Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa 2 Wathesalonike

Sehemu 1: Utangulizi wa jumla

Muhtasari wa kitabu cha 2 Wathesalonike

  1. Salamu na kushukuru (1:1-3)

  2. WaKristo wanaoumia kwa mateso

    • Wanastahili ufalme wa mbinguni na ahadi yake ya msaada kutoka kwa majaribio (1:4-7)
    • Mungu atawahukumu wale wanaowatesa Wakristo (1:8-12)
  3. Kutoelewa kwa waumini wengine kuhusu kuja kwa Kristo kwa mara ya pili

    • Kurudi wa Kristo haujatokea 2:1-2)
    • Maelekezo kuhusu matukio yatakayotangulia kurudi kwake Kristo (2:3-12)
  4. Imani ya Paulo kwamba Mungu atawaokoa Wakristo Wathesalonike

    • Mwito wake "kusimama imara" (2:13-15)
    • Maombi yake kwamba Mungu atawafariji (2:16-17)
  5. Paulo anatoa ombi la kuombewa na waumini Wathesalonike (3:1-5)

  6. Paulo anatoa amri kuhusu waumini wasiofanya kazi (3:6-15)

  7. Kumalizia (3:16-17)

Nani aliandika 2 Wathesalonike?

Paulo aliandika Wathesalonike 2. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika ufalme nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu.

Paulo aliandika barua hii akiwa anaishi katika mji wa Korintho.

Kitabu cha 2 Wathesalonike kinahusu nini?

Paulo aliandika barua hii kwa waumini katika mji wa Thesalonike. Aliwatia moyo waumini hawa kwa sababu walikuwa wanateswa.Aliwaambia kuendelea kuishi kwa njia inayompendeza Mungu. Alitaka kuwafundisha tena kuhusu kurudi kwa Kristo.

Kichwa cha Kitabu hiki kinastahili kutafsiriwa namna gani?

Watafsiri wanaweza amuru kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha kitamaduni, "2 Wathesalonike" ama " Wathesalonike wa pili." ama wanaweza chagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama, "Barua ya pili kwa kanisa la Thesalonike," ama "Barua ya pili kwa Wakristo wa Thesalonike," (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Nini maana ya "ujio wa pili wa Yesu"?

Paulo aliandika maswala mengi katika barui hii kuhusu kurudi kwake Yesu Kristo duniani.Yesu akirudi, atawahukumu wanadamu wote. Pia atahukumu viumbe wote. Atasababisha kuwepo kwa amani duniani. Paulo pia alieleza kwamba "mwanaume mhalifu" atakuja kabla ya kurudi kwa Kristo.Mtu huyu atamtii Shetani na kufanya watu wengi kumuasi Mungu.Lakini Yesu atamuangamizi huyu mtu atakaporudi.

Sehemu 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Paulo alimaanisha na maelezo "ndani ya Bwana," na "ndani ya Kristo,' na kadhalika?

Paulo alitaka kuasilisha swala la muungano wa karibu kati ya Kristo na waumini. Tazama utangulizi wa kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi kuhusu aina hii ya maelezo.

Ni maswala gani makuu ya maandishi ya kitabu cha 2 Wathesalonike?

Katika mistari ifuatayo, matoleo ya kisasa yanatofautiana na matoleo ya kale.ULB ina masomo ya kisasa na huyaweka masomo ya awali kama maelezo ya chini.Iwapo kuna tafsiri ya Bibilia katika eneo jumla, watafsiri wazingatie kutumia masomo yanayopatikana katika hayo matoleo. Kama sivyo, watafsiri wanashauriwa kufuata masomo ya kisasa.

  • "Na yule mtu wa kuasi anatambulishwa" (2:3). ULB na UDB na matoleo mengi ya kisasa husoma hivi.Matoleo ya awali yanasoma, "na yule mtu wa dhambi anatambulishwa."
  • "Kwa maana Mungu aliwachagua kama matunda ya kwanza ya wokovu" (2:13) ULB, UDB, na matoleo mengine husoma hivi. Matoleo mengine yanasoma, "Kwa vile Mungu aliwachagua "kutoka mwanzo kwa ajili ya wokovu."

