Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa 2 Petero

Sehemu ya 1: Maelezo kwa jumla

Muhtasari wa kitabu cha 2 Petero

  1. Utangulizi (1:1-2)
  2. Kukumbusha kuishi maisha mema kwa sababu Mungu ametuwezesha (1:3-21)
  3. Onyo kuhusu walimu wa uongo (2:1-22)
  4. Kutia moyo kujiandaa kwa ujio wa pili wa Yesu (3:1-17)

Nani aliandika kitabu cha 2 Petero?

Mwandishi anajitambulisha kama Simoni Petero. Petero alikuwa mtume. Pia aliandika 1 Petero. Kuna uwezekano Petero aliandika barua hii akiwa gerezani Roma muda mfupi kabla ya kifo chake. Petero aliita barua hii kama barua ya pili na kwa sababu hiyo tunaiorodhesha baada ya 1 Petero. Aliandikia barua hii kwa hadhira moja ya barua yake ya kwanza. Kuna uwezekano hadhira hii ilikuwa ni Wakristo waliotawanyika katika inchi za Asia Ndogo.

Kitabu cha 2 Petero kinahusu nini?

Petero aliandika barua hii kuwapa moyo waumini waishi maisha mema. Aliwaonya kuhusu walimu waongo waliosema Yesu alikuwa anachukua muda mrefu kurudi. Aliwaambia Yesu hakuchelewa kurudi ila ni Mungu alikuwa anawapatia watu muda wa kutubu ili waokolewe.

Kichwa cha kitabu hiki kinastahili kutafsiriwa namna gani?

Watafsiri wanaweza kukiita kitabu hiki kutumia jina lake la kitamaduni, "2 Petero" ama "Petero wa Pili" ama wanawezatumia kichwa kinachoeleweka zaidi kama, "Barua ya Pili kutoka kwa Petero" ama "Barua ya pili aliyoandika Petero" (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Ni watu gani Petero aliwakemea?

Labda watu Petero aliwakemea ni watu waliojulikana kwa jina la Wagnostiki. Walimu hawa waliharibu mafundisho ya maandiko matakatifu kwa manufaa yao wenyewe. Waliishi maisha maovu na wakafundisha watu kuishi hivyo .

Nini maana ya kwamba Mungu aliongoza maandiko?

Mafundisho ya Maandiko ni muhimu sana. 2 Petero inawasaidia wasomaji kuelewa kwamba ingawa kila mwandishi wa maandiko ana njia yake ya kipekee ya kuandika, Mungu ndiye mwandishi wa kipekee wa maandiko. (1:20-12)

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Umoja na wingi wa "Wewe" na "Nyinyi"

Katika kitabu hiki, neno "mimi" linaashiria Petero. Pia neno "Nyinyi" linaashiria hadhira ya Petero. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-exclusive and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-you)

Ni maswala gani muhimu katika maandiko ya kitabu cha 2 Petero?

Katika mistari ifuatayo, matoleo ya kisasa ya Bibilia yanatofautiana na matoleo ya kale. Toleo la ULB lina masomo ya kisasa na linaweka masomo ya zamani kama maelezo ya chini. Kama tafsiri ya Bibilia iko katika eneo kwa ujumla, watafsiri wanapaswa kuzingatia masomo ya matoleo hayo. Kama si hivyo, wanapaswa kufuata masomo ya kisasa.

  • "Kuwekwa katika minyororo ya giza la chini hadi hukumu" (2:4) Matoleo mengine ya kisasa na ya zamani yana, "Kuwekwa katika mashimo ya giza la chini mpaka hukumu".
  • "Wanafurahia matendo ya uongo wakati wakiwa katika karamu na nyinyi" (2:13) Matoleo mengine yana, "Wanafurahia matendo yao wakati wanasherehekea nanyi katika karamu za upendo."
  • "Beori"(2:15) matoleo mengine yanasoma, "Bosori".
  • "Vitu vya asili vitachomwa kwa moto na ardhi na matendo yao yatatambulishwa" (3;10). Matoleo mengine yana, "Vitu vya asili vitachomwa kwa moto na ardhi na matendo yaliyomo vitachomeka."

