Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Micah 1

Micah 1:1

neno la Yahwe likanijia

"neno la Yahwe Mungu ameongea"

Yahwe

Hili ni jina la Mungu ambalo alilojifunua kwa watu wake katika Agano la Kale.

Mmorashti

Hii inamaana anatoka Morashti ambao ni mji katika Yuda.

katika siku za Yotahamu, Ahazi, na Kezekia, wafalme wa Yuda

"wakati Yotahamu, Ahazi, na Hezekia walipokuwa wafalme wa Yuda"

lile neno aliloliona kuhusiana na Yerusalemu

"Ono aliloliona kuhusiana na watu wa Samaria na Yerusalemu"

Micah 1:2

Maelezo ya jumla:

Inazungumzia kuhusu hukumu juu ya Samaria.

Sikilizeni, ninyi watu wote. Sikilizeni Dunia, na vyote vilivyomo ndani yako

Sentensi zote hizi zinamaanisha kitu kimoja na kusisitiza kwamba kila mtu aliye duniani anapaswa kusikiliza. Mika anaongea kana kwamba watu wote wa dunia walikuwa pale wakimsikiliza.

atashuka chini na kupakanyaga mahali pa juu ya ya nchi

atapaharibu mahali pa juu kabisa juu ya nchi kana kwamba alikuwa akiwakanyaga kwa miguu yake"

Milima itayeyuka chini yake; mabonde yatapasuka vipande kama mshumaa mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika chini ya mteremko mkali.

Hii inamaana wakati Mungu atakapokuja kuziharibu madhabahu za wapagani hakuna jambo litakalomzuia.

Micah 1:5

Haya yote ni kwa sababu ya uasi wa Yakobo, na kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli

Hivi vifungu vya maneno kimsingi vinamaanisha kitu kimoja na kukazia kwamba Yahwe anatenda kwa sababu ya dhambi za falme zote mbili yaani kaskazini na kusini .

Haya yote ni

"Bwana Mungu atakuja na kuhukumu"

Je! Sababu ilikuwa nini kwa uasi wa Yakobo? Je! Haikuwa Samaria? Je! Haikuwa Samaria?

Hapa "Yakobo" anarejelea kwa ufalme wa kusini mwa Israeli. Mika anatumia maswali kuwasisitiza hao watu wa Samaria ni sababu ya Mungu kuuhukumu ufalme wa Israeli.

Je! Sababu ilikuwa nini kwa mahali pa juu pa Yuda? Je! Haikuwa Yerusalemu?

Mika anatumia maswali kuwasisitiza hao watu wa Yerusalemu ndio sababu Mungu ya kuja kuuhukumu ufalme wa Yuda.

Micah 1:6

Nitafanya

Hapa "Mimi" inarejelea kwa Yahwe.

itakanyagwa kuwa vipande vipande...itachomwa

"Nitakanyaga kuwa vipande vipande...nichoma"

Nitayavuta mawe ya jengo lake

Hapa "yeye" inarejea kwa mji wa Samaria.

Kwa kuwa zawadi zake za ukahaba amezikusanya, na malipo ya ukahaba yatarudi

Mara nyingi kuabudu sanamu pamoja na kulala na kahaba kwenye hekalu la wapagani.

Micah 1:8

Maelezo ya jumla

Mika 1:8-16 inazungumzia hukumu juu ya Yuda.

Nitaomboleza

Hapa "mimi" inamrejea Mika.

Nitaenda peku na uchi

Hii ni ishara ya maombolezo makali mno na kujitesa.

uchi

Mara nyingi, Mika hakuwa uchi mwili mzima. Alikuwa amevaa msuli.

Nitalia kama mbweha na kuomboleza kama bundi

Hawa ni wanyama wajulikanao kwa sauti na kilio chao kisichopendeza

Kwa kuwa jeraha lake haliponi

Hapa "yeye" inarejea kwa mji wa Samaria. Hii inamaana hakuna kitu kinachoweza kuzuia jeshi la adui ambalo ninalokuja kuwaharibu watu wa Israeli.

kwa kuwa imefika kwa Yuda

Hapa "hiki" inarejea kwa "jeraha," ambayo ni, kwa jeshi ambalo Mungu atakalolitumia kuiharibu Samaria.

Beth Leafra

Unaweza kutaka rejea kusema, "Jina la huu mji linamaana ya 'nyumba ya vumbi."'

Najibiringisha mimi mwenyewe kwenye mavumbi

Watu chini ya hukumu ya Mungu wanaweka wazi huzuni yao katika njia imara.

Micah 1:11

Maelezo ya Jumla:

Kwa kuwa maana za vijiji na miji, unaweza kutaka kuingiza hiyo habari katika rejea.

Shafiri

Jina la huu mji linatamkika kama maana moja "uzuri." Lipo kinyume na "Utupu na aibu."

katika uchi na aibu

Adui wa majeshi mara nyingi waliwafanya wafungwa wao kutembea uchi kabisa. Na kulikuwa na aibu katika kuanza kuwashinda watu.

Zaanani

Jina la huu mji linamaanisha "kutoka nje." Wanaogopa kutoka nje na kusaidia.

