Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa injili ya Marko

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha Marko

  1. Utangulizi (1:1-13)

  2. Huduma ya Yesu huko Galilaya

    • Huduma ya awali (1:14-3:6)
    • Yesu anakuwa maarufu zaidi kati ya watu (3:7-5:43)
    • Kuondoka Galilaya na kurudi (6:1-8:26)
  3. Kuelekea Yerusalemu, nyakati mara nyingi ambapo Yesu anatabiri kifo chake mwenyewe; wanafunzi wanakosa kuelewa na Yesu anawafundisha jinsi itakuwa vigumu kumfuata (8:27-10:52)

  4. Siku za mwisho za huduma na maandalizi ya migogoro ya mwisho huko Yerusalemu (11:1-13-13:37)

  5. Kifo cha Kristo na kaburi tupu (14:1-16:8)

Je, kitabu cha Marko kinahusu nini?

Injili ya Marko ni moja ya vitabu vinne katika Agano Jipya ambavyo huelezea baadhi ya maisha ya Yesu Kristo. Waandishi wa Injili waliandika juu ya mambo mbalimbali kuonyesha kuwa Yesu alikuwa nani na ni nini alichofanya. Marko aliandika mengi juu ya jinsi Yesu aliteseka na kufa msalabani. Alifanya hivyo ili kuwatia moyo wasomaji wake ambao walikuwa wakiteswa. Marko pia alielezea desturi za Wayahudi na maneno mengine ya Kiaramu. Hii inaweza kuonyesha kwamba Marko alitarajia wengi wa wasomaji wake wa kwanza kuwa kuwa watu wa mataifa.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake asilia, "Injili ya Marko" au "Injili Kulingana na Marko." Wanaweza pia kuchagua kichwa ambacho kinaweza kuwa wazi, kama vile "Habari Njema Kuhusu Yesu ambayo Marko Aliandika." (Angalia: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Nani aliandika Kitabu cha Marko?

Kitabo hakitupatia jina la mwandishi. Hata hivyo, tangu wakati wa Kikristo wa kwanza, Wakristo wengi wamefikiri kwamba mwandishi alikuwa Marko. Marko pia alijulikana kama Yohana Marko. Alikuwa rafiki wa karibu wa Petro. Marko huenda hakushuhudia kile Yesu alichosema na kufanya. Lakini wasomi wengi wanadhani kwamba Marko aliandika katika injili yake kile ambacho Petro alimwambia kuhusu Yesu.

Sehemu ya 2: Mawazo muhimu za Kidini na Kitamaduni

Je, ni njia zipi ambazo Yesu alitumia njia gani kwa kufundisha?

Watu walimwona Yesu kama rabi. Rabi ni mwalimu wa sheria ya Mungu. Yesu alifundisha kwa njia sawa na walimu wengine wa kidini huko Israeli. Alikuwa na wanafunzi ambao walimfuata kila mahali alipoenda. Wanafunzi hawa waliitwa wanafunzi. Mara nyingi aliwaambia mifano. Mifano ni hadithi zinazofundisha masomo ya maadili. (Angalia: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#disciple na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#parable)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Je, vitabo vinavyoitwa sinoptiki ni vipi vya Injili ni vipi?

Vitabu vya Mathayo, Marko na Luka huitwa Injili za sinoptiki kwa sababu vina vifungu vingi vinavyofanana. Neno "synoptic" linamaanisha "kuona kwa pamoja."

Maandiko husemekana kuwa "sawa" wakati ambapo injili mbili au tatu zinafanana au zinakaribia kufanana. Wakati wa kutafsiri vifungu sambamba, wafasiri wanapaswa kutumia maneno sawa na kuyafananisha iwezekanavyo.

Je, kwa nini Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu"?

Katika Injili, Yesu anajiita mwenyewe "Mwana wa Binadamu." Ni kumbukumbu ya Danieli 7:13-14. Katika kifungu hiki kuna mtu anayeelezewa kuwa "Mwana wa binadamu." Hiyo ina maana kwamba mtu huyo alifanana na mwanadamu. Mungu alitoa mamlaka kwa mwana wa binadamu kutawala mataifa milele. Na watu wote watamwabudu milele.

Wayahudi wa wakati wa Yesu hawakutumia "Mwana wa Binadamu" kama jina la mtu yeyote. Kwa hiyo, Yesu aliitumia kwa ajili yake mwenyewe ili kuwasaidia kuelewa yeye alikuwa nani kweli. (Angalia: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sonofman)

Kutafsiri jina "Mwana wa Binadamu" kunaweza kuwa vigumu kwa lugha nyingi. Huenda wasomaji hawaelewi tafsiri halisi. Watafsiri pia wanaweza kutumia jina mbadala, kama vile "Yule aliye Mtu." Inaweza pia kusaidia wanapoingiza maelezo ya chini ili kulielezea.

Je, kwa nini Marko mara nyingi hutumia maneno ambayo yanaashiria muda mfupi?

Injili ya Marko inatumia neno "mara moja" mara arobaini na mbili. Marko hufanya hivyo ili kufanya matukio kuwa ya kusisimua na ya wazi. Inamtoa msomaji haraka kutoka tukio moja hadi linalofuata.

Je, ni yapi masuala makuu katika maandishi ya Kitabu cha Marko?

Aya zifuatazo zinapatikana katika matoleo ya kale ya Biblia lakini hazijajumuishwa katika matoleo ya kisasa zaidi. Watafsiri wanashauriwa kutojumuisha aya hizi. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri, kuna matoleo ya zamani ya Biblia ambayo yanajumuisha moja au zaidi ya mistari hii, watafsiri wanaweza kuijumuisha. Ikiwa imejumuishwa, inapaswa kuwekwa ndani ya kifungo cha mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yao haikuwa Injili ya Marko.

  • "Mtu yeyote aliye na masikio ya kusikia, na asikie." (7:16)
  • "ambapo mdudu wao hafi na moto hauzimiki" (9:44)
  • "ambapo mdudu wao hafi na moto hauzimiki" (9:46)
  • "Na maandiko yalitimizwa yaliyonena kwamba, 'Alihesabiwa pamoja na watu waovu'" (15:28)

Kifungu kinachofuata hakipatikani katika maandiko ya awali. Biblia nyingi zinajumuisha kifungu hiki, lakini Biblia za kisasa zimekiweka katika mabango ([]) au zinaonyesha kwa namna fulani kwamba kifungu hiki huenda si mfano ya kitabo cha asili cha Marko ya Injili ya Marko. Watafsiri wanashauriwa kufanya jambo sawa na matoleo ya kisasa ya Biblia.

  • "Mwanzoni mwa siku ya kwanza ya juma, baada ya kufufuka, alionekana kwanza kwa Maria Magdalene, ambaye alikuwa amemtoa pepo saba. Akaenda akawaambia wale waliokuwa pamoja naye, walipokuwa wanaomboleza na kulia. Walisikia kuwa alikuwa hai na kwamba yeye alikuwa amemwona, lakini hawakuamini. Baada ya hayo, Yesu alionekana kwa njia tofauti kwa wawili kati yao, walipokuwa wakitembea. Wakaenda kuwaambia wanafunzi wengine , lakini hawakuamini. Baadaye Yesu aliwatokea wale kumi na moja walipokuwa wameketi mezani, na akawakemea kwa kutoamini na ugumu wa moyo, kwa sababu hawakuamini wale waliomwona baada ya kufufuka kutoka kwa wafu. Akawaambia, 'Nendeni ulimwenguni kote, mkahubiri Habari Njema kwa viumbe vyote, yeye anayeamini na kubatizwa ataokolewa, na asiyeamini atahukumiwa. Ishara hizi zitawaongoza wale wanaoamini: Kwa jina langu watawatoa pepo. Watazungumza kwa lugha mpya. Watachukua nyoka kwa mikono yao, na ikiwa watakunywa kitu chochote cha mauti, hakitawaumiza. Wao wataweka mikono juu ya wagonjwWanafunzia, nao watapona.' Baada ya Bwana kuwazungumzia, alipelekwa mbinguni na akaketi kwenye mkono wa kuume wa Mungu. waliondoka na kuhubiri kila mahali, wakati Bwana alifanya kazi pamoja nao na kuthibitisha neno kwa ishara zilizowaongoza."(16:9-20)

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

Mark 1

Marko 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi kwa upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hii kwa mashairi katika 1:2-3, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

"Unaweza kunifanya kuwa safi"

Ukoma ulikuwa ugonjwa wa ngozi ambao ulimfanya mtu asiwe msafi na asiweze kumwabudu Mungu vizuri. Yesu anaweza kufanya watu kuwa "safi" au wenye afya kimwili au pia kuwa "safi" au wenye haki na Mungu kiroho . (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#clean)

"Ufalme wa Mungu umekaribia"

Wasomi wanajadiliana ikiwa "Ufalme wa Mungu" ulikuwapo wakati huu au bado unakuja. Tafsiri za Kiingereza mara nyingi hutumia maneno "karibu," lakini hii inaweza kusababisha ugumu kwa watafsiri. Matoleo mengine hutumia "unakuja" na "umekaribia."

| >>

Mark 1:1

Sentensi ya unganishi

Kitabu cha Marko huanza na nabii Isaya kusema ujio wa Yohana mbatizaji aliye mbatiza Yesu.

Maelezo ya jumla

Mwandishi wa Marko, pia aliyeitwa Yohana Marko, ambaye ni mwana wa mmoja wa wanawake aliyeitwa Mariam aliyetajwa katika injili nne. Pia ni mpwa wa Barinaba.

Mwana wa Mungu

Hii ni jina la muhimu sana kwa Yesu.

Mbele ya uso wako

Hii ni lugha inayomaanisha "mbele yako"

Uso wako... njia yako

Hapa neno "yako" urejea kwa Yesu na liko katika umoja. Pindi unapotafasiri, tumia nomino "yako" kwa sababu ni maneno ya mtu mwingine nabii, na hakutumia jina la Yesu.

Yule

Hii urejee kwa mtumwa.

ataandaa njia yako

Kufanya hivi humaanisha kuandaa watu kwa ajili ya ujio wa Bwana. AT:"nitaandaa watu kwa ajili ya ujio wako"

Sauti ya yule aitae toka jangwani.

Hii inaweza kuelezwa kama sentesi. AT: "Sauti ya yule aitae toka jangwani imesikiwa" au " Wanasikia sauti ya mtu anaita toka jangwani"

Andaa njia ya Bwana... yanyoshe mapito yake

Haya maneno humaanisha kitu kile kile.

Ifanye tayari njia ya Bwana

"Iweke njia tayari ya Bwana." Kufanya hivi humaanisha kuwa tayari kusikia ujumbe wa Bwana unapokuja. Watu hufanya hivi kwa kutubu dhambi zao. AT: "Jiandae kusikia ujumbe wa Bwana unapokuja" au " Tubu na uwe tayari kwa ajili ya Bwana anapokuja"

Mark 1:4

Maelezo ya jumla

Katika mistari hii maneno "yeye" mwanaume, "yule" mwanaume, na "ake" mwanaume urejee kwa Yohana.

Yohana alikuja

Hakikisha wasomaji wako wanaelewa kwamba Yohana alikuwa mtumwa aliyekuwa amenenwa na nabii Isaya katika mistari ya awali.

Nchi yote ya Yuda na watu wote Yerusalemu

Maneno "yote" na "wote" hapa ni maneno ya zaidi hutumiwa kusisitiza kwamba kulikuwa na idadi kubwa ya watu. AT: "Watu wengi kutoka Yuda na Yerusalemu"

Walibatizwa na yeye...kukiri dhambi zao

Haya matendo mawili yalitokewa wakati ule ule. Watu walibatizwa kwa sababu walitubu dhambi zao. AT: "Pindi walipotubu dhambi zao, Yohana aliwabatiza katika mto wa Yordani"

Mark 1:7

Alihubiri

Yohana alihubiri

Sina hadhi hata ya kuinama chini na kufungua kamba za viatu vyake

Yohana anajilinganisha mwenyewe kama mtumishi kuonyesha jinsi gani Yesu ni mkuu. AT:"Sina hadhi na hata kufanya jukumu la chini la kumvulisha viatu vyake.

Ukanda wa ndara zake

Wakati Yesu alipokuwa hai, watu walivaa ndara zilizotengenezwa kwa ngozi na kufungwa kwa ukanda wa ngozi.

Kuinama chini

ni kupinda kwa kuelekea chini

lakini atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu

Ubatizo wa kiroho umelinganishwa kwa ubatizo wa maji. Ubatizo wa kiroho huwaleta watu katika mahusiano na Roho Mtakatifu kama ilivyo katika ubatizo wa maji unamleta mtu kuwa uhusiano na maji

Mark 1:9

Wewe ni mwanangu mpendwa

Baba, Mwana, na Roho wote wanajidhihirisha pamoja, kwa wakati mmoja.

alibatizwa na Yohana

Hii inaweza kutajwa katika hali tendaji. AT: " Yohana alimbatiza yeye"

Roho anamshukia kama njiwa

Maana zinazoweza kuwa sahihi ni: 1)huu ni mfanano, na Roho alimshukia Yesu kama ndege anavyoshuka toka mbinguni kuelekea ardhi au 2) Roho kiuhalisia alionekana kama njiwa alivyoshuka juu ya Yesu.

sauti ilisikika toka mbinguni

Hii inawakilisha Mungu anazungumza. Wakati mwingine watu hukwepa kurejea moja kwa moja kwa Mungu kwa sababu wana mheshimu yeye. AT: "Mungu alizungumza toka mbinguni."

mwana mpendwa

Ni neno la cheo kwa Yesu. Baba anamwita Yesu "mwana" kwa sababu ya upendo wa milele kwake.

Mark 1:12

Sentensi unganishi

Baada ya ubatizo wa Yesu, anakuwa nyikani kwa siku arobaini na badae kwenda Galilaya kufundisha na kuita wanafunzi wake.

alimlazimisha kwenda nyikani

"alimwongoza Yesu nje kwa shinikizo"

Alikuwako nyikani

"Alikaa nyikani"

siku arobaini

"muda wa siku arobaini"

Alikuwa pamoja na

"alikuwa miongoni mwa"

Mark 1:14

baada ya Yohana kukamatwa

"Baada ya Yohana kuwa ametiwa gerezani" Hii inaweza kutajwa katika kauli tendaji. AT: " baada ya kumshika Yohana."

alitangaza

"Alihubiri"

Wakati umetimia

"Huu sasa ni wakati"

Mark 1:16

Alimwona Simoni na Andrea

"Yesu alimuona Simoni na Andrea"

kutupa nyavu baharini

Maana pana ya sentensi hii inaweza kuwekwa wazi. AT: "kutandaza wavu katika maji kushika samaki"

Njoo, nifuate mimi

"Nifuate mimi" au "njoo nami"

Nitawafanya kuwa wavuvi wa watu

Huu mfano humaanisha Simoni na Andrea watawafundisha watu ujumbe wa kweli wa Mungu, ili wengine wamfuate Yesu. AT: "Nitakufundisha namna ya kuwapata watu"

Mark 1:19

ndani ya mtumbwi

"ndani ya mtumbwi wao"

kutayarisha nyavu

"kushona nyavu"

aliwaita wao

Inaweza kuwa msaada kusema wazi kwanini Yesu alimwita Yakobo na Yohana. AT: "aliwaita wao waje naye"

watumishi waliokodiwa

"watumishi ambao walifanya kazi kwa ajili yao"

walimfuata

"Yakobo na Yohana walikwenda pamoja na Yesu"

Mark 1:21

Sentensi unganishi

Katika mji wa Kaperinaumu siku ya Sabato Yesu anafundisha katika sinagogi. Anaondoa pepo kwa mtu, ambayo inashanganza watu walio maeneo ya karibu ya Galilaya.

alikuja Kaperinaumu

"alifika Kaperinaumu"

kama mtu aliye na mamlaka na wala siyo mwandishi

Kuna maneno yaliyo achwa katika sentensi hii ambayo yanaweza kuongozwa. AT: "kama mtu aliye na mamlaka alifundisha na siyo kama waandishi wafundishavyo"

Mark 1:23

Tuna nini cha kufanya na wewe, Yesu wa Nazareti?

Mapepo wanauliza swali wakimaanisha kuwa hakuna sababu ya Yesu kuwaingilia na wanatamani yeye aondoke. " Yesu wa Nazareti, tuache sisi peke yetu! Hakuna sababu ya wewe kutuingilia sisi."

Je! Umekuja kutuangamiza sisi?

Mapepo wanauliza swali kumsihi Yesu asiwadhuru. "Usi tuharibu sisi!"

alimtupa yeye chini

Hapa neno "yeye" lina rejea kwa mtu aliye pagawa na mapepo.

wakati analia kwa sauti kubwa

Pepo ndiye anayelia, wala siyo mtu.

Mark 1:27

waliulizana wao kwa wao, "Hiki ni nini? Mafundisho yaliyo na mamlaka?

Mwitikio wa watu unaweza kuandikwa na sentensi hizi badala ya maswali. "walisema wao kwa wao, "Hii ina shanganza! Anatoa mafundisho mapya, na huzungumza na mamlaka!"

Pia ana amru

Neno "yeye" ulerejea kwa Yesu.

Mark 1:29

Sentensi unganishi

Baada ya kumponya mtu aliye pagawa na pepo, Yesu alimponya mama mkwe wa Simoni pamoja na watu wengi wengine.

Sasa mama mkwe wa Simoni alikuwa amelala akiumwa na homa

mkwe alikuwa mgonjwa na homa. Neno "sasa" hutambulisha mama mkwe wa Simoni katika hadidhi na kutupa maelezo ya nyuma kuhusiana yeye.

wachache waliondoka

Inaweza kuonyeshwa waziwazi nani aliye mponya. "Yesu alimponya homa yake"

alianza kuwahudumia

Inamaamisha chakula kilitengwa. "Aliwahudumia chakua la vinywaji"

Mark 1:32

Sentensi unganishi

Hapa maneno "yeye" na "yeye" urejea kwa Yesu.

wote waliokuwa wagonjwa au kupagawa na mapepo

Hapa neno "wote" ni maelezo zaidi na linatumiwa kusisitiza idadi kubwa ya watu waliokuja. "wengi waliokuwa wagonjwa au kupagawa na mapepo."

Mji wote walikusanyika pamoja katika mlango

Neno "wote" linaelezea namba ya watu waliokuwa wakimtafuta Yesu. "Watu wengi kutoka mjini walikusanyika nje ya mlango"

Mark 1:35

Sentensi unganishi

Yesu anachukua muda kuomba katikati ya wakati wake wa kuponya watu. Badae anaenda mjini kupitia Galilaya kuhubiri, kuponya na kutoa mapepo.

Maelezo ya jumla

Hapa maneno "yeye" na "yeye" urejea kwa Yesu

Mahali pa faragha

"mahali ambapo anaweza kuwa peke yake"

Simoni na wale walikuwa naye

Hapa "yeye" urejee kwa Simoni. Pia, wale waliokuwa pamoja naye akiwemo Andrea, Yakobo, Yohana, na inawezekana watu wengine.

Kila mmoja anakutafuta wewe

Neno "kila mmoja" linafafanua namna watu wengi waliomtafuta Yesu. "Watu wengi wanakutafuta wewe"

Mark 1:38

Maelezo ya jumla

Hapa maneno "yeye" na "mimi" urejea kwa Yesu.

Twendeni mahali pengine

"Tunapaswa kwenda mahali pengine." Hapa Yesu anatumia neno "sisi" kurejea kwake, akiwemo Simoni, Andrea, Yakobo, na Yohana.

Alienda akipitia Galilaya yote

Neno "kupitia" linaelezea Yesu alikwenda maeneo mengi wakati wa huduma yake. "Alikwenda maeneo mengi ya Galilaya."

Mark 1:40

Mwenye ukoma alikuja kwake; alikuwa akimsihi wakati amepiga magoti na kumwambia

"Mwenye ukoma alikuja kwa Yesu; mwenye ukoma alikuwa akimsihi Yesu akiwa amepiga magoti chini. Mwenye ukoma alisema kwa Yesu"

Kama unataka, unaweza kunifanya safi

Kikundi cha maneno "kunifanya safi" kinaeleweka kutoka kwenye kikundi kingine cha maneno. "Kama unataka kunifanya safi, basi unaweza kunifanya safi."

uko tayari

"nataka" au "hamu"

unaweza kunifanya niwe safi

Nyakati za Biblia, mtu aliye kuwa na ugonjwa wa ngozi alihesabika siyo msafi mpaka pale ngozi ilipo ponywa na kubaki bila kuwa na maambukizi. "unaweza kuniponya"

Alisukumwa na huruma, Yesu

Hapa neno " kusukumwa" ni lugha inayo maanisha kuwa na hisia juu ya hitaji la mtu mwingine. "Kuwa na huruma kwa ajili yake, Yesu "au" Yesu alipatwa na huruma kwa ajili ya mtu.

Nina utayari

Inaweza kuwa msada kutaja kitu gani Yesu ana utayari kufanya"Ninatamani kukufanya uwe safi"

Mark 1:43

Maelezo ya jumla

Neno "yeye" ni limetumiwa kurejea kwa yule mkoma aliyeponywa na Yesu.

Uwe na uhakika kutosema chochote kwa yoyote.

"Uwe na uhakika kutosema chochote kwa yoyote"

jionyeshe mwenyewe kwa kuhani

Yesu alimwambia mtu kujionyesha mwenyewe kwa kuhani ili kuhani aweze kumuona ngozi yake kama kwamba ukoma wake umekwisha. Ilihitajika katika sheria ya Musa mtu kujionyesha kwa kuhani kama amekuwa safi.

jionyeshe mwenyewe

Neno "mwenyewe" linawakilisha ngozi ya mwenye ukoma. "jionyeshe ngozi yako"

ushuhuda kwao

Ni vizuri kutumia nomino "wao", kama inawezekana, katika lugha yako. Maana zinazowezekana ni 1) "ushuhuda kwa makuhani" 2) "ushuhuda kwa watu"

Mark 1:45

Lakini alienda

Neno "yeye" urejea kwa mtu aliyeponywa na Yesu.

mwambie kila mmoja...sambaza neno

vivumishi vya maneno haya mawili yana maana inayofanana na yanamwelezea yule mtu aliyewaambia watu wengi.

kila mmoja

Neno "kila mmoja" linafafanua, "Watu wengi aliokutana nao."

Yesu hakuweza tena kuingia mjini kwa uhuru

Hii ina maanisha kwamba makundi makubwa yalimzuia Yesu kuingia mjini kwa sababu makundi yalifanya ugumu kwake kutembea katika mji. "makundi yalimzuia Yesu kutembea kwa uhuru mjini."

mahali pa faraga

"mahali pa utulivu" au "mahali ambapo hakuna mtu aliye ishi"

kutoka kila mahali

Neno "kila mahali" linafafanua kuwa, "kutoka maeneo yote ya mkoa"

Mark 2

Marko 02 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Wenye dhambi"

Watu wa wakati wa Yesu walipozungumza juu ya "wenye dhambi," walikuwa wakiongea juu ya watu ambao hawakuitii sheria ya Musa na badala yake wakatenda dhambi kama kuiba au dhambi za ngono. Wakati Yesu alisema kwamba alikuja kuwaita "wenye dhambi," alimaanisha kwamba watu pekee wanaoamini kuwa wao ni wenye dhambi wanaweza kuwa wafuasi wake. Hii ni kweli hata kama wao sio wale ambao watu wengi wanafikiria kuwa "wenye dhambi." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

Kufunga na Karamu

Watu wangeweza kufunga, au kutokula chakula kwa muda mrefu, walipokuwa na huzuni au wakimwonyesha Mungu kwamba walijutia dhambi zao. Wakati walipokuwa na furaha, kama wakati wa harusi, wangekuwa na karamu, au mlo ambapo wangeweza kula chakula kikubwa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#fast)

Takwimu muhimu za hotuba katika sura hii

Maswali ya uhuishaji

Viongozi wa Kiyahudi walitumia maswali ya uhuishaji ili kuonyesha kwamba walikuwa wamekasirika kwa sababu ya kile Yesu alichosema na kufanya na kwamba hawakuamini kwamba alikuwa Mwana wa Mungu (Marko 2:7). Yesu aliyatumia kuonyesha viongozi wa Kiyahudi kwamba walikuwa wenye kiburi (Marko 2:25-26). (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion)

<< | >>

Mark 2:1

Sentensi unganishi

Baada ya kuhubiri na kuponya watu kote Galilaya, Yesu anarudi Kaperinaumu anako mponywa na kumsamehe dhambi mtu aliye pooza

Ilisikika kwamba alikuwa nyumbani

Hii inaweza kutajwa katika kauli tendaji. watu wa pale walisikia kwamba alikuwa katika nyumba ile ile.

wengi walikusanyika hapo

Hii inaweza kutajwa kama kauli tendaji. "kwa hiyo watu wengi walikusanyika" au "watu wengi walikuja nyumbani"

haikuwepo nafasi ya ziada

Hii inarejea hapakuwa na nafasi ndani ya nyumba. "haikuwepo nafasi tena kwa ajili yao mule ndani"

Mark 2:3

watu wanne walimbeba yeye

"wanne wao walimbeba yeye." Inawezekana kulikuwa na watu zaidi ya wanne ndani ya kundi waliomleta mtu kwa Yesu.

walimletea mtu aliyepooza

walimletea mtu asiyeweza kutembea wala kutumia mikono yake.

