Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

1 Chronicles 1

1 Chronicles 1:1

Wana wa Nuhu walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi

Tafsiri zingine, pamoja na ULB na UDB, za usisha "Wana wana" ili kuweka wazi kuwa Shemu, Hamu, na Yafethi walikuwa ni ndugu na wana wa Nuhu. Lasihivyo, msomaji ata dhani kila mtu aliwakilisha kizazi kimoja mbali na Nuhu, babu yao.

Enoshi, Kenani, Mahalaleli, Yaredi ... Methusela

Haya majina ni orodha ya mababu.

1 Chronicles 1:5

Gomeri ... Dodanimu

Tafsiri haya majina jinsi ungetafsiri majina kwenye lugha yako. Haya yote ni majina ya wanaume.

Dodanimu

Hili jina uwa latafsiriwa "Rodanimu" kama kwenye UDB.

1 Chronicles 1:8

Mizraimu ... Nimrodi

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 1:11

kwa yeye ambaye Wafilisti walitoka

"mababu wa Wafilisti"

1 Chronicles 1:13

Hethi

Hili ni jina la mtu.

Mwarki ... Mhamathi

Haya ni majina ya vikundi vya watu

1 Chronicles 1:17

Arfaksadi ... Yoktani

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 1:20

Yoktani ... Yobabu

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 1:24

Shemu ... Serugi

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 1:28

Nebayothi ... Kedema

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 1:32

Ketura ... Elda

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 1:34

Elifazi ... Miza

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 1:38

Lotani ... Ana

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 1:41

Ana ... Arani

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 1:43

Bela ... Beori ... Yobabu .. Zera .. Hushamu

Haya ni majina ya watu.

Dinhaba ... Bozra

Haya ni majina ya sehemu

Hushamu wa nchi ya Watemani akatawala badala yake

'Hushamu, kutoka nchi ambayo uzao wa Temani waishi, alitawala baada yake."

Watemani

Hili ni jina la kundi la watu

1 Chronicles 1:46

Hushamu ... Hadadi ... Bedadi ... Samla ... Shauli

Haya ni majina ya watu.

Avithi ... Masreka ... Rehobothi

Haya ni majina ya sehemu

1 Chronicles 1:49

Shauli ... Baali Hanani ... Akbori ... Hadari ... Mehetabeli ... Matredi ... Me Zahabu

Haya ni majina ya watu.

Pai

Hili ni jina la sehemu.

1 Chronicles 2

1 Chronicles 2:1

Rubeni ... Asheri

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 2:3

Yahweh

Hili ni jina la Mungu alilo lirihidhisha kwa watu wake wa Agano la Kale.

alimzalia Peresi na Zera

"aliza wana wake Perezi na Zera"

wana wa tano

"wana wa 5"

macho ya Yahweh

"kwa mujibu wa Yahweh|"

Yahweh akamwua

Hii inamaanisha Yahweh aliruhusu Eri auliwe.

mkwe wake

Hii ina maana ya mke wa mwanae.

1 Chronicles 2:13

wa pili ... wa tatu

"mwanae wa pili ... mwanae wa tatu"

1 Chronicles 2:16

Yetheri Mwishmaeli

Hii ina maanisha kuwa Yetheri alikuwa uzao wa Ishmaeli.

1 Chronicles 2:18

aliye mzalia

"alimzaa"

1 Chronicles 2:21

aliye mzalia

"alimzaa"

1 Chronicles 2:23

aliye mzalia

"alimzaa"

1 Chronicles 2:25

Atara

Hili ni jina la mwanamke.

1 Chronicles 2:34

aliye mzalia

"alimzaa"

1 Chronicles 2:42

Wana wa Kalebu ... Maresha

Tafsri tofauti zinaelewa mahusiano miongoni mwa hawa watu kwa njia tofauti. Baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba "baba wa Hebroni ... baba wa Rahama, baba wa Yorkeamu ... baba wa Shamai" ya maanisha "mzinduzi wa ukoo wa Hebroni," nk. Baadhi ya tafsiri za weza tumia hii lugha.

1 Chronicles 2:48

alimzaa

"alimzalia"

1 Chronicles 2:52

Wanuthi ... Waithri, Waputhi, Washumathi, na Wamishrai. Wazora na Waeshtaoli

Haya ni majina ya koo.

1 Chronicles 2:54

Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi na Wazori ... Watirathi, Washimeathi, na Wasukathi ... Wakeni ... Warekabu

Haya ni majina ya koo.

1 Chronicles 3

1 Chronicles 3:1

Daudi

Daudi alikuwa mwana wa Yese, aliye kuwa uzao wa Yuda.

Ahinoamu ... Abigail ... Maaka ... Hagithi ... Abitali ... Egla

Haya ni majina ya wanawake.

Talmai ... Shefatia ... Ithraeamu

Haya ni majina ya wanaume.

Danieli

Huyu mtu ana jina kama la nabii wa Israeli lakini ni mtu tofauti.

Egla mkewe

"Egla, mke wa Daudi." Daudi alikuwa na zaidi ya mke mmoja. "Mke wa Daudi Egla"

1 Chronicles 3:4

alipo tawala miaka saba na miezi sita

Hii ya weza tafsiriwa kama sentensi yenyewe: "Daudi alitawala huko miaka saba na miezi mitatu."

miaka thelathini na mitatu

miaka mitatu - " miaka 33"

Ammieli ... Shammua ... Shobabu ... Nadhani

Haya ni majina ya watu.

1 Chronicles 3:6

Ibhari ... Elishama ... Elifeleti ... Noga ... Nefegi ... Yafia ... Eliada

Haya ni majina ya wanaume.

Elishama ... Elifeleti

Haya majina yametumika kwa wana wawili.

1 Chronicles 3:10

Maelezo ya jumla:

Huu ni mwanzo wa orodha ya uzao wa Daudi ya walio kuwa wafalme.

Mwana wa Sulemani alikuwa ni Rehoboamu. Mwana wa Rehoboamu alikuwa Abiya

Sulemani alikuwa na zaidi ya mwana mmoja. Hii ni kweli kwa kwa wanaume wengine kwenye orodha. "Sulemani alikuwa baba wa Rehoboamu. Rehoboamu alikuwa baba wa Abiya"

Azaria

Hili ni jina lingine la Uzia, jina linalo julikana vizuri kwa huyu mfalme. Wafasiri wanaweza amua kutumia "Uzia" kila sehemu kwa huyu mfalme.

1 Chronicles 3:13

Maelezo ya Jumla

Huu ni mwendelezo wa orodha ya uzao wa Daudi ya walio kuwa wafalme. Tunga hizi sentensi kama ulivyo fanya kuanzia 3:10.

Amoni

Hili ni jina la mwanaume.

1 Chronicles 3:15

Maelezo ya Jumla

Huu ni mwendelezo wa orodha ya uzao wa Daudi ya walio kuwa wafalme. Tunga hizi sentensi kama ulivyo fanya kuanzia 3:10.

Yohanani ... Shalumu ... Yehoyakini

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 3:17

Yehoyakini

Baadhi ya tafsiri zina "Yekonia," ambayo ni mbadala wa "Yehoyakini."

watekwa

Hii inaweza kuwa cheo kilichopewa Yehoyakini kwasababu alichukuliwa matekani. Ingawa, baadhi ya tafsiri za eleza hilo neno kama "Asiri," jina la mmoja wa wanae.

YehoYakini ... Shealtieli, Malkiramu, Pedaya, Shenezari, Yekamia, Hoshama, na Nedabia

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 3:19

Pedaya ... Shimei ... Meshulamu ... Hanania ... Hashuba ... Oheli ... Berekia ... Hasadia ... Yushabu Hesedi ... Pelatia ... Yeshaia ... Refaya ... Arnani ... Shekania

Haya ni majina ya wanaume.

Shelomithi

Hili ni jina la mwanamke.

Obadia

Huyu mwanaume ana jina sawa na nabii wa Israeli Obadia lakini ni mtu tofauti.

uzao wake zaidi walikuwa ni Arnani, Obadia, na Shekania.

Tafsiri tofauti zinawaweka hawa watu katika mahusiano tofauti wao kwa wao, kwasababu lugha ya Kiebrania haijafafanua kuwahusu.

1 Chronicles 3:22

Shemaia ... Hatushi ... Igali ... Baria ... Nearia ... Shafati ... Elionai ... Hizekia ... Azrikamu ... Hodavia ... Eliashibu ... Pelaya ... Akubu ... Delaia ... Anani

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 4

1 Chronicles 4:1

Perezi ... Hezroni ... Karmi ... Huri ... Shobali ... Reaia ... Yahathi ... Ahumai ... Lahadi

Haya ni majina ya wanaume

Zora

Hili kundi la watu liliitwa kwa jina la mji wa Zora walipoisi

1 Chronicles 4:3

Hawa walikuwa mababu

Hii ya husu orodha ya mistari ya awali. Ingawa, baadhi ya tafsiri ya husisha haya majina katika mahusiano ya baba-mwana. Katika namna hii, baadhi ya tafsiri ya husisha Penueli kama baba wa Gedori, badala ya muanzilishi wa ukoo wa Gedori.

Etamu ... Gedori ... Husha

Hay ni majina ya miji.

Ishma ... Idbashi ... Penueli ... Ezeri ... Efrathi

Haya ni majina ya wanaume.

Haselelponi

Hili ni jina la mwanamke.

Hawa walikuwa uzao wa Huri

"Penueli na Ezeri walikuwa uzao wa Huri." Hii ya tanguliza orodha itayofuata.

1 Chronicles 4:5

Ashuri ... Tekoa ... Ahuzamu ... Heferi ... Serethi ... Ishari ... Ethnani ... Kozi ... Anubu ... Zobeba ... Aharheli ... Harumu

Haya ni majina ya wanaume.

Temeni ... Ahashatari

Haya hapa yana fahamika kama majina ya wanaume. Ingawa, baadhi ya tafsiri inayaelewa kama majina ya koo zilizo anzishwa na Ashuri.

Hela ... Naara

Haya ni majina ya wanawake.

alimzalia

"aliwaza wana wake"

a koo zilizotoka kwa Aharheli mwana wa Harumu

Sentensi mpya ya anza hapa. "Kozi pia akawa babu wa Harumu na koo zilizotoka kwa Harumu mwana wa Aharheli"

1 Chronicles 4:9

Yabesi

Hili ni jina la mwanaume.

ongeza mipaka yangu

"nipe mimi eneo zaid"

mkono wako ukuwa juu yangu

Baadhi ya maana ni kwamba mkono wa Mungu wa wakilisha 1) muongozo wake, 2) nguvu zake, au 3) ulinzi wake. "nilinde mimi" au "nifanye ni fanikiwe" au "nilinde." Pia yaweza tafsiriwa kwa ujumla kama "kuwa na mimi."

akamjalia maombi yake

"akafanya sawa na maombi yake"

1 Chronicles 4:11

Kelubu ... Shuha ... Mehiri ... Eshtoni ... Bethi - Rafa ... Pasea ... Tehina

Haya ni majina ya wanaume.

Tehina, ambaye alianzisha mji wa Nahashi

"Tehina, mwanzilishi wa mji wa Nahashi"

Nahashi

Hili ni jina la mji.

Reka

Hili ni jina la sehemu.

1 Chronicles 4:13

Maelezo ya jumla

Itasaidia kutengeneza muunganiko wa mstari na kuweka mstari wa 15 pamoja na mstari wa 13 maana Kenazi alikuwa mzao wa Yefune na Kalebu.

Kenazi ... Othinieli ... Seraia ... Hathathi ... Meonothai ... Ofara ... Yoabu ... Yefune ... Iru ... Ele ... Namu ... Yehaleli ... Zifi .. Zifa ... Tiriya ... Asareli

Haya ni majina ya wanaume.

Ge Harashimu, ambaye watu wake walikuwa wahunzi

Ge Harashimu ina maana ya "Bonde la Wahunzi". Maana ya jina ya weza tafsiriwa au ya weza kufanywa kama lilivyo na maelezo yake: "Ge Harashimu, lenye maana ya 'Bonde la Wahunzi.' Liliitwa hivi sababu watu wake walikuwa wahunzi."

Wahunzi

watu walio na ujuzi wa kutengeneza au kujenga vitu

1 Chronicles 4:17

Maelezo ya Jumla

Maelezo ya 4:17 yamepangiliwa tena ili maana yake ieleweke kwa urahisi zaidi.

Ezra ... Yetheri ... Meredi ... Eferi ... Yaloni ... Miriamu ... Shamai ... Ishibahi ... Eshitemoa ... Yeredi ... Gedori ... Heberi ... Soko ... Yekuthieli ... Zanoa

Haya ni majina ya wanaume.

Hawa walikua wana wa Bithia

Neno "hawa" la mtaja Miriamu, Shamai, na Ishibahi. Walikuwa wana Bithia aliye mzalia mme wake Meredi.

Bithia

Hili ni jina la mwanamke.

Mke wa Kiyahudi wa Meredi

Maandishi ya Kiebrania yasema, "Mke wake wa Kiyahudi," lakini tafsiri nyingi za elewa "wa" ya mhusu Meredi. Hii ya taja mke tofauti wa Meredi, ukiongeza kwa Bithia

1 Chronicles 4:19

Hodaia ... Nahamu ... Keila ... Eshtemoa ... Shimoni ... Amnoni ... Rina ... Ben Hanani ... Tiloni ... Ishi ... Zohethi ... Beni Zoheti

Haya ni majina ya wanaume.

Mgarimi

mtu wa kundi la wa Gari

Mmakathi

mtu kutoka eneo la Maka, linalo itwa pia Makathi.

1 Chronicles 4:21

Shela ... Er ... Leka ... Laada Maresha ... Yoakimu ... Yoashi ... Sarafi

Haya ni majina ya watu

wafinyanzi

watu wanao tengeneza mikebe kutokana na udogo

Bethi Ashbea ... Kozeba ... Netaimu ... Gedera

Haya ni majina ya wanaume

1 Chronicles 4:24

Nemueli ... Yamini ... Yaribu .. Zera ... Shauli ... Shalumu ... Mibsamu ... Mishima ... Hamueli ... Zakuri ... Shimei

Haya ni majina ya wanume

mjukuu

mwana wa mtoto wa mtu

kitukuu

mjukuu - mwana wa mjukuu wa mtu au mjukuu wa kike

1 Chronicles 4:27

wana kumi na sita na mabinti sita

"wana 16 na mabinti 6"

Molada ... Hazari Shuali

Haya ni majina ya miji.

1 Chronicles 4:29

Maelezo ya Jumla

Orodha ya miji ya uzao wa Simeoni uliishi ya endelea

Bilha, Ezemu, Toladi, Bethueli, Horma, Zikilagi, Bethi Markabothi, Hazari Susimi, Bethi Biri, Shaaraimu

Haya ni majina ya miji.

1 Chronicles 4:32

Maelezo ya Jumla

Orodha ya sehemu uzao wa Simeoni uliishi yaendelea.

Etamu ... Aini .. Rimoni ... Tocheni ... Ashani

Haya ni majina ya vijiji.

mipaka

mbali na idadi kubwa ya watu

1 Chronicles 4:34

Meshobabu, Yamileki, Yoshahi mwana wa Amazia, Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia mwana wa Seraia, Asieli, Elioenai, Yaakoba, Yeshohaia, Asaia, Adieli, Yesimieli, Benaia, Ziza, Shifi, Aloni Yedaia Shimiri Shemaia

Haya ni majina ya wanaume

Hawa walio orodheshwa kwa majina walikua viongozi

"Hawa wanaume walikuwa viongozi"

koo zao ziliongezeka sana

idadi ya watu kwenye koo zao iliongezeka sana"

1 Chronicles 4:39

Gedori

Hili ni jina la mji

malishoni

eneo ambao wanyama wana kula nyasi

mengi

kiasi kikubwa

Wahami

uzao wa Hamu

Wameuni

Hili ni jina la kundi la watu. "uzao wa Meuni"

1 Chronicles 4:42

Wanaume mia tano

"wanaume 500"

Pelatia, Nearia, Refaia, Uzieli, Ishi

Haya ni majina ya watu.

wakimbizi wa Waamaleki waliobakia

"wakimbizi walio baki"

wakimbizi

watu walio lazimishwa kuondoka nchini kwao

hadi siku hii

"kutoka kwao hadi sasa"

1 Chronicles 5

1 Chronicles 5:1

sasa Ruben

Neno "sasa" limetumika hapa kuweka alama ya mabadiliko kutoka orodha ya uzao hadi maelezo ya awali ya Rubeni

lakini haki yake ya mzaliwa wa kwanza ilipewa kwa wana wa Yusufu mwana wa Israeli

"lakini Israeli aliwapa haki ya mzaliwa wa kwanza ya Rubeni kwa wana wa Yusufu, mwengine wa watoto wa Israeli"

Rubeni alinajisi kochi la baba yake

Hii ni namna ya adabu ya kusema kuwa Rubeni alilala na mke wa pili wa baba yake. Kochi ni sehemu mwanaume na mke wake walilala pamoja.

