Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa Yuda

Sehemu ya 1 Maelezo ya Jumla

Muhtasari wa kitabu cha Yuda

  1. Utangulizi (1:1-2)
  2. Onyo kuhusu walimu wa uongo (1:3-4)
  3. Mifano ya Agano la Kale(1:5-16)
  4. Jibu linalostahili (1:17-23)
  5. Utukufu kwa Mungu (1:24-25)

Nani aliandika kitabu cha Yuda?

Mwandishi anajitambulisha kama Yuda nduguye Yakobo. Yuda na Yakobo walikuwa ndugu wa kambo wa Yesu Kristo. Haijulikani iwapo barua hii ilipaswa kuwa ya kanisa fulani.

Kitabu cha Yuda kinahusu nini?

Yuda aliaandika barua hii kuwaonya waumini kuhusu walimu wa uongo.Yuda alinukuu mara nyingi kutoka Agano la Kale. Hii inaweza ashiria kwamba Yuda aliandikia hadhira ya Wakristo wa Kiyahudi. Barua hii na 2 Petero zina ujumbe wenye kufanana. Barua zote zinazungumzia malaika, Sodoma na Gomorah na walimu wa uongo.

Kichwa cha kitabu hiki kitafsiriwe namna gani?

Watafsiri wanaweza kuchagua kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha kitamaduni, "Yuda." ama wanaweza chagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama "Barua kutoka kwa Yuda" ama "Barua aliyoandika Yuda." (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni.

Ni watu gani Yuda aliwakemea?

Kuna uwezekano Yuda aliwakemea watu watajulikana kwa jina Wagnostiki. Walimu hawa waliharibu mafundisho ya maandiko matakatifu kwa manufaa yao wenyewe. Waliishi maisha maovu na wakafundisha watu kuishi hivyo .

Jude 1

Jude 1:1

maelezo ya jumla

Yuda anajitambulisha kama mwandishi wa hii barua na anawasalimu wasomaji wake. Yawezekana alikuwa kaka yake Yesu wakambo. Kuna Yuda wengine wawili katika Agano Jipya.

maelezo ya jumla

Neno "wewe" katika hii barua ya husu waKristo ambao Yuda alikuwa akiwandikia na ni katika wingi.

Yuda, mtumishi wa

Yuda ni kaka wa Yakobo. Tafsiri mbadala: "Mimi ni Yuda, mtumishi wa."

Na kaka yake na Yakobo

Yakobo na Yuda ni nusu kaka wa Yesu

wapendwao katika Mungu Baba

"Mungu baba anawapenda ninyi"

huruma na iwe kwenu na amani izidishwe

"kwenu" ina rejea kwa Wakristo wote waliopaswa kupokea barua hii.Tafsiri mbadala: "huruma, neema na upendo na uongezwe mara nyingi kwa ajili yenu."

Jude 1:3

kauli unganishi

Yuda anawapa waamini sababu yake ya kuandika hi barua

maelezo ya jumla

Neno "sisi" la muhusu yuda na waamini katika hii barua

Nilikuwa nafanya kila juhudi kuwaandikia ninyi

"Nilikuwa na shauku ya kuwaandikia ninyi"

wokovu wa kawaida

"tunashiriki wokovu uleule"

Ilinilazimu kuandika

"Nilijisikia uhitaji mkubwa kuandika" au "Nilijisikia hitaji muhimu kuandika"

kuwahimiza mshindanie kwa uaminifu kwa ajili ya imani

"kuwatia moyo kutetea mafundisho ya kweli"

kabidhiwa

Mungu alitoa mafundisho haya ya kweli"

kwa sababu watu fulani wamejiingiza kwa siri

"kwa kuwa baadhi ya watu wamekuja miongoni mwa walioamini pasipo kujijulisha wenyewe"

ambao hukumu yao ya dhambi ilikwisha andikwa tangu zamani

"zamani sana iliandikwa kwamba watu hawa watahukumiwa dhambi"

ambao hubadilisha neema ya Mungu kuwa zinaa

"ambao hufundisha kwamba neema ya Mungu inaruhusu mtu kudumu katika maisha ya dhambi ya zinaa"

ambao humkataa Mkuu wetu wa pekee na Bwana, Yesu Kristo

watu hawa hufundisha kwamba Yesu Kristo sio njia ya kweli au pekee ya kwenda kwa Mungu.

Kataa

kusema kwamba jambo fulani si kweli.

