Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa Wathesalonike 1

Sehemu 1: Utangulizi wa Jumla

Muhtasari wa kitabu cha Wathesalonike 1

  1. Salamu (1:1)

  2. Sala ya Paulo ya shukrani kwa Wakristo wa Thesalonike (1:2-10).

  3. Huduma wa Paulo Thesalonike (2:1-16).

  4. Paulo anashughulikia ukuaji wao wa kiroho

    • Kama mama (2:7)
    • Kama baba (2:11)
  5. Paulo anamtuma Timotheo kwa Wathesalonike na Timotheo anaripoti kwa Paulo kuhusu huduma huo.

  6. Mshauri yanayotekelezeka

    • Maisha ya kumfurahisha Mungu (4:1-12).
    • Starehe ya waliokufa (4:12-18)
    • Kurudi kwa Kristu ni motisha ya maisha ya umungu (5:1-11)
  7. Baraka za mwisho, shukrani na sala.

Nani aliandika Wathesalonike 1

Paulo aliandika Wathesalonike 1. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika ufalme nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu.

Paulo aliandika barua hii akiwa bado anakaa katika mji wa Korinto. Wasomi wengi wanaamini ya kwamba hii ndiyo ilyokuwa barua ya kwanza ya Paulo miongoni mwa barua alizoziandika nyingi.

Kitabu cha Wathesalonike 1 kinahusu nini?

Paulo aliwaandikia barua hii Waumini katika jiji la Thesalonike. Aliandika barua hii baada ya kulazimishwa na Wayahudi kuondoka jiji hilo. Katika barua hii anasema anachukulia ziara yake jijini humu kama iliyozaa matunda ingawa alilazimishwa kuondoka.

Paulo anajibu kwa habari iliyoletwa na Timoteo kuhusu waumini wa Thesalonike.Waumini wa huko walikuwa wanateswa sana. Paulo aliwahimiza kuendelea kuishi maisha yaliyompendeza Mungu. Pia aliwapa moyo kwa kuwaambia kinachofanyika watu wakufapo kabla ya Kristo kurudi.

Kichwa cha kitabu hiki kitafsiriwe vipi?

Watafsiri wanaweza chagua kichwa cha asili kama "Wathesalonike 1" ama "Wathesalonike wa kwanza". Wanaweza pia kuchagua kichwa cha kueleweka zaidi kama "Barua ya Kwanza ya Paulo kwa Wakristo waThesalonike," ama "Barua ya Kwanza kwa Wakristo wa Thesalonike." Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Nini maana ya "kuja kwa pili kwa Kristo?"

Paulo ameandika mengi kuhusu ujio wa pili wa Kristo duniani. Kristo atakaporudi atawahukumu watu wote duniani. Atatawala vyumbe vyote na kutakuwa na amani kila mahali.

Nini huwafanyikia wanaokufa kabla ya kurudi kwa Kristo?

Paulo aliweka wazi kwamba wote wanaokufa kabla ya kurudi kwa Kristo watafufuka na kuwa na Yesu.Hawatakuwa wafu milele.Paulo aliandika haya kutia moyo Wathesalonike. Hii ni kwa sababu wengi wao walikuwa na wasiwasi kwamba waliokufa wangeachwa nyuma siku kuu ya kurudi kwa Yesu.

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Paulo alimaanisha nini na matamshi "ndani ya Kristo" na "ndani ya Bwana?"

Paulo alitaka kuelezea dhana ya Mkristo kuwa karibu na Kristo. Tazama utangulizi katika kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi kuhusu swala hili.

Ni maswala gani muhimu katika maandishi ya kitabu cha Wathesalonike 1?

Katika mistari ifuatayo, matoleo ya kale yanatofoautiana na ya kisasa. Toleo la ULB lina masomo ya kisasa na limeweka ya zamani katika maelezo ya chini. Ikiwa kuna utafsiri wa Bibilia katika eneo jumla, watafsiri wanafaa watumie masomo kwenye tafsiri hizo.Kama siyo hivyo Watafsiri wanaombwa kufuata masomo ya kisasa.

