli.

Nitakuandaa kwa ajili ya vita

Maana zaweza kuwa 1) "Nitakuimarisha kwa ajili ya vita" au 2) "Nitakuandaa kwa ajili ya vita"

kutoka katika kuchomoza kwa jua, na kutoka magharibi

Kwa kuwa jua huzama mashariki, msemo huu unaunda neno kwa ajili ya maneno mengine na ina maana ya kila sehemu juu ya dunia. "kutoka kila sehemu duniani"

Isaiah 45:7

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Ninaunda nuru na kuumba giza; Ninaleta amani na kuumba maafa

Misemo hii miwili inaunda neno kwa ajili ya maneno mengine ambayo inasisitiza ya kwamba Yahwe ni muumba wa enzi wa kila kitu.

Enyi mbingu, nyesha chini kutoka juu ... haki huruka juu pamoja nayo

Yahwe anazungumzia haki yake kana kwamba ilikuwa mvua ambayo huanguka juu ya ardhi, na ya haki yake na wokovu kama mimea ambayo huota juu ya dunia.

Enyi mbingu

Yahwe kwa muda anageuza akili yake kutoka kwa watu wake na kuanza kuzungumza kwa mbingu.

Isaiah 45:9

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

chungu kingine cha duniani kati ya vyungu vya duniani katika ardhi

Yahwe anazungumza juu yake kana kwamba alikuwa mfinyanzi, na kwa yule ambaye angebishana naye kana kwamba mtu huyo na binadamu waliosalia waliikuwa vyungu vya udongo. "kama kipande kimoja cha ufinyanzi katika vipande vingi vingine vya ufinyanzi vilivyosambaa juu ya ardhi"

chungu cha dunia

Maana zaweza kuwa 1) "chungu cha udongo" au 2) "kipande kilichovunjika cha ufinyanzi wa udongo".

Je! udongo husem kwa mfinyanzi ... juu yake'?

Yahwe anauliza swali hili kukarpia wle ambao hubishana naye juu ya kile anachofanya. "Udongo haupaswi kusema kwa mfinyanzi ... juu yake!"

Isaiah 45:10

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kukaripia wale ambao hubishana na yeye kuhusu kile anachofanya.

Ole wake asemaye kwa baba, ... 'Unazaa kitu gani?'

Yahwe anazungumzia wale ambao wangebishana naye kana kwamba walikuwa watoto ambao hawajazaliwa ambao hubishana na wazazi wao wenyewe.

Unalea kitu gani? .... Unazaa kitu gani?

Mtoto ambaye hajazaliiwa anauliza maswali haya ya balagha kukaripia wazazi wake kwa kumzaa. Hii naweza kutafsiriwa kama kauli. "Hautakiwi kuwa baba yangu ... Hautakiwi kunizaa mimi" au "Haunileii kwa usahihi ... Haunizai kwa usahihi".

Isaiah 45:11

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

Kwa nini unauliza maswali kuhusu kile nitakachofanya kwa ajili ya watoto wangu? Je! utaniambia nini cha kufanya kuhusu kazi ya mikono yangu?

Yahwe anatumia maswali kukaripia wale ambao wanabishana naye kuhusu kile anachofanya. "Usiniulize mimi kuhusu kile ninachofanya kwa ajili ya watoto wangu. Usiniambie ... mikono yangu".

watoto wangu

Hii ina maana ya watu wa Israeli.

kazi ya mikono yangu

Hapa neno "mikono" linawakilisha Yahwe. "vitu ambavyo nimevitengeneza"

Isaiah 45:12

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Ilikuwa mkononi mwangu ya kwamba

Hapa neno "mikono" inawakilisha Yahwe. "Ilikuwa mimi ambaye"

iliyotandaza mbingu

Yahwe anazungumza kuumba mbingu kana kwamba zilikuwa kitambaa ambacho alikitandaza nje.

Isaiah 45:13

Taarfa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Nilimwamsha Koreshi wima katika haki

Hapa neno "haki" lina maana ya matendo sahihi. Maana zaweza kuwa 1) ambayo Yahwe amemwamsha Koreshi kufanya jambo sahihi au 2) ambalo Yahwe alikuwa sahihi kumwasha Koreshi

Nilimwamsha Koresh

Yahwe anazungumzia kusababisha Koreshi kutenda kana kwamba alikuwa akiamshwa kutoka usiingizini

Nitalaiinsha njia zake zote

Yahwe anazungumzia kuondoa vikwazo na kusababisha Koreshi kuwa na mafanikio kana kwamba alikuwa akitengeneza njia laini ambazo Koreshi anatembelea.

Atajenga mji wangu

Hii ina maana ya Yerusalemu.

na sio kwa gharama wala rushwa

Hapa maneno "gharama" na "rushwa" hutumia maana moja. Koreshi hatafanya vitu hivi kwa ajili ya faida ya mapato. "na hatafanya vitu hivi kwa ajili ya fedha"

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli

Isaiah 45:14

Mapato ya Misri na bidhaa za Ethiopia pamoja na Waseba, wanaume wa maumbile marefu, wataletwa kwako

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "'Watu wa Misri, Ethiopia, na watu warefu wa Seba, watakuletea mapato yako na bidhaa zao"

Mapato ya Misri

"Faida za Misri"

Waseba

Watu hawa kutoka taifa la Seba.

kwako

Hapa "kwako" ina maana ya watu wa Yerusalemu.

Isaiah 45:16

Wataaibika na kufeheshwa pamoja; wale wanaochonga sanamu watatembea kwa aibu

Mistari hii miwili inatumia maana moja, na wa pili kufafanua neno la mstari wa kwanza

Wataaibika na kufeheshwa pamoja

Maneno "aibishwa" na "fedheheshwa" kwa msingi yana maana moja na husisitiza ukali wa aibu. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Sanamu zao zitawaacha wote na aibu kabisa"

watatembea kwa aibu

Kuishi katika aibu ya muendelezo inazungumziwa kana kwamba ilkuwa kutembea katika aibu. "ataendelea kuabishwa"

Israeli ataokolewa na Yahwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. 'Yahwe atawaokoa watu wa Israeli"

hautakuwa tena na aibu au fedheha

Hapa "hautakuwa" ina maana ya watu wa Israeli. Maneno "aibu" na "fedheha" ina maana ya kitu kimoja. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Hakuna mtu atakayekuaibisha tena"

Isaiah 45:18

sio kama takataka

"ili isiwe tupu". Hapa neno "takataka" lina maana ya sehemu tupu, isiyozaa.

lakini aliiunda ili ikaliwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "lakini aliiunda ili watu waweze kuishi juu yake"

Isaiah 45:19

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Isaiah 45:20

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

wakimbizi

watu ambao wametoroka kutoka katika nyumba zao ili adui wasiwakamate au kuwaua

Isaiah 45:21

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa wakimbizi.

Na waache waungane pamoja

Hapa neno "waache" na maana ya wakimbizi kutok miongoni mwa mataifa ambao huabudu sanamu.

Ni nani ameonyesha hili kutoka zamani? Nani amelitangaza? Je! haikuwa mimi, Yahwe?

Yahwe anatumia maswali kusisitiza ya kwamba yeye ndiye aliyewaambia vitu hivi vingetokea. "'Nitawaambia ni nani aliyewaonyesha haya tangu zamani. Nitawaambia ni nani aliyeitangaza. Ilikuwa ni mimi, Yahwe"

Isaiah 45:22

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Geukia kwangu na ukolewe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "'Geuka kwangu nami nitakuokoa"

mwisho wote wa dunia

Sehemu za dunia ambazo zipo mbali sana zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa sehemu ambapo dunia hufika mwisho. Msemo huu pia hunda neno kwa ajili ya maneno mengine kwa ajili ya kila seheu katikati ya mwisho. "sehemu zote za mbali za dunia" au "dunia nzima"

mwisho wote wa dunia

Hapa msemo huu unawakilisha watu ambao wanaishi katika "mwisho wa dunia". "nyie ambao mnaishi katika sehemu za mbali za dunia" au "'nyie wote mnaoishi juu ya dunia"

Kwangu kila goti litainama, kila ulimi utaapa

Maneno "goti" na "ulimi" yanawakilisha watu. "Kila mtu atapiga goti mbele yangu, na kila mtu ataapa"

Isaiah 45:24

Wanasema

Watu wote wa dunia wanazungumza

Katika Yahwe vizazi vyote wa Israeli watafanywa kuwa haki

Hapa neno "kufanywa kuwa haki" haimaanisha Yahwe kusamehe dhambi zao, lakini kuthibitisha kwa mataifa ambayo Israeli alikuwa sahihi kumwabudu yeye. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atavifanya kuwa haki vizazi vyote vya Israeli" au "Yahwe atathibitisha vizazi vyote vya Israeli"

Isaiah 46

Isaiah 46:1

Beli anainama chini, Nebo anajishusha; sana zao ... kwa wanyama waliochoka kuishi

Isaya anazungumzia watu kuweka sanamu ya Beli na Nebo katika mkokoteni wa wanyama kusafirisha kana kwamba bidhaa hizi zilifanywa "kuinama chini" na "kujishusha". Hii yote ni mikao miwili ya kufedhehesha.

Beli ... Nebo

Hawa walikuwa miungu miwili wa msingi ambao Wababeli waliwaabudu.

sanamu zao

sanamu ambazo ziliakilisha Beli na Nebo

hawawezi kuokoa sanamu

"Beli na Nebo hawawezi kuokoa sanamu zao"

wao wenyewe wamekwenda katika kifungo

Isaya anazungumzia watu kubeba sanamu hizi kana kwamba miungu ya uongo ambayo inawakilisha inabebwa katika kifungo.

Isaiah 46:3

Nisikilize mimi

Hapa "mimi" ina maana ya Yahwe

ambao wamebebwa na mimi kabla ya kuzaliwa kwako, kubebwa kutoka tumboni

Yahwe anazungumzia taifa la Israeli kana kwamba lilikuwa mtu, na mwanzo wa taifa kana kwamba ni kuzaliwa kwake.

ambao wamebebwa na mimi

Yahwe anazungumzia kusaidi na kuokoa watu wa Israeli kana kwamba alikuwa akiwabeba. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambao nimewabeba"

Hata katika uzee wako mimi ndiye, na mpaka nywele zako ni mvi nitakubeba

Yahwe anazungumzia taifa la Israeli kuwa zee sana kana kwamba likikuwa mwanamume mzee mwenye mvi.

Isaiah 46:5

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Utanilinganisha na nani? Ni nani unadhani nafanana naye, ili kwamba tuweze kulinganishwa?

Yahwe anatumia swali kusisitiza ya kwamba hakuna mtu kama yeye. "hakuna mtu ambaye mnaweza kunilinganisha naye. Sifanani na mtu, ili tuweze kulinganishwa"

ili kwamba tuweze kulinganishwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ili uweze kutulinganisha"

Isaiah 46:7

Wanaiinua

"Wana..." ina maana ya watu ambao hutengeneza sanamu na "..iinua" ina maana ya sanamu ambayo wametengeneza.

Isaiah 46:8

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wake.

Isaiah 46:10

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wake.

Ninatangaza mwisho kutoka mwanzo, na kabla ya muda kile ambacho hakijatokea

Hii kwa msingi inarudia wazo hilo hilo kwa msisitizo. Kitenzi kutoka katika msemo wa kwanza unaweza kutumika kwa msemo wa pili. "Ninatangaza mwisho kutoka mwanzo, na ninatangaza kabla ya muda kile ambacho bado hakijatokea"

Ninamwita ndege wa mawindo kutoka mashariki

Yahwe anazungumzia Kipro kana kwamba ilikuwa "ndege wa mawindo". Kama ndege anavyokamata kwa haraka windo lake, kwa hiyo Kipro itatimiza kusudi la yahwe kushinda mataifa.

Nimesema; Nitaitimiza pia; Nimekusudia, nitaifanya pia.

Hii inarudia wazo hilo hilo kwa ajili ya msisitizo.

Isaiah 46:12

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

ambao wako mbali na kufanya kilicho sahihi

Yahwe anazungumzia watu kufanya mabaya kwa ukaidi kana kwamba walikuwa mbali kihalisia na kufanya kilicho chema.

wokovu wangu hausubiri

Yahwe anazungumzia kuokoa watu wake mapema kana kwamba wokovu wake ulikuwa mtu ambaye hasubiri kutenda. "Sitasubiri kukuokoa"

Isaiah 47

Isaiah 47:1

Taarifa ya Jumla

Katika sura hii, Yahwe anazungumza na Babeli kuhusu anguko lake kana kwamba alikuwa malkia ambaye ameaibishwa.

keti katika vumbi, binti bikira wa Babeli; keti juu ya ardhi ... binti wa Wakaldayo.

Misemo hii miwili ina maana moja. Kuketi katika mavumbi ni ishara ya aibu.

binti bikirawa Babeli ... binti wa Wakaldayo

Misemo hii miwili ina maana ya mji, Babeli, ambao unazungumziwa kana kwamba ilikuwa binti. Ya kwamba mji ni "binti" ikionyesha jinsi watu wanavyofikiri kwa kubembeleza juuyake.

bila kiti cha enzi

Hapa "kiti cha enzi" ina maana ya nguvu ya kutawala. "bila nguvu ya kutawala"

Hautaitwa tena mrembo na wa kuvutia

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Watu hawatakuita tena mrembo na wa kuvutia"

mrembo na mzuri

Maneno haya mawili yanatumia maana moja. Wanafafanua yule ambaye ni mzuri na anaishi katika starehe. "mzuri sana" au "mwenye starehe sana"

jiwe la kusaga

jiwe kubwa linatumiwa kusaga nafaka

Isaiah 47:3

Kauli Kiunganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza na Babeli kuhusu anguko lake kana kwamba alikuwa malkia ambaye ameaibishwa.

Uchi wako utafunuliwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Utakuwa uchi"

aibu yako itaonekana

Hapa neno "aibu" ni tasifida kwa ajili ya sehemu za siri za mtu. Hii inaweza kutafsiriwa katika hali ya kutenda. "watu wataona aibu yako" au "watu wataona sehemu zako za siri"

Mkombozi wetu

"wetu" ina maana ya Isaya na watu wa Israeli.

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli

Mtakatifu wa Israeli

Mungu wa Israeli

binti wa Wakaldayo

Msemo huu una maana ya mji, Babeli, ambao unazungumziwa kana kwamba ulikuwa binti. Ya kwamba mji ni "binti" inaashiria jinsi Wakaldayo wanavyomfikiria yeye.

kwa maana hautaitwa tena

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kwa maana watu hawatakuita tena"

malkia wa falme

Yahwe anazungumzia Babeli kuwa mji mkuu wa Falme ya Babeli kana kwamba ilikuwa malkia aliyetawala falme nyingi.

Isaiah 47:6

Kauli Kiunganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza na Babeli kuhusu anguko lake kana kwamba alikuwa malkia ambaye ameaibishwa.

Nilikasirishwa

Hapa "nilikasirishwa" ina maana ya Yahwe.

nilitia unajisi urithi wangu

Yahwe anazungumzia watu wa Israeli kuwa milki yake maalumu kana kwamba walikuwa urithi wake. "Niliwanajisi watu wangu, ambao walikuwa milki yangu maalumu"

kuwakabidhi mikononi mwako

Hapa neno "mkononi" inawakilisha nguvu na utawala wa Babeli. "Ninawaweka chini ya nguvu yako"

umeweka nira nzito sana juu ya watu wazee

Yahwe anazungumzia Wababeli kuwakandamiza watu wazee kana kwamba wamewatendea watu wazee kama ng'ombe na kuweka nira nzito juu ya shingo zao.

nitatawala milele kama malkia wa enzi

Babeli inazungumzia kutawala kwa kudumu juu ya mataifa mengi kana kwamba ilikuwa malkia ambaye atatwala milele.

Hukuviweka vitu hivi moyoni

Yahwe anazungumzia juu ya kufikiria kwa makini kuhusu kitu kana kwamba ilikuwa ni kuweka kitu hicho ndani ya moyo wa mtu. "Haukufikiria vitu hivi"

Isaiah 47:8

Kauli Kiunganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza na Babeli kuhusu anguko lake kana kwamba alikuwa malkia ambaye ameaibishwa.

wewe upendaye anasa

"wewe mwenye starehe". Hii ina maana ya starehe nyingi ambazo Babeli alifurahia.

kwa imara

Hii ina maana ya dhana ya usalama ya uongo ya Babeli katika kuwaza ya kwamba hatapoteza nafasi yake ya utajiri na heshima. "unayedhani upo salama"

Sitawahi kukaa kama mjane ... kupotewa kwa watoto

Babeli kuamini ya kwamba mataifa mengine hawataweza kumshinda inazungumziwa kana kwamba hatawahi kuwa mjane au hatawahi kufiwa na watoto.

Sitawahi kukaa kama mjane

"Sitawahi kuwa mjane"

katika muda mmoja katika siku moja

"ghafla katika wakati mmoja"

Isaiah 47:10

Kauli Unganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza na Babeli kuhusu anguko lake kana kwamba alikuwa malkia ambaye ameaibishwa.

unasema moyoni mwako

Hapa neno "moyoni" lina maana ya utu wa ndani. "unasema kwako mwenyewe"

Maafa yatakuzidi

Yahwe anazungumzia balaa kana kwamba ilikuwa mtu ambaye anakamata Babeli. "Utapitia maafa"

Uharibifu utaanguka juu yako

Yahwe anazungumzia Babeli kuharibiwa kana kwamba uharibifu ulikuwa kitu ambacho huanguka juu ya mji. "Utapitia uharibifu" au "Wengine watakuangamiza"

Janga litakupiga

Yahwe anazungumzia Babeli kupitia janga kana kwamba janga lilikuwa mtu ambaye anapiga Babeli. "Utapitia janga"

Isaiah 47:12

Kauli Unganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza na Babeli kuhusu anguko lake kana kwamba alikuwa malkia ambaye ameaibishwa.

Ng'ang'ania kurusha laana zenu ... huenda utatisha mbali maafa

Yahwe anakejeli Babeli kwa kumwambia kuendelea kufanya uchawi wake kuweka mambo mabaya mbali, lakini anajua ya kuwa haitawasaidia.

Isaiah 47:14

Kauli Unganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza na Babeli kuhusu anguko lake kana kwamba alikuwa malkia ambaye ameaibishwa.

watakuwa kama mashina ya mabua. Moto utawaunguza

Yahwe analinganisha waganga na wachawi na mabua ambayo huwaka haraka katika moto. Hii ina maana Yahwe atawaangamiza kwa urahisi kama vile moto unavyochoma mashina ya mabua, na kwa hiyo hawana nguvu ya kuokoa Babeli.

mkono wa mwale wa moto

Hapa neno "mkono" unawakilisha nguvu. "nguvu ya mwale wa moto"

Hakuna mkaa wa kuwapa joto na hakuna moto kwa ajili yao kukaa karibu

Yahwe anasisitiza ya kwamba huu ni moto wa kuharibu kwa kusema kwamba sio moto ambao watu hutumia kujipatia joto.

Isaiah 48

Isaiah 48:1

Sikia haya

"Sikiliza ujumbe wangu". Yahwe anazungumza.

nyumba ya Yakobo

Hapa "nyumba" ina maana ya vizazi vya Yakobo. "vizazi vya Yakobo"

ambao wameitwa kwa jina la Israeli

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambao kila mtu huwaita watu wa Israeli"

wametokana na mbegu ya Yuda

Msemo huu unasisitiza ya kwamba ni vizazi vya moja kwa moja, vya kimwili vya Yuda. "ni vizazi vya Yuda"

kumsihi Mungu wa Israeli

"kumwita Mungu wa Israeli"

wanajiita wenyewe

Hii ina maana ya wtu wa Israeli. "mnajiita wenyewe"

mji mtakatifu

Hii ina maana ya Yerusalemu.

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli

Isaiah 48:3

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

walitoka kutoka kwa kinywa changu

"Kinywa" ina maana ya mtu kuzungumza. "nilizungumza mambo haya"

musuli wako wa shingoni hukazika kama chuma, na kipaji chako cha uso kama shaba

Yahwe analinganisha kukazwa kwa misuli ya shingo zao na ugumu wa vipaji vyao vya uso kwa ugumu wa chuma na shaba. Hapa, kuwa na shingo iliyokazwa au kipaji cha uso kigumu ni sitiari ambayo ina maana ya watu kuwa wakaidi. "ni kana kwamba shingo zenu ni chuma na vichwa vyenu ni shaba"

nilitamka mambo haya kwako mapema; kabla havijatokea nilikujulisha

Huku ni kusema kitu hicho hicho mara mbili kwa ajili ya msisitizo.

Isaiah 48:6

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

hautakiri kuwa kile nilichosema ni ukweli?

Yahwe anatumia swali kukaripia watu wa Israeli kwa kutokiri kile wanachopaswa kujua ni ukweli. "wewe ni kaidi na hautakiri kile nilichosema ni kweli"

Isaiah 48:8

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

mambo haya hayakufunuliwa kwa masikio yako mapema

Yahwe anazungumzia kufafanua kitu kana kwamba alikuwa akikunjua. Neno "masikio" yanawakilisha watu ambao wanasikiliza. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Sikuelezea mambo haya kwako kabla"

tangu kuzaliwa

Yahwe anazungumzia mwanzo wa mataifa kana kwamba ulikuwa kuzaliwa kwao.

Isaiah 48:9

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli

Kwa ajili ya jina langu nitasitisha hasira yangu

Hapa neno "jina" lina maana ya sifa ya Yahwe. "Kwa ajili ya sifa yangu nitakawiza hasira yangu"

na kwa ajili ya heshima yangu nitajizuia kukuangamiza

Sehemu hii ya sentensi ina maana moja kama sehemu ya kwanza.

