Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa Wagalatia

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha Wagalatia

  1. Paulo anatangaza mamlaka yake kama mtume wa Yesu Kristo; anasema kwamba anashangazwa na mafundisho ya uongo ambayo Wakristo wa Galatia wamekubali kutoka kwa watu wengine (1:1-10).
  2. Paulo anasema kwamba watu wanaokolewa kwa kumtegemea Kristo pekee, si kwa kushika sheria (1:11-2: 21).
  3. Mungu anaweka watu kuwa haki na yeye wakati wanapomwamini Kristo tu; mfano wa Abrahamu; laana ambayo sheria huleta (na sio njia ya wokovu); utumwa na uhuru uliolinganishwa na kuonyeshwa nao Hagari na Sara (3:1-4:31).
  4. Watu wanapojiunga na Kristo, huwa huru kutokana na kuzingatia sheria ya Musa. Wao pia wako huru kuishi kama Roho Mtakatifu anavyowaongoza. Wao wako huru kukataa madai ya dhambi. Wao wako huru kubeba mizigo ya wenzao (5:1-6:10).
  5. Paulo anawaonya Wakristo wasiamini katika kutahiriwa na kufuata sheria ya Musa. Lakini, wanapaswa kumtegemea Kristo (6:11-18).

Nani aliandika Kitabu cha Wagalatia?

Paulo aliandika 1 Wakorintho. Paulo alitoka mji wa Tarso. Alikuwa alijulikana kwa jina la Sauli katika maisha yake ya awali. Kabla ya kuwa Mkristo, Paulo alikuwa Mfarisayo. Aliwatesa Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara kadhaa katika Ufalme wa Roma akiwaambia watu kuhusu Yesu.

Haijulikani wakati gani Paulo aliandika barua hii na mahali gani alikuwa wakati wa kuandika. Wasomi wengine wanafikiri Paulo alikuwa katika mji wa Efeso na aliandika barua hii baada ya safari yake ya pili kuenda kuwaambia watu kuhusu Yesu. Wasomi wengine wanafikiri Paulo alikuwa katika mji wa Antiokia huko Siria na akaandika barua baada ya safari yake ya kwanza.

Kitabu cha Wagalatia kinahusu nini?

Paulo aliandika barua hii kwa Wakristo Wayahudi na Wayunani katika eneo la Galatia. Alitaka kuandika dhidi ya walimu wa uongo ambao walisema kwamba Wakristo wanahitaji kufuata sheria ya Musa. Paulo alitetea injili kwa kueleza kwamba mtu anaokolewa kwa kuamini Yesu Kristo. Watu wanaokolewa kama matokeo ya Mungu kuwa wema na sio matokeo ya watu wanaofanya kazi nzuri. Hakuna mtu anayeweza kumtii kikamilifu sheria. Jaribio lolote la kumpendeza Mungu kwa kuitii sheria ya Musa litasababisha Mungu kuwahukumu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#goodnews, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#save, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#works)

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha jadi, "Wagalatia." Au wanaweza kuchagua kichwa cha wazi zaidi, kama "Barua ya Paulo kwa Kanisa la Galatia." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Ina maana gani "kuishi kama Wayahudi" (2:14)?

"Kuishi kama Wayahudi" inamaanisha kutii sheria ya Musa, ingawa mtu anategemea Kristo. Watu kati ya Wakristo wa kwanza ambao walifundisha kwamba hii ilikuwa muhimu waliitwa "Wayudaiza".

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Paulo alitumiaje maneno "sheria" na "neema" katika Kitabu cha Wagalatia?

Maneno haya hutumiwa kwa njia ya pekee katika Wagalatia. Kuna fundisho muhimu katika Wagalatia kuhusu maisha ya Kikristo. Chini ya sheria ya Musa, maisha ya haki au matakatifu yalihitaji mtu kuitii kanuni na masharti. Kama Wakristo, maisha matakatifu sasa yamehamasishwa na neema. Hii inamaanisha kwamba Wakristo wana uhuru katika Kristo na hawatakiwi kutii masharti ya binadamu. Lakini Wakristo wanapaswa kuishi maisha matakatifu kwa sababu wanashukuru kwamba Mungu amekuwa mwenye huruma kwao. Hii inaitwa "sheria ya Kristo." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#holy)

Paulo alimaanisha nini kwa maneno "katika Kristo," "katika Bwana," nk?

Aina hii ya kujieleza ipo katika 1:22; 2:4, 17; 3:14, 26, 28; 5:6, 10. Paulo alijaribu kueleza wazo la muungano wa karibu sana sana kati ya Kristo na waumini. Lakini, aldhamiria maana maana nyingine pia. Angalia, kwa mfano, "tunapomtafuta Mungu kutuhakikisha katika Kristo" (2:17), ambako Paulo alizungumzia kuwa mwenye haki kwa njia ya Kristo.

Tafadhali angalia utangulizi wa Kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi juu ya aina hii ya kujieleza.

Je, ni masuala gani muhimu katika Kitabu cha Wagalatia?

Kifungu kinachofuata ni suala la maana zaidi katika Kitabu cha Wagalatia:

  • "Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? " (3:1) ULB, UDB, na matoleo mengine ya kisasa yana somo hili. Hata hivyo, matoleo ya kale ya Biblia yanaongeza, "ili msipaswe kuutii ukweli." Watafsiri wanashauriwa kutoingiza maneno haya. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri kuna matoleo ya kale ya Biblia ambayo yana kifungu hicho, watafsiri wanaweza kukijumuisha. Ikiwa imetafsiriwa, inapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yao sio Wagalatia. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

Galatians 1

Wagalatia 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Paulo alianza barua hii tofauti na barua zake zingine. Anaongezea kwamba yeye "hakuwa mtume kutoka kwa wanadamu wala kwa shirika la kibinadamu, bali kupitia Yesu Kristo na Mungu Baba, aliyemfufua kutoka kwa wafu." Paulo labda alijumuisha maneno haya kwa sababu walimu wa uongo walimpinga na kujaribu kushusha mamlaka yake.

(note title)

Dhana maalum katika sura hii

Uzushi

Mungu milele huwaokoa watu kupitia injili ya kweli, ya kibiblia, tu. Mungu anakataa namuna lolote lingine la injili. Paulo anamwomba Mungu kuwalaani wale wanaofundisha injili ya uwongo. Huenda wasiokolewe. Wanapaswa kutendewa kama wasio Wakristo. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#save, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#eternity, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#goodnews and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#condemn and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#curse)

Tabia za Paulo

Watu wamoja katika kanisa la kwanza walikuwa wakifundisha kwamba Wayunani walistahili kutii sheria ya Musa. Ili kukataa mafundisho haya, katika mistari ya 13-16 Paulo anaeleza jinsi zamani alikuwa Myahudi mwenye bidii. Lakini Mungu bado alikuwa anahitaji ya kumwokoa na kumwonyesha injili ya kweli. Kama Myahudi, na mtume kwa Wayunani, Paulo alikuwa na tabia ya sifa ya pekee ya kukabiliana na suala hili. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Mnaacha upesi hivi na mnafuata injili ya namuna nyingine"

Kitabu cha Wagalatia ni mojawapo ya barua za kwanza za Paulo katika Maandiko. Inaonyesha kwamba vita vya uzushi vilikuwepo hata katika kanisa la kwanza. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

| >>

Galatians 1:1

Sentensi unganishi

Mtume Paulo, mwandishi wa barua hii kwa makanisa yaliyoko katika maeneo ya Galatia.

Maelezo ya jumla

Maneno 'ninyi,' 'nanyi' au 'yenu' hurejelea watu wa Galatia katika wingi wao.

Aliyemfufua yeye

"Aliyemfufua Yesu Kristo"

Kufufuliwa

Hapa inamaanisha ni kitendo cha kumfanya mtu aliyekuwa amekufa kuwa hai tena.

Ndugu

Hapa inamaanisha Wakristo, kwa kujumuisha wanaume na wanawake wote, kwa kuwa waumini wote ndani ya Kristo ni washirika wa familia moja, na Mungu ndiye Baba yao wa mbinguni.

Galatians 1:3

kwa dhambi zetu

"dhambi" huwakilisha hukumu ya dhambi. "kuchukua hukumu tuliyostahili kwa sababu ya dhambi zetu"

ili kwamba atukomboe na nyakati hizi za uovu

Hapa neno, "Nyakati...hizi" huwakilisha nguvu zinazotenda kazi katika nyakati husika. "ili kwamba atuweke huru kutoka katika kazi za nguvu ya uovu ndani ya ulimwengu wa leo"

Mungu wetu na Baba

Hii inarejeleaa kwa " Mungu Baba yetu." Ni Mungu wetu na Baba yetu.

Galatians 1:6

Sentensi Unganishi:

Paulo anatoa sababu yake ya kuandika barua hii-anawakumbusha kuendelea kuielewa injili.

Ninashangaa

"Ninashangazwa" au "Nimeshitushwa." Paulo alisikitishwa na mambo haya waliyokuwa wanayafanya.

kwamba mmegeuka haraka sana kutoka kwake... na kwenda kwenye injili nyingine

Maana nyingine zaweza kuwa ni 1) " Mmeacha kwa haraka sana kumtumaini Yeye au 2) "mmeacha kwa haraka sana kuwa waaminifu kwake."

