Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa injili ya Yohana

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Injili ya Yohana

  1. Utangulizi kuhusu Yesu ni nani (1:1-18)

  2. Yesu anabatizwa, na kuwachagua wanafunzi kumi na wawili (1:19-51)

  3. Yesu anahubiri, anafundisha, na kuwaponya watu (2-11)

  4. Siku saba kabla ya kifo cha Yesu (12-19

    • Maria anapaka mafuta miguu ya Yesu (12:1-11))
    • Yesu anampanda punda kwenda Yerusalemu (12:12-19)
    • Baadhi ya watu wa Kiyunani wanataka kumwona Yesu (12:20-36)
    • Viongozi wa Kiyahudi wanamkataa Yesu (12:37-50)
    • Yesu anawafundisha wanafunzi wake (13-17)
    • Yesu anakamatwa na kujaribiwa (18:1-19: 15)
    • Yesu anasulubiwa na kuzikwa (19:16-42)
  5. Yesu anafufuka (20:1-29)

  6. Yohana anasema kwa nini aliandika injili yake (20:30-31)

  7. Yesu anakutana na wanafunzi (21)

Je, kitabu cha Yohana kinahusu nini?

Injili ya Yohana ni moja ya vitabu vinne katika Agano Jipya ambavyo huelezea baadhi ya maisha ya Yesu Kristo. Waandishi wa Injili waliandika juu ya mambo mbalimbali kuonyesha kuwa Yesu alikuwa nani na ni nini alichofanya. Yohana alisema kwamba aliandika injili yake "ili watu waweze kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai" (20:31).

Injili ya Yohana ni tofauti kabisa na Injili nyingine tatu. Yohana hajumuishi baadhi ya mafundisho na matukio ambayo waandishi wengine walijumuisha katika injili zao. Pia, Yohana aliandika juu ya baadhi ya mafundisho na matukio ambazo hazipo katika injili nyingine.

Yohana aliandika mengi juu ya ishara alizofanya Yesu ili kuthibitisha kwamba kile Yesu alisema juu yake mwenyewe ni kweli. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sign)

e, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake asilia, "Injili ya Yohana" au "Injili kama ilivyoandikwa na Yohana." Au wanaweza kuchagua kichwa ambacho kinaweza kuwa wazi, kama vile "Habari Njema Kuhusu Yesu ambayo Yohana Aliandika." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Nani aliandika Kitabu cha Yohana?

Kitabu hiki hakitupi jina la mwandishi. Hata hivyo, tangu wakati wa Kikristo wa kwanza, Wakristo wengi wamefikiri kwamba Mtume Yohana ndiye aliyekuwa mwandishi.

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za desturi

Kwa nini Yohana anaandika mengi kuhusu wiki ya mwisho ya maisha ya Yesu?

Yohana aliandika mengi kuhusu wiki ya mwisho ya Yesu. Alitaka wasomaji wake kufikiri sana juu ya wiki ya mwisho ya Yesu na kifo chake msalabani. Alitaka watu waelewe kwamba Yesu kwa hiari alikufa msalabani ili Mungu awasamehe kwa ajili ya kutenda dhambi. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Maneno "kubaki," "kuishi," na "kukaa" yana maana gani katika injili ya Yohana?

Mara nyingi Yohana alitumia maneno "kubaki," "kuishi", na "kukaa" kama mifano. Yohana alizungumuza juu ya mwamini kuwa mwaminifu zaidi kwa Yesu na kumjua Yesu vizuri kama neno la Yesu "lilibaki" ndani ya yule mwamini. Pia, Yohana alizungumuza juu ya aliyejiunga kiroho na mtu mwingine kwa kusema "alibaki" ndani yake. Wakristo wanasema "kubaki" katika Kristo na kwa Mungu. Baba anasemwa "kubaki" ndani ya Mwana, na Mwana anasemwa "kubaki" ndani ya Baba. Mwana anasemwa "kubaki" katika waumini. Roho Mtakatifu pia anasemwa "kubaki" ndani ya waumini.

Watafsiri wengi wataona vigumu kwa kutafsiri mawazo hayo katika lugha zao kusema maneno sawasawa kabisa. Kwa mfano, Yesu alitaka kuelezea wazo la Mkristo kuwa kiroho pamoja naye wakati aliposema, "Yeye anayekula mwili wangu na kunywa damu yangu anakaa ndani yangu, na mimi ndani yake" (Yohana 6:56). UDB hutumia wazo la "ataunganishwa na mimi, nami nitaunganishwa naye." Lakini watafsiri wanaweza kutumia maneno nyingine za kueleza wazo hilo.

Katika kifungu hicho, "Ikiwa maneno yangu yanakaa ndani yenu" (Yohana 15:7), kulingana na UDB wazo hili linatafsiriwa kama, "Ikiwa unaishi katika ujumbe wangu." Watafsiri wanaweza kutumia tafsiri hii kama mfano.

Je, kuna maswali makuu gani katika maandishi ya Kitabu cha Yohana?

Haya ni masuala muhimu zaidi ya maandishi katika Kitabu cha Yohana:

  • "wakingoja maji kuchemka. Malaika wa Bwana mara na mara alishuka ndani ya bwawa na kuchochea mara na mara." (5:3-4)

Watafsiri wanashauriwa kutotafsiri kifungu hiki. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri, kuna matoleo ya zamani ya Biblia ambayo yanajumuisha kifungu hiki, basi watafsiri wanaweza kukijumuisha. Ikiwa inatafsiriwa, inapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yake sio Injili ya Yohana. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

  • Habari ya mwanamke mzinzi (7:53-8:11)

Kifungu hiki kinajumuishwa katika matoleo mengi ya kale na ya kisasa ya Biblia. Lakini hakiko katika nakala za kwanza za Biblia. Watafsiri wanashauriwa kutafsiri kifungu hiki. Kinapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) kuonyesha kwamba labda asili yake sio Injili ya Yohana. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

  • Baadhi ya matoleo ya zamani pia yana kifungu hiki:

"kupitia katikati yao, na hivyo kupitia" (8:59)

Lakini ni hakika kwamba kifungu hiki hakikuwa hapo awali kwa Injili ya Yohana. Hakipaswi kuingizwa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

John 1

Yohana 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka mbele kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari ya 1:23, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

"Neno"

Hili ni neno la kipekee unaotumiwa kumtaja Yesu. Yeye ni "Neno la Mungu" katika hali ya kimwili na ufunuo wa mwisho wa Mungu mwenyewe duniani. Ingawa hii inaweza kuonekana kuwa mafundisho magumu, ni rahisi sana: Yesu ni Mungu, aliyeumba mbingu na dunia. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#wordofgod, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#flesh, and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#reveal)

Mwanga na Giza

maneno haya ni mifano ya kawaida katika Agano Jipya. Mwangaza hutumiwa hapa ili kuonyesha ufunuo wa Mungu na haki yake. Giza ni mfano wa dhambi na dhambi hupenda kufichwa kwa macho ya Mungu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#light, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#darkness and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

"Watoto wa Mungu"

Wakati watu wanpomwamini Yesu, wanaacha kuwa "watoto wa ghadhabu" na kuwa "watoto wa Mungu." Wanaingizwa katika "familia ya Mungu." Huu ni mfano muhimu ambayo itafunuliwa katika Agano Jipya. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#adoption)

Mifano muhimu za usemi katika sura hii

Mifano

Ingawa vitabu vingine vya Injili mara nyingi vinatumia mifano katika mafundisho ya Yesu na katika unabii, sura ya kwanza ya injili hii inatumia mifano kwa kielelezo cha maana ya maisha ya Yesu. Kwa sababu ya mifano hizi, msomaji anaonyeshwa kwamba injili hii italeta ufahamu zaidi juu ya maisha ya Yesu kwa kitheolojia. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Mwanzoni kulikuwa neno"

Sehemu ya kwanza ya sura hii inafuata taratibu ya kanuni za ufahamuna muundo wa kishairi. Kutafsiri taratibu hizi itakuwa vigumu sanai.

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.' (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sonofman)

| >>

John 1:1

Hapo mwanzo

Ina maanisha mwanzoni kabisa ya wakati kabla Mungu hajaumba mbingu na nchi.

Neno

Iina maanisha Yesu. Kama inawezekana litafsiri kama "Neno" Kama katika lugha yako "Neno" ni ngeli ya kike, inawe kufasiriwa kama "yule anayeitwa "Neno."

Vitu vyote viliumbwa kwa yeye

Hii inaweza kufasiriwa katika hali tendaji. "Mungu alivifanya vitu vyote kwa yeye."

pasipo yeye hakuna hata kitu kimoja kilichofanyika ambacho kilichofanyika.

Hii inaweza kufasiriwa katika hali tendaji. "Mungu hakufanya kila kitu chochote pasipo yeye" au " Mungu alifanya vitu vyote akiwa naye."

John 1:4

Ndani yake kulikuwa uzima

Hapa "uzima"ni mfano kwa kusababisha kila kitu kuishi. A: "Yeye anayeitwa Neno ndiye aliyesababisha kila kitu kuishi.

Uzima

hapa tumia neno la jumla kwa "uzima." Kama utatafasiri moja kwa moja unaweza kufasiri kama "uzima wa kiroho".

Uzima huo ulikuwa nuru ya wanadamu wote

"Nuru" ni mfano ambao ambao unamaanisha ufunuo wa Mungu.AT: aliifunua kweli kwetu kama vile nuru ifunuavyo kile kilichomo gizani.

NUru yang'ara gizani wala giza halikuliweza

Kama vile ambavyo giza lisivyoweza kuizima nuru, watu wabaya hawajaweza kumzuia yeye ambaye ni kama nuru katika kuifunua kweli ya Mung.

John 1:6

Kuishuhudia nuru

Hapa "Nuru" ni mfano kwa ajili ufunuo wa Mungu katika Yesu. AT: "onyesha jinsi ambavyo Yesu alivyo kama nuru halisi kutoka kwa Mungu."

John 1:9

Niru ya kweli

Hapa "nuru" ni mfano ambao unamwakilisha Yeus kama ufunuo wa kweli kutoka kwa Mungu.

hutia nuru

"hutoa nuru kwa"

John 1:10

Alikuwapo duniani, na kwa yeye ulimwengu ulipata kuwepo, lakini ulimwengu haukumjua

AT: "Lakini pamoja kwamba alikuwa ulimwenguni, na kwamba Mungu aliumba vitu vyote kwa yeye, bado watu hakumtambua."

alikuja kwa vitu vyake, na watu wake hawakumpokea

AT: "Alikuja kwa wenzake , na wenzake hwakumpokea."

John 1:12

Amini juu ya

Hii ina maanisha Yesu kuwa Mwokozi na kuishi kwa jinsi ambayo inamtukuza.

Jina

Neno 'jina" ni neno ambalo linaelezea utamblisho wa "Yesu" na kila kitu kitu kuhusu yeye.

aliwapa uwezo

aliwapa mamlaka" au "aliwezesha kwa ajili yao"

Wana wa Mungu

Neno "watoto"ni mfano ambao unawakilisha uhusiano wetu na Mungu, ambao ni kama vile watoto na baba.

John 1:14

Neno

Huu ni mfano ambao unamaanisha kwa Yesu. Yeye ndiye aliye mfunua Mungu alivyo.

Baba

Hiki ni cheo muhimu kwa cha Mungu.

amejaa neema

AT: "ambaye mara zote hufanya kwa wema kwa ajili yetu katika njia mbazo hatustahili."

yeye ajaye baada yangu

Yohana anaongea kuhusu Yesu. Neno "anakuja baada yagu" linamaanisha kwamba huduma ya Yohana ilikuwa tayari imeanza na huduma ya Yesu itaanza baadaya, baada ya Yohana.

ni mkuu kuliko mimi

"ni mkuu zaidi yangu" au" ni muhimu zaidi"

kwa sababu amekuwapo kabla yangu

Kuwa mwangalifu usitafsiri kwamba Yesu ni wa muhimu zaidi kwa sababu ni mzee kuliko Yohana. Yesu ni mkuu zaidi ya Yohana kwa sababu yeye ni Mungu Mwana, ambaye amekuwepo na kutawala juu ya vitu vyote pamoja na Mungu.

John 1:16

utimilifu

Huli neno linamaanisha kwa neema ya Mungu ambayo haina mwisho.

kipawa cha bure baada ya kingine

"baraka baada ya baraka"

aliye mwanadamu pekee, ambaye ni Mungu

Hii inaweza kumaanisha1)aliye Mungu wa wa pekee" au" 2) yeye aliye Mwana wa pekee,"

aliye katika kifua cha Baba

Neno "kifua" ni mfano . Hii inamaanisha kuwa Yesu ndiye aliye karibu na Baba" ikimaanisha ushusino wa karibu.

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.

John 1:19

Wayahudi walitumwa kwake kutoka Yerusalemu

Hapa mwandishi anatumia mfano. Neno "Wayahudi" limetumika kwa kuwakilisha "Viongozi wa Kiyahudi." AT:" Viongozi wa Kiyahudi waliwatuma kwake kutoka Yerusalemu.

Yeye alisema wazi, wala hakukana

Neno la pili linaeleza maneno hasi ambayo neno la kwanza linachokisema katika mtazamo chanya. Hii inasisitiza kuwa Yohana alikuwa akisema kweil.AT: "Aliwambia ukweli bila woga".

U nani?

AT: "U nani ni kama sio Masihi"? au " Nini kinachoendelea?" au " Unafanya nini."

John 1:22

Kiunganishi cha sentesi:

Johana anaendela kuongea na makuhani na walawi.

wakamwambia

"makuhani na Walawi wakamwambia Yohana>"

sisi...sisi

Makuhani na Walawi, sio Yohana.

Akasema

"Yohana akasema"

Mimi ni sauti aliaye nyikani

Neno "sauti" ni mfano ambao unamwakilisha Yohana na ujumnbe wake. AT: Mimi ni kama mtu ongea kwa sauti mbapo hakuna mtu yeyote anaweza kunisikia.

Inyosheni njiai ya Bwana

Hapa neno "njia" limetumika kama mfanoAT: Jiandae mwenyewe kwa ajili ya ujio wa Bwana kama vile ambavyo watu waandaavyo barabara kwa ajili ya ujio wa mtu muhimu.

John 1:24

Basi kulikuwa na mtu ametumwa kutoka kwa Mafarisayo

Haya ni habari ya nyuma kuhusu watu waliomuuliza Yesu kutoka kwa Mafarisayo.

John 1:26

Maelezo kwa jumla:

mstari wa 28 unatwambia habari za nyuma kuhusu mwanzo wa hadithi.

Huyu ndiye ajaye baada yangu

AT: " Atawahubiri baada ya mimi kuondoka"

Mimi sisitahili "kufungua gidamu ya viatu vyake

kazi ya kufungua viatu vyake " ambayo ni kazi ya mtumwa au mja kazi ni fumbo. Johana nasema kuwa hasitahili kumfanyia Yesu kazi hata ile ya chini kabisa liyofanywa na watumwa.

John 1:29

Mwanakondoo wa Mungu

Huuu ni mfano ambao unawakilisha Utimilifu wa dhabihu kamilifu ya Mungu. Yesu anaitwa "Mwanakondoo wa Mungu" kwa sababu alikuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi za watu.

dunia

neno "dunia" ni neno ambalo linalojumuisha watu wote duniani.

ajaye nyuma yangu, ni mkuu, kwa maana amekuwapo kabala yangu

Tafsili hili kama ulitafsiri 1:14:1:15

John 1:32

shuka

"shuka chini"

kama njiwa

hili ni neno lenye lugha ya picha . "Roho " anashuka chini kama vile ambavyo njiwa ashukavyo kwa mtu.

mbinguni

Neno "mbingu" linamaanisha "anga."

Mwana wa Mungu

Baadhi ya nakala za kifungu hiki husema "Mwana wa Mungu": wengine husema " mchaguliwa wa Mungu."

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.

John 1:35

Tena, siku iliyofuata

Hii ni siku nyingine. Ilikuwa ni siku ya pili Yohana alipomwona Yesu.

Mwanakondoo wa Mungu

Huu ni mfano ni mfano ambao unawakilisha dhabihu timilifu. Yesu ni Mwanakondoo wa Mungu kwa sababu alidhabihiwa kulipa dhambia za watu.

John 1:37

muda wa saa kumi

Neno linaonyesha wakati wa mchana, kabla ya giza, ambao usinge ruhusu kusafiri kwenda katika mji mwingine, yawezekana 10 za jioni.

John 1:40

Maelezo kwa Ujumla:

Mistari hii utupa maelezo kuhusu Andrea na jinsi alivyomleta ndugu yake Petro kwa Yesu. Hii ilitokea kabla hajaenda mahali ambapo Yesu alikuwa akikaa.

mwana wa Yohana

Huyu ni Yohana Mbatizaji. " Yohana lilikuwa jina la kawaida.

John 1:43

Basi Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mji wa Andrea na Petro

Hii ni habari ya nyuma kuhusu Filipo.

John 1:46

Nathanaeli akamwambia

"Nathaneli akamwambia Filipo."

Je jambo jema laweza kutoka Israeli?

Neno hili lijitokeza kama swali kuonyesha msisitizo.AT: "Hakuna kitu kizuri kinaweza kutoka Nazarti."

ambaye ndani yake hakuna udanganyifu

Hili linaweza kusema katika mtazamo chanya. AT: "mtumkweli aliyekamilika."

John 1:49

Rabbi, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni mfalme wa Israeli!

Nathanaeli anasema Yesu ni "Mwana wa Mungu" kwa sababu Yesu amjua Nathanaeli pasipo kukutana naye awali.

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu.

Kwa sababu nilikuambia.. je unaamini?

Hili jibu linaonekana katika jinsi ya swali kuonesha msisitizo. unaweza kuifasili kama sentesi. AT: "Unaamini kwa sababu nilisema, nilikuona chini ya mtini'!

Amini, amini

Tafsiri hili jinsi ambavyo lugha yako inavyosisitiza kuwa kile kinachofuata ni kweli.

John 2

Yohana 02 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Divai

Ilikuwa ni desturi ya divai kutumiwa wakati wa sherehe. Haikuchukuliwa uovu kunywa divai.

Kuwafukuza wanaobadili pesa

Hii ndiyo maelezo ya kwanza juu ya Yesu kuwafukuza nje ya hekalu wanaovunja pesa. Tukio hili lilionyesha mamlaka ambayo Yesu alikuwa nayo juu ya hekalu na juu ya Israeli yote.

"Alijua yaliyokuwa ndani yao"

Yohana anajua kwamba inawezekana kwa Yesu kuwa na aina hii ya ujuzi kwa sababu tu ya Yesu kuwa Mungu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Wanafunzi wake wakakumbuka"

Maneno haya hutumiwa kama ufafanuzi wa matukio yanayotokea katika sura hii. Maneno haya hayajulikani wakati ambapo matukio hutokea, lakini yamejulikana wakati kitabu kilipoandikwa. Watafsiri wanaweza kuchagua kutumia mabano ili kutenga maelezo au ufafanuzi wa mwandishi juu ya matukio yaliyopita.

<< | >>

John 2:1

Maelezo kwa Jumla:

Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini. Mstari huu unaonyesha habari ya nyuma juu ya habari inavyoanza.

Siku tatu baadaye

Wafaasili wengi husoma hili kama siku ya tatu baada ya Yesu kumwiita Filipo and Nathanaeli kuja kwake. Siku ya kwanza inaonekana katika Yohana 1:35 na siku ya pili ni 1:43

Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa harusini

Hii inaweza kutamkwa kama tendaji. AT: " Mtu alimwalika Yesu na wanafunzi wake katika arusi."

John 2:3

Mwanamke

Hii inaa mweelezea Mariamu. Kama ni neno lenye ukakasi katika lugha yako kwa mwana kumwiita mama mwanamke, tumia neno jingine.

hiyo inanihusu nini?

Hili linaonekana katika muundo wa swali ili kuonesha msisitizo . unaweza kukuifasili kama sentensi. AT: " hii haimaanishi kufanya nami" au " usiniambie nini cha kufanya."

Muda wangu bado haujatimia

Neno "muda" ni neno ambalo inawakilisha kuwa tukio maalumu kwa Yesu kuonesha kwamba yeye ni Masihi kwa miujiza.AT: "Sio muda mwafaka kwangu kufanya matengo makuu."

John 2:6

nzio mbili hadi tatu

"lita 80 hadi 120." nzio moja lilikuwa was

hadi juu

hii inamaanisha "juu sana' au "iliyojaa kabisa."

mhudumiaji mkuu

Hii ina maanisha mtu aliye na mamlaka juu ya chakula na kinywaji.

John 2:9

(lakini watumishi waliochota maji walifahamu)

hii ni habari ya nyuma.

kulewa

kutokuweza kuelewa pombe ghali na isiyo ghali kwa sababu ya kunywa kiasi kingi cha kileo.

John 2:11

Viunganishi vy maneno:

Hii si mwenendelezo wa hadithi kuu, badala yake inashamilisha hadithi.

Kana

Jina la sehemu

akifunua utukufu wake

Hapa "utukufu" ni neno linaonesha nguvu za Yesu.

John 2:12

akateremka

Hii inamaanisha kwamba walisafiri kutoka sehemu ya mwinuko kuelekea bondeni. Kana in kusini magaharibi ya Kaperanaumu na iko juu.

ndugu zake

Neno "ndugu"linajumisha kaka na dada. Kaka na dada wa Yesu walikuwa wadogo kuliko alivyokuwa.

John 2:13

Maneno ya jumla:

Yesu na wanafunzi wake wanapanda kwenda Yerusalemu kwenye hekalu.

juu hadi Yerusalemu

Hii inamaasha kuwa walisafiri kutoka kwenye mwinuko kwenda chini. Yerusalemu imejengwa juu ya kilima.

ndani ya hekalu

inamaanisha sehemu ya nje ya hekalu mahali ambapo wasio wayahudi waliruhusiwa kuabudu.

wale waliouza

watu waliweza kununua hekaluni na kuwadhabihu kwa ajili ya kumuheshimu Mungu.

wabadili fedha

Mamlaka ya Kiyahudi iliitaji watu ambao walihitaji kununua wanyama kwa ajili ya dhabihu kubadilisha pesa zao kutoka kwa wabadilishaji wa fedha.

John 2:15

Basi

Neno hili linaonyesha tukio lililotokea kwa sababu ya kile kilichotokea mwanzoni. Katika hali hii, Yesu aliwaona wabadili fedha wamekaa katika hekalu.

Acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu soko

Yesu, Mwana wa Mungu, anawafukuza wafanyabiashara kutoka mahali palipoandaliwa kwa ajili ya ibada ya Baba yake, Mungu Baba, kumuheshimu.

nyumba ya Baba yangu

Haya ni maneno ambayo Yesu aliyasema yakimaanisha hekalu.

Baba

Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu.

John 2:17

iliandikwa

Hii inaweza kusema katika muundo wa kutenda. Kuna mtu alikuwa ameandika."

nyumba yako

Neno hili linamaanisha, nyumba ya Mungu.

maliza

Neno hili "maliza" linaelekeza kwenye "moto." Upendo wa Yesu kwa ajili ya hekalu ni kama moto unaowaka ndani yake.

ishara

Hili ni tendo ambalo linalothibitisha kuwa ni jambo la kweli.

mambo haya

Haya yanamaanisha matendo ya Yesu aliyokuwa kinyume na wabadili fedha ndani ya hekalu.

