Key Terms

Abudu

Ufafanuzi

"Kuabudu" ni kuheshimu, kusifu na kumtii mtu hasa Mungu.


Adili, uadilifu

Ufafanuzi

Adili au uadilifu ni wema wa Mungu, haki, uaminifu na upendo. Kwa sababu Mungu ni wa adili hukemea dhambi.


Agano

Ufafanuzi

Agano ni makubaliano kati ya pande mbili kuwa upande mmoja au zote unapaswa kutekeleza.


Ahadi

Ufafanuzi

Ahadi ni hali ya kuahidi kufanya jambo fulani. Mtu anapokuahidi kitu inamaana yupo tayari kufanya jambo hilo.


Aliye Juu

Ufafanuzi

Neno "Aliye Juu" ni cheo cha Mungu. kina husu ukuu wake au mamlaka.


Aliyechaguliwa, chagua, watu waliochaguliwa, Aliyechaguliwa, Mteule

Ufafanuzi

Msemo, "wateule" una maana ya "waliochaguliwa" au "watu waliochaguliwa" na una maana ya wale ambao Mungu amewateua au chagua kuwa watu wake. "Aliyechaguliwa" au "Aliyechaguliwa na Mungu" ni jina ambalo lina maana ya Yesu, ambaye ni Masihi aliyechaguliwa.

Msemo "chagua" una maana ya kuchagua kitu au mtu au kuamua jambo. Mara kwa mara hutumika kumaanisha Mungu kuteua watu wawe wake na wamtumikie.

"Kuchaguliwa" ina maana ya "kuchaguliwa" au "kuteuliwa" kuwa au kufanya jambo.

Mungu alichagua watu kuwa wasafi, kutengwa kando na yeye kwa kusudi la kuzaa matunda mema ya kiroho. Hiyo ni sababu kwa nini wanaitwa "wateule" au "waliochaguliwa".

Msemo "aliyechaguliwa" hutumika mara nyingine katika Biblia kumaanisha baadhi ya watu kama Musa na Mfalme Daudi ambao Mungu aliwateua kama viongozi wa watu wake. Pia inatumika kumaanisha taifa la Israeli kama watu waliochaguliwa na Mungu.

Msemo "wateule" ni msemo wa zamani ambao humaanisha "waliochaguliwa" au "watu waliochaguliwa". Msemo huu katika lugha asili ni wingi inapomaanisha waumini wa Kristo.

Katika tafsiri za Biblia ya Kingereza za zamani, msemo "mteule" unatumika pote katika Agano la Kale na Jipya kutafsiri neno kwa ajili ya "waliochaguliwa". Tafsiri zaidi za kisasa hutumia "mteule" katika Agano Jipya pekee, kumaanisha watu ambao wameokolewa na Mungu kupitia imani kwa Yesu. Kwingineko katika Biblia, wanatafsiri neno hili kwa uwazi zaidi kama "waliochaguliwa".

Mapendekezo ya Tafsiri

Ni bora kutafsiri "mteule" kwa neno au msemo ambao una maana ya "waliochaguliwa" au "watu waliochaguliwa". Hizi zinaweza kutafsiriwa kama "watu ambao Mungu amechagua" au "wale ambao Mungu ameteua kuwa watu wake".

Msemo, "ambao wamechaguliwa" unaweza kutafsiriwa kama "ambao wameteuliwa" au "ambao waliteuliwa" au "ambao Mungu amewachagua".

"Ninakuchagua" inaweza kutafsiriwa kama, "ninakuteua" au "ninakuchagua".

Kwa kulinganisha na Yesu, "Aliyeteuliwa" inaweza pia kutafsiriwa kama, "Aliyechaguliwa na Mungu" au "Masihi aliyeteuliwa mahsusi na Mungu" au "Yule ambaye Mungu alimteua"


Amina, kweli

Ufafanuzi

Neno "Amina" hutumika kusisitiza au kuweka mkazo jambo ambalo mtu amesema. Mara nyingi hutumika mwisho wa sala. Mara nyingine hutafsiriwa kama "kweli."


amri, kuamuru

Ufafanuzi

Kuamuru ni kutoa amri kwa mtu afanye jambo fulani. Amri ni jambo ambalo mtu ameamriwa afanye.


Batiza, ubatizo

Ufafanuzi

Katika Agano Jipya, maneno "batiza" na "ubatizo" kwa kawaida utaratibu wa kuoshwa kwa Mkiristo kwa kutumia maji kuonesha kwamba ameoshwa kutoka katika dhambi na ameungana na Kristo.

Maono ya Kutafasiri


baya, ovu, uovu

Ufafanuzi

Msemo "baya" na "uovu" yote ina maana ya chochote ambacho kinapingana na tabia takatifu na mapenzi ya Mungu.

Wakati "ubaya" unaweza kuelezea tabia ya mtu, "ovu" unaweza kumaanisha zaidi ya tabia ya mtu. Hata hivyo, misemo yote inafanana maana.

Msemo "uovu" una maana ya hali ambayo watu hufanya maovu.

Matokeo ya uovu yanaonywesha kwa uwazi kwa jinsi watu wanavyotenda vibaya wengine kwa kuwaua, kuiba, kusengenya au kuwa katili na kutokuwa mwema.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, misemo "uovu" na "ovu" inaweza kutafsiriwa kama "ubaya" au "dhambi" au "kinyume na maadili".

Njia zingine za kutafsiri hii zinaweza kujumuisha "isiyo nzuri" au "sio takatifu" au "sio adilifu".

Hakikisha maneno au misemo ambayo inatumika kutafsiri misemo hii kutosha muktadha ambayo ni kawaida katika lugha husika.


Bila mawaa

Ufafanuzi

Neno "bila mawaa" kwa kawaida linamaanisha "bila lawama". Linatumika kumtaja mtu anayemtii Mungu kwa moyo wake wote, lakini haimaanisha kwamba hana dhambi.

Maoni ya Ufasiri


Binti Sayuni

Ufafanuzi

"Binti Sayuni" ni njia ya kitamathali inayomaanisha watu wa Israeli. Inatumika haswa katika unabii.

Katika Agano la Kale, "Sayuni" hutumika sana kama jina jingine la mji wa Yerusalemu.

"Sayuni" na "Yerusalemu" zote zina maana ya Israeli.

Msemo "Binti" ni msemo wa ubembelezi au mapenzi. Ni sitiari ya uvumilivu na utunzaji ambao Mungu anao kwa watu wake.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia za kutafsiri hili yaweza kuwa, "binti yangu wa Israeli, kutoka Sayuni" au "watu kutoka Sayuni, ambao ni kama binti kwangu" au "Sayuni, watu wangu wapendwa Israeli".

Ni vyema kubaki na msemo "Sayuni" katika usemi huu kwa maana unatumika mara nyingi katika Biblia. Maandishi yanaweza kuwekwa katika tafsiri kuelezea maana yake ya kitamathali na matumizi ya kinabii.

Ni bora kukaa na msemo "Binti" katika tafsiri ya usemi huu, ikiwa inaeleweka kwa sahihi.


Busara, hekima

Ufafanuzi

Busara inamuelezea mtu anayeelewa jambo la haki na mambo ya maadili na akayafanya. Hekima ni uelewa na kutenda yaliyo sahihi na maadili ya haki.


Bwana wa Majeshi, Mungu wa majeshi, Majeshi

Ufafanuzi

Bwana wa majeshi ay Mungu wa majeshi ni vyeo vinavyoelezea mamlaka ya Mungu juu ya malaika maelfu wanaomtii yeye.


Bwana Yahwe, Yahwe Mungu

Ufafanuzi

Katika Agano la Kale, "Bwana Yahwe" inatumika mara kwa mara kumaanisha Mungu mmoja wa kweli.

Neno "Bwana" ni cheo cha Mungu na "Yahwe" ni jina la Mungu mwenyewe. "Yahwe" mara nyingi huunganishwa na neno "Mungu" kuunda "Yahwe Mungu."


bwana, mkuu

Ufafanuzi

Neno "bwana" linamaanisha mtu anayemiliki na mwenye mamlaka juu ya watu wengine.

Neno hili wakati mwingine linatafsiriwa kama "mkuu" wakati wakumuita Yesu au wakati wakumaanisha mtu anayemiliki watumwa.


chakula cha Bwana

Ufafanuzi

Msemo "Chakula cha Bwana" unatumika na mtume Paulo kumaanisha mlo wa Pasaka ambao Yesu alikula na wanafunzi wake usiku alipokamatwa na viongozi wa Kiyahudi.

Katika mlo huu, Yesu aliuvunja mkate wa Pasaka katika vipande na kuuita mwili wake ambao punde utapigwa na kuuliwa pia. Aliita kikombe cha divai damu yake, ambayo itamwagwa hapo punde atakapokufa kama sadaka ya dhambi. Yesu aliamuru kila mara wafuasi wake wanapokula mlo huu pamoja, wanapaswa kukumbuka kifo chake na ufufuo. Katika barua yake kwa Wakorintho, mtume Paulo aliendeleza kuimarisha zaidi chakula cha Bwana kama zoezi la mara kwa mara la waumini wa Yesu. Makanisa siku hizi husema "ushirika" kumaanisha chakula cha Bwana. Usemi "Meza ya Bwana" hutumika wakati mwingine.


Chukizo, mbaya

Ufafanuzi

Neno "chukizo" hutumika kuelezea jambo linalosababisha karahaau chuki iliyokithiri. Wamisri waliwaona Waebrania kama "chukizo." Hii ina maana kuwa Wamisri waliwachukia Waebrania na hawakutaka kushirikiana nao au kuwa karibu nao. Vitu ambavyo Biblia imeviona kama "Chukizo kwa Yahweh" ni; uongo, kujivuna, kafara za binadamu, kuua na dhambi za zinaa kama uzinzi na matendo ya zinaa kinyume na maumbile. Katika kuwafundisha wanafunzi wake kuhusu siku za mwisho, Yesu anarejea unabii wa nabii Danieli kuhusu "chukizo la uharibifu" kwamba itakuwa kama uasi dhidi ya Mungu, Kuchafua sehemu yake ya kuabudia.


damu

Ufafanuzi

Neno "damu" linamaanisha kimiminika chekundu kinachotoka katika ngozi ya mtu panapokuwa na jeraha au kidonda. Damu inaleta viini lishe vya uhai katika mwili wote wa mtu.

Maoni ya Kutafasiri


dhambi,yenye dhambi, mwenye dhambi, kufanya dhambi

Ufafanuzi

Neno "dhambi" la husu matendo, mawazo, na maneno yaliyo kinyume dhidi ya mapenzi ya Mungu na Sheria. Dhambi yaweza maanisha kutofanya kitu Mungu alicho tuambia tufanye.


Dhamira

Ufafanuzi

Dhamira ni sehemu ya fikra za mwanadamu ambazo Mungu anamfanya atambue kuwa anafanya dhambi.


Dunia, kidunia

Ufafanuzi

Dunia ni sehemu ya ulimwengu ambapo watu wanaishi ndani yake. Kidunia inaelezea maadili na tabia mbaya za watu wanaoishi kwenye hii dunia.


fadhila, yenye kufaa, upendeleo

Ufafanuzi

Msemo "fadhila" una maana ya kufanya jambo kumnufaisha mtu ambaye anachukuliwa ki chanya. Kitu ambacho "kinafaa" ni chanya, kinakubalika, au kina manufaa.

Msemo "upendeleo" ina maana ya kutenda kwa upendeleo kwa baadhi ya watu lakini sio wengine kuonyeshwa kwa watu ambao ni matajiri au wanafikiriwa.

Yesu alikua "kwa fadhila za" Mungu na wanadamu. Hii ina maana walimkubali silika na tabia yake .

Msemo "kupata fadhila" ina maana ya kwamba mtu anakubalika na mtu mwingine.

Mfalme anapoonyesha upendeleo kwa mtu, mara nyingi humaanisha anakubali maombi ya huyo mtu na kumpatia.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia zingine za kutafsiri msemo "fadhila" zinawvza kujumuisha "baraka" au "faida".

"Mwaka wa baraka wa Yahwe" unaweza kutafsiriwa kama "mwaka


Farisayo.

Ufafanuzi

Mafarisayo walikuwa watu wa muhimu sana, kundi la watu lenye nguvula dini ya Kiyahudi katika nyakati za Yesu.


Fidia

Ufafanuzi

Fidia ni kiasi cha pesa au malipo mengine yanayohitajika kwa ajili ya kumuachia mtu aliyefungwa.


funga

Ufafanuzi

Neno "funga" linamaanisha kukaza kitu kwa usalama. Kitu kilichofungwa au kuunganishwa pamoja kinaitwa "muungano". Neno "kufunga" ni sehemu ya neno hili katika wakati uliopita.

Maoni ya Tafasiri

Neno "funga" laweza pia kutafasiriwa kama "kaza" au "zungushia"


ghadhabu, hasira

Ufafanuzi

Ghadabu ni hasira kali ambayo mara nyingine hudumu kwa mda mrefu. Hii maranyingi huelezea hukumu ya Mungu ya haki na adhabu ya watu walioasi dhidi yake.


habari njema, injili

Ufafanuzi

Msemo "injili" una maana ya "habari njema" na una maana ya ujumbe au tangazo ambalo linawaambia watu jambo ambalo lina manufaa kwako na kuwapa furaha.

Katika Biblia, msemo huu humaanisha ujumbe kuhusu wokovu wa Mungu kwa watu kupitia sadaka ya Yesu msalabani.

Katika Biblia nyingi za Kiingereza, "habari njema" mara nyingi hutafsiriwa kama "injili" na pia hutumika katika misemo kama vile "injili ya Yesu Kristo" au "injili ya Mungu" na "injili ya ufalme".

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia tofauti za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha "jumbe mzuri" au "tangazo zuri" au "ujumbe wa Mungu wa wokovu" au "mambo mazuri Mungu anayofundisha kuhusu Yesu".

Kulingana na muktadha, njia za kutafsiri msemo "habari njema ya" inaweza kujumuisha "ujumbe/havbari njema" au "ujumbe mzuri kutoka" au "mambo mazuri Mungu husema juu ya" au "kile Mungu anasema kuhusu jinsi anavyookoa watu".


Haki ya uzaliwa

Ufafanuzi

Neno "haki ya uzaliwa" inamaanisha heshima katika Biblia, jina la familia, na mali iliyokuwa ikitolewa kwa mzaliwa wa kwanza katika familia.

