Other

Adui

Ufafanuzi

"Adui" ni mtu au kundi lililo kinyume na mtu au kitu fulani.


agano jipya

Ufafanuzi

Neno "agano jipya" la husu kujitolea au makubaliano Mungu aliyo fanya na watu wake kupitia dhabihu ya Mwanae, Yesu.


agizo

Ufafanuzi

Agizo ni sharti au sheria ya hadhara inayo toa amri au maelekezo ya watu kufuata. Hili neno lina maana sawa na "kisimika"


Ahadi

Ufafanuzi

"Ahadi" hii ni ya kuweka matumaini ya kufanya kitu au kutoa kitu.


aibisha, ya kuaibisha

Ufafanuzi

Msemo wa "aibisha" una maana ya kufanya kitu ambacho si cha heshima kwa mtu. Hii inaweza pia kumsababishia mtu huyo aibu au fedheha.

Msemo "ya kuaibisha" inaelezea tendo ambalo ni la aibu au litasababisha mtu kupungukiwa na sifa.

Mara nyingine "kuabisha" inatumika kumaanisha vyombo ambavyo havina kazi kwa jambo lolote muhimu.

Watoto wanaamuriwa kuwaheshimu na kuwatii wazazi wao. Pale ambapo watoto hawatii, wanakuwa hawaheshimu wazazi wao. Wanawafanya wazazi wao kwa njia ambayo haiwapi heshima kwao.

Waisraeli walipunguza sifa kwa Yahwe walipoabudu miungu ya uongo na kutenda mwenendo muovu.

Wayahudi hawakumheshimu Yesu kwa kusema ya kwamba alikuwa amepagawa na pepo.

Hii inaweza kutafsiriwa kama "kutoheshimu" au "kutenda bila heshima.

Nomino ya "kutoheshimu" inaweza kutafsiriwa kama "kutoheshimu" au "kupotea kwa sifa".

Kutegemea na muktadha, "ya kuaibisha" inaweza kutafsiriwa kama "siyo na heshima" au "ya aibu" au "haifai" au "haina thamani".


aibu, fedhehesha

Ufafanuzi

Msemo "aibu" una maana ya kupotea kwa utukufu na heshima.

Mtu anapofanya jambo la dhambi, inaweza kumsababisha awe katika hali ya aibu au kupoteza heshima.

Msemo "fedhehesha" unatumika kuelezea tendo la dhambi au mtu aliyeifanya..

Mara nyingine mtu anayefanya mambo mema anatendewa kwa njia ambayo inamsababishia mtu fedheha au aibu.

Kwa mfano, Yesu alipouwawa msalabani, hii ilikuwa njia ya fedheha kufa. Yesu hakufanya jambo lolote baya kustahili fedheha hii.

Njia za kutafsiri "fedheha" zinaweza kujumuisha "aibu" au "kutokuwa na heshima.

Njia za kutafsiri "fedhehesha" zinaweza kujumuisha "aibu" au kutokuwa na heshima.


aina

Ufafanuzi

Neno "aina" linamaanisha makundi ya vitu vilivyoungana kwa kugawana tabia.

Katika Biblia, usemi huu unatumika bayana kumaanisha aina tofauti za mimea na wanyama ambao Mungu alivyotengeza alipoumba ulimwengu. Mara nyingi kuna tofauti nyingi za spishi katika kila "aina." Kwa mfano, farasi, punda milia, na punda zote ni sehemu ya "aina" moja lakini ni spishi tofauti. Kitu kikuu kinachotofautisha kila "aina" kama kundi tofauti ni kwamba kila mmoja wa hilo kundi anaweza kuzaa zaidi wa "aina" hiyo. Viumbe wa aina tofauti hawawezi kufanya hivyo pamoja.


Amani

Ufafanuzi

Amani ni kitendo cha kutokuwa na migogoro au hofu. Mtu mwenye amani anahisi shwari na ana uhakika wa kuwa salama.


amri

Ufafanuzi

Amri ni tamko au sheria ambayo inatolewa kwa umma kwa watu wote.

Sheria za Mungu pia zinajulikana kama makataa, maagizo au amri.

Kama sheria na amri, makataa lazima yanapaswa kufuatwa.

Mfano wa makataa ya mtawala wa kibinadamu ulikuwa ni tangazo la Kaisari Augusto ya kwamba kila mmoja aliyeishi katika milki ya Roma alipaswa kurudi nyumbani kwake ili ahesabiwe katika sensa.

Kutoa amri juu ya jambo ina maana ya kutoa amri ambayo ilikuwa lazima kuitii. Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kuamuru" au "kuamrisha" au "kutaka rasmi" au "kuweka sheria kwa umma".

Jambo linalofanywa kuwa "amri" kufanyika ina maana ya kwamba "lazima ifanyike" au "imeamuliwa na haitabadilishwa" au "kutamkwa kwa uhakika ya kuwa itafanyika"


amri

Ufafanuzi

Amri ni sheria maalumu iliyo andikwa inayo toa muongozo watu kuishi.


Amri kumi

Ufafanuzi

"Amri Kumi" zilikuwa amri ambazo Mungu alimpa Musa Mlima Sinai wakati Waisraeli waliishi jangwani wakiwa njiani kwenda nchi ya Kanani. Mungu aliandika hizi amri kwenye mawe makubwa mawili.


Angalia, Mlinzi

Ufafanuzi

"Angalia" inamaanisha kuwa kutazama kitu kwa ukaribu na kwa makini. "Mlinzi" ni mtu ambaye kazi yake ni kuulinda mji kwa kuangalia kwa makini vyote vinavyomzunguka kama kuna hatari yoyote kwa watu wa mji ule.


angika au nyonga

Ufafanuzi

Neno hili nyonga au angika lina maana ya ninginiza au tundika kitu au mtu. kifo cha kunyongwa au kujinyonga hufanyika kwa kutumia kamba ambayo mtu humfungwa shingoni na kumning'niza kwa kitu kilicho juu kama vile mti. Yuda alijiua mwenyewe kwa kujinyonga. Kifo cha Yesu kwa kuangikwa kwenye msalaba wa mbao kilifanyika kwa utofauti: askari walimtundika Yesu kwa kumpigilia misumali miguuni na mikononi katika msalaba. kuangika au kunyonga mtu mara zote ni njia ya kumwua mtu kwa kumnyonga kwa kutumia kamba inayofungwa shingoni mwa mtu.


Asali, sega la asali

Ufafanuzi

Asali ni kimiminika kitamu kinachotengenezwa na nyuki kutokana na maua. Sega ni fremu ya nta ambayo nyuki hutumia kutunzia asali. Asali inaweza kuwa na rangi ya njano au kikahawia kutegemea na aina. Asali yaweza kupatikana mstuni hasa katika mashimo ya miti au mahali popote ambapo nyuki zaweza kuweka makao. Watu pia hutunza asali katika mizinga ili kuzalisha asali za kula au kuuza, lakini huenda asali inayotajwa kwenye Biblia ni asali ya msituni. Biblia inawataja watu watatu walioishi kwa kula asali, watu hawa ni Yonathani, Samsoni na Yohana Mbatizaji. Neno hili 'asali' hutumika pia kimfano kumaanisha kitu kitamu au kitu cha kustarehesha. Mfano, Maneno na sheria za Mungu husemwa kuwa ni tamu sana kuliko asali. Wakati mwingine maneno ya mtu yanaweza kusemwa kuwa ni matamu kama asali, lakini matokeo yake huwa ni udanganyifu na kuwaumiza watu wengine.


asiye amini, kuto amini

Ufafanuzi

Neno "kuto amini" la eleza kuto kuwa na imani ya kitu au mtu.


Balozi, mwakilishi

Ufafanuzi

Balozi ni mtu aliyechaguliwa rasmi kuwakilisha nchi yake katika mataifa ya kigeni. Mara nyingine hutafsiriwa kama mwakilishi.


barua, waraka

Ufafanuzi

Barua ni ujumbe wa kuandikwa unaotumwa kwa mtu au kundi la watu ambaokwaida wako mbali kutoka kwa mwandishi. Waraka ni barua maalum, mara nyingi huandikwa kwa njia rasmi, kwa kusudi maalum, kama kufundisha.

Katika nyakati za Agano Jipya, waraka na aina zingine za barua ziliandikwa kwenye kartasi zilizotengenezwa kwa ngozi ya wanyama au kwenye karatasi za mafunjo ilitengenezwa kutoka kwenye ufumwele wa mimea. Nyaraka za Agano Jipya kutoka kwa Paulo, Yohana, Yakobo, Yuda na Petro ni barua za maelekezo walizoandika kuwatia moyo, kuwasihi, na kuwafundishia Wakristo wa kwanza katika miji tofauti katika ufalme wa Rumi. Njia za kutafsiri hili neno ni pamoja na, "ujumbe wa kuandikwa" au " maneno yalioandikwa" au "maandishi."


Bibi harusi

Ufafanuzi

Bibi harusi ni mwanamke ambaye katika sherehe ya harusi anaolewa kwa mmewe, ambaye ni bwana harusi.


Bikira

Ufafanuzi

Bikira ni mwanamke ambaye hajawahi kuwa na mahusiano ya ngono.


Bure, ubatili

Ufafanuzi

Neno "bure" linaelezea kitu ambacho hakina maana au hakifai. Vitu vilivyo bure ni vitu tupu au vitu visivyo na maana.


Busara

Ufafanuzi

Neno "busara" humuelezea mtu anayefikiri kwa makini kuhusu matendo yake na kufanya maamuzi ya hekima.


Busu

Ufafanuzi

Busu ni tendo ambalo mtu mmoja anaweka mdomo wake juu ya mdomo wa mwingine au uso. Msemo huu unaweza pia kutumika kitamathali.

Tamaduni zingine hubusiana kwenye shavu kama ishara ya salamu au kuaga. Busu linaweza kupitisha ujumbe wa upendo mkubwa kati ya watu wawili, kama mme na mke. Usemi "kumbusu mtu kwaheri" inamaanisha kumuagamtu kwa busu. Wakati mwingine neno "busu" linatumika kumaanisha "kusema kwaheri kwa." Wakati Elisha aliposema kwa Eliya, "Niache niende kumbusu baba na mama yangu," alitaka kuwaaga wazazi wake kabla yakuwaacha na kumfuata Eliya.


Bwana

Ufafanuzi

Neno "Bwana" linamaanisha mtu anayemiliki na mwenye mamlaka juu ya watu wengine. Inapokuwa na herufi kubwa, ni jina linalomaanisha Mungu. (Noti hata hivyo inapotumika kama njia ya kumtambua mtu mwanzo mwa sentesi inaweza kuwa na herufi kubwa na kuwa na maana ya "mkuu.")

Katika Agano la Kale, msemo huu pia unatumika maneno kama, "Bwana Mungu Mkuu" au "Bwana Yahwe" au "Yahwe Bwana wetu." Katika Agano Jipya, mitume walitumia neno hili katika misemo kama, "Bwana Yesu" na "Bwana Yesu Kristo," illiyoonyesha kuwa Yesu ni Mungu. Neno "Bwana" katika Agano Jipya pia linatumika peke yake kama njia ya moja kwa moja ya kumtambua Mungu, hasa katika nukuu za kutoka Agano la Kale. Kwa mfano, maandishi ya Agano la Kale ya, "Amebarikiwa ajaye kwa jina la Yahwe" na Agano Jipya lina, "Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana." Katika ULB na UDB, jina "Bwana" linatumika tu kutafsiri maneno halisi ya Kihebrania na Kigriki yanayomaanisha "Bwana." Halitumiki kama tafsiri ya jina la Mungu (Yahwe), kama inavyofanywa na tafsiri zingine.


Bwana harusi

Ufafanuzi

Bwana harusi ni mtu anayemwoa bibi arusi katika sherehe ya harusi.


chafu

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "chafu" utumika kama fumbo kueleza vitu ambavyo Mungu alitangaza sio sahihi kwa watu wake kugusa,kula, au kutoa dhabihu.


chemchem, kisima

Ufafanuzi

Msemo wa "chemchem" na "kisima" mara kwa mara una maana ya kiasi kikubwa cha maji ambacho kinatiririka kiasili kutoka kwenye ardhi.

Maneno haya yanatumika kitamathali katika Biblia kumaanisha baraka inayotiririka kutoka kwa Mungu au kumaanisha kitu ambacho kinasafisha au kutakasa.

Katika muda wa sasa, chemchem mara nyingi ni chombo kilichoundwa na mtu ambacho kina maji yakitiririka kutoka kwake, kama vile chemchem ya maji ya kunywa. Hakikisha ya kwamba tafsiri ya msemo huu una maana ya chanzo cha asili ya maji yanayotiririka.

Fananisha tafsiri ya msemo huu na jinsi msemo "mafuriko" unavyotafsiriwa.


chinja, chinjwa

Ufafanuzi

Neno "chinja" lina maana ya kuua mtu au mnyama. Mara nyingi ina maana ya kuua kwa vita au vurugu.


Chochea

Ufafanuzi

Neno "kuchochea" linamaanisha kumsababisha mtu apate hisia hasi.


chui

Ufafanuzi

Chui ni mnyama pori mkubwa kama paka, mwenye rangi ya kahawa na madoa meusi.

Chui ni aina ya mnyama anayeshika wanyama wengine na kuwala. Katika Biblia, ughafla wa maafa unalinganishwa na chui anaye shambulia mawindo yake ghafla. Nabii Danieli na mtume Yohana wanazungumzia maono ambayo waliona mnyama aliyefanana na chui.


chukiza, chukia

Ufafanuzi

Msemo "chukiza" unaelezea jambo ambalo linapaswa kutopendwa na kukataliwa. "Kuchukia" kitu ina maan ya kutokipenda kabisa.

Mara nyingi Biblia huzungumzia kuhusu kuchukia uovu. Hii ina maana kuchukia uovu na kuukataa.

Mungu alitumia neno "chukiza" kuelezea matendo maovu ya wale waliomwabudu miungu ya uongo.

Waisraeli waliamriwa "kuchukia" matendo ya dhambi, na kinyume na maadili ambayo baadhi ya makundi ya watu majirani waliyafanya.

Mungu aliyataja matendo yote ya uasherati kuwa "chukizo".

Uaguzi, uchawi, na sadaka za mtoto yote yalikuwa "chukizo" kwa Mungu.

Msemo "chukizo" unaweza kutafsiriwa kama "uovu mbaya" au "inayochukiza" au "inayostahili kukataliwa".

Inapotumika na kiumbe takatifu "chukizo kwa" waovu, hii inaweza kutafsiriwa kama "kuchukuliwa kutotamanika kwa" au "kutokuwa na ladha" au "kukataliwa na"

Mungu aliwaambia Waisraeli "kuchukia" aina kadhaa ya wanyama ambao Mungu alitamka kuwa "wachafu" na kutofaa kwa chakula. Hii inaweza kutafsiriwa kama "kuchukia kwa uzito" au "kukataa" au "kuchukua kama kutokubalika".


dada

Ufafanuzi

Dada ni mtu wa jinsi ya kike anaye shiriki wastani wa mzazi mmoja na mtu mwingine.


desturi

Ufafanuzi

Neno "desturi" la eleza tamaduni na mapokeo yaliyo tunzwa kwa muda na yanayo pokelewa na vizazi vijavyo.


dhabihu, sadaka

Ufafanuzi

Katika Biblia, maneno "dhabihu" na "sadaka" ya husu zawadi maalumu anazopewa Mungu kama kitendo cha kumuabudu. Watu pia walitoa sadaka kwa miungu ya uongo.


dhahabu

Ufafanuzi

Dhahabu ni chuma cha manjano, cha ubora wa juu sana kinachotumika kutengeneza vito na vyombo vya dini. Ilikuwa chuma ya thamani zaidi katika kipindi cha zamani.

Katika kipindi cha Biblia, aina nyingi tofauti ya vyombo vilitengezwa kwa dhahabu ngumu au kufunikwa na safu nyembamba ya dhahabu.

Vyombo hivi vilijumuisha heleni na vito vingine, sanamu, madhabahu, na vyombo vingine vilivyotumika katika tabenakulo au hekalu, kama vile sanduku la agano.

Katika Agano la Kale, dhahabu ilitumika kama njia ya kubadilishana katika kununua na kuuza. Ilipimwa juu ya mizani kupata thamani yake.

Baadaye, dhahabu na vyuma vingine kama vile fedha vilitumika kutengeneza sarafu kutumiwa kununua na kuuza.

Pale inapomaanisha kitu ambacho sio dhahabu ngumu, lakini ina safu nyembamba tu ya dhahabu, msemo "ya dhahabu" au "kufunikwa kwa dhahabu" inaweza kutumika.

Mara nyingi chombo kinaelezewa kama "rangi ya dhahabu" ambayo ina maana ina rangi ya njano ya dhahabu, lakini haijatengenezwa kwa dhahabu.


dhalimu, kwa dhalimu, udhalimu

Ufafanuzi

Maneno "dhalimu" na "kwa dhalimu" yanaeleza kutendea watu pasipo haki, na mara nyingi, namna ya kudhuru.


Dharau, kudharauliwa

Ufafanuzi

Dharau ni kitendo cha kutokuheshimu kinachooneshwa kwa mtu au kitu. Kitu kisichoheshimiwa kinaitwa kilichodharauliwa.


Dhifa

Ufafanuzi

Dhifa ni sherehe maalumu ya mlo ambayo kwa kawaida inahusisha aina tofauti ya vyakula.


dhihaki

Ufafanuzi

Neno kudhihaki ni kumtania mtu, kwa namna mbaya.


dhiki

Ufafanuzi

Neno "dhiki" la husu kipindi cha ugumu, mateso, na msongo wa mawazo.


Divai, kiriba, divai mpya

Ufafanuzi

Katika nyakati za Biblia "divai" ni kinywaji kilichotengenezwa na maji ya matunda yanayoitwa zabibu. Divai ilihifadhiwa kwenye viriba ambayo ni vyombo vilivyotengenezwa kwa ngozi ya wanyama.


Dubu

Ufafanuzi

Dubu ni mnyama mkali mkubwa mwenye miguu minne na ana manyoa meusi, meno na makucha makali. Dubu walikuwa wamezoeleka katika Israeli nyakati za Biblia.


dunia, kidunia

Ufafanuzi

Msemo "dunia" una maana ya dunia ambayo wanadamu wanaishi, pamoja na kila aina ya viumbe hai.

"Dunia" pia inaweza kumaanisha ardhi au udongo ambayo hufunika nchi.

Msemo huu mara kwa mara hutumika kitamathali kumaanisha watu wanaoishi juu ya dunia.

Misemo, "acha dunia iwe na furaha" na "Atahukumu dunia" ni mifano ya matumizi ya tamathali ya msemo huu.

Msemo "kidunia" mara kwa mara humaanisha vitu vya kimwili kinyume na vitu vya kiroho.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao lugha ya taifa hutumia kumaanisha sayari ya dunia ambayo tunaishi.

Kulingana na muktadha, "dunia" pia inaweza kutafsiriwa kama, "ulimwengu" au "ardhi" au "udongo".

Unapotumika kitamathali, "dunia" inaweza kutafsiriwa kama, "watu wa dunia" au "watu wanaoishi juu ya dunia" au "kila kitu juu ya dunia".

Njia za kutafsiri "kidunia" zinaweza kujumuisha, "kimwili" au "vitu vya dunia hii" au "vinavyoonekana".


elekeza, maelekezo

Ufafanuzi

Usemi "elekeza" na "maelekezo" yanamaanisha kutoka uongozo bayana ya nini cha kufanya.

"Kutoa maelekezo" inamaanisha kumuambia mtu bayana kitu anachotakiwa kufanya. Yesu alipowapa wanafunzi wake mikate na samaki kuwapa watu, aliwapa maelekezo bayana ya jinsi ya kuifanya. Kulingana na mazingira, neno "elekeza" inaweza kutafsiriwa kama "kumuambia" au "kuongoza" au "kufundisha" au "kutoa maelekezo kwa." Neno "maelekezo" inaweza kutafsiriwa kama "uongozo" au"ufafanuzi" au "kitu alichokuambia kufanya." Mungu akikupa maelekezo, huu usemi wakati mwingine unatafsiriwa kama "kuamuru" au "kuamrisha."


erevu

Ufafanuzi

Neno "erevu" la elezea mtu enye akili na mahiri, hususani katika mambo ya utendaji.


fagia

Ufafanuzi

Neno "fagia" mara nyingi ueleza maana pana, ya kuondoa kwa haraka uchafu kwa kutumia ufagio.


fahamu, ufahamu

Ufafanuzi

Neno "fahamu" lina maana ya kusikia ua kupokea taarifa na kuelewa ina maana gani.


Faida

Ufafanuzi

Kwa ujumla "faida" ni kitendo cha kupata kitu kizuri kwa kufanya jambo fulani au kitu fulani kizuri ambacho mtu anakipata. Kitu kina faida kwa mtu ikiwa kinaleta mambo mazuri au kinasaidia kuleta mambo mazuri kwa watu wengine.


familia

Ufafanuzi

Msemo "familia" una maana ya kundi la watu ambao wana uhusiano wa damu na mara nyingi hujumuisha baba, mama, na watoto wao. Mara kwa mara pia hujumuisha ndugu wengine kama babu na bibi, wajukuu, wajomba na shangazi.

Familia ya Kiebrania ilikuwa jamii ya kidini inayopitisha utamaduni kupitia ibaada na maagizo.

Mara kwa mara baba alikuwa mwenye mamlaka ya familia.

Familia pia inaweza kujumuisha watumishi, masuria, na hata wageni.

Baadhi ya lugha zina neno pana kama vile "ukoo" au "nyumba" ambayo litafaa zaidi kwa muktadha ambapo zaidi ya wazazi na watoto wanatajwa.

Msemo "familia" pia unatumika kumaanisha watu ambao wana uhusiano wa kiroho, watu kama hawa ambao ni sehemu ya familia ya Mungu kwa sababu wanmwamini Yesu.


Faraja, mfariji

Ufafanuzi

Faraja ni kumsaidia mtu anayeteseka kimwili au kihisia.


Farasi

Ufafanuzi

Farasi ni mnyama mkubwa mwenye miguu minne ambaye katika kipindi cha Biblia alitumiak katika kufanya kazi za shambani na katika usafirishaji. Baadhi ya farasi walitumika katika kuvuta gari, na wengine walipandwa na mpanda farasi binafsi. Farasi walivalishwa hatamu katika vichwa vyao ili waweze kuongozwa Katika Biblia, farasi walihesabiwa kama mali ya thamani, na kipimo cha utajiri, hasa hasa kwa ajili ya matumizi yake katika vita. Wanyama walikuwa wanafanana na farasi ni punda.


fedha

Ufafanuzi

Fedha ya ng'aa, ni ya chuma ya kijivu inayo tumika kufanya sarafu, mikufu, vyombo, na mapambo.


fedhehesha. fedheha

Ufafanuzi

Neno 'fedhehesha' lina maana ya kumfanya mtu aaibike au adhalilike. Hii ni kwasababu mara kwa mara hufanyika hadharani. Tendo la kumwaibisha mtu huitwa " fedheha." KIpindi ambacho Mungu humshusha mtu, humaanisha kwamba Mungu humfanya mtu apate mambo mabaya ili kumsaidia mtu aachane na kiburi. Hii ni tofauti na kumdhalilisha mtu, maana fedheha ni kitendo ambacho hufanywa ili kumuumiza mtu. Kumfedhehesha mtu yaweza kutafsiriwa kama 'kumwaibisha' au kumdhalilisha mtu. kuna njia nyingi za kutafsiri neno 'fedheha' kwa kutegemea na Muktadha. Maneno kama 'udhalilishaji' na aibu,''


filimbi, zumari

Ufafanuzi

Katika kipindi cha Biblia, zumari ilikuwa vyombo vya muziki iliyotengenezwa kwa mfupa au mbao na mashimo inayoruhusu sauti kutoka nje. Filimbi ilikuwa aina ya zumari.

Zumari nyingi ilikuwa na matete yaliyotengenezwa kutoka kwa nyasi nene ambayo hutikisika pale hewa inapopulizwa kwake.

Zumari bila matete mara kwa mara ilijulikana kama "filimbi".

Mfugaji alicheza filimbi kutuliza mifugo yao ya kondoo.

Zumari na filimbi ilitumika kucheza muziki wa huzuni na furaha.


Fimbo

Ufafanuzi

Fimbo hiki ni kifaa chembamba kama fimbo kinachotumika kwa njia mbali mbali.


fimbo ya kifalme

Ufafanuzi

Neno "fimbo ya kifalme" ina husu gongo zuri linalo shikiliwa na mtawala, kama mfalme.


fundisha, kufundisha, mwalimu, fundishwa

Ufafanuzi

Haya maneno "fundisha" na "kufundisha" yanaeleza kuambia watu wengine taarifa wasiyo ijua kabla. Mara nyingi maelezo utolewa rasmi au kwa utaratibu.


funga

Ufafanuzi

Msemo "kufunga" una maana ya kuacha kula chakula kwa kipindi fulani, kama vile siku moja au zaidi. Mara nyingi inajumulisha kutokunywa.

Kufunga kunaweza kusaidia watu kumlenga Mungu na kuomba bila kutolewa mawazo kwa kuandaa chakula na kula.

Yesu aliwalaani viongozi wa dini wa Kiyahudi kwa kufunga kwa sababu ambazo sio sahihi. Walifunga ili kwamba wengine wafikiri kuwa wao ni watakatifu.

Mara nyingi watu walifunga kwa sababu walikuwa na huzuni sana au majonzi juu ya jambo.

Kitenzi cha "kufunga" kinaweza kutafsiriwa kama "kujizuia kula" au "kutokula".

Nomino ya "funga" inaweza kutafsiriwa kama "muda wa kutokula" au "muda wa kujizuia na chakula"


funga

Ufafanuzi

Msemo "funga" una maana ya kufunga kitu kuzunguka kitu kingine. Mara kwa mara humaanisha kutumia mkanda kuzunguka kiuno kuweka kanzu au gwanda mahali pake.

Msemo wa kibliblia unaojulikana, "funga kiuno" una maana ya kuchomekea chini ya vazi ndani ya mkanda kuruhusu mtu kusogea kwa uhuru zaidi, mara nyingi kufanya kazi.

Msemo una maana ya kujiweka tayari kufanya kazi au kujiandaa kufanya kitu kigumu.

Msemo "funga kiuno" unaweza kutafsiriwa kutumia msemo katika lugha husika yenye maana moja. Au inaweza kutafsiriwa bila tamathali kama "jiandae kwa ajili ya tukio" au "jiandae"

Msemo "kufngwa na" inaweza kutafsiriwa kama "kuzungushwa na" au "kufungwa na".


Furaha

Ufafanuzi

"Furaha" ni jambo ambalo linamfurahisha mtu sana na kuleta furaha kubwa.

"Kufurahishwa" na jambo ina maana ya "kuwa na furaha" au "kufurahia juu ya" kitu.

Pale ambapo kitu kinakubalika sana au kupendeza kinasemekana kama "furahisha".

Kama furaha ya mtu ipo katika kitu ina maana ya kwamba anakifurahia sana.

Msemo wa, "furaha yangu ipo katika sheria ya Yahwe" inaweza kutafsiriwa kama, "sheria ya Yahwe inanipa furaha kubwa" au "Ninapenda kutii sheria za Yahwe" au "Nina furaha kutii amri za Yahwe".

Misemo "kufurahia" na "kuwa na furaha katika" inaweza kutafsiriwa kama "sifurahishwi kabisa na" au "sina furaha juu ya".

Msemo "kufurahishwa mwenyewe na" ina maana, "anafurahia kufanya" kitu au "ana furaha sana juu ya" kitu au mtu.