Hivyo hajanakiliwa kama mwana wa kwanza

"Hivyo historia ya familia ya haimuorodheshi Rubeni kama mwana mkubwa"

Hanoki, Palu, Hezroni, Karmi

Haya ni majina ya wanaume

1 Chronicles 5:4

Yoeli ... Shemaia ... Gogi ... Shimei ... Mika Reaia ... Reaia ... Baali ... Bera ... Tiligathi Pileser

Haya ni majina ya wanaume

Tiligath Pileseri

Hili jina limeandikwa pia kama Tiglathi Pileaseri katika sehemu zingine za Biblia

1 Chronicles 5:7

wameorodheshwa katika nakala za uzao wao

Hii yaeza anza sentensi mpya: "Nakala zao za uzao zimewaorodhesha kama"

nakala za uzao

nakala zinazoonyesha jinsi watu katika familia wanavyo husiana wao kwa wao

Yeieli ... Zekaria ... Bela ... Azazi ... Shema

Haya ni majina ya wanaume

Aroeri ... Nebo ... Baali Meoni

Haya ni majina ya miji

1 Chronicles 5:10

Wahagiri

Haya ni majina makundi ya watu.

1 Chronicles 5:11

Saleka

Hili ni jina la mji

Yoeli ... Shafamu ... Yanai ... Shafati ... Mikaeli ... Meshulamu ... Sheba ... Yorai ... Yakani ... Zia ... Eberi

Haya ni majina ya wanaume

1 Chronicles 5:14

Abihaili ... Huri ... Yaroa ... Gileadi ... Mikaeli ... Yeshishai ... Yado ... Buzi ... Ahi ... Abdieli ... Guni

Haya ni majina ya wanaume

1 Chronicles 5:16

Waliishi

"Kabila la shule liliishi"

nchi za malisho

maeno wanyama wanayo kula nyasi

Hawa wote waliorodheshwa katika nakaka za uzao

"Nakala za uzao ziliwaorodhesha wote" au "Nakala zao familia za mababu ziliwaorodhesha"

Hawa wote

Haiko wazi ni idadi gani ya watu walio tangulia imetajwa

1 Chronicles 5:18

Warubeni

Hii ya husu watu kutoka kabila la Rubeni

Wagadi

Hii ya husu watu kutoka kabila la Gadi

wana jeshi elfu arobaini na nne

wana jeshi elfu nne "44, 000 soldiers"

walio beba ngao na upanga, na pinde na mishale

Wanajeshi wanaelezwa kama wenye ujuzi vitani kwa silaha walizo beba. "Walifunzwa kupambana vizuri vitani"

Wahagri ... Yeturi ... Nafishi ... Nodabu

Haya ni majina ya makundi ya watu.

1 Chronicles 5:20

Waisraeli walipaza sauti kwa Mungu

"Waisraeli walimuomba Mungu kwa sauti kwa ajili ya Msaada"

Walikamata

"Waisraeli walikamata Wahagri"

ngamia elfu hamsini

"ngamia 50,000"

punda elfu mbili

"punda 2,000"

Kwa sababu Mungu aliwapigania

Msaada wa Mungu waelezwa kama mwanajeshi aliye pigana vitani. "Kwasababu Mungu aliwasaidia"

1 Chronicles 5:23

Baali Herimoni ... Seniri

Haya ni majina ya milima

Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia, na Yahdieli

Haya ni majina ya wanaume

1 Chronicles 5:25

Puli ... Tiligathi Pileseri

Haya ni majina ya wanaume

Warubeni ... Wagadi

Haya ni majina ya makundi ya watu

Hala ... Habori ... Hara

Haya ni majina ya miji

Gozani

Hili ni jina la mto

1 Chronicles 6

1 Chronicles 6:1

Gerishoni ... Kohathi ... Merari ... Amramu ... Izhari ... Hebroni ... Uzieli ... Nadabu ... Abihu ... Eleazari ... Ithamari

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 6:4

Eleazari ... Abishua ... Buki ... Uzi ... Zerahia ... Meraioti

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 6:7

Meraioti ... Amaria ... Ahitubi ... Zadoki ... Ahimazi ... Yohanani

haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 6:10

Amaria ... Ahitubi ... Zadoki ... Shalumu

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 6:13

Hilikia ... Seraia ... Yehozadaki

Haya ni majina ya wanaume.

wapeleka utumwani Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Nebukadneza.

Nguvu ya Nebukadneza kupitia jeshi lake inafafanuliwa kama sehemu ya mwili wake ("mkono") alitumika kuongoza jeshi lake. " aliruhusu jeshi la Nebukadneza kushinda majeshi ya Yuda na Yerusalemu na kuchukua watu kwenda matekani."

1 Chronicles 6:16

Gershomi ... Kohathi ... Merari

Ona jinsi ulivyo tafsiri haya majina 6:1

Libni ... Shimei

Haya ni majina ya wanaume

Amramu ... Izhari ... Hebroni ... Uzieli

Ona jinsi ulivyo tafsiri haya majina 6:1

1 Chronicles 6:19

Merari ... Mahili ... Mushi ... Yahathi ... Zima ... Yoa ... Ido ... Zera ... Yeatherai ...

Haya ni majina ya wanaume

1 Chronicles 6:22

Aminadabu ... Kora ... Asiri ... Elikana ... Ebiasa ... Tahathi ... Urieli ... Uzia ... Shauli

Haya ni majina ya wanaume

1 Chronicles 6:25

Elikana ... Amasai ... Ahimothi ... Zofai ... Nahathi ... Eliabu .. Yerohamu

Haya ni majina ya wanawake

1 Chronicles 6:28

Yoeli ... Merari ... Mahli ... Libni ... Shimei ... uza ... Shimea ... Hagia ... Asaia

Haya ni majina ya wanaume

mzaliwa wa pili

"wana wa pili kuzaliwa"

1 Chronicles 6:31

sanduku kuja hapo

"watu wa Israeli walieka sanduku kule"

hema, hema la kukutania

Maana kadha ni 1) kwamba "hema la kukutania" la eleza jina lingine la "maskani" (UDB) au 2) "eneo takatifu la hema la kukutani"

Walikamilisha wajibu wao kwa kadiri ya maelekezo waliopewa

"Waimbaji walitii maelekezo ya Daudi"

1 Chronicles 6:33

Hawa

"Hawa walikuwa wana muziki"

Wakohathi

Hili ni jina la kundi la watu

kurudi nyuma ya wakati

Hii ina maana orodha inaenda kutokana na wa hivi karibuni na wa zamani.

Hemani ... Yerohamu ... Elieli ... Toa ... Zufi ... Mahathi

Haya ni majina ya wanaume.

Elikana ... Amasai

Ona jinsi ulivyo tafsiri haya majina ya hawa wanaume 6:25

1 Chronicles 6:36

Tahathi ... Asiri ... Ebiasa .. Izhari ... kohathi

Haya ni majina ya watu

1 Chronicles 6:39

Berekia ... Shimea ... Mikaeli ... Baaseia ... Malikiya ... Ethani ... Zima ... Shimei Yahathi ... Gerishomu

Haya ni majina ya watu

Msaidizi

"mfanya kazi mwenza"

aliye simama mkono wake wa kuume

Mamlaka ya mtu yaelezwa kama kwa wapi wanapo simama. Mkono wa kulia wa mtu ni sehemu mtu mwenye mamlaka alisimama.

1 Chronicles 6:44

mkono wa koshoto wa Heman

"Kusimama mkono wa kushuto wa Hemani"

Msaidizi

"Mfanya kazi mwenza"

1 Chronicles 6:48

Walawi, alipangiwa kufanya

"Ilikuwa ni kazi ya wafanya kazi wenza, Walawi, kufanya"

1 Chronicles 6:49

izi sadaka zilifanya maombezi kwa ajili ya Waisraeli

"Hizi sadaka zilikuwa za kufanya maombezi kwa dhambi za watu wa Israeli"

1 Chronicles 6:50

Uzao wa Aruni una kumbukwa kama ifuatavyo

"Hawa walikuwa uzao wa Aruni"

1 Chronicles 6:54

Hizi ni sehemu ambazo wazao wa Aruni walipangiwa kuishi, wazao wa Aruni ambao walitoka katika koo za Wakohathi (maeneo ya kwanza yalikuwa yao)

"Haya ndiyo maeno ambayo uzao wa Aruni, koo za Wakohathi, waliishi (kura zilpigwa kujua wapi wataishi)"

Wakohathi

Ona jinsi ulivyo tafsiri 6:33

Walipewa Hebron

"Waliwapatia Hebroni kuwa yao"

lakini maeneo ya mji na vijiji alipewa Kalebu mwana wa Yefune

"Kalebu na familia yake walienda kuishi kwenye mashamba ya Hebroni na vijiji vizungukavyo"

nchi ya malisho

Hii ni sehemu ya nyasi ambapo wanyama wanakula.

1 Chronicles 6:59

Jumla ya miji yao ilikuwa kumi na tatu

"Walikuwa na jumla ya miji kumi na tatu"

1 Chronicles 6:61

Gerishomu kwa koo zao tofauti walipewa miji kumi na tatu

"Koo za Gerishomu uzao wake ulipata miji 13"

Kohathi ... Gerishomu

Ona jinsi ulivyo tafsiri 6:1

1 Chronicles 6:63

Merari

Ona jinsi ulivyo tafsiri 6:1

miji iliyo tajwa awali kutoka

"hiyo miji kutoka"

1 Chronicles 6:66

Wakohathi

Ona jinsi ulivyo tafsiri 6:33

1 Chronicles 6:71

Gerishomu

Ona jinsi ulivyo tafsiri 6:1

1 Chronicles 6:77

Merari

Ona jinsi ulivyo tafsiri 6:1

Merari ... nchi ya malisho

"kabila la Zebuluni ili wapa uzao wa Merari Rimono na nchi yake yamalisho na Tabori na nchi yake ya Malisho"

Kwa wao pia walipewa ... kabila la Rubeni

Maelezo katika 6:77 yamepangiliwa tena ili maana yake iweze kueleweka kwa uraisi.

Kwa wao pia walipewa

"Pia walipata zaidi"

1 Chronicles 7

1 Chronicles 7:1

walikua na idadi ya 22,600

"Walikuwa wanaume elfu ishirini na mbili na mia sita"

Katika siku za Daudi

"kipindi cha maisha ya Daudi

1 Chronicles 7:4

Pamoja nao walikua na

"Miongoni mwao walikuwa"

jeshi la watu elfu thelathini na sita kwa mapambano

wana jeshi elfu sita kwa pambano - "wana jeshi 36,000 walio kuwa tayari kwa pambano"

1 Chronicles 7:6

waanzilishi

"baba" au "mababu"

1 Chronicles 7:11

Yedieli ... Iri ... Aheri

Haya ni majina ya wanawake

Waliorodheshwa katika ukoo orodha ilikuwa 17,200

"Orodha ya ukoo ilikuwa na elfu kumi na saba na mia mbili"

Shupimu ... Hupimu ... Hushimu

Haya ni majina ya wanaume

1 Chronicles 7:13

Yazieli, Guni, Yezeri, na Shalumu

Haya ni majina ya wanaume

wajukuu wa Bilhahi

"wana wa wana wa Bilhahi"

1 Chronicles 7:14

Waarami

Hii yaeleza mtu wakutoka Aramu, eneo la Syria

suria wake wa Kiaramia alimzalia

"Suria wa Kiaramia alimza"

1 Chronicles 7:20

Eza na Eleadi waliuawa na wanaume wa Gati, wenyeji wa nchi

"Wanaume wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua Eza na Eleadi"

walipoenda kuiba mifugo yao

"ndugu walienda kuiba mifugo kutoka kwa watu wa Gathi"

1 Chronicles 7:23

Akapata mimba akamzaa mwana

"Alishika mimba na kuzaa mwana"

akamuita

"alimpa jina"

Beria ... Sheera

Haya ni majina ya watu

juu na chini Beth Horon na Uzzen Sheerah

Haya ni majina ya sehemu.

1 Chronicles 7:28

makazi yao yalikuwa

"nyumbani kwao kulikuwa"

atika huu mji waliishi uzao wa Josefu mwana wa Israeli

"Uzao wa Yusufu, mwana wa Israeli, waliishi kwenye hii miji"

1 Chronicles 7:39

wananume wa kipekee

"wanaume muhimu"

Kulikuwa na wanaume elfu ishirini na sita walioorodheshwa waliokuwa imara kwa kazi ya jeshi, kwa mujibu wa idadi iliyo orodheshwa

wanaume elfu sita waliorodhesha walikuwa tayari kwa ajili ya kazi ya jeshi, kwa mujibu wa idadi ya orodha* "Kwa mujibu wa nakala za koo, walikuwa 26,000 wanaume wanao weza kutumika kwenye jeshi.

1 Chronicles 8

1 Chronicles 8:6

walihimizwa kuhamia

"waliitaji kuhama" au "waliitaji kuhama"

1 Chronicles 8:8

Shaharaimu ... Yobabu ... Zibia ... Mesha ... Malkamu ... Yeuzi ... Shachia ... Mirima ... Abitubi ... Elipaali

Haya ni majina ya wanaume

Hushimu ... Baara ... Hodeshi

Haya ni majina ya wanawake

kwa mke wake Hodeshi, Shaharaimu akawa baba wa

"Shaharaimu na mkewe Hodeshi walikuwa na wana wafuatao"

1 Chronicles 8:12

Elipaali ... Eberi ... Mishamu ... Shemedi ... Beria ... Shema

Haya ni majina ya wanaume.

Ono ... Lodi ... Aijaloni

Haya ni majina ya sehemu

1 Chronicles 8:14

Elipaali ... na Yobabu

Maelezo katika 8:14 yamepangiliwa tena ili maana yake ieleweke kwa urahisi zaidi.

1 Chronicles 8:19

Maelezo ya Jumla

Maelezo katika 8:19 yamepangiliwa tena ili maana yake ieleweke kwa urahisi zaidi.

1 Chronicles 8:22

Maelezo ya Jumla

Maelezo katika 8:22 yamepangiliwa tena ili maana yake ieleweke kwa urahisi zaidi.

1 Chronicles 8:26

Hawa walikuwa vichwa vya koo na viongozi

Maneno "vichwa vya familia" na "viongozi" ina maana moja.

1 Chronicles 8:29

Baba wa Gibeoni, Jeieli, ambaye mke wake aliitwa Maaka, aliishi ndani ya Gibeoni

Hapa "baba wa" ya husu hali ya Wayahudi kama kiongozi wa mji wa Gibeoni. "Yeieli, kiongozi wa Gibeoni, aliishi Gibeoni. Jina la mkewe lilikuwa Maaka"

Uzao wake wa kwanza

"mzaliwa wa kwanza wa Yeieli"

1 Chronicles 8:38

Yeushi wa pili, na Elifeleti wa tat

"Yeushi mwana wa 2, na Elifeleti wa tatu"

Walikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla ya 150

"Walikuwa na jumla ya wana mia na hamsini na tano na wajuu"

1 Chronicles 9

1 Chronicles 9:1

Kwa hivyo watu wote wa Israeli walinakiliwa ki uzao

Nakala ya uzao yaeleza kumbukumbu ya uzao wa familia au mababu wa mtu.

