Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa 1 Yohana

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha 1 Yohana

  1. Utangulizi (1:1-4)
  2. Kuishi Kikristo (1:5-3:10)
  3. Amri ya kupendana (3:11-5:12)
  4. Hitimisho (5:13-21)

Nani aliandika Kitabu cha 1 Yohana?

Kitabu hiki hakitaji mwandishi. Hata hivyo, tangu wakati wa Kikristo wa kwanza, Wakristo wengi wamefikiri kwamba Mtume Yohana ndiye aliyekuwa mwandishi. Yeye pia aliandika Injili ya Yohana.

Je, kitabu cha 1 Yohana kinahusu nini?

Yohana aliandika barua hii kwa Wakristo wakati ambapo walimu wa uongo walikuwa wakiwasumbua. Yohana aliandika barua hii kwa sababu alitaka kuzuia waumini wasitende dhambi. Alitaka kuwalinda waumini dhidi ya mafundisho ya uongo. Na alitaka kuwahakikishia waumini kwamba walikuwa wameokolewa.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha jadi, "1 Yohana" au "Yohana wa Kwanza." Au wanaweza kuchagua kichwa cha wazi, kama "Barua ya Kwanza Kutoka kwa Yohana" au "Barua ya Kwanza Aliyoandika Yohana." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Ni watu wapi ambao Yohana alizungumza dhidi yao?

Watu ambao Yohana alizungumza dhidi yao inawezekana kwamba walikuwa wale ambao wangejulikana kama Wagnostiki. Watu hawa waliamini kwamba dunia ni uovu. Kwa kuwa waliamini kwamba Yesu alikuwa wa kiungu, walikanusha kwamba alikuwa mwanadamu kweli. Hii ni kwa sababu walidhani Mungu hawezi kuwa mwanadamu kwa sababu mwili ni uovu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#evil)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Maneno "kubaki" na "kuishi" na "kukaa" yana maana gani katika 1 Yohana?

Yohana mara nyingi alitumia maneno "kubaki," "kuishi," na "kukaa" kama sitiari. Yohana alizungumzia muumini kuwa mwaminifu zaidi kwa Yesu na kumjua Yesu vizuri ikiwa neno la Yesu "lilibaki" ndani ya muumini huyo. Pia, Yohana alizungumzia mtu aliyejiunga kiroho na mtu mwingine kana kwamba mtu "aliyebaki" katika mtu mwingine. Wakristo wanasema "kubaki" katika Kristo na kwa Mungu. Baba anasemekana "kubaki" ndani ya Mwana, na Mwana anasemekana"kubaki" ndani ya Baba. Mwana anasemekana "kubaki" katika waumini. Roho Mtakatifu pia anasemekana "kubaki" ndani ya waumini.

Watafsiri wengi wataona kuwa ni vigumu kuwakilisha mawazo haya katika lugha zao kwa njia hiyo hiyo. Kwa mfano, Yohana alitaka kueleza wazo la Mkristo kuwa pamoja na Mungu kiroho wakati alisema, "Yeye asemaye anakaa katika Mungu" (1 Yohana 2: 6). UDB inasema, "Ikiwa tunasema kuwa sisi tuna umoja na Mungu," lakini watafsiri mara nyingi wanapaswa kutumia maneno mengine ambayo yanawasilisha mawazo haya vizuri.

Katika kifungu hicho, "neno la Mungu linakaa ndani yenu" (1 Yohana 2:13), UDB inaelezea wazo hili kama, "unaendelea kutii kile ambacho Mungu anaamuru." Watafsiri wengi wataona kuwa inawezekana kutumia tafsiri hii kama mwongozo.

Je, ni masuala gani muhimu katika Kitabu cha 1 Yohana?

Yafuatayo ni masuala muhimu zaidi ya maandishi katika 1 Yohana:

  • "Na tunawaandikia mambo haya ili furaha yetu iwe kamili." (1:4) ULB, UDB, na matoleo ya kisasa zaidi husoma hivi. Baadhi ya matoleo ya zamani yana, "Na tunawaandikia mambo haya ili furaha yenu iwe kamili."
  • "Na ninyi nyote mnajua ukweli." (2:20) ULB, UDB, na matoleo ya kisasa zaidi yasoma hivi au ifuatavyo: "Na ninyi nyote mna ujuzi." Baadhi ya matoleo ya zamani yana, "na mnajua vitu vyote."
  • "na hivi ndivyo tulivyo!" (3:1). ULB, UDB, na matoleo ya kisasa zaidi kusoma hivi. Baadhi ya maandishi ya zamani yameacha maneno haya.
  • "na kila roho isiyokubali Yesu haitoki kwa Mungu." (4:3) ULB, UDB, na matoleo ya kisasa zaidi yana somo hili. Baadhi ya maandishi ya kale yanasoma, "na kila roho isiyokubali kwamba Yesu amekuja katika mwili sio ya Mungu."
  • "Kwa maana kuna watatu wanaoshuhudia mbinguni: Baba, Neno, na Roho Mtakatifu, na hawa watatu ni mmoja.Nao kuna watatu ambao wanashuhudia duniani: Roho, maji, na damu; na hawa tatu ni kama moja." (5:7-8). ULB, UDB, na matoleo mengine mengi hayasomi hivi. Watafsiri wanashauriwa kutafsiri hii kama ULB inavyofanya. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri, kuna matoleo ya zamani ya Biblia ambayo yanajumuisha kifungu hiki, watafsiri wanaweza kukijumuisha. Ikiwa imejumuishwa, inapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda haipo katika toleo la awali la 1 Yohana. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

1 John 1

1 Yohana 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Hii ni barua ambayo Yohana aliwaandikia Wakristo.

Dhana maalum katika sura hii

Wakristo na dhambi

Katika sura hii Yohana anafundisha kwamba Wakristo wote bado ni wenye dhambi. Lakini Mungu anaendelea kusamehe dhambi za Mkristo. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#forgive)

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Mifano

Katika sura hii Yohana anaandika kwamba Mungu ni mwanga. Mwanga ni mfano ya ufahamu na uadilifu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous)

Yohana pia anaandika kuhusu watu wanaotembea katika nuru au katika giza. Kutembea ni mfano ya tabia au kuishi. Watu wanaotembea katika mwanga huelewa kilicho haki na kukifanya. Watu wanaotembea katika giza hawawezi kuelewa yaliyo sawa, na wanatenda dhambi.

| >>

1 John 1:1

Sentensi Unganishi

Kitabu hiki kinaanza makusudi yake mawili - Ushirika na Furaha.

Maelezo ya Jumla

Mtume Yohana aliandika waraka huu kwa Waamini. Mifano yote ya "nyinyi" na "yenu," hujumuisha waaminio wote na yako katika wingi. Maneno "sisi" na "tu" hapa humaanisha Yohana na walie waliokuwa wameishi na Yesu. Mstari wa 1 ni nusu sentensi, unatakiwa usomwe pamoja na msitari 2. na Sentensi kamili huishia 1:3

Lile lililokuwako tangu mwanzo

Kifungu cha maneno "lile lililokuko tangu mwanzo" humaanisha Yesu, aliyekuwako kabla ya kila kitu kilichofanyika.:Tunawaandikia juu ya yule alikuwako kabla ya uumbaji wa vitu vyote

Neno la uzima

"Neno la uzima" ni Yesu Kristo. Yesu, yule anayesababisha watu waishi milele.