Yeye aliyewaita

"Mungu, aliyewaita ninyi"

kuitwa

Hapa inamanisha Mungu amewateua or kuwachagua watu kuwa watoto wake, kumtumikia na kuutangaza wa ujumbe wa wokovu kupitia kwa Yesu.

kwa neema ya Kristo

" kwa sababu ya neema ya Krsto" au "kwa sababu ya dhabihu ya neema ya Kristo"

Mnageukia injili nyingine

Mnaamini injili nyingine

watu

watu wote au binadamu

Galatians 1:8

anapaswa kutangaza

Hii inaelezea kitu ambacho hakijatokea na hakipaswi kutokea. "wangetangaza" au "walipaswa kutangaza"

tofauti na ile

"tofauti na injili" au "tofauti na ujumbe"

na alaaniwe

"Mungu anapaswa kumwadhibu mtu yule milele yote." na kama lugha yako ina neno au njia inayotumika kutoa laana kwa mtu, unaweza kutumia hiyo.

Kwani sasa hivi ninatafuta uthibitisho wa watu au Mungu? Ninatafuta kuwafurahisha wanadamu?

Maswali haya hutarajia jibu ambalo ni " hapana" Hii ni sawa na kusema "sitafuti kukubaliwa na wanadamu, bali ninatafuta kukubaliwa na Mungu. sitafuti kuwafurahisha wanadamu."

Kama ninaendelea kujaribu kuwafurahisha wanadamu, mimi sio mtumishi wa Kristo

Neno 'kama' linaonesha ukweli kuwa "mimi siwafurahishi wanadamu, mimi ni mtumishi wa Kristo." au " kama ningekuwa bado naendelea kuwafurahisha wanadamu, basi nisingekuwa mtumishi wa Mungu

Galatians 1:11

Sentensi Unganishi

Paulo anaeleza kuwa hakujifunza injili kutoka kwa wengine; alijifunza kutoka kwa Yesu Kristo.

Ndugu

Hapa inamaanisha Wakristo, kwa kujumuisha wanaume na wanawake wote, kwa kuwa waumini wote ndani ya Kristo ni washirika wa familia moja, na Mungu ndiye Baba yao wa mbinguni.

haitokani na watu (si injili ya watu)

kwa kutumia maneno haya, Paulo hasemi kuwa Yesu Kristo mwenyewe si mwanadamu. kwa sababu Kristo ni mtu na ni Mungu, ingawa Yeye si mwanadamu mwenye dhambi. Paulo anaandika juu ya kule injili ilikotoka, kwamba haikutoka kwa watu wenye dhambi, bali ilitoka kwa Yesu Kristo.

kilikuwa ni kwa ufunuo wa Yesu Kristo kwangu

Maana zinazokubalika ni 1) Yesu Kristo mwenyewe aliifunua injili kwangu 2)Mungu alinifanya mimi niijue injili wakati aliponionesha jinsi Yesu Kristo alivyo.

Galatians 1:13

Maisha ya nyuma

"Tabia katika kipindi fulani" au " maisha ya kipindi kilichopita" au " maisha ya mwanzo"

NIlikuwa nimeendelea

Hii ni sitiari ( lugha ya picha) inayoonesha jinsi Paulo alivyokuwa mbele ya wayahudi wengine wa umri wake katika kusudi lao la kuwa wayahudi kamili.

wale wenye umri kama wangu

"Wayahudi wenye umri sawa na wa wangu"

baba

"mababu", au "wazazi wa zamani"

Galatians 1:15

Aliniita kupitia neema yake

Maana zinazokubalika ni 1)"Mungu aliniita kumtumikia kwa sababu Yeye ni wa neema" au 2) " Aliniita kwa njia ya neema yake."

kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu

Maana zinazokubalika 1)" kuniruhusu mimi nimjue Mwana wake" 2) "Ulimwengu umwone Yesu Mwana wa Mungu kupitia kwangu."

Mwana

Hili ni jina muhimu la Yesu, Mwana wa Mungu

kumtangaza Yeye

Kumtangaza kuwa Yeye ni Mwana wa Mungu" au "kuhubiri habari njema kuhusu Mwana wa Mungu"

Wala sikutafuta ushauri wa mwili na damu

Haya maelezo yanamaanisha kuzungumza na watu wengine. AT: " kuwaomba watu wanisaidie kuelewa ujumbe."

kupanda

AT: "Kusafiri" Mji wa Yerusalem ulikuwa katika mkoa ulikuwa na milima mingi, ambayo ilimlazimu mtu kupanda milima mingi ili kufika huko, na hivyo ilikuwa kawaida kueleza kitendo cha kusafiri kwenda Yerusalemu kama "kupanda kwenda Yerusalemu."

Galatians 1:18

Lakini sikuona mitume wengine isipokuwa Yakobo

Vikanushi viwili vinatilia mkazo kwamba Paulo alimwona mtume Yakobo tu. AT: Mtume pekee niliyemwona ni Yakobo."

Mbele za Mungu

Paulo anawataka Wagalatia kuelewa kuwa Paulo alikuwa amedhamiria kweli na kwamba Mungu husikia kile anachokisema na kuwa atahukumiwa kama hatausema ukweli.

Tazama, mbele za Mungu, sidanganyi kwa kile niandikacho kwenu

Paulo anatumia msemo huu kuweka mkazo kuwa anausema ukweli. AT: " katika ujumbe huu ninaowaandikia, Siwadanganyi" au " ninasema ukweli katika mambo niliyowaandikia ."

Galatians 1:21

Mikoa ya

"Sehemu ya ulimwengu inayoitwa..."

Walikuwa wakisikia tu

"Bali walikuwa wakijua tu kile wachokisikia kwa wengine kunihusu mimi"

Sikuwa najulikana kwa macho kwa makanisa ya Uyahudi yale yaliyokuwa katika Kristo,

"Hakuna mtu yeyote ambaye alishawahi kukutana nami miongoni mwa makanisa ya Uyahudi yaliyokuwa katika Kristo."

Galatians 2

Wagalatia 02 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Paulo anaendelea kutetea injili ya kweli. Hii ilianza katika Wagalatia 1:11.

Dhana maalum katika sura hii

Uhuru na utumwa

Katika barua hii, Paulo anatofautisha uhuru na utumwa. Mkristo ana uhuru katika Kristo kufanya mambo mengi tofauti. Lakini Mkristo ambaye anajaribu kufuata sheria ya Musa anahitaji kufuata sheria nzima. Paulo anaelezea kwamba kujaribu kufuata sheria ni kama aina ya utumwa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses)

hangamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Siibatili neema ya Mungu"

Paulo anafundisha kwamba, ikiwa Mkristo anajaribu kufuata sheria ya Musa, haelewi neema ambayo Mungu amemwonyesha. Hii ni kosa la msingi. Lakini Paulo anatumia maneno "Siibatili neema ya Mungu" kama aina ya hali ya mawazo. Shabaha ya neno hili inaweza kuonekana kama, "Ikiwa ungeweza kuokolewa kwa kufuata sheria, basi hiyo ingeweza kupuuza neema ya Mungu." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#grace and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-hypo)

<< | >>

Galatians 2:1

Sentense Unganishi

Paulo anaendelea kuwapa historia ya jinsi alivyojifunza injili kutoka kwa Mungu, na siyo kwa mitume.

Alienda

"Alisafiri" Yerusalemu ilikuwa katika nchi ya vilima. Wayahudi pia waliutazama Yerusalemu kama sehemu ya duniani iliyokaribu na mbinguni, hivyo Paulo inawezekana alikuwa akizungumza kwa mfano, au alikuwa akionesha ugumu, kupanda na kusafiri kufika Yerusalemu.

wale waliosemekana kuwa viongozi muhimu

Hawa ni "viongozi muhimu miongoni mwa waumini"

Sikukimbii, au nilikuwa nimekimbia bure

Paulo anatumia neno kukimbia kama lugha ya picha kumaanisha kazi. Na alitumia vikanushi viwili kukazia kuwa kazi aliyokwisha kuifanya ili na faida. AT: "Nilikuwa ninafanya, au nilifanya kazi inayofaa."

kwa bure

"kwa bila faida" au "bila kitu "

Galatians 2:3

Ndugu wa uongo waliotumwa kwa siri

"Watu waliokuja kanisani wakijifanya kuwa ni Wakristo' au watu waliokuja miongoni mwetu wakijifanya kuwa ni wakristo"

Kutahiriwa

Neno hili laweza kuelezwa kwa muundo tendaji. AT " kuwa na mtu wa kumtahiri."

Peleleza uhuru

Hii ina maanisha kuwatazama watu kwa siri ili kuona wanavyoishi katika uhuru.

Uhuru

"uhuru" hali ya kutokuwa chini ya...au utawala wa ..."

