Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa Yakobo

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Jumla

Muhtasari wa Kitabu cha Yakobo

  1. Salamu (1:1)

  2. Kujaribiwa na ukomavu (1:2-18)

  3. Kusikia na kulitenda neno la Mungu

  4. Imani ya kweli inaonekana kwa matendo

    • Neno la Mungu ( 1:19-27)
    • Sheria ya kifalme ya upendo (2:1-13)
    • Matendo (2:14-26).
  5. Matatizo katika jumuiya

    • Hatari za ulimi (3:1-12)
    • Hekima kutoka juu (3:13-18)
    • Tamaa za kidunia (4:1-12)
  6. Mtazamo wa Mungu kuhusu maamuzi yako

    • Majivuno juu ya kesho (4:13-17)
    • Onyo kuhusu utajiri(5:1-6)
    • Kuteseka na uvumilivu (5:7-11)
  7. Maonyo ya kumalizia

    • Viapo (5:12)
    • Sala na uponyaji (5:13-18)
    • Kujali kila mmoja (5:19-20)

Nani alikiandika kitabu cha Yakobo?

Mwandishi wa kitabu hiki anajitambulisha kama Yakobo. Kuna uwezekano Yakobo alikuwa ndugu wa kambo wa Yesu. Yakobo alikuwa kiongozi wa kanisa la mwanzo na mwanachama wa baraza la Yerusalemu. Mtume Paulo pia alimuita "mhimili" wa kanisa.

Huyu siye mtume Yakobo. Mtume Yakobo aliuwawa kabla ya barua hii haijaandikwa.

Kitabu cha Yakobo kinahusu nini?

Katika barua hii Yakobo anawapa moyo waumini waliokuwa wanateseka. Aliwaeleza kwamba Mungu hutumia mateso kuwafanya wawe Wakristo wakomavu. Yakobo pia anawaelezea umuhimu wa waumini kutenda mema. Aliandika mengi kuhusu jinsi waumini wanapaswa kuishi na kuwatendea wengine. Kwa mfano aliwaamuru watendeane haki, kutopigana na kutumia mali kwa hekima.

Yakobo aliwafunza wasomaji wake kutumia mifano mingi kutoka kwa mazingira. Kwa mfano katika 1:6, 11 na 3:1-12. Pia sehemu nyingi za barua hii zinafanana na yale Yesu aliandika kwenye Hotuba mlimani (Mathayo 5-7).

Akina nani walikuwa "Makabila kumi na mbili yaliyotawanyika?"

Yakobo alisema alikuwa anawaandikia "makabila kumi na mbili yaliyotawanyika"(1:1) Wasomi wengine wanafikiri kwamba Yakobo aliwaandikia Wakristo Wayahudi. Wasomi wengine wanafikiri kwamba Yakobo aliwaanndikia Wakristo wote kwa ujumla. Barua hii ni mojayapo ya "barua za jumla" kwa vile haikuandikiwa kanisa fulani ama mtu fulani.

Kichwa cha Kitabu hiki kitafsiriwe namuna gani?

Watafsiri wanaweza kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha asili "Yakobo" ama wanaweza kuchagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama "Barua kutoka kwa Yakobo" ama "Barua iliyoandikwa na Yakobo" (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamatudi

Je, Yakobo alitofautiana na Paulo kuhusu jinsi ya mtu kuhesabiwa haki mbele za Mungu?

Paulo alifundisha kwamba Wakristo wanahesabiwa haki kwa imani na siyo kwa vitendo. Inaonekana Yakobo anawafundisha Wakristo kwamba Wakristo wanahesabiwa haki kwa vitendo vyao. Hali hii inaweza kutatanisha. Lakini kuelewa kuzuri kuhusu kile Paulo na Yakobo walifundisha kunaonyesha kwamba hawakutofautiana. Wote walifundisha kwamba mtu anahitaji imani "ili ahesabiwa haki. Wote walifundisha pia kwamba imani ya kweli itamfanya mtu kutenda mema. Paulo na Yakobo waliyafundisha mambo haya kwa njia tofauti kwa sababu walikuwa na hadhira tofauti zilizotaka kujua vitu vingi kuhusu kuhesbiwa haki. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#justice and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#works)

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Watafsiri wanatakiwa kuashiria namna gani mipito kati ya mada za kitabu cha Yakobo?

Barua hii inabadilisha mada haraka. Wakati mwingine Yakobo hawaelezi wasomaji kwamba karibu anabadilisha mada. Inakubalika kuacha mistari kuonekana haina uhusiano. Ni busara kuweka kando aya kwa kuanzisha mistari mipya ama kuacha nafasi katikati ya mada.

Ni maswala gani muhimu katika maandishi ya kitabu cha Yakobo?

  • "Usitake kujua, mpumbavu, kwamba imani bila matendo ni bure."(2:20). Matoleo ya ULB, UDB na ya kisasa husoma hivyo. Lakini matoleo mengine ya zamani husoma, "Unataka kujua, Mpumbavu, kwamba imani bila matendo imekufa?" Kama kuna tafsiri ya Bibilia katika eneo kwa ujumla, watafsiri wanapaswa kuzingatia kutumia masomo yanayopatikana katika matoleo hayo.La sivyo, watafsiri wanashauriwa kufuata masomo ya kisasa.

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/Translate.html#translate-textvariants)

James 1

Yakobo 01 Maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Majaribio na vishawishi

Maneno haya mawili yanatokea pamoja katika (Yakobo: 1:12-13) Maneno yote "yanasema juu ya mtu anayeweza kuchagua kutenda mazuri na kutenda mabaya. Tofauti yao ni muhimu. Mungu anamjaribu mtu na anahitaji atende mema. Shetani anamshawishi mtu huyo na anataka atende maovu.

Mataji

Taji ambalo mtu hupewa baada ya kuyashinda majaribio ni tuzo. Hiki ni kitu amabaco watu wafanyacho kitu kizuri hupokea. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#reward)

Mifano muhimu za usemi katika sura hii

MIfano

Yakobo anatumia mifano nyingi na "unastahili kuelewa maswala yaliyo kwenye https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor kabla ya kuzitafsiri vizuri.

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Kwa Makabila kumi na mbili yaliyotawanyika"

Haikuwa wazi kama Yakobo aliwaandikia wa nani katika barua hii.Anajiita mwenyewe kama mtumishi wa Bwana Yesu Kristo, na kwa hivyo kuna uwezekano alikuwa akiwaandikia Wakristo. Lakini anawaita wasomaji wake "Makabila kumi na mbili yaliyotawanyika", maneno yatumikayo kuashiria Wayahudi. Kuna uwezekano ametumia maneno hayo kama mfano ya "wengi ambao Mungu amewachagua" ama aliandika barua hii wakati Wakristo wote walikuwa wamekomaa kama Wayahudi.

| >>

James 1:1

Sentensi unganishi

Baada ya salam zake za ufunguzi, Yakobo anawaambia waamini kwamba kusudi la majaribu ni kupima imani.

Yakobo, mtumishi wa Mungu na Bwana Yesu Kristo.

Neno "Niko" linamaanisha " Mimi, Yakobo ni mtumishi wa Mungu na Bwna Yesu Kristo"

Yakobo

Yakobo alikuwa ndugu yake na Yesu.

Kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika.

Hii inaelezea eidha wayahudi wote wa Kikiristo waishio nje ya Israeli au Wakristo wote waishio popote duniani.

Makabila kumi na mbili.

Neno "makabila "kumi na mbili" yanamaanisha watu wote wa Israeli kwa kuwa waligawanywa katika makabila "kumi na mbili". Kwenye mistari hii makabila kumi na mbili yanamaanisha Wayahudi wote wa Kikristo au Wakristo wote duniani. Hapa neno "kumi na mbili" hutumika kama jina na namba "kumi na mbili" inapaswa kuandikwa kama neno sio kama namba.

Kutawanyika

Neno "kutawanyika" kunamaanisha Wayahudi wote waliotawanyika kwenye nchi nyingine mbali na nyumbani kwao Israeli. Kenye mistari hii "kutawanyika" linamaanisha Wakristo wa kiyahudi waishio nje ya Israeli au Wakristo wote waliopo popote duniani.