Beth Ezeli

Jina la huu linamaanisha "nyumba ya kuchukuliwa."

kwa kuwa ulinzi wao umechukuliwa

"kwa kuwa nimechukua kila kitu ambacho kingeweza kuwalinda"

Marothi

Jina la huu mji linamaanisha "uchungu."

kwa sababu janga umetoka kwa Yahwe

"Janga" ni neno la msingi katika Mika ambalo litakalojitokeza tena.

Micah 1:13

Lakishi

Kuna kucheza na neno hapa kama Lakishi inatamkika kama "kwenye magari ya farasi" katika Kiebrania. Watu wanaofungia magari ya farasi kukimbia, sio kupigana. Lakishi ilikuwa ya pili kwa Yerusalemu katika umuhimu katika Yuda.

binti Sayuni

"Binti" wa mji inamaanisha watu wa mji. Tafsiri za kubadilishana: "watu wa Sayuni wale waishio katiaka Sayuni."

kwa kuwa makosa ya Israeli yalionekana kwako

"kwa kuwa hamjatii kama watu wa Israeli walivyofanya"

Moreshethi Gathi

Unaweza kutaka kuongeza rejea kusema "Jina 'Moreshethi' maana yake 'kuondoa' na inalingana katika kutamkwa kwenye neno kwa ajili ya 'mchumba."' Iko kama Moreshethi ni bibi harusi ambaye Ashuru amchukuaye "zawadi za kuagana" ni vitu vitolewavyo na bibi harusi kwenda kwa bwana harusi. Moreshethi Gathi kilikuwa kijiji cha nyumbani kwa Mika.

Akzibu

Unaweza kuongeza rejea kusema "Jina la huu mji linatamkika karibu sawa kama Kiebrania kueleza kwa ajili ya 'kitu cha udanganyifu."'

Micah 1:15

Nitaleta tena

Hapa "mimi" inarejea kwa Yahwe.

Mareshi

Unaweza kutaka kuweka rejea kusema, "Kuna kucheza juu ya maneno hapa pamoja na jina la hiki kijiji na neno la Kiebrania kwa ajili ya 'kushinda."' Huu msemo ulitumika katika kushinda Israeli Kanaani; sasa Israeli itashinda. Hiki kijiji ni kama kilikuwa karibu na kijiji cha nyumbani kwa Mika mwa Moreshethi Gathi.

Adulamu

Hii inarejea kwa mji wa kifalme wa Wafilisti.

Nyoa kichwa chako na kata kipara

Wale waliokuwa wakinyoa kichwa ilikuwa alama ya kuomboleza kwa ajili ya Waisraeli.

Micah 2

Micah 2:1

Maelzo ya Jumla:

Sasa Mika 2:1-11, lengo liondoalomiji kuhukumiwa kwa wakuu katika Israeli ambao wanaochukulia manufaa kwa maskini na sio kufuata maagizo ya Mungu.

Micah 2:3

huu ukoo

Huu "ukoo" inaihusu jamii nzima ya Israeli, ambayo watu matajiri wanawakandamiza maskini. Dhambi za wakuu zinarudi juu ya taifa zima.

ambazo hamtazitoa shingo zenu

Yahwe inamaanisha adhabu yake ni kama nira kuzunguka shingo zao. Ni kitu ambacho kitashusha chini kiburi cha tajiri.

kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni

"watalia kwa sauti"

Je! Ataondoaje kutoka kwangu?

adui hutumia swali katika wimbo wao kuwaelezea wakuu mshangao wa Israeli waliojisikia kwa sababu Mungu aliikuchukua nchi yao na kuitoa kwa mtu mwingine kama walivyokuwa wameochukua kutoka maskini. "Ameichukua kutoka kwangu!"

Kwa hiyo, ninyi watu matajiri hamtakuwa na uzao kugawanya eneo kwa kupiga kura katika mkutao wa Yahwe.

Wale ambao walioichukua nchi kutoka maskini hawatapokea urithi wamewakataa wengine.

Micah 2:6

Maelezo ya jumla:

Mika 2:6-11 inawatambulisha manabii ambao hawajahubiri kwa ufasaha, wale waliomkataa Mika, na njia nyingi tajiri amezitumia vibaya nguvu zao.

wanasema

"watu wa Israeli husema"

Hawatahubiri

"Manabii hawatatabiri"

Je! Roho wa Yahwe amekasirika? Je! haya ni matendo yake kweli?

Watu hutumia maswali kusisitiza kwamba hawajaelewa na kutomwamini Mungu atawaadhibu kweli.

Maneno yangu sio mazuri kwa kila mtu atembeaye kwa unyoofu?

Mika anatumia swali kuwafundisha watu. "Ujumbe wangu ni mzuri kwa wale wanaohusika kwa kufanya yale mazuri."

watu wangu

Hapa "wangu" linamrejea Yahwe.

