Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

UTANGULIZI WA WAKOLOSAI

Sehemu ya 1: Utangulizi kwa ujumla

Muhtasari ya kitabo cha Wakolosai

  1. Salamu, kushuhuru na sala (1:1-12)

  2. Yesu na kazi yake

    • Wokovu na ukombozi (1:13-14)
    • Kristu: Taswira ya Mungu asiyeonekana, na Yule asimamiye vyote vilivyoumbwa(1:15-17)
    • Kristu ndiye kichwa cha kanisa na kanisa linamwamini (1:18-2:7)
  3. Majaribu ya uaminifu

    • Maonyo kuhusu walimu wapotovu (2:8-19)
    • Utiifu wa Mungu siyo sheria kali ama mila zisizovunjika (2:20-23)
  4. Mafunzo na maisha

    • Maisha katika Kristu (3-14)
    • Maisha ya kale na ya kisasa (3:5-17)
    • Familia ya Kikristo (3:18-4:1)
  5. Tabia ya Kikristo (4:2-6)

  6. Kumalizia na salamu

    • Paulo anamshukuru Tikiko na Onesimo (4:7-9)
    • Paulo anatuma salamu kutoka kwa washirika wake (4:10-14)
    • Paulo anatoa mwelekeo kwa Arkipo na Wakristu wa Laodikia (4:15-17).
    • Salamu za kibinafsi za Paulo (4:18)

Nani aliandika kitabu cha Wakolosai?

kitabu cha Wakolosai kiliandikwa na Paulo.Paulo alitoka katika mji wa Tarso. Hapo awali alijulkana kama Saulo. Kabla ya kuwa Mkristo, Paulo alikuwa Mfarisayo. Aliwatesa Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika eneo lote la ufalme wa Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu.

Paulo aliandika barua hii akiwa jela la Roma.

Kitabu cha Wakolosai kinahusu nini?

Paulo aliandika waraka huu kwa waumini wa Asia Ndogo walioko katika jiji la Kolosai. Lengo kuu la barua hii ni kuittetea injili kutokana na walimu wa uongo. Alifanya hivi kwa kumsifu Yesu kama taswira ya Mungu, anayekidhi vitu vyote na kuwa mkuu wa Kanisa. Paulo alitaka wafahamu kwamba Kristo ndiye alyehitajika ili wakubaliwe na Mungu.

Kichwa cha Kitabu hiki kitafsiriwe namna gani?

Watafsiri wanaweza amua kukiita kitabu hiki na jina lake la asili, "Wakolosai," ama wanaweza kutumia kichwa cha kueleweka zaidi kama "Barua ya Paulo kwa kanisa la Kolosai", ama "Barua kwa Wakristo wa Kolosai." (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names).

Sehemu ya 2: Maswala muhimu ya kidini na Kitamaduni

Maswala gani ya kidini yalitatanisha kanisa la Kolosai?

Kanisa la Wakolosai lilkuwa na walimu wa uongo. Mafundisho yao kamili hayajulikani. Kuna uwezekano waliwafundisha wafuasi wao kuwaabudu malaika na kufuata sheria kali za sherehe za kidini.Kuna uwezekano mkubwa kwamba walifundisha kwamba lazima wanaume watahiriwe na pia kuepuka aina fulani za chakula. Paulo pia alisema kwamba mafundisho ya uongo pia yalitoka kwa akili ya watu na siyo Mungu.

Paulo alitumiaje istiara ya mbingu na nchi?

Kwenye waraka huu, Paulo amezungumzia mara nyingi mbingu kama iliyo juu akiitofautisha na ardhi inayozungumziwa kama iliyo chini. Lengo la istiara hii ni kufundisha Wakristo waishi kwa njia inayomheshimu Mungu aishie juu mbinguni. Paulo hafundishi kwamba dunia hii iliyeumbwa ina uovu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#evil).

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya Tafsiri

Namuna gani Maswala ya 'takatifu' na 'kutakasa' yamewakilishwa katika Wakolosai ndani ya ULB?

Maandiko yanatumia maneno haya kuashiria baadhi ya maswala mengi. Kwa sababu hii ni vigumu kwa Watafsiri kuyawakilisha vema katika matoleo yao. Katika Wakolosai, maneno haya hutumika kuashiria WaKristo bila kuelezea majukumu yao. Kwa hivyo Wakolosai katika ULB hutumia "Waumini" ama "Walio na imani ndani yake." (Tazama: 1:2,12,26).

Je, Yesu aliumbwa ama alikuwepo tangu mwanzo?

Yesu hakuumbwa lakini amekuwa akiishi kama Mungu.Yesu pia alichukua umbo la binadamu. Kuna uwezekano mkuu wa kutatanisha katika Wakolosai 1:15 inayosema " Yeye ndiye mzaliwa wa kwanza wa viumbe wote."Kauli hii inamaanisha kwamba Yesu ni mkuu kwa vyumbe wote. Haimaanishi kwamba Yesu ndiye kiumbe wa kwanza kuumbwa na Mungu. Watafsiri wawe makini wasimaanishe Yesu ni kiumbe.

Paulo anamaanisha nini na maelezo "ndani ya Kristo,"Ndani ya Bwana," na kadhalika?

Paulo alitaka kueleza juu ya muungano wa karibu sana kati ya Kristo na waumini. Angalia utangulizi wa kitabo cha Waroma kwa maelezo mengine kuhusu maneno haya.

Ni maswala gani muhimu katika maandishi ya kitabu cha Wakolosai?

Matoleo mengine ya kisasa yanatofautina na ya kale kwenye mistari ifuatayo. Toleo la ULB lina maandishi ya kisasa na imeweka maandishi ya kale kama maelezo ya chini ya tanbihi.Iwapo kuna Biblia katika eneo kwa ujumla, watafsiri wanafaa kuamua kutumia maandishi kwenye matoleo hayo. Kama sivyo, watafsiri wanashauriwa kufuata maandishi ya kisasa.

