Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa 1 Timotheo

Sehemu ya 1 Utangulizi kwa ujumla

Muhtasari wa kitabu cha 1 Timotheo

  1. Salamu (1:1,2)

  2. Paulo na Timotheo

    • Onyo kuhusu walimu wa uongo (1:3-11)
    • Paulo anashukuru kwa kile Kristo amemfanyia katika utume wake (1:12-17).
    • Anamuomba Timotheo kupigania katika vita hivi vya kiroho (1:18-20).
  3. Sala kwa wote (2:1-8)

  4. Wajibu na majukumu kanisani (2:9-6:2)

  5. Maonyo

    • Onyo la pili kuhusu walimu wa uongo (6:3-5)
    • Pesa (6:6-10).
  6. Maelezo kuhusu mtu wa Mungu (6:11-16)

  7. Maelezo kwa Matajiri (6:17-19)

  8. Maneno yakufunga kwa Timotheo (6:20-21)

Nani aliandika kitabu cha 1 Timotheo?

Paulo alikiandika kitabu cha 1 Timotheo. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika himaya nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu.

Kitabo hiki ni barua ya kwanza ya Paulo kwa Timotheo. Timotheo alikuwa mwanafunzi wake na rafiki wake wa karibu. Kuna uwezekano kama Paulo aliandika barua hii akikaribia kufa.

Kitabu cha 1 Timotheo kinahusu nini?

Paulo alikuwa amemwacha Timotheo katika jiji la Efeso kuwasaidia waumini wa huko. Paulo aliandika barua hii kumshauri Timotheo kuhusu maswala mengi. Kati ya maswala aliyoangazia ni swala la kuabudu katika kanisa, na masherti ya waongozi wa kanisa na maonyo kuhusu walimu wa wongo. Barua hii inaonyesha namuna Paulo alifundisha Timotheo kuwa mwongozi wa makanisa.

Kichwa cha kitabu hiki kitafsiriwe namna gani?

Watafsiri wanaweza amua kukiita kitabu hiki kutumia jina lake la kiasili, "1 Timotheo" ama "Timotheo wa Kwanza" ama wanaezatumia kichwa kinachoeleweka zaidi kama "Barua ya Kwanza kwa Timotheo" (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Uanafunzi ni nini?

Uanafunzi ni hali ya kuwafanya watu wawe wanafunzi wa Kristo. Lengo kuu la uanafunzi ni kuwafanya Wakristo kuwa kama Kristo. Barua hii inatoa mwelekeo jinsi kiongozi anatakiwa kumfunza Mkristo ambaye hajakomaa. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#disciple)

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Wingi na umoja wa "wewe"

Neno "mimi" katika kitabu hiki linaashiria Paulo. "Wewe" inamaanisha Timotheo. Tofauti ya haya ni 6:21 (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-exclusive and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-you)

Paulo alimaanisha nini na maelezo "ndani ya Kristo" na "ndani ya Bwana" na kadhalika?

Paulo alitaka kuelezea wazo la kuwa na ushirika wa karibu sana kati ya muumini na Kristo. Tafadhali tazama utangulizi wa kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi kuhusu kauli hii.

Ni maswala gani kuu ya kimaandishi katika kitabu cha 1 Timotheo?

Katika aya ifuatayo,matoleo ya kisasa yanatofautiana na matoleo ya kale. Toleo la ULB lina masomo ya kisasa na imeweka masomo ya zamani kwenye tiniwayo(maelezo ya chini). Iwapo tafsiri ya Bibilia inapatikana eneo kwa ujumla, watafsiri wanashauriwa kuzingatia matumizi ya masomo yaliyoko katika matoleo hayo. Kama sivyo, watafsiri wanashauriwa kutumia masomo ya kisasa.

  • "Utauwa ndiyo njia ya kupata pesa zaidi" Matoleo mengine ya kale yanasoma, "Utauwa ni njia ya kupata pesa zaidi. Jiepushe na vitu hivyo." (6:5).

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

1 Timothy 1

I Timotheo 01 Maelezo kwa jumla

Dhana kuu katika sura hii

Watoto wa Kiroho

Katika sura hii, Paulo anamwita Timotheo "Mwanawe wa Kiume" na "mwanawe"..Paulo alimfanya Timotheo kuwa Mkristo na kiongozi wa kanisa. Kuna uwezekano Paulo pia alimwongoza kumwamini Kristo. Kwa maana hiyo Paulo akamwita Timotheo "mwanangu katika Kristo".

Orodha ya ukoo

Orodha ya ukoo ni orodha ya rekodi ya mababu na wazawa wa mtu. Wayahudi walitumia orodha ya ukoo kuwachagua watu kuwa wafalme. Walifanya hivi kwa sababu ni mtoto tu wa kiume wa mfalme ambaye alistahili kuwa mfalme.Walionyesha pia kabila na familia familia yao. Kwa mfano makuhani walitoka kwa ukoo wa Walawi na wana wa Aruni. Maarufu wengi walikuwa na rekodi za ukoo yao.

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Maneno yanayohusu jambo moja

Kauli "Sheria ni nzuri mtu akiitumia kisheria" ni maneno yanayoashiria kitu kimoja. Maneno "sheria" na "kisheria" yana usemi sawa katika lugha ya awali.

| >>

1 Timothy 1:1

Maelezo ya jumla

Katika kitabu hiki, neno "Yetu" linamaanisha Paulo na Timotheo.

Paulo

"Mimi, Paulo, nimeandika barua hii." Lugha yako inaweza kuwa na njia tofauti ya kumtambulisha mwandishi wa barua. Tumia njia iliyo sahihi kwenu.

kulingana na amri ya

"kwa amri ya" au "kwa mamlaka ya"

Mungu Mwokozi wetu

"Mungu ambaye alituokoa sisi"

Kristo Yesu tumaini letu

Hapa neno "tumaini letu" humaanisha mtu ambaye tunaweka tumaini letu kwake. "Kristo Yesu, ambaye ni tumaini letu" au "Kristo Yesu katika yeye tunaweka ujasiri wetu"

mtoto wa kweli katika imani

Paulo anaongea juu ya uhusiano wa karibu kati ya Timotheo na Paulo kama ule wa baba na mtoto. Paulo anamchukulia Timotheo kuwa ni mtoto wake kwa kuwa alimfundisha kuwa na imani katika Kristo. Mfano wa tafasiri: "ambaye ni sawa na mtoto kabisa kwangu"

Neema, rehema, na amani

"Basi neema, rehema, na amani iwe kwenu," au "Basi ninyi mpate wema, rehema, na amani"

Mungu Baba

"Mungu, ambaye ni Baba yetu" ni jina la muhimu la Mungu.