Walishindwa kumkaribia yeye

"walishindwa kukaribia pale Yesu alipokuwa Yesu"

waliondoa paa juu alipokuwa...kutoboa tundu ndani yake

Nyumba alizoishi Yesu zilikuwa na paa za wima zilizo tengenezwa kwa udongo na kufunikwa kwa vigaye. Hatua ya kutengeneza tundu juu ya paa inaweza kuelezwa zaidi kwa uwazi au kufanywa zaidi kwa ujumla ili kwamba iweze kueleweka katika lugha yako. "waliondoa vigaye sehemu ya paa juu alikokuwa Yesu. Na walipotoboa katika paa ya udongo "au" walipotengeneza tundu juu ya paa alipokuwa Yesu, na kisha walimshusha"

Mark 2:5

alipoiona imani yao.

"Akijua kwamba watu hao wana imani." Hii inaweza kumaanisha 1) kwamba ni wale watu waliokuwa wamembeba aliyepooza ndio waliokuwa na imani au 2) kwamba aliyepooza na watu wamembeba wote walikuwa na imani.

Mwana

Neno "mtoto" hapa linaonesha kwamba Yesu alimjali huyo mtu kama baba anavyomjali mwana.

dhambi zako zimesamehewa

Maana zinayowezekana 1) "Mungu amekwisha kukusamehe dhambi zako" (Taz 2:7) au 2) "Nimekusamehe dhambi zako."

walijihoji mioyoni mwao

Hapa "mioyo yao" ni mbadala wa mawazo ya watu. "walikuwa wanafikiri wao wenyewe"

Anawezaje mtu huyu kusema hivi?

Hili swali liliulizwa kuonyesha kwamba waandishi walitilia shaka uwezo wa Yesu kusamehe dhambi. "Mtu huyu hapaswi hivi!"

Nani anayeweza kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?

Swali hili liliulizwa kuonyesha kwamba waandishi walitia shaka kwamba Yesu ni Mungu. "Mungu peke yake ndiye anaweza kusamehe dhambi!"

Mark 2:8

katika roho yake

"ndani ya utu wa ndani" au"ndani yake"

walikuwa wakifiri miongoni mwao wenyewe

Waandishi walikuwa wakifiri kila mmoja nafsini mwake; walikuwa hawaongeleshani kila mmoja na mwenzake.

Kwa nini mnafikiri hivi mioyoni mwenu?

Yesu aliuliza swali hili kuwakemea waandishi kwa kutilia mashaka mamlaka yake. NI kama alitaka kusema kuwa, "Hampaswi kuonea shaka mamlaka yangu!"

hii iko ndani ya mioyo yenu

Neno "mioyo" linatumika mara kwa mara kurejea kwenye mawazo, hisia, matamanio, au mapenzi ya mtu

Lipi ni jepesi kusema kwa mtu aliyepooza... chukua kitanda, na utembee?

Yesu aliuliza swali hili kwa sababu waandishi waliamini kwamba mtu huo alikuwa amepooza kwa sababu ya dhambi zake na ikiwa dhambi za mtu huyo zingesahewa, angeweza kutembea. Kama Yesu alimponya mtu aliyepooza, waandishi walipaswa kukiri kwamba Yesu anaweza kusamehe dhambi. Sawa na kusema "Ni rahisi kumwambia mtu aliyepooza dhambi zako zimesamehewa!" [Hili ni swali lisihitaji jibu]

Mark 2:10

Lakini ili kwamba umjue

"Lakini ili kwamba umjue." Neno "wewe" urejea kwa waandishi na kundi.

kwamba Mwana wa Adamu ana mamlaka

Yesu ujirejea yeye mwenyewe kama "Mwana wa Adamu." "Kwamba mimi ni Mwana wa Adamu na nina mamlaka."

mbele ya kila mmoja

"wakati watu walipokuwa wakitazama"

Mark 2:13

Sentensi unganishi

Yesu anafundisha kundi kando ya bahari ya Galilaya, na anamwita Lawi kumfuata yeye.

ziwa

Hili ni bahari la Galilaya, ambayo linajulikana kama ziwa la Gennesareti.

mkutano ulikuja kwake

watu walikwenda pale alipokuwa

Lawi mwana wa Alfayo

Alfayo ni baba wa Lawi

Mark 2:15

Sentensi unganishi

Ni badae sasa kwa siku hiyo, na Yesu anakuwa katika nyumba ya Lawi kwa ajili ya chakula.

Nyumba ya Lawi

"nyumba ya Lawi"

watu wenye dhambi

Mafarisayo walitumia kikundi cha maneno "watu wenye dhambi" kurejea kwa watu walioshindwa kutunza sheria kama walivyo fikiri Mafarisayo wangefanya.

kwa kuwa kulikuwa na wengi na walimfuata

Maana zinazowezekana ni 1) "kulikuwa na watoza kodi wengi na watu waovu waliomfuata Yesu

kwa nini anakula na wakusanya kodi na watu wenye dhambi?

Waandishi na Mafarisayo waliuliza swali hili konesha kwamba walikataa ukarimu wa Yesu. "Hakupaswa kula na kunywa na wenye dhambi na watu wanaokusanya kodi."

Mark 2:17

Sentensi unganishi

Yesu aliitikia kwa kile walichokuwa wamesema waandishi kwa wanafunzi wake kuhusu kula na watoza kodi na watu wenye dhambi.

aliwaambia

aliwaambia waandishi

Watu walio na nguvu katika mwili hawamhitaji tabibu; ni wagonjwa pekee ndio wanamhitaji

Yesu aliwalinganisha wale wanajijua kuwa ni wenye dhambi na wale wale wanaojijua kuwa ni wagonjwa. "Watu wanaofikiri kuwa wao ni wenye haki hawahitaji msaada; ni wale tu wanaojijua kuwa ni wagonjwa ndio wanaohitaji msaada!

nguvu katika mwili

"afya"

Sikuja kuwaita watu wenye haki, lakini watu wenye dhambi

Yesu alitegemea kuwa wasikilizaji wake wangeelewa kwamba alikuja kwa wale wanaohitaji msaada. "Nilikuja kwa watu wanaojielewa kuwa ni wenye dhambi, siyo kwa watu wanaoamini kuwa wao ni wenye haki."

lakini watu wenye dhambi

Inaweza kuwa msaada kutaja kwamba hii inarejea kwa watu ambao Yesu aliwaita. "lakini nilikuja kuwaita watu wenye dhambi"

Mark 2:18

Sentensi unganishi

Yesu anasema mifano kuonyesha kwa nini wanafunzi wake hawakuweza kufunga pindi alipokuwa nao.

Mafarisayo walifunga...wanafunzi wa Mafarisayo

Haya maneno yanarejea kwa kundi lile lile la watu, lakini la pili liko bayana zaidi. Yote urejea kwa wanafunzi wa Mafarisayo, lakini hayalengi kwa viongozi wa Mafarisayo. "wanafunzi wa Mafarisayo walikuwa wakifunga... wanafunzi wa Mafarisayo"

baadhi ya watu

"baadhi ya watu." Ni vizuri kutofasiri kikundi cha maneno bila bayana hawa walikuwa watu akina nani. Kama katika lugha yako unapaswa kuwa bayana, maana zinazowezekana ni 1)hawa watu hawakuwa miongoni mwa wanafunzi wa Yohana au wanafunzi wa Mafarisayo au 2) hawa watu walikuwa miongoni mwa wanafunzi wa Yohana

Je waliohudhuria harusini wanaweza kufunga wawkati bwana harusi akiwa yuko bado pamoja nao?

Yesu aliuliza swali hili kulinganisha kati yake mwenyewe na wanafunzi wake na bwana harusi na marafiki wake.'' wanafunzi wangu husherekea kwa kuwa niko pamoja nao!''

Mark 2:20

bwana harusi atakapoondolewa

Yesu anajilinganisha mwenyewe na bwana harusi anapoongelea kuhusu kifo chake, ufufuo na kupaa kwake. Kama lugha yako inakulazimu kuchanganua mtendaji, fanya kwa ujumla kama iwezekanavyo. Kauli ya kutenda inachukua nafasi kama lugha yako haiwezi kutumia kauli ya kutendewa. "Watamwondoa bwana harusi" au bwana harusi ataondoka."

mbali nayo... wao watafunga

Neno "kwao" na "wao" urejea kwa washiriki wa harusi.

Hakuna mtu ashonaye kipande kipya cha nguo kwenye vazi kuukuu

Kushona kipande kipya cha nguo kwenye vazi kuukuu kitasababisha tundu kwenye vazi kuukuu kuwa baya zaidi kama kipande cha nguo mpya hakitabadilika. Vyote viwili, nguo mpya na vazi kuukuu vitapotea.

Hakuna mtu

"Hakuna yoyote." Kikundi cha maneno urejea kwa watu wote, wala siyo watu.

Mark 2:22

Hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu

Yesu analinganisha mafundisho yake na wanafunzi wake na divai mpya na viriba vipya. Mfano huu hujibu swali "Kwa nini wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi? Hapa "Hakuna mtu akabidhiye mafundisho mapya kwa wale waliozoea mafundisho ya zamani."

Divai mpya

"juice ya zabibu." Hii ina maana ya mvinyo ambayo haijaumuka bado. Kama zabibu hazijulikani katika eneo lako, tumia neno la jumla kwa matunda.

virriba vikuukuu

Hii inamaanisha viriba ambavyo vimetumika mara nyingi

viriba

Hii ilikuwa mifuko iliyotengenezwa kwa kutumia ngozi za wanyama. Pia inaweza kuitwa "mifuko ya divai" au "mifuko ya ngozi" (UDB)

divai itaweza kuvipasua viriba

Wakati divai mpya inapoumuka na kupanuka, inaweza kupasua na kutoka nje kwa sababu havitaweza tena kunyooka kwa nje.

kupotea

kuharibika

viriba vipya

"viriba vipya" au "mifuko mipya ya divai." Hii inarejea kwa viriba vipya ambavyo havijawahi kutumika.

Mark 2:23

Sentensi unganishi

Yesu anawapa Mafarisayo mfano kutoka katika maandiko kuonyesha kwanini wanafunzi hawakuwa sahihi kuchukua masuke ya ngano siku ya Sabato.

kuchukua masuke ya ngano...kufanya kitu ambacho siyo sawa kisheria katika siku ya Sabato

Kuchukua ngano katika mashamba ya wengine na kula haikuhesabiwa kuwa wizi. Swali lilikuwa kama ilikuwa sawa kufanya jambo kama hilo siku ya Sabato

kuchukua masuke ya ngano

Wanafunzi walichukua masuke ya ngano kuyala. Hii inaweza kuelezwa kwa maneno kuonyesha maana kamili. "chukua na kula masuke ya ngano"

masuke ya ngano

Hii ni sehemu nyeti ya zao la ngano, ambayo ni aina ya nyasi pana. Hushikiria ngano iliyokomaa au mbegu za mmea

Tazama, kwanini wanafanya kitu ambacho ni kinyume na sheria katika siku ya Sabato?

Mafarisayo wanamuuliza Yesu swali kumlaani. Hii inaweza kutofasiriwa kama sentensi. "Tazama! Wanavunja sheria ya kiyahudi kuhusu Sabato"

Tazama

"Uwe makini kusikiliza kile ninachotaka kukuambia"

Mark 2:25

Aliwambia

"Yesu aliwambia Mafarisayo"

Hamjasoma kile alichofanya Daudi pamoja naye? Jinsi alivyokwenda

Yesu alijua kwamba Waandishi na Mafarisayo walikuwa wamesoma simulizi. Aliwashutumu kwa kukuielewa kwa makusudi. Tafsiri mbadala: "Kumbukeni kile Daudi alichofanya...pamoja naye na jinsi alivyokwenda" au "Kama mnakumbuka kile Daudi...naye, mngejua kwamba alikwenda"

Hamkusoma kile alichofanya Daudi alipokuwa katika uhitaji na njaa-- yeye pamoja na watu waliokuwa pamoja naye

Hii inaweza kusema kama amri. "Kumbuka ulichosoma kuhusu alichofanya Daudi wakati ambapo alikuwa na watu wakiwa na uhitaji na njaa"

soma nini Daudi

Yesu anarejea kwa kusoma kuhusu Daudi katika Agano kale. Hii inaweza kutofasiriwa kuonyesha taarifa thabiti.

Jinsi alivyokwenda katika nyumba ya Mungu...kwa wale walikuwa naye?

Hii inaweza kuelezwa kama sentensi iliyotengenishwa na mstari wa 25. "Alienda aliingia katika ya Mungu...kwa wale walikuwa naye" (UDB)

namna gani alienda

Neno "a" urejea kwa Daudi

mkate uliowekwa mbele

Hii urejea kwa mikate kumi na miwili ambayo ilikuwa imewekwa kwenye meza ya dhahabu ndani ya hema au jengo la hekalu kama dhabihu kwa Mungu nyakati za kipindi cha Agano la Kale.

Mark 2:27

Sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu

"Mungu aliweka Sabato kwa ajili ya mwanadamu"

mwanadamu

"mtu" au "watu" au "mahitaji ya watu" Hii urejea kwa wanaume na wanawake.

siyo mwanadamu kwa ajili ya Sabato

'Mungu hakumuumba mtu kwa ajili ya uzuri wa Sabato"

Mark 3

Marko 03 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Sabato

Ilikuwa kinyume cha sheria ya Musa kufanya kazi siku ya sabato. Mafarisayo waliamini kumponya mtu mgonjwa siku ya Sabato ilikuwa "kazi," hivyo wakasema kwamba Yesu alifanya makosa wakati alimponya mtu siku ya Sabato. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses)

"Kukufuru dhidi ya Roho"

Hakuna mtu anayejua kwa hakika hatua ambazo watu hufanya au maneno gani wanayosema wanapotenda dhambi hii. Hata hivyo, labda wao humtusi Roho Mtakatifu na kazi yake. Sehemu ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwafanya watu kuelewa kuwa wao ni wenye dhambi na wanahitaji kusamehewa na Mungu. Kwa hiyo, yeyote asiyejaribu kuacha dhambi huenda anakufuru Roho. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#blasphemy and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#holyspirit)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Wanafunzi kumi na wawili

Yafuatayo ni orodha ya wanafunzi kumi na wawili:

Katika Mathayo:

Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo, Yohana mwana wa Zebedayo, Filipo, Bartholomeo, Tomasi, Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Tadayo, Simoni wa Zeloti na Yuda Isikariote.

Katika Marko:

Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana mwana wa Zebedayo (ambao aliwaita Boanerge, yaani, wana wa ngurumo), Filipo, Bartholomeo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alifayo, Tadayo Simoni wa Zeloti na Yuda Isikariote.

Katika Luka:

Simoni (Petro), Andrea, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomeo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alifayo, Simoni (aitwaye Zeloti), Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda Isikariote.

Thadayo labda ni Yuda, mwana wa Yakobo.

Ndugu na Dada

Watu wengi huwaita wale ambao wana wazazi sawa "ndugu" na "dada" na kuwafikiria kama watu muhimu zaidi katika maisha yao. Watu wengi pia huita wale walio na babu na nyanya sawa "ndugu" na "dada." Katika sura hii Yesu anasema kwamba watu muhimu zaidi kwake ni wale wanaomtii Mungu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#brother)

<< | >>

Mark 3:1

Sentensi unganishi

Yesu amponya mtu siku ya Sabato katika Sinagogi na kuonyesha jinsi anavyojisikia walivyofanya Mafarisayo kuhusiana na sheria za Sabato. Mafarisayo na Maherode wanapanga kumua Yesu.

Baadhi ya watu

"Baadhi ya Mafarisayo." Badae, katika 3:5, hawa watu wanaonyeshwa kama Mafarisayo.

mtu aliye na mkono uliopooza

"mtu aliye na mkono uliopooza"

Baadhi ya watu walimtazama kuona kama atamponya

"Mafarisayo walimtazama Yesu kwa karibu sana kuona kama atamponya na mkono uliopooza"

mshtaki

Mafarisayo walitaka kumshtaki Yesu kwa kuvunja sheria kwa kufanya kazi siku ya Sabato, je amponye mtu. "kumshtaki yeye kwa kufanya kosa" au " kumshtaki yeye kwa kuvunja sheria"

Mark 3:3

katika ya umati

"katika ya umati huu"

Je ni halali kutenda tendo jema siku ya Sabato... au kutenda yasiyo haki?

Yesu alisema changamoto hii. Alitaka wao wakiri kuwa ni halali kumponya mtu siku ya Sabato.

kutenda tenda jema siku ya Sabato au kutenda isivyo haki... kuokoa maisha au kuua.

Haya makundi ya maneno yanafanana katika maana, tofauti ya pili imeenda ndani zaidi.

kuokoa maisha, au kuua

Inaweza kuwa ni msaada kutubu "ni halali," kama lilivyo swali analouliza Yesu tena kwa njia nyingine. "ni halali kuokoa maisha au kuua"

maisha

Hii urejea kwa maisha ya kimwili kama neno mbadala kwa mtu. "mmoja wapo anakufa" au maisha ya mmoja wapo"

Lakini walikuwa kimya

"Lakini walikataa kumjibu"

Mark 3:5

Aliangalia

"Yesu aliangalia"

alihuzunika

"alikuwa na huzuni kubwa"

ugumu wa mioyo yao

Huu mfano unaelezea jinsi Mafarisayo hawakuwa tayari kuwa na huruma kwa huyo mtu aliye kuwa na mkono uliopooza. "hawakuwa tayari kuwa na huruma kwa mtu huyo"

Nyosho mkono wako

"Nyosha mkono wako"

mkono wake uliponywa

Hii inaweza kutajwa na kauli tendaji. "Yesu alimponya mkono wake" au Yesu aliufanywa mkono wake kama ulivyo kuwa awali"

wakafanya njama

walianza kufanya mpango

Maherode

Hili ni jina la kisiasa lilompa nguvu Herode wa Antipasi

kwa namna gani watamuua

"kwa namna gani watamuua Yesu"

Mark 3:7

Sentensi unganishi

Yesu aliendelea kuponya watu kama alivyofuatwa na umati mkubwa pindi alipotaka kuwa mbali nao.

bahari

Hii urejea bahari ya Galilaya

Idumaya

Huu ni mkoa, hapo awali ulijulikana kama Edomu, ambao ulikuwa mpaka nusu ya kusini mwa mkoa wa Uyahudi.

mambo aliyokuwa anafanya

Hii inarejea kwa miujiza ya Yesu aliyokuwa akifanya. "miujiza mikubwa aliyokuwa akifanya"

alikuja kwake

"alikuja alipokuwa Yesu"

Mark 3:9

Na aliwaambia wanafunzi wake kuwa na mtubwi mdogo... ili kwamba wasije wakamsonga.

Kama ilivyokuwa umati mkubwa ulikuwa unamsonga Yesu, alikuwa katika hatari ya kusongwa. Katika mstari wa 9-10 yameunganishwa na kusemwa taarifa dhabiti kwa usahihi.

aliwauliza wanafunzi wake

"Yesu aliwambia wanafunzi wake"

Kwa kuwa aliponya wengi, ili kwamba

Neno "wengi" umaanisha idadi kubwa ya watu waliokwisha ponywa na Yesu. "Kwa sababu Yesu alikuwa ameponya tayari watu wengi, kila mmoja"

yeyote aliyekuwa na mateso alikuwa na shauku ya kumsogelea ili kwamba amguse.

"wagonjwa wote walimsonga wakiwa na shauku ya kumgusa"

Mark 3:11

muone yeye

"muone Yesu"

walianguka...wakalia na kusema

Hapa "wao" urejea kwa roho chafu. Ni zile zinazosababisha watu wanao wamiliki kufanya mambo. Hii inaweza kufanywa dhabiti. "ziliwasababisha watu wanao wamiliki kuanguka chini mbele yake na kulia.

walianguka mbele yake

Roho chafu hazikuanguka mbele yake Yesu kwa sababu zilimpenda au zilitaka kumwabudu yeye. Zilianguka chini mbele yake kwa sababu zilimuogopa.

Wewe ni Mwana wa Mungu

Yesu ana nguvu juu ya roho chafu kwa sababu ni yeye ni "Mwana wa Mungu"

Mwana wa Mungu

Hili ni jina la muhimu sana kwa Yesu

Aliwaamuru kwa msisitizo

"Yesu aliwaamuru kwa msisitizo roho hizo chafu"

si kumfanya yeye ajulikane

"si kumfunua yeye ni nani"

Mark 3:13

Sentensi unganishi

Yesu awaita rasmi wanafunzi wake kabla hajaenda nyumbani, pale aliposhitakiwa kuwa wazimu na aliyetawaliwa na Beelzebuli.

ili kwamba wawe pamoja naye na aweze kuwatuma kuhubiri

"ili kwamba wawe pamoja naye na aweze kuwatuma kuhubiri"

Simoni, aliyempa jina la Petro

Mwandishi anaanza kuwataja orodha ya majina ya mitume kumi na mbili. Simoni ni mtu wa kwanza aliye kutajwa.

Mark 3:17

kwa wale aliowapa

Kikundi cha maneno "kwa wale" urejea kwa wote Yakobo mwana wa Zebedayo na ndugu yake Yohana.

jina la Bonagesi, hao ni, wana wa ngurumo

"Jina Bonagesi, ambalo lina maanisha wana wa ngurumo" Maana ya jina "Bonagesi" inaweza kuwa dhabiti zaidi. "jina jipya 'wanaume wanaofananishwa kama ngurumo"

Thadayo

Hili ni jina la mwanaume

ambaye atamsaliti

"ambaye atamsaliti Yesu" Neno "ambaye" urejea kwa Yuda Iskariote.

Mark 3:20

Kisha alienda nyumbani

"Kisha Yesu alienda nyumbani kule alikokuwa anaishi"

kula mkate

Neno "mkate" usimama badala ya chakula. "kule wote" au " kula chochote"

walienda kumkamata

Familia yake walienda nyumbani, ili kwamba wamkamate na kumlazimisha aende nao.

kwani walisema

Maana za neno "wao" ni 1) ndugu zake au 2) baadhi ya watu katika umati

amerukwa na akili zake

"Familia ya Yesu inatumia lugha hii kueleza kwa namna gani wanafikiri anavyofanya. "uazimu" au kichaa"

Kwa mtawala wa mapepo anatoa mapepo

"Kwa nguvu za Beelzebuli ambaye ni mtawala wa mapepo, Yesu anatoa mapepo

Mark 3:23

Sentensi unganishi

Yesu aeleza kwa mifano kwanini hatawaliwi na Shetani na wale wanaofanya mapenzi ya Mungu wako vile vile kama kuwa kaka yake, na dada, na mama.

Yesu aliwaita kwake

"Yesu aliwaita watu waje kwake"

Inawezekanaje Shetani kumtoa Shetani?

Yesu aliuliza swali hili katika kuwajibu waandishi kusema kwamba anatoa mapepo kwa Beelzebuli. " "Shetani hawezi kujitoa yeye mwenyewe!" au " Shetani hawezi kwenda kinyumbe na roho zake chafu!"