Mmelivua joho, nguo, kutoka wale wapitao wasioshutumiwa

Maana ziwezekanazo 1) Mika anamaanisha watu matajiri waovu ni kweli wanaiba majoho kutoka maskini, lakini hii ni tofauti. Au 2) Mika anarejea kwa watunzaji wa mapato ya mawia mavazi ya nje ya maskini wajao kuazima pesa na kutoa mavazi kama dhamana warudishapo. Kulingana na sheria kwenye Kutoka, walitakiwa kurudisha kabla ya kuchwa kwa sababu inaweza kuwa jambo pekee la mtu maskini kuwekwa joto usiku

Micah 2:9

Maelezo ya Jumla:

Yahwe anaendelea kuongea na watu matajiri waovu katika Israeli.

mnachukua baraka zangu kutoka kwa watoto wao wadogo milele.

Hii inarejea , kwa ujumla, kwa baraka Mungu alizowawapati watu wake. Inaweza kurejea kwa 1) kuwa wamiliki wa nchi katika Israeli, 2) ahadi ya baadaye au 3) kwa mababa wa wana, wakulima waliofanya kazi kwa bidii kuanzisha taifa.

imeangamizwa kwa maangamizo kabisa

"Nitaiangamiza kabisa"

angefikiriwa

"ungemfikiria"

Micah 2:12

Maelezo ya Jumla:

Yahwe anaendelea kuongea. Mwishoni mwa hii sura, Yahwe anajionyesha yeye mwenyewe kuwa mchungaji ambaye awachungaye watu wake. Anaweza hasa kuwatambulisha wale walio katika Yerusalemu ambaye amerudi kutoka Ashuri.

Mtu avunjaye hufungua njia...Yahwe atakuwepo kwenye vichwa vyao.

Hii ni picha ya Mfalme akiwaongoza watu wake mbali na mji uliozungushiwa ukuta.

Micah 3

Micah 3:1

Maelezo ya Jumla:

Sura ya 3 inawalenga wakuu wapotoshaji katika Israeli.

Nimesema

Hapa "mimi" inamrejea Mika.

Je! Sio sahihi kwenu kuifahamu haki?

Mika anatumia swali kuwakemea wakuu kwa sababu hawakuwa wanawalinda watu au kuwatendea haki.

ninyi manaorarua ngozi yao, miili yao kutoka mifupa yao...kama nyama katika chungu

Mika anatumia hii picha mbaya ya bucha kuwakata wanyama kuwa nyama kusisitiza jinsi Mungu alivyo fadahaishwa na wakuu kwa sababu ya jinsi walivyo wakatili kwa wale waliotakiwa kulindwa.

Micah 3:4

Maelezo ya Jumla:

Mika anaendelea kuongea.

lia kwa Yahwe

"piga kelele kwa Yahwe kwa ajili ya msaada"

Atauficha uso wake kutoka kwenu

Hii inamaanisha Mungu hatasikia vilio vyao. Hawatasikia vilio vya maskini, na hivyo wapokee kama walivyofanya kutoka kwa Mungu.

Micah 3:5

Maelezo ya Jumla:

Mika anaendelea kuongelea hukumu juu ya manabii wa uongo.

itakuwa usiku kwenu...siku itakuwa giza juu yao

Yahwe anasema katika 3:6 hawa manabii wa uongo hawatapokea tena ujumbe wa Mungu kwa watu wa Israeli. Wakati mwingine manabii walipata ujumbe kutoka kwa Mungu kupitia maono, au ndoto usiku.

Waonaji watawekwa kuwa aibu, na waaguzi watachanganyikiwa

"Nitawafanya waonaji kuwa aibu, na nitawachanganya waaguzi"

Wote watafunga midomo yao

"Hawataongea tena"

kwa kuwa hakuna jibu kutoka kwangu

Hii inamaanisha Mungu atakuwa kimya kama sehemu ya adhabu yao.

Micah 3:8

Lakini kwangu

"Mimi" hapa inamrejea Mika, nabii wa kweli amejitenga kutoka manabii wa uongo.

Nimejaa uwezo kwa Roho ya Yahwe, na nimejaa haki na uweza

Roho wa Yahwe alichagua kumpatia Mika nguvu, haki, na uweza katika uhodari, njia ya aina yake. "Roho wa Yahwe amenijaza nguvu, haki, na uweza" au "Roho wa Yahwe amenipa nguvu, haki, na uweza"

kumtangazia Yakobo kosa lake, na kwa Israeli dhambi yake

Hivi virai vyote vinamaana moja na kusisitiza hao watu wote wa falme zote kaskazini na kusini wamefanya dhambi.

Micah 3:9

Mmeijenga Sayuni kwa damu na Yerusalemu kwa uovu

Matajiri walikuwa wakijijengea wenyewe nyumba nzuri mara nyingi kwa gharama na kuwatenda vibaya maskini.

damu

Hapa "damu" inarejea kuua.

Je! Yahwe yu pamoja nasi? Hakuna uovu utakaokuja juu yetu.

Mika anawanakuu watu wafikiriao tofauti Yahwe hatawaadhibu kwa matendo yao maovu. Neno la Kiebrania la "uovu" hapa ni sawa kama "janga" katika 2:3, neno kuu katika kitabu.

Micah 3:12

kwa sababu yenu

Hapa "ninyi" inawarejea makuhani, manabii, na wakuu wa wa mstari uliopita.

Sayuni italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa rundo la kifusi, na mwinuko wa hekalu utakuwa kama mwinuko wa msitu.

