Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Habakkuk 1

Habakkuk 1:1

Ujumbe ambao Habakuki nabii aliuokea

Maneno haya yanatambulisha sura mbili za mwanzo wa kitabu. Kama lugha yako inahitaji sentensi kamili hapa, "Huu ni ujumbe ambao Habakuki nabii aliupokea kutoka kwa Mungu."

kwa muda gani nitalilia msaada, na hutasikia?

NI: "Nimekuwa nikilia kwaajili ya msaada kwa muda mrefu, ingawa lakini unajifanya kama hunisikii!"

Habakkuk 1:3

Taarifa kwa ujumla:

Habakuki anaendeleza maombi yake kwa Mungu.

ugomvi unainuka

"mapigano kati ya watu yanakuwa kawaida zaidi"

Uovu unawazunguka wenye haki

Hii inaweza kuwa na maana kwamba watu wenye haki wanateseka si kwa halali 1) "waovu wananguvu zaidi kuliko watu wenye haki" au 2)"kuna watu waovu zaidi kuliko watu wenye haki."

uadilifu wa uongo unaenea

NI: "uovu unatokea badala ya uadilifu" au "kukosa haki kunaongezeka"

Habakkuk 1:5

Taarifa kwa ujumla:

Yahwe anajibu maombi ya Habakuki.

Angalia mataifa na uyachunguze

"Jifunze mambo yanayoendelea katika mataifa mengine"

upana wa nchi

Hii inaweza kuwa namaana 1) kila mahali katika Yuda au 2) kila mahali duniani

nyang'anya

chukua kwa nguvu au iba kutoka kwa mmiliki halali

masikani

"nyumba"

wao ... wao ... wao wenyewe

Maaskari Wakaldayo. Mungu atainua taifa la Wakaldayo, na maaskari Wakaldayo watavamia Uyahudi.

Wanatisha na kuogofya

Maneno "kutisha" na "ogofya" kimsingi yanamaana kitu kile kile na kusisitiza kwamba kuwafanya wengine waogope sana, NI: "Wanawafanya wengine waogope sana."

endelea

"kuja"

Habakkuk 1:8

Farasi zao ... farasi zao

farasi za askari wa Wakaldayo

haraka kuliko mbwa mwitu wa jioni

Farasi za Wakaldayo wanalinganishwa na mbwa mwitu wakali ambao wanakimbilia mawindo yao wakati wa jioni wanapokuwa na njaa sana kwasababu hawajala siku nzima.

wapanda farasi wao

Askari wa Wakaldayo wanapanda farasi.

chui

kubwa, paka wepesi

wanaruka kama tai

"wapanda farasi wanaendesha kwa haraka kama tai wanavyopaa"

umati wao unakwenda kama upepo wa jangwani, na wanakusanya mateka kama mchanga

Wakaldayo ni wengi, na kama chembe chembe za mchanga upepo hubeba katika mawimbi wengi hawahesabiki, hivyo hakuna mtu anayeweza kuhesabu watu wanaokamata na kuwafanya wafungwa.

Habakkuk 1:10

Taarifa kwa ujumla:

Yahwe anaendelea kuwaeleza askari wa Wakaldayo.

upepo utatimua

majeshi ya Wakaldayo yanayovamia yanalinganishwa na upepo unaotimua kupitia upande mmoja na kwa haraka unaendelea katika eneo lingine.

Habakkuk 1:12

Taarifa kwa ujumla:

Habakuki anazungumza kwa Yahwe kuhusu Wakaldayo.

Wewe si kutoka nyakati za kale, Yahwe Mungu wangu, Mtakatifu wangu?

NI: "Wewe ni wa milelel, Yahwe Mungu wangu, Mtakatifu wangu."

wao ... wao

Wakaldayo

Mwamba

kinga ya Israeli

Waliwekwa kwaajili ya lengo la kuisahihisha Israeli

"Wao waliwekwa kwa lengo la kuisahihisha Israeli"

Habakkuk 1:13

Taarifa kwa Ujumla:

Habakuki anaendelea kuongea kwa Yahwe kuhusu Wakaldayo.

