Kiswahili: translationNotes Print

Updated ? hours ago # views See on WACS

Utangulizi wa 1 Wakorintho

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha 1 Wakorintho

  1. Mgawanyiko katika kanisa (1:10-4:21)
  2. Dhambi na makosa (5:1-13)
  3. Wakristo kuwapeleka Wakristo wengine mahakamani (6:1-20)
  4. Ndoa na mambo yanayohusiana nayo (7:1-40)
  5. Uovu wa uhuru wa Kikristo; chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu, kukimbia ibada ya sanamu; kufunika kwa vichwa vya wanawake (8:1-13; 10:1-11:16)
  6. Haki za Paulo kama mtume (9:1-27)
  7. Meza ya Bwana (11:17-34)
  8. Vipaji vya Roho Mtakatifu (12:1-31)
  9. pendo (13:1-13)
  10. Vipaji vya Roho Mtakatifu: unabii na lugha (14:1-40)
  11. Ufufuo wa waumini na ufufuo wa Kristo (15:1-58)
  12. Kufunga: mchango wa Wakristo huko Yerusalemu, maombi, na salamu za kibinafsi (16:1-24)

Nani aliandika Kitabu cha 1 Wakorintho?

Paulo aliandika 1 Wakorintho. Paulo alitoka mji wa Tarso. Alikuwa anajulikana kama Sauli katika maisha yake ya awali. Kabla ya kuwa Mkristo, Paulo alikuwa Mfarisayo. Aliwatesa Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara kadhaa katika Ufalme wa Roma akiwaambia watu kuhusu Yesu.

Paulo alianzisha kanisa lililokutana huko Korintho. Alikuwa akiishi katika mji wa Efeso wakati aliandika barua hii.

Je, kitabu cha 1 Wakorintho kinahusu nini?

1 Wakorintho ni barua ambayo Paulo aliwaandikia waumini waliokuwa katika mji wa Korintho. Paulo alikuwa amesikia kwamba kuna matatizo kati ya waumini huko. Walikuwa wakigombana. Baadhi yao hawakuelewa baadhi ya mafundisho ya Kikristo. Na baadhi yao walikuwa na tabia mbaya. Katika barua hii, Paulo aliwajibu na kuwahimiza kuishi kwa njia iliyopendeza Mungu.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha jadi, "Wakorintho wa Kwanza." Au wanaweza kuchagua kichwa wazi, kama "Barua ya kwanza ya Paulo kwa Kanisa la Korintho." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Mji wa Korintho ulikuwaje?

Korintho ilikuwa mji mkuu katika Ugiriki wa kale. Kwa sababu ulikuwa karibu na Bahari ya Mediterane, wasafiri wengi na wafanyabiashara walikuja kununua na kuuza bidhaa huko. Hii ilisababisha mji kuwa na watu kutoka tamaduni nyingi tofauti. Mji huo ulijulikana kwa kuwa na watu waliokuwa wameishi katika njia za uasherati. Watu waliabudu Afrodito, mungu wa kike wa Kigiriki wa upendo. Kama sehemu ya sherehe za kuheshimu Afrodito, waabudu wake walifanya ngono na makahaba wa hekalu.

Tatizo lilikuwa nini kwa nyama iliyotolewa kwa sanamu?

Wanyama wengi waliuawa na kutolewa dhabihu kwa miungu ya uongo huko Korintho. Wakuhani na waabudu walishika sehemu ya nyama hizo. Sehemu kubwa ya nyama hizo ilikuwa ikiuzwa katika masoko. Wakristo wengi hawakukubaliana iwapo ilikuwa ni sawa kula nyama hii, kwa sababu ilikuwa imetolewa kwa mungu wa uwongo. Paulo anaandika juu ya shida hii katika 1 Wakorintho.

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Je, mawazo ya "takatifu" na "kutakasa" yamewakilishwa vipi katika 1 Wakorintho kwenye ULB?

Maandiko hutumia maneno kama haya ili kuonyesha moja kati ya mawazo mbalimbali. Kwa sababu hii, mara nyingi ni vigumu kwa watafsiri kuyawakilisha vizuri katika tafsiri zao. Katika kutafsiri kwa Kiingereza, 1 Wakorintho kwenye ULB hutumia kanuni zifuatazo:

  • Wakati mwingine maana katika kifungu inaashiria utakatifu wa maadili. Hasa muhimu kuelewa katika injili kuwa ni ukweli kwamba Mungu anawaona Wakristo kuwa wasio na dhambi kwa sababu wameungana na Yesu Kristo. Ukweli mwingine unaohusiana na haya ni kwamba Mungu ni mkamilifu na hana hatia. Ukweli wa tatu ni kwamba Wakristo wanapaswa kujiendesha kwa njia isio na hatia na isiyo na hatia katika maisha. Katika hali hizi, ULB inatumia "takatifu," "Mungu mtakatifu," "watakatifu," au "watu watakatifu." (Angalia: 1:2; 3:17)
  • Wakati mwingine maana katika kifungu inaonyesha rejeo rahisi kwa Wakristo bila kuashiria jukumu fulani wanayopaswa kufanya. Katika nyakati hizi, ULB hutumia "mwamini" au "waumini." (Angalia: 6:1, 2, 14:33; 16:1,15)
  • Wakati mwingine maana katika kifungu hiki inaashiria mtu au kitu kilichowekewa Mungu peke yake. Katika matukio haya, ULB inatumia "kuwekwa kando," "kujitolea," "iliyohifadhiwa," au "kutakaswa." (Angalia: 1:2; 6:11; 7:14,34)

UDB mara nyingi husaidia ikiwa wafasiri wanafikiria juu ya jinsi ya kuwakilisha mawazo haya katika tafsiri zao wenyewe.

Nini maana ya "mwili"?

Paulo mara nyingi alitumia maneno "mwili" au "kimwili" kwa kutaja Wakristo ambao walifanya mambo ya dhambi. Hata hivyo, sio ulimwengu wa kimwili ambao ni mbaya. Paulo pia alielezea Wakristo ambao waliishi kwa njia ya haki kama "kiroho." Hii ni kwa sababu walifanya kile Roho Mtakatifu aliwafundisha kufanya. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#flesh, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#spirit)

Paulo alimaanisha nini kwa maneno "katika Kristo," "katika Bwana," na kadhalika?

Maneno haya hutokea katika 1:2, 30, 31; 3:1; 4:10, 15, 17; 6:11, 19; 7:22; 9:1, 2; 11:11, 25; 12: 3, 9, 13, 18, 25; 14:16; 15:18, 19, 22, 31, 58; 16:19, 24. Paulo alijaribu kueleza wazo la muungano wa karibu kati ya Kristo na waumini. Wakati huo huo, mara nyingi alitaka kuelezea maana nyingine pia. Ona, kwa mfano, "wale ambao wamejitolea katika Kristo Yesu" (1:2), ambako Paulo alimaanisha hasa kwamba waumini Wakristo wamejitolea kwa Kristo.

Tafadhali angalia utangulizi wa Kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi juu ya maneno haya.

Je, ni masuala gani muhimu katika Kitabu cha 1 Wakorintho?

Kwa aya zifuatazo, matoleo ya kisasa ya Biblia yanatofautiana na matoleo ya zamani. Watafsiri wanashauriwa kufuata matoleo ya kisasa ya Biblia. Hata hivyo, ikiwa katika wilaya ya watafsiri kuna Biblia ambazo zinasomwa kulingana na matoleo ya kale ya Biblia, watafsiri wanaweza kufuata hayo. Ikiwa ni hivyo, mistari hii inapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yao sio 1 Wakorintho.

  • "Basi, tukuzeni Mungu kwa miili yenu." Baadhi ya matoleo ya zamani husema "Kwa hiyo, tukuzeni Mungu kwa miili yenu na katika roho zenu, ambayo ni ya Mungu." (6:20)
  • "Nilifanya hivyo ingawa mimi sikuwa chini ya sheria." (9:20) Baadhi ya matoleo ya zamani hayana kifungu hiki.
  • "kwa ajili ya dhamiri - dhamiri ya mtu mwingine." Baadhi ya matoleo ya zamani husoma "kwa sababu ya dhamiri: kwa maana dunia na kila kitu kilicho ndani yake ni ya Bwana: dhamiri ya mtu mwingine." (10:28)
  • "na kwamba mimi hutoa mwili wangu kuchomwa moto." (13: 3) Baadhi ya matoleo ya zamani yanasema, "na kwamba ninatoa mwili wangu ili nipate kujivunia."
  • "Lakini kama mtu hajui jambo hili, asitambuliwe." (14:38) Baadhi ya matoleo ya zamani husema, "Lakini ikiwa kuna mtu yeyote asiyejua jambo hilo, basi asijue."

(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/jit.html#translate-textvariants)

1 Corinthians 1

1 Wakorintho 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Aya tatu za kwanza ni salamu. Katika inchi za kale za Mashariki ya Karibu, hii ilikuwa njia ya kawaida ya kuanzisha barua.

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB hufanya hivi kwa maneno ya mstari wa 19, ambayo yanayotoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Mgongano

Katika sura hii, Paulo anakaripia kanisa kwa kugawanyika na kwa kufuata mitume tofauti. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#apostle)

Vipaji vya kiroho

Vipaji vya kiroho ni uwezo usio wa kawaida wa kusaidia kanisa. Roho Mtakatifu anatoa vipaji hivi kwa Wakristo baada ya kumwamini Yesu. Paulo anaorodhesha vipaji vya kiroho katika Sura ya 12. Wasomi wengine wanaamini kwamba Roho Mtakatifu alitoa baadhi ya vipaji hivi katika kanisa la kwanza tu ili kusaidia kuanzisha kanisa. Wasomi wengine wanaamini kwamba vipaji vyote vya Roho bado vinapatikana ili kuwasaidia Wakristo wote katika historia ya kanisa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#faith)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Misemo

Katika sura hii, Paulo anaelezea kurudi kwa Kristo kwa kutumia maneno mawili tofauti: "ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo" na "siku ya Bwana wetu Yesu Kristo." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-idiom)

Maswali ya uhuishaji

Paulo hutumia maswali ya uhuishaji ili kuwakaripia Wakorintho kwa kugawanyika katika vikundi na kwa kutegemea hekima ya kibinadamu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kikwazo

Kikwazo ni mwamba ambamo watu wanajikwaa. Hapa ina maana kwamba Wayahudi wanaona vigumu kuamini kuwa Mungu alimruhusu Masihi wake kusulubiwa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

| >>

1 Corinthians 1:1

sentesi unganishi

Paulo na Sosthenes wanato salamu za kwa waumini wa kanisa la Korintho

Maelezo ya Jumla

Maneno kama vile "ninyi" and "yanu" yanahusiana na wale ambao paulo aliwaandikia na alitumia kiwakilisha cha wingi.

Paulo...kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho

Hii ilikuwa ni namna ya mwandishi wa barua kujitambulisha kwa wasomaji wake : " mimi, Paulo niliwaandikia barua hii ninyi munaomwamini Mungu mlioko Korintho"

Sosthene ndugu yetu

Hii inaonesha kuwa Paulo na Wakorintho wanamfahamu vema Sosthene:" Sosthene ndugu yetu ambaye mimi na ninyi tunamfahamu"

wale ambao wamewekwa wakfu katika Yesu Kristo

Neno "kuwekwa wakfu" linamaana ya watu ambao Mungu amewapa kibali cha kumtukuza yeye. " hii ni kwa wale ambao Yesu Kristo amaewatenga kwa ajili ya Mungu" au " watu ambao Mungu amaewachukua na kuwatenga kwa ajili yake mwenyewe kwa wanamwamini Yesu Kristo"

ambao wameitwa kuwa watu watakatifu

Hii inaweza kuelezewa kwa kitenzi tendaji: " ambao Mungu amewaita kuwa watu watakatifu" kuna maana mbili zinazokubalika. 1) " wale ambao Mungu amewatenga kwa ajili yake mwenyewe" 2) wale ambao Mungu amewaita kujitenga na dhambi" au ambao Mungu amewaita wajitenge na matendo ya dhambi"

Bwana wao na wetu

Yesu ni Bwana kwa Paul na kwa Wakorintho na ni Bwana kwa makanisa yote na watu wote

1 Corinthians 1:4

Sentensi Unganishi

Paulo anaelezea mwenendo na ushirika wa waumini katika Krito wanaposubiri kurudi kwake mara ya pili

kwa sababu ya neema ya Mungu ambayo Kristo Yesu aliwapa

Paulo anazungumzia neema kana kwamba ni kitu chenye umbo ambacho Yesu amewapa wakristo kama zawadi. " hii ni kwa sababu Yesu amefanya iwezekane kwa Mungu kuwa mwema kwako"

Amewafanya kuwa matajiri

Yawezekana maana ni 1)"Kristo amekufanya wewe tajiri" au 2) "Mungu amekufanya wewe tajiri."

Amewafanya kuwa matajiri katika kila njia

inatumia lugha ya makazo kumaanisha" aliwafanya matajiri wenye baraka nyingi za rohoni"

katika usemi

Mungu amekupa uwezo wa kuwaambia na kuwashirikiwe wengine kuhusu ujumbe kwa namna mbalimbali.

pamoja maarifa yote.

Mungu amekuwezesha kuelewa ujumbe wake kwa namna mbalimbali.

ushuhuda kuhusu Kristo ya kwamba amethibitishwa kuwa kweli miongoni mwenu.

maneno haya yanaweza kumaanisha: 1) ninyi wenyewe mliona tulichokise kwenu kuhusu Kristo ilikuwa ni kweli 2) watu wengine walijifunza kwa kuona ninyi na sisi tunavyoishi katika Kristo.

1 Corinthians 1:7

Kwa hiyo

"Kama matokeo"

hampungukiwi karama za kiroho

"kuwa na kila uwezo wa rohoni"

Ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo

Yawezekana maana ni 1)Wakati Mungu atakapo mfunua Bwana Yesu Kristo" au 2)"Wakati Bwana wetu Yesu Kristo atakapojidhihirisha yeye mwenyewe."

msilaumiwe

Kusiwepo sababu yoyote ya kulaumiwa na Mungu

Mungu ni mwaminifu

Mungu atatimiza jambo lolote ambalo ameahidi kufanya.

mwana wake

Ni cheo cha Yesu Kristo, yaani "Mwana wa Mungu"

1 Corinthians 1:10

sentensi unganishi

Paulo anawakumbusha waumini wa Korintho kwamba wanapaswa kuishi katika umoja na katika ujumbe wa msalaba wa Kristo, siyo ubatizo wa watu unaoleta wokovu.

kaka na dada zangu

Hii inamaana washirika wote wakristo, ikijumuisha wote wanawake na wanaume.

kwamba wote mkubali

" kuishi katika hali ya upatanifu na ushirikiano"

kwamba kusiwe na migawanyiko miongoni mwenu

" kusiwe na migawanyiko ya makundi makundi miongoni mwenu"

kwamba muungane pamoja katika nia moja na katika kusudi

" muishi katika hali ya umoja"

watu wa nyumba ya Kloe

Hii inahusu wanafamilia, wafanyakazi, na watu wengine ambao ni sehemu ya kaya ambayo Chloe ni mwanamke kiongozi.

kuna mgawanyiko unaoendelea miongoni mwenu

" kuna makundi yenye migogoro na kugombana kati yenu"

1 Corinthians 1:12

Kila mmoja wenu husema

Paulo anaelezea kwa ujumla tabia ya mgawanyiko

Je! Kristo amegawanyika?

Paulo ataka kuweka makazo kuhusu ukweli kwamba Kristo hajagawanyika lakini ni mmoja. "Haiwezekani kumgawanya Kristo katika namna mnayofanya."

Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu?

Paulo anapenda kuweka mkazo kwamba alikuwa Kristo aliyesulubiwa wala si Paulo au Apolo. " ni ni ukweli uliowazi kuwa hawakumuua Paulo pale msalabani kwa ajili ya wokovu wenu."

Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

Paulo anaweka mkazo kwamba wote tunabatizwa katika jina la Kristo. " Na Watu hawakuwabatiza ninyi katika jina la Paulo."

1 Corinthians 1:14

Namshukuru Mungu

Paulo anafurahia kuwa hakuwabatiza watu wengi wa pale Korintho

sikumbatiza yeyote isipokuwa

"pekee"

Krispo

Alikuwa kiongozi wa sinagogi ambaye alibadilika kuwa Mkristo.

Gayo

Alisafiri pamoja na Mtume Paulo

Hii ilikuwa hivyo kwamba hakuna hata mmoja angesema kwamba mlibatizwa katika jina langu.

"Nilijizua katika kubatiza watu zaidi kwasababu niliogopa kwamba wange jivuna baadaye kwamba nimekwisha kuwabatiza wao."

Nyumba nzima ya Stephania

Hii inahusu wanafamilia na watumwa katika nyumba(kaya) mahali Stephania, mwanaume, na kiongozi wa kaya.

1 Corinthians 1:17

Kristo hakunituma mimi kubatiza

Hii inamaanisha kwamba ubatizo halikuwa lengo la msingi la Paulo katika huduma yake.

maneno ya hekima ya kibinadamu...msalaba wa Kristo usionekane kuwa kitu kisichokuwa na nguvu

Paulo anazungumza kwa " maneno ya hekima ya kibinadamu" ni kama vile walikuwa watu, na msalaba ulikuwa kama chombo, ambacho Yesu aliweka nguvu yake ndani ya chombo hicho. Hii ilimaanisha kuwa " maneno yanayotokana na hekima ya kibinadamu ... yasije kuondoa nguvu ya msalaba wa Kristo" au " maneno ya hekima ya kibinadamu... yasiwafanye watu washindwe kuamini ujumbe kuhusu Yesu na kuanza kujidhania kuwa wao ni wamuhimu zaidi kuliko Yesu.

1 Corinthians 1:18

Sentensi Unganishi

Paul anasisitiza Hekima ya Mungu dhidi ya hekima ya kibidamu

ujumbe wa msalaba

"Mahubiri kuhusu kusulubiwa"au "ujumbe kuhusu kufa kwa Kristo msalabani."

ni upuuzi

"haina maana" au "ni upumbavu"

Kwa wale wanaokufa

Hapa "kufa" inamaanisha hatua ya kifo cha kiroho.

ni nguvu ya Mungu

" Mungu anafanya kazi katika utu wetu wa ndani"

Nitaiharibu hekima ya wenye busara

" nitaharibu busara za watu" au " nitaifanya mipango ya watu wenye busara isifanikiwe kabisa"

1 Corinthians 1:20

Yuko wapi mtu mwenye busara?Yukowapi msomi? Yuko wapi mpingaji wa dunia hii?

Paulo anafafanua kwamba watu wenye busara ya kweli hawatapatikana popote. " ukiwalinganisha na busara inayopatikana kupitia Injili , hakuna watu wenye busara, hakuna wasomi, hakuna waleta hoja!"

Msomi

Ni mtu aliyefahamika kuwa na mafunzo ya hali ya juu.

Mpingaji

Ni mtu anayeleta hoja ya kupinga kulingana na anachojua au ni mtu mweye ujuzi wa kufanya mabishano mbalimbali

Mungu hakuigeuza hekima ya dunia hii kuwa ujinga?

Paulo anatumia swali hili kufafanua kile Mungu amefanya kinyume na hekima ya dunia hii. "Mungu ameonesha kuwa kila kitu kilichokuwa ni hekima kwa watu kilikuwa ni upumbavu kabisa"

wale wanaoamini

Inaweza kumaanisha: 1)Wote wanaoamini ujumbe wa Injili" au 2)wote wanaoamini katika Kristo."

1 Corinthians 1:22

Maelezo kwa Ujumla

Hapa neno "sisi" linawakilisha Paulo na walimu wengine wa Biblia.

Kristo aliyesulubiwa

"Kuhusu Kristo, ambaye alikufa msalabani."

