Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa Tito

Utangulizi wa Jumla

Muhtasari wa kitabu cha Tito

  1. Paulo anamshauri Tito kuwateua viongozi wanaomcha Mungu (1:1-16)
  2. Paulo anamshauri Tito kuwafundisha watu kuishi maisha ya kumcha Mungu (2:1-3:11)
  3. Paulo anamalizia kwa kuelezea baadhi ya mipango yake na kutuma salamu kwa waumini. (3:12-15)

Nani aliandika kitabu chaTito?

Paulo aliandika Kitabu cha Tito. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika himaya nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu

Kitabu cha Tito kinahusu nini?

Paulo alimwandikia barua hii Tito, mfanyakazi mwenza aliyekuwa anayaongoza makanisa ya Kisiwa cha Krete.Paulo alimwelekeza jinsi ya kuwachagua viongozi wa kanisa.Paulo pia alifafanua jinsi waumini walipaswa kutendeana.Na akawahimiza wote waishi maisha yanayompendeza Mungu.

Kichwa cha kitabu hiki kinafaa kitafsiriwe vipi?

Watafsiri wanaweza kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha kitamaduni, "Tito" ama wanaweza kuchagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama, "Barua ya Paulo kwa Tito," ama "Barua kwa Tito." (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Watu wanaweza tumikia kanisa katika majukumu gani?

Kuna mafundisho fulani katika kitabu cha Tito kuhusu iwapo mwanamke ama mwanamume waliopeana talaka wanaweza kutumikia katika nafasi za uongozi kwenye kanisa. Wasomi wanatofautiana kuhusu maana ya mafundisho haya.Mafundisho zaidi kuhusu haya mambo yatakuwa ya muhimu kabla ya kukitafsiri kitabu hiki.

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Umoja na wingi wa "wewe" na "ninyi"

Katika kitabu hiki, neno "mimi" linaashiria Paulo. Mara nyingi neno "wewe" inaashiria mtu moja, ndiye Tito, isipokuwa katika 3:15. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-exclusive and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-you)

Ni nini maana ya "Mungu mkombozi wetu"?

Hili ni tamko la kawaida katika barua hii. Paulo alitaka wasomaji wafikirie jinsi Mungu aliwasamehe kupitia kwa Kristo baada ya hao kumtendea dhambi. Na kwa kuwasamehe aliwaokoa kutoka kuadhibiwa wakati atakapowahukumu watu wote. Tamko sawa na hili katika barua hii ni, "Mungu wetu mkuu na Mkombozi Yesu Kristo."

Titus 1

Tito 01 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Paulo anaanzisha barua hii kirasmi katika mistari 1-4. Waandishi walianzisha barua kwa njia hii hapo kale Mashariki ya Karibu.

Katika mistari ya 6-9, Paulo anaorodhesha sifa za mwanaume anayetaka kuwa mzee wa Kanisa. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-abstractnouns) Pauo anapeana orodha sawa katika 1 Timotheo 3.

Dhana muhimu katika sura hii

Wazee

Kanisa limetumia vyeo tofauti kuashiria viongozi wa kanisa. Baadhi ya vyeo hivi ni: Mwangalizi, mzee, mchungaji na askofu.

Maswala mengine tata katika tafsiri ya sura hii

Wanapaswa, wanaweza, Inawalazimu

ULB hutumia maneno tofauti kuwashiria mahitaji ama mambo ya lazima. Maneno hayo yana matumizi ya viwango tofauti vya misisitizo. Tofauti ndogo ya maana ya hayo maneno inaweza kuwa ngumu kutafsiri. UDB inatafsiri maneno hayo kwa njia ya jumla.

| >>

Titus 1:1

kwa imani ya

kuimarisha imani ya

inayokubaliana na utauwa

"inayofaa katika kumheshimu Mungu"

tangu milele (kabla ya nyakati zote)

"Kabla ya kuanza kwa wakati"

Katika wakati muafaka

"katika wakati unafaa"'

alilifunua neno

Paulo anaongea juu ya ujumbe wa Mungu kana kwamba ni kitu ambacho chaweza kudhihirishwa dhahiri kwa watu. "Alitangaza neno lake."

aliniamini mimi kuufikisha

"Niliaminiwa kutangaza" au "alinipa wajibu wa kuhubiri"

