Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Hosea 1

Hosea 1:1

Neno la Bwana lililofika

"Neno ambalo Bwana Mungu aslilisema"

Beeri.

Hili ni jina la mwanaume.

Uzia ... Yothamu ... Ahazi ... Hezekia ... Yeroboamu ... Yoashi

Matukio yaliyopo katika kitabu hiki yalitokea katika kipindi cha wafalme hawa.

Ukahaba mkubwa

"ukahaba" inawakilisha watu wanavyokuwa sio waaminifu kwa Mungu.

Hosea 1:3

Gomeri ... Diblaimu

Haya ni majina ya watu.

Nyumba ya Yehu

"nyumba" inamaanisha "familia" wakiwemo Yehu na uzao wake.

Nyumba ya Israeli

Maeliezo haya yanamaana ya ufalme wa Israeli.

Upinde wa Israeli.

Hapa "upinde" inamaana ya nguvu za jeshi. "nguvu za jeshi la Israeli"

Hosea 1:6

Lo Ruhama

Jina hili lina maana ya "sitawahurumia."

Hosea 1:8

Lo Ruhama

Jina hili lina maana ya "sitawahurumia."

Lo Ami

Jina hili lina maana ya "si watu wangu"

Hosea 1:10

Taarifa ya jumla

Bwana anazungumza na Hosea.

kama mchanga wa bahari

Hii inasisitiza idadi kubwa ya Waisraeli.

ambayo haiwezi kupimwa au kuhesabiwa

"ambayo hamna hata mmoja anayeweza kupima au kuhesabu"

Itakuwa pale ambapo waliambiwa

"Ambapo Mungu aliwaambia"

pale ambapo waliambiwa

Yamkini maneno haya yanaelekezwa kwa Yezreeli, mji ambao makosa yalifanywa na wafalme wa Israeli na ambayo ilikuwa ishara ya adhabu ya Mungu juu yao.

Wataambiwa

"Mungu atawaambia"

watakusanyika pamoja

"Mungu atawakusanya pamoja"

watatoka kutoka nchi

Hii inamaanisha nchi ambayo watu wa Israeli walichukuliwa mateka.

siku ya Yezreeli

Mungu atawaweka watu wake nyuma katika nchi ya Israeli.

Hosea 2

Hosea 2:1

Sentensi unganishi:

Bwana anazungumza na Hosea.

Watu wangu!

"Ninyi ni watu wangu"

umeoneshwa huruma.

"Bwana amewaonesha huruma"

Huruma

"wema" au "rehema"

Hosea 2:2

Taarifa ya jumla

Bwana anazungumza na Hosea.

Mashtaka

Haya ni malalamiko ya mtu mmoja dhidi ya mtu mwingine mahakamani.

Mama yako

Hapa "mama" inamaanisha taifa la Israeli.

kwa kuwa yeye si mke wangu

Bwana anaeleza kuwa Israeli inazungumzwa kama mwanamke ambaye hatendi kama mke kwa Bwana. Badala yake Israeli amegeuka na kuacha kumfuata na kumwabudu yeye.

wala mimi si mumewe

Bwana hawezi kuendelea kuwa na uhusiano na taifa la Israeli kama mume kwa mke wake.

na matendo yake ya uzinzi

Mke ambaye ni mzinzi anamuacha mume wake na kulala na mwanaume mwingine. Hivi ndivyo Israeli alivyofanya mbele ya Bwana.

kati ya matiti yake

Israeli wanategemea miungu na sio Bwana.

nitamvua nguo na kumuonyesha uchi wake kama siku aliyozaliwa

Bwana hataendelea kuwalinda na kuwasaidia Israeli kwa sababu taifa limemwacha.

nitamfanya kama jangwa

Bwana ataibadilisha Israeli ifanane na jangwa ambao nii mji usiozalisha.

nitamfanya afe kutokana na kiu

Hapa "kiu" inamaana ya uhitaji wa kumwabudu Bwana na sio miungu mingine, au Israeli hawatatweza kuishi kama taifa.

Hosea 2:4

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza na Hosea.

kwa maana wao ni watoto wa ukahaba.

Waisraeli wanafanya kama vile sio wa Bwana. Kama wazazi wao walivyofanya hawakumwabudu Mungu, na wao pia.

Maana mama yao amekuwa kahaba

Kizazi kilichopita waliitumikia miungu mingine na kuonekana kuwa ni makahaba kwa kuwa hawakuwa waaminifu kwa Mungu.

Nitawafuata wapenzi wangu, kwa maana wananipa mkate wangu na maji, sufu yangu na kitani, mafuta yangu na kinywaji.

Hapa "wapenzi wangu" inamaanisha Baali na miungu mingine ya uongo ambao Israeli walichagua kuiabudu badala ya Bwana.

Hosea 2:6

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza na Hosea.

Kwa hiyo nitajenga ua wa kuzuia njia yake kwa miiba. Nitajenga ukuta dhidi yake ili asiweze kupata njia

Maneno haya yanaonesha kuwa Bwana atawazuia watu wake wasipate mafanikio kwa sababu wanaiabudu miungu.

Kisha atasema, "Nitarejea kwa mume wangu wa kwanza, kwa maana ilikuwa ni bora kwangu zamani kuliko sasa."

Israeli watarejea kwa Bwana sio kwa sababu ya upendo wao kwake lakini kwa sababu wameumizwa kwa kumwabudu Baali.

Hosea 2:8

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza na Hosea.

Nitachukua sufu yangu na kitambaa kilichotumiwa kufunika uchi wake

Hii ina maana ya kwamba mavuno ya Israeli hayatakua. Bwana ataondoa baraka toka Israeli na watu wataachwa peke yao katika hatari.

kilichotumiwa kufunika uchi wake

"kitu ambacho watu hutumia kujifunika wenyewe"

Hosea 2:10

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza na Hosea.

nitamvua nguo machoni pa wapenzi wake

Hii inamaanisha Mungu atawaaibisha watu wa Israeli mbele ya mataifa mengine.

hakuna mtu atakayemwokoa mkononi mwangu

Hakuna mtu atakayewasaidia Israeli. Hapa "mkono" inamaana ya nguvu ya Mungu kuhukumu.

Hosea 2:12

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza na Hosea juu ya kile atakachokifanya kwa Israeli.

Hii ni mishahara ambayo wapenzi wangu walinipa

"huu ndio mshahara ambao atapewa na wapenzi wake"

Nitawafanya kuwa msitu

Bwana ataangamiza mizabibu na miti yake ya matunda kwa kuruhusu miti mingine na magugu kukua pamoja.

tamko la Bwana

"ambalo Bwana anasema"

Hosea 2:14

Sentensi unganishi:

Bwana anazungumza kuhusu Israeli.

hiyo nitaenda kumshawishi

"Mimi, Bwana nitamrudisha kwangu"

bonde la Akori kama mlango wa tumaini

Bwana atawaongoza Israeli tukoka Misri, atawaongoza Israeli katika bonde la Akori ili wamtumaini tena Bwana.

Yeye atanijibu huko kama alivyofanya katika siku za ujana wake, kama katika siku ambazo alitoka katika nchi ya Misri

Bwana anatumaini kwamba taifa la Israeli litatubu na kuchagua kumwabudu yeye kama Mungu wao.

Atajibu

Baadhi ya matolea ya kisasa ya kiebrania maneno haya yana maana ya "Ataimba."

Hosea 2:16

Itakuwa katika siku hiyo

Hii inamaanisha siku ambayo Israeli walichagua kumwabudu Bwana pekee.

tamko la Bwana

"Kitu ambacho Bwana amezungumza"

Mungu wangu

Hii inamaanisha watu wa Israeli watampenda na kuwa waaminifu kwa Bwana kama vile mke kwa mume wake.

Baali wangu

"Baali" inamaanisha miungu ya uongo ambayo Wakaanani wanaabudu.

Kwa maana nitaondoa majina ya Baali kinywani mwake

Waisraeli hawatataja majina ya Baali na miungu mingine.

Hosea 2:18

Sentensi unganishi:

Bwana anazungumza na Hosea kuhusu namna atakavyowafanyia Israeli.

Siku hiyo

Hii inazungumzia kuhusu urejesho wa baadae kati ya Israeli na Bwana.

Nitafanya agano kwao

Agano la Bwana litajumuisha amani kwa wanyama.

Nitaondoa upinde, upanga, na vita katika nchi, nami nitakufanya ulale kwa usalama.