Msemo "hufurahia" una maana ya vitu ambavyo mtu hufurahia. Hii inaweza kutafsiriwa kama "starehe" au "vitu vinavyoleta furaha".

Msemo kama wa, "Ninafurahi kufanya mapenzi yako" unaweza kutafsiriwa kama, "Ninafurahi kufanya mapenzi yako" au "Nina furaha sana ninapokutii".


furaha, mwenye furaha

Ufafanuzi

Furaha ni hisia ya kupendezwa au kuridhika inayotoka kwa Mungu. Maana inayokaribiana, "mwenye furaha" inaelezea mtu anayejisikia vizuri sana na mwenye furaha nyingi.

Mtu anasikia furaha anapokua anahisi kuwa anachopitia ni chema sana. Mungu ndiye anayegawa furaha ya kweli kwa watu. Kuwa na furaha hakutegemei hali nzuri. Mungu anaweza kuwapa watu furaha hata kama vitu vigumu kabisa vinatokea katika maisha yao. Sehemu zingine zinaelezwa kama za furaha, kama nyumba na miji. Hii inamaanisha kuwa watu waiishio humo ni wenye furaha.


furahia sana, mwenye furaha

Ufafanuzi

Msemo "furahia sana" na "mwenye furaha" una maana ya kuwa na shangwe sana kwa sababu ya mafanikio au baraka maalumu.

"Kufurahia sana" kunajumuisha hisia za kushangilia jambo zuri.

Mtu anaweza kufurahia sana ndani ya wema wa Mungu.

Msemo "mwenye furaha" unaweza kujumuisha kuwa na kiburi ndani ya hisia za furaha juu ya mafanikio au utajiri.

Msemo "furaha sana" unaweza kutafsiriwa kama "kushangilia kwa furaha" au "kusifu na furaha kubwa".

Kulingana na muktadha, msemo "mwenye furaha" unaweza kutafsiriwa kama "kusifu kwa kishindo" au "kushangilia na sifaf binafsi" au "kiburi"


fuvu

Ufafanuzi

Neno "fuvu" la eleza kichwa cha mifupa kisicho na nyama cha mtu au mnyama


Gari

Ufafanuzi

Zamani za kale magari yalikuwa mepesi, yenye matairi mawili yalioendeshwa na farasi.


gavana, kutawala, mtawala, serikali

Ufafanuzi

"Gavana" ni mtu anayetawala mkoa, eneo au mahali. Neno "kutawala" lina maana ya koungoza au kusimamia watu.

Msemo "mtawala" ilikuwa jina mahususi kwa gavana aliyetawala juu ya mkoa wa Kirumi.

Katika kipindi cha Biblia, magavana waliteuliwa na mfalme au mfalme mkuu na walikuwa chini ya mamlaka yake.

"Serikali" inaundwa na viongozi wote ambao wanatawala nchi au ufalme fulani. Watawala hawa hutengeza sheria ambazo huongoza tabia ya wanachi il kwamba kuwepo na amani, ulinzi, na mafanikio kwa watu wato wa taifa hilo.


Gereza, mfungwa , jela

Ufafanuzi

Gereza nisehemu ambayo wahalifu huwekwa kama adhabu kwa uhalifu waliofanya. Mfungwa ni mtu anayewekwa gerezani.


geuka, geuka kando, geuka nyuma

Ufafanuzi

"Kugeuka" kuna maana ya kubadili mwelekeo wa mwili au kusababisha kitu kingine kubadilisha muelekeo.


Ghadhabu

Ufafanuzi

Ghadhabu ni hasira iliyopitiliza isiyoweza kuzuilika. Mtu anapokuwa na ghadhabu inamaana mtu anaonesha hasira yenye uharibifu.


Giza

Ufafanuzi

Msemo "giza" una maana ya kutokuwepo kwa nuru. Kuna maana kadhaa za kitamathali za msemo huu:

Kama sitiari, "giza" ina maana ya "uchafu" au "uovu" au "upofu wa kiroho".

Pia ina maana ya jambo lolote linalohusu dhambi au uharibifu wa maadili.

Msemo, "mamlaka ya giza" una maana ya kila kilicho kiovu na kinachotawaliwa na Shetani.

Msemo "giza" unaweza pia kutumika kama sitiari ya kifo.

Watu wasiomjua Mungu wanasemekana kuwa "wanaishi gizani", ambayo ina maana hawaelewi au hawatenda haki.

Mungu ni nuru (utakatifu) na giza (uovu) haliwezi kushinda nuru hiyo.

Mahali pa adhabu kwa wale wanaomkataa Mungu mara nyingi hujulikana kama "giza la nje".

Mapendekezo ya Tafsiri

Ni bora kutafsiri msemo huu kihalisia, kwa neno la lugha ya mradi ambalo lina maanisha kutokuwepo kwa nuru. Huu unaweza kuwa msemo wenye maana ya giza la chumba ambalo halina mwanga au wakati wa siku ambapo hakuna mwanga.

Kwa matumizi ya kitamathali, ni muhimu kuweka picha ya giza kwa kutofautisha na mwanga, kama njia ya kuelezea uovu na udanganyifu kulinganisha na wema na ukweli.

Kutegemea na muktadha, njia zingine za kutafsiri hili zaweza kuwa, "giza la usiku"


gongo

Ufafanuzi

Ngo ni fimbo ndefu ya mbao, utumika kama fimbo ya kutembelea.


gumia

Ufafanuzi

Msemo "gumia" una maana ya kutoa sauti ya chini, nzito ambayo inasababishwa na mateso ya kihisia au kimwili. Mara kwa mara gumia hutengenezwa bila maneno.

Mtu anaweza kugumia kwa sababu ya kuhisi majonzi.

Kugumia inaweza kusababishwa kwa kujisikia vibaya, mzigo wa kundamiza.

Njia zingine za kutafsiri "gumia" zinaweza kujumuisha "kutoa sauti ya chini ya maumivu" au "kulia kwa kulalamika".

Kama nomino, hii inaweza kutafsiriwa kama "kilio cha chini cha mateso" au "mnung'uniko wa chini wa maumivu"


hakimu

Ufafanuzi

Hakimu ni mtu anayeamua nini kiko sawa au la ukiwepo ugomvi kati ya watu, mara nyingi katika mambo yanayofungamana na sheria.

Katika Biblia, Mungu mara nyingi anatajwa kama hakimu kwa sababu yeye ndiye hakimu aliye kamili anayefanya maamuzi ya mwisho kuhusu nini kiko sawa au kisicho sawa. Baada ya watu wa Israeli kuingia nchi ya Kanaani na kabla hawajawa na wafalme wa kuwatawala, Mungu aliwapa viongozi waitwao "waamuzi" kuwaongoza nyakati za shida. Mara nyingi waamuzi hao walikuwa viongozi wa kijeshi waliowaokoa Waisraeli kwa kuwaangamiza maadui zao. Neno "hakimu" linaweza pia kuitwa "muamuzi" au "kiongozi" au "mkombozi" au "gavana," kutegemea na mazingira.


halali, ipasavyo, kinyume na sheria

Ufafanuzi

Msemo "halali" unamaanisha kitu kinachoruhusiwa kufanywa kulingana na sheria au mahitaji mengine. Kinyume cha hiki ni "kinyume na sheria" inyomaanisha "sio halali."

Katika Biblia, kama kitu kinasemwa kuwa "halali" inamaanisha inaruhusiwa na sheria ya kimaadili ya Mungu, au kwa sheria ya Musa au sheria zingine za Kiyahudi. Kitu ambacho "sio halali" "hakiruhusiwi" na sheria hizo. Kufanya kitu "ipasavyo" inamaanisha kuifanya "sawa" au "katika njia sahihi." Mambo mengi Wayahudi waliyoona ni halali au sio halali hayakuwa kwenye makubaliano na sheria za Mungu kuhusu kuwapenda wengine. Kulinga na mazingira, njia za kuafsiri "halali" ni pamoja na, "kuruhusu" au "kulingana na sheria ya Mungu" au "kufuatana na sheria zetu" au "sawa" au inafaa." Msemo "Je ni halali" inaweza pia kutafsiriwa kama "Je, sheria zetu zinaruhusu" au "Hilo ni jambo ambalo sheria zetu zinaruhusu?"


hali ya chini, kuwa chini

Ufafanuzi

Misemo "wa hali ya chini" na "kuwa chini" inamaanisha kuwa maskini auna hadhi ya chini. Usemi huu pia unaweza kuwa na maana ya kuwa mnyenyekevu.

Yesu alijinyenyekesha hadi nafasi ya chini ya kuwa binadamu na kuwatumikia wengine. Kuzaliwa kwake kulikuwa kwa hali ya chini kwa sababu alizaliwa mahali ambapo wanyama walitunzwa; sio katika nyumba ya kifalme. Kuwa na mtazamo wa chini ni kinyume na kuwa na majivuno. Njia za kutafsiri "hali ya chini" ni pamoja na , "unyenyekevu" au "hadhi ya chini" au "kutokua muhimu." Msemo "kuwa chini" unaweza pia kutafsiriwa kama "unyenyekevu" au "umuhimu mdogo."


Halmashauri

Ufafanuzi

Halmashauri ni kundi la watu wanaokutana kujadili, kutoa ushauri na kufanya maamuzi juu ya masuala ya muhimu.


Hamira, Chachu

Ufafanuzi

"Chachu" ni neno la jumla la kitu kinachosababisha unga wa mkate kuumuka. "Hamira" ni aina ya chachu.


Hasira

Ufafanuzi

"Kukasirika" au "kupata hasira" ina maana ya kutofurahishwa au kuhangaishwa juu ya jambo fulani au mtu fulani.


hati

Ufafanuzi

Zamani za kale, hati ilikuwa aina ya kitabu kilicho tengenezwa kwa karatasi ndefu ya mafunjo au ngozi.


haya, aibu

Ufafanuzi

Neno "haya" la husu hali ya maumivu ya kuumizwa kihisia kwa kuaibishwa kwasababu ya kitu cha fedheha ambacho yeye au mtu mwingine amefanya.


hema

Ufafanuzi

Hema ni hifadhi linalo hama lililo tengenezwa na uzi uliyo zungushiwa kwenye nguzo pamoja.


hema la kukutania

Ufafanuzi

Neno "hema la kukutania" la husu hema ambalo lilikuwa la muda mfupi Mungu alipo kutana na Musa kabla ya maskani kujengwa.


Heshima

Ufafanuzi

Heshima ni hisia za kumuheshimu mtu au kitu kwa hali ya juu.


hudumu, huduma

Ufafanuzi

Neno "hudumu" lina maana kufanya vitu kusaidia watu wengine. Linaweza pia maanisha "kuabudu."


huru, uhuru

Ufafanuzi

Msemo "huru" au "uhuru" una maana ya kutokuwa katika utumwa au aina yoyote ya kifungo.

Msemo "kumweka mtu huru" au "kumweka huru mtu" ina maana ya kutoa njia kwa mtu ili asiwe katika utumwa au kifungo.

Katika Biblia, misemo hii mara kwa mara hutumika kitamathali kumaanisha jinsi gani muamini katika Yesu hayupo chini ya nguvu ya dhambi.

Kuwa "huru" au "uhuru" inaweza kumaanisha kutohitajika kutii Sheria ya Musa, lakini badala yake kuwa huru kuishi kwa mafunzo na uongozi wa Roho Mtakatifu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "huru" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana ya "kutofungwa" au "kutokuwa katika utumwa" au "kutokuwa katika kifungo".

Msemo "ukuru" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana, "hali ya kuwa huru" au "hali ya kutokuwa mtumwa" au "kutofungwa".

Msemo "kuweka huru" unaweza kutafsiriwa kama "kusababisha kuwa huru" au "kukomboa mtu kutoka utumwani" au "kumwachia kutoka kifungoni".

Mtu ambaye "amewekwa huru" atakauwa "ameachiliwa" au "kutolewa kutoka" katika kifungo au utumwa.


iga, mwigaji

Ufafanuzi

Maneno "iga" na "mwigaji" yanamaanisha kumuiga mtu mwingine na kuigiza sawa na mtu huyu afanyavyo.

Wakristo wanafundishwa kumuiga Yesu Kristo kwa kumtii Mungu na kuwapenda wengine, kama Yesu alivyofanya. Mtume Paulo aliliambia kanisa la awali kumuiga yeye, kama yeye alivyomuiga Yesu.


Ikulu

Ufafanuzi

Neno "ikulu" linamaanisha jengo au nyumba ambayo mfalme aliishi pamoja na familia yake na watumishi wake.


Imeandikwa

Ufafanuzi

maneno haya "Kama ilivyoandikwa" au "kilichoandikwa" yametokea mara nyingi katika agano jipya na yameelezea amri au unabii ulioandikwa katika maandiko ya Kiebrania.


inua, inuka

Ufafanuzi

Inua, inua juu inamaana ya kuinua kitu juu au kukuweka juu.


jamaa wa karibu

Ufafanuzi

Usemi "jamaa wa karibu" unamaanisha ndugu wa damu wa mtu. Mara nyingi neno hili hutumika zaidi kumaanisha ndugu wa kiume.

Usemi huu unaweza kumaanisha ndugu wa karibu, kama vile mzazi au kaka, au kwa ndugu wa mbali zaidi, kama vile shangazi, mjomba au binamu. Katika Israeli ya zamani, kama mwanamme akifa, ndugu yake wa karibu wa kiume alitarajiwa kumuoa mjane wake, kutunza mali zake, na kusaidia kulibeba jina la familia yake. Ndugu huyu alikuwa anaitwa "jamaa mkombozi." Usemi unaweza pia kutafsiriwa kama, "ndugu" au "mwana familia."


jangwa, njika

Ufafanuzi

jangwa, au nyika, ni sehemu iliyokauka, isiyokuwa na mazao ambayo mimea na miti michache inaweza kuota pale.

Jangwa ni eneo la ardhi lenye tabia ya nchi ya ukavu na mimea na wanyama wachache.

Kwa sababu ya mazingira magumu, watu wachache sana wanaweza kuishi katika jangwa, kwa hiyo pia inajulikana kama "nyika".

"Nyika" inaleta maana ya sehemu iliyojitenga, ya kipekee mbali na watu.

Neno hili pia linaweza kutafsiriwa kama "sehemu ya jangwa" au "sehemu iliyojitenga" au "sehemu isiyokaliwa".


jasiri, ujasiri, ushujaa

Ufafanuzi

Maneno yote haya yanamaanisha kuwa na ujasiri na ushujaa kwa kuongea ukweli kuhusu jambo halali hata kama ni vigumu na hatari.


jikwaa

Ufafanuzi

Neno "jikwaa" lina maana ya "karibu kuanguka" wakati wakutembea au kukimbia. Kujikwaa juu ya kitu.


jirani

Ufafanuzi

Neno "jirani" mara kwa mara la mueleza mtu anaye ishi karibu. Pia yaweza kueleza kwa ujumla mtu anaye ishi katika jamii moja au kundi la watu.


jitu

Ufafanuzi

Jitu mara nyingi ilimaanisha mtu ambaye alikuwa na ukubwa usio wa kawaida wa urefu na nguvu.

Goliati, mwanajeshi wa Kifilisti aliyepigana na Daudi, aliitwa Daudi kwa sababu alikuwa mrefu sana, mkubwa, na mtu mwenye nguvu.

Wapelelezi wa Israeli waliotafiti nchi ya Kaanani walisema ya kwamba watu wanaoishi pale walikuwa kama majitu.


jiwe la kujikwaa

Ufafanuzi

Neno "jiwe la kijikwaa" la eleza kitu cha kimwili kinacho msababisha mtu kijikwaa na kuanguka.


joho

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "joho" uleza vazi lililo valiwa chini ya ngozi, chini nguo nyingine.


juma

Ufafanuzi

Neno "juma" kwa kawaida lamaanisha kipindi cha kuishia siku saba.


juu, juu sana

Ufafanuzi

Maneno " juu" na " juu sana" ni misemo inayo maanisha, "mbinguni."


kabila

Ufafanuzi

Kabila ni kundi la watu waliyo toka kwa babu mmoja.


kaburi

Ufafanuzi

Neno "kaburi" ni sehemu watu wanapo weka mwili wa mtu aliye kufa.


Kahaba

Ufafanuzi

"Kahaba" ni mtu anayefanya vitendo vya uzinzi kwa sababu ya pesa au ibada za kidini. Mara nyingi kahaba huwa mwanamke ila kuna wanaume pia.


kama, mfano

Ufafanuzi

Misemo "kama" na "mfano" inamaanisha kitu kuwa sawa au kufanana na kitu kingine.

Neno "kama" pia inatumika katika mithali zinazoitwa "mfanano" ambapo kitu kinalinganishwa na kitu kingine, kawaida huonyesha tabia zinazolingana. Kwa mfano, "nguo zake zinang'aa kama jua" na "sauti ilivuma kama ngurumo." "Kuwa kama" au "kusikika kama" au "kuonekana kama" kitu au mtu inamaana kuwa na sifa zinazofanana na kitu anacholinganishwa nacho au mtu anayelingishwa naye. Watu waliumbwa katika "mfano" wa Mungu. Inamaanisha wana sifa au tabia ambazo ni "kama" au "zizafanana" na sifa ambazo Mungu anazo, kama uwezo wakufikiri, kuhisi na kuwasiliana. Kuwa na "mfano" wa kitu au mtu inamaana kuwa na tabia zinazofanana na hicho kitu au mtu.


Kamanda, amri

Ufafanuzi

Kamanda ni kiongozi wa jeshimwenye jukumu la kuongoza kundi fulani la askari.


kamata

Ufafanuzi

Neno "kamata" la maanisha kuchukuwa au kumteka mtu au kitu kwa nguvu. Inaweza maanisha ya kumzidi nguvu au kumtawala mtu.


Kamili

Ufafanuzi

Katika Biblia neno kamili linamaana ya kukua katika maisha yetu ya Kikristo. Kukifanya kitu kuwa kamili ni kitendo cha kukifanyia kazi mpaka kikamilike bila dosari.


kanuni

Ufafanuzi

Neno "kanuni" lina maana ya "kufundisha". Mara nyingi lina maana ya mafunzo ya dini.

Katika muktadha wa mafunzo ya Kikristo, "kanuni" ina maana ya mafundisho yote kuhusu Mungu - Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu - ikijumlisha silika yake yote na kila kitu alichofanya.

Pia ina maana ya kila kitu Mungu anafundisha Wakristo juu ya namna ya kuishi maisha matakatifu ambayo yanaleta utukufu kwake.

Neno "kanuni" mara nyingnie linatumika kumaanisha mafunzo ya dini ya kidunia ya uongo ambayo hutoka kwa wanadamu. Muktadha hufanya maana wazi.

Msemo huu pia unaweza kutafsiriwa kama "mafunzo".


kanyaga

Ufafanuzi

"Kanyaga" ina maana ya kukanyaga kitu na kukisaga kwa mguu. Neno pia utumika kimfano katika Biblia kumaanisha "haribu" au "shinda" au "aibisha."


kanzu au vazi

Ufafanuzi

Kanzu ni vazi la mikono mirefu ambalo laweza kuvaliwa na mwanamke au mwanaume. Inafanana na koti.


karamu

Ufafanuzi

Msemo "karamu" una maana ya tukio ambapo kundi la watu hula chakula kingi sana pamoja, mara nyingi kwa kusudi ya kusherehekea kitu. Tendo "kula karamu" lina maana ya kula kiasi kikubwa cha chakula au kushiriki katika kula karamu pamoja.

Mara nyingi kuna aina maalumu za chakula ambavyo huliwa katika karamu maalumu.

Sherehe za kidini ambazo Mungu aliamuru Wayahudi kusherehekea mara kwa mara zilijumuisha kuwa na karamu ya pamoja. Kwa sababu hii sherehe hizo mara nyingi zilijulikana kama "karamu".

Katika kipindi cha Biblia, wafalme na watu wengine matajiri na wenye nguvu walifanya karamu kuwafurahisha familia zao au marafiki.

Katika simulizi kuhusu mwana mpotevu, baba yake alikuwa na karamu iliyoandaliwa kusherehekea ujio wa mwanawe.

Karamu mara zingine hudumu siku kadhaa au zaidi.

Msemo "kusherehekea" unaweza kutafsiriwa kama "kula kwa wingi mno" au "kusherehekea kwa kula chakula kingi" au "kula chakula kingi maalumu".

Kulingana na muktadha, "karamu" inaweza kutafsiriwa kama "kusherehekea pamoja kwa chakula kingi" au "mlo wenye chakula kingi" au "mlo wa sherehe"


kashfa, mtoa kashfa

Ufafanuzi

Kukashifu ina maana ya kusema kitu hasi, cha kudhalilisha kwa mtu mwingine.


kaya/famlia

Ufafanuzi

Istilahi 'kaya' hurejelea watu wote wanaoishi pamoja katika nyumba, ikijumuisha wana familia pamoja na watumishi walio nao. Mtu anaposimamia kaya, hujumuisha kuwaelekeza watumishi pamoja na kuangalia na kulinda mali. Wakati mwingine neno ' kaya' laweza kutumika kimfano kumaanisha ''ukoo wa mtu, hasa hasa wazao wake''


kazi, mfanyakazi

Ufafanuzi

Neno "kazi" linamaanisha kufanya kazi ngumu ya aina yoyote.

Kwa ujumla, kazi ni shughuli inayotumia nguvu, mara nyingi inaashiria kuwa shughuli ni ngumu. Mfanyakazi ni mtu afanyae aina yoyote ya kazi.


kereza meno, saga meno

Ufafanuzi

Kukereza au kusaga meno ina maana ya kukaza meno na kuyakwangua kwenda na kurudi dhidi yao. Hii mara kwa mara huonyesha maumivu na hasira kubwa mno.

Biblia inatuambia ya kwamba kusaga meno ni jambo moja ambalo wale walio jehanamu watafanya katika dhiki yao kuu.

Msemo huu pia unaweza kutafsiriwa kama "kukwangua meno dhidi yao" au "kama haipo wazi nini tendo hili linamaanisha "kusaga meno kwa maumivu" au "kusaga meno katika uchungu".


kiapo, kuapa,

Ufafanuzi

Katika Biblia, kiapo ni ahadi rasmi ya kufanya kitu. Mtu anaye kiapo anapswa kutimiza hiyo ahadi. Kiapo kinahusu kuwa mwaminifu na wa kweli.


kiasi

Ufafanuzi

Kiasi ni uwezo wa kutawala tabia ya mtu ili kuepusha kutenda dhambi.


Kiburi

Ufafanuzi

Kiburi maana yake ni kujivuna.


Kiburi

Ufafanuzi

Neno 'Kiburi' lina maana ya kuwa mwenye kujisifu, kujigamba au kujiona. Inarejelea mtu ambaye hujiona mwenyewe kuwa ni wa juu sana kuliko wengine. Mara nyingi neno hili humzungumzia majivuno ya mtu ambaye huendelea kufanya dhambi kinyume na Mungu. Mara kwa mara mtu mwenye kiburi hujivuna na kujiinua yeye mwenyewe Mtu mwenye kiburi ni mpambavu, hana hekima. Neno 'kiburi' laweza kutafsiriwa kama 'majivuno' ' majigambo' 'kujiinua' au kujiona. Maneno "macho ya kiburi'' ni Lugha ya picha ambayo yaweza kutafsiriwa kama "kuangalia kwa kiburi'' au " kuwaangalia wengine kama watu wasio na umuhimu'' au ''mtu mwenye kiburi anayewadharau wengine kwa kuwaona kuwa wako chini.''


Kiburi

Ufafanuzi

Kiburi ni hali ya mtu kujifikiria mwenyewe na kudhani kuwa yeye ni bora kuliko wengine.


Kichwa

Ufafanuzi

Katika Biblia neno 'kichwa' lilmetumika kama tamathali ya semi likiwa lina maana nyingi: Mara nyingi neno hili limetumika kurejelea hali ya kuwa na mamlaka juu ya watu , kwa mfano, "mmenifanya kichwa cha mataifa" Sentensi hiyo yaweza kutafsiriwa kuwa "mmenifanya kuwa mtawala" au "mmenipa mamlaka juu ya..." Yesu anaitwa 'kichwa cha kanisa.' Kama ambavyo kichwa cha mtu huongoza viungo vingine vya mwili, hivyo na Yesu huongoza na huelekeza viungo vingine vya mwili wake, yaani kanisa. Agano la Jipya linatufundisha kuwa mme ni "kichwa'' au mwenye mamlaka kwa mkewe. Amepewa wajibu wa kumwongoza na kumwelekeza mkewe na familia. Maneno yanayosema "wembe hautagusa kich chake" maana yake ni kwamba" hatakata au hatanyoa nywele zake. Neno 'kichwa' laweza pia kurejelea mwanzo au asili ya kitu fulani, mfano 'kichwa cha mtaa" Maneno kama "kichwa cha nafaka" hurejelea sehemu ya juu ya ngano au mche wa shayiri ambao una mbegu ndani yake. Mfano mwingine wa 'kichwa' ni pale unapotumika kuwakilisha mtu mzima. Mfano, 'kichwa cheupe' humrejelea mtu mzee au tunaposema ' kicha cha Yusufu, tunamaanisha Yusufu mwenyewe. Msemo unaosema 'acha damu yao iwe juu ya kichwa chake' humaanisha kuwa mtu yule anawajibika kwa vifo vyao na atapokea adhabu/hukumu yake.

Mapendekezo ya tafsiri Neno 'kichwa' laweza kutafsiriwa kama 'mamlaka' au 'mtu anayeongoza na kuelekeza' au 'mtu anayewajibika kwa..' kwa kutegemea na muktadha wenyewe. Maneno kama ' kichwa cha' hurejelea mtu mwenyewe mzima, na hivyo maneno hayo yaweza kutafsiriwa kwa kutumia jina la mtu husika. kwa mfano ''kichwa cha Yusufu'' ina maana ya 'Yusufu' Maelezo kama ' itakuwa juu ya kichwa chake' yanaweza kutafsiriwa kama " itakuwa juu yake'' au 'ataadhibiw'a kwa ajili ya' au 'atawajibika kwa ajili ya... Kwa kutegemea na muktadha wenyewe, maana zingine za neno kichwa zaweza kuwa "mwanzo' au "asili'' au ''chanzo'' au "mtawala" au ''juu ya''


kifo, kufa, mfu

Ufafanuzi

Msemo huu unatumika kumaanisha vyote kifo cha kimwili na kiroho. Kimwili, ina maana ya mwili wa kihalisia wa mtu kukoma kuishi. Kiroho, ina maana ya wenye dhambi kutengwa na Mungu mtakatifu kwa sababu ya dhambi yao.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kutafsiri msemo huu, ni vyema kutumia neno la kila siku au usemi ambao una maana ya kifo katika lugha husika.

Katika baadhi ya lugha, "kufa" inaweza kuelezwa kama "kutokuishi". Msemo "kufa" unaweza kutafsiriwa kama "kutokuwa hai" au "kutokuwa na uhai wowote" au "kutokuishi".

Lugha nyingi zinatumia msemo wa tamathali kuelezea kifo, kama "kuondoka" kwa Kiingereza. Ila katika Biblia ni bora kutumia msemo wa moja kwa moja kwa ajili ya kifo ambao unatumika kila siku katika lugha.

Katika Biblia, uhai na kifo wa kimwili mara kwa mara hulinganishwa na uhai na kifo cha kiroho. Ni muhimu katika tafsiri kutumia neno moja au msemo kwa ajili kifo cha kimwili na kifo cha kiroho.

Katika baadhi ya lugha inaweza kuwa wazi zaidi kusema, "kifo cha kiroho" ambapo muktadha unahitaji maana hiyo. Watafsiri wengine wanaweza kuhisi ni bora kusema, "kifo cha kimwili" katika muktadha ambapo unalinganishwa na kifo cha kiroho.