Kikwazo

Ni kama mtu anaweza kujikwaa juu yakizuizi barabarani, vile vile ujumbe wa wokovu kupitia kusulubiwa kwa Kristo ulikuwa kikwazo kwa Wayahudi wasiweze kuamini katika Yesu. "Kutopokelewa" au "Kikwazo sana"

1 Corinthians 1:24

kwa wale ambao waliitwa na Mungu

"Kwa watu walioitwa na Mungu"

Tunamhubiri Kristo

"Tuna fundisha kuhusu Kristo" au "Tunawaambia watu wote kuhusu habari za Kristo."

Kristo kama nguvu na hekima ya Mungu

Inaweza kumaanisha: 1) "Mungu alitenda kwa uweza na hekima kwa kumtuma Kristo kufa kwa ajili yetu" au 2) kupitia Kristo Mungu amethihilisha jinsi alivyo na nguvu na hekima.

nguvu...ya Mungu

Maana nyingine ni kwamba Kristo ni mwenye nguvu na kupitia Kristo, Mungu anatuokoa.

hekima ya Mungu

Maana nyingine ni kuwa Mungu aweka wazi hekima yake kupitia kwa Kristo

ujinga wa Mungu una hekima wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.

"kile ambacho watu huita upumbavu wa Mungu ni hekima ya kweli kuliko busara ya wanadamu, na kile watu huita udhaifu wa Mungu ni nguvu iliyo imara zaidi ya nguvu ya wanadamu"

1 Corinthians 1:26

Sentensi unganishi

paulo anasisitiza nafasi ya waumini Mbele za Mungu

Si wengi wenu

"Wachache tu kati yenu."

hekima katika viwango vya kibinadamu

"jambo linalokubalika kwa watu wengi kuwa ni busara"

mlizaliwa katika ukuu

"maalum kwa sababu familia yako ni muhimu" au '"kifalme"

Mungu alichagua vitu vijinga vya dunia ili kuviaibisha vyenye hekima

Mungu alichagua kutumia watu wanyenyekevu ambao viongozi wa Kiyahudi waliamini kuwa si muhimu kuthibitisha kwamba hawa viongozihawakuwa wa muhimu zaidikuliko wengine kwa Mungu.

Mungu alichagua kilicho dhaifu katika dunia kukiaibisha chenye nguvu

"Mungu aliwachagua wale ambao ulimwengu hufikiri ni dhaifu ili awaaibishe wale ambao ulimwengu hufikiri wapo imara"

1 Corinthians 1:28

hali ya chini na kilichodharauliwa

watu ambao dunia imewakataa."Watu ambao ni wanyenyekevu na kukataliwa."

Vitu ambavyo vimehesabiwa kuwa hakuna kitu

"Vile ambavyo watu kawaida huhesabiwa havithaminiwi"

vitu vilivyo na thamani

"Vitu ambavyo watu kwa kawaida huvithamini"au "Vitu ambavyo watu hudhani vina thamani au vinathaminiwa."

Alifanya hivi

"Mungu alifanya hivi"

1 Corinthians 1:30

Kwa sababu kile Mungu alichofanya

Hii inaonyesha kazi ya Kristo msalabani.

Sisi... yetu

Paulo anajumlisha wale waliotumika naye, pamoja na wakorintho

Kristo Yesu, ambaye amefanyika hekima kwa ajili yetu kutoka kwa Mungu

Hapa inaweza kumaanisha: 1) " Kristo Yesu aliyedhihirisha wazi kwetu jinsi Mungu alivyo wa Hekima" au 2) Kristo Yesu aliyetupatia Hekima ya Mungu"

Anayejisifu, ajisifu katika Bwana

"Kama mtu anajisifu, anapaswa kujisifu kuhusu jinsi Bwana alivyo mkuu."

1 Corinthians 2

1 Wakorintho 02 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB hufanya hivi kwa maneno ya mistari ya 9 na 16, ambayo yanatoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Hekima

Paulo anaendeleza majadiliano kutoka sura ya kwanza ambayo yanalinganisha hekima ya binadamu na hekima ya Mungu. Kwa Paulo, hekima inaweza kuwa rahisi na mawazo ya kibinadamu kuwa pumbavu. Alisema hekima kutoka kwa Roho Mtakatifu ndiyo hekima pekee ya kweli. Paulo anatumia neno "hekima iliyofichwa" wakati anapozungumzia ukweli uliojulikana hapo awali. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#wise and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#foolish)

<< | >>

1 Corinthians 2:1

Sentensi Unganishi

Paulo anatofautisha kati ya hekima ya kibinadamu na hekima ya Mungu. anaeka mkazo kuwa hekima ya kiroho hutoka kwa Mungu.

kaka na dada zangu

Hii inamaanisha washirika wote(wakristo), wanaume na wanawake.

Niliamua kutojua chochote...isipokuwa Yesu Kristo

Paulo alilenga katika kusulubiwa kwa Kristo badala ya mawazo ya kibinandamu: " niliamua kuzungumza zaidi... kuhusu Kristo Yesu

1 Corinthians 2:3

Nilikuwa pamoja nanyi

"Nili kuwa nina watembelea

Katika udhaifu

Inawezekana maana ni 1) "udhaifu wa kimwili" au 2) "Kujisikia kupungukiwa."

maneno ya ushawishi

Ni maneno yanayoonekana kuwa ya busara, na msemaji anategemea watu wafanye anachosema au waamini.

1 Corinthians 2:6

Maelezo ya Jumla

Paulo anaanza kufafanuao hoja yake, kwamba anaposema hekima anamaana gani kwa wasomaji wake.

Sasa tunaizungumza

Neno "sasa" limetumiwa hapa kama alama ya kuonesha fundisho kuu. Paulo anaelezea kuwa hekima ya kweli ni ile hekima ya Mungu.

watu wazima

"Waumini walikomaa kiimani"

kabla ya nyakati

" Kabla Mungu hajaumba chochote"

za utukufu wetu

" ili kudhibitisha ujio wa kutukuzwa kwetu"

1 Corinthians 2:8

Bwana wa utukufu

"Yesu, Bwana wa utukufu."

Mambo ambayo hakuna macho...hayakufikiri, mambo ambayo ...wampendao Mungu

Inataja sehemu tatu za mwili wa mtu kumaanisha kwamba hakuna mtu aliyekwisha kuwa na ufahamu wa kina kwa vitu ambavyo Mungu ameandaa.

Mambo mbayo hakuna jicho limeyaona, hakuna sikio lililoyasikia, mawazo hayakufikiri

Inataja sehemu tatu za mwili wa mtu kumaanisha kwamba hakuna mtu aliyekwisha kuwa na ufahamu wa kina kwa vitu ambavyo Mungu ameandaa.

Vitu vile Mungu amekwisha andaa kwa wale wanampenda yeye.

Bwana amekwisha umba mbinguni vitu vya ajabu kwa wote wanaompenda yeye.

1 Corinthians 2:10

Hivi ni vitu

Paulo anazunguza kuhusu uhalisia wa Yesu na msalaba. mambo ambayo hakuyaeleza kwa kina 2:8 anayafafanua sasa.

Nani ajuaye mawazo ya mtu isipokuwa ni roho ya mtu katika yeye?

Paulo alitumia swali kufafanua kwamba hakuna yeyote ajuaye ni nini mtu anawaza isipokuwa mtu mwenyewe. "Hakuna yeyoteajuaye ni nini mtu anawaza isipokuwa roho ya mtu."

Roho ya mtu

Hii inaonyesha ndani ya mtu,asili ya kiroho yeye

Hakuna yeyote ajuaye vitu vya ndani ya Mungu isipokuwaRoho wa Mungu

"Roho wa Mungutu ajuaye vitu vya ndani ya Mungu"

1 Corinthians 2:12

Maelezo ya Jumla

Hapa "sisi" inajumlisha Paulo na wasikilizaji wake.

tuliyopewa na Mungu

"Kwamba Mungu alitupatia bure " au "kwamba Mungu ametupa kabisa bila malipo"

Roho hutafasiri maneno ya kiroho kwa hekima ya kiroho

Roho Mtakatifu huwasiliana kweli wa Mungu kwa waumini katika maneno ya rohoyenyewew na hutupa yenyewe hekima yake yenyewe.

hutafasiri

"fafanua"

1 Corinthians 2:14

Maelezo ya jumla

hapa neno "sisi" linajumuisha Paulo pamoja hadhira (watu anaowaandikia)

Mtu si wa kiroho

Mtu asiye mkristo,ambaye bado hajapokea Roho Mtakatifu.

yanatambuliwa kiroho.

"Kwa sababu kufahamu mambo haya kuanatokana na msaada wa Roho"

Kwa yule wa kiroho

"Muumini, aliyepokea Roho"

Ni nani anaweza kuyajua mawazo ya Bwana, ambaye anaweza kumfundisha yeye?

Paulo alitumia hili swali kufafanua kwamba hakuna yeyote ajuaye mawazo ya Bwana. "Hakuna yeyote anaweza kujua mawazo ya Bwana.Hivyo hakuna yeyote anaweza kumfundisha Bwana kitu chochote ambacho hakukifahamu kabla."

1 Corinthians 3

1 Wakorintho 03 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka nukuu kutoka kwa Agano la Kale upande wa kulia zaidi kwenye ukurasa ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivyo kwa maneno yaliyotajwa kwenye mistari ya 19 na 20.

Dhana maalum katika sura hii

Watu wa kimwili

Waumini wa Korintho walikuwa hawajakomaa kwa sababu ya vitendo vyao vibaya. Anawaita "wa kimwili," maana matendo yao ni kama ya wasioamini. Neno hili linatumika kwa kinyume na wale ambao ni wa "kiroho." Wakristo wanaofuata "mwili" wao wanatenda upumbavu. Wao wanafuata hekima ya ulimwengu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#righteous, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#flesh, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#spirit and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#foolish and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#wise)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Mifano

Kuna mifano nyingi katika sura hii. Paulo anatumia "watoto" na "maziwa" ili kuonyesha kutokomaa kwa kiroho. Anatumia mifano nyingi na kumwagilia maji ili kuelezea majukumu yake na Apolo katika kukuza kanisa la Korintho. Paulo anatumia mifano mingine katika kusaidia kufundisha ukweli wa kiroho kwa Wakorintho na kuwasaidia kuelewa mafundisho yake. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

<< | >>

1 Corinthians 3:1

Sentensi Unganishi

Paulo sasa anawakumbusha waumini wa Korintho juu maisha yao halisi badala ya kuishi kwa kujiheshimu kuzingatia nafasi yao mbele za Mungu. pia anawakumbusha kuwa mtu anayewapa mafundishi hawezi kuwa na unuhimu kama Mungu ambaye anawawezesha kukua.

kaka na dada zangu

hii inamaanisha washirika wote(wakristo) wanaume na wanawake

Watu wa kiroho

Watu wanaoishi kwa kumtii Roho

Watu wa mwilini

Watu ambao hufuata matakwa yao wenyewe

Kama watoto wachanga katika Kristo

Wakorintho wanalinganishwa na watoto wachanga katika umri na katika ufahamu. "Kama waumini wachanga katika Kristo"

Niliwanywesha maziwa na siyo nyama

Wakorintho wanaweza kuelewa mafundisho rahisi kama watoto wachanga ambao wanaweza kunywa maziwa tu. Hawajawa watu wazima kuelewa mafundisho ya kina kama watoto wakubwa ambao sasa wanaweza kula chakula kigumu.

Hamko tayari

"Hamko tayari kuelewa mafundisho magumu kuhusu kumfuata Kristo."

1 Corinthians 3:3

Bado wa mwilini

bado wanatabia ya dhambi au wanamatamanio ya kidunia

hamuishi kulingana na mwili, na je, hamtembei kama kawaida ya kibinadamu?

Paulo alikuwa anawaonya wakorintho kwa tabia zao za dhambi. "Mnapaswa kuona aibu kwa sababu munaishi kwa kufuata tamaa zenu mbaya na munaishi kwa kufuata desturi za kibinadamu.

Hamuishi kwa kawaida ya kibinadamu?

Paulo alikuwa anawaonya wakorintho kwa tabia zao za dhambi. "Mnapaswa kuona aibu kwa sababu munaishi kwa namna ileile wanayoishi watu wasio na Roho.

Apolo ni nani? Na Paulo ni nani?

Paulo alikuwa anafafanua kwamba yeye na Apolo hawakuwa chanzo cha injili na ndipo hawastahiri kufuatwa. "Ni mbaya kuunda makundi kufuata Apolo au Paulo!"

Paulo ni nani?

Paulo anaongelea habari zake mwenyewe kana kwamba anazungumzia habari za mtu mwingine. ni kama vile anauliza: "mimi ni nani?" au anasema "mimi siyo wa muhimu!"

Watumishi wa yule mliyemwamini

Paulo ajibu swali lake kwa kusema kwamba yeye na Apolo ni watumishi wa Mungu. "Paulo na Apolo ni watumishi wa Kristo, na mmeamini katika Kristo kwa sababu tunamtumikia yeye".

mliyemwamini, kwa kila ambaye Bwana alimpa jukumu.

" Sisi ni watu tu wa Bwanamuliyemwamini ambaye ametupatia majukumu."

1 Corinthians 3:6

Nilipanda

Ufahamu wa neno la Mungu unalinganishwa na mbegu ambayo lazima iwe imepandwa ili istawi

akatia maji

Kama vile mbegu huhitaji maji,imani inahitaji mafundisho zaidi ili iweze kukua.

Kukua

Kama mmea hukua na kuendelea,pia imani na ufahamu katika Mungu hukua nakuwa na kuwa na kina na uimara.

Kwa hiyo, si aliye panda ... anachochote. Lakini ni Mungu anayekuza.

Paulo anaeleza kwamba si yeye wala Apolo aliye nawajibu kwa ajili yakukua kiroho kwa wakristo, lakini ni utendajiwa Mungu.

anayekuza.

Paulo anaelezea kwa kielelezo cha ukuaji wa miti kuhusu ukuaji wa imani ya Wakoritho. : Anawezasha miti kukua" au " Mungu huwawezesha wakristo kumfahamu na kumjua Yeye kwa undani"

1 Corinthians 3:8

Anayepandana anayemwagilia ni sawa

Upandaji na umwagiliaji maji inahesabika ni kazi moja,ambayo Paulo analinganisha yeye mwenyewe na Apolo katika kuwahudumia kanisa la Wakorintho.

Ujira

Kiasi cha fedha ambacho mfanyakazi analipwa, kinalinganishwa kwa kiasi gani alichofanya kazi.

Sisi

Hii inaonyesha kwa Paulo na Apololakini si kanisa la Korintho

Wafanyakazi ya Mungu

Paulo anajitambulisha yeye na Apolo kuwa ni watendakazi pamoja.

bustani ya Mungu

Mungu anawajali waumini wa Korintho, Kama vile mtu ahudumiaye bustani yake ili kuzalisha matunda.

Jengo la Mungu

Mungu amewafanyia usanifuna kuwaumba waumini wa Korintho,kama vile mtu anayejenga jengo.

1 Corinthians 3:10

Kulingana na neemaya Mungu ambayo nimepewa

"Kulingana na uwezo ambao Mungu kweli amenipa kufanya."

Niliweka msingi

Paulo alianzisha mafundisho yake ya imani na wokovu katika Yesu Kristo, hii ilikuwa kama kuweka msingi wa jengo.

Mwingine anajenga juu yake

Paulo anamzungumzia mtu au watu wanaowafundisha Wakorintho kuwa kama maseremala wanaofanya ujenzi juu ya msingi aliokwisha kuujenga.

Kila mtu

Hii inaonyesha kwa wafanyakazi wa Mungu kwa ujumla. "Kila mtu anayemtumikia Mungu."

Hakuna mwingineanaweza kuanzisha msingi mwingine zaidi ya ule ambao umekwisha anzishwa.

hii inaweza kumaanisha " Tayari nimekwisha anzisha msingi ambao yeyote anaweza kujenga" au " hakuna awezaye kujenga Msingi zaidi ya ule niliojenga mimi, Paulo"

1 Corinthians 3:12

Maelezo ya Jumla

Paulo anazungumzia shughuli ambazo wajenzi hufanya wanapojenga jengo akifananisha na kile wanachofanya walimu wa Korintho. Wjenzi mara nyingi hutumia dhahabu, fedha, au mawe ya thamani kama mapambo ya majengo.

Sasa kamayeyote anajengajuu ya msingi kwa dhahabu,fedha, mawe ya thamani, miti,manyasi, au majani

Vitu vya ujenzi yamelinganishwa na thamani ya kiroho yatumikayo kwa kujenga tabia ya mtu na shughuli wakati wa maisha yake. "Hata mtu anajenga kwa thamani, vitu vya kudumu au vya chini,vitu vya kung'aa."

Mawe ya thamani

"Mawe ya gharama kubwa"

Kaziyake itafunuliwa

" Mungu ataweka wazi kila kazi aliyoifanya mjenzi."

kwa mwanga wa mchana utaidhihirisha

Neno "mwanga" ni sitiari kumaanisha wakati Mungu atakapomuhukumu kila mtu. Mungu atakapo weka wazi mafundisho ya walimu hawa, itakuwa kama nuru ya jua juu ya giza la usiku.

Kwa kuwa itadhihirishwa na moto. Moto utajaribu ubora wa kazi wa kila mmoja alichofanya.

Kama moto utadhihirisha uimara au kuharibu udhaifu wa jengo,Moto wa Mungu utahukumu juhudi ya mtu na shughuli. "moto utaonyesha thamani ya kazi yake."

1 Corinthians 3:14

Maelezo ya Jumla

Maneno "mtu" , "chochote mtu" "yeye" na " yeye mwenyewe" yanahusiana na washirika( waumini)

kitabaki

"Salia" au "kubakia"

Kama kazi ya mtu itateketea

"Kama moto utaharibu kazi ya mtu yeyote" au "Kama moto utahapoteza kazi ya mtu yeyote."

Yeyote...yeye...mwenyewe

Haya maneno yanaonyesha "mtu""mtu" au "yeye"

Atapata hasara.Lakini yeye mwenyewe ataokolewa

"Atapoteza kazi ile na tuzo yoyote anaweza kupata kama kazi ile itastahimili katika moto, lakini Mungu atamwokoa."

1 Corinthians 3:16

Hamjuwi kuwa ninyi ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

Paulo anawakalipia Wakorintho: "Mnafanya kana kwamba hamjui kuwa ninyi ni hekalu la Mungu na Roho wa Mungu anakaa ndani yenu!"

Haribu

"haribu" au "hasara"

Mungu atamharibu mtu yule,Kwan hekalu la Mungu ni takatifu, na ni ninyi.

"Mungu atamharibu mtu yule kwasababu hekalu la Mungu ni takatifu na ninyi ni watakatifu piaa."

1 Corinthians 3:18

Mtu asijisifu mwenyewe

Mtu yeyote hanapaswa kuamini kwa kujidanyanya mwenyewe kwamba ni mwenye hekima katika ulimwengu huu.

