Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa Ufunuo wa Yohana

Sehemu ya 1: Utangulizi wa jumla

Muhtasari wa Kitabu cha Ufunuo wa Yohana

  1. Mwanzo (1:1-20)
  2. Barua kwa makanisa saba (2:1-3:22)
  3. Maono juu ya Mungu akiwa mbinguni na maono ya Yule Mwanakondoo (4:1-11)
  4. Mihuri saba (6:1-8:1)
  5. Baragumu saba (8:2-13:18)
  6. Waabudu wa Mwanakondoo, wafia dini na mavuno ya hasira (14:1-20)
  7. Vitasa saba (15:1-18:24)
  8. Ibaada mbinguni (19:1-10)
  9. Hukumu ya Mwanakondoo, kuangamizwa wa yule mnyama, miaka elfu moja,kuangamizwa wa shetani na hukumu ya mwisho (20:11-15)
  10. Uumbaji upya na Yerusalemu mpya (21:1-22:5)
  11. Ahadi ya Yesu ya kurudi, ushuhuda wa malaika, maneno ya kumalizia ya Yohana, Ujumbe wa Kristo kwa kanisa,Mwaliko na onyo (22:6-21)

Nani aliandika kitabu cha Ufunuo wa Yohana?

Mwandishi anajitambulisha kama Yohana. Labda huyu ni Mtume Yohana. Aliandika kitabu cha Ufunuo akiwa katika kisiwa cha Patmosi. Warumi walikuwa wamempeleka huko kuishi uhamishoni kwa sababu ya kuwafundisha watu kumhusu Yesu.

Kitabu cha Ufunuo kinahusu nini?

Yohana aliandika kitabu cha Ufunuo kuwatia moyo waumini ili wabaki waaminifu ingawa walikuwa wanateseka. Yohana alifafanua maono aliyopata kumhusu shetani na wafuasi wake wakiwapinga na kuwaua waumini. Katika maono haya, Mungu anasababisha vitu vingi vibaya kutokea duniani na kuwaadhibu watu wabaya. Kwa mwisho Yesu anamshinda Shetani na wafuasi wake. Kisha Yesu anawafariji wale waliokuwa waaminfu. Na waumini wataishi milele pamoja na Mungu katika mbingu mpya na dunia mpya.

Kichwa cha kitabu hiki kinastahili kutafsiriwa namna gani?

Watafsiri wanaweza amua kukiita kitabu hiki na mojawapo wa vichwa vyake vya kitamaduni kama, "Ufunuo," "Ufunuo wa Yesu Kristo,"Ufunuo kwa Mtakatifu Yohana," ama "Apokalipi wa Yohana."Ama wanaweza kuchagua kichwa cha kueleweka zaidi kama "Vitu alivyovionyesha Yesu Kristo kwa Yohana." (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Ni aina gani ya uandishi wa kitabu cha Ufunuo?

Yohana alitumia aina maalum ya uandishi kufafanua maono yake. Yohana anafafanua alichokiona kutumia alama nyingi. Mfumo huu wa uandishi unaitwa unabii wa alama ama fasihi ya kiapokalipti (inayozungumzia maangamizo yajayo). (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Je, matukio ya Ufunuo ni ya kipindi cha sasa ama kipindi kijacho?

Tangu wakati wa kwanza wa Ukristo, wasomi wamekuwa wakifafanua ufunuo tofauti. Wasomi wengine wanafikiri Yohana alifafanua matukio yaliyotokea nyakati zake. Wasomi wengine wanafikiri Yohana alifafanua matukio yaliyofanyika wakati wake hadi wakati Yesu atakaporudi. Wasomi wengine wanafikiri Yohana alifafanua matukio ambayo yangetokea muda mfupi kabla ya kurudi kwake Kristo.

Watafsiri hawatahitajika kuamua jinsi ya kukifafanua hiki kitabu hiki kitabu kabla ya kukitafsiri. Watafsiri waache unabii huo katika vitenzi vinavyotumika kwenye ULB.

Je, Kuna vitabu vingine kwenye Bibilia kama Ufunuo?

Hakuna kitabu kingine cha Bibilia kinachofanana na Ufunuo. Lakini aya katika vitabu vya Ezekieli, Zakaria na hasa Danieli zina mafundisho na aina sawa ya uandishi kama Ufunuo. Itakua na umuhimu kukitafsiri Ufunuo wakati sawa na Danieli kwa sababu vitabu hivi vina tamathali sawa za usemi na namna ya uandishi.

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya kitafsiri

Je, mtu anahitajika kukifahamu kitabu cha Ufunuo ili kukitafsiri?

Mtu hahitaji kufahamu alama zote katika kitabu cha Ufunuo ili kukitafsiri ipasavyo. Watafsiri wasitoe maana ya alama ama nambari katika tafsiri zao. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Maswala ya "takatifu" na "takasa" yameakilishwa vipi katika Ufunuo ndani ya ULB?

Maandiko yanatumia maneno haya kuashiria mojawapo ya wawazo. Kwa sababu hii, ni vigumu kwa watafsiri kuyatumia vyema katika matoleo yao. Wakati wa kutafsiri Ufunuo kwa Kiingereza, ULB hufuata sheria zifuatazo:

  • Maana katika aya mbili inaashiria utakatifu wa kitabia. Hapa ULB inatumia "takatifu" (Tazama: 14:12; 22:11)
  • Mara nyingi maana yanaashiria Wakristo bila kufafanua majukumu watekelezayo. Katika hali kama hizi, ULB inatumia "Mwumini" ama "waumini". (Tazama:5:8; 8:3, 4; 11:18; 13:7; 16:6; 17:6; 18:20, 24; 19:8; 20:9)
  • Wakati mwingine maana yake inaashiria swala la mtu ama kitu kilichotengwa kwa ajili ya Mungu pekee. Katika hali kama hizi, ULB inatumia "takasa", "tenga kando", "kutabaruku kwa", ama "hifadhiwa kwa."

UDB itakuwa ya msaada kwa watafsiri kwa mara nyingi jinsi ya kuakiisha mawazo haya katika matoleo yao wenyewe.

Vipindi vya muda

Yohana aliashiria vipindi vingi vya muda katika Ufunuo. Kwa mfano kuna uashiriaji mwingi wa miezi arobaini na mbili, miaka saba, na miaka mitatu na nusu. Wasomi wengine wanafikiri vipindi hivi ni alama ya kitu fulani.Wasomi wengine wanafikiri kwamba hivi ni vipindi vya ukweli vya muda. Watafsiri wanatakikana kuvichukulia hivi vipindi kama vinavyoashiria vipindi kamili vya muda. Ni juu ya mtafsiri kuamua umuhimu wavyo ama vitu vinavyowakilishwa na vipindi hivi.

Ni maswala gani ya muhimu ya utafsiri katika kitabu cha Ufunuo?

Yafuatayo ni maswala muhimu ya uandishi katika Kitabo cha Ufunuo.

  • "Mimi ni alfa na omega,' asema Bwana Mungu, 'Yule aliye, na aliyekuwa, na atakayekuja, Mwenyezi'" (1:8). ULB,UDB na matoleo mengine ya kisasa husoma hivi. Matoleo mengine yanaongezea kauli "Mwanzo na Mwisho."
  • "Wazee wakasujudu wakaabudu" (5:14). ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa yanasoma namna hivi. Matoleo mengine ya kale yanasoma, "Wale wazee ishirini na nne wakaanguka na kumwabudu yule anayeishi milele na milele."
  • "Mpaka sehemu ya tatu yake (dunia) ikachomeka" (8:7). ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa yanasoma hivi.Matoleo mengine ya zamani hayana fungu hili la maneno.
  • Maandiko mengine yanaongezea fungu hili "na atakayekuja" (11:17). Lakini ULB, UDB na matoleo mengi ya kisasa hayafanyi hivyo.
  • Maanidko mengine yanaongezea fungu hili "mbele ya kiti cha enzi ya Mungu" (14:15)

lakini ULB, UDB na matoleo mengi ya kisasa hayafanyi hivyo."

  • "Aliyeko na aliyekuwepo, Yule Mtakatifu"16:5). ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa yanasoma hivi. Matoleo mengine ya zamani yanasoma, "Ee Bwana, Yule aliye na aliyekuwa na atakayekuwa."
  • "Mataifa watatembea kwa mwanga wa jiji hilo" (21:24). ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa husoma hivi. Matoleo mengine ya zamani husoma, "Mataifa yaliyookoka watatembea kwa mwanga wa "jiji hilo."
  • "Heri wazifuao nguo zao" (22:14). ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa husoma hivi. Maandiko mengine ya zamani husoma hivi, "Heri wal wanaofuata amri zake."
  • "Mungu atamwondolea sehemu yake katika mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu" (22:19).ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa husoma hivi.Maandiko mengine ya kale husoma, "Mungu atachukua sehemu yake katika kitabu cha uzima na kwenye mji ule mtakatifu."

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

Revelation 1

Ufunuo 01 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii inaelezea jinsi kitabu hiki ni kumbukumbu ya maono Yohana alipokea katika kisiwa cha Patmosi.

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo nukuu kutoka Agano la kale. ULB hufanya hivi na nukuu kutoka 1:7.

Dhana muhimu katika sura hii

Makanisa saba

Barua hii iliandikiwa makanisa saba halisi katika nchi inayotiwa sasa Uturuki.

Nyeupe

Rangi nyeupe huashiria utakatifu ama uadilifu katika maandiko. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#holy and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous)

Tamathali muhimu za usemi katika sura hii

"Yeye aliye, Aliyekuwepo, na atakayekuja"

Maneno haya yanaeleza kwamba Mungu amekuwepo, yupo sasa na atakuwepo milele. Siyo lugha zote zina njia ya kutafsiri kwa urahisi kipindi kilichopita, kipindi cha sasa na kipindi kijacho kwa kitenzi.Inaonekana huu ni mnyambuliko wa jina la Mungu, Yahweh, lenye maana "Mimi niko".

Damu yake

Hii inaashiria kifo cha Yesu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metonymy)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii.

"Anakuja na mawingu"

Wasomi wengi wanaamini kwamba Yesu atarudi kwa awamu mbili. Kurudi kwa kwanza kwa Yesu kutakua wa kisiri kama "Mwizi wa usiku." Halafu Mungu atakuja kwa njia ya uwazi ambapo kila mtu atamuona. Huu ndio ujio wa mwisho uzungumzao kitabu cha Ufunuo.

Yesu

Taswira ya yule mwanaume aliye mbinguni ni ya Yesu. Kwa mtazamo wa jumla, taswira hii ni maelezo kuhusu Yesu katika utukufu yake. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#glory na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

"Malaika wa makanisa saba"

Neno la Kigiriki linalotafsiriwa kama "malaika" linaweza kutafsiriwa pia kama "wajumbe." Kuna uwezekano hii inaashiria wajumbe ama viongozi wa makanisa haya saba.

| >>

Revelation 1:1

Taarifa ya Jumla:

Huu ni utangulizi wa kitabu cha Ufunuo. Unaeleza kuwa ni ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo na unawabariki wote wausomao.

watumishi wake

Hii humaanisha watu wamwaminio Kristo

Nini lazima kitokee hivi punde

"matukio ya lazima kutokea hivi punde"

Kufanywa kujulikana

"kufanywa mawasiliano"

Kwa mtumishi wake Yohana

Yohana aliandika kitabu hiki na alikuwa akijitaja yeye mwenyewe: "kwangu, Yohana, mtumishi wake"

Neno la Mungu

Hii humaanisha ni ujumbe Yohana aliopewa na Mungu.

Yule anayesoma kwa sauti

Hii haihusishi mtu bayana. Inahusisha mtu yeyote anayesoma kwa sauti. "Yeyote anayesoma kwa sauti"

Tii kilichoandikwa ndani

"amini kilichoandikwa humo na kutii amri zilizomo"

Muda umekaribia

"vitu ambavyo lazima vitokee vitatokea karibuni"

Revelation 1:4

Taarifa ya Jumla:

Huu ni mwanzo wa barua ya Yohana. Hapa ajitaja kama mwandishi na kuwasalimu watu anaowaandikia.

neema iwe kwenu na amani kutoka kwake aliyepo...na kutoka kwa roho saba...na kutoka kwa Yesu Kristo

Haya ni matamanio au baraka. Yohana anazungumza kana kwamba hivi ni vitu ambavyo Mungu anaweza kugawa, ingawa ni njia ambazo anatumaini Mungu atawatendea watu wake. "Yule aliyepo...na roho saba...na Yesu Kristo awatendee kwa huruma na kuwawezesha kuishi kwa amani na usalama."

Kutoka kwake aliyepo

"kutoka kwa Mungu, aliyepo"

Atakayekuja

Atakayekuwapo baadaye ananenwa kama anayekuja.

roho saba

Namba saba ni alama ya ukamilifu na utimilifu. "Roho saba" humaanisha mojawapo kati ya Roho ya Mungu au roho saba zinazomtumikia Mungu.

Mzaliwa wa kwanza wa waliokufa

"mtu wa kwanza kufufuliwa kutoka mautini"

ametuweka huru

"ametukomboa"

ametufanya kuwa ufalme, makuhani

"ametuweka kando na kuanza kututawala na kutufanya makuhani"

Mungu na Baba yake

Huyu ni mtu mmoja. "Mungu na Baba yake"

Baba

Hili ni jina muhimu la Mungu linaloeleza uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

kwake kuwa utukufu na nguvu

Haya ni matamanio au baraka. Maana zinazowezekana ni 1)"Watu waheshimu utukufu wake na nguvu" au 2) "awe na utukufu na nguvu". Yohana anaomba kwamba Yesu Kristo ataheshimiwa na ataweza kutawala kabisa juu ya kila mtu na kila kitu.

nguvu

hii inaweza kumaanisha mamlaka yake kama mfalme.

Revelation 1:7

Taarifa ya Jumla:

Katika mstari wa 7, Yohana ananakiri kutoka kitabu cha Danieli na Zekaria.

Kila jicho

Kwa kuwa watu huona kwa macho, neno "jicho" limetumika kuashiria watu. "kila mtu" au "watu wote"

pamoja na wote waliomchoma

"na wale waliomchoma pia watamuona"

waliomchoma

Mikono na miguu ya Yesu ilichomwa wakati aliposulibiwa msalabani. Hapa inamaanisha watu wakimuua. "walimuua"

mchoma

kutengeneza tundu katika

Alfa na Omega

Hizi ni herufi za kwanza na mwisho katika alfabeti ya Kigriki. Maana zinazowezekana ni 1) "yule aliyeanzisha vitu vyote na anayevileta mwisho vitu vyote" au 2)"yule ambaye alikuwepo na ataendelea kuwepo". "Yeye ni A na Z" au "mwanzo na mwisho"

ambaye anakuja

Atakayekuwapo baadaye ananenwa kama anayekuja.

asema Bwana Mungu

Baadhi ya lugha huweka "Bwana Mungu asema" mwanzoni au mwishoni mwa sentesi nzima.

Revelation 1:9

Taarifa ya Jumla:

Yohana anaeleza jinsi maono yake yalivyoanza na maelekezo aliyopewa na Roho.

yenu...nanyi

Hii humaanisha waumini katika makanisa saba

anayeshiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu thabiti ulio katika Yesu

"aliye na fungu katika ufalme wa Mungu. Ninateseka pia na kuvimilia majaribu pamoja nanyi kwa sababu sisi ni mali ya Yesu"

kwa sababu ya neno la Mungu

"kwa sababu niliwaambia wengine kuhusu neno la Mungu"

katika Roho

Yohana anazungumzia kuvutwa na Roho ya Mungu kana kwamba alikua katika Roho. "kushawishika na Roho" au "Roho alinishawishi"

siku ya Bwana

siku ya kuabudu kwa waumini wa Kristo

sauti ya juu kama ya tarumbeta

Sauti ilikua na sauti kuu sana ikafanana na tarumbeta

tarumbeta

Hii humaanisha chombo cha kutengeneza muziki au kuwaita watu kwa ajili ya tangazo au mkutano.

kwenda Smirna, kwenda Pergamo, kwenda Thiatira, kwenda Sardi, kwenda Philadelphia, na kwenda Laodikia

Haya ni majina ya miji uliko Asia ambayo ni Uturuki ya leo

Revelation 1:12

Kauli unaganishi:

Yohana anaanza kueeleza alichokiona katika maono.

sauti ya nani

hii humaanisha mtu anayezungumza. "ambaye"

Mwana wa Adamu

Huu msemo unaelezea umbo la binadamu, mtu anayefanana na binadamu.

mkanda wa dhababu

kipande cha nguo kilichovaliwa kifuani. Inawezekana kuwa ilikua na nyuzi za dhahabu ndani yake.

Revelation 1:14

Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe kama theluji

Sufu na theluji ni mifano ya vitu ambavyo ni viupe sana. Kurudiwa kwa "nyeupe kama" huonesha msisitizi kuwa zilikua nyeupe mno.

sufu

Haya na manyoya ya kondoo au mbuzi. Zilikua zinajulikana kuwa nyeupe mno.

macho yake yalikuwa kama mwali wa moto

Macho yake yanaelezwa kuwa na mwanga kama mwali wa moto. "macho yake yaling'ara kama mwali wa moto"

Nyayo zake zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana

Shaba hung'arishwa kuifanya ingae na kurudisha mwanga. "Miguu yake iling'ara sana kama shaba iliyosuguliwa"

kama shaba iliyosuguliwa sana, kama shaba ambayo imekwisha pitishwa katika moto

Shaba ilisafishwa kwanza kisha kusuguliwa. "Kama shaba iliyosafishwa kwenye tanuu la moto na kusuguliwa"

tanuu

chombo imara kwa ajili ya kutunzia moto mkali sana. watu huweka vyuma ndani yake na ule moto huunguza takataka zote zilizomo katika chuma.

sauti ya maji mengi yanayotiririka kwa kasi

Hii ina sauti kuu sana kama sauti ya mto mkubwa unaotiririka kwa kasi, maporomoko ya maji, au ya mawimbi yenye sauti kali baharini.

kinywani mwake kulikuwa na upanga mkali

Ubapa wa upanga ulikuwa unchomoza kinywani mwake. Upanga wenyewe haukua ukisogea.

upanga mkali wenye makali kuwili

Hii humaanisha upanga wenye makali mawili, ambao umechongeka pande zote ili kukata pande zote.

Revelation 1:17

nikaanguka miguuni pake

Yohana alilala chini akitazama ardhi. Inawezekana alikuwa ameogopa sana na alikuwa akimpa Yesu heshima.

Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu

"Alinigusa na mkuno wake wa kulia"

Mimi ni wa kwanza na wa Mwisho

Hii inamaanisha uasili wa Yesu wa milele.

ninazo funguo za mauti na kuzimu

Kuwa na nguvu juu ya jambo au kitu huzungumziwa kama kuwa na funguo zake. Maana inayooneshwa ni kwamba anaweza kuwapa uhai wale waliokufa na kuwatoa kuzimu. "Nina nguvu juu ya kifo na kuzimu" au "nina uwezo wa kuwapa uhai waliokufa na kuwatoa kuzimu".

Revelation 1:19

Kauli unaganishi:

Mwana wa Adamu aendelea kuzungumza

nyota

Hizi nyota ni ishara. Zinaonekana kuashiria wale malaika saba na makanisa saba.

vinara vya taa

Vinara vya taa ni ishara zinazomaanisha makanisa saba.

malaika wa yale makanisa saba

Maana zinazowezekana ni 1) malaika wa mbinguni wanaolinda yale makanisa saba au 2) wajumbe binadamu katika makanisa saba.

makanisa saba

Hii humaanisha makanisa saba ambayo yalikuwepo Asia ndogo wakati huo.

Revelation 2

Ufunuo 02 Maelezo kwa Jumla

Muundo na mpangilio

Sura ya 2 na ya 3 pamoja zinaunda kitenge kimoja.Hii sehemu mara nyingi hujulikana kama "barua saba kwa makanisa saba."Mtafsiri anaweza amua kuzitenganisha barua hizi moja kwa nyingine ili kuzitofautisha.

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo nukuu kutoka Agano la kale. ULB hufanya hivi na nukuu kutoka 2:27

Dhana muhimu katika sura hii

Umaskini na Utajiri

Sura hii inatoa maana mbili ya kuwa maskini na kuwa tajiri.Waefeso walikuwa maskini wa kifedha kwa sababu hawakuwa na pesa nyingi. Hawakuwa maskini wa kiroho kwa sababu ya "utajiri mwingi" waliokuwa nao ndani ya Kristo. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#spirit)

"Shetani ako karibu kufanya"

Kitabu cha Ufunuo kinahusu mambo ambayo Shetani atakuja kuyafanya duniani. Hata hivyo kinahusu kile ambacho Mungu atafanya mwishowe kumshinda Shetani.

Balaamu, Balaki na Jezebeli

Haya mafundisho juu ya Balaamu ni ngumu kuyaelewa iwapo vitabu vya Wafalme havijatafsiriwa. Kuna uwezekano kwamba hii inaashiria kuongoza watu wa Israeli kwa uzinzi na kwa kuabudu miungu wa uongo. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#falsegod)

Tamathali muhimu za usemi katika sura hii

Mfano

Wasomi wengine wanachukulia sura ya 2 na 3 kama mfano. Wanaelewa kama makanisa haya ni aina ya makanisa ama vipindi vya kihistoria vya kanisa. Ni vema kutafsiri hii kama maelekezo ya makanisa ya kale katika miji hii. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

"Kama una sikio, sikia kile Roho anawaambia makanisa"

Maneno haya ni mwito wa kutubu kwa watu walio ndani ya kanisa. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#repent)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Malaika wa makanisa saba"

Neno la Kigiriki "Malaika" linaweza pia kutafsiriwa kama "wajumbe."Kuna uwezekano hii inaashiria wajumbe ama viongozi wa makanisa haya saba.

"Haya ni maneno yake yule"

Haya maneno yanatumika kutanguliza barua hizi. Kuna uwezekano kama inaashiria Yesu. Kila barua basi inafafanua kipengele juu ya Yesu ambacho ni muhimu kwa barua nzima.

<< | >>

Revelation 2:1

Taarifa ya Jumla:

Huu ni mwanzo wa ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa kanisa la Efeso.

malaika

Maana zinazowezekana ni 1) malaika wa mbinguni anayelinda kanisa au 2) mjumbe binadamu kwa makanisa.

nyota

Hizi nyota ni ishara. Zinaonekana kuashiria wale malaika saba na makanisa saba.

Vinara vya taa

Vinara vya taa ni ishara zinazomaanisha makanisa saba.

Najua ... bidii yako ya kazi na uvumilivu wako thabiti

"Bidii" na "uvumilivu" ni nomino dhahania na zinaweza kutafsiriwa na kitenzi "fanya kazi" na "vumilia". Ninajua ... kwamba mnafanya kazi sana na unavumilia"

na kumbe siyo

"lakini sio mitume"

na wameonekana kuwa waongo

"umetambua kuwa kuwa hao watu ni mitume wa uongo"

Revelation 2:3

kwa sababu ya jina langu

"kwa sababu unaamini jina langu" au "kwa sababu unaniamini"

na haujachoka bado

Kuvunjwa moyo inazungumziwa kama kuwa na uchovu. "haujavunjika moyo" au "haujakata tamaa"

nililonalo dhidi yako

"sikukubali kwa sababu hii" au "nina hasira na wewe kwa sababu hii"

umeuacha upendo wako wa kwanza

Kuacha kufanya kitu inazungumziwa kama kukiacha nyuma. Upendo unazungumziwa kama kitu ambacho kinaweza kuachwa nyuma. "umeacha kunipenda kama ulivyokuwa ukinipenda mwanzoni"

Kwa hiyo kumbuka ulipoanguka

Kutokupenda kama hapo mwanzo inazungumziwa kama kuanguka. "kiasi gani mlivyobadilika" au "jinsi gani mlivyonipenda"

Usipotubu

"usipoomba msamaha"

kukiondoa kinara chako

Vinara vya taa ni ishara zinazomaanisha makanisa saba.

Revelation 2:6

Wanikolai

Watu waliofuata mafundisho ya mtu aitwaye Nikolai

Mwenye sikio asikie

Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asikilize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"

Na kwa yule ashindaye

Hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa wale ambao hawatakubali kufanya uovu"

paradiso ya Mungu

"Bustani ya Mungu". hii ni ishara ya mbinguni.

Revelation 2:8

Taarifa ya Jumla:

Huu ni mwanzo wa ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa kanisa la Smirna.

Smirna

Hili ni jina la mji ulioko Asia ambayo ni Uturuki ya leo.

mwanzo na mwisho

Hii humaanisha asili ya milele wa Yesu.