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

2 Peter 1

2 Petero 01 Maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Kumjua Mungu

Kumjua Mungu inamaanisha kumilikiwa naye ama kuwa na uhusiano naye. Hapa "ujuzi" ni zaidi ya kumjua Mungu na akili. Ni ujuzu unaomfanya Mungu kumuokoa mtu na kumpa neema na amani. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#know)

Kuishi maisha ya ya kumcha Mungu

Petero anafundisha kwamba Mungu amewapa waumini yote wanayohitaji kuishi maisha ya kumcha Mungu. Kwa hivyo waumini wafanye kila waezalo kumtii Mungu zaidi. Waumini wakiendelea kufanya hivyo watakuwa imara na wenye manufaa kupitia uhusiano wao na Yesu. Lakini waumini wasipoendelea kuishi maisha ya kumcha Mungu, watakuwa ni kama wamesahau walichofanyiwa na Mungu kupitia kwa Kristo kuwaokoa. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#godly and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#save)

Maswala mengine ya utata ya kutafsiri katika sura hii

Ukweli wa Maandiko

Petero anafundisha kwamba unabii wa maandiko haukutolewa na binadamu. Roho Mtakatifu alifunua ujumbe wa Mungu kwa watu waliouandika kwa kitabu. Petero pia na Mitume wengine hawakubuni hadithi walizowapa watu kuhusu Yesu. Walishuhudia chenye Yesu alifanya na wakamsikia Mungu akimwita Yesu mwanawe.

| >>

2 Peter 1:1

Simon Petro

"Kutoka Kwa Simoni Petro." Lugha Yako inaweza kuwa na namna fulani ya kumtambulisha mwandishi wa barua. Mimi Simon Petro niliandika barua hii.

Mtumwa na Mtume waYesu Kristo

Petro anaongelea mtazamo wake wa kuwa mtumwa wa Yesu Kristo. Pia alipewa nafasi na mamlaka ya kuwa mtume wa Kristo

Kwa wale

Petro anaonekana kuwaandikia waumini wote watakaosoma waraka huu. Kwenu waumini.

Tumepokea

Sisi mitume tumepokea

Neema iwe kwenu

Neno "ninyi" linamaanisha waumini wote kwa ujumla

Yesu Bwana wetu

Yesu Bwana wa waumin na Mitume

Neema na iwe kwenu;amani iongezeke kupitia maarifa ya Mungu na Yesu Bwana wetu.

Upole wenu na amani uongezeka kwa sababu mnamjua Mungu na Yesu Bwana wetu.

2 Peter 1:3

Aliyetuita

Kwanza Mungu alitufikia. "Sisi" Neno hili linamanisha Petrop pamoja na wasikilizaji wake.

Kwa ajili ya uzuri wa utukufu wake

"kwa njia ya heshima yake na uzuri wa maarifa"

Kwa njia hii alitutumainishi ahadi kuu za thamani

"Ahadi za thamani za Mungu zilikuja njia ya heshima na uzuri wa maarifa"

asili ya Mungu

"tabia ya ukamilifu wa Mungu"

kwa kadiri tunavyoendelea kuachc uovu wa dunia

kadiri unavyoendelea kuziacha tamaa mbaya za dunia."

2 Peter 1:5

Kwa sababu hii

Kwa sababu ya kile ambacho Mungu amefanya

maarifa

"uzuri wa maarifa"

Kwa sababu ya uzuri maarifa

kwa kutumia uzuri wa maarifa uongeze ufahamu

kupata upendo wa ndugu

kuwa wapole kwa sisi kwa sisi

2 Peter 1:8

mambo haya

haya mambo ni:- imani, uzuri, maarifa, kiasi, uvumilivu, utauw, upendo wa ndugu, na upendo.

