Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

UTANGULIZI WA KITABU CHA MATENDO YA MITUME

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Jumla

Muhtasari wa Kitabo cha Matendo ya Mitume

  1. Mwanzo wa kanisa na huduma yake(1:1-2:2:41)
  2. kanisa la kwanza Yerusalemu (2:42-6:7)
  3. kuongezeka kwa upinzani na mauaji ya kishujaa ya Stefano (6:8-7:60)
  4. Mateso ya Kanisa na utume wa Filipo (8:1-40)
  5. Paulo anakuwa Mtume (9:1-131)
  6. Utume wa Petro na Wakristo wa Kwanza Wayunani (9:32-12:24),
  7. Paulo, mtume wa Wayunani, Sheria ya Wayahudi na baraza la viongozi wa kanisa Yerusalemu.
  8. Ongezeko la kanisa katikati mwa inchi za karibu ya bahari Mediterane na Asia Ndogo (16:6-19:20)
  9. Paulo anasafiri Yerusalemu na kuwa mfungwa Roma (19:21-28:31)

Kitabu cha Matendo Ya Mitume kinazungumzia nini?

Kitabu cha Matendo Ya Mitume kinazungumzia habari ya Kanisa la Mwanzo kadiri ya lilivyoongezeka. Kinaashiria vile nguvu za Roho Mtakatifu zilivyosaidia kanisa la Kwanza. Matendo haya yanaanza pindi Yesu alipopaa mbinguni hadi miaka thelathini kutoka hapo.

Ni Jinsi gani jina la kitabo hiki kinafaa kutafsiriwa?

Watafsiri wanaweza kuchagua jina liliyotumiwa zamani kwa mfano, 'Matendo ya Roho Mtakatifu' Ama watafsiiri wanaweza kuchagua jina la waziwazi, kama 'Matendo ya Roho Mtakatifu kupitia kwa mitume'.

Nani aliandika kitabu cha Matendo ya Mitume?

Kitabu hakijamtaja mwandishi ingawa kinaelekezewa Tiofila, yule ambaye Mwinjili Luka anamzungumzia. Kitabu kinazungumzia "sisi" kuashiria kwamba mwandishi wake alisafiri na Paulo. Wasomi wengi wengi wa Biblia wanaamini kwamba ni Luka aliyekuwa akisafiri na Paulo. Ndio maana watu wengi wanaamini kwamba Luka ndiye mwandishi wa hiki kitabu na cha Injili Ya Luka.

Luka alikuwa daktari wa matibabu. Mfumo wake wa maandishi unamuashiria kama mtu aliyekuwa na masomo ya juu sana. Kuna uwezekano mkubwa hakuwa Myahudi. Aliyashuhudia matukio mengi yaliyotajwa katika kitabu cha Matendo.

SEHEMU YA 2:maswala muhimu ya kidini na kitamaduni

Kanisa ni nini

Kanisa na kundi la watu wanaomwamini kristu. Kanisa linajumlisha Wayahudi na wasiyo wayahudi (Wayunani). Matukio ya kitabu hiki kinaonyesha jinsi Mungu anavyolisaidia Kanisa ni. Aliwapa uwezo waumini kuishi kiadilifu kupitia kwa Roho wake Mtakatifu.

SEHEMU YA 3: Maswala muhimu ya Tafsiri

Ni mambo gani muhimu katika maandiko ya Matendo ya Mitume?

Yafuatayo ndio maswala muhimu katika Matendo ya Mitume:

Mistari ifuatayo inapatkana katika tafsiri za kitambo za Bibilia, lakini haiko katika nyaraka bora za kitambo za Bibilia. Tafsiri zingine za kisasa huweka mistari hii kwa mabano (). tafsiri za ULB na UDB huiweka kwa maelezo ya chini (footnote)

  • Fililpo alisema, "Ukiamini na moyo wako wote, unaweza batizwa." Muethiopia akajibu, "Naamini kwamba Yesu ni mwana wa Mungu" (Matendo 8:37).
  • "Lakini Sila aliona vema kubaki pale."(Matendo 15:34)
  • "Tulitaka kumhukumu kwa mujibu wa sheria.Lakini Lisia jemadari akafika akamwondoa mikononi mwetu kwa nguvu." (Matendo 24:6b-8a).
  • " Alipokwisha kusema hayo, Wayahudi wakaenda zao, wakiulizana mengi wao kwa wao." (Acts 28:29).

Katika maandiko yafuatayo,haijulikani yaliyosema maandiko ya awali, Watafsiri watahitajika kuchagua masomo yepi ya kutafsiri. ULB ina masomo ya kwanza lakini masomo yake ya pili yamewekwa kwenye maelezo ya chini.

  • "wakarejea kutoka Yerusalemu" (Matendo 12:25). Matoleo mengine ya Bibilia husema, "Walirudi Yerusalemu (ama huko)."
  • "Aliwavumilia" (Matendo 13:18). Matoleo mengine husema, "Aliwahudumia".
  • "Haya ndiyo Bwana asema, yeye aliyeyatenda haya mambo yaliyojulikana tangu zamano."(Matendo 15:17-18). Matoleo ya awali yasema, "Bwana asema, kwake ambako matendo yake yanajulikana kwanzia zamani."

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants

Acts 1

Matendo 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii inarekodi tukio,kawaida linajulikana kama "kupaa", wakati Yesu alirudi mbinguni baada ya ufufuko wake. Hatarudi tena mpaka "Ujio wake wa pili." (rejelea: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#heaven and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#resurrection).

Toleo la UDB limeweka maneno "Kwa mpendwa Theofila" kando na maneno mengine. Hii ni kwa sabau Waiingereza huanza kuandika barua namna hivi. Unaeza anza kitabu hiki jinzi watu huanza kuandika waraka katika mila yako.

Tafsiri zingine zinanukuu kutoka Agano la Kale kwenye kulia kwa ukurasa kuliko maandiko yote kwa jumla. ULB hufanya hivi kupitia nukuu mbili kutoka Zaburi 1:20

DHANA MAALUM KATIKA SURA HII

BATIZA

Neno "batiza" lina maana mbili katika sura huu. Inaashiria ubatizo wa Yohana na ubatizo wa Roho Mtakatifu (Matendo 1:5). (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#baptize)

"Alizungumza kuhusu ufalme wa Mungu"

Wasomi wengine huamini kuwa wakati Yesu "alipozungumzuia kuhusu ufalme wa Mungu," aliwaeleza wanafunzi wake ni kwa nini ufalme wa Mungu haukuja kabla ya kifo chake. Wengine huamini kwamba ufalme wa Mungu ulianza wakati Yesu alikuwa hai na ya kwamba hapa Yesu alikuwa anafafanua kwamba huu ulikuwa mwanzo kwa umbo jipya.

Matatizo mengine ya tafsiri katika sura hii.

wanafunzi kumi na wawili

yafuatayo ni majina ya wanafunzi kumi na wawili

Katika Injili ya Matayo

Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye; Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Thadayo;Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote

Katika injili ya Marko

Simoni (Petro),Andrea,na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo; na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote.

Katika injili ya Luka

Simoni(Petero),Andrea,Yakobo,Yohana,Filipo,Bartholomayo,Matayo,Tomaso,Yakobo wa Alfayo,Simoni Mkananayo,Yuda wa Yakobo na Yuda Iskariote.

Kuna uwezekano ya kwamba Thadayo na Yuda wa Yakobo ni mtu mmoja

Akeldama

Hili ni neno la Kihebrania au Kiaramaiki. Luka alitumia maneno ya Kigiriki ili wasomaji wake wajue lilivyotamkua,kisha akawaeleza maana yake. Unatakikana kulitamka jinsi linalatamkwa kwa lugha yako kisha ukaeleza maana yake.(Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-transliterate)

| >>

Acts 1:1

Sentensi unganishi.

Luka anaelezea ni kwasababu gani anamwandikia Theofilo

Kitabu cha zamani nilikiandika

Kitabu cha zamani ni Injili ya Luka.

Theofilo

Luka aliandika kitabu hiki kwa mtu anayeitwa Theofilo. Baadhi ya watafsiri hufuata mfumo wa tamaduni zao za kuelezea barua na huandika "Mpendwa Theofilo" mwanzoni mwa sentensi. Theofilo humaanisha "rafiki wa Mungu.

Mpaka siku alipopokelewa juu

Hii inarejesha kwenye kupaa kwa Yesu mbinguni

Amri kupitia kwa Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu kuwaelekeza mitume wake juu ya vitu fulani.

Baada ya kuteswa kwake

Hii inahusu mateso ya Yesu na kifo chake msalabani.

Alijidhihirisha Yeye mwenyewe akiwa hai

Yesu alionekana kwa mitume wake na kwa wanafunzi wengi wengine.

Acts 1:4

Sentensi unganishi

Tukio hili lilitukia wakati wa siku arobaini ambazo Yesu alionekana kwao baada ya Yeye kufufuka toka katika wafu.

Alipokuwa akikutana pamoja nao

Wakati Yesu alipokutana pamoja na mitume wake.

Ahadi ya Baba

Roho Mtakatifu ambaye Baba aliahidi kumtuma.

ambayo, alisema

Roho Mtakatifu ambaye Yesu alisema habari zake.

Yohana alibatiza kabisa kwa maji,

Yesu anatofautisha ubatizo wa Yohana wa maji, na ule ubatizo wa Mungu ambao utakuwa ni wa Roho Mtakatifu.

Yohana alibatiza kwa maji kabisa

"Yohana hasa alibatiza watu kwa maji"

ninyi mtabatizwa

"Mungu atawabatiza ninyi"

Acts 1:6

huu ni wakati wa utakaorudisha ufalme kwa Israeli

"Sasa Utafanya Israeli taifa lenye nguvu tena?"

nyakati au majira

"nyakati au tarehe"

mtapokea nguvu... na mtakuwa mashahidi wangu

Mitume watapokea nguvuitakayowasaidia kumshuhudia Yesu. "Mungu atawatia nguvi... kuwa mashahidi wake.

hadi miisho ya nchi

"kote duniani" au" mpaka sehemu za mbali sana za dunia"

Acts 1:9

wakiwa wanatazama juu

"mitume wakiwa wanaangalia juu mawinguni" wakati Yesu akiinuliwa na mawingu kwenda juu.

Yeye aliinuliwa juu

Mungu alimwinua juu ya anga

wingu likamficha toka katika macho yao

" na wingu liliwazuia kumwona hivyo wasingelimwona tena"

kuangalia kwa makini mbinguni

"Kutazama mawinguni" au "kukaza macho kwenye mawingu"

Ninyi wanaume wa Galilaya

Malaika anazungumza na mitume kama watu waliotoka Galilaya.

atarudi kwa namna ile ile

Yesu atarudi katika mawingu , kama ilivyokuwa wakati wa kupaa kwake kwenda mbinguni.

Acts 1:12

Ndipo wao wakarudi

"Mitume wakarudi"

mwendo wa siku ya sabato

Hii inaelezea umbali ambao kutokana na desturi za walimu wa sheria wa kiyahudi, mtu aliruhusiwa kutembea mwendo wa sabato ambao yapata kilomita moja hivi.

Walipowasiri

"Walipofika mwisho wa safari yao. Mstari wa 12 unasema, "Ndipo wakarudi Yerusalemu kutoka kwenye mlima wa mizeituni"

chumba cha juu

"chumba ambacho kipo juu kwenye nyumba"

Walikuwa wameungana kama mtu mmoja

Kikundi kiliungana na hakikuwa na mgawanyiko au migongano.

wakiwa na juhudi wakiendelea katika kuomba

Wanafunzi waliomba kwa pamoja kwa kawaida na mara kwa mara.

Acts 1:15

Sentensi unganishi

Tukio hili lilitukia wakati Petro na waumini wengine walikuwa pamoja katika chumba cha juu.

Katika siku zile

Maneno haya yanaashiria mwanzo mpya wa historia. Yanaelezea kipindi baada ya Yesu kupaa na wakati wanafunzi wakiwa katika chumba cha juu wamekutanika kuomba.

katikati ya ndugu

Neno "ndugu" Linaelezea ndugu waumini likiunganisha wanawake kwa wanaume.

ilikuwa lazima kwamba maandiko yatimizwe

Yale mambo tunayoyasoma katika maandiko lazima yatimizwe

kwa kinywa cha Daudi

Neno "kinywa" Linaelezea yale maneno aliyoyasema Daudi.

Acts 1:17

Sentensi unganishi

Katika mstari 17 Petro anaendelea na hotuba yake kwa waumini.

Maelezo ya Jumla:

Ingawa Petro anaongea na kundi lote la waumini waliokuwa chumba cha juu, lakini neno "sisi" analitumia kwa kuwataja mitume pekee waliotembea, kuketi, kuongea na Yesu tangu mwanzo wa huduma yake hadi kupaa kwake mbinguni.

Sasa mtu huyu

Neno "mtu huyu" linaelezea juu ya Yuda Iskariote.

alichokipokea kwa uovu wake

"pesa alizopokea ni malipo ya ya uovu alioufanya"

hapo alianguka akitanguliza kichwa, mwili ukapasuka na matumbo yake yote yakawa wazi yakamwagika.

Kuanguka kwa Yuda kulisababisha mwili wake kupasuka na matumbo kumwagika.

shamba la damu.

Watu waliokuwa wakiishi Yerusalemu waliposikia habari za Yuda na kifo chake, wakaliita jina lile shamba lililonunuliwa kwa fedha hizo kuwa ni shamba la damu.

Acts 1:20

Sentensi unganishi:

Petro anaendeleza hotuba yake kwa waumini ambayo alikuwa ameianza.

Maelezo ya Jumla:

Ujumbe wake unasimulia vile Yuda alivyotenda akiunganisha na unabii wa maandiko, Petro anarejea ujumbe katika kitabu cha Zaburi kwamba anaamini inahusiana na tukio hilo.

Kwa sababu imeandikwa katika Kitabu cha Zaburi

Petro anathibitisha kuwa, "Daudi aliandika katika kitabu cha Zaburi".

'Ngoja eneo lake liwe hame na isiruhusiwe hata mmoja kuishi pale

Ni hali ya eneo kuachwa ukiwa kutokana na chanzo cha historia yake.

na isiruhusiwe hata mtu mmoja kuishi pale

Kiwanja ni najisi (mwiko/haramu) au haifai kuishi juu yake.

Ngoja mtu mwingine achukue nafasi yake ya uongozi

"Anaweza akarithiwa katika nafasi ya uongozi"

Acts 1:21

Sentensi Unganishi:

Petro anamaliza hotuba yake kwa waumini aliyoianza

Maelezo ya jumla

Neno "sisi" Petro analitumia akimaanisha mitume na siyo waumini wote.

lazima awe shahidi wa ufufuo pamoja nasi

Petro anawaambia mtu atakayechukua nafasi awe na sifa hizo.

watu walioabatana nasi ... mmoja wao hao lazima awe shahidi pamoja nasi wa kufufuka kwake

Petro anafafanua sifa kwaajili ya mtu ambaye atamrithi Yuda kama mtume.

Wakaweka mbele watu wawili

Walipendekeza majina ya watu wawili waliokuwa na sifa sawa na hotuba ya Petro.

Yusufu aliyeitwa Barsaba, ambaye pia aliitwa Yusto

Yusufu pia alijulikana kwa majina Barsaba na Yusto alitwaa nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Yuda Iskariote.

Acts 1:24

Waliomba wakisema

"Ndipo waumini waliomba" Inamaanisha wote waliokuwemo chumba cha juu waliomba, pengine kwa kuongozwa na mtume mmoja.

Wewe, Bwana, wajua mioyo ya watu wote

"Bwana, Wewe wajua msukumo wa ndani na mawazo ya kila mmoja"

hivyo funua yupi kati ya hawa wawili ndiye uliye mteua kuchukua nafasi katika huduma hii ya kitume

"Kwa sababu hiyo, Mungu, tuoneshe sisi yupi kwenye watu hawa wawili umemteua kujaza nafasi hii wazi katika matume"

Kutokana na Yuda kukosea na kwenda njia yake mwenyewe

Nafasi iliachwa wazi sababu Yuda alimsaliti Yesu, aliondoka, na akafa.

Wakawapigia kura

Walitumia kura kuamua kati ya Yusufu na Mathiasi

Kura ikamwangukia Mathiasi

Kura iliashiria kwamba Mathiasi alikuwa amechaguliwa kuchukua nafasi ya Yuda

Alihesabiwa pamoja na mtume kumi na mmoja

"wanafunzi walimchukulia kuwa ni mmoja wa mitume"

Acts 2

Matendo 02: Maelezo ya Jumla

Muundo na mpangilio

Tafsiri zingine zimesongeza kila mstari wa ushairi mbali kulia kuliko maandiko mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi kutumia ushairi ulionukuliwa kutoka Agano La Kale katika 2:17-21,25-28 na 34-35.

Tafsiri zingine zimenukuu kutoka Agano la Kale katika mkono wa kulia wa ukurasa mbali na maandishi mengine. ULB hufanya hivi kutumia nukuu ya 2:31

Matukio yanayofafanuliwa katika sura hii huitwa "Pentekoste." Watu wengi huamini kwamba kanisa lilianza wakati Roho Mtakatifu alikuja kuishi ndani ya waumini katika sura hii.

HANA MAALUM KATIKA SURA HII

NDIMI

Neno "ndimi" lina maana mbili katika sura hii. Luka anaelezea kilichoshuka kutoka mbinguni (Matendo 2:3) kama kilichofanana na ndimi za moto. Hii ni tofauti na "ulimi wa mwale," ambao ni moto unaofanana na ulimi. Luka pia anatumia neno "ndimi" kuelezea lugha walizozungumza watu baadaya kujazwa na Roho Mtakatifu (Matendo 2:4-6).

SIKU ZA MWISHO

Hakuna ajuaye wakati "Siku za mwisho" (Matendo 2:17) zilipoanza. Tafsiri yako lazima isielezee zaidi ya ULB inavyoeleza. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lastday)

Batiza

Neno "batiza" katika sura hii linaashiria ubatizo wa Wakristo (Matendo 2:38-41). Ingawa tukio lililotajwa katika Matendo 2:1-11 ni ubatizo wa Roho Mtakatiu ambao Yesu aliahidi katika Matendo (1:5, neno "batiza" hapa halikuashiria hilo tukio (tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#baptize).

Unabii wa Yoeli

Utabiri mwingi wa Yoeli ulitimilika katika siku ya Pentekoste (Matendo 2:17-18), lakini vitu vingine alivyosema Yoeli havikutendeka (Matendo 2:19-20). (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet)

Maajabu na ishara

Haya maneno yanaashiria mambo ambayo Mungu pekee yake angeyatenda kuonyesha kwamba Yesu ndiye yule wanafunzi wake walinena juu yake.

<< | >>

Acts 2:1

Maelezo ya Jumla

Hili ni tukio jipya; hii sasa ni siku ya Pentekoste, siku 50 baada ya pasaka.

Maelezo ya jumla

Neno "wao" huenda linarejea kwenye kundi la mitume na waumini wengine 120 ambao walikuwa pamoja katika. Luka 1:15 ametaja vile.

Ghafla

Neno hili linatumika hapa kuonesha tukio lililotokea pasipo kutegemea.

hapo ikaja sauti kutokea mbinguni

"kelele ilitokea mawinguni mahali pa makao ya Mungu"

Sauti kama uvumi wa nguvu wa upepo

"kama uvumi wa upepo wa nguvu sana" au kama mvumo wa nguvu"

Nyumba yote

Hii inaweza ikawa nyumba au jengo kubwa.

Kulionekana kwao ndimi kamaza moto

Hizi si ndimi hasa au moto 1) ndimi zilizoonekana kama za moto au 2) mwale mdogo wa moto ulioonekana kama ndimi wakati unawaka katika sehemu ndogo, kama vile chemli , mwale unaweza ukajitengeneza kama ulimi.

Wote walijazwa na Roho Mtakatifu

Hii inaweza kutafsiriwa kama kitenzi tendaji. Roho Mtakatifu aliwajaze wote waliokuwa kwenye hicho chumba.

Acts 2:5

Maelezo ya jumla

Mstari wa 5 unatoa taarifa ya nyuma kuhusu idadi kubwa ya wayahudi ambao walikuwa wanaishi Yerusalemu, wengi wao walikuwapo wakati wa tukio hili.

Maelezo ya jumla

Hapa neno "wao" linajumuisha waumini na neno "yake" linataja kila mtu katika kundi.

watu wa Mungu

watu waliotaka kuheshimu na au kumwabudu Mungu

kila taifa chini ya mbingu

"kila taifa duniani" Watu kutoka mataifa mbalimbali walikuwa wamekuja Yerusalemu.

Wakati sauti hii iliposikika

Hii inarejea sauti ambayo ilikuwa kama upepo wa nguvu kuwa: "Waliposikia sauti hii"

Mkusanyiko

"kundi kubwa la watu"

Walishangaa kwa mshangao mkuu

Maneno haya yana maana moha. Mshangao wao ulikuwa mkuu sana.

Kweli, hawa wote wanaoongea siyo Wagalilaya?

Watu waliuliza swali wakionyesha mshangao wao kuwa hawa ni wa eneo moja na lugha yao ni moja iweje waongee na lugha za mataifa yetu?

Acts 2:8

Kwa nini sisi tunawasikia, kila mmoja katika lugha tulizozaliwa nazo?

Inawezekana ikamaanisha 1) ni swali halisi ambalo watu walihitaji jibu lake kutokana na mshangao wao au 2) swali lisilohitaji jibu lililodhihirisha jinsi walivyoshangaa.

Waparthi ... Waelamu

Hii inaorodhesha baadhi ya mataifa, mikoa na miji ambayo watu walitoka.

Wabadili dini kufuata desturi za kiyahudi

"watu wasio Wayahudi ambao wamekuwa Wayahudi" au "waliogeukia dini ya Kiyahudi"

Acts 2:12

wameduwaa na kutatanishwa;

Watu hawakujua nini cha kufikiri kuhusu kilichokuwa kinatokea. "shangazwa na kuchanganyikiwa."

Hawa wamejazwa kwa mvinyo mpya."

Baadhi ya watu waliwatuhumu waumini kwa kile kilichotokea wakidai wamelewa na mvinyo.

mvinyo mpya

Linaelezea mvinyo unaoandaliwa kuwa na nguvu kuliko mvinyo ya kawaida

Acts 2:14

Sentensi unganishi:

Petro anaanza kuwasilisha hotuba yake kwa Wayahudi siku ya Pentekoste.

alisimama pamoja na wale kumi na mmoja

Mitume wote walisimama kuunga mkono hoja ya Petro

hili lijulikane kwenu, sikilizeni kwa makini

Petro anaelezea tukio ambalo watu wamelishuhudia likiendelea. Wamsikilize kwa makini

saa hizi ni asubuhi saa tatu.

"saa tatu za asubuhi. Petro anawafikirisha wasikilizaji wajue kuwa watu hawanyi wala hawalewi muda huo wa mapema katika siku.

Acts 2:16

Maelezo ya jumla

Petro anaendelea na hotuba yake kwa Wayahudi akiwakumbusha unabii wa nabii Yoeli katika Agano la Kale kwamba tukio hilo linalingana na utabiri huo.

Hiki ndicho kilichosemwa kupitia nabii Joeli

"hiki ni kile ambacho Mungu alisema na alimwabia Nabii Yoeli aandike mambo ambayo Mungu alikwishasema"

kumimina Roho wangu juu ya miili yote

Hii ni tamathali ya usemi ikizungumzia jinsi Mungu siku za mwisho atamtoa Roho Mtakatifu kwa wingi kwa watu wote.

Acts 2:18

Sentensi unganishi

Petro anaendelea kumnukuu nabii Joeli.

watumishi wangu na watumishi wangu wa kike

Wote waume kwa wake ni watumishi. Mungu atamwaga Roho wake kwa watumishi wake wote kwa wanaume na kwa wake.

Nitammimina Roho wangu

Mungu anamtoa Roho wake kwa ukarimu kwa watu wote.

toa unabii

Mungu anawatia msukumo kuizungumza kweli ya Mungu.

mafusho ya moshi.

"umande" au "ukungu"

Acts 2:20

Sentensi unganishi

Petro anahitimisha kumnukuu nabii Joeli.

Jua litageuzwa kuwa giza

Inamaanisha kwamba, jua litaonekana kuwa jeusi badala ya kutoa nuru.

na mwezi kuwa damu

Inamaanisha kwamba, mwezi utaonekana mwekundu kama damu.

Ya ajabu

"Si ya kawaida" au "muhimu"

kila mmoja ambaye huliitia jina la Bwana ataokoka

"Bwana atamwokoa kila mmoja ambaye anamwita"

Acts 2:22

Sentensi unganisha

Petro anaendelea na hoja yake kwa Wayahudi aliyoianza

sikieni maneno haya

"Sikilizeni kwa yale ninayotaka kuwaambia"

aliyethibitishwa na Mungu kwenu kwa matendo ya uweza na maajabu, na ishara

Inamaanisha Mungu anathibitisha kuwa alimchagua Yesu kwa huduma yake ya kudhihirisha matendo makuu ya miujiza.

mwanadamu aliyethibitishwa na Mungu kwenu

"Mtu ambaye Mungu alimdhibitisha kwenu"

Kwa sababu ya mpango uliokusudiwa tangu mwanzo, na maarifa ya Mungu

Inamaanisha kuwa, Mungu alipanga na kujua tangu zamani kwamba yangetokea nyakati za Yesu

ambaye Mungu alimwinua

Maana yaweza kuwa: 1) "Mlimtia Yesu katika mikono ya maadui" au 2) Yuda alimsaliti Yesu kwenu"

kwa mikono ya watu wahalifu, mlimsulibisha na kumuua

Ingawa watu wahalifu kweli walimsulibisha Yesu, hapa Petro anawashitaki kundi lote kwa kumwua kwasababu walikuwa wamekusudia Yesu auawe.

akauondoa uchungu wa mauti kwake, kwasababu haikuwezekana kwake kumilikiwa na huo.

etro anazungumzia kifo kama mfano wa binadamu anayeshikilia wafungwa hara kusababisha mateso makali.

Acts 2:25

Maelezo ya jumla

Petro ananukuu kifungu ambacho Daudi alikiandika katika Zaburi kinachotaja kuteswa kwa Yesu na kufufuka kwake.

Maelezo ya jumla

Tangu Petro ataje kwamba Daudi alitangulia kusema maneno kuhusu Yesu, maneno "Mimi na Yangu" yanamtambulisha Yesu. Na maneno Bwana na Yeye" yanamtambulisha Mungu.

mbele ya uso wangu

Linamaanisha, "Mbele yangu au mbele ya uwepo wangu"

pembeni mkono wangu wa kulia

Mkono wa kulia ulifikiriwa kuwa ni wa nguvu sana. Mtu aliye mkono wa kuume alikuwa ama mtumishi mwenye nguvu sana au msaidizi mwenye uwezo sana.

moyo wangu ulikuwa na furaha na ulimi wangu ulishangilia.

NI: "Nilikwa na furaha na kushangilia"

mwili wangu utaishi katika ujasiri

"Ingawa hata mimi ni wa kufa tu, nitakuwa na ujasiri kwa Mungu"

Acts 2:27

Sentensi unganishi

Petro anamaliza nukuu ya Daudi.

Maelezo ya jumla

Petro anasema, Daudi alisema maneno kuwa Mtakatifu wangu akimaanisha Yesu na maneno "wako" akimaanisha Mungu.

wala hutaruhusu Mtakatifu wako kuona uozo

Mwili wake Masihi hautabaki maiti muda mrefu mpaka uoze. au "kuchakaa"

njia za maisha

"kweli yenye-kuhuisha"

nijae furaha mbele ya uso wako.'

Neno "Uso" anamaanisha uwepo wa Mungu.

furaha

"Shangwe au Kicheko"

Acts 2:29

Sentensi unganishi

Petro anaendelea na hotuba yake aliyoianzisha kwa Wayahudi wanaomzunguka na kwa waumini wengine wa Yerusalemu.

yeye alikufa na akazikwa

"He died and people buried him"

kwamba ataweka mmoja katika uzao wake kwenye kiti cha enzi

"Mungu angemtuma mmoja wa uzao wa Daudi juu ya kiti cha enzi cha Daudi"

Aliliona hili mapema

Mungu alijua hata kabla lilikuwa halijatokea.

wala alikuwa hakuachwa kuzimu

Mungu hakumwacha Yesu kuzimu.

wala mwili wake haukuoza.'

Mwili kuoza kunamaanisha kuteketea baada ya kifo. hivyo Mungu hakumwacha Yesu muda ambao hatA mwili wake uteketee.

Acts 2:32

Maelezo ya Jumla

Neni "sisi" linaelezea wanafunzi na wale wotewaliokuwa mashahidi wa kufufuka kwa Yesu baada ya kifo chake.

Mungu alimfufua

Neno "alimfufua" Linaelezea kuwa Mungu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu.

akiwa ameinuliwa katika mkono wa kuume wa Mungu

Mungu alimwinia Yesu juu katika mkono wake wa kuume.

yeye amemimina hii ahadi,

Neno "mimina" lina maana Yesu ambaye ni Mungu amefanya tukio hili litokee la kumtoa Roho Mtakatifu kwa waumini.

Acts 2:34

Sentensi unganishi

Petro anamaliza hotuba yake kwa Wayahudi aliyoianza

Maelezo ya jumla

Petro tena ananukuu moja ya Zaburi za Daudi. Daudi hazungumzi kwa nafsi yake mwenyewe katika zaburi hii bali anazungumzia juu ya Yasu Masihi.

mpaka nitakapowafanya adui zako kigoda kwa ajili ya miguu yako

Inamaanisha Mungu atafanya ushindi mkamilifu wa maadui wa Masihi na kuwaweka chini yake.

nyumba yote ya Israeli

Inamaanisha taifa zima la Israeli.

Acts 2:37

Sentensi unganishi

Wayahudi wanaitikia hotuba ya Petro na Petro anawajibu.

waliposikia hivyo

"wakati watu waliposikia Petro akisema"

wakachomwa katika mioyo yao

"Maneno ya Petro yaliwachoma mioyo yao" au "kusikia hatia moyoni na kujawa na huzuni"

kubatizwa

"Turuhusu tupate kubatizwa"

Ni ahadi kwaajili yako

"Ahadi ni kwaajili yako"

wale wote walioko mbali

"WAtu wote waliombali na Mungu mioyoni mwao.

Acts 2:40

Sentensi unganishi

Huu ni mwisho wa sehemu ya habari kwa tukio la siku ya Pentekoste. Inaanza sehemu nyingine inayoelezea jinsi gani waumini waliendelea kuishi baada ya siku ya Pentekoste.

alishuhudia na kuwasihi

"Aliwaambia waziwazi na kuwasihi waitikie kwa ujumbe alioutoa kwao.

Jiokoeni mtoke katika kizazi hiki kiovu

Wajiokoe kutoka katika adhabu ya Mungu itakayowapata watu waovu.

wakayapokea maneno yake

Inamaanisha wakayapokea maneno aliyoyasema Petro kuwa yalikuwa ya kweli.

Walibatizwa

Wote walioamini walibatizwa.

hapo wakaongezeka katika siku hiyo kama watu elfu tatu

"watu wapatao elfu tatu waliongezeka"

katika kuumega mkate

Walishiriki na kula chakula kwa pamoja

Acts 2:43

Hofu ikaja juu ya kila nafsi

watu walijawa na hofu na kicho cha Mungu ndani yao

maajabu mengi na ishara zikafanyika kupitia mitume

Mungu alifanya miujiza na ishara nyingi kupitia wanafunzi wake.

wote walikuwa pamoja

Inaweza kuwa, "wote waliamini jambo hilo moja" au " waumini wote walioamini walikuwa pamona katika sehemu moja"

walikuwa na vitu vyote kwa ushirikiano

"walitumia mali zao kwa kumgawia kila mmoja na mwenzake"

mali walizo miliki

Mashamba na vitu vingine vilivyokuwa wanavimiliki.

kugawanya kwa wote kulingana na hitaji la kila mmoja.

Kila mmoja aligawiwa kulingana na uhitaji wake.

Acts 2:46

waliendelea wakiwa na lengo moja

Waumini waliendelea kukutana pamoja, kwa kusudi moja.

walimega mkate kwenye nyumba zao

walishirikiana kula chakula chao katika nyumba zao na pia kula chakula cha Bwana kwa pamoja.

kwa furaha na unyenyekevu wa moyo

Hii inamaana bila kiburi, kwa furaha, bila choyo na bila kuangalia cheo au upendeleo.

wakiwa na kibali na watu wote

"Watu wote waliwakubali"

ambao walikuwa wakiokolewa

Ambao Bwana alikuwa akiwaokoa

Acts 3

Matendo 03 Maelezo kwa jumla

Dhana maalum katika sura hii

Agano Mungu aliagana na Abrahamu

Sura hii inaeleza kwamba Yesu alikuja kwa Wayahudi kwa sababu Mungu alikuwa akitimiza sehemu yake ya agano lake na Abrahamu. Petero alifikiri kwamba Wayahudi ndio waliokuwa na hatia ya kumuua Yesu.

Tafsiri zingine za utata katika sura hii

"Mliyemtia mikononi mwa wakuu"

Warumi ndio waliomuua Yesu, lakini walimuua kwa sababu Wayahudi walimkamata, wakamleta kwa Warumi, wakawaambia wamuue. Kwa sababu hii, Petero alifikiri kwamba hao ndio waliokuwa na hatia ya kumuua Yesu. Lakini anawaeleza yakwamba hao ndio wa kwanza ambao Mwenyezi Mungu ametuma wafuasi wa Yesu kuwakaribisha watubu (Luka 3:26). (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#repent)

<< | >>

Acts 3:1

Sentensi unganishi

Siku moja; Petro na Yohana wanakwenda hekaluni

Maelezo ya jumla

Mstari wa 2 unatoa mazingira juu ya mtu aliyekuwa kiwete.

ndani ya hekalu

"katika eneo la hekalu" au "katika hekalu." walikuwa hawakuenda ndani ya jengo la hekalu ambamo makuhani waliotumika tu ndio walikuwa wanaruhusiwa.

Mtu fulani, kiwete tangu kuzaliwa, alikuwa akibebwa kila siku na alikuwa akilazwa katika mlango wa hekalu.

Kila siku watu walikuwa wakimbeba mtu huyo na kumlaza karibu na mlango wa hekalu.

Kiwete

Asiyeweza kutembea

mlango wa hekalu ulioitwa mzuri

Mlango wa hekalu uliokuwa ukiitwa mzuri.

Acts 3:4

Petro, akimkazia macho

"Petro na Yohana walimwangalia mtu huyo kwa makini na Petro akaongea"

Kiwete akawaangalia

"kiwete aliwatazama Petro na Yohana kwa makini"

Fedha au dhahabu

Fedha au dhahabu ilitimika kuwakilisha pesa.

kile nilichonacho

Inafahamika kuwa Petro alikuwa na uwezo wa kumponya yule mtu.

katika jina la Yesu Kristo

"Kupitia mamlaka na nguvu ya Jina la Yesu Kristo" lilimponya mtu yule.

Acts 3:7

aliingia ... katika hekalu

Hakuingia ndani ya hekalu mahali makuhani pekee wanaruhusiwa kuingia. Yeye aliingia kwenye uwanda wa hekalu

Acts 3:9

Wakatambua kwamba alikuwa ni yule mtu

Kila mmoja alishuhudia kuwa aliyeponywa ndiye alikuwa mtu yule.

Lango la uzuri

Hili lilikuwa moja ya jina la milango ya kuingia kwenye eneo la hekalu.

walijawa na mshangao na kustaajabu

Watu walishikwa na mshangao mkubwa.

Acts 3:11

Sentensi unganishi

Baada ya kuponywa kwa mtu aliyekuwa hawezi kutembea, Petro anaongea na umati.

Maelezo ya jumla

Katika ukumbi uluokuwa ukiitwa Solomoni. Hapa iko wazi kuwa Petro alitumia eneo hili kutoa hotuba yake, haikuwa ndani ya hekalu ambamo ni makuhani tu walioruhusiwa kuingia.

maajabu makuu

"kujawa na mshangao" au "Kaduwaa"

Wakati Petro alipoona hiki

"Petro alipoona mkutano unaongezeka na kuzidi kushangaa.

Ninyi watu wa Israeli

"Waisraeli wenzangu". Petro akizungumza na mkutano. Neno "watu" katika mkutadha huu inahusisha kila mmoja aliyepo.

kwa nini mnashangaa?

Petro anauliza swali hili ili kuwaambia watu wasishanganzwe na kile kimetokea.

Kwa nini mnayaelekeza macho yenu kwetu, kama kwamba tumemfanya huyu atembee kwa nguvu zetu wenyewe au uchaji wetu?

Petro anawauliza swali hili ili kuwathibitishia kuwa tukio hilo halikutendwa na wao yaani Petro na Yohana, hivyov wasiwatazame wao kama ndiyo waliomponya yule kiwete.

Acts 3:13

Sentensi unganishi

Petro anaendelea na hotuba yake kwa Wayahudi aliyoianza

ambaye mlimkabidhi

"ambaye mlimkamata na kumkabidhi kwa Pilato"

na kumkataa mbele ya uso wa Pilato

"yeye mlimkataa mbele ya Pilato "

yeye alipoamua kumweka huru

"Pilato alipoamua kumweka Yesu huru"

badala yake mkataka muuaji aachwe huru.

"Mlimtaka Pilato amfungulie muuaji"

Acts 3:15

Maelezo ya jumla

Neno "sisi" linawajumuisha Petro na Yohana.

Mfalme wa uzima

Neno hili linamtaja Yesu "Ni mmoja awapaye watu uzima wa milele au "Mtawala wa maisha"

Sasa

Neno hili lilitumika kuhamisha usikivu wa mkutano kwa yule kiwete

kwa imani katika jina lake

Kiwakilishi "Jina" ni jina la Yesu.

amempatia mtu huyu nguvu

"amemfanya mtu huyu nguvu ya kupona"

Acts 3:17

Sasa

Hapa Petro anageuza usikivu wa mkutano kutoka kwa kiwete na anaendelea kuwaambia moja kwa moja.

kwamba mlitenda katika ujinga

Maana inayowezekana 1) Hao watu hawakujua kuwa Yesu alikuwa Masihi au 2) Watu hawakujua maana ya kile walichokuwa wakifanya.

Mungu aliwaambia mapema kwa vinywa vya manabii wote

Manabii waliponena, ilikuwa kama Mungu mwenyewe aliyenena kwasababu aliwaambia nini cha kusema.

kwa mdomo wa manabii wote

Inamaanisha yale yote yaliyonenwa "kupitia manabii" na kuyaandika.

Acts 3:19

Tubuni ... na kugeuka

"Kutubu na kugeuka kunamaanisha kubadirisha njia ya mtazamo na fikra zao kutoka katika dhambi na wamgeukie Mungu"

ili kwamba dhambi zenu ziweze kuondolewa kabisa

"kufuta" au "iliyoondolewa" ili Mungu aweze kuzifuta dhambi zao.

kusudi zije nyakati za kuburudika kutokana na uwepo wa Bwana

"Muda wa kuburudishwa katika uwepo wa Bwana inaweza kuwa; 1) Muda ambao Mungu anaziimarisha roho za watu wake; 2) Muda ambao Mungu analeta uamsho kwenu.

kwamba aweze kumtuma Kristo

"Kwamba anaweza tena kumtuma Kristo". Huu ni ujio mwingine wa Yesu Kristo.

ambaye ameshateuliwa kwa ajili yenu

Mungu alishamteua Yesu kwa ajili yao.

Acts 3:21

Sentensi ungaishi:

Petro anaendelea na hotuba yake kwa Wayahudi waliokuwa wamesimama kwenye eneo la hekalu.

Maelezo ya Jumla

Katika mistari ya 22-23 Petro ananukuu mambo fulani Musa alisema mapema kuhusu Masihi.

mbingu lazima zipokee

Ni mmoja ambaye mbingu lazima zimpokee. Petro anazungumza na mbingu kama anaongea na mtu aliyempokea Yesu nyumbani mwake.

mpaka wakati wa kurejeshwa kwa vitu vyote

"hadi wakati ambao Mungu atarejesha vitu vyote"

ambavyo Mungu alizungumzia zamani za kale kwa vinywa vya manabii watakatifu

"Mungu aliwaambia watakatifu wake manabii kuzungumzia habari zao"

manabii watakatifu ambao wamekuwapo tangu zamani za kale

"manabii wake watakatifu ambao waliishi zamani sana"

atainua nabii

"atateua mmoja kuwa nabii"

Itatokea kwamba kila mtu ambaye hasikilizi kwa nabii huyo ataangamizwa kabisa

mtu asiyemsikiliza Nabii ambaye Mungu amemtuma atamwangamiza kabisa.

Acts 3:24

Sentensi unganishi

Petro anahitimisha hotuba yake kwa Wayahudi aliyoianza

Ndiyo, na manabii wote

"Ni dhahili manabii wote" Neno hapa "ndiyo" linaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata.

tokea Samweli na wale waliofuata baada yake

"wale manabii ambao walifuata baada ya uhai wa samweli"

siku hizi

"siku hizi" au "mambo ambayo yanatokea sasa"

Ninyi ni wana wa manabii na wa agano

"ninyi ni warithi wa manabii" na "ninyi ni warithi wa agano."

katika mbegu yako

"kwasababu ya uzao wako"

familia zote za dunia zitabarikiwa.'

Anamaanisha mataifa mbalimbali yatabarikiwa kwa ajili yake.

Baada ya Mungu kumwinua mtumishi wake,

"Baada ya Mungu kumchagua mtumishi wake" au "Baada ya Mungu kutoa mamlaka kwa mtumishi wake"

mtumishi wake

Hii inarejea kwa Masihi wa Mungu, Yesu.

Acts 4

Matendo 04 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Tafsiri zingine zimetenga kila mstari wa ushairi kulia zaidi kuliko maandishi mengine ili isomeke vyema.ULB hufanya hivi na ushairi ulionukuliwa kutoka Agano la kale 4:25-26

DHANA MAALUM KATIKA SURA HII

umoja

Wakristo wa kwanza walitamani sana kuwa na umoja, Walitaka kuamini mambo sawa na kusaidiana kwa kila kitu walichokimiliki huku wakisaidia pia waliohitaji.

"Ishara na Maajabu"

Maneno haya yanaashiria vitu ambavyo vinaeza kufanywa tu na Mungu. Wakristo walitaka Mungu afanye yale tu ambayo angeweza kuyafanya ili watu waamini kwamba waliyoyanena kumhusu Yesu yalikuwa ya ukweli.

Mifano muhimu kwenye hii sura

Jiwe la pembeni

Jiwe la pembeni lilikuwa kipande cha jiwe kilichowekwa chini wakati wa ujenzi wa jengo. Neno hili limetumika kumaanisha sehemu muhimu ya kitu,ile sehemu tegemeo. Kusema ya kwamba Yesu ni jiwe kuu la pembeni la kanisa ni kusema kwamba hakuna kitu ndani ya kanisa kilicho na umuhimu kuliko Yesu na ya kwamba kila kitu ndani ya kanisa kinamtegemea, (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith)

Sehemu zingine zenye utata katika tafsiri ya sura hii.

Jina

"Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo" (Matendo 4:12). Kwa maneno haya Petro alimaanisha kwamba hamna mtu yeyote ambaye amewahi kuwa duniani ama atakayekuja duniani kuwaokoa watu.

<< | >>

Acts 4:1

Sentensi unganishi

Viongozi wa dini walimkamata Petro na Yohana baada ya Petro kumponya yule mtu aliyezaliwa kiwete.

wakaja kwao

"waliwasogelea" au "walikuja kwao"

Walikuwa wameudhika sana

Walikuwa na hasira. Masadukayo kwa upekee wao wangekuwa na hasira kwa Petro na Yohana kwasababu hawakuamini ufufuo.

walikuwa wanawafundisha watu kuhusu Yesu na kutangaza juu ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu

Petro na Yohana walikuwa wakisema Mungu angewainua watu kutoka mautini sawa na vile Yesu alivyoinuliwa kutoka miongoni mwa wafu. Petro anazungumzia ufufuo wa Yesu na ufufuo wa watu wote kwa ujumla.