  • "Neema na amani viwe nanyi."Matoleo mengine ya zamani husema, "Neema na amani kutoka kwa Baba Mungu wetu na Bwana wetu Yesu Kristo viwe nanyi."1:1
  • "Badala yake tulikuwa wapole miongoni mwenu kama mama anavyowafariji watoto wake." (2:7).Matoleo mengine ya kisasa na ya zamani yanasoma,"Tulikuwa kama watoto wachanga miongoni mwenu, jinsi mama hufariji watoto wake."
  • "Timotheo ndugu yetu na mfanyikazi mwenzetu wa Mungu" (3:2)Matoleo mengine husema, "Timotheo, ndugu na mtumishi wa Mungu."

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

1 Thessalonians 1

1 Wathesalonike 01 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Mstari wa kwanza unatanguliza barua hii kirasmi. Barua za kale katika Mashariki ya Karibu yalikuwa na utangulizi wa aina hii.

Dhana maalum katika sura hii

Ugumu

Watu wengine waliwatesa sana Wakristo wa Thesalonike. Lakini Wakristo hao waliyachukulia mateso hayo kwa njia nzuri. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

| >>

1 Thessalonians 1:1

Maelezo ya Jumla

Paulo anajitambulisha kama mwandishi wa barua na analisalimu kanisa la Watheselonike.

Paulo, Silivanus na Timotheo kwa kanisa.

Paulo ndiye mwandishi wa barua hii

Neema na amani iwe kwenu

Neno "neema" na "amani" ni maumbo kwa mtu anayeishi na watu kwa ukarimu na amani. "Mungu awe mkarimu kwenu na awape amani"

Amani iwe nanyi.

Neno "Nanyi" linaelezea waumini wa Thesalonike.

1 Thessalonians 1:2

Maelezo ya jumla

Katika hii barua "tu" ya husu Paulo Silvana, na Timotheo, isipo kuwa tu imeelezwa vinginevyo.

Huwa tunamshukuru Mungu.

Tunamshukuru Mungu kila wakati.

Tumekuwa tukiwa taja katika maombi yetu.

" Tunawaombea"

Kazi ya Imani

"Matendo ya Imani" au "Kazi yenu kwa Mungu kwa sababu mnamwamini yeye"

1 Thessalonians 1:4

sentensi unganishi

Paulo anaendelea kutoa shukurani kwa waamini walio Theselonike na ana washukuru kwa imani yao kwa Mungu

Ndugu.

"Waumini"

Tunajuaa.

Neno "sisi" linawaelezea Paulo, Silivanus na Timotheo lakini sio Waumini wa Thesalonike.

si kwa neno tu

si kwa kupitia kuhubiri tu

Ila kwa nguvu za Roho Mtakatifu.

Maana halisi zinaweza kuwa, 1. " Paulo na rafiki zake walihubiri kwa nguvu kwa kuwezesha na Roho Mtakatifu" au " 2. Injili inamatokeo makubwa kwa waaminio kupitia kazi ya Roho Mtakatifu".

Wanaume wa namna gani.

"Kwa namna ambavyo tulijitoa kwenu".

1 Thessalonians 1:6

Mmekuwa mfano wa kuigwa.

Kuiga maana yaake ni kutenda kama au kufataa. " mlituiga sisi".

"kulipokea neno"

"kuyapokea mafundisho" au "kuyakubali mafundisho".

Kwa taabu nyingi.

"katika wakati wa mateso makali" au " katika maudhi mengi".

Akaiya

Hii ilikuwa ni wilaya katika kipindi cha nyuma, na kwa sasa inaitwa Ugiriki.

1 Thessalonians 1:8

Limeenea kote

"Limesambaa pote"

Akaiya

Hii ilikuwa ni walaya katika kipindi cha nyuma, na kwa sasa inaitwa Ugiriki.

Kila mahali.

"Sehemu nyingi na kila Mikoa"

Kwa wao wenyewe.

Paulo anaelezea makanisa ambayo yaliwahi kuwapo katika Mikoa iliyokuwa karibu, waliokuwa wamesikia juu ya Waumini wa Thesalonike.

Wao wenyewe.

Kwa hapa "wenyewe" limetumika kusisitiza wale watu waliokuwa wamesikia juu ya waumini wa Thesalonike.