Nyakati hizi

hii inahusu namna ambavyo watu wasioamini hufanya maamuzi

awe kama "mjinga"

"Yule mtu anapaswa kukubali kile ulimwengu hufikiri ni ujinga kwa ajili ya kupata hekima ya kweli ya Mungu"

Huwanasa wenye hekima kwa hila zao

Mungu huwatega watu ambao wanafikiri kuwa wana akili na anatumia mipango yao kuwatega wao

Bwana anajua mawazo ya wenye busara ni ubatili

"Bwana anajua kwamba mipango ya watu ambao hufikiri wana busara ni" au "Bwana anaelewa mipango yote ya wenyebusara na anajua yote ilivyo."

ubatili

"hayatumiki" "hakuna thamani"au "Hakuna pointi"

1 Corinthians 3:21

ninyi ni wa Kristo na Kristo ni wa Mungu

" Ninyi ni mali ya Kristo na Kristo ni mali ya Mungu"

1 Corinthians 4

1 Wakorintho 04 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Kiburi

Paulo analinganisha Wakorintho walio na kiburi na mitume walio wanyenyekevu. Waumini wa Korintho hawakuwa na sababu ya kuwa na kiburi. Yote waliyokuwa nayo, na waliyokuwa; yalikuwa zawadi kutoka kwa Mungu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#apostle)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Mifano

Paulo anatumia mifano nyingi katika sura hii. Anaelezea mitume kama watumishi. Paulo anazungumza juu ya gwaride la ushindi ambapo mitume watakuwa ni wafungwa ambao watauawa. Anatumia fimbo ili kumaanisha adhabu. Anajiita baba yao kwa sababu yeye ni "baba yao wa kiroho." (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#spirit)

Kinaya

Paulo anatumia kinaya kuwaaibisha Wakorintho kwa kuwa na kiburi. Waumini wa Korintho wanatawala lakini mitume wanateseka. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-irony)

Maswali ya uhuishaji

Paulo anatumia maswali kadhaa ya uhuishaji katika sura hii. Anayatumia kusisitiza neno muhimu anapofundisha Wakorintho. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion)

<< | >>

1 Corinthians 4:1

sentensi unganishi

baada ya kuwakumbusha watu kuwa wasiwe na majivuno juu ya nani aliwafundisha habari za Bwana na kuwabatiza, pia anawakumbusha washirika(waumini) wa Korintho kuwa wanapaswa kuwa wanyenyekevu.

Katika hili

"Kwa sababu sisi ni mawakili"

kinachotakiwa kwa uwakili ni kwamba wawe

" tunatakiwa kuwa"

1 Corinthians 4:3

Ni kitu dogo sana kuwa ninahukumiwa na ninyi

Paulo analinganisha kati ya hukumu ya kibinadamu na hukumu ya Mungu. Hukumu ya binadamu ni ya kubahatisha kulinganisha na hukumu ya kweli ya Mungu juu ya binadamu

Sijihukumu mimi mwenyewe

"Sijasikia lawama yoyote juu yangu kwamba nilifanya maovu"

hii haina maana kuwa mimi ni mwenye haki. Ni Bwana anihukumuye

"kule kutosikia lawama siyo uthibitisho kuwa mimi sina hatia. Bwana anajua kama mimi sina hatia au nina hatia.

1 Corinthians 4:5

Kwa hiyo,msitamke hukumu

Kwa kuwa Mungu atahukumu atakaporudi, tusihukumu.

atayaleta nuruni mambo yaliyofichika gizani na kufunua makusudi ya mioyo

Mungu ataweka wazi mawazo na dhamira za watu. Hakuna kitakachofichika mbele za Bwana.

ya mioyo

"ya mioyo ya watu"

1 Corinthians 4:6

kaka na dada zangu

Hii inamaanisha washirika/ wakristo (waumini)wote wanaume na wanawake

kwa ajili yenu

"kwa ajili ya ustawi wenu, au mafaa yenu"

tofauti kati yenu...Ni nini ulicho nacho hukukipokea... kupokea bure, kwa nini mnajivuna kama hamkufanya hivyo

Paulo anawaongelea Wakorintho kana kwamba anazumgumza na mtu mmoja, ndiyo maana katika matukio yote anatumia kiwakilishi cha "wewe".

ni nani aonaye tofauti kati yenu na mwingine?

Paulo aliwaonya Wakorintho ambao wanafikiri wao ni bora kwa kuwa wameamini injili kwa Paulo au kwa Apolo. "Hamko bora zaidi ya watu wengine."

Ni nini ulicho nacho hukukipokea bure?

Paulo alieleza kwamba Mungu aliwapa kile walicho nacho kwa bure. "Kila kitu mlichonacho, Mungu amewapa bure, bila malipo yoyote!"

Kwa nini mnajivuna kama hamkufanya hivyo?

Paulo alikuwa anawaonya kwa kujivuna kwa kile walichopokea. "Hamna haki ya kujivuna" au "Msijivune kabisa."

1 Corinthians 4:8

Maelezo ya Jumla

Paulo anatumia msemo wa kejeli ili kuwafanya Wakorintho waone aibu na kutambua kuwa walikuwa wakitenda dhambi walipojisifu wenyewe pamoja na kuwasifia walimu wao.

Mungu ametuweka sisi mitume kama kutuonyesha

Paulo anaeleza njia mbili jinsi Mungu amekwisha weka mitume kwa kuonyesha wazi kwa ulimwengu uone

ametuweka sisi mitume kama kutuonyesha

Mungu ameonyesha wazi mitume kama tu wafungwa wakti wa mwisho wa gwaride la jeshi la Kirumi,ambao tunaabishwa mbele ya kutekeleza kwao.

kama watu waliohukumiwa kuuawa

Mungu ameweka mitume kuonyesha wazi kama watu waliotayari kutekelezwa.

kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa wanadamu

Neno "ulimwengu" ni jumla ya viumbe vya kiroho (malaika) na viumbe vya asili (wanadamu). kwa hiyo anataja vitu vitatu: kwa ulimwengu, kwa malaika, na kwa wanadamu

1 Corinthians 4:10

Sisi tu wajinga kwaajili ya Kristo, lakini mna busara katika Kristo.

Paulo anatumia kinyume kutofautisha mtazamo wa dunia na mtazamo wa Kikristo wa kuamini katika Kristo.

Sisi ni wadhaifu, lakini ninyi mna nguvu

Paulo anatumia kinyume kutofautisha mtazamo wa kidunia na mtazamo wa kikristo wa kuamini katika Kristo.

Mmeheshimiwa

"Watu wanawahesabu Wakorintho katika nafasi ya heshima."

Tunasika katika hali ya kutoheshiwa

"Watu wanatuhesabu sisi mitume katika nafasi ya kutoheshiwa."

Hata kwa saa hii iliyopo

"Mpaka sasa" au "Kufikia sasa"

Tumepigwa vibaya

"Adhibiwa kwa mapigo makaliya mwili"

1 Corinthians 4:12

Tunapodharauliwa, tunabariki

"Wakati watu wanapotudharau, sisi tunawabariki."

Dharau

"Beza"inawezekana "onea" au "laani"

Tunapoteswa

"Wakati watu wanapotutesa"

Tunapokashifiwa

"Wakati watu wanatukashifu"

Tumekwisha kuwa,na tunasubiriwa kuwa, kukataliwa na dunia

"Tumekuwa, na watu bado wanatusubiri kuwa, takataka za dunia."

1 Corinthians 4:14

Siandiki vitu hivi kuwaaibisha ninyi, lakini kuwarudi ninyi

Sifanyi kuwaaibisha, lakini kuwathibitisha" au Sijaribu kuwaaibisha, lakini nataka kuwarudi."

Sahihisha

"thibitisha"au "fanya bora"

Waalimu makumi elfu

Huu ni ukuzaji wa idadi ya watu wanao waongoza,Kuelezea umuhimu wa wa baba mmoja wa kiroho.

watoto...baba

Kwa sababu Paulo amewaongoza kwa Kristo,yeye ni kama baba kwa Wakorintho

sihi

"Kuwatia moyo kwa nguvu" au "Kuthibitisha kwa nguvu"

1 Corinthians 4:17

Sasa

Hili neno linaonyesha kwamba Paulo anabadilisha mada yake kwa kuwarudi wenye tabia ya majivuno walio waumini wa Korintho.

1 Corinthians 4:19

Nitakuja kwenu

"Nitawatembelea"

haitegemeikatika kusema

"haitendwi kwa maneno" au "Si nini usemacho"

Nini unachotaka?

Paulo alikuwa anawasihi kwa mwisho Wakorintho, kamaamekwisha warudi kwa makosa waliyokwishafanya. "Niambieni nini mnataka kitokee sasa."

Nije kwenu na fimbo au na upendo na roho ya upole.

Paulo anatoa tabia mbili tofauti kwa Wakorintho, atakazotumia atakapofika kwao. "Mnataka nije kuwafundisha ninyi kwa lazima, au mnataka nionyeshe upendo na kwa upole?"

upole

"wema au "uzuri"

1 Corinthians 5

1 Wakorintho 05 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka nukuu kutoka kwa Agano la Kale upande wa kulia zaidi kwenye ukurasa ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivyo kwa maneno yaliyotajwa kwenye mstari wa 13.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Maneno ya badla ya kupunguza uzito

Paulo anatumia maneno ya rahisi ya kupunguza uzito kuelezea mada nyeti. Sura hii inahusika na uasherati wa kijinsia wa mwanachama mmoja wa kanisa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-euphemism and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#fornication)

Mfano

Paulo anatumia ulinganisho uliopanuliwa kwa kutumia sitiari nyingi. Chachu inawakilisha uovu. Mkate labda inawakilisha kanisa nzima. Mikate isiyotiwa chachu inawakilisha kuishi kwa utakatifu. Basi kifungu hiki kina maana: Je, hujui kwamba uovu mdogo utaathiri kanisa lote? Hivyo basi uondoe uovu huu ili uweze kuishi kwa utakatifu. Kristo ametolewa kama sadaka kwa ajili yetu. Kwa hiyo tuwe waaminifu na wa kweli na sio waovu na wanaofanya mabaya. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#evil, https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#unleavenedbread and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#purify and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#passover)

Maswali ya uhuishaji

Paulo anatumia maswali ya uhuishaji katika sura hii. Anayatumia ili kusisitiza maneno muhimu anapofundisha Wakorintho. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion)

<< | >>

1 Corinthians 5:1

Sentensi Unganishi

Paulo anaelezea kwa ufasaha kwamba amesikia kuna dhambi miongoni mwa waumini wa Wakorintho, na namna Wakorintho walivyojisifu na kukaa pamoja na mtu aliyetenda ile dhambi.

Ile hairuhusiwi hata miongoni mwa mataifa

Katika muundo tendaji " hata watu wa wasioamini hawawezi kuruhusu"

Mke wa baba

mke wa baba yake, lakini yawezekana si mama yake wa kumza

Hampaswi kuhuzunika badala?

Hili ni swali lenye jibu limetumika kuwakemea Wakorintho. "Mnapaswa kuhuzunika kwa hili jambo!"

Yeye aliyefanya hivi lazima awe ameondolewa miongoni mwenu

Katika hali ya muundo tendaji:- "Ni lazima aondolewe miongoni mwenu aliyefanya jambo hili ."

1 Corinthians 5:3

...nipo nanyi kiroho

"... kila wakati nafikiri juu yenu."

nimekwisha mhukumu yeye aliyefanya hivi

"Nimekwisha ona huyu mtu ana hatia"

Mnapokutanika pamoja

"kutana"

katika jina la Bwana Yesu

lugha ya kuelezea tendo la kukusanyika pamoja kumwabudu Yesu Kristo

Nimekwisha

" tayari nimemhukumu mtu huyo"

kumkabidhi mtu huyu kwa Shetani

Hii inaonyesha kumfukuza mtu kutoka kwa watu wa Mungu,ili aishi katika utawala wa Shetani, ulimwengu nje ya Kanisa.

ili kwamba mwili wake uharibiwe

ili kwamba mwili wa mtu huyo upate maradhi kwa kurudiwa na Mungu kwa dhambi yake

1 Corinthians 5:6

Majivuno yenu si kitu kizuri

"Majivuno yenu ni mabaya"

Hamjui chachu kidogo huharibu donge zima?

Kama hamira kidogo husambaa kwa mkate mzima, hivyo dhambi ndogo inaweza kuathiri ushirika wote wa waumini.

Kristo, Mwana Kondoo wetu wa pasaka amekwisha kuchinjwa

"Bwana Mungu amemtoa KristoYesu, mwanakondoo wetu wa Pasaka"

1 Corinthians 5:9

wazinzi

Hii inahusu watu wanaokiri kuamini katika Kristo lakini wana tabia mbaya.

Wazinzi wa dunia hii

Watu waliochagua kuishi katika maisha uzinzi,ambao si waumini

wenye tamaa

"Wale walio na tamaa" au "Wale waliotayari kupoteza heshima ili kupata kitu wanchotamani"

Wanyang'anyi

Hii ina maana watu ambao"wanadanganya au tapeli mali za watu wengine"

basi ingewapasa mtoke duniani.

" ingeliwabidi kukaa mbali na watu wote"

1 Corinthians 5:11

Sentensi Unganishi

Paulo anawaambia namna ya kukaa na waumini waliopo kanisani ambao hawataki kukosolewa juu ya matendo yao ya zinaa na dhambi zilizo wazi kwa wengine.

yeyote aliyeitwa

" yeyote anayejiita mwenyewe"

Kaka au Dada

Hii inamaanisha mshirika katika ukristo ama wanamke au mwanaume

Kwa hiyo nitajihusishaje kuwahukumu walio nje ya Kanisa?

Paulo anasisitiza kwamba yeye siyo hakimu wa watu walio nje ya kanisa. kwa maneno mengine "Sipaswi kutoa hukumu kwa watu ambao si wa kanisani"

ninyi hamkuwahukumu walio ndani ya kanisa?

"Mnapaswa kuwahukumu wale wako ndani ya kanisa."

1 Corinthians 6

1 Wakorintho 06 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mashtaka

Paulo anafundisha kwamba Mkristo hapaswi kuchukua Mkristo mwingine kwa mahakamani mbele ya hakimu asiye Mkristo. Ni bora zaidi kudanganywa. Wakristo watawahukumu malaika. Kwa hiyo wanapaswa kuwa na uwezo wa kutatua matatizo kati yao wenyewe. Ni mbaya sana kutumia mahakama kumdanganya mwamini mwingine. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#judge)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Mfano

Hekalu la Roho Mtakatifu ni mfano muhimu. Inaelezea mahali ambapo Roho Mtakatifu anakaa na kuabudiwa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Maswali ya uhuishaji

Paulo anatumia maswali kadhaa ya uhuishaji katika sura hii. Anayatumia kusisitiza manen muhimu anapofundisha Wakorintho. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion)

<< | >>

1 Corinthians 6:1

Sentensi Unganishi

Paulo anaelezea jinsi waumini wanavyoweza kusuruhisha migogoro miongoni mwao

Tatizo

"Kutokubaliana" au "Mabishano"

je anathubutu kwenda kwa mahakama ya dunia mbele ya hakimu asiyeamini, kuliko mbele ya waumini?

Paulo asema kwamba Wakristo lazima wamalize matatizo miongoni mwao wenyewe. " Asithubutu kwenda.... waumini" au " anapaswa kuwa na hofu ya Mungu na asiende...waumini!"

mahakama ya wasio haki

Ni sehemu ambapo hakimu wa serikali huamua kesi na kuamua nani aliye na haki.

Hamjuwi kwamba waumini watauhukumu ulimwengu?

Paulo anawafanya Wakoritho wapate aibu kwa kutenda kana kwamba hawajui

Kama mtauhukumu ulimwengu, hamuwezikuweka sawa mambo yasiyo ya muhimu?

Paulo anasema baadaye watapewa wajibu mkubwa, hivyo kwa sasa lazima kushughulikia haya maswala madogo. "Mtauhukumu ulimwengu wakati ujao, hivyo mnaweza kusuruhisha tatizo hili kwa sasa."

Je mnajui kwamba tutawahukumu malaika?

Paulo anashangaa maana wanaonekana hawajui "Mnajua kwamba tutawahukumu malaika."

Kwa kiasi gani zaidi, tunaweza kuamua mambo ya maisha haya?

"Kwa sababu tunajua kuwa tutawahukumu malaika, na katika maisha haya tunauhakika kuwa Mungu anauwezo wa kuhukuma mambo mbali mbali."

1 Corinthians 6:4

Kama tunaweza kuhukumu mambo ya maisha haya, kwa nini mnathubutu kupeleka mashitaka mbele ya wasiosimama kanisani?

Inaweza kumaanisha 1) hili ni swali lisilohitaji jibu au 2) hii ni sentensi " Mliwahi kusuruhisha migogoro inayohusu maswala ya muhimu maishani, hamkuruhusu matatizo ya Wakristo yasuruhishwe na wasioamini" au 3) Hii ni amri "mnaposuruhisha juu ya maswala muhimu ya maisha, pia suruhisheni migogoro ambayo ipo kanisani " "Kama umeitwa kufanya maamuzi kuhusu maisha ya kila siku." au "Kama una ulazima wa kuweka sawa mambo ambayo ni muhimu katika maisha haya."

Kama tunaweza kuhukumu mambo ya maisha haya

" kama mmeitwa kufanya maamuzi kwa maisha ya kila siku" au " kama mtasuruhisha maswala ya muhimu katika maisha haya"

kwa nini mnathubutu kupeleka mashitaka

" msipeleke mashitaka hayo"

mbele ya wasiosimama kanisani?

Maana zinazokubalika 1) " acheni kupeleka mashitaka hayo kwa watu walio nje ya kanisa" au 2) " mngeweza kupeleka mashitaka hayo hata kwa waumini wasioamika kwa waumini wenzao"

kwa aibu yenu

" kwa kukosa heshima" au "kwa kuonyesha kuwa mmeshindwa katika swala hili"

Hakuna mwenye busara miongoni mwenu wa kutosha kuweka mambo sawa kati ya ndugu na ndugu?

" mnapaswa kuona aibu kwamba hamuwezi kupata muumini wenye hekima kumaliza mibishano miongoni mwa waumini"

ndugu

hapa inamaanisha waumini wote

mashitaka

" mabishano" au " kushindwa kukubaliana"

Lakini kama ilivyo

" namna ilivyo sasa" au " lakini badala "

mwamini mmoja huenda mahakamani dhidi ya muumini mwingine, na mashitaka hayo huwekwa mbele ya hakimu asiyeamini!

" waumini wenye mgogoro wanaomba usuruhishi kwa mahakimu wasioamini kufanya maamuzi juu yao"

mashitaka hayo huwekwa

" muumini anapeleka mashitaka"

1 Corinthians 6:7

usumbufu

"shindwa" au "poteza"

Kwanini msumbuke kwa mabaya? Kwaninimruhusu ninyi wenyewe kudanganywa?

"Ni bora kuacha wengine kuwafanyia mabaya na kuwadanganya kuliko kuwapeleka mahakamani,"

kaka na dada zenu wenyewe

Waumini wote katika Kristo ni kaka na dada kwa kila mmoja. "Waumini wenzako"

1 Corinthians 6:9

Hamjui kwamba

Paulo anaelezea kwamba wanapaswa tayari kuwa wanaujua ukweli huu. "Tayari umejua vile"

Wasio haki hawatarithi

"wenye haki tu watarithi"

kurithi ufalmewa Mungu

Mungu hatawahukumu kama wenye haki katika hukumu, na hawataingia katika uzima wa milele.

Wafiraji

Hawa ni malaya ambao ni wanaume hulala na wanaume wengine.

Wale wanaofanya uzinzi

Wanaume ambao hulala na wanumewengine(Walawiti)

wenye tamaa

watu walio tayari kutumia njia mbaya kujipatia mali

wadhalimu

"matapeli"

mlisafishwa

Mungu amewasafisha

mliwekwa wakfu kwa Mungu

Mungu amewatenga kwa ajili yake.

Mmefanywa haki pamoja na Mungu

Mungu amewafanya haki pamoja na yeye

1 Corinthians 6:12

Sentensi Unganishi

Paulo anawakumbusha waumini wa Korintho kuwa Mungu anataka wawe watakatifu kwa sababu Kristo aliwanunu kwa kifo chake.

Kila kitu ni halali kwangu

Mungu ameniruhusu kufanya kila kitu.

lakini si kila kitu kina faida

Lakini si kila kitu ni kizuri kwangu

Sitatawaliwa na chochote kati hivyo

Sitaruhusu vitu hivi vinitawale

"Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa chakula," lakini Mungu atavitowesha vyote

""Wengine husema 'chakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa chakula; ' lakini Mungu atavitowesha vyotetumbo na chakula"

kutowesha

"kuharibu"

1 Corinthians 6:14

alimfufua Bwana

sababisha Yesu kuishi tena

Hamjuwi kwamba miili yenu ni muunganiko wa Kristo?