Walinakiliwa katika vitabu vya kifalme vya Israeli

Hii ya husu kitabu ambacho hakipo tena.

1 Chronicles 9:4

Washiloni

Hili ni jina la group lilitoka Shela.

1 Chronicles 9:12

Walikuwa ni wanaume wenye uwezo sana wa kufanya kazi katika nyumba ya Mungu

Hawa wanaume wenye uwezo walifanya kazi katika nyumba ya Mungu"

1 Chronicles 9:14

Shemaia ... Elikana

Haya ni majina ya wanaume

kati ya uzao

"mmoja wa uzao"

Wanetofa

Hili ni jina la kundi la watu.

1 Chronicles 9:17

Walinzi wa lango

"askari" au "walinzi wa lango"

Awali walisimama kulinda katika geti la mfalme upande wa mashariki wa kambi ya uzao wa Walawi

"Uzao wa Walawi ulilinda lango la mfalme upande wa mashariki ya kambi"

mlango wa hema ... ango la kuingilia

Haya maneno yote yanaelezea mwingilio wa hema ya kukutania, au maskani

1 Chronicles 9:20

aliwaongoza

"aliwaongoza maaskari"

1 Chronicles 9:22

Majina yao yaliandikwa kwenye kumbukumbu za watu katika vijiji vyao

"Nakala zao katika vijiji vya hawa watu vilijumuisha majina ya hawa wanaume

watoto wao

"uzao wao"

Walinzi wa mageti waliwekwa

"wanaume walilinda miingilio"

pande zote nne, upande wa mashariki, magharibi, kaskazini, na kusini

"pande zote"

1 Chronicles 9:25

Kaka zao

"kaka za walinzi"

walikuja kuwasaidia baada ya mzunguko wa siku saba

mzunguko wa siku, wa awamu "walikuja kusaidia kwa mzunguko wa siku 7, wakipeana awamu"

walipangiwa kulinda vyumba

"walilinda vyumba"

1 Chronicles 9:28

Baadhi yao

"Baadhi ya askari"

walihesabu makala zilizo ingizwa ndani na zilizo tolewa nje

"walihesabau makala watu waliotoa nje kutumia, na wakahesabu makala watu walipo rudisha"

waliwekwa kutunza

"kutunza" au "kujali"

1 Chronicles 9:30

Matithia ... Shalumu

Haya ni majina ya watu.

Wakorahi ... Wakohathi

Haya ni majina ya makundi ya watu.

mikate ya uwepo

Ona kurasa ya neno kuhusu "mkate" kwa maelezo fasii kuhusu "mkate wa uwepo"

1 Chronicles 9:33

walipo kuwa hawafanyi kazi

"hawakuwa na haja ya kufanya kazi nyingine"

kufanya kazi walio pangiwa

"waliitaji kukamilisha kazi yao ya kupangiwa"

usiku na mchana

Hii ina maanisha "wakati wote" na ya weza kufasiriwa kwa kutumia maneno au neno kutoka lugha yako au tamaduni yako yenye kuleta maana moja

Hawa walikuwa viongozi wa familia miongoni mwa Walawi, kama ilivyo orodheshwa katika kumbukumbu za uzao wao

" Historia ya familia orodha yake yataja majina ya Walawi viongozi wa familia"

1 Chronicles 9:35

Gibeoni

Maelezo ya kwanza ya Gibeoni ya eleza mtu lakini ya pili ya taja mji.

1 Chronicles 10

1 Chronicles 10:1

Kila mwanaume wa Israeli alikimbia Wafilisti

"Jeshi la Waisraeli liliwakimbia kutoka"

kuanguka na kufa

"kufa"

1 Chronicles 10:4

unichome nao

"niue nao"

Lasihivyo, hawa wasio tahiriwa watukuja

Maelezo kuhusu "wasio tahiriwa" hapa ni kashfa, ikihashiria kuwa hawa watu ni wageni na hawana mahusiano na Mungu.

kuangukia

"alijiua nao"

1 Chronicles 10:5

a wana wake watatu

"na wana wake wa 3 wakafa"

1 Chronicles 10:7

Kila mwanaume wa Israeli

"Wanaume wa Israeli walipo"

kuishi humo

"waliishi katika miji ya Waisraeli"

Ikawa siku

Hili neno hapa la tumika kueka alama ya tukio muhimu katika historia. Kama lugha yako ina namna ya kufanya hivi, fikiria kutumia hapa.

kukagua wafu

"kuchukuwa kila kitu cha thamani miilini mwa wafu"

Sauli na wana wake wameanguka

"Sauli na wana wake wamekufa"

1 Chronicles 10:9

Wakamvu

"Wafilisti waliondoa kutoka mwilini mwa Sauli"

Ngao yake wakaeka

"Wafilisti wakachukuwa ngao ya Sauli"

Dagoni

Hili ni jina la mungu wa uongo.

1 Chronicles 10:11

Yabeshi Gileadi yote ilipo sikia Wafilisti waliyo

"Watu wa Yabeshi Gileadi walipo sikia nini wana jeshi wa Wafilisti"

mifupa yao

"miili yao" au "mabaki yao"

1 Chronicles 10:13

ushauri

Hii ni maoni au pendekezo kuhusu nini mtu afanye.

ngea na wafu

"alidai kuongea na hao walio kufa"

mwongozo

Hii ni msaada au ushauri kuhusu nini tufanye.

akamua na kupindua ufalme

"kuwapa uongozi wa watu wa Israeli kwa"

1 Chronicles 11

1 Chronicles 11:1

sisi ni nyama na mifupa yako

"sisi ni ndugu zako" au "tuna mababu sawa na wewe"

neno la Yahweh

"ujumbe wa Yahweh"

1 Chronicles 11:4

Yebusi

Hili lilikuwa jina fupi la Yerusalemu baada ya Wayebusi kuuteka mji, kabla ya Waisraeli kuchukuwa.

Daudi alichukuwa

"Lakini jeshi la Daudi lilishinda"

mji wa Daudi

"na wakauita mji wa Daudi"

hivyo akafanywa mkuu wa jeshi

"Hivyo Daudi akamfanya Yoabu mkuu"

1 Chronicles 11:7

Akaimarisha mji

"Waisraeli wakafanya ukuta kuuzunguka mji imara"

kutoka Milo

Hii yaeleza ngome ya Yerusalemu, labda iliyo tengenezwa na Wayebusi.

alikuwa naye

"alimsaidia"

1 Chronicles 11:10

viongozi Daudi aliyo kuwa nao

"viongozi chini ya Daudi"

waliyo jionyesha imara katika ufalme wake

"aliyo saidia uongozi wa Daudi kubaki imara"

thelathini

"wanaume hodari 30"

katika sehemu moja

"kwa wakati mmoja"

1 Chronicles 11:12

na kuwakata Wafilisti

"na kuwaua wafilisti wengi"

1 Chronicles 11:15

watatu wa viongozi thelathini

"3 wa 30"

Kwa wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, Wafilisti walikita kambi yao Bethilehemu

Daudi alikuwa sehemu salama katika pango wakati wana jeshi Wafilisti wakilinda Bethlehemu"

Wafilisti walikita kambi yao Bethilehemu

"Wafilisti waliweka wana jeshi Bethilehemu"

1 Chronicles 11:18

wanaume hodari watatu

wanaume hodari 3"

kisima cha Bethilehemu, kisima pembeni mwa lango

Haya maneno mawili yanahusu kisima kimoja. Ya pili ya husu kisima gani Bethilehemu.

Yahweh, iwe mbali na mimi, kwamba ni yanywe haya maji

Mungu, tafadhali usiniache ninywe dhabihu kama hii kwa gharama ya wanaume wangu"

Je ninywe damu ya wanaume walio hatarisha maisha yao?

Daudi anasema kwa swali kuwa maji yana dhamani kwasababu ya dhabihu iliyo tolewa na hao walioenda kufuata. "Sitakunywa damu ya wanaume walio radhi kufa kwa ajili yangu" au "Sitakunywa maji wanaume walio hatarisha maisha yao kuyapata"

1 Chronicles 11:20

wa watatu

"mashujaa Watatu"

alikuwa kiongozi wa watatu

"Abishai alikuwa kiongozi wa mashujaa watatu

yeye alipewa heshima mara mbili na akawa kiongozi wao

"wana jeshi walikuwa na heshima kubwa kwa Abishai na wakamfanya kiongozi, japo hawaku mhesabu kama kiongozi wa mashujaa Watatu"

1 Chronicles 11:22

mambo makuu

Haya ni matendo yanayoonyesha ujasiri, uweza, au ujuzi.

theluji ikianguka

"wakati wa dhoruba ya theluji"

lakini alimfuata chini

"Benaia alikutana na Mmisri"

mkuki kama gongo la mshonaji

"mkuki mkubwa sana"

1 Chronicles 11:24

akatajwa miongoni mwa wale wanaume hodari watatu

"alikuwa maarufu kama wanaume hodari 3"

Alisifika zaidi ya wale wanajeshi thelathini kwa ujumla, lakini hakuwa pewa hadhi ya wale wanajeshi watatu hodari

"Watu walimheshimu kuliko wana jeshi wale 30, lakini sio zaidi ya wale 3 wenye ujuzi wa juu"

walinzi

Huyu ni mtu au kundi la watu wenye wajibu wakumlinda mtu muhimu.

1 Chronicles 11:42

thelathini pamoja nae

"wanaume 30 pamoja nae"

1 Chronicles 12

1 Chronicles 12:1

wakati akiwa bado amefukuzwa katika uwepo wa

"wakati alipo kuwa hawezi kuwa katika uwepo wa"

Walikuwa wana upinde na waliweza kutumia mkono wa kuume na wakushoto

"Silaha zao zilikuwa upinde, na waliweza kutumia upinde kwa mkono wa kulia au wakushoto"

mawe na manati

Manati ilizungushiwa ngozi iliyo mruhusu mtu kutupa jiwe kwa umbali mrefu. Jiwe liliwekwa katikati wakati mtu alishika miisho na kuzungusha kwa duara. Alipo achilia, jiwe liliruka palipo lengwa.

1 Chronicles 12:3

wale thelathini

"wale wana jeshi 30"

1 Chronicles 12:8

ambao nyuso zao zilikuwa kali kama za simba

"walio kuwa wakali sana"

Walikuwa wepesi kama swala

"Walikuwa wana mbio sana"

swala

Hawa ni wanyama walio wa pole na wepesi, mfano wa ayala.

1 Chronicles 12:9

wapili ... wakumi na moja

Hii ya waorodhesha hawa wanaume kwa vyeo vya uongozi. "2 ... 3 ... 4 ... 5 ... 6 ... 7... 8 ... 9 ... 10 ... 11"

1 Chronicles 12:14

Wamwisho aliongoza mia moja

Hii ina maana kuwa kundi dogo kiongozi alilo ongozi ni 100.

mkubwa aliongoza elfu moja

Hii ina maana kuwa kundi kubwa kiongozi alilo ongozi ni 1000.

mwezi wa kwanza

Huu ni mwezi wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Machi na sehemu ya kwanza Aprili kwa kalenda za magharibi. Ni mwanzo wa masika mvua za mwisho zaja.

1 Chronicles 12:16

wanaume wa Benjamini na Yuda

"wanaume kutoka kabila la Benjamini na Yuda"

1 Chronicles 12:18

roho ikaja juu ya

"Roho ikampa nguvu"

wale thelathini

"wale 30"

Sisi ni wako, Daudi. Sisi tupo upande wako, mwana wa Yesse

Haya maneno ya shiriki maana moja na mkazo wa kumfuata Daudi.

1 Chronicles 12:19

Atamwendea

"kuwaacha viongozi wao kujiunga na"

wa maelfu

"Zaidi ya wanaume 1000"

1 Chronicles 12:21

kikundi cha wezi

"makundi ya watu waliyo wapora nchi nzima"

kama jeshi la Mungu

Hii inalinganisha ukubwa wa jeshi la Daudi kwa jeshi la malaika wa Mungu.

1 Chronicles 12:23

uupindua ufalme wa Sauli kwake

"kumpa utawala wa Sauli kwa Daudi"

ilikutimiza neno la Yahweh

"walifanya neno la Yahweh kweli" au "kutimiza neno la Yahweh"

Kutoka Yuda

"Kutoka kabila la Yuda"

1 Chronicles 12:29

Kutoka kwa Benjamini, kabila la Sauli

"Kutoka kabila la Yuda, kabila la Benjamini"

nusu kabila

Ona jinsi ulivyo tafsiri 5:18

1 Chronicles 12:36

wameandaliwa na silaha za kila namna

"wabeba silaha za kila namna"

1 Chronicles 12:38

dhumuni maalumu

"mipango"

waliandaliwa kwa pambano

"kwa silaha zao kwa ajili ya vita"

siku tatu

"siku 3"

zabibu kavu

Haya ni mizabibu iliyo kaushwa, tunda dogo linalo kuwa kwenye mzabibu

1 Chronicles 13

1 Chronicles 13:1

maelfu na mamia

Jeshi lilikuwa na wakuu walio waongoza makundi ya wana jeshi wa kila kimo. "zaidi ya wanaume 1000 na zaidi ya wanaume 100"

yalionekana sawa machoni pa watu wote

Hapa "macho yana wakilisha mawazo na maoni ya watu. "watu wote walidhani haya ni mambo sahihi ya kufanya"

1 Chronicles 13:5

Baala

Hili ni jina lingine la Kiriathi Yearimu.

ambaye ameketi juu ya makerubi

"anaye tawala kutoka amri za viumbe wenye mabawa katika sanduku la agano"

1 Chronicles 13:7

chombo kipya cha matairi

Hili ni gari la matairi linalo vutwa na mnyama ambaye hajawai kutumika.

tari

chombo cha muziki chenye kichwa cha ngoma kinacho weza kupigwa na chenye vipande vya chuma vilivyo zunguka vinavyo toa sauti ngoma inapo pigwa.

upatu

nyembamba, sahani za chuma zinazo gonganishwa pamoja kufanya sauti kubwa

1 Chronicles 13:9

Hasira ya Yahweh ikawaka juu ya Uza

"Yahweh alikuwa na hasira sana kwa Uza"

mbele za Mungu

"katika uwepo wa Mungu"

Daudi alipatwa na hasira

Daudi alishikwa na hasira dhidi ya Yahweh

hadi leo

Ona ulivyo tafsiri 4:42

1 Chronicles 13:12

Nawezaje kuleta sanduku la Mungu nyumbani mwangu?

Daudi anaeleza hasira yake kuhusu kifo cha Uza alipo kuwa ana jaribu kurudisha sanduku kwenye mji wake. "Siwezi kurudisha sanduku la Mungu kwenye mji wangu" au "Niambie Sheria za kurudisha sanduku, sijui jinsi ya kufanya hivi"

miezi mitatu

"miezi 3"

1 Chronicles 14

1 Chronicles 14:1

Hiramu

Jina la mfalme

maseremala

Hawa ni watu ambao kazi yao ni kufanya vitu vya mbao.

wajenzi

Hawa ni watu wa kufanya vitu kwa mawe au tofali.

alimfanya kuwa

"kumfanya"

ufalme wake ulitukuzwa juu sana kwa ajili ya watu wa Israeli

"Yahweh alimpa Daudi heshima katika ufalme wake kuwasaidia watu wa Israeli"

1 Chronicles 14:8

Daudi amepakwa mafuta kama mfalme juu ya Waisrael

"watu wa Israeli walimpaka mafuta Daudi kuwa mfalme wao"

bonde la Refaimu

Hili ni jina la sehemu

1 Chronicles 14:10

nitawakabidhi kwako

"nitakupa ushindi juu yao"

Baali Perazimu

Hili ni jina la sehemu

kwa mkono wangu

Hii ya husu vifaa vya Daudi. "kutumia jeshi langu"

kama vile mpasuko wa mafuriko ya maji.