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

2 Thessalonians 1

2 Wathesalonike 01 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Mistari 1-2 huanzisha kirasmi barua hii. Barua za kale katika Mashariki ya Karibu zilikuwa na utangulizi wa aina hii.

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

Kitendawili

Kitendawili ni kauli ya ukweli ambayo inaonekana kufafanua kitu kisichoezekana. Kitendawili untaokea katika mistari 4-5: "Tunazungumzia uvumilivu wenu na imani yenu katika mateso yenu yote.Tunazungumzia mateso mnayostahimili.Hii ni ishara ya hukumu ya kweli ya Mungu." Watu kila mara hawangefikiria kwamba kumuamini Mungu wakati wa kuteswa ni ishara ya hukumu ya kweli ya Mungu.Lakini katika mistari ya 5-10, Paulo anaelezea jinsi Mungu atawapatia tuzo wale ambao wanamwamini na jinsi atakavyuwahukumu wanaowatesa. (2 Wathesalonike 1:4-5)

2 Thessalonians 1:1

Maelezo ya Jumla:

Paulo ndiye mwandishi wa barua hii, lakini anawajumuisha Silwano na Timotheo kama wapelekwaji wa barua. Anaanza kwa kusalimia kanisa la Thesalonike.

Maelezo ya Jumla:

Maneno "sisi" linamaanisha Paulo, Silwano naTimotheo, au kama limetumika vinginevyo. Pia neno " ninyi" ni wingi na lina maanisha waumini wa kanisa la Wathesalonike.

Silwano

Huu ni muundo wa Kilatini "Silas." Ni mtu yule yule aliyeorodheshwa katika kitabu cha Matendo kama msafiri mwenzi wa Paulo.

Neema iwe juu yenu

Paulo kawaida anatumia salamu hii katika barua zake.

2 Thessalonians 1:3

Maelezo ya Jumla:

Paulo anatoa shukrani kwa ajili ya waumini katika kanisa la Thesalonike.

kupaswa kutoa shukrani kwa Mungu

Paulo anasema anapaswa kumshukuru Mungu mara kwa mara.

ndugu

Hapa "ndugu" inamaanisha Wakristo wenzetu, ikijumuisha wanaume kwa wanawake.

Hivi ndivyo ipasavyo

"kwa kuwa hiki ni kitu sahihi cha kufanya" au " ni vyema"

Upendo ambao kwa kila mmoja amefungamanishwa na mwenzake

"mnapendana nyinyi kwa nyinyi"

kila mtu na mwenzake

Kila mtu na mwenzake lina maanisha Wakristo wenzetu."

sisi wenyewe

Hapa "wenyewe" limetumika kusisitiza kujisifu kwa Paulo.

kwamba mpate kuhesabiwa kuwa mnastahili kwa ajili ya ufalme wa Mungu.

Hii inakwemwa katika muundo tendaji. AT: "kwamba Mungu atawahesu kuwa wa sehemu ya ufalme wa Mungu."

2 Thessalonians 1:6

Sentensi Unganishi:

Paulo anapoendelea, anaoongea kuhusu Mungu kuwa mwenye haki.

ni haki kwa Mungu

"Mungu yuko sahihi" au "Mungu ni wa haki"

na raha kwenu

Unaweza kuifafanua kwamba Mungu ndiye arudishae raha. AT:" na kwamba Mungu arudishe raha kwenu."

malaika wa nguvu zake

"Malaika wa Mungu wenye nguvu"

Katika mwali wa moto atalipiza kisasi kwa wale wasiomjua Mungu na wale

"Bwana Yesu atawaadhibu kwa mwali wa moto wale wasiomjua Mungu na wale" au "Kisha kwa mwali wa moto atawaadhibu wale wote wasiomjua Mungu na wote ambao hawamtii Bwana Yesu" (UDB)

2 Thessalonians 1:9

watateseka

Neno "wataseka" wanamaanishwa watu wasioitii injili.