Waliwakamata

Makuhani na mlinzi wa hekalu pamoja na Masadukayo waliwakamata Petro na Yohana.

Kwavile ilikuwa jioni sasa

Ilikuwa tendo la kawaida kutowahoji watu wakati wa usiku.

na idadi ya wanaume waliokuwa wameamini

Hii inamanisha kwa idadi ya wanaume tu, wanawake na watoto walioamini hawakuhesabiwa.

Walikuwa yapata elfu tano

"walikuwa kama elfu tano" au "iliongezeka hadi elfu tano"

Acts 4:5

Sentensi unganishi

Petro na Yohana wanajibu swali wa viongozi bila ya kuwa na woga.

Maelezo ya jumla

Neno "wao" linafafanua juu ya Wayahydi kwa ujumla wao.

Hata ilipofika asubuhi siku iliyofuata, kwamba

Kipengere hiki kilitumika hapa kuonyesha tukio lilipoanzia.

wakuu wao, wazee na waandishi

Hii ni rejea kwa Sanhendrini, mahakama ya wazee wa kiyahudi kilichounganisha makundi haya matatu ya wayahudi.

Yohana, na Alexander

Wanaume hawa wawili walikuwa wajumbe wa familia ya Kuhani mkuu. Huyu siye yule Yohana Mtume.

Kwa nguvu gani

"nani aliyewapa nguvu" au "kitu gani kiliwapa nguvu." Walijua Petro na Yohana wasingemponya mtu kwa nguvu zao wenyewe.

Kwa jina gani

"ni nani aliyewapa mamlaka"

Acts 4:8

Kisha, Petro, akiwa amejaa Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu akiwa amemjaza Petro.

kama sisi siku ya leo tunahojiwa kuhusu tendo jema lililofanywa kwa mtu huyu mgonjwa - kwa namna gani mtu huyu alifanywa mzima?

Petro aliuliza swali hili kufafanua kwamba ilikuwa sababu halisi ya kuteswa kwao. Mnatuuliza leo kwa namna gani mtu huyu amepata kupona.

Hebu lijulikane hilo kwenu na kwa watu wote katika Israel

Na ijulikane kwenu na watu wote wa Israel kujua hili.

kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,

Neno "Jina" linafafanua nguvu na mamlaka ya jina hilo. Kwa mamlaka ya Jina la Yesu Kristo wa Nazarethi.

Acts 4:11

Sentensi unganishi

Petro anahitimisha hotuba yake kwa viongozi wa dini ya kiyahudi aliyoianza

Yesu Kristo ni jiwe ambalo ninyi wajenzi mlilidharau, lakini ambalo limefanywa kuwa jiwe kuu la pembeni.

Petro ananukuu kutoka Zaburi, akimaanisha viongozi wa Kiyahudi, kama wajenzi, waliomkataa na Yesu, lakini Mungu alimfanya kuwa wa muhimu zaidi katika ufalme wake, kama jiwe la pembeni katika ujenzi lilivyo la muhimu.

ninyi wajenzi mlilidharau

"Ninyi wajenzi mlimkataa"

Hakuna wokovu katika mtu mwingine awaye yote

Yesu ni mtu pekee aliye na uwezo wa kuokoa

Kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa watu

Hii inamaanisha, hakuna Jina jingine chini ya mbingu Mungu amswapa wanadamu.

ambalo kwa hilo tunaweza kuokolewa.

J"ina ambalo laweza kuokoa au ambaye aweza kuokoa"

Acts 4:13

Maelezo ya jumla

Paulo anaendelea kuzungumzia Wayahudi Viongozi.

Wakati walipoona ujasiri wa Petro na Yohana

Neno "Ujasiri" linaelezea njia ambayo Petro na Yohana wameitumia kujibu za viongozi Wayahudi.

wakagundua kwamba walikuwa ni watu wakawaida wasio na elimu

Wayahudi viuongozi walitambua hivi kwasababu ya njia ambayo Petro na Yohana waliinena.

Walikuwa ni watu wa kawaida, wasio na elimu

Neno "kawaida" na "wasio na Elimu" ni maneno yanayogawana maana moja. Petro na Yohana hawakupata mafunzo ya elimu katika sheria ya kiyahudi

mtu aliyeponywa

Mtu ambaye alikuwa ameponya na Yesu kupitia Petro na Yohana

hawakuwa na kitu cha kusema dhidi ya hili.

Hawakuwa na cha kusema dhidi ya Petro na Yohana juu ya kuponywa kwa huyo.

Acts 4:15

Mitume

Linaelezea juu ya Petro na Yohana.

tutawafanyaje watu hawa?

Wayahudi viongozi wanauliza swali kama wamechanganyikiwa kwasababu kwa kuwa hawakufikiri nini cha kuwatendea Petro na Yohana. "Hakuna cha kuwatendea hawa wanaume"

Ni kweli kwamba muujiza wa ajabu umefanyika kupitia wao unajulikana na kila mmoja anayeishi Yerusalemu

Inamaanisha; kila mtu anayekaa Yerusalamu anajua juu ya muujiza uliotendwa na hawa wanaume.

ili kwamba jambo hili lisienee miongoni mwa watu

Neno "jambo" linamaanisha muujiza wowote au mafundisho ya Petro na Yohana yanaweza kuendelea kusambaa.

kamwe wasinene wala kufundisha kwa jina la hili.

Neno "Jina" linamaanisha ubinadamu wa Yesu. Wasinene tena kwa yeyote kuhusu huyu mtu, Yesu.

Acts 4:19

Maelezo ya jumla

Neno "sisi" linaelezea Petro na Yohana, lakini si kwa wale ambao waliokuwa wakiwaelezea.

Kama ni sahihi machoni pa Mungu

Neno "machoni pa Mungu" linamaanisha maoni ya Mungu. Kama Mungu anafikiri ni sawa kuwatii watu kuliko Mungu.

hatuwezi kuacha kuyanena

"Lazima tutaendelea kunena" au "Hatutaacha kunena"

Acts 4:21

Maelezo ya jumla

Msitari wa 22 unatoa habari ya nyumba kuhusu umri wa mtu kiwete aliyeponywa.

Baada ya maonyo zaidi

Wayahudi Viongozi waliwatishia Petro na Yohana kuwapa adhabu tena.

Hawakuweza kupata sababu yoyote ya kuwaadhibu

Viongozi hawakuweza kupata kujua kwa namna gani wawaadhibu Petro na Yohana bila ya kusababisha vurugu miongoni mwa watu waliomwona mtu aliyeponywa.

kwa kile kilichokuwa kimetendeka

Kwa kile Petro na Yohana walichokuwa wametenda

Mtu aliyekuwa amepokea muujiza wa uponyaji

Mtu yule ambaye Petro na Yohana walikuwa wamemtendea muujiza wa uponyaji.

Acts 4:23

Maelezo ya jumla

Wakinena pamoja, watu walinukuu Zaburi ya Daudi kutoka Agano la Kale.

Maelezo ya jumla

Neno "wao" linamaanisha baadhi ya waumini, lakini si Petro na Yohana.

Walikuja kwa watu wao

Walikwenda kwa waumini wenzao.

kwa Roho Mtakatifu, kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ulisema

Hii inamaanisha Roho Mtakatifu alisababisha Daudi kunena au kuandika kile Mungu alichosema.

Kwa kinywa cha baba yetu Daudi

Neno "kinywa" linaelezea yale maneno ambayo Daudi aliyasema ama aliyaandika "Kwa maneno ya baba yetu Daudi"

Kwanini watu wa mataifa wamefanya ghasia, na watu wametafakari mambo yasiyofaa?

Hili ni swali lenye jibu linaloelezea maneno yenye ubatili ya kumpinga Mungu.

watu wametafakari mambo yasiyofaa

Watu wanatafakari maneno ya ubatili yaliyo kinyume na Mungu.

Acts 4:26

Sentensi unganiishi:

Waumini wanakamilisha nukuu yao kutoka kwa mfalme Daudi katika zaburi walizozianza

Wafalme wa dunia wamejipanga pamoja, na watawala wamekusanyika kwa pamoja dhidi ya Bwana

Mistari hii miwili, Wafalme na Watawala kimsingi ni jambo moja kuonyesha unganiko la kufanya biidi katika kupinga kazi ya Mungu

wamekusanyika kwa pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya masihi wake

Waliunganisha majeshi yao pamoja kupigana vitani. Au kuwa kinyume na Masihi wa Mungu.

Acts 4:27

Sentensi unganishi

Waumini wanaendelea na maombi.

Katika mji huu

"Katika Yerusalemu"

mtumishi wako mtakatifu Yesu

"Yesu anayekutumikia kwa uaminifu"

kufanya yote ambayo mkono wako na mapenzi yako yaliyaamuru

Neno "Mkono" limetumika kwa maana ya nguvu za Mungu.

Acts 4:29

Maelezo unganishi

Waumini wanakamilisha maombi yao waliyoyaanza

yaangalie matisho yao,

Neno, "Yaangalie" Ni ombi kwa Mungu kuchukua hatua dhidi ya vitisho vya Wayahydi viongozi kwa vitisho vyao kwa waumini.

kwamba unaponyosha mkono wako kuponya

Neno "Mkono" unaelezea nguvu za Mungu katika kuponya watu.

kupitia jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu

Neno "Jina" Linamaanisha nguvu na mamlaka ya Mtakatifu Yesu

eneo ambalo walikusanyika kwa pamoja likatikiswa

Eneo walipokuwa wakifanyia maombi pakatikisika.

na wote wakajazwa na Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu aliwajaza wote, na kuanz kulinena neno la Mungu kwa ujasiri

Acts 4:32

Walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja

Neno "Moyo" linaelezea mawazo kuwa wote waliwaza kitu kimoja na moyo mmoja.

walikuwa na vitu vyote shirika

Waligawana vitu vyao kila mmoja na mwenzake.

na neema kubwa ilikuwa juu yao wote.

Pengine maana yake 1) Mungu aliwabariki waumini zaidi; au 2) Watu katka Yerusalemu waliwasaidia waumini katika hali ya juu.

Acts 4:34

waliokuwa na hati za viwanja au nyumba

Umiliki wa hati za viwanja na nyumba kwa waliokuwa wanamiliki Yerusalemu

waliviuza na kuleta pesa ya vitu waliyokuwa wameuza

Fedha ambayo walilipwa kutoka vitu walivyoviuza.

Waliweka chini ya miguu ya mitume

Hii ilikuwa ni njia ya waumini: 1) kuonyesha waziwazi mabadiliko ya mioyo na 2) kuwapa mitume mamlaka juu ya namna zawadi inavyopaswa kutumika.

mgawanyo ulifanywa kwa kila muumini, kulingana na kila mmoja alivyokuwa na hitaji.

Waligawanya pesa kwa waumini kwa aliyekuwa na uhitaji

Acts 4:36

Maelezo ya jumla

Luka anamwelezea historia ya Barnaba

Yusufu, mlawi, mtu kutoka Kipro, alipewa jina la Barnabasi na mitume

Mitume walimpa Yusufu jina jingine Barnaba

hiyo ikitafasiriwa

ambalo linaweza kupewa tafasiri

mwana wa faraja

Mitume walitumia hivyo kuonyesha kwamba Yusufu alikuwa mtu wa kutia moyo wengine

akaziweka chini ya miguu ya mitume

Aliwasilisha pesa kwa mitume.

Acts 5

Matendo 5 Maelezo kwa jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu"

Hakuna anayejua kwa ukamilifu iwapo Anania na Safira walikuwa Wakristo wa ukweli walipoamua kudangaya kuhusu kipande cha ardhi walichokiuza (Matendo 5:1-10), kwa maana Luka hataji swala hili. Anasema tu kwamba walikuwa "miongoni mwa walioamini" (Luke 4:32).Hata hivyo, Petero alifahamu kwamba walidanganya waumini, na alijua kwamba walikuwa wamsikiliza na kumtii shetani.

Walipowadanganya waumini, pia walimdanganya Roho Mtakatifu kwa sababu anaishi ndani ya Waumini.

Gereza

"Gereza ya uma" ambamo Baraza la Wayahudi walimueka ndani Petero (Matendo 5:18) huenda lilikuwa gereza.

<< | >>

Acts 5:1

Sentensi unganishi

Maelezo ya namna wakristo walivyokuwa wakishirikiana mahitaji kwa baadhi ya wakristo kuuza mali zao. Luka anatuambia habari za waumini wawili Anania na Safira walivyohusika katika ushirika huo.

Sasa

"Lakini sasa." Hii inaonyesha sehemu kumalizika na kuanza kwa maelezo ama habari mpya.

Mke wake pia alilijua

"Mke wake pia alijua kuwa Mmewe alikuwa ametunza nyumbani sehemu ya fedha kwa mauzo ya shamba lao".

kuiweka kwenye miguu ya mitume.

Inamaanisha kwamba waliwasilisha hiyo fedha kwa mitume.

Acts 5:3

Maelezo ya jumla

Kama lugha yako unayotumia haina haitumii maswali yenye majibu ndani ya swali, unaweza kutumia kame sentensi tu.

Kwanini Shetani ameujaza moyo wako...ardhi?

Petro alitumia swali hili kumkemea Anania. "Kwa namna gani umemruhusu Shetani kukushawishi ili kudanganya juu ya kiasi cha mauzo ya ardhi yenu."

kusema uongo kwa Roho Mtakatifu na kuficha sehemu ya mali ya shamba

Inaonyesha Anania alikuwa amewaambia mitume kuwa alichotoa kilikuwa kiasi chote cha mauzo ya shamba lake

Wakati lilipokuwa halijauzwa, halikuwa ni mali yako?

Petro alitumia maswali haya kumkumbusha Anania kwamba alikuwa na uwezo juu ya pesa yake. "Alikuwa na wajibu wa kusimamia pesa yake kwa uadilifu."

Ilikuwaje uwaze jambo hili moyoni mwako?

Petro alitumia swali hili kumkemea Anania. "Hukupaswa kuamua kuwa mwongo juu ya jambo hili."

Anania alidondoka chini na akakata roho

Anania alianguka chini kwasababu alikufa. Hakufa kwasababu alianguka chini bali alikufa na kisha akaanguka chini.

Acts 5:7

mke wake aliingia ndani

Mke wa Anania naye aliingia ndani ya nyumba walimokuwa mitume.

Kilichokuwa kimetokea

"Kwamba mme wake alikuwa amekufa"

kwa thamani hiyo

"Kwa thamani hiyo" linalenga kuthibitisha kama Anania alileta fedha kwa mitume yenye thamani sawa na thamani ya shamba lililouzwa.

Acts 5:9

Sentensi unganishi:

Huu ni mwisho wa sehemu ya habari kuhusu Anania na Safira.

Inakuwaje kwamba mmepatana kwa pamoja kumjaribu Roho wa Bwana?

Petro aliuliza hili kuonyesha hawa wawili kwamba walikubaliana kutenda dhambi kwa pamoja. "Mmekubaliana kwa pamoja kumjaribu Roho!"

miguu ya wale waliomzika mme wako

Hapa "Miguu" inamaanisha wanaume waliomzika Anania.

akadondoka miguuni pa Petro

Inamaanisha Safira alipokufa alidondoka mbele yamiguu ya Petro

Akapumua pumzi ya mwisho

Hii ni namna ya kusema kwamba "alikufa."

Acts 5:12

Sentensi unganishi

Luka anaendelea kuwaambia wasomaji kile kilichotokea siku za mwanzoni mwa kanisa Yerusalemu.

Ishara nyingi na maajabu vilikuwa vinatokea miongoni mwa watu kupitia mikono ya mitume

Miujiza na ajabu nyingi ilitendwa miongoni mwa watu kupitia mikono ya mitume.

ukumbi wa Sulemani.

Hili lilikuwa ni eneo Njia ya kutembea lililokuwa limezungukwa na nguzo zilizojengwa kushikilia paa ambalo watu waliliita Mfalme Sulemani.

walipewa heshima ya juu na watu.

Watu waliwaonyesha waumini heshima ya juu.

Acts 5:14

Maelezo ya jumla

Luka anatoa maelezo juu ya watu waliokuwa wakiishi Yerusalemu

waamini wengi walikuwa wakiongezeka kwa Bwana

Watu wengi walikuwa wakimwamini Bwana.

ili kwamba Petro akiwa anapita, kivuli chake kiweze kushuka juu yao

Inamaanisha kuwa Mungu angeweza kuwaponya wagonjwa kama kivuli cha Petro kingewagusa.

wote waliopagawa na roho wachafu,

"Wale ambao roho wachafu walikuwa wamewapagaa. Waliokuwa wakiteswa na roho wachafu"

wote waliponywa.

Mungu aliwaponya wote kwa njia ya mitume

Acts 5:17

Sentensi unganishi

Viongozi wa dini walianza kuwatesa waumini

Lakini

Neno "lakini" linaanzisha habari kinzani. Unaweza kutafasiri hii kwa namna ambavyo lugha yako hutambulisha habari kinzani.

kuhani mkuu aliinuka,

Neno "kuinuka" linamaanisha Kuhani mkuu aliamua kuchukua hatua, si kwamba aliinuka tu kutoka kwenye kiti chake alichokikalia.

na walijawa na wivu

Inamaanisha walijawa na wivu sana

wakanyosha mikono yao kuwakamata mitume

Waliwakamata mitume kwa nguvu, kwa kuwa walikuwa wameagiza walinzi wao wapate kuwakamata mitume.

Acts 5:19

Nendeni, mkasimame hekaluni

Mitume walikwenda kusimama hekaluni katika ile sehemu ya wazi, hawakuingia ndani ambamo hawaruhusiwi kuingia ispokuwa kwa makuhani tu.

maneno yote ya Uzima huu.

Hii inamaanisha ujumbe wa Injili ambao mitume walikuwa wakiutangaza.

wakati wa kupambazuka

Ilipoanza kuwa nuru, "Ingawa malaika alikuwa amewatoa mitume jela wakati wa usiku, hivyo kulipoanza kupambazuka mitume walikuwa tayari wamefika hekaluni.

kuwatuma gerezani ili kuwaleta mitume.

Inamaanisha kuhani alituma mmoja wao kwenda gerezani kuwachukua mitume na kuwaleta mbele ya baraza.

Acts 5:22

lakini tulipokuwa tukifungua, hatukuona mtu ndani

eno "hatukuona mtu" linawakilisha Mitume kwamba hawakuwakuta wakiwa ndani ya gereza.

Acts 5:24

Walishikwa na butwaa

"walishtushwa" au "walichanganyikiwa"

Kuhusu wao

"kuhusu maneno waliyokuwa wamesikia" (taarifa kwamba mitume hawakuwa katika gereza)

litakuwaje jambo hili

Nini kimefanyika hata watu hawa kutoka nje alihali milango imefungwa na walinzi wakiwepo.

wamesimama hekaluni

Mitume hawakuwa ndani ya hekalu wanamoruhusiwa kiungia makuhani tu, bali walikuwa wamesimama kwenye ukumbi wa nje wa hekalu.

Acts 5:26

Sentensi unganishi

Mlinzi na maafisa waliwaleta mitume mbele ya baraza la viongozi wa dini.

waliwaogopa watu

Mitume walipelekwa bila vurugu mbele ya baraza, viongozi walikuwa wamewahofia watu juu ya kitendo chochote wangekifanya kwa mitume.

Katika jina hili

Neno "Jina" linamaanisha Yesu Kristo. Mitume walizuiliwa wasinene neno lolote kupitia Jina la Yesu.

mmeijaza Yerusalemu kwa fundisho lenu

Inamaanisha wamewafundisha watu wote wa Yerusalemu habari za Yesu.

na kutamani kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.

Neno "Damu" linamaanisa kifo cha Yesu na damu yake. Kwamba Viongozi hao walipaswa kuwajibika kwa kuhusika kwao kumwua Yesu Kristo.

Acts 5:29

Petro na mitume wakajibu

Petro alizungumza kwa niaba ya mitume wote kwa maneno yafuatayo.

kwa kumtundika juu ya mti

Petro anatumia neno "mti" kuonyesha kuwa msalaba ulitengenezwa kutokana na mti. "Kwa kumtundika juu ya msalaba"

kutoa toba kwa Israeli, na msamaha wa dhambi

Neno "toba" na "msamaha" yanamaanisha kuleta msamaha kwa watu wa Israeli kwa njia ya toba na kisha Mungu kuwasamehe dhambi zao.

Israeli

Linamaanisha Wayahudi wote.

kwa wale wanaomtii

"Wote wanaojikabidhi chini ya mamlaka ya Mungu"

Acts 5:33

Sentensi unganishi

Gamalieli anatoa maelezo mbele ya wajumbe wa baraza

Gamalieli, mwalimu wa sheria, aliyeheshimiwa na watu wote

Luka anamwelezea Gamarieli juu ya historia yake.

aliyeheshimiwa na watu wote

Alikuwa anaheshimiwa na watu wote

alisimama na kuwaamuru mitume wachukuliwe nje

Gamalieli aliwaagiza walinzi wawatoe nje mitume kwa muda.

Acts 5:35

Wanaume wa Israeli, iweni makini sana na kile mnachopendekeza kuwafanyia watu hawa

Gamarieli anawaeleza majumbe wa baraza wasifanye jambo lolote juu ya hao mitume litakalowaletea majuto baadaye

Theuda aliinuka na kujidai kuwa mtu mkuu

Theuda alikuwa ameasi na kujitwalia idadi kubwa ya wafuasi

Aliuawa, na wote waliokuwa wanamtii walitawanyika

Watu walimwua na jamii ikatawanyika.

Baada ya mtu huyu, Yuda mgalilaya, aliinuka siku zile za kuandikwa sensa, akavuta watu wengi nyuma yake.

Yuda Mgalilaya naye vilevile alitokea wakati wa sensa ya Kaisari, aliwavuta wengi kuasi dhidi ya utawala wa dola ya Kirumi kisha naye kapotea.

Acts 5:38

Sentensi unganishi:

Gamarieli anamaliza kuwaeleza wajumbe wa baraza. Pamoja na kuwapiga wale mitume na kuwaamuru wasizidi kunena habari za Yesu na kuwaachia huru, lakini wanafunzi walizidi kufundisha na kuhubiri habari za Yesu.

jiepusheni na watu hawa na muwaache wenyewe,

Gamalieli anawaambia Wayahudi viongozi wasiwaadhibu hao mitume na wasiwatie tena gerezani.

kama mpango huu au kazi hii ni ya watu itatupwa

Kama jambo hili wanalolitenda chimbuko lake ni mwanadamu litakoma tu.

Lakini kama ni ya Mungu, hamtaweza kuwazuia

Kama kazi hii wanayoifanya chimbuko lake ni Mungu, kazi hii itaendelea.

Hivyo, walishawishika na maneno yake.

Gamalieli alifanikiwa kuwashawishi Viongozi Wayahudi na kukubaliana na ushawishi wake.

Acts 5:40

Kisha, waliwaita mitume ndani na kuwachapa

Wajumbe wa baraza waliwaamru walinzi wa hekalu kuwachapa viboko mitume.

kuwaamuru wasinene kwa jina la Yesu

Wasinene tena juu ya jina la Yesu lenye mamlaka.

wamehesabiwa kuwa wamestahili kuteseka na kutoheshimiwa kwa ajili ya Jina hilo

Ilikuwa ni faida kuteswa na kudharauliwa kwa ajili ya Yesu.

Baada ya hapo kila siku

"Baada ya siku hiyo, kila siku." Kifungu hiki kinaonyesha kile walichokifanya mitume kila siku kwa siku zilizofuata. Walitiwa moyo kufanya hili kwasababu ya kile kilichotokea katika tukio hilo la kuadhibiwa kwao.

Waliendelea kufundisha

"Hawakuacha kufundisha" Hekaluni na katika nyumba za waumini.

Acts 6

Matendo 06 Maelezo kwa jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mgao kwa wajane

Waumini wa Yerusalemu waliwapa wajane chakula kila siku. Wote walikuzwa kama Wayahudi ingawa wengine wao walikua wameishi Yudea na walizungumza Kihebrania, na wengine walikuwa wameishi kwa Mataifa na walizungumza Kigiriki. Waliogawa chakula walikigawa kwa wajane waliozungumza Kihebrania na kuwaacha wale ambao hawakukizungumza. Kumfurahisha Mungu, viongozi wa kanisa waliwateua wanaume waliokifahamu Kigiriki kwa kugawa sehemu ya chakula kwa wajane waliokifahamu Kigiriki Mmoja wa" hao wanaume alikuwa Stefano.

Utata mwingine katika tafsiri ya sura hii

"Uso wake ulikuwa kama wa malaika"

Hakuna ajuaye vile uso wa Stefano ulivyokuwa kama uso wa malaika kwa maana Luka hatuambii hilo. Ni vema tafsiri hii kusema tu kuhusu kinachosema ULB kuhusu haya.

<< | >>

Acts 6:1

Maelezo ya jumla:

Huu ni mwanzo wa sehemu mpya ya habari. Luka anatoa habari muhimu ya kuweza kujifunza.

Sasa katika siku hizi

Hii inaonyesha mwanzo wa sehemu mpya ya habari. Zingatia namna ambavyo sehemu mpya ya habari zinavyotambulishwa katika lugha yako.

Kuongezeka

"Kuongezeka kukubwa"

Wayahudi wa Kiyunani

Hawa walikuwa ni wayahudi ambao walikuwa wakiishi maisha yao zaidi sehemu fulani katika utawala wa kirumi nje ya Israel, na walikuwa wakiongea Kigiriki. Lugha na utamaduni wao vilikuwa kidogo tofauti na wale waliokulia Israeli.

Wahebrania

Hawa walikuwa ni wayahudi waliokuwa wamekulia Israel wakiongea Kiaramaiki. Kanisa liliwaangalia tu wayahudi na wafuasi wa kiyahudi mpaka hapo.

Wajane

Mjane wa kweli alikuwa ni mwanamke ambaye mme wake alikuwa amekufa, na hakuna jamaa wowote wa kumtunza.

wajane wao walikuwa wanasahaulika

"kupuuzwa" au "kusahaulika." Kulikuwa na wengi sana waliohitaji msaada kiasi kwamba baadhi walikoswa hasa Wayahudi wa Kiyunani.

Mgawanyo wa kila siku wa chakula

Pesa ambayo ilitolewa kwa mitume ilitumika kwa sehemu kununua chakula kwa ajili ya wajane wa kanisa la kwanza.

Acts 6:2

Mitume kumi na wawili

Hapa wanazungumziwa mitume kumi na moja pamoja na Mathias aliyekuwa amechaguliwa.

kusanyiko lote la wanafunzi

"Wanafunzi wote" au "Waumini wote"

Siyo sahihi kwetu kuliacha neno la Mungu

Ni neno lenye msisitizo wa muhimu wa kutokuacha huduma ya kufundisha neno la Mungu

Kuhudumia meza

Hili ni neno kwa ajili ya kuhudumia chakula kwa watu.

Wanaume wema, waliojawa na Roho na hekima

Uwezekano wa maana waweza kuwa 1) Wanaume wana sifa tatu- wema, kujazwa na Roho, na kujazwa na hekima au 2) wanaume wana tabia njema kwa sifa mbili- kujazwa na Roho, na kujawa na hekima.

kuwakabidhi huduma hii.

Kuwa na wajibu kwa huduma hiyo muhimu.

huduma ya neno

Ni huduma ya kufundisha na kuhubiri habari njema.

Acts 6:5

Hotuba yao ikaupendeza mkutano wote

Hotuba yao ilikubaliwa, pendekezo lilikubaliwa na jamii yote ya waumini.

Stefano...na Nikolao

Haya ni majina ya kigiriki, na mapendekezo yalikuwa kwamba wanaume walioteuliwa walikuwa zaidi au wote kutoka kundi la waumini wa wayahudi wa kigiriki.

Mwongofu

"Mtu wa mataifa aliyeamini dini ya kiyahudi"

Waliweka mikono yao juu yao

Kuwapa baraka na kuwakabidhi wajibu na mamlaka kwa kazi ya watu saba

Acts 6:7

Maelezo ya jumla:

Msitari huu ni neno linalotoa taarifa mpya juu ya ukuaji wa kanisa.

Neno la Mungu liliongezeka

Idadi ya watu walioliamini neno la Mungu iliendelea kuongezeka. hivyo kwa lugha nyingine neo la Mungu liliongezeka.

Wakawa watii kwa imani

"Walikubali kuifuata njia mpya ya imani"

Imani

Hii inaweza kuwa; 1) Ujumbe wa Injili wa matumaini katika Yesu; au 2) Mafundisho ya kanisa; au 3) Mafundisho ya kikristo.

Acts 6:8

Sentensi unganishi

Huu ni mwanzo wa sehemu mpya ya hadithi.

Maelezo ya jumla

Mistari hii inatupa maelezo ambayo Stefano na watu wengine hali ilivyoendelea kuwa.

Na Stefano

Luka anamwelezea Stefano kama kinara wa sehemu ya simulizi hii.

Stefano, aliyejaa neema na nguvu, alikuwa akifanya

Neno "Neema" na "Nguvu" yanaelezea nguvu kutoka kwa Mungu. Yaani Mungu alikuwa akimpa nguvu Stefano za kutenda.

Sinagogi la Mahuru

"Mahuru" walikuwa yumkini watumwa huru kutoka sehemu hizi tofautitofauti. Haijulikani kama watu wengine walioorodheshwa walikuwa sehemu ya Sinagogi au walishiriki tu katika mdahalo na Stefano.

Kufanya mdahalo na Stefano

"kubishana na Stefano" au "kujadiliana na Stefano"

Acts 6:10

Sentensi unganishi:

Taarifa za nyuma zilizoanza zinaendelea katika mstari wa 10.

Hawakuweza kushindana

"Wasingeweza kuthibitisha uongo kwa kile Stefano alichosema"

Waliwashawishi kwa siri

Kwa kuwa jambo lilifanywa kwa siri, inathibitisha kwamba ushuhuda wao ulikuwa wa uongo.

Maneno ya kukufuru

"maneno kinyume na sheria ya Mungu na Musa"

Acts 6:12

Kuwashurutisha watu

"kuwahamasisha watu kwa kiwango cha kuwa na hasira"

na kumwendea Stefano

Kisha wote wakamwendea kwa nguvu

Kumkamata

"kumshika kwa nguvu"

mtu huyu haachi kunena

anaendelea kunena mara zote.

Kila mmoja aliyekuwa katika baraza, akaelekeza macho yake kumwangalia Stefano

"kuangalia kwa shauku kwake." Hii ni msemo ukimaanisha kuelekeza macho kwake."

Alikuwa kama uso wa malaika

Hii ni tabasamu kama kulinganisha na kiwango cha mfanano unaofanana na kuwa "mng'ao" ambao haujasemwa. "alikuwa anang'aa kama uso wa malaika"

Acts 7

Matendo 07 Maelezo kwa Jumla

Muundo na Mpangilio

Tafsiri zingine zimeweka kila mstari wa ushairi mbele ya kulia kuliko maandishi mengine ili kurahisisha kusoma. ULB hufanya hivi na ushairi ambao umenukuliwa kutoka Agano la Kale 7:42-43 na 49-50.

Inaonekana kwamba 8:1 ni sehemu ya utungo wa sura hii.

Dhana maalum katika sura hii

"Stefano alisema"

Stefano alihadithia historia ya Israeli kwa ufupi. Alisisitiza ule muda Wana wa Israeli walikuwa wamewakataa watu Mungu alikuwa amechagua kuwaongoza. Mwisho wa habari, alisema viongozi wa Wayahudi aliokuwa akiwazungumzia walikuwa wamemkataa Yesu jinsi Waisraeli watenda dhambi walikuwa wakiwakataa viongozi walioteuliwa na Mungu.

"Jazwa na Roho Mtakatifu"

Roho Mtakatifu alimwongoza Stefano kana kwamba alisema tu kile Mungu alitaka aseme.

Kuashiria yajayo

Mwandishi anapolizungumzia jambo ambalo si muhimu kwa wakati huo lakini litakuja kuwa muhimu baadaye katoka hadithi hiyo, hii huitwa kuashiria yajayo. Luka anamtaja Saulo, aliyejulikana kama Paulo kwa hii hadithi ingawa si mhusika wa maana kwenye habari hii. Hii ni kwa maana Paulo ni mtu muhimu katika sehemu zilizobaki kwenye hiki kitabu cha Matendo ya Mitume.

Mifano muhimu za usemi katika Sura hii

Mawasiliano yaliyolengwa

Stefano alikuwa akizungumza na Wayahudi walizifahamu vyema sheria za Musa na kwa hivyo hakufafanua vitu ambavyo wasikilizaji wake walikuwa wanajua mbele. Lakini utahitajika kueleza baadhi ya vitu hivi ili wasomi wako waweze kuelewa alichokuwa anasema Stefano. Kwa mfano labda utaeleza vizuri kwamba wakati ndugu zake Yusufu "walimuuza Misri" (Matendo 7:9), Yosufu alikuwa anaenda kuwa mtumwa Misri, (tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metonymy)

Metonymy

Stefano alizungumzia Yusufu kuongoza "Juu ya Misri" na juu ya nyumba ya Farao. Hapa alimaanisha ya kwamba Yusufu aliongoza watu wa Misri na watu na mali yote iliyokuwa ndani ya nyumba ya Farao (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metonymy).

Matatizo mengine ya tafsiri katika sura hii

Maelezo ya awali

Viongozi wa Wayahudi ambao Stefano aliwazungumzuia walikuwa wanafahamu mbele matukio aliyokuwa akiwazungumzuia. Walifahamu kwamba Musa aliandika Kitabu cha Mwanzo. Kama kitabu cha mwanzo hakikutafsiriwa katika lugha yako, itakuwa vigumu kwa wasomaji wako kuelewa alichosema Stefano.

<< | >>

Acts 7:1

Sentensi unganishi

Sehemu ya habari kuhusu Stefano iliyoanzia sura 6:8 inaendelea. Stefano anaanza kumjibu Kuhani Mkuu na baraza kwa kuanza kuzungumzia mambo yaliyotukia katika historia ya Israeli. Maelezo mengi ya Stefano yanatoka kwenye vitabu vya sheria vya Musa.

Maelezo ya ujumla

Kwenye mstari wa 2,Stefano anaanza hotuba yake kumjibu kuhani mkuu na baraza.Anaanza hotuba yake kwa kuongelea mambo yaliyotokea katika historia ya Israeli.

Ndugu na baba zangu,nisikilizeni mimi.

Stefano alikuwa akiheshimika sana kwenye baraza kwa salamu yake ya kifamilia.

Acts 7:4

Hakumpa chochote kama urithi wake

Hakuweza kutoa chochote katika hiyo.

hapakuwa na sehemu hata ya kuweka mguu

Inaweza kuwa na maana ya; 1) Eneo pana la kuweza kusimama; au 2) Aridhi ya kutosha kuweza kutembea kwa hatua kadhaa.

kama miliki yake na uzao wake

Kwamba nchi itakuwa mali yake milele yeye na uzao wake.

Acts 7:6

Mungu alinena naye hivi

Badaaye Mungu alimwambia Ibrahimu.

miaka mia nne.

Miaka mia nne (400).

nitalihukumu taifa

Neno "taifa" linamaanisha watu walio ndani yake. Mungu atawahukumu watu wa taifa.

ambalo litawafanya mateka

Nchi ambayo uzao wako watakuwa mateka.

akampa Abrahamu agano la tohara

Mungu alifanya Agano na Abrahamu la tohara kwa watoto wake wote wa kiume.

Abrahamu akawa baba wa Isaka

Ni habari inayoelezea Uzao wa Abrahamu.

na Yakobo akawa baba

Na Yakobo akawa baba, Stefana anaelezea kwa ufupi.

Acts 7:9

Mababu

Wana wakubwa wa Yakobo " "au" ndugu wakubwa wa Yusufu"

wakamwonea wivu Yusufu

Ndugu zake wakubwa na Yusufu walijawa na wivu dhidi yake.

wakamuuza katika nchi ya Misri

Wayahudi walijua kuwa mababu zao walimwuza Yusufu na kuwa mtumwa katika nchi ya Misri.

Na Mungu

Inafaa kutumika kiuhalisia kuwa; "lakini Mungu" alikuwa pamoja naye huko.

Juu ya Misri

Yusufu akawatawala watu wote wa Misri

na juu ya nyumba yake yote

linaelezea; na kila kitu Farao alichokuwa anakimiliki nyumbani kwake.

Acts 7:11

Kukawa na njaa

"Kukawa na njaa."ardhi ikaacha kutoa chakula

Mababa zetu

"Ndugu zake wakubwa Yusufu"

Nafaka

"Chakula"

aliwatuma baba zetu...Kaka zake

Yakobo aliwatuma baba zetu, ndugu zake na Yusufu.

Katika safari ya pili

Katika safari yao ya pili ya kufuata chakula huko Misri.

Akajionyesha

Yusufu akajifunua kwa ndugu zake na kujitambulisha kama ndugu yao.

familia ya Yusufu ikajulikana kwa Farao.

Kwa maana nyingine; Farao akafahamu kuwa hao walikuwa ndugu zake na Yusufu.

Acts 7:14

Yusufu akawatuma ndugu zake kwenda

liwatuma ndugu zake kwenda Kanaani, nyumbani kwa kaka zake.

Yakobo akafa yeye na baba zetu,

"Yakobo na ndugu zake, baba zetu" wote walikufa.

Wakachukuliwa hata Shekemu wakazikwa

"Uzao wa Yakobo walimchukua na kwenda kumzika katika makaburi walikozikwa ndugu zake.

kwa vipande vya fedha

"kwa fedha"

Acts 7:17

Wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimwahidi Abrahamu ulipokaribia, watu wakiwa wameongezeka huko Misri,

Katika baadhi ya lugha zingine inaweza kuwa msaada ikisomeka; Idadi kubwa ya watu ilipoongezeka, badala ya kusema; muda wa ahadi ulipowadia.

Muda wa ahadi ulipokaribia

Ulikuwa umekaribia muda ambao Mungu angetimiza ahadi yake kwa Ibrahimu.

aliinuka mfalme mwingine

falme mwingine alianza kutawala

Juu ya Misri

"Misri" inasimama badala ya watu wa Misri. "Watu wa Misri"

Nani asiyejua kuhusu Yusufu

"Yusufu"inarejea sifa njema ya Yusufu. "Nani hakujua kuhusu mamlaka ya Yusufu huko Msri."

Waliwatenda mabaya baba zetu.

"Waliwatenda mababu zetu kimaskini"au" "walichukua faida kwa mababu zetu"

Waliwatupa watoto wao wachanga

kuwatupa watoto wao wachanga ili wasiishi

Acts 7:20

Katika kipindi kile Musa alikuwa amezaliwa

Haya ni maelezo ya kumtambulisha mtu mpya, Musa.

Alikuwa mzuri mbele za Mungu

Musa alikuwa kijana mzuri

Akalelewa miezi mitatu

Wazazi wake walimlea Musa miezi mitatu.

Wakati alipotupwa nje

Musa "alitupwa" kwa sababu Farao alikuwa ameamuru kila mtoto wa kiume azaliwapo lazima atupwe. Wazazi wake walilazimika kumweka nje ya nyumba yao.

Binti Farao alimchukua na kumfanya kama mwana wake

kama vile alikuwa mwanaye wa kiume wa kuzaa

Acts 7:22

Musa alifundishwa

"Wamisri walimfundisha Musa"

Mafundisho yote ya kimisri

hii inaongezea ,"vitu vyote walivyovijua Wamisri."

alikuwa na nguvu katika maneno na matendo

"alikuwa na uwezo katika maneno na matendo yake"

ikamjia katika moyo wake

Musa alitafakari na kisha akaamua

kutembelea ndugu zake, Wana wa Israeli

Kuona jinsi gani ndugu zake, wana wa Israeli wanaendeleaje.

Alipomwona Mwisraeli akitendewa mabaya

Alipomwona Mmisri anamtesa mwisraeli, Musa alimtetea na akalipiza kisasi kwa kumpiga hadi kufa yule Mmisri.

Musa alifikiri

" Musa alidhani kuwa, alichokifanya ndugu zake watajua kuwa ni Mungu anawapigania"

kwa mkono wake

kupitia yeye Mungu alikuwa akiwaokoa ndugu zake.

Acts 7:26

baadhi ya Waisraeli

Waisraeli wawili aliwaona wanaogombana wao kwa wao.

akajaribu kuwapatanisha

Alijaribu kuwazuia wasipate kuendelea na ugomvi.

Mabwana, Ninyi ni ndugu;

Musa alikuwa akizungumza na hao waisraeli waliokuwa wakigombana

mbona mnakoseana ninyi kwa ninyi,?

Musa aliuliza swali kuwatia moyo waache kugombana. Msizidi kugombana tena

Nani kakufanya mtawala na mwamuzi wetu?

Hili swali lilitumika kumkemea Musa."Huna mamlaka juu yetu"!

Wewe unataka kuniua , kama ulivyomuua Mmisri jana?"

Mtu yule alitumia swali hilo kumwonya Musa aanze kuzani yawezekana wengi wao walimwona akimwua yule Mmisri.

Acts 7:29

Maelezo ya jumla

Jamii iliyokuwa inamsikiliza Stefani ilikuwa inajua kuwa Musa alikuwa amemwoa mwanamke wa kimidiani alipokimbia kutoka Misri.

Baada ya kusikia haya

Musa alipotambua kuwa Waisraeli wanajua kuwa alikuwa amemwua Mmisri siku moja kabla.

Baada ya miaka arobaini kupita

Wakati miaka arobaini imepita baada ya Musa kutoka Misri.

malaika akamtokea

Stefano alikuwa akiongea na kungi ambalo lilijua pia kuwa Mungu aliongea na Musa kwa njia ya Malaika.

Acts 7:31

alishangaa na kustaajabia kile alichokiona

Musa alishangaa kwamba kichaka hakiungui moto. Hii ilijulikana na watazamaji wa Stefano.

Aliposogelea kwenda kutazama ....Musa alitetemeka na hakuthubutu kuangalia

Hii inamaanisha Musa alikisogelea kichaka kwa karibu ili kuchunguza kilichokuwa kinatokea, lakini ghafla akarudi nyuma kwa hofu aliposikia sauti ikitoka ndani ya kichaka.

Mimi ni Mungu wa baba zako

"Mimi ni Mungu ambaye baba zako waliniabudu"

Musa alitetemeka

Musa alitetemeka kwa hofu.

Acts 7:33

Vua viatu vyako

Mungu alimwambia Musa hivyo ili kumweshimu Mungu.

Sehemu unayosimama ni mahali patakatifu

Musa, eneo unalosimama sasa ni Mungu amelifanya kuwa takatifu, Uwepo wa Mungu ukpo katika eneo hili.

Nimeona

Nimeona kwa hakika pasipo shaka.

Watu wangu

Watu wa Mungu "Uzao wa Abraham,Isaka na Yakobo"

Nimeshuka ili niwaokoe

"nami nimeshuka ili kuwaondolea vifungo"

sasa njoo

"Jiandae" au "KUwa tayari" kwenda. Mungu anatumia amri, anamwamrisha.

Acts 7:35

Maelezo ya jumla

Baada ya Waisraeli kutoka Misri, walikaa miaka 40 wakizunguka zunguka jangwani kabla Mungu hajawaongoza kuingia katika nchi aliyokuwa amewaahidi kuwapa.

Huyu ni Musa ambaye walimkataa

Hii inarejesha nyuma matukio yaliyotunzwa

Nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi ?

Hili swali lilitumika kumkemea Musa."Huna mamlaka juu yetu"!

Mtawala na mkombozi

"Kutawala juu yao na kuwaweka huru kutoka kuwa watumwa"

Kwa mkono wa malaika

"Kwa nguvu ya malaika"

Kipindi cha miaka arobaini

"kipindi cha miaka arobaini ambacho watu wa Israeli waliishi jangwani"

Kutoka miongoni mwa ndugu zenu

"kutoka miongoni mwa watu wenu kuwa Nabii"

Acts 7:38

Maelezo ya jumla

Mstari wa 40 ni nukuu kutoka katika vitabu vya sheria vya Musa.