Uzima

Neno "uzima" mwote katika barua hii humaanisha zaidi ya uzima wa kimwili. Hapa linasimama badala ya Yesu, aliye uzima wa milele.

Na ule uzima ulifanywa kujulikana wazi

Hili linaweza kutamkwa katika mtindo tendaji. :"Mungu aulifanya uzima wa milele ujulikane kwetu" au Mungu alitufanya sisi tuweze kumjua yeye, aliye uzima wa milele"

na tumeuona

"na tumemwona yeye"

na kuushuhudia,

"na tunawatangazia na wangine kwa dhati kuhusu yeye"

uzima wa milele

"Uzima wa milele," hapa humaanisha yule ambaye hutoa uzima, Yesu. : "Yule anayetuwezesha sisi kuishi milele"

ambalo lilikuwa pamoja na Baba

"aliyekuwa na Mungu Baba"

na lilifanywa kujulikana kwetu

Huu ulikuwa ni wakati alioishi duniani. :"na alikuja kuishi miongoni mwetu"

1 John 1:3

Maelezo ya Jumla

Hapa maneno "tu...," "nasi" na "yetu" humaanisha Yohana na wale ambao wamekuwa pamoja na Yesu.

Lile ambalo tumeliona na kulisikia twalitangaza pia kwenu

Tunawaambieni pia nanyi tuliloliona na kulisikia"

muwe na ushirika pamoja nasi. Ushirika wetu ni pamoja na Baba

"muwe rafiki zetu wakaribu. Tu marafiki wa Mungu Baba"

Ushirika wetu

Hako wazi kama Yohana anawaingiza ama anawaacha wasomaji wake.

Baba...Mwana

Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea uhusiano ulioko baina ya Mungu na Yesu.

ili kwamba furaha yetu iwe kamili.

"kuifanya furaha yetu ikamilike" au kutufanya sisi tufurahi kikamilifu kabisa"

1 John 1:5

Sentensi Unganishi

Tangu hapa hata sura inayoofuata, Yohana naaandika kuhusu ushirika - uhusiano wa karibu pamoja na Mungu na aamini wengine.

Maelezo ya Jumla

Hapa maneno "sisi" na "yatu.." humaanisha waaminio wote, kumlisha watu ambao Yohana alikuwa akiwaandikia. Ispokuwa imetamkwa vinginevyo, hiyo ndiyo maana kwa ukumbusho wa kitabu hiki.

Mungu ni nuru

Hii humaanisha kwamba Mungu ni safi na mtakatifu kikamilif. Zile tamaduni zinahusianisha weme na nuru zinaweza kulishika wazo hili bila ya kulifafanua fumbo lenyewe. "Mungu ni kwa uhalisia Mungu ni mwenye haki na kama nuru halisi"

ndani yake hakuna giza hata kidogo

Hii humaanisha kwamba MUngu hawezi kutenda dhambi na siyo mwovu kwa namna yo yote.Zile tamaduni zinahusianisha uovu na giza zinaweza kulielewa wazo hili bila kulielezea fumbo lenyewewe. : "Ndani yake hakuna giza la dhambi"

twatembea gizani,

Hii humaanisha "kujizoweza uovu na kutenda uovu"

damu ya Yesu Kristo,

Hii hurejelea kifo cha Yesu.

Mwanawe

Cheo hiki ni muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.

1 John 1:8

Malezo ya Jumla

Hapa neno "yeye" "lake" humaanisha Mungu.(Tazama 1:5)

hatuna dhambi

"hatutendi dhambi"

twajidanganya

"Twajilaghai wenyewe" au "tunajiambia uongo wenyewe"

kweli haimo ndani yetu

Ile kweli imezungumziwa kana kwamba lilikuwa ni jambo au kitu kambacho kingeweza kuwa ndani ya waamini.

kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote

Virai hivi viwili kimsingi vinamaanisha jambo lile lile. Yohana anavitumia kusisitiza kwa hakika Mungu atasamehe dhambi dhambi. : "na atazisamehe kabisa kabisa ubaya ambao tumeufanya"

twamfanya yeye kuwa muongo,

tunadai kwamba yeye ni mwongo: "ni sawasawa na kumwita yeye mwongo, kwa sababu amesema sisi sote tumetenda dhambi"

neno lake halimo ndani yetu

Kutii kuheshimu neno la Mungu kumezunguziwa kana kwamba neno lake lilikuwa ndani ya waamini. : "hatulielewi neno la Mungu wala hatutii linachokisema"

1 John 2

1 Yohana 02 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mpinga Kristo

Katika sura hii Yohana anaandika juu ya mpinga Kristo maalum na wapinga Kristo wengi. Neno "mpinga Kristo" linamaanisha "anayepinga Kristo." Mpinga Kristo ni mtu atakayekuja siku za mwisho na kuiga kazi ya Yesu, lakini ataifanya kwa uovu. Kabla ya mtu huyu kuja, kutakuwa na watu wengi wanaofanya kazi dhidi ya Kristo; wao pia huitwa "wapinga Kristo." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#antichrist and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lastday and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#evil)

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Mfano

Kuna makundi kadhaa ya ya mifano yenye kufanana ambao yanatumiwa katika sura hii.

Kuwa ndani ya Mungu ni mfano ya kuwa na ushirika pamoja na Mungu, pia neno la Mungu na ukweli kuwa ndani ya watu ni mfano ya watu kujua na kutii neno la Mungu.

Kutembea ni mfano ya tabia, kutojua ambapo mtu anaenda ni mfano ya kutojua jinsi ya kuishi, na kujikwaa ni mfano ya dhambi.

Nuru ni mfano wa kujua na kufanya kile kilicho sahihi, na giza na upofu ni mfano ya kutojua kilicho sahihi na kutenda mabaya.

Watu wanaopotosha wengine ni mfano ya kufundisha watu mambo yasiyo ya kweli. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

<< | >>

1 John 2:1

Sentensi Unganishi

Yohana anaendelea kuandika juu ya ushirika na anaonyesha kwamba inawezekana kwa sababu Yesu yuko kati ya waaminio na Baba.

Maelezo ya Jumla

Hapa maneno "tunaye' na "zetu" humaanisha Yohana na waaminio wote. Neno "Yeye" na "zake" yaweza kumaanisha Mungu Baba au Yesu.

Watoto

Yohana alikuwa mzee na kiongozi wao. Alitumia maelezo haya kuonyesha pendo lake kwao. : "Watoto wangu wapendwa katika Kristo" au "Ninyi mliowapendwa kwangu kama watoto wangu mwanyewe"

ninawaandikia mambo haya

"Ninaandika barua hii"

Lakini kama mmoja wenu akitenda dhambi

"Lakini mmoja wenu anapotenda dhambi." Hili ni jambo ambalo inawezekana likatokea"

tunaye wakili aliye pamoja na Baba,

Neno "wakili" hapa humaanisha Yesu. : "mtu anayezungumza kwa Mungu Baba na kumsihi yeye apate kutusamehe sisi"

eye ni upatanisho kwa dhambi zetu, na siyo kwa dhambi zetu

"Aliyatoa dhabifu maisha yake mwenyewe kwa ajili yetu, na kwa sababu ya hilo Mungu husamehe dhambi zetu"

Kwa hili twajua kwamba , kama tukizishika amri zake.