atakapokuja sike ile

Hapa "siku ile" ni siku Yesu atakaporudi duniani.

ili atukuzwe na watakatifu wake

Hii inaweza kusemwa katika hali halisi. AT: "watu wake waliomwamini watamtukuza "

watastaajabishwa na wale wote walioamini

Hii inaweza kuwa katika hali tendaji. "wale wote walioamini watashangaa" au "wale wote walioamini watamshangaa yeye"

2 Thessalonians 1:11

Pia tunaendelea kuomba kwa ajili yenu

Paulo anasisitiza jinsi anavyoomba mara nyingi kwa ajili yao. AT: Pia mara kwa mara tunaomba kwa ajili yenu.

kuita

Neno "kuita" lina maanisha Mungu anateua au anachagua watu kuwa watoto wake, kuwa watumishi wake na wahubiri wa ujumbe wa wokovu kwa njia ya Yesu.

kutimiza kila haja ya wema

"awawezeshe kufanya mema kwa kila namna mnavyo tamani" (UDB)

ili kwamba mpate kulitukuza jina la Bwana wetu Yesu

Hili linaweza kuelelezewa katika muundo tendaji. AT: "ili kwamba mweze kulitukuza jina la Bwana wetu Yesu"

Ili mtukuzwa na yeye

Hili linaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: "Yesu atawatukuza ninyi"

kwa sababu ya neema ya Mungu wetu

kwa sababu ya neema ya Mungu"

2 Thessalonians 2

2 Wathesalonike 02 Maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

"Kukusanyika pamoja "ili tukae naye"

Kifungu hiki kinaashiria wakati ambapo Yesu anawaita wale wanaomwamini. Wasomi wanatofautiana iwapo hii inaashiria kurudi kwa Yesu kwa mwisho kwa utukufu ama kama si hivyo.(Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe)

Mtu muasi

Hii ni sawa na "mwana wa uharibifu" na "yule muasi" katika sura hii.Paulo anamhusisha na Shetani ambaye anafanya kazi kwa bidii duniani. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#antichrist)

Anakaa ndani ya hekalu la Mungu

Huenda Paulo anarejelea hekalu la Yerusalemu ambalo liliharibiwa na Warumi miaka chache baada ya kuandika hii barua. Ama anarejelea kwa hekalu lijalo la ukweli, ama kanisa kama hekalu la kiroho la Mungu.(Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

<< | >>

2 Thessalonians 2:1

Maelezo ya Jumla:

Paulo anawaasa waumini wasidanganywe kuhusu siku ambayo Yesu atarudi.

Sasa

Neno "Sasa" linaonyesha kubadilika kwa mada katika maelekezo ya Paulo.

Ndugu

Neno "ndugu" linamaanisha Wakristo wenzetu, linajumuisha wote wanaume na wanawake. AT: " kaka na dada"

Kwamba msisumbuliwe au kuhangaishwa kwa urahisi

kwamba msiruhusu mambo yawasumbue kwa urahisi.

kwa ujumbe au barua ambayo inadhaniwa kutoka kwetu

"kwa maneno au barua iliyoandikwa ambayo inadhaniwa kutoka kwetu.

kwa tokeo kwmba

"kusema kwamba'

siku ya Bwana

Hii inamaanisha wakati atakaporudi duniani kwa ajili ya waumini.

2 Thessalonians 2:3

Maelezo ya Jumla:

Paulo anafundisha kuhusu mtu wa uasi.

haitakuja

"siku ya Bwana haitakuja"

anguko

hii inamaanisha wakati ujao ambao watu wengi watampa Mungu kisogo.

na mwana wa uasi amefuniuliwa

Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: na Mungu anamfunua mtu wa uasi

mwana wa uaharibifu

Paulo anaongea uharibifu kama mtu alizaa mwana ambaye lengo lake ni kuharibu kila kitu. AT: "yeye aharibuye kila kitu anachoweza"

vyote vinavyoitwa Mungu au vivavyoabudiwa

Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: "kila kitu ambacho watu hukifanya kuwa Mungu au kila kitu ambacho watu huabudu"

anajiinua mwenyewe kama Mungu

"anajionyesha mwenyewe kama Mungu"

2 Thessalonians 2:5

Hamuyakumbuki...mambo haya?