Nguvu na ushindi wa jeshi la Daudi wafananishwa na mpasuko wa mafuriko ya maji. "kwa urahisi"

wateketezwe kwa moto

"kuchoma miungu yao ya uongo"

1 Chronicles 14:13

bonde

"bonde la Refaimu"

Usiwashambulie kwa mbele

"kushambulia kwa mbele"

wazunguke kwa nyuma yao na uwajie kupitia misitu ya balisamu

"nenda kupita msitu wa balisamu na kuwashumbulia kwa nyuma"

balisamu

Huu ni aina ya mti

1 Chronicles 14:15

Maelezo ya Jumla

Mungu anaendelea kumjibu Daudi kwa swali lake.

atakutangulia kwenda

"ataenda mbele yako kukupigania"

Gezeri

Hili ni jina la mji

umaarufu wa Daudi ukaenda katika nchi zote

"Watu wa mbali wakaskia ushinde wa Daudi dhidi ya Wafilisti"

1 Chronicles 15

1 Chronicles 15:1

Daudi akajingea nyumba zake

"Watu wakamjengea nyumba Daudi"

Akaanda sehemu

"akaamuru sehemu maalumu iandaliwe"

akakusanya Israeli yote

"akaamuru watu wote wa Israeli waje pamoja"

kuleta sanduku

"kusherehekea wakati Walawi wakibeba sanduku"

1 Chronicles 15:4

ndugu

watu walio wa sehemu ya familia au kabila moja

1 Chronicles 15:11

niliyo iandaa.

"Nimewaamuru Walawi kuianda"

1 Chronicles 15:13

Mara ya kwanza hamkubeba

"Hamkubeba sanduku kabla"

hatuku mtafuta

"hatukumuliza kwa maelekezo"

akawa na hasira kwetu

"akatuadhibu sisi"

Walawi waka jiweka wakfu iliwaweze kuleta

"Walawi walijisafisha ili kuweza kubeba"

1 Chronicles 15:16

upatu

Ona ulivyo tafsiri 3:7

wakipaza sauti zao

"kuimba"

daraja la pili

"mamlaka ya chini" au "darja la 2"

mlinzi wa lango

watu waliyo linda lango

1 Chronicles 15:19

upatu

Ona ulivyo tafsiri 3:7

waliongoza njia

"waliwaongoza wana muziki wengine" ua "waliongoza msafara"

1 Chronicles 15:25

wa maelfu

"zaidi ya wanaume 1000"

Obedi Edomu

Hili ni jina la mwanaume.

1 Chronicles 15:27

Daudi alivishwa joho safi la maridadi, pamoja na Walawi walio beba sanduku, waimbaji, na Kenania, kiongozi wa nyimbo na waimbaji

"Daudi, Walawi, na waimbaji wote walivaa mavazi safi ya majoho"

Joho

Hii ni aina nyororo, ya kitamba kigumu.

Kenania

Hili ni jina la mwanaume

Hivyo Israeli yote wakaleta sanduku la agano la Yahweh

"Hivyo umati mkubwa wa Waisraeli walileta sanduku la agano la Yahweh kutoka nyumba ya Obedi Edomu hadi Yerusalemu"

upatu

Ona jinsi ulivyo tafsiri 13:7

1 Chronicles 15:29

sanduku la Yahweh lilivyokuja kwa mji wa Daudi

"watu walileta sanduku la agano la Yahweh kwenye mji wa Daudi"

Mikali

Hili ni jina la mke wa Daudi

akamdharau moyoni mwake

"alimdharau sana katika fikra zake"

1 Chronicles 16

1 Chronicles 16:1

Wakaleta ndani Sanduku

"Waisraeli wakaleta sanduku"

kipande cha mkate

kipande kimoja cha mkate wa kuoka, wenye hamira

zabibu kavu

Hizi ni zabibu zilizo kavu, tunda dogo linalo ota kwenye mizabibu.

1 Chronicles 16:4

upatu

Ona ulivyo tafsiri 13:7

1 Chronicles 16:7

Kisha katika hiyo siku

Hii ya husu siku sanduku la agano liliamishwa kutoka nyumba ya Obedi Edomu kwenda Yerusalemu.

nyimbo ya shukurani

"nyimbo ya kutoa shukrani"

liitieni jina lake

"omba kwa Yahweh"

1 Chronicles 16:10

katika jina lake takatifu

"vile Mungu alivyo"

mioyo ya wanao mtafuta Yahweh

"acha hao wanaotaka kumjua Yahweh zaidi"

Mtafute Yahweh na nguvu zake; tafuteni uwepo wake siku zote

Haya maneno yanashiriki maana moja na yanatumika kutia mkazo. "Mtafute Yahweh na nguvu zake; tafuta kuwa karibu naye daima"

1 Chronicles 16:12

Kumbukeni matendo

"Kumbuka mambo mazuri"

kinywa chake

"aliyo nena"

3enyi uzao wa Israeli mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wateule wake

Haya maneno yanashiriki maana moja na yanatumika kutia mkazo.

Amri zake zipo duniani kote

"Amri zake ni za watu wote wa dunia"

1 Chronicles 16:15

Tunzeni agano lake akilini mwenu

"Kumbuka agano la Yahweh"

vizazi elfu moja

"vizazi 1,000"

Anakumbuka

"Yahweh anakumbuka"

kama sehemu

"kama sehemu yako"

1 Chronicles 16:19

Nilisema hili mlipo kuwa wachache kwa idadi, wachache sana

"Yahweh alisema hili Waisraeli walipo kuwa kundi dogo la watu"

wageni katika nchi

"wageni katika nchi"

Walienda taifa hadi taifa, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine

Haya maneno yanashiriki maana moja na kutilia mkazo umbali Waisraeli walivyo tanga.

kwa ajili yao

"kwa sababu yao"

1 Chronicles 16:23

dunia yote

Kila kitu kwenye dunia cha leta utukufu kwa Mungu.

siku hadi siku

"kila siku"

1 Chronicles 16:25

Uzuri wa ajabu na utukufu upo uweponi mwake

"Uzuri na ajabu vimemzunguka"

Uwezo na furaha upo kwake

"Yahweh anaonyesha nguvu na furaha yake"

1 Chronicles 16:28

Mpeni sifa Yahweh

"Mpe sifa Yahweh kwa"

upasao jina lake

"anastahili au anastahili kupokea"

1 Chronicles 16:30

Mtetemeke mbele zake

"Onyesha hofu ya heshima kwa wazo lake"

Mbingu nazo ziwe nafuraha, na dunia ifurahi

"Acha kila mtu afurahi"

1 Chronicles 16:32

Bahari na ingurume

"Bahari itafanya sauti kubwa sana"

na inayo ijaza

"viumbe wa bahari"

miti iliyopo misituni ipige kele

Hii ina zungumzia miti kama ni watu wanao weza kupiga kelele kwa furaha.

1 Chronicles 16:34

Chema, wema

Neno "wema" lina maana tofauti kulingana na muktadha. Lugha nyingi zitatumia maneno tofauti kutafsiri hizi maana tofauti.

  • Kwa ujumla, kitu ni chema kama kinalingana na tabia ya Mungu, kusudi, na mapenzi.
  • Kitu ambacho ni "chema" cha weza pendeza, bora, saidia, kufaa, faidisha, au kubalika kimaadili.
  • Ardhi iliyo "njema" yaweza itwa "rotubisha" au "inayozalisha."
  • Zao "jema" la weza kuwa zao "tele"
  • Mtu anaweza kuwa "mwema" kwa kile anachofanya kama wana ujuzi kwa kazi yao au ajira, kama, "mkulima mwema."
  • Katika Biblia, maana ya jumla ya "jema" mara nyingi utofautishwa na "uovu"
  • Neno "wema" mara kwa mara la husu kuwa na maadili mema au wenye haki katika mawazo na matendo.
  • Wema wa Mungu wa husu jinsi anavyo bariki watu kwa kuwapa vitu vyema na vya faida. Yaweza pia kumaanisha ukamilifu wake wa adili.

uaminifu wa agano, utii wa agano, upendo mwema, upendo usio shindwa

Hili neno la tumika kuelezea kujitolea kwa Mungu kutimiza ahadi alizo ziweka kwa watu.

  • Mungu alifanya ahadi kwa Waisraeli katika makubaliano rasmi yani "maagano"
  • "uaminifu wa agano" au "utii wa agano" la Yahweh ya husu ukweli kwamba Yahweh ana shika ahadi zake kwa watu wake.
  • Uaminifu wa Mungu wa kushika ahadi za agano lake ni muonekano wa neema yake kwa watu wake.
  • Neno "utii" ni neno lingine linalo husu kuwa muhusika na kutegemewa kufanya na kusema yale yaliyo ahidiwa na kumsaidia mtu mwengine.

dumu, kudumu

Neno "dumu" la maanisha kubaki kwa kipindi kirefu au kuvumili kitu kigumu kwa subira.

  • Lina maana pia ya kusimama imara kipindi majaribu yanapo kuja, bila kukata tamaa.
  • Neno "kudumu" la weza maanisha "subira" "kustahimili mapito" au "kuvumilia wakati wa dhiki"
  • Faraja ya kwa Wakristo "kudumu ata mwisho" ya waeleza wa mtii Yesu, ata kama hili litawa sababisha wateseke.
  • Ku "vumilia mateso" ya weza maanisha pia "kupitia mateso"

milele

Kwenye Biblia, neno "milele" la eleza muda usio kwisha. Wakati mwengine la tumika kifumbo kumaanisha, "muda mrefu sana"

  • Neno "milelel na milele" la tilia mkazo kwamba kitu kita kuwepo tu.
  • Maneno "milele na milele" ni namna ya kueleza umilele au uzima wa milele ni nini. Pia lina wazo la muda usio kwisha.
  • Mungu alisema kuwa kiti cha Daudi kitadumu "milele". Hili linahusu ukweli kwamba mzao wa Daudi Yesu ata tawala kama mfalme hadi mwisho.

Mungu

Katika Biblia, neno "Mungu" la husu kiumbe wa milele aliye umba ulimwengu bila chochote. Mungu yupo kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Jina la Mungu la binafsi ni "Yahweh"

  • Mungu amekuwepo daima; amekuwepo kabla ya chochote kuwepo, na ataendelea kuwepo milele.
  • Yeye ndie Mungu pekee wa kweli na ana mamlaka juu kila kitu katika ulimwengu.
  • Mungu ni mwenye haki kamilifu, wa hekima isiyo na mwisho, mtakatifu, wa haki, wa rehema, na wa upendo.
  • Yeye ni Mungu mtunza agano, anaye timiza maagano yake.
  • Watu waliumbwa wamuabudu Mungu na ni yeye tu wamuabudu.
  • Mungu alirihidhisha jina lake kama "Yahweh" lenye maana ya, "yupo" au "Mimi ndiye" au "Yeye ambaye (daima) yupo."
  • Biblia ya fundisha kuhusu "miungu" ya uongo ambayo ni sanamu isio ishi watu waabuduo kwa makosa.

wokovu

Neno "wokovu" la husu kuokolewa au kukombolewa kutoka kwenye uovu na hatari.

  • Katika Biblia, "wokovu" wa husu ukombozi wa kiroho na wa milele unao tolewa na Mungu kwao wanao tubu dhambi zao na kumuamini Yesu.
  • Biblia pia ya zungumzia Mungu kuokoa au kukomboa watu kwa adui zao wa mwilini.

jina

Katika Biblia, neno "jina" linatumika kwa mfumbo kadhaa.

  • Baadhi ya Muktadha, "jina" la weza husu sifa ya mtu, kama vile, "acha tujfanyie jina"
  • Neno "jina" la weza pia kuhusu kumbukumbu ya kitu. Kwa mfano, "kata majina ya sanamu" maana yake kuharibu hizo sanamu ili kwamba wasiendelee kukumbukwa au kuabudiwa.

Kuzungumza "katika jina la Mungu" ya maanisha kusema kwa nguvu na mamlaka, au kama mwakilishi wake.

  • "Jina" la mtu la weza husu huyo mtu kwa ujumla, kama "hakuna jina chini ya mbingu ambalo la tupasa kuokolewa."

ufukufu

Kwa ujumla, neno "utukufu" la maanisha heshima, uzuri, na ukubwa wa ajabu. Chochote chenye utukufu cha semekana kuwa na "utukufu"

  • Wakati mwengine "utukufu" ya husu kitu cha dhamani kubwa na umuhimu. Katika muktadha mengine ina eleza uzuri, mwanga, au hukumu.
  • Kwa mfano, msemo "utukufu wa wachungaji" ya husu malisho tele kondoo wao walipo kuwa na nyasi nyingi ya kula.
  • Utukufu wa tumika sana kumueleza Mungu, ambaye ana utukufu kuliko mtu au kitu chochote katika ulimwengu. Kila kitu katika tabia yake ya rihidhisha utukufu na uzuri wake.
  • Msemo "kufurahia utukufu" una maana ya kugamba kuhusu au kujivunia kitu.

sifa

Kumsifu mtu ni kuonyesha matamanio na heshima kwa huyo mtu.

  • Watu wanamsifu Mungu kwasababu kwa jinsi alivyo mkuu na kwasbabu ya matendo makuu aliyo fanya kama Muumbaji na Mwokozi wa ulimwengu.
  • Sifa kwa Mungu muda mwing ya jumuisha kuwa na shukurani kwa aliyo ya fanya.
  • Muziki na kuimba mara nyingi ya tumika kama njia ya kumsifu Mungu.
  • Kumsifu Mungu ni sehemu ya maana ya kumuabudu.
  • Neno "kusifu" la weza tafsiriwa kama, "kumzungumzia vizuri" au "kumheshimu sana kwa maneno" au "kusema mambo mazuri kuhusu"
  • Jina "sifa" la weza tafsiriwa kama, "heshima ya kusema" au "hotuba inayo heshimu" au "kuzungumza mambo mazuri kuhusu"

1 Chronicles 16:36

kutoka milele na milele

"milele"

Watu wote

"Watu" au "Kila mtu aliyepo hapo"

1 Chronicles 16:37

kama kazi za kila siku zilivyo itaji

"kama ilivyo itajika kila siku katika sheria ya Musa"

watumike mbele ya hema

"kutumika ndani au karibu na hema ya kukutani"

1 Chronicles 16:40

Walikuwa

"Makuhani"

1 Chronicles 16:42

upatu

Ona ulivyo tafsiri 13:7

1 Chronicles 17

1 Chronicles 17:1

kuwa katika nyumba yake

kuridhika na kuwa na furaha, bila tamanio la kuhama wala kubadilika.

nyumba jengwa na mierezi

Mbao za kutoka kwenye miti ya mierezi ili hesabiwa kuwa mbao bora ya ujenzi.

fanya yalio moyoni mwako

Daudi anaelezwa afanye sawa na sehemu ya mwili yenye hisia. "fanya utakacho taka kufanya"

Mungu yupo nawe

Kuwa katika makubaliano na Mungu ni kama kufanya kazi naye kwasababu Mungu atakusaida kufanikiwa. "Mungu akubaliana na unacho taka kufanya"

1 Chronicles 17:3

neno la Mungu lilimjia

"Mungu alizungumza neno lake"

niliyo ileta Israeli

"kwamba nili waleta Waisraeli kwenye nchi ya ahadi kutoka Misri"

hema, hema la kukusanyikia

Yote haya maneno "hema" na "hema la kukusanyikia" ya eleza kitu kimoja na kutia mkazo kwamba aliishi katika jengo lisilo la kudumu.

Kwa nini haujanijengea mimi nyumba ya mierez?

"Ungenijenga nyumba yenye mbao za gharama."

1 Chronicles 17:7

Nilikuchugua kutoka malishoni

Kazi ya Daudi kama mchungaji ya taja kwa sehemu aliyo chunga kondoo zake. "Nilikutoa kwenye kazi yako kama mchungaji"

malishoni

Ona jinsi ulivyo tafsiri 4:39

1 Chronicles 17:9

Maelezo ya Jumla

Mungu anaendelea kuzungumza ujumbe Nathani anao paswa kumpa Daudi.

nitawapanda hapo

Mungu ana taja kuwaweka Waisraeli kwenye nchi ya ahadi kama mmea aliyo uotesha kwenye ardhi. "Nitawapandikisha hapo"

siku zile nilipo waamuru

Kipindi cha vizazi vingi kina tajwa kama siku. "nilipo amuru" au kutoka vizazi nilivyo amuru"

kuwa juu ya watu wangu Waisraeli

Kuwa katika mamlaka yaelezwa kama kua juu ya mtu. "kuwaamuru watu wangu Israeli"

maadui zako wote ... nina kwambia

Maneno "zako" na "nina kwambia" ya muhusu Daudi.

nitawatiisha

kumfanya mtu au mnyama asiweze kutembea.

nitakujengea nyumba

Yahweh anaeleza kumpa Daudi wazao wengi kutawala juu ya Israeli kama kumjenga nyumba.