Huyu ni miongoni mwa mtu ambaye alikuwa katika mkutano

"Huyu ni Musa mtu ambaye ni miongoni mwa Waisraeli.

Huyu ni mtu ambaye Mungu aliongea naye maneno yaliyo hai na kutupa sisi

"Huyu ni mtu ambaye Mungu aliongea naye neno lililo hai kutupa sisi"

Neno lililo hai

Maana sahihi ni 1) "ujumbe ambao uliopo" au 2) "maneno yaletayo uzima."

Walimsukuma mbali nao

Mfano huu unaonyesha kukataliwa kwa Musa, "walimkataa yeye kama kiongozi wao"

katika mioyo yao waligeukia Misri

"WAlikusudia kurejea tena Misri"

Wakati huo

"Walipoamua kurudi Misri"

Acts 7:41

Maelezo ya Jumla

Hapa nukuu ya Stefano inatoka kwa Nabii Amosi

Walitengeneza ndama

walitengeneza sanamu mfano wa ndama ili waiabudu.

ndama... hiyo sanamu kazi ya mikono yao

Fungu lote hili linafafanua ndama yule aliyetengenezwa.

Mungu aligeuka

Mungu aligeukia mbali kwa kuwa hakupendezwa na watu hao na kutokuwasaidia tena. Mungu aliacha kuwarekebisha.

Akawaacha

"Akajiondoa kwao

waabudu nyota za angani,

Inaweza kuwa; 1) Nyota pekee au 2) Jua, Mwezi na Nyota.

kwenye kitabu cha manabii

Ni muunganiko wa maandiko kutoka Manabii wa Agano la Kale.

Je mnanitolea mimi sadaka za wanyama mliowachinja .....Israeli

Mungu aliwauliza Waesraeli swali kuonyesha kuwa walikuwa hawamwabudu yeye wala kumtolea dhabihu zao. "Hamkuniheshimu mimi wakati mlipochinja wanyama wasiofaa na kutoa dhabihi .... Israeli".

Nyumba ya Israeli

Hii ni ujumla wa Taifa la Israeli

Acts 7:43

Sentensi unganishi

Stefano anaendeleza majibu yake kwa Kuhani Mkuu na wajumbe wa baraza

Maelezo ya Jumla.

Hii ni nukuu Stefano anaiweka kutoka kwa Nabii Amosi

Mliipokea

Inamaanisha waliitwaa hiyo miungu pamoja nao wakasafiri pamoja nayo huko Jangwani

Hema ya kukutania ya Moleki

Hema ya kukutania au hema ambalo lilijengwa kumwabudu mungu Moleki

Nyota ya mungu Refani

nyota ambayo ilimtambulisha mungu wa uongo Refani

picha ambayo mliitengeneza

Walitengeneza picha ya mungu Moleki na Refani kwa kusudi la kumwabudu.

nitawapeleka mbali zaidi ya Babeli.'

Nitawaondoa kwenye maeneo hata mbali zaidi ya Babeli. Huu ni mwitikio wa hukumu ya Mungu.

Acts 7:44

Hema la kukutania la ushuhuda.

hema ambalo lilijengwa kulifunika sanduku lililokuwa na amri kumi zilizochorwa kwenye mawe na kuwekwa ndani ya sanduku.

Kumiliki Taifa

Hii itajumuisha nchi ,majengo,wanyama na vyote na miliki zote za taifa ambalo Israeli walikuwa wakiwashinda maadui na kuchukua nyara.

Hii Ilikuwa hivi mpaka siku za Daudi

Sanduku la agano lilibaki kwenye hema na ilijumuisha muda wa Daudi, mfalme wa Israeli

Mahali pa makao ya Mungu wa Yakobo

Daudi alitaka sanduku la agano likae Yerusalemu, siyo litangatange kwenye hema kuwazunguka Israeli

Acts 7:47

Maelezo ya jumla

Mistari ya 49-50, Stefano ananukuu maneno kutoka kwa Nabii Isaya. Katika nukuu, Mungu anaongea kuhusu yeye mwenyewe.

zilizojengwa kwa mikono

zilizotengenezwa na watu

Mbinguni ni kiti changu cha enzi ....na duniani ni sehemu ya kuwekea miguu yangu.

Nabii analinganisha ukuu wa Mungu na jinsi isivyowezekana kwa mtu sehemu kwa Bwana kupumzika katika nchi tangu dunia ilipokuwa utupu lakini ni sehemu ya Mungu kuwekea miguu tu.

Ni nyumba ya aina gani mnaweza kunijengea?

Mungu anauliza swali ili kuonesha namna gani mwanadamu ana mapungufu kufikia uumbaji wake. Huwezi kujenga nyumba ambayo itanitosha mimi!

Wapi sehemu yangu ya kupumzikia

Mungu anauliza hili swali kumwonyesha mwanadamu kwamba hawezi kumpatia Mungu mapumziko. "Hakuna sehemu nzuri ya kumtosha Mungu kupumzikia!"

Siyo mikono imefanya haya yote?

Mungu anauliza hili swali kuonyesha kwamba mwanadamu hatengenezi chochote. "Mkono wangu umefanya hivi vitu vyote!

Acts 7:51

Sentensi unganishi

Kwa karipio kali, Stefano anamalizia kumjibu Kuhani Mkuu na baraza kwa staili ile aliyoanza nayo sur 7:1.

Enyi watu wenye shingo ngumu

Shingo ngumu -Stefano alibadilisha kutoka utambulisho wa viongozi wa Kiyahudi na kuwakemea

shingo ngumu

Shingo ngumu -Hii haina maana walikuwa na shingo ngumu, lakini anawaambia kuwa walikuwa wasumbufu.

moyo usiotahiriwa

Moyo usiomtii Mungu. Wayahudi walilitumia neno kwa watu wasio na tohara ni sawa na watu wasiomtii Mungu. Stefano alitumia "moyo' na "masikio" kuwakilisha Wayahudi viongozi waliotenda kwa namna ya watu wa mataifa walivyokuwa wakitenda. Viongozi hawa hawakumtii na wala kumsikiliza Mungu.

Ni manabii wapi baba zenu hawakuwatesa?

Stefano aliuliza swali kuwaonyesha kwamba hakujifunza chochote katika makosa ya baba zao. "Baba zao waliwatesa kila nabii"!

Mmoja mwenye Haki

Anamaanisha juu ya Kristo, Masihi.

mmekuwa wasaliti na wauaji wake pia,

"Mlimsaliti na kumwua"

sheria ile iliyoagizwa na malaika lakini hamkuishika.

"Sheria ambazo Mungu alizituma kwa Malaika kuwaba baba zetu.

Acts 7:54

Sentensi unganishi

Baraza lilimjia juu Stefano kutokana na ujumbe wake.

wajumbe wa baraza waliposikia mambo haya,

Hii ni hatua ya kugeuka; mahubiri yalifikia mwisho na baraza likachukua hatua.

wakachomwa mioyo

Hii ni fumbo kwa, "kujawa na hasira"

wakamsagia meno

Hili ni fumbo linaloelezea hasira nzito au chuki. "walikuwa na hasira ambayo walisaga meno yao kwa pamoja."

Aliangalia mbinguni kwa makini

"Aliangalia juu kwenye mawingu."Inatokea kwamba Stefano peke yake aliona maono siyo mwingine yeyote katika mkutano.

akaon utukufu wa Mungu

Kwa kawaida watu walizoea kuuona utukufu wa Mungu kwa ishara ya nuru." :mwanga mkali kutoka kwa Mungu". Stefano katika maono yake alimwona Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wangu.

Mwana wa Adam

Stefano alimtambulisha Yesu kwa cheo cha "Mwana wa Adam."

Acts 7:57

wakaziba masikio yao

Waliziba masikio yao wasiweze kusikia zaidi alichokuwa akisema Stefano.

Nguo za nje

mavazi ya nje au nguo mojawapo walizokuwa wakivaa juu ya nguo zingine.

Wakamtupa nje ya mji

baraza la wazee wakampiga Stefano wakamkamata kwa nguvu na kumtupa nje ya mji

miguuni mwa

"mbele ya "kwa kusudi la kuzilinda

kijana

Sauli alikuwa na umri wa kati ya miaka 30 wakati ule.

Acts 7:59

Sentensi unganishi

Maelezo ya Stefano yanakomea katika sura hii ya 7.

"Pokea roho yangu"

"Chukua Roho yangu" Hili lilikuwa ni ombi toka kwa Stefano.

Akapiga magoti

Hii ni namna ya kuonyesha unyenyekevu kwa Mungu.

usiwahesabie dhambi hii

Inamaanisha; Uwasamehe dhambi hii.

akakata roho

Ni lugha nyingine kuonyesha umauti wa mtu.

Acts 8

Matendo 08 Maelezo ya jumla

Muundo na Mpangilio

Tafsiri zingine zimeweka kila mstari wa ushairi mbele ya kulia kuliko maandishi mengine ili kurahisisha kusoma. ULB hufanya hivi na ushairi ambao umenukuliwa kutoka Agano la Kale 8:32-33

Sentensi ya Kwanza ya mstari wa 1 inaishia na maelezo ya matukio ya sura ya 7: Luka anaanza sehemu mpya ya historia yake na maneno "Hapo ikaanza".

Dhana maalum katika sura hii.

upokea Roho Mtakatifu

Katika sura hii, Luka anawazungumzia kwa mara ya kwanza juu ya watu wanaopokea Roho Mtakatifu (Matendo 8:15-19).Roho Mtakatifu alikuwa mbele amewawezesha waumini kunena kwa lugha, kuwaponya wagonjwa na kuishi kama jumuia na alikuwa amemjaza Stefano pia. Lakini wakati Wayahudi walipoanza kuwafunga waumini katika gereza waumini walioweza kutoroka Yerusalemu walitoroka na walipokuwa wakiondoka waliwahubiria watu kumhusu Yesu. Wakati watu waliosikia ujumbe kuhusu Yesu walipokea Roho Mtakatifu, viongozi wa kanisa walijua kwamba watu hao walikuwa waumini wa ukweli.

Ilitangazwa

Sura hii inazungumzia waumini wakitangaza neno, habari njema na kumtangaza Yesu kwamba ndiye Kristu kuliko sura zingine za kitabo cha Matendo. Neno "tangaza" ni tafsiri ya neno la Kigiriki linalomaanisha kusema habari njema kuhusu jambo ama kitu.

<< | >>

Acts 8:1

Sentensi unganishi

Simlizi inamalizika kumhusu Stefano, kuanzia sura hii ya 8 simlizi inaanza kumtaja Sauli.

siku hiyo ndipo alipoanza... isipokuwa mitume.

Sehemu ya mstari huu wa 1 ni habari inayoeleza kuanza kwa mateso kwa watu wa njia ile baada ya kifo cha Stefano. Unaelezea sababu za Paulo kuanzisha mateso hayo kwa waumini.

Siku hizo

Hii inahusu siku ambayo Stefano aliuawa,

Waaminio wote walitawanyika

Hii ni inavumisha wengi au zaidi ya waamini wa Yerusalem waliyakimbia mateso.

Isipokuwa mitume

Inadhihirisha kwamba mitume walibaki Yerusalem ingawa hawakuyazoea hayo mateso makubwa

Watu wacha Mungu

"Watu wenye hofu ya Mungu" au "Watu waliomuogopa Mungu

Wakafanya maombolezo makubwa

"Wakalia sana ...juu yake"

Aliwaburuza wanaume na wanawake

Sauli aliwachukua kwa nguvu Wayahudi waamini na kuwatoa nje ya nyumba zao na kuwatupa gerezani.

Wanaume na wanawake

inaelezea juu wanaume na wanawake ambao waliokuwa wamemwamini Yesu.

Acts 8:4

Sentensi unganishi

Hapa panaanzia simlizi inayomhusu Filipi, ambaye watu walikuwa wamemchagua kuwa shemasi,

Ambao walikuwa wametawanyika

" waumini ambao walikuwa wametanyika kwa mateso makubwa".

Alienda mpaka Mji wa Samaria

"Kwenda chini" Neno limetumika hapa kwasababu Samaria iko kwenye ukanda wa chini zaidi ya Yerusalemu.

Mji wa Samaria

Haiko wazi kama ni mji wa Samaria katika mji wa Samaria.

akamtangaza Kristo huko

Cheyo "Kristo" kinamwelezea Yesu, Masihi.

Acts 8:6

Wakati makutano ya watu

"Wakati makutano ya watu kutoka mji wa Samaria." Lilikuwa eneo lililobainishwa huko nyuma

Wakaweka umakini

Sababu ya watu kuweka umakini ilikuwa ni uponyaji wote alioufanya Filipo.

Kutoka hapo watu wengi waliosikia, pepo wachafu waliwatoka watu huku wakilia kwa sauti kubwa

"roho wachafu walikuwa wakipaza sauti na kutoka kwa watu waliokuwa nayo.

Na kulikuwa na furaha kubwa katika mji.

Watu wa mji walikuwa na furaha kubwa

Acts 8:9

Maelezo ya jumla

Simoni ametajwa kwenye simlizi hii ya Filipo. Mistari ya 9-11ni maelezo yanayomhusu Simoni ya kuwa alikuwa nani miongoni mwa wasamaria.

Lakini palikuwana mtu mmoja ...jina lake Simoni

Hii ni njia ya kumtambulisha mtu mgeni katika simulizi. Lugha yako pengine inaweza kutumia maneno tofauti kumtambulisha mtu mgeni katika simulizi.

Mji

"Mji wa Samaria"

Wasamaria wote tangu mdogo hata mkubwa

Hii inaongeza chumvi. "Wasamaria wengi katika mji wa Samaria.:

Huyu mtu ni ile nguvu ya Mungu ambayo ni Kuu.

Watu walikuwa wanasema kwamba Simoni ni nguvu ya Mungu inayojulikana Nguvu Kuu.

Acts 8:12

Sentensi unganishi

Mistari hii anatoa maelezo zaidi kuhusu Simoni na baadhi ya Wasamaria waliokuwa wakimwamini Yesu.

Wakabatizwa.

Filipo aliwabatiza waamini wapya

Na Simoni mwenyewe aliamini

Neno "mwenyewe" linatumika kumwelezea Simoni naye aliamini.

Naye alibatizwa

Filipo alimbatiza Simoni pia.

Wakati alipoona ishara na miujiza iliyokuwa ikitendeka, alishangaa

Simoni alishangaa pale alipoona Filipo anafanya ishara na miujiza mikubwa

Acts 8:14

Sentensi unganishi

Luka anaendeleza habari ya kile kilichokuwa kinatokea huko Samaria.

Wakati mitume wa Yerusalemu waliposikia

Alama hii ni ya mwanzo wa sehemu mpya ya simlizi ya waumini walivyokuwa wakiendelea huko Samaria.

Samaria

"Samaria" Neno linaloelezea juu ya watu wengi waliokuwa waumini katika wilaya yote ya Samaria.

Pale waliposhuka chini

"Pale Petro na Yohana waliposhuka chini" kwenda Samaria.

Waliomba kwa ajili yao

"Petro na Yohana waliwaombea waamini wa Samaria"

Kwamba wangepokea Roho Mtakatifu.

"Kwamba Wasamaria wanaoamini wangeweza kupokea Roho Mtakatifu"

Walikuwa tu wamebatizwa

"Filipo alikuwa tu amewabatiza katika Jina la Bwana Yesu Wasamria walioamini"

Ndipo Petro na Yohana wakaweka mikono yao kwao

"Kwao" linahusu watu wa Wasamaria ambao waliamini ujumbe wa injili kutoka kwa Filipo".

Acts 8:18

Roho Mtakatifu ametolewa kupitia kuwekewa mikono ya mitume.

"Mitume waliwapa Roho Mtakatifu kwa kuweka mikono yao juu ya watu"

Kila nitakae mwekea mikono apokee Roho Mtakatifu.

"Kwamba wakati ninaweka mikono yangu juu ya watu, wapokee Roho Mtakatifu"

Acts 8:20

Maelezo ya jumla

Viwalilishi vya majina katika habari hii vinamwakilisha Simoni

pesa yako pamoja na wewe ipotelee mbali

Wewe na pesa yako muangamizwe

Karama ya Mungu

"Karama" ni neno linaelezea uwezo wa kutoa Roho Mtakatifu kwa njia ya kuweka mikono juu ya mtu mwingine.

Hauna sehemu katika jambo hili

Neno "huna sehemu" linaonyesha kuwa Simoni huna sehemu ya kushiriki katika kazi hii.

Moyo wako si mnyoofu

"Kufikiri kwako si sahihi"

Kwa namna ulivyotamani

"Kutaka kununua uwezo wa kutoa nguvu ya roho kwa wengine"

Uovu huu

"Mawazo haya maovu"

labda utasamehewe

"Anaweza kuwa tayari kukusamehe"

Sumu ya uchungu

Haya ni maelezo ya fumbo yanayomaanisha wivu uliokidhiri.

Vifungo vya dhambi

"mtumwa wa dhambi" au "atafanya dhambi tu"

Acts 8:24

Mambo yote mliozungumza yaweza kunitokea

Ujumbe unaweza kuzungumzwa kwa namna nyingine; "Mambo mliyoyazungumza yasiweze kutokea kwangu"

Mambo yote mliozungumza yaweza kunitokea

Ni kemeo la Petro juu ya Simeoni kuadhibiwa kwake na pesa yake pia.

Acts 8:25

Sentensi unganishi

Hapa ni hitimisho la simulizi kuhusu Simoni na wasamaria.

Ushuhuda wa kuzaliwa

Petro na Yohana waliwaeleza wasamaria juu ya wao walivyomfahamu Yesu.

Kunena maneno ya Bwana

Petro na Yohana walielezea juu ya maandiko ambayo Yesu alizungumza kwa wasamaria.

Katika vijiji vingi vya wasamaria

Kwa watu wengi katika vijiji vya Samaria.

Acts 8:26

Sentensi unganishi

Huu ni mwanzo wa simulizi kuhusu Filipo na mwanaume kutoka Ethiopia.

Maelezo ya jumla

Mstari wa 27 unaonyesha taarifa za mwanaume kutoka Ethiopia.

njia iendayo chini ya Yerusalemu kuelekea Gaza

"Iendayo chini" hapa linatumika kwasababu Yerusalemu iko juu zaidi ya Gaza

Sasa

Neno "sasa" ni neno la kiunganishi cha simulizi.

Njia hii iko katika jangwa

Wasomi wengi wanaamini Luka aliongeza mkazo wa kuelezea eneo ambalo Filipo angeweza kupitia.

Tazama

Neno "tazama" linatutahadharisha kwa mtu mpya katika simulizi. Lugha yako inaweza ikawa njia ya kufanya hivi. Kingereza linatumia "Palikuwa na mtu ambaye alikuwa."

Towashi

Mkazo"towashi" hii ni kwamba, Mwethiopia aliyekuwa katika ofisi za serikali kuu.

Kandake

Hiki ni cheo kwa malkia wa Ethiopia . Ni sawa na jinsi "farao" alitumika kuwa mfalme wa Misri.

Kumsoma nabii Isaya

Hili ni agano la kale la Isaya.

Acts 8:29

Sogea karibu na gari hili

Filipo alifahamu kuwa ni muhimu kuwa karibu na mtu yule aliyepanda kwenye mkokoteni.

akamsikia akisoma katika chuo cha nabii Isaya

Hiki ni kitabu cha Agano la Kale cha Nabii Isaya.

Je unafahamu unachosoma?"

Mwethiopia alikuwa mtu mwenye akili na aliweza kusoma, lakini alikuwa na upungufu wa ufahamu wa kiroho. Filipo alimwulija, "Je! Unafahamu maana ya habari unayoisoma?

Nitawezaje, isipokuwa mtu aniongoze kuielewa?"

Swali hili liliulizwa kusisitiza kuwa hakuweza kuelewa bila msaada. ''siwezi mpaka mtu aniongoze"

Alimuomba filipo akae nae

Filipo alikubali kutembea naye akiwa chini ya barabara pamoja naye akiyafafanua maandiko.

Acts 8:32

Maelezo ya jumla

Hiki ni kifungu kutoka katika kitabu cha Isaya

Kama kondoo mbele ya mchungaji akiwa kimya

Mkata manyoya ni mtu ambaye anakata manyoya ya sufu za kondoo ili zitumike.

Kwa kuhuzunishwa kwake hukumu yake iliondolewa

Alidharauliwa na kuhukumiwa bila haki.

Nani ataeleza kizazi chake?

Swali hili lilitumika kuelezea kuwa hatakuwa na uzao. Kwamba; "Hakuna hata mmoja atakayeweza kuzungumzia habari za uzao wake"

maisha yake yameondolewa katika nchi."

Hii inaelezea kifo chake. "Watu walimwua" au "Watu waliyaondoa maisha yake hapa duniani"

Acts 8:34

Nakuomba

"Tafadhari niambie"

ni kuhusu yeye, au za mtu mwingine"

"Je, Ni nabii anazungumzia habari zake mwenyewe, au anamzungumzia mtu mwingine"

katika Isaya

Inamaanisha maandiko ya Nabii Isaya.

Kumhubiria kuhusu Yesu

"kufundisha habari njema kuhusu Yesu kwa matoashi'

Acts 8:36

Wakati wakiwa njiani

Waliendelea na safari njiani

wakafika penye maji

Haiko wazi kama haya "Maji" yalikuwa ya kijito au bwawa la maji au maji mengi. tunachofahamu yalikuwa na kina cha kutosha kuwaza kwenda chini yake.

"Tazama, pana maji hapa nini kinazuia nisibatizwe?,

Towashi alitumia swali hili kumwomba Filipo amruhusu kubatizwa. "Tafadhali niruhusu nibatizwe"

akaamuru gari lisimame.

Akamwambia dereva wa mkokoteni asimame.

Acts 8:39

Sentensi unganishi

Huu ni mwisho wa simulizi kuhusu Filipo na mtu kutoka Ethiopia.

Toashi hakumwona tena

Filipo alitoweka machoni pa Towashi hivyo hakumwona tena.

Filipo akatokea Azoto.

Kulikuwa hamna dalili za Filipo kusafiri kati ya alipokutana na Ethiopia na Azoto. Ghafla alipotelea katika barabara ya Gaza na kuzuka tena Azoto.

Mpaka alipokuja Kaisaria.

Simulizi ya Filipo inaishia Kaisaria.

Acts 9

Matendo 09 Maelezo kwa jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Njia"

Hakuna anayefahamu aliyeanza kuwaita Waumini wafuasi wa Njia. Labda Waumini walijiita hivyo kwa vile Bibilia kwa mara nyingi humzungumzia mtu anayeishi maishi yake kama mtu atambeaye njiani. Kama huu ni ukweli, Waumini walikuwa "Wakifuata njia ya Bwana" kwa kuishi kwa njia inayompendeza Mungu.

"Barua kwa Masinagogi ya Dameski"

Kuna uwezekano "Barua" alizoomba Paulo zilikuwa nyaraka za Kisheria zilizoruhusu kuwafunga gerezani. Viongozi wa masinagogi wa Dameski waliiheshimu hiyo barua kwa vile iliandikwa na kuhani mkuu.Iwapo Warumi wangekuwa wameiona hiyo barua, wangemruhusu pia Saulo kuwatesa Wakristo kwa vile waliwaruhusu Wayahudi kuwafanyia watakavyo wale walovunja sheria zao za kidini.

Matatizo mengine ya tafsiri katika sura hii

Alichoona Saulo alipokutana na Yesu

Ni wazi kwamba Saulo aliuona mwanga na kwamba hii ni kwa sababu ya huu mwanga "alianguka chini" Watu wengine hufikiri kwamba Saulo alifahamu ni Bwana alikuwa akimzungumzia bila kuona kiwili cha binadamu kwa vile Biblia huzungumzia kila mara Mungu kama mwanga na kwamba huishi ndani ya Mwanga. Watu wengine hufikiri kwamba baadaye katika maisha yake aliweza kusema,"Nimemuona Bwana Yesu" kwa vile ni umbo la binadamu aliona hapo.

<< | >>

Acts 9:1

Sentensi unganishi

Simulizi inarudi nyuma kwa Sauli na wokovu wake.

Maelezo ya jumla

Mistari hii inatupatia picha kwa kutujulisha kuwa Sauli alikuwa akiendelea na kazi zake tangu Stefano alipouawa kwa kupondwa kwa mawe.

kuendelea kuongea maneno ya mauaji dhidi ya wanafunzi

Kiwakilishi cha jina "mauaji" linaweza tafsiriwa kama kitendo: aliendelea kuongelea vitisho, hata kwa kuwaua wanafunzi.

kwa ajili ya masinagogi

Inazungumzia juu ya watu katika Sinagogi. "Kwa watu wa Sinagogi" au "Kwa viongozi wa Sinagogi"

ili kwamba akimpata

Kama akimpate mtu yeyote

aliye katika Njia ile

"anayeyafuata mafundisho ya Yesu"

Anaweza akawapeleka Yerusalemu

Anaweza akawapeleka kama wafungwa.' "ili viongozi wa wayahudi wapate kuwahukumu na kuwasulubisha".

Acts 9:3

Sentensi unganishi

Baada ya Kuhani Mkuu kumpatia Sauli barua, Sauli alisafiri kuelekea Dameski.

Hata alipokuwa akisafiri

Sauli aliondoka Yerusalemu na kuelekea Dameski.

Ilitokea kwamba

Haya ni maelezo yanayobadisha simulizi kuonyesha kwamba jambo la tofauti litatokea.

ikaangaza kotekote nuru kutoka mbinguni

"nuru kutoka mbinguni ikawangaza kotekote"

Kutoka mbinguni

Inaweza kuwa na maana kuwa; 1) Mbinguni, mahali Mungu anaishi au 2) Anga.

Akaanguka chini

Inawezekana kwamba 1)"Sauli alianguka pekee yake chini"au 2)"Mwanga ulisababisha yeye kuanguka chini"au 3)Sauli alianguka chini kama yeyote ambaye huanguka,"Sauli hakuanguka kwa bahati mbaya.

Kwa nini unaniudhi ?

Bwana alimkemea Sauli katika hali ya swali. "Unaniudhi mimi!"

Acts 9:5

Maelezo ya jumla

Kila kuwakilishi cha neno "wewe" linamaanisha umoja.

Wewe u nani, Bwana

Sauli hakupata kumjua Yesu kama Bwana. Hii ilikuwa ni tatizo kwamba alikuwa kwenye nguvu za ajabu

Lakini inuka ,ingia mjini

"inuka na uende katika mji wa Dameski"

utaambiwa yakupasayo

Mtu mmoja atakuambia

wakisikiliza sauti, wasione mtu

Waliisikia sauti, lakini hawakumwona mtu yeyote.

Bila kumuona yeyote

"Lakini hakumwona yeyote" Bali Sauli aliona mwanga tu.

Acts 9:8

alipofungua macho

Hii inamaanisha Sauli aliyafunga macho kwasababu ya mwanga ulikuwa mkali.

Hata asionne chochote

Sauli alikuwa kipofu.

hakuweza kuona kitu

"Alikuwa kipofu" au "hakuweza kuona chochote"

Hakuweza kula wala kunywa

"hakuweza kula wala kunywa hakuwa na njaa"

Acts 9:10

Maelezo ya jumla

Simulizi inabadilika na kuanza kumtaja mtu aliyeitwa Anania ambae anatambulishwa kwenye simulizi. Huyu sio Anania yule aliyetajwa katika matendo ya mitume 5:1, 3.

Basi palikuwa

Hii inatambulisha wahusika wapya, Anania

Naye alisema

Anania alisema

Inuka uenda zako katika mtaa uitwao Nyofu

Nenda kwenye barabara inayoitwa nyoofu.

Katika nyumba ya Yuda

Yuda si yule mwanafunzi aliyemsaliti Yesu. Yuda alikuwa ndio mmiliki wa nyumba uko Dameski ambapo Anania alikuwa akiishi.

Mtu wa Tarso aitwaye Sauli

"Mtu kutoka katika mji wa Tarso"

kumwekea mikono juu yake

Hii ilikuwa alama ya kumpatia Sauli baraka za kiroho.

Kwamba apate kuona

"Aweze kuona kwa mara nyingine tena"

Acts 9:13

Watu wako watakatifu

Neno "Watu watakatifu" linamaana ya Wakristo. "Watu wa Yerusalemu waliokwisha kumwamini Yesu"

ana mamlaka kutoka kwa kuhani mkuu kumkamata kila mmoja

Inamaana Sauli amepewa nguvu na mamlaka na Kuhani Mkuu, lakini yalikuwa na mipaka kwani ilikuwa ni kwa Wayahudi tu.

Yeye ni chombo teule kwangu

"chombo teule" ni hali ya kutengwa maalumu kwa ajuli ya huduma. "Nimemchagua yeye ili anitumikie.

Kubeba jina langu

Hii ni hali ya kumuelezea na kuongelea kuhusu Yesu. ili anipeleke mimi kwa watu.

Kwa ajili ya jina langu

Hii ni hali ya kuwaelezea watu kuhusu mimi (Yesu).

Acts 9:17

Sentensi unganishi

Anania anaenda katika nyumba ambapo Sauli anaishi. Baada ya kuponywa , simulizi inabadilika kutoka kwa Anania kwenda kwa Sauli.

Anania akaenda, akaingia mle nyumbani;

Anania likwenda kwenye na baada ya kuipata ile nyumba mahali alipokuwepo Sauli akaingia ndani.

Kumwekea mikono

Anania aliweka mikono yake juu ya Sauli

amenituma ili upate kuona na kujazwa roho mtakatifu

"Amenituma ili upate kuona tena na Roho Mtakatifu akujaze"

Kitu kama magamba

"Kitu kilitokea kama magamba ya samaki na kuanguka toka machoni"

akapata kuona

Alikuwa na uwezo wa kuona tena

Aliinuka na akabatizwa

"Sauli aliiuka na Anania akambatiza"

Acts 9:20

Wakati huo huo akamtangaza Yesu

ukumu la kumtangaza Yesu, punde alianza kulifanya.

Akisema kuwa Yeye ni mwana wa Mungu

"Yeye" inaashiria kuwa ni Yesu. Sauli, Baada ya kumwamini Yesu na kumjua Yesu kama 'mwana wa Mungu"

Wote waliomsikiliza

Wengi walipata kusikia habari zake.

Sio mtu yule aliyewaharibu wote wa Yerusalemu walioliitia jina hili?

Hii ni kejeli na swali hasi linalomwelezea Paulo kuwa hakika alikuwa mtu ambaye aliwatesa waamini. "Huyo ni mtu ambaye aliwaharibu wote wa Yerusalemu walioliitia jina hili la Yesu!"

Acts 9:23

Wayahudi

Inamaanisha Wayahudi viongozi.

lakini mpango wao ukajulikana na Sauli

"Lakini mtu mmoja akawaambia mpango wao kwa Sauli" au "Lakini Sauli akafahamu mipango yao juu yake"

Wakamvizia mlangoni

Mji huu ulikuwa na ukuta uliouzunguka.Watu waliingia na kutoka katika mji huo kupitia mlango.

Wanafunzi wake

Watu walioamini ujumbe wa Sauli kuhusu Yesu na walifuatilia mafundisho yake

wakamshusha kupitia ukutani, wakamtelemsha chini katika kapu

Kwa kutumia kamba walimshusha Sauli katika kikapu kikubwa kupitia tundu katika ukuta.

Acts 9:26

Lakini wote walikuwa wakimuogopa

"Walikuwa wote" ni kuimba kwa wingi "karibia wote"

Sauli alihubiri kwa ujasiri katika jina la Yesu

Huu ni mfano wa Sauli anahubiri au anafundisha ujumbe wa injili ya Yesu Kristo.

Acts 9:28

Katika jina la Bwana Yesu

Hii ni injili ya mfano wenye ujumbe wa Yesu Kristo.

Mahojiano na wayahudi wa kiyunani

Sauli alijaribu kutafuta sababu za wayahudi wa kiyunani.

Kumleta chini mpaka Kaisaria

Kaisaria iko chini zaidi ya Yerusalemu. Hata hivyo,ilikuwa kawaida kusema kwamba mmoja alipanda juu Yerusalemu.

na wampeleke aende Tarso.

Kaisari ilikuwa bandari, yawezekana walimpeleka Sauli Tarso kwa njia ya meri.

Acts 9:31

Sentensi unganishi

Katika mstari wa 32, habari inabadirika kutoka simlizi ya Sauli na kuanza simlizi mpya juu ya Petro.

Maelezo ya jumla

Mstari wa 32 ni habari inayotupatia taarifa za kukua kwa kanisa.

kanisa lote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria

Hapa ni kiwakilishi cha "kanisa" kama umoja likiwakilisha zaidi ya kusanyiko la waumini. Linaelezea waumini wote katika jumuia zote za Israeli.

lilikuwa na amani

ilikaa kwa amani". Linamaanisha kuwa yale mateso yaliyoanza kwa mauaji ya Stefani yalikuwa yamekoma.

Likajengwa

Hapa mwezeshaji wake ni "Mungu" au "Roho Mtakatifu". "Mungu aliwasaidia wakue" au "Roho Mtakatifu aliwajenga na kuwa imara".

Kutembea katika hofu ya Mungu

"waliendelea kumheshimu Bwana'

Katika faraja ya Roho Mtakatifu

"Roho Mtakatifu aliwaimarisha na kuwapa ujasiri"

Pande zote za mkoa

Hii ni fahari kwa Petro kutembelea waumini wengi pande za Yuda, Galilaya, na Samaria.

Alitelemkia

Neno "Alitelemkia" ilieleza kuelekea Lida iliyo upande wa chini kulinganisha na maeneo mengine alikotembelea Petro.

Lida

Lida ni mji ulioko kati ya kilomita 18 kaskazini mashariki mwa Jafa. Huu mji ulikuwa ukiitwa Lod kwenye Agano la Kale,na katika Israeli ya sasa.

Acts 9:33

Akamuona huko mtu mmoja

Petro hakuwa makini kumtafuta mtu aliyepooza lakini ilimtokea. "Hapo Petro akakutana na mtu."

mtu mmoja jina lake Ainea

Hapa anatambulisha Ainea kama mtu mpya katika simlizi.

Ambaye amekuwa kitandani ...amepooza

Hii ni historia ya nyuma kuhusu Ainea

Aliyepooza

hana uwezo wa kutembea, pengine hakuwa na uwezo wa kujisogeza chini ya kiuno

jitandikie kitanda chako

"jitwike godoro lako"

kila mtu aliyekaa Lida Sharon

Hii inaimarisha maana " watu wengi walioishi maeneo ya Lida na Sharoni.

Wakamwona yule mtu.

Inaweza kuwa msaada kuelezea kuwa walimwona mtu akiwa mtu ameponywa. "Walimwona mtu ambaye Petro alikuwa amemponya".

Acts 9:36

Sentensi unganishi

Luka anaendelea na simlizi ya tukio jipya kuhusu Petro.

Maelezo ya jumla

Mistari hii inatupa historia ya mwanamke aliyeitwa Tabitha.

Palikuwa

Hili linamtambulisha sehemu mpya katika simulizi.

Tabitha, ambalo lilitafsiriwa kama "Dorcas."

Tabitha ni jina lake katika lugha ya kiaramaiki,na jina la Dorcas katika lugha ya Kigiriki. Majina yote yalikuwa na maana ya "paa."

alijaa matendo mema

"anafanya mengi mazuri ya kweli"

Ilitokea katika siku hizo

"Ilitokea wakati Petro alipokuwa Lida".

walipomsafisha

Waliusafisha mwili ikiwa ni maandalio ya maziko yake.

walimpandisha chumba cha juu na kumlaza.

Huu ilikuwa ni utaratibu wa muda wa kuuonyesha mwili wakati wa maandalizi ya mazishi.

Acts 9:38

Waliwatuma watu wawili kwake

"Wanafunzi waliwatuma watu wawili kwake"

Katika chumba cha juu

Chumba cha juu mahali mwili wa Dorkas ulikuwa umelazwa.

Wajane wote

Inawezekana kuwa wajane wote wa mji ule walikusanyika pamoja kwani haukuwa mji mkubwa.

Wajane

wanawake ambao waume zao walifariki na walikuwa wanahitaji kusaidiwa.

Wakati akiwa pamoja nao

"wakati akiwa hai pamoja na wanafunzi"

Acts 9:40

Sentensi unganishi

Simlizi ya Tabitha inaishia katika mstari 42, na mstari 43 unatuambia kilichokuwa kinaendelea kwa Petro baada ya simlizi ya Tabitha kumalizika.

Akawatoa wote nje

Kwa shauri hili, Petro aliwafanya kila mmoja kuondoka ili aweze kuwa pekee yake na kuomba kwa ajili ya Thabitha.

akampa mkono wake akamwinua

Petro alimshika mkono wake na kumsaidia kuinuka.

waumini na wajane,

Hata wajane yawezekana walikuwa waumini, lakini hapa wametambulishwa kwa jina la wajane kwasababu Tabitha alikuwa mtu muhimu kwao.

Jambo hili kujulikana Yafa yote

Muujiza wa Petro kumfufua Tabitha kutoka kwenye kifo ukajulikana na watu wote wa Yafa.

Walimwamini Bwana

"waliiamini injili ya Bwana Yesu."

Ikatokea kwamba Petro alikaa

"Ikatokea kuhusu kwamba Petro akakaa huko kwa muda"

Acts 10

Matendo 10 Maelezo kwa Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Chafu(Najisi)

Wayahudi waliamini kwamba waliamini walitembelea ama kula na watu wa mataifa. Hii ni kwa sababu Wafarisayowalikuwa wameunda sheria kinyume nayo kwa vile walitaka watu wasikule chakula ambacho sheria Musa ilisema ni najisi. Sheria ya Musa ilisema kwamba chakula kingine kilikuwa najisi lakini haikusema kwamba watu hawakustahili kutembelea ama kula na watu wa mataifa. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#clean and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses)

Ubatizo na Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu aliwakujia waliokuwa wakimsikiza Petero. Hii inaonyesha Waumini Wayahudi kwamba watu wa Mataifa wangepokea neno la Mungu na kupokea Roho Mtakatifu vile waumini Wayahudi walivyopokea. Baada ya hiyo,Watu wa Mataifa walibatizwa.

<< | >>

Acts 10:1

Sentensi unganishi

Huu ni mwanzo wa sehemu juu ya habari inayohusu Kornelio.

Maelezo ya jumla

Mistari hii inatupa mrejesho wa taarifa kuhusu yeye.

Kulikuwa na mtu fulani

Hii ilikuwa ni njia ya kutambulisha mtu mwingine katika habari.

jina lake aliitwa Cornelio, alikuwa mkuu wa kikosi cha Kiitalia

"jina lake aliitwa Kornelio. alikuwa ni mtu mwenye cheo wa maaskari 100 kutoka Italia katika sehemu ya jeshi la Rumi"

Alikuwa mcha Mungu na alimwabudu Mungu

"Aliamini katika Mungu na alitaka kumtii Mungu na kumwabudu Mungu katika maisha yake"

na nyumba yake yote

"na watu wote wengine wa nyumbani kwake ambao pengine walikuwa wa mataifa walimcha Mungu"

aliomba kwa Mungu siku zote.

Alikuwa akimwomba Mungu wakati wote.

Acts 10:3

saa tisa

Hii ni muda wa Alasiri wa kawaida uliokuwa ukitumiwa na wayahudi kwa maombi.

akaona kwa wazi

Kornelio aliona kwa wazi"

Maombi yako na zawadi zako kwa masikini zimepanda juu kama kumbukumbu kwenye uwepo wa Mungu

Inamaanisha kuwa Misaada ya Kornerio kwa wahitaji pamoja na maombi yalimpendeza Mungu na kuwa ukumbusho kwake.

mtengenezaji wa Ngozi

Mtu mtaalamu wa kutengeneza ngozi za wanyama.

Acts 10:7

Baada ya Malaika aliyekuwa akisema naye kuondoka

"Baada ya maono ya Kornelio kufika mwisho"

Askari aliyekuwa akimwabudu Mungu kutoka miongoni mwa maaskari waliokuwa wakimtumikia.

Moja ya maaskari waliokuwa wakimtumikia Kornelio ambao pia walikuwa wakimwabudu Mungu. Ilikuwa mara chache sana jeshi la kirumi, ambapo Kornerio na maaskari wengine kumcha Mungu, alihali wenginge hawamchi Mungu.

aliwaambia yote yaliyotokea

Kornerio alielezea maono yake kwa watumishi wake wawili na kwa mmoja wa maaskari wake.

akawatuma Yafa

"aliwatuma wawili wa watumishi wake na askari mmoja huko Yafa"

Acts 10:9

Sentensi unganishi:

Habari inabadilika kutoka kwa Kornelio kutuambia kile Mungu alikuwa anakifanya kwa Petro.

Wakati wa saa sita

"Ilikuwa saa sita mchana"

juu darini

Mapaa ya nyumba yalikuwa tambarare, na watu mara nyingi walifanya kazi mbalimbali juu yake.

wakati watu wanapika chakula,

"Kabla watu hawajamaliza kutayarisha chakula cha mchana"

Aliona maono

"Mungu alimpa Petro maono" au "Aliona maono"

akaona anga limefuguka

Huu ulikuwa ni mwanzo wa Maono ya Petro.

kitu fulani kama nguo kubwa ikishuka chini kwenye ardhi katika kona zake zote nne

Ndani ya chombo kilikuwa na wanyama na mwonekano wake ni kama nguo kubwa ya pembe nne.

kikishuka chini katika pembe zake nne.

"Kitambaa kikiwa na pembe zake nne juu zaidi ya kingine.

aina zote za wanyama wenye miguu minne na watambaao juu ya ardhi, na ndege wa angani

Wanyama wenye miguu... ndege wa angani. Mwitikio wa Petro kwa maono yale mstari unaofuata unaonyesha Wayahudi walikuwa wamepewa amri ya kutokula baadhi ya hao wanyama. "Wanyana na ndege ambao sheria ya Musa ilizuia wasipate kuliwa"

Acts 10:13

sauti ikasema kwake

Mtu anayeongea hajulikani. Pengine "sauti" alikuwa Mungu mwenyewe, ingawa inawezekana alikuwa Malaika kutoka kwa Mungu.

Siyo hivyo

Petro anaapa "Sitafanya hivyo"

sijawahi kula kitu chochote najisi na kichafu

Imetafsiriwa kuwa wanyama wanawakilisha wasio safi kama ilivyoelezwa na sheria ya Musa na walikuwa hawaliwi na waumini walioishi kabla ya kifo cha Kristo.

Alichokitakasa Mungu

Kama Mungu ndiye msemaji, anajipambanua mwenyewe kwa nafsi ya tatu; "Kile ambacho Mungu alikitakasa"

Hii ilitokea mara tatu

Si kwamba kila kitu alichokiona Petro kilitokea mara tatu. Hii inaweza kuwa na maana; "Kile ambacho Mungu alikitakasa" neno hili ndilo lilijirudia mara tatu mfurulizo.

Acts 10:17

Petro akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa

Inamaana kuwa Petro alikuwa na wakati mgumu kuelewa maana ya maono hayo.

Tazama

Neno "Tazama" hapa linatutazamisha sisi kuwa makini katika taarifa za ajabu ambazo zinafuata, kwa jambo hili, wanaume wawili walisimama mbele ya geti.

wakasimama mbele ya geti

"kusimama mbele ya geti la kuingilia ndani." hii inamaanisha kuwa hii nyumba ilikuwa na ukuta na geti la kuingilia kwenye nyumba hiyo.

wakiuliza njia ya kwenda kwenye nyumba

Hili nitukio lilitendeka kabla ya kufika kwenye nyumba alipokuwa Petro. Hili tukio lingeripotiwa mapema kabla.

Na wakaita

Watu wa Karnelio walibaki nje ya Geti wakati wakiulizia kuhusu Petro.