Walitaka

Kama: "Wapelelezi hawa walitamani" au "Ndugu hawa wa uongo walitaka"

Kutufanya kuwa watumwa wa sheria

"Kutufanya kuwa watumwa wa sheria." Paulo anazungumzia kuhusu kuwalazimisha kufuata desturi za kiyahudi kama zilivyoamriwa katika sheria. Analizungumzia jambo hili kama ni utumwa. Jambo muhimu la kidesturi hapa ni tohara. "kutulazimisha kutii sheria"

kujitoa katika utii

"kutii" au "kusikia"

Galatians 2:6

Hawakuchangia chochote kwangu

Neno 'kwangu' linawakilisha kile ambacho Paulo alikuwa akifundisha. "halikuongeza chochote kwa kile ninachofundisha" au " hawakuniambia niongeze kitu chochote kwa kile ninachofundisha."

Badala yake

"kinyume"

Nimeaminiwa

Neno hili laweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mungu ameniamini mimi."

Galatians 2:9

Kujenga kanisa

Ni watu waliwaofundisha watu kuhusu Yesu na kuwashawishi wamwamini Yesu.

Neema niliyopewa mimi

"kwamba Mungu amekuwa mwema kwangu"

kutupokea....mkono wa kulia wa ushirika

"Waliwakaribisha...kama watendakazi wenzao" au "waliwakaribisha...kwa heshima"

Mkono wa kulia

"Mikono yao ya kuume"

Kuwakumbuka masikini

"kushughulikia au kujali mahitaji ya masikini"

Galatians 2:11

Nilipingana waziwazi ( usoni pake)

Maneno "kwa usoni pake" ni lugha ya picha likimaanisha "mahali atakapoweza kuona na kusikia." "Nilikabiliana naye" au "Niliyakosoa matendo yake"

Kabla

Katika uhusiano na wakati/muda

Aliacha

"Aliacha kula pamoja nao"

Alikuwa anawaogopa watu wale

"Alikuwa na hofu na watu hawa waliotaka tohara wangemhukumu kwamba alikuwa akifanya kitu kibaya" au "aliogopa kwamba watu hawa wangemlaumu kwa kufanya jambo fulani baya." kimakosa"

Watu waliotaka tohara

Wayahudi waliokuwa Wakristo, lakini walilazimisha kwamba wale waliomwamini Kristo wanapaswa kuishi kwa kufuata desturi za Kiyahudi.

Kuweka mbali kutoka

"kukaa mbali kutoka" au kuepukwa"

Galatians 2:13

hawafuati injili ya kweli

"Walikuwa wanaishi kama watu ambao hawajaiamini Injili" or " walikuwa wanaishi kana kwamba hawaiamini injili"

Kwa jinsi gani mnaweza kuwalazimisha Watu wa mataifa kuishi kama Wayahudi?

Hili swali linaonesha hali ya kukemea na linaweza kutafsiriwa kama, "mnakosea kuwalazimisha wamataifa kuishi kama Wayahudi." Neno "wewe" linamrejelea Petro na liko katika umoja.

lazimisha

Maana zinakubalika: 1) kulazimisha kwa kutumia maneno or 2) Kushawishi.

Galatians 2:15

Sentensi Unganishi:

Paulo anawaambia waumini kwamba Wayahudi wanaojua sheria na Wamataifa ambao hawaijui sheria, wameokolewa kwa imani peke yake ndani ya Kristo na siyo kwa kutunza sheria.

si watu wa mataifa wenye dhambi

"siyo wale watu wa mataifa ambao wayahudi huwaita wenye dhambi"

Tulikuja katika imani ndani ya Kristo Yesu

"Tuliamini katika Kristo Yesu"

sisi

Huenda pengine hii inamrejelea Paulo na wengine, na si Wagalatia.

hakuna mwili

Neno mwili limetumika kuwakilisha mtu yaani "hakuna mtu"

Galatians 2:17

Lakini kama tunapomtafuta kuhesabia haki ndani ya Kristo

Hii inamaanisha kwamba tumehesabiwa haki kwasababu tumeungana na Kristo na kuhesabiwa haki kwetu kwa njia ya Kristo.

tunajikuta sisi wenyewe pia kuwa wenye dhambi

Maneno "tunajikuta wenye dhambi" yanatilia mkazo kuwa kwa kweli sisi ni wenye dhambi.

sivyo hivyo! La hasha

"Bila shaka hiyo siyo kweli!" Maelezo haya yanatupa jibu hasi kwa swali lililotangulia, Je Yesu alifanyika mtumwa wa dhambi? Unaweza kuwa na maelezo yenye maana sawa katika lugha yako ambayo unaweza kuyatumia hapa.

Galatians 2:20

Mwana wa Mungu

Hili ni jina la muhimu la Yesu

Siikani neema

Paulo anatumia neno hasi katika kutilia mkazo wa ukweli chanya. "ninahakikisha uthamani wa..."

kama haki ingeweza kupatikana kwa.... basi Kristo asingekufa

Paulo anaelezea hali ambayo haipo, haitatokea. "lakini kama haki haipo....basi Kristo hakufa"

kama haki ilikuwepo kupitia sheria, basi Kristo angelikuwa amekufa bure

"kama mtu angeweza kuwa mwenye haki kwa kushika sheria"

angelikuwa amekufa bure

"Kristo angekuwa hajafanya chochote kwa kufa kwake"

Galatians 3

Wagalatia 03 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Usawa katika Kristo

Wakristo wote wameungana kwa usawa na Kristo. Wala uzazi, wala jinsia, wala cheo, vyote havijalishi. Wote wako sawa na wenzake. Wote wako sawa machoni pa Mungu.

Mfano muhimu ya matamshi katika sura hii

Maswali ya uhuishaji

Paulo hutumia maswali tofauti mengi ya uhuishaji katika sura hii. Anayatumia kuwashawishi Wagalatia juu ya dhambi zao. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Mwili

Hili ni suala ngumu. "Mwili" inaweza kuwa mfano ya asili yetu ya dhambi. Paulo hafundishi kwamba sehemu ya kimwili ya mwanadamu ni ya dhambi. "Mwili" hutumiwa katika sura hii kutofautisha na yale ambayo ni ya kiroho. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#flesh)

"Wale wa imani ni watoto wa Abrahamu"

Wasomi wamegawanyika juu ya maana ya maneno haya. Baadhi yao wanaamini kama Wakristo wanarithi ahadi ambazo Mungu alimpa Abrahamu, kwa hiyo Wakristo wanachukua nafasi ya wazao wa Israeli. Wengine wanaamini kama Wakristo hufuata Abrahamu kiroho, lakini hawarithi ahadi ambazo Mung alimpa Abrahamu. Kwa kuzingatia mafundisho mengine ya Paulo na muktadha hapa, Labda Paulo anaandika hivi kuhusu Wakristo wa Kiyahudi na wa Mataifa walio na imani sawa na Abrahamu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#spirit and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

<< | >>

Galatians 3:1

Sentensi unganishi:

Paulo anawakumbusha waumini wa Galatia kwamba Mungu aliwapa Roho wa Mungu wakati walipoamini injili kwa imani, siyo kwa matendo yao ya kushika sheria

Maelezo ya jumla

Paulo anawakemea Wagalatia kwa kuwauliza swali la uchokozi na Kejeli

Nani amewawekea uchawi?

Paulo anatumia swali la uchokozi kwa kusema kuw Wagalatia wanatenda kama kuna ameweka laana au uchawi. Haamini kwa hakika kwamba mtu mmoja ameweka uchawi kwao. "Mnaenenda kana kwamba mtu amewawekea uchawi"

Mimi nataka tu kufahamu hili kutoka kwenu

Huu ni mwendelezo wa hoja kutoka mstari 1. Paulo anajua majibu ya maswali anayoyauliza.

Mlimpokea Roho kwa matendo ya sheria au kwa imani ambayo mliisikia?

"Mlimpokea Roho, si kwa matendo kama sheria isemavyo, lakini kwa kuamini kile mlichosikia."

Je ninyi ni wajinga?

Swali hili lenye jibu linaonesha mshangao wa Paulo na hata hasira yake kwa Wagalatia Wagalatia ni wajinga. "Ninyi (wingi) mu wajinga kweli!" .

katika mwili

Neno mwili ni lugha ya picha linalomaanisha juhudi. "kwa juhudi zako" au "kwa kazi yako mwenyewe."

Galatians 3:4

Je mmeteseka kwa mambo mengi bure?

Paulo anauliza swali hili kuwakumbusha Wagalatia kwamba wakati walikuwa wakiteseka, wal wakiamini kuwa watakakalenye jibu kuwakumipoamibusha Wagalatia kwa maisha magumu waliyoteswa nayo.

Mmteseka sana na mambo mengi kwa bure

inaweza kuelezwa kwa uwazi kuwa waliteseka kwa mambo haya kwasababu ya watu waliopinga imani yao ndani ya Yesu. "Je umeteseka bure kwa mambo mengi kwa ajili ya ya wale wanaowapinga nyie kwasababu ya imani yenu katika Kristo." "Mlimwamini Yesu, na mmeteseka kwa mambo mengi kutoka kwa wale wanaomping Kristo." "Je imani na mateso yenu ni bure"

kwa bure

"isiyofaa" au "pasipo na matumaini ya kupokea kitu chochote"

kama kweli ilikuwa bure?