Wao ambao wanasaliti

"Wakaldayo, ambao hakuna mmoja atakayewaamini"

meza

"haribu"

kama samaki baharini ... kama vitu vitaambaavyo

Hizi kauli mbili zinadhihirisha wazo lilelile kwamba Mungu ameruhusu Wakaldayo kuwashughulikia Israeli kama viumbe wenye thamani ndogo sana, na si kama watu wanavyotakiwa kushughulikiwa.

Habakkuk 1:15

Taarifa kwa Ujumla:

Habakuki anaendelea kuongea kwa Yahwe kuhusu Wakaldayo.

ndowano ya samaki ... wavu wa samaki

vifaa vilitumika kuvua samaki

wavu

"kifaa kilitumika kuvulia "vitu vitaambaavyo"

Wanyama walionona ni sehemu yao, na nyama nene ni chakula chao

badilishana tafsiri: "wanyama wazuri sana na nyama nzuri sana ni fungu la chakula chao"

fungu

sehemu ndogo ya kitu fulani kikubwa ambacho kinatumika kati ya watu wengi

wanamaliza nyavu zao za kuvulia

wavuvi wanawamaliza samaki kwenye nyavu ili kwamba wazitupe tena na wavue samaki wengi zaidi.

Habakkuk 2

Habakkuk 2:1

mimi ... yangu ... mimi

Habakuki

yeye

Yahwe

Nitasimama katika nguzo yangu ya ulinzi na kuweka kituo changu mwenyewe juu ya mnara wa mlinzi.

Kauli hii inasema kitu kilekile kwa namna mbili tofauti. "nitazimama katika nguzo yangu juu ya mnara wa mlinzi." Habakuki anatumia kauli hii akijilinganisha yeye mwenyewe anasubiri kusikia kutoka kwa Mungu kwa askari mlinzi asimamaye kulinda juu ya mnara.

Nitageuka kuondokana na lawama zangu

Neno "geuka" linazungumzia mtu kubadilisha mawazo yake kama nikuondoka kutoka kitu kimoja kwenda kingine. NI: "Nitaacha kulaumu na kukubaliana na Mungu"

Habakkuk 2:2

Taarifa kwa Ujumla:

Yahwe anamjibu Habakuki.

Tunza maono haya, na uandike kwa dhahiri kwenye vibao

Kauli zote mbili zinasema kitu kile kile katika njia mbili tofauti. Badilisha tafsiri: "Andika kwa wazi juu vibao ambacho Mungu anakwenda kukwambia"

vibao

hivi ni vipande bapa vya mawe au udongo mfinyanzi ambao uliotumika kwaajili ya kuandika.

yule anayesoma anaweza kukimbia

Hii inaweza kumaanisha 1) mtu fulani atakimbia pamoja na vibao na kuwasomea au 2) mtu yeyote ambaye anayesoma ataweza kusoma kwa urahisi

na mwisho kuongea

kile kilichoandikwa kitatokea au kuja kuwa halisi.

na hakitakawia

Maana zinazowezekana 1) "na hakitasubiri" au 2) "na hakitakuja kwa taratibu"

Habakkuk 2:4

Taarifa kwa Ujumla:

Yahwe anaendelea kumjibu Habakuki.

Angalia!

Neno "angalia!" hapa linaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata.

Yule ambaye anatamani hayuko sawa ndani yake ... kijana mwenye kiburi ... yeye hatastahimili, lakini hukuza hamu yake ... hukusanyika kwake mwenyewe ... anakusanyika kwaajili yake.

Yahwe anazungumzia Wakaldayo ingawa kama wako mtu mmoja. "Yeye" inarejerea kwa Wakaldayo ingawa kama wako mtu mmoja.

Hukusanya kwake kila taifa na hukusanya kwaajili yake mwenyewe watu wote.

Hapa kinasemwa kitu kimoja katika namna mbili tofauti. "Anawakusanya watu wote kutoka kila taifa" (Angalia:

Kusanya

leta pamoja

kila ... wote

idadi kubwa sana

Habakkuk 2:6

Taarifa kwa Ujumla:

Yahwe anaendelea kumjibu Habakuki. Ingawa narejerea kwa Wakaldayo kama wako mtu mmoja.

Kwa muda gani utaongeza uzito wa dhamana uliyochukua?

