Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa Waefeso

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha Waefeso

  1. Salamu na sala kwa baraka za kiroho katika Kristo (1:1-23)
  2. Dhambi na wokovu (2:1-10)
  3. Umoja pamoja na amani (2:11-22)
  4. Siri ya Kristo ndani yenu, amejulishwa (3:1-13)
  5. Maombi kwa ajili ya utajiri wa utukufu wake ili kuwafanya kuwa na nguvu (3:14-21)
  6. Umoja wa Roho, kujenga Mwili wa Kristo (4: 1-16)
  7. Maisha mapya (4:17-32)
  8. Waigaji wa Mungu (5:1-21)
  9. Wake na waume; watoto na wazazi; watumwa na mabwana (5:22-6:9)
  10. Silaha za Mungu (6:10-20)
  11. Salamu ya mwisho (6:21-24)

Nani aliandika kitabu cha Waefeso?

Paulo aliaandika Waefeso. Paulo alikuwa anatoka mji wa Tarso. Alijulikana pia kama Saulo mwanzoni. Kabla kuwa Mkristo, alikuwa Mfarisayo na kuwatesa Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo alitembea mara kadhaa kwa ardhi ya Warumi huku akiambia watu kuhusu Yesu.

Mtume Paulo alisaidia kuanzisha kanisa la Efeso wakati moja wa safari zake. Pia akaishi na Waefeso kwa mwaka moja na nusu akiwasaidia waumini. Pengine Paulo aliandika barua hii angali kwenye jela wa Roma.

Kitabu cha Waefeso ni kuhusu nini?

Paulo aliwaandikia barua hii Wakristo wa Waefeso kuwaeleza upendo wake Mungu kwao kupitia Yesu Kristo. Alieleza baraka Mungu alikuwa anawapa kwa sababu walikuwa wameunganishwa pamoja na Kristo. Aliwaeleza waumini wote kwamba walikuwa umoja na haikujari kama mtu ni Myahudi au Wayunani.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha asili, "Waefeso." Au wanaweza kuchagua kichwa wazi, kama "Barua ya Paulo kwa Kanisa la Efeso" au "Barua kwa Wakristo huko Efeso." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Je, ni nini "ukweli uliofichwa" katika Kitabu cha Waefeso?

Maneno yaliyotafsiriwa katika ULB kama "ukweli uliofichwa" au "uliofichwa" hutokea mara sita. Kwa hiyo Paulo alimaanisha kitu ambacho Mungu alipaswa kuwafunulia wanadamu kwa sababu hawakuweza kukijua wenyewe. Daima ilikuwa inahusu jinsi Mungu alivyopanga kuokoa wanadamu. Wakati mwingine ilikuwa juu ya mpango wake wa kufanya amani kati yake na wanadamu. Wakati mwingine ilikuwa juu ya mpango wake wa kuunganisha Wayahudi na Wayunani kupitia Kristo. Wayunani sasa wanaweza kufaidika na ahadi za Kristo wakiwa sawa na Wayahudi.

Je, Paulo alisema nini juu ya wokovu na kuishi kwa haki?

Paulo alisema mengi juu ya wokovu na kuishi kwa haki katika barua hii na katika barua zake nyingi. Alisema kuwa Mungu amekuwa na wema na kuwaokoa Wakristo kwa sababu wanaamini Yesu. Kwa hiyo, baada ya kuwa Wakristo, wanapaswa kuishi kwa njia ya haki ili kuonyesha kuwa wana imani katika Kristo. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

"Wewe" kutumika kwa umoja na wingi

Katika kitabu hiki, neno "Mimi" linamaanisha Paulo. Neno "nyinyi" ni karibu kila mara na linawakilisha waumini ambao wanaweza kusoma barua hii, isipokuwa: 5:14, 6:2, na 6:3. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-you)

Je, Paulo alimaanisha nini na "Upekee

Wakati Paulo alizungumza kuhusu "nafsi mpya" au "mtu mpya," alimaanisha hali mpya ambayo muumini anapokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hali hii mpya iliumbwa kwa mfano wa Mungu (Angalia: 4:24). Maneno "mtu mpya" hutumiwa pia kwa ajili ya Mungu kuleta amani kati ya Wayahudi na Wayunani. Mungu aliwaunganisha kama watu mmoja ambao ni wake (Tazama: 2:15).

Paulo alimaanisha nini na "nafsi mpya" au "mtu mpya"?

Wakati Paulo alizungumza kuhusu "nafsi mpya" au "mtu mpya," alimaanisha hali mpya ambayo muumini anapokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hali hii mpya iliumbwa kwa mfano wa Mungu (Angalia: 4:24). Maneno "mtu mpya" hutumiwa pia kwa ajili ya Mungu kuleta amani kati ya Wayahudi na Wayunani. Mungu aliwaunganisha kama watu mmoja ambao ni wake (Tazama: 2:15)

Je, mawazo ya "takatifu" na "takasa" yanawakilishwa vipi katika Waefeso katika ULB?

Maandiko hutumia maneno kama hayo ili kuonyesha yoyote kati ya mawazo mbalimbali. Kwa sababu hii, mara nyingi ni vigumu kwa watafsiri kuyawakilisha vizuri katika tafsiri zao. Katika kutafsiri kwa Kiingereza, ULB inatumia kanuni zifuatazo:

Wakati mwingine maana katika kifungu ina maana ya utakatifu wa maadili. Hasa muhimu kwa kuelewa injili ni matumizi ya "takatifu" kuonyesha ukweli kwamba Mungu anawaona Wakristo kama wasio na dhambi kwa sababu wameungana na Yesu Kristo. Matumizi mengine ya "takatifu" ni kueleza wazo kwamba Mungu ni mkamilifu na hana hatia. Matumizi ya tatu ni kueleza wazo kwamba Wakristo wanapaswa kuwa na mwenendo isiyo na hatia, na kasoro katika maisha yao. Katika hali hizi, ULB inatumia "takatifu," "Mungu mtakatifu," "watakatifu," au "watu watakatifu." (Angalia: 1:1, 4)

Wakati mwingine maana katika kifungu inaonyesha Wakristo bila kuashiria jukumu fulani wanalopaswa kufanya. Katika hali hizi, ULB inatumia "mwumini" au "waumini."

Wakati mwingine maana katika kifungu kinaashiria wazo la mtu au kitu kiichowekwa wakfu kwa Mungu pekee. Katika hali hizi, ULB inatumia "kutenga," "kukusudia," au "kuhifadhiwa kwa." (Angalia: 3:5)

UDB mara nyingi husaidia wakati watafsiri wanafikiri juu ya jinsi ya kuwakilisha mawazo haya katika tafsiri zao wenyewe.

Je, Paulo alimaanisha nini kwa maneno "katika Kristo," "katika Bwana," nk?

Aina hii ya usemi hutokea katika 1:1, 3, 4, 6, 7, 9, 10, 11, 12, 13, 15, 20; 2:6, 7, 10, 13, 15, 16, 18, 21, 22; 3:5, 6, 9, 11, 12, 21; 4:1, 17, 21, 32; 5:8, 18, 19; 6:1, 10, 18, 21. Paulo alimaanisha kueleza wazo la muungano wa karibu sana kati ya Kristo na waumini. Tafadhali angalia utangulizi wa Kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi juu ya aina hii ya usemi.

Je, ni masuala gani muhimu katika Kitabu cha Waefeso?

  • "katika Efeso" (1:1). Kadhaa ya maandiko ya awali hayajajumuisha maneno haya, lakini labda yamo katika barua ya awali. ULB, UDB, na tafsiri nyingi za kisasa zinayajumuisha.
  • "kwa sababu sisi ni viungo vya mwili wake" (5:30). Tafsiri nyingi za kisasa, ikiwa ni pamoja na ULB na UDB, husoma kwa njia hii. Baadhi ya matoleo ya zamani yanasoma, "kwa sababu sisi ni viungo vya mwili wake na mifupa yake." Watafsiri wanaweza kuamua kuchagua usomaji wa pili ikiwa matoleo mengine katika eneo lao yanafanana hivyo. Ikiwa watafsiri wanachagua usomaji wa pili, wanapaswa kuweka maneno ya ziada ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yao sio Kitabu cha Waefeso.

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

Ephesians 1

Waefeso 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

"Naomba"

Paulo amepanga sehemu ya sura hii kama sala ya sifa kwa Mungu. Lakini Paulo hazungumzi na Mungu pekee. Anafundisha kanisa huko Efeso. Pia anawaambia Waefeso jinsi anavyowaombea.