Msemo wa "wafu" ni kivumishi chenye maana ya watu waliokufa. Baadhi ya lugha zitatafsiri hili kama, "watu waliokufa" au "watu ambao wamekufa"


kifuko cha kifuani

Ufafanuzi

Neno "dirii" ni kipande cha silaha kinachofunika kifua kumlinda askari wakati wa vita. Neno "kifuko cha kifuani" linamaanisha kipande maalumu cha nguo ambacho kuhani mkuu wa Kiisraeli alivaa katika sehemu yake ya mbele kifuani.


kikapu

Ufafanuzi

Neno "kikapu" linamaanisha chombo kilichotengenezwa kwa kusukwa.


Kimbia

Ufafanuzi

Kukimbia ni kitendo cha kutembea haraka kwa miguu, haraka zaidi ya kutembea. Pia kukimbia yaweza kuwa na maana zifuatazo.


Kimbilio, malazi

Ufafanuzi

"Kimbilio" ni sehemu au hali ya usalama na ulinzi. "Malazi" ni sehemu yenye muundo wa kimwili ambayo inakulinda kutokana na hali ya hewa au hatari.


kinanda, kinubi

Ufafanuzi

Kinanda na kinubi ni vyombo vidogo vya muziki vyenye nyuzi zilizotumika na Waisraeli kumuabudu Mungu.

Kinanda kinafanana sana na gita la siku hizi, lina sanduku ya mbao na shingo ndefu ambapo nyuzi zimefungwa. Kucheza kinanda au kinubi, nyuzi flani zinashikiliwa na mkono mmoja wakati nyuzi zingine zinapigwa na mkono mwingine. Kinanda na kinubi zote zinachezwa kwa kupigwa au kuvutwa nyuzi. Idadi ya nyuzi ilitofautiana, lakini Agano la Kale lilitaja bayana vyombo vyenye nyuzi kumi.


kinara cha taa.

Ufafanuzi

Katika Biblia, usemi "kinara cha taa" kwa ujumla inamaanisha umbo ambapo taa inawekwa ili kutoa mwanga kwa chumba.

Kinara cha taa cha kawaida kilibeba taa moja na kilitengenezwa kwa udongo, mbao au chuma (kama shaba, fedha, au dhahabu.) Katika hekalu la Yerusalemu kulikuwa na kinara cha taa maalumu cha dhahabu kilichokuwa na matawi saba kwa kushikilia taa saba.


kinubi

Ufafanuzi

Kinubi ni chombo au kifaa cha muziki mara nyingi huwa na muundo ulio na uwazi mkubwa na nyuzi za wima. Katika Biblia, mbao za msonobari zilitumika kutengenezea vinubi pamoja na vyombo vingnei vya muziki. Vinubi mara kwa mara vilishikiliwa mikononi na kupigwa wakati mtu akiwa anatembea. Sehemu nyingi katika Biblia, vinubi vilikuwa vikitumika katika kumsifu na kumwabudu Mungu. Daudi aliandika Zaburi kadhaa ambazo zilikuwa zimepangwa kwa muziki wa kinubi. Daudi pia alicheza kinubi kwa mfalme Sauli ili kutuliza na kuburudisha roho ya mfalme iliyotaabika.


kinyume cha sheria

Ufafanuzi

Maneno "kinyume cha sheria" na "sio kisheria" yanatumika kueleza matendo yanayo vunja sheria.


kinywaji kikali

Ufafanuzi

Neno "kinywaji kikali" ina eleza vinywaji vilivyo zindikwa na vina vilevi.


Kisasi

Ufafanuzi

"Kisasi" ni kitendo cha kumuadhibu mtu kama malipo ya yale mabaya aliyoyatenda.


Kisima,birika

Ufafanuzi

Kisima na birika ni vyanzo viwili tofauti vya maji katika nyakati za Biblia.


Kitabu cha uzima

Ufafanuzi

Neno "Kitabu cha uzima" linatumika kumaanisha Mungu alipoandika majina ya watu aliowakomboa na kuwapa uzima wa milele.


kiti cha enzi

Ufafanuzi

Kiti cha enzi ni kiti ambacho mfalme ana keti kuamua mambo muhimu na kusikiliza maombi ya watu wake.


Kiumbe

Ufafanuzi

Kiumbe ni kila kitu kilicho hai ambacho Mungu alikiumba, binadamu na wanyama.


Kivuli

Ufafanuzi

Neno "kivuli" lina maana ya giza linalo sababishwa na kitu kinacho ziba mwanga. Pia lina maana kadhaa ya mafumbo.


kizazi

Ufafanuzi

Msemo "kizazi" una maana ya kundi la watu ambao wote wamezaliwa katika kipindi cha kufanana.

Kizazi pia kinaweza kumaanisha kipindi cha muda. Katika kipindi cha Biblia, kizazi kilichukuliwa kuwa kama miaka 40.

Wazazi na watoto waoo wanatoka katika vizazi viwili tofauti.

Katika Biblia, msemo "kizazi" pia hutumika kitamathali kumaanisha kwa ujumla watu ambao huwa na tabia za kufanana.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo " kizazi hiki" au "watu wa kizazi hiki" unaweza kutafsiriwa kama "watu wanaoishi sasa" au "nyie watu".

"Kizazi hiki kiovu" inaweza kutafsiriwa kama "watu hawa waovu wanaoishi sasa".

Msemo "kutoka kizazi hadi kizazi" au "kutoka kizazi kimoja hadi kingine" inaweza kutafsiriwa kama "watu wanaoishi sasa, pamoja na watoto na wajukuu wao" au "watu katika kipini chote" au "watu wa kipindi hili na vipindi vya baadaye" au "watu wote na uzao wao".

"Kizazi kinachokuja kitamtumikia; watawaambia kizazi kifuatacho juu ya Yahwe" inaweza kutafsiriwa kama "Watu wengi hapo baadaye watamtumikia Yahwe na kuwaambia watoto na wajukuu wao juu yangu".


kizingiti

Ufafanuzi

Neno "kizingiti" la eleza sehemu ya chini ya mlango au sehemu jengo ambayo ipo ndani ya mlango.


Komamanga

Ufafanuzi

Komamanga ni aina ya tunda nene lenye ngozi ngumu lililojaa mbegu nyingi ndani zilizozungukwa na chakula chenye rangi nyekundu.


komboa, mkombozi, ukombozi

Ufafanuzi

"Kukomboa" mtu ina maana ya kumukokoa mtu huyo. Msmo "mkombozi" una maana ya mtu ambaye hukomboa au kuweka huru watu kutoka utumwani, mateso au hatari zingine. Msemo "ukombozi" una maana ya kile kinachotokea pale mtu anapookoa au kuweka watu huru kutoka utumwani, matesoni, au hatari zingine.

Katika Agano la Kale, Mungu aliwaweka wakombozi kuwalinda Waisraeli kwa kuwaongoza katika vita dhidi ya makundi ya watu wengine waliokuja kuwashambulia.

Wakombozi hawa pia walijulikana kama "waamuzi" na kitabu cha Agano la Kale cha Waamuzi kimeweka kumbukumbu ya kipindi katika historia ambapo waamuzi hawa walikuwa wakitawala Israeli.

Mungu pia anaitwa "mkombozi". Kote katika historia ya Israeli, aliwakomboa au kuwaokoa watu wake kutoka kwa maadui zao.

Msemo "kutoa kwa" ina maana tofauti kabisa ya kumtoa mtu kwa adui, kama pale Yuda alipomtoa Yesu kwa viongozi wa Kiyahudi.

Mapendekezo ya Tafsiri

Katika muktadha wa kusaidia watu kutoroka kutoka kwa adui zao, msemo "komboa" unaweza kutafsiriwa kama "okoa" au "kuweka huru" au "nusuru".

Pale inapomaanisha kukabidhi mtu kwa adui, "kukabidhi" inaweza kutafsiriwa kama "kusaliti" au "kumpatia" au "kutoa kwa".

Neno "mkombozi" linaweza kutafsiriwa kama, "mkombozi" au "mweka huru".

Pale ambapo msemo "mkombozi" una maana ya waamuzi waliongoza Israeli, inaweza pia kutafsiriwa kama "bosi au "mwamuzi" au "kiongozi"


kondoo, kondoo dume, kondoo jike

Ufafanuzi

"kondoo" ni mnyama wa saizi ya kati wa miguu minne mwenye manyoya mwili mzima.


Kosa, mateso, kuumiza

Ufafanuzi

"kumkosea" mtu inamaanisha kumfanyia mtu isivyo haki na kwa udanganyifu.


kuachwa, kuacha

Ufafanuzi

Msemo wa "kuachwa" na "kuacha" ina maana ya kuangamiza sehemu isiyokuwa na watu ili kwamba isiwe ya makazi.

Inapomaanisha mtu, msemo "kuachwa" inaelezea hali ya uharibifu, upweke, au majonzi.

Msemo "kuacha" ni hali ya kuachwa.

Iwapo shamba ambapo mimea inaota linaachwa, ina maana kitu kimeaangamiza mimea, kama wadudu au uvamizi wa jeshi.

"Eneo lilioachwa" lina maana ya eneo ya ardhi ambapo watu wachache wanaishi kwa sababu kuna mazao machache au mimea mingine inayoota pale.

"Ardhi iliyoachwa" au "nyika" mara kwa mara ilitengwa kwa watu waliotengwa na jamii (kama wakoma) na wanyama wa hatari.

Kama mji "unatengwa" ina maana ya kwamba majengo yake na mali vimeharibiwa au kuibiwa, na watu wake wameuwawa au kukamtwa. Mji unakuwa "tupu" na "kuharibika". Hii ni sawa na maana ya "teketeza" au "teketezwa", lakini kwa msisitizo zaidi kwa utupu.

Kutegemea muktadha, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "kuharibiwa" au "kuangamizwa" au "kuwekwa kama takataka" au "mpweke/iliyotengwa" au "kutelekezwa"


Kuadhibu, adhabu

Ufafanuzi

"Kuadhibu" inamaana ya kusababisha mtu ateseke baada ya kufanya makosa. Adhabu ni matokeo hasi anayopewa mtu baada ya kufanya jambo baya.


kubeba

Ufafanuzi

Neno "kubeba" linamaanisha "kubeba" kitu fulani. Lakini pia kuna kuna matumizi ya tamathari mbalimbali ya neno hili.


kuchinja

Ufafanuzi

Neno "kuchinja" Maneno waliyo chinjwa ya weza pia tumika kutafsiri watu waliyo chinjwa au watu waliyo uawa. Pia la weza tumika kumaanisha mkua mnyama kwa kusudi la kumla.


kudanganya, udanganyifu, hila, mdanganyifu

Ufafanuzi

Msemo wa"kudanganya" una maana ya kumfanya mtu aamini jambo ambalo sio la kweli. Tendo la kumdanganya mtu linajulikana kama "udanganyifu".

Msemo mwingine, "udanganyifu" pia una maana ya tendo la kumfanya mtu aamini jambo ambalo sio kweli.

Mtu anayefanya wengine kuamini jambo la uongo ni "mdanganyifu". Kwa mfano, Shetani anaitwa "mdanganyifu". Roho chafu anazoziongoza pia zinajulikana kama wadanganyifu.

Mtu, tendo, au ujumbe ambao sio wa kweli unaweza kuelezwa kama "udanganyifu".

Misemo ya "udanganyifu" na "hila" zina maana moja, lakini kuna tofauti kadhaa ndogo jinsi zinavyotumika.

Misemo inayojieleza ya "udanganyifu" na "hila" ina maana moja na hutumika katika muktadha moja.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia zingine za kutafsiri "kudanganya" zinaweza kujumuisha "uongo" au "kusababisha kuwa na na imani potofu" au "kusababisha mtu afikiri jambo sio la kweli".

Msemo "kudanganywa" unaweza kutafsiriwa kama "kusababisha kufikiri jambo ni la uongo" au "alidanganywa" au "alifanyiwa hila" au "alipumbazwa" au "alipotoshwa".

"Mdanganyifu" inaweza kutafsiriwa kama, "mwongo" au "mtu mpotoshaji" au "mtu anayedanganya".

Kulingana na muktadha, msemo wa "udanganyifu" au "hila" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo unaomaanisha "uongo" au "kudanganya" au "upotoshaji" au "kutokuwa na uaminifu".

Msemo "kudanganya" au "udanganyifu" unaweza kutafsiriwa kwa "uongo" au "upotoshaji" au "kudanganya" kumuelezea mtu anayezungumza au kutenda kwa njia ambayo inasababisha watu wengine kuamini mambo ambayo sio ya kweli.


Kufanikiwa, mafanikio

Ufafanuzi

"Kufanikiwa" ni kitendo cha kuishi vizuri na kuwa na mafanikio kimwili na kiroho. Nchi inayofanikiwa inamaanisha wana utajiri na wanakila kitu wanachohitaji.


Kufanya, nia, kujituma

Ufafanuzi

Kufanya au kujituma ni kitendo cha kufanya maamuzi au kuahidi kufanya jambo fulani.


kufanywa haki

Ufafanuzi

Usemi "kufanywa haki" inamaanisha kumfanya mtu mwenye hatia kuwa mwenye haki. Mungu pekee ndiye awezaye kuwafanya watu kuwa na haki.

Mungu anapowafanya haki watu, huwasamehe dhambi zao na kuwafanya kana kwamba hawana dhambi. Huwafanya haki watenda dhambi wanaotubu na kumuamini Yesu kuwaokoa kutoka dhambi zao. "kufanywa haki" inamaanisha kile Mungu anachofanya anaposamehe dhambi za mtu na kutamka kuwa mtu huyo ni mwenye haki machoni pake.


kufinyanga

Ufafanuzi

Kufinyanga ni kutengeneza mbao, chuma, au udogo ilikutimia kuunda umbo kutokana na dhahabu, fedha, au vitu vingine vinavyo weza kumika kwa kufinyangwa.


Kufurani

Ufafanuzi

Kufurahi inamaana ya kuwa na furaha.


kufuru

Ufafanuzi

Neno la "kufuru" lina maana ya kuharibu au kuchafua sehemu takatifu au kitu katika namna ambayo haikubaliki kutumika katika kuabudu.

Mara kwa mara kukufuru kitu inahusisha kuonyesha okosefu mkubwa wa keshima kwake.

Kwa mfano, wafalme wa kipagani walikufuru vyombo maalumu kutoka hekalu la Mungu kwa kuvitumia kwa ajili ya sherehe katika kasri zao.

Mifupa kutoka watu waliokufa ilitumika na maadui kukufuru madhabahu katika hekalu la Mungu.

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama, "kusababisha kutokuwa mtakatifu" au "kumvunjia heshima kwa kufanya asiwe mtakatifu" au "kukufuru kwa kuvunja heshima" au "kusababisha kutokuwa msafi".


kufuta

Ufafanuzi

Maneno "kufuta" au "kuondoa" ni vifungu vinavyomaanisha kuondoa kabisa au kuangamisa kitu au mtu.

Maone ya Kutafasiri


Kugawa, kupewa

Ufafanuzi

Kugawa au kupewa ni kitendo cha kumteua mtu kwa ajili ya kufanya kazi maalumu.


kuhamisha, Uhamisho

Ufafanuzi

Msemo "kuhamisha" una maana ya watu waliolazimishwa kuishi mahali mbali na nchi yao ya nyumbani.

Watu mara kwa mara hutumwa uhamishoni kwa ajili ya adhabu au sababu za kisiasa.

Watu walioshindwa wanaweza kupelekwa uhamishoni katika nchi ya jeshi iliyowashinda ili kuwafanyia kazi.

"Uhamisho wa Babeli" (au "Uhamisho") ni kipindi katika historia ya Biblia ambapo raia wengi wa Kiyahudi wa eneo la Yuda walichukuliwa kutoka nyumbani mwao na kulazimishwa kuishi Babeli. Ilidumu miaka 70.

Msemo "waliohamishwa" una maana ya watu ambao wanaishi katika uhamisho, mbali na nchi yao ya nyumbani.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo wa "kuhamisha" unaweza kutafsiriwa kama "kufukuza" au "kulazimisha kutoka nje" au "kuondoa".

Msemo "Uhamisho" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana "muda ambao walifukuzwa" au "muda wa kufukuzwa" au "muda wa kulazimishwa kutokuwepo" au "kuondolewa".

Njia za kutafsiri "waliofukuzwa" zinaweza kujumuisha, "watu waliofukuzwa" au "watu ambao waliondolewa" au "watu walifukuzwa kwenda Babeli"


Kuhani mkuu

Ufafanuzi

Kuhani mkuu alikuwa kiongozi wa muhimu sana katika dini ya kiyahudi wakati ambao Yesu aliishi duniani.


Kuharibu

Ufafanuzi

Kuharibu kitu ni hali ya kuangamiza, kukiteketeza au kukifanya kisiwe na maana tena.


Kuhitimu, waliohitimu

Ufafanuzi

Neno "kuhitimu" ni kitendo cha kupata haki ya kupokea faida fulani au kujulikana kwa kuwa na ujuzi fulani.


Kuhubiri

Ufafanuzi

Kuzungumza na kundi la watu kuwafundisha kuhusu Mungu na kuwasihi wamtii Mungu.


Kuinama chini

Ufafanuzi

Kuinama maana yake kujikunja kwa unyenyekevu kuonesha heshima kwa mtu. "Kuinama chini" inamaanisha kupiga magoti chini sana, kwa kawaida uso na mikono ikielekea ardhini.

Maoni ya Kutafasiri


kujiamini, ujasiri

Ufafanuzi

Kujiamini ni kuwa na uhakika kuwa jambo fulani ni la kweli au litatokea.


Kujivuna

Ufafanuzi

Kujikweza ni kitendo cha mtu kujivuna au kuwa na majivuno.


Kujua kabla

Ufafanuzi

Msemo "kujua kabla" unatokana na maana ya kujua jambo kabla halijatokea.

Mungu hazuiliwi na muda. Anajua kila kitu ambacho hutokea kipindi cha nyuma, sasa na baadaye.

Neno hili mara kwa mara hutumika katika muktadha ya Mungu kujua tayari nani ataokolewa kupitia kumpokea Yesu Kristo.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "kujua kabla" unaweza kutafsiriwa kama "kujua kabla" au "kujua kabla ya wakati" au "kujua kabla ya" au "kujua tayari".


kujua, ufahamu, kufanya kujulikana

Ufafanuzi

"Kujua" inamaanisha kuelewa kitu au kuwa na ufahamu wa jambo. Usemi "kufanya kujulikana" ni usemi unaomaanisha kutoa taarifa.

Neno "ufahamu" linamaanisha taarifa ambazo watu wanajua. Inaweza kuwa kujua vitu katika dunia ya kimwili na kiroho. "Kujua kuhusu" Mungu inamaanisha kuelewa mambo kumhusu kwa sababu ya yale aliyotufunulia. "Kumjua" Mungu inamaanisha kuwa na uhusiano naye. Hii inamaanisha pia kuwajua watu wake. Kujua mapenzi ya Mungu inamaanisha kuwa na ufahamu wa yale aliyetoagiza, au kuelewa ni nini anataka mtu afanye. "Kujua Sheria" inamaanisha kuwa na ufahamu wa yale Mungu aliyoagiza au kuelewa yale Mungu aliyoagiza katika sheria alizompa Musa. Wakati mwingine "ufahamu" unatumika kama neno lingine la "hekima," linalojumuisha kuishi katika njia inayompendeza Mungu. "Ufahamu wa Mungu" wakati mwingine unatumika kama njia nyingine ya kusema hofu ya Yahwe.


kukandamiza, ukandamizaji, mkandamizaji

Ufafanuzi

Meneo, "kukandamiza," "ukandamizaji," "mkandamizaji" ya husu kumtendea mtu kwa ukali. "mkandamizaji" ni mtu anaye kandamiza watu.


Kukataa

Ufafanuzi

"Kukataa" kitu au mtu inamaana kuacha kumkubali mtu au kitu.


Kukatwa

Ufafanuzi

Kukatwa ni kitendo cha kuondolewa, kufukuzwa au kutengwa toka kwenye kundi. Pia inaweza kuwa na maana ya kuuawa kama tendo la hukumu kwa ajili ya dhambi.


Kukemea

Ufafanuzi

Kukemea ni kitendo cha kumrekebisha mtu ili kumsaidia mtu yule kuacha dhambi.


kukesha

Ufafanuzi

Katika nyakati za Biblia, "kukesha" ulikuwa wakati wa usiku ambao katika huo mlinzi au mwangalizi wa mji alikuwa kazini akiangalia hatari yoyote kutoka kwa maadui.


Kula

Ufafanuzi

Kula ni kitendo cha kutumia kitu fulani. Pia ina maana nyingine.


kulala na, kuwa na mahusiano na, fanya mapenzi

Ufafanuzi

Katika Biblia, haya maneno ni tafsida yanayo eleza kufanya ngono.


kulewa, mlevi

Ufafanuzi

Msemo "kulewa" ina maana ya kuleweshwa kutokana na kunywa kileo.

"Mlevi" ni mtu ambaye hulewa mara kwa mara. Mtu wa aina hii anajulikana kama "mlevi".

Biblia inawaambia waumini kutolewa na vilevi, lakini kutawaliwa na Roho Mtakatifu wa Mungu.

Biblia inafundisha ya kwamba ulevi sio busara na inamshawishi mtu kutenda dhambi kwa njia zingine.

Njia zingine za kutafsiri "kulewa" zinaweza kujumuisha "levya" au "kulewa" au "kupata kilevi kingi sana" au "kushiba kwa kinywaji chachu"


kumbukumbu, sadaka ya kumbukumbu

Ufafanuzi

Neno "kumbukumbu" la husu tendo au kitu kinacho msababisha mtu au kitu kukumbukwa.


Kumiliki, Miliki

Ufafanuzi

"Kumiliki" au "miliki" ni kitendo cha kuwa na kitu fulani. Pia inaweza kuwa na maana ya kuwa na mamlaka juu ya kitu fulani au kumiliki eneo la ardhi.


Kumuachia

Ufafanuzi

Neno "kumuachia" lina maana ya kukiri wazu kuwa mtu fulani hana hatia kwa kosa fulani au tabia fulani alikuwa ameshitakiwa.


kumwaga damu

Ufafanuzi

Neno "kumwaga damu" linamaanisha kifo cha mwanadamu kwa sababu ya mauaji, vita, au sababu nyingine ya kikatiri.

Maoni ya Kutafasiri


Kundi la watu, watu

Ufafanuzi

"Watu" au "kundi la watu" linamaana ya makundi ya watu wenye lugha moja na utamaduni mmoja. Pia yaweza kuwa na maana ya watu waliokusanyika sehemu fulani au kwa ajili ya tukio fulani.


kundi, mifugo

Ufafanuzi

Katika Biblia "kundi" ina maana ya kundi la kondoo na mbuzi na "mifugo" ina maana ya kikundi cha ng'ombe, maksai, au nguruwe.

Lugha tofauti zinaweza kuwa na njia tofauti za kutaja makundi ya wanyama au ndege.

Kwa mfano, katika Kiingereza msemo "kundi" unaweza pia kutumika kwa ajili ya kondoo au mbuzi, lakini katika maandishi ya Biblia haitumiki kwa njia hii.

Msemo "kundi" katika Kiingereza pia hutumika kwa ajili ya kundi la ndege, lakini unaweza kutumika kwa ajili ya nguruwe, maksai au ng'ombe.

Fikiria ni misemo gani inatumika katika lugha yako kumaanisha makundi tofauti ya wanyama.

Kwa mistari ambayo ina maana ya "makundi au mifugo" inaweza kuwa bora kuongeza "ya kondoo" au "ya ng'ombe" kwa mfano, kama lugha haina maneno tofauti kumaanisha aina tofauti za makundi ya wanyama.


kuomba

Ufafanuzi

Neno "kuomba" lamaanisha kumwomba mtu kitu fulani kwa umuhimu. Mara kwa mara inamaanisha kuomba pesa, lakini pia limetumika kuonesha kuombeleza jambo fulani.


kuomboleza

Ufafanuzi

"Kuomboleza" kwa husu huzuni ya ndani, mara nyingi wakati wa kifo cha mtu.


kupiku

Ufafanuzi

Neno "kupiku" ina maana ya kupata uweza juu ya mtu au kitu. Mara nyingi ina maana ya kufikia kitu na kukipita baada ya kukufukuzia.


Kupokea

Ufafanuzi

Kupokea ni kupata au kukubali kitu unachopewa au kuletewa.


Kupotea, akipotea, kupotoshwa

Ufafanuzi

Kupotea ina maana ya kutomtii Mungu. Watu wanaopotoshwa wamewaruhusu watu wengine kuwasababisha wasimtii Mungu.


kupumua, pumzi

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "kupumua" na "pumzi" yanatumika mara kwa mara kitamathari kumaanisha kutoa uhai au kuwa na uhai.

Maoni ya Kutafasiri


kura, kupiga kura

Ufafanuzi

"Kura" ni kitu kilichowekwa alama kinachochaguliwa miongoni mwa vitu vya kufanana kama naamna ya kuamua jambo. "Kupiga kura" inamaanisha kurusha vitu vilivyo wekwa alama kwenye sakafu au ardhi yoyote.

Mara nyingi kura yalikuwa mawe madogo yenye alama au vipande vidogo vilivyovunjika vya udongo. Tamaduni zingine zinafanya "bahati nasibu" au "kuvuta" kura kwa kutumia majani makavu. Mtu anayashikilia majani makavu ili asiwepo wakuona yana urefu gani. Kila mtu anavuta jani na yule atakayepata jani kavu refu zaidi (au fupi) ndiye atakayekuwa amechaguliwa. Zoezi la kupiga kura lilitumika na Waisraeli kujua ni nini Mungu aliwataka wafanye. Kama nyakati za Zekaria na Elisabeti, ilitumika pia kuchagua ni kuhani yupi atatenda jukumu bayana hekaluni katika muda maalumu. Askari walio msulubisha Yesu walipiga kura kuamua ni nani atakaa na joho la Yesu. Usemi "kupiga kura" inawezakutafsiriwa kama "kufanya bahati nasibu" au "kurusha kura". Kulinga na mazingira, neno "kura" inaweza pia kutafsiriwa kama "jiwe lenye alama" au "kipande cha udongo" au "kijiti" au "kipande cha jani." Kama maamuzi yakifanyika "kwa kura" hii inaweza kutafsiriwa kama "kufanya bahati nasibu (au kurusha) ya kura."


kusaliti

Ufafanuzi

Neno "kusaliti" lamaanisha tendo la kumdanganya na kumdhuru mwingine. "Msaliti" ni mtu amsalitiye rafiki yake mwenye kumwamini.

Maoni ya Tafasiri


kusanya, kukusanya

Ufafanuzi

Msemo "kusanya" una maana ya kupita katika shamba au shamba la matunda kuokota nafaka yoyote au tunda ambao wavunaji wameacha nyuma.

Mungu aliwaambia Waisraeli kuruhusu wajane, watu maskini, na wageni kukusanya mabaki ya nafaka ili kwamba wapate chakula kwa ajili yao.

Mara nyingine mmiliki wa shamba angeruhusu wakusanyaji kwenda moja kwa moja nyuma ya wavunaji kukusanya, ambayo iliwawezesha wao kukusanya nafaka zaidi.

Mfano wa wazi ni jinsi hii ilivyofanya kazi katika simulizi ya Ruhtu, ambaye aliruhusiwa kwa ukarimu kukusanya miongoni mwa wavunaji katika mashamba ya ndugu wa Boazi.