Acts 10:19

akiwaza juu ya hayo maono

"Wakati Petro alipokuwa akifikri juu ya haya maono"

Roho

"Roho Mtakatifu"

Tazama

Uwe macho" au "Amka"

watu watatu wanakutafuta

Baadhi ya nyaraka za kale zinasema idadi tofauti ya wale watu.

Shuka chini

"Shuka chini kutoka dari ya nyumba"

Usiogope kwenda nao

Ingekuwa kawaida kwa Petro kutokwena na hao watu; 1) Kwa vile walikuwa wageni kwake na 2) Walikuwa wa mataifa ambapo Wayahudi walikuwa hawachangamani na wao.

Mimi ni yule mnayemtafuta

"Mimi ndiye mtu yule mnayemtafuta"

Acts 10:22

Wakasema

"Wale wajumbe watatu kutoka kwa Kornelio wakasema kwa Petro"

hupenda kumwabudu Mungu

Neno "Kumwabudu" Lina maana ya nia ya ndani kuheshimu na kicho cha kweli.

taifa lote la kiyahudi

Hii ni mfano kwa ajili ya tabia nzuri ya Kornelio ilikuwa inajulikana vizuri kwa watu wengi wa Kiyahudi.

Petro akawakaribisha kuingia ndani na kukaa pamoja naye

Safari ya kuelekea Kaisaria ilikuwa ndefu sana kwa wao kuanza muda wa mchana.

kukaa pamoja naye

"Wajumbe wa Kornerio wakawa wageni wake"

ndugu wachache kutoka Yafa

Hii inaelezea juu ya waumini waliokuwa wakiishi Yafa.

Acts 10:24

Siku iliyofuata

Hii ilikuwa ni siku moja baada ya wao kuondoka Yafa. Safari ya kwenda Kaisaria ilikuwa ndefu zaidi ya siku moja.

Kornelio alikuwa akiwasubiri

Kornerio alikuwa akiwatarajia. Akiwa amewaita pamoja ndugu zake na marafiki zake wa karibu

Acts 10:25

Wakati Petro akiingia ndani

"Mara Petro alipoingia ndani ya nyumba"

Kornerio akainama hadi chini kwenye miguu yake

Ingawa kuinama lilikuwa ni tendo la kawaida katika utamaduni wao, Kornerio yeye aliinama kwa Petro kama ishara ya kumsujudia.

Simama; mimi mwenyewe pia ni mwanadamu

Hili ni kukemea vikali au marekebisho kwa Kornelio kuwa asimwabudu Petro.

Acts 10:27

Sentensi unganishi:

Petro anawaelekea watu waliokuwa wamekusanyika kwenye nyumba ya Kornelio.

watu wengi wamekusanyika pamoja

"akakuta wamataifa wengi wamekusanyika pamoja." hii inamaanisha kuwa watu ambao Kornelio alikuwa amewaalika walikuwa wamataifa.

Ninyi wenyewe mnajua

Petro anamlenga Korneria na wageni aliokuwa amewaalika.

siyo sheria ya kiyahudi

"imefichika kwa wayahudi"

mtu ambaye si wa taifa hili.

Anaelezea watu ambao hawakuwa wayahudi, bila kutaja maeneo maalumu walikokuwa wanaishi.

Acts 10:30

Sentensi unganishi:

Kornelio akajibu swali la Petro.

Maelezo ya jumla:

Mstari wa 31na 32 Kornelio ananukuu kile malaika alisema alipojitokeza kwake wakati wa saa tisa.

Siku nne zilizopita

Kornerio anafafanua juu ya siku kabla ya usiku wa siku kabla ile kabla hajaongea na Petro. Utamaduni wa Kibiblia unahesabu siku hiyo. Hivyo kabla ya siku tatu zilizopitz za usiku ilihesabiwa kuwa "siku ya nne iliyopita." Mila za Magharibi ya sasa, hii inawezakuwa, "Siku tatu zilizopita."

Wakati nikiomba

maandiko ya kale yanasema "kufunga na kuomba" badala ya kuomba tu"

muda wa saa tisa

Mchana wa kawaida ni wakati wa Wayahudi kuomba kwa Mungu.

maombi yako yamesikiwa na Mungu

Inamaanisha Mungu amesikia maombi yako

ukumbusho mbele za Mungu

"Mungu amekuletea ukumbusho" Hii haimanishi kuwa Mungu alikuwa amesahau.

akamwite mtu mmoja anayeitwa Simoni aje kwako

"Mwambie Simoni anayeitwa Petro kuja kwako"

Umetenda wema kuja

Hii ni namna ya heshima ya kumshukuru Petro kwa kuja kwake.

katika macho ya Mungu

Hii inadhihirisha uwepo wa Mungu.

Acts 10:34

Sentensi unganishi

Petro anaanza hotuba kuongea na kila mtu ndani ya nyumba ya Kornelio.

Ndipo Petro akafungua mdomo wake na kusema

"Petro alianza kuzungumza kwao"

Hakika

Hii inamaanisha kile anachokwenda kukisema kina umuhimu wa kukijua

Mungu hawezi kuwa na upendeleo

"Mungu hapendelei watu maalumu"

kila mtu yeyote anayemwabudu na kufanya matendo ya haki anakubalika kwake

"anamkubali kila mtu anayemwabudu na kufanya matendo ya haki"

Ibada

Neno "Ibada" linamaanisha nia ya ndani ya heshima na kicho cha kweli.

Acts 10:36

Sentensi unganishi

Petro anaendelea na Kornerio pamoja na wageni wake.

ambaye ni Bwana wa wote

"Wote" maana yake watu wote"

Yudea yote

"Katika maeneo mbalimbali ya Yudea"

baada ya ubatizo ambao Yohana alitangaza

"Baada ya Yohana kuhubiri kwa watu kurubu na kubatizwa"

Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu

Roho Mtakatifu na nguvu za Mungu zimenenwa kana kwamba ni vitu vinaweza kumiminwa juu ya mtu.

wote walioteswa na ibilsi

"Watu wengi waliokuwa wanapitia mateso ya shetani"

Mungu alikuwa pamoja naye.

Inamaanisha; "Mungu alikuwa akimtia nguvu kuzitenda kazi zote"

Acts 10:39

Maelezo ya jumla

Petro na Mitume na waumini ambao walikuwa pamoja na Yesu wakati akiwa hapa duniani.

Katika nchi za Wayahudi

Inaelezea zaidi Yudea ya wakati huo.

ambaye waliyemuua

"ambaye viongozi wa kiyahudi walimwua''

Wakamtundika juu ya mti

Inamaanisha, "kumuwamba Yesu katika mti wa msalaba"

Huyu mtu

"Huyu mtu Yesu"

Mungu alimfufua

"Mungu alimfanya kuishi tena"

siku ya tatu

"Siku ya tatu baada ya kufa kwake"

kumpa kujulikana

"alimpa kujulikana na wengi"

kutoka kwa wafu

"Kutoka miongoni mwa waliokwisha kufa" Linafafanua juu ya roho za watu waliokwisha kufa. Kurejea kutoka miongoni mwa hizo roho ni kuwa mzima tena.

Acts 10:42

Sentensi unganishi

Petro anamalizia hotuba yake katika nyumba ya Kornerio aliyokuwa ameianza.

kuwa huyu ndiye ambaye Mungu alimchagua

Mungu alikuwa amemchagua Yesu Kristo.

walio hai na waliokufa

Anamaanisha, " Watu walio hai na watu waliokwisha kufa

Katika yeye manabii wote washuhudie

"Manabii wote walishuhudia habari za Yesu".

kila anayeamini katika yeye atapokea msamaha wa dhambi

Mungu atasamehe dhambi za kila mmoja anayemwamini Yesu kwasababu ya kile Yesu ametenda.

kupitia jina lake

Neno "jina" Linaelezea matendo ya Yesu. Jina lake linamaanisha Mungu huokoa.

Acts 10:44

Roho Mtakatifu akawajaza wote

Neno "Kuwajaza" maana yake ni kutokea ghafla. "Roho Mtakatifu ghafla alishuka".

wote waliokuwa wakisikiliza

Neno "wote" linaelezea kuwa; "Wamataifa ndani ya nyumba waliokuwa wakimsikiliza Petro".

Watu wale wanaohusika na kikundi cha waamini waliotahiriwa

Hii ni namna nyingine ya kuzungumzia juu ya Waumini Wayahudi

Karama ya Roho Mtakatifu

Inaelezea juu ya Roho Mtakatifu mwenyewe aliyetolewa kwao.

Roho Mtakatifu aliyemwagwa

Mungu alimtoa Roho Mtakatifu. "Zawadi ya bure"

Pia na kwa mataifa

Neno "pia" linaonyesha ukweli kuwa Roho Mtakatifu alikuwa tayari ametolewa kwa Wayahudi waumini

Acts 10:46

Sentensi unganishi

Huu ni mwisho wa sehemu ya simlizi kuhusu Kornerio.

wamataifa wanaongea kwa lugha zingine na kumwabudu Mungu

Zilijulikana kuwa ni lugha zilizokuwa zinatamkwa na waliojazwa na Roho Mtakatifu, kilichofanya Wayahudi kukubali kwamba wamataifa nao walikuwa wakimtukuza Mungu.

Kuna mtu yeyote anaweza kuzuia maji ili watu wasibatizwe, Watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi?

Petro alilitumia swali hili kuwashawishi Wayahudi wakristo kwamba Wamataifa walioamini wanaweza kubatizwa.

Ndipo akawaamuru wabatizwe

Inamaanisha kwamba Wayahudi wakristo ndio waliowabatiza Wamataifa siku hiyo.

wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo

"Kwa Jina la Yesu Kristo" Linaelezea kuwa sababu ya kubatizwa kwao ni kwa kumwamini Yesu Kristo.

Acts 11

Matendo 11 Maelezo kwa Ujumla

Dhana Maalum katika sura hii

"Watu wa mataifa pia walipokea neno la Mungu"

Karibu waumini wote wa kwanza walikuwa Wayahudi. Luka anaandika katika sura hii kwamba watu wengi wa mataifa walianza kumwamini Yesu. Waliamini kwamba habari ya Yesu ilikuwa habari ya kweli, vile wakaanza "kulippokea neno la Yesu." Baadhi ya waumini katika Yerusalemu hawakuamini kwamba watu wa Mataifa pia wangekuwa wafuasi halisi wa Yesu. Kwa hivyo Petero alienda akawaambia kilichokuwa kimemtendekea na jinsi alivyowaona watu wa mataifa wakilipokea neno la mungu na kupokea Roho Mtakatifu.

<< | >>

Acts 11:1

Sentensi unganishi

Petro anaingia Yerusalemu na anaanza kuongea na Wayahudi wa huko.

Maelezo ya jumla

Huu ni mwanzo wa tukio jipya katika simlizi

Sasa

Linaashiria sehemu mpya ya simlizi

Ndugu

"Ndugu" Linamaanisha waumini katika Yudea.

waliokuwa Yudea

"Waliokuwa wakiishi mkoa wa Yudea"

Walikuwa wamelipokea neno la Mungu

Linamaanisha kuwa Wamataifa walikuwa wameupokea ujumbe wa Injili kuhusu Yesu. "Waliamini ujumbe wa Mungu kuhusu Yesu Kristo".

Walikuwa wamepanda kwenda Yerusalemu

Yerusalemu ilikuwa juu zaidi ya kila eneo la Israeli. hivyo ilikuwa kawaida kwa Waisraeli kusema wanapanda juu kwenda Yerusalemu.

lile kundi la watu waliotahiriwa

Wayahudi walioamini kwamba kila anayeamini lazina atahiriwe.

watu wasiotahiriwa

Linamaanisha, "watu wa Mataifa"

Alikula pamoja nao

Ilikuwa kinyume kwa utamaduni wa Wayahudi, Wauahudi kula na Wamataifa.

Acts 11:4

Sentensi unganishi

Petro anawajibu Wayahudi kwa kuwaambia juu ya maono na kile kilichotokea katika nyumba ya Kornerio.

Petro alianza kueleza

Petro hakujaribu kusema maneno ya kuwapinga Wayahudi waumini, bali alijibu kwa maelezo ya kirafiki na hekima.

Kwa undani

"Hakika ya kile kilichotokea"

Kama kitambaa kikubwa

Chombo kilichoshikilia wanyama kilionekana kitambaa kikubwa.

Chenye pembe nne

"Kikubwa chenye pembe nne"

wanyama wenye miguu minne waishio katika nchi,

"Wanyama wa miguu" Mwitikio wa Petro ulilenga sheria ya Musa iliyokuwa inazuia kula baadhi ya wanyama.

Wanyama wa mwitu

Pengine ni wanyama wasioweza kufugwa.

wanyama watambaao

Hawa ni wale waendao kwa kutambaa.

Acts 11:7

nikasikia sauti

Sauti ilinena lakini bila yeyote kujidhihirisha. "Sauti" yawezekana ni Mungu, ingawa inawezekana kuwa ilikuwa sauti ya Malaika.

Siyo hivyo

"Siwezi kufanya hivyo" linganisha na sura 10:13.

mdomoni mwangu hakujawahi kuingia kitu chochote kisicho kitakatifu

Wanyama waliokuwa kwenye kitambaa walikuwa ni wanyama ambao sheria ya Wayahudi katika Agano la Kale iliwazuia wasiweze kuwala.

Kichafu

Katika Agano la Kale Sheria ya Wayahudi, mtu alionekana mchafu katika njia mbalimbali, kama vile kula wanyama waliokuwa hawaruhusiwi kuliwa.

kile Mungu alichokitangaza kuwa ni safi, usikiite najisi

Sentensi hii inaelezea juu ya wanyama waliokuwa kwenye kitambaa kikubwa cha pembe nne.

Hii ilitokea mara tatu

Si kila tukio lilirudiwa kuonekana mara tatu, Hata hivyo neno; "Kile Mungu alichokitakasa usikiite najisi" Ni neno lilijirudia mara tatu kwa Petro. Linganisha na sura 10:13.

Acts 11:11

Tazama

Hili neno linaashiria kuanza kutajwa watu wengine kwenye simlizi hii.

Mara moja

"Mara hiyo bila kuchelewa"

Walikuwa wametumwa

"Mtu fulani alikuwa amewatuma"

na nisitofautiane nao.

"Kwamba nisipate cha kunitofautisha nao kwamba walikuwa wamataifa"

Hawa wanaume sita wakaenda pamoja na mimi

anaume sita wakaenda nami mpaka Kaisaria.

Hawa ndugu sita

"Hawa sita Wayahudi waumini"

Ndani ya nyumba ya mtu mmoja

Linaelezea nyumba ya Kornerio

Simoni aliyeitwa Petro

"Simoni ambaye pia aliitwa Petro"

utaokoka

Inaweza kuwa "Mungu atakuokoa"

Na wote wa nyumba yako

Linamaanisha; Wote wataokolewa walioko nyumbani mwako"

Acts 11:15

Maelezo ya jumla

Hapa Petro anajumuisha yeye, Mitume na Wayahudi waumini wote waliopokea Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste.

Nilipoanza kusema nao, Roho mtakatifu akaja juu yao

namaanisha kwamba, "Petro kabla hajamaliza kunena, kwa vile alikuwa amenuia kusema nao zaidi, Roho Mtakatifu akaingilia kati kwa kuwashukia.

Roho mtakatifu akaja juu yao kama alivyokuja kwetu mwanzoni.

Roho Mtakatifu alishuka kwa wamataifa walioamini kama vile alivyofanya kwetu siku ya Pentekoste.

mtabatizwa katika Roho mtakatifu

Mungu atawabatizeni ninyi katika Roho Mtakatifu.

Acts 11:17

Sentensi unganishi

Petro anamalizia hotuba yake aliyokuwa ameianza katika sura 11:4 kwa Wayahudi juu ya maono yaliyotokea katika nyumba ya Korinerio.

Pia kama Mungu ametoa zawadi... mimi ni nani, kwamba naweza kumpinga Mungu?

Petro anatumia swali hilikueleza kuwa yeye alikuwa anafanya vile kwa kumtii Mungu.

Zawadi sawa

Petro anaelezea zawadi ya Roho Mtakatifu.

Waliposikia mambo haya, hawakurudisha,

"Walinyamaza, hawakuweza tena kumshambulia Petro.

Mungu ametoa toba kwa ajili ya uzima.

"Ametoa toba kwa wote kuwaongoza katika uzima wa milele"

Acts 11:19

Sentensi unganishi

Luka anaelezea kuhusu kile kilichotokea kwa waumini waliokimbia baada ya kuuawa kwa Stefano kwa mawe.

Sasa

Luka anatambulisha simlizi mpya

waamini ambao mateso yalianzia kwenye kifo cha Stephano walitawanyika kutoka Yerusalemu-waamini hawa walienda mbali,

Mateso yaliyoanza na kifo cha Stefano yalisababisha waumini kukimbia na kusambaa maeneo mbalimbali.

Wayahudi peke yake

Waumini walidhani ujumbe wa Mungu ulikuwa kwa ajili ya Wayahudi pekee na siyo kwa wamataifa pia.

na kusema na wayunani

Watu aliokuwa wakiongea kiyunana nao walikuwa ni watu wa mataifa hawakuwa Wayahudi.

Na mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao

Mkono wa Mungu unamaanisha nguvu zake. "Mungu alikuwa na nguvu kuwawezesha wale waumini kuhubiri kwa ujasiri".

na kumgeukia Bwana

Wengi waliacha kuiamini miungu yao ya zamani, na walimwamini Yesu.

Acts 11:22

Maelezo ya jumla

Katika mistari hii Luka anaanza kumtaja Barnaba na wakati huo huo akiwataja waumini wa kanisa la Yerusalemu.

masikioni mwa kanisa

apa neno "masikio" linamaanisha Waumini walisikia habari za matukio.

kuona karama ya Mungu

"Kuona neema ya Mungu" au "Namna gani Mungu ametenda kwa ukarimu juu ya waumini".

aliwatia moyo wote

"Aliendelea kuwatia moyo"

kubaki na Bwana

"kubaki waaminifu katika Bwana" au"Kuendelea kumtumaini Bwana"

Kwa miyo wao wote

"Kwa utimilifu; au Bila kupungukiwa"

amejazwa na Roho Mtakatifu

Barnaba aliongonzwa na Roho Mtakatifu kwa vile alikuwa amemtii.

watu wengi wakaongezeka katika Bwana

"Kuongezeka" Walioamini walizidi kuongezeka.

Acts 11:25

Maelezo ya jumla

Luka anazungumzia kuhusu Barnaba na Sauli.

Kwenda Tarso

"Alitoka kuelekea Tarso"

kumwona Sauli...Alipompata, akamleta Antiokia

Inaonyesha Barnaba alichukua muda na bidii kumtwaa Sauli kutoka Tarso.

Ikawa

neno linaonyesha mwanzo wa tukio jingime katika simlizi hiyo.

wakakusanyika pamoja na kanisa

"Barnaba na Sauli wakakusanyika pamoja na kanisa."

Na wanafunzi wakaitwa wakristo kwa mara ya kwanza

Inamaanisha kuwa watu wengine walikuwa wakiwaita waumini kwa jina hili. "Watu wa Antiokia waliwaita wanafunzi wakristo"

Kwa mara ya kwanza

"Kwa mara ya kwanza huko Antiokia"

Acts 11:27

Maelezo ya jumla

Luka anaelezea historia kuhusu unabii huko Antiokia.

Sasa

Neno hili linatumika kuweka kituo katika simlizi hiyo kuu.

manabii wakashuka kutoka Yerusalemu mpaka Antiokia

Yerusalemu ilikuwa juu zaidi ya Antiokia, hivyo ilikues kawaida ya Waisraeli kusema wanapanda kwenda Yerusalemu

Agabo ndilo jina lake

"Jina lake alikuwa akiitwa Agabo

akiashiriwa na Roho

"Roho Mtakatifu alimwezesha kutoa unabii"

njaa kali itatokea

"Upungufu mkubwa wa chakula utatokea"

Juu ya dunia yote

Akimaanisha, "Katika dola yote ya Kirumi"

wakati wa siku za Klaudio.

Wasikilizaji wa Luka wangejua kwamba Klaudio alikuwa Mtawala wa Rumi wakati huo.

Acts 11:29

Maelezo ya Jumla

Sura hii wanaotajwa ni waumini wa kanisa huko Antiokia

Kwa hiyo

Neno linaloelezea kuwa jambo lililotokea kwasababu ya kitu kingine pia

kila mmoja alivyo fanikiwa,

atu matajiri walituma misaada zaidi, na wale masikini walituma kwa kiasi chao.

kwa ndugu walioko Uyahudi

"Kwa wakristo waliokuwa huko Yudea"

kwa mkono wa Barnaba na Sauli.

"Chini ya usimamizi wa Barnaba na Sauli"

Acts 12

Matendo 12 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Sura ya 12 inatuelezea kilichomtendekea mfalme Herode wakati Barnabas alikuwa anamrudisha Saulo kutoka Tarshishi na wakipeleka pesa kutoka Antiokia kwa watu wa Yerusalemu (11:25-30). Aliwaua viongozi wengi akamfunga Petero gerezani. Baada ya Mungu kumsaidia Petero kutoroka gerezani, Herode aliwaua walinzi wa gereza kisha naye akauwawa na Mungu. Luka anatuelezea katika mstari wa mwisho wa sura hii jinsi Barnaba na Saulo waliyorudi kutoka Antiokia.

Mifani ya usemi muhimu katika hii sura

Kuwa na mfano wa kibinadamu

"Neno la Mungu" linazungumziwa kana kwamba ni kiumbe kinachoweza kumea na kuzaana. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#wordofgod and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-personification)

<< | >>

Acts 12:1

Sentensi unganishi

Hapa tena panaanza mateso upya. tukio la kwanza ni la kuuawa kwa Yakobo na kisha kukamatwa kwa Petro na kutiwa gerezani na baadaye kuwa huru.

Maelezo ya jumla

Hii ni historia kuhusu Herode kumwua Yakobo.

Sasa

Hii inaanzisha mwanzo wa simulizi.

Wakati huo

Neno linalotambulisha wakati au kipindi cha njaa.

akanyosha mkono wake

Inamaanisha Herode alikuwa ameanza kuwakamata waumini.

wale wanaotoka kwenye kusanyiko

Ni Yakobo na Petro pekee wanatajwa kuashiria huwa hawa walikuwa viongozi wa kanisa la Yerusalemu.

ili kuwatesa

"Kusababisha mateso kwa waumini"

Akamwuua Yakobo nduguye Yohana kwa upanga.

Hii inaonyesha namna Yakobo alivyouawa.

Akamwua

Inamaanisha ama "Herode Mfalme alimwua" au "Herode Mfalme aliagiza kuua."

Acts 12:3

Maelezo ya jumla

Neno la kiwakilishi hapa linamaanisha Mfalme Herode.

Baada ya kuona kuwa inawapendeza Wayahudi

erode alitambua kuwa mauaji ya Yakobo yalikuwa yamewafurahisha Wayahudi"

Kuwapendeza Wayahudi

"Wayahudi viongozi walipendezwa na tukio hilo"

Hiyo ilikuwa

"Herode alifanya hivi" au "Hii ilitokea"

Siku za mikate isiyochachwa

Inadokeza sikuku ya dini ya Kiyahudi ya Pasaka. "Ni muda huu Wayahudi walikuwa wakila mkate usiotiwa chachu."

vikosi vinne vya askari

"Vikosi vinne vya askari". Kila kikosi kilikuwa na askari wanne vilivyo mlinda Petro. Kila kikosi kimoja baada ya muda uliogawanywa katika saa ishrini na nne. kila mara askari wawili wangekuwa karibu na Petro alihali askari wawili wakiwa kwenye lango.

alikuwa akitarajia kumpeleka kwa watu

Herode alikuwa amepanga kumhukumu Petro mbele ya macho ya Wayahudi.

Acts 12:5

Petro akawekwa gerezani,

Inamaanisha Maaskari waliendelea kumlinda Petro ndani ya gereza.

lakini maombi yakafanywa kwa bidii na kusanyiko kwa ajili yake

Kundi la waumini wa Yerusalemu kwa nia moja walimwomba Mungu kwa ajili yake.

Kwa nia moja

"Walizidi kujikabidhi" au "Kwa nia moja bila kukatisha maombi"

Herode alikuwa anatarajia kumtoa nje

Herode alikuwa amepanga kumtoa Petro nje ya gereza ili kumhukumu.

amefungwa na minyororo miwili,

"alifungwa kwa minyororo miwili". Kila mnyororo ulikuwa umeunganishwa kwa walinzi wawili walioketi karibu na Petro.

Wakilinda gereza.

"Wakifanya kazi yao ya ulinzi"

Acts 12:7

Tazama

Neno linaloashiria kuzingatia kwa taarifa za kushangaza zilizokuwa zinakwenda kutokea.

Upande wake

"Anayefuata" au "Upande wake"

Ndani chumbani

"ndani ya chumba cha gereza"

Akampiga Petro ubavuni

"Malaika alimpiga ili kumwamsha Petro" Petro alikuwa na usingizi mzito kiasi kwamba ilikuwa inahitajika kuamshwa.

minyororo aliyokuwa amefungwa ikafunguka

Malaika alisababisha minyororo kuanguka kutoka kwa Petro bila ya kuigusa.

Petro akafanya hivyo

Petro alifanya kile aliagizwa kufanya na Malaika. Petro alitii.

Acts 12:9

Hakujua

"Hakuwa anajua kilichokuwa kinaendelea"

kilichofanywa na malaika kama ni cha kweli

Tukio la Malaika kwa Petro lilikuwa la kweli.

Baada ya kupita lindo la kwanza na la pili

Askari hawakuwa na uwezo wa kumwona Petro na malaika wakitembea mpaka kutoka lango la nje.

walipita

"Waliweza kupita"

Lindo la pili

"Katika lindo la pili nako wakapita"

Wakafika

"Walilifikia lango kuu"

Lililoelekea mjini

"Lilifunguka kutoka gerezani kuelekea mjini"

likafunguka lenyewe

Si Petro wala Malaika aliyelifungua lango hilo.

wakashuka kwenye mtaa,

"Wakatembea wakiwa barabarani"

Malaika akamwacha.

"Mara Malaika akamwacha" au "Ghafla akatoweka"

Acts 12:11

Petro alipojitambua

"Petro alipopata ufahamu alitambua kuwa tukio lilikuwa halisi"

ili kunitoa katika mikono ya Herode,

ungu ameniokoa na mkono mbaya wa Herode uliopangwa kwa ajili yangu"

na kwa matarajio ya watu wote wa uyahudi

"Kwamba Wayahudi viongozi walidhani ingefanikiwa kwa Petro kuuawa"

Baada ya kujua haya

Herode alitambua kuwa Mungu alikuwa amemwpusha Petro na hukumu ya yake.

Yohana ambaye ni Marko

"Yohana ambaye pia aliitwa Marko"

Acts 12:13

Maelezo ya jumla

Maelezo haya yanawataja binti Rhoda pamoja na wote waliokuwa wakiomba mle chumbani.

Alibisha mlangoni

"Petro alibisha mlangoni" Alizidi kugongagonga kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi ili kuruhusu waliopo kujua kuwa wametembelewa.

kwenye mlango wa kizuizi

"Katika mlango wa nje" au "Katika mlango wa kuingilia kutoka barabarani hadi kwenye yadi ya nyumba"

Akaja kufungua

"Alikuja getini kuuliza ni nani aliyekuwa anabisha hodi"

Kwa furaha

"Kwa vile alijawa na furaha" au "Furaha kupita kiasi"

Alishindwa kuufungua mlango

"Hakuweza kuufungua mlango" au "Alisahau kufungua mlango"

akakimbia ndani ya chumba

"Alikwenda mbio kwenye chumba cha nyumba ile"

na kuwajulisha

liwajulisha au "Alisema"

Petro amesimama mbele ya Mlango

"Amesimama nje mbele ya mlango"

Wewe ni mwendawazimu

Watu siyo tu hawakumwamini, bali walimkemea pia kwa kusema maneno ya kipuuzi.

lakini alikazia kuwa ni kweli

"Alisisitiza kusema alichowaambia kilikuwa cha kweli"

Wakamwambia

"Walimwambia"

Ni malaika wake

"KIle ulichokiona ni malaika wa Petro" Wayahudi waliamini kuwa na malaika mlinzi na inawezekana walifikiri kwa Petro hivyo, kuwa malaika wa Petro alikuwa amekuja kwao.

Acts 12:16

Maelezo ya jumla

Ingawa Herode alikuwa amemwua Yakobo sura 12:1, hata hivyo kulikuwa na Yakobo zaidi ya mmoja.

Lakini Petro aliendelea kubisha

Neno "Kuendelea" linamaanisha Petro alifuluriza kubisha kwa mudo wote wale wa ndani wakiwa wanazungumza habari zake.

Wajulishe haya mambo

"Waambieni habari hizi"

Ndugu zake

"Waumini wengine"

Acts 12:18

Sasa

Hili limetumika kutenganisha simulizi. Muda umekwishapita, sasa ni siku nyingine.

Kulipokuwa mchana,

"Saa ya asubuhi"

kukawa na huzuni kubwa

Kinyume cha huzuni kubwa ni "Furaha kubwa" Askari hao hawakuwa na furaha hiyo tena.

Furaha kubwa

Hili linaelezea kinyume cha furaha kama; Msongo wa mawazo, mashaka, hofu na kuchanganyikiwa.

kuhusu

"Kuhusiana na"

Baada ya Herode kumtafuta na hakumwona

"Herode alimtafuta Petro na kushindwa kumpata"

akawauliza walinzi na akaamuru wauawe

Ilikuwa ni adhabu ya kawaida kwa serikali ya Rumi kuua walinzi kama mfungwa wao aliwatoroka.

Akaenda kutoka uyahudi mpaka Kaisaria

Kaisaria ilikuwa chini zaidi ya Yudea.

Acts 12:20

Sentensi unganishi

Luka anaendelea na simlizi nyingine juu ya maisha ya Herode.

Sasa

Neno linaloweka daraja la kuelekea kwenye tukio jingine.

Wakaenda kwa pamoja kwake.

Ni tukio lisilofurahisha kwamba wote walikwenda kwa Herode. "Wanaume waliowawakilisha watu wa Tiro na Sidoni walienda kwa pamoja kufanya mazungumzo pamoja na Herode.

Wakawa na urafiki na Blasto

"Hawa watu walimfanya kuwa rafiki yao"

Blasto

Blasto alikuwa msaidizi au ofisa wa Mfalme Herode.

wakaomba amani,

"Wanaume wale waliomba kuwe na amani"

nchi yao ilipokea chakula kutoka katika nchi ya mfalme.

Yawezekana walinunua chakula hiki. "Watu wa Tiro na Sidoni walikuwa wakinunua chakula chao chote kutoka kwa watu waliotawaliwa na Herode."

nchi yao ilipokea chakula

Inaonekana Herode alikuwa amezuia nchi yake kutoa chakula kwa Tiro na Sidoni kwasababu alikuwa amewakasirikia watu wa nchi hizo.

Siku iliyokusudiwa

Hii inawezekana ilikuwa ni siku ambayo Herode alikubali kukutana na wawakilishi wa miji ya Tiro na Sidoni.

mavazi ya kifalme

Mavazi ya gharama ambayo yangemdhihirisha kuwa alikuwa mfalme.

kukaa kwenye kiti chake cha kifalme,

Hii ilikuwa ni kawaida ya Herode kufanya wakati watu walikuja kumwona.

Acts 12:22

Sentensi unganishi

Hii ni sehemu ya mwisho ya simlizi ya Mfalme Herode.

Ghafla

"Wakati huo huo" au "Wakati watu walipokuwa wakimsifia Herode"

akampiga,

"Herode aliharibiwa" au " kikasababisha Herode kuwa mgonjwa sana"

hakumpa Mungu utukufu

Herode akawaruhusu watu wamwabudu yeye badala ya kuwaambia wamwabudu Mungu.

akaliwa na chango na akafa

"Chango" inaonyesha na wadudu ndani ya mwili, labda minyoo katika utumbo.

Acts 12:24

Maelezo ya jumla

Hii ni taarifa inayotoa mrejesho juu ya kuenea kwa neno la Mungu na kwa vile Barnaba na Sauli walikuwa wakifanya.

neno la Mungu likakua na kusambaa

Neno la Mungu likahubiriwa kama vile mti mbichi uliokuwa na uwezo wa kustawi na kuzaa matunda. "Neno la Mungu likasambaa katika maeneo mbalimbali na watu wakamwamini."

Neno la Mungu

Watu wengi walisikia habari za neno la Mungu na kuupokea wokovu kwa njia ya Yesu.

kukamilisha huduma yao wakatoka pale wakarejea Yerusalemu,

Inaelezea wakati walipopeleka fedha kutoka kwa waumini wa Antiokia sura 11:29.

walirudi kutoka kule

Walirudi kwenda Antiokia. "Baraba na Sauli walirudi Antiokia"

wakamchukua na Yohana

"Baraba na Sauli walimchukua Yohana pamoja nao"

ambaye jina la kuzaliwa ni Marko

"Alikuwa akiitwa jina jingine Marko"

Acts 13

Matendo 13 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Tafsiri zingine zimeweka nukuu kutoka Agano La Kale kwenye mkono wa kulia mbali na maandiko mengine. ULB hufanya hivi kwa kutumia nukuu tatu kutoka Zaburi 13:33-35

Tafsiri zingine zimeweka kila mstari wa ushairi mbele ya kulia kuliko maandishi mengine ili kurahisisha kusoma. ULB hufanya hiv na ushairi ambao umenukuliwa kutoka Agano la Kale 13:41

Nusu ya pili ya kitabu cha Matendo inaanzia katika sura hii. Luka anaandika zaidi kumhusu Paulo kuliko Petero, na inelezea jinsi watu wa mataifa, na siyo Wayahudi, wanafunuliwa habari ya Yesu na waumini.

Dhana Maalum katika sura hii.

Mwanga kwa watu wa mataifa

Mara nyingi Biblia huzungumzia watu wasio wanyoofu, watu wasiotenda yanayomfurahisha Mungu,kana kwamba ni watu watembeayo kwa giza. Inazungumzia mwanga kana kwamba ndio unaweazesha wenye dhambi kubadilika ili wafahamu kwamba wanachotenda ni kibaya na waanze kumtii Mungu. Wayahudi waliwachukulia watu wote wa mataifa kama watembeao kwa giza lakini Paulo na Barnaba wakazungumzia watu wa mataifa kumhusu Yesu kama watakaoenda kuwaletea mwanga wa kawaida. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous) Jesus as if they were going to bring them physical light. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#figs-metaphor and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous)

<< | >>

Acts 13:1

Sentensi unganishi

Luka anaanza kuzungumzia habari za safari za huduma ambazo kanisa la Antiokia liliwatuma Barnaba na Sauli.

Maelezo ya jumla

Mstari wa 1 unatupatia maelezo kuhusu watu wa kanisa la Antiokia.

Sasa katika kanisa la Antiokia,

"Kwa wakati, kanisa la Antiokoa"

Simeoni (aliyeitwa Nigeri). Lukio wa Kirene, Manaen

"Majina ya baadhi ya waliokuwepo katika kanisa la Antiokia

ndugu asiye wa damu wa Herode kiongozi

"Manaeni alikuwa pengine rafiki yake na Herode waliocheza michezo ya ujana pamoja naye"

kiongozi wa mkoa

"Mtawala wa sehemu au robo ya nchi"

Wakati

Neno hili linatambulisha matukio mawili yaliyokuwa yanatendeka kwa wakati mmoja.

Niteengeeni pembeni

"Nitengeeni hao kwa kunitumikia mimi"

kazi niliyo waitia.

Linamaanisha, Mungu amewachagua kufanya hazi hii.

na kuweka mikono yao juu ya watu hawa

"Wakaweka mikono juu ya manaume hao ambao Mungu alikuwa amejitengea kwa kazi yake. Tendo hili lilionyesha kwamba viongozi walikubali kuwa Roho Mtakatifu alikuwa amewaita Barnaba na Sauli kwa kuifanya kazi hii."

wakawaacha waende.

"Wakawaacha waende zao" au "Wakawatuma wanaume hao kutenda kazi ambayo Roho Mtakatifu alikuwa amewatuma kuitenda"

Acts 13:4

Maelezo ya jumla

Luka anandika kuwaelezea Barnaba na Sauli

Sasa

Neno hili linatambulisha tukio lililotendeka kwasababu ya lile lililokuwa limetangulia kutukia. Tukio la mwanzo lilikuwa la kutengwa na Roho Mtakatifu kwa Barnaba na Sauli

walitelemka

Neno "Kutelemka" linatumika hapa kwasababu Seleukia ni mji ulio chini zaidi ya Antiokia.

Seleukia

Mji ulio kandokando ya ziwa.

Mji wa Salami

Mji wa Salami ulikuwa katika kisiwa cha Kipro.

Sinagogi la Wayahudi

Maana inayowezekana; 1) "Kulikuwa na masinagogi mengi ya Wayahudi katika mji wa Salami mahali Barnaba na Sauli walihubiri" au 2) Barnaba na Sauli waliaza kuhubiri ndani ya Sinagogi katika mji wa Salami na kuendelea kuhubiri katika Masinagogi waliyoyaona wakati wakisafiri kuzunguka kisiwa hicho cha Kipro

walikuwa pamoja na Yohana Marko kama msaidizi wao.

"Yohana Marko alisafiri pamoja nao na alikuwa akiwasaidia"

Msaidizi

"Aliyewahudumia"

Acts 13:6

Maelezo ya jumla

Mistari hii imetaja viwakilishi vingi vya majina kuelezea watu mbalimbali walio tajwa na mwandishi Luka.

katika kisiwa chote

Walitembelea kisiwa chote kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wakiunena ujumbe wa Injili katika kila mji walimopita.

Pafo

Ni mji Mkuu wa kisiwa cha Kapro mahali Liwali alikuwa akiishi.

Walimkuta

Neno "Kumkuta" linamaanisha kuwa walimfikia bila ya kumtafuta.

Mtu fulani mchawi

"Mtu aliyekuwa akifanya kazu ya uchawi" au "Mtu aliyekuwa akifanya mambo yasiyo ya kawaida katika fani ya kimazingaombwe"

ambaye jina lake lilikuwa Bar Yesu

"Bar - Yesu" maana yake "Mwana wa Yesu". Hakukuwa na mahusiano yoyote ya karibu na Yesu Kristo". Jina Yesu lilikuwa ni jina la kawaida katkia wakati ule.

Mchawi huyu alishirikiana

"Alikuwa mara kwa mara pamoja na" au "Alikuwa mara kwa mara akiambatana na"

Liwali

Huyu alikuwa Kiongozi mtendaji Katika utawala mkoa wa dola ya Rumi.

aliyekuwa mtu mwenye akili

Hii ni historia ya maisha ya Liwali Sergio Paulus.

Lakini Elima "yule mchawi"

Huyu alikuwa Bar- Yesu, ambaly aliyekuwa akiitwa mchawi.

hivyo ndivyo jina lake lilivyo tafsiriwa

"Hivyo ndivyo jina lake katika lugha ya kigriki"

aliwapinga; alijaribu kumgeuza

"Aliwazuia akijaribu kumgeuza"

alijaribu kumgeuza yule liwali atoke kwenye imani

"Alijaribu kumshawishi Liwali kuiacha imani ya ujumbe wa Injli"

Acts 13:9

Sentensi unganishi

Wakati wakiwa katika kisiwa cha Pafo, Pauli alianza kuzungumza na Elima.

Lakini Sauli aliyeitwa Paulo

"Sauli" ambalo ni jina la Kiyahudi, na "Paulo" ambalo ni jina la Kirumi. Wakati alipokuwa akizungumza na mtawala wa Rumi, alikuwa akitumia jina la Kirumi.

akamkazia macho

"Akamkazia macho kwa makini"

Ewe mwana wa Ibilisi

Paulo anasema yule mtu alikuwa akitenda kama Ibilisi. "Wewe sawa na shetani" au "Unatenda kama Shetani"

umejazwa na aina zote za udanganyifu na uovu

"Wakati wote unatenda kwa kusababisha wengine waamini ambacho si kweli kwa kutumia udanganyifu na mara zote unatenda mabaya"

Uovu

Inamaanisha kuwa mzembe na kutokufuata sheria ya Mungu kwa dhati.

Wewe ni adui wa kila aina ya haki

Paulo anamwunganisha Elima pamoja na Ibilisi. Kama vile Ibilisi ni adui wa Mungu kwa kuwa kinyume na haki, ndivyo ilivyo kwa Elima pia.

Hautakoma kuzigeuza njia za Bwana, zilizonyooka, je utaweza?

Paulo anatumia swali kumkemea Elima kwa upinzani wake kwa Mungu.

njia za Bwana, zilizonyooka

Hapa "njia zilizonyoka" linamaanisha njia zilizo za kweli katika Bwana.

Acts 13:11

Sentensi unganishi

Paulo anamalizia majadiliano na Elima.

mkono wa Bwana upo juu yako

Neno "mkono" unawakilisha nguvu za Mungu na neno "juu yako" linamaanisha adhabu . "Mungu atakuadhibu"

utakuwa kipofu.

Hii inaweza kutafsiriwa kuwa; "Mungu atakufanya kipofu"

Hautaliona Jua

Elima atakuwa kipofu kabisa kwamba hataweza kuliona jua.

kwa muda

"Kwa kipindi fulani" au "Mpaka muda wa Mungu aliouamru"

mara moja ukungu na giza vilianguka juu ya Elimas

"Macho ya Elima yakapata ukungu na giza" au "Elima uoni ulikuwa hafifu na kisha hakuweza kuona kabisa"

alianza kuzunguka pale

"Elima alianza kutangatanga"

Liwali

Huyu alikuwa ni mtumishi wa serikali katika jimbo la Rumi.

Aliamini

"Alimwamini Yesu"

alishangazwa kwa mafundisho kuhusu Bwana.

"Mafundisho kuhusu Bwana Yesu yalimshangaza mno"

Acts 13:13

Sentensi unganishi

Hii ni sehemu mpya ya simlizi kuhusu Paulo akiwa Antiokia ya Pisidia

Maelezo ya jumla

Mistari ya 13 na 14 inatupa inatupa ufafanuzi wa simlizi hiyo.

Maelezo ya jumla

"Paulo na rafiki zake" Walikuwa Barnaba na Yohana Marko (aliyeitwa Yohana). Kutokea hapa na kuendelea, Sauli akaitwa Paulo katika Matendo ya Mitume. Jina la Paulo limeorodheshwa kwanza kuonyesha kuwa alikuwa kiongozi wa kundi. Ni muhimu kutunza mtiririko huu katika tafasiri.

Sasa

Linaonyesha mwanzo wa kipengere na simlizi mpya.

walisafiri majini kutoka Pafo

"Walisafiri kwa kutumia jahazi kutoka Pafo"

wakafika Perge katika Pamfilia.

"Walifika Perge iliyo Pamfilia"

Lakini Yohana aliwaacha

"Lakini Yohana Marko akawaacha Paulo na Barnaba"

Antiokia ya Pisidia.