Kama ufalme umegawanyika yenyewe

Neno "ufalme" ni neno mbadala kwa watu wanaoishi katika ufalme. "kama watu wanaoishi katika ufalme wamegawanyika wao wenyewe"

haiwezi kusimama

Kikundi hiki cha maneno ni mfano wa maana kwamba watu hawataunganishwa na wataanguka. "hawatavumilia" au "wataanguka"

nyumba

Haya ya maneno mbadala kwa watu wanaoishi ndani ya nyumba. "familia" au "kaya"

Mark 3:26

Kama Shetani atainuka kinyume chake mwenyewe na kugawanyika

Neno "mwenyewe" ni nomino tendaji ambayo inarejea tena kwa Shetani, na mfano mbadala wa roho chafu zake. "Kama Shetani na roho zake chafu waligombana" au "kama Shetani na roho zake chafu wameinukiana dhidi ya mwenzake na wamegawanyika"

hawezi kusimama

Huu ni mfano unamaanisha ataanguka na hawezi kuvumilia. "atakoma kuwa pamoja" au "hawezi kuvumilia na amefika mwisho" au "ataanguka na amefika mwisho.

mnyang'anyi

kuiba vitu vya dhamani vya mtu

Mark 3:28

Kweli nawambieni

Hii huonyesha kwamba sentensi inayofuata ni ya kweli na muhimu

wana wa watu

"wale waiokwisha zaliwa." Sura hii imetumiwa kusisitiza ubinadamu wa watu. "watu"

tamka

"zungumza"

walikuwa wakisema

"watu walikuwa wakisema"

ana roho chafu

Hii ni lugha inayo maanisha kumilikiwa na roho chafu. "anamilikiwa na roho chafu"

Mark 3:31

ndugu

Hii inarejea kwa ndugu zake Yesu

Wakamtuma mtu, kumwita

"Wakamtuma mtu ndani kumwambia kwamba walikuwa nje na kwamba yeye anapaswa kuja kwao"

wanakutafuta wewe

"wanakuulizia wewe"

Mark 3:33

huyu ndugu yangu, dada, na mama

"hawa ni ndugu, dada yangu, na mama yangu"

Mark 4

Marko 04 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Marko 4:3-10 huunda mfano mmoja. Mfano huo umeelezwa katika 4:14-23.

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivyo kwa mashairi katika 4:12, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Mifano

Mifano ni hadithi fupi ambayo Yesu aliwaambia ili watu waweze kuelewa kwa urahisi somo alilojaribu kuwafundisha. Pia aliwaambia hadithi ili wale ambao hawakutaka kumwamini wakose kuelewa kweli.

<< | >>

Mark 4:1

Sentensi unganishi

Yesu alipokuwa anafundisha akiwa kwenye mtumbwi kandokanod ya bahari, aliwambia mfano wa udongo

bahari

Hii ni bahari la Galilaya

na kukaa chini

"na akaketi ndani mwa mtumbwi"

Mark 4:3

Sikilizeni

"Zingatia"

Alipokuwa akipanda

"Alipokuwa akipanda mbengu juu ya udongo." Kwa tamaduni zingine watu walipanda mbingu kwa utofauti. Katika mfano huu mbengu zilipandwa kwa kutupwa juu ya ardhi iliyokuwa imeandaliwa kwa kukuza.

ziliota

"zilianza kuota kwa haraka"

udongo

Hii inarejea kupoteza uchafu juu ya ardhi ambapo utapanda mbengu.

Mark 4:6

zilinyauka

Hii urejea kwa mimea midogo. Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "inanyausha mimea midogo"

sababu hazikuwa na mzizi

"sababu mimea midogo haikuwa na mizizi, zilinyauka"

na ikazisonga

Neno ika -"zi"-songa urejea kwa mimea midogo

Mark 4:8

zingine zilizaa mara thelathini zaidi

Kiasi cha nafaka kilichotokana na kila mmea inalinganishwa na mbengu moja iliyoota. "Mimea baadhi ilizaa mara thelathini zaidi kama mbegu ilivyopandwa na mtu"

thelathini...sitini...na mia

"30...60...100." Hizi zinaweza kuandikwa kama hesabu

na baadhi sitini, na baadhi mia

Yesu anaendelea kueleza kiasi cha nafaka iliyopatikana. Udondoshaji wa maneno umetumika hapa kufupisha kikundi cha maneno lakini yanaweza kuandikwa. "na baadhi zilizaa sitini zaidi ya nafaka na baadhi zilizaa mia zaid ya nafaka"

Yeyote aliye na masikio kusikia

Hii ni njia ya kurejea kwa yeyote asikilizae. "Yeyote anayenisikiliza mimi"

acha asikilize

Hapa neno "kusikiliza" humaaanisha kuwa makini. "unapaswa kuwa makini kwa kila ninachosema"

Mark 4:10

Yesu alipokuwa peke yake

Hii haimaanishi kwamba Yesu alikuwa kabisa peke yake, hapa, umati wa watu ulikuwa umeenda na Yesu alikuwa na wanafunzi kuma na wawili na wafuasi wengine baadhi.

Kwenu mmepewa

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu amekupa wewe" au "Nimekwisha kukupa wewe"

kwa walio nje

"lakini kwa wale hawako miongoni mwenu" Hii urejea kwa wote wale hawakuwa miongoni mwa wanafunzi kumi na wawili au wafuasi wengine wa Yesu.

kila kitu kiko katika mifano

Inaweza kusemwa kwamba Yesu anatoa mifano kwa watu. " Nimezungumza vyote katika mifano"

wanapotazama... wanaposikia

Inakisiwa kwamba Yesu anazungumza kuhusu watu akitazama kwa kile anacho waonyesha na kusikia kile anacho wambia. "wanapotaza kile nafanya... wanaposikia kile nachosema "

wanatazama, lakini hawaoni

Yesu anazungumzia watu wanaoelewa wanachokiona kwa uhalisia. "wanatazama na hawaelewi"

geuka

Hii inamaanisha kugeuka mbali na dhambi

Mark 4:13

Sentensi unganishi

Yesu anaelezea mfano wa udongo kwa wafuasi wake na kisha anawambia kuhusiana na taa kuonyesha vitu vilivyo jificha vitajulikana.

Na akasema kwao

"Na Yesu akasema na wanafunzi wake"

Je hamuelewi mfano huu? Mtawezaje kuelewa mifano mingine ?

Yesu alitumia maswali haya kuonyesha jinsi alivyokuwa na huzuni kwamba wanafunzi wake hawakuweza kuelewa mfano wake. "kama hautaweza kuelewa mfano huu, fikiri jinsi ilivyo ngumu kwa wewe kuelewa mifano mingine"

Mkulima anayepanda mbegu zake

"Mkulima anayepanda mbegu zake huwakilisha"

kwa yule anayepanda neno

"Neno" huwakilisha ujumbe wa Mungu. Kupanda ujumbe huwakilisha kufundisha. "yule anayefundisha watu ujumbe wa Mungu"

Baadhi huanguka kandokando mwa njia

"Baadhi ya watu ni kama mbegu huanguka kandokando mwa njia" au "Baadhi ya watu ni kama njia ya miguu ambapo mbegu huangukia"

njia

"njia ya miguu"

wanapoisikia

Hapa wanapo-"i" sikia urejea "neno" au "ujumbe wa Mungu"

Mark 4:16

Na baadhi ni wale

"Na baadhi ya watu ni kama mbegu." Yesu anaanza kuelezea ni kwa namna gani wanafanana kama mbegu zinazoangukia udongo wa mawe.

Na hawana mizizi yoyote ndani yao

Hii ni ulinganishi wa mimea midogo kuwa inakuwa na mizizi mifupi. Mfano huu humaanisha kwamba watu kwa mara kwanza husimumika pindi wapokeapo neno, lakini hawakujitoa kwa nguvu kwalo. "Nao wanakuwa kama miche midogo isiyokuwa na mizizi"

hakuna mzizi

Hii siyo ya kutia chumvi sana katika kuelezea, tiachumvi, kusisitiza jinsi mizizi ilivyokuwa na kina kidogo.

vumilia

Katika mfano huu, "vumilia" humaanisha "kuamini" "kuendelea katika imani"

sababu ya neno

Inaweza kuwa msaada kueleza kwanini taabu huja. Ilikuja kwa sababu watu waliliamini neno. "sababu waliliamini neno"

walijikwaa

Katika mfano huu, "kujikwaa" humaanisha "kuacha kuamini ujumbe wa Mungu"

Mark 4:18

Na wengine ni wale waliopandwa katika miiba

Yesu anaanza kueleza kwa namna gani watu wanakuwa kama mbegu zinazoanguka kwenye miiba. "Na watu wengine wanakuwa kama mbegu zilizopandwa katika miiba"

wanaujali ulimwengu

"masumbufu ya maisha" au "mambo yanayo husiana na maisha ya sasa"

udanganyifu wa mali

"tamaa ya mali"

huwaingia na kulisonga neno

Kama Yesu anavyoendelea kusema kuhusu watu walio kama mbegu zinazoanguka katika ya miiba, anaeleza tamaa na masumbufu yanavyofanya kwa neno katika maisha kama miiba inavyoisonga mimea midogo.

halizai

"neno hakuna kuzaa tunda lolote katika wao"

yule aliyepanda katika udongo mzuri

Yesu anaanza kueleza namna gani baadhi ya watu wako kama mbegu zilizopandwa katika udongo mzuri. "kama mbegu zilizopandwa katika udongo mzuri"

baadhi thelathini, na baadhi sitini, na baadhi mia

Hii inarejea kwa nafaka ilitokana na mimea. "baadhi huzaa nafaka thelathini, baadhi nafaka sitini, na baadhi nafaka mia" au baadhi 30 nafaka, baadhi nafaka 60, na baadhi nafaka 100"

Mark 4:21

Yesu akawambia

"Yesu alisema na umati"

Je huwa unaleta taa ndani ya nyumba na kuiweka chini ya kikapu, au chini ya kitanda?

Swali hili linaweza kuandikwa kama sentensi. "Unaleta taa ndani ya nyumba na kuiweka chini ya kikapu, au chini ya kitanda!"

Kwa kuwa hakuna chochote kilichojificha ambacho hakitajulikana...njoo nje kweupe

Hii inaweza kusemwa kwa namna chanya. "Kwa kila kitu kilichojificha kitafanywa kujulikana, na chochote kilicho sirini kitakuwa peupe"

hakuna kilichojificha... hakuna siri

"hakuna kilichojificha... hakuna siri" Vifungu vyote vina maana ile ile. Yesu anasisitiza kwamba kila kilichojificha kitawekwa wazi.

Akiwapo mwenye masikio ya kusikia, na asikie!"

Hapa neno "kusikiliza" humaaanisha kuwa makini. "unapaswa kuwa makini kwa kila ninachosema"

Mark 4:24

Akawambia

"Yesu akawambia umati"

kwa kuwa kipimo mpimacho

maana zinazowezekana ni 1) Yesu anazungumza kipimo halisi na ukarimu kwa wengine au 2) huu mfano ambao Yesu anazungumzia wa "kuelewa" kama ilikuwa ni "kupima"

ndicho mtakachopimiwa, na itaongezwa kwenu

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu atakupima, na atakuongezea"

yeye atapokea zaid...na yule vitachukuliwa

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "kwa yeye Mungu atampa zaidi...kutoka kwake Mungu atavichukua"

Mark 4:26

Sentensi unganishi

Yesu basi anawambia watu mfano kueleza ufalme wa Mungu, ambapo kwa badae anawaeleza wanafunzi wake.

kama mtu aliyepanda mbegu

Yesu hufanananisha ufalme wa Mungu kwa mkulima anayepanda mbegu. "kama mkulima anayepanda mbegu"

Alipolala usiku na kuamka asubuhi

"Anamka asubuhi na kulala usiku"

jani

shina au kuchipuka

sikio

kichwa katika shina au sehemu ya mmea inashika tunda

mara hupeleka mundu

Hapa "mundu" ni maneno mbadala yanayosimama kwa mkulima au watu wanaotumwa na mkulima kwenda kuvuna nafaka. "mara huenda na mundu kuvuna nafaka" au "mara hutuma watu na mundu kuvuna nafaka"

mundu

ni upanga uliojikunja au ndoano iliyo na makali inatumiwa kuvunia nafaka

sababu mavuno ni tayari

Hapa maneno "ni tayari" ni lugha kwa ajili ya nafaka iliyo tayari kuvunwa. "sababu nafaka iko tayari kuvunwa"

Mark 4:30

tuufananishe ufalme wa Mungu na kitu gani, au tutumie mfano gani kuuelezea?

Yesu aliuliza swali hili kusababisha wasikilizaji wake kufikiri kuhusu ufalme wa Mungu. "Pamoja na mfano huu naweza kueleza ufalme wa Mungu ukoje"

pindi inapopandwa

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "wakati yoyote anapanda mbegu" au "wakati yoyote anapanda mmea"

inafanya matawi makubwa

Mti wa haradali unaelezwa kama unasababisha matawi kukua makubwa. "pamoja na matawi makubwa"

Mark 4:33

alisema neno kwao

Neno "kwao" urejea kwa umati

kwa kadiri walivyoweza kuelewa

"na kama waliweza kuelewa baadhi, aliendelea kuwaambia zaidi"

wakati alipokuwa peke yake,

Hii inamaanisha kuwa alikuwa mbali na umati, lakini wanafunzi bado walikuwa naye.

akawaelezea kila kitu

Hapa "kila kitu" ni kutia chumvi sana katika kueleza kitu au tia chumvi. Aliezea mifano yake yote. "alielezea mifano yake yote"

Mark 4:35

Sentensi unganishi

Kama Yesu na wanafunzi wake wanachukua mtumbwi kukwepa umati wa watu, upepo mkali wa dhoruba ukajitokeza. Wanafunzi wake wanaogopa wanapoona hata upepo na bahari unamtii Yesu.

akasema kwao

"Yesu alisema kwa wanafunzi wake"

upande wa pili

"upande wa pili wa bahari ya Galilaya" au "upande wa pili wa bahari"

upepo mkali wa dhoruba ukajitokeza

Hapa "ukajitokeza" ni lugha inayotumiwa kwa "kuanza" " upepo mkali wa dhoruba kuanza"

mtumbwi ulikuwa umejaa

Inaweza kuwa msaada kusema kwamba mtumbwi ulikuwa umejaa maji. "mtumbwi ulikuwa umejaa maji"

Mark 4:38

Yesu mwenyewe

Hapa "mwenyewe" husisitia kwamba Yesu alikuwa peke yake kwenye shetri"

shetri

Hii inakuwa mwishoni mwa mtumbwi. "shetri ya mtumbwi"

Wakamwamsha

Neno "waka" urejea kwa wanafunzi

haujali sisi tunakufa?

Wanafunzi waliuliza swali hili kuonyesha uoga wao. Swali hii linaweza kuandikwa kama sentensi. "unapaswa kuwa makini kwa kile kinachotokea, wote tunakufa"

tunaelekea kufa

Neno "tuna" inajumuisha wanafunzi na Yesu.

Amani, shwari

Haya maneno mawili yanafanana na yanatumiwa kwa kusisitiza

utulivu mkubwa

"ukimya mkubwa juu ya bahari" au utulivu mkubwa juu ya bahari"

Mark 4:40

Na akasema kwao

"Na Yesu akasema kwa wanafunzi wake"

Kwa nini mnaogopa? Je hamna imani bado?

Yesu anauliza maswali haya kuwafanya wanafunzi kufikiri kwanini wanaogopa wakati yuko pamoja nao. Haya maswali yanaweza kuandikwa kama sentensi. "Haupaswi kuogopa. Unahitaji imani zaidi"

Huyu ni nani tena, kwa sababu hata upepo na bahari vya mtii?

Wanafunzi wanauliza swali katika hali ya kushangaa kwa yale Yesu alifanya. Hili swali linaweza kuandikwa kama sentensi. "Huyu mtu si kama watu wengine wa kawaida; hata upepo na bahari unamtii!"

Mark 5

Marko 05 Maelezo ya Jumla

Changamoto za kutafsiri katika sura hii

"Talitha, koum"

Maneno "Talitha, koum" (Marko 5:41) yanatoka kwa lugha ya Kiaramu. Marko anayaandika jinsi yanavyosikika na kisha kutafsiri. (See: rc://*/ta/mtu/translate/translate-transliterate)

<< | >>

Mark 5:1

Sentensi unganishi

Baada ya Yesu kutuliza dhoruba kubwa, anamponywa mtu aliyekuwa na mapepo mengi, lakini wenyeji wa Gerasi hawakufurahi kwa uponyaji wake, na walimuomba Yesu aondoke.

Walikuja

Neno "Wali" urejea kwa Yesu na wanafunzi wake.

bahari

Hii urejea kwa Bahari ya Galilaya

Gerasenes

Hili jina urejea kwa watu wanaoishi Gerasi.

akiwa na roho chafu

Hii lugha inayomaanisha kwamba mtu "ametawaliwa" au "kumilikiwa" na roho chafu. "kutawalia na roho chafu" au roho chafu kumiliki"

Mark 5:3

Alikuwa amefungwa nyakati nyingi

Hii inaweza kuandikwa katika kauli tendaji. "Watu walimfunga mara nyingi"

viungo vyake viliharibika

Hii inaweza kuandikwa katika kauli tendaji. "kuharibika kwa viungo vyake"

Viungo

"kamba kwenye miguu yake" au "minyororo iliyofungwa kifundoni kumzuia"

minyororo

"pingu" au "minyororo ilifungwa kwenye kifundo cha mkono kumzuia"

kumshinda

"mwenye kumzuia" Mtu mwenye pepo mchafu hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu za kumshinda

kumshinda

"kumtawala"

Mark 5:5

alijikata yeye mwenyewe kwa mawe makali

Mara nyingi wakati ambapo mtu anamilikiwa na pepo, pepo atamsababisha mtu huyo kufanya vitu vya uharibifu, kama vile kujikata mwenyewe.

Alipomwona Yesu kwa mbali

Wakati ambapo mtu huyu alipomwona Yesu, Yesu alikuwa anatoka mtumbwini.

kuinama

Hii inamaanisha aliinama mbele za Yesu kwa hofu na heshima, na wala si kwa kuabudu.

Mark 5:7

Akapiga kelele

"Roho chafu ikapiga kelele"

Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu?

Roho chafu inauliza swali hili kwa uoga. Hii inaweza kuandikwa kama sentensi. "Niache peke yangyu, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu! Hakuna sababu ya wewe kuniingilia mimi"

Yesu...usinitese.

Yesu, "Mwana wa Mungu aliye juu,"ana uwezo kuzitesa roho chafu.

Mwana wa Mungu aliye juu

Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu.

Nakuombwa kwa Mungu mwenyewe

Hapa roho chafu anaapa kwa Mungu kama anafanya ombi la Yesu. Angali namna gani ya ombi hili linafanywa katika lugha ya kwenu.

Mark 5:9

Alisema kwake, "Jina langu ni Jeshi, kwa kuwa tuko wengi."

roho zilizokuwa ndani ya mtu zilisema kwa Yesu kwamba haimo roho chafu moja tu ndani ya mtu huyu, bali roho wengi wachafu.

Mark 5:11

nao walimsihi

"roho chafu walimsihi Yesu"

Aliwaruhusu

"Yesu aliziruhusu roho chafu" zikawaingie nguruwe

na walikimbilia

"na nguruwe walikimbilia"

nao walikimbilia chini ya kilima mpaka baharini, na karibia nguruwe elfu mbili walizama baharini

Unaweza kuifanya hii sentensi kujitegemea: "mpaka baharini. Kuliwakuwako na nguruwe elfu mbili, na walizama baharini."

Yapata nguruwe elfu mbili

"Yapata nguruwe 2000 " walizama baharini

Mark 5:14

katika mji na nchi

Inaweza kusemwa kwa usahihi kuwa watu walitoa taarifa yao kwa watu walikuwa katika mji na nchi.

Jeshi

Hili lilikuwa jina la mapepo mengi ambayo yalikuwa ndani mwa mtu.

katika akili yake timamu

Hii ni lugha inayoamaanisha kuwa anafikiri vizuri. "kwa akili timamu" au "kufikiri kwa usahihi.

waliogopa

Neno "wa" urejea kwa kundi la watu walioenda nje kuona nini kimetokea.

Mark 5:16

Mtu aliyekuwa akitawaliwa na mapepo

"Mtu ambaye mapepo yalimtawala"

Mark 5:18

mapepo-aliyekuwa amepagawa na mapepo

amepagawa na mapepo- Ijapokuwa mtu hajapagawa na mapepo tena, bado anaelezwa katika hali hiyo. "mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo"

Lakini hakumruhusu

Alichofanya Yesu hakikumruhusu mtu kufanya inaweza kusema kwa usahihi. "Lakini hakumruhusu mtu kuja nao"

Dekapoli

Mkoa uliokuwa kusinimashariki mwa Bahari ya Galilaya

kila mmoja alistaajabu

Inaweza kuwa msaada kusema kwanini watu walistaajabu. "watu wote waliosikia alichosema walistaajabu"

Mark 5:21

Sentensi unganishi

Baada ya kumponya mtu aliyemilikiwa na pepo katika mji wa Gerasenes, Yesu na wanafunzi wake wanarudi kupitia ziwa Kaperinaumu ambapo mmoja wa watawala wa sinagogi anamuuliza Yesu kumponya binti yake.

upande mwingine

Inaweza kuwa msaada kuongoza taarifa kwa maneno haya. "upande wa pili wa bahari"

kando mwa bahari

"ufukoni mwa bahari" au "katika ufuko"

bahari

Hili ni bahari la Galilaya.

Yairo

Hili ni jina la mwanaume.

Kwa hiyo alienda kwake

"Hivyo Yesu alienda pamoja na Yairo." Wanafunzi wa Yesu walienda pia naye. "Hivyo Yesu na wanafunzi walienda na Yairo"

weka mikono yako

"Kuweka mikono" urejea kwa nabii au mwalimu kuweka mkono wake kwa mtu na kugawa aidha uponyaji au baraka. Katika jambo hili, Yairo anamuomba Yesu kumponya binti yake.

kwamba afanywe mzima na aishi

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "na mponye na kumfanya hai"

na walimzonga karibu wakimzunguka.

Hii inamaanisha umati walimzunguka Yesu na kujisonga wenyewe kuwa karibu na Yesu.

Mark 5:25

Sentensi unganishi

Wakati Yesu akiwa katika njia kumponya mtoto wa miaka 12 wa mtu mmoja, mwanamke aliyekuwa anaumwa miaka 12 anaingilia kati kwa kumgusa Yesu kwa ajili ya uponyaji.

Sasa kulikuwa na mwanamke

"Sasa" inaonyesha kuwa huyu mwanamke ambaye ametambulishwa kwa simulizi katika lugha yako.

ambaye damu yake ilitoka kwa muda miaka kuma miwili

Mwanamke hakuwa na kidonda kilichokuwa wazi; badala yake, kutokwa kwa damu yake kwa kila mwezi hakukukoma. Lugha yako inaweza kuwa na njia ya heshima kurejea kwa hali hii.

kwa miaka kumi na miwili

"kwa miaka 12"

alikuwa vibaya

"ugonjwa wake ilikuwa mbaya" au "kutokwa damu kuliongezeka"

taarifa kuhusu Yesu

Alikuwa amesikia taarifa kuhusu Yesu kwa jinsi alivyoponya watu. " Kuwa Yesu aliponya watu"

vazi

vazi la nje au mkoti

Mark 5:28

nitakuwa mzima

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "itaniponywa mimi" au "nguvu yake itaniponywa mimi"

aliponywa kutoka kwenye mateso yake.

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "ugonjwa ulimwacha" au " hakuwa tena na ugonjwa"

Mark 5:30

na unasema, 'Ni nani aliyenigusa?'

"tulishangaa kusikia ukisema kwamba mtu fulani alikugusa."

umati huu ulimsonga

Hii inamaanisha walimsonga Yesu na kusukuma wenyewe kwa pamoja kuwa karibu na Yesu.

Mark 5:33

alianguka chini mbele yake

"alipiga magoti mbele zake." Alipiga magoti mbele ya Yesu kama tendo la heshima na utii.

kumwambia ukweli wote

Maneno "ukweli wote" urejea kwa namna alivyomgusa na kupona. "kumwambia ukweli wote kuhusu alivyomgusa"

Binti

Yesu alikuwa akiitumia istilahi hii kwa mfano kurejea kwa mwanamke kama muumini.

imani yako

"imani yako kwangu"

Mark 5:35

Wakati alipokuwa akiongea

"Wakati Yesu alipokuwa akizungumza"

baadhi ya watu walikuja kutoka kwa kiongozi wa Sinagogi

Maana zinazowekana ni 1) watu hawa walitokea nyumbani mwa Jarius au 2) Jarius alikuwa amewapa watu hawa maagizo kwenda kumuona Yesu au 3) watu hawa walikuwa wametumwa na mtu aliyekuwa kama mwenyekiti na kiongozi wa Sinagogi kwa kukosekana kwa Jarius.

kiongozi wa Sinagogi

"kiongozi wa Sinagogi" ni Jarius

kuzungumza

"kuzungumza na Jairus

Kwa nini kuendelea kumsumbua mwalimu zaidi?

"Hatupaswi kumsumbua mwalimu zaidi"

mwalimu

Hii inarejea kwa Yesu

Mark 5:36

Amini tu

Kama ni muhimu, unaweza kusema kuwa Yesu anamuamru Jarius kuamini. "Amini tu naweza kumfanya binti yako kuwa hai"

hakuwa...aliona

Katika mistari hii neno "a" urejea kwa Yesu.

kuongozana naye

"kwenda naye" Inaweza kuwa msaada kusema wakati walipokuwa wakienda. "kuongozana naye kwa nyumba ya Jarius"

Mark 5:39

aliwaambia

"Yesu aliwaambia watu walikuwa wakilia"

Kwa nini mnafadhaika na kwa nini mnalia?