Paulo anatumiwa swali lisilohitaji kujibiwa kuwakumbusha mafundisho ambayo aliwafundisha awali alipokuwa nao. Hii inaweza kuelezewa kama. AT: " Ninauahakika kuwa mnakumbuka... haya mambo."

mambo haya

Hii ina maanisha kurudi kwa Yesu, siku ya Bwana , na mtu wa kuasi.

atafunuliwa tu kwa wakati muafaka

Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: "Mungu atamfunua mtu wa uasi kwa muafaka"

siri ya kuasi

Hii ina maanisha kwa siri ambayo Mungu mwenyewe anaifahamu.

anayemzuia

kumzuia mtu ni kuwashikilia nyuma au hali kutowafanya kuendelea na kile wanachotaka kufanya.

2 Thessalonians 2:8

ndipo mwenye kuasi atakapofunuliwa

Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: Halafu Mungu atamruhusu mwenye kuasi ili kujionyesha mwenyewe.

kwa pumzi ya kinywa chake

Hapa neno "pumzi" linamaanisha nguvu ya Mungu. AT: "kwa nguvu ya neno lake lilotamkwa"

Ufunuo wa kuja kwake utamfanya kuwa sio chochote

Wakati Yesu atakaporudi duniani na kujionyesha, atamshinda yule mwenye kuasi.

kwa nguvu zote, ishara, na maajabu ya uongo

"kwa nguvu zote, ishara, na maajabu ya uongo"

na uongo wote wenye udharimu

Mtu huyu ataumia kila aina ya ubaya kuwadanganyawatu ili wamwamini yeye badala ya Mungu.

Mambo haya yatakuwepo kwa wale wanaopotea

Huyu mtu atapewa nguvu na shetani na atadanganya kila mtu ambaye hakuamini katika Yesu.

wanaopotea

Hapa "potea" lina wazo la milele au uangamivu wa milele

2 Thessalonians 2:11

Kwa sababu hii

" Kwa sababu watu hawapendi kweli"

Mungu anawatumia kazi yenye uongo ili waamini uongo

Paulo anaongea kuwa Mungu anaruhusu kitu kutokea kwa watu kana kwamba anawatumia. AT: "Mungu anaruhusu mtu wa kuasi awadanganye"

wote watahukumiwa

Hii inaaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT:" Mungu atawahukumu wote"

wale ambao hawakuamini kweli badala yake wakajifurahisha katika udhalimu

"wale ambao walifurahia udhalimu kwa sababu hawakuiamini kweli"

2 Thessalonians 2:13

Sentence Unganishi

Paulo sasa anabadilisha mada.

Maelezo ya Ujumla:

Paulo anatoa shukrani kwa Mungu kwa ajili ya wakristo na anawatia moyo.

Lakini

Paulo anatumia neno hili hapa kuanzisha kubadili mada.

inatupasa kumshukuru Mungu wakati wote

Hii ni hali ya kukuza tukio au jambo la kawaida na kulifanya kuwa kubwa zaidi kuliko uhalisia wake. AT: "tunapaswa kuendelea kutoa shukrani"

tunapaswa

Neno tunapaswa linamaanisha Paulo, Silwano, na Timotheo.

ndugu mpendwao na Bwana

Hili linaweza kulezwa katika muundo tendaji. AT: "kwa kuwa ndugu Bwana anawapenda"

ndugu

Hapa "ndugu" linamaanisha wakristo wenzangu, inajuisha wanaume na wanawake. AT: "ndugu wa kiume na wakike.

malimbuko kwa ajili ya wokovu

"kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuamini katika Yesu na kuokolewa.