"Mji wa Antiokia ni wilaya ya Pisidia"

Baada ya kusoma sheria

"Sheria na Manabii" Inamaanisha sehemu ya maandiko ya Wayahudi ambayo yalisomwa. 'Baada ya mtu mmoja kusoma kutoka vitabu vya sheria na maandiko ya Manabii"

waliwatumia ujumbe wakisema

"Wakiwaomba mmoja wao aseme neno"

Ndugu

Neno "ndugu" lilitumika wa watu katika Sinagogi kuwazungumzia Paulo na Barnaba kama Wayahudi wenzao.

kama mnao ujumbe wa kutia moyo

"Kama mnataka kutuambia jambo lolote la kututi moyo"

semeni

"Tafadhali mnaweza kunena"

Acts 13:16

Sentensi unganishi

Paulo anaanza hotuba yake kwa watu waliokuwamo kwenye Sinagogi huko Antiokia ya Pisidia. Anaanza kwa kuzungumzia mambo ambayo yalitokea katika historia ya Israeli.

alisimama na kuwapungia mkono

Inamaanisha kutoa ishara kwa mikono kwamba yuko tayari kuanza kusema.

enyi mnao mtii Mungu

Anamaanisha, Wamataifa ambao wanafuata desturi na dini ya Kuyahudi. "Ninyi msio Waisrael, lakini mnamwabudu Mungu"

sikilizeni

"Nisikieni mimi" au "Sikieni ambacha nataka kuwaambia"

Mungu wa hawa watu wa Israeli

"Mungu ambye anaabudiwa na Waisraeli

baba zetu

"Mababa wa Wayahudi"

na kuwafanya watu wengi

"Aliwawezesha wao kuwa watu wengi sana"

kwa mkono wake kuinuliwa

anamaanisha Mkono wa Mungu wenye uweza.

aliwaongoza nje yake

"Kutoka katika nchi ya Misri"

aliwavumilia

linamaanisha "Aliwajali" na "Aliwavumilia katika kutokutii kwao"

Acts 13:19

Maelezo ya jumla

Mwinjilisti Luka katika kuandika kwake anatumia viwakilishi vingi vya majina kuelezea wale ndugu wanaotajwa katika vifungu hivi.

Mataifa

Neno "Mataifa" linafafanua tofauti ya makundi ya watu na siyo mipaka ya mataifa kijiografia.

yalitokea zaidi ya miaka mia nne na hamsini

lichukua muda wa miaka mia nne na hamsini kuikamilisha kazi ya kuyaondoa mataifa Kanaani.

mpaka Samweli Nabii

"Muda huo ulifikia hata kipindi cha Nabii Samweli"

Acts 13:21

Maelezo ya jumla

Nukuu katika simlizi hii inatoka katika kitabu cha Samweli na katika Zaburi za Ethani katika Agano la kale.

kwa miaka arobaini

"Kuwa mfalme wao kwa miaka arobaini"

kumuondoa katika ufalme

Inamaanisha kuwa Mungu alisababisha Sauli asiendelee kuwa Mfalme. "Alimkataa asiwe Mfalme"

alimwinua Daudi kuwa mfalme wao

"Mungu alimchagua Daudi kuwa Mfalme wao."

Mfalme wao

"Mfalme wa Israeli" au "Mfalme juu ya Waisreli"

Ilikuwa ni kuhusu Daudi kwamba Mungu alisema

"Mungu alisema hivyo kuhusu Daudi"

Nimempata

"Nimeshaona kwamba"

kuwa mtu apendezwaye na moyo wangu

namaanisha kuwa "Yeye ni mtu anayetaka kutenda ambayo mimi nataka"

Acts 13:23

Maelezo ya jumla

Nukuu hii inatoka katika vitabu vya Injili.

Kutoka kwenye ukoo wa mtu huyu

"KUtoka katika ukoo wa Daudi." Hii imewekwa mwanzoni mwa sentensi kuelezea kuwa Mwokozi angekuwa nduye aliyetoka katika ukoo wa Daudi.

ameiletea Israeli

Inamaanisha watu wa Israeli.

kama alivyoahidi kufanya

"Kama vile Mungu alivyoahidi angefanya"

Ubatizo wa toba

Unaweza kulitafasiri neno "toba" kama kitenzi kama vile; "Ubatizo kwa watu waliotakiwa kutubu kwa ajili ya dhambi zao."

"Mwanifikiri mimi ni nani?"

Yohana aliuliza swali kuwafanya watu wafikirie Yohana alikuwa nani.

mimi si yule

Yohana alikuwa anamwelezea Masihi, ambaye watu walikuwa wanamtegemea kuja.

Lakini sikilizeni

Neno linalo elezea umuhimu wa kile ambacho atakwenda kusema.

ajaye nyuma yangu

Hii pia inazungumzia kuja kwa Masihi. "Masihi atakuja Mapema"

sisitahili kulegeza viatu vya miguu yake.'

"Mimi sistahili hata kungua kamba za kiatu chake."

Acts 13:26

Maelezo ya jumla

Viwakilishi vya majina hapa vinamuwakilisha Paulo na kundi lote la watu waliokuwemo kwenye Sinagogi.

Ndugu, watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wale ambao kati yenu mnamwabudu Mungu

Paulo analielezea kundi la Wayahudi na wale wa mataifa walioungia katika dini ya kiyahudi ili kubaki na hali yao waliyoichagua ya kumwabudu Mungu wa kweli.

ujumbe huu wa ukombozi umetumwa

Kwa maneno mwngine; "Mungu ameshatuma ujumbe wake wa wokovu"

Ukombozi huu

Neno hili linamaanisha kwamba; "Mungu atawaokoa watu"

hawakumtambua

"Hawakuweza kabisa kumtambua huyu mtu Yesu alikuwa ni mmoja ambaye Mungu alimtuma kuwakomboa."

Ujumbe wa manabii.

Unawakilisha; "Maandiko ya manabii" au "Ujumbe wa manabii."

ambao unasomwa

"Ambao mtu anausoma"

walitimiliza ujumbe wa manabii

"Hakika walitenda kama vile Manabii walivyosema."

Acts 13:28

Maelezo ya jumla

Viwakilishi vya majina, vinawakilisha Wayahudi na Viongozi wa dini zao katika Yerusalemu.

hawakupata sababu nzuri kwa kifo ndani yake

"Hawakupata sababu zenye maana kwanini Yesu alipaswa auawe"

Walimwomba Pilato amwue

Neno "Kumwomba" ni neno lenye nguvu likimaanisha "Kutaka, kulazimisha, kudai"

Walipomaliza mambo yote yaliyoandikwa kuhusu yeye

"Wakati walipomtendea Yesu, kila kitu walichokuwa wamekisema manabii kilitimia.

walimshusha kutoka mtini

"Walimwua Yesu na kuuondoa mwili wake kutoka kwenye msalaba baada ya kufa."

kutoka mtini

"Kutoka msalabani"

Acts 13:30

Lakini Mungu alimfufua

"Lakini" ni neno linaloonyesha nguvu ya kutofautisha usemi uliotangulia na ule unaofuata kama vile; "Watu walimwua Yesu lakini Mungu alimfufua Yesu"

alimfufua kutoka wafu.

"Alimfufu kutoka miongoni mwa wale waliokuwa wamekufa"

kufufuliwa

"Kufanywa mzima tena"

Alionekana... Galilaya kuelekea Yerusalemu.

"Wanafunzi waliotembea pamoja na Yesu kutoka Galilaya mpaka Yerusalemu wakimwona kwa siku nyingi."

Siku nyingi

"Tunajua kutoka maandiko mengine kwamba, muda wa siku arobaini"

hawa sasa ni mashahidi wa watu.

"Sasa wanashuhudia kwa watu habari za Yesu"

Acts 13:32

Maelezo ya jumla

Nukuu ya pili hapa inatoka katika kitabu cha nabii Isaya.

Hivyo

Kiunganishi cha neno kinachoonyesha tukio kwamba tukio lililokwisha kupita ni kwasababu ya tukio lililokuwa limetangulia kutukia. Tukio la nyuma kabla ya lile lililofuata ni la kumfufua Yesu kutoka kwa wafu.

mababu zetu.

"mababu zetu" Paulo bado anaongea na Wayahudi na watu wa mataifa waliofuata desturi za Kiyahudi huko Antiokia Pisidia. Hawa walikuwa mababu wa kimwili wa Wayahudi na Mababu wa kiroho wa wakristo wa mataifa waliofuata desturi za Kiyahudi.

Mungu aliweka ahadi hizi

"Mungu amekwisha timiza hizo ahadi"

kwetu, watoto wao,

"Kwetu" inamaanisha wale watoto wa hao mababu"

katika hilo alimfufua Yesu na kumrudisha tena katika uhai

"Kwa kumfanya Yesu kuwa mzima tena"

Hili pia liliandikwa katika Zaburi

kweli huu umeandikwa pia na Zaburi ya pili."

Mwanangu, leo nimekuwa Baba yako

Hivi ni vyeo muhimu vinavyoeleza ule uhusiano kati ya Yesu na Mungu.

kwamba alimfufua kutoka wafu ili kwamba mwili wake usiharibike, ameongea hivi

"Mungu alinena haya maneno juu ya kumfanya Yesu kuwa mzima tena ili asionekane na mauti tena"

Kutoka kwa wafu

"Wafu" ni neno linalowakilisha watu waliokwisha kufa. Atamfufua kutoka miongoni mwao na kumfanya kuwa mzima tena"

baraka halisi

"Baraka za kipekee"

Acts 13:35

Hii ndiyo sababu kasema pia katika zaburi nyingine

Wasikilizaji wa Paulo wangeweza kufahamu kuwa Zaburi hii ilikuwa inamtaja Masihi.

Anasema pia

"Daudi pia alisema." Daudi ni mwandishi wa Zaburi ya 16 ambapo nukuu hii imechukuliwa.

'Hautaruhusu mtakatifu wako kuuona uozo.'

Neno "kuona uozo" ni neno linalofanana na "kuharibika." Hutaruhusu mwili wa mtakatifu wako kuharibika."

Hutaruhusu

Hapa Daudi anamwambia Mungu.

Katika kizazi chake

"Katika kipindi cha uhai wake"

kutumika katika nia ya Mungu

"alifanya kile alichomtaka Mungu kufanya"

alilala,

Hii ilikuwa lugha laini iliyokwa inazungumzia kifo.

alilazwa pamoja na baba zake

"Alizikwa pamoja na baba zake waliokuwa wamekufa"

aliuona uaharibifu

"Kuona uharibifu" ni kusema kuwa "Mwili wake uliharibiwa"

Lakini aliyefufuliwa

"Lakini Yesu ambaye"

hakuuona uharibifu

"Yesu hakuona uharibifu"

Acts 13:38

Maelezo ya jumla

Kiwakilishi cha jina "yeye" linaelezea juu ya Yesu.

na ifahamike kwenu

"Fahamu hivi" au "Hii ni muhimu kwako kujua"

Ndugu

Paulo anatumia lugha ua ndugu kuona Wayahudi na wafuasi wa dini ya kiyahudi wote ni ndugu.

ifahamike kwenu, ndugu, kupitia mtu huyu, msamaha wa dhambi

"tunawatangazia kuwa dhambi zenu zinaweza kusamehewa kupitia Yesu."

Msamaha wa dhambi

"Msamaha" inaweza kutafasiriwa kuwa; Mungu anaweza kusamehe dhambi zako"

Kwa yeye kila aaminiye

"Kila mmoja anayemwamini yeye"

Kwa yeye kila aaminiye anahesabiwa haki

"Yesu anamhesabia haki kila mmoja anayemwamini"

Kila kitu

"dhambi zote"

Acts 13:40

Sentensi ungsnishi

Paulo anamalizia hotuba yake katika Sinagogi la Antiokia ya Pisidia aliyoianza katika sura 31:16.

Maelezo ya jumla

Katika ujumbe wake kwa watu wa Sinagogi, Paulo ananukuu nukuu ya Nabii Habakuki.

Kuweni waangalifu

"Iweni waangalifu kwa mambo ambayo nimekwisha waelezeni."

kwamba kitu walichokiongelea manabii

"Kwa kile manabii walishawahi kuzungumzia"

Tazama, enyi mnaodharau

"Mnaofanya mizaha, dharau"

mkashangae

"Mkashitushwe"

mkaangamie

"Kisha kufa"

Ninafanya kazi

"Ninatenda kitu"

Katika siku zenu

"Kipindi cha uhai wenu"

Kazi ambayo

"Ninafanya kitu ambacho"

hata kama mtu atawaeleza."

"Hata ikiwa mtu mmoja kuwaanbia habari yake"

Acts 13:42

Paulo na Barnaba walipoondoka

"Wakati Paulo na Barnaba walipokuwa wakiondoka"

wakawaomba waongee

"Wakawaomba"

Maneno yale yale

"Maneno ambayo Paulo alikuwa ameyatamka kwenye hotuba yake"

Wakati mkutano wa sinagogi ulipokwisha

Inaweza kuwa; 1) Wakati Paulo na Barnaba walipoondoka mstari 42: au 2) Paulo na Barinaba waliopouacha mkutano kabla ya kuhitimisha.

Wongofu

"Hawa walikuwa si Wayahudi ambao hawakufuata utamaduni wa Kiyahudi"

waliongea nao na waliwahimiza

"Na Paulo na Barnaba walinena nao hao na kuwasihi"

waendelee katika neema ya Mungu.

"Waendelee kumtumaini Mungu ambaye husamehe dhambi kwasababu ya kile Yesu alifanya kwao"

Acts 13:44

Karibu mji mzima

"Mji" Ni neno linaliwakilisha watu wa mji huo.

kusikia neno la Mungu.

"Kuwasikia Paulo na Barnaba wakinena neno la Bwana Yesu.

Wayahudi

:Hawa ni Wayahudi Viongozi"

walijawa na wivu

"Hali ya wivu ikawajia"

Wakaongea masneno ya kupinga

"Maneno yaliyopinga ujumbe wao"

maneno yaliyopinga vitu vilivyosemwa na Paulo

"Mambo yale yaliyosemwa na Paulo"

Acts 13:46

Maelezo ya jumla

Paulo ananukuu nukuu ya Nabii Isaya katika Agano la Kale.

Ilikuwa ni muhimu

"Mungu alikuwa ameagiza kile cha kufanya"

kwamba neno la Mungu liongelewe kwanza kwenu

"Kwamba tulinene neno la Mungu kwenu kwanza"

kuwa mnalisukumia mbali kutoka kwenu

"Kulipinga neno la Mungu lililonenwa"

nakujiona kuwa hamkusitahili uzima wa milele

Mmeonyesha kuwa hamkuuthamini uzima wa milele"

tutawageukia Mataifa.

"Tutawaambia watu wa Mataifa habari za Yesu"

kama nuru

Hapa ni ukweli kuhusu Yesu kwamba Paulo alikuwa akihubiri kana kwamba kulikuwa na nuru iliyokuwa ikiruhusu watu kuona.

kwamba mlete wokovu kwa pande zote za dunia

"Kuwaambia watu mahali pote katika dunia kwamba ninataka kuwaokoa"

Acts 13:48

kulisifu neno la Bwana.

"Kumsifu Mungu kwa ujumbe kuhusu Bwana Yesu"

Wengi waliochaguliwa kwa uzima wa milele

"Watu wote ambao Mungu alikuwa amewachagua kupokea uzima wa milele"

Neno la Bwana lilienea nchi yote

"Wale alioliamini jina la Yesu walienda kila mahali katika jimbo hilo na kuwaambia wengine habari za Yesu"

Acts 13:50

Sentensi unganishi

Huu ni muda wa mwisho wa Paulo na Barnaba kukaa Antiokia ya Pisidia na wakaenda ikonia.

Wayahudi

Hii yawezekana kuzungumzia viongozi wa Kiyahudi.

Waliwasihi

"Kushawisha" au "kuhamasisha"

Wanaume viongozi

"Wanaume mashuhuri"

Haya yalichochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba

"Walishawishi wanaume mashuhuri na wanawake kuwatesa Paulo na Barnaba"

waliwatupa nje ya mipaka ya mji.

"Waliwatoa Paulo na Barnaba kutoka nje ya mji"

walikung'uta mavumbi ya miguu yao.

"Huu ulikuwa tukio la mfano kuonyesha kwa watu wasioamini kwamba Mungu alikuwa amewakataa na angeweza kuwahukumia"

Wanafunzi

"Yawezekana ni wale waumini wapya walioamini huko Antiokia Pisidia ambao Paulo na Barnaba waliwaacha"

Acts 14

Matendo 14 Maelezo kwa jumla

Dhana Maalum katika sura hii

"Ujumbe wa neema yake"

Ujumbe wa Yesu ni ujumbe wa Mungu ambao huwapa neema wanaomuamini Yesu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#grace and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe)

Zeu na Herme

Watu wa mataifa katika himaya ya Warumi waliabudu miungu wengi ambao hawakuwepo. Paulo na Barnaba waliaambia kuamini katika "Mungu aliye hai" Yahwe. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#falsegod)

Maswala mengine tata kwenye tafsiri ya sura hii.

"Lazima tuingie kwenye ufalme wa Mungu kupitia mateso mengi"

Yesu aliwaambia wafuasi wake kabla hajafa kwamba kila anayemfuata angepata mateso. Paulo anayarudia maneno hayo kupitia maneno tofauti na hayo.

<< | >>

Acts 14:1

Maelezo ya jumla

Habari ya Paulo na Barnaba Ikonia inaendelea.

Ikatokea katika Ikonia ya kwamba

Maana hapa yawezekana kuwa 1) "ilitokea Ikonia ya kwamba" au 2) "Kama kawaida ndani ya Ikonia"

alizungumza kwa namna ambayo

"alizungumza kwa namna ambayo." Inaweza kusaidia kutamka kwamba walizungumza ujumbe kuhusu Yesu. "walizungumza ujumbe kuhusu Yesu kwa nguvu"

Wayahudi waliokuwa hawatii

Hii inalenga kikundi cha Wayahudi ambao hawakumuamini ujumbe wa Yesu.

kutikisa akili za Wayunani

kusababisha Wayunani kuwa na hasira inazungumzwa kana kwamba maji yaliyotulia kuchafuliwa.

akili

hapa neno "akili" linamaanisha watu

ndugu

hapa "ndugu" linamaanisha Paulo na Barnaba na waumini wapya.

Acts 14:3

Maelezo ya jumla

Hapa neno "Yeye" linamaanisha Bwana.

Kwa hiyo wakabaki kule

"Hata hivyo walibaki kule." Paul na Barnaba walibaki ikonia kuwasaidia watu wengi walioamini katika 14:1. "Kwa hiyo" inaweza kuondolewa kama itaongeza mchanganyiko kwenye maandishi.

kutoa uthibitisho kuhusu ujumbe wa neema yake

"kuonesha kwamba ujumbe kuhusu neema yake ni kweli"

kuhusu ujumbe wa neema yake

"kuhusu ujumbe wa neema ya Bwana"

kwa kuruhusu ishara na maajabu kufanywa na mikono ya Paulo na Barnaba.

HIi inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa kuwawezesha Paulo na Barnaba kufanya ishara na maajabu"

kwa mikono ya Paulo na Barnaba

Hapa "mikono" inamaanisha nia na juhudi za wanaume hawa wawili kulingana na walivyoongozwa na Roho Mtakatifu. "kwa huduma ya Paulo na Barnaba"

sehemu kubwa ya mji uligawanyika

Hapa "mji" inamaanisha watu waliomo kwenye mji. "watu wengi wa mji waligawanyika" au "watu wengi wa mji hawakukubaliana"

walikuwa upande wa wayahudi

"waliaunga mkono Wayahudi" au "walikubaliana na Wayahudi." Kundi la kwanza lililotajwa halikukubaliana na ujumbe kuhusu neema.

na mitume

Kundi la pili lililotajwa lilikubaliana na ujumbe kuhusu neema. Inaweza kusaidia kutaja tena kitezi. "walijiunga na mitume"

mitume

Luka anamaanisha Paulo na Barnaba. Hapa "mitume" inaweza kutumika katika hali ya ujumla ya "wale waliotumwa nje."

Acts 14:5

Taarifa ya Jumla:

Hapa waliopata habari ni Paulo na Barnaba.

walijaribu kuwashawishi viongozi wao

"walijaribu kuwashawishi viongozi wa Ikonio." Hapa "walijaribu" inaashiria hawakuweza kuwashawishi kikamilifu kabla ya mitume kuondoka katika mji.

kuwatesa na kuwapiga mawe Paulo na Barnaba

"kuwapiga Paulo na Barnaba na kuwaua kwa kuwaponda mawe"

Likaonia

Wilaya ndani ya Asia Ndogo

Listra

Mji ndani ya Asia Ndogo kusini mwa Ikonio na Kaskazini mwa Derbe

Derbe

Mji ndani ya Asia Ndogo kusini mwa Ikonio na Listra

huko walikuwa wakihubiri injili

"Paulo na Barnaba walihubiri injili pia huko"

Acts 14:8

Kauli Unganishi:

Paulo na Barnaba sasa wako Listra.

Taarifa ya Jumla:

Taarifa ya Jumla: Anayezungumziwa kuwa na imani ni yule kiwete; na aliyemsemesha ni Paulo. Yule aliyesemeshwa ni kiwete.

mtu fulani aliketi

Hii inatambulisha mtu mpya katika simulizi.

dhaifu miguuni mwake

"kutokuweza kusogeza miguu yake" au "kutokuweza kutembea kwa miguu yake"

kiwete

"kilema"

kiwete tangu tumboni mwa mama yake

"kiwete tangu kuzaliwa"

Paulo alimkazia macho

"Paulo alimtazama moja kwa moja"

alikuwa na imani ya kufanywa mzima

Nomino "imani" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi "amini." "aliamini kwamba Yesu anaweza kumponya" au "aliamini kuwa Yesu anaweza kumfanya mzima"

akaruka juu

"akaruka hewani." Hii inaashiria kwamba miguu yake ilikuwa imeponywa kikamilifu.

Acts 14:11

alichokifanya Paulo

Hii inamaanisha uponyaji wa Paulo kwa kiwete.

miungu imeshuka kwetu

Idadi kubwa ya watu iliamini kuwa Paulo na Barnaba walikuwa miungu ya kipagani walioshuka toka mbinguni. "miungu wameshuka toka mbinguni kuja kwetu"

katika lahaja ya Likaonia

"katika lugha yao ya Kilikaonia" (UDB). Watu wa Listra walizumngumza Kilikaonia na Kigriki pia.

katika mfano wa mwanadamu

Watu hawa waliamini kuwa miungu walihitaji kubadili mionekano yao ili wawe kama binadamu.

walimuita Barnaba "Zeu"

Zeu alikuwa mfalme juu ya miungu wengine wote wa kipagani.

Paulo, Herme, kwa sababu alikuwa msemaji mkuu

Herme alikuwa mungu wa kipagani aliyeleta ujumbe kutoka kwa Zeu na miungu wengine.

Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje tu ya mji, alileta

Inaweza kusaidia kuweka taarifa ya ziada kuhusu kuhani. "Kulikuwa na hekalu nje tu ya mji ambapo watu walimwabudu Zeu. Kuhani aliyehudumu katika hekalu aliposikia kile ambacho Paulo na Barnaba walichokifanya, alileta

ng'ombe na mashada ya maua

Ng'ombe walikuwa ni wakutolewa sadaka. Mashada yalikuwa mojawapo kati ya kuwawekea mataji Paulo na barnaba, au kuwawekea ng'ombe kwa ajili ya sadaka.

milangoni

Milango ya miji mara nyingi ilitumika kama sehemu ya kukutana kwa watu wa mji husika.

walitaka kutoa sadaka

"walitaka kutoa sadaka kwa Paulo na Barnaba kama miungu Zeu na Herme.

Acts 14:14

mitume, Barnaba na Paulo

Inawezekana Luka anatumia "mtume" katika hali ya ujumla ya "yule ambaye ametumwa."

walichana nguo zao

Hili ni tendo la ishara kuonesha kuwa walihuzunishwa na kukasirishwa kwamba kundi lilitaka kuwatolea wao sadaka.

Watu, kwa nini mnafanya hivi vitu?

Barnaba na Paulo wanawakaripia watu kwa kujaribu kuwatolea sadaka. "watu, hampaswi kutuabudu!"

Sisi pia ni binadamu wenye hisia kama nyie

Kwa kauli hii, Baranaba na Paulo wanasema kuwa wao sio miungu. "Sisi ni binadamu tu kama nyie.. Sisi sio miungu!"

wenye hisia sawa na nyie

"kama nyie kwa kila hali"

mgeukieni Mungu aliye hai kutoka kwa vitu hivi visivyo na maana

"acheni kuabudu miungu ambayo haiwezi kuwasaidia, na badala yake anzeni kumuabudu Mungu aliye hai"

Mungu aliye hai

"Mungu ambaye kweli yupo" au "Mungu anayeishi"

Siku za nyuma

"katika nyakati za zamani" au "Hadi sasa"

kutembea katika

"kuishi kulingana na"

Acts 14:17

Kauli Unganishi:

Paulo na Barnaba wanaendelea kuzungumza na kundi nje ya mji wa Listra.

hakujiacha mwenyewe bila ya shahidi

Hii inaweza pia kuwekwa katika hali chanya. "hakika Mungu ameacha shuhuda" au "hakika Mungu ameshuhudia"

kwa kuwa

"kama inavyooneshwa na ukweli kuwa"

akiwajaza mioyo yenu kwa chakula na furaha

Hapa "mioyo yenu" inamaanisha watu. "akiwapa cha kutosha kula na vitu ambavyo vitawapa furaha"

Paulo na Barnaba wakawazuia makutano kuwatolea sadaka kwa nadra

Paulo na Barnaba waliwazuia makutano kuwatolea sadaka, lakini ilikuwa ni taabu kufanya hivyo.

wakawazuia ... kwa nadra

"walikuwa na wakati mgumu kuwazuia"

Acts 14:19

Taarifa ya Jumla:

Aliyedhaniwa kuwa amekufa ni Paulo.

kuwashawishi makutano

Inaweza kusaidia kueleza wazi alichowashawishi umati kufanya. "kuwashawishi watu kutowaamini Paulo na Barnaba, na kuwegeukia"

makundi

Hii inaweza kutokuwa kundi moja na "makutano" katika mstari uliopita. Muda umepita, na hili linaweza kuwa kundi tofauti lililokusanyika pamoja.

wakidhani kuwa amekufa

"kwa sababu walifikiri kuwa ameshakufa"

wanafunzi

Hawa walikuwa waumini wapya katika mji wa Listra.

kuingia katika mji

"Paulo aliingia tena Listra na waumini"

alienda Derbe na Barnaba

"Paulo na Barnaba walienda katika mji wa Derbe"

Acts 14:21

Taaarifa ya Jumla:

Hapa waliotangaza ijili na kuwatia mioyo wanafunzi wao inamaanisha Paulo.

Taaarifa ya Jumla:

Wanaposema "Tunapaswa" inajumuisha Paulo, Barnaba na waumini.

mji huo

"Derbe"

Waliendelea kutia nguvu nafsi za wanafunzi

Hapa "nafsi" inamaanisha wanafunzi. Hii inatia mkazo katika mawazo ya ndani na imani. "Paulo na Barnaba waliwasihi waumini kuendelea kuamini ujumbe kuhusu Yesu" au "Paulo na Barnaba waliwasihi waumini kuendelea kukua imara katika mahusiano yao na Yesu.

kuwatia mioyo kuendelea katika imani

"kuwatia mioyo waumini kuendelea kumwamini Yesu"

Acts 14:23

Taarifa ya Jumla:

Waliowachagua na kuwakabidhi kwa Bwana ni Paulo na Barnaba na walioamini ni wale walioongozwa kwa Bwana na Paulo na Barnaba.

Walipowachagua wazee katika kila kanisa

"Paulo na Barnaba walipochagua viongozi katika kila kundi jipya la waumini"

wakawakabidhi

Maana zinazowezekana ni 1) "Paulo na Barnaba wakawakabidhi wazee waliowachagua" au 2) "Paulo na Barnaba wakawakabidhi wazee na waumini wengine" (UDB)

ambaye walimwamini

Wale walioamini inategemea na chaguo lako la ni kina nani waliokuwa wanazungumziwa katika maelezo yaliyopita (mojawapo kati ya wazee au viongozi na waumini wengine).

wakaenda chini Atalia

Usemi "wakaenda chini" unatumika hapa kwa sababu Atalia iko chini kwa kimo kuliko Perge.

ambapo walikabidhiwa katika neema ya Mungu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambapo waumini na viongozi Antiokia waliwakabidhi Paulo na Barnaba kwa neema ya Mungu" au "ambapo watu wa Antiokia waliomba kwamba Mungu awatunze na kuwalinda Paulo na Barnaba"

Acts 14:27

Taarifa ya Jumla:

Waliofika Antiokia na kutoa taarifa ni Paulo na Barnaba. Aliyefungua mlango ni Mungu.

kusanya kanisa pamoja

"wakawaita waumini wa palepale kukusanyika pamoja"

alifungua mlango wa imani kwa Mataifa

Mungu kuwawezesha Mataifa kuamini inazungumziwa kana kwambaaliwafungulia mlango uliokuwa unawazuia kuingia katika imani. "Mungu alifanye iwezekane kwa Mataifa kuamini"

Acts 15

Matendo 15 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Tafsiri zingine zimeweka kila mstari wa ushairi mbele ya kulia kuliko maandishi mengine ili kurahisisha kusoma. ULB hufanya hivi na ushairi ambao umenukuliwa kutoka Agano la Kale 15:16-17

Mkutano unaoelezwa na Luka katika sura hii huitwa "Baraza la Yerusalemu." Huu ulikuwa nimuda ambapo viongozi wengi wa kanisa walikuja pamoja kuamua iwapo waumini walihitaji kufuata sheria zote za Musa.

Dhana maalum katika sura hii

Ndugu

Katika sura hii, Luka anaanza kwa kutumia neno "ndugu" kumaanisha Wakristo wenzake badala ya Wayahudi wenzake.

Kutii sheria za Musa

Waumini wengine walitaka watu wa mataifa watahiriwe kwanza kwa vile Mungu alimuambia Abarahamu kwamba yeyote aliyetaka kuwa wake lazima angepashwa tohara na hii sheria ingedumu. Kwa upande mwingine Paulo na Barnaba walikuwa wameshuhudia Mungu akiwapa watu wa Mataifa kipaji cha Roho Mtakatifu na kwa hivyo hawakusisitiza watu wa mataifa watahiriwe. Makundi yote mawili yalienda Yerusalemu kwa uamuzi wa viongozi wa kanisa kuhusu swala hilo.

"Mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati."

Kuna uwezekano ya kwamba viongozi wa kanisa walitoa uamuzi kwa hizi sheria ili Wayahudi pamoja na watu wa Mataifa waweze kuishi pamoja na kula chakula kimoja pamoja.

<< | >>

Acts 15:1

sentensi unganishi:

Paulo na Barnaba bado wapo Antiokia wakati kulikuwa na malumbano kuhusiana na kutahiriwa kwa watu wa Mataifa

waliwafundisha ndugu

ndugu ina maana ya watu walioamini

Acts 15:3

ujumbe wa jumla

maneno yeye au wao yanamtaja Paulo

kwa kutumwa kwao na kanisa

kanisa hapa linamaanisha watu waliokuwa sehemu ya kanisa

Acts 15:5

lakini watu fulani

hapa Luka anatofautisha watu wanaoamini kuwa wokovu ni kwa Yesu pekee na wale wanaoamini kuwa wokovu ni kwa Yesu lakini pia wanaamini juu ya kutahiriwa kuwa ni muhimu kwa ajili ya wokovu

kutunza sheria ya Musa

kutii sheria ya Musa

Acts 15:7

kwa mdomo

mdomo hapa unamaanisha Petro

aliwapa wao Roho Mtakatifu

alimwacha Roho Mtakatifu aje juu yao

Acts 15:10

sentensi unganishi:

Petro anamaliza mazungumzo yake na mitume pamoja na wazee

baba zetu

hii inamaanisha wazee wa Kiyahudi

Acts 15:12

Ujumbe wa jumla:

neno wao hapa linamaanisha Paulo na Barnaba

kusanyiko lote

kila mtu, au kundi lote

Mungu alifanya

Mungu alitenda, au Mungu alisababisha

Acts 15:13

Sentensi unganishi:

Yakobo anaanza kuongea na mitume na wazee

kwa ajili ya jina lake

kwa ajili ya jina la Mungu

Acts 15:15

Sentensi unganishi:

Yakobo anamnukuu nabii Amosi kutoka Agano la Kale

kubaliana na hili

thibitisha ukweli

jina langu

hii inamaanisha Mungu

Acts 15:19

wanaomgeukia Mungu

Mtu anayeanza kumtii Mungu

kumsoma Musa

hii ina maana ya kusoma sheria za Musa

Acts 15:22

kanisa lote

hii ina maana ya watu wote waliopo kanisani

Sisilia

Hili ni jina la kisiwa katika jimbo la Asia ndogo

Acts 15:24

kuchagua wanaume

watu waliotumwa walikuwa Yuda aitwaye Barsaba na Sila

Acts 15:27

Damu

hii inamaanisha kunywa damu au kula nyama yenye damu

kwa heri

hii inamaanisha mwisho wa barua

Acts 15:30

manabii pia

manabii walikuwa ni walimu walioidhinishwa na Mungu kuongea kwa niaba yake

ndugu

walioamini wenzake

Acts 15:33

neno la Bwana

hii ina maana ya ujumbe wa Mungu

Acts 15:36

turudi sasa

nashauri turudi sasa

Pamfilia

hili ni jimbo katika Asia ndogo

Acts 15:39

na kisha akaenda

hii inamaanisha kuwa Sila alikuwa na Paulo na kisha akaondoka

alipita Siria na Sisilia

Haya ni maeneo katika Asia ndogo

Acts 16

Matendo 16 Maelezo kwa jumla

Dhana maalum katika sura hii

Kutahiriwa kwa Timotheo

Paulo alimtahiri Timotheo kwa vile walikuwa wanahubiri ujumbe wa Yesu kwa Wayahudi na watu wa Mataifa. Paulo alitaka Wayahudi wajue kwamba aliheshimu sheria za Musa ingawa viongozi wa kanisa Yerusalemu walikuwa wameamua kwamba Wakristo hawana haja ya tohara.

Mwanamke aliyekuwa na pepo wa uaguzi

Watu wengi hupenda sana kujua yanayojiri siku za usoni, lakini sheria za Musa zilisema kwamba ni dhambi kuongea na roho za wafu ili kujua yajayo. Inaonekana huyu mwanamke alijua kutabiri yajayo vyema.Alikuwa mtumwa aliyetumiwa na wenyeji wake kujitajirisha kutokana na kazi hii yake. Paulo alitaka aache kutenda dhambi, na kwa hivyo aliamuru huyo pepo amtoke. Luka hatuelezi iwapo alianza kumfuata Yesu ama hata jambo lingine kumhusu.

<< | >>

Acts 16:1

Sentensi ungsnishi

Hii sehemu ya hadithi ni kuhusu safari ya Paulo na Sila. Hapa Timotheo alitambuisha kwenye hadithi na kujiunga na Paulo na Sila. Mstari wa 1 na 2 hutoa taarifa za msingi kuhusu Timotheo

Tazama

Neno "Tazama" inatutaadharisha juu ya mtu mpya katika simulizi. Lugha yako huenda ikawa na njia ya kufanya hivyo.

Kijana aliyezaliwa na mama wa Kiyahudi ambaye ni muumini

"Kijana aliyezaliwa na mama wa Kiyahudi ambaye anamwamini Kristo.

Aliongelewa vizuri

"Timotheo alikuwa na tabia nzuri" au "Walioamini walisema mambo mazuri juu ya Timotheo"

Paulo alimtaka ili asafiri naye, hivyo akamchukua

"Paulo alimtaka Timotheo asafiri naye hivyo Paulo akamchukua" maneno mengine kama (yeye, yake) yanamrejea Timotheo.

baba yake ni Mgiriki

Kama Mgiriki, baba yake Timotheo hangeweza binafsi kumtahiri Timotheo hivyo Paul alimtahiri. Tohara mara nyingi ilifanywa na Mwalimu wa Kiyahudi, kama vile Paulo.

Acts 16:4

walipo kuwa wakienda

"Walipo kuwa" hii inamaanisha Paulo, Sila na Timotheo.

ili kuyatii

'Kwa washiriki wa kanisa kutii' au 'kwa waumini kutii'

yaliandikwa na mitume na wazee huko Yerusalemu

"ambayo imeandikwa na mitume na wazee huko Yerusalemu"

Makanisa yakaimarishwa

"Paulo , Sila na Timotheo waliimarisha makanisa"

Acts 16:6

Firigia na Galatia

Haya ni majimbo huko Asia

walikatazwa na Roho Mtakatifu

"Roho Mtakatifu aliwakataza wao" au " Roho Mtakaifu hakuwaruhusu"

Misia....Bithinia

Haya ni majimbo mengine mawili zaidi huko Asia

Roho wa Yesu

"Roho Mtakatifu"

Acts 16:9

Maono yalimtokea Paulo

Maono ni tofauti na ndoto.

akimwita yeye

"akimuomba Paulo" au "akimsihi Paulo"

mtusaidie

"Unisaidie na watu wengine wa Mekedonia"

kujiandaa kwenda

Neno "tukajiandaa" inajumuisha Paulo pamoja na wale waliokuwa naye, hii ni pamoja na Luka ambaye ndiye muandishi wa kitabu cha Matendo ya Mitume.

Mungu alituita

Alituita, hii inajumuisha Paulo pamoja na wale waliokuwa naye, hii ni pamoja na Luka ambaye ndiye muandishi wa kitabu cha Matendo ya Mitume.

Kuwahubiria injili

"kuhubiri injili kwa watu wa Makedonia"

Acts 16:11

Sentensi unganishi

Msatri wa 13, ni mwanzo wa hadithi ya Lidia. Hii ni hadithi fupi iliyotokea wakati wa kusafiri kwa Paulo

tukaenda

"tukaenda" hii inajumuisha Paulo pamoja na wale waliokuwa naye, hii ni pamoja na Luka ambaye ndiye muandishi wa kitabu cha Matendo ya Mitume.

Somathrake ...Neapoli

Hizi ni miji ya mwambao karibu na Philipi.

Utawala wa Kirumi

ni sehemu ambayo Warumi waliteka na kuishi kwa muda huo, hasa maaskari

Acts 16:14

Sentensi unganishi

Hii ndyo mwishowa hadithi ya Lidia

Mwanamke mmoja aitwaye Lidia

"Kulikuwa na Mwanamke aitwaye Lidia"

muuzaji wa zambarau

"Mfanya biashara aliyeuza nguo za zambarau"

kumuabudu Mungu

Mwenye kumuabudu Mungu ni Mataifa ambaye hutoa sifa kwa Mungu na kumfuata Yeye, lakini hafuati sheria zote za Kiyahudi.

alitusikiliza

"Yeye alitusikiliza"

mambo yaliyozungumzwa na Paulo

"Mambo ambayo paulo aliyasema "

Baada ya kubatizwa yeye na nyumba yake

"walipo mbatiza Lidia na watu wa nyumbani mwake"

Acts 16:16

Sentensi unganishi

Hii ni hadithi nyingi inayotokea wakati wa kusafiri kwa Paulo. Hii ni tukio la kwanza katika hadithi, ni habari ya mbashiri mdogo.

msichana mmoja

"kulikuwa na mwanamke mdogo"

pepo la utambuzi

roho mbaya huongea naye kuhusu habari ya maisha ya watu ya baadaye.

Alimletea bwana wake faida vyingi kwa kubashiri

hii ni habari ya nyuma kuhusu mchana huyo

akiwa amekasirishwa na yeye

"alisumbuliwa na yeye" au " alijisikia vibaya kwa kile kitu anachokifanya"

aligeuka

"Paulo aligeuka nyuma" au " alikwenda kumkabili yule msichana nyuma yake"

akatoka na kumuacha mara moja

"na pepo akatoka mara moja"

Acts 16:19

mabwana zake

wale wanao mmiliki yule msichana mtumwa

tumaini la faida

Hii inamaanisha ule uwezo wa kubashiri aliokuwa nao yule msichana na watu kumlipa kwa kuwabashiria.

kuwaburuza wao

Mabwana waliwaburuza "Paulo na Sila" lakini siyo kundi lote akiwemo Luka na Timotheo.

mbele ya wenye mamlaka

'Katika uwepo wa mamlaka' au 'kuhukumiwa na mamlaka

Walipowafikisha kwa mahakimu, walisema,

"Baada ya mabwana kuwaleta Paulo na Sila mbele ya mahakimu, mabwana wale wakasema"

Wanafundisha

"Paulo na Sila wanafundisha"

siyo ya kisheria

mabwana wanajumuisha mambo ya kitawala katika madai yao kwani wao pia walikuwa raia wa Kirumi

Acts 16:22

mahakimu wakararua nguo zao na kuwavulia

Mahakimu walirarua nguo za Paulo na Sila na kuwavulia"

na kuwaamuru wachapwe na viboka

"Kumuamuru maaskari kumchapa Paulo na Sila kwa viboko"

waliwatupa

"mahakimu waliwaweka Paulo na Sila" au " mahakimu waliwaamuru maasakari kumuweka Paulo na Sila"

na kumuamuru askari wa gereza kuwalinda vema

Askari wa gereza ni mtu anayehusika na wafu wote waliowekwa jela au gerezani. "kumuambi mlinzi wa gereza ahakikishe kuwa hawatoki nje"

kuwafunga

"kuwafungia imara katika sehemu"

nguzo

ni kipande cha mti iliyo na matobo kwa ajili ya kuwekea miguu ya mtu ili imzuiye mtu huyo asiweze kwenda.

Acts 16:25

Sentensi unganishi

Hii ni tukio lingine katika hadithi; inahusu Paulo na Sila gerezani na mlinzi wa gereza

wakiwasikiliza wao

"Neno wao" linamaanisha Paulo na Sila, ambao walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu.

na misingi ya gereza ikatikiswa

"ambayo ilitikisa misingi ya gereza"

minyororo yao ikalegezwa

"minyororo yao waote ilifunguka"

Acts 16:27

ili kujiuwa

Mlinzi wa gereza alichagua kujiuwa kuliko kukabiliana na aina ya mateso yatakayo mpata kwa kuwaruhusu wafungwa kutoroka.

wote tuko mahali hapa

Neno "wote" linajumuisha Paulo, Sila na wafungwa wengine wote.

Acts 16:29

kwa haraka

"aliingi kwa haraka ndani ya gereza"

akawaangukia Paulo na Sila

"Mlinzi wa gereza alijinyenyekesha kwa kuinama mbele ya Paulo na Sila.

na kuwatoa nje

"kuwaongoza nje ya gereza"

Acts 16:32

Sentensi unganishi

wakanena, hapa inamaanisha Paulo na Sila..

nyumbani mwake

Mlinzi wa gereza aliwaleta Paulo na Sila nyumbani kwake"

yeye pamoja na watu wa nyumbani mwake wakabatizwa

"Paulo na Sila walimbatiza Mlinzi wa gereza pamoja na watu wote wa nyumbani kwake"

yeye...naye

Maneno haya yanamaanisha Mlinzi wa gereza

kwasababu wote waliamini

"kwasababu watu wote wa nyumbani kwake waliamini"

Acts 16:35

Sentensi unganishi

Hii ni tukio la mwisho kwenye hadithi. Inahusu Paulo na Sila kuwachiwa kutoka gerezani

ilipokuwa mchana

Hii ni mwanzo wa habari nyingine

walituma ujumbe

"kutuma ujumbe" au Kutuma amri"

waruhu hao wanaume

"waruhusu hao wanaume" au "waruhusu hao wanaume waende"

tokeni nje

"tokeni nje ya gereza"

Acts 16:37

akawaambia

"kusema na walinzi"

Hadharani

"mahakimu walifanya hatharani"

walitupiga , wanaume ambao

Neno "walitupiga", lina maanisha Paulo na Sila

hapana,

Paulo hapa anawajibu mahakimu au wakuu wa mji, japo anaongea na mlinzi wa gereza. " Haitawezekana"

Warumi

Hii ina maana ya wananchi wa kisheria ya Dola. Uraia zunatoa uhuru wa kutoteswa na haki katika kesii. Viongozi wa mji walikuwa na hofu kuwa inaweza kufahamu jinsi viongozi wa jiji walivyo wanyanyasa Paulo na Sila.

wao wenyewe waje

"watawala wa mji waje"

Mahakimu wakaja na kuwasihi

"mahakimu walikuja na kumsihi Paulo na Sila"

baada ya kuwatoa

"baada ya mahakimu kuwaondoa Paulo na Sila"

Acts 16:40

Sentensi unganishi

"Hii ni mwisho wa hadithi ya Paulo na Sila kuwa gerezani"

Taarifa za ujumla

Fungu hili linazungumzia habari a Paulo na Sila pamoja na Waumini wa mji wa Philipi.