"Kwa wakati fulani utakuwa huwezi kuchukua dhamana kutoka kwa watu." Hii inaweza kumaanisha 1) Wakaldayo wanafanana na wanyang'anyi waliobeba dhamana wamewalazimisha watu wengine kutia saini au 2) Yahwe anatunza adhabu kwamba Wakaldayo wameiba na siku fulani atawahitaji kuwajibika.

dhamana

ahadi ya kuzingatia imetolewa kwaajili ya deni ambalo linadaiwa, daima iliandikwa kwenye udongo wa mfinyanzi

wale watakao kuwa wakikudai hawatainuka kwa ghafula, na wanaokusumbua kuamka

swali hili linaulizwa ili kwamba kuwafanya Wakaldayo wafikiri kuhusu jibu. "Wale ambao wanakukasirikia watakuja kinyume chako, wale unaowaogopa wataanza kushambulia"

wale wanaodai kwako

Nahau hii inamaanisha wale ambao wanakudeni kwamba lazima walipe. Hivyo, baadhi ya tafsiri za kisasa hutafsiri kauli hii kumaanisha wanaodai, siyo wanaodaiwa.

wale wanaokutisha

Hii inarejerea kwa walewale wadaiwa. Watawatisha Wakaldayo kwa kuwashambulia kulipa kisasi kwa deni lisilo la haki kwamba walikuwa wamelazimishwa kuwa nalo.

inuka juu

"kuongezeka zaidi" au "kuwa na nguvu zaidi"

iliyotekwa nyara

kuibiwa au kuchukuliwa kwa nguvu.

Habakkuk 2:9

Taarifa kwa Ujumla:

Yahwe anaendelea kumjibu Habakuki. Ingawa narejerea kwa Wakaldayo kama kwa mtu mmoja.

ambaye gawa mapato mabaya nyumbani mwake

"ambaye anafanya kazi kupata faida isiyo ya uaminifu kwaajili ya familia yake"

weka kiota chake juu

"jenga nyumba yake mbali na matatizo"

mkono wa mwovu

NI: "mkono wa mwovu" Kutenda "uovu" kama mtu au "watu waovu"

Umebuni aibu kwaajili ya nyumba yako kwa kuondoa watu wengi

"Kwasababu umeondoa watu wengi, familia yako itakuwa inateseka kwa aibu"

Wewe

Umoja

Kuondoa

Kuharibu

umetenda dhambi kinyume chako wewe mwenyewe

"umiza wewe mwenyewe"

mawe ... pao la mbao

"mawe" na "pao la mabo" kuwakilisha watu walioumizwa katika jengo la nyumba, ambao kinyume chake wanawakilishwa watu walioharibiwa na Wakaldayo.

paza sauti

fanya mashitaka kwa Mungu kinyume wajenzi wa nyumba

wajibu

kubaliana na mashitaka

Habakkuk 2:12

Taarifa kwa Ujumla

Yahwe anaendelea kumjibu Habakuki. Ingwa anarejerea kwao Wakaldayo kama kwa mtu mmoja.

Ole kwa yule ambaye anajenga jiji kwa damu, na ambaye anaimarisha mji katika uovu

Kauli hizi mbili zinasema kitu kile kile katika njia mbili tofauti. Tafsiri zinazoingiliana: "Onyo kwa Wakaldayo ambao wanajenga miji yao kwa vile walivyoiba kutoka kwa watu ambao wamewaua"

pamoja na damu

kwa kuua watu. Tafsiri inayopokezana: "yule anayeua watu na kuiba mali zao ili kwamba ajenge mji."

Anayeanzisha mji katika uovu

"Yule anayeanza mji kupitia tabia mbovu." Wakaldayo wanajenga miji yao wakitumia mali zilizoibwa kutoka kwa watu waliowaua.

Hii haikutoka kwa Yahwe wa majeshi kwamba watu wafanye kazi kwa moto na mataifa yote mengine yachoke bila kitu?

Mungu amesababisha uharibifu wa kile watu walichojenga. Ilisemwa katika njia mbili tofauti ili kufanya iwe wazi zaidi. Tafsiri inayobadilishana: "Yahwe ndiye yule anayesababisha watu wanaofanya kazi ngumu ya kujenga kuharibiwa kwa moto na matokeo ni hakuna."