Dhana maalum katika sura hii

Kujaaliwa

Wasomi wengi wanaamini kwamba sura hii inafundisha juu ya somo inayojulikana kama "kujaaliwa." Hii inahusiana na dhana ya Biblia ya "kujaaliwa." Wasomi wengine huchukua hii kuonyesha kwamba Mungu amechagua, tangu kabla ya msingi wa dunia, baadhi ya watu ili kuwaokoa milele. Wakristo wana maoni tofauti juu ya kile Biblia inafundisha juu ya suala hili. Kwa hivyo watafsiri wanahitaji kuwa makini zaidi wakati wa kutafsiri sura hii, hasa kuhusiana na mambo ya usababisho. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#predestine)

| >>

Ephesians 1:1

Sentensi Unganishi

Majina ya Paulo peke yake kama mwandishi wa hii barua kwa waamini wa kanisa la Efeso

Maelezo ya Jumla

Bila kutajwa vinginevyo, pote palipo na " kwenu" na "Yako" ya husu waamini wa Efeso pamoja na waamini wote na kwa hiyo ni wingi.

Paulo, Mtume ... Kwa watakatifu wa Mungu Efeso

Lugha yako yaweza kuwa na namna ya kumtambulisha mwandishi wa barua na waliokusudiwa. " Mimi, Paulo, Mtume na waandikia hii barua kwenu, watu watakatifu wa Mungu Efeso.

Walio waaminifu katika Kristo

"Katika Kristo Yesu" na misemo kama hiyo ni mifano inayo jitokeza kwenye barua za agano jipya. Zinaeleza mahusiano madhubuti sana kati ya Kristo na ao wanao mwamini.

Neema kwenu na amani.

Hii ni salamu zoefu na baraka ambayo Paulo utumia kwenye barua zake.

Ephesians 1:3

Sentensi unganishi

Paulo anafungua barua kwa kuongea kuhusu nafasi ya waamini na usalama wao mbele za Mungu.

Maelezo ya Jumla

Katika hiki kitabu, vinginevyo kuelezwa, maneno "sisi" na "wote" ya husu Paulo, waamini wa Efeso, na waamini wote.

Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo apewe sifa.

'Hii pia yaweza ekwa hali tendaji. " Acha tumsifu Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Aliyetubariki

"kwa kuwa Mungu ameyubariki sisi"

Kila baraka za rohoni

"Kila baraka zinakuja kutoka katika Roho wa Mungu"

Katika maeneo ya bingu

"katika ulimwengu wa roho". Neno "bingu" la husu mahali Mungu alipo.

Ndani ya Yesu

"Ndani ya Yesu " sawa na maelezo ambayo ni mafumbo kila mara hutokea kwenye barua za Agano jipya. Zinaeleza aina ya mahusiano mazito yanayowezekana kati Kristo na wote wanaomwamini.

Tuwe watakatifu na tusiwe na lawama

Paulo anatumia maneno mawili yenye kufanana akisisitiza uadilifu.

Ephesians 1:5

Maelezo ya Jumla

Maneno "wake", "Yeye", na "yeye" yamuhusu Mungu.

Mungu ametutangazia sisi kuwa warithi wake

Neno' sisi' linamhusu Paulo, Kanisa la Efeso, na waamini wote ndani ya Kristo."Mungu alipanga muda mrefu kuturithi."

Kuwa urithi

Hapa " warithi" inahusu kuwekwa ndani ya familia ya Mungu.

Kupitia Yesu Kristo

Mungu aliwaleta waamini kwenye familia yake kupitia kazi ya Yesu Kristo.

Mpendwa wake wa kipekee

"Mpendwa wake pekee, Yesu Kristo" au "Mwanae, anaye mpenda"

Ephesians 1:7

Kwa mwana wake wa kipekee

"kwa mwana wa Mungu wa kipekee, Yesu Kristo"

Utajiri wa neema yake

Paulo anazungumzia neema ya Mungu kana kwamba ilikuwa ni vitu vya thamani: "ukuu wa neema ya Mungu" au "kushikamana na neema ya Mungu"

Ametumwagia hii neema kwa sana

"Ametupa sisi hiki kiasi kikubwa cha neema" au " Amekuwa mkarimu sana kwetu"

katika hekima na ufahamu

Yamkini tafsiri zilizopo ni 1) "sababu anayo hekima zote na ufahamu" 2) "ilituwe na hekima kubwa na ufahamu"

Ephesians 1:9

kwa kadiri ya alivyo pendezwa

Yamkini tafsiri zilizopo ni 1) "sababu alitaka kutufahamisha" au 2) " ndivyo alivyo taka"

na aliyo ionyesha katika Kristo

"na alionyesha kusudi hili ndani ya Kristo

katika Kristo

"kwa njia ya Kristo"

kwa lengo la kuwa na mpango

Sentensi mpya ya weza anza hapa. " Alifanya hivi kwa lengo la kuwa na mpango" au "Alifanya hivi, akifikiria kuhusu mpango.

kwa wakati timilifu

"Kwa kuwa wakati ukiwa mwafaka" au "kwa wakati aliyo uteuwa"

Ephesians 1:11

Tulichaguliwa kuwa warithi

Hii yaweza nenwa kama kauli tendaji. "Mungu ametuchagua sisi kuwa warithi"

Tumechaguliwa... ni sisi ambao ni wa kwanza

"Mungu alituchagua hapo awali"

Ili kwamba tuwe wa kwanza

Hapa neno "sisi" la husu wa Yahudi waamini walio sikia habari njema, sio waamini wa Efeso.

Ili kwamba tuwe sifa za utukufu wake

"ili kwamba tuishi kumsifu kwa utukufu wake.

Ephesians 1:13

Tumetiwa mhuri na ahadi ya Roho Mtakatifu

Nta ilikuwa ya wekwa kwenye barua na kuchapwa na alama inayowakilisha nani katuma barua. Paulo anatumia huu utamaduni kutuonyesha picha jinsi gani Mungu amemtumia Roho Mtakatifu kutu hakikishia kwa sisi ni wake. "Mungu aliweka mhuri wokovu wetu na Roho Mtakatifu akionyesha umiliki wake."

Dhamana ya urithi wetu

Kupokea ahadi ya Mungu ya zungumziwa hapa kama vile mtu anavyo rithi mali au utajiri kutoka katika familia. "ahadi ya kuwa tutapokea kile ambacho Mungu ametuahidi"

Ephesians 1:15

Sentensi unganishi

Paulo anaomba kwa ajili ya waamini wa Efeso na anamsifu Mungu kwa ajili ya nguvu waliyo nayo kupitia Kristo.

Sijaacha kumsifu Mungu

Paulo anatumia "sijaacha" kusisitiza kuwa anaendelea kumsifu Mungu. "Naendelea kumshukuru Mungu"

Ephesians 1:17

roho ya hekima na mafunuo ya ufahamu wake

":hekima ya kiroho ya kufahamu mafunuo yake"

macho yenu ya moyoni yatiwe nuru

"kipengele macho ya rohoni "inaelezea uwezo wa mtu kupata ufahamu.'kwamba upate ufahamu na kutiwa nuru."

macho yenu ya moyoni yatiwe nuru

Hii yawezwa tajwa kama njeo tendaji. Ili Mungu awatie nuru mioyo yenu" au "kwamba Mungu awatie nuru ufahamu wenu"

kutiwa nuru

"kufanywa kuona"

urithi

Kupokea kile ambacho Mungu amewaahidi waamini, ya elezewa kana kwamba mtu anarithi mali na utajiri kutoka kwa nduguye wa familia.

watakatifu wote wa Mungu

Hii yawezwa tajwa kama njeo tendaji. "Wote wale ambao amewatenga kwa ajili yake" au "wote wale ambao ni wake kabisa"

Ephesians 1:19

ukuu uzidio wa nguvu yake

Nguve za Mungu za pita sana nguvu zingine.

ndani yetu

"kwa faida yetu" au "kwa uhusiano nasi"

kufanya kazi katika nguvu zake

"nguvu yake kubwa ambayo ya fanya kazi ndani yetu"

alimfufua kutoka kwa wafu

"alimfufua kutoka kwa wafu" au "alimfanya kuishi tena"

kumketisha katika mkono wake wa kuume

"Kristo aliye keti mkono wa kuume wa Mungu" au "kristo aliye keti sehemu ya adhama"

mahali pa mbingu

"katika ulimwengu wa roho". Neno "mbingu" la husu sehemu Mungu alipo. Ona jinsi illivyo tafsiriwa katika 1:3

juu mbali na utawala, mamlaka, nguvu, enzi

Hii ni misemo tofauti ya matabaka ya viumbe wa rohoni, kwa malaika na mapepo. " mbali zaidi ya aina tofauti za viumbe wa rohoni"

kila jina litajwalo

Hii ya weza tajwa katika kauli tendaji. Tafsiri zilizopo ni 1) "Kila jina mwanadamu atoalo" au 2) "Kila jina Mungu atoalo"

Jina

Tafsiri zilizopo ni 1) Cheo au 2)nafasi ya mamlaka.

wakati huu

"Katika wakati huu"

wakati ujao

"hapo baadae"

Ephesians 1:22

Mungu amevitiisha

Mungu ameweka" au "Mungu ameweka"

vitu vyote chini ya miguu ya Kristo

Hapa miguu inawakisha ubwana wa Kristo,mamlaka,na nguvu:"vitu vyote chini ya nguvu ya Kristo"

alifanya yeye kichwa ...ambacho ni mwili wake

kama mwili wake ,kichwa hutawala vitu vyote vinavyohusu mwili wake hivyo ni Kristo kichwa cha mwili wa kanisa.

