Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Zephaniah 1

Zephaniah 1:1

neno la Yahweh lililokuja

"neno ambalo Yahweh Mungu alilisema"

Nitaangamiza kabisa kila kitu kutoka usoni mwa dunia...Nitamkata mwanadamu kutoka katika uso wa dunia

Haya ni makusudi kwa ukuzaji wa Yahweh kueleza hasira yake kwa dhambi za watu.

Kukata

Kuangamiza limezungumzwa kama kilikuwa kikikatwa kitu fulani kutoka mahali pake.

Zephaniah 1:4

Milcom

"Milcom" labda ni jina lingine kwa sanamu "Molech."

Zephaniah 1:7

Yahweh ameandaa sadaka na amewatenga wageni wake

Lugha hii inaonyesha mwisho wa mpango wa Mungu na jinsi anavyowatumia adui za watu wake kukamilisha makusudi yake.

Katika siku ilie

"Katika siku ya Yahweh"

kila mmoja amevaa mavazi ya kigeni

maneno haya yanaonyesha kwamba Waisraeli walivaa nguo sawa na za wageni kuonyesha huruma kwa mila zao na kwa ibada zao kwa miungu ya kigeni.

Katika siku ile

"Katika siku ya Yahweh"

Zephaniah 1:10

Tamko la Yahweh

"Yahweh ametamka nini" au "Nini Yahweh amesema kwa makini"

Lango la Samaki

Lango la Samaki lilikuwa mojawapo la malango ukutani mwa mji.

Kuomboleza kutoka kwenye Wilaya ya Pili

"Kuomboleza kwa sauti kubwa kutoka kwenye Wilaya ya Pili." Wilaya Pili ilikuwa karibu sehemu ya Yerusalemu.

kutoka milimani

Hii inahusu milima inayozunguka Yesusalemu. "kutoka milima inayozunguka Yerusamu."

kwa wafanyabiashara wote watakuwa wameharibiwa; wale wote wanaopima fedha watakuwa wamekatiliwa mbali

"kwa wale ambao hununua na kuuza bidhaa, wafanyabiashara, watakuwa wameuwawa."

Zephaniah 1:12

Nitaichungua Yerusalemu kwa taa

Hakuna hata mmoja atakayeweza kujificha kutoka kwa Mungu.

makazi kwenye mvinyo yao

Watajisikia salama kutoka kwenye shida

na kusema moyoni mwao

Watasema kwa uhakika

Zephaniah 1:14

karibu, karibu na inaharakisha haraka

Marudio ya neno "karibu," pamoja na maneno "inaharakisha haraka" inasisitiza kwamba siku wakati Yahweh anahukumu watu haraka itatokea. "karibu na itakuwa hapa haraka."

Siku hiyo itakuwa siku ya ghadhabu ... buruji

Kauli hii ni kusisitiza jinsi hukumu ya Mungu itakavyokuwa ya kutisha. Namba nyingi za hotuba zinaongezeka na kuonyesha uharibifu wa asili ya hukumu hii ya mwisho ya Mungu. Inajenga mkazo.

siku ya shida na uchungu

Neno "shida" na "uchungu" inamaanisha kuhusu kitu kilicho sawa na kusisitiza ukali wa shida za watu.

siku ya dhoruba na uharibifu

Hapa neno "dhoruba" inahusu hukunu ya Mungu. Neno "uharibifu" inaelezea madhara ya hukumu ile. "siku ya inayoharibiwa na dhoriuba" au siku ya kuharibiwa na hukumu." (na

siku ya giza na viza

Neno "giza" na "viza" linashiriki maana sawa na kusisitiza kiwango giza. Maneno yote yanalejea kwenye wakati wa maafa au hukumu ya Mungu. "Siku ambayo imejaa giza." au "siku ya hukumu ya kutisha."