1 Chronicles 17:11

siku zako zitapo timia

Maisha yana tajwa kama idadi kadhaa za siku. "utakapo kufa"

kwenda kwa baba zako

Haya maneno yaeleza kifo kama sehemu mababu wa Daudi walipo kwasababu wamekufa tayari.

nitainua uzao wako

Kumueka mtu katika uongozi ya tajwa kama kumuinua juu sana.

nitaimarisha kiti chake cha enzi

Haki ya kutawala kama mfalme imeelezwa kama sehemu ya mfalme kuishi.

1 Chronicles 17:13

na kiti chake cha enzi

Haki ya kutawala kama mfalme imeelezwa kama sehemu ya mfalme kuishi. "na haki yake ya kutawala"

na kumtaarifu

"kumwabia"

1 Chronicles 17:16

akasema

"Daudi akasema"

Mimi ni nani, Yahweh Mungu, na familia yangu ni nini, hadi unilete umbali huu?

Daudi anauliza ili swali kuonyesha shukurani kuwa Mungu amemchagua kumbariki ata kama hastahili.

Hili lilikuwa jambo dogo

Kitu kisicho cha muhimu cha elezwa kuwa kidogo.

machoni pako

Machoni pa Yahweh ya husishwa na ufahamu wake.

Nini zaidi mimi, Daudi, niseme?

Daudi anatumia hili swali kuonyesha kuwa hawezi kueleza kabisa shukrani zake kwa Mungu. "Kama ningeweza sema zaidi kuonyesha shukurani zangu kisha ningefanya lakini sijui nini tena niseme"

mtumishi wako

Daudi anaeleza kuwa yeye ni mtumishi wa Yahweh.

Umemheshimu mtumishi wako. Umemtambua kwa kipekee mtumishi wako

Maneno yote mawili yana maana moja. Kama lugha yako ina maana moja ya kueleza "heshima" na "utambuzi" kisha hii yaweza tafsiriwa kama neno moja.

1 Chronicles 17:19

wa ajili ya mtumishi wako

"faida yangu"

uliwaokoa kutoka Misri

"kuwaokoa kutoka utumwani Misri"

matendo makuu na yahajabu

Maneno "makuu" na "ya ajabu" yana maana moja na kukazia uzito wa ukuu. "matendo mazuri ya ajabu"

1 Chronicles 17:22

itimizwe milele

"iendele milele"

1 Chronicles 17:25

utamjengea nyumba

Kuwa na watoto na kukuza familia kubwa yaelezwa kama kujenga nyumba.

nimepata ujasiri

"kuwa mjasiri wakutosha"

umeibariki, na itabarikiwa milele

Ina maana moja, imerudiwa kwa mkazo.

1 Chronicles 18

1 Chronicles 18:1

Baada ya haya

"Baada ya Mungu kuahidi kumbariki Daudi"

1 Chronicles 18:3

Hadadezeri

Hili ni jina la mwanaume.

Zoba

Hili ni jina la nchi.

magari ya farasi elfu

"magari ya farasi 1000"

wanaume wa farasi elfu saba

Hawa ni wana jeshi walio endesha farasi. "wanaume wa farasi 7000"

wanajeshi wa miguu elfu ishirini

Hawa ni wana jeshi waliyo tembea. "wanajeshi wa miguu 20,000"

aliwajeruhiku

kulemaza mtu au mnyama kwa kumkata msuli wa nyuma ya paja

akahifadhi

kutunza kwa matumiza maalumu

magari ya farasi mia moja

"magari ya farasi 100"

1 Chronicles 18:5

aliua wanaume elfu ishirini na mbili

elfu mbili - "aliua 22,000"

vikosi

kundi la wana jeshi waliyo pangiwa eneo fulani.

1 Chronicles 18:7

Hadadezeri

Ona jinsi ulivyo tafsiri jina lake 18:3

Tibhathi ... Kuni

Haya ni majina ya miji.

saani ya shaba

Hii ni bakuli kubwa ya shaba, kiasi cha mita 5 upana, hiliyo wekwa hekaluni kwa kunawia kipindi cha sherehe.

1 Chronicles 18:9

Toi ... Hadoramu

Haya ni majina ya wanaume

amepigana

"amekuwa katika vita na"

1 Chronicles 18:12

Abishai ... Zeruia

Haya ni majina ya wanaume.

Waedomi elfu kumi na nane

"Waedomi 18,000"

Bonde la Chumvi

Hili ni jina la bonde katika ya Edomu na Yuda uliyo tumika kama uwanja wa pambano.

vikosi

makundi ya wana jeshi yaliyo pangwa sehemu maalumu.

Waedomi wote wakawa watumishi wa Daudi

"watu wa Edomi walilazimishwa kumkubali Daudi kama mfalme na kulipa pesa kwa serikali ya Daudi kila mwaka"

1 Chronicles 18:14

Zeruia ... Ahiludi ... Ahitubi ... Abiathari ... Shavisha ... Benaia ... Yehoiada

Haya ni majina ya wanaume.

mtunza kumbukumbu

mtu anaye fanya kazi ya kuandika maelezo ya maalumu ya matukio.

Ahimeleki

Hili jina linawakilisha sahisho la "Abimeleki," ambalo tafsiri zingine zinatumia. Sahisho hili linafanya huu mstari ukubaliane na 8:15.

Zadoki mwana wa Ahitubi na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani

Baadhi ya tafsiri ina sahisha hili kusema kwamba Ahitubi na Ahimeleki walikuwa makuhani wa kuu.

Wakerethi ... Wapelethi

Haya ni majina ya makundi ya watu.

1 Chronicles 19

1 Chronicles 19:1

Nahashi ... Hanuni

Haya ni majina ya wanaume.

Nitaonyesha ukarimu ... alionyesha ukarimu

"Nitakuwa mkarimu ... alikuwa mkarimu"

kumfariji

"kuliwaza"

Unadhani Daudi anamheshimu baba yako sababu ametuma watu kukufaraji?

"Usidhani kuwa Daudi ana muheshimu baba yako kwasababu ametuma wanaume kukufariji."

Je watumishi wake hawajaja kutadhimini nchi iliwaipindue?

"Hakika watumishi wanakuja kwako kudadisi nchi ili waipindue."

1 Chronicles 19:4

mavazi

"nguo"

alienda kukutana nao

"alituma wajumbe kwenda kuwafariji"

walifedheeka sana

Fedhea yaelezewa kubwa sana kuonyesha jinsi ilivyo wahadhiri. "aibika sana"

1 Chronicles 19:6

wamekuwa kikwazo kwa Daudi

Neno "uvundo" la elezea harafu mbaya. Hii yaelezea Waamoni kama kitu kibaya na hakitakiwi.

talanta elfu moja

"talanta 1,000"

Naharaimu .. Maka ... Zoba ... Medeba

Haya ni majina ya miji.

1 Chronicles 19:8

alipo sikia

"alisikia Waamoni walikuwa wanakuja kwa vita"

kukutana nao

"kupigana dhidi yao"

1 Chronicles 19:10

Abishai

Hili ni jina la kaka wa Yoabu.

1 Chronicles 19:12

Kuwa thabiti

"Kuwa shupavu"

natujionyeshe kwa watu wetu kuwa ni wenye nguvu

"tutende kwa ujasiri"

1 Chronicles 19:14

wasogea kwenye pambano

"alienda mbele kwenye pambano" au "aliwafuata maadui wana jeshi kwenye pambano"

1 Chronicles 19:16

Waaremi walipoona

"Waaremi walielewa"

msaada

"wana jeshi zaidi"

Shofaki ... Hadadezeri

Haya ni majina ya wanaume.

Daudi alipo ambiwa haya

Wajumbe wake walipo mwambia Daudi hili.

Alipanga

"kuweka vizuri"

wakapigana nao

"Waaremi wakapigana na Daudi na wana jeshi wake"

1 Chronicles 19:18

akaua elfu saba

"akaua 7,000"

wanajeshi wa miguu elfu arobaini

wanajeshi wa miguu 40,000"

Shofaki ... Hadadezeri

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 20

1 Chronicles 20:1

kusikitisha nchi

"kuharibu nchi" Hii yaeleza jeshi linapo haribu nchi maadui zao wanapo otesha chakula

1 Chronicles 20:2

Taji liliwekwa kichwani mwa Daudi

"Wanaume wa Daudi wakaeka taji kichwani kwake"

akaleta mali

vitu vya thamani vilivyo chukuliwa vitani.

Daudi aliwataka watu wote wa mji

Watu wanatajwa kwa miji yao. "Daudi aliwataka watu wote wa miji"

1 Chronicles 20:4

Gezeri ... Gobu

Haya ni majina ya miji

Sibekai ... Sipai ... Elhanani ... Lahmi

Haya ni majina ya wanaume.

Mhushathi ... Refaimu ... Mbethilehemu ... Mgiti

Haya ni majina ya makundi ya watu.

wakazidiwa

kumtawala mtu au kitu kwa kutumia nguvu.

gongo

mbao ndefu na nyembamba

gongo la mshonaji

aina ya mbao inayo tumika kunyoosha mapindo wakati nyuzi za zuria zinashonwa pamoja kuzunguka.

1 Chronicles 20:6

Refaimu

Hilo ni jina lililo pewa jamii ya watu ambao walikuwa warefu na imara.

Yehonadabu ... Shimea

Haya ni majina ya wanaume.

waliuawa na mkono wa Daudi na mkono wa wanajeshi wake

Daudi na wana jeshi wake wana tajwa kwa sehemu ya miili yao inayo tumika kushikilia upanga. "Daudi na wana jeshi wake waliua wazao wa Refaimu"

1 Chronicles 21

1 Chronicles 21:1

Adui akainuka dhidi ya Israeli

Kuwa juu kunafafanua kuwa na nguvu zaidi. "'Adui wa Israel walikuwa na nguzu zaidi"

Kumchochea

Kumsababisha mtu afanye kitu.

Kutoka Beerisheba mpaka Dani

Waisraeli waliichukulia hii miji miwili miji yao ya kusini zaidi na kaskazini zaidi. Daudi alitumia hii miji miwili kufikia Waisraeli wote.

Mara mia zaidi ya lilivyo

Yoabu alieleza matamanio ya kuwa na jeshi lenye ukubwa wa watu 100 kwa kusema angependa jeshi liwe na wanajeshi zaidi na lenye nguvu.

Lakini bwana wangu mfalme, kwani wote hawamtumikii bwana wangu? kwanini bwana wangu anataka hili? Kwanini ulete hatia kwa Israeli?

Lakini bwana wangu mfalme, wote wanakutumikia tayari. Bwana wangu asiombe hili. Utaleta tu hatia kwa watu wa Israeli kwa matamanio yako ya nguvu ya kijeshi.''

Kwanini bwana wangu analitaka hili?

Neno ''hili'' limemaanisha mpango wa Daudi kuhesabu wanaume waote wa Israeli.

1 Chronicles 21:4

Neno la mfalme halikubadilika

Mstari huu wahusu amri ya mfalme Daudi kuwa ya mwisho kwasababu hatabadili amri yake baada ya kuitoa. "amri ya mfalme haitakuja kubadilika"

wanaume waliobeba upanga

Maaskari wa Israeli walielezewa kwa kitendo cha kuvuta upanga na kupigana nao.

1 Chronicles 21:6

Lakini Levi na Benjamini hawakus hesabiwa miongoni mwao

" Lakini Yoabu hakuwa hesabu wanaume kutoka makabila ya Levi na Benjaminini"

kwa hili tendo

"tendo hili" limemaanisha katika mpango wa Daudi kuhesabu wanaume wote wa Israeli wenye uwezo wa kupigana.

chukua hatia ya mtumishi wako

Msamaha unafafanuliwa kama kuwa na hatia halafu ikaondolewa. "Nisamehe mimi"

hatia ya mtumishi wako

Daudi anajitaja mwenyewe kama mtumishi wa Mungu. "hatia yangu"

1 Chronicles 21:9

Yahweh

Neno "Yahweh" ni jina binafsi la Mungu ambalo alilidhihirisha alipokuwa anazungumza na Musa kwenye kichaka cha moto.

  • Jina "Yahweh" limetokana na neno linye maana, "Kuwa" au "kuwepo."
  • Maana inayowezekana kuwa ya "Yahweh" inajumuisha, "ndiye" au "Ndimi" au "anaye sababisha kuwa."
  • Jina hili linadhihirisha kuwa Mungu anaishi na ataendelea kuishi milele. pia linamaanisha yupo siku zote.
  • Kufuata mila, tafsiri nyingi za Biblia zinatumia neno "BWANA" kuwakilisha "Yahweh." Mila hii ni matokeo ya ukweli kihistoria, kwamba watu wa Kiyahudi walikuwa na uwoga wa kutamka jina Yahweh na kuanza kusema "Bwana" kila muda neno "Yahweh" lilitokea katika nakala. Biblia za kisasa zimeandika "BWANA" kwa herufi kubwa zote kuonesha heshima kwa jina la Mungu binafsi na kulitofautisha na "Bwana" ambalo na tofauti na neno la Kiebrania.
  • Neno "Yahweh" halitokei kamwe katika nakala halisi ya agano jipya; neno pekee la kiyahudi la "Bwana" ndo linalotumika, hata kwenye nukuu za agano la kale.

Gadi

Gadi ni moja ya wana wa Yakobo, ambaye ni, Israeli.

  • Familia ya Gadi ilikuwa moja ya makabila kumi na mbili ya Israeli.
  • Mwanamume mwingine katika Biblia aliye itwa Gadi alikuwa nabii aliye mkabili Daudi kwa dhambi yake ya kuchukuwa takwimu ya watu Waisraeli.
  • Miji, Baaligadi na Migdalidadi yote ni maneno mawili katika nakala halisi na wakati mwengine uandikwa, "Baali Gadi" na "Migdali Gadi."

nabii, unabii, kutoa unabii, muonaji, nabii wa kike

"nabii" ni mwanaume anaye ongea jumbe za Mungu kwa watu. Mwanamke anaye fanya haya anaitwa "nabii wa kike"

  • Mara nyingi manabii waliwaonya watu wa geuke toka dhambi zao na kumtii Mungu.
  • "unabii" ni ujumbe nabii anauzungumza. "Kutoa unabii" ni kuzungumza jumbe za Mungu.
  • Mara nyingi ujumbe wa unabii ulikuwa kuhusu jambo litakalo tokea mbeleni.
  • Unabii nyingi katika Agano la Kale zimeshatimia.
  • Katika Biblia mkusanyiko wa vitabu vilivyo andikwa na manabii wakati mwingine vinatajwa kama "manabii"
  • Kwa mfano, maneno, "sheria na manabii" ni namna ya kutaja maandiko yote ya Kiebrania, ambayo yanajulikana kama "Agano la Kale"
  • Jina la kale la nabii lilikuwa "muonaji" au "mtu anaye ona"
  • Wakati mwengine neno "muonaji" la husu nabii wa uongo au mtu anaye tumia uganga.

1 Chronicles 21:11

kupatwa na upanga wao

Haya maneno ni namna nyepesi ya kueleza kuuliwa na adui.

kupatwa na upanga wao

Haya maneno ni eleza mbinu ya Yahweh ya kuua kwa kifaa mwanajeshi angetumia kuua.

akiharibu

"akiua"

1 Chronicles 21:13

Nipo katika shida kubwa

"Nipo kwenye shida nyingi"

Acha nianguke katika mikono ya Yahweh kuliko kuangukia mikono ya mwanadamu, sababu matendo yake ya rehema ni makubwa mno

"Acha nije katika utawala wa Yahweh, kuiko chini ya utawala wa watu, kwa kuwa Yahweh ni wa rehema sana"

na watu elfu sabini wakafa

"na watu 70,000 wakafa"

kubadili nia yake

Kubadili uamuzi.