Kichwa cha vitu vyote katika kanisa

Hapa "kichwa" kinahusu kiongozi au mmoja ambaye yupo kwenye madaraka "mtawala juu ya vitu vyote ndani ya kanisa."

ambacho ni mwili wake

Kanisa kila mara hurejea mwili wa Kristo.

"ukamilifu wake ambao hujaza vitu vyote katika njia zote"

"Kristo hujaza kanisa na kwa mwili wake na nguvu ambazo hutupatia na kuzuilia maisha na vitu vyote"

Ephesians 2

Waefeso 02 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Sura hii inazingatia maisha ya Mkristo kabla ya kumwamini Yesu. Kwa hiyo Paulo anatumia habari hii kuelezea namna maisha ya zamani ya mtu ilivyo tofauti na utambulisho mpya wa Mkristo "katika Kristo." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith)

Dhana maalum katika sura hii

Mwili mmoja

Paulo anafundisha kuhusu kanisa katika sura hii. Kanisa lina makundi mawili tofauti ya watu (Wayahudi na Wayunani). Wao sasa ni kundi au "mwili" mmoja. Kanisa linajulikana pia kama mwili wa Kristo. Wayahudi na Wayunani wameunganishwa katika Kristo.

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Wamekufa katika makosa na dhambi"

Paulo anafundisha kwamba wale ambao si Wakristo "wamekufa" katika dhambi zao. Dhambi huwafunga au huwafanya kuwa watumwa. Hii inawafanya kuwa "wamekufa" kiroho . Paulo anaandika kwamba Mungu huwafanya Wakristo kuwa hai katika Kristo. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#death, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Maelezo ya kuishi kidunia

Paulo anatumia njia nyingi za kuelezea jinsi ilivyo dunia ya wasio Wakristo. "Waliishi kulingana na njia za ulimwengu huu" na "wanaishi kulingana na kiongozi wa mamlaka ya hewa," "kutimiza matamanio mabaya ya asili yetu ya dhambi," na "kutekeleza matamanio ya mwili na ya akili. "

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"(hilo) Ni zawadi ya Mungu"

Wasomi fulani wanaamini "hilo" hapa linamaanisha kuokolewa. Wasomi wengine wanaamini kwamba ni imani ambayo ni zawadi ya Mungu. Kwa sababu ya maandishi ya Kigiriki, "hilo" inamaanisha kuokolewa na neema ya Mungu kupitia imani.

Mwili

Hii ni suala ngumu. "Mwili" ina uwezekano wa kuwa mfano wa asili ya dhambi ya mtu. Maneno ya "Wayunani kimwili" yanaonyesha Waefeso wakati mmoja waliishi bila ya kumjali Mungu. "Mwili" pia hutumiwa katika aya hii kutaja sehemu ya kimwili ya mwanadamu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#fles)

<< | >>

Ephesians 2:1

Sentensi Unganishi:

Paulo anawakumbusha waamini walivyokuwa hapa mwanzo na sasa namna walivyo mbele za Mungu.

Na ninyi mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu

Hii inaonyesha ni kwa namna gani watu wana dhambi kiasi cha kushindwa kumtii Mungu kwa namna ile ile wafu wasivyoweza kujishughulisha kimwili tena.

makosa na dhambi zenu

Maneno "makosa" na "dhambi" kimsingi yanamaanisha kitu kile kile. Paulo anayatumia yote pamoja kuweka mkazo wa ukubwa wa dhambi ya watu.

hapo mwanzo mlienenda

Hii inaelezea tabia ya namna watu walivyoishi

kwa kumfuata mtawala wa mamlaka ya anga

Mtume Paulo anatumia neno "anga" kumaanisha tabia za ubinafsi na ufisadi wa watu waaishio humu duniani.

mtawala wa mamlaka ya anga

Hii inamaanisha ibilisi au shetani

roho yake yule

Sentensi "roho yake yule" inamaanisha ibilisi au shetani.

Tulikuwa tukitenda kwa namna ya tamaa mbaya za miili yetu, tulikuwa tukifanya mapenzi mwili na ya akili.

Maneno "mwili" na "nia" yanawakilisha mwili wote.

wana wa ghadhabu

Watu ambao Mungu amewakasirikia

Ephesians 2:4

Mungu ni mwingi wa rehema

"Mungu amejaa rehema" au "Mungu ni mwema sana kwetu"

kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi

"kwa sababu ya pendo lake kubwa kwetu" au "kwa sababu anatupenda sana"

wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya

Hii inaonyesha ni jinsi gani mtu mwenye dhambi hawezi kumtii Mungu mpaka pale anapopewa maisha mapya ya kiroho kama tu vile mtu mfu asivyoweza kujishughulisha na maisha ya mwili huu isipokuwa amefufuliwa kutoka katika wafu.

alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo

"Ndani ya Kristo" na maelezo kama hayo ni mifano ambayo mara nyingi hutokea katika barua au nyaraka za Agano Jipya. Inaelezea aina nzito kabisa ya mahusiano inayoweze kuwepo kati ya Kristo na wote wanaomwamini.

alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo Yesu.

Kama alivyokwisha kumfufua Kristo, atatufufua na sisi na tutakuwa na Kristo mbinguni.

ndani ya Kristo Yesu

"Ndani ya Kristo" na maelezo kama hayo ni mifano ambayo mara nyingi hutokea katika barua au nyaraka za Agano Jipya. Inaelezea aina nzito kabisa ya mahusiano inayoweza kuwepo kati ya Kristo na wote wanaomwamini.

katika nyakati zijazo

"huko baadaye"

Ephesians 2:8

Kwa maana ni kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani

Wema wake Mungu kwetu ni sababu iliyotuwezesha sisi kuokolewa kutoka katika hukumu kama tu tutamwamini Yesu.

Haitokani na

Neno "haitokani" linahusu au linarejea kwamba "kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani"

...kutoka kwetu

Neno "kwetu" linaelezewa kumaanisha Paulo na waamini wote katika Efeso.

sisi tu kazi ya Mungu

Neno "sisi" linaelezewa kumaanisha Paulo na waamini wote katika Efeso

katika Yesu Kristo

"Ndani ya Kristo" na maelezo kama hayo ni mifano ambayo mara nyingi hutokea katika barua au nyaraka za Agano Jipya. Inaelezea aina nzito kabisa ya mahusiano inayoweza kuwepo kati ya Kristo na wote wanaomwamini.

Ephesians 2:11

Maelezo au Sentensi unganishi:

Paulo anawakumbusha hawa waamini kwamba Mungu aliwafanya watu wamataifa na Wayahudi kuwa mwili mmoja kupitia Kristo na msalaba wake.

wamataifa kwa jinsi ya mwili

Hii inaongelea juu watu ambao hawakuzaliwa Wayahudi.

msiyotairiwa

Watu ambao si Wayahudi hawakutairiwa walipokuwa watoto na hivyo Wayahudi waliwaona hao kama watu wasiomfuata Mungu.

tohara

Hili lilikuwa neno lingine linaloelezea juu ya Wayahudi kwa sababu watoto wote wachanga wa kiume walitairiwa walipokuwa na umri wa siku nane.

tohara ya mwili

Kutahiriwa kulifanywa juu ya miili ya watoto wadogo wa kiume.

watu wa Israel

"jamii ya watu wa Israel"

wageni kwa agano la ahadi

Tafsiri mbadala: "hamkujua ahadi za agano la Mungu"

Ephesians 2:13

Sasa katika Kristo Yesu

Paulo anawatofautisha Waefeso kabla ya kumwamini Kirsto na baada ya kumwamini Kristo

ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu, mmeletwa karibu na Mungu

Kwa sababu ya dhambi za waamini, walikuwa wametengwa na Mungu. Hata hivyo, sasa Yesu amewaleta karibu na Mungu kwa damu yake.