"Kama tunafanya anayotuambia kufanya, kisha tutakua na uhakika kwamba tunao uhusiano na yeye"

tunamjua yeye

"tunao uhusiano na yeye"

1 John 2:4

Yeye asemaye

"Yeyote anayesema" au "mtu anayesema"

Namjua Mungu,

"Nina uhusiano mwaema na Mungu

lakini hazishiki

"hatendi" au "hatii"

amri zake

"kile mabacho Mungu anamwambia kutenda"

kweli haimo ndani yake

Kweli imezungumziwa kana kwamba ni jambo lingeweza kuwa ndani ya waaminio. : " Haamini ambacho Mungu anasema kuwa ndiyo kweli"

ashikaye

"hutenda" au "hutii"

neno lake

"kile Mungu anachombia yeye kutenda"

upendo wa Mungu

Maana zinzowezekana kuwa ni 1) "upendo wetu kwa Mungu au 2) "upendo wa Mungu kwetu."

kweli katika mtu yule upendo wa Mungu umeshakamilishwa

Hili linaweza kutamkwa kwatika muundo tendaji. : "Mungu amekamilisha pendo wa Mungu ndani ya mtu huyo," "Kwa hakika, wale wanaotii amri za Mungu ni watu wanaommpenda Mungu katika njia zote," au "upendo wa Mungu kwa watu hutimiza lengo lake wanapotenda analowaambia kutenda"

Katika hili twajua kwamba tuko ndani yake

Kirai "tuko ndani yake" humaanisha mwamini ana muuu ngano na Mungu daima au ana ushirika na Mungu unaoendelea. Katika 1Yohana, kiari/kifungu "kaa ndani yake" mara kwa mara limetumika kumaanisha kitu kile kile. : "Tunapotii analotuambia Mungu, tunaweza kuwa na uhakika kwamba tuna ushirika na yeye"

tuko ndani yake

"tuna uhusiano na Mungu"

imempasa yeye mwenyewe pia kuenenda kama vile Yesu Kristo alivyoenenda.

Unayafanya maisha ya mtu kana kwamba yalikuwa yakitembea. : "ni lazima aishi kama Yesu Kristo alivyoishi' au "inampasa pia kumtii Mungu kama tu vile Yesu Kristo alivyotii"

1 John 2:7

Sentensi Unganishi

Yohana anawapa waaminio kanuni za msingi za ushirika - utii na upendo

Wapendwa

"Ninyi watu niwapendao" au "Rafiki wapendwa"

siwaandikii ninyi amri mpya, bali amri ya zamani

"Ninaaandikia kupendana nyinyi kwa nyinyi, ambalo siyo jambo jipya kutenda bali ni amri ya zamani amabayo mmishaisikia." Yohana anamaanisha amri ya Yesu ya kupendana kila mtu na mwenzake

tangu mwanzo

Hapa, neno 'mwanzo" humaanisha wakati walipoamua kumfuata Kristo. "tangu mlipoanza kuamini katika Kristo"

Hata hivyo ninawaandikia ninyi amri mpya,

Lakini kwa namna nyingine amri ninayowaandikia ni mpya"

ambayo ni kweli katika Kristo na kwenu,

Hapa neno "Katika" humaanisha "kwa sababu ya." : "ambayo ni kweli kwa sababu ya alichotenda Kristo, na kwa sababu ya mnchotenda nyinyi"

giza linapita, na nuru ya kweli iko tayari inaangaza

"giza," hapa humaanisha uovu na "nuru" humaanisha wema. ; "kwa sababu mnaacha kutenda ovu na mna zidi kutenda jema zaidi na zaidi.

1 John 2:9

Maelezo ya Jumla

Hapa, neno "ndugu" humaanisaha Mkristo mwenza

Yeye asemeye

"Yeyote asemaye" au "Wale wanaodai." Hiaimanishi mtu yeyote.

yuko kwenye nuru

Hii ni picha ya kuishi kwa haki. Watu wanapofanya lililo haki, wanaweza kulifanya nuruni siyo kwa kificho gizani.: "hufanya lililo sahihi"

yuko katika giza hata sasa

Hii ni picha ya kuishi maisha ya dhambi. Watu wanapofanya yaliyo maovu, hupenda kujificha gizani. : "yuko gizani, akitenda lililo ovu"

hakuna jambo lolote liwezalo kumkwaza.

hakuna litakalomsababisha kujikwaa." Neno "kujikwaa" ni fumbo linalomaanisha kuanguka kiroho au kimaadili. : " hakuna litakalomsababisha kutenda dhambi" au "hatashindwa lipendezalo kwa Mungu"

yuko gizani na anatembea gizani

wazo hili linalofanana limesemwa mara mbiili kusisitiza kulivyo uovu kumchukia mwamini mwenzako. "anaishi gizani au anaishi katika giza la dhamb

hajui wapi aendako

Hii ni picha ya Mwamini anayeishi isivyompasa Mkristo kuishi. : "hata hajui kwamba analofanya ni ovu"

giza limeyapofusha macho yake

"giza limemfanya asiweze kuonona." giza ni fumbo au mfano kwa ajili ya dhambi au uovu. : "dhambi imefanya isiwezekane kwake kuielewa kweli"

1 John 2:12

Maelezo ya Jumla

Yohana anaelezea sababu inayomfanya kuandika barua yake ama kwa vikundi vyenye umri mbalimbali au kwa waamini wanaotofautiana katika ukomavu. Barua yenyewe imeandikwa kwa mtindo wa kishairi.

watoto wapendwa

Yohana ni mzee na kiongozi wao. Alitumia maelezo haya kuonyesha upendo kwa aji yao. : "Watoto wangu wapendwa katika Kristo" au "ninyi mlio wapendwa kama watoto wangu mwenyewe." Tazama maelezo katika sura ya 2:1 uone linavyofafanuliwa.

dhambi zenu zimesamehewa

"Mungu husamehe dhambi zenu"

kwa ajili ya jina lake.

"jina lake" humaanisha Kristo na alivyo yeye. :"kwa sababu ya kile Kristo amefanya kwa ajili yenu"

Nawaandikia ninyi, akina baba,

Neno "akina baba" hapa linaweza kuwa fumbo au mfano ukimaanisha waamini waliokomaa. : "Ninawaandikia ninyi, waamini mlikoamaa

mnamjua

"mna uhusiano na"

yeye aliye wa tangu mwanzo.

"yeye ambaye amekuwa akiishi siku zote" au "yeye ambaye amekuwako siku zote." humaanisha Yesu au Mungu Baba."

vijana,

Hili inawezekana kumaanisha wale wasio waamini wapya tena, bali ni wale wanokua katika ukomavu wa kiroho

mko imara,

Hapa neno "imara" halimaanishi nguvu za kimwili za waamini, bali ni ule uaminifu wao kwa Kristo.

neno la Mungu linakaa ndani yenu

Mwandishi anamaanisha lile ongozeko la uaminifu wa waaminio kwa Kristo na ufahamu wao juu Yake kana kwamba alikuwa akiongelea neno la Mungu likiishi ndani yao. : "Ninyi mnaolijua neno la Mungu"

mmemshinda

Mwandishi anazungumzia juu ya maaminio kukataa kumfuata Shetani na kuipinga kwao mipango yake kana kwamba mambo hayo yamekuwa ni jambo la kumshinda yeye.

1 John 2:15

Msiipende dunia

Neno "dunia" katika 2:15-17 humaaniha mabo yote watu hutaka kufanya , mambo ambayo hayamtukuzi Mungu. : "Msienende kama watu wa duniani wasiomheshimu Mungu"

wala mambo yaliyo katika dunia

"msitake mambo yale yale wanayoyataka wale wasiomheshimu Mungu"

Kama kuna yeyote ambaye huipenda dunia, upendo wa Baba haumo ndani yake.