  • "Tunawatakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba wetu" (1:2). Matoleo ya zamani yana maandishi marefu: "Neema na amani kutoka kwa Baba yetu Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo viwe nanyi."
  • "Epafra, Mtumishi mwenzetu mpendwa, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Kristu kwa niaba yetu"(1:7). Matoleo mengine ya kale yanasema "kwa ajili yenu": Epafra, Mtumishi wetu mpendwa, Mtumishi mwaminifu wa Christu kwa ajili yenu."
  • "Baba aliyewafanya mustahili kushiriki uridhi wa waumini walio kwa mwanga.(1:12). Matoleo mengine ya zamani yanasoma, "Baba,aliyetuwezesha kushiriki katika mwanga wa uridhi."
  • "Katika Mwanawe tumepata ukombozi"(1:14). Matoleo mengine ya kale yanasema, "Katika Mwanawe tumepata ukuombozi katika damu yake."
  • "na akatusamehe dhambi zetu zote"(2.13). Matoleo mengine ya zamani yanasoma: "na akawasamehe dhambi zenu zote."
  • "Kristu, uhai wako, atakapotokea"(3:4). Matoleo mengine ya zamani yanasema, "Kristo, uhai wetu, atakapotokea."
  • "Ni kwa sababu ya mambo haya ndipo hasira ya Mungu inakuja kwa wana wasiotii" (3:6). Matoleo ya ULB,UDB ,na mengineyo ya kisasa husema hivi. Hata hivyo, kuna baadhi ya matoleo ya kisasa na ya kale ambayo husema, " Ni kwa sababu ya mambo haya ndipo hasira ya Mungu inakuja."
  • 'Ni kwa sababu ya haya mambo nikamtuma kwenu ili myafahamu mambo kutuhusu sisi"(4:8). Matoleo mengine yanasem, "Nilimtuma kwenu "ili ayafahamu mambo kuhusu nyinyi."

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

Colossians 1

Wakolosai 01 Maelezo kwa ujumla

Muundo na Mpangilio

Kama barua ya kawaida, Paulo ananza barua yake katika mistari ya 1-2 kwa kumtambulisha Timotheo na kujitambulisha kwa Wakristo wa Kolosai.

Paulo anazungumzia maswala mawili katika sura hii: Kristo ni nani na amefanyia Wakristo nini.

Dhana maalum katika sura hii

Ukweli wa siri

Paulo anaashiria ukweli wa siri katika sura hii. Jukumu la kanisa katika mipango ya Mungu halikujulikana hapo mwanzo. Lakini sasa Mungu amelitambulisha. Moja ya siri hii inahusisha watu wa Mataifa kuwa na nafasi sawa na Wayahudi katika mipango ya Mungu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#reveal).

Mifano muhimu katika sura hii

Picha za maisha ya Kikristo

Paulo anatumia picha nyingi kuelezea maisha ya Kikristo katika sura hii. Anatumia mifano ya "kutembea" na "Kuzaa matunda." (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#fruit

Sehemu zingine zenye utata katika tafsiri ya sura hii

Kitendawili

Kitendawili ni kauli ya ukweli inayaonekana kuelezea kitu kisichowezekana. Mstari wa 24 ni kitandawili: "Sasa ninafurahia katika mateso yangu kwa ajili yenu." Mara nyingi watu hawafurahi wakati wanapoteseka. Lakini katika mistari ya 25-29 Paulo anaelezea ni kwa nini mateso yake ni mazuri. (Wakolosai 1:24)

| >>

Colossians 1:1

Sentensi Unganishi:

Kupitia barua hii ni kutoka kwa Paulo na Timotheo kwa waumini wa Kolosai, baadaye kwenye barua Paulo anaweka bayana kwamba yeye ndiye mwandishi. Huenda alikuwa na Timotheo na kuandika maneno chini Paulo kama mzungumzaji.

Maelezo ya Jumla:

Kupitia hii barua maneno "sisi," "yetu," na "yakwetu" pamoja na Wakolosai vingenevyo yameandikwa tofauti. Neno "ninyi," "yenu," "yakwenu" yanawahusisha waumini Wakolosai na hivyo ni katika wingi vinginevyo yameandikwa tofauti.

Mtume wa Yesu Krist kwa mapenzi ya Mugu

"Aliyechaguliwa na Mungu kuwa mtume wa Yesu Kristo"

Tunatoa...Bwana wetu...sisi mara kwa mara

Haya maneno hayawajumuishi Wakolosai.

Colossians 1:4

Tumeshasikia

Paulo anajiondoa katika wasikilizaji anasemapo "sisi"

Imani yenu katika Kristo Yesu

"Kuamini kwenu katika Kristo Yesu"

kwa sababu ya tarajio la uhakika lililohifadhiwa kwa ajili yenu mbinguni

Ambalo ni matokeo ya uhakika wenu wa tumaini kwa kile Mungu ametunza mbinguni

kuzaa tunda na kuenea

Hapa Paulo anazungumzia kana kwamba kulikuwa mti au mche/mmea ambao ukuapo na kuzalisha chakula.

ulimwenguni kote

Injili inaene na kukua kupitia dunia iliyojulikana.

neema ya Mungu katika kweli

"neema ya Mungu ya kweli"

Colossians 1:7

mpendwa wetu...mwenzetu...kwa niaba yetu

Neno "yetu" na "sisi" sio pamoja na Wakolosai.

injili mliyojifunza kutoka kwa Epafradito, mpendwa wetu mtumishi mwenzetu, ambaye

"injili. Ambayo hasa umejifunza kutoka kwa Epafradito, ambaye in mpendwa mtumishi mwenzetu na ambaye" au "injili. ni sahihi kile Epafra, mtumishi mwenzetu mwenzetu, aliwafundisha. Yeye"

Epafra, tumishi mpendwa wetu, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Kristo kwetu

Hii ina maana kwamba Epafraalikuwa anafanyakazi kwaajili ya Kristo ambayo Paulo mwanyewe angeliifanyakama asingekuwa gerezani.

Epafra

Epafra alikuwa mwanaume aliyehubiri Injili kwa watu wa Kolosi

mpendwa wenu katika Roho

Roho Mtakatifu amewazesha kupenda waumini

Colossians 1:9

Sentensi Unganishi:

Kwa sababu Rohi amewawezesha kuwapenda wengine, Paulo anawaombea na kuwaambia hapa vile aombavyo kwa ajili yao.

Kwa sababu ya upendo huu

"Kwa sababu Roho Mtakatifu amewawezesha kupenda waumini wengine."