"Ninyi hamtakuwa tasa au msiozaa matunda"

mtazaa matunda

yeyote asiyekuwa na mambo haya

mtu yeyote asiyekuwa na mambo haya

huyaona mabo ya karibu tu, yeye ni kipofu

usemi huu unamfananisha mtu anayefikiria mambo ya duniani tu kuwa yako vizuri mbele yake, kama mtu asiye na macho.

2 Peter 1:10

kwa hiyo

Neno "kwa hiyo" linaanzisha mwitikio wa waumini kwa kile kilichosemwa mapema.

kujihakikishia uteule na wito kwa ajili yenu

Neno " wito" linamaanisha mwaliko wa ujula waMungu kwa watu wote. Neno "uteule" linamaanisha watu maalumu ambao Mungu amewchagua. Maneno haya mawili yana maana sawa.

hamtajikwaa

hamtashindwa kiroho na katika tabia njema

2 Peter 1:12

Kwa hiyo

Mwandishi anataka kutengeneza maelezo ambayo yanatokana na kile alichoandiaka mwanzoni.

Nitakuwa tayari kuwakumbusha mambo haya

Petro anaonyesha kuwa ataendelea kuwakumbusha waumini jinsi ya kumfuata Kristo

juu ya mabo haya

jinsi waumini inavyowapasa kukua katika imani

kuwaamsha

huu ni ufafanuzi unaomaanisha "kuwaandaa ili wawe tayari"

nimo katika hema hii

Haya maelezo yanaytumika badala ya "kwa sababu bado ninaishi"

Nitajitahidi kwa bidii kwa ajili yenu ili mkumbuke mambo haya

"Ntatumia juhudi zangu kuwafundish mambo haya ili muyakumbuke"

Nitaiondoa hema yangu

huu nu ufafanuzi wa "Nitakufa"

Baada yakuondoka Kwangu

Maelezo haya yanaonyesha "baada ya kufa kwangu"

2 Peter 1:16

Pale sauti iliposikika toka katika utukufu mkuu

Petro anamaanisha yeye mwenyewe na yule mwanafunzi mwingine, Yakobo, na Yohana waliposikia ile sauti ya Mungu.

Kwa kuwa sisi hatukufuata hadithi zilizoingizwa kwa ustadi

Kwa kuwa sisis mitume hatukufuata hadtibzilizotengenezwa kwa ustadi

Yetu

waumini wote ikijumuisha sisi mitume

Pale tulipokuwa naye kwenye ule mlima matakatifu

Petro anamaanisha wakati ule Yesu alipobadilika sura yake ikang'aa mbele ya Petro, Yakobo na John (Tazama Mathayo)

2 Peter 1:19

Tunalo hili neno la unabii lililothibitika

Perto anamaanisha wale Mitume. Mitume wnaujumbe kutoka kwa malaika ambao wanajua kuwa ndiyo ukweli kutoka kwa Mungu

Ambalo kwalo mwafanya vyema kulitekeleza

Petro anawaelekeza waumini kuwa na utayari kwa jumbe za kinabii

Ni kama taa ing'aayo gizani mpaka kunapokucha

Ujumbe wa kinabii umelinganishwa na taa inayotoa Mwanga gizani mpaka mwanga unapowadia asubuhi.

Na nyota za mawio zionekanapo katika mioyo yenu

Nyota ya asubuhi ni Kristo anayekuja kuishi kwenye mioyo yetu.

isipokuwa wanadamu waliwezeshwa na Roho mtakatifu aliyeongea toka kwa Mungu

Roho mtakatifu aliwaongoza watu hawa, kwa hiyo waliongea ambacho Mungu alitaka waongee.