Nayajua mateso yako na umasikini wako

"Mateso" na "umasikini" zinaweza kutafsiriwa kama vitenzi. "ninajua ulivyoteseka na jinsi gani ulivyo masikini"

na uongo wa wale wanaojiita ni wayahudi

"uongo" unaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "Ninajua jinsi gani wale wanaojiita wayahudi walivyowasema vibaya" au "Ninawajua wale wanaojiita wayahudi na wamesema vitu vibaya juu yenu"

lakini siyo

"lakini sio wayahudi wa kweli"

sinagogi la Shetani

Watu wanaokusanyika kumtii au kumtukuza Shetani awnazungumziwa kama sinagogi, mahali pa wayahudi pa kuabudu na kufundishia.

Revelation 2:10

Ibilisi anataka kuwatupa baadhi yenu gerezani

"Ibilisi atasababisha hivi punde wengine wawaweke baadhi yenu gerezani"

Iweni waaminifu hadi kufa

"Kuweni waaminifu kwangu hata kama watawaua". Matumizi ya neno "hadi" haimanishi kuwa uache kuwa mwaminifu wakati wa kifo.

taji

"taji la ushindi." Hili lilikua shada ambalo asili yake ilikua ya matawi ya mizeituni au majani ya laurusi ambayo yaliweka kwenye kichwa cha mwanariadha mshindi.

taji la uzima

Maana zinazowezekana ni 1)"taji linaloonesha kuwa nimekupa uzima wa milele" au 2)"uzima wa kweli kama dhawabu kama taji la mshindi"

Mwenye sikio asikie

Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asiklize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"

Yeye ashindaye

hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa wale ambao hawatakubali kufanya uovu"

hatapata madhara ya mauti ya pili

"hatapitia kifo cha pili" au "hatakufa mara ya pili"

Revelation 2:12

Taarifa ya Jumla:

Huu ni mwanzo wa ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa kanisa la Pergamo.

Pergamo

Huu ni mji ndani ya Asia ambapo ni Uturuki ya leo.

upanga mkali, wenye makali kuwili

Hii humaanisha upanga wenye makali mawili, ambao umechongeka pande zote ili kukata pande zote.

kiti cha enzi cha shetani

Maana zinazowezekana ni 1) nguvu ya Shetani na ushawishi wake juu ya watu, au 2) mahali ambapo Shetani hutawala.

wewe walishika sana jina langu

Kuwa na imani dhabiti inazungumziwa kama kushikilia kwa nguvu. "Unaniamini kwa dhabiti"

hukuikana imani yako iliyo kwangu

"Imani" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi "kuamini". "hukuacha kuniamini"

Antipasi

Hili ni jina la mtu.

Revelation 2:14

Lakini nina mambo machache dhidi yako

"sikukubali kwa sababu ya vitu vichache ulivyofanya" au "nina hasira na wewe kwa sababu ya vitu vichache ulivyofanya"

washikao mafundisho ya Balaamu

Maana zinazowezekana ni 1)"wafundishao alichofundisha Balaamu" au 2)"wanaofanya alichofundisha Balaamu".

Balaki

Hili ni jina la mfalme.

aliyemfundisha Balaki kuweka vikwazo mbele ya wana wa Israel

Jambo linalowapelekea watu kutenda dhambi huzungumziwa kama jiwe barabarani ambalo watu hujikwaa nalo. "aliyemuonesha Balaki jinsi ya kuwafanya watu wa Israeli kutenda dhambi".

Uasherati

"kutenda dhambi ya zinaa".

Wanikolai

Hili ni jina la kundi la watu waliofuata mafundisho ya mtu aitwaye Nikolai

Revelation 2:16

Basi tubu

kwa hiyo tubu

usipofanya hivyo

"usipotubu"

nitafanya vita dhidi yao

"kupigana dhidi yao"

kwa upanga utokao katika kinywa changu

Hii humaanisha upanga katika 1:14. Ingawa alama za lugha za ufunuo kawaida hazitakiwi kutafsiriwa, watafsiri wanaweza kuchagua kama waifafanue hii alama kama alama ya neno la Mungu, kama UDB ilivyofanya. Hii alama inaonesha kwamba Kristo atawashinda maadui zake kwa kutoa amri tu.

Mwenye sikio na askie

Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asikilize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"

Yeye ashindaye

Hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa wale ambao hawatakubali kufanya uovu"

Revelation 2:18

Taarifa ya Jumla:

Huu ni mwanzo wa ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa kanisa la Thiatra.

Thiatra

Hili ni jina la mji ndani ya Asia ambapo ni Uturuki ya leo.

Mwana wa Mungu

Hili ni jina muhimu la Yesu Kristo.

macho yake kama mwali wa moto

Macho yake yanaelezwa kuwa na mwanga kama mwali wa moto. "macho yake yaling'ara kama mwali wa moto"

nyayo kama shaba iliyosuguliwa

Shaba hung'arishwa kuifanya ingae na kurudisha mwanga. "Miguu yake iling'ara sana kama shaba iliyosuguliwa"

upendo wako na imani na huduma na uvumilivu wako thabiti

Hizi ni nomino dhahania ambazo zinaweza kutafsiriwa na vitenzi. "jinsi unavyopenda, kuamini, kuhudumu na kuvumilia kwa thabiti.

upendo wako na imani na huduma na uvumilivu wako thabiti

Maana ya mambo ya hivi vitenzi vinaweza kuweka bayana. "jinsi unavyonipenda na wengine, unavyoniamini, unavyohudumia wengine, na kustahamili tabu kwa uvumilivu".

Revelation 2:20

Lakini ninalo hili dhidi yako

"Lakini sikubali baadhi ya vitu ulivyofanya" au "Lakini nina hasira na wewe kwa sababu ya jambo ulilofanya".

mwanamke Yezebeli

Yesu alimzungumzia mwanamke mmoja kanisani mwao kana kwamba alikua Malkia Yezebeli kwa sababu alifanye vitendo vya dhambi kama vile alivyofanya Malkia Yezebeli zamani kabla ya huo wakati.

Nilimpa muda wa kutubu

"Nilimpa nafasi ya kutubu" au "nilisubiri atubu"

Revelation 2:22

Nitamtupa kwenye kitanda cha maradhi

Yeye kulazimika kulala kitandani itakua matokeo ya yesu kumfanya kuwa mgonjwa sana. "Nitamfanya alale kitandani akiumwa" au "nitamfanya aumwe sana"

na wale watendao uzinzi naye kwenye mateso makali

Yesu anazungumzia watu kuteseka kama kuwatupa katika mateso. "na nitawafanya watakaozini naye kuteseka sana"

Kuzini

"kufanya uzinzi"

hadi watakapotubu dhambi zao

"kama hawatatubu dhambi zake anazozifanya".

Nitawapiga wanawe wafe

"Nitawaua watoto wake"

watoto wake

Yesu alizungumzia wafuasi wake kama vile walikuwa watoto wake. "wafuasi wake" au "watu wanaofanya anachofundisha"

mawazo na mioyo

Neno "moyo" mara nyingi humaanisha hisia na tamaa. Haya mawazo mawili yaweza kutafsiriwa kama vitenzi. "nini ambacho watu wanawaza na kutaka".

Nitampa kila mmoja wenu

Huu ni udhahiri kuhusu adhabu na thawabu. "Nitawaadhibisha au kuwazawadia kila mmoja wenu"

Revelation 2:24

kwa wale wote msioshika fundisho hili

Kuamini fundisho inazungumziwa kama kulishika fundisho. "watu wote wasioamini fundisho hili"

fundisho hili

jina "fundisho" linaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "anachofunza"

mafumbo ya Shetani

"vitu vya kina afundishavyo Shetani"

vitu vya kina

Vitu vya siri huzungumziwa kama vile ni vya kina. "vitu vya siri"

baadhi huita mafumbo ya Shetani

Maana zinazowezekana ni 1) wale walioviita vitu vya kina walielewa kuwa vilitoka kwa Shetani au 2) watu wengine waliviita vitu vya kina lakini Yesu alichokua anasema ni kwamba ni vya kutoka kwa Shetani. "vitu vya Shetani, ambavyo baadhi ya watu huita vitu vya kina"

Revelation 2:26

Yule ashindaye

Hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa yule ambaye hatakubali kufanya uovu"

Atawatawala ... atawavunja vipande

Huu ni utabiri kutoka Agano la Kale kuhusu mfalme wa Israeli, lakini Yesu alimaanisha hapa kwa wale atakaowapa mamlaka juu ya mataifa.

Atawatawala kwa fimbo ya chuma

Kutawala kwa ukali kunazungumziwa kama kutawala kwa fimbo ya chuma. "Atawatawala kwa ukali kama vile anawapiga na fimbo ya chuma."

kama mabakuli ya udongo, atawavunja vipande vipande

Kuwavunja katika vipande ni picha inayoonesha 1) kuwateketeza watenda maouvu au 2)kuwashinda maadui. "Atawashinda kabisa maadui wake kama vile kuvunja vipande vipande mabakuli ya udongo."

Kama nilivyopokea kutoka kwa Baba yangu

Lugha zingine zinaweza kuhitaji kuonesha kilichopokelewa. Maana zinazowezekana ni 1)"Kama vile nilivyopokea mamlaka kutoka kwa Baba yangu" au 2) Kama nilivyopokea nyota ya asubuhi kutoka kwa Baba yangu.

Baba yangu

Hili ni jina muhimu la Mungu linaloeleza mahusiano kati ya Mungu na Yesu.

nitampa pia

Hapa inamaanisha yule atakaye shinda.

nyota ya asubuhi

Hii ni nyota inayoonekana asubuhi kabla ya kupambazuka. Ilikua pia ni ishara ya ushindi.

Mwenye sikio asikie

Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asikilize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"

Revelation 3

Ufunuo 03 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Sura ya 2 na ya 3 zinaunda kitenge kimoja. Sehemu hii mara nyingi hujulikana kama "barua saba kwa makanisa saba."Mtafsiri anaweza amua kuzitenganisha barua hizi moja kwa nyingine ili kuzitofautisha.

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 3:7

Dhana muhima katika sura hii.

Roho saba za Mungu

Maana halisi ya maneno haya haiko wazi. Kuna uwezekana kama hii inaashiria Roho Mtakatifu na nambari saba inaashiria "ukamilifu". Inawezekana pia kama inaashiria roho saba ambazo zinazunguka kiti cha enzi cha Mungu. Sio ya lazima kufafanua hili kwenye tafsiri.

Nyota saba

Kuna uwezekano kama hii inaashiria viongozi wa makanisa. (Tazama:Ufunuo 1:20)

Tamathali muhimu za usemi katika hii sura

Mfano

Wasomi wengine wanachukulia sura ya ya 2 na ya 3 kama mfano. Wanaelewa haya makanisa kama aina ya makanisa ama vipindi vya kihistoria vya kanisa.Ni vyema kutafsiri hii kama maelekezo ya makanisa ya kale katika miji hii. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Maneno,"Tazama, nasimama mlangoni na kubisha" ni mfano mungine inayoelezea utayari na kukubali kwake Yesu kumpokea mtu yeyote anayetubu na kumuamini. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#repent and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe)

"Kama una sikio, sikia kile Roho anawaambia makanisa"

Maneno haya ni mwito wa kutubu kwa watu walio ndani ya kanisa.

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Malaika wa makanisa saba"

Neno la Kigiriki "Malaika" linaweza pia kutafsiriwa kama "wajumbe."Kuna uwezekano hii inaashiria wajumbe ama viongozi wa makanisa haya saba.

"The words of the one who"

The verses with these words can be difficult to translate. They do not make complete sentences. You may need to add "These are" to the beginning of these verses. Also, Jesus used these words to speak of himself as if he were speaking of another person. Your language may not allow people to speak of themselves as if they were speaking of other people. Jesus began speaking in Revelation 1:17. He continues to speak through the end of Chapter 3.

<< | >>

Revelation 3:1

Taarifa ya Jumla:

Huu ni mwanzo wa ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa kanisa la Sardi.

Sardi

Hili ni jina la mji ndani ya Asia ambayo ni Uturuki ya leo.

roho saba

Namba saba ni alama ya ukamilifu na utimilifu. "Roho saba" humaanisha mojawapo kati ya Roho ya Mungu au roho saba zinazomtumikia Mungu.

nyota saba

Nyota hizi ni alama. Zinaonekana kuasharia wale malaika saba wa makanisa saba.

hai ... mfu

Kumtii na kumheshimu Mungu inazungumziwa kama kuwa hai; kutomtii na kutomheshimu inazungumziwa kama kuwa mfu.

Amka

Kuwa makini na hatari inazungumziwa kama kuamka. "Kuwa makini" au "kuwa mwangalifu"

kuimarisha yaliyosalia, lakini yako karibu kufa

Matendo mema yaliyofanywa na waumini wa Sardi yanazungumziwa kama vile yako hai lakini yako hatarini kufa. "kamilisha kazi iliyosalia au kile ulichokifanya hakitakua na maana" au "kama hautakamilisha ulichoanza kufanya, kazi yako ya nyuma itakua batili"

Revelation 3:3

yale uliyoyapokea na kusikia

Hii humaanisha neno la Mungu ambalo waliamini. "neno la Mungu mlilosikia na ukweli mlioamini"

usipoamka

Kuwa makina na hatari huzungumziwa kama kuamka. "Kuwa makini" au "Kuwa mwangalifu."

nitakuja kama mwivi

Yesu atakuja wakati watu hawatarajii kama vile mwizi ajavyo asipotarajiwa.

majina machache ya watu

Hii humaanisha watu wenyewe. "watu wachache"

hawakuchafua nguo zao

Yesu anazungumzia dhambi katika maisha ya mtu kama vile ni nguo chafu. "hawajafanya maisha yao yawe yenye dhambi kama nguo chafu"

Watatembea pamoja nami

Watu kawaida walizungumzia kuishi kama "kutembea."

wamevaa nguo nyeupe

Nguo nyeupe huashiria maisha masafi bila dhambi. "na watavikwa nguo nyeupe ambayo inaonesha waso ni wasafi"

Revelation 3:5

Yeye ashindaye

Hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa wale ambao hawatakubali kufanya uovu"

atavikwa mavazi meupe

Hii inaweza kutafsiriwa na kitenzi. "atavaa mavazi meupe" au " Nitampa ngu nyeupe"

nitalitaja jina lake

Hata taja jina lake tu bali atatangaza kuwa huyu ni mtu wake. "Nitatangaza kuwa ni mali yangu"

Baba yangu

Hili ni jina muhimu la Mungu linaloeleza uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

Mwenye sikio asikie

Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asikilize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"

Revelation 3:7

Taarifa ya Jumla:

Huu ni mwanzo wa ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa kanisa la Filadefia.

ufunguo wa Daudi

Yesu anazungumzia mamlaka yake kuamua nani aingie katika ufalme wake kama vile ni ufunguo wa Mfalme Daudi.

hufungua na hakuna afungaye

"anafungua mlango wa ufalme na hakuna awezaye kuufunga.

hufunga na hakuna awezaye kufungua

"hufunga mlango na hakuna awezaye kuufungua"

nimekuwekea mbele yako mlango uliofunguliwa

"Nimekufungulia mlango"

jina langu

neno "jina" mara nyingi hutumika kuonesha mtu mwenye hilo jina. "mimi"

Revelation 3:9

sinagogi la Shetani

Watu wanaokusanyika kumtii au kumtukuza Shetani wanazungumziwa kama sinagogi, mahali pa wayahudi pa kuabudu na kufundishia.

kusujudu

Hii ni ishara ya unyenyekevu, sio kuabudu. "Sujudu kwa unyenyekevu"

mbele ya miguu yako

"mbele yako"

watajua

"watajifunza" au "watakiri"

nitakulinda pia katika saa ya kujaribiwa

"nitakutunza pia katika saa ya kujaribiwa"

saa ya kujaribiwa

"muda wa kujaribiwa." Hii inaweza kumaanisha "wakati ambapo watu watajaribu kukufanya usinitii.

inakuja

Iliyo siku za usoni inazungumziwa kama ijayo.

Naja upesi

Inaeleweka kuwa anakuja ili ahukumu. "Ninakuja kuhukumu hivi punde"

Shikilia sana

"Endelea kuamini"

taji

Taji ilikua ni shada ambalo asili yake ilikua ya matawi ya mizeituni au majani ya laurusi ambayo yaliweka kwenye kichwa cha mwanariadha mshindi.

Revelation 3:12

yeye ashindaye

hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa wale ambao hawatakubali kufanya uovu"

nguzo katika hekalu la Mungu wangu

"Nguzo" inaonesha kuwa sehumu muhumi na ya kudumu katika ufalme wa Mungu. "imara kama nguzo katika ufalme wa Mungu wangu"

Mwenye sikio asikie

Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asikilize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"

Revelation 3:14

Taarifa ya Jumla:

Huu ni ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa kanisa la Laodikia.

Maneno yake aliye Amina

Hape "aliye Amina" ni jina la Yesu Kristo. Athibitisha ahadi za Mungu kwa kusema amina.

mtawala juu ya uumbaji wa Mungu

Maana zinazowezekana ni 1)"yule ambaye antawala vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu" au 2)"yule ambaye Mungu aliumba vitu vyote kupitia kwake."

wewe si baridi wala moto

"Baridi" na "moto" inaonesha kuvutiwa kwa mambo ya kiroho au kumpenda Mungu kwa pande mbili tofauti kabisa. Kuwa "baridi" ni kuwa kinyume kabisa na Mungu na kuwa wa "moto" ni kuwa na uchu wa kumtumikia.

vuguvugu

"joto kidogo." Hii humuelezea mtu aliye na hamu ndogo ya mambo ya kiroho.

nitakutapika utoke kinywani mwangu

Kuwakataa inazungumziwa kama kuwatapika kutoka kinywani. "Nitawakataa kama vile nitemavyo maji ya uvuguvugu."

Revelation 3:17

wewe ni duni sana, wakuhuzunikiwa, maskini, kipofu na uchi

Yesu anazungumzia hali yao ya kiroho kama vile anazungumzia hali yao ya kimwili. "Nyie ni kama watu duni sana, wakusikitisha, maskini, vipofu, na uchi."

Nunua kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto

Dhahabu iliyo safishwa katika moto ni safi na ya dhamani sana. Hapa wokovu ambao Yesu anawapa binadamu unazungumziwa kama dhahabu. "Pokeeni kutoka kwangu kilicho cha dhamani zaidi kama vile ni dhahabu iliyotakaswa katika moto."

upate kuwa tajiri

Hii humaanisha utajiri wa kiroho, kuishi maisha yenye dhamani sana mbele za Mungu. "wawe matajiri kiroho" au "aishi maisha ya dhamani zaidi"

nguo nyeupe za kumetameta

Nguo nyeupe zinaonesha utakatifu. "utakatifu kama nguo nyeupe"

upate kuona

Kuona inamaanisha kuelewa ukweli.

Revelation 3:19

kuwa mkweli na utubu

"kuwa makini na utubu"

nasimama katika mlango na kubisha

Yesu anazungumzia watu kutaka kuhusiana naye kama vile wanataka kumkaribisha nyumbani mwao. "Mimi ni kama yule asimamaye mlangoni akibisha hodi"

na kubisha

Watu hubisha hodi wakitaka kukaribishwa kwenye nyumba ya mtu. "na ninataka mniruhusu niingie ndani"

asikiaye sauti yangu

Msemo wa "sauti yangu" huonesha Yesu akizungumza. "anayesikia nikizungumza" au "anayesikia nikiita"

nitakuja na kuingia nyumbani kwake

Lugha zingine zinaweza kupendelea kitenzi cha "nenda". "Nitaenda nyumbani kwake"

na kula naye

Hii huonesha kuwa pamoja kama marafiki.

Revelation 3:21

Kauli unganishi:

Huu ni mwisho wa ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa makanisa saba.

Yeye ashindaye

hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa wale ambao hawatakubali kufanya uovu"

ukaa chini pamoja nami juu ya kiti changu cha enzi

Kukaa katika kiti cha enzi humaanisha kutawala. "kutawala pamoja nami" au "kuketi na mimi katika kiti changu cha enzi na kutawala na mimi"

Baba yangu

Hili ni jina muhimu la Mungu linaloeleza mahusiano kati ya Mungu na Yesu.

Mwenye sikio asikie

Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asikilize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"

Revelation 4

Ufunuo 04 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 4:8,11

Sura hii inaanzisha sehemu iliyobaki ya kitabu cha Ufunuo na ni tofauti na sura tatu za kwanza. Inaelezea kufumbuliwa kwa picha Yohana anaona kwenye maono yake.

Dhana muhimu katika sura hii

Utukufu

Sura hii yote ni picha inayofafanua onyesho fulani mbinguni ambapo kila kitu kinampatia Mungu utukufu kila wakati. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#heaven and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#glory)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Mfano

Ufafanuzi wa mtu akaliaye kwenye kiti cha enzi una mifano nyingi sana. Tamaduni nyingi hazina haya mawe maalum ya thamani na kuna uwezekano yanaashiria kitu fulani chenye umuhimu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-simile and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-unknown)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii.

Picha ngumu

Kuna picha nyinga ambazo zisizo wezekana kuwa ngumu ama zisizoezekana.Kwa mfano,mwanga utokapo kwenye kiti cha enzi, taa ambazo ni roho saba za Mungu "ama mfano wa bahari iliyo mbele ya kiti cha enzi.Ni vyema kuacha ugumu huu kubaki katika tafsiri yako. (Tafsiri: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

<< | >>

Revelation 4:1

Taarifa ya Jumla:

Yohana aanza kueleza maono yake ya kiti cha enzi cha Mungu.

Baada ya mambo haya

"baada ya vitu ambavyo Yohana ametoka kuona"

mlango ulikuwa umefunguliwa mbinguni

Msemo huu humaanisha uwezo ambao Mungu alimpa Yohana kuona mbinguni, angalau kwa njia ya maono.

ikizungumza nami kama tarumbeta

Jinsi sauti ilikuwa kama tarumbeta inaweza kuainishwa vizuri. "kuzungumza na mimi kwa sauti kama sauti ya tarumbeta"

tarumbeta

Hii humaanisha chombo cha kutengeneza muziki au kuwaita watu kwa ajili ya tangazo au mkutano.

nilikuwa katika Roho

Yohana anazungumzia kuvutwa na Roho ya Mungu kana kwamba alikua katika Roho. "kushawishika na Roho" au "Roho alinishawishi"

yaspi na akiki

Mawe ya thamani. Yaspi inawezekana ilikua nyeupe kama kioo

zumaridi

Jiwe la thamani la kijani

Revelation 4:4

wazee ishirini na wanne

wazee wanne -"wazee 24"

taji za dhahabu

Hizi zilikua kama mashada ya matawi ya mizeituni na majani ya laurusi zilizopondwa katika dhahabu. Taji za naamna hii za majani walipewa wanariadha washindi vichwani mwao.

miale ya radi

Mwanga unaotokea wakati radi ikipiga.

muungurumo ya radi

Hii ni miungurumo ya sauti ambayo radi husababisha.

roho saba

Namba saba ni alama ya ukamilifu na utimilifu. "Roho saba" humaanisha mojawapo kati ya Roho ya Mungu au roho saba zinazomtumikia Mungu.

Revelation 4:6

bahari ya kioo

Inaainisha wazi jinsi ilivyokua kama kioo au bahari. Maana zinazowezekana ni 1) bahari linazungumziwa kama vile ni kioo. "bahari lililo laini kama kioo" au 2) kioo kinazungumziwa kama vile ni bahari. "kioo kilichosambazwa kama bahari"

kama kioo

Inaainishwa wazi jinsi ilivyokua kama kioo. "nyeupe kama kioo"

Katikati ya kiticha enzi na kukizunguka

"Hapo hapo karibu na kiti cha enzi" au "Karibu na kiti cha enzi na kukizunguka"

wenye uhai wanne

"viumbe wanne" au "vitu vinne vyenye uhai"

Revelation 4:7

Kiumbe hai

"kiumbe hai" au "kitu hai".

wamejaa macho juu na chini

Juu na chini ya kila bawa kulijaa macho.

atakayekuja

Aliyepo wakati wa usoni azungumziwa kama ajaye

Revelation 4:9

aliyekuwa ameketi kwenye hicho kiti cha enzi, yeye aishiye milele

Huyu ni mtu mmoja. Yule ambaye ameketi kwenye kiti cha enzi anaishi milele na milele.

milele na milele

Maneno haya yana maana moja na yanarudiwa kuonesha msisitizo. "milele yote"

wazee ishirini na wanne

wazee wanne -"wazee 24"

walisujudu wenyewe

Kulala chini kwa kutazama ardhi.

kutupa chini taji zao mbele ya kiti cha enzi

Hizi zilikua mfano wa taji za matawi ya mizeituni au majani ya laurusi yaliopondwa katika dhahabu. Mifano ambayo iliundwa kwa majani walipewa wanariadha washindi kuvaa kichwani. Wazee walikua wakionesha kuwa wanatii utawala wa Mungu. "walitupa chini mataji yao mbele ya kiti cha enzi kuonesha kumtii yeye"

Bwana wetu na Mungu wetu

"Bwana wetu na Mungu." Huyu ni mtu mmoja yule ambaye ameketi kwenye kiti cha enzi.

kupokea utukufu na heshima na nguvu

Hivi ni vitu ambavyo Mungu anavyo siku zote. Kusifiwa kuwa navyo inazungumziwa kama kuvipokea. "kusifiwa kwa utukufu wake, heshima, na nguvu" au "kwa kila mmoja kumsifu kwa sababu yeye ni mtukufu, mwenye heshima, na mwenye nguvu.