Tulisikia...hatujaacha...tumekuwa tukiuliza...tumekuwa tukiomba

Hii inaonyesha Paulo na Timotheo lakini si waumini wakolosai

tangu siku tuliposikia hivi

"tangu siku Epafra alipotuambia haya mambo"

kwamba mtajazwa na maarifa ya mapenzi yake

Paulo anazungumzia waumini wa Kolosai kana kwamba walikuwa chombo cha kubebea. "kwamba Mungu atawajaza kwa kile mnachohitaji kukijua hivyo basi mtafanya mapenzi yake"

Katika hekima yote na ufahamu wa kiroho

"Hekima na ujuzi mmpewa kwa Roho Mtakatifu"

kwamba mtembee katika ustahimilivu wa Bwana katika yeye

"Kwamba muishi katika njia ambayo Ingempendeza Mungu"

katika njia zinazompendeza

"katika njia ambazo zitampendeza Bwana"

Mzae matunda

Hii inalingashwa na mti uzaao matunda kwa kazi nzuri ya waumini.Kama mmea ukuao nakuzaa matunda, hivyo pia waaumini ni kukua katika kumjua Mungu na katika kutenda matendo mema.

Colossians 1:11

Tunawaombea

Neno 'sisi' linaonyesha Paulo naTimotheo lakini si Wakolosai

katika uvumilivu na ustahivu

Paulo anawazungumzia waamini Wakolosai kana kwamba Mungu atawahamishia eneo la uvumilivu. Katika uhalisia, anaomba kwamba hataacha kumwamini Mungu na kwamba watakuwa wavumilivu kikamilifu kadiri waendeleavyo kumhesimu.

aliyewafanya muweze kuwa na sehemu

"amewaruhusu kuwa na sehemu"

mmestahilishwa

Hapa Paulo analenga kwa wasomaji wake kama wapokeaji wa baraka za Mungu.Hamanishi kuwa yeye mwenyewe hana ushirika katikabaraka zile.

Kwa ushirikakatika urithi

Kupokea ambacho Mungu amewaahidi waamini kinazungumziwa kana kwamba kulikuwa na kitu cha kurithi na wanafamilia kurithishwa.

Katika Mwanga

"Kaika utukufu wa uwepo wake"

Colossians 1:13

Sentensi Unganishi:

Paulo anazungumzia kuhusu njia katika Kristo ni nzuri.

Ameokoa

"Mungu Baba amekwisha kuokoa"

katika utawala wa giza

Giza ni picha ya kawaida kwenye maandiko kwa uovu. "nguvu ya uovu"

Mwanae mpendwa

"Mungu ni Baba wa mwana mpendwa, Yesu Kristo"

Katika mwanae tuna ukombozi

mara nyingi Paulo anawaongelea waamini wapi "katika" Yesu Krsto au "katika" Mungu. "Mwanae ametukomboa sisi"

Msamaha wa dhambi

"Mwanae ametusamehe dhambi" au "Baba

Colossians 1:15

Mwana ni mfano wa Mungu asiyeonekana

Kwa kujua kwamba Yesu mwana ni kama, tunaweza kujua Mungu Baba alivyo.

Mwana

hili ni jina muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.

Ni mzaliwa wa kwanza

"Mwana n i mzaliwa wa kwanza."Yesu ni muhimu sana na ni wa pekee, "mwana" wa Mungu. Ni Mungu.Neno "Mwana"inaonyesha uhusiano wa ndani na Baba.Uhusiana huu haufahamiki mpaka na vinginevyo uelezwe katika maneno ya lugha kwa 'mwana' na 'baba.'

Kwa sababu ya yeye vitu vyote viliumbwa

"Kwa sababu mwana aliumba vitu vyote"

Hata enzi au mamlaka au utawala vitu vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake

Mwana aliumba vitu vyote kwa ajili yake, kujumlisha kiti cha enzi, utawala, ya kifalme na mamlaka.

Yeye ni mtangulizizwa vitu vyote

"Amekuwepo kabla yavitu vyote"

Katika yeye vitu vyote hushikamanishwa pamoja

"Anashikamanisha kila kitu pamoja"

Colossians 1:18

Yeye ni kichwa

"Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ni kichwa."

Yeye ni kichwa cha kanisa, yaani mwili wake

Hii inalinganisha nafasi ya Yesu kwa kanisa kama kichwa katika mwili wa kibinadamu.

Mwanzilishi

yeye ni mtawala wa kwanza au mwanzilishi. Yesu alianzisha wa kanisa

Mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu

Yesu ni mtu wa kwanza kufa na kurudi katika uhai, hatakufa tena.

Mwana

Hii ni jina muhimu sana kwa Yesu, mwana wa Mungu.

Kupitia damu ya mwana ya msalaba wake

asili yaneno "Kupitia" ni wazo la mtiririko au njia, inaonyesha kwamba Mungu huleta amani na upatanisho kwa watu kwa damu ya Yesu alipokufa msalabani.

damu ya msalaba wake

Hapa "damu" inasimama badala kifo cha Kristo msalabani.

Colossians 1:21

Sentensi Unganishi:

Kristo hubadilisha dhambi za waumini wa mataifa kwa utakatifu wake.

Na wewe pia

"Na ninyi Waamini wa Kolosai pia"

Mlikuwa wageni kwa Mungu

"Mlikuwa mmtengwa kutoka kwa Mungu" au "mlikuwa mmesukumwa mbali naMungu."

kuwaleta ninyi watakatifu, wasio na lawama mbele yake

Paulo anawaeleza Wakolosai ingawa Yesu aliwasafisha, kuwaweka katika nguo safi, na kuwaleta kusimama mbele ya Mungu Baba.

bila lawama, na bila dosari

Paulo anatumia maneno mawili yenye maana zinazokaribiana kusisitiza wazo la ukamilifu. "kamili"

mbele yake

"katika mtazamo wa Mungu" au "fikra ya Mungu"

iliyotangazwa

ambayo waumini walitangaza

kwa kila mtu aliyeumbwa chini ya mbingu

"kwa kila mtu katika dunia"

injili ambayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi

Paulo alikuwa mtumishi wa Mungu halizi. "injili ambayo mimi, Paulo, akimtumikia Mungu kwa kutaingaza"

Colossians 1:24

Natimiliza katika katika mwili wangu kile kinachopungua kwa mateso ya Kristo

Paulo anazungumzia mateso anayoendelea kuyapata. Yawezekana alikuwa anateseka mno ambapo yeye na Wakristo wote lazima wapitie kabla Kristo hajaja tena, na kwamba Krsito hupata pamoja nao kiroho haya magumu.

Natimiliza katika mwili wangu

Paulo anazungumzia mwili wake kana kwamba kilikuwa chombo cha kubebea ambacho kingeweza kubebea mateso.

kwa ajili ya ajili mwili wake , ambao ni kanisa

mara nyingi Paulo anazungumzia kanisa, kundi la waamini wote, kana kwamba ulikuwa mwili wa Kristo.

kulijaza neno la Mungu

Hii inamaana kuleta lengo la ujumba wa injili ya Mungu, ambayo inatakiwa kuhubiriwa na kuaminiwa.