Mika anamaanisha kwamba Yerusalemu itaharibiwa kabisa. Mji mkubwa pamoja na watu wengi waishio huko wakuwa wametelekezwa na kukomaa kama shamba au msitu.

Sayuni atalimwa kama shamba

Baada ya uharibifu wake, Yerusalemu atapatikana kwa kulimwa. "Watu wengine watailima Sayuni kama shamba."

na mwinuko wa hekalu utakuwa kama mwinuko wa msitu.

Hakuna hata eneo la hekalu litakaloacha kuharibiwa. Wakuu wamelipotosha, na litaharibiwa pia.

Micah 4

Micah 4:1

mlima wa nyumba ya Yahwe utakuwa imara

"Yahwe atauimarisha mlima ambapo hekalu lake lilipojengwa"

juu ya milima mingine

Hii inamaanisha Mlima Sayuni utakuwa wa muhimu zaidi ya milima yote. Pia inaweza kumaanisha kwamba huu mlima utakuwa mrefu zaidi katika dunia, sio katika eneno pekee.

utakuwa imara juu ya milima mingine

"utaheshimiwa zaidi kuliko mlima mwingine wowote"

watu watatiririka kuuendea

Watu wa mataifa wataenda kwenye mlima wa Yahwe kama mkondo utiririkiao. Hii inamaanisha kwamba watu wengi wataenda. "watu wa mataifa watatiririka kama mto kuuendea" au "watu wa mataifa watauendea"

Micah 4:2

njooni tuupande mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo

Vyote mlima na nyumba ni kumbukumbu kwa hekalu la Yerusalemu.

Atatufundisha njia zake, na tutaenenda katika njia zake

Hapa "njia zake" na "njia zake" zinarejea kwa kile ambacho Mungu ataka watu wakifanye. Pia, "kuenenda" maana yake watatii kile asemacho.

Kwa kuwa kutoka Sayuni sheria itatoka, na neno la Yahwe kutoka Yerusalemu

Hapa maneno "sheria" na "neno" yanazungumzia jambo moja. Mataifa ya dunia watasikiliza sheria ya Mungu katika Yerusalemu.

plau

Plau ni kengee ambayo watu hutumia kulimia kwenye udongo ili wapande mbegu.

Watazipiga panga zao kwenye plau na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea

Virai hivi vyote vinamaanisha kwamba watarudisha silaha zao za vita kwenye vifaa watakavyovitumia kuandalia chakula.

miundu ya kupogolea

Mundu wa kupogolea unatumika kukatia matawi au au visiki kutoka kwenye mmea kuufanya uzae vema.

Micah 4:4

Maelezo ya Jumla:

Mika anaendelea kuelezea "siku za mwisho" wakati watu watakapojifunza na kuitii sheria ya Yahwe.

chini ya mzabibu na chini ya mtini wake

Hii ni picha ya watu waishio katika amani.

kwa kuwa kinywa cha Yahwe wa majeshi kimenena hivi

"kwa kuwa Yahwe wa majeshi amenena"

enenda...katika jina la

Hiki kirai kinamaanisha kuabudu na kutii

Micah 4:6

Maelezo ya Jumla:

Yahwe anaelezea "siku za mwisho" wakati watu watakapojifunza na kutii sheria ya Yahwe.

Siku hiyo

"Katika siku zijazo"

Nitamkusanya achechemeaye

"Nitawaleta pamoja wale ambao ni wadhaifu"

na kumkusanya aliyefukuzwa

"na kuwakusanya wale ambao nimewafanya kuwatoka"

na wale waliotupwa mbali kwenye kwenye taifa imara

"na wale niliowatupa mbali nitalifanya taifa imara"

mnara wa saa kwa ajili ya kundi

Yahwe anatumia hiki kirai kusisitiza kwamba watu wa Yerusalemu walitakiwa kuulinda na kuuangalia kwa ajili ya watu wengine wa Israeli.

kilima cha binti Sayuni

"Binti" wa mji inamaanisha watu wa mji. "kilima ambacho watu wa Sayuni huishi"

kilima

Baadhi ya matoleo ya kisasa yanaelewa hili neno la Kiebrania kumaanisha "boma" au "ngome" hapa.

Micah 4:9

Sasa, kwa nini unapiga kelele kwa sauti kuu?

Mika anawatania watu, kujaribu kuwafanya kufikiria kuhusu kwa nini Mungu anashughulika nao katika njia hii. "Sasa, unapiga kelele kwa sauti kuu."

Je! Hakuna mfalme miongoni mwenu? Je! Mshauri wako amekufa? Je! Hii ndiyo sababu uchungu umekushika kama yule mwanamke katika kuzaa?

Mika anaendelea kuwahutubia watu katika sauti ya mzaha. Jibu la haya maswali ni hapana. Mfalme na washauri bado wapo huko, lakini wako kama hawana maana na wasio na matumaini. "Hivyo kwa nini unaomboleza sasa? Je! Ni kwa sababu hauna mfalme? Je! watu wako wenye hekima wamekufa? Unalia kwa sauti kuu kama mwanamke anayezaa mtoto."