Kristo Yesu Bwana wetu

"Kristo Yesu, ambaye ni Bwana wetu"

1 Timothy 1:3

Kauli Unganishi

Paulo anamtia moyo Timotheo kukataa matumizi mabaya ya sheria na atumie vizuri mafundisho kutoka kwa Mungu.

Kama nilivyokusihi wewe

"Kama nilivyokuhimiza wewe," au "Kama nilivyokuomba kwa bidii"

kaeni Efeso

"nisubirini mimi hapo katika mji wa Efeso"

mapokeo mengine

mafundisho mengine tofauti na yale tuliyofundisha sisi.

wala hawatasikiliza kwa makini

"Pia nataka ninyi muwaamuru wasisikilize kwa makini"

hadithi

zinaweza kuwa ni hadithi kuhusu mababu zao.

vizazi visivyo na mwisho

Paulo anatumia "isiyo na mwisho" kusisitiza kwamba vizazi ni vingi.

Hizi husababisha malumbano

"Hizi huwafanya watu kutokubaliana." Watu walijadili kuhusu hadithi na nasaba ambamo hakuna angeweza kujua ukweli wake.

badala ya kusaidia mpango wa Mungu, ambao ni kwa imani

Maana: 1) badala ya kutusaidia sisi kujua mpango wa Mungu wa kutuokoa, ambao tunajifunza kwa imani 2) badala ya kutusaidia sisi kufanya kazi ya Mungu, ambayo tunaifanya kwa imani

1 Timothy 1:5

sasa

Neno limetumika hapa kuonesha kituo kwenye mafundisho ya msingi. Hapa Paulo anaeleza lengo la kile anachomwamuru Tithotheo.

amri

Hii haimaanishi Agano la Kale au Amri Kumi lakini zaidi ni wajibu uliotolewa na Paulo kwenye 1:3.

ni pendo

Inawezekana kumaanisha 1) upendo kwa Mungu au 2) kuwapenda watu.

kutoka moyo safi

Hapa "safi" inamaanisha kuwa mtu hana nia ovu ya kufanya mabaya. Na "moyo" hapa inamaanisha akili na mawazo ya mtu.

dhamiri nzuri

"dhamiri ambayo imechagua haki juu ya mabaya"

imani thabiti

"uaminifu" au "ukweli" au "isiyo na unafiki"

baadhi ya watu wamekosea

Paulo anaongelea imani ndani ya Kristo kuwa shabaha yetu.

na wameasi vitu hivi

"kuasi" kama ilivyotumika hapa ni msemo unaomaanisha kuwa watu wameacha kufanya maagizo ya Mungu.

walimu wa sheria

Hii inamaanisha "sheria za Musa"

Lakini hawaelewi

"ingawa hawaelewi" au "lakini hawaelewi"

1 Timothy 1:9

Na tunajua hiki

"Hiyo ni, sisi tunaelewa hiki" au "Kwasababu tunatambua hili" au "Sisi pia tunajua hili"

haikutengenezwa kwaajili ya mtu mwenye haki

"haikutolewa kwa mtu mwenye haki" au "haikuwekwa kwa mtu anaye tii" au "hakupewa mtu ambaye ni mwenye haki mbele za Mungu"

kwaajili ya wale wauao baba na mama zao

"wauaji wa baba zao na mama zao" au "wale ambao huwaumiza kimwili baba na mama zao"

watu wasio na maadili kingono

Huu ni mfumo wa neno la kiume kwaajili ya malaya wa kike. Kwenye maeneo mengine ilitumika kama sitiari kwa watu wasiowaaminifu kwa Mungu, lakini katika suala hili maana inaonekana kuhusisha mtu yeyote ambaye analala na mtu mwingine nje ya ndoa.

mashoga

"wanaume ambao wanalala na wanaume wengine."

wale ambao wanateka watu kwaajili ya utumwa

"wale ambao wanateka watu kuwauza kama watumwa" au "wale ambao wanachukua watu kuwauza kama watumwa"

injili ya utukufu wa Mungu wa baraka

"injili ya kuhusu utukufu ambao ni mali ya Mungu wa baraka" au "injili ya utukufu na Mungu mbarikiwa"

ambayo nimeaminiwa

"ambayo Mungu amenipa mimi na akanifanya kuwajibika kwayo"

1 Timothy 1:12

Kauli Unganishi:

Paulo anazungumza jinsi alivyotenda zamani na anamtia moyo Timotheo kumtumaini Mungu.

Nashukuru

"Ninashukuru" au "mimi nashukuru kwa"

yeye aliniona mimi mwaminifu

"yeye alinitazama mimi mwaminifu" au "alifikiria kuwa ninafaa"

na akaniweka katika huduma

"na kuniweka katika nafasi ya kutumika" au "hivyo aliniteua katika huduma"

mimi, mtukana Mungu wa zamani

"mimi, ambaye alisema maovu kinyume na Kristo" au "mimi, ambaye nilikuwa mtukana Mungu hapo zamani"

mtu wa vurugu

"mtu ambaye anaumiza wengine." Huyu ni mtu anayeamini anayo haki kuumiza wengine.

Lakini nilipokea neema kwa sababu nilitenda kwa ujinga katika kutoamini

NI: "Lakini kwa sababu sikuamini katika Yesu, na nilikuwa sijui nilichokuwa nikifanya, nilipokea neema kutoka kwa Yesu"

Nilipokea neema

NI: "Yesu alinionesha neema" au "Yesu kashatoa neema kwangu"

Lakini neema

"Na neema"

ilibubujika kwa imani na upendo

"ilikuwa kwa wingi sana" au "ilikuwa zaidi kuliko ile ya kawaida"

1 Timothy 1:15

Ujumbe huu ni wa kweli

"Kauli hii ni ya kweli"

unaofaa kukubalika

"unaweza kupokelewa bila mashaka yoyote" au "unatakiwa kukubalika kwa ujasiri wote"

kwanza nilikuwa nimepata rehema

"kwanza Mungu alinionesha neema" au "Nilipewa neema kutoka kwa Mungu kwanza"

mfalme mkongwe

"mfalme wa milele" au "mtawala mkuu wa milele"

iwe heshima na utukufu

"aweze kuheshimiwa na kupewa utukufu" au "watu waweze kumweshimu na kukupa utukufu"

1 Timothy 1:18

Nimeweka amri hii mbele yenu

"Amri hii naitoa kwenu" au "Amri hii naiweka kwenu"

mtoto wangu

Hili ni neno la ujumla sana kuliko "mwana" au "binti", lakini bado bado linaonesha uhusiano na baba. Paulo antumia hii kama sitiari kwaajili ya upendo wake kwa Timotheo.