Habakkuk 2:15

Taarifa kwa Ujumla:

Yahwe anaendelea kumjibu cssdved Habakuki. Yeye anarejerea kwa Wakaldayo ingawa kama wako mtu mmoja.

ongeza sumu yako

"ongeza sumu yako kwenye kinywaji"

Utavimbiwa na aibu zaidi kuliko utukufu

"Kama unatafuta utukufu mkuu, Mungu ataleta juu yake aibu kuu"

Wewe

umoja

Kuinywa

Kunywa kikombe cha sumu

Kikome cha mkono wa kuume wa Yahwe kitakugeukia wewe

"Kama Yahwe amehukumu mataifa mengine na uweza wake wote, hivyo atakuhukumu wewe na uweza wake wote"

Kikombe

Divai iliyotiwa sumu

Mkono wa kuume

mkono wa nguvu zaidi

utakuja katika hali yake kukugeukia wewe

"utakuja kwako kama ulivyofanya kwa wengine"

Aibu itafunika heshima yako

"kila mmoja ataona aibu yako na hakuna atakayeona heshima yako"

Habakkuk 2:17

Taarifa ya Ujumla:

Mungu anaendelea kuongea jinsi yaye atakavyo wahukumu Wakaldayo

Kuharibiwa kwa wanyama kutakutisha wewe

"vifo vya wanyama vitakufanya wewe uogope"

Habakkuk 2:18

wewe

neno "wewe" linarejerea kwa Wakaldayo.

subu sanamu

Hii ni kazi ya kuunda sanamu kwa kimiminiko cha chuma katika kitu kilichochongoka katika muundo unaohitajika. chuma kitachukua mwonekano uliosubu na gumu kama picha au sanamu.

metali

Hili ni neno chuma ikiwa katika hali ya majimaji.

mwalimu wa waongo

Kauli hii inarejerea kwa yule aliyechonga au kusubu sanamu. Kwa kutengeneza mungu wa uongo, yeye anafundisha uongo.

Habakkuk 3

Habakkuk 3:1

Nimesikia taarifa zako

Hii inaweza kumaanisha 1) "nimesikia watu wanasema kuhusu kile ulichofanya" au 2) "nilisikia kile ulichosema."

fufua kazi yako

"huisha tena kazi yako" au "fanya tena ulichofanya"

fanya ijulikane

"fanya kazi yako ijulikane"

Habakkuk 3:4

Taarifa kwa ujumla

Habakuki anaendelea kufafanua maono yake ya Yahwe.

miali

Hii ni mistari inayotoka kwenye kitovu cha kitu cha mwanga ambayo inatokea kwenye mwanga asili kama vile jua.

yeye ... yeye ... yeye

Yahwe

Habakkuk 3:6

Taarifa kwa ujumla:

Habakuki anaendelea kufafanua maono yake ya Yahwe.

alipima dunia

Hii inaweza kumaanisha 1) yeye kaikagua kama ambavyo mwenye mamlaka angelifanya kabla hajagawa maeneo kwa watawala au 2) ameitikisa

milima ya milele ... vilima visivyo na mwisho

"milima ambayo imekuwepo tangu mwanzo wa wakati ... vilima ambavyo vitakuwapo mpaka mwisho wa wakati. kama lugha yako haina maneno tofauti kwa "vilima" na "vilima" au kwa "milele" na "usiomwisho" unaweza ukayaweka pamoja kama ilivyo kwenye ULB.

inama chini

katika kumwabudu Mungu. "walilala chini ya ardhi"

Habakkuk 3:7

Taarifa kwa Ujumla:

Habakuki anaendelea kufafanua maono yake ya Yahwe.

mahema ya wakushi katika mateso, na kitambaa cha mahema ... ya Midiani yanatetemeka.

Watu wa Midiani na Wakushi wanao tetemeka na tikisika kwa woga wanafanana na hema ya nguo ambavyo inaenda wakati upepo unavuma.

wakushi

Hii inaweza kuwa 1) jina la kikundi cha watu wasiojulikana vinginevyo au 2) Kushi ile ile.