Yesu aliuliza swali hili kuwasaidia kuona imani yao ndogo. Hii inaweza kuandikwa kama sentensi "Hampaswi kufadhaika na kulia."

aliwatoa wote nje

"watoe watu wengine wote nje ya nyumba"

wale waliokuwa pamoja naye

Hii inarejea kwa Petro, Yakobo, na Yohana

alienda alipokuwa mtoto

Inaweza kuwa msaada kusema alipokuwa mtoto. "alienda chumbani pale alipokuwa amelala mtoto."

Mark 5:41

Talitha koum

Hii ni sentensi ya kiaramu, ambayo Yesu alimwambiaa binti katika lugha yake.

Alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili

"alikuwa na miaka 12"

Aliwaamuru kwa nguvu kwamba hakuna yeyote anapaswa kujua kuhusu hili

"Aliwaamuru kwa nguvu, hakuna yeyote anapaswa kujua hili" au "Aliwaamuru kwa nguvu, Wasimwambie yeyote kuhusu aliyoyafanya!"

Aliwaamuru kwa nguvu

"Aliwaamuru kwa nguvu"

Na aliwaambia wampatie yule binti chakula

Na aliwaambia, 'mpeni chochote ale"

Mark 6

Marko 06 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Watiwa mafuta"

Katika inchi ya Mashariki ya Karibu wakati wa kale, watu walijaribu kuponyesha wagonjwa kwa kuwawekea mafuta ya mizeituni.

<< | >>

Mark 6:1

Sentensi unganishi

Yesu anarudi kwa mji wa nyumbani ambapo anakataliwa.

mji wake wa nyumbani

Hii inarejea kwa mji wa Nazarethi ambao Yesu alikulia na familia yake inaishi. Hii hana maana ya kuwa anamiliki ardhi.

Ni hekina gani aliyopewa?

Hili swali, ambalo lina muundo wa tulivu, inaweza kuulizwa katika kauli tendaji. "Hii ni hekima ya namna gani aliyopata?"

kwamba anafanya kwa mikono yake

Haya maneno yanasisitiza kuwa Yesu mwenyewe anafanya miujiza.

Huyu si seremala, kijana wa Mariamu, na ndugu yake Yohana na Yose na Yuda na Simoni? Dada zake zake hawapo hapa kati yatu?

Si huyu ni seremala, kijana wa Mariamu, na kaka yake Yohana na Yose na Yuda na Simoni? Dada zake hawapo hapa kati yetu?

Mark 6:4

kwao

"kwa umati"

Nabii hakosi heshima ila

Ni hakika kabisa kwamba wananiheshimu na manabii wengine wa sehemu nyingine,lakini si ndani ya miji tuliozaliwa! Hata kidogo na watu wanaoishi katika nyumba zetu hawatuheshimu!"

aliwawekea mikono wagonjwa wachache

"kuwawekea mikono" inarejea kwa nabii au mwalimu kuweka mikono yake kwa yeyote na kutoa aidha uponyaji au baraka. Katika jambo hili, Yesu anaponya watu.

Mark 6:7

Sentensi unganishi

Yesu anatuma wanafunzi wake nje wawili wawili kuhubiri na kuponya.

aliwaita kumi na wawili

Hapa neno "aliwaita" linamaanisha kuwa aliwaita kumi na wawili waje kwake.

Wawili wawili

" 2 kwa 2" au "jozi" msivae kanzu mbili msichukue shuka nyingine."

hapana mkate

Hapa "mkate" ni neno yenye maana sawa na chakula kwa ujumla.

hapana pesa katika mkoba

Katika utamaduni, wanaume walibeba pesa zilizowekwa katika mkanda. "hapana pesa iliwekwa kwenye mfuko wa pesa"

Mark 6:10

akawaambia

"Yesu akawaambia kumi na wawili"

kaeni hapo mpaka mtakapoondoka

"kaeni katika nyumba ile mpaka mtakapoondoka katika mji ule."

kama ushuhuda kwao

"kama ushuhuda kinyume nao." Inaweza kuwa msaada kueleza namna hili tendo lilikuwa ushuhuda kwao. "kama ushuhuda kwao. Kwa kufanya hivyo, utaweza kushuhudiwa kuwa hawakuwakaribisha"

Mark 6:12

Nao wakaenda

Neno "waka" urejea kwa kumi na wawili na haimjumuishi Yesu. Pia, inaweza kuwa msaada kusema kwamba walienda katika miji baadhi. "

kuacha dhambi zao

"tubu dhambi zao"

Waliwafukuza pepo wengi

Inaweza kuwa msaada kusema kwamba walifukuza pepo nje ya watu. "Walifukuza pepo wengi nje ya watu"

Mark 6:14

Sentensi unganishi

Wakati Herode anasikia kuhusu miujiza ya Yesu, anakuwa na wasiwasi, kufikiri kwamba mtu fulani amemfufua Yohana Mbatizaji kutoka kwa wafu. (Herode alisababisha Yohana Mbatizaji kuuwawa.)

Mfalme Herode aliposikia hayo

Neno "hayo" urejea kwa kila kitu ambacho Yesu na wanafunzi wake walikuwa wakifanya katika miji baadhi, ikiwemo na kukemea mapepo na kuponywa watu.

Baadhi walikuwa wakisema, "Yohana mbatizaji

Baadhi ya watu walikuwa wakisema kuwa Yesu alikuwa ni Yohana Mbatizaji. Hii inaweza kusemwa kwa uwazi zaidi. "Baadhi yao walikuwa wakisema, 'Ni Yohana Mbatizaji alie rejea"

Yohana mbatizaji amefufuliwa

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu alimfufua Yohana Mbatizaji"

Baadhi yao wakasema, "Huyu ni Eliya."

Inaweza kuwa msaada kusema kwanini baadhi ya watu walifikiri kuwa ni Eliya. "Baadhi wao walisema, ni Eliya, ambaye Mungu aliahidi kumtuma tena."

Mark 6:16

Maelezo ya ujumla

Katika mstari wa 17 mwandishi anaanza na kutoa maelezo ya nyuma kuhusu Herode na kwanini alimkata kichwa Yohana Mbatizaji.

yupi alimkata kichwa

Hapa Herode anatumia neno "Ni" ikirejea kwake mwenyewe. Neno "Ni" mbadala linalotumika kwa maaskari wa Herode. "ambao niliamuru maaskari wangu kumkata kichwa."

amefufuliwa

Hiii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "amekuwa hai tena"

Herode aliagiza Yohana akamatwe na alimfunga gerezani

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Herode alituma maaskari wake kumshika Yohana na kumfunga gerezani"

kutumwa kumshika

"amri ya kumshika"

kwa ajili ya Herode

"kwa sababu ya Herode"

ndugu wa mke wa Filipi

"mke wa ndugu yake Filipo." Ndugu wa Herode ambaye ni Filipo siyo sawa na Filipi ambaye alikuwa mwinjilisti katika kitabu cha Matendo ya mitume aur Filipi aliyekuwa mmoja wa wanafunzi wa Yesu.

kwa sababu alikuwa amemuoa

"kwa sababu Herode alikuwa amemuoa"

Mark 6:18

alitaka kumuua, lakini hakuweza

Binti wa Herode ni mtendaji mkuu katika kifungu hiki na "binti" ni maneno mbadala kama anavyotaka mtu fulani amuuwe Yohana. "alitaka mtu fulani amuuwe, lakini asinge muuwa"

maana Herode alimwongopa; alimjua

Hivi vifungu viwili vinaweza kuunganishwa tofauti kuonyesha zaidi kwanini Herode alimwogopa Yohana. "maana Herode alimwogopa Yohana kwa sababu alimjua"

alijua kwamba ni mwema

"Herode alimjua kuwa Yohana alikuwa mwema"

Msikilize yeye

"Msikilize Yohana"

Mark 6:21

Sentensi unganishi

Mwandishi anaendelea kutoa maelezo ya nyumba kuhusu Herode na kukatwa kichwa Yohana mbatizaji.

akawaandalia moafisa wake karamu... Galilaya

Hapa neno "aka" urejea kwa Herode na maneno mbadala kwa mtumwa wake ambaye angeweza kumwamuru kuandaa karamu. " alikuwa na chakula kilichokuwa kimaandaliwa kwa ajili ya maofisa... wa Galilaya" au alikuwa amealika maofisa wake... wa Galilaya kuwa na kufurahi pamoja naye"

Chakula

chakula cha kawaida au dhifa

Binti wake mwenyewe Herode

Neno "wake mwenyewe"ni nomino inayotumiwa kusisitiza kwamba ilikuwa ni muhimu alikuwa ni binti wake Herode aliye cheza wakati wa karamu.

alikuja ndani

"alikuja ndani ya chumba"

Mark 6:23

chochote utakachoniomba...ufalme wangu

Hii inaweza kuwa msaada kuongeza maelezo yanayokosekana. "Nitakupa nusu ya kile ninachomiliki na kutawala, kama utaniomba"

akatoka nje

"akatoka nje ya chumba"

mara moja

"sasa hivi"

ndani ya sahani

juu ya kisahani

Mark 6:26

kwa sababu ya kiapo chake, na kwa wageni wake

"kwa sababu ya wageni wake waliosikia akitoa ahadi,"

juu ya sahani

"juu ya kisahani"

Na wanafunzi wake

"Na wanafunzi wa Yohana"

Mark 6:30

Sentensi unganishi

Baada ya wanafunzi kurudi toka kuhubiri na kuponya, wanaenda sehemu nyingine kuwa na faragha, lakini kuna watu wengi wanakuja kumsikiliza Yesu anafundisha. Wakati ambapo kunakuwa jioni, anawalisha watu na kisha anawatuma kila mmoja wakati akiomba peke yake.

eneo la jangwa

eneo ambalo halikuwa na watu

wengi walikuwa wanakuja na kwenda

Hii inamaanisha kwamba watu waliendelea kuja kwa mitume na kisha kwenda mbali nao.

hata hawakuwa

Neno "hawa" urejea kwa mitume.

Hivyo walienda zao

Hapa neno "wali" inawajumuisha mitume na Yesu.

Mark 6:33

waliwaona wakiondoka

"watu walimuona Yesu na mitume wakiondoka"

kwa miguu

Watu walienda kwa miguu kutoka miji yote, ambapo inajipinga na namna wanafunzi walienda kwa mtumbwi.

aliona umati mkubwa

"Yesu aliona umati mkubwa"

walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji

Yesu analinganisha watu kwa kondoo waliochanganyikiwa pindi wanapokosa mchungaji wao wa kuwaongoza.

Mark 6:35

Muda ulipoendelea sana

Hii inamaanisha ilikuwa ni jioni. "Wakati ambapo kulikuwa kumeendelea" au " kuendelea jioni"

eneo la jangwa

Hii inarejea kwa eneo ambalo hakuna watu. Ona kama ilivyo tofasiri katika 6:30

Mark 6:37

Lakini akawajibu na akisema

"Lakini Yesu aliwajibu na akisema kwa wanafunzi wake"

Tunaweza kwenda na kununua mikate yenye thamani ya dinari mia mbili na kuwapa?

Wanafunzi wanauliza swali hili kusema kwamba hakuna njia wanaweza kununua chakula cha kutosha kwa umati huu. "Hatuwezi kununua mikate ya kutosha kulisha umati huu, hata kama tungekuwa na dinari mia mbili!"

dinari mia mbili

"200 dinari." Dinari ni sarafu za Kirumi.

mikate

"mikate" Mikate ni donge la unga lilotengenezwa na kuokwa.

Mark 6:39

nyasi za kijani

Eleza nyasi kwa rangi ya neno inavyotumika katika lugha yako kwa nyasi zenye afya, ambayo inaweza ua isiwe rangi ya kijani.

makundi ya mamia na hamsini

Hii urejea kwa namba ya watu katika kila kundi. "wapatao watu hamsini katika baadhi ya makundi na wapatao watu mia kwa makundi mengine"

kutazama mbinguni

Hii inamaanisha kwamba alitazama juu mbinguni, ambako kunausishwa na sehemu anayoishi Mungu.

alibariki

"alizungumza baraka" au "alishukuru"

aligawa samaki wawili kwa watu wote

"aliwagawa samaki wawili ili kwamba kila moja apate kitu"

Mark 6:42

Walichukua

Maana zinazoweza ni 1) "Wanafunzi walichukua au 2) "Watu walichukua"

vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili

"vikapu kumi na viwili vilijaa vipande vya mkate"

vikapu kumi na mbili

"12 vikapu"

wanaume elfu tano

"5,000 wanaume"

Na walikuwa wanaume elfu tano waliokula mikate

Hesabu ya wanawake na watoto haikuhesabiwa. Kama isingeelewaka kuwa wanawake na watoto walikuwapo, inaweza kuwekwa kwa usahihi. "Na kulikuwa na watu elfu tano walio kula mikate. Hawakuwahesbau wanawake na watoto"

Mark 6:45

sehemu nyingine

Hii inarejea kwa Bahari ya Galilaya.

Bethsaida

Huu ni mji uliopo pwani ya kaskazini katika bahari ya Galilaya.

Walipokuwa wamekwisha kuondoka

"Walipokuwa watu wamekwisha kuondoka"

Mark 6:48

Sentensi unganishi

Dhoruba inajitokeza wakati wanafunzi wanajaribu kuvuka ziwa. Kumuona Yesu anatembea juu ya maji kunawaogopesha. Hawaelewi namna gani Yesu anaweza kutuliza dhoruba.

kuangilia mara ya nne

Huu ni wakati kati ya saa tatu asubuhi na jua linajomoza.

Mzimu

roho ya mtu aliyekufa au aina zingine za roho

Muwe wajasiri!...Msiwe na hofu!

Sentensi hizi mbili zinafanana katika maana, zinasisitiza kwa wanafunzi kwamba hawakupaswa kuogopa.

Mark 6:51

Wakamshangaa kabisa

Kama unataka kuwa mahususi zaidi, inaweza kusemwa nini walikuwa wakishangaa. "Walishangazwa na kila alichokuwa amekifanya"

mikate ilimaanisha nini

Neno "mikate" urejea wakati Yesu alipoizidisha mikate.

mioyo yao ilikuwa migumu

Kuwa na mioyo inawakilisha kuwa wagumu kuelewa.

Mark 6:53

Sentensi unganishi

Wakati Yesu na wanafunzi wake wanafika Genesareti wakiwa katika mtumbwi wao, watu wanamuona na kumletea watu awaponye. Hii inatokea kokote waendako.

Genesareti

Hili ni jina la mkoa kaskazi mwa magharibi mwa Bahari ya Galilaya.

mara wakamtambua

"watu pale walimtambua Yesu"

walikimbia...waliposikia

Neno "wa" urejea kwa watu waliomtambua Yesu, wala si kwa wanafunzi.

wagonjwa

Neno hili urejea kwa watu. "watu wagonjwa"

Mark 6:56

Popote alipoingia

"Popote Yesu alipoingia"

waliwaweka

Hapa "wa" urejea kwa watu. Haaina maana ya kurejea kwa wanafunzi wa Yesu

mgonjwa

Hii urejea kwa watu. "watu wagonjwa"

wakamsihi

Maana zinazowekana ni 1)"mgonjwa alimsihi" au 2) "watu walimsihi"

waache waguse

Neno "wa" urejea kwa mgonjwa.

pindo la vazi lake

"pindo la vazi lake" au " pindo la vazi lake"

wengi

"wote"

Mark 7

Mark 07 General Notes

Structure and formatting

Some translations set poetry farther to the right than the rest of the text to show that it is poetry. The ULB does this with the poetry in 7:6-7, which is from the Old Testament.

Special concepts in this chapter

Hand washing

The Pharisees washed many things that were not dirty because they were trying to make God think that they were good. They washed their hands before they ate, even when their hands were not dirty, though the law of Moses did not say that they had to do it. Jesus told them that they were wrong and that people make God happy by thinking and doing the right things. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#clean)

Other possible translation difficulties in this chapter

"Ephphatha"

This is an Aramaic word. Mark wrote it the way it sounds using Greek letters and then explained what it means. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-transliterate)

<< | >>

Mark 7:1

Sentensi unganishi

Yesu anawakemea Mafarisayo na waandishi

walikusanyika kumzunguka yeye

"walikusanyika kumzunguka Yesu"

Mark 7:2

Na waliona

"na Mafarisayo na wandishi waliona"

kwa mikono najisi

Inaweza kuwa msaada kuongeza maelezo yanayokosekana. "kwamba, walikula na mikono najisi"

wazee

Wazee wa kiyahudi walikuwa viongozi katika jamii zao na pia walikuwa waamuzi wa watu.

vyombo vya shaba

"mabirika ya shaba" au "vyombo vya vyuma"

viti vinavyotumika wakati wa chakula

"benchi" au "vitanda". Kwa wakati huo, Wayahudi wange egemea kitu wakati wa kula.

Mark 7:5

Kwa nini wanafuni wako hawaishi kulingana na tamaduni za wazee, kwani wanakula mikate yao kwa mikono isiyooshwa?

"Wanafunzi wako hawatii tamaduni za wazee wetu! Wanapaswa kuosha mikono yao kwa kutumia ibada zetu!"

Mark 7:6

Maelezo ya ujumla

Hapa Yesu ananukuu kwa nabii Isaya, ambaye aliandika maandiko miaka mingi kabla.

kwa midomo yao

Hapa "midomo" ni kirai cha kuzungumza. "kwa kile wanachosema"

lakini mioyo yao iko mbali nami

Hapa "moyo" urejea kwa mawazo ya watu au hisia. Hii ni njia kusema kuwa watu hawajitoa kwa Mungu. "lakini hawanipendi kabisa"

Wananifanyia ibaada zisizo na maana

"Wananifanyia ibada zisizo na maana" au wananiabudu kwa utupu"

Mark 7:8

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwakemea wandishi na Mafarisayo

kuacha

"kata kumfuata"

Anayesema mabaya juu ya

"Anaye laani"

kushikilia kwa wepesi

"shikiliza kwa nguvu" au "weka"

Mmeikataa amri...mtunze tamaduni zenu

Yesu anatumia sentensi za kejeli kuwakemea wasikilizaji wake kwa kuziacha amri za Mungu. "Mnafikiri mmefanya vizuri kwa jinsi mmemkataa amri za Mungu ili kwamba mtunze tamaduni zenu, lakini mlichofanya si vizuri kabisa!"

Mmeikataa

"mu uhodari kiasi gani kumkataa"

asemaye mabaya

"anaye laani"

hakika atakufa

"anapaswa kuuwawa"

'Yeye asemaye mabaya juu ya baba yake au mama yake hakika atakufa

Yeye asemaye mabaya juu ya baba yake au mama yake hakika atakufa hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mamlaka yanapaswa kumwadhibu kifo mtu anasema vibaya juu ya baba yake au mama"

Mark 7:11

Msaada wowote ambao mngeupokea kutoka kwangu ni hazina ya Hekalu.

Tamaduni za waandishi zilisema kwamba pindi pesa au vitu vingine vilipoahidiwa kanisani, visingetumika kwa lengo lingine lolote.

Hazina ya Hekalu

Mwandishi anataka msomaji ajue jinsi neno linavyo sikika, kwa hiyo andika hii kwakutumia alfabeti za lugha yako lisikike kama hili kwa kadri uwezavyo.

Hazina ya Hekalu

Hapa mwandishi anarejea kwa kitu fulani katika neno la Kiebrania. Hili neno linapaswa kunakiriwa kama ilivyo katika lugha yako kutumia alfabeti.

imetolewa kwa Mungu

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Nimeitoa kwa Mungu"

hivyo haumruhusu kufanya jambo lolote kwa ajili ya baba au mama yake

Kwa kufanya hivi, Mafarisayo wanawaruhusu watu kutowapatia wazazi wao, kama wanatoa ahadi kumpa Mungu kila wangetoa kwao

bure

kualishwa au kuachana nayo

Na mambo mengi ya jinsi hiyo mnayoyafanya."

"Na mnavyofanya inaweza vitu vingine kufanana na hiki"

Mark 7:14

Sentensi unganishi

Yesu anazungumza mfano kwa umati kuwasaidia kuelewa alichokuwa akiwaambia waandishi na Mafarisayo.

Aliita

"Yesu aliita"

Nisikilizeni mimi, ninyi nyote, an mnielewe

Neno hili "Sikiliza" na "elewa" yanashabiana. Yesu anayatumia yote pamoja kusisitiza kwamba wasikilizaji wake lazima wawemakini kwa kile anachokisema.

kuelewa

Inaweza kuma msaada kusema nini Yesu anawaambia kuelewa. "jaribu kuelewa ninachoenda kukuambia"

Hakuna chochote kutoka nje ya mtu

Yesu anazungumza kuhusu anachokula mtu. Hii ni kinyume na "kile kitokacho mwa mtu"

Ni kile kimtokacho mtu

"Ni utu wa ndani" au "Ni kile mtu anachofikiri, anachosema, au dkufanya"

Mark 7:17

Sentensi unganishi

Wanafunzi bado hawajaelewa nini Yesu alichosema kwa waandishi, Mafarisayo, na umati. Yesu anaeleza maana zaidi kwa utoshelevu kwao.

Sasa

Neno hili limetumika hapa kuanzisha wazo jingine katika hadithi. Sasa Yesu yuko mbali na umati, yuko ndani na wanafunzi wake.

Bado hamjaelewa?

Yesu anatumia swali hili kueleza kukatishwa tamaa kwake kwamba hawaelewi. Hii inaweza kuelezwa kama sentensi. "Baada ya yote nimekwisha sema na kufanya, ningetegemea muelewe"

Hamuoni kwamba chochote kimuingiacho mtu hakiwezi kumchafua

Yesu anatumia swali hili kufundisha wanafunzi wake kitu fulani ambacho walipaswa kuwa wanakijua tayari. Inaweza kusemwa kama sentensi "Chochote kiingiacho...huchafua

kwa sababu hakiwezi

Hapa "haki" urejea kwa kile kimwingiacho mtu, kwamba, kila mtu anakula.

Yesu alifanya

"Yesu alitangaza"

vyakula vyote safi

Inaweza kuwa msaada kueleza kwa usahihi nini maana ya maneno haya. "vyakula vyote safi, inamaanisha kuwa watu wanaweza kula chakula chochote pasipo Mungu kumhesabia mlaji kuwa najisi

Mark 7:20

Alisema

"Yesu alisema"

Ni kile ambacho kinamtoka

Inaweza kuwa msaada kusema kwa ufasaha "kile" urejea kwa. "Ni mawazo na matendo yanayomtoka mtu."

kupenda anasa

kushindwa kutawala tamaa za mwili

yanatoka ndani

Hapa neno "ndani" huelezea moyo wa mtu. "hutoka ndani mwa moyo wa mtu" au "hutoka ndani mwa mawazo ya mtu"

Mark 7:24

Sentensi unganishi

Wakati Yesu anaenda Tiro, anamponya binti wa mwanamke wa kimataifa akiwa na imani ya ajabu.

alikuwa na roho chafu

Hii ni lugha inayomaanisha kuwa alikuwa amilikiwa na roho chafu.

Anguka chin

"piga magoti"

Mwanamke huyo alikuwa Myunani, wa kabila la Kifoeniki

Neno "sasa" utambulisha wazo jingine katika hadithi, kama ilivyo sentensi hii hutoa maelezo ya nyuma kuhusu mwanamke.

Kifoeniki

Hili ni jina la mwanamke la kitaifa. Alizaliwa mkoa wa Kifoeniki Syria.

Mark 7:27

Waache watoto kwanza washibe

"Watoto lazima wale kwanza" au "Lazima nilishe watoto kwanza."

Watoto

Wayahudi. AT: "Lazima nitumikie Wayahudu kwanza."

Mkate

Chakula

Mbwa

Watu wa mataifa

hata mbwa hula mabaki ya watoto chini ya meza.

"unaweza kunitumikia, mtu wa mataifa, katika njia ndogo hii.

Mabaki

Vipande vidogo vidogo sana ya mkate

Mark 7:29

uko huru kwenda

"unaweza kwenda sasa" au "nenda nyumbani"

Pepo ameshamtoka binti yako

Yesu amesababisha pepo mchafu kumtoka binti wa mwanamke. Hii inaweza kueleza kwa usahihi. "Nimesababisha roho mchafu kumwacha binti yako"

Mark 7:31

Alikuja kupitia

"Alisafiri kupitia"

Dikapoli

"miji kumi," kanda ya kusini mashariki ya Bahari ya Galilaya.