Namna gani ya mapokezi tuliyokuwa nayo pamoja nanyi.

"Kwa namna ya ukalimu mliyotukaribisha".

Mwanae

Hii ni anwani mhimu ya Yesu inayoeleza mahusiano yake na Mungu.

Aliemuinua.

"Ambaye Mungu alimuinua"

Alietuokoa

Paulo anawahusisha waumini aliokuwa akiwaandikia kwenye neno "sisi"

1 Thessalonians 2

1 Wathesalonike 02 Maelezo kwa ujumla

Dhana muhimu katika sura hii

Shahidi ya Mkristo

Paulo anathamini "Shahidi yake ya Kikristo" kama dhihirisho kwamba injili ni ya ukweli. Paulo anasema kwamba kuwa mtakatifu ama kuishi uungu unashuhudia wasio Wakristo. Paulo anatetea tabia yake ili shahidi wake isiathiriwe. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#testimony and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#godly and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#holy)

Kuishi Kikristo

Sheria ya Musa ilihitaji watu kutoa dhabihu ya wanyama au ya nafaka ndani ya hekalu. Mungu hahitaji dhabihu nyakati hizi. Mungu anahitaji watu waishi kama sadaka.Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses)

<< | >>

1 Thessalonians 2:1

sentensi unganishi

Paulo aeleza waamini huduma yao na thawabu.

ninyi wenyewe

neno 'wewe' inahusu wa Wathesalonike wauminio.

ndugu

Hapa hii ina maana Wakristo wenzake, ikiwa pamoja na wanaume na wanawake, kwa sababu waumini wote katika Kristo ni wanachama wa familia moja ya kiroho, na Mungu kama Baba yao wa mbinguni.

ujio wetu

neno 'wetu' inahusu Paul, Silvanusi na Timotheo lakini si waumini wa Wathesalonike.

haikuwa haina maana

ilikuwa na thamani sana

mateso na walikuwa jeuri

Paulo alipigwa na kuweka katika jela la Filipi. 'walikuwa wakinyanyaswa na kutukanwa.

miongoni mwa mgogoro uliyokithiri

"pindi mkutano ukiwa na upinzani mkubwa"

1 Thessalonians 2:3

wala hayatoki kwa Ubaya, wala kwa uchafu, wala kwa udanganyifu

Alikuwa mkweli, safi na mwaminifu

tulivyokubalika na Mungu na kuaminiwa

Paulo alijaribiwa na kithibitishwa mwaminifu na Mungu

tunanena

Paulo azungumza kuhubiri injili

"Mungu, ambaye huipima mioyo yetu

"Mungu, ambaye huchunguza mawazo na matendo yetu"

1 Thessalonians 2:5

maelezo ya jumla

Paulo anawambia Watheselonike waamini kuwa mwenendo wake haukuwa katika maneno ya kujipendekeza, ulafi, au kujitukuza

tumia maneno ya kujipendekeza

"Kuongea na wewe kwa sifa za uongo

wala kama kisingizio cha tamaa

"wala sisi hakutumia maneno kama kisingio cha uchoyo ili wewe utupatie vitu

inaweza kudai upendeleo

inaweza kuwa alifanya wewe kutupatia vitu

1 Thessalonians 2:7

kama mama awezavyo kuwafariji watoto wake mwenyewe.

Kama vile mama mpole anavyowafariji watoto wake, hivyo Paulo, Silvanusi na Timotheo alizungumza kwa upole kwa Wathesalonike

tulikuwa na shauku na wewe

"sisi tulikupenda wewe"

Wewe umekuja kuwa mpenzi mwema kwetu

sisi tunamjali kwa ajili yenu kiundani

Ndugu

Hapa hii ina maana Wakristo wenzake, ikiwa ni pamoja na wanaume na wanawake, kwa sababu wote waaminio katika Kristo ni wanachama wa familia moja ya kiroho na Mungu kama Baba yao wa mbinguni.