Jude 1:5

kauali unganishi

Yuda antoa mifano ya kale ya wale ambao hawakumfuata Bwana.

Ngpenda kuwakumbusha

"Ninataka ninyi mkumbuke"

mnajua kila kitu

Yuda hasa anarejea kwenye maandiko ya Musa ambayo wamekwisha kufundishwa. Tafsiri mbadala: "mnayajua maandiko ya Musa."

Bwana aliwaokoa mara moja watu kutoka nchi ya Misri

"Bwana aliwaokoa Waisraeli hapo zamani kutoka Misri"

lakini baadaye

"muda ulivyo endelea " au " baada ya jambo fulani kutokea"

enzi yao wenyewe

"nafasi zao" au "majukumu yaliowekwa kwao"

wakaacha wakazi yao maalum

"waliacha nafasi zao wenyewe"

Mungu amewaweka katika vifungo vya milele katika giza

"Mungu amewafunga malaika hawa ndani ya giza"

siku ile kuu

siku ya mwisho ambayo Mungu huukumu watu wote

Jude 1:7

katika namna ileile walijiingiza wenyewe kwenye

Sodoma na Gomora waliishi katika dhambi ya zinaa katika namna hihyo hiyo kama malaika walivyo fuata njia za uovu.

kama mifano ya wale ambao huteseka katika hukumu ya moto wa milele

Uharibifu wa watu wa Sodoma na Gomora ulifanyika mfano wa hatima ya wote wanao mkataa Mungu.

hawa pia walichafua

"Hawa" ina rejea kwa watu wanaomkataa Mungu ambao huchafua miili yao kwa uasherati kwa namna hiyo wakitupa takataka kwenye mkondo inaweza kusababisha maji kuwa mabaya kunywa.

kuhusu wenye utukufu

"kuhusu malaika wazuri wa Mungu"

Jude 1:9

maelezo ya jumla

Balaamu ni Nabii aliye kataa kulahani Israel kwa ajiili ya adui lakini akamfundisha huyo adui kuwafanya watu waoe wasio amini na wawe waabudu sanamu.

maelezo ya jumla

Kora alikuwa ni muIsraeli aliye asi uongozi wa Musa na ukuhani wa Aruni.

bishana kuhusu mwili

walibishana juu ya nani atachukua milki ya mwili. "bishana kuhusu nani angechukua milki ya mwili."

Mikaeli...hakuthubutu kuleta kinyume naye

"Mikaeli...alijizuia mwenyewe kumkemea ibilisi

hukumu au kuleta maneno ya matusi

"upinzani wa nguvu au maneno yasiyo na heshima"

Lakini watu hawa

"watu hawa" ni watu waovu waliotajwa mapema.

tusi mambo yote ambayo hawayaelewi

"kuongea pasipo heshima kinyume na chochote ambacho hawakijui maana yake"

njia ya Kaini

Kaini alimuua kaka yake Abeli.

kosa la Balaam kwa ajili ya mshahara

Balaamu alijaribu kulaani Israeli kwa ajili ya pesa.

uasi wa Kora

Kora aliasi dhidi ya uongozi wa Musa na ukuhani wa Aron.

Jude 1:12

sentensi unganishi

Yuda anatumia mifano mingi kumfafanua mtu asiye na utaua. Anawambia waamini jinsi wanvyo paswa kumtambua mtu huyu miongoni mwao.

Hawa ni wale

"Hawa" ina rejea kwa watu waovu.

miti iliyopukutika isiyo na matunda

Kama baadhi ya miti isiyozalisha matunda katika mwisho wa majira ya joto, hivyo watu hawa waovu hawana imani na kazi za haki.

bila matunda, kufa mara mbili

Kama miti ambayo imeuawa mara mbili kama vile kwa baridi usingeweza kutoa matunda, kwa hiyo watu waovu hawana thamani na hawana maisha ndani yao.

iliyong'olewa na mizizi

Kama miti ambayo imeng'olewa kwenye udongo na mizizi yake, watu waovu wametenganishwa kutoka kwa Mungu ambaye ni chanzo cha maisha.

pori la mawimbi ya bahari

Kama mawimbi ya bahari yanayosukumwa na upepo mkali, hivyo watu waovu hawakuwa na msingi wa imani na walihamishwa kwa urahisi katika mwelekeo mwingi.

yakitoa aibu yao wenyewe

Kama upepo usababishao pori la wimbi kukoroga povu chafu, hivyo watu hawa kwa kupitia mafundisho ya uongo na matendo huwa aibisha wenyewe. AT: "kama vile wimbi huleta povu na uchafu, watu hawa wanachafua wengine kwa aibu yao."