Maoni ya Kutafasiri.


haki, adilifu

Ufafanuzi

Maneno haya yanamaanisha kuwatendea watu vyema kulingana na sheria za Mungu. Sheria za binadamu zinazo onesha kiwango cha Mungu cha tabia sawa kwa watu wengine.

Kuwa wa "haki" ni kutenda ya haki na mema kwa mtu mwingine. Pia inaashiria uaminifu na msimamo kufanya kilicho adilifu machoni pa Mungu. Kutenda kwa "haki" inamaanisha kuwatendea watu kwa njia iliyo sawa, nzuri na ya kufaa kulingana na sheria za Mungu. Kupokea "haki" inamaanisha kutendewa vyema chini ya sheria, aidha kulindwa kwa sheria au kuadhibiwa kwa kuvunja sheria. Wakati mwingine neno "haki" lina maana pana ya "utakatifu"au "kufuata sheria za Mungu."


hatia, mwenye hatia

Ufafanuzi

Msemo "hatia" una maana ya ukweli wa kufanya dhambi au kutenda kosa.

Kuwa na "hatia" ina maana ya kuwa umefanya kitu kiouvu kimaadili, yaani, kutomtii Mungu.

Kinyume cha "mwenye hatia" ni "asiye na hatia".

Mapendekezo ya Tafsiri

Baadhi ya lugha zinaweza kutafsiri "hatia" kama "uzito wa dhambi" au "hesabu ya dhambi".

Njia za kutafsiri "kuwa na hatia" inaweza kujumuisha neno au msemo ambayo ina maana ya "kuwa katika kosa" au "kuwa umefanya jambo ovu kimaadili" au "kuwa umefanya dhambi".


hekalu

Ufafanuzi

Hekalu lilikuwa ni jengo lililo zungukwa na kuta za nyuani ambapo Waisraeli walikuja kuombaa na kutoa dhabihu kwa Mungu. Lilikuwa Mlima Moria katika mji wa Yerusalemu.


heshima, kuheshimu

Ufafanuzi

Istilahi 'heshima' na 'kuheshimu' hurejelea kitendo cha kumpa mtu heshima au kumstahi mtu. Heshima mara kwa mara hutolewa kwa mtu mwenye hadhi ya juu na umuhimu wa juu kama vile mfalme au Mungu. Mungu pia huwaagiza Wakristo wote kuwaheshimu watu wengine, lakini si kutafuta heshima zao wenyewe. Watoto wameagizwa kuwatii wazazi wao na kuwatii. Maneno kama 'heshima' na 'utukufu' ni maneno yanayoenda kwa pamoja hasa yanapomrejelea Yesu. Heshima kwa Mungu inajumuisha kumshukuru na kumsifu Mungu, na kuonesha heshima kwa kumtii Mungu na kuishi katika njia inayoonesha kuwa Mungu ni Mkuu.

Mapendekezo Njia nyingine za kutafsiri neno 'heshima' linajumuisha 'staha' Neno 'kuheshimu' laweza kutafsiriwa kama 'kuonesha heshima maalumu kwa au kuonesha mtu thamani ya juu.


hukumu

Ufafanuzi

Neno "hukumu" mara nyingi humaanisha kufanya maamuzi kama jambo liko sawa kimaadili au kama haliko sawa.

"Hukumu ya Mungu" mara nyingi humaanisha uamuzi wake kulaani kitu au mtu muovu. Hukumu ya Mungu mara nyingi huhusisha kuwaadhibu watu kwa dhambi zao. Neno "hukumu" inaweza pia kumaanisha "kulaani." Mungu anawaagiza watu wake kutowahukumu wengine kwa naamna hii. Maana nyingine ni "uamuzi kati ya" au "kuhukumu kati ya", yaani kuchagua ni mtu gani yuko sahihi katika ugomvi kati yao. Katika mazingira mengine, "hukumu" za Mungu ni yale aliyeamua ni mema na yenye haki. Zinafanana na amri, sheria na maagizo yake. "Hukumu" inaweza kumaanisha uwezo wa busara wa kufanya maamuzi. Mtu anayekosa "hukumu" hana hekima kufanya maamuzi ya busara.


Huruma

Ufafanuzi

Huruma ni hisia za kujali wengine hasa wanaoteseka. Pia huruma ni kujali wengine na kuwasaidia.


imani

Ufafanuzi

Kwa ujumla, msemo "imani" una maana ya imani, au matumaini ndani ya mtu au jambo.

"Kuwa na imani" na mtu ni kuamini ya kwamba kile anachosema na kufanya ni kweli na kuaminika.

"Kuwa na imani na Yesu" ina maana ya kuamini mafundisho yote ya Mungu kuhusu Yesu. Ina maana haswa ya kwamba watu wanamuamini Yesu na sadaka yake kuwasafisha kutoka kwa dhambi zao na kuwakomboa kutoka na adhabu wanayostahili kwa sababu ya dhambi yao.

Imani ya kweli kwa Yesu itamsababisha mtu kuzaa matunda mazuri ya kiroho au tabia kwa sababu ya Roho Mtakatifu anayeishi ndani yake.

Mara kwa mara "imani" kwa ujumla ina maana ya mafundisho yote kuhusu Yesu, yaani kama msemo, "ukweli wa imani".

Katika muktadha kama wa "tunza imani" au "telekeza imani", msemo "imani" una maana ya hali ya kuamini mafundisho yote kuhusu Yesu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Katika baadhi ya muktadha, "imani" inaweza kutafsiriwa kama "imani" au "hatia" au "kujiamini" au "kuamini".

Kwa baadhi ya lugha misemo hii inaweza kutafsiriwa kutumia aina za kitenzi cha "imani".


imani, aminifu,

Ufafanuzi

Neno "imani" la eleza kuamini kwamba kitu au mtu ni wa kweli au tegemeo. Mtu "mwaminifu" na weza kuwa tegemevu kufanya kitu na kusema kilicho sawa na kweli.


ingia bila ruhusa

Ufafanuzi

"Ingia bila ruhusa" ina maana ya kuvunja sheria au kukosea haki za mtu mwingine.


ishara, kithibitisho, ukumbusho

Ufafanuzi

Ishara ni kitu, tukio, au kitendo kinacho wasilisha maana maalumu.


Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli

Ufafanuzi

Neno "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpa Yakobo. Linamaanisha, "anashindana na Mungu."

Uzao wa Yakobo walijulikana kama "watu wa Israeli," "taifa la Israeli" au "Waisraeli." Mungu aliunda agano lake na watu wa Israeli. Walikuwa watu wake aliowachagua. Taifa la Israeli liliundwa na makabila kumi na mbili. Mara baada ya mfalme Sulemani kufa, Israeli iligawanyika katika falme mbili: ufalme wa kusini, uliitwa "Yuda" na ufalme wa kaskazini, uliitwa "Israeli."


Jehanamu, ziwa la moto

Ufafanuzi

Jehanamu ni sehemu ya mwisho iliyo na maumivu na mateso yasiyokoma, mahali ambapo Mungu atamhukumu kila mmoja anayemwasi Yeye na kuukataa mpango wake wa kuwaokoa kupitia kwa sadaka ya Yesu. Pia inarejelewa kama 'ziwa la moto. Jehanamu au Kuzimu kunatajwa kama sehemu ya moto na mateso makali. Shetani na roho chafu zinazomfuata zitatupwa katika Jehanamu kwa ajli ya hukumu ya milele. Watu wasioamini sadaka ya Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi zao, na wasiomtumaini Yeye, watahukumiwa Jehanamu milele

Mapendekezo ya tafsiri Maneno haya yanapaswa kutafsiriwa tofauti tofuauti kwasababu yanatokea tofauti katika muktadaha tofauti. Katika baadhi ya lugha haziwezi kutumia neno 'ziwa' kwa sababu kwao ziwa ni 'maji' Neno Jehanamu laweza kutafsiriwa kama 'sehemu ya mateso au sehemu yenye giza na maumivu' Maneno 'ziwa la moto' yanaweza pia kutafsiriwa kama 'bahari ya moto' au 'moto mkubwa.'


Jemadari

Ufafanuzi

Jemadari ni afisa wa jeshi la Rumi aliyekuwa na kundi la askari 100 juni ya amri yake.


jina

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "jina" linatumika kwa mifano kadhaa.


Jiwe la pembeni

Ufafanuzi

"Jiwe la pembeni" ni jiwe kubwa mabalo limekatwa na kuwekwa katika kona ya msingi wa jengo.


jiwe, kupiga jiwe

Ufafanuzi

Jiwe ni mwamba mdogo. Neno "kupiga jiwe" la husu kurusha mawe na majabali makubwa kwa mtu kuweza kumuua.


Kanisa

Ufafanuzi

Katika agano jipya kanisa ni kundi la watu wanaomwamini Yesu wanaokutana na kuomba pamoja na kusikiliza mafundisho ya Mungu.


katika Kristo, katika Yesu, katika Bwana, katika yeye

Ufafanuzi

Usemi "katika Kristo" na maneno ya kukaribiana yanamaanisha hali ya kuwa na uhusiano na Yesu Kristo kwa imani katika yeye.

Maneno mengine ya kukaribiana ni pamoja na, "katika Kristo Yesu, katika Yesu Kristo, katika Bwana Yesu, katika Bwana Yesu Kristo." Maana zinazowezekana kwa ajili ya maneno "katika Kristo" yanaweza kuwa pamoja na, "kwa sababu wewe ni wa Kristo" au "katika uhusiano ulionao na Kristo" au "kutokana na imani yako katika Kristo." Maneno haya ya kukaribiana yote yana maana sawa ya kuwa katika hali ya kumuamini Yesu na kuwa mwanafuzi wake. Noti: Wakati mwingine neno "katika" lina paswa kuwa na kitenzi. Kwa mfano, "gawana katika Kristo" inamaana "kugawana katika" faida zinazokuja kwa kumjua kristo. "Kusifu katika" Kristo inamaana kuwa na furaha na kutoa sifa kwa Mungu ambavyo Yesu alivyo na alichofanya. "Kuamini katika" Kristo inamaanisha kumuamini yeye kama Mwokozi na kumjua.


kazi, vitendo, matendo

Ufafanuzi

Katika Biblia maneno kazi, vitendo, matendo ni vitu ambavyo Mungu au watu hufanya.


Kiapo

Ufafanuzi

Kiapo ni ahadi ambayo mtu anaiweka kwa Mungu. Mtu anaahidi kufanya jambo fulani kwa ajili ya kumuheshimu Mungu na kuonesha ibada kwake.

Lakini Mungu hatakiwi kutimiza ombo la mtu aliloomba katika kiapo.


kicho, uchaji

Ufafanuzi

Maneno "kicho" na "uchaji" yanamaanisha kujitoa kwa nguvu zote kumuunga mkono mtu au wazo.

Maoni ya Ufasiri


Kipatanisho

Ufafanuzi

"Kipatanisho" ni sadaka inayotolewa ili kutimiza haki ya Mungu au kutuliza hasira yake.


Kristo, Masihi

Ufafanuzi

Masihi na Kristo inamaana ya mpakwa mafuta na inamuelezea Yesu mwana wa Mungu.


Kuamini, kuamini katika

Ufafanuzi

Neno "kuamini" na "kuamini katika" yanahusiana kwa karibu, lakini yana maana tofauti:

Maoni ya Kutafasiri


Kuasili

Ufafanuzi

Neno "kuasili" ni hatua za kisheria za mtoto kuwa na wazazi fulani ambao sio wazazi wake wa kumzaa.


Kubariki

Ufafanuzi

"kubariki" mtu au kitu maana yake ni kusababisha mema na mambo ya manufaa kufanyika kwa mtu au kitu kinachobarikiwa.

//kutokana na maoni hapa chini: Ni mhimu kutoa maana, lengo, au kuzingatia matumizi ya mzizi wa neno "bariki" ambalo kimsingi linapendekea kustawi au kuwa na wingi wa vitu au utajiri. Kwa kuzingatia wingi wa mafundisho ya kimaandiko juu ya upendo wa Mungu, rehema na neema ambayo siyo ya kale tu bali hata sasa. Kwa kuzingatia uangalizi, ulinzi, na uwepo wa Roho wa Mungu. Na kwa ajili yetu kumbariki Mungu, kwa kutoa shukurani, kuthamini, na kuelewa kama tunavyojifunza na kumfuata(kumtii)//

Maoni ya Kutafasiri


Kuchaguliwa tangu asili

Ufafanuzi

Kuchaguliwa tangu asili nikitendo cha kuamua au kupanga kabla ya jambo hilo kutokea.


kuhani mkuu

Ufafanuzi

Neno 'kuhani mkuu' hurejelea kuhani maalumu aliyekuwa ameteuliwa kutumika kwa mwaka mmoja kama kiongozi wa makuhani wote wa Wayahudi. Kuhani mkuu alikuwa na majukuu mahususi. Alikuwa ni mtu pekee aliyeruhusiwa kuingia mahali patakatifu sana katika hekalu ili kutoa sadaka maalumu mara moja kwa mwaka. Waisraeli walikuwa na makuhani wengi sana, lakini walikuwa na kuhani mkuu mmoja kwa muda fulani. Kipindi alichokamatwa Yesu, Kayafa alikuwa kuhani mkuu. Anasi, Baba mkwe wa Kayafa anatajwa mara kadhaa kwasababu alikuwa kuhani mkuu hapo awali, huenda alikuwa bado na mamlaka na nguvu fulani juu ya watu.

Mapendekezo ya tafsiri 'Kuhani mkuu" tunaweza kutafsiri kama "kuhani wa daraja la juu"


Kuhani, ukuhani

Ufafanuzi

Katika Biblia Kuhani alikuwa mtu aliyechaguliwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa Mungu kwa niaba ya watu wa Mungu. Ukuhani lilikuwa jina au masharti ya kuwa kuhani.


Kuhukumu, hukumu

Ufafanuzi

"Kuhukumu" au "hukumu" ni kitendo cha kumpa mtu kumhukumu mtu baada ya kufanya jambo baya.


kujaribu, jaribu

Ufafanuzi

Kumjaribu mtu ni kufanya huyo mtu kufanya kitu kibaya.


kujazwa kwa Roho

Ufafanuzi

Msemo "kujazwa kwa Roho" ni msemo wa kitamathali ambao una maana ya Roho Mtakatifu kumwezesha kufanya mapenzi ya Mungu.

Msemo "kujazwa na" ni msemo ambao hutumika mara kwa mara kumaanisha "kutawalwa na".