Livunjenihili hekalu, na nitaliinua baada ya siku tatu

Yesu anamaanisha mwili wake kama hekalu kwamba atakufana kwamba atakuwa mzima tena baada ya siku tatu. Lakini, ni muhimu kutafasili haya maneno kuwa yameelezwa kuelezea kuvunja na kujenga jengo. Yesu hawaamuru wanafunzi wake kuvunja jengo la hekalu.

nitaliinua

Hii inamaanisha "kujenga" au 'kurudisha"

John 2:20

Yohana 2: 20- 22

Maelezo ya jumla: ilichukuwa miaka arobaini na sita...utaijenga kwa siku tatu? Miaka arobaini na sita... siku tatu aliamini/ waliamini hii sentesi

John 2:23

Basi alikuwa Yerusalemu

Neno basi linatutambulisha katika tukio jingine katika hadithi

wakaalimini jina lake

Hapa "jina" ni neno linalowakilisha utu wa Yesu. "aminini" au "kuamini katika yeye."

ishara za maajabu

Miujiza inaweza kuitwa "ishara" kwa sababu yanatumiwa kama ushahidi kwamba Mungu ni mwenye nguvu ambaye aliye na mamlaka kamili juu ya dunia.

John 3

Yohana 03 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mwangaza na Giza

Hizi ni taswira za kawaida katika Agano Jipya. Mwangaza hutumiwa hapa ili kuonyesha ufunuo wa Mungu na haki yake. Giza linaelezea dhambi na dhambi hubakia kufichwa kwa macho ya Mungu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#light, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#darkness and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Tunajua kwamba wewe ni mwalimu anayetoka kwa Mungu"

Ingawa hii inaonekana kuwa inaonyesha imani, sivyo. Sababu kumwamini Yesu kama "mwalimu tu" inaonyesha ukosefu wa ufahamu wa kuwa yeye hakika ni nani. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.' (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sonofman)

<< | >>

John 3:1

Maneno kwa Ujumla:

Nikodemo anakuja kumwona Yesu.

sasa

Neno hili lintumika hapa kutambulisha sehemu nyingine ya hadithi na kumtambulisha Nikodemo.

mjumbe

sehemu ya kundi

Halimashauli ya Wayahudi

hHalimashauli ya Kiyahudi inaitwa "Sanihedrini." Hili lilikuwa ndilo baraza muhimu kwa mabaraza yote ya Kiyahudi.

twafahamu

hapa "sisi" linajumuisha, likimaanisha tu kwa Nikodemo na wanachama wengine wa halimashauli ya Kiyahudi.

John 3:3

Kiunganishi cha sentesi:

Yesu na Nikodemo wanaendelea kuongea.

Amini, amini

Tafsiri haya kama ulivyotafsiri 1:49; 1:51.

zaliwa mara ya pili

"kuzaliwa kutoka juu" au kuzaliwa na Mungu."

ufalme wa Mungu

Neno "ufalme" ni mfano kwa utawala wa Mungu." 'Sehemu ambayo Mungu anatawala."

Je mtu anaweza kuzaliwa awapo mzee?

Nikodemo alitumia swali hili kusisitiza kwamba hili lisingelitokea. "Ni kweli mtu hawezi kuzaliwa tena wakati akiwa mzee!"

Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili ili azaliwe, je anaweza kufanya hivyo?

Pia Nikodemo anatumia swali hili kusisitiza imani yake kuwa imani yake kuwa kuzaliwa mara ya pili ni jambo lisilowezekana." Ni kweli, hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili!"

mara ya pili

"tena"au "mara mbili"

tumbo

sehemu ya tumbo la mwanamke ambapo mtoto hukulia.

John 3:5

amezaliwa kwa maji na kwa roho

kuna maana mbili: 1)"kubatizwa ndani ya maji na katika Roho" au 2)"kuzaliwa kimwili na kiroho"

Amini, amini

unaweza kufasiri mane haya kama yalivyotumika katika tafsiri za hapo mwanzo.

ufalme wa Mungu

Neno "ufalme" ni fumbo kwa ajili ya utawala wa Mungu katika maisha ya mtu.

John 3:7

Kiunganishi cha Sentesi:

Yesu anaendelea kuongea na Yesu.

Ni lazima uzaliwe mara ya pili

"unapaswa kuzaliwa kutoka juu"

upepo huvuma popote upendako

Katika lugha ya mwanzo, maneno. upepo na Roho ni maneno sawa. Mwongeaji anamaanisha upepo kama ni mtu. "Roho Mtakatfu ni kama upepo ambao unavuma popote upendapo."

John 3:9

Mambo haya yanawezekanaje?

hili ni swali mbalaga ambalo linalosisitiza sentesi. "Hii hawezekani!" au" Hili haliwezi kutokea!"

Wewe ni mwalimu wa Israeli na hauyajui mambo haya?

Hili ni swali mbagala ambalo linaonyesha msisitizo. "weweni mwalimu wa Israeli , na ninashangaa kwamba haufahamu maneno haya!"

Amini, amini

Tafsiri kama ulivyotafsiri.

twazungumza

Yesu aliposema "sisi' hakuwa anamjumuisha Nikodemo.

John 3:12

Kiunganishi cha Maneno:

Yesu anamjibu Nikodemo

mtawezaje kuamini kama nitawaeleza mambo ya mbinguni?

katika sehemu "wewe" ni umoja.

mtawezaje kuamini kama nikiwambiamambo ya mbinguni

"Hautaamini kama nikiwambia mambo ya mbinguni."

mbinguni

hii inamaanisha mahali ambapo Mungu anaishi.

John 3:14

Kama vile Musa alivyomwinua juu yule nyoka jangwani

hili ni fumbo baadhi ya watu "watainua" Yesu kama Musa alivyoinuliwa nyoka wa shaba katika jangwa.

Vivyo hivyo Mwana wa Adamu ni lazima ainuliwe juu

Jangwani ni sehemu kavu lakini hapa anamaanisha mahali walipotembea Musa na Waisraeli.

katika jangwa

Jangwani ni sehemu kavu, sehemu ya jangwa, lakini hapa wanamaanisha mahali ambapo Musa na Waisraeli walizunguka."

John 3:16

Mungu aliupenda ulimwengu

Neno "dunia" hapa ni neno linalojumuisha kila kitu duniani.

alipenda

hii ni aina ya upendo ambao unatoka kwa Mungu na unatakia mema wengine, hata kama mtu hanufaiki. Mungu mwenyewe ni upendo na ndiye chanzo cha upendo wa kweli.

mwana wa pekee

"mmoja na Mwana wa pekee"

kwa sababu Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu, bali ulimwengu uokolewe kwa yeye

maneno mawili yanaweza kuwa yanamaanisha na yametajwa mara mbili ili kwamba kusisitiza kwanza katika mtazamo hasi na chanya. Baadhi ya lugha inaweza kuonyesha msisitizo kwa namna nyingine. Kusudu la Mungu kumtuma Mwanae ni kwamba ulimwengu uokolewe katika yeye.

ahukumiwi

anachiwa huru

hukumu

adhibu

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu.

John 3:19

Kiunganishi cha Sentesi:

Yesu anamaliza kumjibu Nikodemo.

nuru imekuja ulimwenguni

Neno "nuru" ni fumbo kwa kweli ya Mungu iliyofunuliwa katika Yesu. Dunia ni neno linalojumisha vitu vyote vilivyomo duniani. Yeye ambaye ni kama nuru ameifunua kweli ya Mungu kwa watu."

watu wakalipenda giza

"giza" ni fumbo linalomaanisha mahali ambapo hawajapokea nuru" ya ufunuo wa Mungu katika Kristo.

ili kwamba matendo yake yasiwe dhahili

inaweza kutamkwa katika muundo wa kutenda. "ili kwamba nuru isioneshe mambo ayafanyayo" au " kwamba ili nuru isifunue matendo yao.

matendo yake yaonekane wazi

Hili linaweza kutamkwa katika muundo tenda. " Watu wanaweza matendo yake" au "kila mtu aweze kuona mambo ahafanyayo.

John 3:22

Baada ya haya

Hii inamaanisha baada ya Yesu kuongea na Nikodemo.

Aenoni

Neno hili linamaanisha "chemuchemi."

Salimu

kijiji au mji ulio karibu na Mto Yorodani.

kwa sababu mahali pale kulikuwa na maji mengi

"kwa sababu kilikuwa na chemuchemi nyingi katika sehemu ile."

walikuwa wakibatizwa

hili linaweza kusemwa kwa muundo wa kutenda. '" Yohana alikuwa akiwabatiza " au " alikuwa akiwabatiza."

John 3:25

kukatokea malalamiko baina ya baadhi ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi

"Tena wanafunzi wa Yohana na Myahudi wakaanza kubishana.

kutoelewana

kugombana kwa maneno

tazama, anabatiza

Katika sentesi hii "tazama" ni amri ikimaanisha tilia manani!" " Tazama! Anabatiza" au " Tazama! anabatiza."

John 3:27

Mtu hawezi kupokea kitu chochote isipokuwa

"Hakuna mtu aliye na nguvu isipokuwa"

amepewa kutoka mbinguni

Neno "mbinguni" likimaanisha Mungu. Hili linaweza kuchukuliwa katika muundo tenda. " Mungu amempa."

ninyi wenyewe

ninyi ni kwa wingi na inamaanisha watu wote ambao Yohana anazungumza nao.

nimetuma mbele zake

"Mungu amenituma kufika kabla yake."

John 3:29

Viunganishi vya maneno:

Yohana Mbatizaji anaendelea kuongea.

Yeye aliye naye bibi harusi ndiye bwana harusi

Hapa bwana na "bibi" "arusi" ni mfano. Yesu ni kama "bwana arusi" na Yohana ni kama rafiki wa bwana arus." "bwana huoa bibi

Hii, tena, furaha yangu imetimilizwa

'' Hivyo tena ninafurahia sana" au nina furahia zaidi."

furaha yangu

hili neno "yangu" lina maanisha Yohana Mbatizaji , ndiye anayeongea.

Ni lazima aongezeke

anamaanisha bwana arusi, Yesu, ambaye ataendelea kuwa wa muhimu.

John 3:31

Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote

Yohana anaongea kuhusu Yesu. "Yeye ajaye kutoka mbinguni ni wa muhimu zaidi yeyote.

Yeye aliye wa chini ni wa chini na huongea mambo ya chini

Yohana anajipinga mwenyewe dhidi ya Yesu. hamaanishi kuwa kwa kuwa alizaliwa duniani ni mwovu. Ana maanisha kuwa Yesu ni mkuu kuliko yeye kwa sababu Yesu alitoka mbinguni na Yohana alizaliwa hapa duniani. "Yeye aliyezaliwa hapa duniani ni kama mtu yeyote na na anaishi na anaongea kuhusu kilichotokea duniani."

hakuna mtu apokeaye ushuhuda wake

Yohana anaongea kwa kuonyesha neno katika hali ya kulikuza neno kwamba ni watu wachache walimwamini Yesu. "Watu wachache walimwamini."

Yeye apokeaye ushuhuda wake

Aliye ina maanisha mtu. " Mtu yeyote anayeamini kile ambacho Yesu alikisema."

amethibitisha

"kuthibitisha" au "inakubaliana"

John 3:34

Kiiunganishi cha Sentesi:

Yohana Mbatizaji anamaliza kuongea."

Kwa maana yeye ambaye Mungu amemtuma "

Huyu Yesu, ambaye Mungu amemtuma kumwakilisha."

kwa kuwa hatoi Roho kwa kipimo

" Kwa sababu yeye ndiye ambaye Mungu amempa nguvu zote za Roho wake."

Baba...Mwana

Hiki ni cheo kinachoelezea uhusiano wake kati ya Mungu na Yesu.

amepewa...katika mikono yake

Hii ina maanisha kuwekwa katika nguvu zake au kuotawala.

Yeye aaminiye

"Mtu aaminiye" au "mtu yeyote aaminiye."

ghadhabu ya Mungu inamkalia

Nomino dhaniwa "ghadhabu" linaweza kufasiriwa kama kitenzi "adhibu." "Mungu ataendelea kumwadhibu."

John 4

Yohana 04 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Yohana 4:4-38 ni habari moja inayozingatia mafundisho ya Yesu kama "maji yaliyo hai," anayewapa wote wanaomwamini uzima wa milele. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe)

Dhana maalum katika sura hii

"Ilikuwa ni lazima yeye apitie Samaria"

Kwa kawaida, Wayahudi wangeepuka kusafiri kupitia eneo la Samaria. Wasamaria walionekana kama watu wasiomcha Mungu kwa sababu walikuwa kizazi cha ufalme wa kaskazini mwa Israeli ambao walioana na wapagani. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#ungodly, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#kingdomofisrael and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

Mahali sahihi pa ibada

Mojawapo ya dhambi kubwa zaidi zilizofanywa na watu wa Samaria katika historia ni kwamba walianzisha hekalu la uongo katika wilaya yao ili kushindana na hekalu huko Yerusalemu. Huu ndio mlima mwanamke anayezungumzia katika Yohana 4:20. Wayahudi walisema kwa haki kwamba Waisraeli wote waabudu huko Yerusalemu kwa sababu ndipo ambapo Yehova aliishi. Yesu anaelezea kwamba mahali pa hekalu hapajalishi tena. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

Mavuno

Taswira ya kuvuna hutumiwa katika sura hii. Hii ni mfano ambayo inawakilisha watu kuwa na imani katika Yesu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith)

"Mwanamke Msamaria"

Mwanamke Msamaria labda ilitumika ili kuonyesha utofauti na hisia za Kiyahudi kumhusu Yesu. "Yesu mwenyewe alinena kwamba nabii hana heshima katika nchi yake" (Yohana 4:44). Kulikuwa na sababu nyingi ambazo Wayahudi wangeweza kumwona mwanamke huyu kama asiyeaminika. Alikuwa Msamaria, mzinzi, na mwanamke. Licha ya hii, alifanya kile alichohitaji Mungu. Alimwamini Yesu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#adultery and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Katika roho na kweli"

Ibada ya kweli haielekezwi tena kwa mahali moja, lakini sasa imeelekezwa kwake Yesu. Mbali na hayo, ibada haifanywi tena kwa kupitia makuhani. Kila mtu anaweza kumwabudu Mungu mwenyewe kwa njia ya moja kwa moja. Kifungu hiki kinamaanisha kwamba ibada sahihi kwa Mungu inaweza sasa kufanywa bila kutoa sadaka ya kuchinjwa na inaweza kufanywa kikamilifu kwa sababu ya ufunuo mkubwa uliotolewa kwa mwanadamu. Kuna ufahamu zaidi wa ziada wa kifungu hiki. Inaweza kuwa bora kuyaacha maneno haya kwa hali ya kawaida kama iwezekanavyo katika tafsiri ili kutoondoa maana nyingine iliyopo. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#reveal)

<< | >>

John 4:1

Maelezo kwa Ujumla:

Huu ni sehemu nyingine ya simulizi ambayo inamuhusu Yesu na mwanake Msamalia. Mstari huu unatoa habari ya mwanzoni kwa ajili ya sehemu ya simulizi

Basi Yesu alipofahamu

Neno "sasa" limetumika hapa kuonyesha kusimama kidogo katika simulizi kuu. Hapa Yohana anaanza kuelezea sehemu mpya ya simulizi.

Yesu mwenyewe hakuwa anabatiza

Nomino hii mwenyewe inongeza msisitizo kwmba sio kwamba Yesu mwenyewe alikuwa akibatiza, bali wanafunzi wake.

John 4:4

eneo la

"sehemu ya ardhi" au "kipande cha ardhi"

John 4:6

Nipe maji

Hili ni ombi la upole, na sio amri.

John 4:9

Kisha mwanamke Msamalia akamwambia

Neno "akamwambia" linamaanisha Yesu.

Inawekanaje wewe uliye Muyahudi unaomba maji ya kunywa?

Hili neno linaonekana katika muundo wa swali kuonesha mshangao wa mwanamke kwa Yesu kuomba maji. "Siamini kama wewe uliye Muyahudi unamwomba mwanamke Msamalia maji!"

hamchangamani na

"hamchangamani na."

maji ya uzima

Yesu anatumia mfano "maji ya uzima" kumaanisha Roho Mtakatifu ambaye anafanya kazi ya kumbadilisha mtu na kuleta maisha mapya.

John 4:11

wewe si mkuu, je wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo... mifugo?

hili neno linaonekana katika muundo wa swali na kuonesha msisitizo, "wewe sio mkuu kama zaidi ya baba yetu... naYakobo... mifugo?

baba yetu yakobo

"babu yetu Yakobo"

alikunya maji ya kisima hiki

alikunywa maji yaliyoka katika kisima

John 4:13

atapata kiu tena

"atahitaji kunywa maji tena.""

maji nimpayo yatakuwa chemchemi ndani yake

Neno "chemchemi" ni fumbo kwa maji yatiayo uzima. "maji nitakayompa yatakua kama chemchemi ya maji ndani yake."

uzima wa milele

hapa "uzima" lina maanisha "uzima wa kiroho" ambao ni Mungu pekee anayeweza kutoa.

John 4:15

Bwana

katika mkitadha huu, mwanamke Msamalia anamwita Yesu "Bwana" ambayo ni neno la upole au unyenyekevu.

teka maji

"pata maji" au "vuta maji kutoka ndani ya kisima" kwa kutumia chombo na kamba

John 4:17

Umenena vyema... Katika hili umenena vyema

Yesu anarudia kauli hii kusisitiza kuwa anafahamu kuwa mwanamke anaongea ukweli.

John 4:19

Bwana

Katika mkitadha huu mwanamke Msamalia anamwelezea Yesu kama "Bwana," ambalo ni neno la heshima na upole.

Naona ya kuwa unabii

"Naelewa kuwa unabii."

mababa

Mababu wa zamani

John 4:21

niamini

Kumwamini mtu ni kukubali kuwa alichokisema ni kweli.

Ninyi mwaabudu msichokijua. Twaabudu kile tukijuacho

Yesu alimaanisha kuwa Mungu amajifunua na amri zake kwa Wayahudi, sio kwa Wasamalia. Kupitia maadiko Wayahudi wanajua Mungu ni nani kuliko Wasamalia.

Mtamwabudu Baba...kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi

Wokovu wa milele kutoka dhambini unatoka kwa Mungu Baba, ambaye ni Yaweh, Mungu wa Wayahudi.

Baba

Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu.

Kwa sababu wokovu watoka kwa Wayahudi

Hii haimaanishi kuwa Wayahudi watawaokoa wengine kutoka dhambini. Ina maanisha kuwa Mungu amewachagua Wayahudi kama watu maalumu ambao watakaowambia watu wengine kuhusu wokovu wake. "kwa sababu watu wote watafahamu wakovu wa Mungu kwa sababu ya Wayahudi.

John 4:23

Kiunganishi cha Sentesi:

kuabudu ka

Ingawa, saa inakuja, na sasa ipo, ambapo waabudu wa kweli wata

"Ingawa, huu ni wakati sahihi kwa waabudu w kweli."

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.

kuabudu katika roho na kweli

"kumwabudu katika njia sahihi."

John 4:25

Ninafahamu kwamba Masihi...Kristo

Haya maneno mawili yana maanisha "mfalme aaliyeahidia na Mungu."

atatwambia kila kitu

Haya maneno "atawambia kila kitu" yanamaanisha mambo yote ambayo watu wanahitaji kujua. "atatwambia kila kitu tunachohitaji kufahamu."

John 4:27

Wakati huo wanafunzi wake wakarudi

"wakati Yesu alipokuwa akiyasema haya wanafunzi wake walirudi kutoka mjini."

nao walikuwa wakishangaa kwa nini alikuwa akiongea na mwanamke

lilikuwa ni jambo la nadra kwa Muyahudi kuongea na mwanamke asiye mfahamu.

John 4:28

Njoni mumwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda

Hii ni hali ya kusema jambo dogo kwa kulikuza. Mwanamke Msamalia anavutiwa na Yesu na kwamba anaamini kuwa Yesu anawelewa mambo yote. "Njooni mumwone mtu anaye fahamu mengi zaidi kunihusu, pamoja kwamba sijawahi kukutana naye!"

Yamkini akawa ndiye Kristo, inawezakana?

Mwanamke hana uhakika kuwa Yesu ni Kristo, kwa hiyo anauliza swali ambalo linahitaji jibu la '"hapana" lakini anauliza swali badala ya kuweka sentesi kwa sababu anataka watu wenyewe waamue wenyewe.

John 4:31

Wakati wa mchana

"Wakati mwananamke alipokuwa akienda mjini"

Wanafunzi walikuwa wakimuuliza

"wanafunzi walikuwa wakimwambia Yesu" au wanafunzi walikuwa wakimtia moyo"

Ninacho chakula ambacho hamkijui

Hapa Yesu haongelei "chakula" bali anawaandaa wanafunzi wake kwa ajili ya fundisho la kiroho.

Hakuna mtu ambaye amemlea kitu chochote

Wanafunzi wanafikiri kuwa anaongelea chakula cha kawaida.Wakaanza kuulizana wakitegemea mwitikio wa hapana. Hakika hakuna mtu aliye mletea chakula tulipokuwa mjini!"

John 4:34

chakula changu ni kufanya mapenzi yake aliyenituma na kutimiza kazi yake

"Chakula" hapa ni lugha ya picha inayowakilisha "kutii mapenzi ya Mugu." Kama vile ambavyo chakula kinavyo mtoshelea mwenye njaa, kutii mapenzi ya Mungu ndich kinachonitosheleza."

Je hamsemi

'Je hii sio miongoni mwa misemo yenu maarufu"

tazameni mashamba, kwa sababu yako tayari kwa mavuno

maneno haya mashamba na mazao yaliyo tayari yana lugha ya picha. Mashamba yanawakilisha watu wa mataifa. Na neno wako tayari linamaanisha utayari wa watu wa mataifu wa kupokea ujumbe wa Yesu kama vile mashamba yalivyo tayari kwa kuvunwa. "tazameni hawa watu wa mataifa!wako tayari kupokea ujumbe wangu, kama vile mazao katika mashamba yalivyo tayari kwa ajili ya kuvunwa."

Yeye avunaye anapokea posho na hukusanya matunda kwa uzima wa milele

Yesu anaonyesha kuwa kuna tuzo kwa wale "wanaofanya kazi katika mashamba" na kuwashirikisha ujumbe wake wengine. Na yule atakaye pokea ujumbe atapokea pia uzima wa milele ambao Mungu anawapa watu.

John 4:37

Kiunganishi cha Sentesi:

Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake.

Mmoja hupanda na mwingine huvuna

Maneno "kupanda" na kuvuna ni maneno ya lugha ya picha. Yeye anayepanda anashirikisha ujumbe wa Yesu. Yeye anayevuna anawasaidia watu kupokea ujumbe wa Yesu." Mtu mmoja hupanda mbegu, na mwingine huvuna mazao."

ninyi wenyewe mmeingia katika kazi zao

ninyi wenyewe hutia msisitizo kwa neno "wewe" tafsiri hili katika lugha yako katika namna ya kumsisitiza mtu.