Rudisha mkono wako

Yahweh ana mwambia malaika wa uharibifu kuacha kuua watu.

malaika wa Yahweh alikua amesimama

Malaika wa Yahweh anaelezwa kama kitu kilicho simama kama mtu anavyo simama.

Orinani

Hili ni jina la mwanaume.

1 Chronicles 21:16

akiwa na upanga mkonono mwake

"tayari kushambulia"

Sio mimi niliye amuru jeshi kuhesabiwa?

"Mimi ndiye niliye amuru jeshi lihesabiwe"

Lakini hawa kondoo

Daudi anawaelezea watu wa Israeli kama aina ya wanyama watao muamini na kumfuata kiongozi.

wamefanya nini?

"Hawaja fanya kitu kinacho stahili adhabu"

1 Chronicles 21:18

Orinani

Ona jinsi ulivyo tafsiri hili jina 21:3

kama Gadi alivyo muelekeza cha kufanya kwa jina la Yahweh

"kama Gadi, akizungumza na mamlaka ya Yahweh, alivyo muambia Daudi afanye"

1 Chronicles 21:21

uso wake ukiwa kwenye ardhi

Haya maneno yaeleza kwamba Orinani aliinama mbele zaidi. Kuina mbele za mtu ni njia ya kuonyesha unyenyekevu na heshima. Kuinama zaidi ya onyesha unyenyekevu mkubwa na heshima.

gharama yote

"Nitalipa gharama yote hili eneo la kupeta lina gharimu"

1 Chronicles 21:23

Chukuwa kama lako

"Chukuwa kama zawadi"

linalo kupendeza

Ufahamu wa Daudi waelezwa kama macho yake. "linalo onekana zuri kwako"

vifaa vya kupeta

kifaa cha mbao na mawe au machuma yaliyo wekwa kwa chini, inatumika kugawa mbegu kutoka kwenye maganda kwa kuvuta juu unga ulioekwa chini.

1 Chronicles 21:25

shekeli mia sita ya dhahabu

"shekeli 600 ya dhahabu"

Akamuita Yahweh

"aliomba kwa Yahweh msaada"

malaika akarudisha upanga kwenye mfuko wake

malaika aliacha kuua watu"

mfuko

mfuniko wa upanga au kisu

1 Chronicles 21:28

Orinani

Ona jinsi ulivyo tafsiri jina lake 21:13

Mungu muelekeo

Mungu amwabie ni afanye"

anaogopa upanga wa malaika wa Yahweh.

"anaoga atauliwa na malaika wa Yahweh"

1 Chronicles 22

1 Chronicles 22:1

wachonga mawe,

Hawa ni watu wanao kusanya mawe makubwa na kuyakata katika kipimo sahihi ili wa jenzi waeze kutumia mawe kwenye kuta na majeng.

1 Chronicles 22:3

zaidi ya kipimo

"kuliko mtu yeyote awezavyo kupima"

nyumba itayo jengwa kwa Yahweh

"nyumva ya Yahweh" au "nyumba atakayo mjengea Yahweh"

1 Chronicles 22:6

kuitwa

"Daudi aliita"

kumuamuru ajenge ... dhamira yangu kujenga

"aliwaamuru wafanya kazi kujenga ... mpango wangu ulikuwa kuajiri wafanya kazi kujenga"

kwa ajili ya jina la Yahweh Mungu wangu

"kumheshimu Yahweh Mungu wangu"

umemwaga damu nyingi

"umeua watu wengi"

Hauta jenga nyumba kwa jina langu

"Hauta jenga hekalu kunitukuza mimi"

kwasababu umemwaga damu nyingi kwenye ardhi machoni pangu

"kwasbabu ninajua umeua watu wengi"

1 Chronicles 22:9

Maelezo ya Jumla

Daudi anaendelea kumuambia Sulemani kile Yahweh alicho mwambia.

kila upande

Hii ina maana ya kila sehemu kuzunguka Israeli.

katika siku zake

"wakati akitawala Israeli yote"

nyumba kwa jina langu, na nitakuwa baba yake

"hekalu la kunitukuza"

Ata kuwa mwana wangu

Mungu ata mtendea Sulemani kama alikuwa ni mwanae wa pekee.

Nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake juu ya Israeli

Hapa "kiti cha enzi" cha husu mamlaka ya kutawala kama mfalme. "Nitafanya uzao wake utawale juu ya Israeli milele"

1 Chronicles 22:11

Maelezo ya Jumla

Daudi anaendelea kuzungumza na Sulemani.

Sasa

Daudi anatumia hili neno kutambulisha kitu muhimu anacho kwenda kusema.

Uweze kujenga

"Uweze kufanikiwa kuelekeza jengo"

ata kapokuweka kiongozi juu ya Israeli

"atakapo kufanya mfalme juu ya Israeli"

1 Chronicles 22:14

Maelezo ya Jumla

Daudi anaendelea kusema na Sulemani.

Ona

Daudi anatumia hili neno kutambulisha kitu muhimu anacho kwenda kusema

talanta

talanta ni kipimo cha uzito. Kinauzito wa kilogramu 33

milioni moja

"1,000,000"

1 Chronicles 22:15

Maelezo ya jumla

Daudi anaendelea kusema na Sulemani.

wachonga mawe

Hawa ni wafanya kazi ambao wanakata mawe na kuandaa kwa ajili ya wajenzi wa kuta na majengo.

maseremala

Hawa ni watu wanao fanya kazi na mbao.

1 Chronicles 22:17

wenu ... nanyi

Yaeleza wingi 22:18-19

amewapa amani kila pande

"amewaopa amani kutoka vitani kila sehemu ya Israeli"

Amewakabidhi mikononi mwangu wenyeji wote mkoa

"Amenipa nguvu juu ya kila mtu anayeishi kwetu"

Mkoa umetiishwa mbele za Yahweh na watu wake

"Yahweh na watu wake wanatawala nchi"

Sasa

Hili neno la tambulisha kitu muhimu Daudi anachoenda kusema.

mtafuteni Yahweh Mungu wenu

"jaribu kumfanya Yahweh Mungu wenu kuwasikiliza"

kwa moyo wenu wote na nafsi

"kwa dhati" au "moyo wote"

Simameni na mjenge sehemu takatifu

"Simameni na muwaelekeze wafanya kazi wanapo jenga sehemu takatifu"

nyumba iliyo jengwa kwa ajili ya jina la Yahweh

"hekalu utakalo jenga kumheshimu Yahweh"

1 Chronicles 23

1 Chronicles 23:1

Maelezo ya Jumla

Daudi anamteua Sulemani kama mrithi wake na anapanga makuhani wa Kiwalawi na wafanya kazi wa huduma za hekaluni

Walawi walio kuwa miaka thelathini na zaidi walihesabiwa

"Baadhi ya wanaume wa Daudi waliwahesabu Walawi walikuwa na miaka 30 na zaidi"

Idadi ya elfu thelathini na nane

elfu nane "Walikuwa 38,000"

1 Chronicles 23:4

Kwa hawa, elfu ishirini na nne

elfu nne "Kwa hawa Walawi, 24,000"

elfu sita

"Walawi 6,000"

maaskari na waamuzi

Hawa Walawi walisikiliza mashtaka ya kisheria na kutoa haki kwa mujibu wa sheria ya Musa.

Elfu nne

"Walawi 4,000

walinzi wa lango

Hawa Walawi walilinda lango ili mtu najisi hasiingie"

kulingana

"kwa mujibu wa" au "kwa uzao wa"

Gerishoni, Kohathi, na Merari

Haya ni majina ya wana wa Walawi.

1 Chronicles 23:7

Maelezo ya Jumla

Haya ni majina ya Walawi kulingana na koo zao.

1 Chronicles 23:10

Maelezo ya Jumla

Hii yaendeleza orodha ya Walawi kwa mujibu wa koo zao.

hivyo walihesabiwa kama ukoo mmoja

"hivyo Daudi akawahesabu kama koo moja"

1 Chronicles 23:12

Maelezo ya Jumla

Hii yaendeleza orodha ya Walawi kwa mujibu wa koo zao.

Palikuwa na wanne wa wana wa Kohathi

"Kohathi alikuwa na wana 4"

Aruni alichaguliwa kuandaa vitu vitakatifu

"Yahweh alimchagua Aruni kuvitoa vitu vitakatifu"

kumpa baraka kwa jina lake

"kuwa bariki watu kama wa wakilishi wa Mungu milele"

wana wake walihesabiwa kuwa Walawi

"wana wake walikuwa sehemu ya ukoo wa Walawi" Wana wa Musa walikuwa Walawi.

1 Chronicles 23:15

Maelezo ya Jumla

Hii yaendeleza orodha ya Walawi kwa mujibu wa koo zao

1 Chronicles 23:19

Maelezo ya Jumla

Hii yaendeleza orodha ya Walawi kwa mujibu wa koo zao

1 Chronicles 23:21

Maelezo ya Jumla

Hii yaendeleza orodha ya Walawi kwa mujibu wa koo zao

1 Chronicles 23:24

Hawa walikuwa uzao wa Lawi kuligana na koo zao. Walikuwa viongozi, wamehesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, kuanzia koo

"Haya yalikuwa majina ya uzao wa Lawi na familia zao, ambao Daudi aliwahesabu na kuwaorodhesha. Walikuwa viongozi wa koo"

kutoka miaka ishirini na zaidi

"kutoka miaka 20 na zaidi"

na vifaa vyake vinavyo tumika kwenye utumishi wake

"na vifaa vyake walivyo tumia kwenye utumishi wake"

1 Chronicles 23:27

Kwa maneno ya Daudi ya mwisho Walawi walihesabiwa

"Amri ya Daudi ya mwisho ilikuwa wanaume wake wa wahesabu walawi"

miaka ishirini na kuendelea

"walio kuwa miaka 20 na kuendelea"

mkate wa uwepo

Ona jinsi ulivyo tafsiri 9:30

unga

unga mtu anaoupata kwa kusaga mbegu

sadaka ziliochanganywa na mafuta

"sadaka mtu alizozichanganywa na mafuta

1 Chronicles 23:30

Pia walisimama

"Walawi Pia walisimama"

na kila wakati sadaka ya kuteketezwa ilipo tolewa kwa Yahweh

"wakati makuhani walipo toa sadaka ya kuteketezwa kwa Yahweh"

sherehe za mwezi mpya

Hizi siku kuu ziliadhimisha mwanzo wa kila mwezi.

Idadi iliyo pangwa, iliyo tolewa kwa amri, ilipaswa kuwa mbele ya Yahweh

"Ilikuwa ni wajibu wa baadhi ya idadi ya watu wa Walawi kuwepo wakati wa kutoa sadaka kwa Yahweh"

1 Chronicles 24

1 Chronicles 24:1

Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari

Ona jinsi ulivyo tafsiri haya majina 6:1

Ahimeleki

Hili ni jina la mwanaume.

waliwagawanya katika makundi

"aliwagawanya wazao wa Eleazari na Ithamari kwenye makundi"

1 Chronicles 24:4

waligawanya

"Daudi, Zadoki, na Ahimeleki waligawanya"

makundi kumi na sita

"makundi 16"

Magawanyo haya yalikuwa nane kwa idadi

"Walikuwa na magawanyo 8 kulingana na koo za uzao wa Ithamari"

1 Chronicles 24:6

Shemaia

Hili ni jina la mwanamume.

Nethaneli

Ona jinsi ulivyo tafsiri 15:22

Ahimeleki

Ona jinsi ulivyo tafsiri 18:14

Ukoo mmoja ulichaguliwa kwa kura kutoka uzao wa Eleazari, na kisha uliofata utachaguliwa kutoka uzao wa Ithhamari

"Walimchagua mmoja kwa kura kutoka uzao wa Eleazari, kisha watachagua kwa kura kutoka uzao wa Ithamari"

1 Chronicles 24:7

Maelezo ya Jumla

Hii ni utaratibu wa huduma ambao Daudi, Zadoki, na Ahimeleki walichagua kwa orodha kwa uzao wa Eleazari na Ithamari.

1 Chronicles 24:11

Maelezo ya Jumla

Hii ni utaratibu wa huduma ambao Daudi, Zadoki, na Ahimeleki walichagua kwa orodha kwa uzao wa Eleazari na Ithamari.

1 Chronicles 24:15

Maelezo ya Jumla

Hii ya hitimisha utaratibu wa huduma ambao Daudi, Zadoki, na Ahimeleki alichagua kwa kura kwa uzao wa Eleazari na Ithamari.

1 Chronicles 24:19

wakifuata utaratibu waliopewa na Aruni babu yao

"wakifuata sheria ambazo Aruni babu yao aliwapa"

1 Chronicles 24:20

Maelezo ya Jumla

Hii inaanza orodha ya majina ya wana wengine wa Lawi. orodha itaisha 24:29

Amramu

Ona jinsi ulivyo tafsiri 6:1

Shebueli

Ona jinsi ulivyo tafsiri 2315

1 Chronicles 24:23

Hebroni ... Yeria ... Amaria ... Yahazieli ... Yekameamu

Ona jinsi ulivyo tafsiri 23:19

Uzieli ... Mika ... Ishia

Ona jinsi ulivyo tafsiri 23:19

Shamiri ... Zakaria

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 24:26

Merari ... Mahli ... Mushi ... Eleazari

Ona jinsi ulivyo tafsiri 23:21

Yaazia, Beno, Shohamu, Zakuri ... Ibrri

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 24:29

Kishi ... Mushi

Ona jinsi ulivyo tafsiri 23:21

Yerameli .. Mahli ... Ederi ... Yerimothi

Haya ni majina ya wanaume.

Ahimeleki

Ona jinsi ulivyo tafsiri 18:14

1 Chronicles 25

1 Chronicles 25:1

Upatu

Ona jinsi ulivyo tafsiri 13:7

Hemani ... Yeduthuni

Ona jinsi ulivyo tafsiri 16:40

Zakuri ... Matithia

Haya ni majina ya wanaume.

sita kwa jumla

"6 kwa jumla"

1 Chronicles 25:4

Maelezo ya Jumla

Hii inaendeleza orodha ya viongozi wa kazi ya hema la kukutania imeanza 25:1

Bukia ... Mahaziothi

Haya ni majina ya wanaume.