Huu ni ukweli wa siri uliokuwa umejificha

Hii inaweza katika muundo kamili. "huu ni ukweli ambao Mungu alikuwa ameuficha"

kwa miaka mingi na vizazi na kwa miaka

Neno "miaka" na "vizazi" inarejelea kwenye kipindi tangu uumbaji wa dunia mpaka kipindi wakati inijili ilipohibiriwa.

sasa imefunuliwa

"sasa Mungu ameifunua"

utajiri wa utukufu wa siri ya kweli

Paulo anazungumzia thamani hii siri ya ukweli Mungu kana kwamba kulikuwa na hazina ya kupata malighafi. "utajiri"

Kristo yumo ndani yenu

Paulo anawazungumzia waamni kana kwamba walikuwa vyombo vya kubebea ambapo Kristo yupo. Hii ni moja ya njia yake kuelezea umoja wa waamini pamoja Kristo.

Ujasiri wa utukufu ujao

"ambao mnaweza utarajiwao kusemwa kwa utukufu wa Mungu"

Colossians 1:28

tunayemtangaza...tunamwonya...tunamfundisha...tunaweza kumleta

Haya maneno hayawajumuishi Wakolosai.

tunamwonya kila mtu

"Tunamwonya kila mmoja"

Kwamba tumfikishe kwa Mungu kila mmoja

"kwamba tumfikishe kwa Mungu kila mmja"

Kikamilifu

"Wazima Kiroho"

Colossians 2

Wakolosai 02 Maelezo kwa ujumla

Maswala muhimu katika sura hii

Tohara na ubatizo

Katika mistari ya 11-12, Paulo anatumia alama ya tohara ya agano la kale pamoja na alama ya ubatizo ya agano jipya kuchora taswira ya jinsi Wakristo wameungana na Kristo na kuokolewa kutoka kwa dhambi,

ehemu zingine zenye utata katika tafsiri ya sura hii"

Nyama

Hili ni swala ngumu. Labda "nyama" inatumiwa kama mfano ya asili yetu ya dhambi. Paulo hasemi kwamba mwili wa binadamu una dhambi. Ni kama Paulo anajaribu kusema kwamba wakati Wakiristo wanaishi ("katika nyama"), tutaendelea kutenda dhambi. Lakini asili yetu mpya itakuwa inapigana na asili yetu ya kale. Paulo anatumia pia "nyama" katika sura hii kumaanisha mwili wa binadamu.

Maana iliyosemwa

Paulo amevitaja vitu vingi katika sura hii kuashiria mambo yaliyokuwa yanalikumba kanisa la Wakolosai. Ni vyema kuacha maandiko yabaki bila kuelezea kwa uwazi kuhusu maswala yenyewe ya ukweli, (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

<< | >>

Colossians 2:1

Sentensi unganishi:

Paulo anaendelea kuwatia moyo walioamini katika Kolosai na Laodekia wapate kuelewa kuwa Kristo ni Mungu na anaishi ndani ya walioamini ili wapate kuishi sawasawa na walivyompokea.

Ni mapambano ya jinsi gani niliyopitia kwa ajili yenu

Paulo amefanya bidii nyingi katika kuendeleza usafi wao na uelewa wa injili.

Wale waliopo Laodekia

Huu ulikuwa mji karibu sana na Kolosai ambamo pia kulikuwa na kanisa ambalo Paulo alikuwa akiliombea.

kama ambavyo wengi hawajaniona uso wangu katika mwili

"wengi ambao mimi binafsi sijawaona" au "wengi ambao sijaonana nao uso kwa uso"

kwamba mioyo yao

"kwamba mioyo ya wote walioamini ambao hawakuwa wamemuona Paulo"

walioletwa pamoja

waliowekwa pamoja katika ushirika halisi wa karibu

utajiri wote wa uhakika kamili wa maarifa

Paulo nazungumza na mtu anauhakika kamili kwamba habari njema ni kweli ingawa huyo mtu alikuwa tajiri katika mwili huu.

siri ya Mungu ya kweli ya Mungu

Huu ufahamu ambao unaweza kufunuliwa na Mungu peke yake.

ambaye ni, Kristi

Yesu Kristo ndiye siri ya kweli iliyofunuliwa na Mungu.

Katika yeye hazina za hekima na maarifa zilizofichika

Kristo pekee ndiye awezaye kufunua hekima ya kweli ya Mungu na maarifa. "Mungu ameficha hazina zote za hekima na maarifa katika Kristo"

hazina ya hekima na ufahamu

Kimsingi Paulo anazungumzia hekima na maarifa ya Mungu kana kwamba vilikuwa malighafi ya utajiri.

hekima na ujuzi

Kimsingi haya maneno hapa haya maneno yanamaanisha vitu viwili. Paulo ametumia yote pomaja kusisitiza kwamba ufahamu wote wa kiroho unatokana na Kristo.

Colossians 2:4

hila

Hii inamaana kwamba kusababisha mwingine aamini kitu ambacho sio kweli, hivyo, anatenda hiyo imani, na madhara ya mateso kama matokeo.

hotuba yenye ushawishi

hotuba ambayo itafanya mtu afikirie tofauti

sio pamoja nanyi katika nyama

"siko pamoja nanyi kimwili"

Niko nanyi katika roho

"Naendelea kufikiri kuwhusu ninyi"

mpangilio mzuri

kufanya vitu kwa mpangilio

nguvu ya imani yako

"kukosaje na hakuna anayeweza kuwasababishia kuacha kuamini"

Colossians 2:6

mwimarishwe...mjengwe...mjengwe...nyingi

Haya maneno yanaeleza inamaana gani "kutembea katika yeye."

kwamba mlimpokea

"kwamba ninyi waamini wa Kolosai mlimpokea Kristo"

mwimarishewe katika yeye

Paulo anamzungumzia mtu mwenye imani ya kweli katika Kristo kana kwamba huyo mtu alikuwa unaokuwa kwenye aridhi mgumu ngumu yenye mizizi mirefu.

muimarike katika imani

"muishi maisha yenu kulingana na imani yenu katika Yesu Kristo"

kama mlivyofundishwa

Huu ni mwanzo mzuri bila kutaja au vinginevyo kuvuta usikivu kwa mwalimu, ambaye alikuwa Epafradito. "kama mlivyojifunza" au "kama walivyokufundisha" au "kama alivyowafundisha"

muwe na shukurani nyingi

"muwe na shukurani kwa Mungu"

Colossians 2:8

Sentensi unganishi:

Paulo anawasihi walioamini wawe makini wasigeukie maneno na taratibu za wengine kwa sababu hakuna kinachoweza kuongezeka katika ukamilifu wa Mungu walio nao walioamini katika Kristo.