John 4:39

muamini katika yeye

"Kuamini katika" maana yake ni "kuamini katika" huyo mtu. Hapa pia ina maanisha kuwa waliamini kuwa alikuwa Mwana wa Mungu.

ameniambia mambo yangu yote niliyofanya

hili ni hali ya kuelezea jambo dogo katika hali kulifanya jambo kuwa kubwa zaidi ya lilivyo. Mwanamke alivutiwa sana na Yesu na akahisi kuwa lazima akuwa anajua kila kitu kumuhusu yeye. "Ameniambia mambo mengi kuhusu maisha yangu."

John 4:41

neno lake

"Neno" hapa lina sisimama kwa kumaanisha ujumbe ambao Yesu alihubiri. "ujumbe wake"

ulimwengu

ulimwengu hapa unasimama kwa kumaanisha watu wote wanaoishi duniani. "Watu wote wanaoishi duniani."

John 4:43

Maelezo kwa Ujumla:

hii ni sehemu ya simulizi ambayo Yesu anatelemka kwenda Galilaya na anamponya kijana.Mstari 44 inatupa habari kuhusu kitu ambacho Yesu alikuwa amekisema mwanzoni.

Kwa kuwa Yesu mwenyewe alitangaza

yeye mwenyewe limeongezwa kwa kutia msisitizo kwamba Yesu alikuwa ametangaza" au alisema haya.. Unaweza kuliweka katika lugha kwa jinsi ya kutia msisitizo kwa mtu.

nabii hana heshima katika nchi yake

Watu haonyeshi heshima au kumuhesimu nabii wa nchi ya kwao" au "nabii haheshimiwi na watu wa jamii yake."

kwenye sikukuu

sikukuu hapa ni Pasaka.

John 4:46

Sasa

Neno hili linaonyesha ukomo wa masimulizi na kuhamia sehemu nyingine ya simulizi. kama katika lugha yako kuna jinsi ya kuweka hili unaweza kuweka.

afisa

mtu ambaye yuko katika huduma ya mfalme

yuko katika hali ya kufa

"kuwa katika hali kufa."

John 4:48

ninyi hamwezi kuamini hadi mwone ishara na maajabu

Msipo...hamwe kuamini" ni mashaka hasi. Katika lugha nyingine hili linatafsiriwa katika mtazamo chanya. "Mtaamini tu pale mtakapoona miujiza."

kuliamini neno

Hapa "neno" lina maanisha ujumbe ambao Yesu alioutoa. "amini ujumbe."

John 4:51

Wakati

hili neno limetumika kuonesha matukio mawili ambayo yanatokea kwa wakati mmoja. Afisa alipokuwa akienda nyumani, wafanya kazi wake wakimpokea njiani.

John 4:53

Kwa hiyo akaamini yeye na nyumba yake yote

yeye mwenyewe imetumika kusistiza neno "yeye" kama katika lugha yako una namna ya kusema unaweza kufikiri namna ya kutumia.

Ishara

Miujiza inaweza kuitwa "ishara" kwa sababu yametumika kama kiilelezo cha ushahidi kuwa Mungu ni mwenye nguvu zaidi na aliye na mamlaka juu ya dunia.

John 5

Yohana 05 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Baraza

Wayahudi wengi waliamini kwamba baraza hizi zilikuwa na uwezo wa kuponya. Hii ilifanyika wakati maji "yalichochewa." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

"Ufufuo wa hukumu"

Haya ni marejeo ya wakati baada ya kifo ambapo watu wote watahukumiwa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#death and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#judge)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Mwana, Mwana wa Mungu

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana," "Mwana wa Binadamu" na "Mwana wa Mungu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujielezea katika 'mtu wa tatu.' (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sonofman and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sonofgod)

"Ameshuhudia juu yangu"

Yesu anazungumza juu ya Agano la Kale kushuhudia kumhusu yeye. Agano la Kale linatoa unabii mwingi kuhusu Masihi ambayo yalielezea kuhusu Yesu kabla ya kuja kwake duniani. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#christ)

<< | >>

John 5:1

Maneno kwa Ujumla:

hili ni tukio linalofuata katika simulizi,ambalo Yesu anapanda kwenda Yerusalemu na anamponya mtu.Mistari hii inatoa mambo ya nyuma kuhusu mwanzoni mwa simulizi.

Baada ya hili

ina maanisha baada Yesu kumponya mwana wa afisa. ona namna ambavo unaweza kufasiri hili.

kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi

"Wayahudi walikuwa wakisherehekea sikukuu"

alipanda kwenda Yerusalemu

Yerusalemu iko juu ya kilima. Mabarabara ya Yerusalemu yalipanda juu na kutelemka katika vilima vidogo . Kama lugha yako ina neno tofauti kwa kupanda juu ya kilima kuliko kuliko kutembea katika tambarare unaweza kuitumia hapa.

dimbwi

hili lilikuwa ni shimo chini ambalo watu walijaza maji. Wakati mwingine walilizungushia kwa vigae na mawe.

Bethzatha

"Bethzatha" maana yake ni nyumba ya huruma.

matao

muundo ulioezekwa angalau pasipo kuwa ukuta mwingine katika jengo.

Idadi kubwa ya watu

"watu wengi"

John 5:5

Maelezo kwa Ujumla:

Mstari wa 5 unatambulisha mtu amelala pembeni mwa dimbwi la simulizi.

kulikuwa

"Kulikuwa kwenye dimbwi la Bethzatha"

amekuwa hawezi

"amepoza"

miaka thelathini na minane

miaka minane - miaka 38

akatambua

"alifahamu" au "alipata kuelewa"

akamwambia

"Y esu akamwambia yule mtu aliye poza"

John 5:7

Bwana, sina

hapa neno "Bwana" ni namna ya kumkabili mtu wa upole. "Bwana, hakuna mtu"

wakati maji yanapotibuliwa

Hii linaweza kufasiriwa katika muundo tendaji. "wakati malaika hutibua maji"

ndani ya dimbwi

hili lilikuwa ni shimo katika chini ambalo watu walijaza maji. wakati mwingine walilizungushia kwa vigae na mawe.

mwingine huenda mbele yangu

watu walishuka kwa hatua kadhaa kuingia ndani ya maji. "mtu mwingine mara zote huingia ndani ya maji kabla yangu.

Inuka

"simama!"

chukua kitanda chako na uende

"Chukua godor lako la kulalia, na utembee!"

John 5:9

mtu aliponywa

"mtu alikuwa na afya tena"

Sasa

Neno "sasa" limetumika hapa kwa ajili ya Yohana kutoa historia ya nyuma kwamba tukio hili linatukia siku ya Sabato.

John 5:10

Basi

hili neno linaonyesha tukio ambalo lilitokea kwa sababu ya kitu fulani kutokea. Katika hili Yesu alikuwa

Yeye aliye nifanya kuwa mzima

"Mtu aliye nifanya mzima."

John 5:12

Wakamuuliza

"Viongozi wa Kiyahudi wakamuuliza mtu aliyeponywa"

John 5:14

Yesu akampata

"Yesu alimpata mtu aliye mponya

Tazama

"Tazama" au "Sikiliza" au "Tilia manani kile ninachokueleza"

John 5:16

Basi

'Basi" linamwonesha Yohana anatoa kwa ufupi kuhusu tabia za viongozi wa Kiyahudi kwa Yesu.

kazi

Hii ina maanisha shughli au kitu chochote kinachofanywa kuwatumikia watu.

akijifanya yeye kuwa sawa na Mungu

"sema kwamba alikuwa sawa na Mungu"au kusema kwamba alikuwa na mamlaka makuu kama Mungu"

Baba yangu

Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu

John 5:19

Kiunganishi cha sentesi:

Yesu anaendelea kuongea na viongozi wa Wayahudi.

Amini, amini

Tafsiri hii kama ulivyo tafsiri 1:49; 1:51

mtashangazwa

"mtashangazwa" au mtasitushwa"

chochote anachofanya Baba, Mwana anayafanya haya mambo pia. Kwa Baba anampenda Mwana

Yesu, kama Mwana wa Mungu, alifuata na kutii uongozi wa Baba yake chini ya nchi kwa sababu Yesu alijua Baba anampenda.

Mwana...Baba

Hivi ni vyeo muhimu ambavyo zinaelezea uhusiano kati ya Yesu na Mungu.

penda

aina hii ya upendo unatoka utokao kwa Mungu unajali mazuri ya wengine, hata kama haina faida yake. Mungu mwenyew ni upendo na chanzo cha upendo wa kweli.

John 5:21

Kama vile Baba afufuavyo wafu na kuwapa uzima...Mwana pia humpa uzima kwa yeyote apendaye

Neno "kwa" ni linganifu Mwan wa Mungu (Mungu Mwana) anatoa maisha kama Mungu Baba anavyotoa uzima.

Baba...Mwana

Hivi ni vyeo ambavyo vinaelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

uzima

ina maanisha "uzima wa kiroho."

Kwa kuwa Mwana Baba hamhukumu mtu yeyote, bali amempa Mwana uwezo wote wa kuhukumu.

Neno "kwa" linaonesha ulinganifu. Mwana wa Mungu ndiye anayehukumu kwa niaba ya Mungu Baba.

mheshimu Mwana kama ...Baba. Yeye amuheshimu Mwana hamheshimu Baba

Mungu Mwana ni lazima aheshimiwe na kuabudiwa kama vile ambavyo Mungu Baba. Kama tukishindwa kumuheshimu, pia tunashindwa kumuheshimu Mungu Baba.

John 5:24

Amini, amini

Tafsiri hii kama ulivyo tafsiri

hatahukumiwa bali

"atahukumiwa kuwa hana hatia na"

John 5:25

Amini, amini

Tafsiri hii kama ulivyotafsiri mahali pengine pa "amini, amini."

wafu wataisikia sauti yangu,Mwana wa Mungu, na wao waisikiao watakuwa hai

Sauti ya Yesu , Mwana wa Mungu, itawafufua wafu kutoka makaburini.

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu.

John 5:26

Kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake, vivyo hivyo amempa Mwana ili awe na uzima ndani yake

Neno "kwa" linaonyesha ulinganifu. Mwana wa Mungu ana uzima sawa kama aliona nao Baba.

Baba...Mwana wa Adamu

Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea ushirika kati ya Mungu na Yesu.

uzima

hii ina maanisha uzima wa kiroho

Baba amempa Mwana Mwana uwezo kufanya hukumu

Mwana wa Mungu ana mamlaka ya Mungu Baba kuhukumu.

John 5:28

sikia sauti yake

"sikia sauti ya Mwana wa Adamu"

John 5:30

kutofanya chochote kutoka

Tafsiri hii kama ulivyo tafsiri 5:19

mapenzi ya aliyenituma mimi

Neno "aliye" lina maanisha Mungu Baba

John 5:33

ushuhuda ninao pokea sio wa mwanadamu

"Sihitaji ushuhuda wa watu"

okolewa

Hii ina maanisha "kuokolewa" ni katika maana ya kiroho. Kama mtu amekwisha "akolewa" ina maanishakwambaMungu amekwisha msamehe na kumuokoa kutoka katika adhabu ya Jehanamu kwa ajili ya dhambi zake.

Yohana alikuwa ni taa iliyokuwa ikiwaka na kung'ara

Yohana anonesha utakatifu wa Mungu kama vile ambavyo taa itoavyo mwanga.

John 5:36

kazi alizonipa Baba kuzitimiliza ...zinashuhudia...kuwa Baba amenituma

Mungu Baba amemtuma Mungu Mwana, Yesu, Mwana wa Mungu, duniani. Yesu anatimiza kile ambacho Baba amempa kufanya.

Baba

Cheo muhimu kwa Mungu

hamana neno lake...ndani yenu, kwa sababu hamumwamini yeye aliyemtuma

"Hamuamini katika yeye aliyetumwa. Hivi ndivyo ninavyofahamu kuwa hamna neno lake ndani yenu." Kumjua Mungu wa kwelikatika Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye Baba amemtuma. Maneno "Baba" na "Mwana" lazima yatafsiriwe katika utambulisho ambaye ni lazima tuamini.

likikaa ndani yenu

"kukaa pamoja nanyi

John 5:39

ndani yao mna uzima wa milele

"mtapata uzima wa milele kama mtasoma maandiko" au "maandiko yatakwambia namna mtakavyo pata uzima wa milele."

Ili mpate uzima

"uzima" hapa ina maanisha "uzima wa milele."

John 5:41

pokea

"pokea"

hamna upendo wa Mungu ndani yenu

Hii ina maanisha 1)"kweli kabisa hamumpendi Mungu" au 2)"kweli hamjapokea upendo wa Mungu."

John 5:43

katika jina la Baba yangu

Hapa neno "jina" lina maanisha mamlaka na nguvu za Baba.

Baba

Cheo muhimu kwa Mungu.

pokea

"pokea"

mtawezaje kuamini, ninyi ambao hupokea ...Mungu?

"Hakuna namna mnaweza kuamini kwa sababu mnapokea sifa... Mungu!"

amini

hii ina maanisha kuamini katika Yesu.

Nimekuja kwa jina la Baba yangu...kutoka kwa Mungu pekee

Yesu amekuja duniani kwa jina la Mungu Baba, Mungu pekee.

John 5:45

Yupo mwingine ambaye anawashitaki

Mungu alitoa sheria, ili kwamba mahitaji ya agano, kwa Israeli kupitia Musa. Hiki ndicho Wayahudi walimaanisha walipokuwa wakisema, "Musa alitupa sheria."Lakini kwa Waisraeliambao hawakutii sheria, Yesu alimaanisha kuwa Musa angewa shitakikwa kutokutii. Lakini "Musa" anasimama hapa kwa niaba ya sheria yenyewe.

matumaini yenu

"ujasiri wenu'

kama hamyaamini maandiko yake, mtawezaje kuamini maneno yangu?

"Hamuamini maandiko , hivyo hamtaamini maneno yangu!"

maneno yangu?

"Ninachosema?"

John 6

Yohana 06 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Wamfanye mfalme"

Ingawa si wasomi wote wanakubaliana juu ya sababu halisi ambayo Yesu hakutaka kuwa mfalme, kwa ujumla walikubaliana kuwa watu hawakuwa na nia nzuri ya kumfanya awe mfalme. Walitaka awe mfalme kwa sababu aliwapa chakula. Walikosa kutambua ukweli kwamba amekwisha kuwa mfalme wa wafalme. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

Mkate

Yesu anatumia taswira ya mkate katika sura hii. Umuhimu wa mkate asili yake ni utoaji wa kila siku ambao Mungu alitoa kwa Israeli jangwani kwa miaka 40 na matukio ya Pasaka. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#passover)

Eating the flesh and drinking the blood

When Jesus said, "Unless you eat the flesh of the Son of Man and drink his blood, you will not have life in yourselves," he knew that before he died he would tell his followers to do this by eating bread and drinking wine. In the event this chapter describes, he expected that his hearers would understand that he was using a metaphor but would not understand what the metaphor referred to. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#flesh and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#blood)

Mimi ndimi

Yohana anatumia maneno haya mara saba katika injili yake. Ni maneno sawa yanayotumiwa na Mungu, alipojidhihirisha pamoja na jina lake Yahweh katika kichaka kilichokuwa kinawaka. Jina "Yahweh" linaweza kutafsiriwa kama Mimi ndimi."

Mfano muhimu za usemi katika sura hii

"Ananipa ... huja kwangu"

Maneno haya hutumiwa kumaanisha kwamba wengi "wataamini Yesu." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

"Kula mwili wangu na kunywa damu yangu"

Hii inapaswa kuonekana wazi kama mfano. Ni marejeo ya mazoezi yaliyoanzishwa wakati wa chakula cha mwisho cha Yesu wakati Yesu alitumia mkate na divai kuwakilisha mwili wake na damu. Hii ni kumbukumbu ya kifo cha Yesu kwa dhambi. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#flesh, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#blood and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Mawazo kwenye mabano

Mara kadhaa katika kifungu hiki, Yohana anaandika maelezo mengine ili msomaji afahamu vizuri habari. Maelezo haya yanalenga kumpa msomaji ujuzi wa ziada bila kudakiza uandishi. Maneno haya yanawekwa ndani ya mabano.

"Mwana wa Binadamu, Mwana"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.'

<< | >>

John 6:1

Maelezo ya Jumla:

Hii ni sehemu ya pili ya simulizi. Mkutano ulikuwa umemfuata Yesu juu ya mlima. Mistari hii inazungumzia mahali ambapo simulizi inaanzia.

Baada ya mambo haya

Neno " haya mambo" ina maanisha matukio katika. "wakati mwingine baadaye."

Yesu akaenda zake

"Yesu akaenda mahali" au "Yesu kasafiri"

John 6:4

Maelezo kwa UJumla:

kitendo katika simulizi kinaanza msitari wa 5.

(Pasaka, sikukuu ya Wayahudi ilikuwa karibu.)

Yohana kwa ufupi anaacha kuongea kuhusu matukio katika simulizi ili kwamba alete hisotia ya nyuma kuhusu lini tukio lilitokea.

(Basi Yesu alisema maneno haya ili kumjaribu Filipo, kwa sababu yeye mwenyewe alifahamu atakachokifanya.)

kwa ufupi Yohana anaacha kuongea kuhusu matukio katika simulizi ili kwamba afafanue kwa niniYesu alimuuliza Filipo mahali pa kunua mkate.

Kwa sababu yeye mwenyewe alifahamu

Neno "mwenyewe" hapa linaweka wazi kwamba neno "yeye" lina maanisha Yesu.Yesu alifahamu nini angefanya.

John 6:7

ya thamani ya dinari

" Mikate ambayo inagharimu mshahara wa siku mia mbili." Dinari ni wingi wa "dinari nyingi."

mikate ya shayili

mkate mdogo wa mvilingo uliotengenezwa kwa nafaka ya kawaida.

Hii itafaa nini kwa watu wengi?

hii"silesi chacheya mikate na samaki haitoshikulisha watu wengi."

John 6:10

kaa chini

au "kaa chini" tegemea na desturi yako

(Basi kulikuwa na nyasi nyingi katika sehemu ile.)

Hii ilikuwa ni sehemu nzuri kabisa kwa ajili ya watu kukaa.

watu... wanaume... watu

Mkutano

elfu tano kwa idadi

wakati mkutano pengine ulijumuisha wanawake na watoto.

akashukuru

Yesu aliomba kwa Mungu Baba na kumshukuru kwa ajili ya mkate na samaki.

aliwagawia

Yesu aliivunja mikate na samaki akawapitishia wanafunzi wake. Kisha wanafunzi wakawapitishia watu mikate na samaki.

John 6:13

Maelezo ya Jumla:

Yesu anajitoa katika mkutano. Hii ni sehemu ya mwisho ya simulizi kuhusuYesu kuwalisha mkutano juu ya mlima.

wakakusanyika

"Wanfunzi wakakusanya"

wakaacha

chakula ambacho hakuna mtu aliye amekila

ishara hii

Yesu anawalisha watu 5000kwa mikate mitani ya shairi na samaki wawili.

John 6:16

Kiunganishi cha Maneno:

ili ni tukio linalofuata katika simulizi;wanafunzi wa Yesu wanaenda ziwani.

(wakati giza lilikuwa limeingia, na Yesu alikuwa bado hajaenda kwa wanafunzi.)

Tumia lugha yako jinsi ya kuonesha hii ni habari ya nyuma ya habari.

John 6:19

wanafunzi wake wakuwa wamepiga makasia

kwa kawaida mitumbwi ilikuwa na watuwawili, au sita watu waliopiga makasia kwa pamoja. Mila yako inaweza ikawa na namna nyingine ya kusababisha mtumbwikukatisha katika maji mengi .

kama makasia ishirini na matanoau thelathini

tano au makasia sita "kama kilometa tano au sita." kasia ni kama makasia, mita 185.

John 6:22

bahari

Bahari ya Galilaya

(Ingawa, palikuwa... Bwana aliposhukuru)

tumia lugha yako kuonesha kuwa hii ni habari ya nyuma.

mitumbwi iliyokuja kutoka Tiberia

siku iliyofuata baada ya Yesu kuwalisha watu, baadhi ya mitumbwi kutoka Tiberia ilikuja na watu ili wamwone Yesu.Ingawa, Yesu na wanafunzi wake walikuwa wametoka usiku mmoja kabla.

John 6:24

Maelezo ya Jumla:

mkutano unaanza kumuuliza Yesu maswali

John 6:26

Amini, amini

tafsiri hili kama ulivyo tafsiri mengine kama haya maneno.

uzima wa milele ambao Mwana wa Adamu atawapa ninyi, Mungu Baba ametia muhuri juu yake

Baba amfanya uthibitisho wake kwa Yesu, Mwana wa Adamu na Mwanawa Mungu, kutoa uzima wa milele kwa wale wanao amini katika yeye. Baba na Mwana wamekwisha timiza msamaha wa milele na uzima.

Mwana wa Adamu, Mungu Baba

Hivi ni vyeo muhimu ambavyo zinaelezea uhusiano kati Mungu na Yesu.

ametia muhuri juu yake

"ametia muhuri" juu ya kitu maana yake kuweka alama juu yake kuonesha ina milikiwa na.Hii ina maana kuwa Mwana anatokana na Baba.

John 6:30

mababa

"mababa wa zamani"

mbingu

Ina maanisha sehemu ambayo Mungu huishi

John 6:32

Amini, amini

Tafsiri hili kama ulivyo tafsiri maneno kama haya.

Baba yangu ndiye awapaye mkate wa kweli kutoka mbinguni

Baba anatupa "mkate wa kweli" kutoka mbinguni, Mwanae Yesu. Pamoja Baba na Mwana pamoja na Roho Mtakatifu wanawapa watu maisha ya kimwili, kiroho na maisha ya milele.

Baba yangu

Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu.

mkate wa kweli

Yesu anajilinganisha na mkate. Kama vile mkate uliyo muhimu kwa ajili ya maisha yetu ya mwili, Yesu ni wa muhimu kwa ajili ya maisha yetu ya kiroho.

uzima

hili lina maanisha uzima wa kiroho.

John 6:35

Mimi ni mkate wa uzima

Yesu anajifananisha na mkate. Kama vile mkate ulivyo muhimu kwa maisha yetu ya mwili, Yesu ni wa muhimu kwa maisha yetu ya kiroho.

aaminiye katika

Hii ina maanisha kuaminia kuwa Yesu ni Mwan wa Mungu, kumtegemea kama mwokozi, na kuishi katika namna ambayo ina mpendeza.

Wale wote anipaye Baba watakuja kwangu

Mungu Baba na Mungu Mwana ni washirika katwa milele kwa wale wanao mwamini Yesu, Mwana wa Mungu.

Baba

Cheo muhimu kwa Mungu.

Yeye ajaye kwangu sitamtupa kamwe nje

"Nitamtunza kila mmoja ambaye ajaye kwangu.

John 6:38

Kiunganishi cha Maneno:

Yesu anaendelea kuongea na mkutano

yeye aliyenituma

"Baba yangu, aliyenituma mimi"

nisimpoteze hata mmoja

"Niwatunze wote"

mapenzi ya Baba yangu...kila amtazamaye

Yesu anafafanua kwamba Mpango wa Baba unatoauzima wa milele kwa walew wanaoamini " Mwana,"Mwana wa Mungu, Yesu Kristo atakaye fufua na kutukuza miili ya wote wanao amini.