Kuwa katika uchungu na kuzaa, binti wa Sayuni, kama mwanamke mwenye uchungu

Mika anatumia picha ya mwanamke katika kuzaa kusisitiza masumbuko makali ya uhamishoni. Anamaanisha kwamba watakuwa katika uchungu kwa sababu Mungu anawaadhibu kwa kuwapeleka mbali na Israeli. Wengi wao hawatakuja nyumbani tena.

Huko utaokoka. Huko Yahwe atakuokoa

"Huko Yahwe atakuokoa"

Micah 4:11

Maelzo ya Jumla:

Yerusalemu itawashinda maadui zake.

Acha atiwe unajisi; acha macho yetu yaitazame Sayuni

"Ngoja tuuangamize mji wa Yerusalemu na kuwaharibu watu wake hivyo tunaweza kuchukua furaha kubwa katika kuanguka kwao."

kwa kuwa amewakusanya kama miganda kupura sakafuni

Hii inamaanisha pia Mungu anajiandaa kuwaadhibu watu wa mataifa.

Micah 4:13

Maelezo ya Jumla:

Yahwe anaonyesha picha ya kupuria sakafu.

Inuka na pura, binti Sayuni

Mungu atawatumia watu wa Sayuni kuwaadhibu watu wa mataifa.

Nitaifanya pembe yako kuwa chuma, na nitazifanya kwato zako kuwa shaba

Yahwe anawalinganisha watu wa Sayuni na ng'ombe shujaa ambaye angepura ngano. Hii inamaanisha Yahwe atawafanya watu wa Israeli hodari tena ili waweze kuwashinda mataifa mengine.

Micah 5

Micah 5:1

kundi la watu, watu, watu, watu, watu

Neno "watu" au "kundi la watu linarejea kwa kundi la watu ambao wanatumia lugha moja wote na utamaduni mmoja. Kirai "watu" mara nyingi inarejea kwa mkusanyiko wa watu katika mahali fulani au katika tukio maalumu.

Yerusalemu

Yerusalemu ilikuwa asili ya mji wa Wakanaani ambao badaye ulikuwa mji muhimu zaidi katika Israeli. Inaonyesha kama kilomita 34 magharibi mwa Bahari ya Chumvi na kaskazini mwa Bethelehemu. Bado ni mji mkuu wa Israeli ya sasa.

Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli

Neno "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpatia Yakobo. Maana yake, "alipambana na Mungu."

ufito

Neno "fimbo" linarejea kwa nyembamba, ngumu, fimbo kama kifaa ambacho kilitumika katika njia nyingi tofauti tofauti. Ilikuwa kama walau mita moja katika urefu.

Micah 5:2

Lakini wewe, Bethelehemu Efrata

Yahwe anazungumza na watu wa huu mji kana kwamba wako pale wanasikiliza.

Efrata

Hili ni mojawapo ya jina la eneo ambalo Bethehemu ilipokuwa au inaitwa kwa jina jingine kwa ajili ya Bethelehemu au inatofautisha Bethelehemu hii kutoka nyingine. Bethelehemu ipo kama maili sita kusini mwa Yerusalemu. Palikuwa ni nyumbani mwa mji wa Mfalme Daudi. Watafsiri wanaweza kuongeza hii rejea: "Jina 'Efrata' maana yake 'kuzaa matunda."'

hata kama uko mdogo katikati ya koo za Yuda

Hii inamaanisha Mungu atafanya mambo makubwa kupitia kidogo na mji usiokuwa na maana.

atakuja kwangu

Hapa "mimi" inamrejea Yahwe.

ambaye mwanzoni ni kutoka nyakati za kale, kutoka milele

Hii inaurejea ukoo mtawala kutoka familia ya zamani ya Mfalme Daudi. Virai "kutoka nyakati za zamani" na "kutoka milele" kimsingi inamaanisha kitu kimoja na kusisitiza jinsi hii safu ya familia ilivyo ya zamani.

Kwa hiyo Mungu atawatoa

"Kwa hiyo Mungu atajitenga na watu wa Israeli"

hadi wakati yeye aliye katika uchungu atakapozaa mtoto

Hii inarejea kipindi wakati mtawala amezaliwa, muda wenye ukomo.

mabaki ya ndugu zake

"mabaki ya jamaa zake Waisraeli." Hawa ni Waisraeli katika uhamisho. Hapa "yeye" inamrejea mtoto ambaye atakuwa mtawala.

Micah 5:4

Maelezo ya Jumla:

Hii mistari inaendelea kumwelezea mtawala kutoka Bethelehemu.

Atasimama na kulichunga kundi lake kwa nguvu za Yahwe

"Atawaongoza watu wake katika nguvu ya Yahwe."

katika ukuu wa enzi ya jina la Yahwe Mungu wake

"katika mamlaka ya nguvu ya Yahwe Mungu wake"

Watabaki

Hapa "wao" inawarejea watu wa Israeli. Neno "Israeli" au "Yerusalemu" imehusika. "Watu watabaki Israeli" au "Watu watabaki katika Yerusalemu"

kwa kuwa atakuwa mashuhuri hata mwisho wa dunia

Hii inamaanisha kwamba mbeleni watu wote kutoka kila taifa watatoa heshima kwa mtawala wa Israeli.