Ona kwamba

"Iweni makini kwamba" au "Angalieni kwamba"

kuwanasa

Paulo anazungumzia vile ambavyo mtu anavyoweza kuamini mafundisho ya uongo (kwa sababu wanaamini mafundisho ya uongo au wanapenda vitu vitu vya uongo)

falsafa

mafundisho ya kidini na imani yasiyotoka katika neno la Mungu lakini yanatokana na mawazo ya ya watu kuhusu Mungu na maisha

maneno matupu ya udanganyifu

haya ni mawazo ya upotoshaji ambayo hayatuongozi katika maisha ndani ya Kristo. Hayazalishi chochote; ni matupu au hayana thamani.

tamaduni za kibinadamu na juu ya mifumo ya dhambi ya dunia

tamaduni zote za Waisraeli na wapagani (watu wa Mataifa) mifumo ya imani haina maana.

kwa kuwa katika yeye ukamilifu wote wa Mungu unaishi kwa jinsi ya mwili

"kwa sababu asili yote ya Mungu inaishi katika mwili wa Kristo"

Colossians 2:10

katika yeye pia mlitahiriwa

Paulo anawazungumzia wale ambao ni wa Kristo kana kwamba walikuwa walikuwa ndani ya mwili Kristo. "wakati ulipojiunga kanisani kwa kubatizwa, God alikubatiza"

mmejazwa katika yeye

Paulo anazungumzia watu ingawa walikuwa chombo cha kubebea kwenye sehemu ambayo Mungu alimuhifadhi Kristo. mmekamilishwa katika Kristo"

Yeye ni kichwa

Kristo ni mtawla

tohara isiyofanywa na wanadamu

katika mfano huu, Paulo anasema kwamba Mungu amewafanya Waamini wa kikristo kukubalika kwa yeye mwenyewe

Mlizikwa pamoja na yeye katika ubatizo

Paulo anazungumzia kuwa na ubatizo na kujiunga na kusanyiko la waamini kana kwamba ilikuwa imezikwa pamoja na Kristo. "Mungu amewazika pamoja na Kristo wakati mlipojiunga na kanisa katika ubatizo"

Katika yeye mlifufuliwa

Kwenye mfano, Paulo anazungumzia maisha mapya ya kiroho ya waamini, walifanywa mitume kwa sababu Mungu alimfanya Kristo kufufuka tena. Hii inaweza kuwa hai. "kwa sababu mmejiunga na wenyewe kwa Kristo, Mungu amewafufua"

Colossians 2:13

wakati mlipokuwa mmekufa

"wakati ninyi waumini wa Kolosai mlikuwa mmekufa kiroho"

mlikuwa mmekufa .... aliwafanya kuwa hai

Fumbo hili linaonesha jinsi gani baada ya kutoka katika maisha ya dhambi kwenda maisha mapya ya kiroho ilivyo kama mtu anayefufuka kutoka kifo.

mmekufa katika hatia zenu na kutokutahiriwa kwa miili yenu

mlikuwa mmekufa katika mambo mawili: 1) mlikuwa mmekufa kiroho, mkiishi maisha ya dhambi dhidi ya Kristo na 2) mlikuwa hamkutahiriwa kulingana na sheria ya Musa.

alitusamehe sisi hatia zetu zote

"Yesu Kristo alitusamehe sisi Wayahudi na ninyi watu wa Mataifa makosa yetu yote"

alifuta kumbukumbu za madeni zilizoandikwa na taratibu zilizokuwa kinyume nasi

Fumbo hili hufananisha jinsi ambavyo Mungu anaweza kuondoa dhambi (deni zetu) na kutusamehe sisi kwa kuvunja sheria za Mungu (taratibu) kama ambavyo mtu anaweza kufuta kitu kilichoandikwa kwenye karatasi.

aliwaongoza katika ushindi na milki

Katika kipindi cha Warumi, ilikuwa kawaida kwa jeshi la Kirumi kuwa na "gwaride la ushindi" waliporudi nyumbani, kuonesha wafungwa wote na mali walizoteka.

kwa msalaba

Hapa "msalaba" unasimama bdala ya kifo cha Kristo msalabani.

Colossians 2:16

katika kula au katika kunywa

Sheria ya Musa ilijumuisha nani anaweza kula au kunywa. "kwa nini mnakula au mnakunywa"

kuhusu siku ya sikukuu au mwezi mpya, au siku za Sabato

Sheria ya Musa ilielekeza siku za kusherehekea, kuabudu, na kutoa sadaka.

kivuli cha vitu vijavyo

"Kivuli" hutoa wazo la mfano wa asili ya kitu halisi. Kwa njia hiyo hiyo, tamaduni za kidini kama vile Sheria za Musa zinaweza kwa kiasi kuonesha uhalisia wa Yesu Kristo.

kiini

Hapa inamaanisha "uhalisia" kitu ambacho kitoacho "kivuli"

Colossians 2:18

mtu yeyote...asidhulumiwe tuzo yake

"mtu yeyote asidanganywe juu ya tuzo yake."

anayetamani unyenyekevu

Neno "unyenyekevu" linasimama badala kwa ajili ya matendo mwingine anawafanya wengine kufikiria kwamba mwingine ni mnyenyekevu. "anayetaka kufanya mambo kuonyesha kwamba wewe ni mnyenyekevu

kuingia kwenye vitu alivyoviona

Hapa Paulo anazungumzia kuhusu watu wanaojiita kuwa na ndoto na maono kutoka kwa Mungu na wanaongea kwa majivuno kuhusu weneyewe.

kushawishiwa na mawazo yake ya kimwili

Hapa Paulo anasema kwamba hali ya kufikiria kaatika hali ya dhambi hufanya mtu awe na kiburi. "anayejiunua kwa maana ya ya mawazo yake ya mwili"

kushawishiwa

Hapa ni mtu anayejivuna anazungumziwa kana kwamba ndani ya chombo ambacho kilichokuwa na hewa kufanya kirefu kuliko kilivyotakiwa kuwa.

mawazo yake ya mwilini

Hii inamaanisha kufikiri kama mtu wa kawaida au mwenye dhambi badala ya kama mtu wa rohoni.

yeye hana shirika na

"Yeye hashikilii kwa nguvu" au "Yeye hatulii katika," kama vile mtoto awategemeavyo wazazi wake

Kristo, aliye kichwa, ambaye katika yeye mwili wote umeunganishwa kwa mishipa na mifupa

Mfano huu hulinganisha mamlaka ya Kristo juu ya kanisa na kichwa cha mwanadamu ambacho kinaongoza na kusimamia mwili wote.