Mwana na kuamini katika yeye awe na uzima wa milele

Yesu anafafanua kwamba mpango wa Mung unaleta uzima wa milele kwa wale wote wanao mwanini "Mwana," Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, ambaye atakaye wafufua na kutukuza miili ya wale wanaoamini.

John 6:41

Kiunganishi cha Maneno:

Viongozi wa Wayahudi wanaingilia kati wakata Yesu anaongea na mkutano.

nung'unika

Kuongea katika hali ya kutokuwa na furaha

Mimi mkate wa uzima

Tafsiri hii kama ulivyotafsiri 6:35

John 6:43

kiunganishi cha maneno:

Yesu anaendela kuongea na mkutano na sasa anaongea na viongozi wa Wayahudi.

kuvuta

hii inaweza kufasiriwa 1) "kuvuta" 2)"kuvutia"

imeandikwa katika manabii

"Manabii waliandika"

Kila aliyekwisha sikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu

Wayahudi walifikiri Yesu alikuwa mwana wa Yusufu" lakini ni Mwana wa Mungu kwa sababu Baba yake ni Mungu Baba , sio Yusufu. Wale wote ambao kweli wanajifunza kwa Mungu Baba wanaamini katika Yesu, Mungu Mwana.

Baba

Cheo muhimu kwa Mungu.

John 6:46

kinganishi cha maneno

Yesu anaendelea kuongea na mkutano na viongozi wa Wayahudi.

Amini, amini

Tafsiri hii kama ulivyo tafsiri maneno mengine ya namna hii.

hakuna mtua yeyote aliyemwona, isipokuwa yeye aliyetoka kwa Mungu

Ingawa hakuna mwadamu aishie katika dunia amemwona Mungu Baba, Yesu, Mwana wa Mungu, amemwona Baba.

Baba

Cheo muhimu kwa mungu.

yeye aaminiye ana uzima wa milele

"uzima wa milele" umeunganishwa katika Yesu, Mwana wa Mungu.

John 6:48

Mimi ni mkate wa uzima

Tafsiri hii kama ulivyotafsiri maneno yanayofanana na haya.

mababa

"mababa wa zamani"

kufa

hii ina maanisha kifo cha kimwili.

John 6:50

Huu ni mkate

tazama notisi 6:35

hakuna kufa

"ishi milele." hapa neno "kufa" lina maanisha kifo cha kiroho.

mkate wa uzima

Hii ina maanisha" mkate ambao una sababisha watu kuishi"

John 6:52

Kiunganishi cha maneno

Baadhi ya Wayahudi waliopo wanaanza kubishana wenyewe na Yesu anajibu kwa swali lao.

Amini, amini

tafsiri hili kama ulivyo tafsiri maneno mengine ya namma hii.

kula mwili wa Mwana Adamu na kunywa damu yake

Kumpokea Mwana wa Adamukwa imani ni sawa kupokea chakula na kinywaji.

John 6:54

Kiunganishi cha Sentesi:

Yesu anaendelea kuongea kwa wote wanao msikiliza.

chakula cha kweli... kinywaji cha kweli

Kumpokea Yesu kwa imani kunaleta uzima wa milele kama vile ambavyo chakula na kinywaji vinavyoawilisha mwili.

John 6:57

Baba mwenye uzima

Hii inaweza 1) "Baba atoaye uzima" au "Baba aishie," kama watu au wanyama wanavyoishi, kinyume cha "kifo"

Baba

hiki ni cheo muhimu kwa Mungu.

Baba mwenye uzima alinituma...kwa sababu ya Baba...yeye anilaye...ata...ishi kwa sababu ya

Yesu alitumwa na Baba, na anaishi kama mwanadamu kwa sababu ya Mungu Baba. Kama Mungu Mwana alivyotumwa na Mungu Baba, Yesu ni chanzo cha uzima wa milele.

mababa

"mababa wa zamani"

Yesu aliyasema mambo haya ndani ya Sinagogi... huku Kaperanaumu

hii ni babari ya nyuma kuhusu wakati tukio hili lilipotukia.

John 6:60

ni nani awezaye kulipokea?

"hakuna mtu anaweza kulipokea." au "halipokeleki."

Je hili lina kukwaza?

"Nin shangazwa kwamba hili lina wakwaza!"

linakukwaza wewe

"linakusababisha kukata tamaa kwa imani yako"

John 6:62

Basi ni vipi kama mkimwona Mwana wa Adamu akishuka kutokakule aliokuwa kabla?

"Labda mtaamini ujumbe wangu kama mkiniona, yeye aliye kuja kutoka mbinguni, akishuka kule nilikokuwa kabla!"

faida

Hii ina maanisha kusababisha vitu vizuri kutokea.

maneno

"Ujumbe" Pengine maana: 1) maneno yake ndani au 2) kila kitu anachofundisha.

maneno niliyokuambia wewe

"Nilichowambia"

roho

Maana zinazo wezekana ni 1)Roho Mtakatifu au2) vitu vya kiroho.

ni roho, na ni uzimaa

maana dhaniwa 1)"karibia Roho na uzima wa milele" au "kutoka kwa Roho na inatoa uzima wa milele" au 3)" ni kuhusuvitu vya kiroho na uzima."

John 6:64

hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amepewa na Baba

Mwana wa Mungu, amepewa na Baba. Mungu Baba na Mungu Mwana kwa pamoja ni njia katika wokovu msamaha wa milele. Yeyote atakaye kuamini ni lazima aje kwa Mungu kwa kupitia Baba na Mwana.

njoo kwangu

"nifuate mimi"

Baba

hiki ni cheo muhimu kwa Mungu

John 6:66

wanafunzi wake

"wanafunzi wake" hapa ina maanisha jumuisho ambao walimfuata Yesu.

kumi na wawili

Hili kundi maalumu ya wanaume 12 walio mfuata Yesu kwa huduma yake yote. Hii inaweza kufasiriwa "wafuasi kumi na wawili."

John 6:70

Je mimi sikuwachagua, ninyi kumi na wawili, na mmja wenu ni shetani?

"mwenyewe niliwachagua wote, lakini mmoja wenu ni mtumishi wa shetani."

John 7

Yohana 07 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

This whole chapter concerns the concept of believing Jesus to be the Messiah. Some people believed this to be true while others rejected it. Some were willing to recognize his power and even the possibility that he was a prophet, but most were unwilling to believe that he was the Messiah. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#christ and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet)

Labda watafsiri watapenda kuandika alama katika mstari wa 53 kumwelezea msomaji kwa nini wamechagua kutafsiri au kutotafsiri mistari 7:53-8:11.

Dhana maalum katika sura hii

"Wakati wangu haujafika"

Kifungu hiki na "saa yake haujafika" hutumiwa katika sura hii kuonyesha kwamba Yesu alikuwa na uwezo juu ya vitu vilikuwa vinatoweka maishani mwake.

"Maji yaliyo hai"

Hii ni mfano muhimu inayotumiwa katika Agano Jipya. Ni mfano. Kwa sababu mfano huu unatolewa katika mazingira ya jangwa, labda inaonyesha kuwa Yesu anaweza kutoa chakula cha kudumisha maisha. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Tamathali muhimu za usemi katika sura hii

Unabii

Yesu anatoa unabii juu ya maisha yake bila kutoa habari yote katika Yohana 7:33-34.

Kinaya

Nikodemo anawaelezea Mafarisayo wengine kwamba Sheria inamlazimisha asikie mtu moja kwa moja kabla ya kutoa hukumu juu yake. Mafarisayo kwa upande wao walifanya hukumu juu ya Yesu bila kuzungumza na Yesu.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Hawakumwamini"

Ndugu za Yesu hawakuamini kwamba Yesu alikuwa Masihi. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe)

"Wayahudi"

Neno hili linatumika kwa njia mbili tofauti katika kifungu hiki. Linatumika hasa kwa kutaja upinzani wa viongozi wa Kiyahudi waliokuwa wakijaribu kumwua (Yohana 7:1). Pia hutumiwa kwa kutaja watu wa Yudea kwa ujumla ambao walikuwa na maoni mazuri ya Yesu (Yohana 7:13). Mtafsiri anaweza kutumia maneno "viongozi wa Kiyahudi" na "watu wa Kiyahudi" au "Wayahudi (viongozi)" na "Wayahudi (kwa ujumla)."

<< | >>

John 7:1

Na baada ya mambo haya

"Na baada ya kumaliza kuongea pamoja na wanafunzi"

Safiri

"tembea"

John 7:3

ndugu

Hili linaelekeza kwa ndugu zake halisi, wana wa Mariamu na Yusufu.

Ulimwengu

"Watu wote" au "kila mmoja"

John 7:5

kaka zake

kaka zake wadogo

Wakati wangu bado haujafika

Yesu anamaanisha kuwa wakati muafaka bado haujafika kwa ajili ya huduma yake

John 7:8

Hawa

wingi

John 7:10

Naye vile vile alienda

Yerusalemu ilikuwa upande wa juu kutoka pale walipokuwa

Siyo kwa wazi bali kwa siri

Mafungu haya mawili yana maanisha jambo moja, iliyorudiwa kwa kuweka mkazo. Lugha zingine huweka mkazo kwa njia tofauti.

John 7:12

Hofu

Hili huchukuliwa katika hisia zisizokuwa za furaha wakati ambapo kuna utisho wa kuumizwa kwake au wengine.

John 7:14

Kwa jinsi gsni mtu huyu anajua mengi hivi?

"Haiwezekani akajua mengi juu ya maandiko."

Ni yeye aliyenituma

Neno "yeye" linamhusu Mungu Baba.

John 7:17

Lakini yeyete atafutaye utukufu wake aliyenituma, mtu huyo ni wa kweli na ndani yake hakuna kutokutenda haki.

"lakini ninafanya mambo ili kwamba wengine wapate kumheshimu yeye aliyenituma, nami ni yule asemaye kweli. Sidanganyi kamwe."

John 7:19

Musa hakuwapa ninyi sheria?

"Ni Musa aliyewapa ninyi sheria."

Kwa nini mnataka kuniua?

"Mnatafuta kuniua."

Una pepo

"Wewe ni kichaa."

Nani anataka kukuua?

"Hakuna yeyote anayetaka kukuua."

John 7:21

Kazi moja

"Muujiza mmoja" au "ishara moja"

(Siyo kwamba inatoka kwa Musa, lakini inatoka kwa mababa)

Hapa mwandishi anatoa maelezo ya nyongeza.

John 7:23

Kwa nini mnanikasirikia mimi kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima katika siku ya Sabato"

"Hamkupaswa kunikasirikia kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima siku ya Sabato."

John 7:25

Siye huyu wanayemtafuta kumwua?

"Huyu ni Yesu wanayemtafuta kumwua."

John 7:28

Ninyi nyote mnanijua na mnajua ninakotoka

"Ninyi" iko katika wingi.

Ni kweli

"Ni shahidi wa kweli."

John 7:30

Kristo atakapokuja, atafanya ishara zaidi ya hizi anazofanya mtu huyu?

"Kristo atakapokuja hataweza kufanya ishara zaidi ya hizi ambazo mtu huyu amefanya."

Ishara

"Hii inamaanisha miujiza inayothibitisha kuwa yeye ni Kristo."

John 7:33

Yeye aliyenituma

Mungu Baba

John 7:35

Mtawanyiko

Wayahudi sehemu mbali mbali katika ulimwengu wa Wagiriki, nje ya Palestina.

John 7:37

Sasa

Neno "sasa" linatumika hapa kuonyesha mkato ndani ya mstari mkuu wa hadithi.

Siku kubwa

Ni "kubwa" kwa sababu ni ya mwisho, au muhimu zaidi siku ya sikukuu.

Ikiwa yeyote ana kiu

Hii inamaanisha hamu ya mambo ya Mungu, kama vile mwingine anavyoweza kuwa na hamu au "kiu" kwa maji.

Na aje kwangu anywe.

Neno "yeye" maana yake "yeyote." Neno "kunywa" hapa linawakilisha utimilifu wa kiroho katika Kristo.

Maandiko

Hapa "maandiko" linasimama kwa unabii wa Masihi kuhusiana na Kristo. Hii siyo nukuu ya moja kwa moja kutoka fungu lolote maalum la Agano la Kale.

kutiririka ito ya maji ya uzima

Kristo atatoa pumziko la "kiu" ya kiroho kwa watu katika kiwango kikubwa kwamba itatiririkia nje kumsaidia kila aliyepo kama

Maji ya uzima

Hii inamaanisha 1) "maji yatoayo uzima" au "maji yanayowafanya watu kuishi au 2) maji ya asili yatiririkayo kutoka kwenye chemchemi, iliyotofautishwa na maji yatokayo kisimani.

John 7:39

Lakini yeye

"Yeye" inamaanisha Yesu

John 7:40

Nini, Kristo anaweza kutokea Galilaya?

"Kristo hawezi kutoka Galilaya."

Maandiko hayasemi kwamba Kristo atatoka katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji alichokuwa Daudi?

"Maandiko yanafundisha kwamba Kristo atatoka katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi alikuwa."

Maandiko hayajasema?

"Manabii waliandika katika maandiko."

John 7:43

Kukainuka mgawanyiko

Makutano hawakuweza kukubaliana juu ya nani au Yesu alikuwa nani.

Lakini hakuna hata mmoja aliyeinua mkono juu yake

"Lakini hakuna aliyemkamata."

John 7:45

Maafisa

"Walinzi wa Hekalu"

Kwa nini nyinyi hamkumleta?

Hapa "nyinyi" inamaanisha walinzi wa hekalu.

John 7:47

Ndipo Mafarisayo walipowajibu

Hapa "wao" inamaanisha walinzi wa hekalu.

Kupotoshwa

Kudanganywa

Kuna yeyote kati ya watawala aliyemwamini, au yeyote kati ya Mafarisayo?

"Si watawala wala Mafarisayo waliomwamini."

Sheria

Hii ilirejea sheria ya Mafarisayo na si sheria ya Musa.

John 7:50

Sheria yetu humhukumu mtu

Nikodemo alimaanisha kuwa wale wanaoifuata sheria hawamhukumu mtu kabla ya kumhoji.

sheria yetu humhukumu mtu... sivyo?

"Sheria yetu ya Kiyahudi haituruhusu kumhukumu mtu

Na wewe pia unatokea Galilaya?

Inawezekana pia na wewe ni mmoja wa watu wa chini kutoka Galilaya

Hakuna Nabii anayetoka Galilaya

Hii pengine ilirejea katika imani kwamba Masihi hawezi kuzaliwa Galilaya

John 7:53

7:53- 8:11

8:11 Maelezo yaliyotangulia hayana mistari hii.

John 8

Yohana 08 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Watafsiri wanaweza kupenda kuandika alama katika mstari wa 1 ili kuelezea msomaji kwa nini wamechagua kutafsiri au kutotafsiri mistari 8:1-11. Kwa sababu hiki ni kifungu cha utata, ni bora kutokuwa na hitimisho la kitheolojia kutoka kwa kifungu hiki.

Dhana maalum katika sura hii

Mwangaza

Mwangaza ni mfano ya kawaida katika Maandiko yaliyotumiwa kuonyesha haki. Mwangaza pia hutumiwa kuonyesha njia ya haki na kuonyesha maisha ya haki. Giza hutumiwa mara nyingi kama mfano zinazowakilisha dhambi au uovu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#light, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous,

Mimi ndimi

Yohana anatumia maneno haya mara saba katika injili yake. Ni maneno sawa yanayotumiwa na Mungu, alipojidhihirisha pamoja na jina lake Yahweh katika kichaka kilichokuwa kinawaka. Jina "Yahweh" linaweza kutafsiriwa kama "Mimi ndimi."

"Mwanamke aliyekamatwa katika kitendo cha uzinzi"

Ikiwa mwanamke huyo alipatwa katika kitendo cha uzinzi, kulikuwa na mwanamume ambaye pia alikamatwa katika kitendo cha uzinzi. Mwanamume huyo hayuko katika maelezo haya. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#adultery and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.'

<< | >>

John 8:1

Watu wote

Watu wengi

Mwanamke aliyekamatwa katika kitendo cha uzinzi

Mwanamke ambaye walimkuta akizini

John 8:4

Sasa katika sheria

"Sasa" ni utangulizi wa kilichotangulia kuwa Yesu na Wayahudi wenye mamlaka walielewa

Watu kama hao

"Watu kama hao" au "watu wafanyao hayo"

Unasemaje kuhusu yeye?

Hii inaweza kutafsiriwa kama amri. "Kwa hiyo tuambie. Tufanyeje kuhusu yeye?"

Kumtega

"Kumtega." Hii inamaanisha kutumia swali la mtego.

Ili kwamba wapate jambo la kumshitaki kwalo

Nini watakachomshitaki nacho inaweza kufanywa wazi. "Ili kwamba wapate kumshitaki kwa kusema jambo baya" au ili kwamba wapate kumshitaki kwa kutoitii sheria ya Musa na sheria ya Warumi.

John 8:7

Wakati walipoendelea

Neno "walipo" linarejea kwa waandishi na Mafarisayo.

Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu

"Kama yeyote kati yenu hana dhambi" au Ikiwa mmoja kati yenu hajatenda dhambi kamwe"

Miongoni mwenu

Yesu alikuwa anaongea na waandishi na Mafarisayo, na pengine makutano ya watu pia.

Mwacheni

Mwacheni mtu huyo

Aliinama chini

Aliinama kufikia chini

John 8:9

Mmoja baada ya mwingine

Mmoja baada ya mwingine

Mwanamke, wako wapi washitaki wako?

Wakati Yesu alipomwita "mwanamke," hakumaanisaha kumdharau au kumfanya ajione mdogo. Ikiwa watu katika makundi yao ya lugha watafikiri kwamba alikuwa akifanya hivyo, hii itafsiriwe bila kutumia neno "mwanamke."

John 8:12

Mimi ni nuru ya ulimwengu

mimi ndiye nitoaye nuru kwa ulimwengu. Maana yake ni kwamba Yesu ameleta ujumbe wa kweli wa Mungu katika ulimwengu uwaokoao wanadamu kutoka giza la dhambi zao.

Ulimwengu

"Watu wa Ulimwengu"

Yeye anifuataye

"Kila mmoja anifuataye." Hii ni njia ya mafumbo isemayo "Kila mmoja atendaye yale ninayofundisha" au " kila mmoja anayenitii."

Uzima

Hii inamaanisha uzima wa kiroho

Unajishuhudia mwenyewe

"Unayasema mambo haya kwa ajili yako mwenyewe."

Ushuhuda wako siyo kweli

"ushuhuda wako siyo kweli" huwezo kuwa shahidi wa kujishuhudia mwenyewe au kile unachokisema juu yako hakiwezi kuwa kweli.

John 8:14

Ingawa najishuhudia mwenyewe

Hata ingawa nasema mambo haya juu yangu binafsi

Mwili

Kanuni za kibinadamu na sheria za watu

Simhukumu yeyote

Maana zuinazowezekana zaweza kuwa 1) Sijamhukumu yeyote bado au 2) Simhukumu yeyote sasa

ikiwa nitahukumu

Ikiwa nitahukumu watu. Maana inawezekana 1) Ninapowahukumu watu ( kwa wakati ujao) au 2) wakati wowote ninapowahukumu watu (sasa) au 3) ikiwa nitahukumu watu.

Hukumu yangu ni kweli

Maana inayowezekana 1) "Hukumu yangu itakuwa sahihi" au 2) Hukumu yangu ni sahihi

Siko peke yangu, lakini niko pamoja na Baba aliyenituma

Yesu, Mwana wa Mungu, anayo mamlaka kwa sababu ya uhusianomwake maalumu na Baba yake, aliyemtuma. Neno "Baba" na "Mwana" linaonyesha uhusiano wa watu wa Mungu kati yao.

Siko peke yangu

Siko peke yangu katika hukumu. "Siko peke yangu jinsi ninavyohukumu" au "sihukumu peke yangu."

Niko pamoja na Baba

"Baba pia anahukumu pamoja na mimi" au "Baba anahukumu kama nihukumuvyo mimi."

Baba

Hiki ni cheo maalumu kwa Mungu

Baba aliyenituma

Neno "aliyenituma" inazungumza jambo zaidi kuhusu Baba. "Baba, yeye pekee aliyenituma."

John 8:17

Ndiyo, na katika sheria yenu

Neno "Ndiyo" inaonyesha kwamba Yesu anaongeza kile alichosema kabla.

Imeandikwa

Musa aliandika

Ushuhuda wa watu wawilini kweli

"Ikiwa watu wawili watasema jambo lile lile, ndipo watu watakapojua ni kweli"

John 8:19

Hamnijui mimi wala Baba yangu, kama mngelinijua mimi, mngelimjua na Baba yangu vile vile."

Yesu anaonyesha kwamba kumjua yeye ni kumjua Baba pia. Wote Baba na Mwana ni Mungu mmoja, kwa hiyo kumjua mmoja ni kuwajua wote.

Baba yangu

Hiki nicheo muhimu kwa Mungu.

John 8:21

Kufa katika dhambi zenu

"Kufa wakati ukiwa mwenye dhambi." au "utakufa wakati ukiendelea kutenda dhambi." Hapa neno "Kufa" linaelezea kifo cha kiroho.

Hauwezi kuja

"Hauna uwezo wa kuja"

Je atajiua mwenyewe, yeye aliyesema

Hii yaweza kutafsiriwa kama maswali mawili yaliyotenganishwa. Atajiua mwenyewe? Hivyo ndiyo sababu anasema"

John 8:23

isipokuwa uamini kwamba MIMI NDIYE, utakufa

Ikiwa hautaamini

kwamba MIMI NDIYE

Kwamba mimi ni Mungu

John 8:25

Walisema

Neno hili linamaanisha viongozi wa Kiyahudi

Baba

Baba yake

John 8:28

Utakapoinuliwa juu

Utakapoinuliwa. Hili halijatokea bado.

Mwana wa Mtu.... Baba

Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea uhusiano wa Yesu na Mungu.

MIMI NDIYE...BABA alinifundisha

kama Mungu Mwana, anavyomjua Mungu Baba tofauti na mwingine yeyote, na divyo ilivyo wakati wote

Kama Baba alivyonifundisha

katika njia ile ile kwamba Baba alinifundisha

Yeye aliyenituma

Neno linamaanisa Baba

Kama Yesu alivyosema

wakati Yesu alipokuwa akisema

John 8:31

baki katika neno langu

Tii kile nilichosema

kweli itakuweka huru

Ikiwa mtautii ukweli, Mungu atawaweka huru"

John 8:34

Amini, amini

Tafsiri hii kama ilivyofanyika Yoh. 1:49

Ni mtumwa wa dhambi

"Ni kama mtumwa wa dhambi." Hii inamaanisha kwamba dhambi ni kama bwana wa mwenye dhambi.

Katika nyumba

Nyumbani mwa

Ikiwa Mwana atawaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli

Kulingana na tamaduni zao, mwana mkubwa anaweza kumweka huru mtumwa katika nyumba yake.

Mwana

Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.

John 8:37

Neno langu

Mafundisho yangu

John 8:39

Baba

Mababa

Ibrahimu hakufanya hili

Ibrahimu kamwe hakujaribu kumwua yeyote aliyemwambia ukweli kutoka kwa Mungu

Hatukuzaliwa katika dhambi ya zinaa

Wote tulizaliwa kutoka ndoa sahihi

John 8:42

Pendo

Huu ni aina ya upendo unaotoka kwa Mungu na unaelekea katika mema ya wengine, hata kama haufaidiki chochote.