Kazi yetu na taabu

Maneno "kazi" na "tabu" kimsingi inamaana moja. Paulo ametumia hayo kusisitiza jinsi gani walifanya kazi ngumu "jinsi walifanya kazi ngumu"

Sisi tulifanya usiku na mchana ili tusiweze kuwa mzigo kwa yeyote kati yenu

"Sisi tulifanya kazi ngumu kufnya maisha yetu wenyewe hivyo haukuwa na haja ya kutusaidia sisi

1 Thessalonians 2:10

Takatifu, haki, na bila lawama

Paulo ametumia maneno matatu ambayo kimsingi ni kitu kimoja na kusisitiza kwamba wao tulipokuwa njia nzuri sana.

Baba na watoto wake mwenyewe

Paulo analinganisha jinsi baba kuwafundisha watoto wake kuishi na jinsi wao kuwahimiza na kuwahamasisha waumini kutembea kwa namna ambayo inamstahili Mungu

sisi kukuhimiza na kukuhamasisha wewe

Maneno "kuwahimiza" na "kukuhamasisha" kimsingia ni kitu kimoja. Paulo anayatumia kusisitiza (passionately) wamewahamasisha Wathesalonike "sisi ni nguvu kukuhamasisha wewe

kwenye ufalme na utukufu wake.

Neno "utukufu" inaelezea neno "Ufalme." "kwa ufalme wake mtukufu".

1 Thessalonians 2:13

maelezo ya jumla

Paulo anaendela kutumia "twa" kumaanisha yeye na anao safiri nao.

Kwa sababu hiyo twamshukuru Mungu kila wakati, kwa

"Sisi tunaendelea kumshukuru Mungu kila wakati kwa sababu"

Mlipokea kama kweli ilivyo neno la Mungu

Wathessalonike waliamini ujumbe wa Paulo aliohubiri kuwa ulikuja kutoka kwa Mungu na sio kutoka kwenye mamlaka ya Paulo mwenyewe

ni hili neno linalo fanya kazi kwenu mnao amini

Paulo anazungumzia injili kana kwamba ni mtu anaye fanya kazi

1 Thessalonians 2:14

ndugu

Hapa hii inamaanisha Wakristo wenzetu

mlikuwa wafuasi wa makanisa

Wao wanauzoefu sawa wa uadui kutoka baadhi yaWathessalonike kama vile waamini wa kwanza wazoefu wa mateso kutoka kwa viongozi wa Wayahudi "Ikawa kama makanisa"

kutoka kwa watu wa Taifa lenu wenyewe

"kutoka kwa Wathessalonike

Nao walituzuia sisi tusiseme

"Wao walijaribu kutufanya kuacha kusema"

daima walitimiza dhambi zao

"kuendelea kutenda dhambi"

Ghadhabu imewawajia kwao

"Adhabu ya Mungu imewajia ndani yao" au"'hasira ya Mungu imewajia ndani yao'

1 Thessalonians 2:17

ndugu

Hapa hii inamaanisha Wakristo wenzetu

katika uso, si kwa moyo

"Kimwili lakini sisi tunaendelea kuomba kwa ajiri yenu"

kuona uso wako

"Kukuona wewe" au "kuwa na wewe"

Mimi Paulo mara moja na tena

"Mimi Paulo, alijalibu mara mbili"

Kwa nini ni matumaini yetu ... wakati wa kuja kwake?

"Kujiamin kwetu kwa baadae, furaha, na taji ya utukufu ni wewe na wengine wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu.'

1 Thessalonians 3

1 Wathesalonike 03 Maelezo kwa ujumla

Dhana muhimu katika sura hii

Kusimama

Katika sura hii Paulo anatumia "simama imara" kuonyesha kuwa imara. Hii ni njia ya kawaida ya kuelezea kuwa imara ama mwaminifu. Paulo anatumia "Kutingizwa" kama kinyume cha kuwa imara. Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faithful)

<< | >>

1 Thessalonians 3:1

sentensi unganishi

Paulo anawambia waamini amemtuma Timotheo kuimarisha imani zao.

Hatukuweza kuvumilia.

Neno "sisi" linawaelezea Paulo, Silivanus na Timotheo lakini sio waumini wa Thesalonike. au " hatukuweza kuwa na uvumilivu tukihofu juu yenu"

Ilikuwa vyema kubaki kule Atheni peke yake.