Salam

Salam ya kawaida kama "habari" au "siku njema".

Furahini ndugu zangu, mpatapo matatizo.

"Waamini wenzangu, yaone matatizo yote uliyonayo kama mambo ya kukufanya ushangilie"

Jaribu la imani yenu inatengeneza uvumilivu.

Maneno "jaribu", "imani yenu", na "kuvumilia" ni maneno yanayosimama kuonyesha matendo. Mungu hutujaribu ili kujua ni kwa namna gani tunamwamini yeye na kumtii. Waamini ("ninyi") mwamini yeye na mvumilie mateso. "Mnapokutana na magumu Mungu anagundua ni kwa kiasi gani unamwamini. Na matokeo yake unakuwa na uwezo wa kushinda majaribu magumu zaidi.

James 1:4

Tuache uvumilivu ukamilishe kazi yake.

Hapa uvumilivu imezungumzwa kama vile mtu yupo kazini. "Jifunze kuvumilia magumu yote"

Kukua kabisa

Kuwa na uwezo wa kumwamini Kristo na kumtii yeye katika hali zote.

Usipungukiwe chochote

Hii inaweza kuwa sentensi chanya "kuwa na uwezo kumtii Mungu kwa kila jambo"

Muombe Mungu, yeye atoaye

"Muombe Mungu. Ni yeye atoaye"

Ukarimu na "bila kukemea

Hii inaweza kuzungumziwa kwa mtazamo chanya "ukarimu au furaha"

Atawapa

"Mungu atawapa" au "Mungu atajibu maombi yenu"

James 1:6

Kwa imani, bila mashaka yoyote

Hii inaweza kuzungumziwa kwa mtazamo chanya. "Kwa uhakika zaidi kuwa Mungu atajibu"

Kwa yeyote mwenye mashaka ni kama mawimbi ya bahari yanavyoendeshwa na upepo na kuchafuka kwa bahari

Yeyote mwenye mashaka kuwa Mungu atamsaidia ni kama maji ndani ya bahari au maziwa makubwa yanayopita katika uelekeo tofauti.

Ana nia mbili

Nia. Neno "nia mbili" linamaanisha mawazo ya mtu pale anaposhindwa kufanya maamuzi. "Anashindwa kuamua amfuate Yesu as la"

Hana msimamo kwenye njia zake zote

Hapa anazungumziwa mtu amabye hawezi kukaa kwenye njia moja badala yake anaenda njia moja baada ya nyingine.

James 1:9

Ndugu masikini

"mwamini asiye na pesa nyingi"

Kujivuna kwa cheo chake cha juu

Mtu ambaye Mungu anembariki anazungumza kama vile amesimama mahali pa juu sana.

Lakini tajiri

"lakini mtu aliye na pesa nyingi." Maana nyingine ni 1) huyu mtu tajiri ni mwamini, au 2) huyu mtu tajiri si mwamini.

Wa cheo cha chini

Mwamini tajiri anapaswa kufurahi kwamba Mungu ameyaruhusu mateso. "anapaswa kuwa na furaha kwamba Mungu amempa nafsi hiyo"

Atapita kama ua la porini kwenye majani

Matajiri wanafananishwa na maua ya porini ambayo yanakuwa hai kwa mda mfupi.

Mtu tajiri atachakaa katikati ya safari zao

Kama ambavyo maua hayafi ghafla lakini yanachakaa kwa mda mfupi , pia matajiri hawatakufa ghafla lakini watachukua mda mfupi kupotea.

Katikati ya kazi yake.

Shughuli za kila siku za tajiri zinazungumzwa kama safari aliyokuwa anaifanya. Hii inaelezea namna ambavyo hakufikiri chochote juu ya kifo chake hapo baadae na hivyo kitakuja ghafla.

James 1:12

Sentensi unganishi.

Yakobo anawakumbusha waamini wanaosema Mungu hasababishi majaribu; anawaambia namna ya kukabiliana na majaribu.

Baraka

Bahati, vizuri.

Kuvumilia majaribu

Kuendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu uwapo katika magumu.

Kushinda majaribu

Amethibitishwa na Mungu.

Kupokea taji ya uzima

Uzima wa milele unazungumziwa kama taji ya maua inayowekwa kwenye kichwa cha washindi. "pokea uzima wa milele kama tuzo"

Imeahidiwa kwa wale wanaompenda Mungu.

Hii imeelezewa katika hali ya utendaji "Mungu aliahidi taji ya uzima kwa wale wampendao"

Anapojaribiwa

"Anapotamani kufanya uovu"

Nimejaribiwa na Mungu

Hii imeelezewa katika hali ya utendaji. "Mungu amesababisha nifanye maovu"

Mungu hajaribiwi na uovu

Hii imeelezewa katika hali ya utendaji. "Mungu hatamani kufanya lolote ovu"

Wala mwenyewe hamjaribu yeyote

"Na Mungu mwnyewe hamsababishi mtu kufanya uovu"

James 1:14

Kila mtu anajaribiwa na tamaa zake mwenyewe

Tamaa za mtu zinazungumzwa kama vile mtu mwingine ameshawishi afanye dhambi.

Zinamshawishi na kumvuta mbali

Tamaa mbaya zinaendelea kuzungumzwa kama mtu anavyoweza kumshawishi mwingine.

Kushawishi

kuvutia, kumshawishi mtu kufanya uovu.

Ndipo baada ya tamaa ya dhambi kubeba mimba, dhambi huzaliwa, na baada ya dhambi kukomaa sawasawa, huishia katika mauti.

Tamaa inaendelea kuzungumzwa kama mtu, na hapa inaelezewa wazi kama mwanamke mwenye mimba ya mtoto. mtoto anaelezewa kama dhambi. Thambi ni mtoto mwingine wa kike ambaye anakuwa na kupata mimba naanazaa kifo. Mtiririko huu ni picha inayoonyesha namna ambavyo mtu atakufa kiroho na kimwili kwa sababu ya tamaa zake mbaya na dhambi.

Msidanganyike

"Msiache mtu yeyote awadanganye" au "msijidanganye wenyewe"

James 1:17

Kila zawadi iliyo nzuri na kila zawadi iliyokamilika

Sentensi hizi mbili zina maana moja. Yakobo alizitumia kusisitiza kuwa kila kizuri alichonacho mtu kinatoka kwa Mungu.

Baba wa nuru.

Mungu, muumbaji wa nuru zote zilizopo juu angani (jua, mwezi na nyota) inajulikana kuwa ni Baba yao.

Kamwe habadiliki kama kivuli kibadilikavyo

Hii inamuelezea Mungu kama mwanga usiobadilika tofauti na jua, mwezi, sayari na nyota ambazo zinapita katikati ya anga na zinabadilisha nuru yake. "Mungu habadiliki kama jua, mwezi na nyota ambazo zinatokea na kupotea"

Kutupa sisi

Neno "sisi" linamaanisha Yakobo na hadhira yake.

Katupa uzima

Mungu aliyetupa uzima wa milele anazungumziwa kana kwamba ametupa uzima.

Neno la kweli

Ujumbe wa kweli wa Mungu.

Kama uzao wa kwanza

Yakobo anatumia utamaduni wa Kiebrania wa zao la kwanza kama njia ya kuelezea thamani ya Mwamini wa Kikristo kwa Mungu. anaelezea kuwa kutakuwa na waamini wengi sana baadae.

James 1:19

Mnajua hili

Yaweza kumaanisha 1) "mnajua hili" kama amri, kuwa makini juu ya lile ninalotaka kuwaandikia au 2) "mnajua hili" kama sentensi kwamba ninataka kuwakumbusha juu ya jambo ambalo mnalijua.

Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea

Watu wanapaswa kusikiliza kwa makini na kuzingatia maneno haya " usiwe mwepesi kuongea" haimaanishi uongee taratibu.

si mwepesi wa hasira

"usishikwe na hasira mapema"

hasira ya mwanadamu haiwezi kutenda haki ya Mungu

Mtu anapokuwa na hasira hawezi kufanya kazi ya Mungu, ambayo ni haki.

wekeni mbali uchafu wa dhambi na ubaya wote

Dhambi na ubaya vimezungumzwa hapa kama vitu ambavyo vinapaswa kuwekwa mbali au kutupwa.

wekeni mbali uchafu wa dhambi na ubaya wote

Hapa uchafu wa dhambi na ubaya vinamaanisha kitu kimoja. Yakobo ameyatumia kusisitiza ni kwa jinsi gani dhambi ilivyo mbaya. "Acheni kufanya aina zote za dhambi"

uchafu wa dhambi

Hapa uchafu inamaanisha dhambi na ubaya.

Kwa unyenyekevu

"Bila kujivuna" au "bila kiburi"

lipokeeni neno lililopandwa

Neno "kupanda" linamaandishwa kuweka kitu flani ndani ya kitu kingine. Hapa neno la Mungu limetumika kama mmea ambao unapaswa kukua ndani ya waamini. "Utii ujumbe wa Mungu aliousema kwako"

lipokeeni neno lililopandwa

"Neno" linamaanisha neno la Mungu linalosimama kama ujumbe wa ukombozi ndani ya Yesu Kristo ambapo Mungu anawaambia waamini. Wakiliamini, Mungu atawaokoa.

kuokoa roho zenu

"Awaokoe ninyi toka kwenye hukumu ya Mungu"

roho

Hapa neno "roho" inamaanisha mtu.

James 1:22

Litiini neno

Wanapaswa kutii amri zilizoamriwa na Mungu.

Mkijidanganya wenyewe

"mnajidanganya wenyewe

Kwa kuwa kama yeyote alisikiaye neno bila kulitendea kazi ni sawa na mtu ajiangaliaye uso wake halisi katika kioo.

Mtu anayesikiliza maneno ya Mungu lakini hayatii anafananishwa na mtu anayejiangalia kwenye kioo na baadae anasahau muonekano wake.

uso wake halisi

Uso wake kama ulivyo.

Hujitathmini uso wake na baada ya mda mfupi husahau

Mtu anayejiangalia uso wake na baadae akasahau muonekano wake ni sawa na mtu aliyesikia neno la Mungu na kusahau alichosikia.

mtu yule anayeiangalia kwa uangalifu sheria kamili.

Hii inaendelea kuelezea picha ya sheria kama kioo.

Sheria kamili ya uhuru

"sheria kamili inayoruhusu watu kuwa huru"

Mtu huyu atabarikiwa katika utendaji wake.

Hii inaweza kuelezewa katika hali ya kutenda "Mungu atambariki huyu mtu kama akiitii sheria"

James 1:26

kujiona mwenyewe kuwa mtu wa dini

"Anadhani anamuabudu Mungu kwa usahihi

Ulimi wake

Kuudhibiti ulimi wa mtu inamaanisha kudhibiti kauli zake.

udanganyifu

"mjinga" au "kupotosha"

Moyo wake

Hapa moyo inamaanisha imani yake au mtazamo wake.

Dini yake ni bure

"Anamuabudu Mungu bure"

Safi na isiyoharibiwa

Yakobo anaizungumzia dini , namna watu wanavyomuabudu Mungu kama kitu amabacho ni safi na kisichoharibiwa. Hii ni utamaduni wa Kiyahudi kuelezea namna ambavyo kitu kimekubalika na Mungu. "kukubalika kabisa"

mbele za Mungu wetu na Baba

Anaelezewa Mungu.

Yatima

Yatima

Wajane katika mateso yao

Wanawake wanaoteseka kwa sababu waume zao wamefariki.

Kujilinda na ufisadi wa dunia

Kutokubali uovu wa dunia hii ukakusababisha ukatenda dhambi

James 2

Yakobo 02 Maelezo ya Jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Mapendeleo

Wasomaji wengine wa Yakobo waliwatendea matajiri na wenye uwezo mazuri na kuwatendea maskini vibaya. Haya ndiyo mapendeleo na Yakobo anawaambia kwamba hii ni mbaya. Mungu anataka maskini kwa matajiri watendewe wema.

Kuhesabiwa haki

Kuhesabiwa haki ni kile hufanyika wakati Mungu anamfanya mtu kuwa mwenye haki.Yakobo anasema Mungu huwafanya wenye haki ama huwahesabu wenye haki watu ambao imani yao huendana na matendo mazuri. (tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#justice na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Alama za nukuu

Maneno "Nionyeshe imani yako bila matendo na nitakuonyesha imani yangu kwa matendo" ni magumu kuelewa. Watu wengine hufikiri ni yale "wengine wagesema" kama maneno yaliyo na alama za nukuu. Matoleo mengi huyatafsiri kama maneno Yakobo anamwelezea "mtu huyo".

"Wewe una..." "Mimi nina..."

Watu wengine hufikiria kwamba maneno "wewe" na "mimi" yametumiwa kumaanisha "baathi ya watu" na "waatu wengine". Iwapo ni sahihi mstari wa 18 unaweza tafsiriwa , "Watu wengine wanaweza sema, "Watu wengine wana imani na baadhi ya watu wana matendo, siyo watu wote wana zote."Iwapo sentensi ifuatayo pia ni yenye watu wangesema," inaweza tafsiriwa "Baadhi ya Watu wanaonyesha imani yao bila matendo na watu wengine wanaonyesha imani yao kwa matendo. Wote wana imani." Katika hali zote mbili, msomaji ataelewa tu ukiongezea sentensi ya ziada. Ni vyema kutafsiri jinsi ULB hufanya. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metonymy and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

<< | >>

James 2:1

Sentensi unganishi:

Yakobo anaendelea kuwaambia waamini wa Kiyahudi waliotawanyika namna ya kuishi kwa kupendana na kuwakumbusha kutowapendelea matajiri juu ya masikini.

Ndugu zangu

Yakobo anawaandikia ndugu zake ambao ni waamini wa Kiyahudi . "waamini wenzangu" au "ndugu zangu katika Kristo"

Ishikeni imani ya Bwana Yesu Kristo

Mwamini Yesu Kristo.

Bwana wetu Yesu Kristo

Neno "wetu" linamaanisha Yakobo na waamini wenzake.

upendeleo kwa watu wengine

shauku ya kumsaidia mtu fulani zaidi ya mwingine

Kama mtu fulani

Yakobo anaanza kuelezea hali ambayo waamini wanamthamini sana tajiri kuliko masikini.

amevaa pete za dhahabu na mavazi mazuri

"amevaa kama mtu tajiri"

keti hapa mahali pazuri

"keti hapa sehemu ya heshima"

simama pale

"hamia sehemu isiyo na heshima"

Kaa chini ya miguu yangu

Hamia sehemu ya kunyenyekea

Je, hamuhukumiani ninyi wenyewe, na kuwa waamuzi wenye mawazo mabaya?

Yakobo alitumia swali kuwakemea wasomaji wake. "Mnahukumiana wenyewe kwa wenyewe na kufanya maamuzi mkiwa na mawazo mabaya"

James 2:5

Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa

Yakobo anawachukulia wasomaji wake kama ndugu. "kuweni makini, ndugu zangu wapendwa"

Mungu hakuwachagua ... wampendao?

Yakobo anatumia swali kuwafundisha wasomaji wake wasiwe na upendeleo. "Mungu aliwachagua ... mpende yeye"

masikini

"watu masikini."

Kuwa tajiri katika imani

Kuwa na imani kubwa ni utajiri. "kuwa na imani thabiti kwa Kristo"

Warithi

Watu ambao Mungu aliwaahidi watairithi mali na utajiri kama vile watu warithipo toka kwa ndugu wa familia.

Lakini ninyi

Yakobo anaongea na hadhira yote.

mmewadharau masikini

"Mmewadhalilisha masikini"

Je, sio matajiri wanaowatesa ninyi

Hapa Yakobo anatumia maswali kuwasahihisha wasomaji wake. "Ni matajiri wanaowatesa ninyi."

tajiri

"watu matajiri"

wanaowatesa

"wanaowatendea mabaya"

Sio wao ... mahakamani?