yeye ndiye amani yetu

Tafsiri mbadala: "Yesu hutupa amani yake"

Kwa mwili wake

Tafsiri mbadala: "Kwa kifo chake juu ya msalaba"

ukuta wa utenganisho

Tafsiri mbadala: "ukuta wa chuki" au "nia mbaya"

umetutenganisha

Herufi za kwanza "ume" zinaelezea kwamba huo ukuta uliwatenganisha wote Paulo na Waefeso, ambao uliwatenga waumini wa Kiyahudi kutoka kwa waumini wasiokuwa Wakiyahudi (wamataifa)

aliiondoa sheria ya amri na kanuni

Damu ya Yesu ilileta utoshelevu wa sheria ya Musa ili kwamba wote Wayahudi na watu wa mataifa wanaweza kuishi kwa amani ndani ya Mungu.

mtu mmoja mpya

Mtu mmoja mpya, mtu wa jamii ya watu waliokombolewa.

ndani yake

Ni muunganiko na Yesu ambao unafanya upatanisho uwezekane kati ya Wayahudi na watu wa mataifa.

kuwapatanisha watu wote

Tafsiri mbadala: "kuwaleta pamoja wote wawili yaani Wayahudi na watu wa Mataifa (wamataifa)"

kupitia msalaba...kwa njia ya msalaba

Hii ni kwamba, kwa njia ya Kifo cha Kristo juu ya msalaba.

aliufisha (aliuua) uadui kwa msalaba

Yesu aliondoa kabisa sababu ambayo iliwafanya Wayahudi na watu wa mataifa kuwa maadui. Hawakuhitajika tena kuishi kulingana na sheria ya Musa.

Ephesians 2:17

Maelezo au Sentensi Unganishi.

Paulo anawaambia waamini wakiefeso kwamba watu wa mataifa walioamini wamefanyika wamoja na mitume na manabii, na ni hekalu kwa Mungu katika Roho Mtakatifu.

amani iliyotangazwa

Tasfiri mbadala: "injili ya amani iliyotangazwa" au "injili ya amani iliyotangazwa kwa uwazi"

ninyi mliokuwa mbali

Hii inazungumzia juu ya watu wa mataifa au wale wasio Wayahudi.

wale waliokuwa karibu

Hii inazungumzia juu ya Wayahudi.

Kwa maana kwa njia ya Yesu sisi sote wawili tuna nafasi.

Hapa "sisi sote wawili" inazungumzia juu ya Paulo, waamini wa Kiyahudi na waamini wasio Wayahudi.

kwa yule Roho Mtakatifu

Waamini wote, yaani Wayahudi na watu wa mataifa, wamepewa haki ya kuingia mbele za uwepo wa Mungu Baba kwa Roho Mtakatifu yule yule.

Ephesians 2:19

ninyi watu wa mataifa si wageni na wasafiri tena. bali ni wenyeji pamoja na wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu na wajumbe wa nyumbani mwa Mungu.

Hii inaelezea hali ya kiroho ya watu wa mataifa kabla na baada ya kuwa waamini kwa namna ile ile ambayo watu wasiokuwa raia wanavyoweza kuwa raia wa taifa fulani.

si wageni tena

" si watu wa nje tena"

na wasafiri

"na watu wasio raia"

mmejengwa juu ya msingi

Paulo analinganisha Familia ya Mungu na jengo. Yesu akiwa jiwe kuu la pembeni, na mitume wakiwa ndiyo msingi na waamini wakiwa boma (jengo lenyewe)

jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukuwa kama hekalu.

Paulo anaendelea kulinganisha Familia ya Kristo na jengo. Kwa namna ile ile ambayo mjenzi anaungamanisha mawe pamoja wakati akijenga, vivyo hivyo Kristo anatuungamanisha pamoja.

ndani yake...ndani ya Bwana

Haya ni maelezo ya mfano juu ya "ndani ya Kristo Yesu". Haya yanatokea mara nyingi katika nyaraka (barua) za Agano Jipya. Yanaelezea uhusiano wa nguvu sana unaoweza kuwepo baina ya Kristo na wale wanaomwamini yeye.

ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho

Hii inaeleza namna waamini wanawekwa pamoja kuwa mahali ambapo Mungu ataishi siku zote kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu

Ephesians 3

Waefeso 03 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

"Naomba"

Paulo amepanga sehemu ya sura hii kama sala kwa Mungu. Lakini Paulo hazunguzi na Mungu pekee. Anaombea na kufundisha kanisa huko Efeso.

Dhana maalum katika sura hii

Siri

Paulo anaashiria kanisa kama "siri". Jukumu la kanisa katika mipango ya Mungu wakati mmoja halikujulikana. Lakini Mungu amelifunua sasa. Sehemu ya siri hii inahusisha Wayunani kuwa sawa na Wayahudi katika mipango ya Mungu.

<< | >>

Ephesians 3:1

kauli unganishi

Kufanya wazi ukweli siri kuhusu kanisa kwa waumini, Paulo anataja nyuma umoja wa Wayahudi na Mataifa na hekalu la ambayo waumini sasa ni sehemu.

Kwasababu ya hii

"Kwasababu ya neema ya Mungu kwako"

mfungwa wa Kristo Yesu

"moja ambaye Kristo Yesu amemuweka katika gereza"

usimamizi wa zawadi ya Mungu kwamba yeye alinipa kwa ajili yenu

"Wajibu Mungu alinipa kusimamia neema yake juu yenu"

Ephesians 3:3

kutokana na jinsi ufunuo ulivyo funuliwa kwangu

Hii inaweza alisema katika fomu ya kazi. AT: "nini Mungu alinifunulia"

nililivyoyokuandikia kwa kifupi kwenye barua nyingine.

Paulo anataja barua nyingine ameandika kwa watu hawa.

Kwa vizazi vingine ukweli huu haukufanywa utambulike kwa watoto wao

"Ambayo Mungu hakufanya anajulikana kwa watu katika siku za nyuma"

Ila kwa sasa umewekwa wazi kwa Roho

"Sasa Roho umebaini" au "sasa Roho imefanya ni maalumu"

mitume wake na manabii wenye kuwekwa wakfu

"mitume na manabii ambao Mungu amewatenga kwa utumishi"

Ephesians 3:6

Watu wa mataifa ni warithi wenzake ... kwa njia ya Injili

Huu ni ukweli ulio fichika Paulo anaanza kuelezea katika mstari uliopita. Watu wa mataifa waliompokea Kristo pia watapokea urithi kama kama waumini wa Kiyahudi.

wanachama wenzake wa mwili

Kanisa ni mara nyingi hujulikana kama mwili wa Kristo.

katika Kristo Yesu

"Katika Kristo Yesu" na maneno kama ni mafumbo ambayo mara nyingi yametokea katika Agano Jipya. Yanaelezeamahusiano ya nguvu inawezekana kati ya Kristo na walio amini katika Yeye.

Kupitia Injili

Maana inawezekana ni 1) kwa sababu ya Injili watu wa mataifa ni washiriki wengine wa ahadi au 2) kwa sababu ya Injili watu wa mataifa ni warithi na viungo vya mwili na washirika wenzake katika ahadi.

Ephesians 3:8

Mungu amenipa zawadi hii japo kuwa mimi ni mtu mdogo kati ya wale wanaopata nafasi kwa Mungu

"Ingawa mimi ni mdogo anastahili watu wote wa Mungu, Mungu amenipa zawadi hii ya neema"

kuleta kila mtu katika mwanga na kuwaambia kuhusu mpango wa siri za Mungu

"kuwafanya watu wote kufahamu mpango wa Mungu"

kuwaambia kuhusu mpango wa siri wa Mungu kwamba Mungu (aliyeviumba vitu vyote) alikuwa amejificha kwa miaka katika siku za nyuma

"kitu ambacho Mungu alikificha kwa mda mrefu uliopita. Alipo umba kila kitu"

wale waliotengwa kwa Mungu

Hii inaweza semwa katika: "wale ambao Mungu amewatenga kwa ajili yake mwenyewe "

usiopimika

haiwezekani kujulikana kabisa

utajiri wa Kristo

Paulo anazungumzia ukweli kuhusu Kristo na baraka yeye huleta kana kwamba vilikuwa utajiri wa mali.

kuwaelimisha watu wote kuhusu mpango wa siri wa Mungu ni nini.

"angaza mwanga kwenye mpango wa Mungu ili watu wote wajue ni nini" au "kuwaambia watu wote ni nini mpango wa siri ya Mungu"

uliofichwa kwa miaka mingi kuanzia mwanzo Mungu alivyoumba kila kitu.