"Ilikuwa vyema kwangu na Silivanus kubaki Atheni.

Vyema

"Vizuri" au "yenye mantiki"

Atheni

Huu ni Mji katika jimbo la Akaiya, ambapo kwa sasa huitwa Ugiriki.

Ndugu yetu.

"Mkristo mwenzetu"

Hakuna ambaye atasumbuliwa

"Hakuna atakayekuwa na matatizo" au hakuna atakaye ondolewa"

Tumeteuliwa.

"Tumekusudiwa"

1 Thessalonians 3:4

Ukweli dhabiti.

"bila shaka" au " uhakika"

Tulikuwa na wewe

Neno "sisi" linawaelezea Paulo, Silivanus naTimotheo lakini sio waumini wa thesalonike.

Kupata mateso.

"kutendewa mabaya na wengine"

Sikuweza kuvumilia.

Kwa hapa " mimi" inamuelezea Paulo: nilitaka kujua.

Nilimtuma.

"Nilimtuma Timotheo"

Bure.

" Isiyofaa"

1 Thessalonians 3:6

sentensi unganishi

Paulo anawambia wasomaji kuhusu taarifa ya Timotheo baada ya kutoka kuwasalimu

Alikuja kwetu

Neno " kwetu" linawaelezea Paulo na Silivanus lakini sio waumini wa thesalonike.

Habari njema ya Imani yako

" Taarifa nzuri juu ya Imani yako"

Mmekuwa na kumbukumbu nzuri

"Mmekuwa na kumbukumbu nzuri mara kwa mara"

Mnatamani kutuona sisi

"Mnashauku ya kutuona sisi"

Ndugu

" kwa hapa " ndugu inamaanisha wakristo wenzao.

Kupitia Imani yenu.

"kupitia imani yenu katika kristo" au "kupitia maendeleo yenu katika kristo"

1 Thessalonians 3:8

kwa sasa tunaishi.

Neno " sisi" linawaelezea Paulo, Silivanus na Timotheo lakini sio waumini wa thesalonike.

Msimame imara.

"Mnaamini kwa sana"

Ni shukurani zipi tumrudishie Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha yote tulinayo juu yenu kwa Mungu wetu?

Swali hili rhetorical huonyesha shukrani. AT 'Hatuwezi kumshukuru Mungu ya kutosha kwa ajili matendo yake kwa ajili yako! Sisi sana kufurahi juu yako wakati sisi kuomba kwa Mungu wetu!

Kwa shukrani tunaweza kutoa kwa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote kwamba tuna mbele ya Mungu juu yako?

Swali hili rhetorical huonyesha shukrani. AT 'Hatuwezi kumshukuru Mungu ya kutosha kwa ajili matendo yake kwa ajili yako! Sisi sana kufurahi juu yako wakati sisi kuomba kwa Mungu wetu!

Usiku na Mchana.

"Mara kwa mara"

Ni ngumu

Bidii

Kuuona uso wako.

"Kukutembelea"

1 Thessalonians 3:11

maelezo ya jumla

katika hii mistari, neno "wetu" halielezei watu wa aina moja kila wakati.

Na Mungu wetu

"Tunaomba ya kuwa Mungu wetu"

Na Mungu wetu...Bwana wetu Yesu.

Neno "wetu' linaelezea waumini wote.

Baba mwenyewe.

"mwenyewe" inamuelezea "Baba" kwa msisitizo.

Zielekeze njia zetu kwako

Neno "zetu" linawaelezea Paulo, Silivanus na Timotheo lakini sio waumini wa Thesalonike.

Pia sisi tunafanya

Neno "sisi" linawaelezea Paulo, Silivanusi na Timotheo lakini sio waumini wa Thesalonike.

Na afanye hivyo

"Tunaomba ya kuwa Mungu atatenda"

Katika ujio wa Bwana wetu Yesu

" wakati Yesu atakapokuja tena duniani"

Na utakatifu wake wote

"Na wale wote waliowakwake"

1 Thessalonians 4

1 Wathesalonike 04 Maelezo kwa ujumla

Dhana muhimu katika sura hii

Uzinzi

Mila mbalimbali zina vipimo tofauti vya uzinzi na kwa hivyo itakuwa vigumu kutafsiri fungu hili.Watafsiri pia ni lazima wafahamu miiko ya kitamaduni. Maneno haya ni maneno yasiofaa kwa adabu sahihi.