Tazama, nilikutakasa, lakinii sio kama fedha; nimekutakasa katika tanuu la mateso

Yahwe anazungumzia kutumia mateso kusafisha watu wake kana kwamba walikuwa vyuma vya thamani na mateso yalikuwa tanuu ambano anawatakasa.

kwa kuwa ninawezaje kuruhusu jina langu kudharauliwa?

Yahwe anatumia swali kusisitiza kuwa hawezi kuruhusu jina lake mwenyewe kudharauliwa. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa maana sitaruhusu yeyote kudharau jina langu"

Isaiah 48:12

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Yakobo, na Israeli

Zote hizi zina maana ya watu wa Israeli.

Mimi ni wa kwanza, mimi pia ni wa mwisho

Msemo huu unasisitiza asili ya milele ya Yahwe. Maana zaweza kuwa 1) "Mimi ndiye niliyeanzisha vitu vyote, na mimi ndiye humaliza vitu vyote" au 2) "Mimi ndiye niliyekuwa nikiendelea kuishi, na mimi ndiye nitakayekuwa nikiendelea kuishi".

mkono wangu umelaza msingi wa dunia, na mkono wangu wa kuume umezinyosha mbingu

Hapa "mkono" una maana ya Yahwe. "Nililaza msingi wa dunia, na nikatandaza mbingu"

msingi wa dunia

Neno "msingi" kawaida ina maana ya umbo la mawe ambalo hutoa mhimili kwa jengo kutoka chini. Hapa inafafanua umbo ambalo ilidhaniwa kushikilia dunia katika nafasi yake.

umezinyosha mbingu

Yahwe anazungumzia kuumba mbingu kana kwmaba zilikuwa kitambaa ambacho Yahwe alinyosha nje.

ninapoziita, zinasimama juu pamoja

Kusimama pale Yahwe anapoita ni sitiari kwa kuwa tayari kumtii. Yahwe anazungumzia dunia na mbingu kana kwamba ziliweza kumsikia na kumtii.

ninapoziita

Maana zaweza kuwa 1) "ninapoziita dunia na mbingu" au 2) "ninapoziita nyota na mbingu"

Isaiah 48:14

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Nani kati yenu ametanganza mambo haya?

Yahwe anatumia swali kusisitiza ya kwamba sanamu hazijawaambia mambo haya. "Hakuna kat ya sanamu zenu zimesema haya kwenu"

Mshirika wa Yahwe atatimiza kusudi lake dhidi ya Babeli. Atatekeleza mapenzi ya Yahwe dhidi ya Wakaldayo

Hapa "mshirika" ina maana ya Koreshi. Sentensi hizi mbili zina maana moja na zinatumika kwa ajili ya msisitizo.

kusudi lake

"kusudi la Yahwe"

Mimi, mimi

Neno "Mimi" linarudiwa kwa ajili ya msisitizo. "Mimi mwenyewe"

Isaiah 48:16

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Sijazungumza kwa siri

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya chanya. "Nimezungumza dhahiri na wazi"

amenituma

Hapa "mimi" ina maana ya mtumishi asiyejulikana wa Yahwe, huenda Isaya au Koreshi au Masihi alyeahidiwa.

Isaiah 48:17

Mkombozi wako ... Mungu wako

Hapa "wako" ina maana ya watu wa Israeli.

Mkombozi

Mkombozi wa Israeli.

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli.

ambaye anakuongoza katika njia unayopaswa kuenenda

Yahwe kufundisha watu jinsi ya kuishi inazungumziwa kana kwamba alikuwa akiwaongoza kutembea katika njia sahihi.

Kama tu ungetii amri zangu

Yahwev anafafanua kitu ambacho kingeweza kutokea lakini hakikutokea.

Kisha amani yako na mafanikio yako yangetiririka kama mto, na wokovu yako kama mawimbi ya bahari

Misemo hii miwili inatumia maana moja. Kwazote, Yahwe anazungumzia Israeli kupitia baraka nyingi kana kwamba baraka hizo zilitiririka kama maji.

wokovu yako kama mawimbi ya bahari

Kitenzi kinaweza kutumika kutoka katika msemo uliopita. "wokovu wako ungeweza kutiririka kama mawimbi ya bahari"

Isaiah 48:19

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kufafanua hali ya kubuni kwa watu wa Israeli.

Vizazi vyako viingekuwa vingi kama mchanga, na watoto kutoka tumboni mwako wengi kama punje za mchanga

Zote hizi mbili zina maana ya watu wangekuwa na uzao mwingi zaidi kuliko ya uwezo wao kuhesabu.

watoto kutoka tumboni mwako

Yahwe anazungumzia vizazi vya watu wa Israeli kana kwamba walikuwa watoto ambao taifa liliwazaa.

jina lao halingekatwa mbali wala kufutwa

Watu wa Israeli kuangamizwa inazungumziwa kana kwamba jina lao limekatwa, kama vile mtu anavyokata kipande cha nguo au kukata tawi kutoka katika mti, au kufutwa. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda.

jina lao

Hapa neno "jina" lina maana ya vizazi ambavyo vingeendelea kubeba jina la Israeli.

halingekatwa mbali wala kufutwa

Misemo hii miwili katikamuktadha hii ina maana ya kuangamiza watu. "kuangamizwa"

Isaiah 48:20

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

hadi kwenye mipaka ya dunia

Sehemu za dunia ambazo zipo mbali sana zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa sehemu ambapo dunia hufikia mwisho. Msemo huu pia huunda neno la kujumuisha maneno mengine na lina maana ya kila seheu katikati ya mipaka. "katika sehemu za mbali kabiisa za dunia" au "katika dunia yote"

mtumishi wake Yakobo

Hii ina maana ya vizazi vya Yakobo. "watu wa Israeli, watumishi wake"

Isaiah 48:21

Hawakupata kiu ...maji yalimwagiika nje

Hii ina maana ya tukio katika historia ya watu wa Israeli pale Yahwe alipowatunza walipokuwa wakiishi jangwani baada ya kutoroka Misri.

Isaiah 49

Isaiah 49:1

Nisikilize mimi

Hapa "mimi" ina maana ya mtumishi wa Yahwe.

nyie nchi za pwani

Hii ina maana ya watu ambao huishi katika nchi za pwani. "wewe ambaye mnaishi katika nchi za pwani"

Amefanya mdomo wangu kama upanga mkali

Hapa neno "mdomo" unawakilisha maneno ambayo anazungumza. Maneno yake yanalinganishwa na upanga mkali kusisitiza ya kwamba yatakuwa yanafaa. "Amefanya maneno yangu kuwa na matokeo yanyofaa kuwa makali kama upanga"

amenificha katika kivuli cha mkono wake

Yahwe kulinda mtumishi wake na kuweka kusudi lake kuwa siri inazungumziwa kana kwamba mkono wa Yahwe uliiweka kivuli juu yake.

amenifanya kuwa mshale uliong'arishwa; katika podo lake amenificha

Mtumishi wa Yahwe kuweza kutekeleza makusudi ya Yahwe kikamilifu inazungumziwa kana kwmba mtumishi alikuwa mshale mkali, na mpya.

katika podo lake amenificha

Yahwe kulinda mtumishi wake na kuweka kusudi lake kuwa siri inazungumziwa kana kwamba Yahwe alimficha katika podo.

podo

mfuko unaotumika kubeba mishale

Isaiah 49:3

Taarifa ya Jumla

Mtumishi wa Yahwe anaendelea kuzungumza.

Alisema

"Yahwe alisema"

Wewe ni mtumishi wangu, Israeli

"Wewe ni mtumishi wangu, ambaye ninakuita Israeli"

Isaiah 49:5

Taarifa ya Jumla

Mtumishi wa Yahwe anaendelea kuzungumza.

kwamba Israeli aweze kukusanywa kwake

Sehemu hii ya sentensi ina maana moja na sehemu kabla yake. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kuleta watu wa Israeli kwake mwenyewe"

Nimeinuliwa katika macho ya Yahwe

Hapa "macho" yanawakilisha mawazo ya Yahwe au fikra. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe ameniinua"

Mungu wangu amekuwa nguvu yangu

Mungu kumpa mtumishi nguvu inazungumziwa kana kwamba Mungu mwenyewe alikuwa nguvu yake. "Mungu wangu amenipa nguvu" au "Mungu wangu ameniimarisha"

nitakufanya kuwa mwanga kwa watu wa mataifa

Mtumishi kuleta ujumbe wa Yahwe kwa watu wa mataifa na kuwasaidia kuelewa inazungumziwa kana kwamba Yahwe alimfanya mtumishi mwanga ambao hung'aa katika watu wa mataifa.

mpaka mwisho wa dunia

Sehemu juu ya dunia ambazo zipo mbali sana zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa sehemu ambapo dunia hufika mwisho. Msemo huu pia huunda neno lenye maana moja na kundi la vitu kumaanisha kila sehemu katikati ya mwisho. "katika sehemu zote za mbali za dunia" au "katika dunia nzima"

Isaiah 49:7

Mkombozi

Mkombozi wa Israeli

kwa yule ambaye maisha yake yanadharauliwa, anayechukiwa na mataifa, na mtumwa wa watawala

Hapa neno "maisha" linawakilisha mtu. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa yule ambaye watu walidharau, ambaye mataifa walichukia na kuwashika kama watumwa"

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

Isaiah 49:8

Katika kipindi ntakapoamua kuonyesha fadhila yangu nitakujibu, na katika siku ya wokovu nitakusaidia

Vishazi hivi viwili vina maana moja.

nitakujibu

Hapa "nitakujibu" ina maana ya mtumishi wa Yahwe.

katika siku ya wokovu

Hapa neno "siku" ina maana ya muda bayana na sio siku ya masaa 24. Neno "wokovu" linaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "pale kipindi kitakapokuja kwangu kukuokoa"

kukupatia kama agano kwa ajili ya watu

Hapa neno "agano" ni mfano wa maneno kwa yule ambaye huanzisha au kupatanisha agano. "kukufanya kuwa mpatanishi wa agano na watu"

kuijenga tena nchi

Hapa neno "nchi" inawakilisha miji katika nchi ambayo ilikuwa imeangamizwa. "kujenga tena sehemu zilizoharibiwa katika nchi"

kugawia tena urithi uliotelekezwa

Yahwe anazungumzia nchi kana kwamba ilikuwa urithi ambao watu wa Israeli walipokea kama milki ya milele. Inadokezwa ya kwamba mtumishi atagawa tena nchi kwa watu wa Israeli. "kugawa tena nchi iliyotelekezwa kama urithi wao"

Isaiah 49:9

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na mtumishi wake.

Watachunga katika barabara, na katika miteremko ya wazi itakuwa malisho yao

Yahwe anazungumzia watu kuishii kwa uhuru na kwa mafanikio kana kwmba walikuwa kondoo ambao walikuwa na malisho mengi ya kuchunga.

Isaiah 49:10

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Hawatakuwa

Hapa "hawatakuwa" ina maana ya watu wa Mungu.

wala joto au jua kupiga juu yao

Hapa neno "joto" linaelezea neno "jua". Watu kuteseka kutoka na joto la jua inazungumziwa kana kwamba joto liliwapiga. "wala hawatateseka kutokana na joto la jua"

kwa maana yeye ambaye ana rehema juu yao ... atawaongoza

Yahwe anazungumzia mwenyewe katika mtu wa tatu. Anazungumzia kuwalinda watu na kuwatunza kana kwamba alikuwa mchungaji wao. "Mim, yule ambaye ana huruma juu yao ... nitawaongoza"

Nitafanya milima yangu yote kuwa njia, na kufanya njia zangu kuu kuwa usawa

Yahwe anazungumza kuwaongoza watu wake kwa usalama na kuondoa vikwazo kutoka katika njia yao kana kwamba aligeuza milima kuwa njia na kusawazisha njia kuu.

Isaiah 49:12

nchi ya Sinimu

Mahali pa eneo hili haipo wazi, lakini inaweza kumaanisha sehemu ambayo ipo kusini mwa Misri.

Imba, mbingu, na uwe na furaha, dunia; funguka katika kuimba, enyi milima!

Isaya anageuza usikivu wake kutoka kwa watu wa Israeli na kuzungumza kwa mbingu, dunia, na milima kana kwamba ilikuwa watu.

Isaiah 49:14

Lakini Sayunii akasema

Neno "Sayuni" ni jina lingine kwa ajili ya Yerusalemu. Isaya anazungumzia mji kana kwamba ulikuwa mwanamke ambaye hulalamika ya kwamba Yahwe amemsahau.

Je! mwanamke anaweza kumsahau mtoto wake, akinyonya katika titi lake, ili asiwe na huruma kwa mwana aliyemzaa?

Yahwe anatuma swali kuwasaidia watu wake kuelewa ya kwamba hatasahau juu yao au kuacha kuwatunza. "Mwanamke hawezi kusahau kunyonyesha mtoto wake au kuacha kumtunza mwana aliyemzaa"

Isaiah 49:16

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa Sayuni.

Nimeandika jina lako juu ya viganja vyangu

Yahwe anazungumzia uaminifu wake usioyumba kwa Sayuni kana kwamba alikuwa ameandika jina lake juu ya viganja vya mkono wake.

kuta zako zipo mbele yangu muda wote

Yahwe anazungumzia kufikiria daima kuhusu Sayuni kana kwamba kuta zake zilikuwa mbele yake daima. Neno "kuta" ni mfano wa maneno kwa ajili ya mji. "Ninaendelea kuwaza juu ya kuta zako" au "Ninakuwaza daima"

Watoto wako wanaharakisha kurudi

Yahwe anazungumzia watu ambao wanarudi kuishi Yerusalemu kana kwamba walikuwa watoto wa mji. "Wakazi wako wanaharakisha kurudi"

Kwa uhakika ninavyoishi

Hiki ni kiapo ambacho Yahwe anatumia kuhakikisha ukweli wa kile anachosema.

tamko la Yahwe

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "tamko" lielezwa kama kitenzi "tamka" au "sema kwa dhati". "hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyotamka" au "hivi ndivyo kile Yahwe wa majeshi alivyosema kwa dhati"

hakika utawavaa kama mapambo ya vito; utawaweka juu yako, kama bibi harusi

Yahwe anazungumzia wakazi wa Sayuni kana kwamba walikuwa mapambo ya viito ambayo mji huvaa kuonyesha uzuri wake na furaha.

utawaweka juu yako, kama bibi harusi

Sehemu ya mwisho ya msemo inaweza kubainishwa kutoka katika mstari uliopita. " utawaweka juu yako, kama bibi harusi anavyovaa mapambo ya vito"

Isaiah 49:19

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na Sayuni kana kwamba ilikuwa mwanamke

Ingawa ulikuwa takataka na uliyetelekezwa

Maneno "takataka" na "telekezwa" ina maana moja na inasisitiza ya kwamba adui ameangamiza Sayuni na kuiacha tupu. "Ingawa ulikuwa umetelekezwa kabisa"

wale ambao walikumeza

Aui kuangamiza Sayuni inazungumziwa kana kwamba walikuwa wameimeza. "wale ambao walikuangamiza"

Watoto waliozaliwa wakati wa kuondolewa kwako

Yahwe anazungumzia kipindi ambapo watu wa Yerusalemu walikuwa uhamishoni kana kwamba mji ulikuwa umeondolewa watoto wake. Wale mbao walizaliwa wakati watu wakiwa uhamishoni inazungumziw kana kwamba ni watoto wa mji. "Wale mbao wataishi kwako, ambao walizaliwa wakati watu wakiwa katika uhamisho"

Sehemu ina nafasi ndogo mno kwetu

Hii ina maana ya kwamba ktakuwa na watu wengi sana mpaka mji utakuwa mdogo sana kwa ajili yao wote kuish ndani yake.

Isaiah 49:21

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na Sayuni kana kwamba ilikuwa mwanamke.

Nani amezaa watoto hawa kwa ajili yangu?

Sayuni anazungumza na watu ambao wanrudi kuishi katika mji kana kwamba watu hao walikuwa watoto wake. Swali la Sayuni linaelezea mshangao wake ya kwamba watoto wengi sana sasa ni wa kwake.

Nilondolewa na kuwa tasa, nikahamishwa na kuachwa

Sayuni anajifafanua kama mwanamke asiyeweza kupata watoto zaidi. Anadokeza sababu ya mshangao wake mkubwa.

Nilondolewa na kuwa tasa

"Nilikuwa nikiomboleza juu ya watoto wangu waliokufa na kutoweza kupata wengine"

nikahamishwa na kuachwa

"Niliondoka, bila mume"

Nani amekuza watoto hawa? Tazama, niliachwa peke yangu; hawa wametoka wapi?

Tena, Sayuni anatumia maswali kuelezea mshangao wake. "Tazama, niliachwa peke yangu; sasa watoto hawa wote ambao sikuwakuza wamekuja kwangu"

Isaiah 49:22

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na Sayuni kana kwamba ilikuwa mwanamke. Anafafanua jinsi atakavyoweza kupata watoto wengi sana.

Nitainua mkono wanu kwa mataifa; nitainua bendera yangu ya ishara kwa watu

Vishazi hivi viwili vina maana moja. "Nitainua mkono wangu na kutoa ishara kwa bendera kwa ajili ya watu wa mataifa kuja"

Wataleta wana wako katika mikono yao na kubeba binti zako juu ya mabega yao

Yahwe anazungumzia watu ambao wataishi Yerusalemu kana kwamba walikuwa watoto wa mji. Pia anazungumza kuhusu watu wa mataifa mengine kuwasaidia Waisraeli kurud Yerusalemu kana kwamba walikuwa wakiwabeba Waisraeli.

Isaiah 49:23

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na Sayuni kana kwamba ilikuwa mwanamke.

Wafalme watakuwa baba zako wa kambo, na malkia wao yaya wako

Yahwe anazungumzia watu ambao wataishi Sayuni kana kwamba walikuwa watoto wa mji. Misemo "baba wa kambo" na "yaya" ina maana y wanamume na wanawake ambao huwajibika kwa utunzaji wa watoto. "Wafalme na malkia wa mataifa mengine watajitoa kwa ajili ya wakazi wako"

watainama chini kwako kwa nyuso zao ardhini na kulamba vumbi la miguu yako

Misemo hii inaelezea ishara ambayo watu walitumia kuelezea kujiweka chini kabisa kwa mkubwa zaidi.

kulamba vumbi la miguu yako

Maana zaweza kuwa 1) ya kwamba hii ni ishara halisi ya kujiweka chini ambapo mtu hulamba vumbi kutoka katika mguu wa mkubwa wake au kutoka ardhini katika mguu wa mkubwa wake au 2) ya kwamba hii ni lahaja ambayo inaelezea mtu kusujudu mbele ya mkubwa wake.

hawataaibishwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hataaibika" au "hatavunjwa matumaini"

Isaiah 49:24

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na Sayuni kana kwamba ilikuwa mwanamke.

Je! mali iliyoibiwa inaweza kuchukuliwa kutoka kwa hodari, au mateka kuokolewa kutoka kwa jeshi kali?

Isaya anatumia swali kuelezea ugumu wa kuchukua kitu chochote kutoka kwa mwanajeshi mwenye uwezo au hodari mwenye nguvu sana. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mtu hawezi kuchukua mali iliyoibiwa kutoka kwa hodari au kuokoa mateka kutoka kwa wanajeshi wakali"

mali iliyoibiwa

vitu vya thamani vilivyochukuliwa kutoka kwa walioshindwa katika vita.

mateka watachukuliiwa mbali kutoka kwa hodari, na mali iliyoibiwa itaokolewa

Yahwe anasema ya kwamba atafanya kile ambacho kawaida hakiwezekani kwa watu kufanya. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nitachukua mateka kutoka kwa hodari, na nitaokoa mali iliyoibiwa"

Nita ... kuokoa watoto wako

Yahwe anazungumzia watu ambao wataishi Sayuni kana kwamba walikuwa watoto wa mji.

Isaiah 49:26

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na Sayuni kana kwamba ilikuwa mtu.

Nitawalisha wakandamizaji wako kwa nyama yao wenyewe

Maana zaweza kuwaa 1) wakandamizaji watakuwa na njaa sana watakula nyama ya rafiki zao waliokufa. "Nitasababisha wakandamizaji wako kula nyama yao wenyewe" au 2) Yahwe anazungumzia wakandamizaji kupigana dhidi yao wenyewe na kujiangamiza kana kwamba walikuwa wakijila wenyewe. "Nitasababisha wakandamizaji wako kujiangamiza wao wenyewe, kana kwamba walikuwa wakila nyama yao wenyewe"

na watalewa katika damu yao wenyewe, kan kwamba ilikuwa divai

Maana zaweza kuwa 1) wakandamizaji watakuwa na kiu sana mpaka watakunywa damu ya rafiki zao ambao wamekufa. "na watakunywa damu ya rafiki zao na kuwa kama watu dhaifu waliolewa divai" au 2) Yahwe anazungumzia wakandamizaji kupigana dhidi yao wenyewe na kujiangamiza kana kwamba walikuwa wakinywa damu ayo wenyewe. "na watamwaga damu nyingi sana ya rafiki zao kana kwamba walikuwa wakilewa na divai"

Isaiah 50

Isaiah 50:1

Hati ya talaka ambayo nilimuacha mama yako iko wapi?

Yahwe anazungumza juu ya Sayuni kana kwamba mji ulikuwa mama wa watu walioishi kule na kutuma watu katika uhamisho kana kwamba alikuwa akitoa talaka kwa mama yao.

Hati ya talaka ambayo nilimuacha mama yako iko wapi?