siku ya mawingu na giza nene

maneno haya yanamaanisha kitu kilicho sawa kama, na linaongezezea wazo la maneno yaliyotangulia. kama maneno haya, yote "mawingu" na "giza nene" inarejea kwenye hukumu ya Mungu. "siku iliyojaa dhoruba lenye mawiingu yenye giza." (na

siku ya panda na kengele

Maneno "panda" na "kengele" kimsingi yanamaananisha kitu kilicho sawa hapa. Yote yanamaanisha kuita askari kujiandaa kwa vita. "siku wakati watu watakapotoa sauti ya kengele ya vita."

mada ni miji na buruji ndefu

Misemo hii miwili yote inarejea kwenye nguvu ya kijeshi inayoshikilia. " mada ni miji mizuri."

Zephaniah 1:17

tembea kama wanaume vipofu ... waliomwagwa kama vumbi ... sehemu zao za ndani kama samadi

misemo hii mitatu inaashiria ulinganifu kuonyesha nini vilicho nacho kikawaida.

moto wa wivu wake

Hii inahusu nguvu ya hasira ya Yahweh.

Zephaniah 2

Zephaniah 2:1

Mkutano wa hadhara ninyi wenyewe pamoja na kusanyikeni

Misemo hii miwili ina maana ya kitu sawa. Pamoja vinaimarisha amri kwa watu kukusanyika pamoja kwa ajili ya kutubu dhambi zao. "kusanyikeni ninyi wenyewe pamoja."

taifa lisilokuwa na aibu

Taifa halina pole kwa dhambi zake.

siku hiyo inapita kama makapi

Makapi hayamaanishi sehemu ya kilichopandwa kuwa kilitupwa mbali na hivyo siku hii itapita haraka.

kabla hasira kali ya ghadhabu ya Yahweh kuja juu yako, kabla ya siku ya ghadhabu ya Yahweh kuja juu yako

Mtume anarudia msemo uleule karibu hasa ili kusisitiza jinsi hukumu ya Yahweh ilivyo ya kutisha itakavyokuwa na uharaka ambao watu lazima watubu.

Ghadhabu ya Yahweh

Hili linasimama kwa dhamira Mungu kuhukumu.

Zephaniah 2:4

Watamtoa nje Ashdod wakati wa mchana, na watamng'oa Ekron!

Watu kwa haraka watakuwepo na kabisa wataondolewa kutoka miji hii.

Mpaka hakuna mwenyeji atakayebakia

"Mpaka hakuna hata mmoja atakayekuwa pale"

Zephaniah 2:6

Hivyo pwani itakuwa ... kalamu za kondoo

Sehemu ya msitari huu maana yake haiko wazi na imetafsiriwa kwa njia tofauti kwa matoleo ya kisasa

Kalamu za kondoo

Kalamu ya kondoo ni sehemu ndogo iliyozungushiwa uzio kuweka kondoo pamoja.

kulala chini

inamaanisha kulala kitandani

Zephaniah 2:8

tamko la Yahweh wa majeshi

"Yahweh wa majeshi ametamka nini" au "Yahweh wa majeshi amesema ameweka nini"

Zephaniah 2:10

fahari, kiburi, kiburi kilichojaa

Swala, "fahari" na "kiburi kilichojaa" linarejea kwa mtu anayefikiria kwa juu zaidi yeye mwenyewe, na hasa, anafikiria kwamba yeye ni bora kuliko watu wengine.