Maana zinazokubalika 1) Paulo anatumia swali hill kuwaonya ili kazi yao isiwe ya bure. "Msiifanye kazi isiyo na faida au msiache kuamini katika Yesu Kristo na mkayacha mateso yenu yakawa ya bure." 2) Paulo anatumia swali hili kuwaaminisha kuwa mateso yao si bure. "kwa kweli si bure."

Je yeye atoaye Roho kwenu na kutenda matendo ya nguvu kati yenu hufanya kwa matendo ya sheria au kwa kusikia pamoja na imani?

Paulo anatumia tena swali kuwakumbusha Wagalatia jinsi watu wanavyompokea Roho. "Hafanyi hivyo kwa matendo ya sheria, anafany kwa kusikia pamoja na imani."

kwa matendo ya sheria

Hii inawakilisha watu wanaofanya matendo yatokanayo na matakwa ya sheria. "Kwasababu unafanya yale unayoagizwa na sheria kufanya."

kusikia kwa imani

Lugha yako yaweza kuhitaji kuwa na maneno ya wazi kuelezea kile watu walichokisikia kutoka kwa mtu wanayemwamini. "kwasababu uliusikia ujumbe na kumwamini Yesu" au " kwasababu uliusikiliza ujumbe na kumtumaini Yesu."

Galatians 3:6

Sentensi unganishi:

Paulo anawakumbusha Waumini wa Galatia kwamba hata Ibrahimu aliipokea haki kwa imani na siyo kwa sheria.

ilihesabiwa kwake mwenye haki

Mungu aliiona imani ya Ibrahimu katika Mungu, hivyo Mungu alimhesabia Ibrahimu haki.

ambao wanaamini ( wenye imani)

"watu walioamini" Maana ya nomino 'imani' laweza kuelezwa kwa kitenzi 'kuamini" "wale wanaoamini"

watoto wa Ibrahimu

inawakilisha watu wale ambao Mungu huwatazama kama alivyomtazama Ibrahimu. "Mwenye haki kwa namna moja kama ya Ibrahimu."

tangulia kuwaona

Kwa sababu Mungu alimwahidi Ibrahimu na ikaandikwa kabla ahadi hiyo kuja kupitia Kristo, maandiko ni kama mtu ambaye huona muda ujao kabla ya kutokea. "Ilitabiriwa" au " kuona kitu kabla hakijatokea."

katika wewe

"Kwa sababu ya kile umekwisha tenda" au "kwasababu nimekwisha kukubariki" Neno wewe humrejelea Ibrahimu katika umoja.

mataifa yote

"makundi ya watu wote duniani". Mungu alikuwa akielezea kwa mkazo kwamba alikuwa hapendelei wayahudi tu, kundi alilolichagua. Mpango wake wa wokovu ulikuwa kwa wote wayahudu na wasio wayahudi.

Galatians 3:10

Wale ambao wanategemea matendo ya sheria wako chini ya laana

Kuwa chini ya laana inamaanisha kuwa umelaaniwa. Hapa inaonesha kuwa ni kuhukumiwa milele. " Wale wanaotegemea matendo ya sheria wamelaaniwa" au "Mungu atawahukumu hukumu ya milele wale ambao wanategemea matendo ya sheria"

Sasa ni wazi kwamba Mungu huhesabia

Kile kilicho wazi huelezwa dhahiri. "Maandiko yako wazi" au "maandiko yanafundisha wazi wazi."

Mungu hamhesabii haki hata mmoja kwa sheria,

kifungu hiki cha maneno kinaweza kuelezwa kwa kitenzi kitendaji. "Mungu hahesabu haki kwa mtu hata mmoja kwa njia ya sheria"

Mungu hamhesabii haki hata mmoja kwa sheria,

Paulo anasahihisha imani yao kwamba kama wangeitii sheria, Mungu angewahesabia haki. "Hakuna hata mmoja ambaye anaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu kwa kutii sheria" au "Mungu hamhesabii mtu haki kwa utiifu wao wa sheria."

wenye haki

Hii inarejelea watu wenye haki. "Watu wenye haki" au "Watu wale ambao Mungu huwaona ni wenye haki"

matendo ya sheria

"Lazima kufanya yote yanayosemwa na sheria "

ishi kwa sheria

Maanza zinazokubalika 1) Ni lazima kutii "ishi kulingana na" au "Jinyenyekeze kwa" au "salia mwaminifu kwa" au "tii" au "tekeleza"

wataishi kwa sheria

Maana zinazowezekana ni: 1) "lazima kuzitii sheria zote" 2) atahukumiwa kwa sababu ya uwezo wake wa kuishi kama vile sheria zinamwagiza kutenda"

Galatians 3:13

Sentensi unganishi:

Paulo anawakumbusha waumini hawa tena kwamba kutunza sheria kusingemwokoa mtu na kwamba sheria hazikuweza kuongeza hali mpya kwenye ahadi ya imani iliyotolewa kwa Ibrahimu.

kutoka laana ya sheria

Nomino "laana" inaweza kuelezwa kwa kitenzi "laani" kutoka katika laana ya sheria" au " Kutoka katika laana ya kutokutii sheria."

alikuwa laana kwa ajili yetu

Nomino "laana" inaweza kuelezwa kwa kitenzi "laani" "Kwa kulaaniwa kwa ajili yetu" au "Wakati Mungu alipomlaani badala yetu."

kutoka katika laana ya sheria wakati alipofanyika laana kwa ajili yetu......, "Amelaaniwa kila mtu ...

Laana katika muktadha huu inawakilisha hukumu. "kutoka katika hukumu ya sheria...alihukumia badala yetu ....amehukumia mtu yeyote"

kuangikwa juu ya mti

Paulo alitarajia hadhira yake kuelewa kwamba alikuwa akielezea kuangikwa kwa Yesu juu ya msalaba.

yaweza

"yawezekana" au "ita"

sisi

Neno 'sisi' linamjuisha Paulo pamoja na watu watakaosoma waraka huu.

Galatians 3:15

ndugu

Hapa inamaanisha Wakristo, kwa kujumuisha wanaume na wanawake wote, kwa kuwa waumini wote ndani ya Kristo ni washirika wa familia moja, na Mungu ndiye Baba yao wa mbinguni.

lugha za kibinadamu

"kama mtu" au "mambo ambayo watu wengi huyaelewa"

Sasa

Paulo anaonesha kuwa amejadili kanuni ya jumla na sasa anatambulisha jambo la kipekee.

kumaanisha wengi

"kumaanisha uzao wa mwingi"

kwa kizazi chako

Neno "chako" ni umoja, na unarejelea kwa mtu mmoja mahususi, ambaye ni uzao wa Ibrahimu ( na uzao huo unaainishwa kama "Kristo")

Galatians 3:17

Kwa kuwa kama urithi ungelikuja kwa njia ya sheria, usingekuwa tena umekuja kwa njia ya ahadi

Paulo anaongelea hali ambayo haipo ili kutia makazo kwamba urithi unakuja tu kwa njia ya ahadi. " Urithi unakuja kwetu kwa njia ya ahadi kwa sababu hatukuweza kutunza matakwa ya sheria za Mungu"

urithi

Ni kupokea kile ambacho Mungu kwa maneno awewaahidi waumini kama ulivyo urithi wa mali na utajiri kutoka kwa mwana familia,na baraka za milele na ukombozi.

Galatians 3:19

Sentensi unganishi:

Paulo anawaambia waumini wa Galatia sababu ya Mungu kuwapa sheria.

Kwanini tena sheria ilitolewa?

Paulo anatua swali katika kutambulisha mada ijayo anayotaka kuijadili. inaweza pia kutafsiriwa kama maelezo. "nitawaambia nini makusudi ya sheria. au "acheni niwaambie kwa kwanini Mungu aliwapa sheria?

Iliongezwa

Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mungu aliiongeza" au"Mungu aliongeza sheria"

Sheria iliwekwa katika shinikizo kupitia malaika kwa mkono wa mpatanishi

Hii inaweza kufasiriwa katika muundo tendaji. Mungu aliweka sheria kwa msaada wa malaika , na mpatanishi akaipisha au kuirasimisha"

Mpatanishi

mwakilishi

mpatanishi anaashiria zaidi ya mtu mmoja, lakini Mungu ni mmoja

Mungu alimwahidi Ibrahimu pasipo mpatanishi, lakini alimpa Musa sheria kupitia kwa mpatanishi. kutokana na hicho, wasomaji wa waraka wa Paulo walifikiri kwamaba sheria imeifanya ahadi isiwe na umuhimu. Paulo anaeleza kile ambacho wasomaji wake wanaweza kuwa wanafikiria. Naye atatoa maelezo yake katika mistari inayofuata.

Galatians 3:21

Maelezo ya jumla

Neno "sisi" linarejelea wakristo wote.

badala ya

"kinyume cha" au "katika mgongano na"

kama sheria ilikuwa imetolewa ilikuwa na uwezo wa kuleta uzima,

Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji, na nomino dhahania "maisha" inaweza kutafsiriwa na kitenzi "ishi" "Kama Mungu angekuwa ametoa sheria inayowawezesha wote walioishika kuishi, tungekuwa wenye haki kwa kushika sheria"

andiko limefunga mambo yote chini ya dhambi. Mungu alifanya hivi ili kwamba ahadi yake ya kutuokoa sisi kwa imani katika Yesu Kristo iweze kupatikana kwa wale wanaoamini.