Watu "wanajazwa na Roho" wanapofuata uongozi wa Roho Mtakatifu na kumtegemea kabisa kuwasaidia kufanya kile Mungu anachotaka.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "kuwezeshwa na Roho Mtakatifu" au "kutawaliwa na Roho Mtakatifu". Lakini haitakiwi kuonekana kana kwamba Roho Mtakatifu analazimisha mtu kufanya kitu.

Sentensi kama "alijazwa na Roho" inaweza kutafsiriwa kama "alikuwa akiishi kikamilifu kwa nguvu ya Roho" au "Roho Mtakatifu alikuwa akimuongoza kikamilifu".

Msemo huu ni sawa kwa maana na msemo "kuishi kwa Roho" lakini "kujazwa na Roho" inasisitiza ukamilifu ambao mtu huruhusu Roho Mtakatifu kuwa na utawala au ushawishi juu ya maisha yake. Kwa hiyo misemo hii miwili inatakiwa kutafsiriwa tofauti, ikiwezekana.


Kujivuna

Ufafanuzi

Neno "kujivuna" humaaanisha kuongea kwa kiburi kuhusu mtu au kitu. Mara kwa mara inamaanisha kujivuna mwenyewe.

Maoni ya Tafasiri


Kukiri

Ufafanuzi

Kukiri inamaana ya kukubali kuwa jambo fulani ni la kweli. Kukiri ni kauli ya kuwa kitu fulani ni kweli.


kukomboa, ukombozi, mkombozi

Ufafanuzi

"Kukomboa" au "ukombozi" ni kununua kitu kilichokuwa kinamilikiwa hapo mwanzo au kilichochukuliwa mateka. "Mkombozi" ni mtu anayekikomboa kitu au mtu.


Kumkufuru

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "kufuru" inamaanisha kuzungumza kwa njia ambayo inaonesha dharau kubwa kwa Mungu au watu. "Kumkufuru" mtu ni kuongea kinyume cha mtu huyo ili watu wafikiri vibaya juu ya mtu huyo.

Maoni ya Tafasiri


Kumtia mafuta

Ufafanuzi

"Kumtia mafuta" ina maana ya kupaka au kummiminia mafuta mtu au kitu. Mara nyingine mafuta haya huchanganywa na viungo ambavyo huleta ladha au harufu ya manukato. Pia hutumika kama lugha ya picha kuonesha namna ambavyo Roho Mtakatifu anawachagua watu na kuwatia nguvu.


Kuomba, maombi

Ufafanuzi

"Maombi" au "kuomba" ni kitendo cha kuongea na Mungu. Neno hili pia laweza kutumika kama kitendo cha watu kujaribu kuongea na miungu ya uongo.


Kupatanisha, maridhiano

Ufafanuzi

Kupatanisha na maridhiano ni kutengeneza amani kati ya watu waliokuwa maadui.


Kupotea, kuharibika

Ufafanuzi

"Kupotea" inamaanisha kufa au kuharibiwa maranyingi huwa ni baada ya mapigano au majanga. Katika Biblia inamaana zaidi ya kuhukumiwa milele jehanamu.


Kurejesha, marejesho

Ufafanuzi

Kurejesha au marejesho ni kusababisha kitu kirudi katika uhalisia wake au katika hali nzuri.


kutenga

Ufafanuzi

Neno "kutenga" lina maana ya kutengwa kutoka kwenye kitu kutimiza aina ya kusudi.


Kuteua, Kuteuliwa

Ufafanuzi

"Kuteua au kuteuliwa" linamaana ya kumchagua mtu ili aikamilishe kazi fulani.


kutokuwa na imani, upotofu wa imani

Ufafanuzi

Msemo "kutokuwa na imani" una maana ya kutokuwa na imani au kutoamini.

Neno hili linatumika kuelezea watu ambao hawamuamini Mungu, ambayo inaonekana kwa njia ya chafu wanayofanya.

Nabii Yeremia alimshtaki Israeli kwa kutokuwa na imani na kutomtii Mungu.

Waliabudi sanamu na kufuata tamaduni zinginge ambazo si za kiungu za kundi la watu ambao hawakumwabudu au kumtii Mungu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, msemo "kutokuwa na imani" unaweza kutafsiriwa kama "upotofu wa uaminifu" au "kutoamini" au "kutomtii Mungu".

Msemo "upotofu wa imani" unaweza kutafsiriwa kama "ukosefu wa imani" au "uasi dhidi ya Mungu"


Kutubu, toba

Ufafanuzi

Kutubu na toba ni hali ya kuacha dhambi na kumrudia Mungu.


Kuwa na mapepo

Ufafanuzi

Mtu ambaye ana mapepo ana pepo au roho chafu ambalo humuongoza kile afanyacho au kufikiri.

Mara kwa mara mtu mwenye pepo hujiumiza mwenyewe au watu wengine kwa sababu peopo husababisha afanye hivyo.

Yesu aliponya watu waliokuwa na mapepo kwa kuwaamuru mapeopo kuwatoka . Hii mara kwa mara hujulikana kama "kutoa" mapepo.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia zingine za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha, "kutawaliwa na pepo" au "kutawaliwa na roho mchafu" au "kuwa na roho mchafu aishiye ndani".


Kuzaliwa upya, kuzaliwa na Mungu, kuzaliwa kwa roho

Ufafanuzi

Neno "kuzaliwa upya" lilitumiwa mara ya kwanza na Yesu kuelezea maana ya Mungu kumbadilisha mtu kutoka kuwa mfu kiroho na kuwa hai kiroho. Neno "kuzaliwa na Mungu" na "kuzaliwa kwa roho" pia hurejerea hali ya mtu kupewa uzima mpya kiroho.

Maoni ya Tafasiri


kuzimu

Ufafanuzi

katika Biblia kuna maneno mawili yametumika, neno la Kiebrania 'sheol' na neno la Kigriki 'hades.' Maneno haya yametumika katika Biblia kumaanisha kifo na sehemu ambako roho za watu waliokufa huenda. katika Kiebrania neno 'sheol' limetumika katika Agano la Kale kurejelea sehemu ya watu waliokufa au sehemu ya kifo. katika agano jipya, neno la Kigriki 'hades" limetumika kumaanisha sehemu ya roho za watu waliomwasi Mungu. Roho hizi hurejelewa kama zinaenda "chini." Wakati mwingine linaweza kutofautishwa na 'kwenda juu' mbinguni mahali ambako roho za watu za watu wanaomwamini Yesu zinaishi.

Mapendekezo ya tafsiri Katika Agano la Kale neno "sheol" linaweza kutafsiriwa kama " sehemu ya wafu" au "sehemu kwa ajli ya roho za wafu" Baadhi ya tafsiri hufasiri neno hili kama "shimo" au "kifo" kwa kutegemea na muktadha. Neno "hades" limetumika sana katika Agano Jipya ambalo laweza kutafsiriwa kama "sehemu kwa ajili ya roho za wafu za watu wasioamini" au " sehemu ya mateso na adhabu ya kwa roho za wafu wasioamini." Baadhi ya tafsiri hutunza neno ''sheol" au ''Hades'' kwa kutumia herufi ambazo zinakubaliana katika mfumo wa sauti wa lugha husika. kwa kiswahili twaweza kusema 'sheoli" na 'hadesi'


kweli, ukweli, kuwa kweli

Ufafanuzi

Maneno "kweli" na "ukweli" yana eleza mambo ambyo ni halisi, matukio yaliyo tukia, na maneno yaliyo semwa.


Laana, kulaaniwa

Ufafanuzi

Laana ni kusababisha mambo mabaya yatokee kwa mtu au kitu kilicholaaniwa.


liwali

Ufafanuzi

Neno "liwali" la eleza afisa wa serikali aliye tawala sehemu ya Serikali ya Rumi. Kila liwali alikuwa chini ya mamlaka ya mfalme mkuu wa Kirumi.


Mabaki

Ufafanuzi

Mabaki ni watu au vitu vilivyosalia toka kwenye kundi kubwa.


Madhabahu

Ufafanuzi

Madhabahu ilikuwa sehemu yenye muundo ulioinuka ambao wana wa Israeli walichoma wanyama na mazao kama sadaka kwa Mungu.


mahali takatifu

Ufafanuzi

Neno "mahali takatifu" ya husu sehemu ambayo Mungu amefanya takatifu. Inaweza maanisha eneo linalo toa ulinzi na usalama.


maisha, uhai, kuishi, kuwa hai

Ufafanuzi

Maneno haya yote yanamaanisha kuwa hai kimwili, sio kufa. Yanatumika pia kimafumbo kumaanisha kuwa hai kiroho. Yanayofuata yanaelezea nini kinamaanishwa na "maisha ya kimwili" na "maisha ya kiroho."

Kulingana na mazingira, "maisha" inaweza kuetafsiriwa kama "kuwepo" au "mtu" au "roho" au "kuwa" au "kupitia." Neno "uhai" inaweza kutafsiriwa kama "kuishi" au "kukaa" au "kuwepo." Msemo "mwisho wa maisha yake" inaweza kutafsiriwa kama, "alipoacha kuishi." Msemo "alinusuru maisha yao" unaweza kutafisiri kama, "aliwaruhusu waishi" au "hakuwaua." Msemo "walihatarisha maisha yao" unaweza kutafsiriwa kama, "walijiweka hatarini" au "walifanya kitu ambacho kingiweza kuwaua." Bibilia inapozungumzia kuwa hai kiroho, "maisha" yanaweza kutafsiriwa kama "maisha ya kiroho" au "maisha ya milele," kulingana na mazingira. Wazo la "maisha ya kiroho" linaweza pia kutafsiriwa kama, "Mungu kutufanya kuwa hai katika roho zetu" au "maisha mapya kwa Roho wa Mungu" au "kufanywa hai ndani yetu." Kulingana na mazingira, msemo "toa maisha" unaweza kutafsiriwa kama, "kusababisha kuishi" au "kutoa uzima wa milele" au "kusababisha kuishi milele."


Malaika, Malaika mkuu

Ufafanuzi

Malaika ni kiumbe chenye roho na chenye nguvu kilichoumbwa na Mungu. Malaika wanamtumikia Mungu kwa kufanya yale wanayoagizwa kuyafanya na Mungu. Malaika mkuu ni malaika anayewaongoza malaika wengine.


Mamlaka

Ufafanuzi

Mamlaka ni nguvu ya kushawishi na kutawala ambayo mtu anakuwa nayo juu ya mtu mwingine.


manemane

Ufafanuzi

Manemane ni mafuta au manukato yanayo tengenezwa kwa majani ya manemane yanayo ota Africa na Asia.


manna

Ufafanuzi

Manna ili kuwa nyeupe, aina ya chakula cha unga ambacho Mungu alikitoa kwa ajili ya Waisraeli kula kipindi cha miaka 40 waliyo ishi nyikani baada ya kutoka Misri.


Mapenzi ya Mungu

Ufafanuzi

Mapenzi ya Mungu ni kitu anachotamani Mungu au mipango.


maskani

Ufafanuzi

Maskani ilikuwa hema muhimu Waisraeli walimuabudu Mungu kipindi cha miaka 40 walipo zunguka jangwani.


Mataifa

Ufafanuzi

Msemo "mataifa" una maana ya mtu yeyote ambaye sio Myahudi. Watu wa mataifa ni watu ambao sio uzao wa Yakobo.

Katika Biblia, msemo "kutotahiriwa" pia hutumika kitamathali kumaanisha watu wa Mataifa kwa sababu wengi wao hawakutahiri watoto wao wa kiume kama Waisraeli walivyofanya.

Kwa sababu Mungu aliwachagua Wayahudi kuwa watu maalumu, walifikiria juu ya watu wa mataifa kama watu wa nje ambao wasingeweza kuwa watu wa Mungu.

Wayahudi pia waliitwa "Waisraeli" au "Waebrania" katika vipindi tofauti vya historia. Waliwajua wengine wote kama "watu wa Mataifa".

Watu wa mataifa pia inaweza kutafsiriwa kama "asiye Myahudi" au "asiye Muisraeli" (Agano la Kale).

Kitamaduni, Wayahudi hawakula na watu wa mataifa au kujihusishanao, ambapo mara ya kwanza ilisababisha matatizo miongoni mwa kanisa la kwanza.


Matumaini

Ufafanuzi

Neno 'matumaini' hurejelea matarajio na hamu kubwa juu ya kitu fulani kitokee. Lakini pia inaweza kumaanisha kutokuwa na uhakika kwamba kitu fulani kitatokea. Katika Biblia, neno matumaini lina maana ya matarajio. mfano, matumaini yangu yako katika Bwana. Ina maana ya kuwa na matarajio ya kupokea kile ambacho Mungu amewaahidi watu wake. Wakati mwingine neno 'matumaini' laweza kutafsiriwa kama 'uhakika' au hali ya kujiamini. Hasa katika Agano Jipya neno uhakika hutumika zaidi kuonesha matumaini waliyo nayo watu waliomwamini Yesu juu ya kupokea ahadi walizoahidiwa na Mungu.

Mapendekezo ya tafsiri katika mazingira tofauti, neno ' tumaini' lina maana ya ' kutaka ' au kutamani' au kutarajia. Maneno kama ' hakuna cha kutumaini' yana maana ya ' hakuna cha kutegemea. Maneno kama 'mtegemee Mungu' yana maana ya 'mtumaini Mungu.


mbingu, anga, mbinguni

Ufafanuzi

Neno linalotafsiriwa kama "mbingu" hurejelea mahali anapoishi Mungu. Neno hilo hilo laweza kumaanisha " anga" kwa kutegemea na muktadha. Neno 'mbingu' hurejelea kila kitu tunachokiona juu mawinguni kama vile jua, mwezi, na nyota. Inaweza pia kujumuisha vitu vingine vya anga la mbali kama vile sayari, vitu ambavyo hatuwezi kuviona tukiwa hapa duniani. Neno "anga' hurejelea anga la bluu lililo juu ya dunia ambalo lina mawingu na hewa tunayopumua. Mara kwa mara, jua na mwezi husemwa kuwa ziko 'juu angani. Neno 'mbingu' laweza kumaanisha 'anga' au sehemu ambako Mungu anaishi' hii hutegemea na muktadha mbalimbali. Wakati neno 'mbingu' linapotumika kama tamathali ya semi, humrejelea Mungu mwenyewe. Kwa mfano, Mathayo anapoandika juu ya 'ufalme wa mbinguni' anarejelea ufalme wa Mungu.

Mapendekezo ya tafsiri Wakati neno 'mbingu' linapotumika kimfano laweza kutafsiriwa kama 'Mungu" Maneno 'mbingu' au " vitu vya kimbingu' yaweza kutafsiriwa kama 'jua, mwezi na nyota. Kirai "nyota za mbinguni" chaweza kutafsiriwa kama " nyota za angani."