Kwa nini hamyaelewi maneno yangu?

Yesu anatumia swali hili hasa hasa kuwakemea viongozi wa Kiyahudi kwa kutomsikiliza yeye.

John 8:45

Nani kati yenu ananishuhudia kuwa ni mwenye dhambi?

Hakuna yeyote kati yenu anayeweza kunishuhudia kuwa mimi nina dhambi." Yesu aliuliza swali hili kuweka mkazo kuwa yeye hana dhambi.

Kwa nini haniamini

Hamna sababu ya kushindwa kuniamini" Yesu alitumia swali hili kuwakemea viongozi wa Kiyahudi kwa kutoamini kwao.

John 8:48

Wayahudi

Neno Wayahudi linatumika kuwakilisha viongozi wa Kiyahudi.

John 8:50

Kuyashika maneno yangu

Tii kile ninachosema

Kifo

Hii inamaanisha kifo cha kiroho

John 8:52

Baba

Mababa

John 8:54

Ni Baba yangu anayenitukuza

Hakuna mwanadamu amjuaye Mungu Baba kama Mungu Mwana, Yesu Mwana wa Mungu. Mungu Baba humtukuza Mwana kwa sababu wote Baba na Mwana ni Mungu wa milele.

Baba

Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu

John 8:57

Haujafikisha bado umri wa miaka hamsini, na umeshamuona Ibrahimu?

Miaka yako ya umri ni chini ya hamsini. Usingelikuwa umemuona Ibrahimu."

Amini, amini

Tafsiri hii kama ulivyofanya katika Yoh. 1:49

John 9

Yohana 09 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Ni nani aliyetenda dhambi?"

Katika Israeli ya kale, mara nyingi waliamini kwamba mtoto alizaliwa na ulemavu kwa sababu ya dhambi ya mmoja wa wazazi wake. Hii haikuwa mafundisho ya sheria ya Musa. Katika mjadala huu, Mafarisayo walikuwa wenye dhambi kwa sababu waliona uwezo wa Yesu na hawakumuabudu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses).

Mimi mdimi

Yohana anatumia maneno haya mara saba katika injili yake. Ni maneno sawa yanayotumiwa na Mungu, alipojidhihirisha pamoja na jina lake Yahweh katika kichaka kilichokuwa kinawaka. Jina "Yahweh" linaweza kutafsiriwa kama "Mimi ndimi."

Mwangaza

Mwangaza ni mfano wa kawaida katika Maandiko yaliyotumiwa kuonyesha haki. Mwangaza pia hutumiwa kuonyesha njia ya haki na kuonyesha maisha ya haki. Giza hutumiwa mara nyingi kama mfano unaonyesha dhambi au uovu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#light, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#darkness, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#unrighteous)

"Yeye haishiki Sabato"

Mafarisayo walimwona Yesu akifanya matope kuwa "kazi" na kukiuka sheria kuhusu Sabato. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sabbath)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Kuona

Katika sura hii kumeandikwa habari ya mtu aliyezaliwa kipofu. Yesu pia anatumia habari hizi kama mfano. Katika Yohana 9:39-40, Mafarisayo wanaitwa vipofu kwa sababu hawawezi kuona ukweli ulio mbele yao. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.' (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sonofman)

<< | >>

John 9:1

Yesu alipopita karibu

hapa inamaanisha Yesu na wanafunzi wake

John 9:3

Sisi

Neno sisi linawahusisha wote Yesu na wanafunzi wake aliokuwa akiongea nao.

Mchana...Usiku

Yesu analinganisha wakati watu wanaweza kufanya kazi wakait wa mchana, wakati ambao kwa kawaida watu hutenda kazi, na wakati wa usiku watu hawawezi kufanya kazi ya Mungu.

Nuru ya Ulimwengu

Yule ambaye aonyeshaye kile kilicho cha kweli kama vile nuru ionyeshacho kilicho halisi.

John 9:6

alifanya udongo kwa kutumia mate

Yesu alitumia vidole kuchanganya udongo na mate.

aliosha

aliosha macho yake kwenye kisima

John 9:8

Huyu siye mtu....mwombaji?

Huyu mtu ni yule ... omba, siyo yeye? au "Huyu ni mtu... omba. Ndiyo ni yeye.

John 9:10

alipakwa... macho

Angalia jinsi ulivyotafsiriwa Yoh. 09:06

John 9:13

siku ya Sabato

Siku ya mapumziko kwa Wayahudi

John 9:16

Hawezi kutunza sabato

Hii inamaanisha kuwa hakutii sheria kuhusu Sabato.

Ishara

Miujiza pia yaweza kuitwa ishara kwa sababu imetumika kama viashirio au ushahidi kwamba Mungu ana uwezo wote aliye na mamlaka kamili juu ya ulimwengu.

John 9:19

Waliwauliza wazazi

hapa inamaanisha viongozi wa Wayahudi

yeye ni mtu mzima

yeye ni mwanaume au yeye si mtoto tena

John 9:22

Hofu

Hii inamaanisha hisia zisizokuwa mzuri anazokuwa nazo mtu kama kuna utisho au madhara kwake au kwa wengine

John 9:24

Walimwita mtu

Hapa, "Walimwita" walimaanisha Wayahudi.

Mtu huyu

Hili linarejea kwa Yesu

Mtu yule

Hili linarejea kwa mtu aliyekuwa kipofu

Awe ni mwenye dhambi, mimi sijui

Sijui kama ni mwenye dhambi au la

John 9:26

Sentensi unganishi:

Wayahudi wanaendelea kuongea na mtu aliyekuwa kipofu

Kwa nini mnataka kusikia tena?

Kauli hii ipo katika mfumo wa swali kuelezea kushangazwa kwa yule mtu aliyeponywa awaelezee tena kuhusu kilichotokea.

John 9:30

Hawasikilizi wenye dhambi...humsikiliza

"Hajibu maombi ya mwenye dhambi...Mungu hujibu maombi yake."

John 9:32

Haijasikiwa kamwe kwamba mtu amefungua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu

"Hakuna aliewahi kusikia mtu amefumbua macho"

Ikia mtu huyu hakutoka kwa Mungu, asingefanya chochote

"Ikiwa mtu huyu hakutoka kwa Mungu, asingefanya chochote, lakini ameniponya, kwa hiyo yamkini ametoka kwa Mungu."

ulizaliwa katika dhambi, na wewe sasa unataka kutufundisha sisi?

"Ulizaliwa kamili katika dhambi. Hauna sifa za kutufundisha.

John 9:35

Kuamini

Hii in maana ya kumwamini Yesu, kuamini kwamba, ni Mwana wa Mungu, kumtumaini yeye kama Mwokozi, na kuishi katika njia iletayo heshima kwake.

John 9:39

Ili kwamba wale wasioweza kuona wapate kuona na kwamba wale wanaoona wawe vipofu.

Ili kwamba wale wasioona kwa macho yao wapate kumtambua Mungu na ili kwamba wale ambao wanaona kwa macho yao wasimtambue Mungu.

John 10

Yohana 10 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Kondoo

Kondoo ni taswira ya kawaida inayotumiwa kutaja watu. Katika kifungu hiki, inahusu hasa watu wanaoamini Yesu na kumfuata. Mafarisayo pia wanalinganishwa na mbwa mwitu wanaoiba na kuharibu kondoo.

Kufuru

Ikiwa mtu hujiita Mungu, basi inachukuliwa kuwa ni kufuru. Katika sheria ya Musa, adhabu ya kufuru ilikuwa kupigwa mawe hadi kufa. Hawakuamini Yesu, kwa hiyo wakachukua mawe ili wamwue. Yesu hakuwa na hatia ya kufuru kwa sababu yeye ni Mungu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#blasphemy and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#lawofmoses)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Zizi la kondoo

Mfano uliotumiwa hapa ni kuhusu mahali ambapo kondoo huchungwa. Kungekuwa na mlango au lango ambalo mchungaji angekuwa ameingia ndani ya zizi la kondoo. Kondoo mara moja humtambua. lakini, wizi angeingia ndani ya zizi la kondoo kwa njia nyingine ambayo hawezi kukamatwa. Kondoo watakimbia kutoka mwizi kwa sababu hawakumtambua. Yesu anatumia hii kama mfano wa huduma yake. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

"Ninatoa maisha yangu ili niipate tena"

Ingawa maneno haya hakuwekwa tofauti na mengine, lakini hakika ni unabii uhusu kifo cha Yesu. Inasisitiza kwamba kwa hiari alikufa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

<< | >>

John 10:1

Amini, amini

Itafsiriwe kama ilivyofanyika katika Yoh. 1:49

zizi la kondoo

Hili ni eneo lenye uzio sehemu ambayo mchungaji huwatunza kondoo wake.

Mwizi na mnyang'anyi

Hili ni tumizi la maneno mawili yanayofanana ili kuongeza mkazo

John 10:3

mlinzi wa geti

huyu ni mtu aliyeajiriwa kulinda getini wakati wa usiku

kondoo husikia sauti yake

kondoo husikia na kuelewa sauti yake

John 10:5

Hawakuelewa

Maana inayowezekana: 1) "Wanafunzi hawakuelewa" au 2) Makutano hawakuelewa." Unaweza pia kuiacha kama "hawakuelewa>"

John 10:7

Amini, amini

Tafsiri kama ulivyofanya katika Yoh. 1:49

Mimi ni mlango wa kondoo

"Mimi ni njia wanayoipitia kondoo kwenda zizini." Yesu anasema yeye ndiye anayeruhusu kuingia. Neno "kondoo" limetumika kumaanisha watu wa Mungu.

Wote waliokuja kabla yangu

Hili linarejea kwa walimu wengine waliofundisha kabla ya Yesu.

wezi na wanyang'anyi

Yesu anawaita "wezi na wanyang'anyi" kwa sababu mafiundisho yao yalikuwa ya uongo, na walikuwa wakkijaribu kuwaongoza watu wa Mungu wakati hawaujui ukweli.

John 10:9

Mimi ni mlango

Alimaanisha yeye mwenyewe kama "mlango," Yesu anaonyesha kwamba anatoa njia ya kweli kupata kile zizi la kondoo linawakilisha.

Malisho

Neno "malisho" linamaanisha eneo lenye nyasi mahali kondoo huenda kula.

Hawezi kuja isipokuwa

Hiki ni kinyume mara mbili. Katika lugha zingine ina uasilia zaidi kwa kutumia sentensi chanya.

Ili kwamba wawe na uzima

Neno "wawe" linamaanisha kondoo. "uzima" linamaanisha uzima wa milele.

John 10:11

Mimi ni mchungaji mwema

Mimi nafanana na mchungaji mwema

Huyatoa maisha yake

Kuweka kitu chini maana yake kuondoa uwezo wake. Ni lugha laini yenye kumaanisha kufa.

John 10:14

Mimi ni mchungaji mwema

Mini nafanana na mchungaji mwema

Baba ananijua mimi, nami namjua Baba

Mungu Mwana na Mungu Baba (na Mungu Roho Mtakatifu) wanafahamiana na wote ni nafsi ya Mungu.

Baba

Hiki ni cheo maalumu cha Mungu

Zizi

Kundi la kondoo linalomilikiwa na mchungaji. Neno hili linatokana na neno "Zizi" mahali ambapo kondoo hukaa.

Nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo

Hii ni njia ya upole ya Yesu kusema kwamba atakufa ilikuwalinda kondoo. "Ninakufa kwa ajili ya kondoo."

John 10:17

Anapenda

Aina hii ya upendo hutoka kwa Mungu, na unaelekezwa kwa ajiliya mema ya wengine, hata kama haimfaidii mtu binafsi. Aina hii ya upendo huwajali wengine, haijalishi wamefanya nini.

Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Nami nautoa uhai wangu

Mpango wa Mungu wa milele ulikuwa kwa Mungu Mwanakuutoa uhai wake ili kulipa kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Kifo cha Yesu Msalabani unafunua wenye nguvu wa Mwana kwa Baba na wa Baba kwa Mwana.

Baba

Hiki ni cheo maalumu cha Mungu.

Ninayatoa maisha yangu ili kwamba nipate kuyatwaa tena

Hii ni njia ya upole ya Yesu kusema atakufa na baadaye kuwa mzima tena. "Najiruhusu mwenyewe kufa ili kwamba ninaweza kujirudisha kuwa mzima tena.

John 10:19

Kwa nini mnamsikiliza?

"Msimsikilize"

Je pepo laweza kufumbua macho ya aliyekuwa kipofu?

"Pepo hawezi kumfanya kipofu apate kuona."

John 10:22

Sikukuu ya kuwekwa wakfu

Hii ni siku ya nane, mapumziko ya wakati wa baridi Wayahudi huitumia kukumbuka muujiza wa Mungu alipofanya mafuta kidogo kubaki katika taa mpaka walipopata mafuta mengine baada ya siku nane baadaye. Taa ilitumika kuweka wakfu hekalu la Kiyahudi kwa Mungu. kuweka wakfu kitu ni ahadi ya kukitumia tu kwa kusudi maalumu.

kibaraza

Huu ni muundo uliounganishwa na jengo, ina paa na inaweza kuwa na ukuta ama isiwe nao.

John 10:25

Katika jina la Baba yangu

Hii inamaanisha kuwa Yesu alifanya mambo haya kwa uwezo na mamlaka ya Baba yake. Yesu ni mkamilifu , mtakatifu Mwana w Mungumwenye uwezo wa milele kutoka kwa Baba ili kulipa kwa ajili ya dhambi zote milele na kuokoa na kuwasamehe wote waliomwamini.

Haya yanashuhudia kuhusu mimi

Miujiza yake ilithibitisha kuhusu yeye kama vile shahidi anavyoshuhudia mahakamani.

Siyo kondoo wangu

"Siyo wafuasi wangu" au "siyo wanafunzi wangu" au "siyo watu wangu"

John 10:29

Baba yangu...amewatoa kwangu...hakuna aliye na uwezo wa kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba.

Mungu Baba na Mungu Mwana kwa uwezo wao huwalinda waliookoka.

Baba yangu

Hiki ni cheo uhimu kwa Mungu

Mkono wa Baba

Neno "mkono" linatumika kumaanisha umiliki wa Mungu au madaraka na ulinzi wake.

Mimi na Baba yangu tu umoja

Yesu, Mungu Mwana,na Mungu Baba ni umoja. Wao ni nafsi za Mungu mmoja na wa kweli (pamoja na Roho). Wana umoja katika makusudi, uwezo, mamlaka, huruma na utakatifu. Wao ni Mungu.

John 10:32

Yesu aliwajibu, "Nimeshawaonyesha kazi nyingi nzuri kutoka kwa Baba

Kazi za Yesu zilifanyika katika uwezo wake kama Mwana wa Mungu, katika umoja na Mungu Baba. Kazi za Yesu ni kazi za Baba vile vile (na Roho Mtakatifu).

Baba

Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu

Unajifanya kuwa Mungu

"Alidai kuwa yeye ni Mungu"

Tuna...kuponda mawe kwa...kukufuru, kwa sababu wewe, uliye mtu, unajifanya kuwa Mungu

Yesu alidai kuwa yeye ni Mwana wa Mungu ilikuwa ni kufuru kwa Wayahudi kwa sababu walidhani kuwa Yesu alikuwa akidai kuwa yeye ni Mungu - na ndivyo alivyokuwa.

John 10:34

Ninyi ni miungu

Kwa kawaida neno "mungu" huonyesha "mungu wa uongo" vinginevyo iwe imeandikwa kwa herufi kubwa "M," imaanishayo kwa mmoja Mungu wa kweli. Lakini hapa, Yesu ananukuu maandiko mahali Mungu anawaita wafuasi wake "miungu" kwa sababu amewachagua kumwakilisha duniani.

Je haikuandikwa...miungu?

"Mnapaswa kujua tayari kuwa imeandikwa...miungu"

Maandiko hayawezi kuvunjwa

Maana inayowezekana ni 1) "hakuna atakayebadilisha maandiko." 2) "Maandiko yataendelea kuwa kweli."

'Unakufuru; kwa sababu nilisema, mimi ni Mwana wa Mungu

Wapinzani wa Yesu waliamini kuwa Yesu alikuwa anakufuru alipojiita "Mwana wa Mungu" kwa sababu kusema hivyo ilikuwa ni kudai kuwa sawa na Mungu.

Baba... Mwana wa Mungu

Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu

John 10:37

Baba

Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu

Niaminini

Hapa neno "amini" maana yake ni kukubali au kutumaini kile ambacho mtu huyo amesema ni cha kweli.

Ziaminini kazi

Hapa "Zizminini" maana yake kutumaini kuwa kitu ni cha kweli na kutenda kwa njia hiyo inayoonyesha imani hiyo.

Baba yu ndani yangu na kwamba mimi ni ndani ya Baba

Mungu Baba yuko ndani ya Yesu, Mwana wa Mungu, kwa sababu Mungu Mwana yu ndani ya Baba. Kama nafsi za Mungu, Baba na Mwana wote ni Mungu mmoja wa milele, pamoja na Mungu Roho.

mkono wao

"ufahamu wao." Hii maana ya ke ni kuwa katika nafasi isiyo salama anapoweza kukamatwa.

John 10:40

Yohana kweli hakufanya ishara, lakini mambo yote ambayo Yohana alisema juu ya mtu huyu ni ya kweli.

Ni kweli kwamba Yohana hakufanya ishara, lakini aliongea ukweli juu ya huyu mtu, anayefanya ishara.

Ishara

Miujiza inayothibitisha kwamba kitu fulani ni cha kweli au kinachompa mwingine kuwa na kibali

John 11

Yohana 11 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mwangaza

Mwangaza ni mfano ya kawaida katika Maandiko yaliyotumiwa kuonyesha haki. Mwangaza pia hutumiwa kuonyesha njia ya haki na kuonyesha maisha ya haki. Giza hutumiwa mara nyingi kama mfano wa kuonyesha dhambi au uovu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#light, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#darkness, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#unrighteous)

Mimi ndimi

Yohana anatumia maneno haya mara saba katika injili yake. Ni maneno sawa yanayotumiwa na Mungu, alipojidhihirisha pamoja na jina lake Yahweh katika kichaka kilichokuwa kinawaka. Jina "Yahweh" linaweza kutafsiriwa kama "Mimi ndimi."

Pasaka

Sura hii inaeleza kuwa Yesu hakutembea tena waziwazi kati ya Wayahudi. Kwa hiyo, Mafarisayo walisubiri kumtafuta wakati wa Pasaka. Ilikuwa ni wajibu wa Wayahudi, waliokuwa na uwezo, kwenda Yerusalemu wakati wa sherehe ya Pasaka. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#passover)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

"Mtu mmoja anapaswa kufa kwa ajili ya watu"

Kayafa akasema, "Ni vyema kwenu kwamba mtu mmoja afe kwa ajili ya watu badala ya kuwa taifa lote lipotee." Ni ajabu kwamba Yesu angekuja kufa kwa ajili ya dhambi za taifa na ulimwengu wote. Maneno haya ni kama unabii kuhusu kifo cha Yesu kwa ajili ya dhambi. Hiki ni kitu ambacho kuhani mkuu pia anatabiri kuhusu baadaye katika sura hii. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-irony and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Kama ungalikuwa hapa"

Maria na Martha walimwamini Yesu lakini hawakuelewa kikamilifu yeye ni nani. Katika kifungu hiki, hawakutambua kwamba alikuwa na nguvu juu ya kifo yenyewe na angeweza kumfufua Lazaro kutoka kwa wafu ikiwa angependa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

<< | >>

John 11:1

Maelezo ya jumla:

Hii ni habari inayomhusu Lazaro. Mistari hii inamtambulisha yeye na kutoa historia fupi juu yake na dada yake Mariamu.

Ni Mariamu ndiye aliyempaka Bwana mafuta...nywele zake

Yohana pia anamtambulisha Mariamu, dada yake na Matha.

John 11:3

aliomba Yesu aje

"alitaka Yesu aje kwake"

upendo

Hapa "upendo" inamaanisha upendo wa ndugu, wa asili, upendo wa kibinadamu kati ya marafiki na ndugu.

Kifo

Hii inamaanisa kifo cha kimwili

badala yake kwa utukufu wa Mungu ili kwamba Mwana wa Mungu apate kutukuzwa katika hilo

Yesu kama Mwana wa Mungu, amepokea utukufu ule ule kama wa Mungu

Mwana wa Mungu

Hili ni jina muhimu kwa Yesu

John 11:5

Sasa Yesu alimpenda Martha na dada yake pamoja na Lazaro

Haya ni maneno ya utangulizi

John 11:8

Rabi, Wayahudi walikuwa sasa wanatafuta kukuponda mawe, na unarudi tena huko?

"Mwalimu, kwa hakika huhitaji kurudi huko! Wayahudi wanajaribu kukuponda mawe.!"

Je hakuna masaa kumi na mbili ya mchana?

"Unajua kwamba siku ina masaa kumi na mbili za mchana

John 11:10

Nuru haimo ndani yake

Maana halisi 1) "hawezi kuona" au 2) hawezi kuona"

Rafiki yetu Lazaro amelala

Lazaro amekufa lakini kwa ajili ya muda mfupi tu.

Lakini ninaenda ili kwamba nipate kumwamsha kutoka usingizini

Yesu anaufunua mpango wake wa kumfufua Lazaro.

John 11:12

Maelezo ya jumla

Katika mustari wa 13 kuna kituo katika mtiririko wa habari kama ambavyo Yohana unaongelea kuhusu wanafunzi wa Yesu kutokuelewa kile ambacho Yesu alimaanisha aliposema kuwa Lazaro amelala.

kama amelala

Wanafunzi walidhani kuwa Lazaro amepumzika tu na baadaye ataamka.

John 11:15

Sentensi unganishi:

Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake

kwa ajili yenu

kwa faida yenu

John 11:17

Maelezo ya jumla:

Kwa sasa Yesu yupo Bethania.

alimkuta Lazaro tayari alikuwa kaburini kwa muda wa siku nne

Unaweza kutafasiri hivi pia, "alijua kwamba watu walikuwa wamekwisha kumweka Lazaro kaburini kwa muda wa siku nne kabla ya yeye kufika"

kuhusiana na kaka yao

Lazaro alikuwa kaka yao mdogo

John 11:21

Kaka yangu asingalikufa

"Kaka yangu angeendelea kuwa mzima"

Fufuka tena

Maana yake kumfanya mtu aliyekufa kuishi tena

John 11:24

Ajapokufa

Hapa "kufa" inamaanisha kifo cha kimwili

Bado ataishi

Hapa "Ishi" linamaanisha uzima wa kiroho

Naye aishiye na kuniamini hatakufa kamwe

Na wote waniaminio mimi hawatatengwa kamwe milele kutoka kwa Mungu.

Hatakufa kamwe

Hapa "kufa" inamaanisha kifo cha kiroho

John 11:27

Ndiyo, Bwana, ninaamini kwamba wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu, yeye... ajaye katika ulimwengu.

Martha aliamini kwamba Yesu ni Bwana, Kristo (Masihi), Mwana wa Mungu.

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo maalumu cha Yesu.