Kushangaa, kushangaza

Ufafanuzi

"Kushangaa" ni hali ya mshangao na heshima kubwa inayokuja baada ya kuona jambo kubwa limefanyika na lenye nguvu.


Kushangaa, mshangao

Ufafanuzi

Maneno haya yote yanamaana ya kushangazwa kwa sababu ya jambo fulani lisilo la kawaida ambalo limetokea.


Kusifu

Ufafanuzi

Kumsifu mtu ni kuonesha pongezi au heshima kwa mtu yule.


Kusihi, ng'ang'ania

Ufafanuzi

"Kusihi" inamaana ya kumuomba mtu afanye jambo fulani. Ng'ang'ania ni ombi la haraka.


kusimika

Ufafanuzi

Kusimika kuna maana ya kuteuwa mtu kwa kazi maalumu au jukumu. Pia ina maana ya kufanya uamuzi au tamko.


Kusujudu

Ufafanuzi

Kusujudu ni kitendo cha kuinamisha uso chini kwenye ardhi.


Kusukuma

Ufafanuzi

Hiki ni kitendo cha kuhamisha kitu kimwili kwa kutumia nguvu. Kuna maana mbali mbali za neno hili


Kutangaza, tangazo

Ufafanuzi

Kutanganza ni kitendo cha kutoa tamko hadharani.


Kutawala

Ufafanuzi

Neno "kutawala" linamaana ya kuongoza kama mfalme juu ya watu wa nchi fulani au ufalme. Utawala wa kifalme ni wakati ambao mfalme alitawala.


Kutoboa

Ufafanuzi

"Kutoboa" ni kitendo cha kuchoma kitu kwa kutumia kitu chenye ncha. Pia hutumika kuelezea tendo la kusababisha maumivu makali ya kihisia kwa mtu.


Kutupwa nje, kutupa nje

Ufafanuzi

"kutupwa nje" mtu au "kutupa nje" kitu inamaanisha kulazimisha kitu au mtu kuondoka.


Kuvika

Ufafanuzi

Kujivika na kitu ni kutafuta kuwa na tabia fulani.


Kuvuna, mvunaji

Ufafanuzi

Kuvuna inamana ya kuvuna mazao kama nafaka. Mvunaji ni mtu anayevuna mazao.


Kuwa "tasa" maana yake ni kutoweza kuzaa.

Ufafanuzi

Ardhi au nchi ambayo ni tasa haiwezi kuotesha mmea wowote. Mwanamke tasa ni yule asiyeweza kuzaa mto.

Maoni ya Tafasiri Neno "tasa" linapotumika kurejerea nchi, lingeweza kutafasiriwa kama "isiyozaa" "isiyozalisha" au "isiyo na mimiea." Linapotumika kumtaja mwanamke mgumba, liliweza kutafasiriwa kama "asiye na mtoto" au "asiyeweza kuzaa watoto" au "asiyeweza kutunga mtoto."


Kuwatesa, mateso

Ufafanuzi

"Kuwatesa" au "mateso" ni kitendo endelevu cha kumfanyia mtu au kundi la watu kitu katika namna mbaya ya kuwasababishia madhara.


kuza

Ufafanuzi

Neno "kuza" lina maana ya kufanya kitu au mtu mkubwa au kuvuta umakini kwa ukuu wa mtu.


kuzidisha

Ufafanuzi

neno "kuzidisha" lina maana ya kuongezeka kiidadi. Pia yaweza kusababisha kitu kuongezeka kwa kiasi, kama vile kuzidisha maumivu.


kuzika, zika

Ufafanuzi

Neno "zika" kwa kawaida linamaanisha kuweka kaburini mwili wa mtu aliyekufa. Neno "kuzika" ni kitendo cha kuzika kitu au linaweza kutumika kueleza sehemu itumikayo kuzikia.


Kuzima

Ufafanuzi

"Kuzima" inamaana kutoa au kusimamisha kitu ambacho kinatakiwa kikamilike.


kwato,

Ufafanuzi

Hizi ni sehemu ngumu za chini katika miguu ya wanyama kama vile ngamia, ng'ombe, farasi, punda, nguruwe, kondoo, mbuzi n.k Kwato za wanyama humlinda mnyama anapokuwa anatembea Baadhi ya wanyama wana kwato zilizogawanyika katika sehemu mbili, na wanyama wengine wana kwato ambazo hazijagawanyika.


la kumi, zaka

Ufafanuzi

Maneno "la kumi" na "zaka" yanaeleza "asilimia ya kumi" au "moja-kati-ya -sehemu- ya-kumi" ya pesa, mazao, mifugo, au mali za mtu anazo mpa Mungu.


lala, kulala, aliye lala

Ufafanuzi

Haya maneno yana maana ya kimafumbo kuhusu kifo.


lango, nguzo ya lango

Ufafanuzi

"Lango" ni kizuizi chenye bawaba katika njia ya kufikia ya uzio au ukuta ambao huzunguka nyumba au mji. "Nguzo ya lango" ina maana ya nguzo ya chuma au mbao ambayo inaweza kusogezwa katika sehemu kufunga lango.

Lango la mji linaweza kufunguliwa kuruhusu watu, wanyama, na mizigo kusafiri ndani na nje ya mji.

Kulinda mji, kuta zake na malango ilikuwa nene na imara. Malango yalifungwa na kukazwa na nguzo ya chuma au mbao kuzuia wanajeshi wa maadui kuingia mji.

Lango la mji mara kwa mara ilikuwa kiini cha habari na katikati ya jamii ya kijiji. Pia ilikuwa mahali ambapo mihamala ya kibiashara hufanyika na hukumu kufanyika, kwa sababu kuta za mji zilikuwa na unene wa kutosha kuwa na njia ambayo ilitoa kivuli cha baridi kutoka kwa jua kali. Raia walifurahia kukaa chini ya kivui na kufanya biashara zao na pia kuhumu masuala ya kisheria.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, njia zingine za kutafsiri "lango" inaweza kuwa "mlango" au "uwazi wa ukuta" au "kizuizi" au "njia ya kuingia".

Msemo "nguzo za lango" unaweza kutafsiriwa kama "komeo za lango" au "mihimili ya mbao ya kufunga lango" au "chuma cha kufunga lango"


Laumu

Ufafanuzi

Kumlaumi mtu ni kumkosoa au kukataa matendo au tabia za mtu. Kulaumu ni maoni hasi kuhusu mtu.


Lia, kupiga kelele

Ufafanuzi

Lia au piga kelele inamaana ya kusema kitu kwa nguvu au ghafla. Kupiga kelele kwa maumivu au hasira.


lsio huru, kuwa chini ya, chini ya

Ufafanuzi

Neno "sio huru" la eleza kuwa chini ya mamlaka ya mtu. Maneno "kuwa chini ya" ni amri inayo maanisha "tii" au "nyenyekea mamlaka ya."


maangamizi

Ufafanuzi

Msemo "maangamizi" una maana ya hukumu ya shutuma ambayo haina uwezekano wa rufaa au utorokaji.

Taifa la Israeli lilipochukuliwa mateka Babeli, nabii Ezekieli alisema, "maangamizi yamekuja juu yao".

Kutegemea na muktadha, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "maafa" au "adhabu" au "uharibifu usio na matumaini".


Madhabahu ya kufukizia.

Ufafanuzi

Madhabahu ya kufukizia ilikuwa sehemu ya samani ambayo kuhani aliitumia kuchoma uvumba kama sadaka kwa Mungu. Ilikuwa inaitwa madhabahu ya dhahabu.


mafuriko

Ufafanuzi

Msemo "mafuriko" ina maana ya kiasi kikubwa cha maji ambacho kinafunika juu ya nchi.

Msemo huu pia hutumika kitamathali kumaanisha kiasi kikubwa cha kitu, haswa kitu ambacho hutokea ghafla.

Katika kipindi cha Nuhu, watu walikuwa waovu hadi Mungu akasababisha mafuriko duniani kote kuwa juu ya uso wote wa dunia, hata kufunika juu za milima. Kila mtu ambaye hakuwa katika mtumbwi pamoja na Nuhu alizama. Mafuriko yote mengine hufunika eneo dogo la nchi.

Msemo huu pia unaweza kuwa tendo kama, "nchi ilifurika na maji ya mto".

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia za kutafsiri maana halisi ya "mafuriko" inaweza kujumuisha, "maji yanayomwagikia" au "kiasi kikubwa cha maji"

Mlinganisho wa kitamathali, "kama mafuriko" unaweza kukaa na msemo halisi, au msemo mbadala unaweza kutumika ambao una maana ya kitu ambacho kina hali ya kutiririka kwake, kama vile mto.

Kwa msemo "kama mafuriko ya maji" pale ambapo maji yametajwa tayari, neno "mafuriko" linaweza kutafsiriwa kama "kiasi kikubwa sana" au "yanayomwagikia".

Msemo huu unaweza kutumika kama sitiari kama, "usiruhusu mafuriko kunizoa juu yangu", ambayo ina maana ya "usiruhusu maafa haya makubwa kutokea kwangu" au "usiniache niteketezwe kwa maafa" au "usiache hasira yako initeketeze".


mafuta

Ufafanuzi

Mafuta ni maji mazito yanayo chukuliwa kutoka kwenye mimea au matunda. Katika Biblia, mafuta yalito kwenye mizeituni.


Maji

Ufafanuzi

Pamoja na maana yake ya kawaida maji yaweza kuwelezea vyanzo vya maji kama vile bahari, mto au ziwa.


majivu, vumbi

Ufafanuzi

Majivu ni vumbi la kijivu linalobaki baada ya kuni kuungua. Hutumika pia kama lugha ya picha kuonesha kitu kisicho na thamani.


Majuto

Ufafanuzi

"majuto" maana yake ni maumivu makali au dhiki.


Makabila kumi na mbili ya Israeli

Ufafanuzi

Makabila kumi na mbili inamaanisha watoto kumi na mbili wa Yakobo na uzao wao. Yakobo alikuwa mjukuu wa Abrahamu. Baadae Mungu alibadili jina lake na kumuita Israeli. Haya ndio majina ya makabila ya Israeli; Rubeni, Simoni, Lawi, Yuda, Naftali, Gadi, Asheri, Isakari, Zabuloni, Yusufu na Benjamini. Kizazi cha Lawi hakikurithi nchi ya Kaanani kwa sababu lilikuwa kabila la Kikuhani waliotengwa kumtumikia Mungu na watu wake. Yusufu alipokea urithi wa ardhi mara mbili ambapo aliwapatia watoto wake wawili Efraimu na Manase. Kuna mahali pengine kwenye Biblia orodha ya makabila kumi na mbili yamenukuliwa tofauti. Sehemu nyingine Lawi, Yusufu na Dani hawakuwekwa kwenye orodha na sehem nyingine watoto wawili wa Yusufu Efraimu na Manase wamewekwa kwenye orodha.


makapi

Ufafanuzi

Makapi ni ganda kavu linalolinda mbegu ya nafaka. Makapi sio mazuri kwa chakula hivyo watu hutenganisha na mbegu na kuyatupa.


Makerubi, Kerubi

Ufafanuzi

Kerubi ni umoja na makerubi ni wingi. Hivi ni viumbe vya pekee vya mbinguni alivyoviumba Mungu. Biblia inawaelezea makerubi kuwa wana mabawa na moto.


Malkia

Ufafanuzi

Malkia ni kiongozi mwanamke wa nchi fulani au mke wa mfalme.


Mambo ya nyakati

Ufafanuzi

Mambo ya nyakati ni kumbukumbu zilizoandikwa kwa kipindi fulani cha wakati.


Maono

Ufafanuzi

Maono ni kitu ambacho mtu anakiona. Mara nyingi kitu hiki huwa sio cha kawaida au huwa chenye nguvu ambapo Mungu humuonesha mtu kwa lengo la kumpa ujumbe.


mateka, kifungo

Ufafanuzi

Neno "mateka" au "kifungo" ni kitendo cha kukamata watu na kuwalazimisha waishi mahali ambapo hawataki kuishi kama kwenye nchi ya kigeni.


Mateso

Ufafanuzi

Mateso ni kitendo cha kumsababishia mtu mateso. Mateso ni ugonjwa, huzuni ya kihisia au majanga mengine yatokanayo na mateso.


Matete

Ufafanuzi

Matete ni mimea nyenye mabua marefu yanayoota katika maji.


maumivu makali

Ufafanuzi

Neno "maumivu makali" yaeleza kutesa sana. Kumtesa mtu ina maana ya kusababisha mtu kuteseka, mara nyingi kwa namna mbaya.


mavi, mbolea

Ufafanuzi

Msemo "mavi" una maana ya takataka ya binadamu au mnyama, na pia kinaitwa kinyesi. Unapotumika kama kirutubisho cha kurutubisha udongo, inajulikana kama "mbolea"

Misemo hii pia inaweza kutumika kitamathali kumaanisha kitu ambacho hakina thamani au sio muhimu.

Kinyesi kilichokaushwa cha mnyama mara kwa mara hutumika kama kichochea.

Msemo "kuwa kama kinyesi katika uso wa dunia" unaweza kutafsiriwa kama "kusambazwa kama kinyesi kisicho na maana juu ya nchi".

"Malango ya Kinyesi" katika Ukuta wa Kusini wa Yerusalemu yawezekana ulikuwa mlango ambapo takataka zote zilichukuliwa nje ya mji.


mavuno/kuvuna

Ufafanuzi

Neno 'mavuno' hurejelea mkusanyiko wa matunda, mazao au mboga zilizoiva au kukomaa kutoka katika mimea iliyokuwa imepanda na kustawishwa. Muda wa mavuno mara kwa mara hutokea mwishoni mwa msimu wa kilimo. Waisraeli walikuwa na 'sherehe za mavuno' au 'sherehe ya ukusanyaji' ili kusherehekea uvunaji wa mazao ya chakula. Mungu aliwaagiza kutoa mazao ya kwanza ya mazao haya kama sadaka kwake. Katika lugha ya picha, neno mavuno laweza kutumika kutumika kurejelea watu wanaomwamini Yesu au kueleza juu ya ukuaji wa kiroho wa mtu. Wazo la mavuno ya mazao ya kiroho hukubaliana na huendana na mfano wa picha wa matunda kama picha ya mwenendo na tabia nzuri.

Mapendekezo ya tafsiri Ni vizuri kutafsiri neno hili pamoja na neno ambalo hutumika mara kwa mara katika lugha husika kurejelea uvunaji wa mazao. Tukio la uvunaji laweza kutafsiriwa kama 'kipindi cha ukusanyaji' au ' kipindi cha ukusanyaji wa mazao' au ' kipindi cha kuchuma matunda' Kitenzi 'kuvuna' chaweza kutafsiriwa kama ' kukusanya' au 'kuchuma' or 'kuweka pamoja.'


mawaa

Ufafanuzi

Neno "mawaa" humaanisha kasoro juu ya mtu au mnyama. Yaweza pia kumaanisha upungufu wa kiroho kwa mtu.


Mawaidha

Ufafanuzi

Neno "mawaidha" linamaana ya kuonya au kumshauri mtu.


Mawindo, kwa mawindo ya

Ufafanuzi

"Mawindo" ni kitu kinachowindwa hasa mnyama anayetumika kwa ajili ya chakula.


mazao ya kwanza

Ufafanuzi

Msemo "mazao ya kwanza" ina maana ya sehemu ya matunda ya kwanza ya mazao na mimea ambayo yalivunwa katika kila majira ya mavuno.

Waisraeli walitoa mazao haya ya kwanza kwa Mungu kama sadaka ya toleo.

Msemo huu unatumika kitamathali katika Biblia kumaanisha mzaliwa wa kiume wa kwanza kuwa mazao ya kwanza ya familia. Yaani, kwa sababu alikuwa mwana wa kiume wa kwanza kuzaliwa katika familia, yeye ndiye aliyekuwa akibeba jina na heshima ya familia.

Kwa sababu Yesu alifufuka kutoka kwa wafu, anaitwa "mzawa wa kwanza" wa waumini wake wote ambao wamekufa lakini ambao hapo baadaye watafufuka.

Waumini katika Yesu pia wanaitwa "wazawa wa kwanza" wa uumbaji wote, kuonyesha faida maalumu na nafasi ya wale ambao Yesu amewakomboa na kuwaita kuwa watu wake.

Mapendekezo ya Tafsiri

Matumizi halisi ya msemo huu yanaweza kutafsiriwa kama "sehemu ya kwanza"


mbawala, paa, paa dume, paa mdogo

Ufafanuzi

Mbawala ni mnyama mkubwa, mwenye madaha, na miguu minne ambaye anaishi katika msitu au milimani. Mnyama wa kiume ana pembe kubwa kichwani mwake.

Msemo wa "paa" una maana ya mbawala wa kike na "paa mdogo" ni jina la mtoto wa paa.

Msemo wa "paa" una maana ya paa wa kiume.

"Paa dume" ni dume wa aina ya "mbawala".

Mbawala wana miguu myembamba na yenye nguvu inayowasaidia kuruka juu na kukimbia kwa kasi.

Nyayo zao ina kwato iliyogawanyika ambayo huwasaidia kutembea au kupanda kwa urahisi kwenye mandhari ya kila aina.


mbegu, manii

Ufafanuzi

Mbegu ni sehemu ya mmea unao oteshwa kwenye ardhi kuzalisha aina moja zaidi ya mmea huo. Pia ina maana kadha ya mafumbo.


mbuzi, mwanakibuzi

Ufafanuzi

Mbuzi ni mnyama wa ukubwa wa kati, mwenye miguu minne ambaye analingana na kondoo na hukuzwa kimsingi kwa ajili ya maziwa yake na nyama. Mtoto wa mbuzi huitwa "mwanakibuzi".

Kama kondoo, mbuzi walikuwa wanyama muhimu wa sadaka, haswa wakati wa Pasaka.

Ingawa mbuzi na kondoo wanaweza kufanana, kuna namna ambavyo wako tofauti.

Mbuzi wanya manyoya ya kukwaruza; kondoo wana sufu.

Mkia wa mbuzi husimama juu; mkia wa kondoo huning'inia chini.

Kondoo mara kwa mara hupenda kukaa katika kundi lake, lakini mbuzi wanajitegemea zaidi na kutembea mbali na kundi lao.

Katika kipindi cha Biblia, mbuzi walikuwa chanzo kikuu cha maziwa Israeli.

Ngozi ya mbuzi ilitumika kwa ajili ya kufunika mahema na kutengeza mifuko ya kubeba divai.

Pote katika Agano la Kale na Jipya, mbuzi alitumika kama ishara ya ukosefu wa utakatifu wa watu, labda kwa sababu ya mazoea yao ya kutangatanga mbali na yule aliyekuwa akiwatunza.

Waisraeli pia walitumia mbuzi kama mfano wa mtu mwenye dhambi. Mbuzi mmoja anapotolewa sadaka, kuhani huweka mikono yake juu ya mbuzi wa pili aliye hai na kumwachilia jangwani kama alama ya mnyama kubeba dhambi ya watu.


mbwa mwitu

Ufafanuzi

Mbwa mwitu ni mnyama mkali, anayekula nyama na anafanana na mbwa.


mchungaji, kuchunga

Ufafanuzi

Mchungaji ni mtu anaye linda kondoo. Kitenzi "kuchunga" ina maana ya kulinda kondoo na kuwapa chakula na maji.


meneja, wakili

Ufafanuzi

Neno "meneja" au "wakili" katika Biblia ya husu mtumishi aliye kabidhiwa jukumu la kutunza mali na biashara.


Methali

Ufafanuzi

Methali ni sentensi fupi zinazoelezea hekima au kweli.


meza

Ufafanuzi

Msemo wa "meza" una maana ya kula au kutumia kwa hali ya fujo.

Kutumia neno hili kwa hisi ya tamathali, Paulo anatahadharisha waumini kutojimeza wao kwa wao, akimaanisha kutojishambulia au kuangamizana wao kwa wao kwa maneno au matendo (Wagalitia 5:15).

Pia katika hisi ya tamathali, msemo "kumeza" mara kwa mara hutumika kwa maana ya "kuangamiza kabisa" kama kuzungumzia juu ya mataifa kumeza mengine au moto kumeza majengo na watu.

Msemo huu pia unaweza kutafsiriwa kama "kumeza kabisa" au "kuangamiza kabisa".


mfalme

Ufafanuzi

Neno "mfalme" linamaanisha mwanamme ambaye ni mtawala mkuu wa mji, jimbo, au nchi.

Mfalme kawaida huchaguliwa kutawala kwa sababu ya uhsiano wake kifamilia na wafalme wa nyuma. Mfalme anapokufa, kawaida mwana wake mkubwa ndiye anayekuwa mfalme mpya. Katika nyakati za zamani, mfalme alikuwa na mamlaka yote juu ya watu katika ufalme wake. Neno "mfalme" halitumiki sana kwa mtu asiye mfalme wa kweli, kama "mfalme Herode" katika Agano Jipya. Katika Biblia, Mungu anajulikana kama mfalme anaye tawala juu ya watu wake. "Ufalme wa Mungu" unamaanisha utawala wa Mungu juu ya watu wake. Yesu aliitwa "Mfalme wa Wayahudi," "mfalme wa Israeli," na "mfalme wa wafalme." Yesu atakaporudi, atatawala kama mfalme wa dunia. Neno hili linaweza kutafsiriwa kama, "mkuu" au "kiongozi kamili" au "mtawala mwenye nguvu." Usemi "mfalme wa wafalme" unaweza kutasiriwa kama "mfalme anayetawala juu ya wafalme wengine wote" au "kiongozi mkuu aliye na mamlaka juu ya viongozi wengine wote."


mgeni, ugeni, mgeni

Ufafanuzi

Msemo, "mgeni" una maana ya mtu anayeishi katika nchi ambayo sio yake.

Katika Agano la Kale, msemo huu haswa humaanisha mtu yeyote ambaye alikuja kutoka kwa kundi tofauti la watu na watu ambao anaishi miongoni mwao.

Mgeni pia ni mtu ambaye lugha yake na utamaduni ni tofauti na ya kwako.

Kwa mfano, Naomi na familia yake alipohama kwenda Moabu, walikuwa wageni kule. Naomi na mkwe wake Ruthu walipohamia Israeli baadaye, Ruthu aliitwa "mgeni" kule kwa saba hakuwa wa Israeli kiasili.

Mtume Paulo aliwaambia Waefeso ya kuwa kabla hawajamjua Kristo, walikuwa "wageni" kwa agano la Mungu.

Mara nyingi, "mgeni" hutafsiriwa kama "mgeni" mtu ambaye hajulikani au hajazoeleka.


mhenga, baba, mababu

Ufafanuzi

Inapotumika kihalisia, msemo "baba" una maana ya mzazi wa kiume wa mtu. Kuna baadhi ya matumizi ya tamathali ya msemo huu.

Misemo "baba" na "babu" hutumika kumaanisha mababu wa mtu fulani au kundi la watu. Hii inaweza kutafsiriwa kama "babu" au "baba wa zamani".

Msemo "baba wa" unaweza kumaanisha kitamathali mtu ambaye ni kiongozi wa kundi la watu wanaohusika au wenye chanzo na kitu. Kwa mfano, katika Mwanzo 4, "baba wa wale wote waishio katika mahema" inaweza kumaanisha "kiongozi wa kwanza wa ukoo wa watu wa kwanza ambao waliishi katika mahema".

Mtume Paulo alijiita kitamathali "baba" wa wale ambao aliwasaidia kuwa Wakristo kupitia kutangaza injili pamoja nao.

Mapendekezo ya Tafsiri

Unapozungumza juu ya baba na mtoto wake halisi, msemo huu unatakiwa kutafsiriwa kutumia neno la kawaida kumaanisha baba katika lugha hiyo.

"Mungu Baba" inatakiwa kutafsiriwa kutumia neno la kawaida la "baba".

Unapomaanisha mababu, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "babu" au "baba wa zamani".

Paulo anapomaanisha mwenyewe kitamathali kuwa baba wa waumini katika Kristo, hii inaweza kutafsiriwa kama "baba wa kiroho" au "baba katika Kristo".

Mara nyingine neno "baba" linaweza kutafsiriwa kama "kiongozi wa ukoo".

Msemo "baba wa uongo wote" unaweza kutafsiriwa kama "chanzo cha uongo wote" au "yule ambaye uongo wote hutokana".


mifugo

Ufafanuzi

Neno "mfugo" linamaanisha wanyama wanaotunzwa kwa ajili ya chakula na mazao mengine ya maana. Aina zingine za mifugo wanafundishwa kuwa wanyama wa kazi.

Aina wa mifugo ni pamoja na kondoo, ng'ombe, mbuzi, farasi, na punda. Katika nyakati za Biblia, utajiri kwa sehemu ulipimwa kwa idadi ya mifudo aliyonayo mtu. Mifugo inatumika kwa kuzalisha vitu kama sufu, maziwa, jibini, vifaa vya ujenzi, na nguo. Hii inaweza pia kutafsiriwa kama "wanyama wa shambani."


milele

Ufafanuzi

Katika Biblia, msemo "milele" una maana ya muda usiofika mwisho. Mara kwa mara hutumika kitamathali kumaanisha, "muda mrefu sana".

Msemo "milele na milele" unasisitiza ya kwamba jambo litakuwepo milele.

Msemo "milele na milele" ni njia ya kuelezea maisha ya milele yakoje. Pia una wazo la muda ambao hauishi.

Mungu alisema ya kwamba ufalme wa Daudi utakuwepo "milele". Hii inamaanisha ukweli ya kwamba uzao wa Daudi Yesu atatawala kama mfalme milele.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "mara zote" au "kutokuwa na mwisho". Msemo, "utadumu milele" unaweza kutafsiriwa kama "kuwepo mara zote" au "hautakoma" au "utaendelea mara zote". Msemo wa kishindo, "milele na milele" unaweza kutafsiriwa kama "kwa mara zote na zote" au "kutomalizika" au "ambayo haifiki mwisho". Ufalme wa Daudi kudumu milele unaweza kutafsiriwa kama, "uzao wa Daudi atatawala milele" au "uzao wangu ataendelea kutawala".


Mimi, Yahwe

Ufafanuzi

Mara nyingi katika Agano la Kale, wakati Mungu akijizungumzia, hutumia jina lake badala ya nomino kiwakilishi.

Kwa mfano, badala ya kusema, "Niheshimu mimi," husema "Mheshimu Yahwe." Kuiweka wazi kuwa ni Mungu anayejizungumzia, ULB kawaida hutafsiri hii kwa kuongezea nomino kiwakilishi kama, "Niheshimu mimi, Yahwe" au "Mimi, Yahwe ninasema." Kwa kuongeza nomino kiwakilishi "mimi", ULB inaashiria kwa msomaji kuwa Mungu ndiye anayezungumza.


Mizabibu

Ufafanuzi

Mizabibu ni bustani kubwa ambayo zabibu zinakua na kulimwa.


Mji mtakatifu

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno mji mtakatifu hurejelea mji wa Yerusalemu. Neno hili hurejelea mji wa zamani Yerusalemu pamoja na Yerusalemu mpya ya mbinguni mahali ambapo Mungu ataishi na kutawala miongoni mwa watu wake. Neno hili laweza kutafsiriwa kwa kuunganisha maneno 'takatifu' na 'mji' tafsiri ambayo imetumika katika tafsiri zote.


mjumbe

Ufafanuzi

Neno, "mjumbe" la husu mtu anaye pewa ujumbe kuwa ambia wengine.


Mkate

Ufafanuzi

Mkate ni chakula kitengenezwacho kutokana na unga uliochanganywa na maji na matuta ili kutengeneza donge. Kisha donge linatengenezwa katika hali ya vipande na kuokwa.