Atakuwa amani yetu

Hapa "yetu" inamrejea Mika na watu wa Israeli. "Atakuwa mtu wa amani"

wachungaji saba na viongozi saba juu ya watu

Hapa "wachungaji" inamaanisha "watawala." pia, unaweza kutaka kuongeza rejea inayosema, "Hesabu 'saba' na 'nane' zimeunganishwa kumaanisha kwamba zitakuwa zaidi za kutosha viongozi kukutana na hitaji."

Micah 5:6

Wataichunga nchi ya Ashuru

Hapa kuwashinda Waashuru inzungumziwa kana kwamba ilikuwa kuwachunga kondoo.

nchi ya Nimrodi

Hili ni jina jingine kwa nchi ya Ashuru. Nimrodi alikuwa muwindaji na kiongozi wa mwanzoni. Watafsiri wanaweza kuongeza hii rejea: "Jina 'Nimrodi' maana yake 'uasi.'"

katika malango yake

Hii sura inaweza kueleweka kama "katika malango yake." Malango ya mji yalikuwa kwenye maeneo ya watu wengi ambapo mara nyingi wakuu walifanya maamuzi muhimu.

Ataokoa

"Mtawala ataokoa"

kama umande utokao kwa Yahwe, kama manyunyu kwenye majani

Hii inasisitiza kwamba watu wa Yuda watakuwa wakijifurahisha, baraka, kwa mataifa.

ambayo hayamsubiri mtu, na hayawasubiri wana wa mwanadamu

"na watasubiri kwa na kumtegemea Mungu"

Micah 5:8

katikati ya mataifa, katikati ya watu wengi

Hivi virai viwili kimsingi vinamaanisha jambo moja na kusisitiza kwamba "mabaki ya Yakobo" wataishi katika mataifa mengi tofauti tofauti.

kama simba katikati ya wanyama wa msitu, kama mwana simba katikati ya kundi la kondoo. Wakati akipita katikati yao, atawakanyaga juu yao na kuwararua kuwa vipande vipande

Hii inasisitiza kwamba watu wa Israeli watakuwa na uwezo na ujasiri wakiwa uhamishoni kuhukumu na kuwaharibu maadui zao.

Micah 5:10

Itatokea siku hiyo

Hii inarejea kwa mda usio dhahiri mbeleni, ni kama kipindi cha uhamisho.

Nitawaharibu farasi wako kutoka miongoni mwenu na nitayavunja magari ya farasi

Watu wa Israeli walitumia farasi na magari ya farasi tu katika vita. Pia ilijumuisha ushirikiano na wageni, nchi zisizomjua Mungu. Mungu hakutaka watu waamini silaha zao za vita kuwalinda zaidi kuliko walivyomwamini yeye.

Micah 5:12

Maelezo ya Jumla:

Yahwe anaendelea kuongea na watu wa Israeli.

Micah 6

Micah 6:1

Inuka na ueleze kesi yako...atapigana katika mahakama juu ya Israeli

Katika 6:1-5 Mika anatumia chumba cha mahakam kama picha. Yahwe anazungumza mbele ya mashahidi kuelezea kwa nini watu wa Israeli wamemwacha mungu na kuanza kuabudu sanamu.

milima...vilele...mivumilivu ya dunia

Mika anaongea na hivi vitu kana kwamba ni wanadamu. Mika anatumia milima, vilele, na misingi ya dunia kama ushahidi wa milele juu ya kuabudu sanamu za watu wake.

Micah 6:3

Maelezo ya Jumla:

Hii inaendelea madai ya Yahwe juu ya watu wa Israeli.

Watu wangu, nimefanya nini kwenu? nimewachosha mara ngapi? shuhudieni dhidi yangu!

Mungu anatumia haya maswali kusisitiza kwamba yeye ni Mungu mwema, na hajafanya kitu kuwafanya watu kukoma kumwabudu yeye. "Watu wangu, nimekuwa mwema kwenu. Sijafanya kitu kuwafanya mnichoke. Kama mnafikiri nimefanya, shuhudieni juu yangu, sasa."

nyumba ya utumwa

"mahali ambapo mlipokuwa watumwa"

kumbukeni

"kumbuka"

Balaki mfalme wa Moabu alivyotunga, na vile ambavyo Balamu mwana wa alivyomjibu

Hii inaonyesha kwenye tukio la nyuma wakati Mfalme Balaki alipompangisha Balamu kuwafanya watu wa Israeli. Aidha, Mungu alimruhusu Balamu kuwabariki watu tu.

Beori

Hili ni jina la baba yake na Balamu.

Shitimu

Hili ni jina la mahali katika Moabu.

kwamba mnaweza kujua matendo ya haki yangu, Yahwe.

"hivyo basi mnaweza kukumbuka mimi ni nani, na nini nimefanya juu yenu"

Micah 6:6

Je nilete nini kwa Yahwe, ninapoenda kumwinamia Mungu aliye juu? Je ninaweza kuja kwake na sadaka za kuteketeza, pamoja na ndama wenye mwaka mmoja?Je Yahwe atapendezwa na maelfu ya kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, tunda la mwili wangu kwa ajili ya dhambi yangu mwenyewe?