Mwalimu

Cheo hiki kinamhusu Yesu

John 11:30

Anguka chini ya miguu yake

Mariamu alilala chini au alipiga magoti katika miguu ya Yesu kuonyesha heshima

Kama ungelikuwa hapa, kaka yangu asingelikufa

Angalia hili ulivyotafsiri katika Yoh. 11:21

John 11:33

alisikitika sana moyoni mwake na roho yake iliumia

Yohana anatumia sentensi hizi mbili kuelezea uzito wa maumivu ya moyo ambayo Yesu aliyapata.

Mme mweka wapi

Hii ni njia nyingine ya kuuliza, "mmemzika wapi?"

Yesu akalia

Yesu alianza kulia

John 11:36

Mpendwa

Hili linamaanisha juu ya upendo wa ndugu au upendo wa kibinadamu kwa rafiki au mtu wa familia.

isingefaa huyu mtu, aliyefungua macho ya yule aliyekuwa kipofu, hakuweza kumfanya mtu huyu asife?

Aliweza kumponya mtu aliyekuwa kipofu, kwa hiyo angeweza pia kumponya mtu huyu ili kwamba asife." au "Hakuweza kumfanya mtu huyu asife, kwa hiyo tunajua kuwa hakumponya kweli mtu aliyezaliwa kipofu kama wanavyosema alifanya."

Kufungua macho

Kuponya macho

John 11:38

Je sikusema kwamba, ikiwa utaamini, utauona utukufu wa Mungu?

"Kumbuka kwamba nilikuambia, ikiwa utaniamini, utaona ni kwa jinsi gani Mungu ni Mkuu

mpaka muda huu mwili wake utakuwa umeoza

mpaka muda huu kutakuwa na harufu mbaya

John 11:41

Baba, ninakushukuru kwamba umenisikiliza

Yesu alikuwa akiomba moja kwa moja kwa Baba kama ushuhuda kwa waliokuwa pamoja naye

Baba

Hiki ni cheo maalumu kwa Mungu

John 11:43

Amefungwa mikono na miguu kwa nguo za kuzikia, na uso wake ulikuwa umefungwa kwa nguo.

Utamaduni wa kuzika kwa wakati huu ulikuwa wa kuufunga mwili wa marehemu kwa nguo ndefu za kitani

Yesu aliwaambia

Neno "wao" linamaanisha juu ya watu waliokuwa pale na kuona muujiza.

John 11:45

Maelezo ya jumla

Mistari hii inatuambia mambo yaliyotokea baada ya Lazaro kufufuliwa kutoka wafu.

John 11:47

Maelezo ya jumla

Hii ni sehemu ya pili ya simulizi. Kuhani mkuu pamoja na Mafarisayo wanakutana kwa ajili ya kikao cha baraza la Kiyahudi

Kisha makuhani wakuu

kisha viongozi kati ya makuhani

wote wataishi ndani yake

Viongozi wa Kiyahudi waliogopa kwamba watu wangemfanya Yesu kuwa mfalme wao.

John 11:49

Haujui chochote kabisa

"Hauelewi ni itu gani kinatendeka" au Haujui nini cha kufanya lakini mimi najua."

mtu mmoja kati yao

Hii ni njia ya kumtambulisha mhusika mpya katika simulizi.

John 11:51

kufa kwa ajili ya taifa

Neno "taifa" linatumika kuonyesha watu wa taifa la Israel.

Watoto wa Mungu

Hili linamaanisha watu wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu na ni watoto wake wa kiroho.

John 11:54

Maelezo ya jumla:

Yesu anaondoka Bethania na kwenda Efraimu.

tembea kwa uhuru mbele ya Wayahudi

Hapa anaongelea viongozi wa Kiyahudi.

nchi

hili ni eneo nje ya mji ambapo watu wachache wanaishi.

John 11:56

Walikuwa wakimtafuta Yesu

Neno "Walikuwa" linawazungumza Wayahudi waliosafiri kuja Yerusalemu.

Unafikiri nini? Kwamba hawezi kuja katika sikukuu?

Mzungumzaji hapa alikuwa akishangaa ikiwa Yesu atakuja katika sikukuu ingawa kulikuwa na hatari ya kukamatwa. Aliwauliza wengine waliomzunguka kuhusiana na mawazo yao. "Mnafikiri Yesu anaweza kuwa woga sana kuja katika sikukuu?"

Sasa wakuu wa makauhani

Haya ni maelezo ya nyuma ambayo yanaelezea kwa nini waabudu wa Kiyahudi walikuwa wakishangaa ikiwa Yesu atakuja katika sikukuu au la. Ikiwa lugha yako inayo njia ya kuweka alama ya maelekezo ya nyuma fanya hivyo.

John 12

Yohana 12 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka nukuu za Agano la Kale. Tafsiri ya ULB na nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari ya 12:38 na 40, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Mstari wa 16 ni ufafanuzi juu ya matukio haya. Inawezekana kuweka mstari huu mzima kwa mabano ili kuonyesha tofauti na maelezo ya habari.

Dhana maalum katika sura hii

Upako

Ilikuwa ni desturi kupaka mafuta mwili katika maandalizi ya kuizika. Hii kwa kawaida haingefanyika mpaka baada ya kifo cha mtu. Hii haikuwa nia ya Maria. Yesu anatumia matendo ya Maria kutabiri kuhusu kifo chake kilichokuwa kinakaribia. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#anoint, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

Punda

Jinsi ambavyo Yesu aliingia Yerusalemu, akiwa amepanda mnyama, ilikuwa sawa na vile ambavyo mfalme angeingia katika mji baada ya ushindi mkubwa. Na kwa wafalme wa Israeli, ilikuwa desturi kupanda punda badala ya farasi. Mathayo, Marko, Luka, na Yohana wote waliandika juu ya tukio hili, lakini hawakupa maelezo sawa. Mathayo aliandika kuhusu kuwepo kwa punda na mwana-punda, lakini haijulikani ni yupi ambaye Yesu alipanda. Ni bora kutafsiri kila moja ya vifungu hivi kama inavyoonekana katika ULB bila kujaribu kuwafanya wote kusema jambo sawa. (Angalia: Mathayo 21: 1-7 na Marko 11: 1-7)

Mwangaza

Mwangaza ni mfano ya kawaida katika Maandiko yaliyotumiwa kuonyesha haki. Mwangaza pia hutumiwa kuonyesha njia ya haki na kuonyesha maisha ya haki. Giza hutumiwa mara nyingi kama mfano ya kuonyesha dhambi au uovu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#light, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#darkness, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#unrighteous)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

"Ili atukuzwe"

Unabii wa Yesu kuhusu kutukuzwa kwake ni maelezo juu ya kifo chake. Wanafunzi hawakuelewa kwamba kifo chake kingemtukuza, lakini kilifanyika vivyo hivyo. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#glory and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-irony)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kitendawili

Kitendawili ni taarifa inayoonekana kuwa ya ajabu, ambayo ni kana kwamba inajikana yenyewe, lakini kwa hakika sio ya ajabu. Kitendawili kinatokea katika 12:25: "Yeye anayependa maisha yake ataipoteza, lakini anayechukia maisha yake katika ulimwengu huu ataichunga kwa uzima wa milele." Lakini katika 12:26 Yesu anaelezea maana ya kuchunga maisha ya mtu kwa ajili ya uzima wa milele. (Yohana 12: 25-26).

<< | >>

John 12:1

Litra

Litra ni kipimo cha uzito - paundi ya Kirumi ni sawa na gramu 327.5

Manukato

Hiki ni kimiminika chenye harufu nzuri kilichotengezwa kwa mafuta ya miti na maua yanayonukia vizuri.

nardo

Haya ni manukato yaliyotengenezwa kutokana na maua yanayopatikana katika milima ya Nepali, China, na India.

nyumba yote ilijaa harufu ya manukato

"harufu nzuri ya manukato yake iliijaza nyumba"

John 12:4

yeye ambaye angemsaliti Yesu

"Yeye ambaye baadaye aliwasaidia maadui wa Yesu kumkamata"

Basi alisema hivi...chukua baadhi ya vilivyomo ndani kwa ajili yako

Yohana anaeleza kwanini Yuda aliuliza swali kuhusu maskini.

aliyasema haya, sio kwasababu aliwahurumia maskini, bali kwasababu alikuwa mwizi

"alisema hivi kwasababu alikuwa mwizi. Hakuwajali maskini"

John 12:7

mwache atunze alicho nacho kwa ajili ya siku ya maziko yangu

Yesu anaeleza kuwa matendo ya yule mwanamke yanaweza kueleweka kama tazamio la kifo na maziko yake

maskini mtakuwa nao siku zote

Yesu anamaanisha kuwa mtakuwa na nafasi ya kuwasaidia maskini siku zote

lakini hamtakuwa na mimi siku zote

Kwa njia hii Yesu anasema kwamba atakufa

John 12:9

Basi

Neno hili limetumika hapa kuonesha kituo katika simulizi. Hapa Yohana anaelezea kundi jipya la watu katika simulizi.

kwasababu yake

Ukweli kwamba Lazaro alikuwa hai kulisababisha Wayahudi wengi wamwamini Yesu.

Walimwamini Yesu

Hii inamaanisha "walimwamini Yesu"; hivi, waliamini kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, kumwamini yeye kama Mwokozi, na kuishi kwa kumheshimu yeye.

John 12:12

Hosana

Hii inamaanisha "Mungu aokoe."

Mbarikiwa

Hii huelezea hamu ya kutaka Mungu afanye mambo mazuri kwa mtu huyo.

ajae kwa jina la Bwana

Kuja kwa jina la mtu fulani humaanisha kutumwa kwa mamlaka na nguvu zake, au kuja kama mwakilishi wake.

John 12:14

binti Sayuni

"Binti Sayuni" ni neno linalomaanisha Israeli, kama vile "wana wa Israeli" au "watu kutoka Yerusalemu."

kama ilivyoandikwa

Unaweza kutafasiri hivi, "kama ambavyo manabii waliandika katika maandiko."

John 12:16

wakati Yesu alitukuzwa

"wakati Mungu alimtukuza Yesu"

walikumbuka ya kuwa mambo haya aliandikiwa yeye

Yohana, mwandishi, anafafanua hapa ili kumpa msomaji taarifa za jinsi mitume walivyoelewa baadaye.

John 12:17

ishara hii

Hili ni tukio au tokeo linalodhihirisha kuwa jambo fulani ni la kweli; kwa hali hii, inathibitika kuwa Yesu ni Masihi.

tazama, ulimwengu umekwenda kwake

"inaonekana kuwa kila mtu anakuwa mwanafunzi wake"

ulimwengu

neno hili limaanisha watu wote duniani

John 12:20

kisha baadhi ya Wayunani

hii inatoa utambulisho wa wahusika wapya katika simulizi

kuabudu katika sherehe

Yohana anamaanisha kuwa Wayunani walikuwa wanaenda kumwabudu Mungu wakati wa Pasaka.

Bethsaida

huu ulikuwa mji katika jimbo la Galilaya

na kisha wakamwambia Yesu

Filipo na Andrea wakamwambia Yesu kuhusiana na Wayunani walioomba kukutana naye.

John 12:23

Maelezo ya jumla:

Yesu anaanza kuwajibu Filipo na Andrea.

Amini, amini, nawaambia, chembe ya ngano isipoanguka katika nchi ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, itazaa matunda mengi.

"Kuwa makini zaidi na mfano huu ninaowaambia. Uhai wangu ni kama mbegu iliyopandwa katika nchi na kufa. Kama isipopandwa, hubakia mbegu moja tu. Lakini ikipandwa, hubadilika na kukua kwa kuzaa mbegu nyingi zaidi."

John 12:25

Yeye apendaye uhai wake ataupoteza; bali yeye auchukiaye uhai wake katika ulimwengu huu atausalimisha hata uzima wa milele.

"Kwa jinsi iyo hiyo, yeyote apendaye mapenzi yake, huyaharibu maisha yake. Bali yeye asiyefuata mapenzi yake, kwasababu ya utii kwangu, ataishi na Mungu milele."

anapenda maisha yake...huchukia maisha yake

Hii inamaanisha uzima wa mwili.

John 12:27

Niseme nini? Baba, niokoe mimi na saa hii?

Hii ni lugha ya balagha. Japokuwa Yesu anatamani kuepuka mateso, bado anachagua kumtii Mungu na kuuawa.

Baba

Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu

saa hii

Hii inamaanisha wakati Yesu atateswa na kufa msalabani.

ulitukuze jina lako

ufunue utukufu wako (Mungu) ili ujulikane

sauti ikaja kutoka mbinguni

Mungu aliongea kutoka mbinguni

John 12:30

Maelezo ya jumla

Yesu anaelezea sababu za sauti kutoka mbinguni

Sasa ni wakati wa hukumu ya ulimwengu

ulimwengu humaanisha watu wote walio duniani

sasa mtawala wa dunia hii atatupwa nje

mtawala wa dunia hii ni Shetani

John 12:32

Maelezo ya jumla:

Katika mstari wa 33 Yohana anaeleza historia ya maneno ya Yesu aliposema habari za kuinuliwa juu.

nitakapoinuliwa juu kutoka katika nchi

Hapa Yesu anamaanisha kusulubiwa kwake.

nitawavuta wote kwangu

Kwa kusulubiwa kwake, Yesu atafanya njia kwa ajili ya kila mmoja kumwamini yeye.

John 12:34

Mwana wa Mtu ni lazima atainuliwa juu

Neno "kuinuiwa juu" maana yake ni kusulubiwa.

Huyu mwana wa Mtu ni nani?

Maana yake ni, sifa za mwana wa mtu ni zipi?

John 12:37

Maelezo ya jumla:

Yohana anaanza kuongelea juu ya kutimizwa kwa unabii ambao nabii Isaya alitabiri.

ili kwamba neno la nabii Isaya litimizwe

kwa ajili ya kutimiza ujumbe wa nabii Isaya

mkono wa Bwana

Hii inamaanisha, uwezo wa Bwana wa kuokoa kwa nguvu.

John 12:39

ameifanya mioyo yao kuwa migumu

Huu ni msemo wenye maana kwamba Mungu amewafanya kuwa wasumbufu

mioyo yao kuelewa

Wayahudi waliamini kuwa moyo ndicho kiungo kinacholeta uelewa

John 12:41

ili kwamba wasifukuzwe katika Sinagogi

ili kwamba watu wasiwazuie kwenda kwenye Sinagogi

Walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu

Walitaka watu wawasifie zaidi kuliko Mungu

John 12:44

Maelezo ya jumla

Huu ni wakati mwingine ambapo Yesu anaanza kuongea na makutano

Yesu alilia na kusema

Hii inamaanisha kuwa Yesu alipiga kelele na kusema

yeye anionaye mimi amemwona yule aliyenituma

"yeye" hapa inamaanisha "Mungu"

John 12:46

Sentensi unganishi:

Yesu anaendelea kuongea na makutano

Nimekuja kama nuru

Hii inamaana ya "Nikuja kuwaonesha iliyo kweli"

wasibaki gizani

"giza" hapa humaanisha kuishi katika ujinga wa kutokujua kweli ya Mungu.

John 12:48

katika siku ya mwisho

wakati ambapo Mungu atahukumu dhambi za watu

Nami najua ya kuwa amri yake ni uzima wa milele

Nami najua ya kuwa maneno aliyoniagiza mimi kusema ni maneno yaletayo uzima milele.

Baba

Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu

John 13

Yohana 13 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Matukio ya sura hii hujulikana kama chakula cha jioni la mwaisho au Meza ya Bwana. Sikukuu ya Pasaka kwa njia nyingi inafanana na dhabihu ya Yesu kama kondoo wa Mungu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#passover)

Dhana maalum katika sura hii

"Kuosha miguu ya wanafunzi"

Miguu ilioneka kuwa chafu sana katika inchi ya kale ya Mashariki ya Karibu. Ilikuwa ni kawaida mtumishi kuwa na jukumu la kuosha miguu ya bwana wake. Hatua hii ingechukuliwa kuwa cha aibu kwake Yesu, na ndiyo sababu wanafunzi hawakutaka afanye hivyo. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-explicit)

Kuosha

Taswira ya kuosha hutumiwa hapa usiku wa kifo cha Yesu. Ni Yesu ambaye anaweza kuwasafisha watu. Taswira hii inawakilisha uwezo wa "kufanya haki." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#clean and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous).

Mimi ndimi

Yohana anatumia maneno haya mara saba katika injili yake. Ni maneno sawa yanayotumiwa na Mungu, alipojidhihirisha pamoja na jina lake Yahweh katika kichaka kilichokuwa kinawaka. Jina "Yahweh" linaweza kutafsiriwa kama "kama Mimi ndimi." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#reveal)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.'

<< | >>

John 13:1

Maelezo ya jumla

Kipindi hiki siyo cha Pasaka lakini tayari Yesu ameketi na wanafunzi wake mezani.

mpendwa

Hii ni aina ya upendo utokao kwa Mungu

Baba

Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu

John 13:3

Sentensi unganishi

Mstari wa 3 unaendelea kutufahamisha mambo ambayo Yesu aliyajua.

alivitoa vitu vyote kwa mkono wake

Hapa 'Mkono" unamaanisha mamlaka

alitoka kwa Mungu na alikuwa anarejea kwa Mungu

Yesu alikuwa na Baba siku zote, na angerudi kwake baada ya kumaliza kazi yake hapa duniani.

John 13:6

Bwana, unataka kuniosha miguu yangu?

Swali la Petro linaonesha kwamba hayupo tayari kuosha miguu yake na Yesu.

Kama sitakuosha miguu, basi hauna shirika nami

Yesu anatumia maneno magumu kumshawishi Petro akubali kuoshwa miguu.

John 13:10

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuongea na Simoni Petro

Maelezo ya jumla:

Yesu anatumia neno "ninyi" kumaanisha wanafunzi wake wote.

John 13:12

Je mwajua nimefanya nini kwenu?

Yesu anajaribu kusisitiza mafundisho yake kwa wanafunzi wake

Ninyi mnaniita mimi 'mwallimu' na 'Bwana'

Yesu anamaanisha kuwa wanafunzi wake wanamheshimu sana.

John 13:16

Sentensi unganishi:

Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake

mkubwa

wa muhimu zaidi

umebarikiwa

kubariki hapa kuna maana ya kusababisha vitu vizuri, vyenye faida kumpata mtu.

John 13:19

nawaambieni sasa kabla haijatokea

Ninawaambieni sasa yale yatakayotokea kabla hayajatokea

mpate kuamini kuwa MIMI NDIYE

mpate kuamini ya kuwa Mimi ndiye niliyesema kuwa Nipo

John 13:21

mwenye shida

nisiye na furaha

amini, amini

Tazama tafasiri katika 1:49

John 13:23

mmoja wa wanafunzi ambao Yesu alimpenda

Hii inamaanisha Yohana

kifua cha Yesu

kuweka kichwa kwenye kifua cha mwingine ilikuwa utamaduni mwingine wa Kiyunani uliomaanisha urafiki wa karibu

John 13:26

Iskarioti

Hii inamaanisha kuwa Yuda alitoka katika kijiji cha Keriothi

Shetani akamwingia

Hii inamaana kwamba Shetani alimteka na kumwongoza

John 13:28

kwamba awape maskini kitu

Unaweza kutafasiri hii kama, "Nenda na uwape maskini fedha"

aliondoka na kwenda haraka. Ilikuwa usiku

Yohana anamaanisha hapa kwamba Yuda angefanya uovu wake gizani wakati wa usiku

John 13:31

sasa mwana wa Mtu ametukuzwa na Mungu ametukuzwa ndani yake

Unaweza kutafasiri hii hivi, "Sasa watu wataona jinsi ambavyo mwana wa Mtu atapokea heshima na jinsi ambavyo Mungu atapokea heshimu kupitia yale anayoyafanya mwana wa Mtu."

watoto wadogo

Yesu anatumia neno watoto wadogo kumaanisha kwamba aliwapenda wanafunzi wake kama watoto wake.

kama nilivyosema kwa Wayahudi

Hii inamaanisha viongozi wa Kiyahudi

John 13:34

Sentensi unganishi:

Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake

upendo

Hii ni aina ya upendo utokao kwa Mungu wenye kuleta mema kwa wengine

kila mtu

Hii ni hali ya kutia chumvi katika usemi kwamba kwa kila mtu aonaye upendo wa wanafunzi wake.

John 13:36

kuweka chini uhai wangu

kuutoa uhai wangu au kufa

Je utautoa uhai wako kwa ajili yangu?

Hii ni hali ya kuweka mkazo katika sentensi kwamba "wewe unasema utautoa uhai wako kwa ajili yangu..."

John 14

Yohana 14 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Nyumba ya Baba yangu"

Hii sio kurejelea hekalu. Lakini, ni kurejelea makao ya Mungu mbinguni. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#heaven)

Mfariji

Hili ni jina lingine la Roho Mtakatifu, pamoja na "Roho wa Kweli." Alikuwa tayari ulimwenguni, lakini angekuja kwa njia maalum, kukaa kati ya Wakristo, milele. Yesu na Roho Mtakatifu wote ni Mungu; kwa sababu ya ukweli huu, mtu anaweza kusema kwamba Yesu atakaa katika Wakristo baada ya kifo chake. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#holyspirit)

<< | >>

John 14:1

Usiruhusu moyo wako kuwa katika mahangaiko.

Huu ni msemo wenye maana kwamba , "acha kuogopa na kuwa na mashaka"

Katika nyumba ya Baba yangu kuna makazi mengi...

Mungu Baba ametayarisha eneo mbinguni kwa kila mtu ambaye ni muumini, kuishi pamoja naye na Mwanawe milele.

Baba

Hiki ni cheo cha muhimu kwa ajili ya Mungu.

John 14:4

Je! Twawezaje kuijua njia?

"Je! Tunawezaje kujua namna ya kufika pale?"

njia

Hii inaweza kuwa 1)"njia kwa Mungu" au 2) "mtu yule awapelekaye watu kwa Mungu."

kweli

Hii inaweza kuwa 2) "mtu wa kweli" au 2) "mtu anayenena maneno ya kweli."

uzima

"mtu ambaye anaweza kuwafanya watu wawe hai."

Yesu alimwambia, "Mimi ni njia, kweli, na uzima; hakuna mmoja wenu huja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu

Yesu, Mwana wa Mungu, ni njia pekee kwenda kwa Mungu Baba.

Baba

Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu.

John 14:8

Je! Sijakuwa pamoja nanyi kwa muda mrefu, na bado hunijui mimi, Philipo?

"Nimekuwa tayari pamoja nanyi wanafunzi kwa muda mrefu sana. Wewe, Philipo ungenijua mimi kwa wakati huu."

Jinsi gani unasema, 'Tuonyeshe Baba?

"hivyo wewe, Philipo, hakika usingekuwa unasema, 'Tuonyeshe Baba."

Bwana, tuonyeshe Baba...

Kumwona Mungu Mwana, Yesu, ni kumwona Mungu Baba.

John 14:10

Hamniamini mimi?

"Hakika mngeamini kuwa Baba yu ndani yangu."

Baba

Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu.

Maneno ninayoyasema kwenu sisemi kwa mamlaka yangu mwenyewe

"Ujumbe ninaowaambia hautokani na mawazo yangu mwenyewe."

Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yangu yu ndani yangu

Kumwamini Yesu, Mwana wa Mungu, ni kuwamini Mungu Baba. Nafsi za Mungu ziko kwa kila yeyote kwasababu kila nafsi ya Mungu na zote katika Mungu, kupitia nafsi hizo zi tofauti kutoka kila moja.

John 14:12

amini, amini

Hii ina maana ya kumwamini Yesu, ndiyo kwamba, Kuamini kwamba ni Mwana wa Mungu, kumtumaini yeye kama Mwokozi, na kuishi katika njia ambayo inamweshimu yeye.

Chochote mkiombacho katika jina langu, nitafanya

Hii ni hali ya kuonesha ukuu na uwezo wa Yesu

Baba...Mwana

Hivi na vyeo muhimu vikielezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

John 14:15

Mfariji

Neno linaelezea Roho Mtakatifu, "ambaye atakuja karibu kuwasaidia." Kuwafundisha wanafunzi

Roho wa Kweli

Roho Mtakatifu

ambaye ulimwengu hautampokea

Hapa neno "ulimwengu" linamaanisha watu wasioamini. Watu walio kinyume na Mungu.

John 14:18

Ulimwengu

Watu ambao hawajamwamini Mungu

mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba

Kuamini kwa kweli katika Kristo, Baba na Mwana huishi ndani ya muumini kupitia Roho.

Baba yangu

Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu

John 14:21

kupenda

Aina ya upendo huu huja kutoka kwa Mungu na unalenga kufanya mema kwa wengine, hata kama hautafaa kwa mhusika. Aina ya upendo huu hujari wengine, haijalishi wanafanya nini.

Yeyote anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu

Wakati mmoja anampenda Yesu, naye Baba ampenda mtu yule.

Baba yangu

Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu.

Yuda (Siyo Iskarioti)

Huyu ni Yuda mwingine si yule aliyemsulubisha Yesu.

John 14:23

Sentensi unganishi:

Yesu anamjibu Yuda (Siyo Iskarioti)

Baba yangu

Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu

Neno ambalo mwasikia silo langu bali la Baba ambaye kanituma.

Yesu anasema kwamba yale ayasemayo yatoka kwa Baba. Ujumbe wa Yesu pia ni ujumbe wa Baba kwasababu Baba na Mwana wanakubaliana kikamilifu siku zote

Neno

Hii inaweza pia kuwa ujumbe

John 14:25

Mfariji

Roho Mtakatifu

Ulimwengu

Neno linaelezea watu wa ulimwengu huu.

Katika jina langu

Neno hapa "Jina" linaelezea juu ya nguvu na mamlaka ya Yesu

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.

John 14:28

Mpendwa

Aina ya upendo huu kutoka kwa Mungu unalenga kuwatendea mema wengine, hata wakati usipomfaidia mwenyewe. Upendo wa aina hii unajali wengine, bila kujali wanafanya nini.

Baba ni mkuu kuliko mimi

Mungu Baba ni mkuu kuliko Yesu, aliyekuwa akipitia kudharauliwa kama mwanadamu, lakini umilele, kama nafsi ya Mungu, wote wako sawa

Baba

Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu

John 15

Yohana 15 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mzabibu

Mzabibu ni mfano muhimu katika maandiko. Sura hii inaunda mfano mgumu na uliopanuliwa. Masuala mbalimbali ya mfano huu na jinsi hutumiwa italetea watafsiraji magumu katika lugha zote. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Mimi ndimi

Yohana anatumia maneno haya mara saba katika injili yake. Ni maneno sawa yanayotumiwa na Mungu, alipojidhihirisha pamoja na jina lake Yahweh katika kichaka kilichokuwa kinawaka. Jina "Yahweh" linaweza kutafsiriwa kama "Mimi ndim." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#reveal)

<< | >>

John 15:1

Sentensi unganishi

Simulizi inaendelea. Yesu anaketi mezani pamoja na wanafunzi wake

Mimi ni mzabibu wa kweli

Yesu anajilinganisha mwenyewe na mzabibu kwa kuwa yeye ni chanzo cha uzima.

Baba yangu ndiye mkulima

Hii inamaanisha "Mungu" ni kama mkulima

John 15:3

kaeni ndani yangu

endeleeni kukaa/kuungana na mimi, nami nitaendelea kukaa na ninyi.

mpaka mtakapokaa ndani yangu

Hii ni hali ya kundelea kumtegmea Yesu

Ninyi

Neno hili limetumika katika wingi

John 15:5

Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi

Mzabibu unamwakilisha Yesu. Matawi yanawakilisha wale wote wanaomwamini Yesu.

Yeye akaaye ndani yangu nami ndani yake

Yesu anajaribu kueleza kuwa wanafunzi wake wameunganisha na yeye kama yeye alivyounganishwa nao

huzaa sana

Hii inamwelezea muumini anayempendeza Mungu kwamba kama vile tawi lizaalo sana.

ombeni lolote mtakalo

Yesu anawaambia waumini kwamba ni lazima wamuombe Mungu ajibu maombi yao.

John 15:8

Baba yangu anatukuzwa katika hili

Unaweza kutafasiri hii kama, "Inawafanya watu wamuheshimu Baba yangu"

Baba yangu

Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu

ya kwamba mzae matunda mengi

hapa matunda yametumika badala ya maisha yanayompendeza Mungu

ni wanafunzi wangu

dhihirisheni ya kuwa mu wanafunzi wangu

dumuni katika pendo langu

endeleeni kupokea upendo wangu

John 15:10

Ikiwa mtazishika amri zangu, mtadumu katika pendo langu kama nilivyozshika amri za baba yangu na kudumu katika pendo lake.

Wanafunzi wanapomtii Yesu, wanaonesha upendo wao kwake.

Baba yangu

Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu

ili kwamba furaha yenu ifanyike kuwa timilifu

Unaweza kutafsiri hii kama, "ili furaha yenu itimie."

John 15:12

Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu

Upendo wa aina hii unatoka kwa Mungu na unawafaidia wengine pasipo kujali matendo yao.

Uhai

uzima wa kimwili

John 15:14

Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo

Mnaonesha ya kuwa mu rafiki zangu ikiwa mtaendelea kufanya yae niliyowaagiza

nimewajulisha mambo yote ambayo nimesikia kutoka kwa Baba

Nimewaambia kila kitu ambacho Baba yangu aliniambia.

Baba yangu

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu

John 15:16

Hamkunichagua mimi

Yesu anasema kuwa wanafunzi wake hawakuchagua wenyewe kuwa wanafunzi

nendeni mkazae matunda

hii inamaanisha kuishi maisha yanayompendeza Mungu

kwamba matunda yenu yapate kukaa

matokeo ya matendo yenu yadumu milele

lolote muombalo kwa Baba kwa jina langu, atawapeni

"jina langu" ni kiwakilishi cha mamlaka ya yesu.

Mambo haya ninawaagiza, kwamba mpendane kila mtu na mwenzake

Upendo wa aina hii unatoka kwa Mungu na unawafaidia wengine pasipo kujali matendo yao.

John 15:18

kama ulimwengu utawachukia....

Yesu anatumia neno Ulimwengu kumaanisha watu ambao hawamwamini Mungu

upendo

Hii inarejea upendo wa kibinadamu, wa undungu, rafiki au mtu wa familia

John 15:20

Kumbukeni neno ambalo niliwaambia

Hii ni sawa na kusema kumbukeni ujumbe niliowaambia

kwa ajili ya jina langu

kwa sababu ni watu wangu

John 15:23

Yeye anichukiaye mimi humchukia Baba yangu pia ..... wameona na wamenichukia mimi na Baba yangu

Kumchukia Mungu mwana ni kumchukia Mungu Baba pia.

wangelikuwa hawana dhambi

wasingekuwa wamefanya dhambi

sheria

Hii inamaanisha Agano la Kale lote ambalo lilikuwa na maagizo yote ya Mungu kwa wanadamu

John 15:26

Mfariji

Hii inamaanisha Roho Mtakatifu

Roho wa Kweli

Roho ambaye atawaambia kweli yote

Ninyi pia mnashuhudia

Kushuhudia ni kuwaambia wengine habari za Yesu

Mwanzo

Hii inamaanisha siku za mwanzo za huduma ya Yesu.

John 16

Yohana 16 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mfariji

Hili ni jina lingine la Roho Mtakatifu, pamoja na "Roho wa Kweli." Alikuwa tayari ulimwenguni, lakini angekuja kwa njia maalum, kukaa kati ya Wakristo, milele. Yesu na Roho Mtakatifu wote ni Mungu; kwa sababu ya ukweli huu, inaweza kusemekana kwamba Yesu atakaa katika Wakristo baada ya kifo chake. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#holyspirit)

"Saa inakuja"

Haya ni maneno ambayo yanaweza pia kutafsiriwa kama "wakati unakuja." Yesu anaelezea wakati baada ya kifo chake kama saa hii itakapokuja. Ukitumia maneno haya, yataweza kuonekana kama unabii. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet)

Mifano muhimu za usemi katika sura hii

Mfan

Yesu analinganisha kifo chake na maumivu ya mwanamke anayezaa. Ni kwa maumivu ambapo maisha mapya huja. wakati wa mfano huu kusemwa, hakuna hakika ya wasikilizaji kuelewa mfano huu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

<< | >>

John 16:1

Sentensi unganishi:

Yesu ameketi chakulani na wanafunzi wake na anaendelea kuwafundisha

hamtaanguka

Hii inamaanisha kuwa hamtaiacha imani ndani ya Yesu.

John 16:3

Watawatendea haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala mimi.

Baadhi ya waamini wanaweza kuuawa kwa sababu wasiomjua Mungu Baba pia hawamjui wala kumuelewa Mungu Mwana, Yesu Kristo.

Baba

Hiki ni cheo cha Muhimu cha Mungu.

Hapo mwanzo

Angalia ulivyotafsiri "tangu mwanzo" kwenye Yohana 15:26

John 16:5

Kama nisipoondoka, mfariji hatakuja

"Mfariji atakuja ikiwa nitaondoka"

Mfariji

Angalia jinsi ulivyotafsiri kwenye Yohana 14:25

John 16:8

Mfariji atauhukumu ulimwengu kutokana...haki...naenda kwa Baba

Yesu alipoondoka duniani na akarudi kwa Mungu Baba, kisha Mungu Roho akaanza kuwaonyesha watu wana dhambi na wanahitaji msamaha unaopatokana kwa Yesu pekee.

Ulimwengu

Inamaanisha watu wanaoishi duniani

kutokana na haki, kwa sababu naenda kwa Baba, na hamtaniona tena

"Atawaambia watu kwamba kwa sababu narudi kwa Baba, hamtaniona tena, mtajua kuwa ni mimi mwenye haki ya kweli"

Baba

Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu.

Mkuu wa ulimwengu

Angalia jinsi ulivyotafsiri kwenye Yohana 12:30

John 16:12

Mambo ya kuwaambia

"ujumbe kwa ajili yenu"

Roho wa kweli

Hili ni jina la Roho Mtakatifu atakayewaambia watu kweli ya Mungu

atawaongoza katika kweli yote

kweli inamaanisha ukweli wa kiroho

John 16:15

Vitu vyote...alivyonavyo Baba ni vyangu...Roho atachukua mambo yangu

Mungu Baba, Mwana, na Roho wote wanamiliki ulimwengu. Kwa pamoja ni wamoja na ni Mungu pekee.

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.

Muda mfupi

"karibu" au "kabla ya muda mrefu"

John 16:17

Maelezo ya jumla:

Wanafunzi wanaulizana kuhusu alichosemaYesu

muda mfupi na hamtaniona tena

wanafunzi hawakuelewa kuwa yesu alikuwa anaongelea kifo chake msalabani

na kisha muda mfupi mtaniona

Hii inaweza kumaanisha kufufuka kwa Yesu, au kuja kwa Yesu mara ya pili

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu

John 16:19

Sentensi unganishi:

Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake

amini, amini nawaambia

tafsiri kwa kuonesha kuwa kifuatacho ni cha muhimu zaidi

lakini ulimwengu utashangilia

lakini watu wanaompinga Mungu watashangilia

John 16:22

Kama mkiomba lolote kwa Baba, atawapa kwa jina langu

Baba na Mwana wanajibu maombi pamoja. Wanaomwamini Yesu wana msamaha wa milele wa dhambi na wanaweza kuomba kwa Baba kupitia kwa Mwana, na Baba atajibu.

Baba

Hiki ni cheo cha Muhimu cha Mungu.

Kwa jina langu

Baba atawapatia mahitaji yao kwa sababu ya mahusiano yao na Yesu. "kwa sababu ni wafuasi wangu" au "kwenye mamlaka yangu"

John 16:25

Kwa lugha isiyoeleweka

"kwa lugha ambayo ni ngumu kueleweka"

Nitawaambia waziwazi kuhusu Baba

Kibinadamu kujifunza kuhusu Mungu Baba kupitia Mwana wa Mungu, Yesu. Kumjua Mwana ni kumjua Baba.

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.

John 16:26

Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi

Mtu akimpenda Yesu, Mwana, pia anampenda baba, kwa sababu Baba na Mwana ni mmoja.

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.

Nilitoka kwa Baba... Naondoka ulimwenguni na ninaenda kwa Baba.

Baba alimtuma mwana msalabani awaokoe waamini toka kwenye dhambi na jehanamu, akafufuka toka kwa wafu, na akarudi Mbinguni.

Ulimwengu

"dunia." Ni mahali ambapo watu wanaishi.

John 16:29

Sentensi unganishi:

wanafunzi wanamjibu Yesu

Sasa mmeamini?

"Hatimaye sasa mmeiweka imani yenu kwangu!"

John 16:32

Sentensi unganishi:

Yesu anaendelea kuongea na wanafunzi wake

nanyi mtatawanyika

"wengine watawatawanya"

Baba yu pamoja nami

Hili jina la muhimu la Mungu

ili kwama ndani yangu muwe na amani

amani ya ndani

nimeushinda ulimwengu

nimezishinda taabu na mateso ya duniani

John 17

Yohana 17 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Sura hii ni sala moja ndefu.

Dhana maalum katika sura hii

Yesu ni wa milele

Sura hii inaonyesha wazi kwamba Yesu alikuwepo kabla ya ulimwengu kuumbwa.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Sala

Sala inaweza kuwa dhana ngumu kutafsiri katika tamaduni ambazo hazijui desturi hii. Kwa kuwa Yesu ni Mungu, sala zake si kama sala za watu wengine. Sura hii inaweza kuwa vigumu sana kuelewa kwa sababu Yesu hakuhitaji kuomba msaada, na sala zake pia zinaweza kuonekana kama amri. Haingekubalika kwa mtu mwingine kuomba kwa namna hii.

<< | >>

John 17:1

Baba ...mtukuze mwanao ili na mwana naye akutukuze wewe

Yesu anamwomba baba yake, Mungu Baba amtukuze, mwana wa Mungu

Baba...Mwana

Hivi ni vyeo vya mhimu amabavyo huelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu

Mbingu

Hii inamaanisha sehemu ya juu

John 17:3

Na uzima wa milelel ndio huu...wakujue wewe Mungu wa kweli, na.. Yesu Kristo

Uzima wa milele ni kumjua Mungu wa kweli na wa pekee, Mungu Baba na Mungu Mwana na Mungu Roho.

Kwamba inawapasa wakujue wewe

Hii inamaanisha kumjua mungu kwa uzoefu na wala si juu ya Mungu

Ile kazi uliyonipa kuifanya

"Kazi"inamaanisha jumla ya huduma ya Yesu hapa Duniani.

Baba, nitukuze mimi...kwa niliokuwa nao nilipokuwa na wewe kabla dunia haijaumbwa

Yesu alikuwa na utukufu pamoja na Mungu Baba '"Kabla ulimwengu haujaumbwa" Kwa sababu Yesu ni Mungu Mwana. Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ndio Mungu wa Kweli ambaye amekuwepo milele yote na ataendelea kuwepo milele ne milele.

Baba...Mwana

Hivi ni vyeo vinavyoonyesha uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

John 17:6

Si wa Dunia

Hapa neno "Dunia" humanisha watu wa dunia. Hii inamaanisha Mungu amewatofautisha na wale wasioamini.

Wamelishika neno lako

Wameyatii mafundisho yako

John 17:9

Mimi siuombei ulimwengu

Hapa neno ulimwengu linamanisha watu waovu duniani au watu wasiomtii Mungu

Duniani

Hii inamaanisha hali ya kuwa duniani na kuwa mmoja wa wale wanaoishi humo.

Baba Mtakatifu, uwalinde... ii wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja

Yesu anamwomba Baba ili awalinde wale wanaoamini. Mungu Baba huwalinda wale wanaomwamini Mungu Mwana na kuwafanya wawe na umoja na Mungu katika utatu wake

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu

Uwalinde kwa jina lako ulilonipa mimi

Hapa neno "jina"linamaanisha ulinzi na usimamaizi wa Mungu. "Uwalinde na kwa ulinzi wa jina lako kama ulivyonilinda mimi" au "uwalinde kwa nguvu za jina lako ulilonipa mimi

John 17:12

Hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa mwana wa upotevu

"mtu pekee aliyepotea ni mwana wa upotevu"

mwana wa upotevu

"yule ambaye tokea awali uliamua kumwamngamiza"

ili kwamba maandiko yatimie

"Ili mambo yaliyoandikwa kwenye maandiko"

John 17:15

ulimwengu

watu wakaao duniani

uwalinde na yule mwovu

uwalinde didi a Shetani

uwaweke wakfu kwako katika kweli

wafanye kuwa watu wako kwa kuwafundisha kweli

Neno lako ndiyo kweli

ujumbe wako ni kweli au unachosema ni kweli

John 17:18

ulimwenguni

kwa kila mtu duniani kote

ili kwamba na wao wajitoe kwako kwa ile kweli

unaweza pia kutafsiri kuwa: "ili kwamba wajitoe kikamilifu kwako"

John 17:20

ili kwamba wote wawe na umoja...kama, vile wewe Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako...ili kwwamba wao pia wawezekuwa ndani yetu

Mungu Baba yumo ndani ya Mungu Mwana na mwanaYumo ndani ya Baba. Wla wamwaminioa Yesu, Mungu mwana huwa na umoja na Baba na mwana wamwaminipo.

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu

Dunia

Hii humanisha watu wa duniani

John 17:22

Utukufu ule ulionipa mimi nimewapa wao

nimewaheshimu wafuasi wangu kama ambavyo wewe umeniheshimu mimi

ili kwamba waweze kuwa na umoja

Unaweza kutafsiri kama: "ili uweze kuwaunganisha kama ambavyo umetuunganisha sisi"

kukamilishwa katika umoja

kuwa kitu kimoja

ili ulimwengu ujue

ulimwengu ni watu

John 17:24

Baba...ulinipenda mimi kabla y kuumbwa kwa isingi ya ulimwengu

Mungu Baba amempenda Mungu mwana. Kabla Mungu hajauumba ulimwengu, nafsi za Mungu hupendana, na zitaendelea kupendana milele yote.

Nilipo mimi

hii inamaanisha mbinguni

ili waweze kuona utukufu wangu

ili waweze kujua ukuu wangu

kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu

Hapa Yesu anamaanisha wakati wa kabla ya uumbaji

John 17:25

Ulimwengu haukukutambua, lakini mimi nakujua; na hawa wanajua kuwa ulinituma

"ulimwengu hauna uzoefu wa kukujua wewe kama ninavyokujua; na hawa wanajua kuwa wewe umenituma"

jina

Hili linamanisha Mungu.

lile pendo...ulilonipenda

Upendo wa jinsi hii hutoka kwa Mungu na hulenga mema ya wengine, hata kama hauna maslahi binafsi. Upendo wa jinsi hii huwajali wengine bila kujali wanachofanya

Mungu mwenye haki

Hiki ni cheo cha muhimucha Mungu

John 18

Yohana 18 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Mistari ya 13 na 14 inasema, "kwa kuwa alikuwa baba mkwe Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu mwaka huo. Sasa Kayafa ndiye aliyewapa Wayahudi ushauri kwamba ingekuwa bora kwamba mtu mmoja afe kwa ajili ya watu . " Hii ni taarifa ya mabano inayotolewa na mwandishi. Inalenga kuelezea taarifa muhimu ya historia. Inawezekana kuweka taarifa hii kwa mabano.

Dhana maalum katika sura hii

"Sio halali kwetu kumwua mtu yeyote"

Ufalme wa Kirumi haukuruhusu Wayahudi kutekeleza adhabu ya kifo kwa mtu yeyote. Kwa hiyo, Wayahudi walipaswa kuwasilisha kesi yao kwa mtawala wa kipagani, Pilato.

Ufalme wa Yesu

Yesu anamwelezea Pilato kwamba ufalme wake sio "wa ulimwengu huu." Wataalamu wengine huchukua hii kumaanisha ya kwamba Yesu anatawala ufalme wa kiroho, lakini wengine wanasema kama maana ya maneno ya Yesu ilikuwa kama ufalme wake haukushindana na ufalme wa Kirumi. Inawezekana kutafsiri maneno haya kama ufalme wa Yesu "haukuanzisha mahali hapa au huanzisha mahali pengine."

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

"Mfalme wa Wayahudi"

Maneno haya hutumiwa kwa njia mbili tofauti katika kifungu hiki. Kwanza, Yesu anasemekana kuwa mfalme wa Wayahudi. Yeye ndiye mfalme wa Wayahudi na ulimwengu wote. Pili, hutumiwa kwa kinaya au kudhihaki na Pilato. Pilato hakumwamini Yesu kuwa mfalme wa Wayahudi. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-irony)

<< | >>

John 18:1

Bonde la Kidron

Hili ni bonde liliko Yerusalem ambalo hutenganisha Mlima wa hekalu na Mlima wa mizeituni

palipokuwaa na bustani

hili lilikuwa shamba la mizabibu

John 18:4

Maelezo ya jumla:

Yesu anaanza kuongea na askari, waheshimiwa, na Mafarisayo

Naye Yesu hali akijua kila kitu kilichokuwa kikifanyika dhidi yake

Yesu alijua mambo yote yaliyopaswa kumpata

John 18:6

Mimi

Hapa neno "yeye" halipo kwenye tafsiri ya asili lakini limefananishwa tu na "mimi ndiye"

kuanguka chini

watu walianguka chini kwa sababu ya nguvu za Yesu

Yesu Mnazareth

Yesu, mtu wa kutoka Nazareth

John 18:8

Mimi ndiye

Hapa neno "yeye" halipo kwenye tasfsiri ya asili lakini limehusishwa tu.

Haya yalikuwa hivyo ili lile neno linalosema

"Neno" linamaanisha maneno ambayo Yesu aliyaomba.

John 18:10

Markusi

Markusi ni mtumishi wa kiume wa Kuhani Mkuu

Ala

Huu ni mkoba wakisu au sime unauzuia kisu kisimkate mwenye nacho

Kikombe

Hii inamaanisha 1) Kiasi cha mateso ambayo Yesu alitakiwa kuyapokea 2) Gadhabu ya Mungu ambayo Yesu ilimlazimu kuivumilia ili kuwalkomboa watu wake.

Je nisikinywee kikombe ambacho Baba yangu amenipa?

Yesu anahoji hili swali kuonesha msisitizo kwamba lazima ateseke.

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu.