Yahwe anauliza swali hili la balagha ili kwamba watu watoa "hati ya talaka" ambayo ingetoa sababu ya Yahwe kuwatuma katika uhamisho. "Nionyesheni hati ya talaka mabyo nilimuacha mama yenu"

Ni wadai wapi wa kwangu nimekuuza?

Yahwe anazungumzia kuwafukuza watu katika uhamisho kana kwamba alikuwa akiwauza.

Ni wadai wapi wa kwangu nimekuuza?

Yahwe anauliza swali hili kusisitiza ya kwamba hakuwauza kwa sababu alikuwa na deni kwa mdaiwa. Inadokezwa ya kwamba hiki ndicho watu walivyofikiri. "Sikuwauza kwa sababu ninadaiwa na mtu"

uliuzwa kwa sababu ya dhambi zako, na kwa sababu ya uasi wako, mama yako alifukuzwa

Yahwe anatoa sababu ya kuwafukuza watu katika uhamisho, ambayo anazungumzia kana kwamba amewauza na kutengana na mama yao. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nilikuuza kwa sababu ya dhambi zako, na nikatengana na mama yako kwa sababu ya uasi wako"

Isaiah 50:2

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzunguza na watu wa Israeli.

Kwa nini nilikuja lakini hapakuwa na mtu kule? Kwa nini niliita lakini hakuna aliyejibu?

Sentensi hizi mbili kimsingi zina maana moja. Yahwe anatumia maswali kusisitiza ya kwamba watu wapo uhamishoni kwa sababu hawakuitikia kwake, sio kwa sababu hakuwa tayari kuwaokoa. "Nilipokuja kwako, ulipaswa kuwa pale, lakini haukuwepo. Nilipokuita, ulitakiwa kujibu, lakini haukujibu". au "Nilipokuja kuzungumza na wewe, haukuniitikia".

Je! mkono wangu ulikuwa mfupi sana kukukomboa? Je! hapakuwa na nguvu ndani mwangu kukuokoa?

Yahwe anatumia maswali mawili ya kufanana kukaripia watu kwa kuamini ya kwamba hakuwa na nguvu ya kutosha kuwaokoa. "Mkono wangu hakika haukuwa mfupi kwangu kukulipia, na nilikuwa na uwezo kukuokoa!" au "Hakika nina uwezo wa kuwaokoa kutoka kwa adui wako"

Je! mkono wangu ulikuwa mfupi sana

Hapa neno "mkono" unawakilisha nguvu ya Yahwe. Yahwe kutokuwa na nguvu ya kutosha inazungumziwa kana kwamba mkono wake ulikuwa mfupi. "Je! sikuwa na nguvu ya kutosha"

Je! hapakuwa na nguvu ndani mwangu

"Je! sikuwa na nguvu"

naifanya mito kuwa jangwa

Yahwe anazungumzia kukausha mito kana kwamba alikuwa akigeuza kuwa jangwa. "Ninafanya mito kukauka kama jangwa"

samaki wao hufa kwa kukosa maji na kuoza

"samaki wao hufa na kuoza kwa kukosa maji". Neno "wao" ina maana ya bahari na mito.

naivisha mbingu kwa giza; naifunika kwa nguo ya gunia

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja. Yahwe inazungumza kusababisha mbingu kuwa na giza kana kwamba alikuwa akiivika kwa nguo ya gunia. "Ninafanya mbingu kuwa giza, kana kwamba ilikuwa ikivaa nguo nyeusi ya gunia"

Isaiah 50:4

Taarifa ya Jumla

mtumishi wa Yahwe anaanza kuzungumza.

Bwana Yahwe amenipatia ulimi kama wale wanaofundishwa

Neno "ulimi" linawakilisha kile anachosema. Maana zaweza kuwa 1) Yahwe amemwezesha kuzungumza kama mtu ambaye amejifunza kuzungumza kwa ustadi. "Bwana Yahwe ameniwezesha kuwa msemaji mwenye ujuzi" au 2) Yahwe kanifundisha kile nachosema. "Bwana Yahwe ameniwezesha kuzungumza kile alichonifundisha"

anaamsha sikio langu kusikia

Hapa "sikio langu" ina maana ya mtumishi wa Yahwe. Yahwe kumwezesha kusikia na kuelewa kile ambacho Yahwe anafundisha inazungumziwa kana kwamba Yahwe aliamsha sikio lake kutoka usingizini. "ameniwezesha kuelewa kile anachosema"

kama wale wanaofundishwa

Mtumishi anajilinganisha na mwanafunzi ambaye hujifunza kutoka kwa mwalimu wake. Maana zawekana kuwa 1) "kama mtu ambaye hujifunza kutoka kwa mwalimu wake" au 2) "kama mtu ambaye amemfundisha"

Isaiah 50:5

Taarifa ya Jumla

Mtumishi wa Yahwe anaendelea kuzungumza.

Bwana Yahwe amefungua sikio langu

Yahwe kumwezesha mtumishi wake kusikia na kuelewa inazungumziwa kana kwamba Yahwe alifungua sikio lake. "Bwana Yahwe ameniwezesha kumsikia na kumwelewa"

na sikuwa muasi, wala sikugeuka kinyume

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja. Kutotii kile ambacho Yahwe alisema inazungumzwa kana kwamba ilikuwa kugeuza mgongo wa mtu kwake. Hii inaweza kuelezwa katika misemo chanya. "na nikatii kile alichosema"

Niliwapa mgongo wale walionipiga, na mashavu yangu kwa wale walionyofoa ndevu zangu

Kuruhusu watu kumpiga na kunyofoa ndevu zake inazungumziwa kana kwamba ilikuuwa kutoa mgongo wake na mashavu kwao. "Niliruhusu watu kunipiga mgongoni na kunyofoa ndevu zangu kutoka mashavuni mwangu"

Sikuficha uso wangu kutoka kwa matendo ya aibu na kutemewa

Kuficha uso wa mtu ina maana ya kujilinda. "Sikujihami pale waliponidhihaki na kunitemea"

Isaiah 50:7

Taarifa ya Jumla

Mtumishi wa Yahwe anaendelea kuzungumza.

kwa hiyo sijaaibika

Ingawa mtumishi ametendewa vibaya, hataaibika kwa sababu amemtii Yahwe. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa hiyo sitaaibika"

kwa hiyo nimefanya uso wangu kama jiwe gumu

Hapa "uso wangu" una maana ya mtumishi. Mtumishi kuwa na nia imara ya kumtii Yahwe inazungumziwa kana kwamba uso wake ulikuwa mgumu kama jiwe. "kwa hiyo nina nia dhahiri"

kwa maana najua sitapatwa na aibu

Mtumishi huyu anatazama muda ujao kwa uhakika, salama katika wito wa Yahwe. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa maana najua ya kwamba maadui wangu hawataweza kunifanya nihisi aibu"

Isaiah 50:8

Taarifa ya Jumla

Mtumishi wa Yahwe anaendelea kuzungumza.

Nani atakayenipinga? Tusimame ... Nani mshtaki wangu? Na aje

Mtumishi anatumia maswali haya kusisitiza uya kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kumshtaki kwa haki kwa ubaya. "Kama mtu yeyote anaweza kunipinga, tusimame ... Kama mtu yeyote atanipinga, na aje"

Nani atanitamka kuwa na hatia?

Mtumishi anatumia swali hili kuweka uzito ya kwamba hakuna mtu wa kumtamka kuwa na hatia. "Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kunitamka kuwa na hatia"

watachakaa kama nguo; nondo utawala

Kule ktokuwa na mtu aliyesalia kumshtaki mtumishi kwa kuwa na hatia inazungumziwa kana kwamba washtaki walikuwa nguo ambazo hupwaya na huliwa na nondo.

Isaiah 50:10

Taarifa ya Jumla

Mtumishi anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Ni nani miongoni mwenu anamwogopa Yahwe? Ni nani anayetii sauti ya mtumishi wake? Ni nani anayetembea katika giza zito bila nuru? Anatakiwa ... Mungu wake.

Mtumishi anatumia maswali haya kuwatambua wale ambao anazugumza nao. "Kama mtu miongoni mwenu anamwogopa Yahwe na kutii sauti ya mtumishi wake, lakini anatembea katika giza zito bila nuru, basi anatakiwa ... Mungu wake"

anayetii sauti ya mtumishi wake

Hapa neno "sauti" linawakilisha kile mtumishiu anachosema. "kumtii mtumishi wake"

anayetembea katika giza zito bila nuru

Mtumishi anazungumzia watu ambao wanateseka na kuhisi kutojiweza kana kwamba walikuwa wakitembea katika sehemu ya giza sana. "anateseka na anajihisi kutojiweza"

tumaini katika jina la Yahwe na mtegemee Mungu wake

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja. Hapa neno "jina" linawakilisha Yahwe mwenyewe. Kumtumaini Mungu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kumuegemea yeye. "mtumaini Yahwe, Mungu wake"

Isaiah 50:11

nyie wote mnaowasha moto ... miale ambayo umeiwasha

Hii inaendeleza sitiari kutoka kwa mstari wa nyuma wa watu ambao hutembea gizani. Hapa watu wanaojaribu kuishi kulingana na hekima yao badala ya kumtumaini Bwana wanazungumziwa kana kwamba wamewasha moto wao na kubeba tochi ili kuona gizani.

utalala chini katika nafasi ya maumivu

Hapa "kulala chini" ina maana ya kufa. Kufa kwa maumivu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kulala chini katika nafasi ambayo watapitia maumivu. "utakufa kwa mateso makubwa"

Isaiah 51

Isaiah 51:1

Nisikilizeni mimi

Hapa neno "mimi" lina maana ya Yahwe.

Utazameni mwamba ... na kwa machimbo

Kutazama kitu inawakilisha kufikiria juu yake. "ninafikiria juu ya mwamba ... na machimbo"

mwamba ambao ulichongwa na kwa machimbo ambayo ulikatwa

Mungu anazungumza kuhusu taifa la Israeli kana kwamba lilikuwa jengo lililotengenezwa kwa mawe kana kwamba mababu zao walikuwa mwamba au machimbo ambayo Mungu aliwakata. Hi inaweza kuwekwa wazi. "mababu zako, ambao n kama mwamba ambao ulichongwa na machimbo ambayo ulikatwa"

mwamba ambao ulichongwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "mwamba ambao nilikuchonga"

ulichongwa

"kukata kwa patasi" au "kukata"

machimbo ambayo ulikatwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "machimbo ambako nimekukata"

Isaiah 51:2

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Abrahamu, baba yako

Mungu anazungumzia mababu zao kana kwamba alikuwa baba yao. "Abrahamu, babu yako" au "Abrahamu, mhenga wako"

Sara, aliyekuzaa

Mungu anazungumzia mke wa Abrahamu kana kwamba alikuwa mama yao na amewazaa wao. "Mke wa Abrahamu, Sara, ambao nyote ni vizazi vyake"

alipokuwa mtu binafsi

Hii ina maana pale alipokuwa bado hana watoto. Hii inaweza kuwekwa wazi. "alipokuwa hana watoto"

kumfanya kuwa wingi

Mungu anazungumzia uzao wa Abrahamu kuwa wengi kana kwamba Abrahamu alikuwa wingi. "alifanya uzao wake kuwa wengi" au "alimfanya kuwa na uzao mwingi"

Isaiah 51:3

Yahwe atafariji Sayuni

Mji wa Sayuni, ambao unaitwa Yerusalemu, hapa unawakilisha watu wa Sayuni. "Yahwe atafariji watu wa Sayuni"

atafariji maeneo yake yote yasiofaa

"atafarijii watu ambao wanashi katika maeneo yake yote yasiyofaa"

maeneo yake yasiofaa ... nyika zake ... jangwa lake tambarare

Neno "yake" ina maana ya Sayuni. Miji mara nyingi huzungumziwa kana kwamba ilikuwa wanawake.

maeneo yasiofaa

sehemu ambazo imeangamizwa

nyika yake alifanya kama Edeni, na jangwa lake tambarare ... kama bustani ya Yahwe

Misemo hii ina maana ya kwamba Mungu atafanya maeneno tupu ya israeli mazuri. Katika unabii, matukio ambayo yatatokea katika siku za usoni mara nyingi kufafanuliwa kama kuwa kipindi cha nyuma. Hii inasisitiza ya kwamba hakika yatatokea. "atafanya nyika zake kama Edeni na jangwa zake tambarare ... kama bustnai ya Yahwe.

shangwe na furaha zitapatikana ndani yake

Shangwe na furaha ina maana moja. Kukutwa kule ina maana ya kuwa kule. "kutakuwa na shangwe na furaha Sayuni tena"

Isaiah 51:4

Maelezo ya Jumla

Yahwe anazungumza na watu wa Israeli.

Kuwa msikivu kwangu ... nisikilizeni mimi

Misemo hii miwili ina maana moja. Kwa pamoja inaimarisha amri ya kusikiliza.

Nitafanya haki yangu kuwa mwanga kwa ajili ya mataifa

Hapa haki ya Mungu inawakilisha sheria yake, na mwanga unawakilisha maarifa ya kilicho sahihi. Hii ina maana watu wa mataifa wataelewa na kutii sheria ya Mungu. "sheria yangu utafundisha mataifa kilicho sahihi" au "mataifa watajua sheria yangu"

Haki yangu ipo karibu

Wazo la "karibu" inawakilisha "hivi karibuni". Haki ya Mung kuwa karibu inawakilisha yeye kuonyesha haki yake hivi karibuni. Atafanya hivi kwa kutimiza ahadi zake na kukomboa watu. "Hivi punde nitaonyesha haki yangu"

wokovu wangu utatoka nje

Mungu anazungumzia kuwaokoa watu kana kwamba wokovu wake ulikuwa kitu ambacho kinaweza kutoka nje kwao. "Nitaokoka watu"

mkono wangu utahukumu matafa

Hapa mkono wa Mungu unawakilisha nguvu yake, na kuhukumu inawakilisha utawala. "Nitatawala mataifa kwa nguvu yangu"

pwani

Hii ina maana ya watu ambao wanaishi katika pwani ya nchi za mbali kupita bahari. "watu amboo wanashi katika pwani" au "watu ambao wanaishi katiak nchi kupita bahari"

watasubiri kwa shauku kwa ajili ya mkono wangu

Hapa mkono wa Mungu unawakilisha kile atakachofanya. Hapa ina maana ya yeye kokoa watu. "watasubiri kwa shauku kwangu kufanya kitu" au "watanisubiri kwa shauku niwaokoe"

Isaiah 51:6

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Inua macho yako mbinguni

Kuinua macho inawakilisha kutazama kitu kilicho juu. "Tazama juu angani"

kama moshi ... kama vazi ... kama nzi

Zote hizi zina maana ya vitu ambavyo hutoweka kwa haraka na kirahisi au kutokuwa na thamani.

wokovu wangu utaendelea milele

"wokovu" wa Mungu hapa unawakilisha matokeo ya wokovu wake, ambayo ni uhuru. "Nitakuokoa, utakuwa huru milele"

haki yangu haitakoma kutumika

"haki" ya Mungu hapa inawakilisha yeye kutawala kwa haki. "utawala wangu wa haki hautakuwa na mwisho" au "nitatawala kwa haki milele"

Isaiah 51:7

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

ambao mna sheria yangu mioyoni mwenu

Kuwa na sheria ya Mungu moyoni inawakilisha kujua sheria ya Mungu na kutaka kuitii. "ambaye anajua na kuinua sheria yangu"

wala msivunjwe mioyo kwa matusi yao

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na usipoteze ujasiri wako watakapokuumiza"

Kwa maana nondo watawala kama vazi, na funza watawala kama sufu

Mungu anazungumzia watu kutukana wale ambao wana haki kana kwamba walikuwa mavazi ya sufu, na kuangamizwa kwao kana kwamba wadudu waliwala.

haki yangu itakuwa milele

"haki" ya Mungu hapa inawakilisha yeye kutawala kwa haki. "utawala wangu wa haki hautakuwa na mwisho" au "nitatawala kwa haki milele"

na wokovu wangu kwa vizazi vyote

"wokovu" wa Mungu hapa unawakilisha matokeo ya wokovu wake, ambayo ni uhuru. Kuwa "kwa vizazi vyote" inawakilisha kudumu milele. "Nitakuokoa, na utakuwa huru milele"

Isaiah 51:9

Amka, amka, jivike kwa nguvu, mkono wa Yahwe

Watu huuliza kwa haraka kwa mkono wa Yahwe kuwasaidia kana kwamba mkono wake ulikuwa mtu. Kama haiwi ajabu kuzungumza kwa mkono, hii inaweza kuwekwa moja kwa moja kwa Yahwe badala yake. "Amka, amka, Yahwe, na jivike mkono wako kwa nguvu"

Amka, amka ... mkono wa Yahwe

Watu wanazungumza kana kwamba mkono wa Yahwe ulikuwa umelala kwa sababu haukuwa unawasaidia. Wanautakaa uwasaidie. Neno "amka" linarudiwa kuonyesha ya kwamba wanahtaji msaada wa Mungu haraka.

jivike kwa nguvu

Nguvu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa aina ya nguo ambayo watu walivaa kujiimarisha vitani. "jiweke uwe na nguvu"

Je! sio wewe uliyemponda jitu wa baharini, wewe uliyemchoma joka?

Msemaji anatumia swali kusisitiza nguvu ya Yahwe kufanya mambo makuu. "Ni wewe ambaye ulimponda jtu wa bahari, wewe ambaye alimchoma joka"

jitu wa bahari ... joka

Zote hizi zina maana moja. Zina maana ya Rahabu, nyoka wa kimithiolojia ambaye anaishi baharini, ambayo inaweza kuashiria taifa la Misri au kuashiria uovu na machafuko.

Je! si wewe uliyekausha bahari ... kwa ajili ya waliokombolewa kupita katikati?

Tena, msemaji anatumia maswali kusisitiza nguvu ya Yahwe kufanya mambo makuu. Hii ina maan Yahwe kufungua Bahari ya Shamu kwa Waisraeli kuvuka na kutoroka jeshi la Misri. "Ulikausha bahari ... kwa ajili ya waliokombolewa kupita katikati".

Isaiah 51:11

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Waliokombolewa wa Yahwe

"kukomboa" ina maana ya "kuokoa". Hii ina maana ya watu ambao Yahwe aliwaokoa. "Wale ambao Yahwe aliwaokoa"

kwa furaha milele juu ya vichwa vyao

Hii inatumia kichwa cha mtu kumaansha mtu kwa ukamilifu. "watakuwa na furaha milele"

furaha na shangwe ... huzuni na majonzi

Maneno "shangwe" na "furaha" yana maana moja, kama vile "huzuni" na "majonzi". Kwa pamoja yanasisitiza ukali wa hisia hizi.

furaha na shangwe zitawapita

Hii inazungumzia watu kuzidiwa na furaha na shangwe kwa kuzipatia hisia hizi sifa za binadamu za kuwa na uwezo wa kumpita mtu. "watazidiwa kabisa na shangwe na furaha" au "watakuwa na furaha na shangwe kabisa"

huzuni na maombolezo zitatoweka

Hii inazungumzia watu kutokuw na huzuni na majonzi tena kwa kuzungumza juu ya hisia hizi kana kwamba zinaweza kutoroka. "hawatakuwa na huzuni na maombolezo tena"

Isaiah 51:12

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Mimi, mimi, ndiye yeye

Neno "Mimi" inarudiwa kwa msisitizo.

Kwa nini unawaogopa wanadamu ... kama nyasi?

Swali hili la balagha linasisitiza ya kwamba watu ambao wana ulinzi wa Mungu wanatakiwa kutowaogopa wanadamu. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Usiogope wanadamu ... kama nyasi"

ambao wametengezwa kama nyasi

Msemo huu unalinganisha wanamume na nyasi kusisitiza ya kwamba maisha yao ni mafupi na kwamba wanakufa upesi. "ambao wanaishi na kufa haraka kama nyasi" au "ambao watanyauka na kutoweka kama nyasi"

ambao wametengezwa kama

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambao ni kama"

Isaiah 51:13

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Kwa nini mmemsahau Yahwe ... dunia?

Yahwe anatumia swali kusisitiza ya kwamba hawatakiwi kumsahau Yahwe. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Haukutakiwa kuwa umemsahau Yahwe ... dunia"

Muumba

Muumba wa mbingu na nchi

aliyezinyosha mbingu

"aliyeinyosha anga". Hii inazungumzia Yahwe kuumba mbingu kana kwamba alikuwa amenyosha kwa njia moja anavyosha vazi kubwa. "ambaye alinyosha mbingu kama vazi"

misingi ya dunia

Neno "msingi" kawaida lina maana ya maumbo ya mawe ambayo hutoa mhimili kwa jengo kutoka chini. Hapa inafafanua umbo linalofanana ambalo inasadikiwa kuwa mhimili na kushikilia dunia katika nafasi yake.

ghadhabu ya moto ya mkandamizaji anapoamua kuangamiza

"ghadhabu ya moto ya mkandamizaji atakapoamua kusababisha uharibifu"

ghadhabu ya moto

Hapa neno "moto" lina maana ya "imara" au "kuu". "ghadhabu kuu"

Iko wapi ghadhabu ya mkandamizaji?