Mika anatumia maswali kuwafundisha watu wa Israeli kusu kile hasa kinachomtukuza Mungu. "Hakika hufikirii kwamba unaweza kumtukuza Mungu kwa kumletea ndama mkubwa mwenye mwaka mmoja, kondoo 1,000, 10,000 mito ya mafuta, au mtoto wako wa uzao wa kwanza kama sadaka kwa ajili ya dhambi zako."

mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, tunda la mwili wangu kwa ajili ya dhambi yangu mwenyewe

Hivi virai viwili vinamaanisha kitu kimoja.

Amekwambia

"Yahwe amekwambia"

Micah 6:9

Sauti ya Yahwe inatangaza kwenye mji

"Yahwe anawatangazia watu wa Yerusalemu"

hata hivyo hekima hukiri jina lako

"na mtu mwenye hekima atamuogopa Yahwe" au "na mtu mwenye hekima atatii kile Yahwe asemacho"

Kuwa tayari kwa ajili ya fimbo, na kwa yule aliyeiweka

Hapa "fimbo" inarejea kwa adui askari ambaye Yahwe atawaadhibu watu wake.

kipimo cha uongo

Hii inataja mizani isiyopima vitu kwa usahihi hivyo mtu anaweza kuwaibia wengine kwa madhumuni na kutengeneza pesa nyingi zaidi kwa ajili yake mwenyewe.

Micah 6:11

Ningeweza kumfikiria mtu kuwa hana hatia kama anatumia kipimo cha ulaghai, pamoja na mfuko wa kipimo cha udanganyifu

Yahwe anatumia swali kusisitiza kwamba anaangalia hatia ya mtu adanganyaye wengine ili kutengeneza pesa zaidi. "Hakika nitamwangalia mtu mwenye hatia kama akitumia kipimo kisicho haki na uzito ili kuwadanganya wengine na kutengeneza pesa zaidi kwa ajili yake mwenyewe.

Watu matajiri wamejawa udhalimu

"Watu matajiri wanawachukulia maskini faida"

makazi yao yamesema uongo, na ulimi wao katika midomo yao unaudanganyifu

Vishazi hivi vyote vinamaanisha kitu kimoja na vimeungana kwa ajili ya msisitizo. "Ninyi nyote ni waongo." Hii itafanya matokeo ya mhemko kwa wasomaji.

Micah 6:13

Kwa hiyo nimekupiga kwa pigo linaloumiza...lakini hutakunywa divai

Yahwe anaelezea adhabu yake ya watu wake kama kumruhusu adui askari kuja na kuchukua kila kitu walichokuza, andaa, na kutunza kwa ajili yao wenyewe.

Micah 6:16

Maelezo ya jumla:

Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Kanuni zilizotengenezwa na Omri zimetunzwa

"Mmefanya kile ambacho Omri alichoamuru"

Omri...Ahabu

Hawa watu wote walikuwa wafalme juu ufalme wa kaskazini mwa Israeli. Mungu aliwahesabu wote kuwa waovu sana.

Mnatembea kwa ushauri wao

"mmefanya mambo maovu ambayo Omri na Ahabu waliwaambia watu kufanya.

jambo la kuzomea

Hicho ni, kitu cha kudhihaki kwa kuzomea kwacho.

Micah 7

Micah 7:1

Kwangu mimi ni kama msimu wa mavuno...matini ya malimbuko

Mika anasisitiza kwamba hakuna tean watu waadilifu, waaminifu kwa Mungu, katika Israeli. "Kwangu mimi watu wa Israeli ni kama shamba la mzabibu baada ya mavuno na kukusanya. Mizabibu imejifunua. Siwezi kupata tunda lolote, lakini bado natamani sana kula tini lililoiva.

Watu waaminifu wamepotelea...kwa wavu

Mika anakuza kuonyesha jinsi ambavyo hali ilivyo mbaya. Anahisi hakuna mtu mwema aliyebaki katika Israeli.

Micah 7:3

Maelezo ya Jumla:

Mika anaendelea kuongea kuhusu watu wa Israeli.

Mikono yao ni mizuri mno

"Watu ni wazuri sana"

Mtu bora kwao ni kama mitemba, mwadilifu sana ni kama miche ya miba

Hii inamaanisha kwamba hata kiongozi mzuri katika Israeli amesababisha maumivu na walikuwa hawafai kitu

Imefika siku iliyosemwa nyuma na walinzi, siku ya adhabu

Hapa "yako" bado inawarejea watu wa Israeli. "Manabii wao wamewaambia kwamba Yahwe angewaadhibu"

Sasa ni muda wa machafuko yao

Hii inaweza kurejea kushinda vita. "Sasa iko hapa, na hawataelewa nini kinaendelea"

Micah 7:5

Maelezo ya jumla:

Mika anaendelea kuongea na watu wa Israeli.

Msimwamini kila jirani...watu wa nyumba yake mwenyewe

Mika anaendelea kuonyesha kwamba hakuna mtu yeyote mzuri, mwadilifu, na mwaminifu kwa Mungu miongoni mwa watu wa Mungu. Hapa anasisistiza kwamba hawawezi hata kuwaamini marafiki au familia.