Hapa Yakobo anatumia maswali kuwasahihisha wasomaji wake. " matajiri ndio wao ... mahakamani."

wanaowaburuza mahakamani

"wanaowapeleka kwa nguvu mahakamani na kuwashitaki kwa hakimu"

Hawalitukani ... mnaitiwa?

Hapa Yakobo anatumia swali kurekebisha na kufundisha wasomaji wake. "Matajiri ... mnaitiwa?

Jina zuri

"jina la Kristo" hii ni njia moja wapo ya kuelezea jina la Yesu. "Kristo ambalo kwalo mnaitiwa"

mnaitiwa

"mnajulikana kwalo"

James 2:8

ninyi mkiitimiza

Neno "ninyi" inamaanisha waamini wa Kiyahudi.

kutimiza sheria ya kifalme

"kutii sheria za Mungu." Mungu alitupa sheria za Musa zilizorekodiwa katika agano la kale.

Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe

Yakobo ananukuu maneno toka kitabu cha mambo ya walawi.

Jirani yako

"watu wote"au "kila mtu"

mwafanya vyema

"mnafanya vyema" au "mnafanya yaliyo sahihi"

Kama mkipendelae

"kutoa huduma ya kipekee" au "kutoa heshima kwa"

kutenda dhambi

"kutenda dhambi" ni kuvunja sheria.

mtahukumiwa kwa shiria kama wavunja sheria.

"mna makosa ya kuvunja sheria"

James 2:10

Kwa kuwa yeyote atiiye

"Yeyoye anayetii"

bado akajikwaa ... sheria yote

Kujikwaa ni kuanguka chini wakati mtu anatembea. kutotii sheria ni sawa na kujikwaa wakati wa kutembea.

katika nukta moja

kwa sababu ya kutotii kwa sheria moja tuu

Kwa kuwa Mungu aliyesema

Hii inamuelezea Mungu aliyempa sheria Musa.

usifanye

"kufanya" ni kuchukua hatua

Kama ninyi .... lakini una ... ume

"ninyi" inamaanisha "kati yenu" Japokuwa Yakobo aliwaandikia waamini wengi wa Kiyahudi kwenye sehemu hii ametumia umoja kama vile alikuwa amzungumzia mtu mmoja.

James 2:12

Kwa hiyo zungumzeni na kutii

"hivyo mnatakiwa muongee na kufanya" Yakobo aliwaamuru watu kufanya hivi.

mko karibu kuhukumiwa na sheria ya uhuru.

"Mungu atawahukumu lwa sheria ya uhuru"

Kwa sheria

Mungu atawahukumu kulingana na sheria

Sheria ya uhuru

"Sheia inayotoa uhuru wa kweli"

Huruma hujitukuza juu

"Huruma ni bora kuliko" au "huruma inashinda" Hapa huruma na haki vimezungumwa kama vile ni mtu.

James 2:14

Sentensi unganishi

Yakobo anawatia moyo waamini waliotawanyika kuonyesha imani yao mbele za watu. Kama vile Abrahamu alivyoionesha imani yake kwa vitendo.

Kuna uzuri gani, ndugu zangu, kama mtu anasema ninayo imani, lakini hana matendo?

Yakobo anatumia swali kuifundisha hadhira yake. "Waamini wenzanhu, sio vizuri kabisa mtu akisema ana imani lakini hana matendo."

anayo imani

Yakobo anazungumzia imani, kumuamini Mungu.

haina matendo

Yakobo anazungumzia matendo kuwa ni kufanya matendo mema.

Je, imani hiyo yaweza kumwokoa?

Yakobo anazungumzia imani kuwa kumuamini Mungu kuna nguvu ya pekee katika kumuokoa mwanadamu lakini Imani haitoshi. "Imani hiyo haiwezi kumuokoa."

kumuokoa

"Kumuokoa toka kwenye hukumu ya Mungu."

mkaote moto

"kuwa na nguo za kutosha kuvaa" au "kuwa na sehemu ya kulala."

mle vizuri

"kuwa na chakula cha kutosha."

ya mwili

kula, kuvaa na kuishi vizuri.

yafaa nini?

Yakobo anatumia swali hili kuifundisha hadhira. "hivi sio vizuri."

wa kiume na wa kike

Waamini wenzangu katika Yesu, wanaume kwa wanawake

imani ... imekufa

Yakobo anaizungumzia imani kuwa ni hai mtu afanyapo matendo mema na imekufa kama mtu hatafanya matendo mema.

imani ... ina matendo

Imani inaambatana na mtu afanyaye matendo mema.

James 2:18

Bado mtu fulani anaweza kusema

Yakobo alikuwa anasahihisha uelewa wa hadhira yake juu ya imani na matendo.

Una imani, na mimi ninayo matendo

"Inakubalika iwapo mtu mmoja ana imani na mwingine ana matendo." Yakobo anaelezea ni kwa namna gani watu wnaweza kulumbana dhidi ya mafundisho yake.

Una imani, na mimi ninayo matendo ... nionyeshe imani yako

Yakobo anazungumzia imani na matendo kama vitu ambavyo watu wanaweza kuwa navyo na kuwaonesha wengine.

nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu

Yakobo anazungumza kuwa imani inaweza kuonekana endapo mtu atafanya matendo mema. "Nitaionesha imani yangu kwa kufanya matendo mema"

mapepo nayo yanaamini hivyo na kutetemeka.

"mapepo nayo yanaamini, lakini yanaogopa kwa hofu. Yakobo anafananisha mapepo na watu wanaosema wana imani lakini hawafanyi matendo mema. Yakobo anasema pepo wana busara maana wanamuogopa Mungu wakati watu hawamuogopi.

Je, unataka kujua, ewe mtu mpumbavu, namna ambavyo imani hiyo pasipo matendo isivyofaa?

Yakobo alitumia swali kuwakemea watu ambao hawakumsikiliza. "Ewe mpumbavu, hautaki kunisikiliza thibitisha namna isivyofaa imani bila matendo.

Je, unataka kujua ... isivyofaa?

"Nitawaonyesha ni jinsi gani ... isivyofaa."

James 2:21

Maelezo ya jumla

Kwa kuwa kulikuwa na waamini wa Kiyahudi walijua habari za Abrahamu ambaye waliambiwa na Mungu zamani.

Je, si baba yetu Abrahamu alihesabiwa haki

Hili ni swali linalotumika kuwakemea wapumbavu walioelezewa toka 2:18 waliokataa kuamini kuwa imani na matendo vinaenda sambamba." Abrahamu baba yenu alihesabiwa haki."

haki kwa matendo

"haki kwa kufanya matendo mema"

Baba

"baba" imetumika kama "mababu"

Mnaona

Neno "wewe" linamaanisha umoja. Yakobo anaongea na hadhira yake kama anaongea na mtu mmoja.

mnaona

kuona inaweza kumaanisha "kuelewa"

imani yake ilifanya kazi na matendo yake

Yakobo anazungumzia imani inafanya matendo mema. Imani ya Abrahamu kwa Mungu kuhusu Isaka inamfanya Abrahamu kumheshimu Mungu kwenye wakati mgumu. Kwa kumheshimu Mungu imani yake ikakuwa.

kwa matendo imani yake ilifikia kusudio lake

Kwa kumwamini Mungu Abrahamu alitimiza kusudi la Mungu. "kwa kuwa Abrahamu alimtii Mungu alimwamini Mungu kabisa"

Maandiko yalitimia

"Hii ilitimiza maandiko"

Akahesabiwa kuwa ni mwenye haki

"Mungu aliiona imani yake kuwa imemfanya kuwa mwenye haki." Imani ya Abrahamu na haki vilimpa thamani.

mnaona

Yakobo tena anazungumza na hadhira yake kwa kutumia wingi toka kwenye umoja "wewe"

kwa matendo mtu huhesabiwa haki, na si kwa imani tu .

"Matendo na imani ndio yanayomfanya mtu kuwa na haki na sio imani tuu."