Colossians 2:20

Ikiwa mmekufa pamoja na Kristo katika mtiririko wa imani ya dhambi za ulimwengu.

Fumbo hili linaonesha kwamba, kama vile mtu anavyokufa kimwili hayatii tena mahitaji ya kimwili ya ulimwengu ( pumzi, kula, sleep), mtu anayekufa kiroho pamoja na Kristo haitaji tena kuyatii mambo ya duniani .

Kwa nini mnaishi kama manawajibika kwa dunia: "msiguse"?

Paulo ametumia swali hili, kukemea Wakolosai kwa ajili ya imani isiyo ya kweli ya ulimwengu. Acheni kujinyenyenyekesha kwa imani za ulimwengu.

ishi kama mnawajibika kwa dunia

"fikiri lazima mzitii tamaa za dunia"

dunia

mawazo, tamaa, na dhana za wingi wa dhambi katika dunia ya watu

yameamriwa kwa ajili ya uharibifu

"kuangamia." Paulo hapa anatumia mfano kuchimbua mwili ("uharibifu") kwenye kaburi.

Sheria hizi zinahekima ya dini zilizotengenezwa kwa ubinafsi na unyenyekevu na mateso ya mwili

kutengeneza dini na unyenyekevu na nguvu ya mwili- "Hizi sheria zinaonekana pana kuamini watu kwa sababu zinawaruhusu wale ambao wanaowafwata kuonekana wanyenyekevu kwa sababu wanaumiza miili yao wenyewe"

hazina thamani dhidi ya tamaa za mwili

"msiache kusaidia kufuata mwili wa tamaa"

Colossians 3

Wakolosai 03 Maelezo kwa Ujumla

Muundo na Mpangilio

Sehemu ya pili ya sura hii inafanana na Waefeso 5 na 6.

Maswala muhimu katika sura hii

Nafsi ya kale na nafsi mpya

Nafsi ya kale na nafsi mpya inamaanisha mtu wa kale na mtu mpya. Neno "Mtu wa kale" humaanisha asili ya dhambi ambayo mtu huzaliwa nayo. "Mtu mpya" ni asili mpya ama maisha mapya ambayo Mungu humpa mtu baada ya kuanza kumwamini Kristu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith)

Sehemu zingine zenye utata katika tafsiri ya "sura hii

Tabia

Maswala mengi Paulo anawahimiza wasomaji wake kufuata ama kuacha siyo matendo bali ni tabia. Kwa sababu ya hii, ni ngumu kutafsiri. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-abstractnouns)

"Vitu vilivyo juu"

Makazi ya Mungu mara nyingi huashiriwa kama "juu." Paulo anasema "Tafuta vitu vilivyo juu" na "fikiria kuhusu vitu vilivyo juu." Hapa anamaanisha Wakristo watafute vitu vya umungu na mbinguni.

<< | >>

Colossians 3:1

Sentensi unganishi:

Paulo anawaonya walioamini kwamba kwa kuwa ni wamoja pamoja na Kristo, kuna mambo ambayo waumini hawapaswi kuyafanya

Mungu amewafufua pamoja na Kristo

Kama vile Mungu alivyo mfufua Kristo kutoka kwa wafu, hivyo anawahesabu waumini wa Kolosai kama waliofufuliwa kwenda mbinguni.

mambo yaliyo juu

"mambo ya mbinguni" au "mambo ya kimungu"

kwa kuwa mmekufa

Kama Kristo alivyokufa, hivyo Mungu anawahesabu waumini wa Kolosai kama wamekufa na Kristo.

maisha yenu yamefichwa pamoja na Kristo

Paulo anazungumzia wale watu waishio kana kwamba walikuwa alama ambayo inayoweza kujificha kwenye chombo cha kubebea.

ambaye ni maisha yenu

Kristo ni yule atoaye uzima wa kiroho kwa waamini.

Colossians 3:5

fisheni, mambo yaliyo katika nchi

Paulo anazungumzia tamaa ya dhambi kana kwamba walikuwa sehemu ya kutumia watu kuwashuhudia.

Uchafu

"tabia zisizo safi"

shauku

"kutamani kwa nguvu"

na tamaa, ambayo ni Ibada ya sanamu

"na tamaa, ambayo ni sawa na ibada ya sanamu" au " na msiwe na tamaa kwa sababu ni sawa na kuabudu miungu"

ghadhabu ya Mungu

hasira ya Mungu kinyume na wale ambao hufanya uovu kama kuonyesha kwa kile anafanyacho kuwaadhibu.

wana wasiotii kutotii.

"mwanadamu kutotii" au "watu ambao hawamtii"

"Ni katika mambo haya kwamba ninyi pia hapo kwanza mlitembea kwayo mlipoishi nao."

"Paulo anazungumzia vile ambavyo tabia ya mtu kana kwamba ilikuwa barabara au njia anayotembelea. "Haya ni yale mliyokuwa mkiyafanya"

mlipoishi kati yao

Inaweza kuwa na maana hizi? 1) "unapokuwa umefanyia mazoezi haya mambo" au 2) "unapokuwa umeishi miongoni mwa watu ambao hawamtii Mungu"

ghadhabu, hasira

Neno "hasira" hapa linamaanisha wakati mtu anapokuwa na hasira kwa wale ambao hawamuheshimu kama kuonyesha kwa matendo yake, ambapo italeta madhara kwa watu.

nia mbaya

"tamaa ya kufanya matendo maovu"

hasira

hasira kali sana

matusi

"kururu" au "lugha chafu." Hii inarejea kwa hotuba ambayo inatumika kwa dhamira ya kuumiza wengine

hotuba ichukizayo

maneno ambayo yasioyofaa katika mazungumzo ya upole

kutoka kinywani kwenu

Hapa "kinywa" inasimama badala ya kuzungumza. "katika mazungumzo yenu"

Colossians 3:9

Sentensi unganishi:

Paulo anaendelea kuwaambia waumini jinsi ya kuishi na anawakumbusha kwamba Kristo alifuta kuta ambazo zingekuwepo kati ya Wamataifa na Wayahudi, watumwa na walio huru.

mmeuvua mballi utu wenu wa kale wenyewe pamoja na matendo yake, na mmevaa utu wenu mpya.