Mtu hawezi kuipenda dunia hii pamoja na wale wote wasiomheshimu Mungu na kumpenda Baba wakati huo huo.

upendo wa Baba haumo ndani yake

"hawa hamendi Baba"

tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima-

Hii ni orodha ya baadhi ya mambo yaliyomo duniani. Nayo huelezea inamaana nini kusema "kila kilichomo dunianai"

tamaa ya mwili

"tamaa kali ya kuwa starehe ovu za kimwili"

tamaa ya macho,

"tamaa kali ya kuwa na vitu tuvionavyo"

kiburi cha uzima

"Kiburi cha uzima." hili laweza kuashiria pande zote mali na nia. "kujivunia alicho nacho mtu au anachotenda" au "kiburi ambacho watu husikia kwa sababu ya vitu vyao na kile mtu amefanya."

uzima

Hili lingeweza kumaanisha vitu walivyo navyo watu ili kuishi, vitu kama vile mali, utajiri pamoja na nia.

hayatokani na Baba

"hayatoki kwa Baba" au "sivyo hivyo Baba alivyotufundisha kuishi"

yapita

"yanapita" au "siku moja hayatakuwepo"

1 John 2:18

Sentensi Unganishi

Yohana anaonya juu ya wale waliokinyume na Kristo

Watoto wadogo

"Wakristo wasiokomaa." Tazama sura 2:1 uone lilivyofafanuliwa

ni wakati wa mwisho

Kile kirai "Wakati wa mwisho" humaanisha muda kabla ya kurudi kwa Yesu. "Karibu Yesu atarudi"

wapingakristo wengi wamekuja,

"kuna watu wengi waliokunyume cha Kristo"

kwa hali hii tunajua

"na kwa sababu ya hili tunajua" au "na kwa sababu wapngakristo wametokea, tunajua"

Walikwenda zao wakatoka kwetu

"walituacha"

kwa kuwa hawakuwa wa kwetu.

"lakini kwa kweli hawakuwa wa kwetu kwa namna yoyote" au "kwa uhalisia hawakuwa sehemu ya kundi letu katika nafasi ya kwanza ." Sababu iliyofanya waondoke ni kwamba, kwa kweli sehemu ya kundi; yaani hawakuwa waaminio katika Yesu Kristo.

Kama wangekuwa wa kwetu wangeendelea kuwa pamoja nasi

"Tunajua hivi kwa sababu wasingekuwa wametuacha kama kwa kweli wangelikuwa waamini.

1 John 2:20

Maelezo ya Julama

Katika Agano La Kale neno kutia "mafuta" lilimaanisha kumimina mafuta juu ya mtu ili kumtenga kwa ajili ya kumtumikia Mungu.

Lakini mumetiwa mafuta na yule Mtakatifu

"Bali Yule Mtakatifu amewatia mafuta ninyi. Hapa "kutia mafuta" humaanisha kazi ya Yesu kuwapa waaminio Roho Mtakatifu ili kuwatenga kwa ajili ya kumtumikia Mungu. : "Lakini Kristo, aliye Mtakatifu, amwapa ninyi Roho wake Mtakaifu"

hakuna uongo kwa ile kweli

Hapa tendo la kuema uongo limzungumzwa kana kwamba ni kitu. : "hakuna uongo ujao kutoka kwa Mungu ambaye ni kweli.

1 John 2:22

Nani ni mwongo bali ni yeye anayepinga kwamba Yesu ni Kristo? Huyu mtu ni mpinga kristo

Nani ni mwongo? ni yeyote akanaye ukweli kwamba Yesu ni Kristo." Yohana alitumia swali kusisitiza waongo ni nani.

anayemkana Baba na Mwana.

"hukataa kusema kweli kuhusu Baba na Mwana" au "humkataa Baba na Mwana."

Baba... Mwana

Hivi ni vyeo muhimu ambavyo huelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

ana Baba

"ni wa Baba"

amkiriye Mwana

Husema kweli kuhusu Mwana"

ana Baba

"ni wa Baba"

1 John 2:24

Sentensi Unganishi

Yohana anawakumbusha waamini kuendelea katika lile walilokisikia hapo kwanza

Maelezo ya Jumla

Hapa neno "ninyi" ni katika wingi nna humaanisha watu ambao Yohana anawaandikia pia na waamin wote.

kile mlilosikia toka mwanzo acha liendelee kuwa ndani yenu.

"Kumbukeni na kuamini lile mlilolisikia tangu mwanzo>" Walilisikiaje, walilolisikia, na mwamwazo humaanisha nini, linaweza kuwekwa wazi. "endeleeni kutumaini tulilowafundisha kuhusu Yesu kama tu vile ambavyo mmetumaini tangu mwe waamini.

Lile mlilolisikia tangu mwanzo

"tulilowafundisha kuhusu Yesu mlipoanza kuwa kuwa waamini"

ikiwa mlilolisikia hukaa ndani yenu

Neno "hukaa" linazungumzia kuhusu uhusiano, siyo wakovu. "ikiwa mtaendelea kutumaini tullowafundisha hapo kwanza"

pia mtakaa ndani ya Mwana na Baba

"pia mwe na uhusiano pamoja na Mwana pamoja na Baba." Tazama maelezo katika 2:4 Uone lilivyofafanuliwa

Na hii ni ahadi aliyotupatia sisi: uzima wa milele.

"na hivi ndivyo alivyotuahidi sisi kutupa - uzima wa milele" au " Na ametusababisha kuishi milele.

uzima

Neno "uzima" katika barua nzima humaanisha zaidi ya uzima wa kimwili. Tazama maelezo katika 1:1 uone lilivyofafanuliwa

wangeliwakosesha

"wanaotaka kuwaondoa njiani." Kuna wale ambao wangejaribu kuwaondoeni kwa Mungu na kweli Yake" "wangewasababisha kuamini uongo"

kosesha

Shawishi mtu kutomtii Mungu limezugumziwa kana kwamba linlikuwa likimtoa mtu kwanya njia sahihi ya kufuata

1 John 2:27

Sentensi Unganishi

Kuazia mstari 29, Yohana anatambulisha wazo la kuzaliwa kwenye familia ya Mungu. Mistari inayotangulia inaonyesha kwamba waaminio huendelea kutenda dhambi, sehamu hii inaonyesha waamini pia wana asili mpya ambayo haitendi dhambi. Inaendelea kuelezea kwamba wanaweza kutambuana kila moja.

Na kwa ajili yenu

Kifungu hiki kinamwonyesha Yohana akiwaambia pia ilivyowapasa kuishi kama wafuasi wa Yesu badala ya kuwafuata wale waliokinyume na Kristo.

yale mafuta

Humaanisha "Roho wa Mungu." Tazama maelezo katika 2:20 uone linavyofafanuliwa

mambo yote

Kirai hiki ni baalagha ambayo hutia chumvi mambo au matukio. : "kila kitu mnachohitaji kukijua"

kaeni ndani yake.

"ishini kwa ajili ajili yake." Tazama uone jinsi kurai hiki kilivyotafsiriwa katika 2:4. Jinsi mtu anavyokaa humaanisha ushirika au uhusiano wake.