Revelation 5

Ufunuo 05 maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 4:8, 11

Dhana muhimu katika sura hii

Kitabo kilichofungwa na mihuri

Katika kitabu kilichofungwa na mihuri kimeandikwa ujumbe uliofichwa ambao unangojelewa kusomwa. Kitabu hiki kinaweza kusomwa tu na mtu aliye na mamlaka ya kukifungua.

Wazee ishirini na wanne

Labda maneno haya yanaashiria viongozi wa kanisa lakini utambulisho ya wazee ishirini na wanne sio na hakika. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Sala za Kikristo

Sala za Wakristo zimeunganishwa na ubani. Sala za Wakristo zina harufu nzuri kwa Mungu. Mungu anafurahi wakati Wakristo wanapoomba.

Roho saba za Mungu

Maana halisi ya maneno haya haiko wazi. Kuna uwezekano kama ni mfano inayoashiria Roho Mtakatifu na nambari saba ikiashiria "ukamilifu." Kuna uwezekano kwamba pia si mfano, lakini inaashiria roho saba zinazozunguka kiti cha enzi cha Mungu.

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Mfano

"Simba wa kabila la Yuda" na "mzizi wa Daudi" inaashiria Yesu. Hizi ni mifano inayotumika kama vyeo vya Yesu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

<< | >>

Revelation 5:1

Kauli unganishi:

Yohana anaendelea kueleza alichokiona katika maono ya kiti cha enzi cha Mungu.

Kisha nikaona

"Baada ya kuona hivyo vitu ,nikaona"

yule aliyekuwa amekaa katika kiti cha enzi

Hii ni sawa sawa na "moja" kama 4:1

gombo lililoandikwa mbele na nyuma

"gombo linye maandishi mbele na nyuma"

lilikuwa limetiwa mihuri saba

"lilikuwa limefungwa na mihuri saba"

Nani astahiliye kulifungua gombo na kuzivunja mihuri yake?

Mtu huyu atahitaji kuivunja mihuri ili kuifungua gombo. "Nani anayestahili kuvunja mihuri na kufungua gombo?"

Nani astahiliye kulifungua gombo na kuzivunja mihuri yake?

Hii inaweza kutafsiriwa kama amri. "Acha yule ambaye anastahili kufanya hivi aje avunje mihuri na kuifungua gombo!"

Revelation 5:3

mbinguni au duniani au chini ya dunia

Hii inamaanisha mahali pote: Mahali ambapo Mungu na malaika huishi, mahali ambapo watu na wanyama huishi, na mahali ambapo wale waliokufa walipo.

Tazama

"Sikiliza" au "kuwa makini na jambo nilotaka kukuambia"

Simba wa kabila ya Yuda

Hili ni jina la mtu kutoka kabila la Yuda ambaye Mungu aliahidi atakuwa mfalme mkuu. "Yule aitwaye Simba wa kabila la Yuda" au "Mfalme aitwaye Simba wa kabila la Yuda"

Simba

Mfalme anazungumziwa kama vile yeye ni simba kwa sababu simba ni mnyama imara sana.

shina la Daudi

Huyu ni mzawa wa kizazi cha Daudi ambaye Mungu aliahidi atakuwa mfalme mkuu. "yule aitwaye shina la Daudi"

shina la Daudi

Huyu mzawa anazungumziwa kama vile familia ya Daudi ni mti na yeye ni shina lake.

Revelation 5:6

Taarifa ya Jumla:

Mwanakondoo aonekana katika chumba cha kiti cha enzi

mwanakondoo

"mwanakondoo" ni mtoto wa kiume wa kondoo. Hapa hutumika kuashiria kuwa ni Kristo.

roho saba za Mungu

Namba saba ni alama ya ukamilifu na utimilifu. "Roho saba" humaanisha mojawapo kati ya Roho ya Mungu au roho saba zinazomtumikia Mungu.

zilizotumwa duniani kote

Hii inaweza kutafsiriwa na kitenzi. "kwamba Mungu alizozituma kote duniani

Akaenda

Akakaribia kiti cha enzi. Lugha zingine zitatumia kitenzi "njoo". "alikuja"

Revelation 5:8

Mwanakondoo

"mwanakondoo" ni mtoto wa kiume wa kondoo. Hapa hutumika kushiria kuwa ni Kristo.

wazee ishirini na wanne

wazee wanne -"wazee 24"

wakainama hadi nchi

Kulala chini kwa kutazama ardhi.

Kila mmoja

Maana zinazowezekana ni 1)"kila mzee ni kiumbe hai" au 2)"kila mzee"

bakuli ya dhahabu iliyojaa uvumba ambayo ni maombi ya waamini

Uvumba hapa ni alama ya maombi ya waumini wa Mungu.

Revelation 5:9

Kwa kuwa ulichinjwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kwa kuwa waliwachinja" au "kwa kuwa watu waliwaua"

kuchinjwa

Hii inaweza kumaanisha kutolewa uhai kwa ajili ya sadaka

na kwa damu yako

Kwa sababu damu huashiria uhai wa mtu, kupoteza damu huashiria kufa. Hii inaweza kumaanisha "kwa kifo chako" au "kwa kufa kwako."

ukamnunulia Mungu watu

"Ulinunua watu ili wawe wa Mungu" au "ulilipia gharama ili watu wawe wa Mungu"

wa kila kabila, lugha, jamaa na taifa

Hii humaanisha watu kutoka kila kabila.

Revelation 5:11

elfu kumi kwa elfu kumi na elfu kwa elfu

Hii huonesha kuwa hii ni idadi kubwa sana ya watu. "mamilioni" au "maelfu mengi sana kuhesabu"

Astahili mwanakondoo

"Mwanakondoo anastahili"

kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu, na sifa

Hivi ni vitu ambavyo Mwanakondoo anavyo. Kusifiwa navyo inazungumziwa kama kuvipokea. "kusifiwa kwa utukufu wake, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu."

Astahili .. kupokea ... sifa

Hii inamaanizha kuwa anastahili kusifiwa na kila mtu.

Revelation 5:13

mbinguni na duniani na chini ya nchi

Hii inamaanisha mahali pote: Mahali ambapo Mungu na malaika huishi, mahali ambapo watu na wanyama huishi, na mahali ambapo wale waliokufa walipo.

Kwake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi na kwa mwanakondoo, kuwe sifa, heshima, utukufu

Kitenzi "toa" kinaweza kutumika kuonesha jinsi sifa, heshima na utukufu "ni" kwake yeye aliye katika kiti cha enzi na kwa Mwanakondoo. "Tunapaswa kumpa sifa, heshima, na utukufu yule aketiye kwenye kiti cha enzi na kwa Mwanakondoo"

na nguvu ya kutawala milele na milele

Kitenzi "kuwa" kinaweza kutumika kuonesha jinsi gani nguvu inaweza kuwa kwake aliye kwenye kiti cha enzi na kwa Mwanakondoo. "na wawe na nguvu kutawala milele na milele"

Revelation 6

Ufunuo 06 Maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Mfano wa hasira ya Mungu katika sura hii imewekwa kutia uoga kwa wale watakayosikia maneno haya. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#fear)

Dhana muhimu katika sura hii

Mihuri saba

Kuna kutoelewana kuhusu jinsi mihuri hii imeambatanishwa kwenye kitabu.Ingekuwa ya kueleweka iwapo iliwekwa upande upande lakini kitabu kingeonyesha kilichomo baada ya muhuri wa mwisho kuvunjwa. Si hivyo sura hii inafafanua kitabu kwa sababu kila muhuri unafunua hukumu fulani. Inaaminika pia kwamba kutokuwepo kwa muhuri wa saba kunafunua baragumu saba za hukumu.(Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#judge na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Bei Inaongezeka

Bei ya vitu fulani vitaongezeka kwa gahfla. Watu hawataweza kununua vitu wanavyohitaji kwa kuishi. Hii ndio inaitwa "mfumuko."

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Yule Mwana-Kondoo

Hii inaashiria Yesu. Katika sura hii, inatumika pia kama cheo cha Yesu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

Mifano

Mwandishi anatumia aina nyingi za mifano. Hii ni kwa sababu anajaribu kufafanua picha ya vitu anavyoona katika maono. Kwa hivyo, analinganisha picha hizi kwenye maono na mambo ya kawaida. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-simile)

<< | >>

Revelation 6:1

Kauli unganishi:

Yohana aendelea kueleza matukio yaliotokea mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Mwanakondoo aanza kufungua mihuri na gombo.

Njoo!

Hii ni amri kwa mtu mmoja, inavyoonekana ni mpanda farasi mweupe anayezungumziwa kwenye mstari wa 2.

akapewa taji

Hii aina ya taji ni mfano wa shada la matawi ya mizeituni na majani laurusi ambazo huwezekana zilipondwa kwenye dhahabu. Mifano ambayo iliundwa kwa majani ilipewa kwa wanariadha washindi kuvaa vichwani mwao. Hii inaweza kutafsiriwa na kitenzi. "alipokea taji" au "Mungu alimpa taji"

Taji

Hili lilikua shada la matawi ya mzeituni na majani ya laurusi kama mashada ambayo wanariadhaa washindi walivyopokea kipindi cha Yohana.

Revelation 6:3

muhuri wa pili

"muhuri unaofuata" au "muhuri namba mbili"

mwenye uhai wa pili

"mwenye uhai afuataye" au "mwenye uhai namba mbili"

mwekundu kama moto

"alikua mwekundu kama moto" au "alikua mwekundu wa kungaa"

Aliye mpanda alipewa ruhusa

Hii inaweza kuelezwa kama kitenzi. "Mungu alimpa ruhusa aliyempanda" au "aliyempanda alipokea ruhusa"

Huyu aliye mpanda alipewa upanga mkubwa

Hii inaweza kuelezwa kama kitenzi. "Huyu aliyempanda alipokea upanga mkubwa" au "Mungu alimpa upanga mkubwa yule aliye mpanda."

Revelation 6:5

muhuri wa tatu

"muhuri unaofuata" au "muhuri namba tatu"

mwenye uhai wa tatu

"mwenye uhai afuataye" au "mwenye uhai namba tatu"

mizani

Chombo kinachotumika kupima uzito wa vitu.

kibaba cha ngano kwa dinari moja

Lugha zingine zingependa kutumia kitenzi kama "gharimu" au "nunua" katika sentesi. "Kibaba cha ngano sasa kina gharimu dinari moja" au "Nunua kibaba cha ngano kwa dinari moja." Kulikuwa na ngano chache kwa watu wote kwa hiyo bei yake ilikuwa juu sana.

kibaba cha ngano

Hii huonesha kipomo bayana ambacho kilkuwa kama lita moja. "lita moja" au "bakuli moja"

dinari moja

Hii sarafu ilikua na dhamani ya mshahara wa siku nzima. "sarafu moja ya shaba" au "malipo ya siku moja ya kazi"

Lakini usiyadhuru mafuta na divai

Kama mafuta na divai yangedhuriwa, basi yangekua machache kwa ajili ya watu kununua na kwa hiyo bei zake zingepanda juu.

mafuta na divai

Hii misemo inawezekana kumaanisha uvunaji wa mafuta ya mizeituni na uvunaji wa zabibu.

Revelation 6:7

muhuri wa nne

"muhuri unaofuata" au "muhuri namba nne"

mwenye uhai wa nne

"mwenye uhai afuataye" au "mwenye uhai namba nne"

kijivu

"kijivu". Hii ni rangi ya maiti kwa hiyo ni rangi ya kuashiria kifo.

robo ya nchi

robo moja ya nchi - Nchi hapa inaonesha watu wa duniani. "robo moja" ya watu duniani"

upanga

Upanga ni silaha na hapa inaashiria vita.

na kwa wanyama wa mwitu katika nchi

Hii inamaanisha kwamba mauti na kuzimu zitasababisha wanyama wa mwitu kuua watu.

Revelation 6:9

muhuri wa tano

"muhuri unaofuata" au "muhuri namba tano"

chini ya madhabahu

Hii inaweza kuwa "katika kitako cha madhabahu."

wale waliokuwa wameuawa

Hii inaweza kutafsiriwa na kitenzi. "wale ambao wameuwawa na wengine"

neno la Mungu na kutokana na ushuhuda

Maana zinazowezekana ni 1) ushuhuda ni ushahidi wa Mungu juu ya ukweli wa neno lake (kama inavyooneshwa kwenye UDB), au 2) ushuhuda ni ushahidi wa aliye amini juu ya ukweli wa neno la Mungu.

walioushika

Kuamini neno la Mungu na ushuhuda wake vinazungumziwa kama vitu ambavyo vinaweza kushikwa mikononi. "ambavyo waliamini"

ulipiza kisasi damu yetu

Neno damu hapa linaonesha vifo vyao. "adhibu waliotuuwa"

hata itakapotimia ... ambao watauawa

Hii inaonesha kuwa Mungu ameshaamua kwamba kuna idadi ya watu ambayo watauwawa na adui zao.

watumishi wenzao na ndugu zao wa kike na wa kiume

Hili ni kundi la watu linalofafanuliwa kwa njia mbili: kama watumishi na kaka na dada. "Kaka zao na dada zao wanaomtumikia Mungu pamoja nao" au "waumini wenzao wanaomtumikia Mungu pamoja nao"

ndugu zao wa kiume na wa kike

Wakristo wanazungumziwa kuwa kama ndugu wa kiume na wa kike. "Wakristo wenzao" au "waumini wenzao"

Revelation 6:12

muhuri wa sita

"muhuri unaofuata" au "muhuri namba sita"

jeusi kama nguo ya magunia

Wakati mwingine nguo za magunia zilitengenezwa na nywele nyeusi. Watu walivaa magunia walipokuwa wakiomboleza. Picha ya magunia inapaswa kuwaongoza watu kuwaza mauti na kuomboleza. "nyeusi kama nguo za kuomboleza"

kama damu

Picha ya damu inapaswa kuwaongoza watu kuwaza mauti. Jinsi ilivyokuwa kama damu inaweza kuainishwa vizuri. "nyekundu kama damu"

kama mtini upukutishavyo matunda yake ya wakati wa baridi unapotikiswa na kimbunga

"kama jinsi matunda mabichi yanvyoanguka kwa wingi kutoka mtini pale upepo mkali unapotikiswa."

Anga ilitoweka kama gombo lililoviringishwa

Kawaida anga lilifikiriwa kuwa bati gumu la chuma lakini sasa lilikuwa dhaifu kama kipande cha kartasi ambacho kinachanwa kirahisi na kukunjwa.

Revelation 6:15

majemadari

Hili neno humaanisha wapambanaji wanao amuru vitani.

mapango

Mashimo makubwa kando kando ya mlima.

uso wake

Hii humaanisha Mungu. Hawakutaka Mungu awaone na kuwaadhibu.

uso

Hapa "uso" unatumilia kuonesha wazo la "uwepo."

siku kuu ya gadhabu yao imewadia

Siku ya ghadhabu yao humaanisha ule wakati ambapo watu waovu wataadhibiwa. "hiki ndicho kile kipindi kibaya watakapowaadhibu watu"

imewadia

Iliyopo sasa inazungumziwa kama vile imefika.

gadhabu yao

"Yao" humaanisha yule aliye katika kiti cha enzi na Mwanakondoo.

nani awezaye kusimama?

Kupona au kuendelea kuwa hai vinazungumziwa kama kusimama. Hili swali linatumika kuonesha huzuni yao kuu na uuoga kwamba hakuna mtu awezaye kupona pale Mungu atakopowaadhibu. "Hakuna awezaye kupona"

Revelation 7

Ufunuo 07 Maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Wasomi wengi wanaamini kwamba nusu ya kwanza ya sura hii inahusu uamusho mkuu miongoni mwa Waisraeli ambapo watu 144,000 watakuja kumuamini Yesu. Nusu ya pili ya sura hii inatuelezea uamusho mkuu miongoni mwa watu wa Mataifa ambapo watu wasiohesabika watakuja kumuamini Yesu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 7:5-8, 15-17

Dhana muhimu katika sura hii

Kuabudu

Watu kwenye sura hii wanaitikia matukio haya kwa kutubu na kuabudu.Hiki ndicho kiitikio cha kweli cha habari iliyoko katika kitabu hiki.(Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#reveal, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#repent na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#worship)

Dhiki kuu

Hiki ni kipindi ambacho watu wa duniani wataadhibiwa vikali na Mungu. Kuna kutoelewana kuhusu kipindi hiki lakini wasomi wengi wanaamini kwamba hiki ni kipindi cha nusu ya mwisho ya miaka saba ya dhiki kuu inayotabiriwa katika Ufunuo 4-19 na katika sehemu zinginezo za maandiko.

Mifano muhimu ya usemi

Mwanakondoo

Hii inaashiria Yesu.Katika sura hii, inaashiria pia cheo cha Yesu.(Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

<< | >>

Revelation 7:1

Taarifa ya Jumla:

Yohana anaanza kueleza maono ya watumishi 144,000 wa Mungu waliotiwa muhuri. Hii inatendeka katikakati ya pale ambapo Mwanakondoo anafungua muhuri wa sita na muhuri wa saba.

kona nne za dunia

Dunia inazungumziwa kama vile ni tambarare na mraba kama kartasi. Usemi "kona nne" humaanisha kaskazini, kusini, mashariki na magharibi.

muhuri wa Mungu aliye hai

Neno "muhuri" hapa humaanisha kifaa kinachotumika kuweka alama katika muhuri wa nta. Na hapa, hiki kifaa kitatumika kuweka alama katika watu wa Mungu. "alama" au "stampu"

tumekwishaweka muhuri katika paji za vichwa

Neno "muhuri" hapa linamaanisha alama. Hii alama inaonesha kwamba hawa ni watu wa Mungu na atawalinda. "weka alama katika paji za vichwa"

paji za vichwa

Paji la kichwa ni juu ya uso, juu ya macho.

Revelation 7:4

waliotiwa muhuri

Hii inaweza kusemwa kama kitenzi. "wale ambao wamewekwa alama na malaika wa Mungu"

144,000

"watu laki moja na elfu arobaini na nne"

Elfu kumi na mbili kutoka kabila

"12,000 kutoka katika kabila"

Revelation 7:7

Kauli unganishi:

Hii inaendeleza orodha ya watu wa Israeli waliowekewa muhuri.

Revelation 7:9

Taarifa ya Jumla:

Yohana anaanza kueleza maono ya pili kuhusu umati ukimsifu Mungu. HIli ni kundi tofauti la watu na wale 144,000 waliotiwa muhuri. Hii pia inachukua nafasi kati ya Mwanakondoo alipofungua muhuri wa sita na wa saba.

umati mkubwa

"kundi kubwa" au " idadi kubwa ya watu"

kanzu nyeupe

Hapa rangi "nyeupe" inaashiria usafi.

Wokovu ni kwa

"Wokovu unatoka kwa"

Wokovu ni kwa ... Mwanakondoo

walikuwa wakimsifu Mungu na Mwanakondoo. Nomini "wokovu" inaweza kuelezwa na kitenzi "kuokoa." "Mungu wetu aketiye katika enzi, na Mwanakondoo wametuokoa!"

Revelation 7:11

Malaika wote ... wenye uhai

"Malaika wote walisimama kuzunguka kiti cha enzi pamoja na wazee na wenye uhai wanne.

viumbe wenye uhai wanne

Hawa ni viumbe wanne waliotajwa katika 4:6

wakainama chini ardhini na wakaweka nyuso zao juu ya ardhi

"walisujudu"

Sifa, utukufu ... kwa Mungu wetu

"Mungu wetu anastahili sifa zote, utkufu, hekima, shukrani, heshima, uwezo na nguvu"

Sifa, utukufu ... shukurani, heshima ... viwe kwa Mungu wetu

Kitenzi "toa" inaweza kutumika kuonesha jinsi gani sifa, utukufu, na heshima "niza" Mungu. "Tunapaswa kumpa sifa , utukufu, shukrani, na heshima Mungu wetu"

hekima ... uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu

"Mungu wetu ana hekima yote, uwezo na nguvu"

milele na milele

Haya maneno mawili yanamaana moja na yanasisitiza kuwa sifa haitaisha.

Revelation 7:13

waliovaa kanzu nyeupe

Hizi kanzu nyeupe zilionesha kuwa ni watakatifu.

waliotoka katika dhiki kuu

"wamepona katika dhiki kuu" au "wamepita katika dhiki kuu"

dhiki kuu

"kipindi cha mateso makubwa" au "kipindi ambacho watu watateseka vibaya sana"

Wamezifua kanzu zao na kuzifanya nyeupe kwa damu ya Mwanakondoo

Kufanywa mtakatifu na damu ya Mwanakondoo inazungumziwa kama kufua kanzu zao na damu yake. "Wamefanywa watakatifu kwa kufua nguo zao katika damu yake"

Wamezifua kanzu zao na kuzifanya nyeupe kwa damu ya Mwanakondoo

Neno "damu" inatumika kuonesha kifo cha Mwanakondoo. Kifo chake kinaweza kuzungumziwa vizuri. "Wamefanywa watakatifu kwa kufua nguo zao katika kifo chake"

Revelation 7:15

Kauli Unganishi:

Mzee aendelea kuzungumza na Yohana.

wako ...yao ... wao

Hizi zote zinamaanizha wale watu waliotoka katika Dhiki Kuu.

usiku na mchana

Sehemu hizi mbili na siku zinatumika pamoja kumaanisha "wakati wote" au " bila kukoma"

atasambaza hema yake juu yao

"ataweka hema yake juu yao." Kuwalinda inazungumziwa kama kuwapa hifadhi ya kuishi. "atawahifadhi" au "atawalinda"

Jua halitawachoma

Joto la jua linalinganishwa na adhabu inayosababisha watu wateseke. "Jua halitawachoma" au "Jua halitawadhoofisha"

Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi

"Mwanakondoo anayesimama katikati ya eneo ya kiti cha enzi" au "Mwanakondoo aliye katika kiti cha enzi"

Kwa kuwa Mwanakondoo ... atakuwa mchungaji wao

Wazee wanamzungumzia Mwanakondoo kuwajali watu wake kama mchungaji anavyojali kondoo wake. "Kwa kuwa Mwanakondoo ... atakuwa kama mchungaji kwao" au " Kwa kuwa Mwanakondoo ... atawajali kama mchungaji anavyojali kondoo wake"

atawaongoza katika chemchemi ya maji ya uzima

Wazee wanakizungumzia kinachowapa uhai kama vile ni chemchemi ya maji safi. "Atawaongoza kama mchungaji awaongozavyo kondoo wake kwenye maji masafi" au "atawaongoza kuelekea maishani kama mchungaji anavyowaongoza kondoo wake kuelekea kwe maji masafi"

Mungu atafuta kila chozi katika macho yao

Machozi hapa yanawakilisha huzuni. "Mungu atafuta huzuni yao kama vile anafuta machozi yao" au "Mungu atawasababisha wasiwe na huzuni tena"

Revelation 8

Ufunuo 08 Maelezo ya jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Mihuri saba

Kuna kutoelewana kuhusu jinsi mihuri hii imeambatanishwa kwenye kitabu.Ingekuwa ya kueleweka iwapo iliwekwa upande upande lakini kitabu kingeonyesha kilichomo baada ya muhuri wa mwisho kuvunjwa. Hivi sivyo sura hii inafafanua kitabu kwa sababu kila muhuri unafunua hukumu fulani. Inaaminika pia kwamba kutokuwepo kwa muhuri wa saba kunafunua baragumu saba za hukumu.(Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#judge na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Mifano muhimu ya usemi

Sauti ya kupita

Sauti ya kupita imetumika mara nyingi katika sura hii kuficha utambulisho wa anayefanya hilo tendo. Itakuwa ngumu kuakilisha hili iwapo lugha ya mtafsiri haina sauti ya kupita. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-activepassive)

Mifano

Mwandishi anatumia mifano nyingi. Hii ni kwa sababu anajaribu kufafanua mifano anayoona kwenye maono. Kwa hivyo analinganisha mifano katika maono haya na vitu vya kawaida. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-simile)

<< | >>

Revelation 8:1

Kauli Unganishi:

Mwanakondoo afungua muhiri wa saba.

muhuri ya saba

Huu ni muhuri wa mwisho katika ukurasa. "muhuri unaofuata" au " muhuri wa mwisho" au "muhuri namba saba"

wakapewa tarumbeta saba

Wote walipewa tarumbeta moja. Maana zinazowezekana ni 1) "Mungu aliwapa tarumbeta saba" au 2) "Mwanakondoo aliwapa tarumbeta saba"

Revelation 8:3

autoe

"autoe uvumba kwa Mungu kwa kuuchoma"

mkononi mwa malaika

Hii inamaanizha bakuli katika mkono wa malaika. "bakuli katika mkono wa malaika"

akalijaza moto

Neno "moto" hapa inaweza kumaanisha kuchoma makaa. "akalijaza na makaa yanayowaka" au " akalijaza na makaa ya moto"

Revelation 8:6

Taarifa ya Jumla:

Malaika saba wapiga tarumbeta saba mmoja baada ya mwingine.