2 Peter 2

2 Peter 02 Maelezo kwa ujumla

Dhana muhimu katika sura hii

Nyama

"Nyama" ni mfano ya asili ya dhambi ya mtu. Siyo sehemu ya kimwili ya binadamu iliyo na dhambi. "Nyama" inawakilisha asili ya binadamu inayokataa vitu vyote vya uungu na kutamani vitu vya kidhambi. Hii ndiyo hali ya binadamu wote kabla ya kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia ya kumwamini Yesu Krsito. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#flesh)

Mafundisho fiche

Kuna ulinganifu katika 2:4-8 ambao ni mgumu kuelewa iwapo Agano la kale halijatafsiriwa. Maelezo zaidi ni muhimu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

<< | >>

2 Peter 2:1

Manabi wa uongo walikuja kwa Israeil, na walimu a uongo watakuja kwenu

Kama ile manabii wa uongo walivyokuja wakiidanganya Isreli, vivyo hivyo walimu wa uongo watakuja wakidanganya uongo juu ya Kristo

Ukengeufu

Haya ni maoni yaliyo kinyume na mafunisho ya Kristo na ya Mitume

Bwana aliyewanunua

Yesu ndiye Bwana aliyelipa kwa ajili ya dhambi za watu wote kwa njia ya kifo chake, na kuzikwa kwake na ufufuo.

nja za aibu

Neno "zao" linawakilisha manabii na walimu wa uongo" jinsi matendo yao yalivyo ya zinaa iliyokidhiri.

2 Peter 2:4

Maana Mungu hakuwaacha malaika waliokengeuka

Hii inaanzisha Mpangilio wa sentensi zinazoanza na "kama"

bali aliwatupa kuzimu ("Tartarus)

"Tartarus

ili wafungwe minyororo mpaka hukumu itakapowajilia

Mungu atawaweka katika gereza wakisubiri hukumu ya mwisho

Wala Mungu hakuuvumilia ulimwengu wa zamani...wakati alipoachilia gharika juu yaulimwengu ulioasi

Mungu aliuhribu ulimwengu wa zamani na watu waasi kwa gharika

Mungu aliihukumu miji ya Sodoma na Gomorra kiasi cha kuwa majivu

Mungu alitumia moto kuwaharibu watu wasi mcha Yeye katika miji ya Sodoma na Gomora

bali alimhifadhi Nuhu

Mungu alimwokoa mtu wa haki Nuhu katika gharika

ili iwe mfano kwa ajili ya watu waovu katika siku za usoni

kama vile Sodoma na Gomora ilivyoharibiwa kwa moto katika siku za usoni Mungu atawaharibu katika ziwa la moto.

2 Peter 2:7

alimwokoa Ltu mtu wa haki

Mungu alimwokoa Lutu aliyeishi maisha ya tabia njema

akitesa nafsi yake kwa ajili ya yale alyosikia na kuyaona

Lutu aliendelea kuteseka na kuhrasiwa na tabia za anasa za wenyeji wa Sodoma na Gomora

tabia chafu za wsiofuata sheria

"anasa na tabia inayoharibika ya watu waliovunja sheria ya Mungu"

mtu wa haki

Hii inamaanisha Lutu mtu wa haki

watu wa Mungu

"watu wanaomtii Mungu"

alikuwa akitesa roho yake

Aliusumbua utu wake wa ndani

jinsi ya kuwavumilia waovu kwa ajil ya hukumu skatika siku ya mwisho

Watu wasio haki hawataiepuka hukumu ya Mungu. Watakapokufa watakataliwa mpaka siku ya hukumu

2 Peter 2:10

kwa hakika huu ndio ukweli

Neno "huu" linamaanisha Mungu kuwalinda watu wasio haki gerezani mpaka siku ya hukumu.

wale wanaoendelea kuishi katika tamaa za mwili huu na kuyadharau mamlaka

Watu wasio haki wanaoendela kuishi katika tamaa ya mwilii na kuwachukia viongozi wao au watawala wao.