Kama tu mikono na miguu ni muunganiko wa miili yetu. Hivyo miili yetu ni muunganiko na mwili wa Kristo- Kanisa. "Miili yenu ni kiungo cha Kristo"

Nitatoa muunganiko wa Kristo na kuungana kwa kahaba?

"Ninyi ni viungo vya Kristo.Sitawaunganisha kwa kahaba."

Haiwezekani!

"Haiwezi kamwe kutokea vile!"

1 Corinthians 6:16

Hamjui kwamba

" nataka niwakumbushe kuwa..."

anayeungana na kahaba amekuwa mwili mmoja naye

" mwanaume anayeunganisha mwili wake kwenye mwili wa kahaba , miili yao inakuwa mwili mmoja"

Lakini anayeungana na Kristo amekuwa roho moja na yeye

" Bwana anapounganisha roho yake kwenye roho ya mtu, roho zao zinakuwa roho moja."

1 Corinthians 6:18

Kimbieni

kukimbia kimwili kwa mtu kutoka kwa hatari kunafanishwa na kiroho kwa mtu kukataa dhambi. "Toka"

"Kila dhambi ambayo mtu hufanya ni nje ya mwili," lakini uzinzi mtu hutenda dhambi kinyume na mwili wake mwenyewe

Dhambi ya uzinzi ni mbaya kwa sababu ni dhambi dhidi ya mwili wa mtenda dhambi

hutenda

"kufanya tendo"

1 Corinthians 6:19

Hamjui...

Nataka niwakumbushe...

Mwili wako

Mwili wa kila Mkristo binafsi ni hekalu la Roho Mtakatifu

Hekalula roho Mtakatifu

Hekalu limewekwa wakfu kwa kusudi maalum, na pia ni mahali anapoishi. Katika njia moja, kila mwili wa muumini wa wakorintho ni kama hekalu, kwa sababu Roho Mtakatifu yupo pamoja nao.

Ninyi mlinunuliwa kwa thamani

Mungu amelipa kwa uhuru wa Wakorintho kutoka katika utumwa wa dhambi. "Mungu alilipa kwa uhuru wenu."

Kwa hiyo

"Hivyo" au "Kwa kuwa hii ni kweli" au "kwa sababu ya ukweli huu."

1 Corinthians 7

1 Wakorintho 07 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Paulo anaanza kujibu mfululizo wa maswali ambayo Wakorintho wanaweza kumwuliza. Swali la kwanza ni kuhusu ndoa. Swali la pili ni kuhusu mtumwa akijaribu kuwa huru, asiye Myahudi kuwa Myahudi, au Myahudi kuwa asiye Myahudi.

Dhana maalum katika sura hii

Talaka

Paulo anasema Wakristo walio katika ndoa hawapaswi kutaliki. Mkristo aliyeolewa na asiyeamini hapaswi kuacha mume au mke wake. Ikiwa mume au mke asiyeamini anaondoka, hii sio dhambi. Paulo anashauri kwamba, kwa sababu ya nyakati ngumu na kuwa muda ambapo Yesu atarudi umekaribia, inakubalika kutoolewa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Maneno ya rahisi ya kupunguza uzito

Paulo anatumia maneno ya rahisi ya kupunguza uzito kwa busara kutaja mahusiano ya ngono. Hii mara nyingi hii ni mada nyeti. Tamaduni nyingi hazitaki kuzungumza waziwazi kuhusu mambo haya. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-euphemism)

<< | >>

1 Corinthians 7:1

Sentensi Unganishi

Paulo anatoa maelekezo mahususi juu ya ndoa

Sasa

paulo anatambulisha mada mpya katika mafundisho yake

Vitu mlivyoandika kwangu

Wakorintho walikwisha andika barua kwa Paulo kuomba kupatiwa majibu kuhusu baadhi ya maswali.

kwa mwanaume

Hapa ina maanisha mwanume mwenzi au mme

Lakini kwa sababu ya majaribu kwa matendo mengi maovu

'Lakini kwa sababu Shetani anawajaribu watu kutenda dhambi ya uzinzi'

1 Corinthians 7:3

haki ya ndoa

Waume na wake wanawajibika kwa kawaida kulala na wenzi wao.

1 Corinthians 7:5

Msinyimane

"Msikatae kulala pamoja wenzi wenu"

Fanyeni hivyo ili kupata muda wa maombi

Ili mpate muda maalumu wa maombi.

Fanyeni hivyo

""Jikabidhi ninyi wenyewe"

kurudiana tena pamoja

"Lala pamoja tena"

Kwa sababu ya kukosa kujitawala wenyewe

tawala- "Kwa sababu baada ya siku, tamaa yako ya zinaa itakuwa ngumu zaidi kuitawala"

Ninasema vitu hivi kwenu zaidi kama hiari nasio kama amri

Hapa inamaanisha 1) kuoana na kulala pamoja 2) kuacha kulala pamoja kwa muda

kama mimi

Labda Paulo hakuwahi kuoa au mke wake alifariki.

Lakini kila mmoja na karama yake kutoka kwa Mungu.Mmoja ana aina hii ya karama, na mwingine karama ile.

Mungu anawawezesha watu kufanya mambo yanayotofautiana.

1 Corinthians 7:8

wasioolewa

Hawa ni wale ambao hawajaolewa.

wajane

" wanawake walifiwa na waume wao"

ni vizuri

Neno "Vizuri"hapa linaonyesha haki na kukubalika. "Ni haki na kukubalika"

kuwaka tamaa

"Kuishi kwa tamaa ya kutaka kulala na mtu fulani"

1 Corinthians 7:10

asitengane

Hakuna tofauti kati ya taraka na kutengana. kutengana ni kuacha kuishi pamoja

apatane na

"Anapaswa kutatua mambo yake pamoja na mme wake na kurudi kwake"

asimpe talaka

"haipaswi kuachana."

1 Corinthians 7:12

anaridhika

"utayari" au "utoshelevu"

Kwa mwanaume asiyeamini atakubaliwa

" Mungu amewakuli wanaume wasioamini"

Mwanamke asiyeamini atakubaliwa

"Mungu ameshamkubali mwanamke asiyeamini"

wamekubaliwa

"Mungu amekwisha wakubali"

1 Corinthians 7:15

Kesi kama hiyo,kaka au dadahafungwi katika viapo vyao.

Kwa kesi hiyo,ndoa ya aaminiye makubaliano hayaendelei"

Unajuaje, mwanamke anaweza kumwokoa mme wake?

"hujuwi kama utamwokoa mwanaume asiyeamini."

Unajuaje, mwanaume anaweza kumwoka mke wake

"Haujuwi kamautamwokoa mkewako asiyeamini."

1 Corinthians 7:17

Kila mmoja

"Kila muumini"

Hii ni kawaida kwa kila kanisa

Paulo alikuwa anafundisha waumini katika makanisa yote kufuata katika njia hii.

yeyote alikuwa ametahiriwa alipoitwa kuamini.

Paulo alikuwa anafikisha ujumbe utahiriaji(Wayahudi) "Kwa waliotahiriwa, Mungu alipowaita kuamini, Mlikuwa tayari mmetahiriwa."

Yeyote alipoitwa kwa imani alikuwa hajatahiriwa.

Paulo alikuwa sasa anafikisha ujumbe kwa wale walikuwa hawajatahiriwa. "Kwa waliokuwa hawajatahiriwa ,Mungu alipowaita kuamini, mlikuwa bado kutahiriwa."

1 Corinthians 7:20

Maelezo ya Jumla

mli..msi.. ni maneneo kuonyesha wingi, yanahusu wakristo wote.

katika wito

Hapa "wito"inaonyesha kwa kazi au nafasi ya jamii katika sehemu uliyokuwa unajihusisha. "ishi na fanya kazi kama ulivyofanya."

Ulikuwa mtumwa ulipoitwa na Mungu?

"Kwa wale amabao walikuwa watumwa walipoitwa na Mungu kuamini."

Mtu huru wa Bwana

Hii mtu huru ni mmesamehewa na Mungu and kwa hiyouhuru kutoka kwa Shetani na dhambi.

Mmeshanunuliwa kwa thamani

"Kristo amewanunuakwa kufa kwa ajili yenu"

Tulipoitwa kuamini

"Wakati Mungu alipotuita kuamini katika yeye"

1 Corinthians 7:25

Sasa kuhusu wote ambao hawajaoa kamwe, sina amri kutoka kwa Bwana

Paulo anajua si mafundisho ya Yesu yale anazungumza kuhusu hali hii."Sina amri kutoka kwa Bwanakuhusu watu ambao hawajoa kamwe."

nawapa maoni

Ninawaambia ninachofikiri.

Kwa hiyo

" Basi hayo ni mawazo yangu"

usumbufu

"Mahangaiko yanayokuja"

1 Corinthians 7:27

Umefungwa na mwanamke katika viapo vya ndoa

Paulo anawaambia wanaume ambao wameoa

Umefungwa kwa mwanamke na kiapo cha ndoa? Usitake

" kama umeoa usitafute"

Una uhuru kutoka kwa mke au hujaolewa?

" Kama hujaoa usitafute kuoa"

Usitafute mke

"Usijaribu kutafuta kuoa"

1 Corinthians 7:29

Muda ni mfupi

"Kuna wakati mfupi" au "Wakati umekwisha"

Huzuni

"Kulia" au "Kutoa machozi"

wote wanaoshughulika na ulimwengu

"Wale ambao wanashughulika kila siku na wasioamini"

wawe kama hawakushughulika nao

Hii ni kwa sababu utawala wa Shetani wa dunia hii utakoma kitambo.

1 Corinthians 7:32

huru kwa masumbufu yote

"tulia" au "kutokuwa na wasi wasi"

anajihusisha

"shughulika"

Amegawanyika

"Anajaribu kumpendeza Mungu na kumpendeza mke wake"

1 Corinthians 7:35

Mtego

"mzigo" au "Kizuizi"

wanaweza kudumu kwa

"weza kushughulikia"

1 Corinthians 7:39

Wakati anapoishi

"mpaka afe."

ambavyo apenda

"Yeyote ampendaye"

Katika Bwana

"Kama mme mpya ni mwamini"

Maamuziyangu

"ufahamu wangu wa Neno la Mungu"

Furaha zaidi

"Kuridhika zaidi, Furaha zaidi"

aishi kama alivyo

"baki bila kuolewa."

1 Corinthians 8

1 Wakorintho 08 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Katika Sura ya 8-10, Paulo anajibu swali hili: "Je, inakubalika kula nyama ambayo imetolewa dhabihu kwa sanamu?"

Dhana maalum katika sura hii

Nyama iliyotolewa dhabihu kwa sanamu

Paulo anajibu swali hili kwa kusema kwamba sanamu ni miungu ambayo haipo. Kwa hiyo hakuna ubaya wowote kwa hiyo nyama. Wakristo wana uhuru wa kula. Hata hivyo, mtu asiyeelewa hii anaweza kuona Mkristo akila. Wanaweza kisha kuhimizwa kula nyama kama kitendo cha ibada kwa sanamu.

<< | >>

1 Corinthians 8:1

Sentensi Unganishi

Paulo anawakumbusha waumini kuwa ingawa sanamu hazina nguvu, waumini lazima wawe makini wasiwaathiri waumini dhaifu wanaoweza kufikiri wanatumikia sanamu. Paulo anawaambia waumini wawe makini katika uhuru walinao kwa Kristo.

Maelezo ya Jumla

"Sisi" inamaanisha Paulo pamoja na waumini wengine.

Sasa kuhusu

Paulo anatumia maneno haya kwenda kwenye sawali lijalo alilokuwa ameulizwa na Wakoritho.

vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu

Watu wa imani ya kipagani walitoa nafaka, samaki, ndege, au nyama, kwa miungu yao. Kuhani alitoa sehemu ya dhabihu ili kuichoma kwenye madhabahu.Paulo anazungumzia sehemu iliyo baki, ambayo ilipaswa kurudishwa kwa waabudu au kuuzwa katika soko.

Tunajua kuwa "wote tuna maarifa"

Paulo ananukuu maneno ambayo baadhi ya Wakoritho waliyatumia. "Wote tunajua, kama vile ninyi wenyewe mnapenda kusema, kwamba 'wote tuna maarifa.' "

Maarifa huleta majivuno

" Watu wenye ujuzi mwingi hufikiri wao ni bora zaidi kuliko hali yao halisi."

upendo hujenga

"Upendo ndiyo msaada wa kweli kwa watu"

mtu huyo anajulikana na yeye

"Mungu anamjua mtu huyo"

anadhani kwamba anajua jambo fulani

" anaamini anajua kila kitu kuhusu jambo fulani"

mtu huyo anajulikana naye

katika muundo tendaji "Mungu anamjua mtu huyo"

1 Corinthians 8:4

Maelezo ya Jumla

"Sisi" inamaanisha waumini wote

wajua kuwa "sanamu si kitu katika dunia hii," na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu

Paulo ananukuu maneno haya ambayo baadhi ya Wakorintho waliyatumia. "Sote tunajua, kama ninyi wenyewe mnavyopenda kusema, kuwa sanamu haina nguvu au maana kwetu' na kwamba hakuna Mungu ila mmoja tu"'

sanamu katika dunia hii si kitu

"sanamu haina nguvu katika dunia hii"

waitwao miungu

waitwao miungu..." vitu ambavyo watu huviita miungu"

miungu na mabwana wengi.

Paulo hana imani kuwa miungu na mabwana wengi wapo na wanaishi, lakini anatambua kuwa wapagani wao wanaamini hivyo.

ijapokuwa kwetu kuna

" Vyovyote watakavyosema na kufikiri watu wengine , sisi tunaamini kwamba kuna... tunaishi"

1 Corinthians 8:7

Maelezo ya Jumla

Paulo anazungumza kuhusu ndugu walio "dhaifu" watu ambao hawawezi kutofautisha kati ya vyakula vilivyotolewa kwa miungu na ibada ya sanamu. Kama mkristo anakula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu, ndugu walio dhaifu wanaweza kufikiri kwamba Mungu amewaruhusu kuabudu miungu kwa kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu hao. Hata kama mlaji hakuabudu miungu bali amekula chakula tu, ataharibu dhamiri ya ndugu yake.

kila mmoja... baadhi

"watu wote...baadhi ya watu miongoni mwa wakristo"

kupotoshwa

"kuharibiwa" au "dhuriwa"

1 Corinthians 8:8

chakula hakitatuthibitisha sisi kwa Mungu

"chakula hakitupi sisi kibali kwa Mungu" au "chakula tunacho kula hakimfanyi Mungu kupendezwa nasi"

Sisi sio wabaya sana kama tusipokula, au wema sana kama tukila

"Baadhi ya watu wanaweza kufikiria kuwa kama hatuli baadhi ya vitu, Mungu atatupenda kidogo. Lakini hawako sahihi. Wale wanao fikiri kuwa Mungu atatupenda zaidi ikiwa tunakula vitu hivyo pia hawako sahihi."

mtu ambaye ni dhaifu

waumini wasio imara katika imani zao

mtu amekuona, wewe uliye

Paulo anaongea kwa Wakorintho kama anaongea na mtu mmoja

Dhamiri yake

mawazo yanayomfanya mtu ajue kati ya jambo zuri na baya.

haitathibitika

" tiwa moyo kula "

1 Corinthians 8:11

ufahamu wako

Paulo anatumia neno "wako" kuongea na Wakorintho wote

aliye dhaifu... anaangamizwa

Kaka au dada asiyekuwa imara katika imani yake atatenda dhambi au kupoteza imani yake.

Kwa hiyo

"kwa sababu nilichoeleza ni kweli"

ikiwa chakula kinasababisha

" chakula" ni picha ya mtu anayekula hicho chakula " kwa kula kwangu kama nitasababisha" au " Ikiwa ninakula na kusababisha"

1 Corinthians 9

1 Wakorintho 09 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Paulo anajitetea katika sura hii. Watu wengine walidai kwamba alikuwa anajaribu kupata fedha kutoka kanisani.

Dhana maalum katika sura hii

Kupata pesa kutoka kanisani

Watu walimshtaki Paulo kwa kutaka fedha tu kutoka kanisani. Paulo alijibu kwamba angeweza kupata fedha kutoka kanisa kwa njia ya haki. Agano la Kale lilifundisha kwamba wale waliofanya kazi wanapaswa kukilisha kutoka kwa kazi zao. Yeye na Barnaba hawakutumia kamwe haki hii kimakusudi ili kujikimu maisha yao wenyewe.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Mifano

Paulo anatumia mifano nyingi katika sura hii. Sitiari hizi hifundisho maneno ya ukweli ngumu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Muktadha

Kifungu hiki ni muhimu kwa sababu Paulo "anaweka katika muktadha" kuhubiri kwa injili kwa watu mbalimbali. Hii ina maana kwamba Paulo hujiweka mwenyewe pamoja na Injili kueleweka, bila matendo yake kuzuia injili. Mtafsiri anapaswa kuchukua huduma ya ziada kuhifadhi nyanja za "kuwekwa katika muktadha" hii ikiwa inawezekana. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#goodnews)

Maswali ya uhuishaji

Paulo anatumia maswali mengi ya uhuishaji katika sura hii. Anayatumia kusisitiza maneno mbalimbali anapofundisha Wakorintho.(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion)

<< | >>

1 Corinthians 9:1

Sentensi Unganisha

Paulo anaelezea anavyotumia uhuru wake katika Kristo

mimi si huru?

Paulo anatumia swali kuwakumbusha Wakorintho juu ya haki alizo nazo. " mimi ni mtu niliye huru."

Mimi si mtume?

Paulo anatumia swali hili kuwakumbusha Wakoritho juu ya vile alivyo na haki aliyo nayo. "Mimi ni mtume."

Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu?

Paulo anatumia swali hili kuwakumbusha Wakoritho juu ya vile alivyo. "Nimemuona Yesu Bwana wetu."

Ninyi si matunda ya Kazi yangu katika Bwana?

Paulo anatumia swali hili kuwakumbusha Wakoritho juu ya uhusiano wao kwakwe. "Imani yenu katika Kristo ni matokeo ya kazi yangu katika Bwana."

ninyi ni uthibitisho wa utume wangu katika Bwana.

" ninyi ni kielelzo ambao naweza kutumia kuthibitisha kuwa Bwana amenichagua kuwa mtume "

1 Corinthians 9:3

Huu ndio utetezi wangu

Hapa inaweza kumaanisha 1) maneno yanayofuata ni maneno ya kujitetea kwa Paaulo au 2) maneno katika 9: 1 ni utetezi wa Paulo, " huu ndio utetezi... wangu ninafanya"

Je hatuna haki ya kula na kunywa?

"Tuna haki kabisa kupokea chakula na kinywaji kutoka makanisani."

Hatuna haki ya kuchukua mke aliye amini, kama wafanyavyo mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?

"Kama tuna wake walioamini, tuna haki ya kuwachukua pamoja nasi kama vile mitume wengine wanavyo wachukua wake zao, na ndugu katika Bwana, na kefa."

Au ni mimi peke yangu na Barnaba ambao tunapaswa kufanya kazi?

Paulo anawatia aibu Wakorintho " Mnafikiri ya kwamba Barnaba na mimi ndiyo watu pekee tunaofanya kazi ili tupate pesa."

1 Corinthians 9:7

Ni nani afanyaye kazi kama askari kwa gharama zake mwenyewe?

" Wote tunajua kuwa askari hatumii vifaa vyake mwenyewe." au " Wote tunajua kuwa kila askari hupokea vifaa kutoka serikalini"

Ni nani apandaye mzabibu asile matunda yake?

" Wote tunajua kuwa yule anayepanda shamba la zabibu atakula matunda yake." au " Wote tunajua kuwa hakuna anayetarajia mtu aliyepanda shamba la zabibu asile matunda yake."