Na sasa

Kirai hiki kimetumika kuunda sehemu mpya ya barua.

watoto wapendwa

Yohana alikuwa mtu mzeena kiongozi wao. Alitumia maelezo haya kuonyesha pendo lake kwao. : "watoto wangu wapendwa katika Kristo" au "ninyi mlio kama wapendwa kwangu kama wato wangu mwenyewe. Tazama ufafanuzi wake katika 2:1

atakapotokea,

"tutamwona yeye"

ujasiri

"kujiamini"

wakati atakapotokea

"atakapokuja tena"

amezaliwa na yeye.

amekuwa mzaliwa wa Mungu" au ni mtoto wa Mungu"

1 John 3

1 Yohana 03 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Watoto wa Mungu

Mungu aliumba watu wote, lakini watu wanaweza tu kuwa watoto wa Mungu kwa kumwamini Yesu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe)

Kaini

Kaini alikuwa mwana wa mtu wa kwanza, Adamu, na mwanamke wa kwanza, Hawa. Alimwonea wivu ndugu yake na kumwua. Wasomaji hawawezi kujua Kaini ni nani ikiwa hawajasoma kitabo cha Mwanzo. Wanaweza kusaidiwa ikiwa unawaelezea hivi.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Kujua"

Kujua" ni neno la kitenzi kinachotumika kwa njia mbili tofauti katika sura hii. Wakati mwingine hutumiwa kuhusu kujua ukweli, kama katika 3:2, 3:5, na 3:19. Wakati mwingine inamaanisha uzoefu na kuelewa mtu au kitu, kama katika 3:1, 3:6, 3:16, na 3:20. Lugha zingine zina maneno tofauti kwa maana hizi tofauti.

"Yeye anayezingatia amri za Mungu anakaa ndani yake, na Mungu anakaa ndani yake"

Wasomi wengi wanaamini kama hii inamaanisha kubaki katika mapenzi ya Mungu wala sio kumaanisha kuokolewa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#eternity and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#save)

<< | >>

1 John 3:1

Angalia ni pendo la namna gani ametupatia Baba.

"Fikiria kuhusu kiasi gani Baba yetu anavyotupenda sisi."

Sisi...Tu.

Katika 3:1-3 viwakilishi nomino hivi, humtaja Yohana, wasikilizaji wake, na waumini wote.

Lazima tuitwe watoto wa Mungu.

Hii inaweza kutafsiriwa kwa kitenzi tendaji: "Baba lazima atuite sisi watoto wake."

Watoto.

Hapa hii inamaanisha watu wa Mungu kwa imani katika Yesu.

Ulimwengu haututambui, kwa sababu hakumtambua Yeye.

Hapa "ulimwengu" humaanisha watu ambao hawamheshimu Mungu. Kile ambacho ulimwengu haukijui, hakiwezi kufanywa dhahili: Wale ambao hawamheshimu Mungu, hawajui kwamba sisi ni wa Mungu, kwa sababu hawakumjua Mungu.

Haijadhihirika bado.

Hii inaweza kutafsiriwa kwa kitenzi tendaji: "Mungu hajadhihirisha."

Na kila mtu ambaye ana ujasiri huu kuhusu wakati ujao ulioelekezwa kwake, hujitakasa mwenyewe kama yeye alivyo mtakatifu.

"Kila mtu ambaye anatarajia kwa ujasiri kumuona Kristo kama alivyo, ataendelea kujitakasa mwenyewe kwa sababu Kristo ni mtakatifu."

1 John 3:4

Anafanya uasi.

"Ana kataa kutii sheria ya Mungu"

Ninyi.

Hapa neno "Ninyi" ni wingi na inawalenga watu ambao Yohana anawaandikia.

Kristo alidhihirishwa.

Hii inaweza kutafsiriwa kwa kitenzi tendaji: "Kristo alitokea" au "Baba alimfunua Kristo."

Kudumu katika yeye.

"Ni kuendelea kufanya anayotaka Yesu."

Hakuna ambaye...amemuona au amemfahamu.

Yohana hutumia neno "amemuona" na "amemfahamu" kusisitiza kwamba mtu ambaye hudumu katika kutenda dhambi hajawahi kukutana na Yesu katika maana ya kiroho. "Hakuna ambaye...hajawahi kabisa kumwamini Yeye."

1 John 3:7

Watoto wapendwa.

Watoto wanaopendwa/waumini wanaopatana naye.

Msiruhusu mtu yeyote kuwapotosha.

"Msikubali mtu yeyote awafanye wajinga" au "msikubali mtu yeyote awadanganye."

Atendaye haki ni mwenye haki, kama Kristo alivyo mwenye haki.

"Anayetenda kilicho sahihi anampendeza Mungu kama Kristo anavyompendeza Mungu."

Hutenda dhambi.

"Huendelea kutenda dhambi"

Ni ya Ibilisi.

"Humilikiwa na shetani au ni kama shetani"

Kutoka mwanzo.

Hii inalenga hasa nyakati za uumbaji kabla ya binadamu hawajaanguka dhambini. "Tangu nyakati za mwanzo za uumbaji."

Mwana wa Mungu alidhihirishwa.

Hii inaweza kutafsiriwa kwa fungu la maneno yanayoonesha kitendo: "Mungu alimudhihirisha Mwanawe."

Mwana wa Mungu.

Hili ni jina mhimu kwa Yesu ambalo hufafanua uhusiano kwa Mungu.

1 John 3:9

Yeyote aliyezaliwa na Mungu.

Hii inaweza kutafsiriwa kwa fungu la maneno lenye kitendo: "Yeyote ambaye Mungu amemfanya kuwa mwana wake."

Hafanyi dhambi.

"Hawezi kuendelea kutenda dhambi."

Mbegu ya Mungu.

Hii inalinganisha mbegu ya kawaida inayo pandwa katika udongo na hustawi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ambaye Mungu humweka ndani ya waumini, Roho huwapa nguvu za kupinga dhambi na kufanya kile kinachomfurahisha Mungu. Hii ingeweza kutafsiriwa kama hivi: "Roho Mtakatifu"

Amezaliwa na Mungu.

Hii inaweza kutafsiriwa kama fungu la maneno yenye kitendo: "Mungu amempa maisha mapya ya kiroho" au "Ni mtoto wa Mungu."

Kwa jinsi hii watoto wa Mungu na watoto wa shetani wanajulikana.

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi yenye kuonesha tendo: "Hivi ndivyo tunavyowajua watoto wa Mungu na watoto wa shetani."

Yeyote asiye fanya mambo ya haki huyo si wa Mungu, wala ambaye hampendi ndugu yake.

Hapa "ndugu" humaanisha Wakristo wapendwa. Wale tu wanaofanya haki ndio wa Mungu, na wale tu ambao huwapenda ndugu zao."

1 John 3:11

Tuna pasa kupenda.

Hapa, neno "tuna" linalenga waumimini wote.

Ndugu.

Katika tukio hili, neno ndugu linamaanisha mdogo wake na Kaini, Abeli.

Na kwa nini alimuua?Kaw sababu

Yohana anatumia swali kuwafundisha wasikilizaji wake. Hii ingeweza kutafsiriwa kama usemi: "Alimuua kwa sababu."

Kazi zake zilikuwa na uovu, na kazi za ndugu yake zilikuwa za haki.

"Kwa sababu daima alifanya mambo maovu na ndugu yake alikuwa akifanya mambo mazuri."

1 John 3:13

ndugu

"Waamini wenzangu."

Kama ulimwengu utawachukia

Hapa neno "ulimwengu" lina maana ya watu ambao hawamheshimu Mungu. "Kama hao wasiomheshimu Mungu watawachukia.

Tumetoka katika mauti kuingia uzimani.

"Hatuko tena wafu kiroho bali tu wazima kiroho."