Maana nyingine zinazowezekana ni: 1) "Kwa sababu wote tumetenda dhambi, Mungu aliweka mambo yote chini ya uongozi wa sheria kama kuwaweka katika kifungo, ili kwamba kile alichoahidi kwa hao ambao wenye imani katika Kristo Yesu aweze kuwapatia ambao wameamini" 2) "kwasababu tunatenda dhambi, Mungu ameweka mambo yote katika kifungo. Alifanya hivi kwasababu ya kile alichokiahidi katika Kristo Yesu awape wale wanaoamini"

maandiko

Paulo anayaona maandiko kama alikuwaa ni mtu anaongea na Mungu, ambaye aliyaandika maandiko "Mungu"

Galatians 3:23

Sentensi unganishi:

Paulo anawakumbushaWagalatia wote kwamba waumini wako huru katika familia ya Mungu, si watumwa chini ya sheria.

tulikuwa tumefungwa na kuwa chini ya sheria

kifungu hiki cha maneno kinaweza kuelezwa kwa kutumia muundo tenda. "sheria ilitufunga na tukawa kifunguni." au "sheria ilitunga gerezani."

tulikuwa tumefungwa na kuwa chini ya sheria

Kwa namna ambavyo sheria zilituongoza ni kana kwamba sheria alikuwa mlinzi wa gereza aliyetushikilia. "sheria zilituongoza mfano wa mlinzi wa gereza"

hadi ufunuo wa imani

Kifungu hiki cha maneno kinaweza kwa muundo tendaji. "mpaka Mungu alipodhihirisha kwamba huwahesabia wale wote wanaomtumaini Kristo" au "mpaka Mungu alipofunua kwamba huhesabia wale wote wenye imani katika Kristo"

mwangalizi

Neno hili ni zaidi ya "mtu yule anayemwangalia mtoto." huyu alikuwa ni Mtumwa aliyewajibika na usimamizi wa kanuni na mwenendo uliotolewa na wazazi, na ambaye alitakiwa kutoa taarifa kwa wazazi juu ya matendo ya mtoto.

mpaka Kristo alipokuja

"mpaka ule muda ambao Kristo alikuja"

ili tuweze kuhesabiwa haki

Mungu alikusudia kutuhesabia haki kabla ya ujio wa Yesu. Yesu alipokuja , alitekeleza kusudi lake la kutuhesabia haki. Inaweza kuelezwa kwa muundo tenda" "Kwamba Mungu angetutangaza kuwa wenye haki"

Galatians 3:27

wenyewe mmejivika Kristo

Maana zinazowezekana ni 1) "mmekuwa sawa kama na ubinadamu wa Kristo" au 2) " mmekuwa na mahusiano sawa na Mungu kama ya Kristo

Hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala huru, mwanaume wala mwanamke,

Mungu anaona kuwa hakuna utofauti kati ya wayahudi na wayunani, mtumwa na mtu huru, mwanamme na mwanamke.

warithi

Watu ambao Mungu amewapa ahadi wanaongelewa kama warithi wa mali na utajiri kutoka kwa mwana familia.

Galatians 4

Wagalatia 04 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivi kwa mstari wa 27, ambao umenukuliwa kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Uwana

Uwana ni suala ngumu. Wasomi wana maoni mengi juu ya uwana wa Israeli. Paulo anatumia uwana wa kufundisha jinsi kuwa chini ya sheria hutofautiana na kuwa huru katika Kristo. Si wote wa uzao wa Abrahamu ambao ni wao waliorithi ahadi za Mungu kwake. Uzazi wake tu kupitia Isaka na Yakobo walirithi ahadi. Na Mungu huweka katika familia yake wale tu wanaomfuata Abrahamu kiroho kupitia imani. Wao ni watoto wa Mungu wenye urithi. Paulo anawaita "watoto wa ahadi." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#inherit, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#promise, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#spirit and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#adoption)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Abba, Baba

"Abba" ni neno la Kiaramu. Katika Israeli ya kale, watu walitumia kwa usawa kutaja baba zao. Paulo "hufasiri" sauti zake kwa kuandika kwa herufi za Kigiriki. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-transliterate)

<< | >>

Galatians 4:1

Kauli Unganishi

Paulo anazidi kuwakumbusha wakristo wa Galatia kwamba Kristo alikuja kukomboa wale waliokuwa chini ya sheria, na kuwafanya wasiwe watumwa tena bali wana.

hakuna utofauti

"kuwa sawa na "

waangalizi

Watu wenye wajibu wa kisheria kuangalia watoto

wadhamini

ni watu wanaoaminiwa na wengine kutunza vitu vyenye thamani

Galatians 4:3

Maelezo ya jumla

neno 'sisi' linarejelea Wakristo wote, na wasomaji wa nyaraka wa Paulo

Kanuni za kwanza za ulimwengu

Maana zinazokubalika ni 1) inarejelea sheria na kanuni za kimaadili za ulimwengu 2) inarejelea nguvu za kiroho, ambazo baadhi ya watu wanadhani zinatawala kile kinachotokea duniani.

kukomboa

Paulo anatumia sitiari ya Mtu aliyenunua tena mali zake alizozipoteza au kumnunulia uhuru mtumwa. hii ni picha ya Yesu aliyelipa deni la dhambi za watu kwa kufa pale msalabani.

Mwana

Hili ni jina muhimu sana la Yesu, Mwana wa Mungu.

Galatians 4:6

ninyi ni wana.....si watumwa tne bali wana

Hapa Paulo anatumia neno la watoto wa kiume kwasababu ya jambo la Urithi.katika utamaduni wa wasomaji wake, urithi mara nyingi, lakini si mara zote, ulikuwa ni wa watoto wa kiume tu. Paulo alikuwa hapendelei watoto wa kiume na kuwatenga watoto wa kike hapa.

Mungu alimtuma Roho wa mwanawe ndani ya mioyo yetu, Roho aitaye, "Abba, Baba."

Mungu Baba amemtuma Roho wa Mwana wa Mungu katika mioyo ya waumini. Sasa wanajua kuwa anawapenda wakati wote kama baba mwema anavyowapenda watoto wake.

Kutumwa kwa Roho wa Mwanawe ndani ya mioyo yetu.

Neno moyo limetumika kuwakilisha sehemu ya mtu inayofikiria na kuhisi. "kutuma Roho ya Mwana wake kutuonyesha jinsi ya kufikiri na kutenda"

Mwana

Hiki ni jina muhimu la Yesu, Mwana wa Mungu.

Anayeita

Roho ndiye anayeita

Abba, baba

Hii ni namna ya mtoto anavyojieleza kwa baba yake katika lugha aliyokuwa akiitumia Paulo, ingawa si katika lugha iliyokuwa ikitumiwa na wasomaji wa Galatia. Ili kutunza lugha hiyo ngeni ni vema kulitafasiri kama linavyosikika kama "Abba" ikiwa lugha yako inavyoruhusu.

wewe si mtumwa tena bali ni mwana

Paulo anawazungumzia wasomaji wake kana kwamba ni mtu mmoja, 'wewe' huu ni umoja.

warithi

Watu ambao Mungu amewapa ahadi wanaongelewa kama warithi wa mali na utajiri kutoka kwa mwana familia

Galatians 4:8

Sentense unganishi

Paulo anawakumbusha tena wasomaji wake kuwa wanajaribu tena kuishi chini ya sheria badala ya kuishi kwa imani.

Maelezo ya jumla

Hapa Paulo anaendelea kuwakemea Wagalatia kwa kuwauliza maswali ya kejeli, yasiyohitaji majibu

Mnajulikana na Mungu

inaweza pia kuelezwa kwa muundo tendaji kama "Mungu anawajua"

kwa nini mnarejea tena... kanuni?

Hili swali la kwanza kati ya maswali mawili yanayo na majibu ndani yake. "Kuwa msirejee tena nyuma katika kanuni za awali."

Kanuni za awali

Maana zinazokubalika ni 1) inarejelea sheria na kanuni za kimaadili za ulimwengu 2) inarejelea nguvu za kiroho, ambazo baadhi ya watu wanadhani zinatawala kile kinachotokea duniani.

Mnataka kuwa watumwa tena?

Swali hili laweza kutafsiriwa kama maelezo tu "Hamtakiwi kuw mtumwa tena" au "Inaonyesha kuwa mnataka kuwa watumwa tena."

Galatians 4:10

mnashika kwa uangalifu siku amaalumu, miandamo ya miezi, majira, na miaka

Paulo anazungumzia juu yao kuwa waangalifu katika kusherehekea vipindi/nyakati fulani, wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wenye haki. "mko makini katika kusherehekea siku na miandamo ya miezi na majira na miaka"

mnajitaabisha bure

"kuwa katika hali ya kutofaa, "bila mafanikio" au "kukosa faida"

Galatians 4:12

Sentensi unganishi

Paulo anawakumbusha waumini wa Galatia jinsi walivyokuwa wema katkia kumhudumia wakati akiwa pamoja nao, na anawatia moyo kuendelea kumtumaini hata wakati asipokuwa pamoja nao.