Au na nani achungaye kundi asiyekunywa maziwa yake?

" Wote tunafahamu kuwa wale wachungao kundi hupata kinywaji chao kutoka kundini."

Je ninasema haya kwa mamlaka ya kibinadamu?

"Mnafikiri kuwa ninasema mambo haya kwa matakwa ya mamlaka ya kibinadamu."

Sheria nayo pia haisemi haya?

"Mnatenda haya kana kwamba hamjui hivi ndivyo imeandikwa katika sheria."

1 Corinthians 9:9

usimfunge

Musa alizungumza na wana wa Israeli kama anazungumza na mtu mmoja, hivyo amri hii ipo katika umoja.

Ni kweli kwamba hapa Mungu anajali ng'ombe?

"Mnapaswa kujua bila kuambiwa kuwa siyo ng'ombe ambaye Mungu anamjali zaidi."

Je hasemi hayo kwa ajili yetu?

" Badala yake, Mungu alikuwa anasema kuhusu sisi."

kwa ajili yetu

Hapa "yetu" inarejea kwa Paulo na Barnabas.

ni neno kubwa tukivuna vitu vya mwilini kutoka kwenu?

"Mlipaswa kufahamu kabla hata ya kuwaambia kuwa si jambo kubwa kwetu tukipokea msaada wa vitu kutoka kwenu."

1 Corinthians 9:12

Ikiwa wengine walipata... kwenu, Je! Sisi si zaidi?

Neno "sisi" hapa linamwakilisha Paulo na Barnaba " Wengine walifanya...nanyi mlipaswa kufahamu hata bila kuambiwa kwamba tuna haki zaidi"

Ikiwa wengine walipata haki hii

Wote Paulo na Wakorintho wanajua kuwa wengine walipata haki "Kwamba wengine walipata haki hii"

Wengine

wahubiri wengine wa injili

haki hii

haki waliyonayo waumini wa Korintho ya kuwapatia mahitaji yao wale waliohubiri habari njema kwao

kuwa kikwazo kwa

"kuwa mzigo kwa" au "kuzuia kuenea kwa"

Hamjui ya kuwa wote wafanyao kazi hekaluni hupata chakula chao kutoka hekaluni?

"Nataka niwakumbushe kuwa wale wanaohudumu hekaluni wanapata chakula chao kutoka hekaluni"

wapate kuishi kutokana na hiyo injili

Neno Injili hapa ni lugha ya picha kwa 1) watu waliwahubiria injili, " wanapokea chakula chao na vitu vingine wavyohitaji kutoka kwa watu wanaowafundisha habari njema" au 2) matokeo ya kufanya kazi ya kueneza injili, "wanapokea chakula chao na mahitaji yao mengine kwa sababu wanafanya kazi ya kueneza habari njema"

1 Corinthians 9:15

haki hizi

"vitu hivi ambavyo wanastahili"

ili jambo lolote lifanyike kwa ajili yangu

Katika muundo wa kitenzi tendaji:- "kwa hiyo mtafanya jambo kwa ajili yangu"

kubatilisha huku kujisifu

"kuondo hii fursa ambayo najisifia"

lazima nifanye hivi

"Lazima nihubiri injli"

ole wangu

"itakuwa bahati mbaya"

1 Corinthians 9:17

kama ninafanya hivi kwa hiari

"kama nitahubiri kwa hiari"

kwa hiari

"kwa furaha" au "kwa sababu ninataka"

Bado nina jukumu nililopewa kuwa wakili

katika muundo wa kitenzi tendaji:- "Lazima nifanye kazi hii ambayo Mungu alinip ili kuikamilisha"

thawabu yangu ni nini?

" Hii ndiyo thawabu yangu."

kwamba nihubiripo, niweze kutoa injili bila malipo

"Thawabu yangu kwa ajili ya kuhubiri ni kuwa nihubiri bila kupokea malipo"

kutoa injili

"kuhubiri injili"

na hivyo situmii haki yangu yote ya injili

"kwa hiyo siwaombi watu kunisaidia ninaposafiri na kuhubiri"

1 Corinthians 9:19

kupata zaidi

"kuwashawishi wengine waamini" au "kuwasaidia wengine kuamini katika Kristo"

nilikuwa kama Myahudi

"nilitenda kama Muyahudi" au "niliishi kulingana kwa tamaduni za Kiyahudi"

nilikuwa kama mmoja wao aliye chini ya sheria

"Nilikuwa kama mmoja niliye jidhatiti kufuata matakwa ya uongozi wa Wayahudi, nikikubali uelewa wao wa maandiko ya Kiyahudi"

1 Corinthians 9:21

nje ya sheria

" watu wasiotii sheria ya Musa"

1 Corinthians 9:24

Sentensi Unganishi

Paulo anaeleza kuwa anatumia uhuru wake kujirudi mwenye.

Mnajui ya kuwa katika mbio wote washindanao hupiga mbio, lakini apokeaye tuzo ni mmoja?

Paulo anawakumbusha Wakorintho kwa kitu ambacho wanakijua ili awapashe habari nyingine mpya. " niwakumbushe kuwa ingawa wakimbiaji wote hushiriki katika mbio ni mkimbiaji mmoja tu anayepokea zaidi"

kimbia mbio

Paulo anafananisha kuishi maisha ya Kikristo na kufanya kazi kwa ajili ya Mungu kukimbia mbio na kuwa mwanamichezo. Kama ilivyo katika mbio, maisha ya Kikristo na kazi zinahitaji nidhamu kwenye sehemu ya mkimbiaji, na kama kwenye mashindano Mkristo analo lengo mahususi.

kimbia kupata tuzo

Paulo anaongea habari za tuzo ambazo Mungu huwapa watu wake waaminifu kana kwamba ni ni wakimbiaji wanaoshindana.

taji iharibikayo...taji isiyoharibika.

Taji ni kitita cha maua yaliyosukwa pamoja. Mataji yalitolewa kama zawadi kwa wakimbiaji walioshinda michezo na mashindano. Paulo anaongelea maisha ya milele kama taji isiyonyauka.

mimi sikimbii bila sababu au napigana ngumi kama kupiga hewa

"najua vizuri kwa nini ninakimbia, na ninajua ninachofanya ninapopigana ngumi"

mimi mwenyewe nisiwe wa kukataliwa

" hakimu atasema kwamba nilitii taratibu."

1 Corinthians 10

1 Wakorintho 10 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Sura za 8-10 pamoja zinajibu swali: "Je, inakubalika kula nyama ambayo imetolewa dhabihu kwa sanamu?"

Katika sura hii, Paulo anatumia kutoka kuwaonya watu kutotenda dhambi. Kisha, anarudi kujadili nyama inayotolewa kwa sanamu. Anatumia Mlo wa Bwana kama mfano. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin)

Dhana maalum katika sura hii

Kutoka

Paulo anatumia uzoefu wa Israeli kutoka Misri na kutembea jangwani kama onyo kwa waumini. Ingawa Waisraeli walimfuata Musa, wote walikufa njiani. Hakuna hata mmoja aliyefikia Nchi ya Ahadi. Wengine waliabudu sanamu, wengine walimjaribu Mungu, na wengine walinung'unika. Paulo anawaonya Wakristo wasitende dhambi. Tunaweza kushinda majaribu kwa sababu Mungu hutoa njia ya kuepuka. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#promisedland)

Kula nyama iliyotolewa dhabihu kwa sanamu

Paulo anazungumzia nyama iliyotolewa kwa sanamu. Wakristo wanaruhusiwa kula, lakini inaweza kuumiza wengine. Kwa hiyo wakati wa kununua nyama au kukula na rafiki, usiulize ikiwa imetolewa kwa sanamu. Lakini ikiwa mtu anakuambia kuwa imetolewa kwa sanamu, usiile kwa ajili ya mtu huyo. Usimkosee mtu yeyote. Jaribu kuwaokoa badala yake. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#save)

Maswali ya uhuishaji

Paulo anatumia maswali mengi ya uhuishaji katika sura hii. Anayatumia kusisitiza maneno mmbalimbali anapofundisha Wakorintho.(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion)

<< | >>

1 Corinthians 10:1

sentensi Unganishi

Paulo anawakumbusha Wakorintho mfano wa tabia ambaya( uovu) na ibada ya sanamu wa baba zao wakongwe wa Kiyahudi

baba zetu

Paulo anarejea kwenye wakati wa Musa katika kitabu cha Kutoka wakati Waisraeli walikimbia kupitia bahari ya chumvi wakati majeshi ya Wamisri yakiwafuatilia. Neno "yetu" linamhusu Paulo mwenyewe pamoja na Wakorintho.

walipita katika bahari

Hii bahari inajulikana kwa majina mawili, Bahari ya chumvi na Bahari ya matete.

walipita

"walipita kwa kutembea" au "walisafiri kupitia"

Wote walibatizwa wawe wa Musa katika wingu

"Wote walimfuata na walijidhatiti kwa Musa"

ndani ya wingu

kwa wingu lililowakilisha uwepo wa Mungu na liliwaongoza Waisraeli wakati wa mchana."mwamba" unawakilisha uimara haswa wa Kristo, ambaye alikuwa pamoja nao wakati wote. Wangetegemea ulinzi na faraja yake.

walikunywa kinywaji kile kile cha roho... mwamba wa roho

" walikunywa maji yale yale ambayo Mungu aliyatoa kwenye mwamba kwa muujiza .... mwamba wa rohoni( mwujiza)

mwamba ule ulikuwa ni Kristo

"mwamba" ulikuwa mwamba wa kawaida ulioonekana kwa macho, hata hivi mwamba huo ulikuwa ukiwakilisha nguvu za Kristo zilizofanya kazi ndani yake " alikuwa Kristo aliyefanya kazi kupitia ule mwamba"

1 Corinthians 10:5

hakupendezwa sana

"kutofurahishwa" au "hasirishwa"

wengi wao

" Mababa wa waisraeli"

maiti zao zilisambazwa

"Mungu alitawanya maiti katika eneo lile" au "Mungu aliwaua na kutawanya maiti za miili yao"

jangwani

eneo la jangwa kati ya Misri na Israeli wakopitia Wisraeli katika safari yao ya miaka 40

1 Corinthians 10:7

waabudu sanamu

"watu wanaoabudu sanamu"

walikaa chini kula na kunywa

" walikaa chini kula chakula"

kucheza

Paulo nukuu maandiko ya kiyahudi. Hapa anataka wasomaji wake wafamu kuwa watu walikuwa wakiabudu miungu (sanamu) kwa kuimba, kucheza na kufanya zinaa. Hii haikuwa sherehe ya kawaida

Wakafa siku moja watu ishirini na tatu elfu

"Mungu aliwaua watu 23,000 kwa siku moja"

kwa sababu hiyo

" kwa sababu walitenda matendo mabaya ya zinaa"

1 Corinthians 10:9

walivyofanya na wakaharibiwa kwa nyoka

Hii inaweza kuelezewa katika muundo tendaji: "matokeo yake, waliangazwa na nyoka"

msinung'unike

kulalamika

kuharibiwa na malaika wa mauti

Hii inaweza kuelezewa katika muundo tendaji: " matokeo yake, malaika wa mauti aliwaharibu"

1 Corinthians 10:11

mambo haya yalitokea kwao

"Mungu aliwaadhibu babu zetu"

mifano kwetu.

Hapa "sisi" ina rejea kwa waumini wote.

Yaliandikwa ili yawe mafundisho kwetu

katika muundo tendaji:- " Mungu alitaka Musa ayaandike ili tujifunze kutenda kwa usahihi"

nyakati za mwisho

" siku za mwisho"

asije akaanguka

hafanyi dhambi au kumkana Mungu

Hakuna jaribu lililowapata ninyi lisilo kawaida ya wanadamu

katika mtazamo chanya "majaribu ambayo yanawaathiri ninyi ni majaribu ambayo yanawapata watu wote."

Hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu

" Mungu ataruhusu mjaribiwe katika namna ambayo mtakuwa imara kiasi cha kutosha kupata ushindi"

Hatawaacha mjaribiwe

maelezo katika muundo tendaji "hataruhusu mtu yeyote awajaribu"

1 Corinthians 10:14

Sentensi Unganishi

Paulo anaendelea kuwakumbusha Wakorintho kuwa wasafi na kujitenga ibada ya sanamu na uchafu, wanapokuwa katika ushirika ambao unawakilisha damu na mwili wa Kristo.

ikimbieni ibada ya sanamu

Paulo anazungumzia tendo la kuabudu sanamu ni kama mnyama hatari " fanyeni kila namna ili kukaa mbali na ibada ya kuabudu sanamu"

kikombe cha baraka

Paulo anatumia maelezo haya kufafanua kikombe kilichowekewa divai ambayo ilitumiwa katika meza ya Bwana.

Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?

" tunamshukuru Mungu kwa ajili ya kikombe"

si ushirika wa damu ya Kristo?

Kikombe cha divai ambacho tunashiriki kinatuunganisha kushiriki katika damu ya Kristo. kwa maneno mengine "tunashiriki katika damu ya Kristo."

Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?

" tunashiriki katika mwili wa Kristo tunaposhiriki mkate"

ushirika wa

"kushiriki katika" au " kushiriki katika hali ya usawa pamoja na wengine"

mkate mmoja

kipande kimoja cha mkate uliookwa na kugawanywa au kukatwa katika vipande vidogo vidogo kabla ya kuliwa.

1 Corinthians 10:18

Wale wote walao dhabihu si washiriki katika madhabahu?

Paulo anawakumbusha Wakorintho jambo wanalolifahamu ili baada ya hapo awape habari mpya. kwa maneno mengine anasema " wale wanaokula sadaka wanashiriki katika shughuli na baraka za madhabahu"

Nasema nini basi?

Paulo anawakumbusha Wakorintho jambo wanalolifahamu ili baada ya hapo awape habari mpya:- " kwa kufanya marudio ya kile nilichosema" au " Hiki ndicho ninacho maanisha"

kuwa sanamu ni kitu?

"Tambueni ninachosema kuwa sanamu siyo kitu halisi"

Au ya kuwa chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu?

" Mnafahamu sisemi chakula kilichotelewa sadaka kwa sanamu si kitu muhimu"

1 Corinthians 10:20

Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mapepo

Paulo anazungumzia habari ya mtu anayenywea kikombe kile kile ambacho mapepo hunywea kuonyesha kuwa mtu huyo ni rafiki wa mapepo. kwa maneno mengine " haiwezekani kuwa rafiki wa kweli kwa wote, Bwana na mapepo"

Hamuwezi kuwa na ushirika katika meza ya Bwana na katika meza ya mapepo

" Haiwezekani kuwa na urafiki wa kweli kwa watu wa Mungu na mapepo pia"

Au twamtia Bwana wivu?

Paulo anataka Wakorintho kujibu swali hili katika mioyo yao " Mnapaswa kujua hata kabla ya kuwaambi ya kuwa haifai kumtia wivu Bwana"

twamtia

kukasirika au kukera

Tuna nguvu zaidi yake?

Paulo anataka Wakorintho kujibu swali hili katika mioyo yao " Mnapaswa kujua hata kabla ya kuwaambi ya kuwa hatuna nguvu kuliko Mungu"

1 Corinthians 10:23

Sentensi Unganishi

Paulo anawakumbusha tena kuhusu sheria ya uhuru na kufanya kila kitu kwa faida ya wengine

Vitu vyote ni halali,

Hapa inaweza kumaanisha 1) Paulo pengine anatoa majibu kutokan na mawazo wanayofikiria Wakorintho " wengine wanasema, 'Naweza kufanya jambo lolote'" au 2) Paulo anasema kile anachodhani ni kweli, " Mungu ameniruhusu nifanye kila kitu."

viwajengavyo watu.

"wasaidie watu"

1 Corinthians 10:25

pasipo kuuliza maswali ya dhamiri.

" Mungu anataka ule chakula kwa dhamiri njema"

1 Corinthians 10:28

Lakini mtu... dhamiri ya yule mwingine

hapa inaweza kumaanisha " kuleni chochote kinawekwa mbele yenu bila kuuliza maswali yanayotokana na dhamira"

Lakini mtu akiwaambia,....msile. Hii ni kwa ajili yake aliyewaambia...ajili ya dhamiri.

Paulo anawaambia Wakorintho "usilile",kana kwamba anaongea na mtu mmoja.Lakini Paulo anatumia umoja kuwapa maelekezo waumini wote wa Korintho.

Maana kwanini...dhamiri? Ikiwa mimi natumia... nimeshukuru kwacho?

Maana zinazowezekana ni 1)" siulizi maswali juu ya dhamiri , je kwanini.. dhamiri? kama nashiriki ... kutoa shukrani?" au 2) Paulo ananukuu kila ambacho Wakorintho walikuwa wakifikiria " baadhi watakuwa wanafikiri , kwa nini ... dhamiri? ikiwa.. nashukuru?"

Maana kwanini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?

msemaji anataka msikilizaji wake ajibu swali katika akili yake " kabla ya kukuambia ulipaswa kufahamu kuwa hakuna mtu anayeweza kusema nafanya jambo baya kwa kuwa anatumia mawazo yake wala si mawazo yangu, kuhukumu baya na zuri, japo mazo yake ni tofauti na ya kwangu"

Ikiwa mimi natumia chakula kwa shukrani, kwanini nitukanwe kwa kitu ambacho nimeshukuru kwacho?

msemaji anataka msikilizaji wake ajibu swali katika akili yake " nashiriki mlo kwa shukurani, hivyo hakuna mtu anayeweza kunishutumu kwa kile ambacho nakitolea shukurani"

natumia

Neno "mimi" linawakilisha wale ambao wanakula nyama kwa shukurani. " ikiwa mtu atashiriki" au "wakati mtu anapokula"

shukrani

" na shukuru Mungu kwa hicho"au " na mshukuru mtu anayenipatia hicho"

1 Corinthians 10:31

Msiwakoseshe Wayahudi au Wayunani

"Msiwachukize Wayahudi au Wayunani" au "Msiwafanye Wayahudi na Wayunani kukasirika"

kuwapendeza watu wote

"wafanye watu wote wafurahi"

Sitafuti faida yangu mwenyewe

"Sifanyi mambo ninayotamani mimi binafsi"

wengi

watu wengi kadri iwezekanavyo.

1 Corinthians 11

1 Wakorintho 11 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Huu ni mwanzo wa sehemu mpya wa barua (Sura za 11-14). Paulo sasa anazungumza kuhusu huduma nzuri za kanisa. Katika sura hii, anahusisha matatizo mawili tofauti: wanawake katika huduma za kanisa (mistari ya 1-16) na Meza ya Bwana (mistari ya 17-34).

Dhana maalum katika sura hii

Mazoezi mema katika huduma ya kanisa

Wanawake wasio na adabu

Maagizo ya Paulo hapa yanajadiliwa na wasomi. Labda kulikuwa wanawake ambao walikuwa wakitumia uhuru wao wa Kikristo vibaya a kuleta fujo ndani ya kanisa sababu hawakukuwa na adabu ya kawaida. Fujo kutokana na vitendo vyao vilimfanya awe na wasiwasi.