Bwana atawaweka adui wa Israeli mbali na wao, hakutakuwa na vita tena watu watakuwa salama.

ulale kwa usalama

Kuishi kwa usalama.

Hosea 2:19

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza na Hosea kuhusu namna atakavyowafanyia Israeli.

Nitakuwa mume wako milele

Bwana atakuwa kama mume na Israeli atakuwa kama mke wa Bwana.

Nitakuwa mume wako kwa uaminifu

Bwana atakuwa mwaminifu kwa agano lake kwa Israeli.

mume kwa uaminifu

"mume mwaminifu"

Nawe utanijua mimi, Bwana

Hapa "kuniju" inamaanisha kumtambua Bwana kama Mungu na kuwa mwaminifu kwake.

Hosea 2:21

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza na Hosea kuhusu namna atakavyowafanyia Israeli.

ndilo tamko la Bwana

"Kitu ambacho Bwana amezungumza"

Dunia itashughulikia nafaka, divai mpya na mafuta, na watajibu Yezreeli.

Nchi itazalisha nafaka na divai mpya na mafuta.

Yezreeli

Jina la bonde hili linasimama kwa watu wa Israeli.

Hosea 2:23

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza na Hosea kuhusu namna atakavyowafanyia Israeli.

Nitatampanda mwenyewe katika nchi

Mungu atawaweka watu wake salama katika nchi yao tena. "Atawajali watu wa Israeli kama vile mkulima anavyopanda mazao yake na kujali"

Lo Ruhama

Jina hili lina maana ya "hakuna huruma."

Lo Ami

Hii ina maana ya "sio watu wangu."

Ami Ata

Jina hili lina maana ya "wewe ni mtu wangu."

Hosea 3

Hosea 3:1

"Nenda tena, mpendeni mwanamke, aliyependwa na mumewe; lakini ni mzinzi.

Bwana anamwambia tena Hosea ampende mwanamke mzinzi.

Mpende kama mimi, Bwana, ninavyowapenda watu wa Israeli

Kwa kumpenda mwanamke mzinzi, Hosea ataonesha mfano wa upendo wa Bwana kwa Israeli.

wanaigeukia miungu mingine na kupenda mikate ya zabibu.

Watu walikula mikate ya zabibu kipindi cha sikukuu walipokuwa wakiabudu miungu yauongo.

vipande kumi na tano vya fedha na homeri na letheki ya shayiri

Hii ndo ilikuwa gharama ya kununua mtumwa.

vipande kumi na tano

"vipande 15"

homeri na letheki

"homeri na nusu ya homeri"

Hosea 3:4

Kwa maana wana wa Israeli wataishi kwa siku nyingi bila mfalme, mtu mkuu, dhabihu, nguzo ya mawe, efodi au sanamu za nyumbani.

Kama vile Hosea hakuishi na mke wake kwa sababu alikuwa mzinzi, Israeli wataishi bila mfalme na bila kumwabudu Mungu kwa sababu wamefanya uzinzi.

kumtafuta Bwana Mungu wao

"kimtafta" inamaanisha kumwomba Mungu kuwakubali wao.

Daudi mfalme wao

"Daudi" inawakilisha uzao wote wa Daudi. "uzao wa Daudi utakuwa mfalme wao"

Na katika siku za mwisho

Hapa "siku za mwisho" inamaanisha kipindi cha baadae.

watakuja wakitetemeka mbele za Bwana na wema wake.

Hapa "kutetemeka" inawakilisha hisia za utu. "Walirejea kwa Bwana wakijinyenyekesha wenyewe, kumtii yeye na kuomba baraka zake"

Hosea 4

Hosea 4:1

Taarifa ya jumla:

Sura hii inaanza kwa kuonesha malumbano ya Bwana dhidi ya Waisraeli wasio waaminifu.

Bwana ana mashtaka dhidi ya wenyeji wa nchi

Bwana anaeleza kuwa wana wa Israeli wamefanya dhambi dhidi yake na kuvunja agano lake hii inazungumzwa kama vile Bwana anawashitaki mahakamani.

Mashitaka

Haya ni malalamiko ya mtu mmoja dhidi ya mtu mwingine mahakamani.

Watu wamevunja mipaka yote

"mipaka" ni mwisho wa vitu ambavyo sheria inaruhusu. "Watu wamevunja sheria kwa namna zote"

damu inakuja baada ya damu

"damu" inasimama kama mauaji.

Hosea 4:3

Kwa hiyo nchi inakauka

Maelezo haya yanamaanisha ukame ambapo mvua haijanyesha kwa muda mrefu.

Anaangamia

kuwa dhaifu na kufa kwa sababu ya ugonjwa au kukosa chakula.

wanaondolewa

"wanakufa"

Hosea 4:4

Taarifa ya jumla:

Mungu anazungumza juu ya Israeli.

Mashitaka

Haya ni malalamiko ya mtu mmoja dhidi ya mtu mwingine mahakamani.

msiruhusu mtu yeyote ahukumu mtu mwingine

Mtu yeyote asimuhukumu mtu mwingine kwa lolote kwa sababu kila mtu ni mkosaji wa jambo fulani.

Ninyi makuhani mtajikwaa

"kujikwaa" inamaanisha kutomtii Mungu na kuacha kumtumaini.

nitamwangamiza mama yako

Hapa "mama" inamaanisha taifa la Israeli.

Hosea 4:6

Taarifa ya jumla:

Katika 4:6 Bwana anazungumza na kuhani kuhusu watu wa Israeli. Lakini katika 4:7 anazungumza kuhusu kuhani na sio kwao.

Watu wangu wanaharibiwa kwa sababu ya ukosefu wa maarifa

"Watu wangu wanaharibiwa kwa sababu yenu, makuhani hamjawafundisha vema kuhusu mimi ili wanitii mimi"

Maarifa

Hapa "maarifa" inamaanisha maarifa juu ya Mungu.

Walibadilisha heshima zao kwa aibu

Yawza kuwa na maana ya 1) "heshima" inawakilisha Bwana, na "aibu" inawkilisha miungu. 2) Baadhi ya maandiko yametafsiri "Nitabadili heshima yao kwa aibu." Hii inamaana kuwa Bwana atachukua vitu ambavyo makuhani wanaviheshimu na kusababisha waaibike.

Hosea 4:8

Taarifa ya jumla:

Bwana anaendelea kuzungumza kuhusu makuhani.

Wanajilisha dhambi ya watu wangu

Watu walipotenda dhambi walitoa sadaka ili Mungu awasamehe. Makuhani waliruhisiwa kula sadaka hizo.

wao ni wenye tamaa zaidi ya uovu wao

Makuhani walitaka watu waendelee kutenda dhambi ili watoe sadaka ambazo makuhani watazila.

Itakuwa sawa kwa watu kama kwa makuhani

"Watu pamoja na makuhani watapewa adhabu ile ile"

matendo yao.

"tabia zao"

Hosea 4:10

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza juu ya Israeli.

lakini hawataongezeka

"lakini hawatakuwa na watoto"

wamekwenda mbali

Watu wameacha kumwabudu na kumfuata Mungu.

Bwana

Mtafsiri yupo huru kubadilisha "Bwana" na kuweka "mimi" kwa sababu Bwana ndiye anayeongea maneno haya.

Hosea 4:11

Taarifa ya jumla"

Bwana anazungumza juu ya Israeli.

uasherati, divai, na divai mpya, ambayo imechukua uelewa wao

Watu wa Israeli wanafanya uzinzi nje ya ndoa na wanakunywa sana mvingo. Kwa kufanya hivi wamesahau amri za Bwana.

fimbo zao za kutembelea huwapa unabii

Waabudu sanamu hutumia fimbo za kutembelea ili kutabiri yajayo.

mawazo ya uasherati yamewadanganya

Kuabudu miungu na kulala na wanawake makahaba wa hekaluni inawzfanya watu wa Israeli watamani kuendelea kutenda dhambi dhidi ya Bwana.

yamewadanganya

"kuwashawishi watu kufanya dhambi"

Hosea 4:13

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza juu ya Israeli.

juu ya milima ... kwenye milima

Ilikuwa ni kawaida watu kuweka miungu kwenye maeneo hayo, mara nyingi huitwa "sehemu za juu" katika agano la kale.

makahaba

Hawa ni wanawake wanaofanya uzinzi na wanaume wanaoenda kuabudu miungu fulani.

Hivyo watu wasiofahamu wataangamizwa.