Vikatupwa chini katika nchi

"Malaika alitupa mvua ya mawe na moto uliochanganyikana na damu chini duniani."

theluthi moja yake iungue, theluthi moja ya miti ikaungua na nyasi zote za kijani zikaungua

"iliunguza theluthi moja ya nchi, theluthi moja ya miti na majani yote ya kijani."

Revelation 8:8

Malaika wa pili

"Malaika afuataye" au "Malaika namba mbili"

na kitu kama mlima mkubwa uliokuwa unaungua kwa moto ukatupwa

"malaika akatupa kitu kama mlima mkubwa unaoungua moto"

Theluthi moja ya bahari ikawa damu

"Ilikuwa kama bahari iligawanywa katika sehemu tatu and sehemu moja ikawa damu"

ikawa damu

Maana zinazowezekana ni 1)"ikawa nyekundu kama damu" au 2) ilikua damu kweli kweli.

theluthi moja ya viumbe hai katika bahari vikafa

"ilikuwa kama vile viumbe vyote baharini viligawanya katika makundi matatu, na viumbe vyote katika kundi moja vikafa."

viumbe hai katika bahari

"vitu vinavyoishi baharani" au "samaki na wanyama wengine walioishi baharini"

Revelation 8:10

na nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, ikimulika kama kurunzi

"na nyota kubwa uliowaka kama tochi ilianguka toka mbinguni." Moto wa ile nyota kubwa ulifanana na moto wa tochi

tochi

kijiti kilichowashwa moto upande moja ilikutoa mwanga

Jina la nyota ni Pakanga

Pakanga ni kichaka kilicho na ladha chungu. watu walitumia kutengeneza dawa na pia waliamini kuwa ilikuwa na sumu. "Jina la nyota ni Uchungu" au "Jina la nyota ni Dawa Chungu"

ikawa Pakanga

Ladha chungu ya maji inazungumziwa ka vile ilkuwa Pakanga. "ikawa chungu kama pakanga" au "ikawa chungu"

wakafa kutokana na maji yaliyokuwa machungu

"wakafa walipokunywa maji machungu"

Revelation 8:12

theluthi moja ya jua ikapigwa

Kusababisha kitu kibaya kutokea kwa jua inazungumziwa kama kulipiga au kuligonga. Hii inaweza kuelezwa na kitenzi. "theluthi moja ya jua ikabadilishwa" au "Mungu alibadili theluthi moja ya jua"

theluthi moja ya vyote ikageuka kuwa giza

Maana zinazowezekana ni 1) "theluthi moja ya muda vilikuwa giza" au 2)"theluthi moja ya jua, theluthi moja ya mwezi na theluthi moja ya nyota vilikuwa giza"

theluthi moja ya mchana na theluthi moja ya usiku havikuwa na mwanga

"mwanga haukuwepo theluthi moja ya siku na theluthi moja ya usiku" au "havikutoa mwanga theluthi moja ya siku na theluthi moja ya usiku"

Revelation 8:13

kwa sababu ya ... tarumbeta iliyosalia ... malaika

"kwa sababu malaika ambao walikuwa bado hawajapuliza tarumbeta walitaka kuzipuliza"

Revelation 9

funuo 09 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii inaendeleza hukumu za baragumu saba. Hii sura na ile iliyopita inajumuisha kitengo kimoja.

Ole

Kuna aina nyingi za "ole" maalum ambazo zimetajwa katika kitabu cha Ufunuo. Sura hii ina ole hizi za kwanza. Kuna uwezekano hizi zina maana ya umuhimu wa kimuundo wa matukio kulingana na wakati katika Ufunuo.

Dhana muhimu katika sura hii

Picha ya mnyama

Mfano ya mnyama ni kawaida katika kitabu hiki na pia kwenye hii sura.Watu wa kale wa mashariki ya karibu huenda waliwatazama hawa wanyama kama wenye walikua na 'tabia fulani' iliyoakilisha wanyama hawa. Kwa mfano simba mara nyingi huonekana kama aliye na nguvu. Mtafsiri asijaribu kutoa maana ya kila picha hizi.

Shimo lisilo na mwisho

Hii ni mfano ya kawaida katika kitabu cha Ufunuo kinachoashiria kuzimu.Inasisitiza kwamba kuzima haiwezi kuepukwa. "Inaelezewa kama iliyoko chini kinyume na mbinguni inayoelezewa kama iliyo juu. Hii inasisitza kwamba hakuna mbinguni wala kuzimu hapa duniani. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#hell)

Abadoni na Apolioni

"Abadoni" ni neno la Kiebrania na neno "Apolioni" ni neno la Kigiriki. Maneno yote yanamaanisha "Mwangamizi". Yohana alitafsiri Mwangamizi neno hilo la Kiebrania kwa kuiandika na herufi za Kigiriki.Watafsiri wa ULB na UDB waliyatafsiri kutumia herufi za Kingereza. Watafsiri wanashauriwa kutafsiri maneno haya kutumia herufi za lugha kusudiwa.Kwa vile wasomaji wa asili wa Wagiriki wangeelewa maana ya "Apoloni," watafsiri wanaweza kutoa maana yake katika maelezo ya tanbihi.

Toba

Sura hii inataja dhamira ya toba. Hata ingawa kuna miujiza mingi, watu wanasemekana kuepuka toba na kubaki dhambini. Si vizuri kusahau dhamira hii ukisoma kitabo cha Ufunuo. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#repent and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii.

Mfano

Shetani mara nyingi anafanuliwa kama malaika aliyeanguka. Sababu nyota ni mfano wa malaika katika kitabu cha Ufunuo,maneno "nyota kutoka mbinguni iliyokuwa imeanguka" huenda inaashiria Shetani. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#satan, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-symlanguage na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Kuna Kuna mifano nyingi katika sura hii. Kazi yao ni kuonyesha picha ngumu ambazo Yohana anaona katika maono yake.Kwa hivyo mifano hii inaangazia maswala yanayowezekana kuliko kuangazia kazi ya kishairi. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-simile)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Wale watu ambao hawakuwa na muhuri wa Mungu"

Ikiwezekana ni vyema kutotoa maana ya maneno haya waziwazi kwa tafsiri.Wasomi wengi wanaamini muhuri ni alama iliyofanywa kuwatofautisha waumini na wasioamini wakati huu wa dhiki. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

<< | >>

Revelation 9:1

Kauli Unganishi:

Malaika wa tano kati ya saba aanza kupiga tarumbeta

Niliona nyota kutoka mbinguni iliyokuwa imeanguka

Yohana aliona nyota ikiwa imeshakwisha anguka. Hakuiona ikianguka.

ufunguo wa shimo linaloelekea kwenye shimo lisilo na mwisho

"funguo ambao unafungua tundu la shimo lisilo na mwisho"

shimo linaloelekea kwenye shimo lisilo na mwisho

Maana zinazowezekana ni 1)"shimo" linaelezea jinsi shimo lilivyo refu na lembamba, au 2)"shimo" linamaanisha uwazi wa mwanzo wa tundu la shimo lenyewe.

shimo lisilo na mwisho

Hili ni shimo refu sana na jembamba. Maana zinazowezekana ni 1)shimo halina mwisho chini; inaendelea kwenda chini zaidi milele au 2) shimo ni refu sana hata linakuwa kana kwamba halina mwisho.

kama moshi kutoka katika tanuru kubwa

Tanuru kubwa linatoa moshi mweusi na mnene. "kama moshi mkubwa utokao kwenye tanuru kubwa"

Revelation 9:3

nzige

Wadudu wanaopaa pamoja katika makundi makubwa. Watu huwahofia kwa sababu wanaweza kula majani yote kwenye bustani na kwenye miti.

nguvu kama ile ya nge

Nge wana uwezo kuwadunga na kuwapa sumu watu na wanyama wengine. "uwezo wakudunga watu kama Nge wafanyavyo"

nge

Wadudu wadogo wenye ncha kali zenye sumu mikiani. Kudungwa nao huacha maumivu makali na yanayodumu muda mrefu.

Waliambiwa kutokudhuru majani katika nchi au mmea wowote wa kijani au mti

Nzige wa kawaida walikuwa tishio kubwa kwa watu walipokuja, waliweza kula nyasi zote na majani ya mimea na miti. Nzige hizi zilikatazwa kufanya hivyo.

isipokuwa tu watu

Neno "kudhuru" au "kuumiza" linaeleweka. "lakini kudhuru watu tu"

muhuri wa Mungu

Neno "muhuri" hapa humaanisha kifaa kinachotumika kuweka alama katika muhuri wa nta. Na hapa, hiki kifaa kitatumika kuweka alama katika watu wa Mungu. "alama ya Mungu" au "stampu ya Mungu"

paji za nyuso

paji la kichwa ni juu ya uso, juu ya macho.

Revelation 9:5

Hawakupewa ruhusa

"Hawa" inamaanisha nzige.

hao watu

watu ambao walikuwa wanang'atwa na nzige.

bali kuwatesa tu

Hapa maneno "walipewa ruhusa" yanaeleweka. "lakini walipewa ruhusa kuwatesa"

kuwatesa

"kuwafanya wateseke maumivu makali"

kuwatesa kwa miezi mitano

Nzige wataruhusiwa kufanya hivi kwa miezi mitano.

kuumwa na nge

Nge ni mdudu mdogo wenye ncha kali yenye sumu mkiani. Kudungwa naye kunaweza kusababisha maumivu makali au hata kifo.

watu watatafuta kifo

Kifo kinazungumziwa kama mtu au kitu kinachoweza kufichwa. "watu watatafuta njia ya kufa" au " watu watajaribu kujiua"

hawatakipata

"hawataweza kupata njia ya kufa" au "hawataweza kufa"

Watatamani kufa

"watataka sana kufa" au "watatamani kwamba wafe"

kifo kitawakimbia

Yohana anazungumzia kifo kama vile ni mtu au mnyama anayeweza kukimbia. "hawataweza kufa" au "hawatakufa"

Revelation 9:7

Taarifa ya Jumla:

Nzige hao hawakufanana kama nzige wa kawaida. Yohana anawazungumzia kwa kueleza jinsi gani sehemu zao zinafanana na vitu vingine.

mataji ya dhahabu

Hizi zilikuwa kama mashada ya matawi ya mizeituni au majani ya laurusi yaliyopondwa katika dhahabu. Mifano iliyotengenezwa kwa majani walipewa wanariadha washindi kuvaa vichwani.

Revelation 9:10

Walikuwa na mikia

Neno "Walikuwa" inamaanisha nzige.

na mikia inayouma kama nge

Nge ni mdudu mdogo wenye ncha kali yenye sumu mkiani. Kudungwa naye kunaweza kusababisha maumivu makali au hata kifo. "na mikia kama mikia ya nge" au "na mikia iwezayo kusababisha maumivu mabaya kama mikia ya nge"

katika mikia yao walikuwa na nguvu ya kudhuru watu kwa miezi mitano

Maana zinazowezekana ni 1) walikuwa na nguvu kwa miezi mitano kudhuru watu au 2) wataweza kuuma watu na maumivu yao yatadumu miezi mitano.

shimo lisilokuwa na mwisho

Hili ni shimo refu sana. Maana zinazowezekana ni 1)shimo halina mwisho chini; inaendelea kwenda chini zaidi milele au 2) shimo ni refu sana hata linakuwa kama vile halina mwisho.

Abadoni ... Apolioni

Majina yote yanamaanisha "maangamizi"

kuna maafa mawili yaja

Ziko katika wakati wa baadae zinazungumziwa kama zinakuja.

Revelation 9:13

Kauli Unganishi:

Malaika wa sita kati ya saba kupuliza tarumbeta.

nikasikia sauti ikitoka

Sauti inamaanisha yule aliyekuwa anazungumza. Yohana hasemi msemaji ni nani, lakini inawezekana ikawa ni Mungu. "Nilisikia mtu akizungumza"

pembe ya madhabahu ya dhahabu

Hizi ni zile zehemu zinazoendeleza kona nne za juu ya madhabahu zinazofanana na pembe.

Sauti ilimwambia

Sauti inamaanisha msemaji. "Msemaji akamwambia"

Malaika wale wanne waliokuwa wameandaliwa kwa ... mwaka huo, waliachiwa

"Malaika akawaachia wale malaika wanne waliokuwa wameaandaliwa kwa ... mwaka huo"

Malaika wale wanne waliokuwa wameandaliwa

"Malaika wanne ambao Mungu aliwaanda"

kwa saa hiyo, siku hiyo, mwezi huo, na mwaka huo

Haya maneno yanatumika kuonesha kuwa kuna muda bayana na siyo muda wowote tu. "kwa muda huo bayana"

Revelation 9:16

Taarifa ya Jumla:

Ghafla, wanajeshi 200,000,000 wajitokeza katika maono ya Yohana. Yohana sasa hazingumzi wale malaika wanne walitajwa katika mstari uliopita.

200,000,000

Njia baadhi zakueleza hii ni : "milioni mia mbili" au " elfu laki mbili" au "elfu ishirini mara elfu"

vyekundu kama moto

"alikuwa mwekundu kama moto" au "alikuwa mwekundu wa kung'aa"

njano isiyoiva

"njano kama salfa"

midomoni mwao ulitoka moto, moshi na salfa

"moto, moshi na salfa zilitoka midomoni mwao"

Revelation 9:18

Kauli Unganishi:

Yohana anaendelea kuelezea farasi na mapigo waliyoleta kwa binadamu.

Theluthi ya wanadamu

"Theluthi moja ya watu."

wa kuwa nguvu ya farasi ilikuwa katika midomo yao na katika mikia yao

Nomino "nguvu" inaweza kutafsiriwa na kivumishi. "Kwa kuwa ilikuwa midomo na mikia ya farasi aliyokuwa na nguvu sana" au "kwa kuwa ilkuwa midomo na mikia ya farasi ilyoweza kuwaumiza watu"

Revelation 9:20

wale ambao walikuwa hawajauawa na mapigo haya

"wale ambao mapigo hayakuwaua"

vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikia au kutembea

Msemo huu unatukumbusha kuwa sanamu hazina uhai na hazistahili kuabudiwa. Lakini watu hawakuacha kuviabudu. "licha ya kwamba sanamu haziwezi kuona, kusikia, au kutembea"

Revelation 10

Ufunuo 10 Maelezo ya jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Ngurumo saba

Haieleweki wazi kilichomaanishwa na ngurumo saba. Inakubalika kwa mtafsiri kutoelewa maneno haya na kuyatafsiri kama "ngurumo saba." (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-personification na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

"Siri la Mungu"

Haieleweki maana ya haya maneno. Siyo siri ambayo Paulo anafafanua kwa maana ya kanisa. Labda inaashiria kitu kilichofichwa na hajulikani sasa, lakini kitakachofunuliwa kimefichika ama hakijulikani kitakachofunuliwa wakati huu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#reveal)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Mfano

Kuna Mifano nyingi zimetumika kuelezea malaika huyo mkubwa. Mifano inatumika kuelezea vitu ambavyo Yohana anaona kwa kuvilinganisha na vitu vya kawaida. Lakini, upinde wa mvua na mawingu vingeeleweka kama vitu vya kawaida sivyo mifano. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-simile)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Vitabu vya msokoto

Kitabu cha msokoto kinachotajwa katika sura hii ni tofauti na vitabu vya msokoto vingine vilivyozungumziwa sana katika kitabu cha Ufunuo kufikia sasa. Kinaitwa "cha msokoto". Mtafsiri anatakikana kuhakikisha kwamba msomaji anafahamu kwamba kuna zaidi ya kitabu kimoja cha msokoto.

<< | >>

Revelation 10:1

Taarifa ya Jumla:

Yohana anaanza kueleza maono ya malaika mkuu akishilia gombo. Katika maono ya Yohana anaona kinachoendelea kutoka duniani. Hii inachukua nafasi katikati ya kupulizwa tarumbeta ya sita na tarumbeta ya saba.

Alikuwa amefungwa katika wingu

Yohana anamzungumzia malaika kama vile alikua amevaa wingu kama nguo yake. Huu usemi unaweza kueleweka kama sitiari. Ijapo, kwa sababu vitu vya ajabu vilonekana katika maono, inaweza kueleweka kama ukweli halisia jinsi ulivyo.

Uso wake ulikuwa kama jua

"uso wake ulikuwa unang'ara kama jua"

miguu yake zilikuwa kama nguzo za moto

"Miguu" inamaanisha nyayo zake. "Nyayo zake zilikuwa kama nguzo za moto"

aliweka mguu wake wa kulia juu ya bahari na mguu wake wa kushoto juu ya nchi kavu

"alisimama na mguu wake wa kulia baharini na mguu wake wa kushoto nchi kavu"

Revelation 10:3

Kisha alipaza sauti

"Kisha malaika akapaza sauti"

ngurumo za radi saba zikasema

Ngurumo ya radi inazungumziwa kama vile ni mtu awezaye kuzungumza. "ngurumo saba za radi zakapiga sauti kali" au "radi iliunguruma kwa sauti sana mara saba"

ngurumo saba za radi

ngurumo za radi kutokea mara saba inazungumziwa kama "radi" saba tofauti.

lakini nilisikia sauti kutoka mbinguni

Neno "sauti" humaanisha msemaji. Sio malaika. "lakini nikasikia mtu akizungumza kutoka mbinguni"

Revelation 10:5

aliinua mkono wake juu mbinguni

Alifanya hivi kuonyesha kuwa aliapa kwa Mungu.

kuapa kwa yule aishiye milele na milele

"na akamuliza yule aishiye milele na milele athibitishe"

yule aishiye milele na milele

Hapa "yule" inamaanisha Mungu.

Hakutakuwepo kuchelewa tena

"Hakutakuwa na kusubiri tena" au "Mungu hatachelewa"

ndipo siri ya Mungu itakuwa imetimizwa

"Mungu atatimiza siri yake" au " Mungu atakamilisha mpango wake wa siri"

Revelation 10:8

Kauli Unganishi:

Yohana anasikia sauti kutoka mbinguni ambayo alisikia 10:3 ikizungumza naye tena.

Sauti niliyosikia kutoka mbinguni

Neno "sauti" inamaanisha msemaji anayenena. "Yule niliyemsikia akizungumza kutoka mbinguni" au "Yule aliyezungumza na mimi kutoka mbinguni"

"niambia, nilikwenda"

Hapa inamaanisha Yohana.

iliniambia

"Malaika aliniamba"

uchungu

"chungu" au "chachu." Hii inamaanisha ladha mbaya kutoka tumboni baada ya kula kitu ambacho sio kizuri kula.

litakuwa tamu kama asali

"Itakuwa na ladha tamu kama asali"

Revelation 10:10

lugha

Hii inamaanisha watu waliozungumza hizo lugha. "jumuia za lugha nyingi" au "makundi mengi ya watu waliozungumza lugha zao" au "wazungumzaji wa lugha nyingi"

Revelation 11

Ufunuo 11 Maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 11:15, 17-18.

ole

Kuna aina nyingi maalum za "ole" ambazo zimetajwa katika kitabu cha Ufunuo.Sura hii ina ole ya pili na ya tatu. Labda ole hizi zina maana muhimu fulani kulingana na matukio ya kitabo cha Ufunuo.

Dhana muhimu katika sura hii

Watu wa mataifa

"Watu wa mataifa katika sura hii wanaashiria watu wa mataifa wasio mcha Mungu na sio watu wa mataifa ambao ni Wakristo. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#ungodly)

Mashahidi wawili

Mashahidi hawa wawili wana umuhimu kama manabii wakati wa kipindi cha Ufunuo. Wasomi wamependekeza vitu vingi kuhusu utambulisho wa hawa wanaume wawili. Haijulikani na haina umuhimu wa kujua hawa walikuwa akina nani.Badalayake, ni asili yao isiyoangamika na ujumbe wao ambao ni muhimu na haikataliki. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet)

Shimo lisilo na mwisho

Hii ni taswira ya kawaida katika kitabu cha ufunuo kinachoashiria kuzimu. Inasisitiza kwamba kuzimu haiepukiki. Inaelezewa kama iliyoko chini lakini mbinguni inayoelezewa kama iliyo juu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#hell)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Hawa manabii wawili waliwatesa watu walioishi duniani"

Hawa manabii wawili wanahusishwa na uharbifu mkubwa utakaosababisha hasara kubwa kwa watu duniani. Hii siyo roho mbaya mbali ni jaribio la kuwaleta watu hawa kwa toba. Lakini hawatatubu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#repent na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

"Wakati umetimia wa wafu kuhukumiwa"

Watu watahukumiwa baada ya kufa.Wale wanaomkataa Yesu watapata mateso ya milele. Lakini Wakristo watatuzwa kwa uaminifu wao walioishi maisha yao kama Wakristo. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#eternity na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faithful)

<< | >>

Revelation 11:1

Taarifa ya Jumla:

Yohana anaanza kueleza maono kuhusu fimbo ya kupimia na mashahidi wawili walioteuliwa na Mungu. Maono yalichukua nafasi kati ya kupulizwa kwa tarumbeta ya sita na tarumbeta ya saba.

Nilipewa mwanzi

"Mtu alinipa mwanzi"

Nilipewa ... Niliambiwa

Aliyepewa na aliyeambiwa anamaanishwa ni Yohana.

na wale wanaoabudu ndani yake

"na hesabu wale wanaoabudu ndani ya hekalu"

Wataukanyaga

kukifanya kitu kama vile hakina dhamani kwa kutembea juu yake.

iezi arobaini na miwili

miezi miwili - "miezi 42"

Revelation 11:3

Kauli Unganishi:

Mungu anaendelea kuzungumza na Yohana.

wamevaa magunia

"wamevaa nguo chafu za maombolezo" au "watavaa nguo zilizokwaruzwa kuonesha kuwa walikuwa na masikito sana"

Hawa mashahidi ni

Yohana anaelezea hawa mashahidi ni kina nani.

Hawa mashahidi ni miti miwili ya mizeituni na vinara viwili

"Hawa mashahidi wawili ndio waliowakilishwa na miti miwili ya mizeituni na vinara viwili"

miti miwili ya mizeituni na vinara viwili

Yohana anategemea wasomaji wake wajue kuvihusu kwa sababu nabii mwingine aliandika kuvihusu miaka mingi kabla. "miti miwili ya mizeituni na vinara viwili vinavyosemwa na maandiko"

moto hutoka vinywani mwao na kuwadhuru adui zao

Kwa sababu hii inahusu matukio ya mbeleni, inaweza kuwekwa katika wakati ujao.."moto utatoka vinywani mwao na kuwateketeza adui zao"

moto ... kuwadhuru adui zao

Moto kuwaka na kuua watu inazungumziwa kana kwamba mnyama anayeweza kuwala. "moto .. utawateketeza adui zao" au "moyo ... utawachoma kabisa adui zao"

Revelation 11:6

kufunga anga ili kwamba mvua isinyeshe

Yohana anazungumzia mbingu kama vile ina mlango unaoweza kufunguliwa na kufungwa ili mvua isipite. "kuzuia mvua isidondoke toka mbinguni"

kuipiga nchi kwa kila aina ya pigo

Yohana anazungumzia mapigo kana kwamba ni kijiti ambacho mtu anaweza kuipigia dunia. "kusababisha kila aina yamatatizo kutokea duniani"

shimo lisilo na mwisho

Hili ni shimo refu sana. Maana zinazowezekana ni 1)shimo halina mwisho chini; inaendelea kwenda chini zaidi milele au 2) shimo ni refu sana hata linakuwa kana kwamba halina mwisho.

Revelation 11:8

Miili yao

Hii inamaanisha miili ya mashahidi wawili.

katika mtaa wa mji mkuu

Mji ulikua na zaidi ya mtaa mmoja. Hii ilikuwa sehemu ya wazi ambapo watu waliweza kuwaona. "kwenye mtaa mojawapo wa mji mkuu" au "kwenye mtaa mkuu katika mji mkuu"

siku tatu na nusu

"Siku 3 kamili na nusu moja ya siku" au "siku 3.5" au "siku 3 1/2"

Bwana wao

Walimtumikia Bwana na kama yeye, watakufa katika huo mji.

hawatatoa kibali kuwekwa katika kaburi

Hii ilikuwa ishara ya dharau.