  • Mtu mwenye fahari mara nyingi hakubali makosa yake* Yeye siyo mnyenyekevu.
  • Kiburi kinaweza kusababisha kumwasi Mungu kwa njia zingine.
  • Swala "fahari" na "kiburi" vinaweza pia kutumika kwa maana chanya, kama vile kuwa "fahari ya" ambacho yoyote yule atakuwa amefanikiwa na kuwa "fahari ya" watoto wako* Elezo hili, "kuwa na kiburi katika kazi yako" inamaanisha kutafuta furaha unapofanya kazi yako vizuri.
  • Mtu yeyote anaweza kuwa na fahari kwa alichokifanya pasipo kuwa na kiburi kuhusu jambo hilo* Lugha zingine zina maneno tofauti kwa maana hizi mbili tofauti za "kiburi."
  • Swala hili "kiburi" mara nyingi ni hasi, ikiwa na maana ya "kiburi" au "kujivuna" au "umuhimu wa mtu binafsi."

dharau, kejeli, mzaha katika

Swala hili "dharau," "kejeli" na "mzaha katika" yote yanahusu kumfanya mtu kuwa na furaha, hasa katika njia ya kikatili.

  • Kudharau mara nyingi inahusisha kuiga maneno ya watu au vitendo kwa dhamira ya kuwadhihaki au kuwadharau.
  • Askari wa Kirumi walimdharau au walimkejeli Yesu walipoweka vazi juu yake na kujifanya kumheshimu kama mfalme.
  • Kundi la watu vijana lilimkejeli au kuonyesha mzaka kwa Elisha wakati walipomwita jina, wakifurahia kipara cha kichwa chake.
  • Suala hili "Mzaha katika" linaweza pia kuhusika kukejeli wazo ambalo lisilofikirika kuaminiwa au muhimu.

hofu, woga, hofu ya Yahweh

  • Suala hili "hofu" na "woga" linahusika na hisia mbaya kwa mtu alizonazo wakati kuna tishio la madhara kwake mwenyewe au kwa wengine.
  • Suala hili "hofu" pia linaweza kuhusika na heshima ya kina na hofu kwa mtu aliye na mamlaka.
  • Neno hili "hofu ya Yahweh," na linahusiana na suala "hofu ya Mungu" na "hofu ya Bwana," linahusika na kumheshimu Mungu kwa kina na kuonyesha heshima kwa kumtii yeye* Hofu hii imepewa motisha kwa kujua kwamba Mungu ni mtakatifu na huchukia dhambi.
  • Biblia inafundisha kwamba mtu anayemwogopa Yahweh atakuwa mwenye busara.

Mapendekezo ya tafsiri

  • Inategemea na mazingira, "kuwa na hofu" inaweza kutafsiriwa kama "kuwa na woga" au "heshima ya kina" au"kustahi" au kuwa na hofu ya."
  • Suala hili "woga" linaweza kutafsiriwa kama "hofu" au "kuogopa" au "waoga."
  • Hukumu hii, "Hofu ya Mungu huanguka juu ya wote" inaweza kutafsiriwa kama, "Ghafla wote waliona hofu ya kina kutoa heshima kwa Mungu" au "Ghafla, wote waliona mshangao sana na walimheshimu Mungu kwa kina" au "Kisha Haki, wote waliona woga kwa Mungu

mungu wa uongo, mungu wa kigeni, mungu, mungu wa kike

Mungu wa uongo ni kitu ambacho watu hukiabudu badala ya Mungu mmoja wa kweli* Suala hili "mungu wa kike" linahusika hasa kwa mungu wa uongo wa jinsia ya kike

  • Hawa miungu wa uongo au miungu wa kike hawakuwepo* Yahweh ni Mungu pekee.
  • Watu wakati mwingine hufanya vitu kuwa sanamu kuabudu kama alama ya miungu yao ya uongo.
  • Katika Biblia, watu wa Mungu mara kwa mara hugeuka kutoka kumtii yeye ili kuabudu miungu ya uongo.
  • Mapepo mara nyingi hudanganya watu katika kuamini kwamba miungu ya uongo na sanamu wanayoiabudu ina nguvu.
  • Baal, Dagon, na Molech walikuwa watatu wa miungu mingi ya uongo ambayo waliiabudu watu katika nyakati za Biblia.
  • Asherah na Artemis (Diana) walikuwa miungu wawili wa kike ambayo watu wa kale waliiabudu.

nchi, kidunia

Suala hili "nchi" linahusika na ulimwengu ambao mwanadamu alikuwa akiishi juu yake, pamoja na wanateolojia wote wa uhai.