Meza ya Bwana

Kulikuwa na matatizo katika Wakorintho kwa jinsi walikula Meza ya Bwana. Hawakutenda kwa umoja. katika Wakorintho kwa jinsi walikula Meza ya Bwana, baadhi yao walikula chakula chao wenyewe bila kushirikiana. Baadhi yao walilewa wakati watu masikini walipokuwa na njaa. Paulo alifundisha kwamba waumini wanadharau kifo cha Kristo kama wanakula Meza ya Bwana na kufanya dhambi au wakati wanavunja ushirika na wenzao. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#sin and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#reconcile)

Mifanyo ya muhimu za matamshi katika sura hii

Maswali ya uhuishaji

Paulo hutumia maswali ya uhuishaji ili kuwakaripia watu kwa kutofuata kwao sheria za ibada aliyopendekeza. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-rquestion)

Kichwa

Paulo anatumia "kichwa" kama kielelezo cha mamlaka katika mstari wa 3 na pia kutaja kichwa halisi cha mtu katika mstari wa 4 na kuendelea. Kwa kuwa hayo ni ya karibu sana, inawezekana kwamba Paulo alitumia "kichwa" kwa makusudi kwa njia hii. Hii inaonyesha kwamba mawazo katika aya hizi ziliunganishwa. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metonymy)

<< | >>

1 Corinthians 11:1

Sentensi Unganisha

Baada ya Paulo kuwakumbusha Wakorintho kumfuata yeye kama navyomfuata Kristo, Paulo anatoa maagizo mahususi jinsi wanawake na wanaume wanavyopaswa kuishi kama waumini

"fikiri juu ya" au " kumbuka"

nataka

inaweza kumaanisha 1) "Kwa sababu ya hili, ninataka" au 2) "Hata hivyo, ninataka."

ni kichwa cha

anamamlaka juu ya

naye mwanaume ni kichwa cha mwanamke

inaweza kumaanisha 1) " wanaume wanamamlaka kwa wanawake" au 2) mume anapaswa kuwa na mamlaka kwa mke"

akiwa amefunika kichwa

" anapofunika au kuweke kitambaa kwenye kichwa chake"

anakiabisha kichwa chake

inaweza kumaanisha 1) " hujitia aibu mwenyewe" au 2) huleta aibu kwa Krito, ambaye ni kichwa cha mwanaume."

1 Corinthians 11:5

mwanamke aombae...anakiaibisha kichwa chake

Hii inaweza kumaanisha 1) "wanamke anayeomba ...hujiaibisha mwenyewe" au 2) mke anayeomba...huleta aibu kwa mume wake"

kichwa chake kikiwa wazi

bila vazi lililovaliwa juu ya kichwa ambalo lilifunika mabega na nywele

kukata nywele zake

ni kana kwamba ameondoa nywele zake zote kwenye kichwa chake kwa wembe

ni aibu mwanamke

Ilikuwa ni ishara ya aibu au uzalilishaji kwa mwanamke kunyoa nywele zake au kuzipunguza

kufunika kichwa chake

Mwanamke kuvaa nguo ambayo ilivaliwa juu ya kichwa iliyofunika mabega pamoja na nywele.

1 Corinthians 11:7

haimpasi mwanamume kufunika kichwa chake

ikielezwa katika muundo tendaji, inaweza kumaanisha 1) "ni lazima mwanaume asifunike kichwa chake" au 2) " mwanaume hahitaji kufunika kichwa chake"

utukufu wa mwanaume

Kama vile mwanaume anavyobeba taswira ya ukuu wa Mungu, mwanamke huonyesha tabia ya mwanaume.

Maana mwanamume hakutokana na mwanamke. Badala yake, mwanamke alitokana na mwanamume

Mungu alimuumba mwanamke kwa mfupa kutoka kwa mwanaume. kwa maneno mengine " Mungu hakumuumba mwanaume kutoka kwa mwanamke . Badala yake Mungu alimuumba mwanamke kutoka kwa mwanaume"

1 Corinthians 11:9

Wala...kwa mwanaume

Maneno haya yanarejea katika 11:7 kumaanisha kuwa " mwanamke ni utukufu wa mwanaume"Maana zinazo wezekana ni 1) "kuonyesha mfano kuwa anaye mwanamume kama kichwa chake" au 2) "kuonyesha mfano kuwa anamamlaka ya kuomba na kutoa unabii."

kuwa na ishara ya mamlaka juu ya kichwa chake,

Hapa inaweza kumaanisha 1) "kuonyesha mfano kuwa anaye mwanamume kama kichwa chake" au 2) "kuonyesha mfano kuwa anamamlaka ya kuomba na kutoa unabii"

1 Corinthians 11:11

Hata hivyo

" Pamoja na kwamba nilichosema ni kweli, swala la muhimu ni hili:"

katika Bwana

Hapa inaweza kumaanisha 1) "kati ya Wakristo, ambao ni wa Bwana" au "katika dunia kama ilivyoumbwa na Mungu."

mwanamke hayupo peke yake pasipo mwanamume, au mwanamume pasipo mwanamke.

Hii inaweza kuelezwa katika mtazamo chanya:- " mwanamke anamtegemea mwanaume, na mwanaume anamtegemea mwanamke"

vitu vyote hutoka kwa Mungu.

" Mungu aliumba kila kitu"

1 Corinthians 11:13

Hukumuni wenyewe

"Hukumuni suala hili kulingana na desturi za ndani na taratibu za kanisa mnazozijua"

Ni sahihi mwanamke amwombe Mungu hali kichwa chake kikiwa wazi?

Ikielezewa katika muundo tendaji:-"Kwa kumheshimu Mungu, mwanamke lazima amwombe Mungu akiwa amefunika kichwa chake."

Je hata asili peke yake haiwafundishi...kwake?

Paulo anatarajia Wakorintho wakubaliane naye kuwa " Hali ya asili huwafundisha" kwa maneno mengine " Mnajua hili kwa kutazama watu wanavyofanya kila mara"

amepewa zile nywele

" Mungu alimuumba mwanamke na nywele"

1 Corinthians 11:17

Sentensi Unganishi

Paulo anapozungumzia ushirika mtakatifu, nawakumbusha kuwa na umoja na tabia njema. Anawakumbusha kuwa wakikosa umoja na tabia njema wakati wa ushirika wataugua na kufa, kama ambayo imekwisha tokea kwa baadhi yao.

atika maagizo yafuatayo, mimi siwasifu

Hapa inaweza kumaanisha "ninapotoa maelekezo haya, kunajambo ambalo siwezi kuwasifia"

maagizo

" maelekezo" au "taratibu (sera)"

mnapokusanyika

" kusanyika pamoja"

sio kwa faida bali kwa hasara

" hamsaidiani badala yake mnaumizana"

kanisani

Paulo hazungumzii kuingia ndani ya jengo bali anazungumzia "waumini"

kuna migawanyiko kati yenu

" mnagawanyika wenyewe katika makundi"

ili kwamba wale waliokubaliwa wajulikane kwenu.

Maana zinazokubalika 1) "ili kwamba watu wajue waumini wanao heshimiwa zaidi kati yenu" au 2) "ili kwamba watu waonyeshe kuwakubali waumini fulani kati yenu."

wale waliokubaliwa

Hapa inaweza kumaanisha1) "walinakubaliwa na Mungu" au 2) " ambao kanisa linawakubali"

1 Corinthians 11:20

mkutanikapo

"kusanyika pamoja"

mnachokula sio chakula cha Bwana.

" mnaaminia kuwa mnakula chakula cha Bwana lakini hamukiheshimu kama inavyostahili"

za kulia na kunywea

"ambapo mnaweza kukutana kula chakula"

mnalidharau

chukia au tendea bila adabu na heshima

kuwafedhehesha

aibisha au sababisha kujisikia aibu

Niseme nini kwenu? Niwasifu?

Paulo anawakemea Wakorintho. Kwa maneno mengine anasema " siwezi kusema neno lolote zuri juu ya hili. Siwezi kuwasifu"

1 Corinthians 11:23

Kwa maana nilipokea kutoka kwa Bwana kile ambacho nimewapa ninyi ya kuwa Bwana

" kwa kuwa nilichosikia kutoka kwa Bwana ndicho niliwaambia ninyi, na ilikuwa hivi: Bwana"

usiku ule aliposalitiwa

kielezwa kwa muundo tenda: "usiku ule Yesu aliposalitiwa na Yuda Iskariote "

aliuvunja

" aliupasua mkate katika vipande vidogo vidogo"

Huu ndio mwili wangu

"Mkate ninaoshikilia ni mwili wangu"

1 Corinthians 11:25

kikombe

Hapa inaweza kumaanisha 1) kikombe cha divai ambacho ambacho kilitegemewa akitumie 2) kikombe cha tatu au cha nne miongoni mwa vikombe vinne ambavyo Wayahudi walitumia kunywa divai wakati wa mlo wa Pasaka.

Fanyeni hivi mara nyingi kila mywapo

"Kunyweni kutoka katika kikombe hiki, na kila mara mnapokunywa kitumieni"

mwaitangaza mauti ya Bwana

fundisheni kuhusu kusulubishwa na ufufuo

mpaka atakapokuja

Yesu atakaporudi itasemwa wazi. Kwa maneno mengine " mpaka Yesu atakaporudi tena duniani"

1 Corinthians 11:27

kula mkate na kuywa kikombe cha Bwana

" kula mkate wa Bwana au kunywa kikombe cha Bwana"

chunguza

Paulo aneleza uhusiano wa mtu na Mungu, jinsi mtu anavyoishi katika maisha yake kwamba anatakiwa ayaangalie maisha yake na kuyatathmini kama mtu ayetaza kitu anapotaka kukinunua.

bila kuupambanua mwili

Inaweza kumaanisha1) "na hatambui kuwa kanisa ni mwili wa Bwana" au 2) "na hafikiri kuwa anashiriki mwili wa Bwana."

wagonjwa na dhaifu

Maneno haya yanamaana zizokaribiana: kuwa nyonge, kuwa na madhara

1 Corinthians 11:31

tunajichunguza

Paulo aneleza uhusiano wa mtu na Mungu, jinsi mtu anavyoishi katika maisha yake kwamba anatakiwa ayaangalie maisha yake na kuyatathmini kama mtu ayetaza kitu anapotaka kukinunua.

hatutahukumiwa

ikielezwa kwa muundo tendaji:" Mungu hatatuhukumu"

tunapohukumiwa na Bwana, twarudiwa, ili tusije tukahukumiwa

ikielezwa kwa muundo tendaji:" Mungu anatuhukumu, anatusahihisha, ili asije akatushutumu"

1 Corinthians 11:33

mkutanikapo mpate kula

kusanyikeni kula chakula pamoja kabla ya kusherekea chakula cha Bwana

ngojeaneni

" Kabla ya kuanza kula wasubirie na wengine hadi wafike"

ale nyumbani kwake

"ale kabla ya kuhudhuria mkutano huu"

isiwe kwa hukumu

" lisiwe tukio la Mungu kuwaadhibu"

1 Corinthians 12

1 Wakorintho 12 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Vipaji vya Roho Mtakatifu

Sura hii inaanza sehemu mpya. Sura za 12-14 zinajadili vipaji vya kiroho ndani ya kanisa.

Dhana maalum katika sura hii

Kanisa, mwili wa Kristo

Hii ni mfano muhimu katika Maandiko. Kanisa lina sehemu nyingi. Kila sehemu ina kazi tofauti. Zinakusanywa kuunda kanisa moja. Sehemu zote tofauti ni muhimu. Kila sehemu inapaswa kujali sehemu nyingine zote, hata zile zinazoonekana kutokuwa muhimu. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Hakuna mtu anayeweza kusema, 'Yesu ni Bwana,' isipokuwa kwa Roho Mtakatifu."

Katika kusoma Agano la Kale, Wayahudi wangeweza kubadilisha neno "Bwana" kwa neno "Yahweh." Sentensi hii ina maana kwamba hakuna mtu anayeweza kusema kuwa Yesu ndiye Bwana, Mungu katika mwili, bila uwezo wa Roho Mtakatifu kuwavuta kukubali ukweli huu. Ikiwa neno hili limetafsiriwa vibaya, linaweza kuwa na madhara ya kitheolojia yasiyotarajiwa.

<< | >>

1 Corinthians 12:1

Sentensi Uganishi

Paulo anawafahamisha kuwa Mungu ametoa karama maalumu kwa waumini. Karama hizi ni kwa ajili ya kuusaidia mwili wa waumini.

Sitaki mkose kufahamu

"Ninataka mfahamu"

mlipotoshwa kufuata sanamu zisizoongea

ikielezwa kwa muundo tendaji: "mliamini uongo na mlibudu sanamu zisizoongea"

kwa njia zozote mliongozwa nazo

ikielezwa kwa muundo tendaji:" na ziliwaongoza kwa namna nyingi"

hakuna yeyote anenaye kwa Roho wa Mungu awezaye kusema

maana zinazowezekana ni 1) "hakuna Mkristo ambaye ana Roho wa Mungu ndani yake, awezaye kusema," au 2) "hakuna atoaye unabii kwa nguvu ya Roho wa Mungu awezaye kusema."

Yesu amelaaniwa.

" Mungu atamwadhibu Yesu" au Mungu atamtesa Yesu"

1 Corinthians 12:4

azitendaye kazi zote katika wote

"humwezesha kila mtu kupokea"

1 Corinthians 12:7

kila mmoja hupewa

Hapa ikielezwa kwa muundo tendaji:- Mungu ndiye anayefanya tendo la upaji au utoaji. kwa maneno mengine "Mungu humpa kila mmoja "

mtu mmoja amepewa na Roho neno

ikielezwa kwa muundo tendaji:- "Kwa njia ya Roho Mungu humpatia kila mmoja neno"

kwa Roho

Mungu hutoa karama kupitia kazi ya Roho

hekima...maarifa

Tofauti kati ya haya maneno mawili siyo muhimu, cha muhimu ni kwamba maarifa na hekima hutoka kwaMungu kwa njia ya Roho yule yule.

neno la hekima

" maneno ya busara"

neno la maarifa

" Maneno yanayoonesha ujuzi"

1 Corinthians 12:9

humpa

Hii inaweza kuelezewa katika muundo tendaji " Mungu hutoa"

kwa Roho mmoja

Mungu hutoa karama kupitia kazi ya Roho Mtakati pekee.

aina mbalimbali za lugha

"uwezo wa kuongea lugha mbalimbali"

tafsiri za lugha

uwezo wa kutoa mafafanuzi ya lugha nyingine inayozungumzwa ambayo si lugha yako.

kufasiri

Hii inamaanisha kufafanua kile anachosema mtu kwa lugha isiyofahamika kwa wengine. au kueleza maana za maneno kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine

Roho ni yule

Paulo anawakumbusha wasomaji wake kuwa " Roho ni yule yule... Roho moja"

1 Corinthians 12:12

Sentensi Unganishi

Paulo anaendelea kusema juu ya karama ambazo Mungu amewapa waumini , Mungu ametoa karama mbalimbali kwa waumini tofauti tofauti, lakini pamoja na hilo waumini wamefanywa kuwa mwili mmoja , ambao unaitwa mwili wa Kristo. Kwa sababu hii waumini wanapaswa kuwa na umoja.

katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi au Wa

Hapa inaweza kumaanisha 1) Roho mtakatifu ndiye anayetubatiza, " kwa Roho moja tunabatizwa" or 2) Roho ni kama maji ya ubatizo ni njia iliyotumika kutubatiza kuwa mwili mmoja, " katika Roho moja tulibatizwa"

wote walifanywa kunywa kwa Roho mmoja

"Mungu alitupa sisi sote Roho mmoja, na tunashiriki Roho kama watu wawezavyo kushiriki kinywaji"

wote tulinyweshwa Roho mmoja

Hii inaweza kuelezewa katika muundo wa kitenzi "Mungu ametupatia Roho mmoja, na tunashiriki katika Roho huyo kama watu wanavyo weza kushiriki kinywaji cha aina moja"

1 Corinthians 12:14

kungekuwa wapi kusikia?...kungekuwa wapi kunusa?

Maneno haya ukiyabadili kuwa sentensi: "usingeweza kusikia chochote...usingeweza kunusa chochote"

1 Corinthians 12:18

kiungo kimoja

Kwa ujumla neno "Kiungo" linarejea sehemu zote za mwili kama vile kichwa, mkono au goti. kwa maneno mengine "sehemu ile ile ya mwili"

mwili ungelikuwa wapi?

"kusingelikuwa na mwili"

Kwa hiyo sasa kuna viungo vingi, lakini

kwa maneno mengine ni kusema "kusingekuwa na mwili"

1 Corinthians 12:21

haliwezi kuuambia mkono, "sina haja na wewe."

Neno "wewe" lipo katika hali ya ummoja

onekana kuwa na heshima kidogo

"siyo muhimu sana"

visivyotajwa

Hii pengine inarejea kwenye sehemu za siri za mwili, ambazo huwa vimefunika.

1 Corinthians 12:25

pasiwepo na migawanyiko katika mwili, bali

"mwili uwe na umoja, na"

kiungo kimoja kinaheshimiwa

katika muundo tendaji ni kwmba " mmoja hutoa heshima kwa mwajuiya mwingine"

Sasa ninyi

Neno "Sasa" linatumika kuvuta usikivu kwenye dokezo muhimu linalofuatia

1 Corinthians 12:28

kwanza mitume

Hii inaweza kumaanisha 1) " ninataja karama ya kwanza kuwa ni ya mitume" au 2) "karama ya muhimu zaidi ni ya mitume"

wale wasaidiao

" wale wanaotoa msaada kwa waumini wenzao"

wale wafanyao kazi ya kuongoza

" wale wanaosimamia kanisa"

wote walio na aina mbalimbali za lugha

Watu wanaozungumza lugha za kigeni moja au zaidi bila kujifunza.

Je sisi wote ni mitume? wote ni manabii? wote ni waalimu? wote wanafanya matendo ya miujiza?

Paulo anawakumbusha wasomaji wake jambo wanalolijua. kwa maneno mengine anasema " baadhi yao tu ni mitume. Baadhi yao tu ni manabii. Baadhi yao tu hufanya matendo ya miujiza"

1 Corinthians 12:30

Je wote mnakarama ya uponyaji?

Kwa maneno mengine " si watu wate wanakarama ya uponyaji"

wote mnaongea kwa lugha?

Kwa maneno mengine " si watu wote hunenea kwa lugha"

wote mnatafasiri lugha?

kwa maneno mengine "si wote hufasiri lugha"

Kufasiri

Hii inamaanisha kufafanua kile anachosema mtu kwa lugha isiyofahamika kwa wengine. au kueleza maana za maneno kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine

Tafuteni sana karama zilizo kuu

Hapa inaweza kumaanisha 1) "tafuteni kwa bidii Mungu awape karama zinazoweza kulisaidia kanisa vizuri zaidi"

1 Corinthians 13

1 Wakorintho 13 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Paulo anaonekana kuacha mafundisho yake kuhusu vipaji vya kiroho. Hata hivyo, labda sura hii hutumika pakubwa katika mafundisho yake.

Dhana maalum katika sura hii

Upendo

Upendo ni sifa muhimu zaidi ya mwamini. Sura hii inaeleza kikamilifu kuhusu upendo. Paulo anaeleza kwa nini upendo ni muhimu zaidi kuliko vipaji vya Roho. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#love)

mifano mhimu ya matamshi katika sura hii

Mifano

Paulo anatumia mifano nyingi tofauti katika sura hii. Anatumia sitiari hizi kuwafundisha Wakorintho, hasa katika mada ngumu. Wasomaji mara nyingi wanahitaji ufahamu wa kiroho kuelewa mafundisho haya. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tm/translate.html#figs-metaphor)

<< | >>

1 Corinthians 13:1

Sentensi Unganishi

Baada ya kuzungumzia karama ambazo Mungu amewapa waumini, Paulo anasisitiza jambo la muhimu zaidi.

lugha...malaika

Hapa inaweza kumaanisha 1) Paulo atumia lugha ya kukuza jambo ili ujumbe wake ueleweke, lakini hamaanishi kwamba wanadamu wanaweza kuongea lugha ambayo malaika hutumia. au 2) Paulo anafikiri kuwa baadhi ya watu ambao hunena kwa lugha huwa wananena lugha inayotumiwa na malaika.

nimekuwa shaba iliayo au upatu uvumao

nimekuwa kama chombo kinachotoa sauti kubwa, sauti inayokera na kusumbua

upatu uvumao

chombo chenye umbo la sinia, kinachofunikwa kwenye kitu kingine na kupigwa ili kutoa sauti.

ninautoa mwili wangu ili nichomwe moto

kwa kutumia kitenzi tendaji ni sawa na kusema "ninawaruhusu watesi wangu wanichome moto hadi kufa"

1 Corinthians 13:4

Upendo huvumilia na hufadhili....huvumilia mambo yote

Paulo anazungumzia upendo kama kitu chenye nafsi hai.

hauoni uchungu haraka,

Hii inaweze kuelezewa katika muundo tendaji kama " hakuna mtu atakayeufanya upendo upate hasira kwa haraka"

Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli

"hufurahia katika uadilifu na kweli"

1 Corinthians 13:8

Upendo

Kumpenda mtu mwingine ni kumjali na kufanya mambo ambayo yatamletea faida au kumnufaisha. Upendo upo aina mbalimbali 1. Upendo unaotoka kwa Mungu huwa unakusudia kuleta mema kwa wengine, huwa haulengi kujinufaisha kwa mtu mmoja. Mungu mwenyewe ni upendo na chanzo cha upendo.