Bwana ataangamiza taifa la Israeli kwa sababu hawakuelewe wala kutii amri za Mungu.

Hosea 4:15

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza juu ya Yuda na Israeli.

Yuda asiwe na hatia

Mungu anajua ni kwa kiasi gani Israeli wamefanya dhambi na hataki Yuda afanye kitu hicho hicho.

Ninyi msiende Gilgali; msiende hadi Beth Aven

Watu wa Yuda wanaonywa wasiende kwenye mji wa Gilgali au Beth Aven kuabudu miungu katika maeneo hayo.

Beth Aven

Huu ulikuwa mji uliokuwa kaskazini mpakati mwa ufalme wa Israeli na kabila la Benyamini lililopo kusini mwa ufalme.

kama ndama mkaidi

Israeli anafananishwa na ndama ambaye hamsikilizi bwana wake.

Je! Bwana anaweza kuwaleta kwenye malisho kama kondoo mahali penye nafasi?

Bwana hawezi kuwalisha watu kama kondoo wakati watu ni waasi.

Hosea 4:17

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza juu ya Israeli.

Efraimu alijiunga na sanamu; mwache peke yake

Efraimu ni watu wa kaskazini mwa ufalme wa Israeli. Walichagua kuabudu miungu badala ya Bwana. Bwana anamuamuru Hosea asijaribu kuwarekebisha maana hawatasikia.

watawala wake hupenda sana aibu yao

Viongozi hawaoni aibu ya kile walichokifanya wanapoabudu miungu na kugeuka dhidi ya Bwana.

Upepo utamfunga kwa mabawa yake

Hapa "upepo" unawakilisha hukumu ya Mungu na hasira juu ya taifa la Israeli. Bwana ataruhusu maadui wawashinde watu wa Israeli na kuwachukua mateka.

Hosea 5

Hosea 5:1

Sentensi unganishi:

Bwana anazungumza kuhusu Israeli.

Mmekuwa mtego huko Mizpa na wavu uliosambazwa juu ya Tabori.

Mtego na wavu ni vifaa vinavotumika kukatatia mawindo. Misoa na Tabori yalikuwa maeneo ya kuabudia miungu katika nchi ya Israeli.

Waasi husimama sana katika mauaji

"waasi" ni wale wote waliomuasi Bwana na mauaji inaelezea namna ambavyo mauaji ya watu wasio na hatia yanafanyika ikiwemo kutoa kafara kwa miungu ya kipagani.

Waasi

Mtafsiri anaweza kuiweka hii kama "ninyi waasi" kwa sababu Mungu anazungumza juu ya watu waasi wa Israeli.

mauaji

Baadhi ya nakala za kisasa za kiebrania neno hili limesimama kama uovu.

nitawaadhibu wote

"Nitawaadhibu ninyi nyote"

Hosea 5:3

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza kuhusu Israeli.

Najua Efraimu, na Israeli hajajificha kwangu

"Efraimu" na "Israeli" ni watu ambao wanaishi kaskazini mwa ufalme wa Israeli. Hapa Mungu anasema kuwa anawafahamu wao ni akina nani na nini wanafanya.

Efraimu, sasa umekuwa kama kahaba

Efraimu amesimama kama kahaba kwa sababu watu sio waaminifu kwa Mungu kama vile kahaba sio mwaminifu kwa mwanaume mmoja.

maana mawazo ya uzinzi yako ndani yao

Hii inamaanisha kuwa wanatamani kutokuwa waaminifu kwa Mungu. Wanataka kuabudu miungu.

kumgeukia Mungu ... hawatamjua Bwana.

"kunigeukia mimi ... hawakunijua mimi" au "kunigeukia mimi ... hawakunijua mimi, Bwana."

na hawatamjua Bwana

Israeli hawakumtii tena Mungu kwa namna yoyote. Hawakumtambua Bwana kama Mungu wao.

Hosea 5:5

Taarifa ya jumla:

Mungu anazungumza juu ya Israeli.

Kiburi cha Israeli kinawashuhudia

Hii inamaanisha kwamba tabia yao ya kiburi inaonesha kwamba wana makosa ya kutomtii Bwana.

hiyo Israeli na Efraimu watajikwaa kwa hatia zao; na Yuda pia wataanguka pamoja nao

Falme mbili zitaacha kumtii Mungu kabisa kwa sababu ya kiburi chao na dhambi yao.

Walikuwa wasio waaminifu kwa Bwana, kwa kuwa wamezaa watoto haramu

Hii yaweza kuwa na maana 1) Waisraeli walioa watu toka mataifa mengine na kuzaa watoto pamoja nao au 2) Wazazi wa Israeli hawakuwa waaminifu na waliwafundisha watoto wao kuabudu miungu.

Sasa sherehe mpya za mwezi zitawaangamiza na mashamba yao.

Wana wa Israeli walipaswa kusherehekea kipindi cha mwezi moya. Maelezo haya yanaonesha kuwa mwezi mpya ni mnyama atakayewala watu na mazao yao. maana ya jumla ni kwamba Mungu atawaadhibu watu kwa kutokuwa waaminifu kwake.

Hosea 5:8

Taarifa ya jumla:

Mungu anazungumza juu ya Israeli.

Piga tarumbeta huko Gibea, na tarumbeta huko Rama.

Amri inatolewa kwa watu wa Gibea na Rama kusistiza kuwa adui anakuja.

Sauti ya kilio cha vita huko Beth Aveni 'Tutakufuata, Benyamini!'

Hili ni ombi kuwa askari wa Benyamini wawaongoze watu katika vita.

Beth Aveni

Huu ni mji uliokuwepo mpakani kati ya ufalme wa kaskazini mwa Israeli na kabila la Benyamini kusini mwa ufalme.

Miongoni mwa makabila ya Israeli nimetangaza habari itakayotokea.

"Nitafanya katika kabila la Israeli yale niliyosema"

Hosea 5:10

Taarifa ya jumla:

Mungu anazungumza juu ya Yuda na Israeli.

Viongozi wa Yuda ni kama wale wanaoondoa jiwe la mipaka

"kuondoa jiwe la mpaka" ni kuondoa alama ya nchi inatoonesha mpaka wa mali ya mtu ambayo ilikuwa ni kosa kwa sheria za Israeli.

nitamwaga ghadhabu yangu juu yao kama maji

Hasira ya Bwana dhidi ya Yuda ni kama maji mengi yenye uwezo wa kuangamiza. Kwenye maandiko hisia na tabia zimefananishwa na kimiminika.

Efraimu ameangamizwa; ameangamizwa kwa hukumu

"Nitawaangamiza watu wa Israeli"

kufuata sanamu

"Kufuata" inawakilisha kitendo cha kuabudu miungu.

miungu

Neno la Kiebrania limetafsiriwa hapa kama "miungu" na katika tafsiri za kisasa limetafsiriwa kwa namna nyingi.

Hosea 5:12

Taarifa ya jumla:

Mungu anazungumza juu ya Yuda na Israeli.

nitakuwa kama nondo kwa Efraimu, na kama uozo kwa nyumba ya Yuda

Bwana ataangamiza mataifa yote.

Nondo ... uozo

Maneno haya yanatafsiriwa kwa njia mbali mbali kwa sababu maana ya kiebrania ni pana sana na isiyo na uhakika.

Efraimu alipoona ugonjwa wake, Yuda akaona jeraha lake

Efraimu na Yuda wote walitambua kuwa wapo kwenye hatari.

Efraimu akaenda Ashuru; Yuda akatuma wajumbe kwa mfalme mkuu

Efraimu na Yuda walimuomba Ashuru msaada badala ya kumuomba Mungu awasaidie.

Lakini hakuweza

Hapa anazungumziwa mfalme wa Ashuru.

Hosea 5:14

Taarifa ya jumla:

Mungu anazungumza juu ya Yuda na Israeli.

Kwa hiyo nitakuwa kama simba kwa Efraimu

Bwana ataenda kuishambulia Efraimu kama simba.

kama mwana simba kwa nyumba ya Yuda

Bwana atawatendea Yuda vivyo hivyo.

Mimi, naam mimi

Bwana anasisitiza kuwa yeye ataleta hukumu kwa watu wake wote.

Nitararua

Kama simba anavyorarua mnyama anayemla hivyo Bwana atawararua watu waketoka kwenye nyumba na nchi yao.