Revelation 11:10

watafurahi kwa ajili yao na kusherekea

"watafurahi kwamba mashahidi wawili wamekufa"

hata kutumiana zawadi

Hili tendo linaonesha jinsi gani watu walivyofurahi.

kwa sababu hao manabii wawili waliwatesa wale walioishi katika nch

Hii ndio sababu watu walifurahi sana kwamba mashahidi wamekufa.

siku tatu na nusu

"Siku 3 kamili na nusu moja ya siku" au "siku 3.5" au "siku 3 1/2"

pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu itawaingia

Uwezo wa pumzi unazungumziwa kama kitu kinachoweza kuingia ndani ya watu. "Mungu atasababisha mashahidi wawili kupumua tena na kuishi"

Hofu kuu itawaangukia wale wanaowaona

Hofu inazungumziwa kama kitu kinachoweza kuwaangukia watu. "Wale watakao waona wataogopa sana"

Kisha watasikia

Maana zinazowezekana ni 1) mashahidi wawili watasikia au 2) watu watasikia kile wanachoambiwa mashahidi wawili.

sauti kuu kutoka mbinguni

Neno "sauti" inammanisha ni yule anayenena. "mtu anazungumza nao kwa sauti kuu toka mbinguni na"

ikiwaambia

"ikiwaambia mashahidi wawili"

Revelation 11:13

atu elfu saba

"Watu 7,000"

watakaobaki

"wale ambao hawatakufa" au "wale ambao bado wanaishi"

kumpa utukufu Mungu wa mbinguni

"kusema kuwa Mungu wa mbinguni ni mtukufu"

Ole ya pili imepita

"Tukio la pili baya limepita."

Ole ya tatu inakuja upesi

Kuwepo kwa kipindi cha mbele inazungumziwa kama kijacho. "Ole ya tatu itatokea punde"

Revelation 11:15

Kauli Unganishi:

Malaika wa mwisho wa wale saba anaanza kupuliza tarumbeta yake.

malaika wa saba

Huyu ni malaika wa mwisho kati ya wale saba. "malaika wa mwisho" au "malaika namba saba"

sauti kubwa zilinena mbinguni na kusema

Usemi "sauti kubwa" huwakilisha wananenaji wanaozungumza kwa sauti kubwa. "Wasemaji mbinguni wakanena kwa sauti kubwa na kusema"

Ufalme wa dunia

Hapa inamaanisha mamlaka ya kutawala ulimwengu. "Mamlaka ya kutawala dunia"

dunia

Hii inamaanisha kila mtu duniani. "kila mtu duniani"

ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake

Neno "ufalme" hapa linamaanisha mamlaka ya Bwana wetu na Kristo wake waliyonayo kutawala.

Ufalme wa dunia umeshakuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake

"Bwana wetu na Kristo wake sasa ni watawala wa dunia"

Revelation 11:16

wazee ishirini na wanne

wazee wanne -"wazee 24"

nyuso zao zimeinama chini

Kulala chini kwa kutazama ardhi.

Mungu mwenye Nguvu, ambaye yupo na ambaye alikuwepo

Hizi zinaweza kuwa sentesi. "Wewe, Bwana Mungu, ndiye mtawala juu ya vyote. Wewe ndiye uliyepo, na wewe ndiye uliyekuwepo"

ambaye yupo

"yule aliyepo" au "yule anayeishi"

alikuwepo

"aliyekuwepo" au "yule ambaye alikuwa anaisha daima"

umetwaa nguvu yako kuu

Mungu alichofanya na nguvu yake kuu inaweza kuwekwa wazi. "umewaangamiza kwa nguvu yako wote waliokuasi"

Revelation 11:18

Kauli Unganishi:

Wazee ishirini na nne wanaendelea kumsifu Mungu.

Taarifa ya Jumla:

Maneno "yako" na "wako" yanamaanisha Mungu.

Walikasirishwa

"walikasirika sana"

ghadhabu yako imekuja

Inakuwepo katika muda wa sasa ikizungumzwa kama imeshatokea. "Upo tayari kuonyesha ghadhabu yako"

Wakati umefika

Inakuwepo katika muda wa sasa ikizungumzwa kama imeshatokea. "Wakati ni sahihi" au "Sasa ni wakati"

manabii, waamini, na wale walio na hofu ya jina lako

Orodha hii inafafanua maana ya "watumishi wako". Haya hayakuwa makundi matatu ya watu tofauti. Manabii walikuwa waamini na walimuogopa Mungu.

Revelation 11:19

sanduku la agano lake llilionekana ndani ya hekalu

"Niliona sanduku la agano lake hekaluni mwake"

miali ya radi

Mwanga unaotokea wakati radi ikipiga.

kelele, ngurumo za radi

Hii ni miungurumo ya sauti ambayo radi husababisha.

Revelation 12

Ufunuo 12 maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Wasomi wengi wanaamini kwamba matukio ya sura hii ni ya kipindi kilichopita na kipindi kijacho. Mwandishi anaweza zungumzia matukio bila kusema ni kipindi gani yalitokea. Hata hivyo, Yohana anayazungumzia matukio haya kana kwamba ndio yanakaribia kutokea.

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo mshororo wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 12:10-12

Dhana muhimu katika sura hii

Nyoka

Kuashiria Shetani kama nyoka inakusudiwa kumfanya msomaji kukumbuka hadithi ya majaribu katika Bustani la Edeni. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Mfano

Mwanamke ametajwa katika mifano nyingi lakini utambulisho wake hauko wazi.Sura hii inazungumzia pia kuhusu kutokea kwa mpinga Kristu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#antichrist)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Ishara kuu ilionekana mbinguni"

Haieleweki iwapo hii ilionekana kwa kila mtu duniani ama ilionekana tu na Yohana katika maono yake. Mtafsiri atakuwa na utata iwapo swala hili haliko wazi. Kwa kiingereza hii hufanyika kutumia sauti ya kupita ingawa siyo kila lugha ina uwezo huu.(Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-activepassive na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

<< | >>

Revelation 12:1

Taarifa ya Jumla:

Yohana anaanza kumuelezea mwanamke anyemuona katika maono.

Ishara kuu ilionekana mbinguni

"Ishara kuu ikatokea mbinguni" au "Mimi, Yohana, niliona ishara kuu mbinguni"

mwanamke aliyefunikwa na jua

"mwanamke aliyelivaa jua"

taji ya nyota kumi na mbili

Hii ilikuwa ni mfano wa shada la majani ya laurusi na matawi ya mizeituni, lakini zikiwa na nyota kumi na mbili.

nyota kumi na mbili

"nyota 12"

Revelation 12:3

Kauli Unganishi:

Yohana anaelezea joka lililotokea kwenye maono yake.

joka

Hili lilikuwa tambaazi kubwa kali, kama mjusi. Kwa wayahudi ilikuwa ni alama ya uovu na machafuko.

Mkia wake ulikokota theluthi moja ya nyota

"Alikokota theluthi moja ya nyota na mkia wake"

theluthi moja

"moja ya tatu"

Revelation 12:5

atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma

Kutawala kwa ukali kunazungumziwa kama kutawala kwa fimbo ya chuma. "Atawatawala kwa ukali kama vile anawapiga na fimbo ya chuma.

Mtoto wake alinyakuliwa juu kwa Mungu

"Mungu alimchukua upesi mtoto wake"

Revelation 12:7

Sasa

Yohana anatumia neno hili kubadili mwenendo wa maelezo yake kutambulisha kitu kingine kinachotokea katika maono yake.

joka

Hili lilikuwa tambaazi kubwa kali, kama mjusi. Kwa wayahudi ilikuwa ni alama ya uovu na machafuko. Joka pia linatambulika katika mstari wa 9 kama "ibilisi au Shetani"

Kwa hiyo haikuwepo tena nafasi mbinguni kwa ajili yake na malaika zake

"Kwa hiyo joka na malaika wake hawakuweza tena kukaa mbinguni"

Joka mkubwa ... akatupwa chini katika dunia ... na malaika zake wakatupwa chini pamoja naye

"Mungu alilitupa joka na malaika wake toka mbinguni na kuwatuma duniani"

ule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani ambaye hudanganya dunia nzima

Hii taarifa inaweza kutolewa katika sentesi tofauti baada ya taarifa ya kutupwa duniani. "Hilo joka ni nyoka wa zamani anaye danganya ulimwengu. Anaitwa ibilisi au Shetani"

Revelation 12:10

"nikasikia"

anayezungumza ni Yohana.

nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni

Neno "sauti" inaonesha mtu anayezungumza. "Nikasikia mtu akinena kwa sauti toka mbinguni"

sasa wokovu umekuja, nguvu

Mungu kuwaokoa watu kwa nguvu zake inazungumziwa kana kwamba wokovu wake na nguvu zake ni vitu vinavyoweza kuja. "Sasa Mungu amewaokoa watu wake kwa nguvu zake"

umekuja

"kuanza kuwepo kabisa" au "kutokea" au "kuwa kweli." Sio kwamba vitu hivi havikuwepo kabala, lakini sasa Mungu anavidhihirisha kwa sababu wakati wake kutokea "umekuja."

ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake

Utawala wa Mungu na mamlaka ya Kristo yanazungumziwa kama vile vinakuja. "Mungu atawala kama mfalme, na Kristo wake anamamlaka yote"

mshitaki wa ndugu zetu ametupwa chini

Huyu ni joka aliyetupwa chini katika 12:10

ndugu zetu

Waumini wenzao wanazungumziwa kana kwamba walikuwa ni ndugu. "waumini wenzetu"

mchana na usiku

Hizi sehemu mbili za siku zinatumika pamoja kumaanisha "wakati wote" au "bila kukoma"

Revelation 12:11

Kauli Unganishi:

Sauti kuu kutoka mbinguni inaendelea kuzungumza.

Walimshinda

"Walimshinda mshitaki"

kwa damu ya Mwanakondoo

Damu inamaanisha kifo chake. "kwa sababu Mwanakondoo amemwaga damu na kuwafia"

kwa neno la ushuhuda wao

Neno "ushuhuda" inaweza kuelezwa na kitenzi "shuhudia." Pia walioshuhudiwa wanaweza kuelezwa vizuri. "kwa yale waliyosema walivyomshuhudia Yesu kwa wengine"

hata kufa

Waumini walisema ukweli kumuhusu Yesu, licha ya kwamba walikuwa wanajua kuwa maadui zao wangeweza kujaribu kuwaua kwa sababu hiyo. "lakini waliendelea kushuhudia licha ya kwamba walijua wangeweza kufa kwa hilo"

Amejawa na hasira sana

Ibilisi anazungumziwa kana kwamba ni chombo na hasira inazungumziwa kuwa kama kimiminiko kinachoweza kuwa ndani yake. "Ana hasira sana"

Revelation 12:13

joka alitambua kuwa ametupwa chini kwenye nchi

"joka alitambua ya kwamba Mungu amemtupa nje ya mbingu na kumtuma duniani"

alimfuata mwanamke

"alimfukuza mwanamke"

joka

Hili lilikuwa tambaazi kubwa kali, kama mjusi. Kwa wayahudi ilikuwa ni alama ya uovu na machafuko. Joka linatambulika pia katika mstari wa 9 kama "ibilisi au Shetani"

wakati, nyakati na nusu wakati

"miaka mitatu na nusu"

nyoka

Hii ni njia nyingine yakumaanisha yule joka.

Revelation 12:15

nyoka

Hiki ni kiumbe kimoja na joka lilotajwa mapema katika 12:7

kama mto

Maji walitiririka toka mdomoni mwake kama mto utiririkavyo. "kwa kiasi kikubwa"

kumgharikisha

"kumuosha"

ardhi ... Ilifunua kinywa chake na kuumeza mto alioutema joka kutoka kinywani mwake

Ardhi inazungumziwa kana kwamba ni kiumbe hai, na shimo linazungumziwa kama kinywa kiwezacho kunywa maji. "Shimo likafunguka kwenye ardhi na maji yakaingia humo"

joka

Hili lilikuwa tambaazi kubwa kali, kama mjusi. Kwa wayahudi ilikuwa ni alama ya uovu na machafuko. Joka linatambulika pia katika mstari wa 9 kama "ibilisi au Shetani"

kushikilia ushuhuda kuhusu Yesu

Neno "ushuhuda" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "waliendelea kushuhudia kuhusu Yesu"

Revelation 13

Ufunuo 13 Maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 13:10 ambayo imenukuliwa kutoka Agano la Kale.

Dhana muhimu katika sura hii

Jeraha ya mauti

Wasomi wengi wanaamini huu ni unabii wa kifo cha mpinga Kristo. Wanaamini mpinga Kristo ataigiza ufufuko wa Yesu ama kuugushi. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#antichrist na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#resurrection)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Yule Mnyama

Wasomi wengi anaamini kwamba hii ni mfano kwa kuelezea mpinga Kristu.Hii ni muhimu kwa kuelewa kikamilifu aya hii.Hii ni kinyume na mwanakondoo ambaye anaashiria Yesu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-personification na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Mnyama mwingine

Wasomi wengi wanaamini kwamba huyu mnyama mwingine ni nabii ama kuhani wa mpinga Kristu. Ana uwezo wa kutenda miujiza mingi na kuwafanya watu wengi kumuabudu mpinga Kristu.

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Wanyama wasiojulikana

Sura hii inatumia idadi kubwa ya wanyama wasiojulikana.Wingi wa wanyama hawa wametumika kiishara ingawa maana yao haielezeki waziwazi. Hii itasababisha utata mkubwa kwa watafsiri. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-unknown)

<< | >>

Revelation 13:1

Taarifa ya Jumla:

Yohana anaanza kueleza mnyama anayetokea katika maono yake. "nikaona" inamaanisha ni Yohana aliyeona.

joka

Hili lilikuwa tambaazi kubwa kali, kama mjusi. Kwa wayahudi ilikuwa ni alama ya uovu na machafuko. Joka linatambulika pia katika mstari wa 9 kama "ibilisi au Shetani"

Yule joka akampa nguvu zake

Joka alimfanya mnyama kuwa na nguvu kama yeye. Ingawa hakupoteza nguvu zake kwa kumpa mnyama nguvu.

nguvu ... kiti chake cha enzi, na mamlaka yenye nguvu sana ya kutawala

Hizi ni njia tatu zakumaanisha mamlaka yake, na pamoja zinasisitiza kuwa mamlaka yake walikuwa makubwa.

kiti chake cha enzi

"kiti cha enzi" hapa inamaanisha mamlaka ya joka kutawala kama mfalme. "mamlaka yake ya kifalme" au "mamlaka yake kutawala kama mfalme"

Revelation 13:3

Lakini jeraha lake likapona

"Lakini hilo jeraha lilipona"

jeraha la kusababisha mauti

"jeraha baya." Hili ni jeraha kubwa linaloweza kusababisha mtu kufa.

dunia yote

Neno "dunia" inamaanisha watu waliomo ndani yake. "watu wote duniani"

ikamfuata mnyama

"ikamtii mnyama"

joka

Hili lilikuwa tambaazi kubwa kali, kama mjusi. Kwa wayahudi ilikuwa ni alama ya uovu na machafuko. Joka linatambulika pia katika mstari wa 9 kama "ibilisi au Shetani"

alimpa mamlaka yule mnyama

"alimfanya mnyama kuwa na mamlaka kama aliyokuwa nayo yeye"

Nani kama mnyama?

Hili swali linaonesha ni jinsi gani walivyostaajabishwa na mnyama. "Hakuna aliye na nguvu kama mnyama!"

Nani atapigana naye?

Hiil swali linaonesha kiasi gani watu walihofia nguvu ya mnyama. "Hakuna mtu atakayeweza kupigana na mnyama na kushinda!"

Revelation 13:5

Mnyama akapewa ... Aliruhusiwa

"Mungu alimpa mnyama ... Mungu alimruhusu mnyama"

Mnyama akapewa mdomo ili azungumze maneno ya kujisifu na matusi

Kupewa mdomo inamaanisha kuruhusiwa kuzungumza. "Mnyama aliruhusiwa kuzungumza maneno ya majivuno na matusi"

miezi arobaini na miwili

mieezi miwili - "miezi 42"

kuongea matusi dhidi ya Mungu

"kusema maneno ya kejeli kuhusu Mungu"

akalitukana jina lake, eneo alililokuwa akiishi na wale wanaoishi mbinguni

Haya maneno yanaonesha jinsi mnyama alivyozungumza maneno ya matusi dhidi ya Mungu.

Revelation 13:7

alipewa mamlaka

"Mungu alimpa mamlaka mnyama"

kila kabila, watu, lugha na taifa

Hii humaanisha watu kutoka kila kabila wanahusika.

watamwabudu

"watamwabudu mnyama"

kila mmoja ambaye jina lake halijaandikwa ... katika Kitabu cha Uzima

maneno haya yanaweka wazi ni nani duniani atakayemwabudu mnyama. "wale ambao majina yao hayakuandikwa na Mwanakondoo ... katika Kitabu cha Uzima" au "wale ambao majina yao hayakuwemo ... katika Kitabu cha Uzima"

toka uumbaji wa dunia

"Mungu alipoumba ulimwengu"

mwanakondoo

Huyu ni mtoto wa kiume wa kondoo. Hapa hutumika kuashiria kuwa ni Kristo.

aliyechinjwa

"yule ambaye watu walimchinja"

Revelation 13:9

Taarifa ya Jumla:

Hii mistari ni mapumziko kutoka kwenye hesabu ya Yohana ya maono yake. Hapa anawaonya watu wanaosoma hesabu yake.

Ikiwa yeyote ana sikio

Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asikilize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"

Ikiwa yeyote amechukuliwa

Usemi huu unamaanisha kuwa imashaamuliwa kuwa mtu atachukuliwa. Kama inahitajika, watafsiri wanaweza kusema dhahiri ni nani aliyeamua. "Kama Mungu ameamua mtu achukuliwe" au "Kama ni mapenzi ya Mungu kwamba mtu achukuliwe"

Ikiwa yeyote amechukuliwa mateka

Nomino "mateka" inaweza kutajwa na kitenzi "kamata" "Kama ni mapenzi ya Mungu kwa adui kumkamata mtu fulani"

kwenye mateka ataenda

Nomino "mateka" inaweza kutajwa na kitenzi "kamata" "adui atamkamata"

Ikiwa yeyote atauawa kwa upanga

"Kama ni mpango wa Mungu kwa adui kumuua mtu fulani kwa upanga"

kwa upanga

Upanga unaashiria vita. "vitani"

atauawa

"adui atamuua"

Huu ni mwito wa utulivu na uvumilivu na imani kwa hao walio watakatifu

"Wale waliowatakatifu ni lazima wadumu katika uvumilivu na uwaminifu"

Revelation 13:11

Kauli Unganishi:

Yohana anaanza kuelezea mnyama mwingine anayetokeza kwenye maono yake.

akazungumza kama joka

Maneno makali yanazungumziwa kana kwamba ni muungurumo wa joka. "akazungumza kwa ukali kama joka azungumzavyo"

joka

Hili lilikuwa tambaazi kubwa kali, kama mjusi. Kwa wayahudi ilikuwa ni alama ya uovu na machafuko. Joka pia linatambulika katika mstari wa 9 kama "ibilisi au Shetani"

dunia na wale walioishi wakimuabudu

"watu wote duniani"

yule ambaye jeraha lake baya limepona

"yule aliyekuwa na jeraha baya lililopona"

jeraha baya

"jeraha baya." Hili ni jeraha kubwa linaloweza kusababisha mtu kufa.

Revelation 13:13

Akafanya

"Mnyama toka katika nchi alitenda"

Revelation 13:15

Aliruhusiwa

"Mungu alimruhusu mnyama kutoka katika nchi"

kutoa pumzi katika ile sanamu ya mnyama

Hapa neno "pumzi" humaanisha uhai. "kuipa uhai sanamu"

sanamu ya mnyama

Hii ni sanamu ya mnyama wa kwanza aliyetajwa.

kusababisha wale wote waliokataa kumwabudu mnyama wauawe

"kuwaua wote waliokataa kumwabudu mnyama wa kwanza"

Pia akalazimisha kila mmoja

"Mnyama kutoka katika nchi pia akamlazimisha kila mmoja"

Ilikuwa haiwezekani kwa kila mtu kuuza au kununua isipokuwa mwenye alama ya mnyama

"watu waliweza kununua na kuuza vitu ingawa tu walikuwa na alama ya mnyama." "Aliamuru kuwa watu wangeweza kununua na kuuza vitu kama tu wana alama ya mnyama"

alama ya mnyama

Hii ilikuwa alama ya kuonesha kuwa aliyekuwa nayo alimwabudu mnyama.

Revelation 13:18

Taarifa ya Jumla:

Huu mstari ni mapumziko kutoka katika hesabu ya maono ya Yohana. Hapa anawapa onyo jingine wasomaji wa hesabu yake.

Hii inahitaji busara

"Hekima inahitajika" au "Unahitaji kuwa na busara kuhusu hili"

Ikiwa yeyote ana ufahamu

Neno "ufahamu" inaweza kutafsiriwa na kitenzi "kuelewa." "Kama yeyote anaweza kuelewa vitu hivi"

mwache aweze kufanya hesabu ya namba ya mnyama

"Anapaswa kutambua maana ya namba ya mnyama" au "anatakiwa kujua maana ya namba ya mnyama"

ni namba ya kibinadamu

Maana zinazowezekana ni 1) namba inawakilisha mtu mmoja au 2) namba inawakilisha binadamu wote.

666

"mia sita sitini na sita"

Revelation 14

Ufunuo 14 Maelezo ya jumla

Dhana muhimu katika sura hii

"Ushindi dhidi ya yule mnyama"

Huu ni ushindi katika vita vya kiroho vinavyotokea wakati huu. Ingawa vita vingi vya kiroho haviezi kuonekana, kitabu cha Ufunuo kinatupa taswira ya wakati vita vya kiroho vitatokea hadharani. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#spirit and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Alama ya yule mnyama

Yohana amechukua muda mrefu kwa kuzungumzia ile alama inayopewa na yule mnyama. Wasomi wengi wanaamini kwamba sura hii inafundisha kwamba wale wanapokea alama hii watapata adhabu ya milele katika kuzimu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#eternity na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#hell)

Dhana muhimu katika sura hii

Mavuno

Mavuna ni mfano ya kawaida katika maandiko. Mavuno huashiria wakati vitu vizuri hutokea. Mara nyingi hutumiwa kuashiria watu kutokea kumwamini Yesu lakini Yohana hamaanishi hivi hapa. Hapa inatumika kufafanua kumalizika kwa mipango ya Mungu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith)

<< | >>

Revelation 14:1

Kauli Unganishi:

Yohana aanza kueleza sehemu ifuatayo katika maono yake. Kuna waumini 144,000 wanaosimama mbele ya Mwanakondoo.

Taarifa ya Jumla:

Neno "nikaona" inamzungumzia Yohana.

Mwanakondoo

Huyu ni mtoto wa kiume wa kondoo. Hapa hutumika kuashiria kuwa ni Kristo.

144,000

"laki moja na elfu arobaini na nne"

wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao

"ambao kwenye vipaji vyao vya nyuso Mwanakondoo na Baba yake waliandika majina yao"

Baba yake

Hili ni jina muhimu la Mungu linaloeleza uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

sauti kutoka mbinguni

"mlio kutoka mbinguni"

Revelation 14:3

Wakiimba wimbo mpya

"Wale watu 144,000 waliimba wimbo mpya." Hii inafafanua sauti aliyosikia Yohana. "Sauti hiyo ilikuwa ni wimbo mpya waliouimba"

wenye uhai wanne

"kiumbe hai" au "kitu chenye uhai"

wazee

Hii inamaanisha wazee ishirini na nne walikuwa wamekizunguka kiti cha enzi"

hawakujichafua wenyewe kwa wanawake

Maana zinazowezekana ni 1) "hawajawahi kuwa na mahusiano mabaya ya kimwili na mwanamke" au 2) "hawajawahi kukutana kimwili na mwanamke." Kujitia najisi na wanawake inaweza kuwa alama ya kuabudu sanamu.

maana walijitunza wenyewe dhidi ya matendo ya zinaa

Maana zinazowezekana ni 1) "hawakukutana na kimwili na mwanamke ambaye hakuwa mke wao" au 2) "ni mabikira."

walimfuata Mwanakondoo popote alipoenda

Kufanya kile afanyacho Mwanakondoo kinazungumziwa kama kumfuata. "wanafanya kile ambacho Mwanakondoo anafanya" au "wanamtii Mwanakondoo"

Hakuna uongo uliopatikana katika vinywa vyao

"kinywa" chao kinamaanisha kile walichosema. "Hawakuwahi kudanganya walipozungumza"

Revelation 14:6

Kauli Unganishi:

Yohana anaanza kuelezea sehemu ifuatayo ya maono yake. Huyu ni malaika wa kwanza kati ya watatu wanaotamkia dunia hukumu.

kila taifa, kabila, lugha, na watu

Hii humaanisha watu kutoka kila kabila.