Hii inaweza semwa kama: "Kwamba Mungu, aliyeviumba vitu vyote, alikuwa ameficha kwa umri mrefu katika siku za nyuma"

Ephesians 3:10

viongozi na mamlaka yaliyopo mbinguni zitakuja kujulikana pande nyingi za asili ya hekima ya Mungu

ilikuwa upande asili ya hekima ya Mungu - "Mungu atafanya hekima yake kubwa ijulikane kwa viongozi na mamlaka katika ulimwengu wa roho kupitia Kanisa "

pande nyingi za asili ya hekima ya Mungu

ilikuwa upande asili ya hekima ya Mungu - hekima ya Mungu tata

watawala na mamlaka

Maneno haya yanashiriki maana sawa. Paulo anatumia yote pamoja na kusisitiza kwamba kila kiumbe cha kiroho watajua hekima ya Mungu.

kulingana na mpango wa milele

"katika kutunza mpango wa milele" au "sambamba na mpango wa milele"

katika Kristo Yesu Bwana wetu

Kwa njia ya Kristo

katika ulimwengu wa roho

Kuona jinsi ya kutafsiriwa hii angalia 1:3

Ephesians 3:12

kauli unganishi

Paul anamsifu Mungu katika mateso yake na anaomba kwa ajili ya waumini hawa wa Efeso.

upatikanaji kwa kujiamini

"upatikanaji katika uwepo wa Mungu kwa kujiamini" au "uhuru wa kuingia katika uwepo wa Mungu kwa ujasiri"

kwa sababu ya imani yetu kwake

"kwa sababu ya imani yetu katika Kristo"

tuna ujasiri

"sisi bila hofu" au "tuna ujasiri"

kujiamini

"hakika" au "uhakika"

Huu ni utukufu wako

Hapa "utukufu wako" kujisikia katika ufalme ujao. Wakristo wa Efeso wanapaswa kujivunia mateso ya Paulo gerezani. "Hii ni kwa manufaa yako" au "unapaswa ujivunie hii"

Ephesians 3:14

Kwa sababu hiyo

"Kwa sababu Mungu amefanya yote haya kwa ajili yenu"

Napiga magoti kwa Baba

"Nina inama chini kwa maombi kwa Baba" au "Mimi kwa unyenyekevu kumwomba Baba"

kwa kupitia kwake kila familia hapa duniani na minguni imetajwa

kitendo cha kumtaja hapa pengine pia inawakilisha kitendo cha kujenga: "aliyeumba na kutaja jina kila familia mbinguni na duniani"

Namwomba Mungu wewe

"kuwa angeweza kukupa"

kwamba akubariki, kutokana na utajiri wa baraka zake, akufanye imara kwa nguvu

"Mungu, kwa sababu yeye ni kubwa sana na myenye nguvu, anaweza kuruhusu wewe kuwa na nguvu kwa uwezo wake"

Awajalieni

"angetoa"

Ephesians 3:17

kauli unganishi

Paulo anaendelea maombi aliyoyaanza

kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yenu kupitia imani. Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake

Hili ni ombi la pili Paulo anaomba kwamba Mungu "awapatie" Waefeso "kulingana na utajiri wa utukufu wake "; kwanza ni kwamba wangeweza "kuimarishwa"

mioyo kwa njia ya imani

hapa "moyo" inawakilisha utu wa ndani, na "kupitia" inaonyesha njia ambayo Kristo anaishi ndani ya muumini. Kristo anaishi katika mioyo ya waumini kwa sababu neema ya Mungu inaruhusu wao kuwa na imani.

imani. Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake. Uwe katika pendo lake ili uweze kuelewa

maana inawezekana ni 1) "Imani. Naomba kwamba utakuwa na mzizi na msingi katika upendo wake ili uweze kuelewa" au 2) "Imani hivyo utakuwa na mzizi na msingi katika upendo wake. Nina omba pia uweze kuelewa "

kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake

Paulo analinganisha imani yao kwa mti wenye mizizi au nyumba iliyojengwa juu ya msingi imara. "kwamba utakuwa kama mti wenye shina zuri na nyumba yenye msingi wa jiwe."

Ili uweze kuelewa

Hili ni ombi la pili ambalo Paulo anapiga magoti yake na kuomba: la kwanza ni, Mungu awape kuimarishwa na kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yao kupitia Imani. na "uelewa" ni kitu cha kwanza kabisa Paulo aliomba kwamba Wafilipi wenyewe waweze kufanya.

waaminio wote

"waaminio ndani ya Kristo" au "watakatifu woote"

upana, urefu, kimo, na kina cha upendo wa Kristo

Paulo anatumia maneno hayo kuelezea kwa namba gani ambayo Kristo anatupenda.

ili upate kujua ukuu wa upendo wa Kristo

Hili ni jambo la pili kwamba Paulo anaomba kwamba Waefeso wataweza kufanya; kwanza ni kwamba wao "waelewa." "kwamba uweze kujua ukuu wa upendo wa Kristo"

ili mpate kujazwa na ukamilifu wote wa Mungu

Hili ni ombi la tatu ambalo Paulo anapiga magoti yake na kuomba: la kwanza ni,mpate "kuimarishwa" na la pili ni kwamba "muweze kuelewa"

Ephesians 3:20

kauli unganishi

Paulo anamalizia sala yake kwa baraka.

Maelezo ya ujumla:

maneno "sisi" na "sisi" katika kitabu hiki yanaendelea kuwahusisha Paul na waaminio wote.

Sasa kwake

"Sasa kwa Mungu, ambaye"

kila kitu mbali, mbali juu

Mungu anaweza kufanya zaidi kuliko tunayoweza milele kuomba au kufikiria.

Ephesians 4

Waefeso 04 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi kuwa upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hii kwa mstari wa 8, ambayo imenukuliwa kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Vipawa vya kiroho

Vipawa vya kiroho ni uwezo usio wa kawaida ambao Roho Mtakatifu huwapa Wakristo baada ya kumwamini Yesu. Paulo anataja hapa baadhi tu ya vipawa vya kiroho. Wasomi wengine wanaamini kwamba Roho Mtakatifu alitoa vipawa vya kiroho kwa waumini katika kanisa la kwanza pekee. Vipawa hivi vya kiroho vilikuwa msingi kwa kuendeleza kanisa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith)

Umoja

Paulo anaona kuwa ni muhimu sana kwamba kanisa lina umoja. Hii ni mada kuu ya sura hii.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Mtu wa kale na mtu mpya

Neno "mtu wa kale" labda linamaanisha hali ya dhambi ambayo mtu huzaliwa. "Mtu mpya" ni asili mpya au maisha mapya ambayo Mungu humpa mtu baada ya kumwamini Kristo.

<< | >>

Ephesians 4:1

kauli unganishi

Kwasababu ya kile Paulo amekuwa akiwaandikia Waefeso, anawatia moyo namna gani kuishi maisha yao kama waamini na tena anasisitiza umoja wa waamini.

Kama mfungwa kwa ajili ya Bwana

"kama mtu ambaye yuko gerezani kwa sababu ya uchaguzi wake wa kumtumikia Bwana"

Nawasihi ninyi kuishi maisha yanayoendana na wito

Neno "ninyi" linamaanisha Waefeso waamini. AT: "Nawatia moyo ninyi kujitunza wenyewe kwa namna nzuri ya wito."

Kwa unyenyekevu mkubwa na upole na uvumilivu, mkichukuliana kila mmoja katika upendo

"jifunzeni kuwa wanyenyekevu, wapole, waumilivu na kuchukuliana kila mmoja katika upendo"

Tunzeni umoja wa Roho katika kifungo cha amani

"tafuteni kuishi pamoja kwa amani kuuhifadhi umoja wa Roho"

Ephesians 4:4

Mwili mmoja

Kanisa mara nyingi linatafasiriwa kama mwili wa Kristo.

Roho moja

"Roho Mtakatifu mmoja tu" (UDB)

Pia mliitwa katika ujasiri wa taraja moja

"Mungu aliwachagua ninyi katika tumaini moja la uhakika"

Baba wa wote ... juu ya wote ... na katika yote ...na ndani ya wote

"Baba wa kila kitu...juu ya kila kitu...kupitia kila kitu...katika kila kitu"

Ephesians 4:7

kauli unganishi

Paulo anawakumbusha waamini juu ya karama ambazo Kristo huwapa waamini kutumia katika kanisa ambalo ni mwili wote wa waamini.

maelezo ya jumla

Nukuu hii imetoka katika wimbo mfalme Daudi aliimba.