Mkoa, wilaya

Ufafanuzi

Mkoa ni sehemu ya nchi au himaya.


mkono, mkono wa kuume,

Ufafanuzi

Neno 'mkono' limetumika katika Biblia kama lugha ya picha kwa njia mbalimbali Kuweka kitu katika mikono ya mtu fulani inamaana ya kukabidhi kitu hicho. Neno 'mkono' limetumika kurejelea uweza au nguvu ya Mungu na matendo yake. kwa mfano, Mungu anaposema "je si mkono wangu uliyoyafanya haya?" Neno "kabidhi" hurejelea maana ya kuweka kitu katika mkono au utawala wa mtu fulani. Kuweka mikono juu ya mtu fulani mara nyingi huambatana na utoaji wa baraka kwa mtu huyo. Pia kitendo cha 'kuweka mikono" juu ya mtu kinamaanisha kumweka mtu huyo wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu au kwa ajili ya kumwombea mtu huyo uponyaji. Baadhi ya lugha za picha za neno mkono ni: Kunyosha mkono juu ya mtu maana yake ni kumdhuru. ''kumwokoa kutoka katika mkono wa..." ni kumzuia mtu ili asimdhuru mtu mwingine. matumizi mengine ya mkono ni kama: "kunyosha mkono" ina maana ya 'kudhuru' au kuumiza" "kumwokoa mtu mikononi mwa" ina maana ya kumzuia mtu ili asimdhuru mtu mwingine. "kuwa karibu na mkono " kuwa 'karibu' "kuwa mkono wa kuume" humaanisha kuwa 'nafasi'' au ''sehemu ya'' au "upande wa kulia" Maelezo yanayosema "kwa mkono wa'' au ''kupitia mkono'' ina maana kuwa kitendo kimefanya na mtu huyo. kwa mfano, "kwa mkono wa Bwana'' ina maana kuwa Bwana ndiye amefanya tendo hilo. Wakati Paulo anasema " imeandikwa kwa mkono wangu" ina maana kuwa sehemu hii ya barua iliandikwa kwa mkono wake kabisa, badala tu kusema na mtu mwingine akayaandika.

Mapendekezo ya tafsiri. Maelezo haya na tamathali hizi za semi zaweza kutafsiriwa kwa kutumia lugha zingine za picha ambazo zina maana sawa. Au maana inaweza kutafsiriwa kwa kutumia lugha ya moja kwa moja.


mkuki

Ufafanuzi

Mkuki ni silaha ndefu ya mbao yenye ncha kali ya chuma mwishoni inayo tupwa umbali mrefu.


Mkutano, kukusanyika

Ufafanuzi

Mkutano ni kundi la watu wanaokusanyika pamoja kujadili matatizo, kupeana ushauri na kufanya maamuzi.


Mkuu

Ufafanuzi

"Mkuu" ni kiongozi wa muhimu na mwenye nguvu sana katika kundi fulani.


Mkuu, Binti wa Mfalme

Ufafanuzi

Mkuu ni mtoto wa kiume wa mfalme. Binti wa mfalme ni mtoto wa kike wa mfalme.


mkuyu

Ufafanuzi

Mkuyu ni mrefu, mti wa kivuli wenye shina kubwa na lenye matawi mapana.


Mnara

Ufafanuzi

Mnara ni jengo refu kwa umbo ambalo hujengwa kwa ajili ya walinzi kuangalia kama kuna hatari yoyote. Minara hii mara nyingi ilijengwa kwa kutumia mawe.


mnyama

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "mnyama" ni njia nyingine ya kusema "mnyama".


Mnyweshaji

Ufafanuzi

Katika agano jipya "mnyweshaji" alikuwa mtumsihi wa mfalme aliyepewa kazi ya kupeleka kwa mfalme kikombe cha mvinyo, huonja mvinyo na kuhakikisha haujawekewa sumu.


moto

Ufafanuzi

Moto ni joto, mwanga na miale ambayo hutokana pale kitu kinapochomwa.

Kuchoma mbao kwa moto hugeuza mbao kuwa majivu.

Msemo "moto" pia hutumika kitamathali, mara kwa mara kumaanisha hukumu au utakaso.

Hukumu ya mwisho ya wasioamini ipo katika moto wa jehanamu.

Moto hutumika kusafisha dhahabu na vyuma vingine. Katika Biblia, hatua hii hutumika kuelezea jinsi Mungu husafisha watu kupitia mambo magumu ambayo hutokea katika maisha yao.

Msemo "kuwabatiza kwa moto" unaweza kutafsiriwa kama "kukusababisha upitie mateso ili kwamba yakusafishe"


mpagao

Ufafanuzi

Mpagao ni hali ya fikra ambayo mtu yupo macho lakini hatambui yanayo mzunguka kwasababu anaona na kupitia vitu tofauti.


Mpanda farasi

Ufafanuzi

katika nyakati za Biblia, istilahi, ' mpanda farasi walikuwa ni wanaume ambao waliendesha farasi katika vita. Mashujaa walioendesha gari la kukokotwa na farasi waliitwa wapanda farasi, ingawa jina hili hurejelea watu ambao kiuhalisia huongoza farasi. Waisraeli waliamini kuwa kwa kutumia farasi katika vita ilitia mkazo katika nguvu zao kuliko kumtegemea Yahweh, hivyo hawakutumia wapanda farasi sana.. Neno hili laweza kutafsiriwa kama ' waendesha farasi


Mpatanishi

Ufafanuzi

Mpatanishi ni mtu anaye saidia watu wawili au zaidi kusuluhisha malumbano yao au ugomvi baina yao. Ana wasaidia na kuwapatanisha.


mpenzi

Ufafanuzi

Neno "mpenzi" linamaanisha "mtu anayependa." Kawaida hii inamaanisha watu walio katika mahusiano ya kimapenzi.

Neno "mpenzi" linapotumika katika Biblia, kawaida lina maana ya mtu aliye na uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye hajamuoa au kuolewa naye. Huu uhusiano mbaya wa kimapenzi hutumika kwenye Biblia kumaanisha kutokutii kwa Israeli katika kuabudu sanamu, Kwa hiyo neno "wapenzi" pia hutumika kimafumbo kumaanisha sanamu ambazo watu wa Israeli waliabudu. Katika mazingira haya, neno hili linaweza kutafsiriwa kuwa, "wenzi waovu" au "wenzi katika kuzini" au "sanamu." "Mpenzi" wa fedha ni mtu anayeweka msisitizo mkubwa sana kupata fedha na kuwa tajiri. Katika kitabu cha Agano la Kale cha Wimbo ulio Bora, neno "mpenzi" linatumika kwa njia nzuri.


Mpiga mishale

Ufafanuzi

Mpiga mishale ni mtu mwenye ujuzi wa kutumia upinde na mshale kama silaha.


Mrithi

Ufafanuzi

Mrithi ni mtu ambaye kisheria hupoke mali au pesa za mtu aliyekufa. Katika nyakati za Biblia, mrithi mkuu alikuwa ni mtoto wa kwanza ambaye alipokea sehemu kubwa ya mali au pesa za baba yake. Biblia hutumia neno mrithi kama lugha ya picha kumaanisha Wakristo wanapopokea baraka za kiroho kutoka kwa Mungu, baba yao wa kiroho. Kama watoto wa Mungu, Wakristo ni warithi pamoja na Yesu Kristo. Hii inaweza kutafsiriwa kama "warithi wenza.'


Msamaha

Ufafanuzi

"Msamaha" ni kusamehe au kutokumhukumu mtu kwa sababu ya dhambi zake.


mshiriki

Ufafanuzi

Neno "mshiriki" la husu sehemu moja ya mwili au kundi.


Mshita

Ufafanuzi

Mshita ni mti uliopatikana katika nchi ya Kaanani katika nyakati za zamani.


msimamizi

Ufafanuzi

Neno "msimamizi" la husu mtu aliye mwangalizi wa kazi na maendeleo ya watu wengine.


msingi, kuanzishwa

Ufafanuzi

Kitenzi cha "kuanzishwa" ina maana ya kujengwa juu ya au kutokana na kitu. Msingi ni sehemu ya chini ambapo kitu kunajengwa.

Msingi wa nyumba or jengo lazima uwe na nguvu na kutegemewa ili kuimarisha umbo lote.

Msemo "msingi" unawvza kumaanisha mwanzo wa jambo au muda ambao kitu kiliumbwa.

Kwa kitenzi cha kitamathali, waumini katika Kristo wanalinganishwa na jengo ambalo limejengwa juu ya mafunzo ya mitume na manabii, na Kristo mwenyewe kuwa jiwe la pembeni la jengo.

"Jiwe la msingi" lilikuwa jiwe ambalo lililazwa kama sehemu ya msingi. Mawe haya yalijaribiwa kuhakikisha yalikuwa na nguvu ya kutosha kuimarisha jengo kamili.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "kabla ya msingi wa dunia" inaweza kutafsiriwa kama "kabla ya uumbaji wa ulimwengu" au "kabla ya muda ambapo dunia ilianza kuwepo".

Msemo "kujengwa juu ya" inaweza kutafsiriwa kama "kujengwa kwa imara juu ya" au "kujengwa kwa imara kwa".

Kulingana na muktadha, "msingi" inaweza kutafsiriwa kama "msingi imara" au "uimara wa kudumu" au "mwanzo" au "uumbaji"


msonobari

Ufafanuzi

Msemo "msonobari" una maana ya aina ya mti ambao hubaki kijani mwaka wote na una pia zenye mbegu kwa ndani.

Miti wa msonobari pia humaanisha mti wa "kijani" daima.

Katika nyakati za zamani, mbao za msonobari zilitumika kutengenezea vyombo vya muziki na kwa ujenzi wa maumbo kama vile mitumbwi, nyumba, na hekalu.

Baadhi ya mifano ya msonobari iliyotajwa katika Biblia ni msonobari, seda, mvinje na mreteni.


Mtamba/Mfarika wa ng'ombe

Ufafanuzi

Neno Mtamba' lina maana ya ng'ombe jike mkubwa ambaye hajazaa bado.


Mtawala, watawala, tawala

Ufafanuzi

"Mtawala" ni mtu mwenye mamlaka juu ya watu wengine kama vile kiongozi wa dini, ufalme au nchi.


mtego

Ufafanuzi

Neno mtego lina maana ya kifaa kinacho tumika kudaka wanyama na kuwazuia wasitoroke. Katika Biblia, hili neno linatumika kifumbo kueleza kuhusu jinsi dhambi na jaribu ni mitego inayo wanasa watu na kuwadhuru.


mtenda uovu

Ufafanuzi

Msemo "mtenda uovu" ni kumbukumbu ya jumla kwa watu ambao hufanya mambo ya dhambi na maovu.

Inaweza pia kuwa neno la jumla la watu ambao hawamtii Mungu.

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kwa kutumia neno kwa ajili ya "uovu" au "ubaya" na neno kwa ajili ya "kufanya" au "kutengeneza" au "kusababisha" kitu.


Mtende

Ufafanuzi

"mtende" ni mti mrefu wenye matawi marefu, rahisi na yanayosambaa kutoka juu.


Mteserusi

Ufafanuzi

Neno Mteserusi ni jina la aina ya mti ambao ulipatikana kwa wingi katika maeneo ambapo waliishi watu nyakati za Kibiblia.


mtini

Ufafanuzi

Tini ni tunda dogo, laini, tamu ambalo huota juu ya miti. Linapoiva, tunda hili linaweza kuwa na rangi nyingi, ikiwemo kahawia, njano na zambarau.

Mitini inaweza kuota kuwa urefu wa mita 6 na matawi yao makubwa hutoa kivuli kizuri. Tunda hili lina urefu wa sentimita 3-5.

Adamu na Hawa walitumia majani ya mtini kutengeneza mavazi kwa ajili yao baada ya kutenda dhambi.

Mitini inaweza kuliwa mibichi, ikiwa imepikwa, au kukaushwa. Watu pia walikata katika vipande vidogo vidogo na kuzikandamiza kuwa keki kuliwa baadaye.

Katika kipindi cha Biblia, mitini ilikuwa muhimu kama chanzo cha chakula na kipato.

Uwepo wa mitini inayozaa mara kwa mara hutajwa katika Biblia kama ishara ya mafanikio.

Mara kadhaa Yesu alitumia mitini kama mfano wa kufundisha wanafunzi wake kweli za kiroho.


mtumishi, mtumwa, utumwa

Ufafanuzi

Neno "mtumishi" la weza pia maanisha "mtumwa" na kumueleza mtu anaye mfanyia mtu mwingine kazi, iwe kwa uwamuzi au kwa lazima. Muktadha wa maneno yaliyo zunguka yanaweka dhahiri kuwa kama mtumishi au mtumwa ndiye anaye tajwa.


muamuzi, waamuzi

Ufafanuzi

Muamuzi ni afisa aliye teuliwa anaye kuwa kama hakimu anaye amua mambo ya sheria.


muda

Ufafanuzi

Katika Biblia neno "muda" utumika sana kama fumbo kueleza wakati maalumu au kipindi cha muda fulani matukio yametokea. Lina maana sawa na "umri" au "wakati."


muhuri, kutia muhuri

Ufafanuzi

Kutia muhuri kitu ina maana ya kufunga kwa kitu ambacho inafanya ngumu kufungua pasipo kuvunja muhuri.


Mvua ya mawe

Ufafanuzi

Mvua ya mawe ni vipande vidogo vidogo au vikubwa vya maji yaliyoganda ambayo hushuka kutoka mawinguni. Mawe ya Mvua hushuka kutoka mawinguni katika umbo la kama mpira au vipande vya barafu. Mawe haya ya mvua mara nyingi huwa ni madogo madogo, lakini wakati mwingine yanaweza kuwa makubwa yenye upana wa sentimita 20 hivi na uzito wa kilogramu moja hivi. Kitabu cha Ufunuo katika Agano la Jipya kinazungumzia juu ya mawe ya mvua makubwa yenye uzito wa kilogramu 50 hivi ambayo Mungu atayashusha juu ya dunia ili kuhukumu watu waovu katika siku za mwisho.


mwaka linapotumika

Ufafanuzi

Neno "mwaka linapotumika, kwa hali ya kawaida katika Biblia linamaanisha kipindi cha muda wa siku 354. Hii ni kulingana na kalenda inayotumia mfumo wa mwezi unaochukua kuizunguka dunia.


mwalimu,Mwalimu

Ufafanuzi

Mwalimu ni mtu anaye toa taarifa mpya. Waalimu wanasaidiana kupata na kutumia maarifa na ujuzi.


mwamini

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "mwamini" larejerea mtu anayeamini na kumtegemea Yesu Kristo kama Mwokozi.

Maoni ya Kutafasiri.


Mwananchi

Ufafanuzi

Mwananchi ni mtu anayeishi katika mji fulani au nchi au ufalme. Ni mtu ambaye anajulikana ni mkazi wa kisheria wa eneo hilo.


Mwangamizi

Ufafanuzi

Msemo wa "mwangamizi" una maana ya, "mtu anayeangamiza".

Msemo huu unatumika mara kwa mara katika Agano la Kale kama mrejesho wa jumla ya mtu yeyote anayeangamiza watu wengine, kama vile jeshi vamizi.

Mungu alipotuma malaika kuua wana wote wa kiume wa kwanza Misri, malaika huyo alijulikana kama, "mwangamizi wa wana wa kwanza". Hii inaweza kutafsiriwa kama, "yule (au malaika) ambaye alwaua wana wa kiume wa kwanza".

Katika kitabu cha Ufunuo kuhusu nyakati za mwisho, Shetani au roho nyingine chafu inajulikana kama, "Mwangamizi". Yeye ni "yule anayeangamiza" kwa sababu kusudi lake ni kuangamiza na kuharibu kila kitu alichoumba Mungu.


mwenzi

Ufafanuzi

Mwenzi ni mtu anayekwenda na mtu mwingine au mwenye ushirika na mtu mwingine kwa mfano urafiki au ndoa.


mwerezi

Ufafanuzi

"Mwerezi" ni mberoshi mkubwa ambao una rangi nyekundu. Kama miberoshi mingine ina umbo la sonobari na majani kama sindano.


mwezi

Ufafanuzi

Neno "mwezi" linataja kipindi cha kuishia karibia majuma manne. Idadi ya majuma katika kila mwezi yalitofautiana kulingana na matumizi ya kalenda iliyotumika kwamba ilikumia jua au mwezi.


mwezi mpya

Ufafanuzi

Neno "mwezi mpya" katika Biblia ya husu mwezi unapo onekana mdogo, wa mwanga wa fedha. Huu ni mwanzo wa mwezi unapo hama na kuzunguka dunia.


mwiba, mbaruti

Ufafanuzi

Vicha vya miba na mbaruti ni majani matawi yaliyo chongoka au maua. Haya majani haya zalishi matunda au chochote kinacho tumika.


mwizi, wezi, jambazi

Ufafanuzi

Haya maneno "mwizi" na "wezi" yanaeleza kwa jumla watu wanao iba pesa au mali kwa wengine. Neno "jambazi" mara nyingi la eleza mwizi anaye dhuru kimwili au kutishia watu anao waibia.


mwokovu

Ufafanuzi

Neno "mwokovu" la husu kuwa umeokolewa au kukombolewa kutoka kwenye uovu au hatari.


Mzabibu

Ufafanuzi

Mzabibu ni mmea unaopandwa na kukua kwa kutambaa ardhini au kwa kusimamisghwa juu ya mtu au kitu kingine. Katika Biblia neno mzabibu ni tunda pekee lililizalisha zabibu na kutoa mvinyo.


mzaliwa

Ufafanuzi

Neno "mzaliwa" ni fahirisi ya jumla kwa wazao wa kibaiolojia ya watu au wanyama.


mzawa wa kwanza

Ufafanuzi

Msemo "mzawa wa kwanza" una maana ya uzao wa watu au wanyama ambao huzaliwa kwanza, kabla ya wazawa wengine kuzaliwa. Mara kwa mara mzawa wa kwanza

Katika Biblia, "mzawa wa kwanza" humaanisha mzaliwa wa kiume ambaye anazaliwa.

Katika kipindi cha Biblia, mzawa wa kwanza wa kiume alipewa nafasi ya kujulikana na mara mbili ya urithi wa familia yake ya wana wengine.

Mara nyingi ilikuwa mzawa wa kwanza wa kiume wa mnyama ambaye alitolewa sadaka kwa Mungu.

Dhana hii inaweza kutumika kitamathali. Kwa mfano, taifa la Israeli linaitwa mzaliwa wa kwanza wa Mungu kwa sababu Mungu aliwapa faida maalumu kuliko mataifa mengine.

Yesu, Mwana wa Mungu anaitwa mzawa wa kwanza wa Mungu kwa sababu ya umuhimu wake na mamlaka juu ya kila mtu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Pale ambapo "mzaliwa wa kwanza" inajitokeza katika maandishi pekee, inaweza kutafsiriwa kama "mzawa wa kiume wa kwanza" kwa maana ndiyo kile kinachokusudiwa.


mzeituni

Ufafanuzi

Mzeituni ni mdogo, tunda la mviringo kutoka mti wa mzeituni, ambayo uota maeneo yanayo zunguka Bahari ya Mediterenia.


mzigo

Ufafanuzi

Mzigo ni kitu kizito. Kwa uhalisia inamaanisha uzito wa kitu ambacho mnyama wa kazi angeweza kubeba. Neno "mzigo" pia linamaana kadhaa za kimafumbo:


nabii wa uongo

Ufafanuzi

Nabii wa uongo ni mtu ambaye hudai kimakosa ya kwamba ujumbe wake unatoka kwa Mungu.

Tabiri za manabii wa uongo mara kwa mara hazitimiliki. Yaani, haziji kuwa kweli.

Manabii wa uongo hufundisha ujumbe ambao kwa juu juu au kwa ukamili hupingana na kile ambacho Biblia husema.

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "mtu ambaye hudai kwa uongo ya kuwa ni msemaji wa Mungu" au "mtu ambaye hudai kimakosa kuzungumza maneno ya Mungu".

Agano Jipya hufundisha ya kwamba kipindi cha mwisho kutakuwa na manabii wengi wa uongo ambao watajaribu kudanganya watu kufikiri ya kwamba wanatoka kwa Mungu.


nafaka

Ufafanuzi

Msemo "nafaka" mara nyingi ulimaanisha mbegu ya mmea wa chakula kama vile ngano, shayiri, mahindi, mtama, au mchele. Inaweza pia kumaanisha mmea wote.

Katika Biblia, nafaka kuu ambayo inazungumziwa ni ngano na shayiri.

Vichwa vya nafaka ni sehemu ya mmea ambao hushikilia nafaka.

Kumbuka ya kwamba baadhi ya tafsiri za zamani za Biblia hutumia neno "mahindi" kumaanisha nafaka kwa ujumla. Hata hivyo katika lugha ya Kiingereza ya sasa, "mahindi" humaanisha aina moja ya nafaka tu.


Najisi

Ufafanuzi

Kukinajisi kitu inamaana ya kufanya jambo kwa namna ya unajisi au kutokukiheshimu kitu ambacho ni kitakatifu.


najisi, kunajisiwa

Ufafanuzi

Msemo wa "najisi" na "kunajisiwa" ina maana ya kuchafuliwa au uchafu. Kitu kinaweza kunajisiwa kihalisia, kimaadili au kwa kaida za dini.

Mungu aliwaonya Waisraeli wasijinajisi kwa kula au kugusa vitu ambavyo vimewekwa wakfu kuwa "chafu" au "kiovu".

Baadhi ya vitu kama maiti na magonjwa ya kuambukiza vilitamkwa na Mungu kuwa vichafu na vinaweza kunajisi mtu iwapo atavigusa.

Mungu aliwaamuru Waisraeli kuacha uasherati. Hivi vingewatia unajisi na kuwafanya kutokubalika kwa Mungu.

Pia kulikuwa na aina kadhaa ya hatua za kimwili ambazo zilimnajisi mtu kwa muda mfupi hadi atakapokuwa safi kwa kaida za dini tena.

Katika Agano Jipya, Yesu alifundisha ya kwamba mawazo ya dhambi na matendo ndiyo haswa yanayomnajisi mtu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo wa "najisi" unaweza kutafsiriwa kama "kusababisha kuwa chafu" au "kusababisha kuwa muovu" au "kusababisha kutokubalika kwa kaida za dini".

"Kunajisiwa" kunaweza kutafsiriwa kama "kuwa mchafu" au "kusababisha kutokubalika kimaadili"


ndara

Ufafanuzi

Ndara ni kiatu chenye soli bapa kilicho shika mguu na kamba iliyo zunguka mguu au kisigino. Ndara zinavaliwa na wanaume na wanawake.


ndoto

Ufafanuzi

Ndoto ni kitu ambacho watu huna au kupitia akilini mwao wanapokuwa wamelala.

Ndoto mara kwa mara huonekana kama zinatokea kihalisia, lakini haziko hivyo.

Mara nyingine Mungu husababisha watu kuota juu ya kitu ili waweze kujifunza kutoka na hicho kitu. Pia anaweza kuzungumza moja kwa moja na watu ndani ya ndoto zao.

Katika Biblia, Mungu alitoa ndoto maalumu kwa baadhi ya watu kuwapa ujumbe, mara nyingi kuhusu jambo ambalo lingetoke hapo baadaye.

Ndoto ni tofauti na maono. Ndoto hutokea wakati mtu amelala, lakini maono mara kwa mara hutokea wakati mtu yupo macho.


Neno

Ufafanuzi

Neno ni kitu ambacho mtu husema.


Neno la kweli

Ufafanuzi

"Neno la kweli" ni njia nyingine ya kuelezea neno la Mungu au mafundisho yake.


ng'ombe

Ufafanuzi

"ng'ombe" lina husu aina ya mifugo waliyo fundishwa kulima mazao.


Ng'ombe, fahali, ndama, mifugo

Ufafanuzi

Mifugo ni kundi kubwa la wanyama wenye miguu minne wanaokula majani na hufugwa kwa ajili ya maziwa na nyama.


Ngamia

Ufafanuzi

Ni mnyama mkubwa mwenye miguu minne na mwenye nundu moja au mbili mgongoni.


Ngano

Ufafanuzi

Ngano ni aina ya nafaka ambayo watu huzalisha kwa ajili ya chakula. Biblia inapotaja ngano au mbegu inazungumza juu ya nafaka ya ngano au mbegu.


ngao

Ufafanuzi

Ngao ni chombo kinacho shikiliwa na mwanajeshi katika pambano kuweza kujilinda hasiumizwe na silaha za maadui.


ngome, kimbilio

Ufafanuzi

Maneno "ngome" na "kimbilio" yote ueleza maeneo yaliyo lindwa dhidi ya shambulio na maadui wanajeshi.


ngumu, ugumu, fanya - gumu

Ufafanuzi

Neno 'ngumu' lina maana nyingi sana kutegemea na muktadha. Mara nyingi hueleza kuwa kitu fulani ni kigumu, kuvumilia au kutotoa/kutozaa. Maelezo kama "moyo mgumu" au " kichwa kigumu" inarejelea watu wakaidi wasiotubu. Maneno haya yanaongelea watu wanaoendelea kumwasi Mungu. Lugha ya picha ya maneno 'ugumu wa moyo" na "ugumu wa mioyo yao' yana maana pia ya kuwa na kiburi na uasi. Kama moyo wa Mtu umefanywa 'kuwa mgumu' hii ina maana kuwa mtu huyo anakataa kumtii na kubaki kuwa mkaidi asiyetaka kutubu. Neno moyo likitumika kama kielezi " kwa moyo" likimaanisha kufanya kazi kwa nguvu na kwa juhudi ili kufanya kitu vizuri.

Mapendekezo ya tafsiri Neno ' -gumu"laweza kufasiriwa kama 'ukaidi' au "ugumu' au 'changamoto' kwa kutegemea na muktadha. Maneno kama 'ugumu' au 'ugumu wa moyo'' .yanaweza kutafsiriwa kama " ukaidi' au kudumu katika uasi' au 'mtazamo wa uasi' au ' uasi' au hali ya kutotubu.
"Usiufanye moyo wako kuwa mgumu" inaweza kufasiriwa kama "usikate kutubu '' au "usiendelee kuasi kwa ukaidi." Maneno kama "kuwatesa watu kwa kazi ngumu" yaweza kutafsiriwa kama "lazimisha watu kufanya kazi ngumu kwa kiwango cha kuwatesa au kusababisha mateso kwa watu kwa kuwalazimsha kufanya kazi ngumu. "kazi ngumu" neno hili huhusishwa zaidi na kazi ngumu au ugumu anaokutana nao mwanamke katika kipindi cha kujifungua mtoto.


nguo ya gunia

Ufafanuzi

Nguo ya gunia ilikuwa ya kukwaruza, nguo iliyo tengenezwa kwa nywele ya mbuzi au nywele ya ngamia.


Nguruwe

Ufafanuzi

Mguruwe ni mnyama mwenye mihuu minne anayefugwa kwa ajili ya nyama. Nyama yake inaitwa nyama ya nguruwe.


nguva

Ufafanuzi

Neno "nguva" ni mnyama mkubwa wa baharini anaye kula nyasi na mimea mingine katika sakafu ya bahari.


nguzo ya mlango

Ufafanuzi

"Nguzo ya mlango" ni mhimili ulio wima katika pande zote za mlango, ambao unategemeza kiunzi cha mlango cha juu.

Kabla tu Mungu hajawasaidia Waisraeli kutoroka kutoka Misri, aliwaelekeza kuua mwanakondoo na kuweka damu yake juu ya nguzo za milango.

Katika Agano la Kale, mtumwa aliyetamani kumtumikia bwana wake maisha yake yote aliweka sikio lake juu ya nguzo ya mlango wa nyumba ya bwana wake na msumari kupigiliwa katika sikio lake katika nguzo ya mlango.