Mungu mwokozi wetu

"Mungu anayetuokoa"

Titus 1:4

Mwana wa kweli

Ingawa Tito hakuwa mwana wa Paulo kimwili, wanashiriki imani moja katika Kristo. Hivyo katika Kristo, Paulo humwona Tito kama mtoto wake. "wewe ni kama mwanangu"

Imani yetu ya kawaida

Paulo anaelezea imani ile ile ambayo wote wanayoshiriki katika Kristo. "Mafundisho yale yale ambayo sisi sote tunaamini"

Neema,huruma na amani

Hii ilikuwa salamu ya kawaida. "Neema,huruma na amani ziwe kwenu" au "mjazwe wema, huruma na amanikwenu."

Yesu Kristo mwokozi wetu

"Yesu Kristo ambaye ni mwokozi wetu"

Kwa kusudi hili

"Hii ni sababu"

Nilikuacha Krete

"Nilikuambia kubaki Krete"

Kwamba uyatengeneze mambo ambayo hayajakamilika

"Ili kwamba ungeamalizia kupanga mambo yaliyohitajika kukamilishwa."

Kuweka wazee

"chagua wazee" au "panga na kudhirisha wazee"

wazee

Katika makanisa ya kwanzaya Kikristo ,Wazee wakikristo walipewa uongozi wa kiroho kwa mkutano wa waumini.

Titus 1:6

Sentensi unganishi

Baada ya kuwa amekwisha kumwambia Tito kuwaweka kazini wazee katika kila mji katika kisiwa cha Krete, Paulo anatoa matakwa yanayohitajika kwa wazee.

Mzee lazima asiwe na lawama

Kutokulaumiwa ni ilie hali ya kujulikana kuwa mtu huyo hatendi mambo mabaya. "Mzee lazima asiwe na sifa mbaya."

Mme wa mke mmoja

"kuwa mme mwaminifu" Maana zinazokubalika 1) Mme ambaye hatafuti mahusiano na wanawake wengine au 2) asiye na mke wa pila au hawala au suria.

Watoto waaminifu

Imaana zinazokubalika ni 1)watoto wanaomwaminiYesu au 2)watoto ambao ni waaminifu

wasio na nidhamu

"waasi" au "ambao hawafuati maagizo"

msimamizi wa nyumba ya Mungu

Paulo anaongelea juu ya wazee kana kwamba walikuwa vichwa vya familia, wakuu wa nyumba ya Mungu"

Asiye...zoelea pombe

"asiwe mtu mwenye kutumia kileo" au "asiwe mnywaji" au "asiwe mlevi sana wa pombe"

Asiwe mgomvi

"Asiwe mtu wa fujo"au "asiwe anapenda kupigana na kugombana"

Titus 1:8

Badala

Paulo anabadili hoja kutoka mada inayohusu mambo yasimpasa mzee kwenda kwa mambo anayopaswa kufanya

Rafiki wa wema

"kukumbatia mambo mazuri na tabia nzuri"

kusimamia (kushikilia kwa nguvu)

Paulo anazungumzia hali ya kujitoa katika imani ya Kikristo kama kushikilia imani katika mikono. "kujitoa kwa " au " kuwa na ufahamu mzuri wa.."

Mafundisho mazuri

Lazima afundishe iliyo kweli kuhusu Mungu na mambo mengine ya kiroho.

Titus 1:10

sentensi unganishi

Kwa sababu ya wale wanaopinga neno la Mungu, Paulo anampa Tito sababu za kufundisha Neno la Mungu na kumwonya kuhusu waalimu wa uongo.

watu waasi

Hawa ni watu waasi waliokuwa wakiupinga ujumbe wa injili ya Paulo.

Wale wa tohara

inarejea wakristo wa Kiyahudi walikuwa wakifundisha kwamba ili kumfuata Kristo, mtu lazima atahiriwe.

Maneno yao ni upuuzi

'Maneno yao hayana faida yoyote"

Ni muhimu kuwakataza

"Ni lazima kuwazuia wasieneze mafundisho yao" au "Ni lazima kuwakataza kwa ushawishi wa maneno yao"

yale wasiyotakiwa kufundisha

Vitu ambavyo si sahihi kuvifundisha kuhusu Kristo na sheria.