  • "Dunia" pia inahusisha ardhi au udongo ambao hufunika nchi.
  • Suala hili mara nyingi lilitumika kimafumbo kuhusisha watu ambao huishi juu ya nchi.
  • Maneno, "basi nchi na ifurahi" na "Ataihukumu nchi" yote ni mifano inayotumiwa kwa mafumbo kwa suala hili.
  • Suala hili "kidunia" mara nyingi linahusisha vitu vya kimwili vinavyotofautiana vitu vya kiroho.

Mapendekezo ya tafsiri

  • Suala hili linaweza kutafsiriwa kwa neno au maneno ambayo ni ya lugha ya asili au karibu na lugha ya kimataifa kutumia kuhusisha sayari ya nchi ambayo juu yake tunaishi.
  • Inategemea na utamaduni, "nchi" inaweza kutafsiriwa pia kama, "ulimwengu" au" nchi" au "uchafu" au "udongo."
  • Wakati ilipotumika kimafumbo, "nchi" inaweza kutafsiriwa kama, "watu juu ya nchi" au "watu huishi juu ya nchi" au "kila kitu juu ya nchi."
  • Njia za kutafsiri "kidunia" inaweza kuhusisha, "kimwili" au "vitu vya nchi" au "vinavyoonekana."

ibada

"Kuabudu" maana yake ni heshima, sifa na kumtii mtu fulani, hasa Mungu.

  • Suala hili mara nyingi linamaana sawasawa, "kuinama chini" au "kujitoa binafsi" kujinyenyekesha kwa heshima ya mwingine.
  • Tunamwabudu Mungu wakati tunapomtumikia na kumheshimu, kwa kumsifu yeye na kumtii yeye.
  • Wakati Waisraeli walipomwabudu Mungu, mara nyingi ilihusisha kutoa sadaka za wanyama juu ya madahabahu.
  • Watu wengine huabudu miungu.

Mapendekezo ya tafsiri

Suala hili "ibada" linaweza kutafsiriwa kama "kuinama chini kwa" au "heshima na kutumika" au "heshima na kutii."

  • Katika mazingira mengine, inaweza pia kutafsiriwa kama, "sifa za unyenyekevu" au "kutoa heshima na sifa."

Zephaniah 2:12

juu ya nguzo zake

Wakati majengo yalipoharibiwa na kuanguka chini, nguzo zilitumika kwa kupamba na msaada mara kwa mara ulibakia umesimama.

mihimili

mihimili ni mirefu na vipande vinene vya mti ambavyo vilitumika kuweka jengo imara.

Zephaniah 2:15

kuzomea na kuitingisha ngumi yake

Kuzomea ni sauti ya ukali. Maneno haya yanaonyesha hasira iliyokithiri ya watu walioelekea Ninawi.

Zephaniah 3

Zephaniah 3:1

Hakuisikiliza sauti ya Mungu

Watu wa Yerusalemu hawakutii ambacho Mungu alikuwa nacho kwa mitume wake chakuwafundisha.

na hawatamkaribia Mungu wao

Watu hawakutamani kumwabudu na kumtii Mungu.

Zephaniah 3:3

Wakuu wao ni simba waungurumao katikati yao

"Viongozi wa Yerusalemu ni wenye vurugu"

Majaji wao ni mbwa mwitu wa jioni wasiobakiza chochote ambacho kitakuwa kimetafunwa mpaka asubuhi

"Majaji wao ni watu waovu ambao huchukua vitu ambavyo ni mali za wengine." Hii pia ni mfano.

Manabii wao ni wadhulumaji na wanaume wahaini."

"Manabii wao siowatii na wanaume wasio waaminifu."

Zephaniah 3:5

Haitafichika nuruni

"haki yake imeonyeshwa wazi kwa wote."