Yahwe alikuwa na hasira pale mtoni? Ghadhabu yako ilikuwa kinyume na mtoni, au chuki yako kinyume na bahari ... magari ya ushindi?

kama lugha yako haina maneno yakutenganisha "hasira" na "ghadhabu" na "chuki" unaweza ukaunganisha misitari: "Yahwe alikuwa na hasira na mito? Chuki yako ilikuwa kinyume na bahari ... magari ya ushindi?" NI: "Yahwe hakuwa na hasira na mito, wala Chuki yako haikuwa kinyume na bahari ... magari ya ushindi."

fimbo yako juu ya farasi na magari ya ushindi

Kama askari aliongoza farasi au gari katika vita, Yahwe alikuja kuokoa watu wa Isrseli.

Habakkuk 3:9

Sela

Neno hili linamaanisha "simama na akisi" au "inua juu, inua"

Milima ilikuona wewe na ikatikisika kwa maumivu

Kama Mungu aliigawa nchi, milima ilihama, kama vile ingeliona matendo ya Mungu na kudhihirisha kwa kugeuka kutoka pale ilipogawanyika nchi.

kina cha bahari kilipaza sauti

sauti ya mawimbi makubwa ya bahari

iliinua juu mawimbi yake

kiwango cha maji kinaiinuka

Habakkuk 3:11

Taarifa kwa Ujumla:

Habakuki anaendelea kufafanua maono yake ya Yahwe.

katika mwanga wa mshale wako

kwasababu ya mwanga (mng'ao)wa mshale wa Yahwe ulikuwa unang'aa sana.

Umetembea katika ardhi kwa uchungu. Katika hasira umepukutisha mataifa.

Sentensi hizi mbili zinashiriki maana sawa. Kwa pamoja zinarejerea Yahwe anahukumu mataifa kwaajili ya uovu wake.

uchungu

hasira kwa kitu furani ambacho ni kosa

Habakkuk 3:13

Taarifa kwa Ujumla:

Habakuki anamfafanua Yahwe.

mteule wako

Hii inaweza kumaanisha pia "Masihi wako" lakini mrejeo ni wazi "kwa watu wako" hivyo tumia nomino ya kawada hapa, siyo kama jina halisi.

Unapondaponda kichwa cha nyumba ya mwovu

"Unaharibu kabisa kiongozi wa watu waovu"

Habakkuk 3:14

Taarifa Kwa Ujumla:

Habakuki anamfafanua Yahwe kuwaharibu Wakaldayo.

Wanakuja sawa na tufani

Nguvu na uharaka wa Wakaldayo walivyowashambulia Israeli unalinganishwa na ujio wa ghafla wa tufani.

Kuchekelea/cheka

"kujigamba"

teketeza maskini katika mahali palipo fichika

tafuta watu maskini ambao wamejificha na huwaua na kuchukua mali zao zote

teketeza/meza

hula kila kitu kwa haraka

Habakkuk 3:16

Taarifa kwa Ujumla:

Habakuki anafafanua hofu yake anapofikiri kuhusu Yahwe angewapa adhabu Wakaldayo.

ndani yangu kulitetemeka! midomo yangu ilitetema ... uozo huja kwenye mifupa yangu ... chini yangu mwenyewe natetemeka.

haya yanarejerea hofu iliyosababishwa na kufikiri kuhusu matukio yajayo. Habakuki anatumia baadhi ya sehemu za mwili wake kudhihirisha kwamba kila kiungo chake kinahofu.

oza

chakaa

Habakkuk 3:17

mti mtini ... mizabibu ... mzaituni ... mashamba ... kundi ... ng'ombe

Hakuna chakula. Karibu aina zote za vyanzo vya chakula vinavyo patikana katika nchi ya Israeli.

Habakkuk 3:18

Taarifa kwa ujumla:

Habakuki anamtukuza Yahwe.

furahia ... uwe na furaha

Maneno yote yanamaanisha "uwe na shangwe," lakini kama lugha yako ina neno maalumu kwaajili ya kufurahia baada ya kushinda vita, litumie hilo "shangilia sana" hapa

hufanya miguu yangu kama kulungu; huniongoza mahali pangu pa juu

Miguu kama ya kulungu ingempa Habakuki uwezo kupanda ulioinuka mwamba majabari. Maneno "mahali pa juu" linarejerea mahali pa nje kufikiwa na hatari. Yeye anasema Mungu anampa yeye uwezo wa kutafuta mahali pa usalama.