Hii inaweza kutafsiriwa kama "nguzo ya mbao iliyo katika kila upande wa mlango" au "pande za viunzi vya mlango" au "nguzo za mbao zilizo pande za mlango".


nguzo, safu

Ufafanuzi

"Nguzo" ni nguzo kubwa zilizosimama wima zinazotumika kushikilia paa au sehemu nyingine ya jengo. Jina lingine la nguzo ni safu.


nia

Ufafanuzi

Neno "nia" la husu sehemu ya mtu inayo fikiri na kufanya maamuzi.


Nira

Ufafanuzi

Nira ni kipande cha mbao au chuma kinachowekwa kwa wanyama wawili au zaidi ili kuwaunganisha kwa ajili ya lengo la kuvuta plau au gari.


njaa

Ufafanuzi

Msemo "njaa" una maana ya upungufu mkubwa sana wa chakula katika nchi au eneo lote, mara nyingi kutokana na kutokuwa na mvua ya kutosha.

Mazao ya chakula yanawvza kushindwa kutokana na sababu za asili kama vile ukosefu wa mvua, magonjwa ya mazao, au wadudu.

Upungufu wa chakula pia unaweza kusababishwa na watu, kama vile adui kuangamiza mazao.

Katika Biblia, Mungu mara nyingi huleta njaa kama njia ya kuadhibu mataifa wanapotenda dhambi dhidi yake.

Katika Amosi 8:11 msemo "njaa" unatumika kitamathali kumaanisha kipindi ambapo Mungu aliadhibu watu wake kwa kutozungumza nao. Hii naweza kutafsiriwa kwa neno moja kwa ajili ya "njaa" kwa lugha yako, au kwa msemo kama wa "upungufu mkubwa".


njiwa, ninga

Ufafanuzi

Njiwa na ninga ni aina mbili ya ndege wadogo wa kijivu na kahawia ambao wanafanana. Njiwa mara nyingi hufikiriwa kuwa na rangi iliyo nyepesi, karibu na nyeupe.

Baadhi ya lugha zina majina mawili tofauti kwa ajili yao, wakati wengine wanatumia jina moja kwa wote wawili.

Njiwa na ninga walitumiwa katika sadaka kwa Mungu, hasa kwa watu ambao hawakuweza kununua wanyama wakubwa.

Njiwa mara nyingine huashiria usafi, sio na hatia, au amani.

Kama njiwa au ninga hawajulikani katika lugha ambayo tafsiri inafanywa, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "ndege mdogo, wa kijivu na kahawia anayeitwa njiwa".

Kama njiwa na ninga wote wanawekwa katika mstari mmoja, ni vyema kutumia maneno mawili tofauti kwa ndege hawa, ikiwezekana.


nuru

Ufafanuzi

Kuna matumizi kadhaa ya kimafumbo ya neno "nuru" katika Biblia. Mara nyingi inatumika kama sitiari ya haki, utakatifu, na ukweli.

Yesu alisema, "Mimi ni nuru ya ulimwengu" kumaanisha kuwa analeta ujumbe wa kweli wa Mungu duniani na kuwaokoa watu kutoka kwenye giza la dhambi zao. Wakristo wanaamriwa "kutembea nuruni," ambayo inamaanisha wanatakiwa kuishi jinsi Mungu anavyotaka waishi na kuacha kutenda maovu. Mtume Paulo alisema kuwa "Mungu ni nuru," na hakuna giza ndani yake. Nuru na giza ni tofauti kabisa. Giza ni ukosefu wa nuru. Yesu alisema kuwa yeye "ni nuru ya ulimwengu" na kwamba wafuasi wake wanapaswa kung'aa kama nuru duniani, kwa kuishi kwa naamna inayoonesha ukubwa wa Mungu. "Kutembea nuruni" inaonesha kuishi njia inayompendeza Mungu, kufanya yaliyo mema na sawa. Kutembea gizani inaonesha kuishi kwa kuasi dhidi ya Mungu, kufanya mambo maovu.


nyakuliwa, nyakuliwa pamoja

Ufafanuzi

Neno "nyakua" mara nyingi linamrejea Mungu akimchukua mtu juu mbinguni ghafula, katika njia ya muujiza.


nyenyekea, kwa unyenyekevu

Ufafanuzi

Neno "nyenyekea" mara nyingi umanisha kumueka mtu chini


nyoka

Ufafanuzi

Neno "nyoka" la husu


Nyumba

Ufafanuzi

Istilahi 'nyumba' hutumika kama tamathali ya semi (mfano) katika Biblia. Mara nyingine hutumika kumaanisha 'kaya' kurejelea watu wanaoishi pamoja katika nyumba. Mara zote neno 'nyumba' humaanisha wazao au watoto au ndugu wengine. Mfano, nyumba ya Daudi huwa na maana ya uzao wa Daudi. Maneno kama 'nyumba ya Mungu' au 'nyumba ya Yahweh' huwa na maana ya hekalu au hema la kukutania au sehemu Mungu alipo. Katika Waebrania 3, "Nyumba ya Mungu" ni sitiari ikimaanisha Watu wa Mungu. Kifungu cha maneno ' nyumba ya Israeli" kwa ujumla huwa na maana ya taifa laote la Israeli au hasa hasa kwa makabila ya ufalme wa Kasikazini wa Israeli.

Mapendekezo ya tafsiri kwa kutegemeana na muktadha, neno, nyumba linaweza kuwa na maana ya 'kaya' ' watu, familia, uzao, hekalu au sehemu ya kukaa.'' "Nyumba ya Daudi' in maana ya ''ukoo wa Daudi, familia ya Daudi au uzao wa Daudi. "Nyumba ya Israeli' ina maana ya watu wa Israeli au wazao wa Israeli au waisraeli. 'Nyumba ya Yahweh' ina maana ya hekalu au sehemu ya kumwabudia Mungu.


nyumba ya ghala

Ufafanuzi

"nyumba ya ghala" ni jengo kubwa linalo tumika kuhifadhi chakula au vitu vingine, mara nyingi kwa muda mrefu.


nzige

Ufafanuzi

Neno "nzige" linamaanisha aina kubwa ya panzi anayepaa ambaye wakati mwingine hupaa katika makundi makubwa ambayo huleta madhara makubwa, wakila mboga zote njiani.

Nzige na panzi wengine ni wakubwa, wenye mabawa yaliyo wima na miguu ya nyuma mirefu inayowapa uwezo wa kuruka mbali. Katika Agano la Kale, makundi ya nzige yanazungumziwa kimafumbo kama alama au picha ya uharibifu mkubwa utakaokuja kama matokeo ya kutokutii kwa Israeli. Mungu alituma nzige kama moja ya mapigo kumi dhidi ya Wamisri. Agano Jipya linasema kuwa nzige walikuwa chanzo kikubwa cha chakula cha Yohana mbatizaji alipokuwa akiishi jangwani.


Onyo

Ufafanuzi

Onyo ni kitu ambacho kinawatahadharisha watu juu ya jambo fulani ambalo linaweza kuwadhuru. "kuonywa" ni kuambiwa juu ya jambo fulani la hatari.


Pagani

Ufafanuzi

Katika nyakati za Biblia neno "pagani" lilitumika kuwaelezea watu ambao waliabudu miungu ya uongo badala ya Bwana.


panda, mpandaji, mmea

Ufafanuzi

"kupanda" ina maana kuweka mbegu kwenye ardhi ilikuweza kuotesha mimea. "Mpandaji" ni mtu anaye mpanda au kupanda mbegu.


Pazia

Ufafanuzi

Katika Biblia pazia ni kitu kinene, chenye nyenzo nzito kinachotumika kutengenezea maskani na hekalu.


Pembe, Mapembe

Ufafanuzi

Mapembe ni sehemu za juu katika kichwa cha mnyama zilizo ngumu, za kudumu na zilizochongoka. Wanyama wa aina nyingi huwa na mapembe, wanyama kama ng'ombe, kondoo, mbuzi, swala n.k. Pembe la kondoo dume lilitumika kutengeneza chombo cha muziki kilichoitwa 'sofari' ambacho kilipulizwa katika matukio maalumu ya sikukuu za kidini. Mungu aliwaambia waisraeli kutengeneza pembe nzuri katika kila kona ya madhabahu ya uvumba. Neno pembe wakati mwingine lilitumika kurejelea chupa iliyokuwa imetengenezwa kwa muundo kama pembe na ilitumika kwa ajili ya kutunza maji au mafuta. Chupa hii ilitumika katika kuwatia mafuta wafalme kama vile Samweli alivyofanya kwa Daudi. Neno hili inabidi litafsiriwe kwa neno tofauti na tarumbeta. Neno hili 'lpembe' hutumika pia kama lugha ya picha kumaanisha ' nguvu, uwezo, na mamlaka


pepeta, chekecha

Ufafanuzi

"Pepeta" na "chekecha" ni kutenganisha ngano na makapi. Katika Biblia maneno yote mawili yametumika yakimaanisha kutenganisha au kuwagawa watu.


Pigo

Ufafanuzi

Mapigo ni matukio yanayosababisha mateso au kifo kwa idadi kubwa ya watu. Mara nyingi pigo laweza kuwa magonjwa yanayosambaa kwa haraka na kusababisha watu wengi kufa kabla ya kuweza kudhibitiwa.


Plau

Ufafanuzi

"Plau" hiki i kifaa cha shambani kinachotumika kuvunjavunja udongo na kuandaa shamba kwa ajili ya kupanda.


Ponya, tibu

Ufafanuzi

Maneno 'ponya' na 'tibu' yote mawili yana maana ya kumfanya mtu aliye mgonjwa, aliyejeruhika na asiyejiweza (mlemavu) kuwa na afya nzuri tena. Mtu aliyeponya au kutibiwa amekuwa amefanywa mzima na mwenye afya nzuri tena. Uponyaji waweza kutokea tu kiuasilia bila kutumia kitu chochote, hii ni kwasababu Mungu alitupa miili yenye uwezo wa kupona na kurudia hali yake ya kawaida hata kama ina vidonda au magonjwa ya aina mbalimbali. Aina hii ya uponyaji hutokea polepole. Hata hivyo hali zingine kama kuwa upofu au ulemavu, na magonjwa mengine kama ukoma hayawezi kupona menyewe tu. Wakati watu wenye magonjwa kama haya wanapoponywa huwa ni muujiza ambao hautokei mara kwa mara. Kwa mfano, Yesu aliponya watu wengi walikuwa vipofu, vilema na wagonjwa na wakapona hapo hapo. Mitume pia waliponya watu kwa miujiza, kwa mfano Petro alimfanya mlevu aweze kutembea mara hiyo.


pukuta, pukuchua

Ufafanuzi

Maneno "pukuta" na "pukuchua" yanaeleza sehemu ya kwanza ya gawanya nafaka ya ngano kutoka kwenye mmea wa ngano.


Pumzika

Ufafanuzi

Pumzika inamaana ya kuacha kufanya kazi kwa nia ya kupumzika na kupata nguvu.


punda, nyumbu

Ufafanuzi

Punda ni mnyama wa kazi mwenye miguu minne, anayefanana na farasi, lakini mdogo kidogo na mwenye masikio marefu zaidi.

Nyumbu ni uzao tasa atokanaye na punda dume na farasi jike.

Nyumbu ni wanyama wenye nguvu sana na kwa hiyo ni wanyama wa kazi wenye thamani sana.

Punda na nyumbu wote wanatumika kubeba mizigo na watu wanaposafiri.

Katika kipindi cha Biblia, wafalme huendesha punda katika wakati wa amani, kuliko farasi, ambaye alitumika katika kipindi cha vita.

Yesu aliendesha kuingia Yerusalemu juu ya punda mdogo wiki moja kabla hajasulubiwa kule.


Ripoti

Ufafanuzi

Ripoti inamaana kuwaambia watu kuhusu kitu kilichotokea kutoa habari juu ya tukio hilo. Ripoti yaweza kutamkwa au kuandikwa.


Rudi

Ufafanuzi

Neno "rudi" linamaanisha kurudi au kurudisha kitu.


rushwa

Ufafanuzi

Neno "rushwa" inamaanisha kumpa mtu kitu cha thamani, kama pesa, kumshawishi afanye jambo bila uaminifu.


Rushwa

Ufafanuzi

Rushwa ni hali ambayo watu wameharibika,hawana maadili na sio waaminifu.


saa

Ufafanuzi

Neno "saa" linatumika mara kwa mara katika Biblia kuonesha muda wa siku jambo fulani lilipotendeka. Pia linatumia tamathari kumaanisha "wakati" au "kitambo"


Saa

Ufafanuzi

Pamoja na kutumika kuonesha wakati au muda gani jambo lilitokea, neno 'saa' hutumika kwa namna nyingi kimfano kama tamathali za semi. Wakati mwingine 'saa' hutumika kuonesha muda maalumu uliopangwa, kwa mfano 'saa ya maombi.' Wakati maandiko yanaposema kuwa saa imefika kwa Yesu kuteswa na kuuawa, ilikuwa na maana ya muda maalumu uliowekwa ambao MUngu alikuwa ameukusudia muda mrefu uliopita kuwa ungetokea. Neno 'saa' laweza kutumika pia kumaanisha 'kitambo' au 'wakati huo' Kifungu kinapozungumzia " saa kuchelwa" in maana kwamba ' ilichelewa katika siku wakati juu lingelikuwa linazama upesi'

Mapendekezo ya tafsiri Neno 'saa' linapotumika kimfano laweza kuwa na maana ya 'muda' kitambo' au 'wakati ulioteuliwa.' Virai kama "katika saa ile" au ''saa ile ile'' vyaweza kutafsiriwa kama "kitambo kile'' au ''muda ule'' au mara'' au '' ghafla'' au ''hapo hapo'' Maelezo kuwa '' saa ilichelewa'' yana maana ya '' ilichelewa katika siku''


Sadaka

Ufafanuzi

"Sadaka" yaweza kuwa ppesa, chakula au chochote ambacho masikini anaweza kupewa kama msaada.


Sadaka ya amani.

Ufafanuzi

Sadaka ya amani ilikuwa moja ya sadaka ambayo Mungu aliwaamuru Waisraeli watoe. Mara nyingine iliitwa sadaka ya shukrani au sadaka ya ushirika.


sadaka ya dhambi

Ufafanuzi

"sadaka ya dhambi" ilikuwa moja ya dhabihu ambazo Mungu aliamuru Waisraeli kutoa.


sadaka ya hatia

Ufafanuzi

Sadaka ya hatia ilikuwa sadaka ambayo Mungu alihitaji kwa Waisraeli kufanya kama walifanya jambo kwa bahati mbaya kibaya kama vile kutomheshimu Mungu au kuharibu mali ya mtu mwingine.

Sadaka hii ilihusisha kutoa mnyama na kulipa faini, kwa pesa ya fedha au dhahabu.

Kwa kuongeza, mtu mwenye kosa alikuwa na wajibu wa kulipa kwa uharibifu wowote ambao ulifanyika.


sadaka ya kinywaji

Ufafanuzi

Sadaka ya kinywaji kilikuwa sadaka kwa Mungu amabyo ilihusisha kumwaga divai juu ya madhabahu. Mara kwa mara ilitolewa pamoja na sadaka ya kuteketeza na sadaka ya mazao.

Paulo anamaanisha maisha yake kama kumwagwa nje kama sadaka cha kinywaji. Hii ina maana ya kwamba aliwekwa wakfu kabisa kumtumikia Mungu na kuwaambia watu juu ya Yesu, hata kama alijua angeteseka na labda kuuwawa kwa sababu ya hiyo.

Kifo cha Yesu juu ya msalaba kilikuwa sadaka ya kinywaji ya mwisho, na damu yake ilimwagwa juu ya msalaba kwa ajili ya dhambi zetu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia nyingine ya kutafsiri msemo huu unaweza kuwa, "saaka ya divai ya mizabibu".

Paulo anaposema anakuwa "anamwagwa kama sadaka" hii inaweza kutafsiriwa kama, "nimejikabidhi kufundisha ujumbe wa Mungu kwa watu, kama sadaka ya divai inavyomwagwa kabisa juu ya madhabahu".


sadaka ya kujitolea

Ufafanuzi

Sadaka ya kujitolea ilikuwa aina ya sadaka kwa Mungu ambayo haikuhitajika kwa Sheria ya Musa. Ilikuwa ni uchaguzi binafsi wa mtu kutoa sadaka hii.

Kama sadaka ya kujitolea ilikuwa mnyama wa kutolewa sadaka, mnyama aliruhusiwa kuwa na kasoro chache kwa kuwa ilikuwa sadaka ya kujitolea.

Waisraeli walikula wanyama waliotolewa sadaka kama sehemu ya sherehe ya karamu.

Pale ambapo sadaka ya kujitolea inaweza kutolewa, hii ilikuwa sababu ya kufurahia kwa Israeli kwa kuwa ilionyesha ya kwamba mavuno yalikuwa mazuri ili kwamba watu wawe na chakula kingi.

Kitabu cha Ezra kinaelezea aina tofauti ya sadaka ya kujitolea ambayo ililetwa kwa kujenga tena hekalu. Sadaka hii ilijumuisha pesa ya dhahabu na fedha, pamoja na mabakuri na vyombo vingine vilivyoundwa kwa dhahabu na fedha.


Sadaka ya kuteketezwa

Ufafanuzi

"Sadaka ya kuteketezwa" ilikuwa ni aina ya sadaka iliyotolewa kwa Mungu kwa njia ya moto juu ya madhabahu. Ilitolewa ili kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu. Hii pia ilikuwa ikiitwa "toleo kwa njia ya moto."


sadaka ya mlo

Ufafanuzi

"Sadaka ya mlo" ilikuwa dhabihu ya Mungu katika umbo la nafaka au mkate uliyo tengenezwa kwa unga.


sadaka ya nafaka

Ufafanuzi

Sadaka ya nafaka ilikuwa zawadi ya unga wa ngano au shayiri iliyotolewa kwa Mungu, mara nyingi baada ya sadaka ya kuteketeza.

Nafaka iliyotumika kwa ajili ya sadaka ya nafaka ilitakiwa kuwa safi kutoka ardhini. Mara nyingi ilipikwa kabla ya kutolewa, lakini muda mwingine iliachwa bila kupikwa.

Mafuta na chumvi yaliongezwa kwa unga wa nafaka, lakini hamira au asali haikuruhusiwa.

Sehemu ya sadaka ya nafaka ilichomwa na sehemu yake kuliwa na makuhani.


sadaka ya ushirika

Ufafanuzi

Katika Agano la Kale, "sadaka ya ushirika" ilikuwa aina ya sadaka ambayo ilitolewa kwa sababu tofauti, kama vile kutoa shukrani kwa Mungu na kutimiza kiapo.

Sadaka hii ilihitaji sadaka ya mnyama, ambaye alikuwa wa kiume au kike. Hii ilikuwa tofauti na sadaka ya kuteketeza ambayo ilihitaji mnyama wa jinsia ya kiume.

Baada ya kutoa sehemu ya sadaka kwa Mungu, mtu aliyeleta sadaka ya ushirika aligawana nyama na makuhani na Waisraeli wengine.

Kulikuwa na mlo unaohusishwa na sadaka hii ambayo hujumuisha mkate usiotiwa chachu.

Hii mara zingine unaitwa "sadaka ya amani"


salfa

Ufafanuzi

Salfa ni kitu chenye rangi ya njano kinacho kuwa kimiminiko kinacho waka moto kinapo chomwa.


sanamu, waabudu sanamu

Ufafanuzi

Sanamu ni kitu ambacho watu hutengeza ili waiabudu. Kitu kinaitwa "kuabudu sanamu" kama kinahusisha kutoa heshima kwa kitu tofauti na Mungu wa kweli.

Watu hutengeneza sanamu kuwakilisha miungu ya uongo wanayo abudu. Miungu hii ya uongo haiko hai; hakuna Mungu tofauti na Yahwe. Wakati mwingine mapepo hufanya kazi kupitia sanamu kuifanya ionekane kama vile ina nguvu, licha ya kuwa haina. Sanamu kawaida huundwa kwa vitu vya dhamani kama dhahabu, fedha, shaba, au mbao ya dhamani. "Ufalme unaoabudu sanamu" inamaanisha "ufalme wa watu wanaoabudu sanamu" au "ufalme wa watu wanaoabudu vitu vya duniani." Neno "umbo la waabudu sanamu" ni neno lingine kwa ajili ya "sanamu ya kuchonga" au "sanamu."


Sauti

Ufafanuzi

Sauti hutumika kumaanisha kuongea au kuwasiliana kitu au jambo.


Sehemu za juu

Ufafanuzi

Maneno 'sehemu za juu' yanarejelea madhabahu na maeneo matakatifu yaliyokuwa yakitumika katika kuabudu miungu. Mara zote maeneo haya yalikuwa sehemu za juu kama vile milimani au sehemu za vilima. Wafalme wengi wa Israeli walitenda dhambi kinyume na Mungu kwa kujenga madhabahu kwa ajili ya miungu katika sehemu hizi za juu. Hii iliwafanya watu kujishughulisha kwa undani katika ibada ya miungu. Wakati mfalme aliyemcha Mungu, alipoanza kutawala juu ya Yuda au Israeli, mara kwa mara waliweza kuonda sehemu hizi za juu na madhabahu ili kuzuia ibada za hizi miungu. Hata hivyo, baadhi ya wafalme wazuri hawakuwa makini sana na hawakuziondoa sehemu hizi za juu, na matokeo yake taifa lote la Israeli liliendelea kuabudu miungu.

Mapendekezo ya tafsiri Namna nyingine ya kutafsiri maneno haya twaweza kusema, " maeneo/sehemu iliyoinuliwa kwa ajili ya ibada ya miungu' au 'kilele cha mlima cha ibada ya miungu.' Hakikisha kuwa maneno unayoyatumia yawe na maana ya madhabahu ya miungu na siyo tu maeneo ya juu zilipo madhabahu hizo.


sela

Ufafanuzi

Neno "sela" ni la Kiebrania lililopo sana katika kitabu cha Zaburi. Lina maana kadhaa.


sensa

Ufafanuzi

Neno "sensa" lilitumika kuhesabu kawaida hesabu ya watu katika taifa au ufalme.


shaba

Ufafanuzi

Neno "shaba" linamaanisha aina ya madini yatengenezwayo kwa kuyeyusha kwa pamoja metali, shaba nyekundu na bati. Ina rangi nyeusi inayoelekea njano, nyekundu kiasi.


shahidi wa uongo, shahidi aliyepotoka, ushuhuda wa uongo, taarifa ya uongo

Ufafanuzi

Misemo ya "shahidi wa uongo" na "shahidi aliyepotoka" ina maana ya mtu anayesema vitu vya uongo juu ya mtu au tukio, mara kwa mara katika mahala rasmi kama mahakamani.

"Ushuhuda wa uongo" au "taarifa ya uongo" ni uongo halisia ambao unaambiwa.

"kutoa ushahidi wa uongo" ina maana ya kudanganya au kutoa taarifa ya uongo kuhusu jambo.

Biblia hutoa habari kadhaa ambapo mashahidi wa uongo waliajiriwa kudanganya kuhusu mtu ili kumfanya mtu huyo kuadhibiwa au kuuwawa.

Mapendekezo ya Tafsiri

"Kuwa shahidi wa uongo" au "kutoa ushahidi wa uongo" unaweza kutafsiriwa kama "kushuhudia uongo" au "kutoa taarifa ya uongo juu ya mtu" au "kuzungumza uongo dhidi ya mtu" au "uongo".

Pale ambapo "shahidi wa uongo" ina maana ya mtu, inaweza kutafsiriwa kama "mtu anayedanganya" au "mtu anayeshuhudia uongo" au "mtu anayesema mambo ambayo siyo ya kweli".


shahidi, Shahidi

Ufafanuzi

Shahidi ni mtu ambaye amepata uzoefu binafsi wa kitu kilichotokea. Maranyingi shahidi ni mtu anayetoa ushahidi wa jambo analijua kuwa ni kweli. Shahidi pia aneweza kuwa mtu aliyekuwepo pale na kuona kilichotokea.


shayiri

Ufafanuzi

Neno "shayiri" limamaanisha aina ya nafaka iliyokuwa ikitumika kutengeneza mkate.


sheria, kanuni

Ufafanuzi

"Sheria" ni amri ambayo kawaida huandikwa chini na kushurutishwa na mtu aliye madarakani. "Kanuni" ni uongozo kwa ajili ya kufanya maamuzi na tabia.

Zote "sheria" na "kanuni" zinaweza kumaanisha amri au imani inayoongoza tabia ya mtu. Maana hii ya "sheria" ni tofauti kwa maana ya kutoka "sheria ya Musa" ambapo inamaanisha amri na maelekezo ambayo Mungu aliwapa Waisraeli. Wakati sheria ya ujumla inapotajwa,"sheria" inaweza kutafsiriwa kama "kanuni" au "amri ya jumla."


Shimo

Ufafanuzi

Shimo ni sehemu yenye kina kwenda chini iliyochimbwa kwenye ardhi.


Shimo lisilo na mwisho

Ufafanuzi

"Shimo lisilo na mwisho" ni shimo kubwa, lenye kina kirefu au pengo lisilo na mwisho.


shingo ngumu, kiburi

Ufafanuzi

Neno "shingo ngumu" ni msemo katika Biblia unao tumika kueleza watu wasio mtii Mungu na wanao kataa kutubu. Wana kiburi na hawata tii mamlaka ya Mungu.


Shinikizo la divai

Ufafanuzi

Katika nyakati za Biblia shinikizo la divai ni vyombo vikubwa au sehemu ya wazi ambapo maji ya zabibu yalitengenezwa na kufanywa kuwa divai.


Shoka

Ufafanuzi

Shoka ni kifaa kinachotumika kukatia miti au mbao.


Shtaki, Mashtaka, Mshtaki

Ufafanuzi

Neno "shtaki au Mashtaka" linamaanisha kumlaumu mtu kwa kufanya jambo baya. Mtu anayeshitaki wengine anaitwa "mshtaki."


shtakio

Ufafanuzi

Neno "shtakiwa" la eleza hali ambayo mtu au kitu kina "jaribiwa."


Shujaa, askari

Ufafanuzi

Shujaa na askari ni mtu anayepigana kwenye jeshi. Lakini pia kuna tofauti kadhaa.


si mcha Mungu, siye na Mungu

Ufafanuzi

Meneno "si mcha Mungu" na "siye na Mungu" ina eleza watu waliyo hasi dhidi ya Mungu. Kuishi kwa uovu, pasipo na wazo la Mungu uitwa "siye mcha Mungu" au "pasipo na Mungu."


si takatifu

Ufafanuzi

Neno "si takatifu" lina maana "kuto kuwa takatifu." Inaelezea mtu au kitu kisicho mtii Mungu.


si wa haki,

Ufafanuzi

Neno "si wa haki" ina maana ya wenye dhambi asiye na maadili.


sifa, mashuhuri

Ufafanuzi

Sifa ni kitendo cha kujulikana na kuwa na sifa.


siku

Ufafanuzi

Neno "siku" kwa kawaida lamaanisha kipindi cha masaa 24 kuanzia kuzama kwa jua. Linatumika pia kitamathari.


sikukuu

Ufafanuzi

Kwa ujumla, sikukuu ni sherehe iliyofanyika na jamii ya watu.

Neno kwa ajili ya "sikukuu" katika Agano la Kale lina maana ya "muda ulioteuliwa".

Sikukuu zinazosherehekewa na Waisraeli zilikuwa nyakati maalumu zilizoteuliwa au nyakati ambazo Mungu aliwaamuru wao kuzifuata.