Nitakwenda na kurudi mahali pangu

Bwana atawaacha waasi.

na kutafuta uso wangu

Kujaribu kwenda katika uwepo wa Mungu kwa njia ya kuabudu na kafara.

Hosea 6

Hosea 6:1

Sentensi unganishi:

Wana wa Israeli wanaonesha uhitaji wao wa kutubu.

ametuvunja ...ametujeruhi

Mungu amewaadhibu wana wa Israeli kwa sababu hawakumtii na waliabudu Miungu.

atatuponya ... atatufunga majeraha yetu

Israeli wanaamini kwamba Mungu atawahurumia wakitubu na atawakomboa kutoka kwenye matatizo yao.

Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua

Hii inawakilisha mda mfupi sana. Israeli wanaamini Mungu atakuja haraka kuwaokoa toka kwa adui zao.

siku mbili ... siku ya tatu

"siku 2 ... siku ya 3"

Nasi tumjue Bwana

"Kumjua" sio tuu kujifunza tabia za Bwana na sheria lakini pia kuwa mwaminifu kwake.

Kuja kwake ni hakika kama asubuhi

Bwana atakuwa kuwasaidia watu wake kama vile hakika jua linavyochomoza asubuhi.

Hosea 6:4

Sentensi unganishi:

Bwana anazungumza.

nikufanyie nini?

Mungu anaelezea kwamba subira yake inakaribia mwisho na kilichobaki ni hukumu.

Kwa hiyo nimewavunja vipande vipande kwa manabii

Kwa kupitia manabii wake, Bwana anatangaza kuangamiza taifa lililoasi.

Maagizo yako ni kama nuru inayoangaza

Hapa nabii Hosea anazungumza na Mungu. Anaweza kuwa na maana ya Mungu kutoa amri ya mtu kufa kama adhabu ni kama mwanga unaopiga. Au inaweza kuwa na maana kuwa Amri za Mungu zinawaruhusu watu kuijua kweli kama mwanga unaofanya vitu vionekane.

Maagizo yako

"Amri za Bwana"

Hosea 6:6

Taarifa ya jumla:

Bwama anazungumza.

natamani uaminifu wala si dhabihu

"kwa kuwa natamani uaminifu zaidi ya dhabihu"

Kama Adamu

Yaweza kuwa na maana ya 1) kumwelezea Adamu kama mtu wa kwanza au 2) inayowakilisha watu walioishi mjini Israeli wanaoitwa Adamu au 3) anawakilisha watu kwa ujumla.

Hosea 6:8

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Gileadi ni jiji ... wenye miguu ya damu

"miguu ya damu" inawakilisha watu waovu na vitendo vyao vya uuaji.

makuhani hujiunga pamoja kufanya mauaji kwa njia ya Shekemu

Hatufahamu maneno haya yanamaanihs nini Hivyo ni vyema kutafsiri sentensi hii kwa namna ambayo itaeleweka zaidi.

Hosea 6:10

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Uzinzi wa Efraimu

"uzinzi" inamaana kuwa Efraimu anaiabudu miungu ya uongo.

Israeli ametiwa unajisi

Israeli hajakubaliwa na Mungu kwa sababu ya vitendo vyake.

Kwa maana wewe, Yuda, mavuno yameteuliwa

"Nimetenga mda wa mavuno kwako pia , Yuda"

Mavuno

"Mavuno" inawakilisha siku ya Mungu ya mwisho ya hukumu kwa Israeli na Yuda.

Urihi

mafanikio na usalama

Hosea 7

Hosea 7:1

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Nataka kuiponya Israeli

Kuifanya Israeli imtii Mungu tena na kitendo cha kupokea baraka kinazungumzwa kama kitendo cha uponyaji.

kwa sababu wanafanya udanganyifu

Watu walikuwa wanauza na kununua bidhaa kwa udanganyifu.

kundi la wanyang'anyi

Hili ni kundi la watu wanaowavamia watu wengine bila sababu.

matendo yao huwazunguka

Haya matendo yao maovu yanafananishwa na watu wanaliotayari kuwashitaki kwa maovu yao.

yapo mbele ya uso wangu.

"Uso" huu ni uwepo wa Mungu.

Hosea 7:3

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Wote ni wazinzi

Watu wamefanya uzinzi wa kiroho kwa kuabudu miungu na kutokuwa waaminifu kwa Bwana. Pia hawakuwa waaminifu kwa wake zao na waume zao kwa kulala na watu wengine.

kama tanuru iliyochomwa na mwokaji

"kama tanuru ambalo mwokaji analichoma"

Kukanda unga

Hii ni moja ya hatua katika utengenezaji wa mkate.

Siku ya mfalme wetu

Yamkini hii ni sikukuu inayofanywa na mfalme.

Alinyoosha mkono wake

Hii inamaana kuwa mfalme ataungana na maofisa ili kuwadhihaki watu wasiopaswa kudhihakiwa na hata Mungu mwenyewe.

Hosea 7:6

Taarifa ya jumla:

Maafisa wa mahakama wanaelezewa. Hasira zao ziliwachochea kumuua mfalme.

kwa mioyo kama tanuru

Hii inamaanisha kuwa watu hawa walikuwa na nia ovu ndani mwao kama moto uwakao kwenye tanuru.

Hasira zao hulala

"hulala" Hii inamaanisha kuwa kitu kinachoungua taratibu.

huwaka juu kama moto

Hii inaonesha kuwa kiwango cha hasira yao ni kama moto mkali.

Wote wamepata moto kama tanuru

Hii inafananisha hasira yao na moto utakao kwenye tanuru.

huwaangamiza wale wanaowatawala

Hii inaonesha kuwa maofisa wa mahakama waliwaua wafalme wao.

Hosea 7:8

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Efraimu anajichanganya mwenyewe kati ya watu

Hii inaelezea namna ambavyo wafalme wa falme za kaskazini walifanya kwa bidii kujichanganya na mataifa mengine kwa ajili ya ulinzi dhidi ya uvamizi.

Efraimu ni mkate ambayo haujawahi kugeuzwa

Efraimu ni ufalme wa Kaskazini wa Israeli. Taifa dhaifu kama mkate ambao haujageuzwa na mwokaji ili uwe na nguvu.

Nywele za mvi hunyunyiza juu yake

"nywele za mvi" zinawakilisha umri mkubwa.

lakini hajui

Huu "umri mkubwa" inaonesha wazi kuwa ufalme wa kaskazini ulikuwa dhaifu siku hata siku lakini mataifa hayajui kuwa inazeeka.

Hosea 7:10

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Kiburi cha Israeli kinawashuhudia

Hii inamaanisha kwamba tabia yao ya kiburi inaonesha kwamba wana makosa ya kutomtii Bwana.

wala hawakumtafuta

Israeli waliacha kumtafuta Bwana.

licha ya hayo yote

Hapa "hayo" inamaanisha kitendo cha Mungu kuwaruhusu wageni wawashinde na kuwafanya dhaifu.

Efraimu ni kama njiwa, baradhuli na asiye na busara

Njiwa wanadhaniwa kuwa ni ndege wajinga.

Misri ... Ashuru

Haya ni mataifa yenye nguvu ambayo Israeli wangeomba msaada.

Hosea 7:12

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

nitasambaza wavu wangu juu yao

Hii ni njia ya kukamata ndege. Bwana anaendelea kuwafananisha Waisraeli na ndege. wakienda Misri kwa ajili ya msaada Bwana atawaadhibu.

nitawaangusha kama ndege wa angani

Bwana anazungumza namna atakavyowaangamiza Israeli kama vile atakavyomkamata ndege kwenye wavu.

katika kusonga kwao pamoja

Maelezo haya yanaendelea kusisitiza mfano wa ndege.

Hosea 7:14

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

wanaomboleza kwenye vitanda vyao

Ilikuwa ni kawaida kwa wanaoabudu sanamu kula nyama za sherehe wakiwa wamelala kwenye vitanda.

nao wananiasi mimi

Hawamwabudu tena Bwana wamegeuka na kumwacha.

Ingawa niliwafundisha na kuimarisha mikono yao

Mungu aliwafundisha Waisraeli kumpenda na kumtii yeye kitendo hiki kinazungumzwa kama kitendo cha kuwafundisha watu wake vita.

Hosea 7:16

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Wao ni kama upinde usiotumainika

Huu upinde hautumiki.

kwa sababu ya udhalimu wa vinywa vyao

Hapa "vinywa" ni maneno yaliyosemwa na maofisa. "Kwa sababu wamenitukana mimi" au "kwa sababu wamenilaani mimi"

Hii itakuwa ni aibu yao katika nchi ya Misri.