Kwa maana muda wa hukumu yake umekaribia

Kuwepo katika wakati wa sasa unazungumziwa kama umekuja. Wazo la "hukumu" linaweza kuoneshwa na kitenzi. "sasa ni muda wa Mungu kuhukumu watu"

Revelation 14:8

Umeanguka, umeanguka Babeli mkuu

Malaika anaizungumzia Babeli kuangamizwa kama vile imeanguka. "Babeli kuu imeangamizwa"

Babebi kuu

"Babeli, ule mji mkuu" au "mji muhimu wa Babeli." Huu unawezekana kuwa ulikuwa ni alama ya mji wa Rumi ambao ulikuwa mkubwa, tajiri na wenye dhambi.

uliwanywesha

Babeli inazungumziwa kana kwamba ni mtu badala ya mji uliojaa watu.

kunywa divai ya tamaa zake mbaya

hii ni alama ya kushiriki katika tamaa zake mbaye za uasherati. "kuwa muasherati kama yeye" au "kulewa kama yeye na dhambi za uasherati"

tamaa mbaya

Babeli inazungumziwa kama vile ni kahaba aliyesababisha watu wengine watende dhambi pamoja naye. Hii inaweza kuwa na maana mara mbili: uasherati halisi na pia kuabudu miungu.

Revelation 14:9

kwa sauti kuu

"kwa sauti"

pia atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu

Kunywa divai ya ghadhabu ya Mungu ni alama ya kuadhibiwa na Mungu. "pia watakunywa sehemu ya divai inayowakilisha ghadhabu ya Mungu.

kumwagwa bila kuchanganywa

"kwamba Mungu amechanganya nguvu kamili"

kumwagwa bila kuchanganywa

Hii inamaanisha divai imechanganywa na divai zingine tu na wala hakuna maji yaliochanganywa humo. Ina nguvu, na mtu atakayeinywa nyingi atalewa sana. Kama alama, inaonesha kuwa Mungu atakuwa na hasira sana, sio hasira kidogo.

kikombe cha hasira yake

Mfano wa kikombe hiki kinashikilia divai inayowakilisha hasira ya Mungu.

malaika zake watakatifu

"malaika watakatifu wa Mungu"

Revelation 14:11

Kauli Unganishi:

Malaika wa tatu anendelea kuzungumza.

Na moshi wa maumivu yao

Maneno "maumivu yao" inamaanisha moto unaowatesa. "moshi kutoka katika moto unaowatesa"

hawakuwa na mapumziko

"hawana nafuu" au "mateso hayakomi"

mchana au usiku

Sehemu hizi mbili za siku zinatumika kumaanisha muda wote. "wakati wote"

Huu ni wito wa subira na uvumilivu kwa walio watakatifu

"Wale ambao ni watakatifu lazima wadumu kwa uvumilivu na kwa uaminifu"

Revelation 14:13

wafu wafao

"wale waliokufa"

wafao katika Bwana

"walioungana na Bwana na kufa." Hii inaweza kumaanisha watu waliouawa na adui zao. "walikufa kwa sababu wameungana na Bwana"

kazi

shida na mateso

matendo yao yatawafuata

Matendo haya yanazungumziwa kana kwamba yako hai na yanaweza kuwafuata waliyoyatenda. Maana zinazowezekana ni 1)"wengine watajua matendo mema waliyotenda watu hawa" au 2)"Mungu atawazawadia kwa matendo yao."

Revelation 14:14

Kauli Unganishi:

Yohana aanza kueleza sehemu inayofuata ya maono yake. Hii sehemu inahusu Mwana wa Adamu anapovuna dunia. Kuvuna nafaka ni ishara ya Mungu kuhukumu watu.

mfano wa Mwana wa Mtu

Huu usemi unafafanua umbo la binadamu, mtu anayefanana na binadamu.

taji ya dhahabu

Hii ilikuwa ni mfano wa shada la matawi ya mizeituni au majani ya laurusi yaliyopondwa kwenye dhahabu. Mifano yake iliyoundwa walipewa wanariadha washini kuvaa vichwani mwao.

mundu

kifaa kikali kama kisu au panga kilicho na mkunjo kwa ajili ya kukatia nyasi, nafaka na mizabibu.

kutoka kwenye hekal

"kutoka kwenye hekalu la kimbinguni"

muda wa mavuno umeshawadia

Kuwepo kwa wakati uliopo inazungumziwa kama umekuja.

dunia ikavunwa

"alivuna dunia"

Revelation 14:17

Kauli Unganishi:

Yohana anaendelea kuelezea maono yake ya dunia kuvunwa.

aliyekuwa na mamlaka juu ya moto

Hapa "mamlaka juu ya" inamaanisha jukumu la kuujali moto.

Revelation 14:19

pipa kubwa la divai ... Chujio la divai

Hii inamaanisha chombo kimoja.

pipa kubwa la divai ya ghadhabu ya Mungu

"pipa kubwa la divai ambapo Mungu ataonesha ghadhabu yake"

hatamu

kifaa kilochotengenezwa na ngozi che kuzungushwa kwenye kichwa cha farasi ili kumuongoza.

stadia 1,600

"kilomita 300" au "maili 200"

Revelation 15

Ufunuo 15 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Matukio na picha zinazofafanuliwa hapa inatokea mbinguni.

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 15:3-4

Dhana muhimu katika sura hii

"Mahali patakatifu, ambamo kulikuwa na hema la mashahidi palifunguka mbinguni"

Maelezo haya yamefanya wasomi wengine kuamini kwamba hekalu la Wayahudi lilikuwa na mandhari ya mbinguni. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#heaven na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Nyimbo

Mbinguni mara nyingi huelezewa kama mahali ambapo watu wanaimba.Hizo ni nyimbo za ibada kwa Mungu. Hii inaashiria kwamba mbinguni ni mahali ambapo Mungu anaabudiwa kila mara.

<< | >>

Revelation 15:1

Taarifa ya Jumla:

Huu mstari ni ufupi wa kitakachotokea katika 15:6-16:21.

kubwa na yenye kushangaza

Maneno haya yanamaana za kukaribiana na yanatumika kwa msisitizo. "jambo lililo nishangaaza sana"

malaika saba wenye mapigo saba

"malaika saba waliokuwa na mamlaka ya kutuma mapigo saba duniani"

ambayo yalikuwa mapigo ya mwisho

"na baada yake, hayatakuwapo mapigo mengine tena"

katika hayo hasira ya Mungu ilikuwa imetimilika

"kwa kuwa mapigo haya yatakamilisha ghadhabu ya Mungu." maana zinazowezekana ni 1) mapigo haya yataonesha hasira yote ya Mungu au 2) baada ya mapigo haya, Mungu hatakuwa na hasira tena.

Revelation 15:2

Taarifa ya Jumla:

Hapa Yohana anaanza kueleza maono yake ya watu waliomshinda mnyama na wanamsifu Mungu.

bahari la bilauri

Inaainisha wazi jinsi ilivyokuwa kama kioo au bahari. Maana zinazowezekana ni 1) bahari linazungumziwa kama vile ni kioo. "bahari lililo laini kama kioo" au 2) kioo kinazungumziwa kama vile ni bahari. "kioo kilichosambazwa kama bahari"

wale waliokuwa washindi dhidi ya mnyama na sanamu yake

Jinsi walivyokuwa washindi inaweza kuelezwa vizuri. "wale waliokuwa washindi dhidi ya mnyama na sanamu yake kwa kutowaabudu."

juu ya namba inayowakilisha jina lake

Jinsi walivyokuwa washindi dhidi ya namba inaweza kuelezwa vizuri. "juu ya namba inayowakilisha jina lake na kwa kutowekwa alama ya namba hio"

namba inayowakilisha jina lake

Hii inamaanisha namba inayoelezwa katika 13:18.

Revelation 15:3

Walikuwa wakiimba

"Wale waliokuwa washindi dhidi ya mnyama walikuwa wakiimba"

Nani atashindwa kukuhofu wewe Bwana na kulitukuza jina lako?

Swali hili linatumika kuonesha kushangazwa kwao na jinsi gani Bwana alivyo mkuu na mtukufu. Inaweza kuelezwa kama mshangao. "Bwana, watu wote watakuogopa na kutukuza jina lako!"

kulitukuza jina lako

Usemi huu "jina lako" inamaanisha Mungu. "na kukutukuza wewe"

matendo yako yamejulikana

"umewafanya watu wote wajue matendo yako mema"

Revelation 15:5

Kauli Unganishi:

Malaika saba na mapigo saba wanatoka katika mahali patukufu zaidi. Zilizungumziwa katika 15:1.

Baada ya mambo hayo

"Baada ya watu kumaliza kuimba"

malaika saba wenye mapigo saba

Malaika hawa walionwa wakishilia mapigo saba kwa sababu walipewa mabakuli yaliojaa ghadhabu ya Mungu katika 15:7.

kitani

nguo ya gharama iliyotengenezwa kwa kitani.

mishipi

Mshipi ni kipande cha nguo cha urembo kinachovaliwa sehemu ya juu ya mwili.

Revelation 15:7

wenye uhai wanne

"viumbe wanne" au "vitu vinne vyenye uhai"

mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu

Picha ya divai katika bakuli inaweza kuelezwa vizuri. Neno "ghadhabu" hapa inamaanisha adhabu. Divai ni alama ya adhabu. "mabakuli saba yaliojaa divai inayoashiria ghadhabu ya Mungu"

mpaka mapigo saba ya malaika saba yalipokamilika

"mpaka malaika saba walipomaliza kutuma yale mapigo saba duniani"

Revelation 16

Ufunuo 16 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii ni hitimisho la sehemu kubwa ya kitabu cha Ufunuo ambayo inamalizia kipindi cha hasira ya Mungu ama hukumu kubwa inaletwa na Mungu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#judge)

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 16:5-7

Dhana muhimu katika hii sura

"Mahali patakatifu sana"

Maelezo haya yamefanya wasomi wengine kuamini kwamba hekalu la Wayahudi lilikuwa na mandhari ya mbinguni. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#heaven na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Hukumu za mabakuli saba

Sura hii inafunua hukumu zinazoitwa hukumu za mabakuli saba. Hukumu hizi zimepewa taswira kama zile ambazo zinamwagwa inje kuashiria haraka na ujumla wa hizo hukumu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Hisia ya sura hii inakusudiwa kumshtua msomaji. Hii isipunguzwe kwenye tafsiri.

Har-Magedoni

Hili ni neno la Kiebrania na linatumika kama jina la mahali. Yohana anatafsiri herufi za neno hili kwa kuziandika kwa herufi za Kigriki. Watafsiri wanashauriwa kulitafsiri kutumia herufi za lugha kusudiwa.

<< | >>

Revelation 16:1

Kauli Unganishi:

Yohana aendelea kuelezea sehemu ya maono kuhusu malaika saba na mapigo saba. Mapigo saba ni mabakuli ya ghadhabu ya Mungu.

Nikasikia

Aliyesikia ni Yohana.

mabakuli ya ghadhabu ya Mungu

Picha ya divai katika bakuli inaweza kuelezwa vizuri. Neno "ghadhabu" hapa inamaanisha adhabu. Divai ni alama ya adhabu. "mabakuli saba yaliojaa divai inayoashiria ghadhabu ya Mungu"

Revelation 16:2

kumwaga bakuli lake

Neno "bakuli" linamaanisha kile kilichomo. "kumwagwa divai kutoka katika bakuli lake" au " kumwaga ghadhabu ya Mungu kutoka katika bakuli lake"

majeraha mabaya

"majeraha yenye maumivu." Haya yanaweza kuwa maambukizo kutoka kwa magonjwa au majeruhi ambayo hayajapona.

alama ya mnyama

Hii ilikuwa alama ya kuonesha kuwa aliyekuwa nayo alimwabudu mnyama.

Revelation 16:3

alimwaga bakuli lake

Neno "bakuli" linamaanisha kile kilichomo. "kumwagwa divai kutoka katika bakuli lake" au " kumwaga ghadhabu ya Mungu kutoka katika bakuli lake"

bahari

Hii inamaanisha maziwa yote ya maji ya chumvi na mabahari.

Revelation 16:4

akamwaga bakuli lake

Neno "bakuli" linamaanisha kile kilichomo. "kumwagwa divai kutoka katika bakuli lake" au " kumwaga ghadhabu ya Mungu kutoka katika bakuli lake"

mito na katika chemichemi za maji

Hii inamaanisha mikusanyiko yote ya maji safi.

malaika wa maji

Maana zinazowezekana ni 1) hii inamaanisha malaika wa tatu aliye juu ya kumwaga ghadhabu ya Mungu katika mito na chemichemi za maji au 2) huyu alikuwa ni malaika mwingine aliyekuwa juu ya maji yote.

Wewe ni mtakatifu

"Wewe" inamaanisha ni Mungu.

Wewe uliyepo na uliyekuwepo

"Mungu aliyepo na aliyekuwepo."

walimwaga damu za waamini na manabii

Hapa "walimwaga damu" inamaanisha kuuawa. "watu waovu waliwaua waamini na manabii"

umewapa wao kunywa damu

Mungu atawafanya watu waovu wanywe maji atakayoyabadili kuwa damu.

Nikasikia madhabahu ikijibu

Neno "madhabahu" hapa inamaanisha mtu madhabahuni. "Nikasikia mtu madhabahuni akijibu"

Revelation 16:8

akamwaga kutoka kwenye bakuli

Neno "bakuli" linamaanisha kile kilichomo. "kumwagwa divai kutoka katika bakuli lake" au " kumwaga ghadhabu ya Mungu kutoka katika bakuli lake"

likapewa ruhusa kuunguza watu

Yohana analizungumzia jua kama mtu. "na akasababisha jua kuwachoma watu kwa ukali"

Waliunguzwa kwa joto lenye kutisha

"Lile joto kali sana liliwachoma vibaya"

wakalikufuru jina la Mungu

Hapa jina la Mungu linamuwakilisha Mungu. "walimkufuru Mungu"

mwenye nguvu juu ya mapigo yote

Usemi huu unawakumbusha wasomaji kuhusu jambo ambalo wanalijua kumhusu Mungu. Linasaidia kueleza kwa nini watu walimkufuru Mungu. "kwa sababu ana nguvu juu ya mapigo yote haya"

guvu juu ya mapigo yote

Hii inamaanisha nguvu ya kusababisha haya mapigo kwa watu, na nguvu ya kuyasitisha mapigo.

Revelation 16:10

akamwaga kutoka kwenye bakuli lake

Neno "bakuli" linamaanisha kile kilichomo. "kumwagwa divai kutoka katika bakuli lake" au " kumwaga ghadhabu ya Mungu kutoka katika bakuli lake"

kiti cha enzi cha mnyama

Hapa ndipo mnyama anapotawalia. Inaweza kumaanisha mji mkuu wa ufalme wake.

giza likaufunika ufalme wake

Giza linazungumziwa kama vile ni kitu kama blangeti. "ikawa giza katika ufalme wake wote" au " ufalme wake wote ukawa giza"

Walisaga ... Wakamtukana

Hapa inamaanisha watu katika ufalme wa mnyama.

Revelation 16:12

limwaga kutoka kwenye bakuli lake

Neno "bakuli" linamaanisha kile kilichomo. "kumwagwa divai kutoka katika bakuli lake" au " kumwaga ghadhabu ya Mungu kutoka katika bakuli lake"

maji yake yakakauka

"Na maji yake yalikauka" au "Na kusababisha maji yake kukauka"

zilizoonekana kama chura

Chura ni mnyama mdogo anayeishi karibu na maji. Wayahudi waliwafikiria kuwa wanyama wachafu.

joka

Hili lilikuwa tambaazi kubwa kali, kama mjusi. Kwa wayahudi ilikuwa ni alama ya uovu na machafuko. Joka pia linatambulika katika mstari wa 9 kama "ibilisi au Shetani"

Revelation 16:15

Taarifa ya Jumla:

Mstari wa 15 ni mapumziko kutoka katika masimulizi makuu ya maono ya Yohana. Haya ni maneno yaliyonenwa na Yesu. Masimulizi yanaendelea mstari wa 16.

Tazama! Ninakuja

Inaweza kuwekwa wazi kwamba Bwana Yesu ndiye aliyesema haya katika UDB. Mabano yanatumika hapa kuonesha kuwa sio sehemu ya masimulizi ya maono.

Ninakuja kama mwizi!

Yesu atakuja wakati watu hawatarajii kama vile mwizi ajavyo asipotarajiwa.

atunzaye mavazi yake

Kuishi njia sahihi inazungumziwa kama mtu kutunza mavazi yake. "kufanya kilicho sahihi kama mtu atunzavyo mavazi yake mwilini"

atunzaye mavazi yake

Tafsiri zingine hutafsiri, "kukaa na mavazi yake"

kuiona aibu yake

Hapa "watakaoina" ni watu wengine.

Waliwaleta pamoja

"roho za mapepo ziliwaleta wafalme na majeshi yao pamoja"

sehemu iliyoitwa

"sehemu watu waitayo"

Amagedoni

Hili ni jina la sehemu.

Revelation 16:17

Kauli Unganishi:

Malaika wa saba amwaga bakuli la saba la ghadhabu ya Mungu.

alimwaga kutoka kwenye bakuli lake

Neno "bakuli" linamaanisha kile kilichomo. "kumwagwa divai kutoka katika bakuli lake" au " kumwaga ghadhabu ya Mungu kutoka katika bakuli lake"

Kisha sauti kuu ikasikika kutoka hekaluni na kutoka kwenye kiti cha enzi

Hii inamaanisha mtu aliyekuwa kwenye kiti cha enzi au karibu na kiti cha enzi alinena kwa sauti ku. Haiko wazi ni nani anayezungumza.

miale ya mwanga wa radi

Mwanga unaotokea wakati radi ikipiga.

ngurumo, vishindo vya radi

Hii ni miungurumo ya sauti ambayo radi husababisha.

Mji mkuu uligawanyika

"Tetemeko liliugawanya mji mkuu"

Kisha Mungu akakumbuka

"Kisha Mungu akawazia" au "Kisha Mungu akaanza kuwa makini na." Hii haimaanishi kuwa Mungu alikumbuka jambo alilosahau.

akaupa mji huo kikombe kilichokuwa kimejaa divai kutoka kwenye ghadhabu yake iliyo kali

Divai ni isharaya ya ghadhabu yake. Kuwafanya watu kuinywa ni ishara ya kuwaadhibu. "aliwafanya watu wa mji huo kunywa divai inayoashiria ghadhabu yake"

Revelation 16:20

Kauli Unganishi:

Hii ni sehemu ya bakuli la saba la ghadhabu ya Mungu.

milima haikuonekana tena

Kutokuweza kuiona milima ni mfano wa maneno yanayoeleza wazo ya kwamba milima haikuwepo tena. "milima haikuwepo tena"

talanta

"kilo 34"

Revelation 17

Ufunuo 17 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii ni uendelezo wa sura iliyopita.

Dhana muhimu katika sura hii

Kahaba

Wayahudi walionyeshwa mara nyingi kama watu wazinzi na wakati mwingine kama mkahaba. Hayo siyo maelezo yalioko hapa. Muktadha huu unamtambulisha shetani kama kahaba lakini mtafsiri ayafanye haya maelezo yasiwe wazi kabisa. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Vilima saba

Huenda hii inaashiria mji wa Roma uliosemekana kujengwa juu ya vilima saba. Hata hivyo, mtafsiri asijaribu kutambulisha hivi vilima saba katika tafsiri.

Tamathali muhimu za usemi katika sura hii

Mifano

Yohana anatumia mifano nyingi katika sura hii. Anapeyana maelezo fulani ya maana yazo lakini anaziacha kubaki kutoeleweka kwa kiwango fulani. Mtafsiri ajaribu kufanya namna hivyo. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Na yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kuja "

Kauli hii imekusudiwa kutoa utofautisho na kauli ya kwamba Yesu "alikuwa na yuko na yu tayari kuja" ambayo imetumika kwingine kwenye maandiko (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

Matumizi ya ukweli kinza

Ukweli kinza ni kauli ambayo inaonekana kujipinga ingawa siyo ya kipumbafu. Sentenzi katika 17:11 ni ukweli kinza"yule mnyama ...ni mfalme wa nane ingawa pia ni mmoja wa wale wafalme saba." Mtafsiri asijali kutatua ukweli huu kinza na ubakie kuwa siri. (Ufunuo 17:11)

<< | >>

Revelation 17:1

Taarifa ya Jumla:

Yohana anaanza kueleza sehemu ya maono yake kuhusu kahaba mkuu.

hukumu ya kahaba mkuu akaaye juu ya maji mengi

Nomino "hukumu" linaweza kuelezwa na kitenzi "kuhukumu". "jinsi gani Mungu atamhukumu kahaba mkuu aliyeketi juu ya maji mengi"

kahaba mkuu

"kahaba ambaye kila mmoja anamfahamu." Anawakilisha mji flani wenye uovu.

juu ya maji mengi

"juu ya mito mingi"

na juu ya mvinyo wa uasherati wake wakaao duniani wameleweshwa

Divai inawakilisha uasherati. "Watu wa duniani walilewa kwa kunywa divai yake, ambayo ni, walikuwa washerati"

uasherati wake

Hii inaweza kuwa na maana mbili: uasherati miongoni mwa watu na pia kuabudu miungu.

Revelation 17:3

akanichukua katika Roho mpaka nyikani

Mazingira yanabadilika kutoka kwa Yohana kuwa mbinguni na kuwa nyikani.

mawe ya thamani, na lulu

"aina nyingi za mawe ya dhamani"

lulu

Shanga nzuri na za dhamani. Zinaundwa ndani ya ganda la mnyama fulani mdogo aishiye baharini.

Juu ya paji la uso wake limeandikwa jina

"Mtu aliaandika jina kwenye paji la uso wake"

Babeli mkuu

Kama inahitajika kuwekwa wazi kwamba jina linamaanisha yule mwanamke, inaweza kuwekwa katika sentesi. "Mimi ni Babeli, yule mwenye nguvu"

Revelation 17:6

Taarifa ya Jumla:

Malaika anaanza kumueleza Yohana maana ya yule kahaba na mnyama mwekundu. Malaika anaeleza mambo haya hadi mstari wa 18.

alikuwa amelewa damu

"amelewa kwa sababu alikunywa damu"

waliokufa kwa ajili ya Yesu

"waumini waliokufa kwa sababu waliwaambia wengine kuhusu Yesu"

mshangao

"staajabu" au "shangazwa"

Kwa nini unashangaa?

Malaika alitumia swali hili kumkemea Yohana kwa upole. "Hautakiwi kushangaa!"

Revelation 17:8

shimo lisilo na mwisho

Hili ni shimo refu sana. Maana zinazowezekana ni 1)shimo halina mwisho chini; inaendelea kwenda chini zaidi milele au 2) shimo ni refu sana hata linakuwa kana kwamba halina mwisho.

Kisha ataendelea na uharibifu

Nomino "uharibifu" inaweza kutafsiriwa na kitenzi. "Kisha ataangamizwa" au "Kisha Mungu atamuangamiza"

ataendelea na uharibifu

Uhakika wa kile kitakachotokea baadae kinazungumziwa kana kwamba mnyama anaendako.

wale ambao majina yao hayakuandikwa

"wale ambao majina yao hayajaandikwa na Mungu"

tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu

"kabla Mungu hajaumba ulimwengu"

Revelation 17:9

Kauli Unganishi:

Malaika anaendelea kuzungumza. Hapa anafafanua maana ya vichwa saba vya mnyama ambavyo mwanamke amepanda.

Wito huu

"hii inaifanya ulazima kuwa"

Wito huu ni kwa ajili ya akili zilizo na hekima

Nomino "akili" na "hekima" zinaweza kuelezwa na "fikiri" na "kwa hekima." Kwa nini akili yenye hekima inahitaji inaweza kuwekwa wazi. "Akili yenye hekima inahitaji ili kuelewa hili" au "Unahitaji kufikiria kwa hekima ili kuelewa hili"

Vichwa saba ni milima saba

Hapa "ni" inamaanisha "kusimamia," "wakilisha."