Yahwe anatumia swali kusisitiza ya kwamba watu wanapaswa kutoogopa wale ambao wanataka kuwakandamiza. Wakandamzaji wao sio tishio kwao tena. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Ghadhabu ya mkandamizaji sio tishio"

Isaiah 51:14

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Yule ambaye ameinamishwa chini

Hii ina maana ya watu wa Israeli ambao ni watumwa wa Babeli. Msemo huu unafafanua namna wanvyofanya kazi. "Mtumwa"

shimo

Hii ina maana ya Kuzimu. "shimo la kuzimu" au "kaburi"

wala hatapungukiwa mkate

Hapa "mkate" unawakilisha chakula kwa ujumla. Hii inaweza kuandikwa kwa hali ya chanya. "wala atakuwa bila chakula"

ambaye huvurugavuruga bahari

Hii inazungumzia Yahwe kusababisha bahari kusogea na mawimbi kuinuka na kuanguka kana kwamba alikuwa akikoroga bahari kama mtu anavyokoroga ujazo wa bakuli kwa kijiko kikubwa. "ambaye anasababisha bahari kuvurugwa" au "ambaye hufanya bahari kusogea juu na chini"

mawimbi yake yaungurume

Muungurumo ni sauti ya juu ya nguvu unayofanywa na kitu chenye uhai, kama vile dubu au simba. Hapa mawimbi yanaelezwa kama kutengeneza sauti ya nguvu. "mawimbi huanguka kwa sauti"

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli.

Isaiah 51:16

Nimeweka maneno yangu kinywani mwako

Hii inazungumzia Yahwe kumwambia Isaya anachotakiwa kusema kana kwamba maneno yake yalikuwa chombo halisi. Yahwe aliweka kinywani mwa Isaya. "Nimekwambia nini cha kusema"

Nimekufunika katika kivuli cha mkono wangu

"mkono" wa Yahwe una maana ya nguvu. Hii inazungumzia Yahwe kumlinda Isaya kana kwamba mkono wake ulikuwa umemfunika kumlinda. "nguvu yangu imekuweka salama" au "Nimekulinda na kukuweka salama"

ili kwamba nipande mbingu

Neno "panda" ina maana ya kuimarisha kitu ardhini. Hapa Yahwe kuimarisha mbingu inazungumziwa kana kwamba mbingu ilikuwa hema ambalo lingesambaa na kuwekwa imara kwa kigingi cha hema. "ili niweze kuimarisha mbingu"

kutandaza misingi ya dunia

Neno "msingi" kawaida lina maana ya maumbo ya mawe ambayo hutoa mhimili kwa jengo kutoka chini. Hapa inafafanua umbo linalofanana ambalo inasadikiwa kuwa mhimili na kushikilia dunia katika nafasi yake.

Isaiah 51:17

Amka, amka, simama, Yerusalemu

Hapa "Yerusalemu" inawakilisha watu wanaoishi pale. Yahwe anazungumzia watu wa Yerusalemu kana kwamba walikuwa wakimsikiliza. "Amka, amka, simama, nyie watu wa Yerusalemu"

Amka, amka, simama

"Uwe tayari na inuka". Kurudia kwa neno "amka" linasisitiza uharaka wa wito kuamsha watu wa Israeli. Hautumiki kuwaamsha kutoka usingizi halisi.

wewe ambaye umekunywa kutoka katika mkono wa Yahwe ... kutoka katika kikombe cha kupepesuka

Yahwe anazungumzia kuwaadhibu watu wake kana kwamba alikuwa amewalazimisha kunywa kutoka katika bakuli ambalo lilijazwa na hasira yake. Na walipokunywa bakuli la hasira yake, walipepesuka kana kwamba walikunywa mvinyo mwingi.

chini mpaka kwenye masimbi

Neno "masimbi" lina maan ya vipande vya chini ya chombo ambacho kinywaji kilkuwemo. "mpaka chini kabisa"

kutoka katika mkono wa Yahwe

Hapa Yahwe anamaanishwa kwa mkono wake kusisitiza ya kwamba yeye ndiye aliyetoa bakuli kwa watu wake. "ambayo alikupatia"

katika kikombe cha kupepesuka

"kutoka katika kikombe ambacho kimesababisha upepesuke kana kwamba ulilewa kwa mvinyo"

kupepesuka

kutotembea wiima, au kujikwaa akiwa anatembea

Hakuna mtu ... wa kumuongoza; hakuna mtu ... kumchukua kwa mkono

Vishazi hivi viwili vina maana moja na vinaweza kujumlishwa. Hii inazungumzia Yerusalemu kutojiweza kana kwamba mji uliikuwa mwanamke mlevi bila mtoto wa kumsaidia kutembea kwa usalama. "Hauna mtu wa kukusaidia! Wewe ni kama mwanamke mzee aliyelewa asiye na mwana kumchukua kwa mkono na kumuongoza"

Isaiah 51:19

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

ni nani atasikitika pamoja na wewe? ... Nani atakufariji?

Isaya anatumia maswali kusisitza ya kuwa sasa hakuna mtu wa kulia pamoja nao au kuwafariji. Maswali haya yanweza kuandikwa kama kauli. "lakini hakuna mtu wa kulia pamoja nawe ... Hakuna mtu w kukufariji"

Shida hizi mbili

Shida hizi mbili zina maana ya "ukiwa na uharibifu" na "njaa na upanga".

ukiwa na uharibifu

Maneno haya yana maana moja na husisitiza uharibifu wa nchi unaosababishwa na jeshi pinzani. "adui zako wameacha miji tupu na kuharibiwa"

njaa na upanga

Maneno "njaa" na "upanga" yanafafanua shida ambazo zitakuja juu ya watu. "Upanga" una maan ya "vita". "wengi wenu mmekufa kutokana na njaa na vita"

wanalala katika kila kona ya mtaa

Huu n ujumla, ambayo ina maana ya watoto wengi watalala mitaani, lakini sio katika kila kona ya mtaa. "wanalala mtaani"

kama paa ndani ya wavu

Hii inazungumzia watoto kuchoka sana na kutojiweza kana kwamba walikuwa paa waliokamatwa katika mtego. "hawajiwezi, kama paa aliyeshikwa katika wavu" au "kutojiweza kama paa aliyetegwa"

paa

Huyu ni mnyama, anayefanana na mbawala, ambaye ana pembe na hukimbia haraka sana.

wamejaa hasira ya Yahwe, karipio la Mungu wako

"hasira ya Yahwe" ina maana ya Yahwe kuadhibu watu wake kwa sababu ya hasira yake dhidi yao. Hii inazungumzia watu kuadhibiwa sana kana kwamba wamejaa hasira ya Yahwe. Pia, neno "karipia" linaweza kuandikwa kama kitenzi. "wameahibiwa sanana Yahwe kwa sababu alikuwa na hasira sana kwao na kuwakaripia"

Isaiah 51:21

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

wewe uliyekandamizwa na wewe uliyelewa

Yahwe anatumia neno "uliyekandamizwa" hapa kumaanisha watu wote waliokandamizwa. "nyie watu mliokandamizwa na walevi"

wewe uliyelewa, lakini sio ulevi wa mvinyo

Hii inazungumzia watu kujifanya wamelewa kwa sababu wanateseka kana kwamba wamelewa kwa kulazimishwa kunywa bakuli ya hasira y Yahwe. "wewe ambaye umelewa kwa kunywa mvinyo wa bakuli la hasira ya Yahwe" au "wewe unayejifanya umelewa, kwa sababu umeteseka sana"

Tazama, nimechukua kikombe cha kupepesuka kutoka mkononi mwako - bakuli, ambalo ni kikombe cha hasira yangu - ili kwamba

Hii inazungumzia Yahwe kutokuwa na hasira na watu wake kana kwamba hasira yake likuwa ujazo wa kikombe ambacho alikuwa akikichukua kutoka kwao. "Sitakuwa na hasira na wewe tena. Tazama, ni kana kwamba nimechukua kutoka kwako kikombe kilichokufanya upepesuke, yaani, kikombe ambacho kilijaa hasira yangu, ili kwamba"

Tazama

Hii ni lahaja inayotumika kuvuta nadhari ya msikilizaji kwa kile kinachosemwa baadaye. "sikiliza"

kikombe cha kupepesuka

Neno "kikombe" ina maana ya kile kilicho ndani ya kikombe. "kikombe cha divai ambacho huwafanya watu wapepesuke"

bakuli, ambalo ni kikombe cha hasira yangu

Yahwe anazungumza kuwaadhibu watu kana kwamba aliwalazimisha kunywa kutoka katika bakuli ambalo lilijazwa hasira yake. "bakuli ambalo lilijazwa hasira yangu" au "kikombe ambacho kilijazwa hasira yangu"

Isaiah 51:23

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Nitakiweka katika mkono wa msumbufu wako

Hii inazungumzia Yahwe kuwaadhibu adui zake kana kwamba alikuwa akienda kuwalazimisha kunywa kutoka katika kikombe kilichojaa hasira yake.

Nitakiweka katika mkono wa msumbufu wako

Inadokezwa ya kwamba kwa kuweka kikombe cha hasira yake katika mkono wao Yahwe atakuwa anawalazimisha kunywa kile kilicho katika kikombe. "Nitawalazimisha wasumbufu wako kunywa kutoka katiika mvinyo wa bakuli la hasira yangu"

msumbufu wako

Neno "wasumbufu" inaweza kuelezwa kwa kitenzi. "wale ambao wamekusumbua" au "wale ambao wamekusababisha kuteseka"

ulifanya mgongo wako kama ardhi na kama mitaa kwa ajili yao kutembea juu

Hii inalinganisha namna adui zake walitembea juu ya migongo yao kwa namna watu wanavyotembea juu ya mitaa. "unalala katika mitaa ili maadui zako waweze kutembea juu ya migongo yako"

Isaiah 52

Isaiah 52:1

Amka, amka

Neno hili linarudiwa kwa msisitizo na kuonyesha uharaka. Isaya kujaribu kuamsha watu inazungumziwa kana kwamba alikuwa akijaribu kuwaamsha kutoka usingizini.

vaa nguvu yako

Kuwa na nguvu tena inazungumziwa kana kwamba nguvu ilikuwa mavazi ambayo mtu huvaa. "uwe na nguvu"

Sayuni ... Yerusalemu

Zote hizi zina maana ya watu ambao huishi katika Yerusalemu. Isaya anazungumzia watu kana kwamba walikuwa wakimsikiliza. "watu wa Sayuni ... watu wa Yerusalemu"

asiyetahiriwa au mchafu

Vivumishi vidogo vinaweza kuwekwa kama vivumishi. "Wale ambao hawajatahiriwa au wale ambao sio wasafi"

wachafu

Hii ina maana ya watu wachafu. Mtu ambaye Mungu humchukulia kutokubalika kiroho au kunajisiwa inazungumziwa kana kwamba mtu alikuwa mchafu kimwili. "wale ambao hawakubaliki kwa Mungu"

ataingia kwako

Hapa "kwako" ina maana ya Yerusalemu ambayo inawakilisha watu wanaoishi pale. Inaeleweka ya kwamba wasiotahiriwa na watu wachafu wataingia katika mji kuwashambulia watu. Maneno ambayo hayapo yanaweza kuongezwa kufanya maana wazi. "ingia mji wako kukushambulia"

Isaiah 52:2

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Jikung'ute kutoka mavumbini; amka na ukae, Yerusalemu

Hapa "Yerusalemu" inawakilisha watu wanaoishi kule. "Watu wa Yerusalemu, simama wima na ukung'ute uchafu kutoka kwako"

ondoa mnyororo kutoka shingoni mwako, mfungwa

Inaonyeshwa ya kwamba watu wa Yerusalemu walikuwa wakivaa minyororo kwa sababu walikuwa watumwa walipokuwa uhamishoni Babeli. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi.

binti Sayuni

Hii ni lahaja. "binti" wa mji ina maana watu wa mji ule. "watu wa Sayuni" au "watu ambao wanaishi Sayuni"

Uliuzwa bure, na utakombolewa bila fedha

Hii inazungumzia kuhusu Yahwe kana kwamba alikuwa mmiliki wa watu wa Israeli. Kwa kuwa ni mmiliki halali anaweza kuwatoa au kuwarudisha atakavyotaka. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. :Nimekuuza bure, na nitakukomboa bila fedha"

Isaiah 52:4

Hapo mwanzo

Hapa "mwanzo" ina maana ya mwanzo wa historia ya Israeli walipoanza kuwa watu.

walikwenda chini mpaka Misri

"walikwenda mpaka Misri". Ilikuwa kawaida kutumia msemo "kushuka chini" pale inapozungumziwa kusafiri kutoka Kaanani mpaka Misri.

Ashuru imewakandamiza

Ashuru ina maana ya watu wa Ashuru. "watu wa Ashuru wamewatendea vibaya"

Isaiah 52:5

Basi sasa nina nini hapa ... kuona ya kwamba watu wangu wanachukuliwa bure?

Yahwe anatumia swali kufanya watu kuzingatia kwa makini kile anachotaka kusema. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriiwa kama kauli. "Basi sasa tazama kile kinachotokea ... watu wangu wanachukuliwa tena bure"

nina nini hapa - hili ni tamko la Yahwe - kuona

Maana zaweza kuwa 1) Yahwe anasema, "hili ni tamko la Yahwe". "Ninalo hapa - hiki ndicho kile nachotamka- kuona" au 2) Isaya anasema, "Hili ni tamko la Yahwe". "Ninalo hapa, anatamka Yahwe, "kuona"

kuona ya kwamba watu wangu wanachukuliwa bure

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Ninaona adui akichukua watu wangu bure"

bure

Maana zaweza kuwa 1) "bure" ina maana Wababeli walichukua watu bila haki na bila sababu au 2) hii inaendelea sitiari kutoka 52:2 ambapo Yahwe anazungumziwa kana kwamba alimiliki watu wa Israeli na anaweza kuwatoa bure.

Wale wanaotawala juu yao wanadhihaki

Hii ina maana ya Wababeli ambao wamewashinda watu. Hata hivyo, baadhi ya tafsiri zina, "Wale ambao hutawala juu yao wanalia". Kwa tafsiri hizi, kipande hiki kina maana ya viongozi wa Waisraeli walio katika kifungo.

jina langu linakashifiwa mfululizo siku nzima

Hapa "jina" inawakilisha sifa ya Yahwe. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wale ambao hutazama aduii akichukua watu wangu wanaendelea kusema mambo mabaya juu yangu"

Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu

Hapa "jina" inawakilisha sifa ya Yahwe. "Kwa hiyo watu wangu watanijua mimi ni nani kiukweli"

Isaiah 52:7

Maelezo ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Israeli

Jinsi iliivyo mizuri juu ya milima ni miguu ya wajumbe wanaoleta habari njema

Hapa "miguu" inawakilisha mjumbe ambaye anatembea. "Ni vizuri kuona mjumbe akija juu ya milima kutangaza habari njema"

kwa Sayuni

Hapa "Sayuni" inawakilisha watu wa Sayuni. "kwa watu wa Sayuni"

paza sauti zao

Hii ni lahaja. "paza sauti"

kila jicho lao

Hapa "macho" yanawakilisha mtu mzima. "kila mmoja wao"

Isaiah 52:9

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

enyi uharibifu wa Yerusalemu

Isaya anazungumzia uharibifu wa Yerusalemu kana kwamba ulikuwa mtu ambaye angeweza kushangilia. Hii inawakilisha watu wa Yerusalemu ambao walishindwa. "nyie watu ambao mnaishi miongoni mwa uharibifu wa Yerusalemu"

amemkomboa Yerusalemu

Hapa "Yerusalemu" inawakilisha watu. "amewakomboa watu wa Yerusalemu"

amafunua mkono wake mtakatifu

Hapa "mkono" inawakilisha nguvu ya Yahwe. Yahwe kuonyesha watu wote wa mataifa ya kwamba ni mtakatifu na mwenye nguvu inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa shujaa aliyetoa joho lake, kufunua mikono yake kwa ajili ya vita. "alionyesha utakatifu wake na nguvu yake kuu"

mataifa yote; dunia yote

Hapa "mataifa" na "dunia" inawakilisha watu wa mataifa yote katika dunia yote.

Isaiah 52:11

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Ondoka, ondoka

Neno hili linarudiwa kusisitiza ya kwamba watu wanapaswa kuondoka haswa, ingawa sio mara hiyo hiyo.

Ondoka kutoka hapa

Inachukuliwa kuwa watu wa Israeli walikuwa watumwa wa Babeli. Hii naweza kuwekwa wazi. "ondoka kutoka katika nchi ambapo ni mtumwa"

usiguse chochote kichafu

Kitu ambacho Yahwe amesema hakifai kuguswa au kuliwa inazungumziwa kana kwamba kilikuwa kichafu kimwili. "usiguse kitu ambacho hakikubaliki kwa Yahwe"

ondoka miongoni mwake

Hapa "mwake" inawakilisha Babelii

Yahwe atakwenda mbele yako; na Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi wako wa nyuma

Yahwe kulinda watu wake kutoka kwa maadui inazungumziwa kana kwamba alikuwa hodari ambao huondoka mbele ya watu na hodari wanaobakii nyuma ya watu kuwalinda.

Isaiah 52:13

atakuwa juu na kuinuliwa, na atainuliwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Misemo hii miwili "juu na kiinuliwa juu" na "atainuliwa" ina maana moja na inasisitiza ya kwamba Yahwe ataheshimu mtumishi wake. "Nitampa mtumishi wangu heshima kubwa"

walivyokuogopa wewe

Hapa "wewe" ina maana ya mtumishi wa Yahwe. Hata hivyo, watafsiri wanaweza kubadili "wewe" kuwa "yeye".

muonekano wake uliharibiwa sana kuliko ule wa mtu yeyote

Inachukuliwa ya kwamba mtumishi anaharibiwa kwa sababu adui walimpiga sana. Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "adui zake hupiga mwili wake vibaya sana hadi hakuonekana kama binadamu tena"

Isaiah 52:15

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya mtumishii wake.

mtumishi wangu atanyunyizia mataifa mengi

Mtumishi kusababisha watu wa mataifa kukubaliika kwa Yahwe inazungumziwa kana kwamba mtumishi alikuwa kuhani anayenyunyizia damu ya sadaka kufanya mtu au kitu kukubalika kwa Yahwe.

atanyunyizia

Neno la Kiebrania lilitafsiriwa "kunyunyizia" hapa linaweza kutafsiriwa kama "mshangao" au "shtusha", ambavyo baadhi ya tafsiri za Biblia hufanya.

mataifa mengi

Hapa "mataifa" yanawakilisha watu wa mataifa.

wafalme watafunga midomo yao

Msemo "kufunga midomo yao" ni lahaja. "wafalme wataacha kuzungumza" au "wafalme watakaa kimya"

kile ambacho hawakuambiwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kile ambacho hakuna mtu alichowaambia" au "kitu ambacho hakuna mtu alichowaambia"

Isaiah 53

Isaiah 53:1

Maelezo ya Jumla

Hapa Isaya anafafanua matukio ambayo yatatokea katika siku za usoni kana kwamba yametokea kipindi cha nyuma. Hii inasisitiza ya kwamba yatatokea hakika.

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua mtumishi wa Yahwe.

Ni nani aliyeamini kile walichosikia kutoka kwetu

Kile ambacho Yahwe amegundua ni ajabu sana hadi anashangaa kama walio uhamishoni wataamini. "walichosikia" inajumlisha yeye na wale walio uhamishoni. "Ni vigumu kw yeyote kuamini kile alichosikia"

na ni kwa nani mkono wa Yahwe umefunuliwa?

Mkono una maana ya nguvu ya Yahwe. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na Yahwe amefunua nguvu yake kwa watu"

Kwa maana alikua mbele ya Yahwe kama mti mchanga

Hapa "alikua" ina maana ya mtumishi wa Yahwe ambaye Isaya anamlinganisha na mti mchanga sana. Hii inasisitiza ya kwamba ataonekana dhaifu.

kutoka katika nchi iliyokauka

"nchi iliyokauka" ni ardhi ngumu na iliyokauka ambayo hairuhusu mimea kuota na inawakilisha wapi mtumishi wa Yahwe atakuja. "kutoka katika hali isiyowezekanika"

Isaiah 53:3

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kufafanua mtumishi wa Yahwe.

Alidharauliwa na kukataliwa na watu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu walimchukulia kuwa si kitu na kumkataa"

mtu mwenye huzuni

"mwanamume ajuaye kila aina ya huzuni"

kwa watu ambao huficha nyuso zao

"Uso" inawakilisha dhamira ya mtu au jumuiya. Kuficha uso wa mtu kugeuka kutoka kwa mtu. "kwa watu ambao wanageuka"

alidharauliwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "walimchukulia kutokuwa na thamani"

Isaiah 53:4

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kumfafanu mtumishi wa Yahwe.

amechukua ugonjwa wetu na kubeba huzuni zetu

"Kuchukua" au kubeba usahaulifu kama ugonjwa na huzuni inawakilisha kuuchukua. "amechukua ugonjwa wetu na huzuni juu yake mwenyewe"

ingawa tulidhani ya kuwa aliadhibiwa na Mungu, alipigwa na Mungu, na kuteswa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ingawa tulidhani Mungu alikuwa akimuadhibu na kumtesa"

Isaiah 53:5

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kumfafanua mtumishi wa Yahwe.

Lakini alitobolewa kwa sababu ya matendo yetu ya uasi; alipondwa kwa sababu ya dhambi zetu

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza ya kwamba mtumishi aliteseka kwa sababu ya dhambi za watu. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu aliwaruhusu maadui kumchoma na kumua kwa sababu ya dhambi zetu"

Adhabu kwa ajili ya amani yetu ilikuwa juu yake

Hii ina maana ya amana na Mungu. Hii inaweza kuwekwa wazi. "Alipokea adhabu hii ili tuweze kuishi katika upatanifu"

kwa majeraha yake tunaponywa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "alituponya kwa mateso ya majeraha yake"

Isaiah 53:6

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kumfafanua mtumishi wa Yahwe.

Sisi wote kama kondoo wamepotoka

Kondoo mara kw mara huacha njia ambayo mchungaji huwaongoza. Isaya ana maana ya kwamba tunafanya kile tunachotaka badala ya kile Mungu anavyoamuru.

udhalimu wetu wote

"Udhalimu" hapa unawakilisha hatia kwa ajili ya dhambi yetu. "hatia kwa ajili ya dhambi ya kila mmoja wetu"

Isaiah 53:7

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kumfafanua mtumishi wa Yahwe.

Alikandamizwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Walimtendea kwa ukatili"

hakufungua kinywa chake

"Kinywa" inawakilisha kile ambacho mtu husema. Kufungua kinywa cha mtu ina maana ya kuongea. "hakupinga"

kama mbuzi ambaye huongozwa machinjioni, na kama kondoo aliye mbele ya wakata manyoya alivyo mtulivu

Isaya analinganisha mtumishi kwa mbuzi na kondoo kusisitiza ya kwamba atabaki kimya wakati watu wakimdhuru na kumuaibisha.

kama mbuzii ambaye huongozwa machinjioni

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kama mbuz alivyo kimya mtu anapomchinja"

Isaiah 53:8

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kumfafanua mtumishi wa Yahwe.

Kwa kuonewa na kuhumiwa alishutumiwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Walimtendea kwa ukatili, wakamhukumu, na wakamshutumu"

kuonewa

Neno la Kiebrania linatafsiriiwa hapa kama "kuonewa" na baadhi ya tafsiri kama "kukamata". Kwa tafsiri hizi, wazo ni kuwa Mtumishii atakamatwa na kisha kuhukumiwa na kushutumiwa.

nani kutoka kizazi hicho alimfikiria tena juu yake?

Swali hili linasisitiza ya kwamba hakuna mtu anayemfikiria. "hakuna mtu kutoka kizazii chake aliyejali nini kilitokea kwake" au "hakuna mtu kati ya walioishi naye walijali nini kilitokea kwake"

nani kutoka kizazi hicho alimfikiria tena juu yake?

Tafsiri nyingi zinatafsiri sehemu hii kwa Kiebrania tofauti. "Nani anaweza kusema jambo juu ya uzao wake? au "Nani anaweza kusema kitu kuhusu hatma yake?"

lakini aliondolewa kutoka katika nchi ya walio hai

"Kuondolewa" hapa ina maana ya kifo. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Lakini alikufa" au "Lakini kifo kikamchukua"

ya watu wangu

"ya watu wa Israeli"

wala hapakuwa na udanganyifu katika kinywa chake

"Kinywa" inawakilisha kile mtu anachosema. "wala hakumdanganya yeyote alipozungumza"

Isaiah 53:10

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kumfafanua mtumishi wa Yahwe.

ataona uzao wake

Hapa "uzao" una maana ya wale watu ambao Yahwe amewasamehe kwa sababu ya sadaka ya mtumishi.

atarefusha maisha yake

Hii inazungumzia kumfanya aishi kwa muda zaidi. "Yahwe atamfanya mtumishi wake kuishi tena"

kusudi la Yahwe litatimizwa kupitia kwake

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atatimiza kusudi lake kupitia mtumishi wake"

Baada ya mateso ya maisha yake

Hapa "maisha yake" ina maana ya mtumishi. "Baada ya mtumishi kuteseka"

ataona nuru

tafsiri nyingi zinaelewa "nuru" hapa kumaanisha uhai. Yaani, mtumishi atakuwa hai tena.

Mtumishi wangu mtakatifu

Hapa "wangu" ina maana ya Yahwe

atabeba udhalimu wao

"kubeba" hapa ina maana ya kubeba na inawakilisha mtumishi wa Yahwe kuchukua hatia ya dhambi yao. "atachukua hatia yao juu yake mwenyewe"

Isaiah 53:12

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kumfafanua mtumishi wake.

Kwa hiyo nitampatia sehemu yake miongoni mwa makundi, na atagawanya marupurupu na wengi

Vishazi hivi viwili vina maana moja. "Sehemu" na "marupurupu" ina maana ya mfalme baada ya ushindi vitani kugawanya vitu vilivyotekwa nyara au zawafi na jeshi lake. Hii ina maana Mungu atamheshimu sana mtumishi wake kwa sababu ya sadaka yake.

makundi

Tafsiri nyingi inatafsiri msemo huu kama "wengi" au "wenye nguvu"

kwa sababu alijiweka wazi kwa kifo

"Kujiweka wazi" ina maana ya kuwa wazi au hatarishi. Mtumishi wa Yahwe alijiweka katika hali ambayo angeweza kufa. "alikubali kwa hiari uwezekano wa kifo"

na alihesabiwa na wavunja sheria

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na kuruhusu watu kumtendea kama mhalifu"

Isaiah 54

Isaiah 54:1

wewe mwanamke tasa ... watoto wa mwanamke aliyeolewa

Yahwe kuwaambia watu wa Yerusalemu kufurahi kwa sababu kutakuwa na watu wengi wakiishi katika Yerusalemu tena inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa akimwambia mwanamke tasa atakwenda kuwa na watoto wengi.

imba kwa shangwe ya furaha na kulia kwa sauti, wewe ambaye hujawahi kuwa katika uchungu

Kauli hii ina maana moja na sehemu ya kwanza ya sentensi.

Kwa maana watoto wa mwenye ukiwa ni zaidi

Tukio ambalo litatokea katiika siku za usoni linazungumziwa kana kwamba limetokea kipindi cha nyuma. Hi inasisitiza ya kwamba tukio hakika litatokea. "Kwa maana watoto wa mwanamke mwenye ukiwa atakuwa zaidi"

mwenye ukiwa

Hapa "mwenye ukiwa" ina maana mume wa mwanamke alimkataa na kumuacha.

Isaiah 54:2

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

Fanya hema lako kubwa ... imarisha vigingi vyako

Hii inaendeleza sitiari ambayo ilianza katika 54:1. Yahwe kuwaambia watu wa Yerusalemu kuandaa kwa sababu Yahwe ataongeza watu wake inazungumziwa kana kwamba anamwambia mwanamke kufanya hema lake kubwa kutengeneza chumba kwa ajili ya watoto wengi.

Kwa maana utasambaa

Hapa "utatawanyika" ni umoja na ina maana ya mwanamke tasa. Anawakilisha vizazi vyake vyote. "Kwa maana wewe na vizazi vyako mtasambaa kote"

vitatawala mataifa

Hapa "mataifa" yanawakilisha watu. "watawashinda watu w mataifa mengine"

Isaiah 54:4

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

utasahau aibu ya ujana wako na fedheha ya kutelekezwa kwako

Yahwe kuwaambia watu ambao wapo katika siku za usoni kuwa hata hawatafikiri juu ya aibu waliyopitia pale adui zao walipowashinda inazungumziwa kana kwmba Yahwe alikuwa akimwambia mwanamke ya kwamba hatafikiri tena juu ya aibu aliyopitia kwa kutoweza kupata watoto na mume wake kumtelekeza.

Isaiah 54:5

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

Kwa maana Muumba wako ni mume wako

Yahwe kuwapenda na kuwatunza watu wake inazungumziwa kana kwamba alikuwa mume wao.

Muumba

Muumba wa watu.

Yahwe wa majeshi

Yahwe wa majeshi ya Israeli.

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

Mkombozi

Mkombozi wa Israeli

anaitwa Mungu wa ulimwengu wote

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "yeye ni Mungu wa dunia nzima"

Yahwe amekuita tena kama mke ... kama mwanamke aliyeolewa kijana na kukataliwa

Yahwe kuwatuma watu wake katika uhamisho na kisha kuwarudisha inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa mume ambaye alimkataa mke wake lakini sasa anampokea.

na kuhuzunika rohoni

Hapa "roho" inawakilisha kiumbe cha ndani cha mtu. "na kuhuzunishwa" au "na kuwa na huzuni"

Isaiah 54:7

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

Katika hasira iliyofurika

Yahwe kuwa na hasira sana inazungumziwa kana kwamba hasira yake ilikuwa mafuriko ambayo yanawazidi watu. "Nilipokuwa na hasira sana"

Nimeficha uso wangu kutoka kwako

Hapa "kuficha uso wangu" ni lahaja ambayo ina maana ya Mungu kutelekeza watu wake na kuwaacha wateseke. "Nilikutelekeza"

lakini kwa agano la uaminifu la milele

Nomino dhahania "uaminifu" inaweza kuwekwa kama "mwaminifu". "lakini kwa sababu mimi ni mwaminifu siku zote kwa agano langu na wewe" au "lakinii kwa sababu mimi ni mwaminifu kufanya kile nilichoahidi kufanya"

anasema Yahwe, ambaye anakuokoa wewe

Hapa Yahwe anazungumzia juu yake katiika mtu wa tatu. Inaweza kuwekwa katika mtu wa kwanza. "hivi ndivyo mimi, Yahwe, mkombozi wako, nasema kwako"

Isaiah 54:9

maji ya Nuhu

Hii ina mana ya mafuriko ambayo Yahwe alisababisha wakati wa kipindi cha Nuhu.

Ingawa milima inaweza kuanguka na vilima kutikiswa, bado upendo wangu wa kudumu

Yahwe anafafanua hali ya kubuni kufafanua kile kitakachotokea hata kama masharti yalifiikiwa. "Hata kama milima ilianguka na vilima kutetemeka, upendo wangu wa kudumu"

vilima kutikiswa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "vilima vinaweza kutikisika"

upendo wangu wa kudumu hautageuka kutoka kwako

Yahwe kuendelea kuwapenda watu wake inazungumziwa kana kwamba upendo wake hautaweza kugeuka kutoka kwa watu. "sitaacha kukupenda"

wala agano langu la amani kutikiswa

Yahwe kutofutilia agano lake na watu inazungumziwa kana kwamba agano lake lilikuwa chombo ambacho kinaweza kutikisika. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na sitafuta agano langu la amani" au "na kwa hakika nitakupa amani kama nilivyoahidi katika agano langu"

anasema Yahwe, ambaye ana rehema juu yako

Hapa Yahwe anazungumza juu yake katika utatu. Inaweza kuwekwa katika mtu wa kwanza. "hivyo ndivyo mimi, Yahwe, nayetenda kwa rehema, nasema"

Isaiah 54:11

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

Aliyeteswa

Hapa Yahwe anazungumzia mji wa Yerusalemu kana kwamba ulikuwa ukimsikiliza. Hapa Yerusalemu inawakilisha watu ambao wanaishi pale. "nyie watu mlioteswa wa Yerusalemu"

aliyeendeshwa kwa dhoruba

kuendeshwa Yahwe anazungumzia watu kana kwamba walipulizwa na kuharibiwa kwa upepo na dhoruba. Hii ina maana ya watu kuumizwa na kukosa uthabiti.

asiyefarijika

"bila faraja"

Nitatengeneza njia yako ya miguu katika rangi ya feruzi ... ukuta wa mawe mazuri

Yahwe anafafanua katika maneno ya kiufundi jinsi atakavyorejesha Yerusalemu na kusababisha iwe nzuri tena. Ingawa lugha inaweza kukuzwa.

feruzi ... johari... rubi

Hivi ni vito vya thamani. Feruzi ni rangi ya bluu ya kijani, johari na bluu iliyoiva, na rubi ni rangi nyekundu iliyopauka.

Isaiah 54:13

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

Kisha watoto wako wote watafundishwa na Yahwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na Yahwe atawafundisha watoto wako wote"

na Yahwe

Yahwe anajizungumzia mwenyewe katika utatu. Inaweza kuwekwa katika mtu wa kwanza. "kwa mimi, Yahwe"

Katika haki nitakuimarisha tena

Nomino dhahania "haki" inaweza kuwekwa kama kivumishi "sahihi". "Nitasababisha uwe na nguvu tena kw sababu utafanya kile kilicho sahihi"

na hakuna kitu cha kutisha kitakuja karibu nawe

Hii ina maana hakuna mtu katika mji au walio nje wataweza kuwatisha wakazii wa Yerusalemu tena

Isaiah 54:15

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

anachokonoa matatizo

Hii ni lahaja. "inasababisha taabu" au "inakutaabisha"

ataanguka katika kushindwa

Hii ni lahaja. "utawashinda katika vita"

Isaiah 54:17

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

Hakuna silaha ambayo inaundwa dhidi yako itafanikiwa

Maadui kutofanikiwa dhidi ya watu wa Yahwe inazungumziwa kana kwamba silaha zao hazitaweza kufanikiwa dhidi ya watu wa Yahwe. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Maadui wanweza kutengeneza silaha kukushambulia lakini hawatakushinda"

Huu ni urithi wa watumishi wa Yahwe

Dhawabu ambayo Yahwe atawapa wale ambao watamtumikia inazungumziwa kana kwamba dhawabu ilikuwa kitu watakachoweza kurithi.

hili ni tamko la Yahwe

Yahwe anajizungumzia katika utatu. Hii inaweza kuwekwa katika mtu wa kwanza. "hivi ndivyo mimi, Yahwe, navyotamka"

Isaiah 55

Isaiah 55:1

Kauli Kiunganishi

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu katika uhamisho kupitia Isaya.

Taarifa ya Jumla

Yahwe anazungumzia kubariki watu kwa uhuru kana kwamba alikuwa akiuza chakula na vinywaji kwa watu wahitaji bure.

Njooni ... njooni

Marudio ya neno hili mara nne linaongeza wazo la uharaka wa mwaliko.

nunua divai na maziwa bila pesa na bila gharama

Kuna fasili ya dhana akilini ya kejeli katika kauli hii kwa maana mtu kawaida anapaswa kutumia pesa kununua kitu. Hii inasisitiza neema ya ajabu ya Yahwe katika kutoa vitu hivi bure.

Isaiah 55:2

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

Kwa nini unapima uzito wa fedha kwa kile kisicho mkate?

Yahwe anauliza swali hili kukaripia watu. Anazungumza juu ya watu kutafuta furaha kando na Yahwe kana kwamba walikuwa wakinunua vitu kula ambavyo havikuwa chakula. "Haupaswi kupima fedha kwa kile ambacho ni mkate"

unapima uzito wa fedha

Hii ina maana ya kuhesabu sarafu za fedha ili kumlipa mtu kwa ajili ya kitu. "lipa pesa"

kwa kile kisicho mkate

Hapa neno "mkate" unawakilisha chakula kwa ujumla. Inadokezwa ya kwamba watu walikuwa wakinunua vitu kula ambavyo havikuwa chakula halisi. "kwa vitu vya kula ambavyo sio chakula halisi"

kwa nini unafanya kazi kwa kile hakiridhishi?

Yahwe anauliza swali hili kukaripia watu. Anawazungumzia kutafuta furaha tofauti na kwa Yahwe kana kwamba walikuwa wakifanya kazi kupata pesa kununua vitu ambavyo haviwezi kuwaridhisha. "haupaswi kufanya kazi kwa ajili ya pesa kutumia kwa vitu ambavyo haviridhishi"

kula kilicho chema, na ufurahie katika unene

Watu kumtumaini Yahwe kwa kumbariki na furaha inazungumziwa kana kwamba wanakula chakula kizuri ambacho kinawafanya wawe na furaha.

katika unene

Neno "unene" lina maana ya nyama ambayo ina mafuta mengi juu yake na ni lahaja kwa chakula kizuri. "kwa vyakula vizuri"

Isaiah 55:3

Geuza masikio yako

Kusikiliza au kuzingatia kwa makini juu ya mtu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kugeuza masikio ya mtu kwa mtu.

upendo mwaminifu ulioahidiwa kwa Daudi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "upendo mwaminifu ambayo nimemuahidi Daudi"

Nimemuweka

Maana zaweza kuwa 1) hii ina maana ya kile Yahwe alifanya kwa Mfalme Daudi kipindi cha nyuma au 2) ina maana ya kile ambacho Mungu atafanya kupitia mmoja wa vizazi vya Daudi.

Isaiah 55:5

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa watu wa Yerusalemu.

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli, yaani Yahwe

Isaiah 55:6

Mtafute Yahwe wakati bado anaweza kupatikana

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mtafute Yahwe wakati bado unaweza kumpata"

Na muovu aache njia yake

Neno "muovu" una maana ya watu waovu. Yahwe anazungumzia watu waovu kutofanya dhambi tena kana kwamba walikuwa wakiacha kutembea katika njia ambayo walikuwa wakisafiria. "Na watu waovu wabadili namna wanavyoishi"

na mwanamume wa dhambi mawazo yake

Kitenzi unaweza kutumika kutoka katika msemo uliopita. "na mwanamume mwenye dhambi aache mawazo yake"

mawazo yake

Maana zaweza kuwa 1) "namna anavyofikiri" au 2) "mipango yake"

naye atamhurumia

"na Yahwe atamhurumia"

na kwa Mungu wetu

Kitenzi kinaweza kutumika kutoka kwa msemo wa kwanza katika sentensi hii. "na mruhusu arudi kwa Mungu wetu"

Isaiah 55:8

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

hili ni tamko la Yahwe

Hii inaweza kutamkwa tofauti ili kwamba nomino dhahania "tamko" linawekwa kama kitenzi "tamkwa" au "kusema kwa dhati". "hiki ndicho Yahwe alichotamka" au "hiki ndicho Yahwe alichosema kwa dhati"

kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, kwa hiyo ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zako, na mawazo yangu kuliko mawazo yako

Yahwe anazungumzia mambo anayofanya na jinsi anavyofikiri kama kuwa bora zaidi au juu zaidi kuliko watu wanavyofanya au kufikiri, kama jinsi mbingu ilivyo juu sana kuliko nchi.

Isaiah 55:10

Taarifa ya jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

Kama vile mvua na theluji ... havirudi kule

Hii inawezekana ni ufafanuzi wa mvua na theluji kuvukiza.

kwa hiyo pia neno langu ... litafanikiwa kwa kile ambacho nimekituma

Yahwe anazungumza juu ya neno lake kana kwamba lilikuwa mtu ambaye anamtuma kama mjumbe wake kuhitimisha kazi.

neno langu litakuwa ambalo linatoka kinywani mwangu

Hapa neno "mdomo" unawakilisha Yahwe mwenyewe. "neno ambalo nazungumza"

halitarudi kwangu bila manufaa

Hapa ufafanuzi wa neno kurudi kwa Yahwe lina maana ya kwamba imemaliza kazi ambayo Yahwe ameituma kukamilisha. Ya kwamba haitarudi "bila manufaa" ina maana ya kwamba haitashindwa kutimiza kazi yake. "Haitashindwa kukamilisha kazi yake"

lakini itatimiza kile ambacho ninachotaka, na itafanikisha kile nilichokituma

Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja na inasisitiza ya kwamba kile Yahwe anasema kitaendelea kufanyika. "lakini nitatimiza kile nachotaka, na mambo nayozungumza nitasababisha yafanyike"

Isaiah 55:12

Taarifa ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yerusalemu.

kuongozwa mbele kwa amani

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nitakuongoza mbele kwa amani"

milima na vilima itabomoka kwa kelele za shangwe mbele yako, na miti yote ya shambani itapiga makofi

Yahwe anazungumzia milima, vilima na miti kana kwamba vilikuwa watu na sauti na mikono, vikisherehekea pale Yahwe anapowaokoa watu wake.

Badala ya miba ya vichaka, mvinje utaota; na badala ya mtemba, mti wa mihadasi utaota

Maneno "miba ya vichaka" na "mvinje" ina maana ya aina ya mimea ambayo ina miba mikali inayoota juu yao. Maneno "mvinje" na "mtemba" una maana ya aina ya miti ya kijani. Mimea ya miba inaashiria ukiwa, wakati ukijani unaashiria uzima na mafanikio.

kwa jina lake

Hapa neno "jina" linawakilisha umaarufu wa Yahwe. "kwa umaarufu wake" au "kwa heshima yake"

ambayo haitakatwa mbali

Kitu kinachokoma kuwepo kinazungumziwa kana kwamba kinakatwa mbali, kama tawi linavyokatwa mbali na mti au kipande cha kitambaa kinavyokatwa kutoka kwenye nguo. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambalo halitafika mwisho" au "ambalo itadumu milele"

Isaiah 56

Isaiah 56:1

kwa maana wokovu wangu upo karibu, na haki yangu inakaribia kufunuliwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Hivi punde nitakuokoa na kukuonyesha ya kwamba nina haki"

ambaye anaishikilia kwa nguvu

Hapa "anaishikilia kwa nguvu" ni lahaja ambayo ina maana ya kuendelea kuchunguza kitu. "ambaye ni mwangalifu kuendelea kufanya hivi"

kuzuia mkono wake kufanya uovu wowote

Hapa "mkono" ina maana ya matendo ya mtu au tabia. "hafanyi mambo maovu"

Isaiah 56:3

Tazama, mimi ni mti mkavu

Hii ina maana matowashi walifikiri wangeweza kuwa sehemu ya watu wa Mungu kwa sababu walibadilishwa kwa kuhanithishwa (na kwa sababu hii hawawezi kupata watoto). Waisraeli hawafanya zoezi la kuhasi, wageni walifanya, mara nyingine kama adhabu. Matowashi ambao walipokea imani ya waebrania walijua ya kwamba kawaida hawakuruhusiwa kuabudu katika hekalu (Kumb. 23.1). Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi.

Isaiah 56:4

katika nyumba yangu na katika kuta zangu

Misemo hii miwili ina maana moja. "ndani ya kuta za hekalu langu"

ambayo hatakataliwa mbali

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambayo haitaisha" au"ambayo haitasahaulika"

Isaiah 56:6

wanaojiunga kwa Yahwe

Hii ina maana ya wageni ambao wamejiunga na watu wa Yahwe.

wanaolipenda jina la Yahwe

"jina" linawakilisha tabia na utu wa Yahwe. "wanaompenda Yahwe"

mlima mtakatifu

"Mlima mtakatifu" ni Mlima Sayuni, katika Yerusalemu. "katika mlima mtakatifu wote wa Yahwe"

zitapokelewa juu ya madhabahu yangu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nitapokea juu ya madhabahu yangu"

nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "nyumba yangu itakuwa nyumba ya maombi"

Isaiah 56:9

Nyie wote wanyama wa mwitu wa shambani, njooni na mmeze, nyie wanyama wote wa msituni

Mungu aliwaita majeshi wa mataifa mengine kwa kuwalinganisha na wanyama kuja na kushambulia watu wa Israeli.