Kufa kabla ya kurudi kwa Kristo

Katika kanisa la mwanzo, watu walijiuliza chenye kingefanyika iwapo mtu angekufa kabla ya kurudi kwake Yesu Kristo. Kuna uwezekano kwamba walikuwa na wasiwasi kama waliokufa kabla ya kurudi kwake Kristo wangejumuishwa kwenye ufalme wake. Paulo anajibu swali hilo.

"Kunyakuliwa mawinguni tumlaki Bwana hewani"

Kifungu hiki kinaashiria wakati Yesu atakapowaita wale waliomwamini. Wasomi wanatofautiana iwapo hii inaashiria kurudi kwake Yesu kwa mara ya mwisho kwa utukufu ama hapana. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe)

<< | >>

1 Thessalonians 4:1

Ndugu

hapa "ndugu" inamaanisha mkristo mwenzako

Tunawatia moyo na kuwasihi

Neno "sisi" linawaelezea Paulo, Silvanus na Timothy lakini sio waamini wa Thesalonike. Neno "kutia moyo" na "kusihi" inamaana moja. Paulo aliyatumia ili kusisitiza ni kwa jinsi gani wanawatia moyo waamini.

Mlipokea maelekezo toka

"mlifundishwa na"

Lazima mtembee

Hapa neno "kutembea" inaelezea namna ambavyo mtu anatakiwa kuishi.

1 Thessalonians 4:3

Epuka tamaa za mwili

"kaa mbali na tamaa za mwili"

Namna ya kumiliki

"kujua namna ya kuishi na"

Tamaa za mwili

"tamaa mbaya za mwili"

Asiwepo mtu

"asowepo yeyote" au "asiwepo mtu"

Atakayevuka mpaka na kumkosea

Hii ni maelezo zaidi inayoelezea wazo lile lile kwa namna mbili.

Bwana ndiye mwenye kulipa kisasi

"Bwana atamuadhibu yule atakayevuka mipaka na atamtetea yule atakayekosewa"

Tulivyowaonya na kuwashuhudia

"Tulivyowaambia kabla ba kuwaonya kwa nguvu"

1 Thessalonians 4:7

Mungu hakutuita kwa uchafu bali kwa utakatifu

Mungu alituita kuwa wasafi na watakatifu.

Mungu hakutuita sisi

Neno "sisi" linamaanisha waamini wote.

Yeye anayelikataa hili

"Yeyote asiyezingatia mafundisho haya" au "yeyote anayeyapuuzia mafundisho haya"

1 Thessalonians 4:9

Upendo wa ndugu

"upendo kwa waamini wenzako"

Mlifanya yote kwa ndugu walioko Makedonia yote.

"mlionesha upendo kwa waamini wa Makedonia"

Ndugu

Hapa "ndugu" inamaanisha Mkristo mwenzako

Mtamani

"Kujiingiza" au "kujitahidi kwa bidii"

Fanya shughuli zako

Hii inamaanisha usiingilie mambo ya watu wengine.

Fanya kazi kwa mikono yako

"mfanye kazi zenu wenyewe ili mpate kile mnachookiitaji"

Tembea kwa usahihi

"Ishi kwa heshima na tabia njema"

Wale walioko nje ya imani

"wale ambao sio waamini wa Kristo"

Usihitaji kitu chochote

"Usipungukiwe na hitaji lolote"

1 Thessalonians 4:13

Maelezo ya jumla

Paulo anaongelea waamini walio kufa, walio hai, na ao watakao ishi Kristo akirudi.

Hatutaki msielewe.

"Tunataka muelewe"

Hatutaki

"Sisi" inawaelezea Paulo, Silvanus na Timotheo lakini sio waamini wa Thesalonike.

Ndugu

Hapa "ndugu" inamaanisha Mkristo mwenzako.

Kulala

Hapa inamaanisha "kufa."