Wafalme watano wameanguka

Malaika anazungumzia kufa kama kuanguka. "Wafalme watano wamekufa"

mmoja yupo

"mmoja ni mfalme sasa" au "mfalme mmoja yu hai sasa"

mwingine hajaja bado; wakati atakapokuja

Kutokuwepo inazungumziwa kama bado hajafika. "mwingine bado hajawa mfalme; akiwa mfalme"

atakaa kwa muda mfupi tu

Malaika anazungumzia kuhusu mtu kuendelea kuwa mfalme kana kwamba anabaki mahali fulani. "atakuwa mfalme kwa muda mfupi tu"

Revelation 17:11

ni mmoja wa wale wafalme saba

Maana zinazowezekana ni 1) mnyama anatawala mara mbili: kwanza kama mmoja wa wafalme saba, na kisha kama mfalme wa nane au 2) mnyama yuko katika kundi la hao wafalme saba kwa sababu ni kama wao.

anaenda kwenye uharibifu

Uhakika wa kile kitakachojiri mbeleni kinazungumziwa kana kwamba mnyama anaendako. "hakika itaangamizwa" au "Mungu hakika ataiangamiza"

Revelation 17:12

Kauli Unganishi:

Malaika anaendelea kuzungumza na Yohana. Hapa anaelezea maana ya mapembe kumi ya mnyama.

kwa saa moja

"kwa muda mfupi sana" au "kwa sehemu ndogo sana ya siku"

Hawa wana shauri moja

"Hawa wote wanawaza kitu kimoja" au "Hawa wote wanakubaliana kufanya kitu cha pamoja"

Mwanakondoo

Huyu ni mtoto wa kiume wa kondoo. Hapa hutumika kuashiria kuwa ni Kristo.

walioitwa, waliochaguliwa, na waaminifu

Hii inamaanisha kundi moja la watu. ""Walioitwa, kuchaguliwa , na waaminifu" au " wale ambao Mungu amewaita na kuwachagua na walio waaminifu kwake"

Revelation 17:15

Yale maji uliyoyaona, hapo alipoketi yule kahaba ni watu, makutano, mataifa na lugha

Hapa "ni" inamaanisha "yanawakilisha"

maji

"mito mingi"

makutano

"makundi makubwa ya watu" au "idadi kubwa ya watu"

lugha

Hii inamaanisha watu wanaozungumza hizo lugha.

Revelation 17:16

watamfanya kuwa mpweke na uchi

"kuiba kila kitu alichonacho na kumuacha bila kitu"

watamla mwili wake

Kumuangamiza kabisa inazungumziwa kama kula mwili wake. "watamuangamiza kikamilifu"

Maana Mungu ameweka mioyoni mwao kubeba kusudi lake kwa makubaliano ... yatakapotimia

Watakubali kumpa mnyama nguvu zao, lakini haitakuwa kwamba wanataka kumtii Mungu. "Kwa kuwa Mungu ataweka mioyoni mwao kukubali kumpa mnyama uwezo wao kutawala hadi maneno ya Mungu yatimie, na kwa kufanya hivi, watakamilisha mpango wa Mungu.

Mungu ameweka mioyoni mwao

Moyo unaashiria hamu. Kuwafanya kutaka kufanya kitu inazungumziwa kama kuweka mioyoni mwao. "Mungu amewafanya watake"

nguvu za kutawala

"mamlaka" au "mamlaka ya kifalme"

mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mpaka Mungu atimize alichosema kitatokea"

Revelation 17:18

Kauli Unganishi:

Malaika amaliza kuzungumza na Yohana kuhusu kahaba na mnyama.

ni

Hapa "ni" inamaanisha "anawakilisha"

mji ule mkubwa utawalao

Inaposema mji unaotawala, inamaanisha kwamba kiongozi wa mji anatawala. "mji mkuu ambaye kiongozi wake anatawala"

Revelation 18

Ufunuo 18 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Sura ya 19 itaendeleza mambo yaliomo kwenye sura hii na sura zote zichukuliwe kama kipengele kimoja.

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 19:1-8

Dhana muhimu katika sura hii

Unabii

Malaika anapeana unabii kuhusu kuanguka kwa Babeli. Inazungumziwa kana kwamba ishatokea ingawa haijatokea. Hii ilikuwa ni kawaida katika unabii na unasisitiza kutokuepuka kwa hukumu ijayo. Inatabiriwa pia watu wataomboleza kuanguka kwa Babeli. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#judge na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#writing-apocalypticwriting)

Tamathali muhimu sa usemi katika sura hii

Mifano

Mifano mara nyingi hutumiwa katika unabii. Sura hii inaachana kidogo na mfumo wa kiapokalipti wa kitabo hiki cha Ufunuo. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

<< | >>

Revelation 18:1

Kauli Unganishi:

Malaika mwingine ashuka toka mbinguni na kuzungumza. Huyu ni malaika tofauti na yule wa sura iliyopita, aliyezungumza kuhusu kahaba na mnyama.

Taarifa ya Jumla:

Anayezungumziwa hapa ni kama mtu ni mji wa Babeli.

Umeanguka, umeanguka, ule mji mkuu Babeli

Malaika anazungumzia Babeli kuangamizwa kama vile kuanguka.

ndege achukizaye

"ndege anayeudhi" au "ndege isyevutia"

mataifa yote

Mataifa ni njia nyingine ya kusema kwa watu wa mataifa hayo. "watu wa mataifa hayo"

yamekunywa mvinyo ya tamaa ya uovu wake

Hii ni ishara ya kushiriki katika tamaa zake za uasherati. "yamekuwa na uasherati kwama yeye" au "yamelewa na uasherati wake"

tamaa ya uovu wake

Babeli inazungumziwa kana kwamba ni kahaba aliyesababisha watu wengi wafanye dhambi pamoja naye. Hii inaweza kuwa na maana mara mbili: uasherati halisi na kuabudu miungu.

Wafanya biashara

Mfanya biashara ni mtu anayeuza vitu.

kwa nguvu ya maisha yake ya anasa

"kwa sababu alitumia pesa nyingi sana kwa ajili ya uasherati"

Revelation 18:4

Kauli Unganishi:

Sauti nyingine kutoka mbinguni inazungumza.

Taarifa ya Jumla:

Anayezungumziwa kama mtu ni mji wa Babeli, ambao unazungumziwa kama vile ni kahaba.

sauti nyingine

Neno "sauti" inamaanisha msemaji, ambaye huwezekana kuwa ni Yesu au Baba. "mtu mwingine"

Dhambi zake zimerundikana juu mpaka mbinguni

Sauti inazungumzia dhambi za Babeli kama vile ni vitu vinavyoweza kuunda rundo. "Dhambi zake ni nyingi sana ni kama rundo linalofika mbinguni"

ameyakumbuka

"akawazia" au "akaanza kuwa makini na." Hii haimaanishi kuwa Mungu alikumbuka jambo alilosahau.

Mlipeni kama alivyowalipa wengine

Sauti inazungumzia adhabu kana kwamba ni malipo. "Muadhibu kama alivyowaadhibu wengine"

mkamlipe mara mbili

Sauti inazungumzia adhabu kana kwamba ni malipo. "muadhibu mara mbili zaidi"

katika kikombe alichokichanganya, mchanganyishieni mara mbili kwa

Sauti inazungumzia kusababisha wengine kuteseka kama kuandaa divai yenye nguvu kwa ajili yao kunywa. "muandalie divai ya mateso ambayo ina nguvu mara mbili zaidi ya ile aliyowaandalia wengine" au "mfanyeni ateseke mara mbili zaidi ya alivyowatesa wengine"

mchanganyishieni mara mbili

Maana zinazowezekana ni 1)"andaa mara mbili ya kipimo" au 2)"ifanye kuwa na nguvu mara mbili zaidi"

Revelation 18:7

Kauli Unganishi:

Sauti ile ile kutoka mbinguni inaendelea kuzungumzia Babeli kana kwamba ni mwanamke.

alivyojitukuza

"watu wa Babeli walijitukuza"

Nimekaa kama malkia

Anadai kuwa mtawala, akiwa na mamlaka yake mwenyewe.

siyo mjane

Anadokeza kuwa hatakuwa tegemezi kwa watu wengine.

sitaona maombolezo

Kupitia maombolezo inatajwa kama kuona maombolezo. "sitawahi kuomboleza"

mapigo yake yatakuja

Kuwepo wakati wa mbeleni inazungumziwa kama yanakuja.

Atateketezwa kwa moto

Kuchomwa na moto inazungumziwa kama kuliwa na moto. "Moto utamchoma kikamilifu"

Revelation 18:9

Kauli Unganishi:

Yohana anasema kile watu wanachosema kuhusu Babeli.

Taarifa ya Jumla:

Hapa anayezungumziwa kama mtu ni mji wa Babeli.

waliofanya uasherati na kuchanganyikiwa pamoja naye

"kutenda dhambi za ngono na kufanya chochote walichotaka kama watu wa Babeli walivyofanya"

hofu ya maumivu makali

Maumivu makali yanaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "wakihofu kuwa watateswa kama Babeli" au "wakihofu kuwa Mungu atawatesa kama anavyoitesa Babeli"

Ole, ole

Hii inarudiwa kwa ajili ya msisitizo.

adhabu yako imekuja

Kuwepo katika wakati wa sasa inazungumziwa kama ilimefika.

Revelation 18:11

kuomboleza kwa ajili yake

"kuomboleza kwa ajili ya watu wa Babeli"

mawe ya thamani, lulu

"aina nyingi za mawe ya dhamani"

kitani nzuri

nguo ya gharama iliyotengenezwa kwa kitani.

zambarau

"nguo ya zambarau"

hariri

Hii ni nguo laini, imara iliyotengenezwa kutoka kwenye nyuzi bora kama nondo wa hariri wanapotengeneza vifukofuko vyao. "nguo ya gharama" au "nguo bora" au "nguo nzuri"

nyekundu

"nguo nyekundu"

kila chombo cha pembe za ndovu

"kila aina ya chombo kilichoundwa na pembe za ndovu"

pembe za ndovu

Mali kigumu na kizuri cheupe ambacho watu wanaotoa kutoka kwenye pembe au meno ya wanyama wakubwa sana kama tembo na sili wa baharini. "mapembe" au "meno ya dhamani ya wanyama"

marumaru

jiwe la dhamani linatumika kwenye ujenzi.

mdalasini

kiungo cha mapishi chenye harufu nzuri na kinatoka katika gome la aina fulani ya mti.

kiungo

kitu kinachotumika kuongeza ladha kwenye chakula au harufu nzuri kwenye mafuta.

Revelation 18:14

Tunda

Wanazungumzia vitu vizuri kama vile ni tunda. "Vitu vizuri"

uliyoyatamani kwa nguvu zako zote

"ulitaka sana"

hayatapatikana tena

Kutokupatikana inamaanisha kutokuwepo. uu ni usemi. "hautayaona tena"

Revelation 18:15

Taarifa ya Jumla:

Katika mistari hii, anayezungumziwa kama binadamu ni mji wa Babeli.

kwa sababu ya hofu ya maumivu yake

Nomino "hofu" na "mateso" zinaweza kuelezwa na misemo inayoweza kuonesha ni nani aliyehisi hofu na maumivu makali. "kwa sababu watahofia jinsi atakavyoteswa"

wakilia na kuomboleza kwa sauti

Hiki ndicho watakachokifanya wafanya biashara. "na watalia na kuomboleza kwa sauti"

mji ule mkuu uliovikwa kitani nzuri

Katika sura hii yote, Babeli inazungumziwa kama vile ni mwanamke. Wafanya biashara wanaizungumzia Babeli kama vile imevaa kitani nzuri kwa sababu watu wake walikuwa wamevaa kitani nzuri. "ule mji mkuu, ulio kama mwanamke aliyevaa kitani nzuri" au "ule mji mkuu, ambao wanawake wake walivaa kitani nzuri"

uliovikwa kitani nzuri

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "uliovaa kitani nzuri"

na kupambwa kwa dhahabu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "na kujipamba mwenyewe kwa dhahabu" au "na kujipamba wenyewe kwa dhahabu" au "na kuvaa dhahabu"

vito vya thamani

"vito vinavyodhaminiwa"

lulu

Shanga nzuri na za dhamani. Zinaundwa ndani ya ganda la mnyama fulani mdogo aishiye baharini.

kipato chao kinatoka baharini

Msemo "kutoka baharini" inamaanisha kile wanachokifanya baharini. "wanaosafiri baharini kujikimu kimaisha" au "wanaosafiri baharini kwenda sehemu tofauti ili kufanya biashara ya vitu"

Revelation 18:18

Taarifa ya Jumla:

Katika mistari hii, neno "wa" inamaanisha mabaharia na wanamaji, na yule mtu mmoja anayezungumziwa ni ule mji wa Babeli.

Ni mji gani unafanana na mji huu mkubwa?

Swali hili linawaonesha watu umuhimu wa mji wa Babeli. "Hakuna mji mwingine kama mji ule mkuu, Babeli"

Mungu ameleta hukumu yenu juu yake

Nomino "hukumu" inaweza kuelezwa na kitenzi "kuhukumu." "Mungu amemuhukumu kwa ajili yenu" au "Mungu amemuhukumu kwa sababu ya maovu aliyowatendea"

Revelation 18:21

Kauli Unganishi:

Malaika mwingine aanza kuzungumzia Babeli. Huyu ni malaika tofauti na yule aliyezungumza awali.

jiwe kuu la kusagia

Jiwe kubwa la duara linatumika kusaga nafaka.

abeli, ule mji mkuu, utatupwa chini kwa nguvu na hautaonekana tena

Mungu atauangamiza ule mji kikamilifu. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu ataitupa Babeli kwa nguvu, ule mji mkuu, na haitakuwepo tena"

hautaonekana tena

"na hakuna mtu atakayeuona tena." Kutokuonekana hapa inamaanisha kwamba haitakuwepo tena. "haitakuwepo tena"

Sauti ya wapiga vinanda, wanamuziki, wacheza filimbi, na tarumbeta hawatasikika tena kwenu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Hakuna mtu katika mji wenu ambaye atasikia tena sauti ya wapiga vinanda, wanamziki, na wacheza filimbi, na sauti ya tarumbeta"

kwenu

Malaika anazungumza kana kwamba Babeli alikuwa hapo akimsikiliza. "ndani ya Babeli"

hawatasikika tena kwenu

"hakuna mtu atakayewasikia tena." Kutosikiwa hapa inamaana ya kutokuepo. "hawatakuwepo katika mji wenu tena"

Hakuna fundi ... hataonekana kwenu

Kutopatikana humo inamaana hawatakuwemo. "Hakuna fundi yeyote atakaye kuwa katika mji wenu"

Hakuna sauti ya kinu itakayosikika tena kwenu

Sauti ya kitu kutokusikika inamaana kwamba hakuna atakaye sikia hiyo sauti. "Hakuna atakaye tumia vinu katika mji wenu"

Revelation 18:23

Kauli Unganishi:

Malaika aliyetupa jiwe la kusagia anamaliza kuongea.

Taarifa ya Jumla:

Maneno "yako," "wako," na yake" inamaanisha ni Babeli.

Sauti ya bwana harusi na bibi harusi hazitasikiwa tena ndani yako

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Hakuna ambaye atasikia tena ndani ya Babeli sauti za furaha za bwana harusi na bibi harusi"

hazitasikiwa tena ndani yako

"hakuna atakaye visikia ndani yenu tena." Kutosikiwa hapa inamaanisha havitakuwepo" "havitakuwa ndani ya mji wenu tena"

wafanyabiashara wako walikuwa wakuu wa nchi

Malaika anazungumzia watu muhimu na wenye nguvu kama vile walikuwa wana wa wafalme. "wafanya biashara wenu walikuwa kama wana wa waflame duniani" au "wafanya biashara wenu walikuwa watu muhimu zaidi duniani"

mataifa, wamedanganywa kwa uchawi wako

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "uliwadanganya watu wa mataifa na uchawi wako"

Ndani yake damu ya manabii na waamini ilionekana, na damu ya wote waliouawa juu ya nchi

Damu kukutwa ndani yake ina maana kuwa watu walikuwa na hatia ya kuua watu. "Babeli inahatia ya kuua manabii na waumini na watu wengine wote waliouawa"

Revelation 19

Ufunuo 19 maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Sura ya 19 inaendeleza maswala yalyomo katika sura ya 18 na kwa hivyo zote mbili zichukuliwe kama kipengele kimoja.

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 19:1-8

Dhana muhimu katika sura hii

Nyimbo

Mbinguni mara nyingi huelezewa kama mahali ambapo watu wanaimba.Hizo ni nyimbo za kumwabudu Mungu. Hii inaashiria kwamba mbinguni ni mahali ambapo Mungu anaabudiwa kila mara. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#heaven)

Sherehe za harusi

Sherehe za harusi ama karamu ni ishara muhimu inayotumika katika maandiko.Katika utamaduni wa Wayahudi, paradiso ama maisha pamoja na Mungu baada ya kifo ilipewa taswira ya karamu. Hapa Yesu anaipatia taswira ya karamu ya harusi ambayo mfalme huandalia mwana wake wa kiume ambaye ameoa sasa hivi. Mbali na hiyo, Yesu anasisitiza kwamba siyo watu wote Mungu hualika watajiandaa vilivyo ili washiriki. Watu kama hawa watatupwa nje ya karamu.

<< | >>

Revelation 19:1

Taarifa ya Jumla:

Hii ni sehemu ya maono ya Yohana ifuatayo. Hapa anaelezea furaha ya mbinguni juu ya kuanguka kwa kahaba mkuu, ambaye ni mji wa Babeli.

nilisikia

Hapa aliyesikia ni Yohana.

Haleluya

Neno hili linamaana "Msifu Mungu" au "Tumsifu Mungu."

kahaba mkuu

Hapa Yohana anamaanisha mji wa Babeli ambao watu wake waouvu wanawatawala watu wote duniani na kuwaongoza kuabudu miungu ya uuongo. Anawazungumzia watu waovu wa Babeli kana kwamba ni kahaba mkuu.

aliyeiharibu nchi

Hapa "nchi" ni njia nyingine ya kusema wakazi. "waliwaharibu watu wa duniani"

damu ya watumishi wake

Hapa "damu" ni njia nyingine ya kuwakilisha mauaji. "kuwaua watumishi wake"

yeye mwenyewe

Hii inamaanisha Babeli. Kurudiwa kwa haya maneno ni kwa ajili ya kuongeza msisitizo.

Revelation 19:3

walisema

Hapa waliosema ni umati wa watu mbinguni.

Haleluya

Neno hili linamaana "Msifu Mungu" au "Tumsifu Mungu."

Moshi hutoka kwake

Huu udondoshaji wa maneno. Unaweze kujumuisha maneno yaliyokosekana ambayo yameonyeshwa bila kutajwa. "Moshi wa moto unaowaka katika mji utainuka"

hutoka kwake milele na milele

"kutoka kwa waabudu sanamu milele na milele" au "kwa wale walioshiriki kwenye ukahaba watateseka milele"

hutoka kwake

Hapa anayezungumziwa ni Babeli.

wazee ishirini na wanne

wazee wanne -"wazee 24"

viumbe hai wanne

"viumbe wanne wenye uhai" au "vitu vinne vyenye uhai"

akaaye kwenye kiti cha enzi

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "aliyeketi kwenye kiti cha enzi"

Revelation 19:5

sauti ilitoka kwenye kiti cha enzi

Hapa Yohana anazungumzia "sauti" kana kwamba ni mtu. "mtu alizungumza kutoka kwenye kiti cha enzi"

Msifuni Mungu wetu

Hapa "wetu" inamaanisha mnenaji na watumishi wote wa Mungu.

ninyi mnaomcha yeye

Hapa ina maana ya kumheshimu Mungu. "wote mnaomheshimu Mungu"

wote wasio na umuhimu na wenye nguvu

Mnenaji anatumia maneno haya pamoja kumaanisha watu wote wa Mungu.

Revelation 19:6

Ndipo nilisikia sauti kama sauti ya kundi kubwa la watu, kama sauti ya ngurumo ya maji mengi, na kama ngurumo ya radi

Yohana anazungumzia anachokisia kama vile ilikuwa sauti iliyotengenezwa na umati mkubwa sana wa watu, maji mengi wanayotiririka kwa kasi, na ngurumo ya radi kubwa.

Haleluya

Neno hili linamaana "Msifu Mungu" au "Tumsifu Mungu."

Bwana ni

"Kwa sababu Bwana"

Revelation 19:7

Kauli Unganishi:

sauti ya umati kutoka mstari uliopita yaendelea kuzungumza.

tushangilie

Hapa wanaoshangilia ni watumishi wa Mungu.

kumpa utukufu

"kumpa Mungu utukufu" au "kumheshimu Mungu"

harusi na sherehe ya Mwana Kondoo ... bibi harusi yuko tayari

Hapa Yohana anazungumzia kuunganishwa pamoja kwa Yesu na watu wake kwama vile sherehe ya harusi.

Mwanakondoo

Huyu ni mtoto wa kiume wa kondoo. Hapa hutumika kuashiria kuwa ni Kristo.

imekuja

Kuwepo katika wakati wa sasa inazungumziwa kama imekuja.

bibi harusi yuko tayari

Yohana anawazungumzia watu wa Mungu kana kwamba ni bibi harusi anayejianda kwa ajili ya harusi yake.

Aliruhusiwa kuvalishwa kitani safi na yenye kung'aa

Hapa aliyevaa ni watu wa Mungu. Yohana anazungumzia matendo ya haki ya watu wa Mungu kana kwamba ni nguo safi za kung'aa ambazo bibi harusi huvaa siku ya harusi yake. Unaweza kueleza hii kwa hali ya kutenda. "Mungu alimruhusu kuvaa nguo kitani ya safi na ya kung'aa.

Revelation 19:9

Taarifa ya Jumla:

Malaika anaanza kuzungumza na Yohana. Hii inawezekana kuwa malaika yule yule aliyeanza kuzungumza na Yohana katika 17:1.

walioalikwa

Unaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "watu ambao Mungu amewakaribisha"

sherehe ya harusi ya Mwana kondoo

Hapa malaika anazungumzia kuunganishwa kwa Yesu na watu wake kama vile ni sherehe ya harusi.

Nilisujudu

Kusujudu ni kula chini kwenye ardhi, uso ukitazama chini, kuonesha heshima na utayari wa kutumika.

ndugu zako

Neno "ndugu" hapa inamaanisha waumini wote wa kiume na wa kike.

wenye kuushika ushuhuda wa Yesu

Hapakushika inamaansiha kuamini au kutangaza. "wanaosema ukweli kuhusu Yesu"

kwa kuwa ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii

Hapa "roho ya unabii" inamaanisha Roho Mtakatifu wa Mungu. "kwa sababu ni Roho wa Mungu anayewapa watu nguvu ya kunena ukweli kuhusu Yesu"

Revelation 19:11

Taarifa ya Jumla:

Hapa ni mwanzo wa maono mengine. Yohana anaanza kuelezea mpandaji wa farasi nyeupe.

Kisha niliona mbingu zimefunguka

Hii picha inatumika kuashiria mwanzo wa maono mapya.

yule aliyekuwa amempanda

Aliyempanda ni Yesu.

Huhukumu kwa haki

Hapa "haki" inamaanisha kile kilicho sahihi. "Anahukumu watu wote kulingana na kile kilicho sahihi"

Macho yake ni kama mwali wa moto

Yohana anazungumzia macho ya mpandaji kama vile yaling'aa kama mwali wa moto.

jina lililoandikwa juu yake

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu ameandika jina juu yake"

asilolifahamu mtu yeyote isipokuwa yeye mwenyewe

"Yeye tu ndiye ajuae maana ya jina hilo"

Amevaa vazi lililochovywa katika damu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Damu imefunika vazi lake"

jina lake anaitwa Neno la Mungu

Unaweza kueleza hii kwa hali ya kutenda. "jina lake pia ni Neno la Mungu"

Revelation 19:14

Kinywani mwake hutoka upanga mkali

Ubapa wa upanga ulikuaunchomoza kinywani mwake. Upanga wenyewe haukua ukisogea.

huyaangamiza mataifa

"huyapiga mataifa" au "anayamudu mataifa"

atawatawala kwa fimbo ya chuma

Yohana anazungumzia nguvu ya mpandaji kama vile anatawala na fimbo ya chuma.

Naye hukanyaga vyombo vya mvinyo kwa hasira kali ya Mungu

Yohana anazungumzia mpandaji kuangamiza adui zake kana kwamba ni zabibu ambazo mtu anakanyaga kwenye chombo cha mvinyo. Hapa "hasira" inamaanisha adhabu ya Mungu kwa watu waovu. "Atawakanyaga adui zake kulingana na hukumu ya Mungu, kama tu binadamu anavyokanyaga zabibu kwenye chombo cha mvinyo"

Naye ameandikwa juu ya vazi lake na katika paja lake jina

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu ameandika jina kwenye vazi lake na kwenye paji:"

Revelation 19:17

Niliona malaika amesimama katika jua

Hapa "jua" ni njia nyingine ya kusema mwanga wa jua. "Kisha nikaona malaika akisimama kwenye mwanga wa jua"

walio huru na watumwa, wasio na umuhimu na wenye nguvu

Malaika anatumia makundi mawili ya maneno yenye tofauti pamoja kumaanisha watu wote.