shiriki katika mashindano mazuri

"shiriki katika mashindano ambayo yanafaidisha juhudi" au "jitahidi kuwashinda maadui" Hii ni sitiari ambayo inamaanisha "fanya juhudi kwaajili ya Bwana" (UDB)

amepiga miamba/mawimbi kwa heshima ya imani

Paulo anatumia sitiari nyingine kulinganisha hali ya imani yao na meli ambayo imezama kwenye mwamba. Sitiari hii inamaanisha "kilichotokea kwenye imani zao ambacho ni maafa" (UDB). Utumie hii au sitiari inayofanana kama itaeleweka kwa lugha yako.

wanaweza kufundishwa

"kwamba Mungu anaweza kuwafundisha"

1 Timothy 2

1 Timotheo 02 Maelezo kwa ujumla

Dhana muhimu katika sura hii

Amani

Paulo anawasihi Wakristo kuwaombea kila mtu. Wanastahili kuwaombea viongozi ili Wakristo waishi kwa amani kwa njia ya kimungu na ya kiheshima

Wanawake katika kanisa

Watafsiri wawe makini zaidi ili watafsiri kikamilifi mistari hii.

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Sala" , "kuombeana" na "shukrani"

Maneno haya yanafanana katika maana yao. Siyo muhimu kuyatazama kama yanayohitilafiana.

<< | >>

1 Timothy 2:1

Kauli unganishi

Paulo anamtia moyo Timotheo kuombwa kwa ajili ya watu wote.

Awali ya yote

"Kitu cha muhimu zaidi" au "Kabla ya kitu chochote"

Nakuomba

"Nakusihi" au "Nakuomba"

Heshima

njia ambayo watu wanaweza kutuheshimu. Iliyoainishwa na "Utauwa", Hii ni njia ambayo watu wengine watamheshimu Mungu na kututii sisi.

1 Timothy 2:5

Mjumbe mmoja kati ya Mungu na mtu

Mjumbe ni mtu anayesaidia kujadili ujumbe wa amani kati ya watu wawili ambao hawaelewani. hapa Yesu anawasaidia wenye dhambikuingia kwenye mahusiano ya Amani na Mungu.

akajitoa mwenyewe

"kufa kwa hiari

Kama fidia

"Kama bei ya uhuru" au "kama malipo ya kupata uhuru"

ushuhuda wa wakati mtimilifu

"Ushuhuda wake ni kwawakati mtimilifu" au "Ushuhuda wa wakati huu"

kwa kusudi hili

"Kwa hii" au "kwa sababu hii" au kwa ushuhuda huu"

nimefanywa kuwa mhubiri

"Nimechaguliwa kuwa mhubiri" au "nimechaguliwa na Kristo kuwa mhubiri"

Natamka ukweli

"Nazungumza ukweli" au "nakuambia ukweli"

Sisemi uongo

"Sidanganyi"

Katika Imani na kweli

"Kuhusu imani na kweli" au "Pamoja na imani na kweli"

1 Timothy 2:8

Kauli unganishi

Paulo anatoa maagizo maalumu kwa wanawake.

wanaume kila mahali

"Wanaume katika kila mahali" au "Wanaume kila sehemu"

Inua juu

"kuongeza"

inueni mikono safi

"Mikono iliyotengwa kwa ajili ya Mungu." hii ni kwa ajili ya mtu anayekwepa dhambi

bila kuwa na hasira wala wasiwasi

"Bila kueleza hasira na mgogoro na wengine" au bila kueleza hasira kuhusu wengine na mashaka juu ya Mungu"

kwa heshima

kwa njia ambayo haitaonyesha kutokuwa na umakini kwao" au "kwa njia ambayo inaonyesha heshima ya wazi kwa watu na kwa Mungu"

si kwa kusuka nywele

"Kufany akazi kwa bidii ili kufanya nywelezionekane kuwasafi". Kusuka nywele ni njia moja ya mwanamke inayompa kutokuwa makini kwenye nywele zake.

wanaokiri uungu kwa kufanya kazi njema

anataka kuonyesha kuwa wao ni mai ya Mungu kwa mambo mazuri wanayoyafanya.

1 Timothy 2:11

katika ukimya

"katika utulivu"

kwakutii

"na wasiulize maswali kuhusu kile wanachokisikia"

simruhusu mwanamke

"simkubalii mwanamke"

1 Timothy 2:13

Adamu aliumbwa kwanza

"Adamu ni mtu wa kwanza ambaye Mungu alimuumba kwanza" au "Adamu aliumbwa kwanza na Mungu"

Baadaye Eva

"Baadaye Eva aliumbwa"

Adamu hakudanganywa

"Na adamu hakuwa wa kwanza kudanganywa na Nyoka"

lakini mwanamke alidanganywa na kukosa kabisa

"Kutotii amri za Mungu kwa sababu alikuwa alikuwa amedanganywa kabisa" lengo kuu katika kifungu hiki ni kuwa alikuwa Eva na siyo Adamu ambaye (Kwanza) hakutii sheria za Mungu.

Ataokolewa kwa kuzaa watoto

"Mungu atamweka salama bila shaka kupitia maisha ya kawaida"

Kama wataendelea

"Kama watabaki" au "Kama wataendelea kuishi"

katika Imani na upendo na utakaso

"Katika kumwamini Yesu na kuwapenda wengine na kuishi maisha matakatifu"

pamoja na uzima na akili njema

"na kuwa na kiasi" au "Na ufahamu wa kujua ni kipi kizuri zaidi"

1 Timothy 3

1 Timotheo 03 Maelezo kwa ujumla

Muundo na Mpangilio

1 Timotheo 3:16 huenda ni wimbo, shairi ama kanuni ya imani kanisa la mwanzo "lililotumia kuorodhesha mafundisho muhimu waumini wote walishiriki.

Dhana muhimu katika sura hii

Waangalizi na Mashemasi

Kanisa lilitumia vyeo tofauti vya viongozi wa kanisa. Vyeo vingine vilijumuisha, mzee, mchungaji na askofu. Neno "Mwaangalizi linaashiria maana ya luga ya awali katika misitari ya 1-2. Paulo anaandika kuhusu "Mashemasi" katika misitari ya 8 na 12 kama aina nyingine ya uongozi wa kanisa.