Sihi

Neno hili linamaanisha kuomba kwa nguvu. Hili si neno lililotumika kuomba pesa, chakula au kitu kingine chochote cha mahitaji.

Ndugu

Hapa linamaanisha wakristo wote wa kike na wakiume, ndugu walio katika Kristo ni washirika wa familia moja ya kiroho, pamoja na Mungu Baba yao wa mbinguni.

Hamjanitenda kosa

kwa kutumia maneno haya, Paulo anatilia mkazo kwa Wagalatia walihudumia vizuri sana "Mlinitunza vizuri sana", au "mlinitunza kama mlivyopaswa"

Ingawa afya yangu iliwaweka katika jaribu

"Ingawa ilikuwa vigumu kuniona mimi wakati nikiwa mgonjwa"

kudharau

kuchukia sana

Galatians 4:15

Nimekuwa adui kwenu kwa kuwambia ukweli?

Mnaonekana kufikiri kuwa nimekuwa adui yenu kwa kusema ukweli kwenu?

Galatians 4:17

Kwa huruma wanawatafuta...muwafuate...

"kuwashawishi ili muungane pamoja nao. Paulo anaonyesha nia ya walimu wa uongo iliyokuwepo, walionyesha huruma kwa Wagalatia ili wawafuate wao kwa lengo la kuwaondoa kwenye kweli.

kuwatenganisha

"kuwatenganisha ninyi na mimi" au "kuwafanya mwache kuwa waaminifu kwangu"

kwa shauku

Shauku ya Kufanya kile wanachowaambia

Galatians 4:19

Sentensi unganishi

Paulo anawaambia waumini kwamba neema na sheria haziwezi kufanya kazi kwa pamoja.

Watoto wangu wadogo

Hii ni sitiari kurejelea wanafunzi au wafuasi. " Ninyi mlio wanafunzi kwasababu yangu."

Nateseka kwa uchungu mkali kama wa mwanamke azaapo mpaka Kristo aumbike ndani yenu.

Paulo anatumia neno 'uchungu" kama lugha ya picha kuonesha namna alivyojihusisha na Wagalatia. "Niko katika mateso ni kana kwamba nimekuwa mwanamke aliyeshikwa na utungu wa kuwazaa, na nitaendelea kuwa katika mateso mpaka Kristo atakapowatawala maisha yenu kikweli kweli.

Galatians 4:21

Niambieni

Ni hali ya kutaka kuuliza swali au ninataka kuwaambia jambo fulani

Hamsikii sheria isemavyo?

Paulo anatoa utangulizi kwa jambo analokusudia kulisema baadaye. "Mnapaswa kujifunza vile sheria isemavyo" ama "niwaeleze sheria isemavyo"

Galatians 4:24

Sentensi unganishi

Paulo anaanza habari kwa kueleza ukweli kuwa neema na sheria haziwezi kuwa sehemu moja kwa pamoja na kwa wakati mmoja.

Mambo haya yanaweza kuelezwa kwa kutumia mfano,

"Habari hii ya wana wawili ni picha hii ya kile ninachowambieni sasa."

mfano

Mfano ni namna ya kiuandishi uliotumika kutoa maana fulani, mfano; watu na vitu vimetumika kuwakilisha vitu vingine au maana fulani. Katika mfano huu wa Paulo, wanawake wawili wametumika kurejelea aina mbili za maagano 4:21.

Mlima Sinai

Mlima Sinai umetumika kama kiwakilishi cha sheria. Ni mahali Musa alipopokea mbao mbili za sheria kwa ajili ya wana wa Waisrael.

Huzaa watoto ambao ni watumwa

Paulo anaiona sheria kama vile ni mtu. Watu waliochini ya agano la sheria ni watumwa wanaopaswa kuitii sheria.

Fananishwa

Ni mifano yenye kutoa picha ya kuleta maana fulani.

Yuko katika utumwa pamoja na watoto wake

Hajiri ni mtumwa na watoto wake wako utumwani pamoja naye. Yerusalemu ni kama Hajiri na watoto wake ni watumwa pamoja naye.

Galatians 4:26

Huru

Hapa huru inamaanisha hali ya kutofungwa, kutokuwa mtumwa.

Furahi

Changamka, shangilia, kuwa na furaha.

uliye tasa, wewe usiye zaa...... wewe ambaye huna uzoefu wa kuzaa.

Neno hili 'wewe' kwa hapa linamrejelea mwanamke tasa na liko katika hali ya umoja.

Galatians 4:28

Ndugu

Neno linalomaanisha wafuasi wa Kristo wote wa kiume na wa kike. Waumini wote wa Yesu Kristo ni jamii moja na familia moja ya kiroho iko pamoja na Mungu Baba yao wa mbinguni.

watoto wa ahadi

Maana zinazokuballika kwa Wagalatia kuwa watoto wa Mungu ni 1) kwa kuziamini ahadi za Mungu 2) kwasababu Mungu anatenda miujiza katika kutimiza ahadi zake kwa Ibrahimu, kwanza kwa kumpa Ibrahimu mwana na pia kwa kuwafanya Wagalatia watoto wa Ibrahimu na wa Mungu pia.

Kutokana na mwili

Neno hili linafafanua kitendo cha Ibrahimu kuwa Baba wa Ishmael kwa kumtwaa Hajiri kuwa mke wake. "Kwa matendo ya kibinadamu" au 'Kwasababu ya kile watu walichokifanya."

Kutokana na Roho

Kwasababu ya uongozi wa Roho katika kutimiza mapenzi yake.

Galatians 4:30

Ndugu

Neno linalomaanisha wafuasi wa Kristo wote wa kiume na wa kike. Waumini wote wa Yesu Kristo ni jamii moja na familia moja ya kiroho iko pamoja na Mungu Baba yao wa mbinguni.

bali ni wa mwanamke huru

Maneno yaliyoachwa nje yanaweza yakapachikwa hapa "lakini badala yake, sisi ni watoto wa mwanamke huru."

Galatians 5

Wagalatia 05 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Paulo anaendelea kuandika juu ya sheria ya Musa kama kitu kinachomtega mtu au kumfanya mtumwa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses)

Dhana maalum katika sura hii

Tunda la Roho

aneno "tunda la Roho" sio wingi, ingawa huanza orodha ya vitu kadhaa. Watafsiri wanapaswa kuweka fomu ya umoja ikiwezekana. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#fruit)

Mfano muhimu ya matamshi katika sura hii

Mifano

Paulo anatumia mifano kadhaa katika sura hii ili kuonyesha pointi zake na kusaidia kuelezea masuala magumu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Ninyi mmekatwa kutoka kwa Kristo, ninyi mtakaohesabiwa haki na sheria, hamna tena neema."

Wasomi wengine wanafikiri kama Paulo anafundisha kwamba kutahiriwa husababisha mtu kupoteza wokovu wake. Wataalamu wengine wanafikiri kama Paulo anamaanisha kwamba kutii sheria ili kujaribu kupata haki na Mungu utamzuia mtu kuokolewa kwa neema. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#grace)

<< | >>

Galatians 5:1

Sentensi Unganishi

Paulo anatumia mfano kwa kuwakumbusha waumini kutumia uhuru wao katika Kristo kwa sababu sheria yote imekamilika katika kumpenda jirani kama sisi wenyewe.

Ni kwa Uhuru

Tafsiri inahitaji kusisitiza "uhuru" kinyume cha utumwa uliozungumzwa katika mistari iliyotangulia

Ni kwa uhuru ambao Kristo ametuweka sisi huru

"ili kwamba tuweze kuwa kuwa huru maana Kristo ametuweka huru"

simameni imara

kusimama imara hapa inawakilisha hali ya kutobadilika. Hali ya kutobadilika inaweza kuelezwa kwa uwazi. "msikubali hoja za watu wengine wanaowafundisha vitu tofauti" au " dhamirieni kuwa huru"

kama mtakuwa mmetahiriwa

Paulo anatumia neno 'tohara' kama lugha ya mfano au picha kumaanisha dini ya kiyahudi. "Kama mtarudi kwenye Dini ya Kiyahudi"

Galatians 5:3

shuhudia

"tangaza" au "tumika kama shahidi"

kwa kila mtu aliyetahiriwa

Paulo anatumia neno 'tohara' kama kwa kumaanisha hali ya kuwa Myahudi. "kwa kila mtu ambaye amekuwa Myahudi"

wajibika

"amefungwa" au "zuiliwa" au "kufanywa kuwa watumwa"

Ninyi mmetengwa ktoka kwa Kristo

"Ninyi mmekomesha au kusitisha uhusiano wenu na Kristo"

ninyi wote "mnaohesabiwa haki" kwa sheria

Paulo anaongea kwa kinyume hapa. Anafundisha hasa kwamba hakuna Myahudi anayeweza kuhesabiwa haki kwa kufanya matendo yanayotakiwa na sheria. "ninyi wote mnaodhani mnaweza kuhesabiwa haki kwa kufanya matendo yanayotakiwa na sheria" au " ninyi mnataka kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria"

Ninyi mmeanguka mbali na neema

Yule anayetoa neema anaweza kuelezwa kwa uwazi zaidi. "Mungu hatawaonesha neema yake kwenu"

Galatians 5:5

Maelezo ya jumla

hapa, neno 'sisi' linarejelea kwa Paulo na wale wanaopinga tohara ya Wakristo. Yeye bila shaka wakiwemo na Wagalatia.