Mchungaji

Ufafanuzi

Mchungaji inatumika kama cheo cha mtu ambaye ni kiongozi wa kiroho wa kundi fulani la waamini.


Mfalme wa Wayahudi

Ufafanuzi

Usemi, "Mfalme wa Wayahudi" ni jina linalomaanisha Yesu, Masihi.

Mara ya kwanza Biblia inaandika hili jina wakati linapotumika na wanaume wenye hekima waliosafiri kwenda Bethlehemu wakimtafuta mtoto aliye "Mfalme wa Wayahudi." Malaika alimfunulia Mariamu kuwa mwanaye, mzawa wa mfalme Daudi, atakuwa mfalme ambaye ufalme wake utadumu milele. Kabla Yesu hajasulibishwa, askari Wakirumi walimdhihaki Yesu kwa kumuita "Mfalme wa Wayahudi." JIna hili liliandikwa pia katika kipande cha mbao na kupigwa msumari juu ya msalaba wa Yesu. Yesu kweli ni Mfalme wa Wayahudi na mfalme wa viumbe vyote.


Mfano

Ufafanuzi

"Mfano" ni simulizi fupi au somo fulani linalotumika kuelezea au kufundisha ukweli wa maadili.


mfano wa Mungu, mfano

Ufafanuzi

Neno "mfano" inamaanisha kitu kinachofanana na kitu kingine au ni kama tabia ya mtu au asili yake. Neno "mfano wa Mungu" inatumika katika njia tofauti, kulingana na mazingira.

Katika mwanzo wa nyakati, Mungu aliwaumba binadamu "katika mfano wake", ambayo ni "kwa kumfanana." Hii inamaanisha kuwa binadamu wana sifa fulani zinazoonesha mfano wa Mungu, kama uwezo wa kusikia hisia, uwezo wa kufikiri na kuwasiliana, na roho inayoishi milele. Biblia inafundisha kwamba Yesu, Mwana wa Mungu, ni "mfano wa Mungu," kwamba yeye ni Mungu mwenyewe. Tofauti na binadamu, Yesu hakuumbwa. Kutoka milele yote. Mungu Mwana ana sifa zote za Mungu kwa sababu ana asili sawa na ya Mungu Baba.


mfuasi

Ufafanuzi

Msemo wa "mfuasi" una maana ya mtu anayetumia muda mwingi na mwalimu, akijifunza kutoka kwa tabia na mafunzo ya mwalimu huyo.

Watu waliomfuata Yesu, wakimsikiliza mafundisho yake na kuyatii, walijulikana kama "wanafunzi" wake.

Yohana Mbatizaji pia alikuwa na wanafunzi.

Katika kipindi cha huduma ya Yesu, kulikuwa na wanafunzi wengi waliomfuata na kusikiliza mafunzo yake.

Yesu alichagua watume kumi na wawili wawe wafuasi wake wa karibu; wanamume hawa wakaja kujulikana kama "mitume" wake.

Watume kumi na wawili waliendelea kujulikana kama "wanafunzi" wake au "wale kumi na wawili".

Kabla tu ya Yesu kwenda juu mbinguni, aliwaamuru wanafunzi wake kuwafundisha watu wengine juu ya kuwa wafuasi wa Yesu pia.

Yeyote anayemwamini Yesu na kumtii mafunzo yake anaitwa mfuasi wa Yesu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "mwanafunzi" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo wenye maana ya "mfuasi" au "mwanafunzi".

Hakikisha ya kwamba tafsiri ya msemo huu haimaanishi mwanafunzi anayejifunza darasani.

Tafsiri ya msemo huu unatakiwa kuwa tofauti na tafsiri ya "mtume".


Mfuniko wa upatanisho

Ufafanuzi

Mfuniko wa upatanisho ulikuwa mfuniko wa dhahabu uliotumika kufunika juu ya sanduku la agano.


milele

Ufafanuzi

Msemo huu "milele" una maana ya kitu ambacho kitaendelea kuwepo au kutadumu daima.

Msemo "milele" una maana ya hali ya kutokuwa na mwanzo au mwisho. Pia inaweza kumaanisha maisha ambayo hayana mwisho.

Baada ya maisha haya ya sasa ya duniani, binadamu wataishi milele aidha mbinguni na Mungu au jehanamu kutengana na Mungu.

Misemo "maisha ya milele" inatumika katika Agano Jipya kumaanisha kuishi milele pamoja na Mungu mbinguni.

Msemo "milele na milele" ina wazo la muda ambao hauna mwisho na huelezea nini milele au maisha ya milele yakoje.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia zingine za kutafsiri "milele" zinaweza kujumuisha "kutokuwa na mwisho" au "kuendelea siku zote".

Msemo "maisha ya milele" unaweza kutafsiriwa kama "maisha ambayo hayana mwisho" au "maisha ambayo yanaendelea bila kikomo" au "kufufua miili yetu kuishi milele".

Kulingana na muktadha, njia tofauti za kutafsiri "milele" zinaweza kujumuisha "kuwepo nje ya muda" au "maisha yasiyo na mwisho" au "maisha mbinguni".

Pia fikiria namna neno hili linatafsiriwa katika Biblia katika lugha ya taifa.


mkate usiyotiwa chachu

Ufafanuzi

Neno "mkate usiyotiwa chachu" una lina maana mkate unatengenezwa pasipo hamira. Aina huu wa mkate ni bapa kwasababu hauna hamira kuufanya uumuke.


Mkono wa kulia.

Ufafanuzi

Mkono wa kulia humaanisha mahali pa heshima au nguvu ya mkono wa kiume wa mtawala au mtu wa muhimu.


Mkristo

Ufafanuzi

Baada ya Yesu kurudi mbinguni watu wakaanza kuitwa Wakristo ikiwa na maana ya wafuasi wa Kristo.


Mnafiki, unafiki

Ufafanuzi

Neno 'mnafiki' humrejelea mtu ambaye hufanya mambo ili aonekane mwema, ingawa kwa siri hufanya mambo maovu. Neno 'unafiki' hurejelea tabia ambayo huwahadaa watu kwa kufikiri kuwa mtu huyo ni mwenye haki. Wanafiki wanapenda kuonekana wakiwa wanafanya mambo mazuri, hivyo watu hufikiri kuwa ni watu wazuri. Mara kwa mara watu wanafiki huwakosoa watu wengine kwa kufanya mambo yale yale ya dhambi ambayo wao wenyewe huyafanya. Yesu aliwaita Mafarisayo kuwa ni wanafiki kwasababu walifanya matendo ya kidini kama vile kuvaa aina fulani ya nguo na kula chakula fulani, lakini hawakuwa wema na wenye haki kwa watu. Mtu mnafiki huweka wazi makosa ya watu wengine, lakini yeye mwenyewe hakubali makosa yake.

Mapendekezo ya tafsiri Baadhi ya lugha huwa na maneno kama "sura mbili" ambayo hutumika kumrejelea mnafiki au matendo ya mnafiki. Namna nyingine ya kutafsiri neno mnafiki ni "mdanganyifu, mtu anayejifanya, mwongo,"


Mnaziri, Naziri

Ufafanuzi

Neno "Mnaziri" ni mtu aliye toa kiapo cha "Naziri." Sana wanaume wana toa hichi kiapo, pia wanawake waliweza kutoa.


Moyo

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno 'moyo' limetumika mara nyingi kimfano kurejelea mawazo ya mtu, hisia, tamaa au utashi. Kuwa na 'moyo mgumu' ni msemo wa kawaida wenye maana ya mtu anayemwasi Mungu kwa ukaidi. Msemo "kwa moyo wote'' au '' kwa moyo wangu wote'' una maana ya kufanya kitu kwa kujitoa kikamilifu na kwa uhiari. Msemo mwingine '' weka moyoni" una maana kuchukulia kitu kwa umakini na kukitumia katika maisha. Maneno " kuvunjika moyo'' humwelezea mtu ambaye ana huzuni. Wamekuwa wameumizwa kihisia za ndani

Mapendekezo ya tafsiri Baadhi ya lugha hutumia sehemu tofauti za mwili kama vile 'tumbo' au 'ini' kurejelea mawazo haya. Lugha zingine zaweza kutumia neno moja kuelezea dhana hizi na neno jingine kueleza dhana zingine. kama 'moyo' au sehemu nyingine ya mwili haina maana hii, lugha zingine zaweza kuhitaji kutumia maneno ya moja kwa moja kama vile 'fikra' au 'hisia' au 'tamaa.' Kwa kutegemeana na muktadha, maneno "kwa moyo wangu wote" yaweza kutafsiriwa kama "kwa nguvu zangu zote" au "kwa kujitoa kimamilfu" Maneno kama "weka moyoni" yaweza kutafsiriwa kama 'shughulikia kwa umakini' au fikiria kwa uangalifu" "kuvunjika moyo" ina maana ya kuwa 'mwenye huzuni' au 'kujisikia kuumizwa kwa ndani"


mpendwa

Ufafanuzi

Neno "mpendwa" ni kifungu cha kitabia kinachomweleza mtu anayependa na mwingine.

Maoni ya Ufasiri


Mpinga Kristo

Ufafanuzi

"Mpinga Kristo" linamaanisha mtu au mafundisho ambayo ni kinyume na Yesu Kristo na kazi zake. Wapo wapinga Kristo wengi sana duniani.


mpumbavu, upumbavu, upuuzi

Ufafanuzi

Msemo "mpumbavu" una maana ya mtu ambaye mara kwa mara hutengeneza uchaguzi mbaya, haswa kuchagua kutokutii. Msemo "upumbavu" unaelezea mtu au tabia ambayo siyo ya hekima.

Katika Biblia, msemo "mpumbavu" mara kwa mara una maana ya mtu ambaye haamini au kumtii Mungu. Mara nyingi hii hutofautishwa na mtu mwenye hekima, ambaye humwamini Mungu na kumtii.

Katika Zaburi, Daudi anaelezea mtu mpumbavu kama mtu ambaye hamwamini Mungu, ambaye hupuuza ushahidi wote wa Mungu na uumbaji wake.

Kitabu cha Agano la Kale cha Mithali pia hutoa maelezo mengi ya mpumbavu ni nani, mtu mpumbavu yukoje.

Msemo "upuuzi" una maana ya tendo ambao sio la hekima kwa sababu ni kinyume na mapenzi ya Mungu. Mara nyingi "upuuzi" pia hujumuisha maana ya kitu ambacho ni cha kudharaulika au hatari.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "mpumbavu" unaweza kutafsiriwa kama "mtu mpumbavu" au "mtu asiye na hekima" au "mtu asiyejitambua" au "mtu asiyemcha Mungu"

Njia za kutafsiri "mpumbavu" zinawvza kujumuisha "upungufu wa uelewa" au "kutokuwa na hekima" au "kutojitambua".


Msalaba

Ufafanuzi

Katika Biblia msalaba ni mbao iliyosimama wima inayochimbiwa kwenye ardhi na yenye mbao nyingine inayopita kwa mlalo na inayoshikizwa karibu na juu.


mtakatifu

Ufafanuzi

Neno "mtakatifu'' ni jina ambalo katika Biblia mara zote humrejelea Mungu. Katika Agano la kale, jina hili mara kwa mara lilitokea katika kirai ''mtakatifu wa Israeli" Katika Agano Jipya, jina mtakatifu lilitumika kumrejelea Yesu Mara nyingine katika Biblia, neno mtakatifu hutumika kumrejelea malaika.


mtukufu

Ufafanuzi

Neno "mtukufu" la husu ukubwa na utukufu, mara nying katika sifa za mfalme.


Mtume, utume

Ufafanuzi

Mitume walikuwa watu waliotumwa na Yesu kuhubiri kuhusu ufalme wa Mungu. Utume ni nafasi au mamlaka ya wale waliochaguliwa kuwa mitume.


muhudumu, huduma

Ufafanuzi

Katika Biblia, maneno "muhudumu" na "huduma" ya husu kutumikia wengine kwa mafundisho kuhusu Mungu na kujali mahitaji yao ya kiroho. Neno "muhudumu" pia laweza eleza mtu anaye tumikia watu kwa namna hii.


Mungu

Ufafanuzi

Katika Biblia, msemo "Mungu" una maana ya kiumbe wa milele ambaye aliumba ulimwengu bila chochote. Mungu alikuwepo kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Jina binafsi la Mungu ni "Yahwe".

Mungu mara zote alikuwepo; alikuwepo kabla ya kitu chochote kuwepo, na ataendelea kuwepo milele.

Yeye ni Mungu mmoja wa kweli na ana mamlaka juu ya kila kitu ulimwenguni.

Mungu ana haki timilifu, hekima isiyo na mwisho, mtakatifu, bila dhambi, wa haki, wa rehema, na upendo.

Ni Mungu wa kutunza agano, ambaye hutimiza ahadi zake daima.

Watu waliumvwa kumwabudu Mungu na ni yeye pekee wanaopaswa kumwabudu.

Mungu alifunua jina lake kama "Yahwe" ambayo ina maana ya "yeye ni" au "Mimi ni" au "Yule anayekuwepo daima".

Biblia pia hufundisha kuhusu "miungu" wa uongo ambao ni sanamu wasioishi ambao watu huabudu kwa makosa.


Mungu Baba, Baba wa mbinguni, Baba

Ufafanuzi

Misemo, "Mungu Baba" na "Baba wa mbinguni" ina maana ya Yahwe, Mungu mmoja wa kweli. Msemo huu hujitokeza kama "Baba" haswa pale Yesu anamaan ya yeye.

Mungu alikuwepo kama Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu. Kila mmoja ni Mungu kamili, na bado wote ni Mungu mmoja. Hii ni siri ambayo binadamu wa kawaia hawezi kuelewa kikamilifu.

Mungu Baba alimtuma Mungu Mwana (Yesu) duniani na yeye humtuma Roho Mtakatifu kwa watu wake.

Yeyote anayemwamini Mungu Mwana anakuwa mtoto wa Mungu Baba, na Mungu Roho Mtakatifu huja kuishi ndani ya mtu huyo. Hii ni siri nyingine ambayo binadamu hawawezi kuelewa kikamilifu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Katika msemo "Mungu Baba" ni bora kutafsiri "Baba" na neno sawa ambalo lugha hutumia kikawaida kumaanisha baba wa kimwili.

Msemo "Baba wa mbinguni" unaweza kutafsiriwa na "Baba anayeishi mbinguni" au "Baba Mungu ambaye anaishi mbinguni" au "Mungu Baba kutoka mbinguni".