Nsni slikuwa kiziwi

"ambaye alikiwa hana uwezo wa kusikia"

alikwa na shida ya kuongea

"hakuweza kuongea vizuri"

Mark 7:33

Alimota nje

"Yesu alimtoa nje"

akaweka vidole vyake kwenye masikio yake

Yesu anaweka vidole kwenye masikio yake.

baada ya kutema mate, aligusa ulimi wake

Yesu anatema mate na kisha anagusa ulimi wa mwanaume.

baada ya kutema

Inaweza kuwa msaada kusema kwamba Yesu alitemea mate vidole vyake.

alitazama juu mbinguni

Hii inamaanisha kuwa alitaza juu mbinguni, ambako kunahusishwa na eneo analoishi Mungu.

Efata

Mwandishi anataka msomaji ajue jinsi neno linavyo sikika, Kwa hiyo andika hii kwa kutumia alfabeti za lugha yako na neno lisike karibu na "effatha" kwa kadri uwezavyo.

Kuvuta pumzi

akavuta pumzi kuonyesha kuwa hakuwa na furaha.

kusema naye

"alisema na mwanaume"

masikio yake yalifunguliwa

Hii inamaanisha alikuwa hawezi kusikia. "masikio yake yalifunguliwa na aliweza kusikia"

Kilichokuwa kimeshikilia ulimi wake kilitolewa.

"Yesu alikitoa kilichokuwa kimeushikilia ulimi wake" au "Yesu aliponya kilichokuwa kimemfanya asiongee vizuri"

kilichokuwa kimezuia ulimi

"kinachomzuia yeye kuongea " au "usemi wake kuwa na kikwazo"

Mark 7:36

kadri alivyowaamuru

Inaweza kuwa msaada kuongeza taarifa iliyokosekana. "kadri alivyowaamuru wasimwambie mtu yoyote."

kadri ya wingi

"kadri ya upana" au " zaidi"

hakika

"kabisa" au "mno"

kiziwi...kimya

Haya urejea kwa watu. "watu viziwi...watu wakimya" au " watu wasioweza kusikia...watu wasioweza kuongea"

Mark 8

Marko 08 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mkate

Wakati Yesu alifanya muujiza na kulisha na mkate kwa umati mkubwa wa watu, labda walikumbuka wakati Mungu alifanya ajabu zamani akalisha watu wa Israeli jangwani.

Chachu ni kiungo kinachosababisha mkate kuwa kubwa kabla ya kuoka. Katika sura hii, Yesu anatumia chachu kama sitiari ya mambo ambayo yanabadili jinsi watu wanavyofikiri, kuzungumza, na kutenda. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

"Kizazi cha uzinzi"

Wakati Yesu aliwaita watu "kizazi cha uzinzi," alikuwa akiwaambia kuwa hawakuwa waaminifu kwa Mungu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faithful and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#peopleofgod)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Maswali ya uhuishaji

Yesu alitumia maswali mengi yauhuishaji kama njia ya kuwafundisha wanafunzi (Marko 8:17-21) na kuwakaripia watu (Marko 8:12). (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kitendawili

Kitendawili ni taarifa ya kweli inayoonekana kuelezea kitu kisichowezekana. Yesu anatumia kitambo wakati anasema, "Yeyote anayetaka kuokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata" (Marko 8:35-37).

<< | >>

Mark 8:1

Sentensi unganishi

Umati mkubwa ambao haukuwa na chakula ulikuwa na Yesu. Anawalisha kutumia mikate saba na samaki wachache mbele za Yesu na wanafunzi wake wakaingia ndani ya mtumbwi kwenda eneo jingine.

Katika siku hizo

Kikundi hiki cha maneno kinatumiwa kutambulisha tukio jipya katika hadithi.

sababu wameendelea kuwa pamoja nami tayari kwa siku tatu.

"kwa sababu hii ni siku ya tatu hawa watu wamekuwa pamoja nami"

wanaweza kuwa dhaifu

Maana zinazofaa ni 1) "wanaweza kupoteza fahamu kwa muda" au 2)wanaweza kuwa dhaifu"

Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwashibisha watu hawa katika eneo hili lililoachwa?

Wanafunzi wanaonyesha mshangao kwamba Yesu angewatazamia kuweza kupata chakula cha kutosha. "Hili ni eneo la jangwa ambako hakuna eneo ambalo tunaweza kupata mikate ya kutosha kuwalizisha watu hawa!"

boflo ya mkate

Boflo ya mkate ni bonge la unga wa ngano ambalo linatengenezwa na kuokwa.

Mark 8:5

Akawauliza

"Yesu aliwauliza wanafunzi wake"

Aliuamuru umati ikae chini.

Hii inaweza kuandikwa kama dondoa ya moja kwa moja. "Yesu aliuamuru umati, 'ukae chini"

kaa chini

Tumia maneno ya lugha ya kwenu kwa namna watu wanakula kimatamaduni kama hakuna meza, aidha kwa kukaa au kujilaza.

Mark 8:7

Pia walipata

Hapa neno "wali..." linatumika kurejea kwa Yesu na wanafunzi wake.

alishukuru

"Yesu alishukuru kwa samaki"

Walikula

"Hawa watu walikula"

walikusanya

"wanafunzi walikusanya"

vipande vilivyo baki, vikapu vikubwa saba

Hii inaweza kuwa msaada kuongeza taarifa zilizokosekana. "vipande vilivyo baki vya mkate na samaki, ambavyo vilijaza vikapu saba vikubwa.

Na aliwaacha waende

Hii inaweza kuwa msaada kufafanua ambapo Yesu anawaacha waende. "Na baada ya kula, Yesu aliwaacha waende"

wakaenda katika ukanda wa Dalmanuta

Hii inaweza kuwa msaada kufafanua namna ya kwenda Dalmanuta. "walipiga mashua kupitia bahari ya Galilaya mpaka Dalmanuta"

Mark 8:11

Sentensi unganishi

Huko Dalmanuta, Yesu anakataa kuwapa Mafarisayo ishara kabla ya yeye na wanafunzi hawajaingia katika mashua na kuondoka.

Walitafuta toka kwake

"Walimuuliza"

kutoka mbinguni

Hapa "mbinguni" urejea kwa eneo ambapo Mungu anaishi, na ni maneno badala ya Mungu. "kutoka kwa Mungu"

kumjaribu yeye

Mafarisayo walimjaribu Yesu kumfanya yeye awathibitishie kuwa anatoka kwa Mungu. Baadhi ya taarifa zinaweza kuwekwa sahihi. "kuhakikisha kuwa Mungu alimtuma yeye"

hema

Hii inamaanisha kuvuta ndani na kisha kupumua.

katika roho wake

"katika yeye"

Kwa nini kizazi hiki kinatafuta ishara?

Yesu anawakaripia. Swali hili linaweza kuandikwa kama sentensi. "Kizazi hiki hakipaswi kutafuta ishara"

kizazi hiki

Wakati ambapo Yesu anazungumza juu ya "kizazi hiki", anarejea kwa watu walio ishi wakati huo. Mafarisayo hawa wanajumuishwa katika kundi hili. "wewe na watu wa kizazi hiki"

hakuna ishara itakayotolewa

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendi. "Sitatoa ishara"

aliwaacha, akaingia ndani ya mtumbwi tena

Wanafunzi wa Yesu walienda naye. Baadhi ya taarifa zinaweza kuwekwa sahihi. "aliwaacha, akaingia ndani ya mtumbwi pamoja na wanafunzi wake"

upande ule mwingine

Hii huelezea bahari ya Galilaya, ambayo inaweza kusemwa kwa ufasaha. "kwa upande mwingine wa bahari"

Mark 8:14

Sentensi unganishi

Wakati Yesu na wanafunzi wake wakiwa ndani ya mtumbwi, walikuwa na majadiliano kuhusu kuelewa kudogo kati ya Mafarisayo na Herode, ijapokuwa walikuwa wamekwisha ona ishara nyingi.

Sasa

Hili neno linatumika kuweka alama ya kutenganisha hadithi. Hapa mwandishi anasema taarifa za nyuma kuhusiana na wanafunzi kusahau kuchukua mkate.

hakuna zaidi ya mkate mmoja

Kikundi cha maneno yaliyo kinyume "hakuna zaidi" hutumiwa kusisitiza namna ya kiasi kidogo cha mkate waliokuwa nao. "mkate mmoja tu"

Kuwa macho na ujilinde

Haya maneno mawili yana maana ya kufanana na yanarudiwa hapa kwa msisitizo. Yanaweza kuanganishwa. "Kuwa macho"

chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.

Hapa Yesu anazungumza kwa wanafunzi wake katika mfano ambao hawauelewi. Yesu analinganisha mafundisho ya Mafarisayo na Herode kwa chachu, lakini hauwezi kueleza hivi unavyo tofasiri sababu wanafunzi wenyewe hawakuuelewa.

Mark 8:16

Ni kwa sababu hatuna mikate

Katika sentensi hii, inaweza kuwa msaada kusema kwamba, "ni" urejea kwa kile Yesu alichokwisha sema. "Angepaswa kuwa amesema kwa sababu hatuna mikate"

hakuna mkate

Wanafunzi walikuwa na mkate mmoja, ambao haikuwa na tofauti kutokuwa na mkate kabisa. "mikate midogo kabisa"

Kwa nini mnasemezana kuhusu kutokuwa na mikate?

Hapa Yesu anawaonywa kwa ulaini wanafunzi wake kwa sababu wangeweza kuelewa alichokuwa anazungumzia. Hii inaweza kuandikwa kama sentensi. "Haupaswi kufikiri kwamba naongelea mkate halisi"

Hamjajua bado? Hamuelewi?

Maswali haya yana maana ile ile na yanatumika kwa pamoja kusisitiza kwamba hawaelewi. Hii inaweza kuandikwa kama swali moja au sentensi. "Hamjajua bado?" au "Mnapaswa kujua na kuelewa kwa sasa mambo ninayo sema na kufanya."

Mioyo yenu imekuwa miepesi?

Mfano huu urejea kwa hao hawako wazi au kuwa tayari kuelewa Yesu alimaanisha nini. Huu unaweza kuandikwa kama sentensi. "Namna gani mioyo yenu haiko wazi kuelewa ninachosema?" au "Mioyo yenu haiko tayari kuelewa."

Mark 8:18

Mna macho, hamuoni? Mna masikio, hamsikii? Hamkumbuki?

Yesu anaendelea kukemea kwa utilivu wanafunzi . Haya maswali yanaweza kuandikwa kama sentensi. "Una macho, lakini hauelewi unachokiona. Una masikio, lakini hauelewi unachosikia. Lazima ukumbuke"

elfu tano

Hii urejea kwa watu 5,000 Yesu aliye walisha

mlichukua vikapu vingapi vilivyo jaa vipande vya mikate?

Hii inaweza kuwa msaada kusema wakati ambapo walichukua vipande vya vikapu. "ni vikapu vingapi vilivyo jaa vipande vya mikate mlichukua baada ya kila mmoja amemaliza kula"

Mark 8:20

elfu nne

Hii urejea kwa watu 4,000 waliolishwa na Yesu.

mlichukua vikapu vingapi

Hii inaweza kuwa msaada kusema wakati ambapo walivichukua. "ni vikapu vingapi vilivyo jaa vipande vya mikate mlichukua baada ya kila mmoja amemaliza kula"

Bado hamuelewi?

Yesu kwa utilivu anawakamea wanafunzi wake kwa kushindwa kuelewa. Hii inaweza kuandikwa kama sentensi. "Lazima uelewe kwa sasa mambo ninayo sema na kufanya."

Mark 8:22

Sentensi unganishi

Wakati ambapo Yesu na wanafunzi wake wanatoka katika mtumbwi wao hukpo Bethsaida, Yesu anamponya mtu kipofu.

Bethsaida

Huu ulikuwa ni mji kaskazini mwa ufuko wa bahari ya Galilaya.

akamshika

Hii inaweza kuwa msaada kusema kwa nini walitaka Yesu amguse mtu huyo. "kumgusa ili kumponya"

Alipotema mate juu ya macho yake ...alimuuliza

"Wakati ambapo Yesu alipotema mate juu ya macho yake... Yesu alimuuliza"

Mark 8:24

Alitazama juu

"Mtu alitazama juu"

Naona watu wanaonekana kama miti inatembea

Mtu anaona watu wanatembea, na bado hawakuwa vizuri kwake, hivyo aliwalinganisha na miti. "Ndiyo, naona watu! Wanatembea, lakini siwaoni vizuri . Wanaonekana kama miti"

Kisha tena

"Yesu tena"

na mtu alifungua macho yake, macho yake yaliona

Kikundi hiki cha maneno "macho yaliona" inaweza kuandikwa katika kauli tendi "Kurudisha uonaji, na mtu akafungua macho yake"

Mark 8:27

Sentensi unganishi

Yesu na wanafunzi wake wakiwa njiani kwenda vijiji vya Kaiseria ya Filipi wanazungumza juu ya Yesu ni nani na nini kitatokea kwake.

Wakamjibu na wakasema

"Wakamjibu, wakasema,"

Yohana mbatizaji

Hili lilikuwa jibu la mwanafunzi, ambalo watu walisema Yesu alikuwa nani. Hii inaweza kuonyeshwa kwa usahihi. "Baadhi ya watu wanasema wewe ni Yohana mbatizaji"

Wengine wanasema

Neno "wengine" urejea kwa watu wengine. Pia, inaweza kuwa msaada kuongeza taarifa zinazokosekana. "Watu wengine wanasema wewe ni ... watu wengine wanasema wewe ni"

Mark 8:29

Akawauliza

"Yesu akawauliza wanafunzi wake"

Yesu akawaonya wasimwabie mtu yeyote kumuhusu Yeye.

Yesu hakutaka wao wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye ni Kristo. Hii inaweza kufanywa kwa usahihi. Pia, hii inaweza kuandikwa kama dondoo ya moja kwa moja. "Yesu aliwaonya wasimwambie mtu yeyote kuwa ye ni Kristo" au " Yesu aliwaonya, 'msimwambie mtu yeyote kwamba mimi ni Kristo"

Mark 8:31

Mwana wa Adamu

Hili ni jina muhimu sana kwa Yesu.

na atakataliwa na viongozi na makuhani wakuu, na waandishi, na atauawa, na baada ya siku tatu atafufuka.

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendi. "na kwamba viongozi na makuhani wakuu na waandishi watamkataa, na watu hao watamuua na baada ya siku tatu atafufuka."

Alisema haya kwa uwazi

"Alisema hivi ili iwe nyepesi kuelewa"

alianza kumkemea

Petro alikemewa na Yesu kwa kusema mambo aliyosema kuwa yangetokea kwa Mwana wa Adamu. Hii inaweza kufanywa kwa usahihi. "alianza kumkemea kwa kusema mambo haya"

Mark 8:33

Sentensi unganishi

Baada ya kumkemea Petro kwa sababu hakutaka Yesu kufa na kufufuka, Yesu anawambia wanafunzi wake na umati namna ya kumfata.

Pita nyuma yangu Shetani! Hujali

Yesu anamaanisha ya kuwa Petro anafanya kama Shetani kwa sababu anajaribu kumzuia Yesu kutimiza alichotumwa na Mungu kufanya. "Pita nyuma Shetani! Nakuita Shetani kwa sababu hujali" au "Pita nyuma yangu, kwa sababu unafanya kama Shetani! Hujali"

Pita nyuma yangu

"Nipishe mimi"

nifuate mimi

Kumfuata Yesu hapa kunawakilisha kuwa mmoja wa wanafunzi wake. "kuwa mwanafunzi" au "kuwa mmoja wa wanafunzi wangu"

ajikane mwenyewe

"hawapaswi kuzitimiza tamaa zake" au "anapaswa kuziacha tamaa zake"

achukue msalaba wake, na anifuate.

"beba msalaba wake na umfuate" Msalaba huu unawakilisha mateso na kifo. Kuchukua msalaba huwakilisha kuwa tayari kutesa na kufa. "unapaswa kunitii mpaka hatua ya kuteseka na kufa"

na nifuate

Kumfuata Yesu hapa uwakilisha kumtii. "na nitii mimi"

Mark 8:35

Kwa kuwa yeyote anayetaka

"Kwa kuwa yeyote anayetaka"

maisha

Hii urejea kwa vyote maisha ya mwili na maisha ya kiroho.

kwa ajli yangu na kwa ajli ya injili

"kwa sababu yangu na kwa sababu ya injili." Yesu anazumguza juu ya watu wanaopteza maish yao kwa ajili ya kumfuata Yesu na injili. Hii inaweza kusema kwa usahihi. "kwa sababu ananifuata mimi na kuwambia wengine injili"

Inamfaidia nini mtu, kupata ulimwengu wote, na kisha kupata hasara ya maisha yake?

Hii inaweza kuandikwa kama sentensi. "Hata kama mtu anapata ulimwengu wote, haitamfaidi kama atapata hasara ya maisha yake"

kupata ulimwengu wote

Yesu anatumia kutia chumvi sana katika kusisitiza kwamba hakuna chochote ulimwenguni unachoweza kupata kwa kupoteza maisha yako. "kama anapata kila kitu katika ulimwengu"

kupoteza

"kupoteza"

Mtu anaweza kutoa nini badala ya maisha yake?

Hii inaweza kuandikwa kama sentensi. "Hakuna chochote mtu anaweza kufanya kutoa badala ya maisha yake." au " Hakuna yoyote anaweza kutoa chochote kwa badala ya maisha yake."

Mtu anaweza kutoa nini

Kama katika lugha yako "kutoa" huitaji mtu kupokea alichopewa, "Mungu" inaweza kusemwa kama mpokeaji. "Nini mtu anaweza kumpa Mungu"

Mark 8:38

Katika kizazi hiki cha zinaa na dhambi

Yesu anazungumza juu ya kizazi hiki kama "wazizi" akimaanisha kwamba si waaminifu katika mahusiano yao na Mungu. "katika kizazi hiki cha watu waliojiingiza katika uzizi kinyume na Mungu na niwazinifu" au "katika kizazi hiki cha watu wasio waaminifu kwa Mungu na ni wenye dhambi"

Mwana wa Adamu

Hili ni jina la muhimu sana kwa Yesu

atakapokuja

"atakapokuja tena"

katika utukufu wa Baba yake

Wakati ambapo Yesu anakuja atakuwa na utukufu ule ule kama wa Baba yake

pamoja na malaika watakatifu

"atafuatana na malaika watakatifu"

Mark 9

Marko 09 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"kugeuka sura"

Maandiko mara nyingi huzungumzia utukufu wa Mungu kama mwanga mkubwa, wenye nguvu. Watu wanapoona mwanga huu, wanaogopa. Marko anasema katika sura hii kwamba mavazi ya Yesu yalikuwa na mwanga huu wa utukufu kiasi cha kuwawezesha wafuasi wake kuona kwamba Yesu kweli alikuwa Mwana wa Mungu. Wakati huo huo, Mungu aliwaambia kwamba Yesu alikuwa Mwana wake. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#glory and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#fear)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Neno la kukaza ukweli la kupita ukweli

Yesu alisema mambo ambayo hakutarajia wafuasi wake kuelewa kwa kweli. Wakati aliposema, "Ikiwa mkono wako unakukosesha, uukate" (Marko 9:43), alikuwa akizidisha sana ili waweze kujua kwamba wanapaswa kuacha mbali na chochote kilichowaanya kutenda dhambi, hata kama ni kitu walipenda au walidhani walihitaji.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Eliya na Musa

Eliya na Musa ghafla wanaonekana kwa Yesu, Yakobo, Yohana, na Petro, na kisha kutoweka. Wote wanne waliona Eliya na Musa, na kwa sababu Eliya na Musa walizungumza na Yesu, msomaji anapaswa kuelewa kwamba Eliya na Musa walionekana kimwili.

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe "Mwana wa Binadamu" katika sura hii (Marko 9:31). Lugha yako huenda haiwezi kuwaruhusu watu kujizungumzia wenyewe kana kwamba wanaongea juu ya mtu mwingine. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sonofman and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-123person)

Kitendawili

Kitendawili ni taarifa ya kweli inayoonekana kuelezea kitu kisichowezekana. Yesu anatumia kitendawili wakati anasema, "Ikiwa mtu anataka kuwa wa kwanza, lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote" (Marko 9:35).

<< | >>

Mark 9:1

Sentensi unganishi

Yesu amekuwa akizungumza kwa watu na wanafunzi wake kuhusu kumfuata. Siku sita badae, Yesu anaenda na wanafunzi watatu juu ya mlima pale alipobadilika, kwa hiyo anaonekana kama siku moja atakavyokuwa katika ufalme wa Mungu.

Na aliwaambia

"Na Yesu aliwaambia wanafunzi wake"

ufalme wa Mungu unakuja na nguvu

Ufalme wa Mungu unakuja kumwakilisha Mungu akijionyesha yeye kama mfalme. "Mungu anajionyesha yeye mwenyewe na nguvu kuu kama mfalme"

peke yao

Mwandishi anatumia "yao" hapa kusisitiza kuwa walikuwa wao wenyewe na kwamba Yesu tu, Petro, Yakobo na Yohana welienda mlimani.

alianza kubadilika

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "alionekana tofauti sana"

kabla yao

"mbele yao"

kung'aa sana

"kung'aa" au "inang'aa" Mavazi ya Yesu yalikuwa meupe yakitoa mwanga.

kubwa

"sana, sana"

meupe zaidi, meupe kuliko mng'arishaji yeyote duniani.

Kupausha kunaelezea mchakato wa kufanya pamba nyeupe ya kiasilia zaidi ya weupe kwa kutumia kemikali ya kupausha au amonia.

Mark 9:4

Eliya na Musa

Inaweza kuwa msaada kusema hawa wanaume ni "manabii wawili walio ishi muda kitambo, Musa na Eliya."

walikuwa wakiongea

Neno "wa" urejea kwa Eliya na Musa

Petro alimjibu na kumwambia Yesu

"Petro alimwambia Yesu." Hapa neno "alimjibu" linatumiwa kumtambulisha Petro katika mazungumzo. Petro alikuwa hajibu swali.

sisi

Hili neno urejea kwa Petro, Yakobo, na Yohana

vibanda

"mahema" Hii urejea kwa makao rahisi ya muda.

Kwa kuwa hakujua nini cha kusema, waliogopa sana

Sentensi hii iliyo kwenye mabano usema maelezo ya nyuma kuhusu Petro, Yakobo, na Yohana.

ogopa

kuogopa sana

Mark 9:7

wingu lilitokea na kuwafunika

"kutokea na kuwafunika"

Ndipo sauti ikatoka mawinguni

"Sauti" ni kirai cha Mungu. Pia, "sauti" inaelezwa kama "inatoka mawinguni", ikimaanisha kuwa walimsikia Mungu akuzungumza kutoka mawinguni. "Kisha Mungu alizungumza toka mawinguni"

Huyu ni mwanangu mpendwa. Msikieni

Mungu Baba aliezea upendo wake kwa mwanae mpendwa, Mwana wa Mungu.

Mwana mpendwa

Hili ni jina muhimu kwa Yesu.Mwana wa Mungu.

walipokuwa wakitazama

Hapa "wa" urejea kwa Petro, Yakobo, na Yohana.

Mark 9:9

aliwaamuru kutokumwambia mtu yeyote yale yote waliyoyaona, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka kwa wafu.

Hii inamaanisha kuwa alikuwa akiwaruhusu wawaambie watu kuhusu kile walichokiona tu baada ya kufufuka kutoka kwa wafu.

Kufufuka kutoka kwa wafu

"Kuwa unaishi tena baada ya kufa"

Waliyatunza mambo wao wenyewe.

"Hivyo hawakusema kuhusu mambo haya kwa yeyote ambaye hakuyaona pia yaliyotokea.

Mark 9:11

Eliya afanya kweli...watu watamchukia yeye?

Ijapokuwa Petro, Yakobo, na Yohana walishangaa nini Yesu angemaanisha na "kufufuka toka kwa wafu," walimuuliza badala ya ujio wa Eliya.

Walimuuliza

Neno "wa" urejea kwa Petor, Yakobo, na Yojhana.

Kwa nini waandishi wanasema kuwa Eliya anapaswa kuwa kwanza?

Unabii unasemswa kwamba Elijah ambaye angekuja toka mbinguni. Kisha Masihi, ambaye ni Mwana wa Adamu, atakuja kutawala na Mwana wa Adamu atakuja kuteseka na kuchukiwa na watu. Wanafunzi wamechanganyikiwa ni kwa namna gani hivi viiwili vinaweza kweli.

kwamba Eliya anapaswa kuja wa kwanza

Waandishi walifundisha kuwa Eliya angerudi tena ulimwenguni kabla ya Masihi kuja.