"Hii ndiyo sababu kwamba Misri itawacheka Waisraeli"

Hosea 8

Hosea 8:1

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza kuhusu ujio wa jeshi la Waashuru kuvamia ufalme wa kaskazini.

Tai anakuja juu ya nyumba ya Bwana

Tai mara nyingine ametumika kuwakilisha maadui wa Israeli.

wamevunja agano langu

Hapa "kuvunja" inamaanisha "kutotii"

tunakujua

Hii ina maana ya kwamba "sisi ni waaminifu kwako"

Hosea 8:4

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

ili wakatiliwe mbali

Hii inaweza kuandikwa "lakini matokeo yake yatakuwa kwamba nitawaharibu watu hao"

Kukatwa

Kuharibiwa

Ndama yako imekataliwa, Samaria

Inaweza kuwa na maana 1) Kuhani anazungumza au 2) Bwana anazungumza. "Mimi mwenyewe nitakataa ndama yako, Samaria."

Ndama wako

Mfalme Yeroboamu wa pili wa Israeli alitengeneza miungu miwili ya dhahabu inayofanana na ndama na kuiweka juu ili watu wa ufalme wake waziabudu.

Hasira yangu inawaka juu ya watu hawa

Hasira inazungumzwa kama moto.

Kwa muda gani watakuwa na hatia?

Bwana anauliza swali ili kuonesha hasira yake kuhusu watu wake walio chafuka. "Nina hasira na watu hawa kwa sababu hawatamani kuwa salama"

Hosea 8:6

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Kwa maana watu hupanda upepo na kuvuna kimbunga

Kupanda upepo ni kitendo cha kufanya jambo kwa njia zisizofaa. Kuvuna kimbunga ni kuteseka kutokana na matendo ya mtu mwenyewe.

Mbegu zilizosimama hazina vichwa

Hapa "kichwa" ni sehemu ya mmea mbayo mbegu zinakuwepo. Mmea ambao hauna kichwa unakuwa hauna chochote cha kumpa mkulima. Matendo ya Waisraeli hayatawapa matokeo mazuri.

Ikiwa itakomaa, wageni watakula.

Ikiwa matendo yoyote ya Waisraeli yatasababisha matokeo mazuri basi adui wa Israeli watayachukua.

Hosea 8:8

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Israeli imemezwa

"imemezwa" inamaanisha imekamatwa na kupelekwa uhamishoni.

kama punda wa mwitu pekee

Hii inamaanisha kuwa wana wa Israeli walikataa kumsikiliza Bwana lakini badala yake wakaenda kwa Ashuru kuimba msaada.

Efraimu ameajiri wapenzi kwa ajili yake mwenyewe

Kitendo cha Efraimu kushirikiana na mataifa mengine kinazungumzwa kuwa ni kitendo cha kuwalipa kuwa makahaba kwa Efraimu. "Wana wa Israeli walijaribu kuwalipa mataifa mengine ili wawalinde"

kwa sababu ya unyanyasaji wa mfalme wa wakuu.

Kwa sababu mfalme wa Ashuru aliitwa "mfalme mkuu" atawafanya watu wateseke.

Hosea 8:11

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Ningeandika sheria yangu kwao mara elfu kumi

Hii inamaanisha kwamba tayari Bwana aliwapa Israeli sheria yake kupitia manabii na kuwaambia ni kitu gani alitarajia kutoka kwao mara nyingi.

Elfu kumi

"10,000"

Hosea 8:13

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Watarudi Misri

Kwa sababu ya uovu wao Mungu atarudisha watu wake wawe watumwa kwa Wamisri.

Hosea 9

Hosea 9:1

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

Lakini sakafu na divai hazitawalisha

Hii inamaanisha kuwa mavuno hayatatoa nafaka ya kutosha kukidhi mahitaji ya watu na hakutakuwa na zabibu za kutosha kutengeneza mvinyo.

safafu ya kupuria

Hii ni sehemu kubwa inayotumika sio tuu kupuria nafaka lakini pia hutumiwa kwa sherehe za jamii na kidini.

divai mpya itampungukia.

Hakutakuwa na zabibu za kutosha kutengeneza mvinyo.

Hosea 9:3

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

Nchi ya Bwana.

Hii inaonesha kuwa Bwana anaendelea kuiona nchi ya Israeli kama mali yake na sio mali ya Waisraeli.

Chakula kichafu.

Hiki ni chakula ambacho Waisraeli hawakula kwa sababu kiliwafanya wasikubalike kwa Bwana.

Dhabihu zao zitakuwa kwao kama chakula cha matanga

Hapa "chakula cha matanga" ni chakula kinacholiwa wakati watu wanaomboleza kwa sababu hawajakubaliwa na Mungu. Hii inamaana kuwa Bwana hataiona dhabihu yao kuwa ni chafu na hata wakubali.

Maana chakula chao kitakuwa chao pekee; hakitaingia nyumbani mwa Bwana.

Watu wa Israeli watakuwa na chakula lakini Bwana hataikubali kama dhabihu.

hakitaingia nyumbani mwa Bwana

Chakula kichafu kimezungumzwa kama kitu kinachoweza kwenda chenyewe. Watu huwa wanaenda nacho.

Hosea 9:5

Taarifa ya jumla

Nabii Hosea anazungumza.

Utafanya nini siku ya sikukuu iliyowekwa rasmi, siku ya sikukuu ya Yahweh?

Hosea anatumia swali hili kusisitiza kuwa watu hawataweza kushuhudia sikukuu zao ikiwa adui watawashinda na kuwashukua mateka.

siku ya sikukuu iliyowekwa rasmi ... siku ya sikukuu ya Yahweh

Zote hizi zina maana moja.

Kama wamekimbia

Hapa wanazungumziwa wana wa Israeli.

Misri itawakusanya, na Nofu itawazika

Misri na Nofu inamaanisha watu wanaoishi pale. "Jeshi la Wamisri litawakamata, mtakufa huko na watu wa mji wa Nofu watawazika"

Maana hazina zao za pesa- michongoma mikali itakuwa nao

Michongoma imeota sehemu ambayo Israeli walihifadhi fedha zao michongoma hii imefananishwa na adui ambaye atakuja kuchukua mali wanazomiliki Waisraeli.

michongoma itakuwa nao, na miiba itajaza hema zao.

"michongoma" na "miiba" inamaana moja. Michongoma na miiba ikiota inamanisha ardhi hiyo ni kama jangwa.

Hema zao

Hapa "hema" inawakilisha nyumba za Waisraeli.

Hosea 9:7

Taarifa ya julma:

Nabii Hosea anazungumza.

Siku za adhabu zinakuja; siku za kulipiza kisasi zinakuja

Hosea amesema kitu kile kile ili kusisitiza kuwa Bwana anakuja kuwahukumu watu wa Israeli kwa matendo yao maovu.

Nabii ni mpumbavu, na mtu aliyevuviwa ni mwendawazimu

Sentensi hii yaweza kuwa na maana 1) watu waliwaona manaabii kama wapumbavu au 2) manabii walichanganyikiwa kwa sababu ya dhambi zilizofanywa na watu.

Nabii ni mpumbavu, na mtu aliyevuviwa ni mwendawazimu

"nabii" na "mtu aliyevuviwa" zote zinamaanisha ni mtu anayesema kuwa amepokea ujumbe kutoka kwa Mungu.

kwa sababu ya uovu wako mkubwa na uadui mkubwa

"uovu mkubwa" na "uadui mkubwa" vina maana moja. Uovu wa watu unapelekea uadui dhidi ya Bwana na manabii wake.

Hosea 9:8

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

Nabii ndiye mlinzi wa Mungu wangu juu ya Efraimu

"Mlinzi" hulinda nje ya mji wake kuangalia kama kuna hatari inakuja.

Nabii ndiye mlinzi wa Mungu wangu juu ya Efraimu

Nakala nyingine zimetafsiri sentensi hii kama "Nabii wa Mungu wangu ni mlinzi juu ya Efraimu.

Nabii ni

Hii inamaanisha manabii kwa ujumla ambao Mungu aliwachagua.

Efraimu

"Efraimu" inawakilisha watu wote wa Israeli.

mtego wa ndege ni juu ya njia zake zote

"mtego wa ndege" ni mtego unaotumika kukamata ndege. Hii inamaanisha kuwa watu wa Israeli walifanya kila wanaloliweza kumzuia nabii wa Mungu.