Hemani

Ona jinsi ulivyo tafsiri 16:40

wana kumi na nne na mabinti watatu

"wana 14 na mabinti 3"

1 Chronicles 25:6

upatu

Ona jinsi ulivyo tafsiri 13:7

Yeduthuni ... Hemani

Ona jinsi ulivyo tafsiri 16:40

idadi ya 288

"walikuwa wanaume mia mbili na themanini na nane"

sawa kwa vijana na kwa wazee, kwa walimua na kwa wanafunzi

Hii yaeleza mkazo "wote hao"

1 Chronicles 25:9

Maelezo ya Jumla

Hii yaanza orodha ya kura 24 zilizo tupwa kuchagua utaratibu za familia gani zitakazo hudumu. Hii orodha yaisha 25:29

ya kwanza ... ya pili

Hii yaonyesha utaratibu wa familia zilizo chaguliwa. "namba 1 ...namba 2 ... namba 3 ... namba 4 ... namba 5" au tumia " wa awali" kwa "wa kwanza" na "akifuatiwa" kwa wote wano fuata.

kura ya kwanza iliangukia katika familia ya Yusufu

Kwa watu wote kwenye orodha, nakala ya eleza kwamba palikuwa "watu kumi na mbili kwa idadi" Kwa maana hii imegusiwa, unaweza ongeza hii sentensi kwa ajili ya Yusufu, kama UDB inavyo fanya. "kura ya kwanza ilimwangukia familia ya Yusufu, watu kumi na mbili kwa idadi"

Yusufu ... Zakuri ... Nethania

Ona jinsi ulivyo tafsiri haya majina 25:1

Gedalia

Ona jinsi ulivyo tafsiri haya majina 25:1

watu kumi na mbili

"watu 12"

Izri

Hili jina limeandikwa Zeri 25:1

1 Chronicles 25:13

Maelezo ya Jumla

Hii ya endeleza orodha iliyo anzishwa 25:9

ya sita ... ya tisa

Hii ya onyesha utaratibu jinsi familia zilivyo chaguliwa. "namba 6" ... namba 7 ... namba 8 ... namba 9"

Bukia

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

watu kumina mbili

"watu 12"

Yesharela

Aina nyingine ya kuandika "Ashareka" 25:1

Yeshaia

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:1

Matania

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

1 Chronicles 25:17

Maelezo ya Jumla

Hii yaendeleza orodha iliyo anzwa 25:9

ya kumi ... ya kumi na tatu

Hii ya onyesha orodha jinsi familia zilivyo chagulliwa. "namba 10 ... namba 11 ... namba 13"

Shimei

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:1

watu kumi na mbili

"watu 12"

Azareli

Hii ni aina nyingine ya kuandika "Uzieli" 25:4

Hashabia

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:1

Shubaeli

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

1 Chronicles 25:21

Maelezo ya Jumla

Hii yaendeleza orodha iliyo anzwa 25:9

ya kumi na nne ... kumi na saba

Hii yaonyesha utaratibu familia zilivyo chaguliwa. "namba 14 ... namba 15 ... namba 16 ... namba 17"

Matithia

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:1

watu kumi na mbili

"watu 12"

Yeremothi

Hii ni aina nyingine ya kuandika "Uzieli" 25:4

Hanania

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

Yoshibekasha

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

1 Chronicles 25:25

Maelezo ya Jumla

Hii yaendeleza orodha iliyo anza 25:9

ya kumi na nane ... ishirini na moja

kwanza Hii yaonyesha utaratibu wa familia zilizo chaguliwa. "namba 18 ... namba 19 ... namba 20 ... namba 21"

Hanani

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

watu kumi na mbili

"watu 12"

Malothi

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

Eliatha

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

Hothiri

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

1 Chronicles 25:29

Maelezi ya Jumla

Hii ya hitimisha orodha illiyo anza 25:9

ya ishirini na mbili ... ya ishirini na nne

ya pili ... ishiri na nne Hii yaonyesha utaratibu wa jinsi familia zilivyo chaguliwa. "namba 22 ... namba 23 ... namba 24"

Gidalti

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

watu kumi na mbili

"watu 12"

Mahaziothi

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

Romamti Eza

Ona jinsi ulivyo tafsiri 25:4

1 Chronicles 26

1 Chronicles 26:1

Maelezo ya Jumla

Hii yaanza orodha ya walinzi wa lango

Wakora

Ona jinsi ulivyo tafsiri 9:17

Meshelemia

Ona jinsi ulivyo tafsiri 9:20

Kore

Ona jinsi ulivyo tafsiri 9:17

Asafu

Hili ni jina mbadala la "Ebiasafu" 9:17

Zekaria

Ona jinsi ulivyo tafsiri 9:20

Yediali ... Zebadia ... Yathnieli ... Elamu ... Yehonani ... Eliehoenai

Haya ni majina ya wanaume

wa pili ... watatu ... ya nne ... wa saba

Hii yaonyesha utaratibu ya wana kuzaliwa. "namba 2 ... namba 3 ... namba 4 ... namba 7" au "afuatae" kwa kila mmoja.

1 Chronicles 26:4

Maelezo ya Jumla

Hii yaendeleza orodha ya walinzi wa lango iliyoanza

Obedi Edomu

Ona jinsi ulivyo tafsiri 9:37

Shemaia ... Yehozabadi ... Yoa ... Sakari ... Nethanieli ... Amieli ... Isakari ... Peulethai

Haya ni majina ya wanaume.

wapili ... wanane

Hii yaonyesha utaratibu jinsi wana walivyo zaliwa. "namba 2 ... namba 3 ... namba 4 ... namba 5 ... namba 6 ... namba 7 ... namba 8 au "afuatae" kwa kila moja.

1 Chronicles 26:7

Maelezo ya Jumla

Hii yaendeleza orodha ya walinzi wa lango iliyo anza

Shemaia ... Obedi Edomu

Ona jinsi ulivyo tafsiri 26:4

ndugu zake

" ndugu wa Shemaia" au "ndugu wa familia ya Shemaia"

Othini, Refaeli, Obedi ... Elizabadi ... Elihu ... Semakia ...

Haya ni majina ya Wanaume.

sitini na mbili

wawili "wanaume 62"

jumla ya kumi na nane

"jumla 18"

1 Chronicles 26:10

Maelezo ya Jumla

Hii inaendeleza orodha ya walinzi wa lango iliyo anza

Hosa ... Merari ... Shimiri ... Hilika ... Tebalia ... Zekaria

Haya ni majina ya wanaume.

wa pili ... watatu ... wanne

Hii yaonyesha utaratibu wana walivyo zaliwa. "namba 2 ... namba 3 ... namba 4" au "anaefuata" kwa kila moja.

Wote wa wana wa Hosa na ndugu walikuwa kumi na tatu kwa idadi

"Hawa walikuwa wana 13 wa Hosa na ndugu zake"

1 Chronicles 26:12

wadogo kwa wakubwa

"kila mtu" au "wanaume wa miaka yote"

Shelemeia

Hii ni aina nyingine kuandika "Meshelemia" 26:1

Zekaria

Ona jinsi ulivyo tafsiri 26:1

Kura ilipo rushwa

"Walipo rusha kura"

mshauri makini

Huyu ni mtu anaye onyesha hukumu nzuri katika kufanya maamuzi.

1 Chronicles 26:15

Obedi Edomu kulipangiwa lango la kusini, na wanae walipangiwa nyumba za ghala

"Obedi Edomu ilikuwa na wajibu wakulinda lango la kusini, na wana wake walilinda nyumba za ghala"

Obedi Edomu

Ona jinsi ulivyo tafsiri 26:4

Shupimu

Hili ni jina la mwanamume

Hosa

Ona jinsi ulivyo tafsiri 26:10

Shalekethi

Hilil ni jina la lango.

Lindo lilikabiidhiwa kwa kila familia.

"Kila familia ilikuwa na wajibu wakulinda kitu"

1 Chronicles 26:17

Walawi sita

"Walawi 6"

wanne walipangwa

"wanaume 4 kila siku"

wawili

"wanaume wa 2" au "wanaume 2 kwa zamu"

Katika ua kuelekea magharibi wanne walipangwa

"wanaume wa 4 walilinda ua la magharibi"

wanne barabarani, na wawili katika ua

Wanaume wa 4 walilinda barabara, na wanaume wawili walilinda ua"

Palijazwa na

"Walikuwa"

Merari

Ona jinsi ulivyo tasfiri 26:10

1 Chronicles 26:20

Wazao wa Ladani, walitoka kwa Gerishoni kupitia kwake na walio kuwa viongozi wa familia za Ladani Mgerishoni, walikuwa Yehieli na wanae

"Yehieli na wanae walikuwa uzao wa Ladani, aliye toka Gerishoni ulio wa Ladani. Yehieli na wana wake walikuwa viongozi wa familia ya Ladani Mgerishoni. Wana wa Yehieli"

Ladani ... Gerishoni

Ona jinsi ulivyo tafsiri haya majina 23:7

Mgerishoni

Wazao wa Gerishoni.

Yehieli ... Zethamu ... Yoeli

Ona jinsi jinsi ulivyo tafsiri haya majina katika 23:7.

aliyesimamia

"aliye kuwa msimamizi"

1 Chronicles 26:23

Kulikuwa na askari walio chukuliwa kwa koo

"Viongozi walichagua askari kutoka koo"

Amramu, Izhari, Hebroni, Uzieli

Ona jinsi ulivyo tafsiri haya majina 23:12

Shebueli ... Gerishomu ... Eliezeri ... Rehabia

Ona jinsi ulivyo tafsiri haya majina 23:15

Yeshaia ... Yoramu ... Zikiri Shelomothi

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 26:26

maelfu na mamia

"zaidi ya wanaume 1,000 na zaidi ya wanaume 100"

vitu walivyo vichukuwa

vitu jeshi linavyo chukuwa baada ya ushindi

Kishi ... Neri ... Zeruia

Haya ni majina ya wanaume

Kila kitu kilicho tengwa

"vitu vyote viongozi walivyo vitenga"

1 Chronicles 26:29

Izhari ... Hebroni

Ona jinsi ulivyo tafsiri haya majina 23:12

mambo ya ndani ya Israeli

Hii ya husu shughuli za watu wa Israeli, haya uhusiano na jeshi wala hekalu. "shughuli za watu wa Israeli"

Kenania ... Hashabia

Haya ni majina ya wanaume.

wanaume wenye uwezo 1,700

"wanaume elfu moja na mia saba wenye uwezo"

kazi ya Yahweh na kazi ya mfalme

"kazi iliyo fanywa ya Yahweh na mfalme"

1 Chronicles 26:31

Hebroni

Ona jinsi ulivyo tafsiri 23:12

Yerija

Namna nyingine ya kuandika "Yeria." Ona jinsi ulivyo tafsiri 23:19

walihesabiwa kutoka orodha

"majina yao yalikuwa kwenye orodha"

Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi

"Daudi alipo kuwa mfalme kwa miaka 40"

Yazeri

Hili ni jina la mwanaume.

ndugu 2,700

"elfu mbili na mia saba ndugu"

1 Chronicles 27

1 Chronicles 27:1

Hii ni orodha

"Haya ni majina"

namna tofauti

"namna za tofauti" au "njia nyingi"

Kila kikosi cha jeshi

"Kila kundi"

wanaume elfu ishirini na nne

wanaume elfu nne "wanaume 24,000"

mwaka mzima

"mwaka wote"

mwezi wa kwanza

Huu ni mwezi wa kwanza wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Machi na mwanzo wa Aprili kwa kalenda za Kimagharibi.

Yashobeamu mwana wa Zabdieli

Haya ni majina ya wanaume.

mhusika

"kiongozi"

1 Chronicles 27:4

mwezi wa pili

Huu ni mwezi wa pili wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Aprili na mwanzo wa Mei kwa kalenda za Kimagharibi.

Dodai ... Amizabadi

Haya ni majina ya wanaume.

kikosi chake

"katika kundi lake la jeshi" au kundi la wanajeshi wake"

wanaume elfu ishirini na nne

wanaume elfu nne "wanaume 24,000"

mwezi wa tatu

Huu ni mwezi wa tatu wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Mei na mwanzo wa Juni kwa kalenda za Kimagharibi.

wale thelathini

Ona jinsi ulivyo tafsiri 11:10

1 Chronicles 27:7

Mkuu kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli kaka wa Yoabu

"Asaheli, kaka wa Yoabu, alikuwa mkuu wa mwezi wa nne"

mwezi wa nne

Huu ni mwezi wa nne wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Juni na mwanzo wa Julai kwa kalenda za Kimagharibi.

Asaheli ... Ikeshi

Haya ni majina ya wanaume.

kikosi chake

"kundi lake la jeshi"

wanaume elfu ishirini na nne

wanaume elfu nne "wanaume 24,000"

mwezi wa tano

Huu ni mwezi wa tano wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Julai na mwanzo wa Agusti kwa kalenda za Kimagharibi.

mwezi wa sita

Huu ni mwezi wa sita wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Agusti na mwanzo wa Septemba kwa kalenda za Kimagharibi.

Tekoa

Hili ni jina la sehemu.

1 Chronicles 27:10

Mkuu kwa mwezi wa saba alikuwa Helezi Mpeloni, kutoka watu wa Efraimu

"Helezi, Mpeloni, kutoka watu wa Efraimu, alikuwa mkuu wa mwezi wa saba"

mwezi wa saba

Huu ni mwezi wa saba wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Septemba na mwanzo wa Oktoba kwa kalenda za Kimagharibi.

Helezi ... Sibekai ... Zera ... Abi Ezeri

Haya ni majina ya wanaume.

Mpeloni ... Mhushathi ... Manathothi

Haya ni majinaya makabila au koo.

wanaume elfu ishirini na nne

wanaume ekfu nne "wanaume 24,000"

mwezi wa nane

Huu ni mwezi wa nane wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Oktoba na mwanzo wa Novemba kwa kalenda za Kimagharibi.

mwezi wa tisa

Huu ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Novemba na mwanzo wa Desemba kwa kalenda za Kimagharibi.

1 Chronicles 27:13

Maharai ... Zera ... Heldai ... Othnieli

Haya ni majina ya wanaume.

mwezi wa kumi

Huu ni mwezi wa kumi wa kalenda ya Kiebrania.

Netofa ... Pirathoni

Haya ni majina ya sehemu. Ni wakati wa mwisho wa mwezi Desemba na mwanzo wa mwezi Januari katika kalenda za Magharibi.

wanaume elfu ishirini na nne

wanaume elfu nne "wanaume24,000"

mwezi wa kumi na moja

Huu ni mwezi wa kumi na moja wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Januari na mwanzo wa Februari kwa kalenda za Kimagharibi.

mwezi wa kumi na mbili

Huu ni mwezi wa kumi na mbili wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Februari na mwanzo wa Machi kwa kalenda za Kimagharibi.

1 Chronicles 27:16

Eliezeri ... Mikaeli

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 27:19

Ishmaia ... Yerohamu

Haya ni majina ya wanaume.

1 Chronicles 27:23

wenye umri wa miaka ishirini au chini zaidi

"watu wenye miaka 20 au chini"

kuongeza Israeli

"kuongeza idadi ya Israeli"

kama nyota za mbinguni

Namba ya watu wa Israeli inalinganishwa na namba ya nyota kuonyesha zilivyo nyingi.

Gadhabu iliangukia Israeli

"Mungu aliwaadhibu watu wa Israeli"

Hii idadi haikuandikwa

"Hakuna aliye andika hii namba chini"

1 Chronicles 27:25

Azimavethi ... Zabdi

Haya ni majina ya wanaume.

mhusika wa

"wajibika kulinda"

minara iliyo imarishwa

"nguzo imara"

walio lima ardhi

Hii ina maana ya kuchimba au kutufua udogo kabla ya kupanda

Shefamu

Hili ni jina la sehemu.

1 Chronicles 27:28

mikuyu

Huu ni aina ya mti

Baali Hanani ... Shitrai ... Adlai

Haya ni majina ya wanaume.

Gederi .. Shafati

Haya ni majina ya sehemu

iliyo kuwa inalishwa

"walio kula nyasi shambani"

1 Chronicles 27:30

Obili ... Yedeia ... Yazizi

Haya ni majina ya wanaume

Mishimaeli ... Mhagri

Haya ni majina ya makabila au koo.

Meronothi

Hili ni jina la sehemu.

Hawa wote

"Hawa wanaume"

1 Chronicles 27:32

Yonathani ... Yehoiada

Haya ni majina ya wanaume.

Waariki

Hili ni jina la kabila la ukoo.

1 Chronicles 28

1 Chronicles 28:1

maafisa

Ona jinsi ulivyotafsiri hii 24:4

kazi walizo pangiwa

Kazi inayohitaji kurudiwa, kwa mfano kila siku au kila mwezi.

wa maelfu na mamia

"1,000s na wa 100s"

mali

Hili neno moja linamaana ya vitu na ardhi mfalme alivyomiliki.

1 Chronicles 28:2

akainuka kwa miguu yake

"alisimama juu"

kaka yangu na watu wangu

Mistari hii miwili inashiriki maana moja na kuweka mkazo kuwa Daudi na watu wa Israeli ni ndugu.

sanduku la agano la Yahweh;stuli ya miguu kwa ajili ya Mungu wetu

Mstari wa pili unaelezea mstari wa kwanza. Yahweh mara nyingi inaelezea "sanduku la agano" kama "stuli yake ya miguu."

hekalu kwa jina langu

"hekalu kwa ajili yangu"

mwanaume wa vita na umemwaga damu

Maelezo yote yanahamasisha kitu kimoja , kwamba Daudi aliuwa watu.

umemwaga damu

"aliuwa watu"

1 Chronicles 28:4

Taarifa za jumla:

Daudi anaendelea kuongea na Waisraeli.

mfalme wa Israeli milele

Maana zinazowezekana ni 1) Daudi na uzao wake utatawala milele au 2)Daudi ataendelea kuwa mfalme wa Israeli baada ya kufufuka kutoka wafu.