Msiomboleze

"Msisikitike"

Kama hao wasiojua mambo yajayo

"Kama watu wasioamini"

Kama tukiamini

Hapa "sisi" linawaelezea Paulo na hadhira yake.

Kufufuka tena

"kufufuka na kuishi tena"

Atawaleta pamoja na Yesu hao waliolala mauti.

"akirudi atawafufua waamini waliokufa wakimwamini Yesu"

Kwa ajili ya hayo twasema

"Sisi" linawaelezea Paulo, Silvanus na Timotheo lakini sio waamini wa Thesalonike.

Hakika hatutawatangulia

"hakika hatutakwenda mbele yao"

1 Thessalonians 4:16

Bwana mwenyewe atashuka.

"Bwana mwenyewe atakuja chini"

Malaika mkuu

Malaika mkuu

Waliokufa katika Kristo watafufuka kwanza

Hapa anamaanisha kifo cha kimwili. "wale waliomwamini Yesu Kristo lakini walikufa watafufuka kwanza"

Sisi tulio hai

Hapa "sisi" linamaanisha waamini wote.

Pamoja nao

Neno "wao" linawaelezea waamini waliokufa.

Tutaungana hewani ili kumlaki Bwana mawinguni.

Kumlaki Bwana Yesu

1 Thessalonians 5

1 Wathesalonike 05 Maelezo kwa ujumla

Muundo na Mpangilio

Paulo anamalizia barua yake kama barua za kawaida nyakati za kale kule Mashariki Ya Karibu.

Dhana Muhimu katika sura hii

Siku ya bwana

Wakati kamili wa ujio wa siku ya Bwana itakuwa ni kwa ghafla pasipotarajiwa. Hii ndiyo maana ya "kama mwizi usiku". Kwa sababu hii, Wakristo waishi wakijiandaaa kurudi kwa Bwana. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#dayofthelord and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-simile)

"Kukata kiu ya Kiroho"

Hii ina maana ya kutojali ama kufanya kinyume na mwongozo na kazi ya Roho Mtakatifu.

__<< | __

1 Thessalonians 5:1

sentensi unganishi

Paulo anazidi kuongelea siku Yesu ata rudi

muda na nyakati

"muda ambayo Bwana Yesu atarudu tena "

Ndugu

Her "ndugu" inamaanisha Wakiristo wengine

mwajua ya kuwa

"kufahamu kabisa" au "kuwa na ufahamu"

kama mwizi ajapo usiku

kama vile ambavyo mtu hajui ni usiku gani mwivi atakuja kuvunja na kuiba, sisi hatujui siku ya Bwana itakuja lini. "bilakutazamia"

Pale wasemapo

"Watu watakaposema"

ndipo uharibifu

"ndipo uharibifu usiotegemewa"

kama utungu umjiavyo mama mwenye mimba.

Kama vile mwanamke mjamzito maumivu ya kujifungua mtoto huja ghafla na wala haichi mpaka kuzaliwa itakapokamilika, ndivyo uharibifu huja na watu hawataweza kuepuka.

1 Thessalonians 5:4

ninyi, ndugu hampo kwenye giza

Hapa "ndugu" inamaanisha Wakristo wenzake. "Ninyi si wa dunia hii ya uovu, ambayo ni kama kuwa katika giza"

hata ile siku iwajie kama mwizi

Siku ambayo Bwana atakuja haitakuwa ya kushitukisha kama vile mwizi anavyo mshitukisha mtu. "Isiwapate pasipo kujiandaa"

ninyi nyote ni wana wa mchana...siyo wana wa usiku

Hapa "wana wa mchana" inamaanisha wafuasi wa Kiristo. "wana wa usiku" inamaanisha wale wote wengine wanaofuata dunia.

tusilale kama wengine wafanyavyo

Paulo anafananisha kulala na ile hali ya kutokujua kuwa Yesu atarudi kuhukumu ulimwengu. " tusiwe kama wengine ambao hawajui kuwa Yesu anarudi tena"

tusilale

neno "tu"inarejea kwa waumii wote .

bali tuendelee kukesha na kuwa na kiasi

Walioamini katika Kristo wanatakiwa wawe katika hali ya tahadhari kwa kurudi kwake na kuwa na kuweza kujizuia,