Nabii, unabii

Nabii ni mtu anayeleta ujumbe kutoka kwa Mungu kwenda kwa watu. Mara nyingi manabii huwaonya watu kutoka katika dhambi ili kumtii Mungu. Unabii ni ujumbe unaotolewa na Nabii

Lugha

Katika Biblia neno Lugha humaanisha, lugha za wanadamu zinazotumiwa na makundi mbalimbali ya watu. Wakati mwingine neno Lugha humaanisha lugha ya kiroho ambayo Roho Mtakatifu huwapa waumini kama moja ya "zawadi au karama za Roho"

kujua, maarifa

kujua ni kuelewa kitu au kufahamu jambo, kutambua. maarifa ni neno linalohusiana na habari ambayo watu wanaifahamu.

Kamili

Katka Biblia neno hili humaanisha kukomaa ua kukua katika maisha ya kiroho. Kufanya kitu kikamilike ni kukifanyia kazi hadi kiwe kizuri bila dosari.

1 Corinthians 13:11

Kwa kuwa sasa tunaona kama kwa kioo

Vioo nyakati alizoishi Paulo vilitengenezwa kwa chuma kilichopakwa rangi hivyo vilionesha taswira yenye giza tofauti na vioo vya glass vya siku hizi

sasa tunaona

Hapa inaweza kumaanisha 1) "sasa tunamwona Kristo" au 2) "sasa tunamwona Mungu"

uso kwa uso

Tutamwona Kristo uso kwa uso. Hapa inamaana kwamba tutakuwa pamoja na Kristo katika hali ya mwili.

nitajua sana

" nitamjua Kristo kwa ukamilifu"

kama na mimi ninavyojulikana sana

katika muundo tendaji inaweza kuelezewa "kama Kristo avyonifahamu kikamilifu"

Lakini sasa mambo haya matatu yanadumu

" Nimuhimu kwamba...sasa"

imani, tumaini lijalo, na upendo

" tunamwamini Kristo, tukijua kwamba atafanya vitu vyote alivyoahidi, tunampenda na tunapendana sisi kwa sisi"

1 Corinthians 14

1 Wakorintho 14 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Katika sura hii, Paulo anaandika tena kuhusu vipaji vya kiroho.

Baadhi ya tafsiri huweka kile kinanukuliwa kutoka kwenye Agano la Kale kwa upande wa kulia zaidi kwenye ukurasa; zaidi ya maandiko yote. ULB inafanya hivyo kwa maneno ya mstari wa 21.

Dhana maalum katika sura hii

Ndimi

Wasomi hawakubaliani juu ya maana halisi ya kipaji cha ndimi. Paulo anaelezea kipaji cha ndimi kama ishara kwa wasioamini. Haitumiki kwa kanisa lote, isipokuwa mtu akielezea kile kinachosemwa. Ni muhimu sana kwamba kanisa linatumia kipaji hiki vizuri.

Unabii

Wasomi hawakubaliani juu ya maana halisi ya unabii kama kipaji cha kiroho. Paulo anasema manabii wanaweza kujenga kanisa lote. Anaelezea unabii kama kipaji kwa waumini. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#prophet)

<< | >>

1 Corinthians 14:1

Sentensi Unganishi

Paulo anataka ifahamike kuwa kufundisha ni muhimu kwa sababu watu wanapata maelekezo kwa njia ya kufundishwa, hivyo kazi ya kufundisha lazima ifanywe kwa upendo.

Utafuteni upendo

" ufuateni upendo" jitahidini kuwapenda watu"

zaidi sana mpate kutoa unabii

" na fanyeni kazi kwa bidii ili muweze kutoa unabii"

kuwajenga

" kuwasaidia watu"

1 Corinthians 14:5

Yeye atoaye unabii ni mkuu

Paulo anasisitiza kuwa karama ya kutoa unabii ni kuu zaidi kuliko karama ya kunena kwa lugha. kwa maneno mengine "Anayetoa unabii karama yake ni kuu zaidi"

tafasiri

Hii inamaanisha kufafanua kile anachosema mtu kwa lugha isiyofahamika kwa wengine. au kueleza maana za maneno kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine

nitawafaidia nini ninyi

kwa maneno mengine "Sitawasaidia" au " nitakuwa sijafanya jambo lolote la kuwasaidia"

1 Corinthians 14:7

visipotoa sauti zilizo na tofauti

Hii inareje sauti tofauti tofauti zinazotokana na midundo inayotoa tuni, haimaani tofauti kati ya sauti ya filimbi na kinubi tu.

itatambulikanaje ni chombo gani kinachezwa

Kwa maneno mengine " hakuna mtu atakaye tambua tuni ya filimbi au kinubi kinapogigwa"

1 Corinthians 14:10

hakuna hata moja isiyo na maana

" Zote zina maana"

1 Corinthians 14:12

uthihirisho wa Roho

" muweze kufanya matendo yanadhihilisha kuwa Roho anawaongoza na kuwatawala"

takeni kwamba mzidi sana kulijenga kanisa

" muwe na mafanikio makubwa katika kuwawezesha watu wa Mungu kumtumikia Yeye zaidi"

kutafasiri

Hii inamaanisha kufafanua kile anachosema mtu kwa lugha isiyofahamika kwa wengine. au kueleza maana za maneno kutoka lugha moja mpaka lugha nyingine. Anagalia 2:12 kwa maelezo zaidi kuhusu "tafasiri"

akili zangu hazina matunda

"Siyafamu maneno ninayoyasema"

1 Corinthians 14:15

Nifanye nini?

Paulo anatoa utangulizi wa maamuzi yake. kwa maneno mengine anasema "hivi ndivyo nitakavyofanya"

Nitaomba kwa roho yangu...nitaomba kwa akili zangu. Nitaimba kwa roho yangu...nitaimba kwa akili zangu

Maombi na nyimbo lazima ziwe katika lugha inayoeleweka kwa watu waliopo

kwa akili zangu

" kwa maneno yanayoeleweka kwangu"

ukimsifu Mungu... utoapo shukurani.. usemayo

Paulo anatumia neno "wewe" kutoa ujumbe kwa kila mtu anayeomba katika roho lakini si katika akili yake.

mgeni ataitikaje "Amina"

kwa maneno mengine " Mgeni hataweza kusema Amina"

ataitikaje "Amina"

" kukubali"

1 Corinthians 14:17

wewe washukuru

Paulo anatumia neno "wewe" kuzungumza na Wakorintho wote.

hajengwi

Paulo anasema swala la kuwasaidia watu ni kama kujenga nyumba. lakini bado " mwingine hasaidiki"

maneno kumi elfu

Inamaanisha "maneno elfu kumi au maneno mengi zaidi ya hayo".

1 Corinthians 14:20

Maelezo ya Jumla

Paulo anawaambia kuwa kunena katika lugha mbalimbali kulitabiliwa tangu zamani na nabii Isaya, hii ilikuwa miaka mingi kabla ya tukio la kunena kwa lugha lilotukia siku ya kuanza kwa kanisa la Kristo.

watoto

" watu wanaoweza kudanganywa kwa urahisi"

Imeandikwa katika sheria

Kwa maneno mengine ni kusema "Nabii aliandika maneno haya katika sheria (Agano la Kale)"

Kwa watu wa lugha nyingine na kwa midomo ya wageni

Vifungu hivi viwili vinamaana moja tu, ili kuweka mkazo.

1 Corinthians 14:22

Sentensi Unganishi

Paulo anatoa maelekezo mahususi kuhusu utaratibu wa kutumia karama katika kanisani.

sio kwa walioamini, bali kwa wasioamini.

Kwa maelezo chanya ni sawa na kusema "kwa waaminio tu"

1 Corinthians 14:24

atashawishiwa na yote asikiayo. Atahukumiwa na yote yasemwayo

Paulo anasema jambo moja mara mbili ili kuweka mkazo. kwa maneno mengine anasema atatambua kuwa anahatia ya dhambi kwa kuwa amesikia mnachosema"

Siri za moyo wake zingefunuliwa

kwa muundo tendaji ni kusema "Mungu angemfunulia siri za moyo wake"

1 Corinthians 14:26

Nini kifuatacho basi,

"kwa sababu kila kitu nilichowaambia ni cha kweli, na hicho ndicho mnapaswa kukifanya"

atafasiri kilichosemwa

katika muundo tendaji ni kusema "tafasirini walichokisema"

kutafasiri...tafasiri

Hii inamaanisha kufafanua kile anachosema mtu kwa lugha isiyofahamika kwa wengine. Anagalia 2:12 kwa maelezo zaidi kuhusu "tafasiri"

1 Corinthians 14:29

manabii wawili au watatu wanene,

inaweza kumaanisha: 1) Manabii wawili au watatu tu wahutubie katika kusanyiko moja au 2)Manabii wawili au watatu tu wapokezane katika kunena kwa wakati mmoja.

kilichosemwa

katika muundo tendaji ni " kile wanachonena"

akifunuliwa jambo

katika muundo tendaji unaweza kusema " Kama Mungu akimpa ufunuo mtu mmoja"

1 Corinthians 14:31

anaweza kutoa unabii mmoja baada ya mwingine

Mtu mmoja tu anaweza kutoa unabii kwa wasaa (watu wawili wasitoe unabii kwa wakati ule ule)

wote waweze kutiwa moyo

kwa muundo tendaji ni kusema "Farijianeni wote kwa pamoja"

Mungu si Mungu wa machafuko,

Mungu huwa haleti machafuko kwa kuwafanya watu wanene(waongee) wote kwa wakati ulele.

1 Corinthians 14:34

wakae kimya

hapa inaweza kumaanisha 1) achani kunena 2) acheni kunena wakati mtu anapotoa unabii au 3) kaeni kimya kabisa wakati wa ibada kanisani

Je neno la Mungu lilitoka kwenu? Je limewafikia ninyi tu?

Paulo anasisitiza kwamba mapenzi ya Mungu kwa Wakristo hakifahamiki kwa waumini wa Korintho peke yake. Kwa maneno mengine ni kusema " Neno la Mungu halikutoka kwenu hapo Korintho; ninyi siyo watu pekee munaofahamu mapenzi ya Mungu.

1 Corinthians 14:37

inampasa ayatambue

Nabii wa kweli au mtu wa kiroho atayakubali maandiko ya Paulo kuwa yanatoka kwa Bwana

mwacheni asitambuliwe

Hapa inaweza kueleza kwa muundo tendaji kuwa "msimtambue mtu huyo"

1 Corinthians 14:39

msimkateze mtu yeyote kunena kwa lugha

Paulo anaweka wazi kuwa kuongea kwa lugha kanisani inawezekana na inakubalika

Lakini mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu

Paulo anasisistiza kwamba makusanyiko ya kanisa( waumini) lazima yafanyike katika utaratibu mzuri. kwa maneno mengine " lakini fanyeni mambo yote kwa uzuri na katika utaratibu" au " lakini fanyeni kila kitu kwa utaratibu mzuri, kwa njia inayofaa"

1 Corinthians 15

1 Wakorintho 15 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Ufufuo

Sura hii inajumuisha mafundisho muhimu kuhusu ufufuo wa Yesu. Watu wa Kigiriki hawakuamini kwamba mtu anaweza kuishi baada ya kufa. Paulo anatetea ufufuo wa Yesu. Anafundisha kwa nini ni muhimu kwa waumini wote. (See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#resurrection and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#believe)

Dhana maalum katika sura hii

Ufufuo

Paulo anaonyesha ufufuo kama ushahidi wa mwisho kwamba Yesu ni Mungu. Kristo ni wa kwanza kati ya wengi ambao Mungu atawafufua. Ufufuo ni muhimu kwa Injili. Mafundisho machache tu ni ya muhimu kama haya.(See: https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/kt.html#goodnews and https://read.bibletranslationtools.org/u/WA-Catalog/*_tw/other.html#raise)

Mifano muhimu za matamshi katika sura hii

Paulo anatumia mifano nyingi za matamshi katika sura hii. Anazitumia kueleza mafundisho magumu ya kitheolojia kwa namna ambayo watu wanaweza kuelewa.

<< | >>

1 Corinthians 15:1

Sentensi Unganishi

Paulo anawakumbusha kuwa ni Injili inayowaokoa na tena anawaeleza Injili ni kitu gani. Kisha anatoa somo fupi la historia kuelezea yatakayotokea hapo baadaye.

Ninawakumbusha

"kuwasaidia ninyi kukumbuka"

kusimama kwayo

Paulo anazungumzia habari ya Wakorintho akiwafananisha na nyumba, na Injili anaifananisha na msingi unaobeba hiyo nyumba

mmeokolewa

Hii inaweza kuelezewa katika muundo tendaji "Mungu atawaokoa"

1 Corinthians 15:3

kwa umuhimu

inaweza kumaanisha 1) muhimu zaidi katika mambo mengi au 2) jambo la kwanza kutokea

kwa ajili ya dhambi zetu

" kulipa kwa ajili ya dhmbi zetu" au " ili Mungu atusamehe dhambi zetu"

kutokana na maandiko

Paulo ana rejea maandiko ya Agano la Kale.

alizikwa

Katika hali tendaji unaweza kusema "Walimzika"

alifufuka

Katika hali tendaji unaweza kusema " Mungu alimfufua" au "alifufuka"

1 Corinthians 15:5

Sentensi unganishi

ukitaka mstari wa (5) uwe sentensi kamili, weka koma kwenye mstari 3 sura ya (15) 15:3, mstari huu wa 5 uweke mbele yake ili kuleta sentensi kamili.

aliwatokea

"alijionyesha mwenyewe kwao"

Mia tano

inamaanisha 500

1 Corinthians 15:8

Mwisho wa yote

"Hatimaye, baada ya kuwa ameonekana kwa wengine"

mtoto aliye zaliwa katika wakati usio sahihi

Paulo anatumia lugha ya nahau na pengine anamaanisha kuwa alimwamini Yesu baadaye sana ukilinganisha na mitume wengine. au anamaanisha kuwa, tofauti na mitume wengine hakushuhudia huduma ya Yesu ya miaka mitatu. kwa maneno mengine "mtu alisiyekuwa na uzoefu walioupata wengine."

1 Corinthians 15:10

kwa neema ya Mungu niko vile nilivyo

neema ya Mungu au wema wa Mungu umemfanya Paulo kuwa kama alivyo.

neema yake kwangu haikuwa bure

Paulo anasisistiza kwa maneno mazuri kwamba Mungu alifanya kazi kupitia kwa Paulo. Kwa maneno mengine ni kwamba " kwa sababu alikuwa mwema kwangu, niliweza kufanya kazi nzuri zaidi"

neema ya Mungu iliyo ndani yangu

Paulo anazungumza juu ya kazi aliyoweza kufanya kwa kuwa Mungu alikuwa mwema kwake, Paulo anasema ilikuwa ni neema iliyokuwa ikifanya kazi ndani yake. Hii inaweza kumaanisha: 1) huu ni ukweli halisi,kuwa Mungu alifanya kazi na kwa wema wake alimtumia Paulo kama chombo au 2) Paulo anatumia sitiari na anasema kuwa Mungu alikuwa mwema kumwezesha Paulo kufanya kazi na kuwezesha kazi za Paulo zifanikiwe vizuri.

1 Corinthians 15:12

iweje baadhi yenu mseme hakuna ufufuo wa wafu?

Paulo anatumia swali hili kuanza mada mpya. Kwa maneno mengine anasema "Hampaswi kuwa mnasema hakuna ufufuo wa wafu"

kama hakuna ufufuo wa wafu, hivyo hata Kristo hajafufuliwa.

Kusema kwamba hakuna ufufuo wa wafu, ni kusema kwamba Kristo hakufufuka kutoka kwa wafu.

1 Corinthians 15:15

Sentensi Unganishi

Paulo anataka kuwathibitishia kuwa Kristo alifufuka kutoka kwa wafu.

Na tumepatikana kuwa mashahidi wa uongo kumuhusu Mungu

Paulo anahoji kwamba kama Kristo hakufufuka kutoka kwa wafu, hivyo wanatoa ushahidi wa uongo kuhusu Kristo kwamba amefufuliwa kutoka kwa wafu.

tumepatikana

"kila mtu anaweza kuona jinsi tulivyo"

imani yenu ni bure na bado mko kwenye dhambi dhambi.

imani yao ni kuwa Kristo alifufuka kutoka kwa wafu, na kama hicho hakikutokea, imani yao haina maana, haiwasaidii chochote.

1 Corinthians 15:18

watu wote

"kila mtu , wote kwa pamoja wanaoamini na wasioamini"

sisi ni wa kuhurumiwa zaidi

"watu lazima watuhurumie zaidi ya ilivyo kwa mwingine yeyote"

1 Corinthians 15:20

sasa Kristo

" hivi ndivyo ilivyo, "Kristo" au " huu ndio ukweli: Kristo"

Kristo amefufuka

katika hali tendaji ni kusema: "Mungu amemfufua Kristo"

1 Corinthians 15:22

Adamu

Adamu alikuwa mtu wa kwanza ambaye aliumbwa na Mungu. Adamu na mke wake Eva waliumbwa katika sura ya Mungu. Mungu alimuumba Adamu kutoka katika mavumbi na kumpulizia pumzi ya uhai.

Kifo, kufa

Maneno haya yametumika kumaanisha kifo cha kimwili na kifo cha kiroho. Kifo cha kimwili inamaanisha mwili wa mtu unapokoma kuwa na uhai. Kifo cha Kiroho, inamaanisha watenda dhambi wanapokuwa wametengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zao.

Kristo

Neno Kristo au Masihi linamaanisha " aliyetiwa mafuta" na neno hili linamhusu Yesu, Mwana wa Mungu.

Hai

Neno hili linamaanisha kuwa na uzima, iliyohai. Wakati mwingine linatumiwa kwa lugha ya picha kuelezea uzima wa kiroho.

matunda ya kwanza

Neno"matunda ya kwanza" linamaana ya sehemu ya mazao,matunda au mboga zilizokuwa za kwanza kuvumwa wakati wa majira ya mavuno. Waisraeli walitoa matunda haya kama sadaka kwa Mungu.

1 Corinthians 15:24

Maelezo ya Jumla

Hapa neno " ata-kapo" ni rejea kwa Kristo.

atakapo komesha utawala wote na mamlaka yote na nguvu

" atawakomesha watu ambao wanatawala, wenye mamlaka, na wenye nguvu ya kufanya yote wanayofanya"

mpaka atakapoweka maadui zake wote chini ya miguu yake

Wafalme walioshinda vita waliweza kuweka miguu yao juu ya shingo za adui zao waliowashinda. Kwa maneno mengine hapa inasema "mpaka Mungu atakapo waharibu kabisa maadui wa Kristo."