Kawaida "Baba" inaandikwa kwa herufi kubwa, kuonyesha ya kwamba hii inamaanisha Mungu.


mungu wa uongo, mungu mgeni, mungu, mungu wa kike

Ufafanuzi

Mungu wa uongo ni kitu ambacho watu huabudu badala ya Mungu mmoja wa ukweli. Msemo "mungu wa kike" una maana haswa kwa mungu wa uongo wa kike.

Miungu hawa wa uongo hawapo. Yahwe ni Mumngu wa pekee.

Watu mara kwa mara hutengeneza vitu kuwa sanamu ili kuabudu kama ishara ya miungu yao ya uongo.

Katika Biblia, watu wa Mungu mara kwa mara waligeuka kutoka kumtii yeye ili kuabudu miungu ya uongo.

Mapepo mara kwa mara hudanganya watu kuamini ya kwamba miungu ya uongo na sanamu wanazoabudu ina nguvu.

Baali, Dagoni, na Moleki walikuwa miungu watatu wa uongo ambao waliabudiwa na watu katika kipindi cha Biblia.

Ashera na Artemi (Diana) walikuwa miungu wa kike wawili ambao watu wa zamani waliwaabudu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kunaweza kuwa tayari na neno kwa ajili ya "mungu" au "mungu wa uongo" katika lugha yako.

Msemo "sanamu" unaweza kutumika kumaanisha miungu wa uongo.

Katika Kiingereza, herufi ndogo ya "m" inatumika kumaanisha miungu wa uongo, na herufi kubwa ya "M" hutumika kwa ajili ya Mungu wa ukweli. Lugha zingine pia hufanya hivi.

Njia nyingine inakuwa kutumia neno tofauti kabisa kumaanisha miungu wa uongo.

Baadhi ya lugha zinaweza kuongeza neno kuelezea kama mungu wa uongo ni wa kiume au wa kike.


muujiza, ajabu, ishara

Ufafanuzi

"Muujiza" ni kitu kinacho shangaza ambacho hakiwezekani pasipo Mungu kusababisha kitokee.


mwaminifu, uaminifu

Ufafanuzi

Kuwa "mwaminifu" kwa Mungu ina maana kuwa na desturi ya kuishi kulingana na mafunzo ya Mungu. Ina maana ya kuwa mwaminifu kwake na kumuamini. Hali ya kuwa mwaminifu ni "uaminifu".

Mtu ambaye ni mwaminifu anaweza kuaminiwa kuweza kushika ahadi zake na kutimiza majukumu yake daima kwa watu wengine.

Mtu mwaminifu huvumilia katika kutenda kazi, hata pale ambapo ni ndefu au ngumu.

Uaminifu kwa Mungu ni matendo ya daima ya kutenda ambacho Mungu anatutaka kufanya.

Mapendekezo ya Tafsiri

Katika muktadha nyingi, "mwaminifu" inaweza kutafsiriwa kama "uaminifu" au "kujitolea" au "kutegemea".

Katika muktadha zingine, "mwaminifu" inaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana ya "kuendelea kuamini" au "kuvumilia katika kuamini na kumtii Mungu".

Njia ambazo "uaminifu" inaweza kutafsiriwa inaweza kumaanisha "kuvumilia katika kuamini" au "uaminifu" au "kuamini na kumtii Mungu".


Mwana wa Adamu, mwana wa adamu

Ufafanuzi

Jina, "Mwana wa Adamu" lilitumika na Yesu akijieleza. Mara nyingi alitumia hili jina badala ya kusema "mimi."


Mwana wa Mungu, Mwana

Ufafanuzi

Neno "Mwana wa Mungu la husu Yesu, Neno la Mungu aliye kuja duniani kama binadamu. Anajulikana kama "Mwana."


mwana, mwana wa

Ufafanuzi

Neno "mwana" la husu mvulana au mwanaume na wazazi wake. La weza eleza mzao wa kiume wa mwanaume au mwana aliye pangwa.


mwanakondoo, Mwanakondoo wa Mungu

Ufafanuzi

Neno "mwanakondoo" linamaanisha kondoo mchanga. Kondoo ni wanyama wenye miguu minne na wana nywele nene ya sufu, waliotumika kwa sadaka kwa Mungu. Yesu anaitwa "Mwanakondoo wa Mungu" kwa sababu alitolewa kulipia dhambi za watu.

Wanyama hawa huongozwa nje ya mstari kirahisi na wanahitaji ulinzi. Mungu anawafananisha binadamu na kondoo. Mungu anawaagiza watu wake kutoa sadaka kimwili kama kondoo na wanakondoo kamili kwake. Yesu anaitwa "Mwanakondoo wa Mungu" aliyetolewa sadaka kwa ajili ya dhambi za watu. Alikuwa sadaka kamili, bila kasoro kwa sababu alikuwa hata dhambi kabisa.


mwandishi, mtaalamu katika sheria ya Kiyahudi

Ufafanuzi

Waandishi walikuwa wasimamizi waliyo wajibika katika kuandika au kunakili nyaraka muhimu za serikali au za kidini kwa mkono. Jina lingine la mwandishi wa Kiyahudi ni "mtaalamu katika sheria ya Kiyahudi."


Mwenyezi

Ufafanuzi

"Mwenyezi" linamaanisha "nguvu yote. Kwenye Biblia inamaanisha Mungu. Cheo "mwenyezi" linamuelezea Mungu na kudhihirisha kuwa ana nguvu zote na mamlaka kwa kila kitu.


mwili

Ufafanuzi

Neno "mwili" kwa kawaida linamaanisha mwili wa binadamu au mnyama. Nene hili hutumika pia kitamathari kurejerea kitu au jumla ya kundi lenye wajumbe.

Maoni ya Tafasiri


mwili

Ufafanuzi

Katika Biblia, msemo "mwili" una maana ya tishu laini ya mwili wa mwanadamu au mnyama.

Biblia pia hutumia msemo "mwili" kitamathali kumaanisha wanadamu wote au viumbe wote.

Katika Agano Jipya, msemo "mwili" unatumika kumaanisha asili ya dhambi ya wanadamu. Hii hutumika mara kwa mara kinyume na asili yao ya kiroho.

Msemo, "mwili na damu yake" ina maana ya mtu ambaye anahusiana kibiolojia na mtu mwingine, kama vile mzazi, ndugu, mtoto au mjukuu.

Msemo "mwili na damu" pia unaweza kumaanisha mababu au vizazi vya mtu.

Msemo "mwili mmoja" una maana ya muungano wa kimwili wa mwanamume na mwanamke katika ndoa.

Mapendekezo ya Tafsiri

Katika muktadha wa mwili wa mnyama, "mwili" unaweza kutafsiriwa kama "mwili" au "ngozi" au "nyama".

Inapotumika kumaanisha viumbe wote hai, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "viumbe hai" au "kila kitu chenye uhai".

Inapomaanisha kwa jumla watu wote, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "watu" au "binadamu" au "kila mtu anayeishi".

Msemo "mwili na damu" unaweza kutafsiriwa kama "jamaa" au "familia" au "ndugu wa karibu" au "ukoo wa familia". Kunaweza kuwa na muktadha ambapo inaweza kutafsiriwa kama "mababu" au "vizazi".

Baadhi ya lugha zinaweza kuwa na msemo ambao unafanana na "mwili na damu".

Msemo "kuwa mwili mmoja" unaweza kutafsiriwa kama "kuungana kimapenzi" au "kuwa kama mwili mmoja" au "kuwa kama mtu mmoja kimwili na roho". Tafsiri ya msemo huu unaweza kuangaliwa kuhakikisha inakubalika katika lugha na utamaduni wako.


mwinjilisti

Ufafanuzi

"mwinjilisti" ni mtu ambaye huwaambia watu wengine habari njema juu ya Yesu Kristo.

Maana halisi ya "mwinjilisti" ni "mtu ambaye anahubiri habari njema".

Yesu aliwatuma mitume wake kusambaza habari njema kuhusu namna ya kuwa sehemu ya ufalme wa Mungu kupitia kumuamini Yesu na sadaka yake kwa ajili ya dhambi.

Wakristo wote wanashawishiwa kutangaza hii habari njema.

Baadhi ya Wakristo wanapatiwa karama maalumu kuwaambia kwa ufasaha watu wengine injili. Watu hawa wanasemwa kuwa na karama ya uinjilisti na wanaitwa "wainjilisti".

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "mwinjilisti" unaweza kutafsiriwa kama, " mtu anayehubiri habari njema" au "mwalimu wa habari njema" au "mtu ambaye anatangaza habari njema"


Mwokozi

Ufafanuzi

Neno "Mwokozi" lina husu mtu anaye okoa au komboa wengine na hatari. Pia yaweza maanisha mtu anaye wapa wengine uwezo au waitaji yao.


Myahudi, Yahudi, Wayahudi

Ufafanuzi

Wayahudi ni watu ambao ni uzao wa mjukuu wa Abrahamu, Yakobo. Neno "Yahudi" linatoka katika neno "Yuda"

Watu walianza kuwaita Waisraeli "Wayahudi" baada ya kurudi Yuda kutoka katika uhamisho kutoka Babeli. Yesu Masihi alikuwa Myahudi. Isipokuwa, viongozi wa dini wa Kiyahudi walitaka kwamba auliwe. Mara nyingi msemo "Wayahudi" inamaanisha viongozi wa Wayahudi, sio watu wote Wayahudi. Kwa mazingira hayo, tafsiri zingine huongeza "viongozi wa" kuiweka wazi.


Nabii, unabii, mwonaji, nabii mwanamke.

Ufafanuzi

"Nabii ni mtu anayesema ujumbe wa Mungu kwa watu. Mwanamke anayefanya hivi anaitwa "nabii mwanamke."


nafsi

Ufafanuzi

Nafsi ni sehemu ya ndani, isiyo onekana ya mtu. Ya husu sehemu isiyo ya kimwili ya mtu.


naivera

Ufafanuzi

Naivera ilikuwa vazi kama aproni iliyovaliwa na makuhani wa Kiisraeli. Ilikuwa na sehemu mbili, mbele na nyuma, amnazo ziliunganishwa pamoja mabegani na kufungwa kuzunguka kiuno na mkanda wa kitambaa.

Aina moja ya naivera ilitengenezwa na sufi ya kawaida na ilivaliwa na makuhani wa kawaida.

Naivera iliyovaliwa na kuhani mkuu ilishonwa maalumu kwa kitani cha dhahabu, bluu, zambarau, na chekundu.

Deraya ya kifua ya kuhani mkuu iliunganishwa na sehemu ya mbele ya naivera. Nyuma ya deraya ya kifuani kulitunzwa Urimu na Thumimu, ambaya yalikuwa mawe yaliyotumiwa kumuuliza Mungu mapenzi yake yalikuwa yapi katika baadhi ya masuala.

Mwamuzi Gideoni kwa upumbavu alitengeneza naivera kwa dhahabu na ikawa kitu ambacho Waisraeli waliabudu kama sanamu.


Nchi ya ahadi

Ufafanuzi

"Nchi ya ahadi" imaonekana tuu katika simulizi za Biblis. Ni namna ya kuelezea nchi ya Kanaani ambayo Mungu aliahidi kumpa Abrahamu na uzao wake.


ndugu

Ufafanuzi

Neno "ndugu" kwa kawaida linamaanisha ndugu wa kiume ambaye wanaunganishwa angalau na mzazi mmoja.

Maoni ya Kutafasiri


neema, mwenye neema

Ufafanuzi

Neno "neema" lina maana ya msaada au baraka ambayo hutolewa kwa mtu ambaye hajastahili. Msemo "mwenye neema" inamwelezea mtu ambaye huonyesha neema kwa wengine.

Neema ya Mungu kwa wanadamu wenye dhambi ni zawadi ambayo inatolewa bure.

Dhana ya neema pia ina maana ya kuwa na huruma na kusamehe mtu ambaye amefanya kosa au mambo ya kuumiza.

Msemo "kupata neema" ni msemo ambao una maan aya kupokea msaada na rehema kutoka kwa Mungu. Mara nyngi inajumuisha maana ya kwamba Mughu anafurahishwa na mtu na kumsaidia.


Neno la Mungu, Neno la Yaweh, Neno la Bwana, maandiko

Ufafanuzi

Katika Biblia neno la Mungu ni kitu chochote ambacho Mungu anawaambia wanadamu. Hii ni pamoja na lililoandikwa au kutamkwa. Yesu pia anaitwa "neno la Mungu.


Nguvu

Ufafanuzi

"Nguvu" ni uwezo wa kufanya jambo au kusababisha mambo yatokee mara nyingi hutumia nguvu. Pia nguvu yaweza kumaanisha watu au roho zenye uwezo wa kusababisha mambo yatokee.


nidhamu, nidhamu binafsi

Ufafanuzi

Msemo wa "nidhamu" una maana ya kufundisha watu kutii maelekezo kadhaa ya tabia za maadili.

Wazazi huwafundisha watoto wao kwa kutoa maelekezo ya kimaadili na mwelekeo kwa ajili yao na kuwafundisha kutii.

Vivyohivyo, Mungu huadhibu watoto wake kuwasaidia kuzaa matunda mazuri ya kiroho katika maisha yao, kama vile furaha, upendo, na uvumilivu.

Nidhamu inashirikisha maelekezo yahusuyo jinsi ya kuishi namna ya kumpendeza Mungu, na pia adhabu kwa tabia ambayo ipo kinyume na mapenzi ya Mungu.

Nidhamu binafsi ni njia ya kutumia kanuni za kimaadili na kiroho kwa maisha ya mtu mwenyewe.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kutegemea na muktadha, "nidhamu" inaweza kutafsiriwa kama, "fundisha na kuelekeza" au "ongoza kimaadili" au "adhibu kwa kutenda mabaya".

Nomino ya "nidhamu" inaweza kutafsiriwa kama "mafunzo ya maadili" au "adhabu" au "marekebisho ya maadili" au "mwongozo na maelekezo ya kimaadili".


nyenyekea, unyenyekevu

Ufafanuzi

Neno 'nyenyekea' humwelezea mtu ambaye hufikirii kuwa ni bora kuliko watu wengine. Ni mtu asiye na kiburi au majivuno. Unyenyekevu ni sifa au hali ya kuwa mnyenyekevu. Kuwa mnyenyekevu mbele za Mungu ina maana ya kujua udhaifu na hali ya kutokamilika, huku ukilinganisha na ukuu , hekima na ukamilifu wa Mungu. Mtu anapojinyenyekesha, hujiweka katika daraja la chini. 'Unyenyekevu' ni hali ya kujali mahitaji ya watu wengi kuliko mahitaji yako binafsi. Kirai 'uwe mnyenyekevu' kinaweza kutafsiriwa kama ' ''usiwe mwenye kiburi/majivuno.'' "Nyenyekea mbele za Mungu'' ina maana ya " wasilisha utashi wako kwa Mungu, kwa kuutambua ukuu wake.