Wamejiharibu wenyewe kama siku za Gibea

"Wana wa Israeli wametenda dhambi na kujiharibu kama walivyofanya huko Gibea zamani"

Hosea 9:10

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Nilipoikuta Israeli

Hii inaonesha mara ya kwanza Bwana alipoanza mahusiano na wana wa Israeli kwa kuwafanya watu wa pekee.

ilikuwa kama kutafuta zabibu jangwani. Kama matunda ya kwanza ya msimu kwenye mtini

Hii ina maana moja kusisitiza namna ambavyo Bwana alikuwa na furaha alipoanza mahusiano na watu wa Israeli.

Baal Peori

Hili ni jina la mlima katika nchi ya Moabu ambapo miungu ya uongo iliabudiwa.

Hosea 9:11

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza

utukufu wao utatoka kama ndege

Watu wa Efraimu watapoteza kila kitu kilichokuwa kinafanya mataifa mengine yawaheshimu. Utukufu wao utapotea haraka kama ndege apaavyo.

nikiwaacha

Mungu akiacha kuusaidia ufalme wa kaskazini itakuwa kama vile ameondoka kabisa kwao.

Hosea 9:13

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

Nimeiona Efraimu, kama vile Tiro, alipandwa katika mlima

"kupandwa" ni kuwa sehemu salama. "Taifa la Israeli lilikuwa zuri kama mji wa Tiro, kama mti uliopandwa na mtu kwenye mlima"

akini Efraimu atatoa watoto wake

"watoto" ni watu toka kwenye taifa hilo.

Wape, Bwana-utawapa nini? Wape

Hosea ametumia swali kusisitiza kuwa anataka Bwana awape wana wa Israeli kile wanachostahili.

tumbo lenye kuharibu mimba

"kuharibu" inamaanisha ujauzito unakoma mapema na mtoto anakufa.

Hosea 9:15

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

nitawafukuza nje ya nyumba yangu

Bwana anasema kuwa atawafukuza Israeli kutoka kwenye nchi yake, nchi ya Kanaani.

Maofisa wao.

Watu wanaomtumikia mfalme.

Hosea 9:16

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza kwenye mstari wa 16. Hosea anaanza kuzungumza mstari wa 17.

Efraimu ni mgonjwa, na mizizi yao imekauka; hawazai matunda

Bwana anawazungumzia wana wa Israeli kama mti wenye ugonjwa usioweza kuzaa matunda na upo tayari kukatwa.

Hosea 10

Hosea 10:1

Taarifa ya jumla:

Hosea anazungumza juu ya Israeli.

Israeli ni mzabibu mzuri ambao huzaa matunda yake

Israeli inazungumzwa kama mzabibu unaozaa matunda.

Mzabibu mzuri

Mzabibu huu unatoa matunda kuliko kawaida.

kwa kadiri matunda yake yanavyoongezeka .... nchi uake inazalisha sana

Hii inamaanisha kuwa watu walinawiri na kuwe wenye nguvu na matajiri.

Moyo wao ni udanganyifu

"Wao ni wadanganyifu"

sasa wanapaswa kubeba hatia yao

"Sasa ni wakati ambao Bwana atawaadhibu"

Hosea 10:3

Taarifa ya jumla:

Hosea anazungumza juu ya Israeli.

Na mfalme-angeweza kutufanyia nini?

Watu watasema kuwa mfalme wao asingeweza kuwasaidia. "Hata tungekuwa na mfalme sasa asingeweza kutusaidia"

Wanasema maneno tupu

"maneno tupu" inamaanisha uongo. "Wanaongea uongo"

Kwa hivyo haki inakuja kama magugu yenye sumu katika mito ya shamba.

"Hivyo maamuzi yao sio ya haki, badala yake yana sumu"

kama magugu yenye sumu katika mito ya shamba

Uongo wao na kutotenda haki kunasambaa kwenye taifa na kuwadhuru watu kama mmea wenye sumu.

Hosea 10:5

Taarifa ya jumla:

Hosea anazungumza juu ya Israeli.

Beth Aveni

Huu ulikuwa mji uliokuwa kaskazini mpakati mwa ufalme wa Israeli na kabila la Benyamini lililopo kusini mwa ufalme.

watachukuliwa kwenda Ashuru

"Waashuru watawachukua"

Efraimu atakuwa na aibu, na Israeli atakuwa na aibu kwa sanamu yake

"Na watu wa Israeli wataaibika sana kwa sababu waliabudu miungu"

Sanamu yake

Nakala nyingi zimetafsiri neno hili la Kiebrania kama "mipango" au "mikakati"

Hosea 10:7

Mfalme wa Samaria ataangamizwa

"Waashuru watamwangamiza mfalme wa Samaria"

kama chipu cha kuni juu ya uso wa maji

Hii ina maana kuwa mfalme wa Samaria atakuwa hawezi kitu kama kipande kidpgo cha kuni kinachoelea juu ya maji"

Sehemu za juu za uovu zitaharibiwa

"Waashuru wataharibu sehemu za juu za Israeli ambazo watu walifanya uovu"

Watu wataiambia milima, "Tufunike sisi!" na kwa vilima, "Tuangukieni!"

"'watu watasema 'tunatamani milima itufunike!' na 'tunatamani vilima vituangukie!'"

Hosea 10:9

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

siku za Gibea

Hapa inaelezea matendo ya kushangaza ya kabila la Benyamini katika kitabu cha Waamuzi.

huko umebaki

Hii inamaanisha kuwa watu wa wakati huo waliendelea kufanya sawasawa na mababu zao walivyofanya huko Gibea.

Je, vita vitawapata wana wa uovu huko Gibea?

Bwana alitumia swali kusisitiza kuwa waliokuwa Gibea wakafanya uovu lazima vita vitawapata.

wana wa uovu

"wale wafanyao uovu"

Hosea 10:10

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Uovu mara mbili

Hii inamaanisha uovu mwingi wa Israeli.

Efraimu ni ndama mwenye mafunzo ambayo anapenda kupura nafaka

Ndama anapenda kupura nafaka kwa sababu wanaweza kutembea kwa uhuru bila nira.

nitaweka nira juu ya shingo yake nzuri. Nitaweka nira kwa Efraimu

"Nira" inamaanisha mateso na utumwa. Bwana amekuwa mwema kwa wana wa Israeli lakini kwa sababu watu hawakuwa waaminifu atawaadhibu na kuwafanya watumwa.

Yuda ataimea; Yakobo atauvuta pigo kwa nafsi yake.

Bwana atasababisha wakati mgumu kwa falme zote za Yuda na Yakobo.

Pigo

Ni kifaa kinachotumika kuifanya ardhi iwe nzuri na kufunika mbegu baada ya kulima.

Hosea 10:12

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

ifanyieni haki, vuneni matunda ya uaminifu wa agano

Haki na agano vimezungumzwa kama mazao ambayo yanapandwa na kuvunwa.

Chimbueni ardhi yenu isiyopandwa

Ardi isiyolimwa haipo tayari kwa kupandwa. Bwana anataka watu watubu ili waanze kufanya mambo yanayofaa.

Mmelima uovu; mmevuna udhalimu.

Uovu na udhalimu vimezungumzwa kama mazao ambayo yanapandwa na kuvunwa.

Mmekula matunda ya udanganyifu

Matokeo ya udanganyifu yanazungumzwa kama chakula ambacho kinaweza kulika.

Hosea 10:14

Itakuwa kama Shalmani aliharibu Beth Arbeli siku ya vita

Vita inayokuja inafananishwa na vita ya zamani.

Shalmani

Hili ni jina la mfalme aliyeangamiza mji wa Beth Arberi miaka ya 740 kabla ya Kristo.

Beth Arberi

Hili ni jina la mji wa kabila la Naftali.

Kwa hiyo itakuwa kwako, Betheli, kwa sababu ya uovu wako mkubwa

Hapa "Betheli" inawakilisha watu wanaoishi pale. Nabii aliwaambia watu wa Betheli kama vile walikuwa wakimsikiliza.

Hosea 11

Hosea 11:1

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza namna anavyowajali Waisraeli kama mzazi anavyomjali mtoto.