Micah 7:7

Lakini kama kwangu mimi

Hapa "mimi" inamrejea Mika

Usifurahi juu yangu

Mika harejelei kwake pekee. Anamaanisha adui hatakiwi kufurahi juu ya kilichotokea kwa watu wote wa Israeli.

Wakati nitakapokuwa nimekaa katika giza, Yahwe atakuwa nuru kwangu

Mika anarejea kwenye janga ambalo linakuja kwa watu wa israeli kama "giza." Anamaanisha ingawa Mungu atamwacha adui kuja kuwaharibu sasa, atakuja kuwaokoa mbeleni.

Micah 7:9

Kwa sababu nimetenda dhambi

Mika hajirejei yeye pekee. Anamaanisha watu wote wa Israeli wametenda dhambi.

hata niteteapo kosa langu, na kutekeleza hukumu kwa ajili yangu

Hii inarejea wakati Mungu aamuapo amewaadhibu watu wake mno. Kisha atawaadhibu watu wa mataifa mengine ambao waliowajeruhi watu wa Israeli.

Atanileta kwenye nuru

" Atakuja na kutuokoa kutoka maadui zetu. Itakuwa kama kumleta mtu katika giza kwenye nuru"

Micah 7:10

Kisha adui yangu

Mika hajirejei yeye pekee. Anamaanisha adui wa watu wote wa Israeli.

Yuko wapi Yahwe Mungu wako?

adui hutumia swali kuwatania watu wa Israeli. "Yahwe Mungu wako hawezi kukusaidia"

Macho yangu

"Mimi" au "sisi"

yatamtazama yeye

Hapa "yeye" inawarejea maadui ambao waliowajerui watu wa Israeli.

atakanyagwa chini

"maadui zao watawakanyaga chini"

Micah 7:11

Siku ya kujenga kuta zako zitakuja

Hapa "kuta" inarejea kwa kuta kuzunguka miji yao, ambzo zimeandaa usalama na ulinzi kutoka maadui zao.

mipaka itasogezwa mbali sana

"Yahwe ataisogeza mipaka ya ukubwa wa nchi yenu" au "Yahwe ataongeza ukubwa zaidi wa ufalme wenu"

Hizo nchi zitakuwa zitakuwa zimejitenga

"Zile nchi zitakuwa tupu" au "Hakuna atakayeishi katika hizo nchi"

Micah 7:14

Chunga watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako

Mika anaomba kwa Yahwe, akimuuliza kuwalinda watu wake wa Israeli tena. Hapa "fimbo" inawarejea wakuu wa Mungu na kuongoza, kama mchungaji atumiavyo fimbo kuongoza na kuzilinda kondoo zake.

Wanaishi wenyewe kwenye msitu

Mika anamaanisha kwamba baadhi ya watu wanaishi ambapo aridhi ni maskini na wamejitenga na hawawezi kujipatia bidhaa zinazohitajiaka.

Waache wachunge katika Bashani na Gileadi

Hii mikoa inajulikana kama nchi tajiri kwa kukuza chakula. Hivyo Mika anauliza upanuzi zaidi wa eneo, ambalo lilikuwa limepotea kwa wavamizi miaka ya nyuma.

kama siku za zamani

Hii inaweza kurejewa wakati Suleimani alipokuwa mfalme.

Nitaonyesha

Hapa "mimi" inamrejea Yahwe.

Micah 7:16

Wataweka mikono yao juu ya midomo yako; masikiio yao yatakuwa kiziwi

Hii inaonyesha jinsi walivyo na hofu, sana hivyo hawawezi kujibu.

Watalamba vumbi kama nyoka, kama viumbe vitambaavyo juu ya nchi

Virai vyote vinamaanisha jambo moja. Maadui wa Mungu wataaibishwa kabisa na kuja kwake katika hofu baada ya kuona mambo yenye nguvu ayafanyayo.

Micah 7:18

Ni nani aliye Mungu kama wewe

Mika anatumia swali kusisitiza kwamba hakuna mwingine afanyaye mambo ambayo Yahwe ayafanyayo.

mabaki ya mrithi wako

"wale walio wakwetu watu wako waliochaguliwa ambao walioponea chupuchupu adhabu yako"

Micah 7:19

Uta

Hapa "wewe" inamrejea Yahwe.

juu yetu

Hapa "sisi" inamrejea Mika na watu wa Isralei.

utayakanyaga maovu chini ya miguu yako. Utazitupa dhambi zetu zote kwenye vilindi vya bahari

Hii inamaanisha Mungu atazisamehe kabisa dhambi za watu na hakutakuwa tena na adhabu ya watu kwa ajili yao.

mpatie ukweli Yakobo na agano aminifu kwa Ibrahimu

Hapa "Yakobo" na "Ibrahimu," ambao ni mambabu wa taifa la Israeli, inarejea kwa watu wa Israeli sasa.

kwa babu zetu

Hii inamrejea Ibrahimu na Yakobo, na labda wengine waliokuwa hai wakati Mungu alipolifanya agano lake pamona na Israeli.