Kwa faida ya aibu

"Hii inarejela faida ambayo watu wanapata kwa kufanya mambo yasiyo na heshima.

Wanaharibu nyumba nzima

"huharibu imani za familia yote"

Titus 1:12

Mmoja wao

"Mmoja wa Wakrete" au mtu fulani kutoka kwa watu wa Krete

Mtu busara

Maana zinazokubalika ni 1) nabii au 2) "mshairi au mwana falsafa au 3) mwalimu

Wakrete wana uongo usio na mwisho

"Wakrete hudanganya kila wakati" Maneno haya yametiwa chumvi kuonesha tabia wa Wakrete ya kudanganya.

wabaya na mnyama wa hatari

Msemo huu unawalinganish Wakrete na hayawani au wanyama hatari.

Wavivu na walafi

Ni msemo unaoonesha watu wasiopenda kufanya kazi yoyote lakini wanakula sana.

kuwazuia kwa nguvu ( kuwarekebisha)

kwa hiyo waambie kwa ujasiri kwamba hawako sahihi (wamekosea)"

Kwamba wanaweza kuwa katika imani ya kweli

"Watakuwa na imani imara" au " kwamba imani yao itakuwa ya kweli"

Titus 1:14

Sentensi kiunganishi

Paulo anaendelea na maagizo yake kwa kumwelekeza Tito kile anachotakiwa kufundisha

Hadithi za Kiyahudi

Hii inaonyesha kwa mafundisho ya uongo ya Wayahudi

kurudisha nyuma ukweli

Paulo anaongelea ukweli kana kwamba ni kitu kilicho katika mwendo ambacho chaweza kurudishwa nyuma. "Kukataa ukweli"

Titus 1:15

Kwa wale walio safi, vyote ni safi.

Kila kitu ni safi kwa yule aliye safi ndani yake. " kila kitu anachofanya kitakuwa safi"

kwa wale walio safi

kwa wale walimpokea Mungu

Kwa wale waliochafuliwa na wasioamini, hakunakilicho safi

Paulo anaongelea watu wenye dhambi kana kwamba ni wachafu kimwili. "Yeyote aliiye najisi kimaadili na ambaye haamini hawezi kuwa safi."

wanamkana kwa matendo yao

"matendo yao yanaonesha kuwa hawamjui"

waovu (wanachukiza)

mbaya, ya kutia kinyaa au isiyofaa

Hawakuthibitishwa kwa tendo lolote jema

"hakuna mtu yeyote anayewatarajia kufanya kitu chochote kizuri"

Titus 2

Tito 02 Maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Majukumu ya kijinsia

Wasomi wanatofautiana kuhusu jinsi ya kuielewa aya hii katika muktadha wake wa kihistoria na kitamaduni. Wasomi wengine wanaamini kwamba wanaume na wanawake wako sawa kwa maswala yote. Wengine wanaamini Mungu aliwaumba wanaume na wanawake kutumikia majukumu ya kipekee katika kanisa na ndoa.Watafsiri wawe makini wasiathiriwe na jinsi wanavyoelewa swala hili wakati wa kutafsiri aya hii.

Utumwa

Katika sura hii, Paulo haandiki iwapo utumwa ni mzuri ama mbaya. Paulo anafundisha kwamba watumwa wawafanyie mabwana wao kazi kwa uaminifu. Anawafundisha waumini wote kumcha Mungu na kuishi vyema katika kila hali.

<< | >>

Titus 2:1

Sentensi unganishi:

Paulo anaendelea kumweleza Tito sababu za yeye kuhubiri Neno la Mungu, na jinsi ambavyo wazee, akina mama wazee, vijana, na watumwa au watumishi wanapaswa kuishi kama waamini.