Israeli alikuwa kijana

Bwana anazungumza juu ya wana wa Israeli kama watoto.

nikamwita mtoto wangu kutoka Misri

"mtoto" inamaanisha watu wa Mungu Baba. "Niliwaongoza watoto wangu kutoka Misri"

Kwa kadiri waliyoitwa, ndivyo walivyoondoka kwangu

"kwa kadiri nilivyowaita kuwa watu wangu ndivyo walivyokataa"

Hosea 11:3

Taarifa ya jumla:

Bwana anasema ni kwa namna gani anawajali Waisraeli.

Lakini mimi ndio niliyemfundisha Efraimu kutembea

Bwana anawaelezea Waisraeli kama watoto wadogo aliowafundisha kutembea.

niliyewainua kwa mikono zao

"kuwajali wao"

Niliwaongoza kwa kamba za ubinadamu, na mafungo ya upendo

Bwana aliwapenda watu wake kwa namna ambayo hakuna binadamu ambaye angeelewa na kujali.

Mimi nilikuwa kama mtu aliyepunguza jozi juu ya taya zao

Bwana anazungumza juu ya taifa la Israeli kama mnyama afanyaye kazi ngumu na kuifanya kazi yake kuwa rahisi.

nikainama na kuwalisha

Hii inamaanisha kuwa Bwana aliwapa mahitaji yao.

Hosea 11:5

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza juu ya Israeli.

Je, hawatarudi nchi ya Misri?

Swali hili linamaanisha kuwa taifa la Israeli watakuwa watumwa tena kama walivyokuwa Misri.

Je, Ashuru haitatawala juu yao kwa sababu wanakataa kurudi kwangu?

Taifa la Israeli litachukuliwa mateka na Ashuru kama matokeo ya kutokuwa waaminifu kwa Bwana.

Upanga utaanguka juu ya miji yao

Hapa "upanga" inawakilisha maadui wa Israeli watakao haribu miji ya Israeli.

kuharibu makomeo ya milango yao

Kuharibu makomeo inamaana ya kuondoa ulinzi wa watu.

ngawa wanaita kwa Aliye Juu

Hapa Mungu anajizungumzia mwenyewe. "Ingawa wataniita mimi, niliye juu"

hakuna mtu atawasaidia

Bwana hataruhusu mtu yeyote awasaidie Israeli kwa sababu wamemuacha.

Hosea 11:8

Taarifa ya jumla:

Bwana anaongea juu ya Israeli.

Ninawezaje kukuacha, Efraimu? Ninawezaje kukupeleka, Israeli?

Bwana anawapenda watu wake sana kiasi kwamba hatawaharibu kabisa.

Ninawezaje kukufanya kama Adma? Ninawezaje kukufanya kama Seboimu?

Bwana anawapenda watu wake sana kiasi kwamba hatawaharibu kabisa. "Sitaki kuwaangamiza kama nilivyoiangamiza Adma na Seboimu miji niliyoiangamiza pamoja na Sodoma"

Kwa maana mimi ni Mungu na wala si mtu

Mungu si kama mwanadamu anayeamua haraka kulipa kisasi.

Moyo wangu umebadilika ndani yangu

Hapa "moyo" unawakilisha mapenzi ya Mungu na maamuzi yake.

sitakuja katika ghadhabu

"Sitakuja kwako na kuwa na hasira na wewe"

Hosea 11:10

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza kuhusu lini atawakomboa watu wake.

Watanifuata, Bwana

Kumuabudu na kumuheshimu Bwana kunazungumzwa kama kitendo cha kumfuata nyuma yake.

Nitanguruma kama simba

Bwana atawafanya watu wake warudi kwenye nchi yake na kitendo hiki kimezungunzwa kama kitendo cha kuitwa.

Watakuja wakitetemeka kama ndege ... kama njiwa

Watarudi nyumbani mapema kama vile ndege anavyorudi kwenye kiota chake.

tamko la Bwana

"ambalo Bwana anasema"

Hosea 11:12

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza kuhusu Israeli na Yuda.

Efraimu ananizunguka kwa maneno ya uongo, na nyumba ya Israeli kwa udanganyifu

Vitendo vya uongo na udanganyifu vinazungumzwa ka vitu ambavyo watu wa ufalme wa kaskazini wamemzunguka navyo Bwana.

Lakini Yuda bado anaendelea nami

Watu wa ufalme wa kusini bado ni waaminifu kwa Mungu.

Hosea 12

Hosea 12:1

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

Efraimu hujilisha upepo

Wana wa Israeli wanafanya mambo ambayo hayatawasaidia ni sawasawa na kujilisha upepo.

kufuata upepo wa mashariki.

Upepo wa mashariki ulikuwa na joto sana na wenye kuharibu. Hii inamaanisha kuwa majeshi kutoka mashariki ambayo Bwana atayatuma kuwaharibu wana wa Israeli.

huchukua mafuta ya Misri

Wana wa Israeli walipeleka mafuta kama zawadi kwa mfalme wa Israeli na kumsihi awasaidie.

Bwana pia ana mashtaka dhidi ya Yuda

Bwana anasema kwamba watu wa Yuda wamemtenda dhambi na kuvunja agano lake.

dhidi ya Yuda ... ataadhibu Yakobo ... kwa yale aliyoyatenda ... atamlipa kwa matendo yake

"Yuda" na "Yakobo" wote wanawakilisha watu wa Yuda.

mashitaka

Haya ni malalamiko ya mtu mmoja dhidi ya mtu mwingine mahakamani.

Hosea 12:3

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza juu ya Yakobo baba wa Israeli.

Katika tumbo Yakobo akamshika ndugu yake kisigino

Yakobo alitaka kuchukua nafasi ya ndugu yake ya uzaliwa wa kwanza.

Alishindana na malaika akashinda

Yakobo alishindana na malaika ili malaika ambariki.

Hosea 12:5

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

ndilo jina lake

"tunaomba kwa jina lake" au "tunaabudu kwa jina lake"

Shika uaminifu na haki la agano

Hii inamaanisha kutii amri za Mungu na kufanya mabo kwa usahihi.

Hosea 12:7

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza juu ya Israeli.

mizani ya uongo

Wafanyabiashara wanatumia mizani kupima uzito wa fedha au bidhaa wanayonunua ua kuuza.

wanapenda kudanganya

Wafanyabiashara wanawadanganya wateja wao kwa kuchukua pesa nyingi kuliko inavyotakiwa.

Kwa hakika mimi ni tajiri sana; Nimepata utajiri kwa nafsi yangu

Sentensi hizi zina maana sawa kuwa watu wa Efraimu wanajiona kuwa wamefanikiwa sana.

Nimepata utajiri

Kuwa tajiri kwa kufanya biashara kunazungumzwa kama kupata utajiri.

hawataona uovu wowote ndani yangu, chochote ambacho kitakuwa dhambi

Watu wa Efraimu wanajiona kuwa ni watu wasio na lawama.

Hosea 12:9

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza na watu wa Israeli.

Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, tangu ulipotoka nchi ya Misri

Hii inaweza kuwa na maana ya 1) "Mimi ni Bwana Mungu wako niliyewatoa baba zako toka nchi ya Misri" au 2) "Nimekuwa Mingu wako tangu ulipokuwa katika nchi ya Misri" au 3) "Nimekuwa Mungu wako ulipokuwa katika nchi ya Misri"

Nitakufanya uishi tena katika hema

Hii inaweza kuwa na maana ya 1) Bwana anawatoa kwa nguvu wana wa Israeli toka kwenye nyumba zao na kuwafanya waishi kwenye hema au 2) Ni ahadi kuwa baada ya uhamishi watu wataishi katika hema tena na Bwana atawatunza kama alivyofanya Misri.

Kwa mkono wa manabii

Hapa "mkono" unawakilisha mtu anayechukua hatua. "kupitia manabii"

Hosea 12:11

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

madhabahu zao zitakuwa kama miundo ya jiwe katika miamba ya mashamba

Madhabahu ambazo watu wataabudia zitaangushwa chini na kuwa vipande vya mawe.

Yakobo akakimbia mpaka nchi ya Aramu; Israeli alifanya kazi ili kupata mke

"Yakobo" na "Israeli" ni majina ya mtu mmoja.

Hosea 12:13

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

kwa nabii

Ambaye ni Musa.

amemkasirisha

Hasira ambayo mtu ameisababisha kwa Bwana ni kubwa mno.