Nyumba ya Lidia

"nyumbani kwa Lidia"

walipowaona ndugu

Neno "ndugu" linamaanisha waumini wa jinsi zote. Waliwaona waumini.

Acts 17

Matendo 17 Maelezo kwa jumla

Dhana Maalum katika sura hii

Kutoelewana kuhusu Maasiya

Wayahudi walimtarajia Kristo ama Maasiya awe mfalme mwenye nguvu kwa vile Agano la Kale limesema hivyo mara nyingi. Agano hilo pia lizungumzia wakati ambapo Maasiya angeteseka na hayo ndio Paulo alikuwa akiwaambia Wayahudi. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#christ)

Dini ya Athene

Paulo alisema kwamba watu wa Athene walikuwa watu wa "Kidini" lakini hawakumuabudu Yahweh. Waliiabudu miungu wengi wasio kweli. Hapo awali waliwaleta watu wengi chini ya utawala wao na baadaye wakaanza kuabudu miungu zao. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#falsegod)

Katika sura hii Luka anafafanua kwa mara ya kwanza jinsi Paulo alivyo waambia ujumbe wa Kristo kwa wale hawakufahamu lololete kuhusiana na agano la kale.

<< | >>

Acts 17:1

Sentensi unganishi

Habari kuhusu Paulo na Sila inaendelea pamoja na Timotheo katika safari yao ya kimisionari. Walifika Thesalonike na Luka hakuwa pamoja nao.

Taarifa za jumla

Ni habari kuhusu Paulo na Sila pamoja na Wayahudi katika Sinagogi huko Thesolanike

Sasa

Ni neno linalogawanya habari iliyokuwa ikiendelea kwa kutaja jambo jingine. Luka anaanza kuelezea sehemu mpya ya tukio.

walipopita

"Kusafiri kupitia"

miji ya Amfipoli na Apolonia

Hii ni miji ya mwambao huko Makedonia

walifika mjini

Neno linaloonyesha kuwa walisafiri hadi kufika mjini.

kama ilivyokuwa kawaida

" kama ilivyokuwa kawaida yake" au "Kama alivyofanya siku zote". Mara kwa mara Paulo alikuwa na ya kuingia kwenye Sinagogi siku ya sabato mahali wayahudi walikusanyuka.

kwa sabato tatu

"katika kila siku ya sabato kwa majuma matatu".

alihojiana nao kutoka kwenye maandiko

"alijadiliana na Wayahudi wa Sinagogi" au walijadili na Wayahudi wa Sinagogi"

alihojiana nao

"aliwapa sababu" au "kuhojiana pamoja nao" au "kuzungumza pamoja nao".

Acts 17:3

Alikuwa akifungulia maandiko

Maana inawezekana ni 1) "Paulo alikuwa akieleza maandiko kwa usahihi ili watu waweze kuwa na uwezo wa kuelewa ni nini alikuwa akifundisha" au 2) "Paulo alikuwa akifungua kitabu au kitabu cha maandiko."

ilimpasa

"ilikuwa ni sehemu ya mipango ya Mungu"

kufufuka tena

"kurudi tena katika uhai"

kutoka wa wafu

"kutoka miongoni mwa wafu" anaelezea juu ya roho za watu ambao wamekwisha kufa. Kurudi kutoka miongoni mwao kunamaanisha kurudi katika uzima tena.

Wayahudi walishawishika

"Wayahudi walishawishika " au "Wayahudi walikubali"

na kuungana na Paulo

"na kuwa na ushirika na Paulo"

Wagiriki wacha Mungu

wale wenye kumcha Mungu lakini hawajabadilishwa kuingia dini ya kiyahudi kwa njia ya kutahiriwa.

umati mkubwa

"ni umati mkubwa wa watu"

Acts 17:5

Maelezo ya jumla

Fungu hili linajadili juu ya Wayahudi wasioamini na wanaume wengine waovu kutoka sokoni.

waliojawa na wivu

"Ni hali ya wivu inayoleta msukumo ndani ya mtu" "Kuwa na wivu sana" au "Kuwa na hasira sana"

kwa wivu

Inaelezwa kuwa hawa Wayahudi walikuwa na wivu kwasababu baadhi ya Wayahudi wa Kiyunani wakiuamini ujumbe wa Paulo.

kundi maalumu la wanaume waovu

"baadhi ya wanaume waovu"

kutoka eneo la sokoni

"Kutoka eneo la wazi la mkusanyiko" Ni eneo la wazi la kufanyia biashara ya kuuza na kununua bidhaa, Ng'ombe au eneo la kutolea huduma.

kuusimamisha mji kwa ghasia

Mji kusimamisha kazi zake kutokana na ghasia.

wakaivamia nyumba

"Kuingia kwa vurugu na kuivamia nyumba kwa nguvu" . Hii inawezekana walikuwa wakiirushia mawe nyumba na kutaka kuvunya mlango wa nyumba.

Jason

Hili ni jina la mtu.

kuwaleta mbele za watu

"Kundi la watu Serikalini au kundi la watu raia wa nchi walikusanyika ili kufanya maamuzi"

mbele ya maofisa

"mbele ya Viongozi"

Hawa wanaume walio

Viongozi wa Kiyahudi waliongea wakimaanisha Paulo na Sila kwa kusema "Hawa wanaume"

walioupindua ulimwengu

Hiki Kifungu inawakilisha namna nyingin ya Kusema Paulo na Sila wanasabisha ghasia. Viongozi wa Kiyahudi wanatia chumvi juu ya ushawishi walionao Paulo na Sila katika mafundisho yao.

waliokaribishwa na Yasoni

Hii kifungu inaashiria kuwa Yasoni alikubaliana na mitume waliokuwa wakieneza ujumbe wa machafuko

Acts 17:8

Taarifa za jumla

Fungu hili linazungumzia wale waheshimiwa wa mji huo.

waliingiwa na wasiwasi

"kufadhaika" au "kuwa na mashaka kiakili"

walikuwa wamaukua fedha ya ulinzi kutoka kwa Jason na baadhi ya watu wengine.

Fedha hii ilikuwa ahadi ya mwenendo mzuri, ambayo inaweza kurudishwa kama mambo yote yataenda vizuri, au kutumika kukarabati uharibifu uliosababishwa na mwenendo mbaya. "walipokea dhamana" au "amana" au "faini"

na wengine

"waumii wengine mbali na Yasoni"

Acts 17:10

Taarifa ya Jumla

Hii ni sehemu nyingine ya habari kuhusu Paulo na Sila safarini. Kwa sasa wako Beroya"

ndugu

Neno "ndugu" linamaanisha wanaume na wanawake walioamini"

Hawa watu walikuwa waungwana mno

Ni watu waliokuwa na utayari wa kufikiri kwa hali ya kupokea mawazo mapya zaidi ya watu wengine'.

walipokea neno

"kusikiliza mafundisho"

kwa utayari wa akili zao

"Hao Waberoya walikuwa wamejiandaa kuchunguza mafundisho ya Paulo kulingana na maandiko"

kuchunguza maandiko kila siku

"kusoma kwa umakini na kupima uhalisia wa kifungu cha maandiko kila siku"

mambo haya yaliendelea hivyo.

"Maneno aliyoyasema Paulo yalikuwa ya kweli.

Acts 17:13

Taarifa ya jumla

Athene ni mji uliokuwa chini ya pwani kutoka Beroya ambayo ni Makedonia. Atheni ulikuwa moja ya miji muhimu zaidi katika Uyunani.

walipogundua

"walipoambiwa" au "walipojulishwa" au "waliposikia"

walikwenda huko na kuchochea

Hii inazungumzia kuhusu watu walioshawishwa kama mtu anayechanganya kemikali ili kutoa mlipuko. Waliwaendea na kuwashawishi kutenda isivyo.

kuanzisha ghasia katika umati

"kusababisha hofu na wasiwasi miongoni mwa watu"

Ndugu

Neno "ndugu" linamaanisha wanaume na wanawake walioamini"

waliompeleka Paulo

"Walioambatana na Paulo" au "waliokwenda pamoja na Paulo"

Walipokea kwake maelekezo kuhusu Silas na Timotheo.

"Aliwaambia wawaelekeze Silas na Timotheo"

Acts 17:16

Taarifa ya jumla

Hii ni sehemu nyingine ya hadithi ya Paulo na Sila wakiwa safarini. Paulo kwa sasa yuko Athene akiwangojea Silas na Timotheo kuungana naye.

roho yake iikasirishwa kuona mji umejaa na miungu ya sanamu.

"alisumbuliwa" au "alifadhaika" au "akawa na huzuni"

akajadiliana

Hili neno linaashiria kuwa kulikuwa na majibizano zaidi kutoka kwa wasikilizaji kuliko katika kuhubiri. "alijadiliana"

sokoni

Hii ni sehemu ambayo watu huuza na kununua vitu, ngombe, au huduma hutolewa. " sehemu ya umma"

Wale waliokuwa wakimwabudu Mungu

Inamaanisha Watu wa mataifa waliokuwa wakimsifu Mungu na kumfuata ingawa hawakuwa wakifuata taratibu za ibada ya Kiyahudi.

Acts 17:18

Waepikureo na Wastoiko.

Watu hawa waliamini mambo yote yalifanywa kwa bahati na kwamba miungu walikuwa na shughli zao na walifurahi kutobuguziwa katika kuiongoza ulimwengu. Walikataa ufufuo na walitaka maisha rahisi ya raha pekee.

Wanafalsafa wa Wastoiko

Watu hawa waliamini uhuru unatokana na kujiwekea mwenyewe hatima yako. Walikataa Mungu anayependa binafsi na ufufuo.

wakamkabili yeye

"walimkabii Paulo"

na baadhi wakasema

"na baadhi ya wanafilosofia wakasema"

Ni nini huyu msengeaji

'Babbler' ilitumika kwa kutaja ndege kuokota mbegu kama chakula. Ilihusu ubaya wa wasengenyaji. Wanafalsafa walisema Paulo alikuwa na baadhi ya habari ambazo hazikuwa na thamani ya kusikiliza

wengine wakasema

"Wanafilosopha wengine wakasema"

Inaonekana ni muhubiri

"Inaonekana ni mtu ayetangaza " au "anaonekana yuko katika umisheni wa kusambaza habari'

Acts 17:19

Wakamchukua

Wanafalsafa wa Waepikureo na Wastoike walimchukua Paulo"

na kumleta Areopago

kilima katika Athene juu ambayo mahakama kuu ya Waethene ambapo huenda walikutana.

Twaweza kujua haya mafundisho mapya unayoyaongea

"Twaweza" hapa inamaanisha mafilosopha peke yao. "'Tunataka kufanya uamuzi juu ya mambo haya unayodai "

wote wa Athene

"Wananchi wa Athene" ni watu kutoka Athene, mji karibu na pwani katika Makedonia (sasa ni Ugiriki)

na wageni

"Mtu mgeni" au "mtu mpya katika jamii ya Athene"

hutumia muda wao kwaq hasara

"walitumia muda wao "au "hutumia muda wao"

kuongea na kusikiliza juu ya jambo jipya

"Kujadili mawazo mapya ya falsafa" au "kuzungumza juu jambo jipya kwao'

Acts 17:22

Taarifa ya Jumla

Paulo alianza mahubiri yake kwa wanafilosofia wa Areopago.

weny dini hasa katika kila namna

Paulo alikuwa akirejea jinsi Waathene wanavyoonyesha hadharani kuheshimu miungu kwa sala, kujenga madhabahu na kutoa dhabihu

kwani nilipokuwa nikipita

"kwasababu nilipotembea na kupita"

KWA MUNGU ASIYEJULIKANA

Inaweza ikawa na maana zifuatazo 1) "mungu fulani asiyejulikana" au 2)"kwa mungu yeyote tusiyemjua

Acts 17:24

Dunia

Kwa hali ya ujumla "dunia" inamaanisha mbingu na ardhi na kila kitu kilichoko ndani yake.

kuwa Yeye ni Bwana

"Yeye" inarejea yule Mungu asiyefahamika ambaye Paulo anawaelezea kuwa ni Bwana Mungu. "kwasababu ni Mungu"

yaliyojengwa na mikono

"kupitia matendo ya watu"

hatumikiwi na mikono ya wanadamu

"Kutumikiwa" ni ile hali ambayo Daktari anapomhudumia mgonjwa ili apone. "kujali kwa"

Kwa mikono ya watu

"kwa mikono ya wanadamu"

Kwani Yeye

"kwasababu Yeye mwenyewe"

Acts 17:26

mtu mmoja

Inaweza kuwa na maana zifuatazo .1) "ni Adamu ambaye Mungu alimuumba" au 2) "Inaweza ikajumuisha Adamu na Hawa ambao Mungu aliwaumba"

alifanya Mataifa

"Mungu,muumbaji, alifanya mataifa yote"

yote ...wao

Hapa inamanisha watu wote waishio juu ya uso wa dunia.

kwahiyo

neno hili ni alama ya kauli kwamba alisema kwasababu ya kile ambacho alisema hapo awali.

kumtafuta Mungu japo hayuko mbali nao

"Kumtafuta Mungu"

wamfikie

"kuona haja ya Yeye"

hayuko mbali

Paulo anasema kinyume ya kile anachozungumza ili kusisitiza jambo. " Yeye yuko karibu sana"

na kila mmoja wetu

Paulo anajiweka mwenyewe, wasikilizaji wake na kila taifa alipotumia neno "kila mmoja wetu"

Acts 17:28

Kwake

"Kwa Mungu"

Tunaishi na Kutembea

Paulo anajumuisha wasikilizaji wake na yeye mwenyewe.

tu wazaliwa wake

Hapa 'tu wazaliwa wake' ni wazaliwa ambao wanaweza kuwa si watoto wa sasa. Wao kushiriki baadhi ya sifa pamoja na babu zao. 'Wake' ni kiwakilishi kisichojulikana katika nukuu hii.

kuwa uungu

Hapa "uungu" inarejea hali ya Mungu au sifa zake.

Acts 17:30

Taarifa unganishi

Paulo alimaliza mazungumzo yake na wanafilosofia wa Areopago, aliyokuwa ameianza.

Kwahiyo

neno hili ni alama ya kauli kwamba alisema kwasababu ya kile ambacho alisema hapo awali

Mungu hakuzijari nyakati za ujinga

Inaweza kuwa na maana zifuatazo 1) "kwamba hawajui kuhusu kitu chochote" au 2) " kumkataa kwa makusudi"

Wakati atakapo wahukumu walimwengu kwa haki kwa njia ya mtu aliyemchagua

hapa, neno "walimwengu" inarejea watu waishio duniani.

kwa mtu ambaye alimchagua

"kwa mtu ambaye Mungu alimchagua"

Mungu alitoa uhakika wa mtu huyu

"Mungu alionyesha uchaguzi Wake kwa mtu huyu"

Acts 17:32

Taarifa unganishi

Hii ni sehemu ya mwisho wa hadithi kuhusu Paulo akiwa huko Athene

na watu wa Athene

Wale watu waliokuwepo pale Areopago wakimsikiliza Paulo

baadhi yao wakamdhihaki Paulo

Wale hawakuamini kuwa inawezekana kwa mtu yeyote kufa na kurudi tena kwenye maisha. "Baadhi walimdharau" au "baadhi walimcheka Paulo"

Sisi tutakusikiliza

"sisi" inarejea watu wa Athene ambao walitaka kumsikiliza Paulo. Waliongea moja kwa moja kwa Paulo lakini si pamoja Paul katika kundi lao."

Dionisio Mwareopago, na Mwanamke anaitwa Damari

Dionysius ni jina la mtu. Areopago ina maana kwamba Dionysius alikuwa mmoja wa majaji katika Areopago.

Acts 18

Matendo 18 Maelezo kwa ujumla

Dhana maalum katika sura hii

Ubatizo wa Yohana

Wayahudi wengine walioishi mbali kutoka Yerusalemu na Judea walisikia kumhusu Yohane Mbatizaji na wakafuata mafundisho yake. Walikuwa bado kusikia habari za Yesu. Mmoja wa hao aliitwa Apollo. Alimfuata Yohane Mbatizaji lakini hakufahamu kwamba Maasiya alikuwa aliisha kuja. Yohane aliwabatiza watu kuonyesha ya kwamba walitubu dhambi zao na lakini ubatizo huu ulikuwa tofauti na ubatizo wa Kikristo. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faithful and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#christ and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#repent)

<< | >>

Acts 18:1

Taarifa ya jumla

Hii ni sehemu nyingine ya hadithi ya safari ya Paulo. Kwa sasa yuko Corintho. Akwila na Priskila wanatambulishwa kwenye hadithi katika mstari 2 na 3 inatoa habari ya nyuma kuhusu wao.

baada ya mambo hayo,

"baada ya matukio hayo kufanyika huko Athene"

Huko akampata

Inaweza kuwa na maana kwamba: 1) "Paulo alitokea kumpata kwa bahati" au 2) "Paulo alimpata baada ya kuwatafuta kwa nia.'

Mtu mmoja aliyeitwa Akwira

Hapa anamtaja mtu yule aliyemwona huko naye ni Akwira.

mzaliwa wa Ponto

Ponto ilikuwa mkoa katika pwani ya kusini ya Bahari ya Nyeusi.

alikuwa amehamia karibuni

"Hii huenda ni muda fulani kwa miaka ya nyuma"

Italia

Jina hili ni la nchi. Roma ni mji mkuu wa Italia.

Klaudia alikuwa ameagiza

Klaudia alikuwa ndiye Kaisari wa Kiroma kwa sasa.

Alikuwa akifanya biashara waliyoifanya

Alikuwa akifanya aina ya kazi waliyoifaya na wao.

Acts 18:4

Taarifa ya jumla

Sila na Timotheo walioungana na Paulo

Kwahiyo Paulo akajadiliana

Hapa "kujadiliana" inamaanisha Paulo alikuwa na maongezi ya pande mbili". "kwa hiyo walijadiliana"

Aliwashawishi

"aliendelea kujaribu kuwashawishi"

Paulo alisukumwa na Roho

Paulo alizidi kusukumwa na Roho.

akakung'uta vazi lake

Hii ni hatua ya mfano zinaonyesha kwamba Paulo alikata mahusiano na Wayahudi wasioamini na kuwaacha kwa hukumu ya Mungu.

Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu wenyewe

Hapa "damu" inalinganishwa na adhabu ya dhambi. Paulo anawaambia Wayahudi hao kuwa watawajibika kwa ajili ya hukumu watakayokabiliana nao kwa sababu ya ukaidi wa kukataa kutubu. "Ninyi peke yenu mtabeba jukumu la adhabu yenu kwa ajili ya dhambi zenu".

Acts 18:7

Kauli ya jumla

maelezo ya fungu hili yanazungumzia habari za Tito Yusta na Krispas

Tito Yusto...Krispo

Ni majina ya wanaume

alimwabudu Mungu

Ni mwabudu Mungu wa kimataifa ambaye alimtukuza Mungu na kumfuata, lakini si kwa njia ya kushika sheria za Kiyahudi.

Kiongozi wa sinagogi

ni mtu wa kawaida ambaye hufadhili na kuhudumia sinagogi, na si lazima awe mwalimu.

na watu wa nyumbani mwake

"watu walioishi na yeye ikiwa ni pamoja na ndugu na jamaa zake"

Watu wengi wa Korintho walibatizwa

"Watu wengi wa Korintho ambao siyo Wayahudi" walibatizwa

Acts 18:9

usiogope, lakini ongea na usinyamaze

Bwana anatoa amri moja katika njia mbili tofauti -"usiwe na hofu" na "Sema na wala usinyamaze"'-kufanya maneno yake kuwa na nguvu. "N lazima kuacha kuwa na hofu, na badala yake endelea kusema na usikae kimya.'

Ongea na usinyamaze

Mungu anamuamuru Paulo kwa nguvu aongee. " Hakika ni lazima uongee"

usinyamaze

"usinyamaze kuongelea kuhusu injili"

kwani Mimi niko pamoja nawe

"Mimi" inamaanisha Bwana, ambaye anaongea na Paulo.

Niko nawe

"nawe" inamaanisha Paulo , ambaye Bwana anaongea naye kwa njia ya maono.

nina watu wengi katika mji huu

"Kuna watu wengi katika mji huu walioweka imani yao kwangu"

Paulo akakaa huko...,akifundisha neno la Mungu miongoni mwao.

Hii ni kauli ya kumalizia kwa sehemu hii ya hadithi.

Acts 18:12

Taarifa ya jumla

Hili ni tukio jipya katika hadithi. Paulo aliletwa kwenye kiti cha hukumu mbele ya Galio.

Galio alipofanywa mtawala wa Akaya

Akaya ilikuwa jimbo la Roma ambao Korintho ilikuwa sehemu yake ambayo sasa inafahamika kama kusini mwa Ugiriki.

kumleta yeye mbele ya kiti cha hukumu

Wayahudi walimshika Paulo kwa nguvu na kumleta Paulo mbele ya mahakama. "walimpeleka ili akahukumiwe na mtawala"

Acts 18:14

Galio akasema

Galio alikuwa gavana wa Kirumi wa Mkoa.

sheria zenu

Hayo yalikuwa ni sheria ya Musa na desturi nyingine za kiyahudi wakati wa Paulo

Mimi sitamani kuwa hakimu kwa habari ya mambo hayo

Mimi nakataa kufanya hukumu kuhusiana na mambo hayo"

Acts 18:16

Taarifa za jumla

Fungu linaelezea watu wamataifa mbele ya baraza. Waliitikia kinyume cha wayahudi waliokuwa wamemleta Paulo mbele ya kiti cha hukumu.

Galio aliwafanya wote waondoke mbele ya kiti cha hukumu

Galio aliwaaga waondoke mbele yake na kiti chake cha hukumu.

wote wakamkamata

Hali hii ya kutia chumvi ni kusisitiza hisia kali watu waliyokuwa nayo . "watu wengi walimkamata" au "wengi wao walimshika"

Hivyo walimkamata Sosthene, kiongozi wa sinagogi, na kumpiga mbele ya kiti cha hukumu.

Inamaanisha 1)"Watu wa Mataifa walimpiga Sosthene mbele ya kiti cha hukumu kwasababu alikuwa kiongozi wa Kiyahudi. Au 2) Sosthene alikuwa Myahudi Mkristo hivyo wayahudi walipandwa na hasira juu ya imani yake na kumwadhibu mbele ya kiti cha hukumu.

wakampiga

Sosthene ilipigwa mwili wake ."kupigwa" au "kuumizwa".

Acts 18:18

Sentensi Unganishi

Huu ni mwendelezo wa safari ya kimisionari ya Paulo, pamoja na Priskila na Akwila waliondoka Korintho.

Taarifa ya jumla

Kenkrea ulikuwa ni bandari katika sehemu ya mji mkuu wa Korintho.

Ndugu

Neno "ndugu" linamaanisha wanaume na wanawake walioamini

kwenda Syria kwa meli pamoja na Priskila na Akila

Paulo alipanda kwenye meli iliyokuwa inaenda Syria . Priskila na Akwila walienda pamoja naye.

Alikuwa amenyoa kichwa chake

Hii ni alama ya mfano wa tendo lililodhihirisha nadhiri kamilifu.

kujadiliana na

" kujadiliana pamoja" au "kujadiliana"

Acts 18:20

Taarifa ya jumla

Hapa wanatambulishwa Wayahudi waliokuwa wakiishi mji wa Efeso

Kuwaaga na kuondoka

"kuwaambia kwaherini"

Acts 18:22

Sentensi unganishi

Paulo anaendelea na safari yake ya kimisionari.

Taarifa ya jumla.

Frigia ulikuwa ni jimbo katika Adsia ambao kwa sasa ni Uturuki.

alipotua Kaisaria

"alifika Kaisaria kwa njia ya Meli"

alipanda kwenda

"Paulo alisafiri kwenda mji wa Yerusalemu" Kupanda kwenda juu kwa vile Yerusalimu ulikuwa nyanda za juu zaidi ya Kaisaria.

Kusalimia Kanisa la Yerusalemu

"kuwasalimia washirika wa kanisa laYerusalemu"

Akashuka kwenda

Alishuka kwenda Antiokia kwa vile Antiokia ulikuwa mji uliochini ya bonde zaidi ya Yerusalemu.

Paulo aliondoka

"Paulo alikwenda zake" au "Paulo aliondoka"

Baada ya kukaa pamoja nao kwa muda fulani.

Unazungumziwa muda alioutumia kukaa nao kabla mtu hajaanza safari nyingine.

Acts 18:24

Sentensi unganishi

Luka anaelezea kile kilichotokea katika Mji wa Efeso wakiwa na Prisila na Akwira

Taarifa ya Jumla

Apolo anatambulishwa kwenye hadithi. Mistari ya 24 na 25 inatoa habari kumuhusu yeye.

Mmoja wa Wayahudi aitwaye Apolo

Hapa Luka anaanza kuelezea habari ya mtu mpya.

Mzaliwa wa Alexandra

"Mtu ambaye alizaliwa katika mji wa Alexandria". Hii inaweza kuwa ni miji ya 1) "Alexandria huko Misiri katika mwambao wa kaskasini. " au 2) Alexandra huko Asia katika mwambao wa magharibi."

ufasaha katika kuongea

"mwongeaji mzuri"

mwenye uwezo katika maandiko

"Alikuwa anayafahamu vema maandiko. Alikuwa anauelewa mzuri wa maandiko ya Agano la Kale.

Apolo alikuwa ameelimishwa vema katika mafundisho ya Bwana.

"Baadhi ya waumini walikuwa wamemfundisha Apolo namna Bwana Yesu alivyokuwa anataka watu wapate kuishi.

Alikuwa na bidii katika roho

Neno "roho" linamtambulisha Apolo kama mtu aliyekuwa mwenye nia thabiti ya roho.

ubatizo wa Yohana

"Ubatizo ambao Yohana alifanya" Huu ni ulinganisho wa ubatizo wa Yohana ambao ulikuwa wa maji na ubatizo wa Yesu ambao ulikuwa wa Roho Mtakatifu.

njia za Mungu

Namna vile anawataka watu waishi.

kwa usahihi

"kwa undani zaidi "

Acts 18:27

Taarifa ya jumla

Akaya lilikuwa jimbo katika sehemu ya Kusini mwa Ugiriki kwa sasa

Kupitia katika Akaya

"Kwenda kupitia katika Mkoa wa Akaya"

Ndugu

Neno "ndugu" hapa linamaanisha wanaume na wanawake walioamini.

kawaandikia wanafunzi

"kuandka barua kwa Wakiristo walioko Akaya"

Wale walioamini kwa neema

"Wale waliokuwa wameamini wokovu wa Yesu wa neema"

Appolo aliwashinda Wayahudi hadharani

Appolo aliwashinda Wayahudi mbele ya watu wengine kwa hoja zake.

Kwa uwezo na ujuzi wake

"Kwa nguvu ya ushindani wa hoja zake na ujuzi wake wa kuongea"

Acts 19

Matendo 19 Maelezo kwa ujumla

Dhana maalum katika sura hii

Ubatizo

Yohane aliwabatiza watu kuwashiria kwamba walikuwa wanatubu dhambi zao. Wafuasi wa Yesu waliwabatiza watu waliotaka kumfuata Yesu.

Hekalu la Diana

Hekalu la Diana lilikuwa na umuhimu kubwa katika jiji la Efeso. Watu wengi walienda Efeso kuliona hili hekalu, na wakanunua sanamu za Diana, mungu we kike, wakati walipokuwa pale. Watu waliouza sanamu hizi za Diana walihofia kwamba watu wasingeamini kwamba Diana ni mungu wa ukweli, wangeacha kununua sanamu kutoka kwa wauzaji.

<< | >>

Acts 19:1

Sentensi unganishi

Paulo anasafiri kwenda Efeso

Taarifa ya jumla

"Nyanda za juu za nchi" lilikuwa ni eneo la Asia ambalo kwa sasa ni Uturuki kaskazini ya Efeso. Paulo alilazimika kusafiri kwa nchi kavu kuzunguka pembezoni mwa bahari ili kuweza kufika Efeso ambao pia ni Uturuki ya sasa.

Ikawa kwamba

Huu ni mwanzo wa habari mpya.

Kupita katikati

"Kusafiri kupitia"

kumpokea Roho Mtakatifu

Hii inamaanisha kuwa na Roho Mtakatifu aliyekuja juu yao.

Hatukuwahi hata kusikia kuhusu Roho Mtakatifu

Sisi hatukusikia kuhusu Roho Mtakatifu

Acts 19:3

Taarifa ya jumla

Paulo anaendeleza mjadala wake pamoja na waumini wapya huko Efeso.

mlibatizwa katika nini?

"Ubatizo wa aina gani mliobatizwa?"

Katika Ubatizo wa Yohana

"Tuliupokea ubatizo kupitia mafundisho aliyokuwa akifundisha Yohana"

Ubatizo wa toba

"Ubatizo ambao watu waliuomba wakati walipotaka kugeuka kutaka kutubu dhambi zao

yule ambaye angekuja

Hapa neno "Yule" linamaanisha Yesu.

kuja baada yake

Hii inamaanisha angekuja baada ya Yohana Mbatizaji.

Acts 19:5

Sentensi unganishi

Paulo anaendelea kuishi huko Efeso

Wakati watu

"Watu" hapa inahusu waumini wa Efeso wakizungumza na Paulo.

Wakabatizwa

Wakapokea ubatizo

Kwa jina la Bwana Yesu

Hapa "Jina" linamaanisha nguvu na mamlaka ya Yesu.

akaweka mikono yake

Akaweka mikono yake juu ya vichwa vyao wakati akiomba'

walinena kwa lugha nyingine, na kutabiri

hakuna maelezo ya ambao wanaweza kuelewa ujumbe wao

Katika yote walikuwa watu wapatao kumi na wawili

Hii ni taarifa za msingi kuhusu wanaume ambao walikuwa wamebatizwa

Acts 19:8

Paulo alikwenda katika sinagogi akasema kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu

Paul mara kwa mara alihudhuria mikutano katika sinagogi kwa miezi mitatu na kusema nao kwa ujasiri

kuwavuta watu

kujaribu kuwashawishi watu kwa ujumbe wa kweli.

kuhusiana na ufalme wa Mungu

Hapa neno "Ufalme" linasimamia uongozi wa Mungu kama Mfalme.

Baadhi ya Wayahudi wengine walikuwa wagumu

Baadhi ya Wayahudi wakaidi walikataa kukubali ujumbe

Kuongea mabaya

Kuongea mambo mabaya

njia ya kristo

wokovu kupitia Yesu Kristo

katika ukumbi wa Tirano

Katika ukumbi mkubwa mahali Tirano alipokuwa akifundishia watu.

Tirano

Hili ni jina la mtu mwanaume

wote waliokuwa wanaishi Asia walisikia

Inaweza kuwa na maana ya 1) 'Paul alishirikisha injili kwa watu wengi katika Asia' au 2) 'Ujumbe wa Paulo uliwafikia wote wa Asia kutoka Efeso kutoka hadi Asia yote.

Neno la Bwana

Hapa "neno" linasimama kwa ujumbe. Ujumbe kuhusu Bwana Yesu.

Acts 19:11

Taarifa ya jumla

Fungu hili linazungumzia juu ya wale waliokuwa wagonjwa.

Mungu alikuwa akitenda makuu kupitia mikono ya Paulo hata waliokuwa wagonjwa waliponywa

Hapa "mikono" linasimamia maisha yote ya Paulo. Mungu alikuwa akimtumia Paulo kutenda miujiza.

walichukua leso na eproni kutoka mwili wa Paulo

Hivi vilikuwa vitambaa ambavyo Paulo alivivaa ama kuvitumia. Walipovigusa vitambaa amabvyo Paulo alivivaa wakati wa huduma.

Acts 19:13

Taarifa ya jumla

Huu ni mwanzo wa tukio jingine lililotokea wakati Paulo akiwa Efeso. Ni kuhusu wapunga mapepo Wayahudi.

Wapunga mapepo

watu ambao hufukuza roho wabaya kutoka kwa watu au maeneo

akilitumia jina la Yesu kwa matumizi yao wenyewe

Ingawa hawakuwa wakimwamini Yesu, walijaribu kutumia jina lake kama moja ya maneno yao ya muujiza

Walinena juu yao walikuwa wapegawa na roho chafu

Walilitaja jina la Yesu kwa roho wachafu zilizokuwa zimewapaa watu

wale waliokuwa na pepo wabaya

wale waliokuwa wakiongozwa na roho wabaya

Kwa Yesu anayehubiriwa na Paulo

"Yesu" lilikuwa ni jina la kawaida wakati ule, hivyo hao wapunga mapepo waliwataka wato kujua waliyekuwa wakimnena.

kwa Yesu

Hii inasimamia nguvu na mamlaka ya Yesu.

Waliofanya vile walikuwa wana saba wa kuhani wa kiyahudi, Skewa.

Hii ni habari inayojadili habari ya wapunga mapepo.

Skewa

Hili ni jina la mtu mwanaume.

Acts 19:15

Yesu namjua na Paulo namjua

"Namjua Yesu na Paulo" au "Nimesikia kuhusu Yesu na Paulo"

lakini ninyi ni nani?

roho aliuliza swali hili kuwathibitishia wapunga mapepo kuwa wao hawakuwa na mamlaka juu ya roho wachafu.

roho mchafu aliyekuwa ndani ya yule mtu akawarukia.

Hii inamaanisha roho mchafu alimsababisha yule mtu aliyekuwa akiongozwa naye kuwarukia hao wapunga mapepo.

Wapunga pepo

Linaelezea juu ya watu waliokuwa wakitoa roho chafu kutoka kwa watu au eneo fulani.

nao walikimbia .............. uchi

Wapunga mapepo walikimbia na kuacha nguo zao. walikimbia uchi.

Jina la Bwana Yesu liliheshimiwa

Waliliheshimu jina la Yesu ama walilifikiria jina la Bwana Yesu kuwa kuu.

Jina

Hili linasimama kwa nguvu na mamlaka ya Yesu.

Acts 19:18

Sentensi unganishi

Huu ni mwisho wa sehemu ya habari inayowahusu Wayahudi wapunga mapepo.

Wakakusanya vitabu vyao

'Walikusanya vitabu vyao'. Neno "vitabu" linaelezea aina ya magombo yaliyokuwa yakitumika kuendeshea manuizio ya uchawi kutokana na mwelekezo wa maneno yaliyoandikwa humo.

mbele ya macho ya kila mtu

mbele ya kila mtu

thamani yake

"thamani ya vitabu" au "thamani ya yale magombo"

Elfu hamsini

50,000.00

vipande vya fedha

"Kipande cha fedha" ilikuwa takriban mshahara wa siku kwa mfanyakazi wa kawaida

Hivyo Neno la Bwana likaenea kwa upana sana katika njia yenye nguvu

"Kwasababu ya matendo makuu haya, watu wengi zaidi waliusikia ujumbe kuhusu Bwana Yesu."

Acts 19:21

Sentensi unganishi

Paulo anazungumzia kuhusu uamuzi wake wa kwenda Yerusalemu, lakini hajaondoka Efeso bado

Paul anakamilisha huduma katika Efeso.

Paul anakamilisha kazi ambayo Mungu alikuwa amemwagiza kuifanya katika Efeso.

Aliamua katika roho

Inawezekana kuwa na maana ya 1) Paulo aliamua kwa msaada wa Roho Mtakatifu au 2) Paulo alikusudia kutokana na uamzi wa roho yake, ambayo inamaana alifanya uamzi wake.

Akaya

Akaya ilikuwa Jimbo la Rumi mahali ambapo Korintho ilipokuwa. Ulikuwa ni mji kubwa kusini mwa Ugiriki na mji mkuu wa jimbo.

Mimi lazima pia nikaone Rumi

Mimi lazima pia kusafiri kwenda Rumi

Lakini naye akabaki kwa muda huko Asia

Ni kufanywa wazi kwa mistari michache inayofuatia kwamba Paulo alikuwa alibakia Efeso

Acts 19:23

Sentensi unganishi

Luka anaelezea juu ya ghasia ambayo ilizuka wakati Paulo akiwa Efeso.

Taarifa ya jumla

Demetrio ametambulishwa kweny habari hii. Mstari wa 24 umeelezea kumhusu Demetrio

Taarifa ya jumla

Efeso kulikuwa na hekalu kubwa lililojengwa kwa ajili ya mungu mke Diana, Wakati mwingine imetafasiriwa kwa jina la kigiriki "Artemi". Diana alikuwa miungu ya uongo ya kurutubisha uzazi.

kuliinuka mvurugano mkubwa

"Watu walikuwa wamechanganyikiwa kabisa"

njia

Hili lilikuwa ni neno lililotumika kutaja Ukristo.

Sonara fulani aliyekuwa akiitwa Demetrio

Matumizi ya neno "fulani" linamwelezea mtu mpya katika habari.

Mfua fedha

Mtu mjuzi anayefanya kazi ya kufua fedha kufanya visanamu na vito vya thamani.

aitwaye Demetrio

Hili ni jina la mtu mwanaume. Demetrio alikuwa mfua dhahabu katika Efeso aliyekuwa kinyume na Paulo na kanisa la mtaa hapo Efeso.

alizalisha fedha nyingi kwa biashara hiyo

"aAlitengeneza pesa nyingi kutoka kwa watu waliotengeneza visanamu.

Acts 19:26

Sentensi unganishi

Demetrio anaendelea kuzungumza na mafundi

munaona na kusikia kwamba

"Mumekuja kwa kujua na kuelewa kwamba"

kuwageuza watu wengi

Paulo anawazuia watu kuacha kuabudu miungu. Paulo anawashawishi watu kufuata mwelekeo mwingine.

Anawaeleza kuwa hakuna miungu ambayo iliyotengenezwa kwa mikono

Neno hapa "Mikono" linaelelzea hali yote ya mtu. Anamaanisha kuwa Hakuna miungu iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu iliyo ya kweli.

kwamba biashara yetu haitaweza kuhitajika tena.

"Kwamba watu hawataweza tena kuhitaji na kununua miungu kutoka kwetu."

hekalu la mungu mkuu mke diana hataonekana na thamani tena.

Hii inaweza kutafsiriwa kuwa; "watu watafikiri kuwa hakuna faida inayoendelea kuabudu katika hekalu ya mungu mke Diana."

Hata atapoteza umaarufu wake

Umarufu wa Diana utapotea kwa kufikiri habari yake.

ambao wote walio Asia na ulimwengu wa waabuduo

hili linakuzwa ili kuonyesha vile Diana alivyokuwa anapendwa na wengi.

Acts 19:28

Taarifa ya jumla

Habari hii inazungumzia mafundi waliokuwa wakifua visanamu. Kundi jingine ni la wale waliokusanyika kuwasikiliza mafunzi wafua visanamu.

Taarifa ya jumla

Gayo na Aristariko walitoka Makedonia lakini walikuwa wakitenda kazi na Paulo katika Efeso katika wakati wake.

walijawa na hasira

"wakawa na hasira sana"

na wakapiga kelele, wakisema

kelele kwa sauti kubwa, akizungumza

Mji wote ulijawa na taharuki

Watu waliokuwemo katika mji wote wakaingiwa na taharuki na kuanza kupiga kelele.

watu wakakimbia kwa pamoja

Kulikuwa na hamasisho la ghasia kubwa

kwenye ukumbi

Ukumbi wa Efeso ilitumika kwa ajili ya mikutano ya hadhara na kwa ajili ya burudani kama vile michezo na muziki

Washirika walioambatana na Paulo

watu waliokuwa wakisafiri pamoja na Paulo

Gayo na Aristarko

Haya ndiyo majina ya watu wanaume

Acts 19:30

Taarifa ya jumla

Efeso ilikuwa sehemu ya utawala wa Rumi katika jimbo la Asia.

kuingia kwenye ukumbi

Ukumbi wa Efeso ulitumika katika mikutano ya wazi na kwa matamasha ya michezo na muziki. Ulikuwa ni ukimbi inje ya mji wenye nusu mduara ukiwa na viti vyenye kubeba watu maelfu.

Acts 19:33

Alexazanda

Hili ni jina la mtu mwanamme

akawapungia mkono ili kuelezea

kutigisha mkono akitoa ishara kwa watazamaji ili wanyamaze na aweze kutoa maelezo.

kufanya maelezo

Alitaka kutoa hotuba, lakini sio wazi nini alichokuwa anakwenda kusema.

bila ya sauti

Kupaza sauti ya watu wote kwa wakati mmoja ilionekana kama sauti moja ikinena.

Acts 19:35

Sentensi jumuishi

Karani wa mji anaongea ili kuunyamazisha umati wa watu

Karani wa Mji

Hii inafafanua juu ya "Karani" au "Mwandishi"

Je, kuna yeyote ambaye hajui kuwa mji wa Efeso ni hekalu mlinzi wa Diana mkuu na ya sanamu iliyoanguka kutoka mbinguni

karani aliuliza swali hili kuwahakikishia umati kuwa walikuwa sahihi na kuwatia moyo.

Nani asiyejua

Karani wa mji anatumia neno "asiye" ili kusisitiza kuwa watu wote wa mji wanajua hili.

Mlinzi wa hekalu

Watu wa Efeso wanatunza na kulinda hekalu la Atemi

sanamu iliyoanguka kutoka mbinguni

Ndani ya hekalu la Diana kulikuwa mfano wa mungu fasheni iliyoanguka kutoka angani, kulikuwa mwamba uliofikiriwa kutoka Zeus

Acts 19:38

Sentensi unganishi

karani wa mji alimaliza kizungumza na umati

Kwa sababu hiyo

Hili neno linaashiria kuwa Karani alisema kwa sababu ya kile ambacho alisema hapo awali. Karani wa mji alikuwa amesema, Gayo na Aristariko alikuwa walikuwa si wezi wala wenye kufuru.

wanamashitaka dhidi ya mtu yetote

Nono "shitaka" na "tuhumu" ni vitendo dhidi ya wengine.

Liwali

Huyu alikuwa ni gavana, mwakilishi wa mambo ya kisheria katika mahakama.

Acha washitakiane wao kwa wao

Hili halimaanishi Demetrio na wale waliokuwa naye watashitakiana wao kwa wao. Hili lilikuwa eneo ambalo kila mtu alikuwa huru kutoa shitaka kwa mtu yeyote.

Lakini kama wewe ukitafuta chochote kuhusu mambo mengine

"Lakini kama kuna matatizo vema kuongea"

yatashughurikiwa katika kikao halali.

"Vema kujadili na kutatua tatizo kwa utaratibu wa kawaida"

katika hatari ya kutuhumiwa kuhusu ghasia siku hii.

"Hii inaweza kusababisha hatari kwa mamlaka ya Rumi tukituhumiwa kuanzisha ghasia kama hii ya leo"

Acts 20

Matendo 20 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Katika sura hii Luka anafafanua safari ya mwisho ya Paulo kwa waumini walioko katika mikoa ya Makedonia na Asia kabla ya Paulo kurudi Yerusalemu.

Dhana maalum katika sura hii

Kupiga mbio

Paulo alifananisha maisha ndani ya Yesu kan kwamba alikuwa kwa mashindano ya kupiga mbio. Alimaanisha kwamba alihitaji kuendelea kufanya bidii sana hata kama mambo hayakumwendea vyema mpaka akataka kuachia njiani. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#discipline)

"Kulazimishwa na Roho"

Paulo alifikiri kwamba Roho Mtakatifu alimhitaji aende Yerusalemu hata kama yeye hakutaka. Huyo Roho Mtakatifu pia aliwaambia watu wengine kwamba Paulo atakapofika Yerusalemu watu watajaribu kumdhuru.