Zephaniah 3:6

Nimeifanya mitaa yao magofu, hivyo hakuna atakayepita juu yao. Miji yao imeharibiwa hivyo hakuna mwanaume atakayekaa humo

Yahweh anaelezea wazo lililo sawa kwa njia mbili tofauti ili kusisitiza ukamilifu wa uharibifu wa miji.

Zephaniah 3:8

Tamko la Yahweh

Hii inamaanisha Yahweh amesema kwa makini.

Inuka kwa waathirika

"Inuka kuangamiza waathirika"

kuyakusanya mataifa, kuzikusanya falme

Maneno haya mawili yanamaanisha kitu sawa na kusisitiza kwamba Yahweh atayahukumu mataifa yote.

hasira yangu, ghadhabu yangu kali yote

Maneno "hasira" na "ghadhabu kali" kimsingi ina maana sawa na inasisitiza kiwango cha hasira ya Yahweh. "hasira yangu kali."

hivyo nchi yote itakuwa imemezwa kwa moto wa hasira yangu

Maneno haya yanaweza kuelezewa kwa mfumo wa kitendo. "kwa hiyo moto wa hasira yangu utameza nchi yote."

kuteketezwa kwa moto wa hasira yangu

Hasira hapa imesemwa kama kutakuwa na moto ambao utateketeza kitu fulani.

Zephaniah 3:9

Nitawapa midomo safi watu

Hii ni njia nyingine ya kusema kwamba Mungu atasababisha watu wake kusema ambacho ni haki.

nitumikieni mimi mkisimama bega kwa bega

Watu wataunganishwa kwa hamu zao kumtumikia Mungu, kama watu wameunganishwa kimwili watakaposimama pamoja kwa mabega yao yakigusana kila mmoja.

Zephaniah 3:12

hakuna ulimi wa udanganyifu utakaoonekana mdomoni mwao

"hakuna hata mmoja atakayeonekana na ulimi wa udanganyifu mdomoni mwake" au "hawatasema vitu vya udanganyifu."

watafunga na kulala chini

Yahweh husema kwa watu wa israeli kama wao ni kundi la kondoo wanaofunga na kupumzika kwa usalama.

Zephaniah 3:14

binti Sayuni

"Hii inamaanisha watu wote wa Yerusalemu.

Usiiache mikono yako ilegee

Hii inamaanisha usijisikie dhaifu au mnyonge unavyokuwa kama mikono yako itakuwa dhaifu kimwili.

Zephaniah 3:17

hodari, nguvu

Masuala haya "hodari" na "nguvu" hurejea kuwa na nguvu kubwa au uwezo. . Mara nyingi neno "nguvu" ni neno lingine kwa "nguvu."Tunapozungumza kuhusu Mungu, inaweza kumaanisha "Uwezo." . Maneno, "wanaume wenye nguvu" mara kwa mara inahusu wanaume ambao ni wajasiri na wanaoshinda vita. Bendi ya Daudi ya wanaume waaminifu iliyomsaidia kumlinda na kumtetea mara kwa mara ilikuwa inaitwa "wanaume hodari."

Zephaniah 3:19

Nitamwokoa kilema na kumkusanya aliyefukuzwa

Hii inaonekana kurejea kwa kilema na kondoo aliyefukuzwa, ambaye anatumika kwa picha ya Waisraeli walioteseka utumwani.

Nitawatengeneza wao kama sifa

Wazo zima hapa ni, "Nitawatengeneza wao kuwa vitu vya kusifiwa," hiyo ni, "Nitawatengeneza wao kusifiwa kwa wengine."

Katika wakati ule nitakuongoza; katika wakati ule nitakukusanya pamoja

Misitari hii miwili kimsingi ina maana ya kitu kilichosawa na kuashiria kwamba Yahweh atawaleta nyuma watu uhamishoni katika nchi yao. "Katika wakati ule nitakukusanya pamoja na kukuongoza nyumbani."