Kudumu katika mauti.

"Ni kuendelea kufa kiroho."

Yeyote anaye mchukia ndugu yake ni muuaji.

Hii ni kumlinganisha mtu anaye mchukia muumini mwingine na muuaji. Kwa kuwa chuki ni chanzo cha mauaji, Mungu humuwazia mtu yeyote mwenye chuki kuwa mwenye hatia kama aliye muua mtu. "Yeyote anayemchukia muumini mwenzake ana hatia kama muuaji."

Uzima wa milele haukai ndani ya muuaji.

"Uzima wa milele" ni uhai ambao Mungu hutupatia waumini baada ya kufa, lakini pia ni nguvu ambayo Mungu huwapatia waumini katika uzima huu, kuwasaidia waache kufanya dhambi na wafanye yale yanayo mpendeza yeye. "Muuaji hana nguvu za uzima wa kiroho zinazofanya kazi ndani yake."

1 John 3:16

Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu.

Maelezo haya humaanisha: "Kristo kwa kupenda kwake mwenyewe aliutoa uhai wake kwa ajili yetu" au "Kristo kwa kupenda kwake alitufia sisi."

Mali za ulimwengu.

"Mali zinazomilikiwa kama vile pesa, chakula, au nguo."

Humuona ndugu yake mwenye uhitaji.

"Na humtambua muumini mwenzake anayehitaji msaada."

Na huufunga moyo wake wa huruma kwa ajili yake.

Maelezo haya humaanisha kwamba, "lakini hamwonei huruma." au lakini hapendi kumsaidia."

Upendo wa Mungu unakaaje ndani ya mtu huyo?

Yohana anatumia swali kuwafundisha wasikilizaji wake. Hii ingeweza kutafsiriwa kama usemi: "Upendo wa Mungu haumo ndani yake."

Watoto wangu wapendwa.

"Watoto au wapendwa waumini wenzi wangu."

Haya tusipende kwa maneno wala kwa mdomo.

Kifungu hiki, "kwa maneno" na "kwa mdomo" yote mawili yanalenga kile ambacho mtu anasema. " Usiseme tu ili mradi kwamba unawapenda watu."

Bali katika matendo na kweli

"Bali onesha kwamba kweli unawapenda watu kwa kuwasaidia."

1 John 3:19

Sentensi Unganishi

Hapa huenda Yohana anamaanisha kwamba uwezo wa waminiowa kumpenda Mungu na kupenda wao kwa wao kwa thati (tazama mstari wa 18) ni in ishara kwamba maisha yao mapya hasa asili yake ni ukweli kuhusu Kristo.

Sisi tunatokana na kweli.

"sisi ni wa hiyo kweli" au :"tunaishi kufuatana na jinsi Yesu alivyotufundisha."

mioyo yetu inathibitika

neno "moyo" humaanisha hisia. "hatutahisi hatia."

Ikiwa mioyo yetu yatuhukumu

Hii ni methali au fumbo. : "kama tuajua kwamba tumefanya dhambi na matokeo yake tunasikia hatia"

Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu.

"Mungu hujua zaidi ya mtu na huhukumu vyema" Athari za ukweli huu labda huenda ni kwamba Mungu ni mwenye rehema zaidi ya dhamiri zetu ambavyo zingesema. Ubora huu wa Mungu umeelezewa kwa neno "mkuu." Mungu hujua zaidi ya tunavyojua.

Wapendwa

"Ninyi watu ninaowapenda" au "rafiki wapendwa." Tazama lilivyotafriwa katika 2:7

na tunafanya mambo yanayopendeza mbele zake.

Maoni ya Mungu yameongelewa kana kwamba yanategemea anayoona yakitokea mbele zake. "na hufanya linalompendeza yeye"

1 John 3:23

Hii ndio amri yake.

"Hiki ndicho ambacho Mungu anataka tufanye."

Mwana

Hili ndilo Jina Mashuhuri la Yesu, Mwana wa Mungu.

Dumuni ndani yake, na Mungu hudumu ndani yake.

Daima kuwa na ushirika endelevu na Mungu.

1 John 4

1 Yohana 04 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Roho

Neno hili "roho" linatumiwa kwa njia tofauti katika sura hii. Wakati mwingine neno "roho" linamaanisha viumbe wa kiroho. Wakati mwingine inahusu tabia ya kitu fulani. Kwa mfano "roho ya mpinga Kristo," "roho ya kweli," na "roho ya hitilafu" inamaanisha kile ambacho ni mfano wa mpinga Kristo, ukweli, na kosa. "Roho" (iliyoandikwa na herufi kubwa "R") na "Roho wa Mungu" inamaanisha Mungu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#antichrist)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kupenda Mungu

Ikiwa watu wanampenda Mungu, wanapaswa kuonyesha katika njia wanayoishi na jinsi wanavyowatendea watu wengine. Kufanya hivyo kunaweza kutuhakikishia kuwa Mungu ametuokoa na kwamba sisi ni wake, lakini kupenda wengine haituokoi. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#save)

<< | >>

1 John 4:1

Maelezo ya Jumla

Yohana anatoa onyo dhidi ya walimu wa uongo ambao hufundisha kinyume cha Kristo kuwa na mwili wa kibinadamu na waalimu huongelea kama wale wanaopenda mazungumzo ya ulimwengu

Wapendwa

"Nyinyi watu ninaowapenda" au "Rafiki wapendwa." Tazama linavyofafanuliwa 2:7

msiiamini kila roho

Hapa, neno "roho" humaanisha uwezo au nguvu zakiroho au nafsi inayompa mtu ujumbe au unabii. "msimtumaini kila nabii anayedai kuwa anao ujumbe kutoka kwa roho"

zijaribuni roho

Hapa, neno "roho" humaanisha uwezo au nguvu zakiroho au nafsi inayompa mtu ujumbe au unabii. : "hakikisheni kwamba mnasikiliza kwa makini kwa anayoyasema nabii"

jaribu

"thibitisha"

kila roho itakayokiri kuwa Yesu Kristo amekuja katika mwili

"amechukua umbo la mwili" au amekuja katika mwili unoonekana"

Hii ni roho ya mpinga kristo

"wao ni walimu wanaliokinyume na Kristo" au "wao ni walimu wanaompinga Kristo"

mpinga kristo, ambayo mliyoisikia kuwa inakuja

"mpingakristo. Mmekwisha kusikia kwamba watu kama hao wanakuja miongoni mwetu"

inakuja, na sasa tayari iko duniani.

"wanakuja. Na hata sasa tayari wako hapa"

1 John 4:4

watoto wapendwa

Yohana alikuwa mzee tena kiongozi wao. Alitumia maelezo haya kuonyesha pendo lake kwao. "watoto wangu wapendwa katika Kristo" au "ninyi mlio kama watoto wangu mwenyewe ninaowapenda." Tazama 2:1lilivyofafanuliwa

mmekwisha washinda

"hamjawaamini waalimu wa uongo"

yeye aliye ndani yenu

"Mungu aliyemo ndani yenu"

yeye aliye katika ulimwengu

Uwezekano wa maana mbili ni 1) "wale waalimu wa kidunia" au 2) "Shetani aliyeko ulimwenguni

ulimwengu

Jina "ulimwengu" humaanisha watu wot wasiomtii Mungu pia humaanisha mfumo uovu ukaao katika ulimwengu wa dhambi

Wao ni wa ulimwengu,

"Wale waalimu wa uongo ni watu wasiomtii Mungu"

kwa hiyo wanachokisema ni cha ulimwengu,

"kwa hiyo hufundisha mawazo yaliyokinye na Mungu"

na ulimwengu huwasikiliza wao.

kwa hiyo watu wasiomtii Mungu huwasikiliza wao"

1 John 4:7

Maelezo ya Jumla

Yohana anaendelea kufundisha kuhusu asili mpya. Anawafundisha wasomaji wake juu ya pendo lamungu na kupendana wao kwa wao

Wapendwa

"Nyinyi watu ambao ninawapenda" au "Rafiki wapendwa" Tazama lilifasiriwa katika 2:7

tupendane sisi kwa si

"waaminio ni lazima wapendane wao kwa wao"

na kila mmoja apendaye amezaliwa na Mungu na kumjua Mungu.