Kwa kila mmoja wetu amepewa karama

Hii yaeza elezwa kwa kutumia kauli tendaji. "Mungu ametoa karama kwa kila mmoja wetu" au "Mungu alitoa karama kwa kila muumini"

Alipopaa juu sana

"wakati Kristo alipokwenda juu mbinguni"

Ephesians 4:9

Alipaa

"Kristo alikwenda juu"

Pia alishuka

"Kristo alishuka pia"

Pande za chini za dunia

Yaweza kumaanisha kwamba 1) "katika maeneo ya chini, ya dunia" au 2) "katika sehemu za chini, za dunia."

Aweze kuvijaza vitu vyote

"iliaweze kuwa kila mahali kwa nguvu zake"

jaza

"kamilisha" au "kuridhisha"

Ephesians 4:11

Kristo alitoa karama kama hizi

"Kristo alitoa karama kwa kanisa kama hizi"

kuwawezesha waamini

"kuwaanda waamini" au "kuwapatia waamini"

Kazi ya huduma

"kuwahudumia wengine"

Kwa ajili ya ujenzi wa mwili wa Kristo

Hii inalinganishwa ukuaji wa kiroho kwa kufanya mazoezi kuongeza nguvu ya mwili wa binadamu."

kuujenga

"uboreshaji"

mwili wa Kristo

"mwili wa Kristo" wa husu waumini mmoja mmoja wa mwili wa Kristo.

Kuufikia umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu

Maarifa ya Yesu Kristo kama mwana wa Mungu ni ya mhimu katika kuufikia umoja wa imani na ukomavu kama waamini.

Kufikia umoja wa imani

"kuwa na usawa wa nguvu katika imani"

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo mhimu cha Yesu.

Kuwa wakomavu

AT: "Kuwa waamini waliokomaa"

mkomavu

"mtu mzima," "amekuwa," au "mkamilifu"

Ephesians 4:14

Kuwa kama watoto

Hii ni kulinganisha waamini ambao hawajakuwa kiroho na mtoto ambaye amekuwa na udhoefu mdogo sana katika maisha."

Kurushwarushwa na kuchukuliwa huku na huku na kila upepo wa fundisho

Hii inamlinganisha muumini ambaye hajakomaa na husikia fundisho potofu na boti ambayo inarushwa na upepo katika mwelekeo usio sahihi juu ya maji.

Kwa hila ya watu katika ujanja wa udanganyifu uliopotoka

"kwa watu wajanja ambao hupotosha waamini kwa uongo wa kiujanja"

Katika yeye aliye kichwa...mwili wote hukua na kujengeka wenyewe juu

Paulo anatumia mwili wa binadamu kuelezea namna gani Kristo husababisha waamini kfanya kazi pamoja katika umoja kama kichwa cha mwili husababisha sehemu za mwili kufanya kazi pamoja ili kukuwa kiafya.

pamoja na kila kiungo

"kiungo" ni ukanda madhubuti unao unganisha mifupa katika mwili.

Ili kwamba mwili wote ukue na kujijenga wenyewe juu katika upendo

"Hivyo, waamini wanaweza kusaidiana kila mmoja na mwenzake kukua katika upendo"

Ephesians 4:17

Sentensi unganishi:

Paulo anawaambia wao kile ambacho hawapaswi kufanya sasa tu kwasababu wao kama waamini wamewekewa mhuri na Roho Mtakatifu wa Mungu.

Hivi nasema kwahiyo, na ninawasihi ninyi katika Bwana

"Kwahiyo, ninawatia moyo kwa nguvu katika Bwana"

Msitembee tena kama wamataifa wanavyotembea katika ubatili wa akili zao

"Acheni kuishi kama wamataifa na fikra zao zisizonamaana"

Kutiwa giza katika fikra

Hawawezi kufikiri au kuhoji kwa usahihi.

kufukuzwa kutoka katika maisha ya Mungu kwa ujinga uliomo ndani yao na kwa ugumu wa mioyo yao

"Hawawezi kuhisi maisha ya Mungu kwa sababu akili zao zimepofushwa na ni wagumu"

Kufukuzwa

"kukatiliwa mbali" au "kutengwanisha"

ujinga

"ukosefu wa maarifa" au "ukosefu wa taarifa"

sababu ya ugumu wa mioyo yao

Wamekataa kumsikiliza Mungu na kufuata mafundisho yake.

wamejikabidhi wenyewe kwa ufisadi katika matendo machafu

Paulo anawaongelea awa watu kama wao ni vitu wanaojikabidhi wao wenyewe kwa watu, na anaongelea jinsi wanavyo taka kuridhisha tamaa zao za mwili kana kwamba ndio mtu wanao jikabidhi kwake. "Wanacho taka tu nikuridhisha tamaa zao za mwili"

jikabidhi

"kujitoa kabisa"

Ephesians 4:20

Lakini hivi sivyo mlivyojifunza kuhusu Kristo

"Lakini hamkujifunza kumfuata Kristo kwa namna hii"

Kama mmesikia kuhusu yeye na mmefundishwa katika yeye, kama ilivyo kweli iliyo ndani ya Yesu

"Kwavile mmesikia kuhusu Yesu na mmejifunza ukweli kuhusu yeye"

Ninyi lazima mvue utu wa kale- ule ambao unakubaliana na tabia zenu za kale, ambao umeharibika sawasawa na tamaa za udanganyifu

AT: "Ninyi lazima mziondoe tabia ambazo zilikuwa za kawaida kwa njia za maisha yenu ya kale, ambazo zilikuwa mbaya kama tamaa zenu mbaya zilivyowadanganya ninyi"

Lazima muuvue utu wa kale

Lazima mwachane na tabia zote za dhambi kama tu kuvua nguo na kuzitupa mbali. AT: "Lazima mbadili tabia zenu."

Zile zinazoendana na mwenendo wenu wa kale

AT: "tabia ambazo zinakubaliana na asili yenu ya kale" au "tabia ambazo zinakubaliana na ukale wenu"

Ambayo imeharibiwa kulingana na tamaa danganyifu

AT: "ambayo inaendelea kukua vibaya kwasababu ya tamaa za mwili zidanganyazo"

Ephesians 4:23

vueni utu wenu wa zamani

Paulo anazungumzia tabia njema kana kwamba ni vipande vya nguo. "Lazima ubadili tabia" au Lazima uweke mbali mtu wa kale"

mfanywe upya katika roho ya akili zenu

Hii ya weza badilishwa katika njeo tendaji. "Mungu anaweza kukusaidia ukuwe karibu na yeye na kufikiri kwa namna mpya"

Ili kwamba mweze kuvaa utu mpya

Mtu asiye mwamini anakuwa mtu mpya anapokuwa muumini katika Kristo kama ilivyo kwa mtu anavyovaa nguo mpya na kuonekana tofauti kabisa.

unaoendana na Mungu

" inayo akisi tabia ya Mungu" au "yenye kuonyesha jinsi Mungu alivyo"

Ephesians 4:25

Wekeni mbali uongo

"Lazima mwache kusema uongo"

Mnene ukweli, kila mmoja na jirani yake

"Waamini lazima wanene ukweli kwa majirani zao"

Sisi ni wajumbe kila mmoja kwa mwingine

"Sisi sote ni wajumbe wa familia ya Mungu"

Mwe na hasira, lakini msitende dhambi

"mnaweza kukasirika, lakini msitende dhambi"

Msiliruhusu jua kuzama mkiwa na hasira zenu

"Lazima mwache kuwa na hasira kabla usiku haujaingia" au "muiondoe hasira yenu kabla ya siku haijaisha"

msimpe ibilisi nafasi

"Msimpe ibilisi fursa ya kukupeleka dhambini"

Ephesians 4:28

Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu

"msiruhusu lugha mbaya itoke kinywani mwenu" au "msiruhusu mazungumzo maovu yatoke kinywani mwenu"

Badala yake maneno ambayo ni msaada kwa kuwajenga wengine

"badala yake neneni maneno ambayo ni msaada katika kutoa afya kwa waamini wengien"

Kuwapa neema wao ambao wanasikiliza

"kwa njia hii mtatoa neema kwa wale ambao wanasikiliza"

faida

"saidia" au "msaada"

Msimhuzunishe

"msitese" au "msiudhi"

Kwa yeye ambaye mmewekewa mhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi

Paulo anasema Roho Mtakatifu amewaakikishia waamini kuwa Mungu atawapatia ahadi aliyo waahidi. Roho ni kama alama ambayo Mungu amewaekea watu wake kuonyesha kuwa anawamiliki. "Ni Roho ambaye Mungu amekupa kuonyesha kuwa anakumiliki na ata kukomboa kwa wakati muafaka"

Ephesians 4:31

sentensi unganishi

Paulo anamaliza maelekezo ya kuhusu yapi waamini wasifanye na anamaliza na yapi wafanye.

lazima muweke mbali

tafsiri zilizopo ni 1) lazima ufanye mwenyewe au 2) "lazima umuruhusu Mungu aondoe"

weka mbali uchungu wote

"acha kuwa na hasira ya mambo mabaya watu walio kufanyia"

ghadhabu

wakati wa hasira nzito

hasira

neno lililo zoeleka la hasira

mwe na huruma

" badala yake, lazima uwe na huruma

msameheane

"upole" au "huruma sana"

Ephesians 5

aefeso 05 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivi kwa maneno ya mstari wa 14.