Maswala mengine ya matata katika tafsiri ya sura hii

Sifa za tabia

Sura hii inaorodhesha sifa chache ambazo lazima mwanaume anayetaka kuwa mwangalizi ama shemasi katika kanisa awe nazo. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-abstractnouns)

<< | >>

1 Timothy 3:1

Kazi njema

Kazi ya kuheshimika

Mume wa mke mmoja

Mwangalizi lazima awe na mke mmoja.Siyo sawa ikiwa hii ninawajumuisha wanaume ambao hapo nyuma walikuwa wajane au wametalikiwa, au hawakuwahi kuoa.

awe na Kiasi

"Asifanye jambo lolote bila kiasi"

Busara

Mtu ambaye anafikiri katika njia ya busara", au"ambaye hutumia sauti ya hukumu"au "busara"mantiki, au "akili"

Mtaratibu

Tabia nzuri

Mkarimu

Mwenye kukaribisha wageni

Asitumie kileo

"Asiwe mlevi" au" asiwe anakunywa sana kileo"

Asiwe mgomvi

"Asiwe mtu ambaye anapenda kupigana na kusemasema"

Asiwe mpenda fedha

Wala mtu ambaye anaiba moja kwa moja au kupitia mitandao siyo mtu ambaye hufanya kazi kwa uwazi kuongeza fedha lakini hajali watu wengine kwa umakini.

1 Timothy 3:4

kwa heshima yote

Maana zinazowezekana ni 1) watoto wa kiongozi waheshimu baba na watu wengine au 2) watoto wa mwangalizi wanapaswa kuwaheshimu watu wote.

Kuongoza nyumba yake

Kuitunza familia yake"au "kulinda watu wanaoishi nyumbani mwake"

Kwa heshima zote

Yote inaweza husika watu wote au katika muda wote au katika shida zozote

Ikiwa mtu hafahamu namna

Kwa sababu ikiwa mtu hafahamu namna ya "au" kwa wakati mtu hawezi "au" lakini kukisia mtu hawezi"

Atawezaje kulitunza kanisa la Mungu

"Hawezi kulitunza kanisa laMungu" au"hatakuwa tayari kuliongoza kanisa la Mungu."

1 Timothy 3:6

Asije akawa mwamini mpya

"Asije akawa mwamini mpya" au " asije akawa mtua mbaye amekuwa mwamini kwa muda mfupi uliopita "au " lazima awe mwamini mchanga"

Asije akaanguka katika hukumu kama mwovu

Kuwa na majivuno kama mwovu anavyofanya na kwa sababu ya kwamba amehukumiwa kama mwovu alivyo.

Lazima pia awe na sifa njema kwa wote wa nje.

"Ni muhimu pia kwa wote ambao hawajamwamini Yesu kufikiri vizuri juu yake"au"Wote wa nje ya kanisa lazima wafikiri vizuri juu yake"

Kuanguka katika aibu

Kuleta aibu juu yake"au"kumpa mtu sababu za kutodhibitishwa kwake"

Kuanguka katika......mtego wa mwovu

Kuruhusu mwovu kumtega." Shetani kutengeneza mtego au kunaswa ni mfano wa shetani kumhadaa kujiingiza katika dhambi bila kujua.

1 Timothy 3:8

Mashemasi vilevile

"Mashemasi, kama kwa waangalizi"

Wawe wakamilifu

Awe anastahili heshima

Asiwe na kauli mbili

Kauli-"siyo kusema kitu kimoja lakini maana ni nyingine"au "siyo kusema kitu kimoja kwa mtu mmoja na kusema vitu vingine tofauti kwa wengine"

Asitumie mvinyo kupita kiasi

"Asitumie mvinyo kupita kiasi"au"asijitoe kutumia mvinyo kupita kiasi"

Wasiwe na tamaa

"Wasiangalie pato lisilo la haki"

Waweze kutunza kweli iliyofunuliwa kwa imani

Lazima waendelee kuamini ujumbe wa kweli uliofunuliwa na Mungu kwetu kwamba tunaamini."Hii inamanisha kwamba kwa kweli iliyoingia kwa muda mrefu lakini Mungu aliionyesha kwao kwa muda huu .

Kwa dhamira njema

"Kwa dhamira njema kujua kwamba hatukufanya chochote kinyume"

Wawe wamedhibitishwa kwanza

Wawe wamedhibitishwa kutadhiminiwa na kuamua ikiwa wanafaa kutumika"au" waweze dhibitisha peke yao kwanza"

Kwa sababu hawana lawama

Ikiwa hakuna mmoja aweza kutafuta chochote kisicho sawa yeye peke yake "au "kwa sababu hawana lawama "au" kwa sababu hawakufanya chochote kisicho sawa"

1 Timothy 3:11

Wanawake vivyo hivyo

Hapa "wanawake"inaweza kutumiwa kama wanawake kwa ujumla, lakini inaonekana inabainisha mashemasi,wake au mashemasi wanawake.Kwenye :"wake vilevile wana mahitaji"au"mashemasi wa kike,pana mahitaji kama mashemasi"

Wawe wakamilifu

"kufanya vizuri"

Wasiwe wasingiziaji

"Ni lazima wasiongee uovu kuhusu watu wengine"

Kiasi

"Wasifanye chochote kwa ziada"

Mume wa mke mmoja

Mtu lazima awe na mke mmoja tu. Siyo sahihi ikiwa hii inajumuisha watu ambao hapo nyuma walikuwa wagane, wamepeana talaka, au hawakuwahi kuoa.

Kutawala vizuri watoto wake na wa nyumbani mwake.

Kutunza na kuongoza vizuri watoto wake na wengine wanaoishi kwenye nyumba yake.

Kwa wote

"Kwa mashemasi wote "au "kwa maaskofu wote. Mashemasi, na mashemasi wa kike"au "kwa viongozi wa makanisa haya"

Wamepata peke yao

"kupokea peke yao "au" kuongezeka peke yao"

1 Timothy 3:14

Kauli Unganishi:

Paulo anamwambia Timotheo sababu iliyomfanya amwndikie barua na kisha anamweleza juu ya uungu wa Kristo.

Na nina tumaini kuja kwako upesi

"ijapokuwa ninatumaini kuja upesi sana"

lakini ikiwa nitachelewa

Lakini ikitokea siwezi kufanya hivyo upesi au "lakini ikiwa kitu chochote kitanizuia kuwa hapo upesi"

katika nyumba ya Mungu

Paulo anaongelea juu ya kikundi cha walioamini kama ni familia moja.

Mungu anayeishi

Msemo huu unamwelezea Mungu kama ndiye atoaye uzima.

Nguzo na mtetezi wa kweli

Paulo anaongea juu ya walioamini na kuibeba kweli kuhusu Kristo kama vile wao ni nguzo na msingi unaoshikilia jengo lote.