Kwa kuwa wale walalao hufanya hivyo usiku

Kama ilivyo usiku wakati watu wamelala na hawajui nini kinachotokea, ndivyo itakavyokuwa kwa dunia, ambao hawajui kuwa Kiristo atarudi.

wale wanao lewa hulewausiku

Paulo anataja kuwa ni usiku ambapo watu huwa wanalewa, hivyo kama watu hawana ufahamu kuwa Kiristo anarudi hawataishi maisha ya kujizuia

1 Thessalonians 5:8

maelezo ya jumla

katika mistari ya 8-10 "sisi" ya husu waamini wote

wana wa mchana

Hii inawakilisha waumini katika Kristo. "waumini katika Kristo" au "watu wa mwanga."

tuwe na kiasi

"tujizoeze katika kujizuia"

kuvaa dirii ya

kama askari anavyo vaa dree kuulinda mwili wake, Mkiristo aliyeamini anayeishi kwa imani na upendo atapata ulinzi. "tujilinde wenyewe kwa"

kofia ya chuma

kama kofia ya chuma inavyo mlinda askari kichwani, hivyo ndivyo uhakika wa waokovu inavyomlinda muumini. "na ujue"

kwamba tumacho au tumelala

"kwamba tuko hai au tumekufa"

kujengana ninyi kwa ninyi

"kufarijiana"

1 Thessalonians 5:12

Ndugu,

Hapa "Ndugu" humaanisha walioamini wenzake

tuwatambue wale wanaotumika

"Kuheshimu na kuthamini wale ambao wanashiriki katika kuongoza"

na wale wanaowaongoza katika Bwana

Hii inamaanisha wale watu ambao Mungu amewaweka kutumika kama viongozi katika vikundi vya waumini sehemu mbalimbali.

muwatambue na kuwapa heshima kwa upendo kwa sababu ya kazi yao

"Waheshimuni na kuwatii kwa kazi yao kwasababu mnawapenda wao"

1 Thessalonians 5:15

Furahini siku sote, Ombeni bila ukomo, Mshukuruni Mungu kwa kila jambo

Paulo anawatia moyo waumini kuendeleza tabia ya kiroho ya kufurahi kwa kila jambo, kuwa na juhudi katika maombi, na kutoa shukurani kwa mambo yote.

kila jambo

katika hali zote

Kwa kuwa haya ni mapenzi ya Mungu

Paulo anaeleza zile tabia alizo zitaja kuwa ni mapenzi ya Mungu kwa waamini wote.

1 Thessalonians 5:19

Msimzimishe Roho

"Msimzuie Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yenu"

Msiudharau unabii

"Msiwe na dharau kwa unabii" au "Msichukie chochote ambacho Roho Mtakatifu atamueleza mtu"

Jaribuni kila Jambo

"Kakikisha kuwa kila unabii ni kweli na unatoka kwa Mungu"

shikilia lililo jema

Paulo anazungumza ujumbe za Roho Mtakatifu kama ni vitu ambavyo mtu anaweza shika mikononi mwake.

1 Thessalonians 5:23

kuatenga kwa ajili yake kabisa

"awatenge" au "kufanya ninyi msiwe na kosa, hivyo kwamba msitende dhambi"

roho, nafsi na miili wote

Hii ni mfanano ambao neno "roho", "nafsi" na "mwili" kuwa na maana sawa lakini hutumiwa hapa kwa msisitizo.

itunzwe pasipo mawaa katika

"itunzwe isifanye dhambi mpaka"

Yeye aliyewaita ni mwaminifu

"Yeye ni Mwaminifu aliyewaita "

ndiye ambaye pia kutenda.

""atawasaidia ninyi"

1 Thessalonians 5:25

maelezo ya jumla

Paulo anatoa kauli zake za kufunga

ndugu

Hapa "ndugu" ya maanisha wa Kristo

nawasihi katika Bwana

"nawauliza, kama ni Bwana anazungumza nanyi"

barua hii isomwe

hii yawezwa tajwa katika kauli tendaji, "ninyi nyote msome hii barua"