Kwa kuwa

"Hii ni kwa sababu"

kwa imani, tunasubiri tumaini la haki

Maana zinazokubalika ni 1) "Tunasubiri kwa imani tumaini la haki" au 2) "tunasubiri tumaini la haki ambalo linakuja kwa imani."

tunasubiri kwa hamu tumaini la haki

"Tunasubiri kwa uvumilivu na kwa shauku kuwa Mungu atatufanya wenye haki pamoja naye milele, na tunamtarajia kuwa Mungu atafanya hivyo.

kutahiriwa au kutokutahiriwa

maneno ya mfano yakimaanisha kuwa Myahudi or Mmataifa yaani asiye myahudi. "si kwa kuwa myahudi au kutokuwa myahudi"

Ni imani pekee inayofanya kazi kupitia upendo

"Badala ya hiyo, Mungu anajishughulisha na imani yetu katika yeye, ambayo tunaionesha kwa kuwapenda wengine

humaanisha kitu

ina thamani

Mlikuwa mnapiga mbio

"Mlikuwa mnafanya kile mlichofunzwa na Yesu"

Ushawishi wa kufanya hivyo hautoki kwake yeye anayewaita ninyi

"Yule anayewashawishi kufanya hivyo siyo Mungu, anayewaita"

yeye anayewaita

kusudi la kuwaita laweza kuelezwa hapa wazi. "yeye aliyewaita muwe watu wake"

ushawishi

Kumshawishi mtu fulani ni kumfanya mtu huyo abadili kile anachoamini na hivyo kutenda tofauti.

Galatians 5:9

hamtafikiri kwa njia nyingine yoyote

"hamtaamini kitu chochote totauti na kile ninachowaambia"

yeyote yule atakayepotosha atabeba hukumu

" Mungu atamwadhibu mtu huyo anayewapotosha na kuwasumbua"

Anayewapotosha ninyi

"anayesababisha ninyi mkose uhakika wa kipi ni kweli" au "kuinua shida miongoni mwenu"

Yeyote awaye

Maana zinazokubalika ni 1) Paulo hajui majina ya watu wanaowaambia Wagalatia kwamba wanahitaji kutii Sheria ya Musa au 2) Paulo hataki Wagalatia washughulike kujua kama wale wanaowasumbua ni matajiri au maskini au wakubwa au wadogo au wenye au wasio na dini

Galatians 5:11

Ndugu, kama naendelea kutangaza tohara, kwa nini bado ninateswa?

Paulo anaelezea hali ambayo haipo kwa kukazia kuwa watu wanamtesa kwasababu hahubiri watu wawe wayahudi. Hii yaweza pia kuelezwa kwa muundo tendaji. " ndugu mwaweza kuona kuwa siendelei kutangaza habari za tohara kwa sababu wayahudi wananitesa"

Ndugu

"Ndugu." Neno la kiswahili "ndugu" linamaanisha watu wa kike na wa kiume.

Kwa suala hilo kile ambacho ni kizuizi cha msalaba kitaweza kuharibiwa

Paulo anaelezea juu ya hali ambayo haipo ili kukazia kwamba watu wanamtesa kwasababu anahubiri kwamba Mungu huwasamehe watu kwasababu ya kazi ya Yesu juu ya msalaba.

jambo hilo

"kama ningekuwa bado ninasema kwamba watu wanatakiwa kuwa wayahudi"

kizuizi cha msalaba kimeondolewa

msemo huu waweza kuelezwa kwa muundo tenda: kwamba ujumbe kuhusu msalaba hauna kizuizi" au " hakuna kizuizi chochote katika mafundisho ya msalaba yanaweza kuwafanya watu wajikwae."

kizuizi cha msalaba kimeondolewa

kujikwaa inawakilisha hali ya kutenda dhambi, na kizuizi inamaanisha kitu kile kinachowafanya watu watende dhambi. katika jambo hili, dhambi ni kuukataa ukweli wa mafundisho kwamba watu wanatakiwa kuamini kuwa Yesus Kristo alikufa msalabani ili watu wawe na haki mbele za Mungu. "Mafundisho juu ya msalaba yanayowafanya watu kuukataa ukweli yamekwisha kuondolewa"

watajihasi wenyewe

Maana zinazokubalika ni 1) kukata viungo vyao vya kiume ili wawe matowashi au 2) kujikata au kujiondoa wenyewe kutoka katika ushirika wa watu wa Mungu

Galatians 5:13

Kwa kuwa

Paulo anatoa sababu kwa maneno yake yaliyo katika 5:11:

Mmeitwa katika uhuru

kifungu hiki cha maneno chaweza kuelezwa katika muundo tendaji. "Mungu amewaita katika uhuru"

Mungu amewaiteni ninyi kwenye uhuru.

Maana zinazokubalika ni 1) Mungu amewachagua ninyi kuwa watu wake ili kwamba muwe huru au 2) Mungu ameamuru ninyi muwe huru.

Ndugu

Ndugu hurejea kwa wakristo wa " kiume na wa kike"

fursa kwa ajili ya mwili

"nafasi ya kufanya kile kinachoridhisha asili yenu ya dhambi," Hii inarejelea hasa vitu ambavyo vinaleta madhara kwa mtu mwenyewe binafsi au majirani

sheria yote imekamilika katika amri moja

Maana zinazokubalika ni 1) "unaweza kueleza sheria yote katika amri moja, ambayo ni hii" au 2) kwa kutii amri moja, unatii amri zote, na hiyo amri ni hii."

Ni lazima umpende jirani yako kama wewe mwenyewe

maneno "wewe," "yako," na "wewe mwenyewe" yote yako katika umoja

Galatians 5:16

Sentensi unganishi

Paulo anaeleza jinsi Roho anavyo na mamlaka dhidi ya dhambi

tembea kwa kwa Roho

Kutembea ni mfano wa kuishi. "enendeni katika maisha yenu katika nguvu za Roho Mtakatifu" au "ishi maisha yako kwa kumtegemea Roho"

hamtazitimiza tamaa za mwili

"hamatazifanya dhambi ambazo mnataka kuzifanya kwa sababu mko binadamu"

hamko chini ya sheria

Hamuwajibiki kutii sheria ya Musa

Galatians 5:19

matendo ya mwili

Paulo anatumia neno "mwili" kama sitiari au mfano unaowakilishi asili ya mwanadamu."mambo yanayofanywa kama matokeo ya utu wa dhambi ya asili ya mtu"

kurithi

Kupokea kile ambacho Mungu amekwisha kuwaahidi waumini kama kurithi mali na utajiri kutoka kwa mwana familia.

Galatians 5:22

tunda la Roho ni upendo...kiasi

Paulo anatumia sitiari kuonesha kile ambacho watu wanaweza kukiona kwa watu wengine. "Watu ambao wanaongozwa na Roho wataonesha upendo ...kiasi kama vile mti unavyozaa tunda."

tunda la roho

Ni kile ambacho Roho huzalisha"

wameusulibisha mwili pamoja na shauku na tamaa zake mbaya

Paulo anaongelea Wakristo ambao huzuia tamaa mbaya kana kwamba tamaa hizo walikuwa ni watu ambao wakristo walikuwa wakiwaua. "tumeua asili yetu ya dunia pamoja na tamaa na hamu zake mbaya kana kwamba tumezisulubisha kwenye msalaba."

Galatians 5:25

Kama tukiishi kwa Roho

"Tangu Roho wa Mungu alipotufanya kuwa hai"

tembea kwa Roho

Neno 'kutembea' ni sitiari kuonesha maisha ya kila siku. "mruhusu Roho Mtakatifu awaogoze ili kwamba tufanye mambo yanayompendeza na kumheshimu Mungu.

tu

"tunapaswa"

Galatians 6

Wagalatia 06 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Sura hii inahitimisha barua ya Paulo. Maneno yake ya mwisho yanashughulikia masuala ambayo hayaonekani kuwa yameunganishwa na barua yake yote.

Ndugu

Paulo anaandika maneno katika sura hii kwa Wakristo. Anawaita "ndugu." Hii inahusu ndugu za Paulo wa Kikristo na sio ndugu zake wa Kiyahudi.

Dhana maalum katika sura hii

Uumbaji Mpya

Watu ambao wamezaliwa tena ni uumbaji mpya katika Kristo. Wakristo wamepewa uzima mpya katika Kristo. Wana asili mpya ndani yao baada ya kuwa na imani katika Kristo. Kwa Paulo, hii ni muhimu zaidi kuliko ukoo cha mtu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#bornagain and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Mwili

Hili ni suala ngumu. "Mwili" inatofautishwa na "roho." Katika sura hii, mwili pia hutumiwa kutaja mwili halisi. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#flesh and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#spirit)

__<< | __

Galatians 6:1

sentensi Unganishi

Paulo alifundisha waamini jinsi wanavyopaswa kuwatendea waamini na jinsi Mungu anavyowapa thawabu.