1 Timothy 3:16

Katika mwili

Paulo anatumia neno "mwili" hapa kumaanisha Binadamu.

akaonekana na malaika

Hii unaweza pia kusema, "Malaika walimwona"

Alidhibitishwa na Roho

"Roho Mtakatifu alituhakikishia Yesu alikuwa ambaye alisema alikuwa"

alitangazwa kati ya mataifa

"watu wa mataifa mengi waliwaambia wengine kuhusu Yesu"

akaaminiwa kweye ulimwengu

"pande nyingi za ulimwengu zilimwamini Yesu"

1 Timothy 4

1 Timotheo 04 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

1 Timotheo 4:1-3 ni unabii Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Siku za baadaye

Hii ni njia nyingine ya kuashiria siku za mwisho( Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lastday)

<< | >>

1 Timothy 4:1

Kauli unganishi

Paulo anamwambia Timotheo kile ambacho Roho anasema kitatokea na anamtia moyo kwa kile ambacho anapaswa kufundisha.

nyakati zijazo

Inaweza kumaanisha 1) nyakati za baadaye kuliko nyakati za Paulo, "katika nyakati zinazokuja" au "wakati ujao" au 2) Katika wakati wa Paulo mwenyewe, "katika wakati wa kipindi hiki kabla ya wakati wa mwisho"

kuacha imani

"kuacha kuamini katika Yesu" au "kuondoka katika kile ambacho walikuwa wanakiamini"

kuwa makini kusikiliza

"kutoa kipaumbele" au "kwa sababu wanasikiliza kwa makini" au "wakati wakisikiliza"

roho zidanganyazo na mafundisho ya kipepo

"roho zinazowalaghai watu na mambo ambayo mapepo yanafundisha"

kwa uongo na unafiki

"yanayofundishwa na wanafiki ambao wanawaambia uongo"

dhamiri zao zitakuwa zimechomwa moto

Huu mfano ni wa mabwana ambao walikuwa wakiweka chuma cha moto katika ngozi za watumwa au wanyama kutengeneza kovu ambalo linaonesha umiliki. Yaweza kumaanisha 1) alama ya kuchomwa kama kitu cha kuleta utambulisho, "Wanafanya hivi hata kama wanajiona kwamba ni wanafiki," au 2) dhamiri zao zimetiwa ganzi, "kana kwamba wameweka chuma cha moto katika dhamiri zao kuzifanya kuwa na ganzi"

1 Timothy 4:3

Wata

"Watu hawa wata"

kataza kuoa

"kuwakataza waumini kuoa" au "kuwazuia waumini kuoa"

kataza...kupokea vyakula

"waliwataka watu...wajiepushe na vyakula" au "kuwakataza watu...kula vyakula" au "kutowaruhusu watu...kula aina ya vyakula." "watu" hapa yaweza kumaanisha waamini.

waaminio na waijuao kweli

"waamini waijuao kweli" au "waamini waliojifunza kweli"

hakuna kinachokataliwa kama kitapokelewa kwa shukurani

"hatukitupi kitu chochote ambacho tunamshukuru Mungu kwacho" au "hatukikatai kitu chochote ambacho tunamshukuru Mungu kwacho" au "kila kitu ambacho tunakila kwa shukurani kinakubalika"

kinatakaswa kupitia neno la Mungu na kwa njia ya maombi

tafsiri mbadala: "tumekitenga kwa ajili ya matumizi ya Mungu kwa kulitii neno la Mungu na kumuomba yeye" au "tumekitenga kwa ajili ya matumizi ya Mungu kwa maombi ambayo yanakubaliana na ukweli ambao Mungu ameufunua"

1 Timothy 4:6

kama utayaweka mambo haya mbele ya ndugu

"uweke fikra hizi ndani ya akili za waumini" au "uwasaidie waumini kuyakumbuka maneno haya." "Fikra" au "maneno" yanamaanisha mafundisho.

unaendelea kulishwa

"kufundishwa". Mungu alikuwa akimfanya Timotheo mwenye nguvu na kumfundisha kuyafanya yampendezayo Mungu.

maneno ya imani

"maneno ambayo yanawasababisha au yanayowafanya watu kuamini"

hadithi za kidunia zinazopendwa na wanawake wazee

"hadithi za kidunia na za wanawake wazee." Maneno "zilizopendwa na wanawake wazee" inaweza kuwa mfano kwa maana ya "za kijinga" au "kipuuzi." Paulo hakusudii kuwatukana wanawake katika kuwaongelea kwake :wanawake wazee." Badala yake, yeye na wasikilizaji wake walijua kwamba wanaume wanakufa wakiwa vijana ukulinganisha na wanawake, kwa hiyo kuna wanawake wengi zaidi kuliko wanaume ambao akili zao zimekuwa dhaifu kwa sababu ya umri mkubwa.

jifunze kutenda kwa namna ambayo inampendeza Mungu

"jifunze kuwa wa kiMungu zaidi" au "jifunze kutenda kwa namna ua njia ambayo inampendeza Mungu" au "jitahidi kuwa wa kiMungu zaidi"

mazoezi ya mwili

"mazoezi ya kimwili"

kutakusaidia maisha ya sasa hapa duniani

"ni ya manufaa kwa maisha haya" au "inasaidia kuyafanya maisha haya kuwa bora"

1 Timothy 4:9

wakuaminiwa kabisa

"unastahili imani yako kamilifu" au "unastahili kuamini kwa hali ya juu kabisa"

Ni kwa sababu hii

"Hii ndiyo sababu"

tunafanya kazi kwa bidii na juhudi sana

Maneno "juhudi" na "kufanya kazi kwa bidii" kimsingi yanamaanisha kitu kilekile. Paulo anayatumia yote pamoja kusisitiza ni kwa namna gani wamefanya kazi hiyo kwa bidii.

tumaini letu liko kwa Mungu aishie

"tumeweka tumaini letu kwa Mungu aliyehai"

lakini hasa kwa waaminio

"lakini yeye hasa ni mwokozi kwa wale watu waaminio"

1 Timothy 4:11

Uyaseme na kuyafundisha mambo haya

"Agiza na fundisha mambo haya" au "Agiza na ufundishe mambo haya ambayo nimeyataja hivi punde"

Mtu yeyote asiudharau ujana wako

"mtu asikuchukulie kwamba wewe si wa muhimu kwa sababu u kijana"

endelea kuyasoma

"soma Maandiko" au "endelea kulisoma Neno la Mungu kwa sauti na kwa uwazi mbele za watu"

endelea...kuyahimiza

"wahimize wengine" au "watie moyo wengine kulifanyia kazi Neno la Mungu katika maisha yao"

1 Timothy 4:14

usiache kutumia karama iliyoko ndani yako

Paulo anamzungumzia Timotheo kuwa ni kama chombo ambacho kimebeba karama za Mungu.

usiache

Hii inaweza kutafasiriwa kama, "hakikisha unatumia"

kuwekewa mikono na wazee

Hii ilikuwa ni sherehe ambayo viongozi wa kanisa waliweka mikono juu ya Timotheo na kumuombea kwamba Mungu atamuwezesha kufanya kazi aliyomwamuru au aliyomwagiza kuifanya.