Nyota zinazo randaranda, ambao weusi wa giza umetunzwa kwa ajili yao milele

Kama vile nyota zitembeavyo angani na kufanya ugumu kuzifuata, hivyo na wewe usiwafuate watu hao.

Jude 1:14

watu hawa...kazi yao...wana

Hawa inarejea kwa watu waovu.

wa saba katika orodha ya Adamu

Kizazi cha saba kutoka kwa Adamu. Baadhi ya tafsiri husema sita katika orodha ya Adamu inategemeana kama Adamu anahesabika kama kizazi.

Tazama, Bwana

"taarifa, Bwana", au "tazama, bwana"

mambo yote magumu

"maneno yote makali"

manung'uniko, walalamikao

Watu walio na moyo usio na utii. Wanung'unikao huwa wanafanya hivi kimya kimya, Walalamikao hufanya hivi kwa uazi zaidi.

wajivunao mno

Watu wanao jisifu wenyewe ili kwamba wengine wawasikie.

Jude 1:17

Watu hawa

"Hawa wadhihaki"

wanatawaliwa na tamaa za asili

Watu hawa wanazungumziwa kama tamaa zao ni wafalme wanao watawala. "Awaachi kumkosea Mungu kwa kuendelea kufanya maovu wanayo tamani kufanya.

hufuata ... tamaa

Tamaa zisizo za kitauwa za ongelewa kama ni njia ambayo huyo mtu kaifuata.

ni wa kidunia

"wenye dharau wanajiingiza kwenye dhambi ya zinaa"

hawana Roho

Roho Mtakatifu anazungumziwa kama ni kitu ambacho watu wanaweza kumiliki.

Jude 1:20

sentensi unganishi

Yuda anawambia waamini jinsi ya kuishi na namna ya kuwa tendea wengine.

kama mjijengavyo wenyewe

Kama muwezavyo kukua imara na afya njema, ili kwamba muweze kuimarika na kukua fahamu zenu na roho katika maarifa ya Mungu

msubiri

"tunatazamia kwa shauku"

jitunzeni katika upendo wa Mungu

Kuweza ;kupokea upendo wa Mungu ya zungumziwa kama vile mtu amejihifadhi sehemu.

rehema za Bwana wetu Yesu Kristo ambayo huwapatia uzima wa milele

Hapa "rehema" ya wakilisha Yesu Kristo mwenyewe, ambaye atawaonyesha rehema zake kwa waaamini kwa kuwafanya wa ishi milele

Jude 1:22

baadhi ya watu, ambao wako katika mashaka

"baadhi ya watu, ambao bado hawajaamini kuwa Mungu ni Mungu"

wanyakueni kutoka katika moto

"ili kwamba wasije wakaenda kwenye ziwa la moto"

na kwa baadhi yao onesheni huruma kwa hofu

"na muwe wakarimu kwa wengine bali ogopeni kutenda dhambi kama wao."

mkichukia hata vazi lililotiwa doa na mwili

"chukieni hata mavazi yao, kwa sababu yamefayika kuwa machafu kwa dhambi." Wamejaa dhambi hivyo hata mavazi yanafikiriwa machafu.

Jude 1:24

sentensi unganishi

Yuda anafunga na baraka

kuwasababisha msimame mbele ya utukufu wake

Utukufu wake ni taa nzuri yenye kuwakilisha ukuu wake. "Na kukuruhusu kufurahia na kuabudu utukufu wake"

bila mawaa

Hapa dhambi ya tajwa kama uchafu kwenye mwili wa mtu au doa kwenye mwili wa mtu. "Utakapo kuwa bila dhambi"

kwake Mungu pekee mwokozi kupitia Yesu Kristo Bwana wetu

"kwa Mungu pekee, aliye tuokoa kwa lili Yesu Kristo alilifanya." Hii ya sisitiza kuwa Mungu baba pamoja na Mwana ndie Mwokozi.

utukufuu uwe kwake, ukuu, uwezo na nguvu kabla ya nyakati zote, na sasa na hata milele. Amina.

Mungu alikuwa nao, na anao, na siku zote atakuwa na utukufu, uongozi kamilifu, na utawala wa mambo yote.