Walinzi wao wote ni vipofu

Hii ina maana ya viongozi wa Israeli hawawezi au labda hawataki kuona kile kinachotendeka katika jamii.

Wote ni mbwa walionyamaza

Viongozi wanatakiwa kufungua vinywa vyao na kuwaonya watu, lakini hawafanyi hivyo. Kulinganisha mtu na mbwa katika jamii hii ni fedheha kubwa.

Wanaota, na kujilaza chini wanapenda kulala

Hii ina maana viongozi hawaleti neno la Mungu la kuwaonya Waisraeli lakini wanapenda zaidi starehe yao.

Isaiah 56:11

Muhtasari wa Jumla

Yahwe anaendelea kufafanua viongozi waovu wa watu wake.

Mbwa wana hamu kubwa ya kula

Yahwe anaendelea kulinganisha viongozi wabaya wa Israeli na mbwa.

Isaiah 57

Isaiah 57:1

watu wa agano la uaminifu

"watu ambao wana haki na kushika sheria ya Mungu" au "watu ambao ni waaminifu kwa Mungu"

wanakusanywa mbali ... wanapumzika katika vitanda vyao

Zote hizi zina maana ya kufa.

ya kwamba mwenye haki anakusanywa mbali kutoka katika uovu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ya kwamba watu wenye haki hufa, na Yahwe huwachukua mbali kutoka kwa chote kilicho kiovu"

Anainga katika amani

"Wenye haki huingia katika amani"

wale wanaotembea katika unyofu

"wale ambao wamefanya kilicho sahihi"

Isaiah 57:3

Lakini njooni hapa

Mungu anawaita watu wote ambao sio waaminifu kuja mbele yake ili awahukumu katika utofauti mkubwa kwa ahadi kwa ajili ya wenye haki waliotangulia.

wana wa mwanamke mchawi

Hii ni fedheha kubwa dhidi ya watu ambao hufanya uchawi kwa sababu uchawi na mazingombwe hujumuisha kuabudu sanamu.

watoto wa mzinzi na mwanamke ambaye amejifanya kuwa kahaba

Hii ina maana ya uzinzi halisia na wa kiroho. Wamemuacha kuabudu Mungu na sasa wanaabudu miungu mingine pamoja na ukahaba halisia katika sherehe za Wakaanani.

Ni nani ambaye unafurahia kumdhihaki? Ni dhidi ya nani unafungua mdomo na kuchomoza ulimi wako?

Yahwe anatumia maswali kukaripia watu ambao wanamdhihaki kupitia kuabudu kwa uongo. "Mnanidhihaki na kunikejeli kwa kufungua mdomo wako wazi na kuchomoza nje ulimi!"

Je! wewe siye watoto wa uasi, watoto wa udanganyifu?

Yahwe anatumia swali lingine kukaripia watu. Hii haimanshi kuzaliwa kwao lakini hali yao ya kiroho. "Nyie ni watoto wa uasi, watoto waa udanganyifu!"

Isaiah 57:5

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wasio waaminifu wa Israeli.

Mnajipatia joto wenyewe ... chini ya mawe yalitokeza

Matendo haya yote yanahusishwa na kuabudu sanamu. Mialoni ilikuwa miti mitakatifu kwa Wakaanani. Watu walidhani matendo haya yangeongeza rutuba kwa watu na kwa nchi.

Isaiah 57:6

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa watu wasio waaminifu wa Israeli.

ambavyo vimegawiwa kwako

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Maana hasa katika iiebrania haipo wazi. "hilo ni fungu lako" au "huo ni urithi wako"

Je! nifurahi katika hivi vitu ?

Yahwe anatumia swali kukaripia watu. "Hakika, vitu hivi havinifurahishi"

Isaiah 57:7

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa watu wasio waaminifu wa Israeli.

Uliandaa kitanda chako

Hii ina maana ya kulala na kahaba kama sehemu ya kuabudu miungu ya uongo.

juu ya mlima wa juu

Watu mara kwa mara walienda juu ya vilima na milima kuabudu miungu ya uongo. Walidhani hizo zilikuwa sehemu bora za kuabudu. Hii inaweza kumaanisha Yerusalemu, pia.

Ulifanya agano pamoja nao

"Ulifanya mkataba na mimi"

Isaiah 57:9

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa watu wasio waaminifu wa Israeli.

ulishuka chini Kuzimu

Watu hawakwenda kuzimu kihalisia, dunia ya wafu. Badala yake, Yahwe anaonyesha ya kwamba watu walikuwa tayari kwenda popote kutafuta miungu wapya wa kuabudu.

Ulipata maisha mikononi mwako

Baada ya kujaribu sana, waabudu sanamu waligundua kuwa bado wana nguvu ya kuendelea. Hapa "mkono" una maana ya "nguvu" au "uwezo"

Isaiah 57:11

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa watu wasio waaminifu wa Israeli.

Ni nani uliye na wasiwasi juu yake? Ni nani unayemuogopa sana ambaye amasababisha kutenda kwa udanganyifu ... juu yangu?

Yahwe anatumia maswali haya kukaripia watu. "Inaonekana unaogopa kabisa sanamu hizi kwako utende kwa udanganyfu ... juu yangu!"

sana mpaka huwezi kunikumbuka au kufikiria juu yangu

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza ya kwamba, ingawa watu walitakiwa kumkumbuka Yahwe, hawakufanya hivyo.

Nitatangaza matendo yako yote ya haki na kusema yote ambayo umeyafanya

Yahwe anawakejeli, kwa kuita matendo yao ya uovu haki.

Isaiah 57:13

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa watu wasio waaminifu wa Israeli.

acha kusanyiko lako la sanamu likuokoe

Yahwe anawadhihaki watu na sanamu zao. Anaziambia sanamu kuwaokoa watu ingawa anajua haziwezi.

upepo utaubeba wote mbali, pumzi itazibeba zote mbali

Hii ni kusema jambo moja kwa njia mbili kusisitiza ya kwamba sanamu hazijiwezi na hazina thamani. "upepo, hata pumzi, itazipuliza mbali"

mlima mtakatifu

"Mlima matakatifu" ni Mlima Sayuni, katika Yerusalemu.

Isaiah 57:14

Jenga, jenga! Safisha njia! Ondoa vitu vyote vya kujikwaa kutoka katika nja ya watu wangu

Yahwe ana nguvu na haraka ya kwamba njia ya wazi na tambarare iweze kuwepo kwa watu kurudi kwake na kufungulia vikwazo kwa kumuabudu Yahwe. Hii inaitikia 40:3.

Kwa maana hiki ndicho Yule aliye juu na kuinuliwa asemavyo

Maneno "juu" na "kuinuliwa" kimsingi ina maana moja hapa na inasisitiza Yahwe kuinuliwa.

kufufua roho ya wanyenyekevu, na kufufua moyo ya wenye majuto makali

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza ya kwamba Yahwe atawatia nguvu na kutia moyo wale ambao wanajishusha mbele yake.

roho ... moyo

Hapa hizi zina maana ya mawazo ya mtu na hisia, sio roho na moyo kihalisia.

Isaiah 57:16

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Nimeficha uso wangu

Hii ina maana ya Mungu alikata tamaa kwa watu wake na hakuwasaidia au kuwabariki.

alikwenda kwa nyuma katika njia ya moyo wake

Hii ina maana ya Waisraeli waliendelea kumkataa Mungu wa kwelii kwa wa uongo. Hapa "nyuma" na "njia" ni maneno ya mahali yanayowakilisha motisha na hisia.

Isaiah 57:18

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

njia zake

"njia zao". Hapa "zake" ina maana ya watu wa Israeli.

fariji na tuliza wale ambao wanaomboleza kwa ajili yake

"Nitabembeleza na kutuliza wale ambao wanahisi huzuni kwa ajili ya mateso ya watu kwa sababu ya tabia yao ya dhambi"

na ninatengeneza matunda ya midomo

Hapa "matunda ya midomo" ina maana ya kile mtu anachosema. "na ninasababisha wao wanisifu na kunishukuru"

Amani, amani, kwa wale ambao wapo mbali sana

"Nimefanya amani pamoja nao ambao wako mbali" Neno "Amani" linarudiwa kwa msisitizo.

Isaiah 57:20

Lakini waovu ni kama bahari inayorusharusha ... takataka na matope

Hii inalinganisha waovu na maji yenye vurugu katika ufuko yanayofanya maji kuwa machafu.

Isaiah 58

Isaiah 58:1

Inua sauti yako kama tarumbeta

Hii ina maana kupiga kelele kwa sauti. Hapa "yako" ina maana ya Isaya.

Wakabili watu wangu kwa uasi wao, na nyumba ya Yakobo kwa dhambi zao

Misemo hii miwili ina maana moja. Kwa pamoja wanaimarisha uharaka kukabili watu wa Yahwe.

Isaiah 58:3

'Kwa nini tumefunga', wanasema, 'lakini hauioni? Kwa nini tumejishusha, lakini hautambui?'

Watu wa Israeli wanatumia maswali kulalamika kwa Mungu kwa sababu wanahisi hawajali.

Isaiah 58:4

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kwa kujibu swali lao la changamoto.

Tazama

"Tazama" or "Zingatia kwa makini". Yahwe anawakabili swali lao kwa kuwaambia kuzingatia kwa makini.

ngumi ya uovu

"ngumi ya uovu". Hii inaonyesha wanapigana kwa ukali. "Ngumi" inawakilisha hasira ambayo ni vurugu ya mwili.

Je! hii ni aina ya kufunga ambayo ningetaka ... chini yake?

Yahwe anatumia swali kukaripia watu. Wanajifanya kana kwamba ni wanyenyekevu mbele ya Mungu, lakini wanawaumiza watu wengine. "Hii sio aina ya kufunga ninayoitaka ... chini yake"

Siku kwa ajili ya mtu yeyote kujishusha, kwake kuinamisha chini kichwa chake kama matete

Hii ina maana mtu anainama chini, lakini sio mnyenyekevu ki ukweli. "Tete" linawakiliisha mmea dhaifu ambao hujikunja kirahisi.

Je! unata hivi kufunga kweli, siku ambayo inampendeza Yahwe?

Yahwe anatumia swali kukaripia watu. "Hakika haufikiri aina hii ya kufunga inanifurahisha!"

Isaiah 58:6

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Isareli.

Je! hii sio kufunga ambayo naichagua ...kuvunja kila nira?

Yahwe anatumia swali kufundisha watu kuhusu aina ya kufunga ambayo inamfurahisha. "Hii ni kufunga ninayochagua ... kuvunja kila nira".

Kufungua vifungo vya waovu, kufungua kamba za nira, kuwaweka waliokanyagwa huru, na kuvunja kila nira

Misemo hii yote ina maana ya kwamba wanatakiw kuwasaidia watu wle ambao waovu na wanawaumiza na kuwakandamiza.

Je! sio ku ... nyumba yako?

Yahwe anatumia swali lingine kuwafundisha watu. "Ni ku... nyumba yako".

vunja mkate wako

Msemo huu unawakilisha kuanza mlo kwa mwenyeji kuchana mkate.

Isaiah 58:8

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Kisha nuru yako itavunjwa wazi kama mapanzuko

"Vunja wazi" ni lahaja ambayo ina maana ya pale ambapo nuru huanza kuwaka kwa mwanga. Hii ina maana ya kwamba kama watawasaidia watu wahitaji, matendo yao yatakuwa kama nuru inayoonwa na wengine, kama jua linavyochomoza baada ya giza la usiku. Au mwanga unaweza kumaanisha nuru ya Bwana, inayowaka juu yao na kuwabariki.

na uponyaji wako utachipuka juu kwa haraka

Hii ina maana Mungu atawabariki na kuwarudisha haraka, kama kidonda kinavyopona haraka.

haki yako itakuwa mbele yako, na utukufu wa Yahwe utakuwa ulinzi wako wa nyuma

Hii ina maana ya kipindi ambapo Mungu aliwalinda watu wa Israeli walipotoroka kutoka Misri. Hii ina Mungu atawalinda tena kutoka kwa adui zao watakapofanya kilicho sahihi.

haki yako

Msemo huu katika Kiebrania unaweza kutafsiriwa kama yule anayetoa haki au hata ushindi. Katika muktadha huu, msemo huu ungemaanisha Mungu. Tafsiri za kisasa zina tafsiri hii.

Isaiah 58:9

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

kisha nuru yako itainuka kutoka gizani, na giza lako litakuwa kama mchana

"Nuru yako" inawakilisha matendo ya wema ambayo yatakuwa mifano kwa kila mtu, na "giza" ni matendo mabaya, yatashindwa kwa matendo yao mema.

Isaiah 58:11

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli

kukuridhisha katika maeneo ambapo hakuna maji

"Maji" inawakilisha kila kitu wanachohitaji kwa ajili ya maisha tele hata kama mazingira yake hayana ya kutosha.

utakuwa kama bustani iliyomwagiliwa

"Bustani iliyomwagiliwa" inawakilisha wingi ili waweze kuwa na yote wanayohitaji.

kama chemchemi ya maji, ambayo maji yake hayakosi

"Chemchemi ya maji" inawakilisha chanzo cha wingi katika nchi ambapo maji ni ya thamani.

Isaiah 58:12

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli

utaitwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu watakuita"

Isaiah 58:13

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli

unageuza miguu yako kutoka na kusafiri katika siku ya Sabato, na kutofanya starehe yako katika siku yangu takatifu

Hapa "miguu" ina maana ya safari na kazi ambayo wtu walifanya katika siku zingine zote. Mungu hakuruhusu safari ndefu au kazi katika siku ya kupumzika. "unaacha kusafiri na kufanya unachotaka kufanya katika siku ya Sabato, siku yangu takatifu"

Isaiah 58:14

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Nitakufanya uendeshe katika vilele vya dunia

Hii ina maana ya Mungu kunua taifa katika sifa na nguvu kwa mwitikio wa kuishi katika haki.

kwa maana kinywa cha Yahwe kimenena

"kinywa" inaashiria kile ambacho Yahwe anasema. "Kwa maana Yahwe amekisema"

Isaiah 59

Isaiah 59:1

Tazama

"Tazama!" "Unapaswa kujua!" Yahwe anawaambia watu kuzangatia kwa makini.

Mkono wa Yahwe sio mfupi sana

"Mkono" unawakilisha nguvu na uwezo. "Mkono mfupi hauna nguvu na uwezo. "Yahwe anaweza kabisa"

yako ...yamekutenga

Viwakilishi hivi vya wingi vina maana ya watu wa Israeli kama kundi moja.

dhambi zako zimemfanya afiche uso wake kwako

"Uso" unawakilisha kuwepo sasa na kutazama juu ya. "dhambi zako zimekufanya ugeuke kutoka kwako"

Isaiah 59:3

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Kwa maana mikono yako imetiwa doa kwa damu na vidole vyako kwa dhambi

Hapa "mikono" na "vidole" ina maana ya matendo yao. Hii ina maana wana hatia ya kufanya mambo makali na ya dhambi. "vyako" ni wingi. "Kwa maana umetenda dhambi kali"

Midomo yako inazungumza uongo na ulimi wako unazungumza kwa nia mbaya

Sehemu za mwili ambazo hutoa maneno na kuwakilisha kile watu wanasema. "Unazungumza uongo na mambo maovu"

wanatunga mimba ya taabu na kuzaa dhambi

"Kupata mimba" na "kuzaa" inasisiitiza jinsi wanavyopanga kwa makini kufanya mambo ya dhambi. Hapa "wanatunga" bado ina maana ya watu wa Israeli. "wanafanya kazi kwa bidii kufanya mambo ya dhambi"

Isaiah 59:5

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kuhusu maovu wanayofanya kwa kutumia sitiari ya nyoka wenye sumu na wavu za buibui.

Wanatotoa mayai ya nyoka wenye sumu

Mayai ya nyoka wenye sumu kutotoa kuwa nyoka hatari zaidi. "Nyoka wenye sumu" inawakilisha uovu ambao watu hufanya ambao unadhuru zaidi na zaidi. "Wanafanya uovu ambao husambaa kutengeneza uovu zaidi"

kufuma wavu wa buibui

Hii inawakilisha matendo ya watu ambayo hayana thamani. "wanazaa vitu na matendo ambayo hayana thamani"

Yeyote anayekula mayai yao hufa, na iwapo yai likipondwa, linatotoa kuwa nyoka wa sumu

Kula yai lenye sumu litamuua mtu ambaye analila na inawakilisha kujiangamiza. Kuvunja yai huruhusu nyoka wadogo wenye sum kutotoa na inawakilisha kusambaa kwa uharibifu. "Matendo wanayofanya yatawaangamiza na kusambaza uharibifu kwa wengine"

iwapo yai likipondwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kama mtu akiponda yai"

Nyavu zao haziwezi kutumiwa kwa ajili ya mavazi, wala hawawezi kujifunika kwa kazi zao

Hii ina maana matendo yao maovu hayawezi kufunikwa na kufichwa, kama vile wavu hauwezi kufanya nguo na kumfunika mtu. "Matendo yao maovu yatafunuliwa kuwa bila thamani"

Nyavu zao haziwezi kutumiwa kwa ajili ya mavazi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Hawawezi kuvaa nguo kwa wavu zao"

Matendo ya vurugu yamo mikononi mwao

"mikono" inawakilisha uwezo na nguvu ya kufanya vitu hivi na kwa hiyo jukumu lao. "wana wajinu kamili kwa vurugu wanayofanya"

Isaiah 59:7

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kzungumza na watu wa Israeli.

Miguu yao hukimbilia uovu

"Miguu" inawakilisha uwezo wa kuondoka na "kukimbia" ina maana ya kufanya jambo kwa haraka. "Wana haraka ya kufanya mambo maovu"

ni njia zao

"njia" inawakilisha njia yao ya maisha. "ni yote wanayofanya"

hakuna haki katika njia zao

"njia" inawakilisha njia yao ya maisha. "kamwe hawafanyi kilicho haki" au "kila kitu wafanyacho sio cha haki"

Wametengeneza njia zilizopinda

"Njia zilizopinda" inawakilisha njia ya maisha ambayo imepotoka. "Wanasema na kufanya mambo yasiyo ya kweli. Ni wajanjawajanja"

Isaiah 59:9

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

haki ipo mbali kutoka kwetu

Hapa "kwetu" ina maana ya Isaya na watu wa Israeli. "Mbali" inawakilisha haki iliyotoweka na ngumu kupata. "haki imetoweka na ngumu sana kupata"

Tunasubiri kwa ajili ya nuru, lakini tunaona giza; tunatafuta mwanga, lakini tunatembea gizani

Kila ya hii misemo ina maana ya kwamba watu wanasubiri wema wa Mungu, lakini inaonekana kana kwamba amewatelekeza.

Tunapapasa ukuta kama vipofu ... kama watu waliokufa

Hii ina maana ya kwamba kwa sababu Mungu haji kwao, wanajisikia bila msaada, kutopata njia sahihi na kukata tamaa na siku za usoni, bila tumaina la maisha ya kusisimua.

Isaiah 59:11

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Tunaunguruma kama dubu na kunung'unika kama njiwa

Hii ina maana ya sauti ambayo watu walifanya kwa sababu walikuwa na dhiki na maombolezo.

Isaiah 59:12

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza.

makosa yetu mengi

Hapa "yetu" ina maana ya Isaya na watu wa Israeli.

mbele zako

Hapa "yako" ina maana ya Yahwe.

dhambi zetu zinashuhudia dhidi yetu

Isaya anafafanua dhambi kama mtu anavyokwenda mbele za Mungu kutamka ya kwamba watu wana hatia.

kwa maana makosa yetu yapo pamoja nasi

"pamoja nasi" inawakilisha kutambua uwepo wao. "kwa maana tunatambua makosa yetu"

Isaiah 59:14

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza.

Haki imerudishwa nyuma

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wanasukuma haki nyuma"

Haki ... haki ... kweli ... uadilifu ... Uaminifu

Haya ni mawazo ambayo Isaya anafafanua kama kujifanya kama watu

Isaiah 59:16

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza.

Aliona ya kwamba hakuna mtu, na akashangaa ya kwamba hapakuwa na mtu wa kuingilia kati.

"Yahwe alishtushwa ya kwamba hakuna mtu alikua kuwasaidia wale waliokuwa wakiteseka" au "Yahwe alishangazwa ya kwamba hakuna mtu aliyekuja kuwasaidia wale waliokuwa wakiteseka"

Kwa hiyo mkono wake mwenyewe ulileta wokovu kwa ajili yake

"'mkono" unawakilisha uwezo na nguvu. "Yahwe alitumia nguvu yake mwenyewe kuwaokoa watu"

na haki yake ikamsaidia

"Haki" ni sifa ambayo hujifanya kama mtu. "na alifanya sahihi kama anavyofanya siku zote"

Isaiah 59:17

Akavaa haki kama dereya ya kifuani na kofia ya chuma ya wokovu juu ya kichwa chake. Alijivisha mavazi ya kisasi na kuvaa ari kama joho

"dereya", "kofia ya chuma", "mavazi", na "joho" ni nguo kwa ajili ya vita na kupigana, Isaya anamfafanua Yahwe kama akivaa haya kuwaadhibu watu wake.

joho

joho lililo huru, linalotiririka

Akawarudishia maliipo

Isaya anafafanua tukio la siku za usoni kana kwamba ilitokea kipindi cha nyuma. Hii ina maana hakika itatokea.