"kwa sababu wale wanaowapenda waamini wenzao wamefanyika watoto wa Mungu na humjua yeye"

kwa sababu pendo latoka kwa Mungu.

"kwa sababu Mungu hutusababisha kupendana sisi kwa sisi"

amezaliwa na Mungu

Hii ni methali au fumbo ambalo humaanisha mtu mtu fulani kuwa na uhusiano na Mungu kama mtoto kwa babaye.

Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo.

"Asili ya Mungu ni kupena watu. Wale wasiowapenda waamini wenzao hawamjui Mungu kwa sababu tabia ya Mungu ni kupenda watu.

Mungu ni upendo

Hii ni mithali au fumbo linalomaanisha "tabia ya Mungu ni upendo"

1 John 4:9

Katika hili pendo la Mungu lilifunuliwa miongoni mwetu,

"Kwa hili Mungu alionyesha kwamba alitupenda"

pendo la Mungu lilifunuliwa

Ule uhalisa kwamba Mungu anampenda kila mtu yamengumzwa kana kwamba yalikuwa kitu ambacho kwacho Mungu angeweza kwao.

ili tungeishi kwa sababu ya yeye

"kutuwezesha kuishi miliele kwa sababu ya kile Yesu alifanya

Katika hili pendo

Mungu alituonyesha sisi hasa pendo ni nini

pendo, si kwamba tulimpenda Mungu, lakini yeye alitupenda, na

"pendo: pendo la kweli siyo namna tuvyompenda Mungu, bali ni jinsi alivyotupenda sisi, na"

akamtuma Mwanawe awe fidia ya dhambi zetu.

Hapa "fidia" hurejelea tukio la ambalo kwalo Mwana alifanyika dhabihu kwa ajili ya dhambi kwa ajili ya dhambi za watu wote. : "An alimtuma Mwanawe kutoa mwenyewe kuwa dhabihu ili kwamba Mungu angeweza kutusamehe dhambi zetu

1 John 4:11

Wapendwa

"Enyi watu niwapendao," au "rafiki wapendwa." Tazama 2:7

ikiwa Mungu alitupenda sisi

"kwa kuwa Mungu alitupenda sisi katika njia hii"

kupendana sisi kwa sisi

Waaminio wanapaswa kuwapenda waamini wengine.

Mungu anakaa ndani yetu... tunakaa ndani yake

"Mungu anao uhusiano nasi... tunao uhusianao na Mungu naye ana uhusiano nasi." Tazama lilivyotafsiriwa 2:4

kwa sababu ametupa

"kwa sababu alitupatia Roho wake" au "amekwisha mweheka roho wake nadani yetu," hata hivyo, kirai hiki hakiashirii Mungu ana kiasi kidogo cha Roho Wake alichobaki nacho baada ya kuwa ametupatia sisi sehemu yake.

Na tumeona na kushuhudia kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa mwokozi wa ulimwengu.Roho wake.

"Nasi mitume tumewona MWana wa Mungu na tunamwambia kila mtu kwamba Mungu, Baba, amemtuma MWana ili kuokoa watu hapa duniani"

Baba...Mwana

Hivi ni vyeo muhimi ambavyo huelezea uhusiano kaika ya Mungu na Yesu.

1 John 4:15

Kila anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu

"Wale wanaousema ukweli kuhusu, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu"

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Yesu kinachoelezea uhusiano wake kwa Mungu.

hukaa ndani yake

"Mungu anauhusiano naye na yeye pia anauhusianao na Mungu. Tazama 2:4

Mungu ni Pendo

Hii ni mithali ambaoy humaanisha kuwa "tabia ya Mungu ni upendo." Tanzama 4:7

na yeye anayekaa ndani ya upendo anakaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

"wale wanaoendelea kupenda wengine wanao uhusianao wa karibu na Mungu, naye Mungu anao uhusiano wa karibu nao"

1 John 4:17

Kwa sababu hii, pendo hili limekwisha kamilishwa miongoni mwetu, ili tuwe na ujasiri

Hili laweza kutamkwa katika mtindo tendaji. (Maana zinazowezekana ni 1) " Kwa sababu kwa sababu hii" hurejea 4:14 : "Kwababu yeyote akaaye katika pendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu ndani yake, Mungu amelifanya pendo lake kamili kwa ajili yetu, na kwa hiyo tunaweza kuwa na ujasiri kamili" au 2) "Kwa sababu hii" hurejea kwa "tuwe na ujasiri." : "Tuna ujasiri kwamba Mungu atatupokea katika siku anayohukumu kila mmoja, kwa hiyo tunajua amelifanya pendo lake kuwa kamili"

pendo hili limefanywa timilifu miongoni mwetu

"hivi ndivyo ambavyo Mungu amelifanya pendo lake kuwa kamili kwa ajili yetu"

kwa sababu kama yeye alivyo, na sisi ndivyo tulivyo katika ulimwenngu huu

"kwa sababu uhusiano alionao Yesu pamoja na Mungu ni uhusiano ule ule tulionao sisi pamoja na Mungu ulimwenguni humu"

pendo kamili huitupa hofu nje

Hapa "pendo" limeelezwa kama nafsi yenye uwezo wa kuondoa hofu. Pendo la Mungu ni kamilifu, haitupasi kuogopa"

kwa sababu hofu huhusiana na hukumu

"kwa sababu tunaogopa kama tunafikiri kwamba Mungu atakapokuja atatuadhibu kila mmoja"

Lakini yeye aogopaye hajakamilishwa katika pendo.

"Mtu anapoogopa kwamba Mungu atamwdhibu yeye, inamaanisha kwamba pendo lake si kamili"

1 John 4:19

1Yohana 4:19-21

Sisi amchukiaye ndugu yake yeyote asiyempenda ndugu yake anayemuona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamuona amri tuliyo nayo kutoka kwake

1 John 5

1 Yohana 05 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Watoto waliozaliwa kutoka kwa Mungu

Watu wanapoamini Yesu, Mungu huwafanya watoto wake na kuwapa uzima wa milele. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe)

Kuishi Kikristo

Watu wanaomwamini Yesu wanapaswa kutii amri za Mungu na kupenda watoto wake.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kifo

Wakati Yohana anaandika juu ya kifo katika sura hii, anaelezea kifo cha kimwili. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#death)

"Ulimwengu wote upo katika uwezo wa mwovu"

Maneno "yule mwovu" yanamaanisha Shetani. Mungu amemruhusu aongoze ulimwengu, lakini hatimaye Mungu ana mamlaka juu ya kila kitu. Mungu anawaweka watoto wake salama mbali na mwovu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#satan)

__<< | __

1 John 5:1

Maelezo ya Jumla

Yohana anaendelea kuwafundisha wasomaji wake kuhusu upendo wa Mungu na upedo ambao waaminio wanapaswa kuwa nao kwa sababu mekuwa na hali hii mpya kutoka kwa Mungu

amezaliwa na Mungu

"ni mwana wa Mungu"

Kwa hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu: tunapompenda Mungu na kutekeleza amri zake.