Nyumba ya Mungu, Nyumba ya Yahweh

Ufafanuzi

Katika Biblia, vifungu vya maneno "nyumba ya Mungu'' na "nyumba ya Yahweh'' hurejelea sehemu ambapo Mungu huabudiwa'' au 'sehemu ya kumwabudia Mungu.' Neno hili piakimahususi laweza kurejelea 'hema la kukutania au hekalu' Wakati mwingine neno 'nyumba ya Mungu' humaanisha ''watu wa Mungu"

Mapendekezo ya tafsiri Wakati neno la nyumba ya Mungu linaporejelea sehemu ya kuabudia ina maana ya 'nyumba au sehemu ya kumwabudia Mungu.


okoa, salama

Ufafanuzi

Neno "okoa" la husu kumzuia mtu kutopitia kitu kibaya au cha hatari. Kuwa "salama" ya maanisha kulindwa na hatari au majanga.


ombea, sala ya kuombea

Ufafanuzi

Msemo "ombea" na "sala ya kuombea" inamaanisha kufanya maombi kwa mtu kwa niaba ya mtu mwingine. Katika Biblia hii kawaida humaanisha kuwaombea watu wengine.

Usemi "kuomba kwa ajili ya" na "kuombea" inamaanisha kufanya maombi kwa Mungu kwa faida ya watu wengine. Biblia inafundisha kuwa Roho Mtakatifu hutuombea, kwamba, humsihi Mungu kwa ajili yetu. Mtu huombea watu wengine kwa mtu mwenye mamlaka.


omboleza, maombolezo

Ufafanuzi

usemi "omboleza" na "maombolezo" yanamaanisha hisia kali ya kulia, majonzi au huzuni.

Wakati mwingine hii ni pamoja na kujuta kwa kina kwa ajili ya dhambi, au huruma kwa watu waliopitia maafa. Maombolezo yanaweza kujumuisha kulia, kutoa machozi au kulia kwa sauti.


Onesha, ufunuo

Ufafanuzi

Kuonesha ni kusababisha kitu fulani kujulikana. Ufunuo ni kitu kilichojulikana.


Pasaka

Ufafanuzi

"Pasaka " ni jina la sherehe ya kidini ambayo Wayahudi walisherehekea kila mwaka kukumbuka mi kwa namna gani Mungu aliwaokoa mababu zao Waisraeli toka utumwani Misri.


Pentekoste au sikukuu za majuma

Ufafanuzi

Sikukuu za majuma ilikuwa ni sikukuu ya Kiyahudi iliyofanyika siku hamsini kabla ya Pasaka. Baadae ilikuja kuitwa Pentekoste.


pepo mbaya, roho ovu, roho chafu

Ufafanuzi

Misemo hii yote ina maana ya mapepo, ambayo ni viumbe vya roho vinavyopingana na mapenzi ya Mungu.

Mungu aliwaumba malaika kumtumikia. Shetani alipomwasi Mungu, baadhi ya malaika pia waliasi na kutupwa kutoka mbinguni. Inaaminika ya kwamba mapepo na roho mbaya ndio hawa "mailak walioanguka".

Mara kwa mara haya mapepo yanajulikana kama "roho chafu". Msemo "chafu" una maana ya "isiyo safi" au "uovu" au "isiyo takatifu".

Kwa sababu mapepo humtumikia shetani, wanafanya mambo maovu. Mara kwa mara wanaishi ndani ya watu na kuwaendesha.

Mapepo wana nguvu kuliko wanadamu, lakini hawana nguvu kama ya Mungu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo wa "pepo" unaweza kutafsiriwa kama "roho mchafu".

Msemo wa "roho mchafu" unaweza kutafsiriwa kama "roho chafu" au "roho iliyoharibika" au "roho mchafu".

Hakikisha ya kwamba neno au msemo unaotumika kutafsiri msemo huu ni tofauti na msemo unaotumika kumaanisha shetani.

Pia fikiria jinsi msemo wa "pepo" unaweza kutafsiriwa katika lugha ya kawaida au ya taifa.


Rabi, Raboni

Ufafanuzi

Rabi ina maana ya bwana wangu au mwalimu wangu.


rehema

Ufafanuzi

Neno "rehema" lina husu kusaidia mtu waliyo na shida, hususani wanapo kuwa chini au hali ngumu.


rithi, urithi, mrithi

Ufafanuzi

Maneno "rithi" na "urithi" zinamaanisha kupokea kitu cha dhamani kutoka kwa mzazi au mtu mwingine kwa sababu ya uhusiano maalumu na huyo mtu. "Mrithi" ni mtu ambaye anapokea urithi.

Urithi wa halisia ambao unapokelewa unaweza kuwa fedha, ardhi, au aina zingine za mali. Urithi wa kiroho ni vyote ambavyo Mungu huwapa watu wanaomuamini Yesu, zikiwemo baraka za maisha ya sasa pamoja na maisha ya milele pamoja naye. Biblia pia inawaiita watu wa Mungu urithi wake, kinachomaanisha kuwa ni wake, ni mali yake ya dhamani. Mungu alimuahidi Abrahamu na uzao wake kuwa watarithi nchi ya Kanaani, kwamba itakuwa yao milele. Kuna maana ya kitamathali na kiroho ya jinsi watu walio wa Mungu wanasemwa "kurithi nchi." Hii inamaanisha kuwa watafanikiwa na kubarikiwa na Mungu kwa mambo ya kimwili na kiroho. Katika Agano Jipya, Mungu anaahidi kuwa wale wanaomuamini Yesu "watarithi wokovu" na "kurithi uzima wa milele." Pia inaelezwa kama, "kurithi ufalme wa Mungu." Huu ni urithi wa milele unaodumu milele. Kuna maana zingine za kitamathali za haya maneno: Biblia inasema kuwa watu wenye hekima "watarithi utukufu" na watakatifu "watarithi vitu vizuri." "Kurithi ahadi" inamaanisha kupokea vitu vizuri ambavyo Mungu ameahidi kuwapa watu wake. Msemo huu pia unatumika kwa njia ya uhasi kumaanisha watu wapumbavu au wasiotii ambao "wanarithi upepo" au "kurithi upumbavu." Hii inamaanisha wanapokea matokeo ya matendo yao ya dhambi, ikiwemo adhabu na maisha yasiyo na maana.


Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu, Roho wa Bwana.

Ufafanuzi

Maneno haya yote humrejelea Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu. Mungu mmoja na wa kweli aishiye milele katika nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu mara zingine hutajwa kama 'Roho' na 'Roho ya Yahweh' au 'Roho wa ukweli' Roho Mtakatifu ni mtakatifu kwa sababu yeye ni Mungu. Yeye yuko kamili na mwadilifu katika kila jambo alifanyalo. Roho Mtakatifu alishiriki kikamilifu katika uumbaji wa ulimwengu pamoja na Baba na Mwana. Wakati Mwana wa Mungu, Yesu aliporudi mbinguni, Mungu alimtuma Roho Mtakatifu kwa watu ili awaongoze, kuwafundisha, kuwafariji na kuwawezesha kufunya mapenzi ya Mungu. Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu na pia anawaongoza wale wanaomwamini Yesu.

Mapendekezo ya tafsiri Neno hili laweza kutafsiriwa tu kwa kutumia maneno yenye kumaanisha 'roho' na 'mtakatifu' Lakini maneno mengine ambayo yaweza kutumika ni kama 'Roho Safi' au 'Roho aliye Mtakatifu' au 'Mungu Roho.'


roho, kiroho

Ufafanuzi

Neno "roho" la eleza sehemu isiyo ya kimwili ya watu isiyo onekana. Mtu anapo kufa, roho yake inaacha mwili wake. "Roho" inaweza eleza tabia au hali ya kihisia ya mtu.


Sabato

Ufafanuzi

Neno "Sabato" la husu siku ya saba ya wiki, ambayo Mungu aliwaamuru Waisraeli waitenge kama siku ya kupumzika na kutofanya kazi.


Sadukayo

Ufafanuzi

Masadukayo walikuwa kikundi cha makuhani wa Kiyahudi kipindi cha Yesu Kristo waliyo unga mkono utawala wa Warumi na ambao hawakuamini ufufuo.


safi, kusafisha

Ufafanuzi

Kuwa "safi" inamaana kutokuwa na mapungufu au kutochanganya kitu ndani ya kitu ambacho hakitakiwi kuchanganywa. Kukisafisha kitu ni kitendo cha kukisafisha na kuondoa chochote kinachoweza kuchafua.


Safi, kusafisha

Ufafanuzi

Neno "safi" inamaana ya kawaida ya kutokuwa na uchafu au doa. Katika Biblia hutumika kuwa na maana ya "takatifu" au "kuwa huru na dhambi."


samehe, kusamehe

Ufafanuzi

Kumsamehe mtu ina maana ya kutokaa na kinyongo dhidi ya mtu ambaye alifanya jambo la kuumiza. "Kusamehe" ni tendo la kumsamehe mtu.

Kumsamehe mtu mara nyingi humaanisha kutomuadhibu mtu huyo kwa jambo ambalo amekosa.

Msemo huu unaweza kutumika kitamathali kumaanisha, "katisha" kama msemo "kusamehe deni".

Watu wanapokiri dhambi zao, Mungu huwasamehe kutokana na sadaka ya kifo cha Yesu msalabani.

Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kusamehe wengine kama jinsi alivyowasamehe wao.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "samehe" inaweza kutafsiriwa kama "omba radhi" au "katisha" au "achilia" au "kutoshikilia dhidi ya"


Sanduku

Ufafanuzi

Maana ya kawaida ya "sanduku" ni sanduku la mbao la mstatili lililotengenezwa kwa ajili ya kushikilia au kulinda kitu fulani. Sanduku laweza kuwa kubwa au dogo kutokana na matumizi yake.


Sanduku la agano, Sanduku la Yahweh.

Ufafanuzi

Sanduku la agano ni sanduku la mbao maalumu lililofunikwa na dhahabu na lenye vibao viwili vya mawe vyenye amri kumi. Pia lina fimbo ya Haruni na mana.


Sayuni, Mlima Sayuni

Ufafanuzi

Hapo awali, neno "Sayuni" au "Mlima Sayuni" lilimaanisha ngome ambayo Mfalme Daudi aliiteka kutoka kwa Wayebusi. Majina haya yakawa njia nyingine ya kuitaja Yerusalemu.


Sehemu takatifu, sehemu takatifu sana (patakatifu pa patakatifu)

Ufafanuzi

Katika Biblia, maneno kama 'sehemu takatifu' na ' sehemu takatifu sana' yanarejelea sehemu mbili za hema la kukutania au jengo la hekalu. 'Sehemu takatifu' ni chumba cha kwanza kilicho na madhabahu ya uvumba na meza iliyo na 'mkate wa uwepo' juu yake. 'Sehemu takatifu sana' (patakatifu pa patakatifu) kilikuwa ni chumba cha pili cha ndani sana kilicho na sanduku la agano. Kulikuwa na pazia kubwa na pana lililotenganisha kati ya chumba cha nje na chumba cha ndani. Kuhani mkuu ndiye pekee aliyeruhusiwa kuingia sehemu takatifu sana yaani Patakatifu pa patakatifu. Wakati mwingine 'sehemu takatifu' hurejelea jengo na sehemu za nje za hekalu au hema la kukutania. Pia neno hili laweza kumaanisha eneo lolote lililotengwa kwa ajili ya Mungu.

Mapendekezo ya tafsiri Maneno 'sehemu takatifu' yanaweza kutafsiriwa kama "chumba kilichotengwa kwa ajili ya Mungu'' au '' chumba maalumu kwa ajili ya kukutana na Mungu'' au chumba kilichotunzwa kwa ajli ya Mungu. ''sehemu takatifu'' yaweza kujumuisha sehemu iliyotakaswa' au hekaluni.


shawishi, ushawishi

Ufafanuzi

Msemo "shawishi" una maana ya kumsihi mtu kwa nguvu na kumbembeleza mtu kufanya kilicho sahihi. Aini hii ya kusihi inaitwa "kushawishi".

Kusudi la kushawishi ni kusihi watu wengine kuepukana na dhambi na kufuata mapenzi ya Mungu.

Agano Jipya hufundisha Wakristo kujishawishi baina yao kwa upendo, sio kwa ukali au ghafula.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "kushawishi" pia inaweza kutafsiriwa kama "kubembeleza kwa nguvu" au "kusihi" au "kushauri".

Hakikisha tafsiri ya msemo huu hainyoeshi ya kuwa anayeshawishi ana hasira. Msemo unatakiwa kuonyesha nguvu na uzito, lakini usionyeshe kauli ya ukali.

Katika muktadha nyingi, msemo "shawishi" unatakiwa kutafsiriwa tofauti na "kutia moyo" ambayo ina maana ya kutia msukumo, aminisha, au kufariji mtu.

Mara kwa mara msemo huu pia unatafsiriwa tofauti na "onya" ambayo ina maana ya kuonya au kusahisha mtu kwa tabia yake mbaya.


shemasi

Ufafanuzi

Shemasi ni mtu ambaye anatumika katika kanisa lake, akiwasaidia waumini kwa mahitaji ya kiutendaji, kama vile chakula au pesa.

Neno "shemasi" limechukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye neno la Kigiriki lenye maana ya "mtumishi" au "mchungaji".

Tangu kipindi cha Wakristo wa awali, kuwa shemasi ilikuwa ni nafasi na huduma iliyobainishwa katika mwili wa Kanisa.

Kwa mfano, katika Agano Jipya, mashemasi walikuwa wanahakikisha ya kuwa kila pesa au chakula ambacho waumini hutoa zingegawanywa sawa sawa kwa wajane miongoni mwao.