James 2:25

Hali kadhalika, ... haki kwa matendo

Yakobo alikuwa anasema kama ilivyokuwa kweli kwa Abrahamu ndivyo ilivyokuwa kweli kwa Rahabu. wote walihesabiwa haki kwa matendo.

hakuwa Rahabu yule kahaba alihesabiwa haki kwa matendo ... barabara nyingine

Yakobo alitumia swali kuwaelekeza watu. "hakuwa Rahabu yule kahaba alihesabiwa ... barabara nyingine."

Rahabu yule kahaba

Rahabu alikuwa mwanamke aliyezungumzwa katika agano la kale na Yakobo alitegema hadhira yake inafahamu.

haki kwa matendo

Yakobo anazungumzia matendo kama kitu cha kumiliki.

wajumbe

Watu wanaoleta habari njema toka sehemu nyingine.

kuwapeleka kwa barabara nyingine

"aliwasaidia kutoroka mjini"

Kwa kuwa kama vile mwili usipokuwa na roho umekufa, vivyo hivyo imani pasipo matendo imekufa.

Yakobo anazungumzia imani imani isiyo na matendo kama mwili uliokufa usio na roho.

James 3

Yakobo 03 Maelezo kwa jumla

Mifano muhimu katika sura hii

Mifano

Yakobo anawafundisha wasomaji wake kwamba waishi kumpendeza Mungu kwa kuwakumbusha kuhusu mambo wanayofahamu ya kawaida katika maisha ya kila siku. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

<< | >>

James 3:1

sio watu wengi

"siyo wengi wenu" Yakobo anatengeneza senyensi ya jumla.

Ndugu zangu

"wapendwa waumini wenzangu."

tutapokea hukumu kubwa sana

"Mungu atatuhukumu sisi kwa nguvu kwa sababu hatuna udhuru, wakati tufanyapo dhambi kwa sababu twajua na kufahamu Neno lake vizuri kuliko watu wengine."

Tutapokea

Yakobo anapanga makundi ya wale ambao hufundisha Maandiko kama yeye. Ingawa baadhi ya waumini ambao wangepokea barua hii, wangekuwa walimu wa Maandiko, wengi wasingeweza.

Kwa kuwa wote tunajikwaa.

Neno "wote" Yakobo amelitumia kumaanisha hadhira yake.

Kujikwaa

Dhambi imezungumzwa kama tendo la kujikwaa wakati wa kutembea. "kuanguka au kutenda dhambi"

Hawezi kujikwaa katika maneno yake.

"Hawezi kufanya dhambi kupitia maneno anayo zungumza."

Ni mtu mkamilifu.

"Amekomaa kiroho"

Kuongoza mwili wake wote.

Yakobo anazungumza juu ya moyo wake, hisia zake, na matendo yake. "kuongoza tabia yake" au "kuongoza matendo yake"

James 3:3

Ikiwa tunaweka rijamu kwenye midomo ya farasi.

Yakobo anazungumza kuhusu rijamu za farasi. Rijamu ni kipande kidogo cha chuma kinaachowekwa katika mdomo wa farasi ili kumuongoza kule anakoelekea.

Sasa ikiwa

"Kama" au "Endapo"

Farasi

"Farasi" ni mnyama mkubwa anayetumika kubeba vitu au watu. "endapo tunaweka rijamu katika vinywa vya farasi"

Tazama pia kwamba meli...huendeshwa kwa usukani mdogo sana.

"Meli" ni kama gari kubwa linaloelea juu ya maji. "Usukani"ni kipande kidogo cha mti au cha chuma kilicho nyuma ya meli kinachotumika kuiongoza meli kule inakoelekea. Neno "usukani" lingeweza kutafsiriwa kama "kifaa".

Maelezo ya jumla

Yakobo anajaribu kukuza mjadala juu ya vitu vidogo kutawala vitu vikubwa.

Zinasukumwa na kwa upepo mkali.

"Upepo mkali unazisukuma"

Zinaendeshwa kwa usukani mdogo sana popote nahodha atakapotaka kugeuka.

"Uwe na kifaa kidogo ambacho mtu anaweza kukitumia kuongozea meli mahali iendakako."

James 3:5

Vivyo hivyo.

Neno hili huashiria mlingano wa ulimi kwa rijamu za farasi na usukani wa meli katika mistari iliyotangulia.

Hujisifia mambo makuu sana

"mambo" ni ujumla wa vitu vyote ambavyo watu hawa wanajisifia.

Angalia

"fikiri kuhusu"

Jinsi msitu ulivyo mkubwa unawashwa na cheche moja!

"Ulimi mdogo wa moto unaweza kuwasha moto utakao unguza miti mingi!"

Ulimi pia ni moto.

Kama moto unavyo uunguza na kuteketeza vyote vinavyochomwa, ulimi, husimama badala ya mambo ambayo mtu huyatamka, yanaweza kuwaumiza watu vibaya. "Ulimi ni kama moto."

Ulimwengu wa uovu umewekwa katikati mwa viungo vya mwili wetu.

"Ni sehemu ndogo ya mwili wetu, lakini una uwezo wa kufanya dhambi katika aina zote za mambo."

Ambao hunajisi mwili wote.

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Inaweza kutufanya sisi tusimpendeze Mungu kabisa" au "Inaweza ikatufanya sisi tusikubalike kwa Mungu."

Na huweka katika moto njia ya uzima.

Msemo huu "njia ya uzima" una maana ya maisha yote ya mtu. "na unaweza kuharibu maisha yote ya mtu."

Na wenyewe unachomwa katika moto katika jehanamu.

Neno "wenyewe" limesimama badala ya ulimi. Pia, hapa neno "jehanamu" limesimama badala ya nguvu za uovu au nguvu za shetani. Hii ingeweza kutafsiriwa kama kishazi kazi: "kwa sababu shetani huutumia kwaajili ya uovu."

James 3:7

Kila aina ya .... na mwanadamu.

Usemi huu "kila aina" humaanisha "aina nyingi." hii inaweza kutafsriwa kama fungu la maneno yanayoonesha kutenda; "Watu wamejifunza kudhibiti aina nyingi za wanyama wa mwitu, ndege, vitambaavyo, na viumbe wa baharini."

Kitambaacho.

Huyu ni mnyama ambaye hutembea juu ya ardhi kwa kujikokota.

Kiumbe wa baharini

Huyu ni mnyama ambaye anaishi majini.

Lakini kuhusu ulimi hakuna hata mmoja miongoni mwa watu awezaye kuchunga ulimi.

Hapa "ulimi" humaanisha kile ambacho mtu hutamka. Maana kamili inaweza kutajwa kwa uwazi kama hivi: "hakuna mtu hata mmoja awezaye kudhibiti ulimi wake pasipo msaada wa Mungu."

Muovu asiyedhibitiwa

Ulimi umezungumziwa kama vile ni uovu usioweza kudhibitiwa. Yakobo anafananisha na tamaa za mtu kuongea mambo maovu.

Umejaa sumu ya kufisha

Yakobo anafananisha uwezo wa mtu kuongea mabaya kama vile nyoka au mmea wenye sumu. Sumu ni maneno yaumizayo ambayo yanaweza kusemwa kwa mtu.

James 3:9

Kwa ulimi tuna.

"Tunatumia ndimi zetu kusema maneno ambayo."

Tunawalaani watu.

Kumuomba Mungu awaumize wengine

Ambao wameumbwa katika sura ya Mungu.

"Ambaye Mungu amemfanya katika sura yake."

Kutoka kinywa kilekile inatoka baraka na laana

Maneno yaliyobeba baraka na laana yanatoka katika kinywa cha mtu.

Ndugu zangu.

"Wakristo wenzangu"

Mambo haya hayapaswi kuwa hivyo.

"Hili ni kosa."

James 3:11

Usemi unaounganisha.

Baada ya kuweka mkazo kwamba maneno ya waumini hayatakiwi kuwa ya baraka na laana, Yakobo anatoa mifano ya kufundisha wasomaji wake kuwa watu wanamheshimu Mungu kwa kuishi katika njia sahihi.