<< | >>

Acts 20:1

Taarifa unganishi

Paulo anaondoka Efeso anaendelea safari zake

baada ya ghasia

"Baada ya ghasia" au "kufuatia ghasia"

Aliwaaga

"alisema kwaheri."

aliwatia moyo waumini sana

"Kwa hali ya dhati aliwatia moyo waumini" au "Alisema mambo mengi ya kuwatia moyo waumini"

Baada ya kuishi miezi mitatu huko

yeye alikaa miezi mitatu huko

njama iliandaliwa dhidi yake na Wayahudi

"Wayahudi waliandaa njama dhidi yake"

wakati alipokuwa karibu kusafiri kwa meli kuelekea Syria

alikua tayari kusafiri kwa meli kwenda Syria

Acts 20:4

Taarifa ya jumla

Luka mwandishi wa Matendo ya Mitume, alikuwa ameungana na timu ya Paulo. Hapa anatumia maneno ya wingi akimtaja Paulo akiwamo na yeye.

kuandamana naye

Kusafiri pamoja na Paul

Sopatro ... Trofimo

Haya ndiyo majina ya watu wanaume

Berea ... Derbe ... Troa

Haya ndiyo majina ya maeneo waliyopitia

Aristarko ... Gayo

Haya ni majina ya watu wanaume

Watu hawa walikuwa wamekwenda mbele yetu

"hawa watu walikuwa wamesafiri mbele yetu"

siku za mikate isiyotiwa chachu

Hii inaelezea juu ya wakati wa sikukuu ya Wayahudi. Kipindi cha Pasaka.

Acts 20:7

Taarifa unganishi

Luka anaelezea huduma ya Paulo ya mahubiri huko Troa na kile kilichotokea juu ya Eutiko

Taarifa ya jumla

Luka bado anaelezea kuwa walikuwa pamoja katika safari hiyo.

kumega mkate

Mkate kilikuwa ni chakula cha kawaida wakati wa saa ya chakula. Kumega mkata hapa, inaweza kuwa walishiriki chakula saa ya chakula.

aliendelea kunena

aliendelea kutoa ujumbe

Chumba cha juu

Hii inaweza kuwa chumba cha juu ghorofa ya tatu.

Acts 20:9

Taarifa ya jumla

Habari hii inazungumzia juu ya Paulo na Eutiko.

katika dirisha

Hii ilikuwa sehemu ya uwazi katika kona ya ukuta wa chumba cha juu. Upana wake ulitosha mtu kuweza kuketi pale.

Eutiko

Hili ni jina la mtu mwanaume

aliyepatwa na usingizi mzito

Hapa inasemea; "Alichoka sana na kupelekea usingizi mzito uliompata"

ghorofa ya tatu na aliokotwa akiwa amekufa

Wakati walipotelemka kwenda kuona hali yake, walimwona akiwa amekwisha kufa.

Ghorofa ya tatu

Hii inamaanisha ghorofa mbili kabla ya tatu inayofuata.

Acts 20:11

Taarifa unganishi

Huu ni mwisho wa sehemu ya hadithi kuhusu mahubiri ya Paulo kule Troa na kuhusu Eutiko

waliumega mkate

Mkate kilikuwa chakula cha kawaida kipindi cha saa ya chakula. Inamaanisha pengine walishiriki chakula kilichokuwa na aina nyingi zaidi ya mkate.

aliondoka

"aliendelea na safari"

Mvulana

Inawezekana kuwa na maana ya; 1) kijana zaidi ya 14, au 2) mtumishi au mtumwa au 3) mvulana kati ya umri wa 9 na 14 miaka.

Acts 20:13

Taarifa unganishi

Paulo na wenzake wakaendelea na safari yao

Taarifa ya jumla

Fungu hili linazungumzia juu ya Luka na wale waliokuwa wakisafiri naye bila Paulo kuwemo kwenye kundi.

Sisi wenyewe tulikwenda

Neno 'wenyewe' linaongeza mkazo na hutenganisha Luka na wasafiri wenzake Paulo, ambaye hakusafiri kwa mashua

tulisafiri kwenda Aso

Aso ni mji uliokuwa chini ya mji wa Behram ya sasa katika Uturuki pwani ya bahari ya Aegean.

yeye mwenyewe alitamani

"yeye mwenyewe" ni kiwakilishi cha jina la Paulo aliyekuwa anatamani

kwenda kwa njia ya bara

Kusafiri kwa nchi kavu

kwenda Mitylene

Mitylene ni mji katika siku ya leo Mitilini, Uturuki katika pwani ya bahari ya Aegeana.

Acts 20:15

Taarifa ya jumla

Habari hii inaelezea Paulo, Mwandishi Luka na wale waliosafiri pamoja nao.

upande wa pili wa kisiwa

"karibu na kisiwa" au " kuvuka kutoka kwenye kisiwa"

Kisiwa cha Chiosi

Chiosi ni kisiwa katika pwani ya Uturuki kwa sasa katika bahari ya Aegean

tulitia nanga kisiwani cha Samos

"Tuliwasili katika kisiwa cha Samos"

kisiwa cha Samos

Samos ni kisiwa cha kusini ya Chios katika pwani ya bahari ya Aegean kwa sasa ni Uturuki.

mji wa mileto

Mileto ulikuwa ni mji wa bandari magharibi mwa Asia Ndogo karibu ni kwenye chanzo cha mto Meander.

Paulo alikuwa ameamua kusafiri kupitia Efeso

Paulo alisafiri majini kusini zamani mji wa bandari wa Efeso, kusini zaidi ili kufika nchi kavu huko Mileto.

ili kwamba asitumie muda wowote

Hii inamaanisha "muda" kama vile ulikuwa bidhaa ambao mtu angeweza kuutumia.

Acts 20:17

Taarifa unganishi

Paulo anawaita wazee wa kanisa la Efeso na kuanza kuzungumza nao.

kutoka Mileto

Mileto ilikuwa ni mji wenye bandari Magharibi ya Asia ndogo karibu na chanzo cha mto Meander.

Ninyi wenyewe

Paulo hapa anatumia msisitizo kwa kile anachowaambia.

kuweka mguu katika Asia

aliingia mkoa huu wa Asia

jinsi nilivyokuwa kwenu muda wote

Anazungumzia muda alioutumia akiwa kwao.

kwa unyenyekevu wote

'Unyenyekevu' au 'kujishusha hadi chini'

kwa machozi

"machozi" wakati mwingine alijisikia hali ya huzuni na kulia machozi.

kwa Wayahudi

Hii haimaanishi kwa kila Myahudi. Anaelezea juu ya baadhi ya wale waliomtendea mabaya.

Mwajua jinsi ambavyo sikujizuia kutangaza kwenu

" Mnajua jinsi ambavyo sikunyamaza, lakini kila mara niliwahutubia."

kwenda nyumba kwa nyumba

Paulo alifundisha watu kwenye makazi yao binafsi yaani nyumba kwa nyumba.

juu ya toba kwa Mungu na imani katika Bwana wetu Yesu

"toba" na "imani" ni maneno yanayoweza kutafsiriwa kwa vitenzi. Kwamba walipaswa kutubu mbele za Mungu na kuamini katika Bwana Yesu Kristo.

Acts 20:22

nikiwa ninamtii Roho Mtakatifu kuelekea Yerusalemu, nisiyajue mambo ambayo yatanitokea mimi huko,

Hapa anaongelea juu ya Roho Mtakatifu akimshawishi Paulo kwenda Yerusalemu kama vile Roho Mtakatifu alikuwa amemfunga mfano wa mtumwa.

Roho Mtakatifu hunishuhudia mimi

Roho Mtakatifu amewasilisha maonyo haya kwangu

minyororo na mateso ndivyo vinavyoningojea

Mimi nahusika kufungwa jela kwa minyororo na kuteswa katika kifungo.

ili niweze kumaliza mwendo wangu na huduma niliyopokea kutoka kwa Bwana Yesu

Paulo anatumia mfano waq mashindano. Ili kukamilisha kazi ambayo Mungu aliiweka kwa ajili ya yake kuifanya

kuishuhudia injili ya neema ya Mungu

"kuwaambia watu habari njema kuhusu neema ya Mungu. Hii ndiyo huduma ambayo Paulo alikuwa ameipokea kutoka kwa Yesu.

Acts 20:25

Taarifa unganishi

Paulo anazidi kuongea na wazee wa Efeso

Na sasa, tazama, najua

"Na sasa, nisikilizeni kwa makini, kwasababu ninajua"

Mimi najua kuwa ninyi nyote

Mimi najua kuwa ninyi kwa ujumla wenu wote.

miongoni mwao nilikwenda kuwahubiri kuhusu Ufalme

kwenu ambao mimi niliwahubiria ujumbe kuhusu ufalme wa Mungu

hamtaniona uso wangu tena

Neno 'uso' hapa inawakilisha mwili wa Paulo.

Mimi sina hatia katika damu ya mtu yoyote

Siwezi kulaumiwa na mtu yeyote kuwa na hatia mbele za Mungu

mtu yeyote

Hapa inamaanisha nafsi ya kila mmoja wao awe mwanaume au mwanamke.

Kwa maana sikujizuia kuwatangazia

"kwamba sikukaa kimya bila kuwatangazia ujumbe wa kweli.

Acts 20:28

Kwa sababu hiyo

Neno hili ni alama ya kauli inayosema kwa sababu ya kile ambacho nilisema hapo awali. Katika kesi hiyo, inaturudisha nyuma kwa yale yote ambayo Paulo amesema hadi sasa katika hotuba yake kuhusu yeye kuondoka kwao.

juu ya kundi lolote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi. Iweni waangalifu kulichunga kusanyiko la Bwana

Waumini wanafananishwa na kundi la kondoo. Viongozi wamepewa wajibu na Mungu kulilinda kundi la waumini kwa uangalifu mkuu dhidi ya mbwa mwitu.

kusanyiko la Bwana, ambalo alilinunua kwa damu yake mwenyewe

kumwaga "damu" ya Kristo hapa inafananishwa na malipo kwa Mungu kwa ajili ya dhambi zetu.

mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, na wasilihurumie kundi.

Ni picha ya waumini ambao ni kondoo kuanza kufundishwa mafundisho ya uongo yatakayoanza kuwavutana kuwatoa katika kweli ya Mungu

ili kuwavuta wanafunzi wawafuate wao

Mwalimu wa uongo anayeweza kuwavuta waumini kwa mafundisho ya uongo, kwa lengo la kuwaondoa waumini kuwa wanafunzi wa Yesu na kuwafanya kuwa wanafunzi wake.

Acts 20:31

kuwa macho. kumbuka

'kuwa macho na kukumbuka' au 'kuwa macho kama unakumbuka' au 'kuwa macho kwa kukumbuka.'

Kuwa macho

kuwa macho na tahadhari 'au' kuangalia nje" au "kukaa macho"

Kumbuka

"Endelea kukumbuka" au "Tahadhari"

kwa miaka mitatu sikuweza kuacha kuwafundisha... usiku na mchana

Paulo hakufuruliza kuwafundisha kwa miaka mitatu, lakini mara kwa mara katika muda wa miaka mitatu.

Sikuweza kuacha kuwafundisha

Maana inawezekana ni 1) 'sikuweza kuacha kuwaonya au 2) "sikuweza kuacha kuhamasisha kwa marekebisho."

kwa machozi

Hapa "machozi" inaelezea kilio cha Paulo kwasababu ya hisia zake kali juu ya vile alivyojihisi wakati akiwaonya hao watu.

Na sasa mimi nawakabidhi kwa Mungu, na kwa neno la neema yake

Hapa "neno" linasimama juu ya ujumbe. Kwamba namwomba Mungu awalinde na kuwasaidia kuendelea kuuamini ujumbe niliosema nanyi juu ya neema yake.

ambalo laweza kuwajenga

Imani ya mtu kuwa imara ni mfano wa ukuta uliojengwa na kuzidi kuimarishwa zaidi na zaidi.

na kuwapa urithi

Hapa pia anazungumzia neno la neema yake Mungu kana kwamba Mungu mwenyewe alikuwa akiwapa urithi watu wake.

Acts 20:33

Taarifa unganishi

Paulo alimaliza hotuba yake kwa wazee wa Kanisa la Efeso, Ambayo alikuwa akiihutubia

Sikutamani fedha ya mtu.

"Sikuwa na tamaa ya fedha za mtu yeyote" au "Mimi mwenyewe sikuhitaji fedha ya mtu yeyote"

fedha ya mtu, dhahabu, au nguo

Mavazi yalidhaniwa kuwa kama hazina; kwa kadri mtu alivyozidi kuwa navyo, ndivyo alivyodhaniwa kuwa na utajiri.

Ninyi wenyewe

Neno "wenyewe" inatumika hapa kwa kuongeza msisitizo.

nimefanya kazi kwa mikono yangu mwenyewe kutimiza mahitaji yangu.

Neno "mikono" hapa inawakilisha roho yote ya Paulo. 'Mimi nilifanya kazi kwa mikono yangu mwenyewe ya kupata fedha na kulipa kwa ajili ya gharama zangu."

Kufanya kazi kuwasaidia wanyonge

"Fanyeni kazi ilikupata fedha kusaidia watu ambao hawawezi kuzipata kwaajili yao wenyewe"

maneno ya Bwana Yesu,

Hapa "maneno" yanafafanua juu ya Yesu alivyosema.

Ni heri kutoa kuliko kupokea

Mtu hupokea neema ya Mungu na uzoefu wa furaha yake zaidi anapotoa

Acts 20:36

Taarifa unganishi

Paul anamalizia muda na hotuba yake kwa wazee wa kanisa la Efeso na kisha kuomba pamoja nao.

alipiga magoti akaomba pamoja nao

Ilikuwa desturi ya kawaida kupiga magoti wakati wa kuomba. Ilikuwa alama ya unyenyekevu mbele za Mungu.

kumwangukia Paulo shingoni

"Aliwakumbatia kwa karibu" au "kuweka mikono yao karibu naye"

walimbusu

Kumbusu mtu kwenye shavu ni usemi wa kindugu au upendo wa kirafiki katika Mashariki ya Kati.

Kamwe hawatauona uso wake tena

Neno "uso" hapa inawakilisha mwili wa Paulo kimwili. 'hamtaniona katika mwili katika dunia hii.'

Acts 21

Matendo 21 Maelezo kwa Jumla

Muundo na Mpangilio

Matendo 21:1-19 Inaelezea safari ya Paulo kwenda Yerusalemu. Baada ya kuasili Yerusalemu,Waumini walimuambia kwamba Wayahudi walitaka kumdhuru .Walimwelezea pia alichopaswa kufanya ili wasimdhuru (Mistari 20-26). Ingawa Paulo alikifanya alichoambiwa na waumini,Wayahudi walijaribu kumuua. Warumi walimuokoa na wakampa nafasi ya kuwaongelesha Wayahudi.

stari wa Mwisho wa sura hii unaishia na sentensi isiyokamilifu kimaana. Tafsiri nyingi huwacha hiyo sentensi kama haijakamilika kama vile ULB hufanya.

Dhana maalum katika sura hii

"Wote wamejitahidi kuilinda sheria"

Wayahudi wa Yerusalemu walifuata sheria za Musa. Hata wale waliomfuata Yesu bado walizizingatia. Makundi yote yalifikiri kwamba Paulo alikuwa akiwaambia Wayahudi walio Uyunani wasifuate hizo sheria. Lakini watu wa Mataifa ndio Paulo alikuwa akiwahutubia.

Nadhiri za kuwafunga wanaume

Nadhiri ambazo Paulo na marafiki wake watatu walichukua ilikuwa ni kama ya Wanaume wa kujifunga kwa Nadhiri kwa vile walinyoa nywele zao (Matendo 21:32)

Watu wa Mataifa kwa hekalu

Wayahudi walimlaumu Paulo kwa kumleta mtu wa Mataifa katika sehemu maalum ya hekalu ambamo Mungu aliwaruhusu Wayahudi pekee kuingia. Wakafikiri kwamba Mungu alitaka wamuadhibu Paulo kwa kumuua. (Tazama: //en/tw/dict/bible/kt/holy)

Uraia wa Urumi

Warumi walidhani kwamba ni Warumi pekee yao waliostahili kuhudumiwa kwa haki. Wangewatenda watakavyo wale ambao hawakuwa raia wa Urumi lakini kwa Warumi waliwatendea kufuata sheria. Watu wamoja walizaliwa raia wa Roma na wengine wakaipa pesa serikali ya Warumi ili wawe raia.

<< | >>

Acts 21:1

Sentensi unganishi

Mwandishi Luka, Paulo na washirika wake wanaendelea na safari yao.

Taarifa ya jumla

Paulo anatumia kiwakilishi cha jina kwa wingi akijitambulisha yeye, Paulo na wenzao wanaosafiri kwa pamoja.

tukafika moja kwa moja kwenye mji wa Kosi,

"tulikwenda moja kwa moja kwenye mji wa kosi" au "tulikwenda moja kwa moja kwenye mji wa kosi bila kupitia sehemu nyingine"

Mji wa Kosi

Kosi ni kisiwa cha pwani ya Ugiriki pwani kwa sasa ni Uturuki mkoa wa kusini mwa Aegean ya bahari.

Mji wa Rhodes

Rhodes ni kisiwa cha pwani ya Ugiriki kwa sasa ni Uturuki kusini mwa bahari ya Aegeani na kosi pia kaskazini ya Krete

Mji wa Patara

Patara ni mji upande wa kusini magharibi mwa pwani ya Bahari ya Aegean kwa sasa ni Uturuki kuelekea bahari ya Mediterraneani.

Tulipopata meli inayovuka kwenda Foinike

Hapa "Meri kuvuka kupitia" linamaanisha kuwa ni wale watumishi wa meri ambao wangesafiri pamoja na meri.

Meri kuvuka kupitia

Hapa hakumaanishi meri ilikuwa inavuka wakati huo, bali ingevuka baadaye.

Acts 21:3

Taarifa ya jumla

Neno 'sisi' linamhusu Luka, Paulo na wale waliokuwa wakisafiri pamoja nao.

tukaiacha upande wa kushoto

"Tulikipita kisiwa upande wa kushoto"

huko ndiko meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake

Hapa "Meri" inasimama kwa nafasi ya watumishi waliokuwa wakisafiri na meri. Wafanyakazi hao wangeshusha mizigo kutoka merini.

Wanafunzi hawa walimwambia Paulo kupitia Roho

"Waumini hawa walimwambia Paulo kile Roho Mtakatifu alikuwa amekidhihirisha kwao"

kwamba yeye asikanyage Yerusalemu

Hapa "Miguu" linamaanisha Paulo mwenyewe asikanyage huko Yerusalemu.

Acts 21:5

Taarifa ya jumla

Fungu hili linazungumzia waumini huko Tiro

Wakati tulipokuwa tumekaa siku kadhaa

Inaonyesha kuwa kuna muda waliokaa katika mji huo.

tukapiga magoti pwani, tukaomba

likuwa desturi ya kawaida kupiga magoti wakati wa kuomba. Hii ilikuwa ni alama ya kuonyesha unyenyekevu mbele za Mungu.

tukaagana kila mmoja

"Alisema 'kwaheri' kwa kila mmoja

Acts 21:7

Sentensi unganishi

Paulo anaanza rariba yake akiwa Kaisaria

tuliwasili Tolemai

Tolemai ulikuwa ni mji wa kusini mwa Tiro, Lebanoni. Tolemai ya sasa ni Acre, Israeli.

ndugu hawa

"waumini wenzake"

mmoja kati ya saba

"Saba" inahusu wanaume waliochaguliwa kusambaza chakula na misaada kwa wajane.

mtu huyu

"Philipo"

Sasa

Neno hili limetumika kama alama ya kumalizika kwa tukio moja na kuanza kwa tukio jingine. Luka anasimulia habari za Philipo na binti zake.

mabinti wanne mabikira ambao walitabiri

"Mabinti bikra wanne ambao kwa kawaida walikuwa wakipokea na kupeleka ujumbe kwa watu kutoka kwa Mungu.

Acts 21:10

Sentensi unganishi

Fungu hili linazungumzia habari ya unabii ulionenwa kumhusu Paulo katika Kaisaria kutoka kwa nabii Agabo.

nabii mmoja aitwaye Agabo

Hii inamtambulisha mtu mpya katika habari hii.

Agabo

Agabo alikua mtu kutoka Yudea

Kuchukua mkanda wa Paulo

"Aliutwaa mkanda wa Paulo kutoka kiunoni mwake"

na kusema, "Roho Mtakatifu asema hivi," "Wayahudi wa Yerusalemu watamfunga mtu anayemiliki mkanda huu

Alimaanisha kuwa Roho Mtakatifu alimjulisha Nabii Agabo kuwa Wayahudi huko Yerusalemu watamfunga Paulo kama alivyojifunga mkanda wa Paulo na kumkabidhi kwa watu wa mataifa.

Wayahudi

Hii haimanishi Wayahudi wote, lakini baadhi ya watu walifanya hivyo.

kumkabidhi mikononi mwa

"Kumkabidhi kwa"

katika mikono ya wamataifa

Neno "Mikono" Linawakirisha udhibiti.

Wamataifa

Neno hili linasimamia mamlaka miongoni mwa wamataifa.

Acts 21:12

Taarifa ya jumla

Fungu hili linaelezea kumhusu Mwandishi Luka na baadhi ya waumini isipokuwa Paulo.

Mnafanya nini, mnataka kuvunja moyo wangu?

Paulo anauliza swali hili kuonyesha waumini wanapaswa kuacha kujaribu kumshawishi. 'Acheni, mnachofanya mnataka kunivunja moyo wangu.'

Kwa jina la Bwana Yesu

Hapa "jina" linamaanisha utu wa Yesu Kristo.

hakutaka kushawishiwa

Hakuweza kujaribu kumshawishi ili asiende Yerusalemu.

mapenzi ya Bwana yafanyike

Inamaanisha kuwa; lolote lile likitokea litakuwa kwa mpango wa Bwana.

Acts 21:15

Sentensi unganishi

Huu ni mwisho wa kipindi cha Paulo kuwa huko Kaisaria.

Taarifa ya jumla

Neno 'sisi' linamhusu Luka, Paulo na wale waliosafiri pamoja nao.

Pamoja walimleta mtu

"Miongoni mwao alikuwemo mtu mwingine"

Mnasoni, mtu kutoka Kupro

Mnasoni alikuwa mtu kutoka kisiwa cha Kupro.

mwanafunzi wa kwanza

Hii inamaanisha Mnason alikuwa muumini wa Yesu aliyeamini mwanzoni mwa huduma.

Acts 21:17

Sentensi unganishi

Paulo na wenzake sasa wanafika Yerusalemu.

ndugu walitukaribisha

Hawa walikuwa waumini wanaume na wanawake, waliowakaribisha.

alitoa taarifa hatua kwa hatua

"Paulo alitoa maelezo ya kina ya mambo yote ambayo Mungu aliyatenda"

Acts 21:20

Sentensi unganishi

wazee katika Yerusalemu wakaanza kumjibu Paulo.

ndugu

Neno "ndugu" linamaanisha waumini wenzao.

Wameambiwa kuhusu wewe... wasifuate desturi za zamani.

Hapa baadhi ya Wayahudi walikuwa wakifuatilia kuharibu mafundisho ya Paulo aliyokuwa amawafundisha waumini wapya, ili wafuate desturi za Musa badala ya kumfuata Yesu.

Wameambiwa

"Watu waliwaambia waumini wa Kiyahudi"

Acts 21:22

Taarifa ya jumla

Fungu hili limawahusu Yakobo na wazee wengine.

watu wanne ambao waliweka kiapo

Hii ilikuwa ni aina ya kiapo ambapo mtu hakutaka kunywa kileo au kukata nywele zao mpaka mwisho wa kipindi cha kuweka muda. "watu wanne ambao walitoa ahadi kwa Mungu."

Wachukue watu hawa na ujitakase mwenyewe pamoja nao

Walikuwa wanapaswa wao wenyewe kujitakasa ili waweze kuabudu ndani ya hekalu.

na uwalipie gharama zao

Lipa kile ambacho watahitaji kulipiwa.

ili waweze kunyoa vichwa vyao

Hii ni ishara ya mtu anayetimiza nadhili yake kwa Mungu.

mambo waliyoambiwa kuhusu wewe

Mambo ambayo yanasemwa na watu kukuhusu wewe.

Kufuata sheria

Inamaanisha utii wa kuzishika sheria za Mungu.

Acts 21:25

Sentensi unganishi

Yakobo na Wazee katika Yerusalemu wanamaliza maswali yao kwa Paulo.

wanapaswa kujiepusha na vitu vilivyotolewa dhabihu kwa sanamu, na damu, kutokana na kile kilichonyongwa

ote hayo yalikuwa sheria za kile wanachotakiwa kula.

kujiepusha na vitu vilivyotolewa dhabihu kwa sanamu

Wajiepushe kula nyama iliyotolewa kwa ibada za sanamu.

kutokana na kile kilichonyongwa

Mnyama ambaye ameuawa bila damu kutoka.

ibada ya kujitakasa pamoja nao

Kabla ya kuingia Hekaluni Wayahudi walitakiwa kuwa sherehe au tohara. Kusafishwa alikuwa na kufanya na Wayahudi kuwa na mawasiliano na watu wa mataifa mengine.

siku ya kujitakasa

Hii ni hatua tofauti ya kujitakasa ambayo ilitakiwa kuitimiza ili waweze kuingia hekaluni.

mpaka sadaka ilipotolewa

"Mpaka walipowasilisha wanyama kwa sadaka"

Acts 21:27

Sentensi unganishi

Huu ni mwanzo wa sehemu ya hadithi kuhusu kukamatwa kwa Paulo.

Taarifa ya jumla

Mstari wa 29 unaelezea habari kuhusu Wayahudi kutoka Asia.

Siku saba

Hizi zilikuwa siku saba kwa ajili ya kujitakasa.

katika Hekalu

Paulo hakuwa ndani ya hekalu lenyewe. Alikuwa kwenye uwa wa nje wa hekalu.

Makutano wote wakashawishika

"Ilisababisha kundi kubwa la watu kuanzisha upinzani.

na wakamnyoshea mikono

Neno Kumnyoshea mikono" lina maana ya watu kuanza kumvamia.

watu, sheria na mahali

"Watu wa Israel, sheria ya Musa, na hekalu

mwanzoni walikuwa wamemwona...walidhani kwamba Paulo alikuwa ameingia na Myunani hekaluni

Mwandishi Luka anaelezea kwanini wayahudi kutoka Asia walimshitaki Paulo kuwa alimleta Myunani

Trofimu

Huyu alikuwa mwanaume Myunani ambaye Paulo alishitakiwa kuwa aliingia naye hekalu

Acts 21:30

Mji wote ulikuwa na taharuki

Neno "wote" hapa ni lugha ya kuumba picha kubwa kwa msisitizo. neno "mji" inawakilisha watu katika mji huo. "Watu wengi katika mji wakawa na hasira juu ya Paulo."

"Walimvamia Paulo"

Paulo alivamiwa

milango mara ikafungwa

Walifunga milango ili kwamba kusije kufanyika maandamano ndani ya hekalu.

habari zilimfikia mkuu wa kikosi cha ulinzi

afisa wa kikosi cha ulinzi au kiongozi wa askari wapatao 600

Yerusalemu yote ilikuwa katika ghasia

Neno "Yerusalemu" hapa inawakilisha watu wa Yerusalemu. neno "wote" ni msisitizo kuonyesha umati mkubwa waliokuwa wamekasirika. "wengi wa watu huko Yerusalemu walikuwa katika ghasia."

Acts 21:32

aliukimbilia umati chini

Kutoka ngome, kuna ngazi kwenda chini katika mahakama.

mkuu wa kikosi

afisa wa kikosi cha kijeshi cha Rumi au kiongozi wa askari wapatao 600

alimkamata Paulo

"Akamshika Paulo" au "Paulo alishikiriwa"

akaamuru afungwe minyororo

Aliwaagiza askari wake kumkamata na kumfunga.

kwa minyororo miwili

Hii inamaanisha kuwa Paulo alifungwa na maaskari wawili kila mmoja upande wake mmoja.

Akamuuliza yeye ni nani na amefanya nini.

Alimwuliza kuwa yeye ni nani?, Amefanya nini?

Akamuuliza yeye ni nani

Mkuu wa ulinzi anazungumza na umati, hazungumzi na Paulo.

Acts 21:34

Jemadari

Huyu alikuwa ni afisa wa kijeshi au kiongozi wa askari wapatao 600.

aliagiza Paulo aletwe ndani

Aliagiza askari wake wamlete Paulo.

ndani ya ngome

Ngome hii ilikuwa imeunganishwa kwenye uwanda wa nje wa hekalu.

Wakati alipofika kwenye ngazi, walimchukua

'Wakati Paulo alipofika kwenye ngazi za ngome, askari wakamchukua'

Muondoeni huyu

Umati wa watu kwa kutumia lugha kiasi fulani kali na lugha halisi ya kuomba Paulo auwawe.

Acts 21:37

Paulo alipokuwa analetwa

"askari walipokuwa tayari kuleta Paulo"

Ngome

ngome ilikuwa imeunganishwa na uwanda wa nje wa hekalu

mkuu wa kikosi cha ulinzi

afisa wa jeshi la Kirumi wa askari wapatao 600.

Je, unajua Kiyunani? Wewe si yule Mmisri ambaye awali aliongoza uasi na alichukua magaidi elfu nne nyikani?

Mkuu wa jeshi anatumia maswali haya kueleza mshangao kwamba Paulo si yule aliyemdhani kuwa. Nilifikiri kuwa ni yule Mmisri ambaye aliongoza uasi katika jangwa na magaidi elfu nne."

wewe si yule Mmisri

Muda mfupi kabla ya ziara ya Paulo, mtu asiyejulikana jina kutoka Misri, alikuwa akizindua uasi dhidi ya Rumi katika Yerusalemu. Baadaye alitorokea "jangwani," 'na kamanda anashangaa kama Paulo atakuwa ndiye na mtu huyo.

aliongoza uasi

Neno "uasi" linamaanisha watu waliasi na kwenda kinyume na serikali ya Rumi"

magaidi elfu nne

"4000 watu wanaoua na kuwadhuru wengine wale wasiokubaliana nao"

magaidi

Ni wale Wayahudi walioiasi serikali ya Rumi na kuanza kuwauaWarumi na kila mmoja ambaye aliyeunga mkono serikali ya Kirumi.

Acts 21:39

Sentensi unganishi

Paulo anaanza kujitetea kwa kile alichukuwa amefanya

Nakuuliza

"nakuomba" au "nakusihi"

nikubalie

"Tafadhali nikubalie" au tafadhali niruhusu"

Jemadari alikuwa amempa kibali

Neno "kibali" linamaanisha kuwa mkuu wa kikosi alikmpa Paulo kibali cha kuzungumza.

Paulo akasimama penye ngazi

Neno "ngazi" linamaanisha hatua ya juu ya kupanda kuelekea kwenye ngome.

akatoa ishara ya mkono kwa watu

Paulo alitoa ishara ya mkono kwa watu kuashiria wanyamaze

kulipokuwa na ukimywa sana

wakati watu waliponyamaza kabisa

Acts 22

Matendo 22 Maelezo kwa Jumla

Muundo na Mpangilio

Hii ndio mara ya pili kusema habari ya Kubadilishwa kwa Paulo kuwa Mkristo katika kitabu cha Matendo.Kwa sababu hili ni tukio muhimu katika kanisa la awali, "kuna mara tatu ya kusema habari ya kubadilishwa kwa Paulo kuwa Mkristo. (Tazama: Matendo 9 na Matendo 26).

Dhana maalum katika sura hii

Katika lugha ya Kihebrania

Wakati huu Wayahudi wengi walizungumza Kiaramea na Kiyunani. Wengi wa waliozungumza Kihebrania walikuwa Wayahudi watu wa elimu. Hii ndio maana watu walimsikiliza Paulo kwa makini alipoanza kuzungumza kwa Kihebrania.

"The Way"

Hakuna anayefahamu aliyeanza kuwaita Waumini wafuasi wa Njia. Labda Waumini walijiita hivyo kwa vile Bibilia kwa mara nyingi humzungumzia mtu anayeishi maishi yake kama mtu atembeaye njiani. Kama huu ni ukweli, Waumini walikuwa "Wakifuata njia ya Bwana" kwa kuishi kwa njia inayompendeza Mungu.

Uraia wa Urumi

Warumi walidhani Kwmaba ni Warumi pekee yao waliostahili kuhudumiwa kwa haki. Wangewatenda watakavyo wale ambao hawakuwa raia wa Urumi lakini kwa Warumi waliwatendea kufuata sheria. Watu wamoja walizaliwa raia wa Roma na wengine wakalipa pesa serikali ya Warumi ili wawe raia. "Kiranja Mkuu" angeadhibiwa kwa kuwatendea raia wa Urumi sawa wale wasiokuwa raia.

<< | >>

Acts 22:1

Sentensi unganishi

Paulo anazungumza na Wayahudi huko Yerusalemu.

Ndugu na baba zangu

Hii ilikuwa ni njia ya kistaarabu ya kuzungumza na watu ambao walikuwa na umri sawa na wa Paulo, na wanaume wazee waliokuwa katika kusanyiko hilo.

Nitakao ufanya kwenu sasa

"Nitakaoueleza kwenu" au "nitakao uwakilisha kwenu"

Lugha ya kihebrania

"lugha ya Kihebrania ilikuwa lugha ya Wayahudi"

Acts 22:3

nilipata elimu katika mji huu, miguuni pa Gamalieli

alikuwa mwanafunzi wa rabi Gamalieli hapa Yerusalemu "

Gamarieli

Gamarieli alikuwa mwalimu mashuhuri wa sheria ya Kiyahudi.

Nilifundishwa kulingana na njia sahihi ya sheria za baba zetu.

"Aliniagiza jinsi ya kutii kwa makini kila sheria ya baba zetu" au "mafundisho niliyopata yalifuatiwa na maelezo halisi ya sheria ya baba zetu"

Nina bidii kwa Mungu

"Nimejitoa kikamilifu kumtii Mungu" au "Mimi nina hamu kuhusu huduma yangu kwa Mungu"

kama ninyi nyote mlivyo leo

"Kama ilivyo kwenu nyote hivi leo". Paulo anajilinganisha na umati wa watu.

njia hii

Hii ilikuwa ni neno lililotumika kutaja Ukristo

hadi mauti

"mauti" inaweza kutafsiriwa na kitenzi "kuua" au "kufa

na kuwatupa gerezani

"Walitupwa gerezani" au "Kuwaweka gerezani"

kutoa ushahidi

"Kushuhudia" au "kutoa ushahidi"

nilipokea barua kutoka kwao

"Makuhani wakuu na wazee nilipokea barua kutoka kwao"

kwa ajili ya ndugu zetu walioko Dameski

Hapa "ndugu" inahusu "Wayahudi wenzake

Ilikuwa niwalete Yerusalemu watu wa njia ile

"Waliniagiza kuwafunga minyororo wale wote wa njia ile na kuwaleta Yerusalemu

ili waadhibiwe

"ili wapate adhabu" au "ili viongozi wa Wayahudi wangeweza kuwaadhibu"

Acts 22:6

Sentensi unganishi

Paulo anazungumzia namna alivyoweza kukutana na Yesu.

Ikatokea ya kwamba

Msemo huu umetumika hapa kama tukio la kwanza. Hapa Paulo anaelezea jinsi alivyokutana na Yesu.

nikasikia sauti ikiniambia

Hapa "sauti" inasimama kwa mtu akizungumza. "Mimi nilisikia mtu akiniambia"

Acts 22:9

ila hawakuielewa sauti ya yule aliye ongea na mimi

Neno "sauti" linasimama badala ya mtu anayeongea. Hawakuelewa kile yule mtu alichokuwa akiongea nami.

huko utaambiwa

"kuna mtu atakuambia" au "huko utafahamu"

Sikuweza kuona kwa sababu ya mwangaza wa ile nuru

"Niliachwa nikiwa sioni kwasababu ya uli mwanga angavu.

nikaenda Dameski kwa kuongozwa kwa mikono ya wale waliokuwa na mimi

Hapa "mikono" anasimama kwa wale waliomuongoza Paul. Hii inaweza ikaanza: "Watu waliokuwa na mimi waliniongoza kwenda Dameski"

Acts 22:12

Taarifa ya jumla

Fungu hili linazungumzia habari za Anania

Anania

Huyu si Anania aliyekufa mapema mwanzoni mwa sura ya 5:3

mtu mwema kwa mujibu wa sheria

Anania ilikuwa makini sana kuhusu kufuata sheria za Mungu.

aliyenenwa vyema na Wayahudi walioishi kule

"Wayahudi walioishi kule walinema mema juu yake"

ndugu Sauli

Hapa "Ndugu" ni njia ya kistaarabu kumuelezea mtu. "Rafiki yangu Sauli"

pokea kuona

neno "kuona" inaweza kutafsiriwa na kitenzi "kuona." "kuona tena"

muda uleule

Hii ni kawaida kama tukio lilitendeka muda mfupi baada ya kuanza kwa tukio.

Acts 22:14

Sentensi unganishi

Paulo anamalizia kuwaambia kile kilichotokea kwake huko Dameski. Ananukuu kile Anania alisema kwake. Hii ni sehemu ya hotuba ya Paulo aliyoitoa huko Yerusalemu.

mapenzi yake

"kile Mungu anapanga na kinaweza kutokea"

kusikia sauti kutoka mdomoni kwake mwenyewe

Vyote "sauti" na "kinywa" rejea kwa nayezungumza. "kumsikiliza akiongea moja kwa moja kwako"

kwa watu wote

Hapa "watu" maana yake watu wote akiwa mwanamume au mwanamke. "kwa watu wote"

Na sasa

Hapa "sasa" haina maana "wakati huu," lakini linatumika kuleta umakini na hatua muhimu ifuatayo.

ubatizwe

Hii inaweza kuanza: "naomba nikupatize" au "kupokea ubatizo"

Kuoshwa na kuondolewa dhambi zako

kama kuoshwa kwa mwili wa mtu ili kuondoa uchafu, akiliitia jina la Yesu kwa msamaha wa dhambi. Omba msamaha wa dhambi zako.

ukiliitia jina lake

Hapa "jina" ni Bwana Yesu. "wito kwa Bwana" au "kuamini katika Bwana"

Acts 22:17

Sentensi unganishi

Paulo anaanza kwa kuwaambia umati wa watu kuhusu maono yake kwa Yesu.

ikatokea kwamba

Kipengere hiki kinaweka alama ya kuonyesha kuanza kwa tukio.

Nilipewa maono

Hii inaweza ikaanza: "nilikuwa na maono" au "Mungu alinipa maono"

Nilimwona akiniambia

"Nilimwona Yesu akiniambia"

hawataukubali ushuhuda wako kunihusu mimi

"Wale ambao wanaishi Yerusalemu hawataamini kile unachowaambia kunihusu mimi"

Acts 22:19

Sentensi unganishi

Huu ni mwisho wa hotuba ya Paulo kwa umati wa Wayahudi waliokuwa kwenye ngome.

Taarifa ya jumla

Fungu hili linazungumzia Wayahudi wasioamini waliokuwa Yerusalemu

wao wenyewe wanajua

"wao wenyewe" ni msisitizo wa neno katika kiwakilishi cha jina

katika kila sinagogi

Paulo alikwenda kwenye masinagogi akiwatafuta Wayahudi waliokuwa wamemwamini Yesu.

damu ya Stefano ... ilikuwa imemwagika

Msemo huu ulikuwa ni desturi ya kusema mtu aliyeuawa. "walimwua Stephen."

Acts 22:22

Mwondoeni mtu huyu katika nchi

Neno "nchi" yanaongeza mkazo "Mwondoeni." : "Mwueni"

Na walivyokuwa

Neno "Walipokuwa" limetimika kwa alama matukio mawili ambayo yanatokea wakati huo huo.

na kutupa mavazi yao na kutupa mavumbi juu

Tukio hili linaonyesha Wayahudi walikuwa wamekasirika kwasababu walijisikia kuwa Paulo alikuwa amenena kinyume cha Mungu.

akaamuru Paulo aletwe

Hii inamaanisha "aliwaamuru askari wake ili kumleta Paulo"

ngome

ilikuwa imeungana na uwanda wa nje wa hekalu

Akaamuru aulizwe huku anapigwa mijeledi

Kamanda alitaka Paul kuteswa kwa kuchapwa viboko ili kuhakikisha anasema ukweli.

Acts 22:25

Taarifa ya jumla

Fungu hili linazungumzia juu ya askari.

Kamba

Hizi zilikuwa na nyuzi nyuzi za ngozi au mnyama.

Je, ni halali kwenu kumpiga viboko mtu ambaye ni raia wa Rumi na hajakuhumiwa bado?

Paulo alitumia swali hili kuuliza juu ya uhalali wa kuchapwa kwake viboko. "Si halali kwenu kumpiga mijeledi mtu ambaye ni raia wa Rumi na hajakuhumiwa!"

Je, unataka kufanya nini?

Swali hili limetumika kuwaomba kamanda kufikiria upya mpango wake wa kumjeledi Paulo. "Hupaswi kufanya hivi!"

Acts 22:27

Taarifa ya jumla

Fungu hili linazungumzia habari za Paulo

Jemedari mkuu akaja

Neno "kuja" linaweza kuwa na maana ya "kwenda"

ilikuwa kiasi kikubwa cha pesa

"Ilikuwa baada ya kulipa kiasi kikubwa cha pesa katika mamlaka ya Kirumi"

ndipo nilipata uraia.

"Nilijipatia uraia" au " Nilipewa uraia"

Mimi ni Mrumi wa kuzaliwa

Baba akiwa raia wa Kirumi, hivyo watoto wake wanakuwa raia wa Kirumi mara wanapozaliwa

wale waliokuwa tayari kwenda kumuuliza

Wanaume waliokuwa wamepanga kumwuliza maswali.

Acts 22:30

Taarifa ya jumla

Mstari huu unazungumzia jemedari mkuu

Jemedari mkuu

afisa wa jeshi mwenye kikosi cha askari wapatao 600

Hivyo akamfungua vifungo vyake

"yawezekana jemedaari mkuu alimfungua Paulo minyororo." au Mkuu wa jeshi aliamuru askari wake kumfungua vifungo Paulo"

Akamleta Paulo chini

Kutoka kwenye ngome, kuna njia ya kutelemka chini mpaka kwenye uwanda wa nje wa hekalu"

Acts 23

Matendo 23 Maelezo kwa Jumla

Muundo na Mpangilio

Tafsiri zingine zinanukuu kutoka Agano la Kale kwenye kulia kwa ukurasa kuliko maandiko yote kwa jumla. ULB hufanya hivi kupitia kilichonukuliwa katika 23:5

Dhana maalum katika sura hii

Ufufuko wa wafu

Wafarisayo waliamini kwamba baada ya watu kufa, wangefufuka tena na Mungu awazawadie ama awaadhibu. Wasadukayo waliamini kwamba pindi watu wanapokufa,hawangefufuka. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#raise and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#reward)

"Waliita laana"

Wayahudi wengine waliahidi Mungu kutokula ama kunywa mpaka Paulo auliwe na wakamuomba Mungu awaadhibu kama hawangetekeleza ahadi yao.

Uraia wa Urumi

Warumi walidhani Kwmaba ni Warumi pekee yao waliostahili kuhudumiwa kwa haki. Wangewatenda watakavyo wale ambao hawakuwa raia wa Urumi lakini kwa Warumi waliwatendea kufuata sheria. Watu wamojf walizaliwa raia wa Roma na wengine wakalipa pesa serikali ya Warumi ili wawe raia. "Kiranja Mkuu" angeadhibiwa kwa kuwatendea raia wa Urumi sawa wale wasiokuwa raia.

Mifano ya usemi muhimu katika sura hii

Chokaa

Hii ni mfano ya kawaida katika Maandiko matakatifu inayoonyesha mtu kuwa mzuri au kitu kuwa kizuri na safi ama mwenye haki lakini yule mtu ni mwovu ama amejinajisi ama si wa haki.

<< | >>

Acts 23:1

Sentensi unganishi

Paulo anasimama mbele ya wakuu wa makuhani na wajumbe wa baraza.

Ndugu zangu

Hii ina maana " Wayahudi."