Fumbo hili linajenga wakristo ambao wanapaswa kuondoa matendo yasiyo ya kimungu na kuanza kutenda kimungu kwa mtu ambaye anaondoa mavazi machafu na kuvaa mavazi mapya yaliyo safi.

picha yake

Hili linamzungumzia Yesu Kristo

hakuna mgriki au myahudi, kutahiriwa au kutokutahiliwa, msomi, asiye msomi, mtumwa, asiye mtumwa

Hii ni kusema kwamba Mungu anamuona kwa sura ileil, sio kwa jamii, dini, utaifa, au tabaka (hai ya kijamii). " jamii, dini, tamaduni, na hali ya ekijamii

mtu wa Scythia

huyu ni mgeni ambaye hajui mila za mahala pale

asiyesoma

Huyu ni mtu kutoka nchi ya Scythia, ambayo ilikuwa nje ya himaya ya Rumi. Wagiriki na Warumi walitumia hili neno kwa mtu aliyekulia katika sehemu ambayo kila mmoja alifanya mambo maovu mda wote.

Kristo ni vitu vyote, na katika vyote

hakuna kilicho tenganishwa au kuachwa kwenye uwepo wa Kristo. "Kristo ni wa muhimu kwa watu wake wote."

Colossians 3:12

Vaeni...moyo wa huruma

Kama vile mtu awezavyo kuvaa nguo anapokuwa amevaa, waumini wanapaswa kuvaa huruma, unyenyekevu, nk. katika tabia zao kwa kila mmoja.

Kwa hiyo

"Kwa sababu kile nilichokisema ni kweli"

kama wateule wa Mungu - watakatifu na wapendwao

"kama watakatifu wa Mungu na wanaopendwa kwa pendo kuu waliochaguliwa."

ukarimu

"mpole" au "mpole"

unyenyekevu

"unyenekevu wa akili" au "upole wa akili"

upole

"upole"

chukulianeni ninyi kwa ninyi

"fanyeni kazi kwa pamoja katika maelewano na upendo. "chukulianeni na kila mmoja" au " vumilianeni na kila mmoja"

Hurumianeni kwa kila mtu

"Heshimu kila mmoja bora kuliko wanavyostahili kuheshimiwa"

ana lalamiko dhidi

"malalamiko dhidi"

ambao ni dhamana ya ukamilifu

"ambao unatufungamanisha kikamilifu pamoja" au "ambao unatufungamanisha pamoja katika maelewano kamili"

Colossians 3:15

Amani ya Kristo iwaongoze katika mioyo yenu

Paulo anazungumzia amani ambayo Kristo atoayo kana kwamba ilikuwa sheria. inaweza kuwa 1) "fanyeni mabo yote ili kwamba muweza kuwa na mahusiano ya amani kwa hiyo mnaweza kuwa na mahusiano ya amani na kila mmoja" au 2) "Mruhusu Mungu akupe amani kwenye mioyo yenu"

katika mioyo yenu

Neno "Yenu" lina rejea kwa waumini wa Kolosai.

Neno la Kristo likae ndani yenu

Paulo anzungumzia neno la Kristo kama lilikuwa mtu anayeweza kuishi ndani ya mtu mwingine. "siku zote tumaini ahadi za Kristo"

peaneni mawaidha ninyi kwa ninyi

"peaneni tahadhari ninyi kwa ninyi"

ni kwa Zaburi na nyimbo na tenzi za roho

"pamoja na aina zote za nyimbo kumsifu Mungu"

shukurani katika mioyo yenu

"mioyo ya shukurani"

katika maneno na katika matendo

kuongea au kufanya

"katika jina la Bwana Yesu"

"kumwabudu Bwana Yesu" au "pamoja na mamlaka ya Bwana Yesu"

kupitia yeye

"kupitia Bwana Yesu"

Colossians 3:18

Sentensi Unganishi:

Paulo anatoa baadhi ya maelekezo muhimu kwa wake, waume, watoto, kina baba, watumwa, na mabwana.

Wake, nyenyekeeni kwa

"Wake, tiini"

ni sahihi

"ni sahihi" au "ni sawa"

msiwe wakali dhidi ya

"msiwe wakali na" "msiwe na hasira juu ya"

msiwachokoze watoto wenu

"msiwachochee watoto wenu"

Colossians 3:22

tiini mabwana zenu kulingana na mwili

"tiini mabwana zenu wa kidunia"

sio kwa huduma ya machoni kama watu wa kufurahisha

"Vitu. msitii pale tu wakati Bwana wenu anawatazama, kama ambavyo mnatakiwa kuwafurahisha watu"

kama kwa Bwana

"kama muwezavyo kufanya kwa Bwana"

"tuzo ya umilikaji"

"zawadi ya urthi"

urithi

Kupokea kile Mungu alichowaahidi waamini kinazungumziwa kana kwamba kulikuwa na mali na utajiri kutoka wanafamilia.

yeyote atendaye yasiyo haki atapokea huku

"Mungu ataadhibu yeyote afanyaye yasiyohaki"

afanyaye uovu

ambaye atendaye makosa yoyote

hakuna upendeleo

"Mungu humuhukumu kila mmoja kwa kiwango kile kile"

Colossians 4

Wakolosai 04 Maelezo kwa ujumla

Muundo na Mpangilio

Wakolosai 4:1 inaonekana kuambatana na sura ya 3 badala ya 4

Maswala Muhimu kwa sura hii

"Kwa mkono wangu mwenyewe"

Ilikuwa kawaida kwa mwandishi wa kale katika inchi za Mashariki ya Karibu kuzungumza na mtu mwingine anaandika chini yanayozungumzwa. Barua nyingi za Agano jipya ziliandikwa namna hivi.Paulo aliandika mwenyewe salamu za mwisho.

Sehemu zingine zenye utata katika tafsiri ya sura hii

Ukweli wa siri

Paulo anaashiria ukweli wa siri katika sura hii. Jukumu la kanisa katika mipango ya Mungu halikujulikana hapo mwanzo. Lakini sasa Mungu amelitambulisha. Moja ya hii siri inahusisha watu wa Mataifa kuwa na nafasi sawa na Wayahudi katika mipango ya Mungu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#reveal).