mwili

Neno "mwili" linamaanisha ubinadamu katika dhambi ya asili ya mwanadamu

wana ujasiri katika dhamiri zao

Neno "dhamiri" linamaanisha wale wanaoendelea katika uharibifu wa tamaa katika dhambi zao za asili na hawaheshimu malaika na mamlaka ya kiroho

Hwaogopi kuwakufuru watukufu

Wasio haki hawaogopi kuwachokoza na kuwanenea maovu malaika

malaika wana uwezo na nguvu kuliko wanadamu

Malaika wana nguvu za mwili na wa mamalka kuliko wanadamu

Lakini hawawezi kuleta hukumu dhidi yao kwa Bwana

"lakini malaika hawaleti humu iumizayo dhidi ya hawa watu kwa Bwana"

2 Peter 2:12

hawa wanyama wasio na akili

Kama vile wanyama wasivyoweza kueleza kwa mantiki, vivyo hivyo hawa watu hawaezi kuwa na mantiki, "Hawa walimu wa uongo wako kama wanyama wasio na akili"

Hawajui wanachotukana

Huongea uovu ambao hawaujui

wataangamizwa

Mungu atwaangamiza watu hawa

Wataumizwa kwa ujira wa maovu yao

"Wanachofikiri kuwa ni kizuri kwao, kiuhalisia ni kibaya kwao"

Wamejaa uovu na uchafu

Neno "uchafu" na "uovu" vinamaanisha maana moja. Waalimu wa uongo hufedhehesha na kutahayarisha amabavyo ni sawa na uchafu na uovu ambavyo mtu hawezi kviondoa

hufurahia udanganyifu wanaposherehekea na wewe

huendele katika furaha ya kuwadanganya watu wasio hatia na katika macho yao hawaonyeshi hatia

macho yao yamefunikwa na uzinzi, hwatosheki kutenda dhambi

"wanatamani kila mwanmke wanayemuona na kamwe hawatosheki"

wana mioyo iliyofunzwa kujaa tamaa

" inawakirisha mtu kama kamili, alifunzwa katika mawazo na na mattendo ya uchoyo. wanatamani utajiri na miliki isiyo haki.

2 Peter 2:15

Wameiacha njia ya kweli, wamepotoka na wamefuata...

"walimu wa uongo .wameiacha...wamepotoka..wamefuata". Walimu wa uongo wamekataa kumtii Mungu kwa kukataa kilicho sahihi

aliyependa kupata malipo yasiyo haki

alipokokea malipo ya anasa na yenye matendo ya dhambi

Lakini alikemwa kwa ajili ya ukosaji wake

alionywa vikali kwa kutokutii kwake

alizuia wazimuwa nabii

Mungu alitumia punda kuzuia upumbavu wa nabii

2 Peter 2:17

Watu hawa ni kama chemichemi zisizo na maji

Kama vile chemichemi zilizokauka na hazitoi maji kwa ajili ya maisha ya kawaida, vivyo hivyo mafundisho yao hayawaongozi watu katka maisha ya kiroho. Ni eneo la uongo kuwafariji waatu, kisima kikavu

Ni kama mawingu yanayotoweshwa na upepo

Mawingi mengine hubeba mvua. Mvua hii huleta maji yanayokuza au maji yagharikishayo. Hawa watu ni kama hayo mawingu yanayobeba uharibifu.

Huongea kwa majivuno matupu

Hotuba zao ni za kujivuna zisizo na maana.

Huangusha watu kwa tamaa ya mwili

Wanawavuta watu ili waingie katika dhambi ya mwili na matendo ya anasa.

Huwaahidi watu uhuru wakati waowenyewe ni watumwa wa dhambi ya ufisadi.

Huahidi uhuru wa uongo, uhuru unaowapeleka watu kutendda dhambi. huu ni utumwa wa dhambi.