Yafanye mambo hayo yote na uyaishi

"Fanya mambo haya yote na uishi kwa kuyafuata"

ili kukuwa kwako kuwe dhahiri kwa watu wote

"hivyo watu wengine waone ukuwaji wako" au "hivyo watu wengine watauona ubora wa maisha yako kwa kuyafanya hayo"

Dhibiti mwenendo wako

"Enenda kwa uangalifu" au "Dhibiti tabia yako"

Endelea kuyafanya mambo haya

"Endelea kufanya mambo haya"

utajiokoa mwenyewe na watu wanaokusikiliza

"utajiokoa wewe na wale wanaokusikiliza kutoka katika kuamini jumbe za uongo na kufanya matendo mabaya. Watu wanaoamini jumbe za uongo na kufanya matendo mabaya wategemee kutesekea kama matokeo yake. Paulo hataki Timotheo na marafiki zake kuteseka kwa kuamini na kutenda vitu au mambo yasiyo sahihi.

1 Timothy 5

1 Timotheo 05 Maelezo kwa ujumla

Dhana muhimu katika sura hii

Heshima na adabu

Paulo anawahimiza Wakristo wachanga kuwaheshimu na kuwaonyesha adabu Wakristo wazee. Mila huwaheshimu na kuwaonyesha adabu watu wazee kwa njia tofauti.

Wajane

Nyakati za zamani katika Mashariki ya Karibu, ilikuwa ni muhimu kuwasaidia wajane kwa vile hawakuwa na uwezo wa kujipatia chakula.

<< | >>

1 Timothy 5:1

Sentensi unganishi:

Paulo anaendelea kumuasa Timotheo awajali wanaume, wanamke, wajane na wanawake wazee ndani ya kanisa.

Taarifa ya jumla:

Paulo alikua anatoa maagizo haya kwa mtu mmoja, Timotheo.

Usimkemee mwanaume mzee.

"Usiongee kwa ukali kwa mzee wa kiume"

Ila msihi kama baba

"Ila mtie moyo kama uongeavyo na baba yako," kwa adabu.

Msihi kijana wa kiume kama ndugu

"Mtie moyo vijana wa kiume kama ndugu zako" au "wafundishe vijana wakiume kama ambavyo ungefundisha ndugu zako," kwa amani.

Wanawake vijana kama dada

"wasihi wanawake vijana kama ambavyo unge wasihi dada zako" au "wafundishe wanawake vijana kama ambavyo ungewafundisha dada zako,"

Kwa usafi wote

"kwa mawazo safi na matendo" au "katika hali ya utakatifu"

1 Timothy 5:3

Waheshimu wajane

"Waheshimu na kuwahudumia wajane"

wajane kwelikweli

"wajane wasio na mtu wa kuwahudumia"

waache kwanza wajifunze

"awali ya yote wanahitaji kujifunza"

katika nyumba zao wenyewe

kwenye familia zao wenyewe au kwa wale wanaoishi kwenye nyumba zao

waache wawalipe wazazi wao

"Waache wawatendee mema wazazi wao kwa sababu ya mambo mazuri ambayo wazazi wao wamewapa."

1 Timothy 5:5

Lakini mjane halisi ameachwa peke yake

"Lakini yule ambaye ni kweli mjane hana familia"

yeye daima husubiri mbele yake kwa maombi na sala

"husubiri kwa uvumilivu kwa maombi yake na sala"

maombi na sala

maneno haya mawili maana kimsingi yana maana moja. Paulo anayatumia kwa pamoja ili kusisitiza kiasi gani wajane hawa huomba.

usiku na mchana

maneno "usiku" na "siku" hutumiwa pamoja kumaanisha "wakati wote."

Hata hivyo

"Lakini"

wafu

mfano Huu unamaana kwamba yeye hana uwezo wa kumjibibu Mungu. "ni kama mtu aliekufa, hana la kujibu kwa Mungu"

hai

Hii ina maana ya maisha ya kimwili.

yeye daima husubiri kwa maombi na sala

"Anaendelea kufanya maombi na sala"

amekufa

Paulo anaongea kuhusu watu ambao hawamtafuti Mungu na kumpendeza kama walikua wafu. "ni kama mtu aliekufa, hana la kujibu kwa Mungu"

bado yu hai

Hii ina maana ya maisha ya kimwili.

1 Timothy 5:7

Na kuhubiri mambo haya

"Waamuru mambo kama haya vizuri"

ili waweze kuwa na zaidi ya aibu

"hivyo kwamba hakuna mtu anayeweza kupata kosa pamoja nao." Maana ya "wao" ni 1) 'wajane hao na familia zao " au 2)" kanisa. " Ni inaweza kuwa bora kuondoka somo kama "wao."

hatoi kwaajili ya ndugu yake

"haitoi kwa mahitaji ya ndugu zake" au " hatoi msaada kwa mahitaji ya jamaa zake '"

kwa ndugu yake

"kwa ajili ya wanafamilia yake yote" au "kwa wale wanaoishi katika nyumba yake"

kwa wale wa nyumbani kwake

"kwa wanafamilia wanaoishi katika nyumba yake"

ameikana Imani

"yeye ametenda kinyume cha ukweli tunaoukubali"

ni mbaya kuliko mtu asiyeamini

"ni mbaya zaidi kuliko wale ambao hawaamini katika Yesu." Paul anamaanisha mtu huyu ni mbaya kuliko mtu asiyeamini kwa sababu hata wasioamini utunzaji wa ndugu zao. Kwa hivyo, muumini anapaswa atunze ndugu zake.

ili waweze kuwa bila aibu

"hivyo kwamba hakuna mtu anayeweza kupata kosa pamoja nao." Maana ya "wao" ni 1) 'hawa wajane na familia zao "(UDB) au 2)" Waumini. " Ni inaweza kuwa bora kuondoka somo kama "wao."

1 Timothy 5:9

aandikishwe kama mjane

inaonekana kulikuwapo na orodha, iliyoandikwa au la, ya wajane. washiriki wa kanisa waliyatimiza mahitaji hayo ya wanawake ya makazi, mavazi, na chakula; na wanawake hawa walitarajiwa kujitolea maisha yao kwa kuwahudumia jumuiya ya kikristo.

aliye juu ya umri wa miaka sitini

Wajane ambao walikuwa wadogo chini ya miaka sitini wanaweza kuolewa tena, na hivyo Kanisa linapaswa kuwatunza tu wajane ambao walikuwa na umri zaidi ya sitini.

mke wa mume mmoja

Maana inawezekana ni 1) yeye alikuwa daima mwaminifu kwa mumewe au 2) na hajapewa talaka na mume wake na kuolewa na mtu mwingine.