Revelation 19:19

Mnyama alikamatwa na nabii wake wa uongo

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mpandaji wa farasi nyeupe alimkamata mnyama na nabii wa uongo"

chapa ya mnyama

Hii ilikuwa alama ya kuonesha kuwa aliyekuwa nayo alimwabudu mnyama.

Wote wawili walitupwa wangali hai

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu alimtupa mnyama na nabii wa uongo wangali hai"

katika ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti

"ziwa la moto liwakalo salfa" au "sehemu ilyojaa moto unaowaka salfa"

Revelation 19:21

Wale waliobaki waliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa mmoja aliyepanda juu ya farasi

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mpandaji wa farasi aliwaua wanajeshi waliosalia wa mnyama kwa upanga uliotoka kinywani mwake"

uliotoka kinywani mwake

Ubapa wa upanga ulikuaunchomoza kinywani mwake. Upanga wenyewe haukua ukisogea.

Revelation 20

Ufunuo 20 Maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii inahusu kipindi kinachojulikana kama "ufalme wa kimilenia" kwa sababu ni ufalme wa miaka elfu moja. Sura hii ni muhimu kuelewa matukio ya siku za mwisho na kitabu cha Ufunuo.(Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lastday)

Dhana muhimu katika sura hii

Miaka elfu ya utawala wa Kristo

Yesu anaelezewa kama anayetawala kwa miaka elfu moja na nabii zote za maandiko kuhusu amani duniani kote lazima zitatimika. Wasomi wanatofautiana kuhusu iwapo huu ni muda wa ekweli ama ni ishara ya mwanzo wa utawala wa Kristo kwenye mioyo ya watu. Ni vizuri kutafsiri kana kwamba Kristo anatawala kimwili duniani kwa miaka elfu moja na siyo kujaribu kuweka taswira ya kimafumbo katika maandiko. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet)

Uasi wa mwisho

Sura hii inafafanua kipindi cha wakati baada ya utawala wa Yesu kinachojulikana kama uasi wa mwisho.Wakati huu,Shetani na watu wengi watajaribu kuasi dhidi ya Yesu. Hii itapelekea ushindi wa mwisho wa Mungu dhidi ya dhambi na uovu kabla ya maisha ya milele kuanza. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#evil na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#eternity)

Kiti kikubwa cheupe cha enzi

Hii ni hukumu muhimu mbinguni baada ya uasi wa mwisho.Wakati wa hukumu hii, watu walio na imani kwa Mungu wanatenganishwa na wale wanaomkataa. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#judge, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#heaven and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith)

Tamathali muhimu za usemi katika sura hii

Kitabu cha uzima

Hii ni mfano wa maisha ya milele. Walio na uzima wa milele wanasemekana kuwa na majina yao yameandikwa katika kitabu hiki cha uzima.. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii.

Kuzimu na ziwa la moto

Hizi zinaoenakana kuwa mahali mbili tofauti. Mtafsiri anaweza kufanya utafiti zaidi kupata jinsi ya kuzitofautisha hizi mahali mbili lakini zisifananishwe katika tafsiri. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#hell)

<< | >>

Revelation 20:1

Taarifa ya Jumla:

Yohana anaanza kueleza maono ya malaika akimtupa ibilisi kwenye shimo lisilo na mwisho.

Kisha niliona

Hapa aliyeona ni Yohana.

shimo lisilo na mwisho

Hili ni shimo refu sana na jembamba. Maana zinazowezekana ni 1)shimo halina mwisho chini; inaendelea kwenda chini zaidi milele au 2) shimo ni refu sana hata linakuwa kana kwamba halina mwisho.

joka

alikuwa mtambaazi mkubwa na mkali, anayefanana na mjusi. Kwa wayahudi, hii ilikuwa ni alama ya uovu na mabaya.

kulitia mhuri juu yake

Malaika alilifunga shimo na kulitia muhuri ili mtu yeyote asifungue. "aliifunga na kuitia muhuri ili mtu yeyote asifungue"

asiwadanganye mataifa

Hapa "mataifa" ni njia nyingine ya kusema watu wa duniani. "asiwadanganye makundi ya watu"

miaka elfu

"miaka 1,000"

ataachiwa huru

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu atamuamuru malaika amuweke huru"

Revelation 20:4

Taarifa ya Jumla:

Hii ni sehemu ifuatayo ya maono ya Yohana. Anaelezea kuona ghafla viti vya enzi na roho za waumini.

walikuwa wamepewa mamlaka ya kuhukumu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wale ambao Mungu aliwapa uwezo wa kuhukumu"

ambao walikuwa wamekatwa vichwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wale ambao vichwa vyao vilikatwa"

kwa ajili ya ushuhuda kuhusu Yesu

"kwa sababu walizungumza ukweli kuhusu Yesu"

Walikuja uzimani

"walifufuka" au "walikuwa hai tena"

Revelation 20:5

Wafu waliobaki

"watu wote wengine waliokufa"

miaka elfu ilipokuwa imeisha

"mwisho wa miaka 1,000"

Mauti ya pili haina nguvu juu ya watu hawa

Hapa Yohana anafafanua "mauti" kama mtu mwenye nguvu. "Watu hawa hawatapitia kifo cha pili"

Mauti ya pili

"kufa mara ya pili." Hii inaelezwa kama adhabu ya milele katika ziwa la moto la 20:13 na 21:7. "kifo cha mwisho ni ziwa la moto."

Revelation 20:7

Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu atamuachia Shetani kutoka katika gereza lake"

kona nne za dunia

Hii ni lugha inayomaanisha "duniani kote"

Gogu na Magogu

Haya ni majina ambayo nabii Hezekia alitumia kuwakilisha mataifa ya mbali.

Watakuwa wengi kama mchanga wa bahari

Huu ni msisitizo wa namba kubwa sana la askari wa jeshi la Shetani.

Revelation 20:9

Walikwenda

"Jeshi la Shetani lilikwenda"

mji upendwao

Hii inamaanisha Yerusalemu.

moto ulikuja kutoka mbinguni na kuwaangamiza

Hapa Yohana anazungumzia moto kana kwamba ukko hai. "Mungu alituma moto toka mbinguni kuwachoma"

Ibilisi, ambaye aliwadanganya, alitupwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu alimtupa Ibilisi aliyewadanganya" au "Malaika wa Mungu walimtupa Ibilisi aliyewadanganya,"

ziwa liwakalo kiberiti

"ziwa la moto liwakalo kiberiti" au "sehemu ilyojaa moto unaowaka kiberiti"

ambamo mnyama na nabii wa uongo walikuwa wameshatupwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambamo alikuwa amemtupa mnyama na nabii wa uongo"

Watateswa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu atawatesa"

Revelation 20:11

Taarifa ya Jumla:

Hii ni sehemu ifuatayo ya maono ya Yohana. Anaelezea kuona ghafla kiti cheupe cha enzi na wafu wakihukumiwa.

Dunia na mbingu zilikimbia mbali kutoka katika uwepo wake, lakini hapakuwako nafasi ya wao kwenda

Yohana anaelezea mbingu na nchi kama vile ni watu wanaojaribu kutoroka hukumu ya Mungu. Hii inamaanisha kuwa Mungu aliaangamiza kabisa mbingu na nchi za zamani.

hodari na wasio wa muhimu

Yohana anaunganisha maneno haya yenye maana tofauti kumaanisha watu wote waliokufa.

vitabu vilifunuliwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mtu alivifunua vitabu"

Wafu walihukumiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu aliwahukumu watu waliokuwa wamekufa na sasa wako hai tena"

kwa kile kilichoandikwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kwa kile alichoandika"

Revelation 20:13

Bahari iliwatoa wafu ... Kifo na kuzimu viliwatoa wafu

Hapa Yohana anazungumzia bahari, kifo na kuzimu kana kwamba ni watu hai.

wafu walihukumiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu aliwahukumu wafu"

Kifo na kuzimu zilitupwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu alizitupa kifo na kuzimu" au "Malaika wa Mungu walizitupa kifo na kuzimu"

kuzimu

Hapa "kuzimu" ni njia nyingine ya kusema mahali ambapo wasioamini wanapokwenda pale wanapokufa ili kusubiri hukumu ya Mungu.

mauti ya pili

"kufa mara ya pili." Hii inaelezwa kama adhabu ya milele katika ziwa la moto katika 20:13 na 21:7. "kifo cha mwisho ni ziwa la moto"

Kama jina la yeyote halikupatikana limeandikwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kama malaika wa Mungu hawakupata jina la mtu"

litupwa ndani ya ziwa la moto

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "malaika alimtupa katika ziwa la moto" au "malaika alimtupa mahali ambapo moto unawaka milele"

Revelation 21

Ufunuo 21 Maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii inatoa maelezo ya kina kuhusu Yerusalemu mpya.

Dhana muhimu katika sura hii

Kifo cha pili

Kifo ni aina ya muachano. Kifo cha kwanza ni kifo cha mwili, kuachana kwa roho kutoka kwa mwili. Kifo cha pili ni utengano wa milele kutoka kwa Mungu. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#death, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#soul na https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#eternity)

Tamathali muhimu za usemi katika sura hii

Kitabu cha uzima

Hii ni mfano wa maisha ya milele. Wale walio na uzima wa milele husemekana kuandikwa majina yao wkenye kitabo hiki cha uzima. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Mbingu mpaya na dunia mpya

Haieleweki iwapo hii ni dunia na mbingu tofauti kabisa ama kama zitatengenezwa kutoka kwa dunia na mbingu za kisasa. Hii ni hali sawa na Yerusalemu mpya. Kuna uwezekano kwamba hii itaathiri tafsiri katika lugha zingine.

<< | >>

Revelation 21:1

Taarifa ya Jumla:

Yohana anaanza kueleza maono yake ya Yerusalemu mpya.

nikaona

Aliyeona ni Yohana.

kama bibi harusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe

Hii inaifananisha Yerusalemu mpya kama bibi harusi anayejipamba kwa ajili ya bwana harusi wake.

Revelation 21:3

Nilisikia sauti kubwa kutoka kwenye kiti cha enzi ikisema

Neno "sauti" inamaanisha yule anayezungumza. "mtu akinena kwa sauti kutoka katika kiti cha enzi akisema"

Tazama!

Nenno "Tazama" inatuweka macho kuwa makini na taarifa za kushangaza zifuatazo.

Makao ya Mungu yapo pamoja na wanadamu, naye ataishi pamoja nao

Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na inasisitiza kuwa, hakika, Mungu ataishi miongoni mwa watu.

Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao

Machozi hapa yanawakilisha huzuni. "Mungu atafuta huzuni yao kama vile anafuta machozi yao" au "Mungu atawasababisha wasiwe na huzuni tena"

Revelation 21:5

maneno haya ni ya hakika na kweli

Hapa "maneno" yanamaanisha ujumbe uliyounda. "ujumbe huu ni wakuaminika na wa kweli"

Alfa na Omega, mwanzo na mwisho

Misemo hii miwili inamaanisha jambo moja na inasisitiza asili ya milele ya Mungu .

Alfa na Omega

Hizi ni herufi za kwanza na mwisho katika alfabeti ya Kigriki. Maana zinazowezekana ni 1) "yule aliyeanzisha vitu vyote na anayevileta mwisho vitu vyote" au 2)"yule ambaye alikuwepo na ataendelea kuwepo". Kama haieleweki kwa wasomaji unaweza kufikiria kutumia herufi katika alfabeti zako. "Yeye ni A na Z" au "mwanzo na mwisho"

mwanzo na mwisho

Maana zinazowezekana ni 1)"yule aliyeanzisha vitu vyote na ambaye atasababisha vyote kufika mwisho" (UDB) au 2) "yule aliyekuwepo kabla ya vitu vyote na atakuwepo baada ya vitu vyote."

Kwa yeyote aonaye kiu ... maji ya uzima

Mungu anazungumzia hamu ya uzima wa mile kama vile ni kiu na mtu anayepokea uzima wa milele ni kama vile anakunywa maji yaletayo uzima.

Revelation 21:7

Kauli Unganishi:

Aliyeketi katika kiti cha enzi aendelea kuzungumza na Yohana.

waoga

"wale wanaoogopa sana kufanya kilicho sahihi"

wachukizao

"wanaofanya vitu vibaya"

ziwa la moto wa kiberiti uunguzao

"ziwa la moto liwakalo kiberiti" au "sehemu ilyojaa moto unaowaka kiberiti"

mauti ya pili

"kufa mara ya pili." Hii inaelezwa kama adhabu wa milele katika ziwa lamoto katika 20:13 na 21:7. "kifo cha mwisho katika ziwa la moto."

Revelation 21:9

bibi harusi, mke wa mwana kondoo

Malaika anazungumzia Yerusalemu mpya kama vile ni mwanamke anayetaka kuolewa na bwana harusi wake, Mwanakondoo. Yerusalemu ni jina jingine la waumini watakao ushimo.

Mwanakondoo

Huyu ni mtoto wa kiume wa kondoo. Hapa hutumika kuashiria kuwa ni Kristo.

alinichukua mbali katika Roho

Mazingira yanabadilika na Yohana anapelekwa kwa mlima mrefu ambapo anaweza kuuona mji wa Yerusalemu.

Revelation 21:11

Yerusalemu

Hii inamaanisha "Yerusalemu kushuka kutoka mbinguni" ambayo ameieleza katika mstari uliopita na sio Yerusalemu halisia.

kama kito cha thamani, kama jiwe la yaspi jeupe kama kioo

yaspi safi - Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja. Ya pili inasisitiza ubora wa Yerusalemu kwa kutaja bayana aina ya yaspi.

jeupe kama kioo

nyeupe* "nyeupe sana"

yaspi

Hili ni jiwe la dhamani. Yaspi inawezakana kuwa ilkuwa nyeupe kama kioo.

milango kumi na miwili

"milango 12"

pameandikwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mtu aliapaandika"

Revelation 21:14

Mwanakondoo

Hii inamaanisha Yesu.

Revelation 21:16

stadia

Kiwanja cha michezo kinaurefu wa mita 185.

dhiraa

dhiraa ni sentimita 46.

Revelation 21:18

Ukuta ulikuwa umejengwa kwa yaspi na mji kwa dhahabu safi

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu aliujenga ukuta kwa yaspi na mji kwa dhahabu safi"

dhahabu safi, kama kioo safi

Dhahabu ilikuwa safi sana hadi inazungumziwa kama vile ilikuwa kioo.

Misingi ya ukuta ilikuwa imepambwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu aliipamba misingi ya ukuta"

yaspi ... zumaridi ... akiki

Haya ni mawe ya dhamani. Yaspi inawezekana ilkuwa nyeupe kama kioo, na akii inawezekana ilikuwa nyekundu. Zumaridi ni kijani.

yakuti samawi ...kalkedon ... sardoniki ... krisopraso ... hiakintho ...amethisto

Hivi vyote ni vito vya dhamani.

Revelation 21:21

lulu

Shanga nzuri na za dhamani. Zinaundwa ndani ya ganda la mnyama fulani mdogo aishiye baharini.

kila mlango ulitengenezwa kutoka kwenye lulu moja

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mtu alitengeneza kila mlango kutoka kwenye lulu moja"

hahabu safi, ikionekana kama kioo safi

Dhahabu ilikuwa safi sana hadi inazungumziwa kama vile ilikuwa kioo.

Bwana Mungu ... na Mwana Kondoo ni hekalu lake

Hekalu liliwakilisha uwepo wa Mungu. Hii inamaanisha Yerusalemu mpya haitahitaji hekalu kwa sababu Mungu na Mwanakondoo watakuwepo humo.

Revelation 21:23

taa yake ni Mwanakondoo

Hapa utukufu wa Yesu , Mwanakondoo, unazungumziwa kama vile ni taa inayotoa nuru kwa ajili ya mji.

Milango yake haitafungwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Hakuna atakayefunga milango yake"

Revelation 21:26

Wataleta

"Wafalme wa duniani wataleta"

hakuna kichafu kitakachoingia ndani yake kamwe

maneno hasi haya mawili yanaweza kusemwa kwa hali chanya kwa kusema "kile kilicho kisafi tu ndio kitaingia."

bali ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "lakini wale tu ambao Mwanakondoo ameandika majina yao katika kitabu cha Uzima"

Mwanakondoo

Huyu ni mtoto wa kiume wa kondoo. Hapa hutumika kuashiria kuwa ni Kristo.

Revelation 22

Ufunuo 22 Maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii inasisitiza kwamba nabii za kitabu cha Ufunuo zinaenda kutimilika hivi karibuni. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet)

Dhana muhimu katika sura hii

Mti wa uzima

Kuna uwezekano kwamba kulinuiwa kulinganisha mti wa uzima katika Bustani ya Edeni na mti wa uzima unaotajwa hapa. Laana ilioanza Edeni itaisha wakati huu.

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Alfa na Omega

Haya ni majina ya herufi za kwanza na za mwisho katika alfabeti ya Kigriki. ULB inafafanua majina yao kwa Kiingereza. Mpangilio huu unweza kuwa kielelezo cha watafsiri wengine. Watafsiri wengine, hata hivyo, wanaweza kuamua kutumia herufi za kwanza na za mwisho katika alfabeti zao, kwa mfano "A na Z " katika Kiingereza.

__<< | __

Revelation 22:1

Kauli Unganishi:

Yohana anaendelea kuelezea Yerusalemu mpya kadri malaika anavyomuonesha.

akanionesha

Hapa anayeoneshwa ni Yohana.

mto wa maji ya uzima

"mto unaotiririka maji yaletayo uzima"

maji ya uzima

Uzima wa milele unazungumziwa kana kwamba ni kinywaji cha maji yaletayo uzima.

Mwanakondoo

Huyu ni mtoto wa kiume wa kondoo. Hapa hutumika kuashiria kuwa ni Kristo.

mataifa

Hapa "mataifa" yanamaanisha watu wanaoishi katika kila taifa. "watu wa mataifa yote"

Revelation 22:3

Wala hapatakuwa na laana yoyote tena

Maana zinazowezekana ni 1) "Hakutakuwa na yeyote humo ... amabye Mungu atamlaani" (UDB) au 2) "Hakutakuwa na yeyote humo aliye chini ya laana ya Mungu."

watumishi wake watamtumikia

Maana zinazowezekana za "wake" ni 1) neno hili linamaanisha Mungu Baba, au 2) linamaanisha Mungu na Mwanakondoo ambao wote wanatawala pamoja kama mtu mmoja.

Revelation 22:6

Taarifa ya Jumla:

Huu ni mwanzo wa mwisho wa maono ya Yohana. Katika mstari wa 6 malaika anazungumza na Yohana. Katika mstari wa 7, Yesu anazungumza, kama ilivyoainishwa katika UDB.

maneno haya ni ya hakika na kweli

Hapa "maneno" yanamaanisha ujumbe uliyounda. "ujumbe huu ni wa kuaminika na wa kweli"

Mungu wa roho za manabii

Maana zinazowezekana ni 1) neno "roho" inamaanisha tabia ya ndani ya manabii na inaashiria kuwa Mungu ndio aliwapa msukumo. "Mungu aliyewaongoza manabii" (UDB) au 2) neno "roho" inamaanisha Roho Mtakatifu amabye aliwaongoza manabii. "Mungu aliyewapa manabii Roho wake"

Tazama!

Hapa Yesu anaanza kuzungumza. Neno "Tazama" inaongeza msistizo kwa kile kinachofuata.

Ninakuja upesi!

Inaeleweka kuwa anakuja ili kuhukumu. "Ninakuja kuhukumu upesi!

Revelation 22:8

Taarifa ya Jumla:

Yohana anawaambia wasomaji wake jinsi alivyomjibu malaika.

kulala kifudifudi

Hii inamaanisha kulala chini na kujinyoosha kwa sababu ya heshima na unyenyekevu. Hii nafasi ilikuwa sehemu muhimu katika kuabudu, kuonesha heshima na utayari wa kutumika.

Revelation 22:10

Kauli Unganishi:

Malaika anamaliza kuzungumza na Yohana.

Usiyatie muhuri ... kitabu hiki

Kutia muhuri kitabu ilikuwa kukifunga na kitu ambacho kilikifanya isiwezekane kwa yeyote kusoma kilichomo ndani hadi ule muhuri uvunjwe. Malaika alikuwa akimwambia Yohana kutoufanya ujmbe kuwa siri. "Usifanye siri ... kitabu hiki"

aneno ya unabii wa kitabu hiki

Hapa "maneno" yanamaanisha ujumbe uliyounda. "Huu ujumbe wa kinabii wa kitabu hiki"

Revelation 22:12

Taarifa ya Jumla:

Kitabu cha Ufunuo kikiwa kinafika mwisho, Yesu anatoa salamu zake za kufunga.

Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho

Misemo hii mitatu inafanana maana na inasisitiza kuwa Yesu alikuwepo na ataendelea kuwepo muda wote.

Alfa na Omega

Hizi ni herufi za kwanza na mwisho katika alfabeti ya Kigriki. Maana zinazowezekana ni 1) "yule aliyeanzisha vitu vyote na anayevileta mwisho vitu vyote" au 2)"yule ambaye alikuwepo na ataendelea kuwepo". Kama haieleweki kwa wasomaji unaweza kufikiria kutumia herufi katika alfabeti zako. "Yeye ni A na Z" au "mwanzo na mwisho"

wa Kwanza na wa Mwisho

Hii inamaanisha uasili wa Yesu wa milele.

Mwanzo na Mwisho

Maana zinazowezekana ni 1)"yule aliyeanzisha vitu vyote na ambaye atasababisha vyote kufika mwisho" (UDB) au 2) "yule aliyekuwepo kabla ya vitu vyote na atakuwepo baada ya vitu vyote."

Revelation 22:14

Kauli Unganishi:

Yesu anaendelea kutoa salamu zake za kufunga.

wale waoshao mavazi yao

Kuwa mtakatifu inazungumziwa kama mtu kuosha nguo zake. "wale waliokuwa watakatifu, kana kwamba wameosha mavazi yao"

Nje

Hii inamaanisha wako nje ya mji na hawaruhusiwi kuingia.

kuna mbwa

Kwenye utamaduni huo, mbwa alikua ni mnyama mchafu anayechukiwa. Hapa neno ni lakumshusha mtu hadhi na linamaanisha watu waovu.

Revelation 22:16

kuwashuhudia

Hapa wanaoshuhudiwa ni wengi.

mzizi wa uzao wa Daudi

Maneno "mzizi" na "uzao" yanamaanisha kitu kimoja tu. Yesu anazungumzia kuwa "mzawa" kana kwamba ni "mzizi" uliota toka kwa Daudi. Kwa pamoja maneno haya yanasisitiza kuwa Yesu anatoka katika familia ya Daudi.

Nyota ya Asubuhi ing'aayo

Yesu anajizungumzia mwenyewe kuwa kama nyota inayoonekana asubuhi kabla ya kupambazuka na inaashiria kuwa siku mpya imekaribia kuanza.

Revelation 22:17

Kauli Unganishi:

Hili ni jibu kwa kile alichosema Yesu.

Bibi harusi

Waumini wanazungumziwa kana kwamba ni bibi harusi anasubiri kuolewa na bwana harusi, Yesu.

Njoo!

Maana zinazowezekana ni 1) kwamba huu ni ukaribisho wa watu kuja na kunywa maji ya uzima. "Njoni mnywe!" au 2) kwamba hili ni ombi la unyenyekevu la kumuomba Yesu arudi. "Tafadhali njoo!"

Yeyote aliye na kiu ... maji ya uzima

Hamu ya mtu kwa ajili ya uzima wa milele inazungumziwa kana kwamba ni kiu na kwa mtu huyo kupokea uzima wa milele kama vile kunywa maji yaletayo uhai.

maji ya uzima

Maisha ya milele yanazungumziwa kama vile ni kinywaji kiletacho uhai.

Revelation 22:18

Taarifa ya Jumla:

Yohana anatoa maneno yake ya mwisho juu ya kitabu cha Ufunuo.

Namshuhudia

Anayeshuhudia ni Yohana.

maneno ya unabii wa kitabu hiki

Hapa "maneno" yanamaanisha ujumbe yaliyounda. "Ujumbe huu wa kinabii wa kitabu hiki."

Kama yeyote ataongeza katika hayo ... Kama mtu yeyote atayaondoa

Hili ni onyo kali la kutobadili chochote kwenye utabiri huu.

yaliyoandikwa katika kitabu hiki

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambayo nimeyaandika ndani ya kitabu hiki"

Revelation 22:20

Taarifa ya Jumla:

Katika mistari hii, Yohana anatoa salamu zake za kufunga pamoja na za Yesu.

Yeye ashuhudiaye

"Yesu, ashuhudiaye"

kila mtu

"kila mmoja wenu"