Isaiah 59:19

Maelezo ya Jumla

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "'ambayo pumzi ya Yahwe huongoza"

wataogopa jina la Yahwe

Hapa "jina" lina maana ya sifa ya Yahwe na tabia. "muogope Yahwe"

kutoka magharibi ... kutoka kwa mawio ya jua

Isaya anaunganisha maneno haya mawili kumaanisha watu katika maeneo yote duniani.

kwa maana atakuja kama kijito kinachokuja kwa kasi

Mabonde membamba ya Yuda yalikuwa yamekauka muda mwingi katika mwaka hadi pale mvua nzito ya ghafla ilipogeuza kuwa maji yanayokwenda kwa kasi. Hicho kilipotokea kulikuwa na kelele nyingi na upepo.

kinachoendeshwa kwa pumzi ya Yahwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambayo pumzi ya Yahwe inaendesha"

tamko la Yahwe

Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "tamko" liwe kitenzi "alitamka" au "alisema kwa dhati". "Hivi ndivyo Yahwe alivyotamka" au "Hiki ndicho Yahwe alichosema kwa dhati"

Isaiah 59:21

maneno yangu ambayo nimeweka kinywani mwako

Hii ina maana ya kumpatia mtu kitu cha kusema. "ujumbe niliokpatia kuzungumza"

Isaiah 60

Isaiah 60:1

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Inuka, angaza; kwa maana nuru yako imekuja, na utukufu wa Yahwe umeinuka juu yako

Hii ina maana ya vtu vitukufu Yahwe amevifanya kwa wakazi wa Yerusalemu. Zipo kwa ajili ya kuonyesha utukufu huo kupitia kile vinavyofanya na kusema na kuwa na tumaini katika siku za usoni.

Isaiah 60:2

Maelezo ya Jumla

Isaya anazungumza na watu wa Israeli. Anaendelea sitiari ju ya "mwanga"

Ingawa giza litafunika dunia, na giza nene mataifa

Misemo hii miwili ina maana moja na inajumlishwa kwa msisitizo. Ina maana ya "giza la kiroho". Hii ina maana watu wengine wote wa dunia hawatamjua Yahwe au namna ya kumpendeza. Hii ni sitiari kwa hukumu takatifu.

bado Yahwe atainuka juu yako

Hii ina maana mwanga wa uwepo wa Mungu utatokea kwa ajili ya watu wa Israeli, na utaonekana njia wanayopaswa kwenda.

na utukufu wake utaonekana juu yako

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na watu wa mataifa wataona utukufu wake juu yako"

Isaiah 60:4

Maelezo ya Jumla

Hapa Yahwe anaanza kuzungumza.

Wote wanajikusanya

"Wote" ina maana ya watu waliobakii wa Israeli ambao watakuja pamoja kurudi Yerusalemu.

binti zako watabebwa mikononi mwao

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watabeba binti zako mikononi mwao" au "watabeba binti zako juu ya viuno vyao"

Kisha utatazama na kung'aa, na moyo wako utashangilia na kumwagikia

Misemo hii inatumia maana moja na kusisitiza ya kwamba watakuwa na furaha sana kwa sababu ya kile kitakachotokea Yerusalemu.

wingi wa bahari

Hii ina maana ya utajiri na bidhaa ambazo zitakuja Yerusalemu kwa njia ya meli, labda kupitia Bahari ya Mediteranea.

utamwagwa nje kwako

Hii inaelezea ya kwamba wingi utakuwa kama maji ambayo yanabubujika nje.

Isaiah 60:6

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

ngamia

"ngamia wadogo"

Efa ... Kedari ... Nebayothi

Haya ni majina ya maeneo ya Uarabuni.

Makundi yote ya Kedari yatakusanywa pamoja kwako

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wa Kedari watakusanya makundi yao kwa ajilii yako"

kondoo wa Nebayothi watatumikia mahitaji yako

Hii ina maana ya hitaji lao la kutoa sadaka.

watakuwa sadaka inayokubalika juu ya madhabahu yangu

Mimi, Yahwe, nitazipokea juu ya madhabahu yangu"

Isaiah 60:8

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Hawa ni kina nani wanaopaa kama wingu, na kama njiwa katika makazi yao?

Yahwe anatumia maswali na picha za kishairi kuvuta nadhari hapa. Analinganisha matanga ya meli kwa mawingu na njiwa. Hii pia ni taswira ya Waisraeli kurudi katika nchi ambapo wanaishi. "Tazama, ninaona kitu kama mawingu yakisogea haraka na kama njiwa wakirudi katika makazi yao"

Pwani

Hii ina maana ya watu ambao wanaishi katika pwani na inafafanua eneo la pwani kana kwamba ilikuwa watu wakiangalia nje. "Watu kutoka pwani"

meli za Tarshishi

Msemo huu kawaida una maana ya meli kubwa za biashara zinazofaa kwa safari ndefu.

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

amekuheshimu

"Yahwe amekuheshimu, watu wa Israeli"

Isaiah 60:10

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

hayatafungwa mchana na usiku

Hapa "mchana" na "usiku" pamoja ina maana ya "wakati wote". Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna atakayeweza kuvifunga"

ili kwamba utajiri wa mataifa uweze kuletwa, na wafalme wake wakiwa wameongozwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ili kwamba watu wa mataifa waweze kuleta utajiri wao, pamoja na wafalme wao"

Isaiah 60:12

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

mataifa hayo yataangamizwa kabisa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nitaangamiza kabisa watu wa mataifa hayo"

utukufu wa Lebanoni

Hii ina maana ya Lebanoni kuwa maarufu kwa miti yake mizuri, haswa mvinje na seda. Utambuzi hasa wa miti yote haujulikani.

sehemu ya miguu yangu

Hii ina maana ya hekalu la Yahwe.

Isaiah 60:14

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Mtakatifu wa Israeli

Mtakatifu wa Israeli

Isaiah 60:15

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

bila mtu yeyote anayepi katikati yako

"na kila mtu akiepuka nchi yako" au "na kila mgeni akiepuka nchi yako"

Pia utakunywa maziwa ya mataifa, na utanyonya katika ziwa la wafalme

Hii ina maana ya utajiri na wing ambao utanyonywa kutoka kwa mataifa ya kigeni. Vishazi vyote vinarudia wazo moja kwa msisitizo.

Mkombozi

Mkombozi wa Israeli.

Mwenye enzi wa Yakobo

Mwenye enzi wa Israeli

Isaiah 60:17

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

badala ya mbao, shaba, na badala ya mawe, chuma

Yahwe atatoa vifaa vya thamani zaidi vya ujenzi kwao sasa. "badala ya mbao, nitaleta shaba, na badala ya mawe, nitaleta chuma"

Nitateua amani kama mkuu wako, na haki watawala wako

Yahwe anafafanua "amani" na "haki" kama watawala wa kibinadamu. Hii ina maana kutakuwa na amani kamili na haki katika nchi ya Israeli.

Vurugu haitasikika tena katika nchi yako

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Hakutakuwa tena na taarifa za vurugu katika nchi yako"

lakini utaita kuta zako Wokovu, na malango yako Sifa

Viumbo vya kihalisia vina majina ya sifa za kiroho. Mji wa Yerusalemu utakuwa eneo salama, na watu pale watamsifu Yahwe.

Isaiah 60:19

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

kwa maana Yahwe atakuwa nuru yako ya mlele

Mistari miwili inarudia wazo hili moja kwa msisitizo.

Jua lako halitazama tena, wala mwezi wako hautaondoka na kupotea

Mwezi hautapotelea kihalisia. Hii ni kusema ya kwamba kulinganisha na mwanga wa Yahwe, mwanga wa jua na mwezi hautakuwa kitu.

Isaiah 60:21

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

tawi la kupanda kwangu, kazi ya mikono yangu

Misemo hii ina maana karibu moja na inarudiwa kwa ajili ya msisitizo.

tawi la kupanda kwangu

Yahwe analinganisha watu kwa mmea mchanga kuota ambao alipanda kana kwamba alikuwa mkulima wa bustani. Yahwe ameweka watu wake katika nchi ya Israeli. Hii inatoa matumaini kwa watu.

kazi ya mikono yangu

Yahwe analinganisha watu wa Israeli kwa kitu kilichoundwa kwa ujuzi wa mkono wake.

ili kwamba niweze kutukuzwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ili kwamba watu wote waweze kunitukuza"

elfu moja

"1,000"

Isaiah 61

Isaiah 61:1

Roho wa Bwana Yahwe yupo juu yangu

"Roho" hapa ni Roho Mtakatifu wa Yahwe ambaye humsukuma au kuhamasisha mtu.

walioteswa

Hii ina maana ya watu maskiniu, wale walio ndani ya huzuni kubwa, au watu walioteswa ambao wana matatizo wanaoshindwa kuyatatua wao wenyewe.

uhuru kwa wafungwa, na kufungua kwa gerez kwa wale waliofungwa

Misemo hii miwili ina maana moja. Inasema ya kwamba Mungu kwa hakika atatoa uhuru kwa wafungwa.

Isaiah 61:2

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza

mwaka wa fadhila ya Yahwe, siku ya kisasi

Misemo hii miwili ina maana ya muda mmoja wa wakati. "Mwaka" na "siku" zote ni mifano bayana ambayo inawakilisha ukubwa kamili.

mwaka wa fadhila ya Yahwe

"wakati ambapo Yahwe atatenda wema kwa watu wake"

Isaiah 61:3

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza.

kuwapa ... kuwapatia

Isaya anarudia hivi kusisitiza.

kilemba

"kilemba cha kichwani" au "kifuniko kizuri cha kinywani". Hii ni kitambaa kirefu cha nguo kinachozunguka kichwa.

mafuta ya furaha ... joho la sifa

Watu huweka mafuta juu yao na kuvaa joho zuri, ndefu wakati wa sherehe na shangwe.

katika nafasi ya roho ya kutojali

"katika nafasi ya huzuni" au "katika nafasi ya maombolezo"

mwaloni wa utakatifu, kupandwa kwa Yahwe

Hii ina maana Yahwe amesababisha watu kuwa na nguvu na imara.

ili aweze kutukuzwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ili kwamba maisha ya watu yaweze kumtukuza yeye"

Isaiah 61:4

Taarifa ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza kutumia usambamba katika kila mstari.

Isaiah 61:6

Taarifa ya Jumla

Mtumishi wa Yahwe anaendelea kuzungumza kwa watu wa Israeli na kila mstari kuwa sambamba.

Utaitwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu watakuita"

utapata mara mbili

Huenda hii ina maana ya fungu mara mbili la nchi.

watafurahi juu ya mgawo wao ... wata ... nchi yao ... itakuwa yao

Hii bado ina maana ya watu wa Israeli. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya mtu wa pili. "utafurahia juu ya gawio lako ... uta ... nchi yako ... itakuwa yako"

Isaiah 61:8

Vizazi vyao vitajulikana miongoni mwa mataifa, na watoto wao miongoni mwa watu

Vishazi hivi viwili vina maana moja. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu kutoka mataifa mengine watajua vizazi vyao"

watoto wao miongoni mwa watu

Kishazi hiki kinachukulia kitenzi hicho hicho kama kilicho nyuma. "uzao wao utajulikana miongoniu mwa watu"

Isaiah 61:10

Nitafurahi sana katika Yahwe

"Nita" ina maana ya watu wa Mungu wakizungumza kama mtu mmoja ambaye Yahwe amerejesha.

amenivisha kwa mavazi ya wokovu; amenivisha na joho la utakatifu

Watu wa Mungu kuzungumza kama mtu mmoja sasa wa wokovu na utakatifu kama muonekano wao tofauti unavyoonekana kwa wote. "Mavazi" na "joho" ni nguo ambazo kila mtu anaweza kuona.

kama bwana arusi anavyojipamba na kilemba, na kama bibi arusi anavyojiremba na vito vyake

Mlinganisho huu unasisitiza ya kwamba mwandishi ana furaha sana, anasherehekea.

kilemba

"kilemba cha kichwani" au "kifuniko kizuri cha kinywani". Hii ni kitambaa kirefu cha nguo kinachozunguka kichwa.

Kwa maana kama nchi izaavyo mimea yake inayochipuka, na kama bustani inavyofanya mimea yake kuota

Huku ni kusema kitu kima kwa njia mbili. Ukweli ya kwamba chochote Mungu anachosema atafanya hakika kitafanyika kinalinganishwa na ukweli kwamba mbegu huchipuka baada ya kupandwa. "Kama vile mbegu zinavyopandwa katika bustani huchipuka kutoka kwenye udongo na kuota"

utakatifu na sifa kuchipuka juu

Msemo huu unaelezea sifa hizi kama kuota kutoka kwa mbegu kama mimea inavyofanya.

Isaiah 62

Isaiah 62:1

Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitakaa kimya

Kauli hizi mbili zina maana moja. Hapa "Sayuni" na "Yerusalemu" zote zinawakilisha watu wanaoishi katika Yerusalemu. "Kwa ajili ya watu wa Yerusalemu sitanyamaza"

sitakaa kimya

Inawezekana ya kwamba "sitakaa" ina maana ya Isaya

mpaka utakatifu wake utakapojitokeza

Vishazi hivi viwili vinaaminisha watu wa Mungu hatimaye kurudi na kuokoa watu wa Israeli na kwamba itakuwa dhahiri kama mwanga ulivyo.

Isaiah 62:3

Pia utakuwa taji la uzuri mikononi mwa Yahwe, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako

Hizi zina maana moja na zinaunganishwa kwa ajili ya msisitizo. Zinasema ya kwamba Yerusalemu utakuwa mji wa kifalme chini ya nguvu na mamlaka ("mkono") ya Mungu.

haitakuwa kwako tena ... kusemwa, "Ukiwa"

Hizi zina maana moja na zinaunganishwa kwa ajili ya msisitizo.

haitasemwa kwako tena

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu hawatasema tena juu yako"

wala nchi yako haitasemwa tena

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wala watu hawatasema tena juu ya nchi yako"

na nchi yako itaolewa

Hii ina maana Yahwe atawapenda watu wa Israeli na atakuwa nao daima kama alivyo mume.

Isaiah 62:5

kama vile mwanamume anavyomuoa mwanamke, vivyo hivyo wana wako watakuoa

Hapa "wana" ina maana ya watu wa Israeli na "wako" ina maana ya Yuda, nchi ya Israeli. Hii ina maana ya kwamba watu watamiliki nchi kama vile mwanamume anavyomiliki mke wake kijana.

kama vile bwana arusi anavyofurahia bibi arusi wake, Mungu wako atafurahi juu yako

Hii inasisitiza furaha ya Mungu juu ya uhusiano wake na watu wake.

Isaiah 62:6

Nimeweka

Hapa "Nimeweka" inaweza kumaanisha Isaya au Yahwe.

walinzi katika kuta zako

Hii ina maana ya manabii, maafisa, au yawezekana malaika, ambao wanaomba kila wakati kwa ajili y watu wa Yerusalemu kama walinzi ambao hulinda mji kila wakati.

hawako kimya mchana na usiku

Hii ina maana wanamsihi Yahwe kwa muendelezo au kujia wao kwa wao. "wanaomba kwa dhati kwa Yahwe katika siku nzima"

Usimruhusu apumzike

Hapa "apumzike" ina maana ya Yahwe.

Isaiah 62:8

kwa mkono wake wa kuume na kwa mkono wa nguvu yake

Mkono wa kuume unawakilisha nguvu na mamlaka. "kwa nguvu na mamlaka yake"

Hakika sitakupatia tena mazao kama chakula kwa ajili ya adui zako

Hii ina maana Yahwe hatawaruhusu adui zake kuwashinda watu wa IUsraeli na kuchukua mazao yao tena. Huenda maadui walichukua mazao kipindi cha nyuma kama ushuru au kulisha majeshi yao wenyewe.

Sitakupatia tena mazao kama chakula kwa ajili ya adui zako ... Wageni hawatakunywa divai yako mpya

Kauli hizi zimewekwa pamoja kwa ajili ya msisitizo au ukamilifu.

wale watakaovuna mazao ... wale wanaochuma mizabibu

Kauli hizi zinawekwa pamoja kwa ajili ya msisitizo na ukamilifu.

Isaiah 62:10

Njoo upite, njoo upite katika malango

Msemo "njoo upite" unarudiwa kuonyesha uharaka.

Ijenge, Ijenge njia

Neno "jenga" linarudiwa kusisitiza ya kwamba Yahwe anataka kwa uharaka barabara kuandaliwa. "Njia" inawakilisha njia ambayo watu watarudi. Hii ni sawa na 40:3 na 57:14.

Kusanya mawe

"Chukua mawe kutoka barabarani kuifanya iwe laini. Mawe yanawakilisha vipingamizi vyote vya safari kuwa haraka.

Nyanyua ishara ya bendera kwa ajili ya mataifa

Bendera ya ishara inawakilisha kitu kuvuta nadhari ya wengine. Hii ina maana Yahwe anawaita watu wa mataifa mengine kugundua nchi ya Israeli na kuona kile Yahwe alichofanikisha kama alivyosema angefanya.

Isaiah 62:11

Tazama

"Gundua"

mwisho wa dunia

Sehemu za dunia ambazo zipo mbali sana zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa sehemu ambapo nchi hufikia kikomo. Msemo huu pia unaunda neno moja kwa kundi la mambo mengi na lina maana ya kila sehemu kati ya miupaka. "sehemu za mbali za dunia" au "dunia nzima"

binti Sayuni

"Binti" inawakilisha watu wa Yerusalemu (Sayuni).

Tazama, dhawabu yake ipo pamoja naye, na fidia yake inakwenda mbele yake

Vishazi hivi vinawakilisha wazo moja kwa msisitizo.

utaitwa

Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda, "watakuita"

Isaiah 63

Isaiah 63:1

Ni nani huyu ajaye kutoka Edomu ... Bosra

Isaya anazungumza kama mlinzi kwa kutumia mfumo wa swali na jibu kuwakilisha taarifa hii juu ya hukumu ya Yahwe kwa Edomu, adui wa Israeli. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Mimi, Yahwe, ninakuja kutoka Edomu, nikiwa nimevaa mavazi mekundu kutoka Bosra"

Bosra

Huu ni mji mkuu wa Edomu.

Ni Mimi

Hapa "Mimi" ina maana ya Yahwe.

Kwa nini nguo zako ni nyekundu, na kwa nini ... kishinikizo cha zabibu

Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Wekundu katika nguo zako zinakufanya uonekane kana kwamba ulikuwa ukikanyaga ju ya zabibu katika kishinikizo cha zabibu"

kishinikizo cha zabibu

Kishinikizo cha zabibu ni sehemu ya chini iliyochongwa kwa jiwe katika ardhi ambapo wafanyakazi hukanyaga zabibu kuziponda kwa miguu yao, ili kutoa juisi ya zabibu.

Isaiah 63:3

Nina zabibu zilizokanyagwa

Hapa "Nina" ina maana ya Yahwe. Picha hii ina maana ya Yahwe kuangamiza adui zake.

Kwa maana ninatazamia siku ya kisasi

Hapa "siku" ina ya kipindi cha muda.

kisasi

Yahwe ataadhibu kwa njia sahihi kuleta haki. Aina yake ya ukombozi inatofautiana na kisasi cha mtu.

mwaka wa ukombozi

Hapa "mwaka" ina maana ya muda bayana uliowekwa na Yahwe kurejesha Israeli.

Isaiah 63:5

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza

lakini mkono wangu wenyewe

Hapa "mkono" unawakilisha uwezo.

na kuwafanya walewe katika hasira yangu

Hii ina maana Yahwe aliwafanya washangae na kutokuwa na ufahamu wa hasira yake kamili na adhabu.

nilimwaga nje damu yao

Hapa "damu" inawakilisha maisha ya adui wa Yahwe ambao walikuw wakimwagika nje ili waweze kufa.

Isaiah 63:7

Nitasema

Hapa "Nitasema" ina maana ya Isaya

alichotufanyia kwetu

Hapa "kwetu" ina maana ya Isaya na watu wa Israeli.

Isaiah 63:9

Katika mateso yao yote

"Katika mateso yao yote". Hapa "yao" ina maana ya watu wa Israeli. Isaya anajumuisha yeye kama mwanajumuiya wa watu.

aliteseka pia

Hapa "aliteseka" ina maana ya Yahwe.

malaika kutoka katika uwepo wake

Hii inawakilisha nani aliyetumwa kutoka katika uwepo wa Mungu.

aliwainua juu na kuwabeba

Hii ina maana ya pale Mungu aliwalinda na kuwaokoa watu wa Israeli kutoka kwa Wamisri miaka mingi mapema. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi.

Isaiah 63:10

Lakini waliasi

"lakini tuliasi". Hapa "waliasi" ina maana ya watu wa Israeli. Isaya anajijumlisha kama mwanajumuiya wa watu.

Roho wake Mtakatifu

"Roho Mtakatifu wa Yahwe"

Isaiah 63:11

Walisema

"tulisema". Hapa "walisema" ina maana ya watu wa Israeli. Isaya anajijumlisha kama mwanajumuiya wa watu.

ambaye aliwatoa kutoka katika baharii

Simulizi ya Yahwe kugawanya maji ya Bahari ya Matete kimiujiza ili kwamba Waisraeli waweze kuvuka na kuwatoroka Wamisri ni taarifa inayosadikiwa.

wchungaji wa kundi lake

Viongozi mara nyingine wanajulikana kama "wachungaji". "viongozi wa watu wake"

Isaiah 63:12

Maelezo ya Jumla

Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza.

ambaye altengeneza nguvu yake tukufu iende pamoja na mkono wa kuume wa Musa

Hapa "mkono wa kuume" inawakilisha nguvu ya Yahwe kupitia Musa. Hii ina maana ilikuwa nguvu ya Mungu ambayo ilimwezesha Musa kugawanya maji katika Bahari ya Matete.