Awe najulikana kwa matendo mema

Hii inaweza andikwa kama "Watu lazima waweze kushuhudia kwa matendo yake mema"

ameniosha miguu

"kufanya kazi kusaidia." Kuosha miguu michafu ya watu ambao wamekuwa wakitembea katika uchafu na matope ni picha ya kukutana na mahitaji ya watu wengine na kufanya maisha yawe yafuraha kwao.

Waaminio

Baadhi ya matoleo hutafsiri "waamini" hapa kama, "Watakatifu" au "watu wa Mungu." Wazo muhimu ni kwa kutaja waumini wa Kikristo.

amefuata kazi zote njema

"ni maalumu kwa ajili ya kufanya matendo mema"

ambaye si mdogo kuliko sitini

Kama Paulo atakapo elezea kwa 5: 11-16, wajane waliokuwa na umri wa miaka midogo kuliko 60 wanaweza kuolewa tena. Kwa sababu hiyo jumuiya ya kikristo walikuwa wakuwatunza wajane ambao walikua na umri zaidi ya miaka sitini.

amekua mkarimu kwa wageni

"amekaribisha wageni katika mji wake"

aliwasaidia watu wenye taabu

Hapa "taabu" linaweza kutumika kama "yeye aliewasaidia wale ambao wanateseka"

amekua akijitoa kwa kila kazi njema

"amejitoa kwa kufanya kila aina ya matendo mema"

1 Timothy 5:11

Lakini kwa habari ya wajane vijana, kataa kuwaandikisha katika orodha

"Lakini msiwaweke wajane vijana kwenye orodha." Orodha ni ya wajane wenye umri wa miaka 60 na zaidi ambao jumuiya ya kikristo ingesaidia.

Kwa kuwa watakaposhindwa na tamaa ya mwili dhidi ya Kristo, watataka kuoa

"ni aliwasihi kutoka kwa Kristo kwa sababu ya tamaa zao za ngono" au "kuwa na tamaa ya mwili inayowafanya watake kutoa dhamira yao ya kiroho"

kutengua ahadi yao ya awali

"wala hawaweki ahadi zao za awali" au "kutokufanya walicho ahidi kukifanya kabla"

dhamira

dhamira ya wajane ilikuwa ni makubaliano yao ya kutumikia jumuiya ya kikristo kwa ajili ya mapumziko ya maisha yao kama jamii angewapa mahitaji yao.

kusengenya

Hawa ni watu ambao hujadili juu ya maisha binafsi ya watu wengine.

mambo wasio paswa kusema

"mambo ambayo si sahihi hata kutaja"

kuwa wamezoea kuwa wavivu

"kuingia katika tabia ya kutokufanya kitu

1 Timothy 5:14

kusimamia nyumba

"kumhudumia kila mtu katika nyumba yake"

wameshamgeukia Shetani

Paulo anazungumzia wanaoishi katika uaminifu kwa Kristo kana kwamba ni njia ya kufuatwa. Hii ina maana mwanamke aliacha kumtii Yesu na kuanza kumtii Shetani. "kuacha njia ya Kristo na kumfuata Shetani" au "aliamua kumtii Shetani badala ya Kristo"

mwanamke yeyote aaminie

"mwanamke yeyote Mkristo" au "mwanamke yeyote ambaye anaamini katika Kristo"

anao wajane

"anao wajane katika jamaa yake"

wajane kweli

"wale wanawake ambao hawana mtu wa kutoa kwa ajili yao"

adui

Inawezekana Maana ni 1) hii inamaanisha Shetani au 2) hii inamaanisha wasio amini.

ili kanisa lisilemewe

Paulo anazungumzia jamii kuwa inasaidia zaidi watu kuliko uwezo wao kama walikuwa wamebeba uzito juu ya migongo yao. Hii inaweza kusemwa "ili kwamba jumuiya ya kikristo haitawasaidia wajane ambao familia inaweza kutoa kwa ajili yao"

1 Timothy 5:17

Sentensi uanganishi:

Paulo tena anazungumzia jinsi wazee (maaskofu) wanapaswa kutunzwa na kisha kumpa Timotheo maelezo binafsi.

watambue wazee wanaoongoza vyema

"Ninyi waumini wote mnapaswa kufikiri kama mnastahili"

Heshima mara mbili

Maana inawezekana ni 1) "ya heshima na malipo" au 2) "heshima zaidi kuliko wengine wapokeavyo"

wale wanaofanya kazi na neno na katika kufundisha

"wale wanaohubiri na kufundisha neno la Mungu"

kufunga

kifaa kianachowekwa kwenye pua na mdomo wa mnyama ili kumzuia kula wakati anafanya kazi.

kupura nafaka

Hii ni njia ya kutenganisha nafaka na makapi kwa kutumia mkokoteni unaovutwa na ng'ombe

anastahili

"inastahili"

1 Timothy 5:19

usipokee mashitaka

Paulo anaongea juu ya mashitaka kama vitu ambavyo vinaweza kushikika au kupokelewa na watu

mbili au tatu

"angalau mbili" au "mbili au zaidi"

wenye dhambi

hii inahusu mtu yeyote kufanya jambo lolote ambalo halimtii au yasiyompendeza Mungu, hata mambo ambayo watu wengine hawayajui.

mbele ya watu wote

"ambapo kila mtu anaweza kuona"

ili wengine wawe na hofu

"ili wengine waweze kuogopa kufanya dhambi"

1 Timothy 5:21

malaika wao wateule

Hii inamaanisha malaika ambao Mungu na Yesu wamewachagua kuwatumikia wao kwa njia maalumu.

weka mikono

Hii ilikuwa sherehe ambapo viongozi wa kanisa moja au zaidi wangeweka mikono juu ya watu na kuomba kwamba Mungu aweze kuwawezesha watu hao kutumikia kanisa kwa njia ambayo Mungu angekuwa radhi. Timotheo alikuwa anasubiri hadi mtu aoneshe tabia nzuri kwa muda mrefu kabla ya kumweka rasmi mtu huyo kuitumikia jamii ya Kikristo.

usishiriki katika dhambi ya mtu mwingine

"kujiunga katika dhambi ya mtu mwingine." Maana inawezekana ni 1) kama Timotheo akichagua mtu ambaye ana dhambi na kuwa mfanyakazi wa kanisa, Mungu angemshikilia Timotheo kuwajibika kwa dhambi ya mtu huyo, au 2) Timotheo hapaswi kutenda dhambi akiona wengine wakitenda.

tunza amri hizi bila ya kuathiri na kwamba wewe usifanye kitu nje ya upendeleo

kwa maneno "upendeleo," Paulo anasisitiza kwamba Timotheo lazima ahukumu kwa uaminifu na kuwa wa haki kwa kila mtu. "kwamba ushike sheria hizi bila ya kuwa sehemu au kuonesha upendeleo kwa mtu yeyote"

tunza amri hizi

Maana inawezekana ni 1) hii inamaanisha sheria ambazo Paulo amemwambia Timotheo au 2) hii inamaanisha sheria ambazo Paulo anataka kumwambia Timotheo.