__<< | __

Colossians 4:1

Sentensi Unganishi:

Baada ya kuongea na mabwana, Paulo anamalizia maelekezo yake maalumu kwa waamini tofauti tofauti katika kanisa la Kolosai.

haki na adili

Haya maneno ni kama kitu kile kile na yametumika kusisitiza vitu ambavyo ni maadili sahihi.

mnaye bwana wa mbinguni

Mungu anataka mahusiano kati ya bwana wa dunia na mtumwa wake wampende Mungu, bwana wa mbinguni, anawapenda watumwa wake wa duniani pamoja na watumwa wa mabwana wa dunia.

Colossians 4:2

Sentensi unganishi

Paulo anendelea kuwapa maelezo waamini juu ya kuishi na kuongea.

Maelezo kwa jumla:

Hapa neno "sisi" linarejea kwa Paulo na Timotheo ila sio Wakolosai.

Endelea kuwa thabiti katika maombi

"endelea kuomba kwa uaminifu" au "endelea kuomba mara kwa mara"

Mungu afungue njia

"Mungu ataandaa fursa"

siri ya kweli ya Kristo

Hii inarejea injili ya Yesu Kristo, ambayo haikueleweka kabla ya kuja Kristo kuja.

Kwa sababu ya lile neno , mimi nilifungwa.

Kwa kutangaza ujumbe ule wa Yesu Kristo sasa nimefungwa.

omba ili niweze kusema kwa uwazi

"omba niwe na nguvu na uwezo wa kutoa ujumbe wa Yesu Kristo kwa uwazi"

Colossians 4:5

Enenda kwa hekima kwa wale walioko nje

Wazo la kuenenda mara nyingi limetumika kwa ajili kungoza maisha ya mtu. "ishi kama kwamba wale ambao sio waamini wataona kwamba mnahekima"

kuokoa mda

"fanya mambo mazuri mnayoweza kwa mda wako" au "weka mda wako kwa busara"

maneno yenu yawe na neema wakati wote. wakati wote ikolee chumvi

"Mazungumzo yenu wakati wote yawe na neema na ya kuvutia."

lazima mjue jinsi ya kuwajibu

" lazima ujue namna ya kujibu maswali ya kila mmoja kuhusu Yesu Kristo"

Colossians 4:7

Sentensi unganishi:

Paulo anafunga na maelekezo maalumu kuhusu watu flani na kwa salamu pia na kwa kila mwamini.

Maelezo kwa jumla:

Onesmo alikuwa mtumwa wa Filimoni katika Kolosai. Alipoteza pesa kutoka kwa Filimoni na kukimbilia Rumi ambako akawa Mkristo kupitia huduma ya Paulo. Sasa Tikiko na Onesmo ndio wanaleta barua za Paulo Kolosai.

Maelezo kuhusu mimi

"kila kitu kilochokuwa kinatokea kuhusu mimi"

watumwa wenzangu

"watumishi wenzangu." Kupitia Paulo mtu aliyehuru, anajiona kama mtumishi wa Kristo na kumwona Tikiko kama mtumishi mwenzake.

kuhusu sisi

Haya maneno hayawajumuishi Wakolosai.

kuweza kutiwa moyo

Moyo ulikuwa katikati ya hisia nyingi. "kuweza kuwatia moyo"

ndugu yetu mpendwa na mwaminifu

Paulo anamwita Onesmo Mkrito mwenzake na mtumishi wa Kristo.

Watamwita

"Tikiko na Onesmo watasema"

kila kitu kilichotokea hapa

Watawaambia waamini wa Kolosai yote yanayochukua nafasi ambapo Paulo napoishi kwa sasa.

Colossians 4:10

Aristarko

Alikuwa amefungwa pamoja na Paulo huko Efeso wakati Paulo alipoandika barua hii kwa Wakolosai.

kama akifika

"kama Marko akija"

Yesu aliyeitwa Yusto

Huyu mtu alikuwa pia mtenda kazi pamoja na Paulo.

"Hao peke yao ni watu wa tohara ni watenda kazi wenzangu katika ufalme wa Mungu.

"Hawa wanaume watatu ni Wayahudi wakristo tunaofanya kazi pamoja nami ya kumtangaza Mungu kama mfalme kupitia Kristo Yesu"

Hawa peke yao wa tohara

"Hawa wanaume Aristarko, Marko na Yusto pekee ni watu waliotahiriwa.

Colossians 4:12

Maelezo kwa Jumla:

Leodekia na Hierapoli walikwa mjini karibu na Kolosai.

Epafra

Epafra alikuwa mtu aliyehubiri injili kwa watu wa Kolosai.

mmoja wenu

"kutoka mji wenu" au "mwanamji mwenzenu"

mtumwa wa Kristo Yesu

"ni kamati ya wanafunzi wa Kristo Yesu"

wakati wote najitahidi kukuweka katika maombi

"Naomba kwa bidii kwa aljili yako"

uweze kusimama kikamilifu na uhakika

"uweze kukomaa na kuwa jasiri"

Mimi ni shahidi yake, kwamba alifanya kazi ngumu kwa ajili yenu

"Nimefanya uchunguzi kwamba alifanya kazi ngumu sana kwa ajili yenu"

Dema

Ni mtendakazi mwingine pamoja na Paulo.

Colossians 4:15

ndugu

Hapa inamaanisha Wakrsto wenzang, kujumuisha wote wanaume na wanawake.

walioko Leokadia

ni mji ulio karibu sana na Kolosai mahali ambapo kulikuwa na kanisa pia

Nimfa, na kanisa lile lililoko ndani ya nyumba yake

mwanamke aliyeitwa Nimfa alitoa nyumba yake iwe kanisa huko Leokadia. "Nimfa na kundi la waumini walikutana nyumbani kwake"

mwambie Arkipo, iangalie huduma ile uliyopewa katika Bwana, kwamba lazima uitimize"

Paulo anatoa mawaidha kwa Arkipo kwa kazi aliyopewa na Mungu na kwamba Arkipo anawajibishwa na Bwana kwa kuitimiza.

Colossians 4:18

Sentensi Unganishi:

Paulo anafunga barua yake kwa salamu zilizoandikwa kwa mkono yake mwenyewe.

Kumbuka minyororo yangu

Paulo anapozungumzia minyororo anamaanisha alipokuwa gerezani. "Nikumbukeni na kuomba kwa ajili yangu wakati nipo gerezani"

Neema na iwe nanyi

Hapa neno "neema" linasimama badala ya Mungu, ambaye huonyesha neema kwa waamini. "Naomba kwamba Bwana wetu Yesu Kristo aendelee kutoa neema kwenu nyote.