Kwa nini imeandikwa...achukiwe

Kama Yesu anafundisha wanafunzi wake, anauliza swali hili na kisha kuwaambia wanafunzi wake jibu. Hii inaweza kama sentensi. "Lakini pia nataka wewe ufikirie kile kilichoandikwa kuhusu Mwana wa Adamu. Maandiko yanasema kuwa anapaswa kuteseka kwa mambo mengi na kufanyiwa vibaya kama aliyechukiwa"

apate mateso mengi na achukiwe?

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "na watu walimtenda kama mtu aliyechukiwa"

na walimfanya kama walivyopenda

Inaweza kuwa msaada kusema nini watu walimfanya kwake. "na viongozi wetu walimfanyia vibaya, kama jinsi walivyo taka kufanya"

Mark 9:14

Sentensi unganishi

Wakati Petro, Yakobo, Yohana na Yesu walipokuja chini kutoka mlimani, waliwakuta waandishi wakibishana na wale wanafunzi wengine.

walirudi kwa wanafunzi

Yesu, Petro, Yakobo na Yohana walirudi kwa wanafunzi wengine ambao hawakuenda nao mlimani.

waandishi walikuwa wakibishana

Waandishi walikuwa wakibishana na wanafunzi ambao hawakuenda pamoja na Yesu.

linashangaa

Inaweza kuwa msaada kusema kwanini walishangaa. "walishangaa kwa kuwa Yesu alikuwa amekuja"

Mark 9:17

Sentensi unganishi

Kueleza nini waandishi na wale wanafunzi walikuwa wakibishania nini, baba wa yule kijana aliye na mapepo anamwambia Yesu kwamba amewauliza wanafunzi kutoa pepo kwa kijana, lakini hawakuweza. Yesu kisha analitoa pepo nje ya mvulana. Baadaye wanafunzi wanauliza kwa nini halishindwa kumtoa pepo.

Ana roho

Hii inamaanisha yule kijana ana roho chafu. "Ana roho chafu"

kutoka povu mdomoni

Wakati mtu anakuwa na mshtuko, wanaweza kuwa na shida ya kupumua au kuvuta hewa. Hii inasababisha kutoka povu mdomoni. Kama lugha yako ina njia kueleza hili, unaweza tumia.

anakuwa mgumu

"kuwa mwenye shingo ngumu" Inaweza kuwa msaada kusema kwamba ni mwili wake unaokuwa mgumu.

hawakuweza

Inaweza kuwa msaada kuongeza maelezo yaliyokosekana. "hawakuweza kutoa roho chafu nje yake"

Aliwajibu

Ijapokuwa alikuwa ni baba wa kijana aliyefanya ombi kwa Yesu, Yesu anaitikia kwa umati wote. Hii inaweza kusemwa kwa usahihi. "Yesu aliitikia kwa umati"

Kizazi cha wasioamini

"Nyie kizazi cha wasioamini" Yesu anaita umati wake hivi, kama anavyoanza kuwajibu.

nitakaa nanyi kwa muda gani?...nitachukuliana nanyi

Yesu anatumia maswali haya kueleza kukatishwa tamaa kwake. Yote maswali yana maana ile ile. Yanaweza kuandikwa kama sentensi. " Nimechoshwa na kutoamini kwenu!" au "Kutoamini kwenu kumenichosha! Nashangaa kwa muda gani nitachukuliana nanyi."

Nitachukuliana nanyi

"nitachukuliwana nanyi" au "kuvumialiana nanyi"

Mleteni kwangu

"Mleteni mvulana kwangu"

Mark 9:20

roho

Hii urejea kwa roho chafu.

tetemeko

Hii ni hali ambayo mtu hana wa uwezo wa kujiongoza juu ya mwili wake, na mwili wake hutikikisika.

Tangu ujana wake

"Tangu alipokuwa mtoto mdogo." Inaweza kuwa msaada kusema kama sentensi nzima. "Amekuwa hivi tangu alipokuwa mtoto mdogo"

Uwe na huruma

"hisi huruma"au " uwe na wema"

Mark 9:23

Kama uko tayari?

Yesu anakemea wasiwasi wa mtu. Hii swali linaweza kuandikwa tofauti au kama sentensi. "Yesy akamwambia, "Kwanini unasema, "kama uko tayari"? au " Yesu alimwambia, 'Usingelikuwa umesema.

unaweza

Inaweza kuwa msaada kuongeza maelezo yaliyokosekana. "unaweza kufanya lolote"

Kila kitu kinawezekana kwa yeyote aaminiye.

Hii inaweza kuandikwa kama dhahania dogo na katika kauli tendaji. "Mungu anaweza kufanya chochote kwa ajili ya watu wanaomwamini yeye"

kwa yeyote

"kwa yeyote mtu"

amini

Hii inarejea kwa kumwamini Mungu.

Nisaidie kutokuamini kwangu

Mwanaume anamuuliza Yesu kumsaidia kushinda kutoamini na kuongezea imani yake. "Nisaidie wakati ninashindwa kuamini" au "Nisaidie kuwa imani zaidi"

kundi linakimbilia kwao

Hii inamaanisha kuwa watu zaidi walikuwa wanakimbilia kule aliko Yesu na kundi lilikuwa linakuwa kubwa.

wewe roho bubu na kiziwi

Maneno "bubu" na "kiziwi" yanaweza kufafanuliwa. "Wewe roho chafu, wewe unaye sababisha kijana kutokuwa na uwezo wa kusikia na kuongea."

Mark 9:26

Alilia kwa nguvu

"Roho mchafu alilia kwa nguvu"

Mvulana alionekana kama aliyekuwa amekufa

Mvulana alionekana kufa" au Mvulana kama amekufa."

kumhangaisha mtoto

"kumtetemesha kijana"

alimtoka

Inaweza kuwa msaada kuongeza maelezo yaliyokosekana. "alitoka nje mwa kijana"

Mtoto alionekana kama amekufa

Muonekano wa kijana unalinganishwa na mtu aliyekufa.

ndipo wengi

"ndipo watu wengi"

alimchukua kwa mkono

Hii inamaanisha kuwa Yesu alimshika mkono mvulana kwa mkono wake.

mwinue juu

"alimsaidia kumwinua juu"

Mark 9:28

faragha

Hii inamaanisha walikuwa peke yao.

mtupe nje

"mtupe roho mchafu nje." Inaweza kuwa msaada kuongeza maelezo yaliyokosekana. "mtupe roho mchafu nje mwa kijana"

Aina hii haiwezi kuondoka isipokuwa kwa maombi

Neno, "haiwezekani" na "isipokuwa" yote yako kinyume. Katika lugha nyingine ni asili zaidi kutumia maelezo mazuri. "Aina hii inawezatu kuondolewa kwa maombi."

Aina hii

Hii inaelezea roho chafu.

Mark 9:30

Sentensi unganishi

Yesu na wanafunzi wake waliiacha nyumba pale walipokuwa na Yesu baada ya kumponya kijna aliyekuwa na pepo. Anatumia muda kuwafundisha wanafunzi wake peke yao.

Kupitia

Kwenda kupitia",au"Kupitia kwa"

Walienda nje ya hapo

"Yesu na wanafunzi wake waliondoka mkoa huo"

kupitia

"alisafiri kupitia"

kwa kuwa alikuwa anafundisha wanafunzi wake

Yesu alikuwa anafundisha wanafunzi wake kwa faragha, mbali na umati.

Mwana wa Adamu

Hapa Yesu anarejea kwake mwenyewe kama Mwana wa Adamu. Hili ni jina muhimu sana kwa Yesu. "Mimi, Mwana wa Adamu,"

katika mikono ya wanaume

Hapa "mikono" ni kirai cha kuthibiti. "katika udhibiti wa wanaume"

Wakati alipouwawa, baada ya siku tatu

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Baada ya kumuua na siku tatu kupita."

walikuwa wameogopa kumuuliza

Walikuwa wameogopa kumuuliza Yesu hii sentensi ilikuwa ina maana gani. "walikuwa wameogopa kumuuliza ilimaanisha nini"

Mark 9:33

Sentensi unganishi

Wakati ambapo wanafika Karperinaumu, Yesu anafundisha wanafunzi wake kuwa watumishi wanyenyekevu.

walikuja

"walifika." Neno "wali" urejea kwa Yesu na wanafunzi wake.

kujadili

"wanajadili wao kwa wao"

walikuwa kimya

Walikuwa kimya kwa sababu waliona aibu kumwambia Yesu walichokuwa wanajadili. "walikuwa kimya kwa sababu waliona aibu"

nani alikuwa mkubwa

Hii inaweza kuwa msaada kuongeza taarifa iliyokosekana. "nani alikuwa mkubwa kati yao"

Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.

Hapa neno "kwanza" na "mwisho" ni maneno yanayo pishana. Yesu anazungumza kuwa "muhumimu zaidi" kama kuwa wa "kwanza" na kuwa "usiye wa muhimu zaidi" kama kuwa wa "mwisho" Kama yeyote anataka Mungu amjali ya kuwa yeye ni wa muhimu zaidi, anapaswa kujiona yeye kuwa asiye na umuhimu zaidi kwa wote"

kwa wote...kwa wote

"kwa watu wote...kwa watu wote"

Mark 9:36

katikati yao

"miongoni mwao" Neno "mwao" urejea kwa umati

Akamchukua katika mikono yake

Hii inamaanisha kuwa alimkumbatia mtoto au kumnyanyua na kumweka katika mapaja yake.

mtoto kama huyu

"mtoto kama huyu"

kwa jina langu

Hii inamaanisha kufanya kitu fulani kwa sababu ya upendo kwa Yesu. "kwa sababu wananipenda" au "kwa ajili yangu"

aliyenituma

Hii urejea kwa Mungu aliyemtuma kwa ulimwengu. "Mungu amenituma mimi"

Mark 9:38

Yohana alimwambia

"Yohana alimwambia Yesu"

fukuza mapepo

"Kuyaondoa mbali mapepo"

kaitka jina lako

Hapa "jina" lina husishwa na mamlaka ya Yesu na nguvu

hanifuati mimi

Hii ina maana kwamba hayuko miongoni mwa makundi ya wanafunzi

Mark 9:40

asiyekuwa kinyume nasi

"asiyetupinga sisi"

yuko upande wetu

Hii inaweza kuelezwa kwa usahihi inavyomaanisha. "ni kujaribu kupata malengo yale yale ambao tunayo"

Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu uko na Kristo

Yesu anazungumza kumpa yeyote kikombe cha maji kama mfano wa mtu anavyoweza kumsaidia mwingine. Huu mfano wa kumsaidia mwingine kwa njia yoyote.

hapotezi

Hii ni sentensi iliyo hasi inasisitiza maana ya chanya. Katika baadhi ya lugha, ni halisia zaidi kutumia sentensi chanya.

Mark 9:42

Jiwela kusagia

Jiwe kubwa juu yake husagwa nafaka kupataunga

kama mkono wako utakuwa kuzuizi

Hapa "mkono" ni kirai cha kutamani kufanya kitu kiovu ambacho utakifanya kwa mkono wako.

kuingia katika maisha bila mkono

"kukosa mkono na kisha kuingia katika masiha"

kuingia katika maisha

Kufa na kisha kuanza kuishi umilele kama inavyosemwa kuingia katika maisha.

bila mkono

kukosekana kwa kiungo cha mwili kwa matokeo ya kutolewa au kuumizwa. Hapa inarejea kwa kukosekana kwa mkono.

moto usiozimika

"mahali ambapo moto usiozimika"

Mark 9:45

na kutupwa kuzimu

na Mungu kuwatupa kuzimuni"

Mark 9:47

funza wake

"funza ambao hula miili ya waliokufa."

Mark 9:49

Kwa kuwa kila mmoja atakolezwa na moto.

Hapa Yesu anazungumzia kila moja atakaswe kwa kupitia mateso. Yesu anazungumzia mateso kama moto na kuwapa mteso watu kama inavyoweza kutumika kwa chumvi kwao. Hii inaweza kusemwa pia katika kauli tendi. "Kama chumvi inavyotakasa dhabihu, Mungu atamtakasa kila mmoja kwa kuwaruhu kuteseka"

ladha yake

"ina ladha ya chumvi"

utaifanyaje iwe na ladha yake tena?

Hii inaweza kuandikwa kama sentensi. "hauwezi kuifanya ladha yake tena."

ladha yake tena

"ladha ya chumvi tena"

Muwe na chumvi miongoni mwenu wenyewe

Yesu anazungumza kufanya mambo mazuri kwa kila mmoja kama hayo mazuri ni chumvi ambayo watu wanakuwa nayo. "Fanya vizuri kwa kila mmoja, kama chumvi iongezavyo ladha kwa chakula"

Mark 10

Marko 10 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka nukuu kutoka kwenye Agano la Kale kwa upande wa kulia zaidi kuliko maandishi yote. ULB inafanya hivyo kwa nukuu zilizotajwa katika 10:7-8.

Dhana maalum katika sura hii

Mafundisho ya Yesu kuhusu talaka

Mafarisayo walitaka kutafuta njia ya kumlazimisha Yesu aseme kwamba ni vizuri kuvunja sheria ya Musa, hivyo wakamwuliza kuhusu talaka. Yesu anaelezea jinsi Mungu aliyepanga ndoa kwa mwanzo, kwa kuonyesha kosa la mafundisho ya talaka ya Mafarisayo.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Mfano

Wasemaji hutumia mifano kama picha ya vitu vinavyoonekana kwa kueleza ukweli usiyoonekana. Wakati Yesu aliposema juu ya "kikombe nitakachokunywa," alikuwa akizungumzia juu ya maumivu atakapoteswa nayo msalabani kuwa mfano wa kinywaji ya uchungu na sumu katika kikombe.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kitendawili

Kitendawili ni taarifa ya kweli inayoonekana kuelezea kitu kisichowezekana. Yesu anatumia kitendawili wakati anasema, "Yeyote anayetaka kuwa mkuu kati yenu lazima awe mtumishi wenu" (Marko 10:43).

<< | >>

Mark 10:1

Sentensi unganishi

Baada ya Yesu na wanafunzi wake kuondoka Karpenaumu, Yesu anawakumbusha Mafarisayo, pamoja na wanafunzi wake, nini Mungu anategemea katika ndoa na talaka

Yesu aliondoka eneo hilo

Wanafunzi wa Yesu walikuwa wakisafiri pamoja naye. Walikuwa wakiondoka Kapernaumu. "Yesu na wanafunzi wake waliondoka Kapernaumu"

na eneo la mbele ya Mto Yorodani

"hii ilikuwa mbele ya Mto Yorodani" au "ilikuwa ng'ambo ya Mto Yorodani"

Aliwafundisha tena

Neno "ali" urejea kwa umati

ilivyokuwa kawaida yake kufanya

"ilikuwa kawaida yake" au "alikuwa desturi yake kufanya"

Musa aliwaamuru nini

Musa alitoa sheria kwa mababu zake, ambazo walipaswa kuzifuata. "Musa aliwaamuru nini mababu wetu katika hili"

cheti cha kuachana

Hii ilikuwa ni karatasi kusema kuwa mwanamke hakuwa tena mke wake.

Mark 10:5

Mioyo yenu migumu

Wakaidi ninyi

Mark 10:7

Sio mwili tena, bali mwili mmoja

Hili ni fumbo kuonyesha muungano wa kimwili wa karibu kama mme na mke.

Mark 10:10

Walipokuwa ndani

"Wakati ambapo Yesu na wanafunzi walikuwa"

ndani ya nyumba

Wanafunzi wake Yesu walikuwa wakizungumza naye kwa faragha. walikuwa peke yao ndani ya nyumba"

wakamwuliza tena kuhusu hili

Neno "hili" urejea kwa mazungumzo aliyokuwa nayo Yesu pamoja na Mafarisayo kuhusu talaka.

Yeyote

"kama mtu yeyote"

anafanya uzinzi dhidi yake

Hapa "yake" urejea kwa mwanamke aliyemuoa kwanza

anafanya uzinzi

Inaweza kuwa msaada kuongeza taarifa zilizosahaulika. "anafanya uzinzi dhidi yake" au "anafanya uzinzi dhidi ya mme wa kwanza"

Mark 10:13

Waruhusuni waatoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie

Sentensi hizi mbili zina maana sawa, zimerudiwa kwa ajili ya msisitizo. Katika luga zingine ni asili zaidi kusisitiza kwa njia nyingine. AT: " Muwe na uhakika wa kuwaruhusu watoto wadogo kuja kwangu."

Msizuie

Hii ni hasi mbili. Katika baadhi ya lugha ni asili zaidi kutumia taarifa chanya. AT: "ruhusu"

Mark 10:15

yeyote

"kama yeyote"

kama mtoto mdogo

Yesu analinganisha namna gani watu wanapaswa kuupokea ufalme wa Mungu na namna watoto wanavyoweza kuupokea. "katika tabia hiyo kama mtoto angefanya"

asiyeupokea ufalme wa Mungu

"hawataweza kumpokea Mungu kama mfalme wao"

hakika hawezi kuuingia

Neno "kuui" urejea kwa ufalme wa Mungu.

Kisha akawachukua watoto mikononi mwake

"aliwakumbatia watoto"

Mark 10:17

Kwanini unaniita mwema

AT: Unapaswa kufikiria kwa umakini unacho ashiria (AU, kile ambacho unaashiria nilivyo) kwa kuniita mwema, kwa sababu Mungu pekee ndiye mwema!

Mark 10:20

Unapungukiwa kitu kimoja

"Kuna kitu kimoja unapngukiwa." Hapa Yesu anazungumza juu ya tendo la kutofanya kitu fulani" kama "kupungukiwa." "Kuna kimoja ambacho haujafanya"

unapungukiwa

hauna kitu fulani

uwape masikini

Hapa neno "u" urejea kwa vitu anavyouza na ni kifungu cha maneno kinachosimama badala ya pesa mtu anayopokea anapouza. "wape masikini pesa"

masikini

Hii urejea kwa masikini. "watu masikini"

hazina

"utajiri"

alikuwa na miliki nyingi

"alimiliki vitu vingi"

Mark 10:23

Ni rahisi kwa Ngamia kupita kwenye jicho la sindano, kuliko tajiri kuingia kwenye ufaulme wa Mungu.

Haiwezekani kwa Ngamia kuingia kwenye jicho la sindano. Ni ngumu zaidi kwa watu matajiri kuamua kumruhusu Mungu atawale maisha yao."

Jicho la sindano

"Jicho la sindano" ni shimo lililo juu ya sindano.

Mark 10:26

Ni nani atakaye okolewa?

"Hivyo hakuna atakaye okolewa."

Mark 10:29

hayupo mmoja ambaye amebaki...ambaye hatapokea

"yeyote aliye acha...atapokea."

kwa ajili yangu

"kwa faida yangu" au "kwa yangu tena"

Dunia hii

"maisha haya" au "umri huu uliopo"

Dunia ijayo

"maisha yajayo" au "umri ujao"

Mark 10:32

Mwana wa Mtu atatolewa

"watu watamtoa Mwana wa Mtu" au "watu watamwachilia Mwana wa Mtu."

Mark 10:35

tu...tu

Haya maneno urejea peke yake kwa Yakobo na Yohana

katika utukufu wako

"wakati ambapo unatukuzwa." Maneno haya "utukufu wako" urejea wakati Yesu anatukuzwa na kutawala katika ufalme wake. "wakati ambapo unaongoza katika ufalme wako"

Mark 10:38

kikombe nitakacho kinywea

Yesu anatumia maneno haya kurejea kwenye mateso ambayo yuko karibu kuyapitia.

ubatizo ambao nitabatizwa kwao

Yesu anatumia maneno haya kurejea kwenye mateso ambayo yuko karibu kuyapitia.

Mark 10:41

wale wanaokusudiwa utawala

"wale wanaofikiriwa kuwa watawala

Kutawala

"kudhibiti" "kuwa na nguvu juu ya"

zoezi

"kufanya matumizi ya"

Mark 10:43

kuwa mkubwa

"kuwa katika heshima" au "Kupongezwa"

yeyote

mtu yeyote

kwa kuwa Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa

"Kwa kuwa Mwana wa Mtu hakuja kwa watu ili wamtumikie"

Mark 10:46

Batimausi

jina la mtu

Timausi

Hili lilikuwa ni jina la baba yake na kipofu mwombaji.

Mark 10:49

aliamuru aitwe

"aliamuru wengine wamwite"

kuwa jasiri

"usiogope"

Mark 10:51

Kuona

"uwezo wa kuona"

Mark 11

Marko 11 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi kwa upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB hufanya hivi kwa mashairi katika 11:9-10,17, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Punda na mwana-punda

Yesu aliingia Yerusalemu juu ya mnyama. Kwa njia hii alikuwa kama mfalme aliyeingia mjini baada ya kushinda vita muhimu. Pia, katika Agano la Kale, wafalme wa Israeli walikuwa wanapanda punda. Wafalme wengine walipanda farasi. Kwa hiyo Yesu alikuwa akionyesha kwamba alikuwa mfalme wa Israeli lakini hakukuwa kama wafalme wengine.

Mathayo, Marko, Luka, na Yohana wote waliandika juu ya tukio hili. Mathayo na Marko waliandika kwamba wanafunzi walimletea Yesu punda. Yohana aliandika kwamba Yesu alipata punda. Luka aliandika kwamba walimletea mwana-punda. Mathayo tu aliandika kwamba kulikuwa punda pamoja na mwana-punda. Hakuna anayejua hakika ikiwa Yesu alipanda punda au mwana-punda. Ni bora kutafsiri kila maneno haya kama yanoyoonekana katika ULB bila kujaribu kuwafanya wote wanasema jambo sawa. (Ona: Mathayo 21:1-7 na Marko 11:1-7 na Luka 19:29-36 na Yohana 12:14-15)

<< | >>

Mark 11:1

Bethfage

ni jina la kijiji

Mark 11:4

Walikwenda

"Wanafunzi wawili walikwenda"

mwanapunda

Hii urejea kwa punda mdogo aliye na uwezo wa kubeba mtu.

Walizungumza

"Waliitikia"

kama Yesu alivyowaambia

"kama Yesu alivyowaambia kuitikia." Hii inarejea namna Yesu alivyokwisha waambia kuitikia kwa maswali ya watu kuhusu kumchukua mwanapunda.

wakawaacha waende

Hii inamaanisha kuwa waliwaruhusu kuendelea kufanya walichokuwa wakifanya"

Mark 11:7

Hosana

Maana ya neno hili haiko wazi, bali kwa uhakika lilitafsiriwa vizuri zaidi kama kuelezea ukaribisho na kusifu, kama ndani "Chini" au"Kumsifu Mungu"

Mark 11:11

wakati ulikuwa umeenda

"kwa sababu ilikuwa jioni"

alikwenda Bethania pamoja nao kumi na wawili

"yeye na wanafunzi wake walikwenda Yerusalemu na kwenda Bethania"

walipokuwa wakirudi kutoka Bethania

"wakati walipokuwa wakirudi Yerusalemu kutoka Bethania"

Mark 11:13

Sentensi unganishi

Hii ilitokea wakatik Yesu na wanafunzi wake wanatembea kuelekea Yerusalemu.

kama angeweza kupata chochote juu yake

"kama kulikuwa na tunda lolote juu yake"

hakupata chochote isipokuwa majani

Hii inamaanisha kuwa hakupata mtini wowote. "alipata majani peke yake na hakuna mtini katika mti"

majira

"wakati wa mwaka"

Aliuambia, "Hakuna yeyote atakayekula tunda kutoka kwako tena

Yesu anauambie kwa mtini na kuulaani. Anazungumza nao ili wanafunzi wake wasikie.

Anauambia mti

"Alizungumza na mtu"

Na wanafunzi wake wakasikia

Neno "wa" urejea kwa Yesu anazungumza kwa mtini.

Mark 11:15

Walikuja

"Yesu na wanafunzi wake walikuja"

kuanza kuwatoa nje wauzaji na wanunuzi ndani ya hekalu

Yesu anawafukuza watu hawa nje ya hekalu. Hii inaweza kuandikwa kwa usahihi. "kuanza kuwatoa wauzaji na wanunuzi nje ya hekalu"

wauzaji na wanunuzi

"watu waliokuwa wakinunua na kuuza"

Mark 11:17

Je haikuandikwa, 'Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote'?

"Imeandikwa ndani ya maandiko kwamba Mungu alisema, 'Ninataka nyumba yangu kuitwa nyumba mahali watu kutoka mataifa yote wanapaswa kusali', lakini ninyi majambazi mmeifanya kama pango mahali mnakoweza kujificha! Ninyi mnajua hivyo!"