Lakini wewe

Paulo anatofautisha "Lakini wewe Tito, kinyume na walimu wa uongo"

na maelekezo ya kuaminika

"mafundisho ya kweli" au "na mafundisho sahihi"

Kiasi

"akili tengefu" au " "inayojijithibiti binafsi"

yenye busara

"inayojithibiti binafsi" au "inayotawala tamaa"

sahihi

"yenye afya"

sahihi katika imani

"yenye afya katika imani" au "sahihi katika imani zao"

Sahihi...katika pendo

"na upendo wenye afya"

sahihi...katika uvumilivu

"imara" au "ya kudumu" au "isiyochoka"

Titus 2:3

vivyo hivyo

"kwa njia iyo hiyo." "Kama unavyowaelekeza wazee, waelekeze akina mama pia."

lazima daima wajioneshe wao wenyewe

"wanapawa kudhihirisha wao wenyewe kuwa" au "Lazima uishi kama..."

kusengenya

Neno hili linarejelea watu wale wanaowasema vibaya wenzao kwa mambo ya kweli au ya uongo.

watumwa wa pombe

Mtu ambaye anatabia ya kuhitaji kunywa pombe mara kwa mara hupenda kunywa pombe nyingi. Paulo anaongelea juu ya watu waliokubuu au kuzoelea ulevi kiasi cha kuwaita watumwa. "watumwa wa pombe"

kuwa wenye busara... wasafi

kuwa na mawazo sahihi au kufikiri vizuri

Titus 2:6

kwa namna iyo hiyo

Tito alitakiwa kuwafundisha wasichana kama alivyokuwa akiwafundisha wazee.

jiwekeni wenyewe

Jioneshe wewe mwenyewe kuwa

mfano katika kazi nzuri

kielelezo cha mtu yule anayefanya mambo sahihi na yenye kufaa.

ujumbe wenye afya

Paulo anaongelea juu ya mahubiri na mafundisho ya Tito kana kwamba ni mtu mwenye afya katika mwili wake.

ili kwamba yeyote apingaye aaibishwe

Hii inawakilisha hali ya kufikirika ya kwamba mtu yeyote atakayempinga Tito ataaibishwa kwa kufanya hivyo. Ilikuwa haizungumzii hali halisi iliyokuwepo dhahiri. Huenda lugha yako yaweza kkuwa na njia fulani ya kuelezea jambo hili.

Titus 2:9

mabwana zao

"mabwana zao wenyewe"

katika kila kitu

"katika kila hali" au "mara zote"

kuwafurahisha

"kuwafanya mabwana zao wafurahi" au "kuwaridhisha mabwana zao"

kuiba

kuwaibia vitu vidogo mabwana zao

kuonesha imani nzuri

"kudhihirisha kuwa wanaaminika kwa mabwana zao"

katika kila njia

"katika kila jambo wanalolifanya"

kupamba mafundisho yetu

Paulo anazungumzia mafundisho ya kikristo kana kwamba ni kitu ambacho chaweza kupambwa. "Yafanyeni mafundisho yetu ili yawavutie watu wengine"

Mungu mwokozi wetu

"Mungu wetu anayetuokoa"

Titus 2:11

Sentensi kiunganishi

Paulo anamtia moyo Tito kuutarajia ujio wa Yesu na kukumbuka mamlaka yake kupitia kwa Yesu.

neema ya Mungu imeonekana.....Inatufundisha

Paulo anaiongelea neema ya Mungu kama ni Mtu anayeenda kwa watu wengine na kuwafundisha jinsi ya kuishi maisha matakatifu.

inatufundisha kukataa mambo yasiyo ya kimungu na tamaa za kidunia

Inatufundisha tusimwasi Mungu

tamaa za kidunia

"Hizi ni tamaa kali kwa ajili ya vitu vya dunia hii" au "tamaa kwa ajili anasa"

katika wakati huu

"wakati bado tunaishi katika dunia hii" au " "muda huu"

tunatarajia kupokea

"Tunasubiri kupokea"

tumaini letu lenye baraka,

Paulo anamaanisha kwamba Mungu atakuja kwetu ambaye ndani yake tumeweka tumaini letu .

mwonekano wa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Paulo anaongelea juu ya utukufu wa Mungu kumaanisha kwamba Mungu mwenyewe atajidhihirisha.

Titus 2:14

alijitoa mwenyewe

"kujitoa mwenyewe afe kwa ajili yetu."

kutukomboa kutoka katika uas

Paulo anamzungumzia Yesu aliyetukomboa kana kwamba anawaweka huru watumwa kutoka katika mikono ya mabwana zao waovu.

watu maalumu

Ni kundi la watu anaowawekezea hazina

walio na hamu

"kuwa na tamaa au hamu kubwa ya ajabu"

Titus 2:15

yaseme na kuyasisitiza mambo haya.