Adui wa mwisho kuharibiwa ni kifo

Paulo anaeleza juu ya kifo kana kwamba anaeleza habari za mtu ambaye Mungu atamuua. Kwa maneno mengine ni kusema "Adui wa mwisho ambaye ataharibiwa na Mungu ni kifo chenyewe"

1 Corinthians 15:27

ameweka kila kitu chini ya miguu yake

Wafalme walioshinda vita waliweza kuweka miguu yao juu ya shingo za adui zao waliowashinda. Kwa maneno mengine hapa inasema " Mungu amewaharibu kabisa maadui wote wa Kristo"

vitu vyote vimewekwa chini yake

Maneno haya yakisemwa kwa kauli tendaji ni kwamba " Mungu amavitiisha vitu vyote chini ya Kristo"

mwana mwenyewe atawekwa chini

Maneno haya yakisemwa kwa kauli tendaji ni kwamba " mwana mwenyewe atatiishwa"

mwana mwenyewe

Katika mistari ya awali neno " mwana" linamaanisha " Kristo" : kwa maneno mengine ni kusema " Kristo ambaye ni Mwana wa Mungu"

Mwana...Baba

Hivi ni vyeo muhimu vinavyofafanua uhusiano kati ya Yesu na Mungu.

1 Corinthians 15:29

Au sivyo watafanya nini wale waliobatizwa kwa ajili wafu?

Kwa ufafanuzi Paulo anasema "vinginevyo ingekuwa haina maana kwa Wakristo kubatizwa kwa niaba ya wafu."

kwa nini tena wanabatizwa kwa ajili yao?

Paulo anataka jambo hili lifahamike kwa Wokorintho hata kabla hajalisema kwao ya kwamba " hakuna sababu yoyote kupokea au kubatizwa kwa niaba ya watu walikwisha fariki"

Na kwa nini tuko katika hatari kila saa?

Kwa maneno mengine ni kusema " hatupati faida yoyote kwa kujiweka katika hatari muda wote"

1 Corinthians 15:31

Nakufa kila siku. Hili nalisema kwa kujisifu kwa ajili yenu

" ninajisifu kwa ajili yenu, hivyo kila mmoja anajua kwamba nasema ninaposema ninakufa kila siku"

Ninakufa kila siku.

Paulo anacho maanisha hapa ni (1)kila siku najipambanua kwa kifo cha Kristo kwa kufisha tamaa mbaya ndani yake 2) kila siku aliishi akijua kuwa kuna watu walikuwa wakitafuta kumuua.

Inanifaidia nini..nilipigana na wanyama wakali huko Efeso... hawafufuliwi?

Paulo anataka Wakorintho wafahamu jambo hilo hata bila kuwaambia. kwa maneno mengine anasema " sikupata chochote...kwa kupigana na wanyama huko Efeso... hawafufuliwi"

kama nilipigana na wanyama katika Efeso

Kuna uwezekano maana ni 1) Paulo alikuwa anaongea kwa mfano kuhusu hoja yake na wapagani waliosoma au mafarakano mbalimbali na watu waliotaka kumuua au 2) Anathibitisha kwamba aliwahi kuwekwa kwenye uwanja kupambana dhidi ya wanyama hatari.

Na tule na kunywa, kwa kuwa kesho tunakufa.

Paulo anahitimisha kwamba kama hakuna maisha mengine baada ya kifo, ni bora kwetu kuyafurahia maisha haya kwa kadri tuwezavyo, kwa kuwa kesho maisha yetu yataisha bila matumaini yoyote

1 Corinthians 15:33

Makundi mabaya huharibu tabia njema

Kama ukiishi na watu wabaya, utatenda kama wao. Hapa Paulo ananukuu msemo unaojulikana

Muwe na kiasi

"Mnapaswa kutafakari kwa undani kuhusu hili"

1 Corinthians 15:35

Sentensi unganishi

Paulo anatoa maelezo mahususi juu ya ufufuo wa miili ya waumini utakavyotokea. Anaeleza juu ya miili ya asili na miili ya kiroho kwa kulinganisha Adamu wa kwanza na Aadamu wa mwisho ambaye ni Kristo.

Lakini mtu mwingine atasema, "Jinsi gani wafu wanafufuliwa? Nao watakuja na aina gani ya mwili?"

Hapa inaweza kumaanisha 1)mtu alikuwa akijiho kwa nia njema au) 2) mtu anauliza swali ili kukejeli swala la ufufuo. kwa maneno mengine ni kusema "Baadhi ya watu watasema kwamba hawapati picha jinsi Mungu atakavyo wafufua wafu, na aina gani ya mwili Mungu atawapa katika ufufuo."

mtu mwingine atasema

"mtu atauliza"

Nao watakuja na aina gani ya mwili

hii ni sawa na kuuliza kwamba, je utakuwa mwili halisi au mwili wa kiroho? je mwili huo utakuwa na umbo gani? je mwili huo utatengenezwa kwa vitu gani?

Wewe ni mjinga sana! Kile ulichopanda

Paulo anaonekana kama vile anazungumza na mtu mmoja "Wewe" ni neno kuonyesha umoja.

Wewe ni mjinga

" hujui kabisa kuhusu mambo haya yote"

Kile ulichopanda hakiwezi kuanza kukua isipokuwa kimekufa.

Kama vile mbegu isivyo weza kuota mpaka ifukiwe ardhini. Vile vile mtu lazima afe kwanza kabla ya kufufuliwa na Mungu

1 Corinthians 15:37

kile ulichopanda sio mwili utakaokuwa

Fumbo la mbegu limetumika tena, kumaanisha kwamba mwili wa mkristo uliokufa utafufuliwa na hautaonekana kama ulivyokuwa.

unachopanda

Paulo anaongea na Wakorintho kana kwamba ni mtu mmoja " unachopanda"

Mungu ataipa mwili kama apendavyo

"Mungu ataamua ni mwili wa aina gani"

mwili

Katika mazingira ya wanyama, "mwili" unaweza kutafasiliwa kama "mwili," "ngozi," au "nyama."

1 Corinthians 15:40

miili ya mbinguni

Kunauwezekano maana ni 1) jua, mwezi, nyota, na mianga mingine ionekanayo katika wingu au 2) viumbe vya mbinguni, kama vile malaika na visivyo vya kawaida.

miili ya duniani

Hii ina rejea kwa wanadamu.

utukufu wa miili ya mbinguni ni wa aina moja na na utukufu wa ulimwenguni ni mwingine.

"utukufu uliopo katika miili ya mbinguni ni tofauti na utukufu uliopo katika miili ya asili ya wanadamu "

utukufu

Hapa "utukufu" unafananishwa na mfano wa mwangaza wa vitu vya angani katika jicho la mwanadamu.

1 Corinthians 15:42

Kinacho pandwa..., na kinacho ota...

Mwandishi anafananisha watu wanaozika maiti kwenye kaburi na watu wanaopanda mbengu itakayo zaa matunda. kwa kitenzi tendaji ni sawa na kusema " Ni kipi kinazikwa kaburini... nikipi kinachotoka kaburini " au watu huzika kitu gani...na Mungu hufufua kitu gani"

kinaharibika... hakiharibiki.

Kina oza... kisichoweza kuoza

1 Corinthians 15:45

Lakini wa kiroho hakuja kwanza bali wa asili, na kisha wa kiroho.

" mtu wa asili alikuja kwanza. mtu wa kiroho alikuja baadaye na anatoka kwa Mungu"

asili

aliumbwa kwa namna ya kidunia, na bado hajawa katika mahusiano na Mungu.

1 Corinthians 15:47

Mwanadamu wa kwanza ni wa dunia, alitengenezwa kwa mavumbi

hapa inaelezea kuwa Mungu alimuumba mtu wa kwanza (Adamu) kutoka katika mavumbi ya ardhi

vumbi

" uchafu"

mtu wa mbinguni

Yesu Kristo

wale ambao ni wa mbinguni

"wale wanaomwamini Kristo"

tumebeba

"kubali kuchukua na kuakisi"

1 Corinthians 15:50

Sentensi unganishi

Paulo anataka wajue kuwa baadhi ya waumini hawatakufa kimwili bali watapata mwili wa ufufuo kupitia ushindi wa Kristo

kwamba mwili na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu

maana zinazokubalika ni: 1) sentensi zote mbili zinamaanisha jambo moja. " Mwanadamu ambao watakufa kabisa hawawezi kuurithi ufalme wa Mungu unaodumu daima" au 2) sentensi ya pili inakamilisha lile wazo linalotangulia hapo mwanzo, kuwa " wanadamu waliodhaifu hawawezi kuurithi ufalme wa Mungu. Wala ambao watakufa hawataweza kuurithi ufalme wa Mungu ambao utadumu milele"

mwili na damu

Ni wale wanafuata tabia za mwili uliohukumiwa kufa.

kurithi tutabadilishwa wote

Ni hali ya kupokea mambo ambayo Mungu ameahidi kwa waumini na Paulo anazungumzia jambo hili kama vile mtu anavyopata urithi wa mali na utajiri kutoka kwa mwanafamilia : "Mungu atatubasilisha sisi sote"

wakuharibika...wakutoharibika

"unaoweza kuoza....usioweza kuoza wala kuharibika"

wote tutabadilishwa

Hii inaonyesha hali tendaji kuwa " Mungu atatubadilisha sisi sote"

1 Corinthians 15:52

Tutabadilishwa

"Mungu atatubadilisha"

katika kufumba na kufumbua kwa jicho

Itatokea kwa haraka kama vile mtu anavyo kufunga na kufungua jicho lake.

katika tarumbeta ya mwisho

"tarumbeta ya mwisho itakapolia"

hali ya kutoharibika

"umbo ambalo halitaharibika ... mwili huu unaweza kuharibika(kuoza).Kupingwa kwa mbiu kunatanguliza matukio makubwa. Katika swala hili, Paulo ana rejea kwenye tukio kubwa la mwisho katika historia ya dunia hii.

huyu binadamu lazima awekwe kwenye milele

Paulo anazungumzia juu ya Mungu kuibadilisha miili yetu ili isife tena ni kana kwamba Mungu anaweka mavazi mapya kwetu.

1 Corinthians 15:54

huu mwili wa kuhalibika...na usioharibika

"mwili huu unaweza kuoza... usioweza kuoza" angalia tafasiri inayofanana na hii katika 15:42

Kifo, ushindi wako uko wapi? Kifo, uko wapi uchungu wako?"

Paulo anasema haya kufanya dhihaka dhidi ya nguvu ya kifo ambayo tayari Kristo amekwisha kuishinda. kwa maneno mengine ni kwamba: " Kifo hakina ushindi. Kifo hakina makali."

1 Corinthians 15:56

Uchungu wa kifo ni dhambi

Ni kwasababu ya dhambi tutakabiliwa na kifo, hivyo tunakufa.

nguvu ya dhambi ni sheria

Sheria ya Mungu iliyopitishwa na Musa inafafanua juu ya dhambi na inatuonyesha jinsi tunavyotenda dhambi dhidi ya Mungu.

atupaye sisi ushindi

" amekwisha kushinda kifo kwa niaba yetu"

1 Corinthians 15:58

Sentensi unganishi

Paulo anataka waumini wakati wanamtumikia Bwana wakumbuke juu ya kugeuzwa na kupata miili ya ufufuo ambayo Mungu atawapatia.

iweni imara na msitikisike.

Paulo anaelezea juu mtu mwenye nguvu za kimwili asiyekubali kushindwa katika kutimiza uamuzi wake. kwa maneno mengine inamaanisha " kufanya uamuzi thabiti"

Daima itendeni kazi ya Bwana

Paulo anaongelea jitihada alizifanya katika kumtumikia Bwana kama vile vitu vya thamani ambavyo kila mtu anapaswa kuvipata. kwa maneno mengine anasema " siku zote mtumikieni Bwana kwa uaminifu"

1 Corinthians 16

1 Wakorintho 16 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Paulo anaeleza kwa kifupi mada nyingi katika sura hii. Ilikuwa ni kawaida katika inchi za kale za Mashariki ya Karibu kwa sehemu ya mwisho ya barua kuwa na salamu za kibinafsi.

Dhana maalum katika sura hii

Maandalizi ya kuja kwake

Paulo alitoa maelekezo ili kusaidia kanisa la Korintho kujitayarisha kwa Paulo kuwatembelea. Aliwaambia waanze kukusanya fedha kila Jumapili kwa ajili ya waumini huko Yerusalemu. Alikuwa na matumaini ya kuja na kukaa pamoja nao wakati wa msimu wa baridi. Aliwaambia wamsaidie Timotheo atakapofika. Alikuwa na matumaini kuwa Apollo angewatembelea, lakini Apolo hadhani kwamba ilikuwa wakati mzuri. Paulo pia aliwaambia wamtii Stephanus. Kwa mwisho, alituma salamu kwa kila mtu.

__<< | __

1 Corinthians 16:1

Sentensi unganishi

Paulo anawakumbusha waumini wa Korintho kukusanya pesa kwa ajili ya waumini wenye mahitaji walioko Yerusalemu. Pia anawajulisha kuwa Timotheo atapitia kwao kabla ya kwenda kwa Paulo.

ya waumini

Paulo alikuwa anakusanya pesa kutoka kwenye makanisa yake kwa ajili ya wakristo masikini wa kiyahudi huko Yerusalemu na Yuda.

kama nilivyo elekeza

"kama nilivyowapa maelekezo mahususi"

aweke kitu fulani kando na kukihifadhi,

Maana zinazowezekana ni: 1) " kitu hicho tunza nyumbani" au 2) "kilete kitunzwe kanisa"

ili kwamba kusiwe na makusanyo wakati nitakapokuja

" kwa hiyo nitakapokuja hakutakuwa na haja ya kukusanya pesa zingine zaidi"

1 Corinthians 16:3

yeyote mtakayemchagua

Paulo anawajulisha kanisa kwamba wanaweza kuteua baadhi ya watu miongoni mwao ili kupeleka sadaka zao Yerusalemu. "yeyote mtakaye mchagua" au " watu mtakaowateua"

nitamtuma pamoja na barua

Maana inayowezekana ni: 1) "Nitatuma na barua ambayo nitaiandika" au 2) "Nitatuma na barua ambayo mtaiandika."

1 Corinthians 16:5

mnaweza kunisaidia katika safari yangu

Hii inamaanisha kwamba wangeweza kutoa fedha au vitu mbalimbali anavyohitaji alivyohitaji Paulo na watumishi wenzake ili waweze kuendelea na safari yao.

1 Corinthians 16:7

kuwa sitarajii kuwaona sasa

Paulo anaeleza kwamba hataki kuwa na ziara ya ya muda mfupi, lakini anapenda kufanya ziara yamuda mrefu hapo baadaye.

Pentekoste

Paulo alitarajia kubakia Efeso hadi sikukuu, iliyoanza mwezi Mei au Juni, siku hamsini baada ya pasaka. Baada ya hapo angesafiri kupitia Makedonia, na kufika Korintho kabla ya majira ya baridi yalioanza mwezi wa Novemba

mlango mpana umefunguliwa

Hii inamaanisha kwamba Mungu amempa nafasi nzuri ya kuwafikia watu kwa injli.

1 Corinthians 16:10

muoneni kwamba yuko na ninyi pasipo kuogopa

" kusiwe na sababu ya kumfanya aogope anapokuwa miongoni mwenu"

Mtu yeyote asimdharau

Timotheo alikuwa kijana sana kuliko Paulo hivyo wakati mwingine hakupewa heshima aliyostahili kama mtumishi wa Injili

ndugu yetu Apolo

Neno "yetu" nilinamhusu Paulo na watu aliowaandikia

1 Corinthians 16:13

Muwe macho, simameni imara, mtende kama wanaume, muwe na nguvu

Paulo anawasisitiza Wakorintho kwa kuwapa maelekezo kana kwamba anatoa amri nne kwa askari wa vita. Hizi amri nne zinamaanisha jambo lilelile.

Muwe macho

Paulo anawaambia watu watambue mambo yanayotokea kama vile walinzi wavyokaa macho wanapolinda mji au Shamba. kwa maneno mengine anasema "muwe makini sana kuhusu kwa yeyote mnayemwamini" au " jilindeni na hatari yoyote"

simameni imara

Paulo anawahimiza waendelee kuamini katika Kristo kulingana na mafundisho yake, wawe kama askari wasiokubali kurudi nyuma wanaposhambuliwa na adui. hii inamaana: 1) " endeleeni kuamini kile tulichowafundisha" au 2) " endeleeni kumwamini Kristo kwa udhabiti wote"

mtende kama wanaume

katika nyakati alizoishi Paulo na watu aliowaandikia barua yake, ilikuwa kawaida kwa wanaume kufanya kazi ngumu kwa ajili ya mahitaji ya familia na kupigana dhidi ya maadui. kwa uwazi zaidi inamaanisha " timizeni wajibu wenu"

yote myafanyayo yafanyike katika upendo

"lazima kila jambo mnalolifanya lioneshe kuwa mnaupendo kwa watu"

1 Corinthians 16:15

Sentensi unganishi

Paulo anaanza kutuma salamu zake anapoelekea kuhitimisha barua yake, anatoa salamu za makanisa mengine, Prisca, Akila na yeye mwenyewe.

kaya ya Sefana

Stefana alikuwa muumini wa kwanza katika kanisa la Koritho.

Akaya

Akaya ni jina la jimbo la Ugiriki

1 Corinthians 16:17

Stefana, Fotunato, na Akiko

Hawa watu pengine walikuwa baadhi ya waumini wa kwanza wa Korintho au wazee wa kanisa ambao waliokuwa watendakazi pamoja na Paulo.

Stefana, Fotunato, na Akiko

Haya ni majina ya watu

Wamesimama mahali ambapo ninyi mgepaswa kuwa

" walisababisha mafanikio yawepo japo ninyi hamkuwepo"Paulo alitiwa moyo kwa ujio wao.

Kwa kuwa wameifurahisha roho yangu

"Paulo alitiwa moyo walipokuja kumtembelea"

1 Corinthians 16:19

Kanisa

katika agano jipya neno " kanisa" lina maana ya kundi la watu wanaomwamini Yesu ambao walikutana pamoja kuomba na kusikia mahubiri ya neno la Mungu. Mara nyingi Neno "kanisa" linamaanisha wakristo wote.

Asia

Nyakati za Biblia, "Asia" ilikuwa ni jina mkoa au jimbo katika dola la Warumi. Hii sehemu ilikuwa upande wa magharibi na kwa sasa inajulikana kama nchi ya Utiruki. Miji kama Efeso, na Kolose ilikuwa katika eneo hili la Asia ambapo Paulo alisafiri na kuhubiri injili.

Akila

Akila alikuwa mkristo wa Kiyahudi kutoka katika jimbo la Ponto, mkoa wa kusini mwa pwani ya bahari nyeusi().

Priska

Priska alikuwa mke wa Akila yeye na mume wake walikuwa wakristo waliofanya kazi ya umisheni pamoja na mtume Paulo.

Bwana

Neno" Bwana" linamaana y mtu mwenye kumikili au mamlaka juu ya watu. Neno hili linapoandikwa kwa herufi kubwa humaanisha Mungu.

takatifu

Neno "takatifu" huzungumzia tabia ya Mungu ambayo ni kamilifu na imejitenga mbali na dhambi. ni Mungu pekee ambaye ni mtakatifu, huwa anawafanya watu na vitu kuwa watakatifu

busu

Busu ni tendo la mtu kuweka mdomo wake kwenye mdomo wa mtu mwingine. Katika Biblia neno hili busu wakati mwingine limetumika kumaanisha kuagana au kuwambia mtu kwahari.

1 Corinthians 16:21

Mimi, Paulo, naandika hivi kwa mkono wangu

Paulo alikuwa anaweka wazi kuwa maelekezo katika ile ya barua alitoka kwake, ingawa Paulo alikuwa akisema na matendakazi mwenza aliandika yale maneno yake. Sehemu ya mwisho wa barua Paulo akaiandika kwa mko wake mwenyewe.

laana iwe juu yake.

"Mungu anaweza kumlaani" angalia tafasiri ya neno laana katika 12:1