Katika baadhi ya tafasiri za Kiingereza, neno "sikukuu" linatumika badala ya karamu kwa sababu sherehe zilijumuisha mlo mkubwa wa pamoja.

Kulikuwa na karamu kadhaa ambazo Waisraeli walisherehekea kila mwaka: Pasaka Sikukuu ya Mkate Usiotiwa Chachu Mavuno ya Kwanza Sikukuu ya Wiki (Pentakuki) Sikukuu ya Tarumbeta Sikukuu ya Kulipia Kosa Sikukuu ya Vibanda Kusudi la sikukuu hizi ilikuwa kumshukuru Mungu na kukumbuka mambo ya ajabu aliyofanya kuwaokoa, kuwalinda na kuwapa watu wake.


Silaha

Ufafanuzi

Silaha ni kifaa anachokitumia askari kupigana akiwa vitani na kujilinda dhidi ya maadui. Pia inaweza kutumika kama lugha ya picha ikimaanisha silaha za kiroho.


simba

Ufafanuzi

Simba ni mnyama mkubwa wa porini anayefanana na paka, mwenye meno yenye nguvu na makucha ya kuulia na kurarua mawindo yake.

Simba wana miili yenye nguvu na kasi kubwa ya kushika mawindo yao. Manyoya yao ni mafupi na yana rangi ya mchanganyiko wa kahawa na dhahabu. Simba dume wana manyoya ya shingoni yanayozunguka vichwa vyao. Simba huua wanyama wengine ili kuwala na pia wanaweza kuwa hatari kwa binadamu. Mfalme Daudi alipokuwa mvulana, aliua simba waliojaribu kuvamia kondoo wake aliokuwa akiwachunga. Samsoni pia aliua simba kwa mikono yake.


sio aminifu, kosa uaminifu

Ufafanuzi

Neno "sio aminifu"la eleza watu wasio fanya kile Mungu alicho amuru wafanye. Hali au ktitendo cha kuwa sio aminifu ni "kuso uaminifu."


sio leta faida

Ufafanuzi

Neno "sio leta faida" ina maana ya kuto kuwa na manufaa.


siotahiriwa, kutotahiriwa

Ufafanuzi

Maneno "siotahiriwa" na "kutotahiriwa" ueleza mwanaume ambaye hajatahiriwa kimwili. Haya maneno utumika pia kifumbo.


siri, ukweli uliyo fichika

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "siri" la husu kitu kisicho julikana au kigumu kuelewa ambacho Mungu sasa anaelezea.


stuli ya mguu

Ufafanuzi

Msemo "stuli ya mguu" una maana ya chombo ambacho mtu huweka miguu yake kwa juu, mara nyingi kupumzisha anapokuwa ameketi. Msemo huu pia una maana za tamathali kwa kujishusha na hadhi ya chini.

Watu katika kipindi cha Biblia walichukulia miguu kuwa sehemu yenye heshima ya chini kabisa ya mwili. Kwa hiyo "stuli ya mguu" ilikuwa heshima ya chini zaidi kwa sababu miguu ilipumzishwa juu yake.

Mungu anaposema "Nitawafanya adui zangu stuli ya mguu kwa ajili ya miguu yangu" anatamka nguvu, utawala na ushindi juu ya watu ambao wanaasi dhidi yake. Watashushwa na kushindwa hadi hatua ya kujishusha kwa mapenzi ya Mungu.

"Kuabudu katika stuli ya mguu ya Mungu" ina maana ya kuinama chini katika kuabudu mbele yake anapokuwa amekaa juu ya kiti chake cha enzi. Hii tena inatoa unyenyekevu na kujishusha kwa Mungu.

Daudi anamaanisha hekalu kama "stuli ya mguu" ya Mungu. Hii inaweza kumaanisha mamlaka yake ya hakika juu ya watu wake. Hii inaweza pia kumpiga picha Mungu Mfalme juu ya kiti chake cha enzi, na miguu yake ikupumzika juu ya stuli ya mguu, ambayo inawakilisha kila kilcho chini yake.


Suria

Ufafanuzi

Suria ni mwanamke ambaye ni mke wa pili wa mwanaume ambaye tayari ana mke. Suria mara nyingi sio mke halali wa mwanaume huyo.


taa

Ufafanuzi

Neno "taa" kawaida inamaanisha kitu kinachotoa mwanga. Taa zilizotumika nyakati za Biblia kawaida zilikuwa taa za mafuta. Aina ya taa iliyotumika katika Biblia ni chombo na sehemu ya kuwekea mafuta, yanayotoa mwanga inapowashwa.

Kawaida taa za mafuta zilitengenezwa kwa chombo cha kawaida cha udongo kilichojaa mafuta ya mzeituni, na utambi ukiwekwa kwenye mafuta ili uwake. Kwa baadhi ya taa, chombo lilikuwa na umbo la yai, na sehemu moja ikiwa imefinywa karibu kuushikilia utambi. Taa ya mafuta iliweza kubebwa au kuwekwa katika kinara ili mwanga wake ujaze chumba au nyumba. Katika maandiko, taa zinatumika kwa njia kadhaa kimithali kama ishara ya mwanaga na uhai.


taabu, mataabiko, taabika

Ufafanuzi

Neno "taabu" ina eleza hali ya maisha ambayo ni ngumu na kusumbua. "Kutaabika" ina maanisha kusikia vibaya au kusongwa na mawazo ya jambo.


tafakari

Ufafanuzi

Neno "tafakari" lina maana ya kutumia muda kufiria jambo kwa umakini na undani.


tafsiri, ufafanuzi

Ufafanuzi

Neno "tafsiri" na "ufafanuzi" inamaanisha kuelewa na kufafanua maana ya jambo ambalo haloki wazi.

Mara nyingi Biblia inatumia misemo hii katika kueleza maana za ndoto na maono. Wakati mfalme wa Babeli alipopata ndoto za kuchanganya, Mungu alimsaidia Danieli kuzitafsiri na kufafanua maana zake. "Tafsiri" ya ndoto ni "ufafanuzi" wa maana ya ndoto. Katika Agano la Kale, wakati mwingine Mungu hutumia ndoto kuwafunulia watu kitakachotokea siku za usoni. Kwa hiyo ufafanuzi wa hizo ndoto zilikuwa ni utabiri. Neno "tafsiri" inaweza pia kumaanisha kuelewa maana ya vitu vingine, kama kuelewa hali ya hewa itakuaje kutokana na ubaridi au joto lililopo, upepo uliopo, na anga ilivyo. Njia za kutafsiri neno "tafsiri" ni pamoja na , "kuelewa maana ya" au "kufafanua" au "kutoa maana ya." Usemi "tafsiri" inaweza kutafsiriwa kama "maelezo" au "maana."


tafuta

Ufafanuzi

Neno "tafuta" la maanisha kutafuta kitu au mtu. Inaweza kuwa na maana ya "jaribu kwa bidii" au "tia juhudi" kufanya kitu.


tai

Ufafanuzi

Tai ni ndege mbua mkubwa sana, mwenye nguvu ambaye hula wanyama wadogo kama vile samaki, panya, nyoka na kuku.

Biblia hulinganisha kasi na nguvu ya jeshi kwa jinsi tai hupaa chini kukamata nyama yake kwa kasi na ghafla.

Isaya anasema ya kwamba wale wanaomtumaini Bwana watapaa juu kama tai afanyavyo. Hii ni lugha ya tamathali inayotumika kuelezea uhuru na nguvu ambao unakuja kutokana na kumuamini na kumtii Mungu.

Katika kitabu cha Danieli, urefu wa nywele za Mfalme Nebukadreza zililinganishwa na urefu wa manyoya ya tai, ambayo yanaweza kuwa zaidi ya sentimita 50.


Taifa

Ufafanuzi

Taifa ni kundi kubwa la watu wanao tawaliwa na serikali. Watu wa taifa mara nyingi wa mababu sawa na ni wajamii moja.


Taji, kuvalisha taji

Ufafanuzi

Taji ni pambo la mviringo linalovaliwa kichwani kwa kiongozi wa juu kama mfalme na malkia. Kuvika taji ni kuweka taji juu ya kichwa cha mtu. Au yaweza kuwa na maana ya "kuheshimu."


takatifu

Ufafanuzi

Neno "takatifu" la elezea kitu kinacho husu kumuabudu Mungu au wapagani wanao abudu miungu ya uongo.


takdiri, majaliwa, jaliwa

Ufafanuzi

Msemo wa "takdiri" una maana ya kile kitakachotokea kwa watu hapo baadaye. Kama mtu ana "takdiri" ya jambo, ina maana ya kwamba kile mtu huyo atafanya hapo baadaye kimepangwa na Mungu.

Mungu anapopanga taifa kupatwa na ghadhabu, hii ina maana ya kwamba ameamua au kuchagua kuwaadhibu taifa hilo kwa sababu ya dhambi yao.

Yuda alikuwa na "takdiri" ya kuangamizwa, ina maana ya kwamba Mungu aliamua ya kwamba Yuda angeangamizwa kwa sababu ya kuasi kwake.

Kila mtu ana takdiri ya mwisho, ya milele, moja wapo mbinguni au jehanamu.

Pale mwandishi wa Mhubiri anaposema ya kwamba kila mtu takdiri yake inafanana, anamaanisha ya kwamba kila mtu hatma yake atakufa.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "kupangwa kwa ghadhabu" unaweza pia kutafsiriwa kama "kuamua ya kwamba utaadhibiwa" au "kuamuliwa ya kwamba utapitia ghadhabu yangu".

Msemo wa kitamathali, "wana takdiri ya upanga" inaweza kutafsiriwa kama, "Mungu ameamua ya kwamba wataangamizwa na adui zake ambao watawaua kwa upanga" au "Mungu ameamua ya kwamba adui wao watawaua kwa upanga".

Msemo, "una takdiri ya" inaweza kutafsiriwa kutumia msemo kama, "Mungu ameamua ya kwamba utakuwa"

Kutegemea na muktadha, "takdiri" inaweza kutafsiriwa kama "hitimisho la mwisho" au "kitakachotokea mwishoni" au "kile alichoamua Mungu kitatokea"


Talaka

Ufafanuzi

Talaka ni tendo la kisheria la kusitisha ndoa. Msemo "kutengana" ina maana ya kutengana rasmi na kihalali kutoka kwa mwenzi wa mtu ili kusitisha ndoa.

Maana halisi ya neno "kutengana" ni "kufukuza" au "kuachana rasmi kutoka kwa". Lugha zingine zinaweza kuwa na misemo ya kufanana yenye maana ya talaka.

"cheti cha talaka" kinaweza kutafsiriwa kama, "karatasi inayosema ya kwamba ndoa imefika mwisho".


tamaa

Ufafanuzi

Tamaa ni hamu kubwa sana, mara nyingi katika mazingira ya kutaka kitu kiouvu au kisicho na maadili mema.

Katika Biblia, "tamaa" mara nyingi inamaanisha hamu ya kimwili kwa mtu mwingine tofauti na mme au mke wake. Wakati mwingine neno hili linatumika kimafumbo kumaanisha kuabudu sanamu. Kulingana na mazingira, "tamaa" inaweza kutafsiriwa kama "hamu mbaya" au "hamu kali" au "hamu mbaya ya kimwili" au "hamu kubwa isiyo ya kimaadili mema" au "kuwa na hamu kubwa ya kutenda dhambi." Msemo "kutamani kitu" inaweza pia kutafsiriwa kama "kuwa na hamu vibaya" au " kuwaza kinyume na maadili kuhusu" au "kuwa na hamu mbaya kimaadili."


Tambua

Ufafanuzi

Neno "tambua" lina maana ya kutambua kwa usahihi kitu fulani au mtu.


tambua, tambuzi

Ufafanuzi

Msemo "tambua" una maana ya kuweza kuelewa jambo, haswa kuweza kujua kama jambo ni sahihi au baya.

Msemo wa "tambuzi" una maana ya kuelewa na kuamua kwa hekima kuhusu jambo fulani.

Ina maana kuwa na hekima na maamuzi mazuri.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "tambua" inaweza pia kutafsiriwa kama "kuelewa" au "kujua tofauti kati ya" au "kutofautisha mema na mabaya" au "kuhukumu sahihi kuhusu" au "kuelewa mema kwa mabaya".

"Tambuzi" inaweza kutafsiriwa kama, "uelewa" au "uwezo wa kuchambua mema na mabaya"


tamka, tamko

Ufafanuzi

Msemo wa "tamka" au "tamko" una maana ya kutoa kauli maalumu kwa umma, mara nyingi kusisitiza jambo.

"Tamko" halisisitizi umuhimu tu wa kile kinachotamkwa, lakini inavuta nadhari kwa yule anayetoa tamko hilo.

Kwa mfano, katika Agano la Kale, ujumbe kutoka kwa Mungu mara nyingi hutanguliwa na "tamko la Yahwe" au "hivi ndivyo Yahwe asemavyo". Msemo huu unasisitiza ya kwamba ni Yahwe mwenyewe anayesema hivi. Ukweli ya kwamba ujumbe unatoka kwa Yahwe unaonyesha jinsi ujumbe ulivyo na umuhimu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "tamka" inaweza pia kutafsiriwa kama "tangaza" au "eneza wazi" au "sema kwa nguvu" au "tamka kwa kishindo".

Msemo "tamko" unaweza kutafsiriwa kama, "kauli" au "tangazo".

Msemo, "hili ni tamko la Yahwe" linaweza kutafsiriwa kama, "hivi ndivyo Yahwe anavyotamka" au "hivi ndivyo Yahwe anavyosema".


tanuu

Ufafanuzi

Tanuu ilikuwa joko kubwa sana liyotumika kuchemsha vyombo katika halijoto la juu.

Katika kipindi cha nyuma, tanuu nyingi zilitumika kuyeyusha vyuma kutengeneza vyombo kama vile vyungu vya kupikia, mapambo ya vito, silaha, na sanamu.

Tanuu zilitumika pia kutengeneza vyungu vya udongo.

Mara nyingine tanuu hujulikana kitamathali kufafanua ya kwamba kitu ni cha moto sana.


Tapanya, nyika

Ufafanuzi

Kutapanya kitu ni kukitupa au kutokukitumia kwa hekima. Nchi ambayo ni nyika ni nchi au mji ulioharibiwa ili kitu chochote kisiishi ndani yake tena.


tarumbeta

Ufafanuzi

Neno "tarumbeta" la eleza chombo cha kutoa mziki au kuita watu pamoka kwa mkutano au kikao.


tawanya, mtawanyiko

Ufafanuzi

Msemo "tawanya" na "mtawanyiko" ina maana ya kutawanya watu au vitu katika pande nyingi tofauti.

Katika Agano la Kale, Mungu anazungumza kuhusu "kutawanya" watu, kusababisha wao wajitenge na kuishi katika maeneo tofauti kati yao. Alifanya hivi kuwaadhibu kwa dhambi yao. Huenda kutawanyika ingeweza kuwasaidia kutubu na kuanza kumwabudu Mungu tena.

Msemo "mtawanyiko" unatumika katika Agano Jipya kumaanisha Wakristo ambao walitakiwa kuacha nyumba zao na kuhamia katika mahali tofauti nyingi kutoroka mateso.

Msemo "tawanyiko" unaweza kutafsiriwa kama "waumini katika maeneo mengi tofauti" au "watu waliohama kuishi katika mataifa tofauti".

Msemo "tawanya" unaweza kutafsiriwa kama "kutuma mbali katika maeneo mengi tofauti" au "kusambaza ng'ambo" au "kusababisha kuhamisha mbali kuishi katika nchi tofauti"


teketeza, uharibifu

Ufafanuzi

Msemo wa "kuteketezwa" au "uharibifu" ina maana ya kufanya mali ya mtu au ardhi kuharibika au kuangamizwa. Pia mara kwa mara hujumuisha kuangamiza au kukamata watu waishio katika ardhi hiyo.

Hii ina maana ya maangamizi kamili na makali sana.

Kwa mfano, mji wa Sodoma uliteketezwa na Mungu kama adhabu kwa dhambi za watu walioishi pale.

Msemo "uharibifu" unaweza kujumuisha kusababisha majonzi ya hisia yatokanayo na hiyo adhabu au uharibifu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "teketeza" unaweza kutafsiriwa kama "kuangamiza kabisa" au "kuharibu kabisa".

Kulingana na muktadha, "uharibifu" inaweza kutafsiriwa kama "maangamizi kamili" au "uharibifu kamili" au "majonzi ya juu sana" au "balaa".


Tembea

Ufafanuzi

Neno "tembea" mara nyingi hutumika ikiwa na maana ya "ishi."


teseka, kuteseka

Ufafanuzi

Maneno "teseka" na "kuteseka" yanaeleza kupitia kitu kisicho pendeza, kama ugonjwa, maumivu, au magumu.


tetemeka

Ufafanuzi

Neno "tetemeka" lina maana ya kutikisika kwa hofu au msongamano wa mawazo.


Thamani

Ufafanuzi

"Thamani" ni watu au kitu kinachoonekana kuwa kina ubora.


theluji

Ufafanuzi

Neno "theluji" ya husu chembe nyeupe za maji yaliyo ganda yanayo anguka kutoka mawinguni sehemu ambazo hali ya hewa ni ya baridi.


thibitisha, uthibitisho

Ufafanuzi

Thibitisha au uthibitisho ni kuwa na hakika kuwa jambo fulani ni la kweli au kuaminika.


tia moyo, kutia moyo

Ufafanuzi

Msemo "tia moyo" na "kutia moyo" ina maana ya kusema na kufanya mambo kusababisha mtu kuwa na faraja, matumaini, kujiamini na ujasiri.

Msemo wa kufanana ni "shawishi", ambao una maana ya kumsihi mtu kukataa tendo ambalo ni baya na badala yake kufanya mambo ambayo ni mazuri na sahihi.

Mtume Paulo na waandishi wengine wa Agano Jipya walifundisha Wakristo wajitie moyo wao kwa wao kupendana na kutumikiana.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, njia za kutafsiri "tia moyo" zinaweza kujumuisha, "kusihi" au "kufariji" au "kusema vitu vya upole" au "kusaidia na kuimarisha".

Msemo, "toa maneno ya faraja" una maana ya "kusema mambo ambayo yatasababisha watu wengine kujisikia kupendwa, kukubalika, na kuwezeshwa".


tia utumwani, katika kifungo

Ufafanuzi

"Kutia utumwani" mtu ina maana ya kumlazimisha mtu huyo kumtumikia bwana au nchi tawala. "Kutiwa utumwani" au "kuwa kifungoni" ina maana ya kuwa chini ya utawala wa kitu au mtu.

Mtu ambaye yupo katika utumwa au kifungoni anatakiwa kutumikia wengine bila malipo; hayupo huru kufanya anavyotaka.

"kutia utumwani" pia ina maana ya kuchukua uhuru wa mtu.

Neno lingine la "kifungoni" ni "utumwa".

Kwa njia ya tamathali, wanadamu ni "wafungwa" wa dhambi hadi Yesu awaweke huru kutoka katika utwala na nguvu yake.

Mtu anapompokea maisha mapya ndani ya Yesu, anasitisha kuwa mtumwa wa dhambi na anakuwa mtumwa wa utakatifu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "tia utumwani mwa" au "kuwa kifungoni mwa" unaweza kutafsiriwa kama "kulazimishwa kuwa mtumwa wa" au "kulazimishwa kumtumikia" au "kuwa chini ya utawala wa".


tii, mtiifu, utiifu

Ufafanuzi

Neno "tii" lina maana ya kufanya unachopaswa au kuamriwa. Neno "mtiifu" la eleza tabia ya mtu anaye tii. Wakati mwengine amri ni kuhusu kutofanya kitu, "usiibe"


totii, mkaidi, kutotii

Ufafanuzi

Msemo wa "totii" una maana ya kutotii kile mtu mwenye mamlaka ameamuru au kuagiza. Mtu anayefanya hivi anakuwa "mkaidi".

Mtu anayefanya jambo aliloambiwa kutofanya anakuwa hatii.

Kutotii pia ina maana ya kukataa kufanya jambo ambalo liliamriwa.

Msemo "mkaidi" pia hutumika kuelezea silika ya mtu ambaye kimazoea hatii au huasi. Ina maana ya kwamba ni wenye dhambi au waovu.

Msemo "ukaidi" una maana "tendo la kutotii" au "tabia ambayo ni kinyume na kile Mungu anataka".

"Mtu kaidi" anaweza kutafsiriwa kwa "watu wanaondelea kutii" au "watu ambao hawafanyi kile Mungu anaamuru"


tukuza

Ufafanuzi

Msemo "tukuza" ina maana ya kuonyesha au kunena jinsi gani kitu au mtu ni mkubwa au muhimu. Ina maana ya "kutoa utukufu".

Watu wanaweza kumtukuza Mungu kwa kunena juu ya mambo mazuri aliyoyafanya.

Wanaweza kumtukuza Mungu kwa kuishi kwa njia ambayo inampa heshima na kuonyesha jinsi alivyo mkuu na wa ajabu.

Biblia inaposema ya kwamba Mungu hujitukuza mwenyewe, ina maana anajifunua kwa watu ukubwa wake wa ajabu, mara kwa mara kupitia miujiza.

Mungu Baba atamtukuza Mungu Mwana kwa kudhihirisha kwa watu ukamilifu wa Mwana, ufaharu na ukuu.

Kila mtu anayemwamini Kristo atatukuzwa na yeye. Wanapofufuliwa katika uzima, watabadilishwa kuakisi utukufu wake na kuonyesha neema yake kwa uumbaji wote.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "kutoa utukufu kwa" au "kuleta utukufu kwa" au "kusababisha kuonekana kubwa".

Msemo "mtukuza Mungu" unaweza kutafsiriwa kama "kumsifu Mungu" au "kuzungumza juu ya ukuu wa Mungu" au "kuonyesha jinsi Mungu alivyo mkuu" au "kumheshimu Mungu"


tuma, kutuma nje, kutumwa

Ufafanuzi

"Kutuma" ni kusababisha mtu au kitu kwenda sehemu. "Kutuma nje" mtu ni kumwambia huyu mtu kwenda na kufanya japo au shughuli.


Tumbo la uzazi

Ufafanuzi

Tumbo la uzazi ni mahali ambapo mtoto hukua ndani ya mama yake.


tunda, kuzaa

Ufafanuzi

Msemo "tunda" lina maana ya sehemu ya mmea ambao inaweza kuliwa. Kitu ambacho "kinazaa" kina matunda mengi. Misemo hii pia hutumika kitamathali katika Biblia.

Biblia mara kwa mara hutumia "tunda" kumaanisha matendo na mawazo ya mtu. Kama vile tunda juu ya mti linavyoonyesha ni aina gani ya mti, vile vile maneno na matendo ya mtu hudhihirisha silika yake ikoje.

Mtu anaweza kuzaa matunda ya kiroho mazuri au mabaya, lakini msemo "kuzaa" mara kwa mara una maana chanya ya kuzaa matunda mema.

Msemo "kuzaa" pia hutumika kitamathali kumaanisha "mafanikio". Hii mara kwa mara humaanisha kuwa na watoto na uzao mwingi, pamoja na kuwa na chakula kingi na utajiri mwingine.

Kwa ujumla, msemo "tunda la" una maana ya kitu chochote ambacho hutoka kwa au ambacho huzalishwa na kitu kingine. Kwa mfano, "tunda la hekima" lina maana ya mambo mazuri ambayo hutokana na kuwa na hekima.

Msemo "tunda la roho" una maana kijumla ya kila kitu ambacho nchi huzaa kwa ajili ya watu kula. Hii inajumlisha sio matunda pekee kama mizabibu au tende, lakini pia mboga, karanga na nafaka.

Msemo wa tamathali "tunda la Roho" una maana ya sifa nzuri ambazo Roho Mtakatifu hutoa katika maisha ya watu ambao humtii yeye.

Msemo "tunda la tumbo" una maana ya "kile ambacho tumbo huzaa" yaani, watotot.


Tunga mimba

Ufafanuzi

Kutunga mimba ni kitendo cha kuwa na mimba ya mtoto. Pia inaweza kutumika kwa wanyama wanapokuwa na mimba.


ua, mahakama

Ufafanuzi

"Ua" ni eneo ambalo liko wazi juu na limezungukwa na ukuta. Neno "mahakama" linamaanisha sehemu ambayo hakimu huamua mambo ya sheria na jinai.


uadilifu

Ufafanuzi

Neno "uadilifu" inamaanisha kuwa mwaminifu, na mwenye msimamo mkali wa maadili na tabia.

Kuwa na uadilifu ni kuchagua kutenda kilicho kweli na sawa hata wakati hakuna mwingine anayetazama. Baadhi ya watu katika Biblia, kama Yusufu na Danieli, walionesha uadilifu walipokataa kufanya uovu na kuchagua kumtii Mungu. Kitabu cha Mithali kinasema kuwa ni bora kuwa maskini na kuwa na uadilifu kuliko kuwa tajiri na mfisadi na muongo.


uaguzi, mwaguzi, kutabiri, mtabiri

Ufafanuzi

Msemo "uaguzi" na "kutabiri" ina maana ya tendo la kujaribu kupata taarifa kutoka kwa roho katika ulimwengu wa rohoni. Mtu anayefanya hivi mara nyingine hujulikana kama "mwaguzi" au "mtabiri".

Katika kipindi cha Agano la Kale, Mungu aliamuru Waisraeli kutofanya uaguzi au utabiri.

Mungu hakuruhusu watu wake kutafuta taarifa kutoka kwake kutumia Urimu na Thumimu, ambayo yalikuwa mawe aliyoyatenga kutumika na makuhani wa juu kwa kusudi hilo. Lakini hakuruhusu watu wake kutafuta taarifa kupitia msaada wa roho chafu.

Waaguzi wa kipagani walitumia taratibu tofauti za kujaribu kutafuta taarifa kutoka kwenye ulimwengu wa roho. Mara zingine walichunguza sehemu za ndani za mnyama aliyekufa au kurusha mifupa ya wanyama juu ya ardhi, wakitafuta violezo ambavyo vingeweza fasiri ujumbe kutoka kwa miungu yao ya uongo.

Katika Agano Jipya, Yesu na mitume pia walikataa uaguzi, uchawi, ulozi na mazingaombwe. Matendo haya yote yalihusisha matumizi ya nguvu kutoka roho chafu na yanalaaniwa na Mungu.


Ubaguzi

Ufafanuzi

"Kuonesha ubaguzi" ni kitendo cha kuamua kuwaonesha watu umuhimu zaidi ya watu wengine.


ubani

Ufafanuzi

Ubani ni harufu nzuri ya kiungo kutoka kwenye mti wa utomvu. Inatumika kutengeneza manukato na udi.

Katika kipindi cha Biblia, ubani ilikuwa kiungo muhimu kilichotumika kuandaa maiti kwa maziko.

Kiungo hiki kilikuwa cha thamani kwa sifa zake za uponyaji na kutuliza.

Wanaume wasomi walipokuja kutoka nchi ya mashariki kumwona mtoto Yesu Bethlehemu, ubani ilikuwa moja ya zawadi tatu walizoleta kwake.


Uchawi, mchawi

Ufafanuzi

Neno "uchawi" lina husu zoezi la kutumia nguvu hisio ya kawaida ambayo haitoki kwa Mungu. "Mchawi" ni mtu anaye tumia uchawi.


uchawi, mchawi, uganga

Ufafanuzi

"Uchawi" au "uganga" umaanisha kutumia mazinga umbwe, inayo maanisha kufanya vitu venye nguvu kupitia msaada wa roho chafu. "Mchawi" ni mtu ni mtu anaye fanya hivi vitu venye nguvu vya kimazinga umbwe.


uchungu wa kuzaa

Ufafanuzi

Mwanamke aliye katika "uchungu" anapitia uchungu unaofatiwa na kujifungua mtoto wake. Huu unaitwa "uchungu wa kuzaa."