Mark 11:20

Mti wa mtini ulikauka mpaka kwenye mizizi yake

"mti wa mtini ulikauka mpaka kwenye mizizi yake na ulikufa."

Mark 11:22

kama hatakuwa na mashaka moyoni mwake lakini huamini

"kutokuwa na mashaka" ina maana mbili hasi "hakika amini." Vifungu hivi vyote vina maana sawa iliyorudiwa kwa mkazo. Lugha zingine zimesisitiza kwa njia tofauti. Wakati: Kama hakika huamini"

Mark 11:24

Wakati mnaposimama na kusali

Ni kawaida kwa desturi za kiyahudi kusimama wakati tusalipo kwa Mungu.

Mark 11:27

Kwa mamlaka gani mnafanya mambo haya

Maneno "mambo haya" yanalejea kwa Yesu kupindua meza za wauzaji hekaluni na kuzungumza dhidi ya vitu walivyofanya na walichofundisha.

Kwa mamlaka gani mnafanya mambo haya, na ni nani aliyewapa ninyi mamlaka ya kuyafanya.

"Hamna mamlaka kufanya mamba haya kwa sababu hatujawapa ninyi mamlaka."

Mark 11:29

Ubatizo wa Yohana, ulitoka mbinguni au ulitoka kwa watu?

Pamoja na kwamba Yesu alilijua jibu la swali hili, aliwauliza kuwajaribu viongozi wa dini sababu ya kumuuliza yeye.

Mark 11:31

Kama tukisema, 'Kutoka mbinguni'

Inaweza kuwa msaada kuongoza taarifa zilizokosekana. "Kama tukisema 'ilitoka mbinguni"

Kutoka mbinguni

Hapa "mbinguni" urejea kwa Mungu. "Kutoka kwa Mungu"

hamkumwamini

Neno "ham" urejea kwa Yohana mbatizaji.

Lakini kama tukisema 'Kutoka kwa wanadamu,'

Inaweza kuwa msaada kuongeza taarifa zinazokosekana katika majibu yao. "Lakini kama tukisema, 'kutoka kwa wanadamu"

Kutoka kwa wanadamu

"Kutoka kwa watu"

Kama tukisema, 'Kutoka kwa wanadamu;...

Viongozi wa dini hawasemi kuwa tatizo lingeweza kuwa kama wangetoa jibu hilo, lakini walifikiri juu yake. "Lakini kama tukisema, 'Kutoka kwa wanadamu, hiyo haitakuwa vizuri" au "Lakini hatutaki kusema kutoka kwa wanadamu"

Waliwaogopa watu

Mwandishi, Mariko, anaeleza kwanini viongozi wa dini hawakutaka kusema kuwa ubatizo wa Yohana ulitoka kwa wanadamu. Hii inaweza kusemwa kwa usahihi. "Walisema wao kwa wao kwa sababu waliwaogopa watu" au "Hawakutaka kusema kuwa ubatizo wa Yohana ulitoka kwa wanadamu kwa sababu waliwaogopa watu.

wote walishika

"watu waliamini"

Hatujui

Hii inaweza kuwa msaada kuongoza taarifa zinazokosekana. "Hatujui ubatizo wa Yohana ilitoka wapi"

Mark 12

Marko 12 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi kwa upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivyo kwa mashairi katika 12:10-11,36, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Hali ya Kudhania

Hali za kudhania ni hali ambazo hazikutendeka. Watu huelezea hali hizi ili waweze kujifunza kile wasikilizaji wao wanafikiri ni nzuri na mbaya au sahihi na zisizo sahihi. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-hypo)

<< | >>

Mark 12:1

pangisha shamba la mizabibu

Mwenye shamba aliwapangisha wengine kuitunza mizabibu.

Mark 12:4

Akamtuma kwao

"mumiliki wa shamba la mzabibu alituma waoteshaji wa mzabibu"

wakamjeruhi kichwani

Hii inaweza kuandikwa kwa usahihi. "walimpiga huyo moja kwenye kichwa, na kumuumiza vibaya"

bado mwingine...wengine wengi

Haya maneno urejea kwa watumishi wengine. "bado mtumishi mwingine...watumishi wengine wengi"

Waliwatendea wengine wengi mambo kama hayo hayo.

Hii inarejea kwa watumishi waliotumwa na mwenye shamba. Maneno "hayo hayo" urejea kwa jinsi walivyotendewa. Hii inaweza kuandikwa kwa usahihi. "Waliwatendea watumishi wengine wengi waliotumwa na mwenye shamba"

Mark 12:6

Watumishi ya shamba

Wakulima wa mizabibi waliokuwa wamapangishwa shamba la mizabibu kutoka kwa mwenye shamba.

Mark 12:8

Kwahiyo, Je! Atafanya nini mmiliki wa shamba la mizabibu?

"Hivyo nitawaambia kile mwenye shamba la mizabibu atakavyofanya."

Mark 12:10

Hamjapata kusoma andiko hili?

"Sasa fikiri kwa uangalifu kuhusu haya maneno, ambayo umeshayasoma katika maandiko."

Mark 12:13

Kwanini mnanijaribu

"Ninajua mnachojaribu cha kunifanya niseme jambo lililo kinyume ili mpate nafasi ya kunishitaki."

dinari

Ni sarafu iliyokuwa na thamani ya mshahara wa siku.

Mark 12:16

Walimletea moja

"Mafarisayo na Maherodia walimletea sarafu ya serikali ya Kirumi"

Mpeni Kaisari kwa vitu vya kaisari

"Toeni kwa serikali ya Roma vitu ambavyo vinamilikiwa na serikali ya Roma

Mark 12:18

Musa alituandikia kuwa, ikiwa ndugu ya mtu...kuwa na mtoto kwa ajili ya ndugu yake.

Musa aliandika kuwa kama ndugu wa mttu akifa... ndugu yake ajipatie mtoto kwa mke aliyeachwa kwa ajili ya ndugu yake.

Mark 12:20

Wakati wa ufufuo, watakapofufuka tena, atakuwa mke wa nani?

"Katika ufufuo, watakapofufuka tena, haitawezekana tena kuwa mke wa hao ndugu saba!"

Mark 12:24

Je! Hii siyo sababu kuwa mmopotoshwa...nguvu za Mungu?

"Mmekoseshwa kwasababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu."

Mark 12:26

wanafufuliwa

"Mungu anawafufua"

Mark 12:28

Sentensi unganishi

Mwandishi anamuuliza Yesu swali la akili, ambalo Yesu analijibu.

Alimuuliza

"Mwandishi alimuuliza Yesu"

iliyo ya muhimu zaidi katika zote..iliyo ya muhimu ni hii

Taarifa inayokosekana inaweza kuongozwa. "amri iliyo ya muhimu zaidi katika zote...amri iliyo ya muhimu anasema"

Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja.

"Sikiliza, Israeli! Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja"

kwa moyo wako yote, kwa roho yako yote

"Moyo" na "roho" ni mifano ya utu wa ndani na tamaa zake na hisia. "kwa chote unachotaka na kujisikia"

kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote

"akili" urejea kwa namna mtu anavyofikiri na "nguvu" urejea kwa nguvu za mtu kufanya mambo. "kwa yote unayofikiri, na kwa yote unayofanya"

umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe

Yesu anatumia mfanano kulinganisha namna watu wanavyopaswa kupendana wao kwa wao kwa upendo ule ule kama wanavyojipenda wenyewe"

zaidi ya hizi

Hapa neno "hizi" urejea kwa amri mbili ambazo Yesu alikuwa amewambia watu.

Mark 12:32

Sentensi unganishi

Yesu anamsifu mwandishi juu ya mawazo yake juu ya kila alichosema Yesu.

Vema

"Jibu zuri"

Mungu ni mmoja

Hii inamaanisha kuwa kuna Mungu mmoja tu.

hakuna mwingine

Iliyokosekana inaweza kuongezewa. "hakuna Mungu mwingine"

kwa moyo wote...kwa ufahamu wote... kwa nguvu zote

"Moyo" ni mfano utu wa ndani wa mtu na tamaa zake na hisia. "Ufahamu" urejea kwa kufikri na "nguvu" urejea kwa nguvu za mtu kufanya.

ule moyo...ule ufahamu...zile nguvu

Neno "ule" limewekwa katika maumbo yai ambapo neno "ako" limeachwa. Linaweza kuongezwa.

kumpenda jirani kama mwenyewe

Mfanano huu unalinganishwa namna watu wanavyopaswa kupendana wao kwa wao kwa upendo ule ule wanavyojipenda wenyewe.

ni muhimu mno kuliko

Lugha hii inamaanisha kuwa kitu fulani ni muhimu mno kuliko kitu kingine. Kwa hali hii, amri hizi mbili ni zaidi ya kumfurahisha Mungu kwamba matoleo ya kuteketeza na dhabihu.

Wewe hauko mbali na ufalme wa Mungu

Hii inaweza kusemwa katika mtindo wa chanya. Hapa Yesu anazungumza juu ya mtu aliye tayari kujitoa kwa Mungu kama mfalme kama aliye karibu kimwili kwa ufalme wa Mungu, kama inavyofananishwa na eneo halisi.

hakuna hata mmoja aliye thubutu

Hii inaweza kusemwa katika mtindo wa chanya. "kila moja aliogopa"

Mark 12:35

Je! Ni kwa jinsi gani waandishi husema Kristo ni mwana wa Daudi?

"Hawa watu hufundisha sheria ya kiyahudi lazima hawako sahihi wanaposema kwamba Kristo ni mtu tu wa kawaida wa uzao wa Mfalme Daudi!"

mwana wa Daudi

Neno "mwana" limetumika hapa kuelezea ukoo.

Ni kwa jinsi gani mwana wa Daudi?

"hivyo hawezi kuwa mwana wa Daudi!"

Mark 12:38

salamu walizopokea kwenye masoko

Nomino "salamu" inaweza kuelezwa pamoja na kitendo "salimu". Hizi salamu zilionyesha kuwa watu waliwaheshimu waandishi. "na kusalimiwa kwa heshima kwenye masoko" au "na kwa watu kuwasalimu kwa heshima kwenye masoko"

Wanakula nyumba za wajane

Hapa Yesu anawaeleza wandishi wakiwadanganya wajane na kuiba nyumba zao kama kula nyumba zao.

Hawa watu watapokea hukumu iliyo kuu

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu hakika atawahukumu kwa hukumu kuu" au "Mungu kwa hakika atawahukumu kwa ukali"

watapokea hukumu kuu kuliko

Neno "kuliko" humaanisha kulinganisha. Hapa kulinganisha ni watu wengine waliohukumiwa. "watapokea hukumu kuu kuliko watu wengine"

Mark 12:41

sarafu ndogo mbili

"sarafu mbili ndogo", ni sarafu yenye thamani kidogo

Mark 12:43

Amini nawaambia

Ni hakika ya kile ninachowaambia

sanduku la sadaka

sanduku hili lilikuwa na kukusanyia sadaka za watu wote hekaluni

vingi

vingi zaidi

umasikini

"upungufu" au "Kutokuwa na chochote"

Mark 13

Marko 13 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivyo kwa mashairi katika 13:24-25, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Kurudi kwa Kristo

Yesu alisema mengi juu ya kile kitatokea kabla ya kurudi kwake (Marko 13:6-37). Aliwaambia wafuasi wake kwamba mambo mabaya yatatokea ulimwenguni na mambo mabaya yatawatokea kabla ya kurudi, lakini walistahili kuwa tayari kwa kurudi kwake wakati wowote.

<< | >>

Mark 13:1

Maelezo ya ujumla

Walipoondoka eneo la hekaluni, Yesu anawambia wanafunzi wake nini kitatokea badae katika hekalu zuri ambalo Herode mkuu alilijenga.

mawe haya yakushangaza na majengo

"Mawe" urejea kwa mawe yaliyotumiwa kujenge. ""majengo yakushangaza na mawe yalitokana nayo"

Unaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja

Hili swali linatumiwa kuleta umakini kwa majengo. Hii inaweza kuandikwa kama sentensi. "Tazama haya majengo makubwa sasa, lakini hakuna jiwe hata moja"

Hakuna hata jiwe moja litakalo salia juu ya jingine ambalo halitaangishwa chini.

Hii inamaanisha kuwa maadui wa kijeshi wataangusha mawe. Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Hakuna jiwe hata moja litakalo salia juu ya jingine, kwa kuwa maadui wa kijeshi watakuja na kubomoa majengo haya."

Mark 13:3

Sentensi unganishi

Katika kujibu maswali ya wanafunzi kuhusu kubomolewa kwa hekalu na nini kitatokea, Yesu anawambia nini kitatokea badae.

Naye alipokuwa amekaa juu ya Mlima wa Mizeituni nyuma ya hekalu, Petro

Walipokuwa wamefika kwenye Mlima wa Mizeituni, na Yesu kuwa amekiti chini. Taarifa zinaweza kufanya kwa usahihi. "Baada ya kufika kwenye Mlima Mizeituni, ambao ulikuwa nyuma ya hekalu, Yesu chini.

faraga

"wakati ambapo walikuwa peke yao"

haya mambo yanatokea...yako karibu kutokea

Hii inarejea kwa kile Yesu amekwisha sema kitatokea kwa mawe ya hekalu. Hii inaweza kufanywa wazi. "haya mambo hutokea kwa majengo ya hekalu... yako karibu kutokea kwa majengo ya hekalu"

wakati ambapo haya yote

"kwamba haya yote"

Mark 13:5

kwao

"kwa wanafunzi wake"

kuwapotosha

Yesu anawaonya wanafunzi wake wasidaganywe na yeyote nini kitatokea. Hapa"kuwapotosha" ni mfano wa kudanganya.

kwa jina langu

Maana talajiwa ni 1)kudai mamlaka yangu" au 2) kudai kuwa Mungu amewatuma"

Mimi ndiye

"Mimi ni Kristo"

watawapotosha wengi

Hapa "kuwapotosha" ni mfano ukimaanisha kudanganya. "nitawadanganya watu wengi"

Mark 13:7

Mtakaposikia vita na tetesi za vita

Maana talajiwa ni 1)"sikia sauti halisi ya vita ikiwa karibu na taarifa za vita kwa mbali" au 2)sikia vita ambavyo ni halisia vinatokea na watu kusema kuwa vita vinaenda kuana"

tetesi

maneno ambayo siyo rahisi kugundua kama yako sahihi au hapana

lakini mwisho bado

Hii inarejea kwa mwisho wa ulimwengu. Taarifa zinazokosekana zinaweza kuongezewa. "lakini siyo mwisho wa ulimwengu. "

litainuka kinyume

Lugha hii inamaanisha kupigana na mtu mwingine. "nitapigana kinyume"

Taifa litainuka kinyume na taifa jingine

Taarifa zinazokosekana zinaweza kuongezwa. "taifa litainuka kinyume na taifa" au "taifa litapigana kinyume na taifa"

Huu ni mwanzo wa utungu.

Yesu anazungumza juu ya maafa kama mwanzo wa utungu kwa sababu mambo makali yatatokea baada ya hayo. "Haya matokeo yatakuwa kama utungu wa kwanza wa mwanamke anaposumbuka wakati anapozaa mtoto. Watasumbuka zaidi baada ya hayo"

Mark 13:9

Iweni macho

"Iweni tayari kwa yale watu watawafanyia"

watawapeleka hadi

Hii inamaanisha kuwafunga watu fulani na kuwaweka chini ya usimamizi wa mtu mwingine.

mtapigwa

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "watu watawapiga"

Mtasimamishwa mbele

Hii inamaanisha kuwekwa katika kujaribiwa na kuhukumiwa. "Mtawekwa katika kujaribiwa kabla" au "Mtaletwa katika kujaribiwa na kuhukumiwa"

kwa ajli yangu

"Kwa sababu yangu" au "kusababishwa na mimi"

kama ushuhuda kwao

Hii inamaanisha watashuhudia kuhusu Yesu. Hii inaweza kufanywa wazi. "na kuwashuhudia kuhusu mimi" au "na mtawambia kuhusu mimi"

Lakini injili lazima kwanza ihubiriwe kwa mataifa yote.

Yesu bado anazungumza juu ya mambo ambayo lazima yatatokea kabla ya mwisho kuja. Hii inaweza kufanywa wazi. "Lakini injili ihubiriwe kwanza kwa mataifa yote kabla mwish haujaja"

Mark 13:11

kuwakabidhi

Hii inamaanisha kuwaweka chini ya usimamizi wa mtu mwingine. Kwa jambo hili, chini ya uzimamizi wa mamlaka.

lakini Roho Mtakatifu

Taarifa zinazokosekana zinaweza kuongezewa. "lakini Roho Mtakatifu atazungumza kupitia wewe"

Ndugu atamshitaki ndugu kuuawa

Ndugu atamshitaki ndugu kuuawa "Ndugu atamshitaki ndugu yake kuuawa" Hii inamaanisha kuwa ndugu atamsaliti ndugu yake na kusaliti huku kutasababisha ndugu yake kuuawa

Ndugu...ndugu

Hii inarejea kwa wote ndugu na dada

baba na mtoto

Hii inamaanisha kuwa baba atamsaliti mtoto wake na kusaliti huku kutasababisha mtoto kuuawa. "baba atamshitaki mtoto wake "auwawe" au baba atamsaliti mtoto wake, kumwaacha auwawe"

Watoto watasimama kinyume cha baba zao

Hii inamaanisha kuwa watoto watawapinga wazazi wao na kuwasaliti.

kuwasababisha kuuawa

Hii inamaanisha kuwa mamlaka yatasema wauwawe. Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji.

Mtachukiwa na kila mtu

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Kila mmoja atawachukia"

kwa sababu ya jina langu

Yesu anatumia kirai "jina langu" kurejea kwake mwenyewe. "kwa sababu yangu" au "kwa sababu mnaniamini mimi"

atakayevumilia mpaka mwisho, mtu huyo ataokoka.

Hii inamaanisha kuwa mwaminifu kwa Mungu mpaka mwisho wa maisha ya mtu. Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu atamuokoa yeyote aliye mwaminifu kwake, kuvumilia majaribu, mpaka mwisho wa maisha yake"

Mark 13:14

chukizo la uharibifu

Haya maneno yanatoka kitabu cha Daniel. Wasikilizaji wake wangekuwa na uelewa wa aya na unabii uhusuo chukizo kuingia katika hekalu kulinajisi. "mambo ya aibu yanayo najisi vitu vya Mungu.

limesimama pale lisipotakiwa kusimama

Wasikilizaji wa Yesu wangekuwa wamejua kuwa hii inarejea kwa hekalu. Hii inaweza kufanywa kwa usahihi. "kusimama katika hekalu pale lisipotakiwa"

asomaye na afahamu)

Si Yesu anazungumza. Mathayo aliongeza kwa hii kupata umakini wa wasomaji, ili waweze kusikiliza onyo hili. "ikiwezekana kila mmoja asomaye awe makini kwa onyo hili"

aliyeko juu ya nyumba

Juu ya nyumba ambapo Yesu aliishi ilikuwa tambarare, na watu wangeweza kusimama juu yake.

asirudi

Hii urejea kwa kurudi nyumbani kwake. Hii inaweza kufanywa kwa usahihi. "hakuna kurudi nyumbani mwake"

kuchukua vazi lake

"kuchukua vazi lake"

Mark 13:17

wana mtoto

Hii njia ya upole kusema kwa mtu kuwa ni mwenye mimba.

Ombeni kwamba

Ombeni kwamba wakati huu" au " Ombeni kwamba mambo haya"

baridi

"majira ya baridi" au " baridi, majija ya mvua" Hii urejea kipindi cha mwaka wakati ambapo ni baridi na isiyofurahisha

hayajawahi kutokea

"kubwa zaidi kuliko haijawahi tokea." Hii inaelezea namna ilivyo kubwa na mbaya mateso makubwa.

hayajawahi kutokea

hayajawahi kutokea "na kubwa zaidi haitatokea tena"

atakapopunguza siku

Inaweza kuwa msaada kuweka wazi "siku" zipi zinaongelewa. "atapunguza siku za mateso" au "atapunguza wakati wa mateso"

atapunguza

Hili neno halimaanishi kuwa siku zitakuwa chini ya masaa 24 kila moja, lakini zitakuwa siku chache za mateso.

hakuna mwili utakaookoka

Neno "mwili" urejea kwa watu. Hapa "kuokoka" urejea kwa wakovu wa kimwili. "hakuna yeyote atakayeokoka" Pia, maneno haya yanaweza kusemwa katika mtindo chanya. "kila mmoja atakufa"

kwa ajili ya

ustawi wa

wateule, ambao aliwachagua

kikundi cha maneno "wale aliowachagua" humaanisha kitu kile kile kama "wateule" Kwa pamoja, wanasisitiza kuwa Mungu aliwachagua watu hawa.

Mark 13:21

Maelezo ya ujumla

Biblia ya UDB hutumia mstari kama daraja kuunganisha mistari ya 21 na 22, kusema maelezo anayowambia watu ili kwamba iwe rahisi kuelewa.

Wakristo wa uongo

"watu wanaodai kuwa wao ni Kristo"

ili kwamba wa kuwadanganya

Neno linalokosekana linaweza kuongezwa. "ili kwamba kuwadanganya watu"

kama inawezekana, hata wateule

Maelezo yanayokosekana yanaweza kuongezwa. "Kama inawezekana, hata wanaweza kuwadanganya wateule" au "hata wataweza kujaribu kuwadanganya watu ambao Mungu amekwisha wachagua."

Iweni macho

"Iweni macho"

Nimwekwisha wambia haya yote kabla ya wakati

Yesu aliwambia mambo haya kuwaonya. "Nimewambia nyinyi haya yote kabla ya wakati kuwaonya"

Mark 13:24

jua litatiwa giza

Hii inaweza kuwa kati hali tendaji. "jua litatiwa giza"

mwezi hautatoa mwanga wake

Hapa mwezi umeongelewa kama ulikuwa hai na waweza kutoa kitu chochote kwa mtu fulani. "mwezi hautato mwanga" au "mwezi utatiwa giza"

nyota zitaangika kutoka angani

Hii haimanishi kwamba zitaanguka chini lakini ni kwamba zitaanguka kutoka pale zilipo kwa sasa.

nguvu zilizoko mbinguni zitatikisika

Hii inaweza kuwa kati hali tendaji. "Mungu ataitingisha nguvu zilizoko mbinguni"

nguvu

Hili ni jina la maelezo juuya sayari na linaweza kuwa pamoja na nyote.

mawinguni

"mawinguni"

Kisha watamuona

"Kisha watu watamuona"

kwa nguvu kubwa na utukufu

"nguvu na utukufu"

atawakusanya

Neno "ata" urejea kwa Mungu na kirai kwa malaika wake, kama wao watakao kusanya wateule. "watawakusanya" au "malaika wake watawakusanya"

pande kuu nne

Ulimwengu wote umesemwa kuwa kama "pande kuu nne" ambazo zinarejea kwa pande nne: kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi.

kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.

Huku kulikokithiri kumetolewa msisitizo kwamba wateule watakusanywa kutoka ulimwengu wote. "kutoka kila eneo ulimwenguni"

Mark 13:28

Sentensi unganishi

Yesu anatoa mifano mifupi hapa kuwakumbusha watu kufahamu lini mambo aliyokuwa anaongelea yanatokea

tawi liwezavyo kutoa

Kifungu "tawi" urejea kwa matawi ya mtini. "matawi yake yanaweza kutoa"

kutoa

"ukijani na laini"

kuweka majani

Hapa majani ya mtini yanaongelewa kama yalikuwa hai na yanaweza kuwa tayari kusababisha majani yake kukua. "majani yake huanza kuchipua"

kiangazi

sehemu ya mwaka ni joto au majira ya kukua

mambo haya

Hii inarejea kwa siku za mateso. "mambo haya nimekwisha kueleza"

yuko karibu

"Mwana wa Adamu yuko karibu"

karibu na malango

Nahau hii inamaanisha kwamba yuko kairba na karibu ameshafika, urejea kwa msafiri kuwa karibu kufika katika mlango. "na yuko karibu hapo"

Mark 13:30

Kweli, nawambieni

Hii huonyesha kwamba sentensi inayofuata hasa ni kweli na muhimu.

hakitapita

Ni njia ya kistaarabu kusema juu ya mtu fulani kufa. "hatakufa" au "hatakoma"

mambo haya hayajatokea

Kifungu "mambo haya" urejea kwa siku za mateso.