katika utakaso wa Roho

"na kuwatenga ninyi kwa ajili ajili yake kwa njia ya Roho"

imani katika kweli

"kuamini katika kweli" au "kuwa na ujasiri katika kweli"

kwa hiyo, ndugu, simameni imara

Paulo anawaasa waumini waendelee kushikilia imani yao katika Yesu.

elewa tamaduni

hapa "tamaduni" linamanisha kwa ukweli wa Kristo ambao Paulo na mitume walifundisha. Paulo anaongea nao kana kwamba wasomaji wake wangeweza kushika neno kwa mikono yao.

uliyofundishwa

Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: tuliyowafundisha"

iwe kwa neno au kwa barua yetu

unaeza kuelezea kwa timilifu zaidi habari. AT: "iwe kwa kile tulichowafundisha gerezani au kile tulichowandikieni kwa barua"

2 Thessalonians 2:16

Sentensi Unganishi:

Paulo anamaliza na baraka kutoka kwa Mungu.

Sasa

Paulo anatumia neno hili kuonyesha badiliko la mada.

Bwana wetu ...aliyetupenda na kutupatia

Neno hili "aliyetupenda" na "sisi" linajumisha waumini wote.

Bwana Yesu Kristo mwenyewe

Neno "yeye mwenyewe" liongeza msisitizo kwa neno "Bwana Yesu Kristo."

awafariji na kuifanya imaramioyo yenu

"mioyo" linamaanisha kwenye sehemu ya hisia. AT: "awafariji na kuwaimarisheni kwa"

2 Thessalonians 3

2 Wathesalonike 03 Maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

watu wasiofanya kazi na wavivu

atika mji wa Thesalonike, inaonekana kulikuwa na shida ya watu katika kanisa ambao walikuwa na uwezo wa kufanya kazi lakini wakakataa kufanya hivyo. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

Utafanya nini ndugu yako akitenda dhambi?

Katika sura hii Paulo anawafundisha Wakristo kwamba wanastahili kuishi kwa njia inayomheshimu Mungu. Wakristo pia wanastahili kuhimizana na kuajibikiana wanachotenda.Kanisa pia lina wajibu wa kuwahimiza waumini kutubu wakati wanatenda dhambi. (Tazama: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#repent and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

__<< | __

2 Thessalonians 3:1

Maelezo ya Jumla:

Paulo anawaomba waumini waombe kwa ajili yake na wenzake

Na sasa

Paulo anatumia neno "sasa" kubadilisha mada.

ndugu

hapa neno "ndugu" linamaanisha wakristo wenzetu, linajumisha wanaume na wanawake. AT: "ndugu wa kiume na wakike"

neno la Bwana liweze kuenea na kutukuzwa

Paulo anaongea kutawanya kana kwamba Neno la Mungu linakimbia toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. AT: "kwamba watu wengi zaidi na zaidi hivi karibuni watasikia ujumbe wetu kuhusu Bwana wetu Yesu na kuuheshimu"

kwamba tuweze kuokolea

Hili linaweza kusemwa katika muundo tendaji: AT: "kwamba Mungu atuokoe" au " kwamba Mungu aweze kutuokoa sisi"

Kwa sababu sio wote wanayo imani

"kwa kuwa watu wengi hawaamini katika Yesu"

ambaye atawaimarisha ninhyi

"ambaye atawaimarisha ninyi"

yule mwovu

"Shetani"

2 Thessalonians 3:4

Tunao ujasiri

' Tunayo imani" au "tunaamini"

kuongoza mioyo yenu

Paulo anamwelezea Bwana kuwahamasishaWakristo wampende Mungu kana kwamba Bwana alikuwa akiwaongoza katika njia

mioyo

Hii ni sitiari kwa ajili ya hisia au takwa, ambayo inaongoza upendo na uaminifu.

kwa upendo wa Mungu na kwa uvumilivu wa Kristo

paulo anaongea upendo wa Mungu na uvumilivu wa Mungu na Kristo kana kwamba kulikuwa na mwisho katika njia. AT:Ni namna gani gani Mungu anawapenda na jinsi gani ambayo Kristo alivyovumilia kwa ajili yetu.