1 Timothy 5:23

Usinywe maji tena

Au "Unapaswa kuacha kuwa mnywaji wa maji," anaekunywa maji tu. Paulo hakatazi maji. Anapendekeza ya kwamba Timotheo atumie mvinyo kama dawa. Maji ya eneo lile husababisha madhara mara kwa mara.

Na huwatangulia hukumuni

"dhambi zao hutangulia mbele ya watu hao hukumuni."

lakini baadhi ya dhambi hufuata baadaye

"Lakini baadhi ya dhambi hufuata watu hao baadaye." Maana inawezekana ni 1) Timotheo hatajua kuhusu baadhi ya dhambi mpaka baadaye, au 2) Kanisa hawataweza kujua kuhusu baadhi ya dhambi mpaka baadaye, au 3) Mungu hata hukumu baadhi ya dhambi mpaka hukumu ya mwisho.

nzuri

Hapa "nzuri" ina maana wao wanaolingawa na tabia ya Mungu, makusudi yake, na mapenzi.

hata wengine hawawezi kujificha

"matendo mema mengine yatajulikana katika siku zijazo"

dhambi za baadhi ya watu zinajulikana wazi

Hii inaweza semwa kama "Dhambi za watu wengine ni dhahiri sana"

baadhi ya matendo mema yanajulikana wazi

"baadhi ya matendo mema ni dhahiri"

1 Timothy 6

1 Timotheo 06 maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

tumwa

Paulo hasemi katika sura hii iwapo utumwa ni mzuri ama ni mbaya. Paulo anaandika kuhusu kuwaheshimu na kuwatumikia kikamilifu mabwana zao. Paulo anawafunza waumini wote kuwa na uungu na kutosheka katika kila jambo.

__<< | __

1 Timothy 6:1

Sentensi unganishi

Paulo anatoa maagizo maalumu juu ya watumwa na bwana zao kisha maelekezo ya namna ya kuishi maisha ya kimungu.

wale wote walio chini ya nira kawa watumwa

Paulo anaongea juu ya watu wanaofanya kazi kama watumwa kwamba ni kama ng'ombe wanaobeba nira

wale wote

kwa kauli hii Paulo anamaanisha walioamini

jina la Mungu

hii inamaanisha asili ya Mungu, au tabia yake

1 Timothy 6:3

afundishaye kwa upotovu

anayefundisha mapokeo tofauti

liongozalo kwenye utaua

inayowasaidia watu kufanya yaliyo ya Mungu

akili zilizoharibika

akili zilizojaa uovu

wanaiacha kweli

kuacha maana yake ni kuacha kufanya kitu

1 Timothy 6:6

utaua na kuridhika ni faida kubwa

ni faida kubwa kwa mtu kufanya mapenzi ya Mungu na kuridhika na alicho nacho

ni faida kubwa

inatupatia faida kubwa au inatufanyia mambo mengi mazuri.

1 Timothy 6:9

kuwa na mali huanguka katika majaribu, katika mtego

Paulo anaongea juu ya wale ambao vishawishi vya pesa vinawafanya waangukie katika shimo ambalo mwindaji amelitumia kama mtego

Huanguka katika upumbavu mwingi na tamaa mbaya

huu ni mwendelezo wa fumbo la mtego. Hii inamaanisha kuwa tamaa zao za kijinga na mbaya zitawashinda.

watu ambao hutamani hiyo

wanaotamani fedha

1 Timothy 6:11

Bali wewe

Hapa "wewe" ipo katika umoja na inamaanisha Timotheo

mtu wa Mungu

mtumishi wa Mungu

huru mabali na hivi vitu

Paulo anaongea juu ya majaribu na dhambi kama vitu ambavyo mtu angeweza kuvikimbia

ulitoa ushuhuda

ulishuhudia

mbele ya mashahidi wengi

Paulo anaelezea wazo la eneo fulani ili kuonesha watu ambao Timotheo aliongea nao.

1 Timothy 6:13

Sentensi unganishi:

Paulo anaongea juu ya ujio wa Kristo, anatoa maelekezo stahiki kwa matajiri, na mwisho anamaliza na ujumbe muhimu kwa Timotheo.

Nakupa amri hii

Hivi ndivyo ninavyokuamuru

mbele ya Mungu

katika uwepo wa Mungu. Inaonekana ni kama Paulo anamwomba Mungu kuwa shahidi wake

mbele ya Kristo

katika uwepo wa Kristo. Inaonekama ni kama Paulo anamwomba Yesu kuwa shahidi wake

pasipo mashaka

Maana tarajiwa 1) Yesu hataona kosa kwa Timotheo au 2) watu wengine hawataona kosa kwa Timotheo

ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo

mpaka Bwana wetu Yesu Kristo atakapokuja tena

1 Timothy 6:15

Mungu atadhihirisha ujio wake

Hii inaweza kumaanisha kuwa Mungu atamdhihirisha Yesu

kwa wakati sahihi

kwa wakati unaofaa/muafaka

mbarikiwa

Anayestahili sifa. Hii inamaanisha Mungu Baba

Peke yake anaishi milele

Yeye pekee ana nguvu ya kuishi milele

akaaye katika mwanga usiokaribiwa

anakaa katika mwaka unaong'aa sana ambao hakuna awezaye kuukaribia

1 Timothy 6:17

waambie matajiri

Hapa "matajiri" kisifa. Inaweza kutafasiriwa kama, waambie wote walio matajiri.

katika utajiri, ambao siyo wa uhakika

katika vitu vingi wanavyovitumaini ambavyo wanaweza kuvipoteza

utajiri wote wa kweli

vitu vyote ambavyo vitatufanya kuwa na furaha ya kweli. Kama vile, upendo, furaha, na amani

watajirike katika kazi njema

Paulo anaongea juu ya baraka za rohoni kama vile ni utajiri wa duniani.

1 Timothy 6:20

linda kile ulichopewa

kwa uaminifu hubiri ujumbe wa kweli ambao Yesu amekupa

epuka majadiliano ya kipumbavu

usitilie maanani majadiliano yasiyofaa

ambayo kwa uongo huitwa maarifa

ambayo kwa ujinga watu wengine huyaita maarifa

wameikosa imani

Paulo anazungumzia imani katika Kristo kama vile shabaha yetu

Neema na iwe pamoja nawe

Mungu awape neema ninyi nyote. Neno "ninyi" limetumiwa katika wingi na linarejelea jamii yote ya Wakristo.