Mbingu na nchi

Huku kulikokithiri kunarejea mbingu zote, pamoja na jua, mwezi, nyote, na sayari na ulimwengu wote.

zitapita

"itakoma kuishi" Kifungu hiki urejea kwa mwisho wa ulimwengu.

maneno yangu hayatapita kamwe

Yesu huzungumza maneno yakutopoteza nguvu zao kama wangekuwa kitu fulani ambacho kamwe hakitakufa. "maneno yangu kwamwe hayatawapotezea nguvu zao"

siku hiyo au saa hiyo

HIi urejea kwa wakati ambapo Mwana wa Adamu atarudi. "siku hiyo au saa hiyo ambapo Mwana wa Adamu atarudi" au " siku hiyo au saa hiyo ambapo nitarudi"

hata malaika wa mbinguni, wala Mwana

Haya yametajwa kati ya wale wasiojua lini Mwana wa Adamu atarudi. "hata malaika mbinguni au Mwana anajua"

malaika mbinguni

Hapa "mbinguni" urejea kwenye eneo ambalo Mungu huishi.

ila Baba

Ni vizuri kutofasiri "Baba" na neno hilo ambalo lugha yako ya asili hutumia kurejea kwa baba wa kibinadamu. Pia, hii ni umboyai ambayo husema kwamba Baba anajua lini Mwana atarudi. "ila ni Baba anajua"

Mark 13:33

muda gani yatatokea

Inaweza kuanishwa waziwazi nini "muda" urejea kwa. "wakati ambapo muda utakuja wakati ambapo matukio yote haya yatatokea"

kila mmoja na kazi yake

"kuwaambia kila moja kazi gani anapaswa kufanya"

Mark 13:35

kama ni jioni

Hii urejea kwa kurudi kwa bwana. "kama atarudi jioni"

jogoo atakapowika

Jogoo ni ndege anayeita asubuhi na mapema. Sauti kubwa anayofanya ni "kuwika"

asikukute umelala

Hapa Yesu anazungumza kutokuwa tayari kama "kulala" "asikukute hauko tayari kwa kurudi kwake"

Mark 14

Marko 14 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi kwa upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivyo kwa mashairi katika 14:27,62, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Kula mwili na damu

Marko 14:22-25 inaelezea chakula cha mwisho cha Yesu na wafuasi wake. Wakati huu, Yesu aliwaambia kwamba kile walichokuwa wakila na kunywa kilikuwa mwili wake na damu yake. Karibu makanisa yote ya kikristo huadhimisha "Meza ya Bwana," "Ekaristi", au "Mkutano wa Kikawa" kukumbuka chakula hiki.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Abba, Baba

"Abba" ni neno la Kiaramu ambalo Wayahudi walitumia kuzungumza na baba zao. Marko analiandika kama linavyotamkwa na kisha kulifasiri. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-transliterate)

"Mwana wa Mwanadamu"

Yesu anajiita mwenyewe "Mwana wa Binadamu" katika sura hii (Marko 14:20). Lugha yako huenda haiwezi kuwaruhusu watu kujizungumzia wenyewe kana kwamba wanaongea juu ya mtu mwingine. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sonofman and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-123person)

<< | >>

Mark 14:1

Sentensi unganishi

Siku mbili tu kabla ya pasaka, makuhani wakuu na waandishi walikuwa wakitafuta kwa hila namba ya kumuua Yesu.

hila

pasipo watu kugundua

Kwa kuwa walisema

Neno "wa" urejea kwa makuhani wakuu na waandishi.

Sio wakati huu wa sikukuu

Inaweza kuwa msaada kuongoze taarifa zilizokosekana. "Hatuwezi kufanya wakati wa sikukuu"

Mark 14:3

Simoni Mkoma

Huyu mtu alikuwa na ukoma hapo awali lakini hakuwa mgonjwa tena.

alabaster

Hili ni laini, "jiwe jeupe."

Nini sababu ya upotevu huu?

Hakuna sababu nzuri kupoteza manukato ghali namna ile.

Manukato haya yangeweza kuuzwa

"Tungeuza manukato haya." au Angeweza kuuza manukato haya

dinari mia tatu

"dinari 300." Dinari ni sarafu za Kirumi.

Mark 14:6

Kwa nini mnampa shida?

Hampaswi kumpa shida

Mark 14:10

Sentensi unganishi

Baada ya mwanamke kumpaka mafuta Yesu kwa manukato, Yuda anaahidi kumkabidhi kwa mahuni wakuu.

ili kwamba apate kumkabidhi kwao

Yuda hakumkabidhi Yesu kwao bado, badala yake alienda kufanya mipango nao. "ili kufanya mpango nao kumkabidhi Yesu kwao"

Wakati wakuu wa Makuhani waliposikia hivyo

Inaweza kuwa msaada kusema waziwazi nini makuhani wakuu walisikia. "Wakati ambapo makuhani wakuu walisikia nini alichotaka kufanya kwa ajili yao"

Mark 14:12

chumba cha wageni

chumba cha ziada kwa ajili ya watembeleaji

Mark 14:15

Fanyeni maandalizi kwa ajili yetu pale

Walipaswa kufanya maandalizi ya chakula cha Yesu na wanafunzi wake kula. "Andaa chakula kwa ajili yetu hapo"

wanafunzi waliondoka

"Wanafunzi wawili waliondoka"

alivyokuwa amewaambia

"kama Yesu alivyokuwa amesema"

Mark 14:17

Karibia meza

Ilikuwa desturi kuwa na meza fupi ikiwa na mito ambapo wageni wangeweza kukaa mbele katika mkao wa nusu kulala kwenye meza wakati wa karamu ya chakula.

mmoja baada ya mwingine

Hii ina maana kwamba "mmoja kwa muda wake" kila mwanafunzi alimwuliza yeye.

Hakika si mimi?

"Hakika, haiwezi kuwa mimi ninayesaidia adui zako kukukamata!"

Mark 14:20

Ni moja wa kumi na wawili kati yetu

"Yeye ni mmoja wa kumi na wawili, mmoja kwa sasa"

anachovya tonge katika bakuli pamoja nami.

Katika utamaduni wa Yesu, wate wangeweza kula mara chache mkate, kuchovyo katika bakuli la mchuzi.

Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakwenda kama vile maandiko yasemavyo juu yake

Hapa Yesu urejea kwa maandiko kutabiri kuhusu kifo chake. Kama una njia ya kistaraabu kusema kuhusu kifo katika kabila lako, tumia hapa. "Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakufa kama yasemavyo maandiko"

kupitia yeye Mwana wa Adamu atasalitiwa

Hii inaweza kuanishwa zaidi moja kwa moja. "nani anamsaliti Mwana wa Adamu"

Mark 14:22

mkate

Huu ulikuwa ni mkate ulio bapa ambao haujatiwa chachu, ambao uliliwa kama sehemu ya chakula cha pasaka

kuumega

Hii inamaanisha kwamba aliumega katika vipande ili kwamba watu wale.

Alichukua kikombe

Hapa "kikombe" ni kirai cha mvinyo. "Alichukua kikombe cha mvinyo"

Hii ni damu yangu ya agano, damu imwagikayo kwa ajili ya wengi

Agano ni kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Hii inaweza kuandikwa kwa uwazi zaidi. "Hii ni damu yangu ambayo inathibitisha agano, damu imwagikayo ili kwamba wengi wapokee msamaha wa dhambi"

Hii ni damu yangu

"Mvinyo huu ni damu yangu. Ni vizuri kutofasiri kihalisia, ijapokuwa wengi huelewa hii kumaanisha kwamba mvinyo unawakilisha damu ya Yesu na huo mvinyo si damu halisi.

Kweli nawaambia

Hii inaonyesha kuwa sentensi inayofuata hasa ni kweli na muhimu.

zao hili la mzabibu

"mvinyo" Hii ni njia ya maelezo inayorejea kwa mvinyo.

mpya

Maana zinazowekana ni 1) "tena" au 2)"kwa njia mpya"

Mark 14:26

wimbo

Wimbo ni aina ya wimbo. Ilikuwa desturi yao kuimba Zaburi toka Agano la Kale katika haua hii.

Mark 14:28

Hata kama wote watajitenga, mimi sitaku

"Sitaku" ni kifupi cha sitajitenga nawe. Maneno "jitenga nawe" yanarudia kinyume chake mara mbili na humaanisha "nitabaki na wewe."

Mark 14:30

kunikana

"sema kwamba hunijui mimi"

Mark 14:32

roho

Neno "roho" limetumika wakati mwingine kimfano kurejea kwa mtu kamili siyo sehemu yake tu.

Mark 14:35

saa hii ingempita

"apewe nguvu ya kushinda mateso aliyokuwa anayapitia.

Aba

Abba ni neno la Kiyunanai ambalo linatumika na watoto kumtaja baba yao. Inaashiria uhusiano wa karibu. Kwa kuwa tayari inamtaja Baba, ni muhimu kuhifadhi neno la Kiyunani "Abba."

Niondolee kikombe hiki

Kikombe hurejea kwenye ghadhabu ya Mungu ambayo ilikuwa lazima Yesu aivumilie.

Alisema, Aba,... Baba, .... Niondolee kikombe hiki. Lakini siyo kwa matakwa yangu, bali matakwa yako."

Yesu alimwomba Baba yake kuondoa mateso ambayo angeweza kuyavumilia juu ya msalaba kufa kwa ajili ya dhambi zote za mwanadamu, kwa muda wote. Lakini Baba alihitaji dhabihu ya Mwana wake, mkamilifu wa pekee kukidhi utakatifu wake wa Kimungu. Kwa hiyo, Yesu alikwenda msalabani.

Baba

Hii ni kichwa muhimu kwa ajili ya Mungu.

Mark 14:37

akawakuta wamelala

"na akamkuta Petro, Yakobo, na Yohana wamelala"

Simoni, je umelala

"Simoni, umelala wakati nilipokuambia kukesha."

Hukuweza kukesha... saa?

"Ungeweza hata kukesha."

Roho inataka kabisa, lakini mwili ni dhaifu.

"Miili yenu haiwezi kufanya kile ambacho akili zenu zinataka ninyi kufanya."

mwili

"mwili unaoonekana"

Mark 14:40

aliwakuta wamelala

"aliwakuta Petro, Yohana, na Yakobo wamelala"

Bado mmelala na kupumzika

bado mmelala! mmepumzika!

Mark 14:43

wakamkamata

wakamkamata kwa nguvu

Mark 14:47

Je mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama mimi ni mnyang'anyi?

mnakuja kwangu, kama dhidi ya mwizi, kwa mapanga na marungu kunikamata

Mark 14:51

shuka zito la kujifunika

nguo nzito iliyotengenezwa kutokana na mmea

Mark 14:53

Sentensi unganishi

Baada ya umati wa makuhani wakuu, waandishi, na wazee kumuongoza Yesu kwa kuhani mkuu, Petro anamtazama kwa mbali wakati wengine wanasimama kushuhudia uongo kinyume na Yesu.

Pale walikusanyika pamoja naye makuhani wakuu wote, wazee, waandishi.

Hii inaweza kupangiliwa kwa upya ili kwamba inakuwa rahisi zaidi kuelewa. "Makuhani wakuu wote, wazee, na waandishi walikuwa wamekusanyika hapa kwa pamoja"

Sasa

Neno hili linatumika hapa kuweka alama ya badiliko katika hadidhi kama mwandishi anavyoanza kusema kuhusiana na Petro.

kuelekea kwenye ua wa kuhani mkuu.

Kama Petro alivyomfuata Yesu, alisimama katika uwanja wa kuhani mkuu. Hii inaweza kuandikwa waziwazi. "na alienda mpaka uwanja wa kuhani mkuu"

Aliketi pamoja na walinzi

Petro aliketi pamoja na walinzi waliokuwa wakifanya kazi katika uwanja. "Aliketi katika uwanja pamoja na walinzi"

Mark 14:55

Sasa

Hili neno limetumika kuweka alama kwa badiliko katika hadithi kama mwandishi anavyoendelea kutuambia kuhusu Yesu kuwekwa kwenye majaribio.

wapate kumwua

Hapakuwa wenyewe ambao wangemwadhibu kifo Yesu; badala yake, wangemuomba mwingine kufanya . "wangemwadhibu kifo Yesu" au "wangeweza kupata mwingine kumwadhibu kifo Yesu"

Lakini hawakuupata

Hawakupata ushuhuda kinyume dhidi ya Yesu ambao wangemtia hatiani na kumwua.

walileta ushuhuda wa uongo dhidi yake

Hapa anaongea ushuhuda wa uongo unoelezwa kama ilikuwa kama kitu halisi ambacho mtu anaweza kubeba. "Mshitaki kwa kusema ushuhuda wa uongo dhidi yake"

hata ushahidi wao haukufanana

Hii inaweza kuandikwa kwa mtindo wa chanya. "lakini ushuhuda wao haukufanana"

Mark 14:57

Tulimsikia

Neno "tu" hurejea kwa watu walioeta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu.

Mark 14:60

alisimama katikati yao

"alisimama kati ya wakuu wa makuhani, waandishi na wazee"

Mimi nipo

Hili ndilo jina Mungu alijiita mwenyewe katika Agano la Kale.

Mark 14:63

alirarua vazi lake

ishara ya hasira juu ya kile ambacho Yesu alikuwa amesema

Wote walimhukumu

"Wajumbe wote wa Baraza walimhukumu Yesu"

Mark 14:66

Sentensi unganishi

Kama Yesu alivyokuwa ametabiri, Petro anamkana Yesu mara tatu kabla ya jogoo hajawika.

chini ya uani

"nje ya uani"

mmoja wa wasichana wa kuhani mkuu

Mtumishi wa kike alimtumikia kuhani mkuu. "moja wa watumishi wa kike waliomtumikia kuhani mkuu"

alimkana

Hii inamaanisha kudai kwamba kitu fulani si sahihi. Katika hali hii, Petor alikuwa akisema kwamba alichosema mtumishi wa kike kuhusu yeye hakikuwa sahihi.

Sijui wala sielewi kuhusu kile unachosema

Ote,"kujua" na "kuelewa" zina maana ile ile hapa. Maana imerudiwa kuongeza msisitizo kwa kile alichokuwa akisema Petor. "Hakika sikuelewi unachoongelea"

Mark 14:69

mmoja wao

mmoja wa wanafunzi wa Yesu

Mark 14:71

naye alihuzunika na kulia

Petro alihuzunika sana na kushitushwa sana na kuanza kulia

Mark 15

Marko 15 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Pazia la hekalu likagawanyika mara mbili"

Pazia la hekalu lilikuwa ni ishara muhimu ambalo lilionyesha kwamba watu walihitaji kuwa na mtu anayeongea na Mungu kwa niaba yao. Hawangeweza kuzungumza na Mungu moja kwa moja kwa sababu watu wote ni wenye dhambi na Mungu huchukia dhambi. Mungu akagawanya pazia ili kuonyesha kwamba watu wa Yesu wanaweza sasa kuzungumza na Mungu moja kwa moja kwa sababu Yesu amelipia dhambi zao.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Kudhihaki

Kwa kujifanya kumwabudu Yesu (Marko 15:19) na kwa kujifanya kuzungumza na mfalme (Marko 15:18), askari na Wayahudi walionyesha kwamba walimchukia Yesu na hawakuamini kwamba alikuwa Mwana wa Mungu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-irony and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#mock)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Eloi, Eloi, lama sabakthani?

Hili ni tamko katika Kiaramu. Marko hutafsiri sauti zake kwa kuandika kwa kutumia herufi za Kigiriki. Halafu anaelezea maana yake. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-transliterate)

<< | >>

Mark 15:1

Wewe umesema hivyo

"Wewe mwenyewe umesema hivyo."

Mark 15:9

funguliwa

"Alimpeleka mbali" au "basi nenda"

Mark 15:14

Walimpiga Yesu

Walimpiga Yesu hasa kwa fimbo

yeye alimtoa

Ona jinsi ulivyotafsiri mstari huu katika

Mark 15:16

kambini

Hii ni sehemu wanaokaa maaskari.

kikosi

"Idadi kubwa" au "wengi"

Wakamvika Yesu vazi la zambarau

Hii ilikuwa tendo la kejeli. Zambarau ilikuwa rangi inayoonesha mamlaka na kumvalisha ni namna ya kudhihaki cheo chake, "Mfalme wa Wayahudi."

Wakaanza kumpigia kumdhihaki na kusema, "salaam, Mfalme wa Wayahudi!"

Maaskari walimdhihaki Yesu kwa sababu hawakuamini kwamba alikuwa Mfalme wa Wayahudi.

Mark 15:25

majambazi

"wezi kila upande"

Mark 15:36

siki mvinyo

"siki"

Pazia la hekalu liligawanyika mara mbili

Mungu aligawa pazia la hekalu mara mbili

Mark 15:39

Mwana wa Mungu

Hii ni cheo muhimu kwa Yesu.

Salome

Ni jina.

Mark 15:45

kaburi lile lililochimbwa katika mwamba

"awali lile kaburi lilichimbwa na mtu katika mwamba imara"

sanda

vazi lililotengenezwa kwa kitani inayopandwa kama ilivyotafsiriwa katika 14:51-52

mahali pale alipozikwa Yesu

"mahali pale ambapo Yusufu na wengine waliuzika mwili wa Yesu"

Mark 16

Marko 16 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Kaburi

Kaburi ambamo Yesu alizikwa (Yohana 19:41) lilikuwa ni aina ya kaburi ambalo familia za Kiyahudi za matajiri zilizika maiti yao. Kilikuwa chumba halisi kilichokatwa kutoka kwenye mwamba. Kilikuwa na eneo bapa upande mmoja ambapo wangeweza kuweka mwili baada ya kuupaka mafuta na manukato na kuufunga kwa nguo. Kisha wangeuweka mwamba mkubwa mbele ya kaburi ili yeyote asiweze kuona ndani au kuingia.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kijana mmoja aliyevalia vazi nyeupe

Mathayo, Marko, Luka, na Yohana wote waliandika juu ya malaika waliovalia nguo nyeupe wakiwa na wanawake katika kaburi la Yesu. Waandishi wawili kati yao waliwaita wanaume, lakini ilikuwa tu ni kwa sababu tu malaika walikuwa katika hali ya kibinadamu. Waandishi wawili kati yao waliandika kuhusu malaika wawili, lakini wale waandishi wengine wawili waliandika juu ya mmoja tu. Ni bora kutafsiri kila moja ya vifungu hivi kama inavyoonekana katika ULB bila kujaribu kufanya vifungu vyote kufanana. (See: Matthew 28:1-2 and Mark 16:5 and Luke 24:4 and John 20:12)

__<< | __

Mark 16:1

Sentensi unganishi

Siku ya kwanza ya wiki, wanawake walikuja asubuhi kwa sababu walitegemea kutumia kitoweo kuupaka mafuta mwili wa Yesu. Walishangaa kumuona kijana ambaye anawambia kuwa Yesu yu hai, lakini wanaogopa na hawamwambii mtu yeyote.

Wakati sabato ilipokwisha

Hii ni kwamba, wakati jua lilipochomoza siku ya saba na siku ya kwanza ya wiki kuanza.

Mark 16:3

jiwe lilikuwa limevingirishwa

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "mtu amekwisha kulivingirisha jiwe"

Mark 16:5

Amefufuka!

Malaika kwa mkazo anatangaza kuwa Yesu amekwishafufuka. Hii inaweza kutofasiriwa katika kauli tendaji. "Alinuka!" au " Mungu alimwinua kutoka mauti!"

Mark 16:8

kaburi,sehemu ya kuzikia

Neno "kaburi" inarejea kwenye eneo ambapo watu wanaweka mwili wa mtu aliyekufa. "Sehemu ya kuzikia" ni neno la kiujumla ambalo linarejea kwa:

  • Wakati mwingine Wayahudi walitumia mapango kama makaburi, na wakati mwingine walichimba mapango kwenye mawe sehemu ya milima.
  • Katika Agano Jipya, ilikuwa ni kawaida kusukuma jiwe kubwa na zito mbele ya kaburi lililo wazi ili kufunga.
  • Kama neno kaburi linaweza kurejea kama shimo ambapo mwili unawekwa chini ya ardhi, njia zingine za kutofasiri inaweza kuwa, "pango" au "shimo" ndani ya sehemu ya mlima"
  • Neno "kaburi" nadra hutumiwa kwa ujumla na kwa usemi urejea kwa hali ya kufa au eneo ambalo roho za watu zinakuwa.

walishangazwa

Haya maneno urejea kwa kushangazwa kwa sababu ya kitu cha ajabu kilichofanyika.

  • Baadhi ya maneno haya yametofasiriwa kwa usemi wa Kigiriki ambayo unamaanisha "kumpiga kwa kushangaza" au "kusimama nje ya mtu" usemi huu unaeleza namna ilivyo ya kushangaza ua mshtuko wa mtu alivyojisikia. Lugha zingine zinaweza kuwa na usemi wa kueleza hili
  • Kawaida tukio ambalo limesababisha maajabu na mshangao lilikuwa na miujiza, jambo ambalo Mungu mwenyewe angelifanya.
  • Maana ya maneno haya inaweza pia kujumuisha hisia za kuchanganyikiwa kwa sababu kilichofanyika hakikutegemewa.
  • Njia zingine za kutofasiri maneno haya inaweza, "kushangazwa kupita kiasi" au "kushitushwa sana"
  • Maneno yanayohusiana hujumuisha: "ajabu"
  • Kwa ujumla, maneno haya ni chanya na yanaeleza kuwa watu walikuwa na furaha kuhusu kilichokwisha tokea.

Mark 16:9

Sentensi unganishi

Yesu anaonekana mara ya kwanza kwa Mariamu Magidalena, ambaye anawambia wanafunzi, kisha anajitokeza kwa wengine wawili kama wanavyokuwa wakitembea, na badae anatokea kwa wanafunzi kumi na mmoja.

siku ya kwanza ya juma

"jumapili"

Walisikia

"Walimsikia Mariamu Magidalena akisema"

Mark 16:12

akajitokeza katika namna tofauti

Yesu alikuwa ni mtu ambaye "wale wawili" waliona, lakini walichokiona hakikuonekana kama Yesu, kwa hiyo hawakujua walikuwa wakimtazama Yesu

wengine wawili

wawili "wale walikuwa naye"

hawakuwaamini

Wanafunzi wengine hawakuwaamini wale wawili walikuwa wakitembea walichosema.

Mark 16:14

Sentensi unganishi

Wakati ambapo Yesu anakutana na kumi na moja, anawakemea kwa kutokuwa na imani na kuwambia waende kwa ulimwengu wote kuhubiri injili.

kumi na moja

Hawa ni wanafunzi kumi na moja ambao walibaki baada ya Yuda kuwaacha.

walikuwa wameegama katika meza

Hiki ni kirai cha kula, ambacho kilikuwa ni njia ya kawaida siku zile wakati wa kula. "walikuwa wanakula chakula"

kueegama

Walikuwa wameegama chini upande wa kushoto, wakitumia mkono wao wa kula chakula kwenye meza.

mioyo migumu

Yesu anakemea wanafunzi wake kwa sababu wasingeweza kumwamini. Tofasiri usemi huu ili ieleweke kuwa wanafunzi hawakumwamini Yesu. "kukataa kuamini"

Nenda katika ulimwengu

Hapa "ulimwengu" ni kirai kwa watu katika ulimwengu. "Nenda kila sehemu kuna watu"

ulimwengu wote

Hii ni kutia chumvi na kirai kwa ajili ya watu "ulimwengu wote"

Yeye abatizae na akabatizwa ataokolewa

Neno "a" urejea kwa yeyote. Sentensi hii inaweza kufanywa katika kauli tendaji."Mungu atawaokoa watu wote ambao wanaamini na kukuruhu wewe uwabatize"

yeye asiye amini atahukumiwa

Neno "a" urejea kwa yeyote. Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. " Mungu atahukumu watu wote ambao hawaamini."

Mark 16:17

Ishara hizi zitaambatana na wote waaminio

Mariko anasema juu ya miujiza kama vile watu wanaenda pamoja na wakristo. "Watu wanawatazama wale wanaomini wataona mambo haya kutokea na kujua niko pamoja na wakristo"

Kwa jina langu

Maana zinaweza kuwa 1) Yesu anataja orodha ya kiujumla: "Katika jina langu watafanya mambo kama haya: Wa" au 2) Yesu anatoa orodha sahihi: "Haya ni mambo watakayo fanya katika jina langu"

Katika jina

Hapa "jina" linahusishwa na mamlka ya Yesu na nguvu. "Kwa nguvu ya jina langu" au " Kwa nguvu za jina langu

Mark 16:19

akachukuliwa juu mbinguni na ameketi

Hii inaweza kuwa kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu alimchukua juu mbinguni, na ameketi"

mkono wa kuume wa Mungu

"sehemu ambapo Mungu umpe kuketi kwa heshima na nguvu"

kulithibitisha neno

"kulionyesha kuwa maneno yake, ambayo yalikuwa yakizunguzwa, yalikuwa kweli"