2 Thessalonians 3:6

Maelezo ya Jumla:

Paulo anawapa waumini maelekezo ya mwisho kuhusu kufanya kazi na sio kukaa bila kufanya kazi.

Sasa

Paulo anatumia neno hili kuonyesha kubadili mada.

katika jina la Bwana Yesu Kristo

"kwa mamlaka ya Yesu"

ndugu

hapa "ndugu" linamaanisha wakristo wenzetu, inajumuisha wote wanaume na wanawake. AT: "ndugu wa kiume na wakike"

Bwana wetu

Neno "wetu" linamaanisha waumini wote.

kuishi bila kufanya kazi

"ni mzembe na anazuia kufanya kazi"

kutuiga sisi

" kufanya kama Paulona wenzake" au " kutenda kama Paulo na watenda kazi wenzake'

Hatukuishi kati yenu kama wale wasio na nidhamu

Paulo anatumia maneno hasi ili kusisitiza maneno chanya. AT: "Tuiishi miongoni mwenu kama waliokuwa na nidhamu sana"

tulifanya kazi usiku na mchana

"tulifanya kazi wakati wa usiku na wakati wa mchana" au "tulifanya kazi muda wote"

katika kazi ngumu na shida

Paulo anasisitizajinsi hali yake ilivyokuwa ngumu. kazi ngumu inamaanisha kazi ambayo inahitaji juhudi kubwa. Ugumu inamaanisha walivumia maumivuna mateso.AT: "katika hali ngumu.

Tulifanya hivi sio kwa sababu hatukuwa ma mamlaka

Paulo anatumia neno hasi kusisitiza upande chanya. Hii inaweza kusemwa kama chanya. AT: "pasina shaka tulikuwa na mamlaka."

2 Thessalonians 3:10

baadhi wanaenenda paipo utaratibu

Hapa "enenda" linasimama kwa kumaanishatabia katika maisha. AT: "baadhi wanaishi maisha ya "kubweteka" au "wengine ni wavivu"

lakini badala yake ni watu wanaoenenda pasipo utaratibu.

Hawa nia watu wanaoingilia mambo ya wengine pasipo kuombwa kufanya hivyo.

kwa utulivu

"katika utulivu, amani utulivu." Paulo anawaasa watu wazembe waiotaka kufanya kazi waache kuchunguza mambo ya wenzao."

2 Thessalonians 3:13

Lakini

Paulo anatumia neno hili kutofautisha kati ya wakristo wavivu na wachapakazi.

ninyi, ndugu

Neno "niny" linamaanisha wakristo wote wa Thesalonike.

ndugu

Neno "ndugu" hapa linamaanisha wakristo wenzangu, inajumuisha wanaume na wanawake. AT: "ndugu wa kiume na wakike"

msizimie roho

"Kuzimia moyo" ni neno linalomaanisha kuchoka, au kukata tama." "msikate tamaa au "msichoke"

muwe makini naye

Mmtambue kuwa ni nani.AT: "mmtambue mbele za watu"

ili kwamba aweze kuaibika

Paulo anawaelekeza waumini kujihadhari nawaumini wavivu kama kitendo cha kuwaadibisha.

2 Thessalonians 3:16

Maelezo ya Jumla:

Paulo anahitimisha maoni/ ufafanuzi wake wakristo wa Thesalonike.

Bwana wa amani mwenyewe awape ninyi

Unaweza kuweka wazi kuwa haya ni maombi ya Paulo kwa Wathesalonike. AT: "Ninaomba kwamba Bwana wa amani mwenyewe awapeni..."

Bwana wa amani mwenyewe

"Mwenyewe" inaelezea kwamba Bwana mwenyewe atawapa amani wakristo.

Hii ni salamu yangu mwenyewe, Paulo, kwa mikono yangu mwenyewe

"Mimi, Paulo, naandika salamu kwa mkono wangu mwenyewe"

Hivi ndivyo niandikavyo

Paul anaweka wazi kwamba hii barua inatoka kwake na sio ya kubumba