Ndugu

Lina maana ya jamaa ya Wakristo ikijumuisha kwa pamoja wanaume na wanawake, kwa kuwa waamini wote ndani ya Kristo ni wana familia moja ya kiroho na Mungu akiwa Baba yao wa mbinguni.

Ikiwa mtu

"ikiwa mtu mmoja" au "mtu mmoja wapo miongoni mwenu"

amekamatwa katika makosa/dhambi

Maana zinazokubalika hapa ni 1) mtu amepatikana katika tendo, " amekamatwa katika kitendo cha dhambi," au 2) mtu amefanya dhambi bila kudhamiria kufanya uovu," ''amefanya dhambi."

ninyi mlio wa kiroho

"wale wanaoongozwa na Roho" au " ninyi mnaoishi chini ya uongozi wa Roho"

mrejeshe huyo mtu

"msahihishe huyo mtu aliyefanya dhambi" au "mtie moyo aliyefanya dhambi aweze kurudia mahusiano sahihi na Mungu."

katika roho ya upole

Maana zinazokubalika 1) Roho anamwelekeza mtu mwenye kutoa masahihisho au 2)" kwa mtazamo wa upole" au kwa njia ya upole" au "kwa hali ya uzuri".

Huku ukijiangalia mwenyewe

maneno haya yanahusu Wagalatia kana kwamba ni mtu mmoja, lengo ni kutilia mkazo kwamba anaongea na mtu mmoja binafsi. "Jiangalie binafsi" au "ninamwambia kila mmoja wenu" "Jiangalie mwenyewe"

ili msijaribiwe

Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. ''ili kwamba kisiwepo kitu cha kuwajaribu ninyi kutenda dhambi"

Galatians 6:3

ikiwa

"Kwa sababu." Hii neno inaonyesha kwamba maneno anayosema baadaye yatoa sababu za kwa nini Wagalatia lazima 1) "kuchukuliana mizigo" 6:1 au 2)kuwa waangalifu ili na wao wenyewe wasije wakajaribiwa (6:1) au " wasije wakajivuna (5:1)

yeye ni kitu

yeye ni mtu muhimu 'au' yeye ni bora kuliko ya wengine

Yeye si kitu

Yeye si muhimu 'au' hana bora kuliko ya wengine

Kila mmoja anapaswa

"Kila mtu lazima"

kila mmoja ataubeba mzigo wake mwenyewe

Kila mtu atahukumiwa kwa kazi yake mwenyewe tu' au 'kila mtu atawajibika kwa kazi yake mwenyewe tu"

kila mmoja ata..

"Kila mtu ata..."

Galatians 6:6

Mmoja wapo

"Mtu"

neno

Hapa hii ina maana kila kitu ambacho Mungu amesema au ameamuru, kama "neno la Mungu" au "ujumbe wa kweli."

Kila apandacho mtu, ndicho atakachovuna pia

kupanda kunamaanisha kufanya jambo fulani ambalo matokeo yake yanafanana na kitendo chenyewe. kuvuna inawakilisha matokeo ya kile ambacho mtu amefanya. "kama vile mkulima avunavyo matunda ya kile kile alichokipanda. hivyo basi, kila mtu atapata matokeo ya kile anachokifanya.

Mtu ... yake

Paulo habainishi wanaume hapa. AT "mtu ... mtu huyo"

kupanda katika mwili wake

Neno 'mwili' ni lugha ya pich kuonesha asili ya dhambi ya mtu. "hupanda mbegu sawa na matakwa ya dhambi ya asili" Anafanya mambo asili yake ya dhambi anataka kufanya"

atavuna uharibifu kutokana na mwili wake

'Atapokea adhabu kwa ajili ya kile kilichofanywa na mwili wake wenye dhambi '

kupanda katika Roho

"Anafanya mambo ya Roho wa Mungu apendayo"

Atavuna uzima wa milele kutoka kwa Roho

'Kupokea uzima wa milele kama zawadi kutoka kwa Roho wa Mungu'

Galatians 6:9

Tusichoke katika kutenda mema

"Tunatakiwa kuendelea kutenda mema"

kutenda mema

kufanya mema kwa ustawi wa watu wengine

wakati wake

"kwa wakati muafaka" au " kwa wakati ambao Mungu ameuchagua"

Hivyo basi,

"kama matoke ya" au "kwasababu ya "

hasa kwa walio

"hasa kwa wale" au "mahususi kwa wale"

walio ndani ya imani

"kwa wale walio wana familia ya Mungu kupitia imani katika Yesu"

Galatians 6:11

Sentensi kiunganishi

Paulo akikaribia kufunga waraka wake, anawakumbusha jambo moja zaidi kwamba sheria haiokoi na kwamba wanatakiwa kuumbuka msalaba wa Yesu

barua kubwa

Hii inaweza kumaanisha kwamba Paulo anasisitiza 1)maelezo yanayofuata au 2) kwamba barua hii ilitoka kwake.

kwa mkono wangu

Maana zinazokubalika 1)Huenda Paulo alikuwa na msaidizi ambaye aliandika mambo mengi katika barua hii kama vile Paulo alimwambia kuandika, lakini Paulo mwenyewe aliandika sehemu hii ya mwisho ya barua au 2) Paulo aliandika barua hii yote yeye mwenyewe.

kufanya mema kwa kuwashawishi

"kuwafanya wengine wawafikirie vizuri" au kuwafany wengine wafikiri kuwa wao ni watu wazuri"

katika mwili

"kwa ushahidi wa kuonekana" au " kwa juhudi zao"

kulazimisha

"kushurutisha" au kushawishi kwa nguvu"

Wanafanya hivyo kwa sababu wasiingie kwenye mateso ya msalaba wa Kristo

"ili kwamba Wayahudi wasiwatese kwa kusema kuwa msalaba wa Kristo pekee huokoa watu"

msalaba

Msalaba hapa unawakilisha kile ambacho Kristo alifanya kwa ajili yetu alipokufa pale msalabani. "Kazi aliyoifanya juu ya msalaba" au " kifo na ufufuo wa Yesu"

wanataka

"watu wale wanaowataka nyie mtahiriwe"

ili waweze kujivunia miili yenu

"ili kwamba wajivune kwa kuwa watakuwa wamewaongeza kwa watu wale wanaoshika sheria."

Galatians 6:14

Isitokee nikajivuna isipokuwa kwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo

"sitaki kujivunia kitu chochote zaidi ya msalaba"

ulimwengu umesulubiwa kwangu

Tungo hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji: "Ninadhani duniani tayari imekwisha kufa" au " naichukulia dunia kama ni mharifu ambaye Mungu amemuua msalabani"

kwa ulimwengu

maneno "nimesulubiwa" yanaeleweka vizuri kutoka na maneno yaliyotangulia kabla ya haya. " na nimesulubishwa katika ulimwengu"

kwa ulimwengu

Maana zinazokubalika ni) Ulimwengu unadhania kuwa mimi tayari nimeshakufa" au "dunia inanichukulia mimi kama mharifu ambaye Mungu amemuua msalabani"

Ulimwengu

maana zinazokubalika ni 1) watu wa dunia, wale ambao hawamjali Mungu au 2) mambo yale ambayo watu wasiomjua Mungu hufikiri ni ya muhimu.

kuwa si kitu

"ni muhimu" kwa Mungu

uzao mpya

maana inawezekana ni 1) muumini mpya katika Yesu Kristo au 2) maisha mapya katika muumini.

amani na rehema juu yao, na Israeli wa Mungu

maana zinazoweza kukubalika ni 1) kwamba waumini kwa ujumla ni Israeli ya Mungu au 2) "amani na rehema ziwe juu ya waamini wa Mataifa na juu ya Israeli ya Mungu " au 3) "amani na iwe juu ya wale wanaofuata kanuni , na inaweza rehema ziwe hata juu ya Israeli ya Mungu. "

Galatians 6:17

Tangu sasa

Hii inaweza kumaanisha "mwisho" au "kwa kuhitimisha barua hii"

mtu yeyote asinitaabishe

Maana zinaweza kukubalika ni 1) Paulo anawaamuru Wagalatia wasimtaabishe "Ninawaamuru kwamba : "msinitaabishe" au 2)Paulo anawaambia Wagalatia kwamba anaagiza watu wote wasimtaabishe. "Ninamwamuru kila mmoja kwamba: usinitaabishe" au 3) Paulo anaeleza matakwa yake, "sitaki mtu yeyote anitaabishe"

kunitesa mimi

Maana zinazokubalika ni 1) "kuniambia mambo haya" au 2) kunisababishia matatizo" au "kunipa kazi ngumu."

maana nimebeba chapa za Yesu mwilini mwangu

"NIna makovuya vidonda katika mwili wangu kwa sababu ya huduma yangu kwa Yesu" au "Bado nina alama ya makovu katika mwili wangu kwasababu mimi ni mali ya Yesu"

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho

"Ninaomba kwamba Bwana Yesu atakuwa mwema katika roho zenu"

ndugu

Hapa neno 'ndugu' linamaanisha Wakristo, kwa kujumuisha wanaume na wanawake wote, kwa kuwa waumini wote ndani ya Kristo ni washirika wa familia moja, na Mungu ndiye Baba yao wa mbinguni.