Msemo wa "shemasi" pia unaweza kutafsiriwa kama, "mchungaji wa kanisa" au "mfanyakazi wa kanisani" au "mtumishi wa kanisani", au msemo mwingine ambo unaonyesha ya kwamba mtu huyu amewekwa mahususi kufanya kazi maalumu ambayo ina manufaa kwa jamii yake ya Kikristo.


sheria, sheria ya Musa, sheria ya Mungu, sheria ya Yahwe

Ufafanuzi

Misemo hii yote inamaanisha amri na maelekezo ambayo Mungu alimpa Musa kwa ajili ya Waisraeli kutii. Misemo "sheria" na "sheria ya Mungu" zinatumika pia kwa ujumla kumaanisha kila kitu Mungu anachotaka watu wake kutii.

Kulingana na mazingira, "sheria" inaweza kumaanisha: Amri kumi ambazo Mungu aliandika katika jiwe kwa ajili ya Waisraeli. sheria zote alizopewa Musa vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale. Agano lote la Kale (pia inajulikana kama "maandiko" katika Agano Jipya). maelekezo yote ya Mungu na mapenzi yake. Usemi "sheria na manabii" inatumika katika Agano Jipya kumaanisha maandiko ya Kihebrania (au "Agano la Kale").


Shetani, ibilisi, yule muovu

Ufafanuzi

Ibilisi ni roho hai Mungu aliyo umba, lakini aliasi dhidi ya Mungu na kuwa adui wa Mungu. Ibilisi anaitwa "Shetani" na "yule muovu."


siku ya Bwana, siku ya Yahwe

Ufafanuzi

Msemo wa Agano la Kale wa "siku ya Yahwe" unatumika kumaanisha kipindi/vipindi maalumu ambapo Mungu angewaadhibu watu kwa dhambi zao.

Msemo wa Agano Jipya wa "siku ya Bwana" huwa una maana ya siku au kipindi ambapo Bwana Yesu atarudi kuwahukumu watu katika wakati wa mwisho.

Huu wakati wa mwisho, wa baadaye wa hukumu na ufufuo, pia hujulikana kama "siku ya mwisho". Kipindi hiki kitaanza pale ambapo Bwana Yesu atakaporudi kuhukumu wenye dhambi na kuunda mamlaka yake ya kudumu.

Neno "siku" katika misemo hii inaweza kumaanisha siku haswa au inaweza kumaanisha "kipindi" au "wakati maalumu" ambao ni mrefu zaidi ya siku moja.

Mara nyingine adhabu huwa ina maana ya "kumwagwa kwa ghadhabu ya Mungu" juu ya wale wasioamini.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, njia zingine za kutafsiri "siku ya Yahwe" zinaweza kujumuisha, "kipindi cha Yahwe" au "kipindi ambapo Yahwe atawaadhibu adui zake" au "kipindi cha hasira ya Yahwe".

Njia zingine za kutafsiri "siku ya Bwana" zinaweza kujumuisha "kipindi cha hukumu ya Bwana" au "kipindi ambacho Bwana Yesu atarudi kuhukumu watu".


siku ya hukumu

Ufafanuzi

Usemi "siku ya hukumu" inamaanisha siku ya usoni ambapo Mungu atamhukumu kila mtu.

Mungu amemfanya Mwanaye, Yesu Kristo, kuhukumu watu wote. Katika siku ya hukumu, Kristo atawahukumu watu kulingana na asili yake ya haki.


siku ya mwisho, siku za mwisho

Ufafanuzi

Usemi wa "siku za mwisho" inamaanisha kwa ujumla kipindi cha mwisho wa muda wa sasa.

Muda huu utakuwa muda usiojulikana. "Siku za mwisho" ni wakati wa hukumu kwa wale waliomgeuka Mungu.


sinagogi

Ufafanuzi

Sinagogi ni jengo la watu wa Kiyahudi wanapo kutania pamoja kumuabudu Mungu.


sio na hatia

Ufafanuzi

Usemi "sio na hatia" unamaanisha kutokuwa na hatia la uhalifu au makosa mengine. Inaweza pia kumaanisha kwa ujumla watu ambayo hawahusiki na matendo maovu.

Mtu anayetuhumiwa kwa kufanya kitu kibaya hana hatia kama hataambatanishwa na hilo kosa. Wakati mwingine usemi "sio na hatia" unatumika kumaanisha watu ambao hawajafanya kosa kustahili ubaya wanaoupata, kama jeshi la adui kushambulia "watu wasio na hatia."


stahili, yenye thamani ya, wasiofaa, isiyo na maana

Ufafanuzi

"Stahili" linaelezea mtu au kitu kinachofaa kupewa heshima. "Kustahilisha" inamaana ya kuwa na thamani au muhimu. "isiyo na maana" inamaanisha isiyo na thamani.


Sulubisha

Ufafanuzi

Sulubisha inamaana ya kumuhukumu mtu kwa kumuweka msalabani na kumuacha ateseke mpaka afe.


tahini, pima

Ufafanuzi

Neno "tahini" yaeleza hali ngumu au inayo umiza yenye kudhihirisha uweza na udhahifu wa mtu.


takasa, utakaso

Ufafanuzi

Kutakasa ni kutenga kando au kufanya takatifu. Utakaso ni hatua ya kufanya takatifu.


takatifu

Ufafanuzi

Msemo "takatifu" una maana ya kitu chochote kinachomhusu Mungu.

Baadhi ya njia ambazo msemo huu unatumika ni, "mamlaka takatifu", "hukumu takatifu", "asili takatifu", "nguvu takatifu", na "utukufu mtakatifu".

Katika sehemu moja ndani ya Biblia, msemo "takatifu" unatumika kuelezea jambo juu ya uungu wa uongo.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia za kutafsiri msemo wa "takatifu" zinaweza kujumuisha "ya Mungu" au "kutoka kwa Mungu" au "fungamana na Mungu" au "huonyesha ni ya Mungu".

Kwa mfano, "mamlaka takatifu" inaweza kutafsiriwa kama "mamlaka ya Mungu" au "mamlaka ambayo yanatoka kwa Mungu".

Msemo wa "utukutufu takatifu" unaweza kutafsiriwa kama "utukufu wa Mungu" au "utukufu ambao Mungu ame" au "utukufu unatoka kwa Mungu".

Baadhi ya tafsiri zinapendelea kutumia neno tofauti wanapofafanua jambo ambalo linafungamana na mungu wa uongo.


takatifu, utakatifu

Ufafanuzi

Maneno 'takatifu' na 'utakatifu' hurejelea tabia ya Mungu ambayo imetengwa na kutofautishwa na kila kitu ambacho ni chenye dhambi na kisicho kamili. Mungu pekee ndiye mtakatifu kweli. Hufawafanya watu na vitu kuwa vitakatifu. Mtu aliye mtakatifu ni mali ya Mungu na ametengwa maalumu kwa kusudi la kumtumika Mungu na kumpa utukufu Yeye. Na kitu ambacho Mungu amekitangaza kuwa ni kitakatifu ni kile ambacho Mungu amekitenga kwa ajili ya utukufu wake na matumizi yake, kwa mfano madhabahu ambayo makusudi yake ni kumtolea Mungu sadaka. Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu, hakuna mtu awezaye kumkaribia Mungu isipokuwa awe ameruhusiwa na Yeye kufanya hivyo, hii ni kwasababu wao ni watu tu, wenye dhambi na wasiokamili. katika Agano la Kale, Mungu alitenga makuhani kama watakatifu kwa huduma maalumu kwake. Walitakiwa kutakaswa kwa sherehe maalumu ili waweze kumkaribia Mungu. Mungu pia aliweza kutenga sehemu na vitu maalumu kuwa vitakatifu vilivyo mali yake au kupitia kwa vitu hivyo aweze kujifunua mwenyewe, vitu hivi ni kama hekalu.

Mapendekezo ya tafsiri Njia za kutafsiri neno 'takatifu' zinaweza kuwa ' kutengwa kwa ajili ya Mungu,' au "kuwa mali ya Mungu" au "hali ya kutokuwa na dhambi" au "kuwa safi." kufanya kitu/kuwa kuwa mtakatifu ina maana ya "kutakasa'' au ''kutenga''


telekeza, kutelekezwa, totoka

Ufafanuzi

Msemo "telekeza" ina maana ya kuacha mtu au kuacha kitu. Mtu ambaye "ametelekezwa" amekuwa ameachwa au kutorokwa na mtu mwingine.

Pale watu "wanapomtelekeza" Mungu, ina maana wanakuwa bila uaminifu kwake kwa kutomtii yeye.

Mungu "anapotelekeza" watu, ina maana ameacha kuwasaidia na kuruhu wapitia mateso ili kwamba kuwafanya wamgeukie na kumrudia yeye.

Msemo huu unaweza kumaanisha kutelekeza vitu, kama vile kuacha, au kutomfuata mafundisho ya Mungu.

Msemo "kutelekezwa" unaweza kutumika katika kisarufi cha nyuma kama vile "amekutelekeza" au kumaanisha mtu ambaye "ametelekezwa".

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia zingine za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha "kuacha" au "kutojali" au "kuachana" au "kuondoka mbali na" au "kuacha nyuma" kulinga na muktadha.

"Kutelekeza" sheria ya Mungu inaweza kutafsiriwa "kutotii sheria ya Mungu". Hii inaweza kutafsiriwa kama "kutenga" au "kukata tamaa juu ya" au "kuacha kutii" mafunzo au sheria zake.

Msemo "kutelekezwa" unaweza kutafsiriwa kama "kuachwa" au "kutengwa".

Lugha ya mradi inaweza kupata kwa uwazi zaidi kutumia maneno tofauti kutafsiri msemo huu, kulingana na maandishi yanaongelea juu ya kutelekeza kitu au mtu.


timiza

Ufafanuzi

Msemo "timiza" una maana ya kukamilisha au fanikisha jambo ambalo lilitarajiwa.

Pale ambapo unabii unatimizwa, ina maana ya kwamba Mungu alisababisha itokee kile kilichotabiriwa katika unabii.

Kama mtu anatimiza ahadi au kiapo, ina maana ya kwamba anafanya kile alichoahidi kufanya.

Kutimiza jukumu ina maana kufanya kazi ambayo ulipangiwa au unapaswa kufanya.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "timiza" unaweza kutafsiriwa kama "fanikisha" au "kamilisha" au "kusababisha kutokea" au "kutii" au "kutenda".

Msemo "imetimizwa" inaweza kutafsiriwa kama "imekuwa kweli" au "imetokea".

Njia za kutafsiri "timiza" kama vile "timiza huduma yako" inaweza kujumuisha, "maliza" au "fanya" au "mazoezi" au "tumikia watu wengine kama vile Mungu amekuita kufanya"


Tohara

Ufafanuzi

Tohara ni kitendo cha kukata govi la mwanaume au mtoto wa kiume. Sherehe ya tohara hufanyika pamoja na tendo hili.


towashi

Ufafanuzi

Mara kwa mara, "towashi" ina maana ya mwanamume ambaye amehanithishwa. Msemo baadaye ukawa msemo wa jumla kumaanisha afisa yeyote wa serikali, hata wale ambao hawana ulemavu huu.

Yesu alisema ya kwamba baadhi ya towashi walizaliwa vile, yawezekana kwa sababu ya uharibifu ya viuongo vya siri au kwa sababu ya kutokuwa kutekeleza jukumu la kuingiliana. Wengine huchagua kuishi kama towashi kwa maisha ya mseja.

Katika nyakati za kale, matowashi mara nyingi walikuwa watumishi wa wafalme ambao waliwekwa kama walinzi katika maeneo ya wanawake.

Baadhi ya matowashi walikuwa maafisa muhimu wa serikali, kama vile towashi wa Ethiopia ambaye alikutana na mtume Filipo katika jangwa.


tukuza, kutukuza

Ufafanuzi

Kutukuza ni kusifu kwa juu sana na kumheshimu mtu. Inaweza kumaanisha kumweka mtu katika nafasi ya juu.

Katika Biblia, msemo "tukuza" unatumika sana kwa ajili ya kumtukuza Mungu.

Mtu anapojitukuza mwenyewe, ina maana anawaza juu yake mwenyewe kwa hali ya kujiinua au namna ya kiburi.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia za kutafsiri "tukuza" zinaweza kujumuisha "kusifu kwa juu" au "kuheshimu sana" au "sifu sana" au "kuzungumza kwa juu sana"

Katika baadhi ya muktadha, inaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana ya "kuweka nafasi ya juu zaidi" au "kutoa heshima zaidi" au "kuzungumza kuhusu kwa kiburi".

"Usijitukuze mwenyewe" inaweza kutafsiriwa kama "Usijiwazie kuwa juu sana" au "Usijidai juu yako mwenyewe".

"Wale wanaojiinua wenyewe" inaweza kutafsiriwa kama "Wale ambao hufikiri kwa kiburi kuhusu wao wenyewe" au "Wale wanaojidai juu yao wenyewe"


Uaminifu wa agano, fadhili, upendo wa kudumu

Ufafanuzi

Maneno haya hutumika kuelezea Mungu alivyijitoa kikamilivu kutimiza ahadi alizoweka kwa watu wake.


ufalme wa Mungu, ufalme wa mbinguni

Ufafanuzi

Usemi wa "ufalme wa Mungu" na "ufalme wa mbinguni" zote zinamaanisha utawala wa Mungu na madaraka yake juu ya watu wake na viumbe vyote.

Wayahudi mara nyingi hutumia neno "mbingu" kumaanisha Mungu, ili kuepuka kutaja jina lake moja kwa moja. Katika kitabu cha Agano Jipya alichoandika Mathayo, aliuita ufalme wa Mungu kama "ufalme wa mbinguni," inawezekana kwa sababu alikuwa akiwaandikia zaidi Wayahudi. Ufalme wa Mungu unamaanisha Mungu kuwatawala watu kiroho pamoja na kuwatawala katika dunia ya kimwili. Manabii wa Agano la Kale walisema kuwa Mungu atamtuma Masihi kutawala kwa haki. Yesu, mwana wa Mungu, ndiye Masihi atakaye tawala juu ya watu wa Mungu milele.


Ufufuo

Ufafanuzi

Ufufuo ni kitendo cha kuwa hai tena baada ya kufa.


uovu

Ufafanuzi

Neno "uovu" ni neno ambalo liko karibu kwa maana na neno "dhambi," lakini inaweza kumaanisha zaidi matendo ya ufahamu mabaya au uovu mkubwa.

Neno "uovu" ina maana halisi ya kupindisha au kupotosha (sheria). Inamaanisha udhalimu mkubwa. Uovu unaweza kuelezwa kama matendo ya kudhuru ya makusudi dhidi ya watu wengine. Maana zingine za uovu ni pamoja na "ukaidi" na "kunyima," ambayo yote ni maneno yanayoeleza hali za dhambi mbaya.