John 18:12

Maelezo ya jumla:

Mstari wa 14 unatoa maelezo yanayomhusu Kayafa

Wayahudi

hii inamaanisha viongozi wa Wayahudi

Walimkamata Yesu na kumfunga

Askari walimfunga Yesu mikono ili asitoroke

John 18:15

mwanafunzi mwingine, na yule mwanafunzi

Huyu ni mtume Yohana, mwandishi wa wa hii injili

John 18:17

Je, wewe si mmoja wa wanafunzi wa huyu mtu?

"Wewe ni mmoja wa wanafunzi wa huyu mtu"

John 18:19

Kuhani mkuu

Huyu alikuwa Kayafa

Nimeumbia waziwazi ulimwengu

Yesu aliifanya huduma yake katika uma wa watu

Hawa watu

Hawa ni wale watu waliomsikia Yesu akifundisha

John 18:22

Je, hivyo ndivo inavyokupas kumjibu kuhani mkuu?

'Hivyo sivyo inavyokupasa kumjibu Kuhani Mkuu"

uwe shahidi kwa ajili ya uovu

"niambie makosa yangu niliyoyasema"

kama nimejibu vyema kwa nini kunipiga?

"kama nimejibu kwa ukweli usinipige"

John 18:25

Maelezo ya jumla:

Hapa habari inarudi kumwelezea Petro.

Je, wewe ni mmoja wa wanafunzi wake?

Swali hili linatoa msisitizo wa ukweli wa jambo

Je si wewe niliyekuona naye kule bustanini?

hapa neno "naye" linamaanisha Yesu

Kisha Petro akamkana tena

Hii inamaanisha kuwa petro alimkana kwa kujua kuwa alikuwa na Yesu.

na papo kwa papo jogoo akawika

Ikumbukwe kuwa Yesu alimwambia Petro kuwa jogoo atawika kabla hajamkana

John 18:28

Maelezo ya jumla:

Askari na washitaki wa yesu wanamleta kwa Kayafa. Mstari wa 28 unaeleza sababu zilizowafanya wasiingie katika Praitorio.

Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako.

Huyu mtu ni mtenda maovu, na ni lazima tumlete kwako ili aadhibiwe"

Kumleta

Hili neno "kumleta" linamaanisha kumkabidhi kwa adui

John 18:31

Maelezo ya jumla:

Kwenye mstari wa 32 mwandishi anaelezea jinsi ambavyo yesu alitabiri kifo chake

Wayahudi wakamwambia

Hawa ni viongozi wa Wayahudi aliompinga Yesu na kumkamata.

sheria haituruhusu sisi kumpa tu adhabu ya kifo

Kulingana na sheria ya Kirumi, Wayahudi wasingweza kumuua mtu.

John 18:33

Mimi siyo Myahudi, au sivyo?

Hapa Pilato anauliza swali kuelezea jinsi ambavyo hana haja na tamaduni za Kiyahudi

watu wako mwenyewe

Wayahudi wenzako

John 18:36

Ufalme wangu si wa ulimwengu huu

Sentesihii yaweza kumaanisha 1) "Ufalme wangu si sehemu ya dunia hii" au 2) "Si hitaji ruhusa ya dunia hii kuwa mtawala wao" au "Si kwa kutokana na ulimwengu huu kwamba nina mamalaka ya kuwa mfalme."

Ili kwamba nisitolewe kwa Wayahudi.

"wangewazuia viongozi wa Kiyahudi kunikamata"

Sauti yangu

"mambo ninayoyaongelea" au "mimi"

John 18:38

kweli ni nini?

"Hakuna awezaye kujua kitu kilicho cha kweli"

Wayahudi

hii inamaanisha viongozi wa Kiyahudi

siyo huyu, ufungulie Baraba

tafsri kuonesha kuwa hawakumtaka Baraba bali Yesu

Baraba alikuwa mnyang'anyi

Hapa Yohana anaeleza Baraba alikuwa mtu wa aina gani

John 19

Yohana 19 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari ya 19:24, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

"Vazi la zambarau"

Rangi ya zambarau ilikuwa ishara ya kifalme Rangi ya zambarau ilikuwa ishara ya kifalme katika Mashariki ya Karibu. Yesu alivikwa kuoneka kama mfalme kwa kumdhihaki. Yesu alikuwa amevaa kuonekana kama mfalme kwa kukejeliwa.

"Wewe si rafiki ya Kaisari"

Pilato hakutaka kumhukumu Yesu kwa kifo, lakini Wayahudi walimlazimisha. Walifanya hivyo ili kuifanya kuonekana kama kuruhusu Yesu kuishi kungeweza kusaliti serikali ya Kirumi.

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Kudhihaki

Maneno yanayofuata yanatakiwa kuchukuliwa kudhihaki: "Salamu, Mfalme wa Wayahudi," "Je, nimsulubishe mfalme wenu?" na "Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi." Kudhihaki ni matumizi ya kinaya kumtukana mtu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-irony)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Gabbatha, Golgotha

Haya ni maneno mawili ya Kiebrania. Baada ya kutafsiri maana ya maneno haya ("Sakafu ya mawe" na "Mahali pa Fuvu"), mwandishi hufasiri sauti zao kwa kuandika kwa herufi za Kigiriki.

<< | >>

John 19:1

Salaam, mfalme wa Wayahudi

Hii "Salaam" inayoambatana na mkono ulioinuliwa ilitumika kwa msalimia Kaisari pekee yake. Wakati asakari wakitumia kofia ya miiba na vazi la dhambarau kwa kumkejeli Yesu, hawakumtambua kwa hakika kuwa ni mfalme.

John 19:4

Mimi sioni hatia yoyote ndani yake

Hii ni sawa na kusema kuwa sioni sababu ya kumwadhibu

taji ya miiba...vazi la dhambarau

taji na vazi la dhambarau ni vitu vinavyovaliwa na wafalme tu.

John 19:7

inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu

Yesu alihukumiwa kufa kwa kifo cha kusulibiwa kwa sababu ya kudai kuwa yeye alikuwa "mwana wa Mungu"

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo cha muhimu cha Yesu

Wewe uatoka wapi?

"Unatoka wapi? Pilato alimuliza Yesu kwa ajili ya kujua utambulisho wake. utamaduni wako unaweza kuwa njia maalumu ya kutambua utamaduni wa mtu.

John 19:10

Je, wewe huongei na mimi?

Pilato anaonyesha kushangazwa na Yesu kwa kutokuitumia nafasi hiyo ya kujiteteta. "Nijibu"

Usingekuwa na nguvu kama usingepewa toka juu

"Una mamalaka kinyume changu kwa sababu tu umepewa"

aliyenitoa

Neno "kutoa" linamaanisha kumkabidhi Yesu kwa adui, kama vile Yuda alivyomtoa Yesu kwa viongozi wa Kiyahudi

John 19:12

ajaifanyaye kuwa mfalme

"madai ya kuwa yeye ni mfalme"

akamleta Yesu nje

Hii inamaanisha kuwa aliwaagiza askari kumleta Yesu nje il ikumwonyesha kwa makutano.

akakaa

Watu wakubwa walikaa wakati watu wengine amabao si wskubwa walisimama.

Kwenye kiti cha hukumu

Hiki ni kiti maalumu ambacho watu mhimu walikaa wakati wa kufanya maamuzi ya kiofisi. Utamaduni wako unaweza kuwa na njia tofauti wautaratibu huu.

Fuvu la kichwa

Hili ni eneo maalumu ambalo watu maalumu ndio wsalioruhusiwa kupaingia, Utamaduni wako unaweza kuwa na maeneo maalumu kama hili.

Kihebrania

Hii ilikuwa lugha ambayo wahebrania waliongea

John 19:14

Sentensi unganishi:

Muda umepita na sasa ni saa la sita, wakati Pilato anawaagiza askari wamsulibishe Yesu.

saa la sita

kama muda wa mchana

Pilato akwaambia Wayahudi

Hapa inamaanisha Pilato aliwaambia viongozi wa Kiyahudi

Je, mimi nimsulibishe mfalme wenu?

Pilato anawauliza Wayahudi ikiwa wanataka askari wake wamsulibishe Yesu.

John 19:17

kwenye eneo liitwalo fuvu la kichwa

Unaweza kutafsiri kama: "kwenye eneo ambalo watu wanaliita fuvu la kichwa"

ambalo kwa Kiebrania huitwa "Golgotha"

Kiebrania ni lugha ya Waisraeli

pamoja naye wanaume wawili

Unaweza kutafsiri kama: "pia waliwasulibisha wahalifu wengine wawili kwenye misalaba yao"

John 19:19

Pilato pia aliandika alama na kuiweka juu ya msalaba

hapa inamaanisha mtu aliyeandika kwa niaba ya Pilato na kuiweka juu ya msalaba wa Yesu

Hapo paliandikwa: YESU MNAZARETHH, MFALME WA WAYAHUDI

Unaweza pia kutafsiri hii kama: "hivyo yule mtu aliandika maneno haya: Yesu ya nazarethi, mfalme wa Wayahudi"

Kiyunani

Hii ni lugha ya serikali ya Kirumi

John 19:21

Kisha wakuu wa makuhani wa Wayahudi wakamwambia Pilato

Wakuu wa makuhani walienda mpaka Ikulu kumshitaki Yesu juu ya maneno na miujiza yake.

Niliyoyaandika nimeandika

Pilato anamaanisha kuwa hawezi kubadilisha maneno katika kibao

John 19:23

Maelezo ya jumla:

Mwishoni mwa mstari wa 24 kuna tofauti kutoka habari kwa kuwa Yohana anaelezea jinsi tukio hili linatimiza maandiko.

kanzu

askari waliweka kando kanzu na hawakuigawa

wakapiga kura

hivi ndivyo askari walivyogawana mavazi ya Yesu.

John 19:25

Yule mwanafunzi aliyempenda

Huyu ni Yohana mwandishi wa injili hii

Mwanamke, mtazame, mwanao huyu hapa

"Mwanamke, tazama na ufifkiri juu huyu mtu kama angekuwa mwano"

Mama yako huyu hapa

"fikiri juu ya huyu mwanamke kama angekuwa mama yako"

John 19:28

Siki

Hiki ni kinywaji cha makomamanga kilchokuwa kimechachushwa kwa muda mrefu

wakaweka

"Hawa" nia walinzi wa Kirumi

Sifongo

Hi ni kiufito kilichokuwa na uwezo wa kunyonya kimiminika

Akaisalimu roho yake

Yesu aliito roho yake kwa Mungu na kuruhusu mwili wake kufa

John 19:31

Wayahudi

Hii inamaanisha viongozi wa Kiyahudi

siku ya maandalio

Huu ni muda uliokuwa kabla ya pasaka ambao ulitumika kuandaa chakula

kuvunja miguu yao na kuiondoa

Unaweza kutafsiri kama, "kuvunja miguu ya waliosulibiwa na kuiondoa miili yao kutoka kwenye misalaba yao"

aliyekuwa amesulibiwa pamoja na Yesu.

Unaweza kutafsiri kama, "ambaye walimsulibisha karibu na Yesu"

John 19:34

Naye aliyeona hili

Sentesi hii inatoa mukhutadha wa habari. Mwandishi ambaye ni (Mtume Yohana) anawafahamisha wasomaji kuwa yeye alikuwepo na kwamba tukiamini alichoandika

John 19:36

Hapana mfupa wake utakaovunjwa

"Hakuna atayevunja hata mmoja ya mifupa yake"

John 19:38

Yusuph wa Arimathaya

Yusuph kutoka mji wa Arimathaya

kwa kuwaogopa wayahudi

"Kwa kuwahofia viongozi wa Kiyahudi"

Nikodemo

Huyu ndiye aliyeenda kwa Yesu wakati wa giza

manemane na udi

Haya ni manukato yaliyo kabla ya mazishitumika kuandaa maiti

Mia moja

Kipimo cha mia moja

Ratli

"Ratli moja" ni sawa na kipimo cha gramu 31

John 19:40

Sasa mahali ambapo Yesu alisulibiwa kulikuwa na bustani....hakuna mtu alikuwa amezikwa humo

Hapa mwandishi Yohana anatoa maelezo kuhusu mahali ambapo kaburi lilikuwa

Kwa sababu ilikuwa siku ya maandalio kwa Wayahudi

Kulingana na sheria ya Kiyahudi, hakuna mtu aliyeruhusiwa kufanya kazi baada ya jua kuzama. Ilikuwa ni mwanzo wa Sabato na Pasaka

John 20

Yohana 20 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Pokea Roho Mtakatifu"

Wanafunzi walikuwa na nguvu maalum waliopewa na Roho Mtakatifu. Aliiwezesha huduma yao.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Raboni

Hii ni neno la Kiebrania. Yohana "alifasiri" sauti zake kwa kubadilisha herufi za Kiebrania na kutumia herufi za Kigiriki. Kisha anaeleza kwamba maana ya neno hili ni Mwalimu." Mtafsiri anatakiwa kufanya hivyo, lakini aifasiri kwa kutumia herufi za lugha inayolengwa.

Mwili wa Yesu wa ufufuo

Kuna siri juu ya mwili wa Yesu wakati huu. Alikuwa kimwili mwenye makovu kutoka kusulubiwa lakini pia aliweza kuingia katika vyumba bila kutumia mlango. Ni vyema kuiacha hii siri mahali pale lakini maelezo yanaweza kuwa muhimu ikiwa tafsiri haieleweki kwa msomaji.

Malaika wawili wenye mavazi meupe

Mathayo, Marko, Luka, na Yohana wote waliandika juu ya malaika waliovalia nguo nyeupe wakiwa pamoja na wanawake katika kaburi la Yesu. Waandishi wawili kati yao waliwaita wanaume, lakini ni kwa sababu tu malaika walikuwa katika hali ya kibinadamu. Waandishi wawili waliandika kuhusu malaika wawili, lakini waandishi wengine wawili waliandika juu ya moja tu. Ni bora kutafsiri kila moja ya vifungu hivi kama inavyoonekana katika ULB bila kujaribu kufanya vifungu vyote kufanana.(Angalia: Mathayo 28: 1-2, Marko 16: 5 na Luka 24: 4 na Yohana 20:12)

<< | >>

John 20:1

Siku ya kwanza ya Juma

Jumapili

Mwanfunzi ambaye Yesualimpenda

Sentesi hii inaonekana kuwa ni njia ambayo Yohana aliitumia kumwonyesha yeye katika kitibu chote. Neno "upendo" linamaanisha upendo wa ndugu au upendo wa rafiki au kwa mwanafamilia

Wamemchukua

Mtu amechukua

John 20:3

mwanafunzi mwingine

Yohana anatumia neno hili kwa kuonyesha unyenyekevu akimaanisha yeye mwenyewe badala ya kutumia jina lake.

Sanda za kitani

Hizi zilikuwa nguo za mazishi zilizotumika kuuzongazonga mwili wa Yesu.

John 20:6

Sanda za Kitani

Hizi ni nguo azazovalishwa mfu kabla ya kuzikwa

leso ilyokuwa kichwani mwake

Hiki ni kitambaa kidogo ambacho hutumika kwa kufutia jasho usoni amabcho pia kilitumika kufunika uso wake

John 20:8

mwanafunzi mwingine

Yohana anatumia neno hili kwa kuonesha unyenyekevu akimaanisha yeye mwenyewe pasipo kutaja jina lake.

aliona na kuamini

Alipoona kuwa kaburi lipo wazi, aliamini ya kuwa yesu alikuwa amefufuka kutoka wafu

bado hawakuyajua maandiko

hapa mwandishi anawaongelea wanafunzi ambao hawakujua bado maandiko yanayosema kuwa Yesu angefufuka tena.

John 20:11

aliwaona malaika wawili na nguo nyeupe

Malaika walikuwa wamevaa nguo nyeupe

wakamwambia

walimuuliza

Kwa sababu wamemchukua Bwana wangu

Kwa sababu wameuchukua mwili wa Bwana wangu

Nami sijui walikomweka

Nami sijui walipouweka mwili

John 20:14

Yesu alimwambia

Yesu alimuuliza

Bwana, kama ni wewe uliyemchukua yeye

neno "yeye" hapa linarejjea kwa yesu

niambiie ulikomweka

niambie ulipokiweka

nami nitamchukua

Maria Magdalena anataka kuchukua mwili wa Yesu na kuuzika tena.

John 20:16

Rabboni

Neno "Rabboni" linamanisha rabi au mwalimu katika Matamushi ya Kiaramaic ya Mariamu

ndugu

Yesu alitumia neno "ndugu" akimaanisha wanafunzi wake

nitapaa kwenda kwa baba amabye pia ni baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.

Yesu alifufuka toka wafu kisha akatabiri kupaa mbinguni, akirudi kwa Baba, Mungu Baba

Baba yangu na Baba yenu

Hivi ni vyeo muhimu vinavyofafanua uhusiano kati ya Yesu na Mungu, na kati ya waumini na Mungu.

John 20:19

Siku hiyo, siku ya kwanza ya juma

hii inamaanisha Jumapili

Amani iwe kwenu

hii ni salamu ya kawaida"

akawaonyesha mikono yake na ubavu wake

"aliwaonyesha vle vidondo mikononi mwake na ubavuni.

John 20:21

amani iwe nanyi

hii nisalamu ya kawaida

Kama vile Baba alivyonituma mimi, vivyo hivyo nami nawatuma ninyi...akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu"

Mungu Baba alimtuma Mungu Mwana anayewatuma waumini katika nguvu ya ya Mungu Roho.

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu

watasamehewa

"Mungu atawasamehe"

Watafungiwa

"Mungu hatawasamehe"

John 20:24

Pacha

Tazama tafsiri tok Yohana 11:15

yule mwanafunzi mwingine walimwambia baadaye

neno "yule" linamaanisha Thomaso

Kma staona alama za misumari sitamini

Nitaamini tu pale nitakapoona alama za misumari na ubavu wake

Mikononi mwake

Neno "mwake" linamaanisha Yesu

John 20:26

Wanafunzi wake walikuwa chumbani tena

Neno "wake" linamaanisha Yesu

Amani na iwe nanyi

Hii ni salamu ya kawaida

asiyeamini

bila imani

John 20:28

umeamini

"umeamini kuwa niko hai"

pasipokuona

"ambao ambao hawajaniona nikiwa hai

John 20:30

ishara

Hii inamanisha miujiza inayotumika kuonyesha ushahidi kuwa Mungu ana nguvu zote na ambaye ana mamalaka kamili juu ya ulimwen

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu

Uzima katika jina lake

"Munaweza kuwa na uzima katika jina lake"

uzima

hii inamaanisha maisha ya kiroho

John 21

Yohana 21 Maelezo ya Jumla

Mifano muhima ya usemi katika sura hii

Mifano

Yesu anatumia mifano mingi ya uchungaji. Kwa mfano, "kulisha kondoo wangu," "chunga kondoo wangu" na "kulisha kondoo wangu." Petro sasa angekuwa mchungaji wa watu wa Mungu.

__<< | __

John 21:1

Baada ya mambo haya

"Baadaye kitambo"

na Tomaso aitwaye Didimasi

unaweza kutafsiri pia kwa kusema, "na Tomaso tuliyemwita Didimasi"

Didimasi

Maana ya jina hili ni "mapacha"

John 21:4

vijana

hii ni hali ya kusema rafiki zangu

mtapata wachache

maana yake, "mtakamata samaki wachache kwenye nyavu zenu"

tupeni ndani

vuteni nyavu ndani

John 21:7

aliyempenda

Huu ni upendo unaotoka kwa Mungu ambao hutazama zaidi mema ya wengine, hata kama hauna maslahi binafsi. Upendo wa aina hii huwajali zaidi wengine bila kujali wanachokifanya

(maana hakuwa amelivaa vizuri)

Hii ni kwa mujibu wa mukhutadha

Kwani hawakuwa mbali na pwani, yapata mita mia moja kutoka ufukweni)

Hii ni kwa mujibu wa mukhutadha

yapata dhiraa miambili

"mita tisini"dhiraa ni ndogo kuliko nusu mita

John 21:10

Simoni Petro kisha akaenda juu

Hii inamaanisha kuwa Petro alirudi kwenye mtumbwi

na akatoa nyavu nchi kavu

na akatoa nyavu na kuziweka ufukweni

nyavu ilikuwa haijararuka

Unaweza kutafsiri hii kama, "nyavu hazikuharibika

John 21:12

kifungua kinywa

mlo wa asubuhi

mara ya tatu

unaweza kutafsiri hii kama muda nambari tatu.

John 21:15

je, unanaipenda...wanipenda mimi

Hapa "upendo" linamanisha aina ya upendo unaotoka kwa Mungu, amabao unaangalia mema ya wengine, hata pale ambapo hakuna maslahi binafsi

wewe wajua kuwa mimi na kupenda wewe

Petro anajibu, anatumia neno kwa "upendo" ambalo linonyesha upendo kwa ndugu au upendo wa urafiki au upendo wa kifamila.

Lisha wanakondoo wangu

"Lisha watu wangu ninaowajali"

Chunga kondoo wangu

"Wajali watu wangu ninaowajali"

John 21:17

Je, wanipenda mimi?

Mara hii Yesu anapouliza swali hili anatumia neno kwa "upendo" ambalo linamanisha upendo wa ndugu au upendo wa urafiki au upendo wa kifamila

Lisha kondoo wangu

"Uwajali watu wangu ninaowajali"

Kweli, kweli

itafsiriwe kama ilivyo kwenye Yohana 1:49, 1:51

John 21:19

Sasa

Yohana analitumia neno hili kuonyesha kuwa anatoa maelezo ya mukhutadha kabla hajaendelea na simulizi

John 21:20

alimpenda

Huu ni aina ya upendo amabao hutoka kwa Mungu ambao huangalia mema ya wengine hata kama hauna maslahi binafsi. Aina ya upendo huu huwajali wengine, bila kujali wanachokifanya

kwenye chakula cha jioni

Hii inakumbushia chakula cha mwisho ambacho Yesu alikula na wanfunzi wake

Petro alimwona

Hapa neno "yeye" linalemlenga "mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda"

John 21:22

nataka abaki

Hapa "yeye", "a...ki", linamanisha "mwanafuzi ambaye Yesu alimpenda" Tazama 21:20

Nitakapokuja

Inamaaninisha kur duniani kwa Yesu mara ya pili, atakapokuja kutoka mbinguni.

hilo linakuhusu nini?

"usijihusishe na jambo hilo"

ndugu

Yesu ana anatumia neno hili kwa wanafuzi wake kama nduguze.

John 21:24

Taarifa za jumla:

Huu ndio mwisho wa Injili ya Yohana. Hivyo mwandishi ambaye ni Yohona anatoa salamu za mwisho na kusema kidogo kuhusiana na yeye mwenyewe.

mwanafunzi

mwanafunzi wa Yohana

ambaye hushuhudia kuhusu mambo yaleyale

neno kushuhudia kama lilivyotumika hapa linamaanisha kuona kitu

sisi tunajua

"sisi" hapa inamaanisha wale wanaomwamini Yesu

kama kila kitu kingeandikwa

unaweza kutafsiri pia kwa kusema, "kama mtu angeandika kila kitu"

hata dunia pia isingeweza kutosha vitabu vyote

Yesu alifanya miujiza mingi kuliko ambavyo watu wangeweza kuandika kwenye vitabu