"Fundisha mambo haya na uwatie moyo wasikilizaji ili wayafanye mambo haya."

Kemea kwa mamlaka yote

Maelezo haya yanaweza kuwekwa wazi kama: " Wakemea au wasahihishe kwa mamlaka yote watu wale ambao hawayafanyi mambo haya"

Usikubali

"Usimruhusu mtu yeyote ku..."

akupuuze

Neno hili linnaweza kuwekwa wazi kumaanisha: " Kataa kusikiliza maneno yako" au "kukataa kukuheshimu"

Titus 3

Tito 03 Maelezo ya jumla

Muundo na Mpangilio

Paulo anampa Tito maelekezo ya kibinafsi katika sura hii.

Mstari wa 15 unamalizia barua hii kirasmi. Hii ni njia ya kawaida ya kumaliza barua siku za kale katika Mashariki ya Karibu.

Dhana muhimu katika sura hii

Orodha ya ukoo

Orodha ya ukoo no orodha inayorekodi mababu wa mtu. Wayahudi walitumia ordha za ukoo kumchagua mtu aliyestahili kuwa mfalme. Walifanya hivi kwa vile mwana wa kiume wa mfalme angekuwa mfalme. Zilionyesha pia ni kabila na familia gani walitokea. Kwa mfano makuhani walitoka katika kabila la Walawi na kwa familia ya Aruni.

__<< | __

Titus 3:1

Sentensi unganishi:

Paulo anaendelea kumpa Tito maelekezo juu ya namna ya kufundisha wazee na watu chini ya uangalizi wake huko Krete.

Uwakumbushe

"Kuwaambia watu wetu tena kile ambacho tayari wanakijua" au "Kuendelea kuwakumbusha"

nyenyekea kwa viongozi na mamlaka, kuwatii

"fanyeni kama watawala wa kisiasa na wenye mamlaka ya kiserikali wasemavyo kwa kuwatii"

watawala na wenye mamlaka

Maneno haya yana maana zinazofanana na yametumika pamoja kumuhusisha kila mmoja ambaye anashikilia mamlaka katika serikari.

muwe tayari kwa kila kazi njema

"muwe rayari kufanya mema wakati wote palipo na fursa"

ubaya

"ongea mabaya juu ya"

waache watu wengine waenende katika njia zao

Paulo anawasihi waumini kufanya mambo kama vile watu wengine wanavyopendelea kufanya, ilimradi tu matakwa yao na matendo yao yasiwe ya dhambi. "

Titus 3:3

kwa kuwa

"kwa sababu"

mwanzo

"zamani" au "kwa wakati fulani" au "awali"

mawazo potofu

"ujinga" au "kutokuwa na hekima"

potoshwa na kumikishwa kwa tamaa nyingi na starehe

Paulo anaongelea juu ya tamaa za dhambi kana kwamba ni watu wanaotupotosha kutoka katika njia ya kweli "tumepotoshwa"

tulifanywa watumwa kwa tamaa nyingi na starehe

Paulo anazizungumzia tamaa zetu mbaya za mwanzo na kuzifananisha na mabwana zetu waliotutumikisha.

shauku

"tamaa" au "hamu"

tuliishi katika uovu na wivu

"uovu na "wivu " ni maneno haya yako sawa kimaana, yaote yanamaanisha "dhambi." "Siku zote tulifanya mambo maovu na kutaka vitu vya watu wengine."

Tulichukiza

"tuliwafanya au tuliwasababisha wengine watuchukie"

Titus 3:4

wakati huruma wa Mungu mwokozi wetu na upendo wake kwa wanadamu ulipoonekana

Paulo anaongelea juu ya wema wa Mungu na Upendo wake kana kwamba walikuwa ni watu waliojitokeza mbele yetu.

kwa huruma yake

"Kwasababu alikuw na rehema juu yetu"

kutuosha kwa kuzaliwa upya

Paulo anazungumzia juu ya msamaha wa Mungu kwa wenye dhambi kwa kuufananisha na kitendo cha kuosha mwili wa mtu. Lakini pia, anaongelea juu ya wenye dhambi kuwa wasikivu mbele za Mungu kama wamezaliwa upya tena.