Je, chemchemi moja hutoa maji matamu na machungu?

Yakobo anatumia swali lisilodai jibu kuwafundisha wasomaji kuhusu sanjari ya mpangilio wa maumbile. "Chemchemi moja haitoi maji matamu na machungu."

Ndugu.

"Waumini wezangu"

Je,mti wa mtini huzaa mizeituni, au mzabibu huzaa matunda ya mtini?

Yakobo anatumia neno la picha ya umbo kuwafundisha wasomaji kuhusu sanjari ya mpangilio wamaumbile. "Mtini hauwezi kuzaa mzeituni, wala mzabibu hauzai matunda ya mtini"

James 3:13

Nani miongoni mwenu ana hekima na ufahamu? Haya mtu huyo.

Yakobo anatumia swali hili kufundisha wasikilizaji wake kuhusu tabia ya unyofu. Maneno " hekima" na "ufahamu" ki-msingi yana maana ileile. "Mtu ambaye ana fikiri kuwa ana hekima sharti"

Onesha maisha mema.

"Onesha tabia njema" au "Ioneshe"

Kwa matendo yake katika unyenyekevu ambao unatoka katika hekima.

"Pamoja na matendo yake mema na unyenyekevu ambao hutokana na kuwa na hekima ya kweli."

Kuwa na wivu mkali na nia ya ubinafsi katika mioyo yenu.

Neno "moyo" hapa lina maana ya jaziba au fikra. "Hutapenda kushiriki jambo na wengine na daima unajiweka mwenyewe katika nafasi ya kwanza."

Usijiinue na kuwa kinyume na ukweli.

"Usiseme uongo na kujifanya kama una hekima."

James 3:15

Hii siyo

"Hii" inarejea katika wivu wa kijinga na nia za ubinafsi kama zilivyoelezwa katika mistari iliyipita.

Hekima ishukayo chini kutoka juu

Ubora wa hekima inayozungumziwa ni kana kwamba ni ile ambayo Mungu aliituma chini toka mbingune

Niya kidunia.

Neno "niya kidunia" humaanisha thamani na tabia za watu ambao hawamheshimu Mungu. "Kutomheshimu Mungu."

Ni ya kishetani.

"Bali ni kutoka kwa mapepo."

Kwa sababu mahali palipo na wivu na nia ya ubinafsi.

"Kwa sababu popote palipo na watu ambao hujihudumia wao binafsi bila kujali wengine."

Kuna ghasia.

"Kuna vurugu" au "kuna mtafaruku."

Kila tabia ya uovu.

"Kila aina ya tabia ya dhambi" au "kila aina ya tendo la uovu."

Kwanza ni safi.

"Kwanza ni takatifu."

Kisha yenye amani na upendo.

Inayopenda- "kisha ni yenye amani."

Yenye wema

Yenye moyo- "wema" au "yenye kujali."

Na tunda jema.

Tunda hili jema linalinganishwa na matendo mema. "matendo mema"

Kamilifu

"Yenye kuaminika" au "yenye ukweli."

Na tunda la haki limepandwa katika amani kwa wote watendao mambo ya amani.

Hii inalinganisha amani na haki katika maisha yetu kama kupanda na kuvuna mazao. "wale ambao huishi katika amani wanafafanya ambacho Mungu husema ni haki."

Si ya kiroho.

"Si ya kutoka kwa Roho Mtakatifu" au "si ya kiroho."

Juu

Hapa "juu" inamaanisha Mungu

James 4

Yakobo 04 Maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Uzinzi

Wandishi katika Bibilia huzungumzia mara nyingi uzinzi kama mfano kwa watu wanaosema wanampenda Mungu lakini wanatenda mambo Mungu huchukia. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#godly)

Sheria

Kuna uwezekano Yakobo analitumia neno hili katika Yakobo 4:11 kumaanisha "sheria ya kifalme" (Yakobo 2:8) na siyo sheria ya Musa(Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Maswali ya kana

Yakobo anauliza maswali mengi kwa sababu anataka wasomaji wake wafikirie jinsi wanavyoishi. Anataka kuwarekebisha na kuwafudisha. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Nyenyekevu

Kuna uwezekano neno hili hutumika kumaanisha watu wasiyo na majivuno. Yakobo analitumia neno hili kuashiria watu wasiyokuwa na majivuno na wanaoeza kumtumainia Yesu na kumtii.

<< | >>

James 4:1

Sentensi unganishi

Yakobo anawakemea waamini waliokosa unyenyekevu. Anawaonya kuwa makini na namna wanavyozungumza na watu wengine.

Maelezo ya jumla

Maneno "ninyi, wewe" imetumika kama wingi kuwaelezea waamini walioandikiwa na Yakobo.

ugovi unatoka wapi ... migogoro

Maneno "ugonvi, migogor" yanamaanisha kitu kimoja. Yakobo anayatumia kusisitiza kuwa nazungumzia juu ya mvutano kati ya watu.

ugonvi na migogoro

Ni tabia zinazotokea katika jamii

Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita

Yakobo anatumia swali kukemea hadhira yake. "ni kwa sababu mna tamaa mbaya" "kwa sababu mnatamani vitu vibaya"

Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita ndani ya washirika wenu?

Yakobo anazungumzia tamaa kama adui anayeleta vita kati ya waamini. kwa hali halisi ni watu ndio wenye tamaa hizi na kugombana wenyewe kwa wenyewe. "mnatamani maovu na mwishoni nmaumizana wenyewe kwa wenyewe"

Ndani ya washirika wenu

Yaweza kuwa na maana kuwa 1) kuna ugonvi kati ya waamini au 2) vita ambayo ni ugonvi upo ndani ya kila mwamini.

Mnauwa na mnafukuzia kile msichoweza kuwa nacho.

"mnauwa" inaelezea ni kwa kiasi gani watu wanaweza kufanya lolote baya ili wawezea kupata wanachokitaka. "Mnafanya uovu wa kila namna ili mpate msichoweza kukipata"

Mnapigana na kugombana

"kupigana na kugombana" zinamaanisha kitu kimoja. Yakobo anatumia kusisitiza namna ambavyo watu wanagombana wenyewe kwa wenyewe.

Mnaomba vibaya

Yaweza kuwa na maana kuwa 1) mnaomba mkiwa na nia mbaya au 2) mnaomba vitu ambavyo hampaswi kuomba au mnaomba vitu vibaya.

James 4:4

Enyi wazinzi

Yakobo anazungumza na waamini akiwafananisha na mke aliyelala na mwanaume mwingine ambaye sio mume wake. "ninyi sio waaminifu kwa Mungu"

Hamjui kwamba ... Mungu?

Yakobo alitumia hili swali kuifundisha hadhira yake. "Mnajua ... Mungu"

urafiki na ulimwengu

Maneno haya yanaelezea uhusiano uliopo kwenye mifumo ya duniani na tabia zake.

urafiki na ulimwengu

Hapa mfumo wa ulimwenguni unaelezewa kama vile ni mtu ambaye watu wengine wanaweza kuwa na urafiki naye.

urafiki na ulimwengu ni uadui dhidi ya Mungu

Kuwa rafiki na ulimwengu inamaanisha kuwa adui wa Mungu. "urafiki na dunia" inamaanisha watu ambao ni marafiki wa dunia na "uadui dhidi ya Mungu" inamaanisha watu ambao wanampinga Mungu. "Marafiki wa ulimwengu ni maadui wa Mungu"

Au mnadhani maandiko hayana maana

Yakobo anatumia swali kueleza kuwa "Kuna maana katika maandiko"

Roho aliyoweka ndani yetu

Tafisi nyingine zinaelezea "roho" kama Roho Mtakatifu. Na tafsiri zingine zinamaanisha roho ya binadamu ambayo kila mtu ameumbwa nayo. Tunapendekeza kuwa utumie maana nyingine ambayo ipo katika tafsiri zinazotumika na wasomaji wako.

James 4:6

Lakini Mungu hutoa neema zaidi

"Japokuwa nafsi zetu hutamani tusivyoweza kuvipata, Mungu atatupa zaidi neema, tukijinyenyekeza wenyewe"

Hutoa neema zaidi

Neema imezungumzwa kama kitu kinachoweza kutolewa.