Maana mwanadamu hufanywa kuwa mtumwa kile kinachmtawala

Mwanadamu hufanya kwa tamaa mabo yale anayopungukiwa kiasi

Huwalaghai watu wanaojaribu kuwakimbia wale waishio katika ukosji

Hujaribu kuwaangamiza watu ambao ni wapya katika imani.

2 Peter 2:20

Yeyote ajiepushaye na uchafu wa ulmwengu kwa kutumia maarifa ya Bwana na mwokozi Yesu Kristo

Mtu yeyote ambaye amempokea Bwana na Mwokozi Yesu Kristo na kugeuka kutoka kwenye uchafu na maisha yasyo matakatifu.

Hali yake huwa mbaya kuliko ile ya mwanzo

Ni wabaya zaidi kwa sababu wana maarif ya maisha matakatifu na wamechagua kurudi kwenye maisha ya dhambi

kama wasingeifahamu njia ya haki

Maisha ya yanayompendza Mungu.

amri takatifu walizopewa

Sheria za Mungu na amri za Mungu ambazo wamepewa wangejua namna ya kuishi kwa ajili ya Mungu

Mithali hii...mbwa huyarudia matapishi yake, Na nguruwe aliyeoshwa hurudi tena kwenye matope."

Ni usemi wa busara unaowalinganisha wale wanaoijua kweli lakini wanrudia maisha ya uasi. "Mbwa huyarudia matapishi yake" imenukuliwa toka Mithali 26:11. Katika namna yeyote maana yake inabaki kuwa "mnyama hawezi kufundishika ili asijnajisi mwenyewe"

2 Peter 3

2 Petero 03 Maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Moto

Watu hutumia moto mara nyingi kuharibu vitu ama kukifanya kitu kiwe safi kwa kuondoa uchafu na vitu visivyofaa. Kwa hivyo Mungu anapowadhibu waovu ama kuwatakaza watu wake, huwa inalinganishwa na moto. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#fire)

Siku ya Bwana

Wakati kamili wa kurudi kwa Bwana itakuwa mshangao kwa wengi. Hii ndiyo maana ya tashbihi "kama mwizi wa usiku". Kwa sababu ya haya Wakristo wanafaa wajiandae kwa ajili ya kurudi kwake Bwana. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#dayofthelord and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-simile)

__<< | __

2 Peter 3:1

Maelezo ya ujumla

Petro anaanza kuzungumza kuhusu siku za mwisho

kukuamsha katika akili

Petro anasema kwa kusababisha wasomaji wake kufikiri kuhusu mambo haya kama alikuwa anawaamsha kutoka kwenye usingizi. "kuwasababisha kufikiri kwa mawazo safi"

maneno yaliyosemwa kabla na manabii watakatifu

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "maneno ambayo manabii watakatifu walisema wakati uliopita"

amri ya Bwana wetu na mwokozi kwa kutumia mitume

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "amri ya Bwana wetu na Mwokozi, ambayo mitume wenu waliwapa"

2 Peter 3:3

Ujue ili kwanza

"Ujue hili kama jambo la muhimu sana."

wakienenda saswasa na matakwa yao

Hapa neno "matakwa" urejea kwa tamaa mbaya ambazo ziko kinyume na mapenzi ya Mungu. "kuishi sawasawa na tamaa zao mbaya"

kuendelea

kitendo, tenda

Iko wapi ahadi ya kurudi kwake?

Wabishi wanauuliza swali la utupu kusisitiza kuwa hawaamini kuwa Yesu atarudi. Neno "ahadi" urejea kwa kutimizwa kwa ahadi kuwa Yesu atarudi. "Ahadi ya kuwa Yesu atarudi sio kweli! Hatarudi!

Baba zetu walikufa

Hapa "Baba" urejea kwa mababu walioishi zamani. "Walikufa" ni lugha ikimaanisha walikufa.

vitu vyote vilikuwa hivyo tangu mwanzo wa uumbaji.