Basi Bwana wake ataachia damu yake

Hapa "damu" ni hatia iliyopo kwa mtu aliyemuua mwenzake. Mungu haitaisamehe dhambi hiyo.

naye atamrudishia aibu yake

"atamfanya ateseke kutokana na matendo yake maovu"

Hosea 13

Hosea 13:1

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Efraimu alipozungumza

Hosea ametumia neno Efraimu kumaanisha ufalme mzima wa kaskazini, japokuwa lilikuwa jina la moja ya makabila kumi na mbili.

kulikuwa na tetemeko

"kulikuwa na tetemeko kati ya watu"

Alijikuza katika Israeli

"kujikuza" ni kujifanya wa muhimu.

lakini akawa na hatia kwa sababu ya ibada ya Baali, naye akafa

Watu wa Efraimu walipoanza kuabudu Baali wakawa dhaifu na adui zao wakawashinda.

Sasa wanafanya dhambi zaidi na zaidi.

Hawa ni watu wa kabila la Efraimu na taifa zima la Israeli.

Watu hawa watoao dhabihu na kumbusu ndama

Sehemu ya kuabudu sanamu ni kwa kuibusu sanamu ambayo ni sanamu ya ndama.

Hosea 13:3

Kwa hiyo watakuwa kama mawingu ya asubuhi ... kama umande ... kama makapi ... kama moshi utokao kwenye bomba.

Maelezo haya yanaonesha kuwa Israeli itapotea kama itaendelea kuabudu sanamu.

yanayotokana na upepo

"ambayo upepo unavuma"

Hosea 13:4

Taarifa ya jumla:

Bwana anawazungumzia watu wake kama kundi la kondoo linalotangatanga jangwani.

Nilikujua jangwani

Bwana anasema kuwa Waebrania ni watu wake wa pekee na anawajali.

Wakati ulipokuwa na malisho, ulishiba

Sura ya kondoo inaendelea kuelezewa.

moyo wako ukainuliwa

"moyo" unawakilisha utu wa ndani wa mtu.

ukainuliwa

Kuwa na kiburi inazungumzwa kama kujiinua.

Hosea 13:7

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

kama simba ... kama chui ... kama dubu ... kama vile mnyama wa mwitu

Hawa ni wanyama wa porini ambao huvamia na kuwaua wanyama wengine.

kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake

"kama dubu ambaye atashambulia mnyama atakayechukua watoto wake"

kama simba

"kama simba atakavyowala"

Hosea 13:9

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

nani atakayekusaidia?

"hakutakuwa na mtu wa kukusaidia wewe"

Mfalme wako yuko wapi, ili akuokoe katika miji yako yote? Wako wapi wakuu, ambao kwao umeniambia hivi, 'Nipe mfalme na wakuu'?

Bwana anauliza swali hili ili kuwaambia Waisraeli kwamba watakapoasi juu yake hakuna mfalme wala kiongozi atakayekuja kuwasaidia.

Hosea 13:12

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Uovu wa Efraimu umehifadhiwa; hatia yake imehifadhiwa.

Sentensi hizi zina maana moja.

imehifadhiwa

Uovu wa ufalme wa kaskazini unazungumzwa kama kitu kinachoweza kuhifadhiwa.

Atakuwa na uchungu wa kujifungua,

Hapa Bwana anazungumzia mateso ya wana wa Israeli kama uchungu wa kuzaa.

lakini ni mwana mjinga, kwa maana wakati wa kuzaliwa, hatatoka tumboni

Bwana anawaelezea wana wa Israeli kama watoto wanaozaliwa. Watu hawataki kutubu na kumtii Bwana.

Hosea 13:14

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Je, nitawaokoa na mkono wa kaburi? Je, nitawaokoa na kifo?

Bwana anatumia swali hili kuwaambia Waisraeli kuwa hatawaokoa na kifo. Lazima atawaadhibu.

Ewe Mauti yako wapi mapigo yako? Ewe kaburi kuko wapi kuharibu kwako?

Bwana anatumia swali kuwaambia kuwa atawaangamiza mda sio mrefu.

Huruma itafichwa

Huruma imezungumzwa kama kitu.

Huruma itafichwa na macho yangu.

"Sina huruma kwao"

Hosea 13:15

Taarifa ya jumla"

Nabii Hosea anazungumza.

Ndugu zake

Neno hili linasimama kuelezea mataifa yanayozunguka ufalme wa kaskazini, hasa Yuda ufalme wa kusini.

upepo wa mashariki utakuja; upepo wa Bwana

Upepo wa mashariki ulikuwa na joto sana na wenye kuharibu. Hii inamaanisha kuwa majeshi kutoka mashariki ambayo Bwana atayatuma kuwaharibu wana wa Israeli.

Kijito cha maji cha Efraimu kitauka, na kisima chake hakitakuwa na maji

Hosea anaendelea kuelezea ni kwa namna gani Mungu atawaadhibu wana wa Israeli.

ghala lake

Hivi ni vitu anavyomiliki mtu.

Hosea 13:16

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

Samaria itakuwa na hatia, kwa sababu ameasi dhidi ya Mungu wake

"Samaria" inamaanisha watu wa mji wa Samaria walio na hatia ya uasi dhidi ya Mungu.

Wataanguka

Watu watakufa.

kwa upanga

Vitani.

watoto wao wadogo watavunjwa, na wanawake wao wajawazito watararuriwa wazi

"adui watawavunja watoto wao wadogo vipande vipande na kuwararua wazi wazi wanawake waajawazito"

Hosea 14

Hosea 14:1

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

kwa kuwa umeanguka kwa sababu ya uovu wako.

Kutenda dhambi kunazungumzwa kama kitendo cha kuanguka.

Chukueni maneno pamoja nanyi

"kirini dhambi zenu"

matunda ya midomo yetu.

Kituatakachosema mtu ndiyo matunda na midomo.

Hosea 14:3

Taarifa ya jumla:

Hosea anazungumza.

kazi ya mikono yetu

"mikono" hii inamaanisha watu wanatengeneza vitu. "kwa sanamu tunazotengeneza"

mtu asiye na baba

Hii inaonesha huruma kubwa ya Mungu kwa watu wake.

hupata huruma

Hapa kitendo cha Mungu kuonesha huruma kinazungumzwa kama ni kitu ambacho mtu amekipata.

Hosea 14:4

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Nitawaponya kugeuka kwao

Kuwafanya watu wasigeuke toka kwa Mungu kunazungumwa kama kitendo cha kuponya.

kugeuka kwao

Watu kushindwa kumtii Mungu kunazungumzwa kama kitendo cha kugeuka toka kwake.

Nitakuwa kama umande kwa Israeli; atachanua kama maua

Bwana anazungumza akijifananisha na umande unaohitajika ili kuupa rutuba mmea na Israeli inafananishwa na ua litakalochanua.

kuchukua mizizi kama mwerezi nchini Lebanoni

Taswira ya Israeli kama mmea inaendelea lakini hapa inafananishwa na mierezi wa Lebanoni.

Matawi yake yataenea ... kama mierezi ya Lebanoni

Sehwmu hii inaendelea kuzungumzia kitu hicho hicho.

Hosea 14:7

Taarifa ya jumla:

Bwana anazungumza.

Watu wanaoishi katika kivuli chake watarejea

Watu wa Israeli tena wataishi kwa kulindwa na Mungu.

watafufuliwa kama nafaka na maua kama mizabibu

Mafanikio ya Israeli yanazungumzwa kwa lugha ya kilimo.

Utukufu wake utakuwa kama divai ya Lebanoni

Kama divai ya Lebanoni ilivyokuwa maarufu pia Israeli itakuwa maarufu.

nifanye nini tena na sanamu?

Sentensi hii inaonesha kuwa Mungu atawakataza Israeli kuabudu muingu.

kama mberoshi majani yake ni ya kijani daima

Mberoshi ni mti ambao majani yake ni ya kijani mwaka mzima. Hii inawakilisha baraka za Bwana juu ya Israeli.

kwangu huja matunda yako

"matunda" inawakilisha kitu kizuri kinachotoka kwa Bwana.

Hosea 14:9

Taarifa ya jumla:

Nabii Hosea anazungumza.

Nani mwenye busara ili aelewe mambo haya? Nani anaelewa mambo haya ili awatambue?

Nabii anatumia maswali haya kusema kuwa watu wenye busara wataelewa na kusikiliza kile atakachokisema.

Kwa kuwa njia za Bwana ni sawa, na wenye haki watatembea ndani yao

Amri za Bwana zinazungumzwa kama njia ya kupitia.

wataanguka

Kutomtii Bwana kunazungumzwa kama kutendo cha kuanguka ukiwa unatembea.