Katika barua yake kwa Wagalatia, mtume Paulo alitumia neno hili kama mithali kuelezea jitihada yake kubwa ya kuwasaidia waumini wenzake kuwa kama Yesu zaidi na zaidi. Mfano wa uchungu wa kuzaa unatumika katika Biblia kuelezea jinsi maafa ya siku za mwisho yatakavyotokea kwa kasi na nguvu.


udaku

Ufafanuzi

Msemo "udaku" una maana ya watu kuzungumza juu ya masuala binafsi ya mtu mwingine, mara nyingi katika hali ya hasi na isiyo na faida. Mara nyingi kile kinachozungumzwa hakijathibitishwa kuwa kweli.

Biblia inasema ya kwamba kusambaza taarifa hasi kuhusu mtu ni kosa. Udaku na kashfa ni mifano ya aina hii ya kauli hasi.

Udaku ni wa madhara kwa mtu anayezungumzwa kwa sababu mara nyingi humuumiza uhusiano wa mtu na watu wengine.


ufalme

Ufafanuzi

Ufalme ni kundi la watu linalotawalwana mfalme. Linamaanisha pia dola au sehemu za kisiasa ambalo mfalme au kiongozi mwingine ana madaraka na mamlaka.

Ufalme unaweza kuwa na ukubwa wowote kijiografia. Mfalme anaweza kutawala taifa au nchi au mji mmoja tu. Neno "ufalme" linaweza pia kumaanisha utawala wa kiroho au madaraka, kama usemi "ufalme wa Mungu." Mungu ni mtawala wa viumbe vyote, lakini usemi "ufalme wa Mungu" kwa mahsusi linamaanisha utawala juu ya watu waliomwamini Yesu na walionyenyekea kwa utawala wake. Biblia pia inazungumzia kuhusu Shetani kuwa na "ufalme" anao tawala kwa muda juu ya vitu vingi duniani. Ufalme wake ni uovu na unajulikana kama wa "giza."


Ufalme

Ufafanuzi

Neno ufalme linawaelezea watu au vitu ambavyo vinahusiana na mfalme au malkia.


ugomvi

Ufafanuzi

Neno "ugomvi" la eleza malumbano ya kimwili au kihisia kati ya watu.


Uhalifu, mhalifu

Ufafanuzi

Uhalifu ni dhambi inayohusisha kuvunja sheria za nchi. Mhalifu ni mtu anayefanya uhalifu.


uhalifu, uasi

Ufafanuzi

Neno "uhalifu" linamuelezea mtu ambaye hatii sheria na maagizo. Wakati nchi au kundi la watu wako katika hali ya "uasi" inamaanisha kuna kutokutii na upotevu wa maadili kulikoenea.

Mtu muasi ni mtu aliyekaidi na hatii amri za Mungu. Mtu Paulo aliandika kuwa katika siku za mwisho kutakuwa na "mwanamme wa uasi," au "yule mhalifu" atakaye shawishiwa na Shetani kufanya mambo maovu.


ujasiri, jasiri

Ufafanuzi

Ujasiri ni kitendo cha kukabiliana au kufanya jambo gumu au la hatari.


ukoma, mkoma

Ufafanuzi

Neno "ukoma" linatumika katika Biblia kumaanisha aina kadhaaza magonjwa ya ngozi. "Mkoma" ni mtu mwenye ukoma. Neno "ukoma" pia linaweza kutumika kuelezea mtu au sehemu ya mwili iliyoadhirika na ukoma.

Aina flani za ukoma zinasababisha ngozi kupoteza rangi na mabaka meupe, kama Miriamu na Naamani walivyokuwa na ukoma. Katika nyakati za sasa, ukoma mara nyingi husababisha mikono, miguu, na sehemu zingine za mwili kuharibika. Kulingana na maelekezo ambayo Mungu aliwapa Waisraeli, mtu akiwa na ukoma, alionekana "mchafu" na ilimbidi kukaa mbali na watu wengine ili asiwaambukize na ugonjwa. Mkoma kawaida angasema "mchafu" ili wengine waonywe wasije karibu yake. Yesu aliponya wakoma wengi, pamoja na aina zingine za magonjwa.


Ukoo

Ufafanuzi

Ukoo ni kundi la wana familia wanaotokana na mababu.


ulimi

Ufafanuzi

Kuna maana kadhaa katika Biblia ya "ulimi."


ulizia

Ufafanuzi

Usemi "ulizia" inamaana kumuomba mtu taarifa. Usemi wa "kuulizia kwa"mara nyingi unatumika kumaanisha kumuomba Mungu hekima au msaada.

Agano la kale limetunza kumbukumbu ya mifano kadhaa ambapo watu walimuuliza Mungu. Neno pia linaweza kutumika kwa mfalme au afisa wa serikalini kufanya utafiti katika kumbukumbu za maandishi rasmi. Kulingana na mazingira, "ulizia" inaweza kutafsiriwa kama "kuomba" au "kuomba taarifa." Usemi "kumuuliza Yahwe" inaewza kutafsiriwa kama "kumuomba Yahwe uongozo" au "kumuuliza Yahwe nini cha kufanya." "Kuulizia juu ya" kitu inaweza kutafsiriwa ka "kuuliza maswali kuhusu" au "kuulizia taarifa kuhusu." Yahwe anaposema, "Sitaulizwa na wewe" hii inaweza kutafsiriwa kama, "Sita kuruhusu wewe uniombe taarifa" au "hautaruhusiwa kutafuta msaada kutoka kwangu."


Umba, Uumbaji, Muumbaji

Ufafanuzi

Kuumba ni kutengeneza kitu au kusababisha kitu kitokee. Kitu kinachoumbwa kinaitwa uumbaji. Mungu anaitwa muumbaji kwa sabau alisababisha vitu vyote vya dunia vikatokea.


umbo, sanamu ya kuchonga, umbo la kuchonga, umbo la chuma

Ufafanuzi

Maneno haya yote yanatumika kumaanisha sanamu ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuabudu miungu ya uongo. Katika mazingira ya kuabudu sanamu, neno "sanamu" ni njia fupi ya kusema "sanamu ya kuchonga."

"Sanamu ya kuchonga" au "umbo la kuchonga" ni kitu cha mbao kilichofanywa kuonekana kama mnyama, mtu, au kitu. "Umbo la chuma" ni kitu au sanamu iliyoundwa kwa kuyeyusha chuma na kuimwaga katika umbo tupu ambalo lina umbo la kitu, mnyama, au mtu. Vitu hivi vya mbao na chuma vilitumika katika kuabudu miungu ya uongo. Neno "umbo" wakati wa kuzungumzia sanamu inamaanisha kati ya sanamu ya mbao au ya chuma.


Umri

Ufafanuzi

"Umri" ni idadi ya miaka aishiyo mwanadamu. pia hutumika kuonesha nyakati kwa ujumla.


unyofu

Ufafanuzi

Neno "unyofu" ueleza kutenda kwa namna inayo fuata sheria za Mungu.]


uongo, ukaidi, kuipotosha

Ufafanuzi

Neno "kilichopotoka" linatumika kumuelezea mtu au tendo fulani ambalo linapotosha kimaadili. Neno "ukaidi" linamaana ya tabia ya kikaidi". Kupotosha kitu inamaana ya kugeuza jambo toka kwenye usahihi wake au uzuri wake.


upanga

Ufafanuzi

Upanga ni silaha ya chuma nyembamba inayo tumika kukata au kuchoma. Ina mshikio na nch ndefu.


upinde

Ufafanuzi

Aina hii ya silaha ambayo inajumuisha mishale ya kurusha kutoka katika upinde. Katika nyakati za Biblia ilitumika kupigana na maadui na kuwindia.


upole

Ufafanuzi

Neno "upole" la elezea mtu aliye mtaratibu, mnyenyekevu, na aliye tayari kuteseka dhuluma. Upole ni uwezo wa kuwa mtaratibu ata kama ukali au nguvu inaonekana ni sahihi.


ushauri, mshauri

Ufafanuzi

Ushauri inamaana ya kumsaidia mtu kuamua kwa busara juu ya jambo fulani. Mshauri mwenye busara ni mtu anayetoa ushauri ambao utamsaidia mtu kuamua kwa usahihi.


ushuru

Ufafanuzi

Ushuru ni pesa au bidha watu wanazo lipa kwa serikali iliyo na mamlaka juu yao.


ushuru

Ufafanuzi

Neno "ushuru" la husu zawadi kutoka kwa mtawala mmoja kwenda kwa mwingine, kwa kusudi la ulinzi na mausiano mema kati ya mataifa yao.


uso

Ufafanuzi

Neno "uso" lina maana ya sehemu ya mbele ya kichwa cha mtu. Msemo huu pia una maana kadhaa za tamathali.

Msemo wa "uso wako" mara kwa mara ni njia ya tamathali ya kusema "wewe". Vivyo hivyo, msemo "uso wangu" mara kwa mara una maana ya "Mimi".

Katika hali ya kimwili, "kumkabili" mtu au kitu ina maana ya kutazama upande wa huyo mtu au kitu.

"Kukabiliana" ina maana ya "kutazamana"

Kuwa "uso kwa uso" ina maana ya kwamba watu wawili wanatazamana katika umbali wa karibu.

Yesu "alipoweka uso wake kuelekea Yerusalemu" ina maana ya kwamba aliamua kwa dhati kwenda.

"Kuweka uso dhidi ya" watu au mji ina maana kuamua kwa nguvu: kutoimarisha tena, au kumkataa mtu au mji huo.

Msemo "uso wa nchi" una maana ya sehemu ya juu ya dunia na mara kwa mara ni kumbukumbu ya jumla ya dunia nzima. Kwa mfano, "njaa inayofunika uso wa dunia" ina maana ya njaa inayosambaa ambayo hugusa watu wengi wanaoishi juu ya nchi.

Msemo wa tamathali, "usifiche uso wako kwa watu wako" una maana "usiwakatae watu wako" au "usiwaache watu wako" au "usiache kuwatunza watu wako".

Mapendekezo ya Tafsiri

Ikiwezekana, ni bora kubaki na msemo au kutumia msemo katika lugha hii ambayo ina maana ya kufanana.

Msemo "kukabili" unaweza kutafsiriwa kama "kugeuka upande wa" au "kutazama moja kwa moja" au "kuangalia uso wa".

Msemo "uso kwa uso" unaweza kutafsiriwa kama "karibu kabisa" au "mbele ya" au "katika uwepo wa".

Kulingana na muktadha, msemo "mbele ya uso wake" unaweza kutafsiriwa kama "kabla yake" au "mbele yake" au "katika uwepo wake".

Msemo "weka uso wake kuelekea" unaweza kutafsiriwa kama "kuanza kusafiri kuelekea" au "aliamua akilini mwake kuondoka".

Msemo "kuficha uso wake kutoka kwa" unaweza kutafsiriwa kama "kugeuka kutoka kwa" au "kuacha kusaidia au kulinda" au "kukataa".

"Kuweka uso wake dhidi ya" mji au watu inaweza kutafsiri kama "kutazama kwa hasira na kushutumu" au "kukataa kukubali" au "kuamua kukataa" au "kulaumu na kukataa" au "kutoa kuhukumu".

Msemo "tamka mbele ya uso wao" inaweza kutafsiriwa kama "sema kwao moja kwa moja".

Msemo " katika uso wa nchi" inaweza kutafsiriwa kama "katika nchi yote" au "juu ya dunia nzima" au "kuishi katika dunia".


Utaji

Ufafanuzi

Utaji ni kipande cha nguo kinachotumika kufunikia kichwa au uso ili usionekane.


Utawala, mtawala

Ufafanuzi

Maneno "utawala" au "mtawala" yana maana ya kusimamia na kuongoza watu wa nchi ili kuwasaidia wafanye sawasawa na inavyotakiwa.


utukufu

Ufafanuzi

Neno "utukufu" la eleza uzuri wa ajabu na umaridadi ambao una ambatana na utajiri na muonekano wa kuvutia.


uvumba

Ufafanuzi

Neno "uvumba" linamaanisha mchanganyiko wa vikolezo vyenye manukato mazuri vinavyochomwa kutoa moshi wenye harufu nzuri.

Mungu aliwaambia Waisraeli kuchoma uvumba kama sadaka kwake. Huu uvumba ulitakiwa kutengenezwa kwa kuchanganya kiwango sawa cha vikolezo maalumu vitano kama Mungu alivyoagiza. Huu ulikuwa uvumba mtakatifu, kwa hiyo hawakutakiwa kuutumia kwa kitu kingine chochote. "Madhabahu ya kufukuzia uvumba" ilikuwa madhabahu maalumu ya kuchomea uvumba. Uvumba ulitolewa angalau mara nne kwa siku, kwa kila saa ya maombi. Ilitolewa pia kila wakati sadaka ya kuteketeza ilipotolewa. Kuchomwa kwa uvumba kunaashiria maombi na kuabudu vinaponyanyuka juu kwa Mungu kutoka kwa watu wake. Njia zingine za kutafsiri "uvumba" zinaweza kuwa, "vikolezo vya manukato mazuri" au "mimea yenye harufu nzuri."


Uvumilivu

Ufafanuzi

Uvumilivu ni kitendo cha kupita katika wakati mgumu na kuwa na subira.


uwezo

Ufafanuzi

Neno "uwezo" la husu kuwa na nguvu nyingi.


uwezo

Ufafanuzi

Neno "uwezo" la husu hali ya kuwa na nguvu kimwili, kihisia, au kiroho.


Uyahudi, dini ya Kiyahudi

Ufafanuzi

Neno "Uyahudi" inamaanisha dini inayofuatwa na Wayahudi. Inajulikana piakama "dini ya Kiyahudi."

Katika Agano la Kale, neno "dini ya Kiyahudi" inatumika wakati katika Agano Jipya neno "Uyahudi" ndio linatumika. Uyahudi inajumuisha sheria zote za na maelekezo ya Agano la Kale ambayo Mungu aliwapa Wasiraeli kutii. Inajumuisha pia desturi na tamaduni zilizoongezwa katika dini ya Kiyahudi kadri muda ulivyoenda. Wakati wakutafsiri, usemi "dini ya Kiyahudi" au "dini ya Wayahudi" zinaweza kutumika katika Agano la Kale au Jipya. Lakini, neno "Uyahudi" linapaswa kutumika tu kwenye Agano Jipya, kwa sababu neno hilo halikuwepo kabla ya wakati huo


uzao, kutokana na

Ufafanuzi

"Uzao" ni mtu ambaye ni ndugu wa damu moja kwa moja wa mtu mwingine nyuma kabisa katika historia.

Kwa mfano, Abrahamu alikuwa uzao wa Nuhu. Uzao wa mtu ni watoto wake, wajukuu, na watukuu, na kuendelea. Vizazi vya Yakobo vilikuwa makabila kumi na mawili ya Israeli.

msemo "kutokana na" ni njia nyingine ya kusema "uzao wa" kama vile "Abrahamu alitokana na Nuhu". Hii inaweza kutafsiriwa kama "kutokana na uzao wa"


viongozi wa Kiyahudi, mamlaka ya Kiyahudi, viongozi wa dini

Ufafanuzi

Usemi "viongozi wa Kiyahudi" au "mamlaka ya Kiyahudi" inamaanisha viongozi wa dini kama makuhani na walimu wa sheria za Mungu. Walikuwa na mamlaka yakufanya maamuzi ya mambo yasiyo yakidini pia.


viuno

Ufafanuzi

Neno "viuno" kinamaanisha sehemu ya mwili ya mnyama au mtu aliyo katikati ya mbavu za chini na mifupa ya nyonga, pia ikijulikana kama tumbo la chini.

Msemo "kaza viuno" unamaanisha kujiandaa kufanya kazi ngumu. Inatokea katika utamaduni wa kuchomekea sehemu ya chini ya joho kwenye mkanda kiunoni ili kusogea kwa urahisi. Neno "viuno" mara nyingi linatumika katika Biblia kumaanisha sehemu ya chini ya mnyama iliyotolewa sadaka. Katika Biblia, msemo "viuno" mara nyingi humaanisha sehemu za siri za mwanamme kimafumbo na kitasifida kama chanzo cha uzao wake. Msemo "atatoka katika viuno vyako" unaweza pia kutafsiriwa kama, "atakuwa uzao wako" au "atazaliwa kutokana na mbegu yako" au "Mungu atasababisha kutoka kwako." Inapozungumzia sehemu ya mwili, hii inaweza pia kutafsiriwa kama "tumbo" au "nyonga" au "kiuno," kulingana na mazingira.


vumilia, uvumilivu

Ufafanuzi

Msemo "vumilia" una maana ya kudumu muda mrefu au kustahamili jambo gumu kwa uvumilivu.

Pia ina maana ya kusimama imara wakati wa mitihani kuwepo, bila kukata tamaa.

Msemo "uvumilivu" unaweza kumaanisha "subira", "ustahamilivu katika majaribu" au "kustahamili pale unapoteswa".

Faraja kwa Wakristo "kuvumilia mpaka mwisho" ni kuwaambia wamtii Yesu, hata kama hili litasababisha wao kuteseka.

"Kuvumilia mateso" pia inaweza kumaanisha "kupitia mateso".

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia za kutafsiri msemo "vumilia" zinaweza kujumuisha "stahamili" au "kuendelea kuamini" au "kuendelea kufanya kile Mungu anachotaka ufanye" au "simama imara".

Katika baadhi ya muktadha, "kuvumilia" kunaweza kutafsiriwa kama, "kupitia jaribu" au "kupitia".

Kwa maana ya kudumu muda mrefu, msemo "vumilia" unaweza kutafsiriwa kama "kudumu" au "kuendelea". Msemo, "hatavumilia" unaweza kutafsiriwa kama, "hatadumu" au "hataendele kuishi".

Njia za kutafsiri "uvumilivu" unaweza kujumuisha "ustahamilivu" au "kuendelea kuamini" au "kubaki mwaminifu".


Vumilia, uvumilivu

Ufafanuzi

"vumilia" au "uvumilivu" ni kitendo cha kuendelea kufanya kitu fulani hatakama ni ngumu sana kufanya au itachukua mda mrefu.


Waasi, uasi.

Ufafanuzi

Uasi ni kukataa kuitumikia mamlaka ya mtu fulani. Waasi ni watu wasiotii na kufanya mambo maovu. Mtu huyu anaitwa muasi.


waheshima, heshima

Ufafanuzi

Neno "heshima" la husu kitu ambacho ni bora na chenye ubora. "mtu wa heshima" ni mtu aliye wa siasa au wa jamii ya juu.


wanaume wasomi, mamajusi

Ufafanuzi

Katika akaunti ya Mathayo ya kuzaliwa kwa Yesu, hawa wanaume "wasomi" au "wenye elimu" walikuwa "wanaume wenye hekima" walioleta zawadi kwa Yesu Bethlehemu muda baada ya kuzaliwa huko. Inawezekana walikuwa "mamajusi," ambao ni watu wanaofuatilia nyota.

Wanaume hawa walisafiri mbali kutoka nchi ya mbali kaskazini mwa Israeli. Haijulikani haswa ni wapi walipotokea na walikuwa kina nani. Lakini ni dhahiri walikuwa wasomi waliozisoma nyota. Wanaweza kuwa wazawa wa wanaume wenye hekima waliowatumikia wafalme wa Babeli wakati wa Danieli na waliofundishwa mambo mengi,ikiwemo kuzisoma nyota na kufafanua ndoto. Kiutamaduni inasemekana kuwa walikuwa wanaume watatu wenye hekima au wanaume wasomi kwa sababu ya zawadi tatu walizoleta kwa Yesu. Lakini, Biblia haisemi walikuwa wangapi.


watoza ushuru

Ufafanuzi

"Mtoza ushuru" alikuwa mfanya kazi wa serikali ambaye kazi yake ilikuwa kupokea pesa watu waliyo paswa kulipa serikali ushuru.


watu wenye busara

Ufafanuzi

Kwenye Biblia watu wenye busara ni watu wanaomtumikia Mungu na kutenda kwa busara na sio wapumbavu. Pia ni neno lililotumika kuwalelezea watu wenye ufahamu wa kipekee na uwezo wanaotumika kama sehemu katika mahakama ya mfalme.


wavuvi

Ufafanuzi

Wavuvi ni wanamume ambao hukamata samaki kutoka majini kama njia ya kupata pesa. Katika Agano Jipya, wavuvi walitumia mitego mikubwa kukamata samaki. Msemo "wavuvi" ni jina lingine la mvuvi.

Petro na mitume wengine walifanya kazi kabla ya kuitwa na Yesu.

Kwa kuwa nchi ya Israeli ilikuwa karibu na maji, Biblia ina kumbukumbu nyingi ya samaki na wavuvi.

Msemo huu unaweza kutafsiriwa na msemo kama "wanamume wanaokamata samaki" au "wanamume wanaopata pesa kwa kukamata samaki"


Wazee

Ufafanuzi

Wazee ni wanamume wa kiroho waliokomaa ambao wana majukumu ya kiroho na uongozi wa utendaji miongoni mwa watu wa Mungu.

Msemo "mzee" umetokana na kweli ya kwamba wazee asili yao walikuwa wanamume wa umri mkubwa ambao, kwa sababu ya umri wao na uzoefu, walikuwa na hekima kubwa.

Katika Agano la Kale, wazee walisaidia kuongoza Waisraeli katika masuala ya haki ya jamii na Sheria ya Musa.

Katika Agano Jipya, wazee wa Kiyahudi waliendelea kuwa viongozi katika jamii zao na pia walikuwa waamuzi kwa watu.

Katika makanisa ya mwanzo ya Wakristo, wazee wa Kikristo walitoa uongozi wa kiroho kwa mikusanyiko ya jamii ya waumini.

Wazee katika makanisa haya walijumuisha wanamume vijana ambao walikomaa kiroho.

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "wanamume wazee" au "wanamume waliokomaa kiroho wanaoongoza kanisa".


Wazee wa ukoo

Ufafanuzi

Katika agano la kale "wazee wa ukoo" ni mababa wa Wayahudi hasa Abrahamu, Isaka na Yakobo.


weka wakfu, kuwekwa wakfu kwa

Ufafanuzi

Kuweka wakfu ni kuweka kando kitu kwa ajili ya kusudi maalumu au shughuli.

Daudi aliweka wakfu dhahabu na fedha zake kwa Bwana.

Mara kwa mara, neno "kujitolea" lina maana ya tukio rasmi au sherehe ya kuweka kando kitu kwa ajili ya kusudi maalumu.

Kuweka wakfu kwa madhabahu ilijumuisha kutoa sadaka kwa Mungu.

Nehemia aliwaongoza Waisraeli katika kuweka wakfu kwa kuta za Yerusalemu zilizotengenezwa kwa ahadi mpya ya kumtumikia Yahwe pekee kwa vyombo vya muziki na kuimba.

Msemo wa "kuweka wakfu" unaweza kutafsiriwa kama "kutenga kusudi maalumu" au "kabidhi kitu kutumika kwa kazi maalumu" au "kabidhi mtu kutenda tendo maalumu".


wivu, tamani

Ufafanuzi

Msemo "wivu" una maana ya kuwa na wivu kwa mtu kwa sababu ya kile ambacho mtu huyo anamiliki au kwa sababu ya sifa za kutamanisha za mtu huyo. Msemo "tamani" una maana ya kumuonea wivu mtu hadi hatua ya kutamani kwa nguvu kuwa na kitu ambacho mtu huyo anacho.

Kwa kawaida wivu ni hisia ya hasi ya kuchukia kwa sababu ya mafanikio, bahati nzuri, au mali za mtu mwingine.

Kutamani ni hamu kali ya kutaka mali ya mtu mwingine, au hata mke au mume wa mtu mwingine.


woga, kutishwa

Ufafanuzi

Istilahi ' hofu' hurejelea hisia kali za woga or kitisho. Mtu aliye na hofu huwa ameogopa. woga ni hali kali na kubwa zaidi ya hofu, zaidi ya hofu ya kawaida. Mara kwa mara mtu anapokuwa ametishwa huwa ameshitushwa na ameshangazwa sana.


woga, kuogopesha

Ufafanuzi

Neno "woga" uelezea hisia ya hofu kuu. "Kuogopesha" mtu ina maana ya kusababisha huyo mtu kujisikia wasi wasi sana.


yayuka, yayushwa

Ufafanuzi

Neno "yayusha" la husu kitu kuwa maji kinapo pashwa. Pia utumika kimfano.


Zabibu

Ufafanuzi

Mzabibu ni tunda dogo, la duara, laini ambalo huota katika vishada vya mizabibu. Juisi ya mizabibu hutumika kutengeneza divai.

Kuna aina tofauti ya rangi ya mizabibu, kama vile kijani iliyoiva, zambarau au nyekundu.

Mizabibu binafsi inaweza kuwa na ukubwa kama sentimita moja au tatu.

Watu huotesha mizabibu katika bustani inayoitwa mashamba ya mizabibu. Hii huwa mistari mirefu ya zabibu.

Mizabibu ilikuwa chakula muhimu sana wakati wa Biblia na kuwa na mashamba ya zabibu ilikuwa ishara ya utajiri.

Ili kukaa na mizabibu isioze, watu mara kwa mara waliikausha. Mizabibu ya kukaushwa iliitwa "zabibu kavu" na ilitumika kutengeneza keki za zabibu kavu.

Yesu alitoa fumbo juu ya shamba la zabibu kuwafundisha wanafunzi wake juu ya ufalme wa Mungu.


Zambarau

Ufafanuzi

Hii ni rangi ambayo ni mchanganyiko kati ya rangu ya bluu na nyekundu.


Zawadi

Ufafanuzi

Zawadi ni kitu anachopokea mtu kwa sababu amefanya jambo fulani liwe baya au zuri. Kumpa mtu zawadi ni kumpa mtu kitu anachostahili.


zinaa

Ufafanuzi

Msemo "zinaa" una maana ya tendo la ngono ambalo hufanyika nje ya mahusiano ya ndoa ya mwanamume na mwanamke. Hii ni kinyume na mpango wa Mungu.

Msemo huu unaweza kumaanisha tendo lolote la kingono ambalo ni kinyume na mapenzi ya Mungu, ikiwemo matendo ya usenge na ponografia.

Aina moja ya zinaa ni uzinzi, ambayo ni tendo la ngono haswa kati ya mtu aliyeoa na mtu ambaye sio mke au mume wake.

Aina nyingine ya zinaa ni "ukahaba" ambayo uhusisha kulipwa kufanya ngono na mtu.

Msemo huu pia hutumika kitamathali kumaanisha ukosefu wa uaminifu wa Israeli kwa Mungu walipoabudu miungu ya uongo.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "zinaa" unaweza kutafsiriwa kama "uzinzi" ikiwa maana sahihi ya msemo inaeleweka.

Njia zingine za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha "matendo mabaya ya ngono" au "ngono nje ya ndoa".

Msemo huu unaweza kutafsiriwa katika njia nyingine kutoka kwa neno "uzinzi".

Tafsiri ya matumizi ya tamathali ya msemo huu unatakiwa kukaa na maana halisi ikiwezekana kwa kuwa kuna ulinganisho wa kufanana katika Biblia kati ya kutokuwa mwaminifu kwa Mungu na kutokuwa mwaminifu katika mahusiano ya kimapenzi.


zingira, kuzingira

Ufafanuzi

Neno "kuzingira" la husu pale jeshi shambulizi linapo zunguka mji na kuusababisha usiweze kupokea maitaji na maji. "Kuzingira" mji ina maana kusababisha mji kuwa chini ya kuzungukwa.