Wabishi wanajadili kwamba hakuna chochote katika ulimwengu kimeweza kubadilika, haiwezi kuwa kweli kwa Yesu kurudi.

tangu mwanzo wa uumbaji.

Hii inaweza kutofasiriwa kama kikundi cha maneno ya kitenzi. "Kwani Mungu aliumba ulimwengu"

2 Peter 3:5

mbingu na nchi vilianza... zamani, kwa amri ya Mungu

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu alianzisha mbingu na nchi... zamani kwa neno lake"

vilianza kutokana na maji na kupitia maji

Hii inamaanisha kuwa Mungu alisababisha ardhi kutoka kwenye maji, kukusanya maji kwa pamoja kufanya ardhi ionekane.

kupitia neno lake

Hapa "neno lake" urejea kwa neno la Mungu na maji

ulimwengu kwa kipindi hicho, ikiwa imejaa maji, iliharibiwa

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu aliujaza ulimwengu na maji kwa kipindi hicho na kuuharibu"

mbingu na dunia zimetunzwa kwa neno hilo hilo kwa ajili ya moto.

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu kwa neno lile lile, ametunza mbingu na nchi kwa ajili ya moto."

kwa neno hilo hilo

Hapa "neno" usimama kwa Mungu, atakaye toa neno.

Vimehifadhiwa kwa ajili ya siku ya hukumu

Hii kusemwa katika kauli tendaji na kuanza sentensi mpya. "Anawatunza kwa ajili ya siku ya hukumu"

kwa ajili ya siku ya hukumu na maangamizi ya watu wasio wa Mungu

Hii inaweza kusemwa pamoja na maneno ya kitenzi. "kwa siku wakati anapohukumu na kuharibu watu wasio wa Mungu"

2 Peter 3:8

Hii haiwezi kuchenga ujumbe wako

"Hauwezi kushindwa kuelewa hili" au "Usipuuze hii"

kwamba siku moja kwa Bwana ni kama miaka elfu moja

"kwamba kutoka kwa mtazamo wa Bwana, siku moja nia kama miaka elfu moja"

Si kwamba Bwana anafanya pole pole kutimiza ahadi

"Bwana si kwamba anafanya pole pole kutimiza ahadi zake"

kama inavyofikiriwa kuwa

Baadhi ya watu wanafikiri kuwa Bwana si kwamba anafanya pole pole kutimiza ahadi zake kwa sababu mtazamo kuhusu wakati ni tofauti na Mungu.

2 Peter 3:10

hata hivyo

Ijapokuwa Bwana ni mvumilivu na anataka watu watubu, hakika atarudi na kuleta hukumu.

siku ya Bwana itakuja kama mwizi

Petro anazungumza juu ya siku ambayo Mungu atamhukumu kila mmoja kama mwizi anayekuja pasipo kutegemewa na kuwashtusha watu.

Mbingu itapita kwa kupaza kelele

"Mbingu zitapita"

Vitu vitateketezwa kwa moto

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu atateketeza kwa moto"

Vitu

Maana zinazowekana ni 1) vitu vya mbinguni kama vile jua, mwezi, na nyota au 2) vinavyofanya mbingu na nch, kama vile mchanga, hewa, moto na maji.

nchi na matendo yatafunuliwa

Mungu ataiona dunia yote na matendo yote ya kila mmoja, na atahukumu kila kitu. Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu ataiweka wazi nchi na kila kitu watu walichofanya."

2 Peter 3:11

Sentensi unganishi

Petro anaanza kwa kuwaambia wakristo namna watakavyo ishi wakati wanasubiri siku ya Bwana.

Kwa kuwa vitu vyote vitateketezwa kwa njii hii.

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Tangu Mungu atahukumu mambo haya yote katika njia hii"

je utakuwa mtu wa aina gani?