Israeli yote

"ardhi yote ya Israeli'' au "Waisraeli wote"

kuketi katika kiti cha enzi

"kutawala" au "kuwa mfalme wa"

ufalme wa Yahweh, juu ya Israeli

"Israeli ambayo ni ufalme wa Yahweh"

1 Chronicles 28:6

Taarifa za jumla:

Daudi anaendelea kuongea na Waisraeli.

Aliniambia

"Mungu aliniambia"

nyumba yangu

Neno "nyumba" linamaana ya hekalu la Yahweh.

Nimemchagua yeye kuwa mwana wangu, nami nitakuwa baba yake

Hii haimaanishi kwamba Solomoni amekuwa kabisa mwana wa Mungu, ila inaeleza mahusiano binafsi kati yake na Mungu watakayo kuwanayo. "Nimemchagua yeye kumtendea kama mwanangu, na nitakuwa kama baba kwake"

amri zangu na sheria

Haya maneno mawili kwa ujumla yana maana moja inayoelezea kila kitu ambacho Yahweh alikiamuru.

kama ulivyo siku ya leo

Neno "ulivyo" hapa linamuelezea Daudi. "kama ulivyokabidhiwa hii siku"

1 Chronicles 28:8

Taarifa za jumla:

Daudi anaendelea kuongea na Waisraeli.

Kisha sasa

Hii ina ashiria kwamba Daudi ameanza awamu mpya katika hotuba yake.

mshike na kufanya

Maneno haya "kufanya" yanamaanisha kitu kimoja na "mshike" Kwapamoja maneno yanahamasisha umuhimu wa kufanya kile Mungu alicho amuru.

watoto wenu baada yenu

" watoto wenu ambao watachukua nafasi zenu baada ya kufa"

1 Chronicles 28:9

Mungu wa baba yako

Daudi anajiita "baba yako" kwasababu hiii ni tafrija maalumu. "Mungu wangu"

moyo wako wote

"kabisa"

anachunguza mioyo yote na kufahamu amasa ya kila wazo la mtu

Hii mistari miwili ina maana moja na kuweka mkazo kwamba Yahweh anajua mawazo na nia za kila mtu.

Ukimtafuta, ataonekana kwako

"ukijaribu kumpata Yahweh akusikilize wewe, atafanya hivyo"

Elewa

"Ona sasa" "Kumbuka" aua "Kuwa na tahadhari"

Kuwa imara na ufanye

Neno "imara" hapa la husu nguvu ya nia na uweza wa tabia.

1 Chronicles 28:11

baraza la hekalu

"baraza ya hekalu" au "mwingilio wa hekalu" hii ina eleza nguzo zilizo saidia dari katika mwingilio wa hekalu.

hazina

vyumba vya hifadhi vya vitu vya thamani

1 Chronicles 28:13

masharti

Haya yalikuwa maagizo maalumu kuhusu jinsi makuhani na Walawi wafanye kazi katika hekalu.

viitengo

Hii ya husu makundi ambayo makuhani na wafanya kazi wengine wa hekalu walikuwa wamepangwa kufanya kazi zao. Ona jinsi ulivyo tafsiri hili neno 24:1

1 Chronicles 28:18

dhahabu ya kutakasika

"dhahabu iliyo safishwa" au "dhahabu yenye thamani"

Nimeeka haya katika maandishi

"Nimeandika yote haya chini"

kunipa kuelewa

"alinisaidia kuelewa maelekezo"

1 Chronicles 28:20

hodari na mjasiri

Haya maneno mawili yanamanisha kitu kimoja na kukazia kuwa Sulemani lazima awe shujaa.

Usiogope au kuwa na wasiwasi

Haya maneno mawili yanamanisha kitu kimoja na kukazia kuwa Sulemani lazima asikate tamaa. "Kuwa hodari" au "Kuwa Mjasiri"

yupo nawe

"nitakusaidia wewe"

Hatakuacha wala kukutelekeza

Haya maneno mawili yanamanisha kitu kimoja na kukazia kuwa Yahweh ata kuwa daima na Sulemani. "Ata kuwa nawe daima"

hivi ni vitengo vya makuhani na Walawi

Ona jinsi ulivyo tafsiri 28:13

1 Chronicles 29

1 Chronicles 29:1

mawe ya shohamu

Haya ni mawe yenye mistari meupe na meusi yanayo tengenezewa mikufu.

kupangwa

Hii ina maana ya mifumo mizuri ya urembo iliyo undwa na mawe.

1 Chronicles 29:3

Maelezo ya Jumla

Daudi anaendelea kuongea na watu kuhusu vitu anavyo toa kwa ajili ya hekalu.

talanta elfu tatu

"talanta 3,000"

dhahabu kutoka Ofiri

dhahabu bora na ya gharama

1 Chronicles 29:8

hazina

Hii ni sehemu ambayo pesa na vitu vya thamani vimeekwa.

Yehieli

Hili ni jina la mwanaume.

Gerishoni

Huyu alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Lawi.

moyo wao wote

kwa utayari, na bila shaka au wasi wasi

1 Chronicles 29:10

Na uabudiwe, Yahweh, Mungu wa Israeli babu wetu, milele na milele

"Na usifiwe, Yahweh baba yetu, Mungu wa Israeli, milele na milele"

1 Chronicles 29:12

Maelezo ya Jumla

Daudi anaendeleza maombi yake sifa kwa Yahweh

Mkononi mwako kuna nguvu na uwezo

Maneno "nguvu na "uwezo" yana maana moja na yanasisitiza ukuu wa nguvu za Yahweh.

1 Chronicles 29:14

Maelezo ya Jumla

Daudi anaendeleza maombi yake sifa kwa Yahweh

Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, tustahili kutoa kwa hiari hivi vitu?

Daudi anamaanisha yeye na watu wake hawastahili sifa kwa kumpa chochote Yahweh.

sisi ni wageni na wasafiri mbele zako

"Unajua sisi si wa muhimu"

Siku zetu katika dunia ni kama kivuli

Vivuli vinatokeza na kutoeka haraka.

1 Chronicles 29:16

kwa unyofu wa moyo wangu

"kwasababu ninataka kuwa mkweli na mwaminifu kwa kila kitu ninachofanya"

1 Chronicles 29:18

hifadhi hili katika fikra za watu wako

"eka hili kwenye mawazo na fikra za watu wako milele"

1 Chronicles 29:20

kusujudu mbele

kulala chini na kutaza ardhi kama njia ya kuonyesha heshima ya hali ya juu

1 Chronicles 29:22

mbele za Yahweh

Hili kumtukuza Yahweh.

mara ya pili

Mara ya kwanza imeelezwa 23:1

kumpaka mafuta ya mamlaka ya Yahweh kuwa mfalme

"alipakwa mafuta kutawala juu ya Israeli kwa niaba ya Yahweh"

1 Chronicles 29:24

utii

"uaminifu wao"

Yahweh alimheshimu sana Sulemani na kumkirimia nguvu kubwa

Hii mistari miwili inasisitiza kuwa Sulemani alipokea upendeleo maalumu kutoka kwa Yahweh, uliyo mfanya mfalme mkubwa na mwenye nguvu wa Israeli.

1 Chronicles 29:26

Daudi

Daudi alikuwa mfalme wa kwanza na alimpenda Mungu na kumtumikia.

  • Daudi alipo kuwa bado kijnana modogo na akichunga kondoo wa baba yake, Mungu alimchagua kuwa mfalme wa Israeli.
  • Daudi alikuwa mpiganaji mkubwa na akaongoza jeshi la Israeli katika mapambano dhidi ya maadui zao. Ushindi wake wa Goliathi Mfilisti wajulikana sana.
  • Mfalme Sauli alijaribu kumuua Daudi, lakini Mungu alimlinda, na kumfanya mfalme baada ya kifo cha Sauli
  • Daudi alitenda dhambi mbaya, lakini alitubu na Mungu akamsamehe.
  • Yesu, Mesia, anaitwa "Mwana wa Daudi" kwasababu ni mzao wa mfalme Daudi.

Yese

Yese alikuwa baba wa Mfalme Daudi, na mjukuu wa Ruthi na Boazi.

  • Yese alitokea kabila la Yuda.
  • Alikuwa "Mefrathi", yenye kumaanisha alikuwa ametoka mji wa Efratha (Bethlehemu)
  • Nabii Isaya alitabiri kuhusu "chimbuko" au "tawai" litakalo toka "shina la Yese" na kuzaa matunda. Hii yamuelezea Yesu aliye kuwa mzao wa Yese.

tawala

Neno "tawala" la maanisha kumiliki kama mfalme juu ya watu wa eneo la nchi au ufalme. Utawala wa mfalme ni kipindi chake cha kwenye madaraka.

  • Neno "kutawala" alatumika kueleza Mungu anavyo tawala kama mfalme juu ya dunia yote.
  • Mungu aliruhusu wafalme watawale juu ya Israeli walipo mkataa kama mfalme.
  • Yesu Kristo atakapo rudi, atatawala wazi kama mfalme juu ya dunia yote na Wakristo watatawala naye.
  • Hili neno laweza pia tafsiriwa kama "madaraka kabisa" au "miliki kama mfalme" au "ongaza kama mfalme"

Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli

Neno "Israeli" ni jina Mungu alilo mpa Yakobo. La maanisha, "anaangaika na Mungu"

  • Wazao wa Yakobo walijulikana kama "watu wa Israeli," "taifa la Israeli", au "Waisraeli."
  • Mungu aliunda agano lake na watu wa Israeli. Walikuwa watu wake aliyo wachagua.
  • Taifa la Israeli liliundwa na makabila kumi na mbili.
  • Baada ya Mfalme Sulemani kufa, Israeli iligawanyika katika falme mbili: ufalme wa kusini , uliitwa "Yuda" na ufalme wa kaskazini, uliitwa "Israeli"
  • Mara nyingi neno "Israeli" laweza tafsiriwa kama, "watu wa Israeli" au "taifa la Israeli," kulingana na muktadha.

mtawala, watawala, tawala

Neno "mtawala" ni jina linalo eleza mtu mwenye mamlaka juu ya watu wengine, kama kiongozi wa nchi, ufalme, au kundi la dini.

  • Katika Agano la kale, mfalme alikuwa anajulikana kwa kujatwa "mtawal," kama katika mstari huu, "alimteua mtawala juu ya Israeli"
  • Mungu anaelezwa kama mtawala mkuu, anaye tawala watala wengine wote.
  • Katika Agano Jipya, kiongozi wa sinagogi aliitwa "mtawala."
  • Aina nyingine ya mtawala alikuwa ni "gavana."
  • Kulingana na muktadha, "mtawala" la weza tafsiriwa kama "kiongozi" au mtu mwenye mamlaka juu ya"
  • Tendo la "kutawala" la maanisha kuongoza "kuwa na mamlaka juu ya." Lina maana moja kama "kumiliki" linapo mtaja mfalme.

Hebroni

Ulikuwa mji eneo la juu, lenye vimilima vya miamba maili ishirini kusini mwa Yerusalemu.

  • Mji ulijengwa katika ya mwaka 2,000 B.C. kipindi cha Abramu. Ulitajwa mara nyingi katika historia ya mambo ya Agano la Kale.
  • Hebroni ilikuwa na nafasi muhimu katika utawala wa mfalme Daudi. Baadhi ya wana wake, pamoja na Absalome, walizaliwa hapo.
  • Umji ulibomolewa kati ya mwaka 70 A.D. na Warumi.

Yerusalemu

Yerusalemu ulikuwa asili mji wa Wakanani zamani badae ukawa mji muhimu wa Israeli. Upo kilomita 34 magharibi mwa Bahari ya Chumvi na kaskazini mwa Bethlehemu. Bado ni mji mkuu wa Israeli.

  • Jina, "Yerusalemu" limetajwa kwanza katika kitabu cha Yoshua. Majina mengine ya Agano la Kale ni "Salemu," "mji wa Yebusi," na "Sayuni." Yote "Yerusalemu" na "Salemu" una shina moja la "amani"
  • Yerusalemu ulikuwa ngome ya Wayebusi uliyo itwa "Sayuni" ambayo mfalme Daudi aliuteka na kuufanya mji wake mkuu.
  • Mwana wa Daudi Sulemani alijenga hekalu la kwanza Yerusalemu, Mlima Moria, ambao ulikuwa mlima Ibrahimu alimtoa mtoto wake Isaka kwa Mungu. Hekalu lilijengwa tena pale lilipo haribiwa na Wababilonia.
  • Kwasababu hekalu lilikuwa Yerusalemu, sherehe kubwa za Wayahudi zilisherehekewa hapo.
  • Watu kawaida walitaja kwenda "juu" Yerusalemu maana ulikuwa juu ya milima.

kifo, kufa, kafa

Haya maneno yanatumika kutaja mauti ya kimwili na kiroho. Kimwili, inaeleza jinsi mwili wa nyama wa mtu unaacha kuishi. Kiroho, inaeleza wenye dhambi wanapo tengwa na Mungu kwasababu ya dhambi.

chema, wema

Neno "wema" lina maana tofauti kulingana na muktadha. Lugha nyingi zitatumia maneno tofauti kutafsiri hizi maana tofauti.

  • Kwa ujumla, kitu ni chema kama kinalingana na tabia ya Mungu, kusudi, na mapenzi.
  • Kitu ambacho ni "chema" cha weza pendeza, bora, saidia, kufaa, faidisha, au kubalika kimaadili.
  • Ardhi iliyo "njema" yaweza itwa "rotubisha" au "inayozalisha."
  • Zao "jema" la weza kuwa zao "tele"
  • Mtu anaweza kuwa "mwema" kwa kile anachofanya kama wana ujuzi kwa kazi yao au ajira, kama, "mkulima mwema."
  • Katika Biblia, maana ya jumla ya "jema" mara nyingi utofautishwa na "uovu"
  • Neno "wema" mara kwa mara la husu kuwa na maadili mema au wenye haki katika mawazo na matendo.
  • Wema wa Mungu wa husu jinsi anavyo bariki watu kwa kuwapa vitu vyema na vya faida. Yaweza pia kumaanisha ukamilifu wake wa adili.

umri

Neno "umri" la husu idadi ya miaka mtu ameishi. Pia ya tumika kumaanisha kipindi cha muda.

  • Maneno mengine yanayo tumika kueleza kipindi kirefu cha muda ni pamoja na, "nyakati" na "majira"
  • Yesu anataja "huu wakati" kama muda uliyopo ambao uovu, dhambi, na uasi vitajaza dunia.
  • Kutakuwa na muda mbeleni wakati haki itatawala juu ya mbingu mpya na nchi mpya.

maisha, ishi, kuishi, hai

Haya maneno yote yanaeleza kuwa hai kimwili, sio kufa. Yanatumika pia kimafumbo kumaanisha kuwa hai kiroho.

heshima, kuheshimu

Maneno "heshima" na kuheshimu yana maana ya kumpa mtu adhama, kukweza, au muabudu

  • Heshima upewa mtu aliye na cheo na muhimu, kama mfalme au Mungu.
  • Mungu pia anawaelekeza Wakristo kuheshimu wengine, lakini wasijaribu kutafuta heshima yao.
  • Watoto wanaelekezwa kuheshimu wazazi wao, inayo jumuisha adhama na utiifu.
  • maneno "heshimu" na "utukufu" yana tumika pamoja mara nyingi, sana yanapo muongelea Yesu. Haya yanaweza kuwa namna moja ya kuzungumzia kitu kimoja.
  • Heshima kwa Mungu ya jumuisha kumshukuru na kumsifu, na kumuonyesha heshima kwa kumtii na kuishi namna inayo onyesha jinsi alivyo mkuu.

1 Chronicles 29:29

yameandikwa katika historia ya Samweli nabii, katika historia ya Nathani nabii, na katika historia ya Gadi nabii

Hii ni kazi isiyo kuwepo tena.

Yalio ekwa kwenye kumbukumbu ni matendo

"Mtu mmoja aliandika hapo matendo"

matendo ya utawala wake

"mambo yaliyo tokea wakati Daudi akiwa mfalme"

mambo yalio mdhuru

"Mambo ya mataifa mengine yaliyo hathiri Israeli"