Kiburi

"mtu mwenye kiburi"

nyenyekea

"mtu mnyenyekevu"

Hivyo

"Kwa sababu hii"

Jitoeni kwa Mungu

"mtii Mungu"

Mpingeni ibilisi

"mpingine ibilisi" au "Msifanye mambo ambayo ibilisi anawaambia mfanye"

atakimbia

"atakimbia mbali"

ninyi

Hii inamaanisha hadhira ya Yakobo.

James 4:8

Taarifa ya jumla.

Neno "ninyi" linamaanisha waamini waliotawanyika ambao Yakobo anawaandikia.

Sogeeni karibu na Mungu, na yeye atakaribia karibu nanyi

Hapa anamaanisha kuwa wakweli na wazi kwa Mungu.

Safisheni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na takaseni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

Hizi ni sentensi mbili zinazoendana.

Safisheni mikono yenu

Hii ni amri kwa watu kufanya mambo ya haki na sio maovu. "Ishini namna ambavyo inampendeza Mungu"

Takaseni mioyo yenu

"mioyo" inamaanisha mawazo ya mtu na hisia zake" Mheshimu Mungu kwa mawazo yako"

nia mbili

"Nia mbili" linamaanisha mtu ambaye hawezi kufanya maamuzi juu ya jambo fulani. "Mtu ambaye hawezi kuamua amtii Mungu au la"

Huzunika, omboleza, na Lia

Maneno haya matatu yana maana moja. Yakobo anayatumia kwa pamoja kuonesha kuwa watu watahuzunika sana kwa kutokumtii Mungu" Yakobo anasema haya kama amri.

Geuzeni kicheko chenu kuwa huzuni na furaha yenu kuwa maombolezo

Hapa kicheko kimezungumzwa kuwa kitageizwa kuwa huzuni na furaha kuwa maombolezo. "Acheni kucheka na mtubu kwa Mungu"

Nyeyekeeni wenyewe mbele za Bwana

"Jinyenyekezeni mbele za Mungu"

Atawainua juu

Yakobo anazungumza namna ambavyo Mungu anamuheshimu mtu mnyenyekevu na kumnyanyua toka chini. "atakuheshimu wewe"

James 4:11

Maelezo ya jumla

Maneno "wewe" au "ninyi" yametumika kuwaelezea waamini walioandikiwa na Yakobo.

Kunena kinyume

"kusema vibaya kuhusu" au "kupinga"

Ndugu

Yakobo anawazungumzia waamini kama ndugu waliozaliwa pamoja. "waamini wenzangu"

bali mnaihukumu

"bali mnafanya kama mtu anayetoa sheria"

Ni mmoja tu ambaye ni mtoa sheria na hakimu

Hapa anamaanisha Mungu. "Mungu ndiye atoaye sheria na ahukumuye"

Wewe ni nani ambaye unamhukumu jirani yako?

Yakobo anatumia swali hili kuikemea hadhira yake. "Ninyi ni binadamu na hamuwezi kuwahukumu binadamu wengine"

James 4:13

kukaa huko mwaka

Yakobo anazungumzia kutumia mda kama pesa. "kaeni huko mwaka mzima"

Ni nani ajuaye nini kitatokea kesho

Yakobo anatumia swali hili kuisahihisha hadhira yake. "Hakuna ajuaye kitakachotokea kesho"

maisha yenu ni nini hasa?

Yakobo alitumia swali hili kufundisha waamini kuwa maisha ya kimwili sio ya muhimu sana. "fikirini juu ya maisha yenu ya kimwili"

Kwa kuwa mnafanana kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi na kisha hupotea.

Yakobo anawafananisha watu na ukungu ambao hutokea na kupotea kwa haraka. "mnaishi kwa muda mfupi na kufa"

James 4:15

Badala yake mngesema

Badala yake, mtazamo wenu uwe?"

sisi tutaishi

Neno "sisi" halimaanishi Yakobo au hadhira yake lakini ni mfano wa namna ambavyo hadhira ya Yakobo inatakiwa iishi.

tutafanya hiki au kile.

"kufanya kile ambacho tumepanga kufanya"

kwake yeye ajuaye kutenda mema lakini hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

Yeyote anayeshindwa kufanya jambo ambalo anapaswa kufanya anatenda dhambi.

James 5

Yakobo 05 Maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Milele

Sura hii inatofautisha vitu vya dunia hii ambavyo havidumu na kuishi kwa ajili ya vitu vitakavyodumu milele. Ni vyema pia kuishi na matarajio kwamba Yesu atarudi karibuni. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#eternity)

Viapo

Wasomi wanatofautiana iwapo fungu hili linafundisha kwamba viapo vyote ni vibaya. Wasomi wengi wanakubaliana kwamba viapo vingine vinakubalika na badala yake Yakobo anawafundisha Wakristo kuwa na maadili.

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Eliya

Hadithi hii itakuwa ngumu kuelewa iwapo vitabu vya 1 Wafalme na 2 Wafalme na 1 Mambo ya Nyakati na 2 Mambo ya Nyakati havijatafsiriwa.

"Okoa roho yake kutoka kwa kifo"

Huenda hii inafundisha kwamba mtu anayeacha maisha yake ya dhambi hataadhibiwa na kifo cha mwili kama athari ya dhambi yake. Kwa upande mwingine, wasomi wamoja wanaamini kwamba hili fungu linafundisha kuhusu wokovu wa milele. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#death and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#save)

__<< | __

James 5:1

Sentensi unganishi

Yakobo anawaonya matajiri juu ya starehe na utajiri.

enyi mlio matajiri

Yaweza kuwa na maana ya 1) Yakobo anawapa onyo kali wale wanaoamini kwenye utajiri au 2) Yakobo anazungumza kuhusu watu wasioamini ambao ni matajiri. "enyi mlio matajiri na mnaosema mnamcha Mungu"

kwa sababu ya taabu inayokuja juu yenu

Yakobo anaelezea kuwa watu hao watateseka sana baadae na taabu yao inakuja. "kwa kuwa mtateseka sana baadae"

Utajiri wenu umeharibiwa na mavazi yenu yametafunwa na wadudu waharibifu. Dhahabu zenu na fedha zenu zimekosa thamani

imetafunwa. Dhahabu zenu na fedha zimekosa thamani. Yakobo anazungumza juu ya matukio haya kama vile yameshatokea. Yakobo anazungumzia utajiri wa duniani haudumu na hauna uzima wa milele. "Utajiri wenu umeharibiwa, nguo zenu zimetafuwa na dhahabu zenu na fedha zimekosa thamani"

utajiri ... nguo ... dhahabu

Hivi vitu vimetajwa kama mifano ya vitu vya thamani kwa mwanadamu.

uharibifu wake utashuhudia dhidi yenu

"uharibifu" ni neno linaloelezea namna ambavyo chuma yaweza haribika. Yakobo anazungumzia kuhusu uharibifu kwa kuwa umesababishwa na watu waovu na matendo yao. "Na Mungu akiwahukumu kuharibiwa kwa mali zenu kutakuwa kama mtu anayewahukumu mahakamani"

Itaangamiza ... kama moto

Uharibifu unazungumzwa kama vile moto ambao utakuja kuwaangamiza watu.

Miili yenu

"mwili" inamaanisha mwili mzima.

Moto

Moto inatumika kuwakumbusha watu kwamba mara nyingi inamaanisha hukumu ya Mungu itakayokuja juu ya waovu.

Katika siku ya mwisho.

Hii inaelezea wakati muafaka wa Mungu kuja kuhukumu ulimwengu. Waovu wanadhani wanahifadhi utajiri kwa ajili ya baadae lakini wanachokifanya wanahifadhi hukumu. "wakati ambao Mungu anataka kuwahukumu"

James 5:4

Sentensi unganishi

Yakobo anaendelea kuwaonya matajiri juu ya starehe na utajiri.

malipo ya watendakazi-wale ambao hamjawalipa kwa kuvuna katika mashamba yenu- wanalia

Pesa ambayo ilitakiwa ilipwe imeelezewa hapa kama mtu anayelalamika juu ya dhuluma aliyofanyiwa. "kwa kuwa hamwalipi mliowaajiri kufanya kazi kwenye mashamba yenu mnafanya makosa"

kilio cha wale waliovuna mazao yenu kimeyafikia masikio ya Bwana wa Majeshi.