Petro anatumia swali la kejeli kusisitiza kile atakachosema badae, kwamba "wanapaswa kuishi maisha ya utakatifu na utaua" "unajua ni aina gani ya watu wanapaswa kuwa"

mbingu itateketezwa kwa moto, na vitu vitayeyushwa katika joto kali

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu ataangamiza mbingu kwa moto, na ataviyeyusha

sehemu ambayo watakatifu wataishi

Petro anazungumza juu ya "utakatifu" kama ilivyokuwa kwa mtu. HIki ni kirai cha watu anaishi au sehemu ya watu watakao ishi kwa utakatifu.

2 Peter 3:14

jitahidi kuwa makini na kutolaumika na kuwa na amani pamoja naye

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "jitahidi kuishi katika njia ili kwamba Mungu asikute doa na kulaumiwa na kuwa na amani na yeye na kila mmoja"

doa na kutolaumiwa

Maneno "doa" na "kutolaumiwa" kimsingi umaanisha kitu kile kile na kusisitiza maadili ya usafi."usafi kamili"

doa

Hii usimama kwa ajili ya "kosa"

zingatia uvumilivu wa Bwana wetu katika wokovu

Kwa sababu Bwana ni mvumilivu, siku ya hukumu bado haijatokea. Hii uwapa watu fursa ya kutubu na kuokolewa, kama alivyo elezea katika 3:8. "Pia, nafikiri kuhusu uvumilivu wa Bwana wetu kama kukupa fursa ya kutubu na kuokolewa"

kutokana na hekima ambayo alipewa.

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "kutokana na hekina ambayo Mungu alimpa"

Paulo anaongelea hayo yote katika barua zake,

"Paulo anaongelea katika barua zake uvumilivu wa Mungu kuwaongoza katika wokovu"

kuna vitu ambavyo ni vigumu kuvielewa.

Kuna vitu katika barua za Paulo ambavyo ni vigumu kuvielewa.

Watu wasio na adabu na uimara wameviharibu vitu hivyo

watu wajinga na wasio na uimara hutofasiri vibaya vitu katika barua za Paulo kwamba ni ngumu kuelewa.

Wajinga na uimara

"Wasio wa kawaida na legarega" Hawa watu hawajafundishwa namba ya kutofasiri maandiko na hawajafanywa imara katika ukweli wa injili.

Kuelekea maangamizi yao.

"matokea yake ni maangamizi yao"

2 Peter 3:17

Sentensi unganishi

Petro anamalizia kuwaelekeza wakristo na kumalizia barua yake.

Hivyo, wapendwa kwa kuwa mnayafahamu hayo.

"Hayo" urejea kwa ukweli kuhusu uvumilivu wa Mungu na mafundisho ya walimu wa uongo.

jilindeni wenyewe

"jilindeni wenyewe"

ili kwamba msipotoshwe na udanganyifu wa walaghai

Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "ili kwamba walaghai wasiwapotoshe kwa maneno yao ya udaganyifu

msipotoshwe...udanganyifu

Kushawishiwa kuto mtii Mungu kunaongelewa kama kuondolewa katika njia sahihi ya kufuata. Udanganyifu na mafundisho ya uongo yanaongelewa kama watu wanaoweza kumoongoza mtu nje ya njia sahihi.

kupoteza uaminifu wako

Uaminifu unaongelewa kama kitu cha kumiliki ambacho wakristo wanaweza kukipoteza. "wewe acha kuwa mwaminifu"

mkue katika neema na ufahamu

"kuongozeka katika neema na ufahamu"

neema na ufahamu wa Bwana na mwokozi Yesu Kristo

Unaweza kutofasiri "neema" na 'ufahamu" kutumia maneno kitenzi. Ona utakavyo tofasiri maneno hayo hayo katika 1:1 na 1:8 na 2:20. "kuwa na uzoefu zaid na zaid na Bwana na Mwokozi Yesu Kristo kukutenda wema wewe, na kwamba unapata kumjua yeye vizuri na vizuri"