Titus 3:6

kwa utajiri

"kwa wingi" au "ukarimu"

alimwaga Roho Mtakatifu juu yetu

imekuwa kawaida kwa Waandishi wa Agano lake kumwongelea Roho Mtakatifu kama kimiminika ambacho humwagwa. "alitupa Roho Mtakatifu kwa ukarimu"

kupitia Mwokozi wetu Yesu Kristo

"Yesu alipotuokoa sisi"

tukiwa tumehesabiwa haki

"Mungu ametutangaza kuwa hatuna dhambi" "Tayari tumefanywa wenye haki na Mungu"

tulifanyika warithi katika uhakika wa maisha ya milele.

Watu walioahidiwa na Mungu waongelewa kama warithi wa mali na utajiri kutoka kwa mwana familia.

Titus 3:8

ujumbe huu

Hii inarejea kwenye maelezo kuhusu Mungu kutupa Roho Mtakatifu kupitia Yesu katika 3:6.

dhamira juu ya kazi nzuri

"kutafuta na kufanya matendo au kazi njema"

ambayo aliweka mbele yao

Paulo anaongelea kuhusu matendo meme kana kwamba ni vitu ambavyo Mungu aliweza kuviweka mbele ya watu. "ambayo Mungu aliyaandaa kwa ajili yao kuyafanya"

Titus 3:9

Sentensi unganishi:

Paulo anaelezea kile Tito anapaswa kuepuka na kuwashughulikia wale ambao wanasababisha ubishi miongoni mwa waumini.

Bali

"lakini wewe, Tito,"

mijadala ya kipumbavu

"mabishano kuhusu mambo yasiyo ya muhimu"

nasaba

mambo yanayohusu habari za uhusiano wa kifamilia au ukoo

ugomvi/mashindano

"kugombana"

sheria

"sheria za Musa"

Kataa/kumkataa

"kujitenga" au "kutoingiliana na" au "msikae na" au "kuepuka"

baada ya onyo moja au mawili

"baada ya kumuonya mtu huyo mara moja au mara mbili"

mtu wa aina hiyo

"mtu kama huyo"

ameiacha njia iliyo sahih

Paulo anamzungumzia mtu yule anayefanya makosa kana kwamba anaiacha njia ambayo amekuwa akiiendea.

anajilaani mwenyewe

"analeta hukumu juu yake mwenyewe"

Titus 3:12

Sentensi unganishi:

Paulo anafunga barua akimwambia Tito cha kufanya baada ya kuchagua viongozi katika Krete na kwa kumpa salamu kutoka kwa wale aliokuwa pamoja nao.

Nitakapo mtuma

"Baada ya kumtuma"

Artemi...Tikiko...Zena

Haya ni majina ya wanaume

harakisha na uje

"fanya haraka na uje" au "njoo haraka"

kukaa kipindi cha baridi

"kukaa wakati wa majira ya baridi"

Harakisha na umtume

"Harakisha" au "Usichelewe kutuma"

na Apolo

"na pia umtume Apolo"

Titus 3:14

Sentensi kiunganishi:

Paulo anafafanua kwanini ni muhimu wa kuwatoa akina Zena na Apolo.

watu wetu

Paulo alikuwa anawarejelea waumini wa Krete.

kujishughulisha wenyewe katika

"washughulike kufanya"

mahitaji muhimu

Haya ni mahitaji ya ambayo yalikuwa hayakupangwa na ya haraka ambayo yalikuwa hayajulikani hapo awali.

ili kwamba wasiweze kuwa wasiozaa matunda

Paulo anaongelea watu ambao hufanya matendo mazuri kama mimea inayozaa matunda ya kula. "ili waweze kuzaa matunda" au "ili maisha yao yawe na maana."

Titus 3:15

maelezo ya jumla

Paulo anahitimisha barua yake kwa Tito.

wote walio

"Watu wote"

wale watupendao katika imani

Maana zinazokubalika hapa ni 1) Waumini wanaotupenda au 2) Waumini wanaotupenda kwasababu tunashiriki imani moja.

Neema na iwe nanyi nyote

Hii ilikuwa ni salamu ya kawaida ya kikristo. "Neema ya Mungu na iwe pamoja nanyi" au "Ninamwomba Mungu awe mwenye neema kwenu ninyi nyote."