Kilio cha wanaovuna kimesikika mbinguni. "Bwana wa majeshi amesikia kilio cha wavunaji"

kwenye masikio ya Bwana wa Majeshi

Mungu anazungumziwa kuwa ana masikio kama mwanadamu. "Bwana wa majeshi amesikia"

Mmejinenepesha mioyo yenu kwa siku ya machinjo

Hapa watu wanaelezewa kama wanyama, wanaolishwa vizuri ili wanenepe na kuchinjwa kwa ajili ya karamu. Japokuwa hamna atakayesherehekea siku ya hukumu. "Tamaa zeni zinawaandaa kwa hukumu ya milele"

mioyo yenu

"Mioyo" imezungumziwa kama kituo cha tamaa za mwanadamu. Neno hili linasimama kumuelezea mtu kwa ujumla.

Mmemhukumu ... mwenye haki

"Mmehukumu" inaweza isiwe na maana ya kisheria ya kupitisha hukumu ya kifo. Bali inawazungumzia watu waovu na wenye nguvu wanaoamua kuwanyanyasa masikini mpaka wanakufa.

mwenye haki

"Mtu anayefanya mambo yanayofaa" Hii sentensi inaelezea watu wenye haki kwa ujumla na sio mtu mmoja.

asiyeweza kuwapinga

"Asiye kinyume na ninyi"

James 5:7

Sentensi unganishi

Yakobo anabadilisha mada toka kwenye kuwakemea matajiri na kuwapa mawaidha waamini.

Maelezo ya jumla

Kwa kufunga Yakobo anawakumbusha waamini kuhusu ujio wa Bwana na kuwapa mafundisho mafupi namna ya kuishi kwa ajili ya Mungu.

Kwa hiyo vumilieni

"Kwa ajili ya hili kuweni na subira na uvumilivu"

mpaka ujio wa Bwana

Sentensi hii inaelezea ujio wa Yesu, atakapoanzisha ufalme wake duniani na kuhukumu watu wote. "Mpaka Kristo atakapokuja"

Mkulima

Katika mazungumzo haya Yakobo anatumia mkulima na mwamini kuelezea namna ya kuwa mvumilivu.

Kazeni mioyo yenu

Yakobo anawataka waamini wawe na mioyo thabiti na kuwa na msimamo. "Kuweni na msimamo" au "Ifanyeni imara mioyo yenu"

kuja kwake Bwana ni karibu.

"Bwana atarudi mapema"

James 5:9

Nsinung'unikiane, ndugu ... ninyi

Yakobo anawaandikia waamini wa Kiyahudi waliotawanyika.

ninyi kwa ninyi,

"kila mmoja na mwenzake"

Hamtahukumiwa

Hii yaweza kuwa "Kristo hatawahukumu ninyi"

hakimu anasimama mlangoni

Yakobo anamfananisha Yesu, kama hakimu kwa mwanadamu na kuelezea ni kuwa bado mda mfupi sana Yesu atarudi kuhukumu ulimwengu"

mateso na uvumilivu wa manabii

"ni kwa namna gani manabii walivumilia mateso na hukumu"

walionena katika jina la Bwana

"Waliongea kwa jina la Bwana kwa watu"

Tazama

"Tazama" inasisitiza "sikiliza kwa makini" au "kumbuka"

wale wanaovumilia

"Wale watakaoendelea kumtii Mungu hata katika hali ngumu"

James 5:12

Zaidi ya yote

"Hii ni muhimu" au "Hasa"

ndugu zangu

"waamini wenzangu"

msiape

"kuapa" ni kusema kuwa utafanya jambo au jambo fulani ni kweli na kuwa na wajibu kwa mamlaka za juu. "Msiape"

aidha kwa mbingu ama kwa nchi

Maneno "mbingu" na "nchi" linamaanisha mamlaka ya kiroho na kibinadamu zilizopo mbinguni na duniani.

"ndiyo" yenu na imaanishe "ndiyo" na "hapana" yenu na imaanishe "hapana

Fanya ulichosema utafanya bila kuapa"

msije kuangukia chini ya hukumu

Kuhukumiwa inazungumzwa kwa mtu aliyeanguka na kulemewa na kitu kizito. "Hivyo Mungu hatawahukumu"

James 5:13

Kuna yeyote miongoni mwenu ana mateso? Lazima aombe

"Kama kuna mtu yeyote anapata mateso yampasa kuomba"

Je, mtu yeyote ni mwenye kuchangamka? Na aimbe sifa

"Mtu yeyote akiwa na furaha, yampasa aimbe nyimbo za kusifu"

Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Na aite

"Mtu yeyote akiwa mgonjwa na aite watu"

maombi ya imani yatamponya mgonjwa, na Bwana atamwinua

Mwamini akimuombea mgonjwa, Mungu atasikia maombi yake na kumponya mtu huyo. "Mungu atasikia maombi ya mwamini aombapo kwa imbani na kumponya mgonjwa.

James 5:16

Maelezo ya Jumla

Kwa kuwa haw walikuwa waamini wa kiyahudi, Yakobo anawakumbusha watu kuomba kwa kukumbuka moja wa manabii na namna walivyoomba.

Kwa hiyo ungameni dhambi zenu

Hii ni kukubali makosa yako kwa waamini wengine ili uweze kusamehewa.

ninyi kwa ninyi,

"kila mmoja na mwenzake"

ili muweze kuponywa

"Ili Mungu awaponye"

Maombi ya mwenye haki huzaa matokeo makubwa

Maombi ni kitu chenye nguvu sana. "Mtu anayemcha Mungu akiomba, Mungu anafanya mambo makuu"

Juhudi

"shauku"

Tatu ... sita

"3 ... 6"

mbingu zilimwaga mvua

Mbingu inamaanisha mawingu ambayo inaelezwa kama chanzo cha mvua. "Mvua ilishuka toka mawinguni"

nchi ikatoa mavuno.

Hapa nchi inaelezwa kama chanzo cha mavuno

Matunda

"Matunda" inamaanisha mazao ya mkulima

James 5:19

Ndugu zangu

"Waamini wenzangu"

kama yeyote miongoni mwenu anapotoka kutoka kwenye ukweli, lakini mtu mwingine akamrejesha

Mwamini ambaye anaacha kumwamini Mungu na kumtii yeye anafananishwa na kondoo aliyeondoka kwenye kundi. Mtu anayemrejesha ili amwamini Mungu tena anafananishwa na mchungaji anayetafuta kondoo aliyepotea. "Mtu yeyote akiacha kumtii Mungu na mwingine akamsaidia kuanza kumtii Mungu tena"

yeyote amwongozaye mwenye dhambi kuondoka katika njia yake ya ukosaji... atafunika wingi wa dhambi.

Yakobo anamaanisha kuwa Mungu atatumia matendo ya huyu mtu ya kumrejesha aliyekosa ili atubu na kuokolewa. Lakini Yakobo anaongea kama vile huyu mtu mwingine ndo ameokoa nafsi ya mwenye dhambi toka kwenye kifo.

ataponya nafsi yake kutoka katika mauti na atafunika wingi wa dhambi.

Hapa "kifo" inamaanisha kufa kiroho, kutengana na Mungu. "Atamuokoa na kifo cha kiroho na Mungu atamsamehe mkosaji dhambi zake zote"

atafunika wingi wa dhambi.

Yawza kumaanisha kuwa 1) Mtu atakayemrejesha ndugu aliyetenda uovu, dhambi zake zitasamehewa. au 2) Ndugu aliyetenda uovu akirudi kwa Bwana , dhambi zake zitasamehewa. Dhambi inazungumzwa kama jambo ambalo Mungu atawasamehe watu wake.