Upatanisho, kulipia

Ufafanuzi

"Upatanisho au kulipia" inaonesha ni jinsi gani Mungu alitoa sadaka ili kulipia dhambi za watu.


upendo

Ufafanuzi

Kumpenda mtu mwingine ni kumjali huyo mtu na kufanya vitu vitakavyo msaidia. Kuna maana tofauti za "upendo" ambazo lugha zingine zinawezakueleza kwa kutumia maneno tofauti:

  1. Aina ya upendo utokao kwa Mungu unalenga kwa ajili ya mema ya wengine, hata kama hayamnufaishi mtu anayependa. Aina hii ya upendo inawajali watu bila kujali wanachokifanya. Mungu mwenyewe ni upendo na ndiye chanzo cha upendo wa kweli.

Yesu alionesha aina hii ya upendo kwa kujitolea maisha yake kama sadak ili kutuokoa kutoka kwenye dhambi na mauti. Aliwafundisha pia wafuasi wake kuwapenda wengine kwa kujitolea. Watu wanapowapenda wengine na aina hii ya upendo, inahusisha matendo yanayoonesha kuwa mtu anafikiria yale yatakomsaidia mtu mwingine kufanikiwa. Aina hii ya upendo inahusisha zaidi kusamehe wengine. Katika ULB, neno "upendo" linamaanisha aina hiiya upendo wa kujitoa, isipokuwa noti ya tafsiri iashirie maana tofauti.

  1. Neno jingine katika Agano Jipya linamaanisha upendo wa kindugu au upendo kwa ajili ya rafiki au mwana familia.

Neno hili linamaanisha upendo wa asili wa binadamu kati ya marafiki na ndugu. Inawezekana kutumika katika mazingira kama, "Wanapenda kukaa kwenye viti muhimu katika sherehe." Hii inamaanisha "wanatamani sana" kufanya hivyo.

  1. Neno "upendo" linaweza pia kumaanisha upendo wa kimapenzi kati ya mwanamme na mwanamke.
  2. Katika hali ya kimithali, "Yakobo nimempenda, lakini Esau nimemchukia", neno "mpenda" linamaanisha Mungu kumchagua Yakobo kuwa katika mahusiano ya maagano na yeye. Hii inaweza pia kutafsiriwa kama "kuchaguliwa." Ingawa Esau alibarikiwa pia na Mungu, hakupewa heshima ya kuwa katika maagano. Neno "kuchukia" linatumika kimithali hapa kumaanisha "kukataliwa" au "kutokuchaguliwa."

ushirika

Ufafanuzi

Kwa ujumla, msemo "ushirika" ina maana ya muingiliano wa kirafiki kati ya wanajumuiya wa kundi la watu ambao huwa na upendeleo na mambo ya kufanana.

Katika Biblia, msemo "ushirika" mara kwa mara humaanisha umoja wa waumini katika Kristo.

Ushirika wa Kikristo na uhusiano ambao waumini wanao baina yao kupitia uhusiano wao na Kristo na Roho Mtakatifu.

Wakristo wa awali walionyesha ushirika wao kwa kusikiliza mafundisho ya Neno la Mungu na kuomba pamoja, katika kugawa vitu vyao, na kula milo pamoja.

Wakristo pia wana ushirika na Mungu kupitia imani ndani ya Yesu na kifo chake cha kujitolea cha msalabani ambacho kilitoa mpaka kati ya Mungu na watu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia za kutafsiri "ushirika" zinaweza kujumuisha "kugawana pamoja" au "uhusiano" au "umoja" au "jamii ya Kikristo"


ushuhuda, shuhudia

Ufafanuzi

Maneno, "ushuhuda" na "shuhudia" yanaeleza kutamka tamko kuhusu kitu ambacho mtu anajua kuwa ni kweli.


utauwa, utauwa

Ufafanuzi

Msemo "utauwa" unatumika kumwelezea mtu ambaye hufanya matendo kwa njia ambayo humheshimu Mungu na kuonyesha jinsi Mungu alivyo. "Utauwa" ni sifa ya tabia ya kumheshimu Mungu kwa kufanya mapenzi yake.

Mtu ambaye ana tabia ya kiutauwa ataonyesha matunda ya Roho Mtakatifu, kama vile upendo, furaha, amani, uvumilivu, upole na kiasi.

Sifa ya utauwa inaonyesha ya kwamba mtu ana Roho Mtakatifu na anamtii.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "watauwa" unaweza kutafsiriwa kama "watu wenye utauwa" au "watu ambao wanamtii Mungu"


utawala

Ufafanuzi

Msemo wa "utawala" una maana ya nguvu, madaraka, au mamlaka juu ya watu, wanyama, au nchi.

Yesu Kristo anasemekana kuwa na utawala juu ya nchi yote, kama nabii, kuhani na mfalme.

Utawala wa Shetani umeshashindwa milele na kifo cha Yesu Kristo juu ya msalaba.

Katika uumbaji, Mungu alisema ya kwamba mtu anatakiwa kuwa na utawala juu ya samaki, ndege, na viumbe wote juu ya nchi.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kutegemea na muktadha, njia zingine za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha "mamlaka" au "nguvu" au "madaraka".

Msemo "kuwa na utawala juu ya" unaweza kutafsiriwa kama "tawala juu ya" au "simamia".


utukufu, fahari

Ufafanuzi

Kwa ujumla, msemo "utukufu" una maana ya heshima, fahari, na ukuu wa hali ya juu sana. Kitu chochote ambacho kina utukufu kinasemekana kuwa na "fahari".

Mara nyingi, "utukufu" ina maana ya kitu chenye thamani kubwa na umuhimu. Katika muktadha zingine inawasilisha ufahari, mwanga, au hukumu.

Kwa mfano, msemo "utukufu wa wafugaji" una maana ya malisho yaliyostawi sana ambapo kondoo wao walikuwa na nyasi nyingi za kula.

Utukufu haswa hutumika kumfafanua Mungu, ambay ana ufahari zaidi ya yeyote au chochote katika ulimwengu. Kila kitu katika tabia yake huonyesha utukufu na ufahari wake.

Msemo "kutukuzwa na" una maana ya kujidai juu ya au kujivunia na kitu.


Uzinzi, zinaa, mzinifu, mzinzi

Ufafanuzi

Neno "uzinzi" hii ni dhambi ambayo inahusisha mwanandoa ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye sio mwenza wake.


vuka mpaka, kosa

Ufafanuzi

Maneno "vuka mpaka" na "kosa" ina eleza kuvunja amri, sheria.


Waebrania

Ufafanuzi

'Waebrania' walikuwa ni watu wa uzao wa Ibrahimu kupitia kwa Isaka na Yakobo. Ibrahimu ni mtu wa kwanza kuitwa 'mwebrania' katika Biblia. Neno 'kiebrania' linarejelea pia lugha ambayo waebrania wanaongea. Agano la kale liliandikwa kwa lugha ya Kiebrania. Katika sehemu mbalimbali za Biblia, Waebrania waliitwa 'Wayahudi,' au 'Waisraeli' Ni vizuri kutunza maneno yote matatu katika muktadha wake, kwa kuwa majina yote matatu yanazungumzia kundi moja la watu.


Wakfu

Ufafanuzi

Kuweka wakfu ni kutenga kitu fulani au watu ili wamtumikie Mungu. Kitu au vitu vinavyowekwa wakfu ni vitakatifu na vinatengwa kwa ajili ya Mungu.


wale kumi na mbili, wale kumi na moja

Ufafanuzi

Neno "wale kumi na mbili" la husu wanaume kumi na mbili Yesu aliyo wachagua kuwa wanafunzi wake wa karibu. Baada ya Yuda kujiua, waliitwa "wale kumi na moja."


wana wa Mungu

Ufafanuzi

Jina, "wana wa Mungu" ni msemo wa mfano wenye maana kadhaa.


watakatifu

Ufafanuzi

Neno "watakatifu" lina maana ya halisi ya "waliyo wasafi" na kueleza waamini wa Yesu.


Watoto, mtoto

Ufafanuzi

Katika Biblia mtoto limetumika kwa namna ya jumla kuelezea mtu ambaye ni mdogo kwa umri. Watoto ni wingi wa neno mtoto.


Watu wa Mungu, watu wangu

Ufafanuzi

"Watu wa Mungu" ni watu ambao Mungu aliwaita toka duniami ili wawe na mahusiano ya kipekee naye.


wema, uzuri

Ufafanuzi

Neno "uzuri" una maana nyingi kutegemea na muktadha. Lugha nyingi hutumia maneno tofauti kutafsiri maana hizi tofauti.

Kwa ujumla, kitu ni kizuri kama kinalingana na tabia ya Mungu, kusudi na mapenzi.

Kitu ambacho ni "kizuri" kinaweza kufurahisha, bora, msaada, kinachofaa, chenye manufaa, au sahihi kimaadili.

Ardhi ambayo ni "nzuri" inaweza kuitwa "yenye rutuba" au "yenye kuzaa".

Zao "zuri" linaweza kuwa zao "la wingi".

Mtu anaweza kuwa "mzuri" katika kile afanyacho kama ana ujuzi katika kazi yao, yaani "mkulima mzuri".

Katika Biblia, maana ya jumla ya "nzuri" mara nyingi hutofautishwa na "uovu".

Msemo "wema" mara nyingi humaanisha kuwa mzuri kimaadili kwa kutoa mambo mazuri na yenye manufaa. Inaweza kumaanisha utimilifu wake wa kimaadili.


wito, kuita, ita

Ufafanuzi

wito, kuita ni kitendo cha kusema kitu kwa nguvu kwa mtu ambaye hayuko karibu. Pia kuna maana mbali mbali kama


wivu

Ufafanuzi

Neno "wivu" inaashiria hamu kubwa ya kulinda usafi wa uhusiano. Inaweza pia kumaanisha hamu kubwa ya kumili kitu au mtu.

Msemo huu mara nyingi unatumika kuelezea hisia ya hasira ambayo mtu anayo juu ya mwenzi wake ambaye amekuwa sio mwaminifu katika ndoa yao. Inapotumika katika Biblia, neno hili huwa humaanisha hamu kubwa ya Mungu kwa watu wake kubaki watakatifu na kutochafuliwa na dhambi. Mungu ana "wivu" kwa ajili ya jina lake, kwamba litunzwe kwa utukufu na heshima. Maana nyingine ya wivu inahusisha kuwa na hasira kwa kuwa mtu mwingine ana mafanikio au ana umaarufu zaidi. Hii ina maana ya kukaribiana na neno "husuda."


woe

Ufafanuzi

Ole ni hisia za dhiki kubwa. Pia inatupa onyo kuwa mtu fulani atapata shida kubwa.


woga, hofu, hofu ya Yahwe

Ufafanuzi

Msemo "woga" au "hofu" ina maana ya hisia zisizo nzuri mtu huwa nazo ambapo kuna tishio la kudhuriwa kwake au kwa wengine.

Msemo "hofu" unaweza kumaanisha heshima kubwa na hofu mtu huwa nayo kwa mamlaka.

Msemo "hofu ya Yahwe" na misemo ya kufanana "hofu ya Mungu" an "hofu ya Bwana" ina maana ya kumheshimu sana Mungu na konyesha heshima kwa kumtii yeye. Hofu hii inahamasishwa kwa kujua ya kwamba Mungu ni mtakatifu na anachukia dhambi.

Biblia inafundisha ya kwamba mtu anayemwogopa Yahwe atakuwa na hekima.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "kuwa na hofu" kunaweza kutafsiriwa kama "kuogopa" au "kuheshimu sana" au "kuhofu" au " kuwa na hofu ya"

Msemo "woga" inaweza kutafsiriwa kama "kuogopa".

Sentensi, "Hofu ya Mungu ilianguka juu yao wote" inaweza kutafsiriwa kama, "Ghafla wote wakapatwa na hofu kuu na heshima kwa Mungu" au "Mara ghafla wote wakahisi kushangazwa sana na kumhofu Mungu sana" au "Wakati huo huo, wote wakapatwa na hofu ya Mungu"


Yaweh

Ufafanuzi

Yaweh ni jina la Mungu alilolithihirisha alipozungumza na Musa katika kichaka kinachowaka moto.


Yesu, Yesu Kristo, Kristo Yesu

Ufafanuzi

Yesu ni mwana wa Mungu. Jina "Yesu" linamaanisha, "Yahwe anaokoa." Neno "Kristo" ni jina linalomaanisha "mtiwa mafuta" na ni jina jingine la Masihi.

Majina mawili mara nyingi yanaunganishwa kama "Yesu Kristo" au "Kristo Yesu." Majina haya yanasisitiza kuwa mwana wa Mungu ndiye Masihi aliyekuja kuwaokoa watu kutoadhibiwa milele kwa dhambi zao. Katika njia za kimiujiza, Roho Mtakatifu alisababisha mwana wa milele wa Mungu kuzaliwa kama binadamu. Wazazi wake wa duniani waliambiwa na malaika kumuita "Yesu" kwa sababu alikusudiwa kuwaokoa watu kutoka katika dhambi zao. Yesu alifanya miujiza mingi iliyoonesha kuwa yeye ni Mungu na ni Kristo, au Masihi.


Zaburi

Ufafanuzi

Zaburi ni nyimbo takatifu ambazo zipo kwenye mfumo wa ushairi zilizoandikwa ili ziimbwe.


zawadi

Ufafanuzi

Msemo "zawadi" una maana ya kitu chochote ambacho hupewa au kutolvwa kwa mtu. Zawadi inatolewa bila matarajio ya kurudishiwa kitu chochote.

Pesa, chakula, mavazi, au vitu vingine zitolewazo kwa watu maskini zinaitwa "zawadi".

Katika Biblia, sadaka itolewayo kwa Mungu pia hujulikana kama zawadi.

Zawadi ya wokovu ni kitu ambacho Mungu anatupatia kupitia imani kwa Yesu.

Katika Agano Jipya, msemo "zawadi" pia hutumika kumaanisha uwezo maalumu wa kiroho ambao Mungu hutoa kwa Wakristo wote kutumikia watu wengine.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo wa jumla wa "zawadi" unaweza kutafsiriwa na neno au msemo ambao una maana ya "kitu ambacho kinatolewa".

Katika muktadha wa mtu kuwa na zawadi au uwezo maalumu ambao unatoka kwa Mungu, msemo "zawadi kutoka kwa Roho" unaweza kutafsiriwa kama "uwezo wa kiroho" au "uwezo maalumu kutoka kwa Roho Mtakatifu" au "kipaji maalumu cha kiroho ambacho Mungu ametoa"