Nimeishi mbele za Mungu na dhamiri njema mpaka leo

"Mimi najua kuwa hata leo nimefanya kila kitu Mungu alichotaka mimi kufanya"

Anania

Ni mtu tofauti na Anania anayetajwa sura ya 5:3

ukuta uliopakwa chokaa

Inamaanisha ukuta uliopakwa chokaa ili uonekane kuwa safi. Paulo anamwambia Anania kuwa anaonekana safi kama ukuta uliopakwa chokaa lakini ndani kumejaa uovu.

Umeketi kuhukumu ... kinyume cha sheria?

Paulo anatumia swali ili kumdhihirisha Anania kuwa ni mnafiki.

Acts 23:4

Je, hii ni jinsi unavyo mtukana kuhani mkuu wa Mungu?

wanaume walitumia swali hili kumkemea Paul kwa nini alisema. "Usimtusi Kuhani Mkuu wa Mungu!

Kwa maana imeandikwa

Paul ananukuu mambo ambayo Musa aliandika katika sheria. Hii inaweza kuwa: "Kwa maana Musa aliandika katika sheria"

Acts 23:6

Ndugu zangu

Hapa "Ndugu zangu" maana yake "Wayahudi wenzake"

mwana wa Mfarisayo

Hapa "mwana" maana yake yeye ni mwana halisi wa Farisayo na pia mtoto wa farisayo. "baba na mababa zake walikuwa mafarisayo"

Kwa ujasiri nakubali ufufuo wa wafu

neno "ufufuo" linaweza kumaanisha "kurudi kwenye maisha." kivumishi cha jina "wafu" inaweza kuwa "wale waliokufa." "Mimi kwa ujasiri nakubali wale waliokufa watarejea katika maisha"

Nimekwisha kuhukumiwa

"Mnanihukumu juu ya jambo hili"

mkutano ukagawanyika

"watu katika umati kwa nguvu hawakukubaliana wao kwa wao"

Kwa maana Masadukayo ... lakini Mafarisayo

Hii ni taarifa za msingi kuhusu Masadukayo na Mafarisayo.

Acts 23:9

Hivyo ghasia kubwa ikatokea

"Walianza kupiga kelele kwa sauti kubwa miongoni mwao." neno "hivyo" inaelezea tukio lililotokea kwa sababu ya kitu kingine kilichotokea hapo awali. Katika kesi hiyo, tukio liliopita ni la Paulo kuzungumzia imani yake juu ya ufufuo.

Vipi kama roho au malaika ameongea na yeye?

Mafarisayo wanawakemea Masadukayo na kudhibitisha kwamba roho na malaika wapo na wanaweza kuzungumza na watu. "Labda roho au malaika amesema naye!"

Wakati mabishano makali yalipotokea

Neno "mabishano makali" linaweza kuwa "Mwanzo wa vurugu"

Jemedari wa kikosi

Afisa wa jeshi la Kirumi au kiongozi wa askari wapatao 600.

Paulo angegawanywa vipande viwili na wao

Inamaanisha Paulo angeweza kuraruliwa vipande na kusababusha maumivu ya mwili.

kumchukua kwa nguvu

"kutumia nguvu za kimwili kumwondoa mahali pale"

ndani ya ngome

Ngome ilikuwa imeunganika na uwanda wa nje wa hekalu.

Acts 23:11

Usiku uliofuata

Hii ina maana usiku baada ya siku Paulo alipokwenda mbele ya Baraza. "Usiku huo"

utashuhudia katika Roma

maneno "kuhusu mimi" yameeleweka. "kutoa ushuhuda juu yangu katika Roma" au "kutoa ushuhuda juu yangu katika Roma"

Acts 23:12

Sentensi unganishi

Wakati Paulo akiwa kifungoni kwenye ngome, Wayahudi wasioamini waliapa kumwua.

Azimio

"kufanya nadhiri" au "kuapa mbele za Mungu"

Azimio

Ni makubaliano ya kawaida ya kufanya jambo fulani.

kuita laana juu yao wenyewe

Neno "laana" Walimwomba Mungu awalaani hama wasingetimiza nadhili yao

wanaume arobaini

wanaume 40

ambao walifanya njama hii

"ambao alipanga kumuua Paulo"

Acts 23:14

Tumejiweka wenyewe chini ya laana kubwa, kutokula kitu chochote hata tumwue Paulo

kuapa na kumwomba Mungu ili awalaani kama hawatatimiza nadhiri zao ni kusema kana kwamba laana ilikuwa kitu walichokibeba juu ya mabega yao. Sisi tumeapa tusile chochote hata tumwue Paulo na tumemwomba Mungu pia atulaani kama hatuwezi kufanya kile tulicho ahidi kufanya"

Sasa

Hii haina maana "wakati huu," lakini imetumika kuweka umakini kwa hatua muhimu ifuatayo.

Kwahiyo

Neno 'kwahiyo" linaonyesha kuna ujumbe uliotangulia kusemwa awali.

mlete chini mbele yako

"Mlete Paulo kutoka ngomeni ili akutane nawe hapa"

kana kwamba mnaamua kesi yake kwa usahihi

"kana kwamba mnataka kujifunza zaidi juu ya kile Paulo amekifanya"

Acts 23:16

kulikuwa na njama

"walikuwa tayari kwa kumshambulia Paulo" au "walikuwa wakisubiri kumwua Paulo"

ngome

Ngome ilikuwa imeunganishwa na uwanda wa nje wa hekalu.

Acts 23:18

Paulo yule mfungwa aliniita akataka nikuletee

Mfungwa Paulo ameniomba kuja kuzungumza nawe.

Yule jemadari mkuu akamshika kwa mkono akajitenga naye kando

Jemedari mkuu alimshika kijana mkono na kwenda naye kando, hii inaonyesha kijana yule alikuwa mpwa wa Paulo mwenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 15.

Acts 23:20

Wayahudi wamekubaliana

Hii haina maana Wayahudi wote. "Baadhi ya Wayahudi wamepatana"

kumleta Paulo chini

"kumleta Paul chini kutoka kwenye ngome"

walikuwa wanakwenda kumwuliza kwa usahihi kuhusu kesi yake

"wanataka kujifunza zaidi juu ya nini Paulo amefanya"

wanaume arobaini

"wanaume 40"

Wamejificha wanamsubiri

"tayari kumwotea Paulo" au tayari kumwua Paulo"

Wameita laana ishuke chini yao wenyewe, kwa kutokula wala kunywa mpaka watakapokuwa wamemwua

"Wao walikuwa wameapa kutokula wala kunywa chochote mpaka wamemwua Paulo. Na kumwambia Mungu awalaani kama hawatafanya walichoahidi kufanya"

Acts 23:22

Taarifa ya jumla

Felix aliyekuwa mkazi wa Kaisaria alikuwa ni Gavana wa sehemu ya Rumi

aliwaita kwake

"aliwaita yeye mwenyewe"

maakida wawili

Maakida wake wawili

wapanda farasi sabini

"Wapanda farasi 70"

askari mia mbili wa mikuki

"Askari 200 ambao wanajilinda kwa mikuki"

saa tatu usiku

Hii ilikuwa yapata 9:00 usiku.

Acts 23:25

Taarifa ya jumla

Jemedari mkuu anaandika barua kwa Gavana Feliki kuhusu kukamatwa kwa Paulo.

Klaudio Lisia kwa Gavana mheshimiwa Felix, salamu

Hii ni njia rasmi ya mwanzo wa barua. Mkuu wa jeshi akimaanisha mwenyewe katika nafsi ya tatu. Nina andika kwa Klaudio Lisia, wewe mheshimiwa Liwali Feliki salamu kwako"

Mheshimiwa Gavana Felix

Feliki alikuwa mtawala wa Kirumi aliyejitakia heshima kuu

Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi

Hapa "Wayahudi" maana yake "baadhi ya Wayahudi." Hii inaweza ikasemwa: "Baadhi ya Wayahudi walimtia mbaroni mtu huyo"

alikuwa karibu kuuawa

"walikuwa tayari kumwua Paulo

nikaenda pamoja na kikosi cha askari

Nilikuwa pamoja na maaskari wangu pale Paulo alipokuwa pamoja na Wayahudi

Acts 23:28

Nilitaka kujua neno

"mimi" inahusu Klaudio Lisia.

alikuwa ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao

Walikuwa wakumtuhumu kwa kumwuliza maswali.

lakini kwamba kulikuwa hakuna tuhuma ambayo ingehitaji mauti ama kifungo.

Maneno "mauti" au "kifungo" yanaweza kuwa; hakukuwa na kitu kinyume cha mamlaka ya Kirumi cha kumwua ama kumtupa gerezani.

Kisha ikajulikana kwangu

"Baadaye nilikuja kubaini"

Acts 23:31

Basi, askari walitii maagizo yao

neno "hivyo" linaweka alama kuwa tukio hilo lilitokea kwasababu ya kitu kingine kilichotokea hapo awali. Katika kesi hiyo, tukio lililopita ni mkuu wa jeshi kuamuru maaskari kumsindikiza Paulo.

walichukua Paul na wakampeleka usiku

Hapa "kuleta" inaweza kutafsiriwa kama "chukua". "walimpata Paulo na kumpeleka wakati wa usiku"

Acts 23:34

aliuliza mkoa gani Paulo alikotokea

"Alimwuliza Paulo mkoa gani aliotokea?"

Alipojua kwamba alikuwa ametoka mkoa wa Kilikia, alisema

"wakati liwali alipotambua kuwa Paulo alikuwa ametoka mkoa wa Kilikia, liwali alisema." Hii yaweza tajwa kama nukuu ya moja kwa moja. "Paulo alisema, 'Mimi nimetokea Kilikia.' Kisha liwali akasema"

Nitasikia kutoka kwako kikamilifu

"Nitakusikiliza kwa yale yote utakayo yasema"

akaamuru awekwe

Hii inaweza ikasemwa: "akaamuru askari amweke Paulo" au "akamwamuru askari amtunze Paulo"

Acts 24

Matendo 24 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Paulo alimwambia mkuu wa mkoa kwamba hakutenda tukio aliloshtakiwa na Wayahudi na kwa hivyo asimwadhibu kwa asilotenda.

Dhana maalum katika sura hii

Heshima

Viongozi wote Wayahudi (Matendo 24:2-4) na Paulo walianza kutoa hotuba zao wakitumia maneno yakudhihirisha heshima kwa mkuu wa mkoa.

Matatizo mengine katika hii tafsiri

Viongozi wa Kiserikali

Maneno "mkuu wa mkoa", Kamanda," na "akida" yanaweza kuwa magumu kutafsiri katika lugha nyingine.

<< | >>

Acts 24:1

Sentensi unganishi

Paulo sasa yuko kwenye misukosuko. Tertulo anawasilisha mashitaka kwa Liwali Feliki dhidi ya Paul.

Baada ya siku tano

"Siku tano baada ya askari wa Kirumi kumchukua Paul kwenda Kaisaria"

Anania

Angalia jinsi gani unaweza kulitafasiri katika 23:1

msemaji

"mwanasheria." Tertulo alikuwa mtaalam wa sheria ya Kirumi. Alikuwa huko kumshtaki Paul mahakamani.

Tertulo

Hili ni jina la mtu mwanamume.

walikwenda huko

"alienda Kaisaria ambako Paulo alikuwa"

alisimama mbele ya Gavana

"mbele ya Gavana ambaye alikuwa jaji wa mahakama"

akaanza kumshtaki

"alianza kuleta ukiukwaji wa sheria ya Kirumi dhidi yake"

tuna amani kubwa

"sisi, raia tulio chini ya utawala wa Felix tuna amani kubwa"

na kwa maono yako yanaleta mageuzi mazuri katika taifa letu

"na kupitia mipango yako mizuri imeleta mabadiliko makubwa katika taifa letu"

Feliki

Angalia jinsi gani unaweza kuitafasili katika

na mtizamo wako huleta mageuzi nzuri kwa taifa letu

"na mipango yako imeboresha sana taifa letu"

Mweshimiwa Felix

Angalia jinsi gani unaweza kuitafasili katika 23:25

Acts 24:4

Taarifa ya jumla

Fungu hili linazungumzia juu ya Anania, baadhi ya wazee na Tetulo

Lakini nisikuchoshe zaidi

Maana inawezekana ni 1) "ili mimi nisichukue sana muda wako" au 2) "Hivyo kwamba nisikufunge."

kwa wema waka nisikilize kwa ufupi

"kusikiliza hotuba yangu fupi"

Tumegundua kwamba mtu huyu mkorofi

neno "sisi" inamaanisha Anania, wazee kadhaa na Tertulo. "sisi tulimshuhudia Paulo" au "tuligundua kwamba Paulo chazo cha matatizo"

Wayahudi wote kila mahali duniani

neno "wote" hapa ni kuongezewa chumvi kama kisingizio cha kumshtaki Paulo. "Wayahudi wote duniani kote"

Tena ni kiongozi wa madhehebu ya Wanazorayo

Neno "dhehebu la Wanazarayo" ni jina jingine kwa wakristo "Mtu huyu anaongoza makundi ya watu wafuasi wa madhehebu ya Wanazarayo""

dhehebu

hili ni kundi dogo ya watu ndani ya kundi kubwa. Tertulo anaona Wakristo kuwa kundi dogo ndani ya Uyahudi.

Acts 24:7

Sentensi unganishi

Tertulo anamaliza kuwasilisha mashtaka ya Paulo kwa Gavana Feliki.

anamshitaki

"kumshtaki Paulo kwa kufanya" au "kumshtaki Paulo kwa kuwa na hatia ya kufanya"

Wayahudi

Hii inamaana ya viongozi wa Wayahudi waliokuwa pale katika kesi ya Paulo.

Acts 24:10

Sentensi unganishi

Paul anaitikia kwa Gavana Feliki kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake.

Gavana alimwashiria

"gavana akitoa ishara"

mwamuzi wa taifa hili

Neno "taifa" linamaanisha watu wa taifa la Kiyahudi. "Mwamuzi wa wa watu wa taifa la Wayahudi"

Kujieleza mwenyewe

"Kuielezea hali yangu"

waweza kuhakikisha

"unauwezo wa kufuatilia na kuthibitisha"

siku kumi na mbili tangu

"Siku 12 tangu"

sikuweza kuhamasisha kusanyiko"

Neno "kuhamasisha" ni kuwafanya watu wasiwe na utulivu"

mashitaka

"Lawama juu ya matendo maovu" au "mashitaka ya uharifu"

Acts 24:14

Nakiri hili kwenu

"Mimi nakiri hili kwako" au "ninatubu hili kwako"

wanaita dini

"wanaita kundi la wazushi"

kwa namna ile namtumikia Mungu wa babu zetu

Hii inamaana kwamba Paulo anadai kufuata dini ya kale, ambayo kwa ufafanuzi si dini mpya, "madhehebu."

kama watu hawa

Hapa "watu hawa" inahusu Wayahudi ambao ndio wanamtuhumu Paulo mahakamani.

ufufuo ujao wa wafu....kwa wote wenye haki na wasio na haki.

neno "ufufuo" linaweza kutumika kama "Kurudishwa katika maisha na Mungu." Na, neno "wafu" linaweza kuwa "wale waliokufa." "wakati Mungu akiwarudisha katika uhai wale wote waliokuwa wamekufa"

wasio wa haki

"wale waliofanya mambo mabaya"

Nafanya kazi

"Nafanyakazi vizuri"

kuwa na dhamiri bila lawama

Hapa "dhamiri" inahusu maadili ndani ya mtu kuwa akiamua kati ya mema na mabaya. "kuwa bila lawama" au "daima kutenda haki"

mbele za Mungu

"Katika uwepo wa Mungu"

Acts 24:17

Sasa

neno hili linaweka alama ya kuhama kutoka katika hoja ya Paulo. Hapa anaanza kuelezea hali katika Yerusalemu wakati baadhi ya Wayahudi walipomweka Paulo nguvuni.

baada ya miaka mingi

"baada ya miaka mingi kutoka Yerusalemu"

Nilikuja kuleta misaada kwa taifa langu na zawadi ya fedha

Hapa "nilikuja" inaweza kutafsiriwa kama "Nilikwenda." "Nilikwenda kusaidia watu wangu kwa kuwapelekea fedha kama zawadi"

katika sherehe ya utakaso katika hekalu

"katika hekalu baada ya kumaliza sherehe ya kujitakasa mwenyewe"

Bila umati wa watu au ghasia

Hii yaweza tajwa kama kauli mpya. "Mimi nilikuwa sijakusanya umati wala sikujaribu kuanzisha ghasia"

wamaume hawa

"Wayahudi kutoka Asia"

kama wanajambo lolote

"Kama wana jambo lolote la kusema"

Acts 24:20

Sentensi unganishi

Paul alimaliza kumjibu Gavana Feliki kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake.

wanaume hawahawa

Hii ina maana ya wajumbe wa baraza ambao walikuwepo Kaisaria katika kesi ya Paulo.

lazima waseme kosa waliloliona kwangu

"waseme iwapo kuna kitu kibaya nilikifanya na kukithibitisha"

Ni kuhusu ufufuo wa wafu

neno "ufufuo" linaweza kutumika kama "Kurudishwa katika maisha na Mungu." Na, neno "wafu" linaweza kuwa "wale waliokufa." "wakati Mungu akiwarudisha katika uhai wale wote waliokuwa wamekufa"

Ninahukumiwa leo na wewe

hii inaweza semwa kama "mnanihukumu mimi leo hii"

Acts 24:22

Taarifa ya jumla

Felix alikuwa Gavana wa Kirumi katika eneo la mji wa Kaisaria.

Njia

Hili lilijuwa jina jingine la ukristo.

Wakati wowote Lisia mkuu wa kikosi anakuja hapa chini

"wakati Lisia mkuu wa kikosi anakuja chini" au "muda Lisia mkuu wa kikosi anakuja chini"

Mimi nitaamua kesi yenu

"Nitafanya uamuzi kuhusu shutuma hizo dhidi yako" au "nitatoa hukumu kama wewe una hatia"

awe na uhuru

"Paulo anapewa uhuru si vinginevyo ni miongoni mwa wafungwa"

Acts 24:24

Baada ya siku kadhaa

"Baada ya siku kadhaa"

Drusila mkewe

Drusila ni jina la mwanamke.

Myahudi

Hii ina maana Myahudi wa kike. "ambaye alikuwa Myahudi"

Felix akajawa na woga

Felix inaweza kuwa aliona uthibitisho wa dhambi zake.

kwa sasa

"kwa wakati huu wa sasa"

Acts 24:26

Paulo angempa fedha

Feliki alikuwa na matumaini Paul atatoa rushwa ili amwachie huru.

hivyo mara nyingi alimwagizia na kuongea naye

"hivyo Feliki mara nyingi alimwagizia Paulo aletwe azungumza naye"

Porkio Festo

Huyu alikua Gavana mpya wa Rumi aliyechukua nafasi ya Feliki.

alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi

Hapa "Wayahudi" inamaanisha viongozi wa Wayahudi. "alitaka viongozi wa Wayahudi wampende"

alimwacha Paulo aendelee kuwa chini ya ulinzi

"alimwacha Paulo gerezani"

Acts 25

Matendo 25 Maelezo kwa jumla

Dhana maalum katika sura hii

Neema/Msaada maalum

Neno hili limetumika kwa njia mbili katika sura hii. Wakati viongozi Wa Wayahudi walipomwomba Festus neema, walikuwa wanamuomba kuwafanyia kitu maalum ambacho hajazoea kukifanya. Wakati Festus "alitaka kupata neema ya Wayahudi", alitaka wakuwe kama yeye na wakuwe" tayari kumtii miezi na miaka inayokuja. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#favor)

Uraia wa Urumi

Warumi walidhani kwamba ni Warumi pekee yao waliostahili kuhudumiwa kwa haki. Wangewatenda watakavyo wale ambao hawakuwa raia wa Urumi lakini kwa Warumi waliwatendea kufuata sheria. Watu wamoja walizaliwa raia wa Roma na wengine wakalipa pesa serikali ya Warumi ili wawe raia. Wafanyakazi wa serikali wangeadhibiwa kwa kuwatendea raia wa Urumi sawa na wale wasiokuwa raia.

<< | >>

Acts 25:1

Taarifa kwa ujumla

Festo ndiye gavana wa Kaisaria

Sasa

Neno hili linaonyesha mwanzo wa tukio linalofuata kwenye simulizi.

Festo akaingia katika jimbo

Inamaanisha 1) Festo aliingia katika eneo au 2) Festo aliingia kwenye eneo ili kuanza kutawala

Alienda toka Kaisaria mpaka Yerusalemu

Hii inamaanisha 1) kwenda juuinaonesha umuhimu wa Yerusalemu au 2) alikwenda mpaka juu kwa kuwa Yerusalemu ipo kilimani.

Walileta mashitaka dhidi ya Paulo

"kumshtaki Paulo kwa kuvunja sheria"

Waliongea kwa nguvu kwa Festo

"walimbembeleza Festo"

Kwamba atamuita..... ili wamuue

"kwamba Festo atamuita Paulo..... ili Wayahudi wamuue"

Anaweza kumuita

Anaweza kumtuma

Wanaweza kumuua njiani

Watamvamia Paulo na kumuua akiwa njiani

Acts 25:4

Paulo alikuwa mfungwa Kaisaria

Paulo ni mfungwa Kaisaria na mimi mwenyewe ntarejea huko baada ya muda mfupi.

Kama kuna jambo lolote baya kwa mtu huyu.

Kama Paulo amefanya jambo lolte baya.

Unaweza kumshtaki

"Unaweza kuleta mashtaka" au "unaweza kumshataki kwa kuvunja sheria"

Acts 25:6

Baada ya kukaa

Baada ya Festo kukaa

Kukaa kwenye kiti cha hukumu

" kukaa juu ya kiti ili afanye kazi ya hakimu"

Paulo aletwe kwake

"kwamba wamlete Paulo kwake"

Alipofika

"Paulo alipofika na kusimama mbele ya Festo"

Jina la Wayahudi

"sheria ya wayahudi"

siyo dhidi ya hekalu

Paulo alisema hajavunja sheria yoyote kuhusu nani aingie kwenye hekalu la Yerusalemu. "siyo dhidi ya sheria za kuingia hekalini"

Acts 25:9

Alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi

Alitaka kuwaridhisha wayahudi

Na kuhukumiwa na mimi juu ya mambo haya huko

"Ntakapokuhukumu kutokana na mashitaka haya"

Sehemu ninayopaswa kuhukumiwa

"Ni sehemu gani ambapo wewe itanihukumu"

Acts 25:11

Maelezo yanayounganisha

Paulo akaendelea kuongea na Festo

Ikiwa nimefanya kinachostahili kifo

"ikiwa nimefanya jambo baya la kustahili adhabu ya kifo"

Ikiwa mashitaka si kitu

"ikiwa mashitaka yao juu yangu si ya kweli"

Hakuna anayeweza kunikabidhi kwao

Hii inamaanisha 1) Festo hana mamlaka ya kisheria ya kumkabidhi Pailo kwa waliomshaki mashitaka ya uongo au 2) Paulo alisema kwamba kama hajafanya kosa lolote basi gavana asisikilize maombi ya Wayahudi.

Namuomba Kaisari

"Naomba kwamba niende mbele ya Kaisari ili nisikilizwe"

Festo aliongea na baraza

Hili ni baraza la kisiasa la serikali ya Roma. "Festo aliongea na washauri wa serikali yake"

Acts 25:13

Maelezo ya jumla

Festo akaanza kuelezea kesi ya Paulo kwa mfalme Agripa.

Sasa

Neno hili linaonyesha mwanzo wa tukio jipya kwenye simulizi.

Mfalme Agripa na Bernike

Agripa alikua mfalme aliyetawala wakati huo na Bernike alikuwa dada yake.

Kumtembelea kiofisi

"kumtembelea Festo kuhusu masuala ya kiofisi.

Mtu mmoja aliachwa na Felix kama mfungwa.

Wakati Felix akiacha ofisi alimuacha mtu gerezani.

Acts 25:17

Kwa hiyo

Neno hili linanyesha maelezo ya kilichosemwa kabla. Hivyo Festo alisema mtu aliyeshitakiwa anatakiwa awakabili washitaki wake na kujitetea.

Walipokuja pamoja hapa

"wakati viongozi wa Kiyahudi walipokuja kuonana na mimi hapa"

Nilikaa kwenye kiti cha hukumu

"Nilikaa juu ya kiti ambacho nilifanya kazi ya hakimu"

Niliamuru mtu huyo aletwe ndani

"Niliamuru askari wamlete Paulo mbele yangu"

Dini yao wenyewe

Neno "dini" linamaanisha mfumo wa imani ya watu juu ya maisha na nguvu.

Kuhukumiwa kule juu ya mambo haya

"ambapo baraza la Wayahudi wataamua kama anamakosa kuhusu masitaka haya"

Acts 25:21

Maelezo yanayounganisha

Festo akamaliza kuelezea kesi ya Paulo kwa mfalme Agripa

Niliamuru awekwe

"Niliwaambia maaskari wamuweke garezani"

"Keso" Festo akasema "utamsikia"

"Festo akasema, 'ntapanga ili usikilize Paulo kesho"

Acts 25:23

Paulo aliletwa kwao

"Walimpeleka Paulo mbele zao"

walinipigia kelele

"Wayahudi waliongea na mimi kwa nguvu"

Asiendelee kuishi

Maelezo haya yanaweka mkazo wa kinyume cha kusema "afe maramoja"

Acts 25:25

Maelezo yanayounganisha

Festo akaendelea kuongea na Mfalme Agripa

Nimemleta kwenu, hasa kwako, Mfamle Agripa

" Nimemleta Paulo kwenu nyote lakini hasa kwako Mfalme Agripa"

Ili nipate cha kuandika zaidi

"ili nipate cha ziada cha kuandika" au "ili nijue niandike nini"

haina maana kumpeleka mfungwa na bila kuonyesha mashitaka yanayomkabili

"itakuwa na maana nikimpeleka mfungwa na kuonyesha mashtaka yanayomkabili"

Mashitaka dhidi yake

inamaanisha kuwa 1) mashitaka yaliyoletwa juu yake na viongozi wa Kiyahudi au 2) mashitaka chini ya sheria za Roma yanayoelezea kesi ya Paulo.

Acts 26

Matendo 26 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Hii ni mara ya tatu kwa kusema habari ya kubadilishwa kwa Paulo. Hii ni kwa sababu hili ni tukio muhimu kwenye Kanisa la awali. Kuna mara tatu ya kusema kubadilishwa kwa Paulo. (Tazama: Matendo 9 na 22)

Paulo alimwelezea Mfalme Agripa kwa nini alikitenda alichokitenda na ya kwamba mkuu wa mkoa asimuadhibu kwa hicho.

Dhana Maalum katika sura hii

Mwanga na giza

Kila mara Biblia huzungumzia watu wasiokuwa waadilifu, watu wasiotenda yanayompendeza Mungu kana kwamba wanatembea gizani. Inazungumzia mwanga kama kinachowawezesha wenye dhambi kuwa waadilifu baada ya kugundua kwamba wanachofanya si kizuri na kumheshimu Mungu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous)

<< | >>

Acts 26:1

Maelezo anayounganisha

Festo alimpeleka Paulo mbele ya Mfalme Agripa. Kwenye mstari wa pili Paulo anaanza kutoa utetezi wake kwa Mfalme Agripa.

Alinyoosha mkono wake

"ilinyoosha mkono wake mbele ya makutano ili apate umakini wao"

Akaweka utetezi wake

Akaakza kujitetea mwenyewe dhidi ya mashitaka"

ninajina mwenye furaha

Paulo alikuwa na furaha akatumia kuwepo kwake mbele ya Agripa kama nafasi ya kuongea juu ya injili.

Acts 26:4

Wayahudi wote

Inamaniisha 1)Mafarisayo walikua na Paulo na walimfahamu kama Mfarisayo au 2)"Paulo alijulikana sana kwa Wayahudi

Kwenye nchi yangu mwenyewe

Ina maanisha 1) kwa watu wake mwenyewe sio lazima wawe kwenye eneo la Israeli au 2) kwenye ardhi ya Israeli.

Acts 26:6

Sasa

Paulo alitumia maneno haya kuonesha utetezi mwingine.

Nimesimama hapa ili nihukumiwe

"Nipo hapa waliponiweka ili nihukumiwe"

Naziangalia ahadi ambazo Mungu aliwapa baba zetu

Paulo ana matumaini na kuja kwa Mesia.

Nategemea kuifikia

"Tunaamini kuwa tutapokea ahadi ambayo Mungu ametuahidi"

Kwa nini mnafikiri ni ajabu kwa Mungu kufufua wafu?

Paulo alisema haya ili kumfanya Agripa aunganishe aliyoyasema Paulo na ambacho Agripa alikiamini juu ya Mungu anavyoweza kufufua wafu. "Wewe mwenyewe unaamini kuwa Mungu anaweza kufufua wafu"

Acts 26:9

Wakati fulani

Paulo alitumia maneno haya kuonesha utetezzi wake mwingine. Sasa anaelezea alivyokuwa anawatesa watakatifu.

Kinyume na jina la Yesu

neno "jina" linasimama kwa ujumbe wa Yesu. "kinyume na ujumbe wa Yesu"

Nipe kura yangu dhidi yao

"Kupiga kura ili kuwaadhibu"

Niliwaadhibu mara kwa mara

Inamaanisha 1)Paulo aliwaadhibu baadhi ya waamini mara nyingi au 2) Paulo aliwaadhibu waamini mbalimbali.

Acts 26:12

Nilipokuwa nafanya hivi

Paulo alitumia maneno haya kuonesha ushahidi mwingine. sasa anaelezea namna Yesu alipomuita toka kwenye kuwatesa watakatifu na kumfuata yeye.

Nilipokuwa

neno hili limetumika kuonesha matukio mawili yanayotokea kwa wakati mmoja. Hapa Paulo alikuwa anawatesa watakatifu alipokuwa akienda Dameski.

Kwa mamlaka na maagizo

Paulo alikuwa na barua toka kwa viongozi wa kiyahudi wakimpa mamlaka ya kuwatesa waamini wa Kiyahudi.

Ni vigumu kwako kuupiga teke mchokoo

Mungu anafananisha kukataa kwa Paulo kuhusu mipango ya Mungu na ng'ombe anayepiga teke fimbo ya mkulima. "ngumu kwako kupambana na maelekezo ya Mungu kwako."

Acts 26:15

Maelezo yanayounganisha

Paulo aliendelea kutoa utetezi wake kwa Mfalme Agripa. Kwenye mistari hii aliendelea kunukuu mazungumzo yake na Bwana.

Nilijitenga mwenyewe

"Nilitengezeza mwenyewe" au "Kuweka wakfu mwenyewe"

kwa imani iliyo kwangu

Hii inaelezea Imani juu ya Mungu kwa waliotengwa na Mungu kwa ajili yake.

Niliowatenga kwa ajili yangu kwa imani iliyo kwangu

Paulo alimaliza kumnukuu Bwana

Acts 26:19

Kwa hiyo

Neno hili linanyesha maelezo ya kilichosemwa kabla. Paulo alielezea ambacho Bwana alimuamuru katika maono.

Sikuyapuuza maono ya mbinguni

"Nilitii ujumbe niliopewa kwenye maono yaliyotoka mbinguni"

Acts 26:22

Maelezo yanayounganisha

Paulo akamaliza kujitetea kwa Mfalme Agripa

Ambayo manabii

Paulo anamanisha maandishi yaliyokusanywa ya Manabii wa Agano la kale.

Kwamba Kristo atateseka

"Kwamba kristo atateseka na kufa"

kutangaza mwanga

Kutangaza ujumbe wa ukombozi"

Acts 26:24

Una wendawazimu

"Unaongea upuuz"i au "umechanganyikiwa"

Mimi sio mwendawazimu

"Mimi ni mzima" au "nina uwezo wa kufikiri vizuri"

Mtupu

"uzito" au "kuhusu jambo lenye uzito"

Naongea kwa uhuru kwake

Naongea kwa uhuru kwa Mfalme Agripa

Haikufanywa kwenye kona

"Haikufanywa kwa siri"

Acts 26:27

Unawaamini managii, Mfalme Agripa?

Paulo alimuuliza swali hili Agripa na Agripa alishaamini waliyosema manabii kuhusu Yesu. "umeshaamini waliyosema manabii wa Kiyahudi Mfalme Agripa!"

Kwa mda mfupi unaweza kunishawishi na kunifanya niwe Mkristo?

Agripa aliuliza hili swali ili kumuonyesha Paulo kwamba haawezi kumshawishi Agripa kirahisi bila kithibitisho. "Unafikiri unaweza kunishawishi kirahisi!"

Acts 26:30

Ndipo Mfalme akasimama na Gavana

Kisha Mfalme Agripa akasemama pamoja na Gavana Festo"

Acts 27

Matendo 27 Maelezo ya jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Kusafiri Majini

Watu walioishi karibu na bahari walisafiri kutumia boti zilizosukumwa na upepo. Wakati wa kipindi fulani mwakani, upepo ungeelekea mwelekeo usiyofaa hadi ikawa vigumu sana kusafiri majini.

Uaminifu

Paulo alimwamini Mungu kama atamwezesha kusafiri kwa usalam hadi atakapofika inchi kavu. Aliwaambia mabaharia na wanajeshi kuamini pia kwamba Mungu atachunga maisha yao. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#trust)

Paulo anaumega mkate

Luka anatumia maneno karibu kuwa sawa na yale aliyotumia kueleza habari ya karama mwisho wa Yesu pamoja na wanafunzi wake. Alichukua mkate, akashukuru Mungu na kuumega na kula. Hata hivyo tafsiri yako isimfanye msomaji kufikiria kwamba Paulo alikuwa anaongoza sherehe ya kidini.

<< | >>

Acts 27:1

Sentensi unganishi

Paulo, kama mfungwa , anaanza safari kwenda Rumi

Taarifa

Neno sisi linamaanisha Luka mwandishi pamoja na Paulo na wasafiri wengine waliosafiri na Paulo

Taarifa

Adramitamu ni mji uliokuwa pwani ya uturuki ya sasa

Wakawaeka Paulo na wafungwa wengine chini ya mashitaka ya Julio wa kikosi cha Agustani

Maaskari wa kirumi wakamweka kwa afisa Julias wa Agustani kwa mkuu wa Paulo na wafungwa wengine.

Acts 27:3

Taarifa kwa ujumla

Neno sisi linamaanisha Luka, Paulo na wote waliosafiri pamoja naye.

Juliasi alimtendea Paulo kwa ukarimu

Julias alimtendea vizuri Paulo

Akasafiri kuzunguka kisiwa cha Kipro ambacho kilikuwa kimeukinga upepo.

Neno Kukinga linaweza kusemwa katika hali tendaji.

Acts 27:7

Tuliposafiri pole pole mwishowe tulifika kwa taabu.

Unaweza kuonesha kuwa kilichofanya wakasafiri kwa taabu ilikuwa ni kwa sababu ya upepo ulivuma dhidi yao.

Karibu na mji wa Lasi

Huu ni mji katika Pwani ya Krete

Acts 27:9

Taarifa kwa ujumla

Maneno kama "sisi" "Tuli" inamaanisha Paulo na wengine waliokuwa katika meli.

Muda wa mfungo wa wayahudi ulikuwa umepita na haikuwa sasa hatari kusafiri.

Mfungo huu ulifanyika katika siku ya utakaso ambayo mara nyingi ilifanyika mwishoni mwa mwezi wa septemba au mwanzoni mwa mwezi wa octoba katika kalenda ya watu wa magharigi. Baada ya muda huo ilikuwa hatari kutokana na vimbunga vya mara kwa mara.

Acts 27:12

Bandari haikuwa sehemu rahisi kukaa wakati wa baridi.

Unaweza kuonesha kwa nini haikuwa rahisi kukaa bandarini. "Bandari haikuweza kutosheleza kuleta usalama kwenye gati za meli wakati wa baridi na vimbunga"

Kaskazini mashariki na Kusini mashariki

Pande hizi hutegemea mahali jua linako chomozea na mahali jua linapozamia. Kaskazini Mashariki inaweza kuwa kushoto kiasi mwa upande unao chomoza jua. Kusini mashariki inakuwa ni kulia kiasi mwa upande wa jua linako zamia.

Acts 27:14

Wakati meli ilipolemewa na kushindwa kuukabili upepo

Upepo ulivuma kwa ukali dhidi ya upande wa kichwa cha meli kiasi kwamba hatukuweza kusafiri.

Acts 27:17

Tulipigwa kwa nguvu sana na dhoruba,

Hii inaweza kusemwa katika hali ya kutenda, Upepo ulivuma kwa nguvu"

mabaharia wakaanza kutupa mizigo kutoka Melini.

Hili lilifanyika ili kupunguza uzitoili meli isizame.

Acts 27:19

Mabaharia wakaanza kutupa vifaa kwa mikono yao wenyewe

Vifaa ina maanisha vyombo maalumu kwa ajili ya mabaharia. Hii inaonesha jinsi hali ilivyokuwa tete.

Bado dhoruba kubwa ilitupiga

Upepo wa kutisha ulitupiga sana.

Acts 27:21

Ili kupata haya madhara na hasara.

Na matokeo yake tumepata madhara na hasara.

Acts 27:23

Lazima usimame mbele ya Kaisari

Neno "Lazima usimame mbele ya Kaisari" Inamaanisha paulo kufika mbele ya mahakama na kuhukumiwa na Kaisari. "Lazima usimame mbele ya Kaisari akuhukumu"

Lakini lazima tuumie kwa kupigwa katika baadhi ya visiwa.

"Upepo lazima utatupeleka ufukweni mwa visiwa fulani."

Acts 27:27

kama usiku wa manane hivi,

Usiku wa manane unaweza kutafsiriwa kama usiku wa saa nane.

wakapata mita thelathini na sita

Mita ni kipimo kama cha urefu wa mikono.

Acts 27:30

Boti ndogo ndogo za kuokolea maisha,

Hizi ni botti au melindogo ambazo hutolewa nyuma ya meli kubwa . boti hizi huwekwa kwa ajili ya kujiokolea wakati meli inataka kuzama

Hamuwezi kuokoka isipokuwa hawa watu wanabaki kwenye meli.

Maneno ya nayayo semwa kinyume yakimaanisha hakuna uwezekano wa kuokoka mpaka watu wabaki melini.

Acts 27:33

33Wakati mwanga wa asubuhi ulipokuwa unajitokeza

Kulipokuwa kukipambazuka

Siku hii ni ya kumi na nne

Siku ya kumi na nne

Hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea

Hii ilikuwa ni njia ya usemi ulio maanisha kwamba hakuna harari yoyote ingewapata. "Kila mmoja atakuwa salama katika dhoruba hii."

Acts 27:36

wote wakatiwa moyo

Hii inaweza kusemwa katika hali tendaji, "Wote walitiwa moyo"

Tulikuwa watu 276 ndani ya meli.

Hii ni taarifa ya nyuma.

Acts 27:39

Nchi kavu majini au Ghuba

Sehemu ya nchi kavu iliyoingia majini iliyokuwa na mchanga mwing

Lakini wakaja mahali ambapo mikondo miwili ya maji inakutana,

Mkondo wa maji unaotiririka kwenda upande mmoja wakati wote. Mara nyingine zaidi ya mkondo mmoja unaweza kutiririka ukiukatisha ule mwingine. Hali hii inaweza kusababisha mchanga kulundikana mahali pamoja na kufanya kina cha maji kuwa kifupi.

Acts 27:42

Mpango wa wale askari ulikuwa

Maaskari walikuwa wanapanga

Angeogelea na kutoroka.

"Kuruka kutoka katika meli na kuingia majini"

wengine juu ya vipande vya mbao

Wengine kwenye vipande vya mbao

Acts 28

Matendo 28 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Hakuna anayefahamu ni kwa nini Luka anamaliza habari hii bila kuwaambia watu kilichomtendekea Paulo baada ya yeye kuwa Roma kwa miaka miwili.

Dhana maalum katika sura hii

"Barua" na "Ndugu"

Viongozi wa Wayahudi walishangaa kwamba Paulo alitaka kuzungumza nao kwa vile hawakuwa wamepokea barua kutoka kwa kuhani mkuu Yerusalemu kusema kwamba Paulo alikuwa anakuja.

Wakati viongozi wa Wayahudi walipozungumza kuhusu "ndugu" walimaanisha Wayahudi wenzao na sio Wakristo.

Matatizo mengine ya utafsiri katika sura hii.

" Alikua mungu"

Wenyeji waliamini ya kwamba Paulo alikuwa mungu, lakini hawakuamini kwamba alikuwa Mungu wa kweli. Hatujui ni kwa nini Paulo hakuwaambia wenyeji kwamba hakuwa Mungu.

__<< | __

Acts 28:1

Sentensi unganishi:

Baada ya meli kuharibika, watu wa kisiwa cha Malta walimsaidia Paulo na wenzake waliokuwa kwenye meli. Walikaa pale miezi mitatu.

kisiwa kilichoitwa Malta

Malta ni kisiwa kilichopo katika kisiwa kingine ambacho kwa sasa kinaitwa Sisili.

watu asilia

wenyeji wa pale

Acts 28:3

shoka mkali alitokea

nyoka mwenye sumu kali alitokea kwenye mzigo wa kuni

haki pia

neno "Haki" lilimaanisha jina la Mungu waliyemwabudu.

Acts 28:5

akamkung'utia yule mnyama motoni

alitikisa mkono wake ili yule nyoka aangukie kwenye moto

walisema kuwa alikuwa mungu

labda kulikuwa na imani kwamba mtu yeyote aliyeishi baada ya kugongwa na nyoka alikuwa sio wa kawaida

Acts 28:7

Ujumbe wa jumla:

Hapa maneno "sisi" ana "sisi" yanamtaja Paulo

alifanywa kuwa mgonjwa

alikuwa mgonjwa

na liponywa

na aliwaponya wote

Acts 28:11

Sentensi unganishi:

Safari ya Paulo kwenda Rumi inaendelea

meli ya Alexandria

meli ambayo ilitoka Alexandria

ambayo ilinyauka kwenye kisiwa

wafanyakazi waliachwa kisiwani majira ya baridi

Acts 28:13

jiji la Regimu

huu ni mji wa bandari uliopo kusini magharibi mwa Italia

jiji la Puteli

Puteli kwa sasa ipo katika mji wa Napoli

Alimshukuru Mungu na kujipa moyo

hii ilimtia moyo sana

Acts 28:16

viongozi kati ya Wayahudi

hawa ni wale viongozi wa Kiyahudi au wa kidini waliopo Rumi

kinyume na watu

kinyume na Wayahudi

Acts 28:19

wayahudi

hii haimanishi Wayahudi wote bali viongozi tu

aliongea kinyume na matakwa yao

alilalamika juu ya mambo ambayo viongozi wa Kirumi walitaka kufanya

Acts 28:21

mnafikiri kuhusu dhehebu hili

dhehebu ni kundi dogo ndani ya kubwa

kwa kuwa tunaijua sisi

kwa sababu sisi tunaijua

Acts 28:23

alitenga siku kwa ajili yake

alichagua siku kwa ajili yake kuongea naye

alishuhudia kuhusu ufalme wa Mungu

ufalme wa Mungu hapa unamaanisha utawala wa Mungu kama mfalme

Acts 28:25

Sentensi unganishi:

Zviongozi wa Kiyahudi walipokuwa tayari kuondoka, Paulo alinukuu maandiko kutoka Agano la Kale kwa ajili yao

lakini hawataelewa...lakini hawatajua

Sentensi hizi mbili zinamaanisha kitu kimoja

Acts 28:27

Sentensi unganishi:

Paulo anamalizia kumnukuu nabii Isaya

na kugeuka tena

kumtii Mungu ni sawa na kumgeukia Mungu

Acts 28:28

Sentesni unganishi:

Paulo anamaliza kuongea na viongozi wa Kiyahudi

nao watasikiliza

baadhi yao watasikiliza

Acts 28:30

Sentensi unganishi:

Luka anakamilisha simulizi ya Paulo katika kitabu cha Matendo ya Mitume

alikuwa anahubiri kuhusu ufamle wa Mungu

ufalme wa Mungu una maana ya utawala wa Mungu