Kama farasi akimbavyoo katika nchi tambarare, hawakujikwaa

Hii ina maana ya kwamba watu wa Israeli walikuwa na miguu ya hakika kama ya farasi katika nchi ya wazi katika safari zao kuelekea Israeli kutoka Misri.

Isaiah 63:14

Maelezo ya Jumla

Watu wa Israeli wnaendelea kuzungumza.

Kama mifugo inavyokwenda chini katika bonde ... pumziko

Picha hii inaonyesha mifugo kushuka katika bonde ambapo kuna nyasi za kijani na maji na inasisitiza ya kwamba Mungu aliwaongoza watu wa Israelii na kuwatunza.

kujifanyia mwenyewe jina la sifa

Hapa "jina la sifa" ina maana ya heshima na sifa ya mtu. "hakikisha una sifa ya kuheshimiwa kwa ajili yako"

Isaiah 63:15

Maelezo ya Jumla

Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza.

Iko wapi ari yako na matendo yako makuu?

Mwandishi anatumia swali kuonyesha hisia za ndani na kujali kwa sababu inaonekaba Mungu hawasaidii. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hatuoni ari yako na matendo yako makuu!"

Huruma yako na matendo yako ya upole yamewekwa kutoka kwetu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Unaficha huruma yako na upole kutoka kwetu"

ingawa Abrahamu hatujui, na Israeli hatutambui

Mababu hawa wa taifa la Israeli wasingeweza kutambua vizazi vyao kwa sababu walibadilika sana. "Abrahamu" na "Israeli" wanawakilisha wakati wa zamani.

Isaiah 63:17

Maelezo ya Jumla

Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza.

Yahwe, kwa nini unatufanya tuzurure kutoka katika njia zako na kuifanya mioyo yetu kuwa migumu, ili kwamba tusikutii wewe?

Hapa mwandishi anatumia swali kuelezea lalamiko la watu wa Mungu. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Yahwe umetufanya tuzurure kutoka katika njia zako na kuwa wakaidi ili kwamba tusikutii"

kwa nini unatufanya tuzurure kutoka katika njia zako

Kutofanya kile ambacho Yahwe anaamuru inazungumziwa kana kwamba mtu anazurura kutoka katika njia sahihi. "kwa nini unatufanya kufanya kilicho kibaya"

kuifanya mioyo yetu kuwa migumu

Hii ina maana kutoweza kukataa mafundisho ya Yahwe kwa kukataa kusikiliza na kutii. Hapa "moyo" unawakilisha nia, hisia na shauku zao.

Isaiah 63:18

Maelezo ya Jumla

Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza.

ambao hawakuitwa kwa jina lako

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "jina" ina maana ya uhusiano wa familia. "ambaye hakuwa mmoja wa familia yako"

Tumekuwa ... hawakuitwa kwa jina lako

Baadhi ya tafsiri za kisasa zinatafsirii sehemu hii tofauti. "Tumekuwa kama watu ambao haujawatawala, kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako"

Isaiah 64

Isaiah 64:1

Taarifa ya Jumla

Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza kwa Yahwe.

O! kama unge

Isaya anatambulisha haja hii kwa uwepo wa Yahwe katika kipindi cha nyuma kwa mshangao mkubwa.

kama ungepasua wazi mbingu

Kama Yahwe amejionyesha kwa mbwembwe kwa kupasua wazi mbingu. Maneno "kupasua wazi" yana maana ya kuchana kipande cha nguo mbalimbali.

milima ingetetemeka

Milima ingeweza kutetemeka kama vile tetemeko.

kama pale moto uwashao misitumisitu, au moto unaofanya maji kuchemka

Hii yawezekana kusisitiza jinsi uwepo wa Mungu ungeweza kusababisha kwa urahisi milima na watu kutetemeka.

Isaiah 64:3

Taarifa ya Jumla

Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza na Yahwe.

wala jicho kuona

"jicho" lina maana ya kuona kitu. "wala hakuna yeyote aliyeona"

Isaiah 64:5

Taarifa ya Jumla

Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza na Yahwe.

kumbukeni

Hii ni lahaja ambayo ina maana na "kumbuka"

Isaiah 64:6

Taarifa ya Jumla

Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza na Yahwe.

na matendo yetu yote matakatifu ni kama kitambaa cha hedhi

"Kitambaa cha hedhi" ni nguo ambayo mwanamke hutumia wakati wa mwezi anapotokwa damu kutoka kwenye tumbo la uzazi wake. Hii ina maana majaribio yao kumfurahisha Mungu yalishindikana. Sentensi hii ilikusudiwa kushtusha.

Tumenyauka wote kama majani

Isaya analinganisha watu wa Israeli na majaniu ambayo hukauka yanapokufa.

Udhalimu wetu, kama upepo, unatubeba mbali

Hii ina maana dhambi zao, kama jamii, ni sababu ya kushindwa kwao. Isaya analinganisha udhalimu na upepo kama nguvu ya mateso yao ya adhabu ya Yahwe.

umeficha uso wako kwetu

Hii ina maana Mungu alikataa tamaa juu ya watu wake na kuwaacha wateseke.

Isaiah 64:8

Taarifa ya Jumla

Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza na Yahwe.

sisi ni udongo wa ufinyanzi. Wewe ni mfinyanzi; na sisi wote ni kazi ya mkono wako

Hii ina maana Mungu aliwaumba watu wa Israeli.

kumbukeni

Hii ina maana ya kukumbuka kipindi cha nyuma.

tutazame sisi sote

Isaya anamuuliza Yahwe kuzingatia kwa makini hali yao.

Isaiah 64:10

Taarifa ya Jumla

Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza na Yahwe.

Miji yako mitakatifu imekuwa nyika

Hii inasisitiza ya kwamba miji imeangamizwa na hakuna aishiye kule.

Hekalu letu takatifu na zuri, ambapo baba zetu walikusifu, limeangamizwa kwa moto

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Adui ameangamiza hekalu letu takatifu na zuri, pale ambapo baba zetu walikusifu, kwa moto"

Unawezaje kujizuia, Yahwe? Unawezaje kukaa kimya na kuendelea kutudhalilisha?

Wanatumia maswali kuelezea kukata tamaa kwao kwa sababu Mungu bado hajaja kuwasaidia. "Tafadhali usijizuie, Yahwe! Tafadhali usikae kimya na kuendelea kutuaibisha!"

Isaiah 65

Isaiah 65:1

Nilikuwa tayari

Hapa "nilikuwa" ina maana ya Yahwe.

Nimetandaza mikono yangu nje siku nzima kwa watu wakaidi

"Kutandaza nje mikono yangu" ni ishara ya mtu kuonyesha kusihi sana au ombi la nguvu. "Nimeendelea kuwaomba watu wakaidi kupokea msaada wangu"

Isaiah 65:3

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

katika bustani ... juu ya vigae vya matofali

Hii ina maana ya maeneo ya Wakaanani kwa ajilii ya kuabudu sanamu. Madhabahu yao matakatifu yalitengenezwa kwa tofali, ambayo Yahwe alikataza kwa ajili ya madhabahu yake. Madhabahu ya Yahwe ilitengenezwa kwa mawe.

wanakaa miongoni mwa makaburi na kulinda usiku kucha

Hii ni kumbukumbu ya kushauriana na wafu, zoezi ambalo Yahwe alikataza.

wanakula nyama ya nguruwe

Yahwe hakuruhusu watu wa Israeli kula nyama kutoka katika nguruwe.

Isaiah 65:5

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa watu wa Israeli n kuhusu wao.

Mambo haya ni moshi puani mwangu

Yahwe analinganisha watu hawa ambao wanaendelea kumuudhi kwa moshi unaosumbua kupumua kwa mtu.

moto unaowaka siku nzima

Yahwe analinganisha watu wa Israeli kwa moto unaowaka taratibu ambao hutuma moshi bila kukoma huku ikisumbua.

Isaiah 65:6

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya watu wa Israeli.

Tazama, imeandikwa

"tambua na zingatia kwa makini"

katika mapaja yao

Hii iina maana Mungu atawaadhibu kikamilifu. Msemo huu unalinganisha Yahwe kuadhibu watu kwa kutupa miguu yao wanapokaa.

Isaiah 65:8

Kama pale juisi inavyopatikana kwenye vishada vya mizabibu

Yahwe analinganisha watu wa Israeli kwa kishada cha mizabibu ambacho bado kina juisi nzuri ndani yake.

pale juisi inavyopatikana kwenye vishada

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "utakapokuta juisi katka kishada"

sitawaharibu wote

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya chanya. "Nitawaacha wale ambao ni wa haki"

Isaiah 65:9

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

milima yangu

Hii ina maana ya maeneo ya juu kabisa ya Yerusalemu na Yuda yote.

Sharoni

Hili lilikuwa eneo lenye rutuba la malisho.

bonde la Akori

Hili ni jina la bonde ambalo huenda linaweza kukiimbia kutoka Yerusalemu mpaka kusini mwa Yeriko. Hili pia lilikuwa eneo lenye rutuba la malisho.

Isaiah 65:11

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

mlima mtakatifu

"Mlima mtakatifu" ni Mlima Sayuni, katika Yerusalemu. "katika mlima mtakatifu wote wa Yahwe"

ambao huandaa meza ... na kujaza vikombe vya divai kwa divai iliyochanganywa

Watu huleta chakula na kinywaji na kuviweka mbele ya sanamu kama sehemu za ibaada yao.

divai iliyochanganywa

divai iliyochanganywa na viungo

Bahati ... Hatma

Haya ni majina ya miungu ya uongo. Pia wanaitwa "Gadi" na "Meni".

Isaiah 65:12

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa wale wa Israeli ambao huabudu sanamu.

amekukusudia kwa ajili ya upanga

"Upanga" inawakilisha silaha za vita ambazo Yahwe atatumia kuafhibu wale ambao hawaitikii wito wa Yahwe.

nilipoita, haukujibu; nilipozungumza, haukusikiliza

Vishazi vyote vina maana moja na vinarudiwa kwa ajili ya msisitizo.

Isaiah 65:13

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa wale wa Israeli ambao huabudu sanamu.

Tazama, watumishi wangu

"Tambua na zingatia kwa makini" Yahwe anarudia hili kwa ajili msisitizo.

lakini utalia kwa sabubu ya maumivu ya moyo, na utaomboleza kwa sababu ya kupondwa kwa roho

Vishazi hivi vina maana moja na marudio ni kwa ajili ya msisitizo.

kupondwa kwa roho

Msemo huu unalinganisha hisia ya kuvunjwa moyo sana na majonzi kwa kitu kuharibika umbo kwa sababu ya shinikizo la juu.

Isaiah 65:15

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kwa wale wa Israeli ambao huabudu sanamu.

atabarikiwa na mimi, Mungu wa ukweli

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mimi, Mungu ambaye huzungumza ukweli daima, nitambariki"

shida za awali zitasahaulika ... zitafichwa

Vishazi hivi inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "watasahau shida zao za awali, kwa maana shida hizi zitatoweka katika kumbukumbu zangu"

zitafichwa kutoka machoni pangu

"kufichwa machoni pangu" inawakilisha uzingatiaji na kumbukumbu ya Yahwe. "Hata sitawaza juu yao tena"

Isaiah 65:17

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Maana tazama

"Tambua! Zingatia kwa makini!"

mbingu mpya na dunia mpya

Tofauti zote ambazo pia huwakilisha kila kitu katikati.

mambo ya awali hayatakumbukwa au kuletwa akilini

Vishazi hivi viwili vina maana moja na zinaungwa kwa ajili ya msisitizo. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hautafikiria juu ya kile kilichotokea kipindi cha nyuma"

Lakini utakuwa na furaha

Hapa "utakuwa" ina maana watumishi wote wa Mungu.

kutoa machozi na vilio vya dhiki havitasikiwa tena kwake

Unaweza kuelewa hii katika hali ya kutenda. "hakuna mtu atasikia machozi na kulia kwa dhiki tena kwake"

Isaiah 65:20

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya watu wake waaminifu.

miaka mia moja

"miaka 100"

atachukuliwa kuwa mtu kijana

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu watamchukulia kuwa mtu kijana"

atachukuliwa kuwa amelaaniwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu watamchukulia mtu huyu kuwa amelaaniwa"

Isaiah 65:22

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya watu wake waaminifu.

kama itakavyokuwa siku za miti ndivyo zitakuwa siku za watu wangu

"Siku" ina maana ya urefu wa maisha yao. "kwa maana watu wangu wataishi kwa urefu kama miti inavyoishi"

wao ni watoto wa wale waliobarikiwa na Yahwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wao ni watoto wa wale ambao Yahwe amewabariki"

Isaiah 65:24

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya watu wake waaminifu.

mliima mtakatifu

"Mlima mtakatifu" ni Mlima Sayuni, katika Yerusalemu. "katika mlima mtakatifu wote wa Yahwe"

Isaiah 66

Isaiah 66:1

Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni kigoda cha miguu yangu

Yahwe analinganisha mbingu kwa kiti cha enzi na dunia kwa kigoda cha miguu kusisitiza jinsi alivyo mkuu.

nyumba utakayoijenga kwa ajili yangu iko wapi basi? Sehemu nayoweza kupumzika iko wapi?

Yahwe anatumia maswali kusisitiza ya kuwa wanadamu hawawezi kujenga sehemu kwa ajili yake kuishi.

Isaiah 66:2

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Mkono wangu umefanya vitu hivi vyote

"Mkono" ina maana ya nguvu na mamlaka ya Yahwe, sio mwili wa kihalisia.

Tamko la Yahwe

Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "tamko" linaelezwa kama kitenzi "kutamka" au "alisema kwa dhati". "hiki ndicho Yahwe wa majeshi alvyotamka" au "hiki ndicho Yahwe wa majeshi alivyosem kwa dhati".

waliovunjika na walio na majuto rohoni

Hapa "kuvunjika" na "kujuta" ina maana ya mtu ambaye ni mnyenyekevu kiukweli na ambaye huteseka kwa ajili ya imani yake.

Isaiah 66:3

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Yule anayechinja ... pia hubariki uovu

Vishazi hivi vnne vyote vinafafanua njia tofauti watu waovu wanavyofanya na kufikia maana moja kwa ajili ya msisitizo.

Wamechagua njia zao wenyewe

"Wamechagua kufanya mambo maovu ambayo hukiuka njia za Yahwe"

Isaiah 66:4

Yahwe anaendelea kuzungumza kuhusu watu waovu.

Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya watu waovu.

Walifanya kilicho kiovu machoni mwangu

Hapa "machoni" ina maana ya Yahwe kuwachukulia tabia zao. "Walifanya kile nilichochukulia kuwa uovu"

Isaiah 66:5

Na atukuzwe Yahwe

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mtukuze Yahwe" au "Na Yahwe ajitukuze mwenyewe"

lakini wataaibishwa

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "lakini nitawatia aibu"

Isaiah 66:6

Yahwe anafafanua adhabu kwa unafiki wa wanaoabudu.

Yahwe anafafanua adhabu kwa unafiki wa wanaoabudu.

Sauti ya ghasia ya vita

Sauti inawakilisha ugomvi wa kweli ambao unaendelea katika hekalu wakati Yahwe anatekeleza adhabu.

Isaiah 66:7

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza.

Kabla hajaingia katika uchungu, anazaa; kabla maumivu hayajaja juu yake, alimzaa mwana wa kiume

Yahwe anazungumza kuhusu Sayuni kana kwamba ilkuwa mwanamke ambaye anataka kuzaa. Ingawa Sayuni iliangamizwa na watu hawakuishi huko tena, Yahwe anaahidi ya kuwa bila kukawia na kwa juhudi kidogo taifa zima litatoka kwake.

Nani amesikia ju ya jambo kama hili? Nani ameona mambo haya? Je! nchi itazaliwa katika siku moja? Je! taifa linaweza kuimrishwa katika muda mmoja?

Yahwe anatumia maswali kusisitiza jinsi tukio hili litakavyokuwa la kipekee. Muendelezo wa maswali unajenga mtanuko hadi Sayuni hatimaye inatajwa.

Isaiah 66:9

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya Yerusalemu kana kwamba ilikuwa mama.

Je! nitamleta mtoto mchanga karibu na uwazi wa kuzaliwa ... kuzaliwa?

Yahwe anatumia maswali kusisitiza ya kwamba hatashindwa kutimiza ahadi zake kwa watu wa Yerusalemu.

Isaiah 66:10

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza kuhusu Yerusalemu kana kwamba ilikuwa mama na wakazi wa Yerusalemu kana kwamba walikuwa watoto wachanga wapya.

Kwa maana utanyonya na kutosheka; kwa matiti yake utafarijiwa

Hii ina maana Yerusalemu itakuwa sehemu ya usalama na faraja kwa watu wa Mungu. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Kwa maana atakuridhisha kwa maziwa yake; atakufariji kwa matiti yake"

Isaiah 66:12

Maelezo ya Jumla

Yahwe anaendelea kuzungumza juu ya Yerusalemu kana kwamba ilikuwa mama.

kama mto ... kama kijito kinachomwagikia

Hii ina maana Mungu atasababisha watu wa mataifa kuleta kiasi kikubwa cha utajiri, ambacho kitakuwa cha kudumu kama mto na wingi.

Utanyonya kando yake, kubebwa mikononi mwake, na kuchezeshwa juu ya magoti yake

Hii ina maana Yerusalemu itakuwa sehemu ya usalama na faraja kwa watu wa Mungu.

kubebwa mikononi mwake, na kuchezeshwa juu ya magoti yake

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "atakubeba mikononi mwake na kukurusha juu ya magoti yake kwa furaha"

kwa hiyo nitakufariji, na utafarijiwa Yerusalemu

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa hiyo nitakufariji katika Yerusalemu"

Isaiah 66:14

Maelezo ya Jumla

Isaya anazungumza kwa watu waaminifu wa Mungu.

mifupa yako itachipuka

"Mifupa" ina maana ya mwili mzima kama sehemu yake.

itachipuka kama nyasi laini

"Nyasi laini" huota haraka na kwa imara na hulinganisha na afya na nguvu ya watu waamniifu wa Mungu.

Mkono wa Yahwe utajulikana kwa watumishi wake

Hapa "mkono" una maana ya nguvu yake. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atadhihrisha nguvu yake kwa watumishi wake"

Isaiah 66:15

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza kwa watu waaminifu wa Mungu.

anakuja na moto

Yahwe kuonekana katika Agano la Kale mara kwa mara huunganishwa na moto ambao huwakilisha hasira ya Yahwe na hukumu.

kama dhoruba ya upepo

Dhoruba inawakilisha matendo yenye nguvu ya Yahwe ya kufanya hukumu yake kuwa na manufaa.

kwa upanga wake

"Upanga" ni silaha ambayo inawakilisha vita zote na mauaji.

Wale watakaouawa na Yahwe watakuwa wengi

Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe ataua watu wengi"

Isaiah 66:17

Maelezo ya Jumla

Isaya anaendelea kuzungumza.

Wanajiweka wakfu

"Wanajiweka" ni wale ambao huabudu Yahwe lakini wanaenda kinyume na sheria zake.

kuingia katika bustani

Hii ni sehemu ambapo watu wataenda kuabudu sanamu.

yule aliye katikati

Hii inafafanua kionogzi wa wale ambao huenda kuabudu sanamu.

tamko la Yahwe

Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "tamko" linaelezwa kama kitenzi "kutamka" au "alisema kwa dhati". "hiki ndicho Yahwe wa majeshi alvyotamka" au "hiki ndicho Yahwe wa majeshi alivyosem kwa dhati"

Isaiah 66:18

Kwa maana mimi ninajua

Hapa "mimi" ina maana ya Yahwe

matendo yao ... mawazo yao

Hapa "yao" ina maana ya wanaoabudu ambao ni wanafiki ambao Yahwe amekwisha wafafanua awali.

Puli ... Ludi ... Tubali ... Yavani

Haya ni majina ya maeneo ambayo yapo mbali kutoka nchi ya Israeli.

Isaiah 66:20

Wataleta

Hapa "wataleta" ina maana ya wageni ambao walisalia na kushuhudia mataifa. Watarudi Yerusalemu na walio uhamishoni wa Israeli.

mlima mtakatifu

"Mlima mtakatifu" ni Mlima Sayuni, katika Yerusalemu. "katika mlima mtakatifu wote wa Yahwe"

Isaiah 66:22

mbingu mpya na dunia mpya

Zote ni utofauti mkubwa mno ambao pia huwakilisha kila kitu katikati.

tamko la Yahwe

Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "tamko" linaelezwa kama kitenzi "kutamka" au "alisema kwa dhati". "hiki ndicho Yahwe wa majeshi alvyotamka" au "hiki ndicho Yahwe wa majeshi alivyosem kwa dhati"

Isaiah 66:24

Maelezo ya Jumla

Yahwe anamaliza kuzungumza.

Watatoka nje

Hapa "watatoka" ina maana ya watu wote, waaminifu wa Israeli na wageni, ambao huja kumwabudu Yahwe.

funza ... na moto

Vishazi vyote viwili vinafafanua wazo moja kusisitiza adhabu ya Yahwe.

funza ambazo zinawala

Funza zinawakilisha utisho wa kuoza ambao ni adhabu ya Yahwe kwa waovu.

moto unaoteketeza

Moto pia unawakilisha hukumu ya Yahwe.

hautazimishwa

Hii inaweza kuelezwa kwa chanya. "utachoma milele"

wote wenye mwili

Msemo huu unawakilisha viumbe vyote hai vilivyoumbwa ambavyo hurudi kutoka kwa wafu.