Dhana maalum katika sura hii

Urithi wa ufalme wa Kristo

Hii ni vigumu kuelewa. Baadhi ya wasomi wanaamini kuwa wale wanaoendelea kufanya mambo haya hawataurithi uzima wa milele. Lakini Mungu anaweza kusamehe dhambi zote zilizotajwa katika aya hii. Kwa hiyo washerati, wasio wasafi, au wenye tamaa wakingali wanaweza kupata uzima wa milele ikiwa wanatubu na kumwamini Yesu. Somo la asili zaidi ni "Hakuna mtu ambaye ni mzinzi au msherati, au mlafi (kwani hii ni sawa na kuabudu sanamu) atakayekuwa kati ya watu wa Mungu ambao Kristo anatawala kama mfalme." (UDB) (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#forgive, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#eternity and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#life and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#inherit)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Wanawake, watii waume zenu

Wasomi wamegawanywa juu ya jinsi ya kuelewa kifungu hiki katika mazingira yake ya kihistoria na ya kitamaduni. Baadhi ya wasomi wanaamini kama wanaume na wanawake ni sawa kabisa katika mambo yote. Wasomi wengine wanaamini kama Mungu aliumba wanaume na wanawake kutekeleza majukumu tofauti katika ndoa na kanisa. Watafsiri wanapaswa kuwa makini wasiweke jinsi wanavyoelewa suala hili kuathiri jinsi wanavyotafsiri kifungu hiki.

<< | >>

Ephesians 5:1

Kauli unganishi

Paulo anaendelea kuwaambia waumini jinsi wanavyotakiwa na wasivyotakiwa kuishi kama watoto wa Mungu.

Kwa hiyo mwe wa kumuiga Mungu

"Hivyo ninyi mfanye mambo ambayo Mungu hufanya"

kama watoto wake wapendwa

Mungu anatamani sisi tumuige yeye maadam sisi ni watoto wake.

tembea katika upendo

"ishi maisha ya upendo"

sadaka na dhabihu, harufu nzuri inayompendeza Mungu

"sadaka inayonukia vizuri na dhabihu kwa Mungu"

Ephesians 5:3

uovu wa kujamiiana au uchafu au tamaa ya anasa lazima usidokezwe kati yenu, kama ilivyo sahihi kwa waumini

"siruhusu hata mawazo ya uovu wa kujamiina au uchafu au urafi kupatikana kati ya watu wa Mungu"

uchafu wowote

"maadili yoyote yasiyosafi"

kupenda anasa kwa ulafi

NI: "kutamaa kwaajili ya walivynavyo wengine"

kama ilivyosawa kwaajili ya waumini

NI: "tabia zenu daima ziwe zinazofaa kama watu watakatifu wa Mungu"

lazima usidokezwe kati yenu

"lazima usitajwe kati yenu" au "lazima usigundulike kati yenu"

Ephesians 5:5

urithi

Kupokea kile Mungu alicho ahidi waamini ni mfano wa mtu kurithi mahali au utajiri kwa familia.

matupu

"Msiruhusu mtu yeyote awadanganye kwa hoja za uongo" au "Msiruhusu mtu yeyote awakoseshe ninyi kwa maneno yasiyokuwa na maana"

Ephesians 5:8

Hapo kale ulikuwa giza

Kama tu mmoja hawezi kuona gizani, ndivyo watu wanaoishi katika dhambi wanapungukiwa ufahamu wa kiroho.

Lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana

Kama tu mmoja anaweza kuona katika nuru, ndivyo watu ambao wanaishi katika haki wanaufahamu wa kiroho.

kwa sababu tunda la haki ni uzuri wote, haki, na kweli

kazi zinazotoka kwenye maisha ya muumini (uzuri, haki, na kweli) zinafanana na tunda zuri linalozalishwa na mti wenye afya.

hazina ushirikiano pamoja na kazi zisizozaa za giza

"Usijihusishe na kazi za dhambi au wasioamini"

kazi zisizozaa za giza

kazi za mtu fulani anayeishi katika giza la kiroho zinafanana na matendo maovu ya watu wanaofanya kazi za uovu wamefichwa na giza usiku.

lakini afadhali uwafichue

"lakini heri uwaweke wazi kuwa wanamakosa"

Ephesians 5:13

sentensi unganishi

Haijulikani kama nukuu hii ni zile za Nabii Isaya au ni nukuu ya nyimbo zilizoo imbwa na waamini.

Kila kitu kimefunuliwa na nuru

Kama vile nuru hufunua vitu ambavyo vilikuwa vimefichwa katika ulimwengu unaoonekana, hivyo nuru ya Kristo inafunua uovu wa matendo ya kiroho ya wasioamini katika ulimwengu wa kiroho.

Amka, wewe uliyelala, na inuka kutoka kwa wafu

Wasioamini wanahitaji kuamka kutoka katika kifo cha kiroho kama vile mtu ambaye amekufa lazima afufuke tena ili kusudi aitikie.

wewe ulalaye ... atang'aa juu yako

"wewe" ya husu "aliyelala"

Kristo ataangaza juu yako

Kristo atamwezesha asiyeaamini kufahamu kiasi cha msamaha kilichotolewa na maisha mapya kama vile nuru inavyoonesha dhahiri kilichoko pale ambacho kilikuwa kimefichwa na giza.

Ephesians 5:15

Hivyo basi uwe makini jinsi mnavyoishi, siyo kama watu wasio na hekima bali kama wenye hekima

Wasio na hekima hawajilindi wenyewe kinyume na dhambi. Kwa hali yoyote watu wenye hekima wanaweza kutofautisha dhambi na kuikimbia. NI: "Hivyo basi ni lazima muwe makini muishi sawa na watu wenye hekima zaidi kuliko mtu mpumbavu" au "Hivyo basi lazima mwe makini kuishi sawasawa na mtu mwenye hekima."

Komboa wakati

Tunalo chaguo la kuishi katika dhambi ambalo ni sawa kama kutumia wakati wetu bila hekima. Au tunaweza kuishi tukifanya ambacho Bwana anataka sisi tufanye na kuutumia muda wetu kwa hekima. KWAMBA: "Tumia muda wako kwa hekima."

kwasababu siku ni mbaya

Neno "siku" linamaanisha ni katika muda unaoishi

Ephesians 5:18

sentensi unganishi

Paulo anamaliza maelekezo yake kwa jinsi gani waamini wapswa kuishi.

Na usilewe kwa mvinyo

"Na usilewe kutokana na kunywa mvinyo"

badala yake uwe umejaa na Roho Mtakatifu

"badala yake uwe uliyejaa na Roho Mtakatifu"

katika zaburi na sifa na nyimbo za kiroho

"pamoja na aina zote za nyimbo za kumsifu Mungu"

daima mkitoa shukrani

"Mtoe shukrani daima"

mkijitoa wenyewe

"Kwa unyenyekevu jitoeni wenyewe"

Ephesians 5:22

sentensi Unganishi:

Paulo anatoa maelekezo kwa mume na wake juu ya jinsi wanavyopaswa kutendeana.

yeye ni mwokozi wa mwili

NI: "Kristo ni Mwokozi wa mwili wa waumini" au "Kristo ni Mwokozi wa waumini wote"

Hivyo pia wake wawe kwa waume zao katika kila kitu

NI: "hivyo wake lazima pia wawe watiifu kwa waume zao katika kila jambo"

Ephesians 5:25

wapendeni wake zenu

Hapa "pendo" linarejea pasipo ubinafsi, kutumika, au kutoa upendo.

kujitoa mwenyewe kwaajili yake, kwamba unaweza kumfanya yeye mtakatifu kwasababu yeye alitusafisha sisi

Maneno "mwenyewe" na "yeye" yanarejea kwa Kristo. Maneno "yeye" na "sisi" yanarejea kwa Kanisa.

kajitoa mwenyewe kwaajili yake

NI: "Kristo alitoa kila kitu kwaajili yake"

yeye alitusafisha sisi kwa kutuosha kwa maji kupitia neno

Maana zinazowezekana ni 1) Paulo anarejea kuwa umekuwa ukisafishwa kwa neno la Mungu na kupitia ubatizo wa maji katika Kristo au 2) Paulo anasema Mungu alitufanya sisi wasafi kiroho kutoka katika dhambi zetu kwa neno la Mungu kama tunavyoifanya miili yetu safi kwa kuiosha kwa maji.

kwamba yeye aweza kujiwasilishia mwenyewe kanisa

"kwamba anaweza kuwasilisha kwake mwenyewe kanisa"

bila waa au kunyanzi

Paulo anasema kuhusu Kanisa kama vazi ambalo ni safi na liko katika hali nzuri. Anatumia wazo lile lile katika namna mbili kusisitiza utakatifu wa Kanisa.

takatifu na bila makosa

Kauli "bila makosa" kimsingi inamaanisha kitu kile kile "mtakatifu." Paulo anatumia viwili pamoja kusisitiza utakatifu wa kanisa.