"Tunapompenda Mungu na kutenda atuamruyo, ndipo tunatambua kwamba tunawapenda watoto wake"

Hivi ndivyo tunavyompenda Mungu kwamba twazishika amri zake.

"Kwa sababu tunapofanya atuamruyo, hilo ndilo pendo la Mungu"

Na amri zake ni nyepesi.

"Na anayotuamru siyo gumu"

nzito

"lenye kuponda," "lenye kukandamiza" au "gumu"

1 John 5:4

kila aliyezaliwa na Mungu

"watoto wote wa Mungu"

huushinda ulimwengu

"wanaushindi juu ya ulimwengu," "hufaulu dhidi ya ulimwengu," au "hukataa kufanya mambo maovu wayafanyayo wasioamini"

Na huu ndio ushindi wa kuushinda ulimwengu: imani yetu

"Imani yetu hupatia nguvu ya kuzuia lolote ambalo lingetutia katika ktenda dhambi dhidi ya Mungu"

Ni nani anayeushinda ulimwengu?

Yohana alitumia swali hili kutambulisha jambo fulani alilotaka kufundisha. "Nitaambia anayeshinda ulimwengu"

ulimwengu

ujumbe huu "ulimwengu? kwa kumaanisha watu wote wenye dhambi na mfumo mwovu wa ulimwengu"

Ni yule aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Hili halimaanishi mtu maalum bali kwa yeyote anayeamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.

Mwana wa Mungu

hiki ni cheo muhimu kwa Yesu kinachoelezea uhusiano wake kwa Mungu

1 John 5:6

Sentensi Unganishi

Yohana anafundisha kuhusu Yesu Kristo na aliyosema Mungu kuhusu yeye.

Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu- Yesu Kristo

"Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji na damu. hapa "maji" ni taashira au mfano labda huenda kwa ajili ya ubatizo wa Yesu, na "damu" husimama kwa niaba ya kifo cha Yesu msalabani. : "Mungu alionyesha kwamba Yesu Kristo ni Mwanawe kwenye ubatizo wa Yesu na kifo chake masalabani"

Hakuja tu kwa maji bali kwa maji na damu

Maji humaanisha ubatizo wa Yesu na damu humaanisha kifo cha Yesu msalabani. : "Mungu hakutuonyesha sisi kuwa Yesu alikuwa Mwanawe kupitia ubatizo wake tu, bali pia kwa njia ya kifo chake msalabani"

1 John 5:9

Kama tunaupokea ushuhuda wa wanadamu ushuhuda wa Mungu ni mkuu

"Kama tunaamini wasemayo watu, basi ni lazima tuamini asemacho Mungu kwa sababu Yeye daima huisema kweli"

tunaupokea ushuhuda wa wanadamu

uhalisia kwamba watu huutoa ushahidi au kushuhudia juu ya mambo mbalimbalia limezungumziwa hapa kana kwamba ni kitu amabacho wengine hukipokea.

ushuhuda wa Mungu ni mkuu

usuhuda wa Mungu ni mkuu na muhimu na wa kutegemewa zaidi

amwaminiye Mwana wa Mungu ana ushuhuda ndani yake m

mtu yeyote anayemwamini Yesu hujua kuwa hakika Yesu ni Mwana wa Mungu"

amemfanya yeye kuwa mwongo,

"anamwita Mungu mwongo"

kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu ameuleta kuhusu Mwanawe.

"kwa sababu haamini kwamba Mungu aliseama kweli kuhusu Mwanawe"

1 John 5:11

Na ushuhuda ndio huu

"Hivi ndivyo Mungu anavyosema"

uzima

Hapa "uzima" husimama badala ya haki ya kuishi milele kwa neema na upendo wa Mungu. Tazama 1:1

uzima huu umo ndani ya Mwanawe.

uzima huu ni kwa njia ya Mwanawe, "Tutaishi milele kama tutaungana na Mwanawe" au "tutaishi milele kama tutakuwa na muungano na Mwanawe"

Mwana

Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.

Aliye naye Mwana ana uzima

Kuwa katika uhusiano wa karibu na Yesu kunazungumzia ni kama kuwa na Mwana. "Yeye aaminiye katka Mwana wa Mungu anao uzima wa milele"

1 John 5:13

Maaelezo ya Jumla

Hii inaanzisha mwisho wa barua ya Yohana. Anawaambia wasomaji wakke kusudi lake la mwisho kwa barua yake na anawapa mafundisho kadha ya mwaisho.

mambo haya

"barua hii"

ninyi mnaoamini katika jina la Mwana wa Mungu

Hapa "jina" ni Taashira au Ishara inayomwakilisha Mwana wa Mungu. : "Ninyi mnaotumaini katika Mwana wa Mungu"

Mwana wa Mungu

Hiki nicheo muhimi sana kwa Ysu ambacho uelezea uhusiano wake kwa Mungu.

uzima

Hapa "uzima" husimama badala ya haki ya kuishi milele kwa neema na upendo wa Mungu. Tazama 1:1

Na huu ndio ujasiri tulionao mbele zake, kwamba

"tuna ujasiri mbele za Mungu kwa sababu tunajua, kwamba"

kama tukiomba kitu chochote sawa sawa na mapenzi yake

"Kama tunaomba mambo ambayo Mungu hutamani"

tunajua kwamba tunacho hicho tulichomwomba.

"tunajua kwamba tutapokea ambacho tumemwomba Mungu"

1 John 5:16

ndugu

Mwamini mwenza

uzima

"uzima" hapa husimama bada ya haki ya kuishi milele kwa neema na pendo la Mungu. Tazama 1:1

Mauti

hii humanisha hauti ya milele, yaani, kutumia muda wote mbali na uwepo wa Mungu.

1 John 5:18

Sentensi Unganishi

Yohana anahitimisha barua yake, akifunua alichokisema kwa kuhusu hali mpya ya waaminio ambayo haiwezi kutenda dhambi na anawakumbusha kulinda na sanamu.

ulimwengu wote

"ulimwengu" ni njia ambayo kwayo baadhi ya waandishi wa Kibiblia huwazungumzia watu waishio watu wote wanaoishi ulimwenguni walio katika uasi dhidi ya Mungu na pia hulitumia kuelezea mfumo wa ulimwengu uliodhiliwa na nguvu ya dhambi yenye kuharibu.

chini ya utawala wa yule mwovu.

yaani, katika nguvu za yule mwovu.

1 John 5:20

Maelezo ya Jumla

Maneno "yeye" na "Aliye" humrejea Yesu Kristo

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu ambacho huelezea uhusiano wake kwa Mungu.

ametupatia ujuzi

"ametuwezesha kumwelewa huyo kweli"

uzima

Hapa, neno "uzima" husimama kwa niaba ya haki ya kuishi milele kwa neema na pendo la Mungu. Tazama maelezo katika1:1.

Yeye ni... uzima wa milele

hili linasimama kwa niaba ya wazo kwamba Kristo hutupatia uzima wa milele.

Watoto

Yohana alitumia maelezo haya kuonyesha kuonyesha upendo wake kwa ajili yao. : "Watoto wangu katika Kristo" au "ninyi mlio wapendwa kwangu kama watoto wangu mwenyewe." Tazama lilivyotafsiriwa katika 2:1.