Ephesians 5:28

kama miili yao wenyewe

NI: "kama wapendavyo miili yao wenyewe"

badala yake anaurutubisha

"badala yake anautunza" au "yeye anaulinda"

sisi tu viungo vya mwili wake

Inawezekana ikamaanisha 1) "sisi ni jumuiya ya mwili wake" au 2) waumini wanashikamana kuutengeneza mwili wa Kristo kama vile viungo vya mwili wa mwanadamu vinavyoshikamana kuunda mtu.

Ephesians 5:31

kwa kisababishi hiki

"kwa sababu hii"

lazima kumpenda mke wake kama yeye mwenyewe

Maneno haya "yeye" na "mwenyewe" yanarejea kwa mwanaume muumini ambaye kaoa.

mke lazima amheshimu mume wake

"mke lazima amtii mume wake"

Ephesians 6

Waefeso 06 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Utumwa

Paulo hajaandika katika sura hii ikiwa utumwa ni nzuri au mbaya. Paulo anafundisha kuhusu kufanya kazi ili kumpendeza Mungu ukiwa mtumwa au bwana. Anachofundisha Paulo hapa juu ya utumwa kingekuwa cha kushangaza. Katika wakati wake, mabwana hawakutarajiwa kuwaheshimu watumwa wao na kutowatisha.

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Silaha za Mungu

Mfano hii inaelezea jinsi Wakristo wanaweza kujikinga wakati wanavamiwa kiroho. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#spirit and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

__<< | __

Ephesians 6:1

sentensi unganishi

Paulo anatoa maelekezo kwa watoto, wababa, wafanya kazi, na mabwana.

Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana

Paulo anarejea kwa watoto kuwatii wazazi wao wa kimwili.

Ephesians 6:4

Na ninyi akina baba msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira

"Ninyi wababa msifanye mambo ambayo yatawafanya watoto wenu wakasirike" au "Ninyi akina baba msiwasababishie wattoto wenu kuwa na hasira"

muwalee katika maonyo na maagizo ya Bwana

"wasaidieni kukua katika mafunzo na mafundisho ya Bwana"

Ephesians 6:5

watumwa, iweni watiifu kwa

"Ninyi watumwa mnapaswa kutii"

kwa heshima kubwa na kutetemeka

Hizi ni njia mbili zinazofanana kuonyesha heshima kuhusu mabwana zao.

kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. Tiini kama vile mnavyomtii kristo

"Nyeyekeeni kwa hofu, kama kumtii kristo"

usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama

"siku zote fanya kazi kama ulivyokuwa ukifanya kazi kwa ajili ya kristo mwenyewe, hata kama mabwana zenu hawawatazami"

kama watumwa wa Kristo

watumikieni mabwana zenu ingawa bwana wenu duniani ni Kristo.

Watumikieni kwa mioyo yenu yote. Kana kwamba kumtumikia Bwana na wala si wanadamu

"fanya kwa furaha maana unafanya kwa ajili ya Bwana na si kuwafurahisha wanadamu."

Ephesians 6:9

fanyeni vivyo hivyo kwa watumwa wenu, na msiwatishie

Msiwatishie watumwa wenu, lakini muwafundishe kama Kristo angeweza kuwafundisha"

mkijua kwamba yeye aliye Bwana wa wote ni yule aliye mbinguni

"kwa sababu mnajua kuwa Krisato ni Bwana wa wote watumwa na Mabwana zao"

Mkijua kuwa hakuna upendeleo kwake

"Na hana upendeleo"

Ephesians 6:10

sentensi unganishi

Paulo anatoa maelekezo kuwafanya waumini kuwa na nguvu katika hii vita tunaishi kwa ajili ya Bwana.

iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake

"Hii inategemea kikamilifu katika Bwana kuwapa nguvu ya ya Kiroho"

Vaeni silaha zote za Mungu zilizo kamili, ili kwamba mpate kusimama kinyume na hila za shetani

Wakristo wanapaswa kutumia raslimali zote ambazo Mungu amewapa ili kusimama kinyume na shetani kama vile maaskari wa wanavyoweka siraha za kujikinga mwenyewe kutoka kwa uvamizi wa maadui.

Ephesians 6:12

damu na nyama

Hii fafanuzi inahusiana na watu, siyo roho ambazo hazina mwili wa Binadamu.

kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu

wakristo wanapaswa kutumia raslimali za kukinga ambazo Mungu amewapa katika kupigana na shetani kwa njia ile askari hubeba silaha ili kujilinda dhidi ya maadui.

Ephesians 6:14

hatimaye simameni imara

maneno "simameni imara" ni lugha yenye maana ya "kuzuia vikali"

mkanda wa kweli

kweli inashika kila kitu pamoja kwa ajili ya muumini kama mkanda unavyoshika nguo zote za askari pamoja.

haki kifuani

Zawadi ya haki inafunika mioyo ya waumini kama kitu cha kulinda kifuaniani kwenye kifua cha Askari.

mkiwa mmevaa utayari miguuni mwenu ili kutangaza injili ya ya Amani

Ni askari pekee anavaa ili kumpa maalifa ya kutembea, muumini anapaswa kuwa na maarifa imara ya injili ya amani ili kuwa tayari kuitangaza.

kila hali mkichukua ngao ya Imani

Imani ambayo Mungu amempa muumini ni lazima itumike kwa ajili ya ulinzi wakati shetani anapovamia kama vile ngao ambayo askari anaitumia kujikinga kutoka katika uvamizi wa maadui.

kuizima mishale ya mwovu Ibilisi

Uvamizi wa shetani katika kumvamia muumini ni kama mishale ya moto inayorushwa kwa askari na adui.

Ephesians 6:17

Na mvae kofia ya wokovu

Wokovu uliopewa na Mungu unalinda mawazo ya muumini kama vile kofia inavyolinda kichwa cha askari.

na upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu

Neno la Mungu, limevuviwa na Roho Mtakatifu, ili litumike kwa kupigana kinyume na kuwalinda waumini kutoka kwa mwovu kama vile askari anavyotumia upanga kupigana na kujilinda dhidi ya adui anayevamia.

pamoja na kusali na kuomba, ombeni kwa Roho

"Ombeni wajati wote katika Roho kama unavyoomba na ufanye maombezi maalumu"

kwa uvumilivu wote na maombi kwa ajili ya waumini wote

"Mara kwa mara tuwe macho kwa kuomba kwa ajili ya waumini wote"

Ephesians 6:19

sentensi unganishi

Paulo anawaomba kuomba kwa ajili ya ujasiri wake katika kusema injili wakati akiwa gerezani na akasema anamtuma Tikiko ili kuwafariji. Kisha alitoa baraka za amani na neema kwa waumini wote wanaompenda Yesu.

ili niweze kupewa ujumbe

"Kwamba Mungu anipe neno" au "Mungu atanipa ujumbe"

ninapofungua mdomo wangu ili kuufanya ujulikane kwa ujasiri

"Ninapoongea kufafanua kwa ujasiri"

kwa sababu hii mimi ni balozi niliyefungwa minyororo

Niko gerezani sasa kwa sababu ya kuwa mwakilishi wa Injili"

kwamba katika kifungo changu niseme kwa ujasiri kama ninavyowiwa kusema

"Kwamba niseme ujumbe wa Mungu kwa ujasiri wakati nikiwa humu gerezani"

Ephesians 6:21

mambo yangu

"Yaliyonipata" au "Hali yangu"

Tikiko

Tikiko alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wakitumika na Paulo.

atawajulisha kila kitu

"Atawaambia kila kitu"

Ephesians 6:23

Sentensi unganishi

Paulo anafunga barua yake kwa wa Efeso na baraka ya amani na neema kwa wote waamini wanao mpenda Kristo.